461
FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA! Nyaraka na Kumbukumbu za Mwanafunzi Apendwaye: Injili ya Yohana, 1, 2 na 3 Yohana NA BOB UTLEY, PROFESA MSTAAFU WA KANUNI ZA UFASIRI (UTAFASILI WA BIBLIA) MWONGOZO WA USOMAJI WA FASIRI MFUATANO AGANO JIPYA, VOL.04 BIBLE LESSONS INTERNATIONAL, MARSHAL, TEXAS 2013

FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

  • Upload
    others

  • View
    46

  • Download
    3

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA

UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA!

Nyaraka na Kumbukumbu za Mwanafunzi Apendwaye:

Injili ya Yohana, 1, 2 na 3 Yohana

NA BOB UTLEY,

PROFESA MSTAAFU WA KANUNI ZA UFASIRI (UTAFASILI WA BIBLIA)

MWONGOZO WA USOMAJI WA FASIRI MFUATANO AGANO JIPYA, VOL.04

BIBLE LESSONS INTERNATIONAL, MARSHAL, TEXAS 2013

Page 2: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

ORODHA YA YALIYOMO Neno Toka kwa Mwandishi:Ni kwa namna gani fasiri hii inaweza kukusaidia! ............................................................ ii

Mwongozo Mzuri wa Usomaji wa Biblia: Utafiti Binafsi kwa Ukweli Uliothibitika ...................................................... iii

Fasiri

Utangulizi wa Yohana ................................................................................................................................................... 1

Yohana 1 ....................................................................................................................................................................... 7

Yohana 2 ..................................................................................................................................................................... 41

Yohana 3 ..................................................................................................................................................................... 55

Yohana 4 ..................................................................................................................................................................... 74

Yohana 5 ..................................................................................................................................................................... 93

Yohana 6 ................................................................................................................................................................... 109

Yohana 7 ................................................................................................................................................................... 133

Yohana 8 ................................................................................................................................................................... 147

Yohana 9 ................................................................................................................................................................... 162

Yohana 10 ................................................................................................................................................................. 171

Yohana 11 ................................................................................................................................................................. 181

Yohana 12 ................................................................................................................................................................. 196

Yohana 13 ................................................................................................................................................................. 213

Yohana 14 ................................................................................................................................................................. 224

Yohana 15 ................................................................................................................................................................. 243

Yohana 16 ................................................................................................................................................................. 253

Yohana 17 ................................................................................................................................................................. 264

Yohana 18 ................................................................................................................................................................. 278

Yohana 19 ................................................................................................................................................................. 292

Yohana 20 ................................................................................................................................................................. 305

Page 3: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

Yohana 21 ................................................................................................................................................................. 316

Utangulizi wa 1 Yohana ............................................................................................................................................. 323

1 Yohana 1 ................................................................................................................................................................ 328

1 Yohana 2 ................................................................................................................................................................ 339

1 Yohana 3 ................................................................................................................................................................ 357

1 Yohana 4 ................................................................................................................................................................ 378

1 Yohana 5 ................................................................................................................................................................ 390

2 Yohana .................................................................................................................................................................. 405

3 Yohana .................................................................................................................................................................. 413

Viambatisho

Maelezo mafupi ya Istilahi za Visarufi vya Kiyunani ................................................................................................. 422

Uhakiki wa Tofauti za Kiuandishi .............................................................................................................................. 431

Ufafanuzi/Faharasa ................................................................................................................................................... 435

Kauli ya Mafundisho ................................................................................................................................................. 444

Page 4: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

MADA MAALUM: ORODHA YA YALIYOMO

Archē ........................................................................................................................................................................... 10

Malaika wa Bwana, ..................................................................................................................................................... 11

Kusadiki, Kuamini, Imani, 1:7 ...................................................................................................................................... 13

Mashuhuda wa Yesu, 1:8 ............................................................................................................................................ 14

Kujua, 1:10 .................................................................................................................................................................. 15

Mwili, 1:14 .................................................................................................................................................................. 17

Utukufu (doxa), 1:14 ................................................................................................................................................... 18

Wema, 1:14 ................................................................................................................................................................. 19

Kusadiki, Amini, Imani na Uaminifu katika Agano la Kale, 1:14 .................................................................................. 20

Msimamo wa Paulo kuhusiana na Sheria ya Musa, 1:17 ............................................................................................ 23

Mafarisayo, 1:24 ......................................................................................................................................................... 28

Chati ya Majina ya Mitume, 1:45 ................................................................................................................................ 34

Yesu Mnazareti, 1:45 .................................................................................................................................................. 36

Amina, 1:51 ................................................................................................................................................................. 38

Mbingu na Mbingu ya Tatu, 1:51 ................................................................................................................................ 39

Mtazamo wa Kibiblia kuhusiana na Kilevi na Matumizi Mabaya ya Kilevi, 2:3........................................................... 43

Uzani na Vipimo vya Mashariki ya Karibu ya Kale, 2:6 ............................................................................................... 46

Pasaka, 2:13 ................................................................................................................................................................ 49

Matumizi ya Yohana ya neno “Kuamini”, 2:23 ........................................................................................................... 53

Wakuu wa Baraza la Sinagogi, 3:1 .............................................................................................................................. 56

Ufalme wa Mungu, 3:3 ............................................................................................................................................... 59

Pumzi, Upepo na Roho, 3:8 ........................................................................................................................................ 62

Mungu Kuelezewa kama Mwanadamu, 3:16 ............................................................................................................. 64

Uchaguzi, Majaliwa na Uhitaji wa Usawa Kithiolojia, 3:16 ......................................................................................... 66

Muhuri/Lakiri, 3:33 ..................................................................................................................................................... 72

Ubaguzi wa Kimbari, 4:4 ............................................................................................................................................. 76

Unabii wa Agano la Kale, 4:19 .................................................................................................................................... 81

Unabii wa Agano Jipya, 4:19 ....................................................................................................................................... 84

Baba, 4:23 ................................................................................................................................................................... 87

Masihi, 4:25 ................................................................................................................................................................ 87

Mapenzi (Thelēma) ya Mungu, 4:34 ........................................................................................................................... 89

Uponyaji, 5:14 ............................................................................................................................................................. 96

Taratibu za Ufafanuzi kwa Ufasiri (Dhambi Isiyosameheka), 5:21 ........................................................................... 100

Page 5: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

Kupelekwa (Apostēllo), 5:24 ..................................................................................................................................... 101

Saa (hōra), 5:25 ......................................................................................................................................................... 101

Mafundisho ya Kanisa la Kwanza, 5:39 ..................................................................................................................... 106

Sarafu zilizotumika Palestina Enzi za Yesu, 6:7 ......................................................................................................... 112

Hesabu ya Kumi na Mbili, 6:13 ................................................................................................................................. 113

Majina ya Uungu, 6:20 .............................................................................................................................................. 115

Dhamana ya Mkristo, 6:37 ........................................................................................................................................ 118

Ukweli (Dhana) katika maandiko ya Paulo, 6:55 ...................................................................................................... 123

Milele (‘olam), 6:58 ................................................................................................................................................... 125

Kupaa, 6:62 ............................................................................................................................................................... 127

Roho (Pneuma) katika Agano Jipya, 6:63 ................................................................................................................. 128

Uasi (Aphistēm), 6:64 ................................................................................................................................................ 129

Ujasiri (parhēsia), 7:4 ................................................................................................................................................ 135

Malaika na Mapepo, 7:20 ......................................................................................................................................... 138

Ustahimivu, 8:31 ....................................................................................................................................................... 154

Ujuzi wa Kipekee, 8:40 .............................................................................................................................................. 157

Wokovu (Njeo za Vitenzi vya Kiyunani vilivyotumika), 9:7 ....................................................................................... 164

Kutubu (Agano Jipya), 9:22 ....................................................................................................................................... 166

Maangamizi, 10:10.................................................................................................................................................... 173

Kutiwa Mafuta katika Biblia, 11:2 ............................................................................................................................. 183

Ibada kwa Walio katika Huzuni, 11:20 ...................................................................................................................... 186

Wanawake katika Biblia, 11:28 ................................................................................................................................. 187

Utaratibu wa Mazidhi, 11:44 .................................................................................................................................... 191

Uovu Binafsi, 12:31 ................................................................................................................................................... 205

Vita huko Mbinguni, 12:31 ....................................................................................................................................... 206

Moyo, 12:40 .............................................................................................................................................................. 209

Amri katika Maandiko ya Yohana, 12:45 .................................................................................................................. 211

Pasaka (Taratibu za Utumishi), 13:2 ......................................................................................................................... 216

Yuda Iskarioti, 13:26 ................................................................................................................................................. 220

Waliokufa Wako Wapi?, 14:3 ................................................................................................................................... 227

Maombi ya Kumaanisha, 14:13 ................................................................................................................................ 232

Jina la Bwana, 14:13 ................................................................................................................................................. 233

Yesu na Roho, 14:16 ................................................................................................................................................. 234

Matumizi ya Pauo ya neno Cosmos, 14:18 ............................................................................................................... 235

Page 6: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

Siku Hiyo, 14:20 ........................................................................................................................................................ 236

Utatu, 14:26 .............................................................................................................................................................. 238

Hulka ya Roho, 14:26 ................................................................................................................................................ 239

Amani (Agano Jipya), 14:27 ...................................................................................................................................... 240

Moto, 15:6 ................................................................................................................................................................ 246

Nuru, 16:13 ............................................................................................................................................................... 257

Uchaguzi/Majaaliwa na Uhitaji wa Usawa Kithiolojia, 17:2 ..................................................................................... 266

Imani katika Mungu mmoja, 17:3 ............................................................................................................................. 267

Kweli katika Maandiko ya Yohana, 17:3 ................................................................................................................... 269

Uchaguzi/Maajaaliwa na Uhitaji wa Usawa Kithiolojia, 18:2 ................................................................................... 281

Yesu Mnazareti, 18:5 ................................................................................................................................................ 282

Mlinzi wa Mfalme, 18:28 .......................................................................................................................................... 287

Pontio Pilato, 18:29 .................................................................................................................................................. 288

Wanawake Waliomfuata Yesu, 19:25 ....................................................................................................................... 299

Manukato ya Mazishi, 19:39 ..................................................................................................................................... 303

Kuonekana kwa Yesu baada ya Ufufuo, 20:16 .......................................................................................................... 309

Muundo (Tupos), 20:25 ............................................................................................................................................ 312

Yohana 1 ukilinganisha na 1 Yohana 1, 1:1 ............................................................................................................... 330

Koinōnia, 1:3 ............................................................................................................................................................. 332

Ukristo ni Jamii Moja,1:3 .......................................................................................................................................... 332

Kukaa katika Maandiko ya Yohana, 2:10 .................................................................................................................. 344

Kujua, 2:13 ................................................................................................................................................................ 347

Serikali ya Wanadamu, 2:5 ....................................................................................................................................... 348

Enzi Hii na Enzi Ijayo, 2:17 ........................................................................................................................................ 350

Aliye Mtakatifu, 2:20 ................................................................................................................................................ 352

Maneno ya Agano Jipya yahusuyo Kurudi kwa Yesu, 2:28 ....................................................................................... 359

Haki,2:29 ................................................................................................................................................................... 361

Ushahidi wa Agano Jipya wa wokovu wa Mtu, 3:1 ................................................................................................... 364

Utakaso katika Agano Jipya, 3:5 ............................................................................................................................... 368

Mwana wa Mungu,3:8 .............................................................................................................................................. 369

Maombi yasiyo na Ukomo lakini Yenye Ukomo, 3:22 .............................................................................................. 375

Hukumu katika Agano Jipya,4:1 ................................................................................................................................ 379

Maneno ya Kiyunani yahusuyo Kupima na Vidokezo Vyake, 4:1 ............................................................................. 380

Mpango wa Ukombozi wa Milele wa YHWH,4:15 .................................................................................................... 386

Page 7: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

Dhamana ya Mkristo, 5:13 ........................................................................................................................................ 395

Maombi ya Kusihi, 5:14 ............................................................................................................................................ 397

Dhambi hadi Mauti, 5:16 .......................................................................................................................................... 400

Mzee, 2:1 .................................................................................................................................................................. 407

Kanisa (Ekklesia), 3:6 ................................................................................................................................................. 417

Page 8: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

i

NENO TOKA KWA MWANDISHI NI KWA NAMNA GANI FASIRI HII ITAKUSAIDIA?

Kutafasiri Biblia ni uwiano wa wastani na wa kiroho ambao unajaribu kumwelewa mwandishi wa kale aliyevuviwa kuandika ili kuwezesha ujumbe wa Mungu uweze kueleweka na kutumiwa katika zama hizi.

Mchakato wa kiroho ni muhimu sana lakini mugumu sana kuelezea. Unahusisha kujitoa na kuwa wazi kwa Mungu. Lazima pawepo na njaa (1) kwa ajili yake (2) ya kumjua yeye na (3) kumtumkia yeye. Mchakato huu unahusisha maombi, ukiri na kuwa tayari kubadili mfumo wa kuishi. Roho Mtakatifu ni wa muhimu sana katika mchakato wa utafasiri, lakini kwa nini wakristo waaminifu, wanaompenda Mungu wanaielewa Biblia tofauti kabisa na kuitafasiri visivyo.

Mchakato wa uwiano huu ni rahisi kuuelezea. Lazima tuwe na msimamo na haki kwa maandiko badala ya kuathiriwa na hali ya upendeleo binafsi au wa ki-madhehebu. Sote tumefungamanishwa ki-historia. Hakuna yeyote mtafasiri miongoni mwetu awezae kubisha. Fahiri hii inatoa kwa uangalifu uwiano ulio sahihi wenye kanuni tatu za tafasiri zilizoundwa kusaidia kudhibiti hali zetu za upendeleo.

KANUNI YA KWANZA

Kanuni ya kwanza ni kuona muundo wa kihistoria ambao kwayo Biblia iliandikwa na tukio zima la kihistoria katika uandishi wake. Mwandishi wa mwanzo alikuwa na kusudi, ujumbe wa kuwakilisha. Andiko haliwezi kumaanisha kitu kwetu ambacho hakikumaanishwa na ile asili, na mwandishi aliyevuviwa wa zama hizo. Kusudi lake na wala sio mahitaji yetu ki-historia, ki-musisimko, ki-tamaduni na mapokeo ya ki-madhehebu yetu ni— ufunguo.

Matumizi ni mbia mkubwa wa tafasiri, lakini tafasiri sahihi lazima ipate kipaumbele kwa matumizi. Lazima isisitizwe kwamba, kila andiko la Biblia lina tafasiri moja tu, na si vinginevyo. Maana hii ndiyo mwandishi wa mwanzo wa Biblia alivyokusudia akiongozwa na roho kuiwasilisha katika enzi zake. Maana hii moja yaweza kuwa na matumizi anwai, katika tamaduni na mazingira tofauti. Matumizi haya lazima yaambatane na ukweli halisi wa mwandishi wa awali. Kwa sababu hii, mwongozo wa fasiri hii imetayalishwa kwa namna ya kutoa utangulizi kwa kila kitabu cha Biblia.

KANUNI YA PILI

Kanuni ya pili ni kuibainisha fasihi moja. Kila kitabu cha Biblia ni hati ya kumbukumbu iliyounganishwa. Wafasiri hawana haki ya kutenganisha hoja moja ya ukweli kwa nyingine. Kwa hiyo hatuna budi kujaribu kuelewa kusudi la kitabu kizima cha Biblia kabla ya kutafasiri fasihi ya kitabu kimoja kimoja. Sehemu moja—sura, aya, au mistari haiwezi kumaanisha ambacho kitabu kizima hakimaanishi. Tafsiri sharti iwiane na mtizamo mzima kuelekea mtimzamo wa sehemu ya vifungu vya Biblia. Kwa hiyo mwongozo huu wa fasiri ya mafunzo haya umelenga kuwasaidia wanafunzi kuchambua muundo wa kila andiko ki-aya. Mgawanyo wa ibara na sura havikuvuviwa bali ni kutusaidia tu ili kubaini mawazo.

Kutafasiri katika ngazi ya aya na sio sentesi, ibara,kifungu au ngazi ya neno ndio ufunguo katika kufuata maana ya mwandishi aliyokusudia. Aya zimejengwa kwenye mada iliyounganishwa pamoja, mara nyingi huitwa sentesi yenye dhamira au mada. Kila neno, kifungu, ibara na sentesi katika aya kwa kiasi fulani vinahusiana na dhamira iliyo pamoja. Aidha haya huweka ukomo, inapanua , kuieleza na/ au kuihoji. Maelekezo sahihi (ufunguo) kwa tafsiri sahihi ni kufuata wazo la mwandishi wa awali aya kwa aya kufuatana na fasihi binafsi ambayo inatengeneza Biblia nzima..Tafsiri hizi zimechaguliwa kwa sababu zinatumia nadharia mbalimbali za tafsiri.

1. Andiko la Kiyunani la United Bible Society ni rekebisho la chapisho la Nne la (UBS4). Andiko hili liliandikwa ki-aya na wasomi wa maandiko ya kisasa.

Page 9: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

ii

2. Toleo la New King James Version (NKJV) ni utafsiri wa fasihi wa neno kwa neno uliosimamia kwenye mapokeo ya machapisho ya Kiyunani yaliyojulikana kama “Upokeaji wa Maandishi”. Mgawanyo wa aya zake ni mrefu kuliko tafasiri zinginezo. Urefu wa aya hizi unamwezesha wasomi kuona mada zilizo pamoja.

3. Toleo la New Revised English Version(NRSV) ni tafsiri ya neno kwa neno lililoboreshwa. Inatengeneza pointi ya kati baina ya matoleo mawili ya kisasa yanayofuata. Mgawanyo wa aya zake ni wa msaada mkubwa katika kubainisha masomo.

4. Toleo Today’s English Version(TEV) ni utafsiri sawia wenye nguvu uliyochapishwa na muungano wa vyama vya Biblia. Unajaribu kutafasiri Biblia kwa njia ya kumwezesha msomaji au mnenaji wa kiingereza cha kisasa kuelewa maana iliyomo katika andiko la Kigiriki. Mara nyingi, hasa hasa katika injili, inagawanya aya kufuatana na mnenaji hata kuliko somo lenyewe, sawa na NIV. Kwa kusudi la mtafasiri, hili halina msaada. Inapendeza kuona kuwa vitabu vya UBS4 na TEV vimechapishwa na mtu yule yule lakini aya zake zinatofautiana.

5. The Jerusalem Bible(JB) ni tafsiri sawia yenye mlinganyo wa nguvu iliyosimamia kwenye tafasiri ya Katoliki ya Ufaransa. Ni nzuri mno katika kufanya ulinganifu wa aya kutoka katika mtizamo wa ki-Ulaya.

6. Chapisho la andiko ni uboreshaji wa mwaka 1995 wa toleo la Biblia New American Standard Bible (NASB) ambalo ni tafasili ya neno kwa neno. Pia maoni ya mstari kwa mstari yanafuata aya hizi.

KANUNI YA TATU

Kanuni ya tatu ni kusoma Biblia tofauti tofauti ili kupata uwezekano mpana wa maana (somo la maana ya maneno) kwamba maneno ya Kibiblia au vifungu yanaweza kuwa nayo. Daima, neno au fungu la maneno katika Kiyunani yanaweza kueleweka kwa njia mbalimbali. Tafsiri hizi tofauti husaidia kubaini na kuelezea utofauti uliopo katika maandiko ya awali ya Kiyunani. Lakini haya hayaathiri mafundisho, bali husaidia katika kujaribu kurejelea maandiko asili yaliyoandikwa na mwandishi wa kwanza aliyevuviwa.

Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni ya utoaji taarifa na udadisi kimawazo. Mara nyingi tafsiri nyingine hutusaidia tusiwe ving’ang’anizi na wafinyu wa mawazo na mapokeo ya kimadhehebu. Watafasili wanapaswa kuwa na upana mkubwa wa kuelewa tafsiri tofauti tofauti na kuweza kubaini ni kwa ugumu upi maandiko ya kale yanaweza kuwa. Inashangaza kuona ni kwa kiasi kidogo kilioje cha makubaliano yaliopo kati ya Wakristo ambao wanadai kuamini biblia kama chanzo chao pekee cha ukweli. Kanuni hizi zimenisaidia kushinda hali yangu ya kufungwa kihistoria na kunifanya nipambane na maandiko ya zama hizo. Ni matumaini yangu kuwa kanuni hizi zitakuwa za Baraka kwako.

Bob Utley Juni 27, 1996 Haki Miliki © 2013 Bible Lessons International

Page 10: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

iii

MWONGOZO KWA USOMAJI MZURI WA BIBLIA:

UTAFITI BINAFSI KWA UKWELI ULIOTHIBITIKA

Kinachofuata ni maelezo mafupi ya Dr. Bob Utley mwana falsafa wa kanuni za ufasili na njia alizotumia katika

fasihi yake.

Tunaweza kuufahamu ukweli? Unapatikana wapi? Tunaweza kuuthibitisha kimantiki? Kweli, kuna mamlaka ya

kimsingi? Kuna imani kamili inayoweza kulinda maisha yetu, na ulimwengu wetu tuliomo? Kuna maana yeyote

katika maisha? Kwa nini tuko hapa? Tunakwenda wapi? Maswali haya yanauliza kwa watu wote wenye tafakuri

zenye uwiano—wameyatawala maarifa ya binadamu tangu mwanzoni mwa nyakati (Mhu. 1:13-18; 3:9-11).

Naweza kukumbuka utafiti wangu binafsi kwa ajili ya ungamanisho la maisha yangu. Nimekuwa mwamini katika

Kristo kwenye umri mdogo, awali kabisa nikizingatia juu ya ushahidi wa watu wengine muhimu kwenye familia

yangu. Nilivyokuwa kufikia utu uzima, maswali juu yangu na ulimwengu ninamoishi ulivyokuwa.Tamaduni za

kawaida na dini hazikuleta maana yeyote kwenye uzoefu niliousoma au kukutana nao. Ulikuwa ni muda wa

kuchanganyikiwa, kutafuta, kutamani, na mara nyingi fikra zisizokuwa na tumaini katika uso wa ulimwengu

mgumu, usiojali nilimoishi.

Wengi walidai kuwa na majibu kwa maswali haya ya msingi, lakini baada ya utafiti na kufikiri nikapata majibu yao yamelenga juu ya (1) falsafa binafsi, (2) hadithi za kubuniwa za kale, (3) uzoefu binafsi, au (4) Saikolojia zilizojichomoza. Nilihitaji digrii fulani ya uthibitisho, baadhi ya vielelezo, kiasi cha busara ambamo ningelenga mtazamo wangu wa kidunia, kiini cha uzima wangu, sababu yangu ya kuishi. Niliyapata haya katika usomaji wangu wa biblia. Nilianza kutafuta ushahidi wa udhamini nilioupata katika (1) utegemezi wa historia ya biblia kama ulivyothibitishwa na elimu kale, (2) usahihi wa Nabii za Agano la Kale, (3) umoja wa jumbe za Biblia zaidi ya miaka 1600 ya kutolewa kwake na (4) shuhuda binafsi za watu ambao maisha yao yalibadilika moja kwa moja baada ya kusoma biblia. Ukristo, kama mfumo wa imani na kuamini uliounganishwa, una uweo wa kukabiliana na maswali magumu ya maisha ya mwanadamu. Siyo haya tu yanaweza kutoa muundo kazi, lakini mwelekeo unaotokana na uzoefu wa imani za kibiblia uliniletea furaha zenye hisia na ustahimili. Nilijiridhisha ya kuwa nimepata kiini cha uzima wa maisha yangu—Kristo, kama ninavyoelewa kupitia maandiko.Ulikuwa ni uzoefu mgumu, msukumo wenye kuweka huru. Ingawa, naweza kukumbuka mshituko na maumivu yalipoanza kunifahamisha juu ya tafasiri ngapi tofauti ya kitabu hiki zimetetewa, wakati mwingine hata ndani ya makanisa hayo ya aina moja. Nikithibitisha mwongozo wa Ki-Mungu na uaminifu wa biblia haukuwa mwisho, lakini ni mwanzo pekee. Ni kwa vipi naweza kuthibitisha au kukataa tafsiri zinazotofautiana na kugongana za kurasa nyingi ngumu ndani ya maandiko kwa wale waliokuwa wakidai mamlaka yake na uaminifu? Kazi hii imekuwa lengo la maisha yangu na hija ya imani. Nilifahamu ya kuwa imani katika Kristo imeniletea furaha na amani kubwa. Mawazo yangu yametamani baadhi ya imani kamili katikati ya nadharia ya utamaduni wangu na mfumo wa imani gonganishi wa dini na majivuno ya kimadhehebu. Katika utafiti wangu wa mitazamo halali kwenye utafsiri wa fasihi ya kale, nilishangaa kuvumbua historia yangu, ya kitamaduni, ya kimadhehebu na uzoefu wa kipendeleo. Kwa kawaida kabisa, mara nyingi, nimesoma Biblia ili kuimarisha mtizamo wangu. Nimeutumia kama chanzo cha mfumo wa imani kuvamia imani nyingine wakati nikijihakikishia usalama wangu na utoshelevu. Ni kwa namna gani utambuzi wa maumivu haya yalikuwa kwangu! Ingawa siwezi kuwa kipingamizi moja kwa moja, naweza kuwa msomaji mzuri wa biblia. Naweza kuweka ukomo wa upendeleo kwa kutambua na kukubali uwepo wao. Sijawaweka huru,lakini nimeukabiri udhaifu wangu. Mtafsiri mara nyingi ndio adui mbaya wa usomaji mzuri wa biblia! Ngoja nitaje baadhi ya dhanio nilizoleta kwenye usomaji wa biblia ili, msomaji, aweze kuzichunguza pamoja nami:

Page 11: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

iv

DHANIO

1. Ninaamini biblia ni uvuvio wa ki-pekee wa ufunuo binafsi wa Mungu mmoja na aliye wa kweli. Kwa hiyo, ni lazima itafsiriwe katika mwanga wa kusudi la Ki-Ungu la mwandishi wa mwanzo (yaani Roho) kupitia mwandishi wa kibinadamu katika muundo wa historia uliokusudiwa.

- Wapokeaji wa mwanzo - Ujumbe ulioandikwa - Kusudi la mwandishi wa mwanzo 2. Ninaamini biblia iliandikwa kwa ajili ya mtu wa kawaida—kwa watu wote! Mungu alilazimika

mwenyewe kuongea kwetu waziwazi kupitia historia na tamaduni zilizomo. Mungu hakuuficha ukweli, anatutaka sisi kuelewa! Kwa hiyo, inalazimika kutafsiriwa katika (uwazi) katika siku hizo, na siku hizi tulizomo. Biblia haitakiwi kumaanisha kwetu yale ambayo hayakumaanisha kwa wale wa mwanzo walioisoma au kuisikia. Inaeleweka kwa wastani wa mawazo ya kibinadamu na kutumia aina ya njeo mbadala za kawaida za mawasiliano ya ki-binadamu.

3. Ninaamini Biblia inakusudi na ujumbe uliowekwa pamoja. Haina mkanganyiko ndani yake, ingawa inajumuisha (njia ngumu na zinazokinzana). Hivyo basi, mtafsiri mzuri wa biblia ni biblia yenyewe.

4. Ninaamini kwa kila kurasa (pasipo kujumuisha unabii) ina maana moja iliyosimama kwenye kusudi la mwanzo la mwaandishi aliyevuviwa. Ingawa hatuwezi kutia shaka kutambua kusudi la mwandishi wa mwanzo, viashirio vingi daima vimeelekeza katika uelekeo wake; a. Aina ya fasihi tanzu uliochaguliwa kuelezea ujumbe b. Mtindo wa kihistoria na/au muda maalumu ulioshawishi maandiko kuandikwa c. Muundo wa fasihi wa kitabu husika pamoja na kila fasihi moja d. Muundo wa maandishi (elezewa kwa fasaha) wa fasihi moja kama zinavyo husiana na ujumbe e. Umbo la kisarufi husika lililowekwa kuwasilisha ujumbe f. Maana zilizochaguliwa kuwakilisha ujumbe

Mafunzo ya kila eneo hili liwe chanzo cha mafunzo yetu katika aya. Kabla sijaelezea njia zangu za usomaji mzuri wa biblia, hebu nielezee angalau njia zisizosahihi zinazotumiwa siku hizi zilizopelekea kuwepo kwa tafsiri tofauti nyingi na hivyo basi zinatakiwa kuepukika.

II. Mbinu zisizofaa 1. Kutojali mazingira ya fasihi ya vitabu vya Biblia na kutumia kila sentesi, ibara, au maneno binafsi kama

maelezo ya kweli yasiyohusiana na kusudi la mwandishi wa mwanzo au mtindo mpana. Hii mara nyingi huitwa “uhakiki wa andiko”

2. Kutoujali muundo wa ki-hisoria wa vitabu kwa kubadilisha muundo wa ki-historia unaodhaniwa kuwa ni mdogo au usiosaidika kutoka kwenye andiko lenyewe.

3. Kutojali muundo wa kihistoria wa vitabu na kusoma kama gazeti la mtaani lililoandikwa asili kwa wakristo binafsi wa kisasa.

4. Kuupa muundo wa kihistoria wa vitabu kwa kuliistiari andiko ndani ya ujumbe wa falsafa/theolojia isioendana na wasikiaji wa kwanza na kusudi la mwandishi wa mwanzo.

5. Kutojali muundo wa mwanzo kwa kubadilisha mtindo wa theolojia ya mtu, mafundisho yanayopendeka, au mambo ya kisasa yasiyoendana na kusudi la mwandishi wa mwanzo na ujumbe uliotolewa. Tabia hii mara nyingi hufuata usomaji wa mwanzo wa biblia kama kigezo cha kuanzisha mamlaka ya mnenaji. Hii mara nyingi hurejewa kama “mwitikio wa msomaji” (utafsiri wa-andiko-lililomaanisha-kwangu). Kwa wastani, vitu vitatu vinavyoendana vinaweza kupatikana katika mawasiliano ya binadamu yalioandikwa.

Kusudi la Mwandishi wa Mwanzo

Andiko lililoandikwa

Wapokeaji wa

Mwanzo

Page 12: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

v

Siku za nyuma, mbinu tofauti za usomaji zimenitazamisha juu ya moja kati ya vitu vitatu. Lakini kweli tunatamka kwa dhati uhuisho wa Biblia wa kipekee na mchora uliofanyiwa mabadiliko unaofaa zaidi: Kwa kweli vitu hivi nyote vitatu lazima

vijumulishwe katika mchakato wa ufasiri. Kwa kusudi la uthibitisho, ufasiri wangu unalenga juu ya moja kati ya vitu viwili: mwandishi wa mwanzo na maandiko. Ninayamkinika kujibu matusi mabaya niliyoyachunguza (1) shutumu au kutakasa maandiko na (2) tafasili ya “mwitikio wa msomaji” (unamaanishwa nini kwangu).Matusi yanaweza kutokea katika kila hatua. Ni lazima kila mara tuchunguze mienendo yetu, upendeleo wetu, mbinu na matumizi. Lakini ni kwa jinsi gani tunaweza kuyachunguza kama hapatakuwepo na mipaka ya ufasihi, ukomo au kigezo? Hapa ni pale kusudi la mwandishi na muundo wa maandiko yaliponipa baadhi ya vigezo kuzuia maeneo ya fasiri zilizo halali. Katika kuangazia hizi mbinu za usomaji zisizofaa, zipi ni baadhi ya mitazamo mizuri ya usomaji mzuri wa biblia ambao unatoa digri ya uthibitisho na misimamo?

III. Mitazamo inayofaa katika usomaji mzuri wa Biblia Katika hatua hii sijadili mbinu pekee za ufasiri wa namna mahususi lakini kwa pamoja kanuni halali kwa aina yote ya maandiko ya kibiblia. Kitabu kizuri kwa namna ya mitazamo mahususi ni How To Read The Bible For All Its Worth, ya Gordon Fee na Douglas Stuart, kilichochapishwa na Zondervan. Utaratibu wangu mwanzoni ulinitizamisha juu ya msomaji aliyemruhusu Roho Mtakatifu kuangaza biblia kupitia kwa miduara minne ya usomaji binafsi. Hii inamfanya Roho, andiko na msomaji wawe kiwango cha mwanzo, na siyo cha juu. Vile vile hii inamlinda msomaji kutokuwa na mwanya wa kushawishiwa na mtoa maoni. Nimesikia ikisemwa: “Biblia inaangazia zaidi katika fasihi”. Hii haimaanishi kukashifu maoni juu ya msaada wa usomaji lakini ni ombi kwa muda unaofaa kwa matumizi yao. Tunalazimika kuusaidia ufasiri wetu kutoka katika andiko lenyewe. Maeneo matatu yanatoa angalau ukomo wa uthibitisho:

1. muundo wa kihistoria 2. mazingira ya fasihi 3. muundo wa kisarufi (vipashio) 4. matumizi ya maneno ya kisasa 5. milango muhimu iliyo sambamba 6. namna tanzu ya uwasilishaji

Tunahitajika kuweza kutoa sababu na mantiki zilizo nyuma ya ufasii wetu. Biblia ndiyo chanzo pekee cha imani yetu na mazoezi. Kwa huzuni, mara nyingi wakristo hawakubali juu ya kile kinachofundishwa au kukiri. Ni kushindwa kudai uhuisho juu ya Biblia na kupelekea waamini washindwe kukubali juu ya kile kinachofundishwa na kutakiwa! Miduara mine ya usomaji imeundwa kutupatia utambuzi wa ufasili ufuatao:

1. Mzunguko wa kwanza wa usomaji a. Soma kitabu katika mkao mmoja. Soma tena katika fasili tofauti , kwa matumaini kutoka katika fasili

tofauti za nadharia 1) Neno kwa neno (NKJV, NASB, NRSV) 2) Mlinganyo wenye nguvu (TEV, JB) 3) Ufafanuzi (Living Bible, Amplified Bible)

b. Angalia kiini cha kusudi la uandishi mzima. Tambua dhamira yake. c. Tenga (ikiwezekana) fasihi moja, sura, ibara au sentesi inayoelezea waziwazi Kiini cha kusudi au

dhamira

Roho Mtakatifu Utofauti wa

maandiko Waamini wa

awali

Kusudi la

Mwandishi wa

Mwanzo

Maandiko

yalioandikwa

wapokeaji wa

mwanzo

Page 13: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

vi

d. Tambua fasihi tanzu yenye nguvu 1) Agano la kale

a) Simulizi za waebrania b) Mashairi ya waebrania (fasihi za hekima, zaburi) c) Unabii wa ki-Ebrania (lugha ya mjazo, shairi) d) Alama za siri za ki-sheria

2) Agano jipya a) Simulizi (Injili, matendo) b) Hadithi za mafumbo (Injili) c) Barua/nyaraka d) Fasihi za mafunuo

2. Mzunguko pili wa usomaji a. Soma kitabu kizima tena, ukitafuta kufahamu mada muhimu au masomo. b. Elezea kwa muhtasari wa mada muhimu na elezea kwa kifupi yaliomo kwa maelezo rahisi c. Angalia kusudi la maelezo yako na eleza kwa mapana kwa msaada wa usomaji.

3. Mzunguko wa tatu wa usomaji. a. Soma tena kitabu kizima, ukitafuta kutambua muundo wa ki-historia na Matukio lengwa kwa ajili ya

uandishi kutoka katika kitabu cha Biblia yenyewe. b. Taja vipengele vya ki-historia ambavyo vinatajwa katika kitabu cha Biblia.

1) Mwandishi 2) Tarehe 3) Wapokeaji 4) Kusudu mahsusi la uandishi 5) Mwelekeo muundo wa kitamaduni unaorandana na kusudi la mwandishi 6) Marejeo toka kwenye matukio na watu wa kihistoria/ kale

c. Panua maelezo yako kwa kiwango cha aya kutoka katika sehemu ya kitabu cha biblia unayotafasiri. Mara nyingi tambua na kuelezea fasihi. Inaweza kuwa na vifungu na aya nyingi. Hii inakuwezesha wewe kufuata wazo na muundo wa maandiko ya mwandishi wa mwanzo.

d. Angalia muundo wako wa kihistoria kwa kutumia msaada wa usomaji

4. Mzunguko wa nne wa usomaji a. Soma tena bayana fasihi moja katika tafasiri nyinginezo nyingi

1) Neno kwa neno (NKJV, NASB, NRSV) 2) Mwenendo linganifu (TEV, JB) 3) Ufafanuzi (Living Bible, Amplified Bible)

b. Angalia fasihi au muundo wa kisarufi 1) Misemo ya kujirudia Waefeso.1:6, 12, 14 2) Muundo wa kisarufi unaojirudia Warumi 8:31 3) Mbinyo wa mawazo (dhana zinazoafikiana)

c. Taja vipengele vifuatavyo:- 1) Istilahi muhimu 2) Istahili zisizo za kawaida 3) Muundo muhimu wa kisarufi 4) Maneno magumu, ibara, na sentesi

d. Angalia njia muhimu zilizosambamba 1) Angalia njia za wazi za ufundishaji kwenye somo lako kwa kutumia

a) Vitabu vya thiolojia b) Biblia za marejeo

Page 14: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

vii

c) Itifaki 2) Angalia maneno mawili yanayokinzana katika somo lako. Kweli nyingi za ki-Biblia zinatolewa

katika rahaja mbili zinazofanana. Migongano mingi ya ki-madhehebu hutokea kutokana nauthibitisho nusu wa maandiko ya Biblia. Biblia zote zimevuviwa. Ni lazima tutafute ujumbe mzima ili kutoa mlinganyo wa ki-maandiko katika tafasiri zetu.

3) Angalia milinganisho ndani ya kitabu, kilekile, mwandishi Yule Yule, au namna ileile, Biblia ina mfasiri wake mzuri kwa sababu ina mwandishi mmoja ambaye ni Roho Mtakatifu.

e. Tumia misaada ya kusoma kuangalia uchunguzi wako wa muundo wa kihistoria na tukio. 1) Soma biblia 2) Ensaikolopidia za biblia, vitabu vya mkononi na kamusi 3) Tangulizi za biblia 4) Fasihi za biblia (katika hatua hii kwenye usomaji wako ruhusu jamii ya waamini, waliopita na

waliopo, kusaidia na kusahihisha usomaji wako binafsi)

IV. Matumizi ya utafasiri wa Biblia. Katika hatua hii tunageukia matumizi, umechukua muda kuelewa andiko katika muundo wake, sasa lazima utumie katika maisha yako, utamaduni wako, na elezea mamlaka ya Ki-biblia kama “uelewa ule mwandishi wa ki-biblia wa mwanzo alivyosema katika zama zake na kutumia ukweli huo katika zama hizi”. Matumizi lazima yafuate utafasiri wa kusudi la mwandishi wa mwanzo katika muda na mantiki. Hatuwezi kutumia njia ya Biblia katika zama zetu mpaka pale tutakapo fahamu kile alichokuwa akikisema katika zama hizo. Njia ya Biblia isimaanishe kile asicho kimaanisha! Maelezo yako kwa kirefu, kwa kiwango cha aya (mzunguko wa usomaji #3) yatakuwa mwongozo wako. Matumizi lazima yafanyike katika kiwango cha aya, na sio kiwango cha neno, maneno yana maana pekee katika mazingira, ibara zina maana pekee katika mazingira na sentensi zina maana pekee katika mazingira. Mtu pekee aliyevuviwa ambaye amejumuishwa katika mchakato wa utafsiri ni mwandishi wa mwanzo. Kipekee unafuata utangulizi wake kwa mwanga wa Roho Mtakatifu. Lakini nuru sio uvuvio. Kusema “asema Bwana”lazima, tufungamane na kusudi la mwandishi wa mwanzo. Matumizi lazima yaendane bayana na kusudi lote la uandishi mzima, maandishi bayana, na muendelezo wa kiwango cha aya. Usiruhusu mambo ya zama hizi yatafasiri Biblia, iruhusu Biblia ijiongee yenyewe. Hii itatuhitaji kuvuta kanuni kutoka kwenye andiko. Hii itakubalika kama andiko litaiwezesha kanuni. Bahati mbaya wakati mwingi kanuni zetu ni “zetu” na si kanuni za ki-maandiko. Katika kutumia Bibilia, ni muhimu kukumbuka kuwa (isipokuwa katika unabii) maana moja na moja pekee itakubalika kwa andiko la Kibiblia pekee. Maana hiyo iendane na kusudi la mwandishi wa mwanzo kama alivyo eleza tatizo au hitaji katika zama zake. Mengi ya matumizi yanayowezekana yanaweza kutolewa kutoka katika maana hii moja. Matumizi yatategemea mahitaji ya wapokeaji lakini ni lazima yaendane na maana ya mwandishi wa mwanzo.

V. Sura ya utafasiri wa kiroho. Zaidi ya hapo nimejadili mantiki na mchakato wa ki-maandiko uliojumuishwa kwenye utafasiri na matumizi. Sasa ngoja nijadili kwa kinaga ubaga mwelekeo wa kiroho wa utafasiri. Mfuatano ufuatao umekuwa wa msaada sana kwangu.

1. Omba kwa ajili ya msaada wa Roho (kama vile 1Kor. 1:26-2:16) 2. Omba kwa ajili ya msaada binafsi na kusafishwa kutoka katika dhambi inayojulikana (kama vile 1 Yohana

1:9) 3. Omba kwa ajili ya hamu kubwa ya kumjua Mungu (kama vile Zab. 19:7-14, 42:1, 119:1) 4. Tumia utambuzi wowote mpya mara moja katika maisha yako. 5. Baki mnyenyekevu na anayefundishika.

Page 15: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

viii

Ni vigumu kuweka mlinganyo kati ya mchakato wa kimantiki na uongozi wa kiroho wa Roho Mtakatifu. Dondoo zifuatazo zimesaidia kulinganisha hizi mbili:

1. Kutoka kwa mwandishi James W.Sire, scripture twisting,kr. 17-18 “Nuru huja kwenye mawazo ya watu wa Mungu na sio tabaka la watu wa kiroho. Hakuna daraja la ualimu katika ukristo wa kibiblia. Hakuna kuongoza, hapana mtu awaye yote ambaye tafsiri zote nzuri zitoke kwake. Na hivyo, wakati roho mtakatifu anatoa karama maalumu ya hekima, maarifa na utambuzi wa kiroho huwa pamoja. Hakutoa hizi kwa wakristo waliokirimiwa kuwa wao ndo pekee watafsiri wenye mamlaka ya Neno lake. Ni juu ya kila watu wake kujifunza, kuamua na kutambua kwa kufanya marejeo kwenye Biblia ambayo inasimama kama yenye mamlaka hata kwa wale ambao Mungu amewapa uwezo pekee. Kwa kufupisha, wazo mnalofanya kupitia kitabu kizima ni kuwa Biblia ni ufunuo wa kweli wa Mungu kwa watu wote, ya kuwa ni mamlaka yetu ya mwisho katika mambo yote ambayo inayaongelea, kuwa sio fumbo lote lakini inaweza kueleweka vya kutosha na watu wa kawaida kwa kila tamaduni.”

2. Juu ya Kierkegaard, inayopatikana toka kwa Benard Ramm,Protestant Biblical Interpretation(tafsiri ya biblia ya ki-protestanti) Uk.75: Kutokana na Kierkegaard, kisarufi, misamiati na usomaji wa kihistoria wa Biblia ulikuwa ni muhimu lakini utangulizi wa usomaji wa kweli wa Biblia na kusoma Biblia kama neno la Mungu mmoja lazima alisome kwa moyo wake wote mdomoni mwake, kutoka ncha ya kidole, na shauku ya matarajio katika mazungumzo na Mungu. Usomaji wa Biblia pasipo tafakari, kutojali au kielimu, au weledi sio usomaji wa Biblia kama neno la Mungu, kama mmojawapo asomavyo barua ya mapenzi isemavyo, tena mmoja asoma kama neno la Mungu.

3. H.H Rawley katika The Relevance of the Bible, Uk.19: Hakuna uelewa mdogo wa kisomi wa Biblia, ingawa yote, inaweza kumiliki hazina yote. Haidharau uelewa huo, kwa kuwa ni muhimu kwa uelewa wote. Lakini ni lazima iongeze uelewa wa kiroho wa hazina ya kiroho ya kitabu hiki kwa ujumla. Kwa huo uelewa wa kiroho kitu fulani ambacho ni zaidi ya hadhari ya kiroho ni muhimu. Mambo ya kiroho ni utambuzi wa kiroho, na wanafunzi wa Biblia wanahitaji fikra za upokeaji wa kiroho. Ile hamu ya kumtafuta Mungu ambayo inaweza kumsababisha ajitoe kwake. Ni kama kupita zaidi ya usomaji wa kisayansi kuingia kwenye urithi wa utajiri wa hiki kitabu kikubwa kuliko vyote.

VI. Njia hizi za Fasiri Study Guide Commentary (Mwongozo wa usomaji) wa fasihi umeundwa kusaidia njia zako za utafsiri katika njia zifuatazo:

1. Maelezo fasaha ya kihistoria yanayotambulisha kila kitabu baada ya kufanya “mzunguko wa usomaji #3” angalia taarifa hizi.

2. Utambuzi wa ki-mazingira unapatikana katika kila kurasa. Hii itakusaidia kuona jinsi gani maandishi/fasihi imeundwa.

3. Katika kila mwanzo wa kifungu au fasihi kubwa inaunganisha mgawawanyo wa aya na maelezo ya kichwa cha makala yanatolewa kutoka katika tafsiri za kisasa. a. United Bible Society Greek Text.Toleo la nne lililobadilishwa (UBC) b. The New American Standard Bible 1995 ya kisasa (NASB) c. The New King James Version (NKJV) d. The New Revised Standard Version (NRSV) e. Today’s English Version (TEV) f. The Jerusalem Bible (JB)

Aya zilizogawanywa hazikuvuviwa. Lazima ziyakinishwe kutoka katika mazingira fulani. Kwa kulinganisha tafsiri nyingi za kisasa kutoka tafsiri nyingi za ki-nadharia na mitizamo ya kitheolojia, tunaweza kuchanganua muundo unaokusudiwa wa mawazo ya mwandishi wa mwanzo, kwani kila aya ina ukweli mmoja mkubwa. Huu uliitwa “mada ya sentensi” au wazo la kati la andiko, hilo wazo lililounganishwa ni ufunguo kwa tafsiri nzuri ya kihistoria na kisarufi. Mmojawapo asitafsiri, kuhubiri au kufundisha chini ya aya, vilevile ukumbuke ya kuwa kila aya inahusiana na aya zingine. Hii ndo maana kiwango cha aya kinachoelezea kitabu kizima ni muhimu. Ni lazima tuweze kufuata mtiririko wa kimantiki wa somo lililotolewa na mwandishi wa mwanzo aliyevuviwa.

Page 16: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

ix

4. Muhtasari wa Bob unafuata mtazamo wa kifungu kwa kifungu kwa utafsiri wake. Hii inatulazimisha kufuata mawazo ya mwandishi wa mwanzo. Muhtasari unatoa habari kutoka sehemu nyingi. a. Mazingira ya fasihi b. Utambuzi wa kihistoria na tamaduni c. Habari za kisarufi d. Usomaji wa neno e. Njia muhimu zilizo sambamba

5. Mahali fulani katika fasihi, andiko lililochapishwa toka toleo jipya la Marekani (1995 mpaka sasa hivi) litaongezewa na tafsiri za matoleo mbalimbali ya kisasa. a. New King James Version (NKJV) ambayo unafuata mswaada wa “Upokeaji wa Maandiko halisi”. b. The New Revised Standard Version (NRSV) ambayo ni rudio la neno-kwa-neno Kutoka katika Umoja

makanisa asili ya Revised Standard Version c. The Today’s English Version (TEV) ambayo ni tafsiri ya mlinganyo wa nguvu Kutoka American Bible

Society. d. The Jerusalem Bible (JB) ambayo ni tafsiri ya Kiingereza inayotegemea kutoka tafsiri ya

Mlinganyo wa nguvu wa Katoriki ya Ufaransa. 6. Kwa wale wote ambao hawasomi ki-giriki, ukilinganisha na tafsiri za kiingereza inaweza kusaidia kutambua

matatizo katika andiko: a. Tofauti za mswada b. Maana ya maneno mbadala c. Muundo na maandiko magumu ya kisarufi Ingawa tafsiri za kiingereza haziwezi kuleta suluhu kwenye

matatizo hayo yanayalenga kama sehemu ya ndani na usomaji kamili. d. Karibia kila kifungu, maswali muhimu ya majadiliano yanatolewa ambayo yanajaribu kulenga maswala

muhimu ya utafsiri wa kifungu hicho.

Page 17: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

1

UTANGULIZI WA YOHANA

MAELEZO YA AWALI

A. Mathayo na Luka walianza na kuzaliwa kwa Yesu, Marko akaanza na ubatizo wake, lakini Yohana akaanza kabla ya uumbaji.

B. Yohana anawasilisha Uungu wote wa Yesu wa Nazareti toka mstari wa kwanza kifungu cha kwanza na akaendelea kusisitiza katika injili yote. Vidokezo vya injili vinaficha kweli hii mpaka baada ya uwasilishaji wao (Siri za Umasihi).

C. Kwa wazi kabisa Yohana alikuza injili yake katika mwanga wa msingi wa uthibitisho wa vidokezo vya injili. Anajaribu kuongezea na kutafasiri maisha na mafundisho ya Yesu katika mwanga wa uhitaji wa kanisa la mwanzo (karne ya mwanzo kabisa)

D. Yohana anajaribu kuunda uwasilishaji wake juu ya Yesu Masiha kwenye 1. Miujiza /ishara saba na utafasili wake 2. Mahojiano ishirini na saba na/au mazungumzo na watu binafsi 3. Kuabudu kiasi fulani na siku za mikate

a. Sabato b. Pasaka (kama vile Yoh. 5-6) c. Sikukuu za vibanda (kama vile Yoh. 7-10) d. Sikukuu za kutabaruku (kama vile Yoh. 10:22-39)

4. Maelezo ya neno “nalikuwepo ” a. Kuhusiana na jina la Uungu (YAHWE)

1) Mimi ndiye (Yoh 4:26; 8:24,28; 13:19; 18:5-6) 2) Kabla ya Ibrahim kuwepo nalikuwepo (Yoh. 8:54-59)

b. Ikiwa na kiima cha kuarifu 1) Mimi ni mkate wa uzima (Yoh. 6:35; 41,48,51) 2) Mimi ni Nuru ya ulimwengu (Yoh. 8:12) 3) Mimi ni mlango wa kondoo (Yoh. 10:7,9) 4) Mimi ndimi mchungaji mwema (Yoh. 10:11,14) 5) Mimi ndimi ufufuo na uzima (Yoh. 11:25) 6) Mimi ndimi njia, kweli na uzima (Yoh. 14:6) 7) Mimi ni mzabibu wa kweli (Yoh. 15:1,5)

E. Tofauti ya injili ya Yohana na injili zingine 1. Ingawa ni kweli kwamba kusudi la awali la Yohana ni la kithiolojia, utumiaji wake wa historia na

kijografia ni sahihi kabisa na wenye maelezo kamilifu. Sababu haswa ya utofauti kati ya mihutasari na Yohana haiku wazi a. Huduma ya mwanzo ya Yudea ( utakaso wa awali wa Hekalu) b. Utaratibu wa kupanga matukio na tarehe ya wiki ya mwisho ya maisha ya Yesu c. Kusudi la uundaji upya wa thiolojia

2. Ingalisaidia kupata wasaa kujadili tofauti ya wazi kati ya Yohana na mihutasari. Napenda ninukuu George Eldon Ladd toka kwenye kitabu A Theology Of a New Testament juu ya tofauti: a. “Injili ya Nne ni tofauti kabisa na mihtasari ya kwamba swali lazima kiukweli likabiliwe hata kama

linatoa kiusahihi taarifa za mafundisho ya Yesu au hata kama imani ya Kikristo imebadilisha sana mapokeo kiasi kwamba historia imemezwa katika utafasili wa kithiolojia” (uk. 215)

b. “Suluhisho linaloangukia karibu mkononi ni kwamba mafundisho ya Yesu yanaelezewa katika nahau za Yohana. Kama hili ndo suluhisho sahihi, na tukifanya hitimisho kwamba injili ya Nne inafundishwa katika nahau za Yohana, swali hili muhimu linafuata; kwa kiasi gani injili ya nne ile ya Yohana ni ya kithiolojia kuliko ile ya Yesu? ni kwa kiasi gani mafundisho ya Yesu yamesimilishwa sana kwenye mawazo ya Yohana kiasi kwamba kile tulicho nacho ni utafasili wa Yohana kuliko uwasilishaji sahihi wa mafundisho yake Yesu” ( uk. 215) .

Page 18: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

2

c. Pia Ladd alimnukuu W. F. Albright toka " uvumbuzi wa karibuni katika Palestina na injili ya Yohana" in The Background of the New Testament and Its Eschatology na kuhaririwa na W. D. Davies na D. Daube. “Hakuna tofauti za kimsingi katika mafundisho kati ya Yohana na mihutasari; Utofauti kati yao ni kule kusimamia katika umakinikiaji wa dhana Fulani juu ya mafundisho ya Yesu, hasa hasa yale yanayokaribia kufanana na mafundisho ya Essene kwa karibu sana. Hakuna kabisa kile kinachoonyesha kwamba mafundisho ya Yesu yamebadilishwa au kupotoshwa, au kitu kipya muhimu kimeongezwa kati yao, ya kwamba uhitaji wa kanisa la mwanzo ulisababisha uchaguzi wa vitu vya kuingizwa ndani ya injili tuweze kuukubali, lakini hakuna sababu ya kudhani kwamba uhitaji wa kanisa hilo ulihusika kwa ugunduzi wowote au uvumbuzi wa umuhimu wa kithiolojia. Moja ya uthibitisho mgeni kabisa wa uhakiki cha wasomi wa Agano Jipya na wanathiolojia ni kwamba fikra za Yesu zilikuwa na ukomo kiasi kwamba tofauti yeyote ya wazi kati ya Yohana na mihutasari lazima iwe ni kwa sababu ya tofauti kati ya Wanathiolojia wa kanisa la mwanzo. Kila mwenye fikra kubwa na nafsi atapelekea kutafasiliwa kitofauti kabisa na marafiki na wasikililizaji tofauti, kile kitakacho wapelekea kuchagua kile kilcho muhimu mbali na kile walichokiona na kukisikia” (kurasa za 170-171)

d. Na tena toka kwa George E.Ladd: “Tofauti kati yao sio kwamba Yohana ni mwanathiolojia na wengine sio lakini wote ni Wanathiolojia katika Nyanja tofauti. Historia iliyotafasiliwa yaweza kuwasilisha ukweli zaidi wa jambo la uhakika kuhusu hali yenyewe kuliko matukio yaliyo andikwa. Kama Yohana ni mtafasili wa kithiolojia, ni utafasili wa matukio yale Yohana alishawishika yatokee katika historia. Ni dhahili kabisa sio kusudio la muhtasari wa injili kutoa taarifa ya maneno yenyewe ya Yesu au habari ya matukio ya maisha yake. Ni taswira ya Yesu na mihutasari ya mafundisho yake. Mathayo na Luke walijisika wao kuwa huru kupanga upya vfaa vya kuandikia maandiko katika Marko na kutoa taarifa ya mafundisho ya Yesu kwa uhuru wa kufikirika. Kama Yohana alitumia uhuru zaidi ya Mathayo na Luka, ni kwa sababu alitamani kutoa zaidi na kuonyesha taswira halisi ya Yesu” (kurasa za 221-222)

MWANDISHI A. Mwandishi wa injili hajulikani lakini inadokeza kwenye uandishi wa Yohana

1. Kama shahidi mwandishi wa wazi (kama vile Yoh. 19:35) 2. Kifungu “wanafunzi wapendwa” ( wote hata wenye majina ya ukoo walimtambua yeye kama Yohana

Mtume). 3. Yohana, mwana wa Zebedayo, hakuwahi kutamkwa kwa jina.

B. Muundo wa kihistorai unadhihirisha ni kutoka kwenye injili yenyewe, suala la uandishi sio kitu muhimu

sana kwenye utafasili. Uthibitisho wa mwandishi aliyevuviwa ni muhimu! Uandishi na tarehe ya injili ya Yohana hauathiri uvuvio, lakini utafasili. Watoa maoni wanatafuta muundo wa kihistoria, sababu ya kufanya kitabu kiandikwe. Je, inalazimu Yohana kulinganisha uwekevu na; 1. Enzi mbili za Wayahudi 2. Mwalimu wa maeneo ya mambo ya kale (Qumran)juu ya haki 3. Dini ya kale ya Uajemi iliyoanzishwa na Zoroaster 4. Mawazo ya kimafunuo 5. Mtazamo wa kipee wa Yesu

C. Mtizamo wa awali wa kimapokeo ni kwamba Yohana Mtume, mwana wa Zebedayo, ni mwanadamu, asili

wa ushuhuda. Hili lazima libainishwe kwa sababu karne ya pili vitu kutoka nje vinaonekana kuunganisha kwenye vitu vingine katika uzalishaji wa injili. 1. Wapendwa wenzake na wazee wa Efeso wakawatia moyo Mtume mwenye umri mkubwa kuandika

(Eusebio akamnukuu Clement wa Iskandria)

Page 19: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

3

2. Mtume mwenza, Andrea (the Muratorian Fragment, 180-200 b.k.,kutoka Rumi)

D. Baadhi ya wasomi wa sasa wamewasadiki waandishi wengine wakisimamia kwenye mawazo tofauti kuhusu mtindo na somo la injili. Wengi walichukulia tarehe za mwanzoni mwa karne ya pili (kabla ya 115 B.K) 1. Iliandikwa na wanafunzi wa Yohana (mzunguko wa ushawishi wa Johannine) ambaye alikumbuka

mafundisho yake (J. Weiss, B. Lightfoot, C. H. Dodd, O. Cullmann, R. A. Culpepper, C. K. Barrett). 2. Iliandikwa na “Yohana mwenye umri mkubwa” (moja ya orodha ya viongozi wa awali toka Asia

waliovutiwa na thiolojia na istilahi ya Yohana Mtume) kilichochukuliwa toka kwenye kifungu kisicho eleweka vizuri katika Papias (70-147 B.K) kilichonukuliwa na Eusebio (280-339 B.K)

E. Ushahidi wa Yohana mwenyewe kama msingi wa asili ya maandiko ya Biblia. 1. Ushahidi wa ndani

a. Mwandishi aliyajua mafundisho ya Wayahudi na matambiko na kushirikishana mtazamo wao wa kidunia wa Agano la Kale

b. Mwandishi aliijua hali yao ya Palestina na Yerusalem kabla miaka ya 70 B.K c. Mwandishi anadai kuwa shahidi wa macho

1) Yohana 1:14 2) Yohana 19:35 3) Yohana 21:24

d. Mwandishi alikuwa mwanajumuiya wa kundi la kitume, kwa vile alijua vizuri; 1) Maelezo ya tarehe na mahali (majaribu ya usiku) 2) Maelezo ya tarakimu (mitungi ya maji katika Yohana 2:6 na samaki katika Yohana 21:11) 3) Maelezo ya watu 4) Mwandishi aliyajua maelezo ya matukio na hatua za kuchukua dhidi yao 5) Mwandishi anaonekana kudhihilisha kama “ mwanafunzi kipenzi”

a) Yohana 13:23,25 b) Yohana 19:26-27 c) Yohana 20:2-5,8 d) Yohana 21:7, 20-24

6) Mwandishi anaonekamna kuwa mwanajumuiya wa ndani ya mduara pamoja na Petro. a) Yohana 13:24 b) Yohana 20:2 c) Yohana 21:7

7) Jina Yohana, mwana wa Zebedayo, halionekani kwenye injili, ambacho kinaonekana sio kitu cha kawaida kwa sababu alikuwa ni mmoja wa wanajumuiya wa mduara wa ndani wa kitume.

2. Ushahidi wa nje a. Injili ilijulikana na

1) Irene (120-202 B.K) ambaye alihusiana na Polycarp, alimjua Yohana Mtume (cf. Eusebio, Mhubiri 5:20:6-7) “Yohana mwanafunzi wa Yesu aliye egama katika kifua chake na mwenyewe kuitoa injili kwa Waefeso katika Asia” ((Haer, 3:1:1, imenukuliwa katika Eusebius' Mhubiri. 5:8:4).

2) Clement wa Iskandria (153-217 B.K) - "Yohana aliyebishiwa na rafiki zake na katika hali ya kiungu akachukuliwa na Roho wa Bwana, akaandika injili ya Kiroho” (Eusebius' Mhubiri 6:14:7)

3) Justine Martyr (110-165 B.K) katika mazungumzo yake na Trypho 81:4 4) Mfuasi wa Tertullia (145-220 B.K)

b. Uandishi wa Yohana uliothibitishwa na mashahidi wa awali 1) Polycarp (70-156 B.K, iliyewekwa kama kumbu kumbu na Irene), ambaye alikuwa Askofu wa

Smyrna (155 B.K)

Page 20: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

4

2) Papias (70-146 B.K,iliyewekwa kama kumbu kumbu ya dibaji ya wale waliokuwa kinyume na Marcion toka Rumi and Eusebio), ambaye alikuwa ni Askofu wa Hierapolis katika Phyrgia na kutolewa taarifa kuwa mwanafunzi wa Mtume Yohana.

F. Sababu zilizopelekea kuutilia shaka uandishi wa kimapokeo 1. Injili iliyojiungamanisha na dhamira ya kimafunuo 2. Kiambatisho dhahili ukurasa wa 21 3. Hitilafu za uwekaji wa kumbukumbu za matukio dhidi ya mihitasari 4. Yohana hakujirejerea mwenyewe kama “ mwanafunzi kipenzi” 5. Yesu wa Yohana alitumia misamiati tofauti kuliko mihitasari

G. Kama tukisadiki kuwa alikuwa Mtume Yohana kwa hiyo tnaweza kusadiki mtu?

1. Kuwa aliandika toka Efeso ( Irene anasema “ ilitolewa injili toka Efeso”) 2. Aliiandika wakati akiwa amezeeka ( Irene anasema aliishi mpaka kwenye utawala wa Trajan 98-117

B.K) TAREHE

A. Kama tukimsadiki Mtume Yohana 1. Kabla ya mwaka 70 B.K, wakati Yerusalemu ilipoharibiwa na kamanda wa Rumi, Titus

a. Katika Yohana 5:2, “Na huko Yerusalem penye mlango wa kondoo pana birika iitwayo kwa Kiebrania Bethzatha, nayo ina matao matano.

b. Utumiaji wa kurudia cheo cha awali “ cha uanafunzi” kudokeza makundi ya Mitume c. Viashilio vya mafunuo vilivyodhaniwa baadaye sasa vimevumbuliwa katika Bahari ya Chumvi,

ambayo yanaonyesha yalikuwa ni sehemu ya istilahi ya kithiolojia ya karne ya kwanza. d. Hakuna palipotajwa uharibifu wa Hekalu na Mji waYerusalem katika mwaka wa 70 B.K e. Mwana Akiolojia mashuhuru wa Kimarekani W.F Albright anathibitisha tarehe ya kuandika injili

mwishoni mwa miaka ya 70 au mwanzoni mwa miaka ya 80 2. Baadaye katika karne ya kwanza

a. Kujitokeza kwa thiolojia ya Yohana b. Kuanguka kwa Yerusalemu hakujatajwa kwa sababu ilitokea miaka ishirini kabla c. Yohana anatumia aina ya mafunuo ya kimafungu na misisitizo d. Mapokeo ya kanisa ya awali ya

1) Irene 2) Eusebio

B. Kama tukisadiki kuwa “Yohana ni Yule wa miaka mingi” kwa hiyo tarehe itakuwa katikati ya karne ya pili. Nadharia hii ilianza kwa kukataliwa na Dionizi juu ya uandishi wa Mtume Yohana (kwa sababu za kifasihi). Eusebio ambaye alikataa uandishi wa Mtume Yohana wa ufunuo kwa sababu za kithiolojia, akahisi amempata “Yohana” mwingine katika wakati muafaka na mahali sahihi katika nukuu ya Papias wa huko Roma (Mhubiri 3:39:5,6), ambayo inaorodhesha “Yohana” wawili (1) wa kwanza Mtume na (2) wa umri mkubwa (mzee wa kanisa)

WAPOKEAJI

A. Mwanzoni kabisa iliandikwa kwa ajili ya kanisa la Jimbo la Rumi ya watu wa chini huko Asia, hasa hasa Efeso.

B. Kwa sababu ya urahisi wa ndani na kina cha uhusika wa maisha na ubinadamu wa Yesu wa Nazareti, hii ikaja kuwa injili pendwa kwa waamini wa mataifa wa Kiyunani na makundi yenye maarifa ya mafunuo.

DHUMUNI

A. Injili yenyewe inathibitisha kuwa na kusudi la uinjilist, Yohana 20:30-31

Page 21: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

5

1) Kwa viongozi wa Kiyahudi 2) Kwa viongozi wa watu wa mataifa 3) Kwa viongozi wa kwanza wa mafunuo

B. Inaelekea kuwa na msukumo wa nguvu wa kuomba radhi 1) Wafuasi waliokithiri wa Yohana Mbatizaji 2) Dhidi ya walimu wa uongo wa mwanzo wenye mafunuo (hasa kwenye dibaji); mafundisho haya ya

mafunuo ya uongo pia yakaunda kwa nyuma vitabu vingine vya Agano Jipya. a. Waefeso b. Wakolosai c. Nyaraka za kichungaji (1Timotheo, Tito, 2Timotheo) d. 1Yohana ( 1Yohana ingalitenda kazi kama barua ya utangulizi ya injili)

C. Kuna uwezekano ya kwamba maelezo ya kusudio la Yohana 20:31 laweza kueleweka kama la kutia moyo ustahimilivu wa mafundisho vile vile na Uinjilisti kwa sababu ya mwendelezo wa njeo za wakati uliopo kuelezea wokovu. Kwa maana hii Yohana, kama Yakobo, anawezakuwa akileta ulinganifu wa thiolojia ya Paulo yenye msisitizo na baadhi ya makundi ya watu wa chini toka Asia (kama vile 2 Petro 3:15-16). Inashangaza kuwa tamaduni za makanisa ya mwanzo yalimtambulisha Yohana kwa Waefeso, na sio Paulo (kama vile F. F. Bruce's Peter, Stephen, James and John: Studies in Non-Pauline Christianity, pp. 120-121).

D. Hitimisho la kazi (Yohana 21) linaonekana kujibu maswali maalumu ya kanisa la mwanzo 1) Yohana anajazilizia uwajibikaji wa mihitasari ya injili, ingawa alikuwa anajitizamisha kwenye huduma

ya Yudea, hasa hasa Yerusalemu. 2) Maswali matatu yaliyoenea katika kiambatisho, Yohana 21

a. Urejesho wa Petro b. Ukaaji wa Yohana wa muda mrefu c. Uchelewaji wa Yesu kurudi mara ya pili

E. Baadhi walimwona Yohana kama hasisitizi juu ya ushirika Mtakatifu kwa makusudi makubwa akiachana nayo na kutoweka kumbu kumbu yeyote au wakijadili maagizo yao wenyewe tofauti na fursa timilifu za kimazingira katika Yohana 3 (kwa ajili ya ubatizo) na Yohana 6 ( kwa ajili ya Ekaristi au Karamu ya Bwana)

MUHTASARI WA SURA YA YOHANA

A. Utangulizi wa kifalsafa/kithiolojia (Yohana 1:1-18) na utangulizi wa kiutendaji (Yohana 21) B. Ishara na maajabu sabu wakati wa huduma ya Yesu iliyofanyika wazi (sura ya 2-12) na utafasili wake.

1. Kubadili maji kuwa divai kwenye harusi ya Kana (Yohana 2:1-11) 2. Alimponya mototo wa Diwani huko Kapernaum (Yohana 4:46-54) 3. Alimponya mtu kiwete katika kisima cha Besthaida huko Yerusalemu (Yohana 5:1-18) 4. Aliwalisha watu 5,000 huko Kana ya Galilaya (Yohana 6:1-15) 5. Alitembea juu ya maji huko Galilaya (6:16-21) 6. Alimponya mtu aliyekuwa kipofu toka tumboni mwa mamaye huko Yerusalemu (9:1-41) 7. Akamfufua Lazaro aliyekufa huko Bethani (Yohana 11:1-57)

C. Mahojiano na mijadala na watu binafsi 1. Yohana Mbatizaji (Yohana 1:19-34; 3:22-36) 2. Wanafunzi wa Yesu

a. Andrea na Petro (Yohana 1:35-42) b. Filipo na Nathanaeli (Yohana 1:43-51)

3. Nikodemu (Yohana 3:1-21) 4. Mwanamke wa Samaria (Yohana 4:1-45) 5. Wayahudi katika Yerusalemu (Yohana 5:10-47) 6. Kusanyiko la watu huko Galilaya (Yohana 6:22-66) 7. Petro na Wanafunzi wa Yesu (Yohana 6:67-71) 8. Nduguze Yesu (Yohana 7:1-13) 9. Wayahudi huko Yerusalem (Yohana 7:14-8:59; 10:1-42)

Page 22: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

6

10. Wanafunzi wa Yesu wakiwa ghorofani (Yohana 13:1-17:26) 11. Kukamatwa kwa Wayahudi na majaribu (Yohana 18:1-27) 12. Majaribu ya Rumi (18:28-19:16) 13. Mazungumzo juu ya ufufuo wake, 20:11-29

a. Akiwa na Mariam Magdalena b. Akiwa na Mitume kumi c. Akiwa na Tomaso

14. Mjadala juu ya hitimisho la kazi, Yohana 21:1-25 15. (Yohana 7:53-8:11, habari juu ya mwanamke mzinzi, kiasilia alikuwa sio sehemu ya injili ya Yohana)

D. Ibada Fulani/ siku za sikukuu 1. Sabato (Yohana 5:9; 7:22; 9:14; 19:31) 2. Pasaka (Yohana 2:13; 6:4; 11:55; 18:28) 3. Sikukuu ya vibanda (Yohana 8:9) 4. Sikukuu ya kutabaruku (kama vile Yohana 10:22)

E. Utumiaji wa maelezo ya “mimi” 1. “mimi ndiye” (Yohana 4:26; 6:20; 8:24,28,54-59; 13:19; 18:5-6,8) 2. "mimi ni mkate wa uzima" (Yohana 6:35,41,48,51) 3. "mimi ni nuru ya ulimwengu" (Yohana 8:12; 9:5) 4. "mimi ni mlango wa kondoo" (Yohana 10:7,9) 5. "Mimi ndimi Mchungaji mwema" (1 Yohana 0:11,14) 6. "Mimi ndimi huo Ufufuo na Uzima" (Yohana 11:25) 7. "Mimi ndimi njia, kweli na Uzima" (Yohana 14:6) 8. "Mimi ndimi mzabibu wa kweli" (Yohana 15:1,5)

MZUNGUKO WA KWANZA WA USOMAJI

Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwa tafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Dhamira ya kitabu kizima 2. Aina ya fasihi iliyotumika (uwasilishaji)

MZUNGUKO WA PILI WA USOMAJI

Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwa tafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Mada ya sehemu ya kwanza ya fasihi 2. Mada ya sehemu ya pili ya fasihi 3. Mada ya sehemu ya tatu ya fasihi 4. Mada ya sehemu ya nne ya fasihi 5. N.k.

Page 23: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

7

YOHANA 1

MIGAWANYO YA AYA YA TAFSIRI ZA KISASA *

UBS4 NKJV NRSV TEV NJB Neno Alikuwa Neno la Milele Utangulizi Neno la Uzima Utangulizi Mwili 1:1-5 1:1-5 1:1-5 1:1-5 1:1-18 Ushahidi wa Yohana Nuru Ya Kweli 1:6-13 1:6-13 1:6-9 1:6-9 1:10-13 1:10-13 Neno Akawa Mwili 1:14-18 1:14-18 1:14-18 1:14 1:15 1:16-18 Ushuhuda wa Sauti toka Nyikani Ushuhuda Ujumbe wa Ushahidi Yohana wa Yohana Yohana wa Yohana Mbatizaji Mbatizaji 1:19-28 1:19-28 1:19-23 1:19 1:19-28 1:20 1:21a 1:21b 1:21c 1:22a 1:22b 1:23 1:24-28 1:24-25 1:26-27 1:28 Mwana Kondoo Mwana Kondoo Mwana kondoo Wa Mungu wa Mungu wa Mungu 1:29-34 1:29-34 1:29-34 1:29-31 1:29-34 1:32-34 Wanafunzi wa Wanafunzi wa Ushuhuda wa Wanafunzi wa Wanafunzi Kwanza Kwanza Wanafunzi wa kwanza wa wa Kwanza Kwanza wa Yesu Yesu 1:35-42 1:35-42 1:35-42 1:35-36 1:35-39 1:37-38a 1:38b 1:39 1:40-42a 1:40-42 1:42b Wito wa Filipo na Yesu Anaita Nathanaeli Nathanaeli Filipo na Wa Ufilipi Nathanaeli

Page 24: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

8

1:43-51 1:43-51 1:43-51 1:43-45 1:43-51 1:46a 1:46b 1:47 1:48a 1:48b 1:49 1:50-51

* Ingawa hazijavuviwa, migawanyo ya aya ndiyo ufunguo wa kuelewa na kufuatilia kusudio la asili la mwandishi. Kila tafsiri ya kisasa imegawanya na kufanya muhtasari wa aya. Kila aya ina mada kuu, kweli au wazo. Kila toleo limebeba hiyo mada kwa namna yake ya pekee. Unaposoma maandiko ya mwandishi jiulize ni tafsiri ipi inawiana na uelewa wako wa somo na mgawanyo wa mistari. Katika kila sura lazima tusome Biblia kwanza na kujaribu kutambua somo (aya), kisha tulinganishe na matoleo ya kisasa. Ni pale tunapoelewa kusudi la asili la mwandishi kwa kufuata mantiki yake na jinsi alivyojieleza tunaielewa kwa Biblia kiukweli. Ni mwandishi wa asili tu aliyevuviwa —wasomaji hawana haki ya kurekebisha ujumbe. Wasomaji wa biblia wana wajibu wa kutumia ukweli uliovuviwa kwenye siku na maisha yao. Fahamu kwamba maneno yote ya kiufundi na vifupisho vimefafanuliwa kwa kirefu kwenye nyaraka zifuatazo: Maelezo Fasaha Ya Muundo Wa Sarufi Za Kiyunani (Brief Definitions of Greek Grammatical Structure),Uhakiki Wa Tofauti Za Kiandishi (Textual Criticism),Ufafanuzi na Maelezo ya Kimaandiko (Glossary).

MZUNGUKO WA TATU WA USOMAJI KUFUATILIA KUSUDIO LA ASILI LA MWANDISHI KATIKA NGAZI YA AYA Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwatafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Aya ya kwanza 2. Aya ya pili 3. Aya ya tatu 4. N.k

UTAMBUZI WA KI-MUKTADHA KWA MISTARI YA 1-18

A. Mhutasari wa Kitheolojia wa ushairi/ wimbo wa kumsifu Mungu/ kanuni za imani 1. Umilele, utakatifu, muumbaji, Kristo mwokozi, Yohana 1: 1-5 (Yesu kama Neno) 2. Ushahidi wa kinabii juu ya Kristo, Yohana 1:4-5, 7-8, 15 ( Yesu kama Nuru) 3. Mungu kumfunua Kristo katika umbo la mwili, Yohana 1:10-18 (Yesu kama Mwana)

B. Muundo wa kitheolojia wa Yohana 1:1-18 na dhamira ya mara kwa mara

1. Yesu alikuwepo kabla akiwa na Mungu Baba (Yohana 1:1a) 2. Mungu alikuwa katika uhusiano wa karibu na Mungu Baba (Yohana 1:1b, 2, 18c) 3. Yesu anashiriki asili yake na Mungu Baba (Yohana 1:1c, 18b) 4. Maana ya Mungu Baba ya ukombozi na ukubalifu (Yohana 1:12-13) 5. Umbo la mwili, Mungu kuwa mwanadamu (Yohana 1:9 14) 6. Ufunuo, Mungu aliyefunuliwa kamili na uelewa (Yohana 1: 18d)

C. Mrejesho wa Kiebrania na Kiyunani wa neno logos

1. Historia ya Kiebrania a. Nguvu ya neno lililonenwa (Isa. 55:11; Zab. 33:6; 107: 20; 147: 15,18), kama katika Uumbaji

(Mwa. 1:3,6,9,11,14,20,24,26,29) na Baraka za kizee(Mwa. 27;1ff; 49:1) b. Mithali 8:12-23 mfano wa “Hekima” kama uumbaji wa kwanza wa Mungu na nguvu za asili za

uumbaji wote (Zab. 33:6 na usiyo wa sheria za kanisa Hekima Ya Suleimani, 9:9)

Page 25: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

9

c. Targums (tafsiri za Kiarama na fasiri) linakaa badala ya kifungu “ Neno la Mungu” kwa neno logos kwa sababu ya usumbufu wake pamoja na maneno ya elimu ihusuyo asili ya mwanadamu

2. Mrejesho wa Kiyunani a. Heracleitus – ulimwengu ulikuwa katika mfululizo wa mabadiliko; utakatifu usioathiriwa na mtu

binafsi na neno logos lisilobadilika likashikamana kwa pamoja na kulinda mchakato wa ubadilikaji b. Pilato - logos neno lisilo athiriwa na hisia za mtu binafsi na lisilo badilika lilizitunza sayari katika

uelekeo na kubainisha majira c. Uvumilivu- logos ilikuwa “sababu ya kidunia” au kiongozi, lakini ilikuwa ni nusu mtu d. Philo – alitoa mfano wa maana ya logos kama “Kuhani Mkuu ambaye anaielekeza nafsi ya

mwanadamu mbele ya Mungu,” au “daraja kati ya mwanadamu na Mungu,” au “mkombo atumiwao na Rubani kuongoza vitu vyote ulimwenguni” (kosmocrater-watawala wa giza)

D. Vitu vya asili vilivyoboreshwa na mifumo ya kitheolojia/falsafa ya mafunuo ya karne ya pili B.K. 1. Asili ya uhai (umilele) pande mbili zilizo kinyume kati ya Roho na vitu 2. Vitu ni viovu na vikaidi; Roho ni kitu kizuri 3. Mfumo wa mafunuo ulidai mtiririko wa kiwango cha kimalaika (aeons) kati ya ukuu, Mungu mwema

na mungu mdogo zaidi ambaye aliweza kuunda kitu. Kisha baadhi walidai kwamba huyo mungu mdogo zaidi alikuwa YHWH wa Agano la Kale (kama Marcion)

4. Wokovu ulikuja kwa a. maarifa ya siri au neno la siri ambalo lilimruhusu mtu kupitia viwango hivi vya kimalaika katika

njia zao na muungano wao kwa Mungu b. dalili ya maisha ya utakatifu katika wanadamu wote, ambao hawana utambuzi hadi wapokee

maarifa ya siri c. mtu maalumu wa nguvu za asili wa ufunuo ambaye anayaleta maarifa haya ya siri kwa

mwanadamu (Roho ya Kristo) 5. Mfumo huu wa fikra ulitetewa na Uungu wa Yesu, lakini ulikataliwa na umbo lake halisi la mwili wa

kudumu na kiini cha nafasi yake ya ukombozi

E. Mpangilio wa Kithiolojia 1. Yohana 1:1-18 ni jaribio la kuhusianisha fikra zote za Kiebrania na Kiyunani kwa kutumia neno

logos. 2. Uasi wa wafuasi wa mafunuo ni mrejesho wa kifalsafa kuelekea muundo huu wa utangulizi mkuu

kuilekea Injili ya Yohana. Yohana 1 imeweza kuwa barua iliyoenea kuilekea Injili. Mfumo wa Kitheolojia wa fikra uliitwa “mafunuo” haukujulikana katika maandishi hadi karne ya pili, hadi pale yaliyopatikana mawazo ya kwanza ya Kimafunuo kwenye Magombo ya Bahari ya Chumvi na katika Philo.

3. Injili zilizofupishwa (hasa Marko) zimeuficha Uungu wa Yesu (siri ya Ki-masihi) hadi baada ya Karvari, lakini Yohana, na maandishi mengi baadaye, yaliukuza ujumbe muhimu wa Yesu kama Mungu kamili na mwanadamu kamili (Mwana wa Adamu, kama vile Ezek. 2:1 na Dan. 7:13) katika sura ya kwanza.

F. Tazama Mada Maalumu: Yohana 1 ikilinganishwa na 1 Yohana 1

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 1:1-5 1Hapo mwanzo kulikuwakoo na Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa kwa Mungu. 2Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. 3Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. 4Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. 5Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza.

Page 26: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

10

1:1 “Hapo mwanzo” Hii inaakisi Mwanzo 1:1 na pia inatumika katika 1 Yohana 1:1 kama marejeo ya umbile la mwili. Inawezekana kwamba Yohana 1 ilikuwa barua ilikuwa ni kitangulizi cha Injili. Yote yalihusika na mafunuo. Yohana 1:1-5 ni ukubalifu wa uwepo wa kabla wa Uungu wa Yesu Kristo kabla ya uumbaji (kama vile Yohana 1:15; 8:56-59; 16:28; 17:5; 2 Kol. 8:9; Fil. 2:6-7; Kol. 1:17; Ebr. 1:3; 10:5-9). Agano Jipya linaelezwa kama

1. Uumbaji mpya, ambao haukuharibiwa na Anguko ( yaani., Mwa. 3:15 uliokamilishwa kwa ajili ya mwanadamu)

2. utekaji mpya (Nchi ya Ahadi) 3. utokaji mpya (unabii uliotimizwa) 4. Musa mpya (mwasilishaji wa sheria) 5. Yoshua mpya (kama vile Ebr. 4:8) 6. muujiza mpya wa maji (kama vile Waebrania 3-4) 7. manna mpya (Yohana 6)

na nyingine nyingi zaidi, hasa katika Waebrania.

MADA MAALUMU: ARCHĒ

Neno la Kiyunani Archē linamaanisha "mwanzo" au "asili" ya kitu. 1. mwanzo wa mpangilio ulioumbwa (kama vile. Yohana 1:1; Ebr. 1:10) 2. mwanzoni mwa injili (kama vile Mko 1:1; Flp. 4:15; 2 The. 2:13; Ebr. 2:3; 1 Yohana 1:1) 3. mwanzo wa jicho la kwanza la ushahidi (kama vile Luka 1:2) 4. mwanzo wa dhambi (miujiza, kama vile Yohana 2:11) 5. mwanzo wa mafundisho (kama vile Ebr. 5:12) 6. mwanzo wa udhihirisho uliojikita katika kweli ya injili (kama vile Ebr. 3:14) 7. mwanzo, Kol. 1:18; Ufu. 3:14

Ilikuja kutumika juu ya "utawala" au "mamlaka" 1. juu ya wanadamu rasmi watawalao

a. Luka 12:11 b. Luka 20:20 c. Warumi 13:3; Tito 3:1

2. juu ya mpangilio wa mamlaka a. Warumi 8:38 b. 1 Kor. 15:24 c. Efe. 1:21; 3:10; 6:12 d. Kol. 1:16; 2:10,15 e. Yuda 1:6

◙ “kulikuwako” (mara tatu) Hii ni njeo ya wakati usiotimilifu (kama vile Yohana 1:2, 4, 10) ambao uliangalia juu ya uwepo endelevu katika wakati uliopita. Huu wakati unatumika kuonyesha Logos kuwepo kabla (kama vile Yohana 8:57-58; 17: 5:24; Kor. 8:9; Kol. 1:17; Ebr. 10:5-7).Linaundwa na njeo za wakati timilifu wa Yohana 1: 3,6 na 14. ◙ “Neno” Neno la Kiyunani logos linarejea ujumbe, na sio neno moja tu. Katika mazingira haya ni kichwa cha ufupisho ambacho kilitumiwa na Wayunani kuueleza “ulimwengu wa kimantiki” na Waebrania kama watu wanaoshabihiana na “Hekima.” Yohana alilichagua hili kutetea kwamba Neno la Mungu linahusiana na mambo yote yaani mtu na ujumbe. Angalia Utambuzi wa muktadha, C. ◙ “Neno alikuwako kwa Mungu” “alikuwako” ingeweza kufasiriwa “ana kwa ana.” Inafafanua ushirika wa karibu. Pia moja kwa moja inagusia hadi dhana ya asili ya Uungu mmoja na udhihirisho wa milele wa nafsi ya tatu (tazama Mada Maalumu: Utatu). Agano jipya linatetea usemi unaodai kwamba Yesu ametenganishwa na Baba, lakini pia Yeye ni mmoja na Baba.

Page 27: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

11

◙ “naye Neno alikuwa Mungu” Kitenzi hiki ni njeo ya wakati usiotimilifu kama katika Yohana 1:1a. Hakuna kifungu (ambacho kinamtambulisha muhusika, tazama F.F Bruce, Answers to Questions, uk. 66) pamoja na Theos, lakini nafasi ya Theos inaondolewa kwanza katika kifungu cha Kiyunani kwa msistizo. Mstari huu na Yohana 18 ni semi zenye nguvu juu ya utimilifu wa Uungu wa Logos iliyokuwepo kabla (kama vile Yohana 5:18; 8:58; 10:30; 14:9; 17:11; 20:28; Rum. 9:5; Ebr. 1:8; 2 Pet. 1:1) Yesu ni Mungu kamili kama mwanadamu kamili (kama vile 1 Yohana 4:1-3). Yeye si sawa na Mungu Baba lakini Yeye ni sawa na asili ya Uungu kama Baba. Agano Jipya linautetea Uungu kamili wa Yesu wa Nazareti, lakini linalinda tofauti ya utu wa Mungu Baba. Asili ya Mungu mmoja inasisitizwa katika Yohana 1:1; 5:18; 10:30; 34-38; 14:9-10; na 20-28, ambapo tofauti zao zimesisitizwa katika Yohana 1:2, 14,18; 5:19-23; 8:28; 10:25, 29;14:11, 12, 13, 16.

1:2 Huu mstari ni sambamba na Yohana 1:1 na inasisitiza tena ukweli wenye kushutua katika nuru ya imani ya Mungu mmoja kwamba Yesu, alizaliwa mnamo 5-6 k.k., mara nyingi amekuwa na Baba na, kwa hiyo ni Mungu.

1:3 “Vyote vilifanyika kwa huyo” Logos ilikuwa asili ya Baba ya uumbaji wa vyote vionekanavyo na visivyoonekana (kama vile Yohana 1:10; 1 Kor. 8:6; Kol. 1:16; Ebr. 1:2). Hii ni sawa sawa na kazi ifanywayo na hekima katika Zab. 104:24 na Mit. 3:19; 8:12-23 (katika Waebrania “hekima” ni nomino jinsia ya kike)

◙ “wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika" Huu ni ukanushaji wa mafundisho ya ufunuo wa uongo juu ya dahari ya kimalaika kati ya ukuu, mungu mwema, na kiumbe kidogo zaidi cha kiroho kilichoumbwa, kitu kilichokuwepo kabla (tazama Mitazamo ya ndani D).

1:4 “Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima” Kifungu hiki kinasisitiza “uzima” ambao kwa huo unatokana na Mwana, Neno. Yohana analitumia neno hili zoe, kuyarejea maisha ya ufufuo, maisha ya milele, maisha ya Kimungu (Yohana 1:4;3:15, 36; 4:14, 36; 5:24, 26, 29,39, 40; 6:27, 33, 35, 40, 47, 48, 51, 53, 54, 63,65 n.k). Neno lingine la Kiyunani lihusulo “uzima,”bios lilitumika kidunia, maisha ya kibaiyolojia (1 Yohana 2:16).

◙ “nao ule uzima ilikuwa nuru ya watu” Nuru ni tafsida ya kawaida aliyoitumia Yohana katika kweli na maarifa ya Mungu (kama vile Yohana 3:19; 8:12;9:5; 12:46). Inafahamika kuwa uzima ulikuwa kwa wanadamu wote (uwezekano uliodokezwa katika Zab. 36:5-9)! Nuru na giza pia zilikuwa ni mawazo ya kawaida katika Magombo ya Bahari ya Chumvi. Mara nyingi Yohana anajieleza mwenyewe katika mfumo wa (uliotofautisha) maneno na namna mbali mbali.

1:5 “Nayo nuru yang’aa gizani” Huu ni wakati uliopo, unaomaanisha tendo endelevu. Yesu amekuwapo mara kwa mara, lakini sasa anadhihirishwa ulimwenguni (Yohana 12:8;9:5; 12:46). Katika Agano la Kale udhihirisho wa mwili au wa kibinadamu wa Mungu mara nyingi ulitambulishwa kupitia malaika wa Bwana(kama vile Mwa. 16:7-13; 22:11-15; 31:11, 13;48:15-16; Kutoka 3,2,4; 13:21; 14:19; Amu. 2:1; 6:22-23; 14; 13:22-23; Zek. 3:1-2. Baadhi wanadai kwamba hii ni Logos ya umbo la mwili lililokuwepo kabla.

MADA MAALUMU: MALAIKA WA BWANA

Ni dhahiri kwamba Mungu alijidhihirisha Mwenyewe kimwili katika muundo wa mwanadamu kwenye. ;Agano la Kale. Swali juu ya Utatu Mtakatifu linakuja mtu gani miongoni mwa Utatu aliyeikamilisha kazi hii. Tangu Mungu Baba (YHWH) na Roho Wake kimwili si dhahiri, inaonekana kuwepo na uwezekano wa kwamba udhihirisho huu ni Masihi aliyekuwepo kabla kimwili. Ili kufafanua ugumu alioupata mtu katika kujaribu kutambua udhihilisho wa Mungu katika hali ya kimwili kutoka mfanano wa kimalaika orodha ifuatayo ina ufafanuzi.

1. yeye malaika wa Bwana kama malaika (mara nyingi "Malaika Wake," "Malaika," "Malaika," "Malaika wa Mungu," hata "nguzo") a. Mwa. 24:7,40 b. Kut. 23:20-23; 32:34 c. Nah. 22:22

Page 28: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

12

d. Fal. 5:23 e. 2 Sam. 24:16 f. 1 Nya. 21:15-30 g. Zek. 1:12-13

2. malaikawa Bwana kujidhihilisha katika hali ya kimwili a. Mwa. 16:7-13; 18:1-33; 22:11,15; 31:11,13; 48:15-16 b. Kut. 3:2,4; 14:19 (13:21) c. Fal. 2:15; 6:22-24; 13:3-23 d. Hos. 12:3-4 e. Zek. 3:1-5 f. Mdo. 7:30,35,38

Ni muktadha tu unaoweza kutofautisha kati ya chaguzi mbili

NASB, NKJV “wala giza halikuiweza” NRSV “nalo giza halikuweza kuushinda” TEV “wala giza halikuweza kulikomesha” NJB “na giza lisingeweza kulitiisha” Mzizi wa maana ya neno hili (katalambanō) ni “kukumbatia.” Hivyo, inaweza kumaanisha aidha (1) kufumbata ili kushinda (kama vile Mt. 16:18) au (2) kufumbata ili kufahamu au kuelewa. Yohana angeliweza kutumia utata huu kupendekeza yote. Injili ya Yohana inabainishwa (mf. “kuzaliwa mara ya pili na/au “kuzaliwa kutoka juu, “ 3:3 na “wingu” na/au roho” 3:8). Kitenzi (katalambanō) kinaonekana mara mbili tu katika maandiko yaYohana (utokeaji wake katika Yohana 8:4,5 sio wa asilia). Katika Yohana 1:5 giza haliwezi kushinda na katika 12:35 giza huikuikataa nuru (Yesu/injili) litapatilizwa. Kukataliwa husababisha machafuko; upokeaji husababisha ibada! Manfred T. Brauch, Abusing Scripture, ukur. 35 anabainisha hali ya mwanadamu.

1. upotevu, Luka 15 2. giza, Yohana 1:15 3. uadui, Rum. 5:10 4. utengano, Efe. 2:15-17 5. kutomcha Mungu, Rum. 1:18 6. kujitenga na maisha ya Kimungu, Efe. 4:17-18 7. ufupisho mzuri zaidi wa dhambi ya mwanadamu unapatikana katika Rum. 1:18:3-23

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 1:6-8 6Palitokea mtu, ametumwa toka kwa Mungu, jina lake Yohana. 7Huyo alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeye. 8Huyo hakuwa ile nuru, bali alikuja ili aishuhudie ile nuru.

1:6-8 Mistari hii na Yohana 1:15 (ilitengwa kwenye mabano kwa ajli ya kurejea) inachukuwa kumbu kumbu ya ushahidi wa Yohana Mbatizaji hadi kwa Yesu. Alikuwa nabii wa Agano la Kale. Ni vigumu kuiweka mistari hii katika mfumo wa kiushairi. Huu ni mjadala mpana baina ya wasomi kama kweli ushairi ni utangulizi au lugha ya mjazo Yohana Mbatizaji alikuwa nabii wa mwisho wa Agano la Kale (katika dhana ya ujumbe na mtazamo wake). Alikuwa mtangulizi aliyesemewa katika Mal. 3:1 na 4:5 (kama vile Yohana 1:20-25). Mtume Yohana anaweza kuwa ameingizwa kwenye Yohana 1:6-8 kwa sababu ya migogoro ya kale iliyoshamiri kipindi cha Yohana Mbatizaji (kama vile Luka 3:15; Matendo 18:25; 19:3). Yohana, akiandika baadaye kuliko waandishi wengine wa Injili, alikuona kukua kwa tatizo hili. Inafurahisha kuona kwamba Kristo anaelezwa katika njeo za wakati usiotimilifu (kuwepo kabla) ambapo Yohana anaelezwa katika kauli (anadhihirishwa kwa wakati) na vitenzi vya wakati timilifu (tukio la kihistoria lenye matokeo ya kudumu) vitenzi (kama vile Yohana 1:6). Yesu amekuwako wakati wote.

Page 29: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

13

1:7 “wote wapate kuamini kwa yeye” Hii ni ibara yenye kusudi. Injili ya Yohana, kama Injili zingine (Mkristo wa namna ya pekee), ni uinjilisti wa vijitabu vidogo vidogo. Huku ni kujitolea kwa ajabu juu ya wokovu kwa wote ambao wamekuwa wakitembea kwa imani katika Kristo, ambaye ni nuru ya ulimwengu (kama vile Yohana 1:12; Yohana 3:16; 4:42; 20:31; 1 Tim. 2:4; tito 2:11; 2 Pet. 3:9; 1 Yohana 2:1; 4:14). 1:7,12 “kuamini” kitenzi hiki kimetumika mara 78 katika Injili ya Yohana, mara 24 katika barua za Yohana. Inatia shauku kwamba Injili ya Yohana kamwe haikutumia mfumo wa nomino, ni kitenzi tu. Imani si mwitikio wa akili au hisia za awali, bali kimsingi ni hiari ya moyo. Neno hili la Kiyunani linatafsiriwa na maneno matatu ya Kiingereza: kuamini, imani na kusadiki. Linafanana na neno “kumpokea Yeye” (kama vile Yohana 1:11), na “kumwamini Yeye” (kama vile Yohana 1:12). Wokovu ni uhuru katika neema ya Mungu na kazi iliyomalizwa na Kristo, lakini inanapaswa kupokelewa na watu wote. Wokovu ni uhusiano wa agano ukiwa na vipaumbele pamoja na majukumu.

MADA MAALUMU: KUSADIKI, KUAMINI, IMANI

A. Hili ni aina ya neno muhimu katika Biblia (kama vile Ebr. 11:1,6). Lilikuwa ni somo la Yesu katika mahubiri ya awali (kama vile Mk. 1:15). Kiwastani kuna mahitaji mapya mawili ya agano: toba na imani (Mk. 1:15; Mdo. 3:16, 19; 20:21)

B. Asili na historia yake ya maneno haya 1. Neno “imani” katika Agano la Kale lilimaanisha mtiifu, mwaminifu au mwaminifu wa kutumainiwa

na yalikuwa ni maelezo ya asili ya Mungu na si yetu. 2. Linatokana na neno la Kiebrania (emun, emunah, BDB 53, yaani., Hab. 2:4), ambalo mwanzo kabisa

lilimaanisha “kuwa na uhakika au imara.” Kuitumikia imani ni a. Kumkaribisha mtu (yaani., imani binafsi, sadiki, kama vile. E.1.hapo chini) b. Kuamini imani kuhusu mtu (yaani., maandiko, kama vile. E.5.hapo chini) c. Kuishi maisha kama ya mtu huyo (yaani., mfano wa Kristo)

C. Matumizi yake katika Agano la Kale Lazima isisitiziwe kuwa imani ya Ibrahim ilikuwa si kwa ajili ya Masiha ajaye, lakini ni kwa ahadi ya Mungu ya kwamba atapata mototo na uzao (kama vile Mwa. 12:2-5; 17:4-8; Rum. 4:1-5). Ibrahimu aliikubali ahadi hii kwa kumwamini Mungu (angalia Mada Maalumu: kuamini, amini, imani na uaminifu katika Agano la Kale) na neno lake. Bado anamashaka na kuhusika juu ya ahadi hii, ambayo ilimchukua miaka kumi na mitano kutimizwa. Imani yake isiyo kamili, hata hivyo, alikubaliwa na Mungu. Mungu anapenda kufanya kazi na mwanadamu mwenye mapungufu anayejongea kwake na katika ahadi zake kwa imani, hata kama kwa kipimo cha chembe ya haradari (kama vile Mt. 17:20) au imani mchanganyiko (kama vile Marko 9:22-24)

D. Matumizi yake katika Agano Jipya Neno “kuamini” linatoka katika neno la Kiyunani pisteuō au nomino pistis, ambayo yanatafasiliwa kwa Kiingereza “kuamini” “amini” au “imani.” Kwa mfano, nomino haijitokezi katika injili ya Yohana, lakini kitenzi kinatumika mara nyingi. Katika Yohana 2:23-25 kuna uwalakini katika uhalisia wa uwajibikaji wa kundi kwa Yesu wa Nazareti kama Masiha. Mifano mwingine wa matumizi ya kubabiya ya neno hili “kuamini” ni katika Yohana 8:31-59 na Mdo. 8:13, 18-24. Imani ya kweli ya Kibiblia ni zaidi ya uwajibikaji wa awali. Lazima ifuatishwe na mchakato wa uwanafunzi (kama vile Mt. 13:20-23, 31-32; 28:19-20)

E. Matumizi yake ikiwa na vivumishi 1. eis inamaanisha “ndani ya.” Muundo huu wa kipekee unasisitizia waumini kuweka imani zao kwa

Yesu a) ndani ya jina lake (Yohana 1:12; 2:23; 3:18; 1 Yohana 5:13) b) ndani yake (Yohana 2:11; 3:15,18; 4:39; 6:40; 7:5,31,39,48; 8:30; 9:36; 10:42; 11:45,48;

12:37,42; Mt. 18:6; Mdo 10:43; Flp. 1:29; 1 Petr. 1:8)

Page 30: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

14

c) ndani yangu (Yohana 6:35; 7:38; 11:25,26; 12:44,46; 14:1,12; 16:9; 17:20) d) ndani ya mwanaye (Yohana 3:36; 9:35; 1 Yohana 5:10) e) ndani ya Yesu (Yohana 12:11; Mdo. 19:4; Gal. 2:16) f) ndani ya nuru (Yohana 12:36) g) ndani ya Mungu (Yohana 14:1)

2. ev inamaanisha “katika” kama ilivyo katika Yohana 3:15; Marko 1:15; Mdo 5:14 3. epi ikimaanisha “katika” au “juu ya” kama ilivyo katika Mt. 27:42; Mdo 9:42; 11:17; 16:31; 22:19;

Rum. 4:5,24; 9:33; 10:11; 1 Tim. 1:16; 1 Petro. 2:6 4. uhusika wa mahali usio na kivumishi kama ilivyo katika Yohana 4:50; Gal.3:6; Mdo. 18:8; 27:25;

1Yoh. 3:23; 5:10 5. hoti likimaanisha “kuamini kwamba,” inatoa kilichomo kama kile kinachotakiwa kuaminiwa

a) Yesu ni Mtakatifu wa Mungu (Yohana 6:69) b) Yesu ni Mimi ndiye (Yohana 8:24) c) Yesu katika Baba na Baba ndani yake (Yohana 10:38) d) Yesu ni Masiha (Yohana 11:27; 20:31) e) Yesu ni mwana wa Mungu (Yohana 11:27; 20:31) f) Yesu alitumwa na Babaye (Yohana 11:42; 17:8,12) g) Yesu ni wamoja na Babaye (Yohana 14:10-11) h) Yesu alikuja toka kwa Babaye (Yohana 16:27,30 i) Yesu anajitambulisha mwenyewe katika jina la Agano la Babaye “Mimi ndiye” (Yohana 8:24;

13:19) j) Tutaishi naye (Rum. 6:8) k) Yesu alikufa na kufufuka tena (1 The. 4:14)

1:8 Inawezekana Mtume Yohana, akiandika baadaye kuliko waandishi wengine wa Injilii, alitambua tatizo lililoshamiri miongoni mwa wafuasi wa Yohana Mbatizaji ambao hawakuwahi kumsikia au kumkubali Yesu (kama vile Matendo 18:25-19:7).

MADA MAALUMU: MASHUHUDA KUMHUSU YESU

Nomino (marturia) na kitenzi chake (martureō) “ushuhuda” ni maneno muhimu katika Yohana. Kuna mashuhuda wengi juu ya Yesu.

1. Yohana Mbatizaji (kama vile Yohana 1:7,8,15; 3:26,28; 5:33) 2. Yesu mwanyewe (kama vile Yohana 3:11; 5:31; 8:13-14) 3. Mwanamke msamaria (kama vile Yohana 4:39) 4. Baba Mungu (kama vile Yohana 5:32,34,37; 8:18; 1 Yohana 5:9) 5. Maandiko (kama vile Yohana 5:39) 6. Kusanyiko la watu kwenye ufufuo wa Lazaro (kama vile Yohana 12:17) 7. Roho Mtakatifu (kama vile Yohana 15:26-27; 1 Yohana 5:10,11) 8. Wanafunzi wa Yesu (kama vile Yohana 15:27; 19:35; 1 Yohana 1:2; 4:14) 9. Mwandishi mwenyewe (kama vile Yohana 21:24)

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 1:9-13 9Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu. 10Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua. 11Alikuja kwake wala walio wake hawakumpokea. 12Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; 13waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.

Page 31: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

15

1:9 “Kulikuwako Nuru halisi” Hili ni neno lenye maana ya “kweli” katika mantiki ya uhalisia, sio kinyume cha uwongo. Hii inaweza kuhusiana na wanathiolojia wa Kikristo wa karne ya kwanza. Hiki ni kivumishi cha kawaida katika maandiko ya Yohana (kama vile Yohana 4:23, 37, 6:32; 7:28; 15:1; 17:3; 19:35; na 1 Yohana 2:8; 5:20 na mara kumi katika Ufunuo). Tazama Mada Maalumu: Ukweli (dhana) katika Maandiko ya Paulo na Mada Maalumu: Matumizi ya Paulo ya Kosmos (ulimwengu). Yesu ni nuru ya ulimwengu (kama vile Yohana 3:19; 8:12; 9:5; 12:46; 1 Yohana 1:5,7; 2:8,9,10). Waamini hawaiakisi nuru Yake (kama vile Flp. 2:15). Hii ni tofauti kubwa na giza halisi ambalo liko katika mpangilio wa uumbaji au kwa sababu ya uasi wa

1. wanadamu 2. malaika

◙ “akija katika ulimwengu” Yohana amelitumia fungu hili mara kwa mara kumrejea Yesu pale alipotoka mbinguni, kwenye ulimwengu wa kiroho, na kuingia katika ulimwengu wa kimwili kwa wakati na muda (kama vile Yohana 6:14; 9:39; 11:27; 12:46; 16:28). Katika msitari huu inaonyesha kurejea juu ya umbile la kibinadamu la Yesu. Hii ni moja ya pande mbili za fasihi ya Yohana ya kawaida (yaani., juu dhidi ya chini). NASB “amwangaziaye kila mtu” NKJV “amtiaye nuru kila mtu,” NRSV “na kuwaangazia watu wote” TEV “umulikao kwa watu wote” NJB “atoaye nuru kwa kila mtu” Kifungu hiki kinaweza kuelezwa katika njia mbili. Kwanza, kwa kufikiri juu ya mpangilio wa utamaduni wa Kiyunani, ambao unarejea juu ya nuru iliyofunuliwa ndani ya kila mtu, mg’ao wa Kimungu. Hii ndio njia waitumiayo Watu wa jamii ya Kikiristo kuutafsiri mstari huu.Hata hivyo, wazo hili halionekani kamwe katika Yohana. Kwa Yohana, “nuru” hufunua uovu wa mwanadamu (kama vile Yohana 3:19-21). Pili, inaweza kuwa harejei juu ya ufunuo wa asili (ambapo Mungu anajulikana kupitia asili [kama vile Zab. 19:1-5; Rum. 1:19-20] au kwa maana ya ndani ya uadilifu [Rum. 2:14-15]), lakini kuliko Mungu kujitolea katika kutoa mwangaza na wokovu kupitia Yesu, nuru halisi ya kipekee. 1:10 “akija katika ulimwengu” Yohana analitumia neno kosmos katika njia tatu tofauti,

1. ulimwengu unao onekana (Yohana 1:10, 11; 11:9; 16:21; 17:5,24; 21:25) 2. wanadamu wote (Yohana 1:10,29; 3:16, 17; 4:42; ; 6:33; 12:29,46-47; 18:20) 3. jamii ya wanadamu walioanguka iliyounganishwa na kufanya kazi tofauti na Mungu (Yohana 7:7; 15:18-

19; 1 Yohana 2:15; 3:1, 13) Katika mazingira haya #2 inatumika. Tazama Mada Maalumu katika Yohana 14:17

◙ “wala ulimwengu haukumtambua” Si Mataifa yaliyoanguka wala taifa teule la Kiyahudi lililomtambua Yesu kama Masihi aliyehaidiwa. Neno “tambua” linaakisi nahau ya Kiebrania ya uhusiano wa karibu sana kuliko wasomi wanavyodai kuhusu uhalisi (kama vile Mwa. 4:1; Yer. 1:5).

MADA MAALUM: KUJUA (hasa kwa kutumia mifano ya Kumbukumbu la Torati kama kielelezo)

Neno la Kiebrania “kujua”(BDB 393) lina maana kadhaa (mazingira ya kimaana) katika Qal.

1. Kuelewa mema na mabaya - Mwa. 3:22; Kumb. 1:39; Isa. 7:14-15; Yohana 4:11 2. Kujua kwa kuelewa - Kumb. 9:2,3,6; 18:21 3. Kujua kupitia mazoea - Kumb. 3:19; 4:35; 8:2,3,5; 11:2; 20:20; 31:13; Yos. 23:14 4. kufikiri - Kumb. 4:39; 11:2; 29:16 5. kujua kibinafsi

a. mtu - Mwa. 29:5; Kut. 1:8; Kumb. 22:2; 28:35,36; 33:9 b. mungu -Kumb. 11:28; 13:2,6,13; 28:64; 29:26; 32:17 YHWH - Kumb. 4:35,39; 7:9; 29:6; Isa. 1:3;

Page 32: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

16

56:10-11 c. kizinaa - Mwa. 4:1,17,25; 24:16; 38:26

6. ujuzi wa kujifunza - Isa. 29:11,12; Amosi 5:16 7. kuwa mwenye hekima - Kumb. 29:4; Mit. 1:2; 4:1; Isa. 29:24 8. maarifa ya Mungu

a. kwa Musa - Kumb. 34:10 b. kwa Israeli- Kumb. 31:21,27,29

1:11 “Alikuja kwake, walio wake hawakumpokea” Neno “Kwake” linatumika mara mbili katika Yohana 1:11. Muundo wa kwanza wa kisarufi ulioko kwenye hali ya uwingi usio na shamirisho na unarejea juu ya (1) uumbaji wote au (2) Jiografia ya kuelekea Yudea au Yerusalemu. Pili ni hali ya wingi ilioko kwenye jinsia ya kiume na inarejea kwa watu wa Kiyahudi.

1:12 “Bali wote walimpokea” Hii inaonyesha sehemu ya mwanadamu katika wokovu (kama vile Yohana 1:16). Wanadamu wanapaswa kuitikia kwenye neema ya Mungu aliyoitoa katika Kristo (kama vile Yohana 3: 16; Rum. 3:24; 4:4-5; 6:23; 10:9-13; Efe. 2:8-9). Hakika Mungu ni mwenye enzi Yeye ameanzisha amri ya uhusiano na binadamu aliyeanguka. Mwanadamu aliye anguka anapaswa kutubu, kuamini, kuitikia, na kustahimili katika imani. Hii dhana ya “kupokea” kithiolojia inafanana na neno “kuamini” na “kutubu, ” ambapo inamaanisha ungamo la watu wote katika Yesu kama Kristo (kama vile Mt. 10:32; Luka 12:8; Yohana 9:22; 12:42; 1 Tim. 6:12; 1 Yohana 2:23; 4:15). Wokovu ni zawadi ambayo inapaswa kupokelewa na kukubaliwa. Wale “waliompokea” Yesu (1: 12) walimpokea Baba ambaye alimtuma Yeye (kama vile Yohana 13: 20; Mt. 10:40). Wokovu ni uhusiano wa mtu binafsi na Mungu wa Utatu!

◙ “aliwapa uwezo” Hili ni neno (yaani., exousia) linaweza kumaanisha (1) utawala wa haki au (2) haki au kipaumbele (kama vile Yohana 5:27; 17:2; 19:10,11). Kupitia uwana wa Yesu na wito wa Kimungu, mwanadamu aliye anguka sasa anaweza kumfahamu na kumkubali Yeye kama Mungu na Baba.

◙ “wa kufanyika watoto wa Mungu” Waandishi wa Agano la Kale kwa uthabiti walitumia stiari za kijamii kuueleza Ukristo: (1) Baba; (2)Mwana (3) watoto; (4) waliozaliwa upya; na (5)kunyakuliwa.Ukristo unafanana na familia, si matokeo (tiketi ya mbinguni, sera ya bima ya moto). Waamini katika Kristo wamefufuliwa upya “watu wa Mungu.” Kama watoto tunapaswa kuakisi tabia ya Baba, kama alivyofanya “pekee” (kama vile Yohana 1:14; 3:16) Mwana (kama vile Efe. 5:1; 1 Yohana 2:29; 3:3). Ni mamlaka gani yenye nguvu kwa wenye dhambi (kama vile Yohana 11:52; Rum. 8:14,16,21; 9:8; Flp. 2:15; 1 Yohana 3:1,2,10; 5:2; Hos. 1:10 ilivyonukuliwa katika Rum. 9:26; na 2 Kor. 6:18). Pia inafurahisha kwamba maneno mawili ya Kiyunani kwa wana, moja linatumiwa kumhusu Yesu (huios), ambapo (teknon, tekna) lingine limetumika kwa waaminio. Wakristo ni watoto wa Mungu, lakini si wa namna moja kama Mwana wa Mungu, Yesu. Uhusiano Wake ni wa pekee, lakini unashabihiana. Neno “kanisa” (ekklēsia) halionekani katika Marko, Luka,au Yohana.Wanatumia stiari za kijamii kwa mwenendo mpya wa mtu binafsi na ushirika wa pomoja wa Roho.

◙ “ndio wale waliaminio” Hii ni kauli tendaji endelevu ya wakati uliopo “wale wanaoendelea kuamini.” Mrejeo wa historia ya neno hili unasaidia kuimarisha maana ya sasa. Katika Kiebrania hili limerejewa kiasili kwa mtu katika mkao imara. Imekuwa ikitumika kistiari kwa yule ambaye alikuwa akitegemewa, mwaminifu, akitumainiwa. Usawa wa Kiyunani unatafsiriwa katika Kiingereza kwa maneno (“imani,” “sadiki,” na “tumaini”). Kibiblia imani au tumaini si jambo la kimsingi tufanyalo, bali yule ambaye katika yeye tunaliweka tumaini. Ni tumaini la Kimungu, si letu, ambalo ni tazamio. Mwanadamu aliye anguka hutegemea tumaini la Kimungu, hutumaini uaminifu Wake, huamini katika Pendo lake. Tazamio haliko juu ya wingi au ongezeko la imani ya mwanadamu, bali tendo la hiyo imani. Tazama Mada Maalum katika Yohana 1:7 na 2:23

Page 33: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

17

◙ “katika jina Lake” Katika Agano la Kale jina la mtu lilikuwa muhimu. Lilikuwa na nguvu/unabii wenye nguvu kuhusu ubainifu au maelezo ya sifa zao. Kuamini katika jina ni kusadiki na kumpokea mtu (kama vile Yohana 2:23; 3:18; 20:31; 1 Yohana 5:13). Tazama Mada Maalumu: Jina la Bwana katika Yohana 14:13-14

1:13 NASB, NKJV, NRSV “ambao walizaliwa si kutokana na uwezo wa kibinadamu wala nguvu za kimwili wala mapenzi ya mtu” TEV “hawakuwa watoto wa Mungu kwa maana ya asili, yaani, kwa kuwa wazawa na watoto wa baba wa mwili.” NJB “ambao walizaliwa si kwa uwezo au msukumo wa mwili au mapenzi ya mtu” Baadhi ya wazee wa kanisa (yaani, Irenaus, Origen, Tertullian, Ambrose, Jerome, Augustine) tazama kifungu hiki kikimrejea Yesu (yaani, katika hali ya umoja), lakini ushahidi wa maandishi ya Kiyunani uliotumiwa mno uko katika hali ya wingi (wingi wa neno hili unapatikana hapa tu katika Agano la Kale; UBS4 kiwango ni alama “A”), ambapo msitari huu unawahusu waamini katika Kristo (kama vile Yohana 3:5; 1 Pet. 1:3,23), hivyo, hauhitaji upendeleo wa asili wala uzao wa mwanadamu wa mwili (kuzaliwa kwa “damu”), lakini kwa Mungu ateuaye na kuwaweka karibu wale waaminio katika Mwana Wake (kama vile Yohana 6:44,65). Yohana 1:12 na 13 inaonyesha usawa wa agano kati ya Ukuu wa Mungu na mahitaji ya muitikio wa wadamu. Kitenzi cha Kiyunani (kauli tendwa yenye hali ya kuonyesha) inaondolewa katika sentensi ya mwisho ya Kiyunani kwa msisitizo. Hii inasistiza asili na kazi ya ukuu wa Mungu katika kuzaliwa mara ya pili (yaani, “bali Mungu,” ambayo ni sehemu ya kifungu cha mwisho, kama vile Yohana 6:44,65).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 1:14-18 14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli. 15 Yohana alimshuhudia, akapaza sauti yake akasema, Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Ajaye nyuma yangu amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu. 16 Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema. 17 Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo. 18 Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.

1:14 “Naye Neno alifanyika mwili” Yohana anayashambulia mafundisho ya uongo juu ya mafunuo, ambayo yalikuwa yanajaribu kuunganisha Ukristo na mawazo ya wapagani wa Kiyunani. Yesu alikuwa mwanadamu halisi na Mungu halisi (kama vile 1 Yohana 4:1-3) katika kuikamilisha ahadi ya Immanueli (kama vile Isa. 7:14). Mungu alichukua nafasi kama mwanadamu mwiongoni mwa wanadamu walioanguka (kifasihi, “aliweka hema lake”). Neno “mwili” katika Yohana kamwe hakugusia asili ya dhambi kama katika maandiko ya Paulo.

MADA MAALUMU: MWILI (SARX)

Neno hili limetumiwa mara kwa mara na Paulo kwa Wagalatia na makuzi yake kithiolojia katika Warumi. Wasomi wana tofautiana juu ya namna gani dokezo la maana ya maneno haya ibainishwe. Kuna uhakika wa baadhi ya mipishano katika maana. Lifuatalo ni jaribio tu la kunukuu uwanja mpana wa maana ya neno.

A. mwili wa binadamu, Yohana 1:14; Rum. 2:28; 1 Kor. 5:5; 7:28; 2 Kor. 4:11; 7:5; 12:7; Gal. 1:16; 2:16,20; 4:13; Flp. 1:22; Kol. 1:22,24; 2:5; 1 Tim. 3:16

B. kushuka kibinadamu, Yohana 3:6; Rum. 1:3; 4:1; 9:3,5,8; 11:14; 1 Kor. 10:18; Gal. 4:23,29 C. mwanadamu, Rum. 3:20; 7:5; 8:7-8; 1 Kor. 1:29; 2 Kor. 10:3; Gal. 2:16; 5:24 D. kuzungumza kibinadamu, Yohana 8:15; 1 Kor. 1:26; 2 Kor. 1:12; 5:16; 10:2; Gal. 6:12 E. udhaifu wa kibinadamu, Rum. 6:19; 7:18; 8:5-6,9; 2 Kor. 10:4; Gal. 3:3; 5:13,16,19-21; Kol. 2:18 F. ghasia ya wanadamu kumwelekea Mungu, inayohusiana na matokeo ya Anguko, Rum. 7:14; 13:14; 1

Page 34: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

18

Kor. 3:1,3; Efe. 2:3; Kol. 2:18; 1 Pet. 2:11; 1 Yohana 2:16 Inasisitizwa ya kwamba "mwili" hautazamwi kama uovu katika Agano Jipya, ni katika fikira za Kiyunani. Kwa wanafalsafa wa Kiyunani "mwili" ulikuwa chanzo cha matatizo ya wanadamu; kifo kilimweka huru mtu kutoka kwenye matakwa yake. Lakini katika Agano Jipya, "mwili" ni uwanja wa mgogoro wa mapambano ya kiroho (kama vile Efe. 6:10-18), tena usio na upande. Mwingine anaweza kutumia umbile lake la mwili kwa mazuri au mabaya.

◙ “akakaa kwetu” Kifasihi, hii ina maana “kuchukua nafasi.” Ilikuwa na mrejesho wa Kiyahudi kutoka kipindi kichokuwa na mpango cha kushangaza wa Hema (kama vile Ufu. 7:15; 21:3). Baadaye Wayahudi waliuita uzoefu wa mpango huu “fungate kati ya YHWH na Israeli. Kamwe Mungu hakuwa karibu na Israeli zaidi katika kipindi hiki. Neno la Kiyahudi kwa wingu mahususi la Mungu ambalo liliwaongoza Israeli katika kipindi hiki lilikuwa “Shekinah," Neno la Kiebrania lenye maana ya “kukaa na.”

◙ “nasi tukauona utukufu wake”Agano la Kale kabod (utukufu) sasa limepewa nafasi, limekuwa mfano. Hii inazungumzia (1) kitu fuani katika maisha ya Yesu kama mabadiliko au kupaa (yaani, ushuda wa kitume, kama vile 2 Pet. 1:16-17) au (2) dhana kwamba YHWH asiyeonekana anaonekana na anafahamika kwa ukamilifu. Huu ni mtazamo sawa kama katika1 Yohana 1:1-4, ambayo pia ni msistizo juu ya ubinadamu wa Yesu katika upinzani wa mtazamo usio sahihi wa ufunuo juu ya uhusiano wa kipinzani kati ya roho na vitu.

Katika agano la kale neno la Kiebrania lililokuwa la kawaida kwa neno “utukufu” (kabod, BDB 458) lilikuwa ni neno la kibiashara (ambalo lilimaanisha jozi ya vipimo) haswa, kuhusu “vitu vizito.” Vile vilivyokuwa vizito ndo vilikuwa na thamani. Mara nyingi dhana ya uangavu iliongezwa kwenye neno kuelezea ukuu wa Mungu (yaani, mwanzoni kwenye Mlima Sinai, shekinah wingu la utukufu, nuru ya kiama, kama vile Kut. 13:21-22; 24:17; Isa. 4:5;

60:1-2). Yeye pekee anasitahili na kupewa heshima. Utukufu wake unang’ara kiasi kwamba mwanadamu hawezi kuushika (kama vile Kut. 33:17-23; Isa. 6:5).Mungu anaweza kujulikana tu kupitia Kristo (kama vile Yohana 1:14, 18; Kol. 1:15; Ebr. 1:3).

MADA MAALUM: UTUKUFU (doxa)

Dhana ya Kibiblia ya “Utukufu" ni ngumu kuitolea maana. Toleo la LXX lilitumia doxa kufasiri zaidi ya maneno ishirini ya Kiebrania. Linatumika mara nyingi katika Agano Jipya kwa namna mbali mbali. Linatumika kwa Mungu, Yesu, wanadamu na Ufalme wa Kimasihi. Katika Agano la Kale neno lililozoeleka zaidi la Kiebrania kumaanisha "utukufu" (kabod, BDB 458, KB 455-458) kiasili lilikuwa neno la kibiashara linalohusiana na jozi za mizani ("kuwa nzito," KB 455). Kitu kilichokuwa na uzito zaidi kilibeba thamani kubwa zaidi na kuthaminiwa. Mara kwa mara dhana ya mg’ao iliongezwa kuelezea Ukuu wa Mungu (kama vile Kut. 19:16-18; 24:17; 33:18; Isa. 60:1-2). Yeye pekee ni mwenye kustahili na mwenye heshima (kama vile Zab. 24:7-10; 66:2; 79:9). Yeye anag’aa sana kwa mwanadamu aliyeanguka kumwona, hivyo anajifunika Yeye Mwenyewe katika wingu, mkono au moshi (kama vile Kut. 16:7,10; 33:17-23; Isa. 6:5). YHWH yeye pekee anaweza kujulikana kupitia Kristo (kama vile Yohana 1:18; 6:46; 12:45; 14:8-11; Kol.1:15; 1 Tim. 6:16; Ebr. 1:3; 1 Yohana 4:12). Kwa mjadala kamili wa kabod, angalia Mada Maalum: Utukufu [Agano la Kale]). Utukufu wa waaminio ni kwamba waielewe Injili na utukufu katika Mungu (kama vile 1 Kor. 1:29-31; Yer. 9:23-24). Kwa mjadala wa ndani zaidi, angalia NIDOTTE, vol. 2, kur. 577-587.

NASB, NKJV “utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba” NRSV “utukufu wake yeye aliye Mwana wa pekee wa Baba” TEV “Utukufu ambao aliupokea kama Mwana wa pekee wa Baba” NJB “utukufu ambao ni kama Mwana wa pekee wa Baba” Neno hili “pekee” (monogenēs) linamaanisha “yenyewe tu,” “aina moja” (kama vile Yohana 3:16,18; 1 Yohana 4:9, tazama F. F. Bruce, Answers to Questions, kr. 24-25). Vulgate alilitafasiri “pokea kipekee”na, kwa bahati

Page 35: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

19

mbaya, tafsiri za Kiingereza cha kale zililifuata hili (kama vile Luka 7:12; 8:42; 9:38; Ebr. 11:17). Mtazamo uko juu ya umoja na upekee, na si uzao wa uasherati. ◙ “Baba” Agano la Kale linatoa utangulizi wa stiari ya ukaribu unaojulikana wa Mungu kama Baba.

1. Taifa la Israeli mara nyingi linatambuliwa kama “mwana” wa YHWH (kama vile Hos. 11:1; Mal. 3:17) 2. Hata zamani katika Kumbukumbu la Torati ufanano wa Mungu baba unatumiwa (Kumbukumb 1:31) 3. Katika Kumbukumbu la Torati 32 Israeli inaitwa “watoto wake” na Mungu aliitwa “Baba yenu” 4. Ufanano huu unaelezwa katika Zaburi 103:13 na kukuzwa katika Zaburi 68:5 (baba wa yatima) 5. Ilikuwa kawaida katika manabii (kama vile Isa. 1:2; 63:8; Israeli kama mwana, Mungu kama Baba, 63:16;

64:8; Yer. 3:4,19; 31:9). Yesu aliuchukuwa ufanano huu na kwenda kwa kina zaidi katika uhusiano wa karibu, hasa katika Yohana 1:14,18; 2:16; 3:35; 4:21,23; 5:17, 18,19,20,21,22,23,26,36,37,43,45; 6:27,32,37,44,45,46,57; 8:16,19,27,28,38,42,49,54; 10:15,17,18, 25,29,30,32, 36 37,38; 11:41;12:26,27,28,49,50;13:14:2,6,7,8,9,10,11,12,13,16,20,21,23,24,26,28,31; 15:1,8,9,10,15,16,23,24,26; 16:3,10,15,17 ,23,25,26,27,28,32; 17:1,5,11,21,24,25; 18:11; 20:17,21!

◙ “amejaa neema na kweli” Uunganishaji huu unafuata maneno ya Agano la Kale hesed (agano la pendo na hadhi) na emeth (uaminifu) ambao unatumika na kuongezwa katika Kut. 34:6; Neh. 9:17; Zab. 103:8, maneno yote yanatokea kwa pamoja katika Mit. 16:6. Hii inaielezea sifa ya Yesu (kama vile Yohana 1:17) katika maneno ya kimaagano ya Agano la Kale. Tazama Mada Maalumu juu ya kweli katika Yohana 6:55 na 17:3

MADA MAALUMU: WEMA (HESED) Neno hili (BDB 338 I, KB 336 II) lina maeneo mapana ya maana.

A. Lilitumika katika kuwaunganisha wanadamu 1. Wema kwa wenzetu (mf. 1 Sam. 20:14; 2 Sam. 16:17; 2 Nya. 24:22; Ayubu 6:14; Zab. 141:5; Mit.

19:22; 20:6) 2. wema kwa maskini na wahitaji (mf. Mika 6:8) 3. upendo wa Israeli kumuelekea HWH (kama vile Yer. 2:2; Hos. 6:4,6) 4. uzuri wa maua ya kondeni (kama vile Isa. 40:6)

B. Lilitumika katika uungaishaji na Mungu 1. uaminifu wa agano na upendo

a. "ukombozi kutoka katika maadui na taabu" (mf. Mwa. 19:19; 39:21; Kut. 15:13; Zab. 31:16; 32:10; 33:18,22; 36:7,10; 42:8; 44:26; 66:20; 85:7; 90:14; 94:18; 107:8,15,21,31; 109:21-22; 143:8,12; Yer. 31:3; Ezr. 7:28; 9:9)

b. "katika ulinzi wa maisha kutokka katika kifo" (mf. Ayubu 10:12; Zab. 6:4-5; 86:13) c. "katika wepesi wa maisha ya kiroho" (mf. Zab. 119:41,76,88,124,149,159) d. "katika ukombozi wa kutoka dhambini" (kama vile Zab. 25:7; 51:1; 130:7-8) e. "katika kutunza maagano" (mfano., Kum. 7:9,12; 2 Nya. 6:14; Neh. 1:5; 9:32; Dan. 9:4; Mik.

7:20) kuzielezea sifa za Mungu (mf. Kut. 34:6; Zab. 86:15; 103:8; Neh. 9:17; Yoel 2:13; Yona 4:2; Mika 7:20)

2. wema wa Mungu a. "utele" (mf. Hes.14:18; Neh. 9:17; Zab. 86:5; 103:8; 145:8; Yoeli 2:13; Yer. 4:2) b. "ukuu katika kiwango chake" (mf. Kut. 20:6; Kum. 5:10; 7:9) c. "umilele" (mf. 1 Nya. 16:34,41; 2 Nya. 5:13; 7:3,6; 20:21; Ezra 3:11; Zab. 100:5; 106:1; 107:1;

118:1,2,3,4,29; 136:1-26; 138:8; Yer. 33:11) d. nguvu zilizo sawa (mf. Zab. 59:17) e. ilihusiana na nguvu za Mungu (mf. Zab. 62:11c-12a)

3. matendo ya wema (mf. 2 Nya. 6:42; Zab. 89:2; Isa. 55:3; 63:7; Omb. 3:22) Neno hili linatafsiriwa kwa njia mbalimbali katika tafsiri za Kiingereza. Nafikiri maelezo bora yaliyo katika ufupisho yangelikuwa "hakuna kamba iliyounganisha utii wa agano la Kimungu” neno hili ni sambamba na neno

Page 36: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

20

la Agano Jipya "upendo" (agapaō). Munguni mwaminifu na mwenye upendo kwa sababu ya Yeye alivyo!!

MADA MAALUMU: Kusadiki, Amini, Imani na Uaminifu katika Agano la Kale (אמן)

I. Maelezo ya awali Inahitajika kuanza kwamba utumiaji wa dhana ya kithiolojia, ni wa muhimu katika Agano Jipya, hauko wazi kama ulivyoelezewa katika Agano la Kale. Hakika upo, lakini umethibitishwa katika aya na watu muhimu waliochaguliwa. Vitu ambavyo havikupatana katika Agano la Kale

A. Watu binafsi na jamii B. Ukabiliano binafsi na utii wa agano

Imani kwa ujumla ni ukabiliano binafsi na stadi ya maisha ya kila siku! Ni rahisi kuelezea katika maisha ya mfuasi mwaminifu kuliko katika muundo wa kinahau (yaani., usomaji wa neno). Dhana hii binafsi imeelezewa vizuri katika

A. Ibrahimu na uzao wake B. Daudi na Israeli

Watu hawa walikutana/kukabiliana na Mungu na maisha yao yalibadilika jumla (sio maisha kamilifu kihivyo, lakini ni kuendelea katika imani). Majaribu yalifichua udhaifu na nguvu ya imani yao ya kukabiliana na Mungu, lakini hatima, uhusiano wa kuamini umeendelea muda wote! Imani ilijaribiwa na kusafishwa, lakini ikaendelea kama ushuhuda kwa moyo wao wa ibada na stadi ya maisha.

II. Asili kuu iliyotumika A. אמן (BDB 52, KB 63)

1. KITENZI a. Shina la neno Qal -kutegemeza, kustawisha (yaani, 2 Fal. 10:1,5; Esta 2:7, matumizi yasio ya

kithiolojia) b. Shina la neno ni phal-kuhakikisha au fanya imara, kuanzisha, kuhakiki, kuwa mwaminifu

1) Kwa watu, Isa. 8:2; 53:1; Yer. 40:14 2) Kwa vitu, Isa. 22:23 3) Kwa Mungu, Kumb. 7:9; Isa. 49:7; Yer. 42:5

c. Shina la neno Hiphil –kusimama imara, kusadiki, kuamini 1) Ibrahimu alimwamini Mungu, Mwa. 15:6 2) Waisrael katika Misri waliamini, Kut. 4:31; 14:31 (ilikanushwa katika Kumb. 1:32) 3) Waisrael wakamwamini YHWH alipoongea kupitia Musa, Kut. 19:9; Zab. 106:12,24 4) Ahazi hakuamini katika Mungu, Isa. 7:9 5) Yeyote aliyeamini katika Yeye, Isa. 28:16 6) Ukweli wa kuamini kuhusu Mungu, Isa. 43:10-12

2. NOMINO (JINSI YA KIUME) –kubaki kuwa mwaminifu (yaani., Kumb. 32:20; Isa. 25:1; 26:2) 3. KIELEZI- kweli kabisa, kweli, nakubali, iwe hivyo (kama vile Kumb. 27:15-26; 1 Fal. 1:36; 1 Nya.

16:36; Isa. 65:16; Yer. 11:5; 28:6). Hii ni namna ya liturujia ya neno “amina” katika agano la kale na agano jipya.

B. אמת (BDB 54, KB 68) nomino jinsi ya kike, uimarifu, kuwa mwaminifu, kweli 1. Kwa watu, Isa. 10:20; 42:3; 48:1 2. Kwa Mungu, Kut. 34:6; Zab. 117:2; Isa. 38:18,19; 61:8 3. Kwenye ukweli, Kumb. 32:4; 1 Fal. 22:16; Zab. 33:4; 98:3; 100:5; 119:30; Yer. 9:5; Zek. 8:16

C. אמונה (BDB 53, KB 62), uimara, kusimama imara, uaminifu 1. Katika mikono, Kut. 17:12 2. Katika muda, Isa. 33:6 3. Katika watu, Yer. 5:3; 7:28; 9:2 4. Kwa Mungu, Zab. 40:11; 88:11; 89:1,2,5,8; 119:138

III. Matumizi ya Paulo juu ya dhana ya Agano la Kale

Page 37: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

21

A. Paulo anaegemea uelewa wake mpya kuhusu YHWH na Agano la Kale juu ya ukabiliano wake na Yesu akiwa njiani kuelekea Dameski (kama vile Mdo. 9:1-19; 22:3-16; 26:9-18).

B. Alipatwa kuungwa mkono na Agano la Kale kwa uelewa wake mpya katika aya mbili muhimu za Agano la Kale ambazo zilitumia asili ya neno (אמן). 1. Mwa. 15:6- ukabiliano binafsi wa Abrahamu ulioanzishwa na Mungu (Mwanzo 12) ukasababisha

maisha matiifu ya imani (Mwanzo 12-22). Paulo analidokeza hili katika Rumi 4 na Wagalatia 3. 2. Isa.28:16- wale walioamini ndani yake (yaani., kujaribiwa kwa Mungu na uwekaji wa jiwe kuu la

pembeni kwa uthabiti) kamwe hautakuwa a) Rum. 9:33 “aibisha” au “katisha tamaa” b) Rum.10:11, kama ilivyo hapo juu

3. Hab. 2:4-wale wote wanaomfahamu Mungu Yule aliye mwaminifu lazima waishi maisha ya uaminifu (kama vile Yer. 7:28). Paulo analitumia neno hili katika Rum. 1:17 na Gal 3:11 (pia angalia Hab. 10:38)

IV. Matumizi ya Petro ya dhana ya Agano la Kale A. Petro anaunganisha

1. Isa. 8:14 – 1 Pet. 2:8 (jiwe la kujikwaa) 2. Isa. 28:16 – 1 Pet. 2:6 (jiwe kuu la pembeni) 3. Zab. 118:22 – 1 Pet. 2:7 (jiwe lililokataliwa)

B. Alibadilisha lugha ya kipekee ambayo iliielezea Israel kama “jamii iliyochaguliwa, ukuhani wa kifalme, taifa teule, watu waliomilikiwa ya Mungu mwenyewe” toka 1. Kumb. 10:15; Isa. 43:21 2. Isa. 61:6; 66:21 3. Kut. 19:6; Kumb. 7:6

Na sasa anatumia kwa minajili ya imani ya kanisa katika Kristo (kama vile 1 Petro. 2:5,9) 1. Matumizi ya Yohana kwenye dhana hii

A. Utumiaji wake kwenye Agano Jpya Neno “aaminiye" linatokana na neno la Kiyunani pisteuō ambalo pia laweza kutafasiliwa “ kuamini,” “sadiki,” au “imani.” Kwa mfano, nomino haionekani kwenye injili ya Yohana, lakini kitenzi kinatumika mara nyingi. Katika Yohana 2:23-25 kuna mashaka kama kwenye uhalisia wa kundi kujitoa kwa Yesu wa Nazareti kama Masiha wao. Mifano mingine wa utumiaji wa kubabiababia wa neno hili “kuamini” unapatikana katika Yohana 8:31-39 na Mdo. 8:31; 18-24. Imani ya kweli ya Kibiblia ni zaidi kuliko ukubalifu wa awali. Lazima uambatane na mchakato wa uanafunzi (Mt. 13:20-22,31-32).

B. Utumiaji wake ukiwa na vivumishi 1. eis inamaanisha “ndani ya” muundo huu wa kipekee unasisitiza waumini kuweka imani yao kwa

Yesu a. ndani ya jina lake (Yohana 1:12; 2:23; 3:18; 1 Yohana 5:13) b. ndani yake (Yohana 2:11; 3:15,18; 4:39; 6:40; 7:5,31,39,48; 8:30; 9:36; 10:42; 11:45 48;

12:37,42; Mt. 18:6; Mdo. 10:43; Flp. 1:29; 1 Pet. 1:8) c. ndani yake (Yohana 6:35; 7:38; 11:25,26; 12:44,46; 14:1,12; 16:9; 17:20) d. ndani ya mwana (Yohana 3:36; 9:35; 1 Yohana 5:10) e. ndani ya Yesu(Yohana 12:11; Mdo. 19:4; Gal. 2:16) f. ndani ya nuru (Yohana 12:36) g. ndani ya Mungu (Yohana 14:1)

2. ev inamaanisha “katika” kama ilivyo katika Yohana 3:15; Mk. 1:15; Mdo. 5:14 3. epi ikimaanisha “katika” au “juu ya” kama ilivyo katika Mt. 27:42; Mdo. 9:42; 11:17; 16:31;

22:19; Rum. 4:5,24; 9:33; 10:11; 1 Tim. 1:16; 1 Petr. 2:6 4. uhusika wa mahali usio na kivumishi kama ilivyo katika Yohana 4:50; Gal.3:6; Mdo. 18:8; 27:25;

1 Yoh. 3:23; 5:10 5. hoti, likimaanisha “kuamini kwamba,” inatoa kilichomo kama kile kinachotakiwa kuaminiwa

Page 38: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

22

a. Yesu ni Mtakatifu wa Mungu (Yohana 6:69) b. Yesu ni Mimi ndiye (Yohana 8:24) c. Yesu ndani ya Baba na Baba ndani yake (Yohana 10:38) d. Yesu ni Masiha (Yohana 11:27; 20:31) e. Yesu ni mwana wa Mungu (Yohana 11:27; 20:31) f. Yesu alitumwa na Babaye (Yohana 11:42; 17:8,12) g. Yesu ni wamoja na Babaye (Yohana 14:10-11) h. Yesu alikuja toka kwa Babaye (Yohana 16:27,30) i. Yesu anajitambulisha mwenyewe katika jina la Agano la Babaye “Mimi ndiye” (Yohana 8:24;

13:19) j. Tutaishi naye (Rum. 6:8) k. Yesu alikufa na kufufuka tena (1 The. 4:14)

V. Hitimisho A. Imani ya Kibiblia ni ukubalifu wa mwanadamu katika neno/agano la Kiungu. Mungu siku zote

huanzisha (yaani., angalia Mada Maalumu: Agano) 1. Toba (angalia Mada Maalumu: Toba) 2. Sadiki/amini (angalia Mada maalumu) 3. Utii 4. Usitahimilivu (angalia Mada maalumu: Usitahimilivu)

B. Imani ya Kibiblia ni 1. Uhusiano binafsi (imani ya awali) 2. Uthibitisho wa kweli wa Kibiblia (imani katika ufunuo wa Mungu, yaani., andiko) 3. Kuwajibika katika utii sahihi (uaminifu wa kila siku)

Imani ya Kibiblia sio tiketi ya kwenda mbinguni au utaratibu wa bima. Ni mahusiano binafsi. Na hili ndio kusudi la uumbaji, mwanadamu aliumbwa katika sura na mfanano (kama vile Mwa. 1:26-27) wa Mungu. Suala hapa ni kwamba “urafiki wa karibu.” Mungu anapendelea ushirika, sio msimamo fulani wa kithiolojia! Lakini ni ushirika na Mungu aliye mtakatifu anataka kuwa wana waonyeshe tabia za “kifamilia” (yaani., utakatifu, kama vile Law. 19:2; Mt. 5:48; 1 Petro. 1:15-16). Anguko (kama vile Mwanzo) liliathiri uwezo wetu kuwajibika kwa usahihi. Kwa hiyo, Mungu akatenda kwa niaba yetu (kama vile Ezek. 36:27-38), akitupatia “moyo mpya” na “roho mpya” inayotuwezesha kupitia imani na toba ili kuwa na ushirika na Yeye na kumtii Yeye! Yote haya matatu ni muhimu. Yote haya matatu yanapaswa kudumishwa. Kusudi ni kumjua Mungu (wote kwa maana ya Wayunani na Waebrania)

C. Uaminifu wa mwanadamu ni matokea (Agano la Jipya), na sio msingi (Agano la Kale) wa uhusiano na Mungu: imani ya mwanadamu katika uaminifu wake; kusadiki kwa mwanadamu katika kuamini kwake. Moyo wa Agano Jipya katika mtazamo wa wokovu ni kwamba mwanadamu lazima mwanzoni kabisa awajibike na aendelea kuwajibika kwenye neema na rehema ya Mungu, iliyoonyeshwa katika Kristo. Alipenda, alitumwa, alitoa, lazima tuwajibike katika imani na kuamini (kama vile Efe. 2:8-9 na 10) Mungu aliye mwaminifu anawahitaji watu waaminifu kujidhihilisha kwao kwa ajili ya ulimwengu usio na imani na kuwaleta wote kwenye imani binafsi katika Yeye.

1:15 “Ajaye nyuma yangu amekuwa mbele yangu” Haya ni mafundisho ya Yohana Mbatizaji ya ukubalifu wa nguvu wa uwepo wa kabla wa Yesu (kama vile Yohana 1:1; 8:56-59; 16:28; 17:5; 2 Kor. 8:9; Flp. 2:6-7; Kol. 1:17; Ebr. 1:3; 10:5-8). Mafundisho ya uwepo wa kabla na maelezo ya unabii yalikiri kwamba kuna Mungu juu na nyuma ya historia, yeye ambaye bado anatenda kazi ndani ya historia. Ni sehemu ya muhimu ya Mkristo/wazo la neno la kibiblia.

Page 39: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

23

◙ Mstari huu ni mgumu na mabadiliko mengi ya waandishi wenye weledi yalifanywa katika hali ya kujaribu kuelezea na kurahisisha andiko. See Bruce M. Metzger, A Textual Commentary on the Greek New Testament, kr. 197-198. Pia ni mfano mzuri unaohusu namna nyakati za vitenzi vya Kiyunani visivyoweza kusanifiwa. Hili ni tendo lilopita likinukuliwa katika wakati ULIOPO. Tazama Kiambatisho cha Kwanza. 1:16-18 Moja ya sifa za Injili yaYohana ni namna mwandishi alivyozigawa katika matukio ya kihistoria, majibizano, au muda wa mafundisho na maoni yake. Mara nyingi haiwezekani kutofautisha kati ya watu wengine wa Yesu, na maneno ya Yohana. Wasomi wengi wanadai kwamba Yohana 1:16-19 ni maoni ya Yohana (kama vile Yohana 3:14-21).

1:16 “utimilifu wake” Hili na neno la Kiyunani pleroma. Waalimu wa uongo wa mafunuo walilitumia kueleza kipindi kirefu kitakatifu kisichopimika kati ya Mungu mkuu na viumbe vidogo vya kiroho. Yesu ni mpatanishi pekee (yaani, kweli na mkamilifu pekee) kati ya Mungu na mwanadamu (kama vile Kol. 1:19; 2:9; Efe. 1:23; 4:13). Tena hapa inaonekana Mtume Yohana anayashambulia mawazo ya kale ya mafunuo kuihusu kweli.

NASB, NRSV “na neema juu ya neema” NKJV “neema kupita neema” TEV “na kutupa sisi baraka moja hadi nyingine” NJB “karama moja ikichukua nafasi ya nyingine” Swali linalotafasirika ni namna ya kuielewa “neema.” Ilivyo

1. Huruma ya Mungu katika Kristo ndani ya wokovu 2. Huruma ya Mungu kwa maisha ya Mkristo 3. Huruma ya Mungu katika agano jipya kupitia Kristo?

Wazo funguzi ni “neema”; neema ya Mungu imetolewa kwa namna ya kushangaza kataka umbile la mwili wa Yesu. Yesu ni “ndiyo” ya Mungu kwa wanadamu walioanguka (kama vile 2 Kor. 1:20).

1:17 “Kwa kuwa torati” Sheria ya Musa haikuwa mbaya, bali ilikuwa maandalio ya kabla na isiyokamilika ili kuuleta wokovu kamili (kama vile Yohana 5:39-47; Gal. 3:23-29; Warumi 4). Waebrania pia walitofautisha na kulinganisha kazi/ufunuo/maagano ya Musa na Yesu.

MADA MAALUMU: MTAZAMO WA PAULO KUIHUSU SHERIA YA MUSA

Ni nzuri na inatoka kwa Mungu (kama vile Rum. 7:12,16). A. Si njia ya kuielekea haki na ukubalifu wa Mungu (inaweza hata kuwa laana, kama vile Gal. 3). Tazama

Mada Maalumu: Sheria ya Musa na Mkristo. B. Bado ni mapenzi ya Mungu kwa waaminio kwa sababu ni ufunuo wa Mungu Mwenyewe (mara nyingi

Paulo amelinukuu Agano la Kale kuwasadikisha na /au kuwatia moyo waaminio). C. Waamini wanafahamishwa naAgano la Kale (kama vile Rum. 4:23-24; 15:4; 1 Kor. 10:6,11), lakini

hawaokolewi na Agano la Kale (kama vile Mdo. 15; Warumi 4; Wagalatia 3; Waebrania). Ina fanya kazi ndani ya utakaso lakini si uthibitisho.

D. Inafanya kazi ndani ya agano jipya ili: 1. kuonyesha dhambi (kama vile Gal. 3:15-29) 2. kuwaongoza wanadamu ndani ya jamii waliokombolewa 3. kumfahamisha Mkristo maamuzi ya kimaadili

Ni mpangilio maalumu unaomulika kithiolojia uliohusiana na Sheria, kutoka katika hali ya kulaaniwa (kama vile Gal. 3:10-13) na badala yake kuwepo baraka za kudumu, jambo ambalo linasababisha tatizo katika kujaribu kuuelewa mtazamo wa Paulo kuihusu Sheria ya Musa. Mwanadamu aliye ndani ya Kristo, James Stewart analionyesha fumbo la fikra na maandiko ya Paulo: "Kwa kawaida ungetarajia kuwepo kwa mwanadamu anayejiendesha mwenyewe ili kuunda mfumo wa fikra na

Page 40: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

24

mafundisho yaliyoimarishwa na kama kitu kisichobadilishwa kama alivyotumia maneno yenye manufaa. Ungetarajia yeye kuulenga usahihi katika kutumia maneno yalioziongoza fikra zake. Ungedai kwamba neno, linapotumiwa na mwandishi wetu katika maana mahususi, linapaswa kuibeba maana hiyo kotekote. Lakini kwa kuangalia muundo huu yakupasa kutomtia moyo Paulo. Matumizi mengi ya maneno yake ni marahisi, si magumu. . . anaandika 'Basi torati ni njema', 'Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani' (kama vile Rum. 7:12,22) lakini ni dhahiri kwamba kipengele kingine cha nomos ndicho kinachomfanya kuzungumza hali hii pengine, 'Kristo alitukomboa katika laana ya torati' (kama vile Gal. 3:13)" (uk. 26).

◙ “neema” Hii inamaanisha kuokolewa chini ya Mungu, pendo lilirithiwa kwa wale walioanguka (kama vile Efe. 2:8). Hili neno neema (charis), ni la muhimu sana katika maandiko ya Paulo, linatumika tu kwenye aya hii katika Injili ya Yohana (kama vile Yohana 1:14,16,17). Waandishi wa Agano Jipya, chini ya uvuvio, walikuwa huru kutumia misamiati yao wenyewe, analojia, na stiari. Yesu alilileta katika kweli "agano jipya" la Yer. 31:31-34; Ezek. 36:22-38.

◙ “kweli”Hii inatumika katika maana ya (1) uaminifu au (2) kweli dhidi ya uongo (kama vile Yohana 1:14; 8:32; 14:6). Nukuu zote neema na kweli zinatoka kwa Yesu (kama vile Yohana 1:14). Tazama Mada Maalumu katika Yohana 17:3

◙ "Yesu" Huu ni utumiaji wa kwanza wa jina la mtu la mwana wa Maria katika Utangulizi. Mwana aliyekuwapo kabla sasa amekuwa Mwana katika Umbile la Mwili!

1:18 "Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote" Baadhi wanasema kwamba hii inachanganya aya ya Kutoka 33:20-23. Hata hivyo, neno la Kiebrania katika kifungu cha Kutoka kinarejea juu ya "baada ya kukua," si mwonekano wa kimwili wa Mungu Mwenyewe. Msukumo wa kifungu hiki ni ule wa pekee wa ukamilifu wa Yesu kufunuliwa na Mungu (kama vile Yohana 14:8ff). Hakuna mwanadamu mwenye dhambi aliyemuona Mungu (kama vile Yohana 6:46; 1 Tim. 6:16; 1 Yohana 4:12,20). Mstari huu unasisitiza ufunuo pekee wa Mungu katika Yesu wa Nazareti. Yeye ni mkamilifu ni mtakatifu pekee aliyejifunua. Kumjua Yesu ni kumjua Mungu. Yesu ni ufunuo wa mwisho wa Baba Mwenyewe. Hakuna uelewa sahihi wa Uungu mbali na Yeye (kama vile Kol. 1:15-19; Ebr. 1:2-3). Yesu "anamuona" Baba na waamini "humuona" Baba kupitia Yeye (masihi wake, maneno, na matendo). Yeye ni ufunuo kamili na timilifu wa Mungu asiyeonekana (kama vile Kol. 1:15; Ebr. 1:3). NASB "yeye aliye wa pekee wa Mungu" NKJV "Mwana pekee" NRSV " Ni mwana pekee wa Mungu" TEV "Mwana pekee" NJB "Ni mwana wa pekee" Tazama nukuu kuhusu monogenēs katika Yohana 1:14. Yesu ni Mungu kamili na mwanadamu. Tazama nukuu kamili katika Yohana 1:1. Kuna machapisho tofauti na Kiyunani hapa. Neno theos/Mungu liko katika machapisho ya Kiyunani cha kale P66, P75, B, na C, ambapo lina maana ya "Mwana" wakati "Mwana" linawekwa badala ya "Mungu" pekee katika MSS A na C3. Toleo la UBS4 linatoa "Mungu" alama ya "B" (karibia na hakika). Neno "Mwana" inawezekana linakuja kutoka kwa waandishi kwa kukumbuka "Mwanangu mpendwa wa Pekee" katika Yohana 3:16, 18 na katika 1 Yohana 4:9 (kama vile Bruce M. Metzger's A Textual Commentary on the Greek New Testament, ukur. 198). Huu ni ukiri wenye nguvu wa ukamili na Uungu wa Yesu mkamilifu! Inawezekana kwamba mstari huu una majina matatu ya Yesu: (1) mpendwa wa pekee, (2) Mungu, na (3) aliyekaribu zaidi na Baba. Kuna mjadala wa kufurahisha wa uwezekano wa kuondolewa kwa makusudi kwa andiko hili kulikofanywa na waandishi wa sheria wa Kiyahudi katika Bart D. Ehrmans' The Orthodox Corruption of Scripture, ukur. 78-82.

Page 41: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

25

◙ "aliye katika kifua cha Baba" Hii iko sawa katika maana ya kifungu cha maneno "alikuwa Mungu" katika Yohana 1:1 na 2. Linazungumzia juu ya uhusiano wa karibu sana. Linaweza kurejea juu ya (1) ushirika wa uwepo Wake wa kabla au (2) uhusiano Wake uliotunzwa (yaani, Kupaa).

NASB "amemweleza kwetu" NKJV "huyu ndiye aliye mfufua" NRSV,NJB "aliiye mfanya ajulikane" TEV "amemfanya wa kujulikana"

Tunalipata neno la Kiingeleza "(exegesis) ufafanuzi wa kimaandiko" (yaani., "kuondoa," kauli ya kati [yenye ushahidi] tendaji) kutokana na neno hili la Kiyunani lililotumika katika Yohana 1:18, ambalo linadokeza ufunuo kamili na timilifu. Nia moja kuu ya Yesu ni kumfunua Baba (kama vile Yohana 14:7-10; Ebr. 1:2-3). Kuona na kumjua Yesu ni kuona na kumjua Baba (anayewapenda wenye dhambi, anayewasaidia wadhaifu, anayewakubali waliotengwa na watu, anayepokea watoto na wanawake)! Neno la Kiyunani lilitumika kwa wale walioeleza au kutafsiri ujumbe, ndoto, au nyaraka. Hapa pia Yohana anaweza kuwa alitumia neno lililo na maana maalumu kwa wote Wayahudi na Mataifa (kama Logos ya Yohana 1:1). Yohana anajaribu kuhusianisha vyote Wayahudi, Wayunani pamoja na utangulizi. Neno lingemaanisha

1. kwa Wayahudi Yule anayeeleza au kuitafasiri Sheria 2. kwa Wayahudi anayeeleza au kuitafasiri miungu.

Katika Yesu, Yesu pekee, wanadamu kamili huona na kumwelewa Baba!

UTAMBUZI WA KIMUKTADHA KUHUSU MSTARI WA 19-51

A. Kifungu hiki kuhusu Yohana Mbatizaji kinahusika na migogoro ya makanisa mawili ya kale: 1. Ni kile ambacho kilishamiri karibu na watu wa Yohana Mbatizaji na kinatetewa katika Yohana 1:6-9,

20,21,25; na 3:22-36; 2. Ni kile ambacho kilimjumuisha mtu wa Kristo na kinajikita katika Yohana 1:32-34. Huu uasi ni sawa

na wa mafunuo unaoshambuliwa na ule ulioko katika 1 Yohana 1. 1 Yohana unaweza kuwa umeenea baadaye katika Injili ya Yohana.

B. Injili ya Yohana imenyamaza kuhusu ubatizo wa Yesu kwa Yohana Mbatizaji. Zana za kanisa, ubatizo na Ekaristi, hazipatikani kwa urahisi katika fikira za Yohana kuhusu maisha ya Kristo. Angalau kuna sababu mbili ziwezekanazo kuhusu ondoleo hili: 1. Kukua kwa sakramenti katika kanisa la kale kulikosababishwa na Yohana ili kusistiza mwelekeo wa

Ukristo. Injili yake iliangalia juu ya uhusiano, na siyo taratibu. Hakujadili au kunakili sakramenti mbili za ubatizo na Karamu ya Bwana hata kidogo. Kukosekana kwa kitu fulani kilichotarajiwa sana kungeli vuta umakini kukihusu.

2. Yohana, akiandika baadaye kuliko waandishi wengine wa Injili, alizitumia fikra hizi za maisha ya Kristo kujazia mengine. Wakati mihitasari yote hii ikienea kwenye taratibu za kidini, Yohana aliziweka taarifa za ziada kuhusu matukio yaliyomzunguka. Kwa mfano yangelikuwa mazungumzo na matukio ambayo yalitukia katika chumba cha juu (Yohana 13-17) lakini si karamu yenyewe halisi.

C. Msistizo wa fikira hizi uko juu ya ushuhuda wa Yohana Mbatizaji kuhusu utu wa Yesu. Yohana anautengeneza usemi ufuatao: 1. Yesu ni Mwana Kondoo wa Mungu, (Yohana 1:29) jina linalotumika hapa kwa Yesu tu na katika

Ufunuo 2. Yesu alikuwepo kabla (Yohana 1:30) 3. Yesu ni mpokeaji na mtoaji wa Roho Mtakatifu (Yohana 1:33) 4. Yesu ni Mwana wa Mungu (Yohana 1:34)

D. Ukweli kumhusu na kazi ya Yesu vilikuzwa na ushuhuda wa mtu binafsi

Page 42: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

26

1. Yohana Mbatizaji 2. Andrea na Simoni 3. Filipo na Nathanaeli

Hii imekuwa mbinu ya kawaida ya kifasihi katika Injili nzima. Ina mazungumzo ishirini na saba au shuhuda kumhusu Yesu au pamoja na Yesu

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 1:19-23 19Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma kwake makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu ili wamwulize, Wewe u nani? 20 Naye alikiri, wala hakukana; alikiri kwamba, Mimi siye Kristo. 21 Wakamwuliza, Ni nini basi? U Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La. 22 Basi wakamwambia, U nani? Tuwape majibu wale waliotupeleka. Wanenaje juu ya nafsi yako? 23 Akasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena nabii Isaya.

1:19 “Wayahudi” Katika Yohana hii inagusia juu ya (1) watu wa Uyahudi ambao walikwa wakorofi kwa Yesu au (2) Viongozi wa Kidini wa Kiyahudi tu (kama vile Yohana 2:18; 5:10; 7:13; 9:22; 12:42; 18:12; 19:38; 20:19). Baadhi ya wasomi wamedai kwamba Myahudi asingewagusia Wayahudi katika namna hii ya aibu. Kisha, upinzani wa Kiyahudi kwa Ukristo ulichochewa baada ya Baraza la Jammina katika 90 B.K

Neno "Myahudi" kimsingi linatokana na mtu kutoka Yuda. Baada ya kutapanywa kwa makabila kumi na mawili mnamo 922 k.k., Yuda lilikuja kuwa jina la makabila matatu ya kusini. Falme zote za Kiyahudi, Israeli na Yuda, walichukuliwa mateka, lakini wachache tu, hasa kutoka Yuda, walirudi tena chini ya utawala wa Koreshi wa 538 k.k. Baadaye neno lilikuja kuwa adimu kwa Yakobo aliyeishi huko Palestina na walisambaa kupitia Mediterrania hadi ulimwengu mzima.

Katika Yohana neno hili liko kinyume haswa, lakini matumizi yake ya jumla yanaweza kuonekana katika Yohana 2:6 na 4:22.

◙ “makuhani na Walawi” Yohana Mbatizaji naye alikuwa ni wa uzao wa kikuhani (kama vile Luka 1:5ff). Neno “walawi” ni neno pekee linalojitokeza katika injili ya Yohana. Yawezekana hawa walikuwa ni maaskari wa Hekalu. Hili lilikuwa ni kundi rasmi la "watafuta kweli" waliotumwa kutoka mamlaka ya kidini toka Yerusalemu (kama vile Yohana 1:24). Makuhani na Watunga sheria mara nyingi walikuwa Masadukayo, ambapo waandishi weledi walikuwa Mafarisayo (kama vile Yohana 1:24). Makundi haya mawili yalijumuishwa katika kumuuliza maswali Yohana Mbatizaji. Wapinzani wa kisiasa na kidini walijiunga kwa nguvu ili kumpinga Yesu na wafuasi Wake.

◙ “Wewe u nani?” Swali hili ni sawa na lile lililoulizwa kumhusu Yesu katika Yohana 8:25. Yohana na Yesu walifundisha na kutenda katika namna ambayo iliwafanya wale viongozi rasmi kutojisikia vema, kwa sababu walitambua ndani mwao maneno na dhamira ya hukumu fulani toka agano la kale. Swali hili, kisha, linahusiana na matarajio ya Kiyahudi ya nyakati za mwisho, Zama Mpya za watu mashuhuri.

1:20 “Naye alikiri, wala hakukana; alikiri kwamba” Usemi huu ni wenye nguvu, kanusho lilirudiwa mara tatu ambalo alilitarajia, Masihi aliye ahidiwa (Kristo). Kwa “kukiri” angalia Mada maalum katika Yohana 9:22-23.

◙ “Mimi siye Kristo” Ni tafsiri ya Kiyunani ya neno la Kiebrania “māšîah,” ambalo lilimaanisha “aliyepakwa mafuta.” Katika Agano la Kale dhana ya kupakwa mafuta ilikuwa njia ya kusisitiza wito maalumu wa Mungu na matayarisho kwa kazi maalumu. Wafalme, makuhani, na manabii walikuwa wamepakwa mafuta. Ilikuja kutambuliwa na yule aliye wa pekee ambaye ilimpasa kuzitekeleza zama mpya za haki. Wengi walifikiri kwamba Yohana Mbatizaji ndiye aliyekuwa Masihi aliyeahidiwa (kama vile Luka 3:15) kwa sababu alikuwa msemaji wa mwanzo kumhusu YHWH tangu wakati ule wa baadhi ya waandishi wa Agano la Kale miaka mia nne iliyopita. Katika maana hii ningependa kuweka pamoja maoni yangu kutoka Dan. 9:26 kuhusu “Masihi”

Page 43: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

27

Danieli 9:26 NASB “Masihi” NKJV “Masihi” NRSV “Aliye pakwa mafuta” TEV “Mungu alimchagua kiongozi" NJB “Aliye Teuliwa” Ugumu katika kutafsiri mstari huu ni kwa sababu ya maana ziwezekanazo zinazohusiana na neno Masihi au aliyepakwa mafuta (BDB 603):

1. Lilitumika juu ya wafalme wa Kiyahudi (m.f. 1 Sam. 2:10; 12:3) 2. Lilitumika juu ya makuhani wa Kiyahudi (m.f. Law. 4:3,5) 3. Lilitumika kwa Koreshi (kama vile Isa. 45:1) 4. #1 na #2 zimejumuishwa katika Zaburi 110 na Zakaria 4 5. Lilitumika juu ya ujio maalumu wa Mungu wa ufalme wa Daudi kuzileta zama mpya za haki

a. katika Yuda (kama vile Mwa. 49:10) b. nyumba ya Yese (kama vile 2 Samueli 7) c. utawala wa ulimwengu (kama vile Zaburi 2; Isa. 9:6; 11:1-5; Mika. 5:1-4ff)

Mimi binafsi navutiwa na utambuzi wa “aliye teuliwa” na Yesu wa Nazareti kwa sababu ya: 1. Utangulizi wa Ufalme wa milele katika Danieli 2 wakati wa dola ya nne 2. Utangulizi wa “mwana wa adamu” katika Danieli 7:13 uliotolewa na ufalme wa milele 3. Mapatano ya wokovu wa Danieli 9:24 ambao unatoa maana kukielekea kilele cha anguko la historia ya

ulimwengu 4. Matumizi ya Yesu ya kitabu cha Danieli katika Agano Jipya (kama vile Mt. 24:15; Marko 13:14)

1:21 “Ni nini basi? U Eliya wewe?” Kwa sababu Eliya hakufa bali alinyakuliwa katika farasi wa moto kwenda mbinguni (kama vile 2 Fal. 2:1), alitarajiwa kuja kabla ya Masihi (kama vile Mal. 3:1; 4:5). Yohana Mbatizaji alitazama na kufanya kazi zaidi kama Eliya (kama vile Zek. 13:4).

◙“Mimi siye” Yohana Mbatizai hakujiona mwenyewe katika jukumu la uhukumiaji juu ya Eliya, bali Yesu alimpa uwezo wa kufanya kama ukamilifu wa unabii wa Malaki (kama vile Mt. 11:14; 17:12).

◙ "Wewe u nabii yule" Musa alitabiri kwamba aliye kama yeye (aliyeitwa “Nabii”) angekuja baada yake (kama vile Mambo ya Walawi 18:15,18; Yohana 1:25; 6:14; 7:40; Mdo. 3:22-23; 7:37). Kuna njia mbili tofauti ambazo kwazo neno hili lilitumika katika Agano Jipya: (1) kama kielelezo tofauti cha mambo ya hukumu toka kwa Masihi (kama vile Yohana 7:40-41) au (2) kama kielelezo kilichomtambua Masihi (kama vile Mdo. 3:22).

1:23 “Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani” Hii ni nukuu kutoka katika tafsiri za Maandiko ya Kale ya Kiyunani ya Isa. 40:3 chenye kidokezo kinachofanana na Mal. 3:1.

◙ “Inyosheni njia ya Bwana” Hii ni nukuu kutoka (Isa. 40:3) muungano wa fasili za Isaya (sura 40-54) ambamo nyimbo za Mtumishi hutoka (kama vile Isa. 42:1-9; 49:1-7; 50:4-11; 52:13-53:12). Kiasili zinairejea Israeli, lakini katika Isa. 52:13-53:12, kifungu kimepambanuliwa. Dhana ya kuyanyoosha mapito ilitumika kwa ajili ya maandalizi ya ugeni wa kifalme. Neno “nyoosha” linahusiana na fasili ya neno “haki.” Angalia katika 1 Yohana 2:29 Hii aya nzima inaweza kuwa imeliokoa kusudi la theolojia ya Mtume Yohana ya kumshusha Yohana Mbatizaji kwa sababu ya kushamiri kwa makundi ya uasi katika karne ya kwanza ambayo yalimuweka Yohana Mbatizaji kama kiongozi wao wa kiroho.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 1:24-28 24 Nao wale waliotumwa walikuwa wametoka kwa Mafarisayo. 25Wakamwuliza, wakamwambia, Mbona basi wabatiza, ikiwa wewe si Kristo, wala Eliya, wala nabii yule? 26 Yohana akawajibu akisema, Mimi nabatiza kwa maji. Katikati yenu amesimama yeye msiyemjua ninyi. 27Ndiye yule ajaye nyuma yangu, ambaye mimi

Page 44: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

28

sistahili kuilegeza gidamu ya kiatu chake. 28 Hayo yalifanyika huko Bethania ng'ambo ya Yordani, alikokuwako Yohana akibatiza.

1:24 “walikuwa wametoka kwa Mafarisayo” Andiko hili ni tata. Linaweza kumaanisha (1) Mafarisayo waliotumwa kwa Yohana (kama vile Yohana 1:19) au (2) wadadisi walikuwa Mafarisayo, ambao walikuwa wa kawaida katika mwangaza wa dhana ambayo makuhani wengi walikuwa Masadukayo (kama vile Yohana 1:9). Inaonekana kurejea juu ya kundi lingine kuliko Yohana 1:19.

MADA MAALUMU: MAFARISAYO

I. Neno lilikuwa na uwezekana wa kuwa na asili moja kati ya hizi zifuatazo: A. “Kujitenga.” Kundi hili lilianza wakati wa ufuasi wa kiongozi wa Kiyahudi Yuda wa karne ya pili ( huu ni

mtizamo mpana sana unaokubalika), na kujitenga wao wenyewe toka kwenye umma wa watu ili kutunza tamaduni simulizi za sheria ya Musa (yaani., mienendo ya kichini chini ya Kiyahudi iliyopatikana karne ya 18).

B. “Kugawa” Hii ni maana nyingine toka kwenye kiini kile kile cha lugha ya Kiebrania (BDB 827, BDB 831 I, KB 976); yoye yakimaanisha “kugawanya.” Baadhi ya wasomi wanasema linamaanisha mfasili (kama vile Neh. 8:8; 2 Tim. 2:15).

C. “Uajemi.” Hii ni maana nyingine toka kwenye kiini kile kile cha lugha ya Kiarama (BDB 828, KB 970). Baadhi ya mafundisho ya mafarisayo yanaingiliana na wafuasi wa dini za Kiislamu za awali toka Uajemi zilizoanzishwa na Zoroaster (angalia maada maalumu Uovu).

II. Pamekuwepo na nadharia nyingi nani alianzisha Ufarisayo. A. Kikundi cha kithiolojia cha dini ya mwanzo ya Kiyahudi (angali., Yusufu) B. Kikundi cha kisiasa toka kipindi kile cha Herode C. Kikundi cha kisomi cha wafasiri wa sheria za musa ambao walitaka kuwasaidia watu wa kawaida

kuelewa Agano la Musa na tamaduni simulizi zilizowazunguka. D. Mienendo ya chini kwa chini ya waandishi, kama vile Ezra na Sinagogi kuu, wakigombea uongozi wa

ukuhani mkuu katika hekalu. Yaliundwa nje ya misigishano na

1. Makabaila wasiokuwa Wayahudi (hasa Antiokia IV). 2. jamii ya watu wakuu dhidi ya watu wa kawaida 3. wale waliojifungamanisha kwenye maisha ya agano dhidi ya Wayahudi wa kawaida toka Palestina

III. Habari zetu kuwahusu wao zinatoka

A. Yusufu, aliyekuwa mfarisayo 1. Vitu vya kale vya Kiyahudi 2. Vita vya Wayahudi

B. Agano Jipya C. Asili ya awali ya Kiyahudi

IV. Mafundisho yao makuu

A. Imani ya kuja kwa Masiha, iliyoshawishiwa na waandishi wa Kibiblia wa Kiyahudi wenye fasihi ya kimaono kama vile Enock.

B. Imani ya kwamba Mungu yu hai katika maisha yetu ya kila siku. Hii moja kwa moja ilikuwa kinyume na Masadukayo (kama vile Mdo 23:8). Mafundisho mengi ya Kifarisayo yalikuwa ni kijazilizo cha yale ya Masadukayo.

C. Imani katika maelekezo ya kimwili baada ya maisha yaliyolenga maisha ya duniani, yaliyojumuisha zawadi na adhabu (kama vile Dan.12:2)

D. Imani katika mamlaka ya Agano la Kale vile vile simulizi za kitamaduni (Talmud). Walitambua kuwa watiifu kwa amri za Mungu za Agano la Kale kama zilivyo tafasiliwa na shule za wasomi wa sheria za

Page 45: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

29

Kiyahudi (Shammai, asiyependa mabadiliko na Hillel, anayependa mabadiliko). Watafasiri wa sheria za Kiyahudi walisimamia juu ya mazungumzo kati ya wanasheria/walimu wa falsafa mbili zinazokinzana, mmoja asiyependa mabadiliko na mwingine anayependa mabadiliko. Mazungumzo haya ya kisimulizi juu ya maana ya andiko hatimaye likaandikwa kwa miundo miwili.: sheria za kiibada za Wababel na sheria za kiibada zisizo kamili za Wapalestina. Waliamini kuwa Musa alipokea hizi sheria za mdomo kwenye Mlima Sinai. Mwanzo wa haya mazungumzo ya kihistoria yalianzishwa na Ezra na watu wa “Sinagogi kuu” (baadaye wakaitwa Sanhedrin)

E. Imani ilioanzishwa juu ya mafundisho ya kithiolojia ya kimalaika. Haya yalijumuisha viumbe wazuri na wabaya. Hili lilianzia huko Uajemi yenye pande mbili na fasihi za Kiyahudi zenye mwingiliano na Biblia.

F. Imani juu ya mamlaka ya kifalme ya Mungu, lakini pia mazoezi ya utashi huru wa binadamu (yetzer).

V. Nguvu ya mabadilko ya Kifarisayo. A. Walipenda , waliheshimu, kuamini mafunuo ya Mungu (yaani., yote, yakijumuisha sheria, Manabii,

Maandiko, na simulizi za kitamaduni) B. Walijitolea kuwa wafuasi wenye haki (yaani., maisha ya kila siku na imani) wa mafunuo ya Mungu.

Walitaka “Israel yenye haki” kutimiza ahadi ya kinabii ya siku mpya yenye mafanikio. C. Walitetea kuwepo usawa na jamii za Kiyuda, ambao unajuisha ngazi zote za watu, kwa maana kuwa,

walikataa uongozi wa kikuhani (yaani., masadukayo) na thiolojia(kama vile Mdo 23:8). D. Walipigania kitu halisi cha mtu kwenye agano la sheria za Musa. Walitetea au kudai mamlaka ya

Mungu, lakini pia wakashikilia kwenye hitaji la utendaji huru wa mwanadamu E. Agano Jipya linataja mafarisayo mbali mbali walioheshimika (yaani., Nikodemu, Mtawala tajili kijana,

Yusufu wa Alimataya).

Walikuwa ni kundi hilo tu la dini ya Kiyahudi ya karne ya kwanza kuhimili uharibifu wa Yerusalem na hekalu toka kwa Warumi mwaka wa 70 B.k. wakawa ni dini ya Kiyahudi ya kisasa

1:25 “Mbona basi wabatiza” Ubatizo wa kubadili imani ulikuwa wa kawaida katika Uyahudi ya kale kwa yale Mataifa yaliyotarajia kubadili dini, lakini ilikuwa si kawaida kabisa kwa Wayahudi wenyewe kubatizwa (Wayahudi wa madhehebu walizoea ubatizo binafsi na wale walioabudu katika hekalu walinawa kabla ya kuingia). Andiko hili linaweza kujumuisha vidokezo vya Kimasihi kutoka Isa. 52:15; Eze. 36:25; Zek. 13:1.

◙ “ikiwa” Hii ni sentensi shurutishi daraja la kwanza ambayo inafikiliwa kuwa sahihi kutoka katika mtazamo wa mwandishi au kusudi lake la fasihi.

◙ “wewe si Kristo, wala Eliya, wala nabii yule?” Inafurahisha kwamba katika upande wa Magombo y Bahari Ya Chumvi, watu hawa watatu mashuhuri waliwakilisha mawazo ya Essene kwamba kungekuwepo na tofauti tatu za vielelezo vya Kimasihi. Pia inashawishi kwamba baadhi ya viongozi wa kanisa wa muda mrefu waliamini kwamba Eliya angekuja katika umbo la kuonekana kabla ya Ujio wa Pili wa Kristo (kama vile Chrysostom, Jerome, Gregory, na Augustine).

1:26 “Mimi nabatiza kwa maji” Kiwakilishi “katika” pia kinaweza kumaanisha “kwa,” Kipingamizi cho chote kilichochaguliwa kinapaswa kuoana usambamba uliopo na 1:33 ihusuyo “Roho.”

◙ “Katikati yenu amesimama yeye” Kuna tofauti kadhaa zihusianazo na nyakati za kitenzi “kusimama.” UBS4 inatathimini njeo ya wakati timilifu katika alama “B” (takribani yenye uhakika). Bruce M. Metzger anadai kwamba wakati uliopo timilifu ni sifa bainifu za Yohana na udokezaji wa nahau ya Kiebrania ya neno “kuna Mtu ambaye amechukua nafasi kati kati yako” (ukr. 199).

1:27 “ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya kiatu chake.” Hii inazungumzia juu ya masumbufu ya mtumwa ya kutofungua kamba za viatu vya bwana wake aingiapo nyumbani mwake (anayechukuliwa kama mtu wa chini,

Page 46: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

30

masumbufu zaidi ya uduni yaliyostahili kufanywa na mtumwa). Sheria za Uyahudi zilidai kwamba mwanafunzi wa rabbi anapaswa kuwa na hiari kufanya kila kitu ambacho mtumwa alikuwa hiari kukifanya isipokuwa kufungua kamba za viatu vyake. Pia kuna kidokezo cha kuondoa viatu na kuvipeleka katika sehemu iliyoteuliwa kwa ajili ya uhifadhi ambacho hakikutajwa. Hii ilikuwa stiari ya unyanyasaji uliokithiri.

1:28 “huko Bethania” Tafsiri ya King James Version ina jina la “Bethabara” (MSS 2א, C2). Hii ilikuwa ni kwa sababu ya mategemeo ya watafasiri kuhusu mgogoro wa Origen (na uwekaji wa istiari za majina ya mahali) wa mahali pa jiji. Usomaji sahihi ni Bethania (Mafunjo ya Bodmen, P66)-sehemu moja ya kusini mashariki mwa Yerusalemu (kama vile Yohana 11:18), lakini mji ulioko ng’ambo ya pili kutoka Yeriko, ng’ambo ya Mto Yordani (upande wa mashariki).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 1:29-34 29 Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu! 30 Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Yuaja mtu nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu. 31 Wala mimi sikumjua; lakini kusudi adhihirishwe kwa Israeli ndiyo maana mimi nalikuja nikibatiza kwa maji. 32 Tena Yohana akashuhudia akisema, Nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake. 33 Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu. 34 Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ni Mwana wa Mungu.

1:29 “Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu” Sikukuu ya Pasaka haikuwa mbali (kama vile Yohana 2:13). Hivyo, huenda hii ikamaanisha mwanakondoo wa Pasaka anayeashiria ukombozi (yaani, wokovu) kutoka Misri (kama vile Kutoka 12). Pia Yohana anakiweka kifo cha Yesu katika siku sawa ya Pasaka ya mwanakondoo aliyechinjwa (yaani,“Siku ya Maandalio”). Hata hivyo, kumekuwa na tafsiri zingine:

1. inaweza kumzungumzia Mtumishi Aliyejitesa katika Isa. 53:7 2. inaweza kumzungumzia mnyama aliyenaswa katika kichaka katika Mwa. 22:8, 13. 3. inaweza kuzungumzia dhabihu yetu ya kila siku katika Hekalu iitwayo “daima” (kama vile Kut. 29:38-46).

Kwa vyovyote vile muungano kamili, ulikuwa kwa ajili ya kusudi la dhabihu ambalo kwa hilo mwana kondoo alitumwa (kama vile Marko 10:45). Stiari hii ya nguvu kuhusu dhabihu ya kifo cha Yesu kamwe haitumiwi na Paulo na mara chache tu na Yohana (kama vile Yohana 1:29,36; pia nukuu Matendo 8:32 na 1 Pet. 1:19). Neno la Kiyunani kwa “mwanakondoo mdogo” (mdogo kwa sababu ulikuwa mwaka mmoja wa kuzaliwa, kipindi chote cha sadaka ya dhabihu). Neno la tofauti linatumiwa na Yohana katika Yohana 21:15 na mara ishirini na nane katika Ufunuo. Kuna uelekeo mmoja zaidi kwa matumizi ya tamathali za semi za Yohana Mbatizaji: mahusiano ya kimaagano, fasili ya kubuni ambapo "mwanakondoo" ni mpiganaji aliye shinda. Kipengele cha sadaka bado kipo, lakini mwanakondoo kama hakimu wa haki ni mshindi (kama vile Ufu. 5:5-6,12-13).

◙“aichukuaye dhambi ya ulimwengu!” Kifungu “achukuaye” kinamaanisha “saidia na beba.” Kitenzi hiki kinafanana sana na dhana ya “kisingizio” katika Mambo ya Lawi 16. Dhana kwamba dhambi ya ulimwengu imetajwa kugusia asili ya ulimwengu wa kazi ya mwana kondoo (kama vile Yohana 1:9; 3:16; 4:42; 1 Tim. 2:4; 4:10; Tito 2:11; 2 Pet. 3:9; 1 Yohana 2:2; 4:14). Tambua kwamba dhambi iko katika hali ya umoja, na si wingi. Yesu ameshughulika na tatizo la “dhambi” ya ulimwengu.

1:30 “kwa maana alikuwa kabla yangu” Hii imerudiwa na Yohana 1:15 kwa msistizo. Huu ni msistizo mwingine juu ya uwepo wa kabla na Uungu wa Masihi (kama vile Yohana 1:1, 15; 8:58; 16:28; 17:5,24; 2 Kor. 8:9; Flp. 2:6-7; Kol. 1:17; Ebr. 1:3).

1:31 “lakini kusudi adhihirishwe kwa Israeli” Hili ni fungu la kawaida la Yohana (kama vile Yohana 2:11; 3:21; 7:4; 9:3; 17:6; 21:14; 1 Yohana 1:2; 2:19,28; 3:2,5,8; 4:9), lakini hili ni fungu dogo katika Ufupisho wa Injili, linaloonekana tu katika Marko 4:22. Ni tendo katika neno la Kiebrania “kujua,” ambalo linauzungumzia ushirika

Page 47: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

31

binafsi kwa mtu fulani zaidi kuliko ukweli kumhusu. Kusudi la ubatizo wa Yohana lilikuwa mara mbili: (1) kuwaandaa watu na (2) kumfunua Masihi. Kitenzi“dhihirishwa” (phaneroō) linaonekana kuchukua nafasi ya “funua” (apokaluptō) katika maandiko ya Yohana. Kwa ufasaha Yesu anamleta katika mwangaza /uelekeo mtu na ujumbe wa Mungu!

1:32-33 Huu ni msistizo wa mara ya tatu wa dhana kwamba Yohana alimuona Roho akija na kukaa juu ya Yesu.

1:32 “akishuka kama hua kutoka mbinguni” Huu ulikuwa usemi wa Isaya (Isaya 40-66) wa kumkiri Masihi (kama vile Isa. 42:1; 59:21; 61:1). Hii haimaanishi kudokeza kwamba Yesu hakuwa na Roho kabla ya wakati wake. Ilikuwa ishara ya uteuzi maalumu wa Mungu na matayarisho. Kimsingi halikuwa la Yesu, lakini lilimhusu Yohana Mbatizaji! Wayahudi walikuwa na mtazamo wa kiulimwengu wa zama mbili (angalia Mada Maalum katika 1 Yohana 2:17), zama za uovu za sasa na zama za haki zijazo. Zama mpya ziliitwa zama za Roho. Maono haya yangekuwa yamezungumzwa na Yohana Mbatizaji kuwa (1) huyu ni Masihi na (2) zama mpya zimepambazuka. ◙ “hua” Hii lilitumika

1. kama alama za sheria za Kiyahudi kwa Israeli (yaani, Hos. 7:11) 2. kidokezo katika Roho kama ndege jike "aatamiaye" juu ya uumbaji katika Mwa. 1:2 katika Targums 3. katika Philo alama ya hekima 4. kama sitiari ya namna ambayo katika hiyo Roho alishuka ( Roho sio njiwa)

◙ “naye akakaa juu yake’’ Tazama MADA MAALUMU: " UTII" KATIKA MAANDIKO YA YOHANA katika 1 Yohana 2:10. 1:33 “Wala mimi sikumjua” Hii inadokeza kwamba Yohana Mbatizaji hakumjua Yesu kama Masihi, sio kwamba hakumjua Yeye kabisa. Kama watu wa karibu, hakika walikutana katika kusanyiko au kusanyiko la kidini miaka yote. ◙ “lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia” Mungu anazungumza na Yohana kama alivyofanya kwa manabii wa Agano la Kale. Yohana alimtambua Masihi kwa matendo haya bayana ambayo yangelitokea katika ubatizo Wake. Ubatizo wa Yohana ulipendekeza mamlaka ya kidini. Mwakilishi maalumu kutoka Yerusalemu (kama vile Yohana 1:19-28) alitaka kujua chanzo cha mamlaka yake. Yohana Mbatizaji aliitambua mamlaka hiyo kwa Yesu. Ubatizo wa Yesu wa Roho ni mkuu kwa ubatizo wa maji wa Yohana. Ubatizo wa Yesu mwenyewe katika maji utakuwa alama ya ubatizo wa Roho, ushirika katika nyakati mpya! ◙ “huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu” Kuanzia 1 Kor. 12:13 inaonekana kwamba dhana hii inahusiana na mjumuisho asilia wa mtu katika familia ya Mungu, anatuombea kwa kuugua kusiko tamkika kwa Kristo, hubatiza katika Kristo, na kumuumba Kristo ndani ya mwamini mapya (kama vile Yohana 16:8-13). Tazama MADA MAALUMU: ALIYE MTAKATIFU katika 1 Yohana 2:20. 1:34 “Nami nimeona, tena nimeshuhudia” Zote hizi ni nyakati zilizopo timilifu zenye kuarifu ambazo zinadokeza tendo lililopita lililowekwa katika utimilifu na kisha kuendelea. Hii inafanana na 1 Yohana 1:1-4. ◙ "ya kuwa huyu ni mwana wa Mungu" Mmoja anashangaa kama neno la Kiyunani paīs, ambalo mara nyingi linatafsiriwa "mtumishi,"likiakisi kiebrania ('ebed, BDB 712) katika maandiko ya kale ya Kiyunani (LXX), lingeweza kuwa mrejeo kwa "Mwana." Kama ni hivyo, kisha Isaya 53 (kama ni “mwana kondoo” wa Mungu katika Yohana 1:29) ni kidokezo cha Agano la Kale badala ya Dan. 7:13. Yesu ni vyote Mwana na Mtumishi! Atabadilisha waamini kuwa “wana,” na sio “watumishi”! Kichwa hiki kinachofanana kinatumiwa na Nathanaeli katika Yohana 1:49. Pia kinatumika na Shetani katika Mt.

4:3. Kuna tofauti ya ushawishi wa maandiko ya Kiyunani unaopatikana katika MSS P5 na אi*, ambao unamaanisha “Aliye Chaguliwa na Mungu” badala ya “Mwana wa Mungu” (UBS4 inatoa “Mwana wa Mungu” “B” inakadiriwa).

Page 48: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

32

Kifungu "Mwana wa Mungu" ni cha kawaida katika Yohana. Lakini, kama mtu akifuata mantiki ya imani za ukosoaji wa maandishi, kisha ukosefu zaidi wa ustadi na uumbuaji wa maneno usio sahihi yamkini ni halisi, kisha kuna uwezekano wa tafsiri ya moja kwa moja kupitia ushahidi wa maandiko hata kama umewekewa mipaka. Gordon Fee anajadili tofauti hii ya maandiko katika makala yake “The Textual Criticism of the New Testament” kur. 419-433, katika utangulizi wa juzuu ya The Expositor's Bible Commentary:

“Katika Yohana 1:34, Yohana Mbatizaji alisema, ‘Huyu ni Mwana wa Mungu’ (KJV, RSV) au ‘Huyu ndiye Aliyeteuliwa na Mungu' (NEB, JB)? Ushahidi wa MS umegawanyika, hata miongoni mwa aina ya maandishi ya kale. ‘Mwana’ linapatikana katika ufunguo wa ushahidi wa Ki-Iskandria (P66, P75, B, C, L copbo) vile vile pia katika OL nyingi (aur, c, flg) na mashahidi waliofuata wa lugha ya Kishamu, ambapo ‘aliyeteuliwa’anaungwa mkono na P5, א, copsa za Ki-Iskandria pamoja na OL MSS a,b,e,ff2, na lugha ya kale ya Kishamu. “Mwishoni swali linapaswa kuamuliwa katika misingi ya ndani. Kama ulivyo uwezekano wa nukuu, kila jambo liko sawa: tofauti iko katika makusudi, si kwa bahati (kama vile Bart D. Ehrman's The Orthodox Corruption of Scripture, kr. 69-70). Lakini karne ya pili inafafanua mabadiliko ya maandishi yanayounga mkono aina ya uasili wa Ukristo, au maana aliyoifanya mwandishi mwenye imani barabara, uwezekano ambao una udhihirisho kwa ‘Aliyeteuliwa’ ungaliweza kutumika kuunga mkono uasilishaji, na hivyo kuubadilisha kwa ajili ya makusudi ya imani thabiti? Katika upande wa uelekeo, baadaye ilionekana kuwa mbali kuliko, hasa tangu pale 'Mwana' hakubadilishwa popote pale katika Injili ili kukudhi maoni ya wale wanaoasilisha. "Lakini maamuzi ya mwisho yanapaswa kujumuisha fasili ya maandiko matakatifu. Tangu kile alicho kisema Yohana Mbatizaji bila shaka alikusudia takribani kuwa wa kimasihi na si usemi wa thiolojia ya Mkristo, swali ni hili ikiwa inatazamisha Umasiha katika aya hii kama ilivyo kwenye Zaburi 2:7 au Isaya 42:1. Katika upande wa mateso, au Pasaka ya Wayahudi, mwana kondoo anayejirudia rudia katika Yohana 1:29, hakika linajadilika kwamba ‘Aliyeteuliwa’ anafaa katika muktadha wa Injili” (kur. 431-432).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 1:35-42 35 Tena siku ya pili yake Yohana alikuwa amesimama pamoja na wawili katika wanafunzi wake. 36 Akamtazama Yesu akitembea, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu! 37 Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu. 38 Yesu aligeuka, akawaona wakimfuata, akawaambia, Mnatafuta nini? Wakamwambia, Rabi, (maana yake, Mwalimu), unakaa wapi? 39 Akawaambia, Njoni, nanyi mtaona. Wakaenda, wakaona akaapo, wakakaa kwake siku ile. Nayo ilikuwa yapata saa kumi. 40 Andrea, nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana na kumfuata Yesu. 41 Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo). 42 Akampeleka kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama, akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohana; nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro, au Jiwe).

1:35 “wawili katika wanafunzi wake” Marko 1:16-20 anaonekana kueleza tofauti ya wanafunzi hawa. Haijulikani ni mara ngapi mawasiiano ya kipindi kilichopita yalitolewa kati ya Yesu na wanafunzi wake wa Galilaya. Kulikuwa na hatua maalumu za ufundishaji zilizohusishwa katika mchakato wa kuwa mfuasi wa rabi katika ya siku zote za Yesu. Hatua hizi zinaelezewa kinagaubaga katika vyanzo vya sheria za Kiyahudi, lakini haikufuatwa haswa katika maelezo ya Injili. Wanafunzi wawili waliotajwa ni Andrea (kama vile Yohana 1:40), na Yohana Mtume (ambaye kamwe hakujitaja mwenyewe kwa jina katika Injili). Neno mwanafunzi linaweza kumaanisha (1) anayejifunza na /au (2) mfuasi. Hili lilikuwa jina la kale la waamini katika Yesu Kristo kama Masihi wa Kiyahudi aliyeahidiwa. Ni muhimu kunukuu kwamba Agano Jipya lina wito kwa wanafunzi, kutokuwa watupu wa maamuzi (kama vile Mathayo 13; 28:18-20). Ukristo ni maamuzi ya awali (toba na imani) hufuatiwa na maamuzi dhahiri ya utii na ustahimilivu. Ukristo si sera ya bima ya majanga ya moto au tiketi ya kwenda mbinguni bali utumishi wa kila siku/ uhusiano wa urafiki na Yesu.

1:37 "Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena” Yohana Mbatizaji alijikinga nyuma ya Yesu (kama vile Yohana 3:30).

Page 49: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

33

1:38 “Rabi, (maana yake, Mwalimu)” Hiki kilikuwa cheo cha kawaida katika karne ya kwanza ya Uyahudi ili kuwatambua wale ambao wange fasili vidokezo na matumizi ya Sheria ya Musa na Tamaduni za Kienyeji (Kitabu cha sheria na maadili ya Kiyahudi). Kifasihi "bwana wangu" linatumiwa na Mtume Yohana likiwa sawa na "mwalimu" (kama vile Yohana 11:8, 28; 13:13-14; 20:16). Dhana kwamba Yohana anaeleza maneno yake (kama vile Yohana 1:38, 41, 42) inaonyesha aliyaandikia Mataifa.

◙ "unakaa wapi?" Hii inaonyesha kufuata taratibu za kitamaduni za kuimarisha mapatano pekee baina ya mwalimu na mwanafunzi. Swali lao linadokeza kwamba watu hawa wawili wataka kuutumia muda zaidi wakiwa na Yesu kuliko ilivyoonekana kuuliza maswali machache wakiwa njiani (kama vile Yohana 1:39). Neno menō (baki) linajitokeza mara tatu katika Yohana 1:38,39. Linaweza kumaanisha mahali asili au sehemu ya kiroho. Matumizi matatu yanaonyesha kudokeza kazi ya neno lingine linalotoa vidokezo vyote kwa pamoja, ambalo ni la kawaida katika Yohana (yaani, Yohana 1:1,5; 3:3; 4:10-11; 12:32). Utata huu uliokusudiwa ni sifa za maandishi ya Yohana!

1:39 "Nayo ilikuwa yapata saa kumi" Haijulikani kama Yohana anatumia wakati wa Kirumi, unaoanza (1) saa 6:00 asubuhi au (2) alafajiri, au muda wa Kiyahudi, unaoanza saa 6:00 mchana (utusiutusi wa asubuhi). Wakati anao ulinganisha Yohana 19:14 na Marko 15:25 inaonekana kudokeza Wakati wa Kirumi. Hata hivyo,wakati anaoangalia katika Yohana 11:9 inaonekana kudokeza wakati wa Kiyahudi. Huenda Yohana alitumia nyakati zote. Hapa inaonekana kuwa wakati wa Kirumi, yaani saa 4:00 usiku.

1:40 "alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana" Mwandishi (Mtume Yohana) hakujitaja kamwe katiika Injili (yaani, 21:2). Inawezekana kwa usahihi kwamba mmoja wa wanafunzi wawili ambaye alimsikia Yohana Mbatizaji akitoa dai hili alikuwa Yohana, Mt. 4:21; Marko 1:19).

1:41 NASB "Alikutana na ndugu yake kwanza" NKJV, NRSV "Huyo akamwona Simoni, ndugu yake mwenyewe" TEV "Alipomwona" NJB "kitu cha kwanza alichokifanya Andrea" Kuna maandishi mbalimbali ambayo yanaathiri tafsiri. Mambo hayo ni

1. jambo la kwanza alilolifanya Andrea 2. mtu wa kwanza aliyekuwepo 3. Andrea alikuwa wa kwanza kwenda na kuzungumza

◙ “Masihi (maana yake, Kristo) ” Tazama nukuu katika Yohana 1:20. 1:42 “Naye Yesu akamtazama” Neno hili linarejea juu ya "mtazamo makini." ◙"Simoni mwana wa Yohana" Kuna baadhi ya mkanganyiko katika Agano Jipya kuhusiana na jina la baba yake Petro. Katika Mt. 16:17 Petro anaitwa "mwana wa Yona" (Iōnas,) lakini hapa anaitwa "mwana wa Yohana"

(Iōannēs). Jina Yohana linapatikana katika MSS P66, P75, א, na L. MS B ana jina sawa lakini likiwa na "n" moja tu (Iōanēs). Jina Yona linatokea katika MSS A, B3, K na maandishi zaidi ya Kiyunani yaliyofuatia. Inaonekana kutokuwa na jibu sahihi la swali hili. Herufi mbalimbali zenye majina kutoka katika Kiaramu ni za kawaida na zimenukuliwa tofauti. Michael Magill, The New Testament TransLine, uk. 303, anasema, "'Yona' na 'Yohana' labda wanabadilisha herufi za Kiyunani za jina sawa la Kiebrania, kama 'Simoni' na 'Simeoni.'" ◙ “nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro, au Jiwe) Neno Kefa ni neno la Kiaramu kwa maana ya mwamba (kepa), ambalo linatokana na neno la Kiyunani kephas. Jina lingelikumbushia kile ambacho ni imara, chenye nguvu na cha

Page 50: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

34

kudumu.Hii ni moja ya maoni mengi kwa mwandishi wa Injili ili kusaidia kueleza maisha na mafundisho ya Yesu kwa wasomaji wa Mataifa katika Yohana 1:38. Inatia shauku kwamba maneno mawili ya mwisho ya kitaalamu (vitenzi) kuhusu Biblia yanaonekana katika sura hii.

1. Fasiri ya maandiko matakatifu, kuongoza, iliyotumika katika Yohana 1:18 2. Kanuni za ufasili, kueleza, kufasili, kutafsiri, iliyotumiwa katika Yohana 1:42

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 1:43-51 43 Siku ya pili yake alitaka kuondoka kwenda Galilaya, naye akamwona Filipo. Yesu akamwambia, Nifuate. 44 Naye Filipo alikuwa mtu wa Bethsaida, mwenyeji wa mji wa Andrea na Petro. 45 Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti. 46 Nathanaeli akamwambia, Laweza neno jema kutoka Nazareti? Filipo akamwambia, Njoo uone. 47 Basi Yesu akamwona Nathanaeli anakuja kwake, akanena habari zake, Tazama, Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake. 48 Nathanaeli akamwambia, Umepataje kunitambua? Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona. 49 Nathanaeli akamjibu, Rabi, wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe Mfalme wa Israeli. 50 Yesu akajibu, akamwambia, Kwa sababu nilikuambia, Nilikuona chini ya mtini, waamini? Utaona mambo makubwa kuliko haya. 51 Akamwambia, Amin, amin, nawaambia, Mtaziona mbingu zimefunguka na malaika wa Mungu wakikwea na kushuka juu ya Mwana wa Adamu.

1:43 “Siku ya pili yake” Yohana aliwajumuisha wapangaji wa matukio katika Injili nzima (kama vile Yohana 1:29,35,43; 2:1; n.k). Mazingira mazima (1) yanaanzia katika Yohana 1:19, ambapo ingekuwa siku ya kwanza; (2) Yohana 1:29,35,43 una "siku inayo fuata"; na (3) 2:1 una " siku ya tatu inayofuata."

◙ “alitaka kuondoka kwenda” Yohana ananukuu kipindi cha kale cha huduma ya Yesu katika Yudea ambacho hakikunukuliwa katika vidokezo vya injili. Injili ya Yohana inatazamia juu ya huduma ya Yesu katika Yudea na hasa Yerusalemu. Hapa, kisha, Yeye alitaka kwenda Galilaya bila shaka katika harusi huko Kana (Yohana 2).

◙ “Nifuate”Hii kauli tendaji tegemezi ya wakati uliopo. Huu ulikuwa ni wito wa kiualimu wa kuwa mwanafunzi wa kudumu. Wayahudi waliupangilia mwongozo ambao unautaja uhusiano huu.

1:44 “Naye Filipo alikuwa mtu wa Bethsaida” Maana ya jiji hili ni "nyumba ya uvuvi." Hii pia ilikuwa nyumba ya Andrea na Petro.

1:45 “Nathanaeli” Hili ni jina la Kiebrania ambalo linamaanisha "Mungu ametoa." Hatajwi na jina hili katika vidokezo vya Injili. Inafikiriwa na wanafunzi wa sasa kwamba ni mmoja aitwaye "Batromayo," lakini hii imebaki makisio tu.

MADA MAALUMU: CHATI YA MAJINA YA MITUME

Mathayo 10:2-4 Marko 3:16-19 Luka 6:14-16 Matendo 1:12-18

Kundi la kwanza

Simoni (Petro) Andrea (Petro nduguye) Yakobo (mwana wa Zebedayo) Yohana (nduguye Yakobo)

Simoni (Petro) Yakobo (mwana wa `Zebedayo) Yohana (nduguye Yakobo) Andrea

Simoni (Petro) Andrea (Petro nduguye) Yakobo Yohana

Petro Yohana Yakobo Andrea

Kundi la Filipo Filipo Filipo Filipo

Page 51: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

35

pili Bartholomayo Thomaso Mathayo (mtunza ushuru)

Bartholomayo Mathayo Thomaso

Bartholomayo Mathayo Thomaso

Thomaso Bartholomayo Mathayo

Kundi la tatu

Yakobo (mwana wa Alfayo) Thadayo Simoni (Mkananayo) Yuda (Iskariote)

Yakobo (mwana wa Alfayo) Thadayo Simoni (Mkananayo) Yuda (Iskariote)

Yakobo (mwana wa Alfayo) Simoni (Zelote) Yuda (wa Yakobo) Yuda (Iskariote)

Yakobo (mwana wa Alfayo) Simoni (Zelote) Yuda (wa Yakobo)

Kutoka katika muhtasari wa Luka 6:14: ◙ “Simoni, aliyemwita jina la pili Petro” Kuna orodha nyingine tatu za mitume kumi na wawili. Kwa kawaida Petro ni wa kwanza; Yuda Iskariote ni wa mwisho daima. Kuna makundi matatu kati ya manne ambayo yamebaki kwa usawa, hata kama mtiririko wa majina ndani ya makundi unageuzwa mara kwa mara (kama vile Mathayo. 10:2-4; Marko 3:16-19; Matendo 1:13). ◙ “Andrea” Neno la Kiyunani linamaanisha “mwenye sifa za kiume.” Kutoka Yohana 1:29-42 tunajifunza kwamba Andrea alikuwa mwanafunzi wa Yohana Mbatizaji na kwamba alimtambulisha nduguye, Petro, kwa Yesu. ◙ "Yakobo" Hili ni jina la Kiebrania “Yakobo” (BDB 784), ambalo linamaanisha "chukua nafasi ya," kama vile Mwa. 25:26). Kuna wanaume wawili wanaitwa Yakobo katika katika orodha ya wale Kumi na wawili. Ni nduguye Yohana (kama vile Marko 3:17) na sehemu ya mzunguko wa ndani (yaani, Petro, Yakobo, na Yohana). Huyu ni nduguye Yohana. ◙ "Yohana" Huyu alikuwa nduguye Yakobo na moja wa mzunguko wa ndani wa wanafunzi. Aliandika vitabu vitano katika Agano Jipya na aliishi kipindi kirefu kuliko mtume ye yote yule. ◙ "Filipo" Jina la Kiyunani linamaanisha "mpenda farasi" Wito wake umeandikwa katika Yohana 1:43-51. ◙ "Bartolomayo" Jina linamaanisha "mwana wa mtawala wa Misri" Anaweza kuwa Nathanaeli wa Injili ya Yohana (kama vile Yohana 1:45-49; 21:20). ◙ "Mathayo" Jina la Kiebrania (kutoka Mattithiah, kama vile 1 Nya. 9:31; 15:18,21; 16:5; 25:3,21; Neh. 8:4) linamaanisha "karama ya YHWH." Hii inarejea katika Lawi (kama vile Marko. 2:13-17). ◙ "Tomaso" Jina la Kiebrania linamaanisha "pacha" au Didimus (kama vile Yohana 11:16; 20:24; 21:2). ◙ "Yakobo wa Alfayo" Hili ni jina la Kiebrania "Yakobo." Kuna wanaume wawili walioitwa kwa jina la Yakobo katika wale Kumi na wawili. Mmoja ni nduguye Yohana (kama vile Luka 6:17) na sehemu ya mzunguko wa ndani (yaani, Petro, Yakobo, na Yohana). Huyu anajulikana kama "Yakobo aliye mdogo" (kama vile Marko 3:17). ◙ "Simoni aitwaye Zelote" Maandishi ya Kiyunani ya Marko yana "Mkananayo" (pia Mathayo. 10:4). Marko, ambaye Injili iliandikwa kwa Warumi, asingetakiwa kutumia “maneno makali” ya kisiasa, Zelote, ambalo linarejea juu ya Wapigania Mabadiliko wa Kiyahudi Waishio mstuni walio kinyume na utawala wa Kirumi. Luka anamtaja kwa istirahi hii `(kama vile Mdo 1:13). Istirahi ya Mkananayo ina minyumbuo mbali mbali.

1. kutoka eneo la Galilaya lijulikanalo kama Kana 2. kutoka matumizi ya Agano la Kale ya Wakanaani kama mfanyabiashara

Page 52: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

36

3. kutoka jina la jumla kama mwenyeji wa Kanaani. Kama jina la jumla alilolitumia Luka ni sahihi, basi Zelote linatokana na neno la Kiaramu "mwenye shauku" (kama avile Mdo. 1:17). Uchaguzi wa Yesu wa wanafunzi kumi na wawili walikuwa wametoka makundi shindani tofauti na mbalimbali. Simoni alikuwa mmoja wa kundi la kizalendo ambalo lilipigania kupinduliwa kwa ghasia za mamlaka ya Kirumi. Mara nyingi Simoni na Lawi (yaani, Mathayo, mtoza ushuru) na kila mmoja .wasingekuwa katika chumba kile kile ◙ "Yuda wa Yakobo" Pia aliitwa "Lebbeus" (kama vile Mat. 10:3) au "Yuda" (kama vile Yohana 14:22). YoteThadayo na Lebbeus inamaanisha "mtoto apendwaye." ◙ "Yuda Iskariote, " Kuna Simoni wawili, Yakobo wawili, na Yuda wawili. Jina Iskariote lina uwezekano wa minyumbuo miwili:

1. mtu wa Kerioth (mji) katika (kama vile Yos. 15:23, ambapo ingemaanisha yeye alikuwa wa Yudea pekee)

2. jina la baba yake (kama vile Yohana 6:71; 13:2,26) 3. "mtu wa uadui" au mwuaji, ambapo ingemaanisha yeye pia alikuwa Zelote, kama Simoni

◙ “torati, na manabii" Hii inarejea juu ya sehemu mbili za sheria za kanisa la Kiebrania: Sheria, Manabii, na Maandiko (ambayo yaliendelea kujadiliwa huko Jamnia katika 90 a.d.). Ilikuwa nahau kwa ajili ya kurejea Agano la Kale zima.

◙ “Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti" Hii inapaswa kueleweka katika upande wa matumizi ya Kiyahudi. Kisha Yesu aliishi katika Nazarethi na baba yake wa nyumbani aliitwa Yusufu. Hii haipingi kuzaliwa kwa Yesu huko Bethlehemu (kama vile Mika 5:2), wala kuzaliwa Kwake na bikra (kama vile Isa. 7:14). Tazama Mada Maalumu ifuatayo.

MADA MAALUMU: YESU MNAZARETI Kuna maneno mbalimbali ya Kiyunani ambayo Agano Jipya hutumia kumzungumzia Yesu.

A. Haya ni maneno ya Agano Jipya 1. Nazarethi – mji katika Galilaya (kama vile Luka 1:26; 2:4,39,51; 4:16; Mdo. 10:38). Mji huu

hautajwi katika vyanzo vya wakati huu, bali umekutwa katika kumbukumbu ya maandishi ya baadaye. Kwa upande wa Yesu kuwa alitoka Nazarethi haikujitosheleza (kama vile Yohana 1:46). Alama ya msalaba wa Yesu ambayo imeliweka jina la eneo hili ilikuwa alama ya aibu kwa Wayahudi.

2. Nazarēnos – pia inataja maeneo ya kijiografia (kama vile Luka 4:34; 24:19). 3. Nazōraios – inaweza kuurejea juu ya mji, lakini pia ingeweza kuwa mwaminifu na mtenda haki

Masihi wa Kiebrania "Utanzu" (netzer, BDB 666, KB 718 II, kama vile Isa. 11:1; maana zinazokaribiana, BDB 855, Yer. 23:5; 33:15; Zek. 3:8; 6:12; iliyodokezwa katika Ufu. 22:16). Luka akilitumia hili kumhusu Yesu katika 18:37 na Mdo. 2:22; 3:6; 4:10; 6:14; 22:8; 24:5; 26:9.

4. Iliyohusiana na #3 nāzir (BDB 634, KB 684), ambalo linamaanisha "aliyewakifishwa kwa maana ya nadhiri."

B. Matumizi ya Kihistoria ya neno nje ya Agano Jipya. 1. Lilimaanisha kundi la ausi la Kiyahudi (Mkristo wa awali) (nāsōrayyā ya Kiaramu). 2. Lilitumika katika mzunguko wa Kiyahudi kuwatambulisha waamini katika Kristo (kama vile

Matendo 24:5,14; 28:22, nosri). 3. Lilikuja kuwa neno la kawaida katika kumaanisha waamini katika makanisa ya Kisiria (Kiaramu).

"Mkisto" lilitumika katika makanisa ya Kyunani kumaanisha waamini. 4. Wakati mwingine baada ya kuanguka kwa Yerusalemu, Wafarisayo walikusanyika huko huko

Page 53: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

37

Jamnia na walichochea utengano rasmi kati ya sinagogi na kanisa. Mfano wa aina ya maapizo ya mazungumzo dhidi ya Wakristo unapatikana katika "the Eighteen Benedictions" from Berakoth 28b-29a, ambayo "Wanazarethi." "Wanazareti na awaasi waliweza kutoweka kwa muda mfupi; walifutwa kutoka katika kitabu cha uzima na kutoandikwa kuwa walikuwa na imani."

5. Ilitumiwiwa na Justin Martyr, Dial. 126:1, ambaye alitumia netzer ya (Isa. 11:1) kumhusu Yesu.

C. Maoni ya Mwandishi Nashangazwa sana na herufi za maneno, Ingawa nafahamu kwamba hili ni jambo geni kusikika katika Agano la Kale "Yoshua" ina herufi mbalimbali katika Kiebrania. Maelezo yafuatayo yananisababisha kubaki na mashaka kama maana yake dhahiri : 1. kama vile maana yake ya karibu na neno la Kimasihi “tawi” (netzer) au neno lililo sawa nāzir

(aliyepakwa mafuta kwa maana ya nadhiri) 2. vidokezo hasi vya eneo la Galilaya kuyahusu mataifa 3. uchache au kutokuwepo kwa uthibitisho wa fasili za sasa kukusu mji wa Nazarethi katka Galilaya 4. inatoka katika kinywa cha pepo katika maana ya hukumu (yaani, "Umekuja kutuangamiza?").

Kwa wasifu kamili wa masomo ya kundi la neno hili, tazama Colin Brown (ed.), New International Dictionary of New Testament Theology, juzuu. 2, uk. 346 au Raymond E. Brown, Birth of the Messiah, kur. 209-213, 223-225.

1:46 "Nathanaeli akamwambia, Laweza neno jema kutoka Nazareti?'" Ni dhahiri kwamba Filipo na Nathanaeli waliwafahamu manabiii wa Agano la Kale; Masihi angekuja Bethlehemu (kama vile Mika 5:2) karibu na Yerusalemu, si Nazareti katika Galilaya ya Mataifa, bali Isa. 9:1-7 inadokeza jambo hili sana!

1:47 NASB, NKJV, NRSV "hamna hila ndani yake" TEV "hakuna kilisicho sahihi kwake" NJB "katika yeye hakuna udanganyifu"

Hii inamaanisha mwanadamu mnyoofu asiye tahayari (kama vile Zab. 32:2), mwakilishi wa kweli wa watu wateule, Israeli.

1:48 "Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona” Ni dhahiri Yesu alitumia maarifa Yake ya kiroho (yaani, Yohana 2:24-25; 4:17-19,29; 6:61,64,71; 13:1,11,27,28; 16:19,30; 18:4) kutoa ishara kwa Nathanaeli ambayo ilikuwa ya Kimasihi. Ni vigumu kuelewa ni kwa namna gani Uungu wa Yesu na ubinadamu ulifanya kazi. Katika baadhi ya mazingira yasiyofahamika kama alitumia nguvu ya "rohoni" au uwezo wa kibinadamu. Hapa mfano ni uwezo wa "rohoni."

1:49 "Nathanaeli akamjibu, Rabi, wewe u wana wa Mungu….Mfalme wa Israeli" Nukuu vichwa hivi vya somo viwili! Vyote vina vidokezo vya uzalendo wa Kimasiha (yaani, Zaburi 2). Wanafunzi hawa wa kale walimwelewa Yesu katika namna za Kiyahudi katika karne ya kwanza. Hawakuuelewa utu Wake kamili na kazi kama Mtumishi Aliyeteswa (kama vile Isa. 53) hadi baada ya Ufufuko.

1:51 NASB “Amini, amini, nawaambieni ninyi” NKJV “Amin, amin, nawaambia” NRSV “Nawaambieni kweli” TEV “Nawaambieni ninyi kweIi” NJB “Katika kweli yote”

Page 54: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

38

Kimaandishi hii ni “Amina! Amina!” Yesu akilirudia mara mbili neno hili linalopatikana tu katika Injili ya Yohana, ambapo limeonekana mara ishirini na tano. "Amina" ni muundo wa neno la Kiyunani kwa imani (emeth) ambalo linamaanisha "kukubaliwa" (tazama Mada Maalumu; Sadiki, Amini, Imani na Uaminifu katika Agano la Kale). Lilitumika katika Agano la Kale kama sitiari kwa uimara na uaminifu. Lilikuja kutafsiriwa kama "imani" au "uaminifu." Hata hivyo, katika wakati mwingine lilikuja kutumika katika ukubalifu. Katika nafasi ya asili ya sentensi hii, ilikuwa njia pekee ya kuuvuta utiyari juu ya umuhimu wa Yesu, semi za tumaini au ufunuo kutoka kwa YHWH (kama vile Yohana 1:51; 2:3,5,11; 5:19,24,25; 6:26,32,47,53; 8:34,51,58; 10:1,7; 12:24; 13:16,20,21,38; 14:12; 16:20,23; 21:18). Angalia mabadiliko ya wingi (kiwakilishi na kitenzi). Hii imepaswa kuwa imetangazwa kwa wote walio simama pale.

MADA MAALUM: AMINA

I. AGANO LA KALE A. Neno “Amina” linatoka kwenye neno la Kiebrania lenye maana ya

1. “ukweli” (emun, emunah, BDB53) 2. “Uaminifu” (emun, emunah, BDB 53) 3. “imani” au “uaminifu” 4. “amini” (dmn, BDB 52)

B. Asili yake ya neno inadokeza mkao wa mwili wa mtu ulivyo imara. Kinyume cha hili kinaonyesha

mwili wa mtu Yule asio imara, unaotereza (kama vile. Zab. 35:6; 40:2; 73:18; Yeremia 23:12) au kizuizi (kama vile. Zab. 73:2). Kutokana na utumiaji huu wa fasihi unatengeneza upanuzi wa kiisitiari wa imani, uaminifu, utiifu na wa kutegemewa (kama vile. Hab. 2:4)

C. Utumiaji maalumu (angalia mada maalumu: kuamini, amini, imani na uaminifu katika agano la kale) 1. Nguzo, 2 Fal. 18:16 (1 Tim. 3:15) 2. Kuthibitika, Kut. 17:12 3. Uimalifu, Kut. 17:12 4. Uthabiti, Isa. 33:6 5. Ukweli, 1 Fal. 10:6; 17:24; 22:16; Mit. 12:22 6. Thabiti, 2 Nya. 20:20; Isa. 7:9 7. Stahili (sheria alizopewa Musa), Zab. 119:43,142,151,160

D. Katika Agano la Kale maneno mawili ya Kiebrania yanatumika kwa ajili ya imani thabiti 1. Bathach (BDB 105), imani 2. Yra (BDB 431), hofu, heshima, abudu (kama vile. Mwa. 22:12)

E. Kwa maana ya kuamini au uaminifu ulioanzishwa kwa matumizi ya liturujia ambao ulitumika

kuthibitisha maelezo ya kweli ya mtu mwingine (kama vile. Hes. 5:22; Kumb. 27:15-26; 1 Fal. 1:36; 1 Nya. 16:36; Neh. 5:13; 8:6; Zab. 41:13; 72:19; 89:52; 106:48; Yer. 11:5; 28:6).

F. Kiongozi cha kithiolojia kwenye neno hili sio uaminifu wa mwanadamu, bali ni wa Mungu mwenyewe (kama vile Kut. 34:6; Kumb. 32:4; Zab.108:4; 115:1; 117:2; 138:2). Tumaini la mwanadamu aliyeanguka ni neema, uaminifu, kutii Agano la Mungu na ahadi zake. Wale wanaomfahamu Mungu wanahitajika kufanana naye (kama vile. Hab. 2:4). Biblia ni historian na kumbu kumbu ya Mungu kurejesha taswira yake (kama vile Mwa. 1:26-27) kwa mwanadamu. Wokovu unarejesha uwezo wa mwanadamu kuwa na ushirika wa ndani na Mungu. Hii ndio sababu ya kuumbwa kwetu.

Page 55: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

39

II. AGANO JIPYA

A. Utumiaji wa neno “amina” kama hitimisho la kiliturujia kwa minajili ya kuthibitisha ukweli wa maelezo/taarifa ni la kawaida katika Agano Jipya (kama vile. 1 Kor. 14:16; Ufu. 1:7; 5:14; 7:12).

B. Utumiaji wa neno kama kifungio cha maombi ni wa kawaida kwenye Agano Jipya (kama vile. Rum. 1:25; 9:5; 11:36; 16:27; Gal. 1:5; 6:18; Efe. 3:21; Flp. 4:20; 2 The. 3:18; 1 Tim. 1:17; 6:16; 2 Tim. 4:18).

C. Yesu ndiye yeye aliyelitumia hili neno (limezidishwa mara 25 katika Yohana, yaani., Yohana 1:51; 3:3,5,11; n.k.) kuyatambulisha maelezo muhimu (kama vile. Luka 4:24; 12:37; 18:17,29; 21:32; 23:43).

D. Linatumika kama cheo kwa Yesu katika Ufu. 3:14 (pia angalia 2 Kor. 1:20, yamkini jina la heshima la Mungu kutoka Isa. 65:16)

Dhana ya kusadiki au sadiki, au kuamini au amini inaelezewa katika neno la Kiyunani pistos au pistis, ambalo linatafasiliwa katika Kiingereza kama “imani”,“sadiki”,“kuamini”(angalia mada maalumu: Sadiki, Kuamini au Imani).

◙ "ninyi, ninyi" Hizi zote ziko katika hali ya wingi. Yesu anawaambia wote ambao walikuwa wamesimama pale, kwa maana ya, wanadamu wote!

◙ "Mtaziona mbingu zimefunguka" Kifungu hiki kina mzunguko wa ufahamu wa mwanadamu juu ya Mungu katika Agano la Kale.

1. Ezekieli, Eze. 1:1 2. Yesu, Mt. 3:16; Marko 1:10; Luka 3:21 3. Stefano, Mdo. 7:56 4. Petro, Mdo. 10:11 5. Ujio wa mara ya Pili, Ufu. 19:11

Hii ni kauli tendaji timilifu ambayo inadokeza aliyebaki kufunuliwa. Neno "mbingu" ni wingi kwa sababu katika Kiyunani ni wingi. Hii inaweza kumaanisha (1) angani juu ya nchi kama katika Mwanzo 1 au (2) uwepo wa wingi wa Mungu.

MADA MAALUMU: MBINGU NA MBINGU YA TATU

Katika Agano la Kale neno “mbingu” mara nyingi iko kwenye hali ya wingi (yaani, shamayim, BDB 1029, KB 1559). Neno la Kiebrania hii inamaanisha “urefu.” Mungu anaishi mahali pa juu. Dhana hii inaakisi utakatifu na uwezo mkuu wa Mungu. Katika Mwa.1:1, wingi, "mbingu na dunia," vimetazamwa kama vitu vilivyoumbwa na Mungu (1) angani juu ya hii sayari au (2) njia ya kuitaja kweli yote (yaani, ya kiroho na ya kimwili). Kutokana na uelewa huu wa kimsingi maandiko mengine yalitajwa kama marejeo kwa viwango vya Kimbingu: "mbingu ya mbingu" (kama vile Zab. 68:33) au "mbingu na mbingu ya mbingu" (kama vile Kumb. 10:14; 1 Fal. 8:27; Neh. 9:6; Zab. 148:4). Wanasheria walidhani kwamba kungekuwa na

1. mbingu mbili (yaani, R. Yuda, Hagigah 12b) 2. mbingu ya tatu (Test. Lawi 2-3; Ascen. ya Isa. 6-7; Midrash Tehillim kwenye Zab. 114:1) 3. mbingu ya tano (III Baruch) 4. Mbingu ya saba (R. Simon b. Lakish; Ascen. ya Isa. 9:7) 5. mbingu ya kumi (II Enoch 20:3b; 22:1)

Hizi zote zilikuwa na maana ya kuonyesha utenganisho wa Mungu kutoka katika uumbaji uonekanao na /au mipaka Yake. Zaidi ya namba za kawaida za mbingu katika sheria za Kiyahudi zilikuwa saba. A. Cohen, Everyman's Talmud (uk. 30), anasema hii ilihusishwa na elimu sayari, lakini nafikiri inataja juu ya saba kama namba timilifu (yaani, siku za uumbaji na kuwakilisha pumziko la Mungu siku ya saba katika Mwanzo 2:2). Paulo, katika 2 Kor. 12:2, anataja mbingu "ya tatu" (Kiyunani ouranos)kama njia ya kuutambulisha upekee wa Mungu,

Page 56: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

40

uwepo wa ukuu. Paulo alikutana na Mungu binafsi

◙ “na malaika wa Mungu wakikwea na kushuka” Hii inaudokeza uzoefu wa Yakobo huko Betheli (kama vile Mwa. 28:10ff). Yesu anadai kwamba Mungu alihaidi kuyatoa mahitaji yote ya Yakobo, Mungu aliyatoa mahitaji Yake yote!

◙ “juu ya Mwana wa Adamu” Hii ni mamlaka ya uteuzi wa Yesu mwenyewe. Kilikuwa kifungu cha Kiebrania kilichomhusu mwanadamu (kama vile Zab. 8:4; Eze. 2:1). Lakini kwa sababu ya matumizi yake katika Dan. 7:13, kilichukuliwa katika viwango vya Uungu. Neno hili halikuwa na vidokezo vya kizalendo au vya kinguvu kwa sababu halikutumiwa na viongozi wa dini ya Kiyahudi. Yesu alilichagua hili kwa sababu limejumuisha namna mbili za asili Yake (mwanadamu na Uungu, kama vile 1 Yohana 4:1-3). Yohana akimtaja Yesu kwa kulitumia kwake Yeye mara kumi na tatu.

MASWALI YA MJADALA

Huu ni mwongozo wa fasiri, ina maanisha kwamba unawajibika kwa tafsiri zako mwenyewe za Biblia. Kila mmoja wetu lazima atembee katika mwanga tulio nao. Wewe, Biblia, na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Hutakiwi uvitelekeze vitu hivi kwa mfasiri. Maswali ya mjadala huu yanatolewa kukusaidia kufikiri juu ya mambo makubwa ya sehemu za kitabu hiki. Yanalenga kukuamsha kimawazo na sio kutoa maana.

1. Kwa nini watu kutoka Yerusalemu walimuuliza Yohana Mbatizaji kama yeye ni mmoja wa watu mashuhuri watatu wa Agano la Kale?

2. Tambua usemi wa Kikristo ambao Yohana Mbatizaji aliutengeneza kumhusu Yesu katika Yohana 1:19-30. 3. Kwa nini vidokezo na injili ya Yohana inatofautisha sana juu ya wito wa wanafunzi? 4. Nini ujumbe ambao watu wanauelewa kumhusu Yesu? Nukuu majina yenye vyeo waliyokuwa wakimuita

Yeye (Yohana 1:38). 5. Yesu alijiitaje? Kwa nini?

Page 57: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

41

YOHANA 2

MIGAWANYO YA AYA YA TAFSIRI ZA KISASA

UBS4 NKJV NRSV TEV NJB Harusi ya Kana Maji kubadilika kuwa Harusi ya Kana Harusi pale Kana Harusi ya Kana Divai 2:1-11 2:1-12 2:1-11 2:1-3 2:1-10 2:4 2:5 2:6-10 2:11 2:11-12 2:12 2:12 2:12 Kulisafisha Hekalu Yesu analisafisha Hekalu kulisafisha Hekalu kulisafisha Hekalu 2:13-22 2:13-22 2:13-22 2:13-17 2:13-22 2:18 2:19 2:20 2:21-22 Yesu anawajua Mtambuzi wa Roho Maarifa ya Yesu juu ya Yesu akiwa watu wote asili ya Mwanadamu Yerusalemu 2:23-25 2:23-25 2:23-25 2:23-25 2:23-25

MZUNGUKO WA TATU WA USOMAJI KUFUATILIA KUSUDIO LA ASILI LA MWANDISHI KATIKA NGAZI YA AYA Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwatafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Aya ya kwanza 2. Aya ya pili 3. Aya ya tatu 4. N.k

UTAMBUZI WA KIMUKTADHA KWA 2:1-11

A. Yesu alikuwa wa tofauti ni viongozi wengine wa dini katika nyakati zake. Alikunywa na kula na watu wa kawaida. Wakati Yohana alikuwa mtu wa faragha toka jangwani, Yesu alikuwa mtu wa wazi akiwa na watu wa kawaida.

B. Muujiza wake wa kwanza ulikuwa wa kawaida uliojulikana! Uliohusika kumjali mtu wa kawaida, unamwainisha Yesu kama hasira yake dhidi ya watu wa kidini wenye kujihesabia haki binafsi

Page 58: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

42

wakiutazamisha upande mwingine wa tabia zake. Kipaumbele cha watu, na sio tamaduni au ibada zilizo muhimu, yalidhihilisha uhuru wa Yesu, na bado yakarejeshwa kwa matarajio ya kitamaduni.

C. Hii ni moja kati ya ishara saba ambazo Yohana alitumia kudhihilisha tabia na nguvu za Yesu (Yohana 2-11) 1. Maji kuwa Divai (Yohana 2:1-11) 2. Uponyaji wa kijana (Yohana 4:46-54) 3. Uponyaji wa kiwete (Yohana 5:1-18) 4. Kuulisha umati wa watu (Yohana 6:16-21) 5. Kutembea juu ya maji (Yohana 6:16-21) 6. Kumponya kipofu (Yohana 9:1-41) 7. Kumfufua Lazaro ( Yohana 11:1-57)

D. Injili ya Yohana haikuundwa kimfumo wa matukio bali uliundwa kimfumo wa kithiolojia. 2 Yohana ni

mfano mzuri. Mwanzoni kabisa, Yohana alishughulika na Yesu akijaribu kuwafikia Wayahudi (kwa ujumla viongozi na watu wa kawaida) lakini hawakuamini/kupokea. Kwa sababu ya kutokuamini kwao na haki binafsi za kidini, Yesu akaikataa Uyahudi. 1. Mabirika sita ya kujitawadhia, yakiwa yamejazwa pomoni, yanawasilisha dini ya Kiyahudi ambayo

Yesu aliibadili. 2. Kulisafisha Hekalu (ambao kiumri lilitokea mwanzoni mwa wiki ya mwisho ya maisha ya Yesu)

kulinukuliwa kabla kama alama ya awali ya kithiolojia ya kukataa kwake uongozi wa Kiyahudi. Mfano mwingine mzuri wa muundo wa kimaandiko wa Yohana ni Nikodemasi (mwana dini) wa Yohana 3 na mwanamke pale kisimani (binti asiye na dini) katika Yohana 4 . Hapa kuna “kishikiza vitabu” kwa watu wote.

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 2:1-11 1Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo. 2Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake. 3Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai. 4Yesu akamwambia, Mama, tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia. 5Mamaye akawaambia watumishi, Lo lote atakalowaambia, fanyeni. 6Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu. 7Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza hata juu. 8Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza. Wakapeleka. 9Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi, 10akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa. 11Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.

2:1 “Palikuwa na harusi” Harusi zilizofanyika vijijini zilikuwa ni tukio kubwa la kijamii. Mara nyingi lilijumuisha jamii nzima na huenda zilidumu hata siku saba.

◙ “Kana” Hili neno limetajwa tu katika injili ya Yohana (Yohana 2:1, 11; 4:46; 21:2). Tunafahamu kitu fulani kuhusu.

1. Mjini kwa Nathanaeli 2. Mahali pa muujiza wa kwanza wa Yesu 3. Karibu na Kapernaumu

Kuna sehemu nne zinazodhaniwa (AB, Vol.1, uk. 827) 1. Ain Qana, maili moja Kaskazini mwa Nazareti 2. Kafr Kanna, yapata maili tatu Kaskazini Mashariki mwa Nazareti 3. Khirbet Qana, umbali yapata mail nane na nusu Kaskazini mwa Nazareti, 4. Kana kwenye uwanda wa Asochis huko Kana ambao umetajwa na Yusufu (life, 86,206).

Page 59: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

43

Mahali pa uwanda palipotajwa panaonekana kwendana na jina la Kana, ambalo ni neno la Kiebrania lenye maana ya “tete/mafunjo” (yaani, ufito wa mwanzi)

◙ “Mama wa Yesu pia alikuwepo” Yawezekana Maria Magdalena alikuwa akisaidiana na waandaji wa harusi. Hili laweza kuonekana katika (1) utoaji wa maelekezo kwa wahudumu (kama vile Yohana 2:5) na (2) uhusika wake kwenye vinywaji (kama vile Yohana 2:3). Hawa yamkini, walikuwa ni ndugu na rafiki wa familia.

2:3 “Hawana divai” Ilikuwa ni lazima kwa taratibu za Kiebrania kwa wageni kupewa mvinyo. Hii mvinyo hakika ilichachushwa, kama tunavyoona (1) maneno ya mshereheshaji, Yohana 2:9-10; (2) taratibu za Wayahudi wakati wa siku za Yesu; au (3) ukosefu wa hatua za kiafya na viungio vya kikemikali.

MADA MAALUM: MTAZAMO WA KIBIBLIA KUHUSIANA NA KILEVI NA MATUMIZI MABAYA YA KILEVI

I. Maneno ya Kibiblia A. Agano la Kale

1. Yayin – Hili ni neno la jumla la divai (BDB 406, KB 409), ambalo limetumika mara 141. Asili ya neno hili si yumkini kwa sababu haitokani na mzizi wa Kiebrania. Hiii mara nyingi inamaanisha juisi ya matunda iliyochacha, mara nyingi tunda aina ya balungi. Baadhi ya vifungu bainishi ni Mwa. 9:21; Kut. 29:40; Hes. 15:5,10.

2. Tirosh – Hiii ni "divai mpya" (BDB 440, KB 1727). Kwa sababu ya tabia ya nchi ya Mashariki ya Karibu, uchachu unaanza ndani ya masaa sita baada ya kutengeneza juisi. Neno hili hurejerea juu ya divai katika hatua ya kuchachusha. Kwa vifungu vibainishi tazama Kut. 12:17; 18:4; Isa. 62:8-9; Hos. 4:11.

3. Asis – Kwa uhalisia hiki ni kinywaji aina ya kileo ("divai mpya," BDB 779, KB 860, m.f. Yoeli 1:5; Isa. 49:26).

4. Sekar – Hili ni neno "kinywaji kikali" (BDB 1016, KB 1500). Mziziz wa Kiebrania unatumika ndani ya neno "kulewa" au "mlevi." Mara nyingi huu unaongezwa katika ndni yake ili kukifanya kileweshe zaidi. Hiki ni sawa na yayin (kama vile Mit. 20:1; 31:6; Isa. 28:7).

B. Agano Jipya 1. Oinos – neno lililo sawa kimaana na yayin 2. Neos oinos (divai mpya) – neno linalofanana la Kiyunani sawa na tirosh (kama vile Marko 2:22). 3. Gleuchos vinos (divai mpya, asis) – ni ile divai inayotengenezwa katika hatua za mwanzo kabla

ya kuchachushwa (kama vile Matendo ya Mitume 2:13).

II. Matumizi ya Kibiblia A. Agano la Kale

1. Mvinyo ni zawadi ya Mungu (Mwa. 27:28; Zab 104:14-15; Mhu. 9:7; Hos. 2:8-9; Yoeli 2:19,24; Amosi 9:13; Zek. 10:7).

2. Divai ni swehemu ya sadaka ya kuteketeza (Kut. 29:40; Law. 23:13; Hes. 15:7,10; 28:14; Kumb. 14:26; Amu. 9:13).

3. Divai inatumika kama tiba (2 Sam. 16:2;Mit. 31:6-7). 4. Divai inaqweza kuwa chanzo cha tatizo (Nuhu –Mwa. 9:21; Lutu – Mwa. 19:33,35; Samsoni –

Waamuzi 16; Nabali – 1 Sam. 25:36; Uria– 2 Sam. 11:13; Amnon i– 2 Sam. 13:28; Ela– 1 Fal. 16:9; Ben-hadad i– 1 Fal. 20:12; Watawala – Amosi 6:6; na Wanawake – Amos 4).

5. Divai inaweza kutumika vibaya (Mit. 20:1; 23:29-35; 31:4-5; Isa. 5:11,22; 19:14; 28:7-8; Hosea 4:11).

6. Divai ilizuiliwa kwa makundi fulani (makuhani waliokuwa katika zamu, Law. 10:9; Eze. 44:21; Wanazareti, Hesabu 6; na watawala, Mit. 31:4-5; Isa. 56:11-12; Hosea 7:5).

7. Divai ilitumika katika mpangilio wa matukio ya siku za mwisho (Amosi 9:13; Yoeli 3:18; Zek. 9:17).

Page 60: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

44

1. Kipindi cha uwazi kati ya Agano laKale na Agano Jipya 2. Divai katika upatanisho ina msaada (Ecclesiasticus 31:27-33). 3. Walimu wa Sheria za Kiyahudi wanasema, "Divai kuu kuliko tiba zote, mahali palipo na uhaba

wa divai, madawa yalevyayo yanahitajika." (BB 58b).

C. Agano Jipya 1. Yesu alikibadili kiwango kikubwa cha maji katika divai (Yohana 2:1-11). 2. Yesu alikunywa divai (Mt. 11:18-19; Luka 7:33-34; 22:17 na kuendelea) 3. Petro alidhihakiwa kwa ulevi "mvinyo mpya" siku ya Pentekoste (Mdo. 2:13). 4. Divai inaweza kutumika kama matibabu (Marko 15:23; Luka 10:34; 1 Tim. 5:23). 5. Watawala hawatakiwi kuwa watumiaji wabaya. Hii haimaanishi kujinyima molja kwa moja (1

Tim. 3:3,8; Tito 1:7; 2:3; 1 Pet. 4:3). 6. Divai ilitumika katika kupangili matukio ya siku za mwisho (Mathayo 22:1na kuendelea; Ufu.

19:9). 7. Divai ililaaniwa (Mt. 24:49; Luka 12:45; 21:34; 1 Kor. 5:11-13; 6:10; Gal. 5:21; 1 Pet. 4:3; Rum.

13:13-14).

III. Utambuzi wa ndani wa Kithiolojia A. Mkazo wa Kiupembuzi

1. Divai ni zawadi kutoka kwa Mungu. 2. Ulevi ni tatizo kubwa. 3. Waamini katika baadhi ta tamaduni yawapasa kuweka uhuru wa mipaka yao kwa ajili ya injili (Mt.

15:1-20; Marko 7:1- 23; 1 Wakorintho 8-10; Warumi 14). B. Mwelekeo wa kwenda nje ya mipaka

1. Mungu ndiye mwanzilishi wa mambo yote. a. chakula– Marko 7:19; Luka 11:44; 1 Kor. 10:25-26 b. mambo yote yasiyo najisi – Rum. 14:14,20; 1 Tim. 4:4 c. mambo yote ya halali – 1 Kor. 6:12; 10:23 d. mambo yote yaliyo safi– Tito 1:15

2. Mwanadamu aliyeanguka ametumia vibaya zawadi ya Mungu kwa kuzitumia nje ya mipaka ya Mungu aliyoitoa.

C. Matumizi mabaya yako ndani yetu, si ndani ya vitu. Hakuna kilicho kiovu ndani ya uuumbaji wa vitu vinanyoonekana (tazama B. 1. Hapo juu).

IV. Utamaduni wa Karne ya kwanza ya Kiyahudi na Chachu A. Chachu hunza ndani ya muda mfupi, takribani ndani ya masaa 6 baada ya barungi kusagwa B. Desturi ya Kiyahudi inasema kwamba povu linapoonekana juu yake (dalili ya uchachu), hii huelekea

kuwa sehemu ya divai iliyo na uchachu (Ma aseroth 1:7). Hiii iliitwa "divai mpya" au "divai tamu." C. Chachu ya kwanza iliyo kali uilikamilishwa baada ya juma moja. D. Chachu ya pili ilichukuwa sku zipatazo 40. Katika hatua hii tendo hili lilifikiriwa kama "divai kukuu" na

ingweza kutolewa madhabahuni (Edhuyyoth 6:1). E. Divai ambayo iliyobakizwa ndani ya machicha (divai kongwe) ilifikiriwa kuwa nzuri, lakini ilitakiwa

kuchujwa vizuri kabla ya kutumiwa. F. Divai ilifikiriwa kuwa kuukuu kwa usahihi baada ya kutunzwa vema kwa ajili ya kuchachushwa. Miaka

mitatu kilikuwa kipindi cha muda mrefu ambapo divai ingetunzwa kwa usalama. Hii iliitwa "divai kuuku" na ilitakiwa kuchanganywa na maji.

G. Ni katika miaka 100 ya mwisho pekee ya ukame wa mazingira na ongezeko la madawa uchachu umetoweka. Ulimwengu wa kale usingeweza kustisha tendo la asili la kuchachusha.

V. Maelezo ya Kiufugaji

Page 61: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

45

A. Hakikisha uzoefu wako, thiolojia, na fasiri ya kibiblia havimkashifu Yesu na ile karne ya kwanza ya Kiyahudi/Utamaduni wa ki- Kristo! Hawa kwa uwazi hawakujinyima moja kwa moja.

B. Mimi sitetei matumizi haya ya kilevi kwa jamii. Hata hivyo, wengi huchochea nafasi ya Biblia juu ya somo hili na sasa wanadai keki kuu iliyojikita katika utamaduni/ubaguzi wa kimadhehebu.

C. Kwangu mimi, Warumi 14 na 1 Wakorintho 8-10 zimetoa utambuzi na mwongozo uliojikita katika upendo na heshima kwa waamini wenetu na kuieneza injili ndani ya utamaduni wetu, si uhuru binafsi au ukosoaji wa hukumu. Ikiwa Biblia ni chanzo pekee cha imani na matendo, bila shaka yatupasa wote kufikiria upya juu ya jambo hili.

Ikiwa tunahimiza kujinyima moja kwa moja kama mapenzi ya Mungu, nini tunachokimaanisha juu ya Yesu, pamoja na zile tamaduni za sasa ambazo kwa hali ya mazoea hutumia divai (m.f. Ulaya, Israeli, Argentina).

2:4 “mwanamke” Katika Kiingereza hii inaashiria ukari, lakini ilikuwa ni nahau ya Kiebrania, cheo cha heshima (kama vile Yohana 4:21; 8:10; 19:26; 20:15). NASB "tuna nini mimi nawe?" NKJV "tunahusianaje mimi nawe?" NRSV "tunahusiana vipi mimi nawe?" TEV "usiniambie nini cha kufanya" NJB "unahitaji nini kwangu?" Hii ni nahau ya ya Kiebrania, hasa ikimaanisha “tuna nini mimi nawe” (kama vile Amu. 11:12; 2 Sam. 16:10; 19:22; 1 Fal. 17:18; 2 Fal. 3:13; 2 Nya. 35:21; Mt. 8:29; Marko 1:24; 5:7; Luk 4:34; 8:28; Yoh. 2:4). Yawezekana huu ulikuwa mwanzo mpya wa uhusiano wa Yesu na familia yake (kama vile Mt. 12:46ff; Luka 11:27-28). ◙ “saa yangu haijawadia” Hii inaonyesha uelewa binafsi wa Yesu kuhusu kusudi lake aliloliweka (kama vile Marko 10:45). Yohana alilitumia neno “saa” katika nyanja tofauti.

1. Juu ya wakati (kama vile Yohana 1:39; 4:6,52,53; 11:9; 16:21; 19:14; 19:27) 2. Juu ya siku ya mwisho (kama vile Yohana 4:21,23; 5:25,28) 3. Juu ya siku zake za mwisho (kukamatwa, majaribu, kifo, kama vile Yohana 2:4; 7:30; 8:20; 12:23,27; 13:1;

16:32; 17:1)

2:5 “lolote atakalowaambia, fanyeni” Maria Magdalena hakujua maoni ya Yesu kama alikuwa akizuia moja kwa moja utendaji kwa niaba yake katika hali hii.

2:6 NASB "kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha" NKJV "kuhusu tabia ya kutawadha" NRSV "kwa kanuni za Kiyahudi za kutawadha" TEV "Wayahudi wana sheria zao kuhusu taratibu za kutawadha" NJB "kwa sababu ya kutawadha ambayo ni kanuni ya Wayahudi" Mabalasi haya ya maji yalitumiwa kwenye siku za kutawadha miguu, mikono, vyombo n.k. Yohana alitoa mawazo haya ili kuwasaidia watu wa mataifa kuuelewa muundo. 2:6-7 “mabalasi sita ya mawe” Kama ilivyo kawaida kwa Yohana, hii inaonekana kuwa alama yenye makusudi mawili.

1. Kuwasaidia maharusi 2. Hatimaye Ilikuwa alama ya uchaguzi dhidi ya Yesu kama utimilisho wa dini ya Kiyahudi. Sababu iliyopo

katika maelezo haya ya mwisho yaweza kuwa a. Namba “6” ni mfano wa jitihada za mwanadamu

Page 62: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

46

b. Hitaji la Yesu kuyajaza mpaka pomoni yawezekana kuwa na maana fulani, sio tu kutoa divai zaidi. c. Uwingi wa divai, ulikuwa mwingi zaidi ya kusanyiko la ile sherehe. d. Divai ilikuwa alama ya utele wa enzi mpya (kama vile Yer. 31:12; Hos. 2:22; 14:7; Yoeli 3:18; Amo 9:12-

14).

◙ “kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu” Kipimo kilichotumika kilikuwa ni neno la Kiebrania bath. Palikuwa na ukubwa wa aina tatu tofauti wa baths uliotumika katika siku za Yesu kwa hiyo jumla yake haijulikani, lakini muujiza huu ulihusisha uwingi wa divai.

MADA MAALUM: UZANI NA VIPIMO VYA MASHARIKI YA KARIBU YA KALE (USOMAJI WA VIPIMO)

Uzani na vipimo vilivyotumika katika masuala ya biashara vilikuwa ni vya muhimu katika uchumi wa kilimo hapo kale. Biblia inawasihi Waisrael kuwa wasiwe na upendeleo kwenye mambo yao wanayoyafanya na wengine (kama vile Law. 19:35-36; Kumb. 25:13-16; Mith. 11:1; 16:11; 20:10). Tatizo kubwa lilikuwa sio tu uaminifu, bali kutokuwepo na istilahi zilizo sawa na muundo uliotumika huko Palestina. Inaonekana kuwa palikuwepo jozi mbili za uzani; moja “nyepesi” na nyingine “nzito” kwa kila idadi (angalia The Interpreter's Dictionary of the Bible, juzuu ya 4, uk. 831). Pia muundo wa desimali (ulioegamia kwenye sehemu ya 10) wa Misri umekuwa ukijumuishwa na sehemu ya 6 huko Mesopotamia.

Wingi wa “vipimo” na “idadi”vilivyotumika vilitokana na sehemu ya mwili wa mwanadamu, wanyama, mizigo, vibebeo vya wakulima, hakuna hata kimoja kilichokuwa sawia. Kwa hiyo, chati hapa chini ni makadilio tu na ya majaribio. Njia rahisi ya kuonyesha uzani na vipimo iko katika jedwali la kimahusiano

I. Maneno ya ujazo yanayotumika mara nyingi A. Vipimo vya vitu vikavu

1. Homeri (BDB 330, yumkini "mzigo wa punda," BDB 331), mf., Law. 27:16; Hosea 3:2 2. Lateki (AU lethech, BDB 547, yumkini inadokeza katika Hosea 3:2) 3. Efa (BDB 35), mf., Kut. 16:36; Law. 19:36; Ezek. 45:10-11,13,24 4. Se'ah (BDB 684), mf., Mwa. 18:6; 1 Sam. 25:18; 1 Fal. 18:32; 2 Fal. 7:1,16,18 5. Homeri (BDB 771 II, yumkini "mganda" [safu ya mbegu zilizoanguka], BDB 771 I), mf., Kut.

16:16,22,36; Law. 23:10-15 6. Hini (BDB 798, "sehemu ya kumi" ya efa), mf., Kut. 29:40; Law. 14:21; Hes. 15:4; 28:5,13 7. Kibaba ( BDB 866), kama vile 2 Fal. 6:25

B. Vipimo vya vimiminika 1. Kori (BDB 499), mf., Ezek. 45:14 (inawezakuwa kipimi cha vitu vikavu, kama vile II Nya. 2:10;

27:5) 2. Bathi (BDB 144 II), mf., I Fal. 7:26,38; II Nya. 2:10; 4:5; Isa. 5:10; Ezek. 45:10-11,14 3. Hini (BDB 228), mf., Kut. 29:40; Law. 19:36; Ezek. 45:24 4. Logi (BDB 528), kama vile Law. 14:10,12,15,21,24

C. Chati (iliyochukuliwa toka kwa Roland deVaux, Ancient Israel, juzuu. 1, uk. 201 na Encyclopedia Judaica, juzuu. 16, uk. 379)

II. I

stila

Homeri (kikavu) =Kori kimiminika au kikavu

1

Efa (kavu) =bathi (kimiminika) 10 1

Se’ah (kikavu) 30 3 1

Hini (kimiminika) 60 6 2 1

Homeri (kikavu) 100 10 - - 1

Kibaba (kikavu) 180 18 6 3 - 1

Logi (kimiminika) 720 72 24 12 - 4 1

Page 63: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

47

hi za uzani zinazotumika mara kwa mara A. Uzani wa aina tatu unaotumika mara nyingi ni talanta, shekeli, na gera.

1. Kipimo kikubwa katika Agano la Kale ni taranta. Toka Kutoka 38:25-26 tunajifunza kuwa taranta moja ni sawa na shekeli 3,000 (yaani., “uzani wa jumla,” BDB 503)

2. Neno shekel (BDB 1053, “uzani”) hutumia mara nyingi kama inavyodhaniwa, lakini hakijaelezewa katika andiko. Kuna thamani mbali mbali za shekeli zilizotajwa katika Agano la Kale. a. "kipimo cha kibiashara" (toleo la NASB la Mwa. 23:16) b. "shekeli ya madhabahuni" (toleo la NASB la Kut. 30:13) c. "kwa uzani wa Mfalme" (toleo la NASB la II Sam. 14:26), pia uliitwa "uzani wa Kifalme"

kwenye mafunjo ya Elephantine. 3. Gera (BDB 176 II) ilithaminiwa na shekeli 20 (kama vile Kut. 30:13; Law. 27:25; Hes. 3:47; 18:16;

Ezek. 45:12). Uwiano ulitofautiana toka Mesopotamia hadi Misri. Israeli ilifuatisha uthaminishaji uliokuwa ukitumika huko Kaanani(Ugariti)

4. Mina (BDB 584) inathaminishwa na shekeli 50 au 60. Neno hili linapatikana hasa katika vile vitabu vya Agano la Kale (yaani Ezek. 45:12; Ezra 2:69; Neh. 7:71-72). Ezekieli ilitumia uwiano wa 1 ya 60, wakati Wakaanani walitumia uwiano wa 1 ya 50.

5. Beka (BDB 132, "nusu ya shekeli," kama vile Mwa. 24:22) imetumika mara mbili katika Agano la Kale (kama vile Mwa. 24:22; Kut. 38:26) na inathaminishwa na nusu shekeli. Jina lake linamaanisha "kugawanya."

B. Chati 1. Imesimamia juu ya Vitabu vitano vya Torati

Taranta 1

Mina 60 1

Shekel 3,000 50 1

Beka 6,000 100 2 1

Gera 60,000 1,000 20 10 1

2. Ikisimamia juu ya Ezekieli

Taranta 1

Mina 60 1

Shekeli 3,600 60 1

Beka 7,200 120 2 1

Gera 72,000 1,200 20 10 1

2:8 NASB "Mkuu wa meza" NKJV "Mkuu wa sherehe" NRSV "Mwandalizi mkuu" TEV "Msimamizi wa sherehe" NJB "Raisi wa sherehe" Mtu huyu awezakuwa (1) mgeni mheshimiwa aliyesimamia sherehe (2) mtumwa aliyehusika kuhudumia wageni.

2:10 Hoja hapa ni kuwa mara zote divai bora ni ile iliyohudumiwa kwanza. Baada ya wageni kuathiriwa, divai ya kiwango cha chini ilitolewa. Lakini hapa ile bora ilitolewa mwisho! Hapa panaonekana kuwepo na utofauti kati ya

Page 64: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

48

agano la kale (divai ya kale) katika dini ya Kiyahudi na agano jipya (divai mpya) katika Yesu (kama vile kitabu cha Waebrania). Kitendo cha Yesu kulisafisha hekalu (kama vile Yohana 2:13-25, inavyonekana inaondoa utaratibu wa kimatukio wa Yohana kwa kusudi la kithiolojia) inaweza maanisha kweli hii.

2:11 “mwanzo huo wa ishara” Injili ya Yohana imezungukwa na ishara saba na tafasiri zake. Hii ndo ya kwanza. Angalia Mada maalumu: Archē katika Yohana 1:1

◙ “akaudhihirisha utukufu wake, na wanafunzi wake wakaamini kupitia yeye” Udhihirisho (angalia dokezo la kitenzi katika Yohana 1:31) wa utukufu wa Yesu (angalia mada maalumu: Utukufu [Agano la Kale]) lilikuwa kusudi la miujiza. Huu muujiza, kama ilivyokuwa mingine, inaonekana kuelekezwa hasa hasa kwa wanafunzi wake! Hii hairejerei tendo la imani la awali, lakini uelewa wao unaoendelea wa mtu wao na kazi. Ishara hii inadhihirisha ukweli wa mtu na kazi ya Masiha. Haifahamiki kama wageni walitambua kilichotokea.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 2:12 12Baada ya hayo akashuka mpaka Kapernaumu, yeye na mama yake na ndugu zake na wanafunzi wake; wakakaa huko siku si nyingi.

2:12 “Kapernaumu” Baada ya watu wa Nazareti kutokumuamini (kama vile Lk. 4:16-30) hapo pakawa makao yake huko Galilaya (kama vile Mt. 4:13; Marko 1:21; 2:1; Lk. 4:23,31; Yoh. 2:12; 4:46-47).

◙ Huu ni muonekano wa pekee ndani ya huduma ya Yesu dhidi ya familia yake, katika kuutazamisha huu muujiza pale cana.

UTAMBUZI WA MUKTADHA WA 2:13-25

A. Pamekuwepo na majadiliano mengi kati ya wasomi wa Agano Jipya kwa namna Yesu alivyolisafisha hekalu. Yohana aliweka kumbu kumbu ya kujisafisha mapema katika huduma ya Yesu, wakati mihutasari ya injili (Mt. 21:12; Marko 11:15 na Luka 19:45) ilielezea juu ya kulisafisha ndani ya wiki ya mwisho ya maisha ya Yesu. Hata hivyo, yawezekana Yohana aliyaangalia matendo ya Yesu kwa kusudi la kithiolojia (yaani, Yohana anathibitisha Uungu kamili wa Yesu toka mlango wa 1). Kila mwandishi wa injili alikuwa na uhuru chini ya uvuvio kuchagua, kujongea, kupanga, na kuyafupisha matendo ya Yesu na mafundisho yake. Siamini kama walikuwa na uhuru kuweka maneno ya kusema mdomoni mwa Yesu au kuweka matukio. Lazima ikumbukwe kuwa injili sio wasifu wa kisasa, bali ni vijitabu vya uinjilisti kwa viongozi waliochaguliwa. Injili sio utaratibu wa matukio, ama uwekaji wa kumbu kumbu ya maneno ya Yesu (kiasi mihitasari). Hii haimanishi kuwa hayako sahihi. Fasihi za kimashariki zililenga kwenye matarajio ya tamaduni tofauti kuliko fasihi zile za magharibi. Angali Gordon Fee na Douglas Stuart, How To Read the Bible For All Its Worth, ukur. 127-148.

B. Tendo la kulisafisha hekalu lilifaa kusudi lote la kithiolojia la Yohana juu ya Yesu kushughulika kwanza na taifa la Kiyahudi. Hili linaweza kuonekana katika majadiliano na Nikodemasi katika Yohana 3 (imani ya dini ya Kiyahudi). Akianza na yule mwanamke msamaria.

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 2:13-22 13Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; naye Yesu akakwea mpaka Yerusalemu. 14Akaona pale hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng'ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi. 15

Akafanya kikoto cha kambaa, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng'ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao; 16akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya;

Page 65: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

49

msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara. 17Wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa imeandikwa, Wivu wa nyumba yako utanila. 18

Basi Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Ni ishara gani utuonyeshayo, kwamba unafanya haya? 19

Yesu akajibu, akawaambia, Livunjeni hekalu hili, nami katika siku tatu nitalisimamisha. 20Basi Wayahudi wakasema, Hekalu hili lilijengwa katika muda wa miaka arobaini na sita, nawe utalisimamisha katika siku tatu? 21Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wake. 22Basi alipofufuka katika wafu, wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa alisema hivi, wakaliamini lile andiko na lile neno alilolinena Yesu.

2:13 “Pasaka” Sherehe hizi za mwishoni mwa mwaka zimeelezea katika kitabu cha kutoka 12 na Kumbu Kumbu la Torati 16:1-6. Sherehe hizi ndo njia pekee tulio nayo ya kuweka tarehe kuhusu huduma ya Yesu. Mihtasari ya injili zinamaanisha kuwa Yesu alihudumu kwa muda wa mwaka mmoja (yaani, pasaka moja imetajwa). Lakini Yohana ametaja Pasaka tatu: (1) Yoh. 2:13,23; (2) Yoh. 6:4 na (3) Yoh. 11:55; 12:1; 13:1; 18:28,39; 19:14. Pia pana uwezekano wa kuwepo ya nne katika Yohana 5:1. Hatufahamu ni kwa muda gani huduma ya Yesu ilidumu, lakini injili ya Yohana inatoa maoni ya kwamba huenda ilidumu kwa muda wa miaka mitatu na yawezekana mine au hata mitano. Yohana aliitengeneza/kuiandika injili yake wakati wa sikukuu za Kiyahudi (Pasaka, Hema Takatifu, na sikukuu za kuwasha mishumaa, angalia Richard N. Longenecker, Biblical Exegesis in the Apostolic Period, 2nd ed., kur. 135-139).

MADA MAALUMU: PASAKA

I. Maelezo ya awali A. Tendo la Kiungu la hukumu ya Wamisri na ukombozi wa Waisrael ni muguso wa upendo wa YHWH na

uimalishaji wa taifa la Israel (yaani, kwa manabii). B. Kutoka kwa Waisrael ni timizo maalumu la ahadi ya YHWH kwa Abraham katika Mwa. 15:12-21. Pasaka

inafanya ukumbusho wa kutoka kwa wana wa Israel. C. Huu ulikuwa wa mwisho, uliosambaa (kijografia, yaani., Misri na Goshen) na uharibifu mkubwa (

wazaliwa wa kwanza wa binadamu na wanyama waliuwawa) kwa mapigo kumi yalitumwa na YHWH kwenda Misri na Musa.

II. Neno lenyewe (BDB 820, KB 947) A. Maana ya nomino haijulikani

1) Iliyohusishwa na “mapigo” pamoja na “kipigo cha maaafa” (yaani., Kut. 11:1); Malaika wa Mungu walipiga wazaliwa wa kwanza wa binadamu na mifugo.

B. Maana ya kitenzi 1) “kuchechemea” au “kuchopea” (kama vile 2 Sam. 4:4), likitumika katika maana ya “ruka juu ya

nyumba zilizotiwa alama” (yaani., Kut. 12:13,23,27, BDB 619, maarufu kama maelezo ya asili ya neno)

2) “kucheza” (kama vile 1Fal. 18:21) 3) Muakkadia-“kuridhisha” 4) Mmisri-“kupiga” 5) Vitenzi vilivyo sambamba katika Isa. 31:5, “kusimama ili kumlinda” kama vile REB ya Kut. 12:13) 6) Milio ya Wakristo wa mwanzo iliyozoeleka kati ya pasha ya Kiebrania na paschō ya Kiyunani,

“kuumwa/kuumia” C. Uwezekano wa mambo ya kihistoria yaliyowekewa umuhimu wa kwanza

1) Sadaka ya mchungaji kwa mwaka mpya 2) Sadaka ya bedui na chakula cha jumuiya wakati wa kuondoa mahema kwenda uwanda wa

malisho kuepuka uovu. 3) Sadaka ya kuijepusha na uovu dhidi ya wachungaji wanao hama hama

D. Sababu ni ngumu kuwa nazo uhakika wa kujua maana ya neno lenyewe, lakini vile vile na asili yake ni kwamba mambo mengi yaliyotofautiana kuhusu pasaka pia yanapatikana katika matambiko

Page 66: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

50

mengine ya kale. 1) Tarehe za majira ya kuchepua 2) Maelezo ya asili na historia ya neno haijulikani 3) Limehusianishwa na walinzi wa usiku 4) Utumiaji wa damu 5) Michoro/sanamu za malaika na mapepo 6) Chakula maalumu 7) Dalili za kilimo (mikate isiyotiwa chachu) 8) Hakuna kuhani, hakuna madhabahu, wala mtizamo wa mahali Fulani

III. Matukio

A. Tukio lenyewe limeandikwa katika kitabu cha Kutoka 11-12 B. Sikukuu za mwaka zimeelezewa katika Kutoka 12 na kujumuishwa ndani ya sherehe ya siku nane

zikiwa na sikukuu za mikate isiyotiwa chachu. 1) Mwanzoni kabisa yalikuwa ni matukio ya kawaida, kama vile Kutoka. 12:21-23; Kumbu. 16:5

(kama vile Hes. 9) a. Hakuna kuhani b. Hakuna madhabahu maalumu c. Utumiaji uliobobea wa damu

2) Lilikuja kuwa ni tukio la madhabahu iliyokuwa kuu 3) Muunganikano huu wa kawaida wa utoaji sadaka (yaani., damu ya mwana kondoo kufanya

ukumbusho wa kifo cha malaika) na sikukuu ya mavuno katika madhabahu kuu ilitimizwa kwenye mwezi wa karibu na mwezi wa tatu au nne 14 na 15-21

C. Mfano wa umiliki wa wazaliwa wote wa kwanza wa watu na wanyama na ukombozi wao umeelezewa katika Kut. 13

IV. Wajibu wa kihistoria wa kushikilia mila na desturi A. Pasaka ya kwanza ilisherehekewa huko Misri, Kutoka 12 B. Katika mlima Horeb/Sinai, Hesabu 9 C. Pasaka ya kwanza ilisherehekewa huko Caanan (Gilgali) Yosh. 5:10-12 D. Kipindi cha Sulemani cha kuwakufisha hekalu, 1Fal. 9:25 na 2Nya. 8:12 (yamkini, lakini haijaelezwa

rasmi) E. Ile moja wakati wa kutawala kwa Hezekia F. Ile moja wakati wa mageuzi ya Yoasi G. Angalia 2 Fal. 23:22 na 2 Nya. 35:18 inatajwa wakati wa Israeli kukataa kuitunza hii sikukuu ya

mwaka. V. Umuhimu wake

1) Hii ni moja kati ya siku tatu za sikukuu ya mwaka iliyohitajika (kama vile Kut. 23:14-17; 34:22-24; Kumb. 16:16):

2) Pasaka/ mikate ilyotiwa chachu 3) Sikukuu za wiki 4) Sikukuu za vibanda

A. Musa alionyeshwa kabla siku itakayoangaliwa katika madhabahu kuu(kwa vile palikuwepo na sikukuu zingine mbili) katika kumbu kumbu la torati

B. Yesu alitumia wasaa la chakula cha pasaka ya mwaka (au siku kabla) kuthihirisha Agano Jipya katika mfano wa mkate na divai, lakini hakutumia mwana kondoo.

1) Chakula cha pamoja 2) Sadaka ya ukombozi 3) Umuhimu wa kuendeleza katika kizazi kijacho

Page 67: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

51

◙ “naye Yesu akakwea mpaka Yerusalemu” Mara zote Wayahudi waliongea kuhusu Yerusalemu katika maana ya kithiolojia zaidi ya maana ya kijografia

2:14 “pale hekaluni” Herode mkuu (Idumaya aliyeitawala Palestina toka 37-4 K.K) hekalu liligawanywa katika mahakama saba tofauti. Mahakama ya nje ilikuwa ni mahakama ya watu wa mataifa, mahali ambapo wafanya biashara waliweka maduka yao ili kuwahudumia wale wote waliohitaji kutoa sadaka na wale walioleta sadaka maalumu.

◙ “ng’ombe, kondoo na njiwa” Watu walitembea umbali mrefu wakihitaji kununua wanyama kwa ajili ya kutoa sadaka itakayokubaliwa. Hata vivyo, familia ya kuhani mkuu ilisimamia maduka haya na kutoza gharama kubwa ya wanyama hawa. Pia tunafahamu kuwa kama watu wataleta mifugo yao kuhani angalisema haifai kwa sababu ina dosari kwenye miili yao. Kwa hiyo, walihitaji kununua mifugo hiyo toka kwa wachuuzi hawa.

◙ “wavunjaji wa pesa” kuna maelezo aina mbili ya uhitaji wa hawa watu: (1) pesa iliyohitajika kuchuliwa hekaluni ilikuwa shekeli tu. Kwa vile shekeli ya Kiyahudi ilikwisha acha kutumika, hekaluni kulikubaliwa shekeli toka Tiro katika siku za Yesu au (2) hakuna sarafu yenye kichwa cha mfalme wa Rumi ilikubaliwa kutolewa. Palikuwepo, na gharama ya kutoa.

2:15 “Akafanya kikoto cha kambaa, akawatoa wote katika hekalu” Mjeredi huu umetajwa hapa tu. Hasira ya Yesu inaweza onekana hapa. Mahali ambapo Mungu angetambuliwa palikuwa tena si mahali pa kuabudia na mafunuo! Hasira kama hasira yenyewe si dhambi! Maelezo ya Paulo katika Efeso 4:26 yamkini inahusiana na hiki kitendo. Kuna vitu ambavyo vinaweza kututia hasira.

2:16 “Yaondoeni haya” Hii ni kauli tendaji timilifu shurutishi yenye kusisitiza, “viondoweni vitu hivi”

◙ “msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara” Hii ni kauli shurutishi ya wakati uliopo ikiwa na kiambata hasi ikimaanisha kuzuia kitendo ambacho tayari kipo katika mchakato. Injili zingine (yaani., Mt. 21:13; Marko 11:17; Luka 19:46) nukuu Isa. 56:7 na Yer. 7:11 katika suala hili, hata hivyo, katika Yohana nabii hizi za Agano la Kale hazikutajwa. Hii yawezekana kuwa kiini macho kwenye unabii wa kimasiha wa Zak. 14:21

2:17 “Wanafunzi wake wakakumbuka” Maelezo haya yanamaanisha kuwa katika mwanga wa huduma ya Yesu na kwa msaada wa Roho, watu hawa wakaona ukweli wa kiroho wa matendo ya Yesu baadaye (kama vile Yoh. 2:22; 12:16; 14:26).

◙ “ya kuwa imeandikwa” Hii ni kauli tendewa timilifu yenye kutumia mafungu badala ya maneno, ambayo kifasihi ni “kama ilivyoandikwa”. Ilikuwa ni njia ya kawaida ya kuthibitisha uvuvio wa Agano la Kale (kama vile Yoh. 6:31,45; 10:34; 12:14; 20:30). Hii ni nukuu toka katika Zab. 69:9 katika maandiko ya kale ya Kiyunani (LXX). Zaburi hii, kama Zaburi ya 22, inafaa katika kusurubishwa kwa Yesu. Ari ya Yesu kwa Mungu na ibada yake ya kweli ikamwongoza kuelekea mauti, ambapo ndo yalikuwa mapenzi ya Mungu (kama vile Isa. 53:4,10; Luka 22:22; Mdo. 2:23; 3:18; 4:28).

2:18 NASB "Ni ishara gani utuonyeshayo, kwamba unafanya haya” NKJV "Ni ishara gani utatuonyesha, tangu uyatende haya” NRSV "Ni ishara gani utatuonyesha kwa kufanya haya” TEV "Ni muujiza gani utaufanya kwetu kwamba una haki ya kuyatenda haya” NJB "Ni ishara gani utatuonyesha kwetu kwamba unayatenda haya” Hili lilikuwa ni swali kuu la Wayahudi kumhusu Yesu. Mafarisayo walidai kuwa nguvu zake zinatoka na shetani (kama vile Yoh. 8:48-49,52; 10:20). Walitarajia masihi kufanya kitu fulani kwa njia fulani (yaani., kama Musa).

Page 68: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

52

Alipoacha kuyatenda haya matendo, walianza kumtilia shaka (kama vile Marko 11:28; Luka 20:2), kama alivyofanya hata Yohana Mbatizaji.

2:19 “Livunjeni hekalu hili, nami katika siku tatu nitalisimamisha” Neno la Kiyunani la hekalu (hieron) katika Yohana 2:14 na 15 unarejerea eneo la hekalu, wakati neno (naos) katika Yohana 2:19,20, na 21 inarejerea madhabahu ya ndani. Kumekuwepo na majadiliano mengi kuhusu maelezo haya. Hasa katika Mt. 26:60ff, Marko 14:57-59; Mdo. 6:14 hii ni nukuu juu ya kuteswa na kufufuka kwa Yesu. Hata hivyo, katika mazingira haya ni lazima pia ihusiane kwa kiasi fulani na hekalu lenyewe lililovunjwa katika mwaka 70 B.K na Tito (kama vile Mt. 24:1-2). Maelezo haya mawili yanahusiana katika kweli ile Yesu alikuwa akitengeneza juu ya ibada mpya ya kiroho ikijitazamisha kwake mwenyewe na siyo dini ya Kiyahudi ya kale (kama vile Yohana 4:21-24). Tena, Yohana alitumia neno kwa maana mbili!

2:20 “Hekalu hili lilijengwa katika muda wa miaka arobaini na sita” Herode Mkuu akaliongeza na kulifinyanga upya hekalu la pili (kutoka siku za Zerubabel, cf. Hagai) kujaribu kuwatuliza Wayahudi kwa kuonyesha tabia za ki-Esau (aliyeuza haki yake ya uzaliwa wa kwanza). Yusufu anatuambia kwamba ilianza katika mwaka wa 20 au 19 B.K. kama hii ni kweli, inamaanisha kuwa tukio hili hasa lilitokea katika mwaka wa 27-28 B.K. Pia tunajua ya kwamba kazi iliendelea hekaluni mpaka 64 B.K. Hekalu hili limekuja kuwa tumaini kubwa la Wayahudi (kama vile Yeremia 7). Mbadala wa hili atakuwa Yesu mwenyewe, hekalu jipya. Katika Yohana 1:14, amechaguliwa kama hema takatifu na sasa hekalu! Ni kishindo kiasi gani toka kwa fundi selemala! Mungu na mwanadamu sasa wanakutana na kufanya ushirika katika Yesu!

2:21 “Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wake” Wakati Yesu akiwa anayaongea maneno haya wanafunzi hawakuweza kuyatambua haya (kama vile Yohana 2:17). Kumbuka Yohana anaandika baada ya mwongo mmoja (miaka kumi). Yesu anafahamu ni kwa nini alikuja. Yawezekana kuwepo na makusudi matatu.

1. Kumthihirisha Mungu 2. Kuutengeneza utu wa kweli 3. Kutoa maisha yake kama mbadala wa wengi

Ni hili kusudi la mwisho ambalo mstari huu unaongelea (kama vile Marko 10:45; Yohana 12:23,27; 13:1-3; 17:1).

2:22 “wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa alisema hivi” Mara nyingi maneno na matendo ya Yesu yalikuwa zaidi kwa faida ya wanafunzi kuliko wale aliokuwa akiwahutubu. Mara zote hawakujua muda huo.

◙ “wakaliamini lile andiko” Ingawa neno lenyewe halisemi ni andiko lipi, yawezekana Zab. 16:10 ni andiko la ufufuko ambalo alikuwa akidokeza (kama vile Mdo. 2:25-32; 13:33-35). Andiko lile lile (au dhana ya kithiolojia ya ufufuo) imetajwa katika Yohana 20:9

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 2:23-25 23 Hata alipokuwapo Yerusalemu kwenye sikukuu wakati wa Pasaka, watu wengi waliamini jina lake, walipoziona ishara zake alizozifanya. 24 Lakini Yesu hakujiaminisha kwao; kwa kuwa yeye aliwajua wote; 25 na kwa sababu hakuwa na haja ya mtu kushuhudia habari za mwanadamu; kwa maana yeye mwenyewe alijua yaliyomo ndani ya mwanadamu.

2:23 “watu wengi waliamini jina lake” Neno “amini” ni kutoka katika neno la Kiyunani (pisteō) ambalo pia laweza kutafasiliwa kama “kuamini,” “imani,” “amini”. Nomino haitokei katika injili ya Yohana, lakini kitenzi mara nyingi kinatumika. Katika mazingira haya kuna uwalakini kwenye uhalisia wa kusanyiko kujitoa kwa Yesu wa Nazareti kama Masiha. Imani ya kweli ya Kibiblia ni zaidi ya uwajibikaji wa awali. Lazima ufuatane na mchakato wa uanafunzi (kama vile Mt. 13:20-22,31-32). Wazi kabisa waamini wa juujuu walivutwa kuja kwa Yesu kwa sababu ya miujiza yake (kama vile Yohana 2:11; 7:31). Kusudi lao lilikuwa kuuthibitisha ubinadamu wa Yesu na kazi zake. Hata hivyo, lazima ijulikane kuwa imani katika kazi kubwa ya Yesu haikutosha, imani stahimilivu (kama vile Yohana 4:38; 20:29). Kitu lazima kiwe Yesu

Page 69: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

53

mwenyewe. Kiwastani miujiza sio alama ya Mungu (kama vile Mt. 24:24; Ufu. 13:13; 16:14; 19:20). Kazi za Yesu zilikuwa kwa ajili ya kuwaongoza watu kuwapeleka kwenye imani katika Yeye (kama vile Yoh. 2:23; 6:14; 7:31; 10:42); mara nyingi watu waliona miujiza lakini wakashindwa kuamini (kama vile Yoh. 6:27; 11:47; 12:37).

MADA MAALUMU: MATUMIZI YA YOHANA YA NENO “KUAMINI”

Kimsingi Yohana anaunganisha “kuamini” na vivumishi. A. eis inamaanisha “ndani ya.” Muundo huu wa kipekee unasisitizia waumini kuweka imani zao kwa

Yesu 1. ndani ya jina lake (Yohana 1:12; 2:23; 3:18; 1 Yohana 5:13) 2. ndani yake (Yohana 2:11; 3:15,18; 4:39; 6:40; 7:5,31,39,48; 8:30; 9:36; 10:42; 11:45,48;

12:37,42; Mt. 18:6; Mdo. 10:43; Fil. 1:29; 1 Pet. 1:8) 3. ndani yangu (Yohana 6:35; 7:38; 11:25,26; 12:44,46; 14:1,12; 16:9; 17:20) 4. ndani ya mwanaye (Yohana 3:36; 9:35; 1 Yohana 5:10) 5. ndani ya Yesu (Yohana 12:11; Mdo. 19:4; Gal. 2:16) 6. ndani ya nuru (Yohana 12:36) 7. ndani ya Mungu (Yohana 14:1)

B. ev inamaanisha “katika” kama ilivyo katika Yohana 3:15 (Marko 1:15) C. uhusika wa mahali usio na kivumishi (1 Yohana 3:23; 4:50; 5:10) D. hoti likimaanisha “kuamini kwamba,” inatoa kilichomo kama kile kinachotakiwa kuaminiwa. Baadhi ya

mifano ni 1. Yesu ni Mtakatifu wa Mungu (Yohana 6:69) 2. Yesu ni Mimi ndiye (Yohana 8:24) 3. Yesu katika Baba na Baba ndani yake (Yohana 10:38) 4. Yesu ni Masiha (Yohana 11:27; 20:31) 5. Yesu ni mwana wa Mungu (Yohana 11:27; 20:31) 6. Yesu alitumwa na Babaye (Yohana 11:42; 17:8,12) 7. Yesu ni wamoja na Babaye (Yohana 14:10-11) 8. Yesu alikuja toka kwa Babaye (Yohana 16:27,30) 9. Yesu anajitambulisha mwenyewe katika jina la Agano la Babaye “Mimi ndiye” (Yohana 8:24;

13:19) Imani ya Kibiblia katika yote ni nafsi na ujumbe! Inathibitishwa na utii, upendo, na usitahimilivu.

2:24-25 Hii ni sentesi moja katika Kiyunani. Umuhimu wa neno “kuamini” (ni kauli tendaji elekezi isiyo timilifu ya “kuamini” inayokanusha) inatumika katika mazingira haya kuelezea matendo ya Yesu na mwenendo. Ina maana zaidi kuliko ukubalifu wa awali. Sentesi pia iandai kuwa maaarifa ya Yesu juu ya kuabdilika na uovu wa moyo wa mwanadamu (unatazamisha maarifa ya Mungu, kama vile Mwa. 6:11-12,13; Zab. 14:1-3). Aya inaelezeawa na Nikodemus katika Yohana 3. Hata “Bwana dini” hakuweza kwa jitihada zake, maarifa, msimamo, aua umri ili kukubalika mbele za Mungu. Haki huja tu kupitia kuamini/imani/amini katika Yesu( kama vile Rum. 1:16-17; 4).

MASWALI YA MJADALA

Huu ni mwongozo wa fasiri, ina maanisha kwamba unawajibika kwa tafsiri zako mwenyewe za Biblia. Kila mmoja wetu lazima atembee katika mwanga tulio nao. Wewe, Biblia, na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Hutakiwi uvitelekeze vitu hivi kwa mfasiri. Maswali ya mjadala huu yanatolewa kukusaidia kufikiri juu ya mambo makubwa ya sehemu za kitabu hiki. Yanalenga kukuamsha kimawazo na sio kutoa maana.

1. Kwa nini Yesu aligeuza maji kuwa divai? Ina maanisha nini? 2. Elezea desturi za ndoa enzi ya Yesu

Page 70: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

54

3. Unaweza kuchora ramani ya hekalu la Herode? Unaweza onyesha mahali penyewe pa wanunuzi na wauzaji

4. Kwa nini mihitasari haikuweka kumbu kumbu juu ya kulisafisha hekalu hapo awali 5. Je Yesu aliwahi kutabiri juu ya uharibifu wa hekalu la Herode 6. Taja na uelezee neno la Kiyunani lenye maana sawa na “amini”, “kuamini” na “imani”

.

Page 71: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

55

YOHANA 3

MIGAWANYO YA AYA YA TAFSIRI ZA KISASA UBS4 NKJV NRSV TEV NJB

Yesu na Nikodemu Kizazi kipya Yesu na mtoto wa afisa Yesu na Nikodemu Mazungumzo na Nikodemu 3:1-15 3:1-21 3:1-10 3:1-2 3:1-8 3:3 3:4 3:5-8 3:9 3:9-21 3:10-13 3:11-15 3:14-17 3:16-21 3:16 3:17-21 3:18-21 Yesu na Yohana Yohana Mbatizaji Shuhuda za zida Yesu na Yohana Yohana anatoa Mbatizaji anamwinua Kristo za Yohana ushuhuda kwa Mara ya kwanza 3:22-30 3:22-36 3:22-24 3:22-24 3:22-24 3:25-30 3:25-26 3:25-36 3:27-30 Ajaye kutoka Ajaye kutoka Mbinguni Mbinguni 3:31-36 3:31-36 3:31-36

MZUNGUKO WA TATU WA USOMAJI KUFUATILIA KUSUDIO LA ASILI LA MWANDISHI KATIKA NGAZI YA AYA Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwatafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Aya ya kwanza 2. Aya ya pili 3. Aya ya tatu 4. N.k

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 3:1-3 1Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi. 2Huyo alimjia usiku,

Page 72: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

56

akamwambia, Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye. 3Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu

3:1 “Mafarisayo” Chanzo cha vyama vya siasa/dini unarejea nyuma kwenye kipindi cha ufuasi wa kiongozi wa Kiyahudi wa Yuda wa karne ya pili. Majina yao yawezekana yalimaanisha “waliotengwa.” Walikuwa waaminifu na waliojitoa kuzitunza sheria za Mungu kama zilivyokuwa zimeandikwa na kuelezewa kwenye buku la taratibu na sheria za Kiyahudi (Talmud). Kama ilivyo leo baadhi yao walikuwa watu wa kweli wa Agano (Nikodemo, Yusufu wa Arimathaya), lakini baadhi walikuwa ni wenye kujidai, wenye kujihalalisha, wenye kuhukumu, “wanavyoonekana” watu wa agano (kama vile Isa. 6:9-10; 29:13). Moyo ndio ufunguo wa kila kitu! “Agano Jipya” (Yer. 31:31-34) linajitazamisha kwenye msukumo wa ndani (yaani, moyo mpya, mawazo mapya, sheria zilizo andikwa moyoni). Utendaji wa kibinadamu umeonyeshwa, haujitosherezi kama ilivyokuwa. Tohara ya moyo katika Kumbu Kumbu la Torati 10:16; 30:6 ni sitiari kwa imani binafsi ambayo inatoa kuelekea kwenye utii na shukrani.

Ushikiliaji wa kidini na/ au msimamo wa kutopenda mabadiliko ni kitu kibaya sana. Wanathiolojia lazima watoe toka kwenye upendo na imani. Angalia MADA MAALUMU: MAFARISAYO Katika Yohana 1:24 ◙ “Nikodemo” Inashangaza kwa Myahudi wa Palestina kuwa na jina moja la Kiyunani (kama alivyofanya Philipo na Andrea, kama vile Yohana 1:40,43). Likimaanisha “mshindi wa watu” (kama vile Yohana 7:50; 19:39)

NASB, NKJV "mtawala wa Wayahudi" NRSV, NJB "kiongozi wa Wayahudi" TEV "kiongozi Myahudi"

Katika muktadha huu, hiki ni kifungu cha kiufundi kwa wanajamii wa Sinagogi kuu (katika mazingira mengine ingalimaanisha kiongozi wa Sinagogi ya mahali maalum), wanajamii sabini wa mahakama kuu ya wananchi wa Kiyahudi katika Yerusalemu. Mamlaka yake yaliwekewa ukomo na Warumi, lakini bado ina alama muhimu kubwa kwa watu wa Kiyahudi. Angalia mada maalum hapo chini. Yamkini inaonekana kuwa Yohana alimtumia Nikodemo kama mwakilishi wa dini ya Kiyahudi yenye imani kamili Katika karne ya kwanza. Wale waliofikiria wamefika kiroho waliambiwa waanze tena. Imani katika Yesu, wasio waminifu katika watawala (hata katika utawala wa Kimungu, kama vile Kor. 2:16-23), wala historia ya nyuma ya kijamii (kama vile Yohana 8:31-59), inaamua uraia wa mtu katika ufalme. Zawadi ya Mungu katika Kristo, sio uaminifu, sio uchaji wa Mungu wa matusi, bali ni mlango katika ukubarifu wa Kimungu. Ukubalifu wa Nikodemu juu ya Yesu kama mwalimu toka kwa Mungu, ingawa ni kweli, lakini ulikuwa haujitoshelezi. Imani binafsi, imani ya kujitenga, imani ya mwisho katika Kristo kama Masihi ni tumaini pekee la binadamu aliyeanguka (kama vile Yohana 1:12)!

MADA MAALUMU: WAKUU WA BARAZA LA SINAGOGI

I. Chanzo cha habari A. Agano Jipya lenyewe B. Flavian Yusufu wa mambo ya kale ya Kiyahudi C. Sehemu ya Mishna juu ya sheria za kiibada za Kiyahudi (yaani eneo la watu wa Sinagogi kuu).

Bahati mbaya Agano Jipya na Yusufu hawakubaliani na maandiko ya sheria za Kiyahudi, ambazo zinaonekana kuwathibitisha watu wawili wa Sinagogi kuu katika Yerusalemu, kuhani mmoja (yaani., Msadukayo), akidhibitiwa na kuhani mkuu na akishughulika na haki za jamii na uhalifu na wa pili ikidhibitiwa na mafarisayo na waandishi, waliohusiana na mambo ya kidini na kitamaduni. Hata hivyo, tarehe za maandiko ya sheria za Kiyahudi toka mwaka 200 B.K na kuangazia hali ya kitamaduni baada ya Yerusalemu kuangukia mikononi mwa kamanda Tito wa Rumi, mwaka wa 70 B.K. wayahudi (yaani., uongozi wa kifarisayo) waliimarisha tena makao makuu yao kwa minajili ya maisha ya kidini katika mji uitwao Jamnia na baadaye (yaani mwaka wa 118 B.K) wakaondoka kwenda Galilaya.

Page 73: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

57

II. Istilahi Tatizo la kumtambua mtu wa kimahakama unahusisha majina tofauti yanayojulikana. Kuna maneno mengi yaliyotumika kuelezea watu wa kimahakama ndani ya jamii ya Kiyahudi ya Yerusalemu.

A. Gerousia-“senati” au “baraza.” Hili ni neno la zamani lililotumika kwenye kipindi cha mwisho cha Uajemi (kama vile vitu vya asili ya kale vya Yusufu 12.3.3 na II Wamakabayo 11:27). Linatumiwa na Luka katika Mdo 5:21 pamoja na “watu wa Sinagogi kuu.” Yaweza kuwa ni njia ya kuelezea neno kwa viongozi wanaoongea Kiyunani (kama vile Wamakabayo 12:35)

B. Synedrion- “watu wa Sinagogi kuu.” Huu ni muunganikano toka syn (pamoja na) na hedra (nafasi). Cha kushangaza neno hili linatumiaka katika lugha ya Kiarama, lakini likitazamisha neno la Kiyunani mwishoni mwa kipindi cha Wamakabayo hili likajakuwa ni neno linalokubalika kuunda mahakama kuu ya Kiyahudi katika Yerusalemu (kama vile Mt. 26:59; Marko 15:1; Luka. 22:66; Yohana 11:47; Mdo 5:27). Tatizo hapa linakuja wakati maneno yale yale yanatumika katika mabaraza ya kimahakama ya mahali fulani nje ya Yerusalemu (kama vile Mt. 5:22; 10:17)

C. Presbyterion- “baraza la wazee” (kama vile Luka 22:66). Huu ni mfumo wa Agano la Kale la viongozi

wa kikabila. Hata hivyo, ilikuja kurejerea mahakama kuu katika Yerusalemu (kama vile Mdo. 22:5) D. Boulē –neno hili “baraza”lilitumiwa na Yusufu (yaani vita 2.16.2; 5.4.2, lakini sio agano jipya) kuelezea

watu mbali mbali wa kimahakama: 1. Seneti kwenye mji wa Rumi 2. Mahakama za kawaida za Rumi 3. Mahakama kuu ya Kiyahudi katika Yerusalemu 4. Mahakama za kawaida za Kiyahudi

Yusufu wa Arimataya ameelezewa kama mwanajumuiya ya watu wa Sinagogi kuu kwa muundo wa neno hili (yaani., bouleutē, likimaanisha “mkuu wa baraza” kama vile Marko 15:43; Luka 23:50)

III. Maendeleo ya kihistoria Mwanzoni kabisa Ezra alisema kulitengeneza Sinagogi kuu (kama vile Targum katika Wimbo ulio Bora 6:1)katika kipindi cha uhamisho, ambacho kilikuja onekana kuwa watu wa sinagogi kuu katika siku za Yesu.

A. Mishna (yaani., sheria za kiibada za Kiyahudi) zimeweka kumbu kumbu kwamba palikuwepo mahakama mbili kuu katika Yerusalem (kama vile Sanh. 7:1) 1. Moja iliyokuwa imeundwa na wanajumuiya 70 (au 71) (sand. 1:6 hata inaelezewa kuwa Musa

alitengeneza hilo baraza la kwanza la watu wa Sinagogi kuu (Sanhedrin) la watu 11, kama vile Hes.11:16-25)

2. Lingine lililokuwa limeundwa na wanajumuiya 23 (lakini yawezekana inarejerea mabaraza ya Sinagogi ya kawaida).

3. Baadhi ya wasomi wa Kiyahudi waliamini kuwa palikuwepo na wanajumuiya 23 waliounda sinagogi kuu huko Yerusalemu. Wakati watatu wanaungana, pamoja na viongozi wawili, likiteua wanajumuiya 71 toka “watu wa sinagogi kuu.”(yaani Nasi na Av Bet Din). a. Kuhani mmoja (yaani Sadukayo) b. Mwanasheria mmoja (pharisayo) c. Mtu wa ukoo bora mmoja (yaani., wazee)

B. Wakati wa ukimbizi toka mahali pao, kizazi cha Daudi kilichorudi ni Zurubabeli na kizazi cha Aroni alikuwa Yoshua. Baada ya kifo cha Zerubabeli, hapakuwepo na kizazi cha Daudi kilichoendeleza, kwa hiyo joho la kimahakama lilipitishwa pasipo kuwajumuisha makuhani (kama vile I Macc. 12:6) na wazee wa mahali (kama vile Neh. 2:16; 5:7).

C. Jukumu la kuhani katika mahakama lilithibitishwa na Diodorus 40:3:4-5 wakati wa D. Jukumu hili la kuhani katika serikali liliendelea mpaka kipindi cha Selucid. Yusufu anamnukuu Antiokia

“mkuu III” (223-187 K.K) katika mabo ya kale 12.138-142. E. Mamlaka ya kuhani yaliendelea mpaka kipindi cha Wamakabayo kutokana na mambo ya kale ya Yusufu

13.10.5-6; 13.15.5 F. Wakati wa kipindi cha utawala wa Warumi gavana wa Syria (yaani Gabinus toka 57-55 K.K) akaanzisha

Page 74: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

58

“sinsgogi kuu” za Kimikoa (kama vile mambo ya kale ya Yusufu 14.5.4; na Vita 1.8.5), lakini baadaye ilitenguliwa na Rumi (yaani., mwaka wa 47 K.K)

G. Watu wa Sinagogi kuu walikuwa na mkabiliano wa kisiasa na Herode (yaani mambo ya kale 14.9.3-5) ambao, mwaka 37 K.K, wakalipiza kisasi na watu wengine wa baraza kuu wakauwawa (kama vile mambo ya kale ya Yusufu 14.9.4; 15.1.2)

H. Chini ya wakili wa Kirumi (yaani., 6-66 B.K) Yusufu anatuambia (kama vile mambo ya kale 20.200,251) kuwa watu wa Sinagogi kuu tena wakapata nguvu na umaarufu (kama vile Marko 14:55). Kuna majaribu matatu yalioandikwa katika Agano Jipya pale watu wa siangogi kuu, chini ya uongozi wa familia ya kuhani mkuu, walitenda haki. 1. Jaribu la Yesu (kama vile Marko 14:53-15:1; Yohana 18:12-23,28-32) 2. Petro na Yohana (kama vile Mdo 4:3-6) 3. Paulo (kama vile Mdo. 22:25-30)

I. Wakati Wayahudi walipoasi katika mwaka wa 66 K.K, Warumi baadaye wakaiharibu jamii yote ya Kiyahudi na Yerusalemu katika mwaka wa 70 K.K. watu wa sinagogi kuu moja kwa moja wakatenguliwa, ingawa Mfarisayo pale Jamnia wakajaribu kurudisha tena baraza kuu la kisheria (yaani Beth Din) katika maisha ya dini ya Kiyahudi (lakini sio kwenye jamii au siasa)

IV. Uanachama A. La kwanza Kibiblia kutajwa kwenye baraza kuu huku Yerusalemu ni lile la 2Nya. 19:8-11. Liliundwa na

1. Walawi 2. Makuhani 3. Wakuu wa familia (yaani., wazee, kama vile I Wamak. 14:20; II Wamak.4:44)

B. Wakati wa kipindi cha Wamakabayo lilimilikiwa na (1) familia ya kikuhani ya Masadukayo na (2) familia ya ukoo bora wa mahali Fulani (kama vile I Wamak. 7:33; 11:23; 14:28). Baadaye katika kipindi hiki “waandishi” (wanasheria wa Musa, ambao mara nyingi walikuwa mafarisayo) waliongezwa, inaonekana na mke wa Alexanda Jannaeus, yaani Salome (76-67 B.K). Hata hivyo alisema kuwafanya mafarisayo kuwa kikundi cha maarufu (kama vile Yusufu, vita vya Wayahudi 1.5.2).

C. Wakati wa siku za Yesu baraza liliundwa na 1. Familia ya kuhani mkuu 2. Watu wa kawaida toka kwenye familia ya watu wenye uwezo 3. Waandishi (kama vile Luka 19:47)

V. Vyanzo vya maoni vikatafuta toka

A. Dictionary of Jesus and the Gospels, IVP, kurasa 728-732 B. The Zondervan Pictorial Encyclopedia of the Bible, vol. 5, kurasa 268-273 C. The New Schaff-Herzog Encyclopedia of Religious Knowledge, vol. 10, kurasa 203-204 D. The Interpreter's Dictionary of the Bible, vol. 4, kurasa 214-218 E. Encyclopedia Judaica, vol. 14, kurasa 836-839

3:2 “usiku” Mwalimu akasema usiku huo ndio ulikuwa mzuri wa kuzisoma sheria kwa sababu hapakuwepo na mwingiliano. Yawezekana Nikodemu hakutaka watu wamwone akiwa na Yesu kwa hiyo (yawezekana na wengine aliokuwa nao) wakamwendea usiku. Kitu kimoja kinachoshangaza kwenye maandiko ya Yohana ni mara ngapi mtafasiri asadiki uwepo wa maana mbili. Yohana anaainishwa na urejeshwaji wa tofauti uliopo baina ya nuru na giza (angalia Biblia Toleo la NET, uk. Wa 1898, #7 sn). ◙ “Rabbi” Katika Yohana hili linamaanisha “mwalimu” (kama vile Yoh. 1:38; 4:31; Marko 9:5; 11:21). Moja ya vitu vilivyo wasumbuwa viongozi wa Kiyahudi lilikuwa ni lile la Yesu kutowahi kuhudhulia moja ya shule za kithiolojia za sheria za Kiyahudi. Hakuwa na ufahamu juu ya sheria za kiibada za Wayahudi baada ya kujifunza katika sinagogi la mahali fulani huko Nazareti.

Page 75: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

59

◙ “umetoka kwa Mungu” Ibara hii imewekwa kwanza kwenye sentesi kwa ajili ya kusisitiza. Hili lawezekana lilidokeza kwenye unabii wa Kumbu kumbu la Torati 18:15,18. Nikodemo alitambua uwezo wa nguvu na maneno ya Yesu, lakini hili halimaanishi alikuwa sawa kiroho na Mungu. ◙ “isipokuwa Mungu yu pamoja nawe” Hii ni sentesi yenye masharti daraja la tatu ikimaanisha ukweli muhimu. 3:3, 5, 11 “Amini, amini” Hii kiuhalisia ni “Amina, amina” Linatoka kwenye agano la kale la neno la “imani.” Linatoka kwenye shina la neno “kuwa imara” au “kuwa na uhakika.” Yesu alilitumia kutanguliza maelezo muhimu. Na baadaye likatumika kama njia ya kuthibitisha maelezo ya kweli. Herufi mbili za kwanza ni za pekee kwenye injili ya Yohana. Hili la kurudia neno “amina” mara mbili inathihirisha hatua iko kwenye mazungumzo kati ya Yesu na Nikodemo. Angalia MADA MAALUMU: AMINA katika Yohana 1:51 3:3 “Asipozaliwa mara ya pili” Hii pia ni sentesi yenye masharti daraja la tatu, kama maelezo ya Nikodemo katika Yohana 3:2 NASB, NKJV, TEV "mara ya pili" NRSV, NJB "amezaliwa toka juu" Hii ni kauli tendewa timilifu yenye hali ya utegemezi. Neno (anōthen) laweza kumaanisha

1. “kimwili amezaliwa mara ya pili” 2. “kazaliwa toka awali” (kama vile Mdo. 26:4) 3. “amezaliwa toka juu,” ambalo linatoshea katika mazingira haya (kama vile Yohana 3:7,31; 19:11)

Hii yawezekana ni mfano mwingine wa matumizi ya Yohana katika neno hili ambalo lina maana mbili (kuingizwa mara mbili), ambazo zote ni za kweli (kama vile Bauer, Arndt, Gengrich na Danker's A Greek-English Lexicon of the New Testament, ukur. 77). Kama ilivyodhihilishwa kutoka katika Yohana 3:4, Nikodemus akalielewa kama uchaguzi # 1. Yohana na Petro (kama vile 1 Pet. 1:23) alitumia sitiari hii ya mazoea kwenye wokovu kama Paulo alivyotumia neno kuasili. Mtazamo uko juu ya 3:21-24; 6:23; Efe. 2:8-9).

◙ “Hawezi kuuona” Kifungu hiki cha kinahau kinaendana sambamba na kile kilichoko katika Yohana 3:5 chenye maelezo “hawezi kuingia”

◙ “Ufalme wa Mungu” kifungu hiki kinatumika mara mbili tu katika Yohana (kama vile Yohana 3:5). Hiki kinaonekana kama kifungu muhimu kwenye mihtasari ya injili. Hotuba za kwanza na mwisho za Yesu, na hasa ile ya mafumbo, ilishughulika na mada hii. Inarejerea utawala wa Mungu katika moyo wa mwanadamu sasa! Inashangaza kuona kuwa Yohana anatumia kifungu hiki mara mbili tu (na kamwe sio kwenye mafumbo ya Yesu). Angalia mada maalumu hapo chini. Kwa Yohana “maisha ya milele” ni neno na sitiari muhimu. Kifungu kinafanana na msukumo wa mafundisho ya Yesu juu ya elimu ya mabo yajayo (siku za mwisho). Hili fumbo la kithiolojia “tayari, lakini bado” linahusiana na dhana ya Kiyahudi ya enzi mbili, enzi ya sasa ya uovu na enzi ya haki ijayo ambayo itazinduliwa na masiha. Wayahudi wanategemea ujio mmoja wa kiongozi wa kijeshi aliyewezeshwa kiroho (kama ilivyo kwa waamuzi katika Agano la Kale). Ujio mara mbili wa Yesu ulisababisha kupishana kwa enzi hizi mbili. Ufalme wa Mungu umevunjiliwa ndani ya historia ya binadamu ikiwa na mfano wa umbo la binadamu pale Bethelehemu. Haya hivyo, Yesu hakuja kama mshindi wa kijeshi kama ilivyo Ufunuo 19, lakini kama mtumishi anayepitia mateso (kama vile Isaya 53) na kiongozi mnyenyekevu (kama vile Zak. 9:9). Ufalme, kwa hiyo, umezinduliwa (kama vile Mt. 3:2; 4:17; 10:7; 11:12; 12:28; Marko 1:15; Luka 9:2,11; 11:20; 21:31-32) lakini haukukamilishwa (kama vile Mt. 6:10; 16:28; 26:64). Waamini wanaishi katika mvutano wa enzi mbili hizi. Wana maisha ya ufufuo, lakini bado wanakufa kimwili. Wamekombolewa toka kwenye nguvu ya dhambi, lakini bado wanatenda dhambi. Wanaishi katika mvutano wa kiama/siku za mwisho ambao ni tayari na ule ambao ni bado!

Page 76: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

60

Maelezo ambayo yaweza kusaidia katika mvutano huu ulioko tayari na ule ambao bado katika kitabu cha Yohana yanapatikana katika Frank Stagg's New Testament Theology: “injili ya Yohana ni ya msisitizo kuhusu ujio wa mbele (14:3,18 f.,28; 16:16,22) na unaongea wazi juu ya ufufuo na hukumu ya mwisho “katika siku ya mwisho”(5:28 f.; 6:39 f., 44,54; 11:24; 12:48); bado injili ya nne, uzima wa milele, hukumu, na ufufuo ndizo kweli zilizopo sasa (3:18 f.; 4:23; 5:25; 6:54; 11:23 ff.; 12:28,31; 13:31.; 14:17; 17:26)" (ukur. 311).

MADA MAALUMU: UFALME WA MUNGU

Katika Agano la Kale Mungu alifikiriwa kama mfalme wa Israel (kama vile 1 Sam. 8:7; Zab. 10:16; 24:7-9; 29:10; 44:4; 89:18; 95:3; Isa. 43:15; 44:6) na Masiha akawepo kama mfalme aliyedhaniwa/kutegemewa (kama vile Zab. 2:6; Isa. 9:6-7; 11:1-5). Na kuzaliwa kwa Yesu pale Bethelehemu (mwaka wa 6-4 K.K) ufalme wa Mungu ukavunjiliwa ndani ya historia ya mwanadamu kwa nguvu mpya na ukombozi (“Agano Jipya,” kama vile Yer. 31:31-34; Ezek. 36:27-36).

1. Yohana Mbatizaji akatangaza kukaribia kwa ufalme (kama vile Mt. 3:2; Mk. 1:15). 2. Yesu wazi wazi akafundisha kwamba ufalme ulikuwa tayari ndani yake mwenyewe na mafundisho yake

(kama vile Mt. 4:17,23; 10:7; 12:28; Luka 10:9,11; 11:20; 17:21; 21:31-32). Na bado ufalme unakuja (kama vile Mt. 16:28; 24:14; 26:29; Marko 9:1; Luka 21:31; 22:16,18).

Katika usambamba wa mihitasari kwenye Marko na Luka tunakipata kifungu, “ufalme wa Mungu.” Hii ilikuwa mada ya kawaida katika mafundisho ya Yesu yakijumisha utawala wa Mungu uliopo kiatika mioyo wa watu, ambao siku moja utakamilishwa katika ulimwengu wote. Huu unaaksishwa kwenye maombi ya Yesu katika Mat.6:10. Mathayo, akiwaandikia Wayahudi, alipendelea kifungu kile ambacho hakitumii jina la Mungu (yaani., Ufalme wa Mbinguni), wakati Marko na Luka, akiwaandikia watu wa mataifa, anatumia usanifu wa kawaida, akiweka jina la Uungu. Hiki ni kile kifungu cha mfano katika mihitasari ya injili. Hotuba za kwanza na za mwisho za Yesu, na zaidi mafumbo yake, yanashughulika na mada. Zinarejerea utawala wa Mungu katika mioyo ya wanadamu sasa! Inashangaza kuona kwamba Yohana anatumia kifungu hiki mara mbili tu (na kamwe sio kwenye mafumbo ya Yesu). katika injili ya Yohana “uzima wa milele” ni sitiari muhimu. Mvutano na kifungu hiki unasababishwa na ujio mara mbili wa Kristo, Agano la Kale linatazamisha kwenye ujio mmoja wa Masihi wa Mungu kama afisa wa kijeshi, ujio wa kiutukufu-lakini Agano Jipya linaonyesha kuwa alikuja kwanza kama mtumishi mwenye mateso katika Isaya 53 na mfalme mnyenyekevu katika Zak. 9:9. Enzi mbili za Kiyahudi (angalia mada maalumu: Enzi hii na Enzi inayokuja), enzi ya uovu na enzi mpya ya haki, zimeingiliana. Kwa sasa Yesu anatawala ndani ya mioyo ya waumini, lakini siku moja atatawala juu ya uumbaji wote. Atakuja kama Agano la Kale lilivyotabiri (kama vile Ufunuo 19)! Waamini wanaishi ndani ya ulimwengu wa Mungu “uliotayari” dhidi ya “ule ambao bado” (kama vile Gordon D. Fee na Douglas Stuart's How to Read The Bible For All Its Worth, kurasa za. 131-134).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 3:4-8 4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? 5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. 6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. 7 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili. 8Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.

3:5 “Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho” Hii ni sentesi nyingine yenye masharti daraja la tatu. Panaweza pakawepo na utofauti (katika maandiko yenyewe ya Yohana) baina ya

1. Wa ki-mwili dhidi ya Wa-kiroho (hakuna kipengere kwenye “roho”) 2. Wa ki-dunia dhidi ya Wa-kimbingu

Page 77: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

61

Utofauti huu unadokezwa katika Yohana 3:6. Nadharia za maana ya “maji”ni 1. Viongozi wa dini ya Kiyahudi walitumia kumanisha mbegu za kiume 2. Maji yaliyotoka wakati wa kuzaliwa kwa mototo 3. Ubatizo wa Yohana unamaanisha toba (kama vile Yohana 1:26; 3:23) 4. Mrejesho wa nyuma wa Agano la Kale unamaanisha kunyunyiziwa kiibada na Roho (kama vile Ezek. 36:25-

27) 5. Ubatizo wa Kikristo (ingawa Nikodemu hangaliweza kufahamu namna hiyo, awali ukitajwa na Yustin na

Irenaus) Katika muktadha wa nadharia #3 – Ubatizo wa Maji wa Yohana na maelezo kuhusu ubatizo wa Masihi wa Roho Mtakatifu-lazima ziwe maana za wazi kabisa za juu. Kuzaliwa, katika muktadha huu, ni wa kisitiari na hatupashwi kuchukulia kutokuelewa kwa Nikodemu kuhusu maneno haya yatawale utafasili.kwa hiyo, nadharia #1 haifai. Ingawa Nikodemu asingalijua maneno ya Yesu kama yalivyokuwa yakirejerea ubatizo wa Mkristo baadaye, Yohana Mtume mara nyingi alichachawiza thiolojia yake ndani ya maneno ya Yesu kihistoria (kama vile Yohana 3:14-21). Natharia #2 ingalistahili umiliki wa Yohana wa vitu viwili vya juu na chini, ufalme wa Mungu na ufalme wa dunia. Katika kutafasiri maneno haya mmoja lazima apime kama yana fofautiana (#1 au #2) au kukamilishana (#4). D.A. Carson, Exegetical Fallacies, anataja uchaguzi mwingine: ambao maneno yote yanarejerea kwenye uzao mmoja, na uzao wa kiama ukifuatia Ezek. 36:25-27, ambao unaelezea “Agano Jipya” kutokana na Yer.31:31-34 (ukr.42) F. F. Bruce, Answers to Questions, pia anaangalia Ezekiel kama kiini macho cha Agano la Kale nyuma ya maneno ya Yesu. Hata ingeweza kuwa nukuu ya kubadili ubatizo, ambao Nikodemu, mwalimu wa sheria za Kiyahudi aliyeangaliwa, lazima afanye pia (ukur.67)

◙ “Ufalme wa Mungu” Moja ya machapisho ya Kiyunani ya kale (yaani., MS א) na wazee wengi wa kanisa, yalikuwa na kifungu “ufalme wa mbinguni” ambao ni wa kawaida katika injili ya Mathayo. Hata hiyo, kifungu “ufalme wa Mungu kinatokea katika Yohana 3:3 (Yohana 3:3 na 5 ndio sehemu pekee kifungu hiki kinatokea katika Yohana). Yohana, akiwandikia watu wa mataifa (kama alivyofanya katika Marko na Luka), haitumii maneno mengi kwa ajili ya jina la Mungu.

3:6 Huu tena ni umiliki wa wima (juu dhidi ya chini) ambao ni wa kawaida katika Yohana (kama vile Yohana 3:11).

3:7 “wewe…….we” Ya kwanza iko katika hali ya umoja, ikirejerea kwa Nikodemu, lakini ya pili iko kwenye hali ya wingi, ikirejerea kanuni ya pamoja inayotumika kwa binadamu wote (mchezo ule ule juu ya hali ya umoja na wingi katika Yohana 3:11).

Mmoja anajaribiwa kutafasiri katika mwanga wa tabia za Kiyahudi kuamini katika urithi wao wa kijamii (kama vile Yohana 4:12; 8:53). Yohana, akiandika kuelekea mwishoni mwa karne ya kwanza, ni dhahili anakabiliana na mafunuo, na pia majivuno ya jamii ya Kiyahudi.

◙ “lazima” Neno la Kiyunani dei (“ni muhimu,“ (BAGD 172), kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo) imetumika mara tatu katika Yohana 3 (Yohana 3:7,14,30). Inadokeza vitu ambavyo lazima vitokee kwa ajili ya mpango wa Mungu kusonga mbele (kama vile Yohana 4:24; 9:4; 10:16; 12:34; 20:9)

3:8 kuna mchezo juu ya neno la Kiebrania (na Kiarama) ambalo ni (ruach) na neno la Kiyunani (pneuma) ambayo yote yakimaanisha “upepo,” “pumzi,” na “roho.” Maana hapa ni kwamba upepo una uhuru, kama ifanyavyo Roho. Hakuna awezae kuuona upepo, mbali na athari zake; vile vile, kwa Roho pia. Wokovu wa mwanadamu hauko kwenye mamlaka yake, lakini uko kwenye udhibiti wa Roho (kama vile Ezek. 37). Yawezekana kuwa Yohana 3:5-7 pia anaangazia kwenye ukweli ule ule. Wokovu ni muunganiko wa uanzilishi wa Roho (kama vile Yohana 6:44,65) na uajibikaji wa imani/toba wa mtu binafsi (kama vile Yohana 1:12; 3:16,18). Injili ya Yohana kipekee inaangazia juu ya mtu na kazi ya Roho (kama vile Yohana 14:17,25-26; 16:7-15). Anaangalia enzi mpya ya haki kama enzi ya Roho wa Mungu. Yohana 3:8 anasisitizia/kazia fumbo la kwa nini baadhi ya watu wanaamini pale wanaposiki/kuona injili na wengine hakuna. Yohana anathibitisha kuwa hakuna awezae kuamini mpaka pale ameguswa na Roho (kama vile 1:13; 6:44,65). Aya hii inaimarisha thiolojia hiyo. Haya

Page 78: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

62

hivyo, swali juu ya uwajibikaji wa agano (yaani., ukubarifu wa mwanadamu juu ya ahadi ya Kiungu) bado unasadiki Roho anagusa kila mtu. Kwa nini baadhi wanakataa kuamini bado ni muujiza mkubwa wa udhalimu (yaani., kiini binafsi cha anguko). Jinsi ninavyozeeka, ndivyo ninavyosoma Biblia, jinsi ninavyowahudumia watu wa Mungu, ndivyo ninaandika “maajabu” niliyopitia maishani. Wote tunaishi katika ukungu mweusi (yaani., 1Kor 13:12) wa uwasi wa mwanadamu! Ukiwa na uwezo wa kuelezea au kuweka katika njia nyingine, kutengeneza mpangilio wa thiolojia, sio muhimu kama kumwamini Mungu katika Kristo.Ayubu hakuambiwa “kwa nini”!

MADA MAALUMU: PUMZI, UPEPO NA ROHO (AGANO LA KALE)

Neno la Kiebrania ruach (BDB 924) na neno la Kiyunani pneuma laweza kumaanisha “roho,” “pumzi” au “upepo” (angalia mada maalumu: Roho katika Biblia). Roho inahusianishwa mara nyingi na uumbaji (kama vile Mwa. 1:2; Ayubu 26:13; Zab. 104:30). Agano la Kale halielezei vizuri uhusiano uliopo kati ya Mungu na Roho wake (angalia mada maalumu: Utatu Mtakatifu) Katika Ayubu 28:26-28; Zab. 104:24 na Mith. 3:19; 8:22-23 Mungu alitumia “hekima” (BDB 315, ni nomino ya jinsia ya kike, kama vile Mith. 8:12) kuumba vitu vyote. Katika Agano Jipya Yesu anasema kuwa wakala wa Mungu katika uumbaji (kama vile Yoh. 1:1-3; 1 Kor. 8:6; Kol. 1:15-17; Ebr. 1:2-3). Kama ilivyo katika ukombozi, hivyo hivyo, hata kwenye uumbaji, wote watatu katika kichwa cha Mungu walitumika. Mwanzo 1 yenyewe haisisitizi sababu ya pili (kama vile Isa. 45:5-7)

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 3:9-15 9Nikodemo akajibu, akamwambia, Yawezaje kuwa mambo haya? 10Yesu akajibu, akamwambia, Je! Wewe u mwalimu wa Israeli, na mambo haya huyafahamu? 11 Amin, amin, nakuambia kwamba, Lile tulijualo twalinena, na lile tuliloliona twalishuhudia; wala ushuhuda wetu hamwukubali. 12Ikiwa nimewaambia mambo ya duniani, wala hamsadiki, mtasadiki wapi niwaambiapo mambo ya mbinguni? 13Wala hakuna mtu aliyepaa mbinguni, ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana wa Adamu. 14Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; 15ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye.

3:9-10 Nikodemo sharti angelipaswa kuelewa maana ya silabi za Yesu katika mwanga wa (1) itikadi ya ubatizo wa dini ya Kiyahudi na (2) mafundisho ya Yohana Mbatizaji. Hii yaweza kuwa kuuchezea kimakusudi ufahamu wa mtu; hata mtu kama Nikodemu, kiongozi wa Wayahudi, hakuelewa kikamilifu mambo ya kiroho. Injili ya Yohana iliandikwa ili kupambana na wapokeaji wa mafunuo, imani ya mafundisho tofauti yanayosisitizia juu ya maarifa ya binadamu kama njia ya wokovu. Yesu pekee ndiyo nuru (kama vile Yohana 3:19) kwa wote, sio kikundi cha tabaka la watu wenye uwezo.

3:11 “lile tulijualo twalinena” wingi wa viwakilishi nomino vinarejerea kwa Yesu na Yohana mtume (kama vile Yohana 3:11) au Yesu na Baba, ambavyo vinafaa vizuri katika mazingira hayo (Yohana 3:12). Injili sio mtizamo, bali ni mafunuo ya Kimungu!

◙ “wala ushuhuda wetu hamkuukubali” Yohana mara nyingi anatumia maneno kubali/pokea (lambanō) na muunganikano wake wa KIVIVUMISHI katika maana ya kithiolojia.

1. Kutokana na kumpokea Yesu a. Katika hali ya kutokukubali (Yohana 1:11; 3:11, 32; 5:43, 47) b. Katika hali ya kukubali (Yohana 1:12; 3:11,33; 5:43; 13:20)

2. Kutokana na kumpokea Roho a. Katika hali ya kutokukubali (Yohana 14:17) b. Katika hali ya kukubali (Yohana 7:39)

3. Kutokana na kupokea maneno ya Yesu a. Katika hali ya kutokukubali (Yohana 12:48) b. Katika hali ya kukubali (Yohana 17:8)

Page 79: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

63

Angalia MADA MAALUMU: SHUHUDA JUU YA YESU katika Yohana 1:8

3:12 “kama…….kama” Hiyo ya kwanza ni sentensi yenye masharti daraja la kwanza ambayo inadhaniwa kuwa kweli kutokana na mtazamo wa mwandishi au kusudi lake kifasihi. Na hiyo ya pili ni sentensi yenye masharti daraja la tatu ambayo inamaanisha kuwepo na kitendo muhimu.

◙ “wewe” Viwakilishi nomino na vitenzi viko katika wingi. Nikodemu huenda alikuwa na wanafunzi au akiwa na mafarisao wengine wakati wakimwendea Yesu, au hii yaweza kuwa ni maelezo ya jumla (yaani., Nikodemu kama mwakilishi wa kundi) kwa wote Wayahudi wasio amini kama Yohana 3:7 na 11.

3:13 Aya hii inakusudia kuthibitisha ufunuo wa Yesu aliopewa na Baba kuwa wa kweli, timilifu, aliopewa kwanza mkononi, na wa kipekee (kama vile Yohana 1:1-14). Huu ni mfano mwingine umiliki mara mbili wa wima katika Yohana: mbingu dhidi ya dunia, vya mwilini dhidi ya vya rohoni, Nikodemu halisi dhidi ya Yesu halisi (kama vile Yohana 1:51; 6:33,38,41,50,51,58,62). Aya hii inathibitisha (1) Uungu; (2) kuishi kabla; (3) ubadilikaji sura ya umilele wa mtu wa pili wa Utatu (kwa ajili ya Utatu angalia Mada Maalumu katika Yohana 14:26

◙ “Mwana wa Adamu” Huu ni usanifu-binafsi wa Yesu; haukuwa na maana ya utaifa, uanajeshi, umasiha katika karne ya kwanza ya Uyahudi. Neno limetolewa toka Ezek. 2:1 na Zab. 8:4, ambapo ilimaanisha “mwanadamu” na Dan.7:13 ambapo ilimaanisha Uungu. Neno linajumuisha fumbo la Yesu kama mtu, Mungu kamili na mtu kamili (kama vile 1 Yohana 4:1-3).

3:14-21 Ni vigumu kujua kwa yakini mazungumuzo mya Yesu na Nikodemu yalipoishia na Yesu au Yohana Mtume baadaye maoni yao yalipoanzia. Yawezekana kuwa mihitasari ya injili yaliweka kumbu kumbu ya huduma ya wazi ya mafundisho ya Yesu, wakati Yohana akiweka kumbu kumbu vipindi vyake binafsi akiwa na wanafunzi wake. Yohana3:14-21 inaweza elezewa kama ifuatavyo.

1. Yohana 3:14-15 inahusiana na Yesu 2. Yohana 3:16-17 inahusiana na Baba 3. Yohana 3:18-21 inahusiana na mwanadamu

Kumbuka kuwa iwe ni Yesu au Yohana hawaathiri ukweli wa maelezo!

3:14 “Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani” Hii ni nukuu toka Hes. 21:4-9 ambayo inasimulia uzoefu wa hukumu wakati wa kipindi cha kutangatanga jangwani. Kweli kuu hapa ni kwamba mwanadamu sharti aamini na kutii neno la Mungu, hata pale ambapo hatalielewa kwa ukamilifu. Mungu alitoa njia kwa Waisrael ili waokolewe kutokana na kuumwa na nyoka pindi tu pale watakapo amini. Kuamini huku kulishuhudiwa na utii wa neno/ahadi yake (kama vile Hes. 21:8)

◙ “kuinuliwa” Neno hili la Kiyunani (kama vile Yohana 8:28; 12:32,34) mara nyingi lilitafasiliwa “kuinuliwa juu” (kama vile Mdo. 2:33; 5:31; Fil. 2:9) na ni neno lingine ambalo Yohana analitumia kwa maana mbili (ingizo mara mbili, kama vile Yohana 1:5; 3:3,8). Kama Mungu alivyo ahidi ukombozi toka katika mauti kutokana na kuumwa na nyoka kwa wale walioamini neno la Mungu kwa kuangalia nyoka wa shaba, vile vile pia, kwa wale walioamini jina lake (injili kuhusu Kristo, Yule aliye inuliwa msalabani) na wale watakao amini katika Yesu wataokolewa toka kuumwa na nyoka(shetani, dhambi) kama vile Yohana 12:31-32.

3:15-18 “Kila mtu” (Yohana 3:15) “kila mtu” (Yohana 3:16) “kila mtu” (Yohana 3:18) upendo wa Mungu ni mwaliko wa watu wote (kama vile Isa. 55:1-3; Ezek. 18:23,32; Yohana 1:29; 3:16; 6:33,51; 2 Kor. 5:19; 1 Tim. 2:4; 4:10; Tit 2:11; 2 Pet. 3:9; 1 Yohana 2:2; 4:14). Zawadi ya wokovu ni ya wote, lakini upokeaji ndio haupo!

3:15 “aaminiye” Hii ni kauli tendaji endelevu ya wakati uliopo. Kuamini ni imani inayoendelea. Angalia dokezo kwenye Yohana 1:12 na Mada Maalum katika Yohana 1:7 na 2:23

Page 80: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

64

◙ “Katika yeye” Hii inarejea sio tu kwenye kweli (ukweli wa thiolojia) kuhusu Yesu, lakini kwenye ushirika binafsi na Yeye. Wokovu ni (1) ukweli wa kuaminiwa; (2) mtu wa kuupokea na kutii; na (3) maisha kama ya Yule mtu aishiye! Muundo wa kisarufi hapa sio wa kawaida. Ni kiwakilishi nomino kikiwa na kivumishi en ambacho kinapatikana tu katika Yohana; mara nyingi ni kivumishi eis. Inawezekana kuwa lazima ihusishwe na “atakuwa na uzima wa milele” (kama vile The New Testament in Basic English cha Harold Greenlee). 3:15,16 “Uzima wa Milele” Neno la Kiyunani (zoē) inarejerea kwenye ubora na wingi (kama vile Yohana 5:24). Katika Mt. 25:46 neno lile lile limetumika kutengana milele. Katika Yohana zoē (limetumika mara 33, hasa hasa mlango 5 na 6) kawaida (kitenzi kimetumika kwenye maisha ya kimwili, yaani., 4:50,51,53) ikirejerea ufufuko, maisha ya kiama, au maisha ya enzi mpya, maisha ya Mungu mwenyewe. Yohana ni kitabu cha pekee kati ya vitabu vya injili kwenye msisitizo juu ya “maisha ya milele.” Ni dhamira na lengo kuu katika injili yake (kama vile Yohana 3:15; 4:36; 5:39; 6:54,68; 10:28; 12:25; 17:2,3).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 3:16-21 16Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. 17 Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. 18 Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu. 19Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. 20 Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa. 21Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika Mungu.

3:16 “Mungu aliupenda” Hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati uliopita usiotimilifu (kama lilivyo neno”kumpa”), ambalo hapa linaongelea kitendo ambacho tayari kilisha tendeka huko nyuma (Mungu akamtuma Yesu). Yohana 3:16-17 kimsingi inashughulika na pendo la Baba (kama vile 1 Yohana 4:7-21, hasa, Yohana 3:9-10). “Aliupenda” ni neno agapaō. Halikutumia sana katika Wayunani wa tabaka la juu. Kanisa la awali likalichukua na kuliingiza likiwa na maana maalumu. Katika mazingira fulani linahusiana na upendo wa Bbaba au Mwana, hata hivyo, linatumika vibaya juu ya upendo wa mwanadamu (kama vile Yohana 3:19; 12:43; 1 Yohana 2:15). Kithiolojia ni kisawe cha hesed katika Agano la Kale, amblo lilimaanisha utii wa Agano na pendo la Mungu. Katika siku za Yohana huko Koine ya Uyunani, neno agapaō na phileō kimsingi ni visawe (linganisha Yohana 3:35 na 5:20). Watafasiri lazima waweke akilini kuwa maneno yote yaliyotumika kumwelezea mungu (lugha ya binadamu kumwelezea Mungu) yanachukua mizigo ya mwanadamu. Lazima tutumie maneno yanayoelezea ulimwengu wetu, fikra zetu, mitazamo yetu ya kihistoria katika kujaribu kuelezea Binadamu wa kiroho, wa milele, wa utakatifu na wa kipekee yaani (Mungu). Misamiati yote ya mwanadamu kwa namna Fulani inashabihiana au inasitirahiana. Kile ambacho kimedhihilishwa ni kweli, lakini sio mwisho. Mwanadamu aliye anguka, wa muda, aliye na kikomo hawezi kupata ukweli.

MADA MAALUM: MUNGU KUELEZEWA KAMA MWANADAMU (lugha ya kibinadamu)

I. Aina hii ya lugha (yaani., Uungu kuelezewa katika maneno ya kibinadamu) ni wa kawaida katika Agano la Kale (baadhi ya mifano) A. Viungo vya mwili

1. Macho - Mwa. 1:4,31; 6:8; Kut. 33:17; Hes. 14:14; Kumb. 11:12; Zak. 4:10 2. Mikono – Kut. 15:17; Hes. 11:23; Kumb. 2:15 3. Viganja – Kut. 6:6; 15:16; Kumb. 4:34; 5:15 4. Masikio – Hes. 11:18; 1 Sam. 8:21; 2 Fal. 19:16; Zab. 5:1; 10:17; 18:6 5. Uso – Kut. 33:11; Law. 20:3,5,6; Hes. 6:25; 12:8; Kumb. 31:17; 32:20; 34:10 6. Vidole – Kut. 8:19; 31:18; Kumb. 9:10; Zab. 8:3

Page 81: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

65

7. Sauti – Mwa. 3:9,11,13; Kut. 15:26; 19:19; Kumb. 26:17; 27:10 8. Miguu – Kut. 24:10; Ezek. 43:7 9. Umbo la mtu – Kut. 24:9-11; Zaburi 47; Isa. 6:1; Ezek. 1:26 10. Malaika wa Bwana – Mwa. 16:7-13; 22:11-15; 31:11,13; 48:15-16; Kut. 3:4,13-21; 14:19; Amu.

2:1; 6:22-23; 13:3-22 B. Matendo ya mwili (angalia mifano)

1. Kuongea kama moja ya mfumo wa uumbaji- Mwa. 1:3,6,9,11,14,20,24,26 2. Kutembea (yaani., sauti ya)- Mwa. 3:8; Law.26:12; Kumb. 23:14; Hab. 23:14 3. Kufunga mlango wa safina ya Nuhu – Mwa. 7:16 4. kunukia dhabihu – Mwa. 8:21; Law. 26:31; Amo. 5:21 5. kurudi chini – Mwa. 11:5; 18:21; Kut. 3:8; 19:11,18,20 6. maziko ya Musa – Kumb. 34:6

C. Mihemuko ya kibinadamu (baadhi ya mifano) 1. Majuto/toba- Mwa. 6:6,7; Kut. 32:14; Amu. 2:18; 1 Sam. 15:29,35; Amo. 7:3,6 2. Hasira- Kut. 4:14; 15:7; Hes. 11:10; 12:9; 22:22; 25:3,4; 32:10,13,14; Kumb. 6:15; 7:4; 29:20 3. Wivu - Kut. 20:5; 34:14; Kumb. 4:24; 5:9; 6:15; 32:16,21; Yosh. 24:19 4. Karaha/chuki- Law. 20:23; 26:30; Kumb. 32:19

D. Maneno ya kifamilia (baadhi ya mifano) 1. Baba

a. Wa Israeli- Kut. 4:22; Kumb. 14:1; Isa. 1:2; 63:16; 64:8; Yer. 31:9; Hos. 11:1

b. Wa Wafalme- 2 Sam. 7:11-16; Zab. 2:7 c. Sitiari za vitendo vya kibaba- Kumb. 1:31; 8:5; 32:6-14; Zab. 27:10; Mith. 3:12; Yer. 3:4,22;

31:20; Hosea 11:1-4; Mal. 3:17 2. Mzazi – Hosea 11:1-4

3. Mama- Isa. 49:15; 66:9-13 (mshabihiano wa unyonyeshaji wa mama) 4. Kijana mpendwa mwaminifu-Hosea 1-3

II. Sababu za kutumia aina hii ya lugha A. Ni muhimu kwa Mungu kujidhihirisha mwenyewe kwa mwanadamu. Hakuna misamiati mingine

kuliko ile ya maneno ya kiulimwengu, ulioanguka. Dhana iliyosambaa ya Mungu kuwa wa jinsia ya kiume ni mfano mmoja wa lugha ya kumwelezea binadamu kwa sababu Mungu ni Roho!

B. Mungu anachukulia dhana ya maana halisi ya maisha ya mwanadamu na kuwatumia ili kujidhihilisha mwenyewe kwa mwanadamu aliyeanguka (Baba, Mama, Wazazi, Wapendwa)

C. Ingawa ni muhimu kwa wakati mwingine (yaani., Mwa. 3:8), Mungu hahitaji kuwekewa pingamizi kwa aina yeyote juu ya umbo la kibinadamu (kama vile Kut. 20; Kumbu. 5)

D. Hatima ya Mungu kuelezewa kama mtu ni kubadilika kwa Yesu katika umbo la kibinadamu! Mungu akawa mtu, mwenye kugusika (kama vile Yohana 1:1-18).

kwa umakinika wa maelezo, angalia G. B. Caird, The Language and Imagery of the Bible, ukurasa 10, "Tabia ya mwanadamu kwa Mungu," katika The International Standard Bible Encyclopaedia, kurasa za. 152-154

◙ “Maana” Hii kifahisi ni “kwa maana hiyo” (yaani., Yohana 7:46; 11:48; 18:22). Inaelezea namna, na sio mihemuko! Mungu analionyesha pendo lake (kama vile Rum. 5:8) kwa kutoa (Yohana 3:16) na kupeleka (Yohana 3:17, ambavyo vyote viko kwenye hali tendaji elekezi ya wakati uliopita usiotimilifu) mwanae kufa kwa mbadala wa mwanadamu (kama vile Isaya 53; Rum. 3:25; 2 Kor. 5:21; 1 Yohana 2:2).

◙ “ulimwengu” Yohana analitumia neno hili la Kiyunani kosmos katika maana tofauti tofauti (angalia kidokezo katika Yohana 1:10 na Mada maalumu: Kosmos). Aya hii pia inakanusha mafunuo ya mara mbili kati ya roho wa (Mungu) na roho ya vitu. Wayunani walijaribu kudhani kuwa uovu ndiyo sababu ya mambo yote. Kwao vitu (yaani., mwili wa mtu) ilikuwa ni nyumba ya wafungwa ya mng’ao wa Kiungu katika wanadamu wote. Yohana hakusadiki juu ya uovu wa vitu au mwili. Mungu

Page 82: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

66

hakupenda ulimwengu (sayari, kama vile Rum. 8:18-22) na wanadamu (mwili, kama vile Rum. 8:23). Huu wawezakuwa utata mwingine wa kimakusudi (mwingiliano mara mbili) ambao ni wa kawaida katika Yohana (kama vile Yohana 1:5; 3:3,8)

◙ “hata akamtoa mwanae pekee” Hii inamaana “wa kipekee, wa aina yake.” Haipaswi kufahamika kama “mwanae pekee” katika (1) kwa maana ya kujamiana au (2) kwa maana kwamba hakuna watoto wengine. Hakuna watoto wengine kama Kristo. Angalia dokezo la mtakasa nguo katika Yohana 1:14

◙ “yeyote amwaminiye” Hii ni kauli tendaji endelevu ya wakati uliopo ambayo inasisitiza juu ya herufi za mwanzo na imani endelevu. Angalia Mada Maalum katika Yohana 1:14 na 2:23. Uthibitisho huu umejirudia katika Yohana 3:15 kwa ajili ya kusisitizia. Tunamshukuru Mungu kwa ajili ya “yeyote”! Hili lazima lilete mlinganyo kuhusu msisistizo wowote juu ya kundi maalumu (kijamii, kisomi, au kithiolojia). Sio kwa kihivyo “Ukuu wa Mungu” na “mapenzi huru ya mwanadamu” yamejitenga kimapatano, yote ni kweli! Mara zote Mungu huanzisha uwajibikaji na kuweka agenda (kama vile Yohana 6:44,65), lakini ameunda uhusiano wake na binadamu kwa njia ya agano. Lazima wajongee na kuendelea kujongea kwenye ahadi na mashariti yake.

MADA MAALUM: UCHAGUZI/MAJAALIWA NA UHITAJI WA USAWA KITHIOLOJIA Uchaguzi ni fundisho la ajabu. Hata hiyo, si wito ulio na upendeleo, lakini ni wito kuwa njia, chombo, au njia za ukombozi kwa wengine! Katika Agano la Kale neno hilo lilitumiwa hasa kwa ajili ya huduma; katika Agano Jipya linatumika hasa kwa ajili ya wokovu unaohusika katika huduma. Biblia hipatanishi kamwe kupingana kati ya Ufalme wa Mungu na mapenzi huru ya mwanadamu, lakini inathibitisha zote mbili! Mfano mzuri wa mvutano wa kibiblia itakuwa Warumi 9 juu ya uchaguziwa Ufalme na Warumi 10 juu ya majibu muhimu ya wanadamu (kama vile Warumi 10:11,13). Umuhimu wa huu muvatano wa kithiolojia unaweza kupatikana katika 1:4. Yesu ni mwanadamu mchaguzi wa Mungu na wote ni uwezo wa kuchaguliwa ndani yake (Karl Barth). Yesu ni Mungu. Yesu "ndio" kwa mahitaji ya mwanadamu aliyeanguka (Karl Barth). Waefeso 1:4 pia husaidia kufafanua suala hilo kwa kuthibitisha kwamba lengo la majaaliwa si mbinguni tu, lakini utakatifu (mapenzi ya kristo). Mara nyingi sisi huvutiwa na faida za injili na kupuuza majukumu! Wito wa Mungu (uchaguzi) ni kwa wakati pamoja na milelel! Mafundisho huja kuhusiana na ukweli mwingine, sio mmoja tu, ukweli usiohusiana. Hali au tabia nzuri inakuwa ni kundi dhidi ya nyota moja. Mugu hutoa ukweli katika mashariki na sio magharibi, mtindo. Hatupaswi kuondoa mvutano unaosababishwa na jozi za lahaja(fumbo la maneno) za kweli za mafundisho:

1. majaaaliwa/mchaguzi dhidi ya mapenzi huru ya mwanadamu 2. Usalama wa wanaoamini dhidi ya mahitaji ya uvumilivu 3. Dhambi ya asili dhidi ya dhambi ya hiari 4. Kutotenda dhambi dhidi ya kutenda dhambi kidogo 5. Udhihirisho na utakaso wa papo kwa papo dhidi ya utakaso endelevu 6. Uhuru wa Kikristo dhidi ya wajibu wa Kikristo 7. Mungu anayeweza kupita uwezo wa binadamu dhidi ya Mungu wa asili 8. Mungu kama hatimaye isiyojulikana dhidi ya Mungu anayejulikana katika maandiko 9. Ufalme wa Mungu kama sasa dhidi ya kukamilishwa baadaye 10. Kutubu kama zawadi ya Mungu dhidi ya jibu muhimu la Agano la kibinadamu 11. Yesu kama Mungu dhidi ya Yesu kama mwanadamu 12. Yesu ni sawa na Mungu Baba dhidi ya Yesu wa kumtumikia Mungu Baba

Dhana ya kitheolojia ya “agano” inaunganisha Ufalme wa Mungu (ambaye daia huchukua hatua kwa kuweka mswada) pamoja na mamlaka ya mwanzo imani ya kuendelea kutubu kujibiwa kutoka kwa mwanadamu (k.v. Marko 1:15; Mdo. 3:16,19; 20:21). Kuwa mwangalifu wa maandishi ya uthibitisho wa upande mmoja wa fumbo la maneno na punguza kwa mwingine! Kuwa mwangalifu wa kuthibitisha mafundisho yako ya mapenzi tu au mfumo wa thiolojia!

Page 83: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

67

◙ “hatapotea” Madhara ni kwamba baadhi watapotea (kitenzi cha kati utegemezi cha wakati uliopita usiotimilifu). Wanapotea (amollumi, kitenzi cha kati utegemezi cha wakati uliopita usiotimilifu) moja kwa moja inahusiana na kupungukiwa kwao na imani kumhusu Yesu (kama vile Yohana 11:25). Mungu hasababishi, au hatabisha kutoamini kwao (kama vile Ezek. 18:23,32; 1 Tim. 2:4; 2 Pet. 3:9). Wengi wamejaribu kulichukulia neno hili kifasihi na kwa hiyo wakapendekeza kuangamiza uovu. Hili lingaliweza kuleta mkanganyiko kati ya Dan. 12:2 na Mt. 25:46. Huu ni mfano mzuri wa waumini watiifu waliolazimisha tamaduni za kitamathali za hali ya juu za kimashariki kuzigeuza kwenye muundo wa ufasiri wa kimagharibi (tafsiri sisisi na ya kimantiki). Kutaka kupata maelezo mazuri ya neno hili angalia Robert B. Girdlestone's Synonyms of the Old Testament, kur. 275-277. Angalia Mada maalumu: Uharibifu (apollumi) katika Yohana 10:10 Tena, chunguza kwa namna gani Yohana anafikiri na kuandika katika hali ya namna mbili (yaani., kuangamia dhidi ya uzima wa milele). Msamiati na uundaji wa kithiolojia wa mafundisho ya Yesu yako tofauti kabisa kati ya mihitasari ya injili na Yohana. Mmoja anashangaa ni uhuru kiasi gani (chini ya uangalizi wa Kimungu, yaani, uvuvio) waandishi wa injili walikuwa nao katika kuandaa uwasilisho wa kiinjilisti juu ya Yesu kwenye umati wa watu. Angalia Gordon Fee na Douglas Stuart, How To Read The Bible For All Its Worth, kur. 127-148. 3:17 “kuhukumu ulimwengu” Kuna aya mbali mbali katika Yohana zinazodhihilisha kwamba Yesu alikuja kama mwokozi, na sio kama hakimu (kama vile Yohana 3:17-21; 8:15; 12:47). Hata hivyo, kuna aya zingine ambazo zinadhihilisha kuwa Yesu alikuja kuhukumu, na atahukumu (kama vile Yohana 5:22-23,27; 9:39; vile vile kama sehemu nyingine ya Agano Jipya, Mdo. 10:42; 17:31; 2 Tim. 4:1; 1 Petr. 4:5). Maoni mbali mbali ya kithiolojia yako katika mtiririko.

1. Mungu alimpa Yesu kazi ya kuhukumu kama alivyofanya kwenye uumbaji na ukombozi kama alama ya heshima (kama vile Yohana 5:23)

2. Mara ya kwanza Yesu hakuja kuhukumu, bali kuokoa (kama vile Yohana 3:17), lakini kwa ukweli wa kwamba watu walimkataa, na kujihukumu wao wenyewe.

3. Yesu atarudi kama mfalme wa wafalme na mwamuzi (kama vile Yohana 9:39)

3:18 Mstari huu unarudia dhamira ya wokovu wa bure kupitia Kristo dhidi hukumu binafsi ya mateso. Mungu hawapeleki watu Kuzimu/Jehanamu. Wanajipeleka wao wenyewe. Imani ina matokeo endelevu (“kuamini,” kauli tendaji endelevu ya wakati uliopo) na kama ilivyo kwenye kutokuamini (“wamekwisha hukumiwa” kauli tendewa timilifu elekezi na “hawakuamini” kauli tendaji timilifu elekezi). Angalia Mada Maalum katika Yohana 2:23 na 9:7

3:19-21 “Na watu wakapenda giza kuliko nuru” Watu wengi walioisikia injili waliikataa, sio kwa sababu ya kitamaduni au kisomi, lakini hasa hasa kwa sababu ya uadilifu (kama vile Ayubu 24:13). Nuru inamaanisha Kristo (kama vile Yohana 1:9; 8:12; 9:5; 12:46) na ujumbe wake kuhusu pendo la Mungu, uhitaji wa mwanadamu, kujitoa kwa Kristo na uhitaji wa kuwajibika, hii ni hali ya kurudia wazo/kipengele toka Yohana 1:1-18.

3:19 “Na hii ndio hukumu” Hukumu, kama wokovu, yote yapo katika ukweli wa sasa (kama vile Yohana 3:19; 9:39) na ni ukamilisho wa mbeleni (kama vile Yohana 5:27-29; 12:31,48). Waamini wanaishi katika wakati uliokwisha kuwa tayari (kiama kilichotambulika) na wakati ambao bado (ukamilisho wa kiama). Maisha ya Kikristo

ni furaha na ujibidishaji wenye msukosuko; ni ushindi baada ya mwendelezo wa ushindwaji; uwepo wa uhakika bado ni mwendelezo wa maangalizo juu ya ustahimilivu!

3:21 “bali atendaye kweli huja kwenye “nuru” (kama vile Yohana 3:19,20 [mara mbili], 21) ni nukuu iliyo dhahili kumhusu Yesu, inawezekana kuwa “kweli” lazima pia iandikwe kwa herufi kubwa. Robert Hanna katika A Grammatical Aid to the Greek New Testament, anamnukuu N. Turner katika Grammatical Insights into the New Testament, ambaye alilitafsiri kama, “ mtu ambaye ni mwanafunzi wa ukweli” (ukr. 144) Kithiolojia mstari huu unaelezea ukweli ule ule kama ulioko kwenye Mathayo 7. Maisha ya milele ni tabia zinazochunguzika. Mtu hakika hawezi kumkabili Mungu mpka katika Kristo, ajazwe Roho Mtakatifu, na kubakia vile vile. Fumbo la udongo alilolitumia Yesu liliangazia juu ya uzaaji wa matunda, na sio uoteshaji (kama vile

Page 84: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

68

Mathayo 13; Marko 4; Luka 8; pia angalia mazungumzo ya Yohana katika Yohana 15:1-11). Utendaji kazi hauleti wokovu, lakini ni ushahidi wake (kama vile Efe. 2:8-9,10)

MASWALI YA MJADALA

Huu ni mwongozo wa fasiri, ina maanisha kwamba unawajibika kwa tafsiri zako mwenyewe za Biblia. Kila mmoja wetu lazima atembee katika mwanga tulio nao. Wewe, Biblia, na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Hutakiwi uvitelekeze vitu hivi kwa mfasiri. Maswali ya mjadala huu yanatolewa kukusaidia kufikiri juu ya mambo makubwa ya sehemu za kitabu hiki. Yanalenga kukuamsha kimawazo na sio kutoa maana.

1. Nini maana ya kifungu “kuzaliwa upya/mara ya pili” 2. Nini unachokifikiria juu ya “maji” yanarejerea nini katika Yohana 3:5 na kwa nini? 3. Neno “kuamini” (imani iokoayo) inahisiana na nini 4. Je Yohana 3:16 ni aya kuhusu pendo la Yesu kwa mwanadamu au kwa Baba 5. Amri ya Mungu inahusianaje na Yohana 3:16? 6. Je neno “kuangamia” lina maana ya kuteketea 7. Elezea maana ya “nuru.”

UTAMBUZI WA KI-MUKTADHA WA MISTARI YA 22-36

A. Msisitizo wa Yohana juu ya utatu kamili wa Yesu Kristo umewasilishwa tokea mwanzoni mwa injili kupitia mazungumzo na ukabiliwaji binafsi. Aya hii inaendeleza muundo huo.

B. Yohana, akiandika injili yake mpaka mwishoni mwa karne ya kwanza, anashughulika na baadhi ya maswali yaliyojitokeza tangu pale mhutasari wa injili ulipoandikwa. Mmojawapo ulipaswa kufanya sehemu kubwa ukifuatiwa hasa imani ya mwanzo tofauti na mafundisho ya Kikrsto yaliyohusishwa na Yohana Mbatizaji (kama vile Mdo. 18:24-19:7). Ni muhimu kuwa katika Yohana 1:6-8, 19-36 na 3:22-36, Yohana Mbatizaji anadhihilisha uhusiano wake dhaifu kwa Yesu wa Nazareti na kuthibitisha jukumu la Kimasiha la Yesu.

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 3:22-24 22 Baada ya hayo Yesu na wanafunzi wake walikwenda mpaka nchi ya Uyahudi; akashinda huko pamoja nao, akabatiza. 23 Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele; na watu wakamwendea, wakabatizwa. 24 Maana Yohana alikuwa hajatiwa gerezani.

3:22 “walikwenda mpaka nchi ya Uyahudi” Huduma hii ya awali kote Uyahudi na Galilaya haijazungumziwa katika mihtasari ya injili. Injili sio wasifu wa kupanga matukio ya Yesu. Angalia Gordon Fee na Douglas Stuart, How to Read the Bible For All Its Worth, kur. 127-148.

◙ “akishinda huko pamaoja nao” Yesu alihubili kwenye makusanyiko lakini mijadala ikasambazwa na wanafunzi wake. Akajimimina mwenyewe ndani yao. Utaratibu huu ni utizamisho wa viatabu viwili vya ajabu vya Robert E.Coleman, The Master Plan of Evangelism and The Master Plan of Discipleship, ambavyo vyote vinasisitiza uhusika binafsi wa Yesu na kundi dogo!

◙ “akabatiza” Tunajifunza kutoka kitabu cha Yohana 4:2 kuwa Yesu mwenyewe hakubatiza, lakini wanafunzi wake walibatiza. Ujumbe wa Yesu hatimaye ukaonekana kufanana na ule ujumbe wa Yohana Mbatizaji. Ulikuwa ni ujumbe wa Agano la Kale wa toba na maandalizi. Ubatizo uliotajwa hapa sio ubatizo wa Kikristo lakini ni ubatizo unaomaanisha toba na upokeaji wa roho.

Page 85: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

69

3:23 “Yohana pia alikuwa akibatiza huko Aenon karibu Salim” Eneo halisi la mahali hapa halijulikani. 1. Wengine wanaamini palikuwa Perea ng’ambo ya eneo la Yorodani 2. Wengine wanaamini palikuwa kasikazini mwa Samaria 3. Wengine wanaamini palikuwa maili tatu mashariki mwa mji wa Shekemu.

Kwa sababu “aenon” inaonekana kumaanisha “kijito,” #3 unafaa zaidi. Haijalishi uhalisia wa mahali, Yesu alikuwa akihudumu Uyahudi na Yohana alikuwa mahali Fulani hatua chache toka alipokuwa Yesu.

3:24 “maana Yohana alikuwa hajatiwa gerezani” Haijulikani ni kwa nini kipengele hiki cha utaratibu wa matukio kiliongezwa hapa. Wengine wanasema lilikuwa ni jaribio la kuoanisha utaratibu wa matukio ya Yohana na ule wa kwenye mihitasari (kama vile Mt. 14:1-12; Marko 6:14-29). Inatenda kazi kama ukumbusho wa matukio katika maisha ya Yesu.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 3:25-30 25Basi palitokea mashindano ya wanafunzi wa Yohana na Myahudi mmoja juu ya utakaso. 26Wakamwendea Yohana, wakamwambia, Rabi, yeye aliyekuwa pamoja nawe ng'ambo ya Yordani, yeye uliyemshuhudia, tazama, huyo anabatiza na watu wote wanamwendea. 27 Yohana akajibu, akasema, Hawezi mtu kupokea neno lo lote isipokuwa amepewa kutoka mbinguni. 28 Ninyi wenyewe mwanishuhudia ya kwamba nalisema, Mimi siye Kristo, bali nimetumwa mbele yake. 29Aliye naye bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi, yeye anayesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi. 30Basi hii furaha yangu imetimia. Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua.

3:25 “Basi palitokea mashindano ya wanafunzi wa Yohana na Myahudi mmoja” “Mashindano” (NASB, NRSV, NJB) ni neno la nguvu la “mabishano” au “makabiliano.” Baadhi ya maandishi ya Kiyunani yana hali ya uwingi ya neno “Wayahudi.” Maandiko ya kale ya Kiyunani yamegawanywa sawa.kwa sababu hali ya umoja ni zaidi ya ukawaida (yaani., MSS P25, 2א, A, B, L, W) yamkini ni ya asili. Toleo la UBS4 linaipa alama “B”. Tabia ya waandishi wa kale kulinganisha andiko. Pia inafurahisha kujua kuwa wanafunzi wa Yohana yamkini walichochea suala hili.

NASB, NKJV NRSV, NJB “kuhusu utakaso” TEV “kuhusu mambo ya matambiko” Pamekuwepo na nadharia mbali mbali lakini kiini cha hili ni maridhiano (NKJV).

1. Yawezekana kuwa wafuasi wa Yohana walikuwa wakijadili uhusiano kati ya ubatizo wa Yohana na ule wa Yesu kama ulivyhusishwa na tamaduni za Kiyahudi za kuosha miguu; neno lile lile limetumika katika Yohana 2:6.

2. Baadhi waliamini linahusiana na mazingira ya moja kwa moja yale ambayo Yesu alikuwa akiyafundisha ya kuwa maisha yake na huduma moja kwa moja yalihusu dini ya Kiyahudi. a. Yohana 2:1-12, harusi ya kana b. Yohana 2:13-22, kulisafisha hekalu c. Yohana 3:1-21, mazungumzo na Nikodemo, mtawala wa Wayahudi d. Yohana 3:22-36, kuoshwa miguu kwa Wayahudi na ubatizo wa Yohana Mbatizaji na Yesu.

Ukweli kwamba mazingira hayapanuki hasa hasa juu ya mazungumzo haya yanaangazia ukweli kwamba yalitoa kipaumbele kingine kwa Yohana Mbatizaji kuushuhudia uwezo wa juu kabisa wa Yesu wa Nazareti.

3:26 “yeye uliyemshuhudia, tazama, huyo anabatiza na watu wote wanamwendea” Wanafunzi waliukumbuka ushuhuda ule wa awali wa Yohana kuhusu Mwana Kondoo wa Mungu (kama vile Yohana 1:19-36), wanaonekana kuwa na husuda ndogo juu ya mafanikio ya Yesu. Yesu pia alikuwa makini juu ya roho yeyote ya ushindani (kama vile Yohana 4:1).

3:27 “Hawezi mtu kupokea neno lo lote isipokuwa amepewa kutoka mbinguni” Huu ni uthibitisho wa moja kwa moja wa kwamba hapana mashindano katika vitu vya rohoni. Kila kitu walichonacho waumini wamepewa kwa

Page 86: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

70

neema ya Mungu. hata hivyo, pamekuwepo na mijadala mingi kama ilivyokuwa kwenye maana ya neno “hiki/kile” na yeye.”

1. Baadhi wanasema “yeye” inarejea juu ya muumini na “hiki/kile” inarejea juu ya ujio mmoja wa Kristo kwa ajili ya wokovu (Mungu anaanzisha, binadamu anaweza kukubali tu, kama vile Yohana 6:44,65).

2. Wengine wanaamini neno “yeye” linamrejea Yesu na neno “hiki/kile” linarejea waumini (kama vile Yohana 6:39; 10:29; 17:2,9,11,24)

Tofauti kati ya mitazamo hii miwili ni kwamba neno “alipewa” linarejea huenda kwenye wokovu wa muumini binafsi au kuwa waumini wote ni zawadi toka kwa Mungu aliyopewa Yesu (kama vile Yohana 17:2).

3:28 “Mimi siye Kristo” Yohana Mbatizaji anathibitisha hasa hasa, kama alivyofanya katika Yohana 1:20, yeye sio Masiha, bali ni mtangulizi. Huu ni mkanganyiko wa dhahiri kwa aya za kinabii za Mal. 3:1; 4:5-6, ukijumuisha na Isaya 40 (kama vile Yohana 1:23). Angalia dokezo juu ya “Masihi” katika Yohana 1:20 na Mada Maalumu katika Yohana 4:25.

3:29 “Aliye naye bibi harusi, ndiye Bwana harusi” Kuna mgongano ya kuwa kuna mkanganyiko mwingi kwenye Agano la Kale juu ya stiari ya ndoa hii ikielezea uhusiano kati ya Mungu na Israel (kama vile Isa. 54:5; 62:4,5; Yer. 2:2; 3:20; Ezek. 16:8; 23:4; Hos. 2:21). Paulo pia anaitumia katika Efe. 5:22ff. ndoa ya Kikristo yaweza kuwa ndio ya mfano wa kisasa ya mahusiano ya Agano.

◙ “Basi hii furaha yangu imetimia” Nomino “furaha” na kitenzi “furahini” vimetumika mara tatu katika mstari huu. Badala ya kuwa na roho ya ushindani, Yohana Mbatizaji dhahili alitambua nafasi yake na kufurahi katika Kristo.

3:30 “Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua” Neno “lazima” (dei) hapa ni la muhimu. Tayari limekwisha tumika katika Yohana 3:14 na 4:4. Huu ni uthibitisho wa nguvu wa uwelewa wa Yohana mwenyewe kama mtangulizi wa huduma yenye nguvu na muhimu zaidi ya Yesu.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 3:31-36 31 Yeye ajaye kutoka juu, huyo yu juu ya yote. Yeye aliye wa dunia, asili yake ni ya dunia, naye anena mambo ya duniani. Yeye ajaye kutoka mbinguni yu juu ya yote. 32 Yale aliyoyaona na kuyasikia ndiyo anayoyashuhudia, wala hakuna anayeukubali ushuhuda wake. 33 Yeye aliyeukubali ushuhuda wake ametia muhuri ya kwamba Mungu ni kweli. 34 Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo. 35 Baba ampenda Mwana, naye amempa vyote mkononi mwake. 36 Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.

3:31-36 Pamekuwepo na mabishano mengi kati ya watoa maoni juu ya mistari hii ikiwa ni

1. Mwendelezo wa uthibitishaji wa mdomo waYohana mbatizaji 2. Maneno ya Yesu 3. Yohana Yule Mtume

Mistari hii inarudi kwenye dhamira ya Yohana 3:16-21. 3:31 “yeye ajaye kutoka juu” Ni muhimu kutambua kuwa vyeo viwili vilivytumika hapa kwa ajili ya Masiha vinasisitiza juu ya uwepo wake kabla na Uungu kamili (imedokezwa katika Yohana 3:31), na kubadilika kwake katika umbo la kibinadamu na mpango aliopewa na Mungu (imedokezwa katika Yohana 3:34). Neno “kutoka juu” ni neno lile lile lililotumika katika kifungu cha neno “kuzaliwa upya” au “aliyezaliwa toka juu” katika Yohana 3:3

Pande mbili za juu na chini, za ufalme wa Mungu na ufalme wa duniani wa mwanadamu, ni uainishaji wa Yohana. Ni tofauti kutoka kwenye hukumu ya pande mbili za Magombo ya Bahari ya Chumvi. Pia ni tofauti toka katika ufunuo wa pande mbili za roho na vitu. Katika maandiko ya Yohana uumbaji wenyewe na mwili wa binadamu havikuainishwa ndani yake na uovu wao wenyewe au dhambi.

Page 87: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

71

◙ “huyo yu juu ya yote” Upande mmoja wa mstari huu unadokeza juu ya Uungu wa Yesu na uwepo wake kabla, akija kutoka juu (kama vile Yohana 1:1-18; 3:11-12). Upande wa pili wa mstari huu unathibitisha ya kuwa yu juu ya uumbaji wa Mungu. Haijulikani kutoka katika andiko la Kiyunani huenda neno “wote” limetumika kwa jinsia ya kiume au pande zote, likirejerea wanadamu wote au vitu vyote. La pili “juu ya vyote” linakosekana katika baadhi ya maneno ya Kiyunani. Toleo la UBS4 haliwezi kuamua katika hitimisho lake, lakini uhakiki wa kimaandiko unadhaniwa kupendelea uingizaji wake.

NASB “Yeye aliye wa dunia, asili yake ni ya dunia, naye anena mambo ya duniani” NKJV “Yeye aliye wa dunia, ni wa dunia na anena ya duniani” NRSV “yule aliye wa dunia, ni mali ya dunia na anena kuhusu vitu vya duniani” TEV “yeye atokaye duniani, ni mali ya dunia na anena kuhusu vitu vya duniani” NJB “yeye aliye wa dunia, ni wa dunia mwenyewe na anena katika hali ya kidunia”

Haya sio maelezo yaliyo kinyume kumhusu Yohana. Neno ya dunia hapa (gē, Yohana 12:32; 17:4; 1 Yohana 5:8, lakini mara 76 katika Ufunuo) sio sawa na neno “ulimwengu” (kosmos), ambalo limetumiwa kinyume na Yohana. Kihalisia, huu ni uthibitisho kuwa Yesu alizungumza kile alichokijua, mbinguni, wakati wanadamu wote wanazungumza kile wanachokijua, duniani. Kwa hiyo, ushuhuda wa Yesu ni wa mbali zaidi kuliko nabii au mhubiri yeyote wa duniani (kama vile Ebr. 1:1-4)

3:32 “yale aliyoyaona na kuyasikia, ndiyo anayashuhudia” Kuna mchezo juu ya njeo za vitenzi katika mstari huu: (1) “aliyoyaona” ni njeo timilifu; (2) “aliyoyasikia” ni njeo ya wakati uliopita usiotimilifu” na (3) kuyashuhudia” ni njeo ya wakati uliopo”. Yesu hatimaye ni ufunuo wa Mungu (kama vile 1 Kor. 8:6; Kol. 1:13-20; Ebr. 1:2-3). Anaongelea juu ya (1) uzoefu wake binafsi na Mungu Babaye na (2) Uungu wake.

◙ “wala hakuna aliye ukubali ushuhuda wake” Haya ni zaidi ya mazungumzo ya awali kwa sababu Yohana 3:23-26 inaonyesha kuwa wengi walikuwa wakija kwake. Kifungu hiki kinarejea dini ya Kiyahudi kwa ujumla (kama vile Yohana 3:11), sio mazingira ya papo kwa papo.

3:33 “Yeye Yule” Hii inaonyesha upendo usiokoma, wa ulimwengu wote kwa wanadamu wote. Hakuna mipaka inayohusishwa na injili ya Mungu; mmoja lazima atubu na kuamini (kama vile Marko 1:15; Mdo. 20:21), lakini ahadi iko wazi kwa kila mtu (kama vile Yohana 1:12; 3:16-18; 4:42; 1 Tim. 2:4; Tit 2:11; 2 Petr. 3:9; 1 Yohana 2:1; 4:14).

◙ “yeye aliyeukubali ushuhuda wake” Yohana 3:33 ni wakati uliopita usiotimilifu wenye hali ya kuendelea, wakati 3:36 wakati uliopo wenye hali ya kuendelea. Hii inaonyesha ya kwamba kuamini katika Mungu kwenye wokovu sio tu uamuzi wa awali, lakini pia ni maisha ya uanafunzi. Uthibitisho ule ule wa hitaji la ukubarifu ulioelezewa huko nyuma katika Yohana 1:12 na 3:16-3:36). Neno “kukubali kama lilivyo neno “imani” ina vidokezo viwili katika Agano Jipya.

1. Kumpokea Kristo kibinafsi na kutembea katika Yeye 2. Kuupokea ukweli na mafundisho yahusianayo (kama vile Yuda,3,20)

NASB “ametia mhuri ya kwamba, Mungu ni kweli” NKJV, NRSV “Ameridhia ya kwamba, Mungu ni kweli” TEV “anathibitisha kwa hili ya kwamba, Mungu ni wa ukweli NJB “anashuhudia ya kwamba mungu ni kweli” Wakati waumini wanaweka imani yao binafsi kwa Yesu, inathibitisha ya kwamba ujumbe wa Mungu juu yake Yeye binafsi, ulimwengu, mwanadamu, na Mwanaye ni wa kweli (kama vile Rum 3:4). Hii ni dhamira ya kujirudia rudia katika Yohana (kama vile Yohana 3:33; 7:28; 8:26; 17:3; 1 Yohana 5:20). Yesu ni kweli kwa sababu alimdhihirisha Mungu aliye Mmoja (kama vile Yohana 3:7,14; 19:11).

Page 88: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

72

Kwa kitenzi cha neno “muhuri” (ni kauli tendaji elekezi ya wakati uliopita usiotimilifu) angalia Mada Maalmu zifuatazo

MADA MAALUMU: MUHURI/LAKIRI

Muhuri au lakiri yawezakuwa ni njia ya kale ya kuonyesha 1. Ukweli (kama vile Yohana 3:33) 2. Umiliki (kama vile Yohana 6:27; 2 Tim. 2:19; Ufu.. 7:2-3; 9:4) 3. Ulinzi (kama vile Mwa. 4:15; Mt. 27:66; Rum. 4:11; 15:28; 2 Kor. 1:22; Efe. 1:13; 4:30; Ufu. 20:3) 4. Yawezakuwa pia ni dalili za ukweli wa ahadi ya Mungu (kama vile Rum. 4:11 and 1 Kor. 9:2)

Kusudi la muhuri huu katika Ufunuo 7:2-4; 9:4 ni kuwatambua watu wa Mungu ili kwamba ghathabu ya Mungu isiwadhuru. Muhuri wa shetani pia huwatambua walio wake, wale walio chombo cha ghathabu ya Mungu. Katika kitabu cha Ufunuo “dhiki kuu” (yaani., thlipsis) mara zote inarejerea wasio waumini wakiwatesa waumini, wakati ghathabu/hasira (yaani., orgē or thumos) mara zote huwa ni hukumu ya Mungu juu ya wale wasioamini ili kwamba wapate kutubu na kuirudia imani katika Kristo. Kusudi hili chanya la hukumu laweza kuonekana katika agano la laana/Baraka katika kitabu cha Mambo ya Walawi 26; Kumbukumbu la Torati 27-28;30; Zaburi 1

3:34 “Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu” Kuna maelezo yanayofanana hapa katika Yohana 3:34 ambayo yanaonyesha kuwa mamlaka ya Yesu yanatoka kwa Mungu.

1. Mungu alimtuma 2. Anao ujazo wa Roho kamili

◙ “kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo” Maelezo haya kifasihi yako katika hali ya kukanusha, lakini kwa wasomaji wa Kiingereza hali ya ukubarifu inashika maana. Kuna njia tofauti za uelewa juu ya ujazwaji wa Roho: baadhi wanaamini kuwa

1. Yesu huwapa ujazo wa Roho waumini (kama vile Yohana 4:10-14; 7:37-39) 2. Ujazo wa Roho hurejea juu ya karama ya Mungu ya Masihi (kama vile Yohana 3:35)

Walimu wa Kiyahudi walilitumia neno “kipimo” kuelezea juu ya Mungu kuwavuvia manabii. Walimu wa Kiyahudi waliongezea pia kuwa hakuna nabii mwenye kipimo kamili cha Roho. Kwa hiyo, Yesu yu juu ya Mnabii (kama vile Ebr. 1:1-2) na kwa hiyo, ni ufunuo wa Mungu kamili. 3:35 “Baba ampenda Mwana” Uthibitisho huu unajirudia katika Yohana 5:20 na 17:23-26. Mahusiano ya waumini kwa Mungu yanapatikana juu ya pendo lake kwa Masihi (Mwanae wa pekee, kama vile Ebr. 1:2; 3:5-6; 5:8; 7:28). Tambua sababu nyingi zilizoelezea katika muktadha huu kwa nini mwanadamu amwami ni Yesu kama Masihi.

1. Kwa sababu atoka juu na yuko juu ya vyote (Yohana 3:31) 2. Kwa sababu alitumwa na Baba kwa mpango wa ukombozi (Yohana 3:34) 3. Kwa sababu Baba anaendelea kumpa Yeye ujazo wa Roho (Yohana 3:34) 4. Kwa sababu Mungu anampenda (Yohana 3:35) 5. Kwa sababu Mungu ameweka kila kitu mikononi mwake (Yohana 3:35)

Kuna maneno mbali mbali ya neno “upendo” ambayo yanadokeza mahusiano tofauti ya mwanadamu. Agapaō na

phileō yana mwingiliano wa elimu-maana. Yote yanatumika kuelezea pendo la Baba kwa Mwana.

1. Yohana 3:35; 17:23,24,26 – agapaō 2. Yohana 5:20 – phileō

Panaonekana kuwepo na utofauti wa kimaandiko katika mazungumzo ya Yesu akiwa na Petro katika Yohana 21:15-17. Kumbuka, “Muktadha, muktadha, muktadha,” na sio misamiati/kamusi, inaamua maana ya neno!

◙ “Amempa vyote mikononi mwake” Hii ni kauli tendaji timilifu elekezi. Hii ni nahau ya Kiebrania kwa maana ya nguvu au mamlaka juu ya mwingine (yaani., Yohana 10:28; 13:3; Mdo. 4:28; 13:11). Hii haswa ni aya

Page 89: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

73

inayofurahisha na yenye mifanano mingi (kama vile Yohana 17:2; Mt. 11:27; 28:18; Efe. 1:20-22; Kol. 2:10; 1 Pet. 3:22).

3:36 NASB "Amwaminiye Mwana yuna Uzima wa Milele; Asiye mwamini hatauona Uzima.” NKJV "Aaminiye Katika Mwana yuna Uzima wa Milele; na asiye Amini Mwana hatauona Uzima” NRSV "Yeye Amwaminiye Mwana yuna Uzima; Yeye asiyemtii hatauona Uzima” TEV "Yeye Amwamiye Mwana yuna uzima wa Milele; Yeye asimwamini hatauona Uzima” NJB "Yeyote Aaminiye katika Mwana yuna Uzima wa Milele; Lakini Yeye akataaye kuamini katika Mwana hatauona Uzima” Maneno haya yote yapo katika kauli tendaji ya wakati uliopo ambayo yanaongelea kitendo kinachoendelea. Kuamini ni zaidi uamuzi wa wakati mmoja haijalishi ni kwa uaminifu au mihemuko gani iliyopo (kama vile Mt. 13:20). Hii inathibitisha kuwa pasipo kumjua Yesu, hakuna awezaye kumjua Baba (kama vile Yohana 12:44-50 na 1 Yohana 5:10). Wokovu huja kupitia mwendelezo wa mahusiano uliyopo na Yesu, Mwana (kama vile Yohana 10:1-18; 14:6). Angalia Mada Maalumu:Njeo za Vitenzi zilizotumika kwa ajili ya Wokovu katika Yohana 9: Njeo ya wakati uliopo sio tu inaongelea kitendo kinachoendelea, lakini ni uhalisia uliopo wa wokovu. Wakati mwingine ni ule waumini walionao, lakini ambao bado kutimilizwa. Pande mbili za neno “uliotayari” dhidi ya “usiotayari” wa enzi mbili (angalia Mada Maalumu: Enzi Hii na Enzi Ijayo katika 1 Yohana 2:17). Angalia Mada Maluum: Njeo za za vitenzi zitumikazo kwa ajili ya wokovu katika Yohana 9:7 Inafurahisha pia kutambua tofauti iliyopo ya neno “kuamini” na “kutii” katika mstari huu. Injili siye tu Yule mtu tunayempokea na kweli tunayoiamini, bali pia ni maisha yale tunayoishi kwayo (kama vile Luka 6:46; Efe. 2:8-10). ◙ “Bali ghadhabu ya Mungu inamkalia” Hii ni sehemu pekee katika maandiko ya Yohana (isipokuwa mara 5 katika Ufunuo) ambapo neno “ghadhabu” (orgē) linajitokeza. Dhana hii ni ya kawaida na mara nyingi inahusiana na neno “hukumu.” Hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo. “Kusadiki,” “utii” na “ghadhabu” ni kweli zilizopo zinazoendelea ambazo zitatimilizwa wakati wa mbeleni. Huu ni mvutano kama ule uliopo wa neno “ulioko tayari” na “usio tayari” juu ya ufalme wa Mungu. Kwa ajili ya mazungumzo kamili ya Kibiblia juu ya ghadhabu ya Mungu soma Warumi 1:18-3:20.

MASWALI YA MJADALA

Huu ni mwongozo wa fasiri, ina maanisha kwamba unawajibika kwa tafsiri zako mwenyewe za Biblia. Kila mmoja wetu lazima atembee katika mwanga tulio nao. Wewe, Biblia, na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Hutakiwi uvitelekeze vitu hivi kwa mfasiri. Maswali ya mjadala huu yanatolewa kukusaidia kufikiri juu ya mambo makubwa ya sehemu za kitabu hiki. Yanalenga kukuamsha kimawazo na sio kutoa maana.

1. Ni kwa namna gani ujumbe wa Yesu wa awali unafanana na wa Yohana 2. Ubatizo huu ni ule kama ubatizo wa Kikristo 3. Kwa nini maneno ya Yohana Mbatizaji yanasisitiza sana katika ufunguzi wa aya ya Yohana? 4. Elezea ni mara ngapi na aina gani ya tofauti zilizopo zile Yohana mwandishi huzitumia kuelezea mahusiano

yaliyopo kati ya Yohana Mbatizaji na Yesu? 5. Ni kwa namna gani neno “ukubalifu” katika Yohana 3:33 linahusiana na neno “kuamini” katika Yohana

3:36? Ni kwa namna gani neno “kutokutii” katika Yohana 3:36 linahusika katika mjadala huu? 6. Orodhesha idadi ya sababu zilizotajwa kwa nini watu wamwamini Yesu wa Nazareti kama tumaini lao

pekee la wokovu? (Yohana 3:31-36) 7. Elezea kwa nini neno “ghadhabu” katika Yohana 3:36 liko katika njeo ya kitenzi cha wakati uliopo.

Page 90: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

74

YOHANA 4

MIGAWANYO YA AYA YA TAFSIRI ZA KISASA UBS4 NKJV NRSV TEV NJB

Yesu na Mwanamke Yesu na Yesu na Yesu anachangamana mwanamke Msamaria kukutana Wasamaria Wasamaria Wasamaria wa Samaria na Masihi wake 4:1-6 4:1-26 4:1-6 4:1-4 4:1-10 4:5-6 4:7-15 4:7-15 4:7-8 4:9 4:10 4:11-12 4:11-14 4:13:14 4:15 4:15-24 4:16-26 4:16-26 4:16 4:17a 4:17b-18 4:19-20 4:21-24 4:25 4:25-26 Mavuno Meupe 4:26 4:27-30 4:27-38 4:27-30 4:27 4:27-30 4:28-30 4:31-38 4:31-38 4:31 4:31-38 4:32 4:33 Mkombozi wa 4:34-38 Ulimwengu 4:39-42 4:39-42 4:39-42 4:39-40 4:39-42 4:41-42 Uponyaji wa Anapokelewa Yesu na watu Yesu alimponya Yesu akiwa Galilaya Mwana wa Galilaya wa Mataifa mwana wa diwani diwani 4:43-45 4:43-45 4:43-45 4:43-45 4:43-45 Mtoto wa Mtoto wa diwani Tajiri aponywa aponywa 4:46-54 4:46-54 4:46-54 4:46-48 4:46-53 4:49 4:50-51 4:52-53 4:54 4:54

Page 91: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

75

MZUNGUKO WA TATU WA USOMAJI KUFUATILIA KUSUDIO LA ASILI LA MWANDISHI KATIKA NGAZI YA AYA Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwatafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Aya ya kwanza 2. Aya ya pili 3. Aya ya tatu 4. N.k

UTAMBUZI WA KI-MUKTADHA WA MISTARI YA 1-54

A. Kuna kusudio la uundaji katika aya 3 na 4 1. Mtu wa dini (Nikodemu) dhidi ya Mwanamke aliyetengwa (Yule mwanamke pale kisimani) 2. Wayahudi wa huko Yerusalemu (Orthodox) dhidi ya Wayahudi wasamalia (walio kinyume na

Orthodox)

B. Ukweli kuhusu yeye binafsi na kazi ya Yesu imedhihilishwa mbele zaidi na 1. Mazungumzo na Yule mama pale kisimani (Yohana 4:1-26); 2. Mazungumzo akiwa na wanafunzi wake (Yohana 4:27-38); 3. Ushuhuda wa wanakijiji (Yohana 4:39-42); 4. Ukaribishwaji na watu wa Galilaya (Yohana 4:43-45); 5. Ishara/maajabu ya nguvu za Yesu juu ya magonjwa, Yohana 4:46-54.

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 4:1-6 1 Kwa hiyo Bwana, alipofahamu ya kuwa Mafarisayo wamesikia ya kwamba, Yesu anafanya wanafunzi wengi kuliko Yohana, na kuwabatiza, 2 (lakini Yesu mwenyewe hakubatiza, bali wanafunzi wake,) 3 aliacha Uyahudi, akaenda zake tena mpaka Galilaya. 4 Naye alikuwa hana budi kupita katikati ya Samaria. 5 Basi akafika kunako mji wa Samaria, uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa Yusufu mwanawe. 6 Na hapo palikuwa na kisima cha Yakobo. Basi Yesu, kwa sababu amechoka kwa safari yake, akaketi vivi hivi kisimani. Nayo ilikuwa yapata saa sita.

4:1 “Bwana” Yohana, akikumbuka tena tukio katika fikra zake (kwa njia ya kiroho) miaka kadhaa baadaye, anatumia neno “BWANA” na “Yesu” katika sentensi moja akimaanisha mtu au nafsi moja. Maandiko kadhaa ya

Kiyunani yana neno “Yesu” mara mbili katika Yohana 4:1 (yaani, א, D, NRSV, NJB, REB) lakini “Bwana” imo katika

MSS P66,75, A, B, C, L (NASB, NKJV). Hata hivyo, pamoja na uhakiki mzuri wa neno “Bwana”, UBS4 anaweka neno “Yesu” katika maandiko na kutoa alama “C” (ngumu kuamua).

◙ “Mafarisayo” Tazama Mada Maalumu katika Yohana 1:24

◙ “wamesikia ya kwamba, Yesu anafanya wanafunzi wengi kuliko Yohana, na kuwabatiza” Yesu akaondoka mahali hapo kutokana na uwezekano wa mvutano kati ya wafuasi wake na wafuasi wa Yohana mbatizaji

Page 92: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

76

uliochochewa na mafarisayo. Ufupisho wa injili unaelezea kuwa aliondoka kwa kuwa Herode Antipas alimkamata Yohana mbatizaji (kama vile Mt. 4:12; Marko 1:14, Luka 3:20)

4:2 “Yesu mwenyewe hakubatiza” Hii sio kuumbua maoni juu ya ubatizo (kama vile Mt. 28;19; Matendo 2:38; 8:12; 16:33; 22:16), bali kutambua asili ya ubinafsi wa mwanadamu (yaani, “nilibatizwa na Yesu” au Paulo, kama vile 1 Kor. 1:17). Kiuhalisia, Yesu alibatiza mwanzoni kabisa mwa kazi yake (kama vile Yn. 3:22), lakini baadaye aliacha. Yohana anarekebisha usemi batili wa Mafarisayo.

4:3 “Aliondoka Yudea akaenda zake tena huko Galilaya” Hizi ni nyakati mbili tendaji elekezi za wakati uliopita usio timilifu zilizotumika kusisitiza miondoko ya Yesu Kijiografia.

4:4 “Naye alikuwa hana budi kupita katikati ya Samaria” “kubali” Neno lililotumika ni kitenzi cha Kiyunani dei, ambalo limetumika mara kadhaa katika maudhui haya (kama vile Yn. 3:7, 14, 30). Kwa kawaida linatafsiriwa kama “lazima” au “si budi”, kuna kusudio la kiroho katika safari au njia hii. Kwamba, Wayahudi wa Yudea walichukia wasamaria, na wangeweza kusafiri kupitia katika ardhi yao, kwa sababu waliwachukulia kuwa ni uzao nusu wa kidini sio uzao halisi.

MADA MAALUM: UBAGUZI WA KIMBARI

I. Utangulizi A. Tabia hii ya kujikuza ni ya watu wote kwa wanadamu walioanguka ndani ya jamii, huu ni ubinafsi wa

mwanadamu ili kujilinda kwa wengine, ubaguzi wa mataifa kwa namna mbalimbali, na kauli ya sasa wakati utaifa (au ukabila) ni mtindo wa kizamani.

B. Utaifa ulianzia Babeli (Mwanzo 11) na mwanzoni ulihusishwa na wana watatu wa Nuhu ambapo neno hili mataifa lilitokana kwalo (kama vile Mwanzo 1-3; Matendo 17:24-26).

C. Ubaguzi wa mataifa ni mojawapo ya aina nyingi za uonevu 1. Kutukuza elimu 2. Ujivuni wa kijamii na kiuchumi 3. Uhalalisho wa haki binafsi ya kidini 4. Msimamo usiobadilika wa kuingiza dini katika siasa

II. Matini ya Biblia A. Agano la Kale

1. Mwa. 1:27 –wanadamu jinsi ya kiume walifanywa kwa taswira na mfano wa Mungu, vitu vinavyomfanya awe wa pekee kuonesha pia uthamani wa mtu na hadhi/ utu (kama vile Yohana 3:18)

2. Mwanzo 1:11-25- inaandika fungu, “… baada ya jinsi yao…” mara kumi. Hii imetumika kusaidia utenganisho wa mataifa. Hata hivyo ni wazi kutokana na mazingira, hii inamaanisha kwa wanyama na mimea na sio kwa watu.

3. Mwa. 9:18-27- Hii imetumika kusaidia utawala wa mataifa. Ikumbukwe kwamba Mungu hakulaani kanani. Nuhu, ambaye ni baba yake, alimlaani kanani baada ya kuzinduka kutoka kwenye ulevi wa pombe. Biblia haioneshi kuwa Mungu alithibitisha kiapo/laana. Hata kama alifanya hivyo haiwaathiri watu weusi. Kaanani alikuwa ni baba wa wote wale waliokuwa wakiishi Palestina na kuta za Misri zilizokuwa zimechorwa zinaonyesha kuwa hawakuwa weusi.

4. Hes. 12:1-Musa alioa mwanamke mweusi 5. Yoshua 9:23- Hii imetumika kuhakiki kuwa taifa moja litatumikia lingine. Hata hivyo katika

uhalisia wa Gibeonite ni wa asili moja na Wayahudi. 6. Ezra 9-10 na Nehemia 13- Hivi vimetumika kwa maana ya mataifa, lakini kiuhalisia inaonesha

kuwa ndoa zilikuwa zimekatazwa, sio kwa sababu ya mataifa (walitoka kwa kaka mmoja Nuhu Mwanzo 10) lakini kwa misingi ya kidini.

B. Agano Jipya 1. Injili

a. Yesu alitumia hali hii ya chuki kati ya Wasamaria na Wayahudi katika mifano kadhaa ambayo

Page 93: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

77

ilionesha kuwa ubaguzi wa kimataifa haufai. 1) Fumbo la Msamaria mwema (Luka 10:25-37) 2) Mwanamke kisimani (Yohana 4) 3) Mgonjwa wa ukoma aliyeshukuru (Luka 17:11-19)

b. Injili ni kwa watu wote 1) Yohana 3:18 2) Luka 24:46-47 3) Waebrania 2:9 4) Ufunuo 14:6

c. Ufalme utawajumuisha wanadamu wote 1) Luka 13:29 2) Ufunuo 5

2. Matendo a. Matendo 10 ni habari kamili kuhusu upendo wa Mungu kwa ulimwengu wote na ujumbe

wa injili kwa walimwengu wote. b. Petro alishambuliwa kwa vitendo vyake katika Matendo 11 na tatizo lake halikutatuliwa

hadi baraza la Yerusalemu katika matendo 15 lilipokutana na kupata ufumbuzi. Mvutano kati ya Wayahudi wa Karne ya kwanza na wapagani ulikuwa umezidi.

3. Paulo a. Hakuna Vipingamizi/vizuizi katika Kristo.

1) Gal. 3:26-28 2) Efe. 2:11- 22 3) Kor. 3:11

b. Mungu haitii watu 1) Rum. 2:11 2) Efe. 6:9

4. Petro na Yakobo a. Mungu hatii watu (1 Petro 1:17) b. Kwasababu Mungu haoneshi upendeleo, vivyo hivyo watu wake Yakobo 2:1

5. Yohana a. Mojawapo ya maelezo marefu kuhusu uwajibikaji wa waamini yanaonekana katika 1

Yohana 4:20. III. Hitimisho

A. Ubaguzi au kwa maana hiyo, uonevu wa aina yoyote haufai kabisa kwa watoto wa Mungu. Hapa kuna nukuu kutoka kwa Henlee Barnette aliyezungumza katika mkutano/kikao Glorieta New Mexico katika kamisheni ya maisha ya mkristo mwaka 1964. “Ubaguzi ni imani dhidi ya dini kwa sababu si wa kibiblia wala Kikristo wala wa kisayansi”.

B. Suala hili linawapa Wakristo fursa ya kuonesha upendo wao wa Kikristo msamaha na uelewa kuhusu ulimwengu uliopotea kuja kwa Kristo. Ubaguzi kwa Wakristo unaonyesha kutokukomaa na ni fursa kwa uovu kuirudisha nyuma imani ya mwamini, uhakika na makuzi. Pia itatenda kazi kama kizuizi kupoteza watu wanaokimbilia kwa Kristo.

C. “Nifanye nini” (Sehemu hii inatolewa katika kamisheni ya maisha ya Mkristo iitwayo “mahusiano ya mataifa”)

“KATIKA KIWANGO CHA MTU”

Kubali kuwajibika binafsi katika kutatua matatizo yanayohusiana na taifa.

Kupitia maombi, kusoma biblia na kushirikiana na mataifa mengine na kupambana na maisha ya uonevu wa mataifa mengine.

Elezea msimamo wako kuhusu ushindani uliopo, hasa pale waliochochea ushindani wa chuki hawakupingwa

Page 94: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

78

“KATIKA MAISHA YA FAMILIA”

Tambua umuhimu wa athari ya familia katika kueneza tabia kwa mataifa mengine.

Jaribu kuendeleza tabia za Kikristo kwa kuzungumza juu ya kile ambacho watoto na wazazi wanasikia kuhusu maswala ya mataifa nje ya nyumbani kwao.

Wazazi wanapaswa kuwa waangalifu kwa kuonesha mifano ya mienendo ya Kikristo kwa kuhusiana na watu wa mataifa mengine

Tafuta fursa kufanya urafiki wa kifamilia kwa watu wa mataifa yote.

“NDANI YA KANISA LAKO”

Kwa mahubiri na mafundisho ya ukweli wa Biblia kuhusiana na mataifa, mkutano unaweza kuhamasisha kuonesha mfano kwa jamii nzima.

Uwe na uhakika kuwa, ibada, ushirikiano na huduma kupitia kanisani viko wazi kwa wote hata vile ambavyo makanisa ya Agano Jipya yalivyoona kutokuwepo kwa vizuizi vya kimataifa (Efe. 2:11-22 Wagalatia 3:26-29)

“KATIKA MAISHA YA KILA SIKU”

Saidia kuondoa ubaguzi wa kimataifa wa aina zote katika ulimwengu wa kazi.

Fanya kazi kupitia katika taasisi za kijamii za aina zote ili kupata haki sawa na fursa ukikumbuka kuwa ni tatizo la kimataifa linalotakiwa kushambuliwa, na sio watu, lengo ni kukuza uelewa na sio kuunda machungu.

Ikionekana inaunda kamati maalumu za wananchi walengwa kwa lengo la kufungua njia za mawasiliano katika jamii kwa ajili ya kuwaelimisha wote katika mambo na vitendo maalumu katika kuboresha mahusiano ya mataifa.

Saidia vyombo vya sheria na watunga sheria katika kupitisha sheria, kukuza haki za kimataifa na kupinga wale karibu haki kwa faida za kisasa.

Pendekeza mtumiaji wa maarifa wa sheria kuitumia bila upendeleo.

Epusha vurugu na hali ya kuheshimu sheria ili kufanya uwezekano wa mambo wa mambo kwenda sana kama raia Mkristo hakkikisha kuwa mfumo wa kisheria haitumiki kama vyombo vya kuwawezesha wanaojenga ubaguzi.

Onesha mfano wa roho na fikra za Kristo kwa mahusiano yote ya wanadamu.

◙ “Kupitia Samaria” Palikuwa na chuki kubwa kati ya Wasamaria na Watu wa Yuda iliyoendelea hadi karne ya nane kabla ya Kristo k.k. Katika 772 k.k. makabila kumi ya kaskazini yaliyokuwa na makao makuu yao katika Samaria, walichukuliwa mateka na Mfalme wa Ashuru wakapelekwa Mji wa Wamedi (kama vile 2 Fal.17:6) ndani ya miaka mingi wapagani hawa walioana na masalia ya Waisraeli. Wayahudi waliwaona wasamaria kama sio kizazi kamili kidini waliwaita nusu kizazi (machotara) (Ezra 4:1-4) Hii inasaidia kuelewa Yohana 4:9.

4:5 “mji wa Samaria, uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa Yusufu mwanawe” (kama vile Mwa. 33:18; 19; Yos. 24:32) wengi wanadhani Sikari ni ndio Shekemu Japo haijasemwa katika kitabu cha Agano Jipya.

4:6 “hapo palikuwa na kisima cha Yakobo” Hili lilikuwa shimo lililochimbwa karibia 100’ kwenda chini. Yalikuwa sio Maji yanayotiririka (chemichemi), lakini yalikuwa ni maji ya mvua. Haijatamkwa katika Agano la Kale japo jina linaunganisha eneo hili na sheria za kimila.

◙ “Yesu, kwa sababu amechoka kwa safari yake” Tunaona wazi asili ya mwanadamu wa Yesu hapa (Luka 2:52) lakini hakuwa amechoka vile kuwapenda watu!

NASB, NKJV, JB “Nayo ilikuwa yapata saa sita” NRSV, TEV “Ilikuwa nyakati za mchana”

Page 95: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

79

Palikuwa na mjadala mrefu kuhusu ni njia gani Yohana aliyoitumia kuzingatia muda katika injili yake. Baadhi ya rejea zinaonyesha alitumia muda wa Kiyahudi, wengine muda wa Kirumi, Wayahudi wanaanza usiku saa 12:00 asubuhi, muda wa Kirumi huanza saa sita usiku 6:00 asubuhi. Kwa hiyo Yesu aliwasili katika kisima mapema asubuhi, (yaani saa 12:00 Asubuhi).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 4:7-14 7Akaja mwanamke Msamaria kuteka maji. Yesu akamwambia, Nipe maji ninywe. 8 Kwa maana wanafunzi wake wamekwenda mjini kununua chakula. 9 Basi yule mwanamke Msamaria akamwambia, Imekuwaje wewe Myahudi kutaka maji kwangu, nami ni mwanamke Msamaria? (Maana Wayahudi hawachangamani na Wasamaria.) 10 Yesu akajibu, akamwambia, Kama ungaliijua karama ya Mungu, naye ni nani akuambiaye, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo hai. 11 Yule mwanamke akamwambia, Bwana, huna kitu cha kutekea, na kisima ni kirefu; basi umeyapata wapi hayo maji yaliyo hai? 12 Je! Wewe u mkubwa kuliko baba yetu, Yakobo, aliyetupa kisima hiki, naye mwenyewe akanywa maji yake, na wanawe pia, na wanyama wake? 13 Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena; 14 walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.

4:7 “Akaja mwanamke Msamaria” Mwanamke huyu alikuwa amekuja umbali mrefu peke yake pale kisimani kwa muda usio wa kawaida kutokana na nafasi yake kijamii kama mwanamke kijijini. ◙ “’Nipe maji ninywe”’ Hii ni kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopita isiotimilifu inayoonyesha hitaji la haraka/dharura. 4:8 Mstari huu unamweka Yesu katika hatua ya kupata mazungumzo ya faragha na huyu mwanamke aliye dhalilishwa kwa sheria za kidini za Dini ya Kiyahudi. Hili nalo ilikuwa ni neno la kumwongezea Yohana utambuzi. 4:9 “Imekuwaje wewe Myahudi kutaka maji kwangu, nami ni mwanamke Msamaria?” Wayahudi hawakuruhusiwa hata kunywa maji kutoka ndoo moja na Msamaria (kama vile sheria/mila za jadi za Kiyahudi kufuatana na Walawi 15). Yesu alipuuza vipingamizi/vikwazo viwili vya kijadi: (1) kuongea na Msamaria. (2) Kuongea au kuzungumza na mwanamke hadharani. ◙ “(Maana Wayahudi hawachangamani na Wasamaria)” Parandesi (NASB, NRSV) ambayo pia ilikuwa nyongeza ya

maelezo ya Yohana, ilikuwa inakosekana katika MSS א na D, lakini ilipatikana katika P63, 66, 75, 76,, 1א, A, B, C, L. UBS4

inajumuisha na alama “A” katika kutoa alama/makadirio (hakika). 4:10“Kama” Hii ni sentensi shurutishi daraja la pili inaonyesha “kunyume na ukweli.” Usemi huu unaonyesha kwamba sio vizuri kuangazia hitimisho ambalo nalo linaonekana kuwa na kasoro. Haya ndiyo matumizi pekee ya neno “zawadi” katika injili ya Yohana. Hapa inamrejea Yesu kama zawadi ya Mungu (kama vile Yoh. 3:16) ambaye anatoa uzima wa milele. Katika Yohana 7:38-39 na Matendo inatumika kwenye utoaji wa Roho Mtakatifu (kama vile Mdo. 2:38; 8:20; 10:45; 11:17). Lengo hapa ni kwa wale wasiostahili neema ya Mungu iliyodhihilisha kwa Kristo na Roho. ◙ “maji yaliyo hai” Neno hili lina ufanano wa kiistiari katika Agano la Kale (kama vile Zab. 36:9; Isa. 12:3; 44:3; Yer. 2:13; 17:13; Zek. 14:8). Yesu anatumia neno hili “maji yaliyo hai” kama kisawe cha neno “maisha ya kiroho.” Hata hivyo mwanamke Msamaria alifikiri kuwa Yesu alikuwa akimaanisha maji yanayotiririka, tofauti na maji ya mvua katika tanki la maji. Ni kawaida ya injili ya Yohana kuwa Yesu (mwanga wa ulimwengu) mara nyingi huwa haeleweki (yaani, Nikodemo). Dunia iliyoanguka, haiwezi kuelewa ukweli wa mbinguni (yaani, ujumbe wa Yesu).

Page 96: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

80

4:11 “Bwana” Hili ni neno la Kiyunani kurious katika muundo wa kauli ya mneni kurie. Laweza kutumika katika kauli ya upole (Bwana) au maelezo ya kithiolojia (BWANA) likimrejerea Yesu kama Mungu kamili kama ilivyo katika Yohana 4:1 na Warumi 10:13. Hapa limetumika kwa upole. 4:12 “Wewe u mkubwa kuliko baba yetu, Yakobo” Lugha sanifu inatarajia jibu la “hapana” huu bila shaka ni usemi unaosisitiza kukanusha usemi fulani. Mwanamke Msamaria alikuwa akionyesha umaarufu wa ukoo atokao ambao wasamaria walitokana na Efraimu na Manase hadi Yakobo huko nyuma. Jambo la kushangaza ni kuwa hadhi ya Yesu ilikuwa sawa kabisa na kile alichokuwa akikidai Mazungumzo haya yanabainisha maswala mawili ya kitheolojia.

1. Upendo wa Mungu/Yesu kwa walio dhalilishwa (yaani, Wasamaria, wanawake) 2. Hadhi/ukuu wa Yesu dhidi ya Uyahudi na majivuno ya kimataifa.

4:13-14 “Kila anywaye maji haya Hataona kiu tena” Yamkini maneno haya bila shaka yalihusisha mambo ya Kimasihi (kama vile Isa. 12:3; 48:21; 49:10). Fungu hili ni ukanushi wa nguvu mara mbili. Pana mchezo katika njeo za vitenzi vya nyakati. kauli tendaji endelevu ya wakati uliopo katika Yohana 4:13 inahusiana na kunywa tena na tena, wakati kitendo tendaji tegemezi cha wakati uliopita usiotimilifu cha Yohana 4:14 kinamaanisha kunywa mara moja. 4:14 “chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele” Hii ni kauli ya wakati uliopo endelevu inayomaanisha “kuendelea kuruka” (kama vile Isa. 58:11 na Yohana 7:38). Kwa watu wa jangwani, maji yalikuwa ni alama ya maisha na upaji wa Kiungu.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 4:15-26 15 Yule mwanamke akamwambia, Bwana, unipe maji hayo, nisione kiu, wala nisije hapa kuteka. 16 Yesu akamwambia, Nenda kamwite mumeo, uje naye hapa. 17 Yule mwanamke akajibu, akasema, Sina mume. Yesu akamwambia, Umesema vema, Sina mume; 18 kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako; hapo umesema kweli. 19 Yule mwanamke akamwambia, Bwana, naona ya kuwa u nabii! 20 Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia. 21 Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu. 22 Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi. 23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. 24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli. 25 Yule mwanamke akamwambia, Najua ya kuwa yuaja Masihi, (aitwaye Kristo); naye atakapokuja, yeye atatufunulia mambo yote. 26 Yesu akamwambia, Mimi ninayesema nawe, ndiye.

4:15 Mwanamke, kama alivyo Nikodemu bado anamwelewa Yesu katika hali ya kimwili. Ni jambo la kawaida hata kwa wanafunzi wake walimtafsiri Yesu kivingine kwa lugha yake mbadala (kama vile Yoh. 4:31-33; 11:11-13). 4:16 Toleo la UBS4 hata haisemi uwezekano wa kuwa jina la “Yesu” liliongezwa (kama vile NKJV, NRSV, NJB, REB),

Biblia ya NET inatoa ushahidi wa maandishi kuhusu hitimisho (uk. 1903, yaani MSS א*,c, A, C2 D, L, na W, lakini unakosekana katika MSS P66,75 B, C) waandishi wa zamani walikuwa wakijaribu kuboresha maandiko na kuwa rahisi kuyafuata. ◙ “Nenda kamwite” Hii ni kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopo ikifuatiwa na kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopita usiotimilifu. 4:17 “Sina mume” dhambi lazima ikabiliwe. Yesu hakatai wala halaumu. 4:18 “umekuwa na waume watano” Yesu anatumia uelewa wa ziada kwa uwezo wake kumtikisa mwanamke kutoka katika mazingira ya kimwili kuwa katika mazingira ya kiroho (kama vile Yoh. 1:48).

Page 97: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

81

4:19 “naona ya kuwa u nabii” Mwanamke alikuwa bado hajapata uelewa wa ukombozi alikuwa anajaribu kuweka swala la uhusiano na Mungu kwa kumsifia (kama Nikodemu katika Yohana 3:2). Watoa maoni wengine wanaiona hii kama ni rejea ya ukombozi kutoka kitabu cha Kumb. 18:15-22.

MADA MAALUMU: UNABII WA AGANO LA KALE

I. UTANGULIZI

A. Maelezo ya Ufunguzi 1. Jamii ya waaminio haiamini namna ya ya kutafsiri unabii. Kweli zingine zimekwisha weka wekwa

bayana kama ilivyo kwa nafasi ya Waorthodox katika karne nyingi, lakini si katika karne hii. 2. Zipo hatua kadhaa za unabii wa Agano la Kale

a. Premornarchial (Kabla ya utawala wa Kifalme) (1) Watu binafsi walioitwa manabii

(a) Ibrahimu – Mwanzo 20:7 (b) Musa – Hesabu 12:6-8; Kumbukumbu la Torati 18:15; 34:10 (c) Haruni – Kutoka 7:1 (Msemaji wa Musa) (d) Miriam – Kutoka 15:20 (e) Medad na Eldad – Hesabu 11:24-30 (f) Debora – Waamuzi 4:4 (g) Wasiokuwa na majina – Waamuzi 6:7-10 (h) Samweli - 1 Samweli 3:20

(2) Rejea ya manabii kama kundi – Kumbukumbu la Torati 13:1-5; 18:20-22 (3) Kundi la Kinabii au ushirika – 1 Samweli 10:5-13; 19:20; 1 Wafalme 20:35, 41; 22:6, 10-

13; 2 Wafalme 2:3,7; 4:1, 38; 5:22; 6:1, na kadhalika. (4) Masihi aitwaye nabii – Kumbukumbu la Torati 13:1-5; 18:20-22

a. utawala wa kifalme usioandikwa (wakimlenga mfalme); (1) Gadi – 1 Samweli 22:5; 2 Samweli 24:11; 1 Mambo ya Nyakati 29:29 (2) Nathani – 2 Samweli 7:2; 1 Wafalme 1:22 (3) Ahijah – 1 Wafalme 11:29 (4) Yehu – 1 Wafalme 16:1, 7, 12 (5) Wasiotajwa – 1 Wafalme 18:4, 13, 22 (6) Eliya – 1 Wafalme 18- 2 Wafalme 2 (7) Mikaya – 1 Wafalme 22 (8) Elisha 2 Wafalme 2:9, 12-13

b. Maandiko ya kale ya manabii (yanayo lenga taifa pamoja na mfalme); Isaya – Malaki (isipokuwa Danieli)

B. ISTILAHI ZA KIBIBLIA 1. Ro'eh = “muonaji” (BDB 906, KB 1157), 1 Samweli 9:9. Rejea hii yenyewe inatuonesha mpito

kutoka katika neno nabi. Ro'eh inatokana na istilahi ya jumla “kuona.” Mtu huyu alizielewa njia za Mungu na mipango yake na aliulizwa kutambua mapenzi ya Mungu katika jambo lolote.

2. Hozeh = "muonaji” (BDB 302, KB 3011), 2 Samweli 24:11. Ni jamii ya neno lenye maana sawa na Ro'eh. Inatokana na neno "kuona." Njeo ya wakati uliopita ya neno hili ni "tazama" ambalo limetumika mara nyingi ikimaanisha manabii.

3. Nabi' = "nabii” (BDB 611, KB 661), inayohusiana na lugha ya Akkadia ya kitenzi Nabu = "kuita" na kiarabu Naba'a = "kutangaza”. Hili ni neno limetajwa mara nyingi katika Agano la kale kumaanisha nabii. Limetumika zaidi ya mara 300. Asili kabisa haijulikana kwa hakika japo "kuita” kwa wakati huu inaonekana kama mbadala mzuri zaidi. Yawezekana uelewa mzuri zaidi unatoka YHWH yanayoeleza mahusiano ya Musa kwa Farao kupitia Haruni (rejea kutoka 4:10-16; 7:1;

Page 98: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

82

Kumbukumbu la torati 5:5). Nabii ni mtu anayezungumza kwa niaba ya Mungu kwa watu wake. (Amosi 3:8; Jeremia 1:7,17; Ezekieli 3:4).

4. Istilahi zote tatu zinatumika katika huduma ya Nabii katika 1 Mambo ya Nyakati 29:29; Samueli – Ro'eh; Nathani – Nabi' na Gadi – Hozeh.

5. Kifungu cha maneno, 'ish ha – 'elohim, “Mtu wa Mungu” pia ni namna pana ya kumaanisha msemaji wa Mungu. Inatumika mara 76 katika Agano la Kale kwa kumaanisha “nabii”

6. Neno "Nabii” kwa asili ni la Kigiriki. Inatokana na neno (1) pro = "kabla” au "kwa niaba ya” na (2) phemi = "kuzungumza.”

II. MAANA YA UNABII A. Neno unabii lilikuwa pana kimaana katika lugha ya kiebrania kuliko Kingereza. Vitabu vya historia vya

Yoshua, Wafalme (isipokuwa Ruthu) vinatajwa na Wayahudi kama “Manabii waliopita”. Wote Ibrahimu (Mwanzo 20:7; Zaburi. 105:15) na Musa (Kumbukumbu la Torati 18:18) wanatajwa kama Manabii (pia Miriam, Kutoka 15:20). Kwahiyo kuwa makini unapokuwa unatazama maana kutoka katika lugha ya Kingereza!

B. "Unabii kisheria kabisa waweza kusema ni ule uelewa wa historia unaokubali maana zile tu zinazohusiana na uungu, kusudi la kiungu, ushirika wa kiungu," Interpreter's Dictionary of the Bible, toleo la. 3, ukurasa wa. 896.

C. "Nabii si mwanafalsafa au mwana taaluma ya Theolojia, bali msaidizi wa agano aletaye neno la Mungu kwa watu wake ili kutengeneza hatima zao kwa kufanya mageuzi ya siku zao za sasa,” Prophets and Prophecy, Encyclopedia Judaica toleo la. 13 ukurasa wa. 1152.

III. KUSUDI LA UNABII

A. Unabii ni njia ya Mungu kuzungumza na watu wake, kuwapa miongozo katika mazingira yao ya sasa na tumaini katika kuyaendesha maisha yao na matukio ya duniani. Ujumbe wao ulikuwa wa jumla. Ilikusudiwa kuonya, kutia moyo, kuhamasisha imani na toba, na kuwafahamisha watu wa Mungu kuhusu Mungu mwenyewe na mipango yake. Iliwashikilia watu wa Mungu katika maagano na Mungu. Katika hili inatakiwa iongezwe kuwa mara nyingi imekuwa ikitumika kufunua uchaguzi wa Mungu wa wasemaji (Kumbukumbu la Torati 13:1-3; 18:20-22). Hii ukiipa umaanani kabisa utagundua ilimaanisha Mesiya

B. Mara nyingi nabii aliichukua historia na migongano ya kithiolojia ya siku zake na kuangazia hayo katika mazingira ya matukio ya siku za mwisho. Namna ya muono huu wa siku za mwisho kihistoria katika Israel ni wa kipekee na katika hali yake ya uchaguzi wa kiungu na ahadi za kiagano.

C. Ofisi ya nabii inaonekana kutengeneza usawa (Yeremia 18:18) na kuchukua ofisi ya Kuhani Mkuu kama njia ya kufahamu mapenzi ya Mungu. Urimm na Thummim inabadilika katika ujumbe wa mdomo kutoka kwa msemaji wa Mungu. Ofisi ya nabii inaonekana pia kupita mbali katika Israeli baada ya Malaki. Haitokei mpaka baada ya miaka 400 baadae kwa Yohana Mbatizaji. Haieleweki namna ambavyo kipawa cha “unabii” kwa Agano Jipya kinavyoshabihiana na Agano la Kale. Manabii wa Agano Jipya (Matendo ya Mitume 11:27-28; 13:1; 15:32; 1 Wakorintho. 12:10,28-29; 14:29,32,37; Waefeso. 4:11) sio vifunuo vya ufunuo mpya au maandiko, bali wasimulizi wa yajayo na wazungumzaji wa mambo ya mbele ya mapenzi ya Mungu katika hali za agano.

D. Unabii hauna msingi sana au hausisitizi katika utabiri kwa asili. Utabiri ni njia mojawapo ya kutthibitisha ofisi yake na ujumbe wake, ila lazima izingatiwe “chini ya asilimia 2% ya unabii wa Agano la Kale ni kuhusu wa kimasiya”. Chini ya asilimia 5% kiuhalisia inafunua nyakati za Agano Jipya. Chini ya asilimia 1% inahusu matukio yajayo. “fee na Stuart, How to Read the Bible For All Its Worth, ukurasa wa 166).

E. Manabii wanamwakilisha Mungu kwa watu, wakati Makuhani wanawawakilisha watu kwa Mungu. Haya ni maelezo ya jumla. Kuna utofauti kwa kama Habakkuki, ambaye anauliza maswali kwa Mungu.

F. Sababu moja inayoleta ugumu kuwaelewa manabii ni kwasababu hatujui muundo wa vitabu vyao.

Page 99: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

83

Havina mfuatano unaoeleweka. Vinaonekana ni vyenye hoja na mada kweli lakini si kama vile mtu angetegemea. Mara nyingi hakuna mazingira ya wazi ya kihistoria wala muda maalumu, au mgawanyiko wa wazi wa mambo ya kiungu. Vitabu hivi ni vigumu 1. Kuvisoma kwa mara moja 2. Kufafanua kwa mada 3. Kug’amua kweli kuu au kusudio la mwandishi katika kila uungu.

IV. TABIA ZA UNABII

A. Katika Agano la Kale inaonekana kukua kwa dhana ya “nabii” na “unabii”. Hapo mwanzo katika Israeli kulitokea ushirika wa manabii, ukiongozwa na viongozi shupavu wenye uvuvio wa Mungu kama Eliya na Elisha. Kuna wakati neno “wana wa manabii,” ilitumika kuzungumzia kundi hili (II Wafalme 2). Manabii walikuwa na tabia ya kujawa na furaha ya kupiliza (1 Samweli 10:10-13; 19:18-24)

B. Hata hivyo kipindi hiki kilipita mara kwa manabii mmmoja mmoja. Kulikuwa manabii (wa kweli na waongo) waliojitambulisha pamoja na mfalme, na waliishi katika Kasri la Kifalme (Gadi, Nathani). Pia, kulikuwa na wale waliojitegemea, wakati mwingine wasiokuwa na hadhi kabisa za jamii ya ki-Israeli (Amosi) walijumuisha wote wanawake na wanaume (2 Wafalme 22:14)

C. Nabii mara nyingi alikuwa mfunuaji ya hatima, anayefanya katika mazingira ya mwanadamu yanavyoenda. Mara nyingi jukumu la nabii ilikuwa ni kufunua mpango wa Mungu kwa uumbaji wake ambao hauathiriwi na mwitikio wa kibinadamu. Huu mpango wa wa ulimwengu wa matukio ya mwisho wa nchi ni wa kipekee katika manabii wa Mashariki ya Karibu ya kale. Utabiri na Agano ni mapacha waendao pamoja katika ujumbe wa kinabii (rejea Fee na Stuart, ukurasa wa 150). Hii inamaanisha manabii husisitiza ujumuishwaji katika lengo. Siku zote, japo si kila eneo, hujielekeza katika kuambia taifa.

D. Mambo mengi ya kinabii yakitolewa kwa njia ya kinywa. Baadae iliunganishwa kwa njia ya mada, mfululizo, au namna nyingine ya uandishi wa Mashariki ya Karibu ambao imepotea huku kwetu. Kwakuwa ilikuwa kwa njia ya kinywa, haikuwa na muundo kama unaokuwa katika kazi iliyo andikwa. Hii inafanya vitabu kuwa vigumu kusoma na ngumu kuelewa bila kuwa na historia ya mazingira halisi.

E. Manabii walitumia namna kadhaa kuwasilisha jumbe zao 1. Matukio ya kimahakama – Mungu anawapeleka watu wake mahakamani, mara nyingi ni kesi ya

kutalikiana ambapo YHWH anamkataa mke wake (Israeli) kwasababu ya kukosa uaminifu wake (Hosea 4; Mika 6).

2. Mazingira ya msiba – mzani haswa kwa jaili ya ujumbe wa namna hii na tabia zake “ole” inajitenga kama aina yake kivyake vyake (Isaya 5; Habbakuki 2)

3. Matamko ya Agano la Baraka - asili ya masharti ya Baraka imesisitizwa na madhara yake, yote ya wema na ubaya, yanatajwa kwa ajili ya baadae (Kumbukumbu la Torati 27-28).

V. MIONGOZO YA KUKUSAIDIA KATIKA KUTAFSIRI UNABII

A. Tafta kujua lengo la kwanza la nabii (mwandishi) kwa kuzingatia mazingira ya kihistoria na muktadha

wa maandishi ya kiungu. B. Soma na tafsiri mambo yote, sio sehemu tu; fafanua na yaliyomo. Angalia inavyoshabihiana na

mazingira ya unabii. Jaribu kufafanua kitabu kizima. C. Endelea na kufanya makisio ya utafsiri wa kawaida wa hadithi mpaka vitu katika habari vikuelekeze

katika matumizi yaliyofichwa kimaana; hivyo badili lugha iliyofichwa katika maandishi. D. Fafanua matendo ya kiishara katika ufahamu wa mazingira ya kihistoria na usambamba wa hadithi.

Kuwa na uhakika wa kukumbuka maanadishi ya kale ya Mashariki ya Karibu si kama yale ya kisasa ya kimagharibi.

E. kuwa mwangalifu wa utabiri 1. Je unahusisha siku za mwandishi? 2. Je uliwahi kutimia katika historia ya Israeli?

Page 100: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

84

3. Je ni kweli yamekwisha kuwa matukio yajayo? 4. Je yana kutimizwa kwa sasa nab ado yanasubiri kutimizwa siku zijazo? 5. Waruhusu waandishi wa Biblia wakuongoze katika majibu na sio waandishi wa kisasa.

F. Vitu vya kuzingatia 1. Je utabiri umekidhi kigezo cha sharti la mwitikio 2. Kuna uhakika kwa Yule ambaye unabii umemlenga? (Na kwa nini)? 3. Je kuna uwezekano, wa kibiblia na/au kihistoria, wa kutimia mara mbili? 4. Waandishi wa Agano Jipya, chini ya uvuvio waliweza kumuona mesiya katika sehemu nyingi

katika Agano la Kale kiasi ambacho hakipo kwetu. Wanaonekana kutumia aina hii ya mchezo. Kwakuwa hatujavuviwa basi ni bora tukawaachia utaratibu huu wao.

VI. VITABU VYA KIMSAADA A. A Guide to Biblical Prophecy by Carl E. Amending and W. Ward Basque B. How to Read the Bible for All Its Worth by Gordon Fee and Douglas Stuart C. My Servants the Prophets by Edward J. Young D. Plowshares and Pruning Hooks: Rethinking the Language of Biblical Prophecy and Apocalyptic by D.

Brent Sandy E. New International Dictionary of Old Testament Theology and Exegesis, vol. 4, pp. 1067-1078 F. The Language and Imagery of the Bible by G. B. Caird

MADA MAALUMU: UNABII WA AGANO JIPYA

I. Sio sawa na Unabii wa Agano la Kale (BDB 611, KB 661; tazama Mada Maalumu: Unabii [Agano la Kale]), ambao una vidokezo vya upokeaji wa sheria za Kiyahudi na kunukuu mafunuo yaliyovuviwa toka kwa YHWH (kama vile Mdo. 3:18, 21; Rum. 16:26). Ni manabii tu waliweza kuandika maandiko.

A. Musa aliitwa nabii (kama vile kumb. 18:15-21) B. Vitabu vya historia (Yoshua – Wafalme [isipokuwa Ruthu]) waliitwa “manabii wa mwanzo”

(kama vile Matendo. 3:24) C. Manabii wanachukua nafasi ya makuhani wakuu kama chanzo cha habari kutoka kwa Mungu.

(kama vile Isaya –Malaki) D. Mgawanyo wa pili wa kanuni za kanisa la Kiebrania ni “Manabii” (kama vile Mt. 5:17; 22:40;

Luka 16:16; 24:25, 27; Rum. 3:21). II. Katika Agano Jipya dhana ya unabii imetumika katika njia kadhaa tofauti tofauti.

A. Kuwarejea manabii wa Agano la Kale na jumbe zao zilizovuviwa (kama vile Mt. 2:23; 5:12 11:13; 13:14; Rum. 1:2).

B. Kuurejea ujumbe kwa mtu mmoja badala ya kikundi kichoungana (yaani, manabii wa Agano la Kale kimsingi waliongelea juu ya Israeli).

C. Kuwarejea wote wawili Yohana mbatizaji (kama vile Mt. 11:9; 14:5; 21:26 Luka 1:76) na Yesu kama mpiga mbiu wa ufalme wa Mungu (kama vile Mt. 13:57; 21:11, 46; Luka 4:24; 7:16; 13:33; 24:19). Yesu pia alidai kuwa mkuu kuliko manabii (kama vile Mt. 11:9; 12:41; Luka 7:26).

D. Manabii wengine katika Agano Jipya 1. Maisha ya awali ya Yesu kama ilivyoandikwa katika injili ya Luka (yaani., kumbu kumbu za

Maria) a. Elizabethi (kama vile Luka 1:41-42) b. Zakaria (kama vile Luka 1:67-79) c. Simoni (kama vile Luka 2:25-35) d. Ana (kama vile Luka 2:36)

2. Ubashiri wa kejeli (kama vile Kayafa, Yohana 11:51) E. Inarejea juu ya mtu anayeitangaza injili (ikijumuishwa kwenye orodha ya kipawa cha utangazaji

katika 1 Kor. 12:28-29; Efe. 14:11)

Page 101: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

85

F. Ikirejea juu ya vipawa vinavyoendelea kanisani (kama vile Mt. 23:34; Mdo. 13:1; 15:32; Rum. 12:6; 1 Kor. 12:10, 28-29; 13:2; Efe. 4:11) wakati mwingine hii inaweza kumaanisha kwa wanawake (kama vile Luka 2:36; Mdo. 2:17; 21:9; 1 Kor. 14:4-5).

G. Ikirejea kwa sehemu mafunuo ya kitabu cha ufunuo (kama vile Ufu. 1:3; 22:7, 10, 18,19)

III. Manabii wa Agano Jipya A. Hawatoi ufunuo uliovuviwa kwa maana sawa kama manabii wa Agano la Kale waliofanya (yaani

mafundisho ya Biblia). Usemi huu unawezekana kwa sababu ya Matumizi ya kifungu cha neno “Imani” (yaani., kwa maana ya injili iliyokamilika) iliyotumika katika Matendo 6:7; 13:8; 14:22; Gal. 1:23; 3:23; 6:10; Flp. 1:27; Yuda 3, 20. Dhana hii iko wazi kutokana na fungu kamili la maneno lililotumika katika Yuda 3, “imani ya mara moja pasipo kujirudia imekabidhiwa kwa watakatifu.” Imani ya “jumla pasipo kujirudia” inarejerea kwenye ukweli, mafundisho, dhana, maoni ya dunia juu ya mafundisho ya ukristo. Msisitizo huu unaotolewa mara moja tu ni msingi wa Kibiblia kwa ajili ya kuzuia uvuvio ulio wa kithiolojia wa maandiko ya Agano Jipya na pasipo kuruhusu maandiko mengine kufikirika kimafunuo (angalia Mada Maalumu: Uvuvio). Kuna maeneo mengi yenye utata, yasiojulikana katika agano jipya (Tazama Mada Maalumu: Fasihi za mashariki [mafumbo ya Kibiblia]), lakini waamini wanathibitisha kwa imani kuwa kila kitu “kinachohitajika” kwa ajili ya imani na utendaji inajumuishwa ikiwa na utosherevu wenye uwazi wa kutosha katika Agano Jipya. Dhana hii inaelezwa kama “ufunuo pembe tatu.”

1. Mungu amejidhihirisha mwenyewe katika historia kwa muda muafaka (UFUNUO) 2. Amechagua baadhi ya waandishi wa kibinadamu kuweka kumbu kumbu na kuelezea

matendo yake (UVUVIO). 3. Alimtoa Roho Wake ili kufungua mawazo na mioyo ya watu wapate kuyaelewa

maandishi haya, si kwa ubora tu bali kwa utoshelevu wa wokovu na maisha ya Mkristo yenye kufaa (NURU, tazama Mada Maalumu: nuru). Hoja iliyopo hapa ni kuwa uvuvio umewekewa ukomo kwa waandishi wa neno la Mungu. Hakuna maandiko mengine, maono au mafunuo yenye mamlaka. Sheria za kanisa zimefungwa. Tuna ukweli wote tunaouhitaji ili kuitikia vizuri kwa Mungu. Ukweli huu unaonekana vizuri katika makubariano ya waandishi wa Kibiblia dhidi ya waumini watiifu wa ki-Mungu wasiokubali. Hakuna mwandishi au mnenaji wa kisasa aliye na kiwango cha uongozi wa ki-Uungu kama ambao waandishi wa neno la Mungu waliokuwa nacho.

B. Kwa namna nyingine manabii wa Agano Jipya ni sawa na wale wa Agano la Kale. 1. Utabiri wa matukio yajayo (kama vile Paulo, Mdo. 27:22; Agabo, Mdo. 11:27-28;

21:10-11; manabii wengine wasiotajwa Mdo. 20:23). 1. Kutangaza hukumu (kama vile Paulo, Mdo. 13:11; 28, 25-28) 2. Dalili za matendo ambayo dhahili yanaonyesha matukio (kama vile Agabo Matendo

21:11). C. Mara zote wananena kweli ya injili, wakati mwingine kwa njia ya utabiri (kama vile Matendo

11:27-28; 20-23; 21:10-11) Lakini kimsingi huu sio mtazamo wenyewe. Unenaji wa unabii katika Wakorintho wa 1 kimsingi unaibainisha injili (kama vile 1 Kor. 14:24,39).

D. Ni Roho wa wakati ule ule akimaanisha kudhihirika wakati ule ule na utumiaji wa kiutendaji wa kweli ya Mungu kwa kila hali, tamaduni mpya au kipindi cha muda (kama vile 1 Kor. 14:3).

E. Walikuwa imara katika makanisa ya mwanzo ya Paulo (kama vile 1 Kor. 11:4-5; 12:28, 29;13:2, 8, 8,9; 14:1 3,4,5,6,22,24,29,31,32,37,39; Efe. 2:20; 3:5; 4:11; 1 The. 5:20) na wametajwa katika Didache (iliyoandikwa katika karne ya mwisho au karne ya pili tarehe haijulikani) na wakati wa mienendo ya Kikristo ya karne ya pili na tatu katika Afrika ya kaskazini.

IV. Je karama za Agano Jipya zimekoma?

A. Swali ni gumu kulijibu. Linasaidia kufafanua jambo kwa kuelezea kusudi la karama. Je

Page 102: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

86

wanamaanisha kuthibitisha mafundisho ya awali ya kuhubiri injili au ni njia endelevu ya kanisa kujihudumia lenyewe kwenye ulimwengu ulipotea?

B. Je mmoja aweza kuangalia kwenye historia ya kanisa kujibu maswali au Agano Jipya lenyewe? Hakuna kiashirio chochote kinachoonyesha katika Agano Jipya kuwa karama za rohoni zilikuwa za muda tu. Wale wote wanaojaribu kutumia 1 Kor 13:8-13 kuelezea habari hii wanatukanisha kusudi la mwandishi wa aya hii, ambayo inadokeza kuwa kila kitu kitatoweka isipokuwa upendo.

C. Nathubutu kusema kuwa tangu Agano Jipya, si historia ya kanisa, ndiyo yenye mamlaka, waamini wanapaswa kuthibitisha kuwa karama zinaendelea. Hata hivyo ninaamini kuwa mila zinaathiri tafsiri za maandiko. Baadhi ya maandiko yalioko wazi hayatumiki tena (yaani busu takatifu, Baibui, makanisa kukutana nyumbani n.k). kama mila zinaathiri maandiko, hivyo kwa vipi zisiathiri historia ya kanisa?

D. Hili ni swali ambalo haliwezi kujibiwa. Baadhi ya waumini wanatetea kuwepo na“ukoma” na wengine watetea “kusiwepo na ukomo”. Katika eneo hili, kama ilivyo kwa mambo mengi yaliyo fasiliwa, moyo wa mwamini unabaki kuwa ndo kiini. Agano jipya ni tata na la kitamaduni zaidi. Ugumu unaweza kuamua ni maandiko yapi yanaathiliwa na mila/historia na yapi yanaathiriwa kwa wakati wote na yapi kwa mila (kama vile Fee na Stuart, How to read the Bible for all its Worth, kur. 14-19 na 69-77 hapa ndipo pale mjadala wa uhuru na kuwajibika, unaopatikana katika Warumi 14:1-15, 13 na Kor. 8-10 unapokuwa wenye umuhimu mkubwa. Namna tunavyojibu swali ni muhimu katika njia mbili. 1. Kila mwamini anapaswa kutembea katika imani yake kwa mwanga walio nao. Mungu

anaona mioyo yetu na nia. 2. Kila mwamini yampasa aruhusu waamini wengine kutembea katika uelewa wa imani.

Lazima pawepo na uvumilivu ndani ya mipaka ya kibiblia. Mungu anatutaka tupendane kama anavyotupenda.

E. Kwa kuhitimisha suala hili, Ukristo ni maisha ya imani na upendo, na sio tu thiolojia kamili. Uhusiano wetu na Yeye unaosababisha kuwepo na uhusiano na wengine ni muhimu zaidi kuliko habari au imani kamili.

4:20 “Baba zetu” Hii inamaanisha Abrahamu na Yakobo (kama vile Mwa. 12:7; 33:20) anatetea maana yake ya ujumuishaji wa kimaagano (kama vile Yohana 8:31-59). ◙ “waliabudu katika mlima huu” Hii inarejea ubishano wa kithiolojia kuhusu wapi Mungu YHWH anapaswa kuabudiwa. Wayahudi walisisitiza Mlima Moria (mahali pa hekalu la Wayahudi). Wakati wasamaria walisistiza Mlima Gelizim (Hekalu la Wasamaria lililoharibiwa mwaka 129 k.k na Yohana Hyrcanus). Kwa nyakati zetu hili lingalikuwa jaribio la watu ambao tunawashuhudia wakiondoka katika mambo yao ya kimahusiano na Kristo kwa kuleta miba ya kithiolojia. Watu hufurahia kujifunza dini na falsafa alimradi haya hayawaathiri kibinafsi (kama vile Yn. 3:19-21). 4:21 “saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu” Hii lazima tu ilikuwa habari ya kumshitua kwake na pia kwa wanafunzi wake.Suala sio wapi bali ni nani! 4:22 “kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi” Huu ni uthibitisho wa awali wa Masihi (kama vile Mwa. 12:2-3; 49:8-12; Isa. 2:3; Rum. 9:4-5). 4:23 “Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo” Hili lawezakuwa ni dokezo kwa Mal. 1:11 kuhusu kuabudu kwa watu wote. Ni wazi kwamba Yesu alileta zawadi ya uzima wa milele wakati wa kipindi chake pia baada ya kifo chake. Usemi huu unaakisi mvutano uliopo kati ya enzi mbili za ujio wa Masihi. Enzi mbili za wayahudi (tazama Mada maalumu: katika 1 Yohana 2:17) sasa zimepishanishwa. Enzi Mpya ya Roho sasa ipo, lakini bado tunaishi katika enzi ya kale ya uovu

Page 103: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

87

na dhambi. Bila shaka Yesu anaweka wazi kuwa enzi mpya imeanza ndani yake. Enzi ya Roho, enzi ya Kimasihi imezinduliwa! ◙ “katika roho na kweli” Neno “Roho” (tazama Mada maalum katika Yohana 3:8) inazungumzia ibada ambayo haiko katika misingi ya kienyeji wala kimwili. Neno “kweli” lilitumika wakati wa ulimwengu wa Kiyunani kuhusu dhana ya kifikra, wakati Waebrania walijari uaminifu na hali ya kuaminika. Tazama Mada maalumu: Kweli katika Yohana 6:55 na 17:3 ◙ “Baba” ilikuwa si kawaida sana kumwita Mungu “Baba” katika Agano jipya bila kuongeza rejea kwa Yesu kama mwana wake wa pekee.

MADA MAALUMU: BABA

Agano la Kale linaanzisha neno mbadala la ndani la Mungu kama Baba. (tazama Mada Maalum: Ubaba wa Mungu):

1. Taifa la Israeli daima linaelezwa kama “mwana” wa YHWH (kama vile. Hos. 11:1; Mal. 3:17) 2. Hata mwanzoni kabisa mwa kitabu cha Kumbukumbu la torati mfanano wa Mungu kama Baba

umetumika (1:31) 3. Katika kumbukumbu la torati 32 Israeli inaitwa “Mwana wake” na Mungu anaitwa “Baba yake” 4. Ufananisho huu unatajwa katika Zab. 103:13 na kuendelea katika Zab. 68:5 (baba wa yatima) 5. Lilikuwa la kawaida katika manabii (kama vile Isa. 1:2; 63:8; Israeli kama mwana, Mungu kama Baba,

63:16; 64:8; Yer. 3:4, 19; 31:9). Yesu alizungumza Kiaramu, ikimaanisha kuwa kuna sehemu nyingi ambapo “Baba” anaonekana, ni Pater Yule wa Kiyunani, na linawezakuwa linaakisi neno Abba la Kiaramu (kama vile Marko 14:36). Neno hili la kawaida “Baba” au “Papa” linaonyesha ukaribu uliopo wa Yesu na Baba. Udhihilisho wake huu kwa wafuasi wake pia kunahamasisha ukaribu wetu na Baba. Neno “Baba” lilitumika kidogo sana katika Agano la Kale kwa YHWH, lakini Yesu analitumia daima na kwa kulieneza. Ni uthibitisho mkubwa wa uhusiano mpya wa Waamini na Mungu kupitia kwa Kristo (kama vile Mathayo 6:9)

◙ “Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu” Mungu anawatafuta kwa bidii wanadamu waliopotea (kama vile Isa. 55; Ezek.18:23, 32; Luka 19:10; Yohana 1:12; 3:16). 4:24 “Mungu ni Roho” Kuna baadhi ya vifungu vidogo vidogo katika maandiko ya Yohana yanayoelezea tabia ya Mungu: (1) Mungu ni pendo (2) Mungu ni nuru (3) Mungu ni Roho. Hili laweza kumaanisha (1) sio kimaumbile (2) sio wa eneo moja (3) hahusishwi na mtiririko wa nyakati au (4) wa duniani dhidi ya mbinguni. 4:25 “Yuaja Masihi” Neno Masihi linajitokeza mara mbili tu katika Agano Jipya, mara zote katika injili ya Yohana (kama vile Yohana 1:41; 4:25).

MADA MAALUMU: MASIHI (toka Dan.9: 26)

Ugumu katika kutafasiri neno hili ni kwa sababu ya matumizi tofauti kuhusiana na neno lenyewe “Masihi” au “aliyetiwa mafuta” (BDB 603, KB 645). Neno lilitumika katika kumwekea mtu mafuta maalumu kuonyesha wito wa Mungu na kumkabidhi majukumu ya uongozi.

1. Lilitumika kwa wafalme wa Kiyahudi (mf. 1 Sam. 2:10; 12:3; 24:6, 10;2 Sam. 19:21; 23;1; Zab. 89:51; 132:10, 17; Wim. 4:20; Hab. 3:13; “Malkia mtiwa mafuta” katika Dan. 9:25)

2. Lilitumika kwa makuhani wa Kiyahudi (yaani, “makuhani walitiwa mafuta,” Kut. 29:7; mf. Law. 4:3, 5, 16; 6:15; 7:36; 8:12; bila shaka Zab. 84:9-10; na 133:2)

3. Lilitumika kwa makasisi, na Manabii (kama vile Mwa. 26:7; 1 Nya. 16:22; Zab. 105:15, iliyomaanisha watu wa Agano kwa pamoja; yumkini Hab. 3:13)

Page 104: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

88

4. Lilitumika kwa manabii (kama vile 1 Fal. 19:16; yumkini 1 Nya. 29:22) 5. Lilitumika juu ya Koreshi (kama vile. Isa. 45 :1) 6. # 1 na # 2 umeunganishwa katika Zab. 110 na Zekaria 4. 7. Lilitumika kwa ujio maalumu wa Mungu, Ufalme wa Daudi kuleta enzi mpya ya haki

a. uzao wa Yuda (kama vile Mwa 49:10) b. nyumba ya Yesse (kama vile 2 Sam 7) c. utawala wa ulimwengu (kama vile. Zaburi 2; Isa. 9:6; 11:1-5; Mik. 5:1- 4 na kuendelea) d. Huduma kwa wahitaji (kama vile Isa. 61:1-3)

Mimi binafsi nimevutiwa na utambulisho wa neno “aliyetiwa mafuta” na Yesu wa Nazareti (kama vile.Yn. 1:41; 4:25) kwa sababu

1. kutambulishwa kwa ufalme wa milele katika Danieli 2 kipindi cha utawala wa nne 2. kutambulishwa kwa “mwana Adamu” katika Dan. 7:13 akipewa ufalme wa milele 3. maneno ya ukombozi wa Dan. 9:24, ambayo yanaashiria mwisho wa historia ya ulimwengu

ulioanguka 4. matumizi ya Yesu ya kitabu cha Danieli katika Agano Jipya (kama vile Mt. 24:15; Marko 13:14)

Lazima kukiri kuwa hii ni mada nadra katika Agano la Kale, bila shaka Dan. 9:25. Lazima pia ifahamike kuwa Yesu haingii sana katika maelezo ya jumla kuhusu Masihi katika Agano la Kale

1. hakuwa kiongozi katika Israeli 2. hakutiwa mafuta rasmi na kuhani 3. sio kama mwokozi wa Israeli 4. sio tu “mwana wa Adamu” lakini kwa mshangao “Mwana wa Mungu”

◙ “Naye atakapokuja, yeye atatufunulia mambo yote” Hii inaonyesha kwamba wasamaria walimtarajia Masihi. Pia inaonesha walimwona Masihi anakuja kudhihilisha utimilifu wa Mungu.

4:26 “Mimi ninayesema nawe, ndiye” Usemi huu unaweza kuwa ni kidokezo kwa Isa. 52:6. Ni uthibitisho uliowazi wa Uungu wake (tofauti kabisa na ufupisho wa injili)! Ni mchezo juu ya neno “mimi ndimi” ulioakisi jina mbadala la Mungu YHWH katika Agano la Kale (kama vile Kut. 3:12, 14).Yesu alitumia jina hilo la Mungu katika Agano la Kale kama njia ya kurejea ufunuo binafsi wa YHWH ulioonekana wazi ndani ya Yesu (kama vile Yohana 8:24; 28, 58, 13:19 18:5 ukilinganisha na Isa. 41:4; 43;10; 46:4) Matumizi haya maalumu ya neno “Ndimi” yapaswa kutofautishwa na “ndimi” ya semi za Yohana 6:35, 51, 8:12; 10:7, 9, 11,14, 11:25; 14:6; 15:1, 5, ambazo zinafuatiwa na NOMINO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 4:27-30 27 Mara hiyo wakaja wanafunzi wake, wakastaajabu kwa sababu alikuwa akisema na mwanamke; lakini hakuna aliyesema, Unatafuta nini? Au, Mbona unasema naye? 28 Basi yule mwanamke akauacha mtungi wake, akaenda zake mjini, akawaambia watu, 29 Njoni, mtazame mtu aliyeniambia mambo yote niliyoyatenda. Je! Haimkini huyu kuwa ndiye Kristo? 30 Basi wakatoka mjini, wakamwendea.

4:27 “wakastaajabu kwa sababu alikuwa akisema na mwanamke” Kitamaduni hili halikuwa likifanywa na Wayahudi wa wenye msimamo wa kidini. ◙ “Lakini hakuna aliyesema, Unatafuta nini? Au, Mbona unasema naye?” Haya ni maoni ya wazi kutoka kwa Yohana. Ni lazima atakuwa amekumbuka vizuri tukio hili la kushitua. 4:28 “Mwanamke akauacha mtungi wake” Huu ni ushuhuda mzuri wa wazi, tukio la kihistoria lililoonyesha mshituko wa mwanamke huyo kwa vile alirudi haraka kijijini mwake kutoa ushuhuda (kama vile Yohana 4:29-30). 4:29 “Huyu kuwa ndiye Kristo?” Kwa muundo wa kisarufi swali hili hutarajia jibu la “hapana” lakini mazingira yanaonyesha kuwa mwanamke huyu kwa hakika aliamini kuwa huyu alikuwa Yesu! Neno hili linasanifu usemi!

Page 105: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

89

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 4:31-38 31 Huko nyuma wanafunzi wakamsihi wakisema, Rabi, ule. 32 Akawaambia, Mimi ninacho chakula msichokijua ninyi. 33 Basi wanafunzi wake wakasemezana, Je! Mtu amemletea chakula? 34 Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake.35 Hamsemi ninyi, Bado miezi minne, ndipo yaja mavuno? Tazama, mimi nawaambieni, Inueni macho yenu myatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha kuwa meupe, tayari kwa mavuno. 36 Naye avunaye hupokea mshahara, na kukusanya matunda kwa uzima wa milele, ili yeye apandaye na yeye avunaye wapate kufurahi pamoja. 37 Kwa maana hapo neno hilo huwa kweli, Mmoja hupanda akavuna mwingine. 38 Mimi naliwatuma myavune yale msiyoyataabikia; wengine walitaabika, nanyi mmeingia katika taabu yao.

4:32 Hili ni dokezo lingine lenye pande mbili za mbingu dhidi ya dunia, za kiroho dhidi ya mwili. Yesu alikuwa kwenye mipango ya uinjilisti. Watu kwake ndio walikuwa kipaumbele! 4:34 “Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake” Yohana 17 ni maelezo ya wazi ya uelewa wa Yesu wa kile Baba alichomtaka Yeye kufanya (kama vile Marko 10:45; Luka 19:10; Yohana 6:29). Tofauti kati ya Yesu aliyetumwa toka juu, toka katika uwepo wa sasa wa Mungu Baba, kama mkakati wa kumdhihilisha Babaye na kufanya kazi ya Baba yake. Hii ni ile hali ya uwepo wa mambo mawili kwa pamoja ambayo ilikuwa ni tabia ya Yohana (yaliyo juu dhidi ya yaliyo chini, Roho dhidi ya mwili). Kuna maneno mawili yametumika kuhusu kutumwa kwa Yesu

1. Pempō (Yohana 4:34; 5:23,24, 30, 37; 6:38, 39, 40, 44; 7:16, 18, 28, 33; 8:16, 18,26, 29; 9:4; 12:44, 45, 49; 14:24; 15:21; 16:5)

2. Apostellō (Yohana 3:17, 24; 5:36, 38; 6:29, 57; 7:29; 8:42; 10:36; 11:42; 17:3, 18, 21, 23, 25; 20:21) Haya ni maneno yanayofanana kama ilivyo katika Yohana 20:21 yanavyoonekana, Inaonyesha pia kwamba waamini wametumwa katika ulimwengu huu uliopotea kama wawakilishi wa Baba kwa lengo la ukombozi (kama vile 2 Kor. 5:13-21).

MADA MAALUM: MAPENZI (thelēma) YA MUNGU

“Mapenzi” ya Mungu yamejikita katika namna mbalimbali.

INJILI YA YOHANA

Yesu alikuja kuyatenda mapenzi ya Baba yake (kama vile Yohana 4:34; 5:30; 6:38)

Kuwafufua siku ya mwisho wale wote Baba aliowampa Mwana (kama vile Yohana 6:39)

Kwamba wote waamini katika Mwana (kama vile Yn. 6:29; 40)

Maombi yaliyojibiwa kuhusiana na kuyatenda mapenzi ya Mungu (kama vileYn. 9:31 na Yn. 5:14)

VIDOKEZO VYA INJILI

Kuyatenda mapenzi ya Mungu ni jambo la muhimu (kama vile. Mt. 7:21)

Kuyatenda mapenzi ya Mungu hutufanya kuwa kaka na dada pamoja na Yesu (kama vile Mt. 12:50; Marko 3:35)

Sio mapenzi ya Mungu kwa yeyote kuangamia (kama vile Mt.18:14; 1 Tim. 2:4; 2 Pet. 3:9)

Kalvari ilikuwa ni mapenzi ya Mungu kwa Yesu (kama vile Mt. 26:42; Luka 22:42)

NYARAKA ZA PAULO

ukomavu na huduma ya waamini wote (kama vile Rum. 12:1-2)

waamini waliondolewa kutoka katika enzi hii ya maovu (kama vile Gal. 1:4)

Page 106: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

90

mapenzi ya mungu ulikuwa ni mpango wake wa ukombozi (kama vile. Efe.1:5, 9,15)

waamini wanapitia na kuishi maisha yaliyojazwa na Roho (kama vile 5:17-18)

waamini wamejazwa na maarifa ya Mungu (kama vile Kol. 1:9)

waamini wanafanywa kuwa imara na wakamilifu (Kol. 4:12)

waamini wanatakaswa (kama vile 1The. 4:3)

waamini watoa shukrani katika vitu vyote (kama vile The.5:18)

NYARAKA ZA PETRO

Waamini wanatenda haki (yaani, kunyenyekea kwenye mamlaka ya chini) na, kwa hiyo wanawanyamazisha watu wajinga, hivyo kuwapa fursa kwa kuijua injili/matendo mema (kama vile 1Pet. 2:15)

Mateso ya waamini (kama vile 1 Pet. 3:17; 4:19)

Waamini hawapaswi kuishi maisha ya ubinafsi (kama vile 1 Pet. 4:2)

NYARAKA ZA YOHANA

waamini kuendelea kudumu milele (kama vile Yohana 2:17) waamini ni kielelezo kwa maombi yaliyojibiwa (kama vile 1 Yohana 5:14)

4:35 “Bado miezi minne, ndipo yaja mavuno?” Hiki ni kifungu cha ki-isitiari kinachoonyesha kwamba fursa ya mwitikio kiroho ni sasa! Watu waliokolewa kwa imani katika Yesu wakati wa maisha yake, Sio tu baada ya kufufuka kwake. 4:36-38 “Mmoja hupanda akavuna mwingine” Mistari hii inarejea kwenye huduma ya Manabii au yumkini Yohana mbatizaji. Hii imetumika katika 1 Kor. 3:6-8 kwa uhusiano kati ya huduma ya Paulo na huduma ya Apollo.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 4:39-42 39Na katika mji ule Wasamaria wengi walimwamini kwa sababu ya neno la yule mwanamke, aliyeshuhudia kwamba, Aliniambia mambo yote niliyoyatenda. 40 Basi wale Wasamaria walipomwendea, walimsihi akae kwao; naye akakaa huko siku mbili. 41 Watu wengi zaidi wakaamini kwa sababu ya neno lake. 42 Wakamwambia yule mwanamke, Sasa tunaamini, wala si kwa sababu ya maneno yako tu; maana sisi tumesikia wenyewe, tena twajua ya kuwa hakika huyu ndiye Mwokozi wa ulimwengu.

4:39 “Wasamaria wengi walimwamini” Yohana anatumia KITENZI “kuamini” katika muunganiko wa maneno mengine: “walimwamini” (en), “amini” (hoti) mara nyingi “amini katika” (eis) au weka imani kwa (kama vile Yohana 2:11, 23; 3:16, 18, 36; 6:29, 35, 40; 7:5, 31, 38, 48; 8:30; 9:35, 36; 10:42; 11:25, 26, 45, 48; 12:11, 37, 42, 44, 46; 14:1, 12; 16:9; 17:20). Kwa asili wasamalia waliamini kwa sababu ya ushuhuda wa mwanamke (Yohana 4:39); lakini baada ya kumsikia Yesu aliuamini ushuhuda wake binafsi (kama vile Yoh. 4:41-42) Yesu alikuja kwa kondoo wa Israeli waliopotea, Lakini injili yake ilikuwa kwa wanadamu wote: Wasamaria, kinamama wa Foenike, na askari wa Rumi (kama vile Rum. 10:12; 1 Kor. 12:13; Gal. 3:28-29; Kol.3:11) Tazama Mada Maalumu katika Yohana 2:23 ◙ “kwa sababu ya neno la yule mwanamke, aliyeshuhudia” Kama Mungu alitumia ushahidi wa mwanamke huyu asiye mwadilifu, Yesu pia anaweza akatumia ushahidi wangu na wa kwako! Mstari huu unaonyesha umuhimu wa ushuhuda binafsi wa mtu. Tazama MADA MAALUMU: MASHUHUDA WA YESU katika Yohana 1:8 4:40 NASB, NRSV “anauliza” NKJV “ushauri”

Page 107: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

91

TEV, NJB “anaomba” Hili ni neno la nguvu la Kiyunani na inabidi litafasiliwe kama “kusihi” au “kuomba.” uzito wa neno hili unaonekana kwenye matumizi yake katika Yohana 4:47 (kama vile Luka 4:38). 4:42 “Mwokozi wa ulimwengu” Cheo hiki cha watu wote kimetumika katka 1 Yohana 4:14. Pia unatumika kwa maana ya upendo wa Mungu kwa wanadamu wote (kama vile 1 Tim. 2:6 Ebr. 2:9 1 Yoh. 2:2). Ahadi ya mwanzo. 3:15 imetimizwa! Katika karne ya kwanza fungu hili lilitumika daima kwa kaisari. Kutiwa hatiani kwa warumi kulitokea kwa sababu walitumia wadhifa huu tofauti na Yesu. Wadhifa huu ulionyesha pia jinsi waandishi wa Agano Jipya walivyoweka sifa za Mungu kwa mwanae. Tito 1:3- Tito 1:4; Tito 2:10- Tito 2:13; Tito 3:4- Tito 3:6. Wayahudi walikuwa wamemkataa Yesu (kama vile Yohana 1:11) lakini Wasamaria kwa haraka na kirahisi tu walimpokea Yesu (kama vile Yoh. 1:12)!

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 4:43-45 43Na baada ya siku mbili hizo akaondoka huko, akaenda Galilaya. 44 Kwa maana Yesu mwenyewe alishuhudia ya kwamba nabii hapati heshima katika nchi yake mwenyewe. 45 Basi alipotoka Galilaya, Wagalilaya walimpokea; kwa kuwa wameyaona mambo yote aliyoyatenda huko Yerusalemu wakati wa sikukuu; maana hao nao waliiendea sikukuu.

4:43 Mstari huu unaonyesha kuwa Yesu alitembea kwa uhuru zaidi na mara nyingi kati ya miji ya Yuda na Galilaya kuliko kile mtu anaweza fikiria toka kwenye mihitasari ya Injili. 4:44 Huu ni mstari usio wa kawaida sana kwa sababu hauendani na muktadha uliotangulia. Waweza kurejerea huduma ya Wagalilaya iliyokaribia kuanza (kama vile Yohana 4:3) mfano halisi pia unapatikana katika Mathayo 13: 57, Marko 6:4, Luka 4:44. Katika mihtasari inarejea Galilaya, lakini hapa inarejeaYudea. 4:45 “Wagalilaya walimpokea” Walikuwa tayari wamezoea mafundisho na miujiza ya Yesu wakati alipotembelea Yerusalemu kipindi cha Pasaka. Wagalilaya pia wanasemekana “kumpokea” Yesu, lakini wengi wao hawakufuatilia mapokeo haya na baadaye walimwacha. “Kuamini” (kama vile Yohana 3:16) na “kumpokea” (kama vile Yohana 1:17) kunahusisha zaidi ya ule upokeaji wa mwanzo (kama vile mfano wa udongo katika Mathayo 13:18-23; Marko 4:12-20; Luka 8:11-15) Tazama Mada Maalumu: Hitaji la Ustahimilivu katika Yohana 8:31. ◙ “maana hao nao waliiendea sikukuu” Biblia ya NET inalitilia alama hili kama maoni mengine ya mwandishi yaliyowekwa kwenye mabano, kama yote yafanywavyo kwenye Yohana 4:44 (kama vile NRSV, NIV).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 4:46-54 46 Basi alifika tena Kana ya Galilaya, hapo alipoyafanya yale maji kuwa divai. Na palikuwa na diwani mmoja ambaye mwanawe hawezi huko Kapernaumu. 47 Huyo aliposikia ya kwamba Yesu amekuja kutoka Uyahudi mpaka Galilaya, alimwendea, akamsihi ashuke na kumponya mwanawe; kwa maana alikuwa kufani. 48 Basi Yesu akamwambia, Msipoona ishara na maajabu hamtaamini kabisa? 49 Yule diwani akamwambia, Bwana, ushuke asijakufa mtoto wangu. 50 Yesu akamwambia, Enenda; mwanao yu hai. Mtu yule akalisadiki lile neno aliloambiwa na Yesu, naye akashika njia.51 Hata alipokuwa akishuka, watumwa wake walimlaki, wakisema ya kwamba mtoto wake yu hai. 52 Basi akawauliza habari ya saa alipoanza kuwa hajambo; nao wakamwambia, Jana, saa saba, homa ilimwacha. 53 Basi babaye akafahamu ya kuwa ni saa ile ile aliyoambiwa na Yesu, Mwanao yu hai. Akaamini yeye na wote wa nyumbani mwake. 54 Hiyo ni ishara ya pili aliyoifanya Yesu, alipokuwa ametoka Uyahudi kufika Galilaya.

4:46 NASB, NRSV,

Page 108: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

92

NJB “mtu wa ukoo wa kifalme” NKJV “mtu fulani maarufu” TEV “mtumishi wa serikali” Huyu alikuwa mtumishi wa serikali akihudumu katika familia ya Herode. 4:48 “Msipoona ishara na maajabu hamtaamini kabisa?” Hii ni sentensi shurutishi daraja la tatu ikiwa na ukanushi mara mbili wenye nguvu. Yesu alimwelezea mtu huyo katika hali ya wingi. Wayahudi walikuwa wakitafuta ishara (kama vile Yohana 2:18; 6:2, 30; Mt. 12:38; 16:1). Lakini huyu mtumishi wa Herode yeye aliaamini kabla ya ishara kutolewa. 4:49 “mtoto” Katika mistari mitatu Yohana anatumia maneno matatu tofauti.

1. Yohana 4:49- paidion (NASB, “mtoto”) 2. Yohana 4:50- hyiōs (NASB, “mwana”) 3. Yohana 4:51- pais (NASB, “mwana”)

Bila shaka maneno haya yalitumika kwa maana sawa.

4:50 Mstari huu unachukua umuhimu wa injili ya Yohana – amini katika Yesu, amini maneno yake, amini matendo yake, mwamini yeye binafsi! Imani ya mtu huyu inathibitika katika kuamini kwake hata bila kuonekana kwa ahadi zake Yesu. 4:53 “Akaamini yeye na wote wa nyumbani mwake” Haya ni maelezo ya kwanza miongoni mwa wengi pale ambapo imani ya mtu binafsi inahusu familia nzima.

1. Kornelio (Mdo. 10:44-48) 2. Lydia (Mdo. 16:15) 3. Askari Jela wa Ufilipino (Mdo. 16:31-34) 4. Krespo (Mdo. 18:8) 5. Stephano (1Kor. 1:16)

Pamekuwa na mjadala mrefu kuhusu mabadiliko haya ya kifamilia. Lakini yapaswa yawekwe wazi kuwa wanafamilia wote walihitaji kila mmoja kumkubali Yesu kwa ajili yao wenyewe. Katika mashariki ya kati watu wana uelekeo wa kikabila na kifamilia zaidi kuliko utamaduni wa kisasa. Na ni kweli pia kwamba wengine wengi katika maisha yetu wanaathiri chaguzi zetu. 4:54 Ishara ya kwanza hadharani ilikuwa kwenye sherehe ya harusi huko Kana ya Galilaya (kama vile Yohana 2:1-11).

MASWALI YA MJADALA

Huu ni mwongozo wa fasiri, ina maanisha kwamba unawajibika kwa tafsiri zako mwenyewe za Biblia. Kila mmoja wetu lazima atembee katika mwanga tulio nao. Wewe, Biblia, na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Hutakiwi uvitelekeze vitu hivi kwa mfasiri. Maswali ya mjadala huu yanatolewa kukusaidia kufikiri juu ya mambo makubwa ya sehemu za kitabu hiki. Yanalenga kukuamsha kimawazo na sio kutoa maana.

1. Kwanini Yesu aliondoka katika eneo la Yuda? 2. Je Yohana anatumia muda/saa za Kirumi au za Kiyahudi? 3. Kwa nini Yesu kuzungumza na mwanamke Msamaria ni muhimu sana? 4. Kwa namna gani Yohana 4:20 anaathiri uhusiano wa madhehebu leo? 5. Elezea usemi wa Yesu wenye utata alioufanya katika Yohana 4:26. 6. Wagalilaya walikuwa na imani ya kweli?

Page 109: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

93

YOHANA 5

MIGAWANYO YA AYA YA TAFSIRI ZA KISASA

UBS4 NKJV NRSV TEV NJB

Uponyaji pale Mtu anaponywa penye Uponyaji wa Mtu Uponyaji pale penye uponyaji wa Mtu penye Birika Birika la Bethzatha kiwete siku ya Birika mgonjwa pale penye Sabato Birika la Bethzatha 5:1-9a 5:1-15 5:1 5:1-6 5:1-9a 5:2-9a 5:7 5:8-9a 5:9b-18 5:9b-18 5:9b-10 5:9b-18 5:11 5:12 5:14 5:16 Kuheshimiwa 5:15-17 Kwa Baba 5:18 na Mwana Mamlaka ya 5:16-23 Mahusiano Mamlaka ya Mwana ya Yesu na Mungu Mwana 5:19-29 5:19-24 5:19-23 5:19-47 Uzima na Hukumu ni kupitia kwa Mwana 5:24-30 5:24-29 5:25-29 Uthibitisho wa Yesu ushuhuda juu Kuhusiana na Mungu ya Yesu 5:30 5:30 5:30 Ushuhuda juu Shuhuda Nne Ya Yesu zimshuhudiazo 5:31-40 5:31-47 5:31-38 5:31-40 Yesu anawakemea waliokataa ahadi yake 5:39-47 5:41-47 5:41-47

Page 110: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

94

MZUNGUKO WA TATU WA USOMAJI KUFUATILIA KUSUDIO LA ASILI LA MWANDISHI KATIKA NGAZI YA AYA Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwatafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Aya ya kwanza 2. Aya ya pili 3. Aya ya tatu 4. N.k

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 5:1-9a 1 Baada ya hayo palikuwa na sikukuu ya Wayahudi; naye Yesu akakwea kwenda Yerusalemu. 2 Na huko Yerusalemu penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiebrania Bethzatha, nayo ina matao matano. 3 Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, nao waliopooza, [wakingoja maji yachemke. 4 Kwa maana kuna wakati ambapo malaika hushuka, akaingia katika ile birika, akayatibua maji. Basi yeye aliyeingia wa kwanza baada ya maji kutibuliwa, akapona ugonjwa wote uliokuwa umempata.] 5 Na hapa palikuwa na mtu, ambaye amekuwa hawezi muda wa miaka thelathini na minane. 6 Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima? 7 Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu. 8 Yesu akamwambia, Simama, jitwike godoro lako, uende. 9 Mara yule mtu akawa mzima, akajitwika godoro lake, akaenda. Nayo ilikuwa ni sabato siku hiyo.

5:1 “sikukuu” Baadhi ya maandishi ya zamani ya Kiyunani, א na C, yana neno “sikukuu” kama neno maalumu, lakini maandishi mengi yana neno “sikukuu” kama neno la kawaida. (P66, p75, A, B na D). Palikuwa na siku tatu za sikukuu kwa mwaka ambazo zilikuwa ni lazima kwa Wayahudi wa kiume kuhudhuria palipokuwepo na uwezekano (kama vile Walawi 23): (1) Pasaka (2) Pentekoste; na (3) Sikukuu ya Vibanda. Kama hii ilimanisha kuwa ni Pasaka, basi Yesu alikuwa na kazi ya hadhara ya miaka mine badala ya mitatu (kama vile Yohana 2:13, 23; 6:4: 12:1) Ni desturi iliyomsababisha Yesu ahudumu miaka mitatu baada ya ubatizo wa Yohana. Hii inathibitishwa tu kwa idadi ya sikukuu za pasaka zilizotajwa katika injili ya Yohana. ◙ “Yesu akakwea kwenda Yerusalemu” Inasemekana Yesu alikwenda katika sikukuu huko Yerusalemu mara kadhaa kama kitabu cha Yohana kinavyoeleza (kama vile Yohana 2:13; 5:1; 7:10; 12:12). Yerusalemu ilikuwa imejengwa juu ya vilima saba na ilikuwa juu zaidi kuliko maeneo mengine yaliyoizingira, kwa hiyo usemi kuwa “alienda juu” kihalisia ilikuwa sahihi. Hata hivyo, inaonekana ilikuwa ni nahau kwa sehemu iliyo inuka zaidi. Yerusalemu, kwa sababu ya hekalu, ilikuwa sehemu ya nchi iliyoinuka juu ya ardhi na katikati (kwenye kitovu) cha nchi. 5:2 “penye mlango wa kondoo” “lango hili la kundi” lilikuwa katika sehemu ya kaskazini- mashariki mwa ukuta wa Yerusalemu. Imetamkwa katika kazi ya Nehemia ya ujenzi mpya wa kuta za jiji (kama vile Neh. 3:1; 32, 12:39) NASB, NKJV “birika ambalo linaitwa Bethzatha Kiebrania” NRSV “liitwalo kwa Kiebrania Bethzatha” TEV “katika Kiebrania linaitwa Bethzatha” NJB “liitwalo kwa Kiebrania Bethzatha”

Page 111: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

95

Kuna namna mbali mbali ya uainishaji wa jina hili. Yusufu pia aliitwa “Bethzasha” ambalo lilikuwa jina katika sehemu hii ya Yerusalemu. Pia linaitwa “Bethsaida” katika maandishi ya Kiyunani. Moja ya magombo ya Bahari ya chumvi yaliyopatikana huko Qumram pia yaliitwa “Bethesda” likimaanisha “Nyumba ya huruma” au “nyumba ya chemi chemi mbili”. Leo hii linajulikana kama dimbwi la Mt. Anna. Katika enzi za Yesu Wayahudi wa Palestina walizungumza lugha ya Kiaramu na Kiebrania. Katika Yohana anaposema “Kiebrania” ana maana ya Kiaramu (kama vile Yohana 5:2; 19:13, 17, 20; 20:26; Law. 9:11; 16:16). Katika semi zote za Yesu:

1. Talitha kum, Marko 5:41 2. Ephphatha, Marko 7:34 3. Eloi, Eloi, lama sabachthani, Marko 15:34 yote ni Kiaramu.

5:4 Mstari huu wa (Yohana 5:36-4) ni fasihi za mwandishi wa kale anayejaribu kueleza:

1. Uwepo wa wagonjwa wote karibu na lile birika 2. Kwa nini mtu Yule alikuwepo pale kwa muda mrefu 3. Kwa nini alitaka mtu amweke katika maji Yohana 5:7

Ni dhahili hizi zilikuwa hadithi za kale za Kiyunani. Haikuwa sehemu ya awali ya injili ya Yohana. Uthibitisho juu ya mstari huu ambao haukujumuishwa ni:

1. Haupo katika maandiko P66, p75, א, B, C*, D 2. Imewekewa alama ya nyota katika maandiko zaidi ya 20 ya Wayahudi yaliyoandikwa baadaye, kuonesha

kuwa andiko lilifikiriwa kutokuwa halisi. 3. Kuna maneno kadhaa yasiyo ya Yohana yaliyotumika katika msitari huu mfupi.

Yamejumuishwa katika maandiko kadhaa ya kale ya Kiyunani A, C3, K na L. Pia yamejumuishwa katika mkusanyiko wa vitabu vine vya injili vilivyowekwa kwenye simulizi moja (Diatessaron) katika miaka ya 180 baada ya kuzaliwa Kristo B.K, na maandiko ya Tertullian Ambrose, Chrysostom, na Cyril miaka 200 b.k. Hii inaonyesha uchakavu wake na sio kujumuishwa kwake katika injili asilia iliyovuviwa. Imejumuishwa katika KJV, NASB (lililoboreshwa 1995, likiwa katika mabano), pia NKJV, lakini likaachwa katika biblia za NASB (1970), NRSV, NJB, REB, NET na NIV. Kwa mjadala mzuri wa maandiko tofauti ya mkosoaji wa maandiko tazama Gordon Fee, To What End Exegesis?, uk. 17-28. 5:5-6. Haswa ni kwa nini Yesu alimchagua mtu huyu haijajulikana kwetu. Yumkini amekuwepo kwa muda mrefu mahali pale. Kuna imani kidogo inahitajika kwa upande wa mtu huyu.Ni dhahiri kabisa Yesu alijaribu kuanzisha migogoro na viongozi wa Kiyahudi. Hii ilimpa fursa ya kuonyesha dai lake la kuwa Masihi. Habari ya kiama ya Isaya 35:6 inawezekana kuhusishwa na uponyaji wa kinabii, miujiza mingi ya Yesu haikuwa inafanyika kimsingi kwa ajili ya mtu mmoja bali kwa wale wote wanaowaangalia.

1. Wanafunzi 2. Mamlaka ya Wayahudi 3. Kundi la wahitaji

Injili zinachagua miujiza kadhaa kuonyesha wazi alikuwa nani. Matukio haya yanawakilisha matendo yake ya kila siku. Yamechaguliwa kuonyesha

1. Nafasi Yake kama mtu 2. Upendo wake kwa wanaoteseka 3. Nguvu zake 4. Mamlaka yake 5. Ufunuo wake wa wazi wa Baba yake 6. Ufunuo wa wazi wa enzi yake ya Kimasihi

5:8 “Simama, jitwike godoro lako, uende” Huu ni mfululizo wa amri.

1. Kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopo 2. Ikifuatiwa na kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopita usio timilifu 3. Baadaye ikifuatiwa na kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopo

Page 112: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

96

Kirago kilikuwa kigodoro cha nguo ambacho maskini alikitumia kulalia. Kwa wagonjwa hawa, vilema, na waliopooza, Kilisaidiwa kama kitu cha kulaliwa wakati wa mchana (kama vile Marko 2:4, 9,11,12; 6:55; Mdo. 9:33).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 5:9b-18 9Nayo ilikuwa ni sabato siku hiyo. 10 Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwambia yule aliyeponywa, Leo ni sabato, wala si halali kwako kujitwika godoro. 11 Akawajibu, Yeye aliyenifanya kuwa mzima ndiye aliyeniambia, Jitwike godoro lako, uende.12 Basi wakamwuliza, Yule aliyekuambia, Jitwike, uende, ni nani? 13 Lakini yule mtu aliyeponywa hakumjua ni nani; maana Yesu alikuwa amejitenga, kwa sababu palikuwa na watu wengi mahali pale. 14 Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi. 15 Yule mtu akaenda zake, akawapasha habari Wayahudi ya kwamba ni Yesu aliyemfanya kuwa mzima. 16 Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwudhi Yesu, kwa kuwa alitenda hayo siku ya sabato. 17 Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi. 18 Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu. Basi Yesu akajibu, akawaambia, Amin, amin, nawaambia,

5:9b “Nayo ilikuwa ni sabato siku hiyo” viongozi wa Kiyahudi hawakufurahia kuhusu mtu aliyeponywa, lakini waliudhiwa kwa Yesu kuvunja mila na utamaduni wao usioandikwa (baadaye ukaandikwa katika kitabu cha sheria za Kiyahudi-Talmud) ikiunganishwa na sabato (kama vile Yohana 5:16,18; Mt.7:1-23) Uponyaji wa Yesu siku ya sabato unaweza kuelezwa katika njia mbili

1. Aliponya kila siku, isipokuwa mabishano yakaibuka juu ya uponyaji siku ya sabato 2. Alichagua siku hii kusababisha ubishi huu kama fursa ili kuwangiza viongozi wa kidini katika mjadala wa

kithiolojia. Yesu daima aliponya siku ya sabato. (kama vile Mt.12:9-14;Marko 1:29-31; 3:1-6; Luka 6:6-11; 14:1-6; Yohana 5:9-18; 9:14). Yesu alitoa mapepo siku ya sabato (kama vile Marko 1:21-28; Luka 13:10-17). Yesu aliwatetea wanafunzi kuhusu kula siku ya sabato (kama vile Luka 4:16-30; Yohana 7:14-24). 5:13 “Yesu alikuwa amejitenga” kwa lugha rahisi “aligeuzia kichwa upande mwingine” Yesu alionekana kuwa sawa na Myahudi wa kawaida wa siku zake. Yesu alipotelea katikati ya kusanyiko. 5:14 NASB, NRSV, NJB "usitende dhambi tena" NKJV "usitende dhambi" TEV "kwa hiyo acha kutenda dhambi" Hii ni kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopo yenye kiambata hasi. Ambayo daima ilimaanisha kuacha tendo ambalo tiyari lilikuwa kwenye mchakato, lakini katika hali hii hili linaonekana kutoweza kutendeka (kama vile NET Bible, uk. 1907 #8). Wanathiolojia wa Kiyahudi wa karne ya kwanza walioona ugonjwa kama unahusiana na dhambi (kama vile Yakobo 5:14-15). Hii haielezi magonjwa yote, kama inavyoonekana Yesu akishughulika na mtu aliyezaliwa kipofu (kama vile Yohana 9) na maneno ya Yesu katika Luka 13:1-4. Yesu alikuwa bado anashugulikia maisha ya kiroho ya mtu huyo. Matendo yetu yanaakisi mioyo yetu na imani. Imani ya kibiblia ni tendo la kujaribu kufanya au ni hisia za kifikra ambayo sio lazima kutokea, ni vyote imani na matendo. Siku hizi kuna kama msisitizo katika kanisa kuhusu uponyaji wa kimwili. Kwa hakika Mungu bado anaponya. lakini uponyaji wa kiimani lazima utokane na badiliko la kiroho kwa badiliko la mfumo wa maisha na vipaumbele. Swali zuri lingeweza kuwa “kwanini unataka kuponywa?”

MADA MAALUM: UPONYAJI

Page 113: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

97

Inanishangaza kuona kuwa si wote walioponywa katika Agano Jipya “waliokolewa” (yaani., walimwamini Kristo na kuwa na uzima wa milele). Uponyaji wa mwili ni mbadala duni kwa ajili ya wokovu wa kiroho. Miujiza inaonekana kuwa ya msaada zaidi pale tu inapoturejeza mbele za Mungu. Wanadamu wote tunaishi katika ulimwengu ulioanguka. Mambo mabaya hutokea. Mara nyingi Mungu huchagua kutoingilia kati, lakini hili halisemi kitu chochote juu ya pendo na uhusika wake. Uwe mwangalifu pale unapotaka Mungu aingilie kati kutenda kimiujiza kwa kila hitaji unalolitaka katika kizazi hiki cha uovu. Yeye ni Mungu Mkuu na hatujui maana yake kamili kwenye hali Fulani inayotolewa.

Kwa maana hiyo ningalipenda kuongeza kumbukumbu za fasiri yangu toka kwa 2 Tim. 4:20 kuhusu Paulo na uponyaji ya kimwili (angalia www.freebiblecommentary.org ): "kuna maswali mengi ambayo tungepaswa kuwauliza waandishi wa Agano Jipya. Somo moja ambalo waaminio wote wanalifikiria ni kuhusu uponyaji wa kimwili. Katika kitabu cha Matendo (kama vile 19:12; 28:7-9) Paulo anaweza kuponya, lakini hapa na katika 2 Kor. 12:7-10 na Fil. 2:25-30, anaonekana kutoweza. Kwa nini baadhi waponywe na sio wote, na kuna muda ambapo dirisha linalohusiana na mambo ya uponyaji huwa linafungwa? Hakika ninaamini kwenye nguvu ya ajabu, Baba mwenye rehema ambaye Yeye huponya kimwili vile vile kiroho, lakini ni kwa nini hii dhana ya uponyaji inaonekana kuwepo na baadaye tena haionekani? Sifikirii kuwa inahusiana na imani ya mwanadamu, kwa hakika Paulo alikuwa na imani (kama vile 2 Wakorintho 12). Nahisi kuwa uponyaji na kuiamini miujiza huthibitisha ukweli na mamlaka ya injili, ambayo bado inatenda katika maeneo ya ulimwengu ambayo mwanzoni ilitangazwa. Hata hivyo, nahisi kuwa Mungu anatuhitaji tutembee katika imani na sio kwa mtazamo. Pia, uponyaji wa kimwili mara nyingi huruhusiwa katika maisha ya watu:

1. kama adhabu ya muda mfupi kwa ajili ya dhambi 2. kama matokeo ya maisha kwenye ulimwengu ulioanguka 3. kuwasaidia waaminio kukuwa kiroho

Tatizo langu ni kuwa sikuwahi kujua ni yupi anahusika! Ombi langu kwa ajili ya mapenzi ya Mungu yaweze tendeka katika kila jambo sio kuwa na uhaba wa imani bali ni jaribio la uaminifu ili kuruhusu Mungu mwenye rehema na mwingi wa fadhira kutenda mapenzi yake katika kila maisha." Hapa kuna hitimisho langu:

1. uponyaji ulikuwa ni dhana ya huduma ya Yesu na Mitume. 2. ulikusudia kimsingi kuthibitisha moja kwa moja ujumbe mpya kuhusu Mungu na ufalme Wake. 3. kuonyesha moyo wa Mungu kwa ajili ya watu wanaoumia. 4. Mungu hajawahi kubadilika (Mal. 3:6) na atatenda kwa upendo, katika uponyaji (karama zote za kiroho

bado zinaendelea, kama vile 1 Kor. 12:9,28,30). 5. Kuna mifano mingi ambapo uponyaji kwa wale wenye imani kubwa haukutenda kazi (kijitabu

kilichonisaidia mimi katika eneo hili ni kile cha Gordon Fee, The Disease of the Health, Wealth Gospel). a. Paulo, 2 Kor. 12:7-10 b. Trofimo, 2 Tim. 4:20

6. dhambi na magonjwa yalihusianishwa kwenye fikra za walimu wa dini ya Kiyahudi (kama vile Yohana. 9:2; Yakobo 5:13-18).

7. Uponyaji sio ahadi ya Agano Jipya. Sio sehemu ya upatanisho wa Mungu ulioelezewa katika Isa. 53:4-5 na Zab. 103:3, ambapo uponyaji ni taswira kwa ajili ya msamaha (angalia Isa. 1:5-6, ambapo magonjwa ni stiari kwa ajili ya dhambi).

8. kuna fumbo la kweli kuhusu ni kwa nini baadhi wanapona na baadhi hawaponi. 9. yawezekana kuwa ingawa uponyaji upo katika kila kizazi, kulikuwepo na ongezeko lenye umuhimu

kipindi cha maisha ya Yesu; hili ongezeko litatokea tena kabla ya kurudi kwake. Mwandishi wa kisasa ambaye amenisaidia mimi kutambua kuwa tamaduni zangu za kimadhehebu zimeshusha utendaji wa Roho, hasa ile ya kimiujiza, iliyoandikwa na Gordon Fee. Ana vitabu mbalimbali, lakini viwili nivipendavyo ni vile vinavyoshughulika na eneo hili ni

1. Paul, the Spirit, and the People of God 2. God's Empowering Presence: The Holy Spirit and the Letters of Paul

Page 114: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

98

Kama yalivyo masuala mengi ya Kibiblia, kuna mawili makubwa. Lazima tutembee katika nuru tulio nayo katika upendo, lakini siku zote tukijifungua katika nuru zaidi toka kwenye Biblia na Roho wa Mungu.

5:15 "Yule mtu akaenda zake, akawapasha habari Wayahudi” Msukumo wake wakuijulisha mamlaka ya wayahudi haifahamiki.

1. Inaonekana kuwa ni tendo lisilo la fikra au jambo lisilokuwa na umuhimu ikimaanisha kuwa uponyaji siku zote uanze na imani au umalizie na imani

2. Yesu alimwambia afanye hivo (kama vile Mt. 8:4; Marko 1:44; Luka 5:14; 17:14) 5:16 "Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwudhi Yesu, kwa kuwa alitenda hayo siku ya sabato” kitenzi hiki kipo katika kauli tendaji elekezi isiyo timilifu kinachoonyesha kitendo kinachoendelea cha wakati uliopita. Kitendo hiki hakikuwa kitendo cha kwanza cha Yesu (wala cha mwisho) kufanya uponyaji siku ya sabato! 5:17 NASB "lakini akawajibu," NKJV, REB, NRSV, NIV "Lakini Yesu akawajibu" NJB "Jibu lake kwao lilikuwa" Waandishi walionakiri maandishi ya awali ya Wayunani walikuwa na uelekeo kwa

1. Kurahisisha sarufi 2. kufanya rejea halisi ya viwakilishi nomino 3. kurekebisha mafungu ya maneno

Ni ngumu kujua ni muundo gani wa Johana 5:17 ulikuwa halisi. 1. "lakini Yeye. . ." - P75, א, B, W 2. "lakini Yesu. . ." - P66, A, D, L 3. "lakini Bwana. . ." au "Bwana Yesu" – Tafsiri za Kisyria

Toleo la UBS4 inatoa nafasi #2 a "C" kiwango (ngumu katika kuamua). ◙ "Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi" Hizi zote zinzonyesha kauli ya kati (yenye kushuhudia) elekezi ya wakati uliopo. Yesu alikuwa anasema kuwa Baba haachi kufanya mazuri siku ya sabato Mwanae kadhalika (kwa mjadala mzuri wa msitari huu tazama Manfred Brauch, Abusing Scripture, uk. 219). Hii kwa uhalisia ulikuwa uthibitisho wa uelewa wa Yesu wa uhusiano wake wa kipee na baba yake (kama vile Yohana 5:19-29). Dhana ya Kiyahudi ya kuamini uwepo wa Mungu mmoja (kama vile Kumb. 6:4) kiutendaji ilioneshwa katika “namna moja" ya maelezo ya matukio katika ulimwengu huu (kama vile Amu. 9:23; Ayubu 2:10; Mhu. 7:14; Isa. 45:7; 59:16; Wimb. 3:33-38; Amos 3:6). Vitendo vyote vilikuwa hatimaye vya Mungu mmoja wa kweli. Yesu alipoonyesha uwakala aina mbili katika vitendo vyake ulimwengu alionyesha sababisho pande mbili la Kiungu.. Hili ndilo tatizo gumu la utatu. Mungu mmoja, lakini katika hali ya nafsi tatu (kama vile Mt. 3:16-17; 28:19; Yohana 14:26; Mdo. 2:33-34; Rum. 8:9-10; 1 Kor. 12:4-6; 2 Kor. 1:21-22; 13:14; Gal. 4:4; Efe. 1:3-14; 2:18; 4:4-6; Tito 3:4-6; 1 Pet. 1:2). Tazama MADA MAALUMU UTATU katika Yohana 14:26 5:18 "kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua" kuna sababu mbili za Wayahudi kutaka kumwua Yesu.

1. Alivunja wazi wazi (kifasihi. "alipoteza," kauli tendaji elekezi isiotimilifu, kama vile Mt. 5:19) mila zao (Talmud) kuhusu sabato

2. Maelezo yake yalionyesha kuwa walimwelewa kwa kudai kwake kuwa sawa na Mungu (kama vile Yohana 8:58-59; 10:33; 19:7).

Page 115: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

99

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 5:19-23 19 Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile. 20 Kwa kuwa Baba ampenda Mwana, naye humwonyesha yote ayatendayo mwenyewe; hata na kazi kubwa zaidi kuliko hizo atamwonyesha, ili ninyi mpate kustaajabu. 21 Maana kama Baba awafufuavyo wafu na kuwahuisha, vivyo hivyo na Mwana awahuisha wale awatakao. 22 Tena Baba hamhukumu mtu ye yote, bali amempa Mwana hukumu yote; 23 ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana hamheshimu Baba aliyempeleka.

5:19,24,25 "Amin, amin" kwa kawaida hii inamaanisha "Amina, amina." Neno "amina" ni tafsiri za kiebrania. Kiasili lilimaanisha hali ya kuaminiwa. Lilikuja kutumika ili kuthibitisha neno la ukweli. Yesu ndiye wa pekee aliyejua kutumia neno hili katika mwanzo wa maelezo yake. Alilitumia kuimarisha maneno yake yaliyokuwa muhimu. Yohana ni wa pekee aliye andika neno hili lililosemwa mara mbili. Tazama MADA MAALUMU: AMINA. 5:19 "Mwana" Kuna umuhimu wa kithiolojia wa kurudia rudia kwa neno hili "Mwana" katika baadhi ya mistari ifuatayo. Imetumika mara nane katika mazingira hayo kwa ufupi. Inaonyesha uelewa wa kipekee wa Yesu kuhusu uhusiano wake na Baba na kuaksi nyadhifa za "Mwana wa Adam" na "Mwana wa Mungu." ◙ "Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe" Kama ambavyo daima ni kweli, Agano Jipya linamwasilisha Yesu katika maelezo yenye mafumbo. Katika baadhi ya maandiko anaonekana

1. Yeye ni wamoja na Babaye (kama vile Yohana 1:1; 5:18; 10:30,34-38; 14:9-10; 20:28) 2. Yeye ni tofauti na Baba yake (kama vile Yohana 1:2,14,18; 5:19-23; 8:28; 10:25,29; 14:10,11,12,13,16;

17:12) 3. Yeye ni mtiifu mno kwa Baba yake (kama vile Yohana 5:20,30; 8:28; 12:49; 14:28; 15:10,19-24; 17:8)

Hii bila shaka ni kuonyesha kuwa Yesu ni Mungu kamili, lakini wa tofauti, na mwenye udhihirisho wa ndani wa utatu. Katika maoni yaliyo boreshwa na John Raymond E. Brown, Toleo la Jerome Biblical Commentary, hoja muhimu inajitokeza: "Uhusishaji mdogo hapa usiondolewe kwa kuyachukulia maneno ya Yesu kufanya marejeo ya asili yake ya kibinadamu…Itapoteza pia hoja nzuri ya Yohana kumhusu Kristo. Badala yake, Yesu anasisitiza juu ya uelewano wa kishughuli kati ya Baba yake na Mwana, ambao bila shaka unahitaji utambulisho wa asili; utaratibu kama huo unaonekana katika Yohana 16:12 na kuendelea kuoanisha Roho mtakatifu na mwana. Lakini katika injili nzima hatuoni utatu ukichukuliwa kama thiolojia ya kufikirika kinadharia; siku zote inatazamwa kama msingi asili wa mantiki yake juu ya mafundisho ya wokovu" (uk. 434). ◙ "lile ambalo amwona Baba analitenda" Mwanadamu hajapata kumwona Mungu (kama vile Yohana 5:37 na 1:18), lakini Mwana anadai kumfahamu binafsi kumhusu Yeye (kama vile Yohana 1:1-3). ◙ "kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile" Katika matendo na mafundisho ya Yesu, mwanadamu kwa wazi kabisa anaomwona Mungu asiyeonekana (kama vile Kol. 1:15; Ebr. 1:3). 5:20 "Baba ampenda Mwana, naye humwonyesha yote ayatendayo mwenyewe" Kauli zote hizi zinaonyesha kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo ambazo zinaongelea kitendo kinachoendelea. Hili ni neno la Kiyunani kwa maana ya upendo, phileō. Mtu angalitegemea kuliona neno agapeō kama lilivyo katika Yohana 3:35. Maneno hayo yote mawili yana elimu-maana pana iliyoingiliana katika lugha ya kawaida ya Kiyunani (tazama D. A. Carson, Exegetical Fallacies, 2nd ed., uk. 32-33 na F. F. Bruce, Answers to Questions, uk. 73). ◙ "kazi kubwa" katika muktadha huu hii inarejea kufufua wafu (Yohana 5:21,25-26) na kutekeleza hukumu (Yohana 5:22,27). ◙ "ili ninyi mpate kustaajabu" kifungu nia hiki wazi wazi kinaonyesha wazi kwamba kusudi la miujiza yake ni kuwa wale wayahudi (WINGI nyinyi) waamini katika Mwana wa pekee (kama vile Yohana 5:23; Mdo. 13:41 [Hab. 1:5]).

Page 116: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

100

5:21 "kama Baba awafufuavyo wafu…, vivyo hivyo na Mwana" Katika Agano la Kale YHWH ndiye pekee awezaye kutoa uzima (kama vile Kumb. 32:39). Ukweli kwamba kwamba Yesu anaweza kufufua wafu ni sawa na usemi ya kuwa wako sawa na YHWH (kama vile Yohana 5:26). Yesu anatoa uzima wa milele sasa (kama vile 2 Kor. 5:17; Kol. 1:13) ambalo linahusianishawa na udhihilisho wa maisha ya kimwili katika enzi mpya kwenye Yohana 5:26 (kama vile 1 The. 4:13-18). Inaonekana kwamba makabiliano yaliyoendelea kati ya Yohana na Yesu lilikuwa ni suala la mtu binafsi, wakati bado kumebakia kuwepo na tukio la pamoja la wakati ujao (vyote hukumu na wokovu). ◙ "vivyo hivyo na Mwana awahuisha wale awatakao" Je ni kwa mtu yupi Mwana anachagua kumpa maisha? Katika muktadha huu sio uhakiki wa andiko kwa muundo wa kithiolojia wa Wa-protestanti wa utoaji haki kwa njia ya imani pekee, bali ni kudhihilisha kuwa imani katika Yesu inaleta uzima (kama vile Yohana 1:12; 3:16). Mvutano unakuja katika Yohana 6:44,65. Je Roho anachagua "wote" au "baadhi"? nadhani ni wazi kwamba wanadamu walioanguka hawaanzii katika ulimwengu wa kiroho, lakini nimesimama kibiblia kwenye ukweli wa kwamba wapaswa kumkubali (na waendelee kukubali) Yule Roho anayeugua kwa ajili yao kwa toba, imani, utii, na ustahimilivu! Ajabu hapa ni kuwa ni kwanini baadhi wanaosikia injili wanasema "Hapana"! Naita hali hii "ajabu ya kutoamini." Katika uhalisia ni “dhambi isiyosameheka” ya Injili na "Dhambi kuelekea Mauti" ya 1 Yohana. Tazama Mada Maalumu katika 1 Yohana 5:16

MADA MAALUMU: Taratibu za kiufafanuzi kwa kufasiri “Dhambi isiyosameheka”

A. Kumbuka kuwa injili inaaksi muundo wa Kiyunani 1. Dhambi za aina mbili (angalia Mada Maalumu:Dhambi isio ya makusudi [Agano la Kale] kama vile

Mambo ya WaLawi 4:2,22,27; 5:15,17-19; Hes. 15:27-31; Kumb. 1:43; 17:12-13) a. Isio ya makusudi b. Ya makusudi

2. Muundo wa Kiyunani wa Kipentekoste kabla (yaani., utimilizaji wa injili[yaani., kifo, ufufuko, kupaa] na zawadi maalumu ya Roho bado haijatokea)

B. Kumbuka mazingira ya fasihi ya Marko 3:22-30 1. Familia ya Yesu mwenyewe kutokumwamini (kama vile Marko 3:31-32) 2. Kutokuamini kwa Mafarisayo (kama vile Marko 2:24; 3:1,6,22)

C. Linganisha mfanano wa injili, mahali ambapo wadhifa wa neno “Mwana wa Adamu” lilipobadilika na kuwa “Wana wa Adamu” 1. Mt. 12:22-37 (yaani 12:32, "Neno dhidi ya Mwana wa Adamu") 1. Luka 11:14-26; 12:8-12 (yaani 12:10, "Neno dhidi ya Mwana wa Adamu") 2. Marko 3:28 (yaani "dhambi zote zitasamehewa kwa Wana wa Adamu"

Dhambi isiosameheka ni mwendelezo wa kumkata yesu wazi wazi kabisa. Mafarisayo wazi kabisa walitambua lakini wakakataa kuamini. Kwa maana hii basi inahusiana na “dhambi mpaka mauti” katika 1 Yohana (angalia Mada Maalumu: Dhambi mpaka Mauti)

5:22 Ukanushi mara mbili wenye nguvu na njeo ya kitenzi timilifu inasisitiza ya kuwa hukumu imekwisha kabidhiwa Mwana (kama mbili Yohana 5:27; 9:39. Matendo 10:42; 17:31; 2 Tim. 4:1; 1 Pet. 4:5). Utata uliopo kati ya msitari huu na Yohana 13:17 unaelezwa kwa ukweli kuwa Yesu, katika “siku hizi za mwisho,” haukumu mtu bali wanadamu wanajihukumu wenyewe kwa jinsi wanavyoenenda na Yesu Kristo. Hukumu ya Yesu kwenye kiama (Kwa wale wasioamini) inategemeana na kumkubali au kumkataa Yesu. Utoaji wa uzima wa milele dhidi ya hukumu ilikuwa ni dhima ya Yohana 3:17-21, 36. Upendo wa Mungu kwa Kristo, anapokataliwa inakuwa laana ya Mungu! Kuna njia mbili tu za kufanya uchaguzi! Na ile moja ya pekee ni kupokea uzima wa milele kwa imani kupitia Yesu Kristo (kama vile Yohana 10:1-18; 14:6; 1 Yohana 5:9-12)!

Page 117: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

101

5:23 "ili watu wote wamheshimu Mwana" Ujumuishwaji wa neno "wote" linaweza kumaanisha mazingira ya hukumu siku ya kiama (kama vile Flp. 2:9-11). ◙ "Asiyemheshimu Mwana hamheshimu Baba aliyempeleka" Usemi huu ni sawa kabisa na 1 Yohana 5:12. Hakuna awezaye kumjua Mungu kama hawezi kumjua Mwana wake, na vivyo hivyo, hakuna anayeweza kumtii na kumtukuza Baba kama hawezi kumtii na kumtukuza Mwana!

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 5:24-29 24 Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.25 Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai. 26 Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake. 27 Naye akampa amri ya kufanya hukumu kwa sababu ni Mwana wa Adamu. 28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. 29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.

5:24 "Amin, amin," Usemi huu wa kipekee mara mbili (kama vile Yohana 5:25) wa maneno ya Yesu ni namna ya kuleta utangulizi kwenye maelezo yake muhimu. Tazama Mada Maalumu: Amina katika Yohana 1:51 ◙ "Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele" Semi hizi tatu ni kauli tendaji zenye vitenzi tendaji vya wakati uliopo. Huu ni msisitizo juu ya kuamini (tazama Mada Maalumu katika Yohana 2:23 katika Baba kunakofanywa kwa kumwamini Mwana (kama vile 1 Yohana 5:9-12). Katika muhtasari wa injili, maisha ya milele daima ni tukio la mbele linalotumainiwa katika imani, lakini katika Yohana ni jambo la kweli lililopo sasa (yaani, Yohana 8:51; 11:25). Inawezekana neno "kusikia" linaakisi neno la Kiebrania shema, lililomaanisha "kusikia ili kutii" (kama vile Kumb. 6:4). ◙ "Yeye aliyenipeleka" Kitenzi apostellō (kauli tendaji endelevu ya wakati uliopita usiotimilifu) ndiyo asili ya muundo wa neno "Mtume” (kama vile Yohana 5:36). Lilitumika na viongozi wa dini kama "aliyetumwa kama mwakilishi rasmi kwa ujumbe aliopewa." Neno hili daima linatumiwa katika Yohana kwa kumaanisha Baba alimtuma mwanaye kumwakilisha. Tazama Yohana 4:34.

MADA MAALUMU: KUPELEKWA (Apostellō) Hili ni neno la kiyunanila kawaida kwa “upelekwa” (yaani apostellō). Neno hili lina matumizi kadha ya kithiolojia:

1. Katika kiyunani cha sasa na kwa Wayahudi waliokuwa na elimu na viongozi wa dini, neno hili hutumiwa kama moja inayoitwa na kutumwa kama mwakilishi rasmi wa mwingine, kitu kama kiingereza chetu “Balozi.” (kama vile 2 Kor. 5:20).

2. Injili daima zinatumia kitenzi hiki kwa Yesu kutumwa na baba yake, katika Yohana, linasikika zaidi kama Masihi (kama vile Mt. 10:40; 15:24; Marko 9:37; Luka 9:48 na hasa Yohana 5:36, 38; 6:29, 57; 7:26; 8:42; 10:36; 11:42; 17:3, 8, 18, 21,23 25; 20:21 (Yote “apostellō” na KISAWE CHAKE pempō inayotumika katika mst. 21). Inatumika kwa Yesu kutuma waumini (kama vile Yn. 17:18; 20:2121 [Yote "apostellō na KISAWE CHAKE ni "pempō" katika Yohana 20:21]).

3. Agano Jipya lilituma jina “Mtume” kwa wanafunzi a. Mitume kumi na wawili wa mwanzo kama mzunguko wa kwanza kati ya wanafunzi wake.

(Marko 6:30; Luka 6;13; Matendo 1:2; 26) b. Kundi maalumu la msaada la Mitume na watumishi wenzie.

1) Barnabasi (kama vile. Matendo 14:4, 14) 2) Andronicus na Junias (KJV, Junia , kama vile. Rum. 16:7) 3) Appollo (kama vile. 1 Kor. 4:6-9)

Page 118: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

102

4) Yakobo ndugu wa Bwana (kama vile. Gal. 1:19) 5) Silvanus na Timotheo (kama vile. 1The. 2:6) 6) Bila shaka Tito (kama vile. 2 Kor. 8:23) 7) Bila shaka Epafrodito (kama vile. Efe. 2:25)

c. Zawadi inayoendelea katika kanisa (kama vile. 1 Kor. 12:28-29; Efe 4:11) 4. Paulo anatumia cheo hiki kwa ajili yake katika barua zake nyingi kama njia ya kuonesha mamlaka

yake aliyopewa na Mungu kama mwakilishi wa Kristo. (kama vile. Rum. 1:1 1 Kor. 1:1; Gal. 1:1; Efe. 1:1; Kol. 1:1; Tim. 1:1 2Tim. 1:1; Tito 1:1).

5. Tatizo tunalokumbana nalo kama waamini wa leo ni kwamba Agano Jipya halitafasiri hii zawadi inayoendelea inahusu nini au vipi inabainishwa kwa waamini. Bila shaka mtu apaswa kutofautisha kati kumi nambaili ya awali (# 3b) na matumizi ya baadaye (# 3b). Tazama Mada Maalumu: Msukumo na Mada Maalumu: Mwangaza. Kama mitume wa leo hawakusukumwa kuandika maandiko mengi matakatifu (yaani, kitabu cha Wayunani kanoni kimefungwa, kama vile. Yuda mst. 3; tazama. Mada Maalumu: kanuni ya kanisa) kisha kipi wanafanya tofauti na Manabii wa Agano Jipya na Wainjilisti (kama vile. Efe. 4:11) hapa kuna uwezekano wa mambo.

a. Waanzilishi wa kanisa la wamisionari huanza katika maeneo yasiyo ya uinjilisti (kutumika kama vile katika Doache)

b. Viongozi wa Wachungaji katika eneo Fulani au madhehebu. c. ?

Napenda # 1.

◙ "bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani" Hii ni kitendo tendaji timilifu elekezi ambacho kilitokea wakati wa nyuma na sasa kipo. Ufalme wa Mungu upo na utakuwepo, hivyo basi, hata uzima na milele (kama vile Yohana 5:25-26; 1 Yohana 3:14). Yohana 5:25 ni ya usemi wa nguvu wa uwepo wa ufalme Mungu wa sasa!

5:25 "Saa inakuja, na sasa ipo," Hii ni namna ya lugha inayoashiria uandishi wa Yohana. Maneno na mafungu siku zote yana maana mbili. Katika hili neno "saa" inamaanisha

1. saa ya wokovu 2. saa ya hukumu

Muda mwafaka ni yote mawili uliopo na ujao (kama vile Yohana 5:29; 6:39,44,54). Kile mtu afanyacho sasa akiwa na Yesu ndicho kitaamua kile kitakachomtokea mbeleni. Wokovu na hukumu vyote ni uhalisia wa sasa na utimilizaji wa wakati ujao (kama vile Yohana 5:28).

MADA MAALUM: SAA (hōra)

Neno "saa" limetumika kwa namna tofauti mbalimbali katika injili, kama 1. Rejea ya wakati (kama vile Mt. 8:13; 26:40; Luka 7:21; Yohana 11:9) 2. Stiari kwa ajili ya wakati wa kujaribiwa na majaribu (kama vile Mt. 10:19; Marko 13:11; Luka 12:12) 3. Stiari kwa ajili ya Yesu kuanza huduma Yake (kama vile Yohana 2:4; 4:23) 4. Stiari kwa ajili ya siku ya hukumu (yaani., ujio wa mara ya pili, kama vile Mt. 24:36,44; 25:13; Marko

13:32; Yohana 5:25,28) 5. Stiari kwa ajili ya wiki ya mateso ya Yesu (kama vile Mt. 26:45; Marko 14:35,41; Yohana 7:30; 8:20;

12:23,27; 13:1; 16:32; 17:1)

◙ "wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu" Yohana 5:25 akizungumza waliokufa kiroho; Yohana 5:29 inazungumza kuhusu ufufuo wa wote waliokufa kimwili. Biblia inazungumzia aina tatu za mauti.

1. Mauti ya kiroho (kama vile Mwanzo 3) 2. Mauti ya kimwili (kama vile Mwanzo 5) 3. Mauti ya milele (kama vile Efe. 2:2; Ufu. 2:11; 20:6,14) au ziwa la moto, kuzimu (Gehenna).

Page 119: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

103

Haya ni matumizi nadra ya kifungu "Mwana wa Mungu." Tazama Mada Maalumu katika 1 Yohana 3:8. Moja ya sababu ya hiki kifungu kutotumika mara nyingi ni kwa sababu ya mitizamo ya kidini ya Kiyunani kuhusu miungu (Mlima Olympus) walichukua wake za watu kama wake zao au wake wa Wafalme. Hadhi ya Yesu kama Mwana wa Mungu haangazii kizazi cha kujamiiana au mfuatano wa muda, bali uhusiano wa karibu. Ni stiari ya kawaida ya Kiyunani. Yesu alikuwa anathibitisha Uungu wake kwa viongozi wa kiyahudi kwa njia iliyo wazi kabisa na mahususi kwa kutumia aina mbalimbali za vitabu vya Agano la Kale (kama vile Yohana 5:21,26). 5:26 "Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake" Hii kimsingi inamaanisha neno YHWH kutoka katika kitabu cha kutoka 3:14. Aina hii ya jina la patano kwa Mungu linatokana na kitenzi cha Kiebrania "kuwa" likimaanisha aliyewahi kuishi kabla na ambaye aishiye pekee Tazama Mada Maalumu katika Yohana 6:20 Katika Agano la Kale YHWH pekee haikuwa na "uzima" (kama vile 1 Tim. 1:17; 6:16) na ndiye pekee aliye weza kuwapa wengine uzima (yaani, Ayubu 10:12; 33:4; Zab. 36:9). Yesu anadai kuwa YHWH anampa Yesu nguvu /mamlaka hiyo hiyo ya kipekee! ◙ "vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake" Ni uthibitisho wa nguvu wa Uunguwa Yesu (kama vile Yohana 1:4; 1 Yohana 5:11). 5:27 Sababu ya kwamba Yesu pia ana uwezo (exousia, ana mamlaka, kama vile Yohana 10:18; 17:2; 19:11) kuhukumu kwa haki kwa sababu yeye ni Mungu kamili lakini pia ni mtu kamili. Hakuna maelezo maalumu kuhusu fungu hili "Mwana wa Adam" (kama vile Ezek. 2:1 na Zab. 8:4). Anatujua zaidi (kama vile Ebr. 4:15); Anamjua Mungu vyema (kama vile Yohana 1:18; 5:30). Inashangaza kuwa katika mazingira ambayo Yesu anajiita "Mwana" (kama vile Yohana 5:19 [mara mbili],20,21,22,23 [mara mbili], 25,26) kwamba katika Yohana 5:27 kichwa cha habari "mwana wa Adamu" (lakini bila makala maalumu) inatumika. Hata hivyo njia hii moja imo katika (1) Yohana 3:13,14 dhidi ya Yohana 3:16,17,18,35,36; (2) Yohana 6:27,53 dhidi ya Yohana 6:40; na (3) Yohana 8:28 dhidi ya Yohana 8:35,36. Yesu alitumia vichwa vyote kwa ajili yake kwa kubadilisha badilisha. 5:28 "Msistaajabie maneno hayo" Ni kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopo ikiwa na kiambata hasi ambayo inamaanisha kuzuia kitendo kilichoko kwenye mchakato. Kama inavyoshangaza maneno ya Yesu ya huko nyuma kwa viongozi hawa wa Kiyahudi yalivyokuwa, maneno yake yatakoyofuata pia yatawashangaza. ◙ "ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti Yake" Hii inaonekana kurudisha kelele za Masihi katika Ujio wa Pili (kama vile 1 The. 4:16). Lazaro (kama vile Yohana 11:43) ni kielelezo madhubuti cha tukio hili. Hii haipingi ukweli wa 2 Kor. 5:6,8. Inadhihilisha hukumu ya ulimwengu na mamlaka ya Mwana. Habari nyingi katika hili zinahusisha uhalisia wa maisha ya kiroho hapa tulipo na wakati wa sasa (kiama kilichokwisha tambuliwa). Lakini fungu hili pia linaonyesha tukio la mwisho la wakati ujao wa kiama. Mvutano huu kati ya ufalme wa Mungu ulio tiyari na ambao bado unatoa picha ya mafundisho ya Yesu katika vidokezo vya injili, lakini zaidi katika Yohana. 5:29 Biblia inazungumzia juu ya ufufuo kwa wote waovu na wenye haki (kama vile Dan. 12:2; Mt. 25:46; Matendo 24:15). Aya nyingi zinasisitiza ufufuo wa wenye haki tu (kama vile Ayubu 19:23-29; Isa. 26:19; Yoh. 6:39-40,44, 54; 11:24-25; 1 Kor. 15:50-58). Hii haimaanishi kurejea hukumu inayotokana na kazi tuzitendazo, bali hukumu kutokana na mtindo wa maisha wa waamini (kama vile Mt. 25:31-46; Gal. 5:16-21). Kuna kanuni ya jumla ya neno la Mungu na ulimwengu, wanadamu huvuna kile walichopanda (kama vile Mith. 11:24-25; Gal. 6:6). Au kuweka nukuu katika Agano la Kale, "Mungu atawahukumu wanadamu kufuatana na matendo yao" (kama vile Zab. 62:12; 28:4; Ayubu 34:11; Mith. 24:12; Mt. 16:27; Rum. 2:6-8; 1 Kor. 3:8; 2 Kor. 5:10; Efe. 6:8 na Kol. 3:25).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 5:30 30 Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka.

Page 120: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

104

5:30 Yesu, nembo ya Mungu ya mwili wa kibinadamu aliwajibika na kunyenyekea kwa Baba. Msisitizo huu wa nguvu juu ya kujitoa pia unajitokeza katika Yohana 5:19 ("Mwana hawezi kufanya kitu"). Hii haimaanishi kuwa mwana alikuwa hana uwezo, bali utatu ulimpa wajibu wa ukombozi miongoni mwa nafsi tatu Baba, Mwana, na Roho.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 5:31-47 31 Mimi nikijishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu si kweli. 32 Yuko mwingine anayenishuhudia; nami najua ya kuwa ushuhuda wake anaonishuhudia ni kweli. 33 Ninyi mlituma watu kwa Yohana, naye akaishuhudia kweli. 34 Lakini mimi siupokei ushuhuda kwa wanadamu; walakini ninasema haya ili ninyi mpate kuokoka. 35 Yeye alikuwa taa iwakayo na kung'aa, nanyi mlipenda kuishangilia nuru yake kwa muda. 36 Lakini ushuhuda nilio nao mimi ni mkubwa kuliko ule wa Yohana; kwa kuwa zile kazi alizonipa Baba ili nizimalize, kazi hizo zenyewe ninazozitenda, zanishuhudia ya kwamba Baba amenituma. 37 Naye Baba aliyenipeleka amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wo wote, wala sura yake hamkuiona. 38 Wala neno lake hamnalo likikaa ndani yenu, kwa kuwa ninyi hammwamini yule aliyetumwa na yeye. 39 Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia. 40 Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima. 41 Mimi siupokei utukufu kwa wanadamu. 42 Walakini nimewajua ninyi ya kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu. 43 Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo. 44 Mwawezaje kuamini ninyi mnaopokeana utukufu ninyi kwa ninyi, na utukufu ule utokao kwa Mungu aliye wa pekee hamwutafuti? 45 Msidhani kwamba mimi nitawashitaki kwa Baba; yuko anayewashitaki, ndiye Musa, mnayemtumaini ninyi. 46 Kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu. 47 Lakini msipoyaamini maandiko yake, mtayaamini wapi maneno yangu?

5:31 Katika Agano la Kale palikuwepo na haja ya kuwa na washuhudiaji wawili ili kukamilisha suala (kama vile Hes. 35:30; Kumb. 19:15). Katika mazingira haya Yesu anatoa shuhuda tano kwake binafsi. 1. Kwa Baba (Yohana 5:32,37) 2. Yohana mbatizaji (Yohana 5:33, kama vile Yohana 1:19-51) 3. kazi binafsi za Yesu (kama vile Yohana 5:36) 4. mafundisho (kama vile Yohana 5:39) 5. Musa (kama vile Yohana 5:46) ambayo inaakisi Kumb. 18:15-22

Tazama Mada Maalum katika Yohana 1:8 ◙ "Kama" Hii ni sentesi shurutishi daraja la kwanza ambayo inazungumzia juu ya tendo muhimu. ◙ "ushuhuda wangu si kweli" Hii inaonekana kupingana na Yohana 8:14. Mazingira yanaonyesha kuwa maneno haya yamesemwa katika mtindo tofauti. Hapa Yesu anaonyesha kuwepo na mashuhuda wengine, lakini katika Yohana 8:14 anaonyesha kuwa ushahidi wake ndio wa muhimu tu! Kwa neno "kweli" tazama Mada Maalumu: Kweli katika Yohana 6:55 5:32 "Yuko mwingine anayenishuhudia" Hii inarejea juu ya Mungu Baba (kama vile 1 Yohana 5:9) kwa sababu ya matumizi ya neno allos, ambalo linamaanisha "mwingine ya aina ile" kwa kujitofautisha na heteros, linalomaanisha “mwingine wa aina tofauti" ingawa utofauti huu uliendelea kufifia katika lugha ya kawaida ya Kiyunani. Tazama MADA MAALUM: MASHUHUDA WA YESU katika Yohana 1:8 5:33 "Ninyi mlituma watu kwa Yohana" Hii inamrejea Yohana mbatizaji (kama vile Yohana 1:19). 5:34 "walakini ninasema haya ili ninyi mpate kuokoka" Hii ni kauli tendewa tegemezi ya wakati uliopita isiotimilifu. Irabu tendewa inadokeza uwakala wa Mungu au wa Roho (kama vile Yohana 6:44,65). Kumbuka Injili

Page 121: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

105

ni matangazo ya kiinjili (yaani, vijitabu vya neno la Mungu), sio wasifu wa kihistoria. Kuna kusudio la kiinjili katika yote yaliyowekwa kwenye kumbukumbu (kama vile Yohana 20:30-31). 5:35 "Yeye alikuwa taa" Huu ni msisitizo mwingine juu ya nuru, hapa kuna ujumbe wa maandalio (kama Yohana 1:6-8). 5:36 "kwa kuwa zile kazi alizonipa Baba ili nizimalize" Matendo ya Yesu yalikuwa utimilifu wa unabii wa Agano la Kale kuhusu Masihi. Wayahudi wale wa siku zake wangalitambua ishara hizi za miujiza za kuponya vipofu, kulisha maskini, kuwafanya viwete watembee (kama vile Isa. 29:18; 32:3-4; 35:5-6; 42:7). Nguvu ya mafundisho ya Yesu, haki ya mtindo wa maisha, msaada kwa wenye shida, na miujiza mikubwa (kama vile Yohana 2:23; 10:25,38; 14:11; 15:24) inaruhusu ushuhuda wa wazi kwamba yeye alikuwa nani, anatoka wapi, na alitumwa na nani. 5:37 “Baba aliyenipeleka amenishuhudia” Neno “Yeye” linamaanisha Baba. Katika mazingira haya kifungu hiki kinaonekana kurejerea maandiko ya Agano la Kale. (kama vile Ebr. 1:1-3) hii ingalihusu rejea zote za masihi katika Agano la Kale (kama vile Yohana 5:39). ◙ “Sauti yake hamkuisikia wakati wowote, wala sura yake hamkuiona” Yesu alikuwa akidhihilisha kuwa ingawa Wayahudi wangelimfahamu Mungu kupitia katika mafundisho na uzoefu binafsi katika kuabudu, kiukweli hawakujua Mungu hata kidogo (kama vile Yohana 8:43 Isa 1:1-15; 6:9-10; 29:13; Yer. 5:21). Katika Agano la Kale, kumwona Mungu ilifikiliwa kuwa kunaleta mauti. Mtu pekee aliyezungumzwa na YHWH uso kwa uso alikuwa Musa na hata hivyo, walikutana katika mawingu yaliyotanda. Wengi wamekuwa wakiwaza kuwa andiko la Kut. 33:23 linapingana na Yohana 1:18. Hata hivyo, maneno ya Kiebrania katika Kutoka yanamaanisha “baada ya utukufu,” sio katika umbo. 5:38 “neno lake hamnalo likikaa ndani yenu” Haya ni maneno mawili mbadala katika maandiko ya Yohana. Neno la Mungu (logos) lazima lipokelewe, mara likisha pokelewa (kama vile Yohana 1:12) lazima libakie (kudumu kama vile Yohana 8:31; 15:4; 5: 6; 7:10 1 Yohana 2:6, 10, 14, 17, 24, 27, 28; 3:6, 14, 15, 24). Yesu ni ufunuo kamili wa Mungu. (kama vile Yohana 1:1-18; Flp. 2:6-11; Kol. 1:15-17; Ebr. 1:1-3). Wokovu unathibitishwa kwa uhusiano unaoendelea (maana ya Kiebrania ya neno “kutambua” kama vile Mwanzo 4:1 Yer. 1:5) na uthibitishaji wa kweli ya injili (maana ya Kiyunani ya neno “kutambua” kama vile 2 Yohana 9). Neno hili “kudumu” linatumika katika maana ya uhusiano wa karibu unaodumu. Kudumu ni ile hali ya wokovu wa kweli (kama vile Yohana 15). Linatumika kwa maana tofauti mbali mbali katika Yohana.

1. Mwana katika Baba (kama vile Yohana 10:38; 14:10, 11, 20, 21; 17:21) 2. Baba katika Mwana (kama vile Yohana 10:38; 14:10, 11, 21; 17:21, 23) 3. Waamini katika Mwana (kama vile Yohana 14:20, 21; 15:5; 17:21) 4. Waamini katika Mwana na Baba (kama vile Yohana 14:23) 5. Waamini katika neno (kama vile Yohana 5: 38; 8:31; 15:7; 1 Yohana 2:14).

Tazama Mada Maalumu katika 1 Yohana 2:10. 5:39 “Mwayachunguza maandiko” Hii yaweza kuwa ni kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo au ni kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopo. kwa kuwa imo kwenye orodha ya shuhuda kuwa wayahudi wameikataa, hii bila shaka ni hali ya kuelekeza. Hapa pana sikitiko la viongozi wa Kiyahudi. Walikuwa na maandiko matakatifu, Waliyasoma, wakayachunguza, wakayatafakari, lakini bado yalikosa kuonyesha ni nani yalimlenga. Bila Roho, hata mafundisho haya hayana maana! Maisha ya kweli yanakuja tu kupitia kwenye mahusiano binafsi na utii katika imani (yaani., Kumb. 4:1; 8:13; 30:15-20; 32:46-47). ◙ “hayo ndiyo yanayonishuhudia” Hii inarejea maandiko matakatifu ya Agano la Kale, ambayo Yesu anatekeleza (yaani, Yohana 1:45; 2:22; 5:46; 12:16; 41; 19:28; 20:9). Mojawapo ya mahubiri ya mwanzo ya Petro (kama vile Matendo 3:18; 10:43) na Paulo (kama vile Matendo 13:27; 17:2-3; 26:22-23, 27) katika Matendo unabii ulitumika kama ushahidi wa umasihi wa Yesu. Aya zote isipokuwa moja tu (1 Pet. 3:15-16) ambayo yanathibitisha mamlaka

Page 122: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

106

ya maandiko yanayopatikana katika Agano Jipya (kama vile 1 Kor. 2:9-13; The. 2:13; 2 Tim. 3:16; 1 Pet 1:23-25; 2 Pet. 1:20-21), rejea katika Agano la Kale. Yesu wazi wazi alijiona kama utimilifu na lengo (na tafsiri sahihi kama vile Mathayo 5:17-48) la Agano la Kale.

MADA MAALUMU: MAFUNDISHO YA KANISA LA KWANZA

Kuna maoni mengi kuhusu Ukristo. Siku zetu hizi ni siku za wingi wa dini, kama ilivyokuwa karne ya kwanza. Binafsi, kwa pamoja nayajuisha na kuyakubali makundi yote yale yanayodai kumfahamu na kumwamini Yesu Kristo. Wote hatukubaliani kuhusu hili au lile lakini kimsingi ukristo ni kumhusu Yesu. hata hivyo, kuna makundi yanayodai kuwa wapo wakristo ambao wanaonekana “kufanana.” Ni kwa vipi naweza kuelezea tofauti ? Sawa, kuna njia mbili:

A. Kitabu kinachoweza kusaidia kujua kile makundi ya madhehebu ya kisasa yanaamini (kutoka katika maandiko yao) The Kingdom of the Cults na Walter Martin.

B. Hotuba ya makanisa ya awali, hasa wale kupitia Mtume Petro na Paulo katika kitabu cha Matendo, wanatupatia maelezo ya msingi kwa vipi waandishi wa karne ya kwanza waliovuviwa waliuelezea Ukristo kwenye makundi. “matamko” haya ya awali au “mafundisho” (ambacho kitabu cha matendo ni mhutasari wake) yanaendana na neno la Kiyunani Kerygma. Ufuatao ni ukweli halisi wa injili kuhusu Yesu katika Matendo ya Mitume: 1. Kutimiliza nabii nyingi za Agano la Kale- – Mdo. 2:17-21,30-31,34; 3:18-19,24; 10:43; 13:17-23,27;

33:33-37,40-41; 26: 6-7,22-23 2. Alitumwa na YHWH kama alivyoahidi- Mdo. 2:23; 3:26 3. Miujiza iliyotendeka kuthibitisha ujumbe wake na kudhihilisha huruma ya Mungu- – Mdo. 2:22;

3:16; 10:38 4. Waliofunguliwa, wasiomilikiwa- Mdo. 3:13-14; 4:11 5. Kusurubishwa – Mdo. 2:23; 3:14-15; 4:10; 10:39; 13:28; 26:23 6. Alifufuliwa kuja uzimani- Mdo. 2:24,31-32; 3:15,26; 4:10; 10:40; 13:30; 17:31; 26;23 7. Ameinuliwa mkono wa kulia wa Mungu Baba- Mdo. 2:33-36; 3:13,21 8. Atakuja tena mara ya pili – Mdo. 3:20-21 9. Alichaguliwa kuwa hakimu- Mdo. 10:42; 17:31 10. Akamtuma Roho Mtakatifu- Mdo. 2:17-18,33,38-39; 10:44-47 11. Mwokozi wa kila aaminiye- Mdo. 13:38-39 12. Hakuna mwingine aliye mwokozi- Mdo. 4:12; 10:34-36

Hapa kuna baadhi ya njia za kukubali kwenye hizi nguzo za ukweli: 1. Tubu – Mdo. 2:38; 3:19; 17:30; 26:20 2. Amini – Mdo. 2:21; 10:43; 13:38-39 3. Ubatizwe – Mdo.2:38; 10:47-48 4. Mpokee Roho – Mdo. 2:38; 10:47 5. Yote yatakujilia- Mdo.2:39; 3:25; 26:23

Mpango huu ulitumika kama tamko la kanisa la mwanzo, ingawa waandishi tofauti wa Agano Jipya wanaweza kuacha sehemu au wakasisitiza wengine hasa katika maandiko yao. Injili yote ya Marko kwa karibu inafuata dhana ya mafundisho. Marko kiutamaduni anaonekana kama kuitengeneza hotuba ya Petro, iliyohubiriwa huko Roma, katika injili iliyoko kwenye maandishi. Injili zote za Mathayo na Luka zinafuata muundo wa Marko.

5:41-44 Mistari hii inaonekana kurejea ukweli kuwa viongozi wa kidini wa Kiyahudi walifurahia na kupongezwa na wenzao. Walisifiwa kwa kuwanukuu viongozi wa dini ya Kiyahudi toka huko nyuma, lakini kutokana na upofu wa kiroho walikosa mkuu wa walimu wote, ambaye alikuwa katikati yao. Hii ni mojawapo ya shutuma za nguvu za Yesu kwa walimu wa sheria ya dini ya Kiyahudi katika karne ya kwanza (pia Taz.. hotuba ya Yesu katika Mt. 21:33-46; Marko 12;1-12; Luka 20:9-19).

5:41

Page 123: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

107

NASB, NRSV “Mimi sipati utukufu kutoka kwa watu” NKJV “Mimi siupokei utukufu kwa wanadamu” TEV “mimi sitafuti sifa za wanadamu” NJB “utukufu wa mwanadamu, hauna maana na mimi” Neno “utukufu,” doxa, ni ngumu kulitafsiri kwa mwendelezo ule ule (taz. Mada Maalumu katika Yohana 1:14). Ni neno lenye kumaanisha kwa Kiebrania “utukufu” yaani kadothi, ambalo lilitumika kama njia ya kuelezea uwangavu, na mng’ao wa Mungu (kama vile Kutoka 16:10; 24:17; 40:34 Matendo 7:2) kwa kumtukuza na kumtii Mungu kwa tabia na matendo yake. Mstari mzuri unaounganisha vidokezo hivi ni 2 Pet 1:17 Swala hili la mng’ao wa uwepo wa Mungu na tabia unahusishwa na

1. Malaika (Luka 2:9; 2 Pet. 2:10) 2. Ukuu wa Yesu (kama vile Yohana 1:14; 8:54; 12:28; 13:31; 17:1-5, 22, 24; 1 Kor. 2:8; Flp. 4:21) 3. Kitokanacho na Waamini (kama vile Rum. 8:18, 21; 1 Kor. 2:7; 15:43; 2 Kor. 4:17; Kol. 3:4; 1 The.

2:12 ; 2 The. 2:14; Ebr. 2:10 1 Pet. 5:1, 4) Inapendeza pia kuona kuwa Yohana anamaanisha kusulubiwa kwa Yesu kuwa ni kutukuzwa (kama vile Yohana 7:39; 12:16; 23, 13:31). Hata hivyo, pia inaweza kutafsiliwa kama “heshima” au “shukrani” (kama vile Luka 17:18; Mdo. 12:23; Rum. 4:20; 1 Kor. 10:31; 2 Kor. 4:15; Flp.1:11; 2:11; Ufu.11:13; 14:7; 16:9; 19:7). Hivyo ndivyo ilivyotumika katika mazingira haya. 5:43 “wala ninyi hamnipokei” Katika injili yote ya Yohana, mtazamo wa kuamini katika Yesu sio imani ya kithiolojia inayoelezwa, bali ni kukutana binafsi kwa mtu na Yesu (yaani, Yohana 5:39-40). Kuamini kunaanza na uamuzi wa kumwamini yeye. Hii inaanzisha kukua kwa mahusiano binafsi ya ufuasi unaoishia katika kupevuka kiimani na kuishi maisha ya Kikristo.

◙ “mwingine akija kwa jina lake mwenyewe” Hii ni sentensi shurutishi daraja la tatu.

◙ “mtampokea huyo” Hii na namna ya njia za kujifunza za viongozi wa dini katika kulinganisha na walimu wengine wa shule za sheria za Kiyahudi, Talmud. Michael Magill, New Testament Transline, ina nukuu nzuri “Viongozi wa Kiyahudi watampokea mwalimu wa kawaida au mwalimu wa dini ya Kiyahudi ambaye anadai kutumwa toka kwa Mungu. Kutokana na mwalimu wa kibinadamu, wako katika mahusiano ya kukubaliana na wenzao wakibadilishana utukufu kwa misingi ya usawa, kwa nabii aliyetumwa toka kwa Mungu wanapaswa kuonekana wa chini, wakisikia na kutii. Hiki kimekuwa ni chanzo cha sababu kwa nini manabii wa Mungu wamekuwa wakitawaliwa (ukr. 318) 5:44 Tazama nukuu katika Yohana 17:3.

5:45-47 Yesu anadhihilisha kuwa maandiko ya Musa yalimthibitisha Yeye. Hii bila shaka inarejewa katika Kumb.18:15;-22. Katika Yohana 5:45 mafundisho matakatifu yanasimama kama mshitaki wetu. Yalikusudiwa kuwa kuwa mwongozo wetu (kama vile Luka 16:31) mwongozo ukakataliwa, ukawa adui wetu (kama vile Gal. 3:8-14 23:29).

5:46,47 “kama…kama” Yohana 5:46 iko katika sentensi shurutishi daraja la pili iitwayo “kinyume cha ukweli” inaonyesha kuwa viongozi wa kiyahudi kwa kweli hawakumwamini yesu ipasavyo, hata katika maandiko ya musa ya kwamba yesu (kiama cha musa [yaani, manabii wa kumb. 18:15-19] atakuwa hakimu wao siku ya mwisho. neno “kama” kwenye yohana 5:47 linaelezea sentensi shurutishi daraja la kwanza ambayo inachukuliwa kama kweli (NIV ina neno “kwa vile”)

MASWALI YA MJADALA

Page 124: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

108

Huu ni mwongozo wa fasiri, ina maanisha kwamba unawajibika kwa tafsiri zako mwenyewe za Biblia. Kila mmoja wetu lazima atembee katika mwanga tulio nao. Wewe, Biblia, na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Hutakiwi uvitelekeze vitu hivi kwa mfasiri. Maswali ya mjadala huu yanatolewa kukusaidia kufikiri juu ya mambo makubwa ya sehemu za kitabu hiki. Yanalenga kukuamsha kimawazo na sio kutoa maana.

1. Kwa nini Yohana 5:4 iliondolewa katika fasili zetu za kisasa? 2. Kwa nini Yesu alimponya mtu huyu binafsi? 3. Kwa nini imani ilihusika katika uponyaji wa mtu huyu? Je uponyaji wa mwili unahusika na uponyaji

wa kiroho? 4. Ugonjwa wake ulihusishwa na dhambi yake binafsi? Je Magonjwa yote yanahusiana na dhambi ya

mtu? 5. Kwa nini Wayahudi walitaka kumwua Yesu? 6. Orodhesha kazi za Mungu katika Agano la Kale zilizotumika kwa Yesu. 7. Maisha ya milele ni ukweli uliopo au ni tumaini la wakati ujao? 8. Hukumu ya mwisho inategemea kazi au imani? Kwa nini?

Page 125: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

109

YOHANA 6

MIGAWANYO YA AYA YA TAFSIRI YA KISASA

UBS4 NKJV NRSV TEV NJB Ulishaji wa watu watu elfu tano watu elfu tano Yesu anawalisha watu miujiza ya mikate Elfu tano wanalishwa wanalishwa elfu tano 6:1-15 6:1-14 6:1-15 6:1-6 6:1-4 6:5:15

6:7 6:8-9

6:10-13 6:14-15

Kutembea juu ya maji Yesu anatembea juu Yesu anatembea juu Yesu anatembea juu Yesu anawajilia Ya bahari ya bahari ya maji anawajilia wanafunzi Wake akitembea juu Ya maji 6:16-21 6:15-21 6:16-21 6:16-21 6:16-21 Yesu mkate wa uzima Yesu mkate ushukao Yesu, mkate wa uzima Watu wanamtafuta Mafundisho katika toka mbinguni Yesu Sinagogi pale Kapernaumu 6:22-33 6:22-40 6:22-24 6:22-24 6:25-40 Yesu mkate wa uzima 6:25 6:28 6:28-40 6:29 6:30-31 6:32-33 6:34-40 6:34 Anakataliwa na 6:35-40 walio wake 6:41-51 6:41-59 6:41-51 6:41-42 6:41-51 6:52-59 6:52-59 6:52 6:52-58 6:53-58 6:59 6:59-62 Maneno ya uzima Wengi miongoni mwa Neno la uzima wa Milele wanafunzi wakarejea nyuma 6:60-65 6:60-71 6:60-65 6:60 6:63 6:61-65

6:64-66 Weredi wa Petro

katika imani 6:66-71 6:66-71 6:66-67

6:66-71 6:68-69 6:70-71

Page 126: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

110

MZUNGUKO WA TATU WA USOMAJI KUFUATILIA KUSUDIO LA ASILI LA MWANDISHI KATIKA NGAZI YA AYA Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwatafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Aya ya kwanza 2. Aya ya pili 3. Aya ya tatu 4. N.k

UTAMBUZI WA KI-MUKTADHA WA YOHANA 6:1-71

A. Injili ya Yohana haikuweka kumbukumbu juu ya maandalio ya meza ya Bwana, ingawa Yoh.13:17 inaweka kumbukumbu ya mazungumzo kati ya watu wawili, na maombi katika chumba cha juu. Ni kwa makusudi tu hili liliachwa. Kanisa la karne ya pili lilianza kuangalia sheria katika maana ya sakramenti. Waliziona kama ni njia za neema. Yohana anaweza kuwa anapinga mtazamo huu wa kisakramenti kwa kutoweka kumbukumbu ya ubatizo wa Yesu, au meza ya Bwana.

B. Yohana 6 imo katika mazingira ya kulisha watu elfu tano, hata hivyo wengi hutumia kufundisha mambo ya

sakramenti ya mwili wa Bwana (ekaristi). Huu ndio mwanzo wa imani ya wakatoloki ya Roma ya kushiriki meza ya Bwana, Yohana 6:53-56.

Swali juu ya kwa namna gani Yohana 6 anahusisha ekaristi takatifu, ikinaonyesha asili mbili ya injili. Bila shaka, injili inahusisha maneno ya Yesu na uzima, lakini yaliandikwa miongo kadhaa iliyopita na yalielezea imani katika jamii ya mwandishi mmoja. Kwa hiyo kuna viwango viwili vya kusudio la waandishi

1. Roho 2. Yesu na wasikilizaji wa mwanzo 3. Waandishi wa injili na wasomaji.

Ni namna gani mtu mmoja atafsiri? Nija pekee itakayothibitika lazima iwe inayozingatia mazingira, sarufi nna misamiati itokanayo na mpangilio wa kihistoria na sio vinginevyo.

C. Lazima tukumbuke kuwa wasikilizaji walikuwa Wayahudi na asili ya kihistoria ni kuwa viongozi wa kidini walimtarajia Masia kama aliye bora kuliko Musa (kama vile Yohana 6:30-31) hasa kwa kuzingatia uzoefu wa kutoka kama “mana” Viongozi wa kidini wanatuymia Zaburi 72:16 kama kielelezo/uthibitisho wa andiko. Maneno ya Yesu yasiyo ya kawaida (kama vile Yohana 6:60-62,66) yalikusudia kutafuta matarajio batili ya umati/makusanyiko ya watu kuhusu Masia. (kama vile Yohana 6:14:15)

D. Baba/uzao wa kanisa la kwanza hawakukubali kuwa habari hii ilimaanisha mlo/chakula cha usiku cha BwanaClement wa Iskandria, Origen, na Eusebius hawataji chakula cha Bwana katika mjadala wao katika habari hii.

E. Sitiari katika habari hii ziko sawa kabisa na maneno yaYesu yaliyotumika kwa mwanamke kisimani” katika Yoh 4. Maji ya dunia na mkate yametumika kama sitiari kwa mambo ya milele, na uhalisia wa kiroho.

F. Kudidisha kwa kwake kwa mikate iliyowatosha watu wote ni muujiza ulio katika kumbukumbu za injili zote (Mathayo 14:13-21: Marko 6:32-44: Luka 9:10-17)

G. Michael Magill – New Testament Transline (ukur. 325) huonesha jambo la kuzingatia linalohusiana na makundi mbalimbali katika Kapernaumu na uhusiano wake na maneno ya Yesu ya kushtua. 1. Umati – Yohana 6:24 2. Wayahudi – Yohana 6:41, 52 3. Mitume – Yohana 6:60, 66

Page 127: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

111

4. Wanafunzi kumi na wawili – Yohana 6:67 Yesu kwa matokeo

1. Aliuzuia umati wa watu uliojaribu kumfanya kuwa mfalme kwa vile aliwalisha (Yohana 6:15) 2. Aliupinga uongozi wa Wayahudi kwa msimamo wake mkali na madai yake. 3. Alisababisha wafuasi wengi waliokuwa pembezoni kuondoka. 4. Alishawishi watu kuendelea kuwa na imani kubwa kwa wanafunzi wake (Yohana 6:68-69)

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 6:1-14 1Baada ya hayo Yesu alikwenda zake ng'ambo ya Bahari ya Galilaya, nayo ndiyo ya Tiberia. 2 Na mkutano mkuu wakamfuata, kwa sababu waliziona ishara alizowafanyia wagonjwa. 3 Naye Yesu akakwea mlimani, akaketi huko pamoja na wanafunzi wake. 4 Na Pasaka, sikukuu ya Wayahudi, ilikuwa karibu. 5 Basi Yesu alipoinua macho yake akaona mkutano mkuu wanakuja kwake, alimwambia Filipo, Tununue wapi mikate, ili hawa wapate kula? 6 Na hilo alilinena ili kumjaribu; kwa maana alijua mwenyewe atakalotenda. 7 Filipo akamjibu, Mikate ya dinari mia mbili haiwatoshi, kila mmoja apate kidogo tu. 8 Wanafunzi wake mmojawapo, Andrea, nduguye Simoni Petro, akamwambia, 9 Yupo hapa mtoto, yuna mikate mitano ya shayiri na samaki wawili, lakini hivi ni nini kwa watu wengi kama hawa? 10 Yesu akasema, Waketisheni watu. Na mahali pale palikuwa na majani tele. Basi watu waume wakaketi, wapata elfu tano jumla yao. 11 Basi Yesu akaitwaa ile mikate, akashukuru, akawagawia walioketi; na kadhalika katika wale samaki kwa kadiri walivyotaka. 12 Nao waliposhiba, aliwaambia wanafunzi wake, Kusanyeni vipande vilivyobaki, kisipotee cho chote. 13 Basi wakavikusanya, wakajaza vikapu kumi na viwili, vipande vya mikate mitano ya shayiri vilivyowabakia wale waliokula. 14 Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni.

6:1 “Bahari ya Galilaya au (Tiberia)” Kusanyiko hili la maji lilifahamika kwa majina mengine mengi. Katika Agano la Kale liliitwa Chinnereth (kama vile Hesabu 34:11). Pia lilijulikana kama ziwa Gennessareti katika Luka 5:1 na kwa jina la Kirumi, Ziwa la Tiberia katika Yohana 21:1. Parandesi ni maoni mengine ya tahariri ya mwandishi. Yanaonyesha kuwa injili ya Yohana ilikuwa kwa watu nje ya Palestina (kama vile Yohana 6:4: 6:64: 71) 6:2 Angalia sababu kwa nini umati ulimfuata.

6:3 Yesu alitumia upazaji sauti ya asili na kilima yake kupaza sauti yake. Ukweli kwamba “aliketi chini” inaonyesha kuwa hiki kilikuwa kipindi rasmi cha mafundisho akiwa na wanafunzi wake. Mtu hushangaa kama mlima ulikusudiwa kumkumbushia mtu juu ya muundo ule wa Musa kama Mathayo 5:7. Katika vipindi hivi vikubwa vya mafundisho ya Yesu daima alizungumza na watu wa makundi mbalimbali. Waliomzunguka miguu pake wangalikuwa ndio wanafunzi wake wa karibu; mbali na wale, watu wenye shauku, matajiri na “watu wa kawaida wa eneo hilo”; Na katika vikundi vidogo, viongozi wa kidini (Mafarisayo, waandishi, Masadukayo bila shaka hata Esene). 6:4 “Pasaka, sikukuu ya Wayahudi” njia pekee ya kubainisha urefu wa huduma ya Yesu ni pasaka iliyotajwa katika injili ya Yohana (kwanza 2:15: pili 6:4 na tatu 11:55 & 13:1). Kama Yoh 5:1 pia anazungumzia habari za Pasaka basi tunazo angalau miaka tatu au miaka mine ya huduma ya Yesu. Kuna mengi hatuyajui juu ya maisha ya Yesu (kama vile Yohana 20:30; 21:25). 6:6 “Hili alisema kujipima mwenyewe” Neno hili la Kiyunani hapa kwa maana ya “kujipima” (peirazo) mara nyingi linabeba kidokezo kiovu (Taz. Mada maalumu katika 1 Yohana 4:1, kama vile Mathayo 4:1). Huu ni mfano mzuri kuonyesha kuwa watafsiri wa sasa wanajaribu kulazimisha maneno ya Agano Jipya kuendana na maelezo ya aina moja tu. Wayunani wa lugha ya kawaida ya koine walikuwa wanapoteza tofauti za kisarufi na lugha za Wayahudi wa mwanzo (ona katika Yohana 5:20). Yesu alikuwa anamjaribu Filipo, lakini kwa vipi?

Page 128: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

112

1. Kuhusu imani yake kwa Yesu kama mpaji? 2. Ufahamu wake juu ya Agano la Kale (kama vile Hesabu 11:13, juu ya swala la Musa kwa Mungu kuhusu

kutoa chakula)? 3. Juu ya uangalizi na kujihusisha kwake kwa halaiki?

6:7 NASB, NKJV, JB “Thamani ya dinari ya mia mbili” NRSV “Mishahara ya miezi sita” TEV “Sarafu ya fedha ya mia mbili”

Dinari moja ulikuwa ndio ujira wa siku wa kibarua (kama vile Mathayo 20:2) na askari. Hii ingeweza kuwa karibu sana na theluthi mbili ya ujira wa mwaka.

MADA MAALUMU: SARAFU ZILIZOTUMIKA PALESTINA ENZI ZA YESU

I. Sarafu za shaba A. cherma – thamani ndogo (kama vile Yohana 2:15) B. chalchos – thamani ndogo (kama vile Mt. 10:9; Marko 12:41) C. assarion –sarafu ya shaba ya Kirumi yenye thamani ya senti 1/16 ya a dēnarius (kama vile Mt.

10:29) D. kodrantes – Sarafu ya shaba ya Kirumi yenye thamani 1/64 ya a dēnarius (kama vile Mt. 5:26) E. lepton – sarafu ya shaba ya Kiyunani yenye thamani ipatayo 1/128 ya dēnarius (kama vile Marko

12:42; Luka 21:2) F. quadrans/farthing – Sarafu ya shaba ya Kirumi yenye thamani ndogo

II. Sarafu za fedha A. arguros ("sarafu ya fedha") – yenye thamani kubwa zaidi kuliko shaba au sarafu za shaba nyeusi

(kama vile Mat. 10:9; 26:15) B. dēnarius – sarafu ya fedha ya Kirumi yenye thamani na ujira wa siku (kama vile Mt. 18:28; Marko

6:37) C. drachmē –sarafu ya fedha ya Kiyunani iliyo na thamani sawa na a dēnarius (kama vile Luka 15:9) D. di-drachmon –sarafu mbili za fedha ya kiyunani ilikuwa sawa na ½ shekeli ya kiyahudi (kama vile

Mt. 17:24) E. statēr –sarafu ya fedha yenye thamani ipatayo dēnarii nne (kama vile Mt. 17:27)

III. Sarafu za dhahabu – chrusos ("sarafu za dhahabu") – zenye thamani zaidi (kama vile Mt. 10:9) IV. Maneno ya jumla kwa uzito wa chuma

A. mnaa – Latini mina, uzito wa chuma uliosawa na 100 dēnarii (kama vile Luka 19:13) B. talanton – Kizio cha Kiyunani cha uzito (kama vile Mt. 18:24; 25:15,16,20,24,25,28)

1. thamani ya fedha 6,000 dēnarii 2. thamani ya dhahabu 180,000 dēnari

A. sheqel – uzito wa fedha ya Kiyunani katika agano la kale(yaani,4 oz., kama ile Mwa. 23:15; 37:28; Kut. 21:32)

1. pīm – 2/3 shekeli 2. beka – ½ shekeli 3. gerah – 1/20 shekeli

Vizio vikubwa 1. maneh – 50 shekels 2. kikkar – 3,000 shekels

6:8 – 9 “Andrea, nduguye Simoni Petro” – mazingira haya yanatoa picha nzuri ya imani ndogo ya Andrea juu ya uweza na u-Mwanadamu wa Yesu.

Page 129: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

113

6:9 “mikate mitano ya shayiri” – Huu ulifikilika kama ni mkate aghali sana na uliopendwa. Kilikuwa ni chakula cha watu maskini. Yesu hakutumia uwezo wake kuwapa chakula cha gharama kubwa!

6:10 “Waketisheni watu” watu wa utamaduni huu kwa kawaida hula wakiwa wameketi sakafuni au wameegemea meza yenye umbo la “U”

◙ “palikuwa na majani tele,” Haya ni maoni yenye ushahidi wa macho wa Kitume (waandishi).

◙ “Basi watu waume wakaketi wapata elfu tano jumla yao” Hii kiukweli kilikuwa ni kioja kusema “kulisha watu elfu tano,”kwa sababu kwa hali ilivyokuwa, palikuwa na watu zaidi ya hao pale siku hiyo. Watu Elfu tano ilikuwa ni idadi ya kukadiriwa, ilimaanisha wanaume pekee (yaani 13 na zaidi;) na haikujumuisha wanawake na watoto (kama vile mathayo 14:21). Hata hivyo hakuna uhakika na idadi ya wanawake na watoto waliohudhuria (Mathayo 14:21).

6:11 “akashukuru, akawagawia” Muujiza wa kuzidisha mikate lazima umetokea katika mikono ya Yesu. Katika mazingira ya matumaini ya Wayahudi kwa Masihi tukio hili lingekuwa ni ishara iliyotegemewa ya Yesu kutoa chakula kama Musa alivyotoa Mana. Neno la Kiyunani kwa “kutoa shukrani” (eucharisteō) baadaye likawa ni jina la karamu ya mwisho (kama vile 1 Kor. 11:23-24) Yohana alilitumia hapa kwa fikra ya maelezo ya kiufundi, kwa nyakati zijazo? Injili zingine ambazo hazina kidokezo chochote kuhusu ekaristi takatifu wanatumia neno tofauti (endogeō, kv. Mathayo 14:19; Marko 6:41). Wanatumia neno eucharisteō (kv.Mathayo 15:36; Marko 8:6; Luka 17:16; 18:11) lakini siyo katika mwendelezo ule ule kwenye karamu ya mwisho. Wanatumia neno lile lile kuelezea maombi ya shukrani ya Yesu katika chumba cha juu (kama vile Mathayo 26:27; Marko 14:23; Luka 22:17-19). Kwa hiyo kwa vile matumizi haya hayafanani, Yohana angalihitaji kuweka vidokezo vyake kuwa mahsusi zaidi endapo baadaye wasomaji walitegemewa kuyatafsiri katika mtindo wa ki-ekaristi.

6:12 “kupotea” Tazama Mada Maalumu: Apollumi kwenye 10:10

6:13 “Basi wakavikusanya, wakajaza vikapu kumi na viwili” Neno “kikapu” hapa kinamaanisha kapu kubwa kabisa. Ni muhimu kujua kuwa Yesu hakupoteza chakula cho chote kilichozidishwa. Wala hakubadilisha asili (au aina) ya mkate. Je neno “kumi na mbili” lilimaanisha kitu muhimu? Ni vigumu kuwa na uhakika. Ilitafsiriwa kuwa ni kama rejea ya makabila kumi na mawili ya Israeli (Yesu analiridhisha Agano la Kale) ai kikapu kimoja kwa kila mtume (Yesu nawaridhisha na kuwapa mitume wake), lakini yaweza kuwa ni maelezo ya ushahidi wa macho (kama Yohana 6:19)

MADA MAALUMU: HESABU YA KUMI NA MBILI

Kumi na mbili mara nyingi imekuwa kiishara (Angalia Mada Maalumu: Namba za Kiishara katika Andiko) namba ya shirika

A. Nje ya biblia 1. Ishara kumi na mbli za ukanda 2. Miezi kumi na miwili ya mwaka

B. Katika Agano la Kale (BDB 1040 kuongeza 797) 1. wana wa Yakobo (Makabila ya Kiyunani) 2. waliotazamishwa kwenye

a. Nguzo kumi na mbili za madhabahu katika Kut. 24: b. Vito kumi na viwili juu ya kifua cha kuhani mkuu (ambayo vinasimama kwa niaba ya makabila)

katika Kut. 28:21 c. unga mwembamba wa mkate kumi na miwili katika sehemu takatifu ya kibanda katika Law.

24:5 d. wapelelezi kumi na wawili waliotumwa huko Kanaani katika idadi ya kabila (mmoja kutoka

katika kila kabila)

Page 130: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

114

e. fimbo kumi na mblili (viwango vya kikabila) katika uhasi wa Kora katika Hes. 17:2 f. mawe kumi na mawili ya Yoshua katika Yos. 4:3,9,20 g. majimbo kumi na mawili ya kiutawala katika utawala wa Suleimani katika 1 Fal. 4:7 h. mawe kumi na mawili ya madhabahu yaYHWH katika 1 Fal. 18:31

C. Katika Agano Jipya 1. Mitume kumi na wawili waliochagulwa 2. Vikapu kumi na iwili vya mikate (kimoja kwa kila Mtume) katika Mt. 14:20 3. Viti kumi na viwili vya enzi ambapo Wanafunzi wa Agano Jipyala wamekaa (vinayorejea juu ya

makabila 12 ya Israeli) katika Mat. 19:28 4. majeshi kumi na mmawili ya malaika wa kumsaidia Yesu katika Mat. 26:53 5. Ishara ya Ufunuo a. Wazee 24 juu ya viti 24 4:4 b. 144,000 (12x12,000) katika 7:4; 14:1,3 c. nyota kumi na mbili juu ya taji la mwanamke katika 12:1 d. malango kumi na mawili, malaika kumi na wawili wakiakisi makabila kumi na mawili katika 21:12 e. Mawe kumi na mawili ya misingi ya Yerusalemu mpya na juu yao majina ya mitume kumi na mawili

katika 21:14 f. Mianzi kumi na mbili elfu katika 21:16 (kipimo cha mji mpya, Yerusalemu Mpya) g. kuta ni dhiraa 144 katika 21:17 h. malango kumi na mawili ya lulu katika 21:21 i. miti mipya katika Yerusalemu yenye aina aina kumi na bili za tunda (moja kwa kila mwezi) katika

22:2

6:14 "Nabii" (Hiki ni kidokezo cha kumaanisha Masihi mrejeo wa Kumb. 18:15-22 (kama vile Mdo. 3:22; 7:37);

umati ukatambua uwezo wa Yesu lakini walielewa asili ya ujumbe na ishara zake.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 6:15 15 Kisha Yesu, hali akitambua ya kuwa walitaka kuja kumshika ili wamfanye mfalme, akajitenga, akaenda tena mlimani yeye peke yake.

6:15 Umati ulishtushwa na muujiza wa ki-Masihi wa kuwapa watu chakula. Mstari huu unaweza kuhusiana na

jaribu la mtu mwovu katika Mathayo 4:3.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 6:16-21

16Hata ilipokuwa jioni wanafunzi wake wakatelemka baharini 17 wakapanda chomboni, wakaanza kuivuka bahari kwenda Kapernaumu. Nako kumekwisha kuwa giza, wala Yesu hajawafikia. 18 Na bahari ikaanza kuchafuka kwa kuvuma upepo mkuu. 19 Basi wakavuta makasia kadiri ya maili tatu nne, wakamwona Yesu anakwenda juu ya bahari na kukikaribia chombo; wakaogopa. 20 Naye akawaambia, Ni mimi, msiogope. 21 Basi wakataka kumpokea chomboni; na mara hiyo chombo kikaifikilia nchi waliyokuwa wakiiendea.

6:17 "Kapernaumu" Hapa ndipo yalikuwa makao makuu ya Yesu wakati wa huduma yake Galilaya kwa sababu ya kutoamini kwa watu wa nyumbani kwao Nazareti (kama vile Luka 4:28-29)

6:19 “Basi wakavuta makasia kadiri ya maili tatu nne” walikuwa takribani nusu ya safari kwenye maji wakati Yesu akiwajilia akitembea juu ya maji. Mathayo anakuza simulizi hii akimjumuisha Petro wakati akitembea juu ya maji kumfuata Yesu.

◙ “Walitishika” Mitume hawa walikuwa bado wanamkadiria Yesu kwa viwango vya kidunia. Hofu ya wanafunzi imeelezwa katika Marko 6:49. Uzito wa pamoja wa “ishara”hizi ukawalazimu kutathmini huyu alikuwa nani?

Page 131: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

115

6:20 “Ni mimi” Hii kwa kawaida (egō eimi) inamaanisha “Mimi Ndimi” (kama vile Yohana 4:26; 8:24, 28, 54-59, 13:1918:5-6) ambazo zinaonyesha jina la Agano la Mungu katika Agano la kale, YHWH katika Kutoka 3:12-15. Yesu anaonekana ni “Mimi Ndimi” Ufunuo kamili wa Mungu, nembo (neno) ya mwanadamu ya Mungu, Mwana wake wa kweli na pekee. Tazama D katika mada maalumu ifuatayo.

MADA MAALUM: MAJINA YA UUNGU Huu ulikuwa ni usemi wa kawaida wa Agano Jipya kwa uwepo binafsi na nguvu itendayo kazi ya utatu wa Mungu katika kanisa.Haikuwa kanuni ya miujiza, bali rufaa kwa tabia ya Mungu. Daima, usemi huu unamhusu Yesu kama Bwana (kama vile Flp.2:11)

1. Weredi wa imani ya mtu katikaYesu wakati wa ubatizo (kama vile Rum 10:9-13; Mdo. 2:38; 8:12,16; 10:48; 19:5; 22:16; 1 Kor 1:13; 15; Yak. 2:7)

2. katika upungaji pepo, (kama vile Mt. 7:22; Mk. 9:38; Luka 9:49; 10:17; Mdo. 19:13) 3. katika uponyaji (kama vile Mdo 3:6,16; 4:10; 9:34; Yak. 5:14) 4. katika tendo la huduma (kama vile Mt. 10:42; 18:5; Luka 9:48) 5. katika muda wa kutekeleza nidhamu kanisani (kama vile Mt. 18:15-20) 6. wakati wa kuhubiria watu wa Mataifa (kama vile Luka 24:47; Mdo. 9:15; 15:17; Rum.1:5) 7. katika maombi (kama vile Yn.14:13-14; 15:2,16; 16:23; 1 Kor. 1:2) 8. kama njia ya kurejea Ukristo (kama vile Mdo. 26:9; 1Kor 1:10; 2 Tim 2:19; Yak. 2:7; 1 Pet. 4:14)

Chohote tukifanyacho kama wahudumu, wasaidizi, waponyaji, watoa mapepo, n.k, tunafanya hivyo kwa tabia yake, nguvu Zake, upaji Wake - katika jina Lake.

6:21 “na mara hiyo chombo kikaifikilia nchi waliyokuwa wakiiendea” Hili hakika lilikuwa tukio lingine la kimiujiza (kama vile Yohana 22-25) kwa vile injili ya Marko inaonyesha kuwa walikuwa wamekwenda nusu ya safari majini (kama vile Marko 6:47). Hata hivyo haujatajwa katika injili zingine (yaani Mathayo 14:32 au Marko 6:51.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 6:22-25 22 Siku ya pili yake mkutano waliosimama ng'ambo ya bahari waliona ya kuwa hakuna mashua nyingine huko ila moja, tena ya kuwa Yesu hakuingia katika mashua ile pamoja na wanafunzi wake, bali wanafunzi wake walikwenda peke yao. 23 (Walakini zikaja mashua nyingine kutoka Tiberia mpaka karibu na mahali pale walipokula mikate, wakati Bwana aliposhukuru.) 24 Basi mkutano, walipoona ya kuwa Yesu hayuko huko wala wanafunzi wake, waliingia mashuani wenyewe, wakaenda Kapernaumu wakimtafuta Yesu. 25 Hata walipomwona ng'ambo ya bahari, walimwambia, Rabi, wewe umekuja lini hapa?

6:23 "Tiberia" Huu mji ulikuwa umejengwa na Herode Antipa katika mwaka wa 22 K.K na kuwa makazi yake.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 6:26-34 26 Yesu akawajibu, akasema, Amin, amin, nawaambieni, Ninyi mnanitafuta, si kwa sababu mliona ishara, bali kwa sababu mlikula ile mikate mkashiba. 27 Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa muhuri na Baba, yaani, Mungu. 28 Basi wakamwambia, Tufanyeje ili tupate kuzitenda kazi za Mungu? 29 Yesu akajibu, akawaambia, Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye. 30 Wakamwambia, Unafanya ishara gani basi, ili tuione tukakuamini? Unatenda kazi gani? 31 Baba zetu waliila mana jangwani kama vile ilivyoandikwa, Aliwapa chakula cha mbinguni ili wale. 32 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Siye Musa aliyewapa chakula kile cha mbinguni, bali Baba yangu ANAWAPA NINYI CHAKULA CHA KWELI KITOKACHO MBINGUNI. 33 Kwa maana chakula cha Mungu ni kile kishukacho kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima. 34 Basi wakamwambia, Bwana, sikuzote utupe chakula hiki.

Page 132: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

116

6:26, 32, 53 “Amin, amin, nawaambieni” “Amina” Hili ni fungu la mambo ya Kiebrania lenye matumizi maalumu yapatayo matatu.

1. Katika Agano la Kale neno hili lilitumika kwa “kuamini” likimaanisha kuwa imara na lilitumika kuelewa imani ya mtu kwa YHWH.

2. Matumizi ya Yesu yaliaksi kuanzisha maneno muhimu. Hatuna maneno mengine yanayoweza kutumika kwa pamoja kwa wakati mmoja, kwa neno “Amina’

3. Katika kanisa la mwanzo, kama lilivyo Agano la Kale, likawa baadaye ni neno la uthibitisho na kufanana. Tazama MADA MAALUM: AMINA katika Yohana 1:51

◙ “Lakini kwa vile ulikula mkate” sababu zake zilikuwa za kimwili na haraka, wala hazikuwa za kiroho na za milele.

◙ “Na zilijazwa” Neno hili linamaanisha “kuvimba,” kawaida lilitumika kwa wanyama (hasa ng’ombe)

6:27 “Msifanye kazi” Ni kauli ya kati shurutishi ya wakati uliopo ikiwa na kiambata hasi ambacho mara kinachomaanisha kusimamisha kitendo ambacho tayari kilikuwa kinaendelea. Mazingira ya nyuma ya Agano la Kale kwenye kifungu hiki ni Isaya 5. Mazungumzo haya yana mambo mengi yanayofanana na yale ya mwanamke pale kisimani katika Yohana 4.

◙ “Kuangamia” Tazama Mada aalum: Apollumi katika 10:10

◙ “Ameweka lakiri yake” Hii kifasihi ni “muhuri.” Hii ilikuwa ishara ya uhalisia, umiliki, mamlaka na usalama (kama vile NEB, na Mathayo 28:18; Yohana 17:2). TEV na NIV waitafasili kama “Idhini” kwa vile inatumika kuonyesha idhini ya Mungu Baba juu ya huduma ya Yesu. Angalia MADA MAALUM: MUHURI katika Yohana 3:33 mahali ambapo inaweza kumaanisha Roho Mtakatifu.

6:28 “tufanye nini, kwamba tuweze kufanya kazi za Mungu” Hili lilikuwa swali la kidini la ndani la dini ya Kiyahudi katika karne ya kwanza (kama vile Luka 18:18). Myahudi mwenye dini alidhaniwa kuwa na haki mbele za Mungu kutokana na

1. Uzao wake na 2. Utekelezaji wake wa sheria za Musa kama zilivyotafsiriwa na tamaduni simulizi (Talmud).

6:29 “Mmwamini yeye aliyetumwa na yeye” Hii ni kauli tendaji tegemezi ya wakati uliopo ikifuatiwa na kauli tendaji elekezi ya wakati uliopita usiotimilifu. Neno “kuamini” ni muhimu kulielewa katika mafundisho ya Agano jipya kuhusu wokovu. Tazama Mada Maalum katika Yohana 2:23. Maelekezo ya awali ya neno hili yalikuwa imani ya hiari. Kundi la maneno ya Kiyunani pistis yanaweza kutafsiriwa kama “kuamini,” “kusadiki” au “imani.” Kitovu cha imani na watu lazima kiwe “ndani yake” (kama vile Yohana 1:2 ; 3:16) na sio katika utii wa mwanadamu, kujitoa au shauku. Maelezo ya haraka ya kifungu hiki ni ya kimahusiano binafsi ya Yesu Kristo, na sio thiolojia ya Orthodox kuhusu Yeye, mitambiko ya kidini inayotegemewa, au hata kuishi kiadilifu. Haya yote yanasaidia lakini sio msingi. Angalia kuwa Yesu anabadilisha wingi wa “kazi” wa maswali yao na kuwa katika hali ya umoja. Kwa neno “kupelekwa” Angalia Mada maalum “Kupelekwa” (Apostellō) katika Yohana 5:24 6:30-33 Inabidi kukumbuka kuwa kundi hili lilishiriki kulisha watu elfu tano. Walikuwa tayari wana ishara yao! Viongozi wa dini ya Kiyahudi walifikiri Masihi angerudia baadhi ya vitendo vya Agano la Kale, kama vile kutuma chakula cha Kimbingu Manna (kama vile 11 Baruch 29:8). Viongozi wa sheria za Kiyahudi walitumia Zaburi 72:16 kama andiko hakiki wa mtazamo huu wa Masihi kuwa bora kuliko Musa (kama vile Kor. 1:22). Kuna taswira muhimu ya kisarufi kati ya neno“atakaye amini” na “atakayekuamini” ya Yohana 6:30. Kiini cha kwanza katika muundo wa kawaida wa “kuamini ndani yaYesu. Ni mtizamo binafsi. Mtizamo wa pili juu ya kuamini maneno ya Yesu ndio mtazamo wa kimaudhui. Kumbuka, injili ni mambo mawili mtu na ujumbe. Tazama Mada Maalumu katika Yohana 2:23 6:31 “Kama ilivyoandikwa” Hii ni kauli tendewa timilifu yenye fungu la maneno ya hali ya kuendelea. Ilikuwa ni njia ya muundo wa kisarufi wa kuwasilisha nukuu za mafundisho kutoka katika Agano la Kale. Ilikuwa ni nahau ya kukiri uvuvio na mamlaka ya Agano la Kale. Nukuu hii ingelimaanisha moja ya maandiko mbali mbali katika Agano la Kale: Zaburi 78:24; 105:40; Kutoka 16:4, 15, au Nehemia 9:15

Page 133: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

117

6:32 Yesu anazungumzia thiologia ya utamaduni wa Wayahudi. Walidai kuwa Masiha lazima atende kazi za ajabu kama Musa kwa sababu ya Kut. 18:15 ; 18. Yesu anasahihisha dhana yao kwa hoja kadhaa

1. Mungu sio Musa – aliyewapa manna. 2. Manna haikutoka mbinguni japo watu walifikiri hivyo (kama vile Zab. 78:23, 25) 3. Mkate wa kweli kutoka mbinguni alikuwa Yesu ambaye hakuwa tendo la wakati uliopita bali uhalisia

uliopo.

6:33 “Hicho ndicho kinashuka chini kutoka mbinguni” Hii ni dhana inayojirudia katika Yohana (kama vile Yohana 3:13) ni maneno ya Yohana ya wima ya pande mbili. Katika mazingira haya kushuka kwa Yesu kunasemwa mara saba (kama vile Yohana 6:33, 38, 41, 42, 50, 51, 58). Inaonyesha asili ya kiungu ya Yesu kabla ya kuwepo (kama vile Yohana 6:33, 38, 41, 42, 50, 51, 58, na 62. Pia ni kitendo kuhusu “manna” iliyotoka mbinguni kama alivyofanya Yesu kuwa Yeye ni mkate wa kweli, na mkate wa uzima. Hii kihalisia ni “mkate wa Mungu ule ushukao chini kutoka mbinguni” Hapa kitenzi tendaji endelevu cha wakati uliopo cha jinsia ya ME kikimaanisha (1) mkate (2) mwanaume Yesu. Daima katika Yohana maneno haya yenye utata ni ya msingi (uhusika mara mbili).

◙ “Anatoa maisha kwa ulimwengu” hili ndilo kusudi kwa nini Yesu alikuja (kama vile Yohana 3:16; Marko 10:45, 2Kor. 5:21) lengo ni “maisha mapya” “maisha ya milele” “maisha ya enzi mpya”maisha ya aina ya Mungu kwa ulimwengu uliopotea na wenye kuasi, sio kwa baadhi ya vikundi maalumu (Wayahudi /watu wa mataifa, wateule/wasio wateule, watu wa mlengo wa kushoto/kulia) bali kwa wote.

6:34 NASB, NKJV "Bwana" NRSV, TEV, NJB, NET, NIV, REB "Bwana" Maneno haya mawili yote yana akisi matumizi ya maana ya Kurios. Katika mazingira haya, la pili ndilo linaonekana kuwa sahihi. Umati haukumwelewa Yesu wala maneno yake. Hawakutambua kuwa ni Masihi (pia taz Yohana 4:11, 5:7).

◙ “Tupate mkate huu kila siku” usemi huu ni sawa na ule wa mwanamke aliyekuwa pale kisimani katika Yohana 4:15. Wayahudi hawa kadhalika wala hawakuelewa maneno mbadala ya kiroho ya Yesu. Hii ndio dhima ya maneno ya kujirudia katika Yohana

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 6:35-40 35Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe. 36 Lakini naliwaambia ya kwamba mmeniona wala hamwamini. 37 Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe. 38 Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka. 39 Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya, ya kwamba katika wote alionipa nisimpoteze hata mmoja, bali nimfufue siku ya mwisho. 40 Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.

6:35 “Mimi ni mkate wa uzima” Haya ni mojawapo ya maneno “Mimi ndimi” ambayo yanaainishwa toka Yohana (kama vile Yohana 6:35, 41, 48, 51, 8:12 ; 10:7, 9, 11, 14 ; 11:25, 14:6 ; 15:1, 5). Injili ya Yohana inazingatia kwenye ubinadamu wa Kristo. Hii inahusishwa na matarajio ya ki-Masihi ya Wayahudi juu ya Yesu kuhusu manna na mtoaji mpya wa sheria ambaye angeleta safari mpya (kutoka dhambini). Tazama nukuu kutoka Yohana 8:12

◙ “Ye yote ajaye kwangu hatakufa na njaa, na ye yote aniaminiye hatakufa kwa kiu” Hizi ni kauli mbili hasi zenye nguvu katika Kiyunani, “kamwe Hapana” (kama vile Yohana 6:37). Kuna mahusiano sambamba kati ya “kuja” na “kuamini” (kama vile Yohana 7:37-38, sawa na “kuona” na “kusikia”). Yote yako kwenye wakati uliopo endelevu.

Page 134: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

118

waumini kuja na kuondoka sio uamuzi wa mara moja, bali ni mwanzo wa ushirika wa mtindo wa maisha, urafiki na ushirika.

◙ “Njaa… kiu” Njaa na kiu siku zote vilitumika kuelezea uhalisia wa kiroho (kama vile Zab. 42:1; Isaya 55:1; Amosi 8:11-12 ; Mathayo 5:6).

6:36 “Kwamba umeniona” Baadhi ya mashuhuda za kale (MSS א, A na machapisho ya Biblia za Kilatini na Kiaramu huko Shamu) zinaacha neno“mimi” zikifanya maneno ya Yesu kumaanisha ishara tu (yaani kulisha umati) kiwakilishi nomino kimejumuishwa katika maandishi mengi ya Kiyunani na tafsiri ambazo UBS4 haingeweza kuamua ni ipi asilia.

6:37 “Yote yale anayonipa Baba yangu yatakuja kwangu” Msisitizo wa msingi wa habari hii uko kwenye ukuu wa Mungu. Vifungu viwili venye uhakika kuhusu ukweli wa kithiolojia unapatikana katika Warumi 9 na Efe. 1:3-14. Inapendeza kuona kuwa katika mazingira yote mwitikio wa mwanadamu unahitajika. Warumi 10 ina mafungu saba yote yakijumuishwa. Hii pia imo katika Waefeso 2, ambapo mijadala ya rehema za Mungu katika Yoh 6:1-7 inakuwa na hoja katika kuwataka wanadamu kuwa na imani katika Yohana 6:8-9. Makusudi ya Mungu ni imani kwa waliokombolewa; sio kikwazo kwa wasiookolewa. Ufunguo wa imani ni upendo na rehema za Mungu, sio tu imani ya milele. Tazama kwa wale wote Mungu aliowapa Yesu pia “wanakuja kwake.” Daima Mungu anachukua hatua (kama vile Yohana 6:44, 65) Lakini wanadamu yawapasa kuitikia (kama vile Yohana 1:12 ; 3:16) .Tazama Mada Maalumu katika Yohana 3:16

◙ “Yeyote ajaye kwangu hakika sitamtupa”Hizi ni kauli mbili hasi zingine zenye nguvu. Hii inasisitiza ukweli kuwa Mungu anawaita na kumkaribisha yeyote kupitia kwa Kristo (kama vile Ezekieli 18:21-23 ; 30-32 ; 1 Tim 2:4; ; 2 Petro 3:9). Mungu daima huchukua uamuzi (kama vile Yohana 6:44, 65) lakini wanadamu lazima waitikie (kama vile Marko 1:15 ; Mt. 3:16, 19:20-21). Ni habari ya ajabu kiasi gani kuhusu usalama? (kama vile Rum. 8:31-39).

MADA MAALUMU: DHAMANA YA MKRISTO

A. Je! Wakristo wanaweza kutambua kwamba wameokolewa (kama vile 1 Yohana 5:13)? Yohana ana majaribio matatu au ushahidi. 1. Kimafundisho (imani, 1 Yohana 1:1,5,10; 2:18-25; 4:1-6,14-16; 5:11-12) 2. Mtindo wa maisha (utii, 1 Yohana 2:2-3; 2:3-6; 3:1-10; 5:18) 3. Kijamii (upendo, 1 Yohana 1:2-3; 2:7-11; 3:11-18; 4:7-12, 16-21)

B. Dhamana imekuwa ni suala la kimadhehebu 1. John Calvin alijikita katika uchaguzi wa Mungu. Amesema kuwa katika maisha haya kamwe

hatuwezi kuwa na uhakika. 2. John Wesley aliegemea juu ya dhamana ya uzoefu wa kidini. Aliamini kuwa tunao uwezo wa kuishi

juu ya dhambi inayofahamika. 3. Waamini wa Kanisa Katoliki na Kanisa la Kristo wanaegemea juu ya Kanisa la kimamlaka. Kundi

alilomo mtu huyu ni jawabu la neno dhamana. 4. Walokole wengi wameweka dhamana zao juu ya ahadi za Biblia, zilizoungamanishwa na tunda la

Roho (kama vile Gal. 5:22-23) katika maisha ya mwamini (yaani, ufanano na Kristo wa kila siku). C. Dhamana ya awali ya waaminio imeungamanishwa na sifa za Mungu wa Utatu

1. Upendo wa Mungu Baba a. Yohana 3:16; 10:28-29 b. Warumi 8:31-39 c. Waefeso 2:5,8-9 d. Wafilipi 1:6 e. 1 Petro 1:3-5 f. 1 Yohana 4:7-21

2. Matendo ya Mungu mwana a. kifo badala yetu

Page 135: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

119

1) Matendo 2:23 2) Warumi 5:6-11 3) Wakorintho 5:21 4) 1 Yohana 2:2; 4:9-10

b. maombi ya kuhani mkuu (Yohana 17:12) c. maombi endelevu ya kusihi

1) Warumi 8:34 2) Waebrania 7:25 3) 1 Yohana 2:1

3. Huduma ya Roho wa Mungu a. wito (Yohana 6:44,65) b. kutia mhuri

1) 2 Wakorintho 1:22; 5:5 2) Waefeso 1:13-14; 4:3

c. hakikisha 1) Warumi 8:16-17 2) 1 Yohana 5:7-13

D. Lakini wanadamu yawapasa kukubali kujitolea kwa Mungu kupiitia agano lake (katika nafasi zote, ya awali na ile endelevu) 1. waamini yawapasa kugeuka kutoka dhambini (toba) na kumwelekea Mungu kupitia Yesu (imani)

a. Marko 1:15 b. Matendo 3:16,19; 20:21

2. waamini yawapasa kukupokea kujitolea kwa Mungu katika Kristo (tazama Mada Maalumu: Je! Kunamaanisha nini "kupokea," "Kuamini," "Kukiri/Kuungama," "Kusihi" a. Yohana 1:12; 3:16 b. Warumi 5:1 (na kwa mfanano 10:9-13) c. Waefeso 2:5,8-9

3. waamini yawapasa kuendelea katika imani (tazama Mada Maalumu: Ustahimilivu) a. Marko 13:13 b. 1 Wakorintho 15:2 c. Wagalatia 6:9 d. Waebrania 3:14 e. 2 Petro 1:10 f. Yuda 20-21 g. Ufunuo 2:2-3,7,10,17,19,25-26; 3:5,10,11,21

E. Dhamana ni ngumu kwa sababu 1. mara kwa mara waamini hutafuta uzoefu fulani ambao haukuhaidiwa katika Biblia 2. mara kwa mara waamini hawaielewi injili kwa ukamilifu 3. mara kwa mara waamini wanaendelea na dhambi kwa makusudi (kama vile Kor. 3:10-15; 9:27; 1

Tim. 1:19-20; 2 Tim. 4:10; 2 Pet. 1:8-11) 4. aina ya mtu fulani (yaani, mtu aaminiye katika kushinda) asiyeweza kamwe kukubali upendo na

ukubalifu usio na masharti wa Mungu 5. katika Biblia kuna mifano ya maungamo ya uongo (kama vile Mt. 13:3-23; 7:21-23; Marko 4:14-20;

2 Pet. 2:19-20; 1 Yohana 2:18-19, tazama Mada Maalumu: Ukanaji wa Imani) Tazama Mada Maalumu: Dhamana ya Mkristo kwa maelezo ya mihtasari tofauti tofauti ya mafundisho haya.

6:38 “Nimeshuka kutoka mbinguni” Hii ni njeo ya wakati timilifu ikimaanisha kubadilika kuwa mwanadamu (kama vile Yohana 1:1; Waef 4:8-10) na matokeo yake kubakia vile vile. Pia inaonyesha asili ya Yesu (kama vile Yohana 6:41, 62)

Page 136: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

120

◙ “sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka” Agano jipya linatetea umoja katika utatu (tazama Mada Maalum katika Yohana 14:26), mfano 14:8-9 na nafsi za watu watatu. Mstari huu ni sehemu ya msisitizo wa Yohana unaoendelea juu ya utii wa Yesu kwa Baba Yake. Tazama nukuu kamili katika Yoh 5:19. Taz Mada Maalum “Kupelekwa”(Apostellō)katika Yohana 5:24

6:39 “kwamba katika wote alionipa nisimpoteze hata mmoja” Kuna mahusiano ya wazi kati ya umoja tasa “vyote ambavyo” katika Yohana 6:37 na umoja tasa katika Yohana 6:39. Yohana natumia mtindo huu usio wa kawaida mara kadhaa (kama vile Yohana 17:2, 24). Ni wazi inasisitiza ushirikiano kwa pamoja (kama vile Yohana 6:40 ; 45). Hii ni ahadi kubwa ya kuhifadhi nguvu ya Mungu, chanzo cha dhamana ya Mkristo (kama vile Yohana 10:28-29; 17:2,24, (tazama Mada Maalumu katika 1 Yohana 5:13.) Zingatia kuwa njeo ya kitenzi katika Yoh 6:37 ni wakati uliopo bali katika Yohana 6:39 ni wakati timilifu. Karama za Mungu hudumu! Pia maneno mawili ya mwisho ya kukiri katika Yohana 6:39 yote yako katika kauli tendaji za wakati uliopita usiotimilifu; Yesu hapotezi cho chote kile alichopewa na Baba yake (Yohana 6:37 na 39) na atawafufua wote wale aliopewa siku ya mwisho (kama vile Yohana 6:44). Hapa kuna ahadi za kiungu za (1). Uchaguzi na (2) ustahimilivu. Dhana hii ya siku ya mwisho (chanya na hasi) inaitwa kwa majina kadhaa;-

1. Siku za mwisho, Yohana 6:39 ; 40, 44, 11:24 ; 12:48 ; 2 Tim 3:1 ; 1 Petro 1:5 ; 2 Petro 3:33. 2. Muda wa mwisho. 1 Yohana 2:18 Yuda 1:18 3. Siku ile. Matendo 17:31 4. Siku, Mdo. 17:31 5. Siku kuu Yuda, 1:6 6. Siku maalum, Luka 17:30, 1 Kor. 3:13, 1 Thes. 5:4, Ebr. 10:25 7. Siku yake, Luka 17:24 8. Siku ya Bwana, 1 Thes. 5:2 ; 2 Thes. 2:2 9. Siku ya Kristo, Flp. 1:10, 2:16 10. Siku ya Bwana Yesu Kristo, 1 Kor. 1:8 ; 5:5 11. Siku ya Bwana Yesu 2 Kor. 1:14 12. Siku ya Krito Yesu, Flp. 1:6 13. Siku ya Mwana wa Adamu, Luka 17:24 (taz pia 7) 14. Siku ya hukumu, Mathayo 20:15, 11:22 ; 24, 12:36 2 Petro 2:9 ; 3:7 1 Yoh 4:17 15. Siku ya ghadhabu, Ufunuo 6:17 16. Siku kuu ya Mungu, Ufunuo 16:14

◙ “Lakini iamshe siku ya mwisho” hii inamaanisha siku ya ufufuo kwa waumini lakini ni siku ya hukumu kwa wasioamini, (kama vile Yoh6:40, 44:54, 5:25, 28 ; 11:24 na 1 Kor. 15. Frank Stagg ana maneno ya msaada katika hatua hii kwenye makala yake, A New Testament Theology: “Injili ya Yoha ni msisitizo kuhusu ujio wa mbele ujao (14:3 18:1, 28, 16:16, 22) na inasema wazi kuhusu ufufuo na hukumu ya Siku ya mwisho (5:28 ikifuata ; 6:39 ikifuata ; 44:54 ; 11:24 ikifuatiwa na ; 12:48); lakini katika injili nzima ya nne, maisha ya milele, hukumu na ufufuo ni uhalisia wa sasa (3:18 ikifuata ; 6:39 ikifuata; 4:23 ; 5:25 ; 6:54 ; 3:18 f ; 4:23, ; 5:25 ; 6:54 ; 11:23 ; 12:28, 31 ; 13:31 f ; 14:17 ; 17:26)” (uk. 311).

6:40 “Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya” Hili ndilo jibu kwa swali la Yohana 6:28 “Tufanye nini basi ili tuweze kufanya kazi ya Mungu? Tazama Mada Maalumu katika Yohana 4:34

◙ “Kwamba kila amtazamaye mwana” Kitenzi tendaji endelevu cha wakati uliopo cha neno “amtazamaye” na “amwaminiye” yanafanana (kama “ajaye” na “aaminiye” katika Yohana 6:35, kama “aonaye” na “asikiaye”). Haya ni matendo yanayoendelea sio matukio ya muda mfupi tu. Neno “amtazamaye” linamaanisha “kuangalia kwa shauku” kwa lengo la kutaka kuelewa au kujua. Hakika nalipenda neno “kila mmoja” (pas), tambua kuwa

1. Wote wapate kuamini katika yeye, 1:7 2. Amtiaye nuru kila mtu, Yohana 1:9 3. Ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye, Yohana 3:15 4. ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele, Yohana 3:16

Page 137: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

121

5. ili watu wote wamheshimu Mwana, Yohana 5:23, 6. -9, Yoh 6:37; 39:40, 45. 10. Naye kila aishiye na kuniamini hatakufa, Yohana 11:26 11. Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu, Yohana 12:32 12. Kila mmoja aliye na imani kwangu hatabaki gizani, Yohana 12:46

Huu ndio muujiza wa ukuu wa Mungu (kama vile Yohana 6:38-39 ; 17:2, 24 dhidi ya (mapenzi ya hiari) yote kwa kiasi Fulani ni kweli kwangu na dhana ya kithiolojia ya “patano” inayaunganisha vizuri zaidi ◙ “Huamini ndani yake” Kumbuka kuwa wokovu kimsingi ni uhusiano wa mtu na sio kanuni za imani, thiolojia sahihi wala mitindo ya maisha iliyo mizuri (kama vile Yohana 3:16 ; 11:25-26). Mkazo uko kwenye imani ya mtu, na sio nguvu, Tazama Mada Maalum katika Yohana 2:23 Tambua ulinganifu wa msisitizo juu ya chaguo la pekee la Mungu mkuu katika Yohana 6:37a,39,44,65 na mwitikio wa imani ya mwanadamu katika Yohana 6:37, 40. Mvutano huu wa Kibiblia unapaswa kudumishwa. Ukuu wa Mungu na hiari ya mwanadamu ndivyo vinavyounda vipengele pacha vya agano la Kibiblia. ◙ “Waweza kupata maisha ya milele” Hili ni tendo tendaji tegemezi la wakati uliopo; mwitikio unahitajika. (kama vile Yohana 5:11). Pia angalia kuwa Yohana 6:39 iko pamoja, bali Yohana 6:40 imejitegemea. Hiki ndilo fumbo la wokovu.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 6:41-51 41Basi Wayahudi wakamnung'unikia, kwa sababu alisema, Mimi ni chakula kilichoshuka kutoka mbinguni. 42 Wakasema, Je! Huyu siye Yesu, mwana wa Yusufu, ambaye twamjua babaye na mamaye? Sasa asemaje huyu, Nimeshuka kutoka mbinguni? 43 Basi Yesu akajibu, akawaambia, Msinung'unike ninyi kwa ninyi. 44 Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka; nami nitamfufua siku ya mwisho. 45 Imeandikwa katika manabii, Na wote watakuwa wamefundishwa na Mungu. Basi kila aliyesikia na kujifunza kwa Baba huja kwangu. 46 Si kwamba mtu amemwona Baba, ila yeye atokaye kwa Mungu; huyo ndiye aliyemwona Baba. 47 Amin, amin, nawaambia, Yeye aaminiye yuna uzima wa milele. 48 Mimi ndimi chakula cha uzima. 49 Baba zenu waliila mana jangwani; wakafa. 50 Hiki ni chakula kishukacho kutoka mbinguni, kwamba mtu akile wala asife. 51 Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu

6:41 “Basi Wayahudi wakamnung'unikia” Hiki ni kitendo cha wakati usiotimilifu, ukimaanisha kuwa walianza kulalamika au walilalamika mara kwa mara na wakaendelea kulalamika tena na tena. Mfanano na kipindi cha kutangatanga nyikani (kama mvile Kutoka na Hesabu) unashangaza. Waisraeli wa zama hizo pia walimkataa Musa, mwakilishi wa Mungu ambaye pia aliwapa chakula. 6:42 Hii inaonyesha kuja Wayahudi waliyaelewa maneno ya Yesu kumhusu. Alikuwa wazi kabisa kwa kutumia nahau za Kiyahudi kudai kuwa Yeye ni wa Mungu aliyewahi kuwepo kabla. Maneno ya Yesu bado yanaendelea kushangaza yakitoka kwa fundi seremala wa ki-Galilaya. Yesu alisema maneno mazito kuhusu Yeye mwenyewe, hivyo basi:

1. Ni mwana wa Mungu kama mwanadamu anayeleta uzima wa milele kwa maneno yake na matendo au 2. Mwongo aliyewahi kuwepo au 3. Kichaa au majinuni – (kutoka Josh McDowell, Evidence That Demands a Verdict)

Madai ya uaminifu Yesu ndiyo suala lenyewe la Ukristo. 6:43 “Msinung'unike ninyi kwa ninyi” Hili ni tendo shurutishi la wakati uliopo likiwa na kiambata hasi kinachomaanisha kusimamisha kitendo ambacho tayari kipo kinaendelea.

6:44 “Hakuna mtu awezaye kuja kwangu asipovutwa na Baba aliyenipeleka” Mungu siku zote anachukua maamuzi (kama vile Yohana 6:65 na Isaya 53:6)

Page 138: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

122

Maamuzi yote ya kiroho ni matokeo ya Roho auguwaye ndani yetu, na sio udini wa mwanadamu (kama vile Isaya 53:9). Ukuu wa Mungu na mwitikio wenye mamlaka kwa mwanadamu ni vitu viwili visivyoweza kutenganishwa vilivyounganishwa pamoja kwa mapenzi na huruma ya Mungu. Hii ni dhana ya patano katika Agano la Kale. Mzania katika hili la “kumsogelea Mungu” umo katika Yohana 12:32 ambapo “Yesu anawavuta watu wote kuja kwake.” Kuvutwa huku kunabadili mpangilio wa watu wa Mungu kutoitikia maneno ya kinabii (mfano; Isaya 6:9-13; 29:13). Mungu sasa anaongea sio kwa kupitia kwa manabii kwa Israeli bali kupitia Mwanawe kwa Wanadamu wote (kama vile Ebr.1:1-3) Angalia Mada Maalumu “Kupelekwa” (Apostellō) katika Yohana 5:24. 6:45 “Imeandikwa katika Manabii” Hii ni nukuu toka Isaya 54:13 au Yer.31:34 ambayo inaelezea dhana ya ndani (moyo mpya, fikra mpya) na “Agano Jipya”

◙ “Kila aliyesikia na kujifunza kwa Baba huja kwangu“Haiwezekani kudai kumfahamu Mungu na ukamkataa Yesu (kama vile 1 Yohana 5:1-12) 6:46 “Sio kwamba mtu amemwona Baba“ Uthibitisho wa Yesu ni kuwa kupitia kwake mtu anaweza kumwelewa na kumtambua Mungu (kama vile Yohana 1:18; 14:6,9). Hata Musa kamwe hakumwona YHWH (kama vile maelezo ya Yohana 5:31)

6:47 Mstari huu unafupisha kuhusu zawadi ya Yesu ya wokovu wa bure kwa wanadamu wote (“aaminiye,” kauli tendaji endelevu ya wakati uliopo; “uzima wa milele,” kama vile Yohana 6:51,58: 15,16,36; 5:24; 11:26; 20:31). Yesu ndio kweli pekee ya ufunuo wa Mungu, mlango wa kweli wa kwenda kwa Mungu (ukiijumuisha na injili, kama vile, Yohana 10:1-6,7-9; 14:6), lakini hili linapatikana kwa wana na binti wote wa Adamu (ukijumuisha na utimilizo wa injili ya Yohana 1:4,7,12; 3:16; Mwa.3:15; 12:3). 6:50 Mstari huu, kama ulivyo wa Yohana 6:31-35, ni wa kitendo kinachotumika kumaanisha mkate, mkate wa kimwili (manna) na mkate wa kimbingu (Yesu). Mmoja hutoa uhai wake na kuyawezesha maisha ya kimwili, lakini lazima kurudiwa na hatimaye kushindwa kuzuia kifo.Mwingine hutoa na kuwezesha uzima wa Milele, lakini ni lazima akubaliwe na kuelishwa na kuweka miisho ya haraka ya mauti ya kiroho(ushirika uliovunjika na Mungu; ushirika wa ndani wa dhambi na mtu mwenyewe) 6:51 “Mimi ndimi chakula chenye uzima“ Haya ni moja ya maelezo yaliyozoeleka “Mimi Ndimi” ya injili ya Yohana (kama vile Yohana 6:35,48,51). Ilikuwa ni fasihi ya kiufundi ya Yesu ya kumakinika juu ya ubinadamu wake. Wokovu, kama ulivyo ufunuo, ni wazi kabisa uko kwenye hali ya ubinadamu.

◙ “Chakula nitakachotoa Mimi ni mwili wangu“Hili ni neno mbadala likisisitiza kuwa Yesu mwenyewe, sio mgawa chakula, ni hitaji laetu kuu. Kifungu hiki kinaturudisha nyuma kwa Yohana 1:14

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 6:52-59 52 Basi Wayahudi walishindana wao kwa wao wakisema, Awezaje mtu huyu kutupa sisi mwili wake ili tuule? 53 Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. 54 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. 55 Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 56 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake. 57 Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi. 58 Hiki ndicho chakula kishukacho kutoka mbinguni; si kama mababa walivyokula, wakafa; bali akilaye chakula hicho ataishi milele. 59 Maneno hayo aliyasema katika sinagogi, alipokuwa akifundisha, huko Kapernaumu.

6:52

Page 139: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

123

NASB "shindana" NKJV "bishana " NRSV "pingana" TEV "maneno ya kushindana" NJB "kushindana" Kauli isiotimilifu inamaanisha mwanzo wa kitu au hali ya kitu kuendelea siku za nyuma. Hili ni neno la nguvu la Kiyunani kwa maana ya kugombana (kama vile Mdo. 7:26; 2 Tim. 2:23-24; Tit. 3:9) na kutumika ki-stiari katika 2 Kor.7:5 na Yak. 45:1-2.

◙ “awezaje mtu huyu kutupa sisi mwili wake ili tuule?” Katika kitabu cha Yohana Yesu anazungumza katika lugha ya ki-stiari ambayo kwa kawaida haieleweki katika maana ya kifasihi: (1) Nikodemu, Yohana 3:4; (2) mwanamke Msamaria, Yohana 4:11; (3) kusanyiko la Wayahudi, Yohana 6:52; na (4) wanafunzi wake, Yohana 11:11.

6:53-57 Maneno katika Yohana 6:53 na 54 yanafurahisha sana. Katika Yohana 6:53, neno “alaye” na “awaye yote” yapo kwenye kauli tendaji tegemezi ya wakati uliopita usiotimilifu ambao inazungumza juu ya matendo anzilishi ya hiari. Maneno katika Yohana 6:54, “alaye” na “awaye yote,” yapo katika kauli tendaji endelevu ya wakati uliopo ambayo inasisitizia kitendo kinachoendelea (kama vile Yohana 6:56,57,58). Inaonekana kuwa hii inathibitisha ukweli kwamba mmoja lazima aitike kwa Yesu na aendelee kuitika. Ikumbukwe kuwa kukitumia kifungu hiki kifasihi ni kupotosha tishio la Kiyahudi la unywaji damu (kama vile Law. 17:10-14). Kurejea vidokezo vya wazi vya Yesu kwenye chakula cha Kimbingu (manna) kule nyikani (kama vile Yohana 6:58), na kuvitumia vidokezo hivyo kama vifungu vya kifasihi vianvyoendana na ekaristi takatifu ni upotoshaji wa muundo wa kihistoria na muktadha wa kifasihi wa kusudi la kirutulujia. 6:54 “mwili……damu” Hili ni namna ya ki-stiari ya Kiyahudi ya kurejerea hali ya utu, kama “moyo.” 6:55 “chakula cha uzima….kinywaji cha uzima” Hii ni tabia ya Yohana kulitumia neno kweli/ukweli (angalia Mada Maalumu hapo chini). Yohana, akiandika mwishoni kuliko waandishi wengine wa Agano Jipya, aliona maendeleo juu ya mafundisho mengi yaliyokuwa yanakwenda kinyume na Ukristo (msisitizo zaidi juu ya Yohana Mbatizaji, msisitizo juu ya sakramenti, msisitizo juu ya ufahamu wa kibinadamu wa mafunuo)

MADA MAALUMU: “UKWELI” (DHANA) KATIKA MAANDIKO YA PAULO Katika maana hii Yohana anaunganisha historia ya nyuma ya Waebrania na Wayunani ya neno alētheia yaani “ukweli” kama alivyofanya kwenye neno logos (kama vile 1:1-14). Waebrania (angalia Mada Maalumu: kuamini, amini, imani na uaminifu katika Agano la Kale) ikidokezwa hivyo ambavyo ni kweli, au uaminifu (mara nyingi linahusianishwa na maandiko ya kale ya Kiyunani ya neno pisteuō). Katika Kiyunani lilihusianishwa na ukweli wa Pilato dhidi uongo; mambo ya kimbingu dhidi ya kidunia. Hili linakaa sawa kuhusiana na uwili wa Yohana. Mungu kwa uwazi ameridhihilisha hili (maana na asili ya neno alētheia ni kuweka wazi, kutokuficha, kudhihilisha wazi) Yeye mwenyewe katika Mwana. Hili limeelezewa katika njia tofauti.

1. Nomino, alētheia, kweli a. Yesu amejaa neema na kweli ya kutosha (kama vile Yohana 1:14,17 – maneno ya patano katika

Agano la Kale) b. Yesu ndiye alikuwa mlengwa kwenye ushuhuda wa Yohana Mbatizaji (kama vile Yohana 1:32-34;

18:37 – nabii wa mwisho wa Agano la Kale) c. Yesu anaongea ukweli (kama vile Yn. 8:40,44,45,46 – ufunuo ni fumbo na kitu binafsi) d. Yesu ni njia, kweli, na uzima (kama vile Yohana 14:6) e. Yesu anawatakasa katika kweli (kama vile Yohana 17:17) f. Yesu (neno Logos, 1:1-3) ni kweli (kama vile Yohana 17:17)

2. Kivumishi, alēthēs, kweli, uaminifu

Page 140: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

124

a. Ushuhuda wa Yesu (kama vile Yohana 5:31-32; 7:18; 8:13-14) b. Hukumu ya Yesu (kama vile Yohana 8:16)

3. Kivumishi, alēthinus, kweli a. Yesu ni nuru ya kweli (kama vile Yohana 1:9) b. Yesu ni mkate wa kweli (kama vile Yohana 6:32) c. Yesu ni mzabibu wa kweli (kama vile Yohana 15:1) d. Yesu ni shuhuda wa kweli (kama vile Yohana 19:35)

4. Kielezi, alēthōs, hakika a. Msamalia mwema anamshuhudia Yesu kama mwokozi wa ulimwengu (kama vile Yohana 4:42) b. Yesu ni chakula na kinywaji cha kweli, kama chakula cha manna kilivyopingwa katika siku za Musa

(kama vile Yohana 6:55) Neno ukweli na unyumbulisho wake pia unaelezea ushuhuda mwingine wa Yesu, kwa neno alēthēs

a. Ushuhuda wa Yohana Mbatizaji ni wa kweli (kama vile Yohana 10:41) b. Ushuhuda wa Yohana (mwandishi wa Injili) ni wa kweli (kama vile Yohana 19:35; 21:24) c. Yesu anaonekana kama nabii wa kweli (kama vile Yohana 6:14; 7:40)

Kwa mazungumzo mazuri kuhusu ukweli katika Agano la Kale angalia George E. Ladd's A Theology of the New Testament, kur.263-269

6:56 “hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake” Ukweli huu ambao ni ule ule umesemwa katika Yohana 15:4-7 ; 1 Yoh 2:6 ; 27:28 ; 3:8 ; 24 ; Tazama Mada Maalum kutii katika 1 Yohana 2:10. Hii ni mwendelezo wa msisitizo wa kudumu katika Agano la Kale (kama vile Gal. 6:9 ; Ufunuo 2:7 ; 11:17 ; 26 ; 3:5 ; 12:21 Tazama Mada Maalum katika Yohana 8:31 Mwitikio wa kweli unahalalishwa kwa kuendelea kuitikia. Msisitizo kuhusu kustahimili ni kitu kinachokosekana katika uenezaji wa injili Marekani. Mtu hapaswi tu kuanza na imani bali kumaliza na imani (Ebr. 11); Jonathan Edwards alisema, “uhakiki wa kweli wa chaguzi ni ule unaodumu mpaka mwisho” – W.T. Conner alisema; ‘Wokovu wa mtu aliyeamua kuingia kwenye wokovu ni toka enzi na enzi bila shaka katika fikra na kusudi la Mungu, lakini ukiwa katika sharti la imani na imani inayostahimili na kushinda”

6:57 “Baba aliye hai” Usemi huu sio wa kawaida, ni wa kipekee, lakini dhana inatumika daima katika Biblia. Kuna namna kdhaa tofauti katika kutafsiri asili ya jina/cheo hiki kwa Mungu.

1. Jina la Mungu wa Agano (kama vile Kutoka 3:12; 14-16 ; 2-3 Mada Maalum katika Yohana 6:20) 2. Viapo vya Mungu, “kuma Naishivyo”, au katika jina la Mungu “kama Bwana anaishi”, (kama vile Hesabu.

14:21, 28; Isaya 49:18 ; Yer. 4:2) 3. Kama maelezo ya Mungu, (kama vile Zab. 42 – 2:84 ; 2; Yoshua 3:10; Yer. 10:10 ; Dan. 6:20, 26 ; Hos. 1:10 ;

Mathayo 16:16; 26:63; Mt. 14:15; Rum. 9:26; 2 Kor. 3:3 ; 6:16 ; 1 Thes. 1:9 ; 1 Tim 3:15 ; 4:10 ; Ebr. 3:12 ; 9:14 ; 10:31 ; 12:23; Ufunuo 7:2.

4. Maelezo katika Yohana 3:26 kwamba Baba anao uzima ndani yake na ameutoa kwa mwana na 5:21 ambapo Baba huwafufua wafu, kama afanyavyo mwana.

6:58 Huu ni ulinganisho wa Agano la Kale na Jipya, Musa na Yesu (Tazama kitabu – Ebr. 3:4)

◙ “si kama mababa walivyokula, wakafa” Hii pia inaweza kuwa imesaidia kazi ya kithiolojia ya kukataa wokovu kupitia uzao (kama vile Yohana 8:33-39) au kupitia sheria za Musa (Torati)

◙ Tazama mada maalum chini

MADA MAALUM: MILELE (‘olam)

Asili ya neno la Kiebrania 'olam, עולם (BDB 761, KB 798) halijulikani (NIDOTTE, juzuu ya 3, uk. 345). Limetumika kwa maana mbalimbali (mara nyingi hutegemea muktadha mzima). Ifuatayo ni mifano michache iliyochaguliwa.

1. vitu vya kale a. watu, Mwa. 6:4; 1 Sam. 27:8; Yer. 5:15; 28:8

Page 141: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

125

b. sehemu mbali mbali, Isa. 58:12; 61:4 c. Mungu, Zab. 93:2; Mith. 8:23; Isa. 63:16 d. Vitu, Mwa. 49:26; Ayubu 22:15; Zab. 24:7,9; Isa. 46:9 e. Muda, Kumb. 32:7; Isa. 51:9; 63:9,11

2. wakati ujao a. Maisha ya mtu, Kut. 21:6; Kumb. 15:17; 1 Sam. 1:22; 27:12 b. Ukosoaji sana juu ya kutoa heshima kwa mfalme, 1 Fal. 1:31; Zab. 61:7; Neh. 2:3 c. Kuendelea kuwepo kwa

1) Dunia, Zab. 78:69; 104:5; Wimb. 1:4 2) mbingu, Zab. 148:5

d. uwepo wa Mungu 1) Mwa. 21:33 2) Kut. 15:18 3) Kumb. 32:40 4) Zab. 93:2 5) Isa. 40:28 6) Yer. 10:10 7) Dan. 12:7

e. Agano 1) Mwa. 9:12,16; 17:7,13,19 2) Kut. 31:16 3) Law. 24:8 4) Hes. 18:19 5) 2 Sam. 23:5 6) Zab. 105:10 7) Isa. 24:5; 55:3; 61:8 8) Yer. 32:40; 50:5

f. Agano maalum na Daudi 1) 2 Sam. 7:13,16,25,29; 22:51; 23:5 2) 1 Fal. 2:33,45; 9:5 3) 2 Nya. 13:5 4) Zab. 18:50; 89:4,28,36,37 5) Isa. 9:7; 55:3

g. Masihi wa Mungu 1) Zab. 45:2; 72:17; 89:35-36; 110:4 2) Isa. 9:6

h. Sheria za Mungu 1) Kut. 29:28; 30:21 2) Law. 6:18,22; 7:34; 10:15; 24:9 3) Hes. 18:8,11,19 4) Zab. 119:89,160

i. Ahadi za Mungu 1) 2 Sam. 7:13,16,25; 22:51 2) 1 Fal. 9:5 3) Zab. 18:50 4) Isa. 40:8

j. Uzao wa Ibrahimu na ahadi ya nchi 1) Mwa. 13:15; 17:19; 48:4 2) Kut. 32:13 3) 1 Nya. 16:17

Page 142: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

126

k. Sherehe za kimaagano 1) Kut. 12:14,17,24 2) Law. 23:14,21,41 3) Hes. 10:8

l. Milele, ya kudumu 1) 1 Fal. 8:13 2) Zab. 61:7-8; 77:8; 90:2; 103:17; 145:13 3) Isa. 26:4; 45:17 4) Dan. 9:24

m. Nini kile Zaburi inakisema waaamini watakifanya milele 1) kutoa shukurani, Zab. 30:12; 79:13 2) kudumu katika uwepo Wake, Zab. 41:12; 61:4,7 3) Imani katika Rehema Yake, Zab. 52:8 4) kumsifu Bwana, Zab. 52:9 5) kuimba sifa, Zab. 61:8; 89:1 6) kuitangaza haki yake, Zab. 75:7-9 7) kulitukuza jina lake, Zab. 86:12; 145:2 8) Kubariki jina lake, Zab. 145:1

n. limetumika katika Isaya kuelezea enzi mpya 1) agano la kudumu, Isa. 24:5; 55:3; 61:8 2) YHWH ni Mwamba wa kudumu, Isa. 26:4 3) furaha ya kudumu, Isa. 35:10; 51:11; 61:7 4) Mungu wa milele, Isa. 40:28 5) wokovu wa kudumu, Isa. 45:17 6) wema wa kudumu, Isa. 54:8 7) ishara ya kudumu, Isa. 55:13 8) jina la kudumu, Isa. 56:5; 63:12,16 9) nuru ya kudumu, Isa. 60:19,20

matumizi yaliyojikita kinyume yahusianayo na hukumu ya milele juu ya wale waovu yanapatikana katika Isa. 33:14, "moto wa milele." Isaya mara nyingi anatumia "moto" kuielezea ghadhabu ya Mungu (kama vile Isa. 9:18,19; 10:16; 47:14), lakini ni katika Isa. 33:14 tu ndiyo inaelezea kama "ya kudumu."

3. ni nyakati zilizopita na zijazo ("toka milele na milele") a. Zab. 41:13 (sifa kwa Mungu) b. Zab. 90:2 (Mungu mwenyewe) c. Zab. 103:17 (wema wa Bwana)

Kumbuka, muktadha ndio unaamua dhima ya maana ya maneno. Maagano ya milele na ahadi ni ya kimashariti (yaani Yeremia 7, angalia Mada Maalum: Agano). Kuwa mwangalifu juu ya usomaji wa maoni yako ya sasa au mpangilio wa thiolojia ya Agano Jipya katka kila utumiaji wa neno lisilo na maana. Kumbuka, sisi pia, agano jipya linajumuisha ahadi zote za Agao la Kale (angalia Mada Maalum: Unabii wa Agano la Kale ya mambo yajayo dhidi ya Unabii wa Agano Jipya).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 6:60-65 60 Basi watu wengi miongoni mwa wanafunzi wake waliposikia, walisema, Neno hili ni gumu, ni nani awezaye kulisikia? 61 Naye Yesu akafahamu nafsini mwake ya kuwa wanafunzi wake wanalinung'unikia neno hilo, akawaambia, Je! Neno hili linawakwaza? 62 Itakuwaje basi, mmwonapo Mwana wa Adamu akipaa huko alikokuwako kwanza? 63 Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima. 64 Lakini kuna wengine miongoni mwenu wasioamini. Kwa maana Yesu alijua tangu mwanzo ni nani wasioamini, naye ni nani atakayemsaliti. 65 Akasema, Kwa sababu hiyo nimewaambia ya kwamba

Page 143: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

127

hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amejaliwa na Baba yangu.

6:60 “watu wengi miongoni mwa wanafunzi” Matumizi ya neno “wanafunzi” ina maana pana. Katika Yohana neno hili na “kuyamini” yanatumika kwa pamoja kwa ajili ya (1). Wafuasi wa kweli (Yohana 6: 68) na (2). Wafuasi wa muda (Yohana 6:64, kama vile Yohana 8:31-47) ◙ “waliposikia…. wakasema” kuna kitendo kwenye neno “waliposikia” Walisikia maneno ya Yesu lakini hawakuyaelewa na kuyafanyia kazi. Kwa maana hii neno hili la Kiyunani linafanya kazi sawa na Kiebrania shema (kama vile Kumb. 4:1; 5:1 ; 6:3-4 ; 27:9-10) 6:62 Hii ni sentensi yenye masharti daraja la kwanza ambayo haijakamilika na haina hitimisho. Uhusishaji hapa ni kama wangeliona (kama vile matendo 1) Baada ya kifo/ufufuo/kupaa na kuja kwa roho, mengi ya mafundisho ya Yesu na matendo yangeonyesha maana kwao. ◙ “Akipaa huko alikokuwako kwanza” Huu ni mwendelezo wa msisitizo juu ya Yesu kuhusu “Kushuka chini kutoka mbinguni” Inazungumzia uwepo wake kabla, na Baba yake mbinguni na ushirikiano wake wa karibu na Baba yake aliye mbinguni (kama vile Yohana 17:5; 24)

MADA MAALUMU: KUPAA

Yesu alipaa kwenda mbinguni (kama vile Flp. 2:6-7; 2 Kor. 8:9). Na sasa amerejeshwa katika utukufu Wake wa awali (kama vile Yohana 1:1-3; 17:5; Efe. 4:10; 1 Tim. 3:16; 1 Yohana 1:2). Yeye amekaa mkono wa kuume wa Mungu (kama vile Zab. 110:1; Luka 22:69; Mdo. 2:33; Rum. 8:34; Efe. 1:20; Kol. 3:1; Ebr. 1:3; 8:1; 10:12; 12:2; 1 Pet. 3:22). Huu ni uthibitisho wa ukubalifu wa Baba kwa uhai na maisha yake! Kuna idadi tofauti tofauti ya maneno ya Kiyunani yaliyotumika kuelezea juu ya kupaa kwa Yesu mbinguni:

1. Mdo. 1:2,11,22; analambanō, kunyakuliwa (kama vile 1 Tim. 3:16) 2. Mdo. 1:9, epairō, kutazama juu, kuinua, kunyakua 3. Luka 9:51, analēpsis (kwa mtindo wa #1) 4. Luka 24:51, diistēmi, kusambaa

Katika Injili ya Yohana kuna vidokezo mbali mbali vya akurudi minguni kwa Yesu (kama vile Yohana 7:33; 8:14,21; 12:33-34; 13:3,33,36; 14:4,5,12,28; 16:5,10,17,28; 26:7) 5. Yohana 3:13; 20:17, ana BeBēken, amekwenda zake 6. Yohana 6:62, anabainō, kupaa Tukio hili halikuchukuliwa kumbukumbu katika Injili ya Mthayo au mwishoni mwa Ijili ya Marko katika 16:8, lakini moja wa maongezeko ya waandishi wa baadaye inaeleza tukio katika Marko 16: 19 (yaani, analambanō). Katika Matendo Kuna vidokezo kadha wa kadha kumhusu Yesu kurudi huko mbinguni.

1. Petro – Mdo. 2:33; 3:21 2. Stefano – Mdo.7:55-56 3. Paulo - Mdo. 9:3,5, 22:6-8; 26:13-15

6:63 Mstari huu kwa sababu ya mazingira mapana ya Yohana 6, unaweza ukahusishwa na tofauti kati ya Agano la Kale na Agano Jipya, Musa na Yesu (kama vile Yohana 6:58; 2 Kor. 3:6; tazama ulinganisho wa maagano mawili katika kitabu cha Waebrania.

◙ “Roho ndiyo itiayo uzima” Hii ni moja ya mafungu mengi yanayotumika kwa wote Yesu na Roho. 1. Mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake (Yohana 7:38-39) 2. Naye angalikupa maji yaliyo hai (Yohana 4:10-14) 3. Ndiye Roho wa kweli (Yohana 14:17 ; 15:26 ; 16:13) 4. Mimi ndimi njia, na kweli (Yohana 14:6) 5. Naye atawapa Msaidizi mwingine (Yohana 14:16 ; 26 ; 15:26 ; 16:17)

Page 144: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

128

6. Na Yesu ni msaidizi (1 Yohana 2:1) Angalia Mada Maaalum katika 14:16 Tazama katika mstari huu kuwa “roho” (pneuma) inatumika katika maana mbili maalum

1. Roho Mtakatifu (kama vile Yohana 4:32 ; 333; 2. Kiroho zaidi (kama vile Yohana 10:24 11:33 ; 13:21

Katika Yohana 3:5, 6, 8 ni vigumu kujua nini kinamaanishwa kuwa ni Yohana, yumkini wote.

MADA MAALUMU: ROHO (pneuma) KATIKA AGANO JIPYA)

Neno la Kiyunani "roho" limetumika katika njia mbali mbali kwenye Agano Jipya. Hapa kuna baadhi ya maelezo yenye upambanuzi na mifano.

A. Mungu wa Utatu (angalia Mada Maalumu: Utatu) 1. wa Baba (kama vile Yohana 4:24) 2. wa Mwana (kama vile Rum. 8:9-10; 2 Kor. 3:17; Gal. 4:6; 1 Pet. 1:11) 3. wa Roho Mtakatifu (kama vile Marko 1:11; Mt. 3:16; 10:20; Yohana 3:5,6,8; 7:39; 14:17; Mdo. 2:4;

5:9; 8:29,35; Rum. 1:4; 8:11,16; 1 Kor. 2:4,10,11,13,14; 12:7) B. wa nguvu ya maisha ya mwanadamu

1. wa Yesu (kama vile Marko 8:12; Yohana 11:33,38; 13:21) 2. wa mwanadamu (kama vile Mat. 22:43; Mdo. 7:59; 17:16; 20:22; Rum. 1:9; 8:16; 1 Kor. 2:11; 5:3-5;

7:34; 15:45; 16:18; 2 Kor. 2:13; 7:13; Flp 4:23; Kol. 2:5) 3. mambo ambayo Roho huzalisha ndani na kupitia roho za wanadamu

a. isio roho ya utumwa dhidi roho ya kuasili - Rum. 8:15 b. roho ya unyenyekevu – 1 Kor. 4:21 c. roho ya imani – 2 Kor. 4:13 d. rohoa ya hekima na ufunuo katika maarifa Yake – Efe. 1:17 e. isio roho ya woga dhidi ya nguvu, pendo, na heshima – 2 Tim. 1:7 f. roho ya ukengeufu dhidi ya roho ya ukweli – 1 Yohana 4:6

C. wa ulimwengu wa kiroho 1. viumbe vya kiroho

a. walio wazuri (yaani, malaika, kama vile Matendo 23:8-9; Ebr. 1:14) b. walio waovu (yaani, pepo wabaya, kama vile Mt. 8:16; 10:1; 12:43,45; Matendo 5:16; 8:7;

16:16; 19:12-21; Efe. 6:12) c. pepo (kama vile Luka 24:37)

2. roho ya utambuzi (kama vile Mt. 5:3; 26:41; Yohana 3:6; 4:23; Mdo. 18:25; 19:21; Rum. 2:29; 7:6; 8:4,10; 12:11; 1 Kor. 14:37)

3. mambo ya kiroho (kama vile Yohana 6:63; Rum. 2:29; 8:2,5,9,15; 15:27; 1 Kor. 9:11; 14:12) 4. karama za kiroho (kama vile 1 Kor. 12:1; 14:1) 5. uvuvio wa Roho (kama vile Mt. 22:43; Luka 2:27; Efe. 1:17) 6. Viungo ya kiroho (kama vile 1 Kor. 15:44-45)

D. uainishaji 1. mtazamo wa ulimwengu (kama vile Rum. 8:15; 11:8; 1 Kor. 2:12) 2. mchakato wanadamu wa kufikiri (kama vile Mdo 6:10; Rum. 8:6; 1 Kor. 4:2)

E. wa ulimwengu wa kimwili 1. wingu (kama vie Mt. 7:25,27; Yohana 3:8; Mdo. 2:2) 2. pumzi (kama vile Mdo. 17:25; 2 The. 2:8)

Ni dhahiri kwamba neno hili linapaswa kufasiriwa katika upande wa mazingira ya sasa. Kuna maana mbalimbali ya vivuli ambavyo vinaweza kurejerewa (1) ulimwengu wa kiroho; (2) ulimwengu usioonekana; (3) pamoja na watu wa ulimwengu huu wa kiroho au ulimwengu dhahiri. Roho Mtakatifu ni sehemu ile ya Utatu ambaye ni mtendaji mkuu katika hatua hii ya historia. Enzi mpya za Roho zimekuja. Vyote vilivyo vizuri, vitakatifu, vya haki, na vinavyohusiana naye kweli kweli. Uwepo Wake,

Page 145: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

129

karama, na huduma ni muhimu katika ukuzaji wa injili na mafanikio ya Ufalme wa Mungu (kama vile Yohana 14 na 16). Havutii upande wake Mwenyewe, bali kwa Kristo (kama vile Yohana 16:13-14). Anasadikisha, hushawishi, hubatiza, anabatiza, na anawakomaza waamini wote (kama vile Yohana 16:8-11).

6:64 Kundi hili la wazi lakini la wafuasi waongo, linapunguzwa toka kwa mfuasi mwongo – Yuda (kama vile Yohana 6:70-71 ; 3:11) Bila shaka kuna miujiza inahusika katika ngazi ya kuamini.

MADA MAALUMU: UASI (APHISTĒMI)

Neno la Kiyunani aphistēmi lina uwanja mpana wa elimu-maana. Hata hivyo, Neno la Kiingereza "uasi" limetokana na neno hili na athari za matumizi yake kwa wasomaji wa sasa. Muktadha, kama iliyo kawaida, ndio ufunguo, sio maelezo ya wakati uliopo. Hili ni neno lililounganishwa kutokana na kihusishi apo, ambacho kinamaanisha "kutokana na" au "mbali na" and histēmi, "kukaa," "kusimama," au "kupachika." Angalia matumizi yafuatayo (yasiyo ya kithiolojia):

1. kuondoa kimwili 1. kutoka Hekaluni, Luka 2:37 2. kutoka katika nyumba, Marko 13:34 3. kutoka kwa mtu, Marko 12:12; 14:50; Matendo 5:38 4. kutoka katika vitu vyote, Mt. 19:27,29

2. kuondoa kisiasa, Matendo 5:37 3. kuondoa kimahusiano, Matendo 5:38; 15:38; 19:9; 22:29 4. kuondoa kisheria (tarakisha), Kumb. 24:1,3 (LXX ) na Agano Jipya, Mt. 5:31; 19:7; Marko 10:4; 1 Kor.

7:11 5. kuondao deni, Mt. 18:7 6. kuonyesha kutokuhusika kwa kuondoka, Mt. 4:20; Yohana 4:28; 16:32 7. kuonyesha kutokuhusika kwa kutoondoka, Yohana 8:29; 14:18 8. kuruhsu au kutoa kibali, Mt. 13:30; 19:14; Marko 14:6; Luka 13:8

Katika maana ya kitheolojia KITENZI pia kina matumizi mapana: 1. kufuta, kusamehe, kuifuta hatia ya dhambi, Kut.32:32 (70) (LXX); Hes. 14:19; Yak. 42:10 na Agano Jipya,

Mat. 6:12,14-15; Marko 11:25-26 2. kujiondoa toka dhambini, 2 Tim. 2:1 3. kukataa kwa kujiondoa toka kwenye

a. Sheria, Mt. 23:23; Matendo 21:21 b. imani, Ezek. 20:8 (LXX ); Luka 8:13; 2 The. 2:3; 1 Tim. 4:1; Ebr. 3:12

Waamini wa sasa wanauliza maswali mengi ya kitheolojia ambayo waandishi wengi wa Agano Jipya wasingalifikiri kuyahusu. Moja ya haya yangeliweza kuhusiana na uelekeo wa sasa wa kuitenga imani (uthibitisho) kutoka kwenye imani (utakaso). Kuna watu katika Biblia walihusishwa miongoni mwa watu wa Mungu na jambo lililotokea na kusababisha wao kuondoka.

I. Agano la Kale A. Wale walioisikia taarifa ya wale wapelelezi kumi na wawili (kumi), Namba 14 (kama vile Heb. 3:16-19) B. Kora, Namba 16 C. Wana wa Eli, 1 Samueli 2, 4 D. Sauli, 1 Samueli 11-31 E. Manabii wa uongo (mifano)

1. Kumb. 13:1-5 18:19-22 (njia za kumtambau nabii wa uongo) 2. Yeremia 28 3. Ezekieli 13:1-7

F. Manabii wa uongo 1. Ezekieli 13:17

Page 146: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

130

2. Nehemia 6:14 G. Uovu wa viongozi wa Israeli (mifano)

1. Yeremia 5:30-31; 8:1-2; 23:1-4 2. Ezekieli 22:23-31 3. Mika 3:5-12

II. Agano Jipya A. Hili neno la Kiyunani kifasihi linamaanisha "kuasi."Vitabu vyote vya Agano la Kale na Agano Jipya

vinathibitisha uchochezi wa uovu na mafundisho ya uongo kabla ya Ujio wa Pili (kama vile Mt. 24:24; Marko 13:22; Matendo 20:29, 30; 2 The. 2:9-12; 2 Tim. 4:4). Neno hili la Kiyunani linaweza kuyaaakisi maneno ya Yesu katika Mfano wa Udongo unaopatikana katika Mathayo13; Marko 4; na Luka 8. Kwa kudhaniwa walimu hawa wa uongo si Wakristo, bali waamini wachanga (kama vile Ebr. 3:12). Swali la kitheolojia ni hili walimu wa uongo wanawapeleka wapi waamini? Hili ni vigumu kulijibu kwa kuwa kulikuwa na walimu wa uongo katika makanisa anzilishi (kama vile 1 Yohana 2:18-19). Mara nyingi tamaduni au madhehebu yetu yanajibu swali hili pasipokuwa na marejeo ya maandiko ya Biblia mahususi (isipokuwa njia ya kuhakiki kwa nukuu mstari ulio nje ya muktadha ili kwa uangalifu kuhakiki madhara yaliyomo).

B. Imani Thabiti 1. Yuda, Yohana 17:1 2. Simoni mchawi, Matendo 8 3. Wale waliozungumziwa katika Mt. 7:13-2 4. Wale waliozungumziwa katika Mathayo 13; Marko 4; 5. Wayahudi wa Yohana 8:31-59 6. Iskanda na Himenayo, 1 Tim. 1:19-20 7. Wale wa 1 Tim. 6:21 8. Himanayo na Fileto, 2 Tim. 2:16-18 9. Dema, 2 Tim. 4:10 10. Walimu wa uongo, 2 Pet. 2:19-22; Yuda 1:12-19 11. Wapinga Kristo, 1 Yohana 2:18-19

C. Imani isiyo kuwa na matunda 1. 1 Wakorintho 3:10-15 2. 2 Petro 1:8-11

Mara chache tunafikiri juu ya haya maandiko kwa kuwa mfumo wa injlili yetu (Ufuatao mtazamo wa Calvin, Arminian, n.k.) unaamuru mwitikio wa kimamlaka. Tafadhari usinihukumu kabla kwa kuwa nafundisha somo langu. Shauku yangu ni hatua ya kiufasiri. Tunapaswa kuipa nafasi Biblia ili izungumze nasi na si kuiumba katika mpangilio wa thiolojia iliyopita. Mara nyingi hii inaumiza na kushtua kwa kuwa thiolojia zetu zilizo nyingi ni za kimadhehebu, kitamaduni, kimahusiano (mzazi, rafiki, mchungaji), si za kibiblia (tazama Mada Maalumu: Nini maana ya neno "Kupokea," "Kuamini," "Kiri/Ungama?). Wengine walio miongoni mwa watu wa Mungu wanarudi nyuma na kutokuwa miongoni mwa watu wa Mungu (m.f. Rum. 9:6).

6:65 Hii inaelezea ukweli ule ule kama katika Yohana 6:44. Mwanadamu aliyeanguka hamtafuti Mungu kwa jitihada zake mwenyewe (kama vile Rum. 39:18 kwa mfululizo wa nukuu za Agano la Kale ambalo linasisitiza hali ya dhambi ya binadamu na uasi).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 6:66-71 66Kwa ajili ya hayo wengi miongoni mwa wanafunzi wake wakarejea nyuma, wasiandamane naye tena.67Basi Yesu akawaambia wale Thenashara, Je ninyi nanyi mwataka kuondoka? 68 Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani Wewe unayo maneno ya uzima wa milele. 69 Nasi tumesadiki, tena tumejua, ya kuwa wewe ndiwe mtakatifu wa Mungu.70Yesu akawajibu, Je!Mimi sikuwachagua ninyi Thenashara, na mmoja wenu ni shetani? 71Alimnenna Yuda, mwana wa Simoni Iskariote;maana huyo ndiye atakayemsaliti;naye ni mmojawapo wa wale Thenashara

Page 147: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

131

6:67 “Kumi na mbili” Haya ni matumizi ya kwanza ya Yohana ya kutumia neno la pamoja kwa ajili ya mitume (kama vile Yohana 6:70; 20:24) Tazama Mada Maalum katika Yohana 6:13 6:68 “Simoni Petro akajibu” Petro ni msemaji wa wale kumi na wawili (kama vile Mathayo 16:16). Hii haimaanishi walimwona yeye kama kiongozi wao (kama vile Yohana 9:34 na Luka 9:4-6 ; 22:24).

◙ “Wewe unayo maneno ya uzima wa milele” Ukristo ni yote mawili (1). Ukweli ulioko katika ujumbe, “maneno ya uzima wa milele.” na (2) Ukweli uliyoelezwa ndani ya nafsi Yesu. Injili, kama hiyo, ni yote mawili ujumbe na nafsi. Neno pistis laweza kuhusiana na yote (1). Ujumbe na (2) Nafsi/mtu (kama vile Yohana 1:12; 3: 15-16) Tazama Mada Maalum katika Yohana 2:23

6:69 “Nasi tumesadiki, tena tumejua” Haya yote ni matendo timilifu tendaji elekezi. Wokovu hapa upo katika wakati timilifu ikimaanisha kitendo kilichopita kikafika mwisho, kimekuja kuwa katika hali ya kuwa mwanadamu. Wokovu hapa upo kwenye wakati timilfu ukimaanisha wakati uliopita, tendo lililofikia kilele limekuwa ni mahali pa watu. Wokovu wa kweli unahusiana na njeo za vitenzi vyote vya Kiyunani. Angalia Mada Maalum: Njeo za Vitenzi Vya Kiyunani Vitumikavyo kwa ajili ya Wokovu katika Yohana 9:7

NASB, NRSV NJB “Wewe u Mtakatifu wa Mungu” NKJV “Wewe ni Kristo mwana wa Mungu aishiye” TEV “Wewe ni Mtakatifu uliekuja toka kwa Mungu” Kuna tatizo la kimaandishi katika pointi hii. Andika (NASB, NRSV, NJB) linasaidiwa na maandishi ya zamani ya Kiyunani p75, א, B, C, D, L, and W. L Waandishi wa baadaye bila shaka walionyesha nyongeza ya maneno kutoka kwa Martha katika Yohana 11:27 au ya Petro na Mathayo 16:16; UBS” inatoa andiko fupi zaidi linalopewa kiwango cha alama“A” (lenye uhakika). Fungu la “mtakatifu pekee wa Mungu” ni kichwa cha habari cha Masiha katika Agano la kale. Imedokezwa katika Luka 4:34. Tazama Mada Maalum katika 1 Yohana 2:20. Huu ni ukiri mwingine ya imani kwa wale kumi na wawili sawa na Mathayo 16. 6:70 “Je! Mimi sikuwachagua ninyi Thenashara” Huu ni msisitizo mwingine katika uchaguzi wa Mungu wa mitume (kama vile Yohana 6:40 na 65. Angalia swali la Yesu katika Yohana 6:67, uchaguzi wa Mungu na hiari ya mwanadamu lazima vibakie katika mvutano wa Kibiblia, kuna pande mbili za ushirika wa agano.

◙ “na mmoja wenu ni shetani” Ni maneno ya kushangaza kiasi gani? Wala hayamlengi mmojawapo wa kikundi cha mitume waliorudi (kama vile Yohana 6:66) lakini ni kwa mmoja wao wa mitume waliochaguliwa waliotangaza imani ndani yake. Wengi wameunganisha hili na Yohana 13:2 au 27. Kuna maswali kadhaa yanayohusiana na uelewa wetu wa mstari huu.

1. Kwa nini Yesu alimchagua ibilisi? 2. Neno lina maana gani katika mazingira haya?

Swali la kwanza linahusiana na ubashiri wa unabii (kama vile Yohana 17:12; Zab 41:9) Yesu alijua nini Yuda angefanya. Yuda ni mfano wa mwisho wa dhambi isiyotubiwa. Alimkataa Yesu baada ya kuwa amemsikia, amemwona na kuwa naye kwa miaka kadhaa. Swali la pili lina uwezekano wa maana mbili

1. Wengine wanalihusisha hili na ibilisi (limetumika pia kama shetani katika Mdo. 13:10 na Ufunuo 20:2) wakaingia Yuda (kama vile Yohana 13:2 ; 27)

2. Bila shaka neno linatumika kwa ujumla (bila kibainishi kama 1 Tim. 3:11; 2 Tim. 33:3 na Tito 2:3) Yuda alikuwa mshitaki, katika maana ya Agano la Kale, kama alivyo shetani (tazama Mada Maalum katika Yohana 12:31. Neno la Kiyunani linamaanisha mzushi, mwenye kashfa au mwenye kisa.

Page 148: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

132

6:71 “Simoni Iskariote” kuna nadharia kadhaa kuhusu neno hili (neno lina herufi tofauti katika maandishi mbalimbali ya Kiyunani, inaweza kuwa ;

1. Mtu wa Kerioth – mji wa Yuda 2. Mtu wa Kartan - Mji wa Galilaya 3. Mfuko wa ngozi uliotumika kubeba pesa 4. Neno la Kiebrania kwa “kujinyonga” 5. Neno la Kiyunani kwa kisu cha kuulia

Kama #1 ni kweli alikuwa M-yudea pekee katika kumi na mbili. Kama ni kweli alikuwa kama Simoni. Hivi karibuni pameandikwa kitabu kinachotafsiri Yuda katika mwanga chanya. Kitabu kinaitwa Judas, Betrayer au Friend of Jesus (Msaliti wa Yuda au rafiki wa Yesu) kilichoandikwa na William Klassen, Fortress Pess 1996. Tatizo langu ni kwamba haichukui maoni kwa dhati kutoka katika injili ya Yohana. ◙ “Kusaliti” Neno hili la Kiyunani linafasiliwa kwa upana na katikia mazingira haya haibainishi kitu/iko katikati/haipendelei upande wo wote. Hata hivyo kufuatana na Yuda kumkabidhi Yesu kwa mamlaka kulibainisha ulaya Taz mada maalum katika Yohana 18:2

MASWALI YA MJADALA

Huu ni mwongozo wa fasiri, ina maanisha kwamba unawajibika kwa tafsiri zako mwenyewe za Biblia. Kila mmoja wetu lazima atembee katika mwanga tulio nao. Wewe, Biblia, na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Hutakiwi uvitelekeze vitu hivi kwa mfasiri. Maswali ya mjadala huu yanatolewa kukusaidia kufikiri juu ya mambo makubwa ya sehemu za kitabu hiki. Yanalenga kukuamsha kimawazo na sio kutoa maana.

1. Je Yohana 6 ni mjadala wa chakula cha usiku cha Bwana? Kwa nini ndiyo au siyo? 2. Yesu alikuwa anadai nini aliposema “Mimi ni mkate wa uzima?” 3. Kwa nini Yesu alitoa maneno yenye utata kiasi kile kwa umati huo?

Page 149: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

133

YOHANA 7

MIGAWANYO YA AYA YA TAFSIRI ZA KISASA

UBS4 NKJV NRSV TEV NJB Kutokuamini Ndugu Ndugu zake Yesu Yesu, Maji ya Uzima Yesu na Ndugu Zake Yesu alikwenda za Yesu hawakumwamini Yerusalemu kwa ajili ya Sikukuu na Kufundisha Huko 7:1-9 7:1-9 7:1-9 7:1-9 7:1 Yesu Katika Sikukuu Shule ya Kimbingu Yesu Katika Sikukuu 7:2-9 ya Vibanda ya vibanda 7:10-13 7:10-24 7:10-13 7:10-11 7:10-13 7:12-13 7:14-24 7:14-18 7:14-15 7:14-24 7:16-19 7:19-24 7:20 7:21-24 Huyu Ndiye Kristo? Huyu Huyu ndiye Masihi Watu Wanajadili Anaweza Kuwa Juu ya Asili ya Kristo? Masihi 7:25-31 7:25-31 7:25-27 7:25-27 7:25-27 7:25-31 7:25-31 7:25-27 7:25-27 7:28-29 7:28-29 7:30-31 7:30 Watumishi Yesu na Viongozi Askali Walitumwa Yesu anatabiri Walitumwa wa Kidini Kumkamata Yesu Kuondoka KumkamataYesu Kwake 7:31-34 7:32-36 7:32-36 7:32-36 7:32-34 7:35-36 7:35-36 Mito yaMaji Ahadi ya Ahadi ya Maji Ya Uzima Roho Mtakatifu ya Uzima 7:37-39 7:37-39 7:37-39 7:37-39 7:37-38 7:39 Matengano baina Ni nani huyu? Matengano baina Ugunduzi ya Watu ya Watu Asili ya Masihi 7:40-44 7:40-44 7:40-44 7:40-44 7:40-44 Kutokuamini Kukataliwa na Kutokuamini kwa kwa Wale walioko Wenye Mamlaka Wakuu wa Makuhani katika Mamlaka 7:45-52 7:45-52 7:45-52 7:45 7:45-52 7:46 7:47-49 7:50-51 7:52

Page 150: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

134

MZUNGUKO WA TATU WA USOMAJI KUFUATILIA KUSUDIO LA ASILI LA MWANDISHI KATIKA NGAZI YA AYA Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwatafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Aya ya kwanza 2. Aya ya pili 3. Aya ya tatu 4. N.k

UTAMBUZI WA MUKTADHA WA MISTARI YA 1-52

A. Mpangilio wa Yohana 5 na 6 ni Sikukuu ya Pasaka. Mpangilio wa Yohana 7:1 kupitia Yohana 10:21 ni Sikukuu ya Mahema (Yohana 7:2 na kuendelea).

B. Sikukuu ya Mahema kimsingi ilikuwa shukrani kwa ajili ya mavuno (iliyoitwa Sikukuu ya Mavuno, kama

vile Kutoka 23:16; 34:22). Pia kilikuwa kipindi cha kukumbuka tukio la Kuhamishwa (iliyoitwa Sikukuu ya Vibanda, kama vile Law. 23:29-44 na Kumb. 16:13-15). Ilitokea mnamo tarehe 15 ya mwenzi Tishri, ambayo inafanana na mwishoni mwa mwezi wetu wa Tisa au mwanzoni mwa mweziwa Kumi.

C. Yohana 7 na 8 uhasama iliohimarishwa na Wayahudi dhidi ya Yesu kuivunja Sabato (Yohana 5:16) na dai

Lake la yeye kuwa mmoja na YHWH (Yohana 5:18). Nukuu majaribio ya dadi ya maandishi ambayo yametajwa 1. Mkamateni, Yohana 7:30,32, 44; 10:39 2. Muuwe, Yohana 7:1,19,25; 8:37,40 (pia Yohana 11:53)

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 1:1-9 1 Na baada ya hayo Yesu alikuwa akitembea katika Galilaya; maana hakutaka kutembea katika Uyahudi, kwa sababu Wayahudi walikuwa wakitafuta kumwua. 2 Na sikukuu ya Wayahudi, Sikukuu ya Vibanda, ilikuwa karibu. 3 Basi ndugu zake wakamwambia, Ondoka hapa, uende Uyahudi, wanafunzi wako nao wapate kuzitazama kazi zako unazozifanya. 4 Kwa maana hakuna mtu afanyaye neno kwa siri, naye mwenyewe ataka kujulikana. Ukifanya mambo haya, basi jidhihirishe kwa ulimwengu. 5 Maana hata nduguze hawakumwamini. 6 Basi Yesu akawaambia, Haujafika bado wakati wangu; ila wakati wenu sikuzote upo. 7 Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi; bali hunichukia mimi, kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovu. 8 Kweeni ninyi kwenda kula sikukuu; mimi sikwei bado kwenda kula sikukuu hii, kwa kuwa haujatimia wakati wangu. 9 Naye alipokwisha kuwaambia hayo, alikaa vivi hivi huko Galilaya.

7:1 "Na baada ya hayo" Hii ni njia ya kifasihi ya kuziendeleza fikra, na si alama ya dunia hii (kama vile Yohana 5:1; 6:1; 7:1; 21:1). ◙ "Wayahudi walikuwa wakitafuta kumwua" Katika Yohana "Wayahudi" mara nyingi wanadokeza uovu (kama vile Yohana 1:19; 2:18,20; 5:10,15,16; 6:41,52; 7:1,11,13,35; 8:22,52,57; 9:18,22; 10:24,31,33; 11:8; 19:7,12; 20:19). Kusudio lao la chuki na mauaji yameandikwa mara kadhaa (kama vile Yohana 5:16-18; 7:19,30,44; 8:37,40,59; 10:31,33,39; 11:8,53).

Page 151: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

135

7:2 "Na sikukuu ya Wayahudi, Sikukuu ya Vibanda" Hii pia iliitwa Sikukuu ya Vibanda (kama vile Law. 23:34-44; Kumb. 16:13-17) kwa sababu wakati wa mavuno wanakijiji waliishi katika majengo madogo madogo yaliyokuwa mashambani, ambayo yalikuwa ukumbusho wa Wayahudi juu ya tukio lao la Kuhamishwa. Taratibu na kanuni zao za ibada za sikukuu hii zinatoa historia ya nyuma ya mafundisho ya Yesu katika Yohana 7:1-10:2, kama ilivyokuwa sikukuu ya Pasaka katika Yohana 5-6. 7:3 “ndugu zake” Hii inataja mwanzo wa familia ya Yesu kuanzia kwa Yohana 2:12. Ni dhahiri kwamba hawakuielewa nia Yake, mbinu, au sababu.

◙ "Ondoka hapa, uende Uyahudi" Hii inarejea juu ya msafara wa kila mwaka waliokuwa wakienda hija (kama vile Luka 2:41-44) ambao waliondoka Galilaya na kutembea umbali mrefu kuelekea Yerusalem. Kumbuka kwamba Injili ya Yohana iliangalia juu ya huduma ya Yesu katika Yerusalemu.

7:4 "kujulikana" Tazama Mada Maalumu ifuatayo.

MADA MAALUMU: UJASIRI (parrhēsia)

Neno hili la Kiyunani ni muungno wa maneno "yote" (pan) na "(rhēsis)”. Uhuru huu au ujasiri katika usemi mara nyingi una maana nyingine ya ushujaa katikati ya upinzani au ukataliwaji (kama vile Yohana 7:13; 1 The. 2:2). Katika maandiko ya Yohana (limetumika mara 13) mara nyingi huonesha tangazo la wazi wazi (kama vile Yohana 18:20, pia katika maandiko ya Paulo, Kol. 2:15). Hata hivyo, wakati mwingine kwa maana ya kawaida ni "kwa uwazi" (kama vile Yohana 10:24; 11:14; 16:25,29). Katika Matendo Mitume wanazungumzia ujumbe unaomhusu Yesu katika namna ile ile (kwa ujasiri) kama Yesu alivyozungumza kumhusu Baba na mipango na ahadi Zake (kama vile Mdo. 2:29; 4:13,29,31; 9:27-28; 13:46; 14:3; 18:26; 19:8; 26:26; 28:31). Pia Paulo ilihitaji msaada wa maombi ambapo kwa ujasili angeliweza kuihubiri injili (kama vile Efe. 6:19; 1 The. 2:2) na kuiishi injili (kama vile Flp. 1:20). Tumaini la Paulo la mambo yahusuyo kifo, hukumu na pepo katika Kristo lilimpa ujasiri na kijiamini katika kuihubiri injili katika zama hizi za sasa za uovu (kama vile 2 Kor. 3:11-12). Pia alikuwa na iamani kwamba wafuasi wa Kristo wangefanya kazi kwa namna ya kufaa sana (kama vile 2 Kor. 7:4). Kuna kipengele kimoja zaidi cha neno hili. Kitabu cha Waebrania kinatumia neno hili katika maana ya kipekee ya ujasiri wa mwamini, kumwendea Mungu na kuzungumza Naye (kama vile Heb. 3:6; 4:16; 10:19,35). Waamini wanakubaliwa na kwa ukamilifu na kukaribishwa katika ukaribu na Baba kupitia Mwana (kama vile 2 Kor. 5:21)! Katika Agano Jipyali linatumika katika njia kadhaa.

1. imani, ujasiri, au moyo wa kujiamini inahusiana na a. wanaume (kama vile Mdo. 2:29; 4:13,31; 2 Kor. 3:12; Efe. 6:19) b. Mungu (kama vile 1 Yohana 2:28; 3:21; 4:12; 5:14; Ebr. 3:6; 4:16; 10:19)

2. kuzungumza wazi, dhahiri, au bila na utata (kama vile Marko 8:32; Yohana 7:4,13; 10:24; 11:14; 16:25; Mdo. 28:31)

3. kwa kuzunza hadharani (kama vile Yohana 7:26; 11:54; 18:20) 4. muundo uhusianao (parrhēsiazomai) unatumika kuhubiri kwa ujasiri katikati ya mazingira magumu

(kama vile Matendo 18:26; 19:8; Efe. 6:20; 1 The. 2:2)

◙ "Ukifanya" Hii ni sentensi shurutishi daraja la kwanza ambayo inadhaniwa kuwa ya kweli kutoka katika mtazamo wa mwandishi.

Page 152: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

136

◙ "basi jidhihirishe kwa ulimwengu" Yesu alichagua juu ya matumizi yao ya neno "ulimwengu" katika Yohana 7:4 na kutoa maoni juu yake katika Yohana 7:7. Ulimwengu haukukubali na kunyenyekea Kwake, bali uadui (kama vile. Yohana 15:18-19; 17:14; 1 Yohana 3:13) kwa sababu aliufunua uasi wake na dhambi (kama vile Yohana 3:19-20). Njia ya ndugu zake Yesu kwa Yesu kujifunua mwenyewe (yaani, miujiza) ilikuwa tofauti sana na njia ya Yesu (msalaba). Hapa ndipo unabii wa Isa. 55:8-11 unaokuja katika mtazamo sahihi! 7:5 "Maana hata nduguze hawakumwamini" Haya ni maoni mengine ya kihariri ya mwandishi. Ilipaswa kuwa vigumu sana kumkubali Yesu kama Masihi ulipokulia katika nyumba hiyo hiyo (kama vile Marko 3:20-21). Yesu aliwatunza maumbu wake. Moja ya mwonekano wa ufufuo wake uliopita ulikuwa kwa kusudi la kujifunua mwenyewe kwao. Walikuja kuamini (kama vile Mdo. 1:14)! Yakobo alikuwa kiongozi wa kanisa la Yerusalemu. Na wote Yakobo na Yuda waliandika vitabu vilivyowekwa katika vitabu vya Agano Jipya. 7:6 "Haujafika bado wakati wangu" Neno "wakati" (kairos) linapatika tu hapa (mara mbili) na Yohana 7:8 katika Injili na nyaraka za Yohana. BAGD inatoa maana tatu za karibu.

1. - Muda wa makaribisho wakati uliokubalika (yaani, 2 Kor. 6:2) - wakati fursa (yaani, Luka 4:13) - wakati uliopangwa (yaani, Marko 13:33; Mdo. 3:20; 1 Pet. 1:11)

2. wakati unafaa na uliokubalika - wakati unaofaa (yaani, Mt. 24:45; Luka 1:20) - wakati kamili (yaani, Yohana 7:8; 2 Tim. 4:6)

3. wakati wa hukumu (yaani, Luka 21:8; Rum. 13:11; 1 The. 5:1; 2 The. 2:6) Namba 2 na 3 zina maana zinazopishana. Yesu aliuelewa ujumbe Wake (kama vile 12:23; 13:1; 17:1-5). Kulikuwa na ratiba ya ki-Uungu kwa matukio haya ya Injili ya kuonyesha (kama vile Luka 22:22; Yohana 7:30; 8:20; Mdo. 2:23; 3:18; 4:28). 7:7 "Ulimwengu" Tazama Mada Maalumu: Kosmos (ulimwengu) katika Yohana 14:17 7:8 NASB "Ninyi nendeni kwenye sikukuu hiyo. Mimi siendi kwenye sikukuu hiyo" NKJV "Kweeni ninyi kwenda kula sikukuu; mimi sikwei bado kwenda kula sikukuu hii, NRSV, NJB "Nendeni wenyewe kwenye hiyo sikukuu. Mimi siendi kwenye hiyo sikukuu" TEV "Ninyi nendeni kwenye sikukuu. Mimi siendi kwenye sikukuu" Machapisho kadhaa ya Kiyunani (א, D, na K) hayana kielezi "bado." Inaonekana kuwa na majaribio ya weredi wa awali ili kuondoa mkanganyiko unaoonekana baina ya Yohana 7:8 na 10. Kielezi kimewekwa katika MSS P66, P75, B, L, T, na W (NKJV, Agano Jipya la karne ya Ishirini, NIV). Usemi huu mfupi ungeweza kueleweka kama

1. Siendi nanyi (si kwa sababu yenu) 2. Naondoka katikakati za siku ya sikukuu ya nane (kufunua kupitia ishara ya sikukuu)

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 7:10-13 10 Hata ndugu zake walipokwisha kukwea kuiendea sikukuu, ndipo yeye naye alipokwea, si kwa wazi bali kana kwamba kwa siri. 11 Basi Wayahudi wakamtafuta kwenye sikukuu, wakasema, Yuko wapi yule? 12 Kukawa na manung'uniko mengi katika makutano juu yake. Wengine wakasema, Ni mtu mwema. Na wengine wakasema, Sivyo; bali anawadanganya makutano. 13 Walakini hakuna mtu aliyemtaja waziwazi, kwa sababu ya kuwaogopa Wayahudi.

7:11 "Wayahudi" Katika sura hii kuna makundi matatu yaliyojitenga na Yesu.

1. Ndugu zake 2. “Wayahudi "kundi ambalo linarejea juu ya viongozi wa kidini

Page 153: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

137

3. "makutano "kundi ambalo linarejea juu ya utaratibu wa kusanyiko la kila mwaka kama njia yao ya kuielekea Sikukuu ya Vibanda

4. "watu wa Yerusalemu," ambao walikuwa watu wa jamii moja waliowajua Wakuu wa Sinagogi na mipango yao ya kumuua Yesu

7:12 "Kukawa na manung'uniko mengi katika makutano juu yake" Huu ndiyo ufanano wa kile injili ilichokifanya katika kila umati. Inaonyesha kutofautiana kwa uwezo wa kiroho na viwango vya uelewa uliopo ndani ya mwanadamu (kama vile Yohana 7:40-44). ◙ "bali anawadanganya makutano" Kitenzi planaō kinatumika kwa

1. waalimu wa uongo (yaani, Mt. 24:11; 2 Tim. 3:13; 1 Yohana 1:8; 2:26; 3:7) 2. Masihi wa uongo (yaani, Mt. 24:4-5,24; katika Yohana kuhusu vile Wayahudi walivyomfikiria Yesu kuwa

(kama vile Yohana 7:12,47; Mt. 27:63) 3. watu wamedanganyika wenyewe (kama vile 1 Kor. 3:18; 1 Yohana 1:8) au 4. kudanganyika (kama vile 1 Kor. 6:9; 15:33; Gal. 6:7; Yakobo 1:16

Neno lilitumika juu ya sayari ambazo hazikufuata mzunguko wake wa kawaida wa kundi. Sayari hizi ziliitwa "sayari zilizozurura”

7:13 “Wayahudi” Umati wote ulikuwa wa Kiyahudi. Kwa usahihi hii inaonyesha matumizi maalumu ya Yohana ya neno hili ili kurejea juu ya Yerusalemu. Tazama nukuu katika Yohana 7:1.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 7:14-18 14 Hata ikawa katikati ya sikukuu Yesu alikwea kuingia hekaluni, akafundisha. 15 Wayahudi wakastaajabu wakisema, Amepataje huyu kujua elimu, ambaye hakusoma? 16 Basi Yesu akawajibu, akasema, Mafunzo yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye aliyenipeleka. 17 Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu. 18 Yeye anenaye kwa nafsi yake tu hutafuta utukufu wake mwenyewe; bali yeye anayetafuta utukufu wake aliyempeleka, huyo ni wa kweli, wala ndani yake hamna udhalimu.

7:14 "Hata ikawa katikati ya sikukuu" Sababu barabara kwa Yesu kusubiri hadi wakati wake haidhihiriki, lakini mtu angeweza kuwaza kwamba wakati huu uliokubaliwa kwa ajili ya kusanyiko na watu wa miji kumjadili na huduma Yake. Pia ni wakati uliokubaliwa kwa viongozi wa Kiyahudi kuufunua kwa uwazi uhasama wao (kama vile Yohana 7:13).

◙ "akafundisha" matukio ya kuzungumza kwa Yesu yanabainishwa kwa 1. kufundisha, Mt. 4:23; 5:2,19; 7:29, n.k. Yohana 6:59; 7:14,28,35; 8:20,28 2. kuhubiri, Luka 4:18; 7:22; 9:6; 20:1

Haya maneno yanaonekana kutumika kwa ufanano ili kurejea juu ya upashaji habari wa Yesu juu ya kweli ya Mungu kwa uumbaji Wake. Mara nyingi ufunuo ulimaanisha kuhabarisha na kuhabarisha tena. Ufunuo huo ulidai maamuzi yenye kuendana na mabadiliko ya vipaumbele vya. Kweli hubadilisha kila kitu! 7:15 "Amepataje huyu kujua elimu, ambaye hakusoma?" Kwa urahisi hii inamaanisha kwamba kamwe hakuwai kuhudhuria katika moja ya shule maalumu za sheria za dini ya Kiyahudi, wala kuwa na dalili ya kuwa moja ya mwnafunzi wa waalimu wa sheria za dini ya Kiyahudi. Kutumika kwa neno "huyu" ina maana ya karibu na kutokuheshimu (kama vile Yohana 18:17,29). Mafundisho ya Yesu yaliwastaajabisha wasikilizaji wake mara kwa mara (kama vile Marko 1:21-22; Luka 4:22) kwa sababu ya (1) maudhui na (2) muundo. Viongozi wengine wa Kiyahudi walinukuu moja baada ya jingine; Yesu alidaiwa kumnukuu Mungu!

7:16 Tena Yesu alizingatia si unyenyekevu Wake (tazama maandiko katika Yohana 5:19) kwa Baba tu, bali pia kwa maarifa Yake ya pekee ya Baba Yake. Walikuwa na waalimu wa kale; Yeye alikuwa na Mwalimu wa kimbingu.

Page 154: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

138

7:17 "akipenda" Hii ni sentensi shurutishi daraja la tatu ambayo kinamaanisha umuhimu au uwezekano wa tendo lenyewe. Hili ni fumbo la zawadi ya injili kwa ulimwengu wote (kama vile Yohana 1:12; 3:16) na Ukuu wa Mungu (kama vile Yohana 6:44,65). Roho anapaswa kuufungua moyo (kama vile Yohana 16:8-13).

7:18 Yesu anautetea upekee wake katika utofuti na mwanadamu aliyeanguka: (1) Yeye hautafuti utukufu Wake mwenyewe; (2) Yeye anautafuta utukufu wa Baba; (3) Yeye ni kweli; na (4) Yeye hana dhambi.

◙ "utukufu wake mwenyewe" tazama maandiko katika Yohana 1:14.

◙ "wala ndani yake hamna udhalimu" Yesu angefia mbele yetu kwa sababu Hakutaka kuifia dhambi Yake mwenyewe (2 Kor. 5:21). Yesu kutokuwa na dhambi ni jambo muhimu la Kithiojia. Jambo hili linaelezwa mara nyingi na katika namna tofauti.

1. Luka 23:41 2. Yohana 6:69; 7:18; 8:46; 14:30 3. 2 Kor. 5:21 4. Ebr. 4:15; 7:26; 9:14 5. 1 Pet. 1:19; 2:22 (Isa. 53:9) 6. 1 Yohana 2:29; 3:5,7

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 7:19-24 19 Je! Musa hakuwapa torati? Wala hakuna mmoja wenu aitendaye torati. Mbona mnatafuta kuniua? 20 Mkutano wakajibu, Ama! Una pepo! Ni nani anayetafuta kukuua? 21 Yesu akajibu, akawaambia, Mimi nalitenda kazi moja, nanyi nyote mnaistaajabia. 22 Musa aliwapa tohara; lakini si kwamba yatoka kwa Musa, bali kwa mababa; nanyi siku ya sabato humtahiri mtu. 23 Basi ikiwa mtu hupashwa tohara siku ya sabato, ili torati ya Musa isije ikavunjika, mbona mnanikasirikia mimi kwa sababu nalimfanya mtu kuwa mzima kabisa siku ya sabato? 24 Basi msihukumu hukumu ya macho tu, bali ifanyeni hukumu iliyo ya haki.

7:19 Utunzi wa kisarufi unatarajia jibu la "ndiyo". ◙ “Wala hakuna mmoja wenu aitendaye torati” Huu ulipaswa kuwa usemi wenye kuogofya kwa Wayunani ambao walikuwa wamehudhuria sikukuu iliyohitajika katika Yerusalemu. Sheria ya Musa kwa usahihi ilizuia mauaji ya kudhamiria, bado hii ni sawa kwa kile walichokuwa wakikipanga. Wenyeji walilijua hili lakini hawakuwa tayari kuiacha mipango au malalamiko yao. ◙ “Mbona mnatafuta kuniua?” Swali la Yohana 7:20 halitoki kwa viongozi wa kidini, bali kutoka kwa umati iliokuwa umekuja kuhiji ambao haukufahamu chochote juu ya njama za kumuua. Baadaye, katika Yohana 7:25, watu wa Yerusalemu walizifahamu njama za kumuua Yesu. Viongozi wa kidini pia walimshtaki Yesu kama mtu aliyekuwa anamilikiwa na mapepo ili kueleza njia ya nguvu Zake na mtazamo (kama vile Mt. 9:34; 11:18; 12:24; Marko 3:22-30; Yohana 8:48-52; 10:20-21). 7:20 “Una pepo!” Ni dhahiri kwa kila mtu ambaye alikutana na Yesu kwamba alikuwa na nguvu. Swali lilikuwa ni wapi nguvu hizi zilitoka? Viongozi wa Kiyahudi wasingelikataa “ishara/miujiza” ya Yesu, hivyo basi wafikiria ni nguvu toka kwa shetani na mapepo (kama vile Yohana 8:48-49,52; 10:20). Katika mazingira haya umati wa watu waliokuwa wamehudhuria katika siku kuu ya Vibanda wanatumia fungu sawa, lakini katika maana tofauti. Walidai kwamba Yesu anatenda katika namna isiyokuwa na mantiki, katika mtindo wa kiwazimu.

MADA MAALUMU: MALAIKA NA MAPEPO

A. Watu wa kale waliamini kwamba viumbe vyote vina uhai. Walifikiri kwamba sifa za mwanadamu ni sawa

Page 155: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

139

na nguvu ya asili, wanyama, na viumbe vya asili. Maisha yalielezeka kupitia mwingiliano wa uwepo wa vitu/viumbe hivi na wanadamu.

B. Mifano hii wakati mwingine ilileta matokeo ya kuabudu miungu mingi (miungu wengi). Kwa kawaida mapepo (genii) ilikuwa miungu midogo au nusu miungu (mizuri au miovu) ambao ilileta matokeo kadha wa kadha katika maisha ya watu binafsi. 1. Machufuko na migogoro huko Mesopotamia, 2. Mpangilio na kazi huko Misri, 3. Kanaani, tazama W. F. Albright's Archaeology and the Religion of Israel, Toleo la Tano, kur. 67-9

C. Agano la Kale halielezi sana au kukuza jambo la miungu wadogo, malaika, au pepo, huenda ni kwa sababu ya msistizo wake mkali unaozungumzia Imani ya Mungu mmoja (tazama Mada Maalumu : Mungu mmoja Imani ya Mungu mmoja kama vile Kut. 8:10; 9:14; 15:11; Kumb. 4:35,39; 6:4; 33:26; Zab. 35:10; 71:19; 86:8; Isa. 46:9;Yer. 10:6-7; Mik. 7:18). Haliizungumzii miungu ya uongo ya mataifa ya wapagani (Shedim, BDB 993, kama vile Kumb. 32:17; Zab. 106:37) na halitaji majina au kufananisha baadhi yao. 1. Se'im (mazimwi au majitu yenye manyoya, BDB 972 III, KB 1341 III, kama vile Law. 17:7; 2 Nya.

11:15; Isa. 13:21; 34:14) 2. Lilith (jike, pepo apotoshaye kizinifu nyakati za usiku, BDB 539, KB 528, kama vile Isa. 34:14) 3. Mavet (neno la Kiebrania liliotumika kumtaja mungu mwovu wa Wakanani, Mot, BDB 560, KB560,

kama vile Isa. 28:15,18; Yer. 9:21; na kwa kadri iwezekavyo Kumb. 28:22) 4. Resheph ( mahali, moto, au mawe yenye kutiririsha mvua ya mawe, BDB 958, KB 958, kama vile

Kumb. 32:24; Zab. 78:48; Hab. 3:5) 5. Dever (uharibifu, BDB 184, kama vile Zab. 91:5-6; Hab. 3:5) 6. Az'azel (jina halina uhakika, lakini huenda akawa pepo wa jangwani au jina la mahali, BDB 736, KB

736, kama vile Law. 16:8,10,26) (Mifano hii inachukuliwa kutoka Encyclopedia Judaica, juzuu l. 5, uk. 1523.).Hata hivyo, hakuna imani ya Mungu wawili au uhuru wa malaika kutoka kwa YHWH katika Agano la Kale. Ibilisi chini ya YHWH (kama vile Ayubu 1-2; Zekaria 3), hayuko huru, ni adui anayejiongoza (kama vile A. B. Davidson, A Theology of the Old Testament, kr. 300-306).

D. Dini ya Kiyahudi iliendelezwa kipindi cha uhamisho wa Babeli (586-538 b.k). Kitheolojia iliathiriwa aina mbili za Kiajemi zilizochukua nafasi kwa wafuasi wa Zoroaster, mungu mkuu na mzuri aliitwa Mazda au Ormazd na mpinga uovu aitwaye Ahriman. Huyu aliruhusiwa ndani ya dini ya Kiyahudi baada ya uamisho na kuwa mfano wa aina mbili kati ya YHWH na malaika Zake na Ibilisi malaika zake au pepo.

Theolojia ya dini ya Kiyahudi yenye kutoa mfano wa uovu inaelezwa na kunakiliwa vema katika Edersheim ya Alfred The Life and Times of Jesus the Messiah, juzuu. 2, kiambatisho XIII (kur. 749-863) na XVI (kur. 770-776). Dini ya Kiyahudi ilitoa mifano ya uovu katika njia tatu.

1. Ibilisi au Malaika wa maangamizi 2. kusudi la uovu (yetzer hara) ndani ya mwanadamu 3. Malaika wa Mauti

Edersheim anayabainisha haya kama 1. Mshitaki 2. Mjaribu 3. Mwadhibishaji (juzuu. 2, uk. 756)

Kuna tofauti zinazodhihirika kitheolojia kati ya dini ya Kiyahudi iliyokuwepo baada ya uhamisho na nanma uwaslilishaji na maelezo ya uovu inavyofanyika ndani ya Agano Jipya.

E. Agano Jipya, haswaa Injili, linadai uwepo na upinzani wa uovu wa viumbe vya kiroho kwa mwanadamu na kwa YHWH (katika dini ya Kiyahudi, Ibilisi alikuwa adui wa mwanadamu, lakini si kwa Mungu). Hawa wanayapinga mapenzi ya Mungu, amri, na ufalme.

Yesu alikabiliana na kuvifukuza hivi viumbe vya kimapepo, pia viliitwa (1) roho chafu (kama vile. Luka 4:36; 6:18) au (2) roho za uovu kama vile. Luka 7:21; 8:2), kutoka kwa wanadamu. Yesu kwa udhihilisho alitengeneza tofauti kati ya maradhi (kimwonekano na kiakili) na hali ya kimapepo. Aliithibitisha nguvu Yake na mtazamo wa

Page 156: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

140

ndani wa kiroho kwa kuwatambua na kuwafahamu hawa pepo wabaya. Mara nyingi walimtambua na kumwita, lakini Yesu aliukataa ushuhuda wao, alihitaji wawe kimya, na kuyafukuzia mbali. Utambuzi wa pepo hawa ni ishara ya kuvunja ufalme wa Ibilisi. Kuna upungufu wa ajabu wa habari ndani ya barua za Kitume za Agano Jipya kuhusiana na somo hili. Utambuzi huu kamwe haukuorodhesha karama za kiroho, wala methodolojia au hatua yake iliyotolewa kwa ajili ya vizazi vijavyo vya huduma au waamini.

F. Mwovu yu dhahiri; mwovu ni mtu binafsi; mwovu yupo. Si asili yake wala kusudi lake linalofunuliwa. Biblia inatetea ukweli wake na kwa ukali inapinga ushawishi wake yule mwovu. Ndani ya ukweli hakuna hatima yenye mitazamo yenye uwili ndani yake. Mungu yu ndani ya utawala wake mwenyewe; mwovu anaangamizwa na kuhukumiwa na ataondolewa kutoka katika uumbaji.

G. Watu wa Mungu yawapasa kumpinga mwovu (kama vile Yakobo 4:7). Hawawezi kutawaliwa na naye (kama vile 1 Yohana 5:18), bali wanaweza kujaribiwa na ushuhuda na ushawishi wake kuangamizwa (kama vile Efe. 6:10-18). Mwovu ni sehemu ya mtazamo wa ulimwengu kwa wakristo uliofunuliwa. Wakristo wa sasa hawana haki ya kueleza wazi kwa mara nyingine (kutafasiri upya maandishi ya Rudolf Baltmann); kuyaua maovu (miundo ya kijamii ya Paul Tillich), wala kujaribu kuelezea kwa ukamilifu katika namna ya kisaikolojia (Sigmund Freud). Ushawishi wake umeenea kote, lakini umeangamizwa. Waamini wanahitaji kuenenda ndani ya ushindi wa Kristo!

7:22 NASB, NKJV "(lakini si kwamba yatoka kwa Musa, bali kwa mababa;)" NRSV "(Si kwamba desturi hiyo ilitoka kwa Mose, bali itoka kwa mababu)" TEV "(ingawa hakuwa Musa bali mababu zenu walioianzisha)" NJB "—si kwamba ilianza naye, inaenda nyuma kwa wazee--"

Kanuni ya tohara haikuanza na Sheria ya Musa (kama vile Kut. 12:48; Law. 12:3), lakini alipewa Ibrahimu kama ishara ya agano maalumu na YHWH (kama ile Mwa. 17:9-14; 21:4; 34:22).

◙ “nanyi siku ya sabato humtahiri mtu" Asili ya ubishi wa Yesu iliuwa kwamba walikuwa tayari kuweka kando sheria zao za Kisabato ili kwamba mtoto atahiriwe (kama vile Shab 132a; Sabh. 18:3; 19:1-6), lakini hawakuwa tayari kuziweka kando sheria za Kisabato kwamba mtu awe mzima. Ni muhimu kutambua kwamba Yesu alikuwa akitumia mantiki na kufikiri miundo ya Sheria za Dini ya Kiyahudi katika sehemu hii yote.

7:23 "ikiwa" Hii ni sentensi shurutishi daraja la kwanza ambayo inadhaniwa kuwa ya kweli kutoka katika mtazamo wa mwandishi au kwa sababu zake za kiuandishi.

◙ “mbona mnanikasirikia mimi kwa sababu nalimfanya mtu kuwa mzima kabisa siku ya sabato?” Hii inarejea aidha juu ya uponyaji wa Yesu ulionukuliwa katika Yohana 5:1-9 au uponyaji ambao haukunukuliwa wakati wa sikukuu. Neno la Kiyunani "hasira" (cholaō) ni neno adimu linalopatikana hapa tu katika gano Jipya. Linapatikana katika hali ya mabishano katika fasiri yote ya Kiyunani (BAGD, uk. 883 na MM, uk. 689). Inahusiana na "chuki" (cholē, kama vile Mt. 27:34). Sababu ya Yesu kulitumia neno hili (yaani, ni la karibu) haijadhihirishwa. Inaweza kumaanisha hasira ya "ki-Uungu" katikamaana kwamba walifikiri kwamba walikuwa wakitetea mapenzi ya Mungu na sharia za Mungu, ambazo Yesu alikuwa akizivunja.

7:24 “msihukumu hukumu ya macho tu, bali ifanyeni hukumu iliyo ya haki" Hii ni kauli shurutishi ya wakati uliopo ikiwa na kiambata hasi, ambacho kinamaanisha kuzuia kitendo kilichoko kwenye mchakato. Ikifuatiwa na kauli shurutishi ya wakati uliopita usio timilifu, ambayo inadokeza UMUHIMU. Hili linaweza kuwa dokezo la Isa. 11:3.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 7:25-31

Page 157: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

141

25 Basi baadhi ya watu wa Yerusalemu wakasema, Je! Huyu siye wanayemtafuta ili wamwue? 26 Na kumbe! Anena waziwazi, wala hawamwambii neno! Yamkini hao wakuu wanajua hakika ya kuwa huyu ndiye Kristo? 27 Lakini huyu twamjua atokako; bali Kristo atakapokuja hakuna ajuaye atokako. 28 Basi Yesu akapaza sauti yake hekaluni, akifundisha na kusema, Mimi mnanijua, na huko nitokako mnakujua; wala sikuja kwa nafsi yangu; ila yeye aliyenipeleka ni wa kweli, msiyemjua ninyi. 29 Mimi namjua, kwa kuwa nimetoka kwake, naye ndiye aliyenituma. 30 Basi wakatafuta kumkamata; lakini hakuna mtu aliyeunyosha mkono wake ili kumshika, kwa sababu saa yake ilikuwa haijaja bado. 31 Na watu wengi katika mkutano wakamwamini; wakasema, Atakapokuja Kristo, je! Atafanya ishara nyingi zaidi kuliko hizi alizozifanya huyu?

7:25 "Huyu siye wanayemtafuta ili wamwue?" Muundo wa kisarufi wa hili swali unatarajia jibu la "ndiyo" (kama vile Yohana 5:47;7:19). Huu ni mpangilio wa kwanza wa maswali kupitia Yohana 7:36.

7:26 NASB, REV, NET "Anazungumza hadharani" NKJV "Anena waziwazi," NRSV, NJB "Anawaonya hadharani"

Tazama Mada Maalumu: Ujasiri (parrhēsia) katika Yohana 7:4

NASB "Wakuu kwa hakika hawajua kwamba huyu ndite Kristo NKJV "Yamkini hao wakuu wanajua hakika ya kuwa huyu ndiye Kristo?" NRSV "Je! Yawezekana kuwa viongozi wametambua kweli kwamba huyu ndiye Kristo" TEV "Yawezekana kuwa walifahamu kwa hakika kuwa alikuwa Masihi" NJB "Inaweza kuwa hakika wakuu walitambua kwamba ni Kristo"

Utunzi huu wa kisarufi unatarajia jibu la "hapana". Hata hivyo, haielezi uwezekano (kama vile Yohana 1:31; 4:29).

7:27 "Lakini huyu twamjua atokako; bali Kristo atakapokuja hakuna ajuaye atokako." Hii inarejea juu ya desturi za sheria za dini ya Kiyahudi za Kimasihi zilizojikita juu ya Mal. 3:1 kwamba yule Masihi angeonekana ghafla ndani ya hekalu. Hii inapatikana katika I Enoko 48:6 na IV Ezra 13:51-52.

7:28 Katika mstari huu Yesu anatoa maelezo ya aina mbili. 1. kwamba Mungu alimtuma Yeye (kama vile Yohana 3:17,34; 5:36,38; 6:29; 7:29; 8:42; 10:36; 11:42;

17:3,18,21,23,25; 20:21) 2. kwamba hawakumjua Mungu (kama vile Yohana 5:37,42; 8:19,27,54-55; 16:3)

Yohana ananakili kwamba Yesu "alipaza sauti" (kama vile Yohana 7:37; 12:44; Mt. 8:29). Yesu alipaza sauti Yake juu. Kwa maana, kazi hii katika maana ya kifasihi ni sawa na na matumizi ya Yesu ya mwanzo "Amina" au "Amina, Amina." Alihitaji semi hizi za kejeli zisisitizwe! Yohana 7:29 inaonyesha tatizo! Walidhani Yeye anatoka Galilaya (kama vile Yohana 7:41), lakini katika uhalisia, Yeye anatoka mbinguni!

◙ "yeye aliyenipeleka ni wa kweli," Yule Baba ni kweli (kama vile Yohana 3:33; 8:26; 1 Yohana 5:20) na hivyo ni Mwana (kama vile Yohana 7:18; 8:16). Tazama Mada Maalum katika Yohana 6:55

7:29 "Mimi namjua, kwa kuwa nimetoka kwake, naye ndiye aliyenituma" Huu ni mfano mwingine wa wima ulio mara mbili katika Yohana. Usemi huu ulifikiliwa na viongozi wa Kiyahudi kuwa ni wa kumkufuru Mungu na ulithibitisha hitaji lao la kuuawa kwa Yesu. Tazama Mada Maalumu: Kupelekwa (Apostellō) katika Yohana 5:24

Page 158: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

142

7:30 "wakatafuta kumkamata" Hii ni njeo ya kitenzi kisicho timilifu ambayo inadokeza (1) walianza kumtafuta ili wamkamate au (2) walijaribu tena kumtia mbaroni lakini hawakutaka kusababisha maandamano miongoni mwa wana-hija waliomwamini Yeye kuwa Masihi.

◙ "kwa sababu saa yake ilikuwa haijaja bado" Hii ni nahau ya kinabii ya sasa ambayo inatetea ratiba ya Uungu (kama vile Yohana 2:4; 7:6,30; 8:20; 12:23,27; 13:1; 17:1).

7:31 "Na watu wengi katika mkutano wakamwamini" Hii ilikuwa imani ya kweli katika Yesu hata kama ilikamilishwa na uelewa mbaya wa kuihusu kazi ya Umasihi Wake. Hakuna aliye na "ukamilifu" imani (kama vile Nuhu, Ibrahimu, Musa, Daudi, wale Kumi na Wawili). Tazama Mada Maalumu katika Yohana 2:23 Mara nyingi hutokea wakati injili inapokuwa inawasilishwa. Wengine walimwamini, wengine waliona mashaka, wengime walipatwa na hasira. Hapa ni mkingamo juu ya fumbo la

1. uteuzi wa Kiungu 2. dhambi ya mwanadamu

Kuna fumbo hapa. Mara nyingi nimekuwa nikitiwa wasiwasi juu ya kutokuamini katika uwepo wa nuru ya kutosha. Huenda hii ikawa asili ya maneno ya amani ya Yesu kwa baadhi na mgogoro kwa wengine! ◙ "Atakapokuja Kristo, je! Atafanya ishara nyingi zaidi kuliko hizi alizozifanya huyu?" Muundo wa sarufi ya Kiyunani unatarajia jibu la "hapana". Katika A Theology of the New Testament, George E. Ladd ana maoni ya kushawishi juu ya matumizi ya "alama" ili kusistiza juu ya imani katika Yesu: "Swali la uhusiano wa ishara na imani si jepesi, kwa sababu takwimu zinaonekana kutazama juu ya uelekeo wa aina mbili tofuti. Wakatik mwingine ishara zinawekwa kwa kuchorwa ili kuielekea imani katika Yesu (2:23; 6:14; 7:31; 10:42). Kwa upande mwingine, kulikuwa na wale ambao waliziona ishara na hawakuziamini (6:27; 11:47; 12:37). Zaidi ya hayo, Yesu aliwakaripia Wayahudi mara kwa mara kwa sababu wasingeamini isipokuwa kwa kuona ishara (4:48; 6:30). Jibu linapaswa kupatikana katika mvutano mkubwa kati ya ishara na imani. Inahitaji imani ili kutambua maana halisi ya ishara na ushuhuda wake kwaYesu; kwa wale ambao hawana imani, ishara ni maajabu tu yasiyokuwa na maana. Kwa wale wenye kuitikia, ishara zina maana ya kuthibitisha na kuichimbua imani kwa kina. Ni sawa kwamba ishara za Yesu hazikubuniwa ili kuishurutisha imani. Kwa upande mwingine, kazi za Yesu ni ushuhuda wa kutosha kwa wale wanaoweza kuona kile kinachotokea katika wito wake. Kazi za Yesu zitasaidia kama ilivyo maana ya shutuma na kuthibitisha kwa wanaume vipofu katika dhambi zao" (uk. 274).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 7:32-36 32Mafarisayo wakawasikia mkutano wakinung'unika hivi juu yake; basi wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakatuma watumishi ili wamkamate. 33 Basi Yesu akasema, Bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; kisha naenda zangu kwake yeye aliyenipeleka. 34 Mtanitafuta wala hamtaniona; nami nilipo ninyi hamwezi kuja. 35 Basi Wayahudi wakasemezana, Huyu atakwenda wapi hata sisi tusimwone? Ati! Atakwenda kwa Utawanyiko wa Wayunani, na kuwafundisha Wayunani? 36 Ni neno gani hilo alilolisema, Mtanitafuta wala hamtaniona; nami nilipo ninyi hamwezi kuja?

7:32 "wakuu wa makuhani na Mafarisayo" Hii inarejea juu ya wale waliokuwa miongoni mwa Wakuu wa Sinagogi (tazama Mada Maalum katika Yohana 3:1). Kulikuwa na makuhani wakuu nane tu, lakini tangu kipindi cha utawala wa Kirumi, ofisi ilikuwa kitu bora kilichotegemewa kwa mali kadhaa, familia za Kiyahudi na zizohidhinishwa kutoka mmoja wa familia moja hadi mwana familia mwingine. ◙ "wakatuma watumishi ili wamkamate" Hii inarejea juu ya "Askari wa Hekalu" ambao wangeweza kuwa Walawi. Walikuwa na mamlaka yenye mipaka nje ya eneo la Hekalu lenyewe (kama vile Yohana 7:45,46; 18:3,12,18,22). 7:33 "Bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi" Hiki ni kifungu cha kawaida katika Yohana (kama vile Yohana 12:35; 13:33; 14:19; 16:16-19). Yesu alifahamu Yeye alikuwa nani?, na lini (kama vile Yohana 12:23; 13:1; 17:1-5).

Page 159: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

143

◙ "naenda zangu kwake yeye aliyenipeleka" Hii inarejea juu ya kuhitimisha matukio ya wito wa Yesu wa ukombozi: kusulibiwa, ufufuo, kupalizwa, na kurejea kwa utukufu uliokuwepo kabla (kama vile Yohana 17:1-5; Matendo 1).

7:34 Hili neno linafanana sana na mjadala wa Yesu na wanafunzi wake katika chumba cha juu (Yohana 13:33; kama vile Yohana 7:36 na 8:21). Hata hivyo, hapa inarejea juu ya wale wasioamini (yaani, umati, wakazi wa Yerusalemu, na viongozi wa Kiyahudi).

7:35-36 "Huyu atakwenda wapi hata sisi tusimwone? Ati! Atakwenda kwa Utawanyiko wa Wayunani, na kuwafundisha Wayunani?” Utunzi wa sarufi ya Kiyunani unatarajia jibu la "ndiyo". Haya ni matumizi mengine ya kejeli. Mara nyingi hii imekuwa ni mapenzi ya Mungu (kama vile Mwa. 3:15; 12:3; Isa. 2:2-4). Wakati wa Sikukuu ya Vibanda, fahari sabini walitolewa kwa ajili mataifa ya ulimwengu. Wayahudi waliwajibika kuombea na kuleta nuru kwa Mataifa. Hii inaweza kuakisi juu ya mpangilio wa kiutamaduni wa usemi huu. Neno "Wayunani" lilitumika katika maana ya "Mataifa." Neno disperia lilirejea juu ya watu wa Kiyahudi walioishi katika nchi za Mataifa (kama vile Yakobo 1:1; 1 Pet. 1:1). Huu ni mfano mwingine wa umati kutoielewa lugha ya kiistiari iliyotumiwa na Yesu. Huu ni mfano mwingine wa Yesu wenye matumizi wima mara mbili. Umati haukumuelewa kwa sababu ulizifafanua semi Zake kifasihi badala ya "juu" na "chini" aina ya mafundisho Yake. Yeye alitoka kwa Baba na angelirudi kwa Baba.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 7:37-39 37 Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe. 38 Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. 39 Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa.

7:37 "Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu," Kuna baadhi ya maswali, kama hii ilikuwa ni sikukuu ya siku ya saba (kama vile Kumb. 16:13), au sikukuu ya siku ya nane (kama vile Law. 23:36; Neh. 8:17; II Wamakabayo 10:60, na Josephus). Inavyoonekana katika nyakati za Yesu ilikuwa siku ya sikukuu, hata hivyo, katika siku ya mwisho maji hayakuchukuliwa kutoka katika birika la Siloamu na kutiririshwa katika sehemu ya chini ya madhabahu kama ilivyokuwa katika siku saba zingine. Tunajifunza juu ya taratibu kutoka Kuelekeza ujenzi wa vibanda kwa ajili ya mafunzo ya Kiyahudi ya Buku la sheria za Kiyahudi, ambazo zinanukuliwa kutoka Isa. 12:3. Hii inaweza kuwa taswira ya maombi kwa ajili ya mvua ya mazao.

◙ “ki...” Hii ni sentensi shurutishi daraja la tatu ambayo inamaanisha tendo lenye umuhimu.

◙ "Mtu akiona kiu" Ni mwaliko wa imani ulimwenguni katika Yesu! Tazama nukuu katika Yohana 7:17

◙ "na aje kwangu anywe" Yesu anatumia sitiari ile ile katika Yohana 4:13-15. Kwa kadri iwezekanavyo hii inarejea juu ya Yesu kama Mwamba wa Kimasihi ambao ni maji yaliyohakikishwa (kama vile Kor. 10:4). Ni dhahiri kwamba hii ilihusika na mwaliko wa Agano la Kale wa Isa. 55:1-3 na fursa za kitamaduni za kutiririsha maji kwa ishara ya wakati wa sikukuu. Baadhi ya machapisho ya kale Kiyunani yanaondoa "kwangu" (kama vile MSS P66, א*, na D). Imewekwa katika P66c, P75, אc, L, T, W, na yanadokezwa mazingira. Ile UBS4 inatoa mjumuisho wake "B" kwa yakini (takribani uhakika). Katika Yohana watu wanasisitizwa kumwamini Yeye. Injili ina mtazamo binafsi.

7:38 "Aniaminiye mimi" Ifahamike kuwa hii ni kauli ya wakati uliopo. Hii inaonyesha msistizo juu ya uhusiano binafsi endelevu uliohusishwa katika kuamini sawa na “utii” ndani ya Yohana 15 Tazama Mada Maalumu: Njeo za Vitenzi vya Kiyunani zilizotumika juu ya Wokovu katika Yohana.

Page 160: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

144

◙ "kama vile maandiko yalivyonena" Ni vigumu kulitambua Andiko mahususi la nukuu hii. Ingeweza kuwa Isa. 12:3; 43:19-20; 44:3; 58:11; Ezek. 47:1; Yoeli 3:18; Zek. 13:1; au 14:8, ambapo kistiari linarejea juu ya maji ya hukumu, kifo na pepo kama ishara ya uwepo wa Uungu. Katika maana hii maji yaliyohaidiwa ya zama mpya za baraka za kilimo ni stiari ya asili ndani ya agano jipya. Roho atakuwa mtendaji mioyoni na akilini (kama vile Ezek. 36:27-38).

◙ "mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake" Kumekuwa na kanuni kadhaa kama kiwakilishi anzilishi. 1. Yesu Mwenyewe (kama vile makasisi wa kanisa la kale) 2. waamini binafsi ambao wamemwamini Kristo 3. Yerusalemu. Katika Kiaramu, "yake” (mwanaume) inaweza kumaanisha "yake” (mwanamke) inaweza

kuzungumzia juu ya mji (hii ilikuwa nafasi ya viongozi wa kidini ya Kiyahudi, kama vile Ezek. 47:1-12 na Zek. 14:8)

Kuna muhtasari mzuri, mjadala uliorahisishwa wa kanuni mbili zilizojikita katika kuangalia namna mtu anvyoweza kuweka alama za kiuandishi katika Yohana 7:37b na 38a katika NIDOTTE, juzuu. 1, uk. 683. Yesu amejiita Mwenyewe maji yaliyo hai (kama vile Yohana 4:10). Sasa katika mazingira haya ni Roho Mtakatifu (kama vile Yohana 7:39) ambaye anayatoa na kuyatengeneza maji yaliyo hai ndani ya wale wamfuatao Yesu. Hii ni sambamba na kazi ya Roho ya kumuumba Kristo ndani ya waaminio (kama vile Rum. 8:29; Gal. 4:19; Efe. 4:13).

7:39 “kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa” Inavyoonekana hii inaakisi fikra za Yohana baadaye (yaani, mawazo ya kitahariri) juu ya umuhimu wa usemi huu (kama vile Yohana 16:7). Pia inaonyesha maana zote za Kalvari na Pentekoste zilizotazamwa kama "utukufu" (kama vile Yohana 3:14; 12:16,23; 17:1,5). Kuna waandishi kadhaa mbali mbali wanaojaribu kuelezea kile Yohana alichomaanisha kwenye usemi huu mfupi.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 7:40-44 40Basi wengine katika mkutano walipoyasikia maneno hayo, walisema, Hakika huyu ndiye nabii yule.41 Wengine walisema, Huyu ndiye Kristo. Wengine wakasema, Je! Kristo atoka Galilaya? 42 Andiko halikusema ya kwamba Kristo atoka katika uzao wa Daudi, na kutoka Bethlehemu, mji ule alioukaa Daudi? 43 Basi kukaingia matengano katika mkutano kwa ajili yake. 44 Baadhi yao wakataka kumkamata, lakini hakuna mtu aliyenyosha mikono yake ili kumshika.

7:40 “Hakika huyu ndiye nabii yule” Hii inagusia juu ya ahadi ya Kimasihi ya Musa ambayo inapatikana katika Kumb. 18:15,18. Wengi walimtambua Yesu kama nabii (kama vile Yohana 4:19; 6:14; 9:17; Mt. 21:11). Waliitambua nguvu za Yesu, lakini hawakuuelewa utu Wake na kazi yake. Waislamu pia wanautumia wadhifa huu kwa Yesu, lakini hawauelewi ujumbe Wake.

7:41 "Wengine walisema, Huyu ndiye Kristo" Hii ianaonyesha kwamba neno "Kristo" ni sawa na neno la Kiebrania "Masihi,"ambalo linamaanisha "aliyepakwa mafuta." Katika Agano la Kale wafalme, makuhani, na manabii walipakwa mafuta kama alama ya wito wa Mungu na maandalio. Tazama MADA MAALUMU: KUTIWA MAFUTA KATIKA BIBLIA (BDB 603).

◙ “Wengine wakasema, Je! Kristo atoka Galilaya?" Muundo wa sarufi ya Kiyunani ulitazamia jibu la "hapana" kwa swali hili. Lakini vipi kuhusu Isa. 9:1? 7:42 Muundo wa swali hili kisarufi unatazamia jibu la "ndiyo" ◙ "uzao wa Daudi" (kama vile 2 Samueli 7; Mt. 21:9; 22:42). ◙ "na kutoka Bethlehemu, mji ule alioukaa Daudi?" Haya ni matumizi mengine ya kejeli (kama vile Mika 5:2-3 na Mt. 2:5-6).

Page 161: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

145

7:43 Yesu na ujumbe Wake siku zote ulisababisha mgawanyiko (kama vile Yohana 7:48-52; 9:16; 10:19; Mt. 10:34-39; Luka 12:51-53). Hili ni fumbo la mfano wa udongo (kama vile Mathayo 13). Wengine wana masikio ya kiroho na wengine hawana (kama vile Mt. 10:27; 11:15; 13:9,15 (mara mbili), 16,43; Marko 4:9,23; 7:16; 8:18; Luka 8:8; 14:35).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 7:45-52 45Basi wale watumishi wakawaendea wakuu wa makuhani na Mafarisayo. Nao wakawaambia, Mbona hamkumleta? 46 Wale watumishi wakajibu. Hajanena kamwe mtu ye yote kama huyu anavyonena. 47 Basi Mafarisayo wakawajibu, Je! Ninyi nanyi mmedanganyika? 48 Ni nani katika wakuu amwaminiye, au katika Mafarisayo? 49 Lakini makutano hawa wasioifahamu torati wamelaaniwa. 50 Akawaambia Nikodemo, (naye ni yule aliyemwendea zamani, maana ni mmoja wao), 51 Je! Torati yetu humhukumu mtu kabla ya kumsikia kwanza, na kujua atendavyo? 52 Wakajibu, wakamwambia, Je! Wewe nawe umetoka Galilaya!

7:46 "Hajanena kamwe mtu ye yote kama huyu anavyonena" Kejeli ya Yohana nyingine! Huu ni ushuhuda wa kushtua sana.

1. hawakutaja woga wao juu ya makutano ambao ungelikuwa kisingizio kizuri kwao 2. Maaskari hawa walikubaliana kwa kauli moja katika maoni yao kuhusu Yesu, ambapo makutano

waligawanyika 3. wanaume hawa walizoea kufuata amri, si kutoa maoni yao.

7:48 "Ni nani katika wakuu amwaminiye, au katika Mafarisayo?" Muundo wa sarufi ya Kiyunani katika Yohana zote mbili yaani Yohana 7:47 na 48 unatatarajia jibu la “hapana”. Neno “wakuu” linarejea juu ya Wakuu wa Sinagogi. Hapa tuna Masadukayo na Mfarisayo (Wakuu wote wa Sinagogi), ambao siku zote walikuwa na chuki miongoni mwao, na pia kuungana katika upinzani dhidi ya Yesu (kama vile Yohana 11:47,57; 18:3). 7:49 "Lakini makutano hawa wasioifahamu torati wamelaaniwa" Hii inarejea juu ya "watu wa nchi" ('am hā'āres) ambao waliangaliwa kwa chuki na viongozi wa kidini kwa sababu hawakutimiza Tamaduni (kama vile Kumb. 27:26). Kejeli ya Yohana inaendelea kuonekana katika Yohana 7:51, ambapo Nikodemo anakazia juu yao kwamba wao pia wanaivunja Torati kwa namna walivyomtenda Yesu. La asha, alikuwa na mshangao juu ya udini. Yule mwenye kulaani (eparatos, anapatikana hapa tu katika Agano Jipya) watu wa kawaida wamelaaniwa wenyewe! Ikiwa nuru imekuwa giza, giza li kuu kwa namna gani! Iweni watu wa kuonywa, wa sasa, wenye kiasi, watu wa dini mlioelimishwa! 7:51"Je! Torati yetu humhukumu mtu kabla ya kumsikia kwanza, na kujua atendavyo?" Utunzi wa sarufi ya Kiyunani unatarajia jibu la "ndiyo” (kama vile Kut. 23:1; Kumb. 1:16). 7:52 "Je! Wewe nawe umetoka Galilaya!" Hii inaonyesha upinzani wa kihisia wa Wakuu wa Sinagogi dhidi ya Yesu. ◙ “Tafuta, ukaone"Tafuta ina maana nyingine ndani ya Dini ya Kiyahudi juu ya usomaji wa Maandiko (kama vile Yohana 5:39). Tena hii inaonyesha matumizi ya Yohana ya kejeli. Vipi kuhusu Eliya (kama vile 1 Fal. 17:1) na Yona (kama vile 2 Fal. 14:25), Hosea na Nahumu? Zilipaswa kuwa zimemaanisha "yule" nabii wa Kut. 18:15,19; Mwa. 49:10; 2 Samweli 7

7:53-8:11 Tazama maelezo ya mwanzoni mwa sura ya 8.

MASWALI YA MJADALA

Page 162: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

146

Huu ni mwongozo wa fasiri, ina maanisha kwamba unawajibika kwa tafsiri zako mwenyewe za Biblia. Kila mmoja wetu lazima atembee katika mwanga tulio nao. Wewe, Biblia, na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Hutakiwi uvitelekeze vitu hivi kwa mfasiri. Maswali ya mjadala huu yanatolewa kukusaidia kufikiri juu ya mambo makubwa ya sehemu za kitabu hiki. Yanalenga kukuamsha kimawazo na sio kutoa maana.

1. Ni yapi maneno ya Yesu aliyoyasema juu ya mazingira ya kishereheu katika Yohana 7? 2. Eleza na fafanua kusudi la "Sikukuu ya Vibanda." 3. Kwa nini viongozi wa kidini walikuwa na uadui sana na Yesu? 4. Orodhesha makundi tofauti ambayo yalitoa hoja kumhusu Yesu katika sura hii.

Page 163: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

147

YOHANA 8

MIGAWANYO YA AYA YA TAFSIRI ZA KISASA

UBS4 NKJV NRSV TEV NJB Mwanamke Mzinifu akabiliana Mwanamke Mwanamke uzinifu Mwanamke aliyekamatwa na Nuru ya aliyekamatwa aliyekamatwa mzinifu katika uzinifu Ulimwengu katika uzinifu katika uzinifu 7:53-8:11 7:53-8:12 7:53-8:11 7:53-8:11 7:53-8:11 Yesu, Nuru ya Yesu Autetea Yesu, Nuru ya Yesu, Nuru ya Yesu, Nuru ya Ulimwengu Ushuhuda Wake Ulimwengu Ulimwengu Ulimwengu 8:12-20 8:12-20 8:12 8:12 Mjadala Kuhusiana na Ushuhuda wa Yesu Mwenyewe 8:13-20 8:13 8:13-18 8:14-18 8:19a 8:19a 8:19b 8:19b 8:20 8:20 Mimi Niendako Yesu Atabiri Hamwezi Kwenda Ninyi Hamwezi Kuondoka Kwake Mimi Niendako Kuja 8:21-30 8:21-29 8:21-30 8:21 8:21 8:22 8:22-24 8:23-24 8:25a 8:25a 8:25b-26 8:25b-26 Kweli Itawaweka Huru 8:27-29 8:27-29 8:30-36 8:30 8:30 Kweli Itawaweka Kweli Itawaweka Yesu na Abraham Huru Huru 8:31-38 8:31-33 8:31-32 8:31-32 8:33 8:33-38 Uzao wa Abraham na Shetani 8:34-38 8:34-38 Baba Yenu Ibilisi 8:37-47 8:39-47 8:39-47 8:39a 8:39-41a 8:39b-41a 8:41b 8:41b-47 8:42-47 Kabla ya Abraham, kabla ya Abrahamu, Yesu na Abrahamu Nalikuweko nalikuweko 8:48-59 8:48-59 8:48-59 8:48 8:48-51 8:49-51 8:52-53 8:52-56 8:54-56 8:57 8:57-58 8:58

Page 164: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

148

8:59 8:59

MZUNGUKO WA TATU WA USOMAJI KUFUATILIA KUSUDIO LA ASILI LA MWANDISHI KATIKA NGAZI YA AYA Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwatafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Aya ya kwanza 2. Aya ya pili 3. Aya ya tatu 4. N.k

HISTORIA YA NYUMA YA 7:53-8:11

A. Yohana 7:53-8:11 haikuwa sehemu ya Injili halisi ya Yohana.

B. Ushahidi wa kifungu hiki (sentensi moja katika Kiyunani) ulioondolewa toka katika Injili ni 1. Ushahidi wa nje

a. Kukosekana katika maandishi ya kale ya Kiyunani 1) Magombo -- P65 (karne ya kale ya tatu), P75 (karne ya tatu) 2) Herufi za Kiyunani -- א (karne ya nne), B (karne ya nne), yamkini haipo toka A na C. katika

kitabu cha Yohana zinaonekana kuathiriwa, bali yale machapisho yanayoonekana kuwepo yanapotoweshwa, yanaonekana kutotoa nafasi ya kifungu hiki.

b. machapisho mengi ya Kiyunani ya kale yaliyowekwa ndani yametiliwa alama maalumu, kialama cha nyota, kuonyesha kuwa hayakuwa ya asili

c. unapatikana katika maeneo mengi tofauti katika machapisho mbalimbali ya kale 1) baada ya Yohana 7:36 2) baada ya Yohana 7:44 3) baada ya Yohana 7:25 4) katika Luka baada ya 21:38 5) katika Luka baada ya 24:53

d. hayapo katika tafsiri za kale 1) Kilatini cha kale 2) Lugha ya Shamu ya kale 3) Nakala za mwanzo za toleo la Biblia ya lugha ya Shamu (Syria ya kale)

e. hakuna hoja dhidi ya andiko hili toka kwa wazee wa Kiyunani (mpaka karne ya kumi mbili) f. yanapatikana katika kitabu cha miswaada ya kale D (codex D), machapisho ya ki-Magharibi ya

karne ya sita, toleo la Biblia ya Kilatini, na baadaye toleo la Biblia ya lugha ya Shamu. 2. Ushahidi wa ndani

a. msamiati na mtindo ulipendwa zaidi sana na Luka kuliko Yohana. Iliwekwa katika baadhi ya machapisho ya Kuyunani baada ya Luka 21:38 na kwa mengineyo baada ya 24:53.

b. Moja kwa moja inaharibu muktadha wa mazungumzo ya Yesu kwa viongozi wa Kiyahudi baada ya sikukuu ya Vibanda, 7:1-52; 8:12- 59.

c. Haufanani katika mihtasari ya injili 3. Kwa majadiliano kamili ya kiufundi tazama Bruce M. Metzger's A Textual Commentary on the Greek

New Testament, kr. 219-221.

Page 165: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

149

C. Uwajibikaji huu waweza kuwa ni simulizi halisi za kitamaduni kutoka katika maisha ya Yesu. Hata hivyo, kuna uwajibikaji mwingi wa maisha ya Yesu ambao waandishi wa Injili walizichagua kutokuuweka kwenye kumbu kumbu (Yohana 20:30-31). Ni waandishi wa Injili wenyewe waliokuwa wamevuviwa. Baadaye Waandishi hawakuwa na haki ya kujumuisha uhusika wa maisha ya Yesu, hata kama ni kweli, kile ambacho hakikujumuishwa na mwandishi wa mwanzo aliyevuviwa. Ni waandishi wa awali pekee ndiyo walikuwa na ufahamu chini ya maongozi ya Roho Mtakatifu kufanya uchaguzi, kupanga, na kubadili kazi na maneno ya Yesu. Kifungu hiki siyo cha asilia na, hivyo basi, hakikuvuviwa na hakipaswi kuwekwa katika Biblia zetu!

D. Nimechagua kutokuchangia hoja katika kifungu hiki kwa sababu sikiamini kuwa ni sehemu ya uwandishi wa kalamu ya Yohana na, hivyo sasa, siyo sehemu ya andiko lililovuviwa (hata kama ni la ki-historia).

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 8:12-20 12Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima. 13 Basi Mafarisayo wakamwambia, Wewe unajishuhudia mwenyewe; ushuhuda wako si kweli. 14 Yesu akajibu, akawaambia, Mimi ningawa ninajishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu ndio kweli; kwa sababu najua nilikotoka na niendako; lakini ninyi hamjui nilikotoka wala niendako. 15 Ninyi mwahukumu kwa kufuata mambo ya mwili; mimi simhukumu mtu. 16 Nami nijapohukumu, hukumu yangu ni kweli; kwa kuwa mimi si peke yangu, bali ni mimi na yeye aliyenipeleka. 17 Tena katika torati yenu imeandikwa kwamba, Ushuhuda wa watu wawili ni kweli. 18 Mimi ndimi ninayejishuhudia mwenyewe, naye Baba aliyenipeleka ananishuhudia. 19Basi wakamwambia, Yuko wapi Baba yako? Yesu akajibu, Mimi hamnijui, wala Baba yangu hammjui; kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba yangu. 20 Maneno hayo aliyasema alipokuwa akifundisha hekaluni, katika chumba cha hazina; wala hakuna mtu aliyemkamata, kwa sababu saa yake ilikuwa haijaja bado

8:12 "Basi Yesu akawaambia tena akasema" "Makutano" hayakutajwa katika sura hii. Yawezekana sikukuu ya Vibanda ilikuwa imepita na Yesu alikuwa angali hekaluni akijaribu kujenga hoja na kuwashuhudia viongozi wa Kiyahudi. Hata hivyo, kama Yesu alivyotumia maji ya ibada kwenye sherehe kujidhihilisha mwenyewe, katika sehemu hii anatumia uangavu wa karamu ya sikukuu kujifunua mwenyewe, katika sehemu hii alitumia taa za ibada za sikukuu kujidhihilisha mwenyewe. Hakika inawezekana kuwa Yohana 8:12-10:21 angali amekitwa katika siku ya mwisho ya Sikukuu ya Vibanda (Mahema). ◙ "Mimi ni nuru" Yohana 6, 7, na 8 inaonekana kuhusiana na kipindi cha Waisraeli kutangatanga nyikani, ambayo ndio chanzo cha stiari ambayo Yesu anaitumia mwenyewe.

1. Yohana 6 anatumia "manna" na "mkate wa uzima" 2. Yohana 7 anatumia "maji" na "maji yaliyo hai" 3. Yohana 8 anatumia "taa" na " utukufu wa Shekinah."

stiari hii ya taa imerudiwa kila mahala katika Yohana (kama vile Yohana 1:4-5, 8-9; 3:19-21; 9:5; 12:46). Pamekuwapo na baadhi ya mijadala kuhusiana na nini hiki kinarejelea.

1. Hofu ya kale juu ya giza 2. Sifa ya Mungu katika Agano la Kale (kama vile Zab. 27:1; Isa. 60:20; 1 Yohana 1:5) 3. Usuli wa Sikukuu ya Vibanda, uwashaji wa vinara katika uga wa mwanamke 4. Kidokezo kwenye wingu la utukufu shekinah katika kipindi cha kutangatanga jangwani lenye kuashiria

uwepo wa Mungu 5. sifa za ki-masihi katika Agano la Kale (kama vile Isaya 42:6, 49:6; Luka 2:32).

Waalimu wa dini ya Kiyahudi pia walitumia "taa" kama sifa ya Masihi. Uwashaji wa taa kubwa katika uga wa mwanamke wakati wa Sikukuu ya Vibanda ni muundo wa wazi juu ya maelezo ya Yesu. Uhusishaji wa taa wa ki-

Page 166: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

150

Masihi na nukuu maalumu katika Yohana 1:4,8, vinashabihiana na sikukuu kwenye hekalu juu ya Yesu kuendelea kuudhihilisha uasili wake wa kweli. Hii ni moja ya zile “Ndimi” saba za semi katika Yohana (ikifuatiwa na shamirisho)

1. Mimi ndimi Mkate wa uzima (Yohana 6:35,41,48,51) 2. Mimi ndimi Nuru ya ulimwengu (Yohana 8:12; 9: 5; kama vile Yohana 1:4,9; 12:46) 3. Mimi ndimi mlango wa wanakondoo (Yohana 10:7,9) 4. Mimi ndimi mchungaji mwema (Yohana 10:11,14) 5. Mimi ndimi ufufuo, na uzima (Yohana 11:25) 6. Mimi ndimi, njia, kweli, na uzima (Yohana 14:6) 7. Mimi ndimi mzabibu wa kweli (Yohana 15:1,5)

Haya maelezo ya kipekee, yanapatikana katika Yohana pekee, zinaelekeza kwenye ubinadamu wa Yesu. Yohana anatizamisha juu ya dhana binafsi ya wokovu. Yatupasa kumtumainia Yeye!

◙ "Ya ulimwengu" Hili neno (kosmos, tazama Mada Maalumu katika Yohana 14:17) linaonyesha nafasi ya ulimwengu wote kwa injili ya Yesu kristo (kama vile Yohana 3:16).

◙ "Yeye anifuataye" Hii ni kauli tendaji endelevu ya wakati uliopo. Ni lazima ikumbukwe kwamba Ukristo sio kanuni ya imani au thiolojia, badala yake, ni uhusiano binafsi unafuatiwa na maisha ya ufuasi (kama vile Mt. 28:18-20; 1 Yohana 1:7).

◙ "Sitaenenda katika giza" Hili ni dokezo la dhana ya kitheolojia ya Shetani "amepofusha fikra zao wasioamini" (kama vile 2 Kor. 4:4). Kuna mitazamo zaidi kwenye vifungu vya kale vya Agano Jipya vinavyozungumzia neno la Mungu kama vile "Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga wa njia yangu" (kama vile Zab. 119:105). Wao waikubalio “Nuru" yawapasa kuishi maisha tofauti (kama vile 1 Yoh. 1:7)!

◙ "Nuru ya uzima" Yesu huumiliki uzima wa Mungu na kuwapa wafuasi Wake (kama vile Mt. 5:14), wao ambao tayari Mungu amempa Yeye.

8:13 "Mafarisayo" Tazama Mada Maalumu katika Yohana 1:24

◙ "Ushuhuda wako siyo kweli" Wayahudi walikuwa wakidai ushahidi halali wa kiufundi (yaani., uhitaji wa mashahidi wawili, kama vile Hes. 35:30; Kumb. 17:6; 19:15-21). Yesu alikua amesema mapema kwa upinzanio huu (kama vile. Yohana 5:31 na kuendelea) na alikua ametoa mashahidi kadhaa. Katika muktadha huu, shahidi wake ni Mungu Baba!

8:14, 16 "ninajishuhudia. . .nijapohukumu" Hizi zote ni sentensi shurutishi daraja la tatu ambazo zina maana ya mambo muhimu. Zaidi ya masharti toka Yohana 8 ni ya aina hii.

◙ "kwa sababu najua nilikotoka na niendako" Huu tena ni uwepo "juu na chini" wa pande mbili. Yesu alikuwa na kumbukumbu kamili ya uwepo wake kabla na Baba, uelewa wa kusudi lake, na dhima ya muda wake wa kinabii (kama vile. Yohana 1:1-4, 14-18; 7:28-29; 13:1; 17:5).

◙ "lakini ninyi hamjui nilikotoka wala niendako" Hii lazima inahusiana na Yohana 7. Hawakujua mahali Yesu alikozaliwa (kama vile Yohana 8:41-42) wala hawakujua wapi alikua anaenda (kama vile Yohana 7:34-36; 8:21). Tazama MADA MAALUMU: MASHUHUDA WA YESU katika Yohana 1:8

8:15 "Ninyi mwahukumu kwa kufuata mambo ya mwili" hii pia ni msisitizo wa sura ya 7 (kama vile Yohana 8:24). Tazama Mada Maalumu: Mwili (sarx) katika Yohana 1:14

Page 167: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

151

◙ "mimi simhukumu mtu" Wengine wanaona hapa kupingana kati ya Yohana 3:17 na 9:39. Yesu hakuja kuhukumu, bali kutoa uzima. Kwa ukweli wa kuja kwake wale wanaomkana kuhukumiwa (kama vile Yohana 3:18-21).

8:16-18 Tena hili lilikuwa suala la mashahidi wawili waliohitajika katika kesi ya kisheria. (kama vile Hes. 35:30; Kumb. 17:6; 19:15). Yesu, kwa maneno yasiyo na uhakika, anathibitisha umoja wake na Baba (kama vile Yohana 7:29; 14:9). Tazama MADA MALUMU: MASHUHUDA WA YESU katika Yohana 1:8

8:16 NASB (1970), NJB, REB "Yeye aliyenituma" NASB (1995), NKJV, NRSV, NIV "Baba aliyenituma" Kama vile kuna kutofautiana kati ya matoleo mawili ya NASB, vivyo hivyo kuna kutokukubaliana kati ya UBS3,4

1. UBS3 inatoa "Baba" alama "C"( MS P39,66,75, אi2, B, L, T, W

2. UBS4 inatoa "Baba" alama "A" ( (MSS א*, D, na baadhi ya matoleo ya Shamu ya zamani yakaondoa)

Yesu hayupo peke yake! Baba huwa naye daima (kama vile Yohana 8:16,29; 16:32), isipokuwa kuwepo msalabani (kama vile Marko 15:34). Furaha na kukamilisha ushirika ndicho kiini cha wokovu. Kusudi la uumbaji lilikuwa kwa Mungu kuwa na Mtu wa kushirikiana naye, kwa hayo (yaani., Kristo, kama vile Yohana. 1:3; 1 Kor. 8:6; Kol. 1:16; Ebr. 1:2) aliwaumba kwa sura na mfano wa YHWH kama vile Mwa. 1:26,27). Upungufu huu wa ushirika ni adhabu ya dhambi. Marejesho yake ni kazi ya utume wa Yesu.

8:19 "Yuko wapi Baba yako" Walikua bado wanamuelewa Yesu kwa kiwango cha kimwili, halisi. Nia zao za awali na za kiburi zilifungwa kwa ukweli (kama vile Yohana 8:27). Kutoelewana huku ni sifa za fasihi za injili ya Yohana.

◙ "kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba yangu" Hii ni Sentensi shurutishi daraja la tatu. Mara nyingi huitwa "kinyume na ukweli." "Mimi hamnijui, wala Baba yangu hammjui; kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba yangu." Madhari hii inarudiwa kutoka Yohana 5:37, tazama maelezo kamili katika Yohana 7:28. Ni vigumu kufafanua injili ya Yohana kwa sababu ni kama mchoro wa mfumo unaoendelea au simfini ya tuni iliyojirudia.

8:20 "aliyasema alipokuwa akifundisha hekaluni" Aya hii inaonekana kuwa na maoni mengine ya wahariri kutokana na ushahidi wa macho. Hekalu halikuwa jengo tofauti. Hadithi za Rabbi (Shekalim 6) zinasema kuwa vyombo vyenye tarumbeta kumi na tatu, kila alama kwa lengo fulani, viko katika uga wa wanawake (kama vile. Marko 12:41), ambapo Wana-kondoo wengi walitengenezwa wakati wa sikukuu ya vibanda.

◙ "saa yake ilikuwa haijaja bado" Tazama maelezo katika Yohana 2:4.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 8:21-30 21 Basi akawaambia tena, Mimi naondoka, nanyi mtanitafuta; nanyi mtakufa katika dhambi yenu; mimi niendako ninyi hamwezi kuja. 22 Basi Wayahudi wakasema, Je! Atajiua! Kwa kuwa asema, Mimi niendako ninyi hamwezi kuja? 23 Akawaambia, Ninyi ni wa chini, mimi ni wa juu; ninyi ni wa ulimwengu huu, mimi si wa ulimwengu huu. 24 Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu. 25 Basi wakamwambia, U nani wewe? Yesu akawaambia, Hasa neno lilo hilo ninalowaambia. 26 Ninayo mengi ya kusema na kuhukumu juu yenu; lakini yeye aliyenipeleka ni kweli, nami niliyoyasikia kwake, ndiyo ninenayo katika ulimwengu. 27 Wala hawakutambua ya kuwa anawatajia Baba. 28 Basi Yesu akawaambia, Mtakapokuwa mmekwisha kumwinua Mwana wa

Page 168: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

152

Adamu, ndipo mtakapofahamu ya kuwa mimi ndiye; na ya kuwa sifanyi neno kwa nafsi yangu, ila kama Baba alivyonifundisha ndivyo ninenavyo. 29 Naye aliyenipeleka yu pamoja nami, hakuniacha peke yangu; kwa sababu nafanya sikuzote yale yampendezayo. 30 Naye alipokuwa akisema hayo, wengi walimwamini.

8:21-22 "Mimi niendako ninyi hamwezi kuja. . . Je! Atajiua! Kwa kuwa asema" Swali la Yohana 8:22 linatarajia jibu la "hapana". Ni dhahiri kwamba kutokana na mazingira ingawa hawakuelewa maneno yake (kama vile. Yohana 7:34-36), waliyahusianisha na kifo chake. Kutoka kwa Yusufu tunajifunza kwamba kujiua kulimhukumu mtu kwenda kuzimu. Swali lao linaonekana kuonyesha walidhani kuwa hapa ndipo Yesu lazima awe.

8:21 "nanyi mtakufa katika dhambi yenu" Hii ni sawa sawa "nanyi mtakufa katika dhambi yenu." Neno "dhambi" ni ummoja katika Yohana 8:21 na wingi katika Yohana 8:24. Hii kimsingi inahusisha walipomkataa Yesu kama Kristo (kama vile Yohana 8:24). Hii ni dhambi isiyoweza kusamehewa ya injili za ufupisho. Viongozi wao wanamkataa Yesu peupe kutoka kwa maneno na ishara zake. Angalia maelezo yafuatayo kutoka kwa ufafanuzi wangu juu ya Marko.

Marko 3:29 "mtu atakayemkufuru roho mtakatifu" Hii lazima ieleweke katika mazingira yake ya kihistoria ya kabla ya wapentekoste. Ilikuwa imetumiwa katika maana ya ukweli wa Mungu kukatailiwa. Mafundisho katika aya hii ni kawaida kuitwa "dhambi isiyoweza kusamehewa." Inatakiwa kutafsiriwa kulingana na vigezo vifuatavyo: 1. Tofauti katika Agano la kale kati ya "makusudi" na "dhambi isiyokuwa na makusudi," (kama vile Hes.

15:27-31) 2. Ukosefu wa imani ya familia ya Yesu mwenyewe ilikuwa tofauti kwa kutoamini kwa mafarisayo katika hali

hii 3. Taarifa ya msamaha katika Marko 3:28 4. Tofauti kati ya uwiano wa injili, hasa mabadiliko ya "mwana wa adamu," (kama vile Mt. 12:32; Luka 12:10)

kwa "mwana wa adamu (kama vile Mt. 12:31; Marko 3:28). Katika ufahamu wa juu, dhambi hiii inafanywa na wale ambao wako katika uwepo na uelewa wa wazi, bado wanakataa Yesu kama njia ya Mungu ya ufunuo na wokovu. Waligeuza nuru ya injili katika giza la shetani (kama vile Marko 3:30). Walikataa kumpokea na kupatikana na hatia (kama vile Yohana 6:44,65). Dhambi isiyosameheka sio ya kukataliwa na Mungu kwa sababu ya tendo moja au neno moja, lakini daima, kuendelea kukataliwa na Mungu katika Kristo kwa hiari ya kutokuamini (yaani, mwandishi na mafarisayo).Dhambi hii inaweza tu kutolewa na wale ambao wamekuwa wazi kwa injili. Wale ambao wamesikia ujumbe kuhusu yesu ni dhahiri sana walihusika na kukataa kwake. Huu ni utamaduni wenye uhalisia wa kisasa ambao daima unapatikana kwenye injili, lakini humkataa Yesu (yaani, Marekani, utamaduni wa Magharibi).

8:23 "Ninyi ni wa chini, mimi ni wa juu " Huu ni mfano mwingine wa Yohana wa uthibiti wa wima wa pande mbili (yaani., chini dhidi ya juu, kama vile Yohana 7:35-36; 18:36). Tofauti ya Yohana kati ya Yesu ambaye katoka juu na Wayahudi ambao ni kutoka chini, inaunda uthibiti wa watu wawili ambao ni wa pekee kati ya injili. Injili za ufupisho (Mathayo, Marko, Luka) imetofautisha umri wa enzi mbili za Kiyahudi, enzi iliyopo ya uovu na enzi ya baadaye ya haki. Tofauti hii inaelezea kati ya pande mbili za ulalo na pande mbili za wima. Je Yesu alifundisha watu katika mazingira tofauti? Bila shaka injili ya ufupisho iliandika mafundisho ya umma ya Yesu wakati Yohana aliandika mafundisho binafsi ya Yesu kwa wanafunzi.

◙ "Ninyi ni wa ulimwengu huu" Ulimwengu uko katika uweza wa yule mwovu (kama vile 2 Kor. 4:4; Efe. 2:2; na 1 Yohana 5:19). Kwa ulimwengu (kosmos) tazama Mada Maalumu katika Yohana 14:17

8:24 "kwa sababu" Hii ni sentensi shurutishi daraja la tatu ambayo ina maana ya kitendo muhimu

NASB, NKJV “msiposadiki ya kuwa mimi ndiye" NRSV, JB "Amini kwamba mimi ndiye "

Page 169: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

153

TEV "Amini kwamba mimi ndiye mimi " NJB "Amini kwamba mimi ndiye" Hii ni mojawapo ya maneno yenye nguvu zaidi ya ufahamu wa Yesu katika asili yake mwenyewe Ki-Uungu (au inawezekana kwamba katika muktadha huu inamrejea"masihi"). Anatumia andiko la Agano la Kale la YHWH (kama vile. "mimi ndiye" katika Kutoka. 3:14). Hii inatofautiana na umaarufu wa neno "mimi ndiye" katika kauli ya Yohana. Hii haina maelezo (kama vile Yohana 4:26; 6:20; 8:24,25,58; 13:19; 18:5,6,8). Tazama Mada Maalumu: Matumizi ya Yohana ya "Kuamini" katika Yohana 2:23 8:25 "U nani wewe" Mamlaka ya Wayahudi wanatafuta mazingira ya kisheria kwa ajili ya malipo ya kukufuru (kama vile Mt. 26:57-68; Marko 14:53-65)! Wanataka auawe. Hawakutaka taarifa lakini walitaka ahukumiwe. Yesu anajionyesha wazi wazi katika Yohana (kinyume na injili za ufupisho)! Maneno yake (yaani, Yohana 8:24) na Matendo yake (yaani, kuponya siku ya sabato) huonyesha wazi mamlaka yake. NASB "Hasa neno lilo hilo ninalowaambia" NKJV "Hasa neno lilo hilo ninalowaambia" NRSV "Kwa nini mimi kamwe nawaambie" TEV "Nimekuambia tangu mwanzo" NJB "Nimekuambia tangu mwanzoni" Mwanzo maandishi ya Kiyunani hayakuwa na nafasi kati ya maneno. Kwa hiyo barua za Kiyunani zinaweza kugawanywa katika maneno tofauti ili kufanya maneno kuendana na muktadha. Ugawanyiko wa tafsiri hausiani na tofauti ya maandishi, lakini mgawanyiko wa neno. Hapa kuna chaguzi.

1. hote – Niwaambieni toka mwanzo (NASB, NKJV, TEV, NJB, NIV) 2. ho ti kama nahau yenye mshangao ya lugha ya Kisemitic – kwamba mimi nazungumza na wewe kabisa

(NRSV, TEV rejeo) Pengine ni juu ya neno la Yohana linalotumia neno hili "mwanzo" linatumika katika tafsiri ya machapisho ya kale ya Mwanzo. 1:1 (uumbaji) na katika Yohana 1:1 (huduma yake). Yesu amekuwepo toka "mwanzo" na amekuwa akiwaambia hivi kila wakati kwa maneno na matendo! 8:26-27 Dhamira hizi zinarudiwa katika Yohanaa kwa msisitizo.

1. Naye Baba ndiye aliyenipeleka (kama vile Yohana 3:17,34; 4:34; 5:36,38; 6:29,44,57; 7:28-29; 8:16,26,42; 10:36; 11:42; 12:49; 14:24; 15:21; 17:3,18,21,23,25; 20:21)

2. Mungu ni kweli (kama vile Yohana 3:33; 7:28) 3. Mafundisho ya Yesu ni kutoka kwa Baba (kama vile Yohana 3:11; 7:16-17; 8:26,28,40; 12:49; 14:24; 15:15) 4. Yesu anamdhihirisha Baba (kama vile Yohana 1:18; 8:26-29; 12:49-50; 14:7,9)

◙ "Ulimwengu" Tazama maelezo katika Yohana 1:10.

8:27 Maoni mengine ya kihariri ni kutoka kwa mwandishi. Ikiwa wangeelewa lugha yake ya sitiari na ya ishara, wao, kama Wayahudi wengine, wangejaribu kumwua (kama vile Yohana 5:18; 8:59; 10:33). Madai yake hayakuwa ya siri!

8:28 "Mtakapokuwa mmekwisha kumwinua Mwana wa Adamu" Hili ni dokezo la agano la kale kwa Hes. 21:4-9, ambalo linajadiliwa katika Yohana 3:14. Neno hili, kama yalivyo maneno mengine katika Yohana, lina maana mbili. Linaweza kumaanisha "kuinuliwa juu" kama msalabani (kama vile Yohana 3:14; 12:32,34), lakini mara nyingi hutumika kwa maaana ya “kuinuliwa” kama katika Mdo. 2:33, 5:31; Fal. 2:9. Yesu alijua kwamba alikuja kufa (kama vile Marko 10:45).

Page 170: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

154

◙ "Mwana wa Adamu" Hii ni sifa pekee ya Yesu iliyochaguliwa ambayo haikuhusianishwa kijeshi wala kitaifa ndani ya sheria za Kiyahudi. Yesu alichagua cheo hiki kwa sababu kinaunganisha dhana zote za ubinadamu (kama vile Ezek. 2:1; Zab. 8:4) na uungu (kama vile Dan. 7:13). ◙ "Ndipo mtakapofahamu ya kuwa mimi ndiye" Hata wanafunzi wake (na familia yake) hawakuelewa kikamilifu mpaka (kama vile Yohana 7:39) baada ya Pentekoste! Roho alikuja na nguvu za kuwafungua macho wote waliokuwa na macho na masikio ya kiroho! Kwa uthibitisho wa kipekee wa kisarufi “Mimi ndiye” tazama maelezo katika Yohana 8:24. Wao watajua

1. Yeye ni nani (yaani., Masihi) 2. kwamba Yeye anamdhihirisha Baba (kama vile Yohana 5:19-20) 3. kwamba Yeye na Baba ni wamoja (Yohana 8:29)

8:29 "Hakuniacha peke yangu" Ushirika wa Yesu na Baba alimsaidia (kama vile Yohana 8:16; 16:32). Hii ndio sababu ushirika uliovunjika pale msalabani ulikuwa mgumu kwake (kama vile Marko 15:34).

8:30 "Wengi walimwamini" Kuna usawa mkubwa katika matumizi ya neno "amini" kwenye kifunguu hiki. Inaonekana kuelezea imani isiyo wazi kwa wasikilizaji fulani (kama vile Mathayo 13; Marko 4). Walikuwa tayari kukubali kwamba alikua Masihi kulingana na ufahamu wao wa nini maana yake. Muktadha wa Yohana 8:30-58 unaonyesha wazi kwamba hawakuwa waamini wa kweli (kama vile. Yohana 2:23-25). Katika Yohana kuna ngazi kadhaa za imani, sio wote huongozwa kwenye wokovu. Tazama Mada Maalumu katika Yohana 2:23

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 8:31-33 30 Naye alipokuwa akisema hayo, wengi walimwamini. 31 Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; 32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru. 33 Wakamjibu, Sisi tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wo wote; nawe wasemaje, Mtawekwa huru?

8:31 "Ninyi mkikaa" Hii ni sentensi shurutishi daraja la tatu ambayo inamaanisha juu ya uwepo wa kitendo muhimu. Msisitizo juu ya imani endelevu pia inaelezwa wazi katika Yohana 15. Hiki ni kitu kinachokosekana katika kuitangaza injili. Neno linatakiwa kuaminiwa (kama vile Yohana 5:24), tii, na kukaa ndani yake. Tazama Mada Maalumu: "Kukaa" katika 1 Yohana 2:10

MADA MAALUM: USTAHIMILIVU

Mafundisho ya Kibiblia yenye kuhusiana na maisha ya Kikristo ni magumu kuyaelezea kwa sababu yanawasilishwa katika jozi halisi ya upembuzi wa kimashariki (angalia Mada Maalum: Fasihi ya Mashariki [mafumbo ya Kibiblia]). Jozi hizi zinakinzana, ingawa bado zote ni za Kibiblia. Wakristo wa Kimagharibi yamejaribu kuchagua ukweli mmoja na kuachana na ukweli wa pili. Ngoja nielezee kwa mifano.

A. je wokovu ni maamuzi ya mwanzo kumwamini Kristo au ni kuyatoa maisha yako yote kwenye uanafunzi?

B. je wokovu ni uchaguzi kwa neema itokayo kwa Mungu Mkuu au kuamini kwa mwanadamu na mwitikio wa toba kwenye ahadi ya Kiungu?

C. je wokovu, mara unapoupata, ni vigumu kuupoteza, au kunahitajika kwa ajili ya kuongeza jitihada? Suala la ustahimilivu limekuwa lenye mkanganyo kwa muda wote wa historia ya kanisa. Tatizo lilianza inavyoonekana na mgongano wa sura za agano Jipya:

A. maandiko juu ya ahadi 1. maelezo ya Yesu (Yohana 6:37; 10:28-29) 2. maelezo ya Paulo (Rum. 8:35-39; Efe. 1:13; 2:5,8-9; Fil. 1:6; 2:13; 2 The. 3:3; 2 Tim. 1:12; 4:18) 3. maelezo ya Petro ( 1 Pet. 1:4-5)

B. maandiko juu ya hitaji la ustahimilivu

Page 171: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

155

1. maelezo ya Yesu (Mt. 10:22; 13:1-9,24-30; 24:13; Marko 13:13; Yohana 8:31; 15:4-10; Ufu. 2:7,17,26; 3:5,12,21)

2. maelezo ya Paulo (Rum. 11:22; 1 Kor. 15:2; 2 Kor. 13:5; Gal. 1:6; 3:4; 5:4; 6:9; Fil. 2:12; 3:18-20; Kol. 1:23; 2 Tim. 3:2)

3. maelezo ya mwandishi wa Waebrania (2:1; 3:6,14; 4:14; 6:11) 4. maelezo ya Yohana (1 Yohana 2:6; 2 Yohana 9) 5. maelezo ya Baba (Ufu. 21:7)

Masuala ya wokovu wa Kibiblia toka kwa pendo, rehema, na neema ya Mungu Mkuu wa Utatu. Hakuna mwanadamu atakaye okolewa pasipo kuanzishwa na Roho (kama vile Yohana 6:44,65).Uungu huja kwanza na kuweka ajenda, lakini huhitaji kwamba lazima wachukue hatua katika imani na toba, kwa hali zote mwanzoni na kuendelea. Mungu hutenda na wanadamu katika ushirika wa agano.kuna faida na uwajibikaji! Wokovu hutolewa kwa wanadamu wote. Kifo cha Yesu kinashughulika na tatizo la dhambi ya uumbaji la mwanadamu aliyeanguka. Mungu amekwisha kutoa njia na kuwataka wale wote walioumbwa kwa sura yake kuitikia kwenye pendo lake katika Yesu. Kama ukihitaji kusoma zaidi juu ya somo hili toka kwenye mtizamo wa wale wasio wafuasi wa Calvin, angalia

1. Dale Moody, The Word of Truth, Eerdmans, 1981 (kur. 348-365) 2. Howard Marshall, Kept by the Power of God, Bethany Fellowship, 1969 3. Robert Shank, Life in the Son, Westcott, 1961

Biblia inayaainisha matatizo mawili tofauti katika eneo hili: (1) kuzichukulia ahadi kama kibali cha kuishi pasipo mafanikio, maisha ya ubinafsi na (2) kuwatia moyo wale wote wanaojitahidi na huduma na dhambi binafsi. Tatizo ni kuwa makundi potofu yanachukua jumbe zisizo sahihi na kujenga miundo ya kithiolojia juu ya sura za Kibiblia .baadhi ya Wakristo huhitaji ujumbe wa ahadi, wakati wengine huhitaji onyo kali! Ni kundi lipi ulilopo wewe?

◙"katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli" Yesu alisisitiza utii kwenye mfumo wa maisha (kwenye amri zake, kama vile Yohana 8:51,52,55; 14:15,21,23,24; 15:10,20; 17:6; Luka 6:46; 2 Yohana 9). Kwa maana mstari huu unaaksi neno shema, neno la Kiebrania linamaanishaa "kusikia ili kutenda" (yaani, Kumb. 6:4-6). 8:32 "mtaifahamu" Hii hutumiwa katika maana ya Agano la Kale ya neno "kujua," ambalo linamaanisha "uhusiano wa kibinafsi," si kwa maana ya "kweli ya utambuzi" (kama vile Mwa. 4:1; Yer. 1:5). Kweli ni Mtu! Aya hii, ambayo mara nyingi hupatikana kwenye taasisi za kujifunzia, hairejerei kwenye ujuzi wa binadamu aliojikusanyia. Hiyo imeonyesha kuwagawa na kufunga, kutowaweka huru wanadamu. "Ukweli" uliosemwa hapa ni injili na ubinadamu wa Yesu kristo. Hakuna ukweli, amani, au tumaini mbali naye! 8:32, 40, 44, 45, 46 "kweli" Hii ni dhana kuu ya muktadha. Neno hili lina vidokezo viwili.

1. Uaminifu 2. kweli dhidi ya uwongo

Vidokezo vyote viwiwli ni kweli juu ya maisha na huduma ya Yesu. Yeye ni vyote maudhui na lengo la injili. Kimsingi ukweli ni Mtu haswa! Yesu anamdhihirisha binafsi baba yake. Aya hii mara nyingi hutolewa katika muktadha na kutumika katika mazingira ya elimu. Ukweli, hata ukweli wa kweli, hata mambo mengi ya kweli yaliyoko kwenye ukweli, hayamweki mtu kuwa huru (kama vile Mhu. 1:18). Tazama Mada maalumu: Kweli (neno) katika Yohana 6:55 na 17:3 8:32 “itawaweka huru" Waumini wako huru kutoka kwenye sheria, taratibu za kidini, ubobeaji wa kiutendaji, ibada za kibinadamu. Hata hivyo waamini huru hujifunga kwa ajili ya injili (kama vile Rum. 14:1-15:6; 1 Kor. 8-10). 8:33 “Sisi tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu" inashangaza kuona ni kwa namna gani fahari ya upofu wa jamii unaweza kuwa. Ni vipi kuhusu Misri, Shamu, Babeli, Uajemi, Uyunani, na Rumi?

Page 172: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

156

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 8:34-38 34 Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi. 35 Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote. 36 Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli. 37 Najua ya kuwa ninyi ni uzao wa Ibrahimu lakini mnatafuta kuniua kwa sababu neno langu halimo ndani yenu. 38 Niliyoyaona kwa Baba ndiyo niyanenayo; nanyi vivyo hivyo mliyoyasikia kwa baba yenu ndiyo myatendayo.

8:34 "Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi" Yesu akijaribu kuwaongoza kwenye ukweli wa kiroho nyuma ya maneno yake ya awali "itawaweka huru" katika Yohana8:32, ambayo taarifa ya Yohana 8:33 inaonyesha kwamba walielewa. Maneno haya yanahusiana na mashtaka ya nguvu ya Yesu katika Yohana 8:21 na 24. Hukumu zake za wafuatiliaji wa pembezoni hizo zinatumiwa katika Yohana 8:44-47. Kama Frank Stagg anasema katika Thiolojia ya Agano Jipya, "jambo la dhiki ya mwanadamu ni matokeo ya jaribu lake la kuwa huru (uk. 32). KitenzI hapa ni kauli tendaji endelevu ya wakati uliopo, "kufanya," ambayo inaashiria dhambi inayoendelea. Kuendeleza dhambi ni ushahidi tosha kwamba mtu "hajui" ukweli (Yesu). Ukweli huu mwingine unaelezwa kwa kutumia kauli ya vitenzi vya wakati uliopo "kutenda dhambi" katika 1 Yohana 3:6,9! Swali ni, "je, waamini wanaendelea kutenda dhambi?" Jibu lazima liwe "ndio" (kama vile Warumi 7; Yohana 1). Wakristo wanakabiliana na dhambi, lakini waliopotea wanajitokeza ndani yake na hawatambui! Biblia ya NET (uk. 1921 #21) huongeza maoni mazuri kwamba mazingira ambayo dhambi hutokea katika Yohana ni "kutokuamini" (dhambi isiyoweza kusamehewa). Hii si mazingira ya kimaadili lakini “Ni kuamini kwenye mazingira ya wokovu." "Dhambi" katika Yohana 1 pia ni kutoamini (dhambi hadi kifo)!

8:35 Aya hii haina uhusiano wa moja kwa moja na Yohana 8:34, lakini ni kwa Yohana 8:36. Yesu, sio yule Musa wa sheria za dini za Kiyahudi, ni mwana wa kweli (kama vile Ebr. 1:2; 3:6; 5:8; 7:28). Imani tu ndani yake, sio utendaji wa sheria na kanuni isiyo na mwisho, inaweza kumweka mmoja huru (kama vile Yohana 8:32).

◙"sikuzote" Tazama Mada Maalumu katika Yohana 6:58

8:36 "kama" Hii ni sentensi shurutishi daraja la tatu ambayo inazungumzia jambo muhimu.

8:37 "lakini mnatafuta kuniua" (kama vile Yohana 5:18; 7:1,19; 8:37,40; 11:53).

◙ "kwa sababu neno langu halimo ndani yenu" Maneno haya yanaweza kueleweka kwa maana kadhaa. Msaada wa utafiti wa manufaa ni The Bible in Twenty Six Translations.

1. "kwa sababu neno langu halina shaka ndani yako" -- American Standard Version 2. "haipatikani kwako" -- The New Testament cha Henry Alford 3. "hufanya njia ndani mwenu" -- The New Testament: A New Translation cha James Moffatt 4. "halina nafasi yoyote ndani yako" -- The Emphasized New Testament: A New Translation cha J. B.

Rotherham 5. "kwa sababu maneno yangu hayana nafasi ndani ya mioyo yenu" -- The Four Gospels cha E. Yohana 8:

Rieu Tena, shida ni kupokea au kutopokea injili. Ni suala la wokovu, sio maendeleo ya kimaadili.

8:38 "Niliyoyaona" Hii ni kauli tendaji timilifu elekezi ambayo inahusuiana na Yesu kabla kuwepo na ushirika wa sasa na Baba yake (kama vile Yohana 8:40,42).

◙ "nanyi vivyo hivyo mliyoyasikia kwa baba yenu ndiyo myatendayo" Kutaja kwa mara ya kwanza kwa neno "Baba" inaweza kuwa ni rejea ya jadi za Kiyahudi (kama vile Isaya 29:13). Hata hivyo, katika Yohana 8:41-44 somo hilo linamfaa shetani/Ibilisi. Matendo yao, nia, na maneno, yanamuunga mkono "Musa," huonyesha wazi uelekeo wao wa kiroho. Binadamu hawana/hawawezi kuanzisha katika ulimwengu wa kiroho. Kuna vyanzo viwili vya

Page 173: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

157

ushawishi (si wa vitu viwili) - Mungu/Kristo/Roho au Shetani/na wake! Jinsi mtu anayeitikia injili (kama vile Yohana 1:12; 3:16; 10:1-18; 14:6) inaonyesha mwelekeo wa kiroho! Kuna chaguo fulani la maandishi lililohusiana na maneno haya.

1. merejeo yote kwa "Baba" yanaweza rejeaYHWH (hakuna kiwakilishi nomino "yako") 2. kitenzi ni endelevu, sio elekezi

(tazama Bruce M. Metzger, A Textual Commentary on the Greek New Testament, ukur.225).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 8:39-47 39 Wakajibu, wakamwambia, Baba yetu ndiye Ibrahimu! Yesu akawaambia, Kama mngekuwa watoto wa Ibrahimu, mngezitenda kazi zake Ibrahimu. 40 Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, mtu ambaye nimewaambia iliyo kweli, niliyoisikia kwa Mungu. Ibrahimu hakufanya hivyo. 41 Ninyi mnazitenda kazi za baba yenu. Ndipo walipomwambia, Sisi hatukuzaliwa kwa zinaa; sisi tunaye Baba mmoja, yaani, Mungu. 42 Yesu akawaambia, Kama Mungu angekuwa baba yenu, mngenipenda mimi; kwa maana nalitoka kwa Mungu, nami nimekuja; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye ndiye aliyenituma. 43 Mbona hamyafahamu hayo niyasemayo? Ni kwa sababu ninyi hamwezi kulisikia neno langu. 44 Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo. 45 Nami, kwa sababu nasema iliyo kweli, hamnisadiki. 46 Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi? Nami nikisema kweli, mbona ninyi hamnisadiki? 47 Yeye aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; hivyo ninyi hamsikii kwa sababu ninyi si wa Mungu.

8:39 "Baba yetu ndiye Ibrahimu" Yesu alithibitisha asili yao ya kimwili kutoka kwa Ibrahamu, lakini alisema kuwa walikuwa na sifa za familia ya shetani (kama vile Yohana 8:38, 44). Uhusiano binafsi wa imani, si utambulisho wa rangi, uliowafanya Wayahudi kuwa sawa na Mungu (kama vile Kumb. 6:5,13; Rum. 2:28-29; 9:6).

◙"Kama" Hii ni sentensi shurutishi daraja la kwanza katika umbo (katika kishazi – kauli tendaji timilifu elekezi pamoja na ei), lakini inaweza kufanya kazi kama sentensi shurutishi daraja la pili (kama vile Yohana 8:19 na 42). Vigezo vya maandishi ya kiyunani vilijaribu kuondoa sura hii ya mchanganyiko wa sentensi shurutishi kwa kubadili kitenzi cha kwanza kwenda kwenye hali isiyo kamili. Ikiwa ndivyo ingeweza kusomwa, "Ikiwa mlikuwa watoto wa Ibrahimu, ambavyo sivyo, mngefanya kile Ibrahimu alichofanya, lakini ninyi sio." UBS4 Toa sura ya mchanganyiko wa hali shurutishi ya alama "B".

8:40 "mtu" Yesu sio tu alijisikia kama mwakilishi wa YHWH, sawa na asili ya Mungu pamoja na YHWH, lakini pia mwanadamu wa kweli. Madai haya yanakataa madai ya mafunuo ya walimu wa uongo wa pande mbili za umilele kati ya roho na vitu vya kimwili (kama vile 1 Yohana 1:1-4; 4:1-4).

MADA MAALUM: UJUZI WA KIPEKEE

Walimu wenye mafunuo ya uongo waliamini kwamba viumbwavyo, ulimwengu (maada) ni ovu, na kwahiyo katika upinzani wa ulimwengu wa roho, na kwamba roho tu ndiyo njema. Walijenga Mungu muovu na viumbe ya Agano la Kale kuelezea uumbaji wa ulimwengu (maada) na kumfanya Yesu Kristo kama Mungu kamili wa kiroho.

Imani za Walimu wajuzi wa uongo zinapingana kiukubwa na mafundisho yanayokubaliwa na mkristo. Ukristo unatufundisha kwamba wokovu unapatikana kwa kila mtu, sio wateule wachache na kwamba inakuja kutoka neema kupitia imani katika Yesu Kristo (Waefeso 2:8-9), na kutoka katika masomo au kazi. Chanzo cha ukweli ni Biblia tu, Ukristo unaelezea.

Walimu wa uongo walimngawanya kwa Yesu. Mtazamo mmoja ni kwamba alitokea tu kuwa na umbo lake la kibinadamu lakini kwamba alikuwa katika roho tu. Mtazamo mwingine uliweka wazi kwamba roho yake ya

Page 174: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

158

kiungu ilikuja juu ya mwili wake katika Ubatizo na kuondoka kabla ya kusulubiwa. Ukristo, kwa upande mwingine unashikilia kuwa Yesu alikuwa mwanadamu kamili na Mungu kamili na asili hizi zote zilikuwepo na muhimu kutoa sadaka ya kupendeza kwa dhambi ya ubinadamu.

8:41 NASB, NKJV "'Sisi hatukuzaliwa kwa zinaa”’ NRSV "'sisi sio watoto haramu'" TEV "'sisi ni watoto halali'" NJB "'hatukuzaliwa kiharamu'" Hii inaweza kushikamana na mashtaka ya Yohana 8:48 ("wewe ni Msamaria"). Inaonekana kwamba Wayahudi walikuwa wanadai kuwa Yesu alikuwa mtoto haramu, sio damu kamili ya Myahudi. Baadaye vyanzo vya mwalimu wa sheria za Kiyunani vinasema kwamba Yesu alizaliwa na Askari wa Kirumi. ◙ "sisi tunaye Baba mmoja, yaani, Mungu" maelezo haya yanafikirisha uwepo wa Mungu mmoja katika Agano la Kale (kama vile Kumb. 4:35,39; 6:4-5) yaliyotajwa kwa maneno ya Kibaba (kama vile Kumb. 32:6; Isaya 1:2; 63:16; 64:8). Hapa alikuwa kwenye mtanziko: Viongozi hawa wa Kiyahudi walithibitisha umoja wa Mungu (kama vile. kumb. 6:4-5) na kwamba utiifu wa sheria ya Musa ulileta uhusiano Mzuri na Mungu (kama vile Kumb. 6:1-3,17,24-25). Yesu alikuja kudai kuwa ni mmoja na Mungu! Yesu alidai kwamba kuwa na haki sawa na Mungu hakutegemei utendaji wa sheria, bali kwa imani binafsi ndani yake. Kuchanganyikiwa na kusita kwao kunaeleweka, lakini hapa ndipo ambapo ufahamu wa kiroho na matendo makuu ya Yesu huleta imani!

8:42 "Kama" Hii ni sentensi shurutishi daraja la pili inaitwa "kinyume na ukweli." "Kama Mungu angekuwa baba yenu, mngenipenda mimi" (kama vile Yohana 8:47).

8:43 "Ni kwa sababu ninyi hamwezi kulisikia neno langu" Hii inahusiana na uelewa na upokeaji kiroho. Walikuwa hawana masikio ya kiroho (kama vile Isaya 6:9-10; Mt. 11:15; 13:9,15-16,43; Marko 4:9,23; 7:16; 8:18; Luka 8:8; 14:35; Mt. 7:51; 28:26-27).

8:44 "Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi" Ni maneno ya kushangaza kwa viongozi wa kidini wa siku zake (kama vile. Yohana 8:47). Dhana hii ya tabia za kifamilia zilizoshirikishwa inaelezwa kwa lahaja ya Kiebrania, "mwana wa. . ." (kama vile Mt. 13:38; Mt. 13:10; Yohana 1. 3:8,10). Kwa "Ibilisi" tazama Mada Maalumu katika Yohana 12:31

◙"mwuaji tangu mwanzo" Hii haikuwa na maana ya kudokeza uovu wa milele (yaani., umiliki wa pande mbili kama ilivyokuwa kwenye dini za kale za huko Uajemi), lakini inaonyesha dhana ya majaribu ya kiroho ya Adamu na Hawa kwa wakala wa roho ya uongo iliyokaa ndani Nyoka (kama vile Mwanzo 3). Angalia tofauti ya kusudi kati ya Mungu ambaye ni kweli, ukweli na ibilisi!

8:46 "Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi" Katika muktadha, hii inahusiana na ushuhuda wa uwongo. Shetani anasema uongo, lakini Yesu anasema ukweli. Yesu anawaalika viongozi hawa wa kiyahudi kukanusha maneno na mafundisho yake, kuthibitisha kama ni muongo! Katika muktadha huu taarifa hii haionekani, inahusiana na dhambi za Yesu kama mafundisho ya Thiolojia yalivyo. Katika Yohana "dhambi" ni zaidi ya kanuni ya uovu katika ulimwengu ulioanguka kwenye uasi dhidi ya Mungu kuliko kitendo fulani cha dhambii. Dhambi ni kila kitu Yesu sio! Hatima ya "Dhambi" ni kutoamini (kama vile. Yohana 16:9).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 8:48-59 48 Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Je! Sisi hatusemi vema ya kwamba wewe u Msamaria, nawe una pepo? 49 Yesu akajibu, Mimi sina pepo; lakini mimi namheshimu Baba yangu, na ninyi mwanivunjia heshima

Page 175: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

159

yangu. 50 Wala mimi siutafuti utukufu wangu; yuko mwenye kutafuta na kuhukumu. 51 Amin, amin, nawaambia, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti milele. 52 Basi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng'amua ya kuwa una pepo. Ibrahimu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti milele. 53 Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani? 54 Yesu akajibu, Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si kitu; anitukuzaye ni Baba yangu, ambaye ninyi mwanena kuwa ni Mungu wenu. 55 Wala ninyi hamkumjua; lakini mimi namjua. Nikisema ya kwamba simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua, na neno lake nalishika. 56 Ibrahimu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi. 57 Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado miaka hamsini, nawe umemwona Ibrahimu? 58 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko. 59 Basi wakaokota mawe ili wamtupie; lakini Yesu akajificha, akatoka hekaluni.

8:48 "wewe u Msamaria, nawe una pepo" kuna uwezekano wa kwamba maana ya kweli ya kimazingira inatazamishwa katika neno la kiarama lililotafsiriwa na neno la Kiyunani "msamaria," ambalo lilimaanisha “ mkuu wa mapepo." Yesu alinena Kiarama. Ikiwa ni kweli hii inaendana na mashtaka ya mara kwa mara na viongozi wa kidini kwamba nguvu za Yesu zimekuja kutokana na chanzo kiovu cha nguvu za giza. Inawezekana kwamba kusema mtu alikuwa na pepo ingemaanisha walikuwa wanadanganya (kama vile Yohana 8:52). Kusema Yesu alikuwa Msamaria (kama vile. Yohana 4:9) au alikuwa na pepo (kama vile. Yohana 7:20; 8:48,49,52; 10:20,21, tazama Mada Maalumu katika Yohana 12:31) ilikuwa njia ya kusema kwamba mtu hapaswi kumsikiliza au kukubali ujumbe wake. Hii, kama "Ibrahimu ni Baba yetu," ilikuwa ni udhuru mwingne kwa kutomjibu Yesu au ujumbe wake. 8:49 Mtu hawezi kumuamini katika Baba na sio katika mwana (kama vile Yohana 1. 5:9-12); mtu hawezi kumjua Baba na kutomheshimu mwana (kama vile Yohana 5:23). Ingawa kwa nje ni watu wawili tofauti, lakini wao ni wamoja (kama vile Yohana 10:30; 17:21-23). 8:50 "utukufu wangu" tazama andiko la Yohana 1:14. 8:51,52 "Amin…. amini" Hizi zote ni sentensi shurutishi daraja la tatu zinazomaanisha kitendo muhimu. Angalia utii unahusianishwa na imani (tazama maandiko ya Yohana 8:48). ◙ "hataona mauti milele" Hili ni kanusho mara mbili lenye nguvu. Dhahili kabisa, hii inahusiana na kifo cha kiroho (kama vile. Yohana 8:21,24), sio kifo cha kimwili (kama vile. Yohana 5:24; 6:40, 47; 11:25-26). Ingaliweza kuhusiana na hofu ya kifo (kama vile 1 Wakorintho 15:54-57). Dhana ya "kifo" (thanatos) inaelezewa katika Biblia katika hatua tatu.

1. kifo cha kiroho, Mwa. 2:17; 3:1-24; Isay. 59:2; Warumi 7:10-11; Yakobo 1:15 (uhusiano na Mungu umevunjika)

2. kifo cha mwili, Mwa. 3:4-5; 5 (uhusiano na dunia umevunjika) 3. kifo cha milele, "kifo cha pili," Ufu. 2:11; 20:6,14; 21:8 (uhusiano uliovunjika na Mungu unafanywa wa

kudumu) Kifo ni kinyume cha mapenzi ya Mungu kwa uumbaji wake wa juu (kama vile Mwa. 1:26-27).

8:52 Hii inaonyesha kwamba hawakuelewa maneno ya Yesu (kama vile Yohana 8:51). Walichukua hili kuhusisha maisha ya kimwili ya Ibrahimu na Manabii.

8:53 Swali hili linatarajia jibu la "hapana". Ni tamako lenye kushangaza! Lakini hii ndiyo hasa Yesu alikuwa anadai. 1. Yeye alikuwa mkuu zaidi kuliko Ibrahimu, Yohana 8:53 2. Yeye alikuwa mkuu zaidi kuliko Yakobo, 4:12 3. Yeye alikuwa mkuu zaidi kuliko Yona, Mt. 12:41; Luka 11:32 4. Yeye alikuwa mkuu zaidi kuliko Yohana mbatizaji, 5:36; Luka 7:28 5. Yeye alikuwa mkuu zaidi kuliko Sulemani, Mt. 12:42; Luka 11:31

Page 176: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

160

Kitabu hicho cha Waebrania kinaonyesha ukubwa wa yesu juu ya Musa, Agano Jipya juu ya Agano la Kale (tazama fasihi yangu juu ya Waebrania www.freebiblecommentary.mobi).

◙ "Wajifanya u nani" Hii lilikuwa ni wazo la uhakika kabisa! Yesu anatoa hitimisho wazi katika Yohana 8:54 na 58 na wanajaribu kumpiga mawe kwa ajili ya kufuru (kama vile Yohana 8:59).

8:54 "kama" Ni sentensi shurutishi daraja la tatu inayomaanisha juu ya kitendo muhimu.

◙ "anitukuzaye" Inatumika hapa kwa maana ya heshima (kama vile Rum. 1:21; 1 Kor. 12:26).

8:55 "namjua. . . namjua" Neno la kiingereza linatafsiri maneno mawili ya Kiyunani katika Aya hii, ginōskō na oida, ambayo yanaonekana katika muktadha kuwa sawa (kama vile Yohana 7:28-29). Yesu anamjua Mungu na kamfunua kwa wafuasi wake. Ulimwengu (hata kwa Wayahudi) hawamjui Mungu (kama vile Yohana 1:10; 8:19,55; 15:21;16:3; 17:25). 8:56 "Baba yako Ibrahimu" Hili ni tamko lenye kushangaza. Yesu anajiondoa kutoka kwa "Wayahudi," "kwenye sheria" (kama vile. Yohana 8:17), "hekaluni," na hata kwa mzee Ibrahimu. Kuna mvunjiko wa wazi kutoka kwa Agano Jipya! ◙ "alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu" Hii ni kauli ya kati elekezi ya wakati uliopita isiotimilifu. Kwa kiasi gani Ibrahimu alimwelewa Masihi? Tafsiri kadhaa hutafsiri hii kwa maana ya baadaye. Chaguzi hizi zinachukuliwa kutoka The Bible in Twenty-Six Translations.

1. "aliinuliwa juu ili apate kuona" -- The Emphasized New Testament: A New Translation cha J. B. Rotherham 2. "alifurahia ili kwamba apate kuiona siku yangu" -- Revised Standard Version 3. "alijawa na furaha kwa matarajio ya kuona -- The Berkeley Version of the New Testament cha Gerrit

Verkuyl 4. "ya kuona kuja kwangu" -- The New Testament: An American Translation cha Edgar J. Goodspeed 5. "alifurahia sana kujua siku yangu" -- The New Testament in the Language of Today cha William F. Bec

Pia, The Analytical Greek Lexicon Revised edited cha Harold K. Moulton iliorodhesha vitenzi kama maana ya "kutamani sana" kutoka kwenye matumizi ya maandishi ya machapisho ya kale ya Kiyunani (uk. 2). ◙"naye akaiona, akafurahi" Hii inahusu moja ya mambo mawili.

1. kwamba Ibrahimu, wakati wa maisha yake,alikuwa na maono ya Masihi (kama II Esdras 3:14) 2. kwamba Ibrahimu alikuwa hai (mbinguni) na anajua kazi ya Masihi duniani (kama vile Ebr. 11:13)

Hoja yote kwenye maelezo ya Yesu ni kwamba Baba wa taifa la Wayahudi alitazamia umri wa Masihi pamoja na furaha kubwa, lakini "mbegu" ya sasa (kizazi) ilikataa kuamini na kufurahi! Ibrahimu ni Baba wa waamini (kama vile Rum. 2:28-29), sio wasioamini!

8:57 Vilevile, wasikilizaji wa Yesu hawakuyaelewa maneno yake kwa maana iliyo halisi! Mchanganyiko huu wawezekana ulikuwa wa makusudi! Hawakuona kwa sababu hawakutaka kuona au labda hawakuweza kuona!

8:58 "Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko" Hii ilikuwa ni kufuru kwa Wayahudi na walijaribu kumpiga Yesu mawe (kama vile Kutoka 3:12, 14). Walielewa kabisa yale aliyokuwa akiyasema, ambayo yalikuwa ni kwamba alikuwepo kabla kwenye ule Utatu (kama vile Yohana 4:26; 6:20; 8:24,28,54-59; 13:19; 18:5,6,8).

8:59 "Basi wakaokota mawe ili wamtupie" Maneno ya Yesu yalikuwa wazi sana. Alikuwa ni Masihi na alikuwa mmoja pamoja na Baba. Wayahudi, hawa katika Yohana 8:31 wanasema kuwa "wanamwamini," sasa wako tayari kumtupia mawe kwa kukufuru (kama vile Law. 24:16). Ilikuwa ni vigumu kwa wayahudi kukubali msingi wa ujumbe mpya wa Yesu.

1. Yeye hakutenda kama vile walivyotarajia Masihi atende 2. Aliwapa changamoto kwenye mila zao takatifu

Page 177: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

161

3. Aliwachanganya kwenye imani yao wa uwepo wa Mungu mmoja 4. Alisema kuwa Shetani, sio YHWH, alikuwa "Baba" yao

Mtu lazima "amponde mawe" au "kumpokea"! Hakuna mazingira ya kuwa pande zote! ◙ "Yesu akajificha, akatoka hekaluni" Hii ni moja ya Aya hiyo ambayo imesababisha wakalimani kutafakari (na kuongeza maneno kwa maandishi ya Kiyunani) kama

1. hii ilikuwa miujiza (kama vile Luka 4:30 na maongezo ya maandishi hapa) 2. Yesu akayeyuka katikati ya umati wa watu kwa sababu alionekana kama Wayahudi wengine wote

waliohudhuria Kulikuwa na ratiba ya ibada takatifu. Yesu alijua kwamba alikuja kufa na anajua, lini na wapi. "Saa yake haijafika"!

MASWALI YA MJADALA

Huu ni mwongozo wa fasiri, ina maanisha kwamba unawajibika kwa tafsiri zako mwenyewe za Biblia. Kila mmoja wetu lazima atembee katika mwanga tulio nao. Wewe, Biblia, na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Hutakiwi uvitelekeze vitu hivi kwa mfasiri. Maswali ya mjadala huu yanatolewa kukusaidia kufikiri juu ya mambo makubwa ya sehemu za kitabu hiki. Yanalenga kukuamsha kimawazo na sio kutoa maana.

1. Je, Yohana 7:53-8:11 ni sehemu ya awali ya injili ya Yohana? Kwa nini au sio? 2. Ni nini chanzo cha kauli ya Yesu "Mimi ni nuru ya ulimwengu"? 3. Kwa nini Wafalisayo walikuwa wapinzani kwa Yesu?

4. Elezea matumizi ya neno "amini" katika Yohana 8:30 kulingana na muktadha unaofuata.

Page 178: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

162

YOHANA 9

MIGAWANYO YA AYA YA TAFSIRI ZA KISASA UBS4 NKJV NRSV TEV NJB

Uponyaji wa mtu Mtu aliyezaliwa kipofu Yesu anajidhihilisha Yesu anamponya mtu Uponyaji wa mtu kipofu Aliyezaliwa Kipofu anapata kuona mwenyewe kama aliyezaliwa kipofu nuru ya uzima 9:1-12 9:1-12 9:1-12 9:1-2 9:1-5 9:3-5 9:6-7 9:8 0:9a 9:9b 9:10 9:11 9:12a 9:12b Mafarisayo Mafarisayo wanamtenga Mafarisayo wanauchunguza Wanauchunguza mtu aliyeponywa uponyaji Uponyaji 9:13-17 9:13-34 9:13-17 9:13-15 9:13-17 9:16a 9:16b 9:17a 9:17b 9:18-23 9:18-23 9:18-19 9:18-23 9:20-23 9:24-34 9:24-34 9:24 9:24-34 9:25 9:26 9:27 9:28-29 9:30-33 9:34 Upofu wa kiroho Nuru halisi na Upofu wa kiroho Upofu halisi 9:35-39 9:35-41 9:35-41 9:35 9:35-39 9:36 9:37 9:37 9:40-41 9:40 9:40-41 9:41

MZUNGUKO WA TATU WA USOMAJI KUFUATILIA KUSUDIO LA ASILI LA MWANDISHI KATIKA NGAZI YA AYA Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwatafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu.

Page 179: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

163

Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Aya ya kwanza 2. Aya ya pili 3. Aya ya tatu 4. N.k

UTAMBUZIWA KI-MUKTADHA WA MISTARI YA 1-41

A. Uponyaji wa kipofu, muujiza wa kawaida ulioonekana hasa katika huduma ya Yesu na ni wa kushangaza uliokamilishwa kwa mbinu nyingi na tofauti.

B. Kumponya kipofu ilikuwa ishara ya Kimasihi (Isaya 29:18, 35:5, 42:7, Mt. 11;5). Umuhimu wa uponyaji huu

unaonekana katika mazingira ya karibu sana ya usemi wa Yesu kwamba Yeye ni nuru ya ulimwengu (Ufu. Yohana 8:12 na 9:50). Wayahudi walitaka ishara; waliziona! Ni YHWH pekee awezaye kuyafungua macho!

C. Sura hii ni mfano tendaji wa upofu wa kimwili kwa mwanadamu na upofu wa kiroho kwa Mafarisayo (kama

vile Yohana 9:39-41; Mt. 6:23).

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 9:1-12 1Hata alipokuwa akipita alimwona mtu, kipofu tangu kuzaliwa. 2Wanafunzi wake wakamwuliza wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu? 3 Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake. 4 Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi. 5 Muda nilipo ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu. 6Alipokwisha kusema hayo, alitema mate chini, akafanya tope kwa yale mate. Akampaka kipofu tope za macho, 7akamwambia, Nenda kanawe katika birika ya Siloamu, (maana yake, Aliyetumwa). Basi akaenda na kunawa; akarudi anaona. 8 Basi jirani zake, na wale waliomwona zamani kuwa ni mwombaji, wakasema, Je! Huyu siye yule aliyekuwa akiketi na kuomba? 9 Wengine wakasema, Ndiye. Wengine wakasema, La, lakini amefanana naye. Yeye mwenyewe alisema, Mimi ndiye. 10 Basi wakamwambia, Macho yako yalifumbuliwaje? 11 Yeye akajibu, Mtu yule aitwaye Yesu alifanya tope, akanipaka macho akaniambia, Nenda Siloamu ukanawe; basi nikaenda na kunawa, nikapata kuona. 12 Wakamwambia, Yuko wapi huyo? Akasema, Mimi sijui.

9.1 “kipofu tangu kuzaliwa” huu ni mfano pekee wa aina hii wa uponyaji. Hapakuwapo na uwezekano wowote wa ulaghai.

9:2 “Wanafunzi wake” Hii ni mara ya kwanza kuwataja wanafunzi wake tangu pale kwenye Yohana 6. Hii ingeweza kurejea juu ya (1) wanafunzi wa Uyahudi waliotajwa katika Yohana 7:3 au (2) Wale kumi na wawili

◙ “ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu” Swali hili limesababisha mjadala mkubwa wa kithiolojia. Tunalazimika kutafsiri katika mfumo wa kale wa dini ya Kiyahudi na sio dini za Mashariki. Kuna uwezekano kadha wa kadha:-

1. Hii inarejea juu ya dhambi awali yaani kabla ya kuzaliwa ambapo viongozi wa dini ya Kiyahudi waliichukulia kutoka Mwa. 25:22

2. Hii inarejea juu ya dhambi za wazazi au wazee ambazo ziliwaathiri watoto ambao walikuwa hawajazaliwa (kama vile Kut. 20:5; Kumb. 5:9)

3. Hii inarejea juu ya uhusiano kati ya dhambi na maradhi, iliyokuwa ya kawaida katika theolojia ya dini ya Kiyahudi (kama vile Yakobo 5:15-16; Yohana 5:14)

Page 180: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

164

Hapa hapana chochote cha kufanyia kazi kuhusiana na ushairi wa kitheolojia wa mashariki wenye imani ya kuwa tena na umbile la kibinadamu au mkusanyiko wa matendo mema au mabaya ya mtu yajulikanayo kama karma. Huu ni muundo wa Kiyahudi. Kwa mjadala mzuri wa jambo hili tazama James W. Sire's Scripture Twisting, kr. 127-144 9:3 Mstari huu unatoa jibu la Yesu kuhusiana na swali la wanafunzi wake katika Yohana 9:2. Kweli nyingi zinadookezwa: (1) dhambi na maradhi havijiunganishi vyenyewe na (2) mara nyingi matatizo huleta fursa na upenyo wa baraka za Mungu. 9:4 “tu. . . ni” Viwakilishi hivi mara nyingi havipatani. Machapisho mbali mbali ya Kiyunani yana madiliko ya namna moja au nyingine ili kuleta ukubalifu wa kisarufi. Yanaonekana kuakisi nafasi ya kithiolojia ambayo kama Yesu alivyo nuru ya ulimwengu, yatupasa kuiakisi nuru hiyo ndani ya maisha yetu (kama vile Mt. 5:14). ◙ “usiku waja” Ulinganifu wa Yohana 9:5 unaoonyesha kwamba hii kwa uhakika ni ya kistiari. Neno usiku linaweza kuwakilisha

1. hukumu ijayo 2. wakati ambapo nafasi haitakuwepo 3. kukataliwa na kusuliibiwa kwa Yesu

9:5 “Muda niliopo ulimwenguni” Hii inaonekana kurejea kipindi cha roho za waliokwisha kufa kufanya kazi ndani ya watu walio hai, wakati wa kutoka Bethlehemu kwenda Kalvari/Milima ya Mizeituni. Yesu alikuwa hapa kwa wakati mfupi tu.Yawapasa wasikilizaji wake sasa kuitikia agizo Lake. Kithiolojia kifungu hiki ni sambamba na Yohana 9:4. Mmoja anaweza kushangaa ni kwa jinsi gani neno “Mimi ndiye” inadokezwa katika mazingira kama haya! ◙ “mimi ni nuru ya ulimwengu” Matumizi ya Yohana ya mara kwa mara ya neno “nuru” na “giza” kama istiari za kweli za kiroho. Yesu kama “nuru ya ulimwengu” (kama vile 1:4-5, 8-9; 3:17-21; 8:12; 9:5; 12:46) inaweza kuakisi uhusika wa Kimasihi wa Agano la Kale (kama vile Isa. 42:6; 49:6; 51:4; 60:1, 3). Tazama nukuu katika Yohana 8:12. 9:6 “akafanya tope kwa yale mate” Mate yalitumiwa na Wayahudi kama tiba ya jadi. Haikuruhusiwa kutumika siku ya Sabato (kama vile Yohana 9:14). Injili inanakili mifano mitatu ya Yesu kuyatumia mate (kama vile Marko 7:33; 8:23; na hapa). Kwa kutumia njia hii ya uponyaji iliyokubaliwa, na hata iliyotarajiwa, Kimwili Yesu alikuwa akimtia moyo mtu huyu mwenye imani, lakini pia akipinga kwa umakini sheria na tamaduni za Mafarisayo!

9:7 “birika ya Siloamu” Siloamu inamaanisha “Aliyetumwa.” Birika hili lilitumiwa katika taratibu na kanuni za Sikukuu ya Vibanda.

◙ “(Ambayo inatafsiriwa, Tumwa)” neno “tumwa” lilihusiana na ukweli kwamba maji ya birika yaliingizwa kutoka katika chemchemi za Gihoni, zilizokuwa nje ya kuta za mji wa Yerusalemu. Viongozi wa dini ya Kiyahudi waliunganisha neno "tumwa" na uhusiano wa Kimasihi. Huu ni mtazamo mwingine wa kihariri uliowasilishwa na mwandishi

◙ “Kunawa” Hili lilikuwa tendo lake la imani. Alitenda kwa neno la Yesu! Hii bado haikuwa "imani iokoayo" (kama vile Yohana 9:11,17,36,38). Ilikuwa ni imani iliyokuwa kwenye mchakato. Kwa Injili zote, Yohana anafunua "viwango" vya imani. Yohana 8 inaonyesha kundi la "waaminio," lakini si ndani ya wokovu (kama vile Mathayo 13; Marko 4; mfano wa udongo).

MADA MAALUM: WOKOVU (NJEO ZA VITENZI VYA KIYUNANI VILIVYOTUMIKA) Wokovu siyo kitu, bali ni uhusiano. Haiishii hapo mtu anapomwamini Kristo; ndiyo safari imeanza! Siyo Sera ya bima ya moto, wala tiketi ya kwenda mbinguni, bali ni kukua kumfanana Kristo. Tunao usemi katika Amerika

Page 181: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

165

unaosema, kadiri wawili katika ndoa wanavyoendelea kuishi, ndiyo wanaendelea kufanana. Hili ndilo lengo la wokovu! WOKOVU KAMA KITENDO KILICHO KAMILISHWA (WAKATI TIMILIFU)

- Matendo 15:11 - Warumi 8:24 - 2 Timotheo 1:9 - Tito 3:5 - Warumi 13:11 (inajumuisha WAKATI TIMILIFU ukiwa na mazingira ya WAKATI UJAO )

WOKOVU KAMA HALI YA KUWA (TIMILIFU)

- Waefeso 2:5,8 WOKOVU KAMA MCHAKATO UNAOENDELEA (WAKATI ULIOPO)

- 1 Wakorintho 1:18; 15:2 - 2 Wakorintho 2:15 - 1 Petro 3:21

WOKOVU KAMA UKAMILISHO UJAO (WAKATI UJAO katika NJEO YA KITENZI au MAZINGIRA)

- Warumi 5:9, 10; 10:9,13 - 1 Wakoritho 3:15; 5:5 - Wafilipi 1:28; - 1 Wathesalonike 5:8-9 - Waebrania 1:14; 9:28 - 1 Petro 1:5,9

Kwa hivyo, wokovu unaanza na uamuzi wa imani ya awali (kama vile Yohana 1:12; 3:16; Rum 10:9-13),lakini hili lazima liendane na mchakato wa imani katika mtindo ya maisha (kama vile Rum. 8:29; Gal. 3:19; Efe.1:4; 2:10), ambao siku moja utakuja kukamilishwa kwa kuonekana (kama vile 1Yoh. 3:2). Hatua hii ya mwisho inaitwa utukufu.Hili linaweza kuelezwa kama

1. Utukufu wa awali – udhihirisho (kukombolewa kutoka katika adhabu ya dhambi) 2. Wokovu endelevu–utakaso (kuokolewa toka katika nguvu ya dhambi) 3. Wokovu wa mwisho – utukufu (kuokolewa kutoka katika uwepo wa dhambi)

9:8 “Majirani zake” Kuna makundi matatu yaliyotajwa ndani ya sura hii kama yenye kubeba ushuhuda wa muujiza huu. : (1) jirani zake (2) mtu mwenyewe (Yohana 9:8) ; (Yohana 9:11); wazazi wake (Yohana 9:18). Kulikuwa na kutokukubaliana miongoni mwa majirani, kama ilivyokuwa miongoni mwa Mafarisayo, juu ya uponyaji huu.

◙ "Je! Huyu siye yule aliyekuwa akiketi na kuomba?" Hili swali la Kiyunani linatarajia jibu la "ndiyo". 9:9 "Mimi ndiye" Nahau hii ni sawa na ile ya Kiyunani iliyotumiwa na Yesu katika Yohana 4:26; 6:20; 8:24,28,58; 13:19; 18:5,6,8. Mazingira haya yanaonyesha kwamba muundo huu haukuwa na maana iliyo karibu na masuala ya Kimungu ndani yake. Kuna utata mwingi ulio sawa ndani ya neno kurios lililotumika katika Yohana 9:36 la neno (bwana) na mara 38 ya neno (Bwana) ndani ya sura hii. 9:11-12 Mazungumzo haya yanaonyesha kwamba uponyaji wa mtu huyu haukubeba wokovu wa kiroho papo kwa papo. Imani ya mtu huyu ilikuwa kupitia katika kukutana kwake na Yesu (kama vile Yohana 9:35).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 9: 13-17 13 Basi wakampeleka kwa Mafarisayo yule aliyekuwa kipofu zamani. 14 Nayo ilikuwa sabato, hapo Yesu alipofanya zile tope na kumfumbua macho. 15 Basi Mafarisayo nao wakamwuliza tena jinsi gani alivyopata

Page 182: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

166

kuona. Akawaambia, Alinitia tope juu ya macho, nami nikanawa, na sasa naona. 16 Basi baadhi ya Mafarisayo wakasema, Mtu huyo hakutoka kwa Mungu, kwa sababu haishiki sabato. Wengine wakasema, Awezaje mtu mwenye dhambi kufanya ishara kama hizo? Kukawa matengano kati yao. 17 Basi wakamwambia yule kipofu mara ya pili, Wewe wasemaje katika habari zake kwa vile alivyokufumbua macho? Akasema, Ni nabii.

9:13 “waka” Hii inalazimu kuwazungumzia majirani. ◙ "Mafarisayo" Viongozi wa Kiyahudi wanaenenda kwa kwa maneno mawili toauti katika Yohana. Kwa kawaida wanazungumziwa kama "Wayahudi" (kama vile Yohana 9:18, 22). Hata hivyo, ndani ya sura hii wanaitwa Mafarisayo katika Yohana 9:13, 15, 16, na 40.Tazama Mada Maalumu katika Yohana 1:24 9:14 "Nayo ilikuwa sabato, hapo Yesu alipofanya zile tope" Sheria za kitamaduni za viongozi wa Kiyahudi (Tamaduni za Agano la Kale zilizowekwa katika mpangilio ulio wazi katika buku la sheria na taratibu za Kiyahudi (Talmud) iliochukua nafasi ya muhimu juu ya mahitaji ya watu (kama vile Yohana 5:9; 9:16; Mt. 23:24). Inaonekana kama vile Yesu alifanya haya siku ya sabato kimakusudi kwa kusudi la kuingia kwenye mjadala na viongozi hawa. Angalia kidokezo katika Yohana 5:9. 9:16 Mafarisayo wangaliweza kusimamia hukumu yao juu ya Yesu toka Kumb. 13:1-5. ◙"Kukawa na matengano kati yao" mara nyingi Yesu alisababisha haya (kama vile Yohana 6:52; 7:43; 10:19; Mt. 10:34-39). 9:17 "Ni Nabii" Aya hii inaonyesha maendeleo ya mtu huyu katika imani (kama vile Yohana 9:36, 38). Kwa neno "Nabii" tazama Mada Maalumu katika Yohana 4:19

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 9: 18-23. 8Basi Wayahudi hawakusadiki habari zake, ya kuwa alikuwa kipofu, kisha akapata kuona; hata walipowaita wazazi wake yule aliyepata kuona. 19Wakawauliza wakisema, Huyu ndiye mwana wenu, ambaye mnasema kwamba alizaliwa kipofu? Amepataje, basi, kuona sasa? 20Wazazi wake wakawajibu, wakasema, Tunajua ya kuwa huyu ndiye mwana wetu, tena ya kuwa alizaliwa kipofu; 21lakini jinsi aonavyo sasa hatujui; wala hatujui ni nani aliyemfumbua macho. Mwulizeni yeye mwenyewe; yeye ni mtu mzima; atajisemea mwenyewe. 22 Wazazi wake waliyasema hayo kwa sababu waliwaogopa Wayahudi; kwa maana Wayahudi walikuwa wamekwisha kuafikiana kwamba mtuakimkiri kuwa ni Kristo, atatengwa na sinagogi. 23Ndiyo sababu wale wazazi wake walisema, Ni mtu mzima, mwulizeni yeye.

9:22-23 "akimkiri kuwa ni Kristo" Hii ni sentensi shurutishi dalaja la tatu ambayo inamaanisha tendo lenye maana. Wazazi waliwaogopa viongozi wa Kiyahudi. Kuna mashahidi mbalimbali waliyothibitisha uponyaji huu: (1) jirani (Yohana 9:8-10); (2) mtu mwenyewe (Yohana 9:11-17, 24-33); na (3) wazazi wake (Yohana 9:18-23).

MADA MAALUMU: KUTUBU (AGANO JIPYA)

Toba (sambamba na imani) ni hitaji la pande zote mbili yaani Agano la Kale (Nacham, BDB 636, KB 688, mf., Kut. 13:17; 32:12,14; Shuv, BDB 996, KB 1427, m.f. 1 Flm. 8:47; Eze. 14:6; 18:30; tazama Mada Maalumu: Toba [Agano la Kale]) na Agano Jipya.

1. Yohana Mbatizaji (Mt. 3:2; Marko 1:4; Luka 3:3,8) 2. Yesu (Mt. 4:17; Marko 1:15; Luka 5:32; 13:3,5; 15:7; 17:3) 3. Petro (Matendo 2:38; 3:19; 8:22; 11:18; 2 Petro. 3:9) 4. Paulo (Matendo 13:24; 17:30; 20:21; 26:20; Rum. 2:4; 2 Kor. 2:9-10)

Lakini Toba ni nini? Ni huzuni ya kiroho? Ni kumaanisha kuacha dhambi? Eneo zuri katika Agano la Jipya katika

Page 183: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

167

kuelewa maana tofauti ya dhana hii ni 2 Wakorintho 7:8-11, ambapo hizo tatu zinanahusiana, lakini ni tofauti, maneno ya Kiyunani yanatumiika.

1. "huzuni" (lupeō, kama vile. mst. 8 [mara mbili], 9 [mara tatu], 10 [mara mbili], 11). Inamaanisha kupata maumivu au kutambua na ina maana ya kitheolojia isiyofungamana na upande wo wote.

2. "toba" (metanoeō, kama vile mst. 9,10). Ni muunganiko wa neno "baada ya" na "kumbukumbu," ambayo inadokeza akili mpya, njia mpya ya kufikiri, mtazamo mpya kuhusu maisha na Mungu. Hii ni toba ya kweli.

3. "majuto" (metamelomai, kama vile mst. 8 [mara mbili], 10). Ni muungano wa "baada ya" na "uangalifu." Linatumika juu ya Yuda katika Mt. 27:3 and Esau katika Ebr. 12:16-17. Linadokeza sikitiko juu ya matokeo, si juu ya matendo. Toba na imani ni matendo ya kimaagano yanayohitajika (kama vile Marko 1:15; Matendo 2:38,41; 3:16,19; 20:21). Kuna baadhi ya maandiko ambayo yanadokeza kwamba Mungu hutoa toba (kama vile Matendo 5:31; 11:18; 2 Tim. 2:25). Lakini maandiko mengi yanalitazama hili kama mwitikio muhimu wa agano la mwanadamu kwa majitoleo ya Mungu ya wokovu huru.

Maelezo ya maneno yote ya Kiebrania na Kiyunani yanahitajika ili kuelewa maana kamili ya toba. Neno la Kiebrania linadai "mabadiliko ya tendo," ambapo neno la Kiyunani linadai "mabadiliko ya akili." Mtu aliyeokolewa anapokea akili na moyo mpya (kama vile Eze. 36:26-27). Anafikiri tofauti na kuishi tofauti. Badala ya "Kilicho ndani ni kwa ajili yangu?" sasa swali ni "Mapenzi ya Mungu ni nini?" Toba si hisia ambazo hufifia au dhambi ya moja kwa moja, bali uhusiano mpya na Aliye Mtakatifu ambaye humbadilisha mwamini kwa uendelevu na kuwa ndni ya utakatifu. Si rahisi mtu akasitisha kufanya kitu au kuachana nacho, bali ni kwa mtazamo na uelekeo mpya katika maisha. Anguko linatusabisha sisi kujitazama wenyewe lakini injili inaturuhusu sisi kumtazama Mungu. Toba ni tendo la kugeuka na imani ni tendo la kugeukia kitu/kifikra!

9:22 “atatengwa na sinagogi” Wazazi waliogopa kutengwa nje ya sinagogi wazi wazi (kama vile Yohana 12:42, 16:2) Hatua hii inaturudisha nyuma kwa Ezra (kama vile Yohana 10:8).

Tunajua kutokana na fasiri ya sheria za Kiyahudi kwamba kulikuwa na aina tatu ya kutoshirikishwa: (1) kwa Juma moja (2) kwa mwezi mmoja; au (3) milele.

Yohana, akiandika hadi miaka iliyokaribia karne ya kwanza, aliyafahamu vema kufukuzwa toka ndani ya Sinagogi kwa sababu ya kumkiri Yesu kuwa Kristo. Hii “miundo ya laana”kihistoria iliendelezwa na Mafarisayo baada ya miaka 70 B.K. baada ya kuinuka tena kwa Wayahudi kutoka Jamnia.

◙ “Atapaswa kutengwa na sinagogi” Hili lilikuwa ni tendo la kutoshirikiana lililochukuliwa kwa umakini (kama vile Yohana 12:42; 16:2).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 9: 24-34. 24 Basi mara ya pili wakamwita yule mtu aliyekuwa kipofu, wakamwambia, Mpe Mungu utukufu. Sisi tunajua ya kuwa mtu huyo ni mwenye dhambi. 25 Basi yule mtu akajibu, Kwamba yeye ni mwenye dhambi sijui. Najua neno moja, kuwa mimi nalikuwa kipofu na sasa naona. 26 Basi wakamwambia, Alikutendea nini? Alikufumbua macho jinsi gani? 27 Akawajibu, Nimekwisha kuwaambia, wala hamkusikia; mbona mnataka kusikia tena? Ninyi nanyi mnataka kuwa wanafunzi wake? 28 Basi wakamshutumu, wakasema, Wewe u mwanafunzi wake yule; sisi tu wanafunzi wa Musa 29. Sisi tunajua ya kuwa Mungu alisema na Musa; bali yule hatujui atokako. 30

Yule mtu akajibu, akawaambia, Hii ni ajabu! Kwamba ninyi hamjui atokako, naye alinifumbua macho! 31 Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo. 32 Tokea hapo haijasikiwa ya kuwa mtu ameyafumbua macho ya kipofu, ambaye alizaliwa hali hiyo. 33 Kama huyo asingalitoka kwa Mungu, asingeweza kutenda neno lo lote. 34 Wakajibu, wakamwambia, Ama! Wewe ulizaliwa katika dhambi tupu, nawe unatufundisha sisi? Wakamtoa nje.

9:24 “Mpe Mungu utukufu” Huu ni muundo wa kula kiapo wenye maana ya kuhakikisha uaminifu (kama vile Yoshua 7:19)

Page 184: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

168

9:25 Jibu hili lazima lirejee katika Yohana 9:16. Mtu huyu hana nia ya kuipinga thiolojia bali anatetea matokeo ya kukutana kwake na Yesu

9:27 “Ninyi mnataka kuwa wanafunzi wake” Muundo wa sarufi ya Kiyunani ulitarajia jibu la “hapana,” lakini kuuliza kwao swali hilo hilo ilikuwa kejeli ya waziwazi na inaonyesha werevu wa huyu kipofu aliyekuwa omba omba.

9:28a “Wewe u mwanafunzi wake yule” Kuna swali halisi kwamba ni kwa kiwango gani katika sura hii mtu huyu alikuwa mwenye Imani. Awali inaonyesha kwamba uponyaji alioufanya Yesu haukuunganishwa na imani ya mtu katika Yeye kama Masihi, ni baadaye pale Yesu alipokabiliana naye kwa madai yake ya Kimasihi (kama vile Yohana 9:36-38). Mwendelezo huu unaonyesha kwamba haikuwa lazima uponyaji wa kimwili kuleta wokovu.

9:28b-29 Hii inaonyesha ugumu ambao viongozi wa dini walikumbana nao. Walijaribu kulinganisha kila kitu kilichoelezwa kwa kina, fasiri maalumu za Tamaduni Simulizi (Talmud) na uvuvio uliofunuliwa kwa Musa. Macho yao yalipofushwa kwa sababu ya chuki zao za kidini (kama vile Mt. 6:23). Walikuwa wanafunzi wa tamaduni za mwanadamu (kama vile Isa. 29:13). 9:29 “hatujui atokako” Huu ni mfano mwingine wa kejeli katika Yohana (Yohana 7:27-28; 8:14). Yesu alitoka kwa Baba (Yohana (kama vile Yohana 8:42; 13:3; 16:28) lakini katika upofu wao wenyewe wanafunzi hawakutambua haya

1. Asili Yake 2. Mahali alipozaliwa

9:30 “Hii ni ajabu Kwamba ninyi hamjui atokako, naye alinifumbua macho” Hii ni aina nyingine ya werevu ulio dhahiri na kejeli kali za huyu kipofu omba omba kama alivyoikanusha mantiki ya Mafarisayo.

9:31-33 Mtu huyu kipofu ombaomba asiyekuwa na elimu alikuwa na theolojia thabiti zaidi kuliko viongozi wa kidini!

9:33 “Kama” Hii ni sentensi shurutishi dalaja la tatu ambayo inaitwa “kinyume cha ukweli.” Inatakiwa kueleweka kwamba “Kama huyo asingalitoka kwa Mungu, asingeweza kutenda neno lo lote.”

9:34 “ulizaliwa katika dhambi tupu” Inashawishi kunukuu kwamba sheria za dini ya Kiyahudi hazina dhana ya “dhambi asilia” (Ayubu 14:1,4, Zab. 51:5) Anguko la Mwanzo 3 halikusistizwa katika sheria za Kiyahudi. Wayahudi walidai kwamba kulikuwa na kusudi jema na baya (yetzer) ndani ya kila mtu. Mafarisayo hawa walikuwa wakidai kwamba ushuhuda na mantiki ya mtu huyu aliyeponywa vilikuwa batili kwa sababu mara nyingi alitenda dhambi hali iliyodhihirishwa kwa kuzaliwa akiwa kipofu.

◙ “Wakamtoa nje” Kifasihi hii ni “wakamrusha nje” Marejeo ni juu ya: (1) ushirika na mahudhurio katika masinagogi maalumu au (2) kutupiliwa mbali kutoka katika mkusanyiko. Katika mazingira haya #2 unaonekana kuwa bora zaidi.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 9:35-41. 35Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; naye alipomwona alisema, Wewe wamwamini Mwana wa Mungu? 36Naye akajibu akasema, Ni nani, Bwana, nipate kumwamini? 37Yesu akamwambia, Umemwona, naye anayesema nawe ndiye. 38Akasema, Naamini, Bwana. Akamsujudia. 39Yesu akasema, Mimi nimekuja ulimwenguni humu kwa hukumu, ili wao wasioona waone, nao wanaoona wawe vipofu. 40Baadhi ya Mafarisayo waliokuwapo pamoja naye wakasikia hayo, wakamwambia, Je! Sisi nasi tu vipofu? 41Yesu akawaambia, Kama mngekuwa vipofu, msingekuwa na dhambi; lakini sasa mwasema, Twaona; basi dhambi yenu inakaa.

9:35 NASB, NRSV,

Page 185: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

169

TEV, NJB "'Wewe wamwamini mwana wa Adamu?" NKJV "'Wewe wamwamini Mwana wa Mungu?"

Machapisho ya Kale ya Kiyunani A na L yana “Mwana wa Mungu” lakini P66, P75, א, B, D, na W yana "Mwana wa Adamu.” Kutoka katika matumuzi ya Yohana na uthibitisho wa machapisho ya "Mwana wa Adamu" yanathaminiwa kwa umbali sana, huenda yakawa ya asili. Chapisho la UBS4 linampa "mtu" alama "A" (kwa yakini). Kisarufi swali linatarajiwa liwe na jibu la “ndiyo.” 9:36 NASB, NKJV, "Bwana" NRSV, TEV, NJB "Bwana" Tunaweza kuona ukuaji wa imani ya mtu huyu kitheolojia ndani ya sura hii, mtu huyu akitoka kumwita Yesu

1. mtu (Yohana 9:11) 2. ya kuwa nabii (Yohana 9:17) 3. kwa jina lenye hashima kubwa la "bwana" (Yohana 9:36) 4. kwa "Bwana," katika hali ya utumiaji wa kitheolojia wa neno hili (Yohana 9:38)

Neno la Kiyunani liko sawa katika Yohana zote yaani 9:36 na 38. Ni mazingira tu yawezayo kutofautisha maana iliyomaanishwa. Tazama MADA MAALUMU: MAJINA YA UUNGU katika Yohana 6:20. Neno la Kiyunani Kurios linaweza kuakisi neno la Kiebrania Adon, ambapo lilitamkika na kusimama badala ya YHWH.

9:38 Hiki ni kilele cha uwajibikaji, kwa namna ya wokovu wa mtu aliyeponywa ahusikavyo. Ni ajabu kwamba mstari huu unakosekana kutoka katika Machapisho ya kale ya Kiyunani (P75, א, W) na muunganiko wa Injili nne za kale (Diatessaron). Yana jumuisha maneno mawili adimu sana: (1) kifungu "alisema" kinatokea hapa tu na Yohana 1:23 na (2) neno "aliabudu" linatokea hapa tu katika Yohana. Yanajumuishwa katika tafsiri nyingi za kisasa. 9:39 “Mimi nimekuja ulimwenguni humu kwa hukumu” Hii inaonekana kufanana na Yohana 5:22, 27 ambayo inazungumzia hukumu ya nyakati za mwisho (mambo yahusuyo kifo, hukumu, na Jehanamu). Hata hivyo, hili linaonekana kuhitilafiana na Yohana 3:17-21 na 12:47, 48. Hili linaweza kusuluhishwa na ukweli kwamba Yesu alikuja kwa kusudi la ukombozi, lakini wanadamu ambao walikataa kujitolea Kwake wanajihukumu wao wenyewe. ◙ “ili wao wasioona waone, nao wanaoona wawe vipofu” Huu ulikuwa utimilifu mara mbili wa unabii hasa kutoka Isaya.

1. Waisraeli wanaojivuna hawatalielewa agizo la Mungu (kama vile Isa. 6:10, 42:18-19; 43:8; Yer. 5:21; Eze. 12:2)

2. walio maskini, waliotengwa na jamii, walioathiriwa kimwonekano wenye majuto na wanyenyekevu watasimama (kama vile Isa. 29:18; 32:3-4; 35:5; 42:7, 16)

3. Yesu ni nuru ya ulimwengu kwa wote waliochagua kuiona (kama vile Yohana 1:4-5, 8-9). 9:40 “Je! Sisi nasi tu vipofu?” Isimu za Kiyunani zinatarajia jibu la "ndiyo" (kama vile Mt. 15:14; 23-24). Mistari hii michache ya mwisho inaonyesha kwamba sura hii ni matokeo ya mfano wa upofu wa kiroho ambao hauwezi kuponywa (dhambi isiyosameheka ya mtu asiyeamini, tazama Mada Maalumu katika Yohana 5:21), na upofu uonekanao ambao unaweza! 9:41 Mstari huu unaeleza kweli yote (kama vile Yohana 15:22,24; Rum. 3:20; 4:15; 5:13; 7:7,9). Wanadamu wanawajibika kusimama katika nuru waliyo nayo au iliyofunuliwa kwao!

MASWALI YA MJADALA

Page 186: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

170

Huu ni mwongozo wa fasiri, ina maanisha kwamba unawajibika kwa tafsiri zako mwenyewe za Biblia. Kila mmoja wetu lazima atembee katika mwanga tulio nao. Wewe, Biblia, na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Hutakiwi uvitelekeze vitu hivi kwa mfasiri. Maswali ya mjadala huu yanatolewa kukusaidia kufikiri juu ya mambo makubwa ya sehemu za kitabu hiki. Yanalenga kukuamsha kimawazo na sio kutoa maana. 1. Je! hii Yohana 9 kimsingi inajihusisha na uponyaji wa kimwili au uponyaji wa kiroho? Upofu kimwili au upofu

wa kiroho? 2. Ni kwa jinsi gani mtu huyu angeweza kutenda dhambi kabla hajazaliwa? 3. Katika Yohana 9 ni kwa maana/kiwango gani mtu huupokea wokovu? 4. Je? Yesu alikuja ulimwenguni kuhukumu ulimwengu au kuuokoa ulimwengu? 5. Toa ufafanuzi wa maana ya neno “Mwana wa Mtu” 6. Orodhesha maana ya kejeli iliyokuwa ndani ya majibu aliyoyatoa mtu kipofu kwa viongozi wa Kiyahudi.

Page 187: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

171

YOHANA 10

MIGAWANYO YA AYA YA TAFSIRI ZA KISASA UBS4 NKJV NRSV TEV JB

Mfano wa zizi la Yesu Mchungaji Yesu, Mchungaji Mfano wa Mchungaji Mwema Kondoo Mwema Aliyeutoa Uhai Mchungaji Wake 10:1-6 10:1-6 10:1-6 10:1-5 10:1-5 10:6 10:6 Yesu Mchungaji Yesu Mchungaji Yesu Mchungaji Mwema Mwema Mwema 10:7-18 10:7-21 10:7-10 10:7-10 10:7-18 10:11-18 10:11-16 10:17-18 10:19-21 10:19-21 10:19-20 10:19-21 10:21 Yesu Alikataliwa Mchungaji Yesu Anadai kuwa na Wayahudi Huwajua Kondoo Yesu Anakataliwa Mwana wa Mungu Wake 10:22-30 10:22-30 10:22-30 10:22-24 10:22-30 Juhudi Nyingine 10:25-30 Za Kumpiga Yesu Mawe 10:31-39 10:31-39 10:31-39 10:31-32 10:31-38 10:33 10:34-38 10:39 10:39 Waamini Ng’ambo Yesu aliondoka Yordani Upande wa Pili wa Yordani 10:40-42 10:40-42 10:40-42 10:40-42 10:40-42

MZUNGUKO WA TATU WA USOMAJI KUFUATILIA KUSUDIO LA ASILI LA MWANDISHI KATIKA NGAZI YA AYA Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwatafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Aya ya kwanza 2. Aya ya pili 3. Aya ya tatu 4. N.k

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

Page 188: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

172

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 10:1-6 1 Yesu aliwaambia, Amin, amin, nawaambieni, Yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo, lakini akwea penginepo, huyo ni mwivi naye ni mnyang'anyi. 2 Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo. 3 Bawabu humfungulia huyo, na kondoo humsikia sauti yake; naye huwaita kondoo wake kwa majina yao, na kuwapeleka nje. 4 Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake. 5 Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni. 6 Mithali hiyo Yesu aliwaambia, lakini wao hawakuelewa na mambo hayo aliyowaambia.

10:1 “Amini, amini” Angalia kidokezo katika Yohana 1:51

◙ “lakini akwea penginepo, huyo ni mwivi naye ni mnyang'anyi” Tambua kuna baadhi walioko zizini wasiohusika kwa Mchungaji Mwema (kama vile Mat. 7:21-23 na “mfano wa magugu katikati ya ngano,“ Mt. 13:24-30). Tatizo hapa ni kwamba baadhi wanajaribu kufikia kupitia juhudi binafsi kile ambacho Mungu amekitoa bure kupitia Christo Yesu (kama vile Rum. 3:19-31; 9:30-33; 10:2-4; Gal. 2:16; 5:4). Mafarisayo katika Yohana 9 ni mfano mzuri

10:2 “Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo” Kuna mkanganyiko wa wazi wa istiari katika aya hii. Yesu kama mlango wa kondoo, Yohana 10:7, na pia Mchungaji wa kondoo (Yohana 10:11 na 14). Hata hivyo, mkanganyiko huu sio wa kawaida katika Yohana na Agano jipya.

1. Yesu ni mkate wa uzima na chakula cha uzima (kama vileYohana 6:35,51) 2. Yesu ndiye kweli na msemaji wa kweli (kama vile Yohana 10:8:45-46 and 14:6) 3. Yesu ndiye njia na anaonyesha njia (kama vile Yohana 14:6) 4. Yesu ni dhabihu na ndiye atoaye dhabihu ( kama vile kitabu cha Waebrania)

Cheo cha “uchungaji” kilikuwa ni cheo cha kawaida katika Agano la Kale kwa Mungu na Masihi (kama vile Zab. 23; Zab. 80:1; Isa. 40:10-11; 1 Pet. 5:1-4). Viongozi wa Kiyahudi wanaitwa “wachungaji wa uongo” katika Yeremia 23; Ezekiel 34 na Isaya 56:9-12. Neno “Mchungaji wa kondoo” linafanana na neno “Mchungaji” (kama vile Efe. 4:11; Tito 1:5,7).

10:3 “kondoo huisikia sauti yake” Kutambua na kutii kunahusika na uhusiano uliopo. Katika Yohana wote “husikia” (kama vile Yohana 4:42; 5:24,25,28-29; 8:47; 10:16,27; 18:37) na "kuona" (kama vile Yohana 3:3; 12:40; 20:8) yanatumika katika kusadiki/kuamini katika Yesu kama Kristo.

◙ “naye huwaita kondoo wake kwa majina yao” Yesu anawajua walio wake binafsi na mmoja mmoja (kama YHWH afanyavyo, kama vile Yohana 10:29-31). Mchungaji wa kondoo huwa ana majina ya wanyama wake, hata kwenye kundi kubwa la mifugo. Kithiolojia inashangaza kwamba Yesu huwaita kondoo wake walio wa kweli toka kati kati ya wale wasio wa kweli wa Taifa la Yuda. Watu wa Agano hawakuwa watu wa kweli wa Mungu. Huu ni kiini cha kashfa katika Agano Jipya. Imani ya mtu, isio na unasaba, inatathimini mambo ya mbele ya mtu! Imani ni kitu binafsi, na sio cha kitaifa. Viongozi wa Kiyahudi waliompinga Yesu walikuwa sio sehemu ya watu wa Mungu (kama vile Yohana 10:26)

◙“na kuwapeleka nje” Hii hairejerei tu kwenye wokovu, bali pia kwenye mwongozo wa kila siku (kama vile Yohana 10:4, 9).

10:4 Hii yaweza kuwa ni nukuu toka sehemu zenye utaratibu wa utunzaji wa mifugo mingi sehemu moja nyakati za usiku. Ifikapo asubuhi Mchungaji huwaita na kondoo humfuata.

10:5 kanisa linapaswa kushughulika na wachungaji waongo (kama vile 1 Tim. 4:1-3; 2 Tim. 4:3-4; 1 Yoh. 4:5-6; 2 Petro 2). 10:6 “Mithali hiyo Yesu aliwaambia” Hili ni sio neno la kawaida lililotafasiliwa kwa “hadithi za mafumbo” (parabolē), lakini linatoka katika mzizi ule ule wa neno (paroimian). Muundo wa namna hii unapatikana hapa tu na katika Yohana 16:25,29 na 2 Pet. 2:22. Ingawa liko katika muundo tofauti, linaonekana kuwa kisawe likiwa zaidi na neno la kawaida la “hadithi za mafumbo” (likitumika katika ufupisho wa injili). Neno “hadithi za mafumbo” mara nyingi linamaanisha kuwa mbadala wa tamaduni za kawaida zilizopo mbali na ukweli wa kiroho ili kwamba

Page 189: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

173

kusaidia katika kuleta uelewa. Inawezekana, hata hivyo, kurejea kwenye ukweli uliofichika toka kwenye upofu wa kiroho (kama vile Yohana 16:29; Marko 4:11-12). ◙ “lakini wao hawakuelewa” Kama Yohana 10 inahusiana katika wakati na Yohana 9, basi neno “wao” lingaliwarejea Mafarisayo. Walidai kuona (kama vile Yohana 9:41), lakini hawakuona (kama vile Yohana 10:20). Dini yaweza kuwa kikwazo, na isiwe daraja la kuunganisha.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 10:7-10 7Basi Yesu aliwaambia tena, Amin, amin, nawaambieni, Mimi ndimi mlango wa kondoo. 8 Wote walionitangulia ni wevi na wanyang'anyi; lakini kondoo hawakuwasikia. 9 Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho. 10 Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.

10:7 “Mimi ndimi mlango wa kondoo” Hii ni moja ya kauli maarufu ya Mimi ndiye” ya Yohana 7. Istiari hii inaangazia ukweli wa kwamba Yesu ndiye njia ya kweli (kama vile Yohana 8, 10; 14:6). Mara nyingi hii huitwa tuhuma ya kuitenga Injili. Kama Biblia ni ufunuo pekee wa Mungu, kwa hiyo kuna njia moja tu ya kuwa sawa na imani ya Mungu katika Kristo (kama vile Mdo. 4:12; 1 Tim. 2:5). Angalia dokezo katika Yohana 8:12 10:8 “Wote walionitangulia ni wevi na wanyang'anyi” Kwa sababu ya mazingira yenyewe ya Yohana 9 na 10, sikukuu ya kutabaruku, Hanukkah (kama vile Yohana 10:22), yawezekana hii inarejea mvutano wa awali kati ya wafuasi wa Maccabeus na kizazi chao wakati wa kipindi cha Agano la Kale. Hata hivyo, yumkini inarejerea aya za Agano la Kale kuhusu wachungaji wa uongo (kama vile Isa. 56:9-12; Yeremia 23; Ezekieli 34; and Zekaria 11). Hii lugha ya hali ya juu ya kitamathali na utangulizi wenye utata ilisababisha waandishi kurekebisha au kupanua maana ya neno katika kujaribu kuelezea maana yake. Chapisho moja la (MSD) liliondoa neno “wote” lililoingizwa na machapisho mengine mbali mbali yakaondoa kifungu “kabla yangu.” 10:9 “mtu akiingia kwa mimi, ataokoka” Hii ni sentesi shurutishi daraja la tatu ikiwa na kitenzi tendewa cha wakati ujao. Yesu ni njia pekee ya kwenda kwa Baba (kama vile Yohana 14:6). Kitenzi cha neno “kuokolewa” katika muktadha huu yumkini kinarejea vidokezo vya Agano la Kale vya ukombozi wa kimwili (yaani, kondoo wako salama). Hata hivyo Yohana mara nyingi alichagua maneno yenye maana mbili zinazoingiliana. Dhana ya wokovu wa kiroho haukosekani pia toka kwenye muktadha huu (kama vile Yohana 10:42). 10:10 “Mwivi” Hii inaonyesha nia iliyofichika ya wachungaji waongo. Pia inaaksi kusudi la mtu mwovu! Mwenendo huu wa kutojali wa wafanyakazi wa mshahara unaonekana katika Yohana 10:12-13 ◙ “kuharibu” angalia mada maalumu ifuatayo.

MADA MAALUMU: MAANGAMIZI (Apollumi))

Neno hili lina elimu-maana pana, ambayo imesababisha mkanganyiko mkubwa katika kuhusianisha na dhana ya kithiolojia juu ya hukumu ya milele dhidi ya maangamizo. Maana halisi ya msingi inatoka kwenye neno apo pamoja na ollumi, likimaanisha kuharibu/angamiza. Tatizo linalokuja kwenye matumizi ya neno hili kitamathari. Hili laweza kuonekana wazi katika toleo la Louw na Nida's Greek-English Lexicon of the New Testament, Based On Semantic Domains, juzuu. 2, uk. 30. Inaorodhesha maana nyingi za neno.

1. Angamiza (mfano Mt. 10:28; Luka 5:37; Yohana 10:10; 17:12; Mdo. 5:37; Rum. 9:22 toka juzuu. 1, uk.

232)

2. Kushindwa kupata (mfano Mt. 10:42, juzuu. 1, uk. 566)

Page 190: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

174

3. kupoteza (mfano Luka 15:8, juzuu. 1, uk. 566)

4. Kutokufahamu eneo (mfano Luka 15:4, juzuu. 1, uk. 330)

5. kufa (mfano Mt. 10:39, juzuu. 1, uk. 266) Gerhard Kittel, Theological Dictionary of the New Testament, vol. 1, ukurasa 394, anajaribu kuonyesha matumizi tofauti kwa kuorodhesha maana Nne:

1. kuangamiza au kuuwa (mfano Mt. 2:13; 27:20; Marko 3:6; 9:22; Luka 6:9; 1 Kor. 1:19) 2. Kupoteza au kupata hasara (mfano Marko 9:41; Luka 15:4,8) 3. kuangamia (mfano Mt. 26:52; Marko 4:38; Luka 11:51; 13:3,5,33; 15:17; Yohana 6:12,27; 1 Kor. 10:9-

10) 4. kupotea (mfano Mt. 5:29-30; Marko 2:22; Luka 15: 4,6,24,32; 21:18; Mdo. 27:34)

baadaye alisema, “kwa ujumla tunaweza kusema kuwa mstari wa #2 na #4 inayaweka chini maelezo yanayohusiana na ulumwengu huu katika mihitasari ya injili, wakati mstari wa #1 na #3 inayashusha chini maelezo yanayohusiana na ulimwengu ujao, kama ilivyo katika kitabu cha Paulo na Yohana” (uk. 394). Ukiangalia ndani humu kuna mkanganyiko. Neno lina elimu-maana pana ya utumiaji ambayo waandishi tofauti wa Agano Jipya wanaitumia katika maana tofauti. Nampenda Robert B. Girdlestone, Synonyms of the Old Testament, ukurasa 275-277. Alihusianisha neno kwa watu wale kimaadili walikuwa wamekwisha haribika na wakisubiri utengano wa milele toka kwa Mungu dhidi ya wale watu wanaomjua Kristo na wana uzima wa milele ndani yao. Kundi la awali ni lile “lililookolewa” na kundi la kwanza ni lile “lililoangamizwa.” Robert B. Girdlestone, katika maaandishi yake yenye maneno yaliyokaribiana maana ya Agano la Kale, uk. 276, anaelekeza kuwa kuna sehemu nyingi ambazo neno hili laweza lisitafasiliwe kama maangamizi, “maumivu kama hayo yanakifanya kitu kiutendaji kionekana kutokuwa na maana kwa kusudi lake la awali.”

1. Upotevu wa marhamu, Mt. 26:8 2. Uharibifu wa kutia divai katika viriba vikuukuu, Mt. 9:17 3. Uharibifu wa nywele, Luka 21:18 4. Uharibifu wa chakula, Yohana 6:27 5. Uharibifu wa dhahabu ipoteayo, 1 Pet. 1:7 6. Uharibifu wa ulmwengu, 2 Pet. 3:6 7. Uharibifu wa kimwili, Mt. 2:13; 8:25; 12:14; 21:41; 22:7; 26:52; 27:20; Rum. 2:12; 14:15; na 1 Kor. 8:11

Neno hili kamwe halirejerei maangamizi ya mtu, lakini mwisho wa uwepo wa kimwili. Pia mara nyingi linatumika katika maana iliyo sawa “watu wote wanahesabika kuharibika kimaadili, yaani, wameshindwa kuchukuliana na kusudi ambalo kizazi kilifanywa kuwa viumbe hai” (uk. 276). Ukubarifu wa Mungu kwenye tatizo ya dhambi hii alikuwa ni Yesu Kristo (kama vile Yohana 3:15-16 na 2 Pet. 3:9). Wale wote walioikataa injili sasa wametizamishwa kwenye uharibifu mwingine, unaojumuisha mwili na roho (kama vile 1 Kor. 1:18; 2 Kor. 2:15; 4:3; 2 The. 2:10). Kwa hoja nyingine iliyokinyume angalifu, moto ulao. Binafsi (kama vile R. B. Girdlestone, Synonyms of the Old Testament, uk. 276) hafikirii kuwa neno hili linadokeza maangamizi (kama vile E. Fudge, The Fire That Consumes). Neno “milele” linatumika pote kwa adhabu ya milele na uzima wa milele katika Mt. 25:46. Kulishusha thamani moja ni kuyashusha yote!

◙ “Nilikuja ili wawe na uzima, na wawe nao tele” Kifungu hiki kimenukuliwa mara nyingi kama ahadi ya vitu, lakini katika muktadha huu unahusiana na kumjua Yesu binafsi na Baraka za rohoni, sio ustawi wa kuwa na vitu, ambao anauleta (unafanana na 4:14 na 7:38). Sio kuwa navyo vingi zaidi katika maisha haya, bali ni kujua na kuwa na maisha ya kweli! Kama vidokezo vya injili vilivyoweka kumbukumbu ya msisitizo wa Yesu juu ya ufalme wa Mungu, Yohana anaweka kumbu kumbu ya msisistizo wa Yesu juu ya maisha ya milele. Mtu anaweza kuwa nayo sasa! Ufalme wa mbingu umefunguliwa!

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 10:11-18 11Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. 12 Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, humwona mbwa-mwitu anakuja, akawaacha kondoo na kukimbia; na mbwa-mwitu huwakamata na kuwatawanya. 13 Yule hukimbia kwa kuwa ni mtu wa

Page 191: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

175

mshahara; wala mambo ya kondoo si kitu kwake. 14 Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi; 15 kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. 16 Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja. 17 Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena. 18Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu.

10:11 “Mimi ndimi mchungaji mwema” Hiki kilikuwa ni cheo cha Kimasihi katika Agano la Kale (kama vile Ezek. 34:23; Zak. 11; 1 Petr. 5:4) na kwa YHWH (kama vile Zab. 23:1; 28:9; 77:20; 78:52; 80:1; 95:7; 100:3; Isa. 40:11; Yer. 23:1; 31:10; Ezek. 34:11-16). Kuna maneno mawili ya Kiyunani yanayoweza kutafasiliwa kama “mwema” (1) agathos, ambalo mara nyingi linatumika katika Yohana kwa kumaanisha vitu, na (2) kalos, ambalo lilitumika katika maandiko ya Kale kurejea kile kilicho chema kwa kupinga kilicho kibaya. Katika Agano Jipya lina maana ya “kizuri” “kilodi”, “adilifu”, “enye thamani.” Maneno haya mawili yanatumika pamoja katika Luka 8:15. Angalia kidokezo katika Yohana 8:12. 10:11 “Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo” Hili linarejea Kristo kama mwakilishi mbadala wa upatanisho (kama vile Yohana 10:11,15,17,18). Alijitolea kuyaweka maisha yake chini kwa ajili ya mwanadamu mwenye dhambi (kama vile Isa. 52:13-53:12; Marko 10:45; 2 Kor. 5:21). Maisha ya kweli, maisha ya utele yakuja tu kupitia kifo chake. Bruce M. Metzger katika kitabu chake cha A Textual Commentary on the Greek New Testament ana jambo la kufurahisha katika kifungu hiki: “ badala ya maelezo ya ‘huutoa uhai wake,’ambao unachagishwa na Yohana (10:15,17; 13:37,38; 15:13; 1 Yohana 3:16), shuhuda mbali mbali (P45, א*, D) zinakuwa mbadala wa maelezo ya ‘huutoa uhai wake,’ amabayo yanaonekana katika kidokezo cha Injili (Mt. 20:28; Mark 10:45)" (uk. 230). 10:14 ”nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi” Hii ni dhana ya Kiebrania ya neno “kujua” (angalia Mada Maalumu: Kujua). Kama vile Mwana amujuavyo Baba na Baba amujuavyo Mwana, pia vile vile, Yesu huwajua wale waaminio katika Yeye na wao wamjua. Wamekwisha “kumwona” na “kumusikia” (kama vile Yohana 10:4) na wakakubali (kama vile Yohana 1:12; 3:16). Ukristo ni uhusiano wa mtu binafsi (kama vile Yohana 17:20-26). 10:15 “kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba” Hii ni dhamira inayojirudiarudia katika Yohana. Yesu anatenda na kunena hatma ya uhusiano wake na Baba yake. Mshabihiano wa kushangaza katika Yohana 10:14-15 ni kuwa undani wa Baba na Mwana unalinganishwa na undani kati ya Mwana na wafuasi wake (kama vile Yohana 14:23). Yohana anaangazia katika kidokezo cha Kiebrania cha neno “kujua” kama hatima ya ushirika, sio ukweli unaotambulika. Yesu anamjua Baba; wale wote wanaomjua Yesu, humjua Mungu! 10:16 “Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili” Hiki ni kidokezo toka Isa. 56:6-8. Mazingira yanaonekana kuhitaji kwamba haya yalikuwa ni marejeo ya (1) Msamaria Mwema (kama vile Yohana 4:1-42) au (2) kanisa la watu wa mataifa (kama vile Yohana 4:43-54). Hii inazungumzia umoja juu ya wale wote wanaoitekeleza imani katika Kristo. Agano Jipya linawaunganisha Wayahudi na watu wa mataifa (kama vile Efe. 2:11-3:13; pia 1 Kor. 12:13; Gal. 3:28; Kol. 3:11)! Mwanzo 3:15 na Yohana 3:16 yanaungana!

◙ “kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja” Hili limekuwa ndo kusudi la Mungu (kama vile Mwa. 3:15; 12:3; Kut. 19:5-6). Dhana ya kithiolojia ya umoja huu umezungumuziwa katika Efe. 2:11-3:13 na 4:1-6.

10:17 “Ndipo sababu Baba anipenda,” Kama ambavyo mwana hakulazimishwa kuutoa uhai wake, ndivyo nae Baba hakulazishwa kumtoa mwanae. Hili lisitafasiliwe kwamba Mungu alimtoa Yesu aliyekuwa mwanadamu kwa ajili ya utii wake (mafundisho haya mara nyingi huitwa Uasilishaji, angalia kwenye fafanuzi).

Page 192: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

176

◙ “nautoa uhai wangu ili niutwae tena” Hii inamaanisha ufufuko. Kawaida katika Agano Jipya Baba ndiye aliyemwinua Mwana (kama vile Yohana 18b) kuonyesha ukubarifu wake wa kujitoa kama dhabihu. Lakini hapa nguvu ya Yesu mwenyewe katika ufufuo imethibitishwa.

Kifungu hiki ni fursa nzuri kuonyesha kuwa Agano Jipya mara nyingi inafikiria kazi ya ukombozi kwa wote watatu wa Utatu.

1. Mungu Baba alimwinua Yesu (kama vile Mdo. 2:24; 3:15; 4:10; 5:30; 10:40; 13:30,33,34,37; 17:31; Rum. 6:4,9; 10:9; 1 Kor. 6:14; 2 Kor. 4:14; Gal. 1:1;Efe. 1:20; Kol. 2:12; 1 Thes. 1:10)

2. Mungu Mwana akajiinua mwenyewe (kama vile Yohana 2:19-22; 10:17-18) 3. Mungu Roho akamwinua Yesu (kama vile Rum. 8:11)

10:18 “Nina mamlaka” Hili ni neno lile lile lililotumika katika Yohana 1:12. Laweza kutafasiliwa “enye mamlaka,” “enye haki ya kisheria” au “enye nguvu.” Huu mstari unaonyesha nguvu na mamlaka ya Yesu

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 10:19-21 19 Kukaingia tena matengano kati ya Wayahudi, kwa ajili ya maneno hayo. 20 Wengi wao wakasema, Ana pepo huyu, tena ana wazimu; mbona mnamsikiliza? 21Wengine wakasema, Maneno hayo siyo ya mtu mwenye pepo. Je! Pepo aweza kuwafumbua macho vipofu?

10:19 Kama kulivyoonekana kuwepo kwa mgawanyiko wa maoni kumhusu Yesu katika Yohana 6:52; 7:12,25,43; 9:16; 10:19-21; 11:36-37 dhamira hii iliendelea mpaka katika Yohana. Maajabu ya baadhi ya watu wanaopokea injili na wengine wanaokataa injili ni mvutano kati ya majaliwa ya mwanadamu na utashi huru wa mwanadamu. 10:20 “Ana pepo huyu, tena ana wazimu” Hili lilikuwa shitaka la kawaida dhidi ya Yesu kwa mitazamo miwili tofauti.

1. Katika Yohana 10:20, kama ilivyo katika 7:20, lilitumika kuelezea kuwa Yesu alikuwa na matatizo ya akili 2. Shitaka kama lile lile linatumika na mafarisayo kujaribu kuelezea chanzo cha nguvu za Yesu (kama vile

Yohana 8:48,52) 10:21 kuna maswali mawili katika Yohana 10:21

1. Yohana 10:21a ina ouk, inayotarajia jibu la “ndiyo” 2. Yohana 10:21b ina mē, inayotarajia jibu la “hapana”

Angalia James Hewett, New Testament Greek, uk. 171. Mstari huu, hata hivyo unaonyesha kwa namna gani sheria zilivyokuwa ngumu huko Koine Uyunani. Muktadha, usio na muundo wa kisarufi, ndio mwamuzi wa mwisho. Uponyaji wa Yule kipofu ulikuwa ni alama ya kimasihi (kama vile Kut. 4:11; Zab. 146:8; Isa. 29:18; 35:5; 42:7). Kuna dhana ambayo upofu wa Waisraeli (kama vile Isa. 42:19) unaonyeshwa hapa kama ilivyo katika Yohana 9.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 10:22-30 22 Basi huko Yerusalemu ilikuwa Sikukuu ya Kutabaruku; ni wakati wa baridi. 23 Naye Yesu alikuwa akitembea hekaluni, katika ukumbi wa Sulemani. 24 Basi Wayahudi walimzunguka, wakamwambia, Hata lini utatuhangaisha nafsi zetu? Kama wewe ndiwe Kristo, utuambie waziwazi. 25 Yesu akawajibu, Naliwaambia, lakini ninyi hamsadiki. Kazi hizi ninazozifanya kwa jina la Baba yangu ndizo zinazonishuhudia. 26 Lakini ninyi hamsadiki, kwa sababu hammo miongoni mwa kondoo wangu. 27 Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata. 28 Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu. 29 Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu. 30 Mimi na Baba tu umoja.

10:22 “Sikukuu ya Kutabaruku” Yusufu aliita “sikukuu ya mishumaa” katika siku zetu za leo inajulikana kama sikukuu ya vibanda. Ilidumu kwa siku nane na ilifanyika katikati ya mwezi wa kumi na mbili. Ilisherehekewa kwa kulitabaruku upya Hekalu katika Yerusalemu baada ya ushindi wa vita vya Yuda Maccabeus mwaka wa 164 K.K. Katika mwaka wa 168 K.K Antiochus IV Epiphanes, moja ya viongozi wa utawala wa kifalme, akajaribu

Page 193: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

177

kuwalazimisha Wayahudi kuingia kutenda tamaduni za Kiyunani (kama vile Dan. 8:9-14). Alilibadilisha Hekalu lililokuwa Yerusalem kuingia katika madhabahu ya kipagani likiwa hata na sanamu ya Zeus katika mahali patakatifu. Yuda Maccabeus, moja ya wana wa kuhani Modin, alimshinda huyu mtawala Ashuru na kulisafisha na kulitabaruku Hekalu upya (kama vile I Macc. 4:36-59; II Macc. 1:18). Yohana alitumia sikukuu za Kiyahudi kama fursa kwa Yesu kutumia alama zao kujidhihilisha mwenyewe kwenye uongozi wa Wayahudi, raia wa Yerusalem, na kwenye kusanyiko la mji wa Mahujaji (kama vile Yohana 7-11). ◙ “katika ukumbi wa Suleimani” Hili lilikuwa ni eneo lililofunikwa kandokando mwa sehemu za mashariki mwa mahakama ya wanawake mahali ambapo Yesu alikuwa akifundisha. Yusufu alisema ukumbi huu uliweza kupona toka kwenye maangamizi ya Babel mwaka 586 K.K 10:23 “Ilikuwa kipindi cha baridi” Haya ni maelezo ya ushahidi wa kuona kwa macho 10:24 “kama” Hii ni Sentesi shurutishi daraja la kwanza inayosadikiwa kuwa kweli kutokana na mtazamo wa mwandishi kwa kusudi lake la kifasihi. Kuna sentesi shurutishi daraja la kwanza nyingi katika muktadha huu (kama vile Yohana 10:24, 35, 37, and 38). Utumiaji huu katika Yohana 10:24 unaonyesha ni kwa namna gani muundo huu unaweza tumika katika maana ya fasihi. Mafarisayo hawa hakika hawakumwamini Yesu kuwa ni Masihi; walikuwa wakimtega. ◙ “Tuambie waziwazi” Kuna vitu vingi vya kuzungumzia katika mstari huu. Kwanza, Yesu aliongea katika mafumbo, lugha ya kitamathari, na maelezo tata yenye sura mbili. Umati huu pale Hekaluni ulimtaka ajieleze mwenyewe wazi. Angalia Mada maalumu: Parrhēsia katika Yohana 7:4 Pili, Wayahudi wa nyakati za Yesu hawakutegemea Masihi kuwa katika hali ya Kiungu. Yesu alionekana kudokeza juu ya kuwa wamoja na Mungu katika matukio mbali mbali (kama vile Yohana 8:56-59), lakini katika mazingira haya wanaomba hasa hasa kuhusu Masihi. Wayahudi walitegemea Mpakwa Mafuta huyu kutenda kama Musa (kama vile Kumb. 18:15,19). Yesu alilitenda hilo sawa sawa katika aya ya sita. Utimilifu wake wa kazi za unabii wa Agano la Kale, hasa uponyaji wa Yule kipofu (Yohana 9). Vyote hivi vilikuwa na ushahidi uliohitajika. Tatizo lilikuwa ni kwamba Yesu hakufaa kwenye jeshi lao la kitamaduni, matarajio ya uzalendo wa Masihi. 10:25 “Kazi hizi ninazozifanya kwa jina la Baba yangu ndizo zinazonishuhudia” Yesu anadhihilisha ya kwamba matendo yake ndo yanathibitisha madai yake (kama vile Yohana 2:23; 5:36; 10:25,38; 14:11; 15:24). 10:26 Ni maelezo ya kushangaza ya namna gani 10:28 “Nami nawapa uzima wa Milele” Uzima wa milele unaainisha na uwingi na ubora kwa pamoja. Ni maisha ya enzi mpya. Unapatikana sasa kwa imani kupitia Kristo (kama vile Yohana 3:36; 11:24-26). ◙ “Wala hawatapotea kamwe; wala hakuna atakayewapokonya katika mikono yangu” Hii ni hali yenye hasi mbili ikiwa katika wakati uliopita usiotimilifu wa kati tegemezi. Hili ni moja ya fungu la maneno yenye nguvu juu ya ulinzi wa muumini kila mahali katika Agano Jipya (kama vile Yohana 6:39). Ni dhahili kwamba mtu awezaye kututenganisha toka katika upendo wa Mungu ni sisi wenyewe (kama vile Rum. 8:38-39; Gal. 5:2-4). Dhamana (angalia Mada maalumu katika 1 Yohana 5:13) lazima uendane na ustahimilivu (angalia Mada maalumu katika Yohana 8:31). Uhakika lazima usimamie juu ya tabia na matendo ya Mungu wa Utatu. Injili ya Yohana inadhihirisha uhakika wa wale wanaoendelea kuweka imani yao katika Kristo. Inaanza na maamuzi ya awali ya toba na imani na masuala katika imani ya mtindo wa maisha. Tatizo la kithiolojia ni pale uhusiano binafsi unapopotoshwa ndani ya kitu tunachokimiliki (“mara moja unapookolewa, mara zote unapookolewa”). Imani inayoendelea ni ushahidi wa wokovu wa kweli (kama vile Waebrania, Yakobo, na 1 Yohana) 10:29

Page 194: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

178

NASB, NKJV "Baba yangu, aliyewapa ninyi, ni mkuu kuliko vyote” NRSV "kile Baba yangu alichonipa mimi ni mkuu kuliko vyote” TEV "kile Baba yangu alichonipa mimi ni mkuu kuliko vyote” NJB "Baba yangu, kwa kile alichonipa mimi, ni mkuu kuliko yeyote Swali ni nini kusudi la kifungu “mkuu kuliko”: (1) watu wale Mungu alioumpa Yesu (NRSV, TEV) au (2) Mungu mwanyewe (NASB, NKJV, NJB). Sehemu ya pili ya mstari huu unadokeza mtu ulani awezajaribu kunyakua wafuasi wa Yesu. Kithiolojia uchaguzi wa mara ya pili unaonekana kufaa. Angalia Mada maalumu: Dhamana katika Yohana 6:37 Hili ni fungu la maneno la ajabu juu ya uhakika wa muumini ukilenga juu ya nguvu ya Baba! Ulinzi wa muumini, kama kweli zote za Kibiblia, unatolewa katika hali ya mvutano, sehemu ya kimaagano. Tumaini na ahadi ya muumini katika wokovu uko katika tabia ya Mungu wa Utatu, neema na rehema zake. Hata hivyo, muumini lazima aendelee katika imani. Wokovu unaanza na mamuzi ya awali ya maongozo ya roho ya toba na imani. Ni lazima pia utoke katika mwendelezo wa toba, imani, utii, na usitahimilivu! Wokovu sio zao (bima ya maisha, tiketi ya kwenda mbinguni), lakini ni uhusiano binafsi unaokuwa pamoja na Mungu kupitia Kristo. Ushahidi wa kuhitimisha wa mahusiano mazuri na Mungu ni mabadiliko na maisha yanayobadilika ya imani na huduma (kama vile Mathayo 7). Kuna ushahidi mdogo wa Kibiblia kwa Wakristo wa mwilini (kama vile 1 Wakorintho 2-3). Suala hapa ni mfanano na Kristo, na sio kwenda mbinguni pale tunapokufa. Hakuna upungufu juu ya ulinzi wa Kibiblia na ahadi kwa wale wanaokuwa, wanaohudumu, hata wale wanaohangaika na dhambi. Lakini, hakuna matunda, pasipokuwepo na mizizi! Wokovu ni kwa neema tu, kupitia imani tu, lakini wokovu wa kweli hutoa “kazi njema” (kama vile Efe. 2:10; Yak. 2:14-26). 10:30-33 “Mimi na Baba tu umoja…… Basi Wayahudi wakaokota mawe tena ili wampige” Haya ni moja ya maelezo ya nguvu ya Umasiha na Uungu wa Yesu (kama vile Yohana 1:1-14; 8:58; 14:8-10, hasa 17:21-26, ambayo pia hutumia neno “umoja”). Wayahudi walielewa moja kwa moja kile ambacho alikuwa akikisema na kuhesabika kuwa ni matusi (kama vile Yohana 10:33; 8:59). Walitaka kumpiga mawe wakisimamia juu ya andiko toka Law. 24:26. Katika mkanganyiko ule wa awali juu ya Kristo kuwa mtu (yaani, Arius – mzaliwa wa kwanza; Athanas – Mungu kamili) Yohana 10:30 na 14:9 yalitumiwa mara nyingi na Athanas (angalia The Cambridge History of the Bible, juzuu. 1, uk. 444). Kwa ajili ya “ufuasi wa Arius” angalia kwenye ufafanuzi.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 10:31-39 31 Basi Wayahudi wakaokota mawe tena ili wampige. 32Yesu akawajibu, Kazi njema nyingi nimewaonyesha, zitokazo kwa Baba; kwa ajili ya kazi ipi katika hizo mnanipiga kwa mawe? 33 Wayahudi wakamjibu, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu. 34 Yesu akawajibu, Je! Haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu? 35 Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka); 36 je! Yeye ambaye Baba alimtakasa, akamtuma ulimwenguni, ninyi mnamwambia, Unakufuru; kwa sababu nalisema, Mimi ni Mwana wa Mungu? 37 Kama sizitendi kazi za Baba yangu, msiniamini; 38 lakini nikizitenda, ijapokuwa hamniamini mimi, ziaminini zile kazi; mpate kujua na kufahamu ya kuwa Baba yu ndani yangu, nami ni ndani ya Baba. 39 Wakatafuta tena kumkamata; lakini akatoka mikononi mwao.

10:31 mstari huu unakaribia kuhusiana na maelezo ya Yohana 10:30. Yesu alijibu mashitaka yao katika hali isio ya kawaida ya mabishano juu ya sheria za kiyahudi. Msingi wake ni wa neno Elohim, ambalo ni neno la Agano la Kale linalomaanisha Mungu (kama vile Mwa. 1), lakini katika muundo liko katika hali ya wingi na mara nyingi lilitumika kwa wote malaika na viongozi wa kimwili (waamuzi). Angalia MADA MAALUMU: MAJINA YA UUNGU katika Yohana 6:20 10:32 Mchungaji (kalos) mwema hufanya kazi (kalos) nzuri toka kwa Baba. 10:33 “bali kwa kukufuru” Yesu alitambua kuwa walielewa kiusahihi madai yake ya kuwa yeye na Baba ni wamoja.

Page 195: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

179

10:34 “katika torati yenu” Yesu ananukuu kutoka katika Zaburi lakini anaiita “torati” (yaani,. Torati inamaanisha “mafundisho,” kama vile Yohana 12:34; 15:25; Rum.3:9-19). Neno sheria mara nyingi linarejerea juu ya maandiko ya Musa (Torati), Mwanzo---Kumbu kumbu la Torati. Hii inaonyesha utumiaji mpana wa neno lilivyoenea katika agano la Kale lote. ◙ “Ndinyi miungu” Yesu alitumia nukuu toka katika Zaburi 82:6. Alitumia elohim akirejea waamuzi wa kibinadamu (angalia Elohim katika Mada maalumu katika Yohana 6:20. Waamuzi hawa (ingawa ni waovu) wanaitwa “wana wa aliye juu.” Wayahudi hawa walikuwa wanamghasi Yesu kwa sababu ingawa alikuwa katika hali ya ubinadamu lakini alidai kuwa (1) Mwana wa Mungu na (2) mmoja na Baba. Bado watu wengine waliitwa “miungu” (kama vile Kut. 4:16; 7:1; 22:8,9; Zab. 82:6; 138:) Hoja ya Yesu juu sheria za Kiyahudi inaonekana kufuata mlolongo huu: Maandiko ni ya kweli, watu wanaitwa elohim, kwa hiyo, kwa nini mwaniita mimi mtu anayekufuru kwa kuthibitisha kwamba mimi ni mwana wa Mungu? Neno Elohim kwa Kiebrania liko katika hali ya uwingi lakini limetafasiliwa katika hali ya umoja na kutumika kama kitenzi cha umoja pale linaporejerea kwenye Uungu wa Agano la Kale. Angalia MADA MAALUMU: MAJINA YA UUNGU katika Yohana 6:20 Hili lawezakuwa haswa ombi la Yohana: (1) Neno lenye vidokezo viwili na (2) swali la Kiyunani lenye kutarajia jibu la “ndiyo.” 10:35 “(na maandiko hayawezi kutanguka)” Yohana mara nyingi alipendekeza juu ya mazungumzo ya Yesu. haijulikani kama hii ilikuwa ni kauli ya Yesu au Yohana. Hata hivyo, tena wote wakiwa wamevuviwa, haikujalisha. Msukumo wa nukuu unategemewa na andiko. Yesu pamoja na mitume waliliangalia Agano la Kale na utafasili wake kama maandiko halisi ya Mungu (kama vile Mt. 5:17-19; 1 Kor. 2:9-13; 1 Thes. 2:13; 2 Tim. 3:16; 1 Pet. 1:23-25; 2 Pet. 1:20-21; 3:15-16). Askofu H. C. G. Moule katika The Life of Bishop Moule anasema “Yeye [Kristo] kiuhalisia aliiamini Biblia, na, ingawa kuna vitu ndani yake visivyoelezeka na kutatiza yale yote yalionichanganya mie, naendelea, lakini sio katika hali ya upofu, lakini kuendelea kukiamini kitabu kwa ajili yake” (uk. 138). 10:36 Katika mstari huu Yesu anadai kwamba Baba amemchagua (au “kumtawaza” au “kumtakasa”) Yeye na kumtuma Yeye (kama Masihi). Kwa hakika sasa anastahili kuitwa “Mwana wa Mungu.” Kama mwamuzi wa Israel aliyemwakilisha Mungu (kama vile Zab. 82:6), alimwakilisha Baba katika maneno na matendo. Angalia Mada maalumu: Kupelekwa (Apostellō) katika Yohana 5:24 10:37 Hiki ni kile Yohana 10:19-21 anachokisema. Miujiza ya Yesu inaangazia kazi za Mungu. 10:37,38 “kama…….kama” Hizi ni sentesi shurutishi daraja la kwanza. Yesu alizifanya kazi za Baba yake. Kama ni hivyo, basi watu wanatakiwa kuamini katika Yeye, wakijiaminisha kuwa Yeye na Baba ni wamoja (kama vile Yohana 10:30,38). Angalia Mada maalumu: “Utiifu” katika 1 Yohana 2:10 10:39 Hivi ni kati ya vitu mbali mbali Yesu alijaribu kuviepuka kwa wale waliotaka kumdhuru (kama vile Lk. 4:29-30; Yohana 8:59). Haijulikani kama kukwepa huku kulisababishwa na (1) tukio la miujiza au (2) ufanano halisi wa Yesu na mtu yeyote, uliomsababisha kutoweka kati kati ya kusanyiko pasipo kuonekana.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 10:40-42 40 Akaenda zake tena ng'ambo ya Yordani, mpaka mahali pale alipokuwapo Yohana akibatiza hapo kwanza, akakaa huko. 41 Na watu wengi wakamwendea, wakasema, Yohana kweli hakufanya ishara yo yote, lakini yote aliyoyasema Yohana katika habari zake huyu yalikuwa kweli. 42Nao wengi wakamwamini huko.

10:40 Hii inarejea ng’ambo ya Yordani kupitia Yeriko, karibu ni mji wa Betany.

Page 196: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

180

10:41 Tena Yohana anamwongelea Yohana Mbatizaji juu ya kumthibitisha Yesu (kama vile Yohana 1:6-8,19-42; 3:22-30; 5:33)! Hii ingalikuwa ni zuio la baadhi ya mafundisho potofu yaliyoenea juu ya Yohana Mbatizaji. 10:42 Kama viongozi wa Kiyahudi walivyomkataa Yesu, ndivyo watu wengi wa kawaida (wazaliwa wa eneo) walivyompokea Yeye katika imani (kama vile Yohana 2:23; 7:31; 8:30). Angalia Mada Maalumu katika Yohana 2:23.

MASWALI YA MJADALA

Huu ni mwongozo wa fasiri, ina maanisha kwamba unawajibika kwa tafsiri zako mwenyewe za Biblia. Kila mmoja wetu lazima atembee katika mwanga tulio nao. Wewe, Biblia, na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Hutakiwi uvitelekeze vitu hivi kwa mfasiri. Maswali ya mjadala huu yanatolewa kukusaidia kufikiri juu ya mambo makubwa ya sehemu za kitabu hiki. Yanalenga kukuamsha kimawazo na sio kutoa maana.

1. Kwa nini Yohana alichanganya sitiari zake mara nyingi (mfano: “Yesu ni mlango wa kondoo na Mchungaji mwema”)

2. Ni upi mrejeo wa nyuma wa Agano la Kale katika Yohana 10? 3. Ni nini umuhimu wa Yesu wa “kuutoa uhai wake?” 4. Kwa nini Wayahudi waliendelea kumshutumu Yesu kuwa amepagawa na mapepo? 5. Kwa nini kazi za Yesu zinaonekana kuwa za muhimu? 6. Tunawezaje kufananisha “ulinzi wa muumini” na “ustahimilivu wa watakatifu?”

Page 197: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

181

YOHANA 11

MIGAWANYO YA AYA YA TAFSIRI ZA KISASA

UBS4 NKJV NRSV TEV NJB Kifo cha Lazaro Kifo cha Lazaro Ufufuo wa Lazaro Kifo cha Lazaro Ufufuo wa Lazaro 11:1-16 11:1-16 11:1-6 11:1-4 11:1-4 11:5-7 11:5-10 11:7-16 11:8 11:9-11 11:11-16 11:12 11:13-15 11:16 Yesu Ndimi Ufufuo Mimi Ndimi Ufufuo Mimi Ndimi Ufufuo na Uzima na zima na Uzima 11:17-27 11:17-27 11:17-27 11:17-19 11:17-27 11:20-22 11:23 11:24 11:25-26 11:27 Yesu alilia Yesu na Kifo Yesu alia Adui wa Mwisho 11:28-37 11:28-37 11:28-37 11:28-31 11:28-31 11:32 11:32-42 11:33-34a 11:34b 11:35-36 11:37 Lazaro anarudishwa Lazaro Kufufuliwa Lazaro anarudishwa uzimani Katika Kifo uzimani 11:38-44 1:38-44 11:38-44 11:38-39a 11:39b 11:40-44 11:43-44 Njama za Njama za Kutaka Njama Dhidi ya Viongozi wa Kiyahudi Kumuua Yesu Kumuua Yesu Yesu Kuamua juu ya Kifo cha Yesu 11:45-53 11:45-57 11:45-53 11:45-48 11:45-54 11:49-52

Page 198: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

182

11:53-54 11:54 11:54 Pasaka Ilikuwa Karibu 11:55-57 11:55-57 11:55-57 11:55-57

MZUNGUKO WA TATU WA USOMAJI KUFUATILIA KUSUDIO LA ASILI LA MWANDISHI KATIKA NGAZI YA AYA Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwatafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Aya ya kwanza 2. Aya ya pili 3. Aya ya tatu 4. N.k

MUHTASARI WA KITHIOLOJIA

Umuhimu wa kithiolojia wa Yohana 11 ni: 1. Kuzionyesha nguvu na mamlaka ya Yesu zinazonaendelea 2. Kifo cha Lazaro kilikuwa katika mpango wa Mungu wa kutoa fursa kwa Yesu ili atukuzwe (kama vile

Yohana 9:3) 3. Mazungumzo ya Martha na Yesu yalitoa fursa kwa ukiri wake mkubwa na ufunuo wa baadaye wa Yesu

Mwenyewe. 4. Yesu anatupatia maisha ya milele sasa (kiama kilichotambuliwa). Hii inaashiria ufufufo wa Lazaro. Yesu

alikuwa na mamlaka juu ya kifo! 5. Hata katika sura ya muujiza huu wenye nguvu, kutokuamini kunaendelea (yaani, dhambiI siyosameheka,

tazama Mada Maalumu katika Yohana 5:21)

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 11:1-16 1 Basi mtu mmoja alikuwa hawezi, Lazaro wa Bethania, mwenyeji wa mji wa Mariamu na Martha, dada yake. 2 Ndiye Mariamu yule aliyempaka Bwana marhamu, akamfuta miguu kwa nywele zake, ambaye Lazaro nduguye alikuwa hawezi. 3 Basi wale maumbu wakatuma ujumbe kwake wakisema, Bwana, yeye umpendaye hawezi. 4 Naye Yesu aliposikia, alisema, Ugonjwa huu si wa mauti, bali ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo. 5 Naye Yesu alimpenda Martha na umbu lake na Lazaro. 6 Basi aliposikia ya kwamba hawezi, alikaa bado siku mbili pale pale alipokuwapo. 7 Kisha, baada ya hayo, akawaambia wanafunzi wake, Twendeni Uyahudi tena. 8 Wale wanafunzi wakamwambia, Rabi, juzijuzi tu Wayahudi walikuwa wakitafuta kukupiga kwa mawe, nawe unakwenda huko tena? 9 Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu. 10 Bali akienda usiku hujikwaa; kwa sababu nuru haimo ndani yake. 11 Aliyasema hayo; kisha, baada ya hayo, akawaambia, Rafiki yetu, Lazaro, amelala; lakini ninakwenda nipate kumwamsha. 12 Basi wale wanafunzi wakamwambia, Bwana, ikiwa amelala, atapona. 13 Lakini Yesu alikuwa amenena habari ya mauti yake; nao walidhania ya kuwa ananena habari ya kulala usingizi. 14 Basi hapo Yesu akawaambia waziwazi, Lazaro amekufa. 15 Nami nafurahi kwa ajili yenu kwamba sikuwako huko, ili mpate kuamini; lakini na twendeni kwake. 16 Basi Tomaso, aitwaye Pacha, akawaambia wanafunzi wenziwe, Twendeni na sisi, ili Itufe pamoja

naye.

Page 199: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

183

11:1 "Basi mtu mmoja alikuwa hawezi" Hii ni njeo ya wakati usio timilifu. Hii inamaanisha kuwa amekuwa mgonjwa kwa kipindi kirefu. Hata hivyo, wakati usio timilifu unaweza kutafsiriwa kama "alianza kuugua." ◙“Lazaro" Hili ni neno la Kiebrania "Eleazer,"linalomaanisha "Mungu husaidia" au "Mungu ni msaidizi."Yohana alifikiri kuwa wasomaji walijua urafiki wa Yesu na Maria, Martha, na Lazaro (kama vile Luka 10:38-42, ambacho ni kitu pekee kilichotajwa katika ufupisho wa injili). ◙ “Bethania"Hii ni sehemu nyingine kutoka Bethania iliyotajwa katika Yohana 1:28 na 10:40, iliyokuwa karibu na Yeriko karibu na mto Yordani. Bethania hii ilikuwa yapata maili mbili kusini–mashariki mwa Yerusalemu juu ya ukingo mmoja na mlima wa mizeituni. Hapa palikuwa mahali Yesu alipopendelea kulala wakati akiwa Yerusalemu. ◙ “Mariamu" Hili ni neno la Kiebrania "Mariamu." ◙ "Martha" Hili ni neno la Kiaramu kwa "mhudumu wa kike."Sio la kawaida kwa Martha, aliyekuwa mkubwa ki-umri hatajwi kwanza, inaweza kuhusishwa na Luka 10:38-42. 11:2 "Mariamu yule aliyempaka Bwana marhamu, akamfuta miguu kwa nywele zake" Yohana 11:2 Ni nyongeza nyingine ya mwandishi Yohana (yaani, TEV, NET). Uhusika huu wa moyo wa kujitoa kwa Mariam (kama vile Yohana 12:2-8) unafanana kwa wote Mathayo (kama vile Yohana 26:6-13) na Marko (kama vile Yohana 14:3-9). Mwanamke aliyetajwa katika utaratibu huu wa kupakwa mafuta katika Luka 7:36 na kuendelea ni mwanamke tofauti. Msitari huu unaelezea tukio ambalo halijapata kuwekwa kwenye kumbukumbu. Limeandikwa katika Yohana 12.Wengi wanahisi kuwa hii inamaanisha kuwa Yohana alitegemea wasomaji wake kuijua familia hii kutoka katika vyanzo vingine.

MADA MAALUMU: "KUTIWA MAFUTA KATIKA BIBLIA" Hata hivyo kitenzi, BDB 602, KB 643 I; nomino, BDB 603)

(kitenzi cha Kiebrania, BDB 602, KB 643 I; nomino, BDB 603) A. Yaliyumika kwa ajili ya urembeshaji (BDB 691 I. kama vile Kumb. 28:40; Ruthu 3:3; 2 Sam. 12:20; 14:2; 2

Nya. 28:15; Dan. 10:3; Mik. 6:15) B. Yalitumika kwa ajili ya wageni (BDB 206, kama vile Zab. 23:5; Luka 7:38,46; Yohana 11:2) C. Yalitumika kwa ajili ya uponyaji (BDB 602, kama vile Isa. 61:1; Marko 6:13; Luka 10:34; Yakobo 5:14)

[yalitumika kwa maana ya tiba na kinga katika Eze. 16:9] D. Yalitumika katika maandalizi ya mazishi (kama vile Marko 16:1; Yohana 12:3,7; 19:39-40; 2 Nya. 16:14,

lakini likiwa bila kitenzi "kutiwa mafuta") E. Yalitumika katika maana ya kidini (ya jambo, BDB 602, cf. Mwa. 28:18; 31:13 [nguzo]; Kut. 29:36

[madhabahu]; Kut. 30:26; 40:9-16; Law. 8:10-13; Hes. 7:1 [hema]) F. Yalitumika kuwasimika viongozi

1. Makuhani a. Haruni (Kut. 28:41; 29:7; 30:30) b. Wana wa Haruni (Kut. 40:15; Law. 7:36) c. waliowekwa wakfu (Hes. 3:3; Law. 16:32

2. Wafalme a. Na Mungu (kama vile 1 Sam. 2:10; 2 Sam. 12:7; 2 Fal. 9:3,6,12; Zab. 45:7; 89:20) b. Na manabii (kama vile 1 Sam. 9:16; 10:1; 15:1,17; 16:3,12-13; 1 Fal. 1:45; 19:15-16) c. Na makuhani (kama vile 1 Fal. 1:34,39; 2 Fal. 11:12) d. na wazee (kama vile Amu. 9:8,15; 2 Sam. 2:7; 5:3; 2 Fal. 23:30) e. juu ya Yesu kama mfalme wa Kimasihi

Page 200: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

184

(kama vile Zab. 2:2; Luka 4:18 [Isa. 61:1]; Matendo 4:27; 10:38; Ebr]. 1:9 [Zab. 45:7]) f. wafuasi wa Yesu (kama vile 2 Kor. 1:21; 1 Yohana 2:20,27 [mafuta)

3. Juu ya manabii kadri iliyowezekana (kama vile 1 Fal. 19:16; Isa. 61:1) 4. Kuvikomboa vyombo visivyoaminika vya ki-Uungu

a. Koreshi (kama vile Isa. 45:1) b. Mfalme wa Tiro (kama vile Eze. 28:14, ambapo alitumia stirahi za Bustani ya Edeni)

5. Neno au cheo "Masihi" maana yake ni "Mtiwa mafuta" (BDB 603), kama vile Zab. 2:2; 89:38; 132:10 Matendo 10:38 ni msitari ambapo nafsi tatu za Uungu zinazwekwa pamoja katika kutiwa mafuta. Yesu alipakwa mafuta (kama vile Luka 4:18; Matendo 4:27; 10:38). Dhana inapanuliwa ili kuwajumuisha waamini wote (kama vile 1 Yohana 2:27). Mpakwa mafuta anakuwa wapakwa mafuta! Hii inaweza kuwa sambamba na Mpinga Kristo na wapinga kristo (kama vile 1Yohana 2:18). Tendo la ishara ya Agano la Kale la kumiminiwa mafuta mwilini (kama vile Kut. 29:7; 30:25; 37:29) linahusiana na wale walioitwa na kuandaliwa na Mungu kwa kazi maalumu (yaani, manabii, makuhani, na wafalme). Neno “Kristo” ni tafsiri ya neno la Kiebrania “mpakwa mafuta” au Masihi.

11:3 "maumbu wakatuma ujumbe kwake" Walituma ujumbe kwa Yesu, aliyekuwa Perea, kuvuka Yordani. ◙ "yeye umpendaye hawezi" Hii inaonyesha uhusiano wa kipekee wa familia hii na Yesu. Hili ni neno la Kiyunani phileō. Hata hivyo katika lugha ya kawaida ya Kiyunani, maneno phileō na agapaō yanabadilika badilika (kama vile Yohana 11:5; 3:35; 5:20). 11:4 "Ugonjwa huu si wa mauti, bali ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu" Hii inamaanisha kwamba Yesu alifahamu kuwa Lazaro alikuwa anaumwa. Atamruhusu afe ili Baba aweze kuonyesha uwezo wake kupitia kwake kwa kumfufua kutoka katika wafu. Magonjwa na mateso wakati mwingine ni mapenzi ya Mungu (kama vile Yohana 9:3; kitabu cha Ayubu; 2 Kor. 12:7-10). ◙ “utukufu wa Mungu" Kazi za Yesu zinabainisha "utukufu wa Mungu." Tazama nukuu katika Yohana 1:14. ◙ "ili Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo" Fungu hili lenye kuonyesha kitu cha “Mungu” halimo katika magombo ya kale ya maandiko ya Kiyunani P45au P66.Ugonjwa unaweza kuleta utukufu kwa wote, Baba na Mwana. Utukufu wa Yesu katika utaratibu huu ni tofauti kabisa kuliko ambavyo mtu angetegemea katika injili nzima ya Yohana. Neno hili limemaanisha kuangikwa msalabani na kupewa utukufu. Kufufuka kwa Yesu kutasababisha uongozi wa Wayahudi kuita watu kwa ajili ya kifo cha Yesu. 11:5 Maoni ya kiuandishi ya Yohana (kama vile Yohana 11:36). 11:6 "alikaa bado siku mbili pale pale alipokuwapo" Yesu alichelewa hadi Lazaro akawa amekufa! Yesu hakufanya upendeleo, palikuwa na kusudi la kiimani katika mgonjwa wake (kama vile Yohana 11:15; 9:3). 11:7 "Kisha, baada ya hayo, akawaambia wanafunzi wake, Twendeni Uyahudi tena" Mjadala ulioendelea unaonyesha kuwa mitume walikuwa wanajua wazi kuwa Wayahudi walitaka kumpiga mawe Yesu (kama vile Yohana 11:8; 8:54; 10:31,39). Wanafunzi wanaonyesha mchanganyiko wa ajabu wa imani na uoga (kama vile Yohana 11:16).Mara zote Thomaso anafikiliwa kuwa mwanafunzi mwenye mashaka, lakini hapa alikuwa tayari kufa na Yesu (kama vile. Yohana 11:16). Michael Magill, NT TransLine (uk. 345 #43) inafanya uchunguzi mzuri kuwa neno"twendeni" la Yohana 11:7 linabadilishwa kuwa neno"lakini ninakwenda" ya Yohana 11:11.Wanafunzi walikuwa wameogopa na kuwa na mashaka lakini Yesu alikuwa imara. Ni Tomaso ambaye anaungana na Yesu (hebu twende) katika Yohana 11:16! 11:9-10 Hii inaweza kuwa ni njia ya kuunganisha sura hadi kurudi kwa Yohana 8:12 na 9:4-5 (kama vile Yohana 12:35). Yohana 11:9 anatarajia jibu la "ndiyo".

Page 201: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

185

Kuna tofauti wa wazi kati ya wale wanaoyafuata mapenzi ya Mungu (yaani, Yesu) na wale wasio fanya hivyo (Yohana 11:10, Wayahudi). Yesu hafanyi makosa kwenda kule Mungu anakomwongoza kwenda kwa vile Yeye ndiye nuru ya ulimwengu! Utofauti huu kati ya nuru na giza ulikuwa ni wa kawaida kwenye Fasihi za Hekima ya Kiyahudi na maandishi ya Mambo ya kale huko Mesopotamia (yaani,"Magombo ya Mwana wa Nuru dhidi ya Giza" au "Vita kati ya Wana wa Nuru dhidi ya Wana wa giza"). ◙ "akienda" Hizi zote ni sentensi shurutishi daraja la tatu zenye kuonyesha tendo lenye uwezekano. 11:11 "Rafiki yetu, Lazaro, amelala" kitenzi kipo kwenye wakati timilifu tendewa elekezi. Wanafunzi daima wallishindwa kumwelewa Yesu kwa vile walimchukulia kama wa kawaida (kama vile Yohana 11:13). Matumizi ya Yesu ya stiari hii katika kifo yanaakisi matumizi yake katika Agano la Kale (kama vile Kumb. 31:16; 2 Sam. 7:12; 1 Fal. 1:21; 2:10; 11:21,43; 14:20, n.k.). Neno la Kiingereza "makaburini"linatokana na neno la Kiyunani "kulala." 11:12 "ikiwa" Hii ni sentensi shurutishi daraja la kwanza iliyochukuliwa kuwa kweli kutokana na mtazamo wa mwandishi au kwa kusudio lake la kifasihi. ◙ "atapona" Hii kihalisia neno "kuokolewa" katika matumizi yake katika Agano la Kale ni "kukombolewa kimwili" (kama vile Yakobo 5:15). Tena mitume hawakumwelewa Yesu kwa sababu waliichukuwa lugha yake ya kutumia sitiari (yaani, kulala) kirahisi tu. Hali hii ya kutoeleweka kwa Yesu kwa wasikilizaji Wake ni tabia ya injili ya Yohana (yaani, Yohana11:23-24). Yeye anatoka juu-wao wanatoka chini. Bila msaada wa Roho. (yaani, Pentekoste), hawawezi kuelewa!

11:13 Haya pia ni maoni ya kimaandishi kutoka kwa Yohana. 11:14 "Yesu akawaambia waziwazi" Tazama Mada Maalumu: Ujasiri (parrhēsia) katika Yohana 7:4 11:15 "Nami nafurahi kwa ajili yenu kwamba sikuwako huko, ili mpate kuamini"Yesu anaonyesha kuwa kufufuliwa kwa Lazaro siyo kwa sababu ya urafiki wake naye au kwa sababu ya kumhuzunikia Mariamu na Martha, bali (1) kuamsha imani ya wanafunzi (mst. 14) na (2) kuwatia moyo Wayahudi kwa imani yao (Yohana 11:42). Imani ni mchakato ndani ya Yohana. Wakati mwingine inaanza (yaani, wanafunzi, kama vile Yohana 2:11), mara nyingine (yaani, watazamaji, kama vile Yohana 8:31-59). 11:16 Mstari huu wazi kabisa unaonyesha imani ya Tomaso. Alikuwa amehiari kufa na Yesu. Mitume walitaka waonyeshwe uwezo wa yesu dhidi ya kifo kitu kilichoogopwa sana na wanadamu. Jina Thomaso linaakisi neno la Kiaramu"mapacha" (maoni mengine ya mwandishi), kama Didymus afanyavyo katika Kiyunani. Injili fupi zina mworodhesha kama Mtume (kama viele Mt. 10:3; Marko 3:18; Luka 6:15); Injili ya Yohana inamzungumza daima (kama vile Yohana 11:16; 14:5; 20:24-29; 21:2). Tazama Mada Maalumu: Jedwali la Majina ya Mitume katika Yohana 1:45

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 11:17-27 17 Basi Yesu alipofika, alimkuta amekwisha kuwamo kaburini yapata siku nne. 18 Na Bethania ilikuwa karibu na Yerusalemu, kadiri ya maili mbili hivi; 19 na watu wengi katika Wayahudi walikuwa wamekuja kwa Martha na Mariamu, ili kuwafariji kwa habari ya ndugu yao. 20 Basi Martha aliposikia kwamba Yesu anakuja, alikwenda kumlaki; na Mariamu alikuwa akikaa nyumbani. 21 Basi Martha akamwambia Yesu, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa. 22 Lakini hata sasa najua ya kuwa yo yote utakayomwomba Mungu, Mungu atakupa. 23 Yesu akamwambia, Ndugu yako atafufuka. 24 Martha akamwambia, Najua ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho. 25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; 26 naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo? 27 Akamwambia, Naam, Bwana, mimi nimesadiki ya kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni.

Page 202: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

186

11:17"alimkuta amekwisha kuwamo kaburini yapata siku nne" Viongozi wa Dini ya Kiyahudi walisema kwamba roho ya mwanadamu inakaa karibu na umbo la mwili kwa siku nne. Yesu alijaribu siku nne kudhihirisha kwamba Lazaro alikuwa amekufa kweli na zaidi ya tumaini la Viongozi wa dini ya Kiyahudi 11:18 "kadiri ya maili mbili hivi" Yohana 11:18 ni maoni mengine tahariri ya Yohana. Kimandishi hii ni "maili kumi na tano." 11:19 "watu wengi katika Wayahudi walikuwa wamekuja kwa Martha na Mariamu" Haya ni matumizi yasioainisha upande wowote wa neno "Wayahudi," ambayo kwa kawaida katika Yohana inarejerea maadui wa Yesu. Hata hivyo katika mazingira haya, inamaanisha tu kuwa ni wakazi wa Yerusalemu walioijua familia hii (kama vile Yohana 11:31,33,45). Yesu aliwapenda watu wa Yerusalemu na alikuwa anajaribu kuwa karibu nao kwa kupitia kufufuliwa kwa Lazaro. 11:20 "Mariamu alikuwa akikaa nyumbani" Mahali pa kawaida kwa waombolezaji wa Kiyahudi ilikuwa ni kuketi sakafuni.

MADA MAALUMU: IBADA KWA WALIO KATIKA HUZUNI

Waisraeli walieleza huzuni kwa mpendwa wao aliyefariki na toba binafsi, pamoja na makosa ya jinai yaliyofanyika kwa ujumla kwa njia kadhaa:

1. Kurarua mavazi, Mwa. 37:29,34; 44:13; Waamuzi. 11:35; 2 Sam. 1:11; 3:31; 1 Fal. 21:27; Ayubu 1:20 2. Kuvaa gunia, Mwa. 37:34; 2 Sam. 3:31; 1 Fal. 21:27; Yer. 48:37 3. Kuvua viatu, 2 Sam. 15:30; Isa. 20:3 4. Kuweka mikono kichwani, 2 Sam. 13:19;Yer. 2:37 5. Kuweka vumbi kichwani, Yos. 7:6; 1 Sam. 4:12; Neh. 9:1 6. Kuketi sakafuni, Omb. 2:10; Ezek. 26:16 (kulala chini, 2 Sam. 12:16); Isa. 47:1 7. Kupiga kifua, 1 Sam. 25:1; 2 Sam. 11:26; Nah. 2:7 8. Omboleza , 1 Sam. 25:1; 2 Sam. 11:26 9. Kata mwili, Kumb. 14:1; Yer. 16:6; 48:37 10. Kufunga, 2 Sam. 1:12; 12:16,21; 1 Fal. 21:27; 1 Nya. 10:12; Neh. 1:4 11. Kuimba na kusifu katika maombolezo, 2 Sam. 1:17; 3:31; 2 Nya. 35:25 12. Upara (nywele zilikatwa), Yer. 48:37 13. Kunyoa ndevu, Yer. 48:37 14. funika kichwa au uso, 2 Sam. 15:30; 19:4

Hizi zilikuwa ishara za nje kutokana na hisia za ndani

11:21, 32 "Basi Martha akamwambia…, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa" Hii ni sentensi shurutishi daraja la pili iitwayo "kinyume cha ukweli." Kwa hiyo, Ingeweza kueleweka kama “kama ungekuwa nasi hapa ambavyo haikuwa hivyo, Ndugu yangu hangalikufa na akafa." Manenno ya Martha na Mariam (kama vileYohana 11:32) kwa Yesu yalikuwa yanafanana, lazima watakuwa wamejadili hili katika siku hizi nne za maombolezo. Wanawake hawa wawili walijisikia kuwa katika hali ya utulivu kabisa walipokuwa na Yesu kiasi cha kumwelezea kilichowasibu na huzuni zao kwamba hakuja mapema. 11:22 "Lakini hata sasa najua ya kuwa yo yote utakayomwomba Mungu, Mungu atakupa" Hapakuwa na uhakika kabisa, nini Martha alikuwa akimwomba Yesu, kwa sababu katika Yohana 11:39 alishangazwa na kufufuliwa kwa Lazaro. 11:23-24 "Ndugu yako atafufuka" Martha alitoa maoni yale yale ya kithiolojia kuhusu maisha baada ya haya kama Mafarisayo walioamini katika ufufuo wa kimwili siku ya mwisho. Kuna ushahidi wa kimafundisho wa kiasi Fulani

Page 203: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

187

katika Agano la Kale kuhusu maoni haya (kama vile Dan. 12:2; Ayubu 14:14; 19:25-27). Yesu anageuza uelewa huu wa Wayahudi katika kukiri uwezo wake na mamlaka (kama vile Yohana 11:25; 14:6). 11:24 "siku ya mwisho" Ingawa kuna ukweli kuwa Yohana anasisitiza uharaka wa wokovu (kiama kinachotambulika), bado anategemea muda wa kuhukumu, hii inaelezwa kwa njia mbalimbali.

1. Siku ya hukumu/kufufuka (kama vile Yohana 5:28-29; 6:39-40,44,54; 11:24; 12:48) 2. "saa" (kama vileYohana 4:23; 5:25,28; 16:32) 3. Ujio wa pili wa Kristo (kama vileYohana 14:3; inawezekana kuwa 14:18-19,28 na 16:16,22 inarejea kwa

kuonekana kwa Yesu baada ya kufufuka na siyo katika kuja wakati wa kiama) 11:25 "Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, nauzima"Haya ni mojawapo ya maneno saba ya Mungu "Mimi ndimi" mbele ya uso wa kifo cha Lazaro, Martha alipewa tumaini la kuamini kuwa angeishi. Tumaini hili linatoka ndani ya mtu na uwezo wa Baba na wa Yesu (kam vile Yohana 5:21).Tazama nukuu katika Yohana 8:12. Chakushangaza, maandiko ya magombo ya kale (yaani P45) na mengine ya Kilatini cha Kale, tafsiri za Kisitiria na Mkusanyiko wa vitabu vya Injili vine katika simulizi moja vinaacha maneno "na uzima."UBS3 inajumuisha kwa kiwango cha alama "B", lakini UBS4 inayajumuisha kwa kiwango cha alama "A" (hakika). 11:26 "naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa" Kuna mambo kadhaa muhimu yanayoonekana katika upangaji wa sarufi katika andiko hili.

1. Kiwakilishi cha wote "wote" 2. Kitenzi cha wakati uliopo endelevu kinachoonyesha imani inayoendelea (Yohana 11:25, 26) 3. Kanushi hasi mbili za nguvu zikiungana na kifo.”kamwe haitatokea wala kufa” ambayo bila shaka

yanaashiria “kifo cha kiroho” Katika Yohana uzima wa milele ni uhalisia uliopo kwa waamini, sio tu kwa matukio kadhaa yajayo. Lazaro ametumika kuelezea kwa mifano maneno ya Yesu! Kwa Yohana maisha ya milele ni uhalisia uliopo. 11:27 "Naam, Bwana, mimi nimesadiki ya kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni" Hii imesemwa katika wakati ulio timilifu. Hili ni ungamo la nguvu binafsi la imani ya mwanamke huyu kwa Yesu kama Masihi aliyeahidiwa. Hii kithiolojia ni sawa na ungamo la Petro katika kaisari (kama ville Mathayo 16). Anatumia majina kadhaa mbalimbali kuelezea imani yake.

1. Kristo (ambayo ilikuwa fasili ya Kiyunani kwa Masihi, Aliyepakwa mafuta) 2. Mwana wa Mungu (jina la Masihi katika Agano la Kale) 3. Yeye ambaye anakuja (wadhifa wa jina lingine la aliyeahidiwa kuleta enzi mpya ya haki, kama vile. Yohana

6:14) Yohana anatumia maana ya mazungumzo ya mabadiishano ya mawazo kama mbinu ya kifasihi kupeleka ukweli. Kuna baadhi ya ukiri wa imai kwa Yesu katika injili ya Yohana (kama vile Yohana 1:29,34,41,49; 4:42; 6:14,69; 9:35-38; 11:27). Tazama Mada Malumu: Matumizi ya Yohana ya Amini katika Yohana 2:23

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 11:28-29 28 Naye alipokwisha kusema hayo, alikwenda zake; akamwita umbu lake Mariamu faraghani, akisema, Mwalimu yupo anakuita. 29 Naye aliposikia, aliondoka upesi, akamwendea.

11:28 "Mwalimu" Biblia ya NASB (ukr. 1540) ina maoni makuu, "maelezo muhimu yaliyopaswa kutolewa na mwanamke. Viongozi wa Dini ya Kiyahudi wasingewafundisha wanawake (kama vile Yohana 4:27), lakini Yesu aliwafundisha mara kwa mara."

MADA MAALUMU: WANAWAKE KATIKA BIBLIA

I. Agano la Kale

Page 204: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

188

A. Katika mila na desturi wanawake walichukuliwa kama ni mali kwa aliyenaye 1. Walijumuishwa katika orodha ya mali (Kutoka 20:17) 2. Walivyotendewa wanawake watumwa (Kutoka 21:7-11) 3. Nadhiri za wanawake kufutwa na waume wenye madaraka (Hesabu 30) 4. Wanawake kama mateka wa vita (kumbukumbu la Torati 20:10-14; 21:10-14)

B. Kiutendaji palikuwa na ushirikiano 1. Mwanaume na mwanamke waliumbwa kwa mfano wa Mungu (Mwanzo 1:26-27) 2. Heshima kwa baba na mama (Kutoka 20:12 [Kumb. 5:16]) 3. heshima kuu kwa baba na mama (Mambo ya Walawi 19:3; 20:9) 4. mwanaume na mwanamke wangeweza kuwa Wanazareti (Hesabu 6:1-2) 5. mabinti wana haki ya urithi (Hesabu 27:1-11) 6. ni sehemu ya watu wa agano (Kumbu kumb. 29:10-12) 7. wanapata mafundisho ya baba na mama (Mithali 1:8; 6:20) 8. wana wa kiume na mabinti wa Hemani (nyumba ya Kilawi) waliongoza muziki ndani ya Hekalu (1

Mambo ya Nyakati 25:5-6). 9. Wana wa kiume na wa kike watatoa unabii katika enzi mpaya (Yoeli 2:28-29)

C. Wanawake katika dhima ya uongozi 1. Dada yake Musa, Miriamu, aliitwa nabii wa kike (Kutoka 15:20-21 vile vile nukuu Mika 6:4) 2. Wanawake walikirimiwa toka kwa Mungu kusokota nguo za aina mbalimbali kwa ajili ya

Vibanda(Kutoka 35:25-26) 3. Mwanamke aliyeolewa, Debora, pia nabii (kama vileWaamuzi. 4:4), aliyaongoza makabila yote

(Amu. 4:4-5; 5:7) 4. Hulda alikuwa nabii ambaye mfalme Yosia alimsihi kusoma na kutafsiri kitabu kipya

kilichotolewa "Book of the Law" (2 Falme 22:14; 2 Nya. 34:22-27) 5. Malkia Esta, mwanamke aliyemcha Mungu, aliwaokoa Wayahudi katika Uajemi

II. Agano Jipya

A. Kwa utamaduni wa dini za Kiyahudi na ulmwengu wa kale wa Kiyunani na Rumi, wanawake walikuwa raia wa daraja la pili wenye haki na vipaumbele vichache (isipokuwa Makedonia).

B. Wanawake katika dhima ya uongozi 1. Elizabeti na Mariamu, wanawake waliomcha Mungu kwa kujihudhurisha mbele za Mungu (Luka

1-2) 2. Ana, nabii mwanamke akihudumu katika Hekalu (Luka 2:36) 3. Lidia, mwamini na kiongozi wa kanisa la nyumbani (Matendo 16:14,40) 4. Mabinti Filipo wanne waliokuwa mabikra na manabii (Matendo 21:8-9) 5. Fibii, shemasi wa kike wa kanisa katika Kenkrea (Rum. 16:1) 6. Priska (Prisila), mtendakazi pamoja na Paulo na mwalimu wa Apolo (Matendo 18:26; Rum. 16:3) 7. Maria, Trifaina, Trifosa, Persisi, Yulia, dada wa Nerea, wanawakae kadhaa watenda kazi amoja

na Paulo (Rum. 16:6-16) 8. Yunia (KJV), bila shaka mwanamke mtume (Rum. 16:7) 9. Euodia na Sintike, watenda kazi pamoja na Paulo (Flp. 4:2-3)

III. Ni kwa namna gani mwamini wa sasa atailinganisha mifano hii tofauti ya kibiblia?

A. Ni kwa namna gani mtu ataupambanua kweli wa kihistoria na kiutamaduni, anaoutumia katika mazingire asilia pekee, kutoka katika ukweli wa milele ulio halali kwa makanisa yote, waamini wa rika zote? 1. Kwa umakini yatupasa kuchukuliana na kusudio la mwandishi asilia aliyevuviwa. Biblia ni neno la

Mungu na njia na chanzo pekee cha imani na matendo. 2. Yatupasa kushughulika dhahiri na maandiko yenye masharti nay a kihistoria yaliyovuviwa.

a. Utaratibu wa ibada (yaani, utaratibi na liturujia) wa Israeli (kama vile Matendo 15;

Page 205: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

189

Wagalatia 3) b. dini ya Kiyahudi ya karne ya kwanza c. semi dhahiri za Paulo zenye masharti kihistoria na katika 1 Wakorintho

1) mfumo wa kisheria wa wapagani katika Rumi (1 Wakorintho 6) 2) kubaki katika hali ya utumwa (1 Kor. 7:20-24) 3) ujane/useja (1 Kor. 7:1-35) 4) mabikra (1 Kor. 7:36-38) 5) chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu (1 Kor. 8; 10:23-33) 6) matendo yasiyofaa katika Karamu ya Bwana (1 Wakorintho 11)

3. Kwa uwazi na kwa ukamilifu Mungu alijifunuaa kwa utamaduni maalumu, siku maalumu. Yatupasa kuuchukua ufunuo kwa umakini mkubwa, sio kufanya marekebisho kwa kila kipengele. Neno la Mungu liliandikwa katika maneno ya mwanadamu, likaelezwa katika utamaduni maalumu kwa wakati maalumu.

B. Tafsiri za kibiblia inapaswa kutafuta kusudi la asilia la mwandishi, nini alichokuwa akikizungumzia katika sihu zake zile? Hili ndilo jambo la kimsingi na la muhimu sana la tafsiri sahihi. Lakini basi yatupasa tulitumie hili kwa wakati wetu huu tulio nao. Tatizo kubwa la kiutafsiri linanaweza kuelezea maana ya neno. Je! Ni wapi palikuwa na huduma nyingi kuliko wachungaji ambao walionekana kama viongozi? Je! Ni wapi wahudumu au mashemasi wa kike na manabii wa kike walionekana kama viongozi? Ni dhahiri sana kuwa Paulo, katika 1 Kor. 14:34-35 na 1 Tim. 2:9-15, anadai kuwa wanawake wasishike nafasi katika ibada ya hadharani! Lakini alitumie kwa namna gani katika siku kama hizi? Nisingetaka utamaduni wa Paulo au utamaduni wangu kunyamazisha neno la Mungu na mapenzi yake. Bila shaka katika siku zile za Paulo palikuwa na mipaka sana, lakini pia katika siku zangu hizi inaweza kuwa wazi mno. Najisikia kukosa amani sana kusema kwamba kuwa maneno na na mafundisho Paulo ni ya kimasharti, karne ya kwanza, ukweli unaoendana na mazingira ya wenyeji hao. Mimi ni nani hata niweze kusababisha akili yangu au utamaduni wangu kumpinga mwandishi aliyevuviwa?! Hata hivyo, nitafanya nini ikiwa kuna mifano ya kibiblia ya wanawake waliokuwa viongozi (hata katika maandiko ya Paulo, kama vile Warumi 16)? Mfano mzuri wa hili ni mjadala wa Paulo kuhusu ibada ya hadharani katika 1 Wakorintho 11-14. Katika 1 Kor. 11:5 anaonekana kuyaruhusu mahubiri na maombi ya wanawake katika ibada za hadharani huku vichwa vyao vikiwa vimefunikwa, lakini bado katika 14:34-35 anawahitaji wawe kimya! Kulikuwa na watoa huduma wanawake (kama vile Rum. 16:1) na manabii wa kike (kama vile Matendo 21:9). Ni utofauti huu unaonipa uhuru wa kutambua maoni ya Paulo (kama inavyohusiana na maagizo kwa mwanamke) kama ilivyozuiliwa huko Korintho na Efeso katika karne ya kwanza. Katika makanisa yote mawili palikuwa na matatizo kwa wanawake katika kutumia uhuru wao mpya uliopatikana (kama vile. Bruce Winter, After Paul Left Corinth), ambapo ingeweza kusababisha ugumu kwa kanisa kuifikia jamii kwa ajili ya Kristo. Uhuru wao ulibidi kupunguzwa ili kwamba injili iweze kuleta matokeo mazuri. Siku zangu ziko kinyume na siku za Paulo. Katika siku zangu injili inaweza kuwekewa mipaka ama ikiwa wanawake wenye uwezo wa kusema, waliofunzwa hawaruhusiwi kuchangia katika injili, hawaruhusiwi kuongoza! Ni nini hatima ya lengo la ibada ya hadharani? Si uinjilisti na nidhamu? Je! Mungu anaweza kuheshimiwa na kufurahishwa na viongozi wa kike? Biblia kwa ujumla wake inaonekana kusema "ndiyo"! Nataka kukubaliana na Paulo; theolojia yangu kimsingi ni ya Kipauline. Sitaki kuathiriwa kwa kiwango kikubwa au kugeuzwa kifikra na sera za kisasa za kupigania haki za wanawake. Hata hivyo, nahisi kwamba kanisa limeenda pole pole katika kuitikia ukweli ulio wazi wa kibiblia, kama matendo yasiyo stahili kuhusu utumwa, ubaguzi, itikadi kali, na ubaguzi wa kijinsia. Hili pia limechelewa kwa kutoitikia vyema masuala ya uzalilishaji wa wanawake katika ulimwengu wa kisasa. Mungu katika Kristo amemweka huru mtumwa na mwanamke. Si thubutu kuruhusu maandiko yenye utamaduni unaopingana na haya.

Page 206: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

190

Hoja moja zaidi: kama mtafsiri ninafahamu kuwa Korintho lilikuwa ni kanisa lililoharibiwa sana. Vipawa vilivyotolewa vilikuwa vya majivuno. Wanawake wangeweza kuwa wameshikwa katika hili. Pia ningeweza kuamini kuwa Efeso ilikuwa imeaathiliwa na walimu wa uongo waliofanikiwa kutumia wanawake kama wasemaji mbadala ndani ya makanisa ya Efeso.

C. Mapendekezo kwa usomaji zaidi 1. How to Read the Bible For All Its Worth by Gordon Fee and Doug Stuart (kur. 61-77) 2. Gospel and Spirit: Issues in New Testament Hermeneutics by Gordon Fee 3. Hard Sayings of the Bible by Walter C. Kaiser, Peter H. Davids, F. F. Bruce, na Manfred T.

Branch (kur. 613-616; 665-667)

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 11:30-37 30 Na Yesu alikuwa hajafika ndani ya kijiji; lakini alikuwa akalipo pale pale alipomlaki Martha. 31 Basi wale Wayahudi waliokuwapo na Mariamu nyumbani, wakimfariji, walipomwona jinsi alivyoondoka upesi na kutoka, walimfuata; huku wakidhania ya kuwa anakwenda kaburini ili alie huko. 32 Basi Mariamu alipofika pale alipokuwapo Yesu, na kumwona, alianguka miguuni pake, akamwambia, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa. 33 Basi Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliofuatana naye wanalia, aliugua rohoni, akafadhaika roho yake, 34 akasema, Mmemweka wapi? Wakamwambia, Bwana, njoo utazame. 35 Yesu akalia machozi. 36 Basi Wayahudi wakasema, Angalieni jinsi alivyompenda. 37 Bali wengine wao wakasema, Je! Huyu aliyemfumbua macho yule kipofu, hakuweza kumfanya na huyu asife?

11:30 Huu ni ushahidi mwinngine wa macho wenye kueleza kila kitu kuhusiana na mwandishi wa Kitume. 11:33 NASB "Alivutwa kwa kina na roho na alisumbuka" NKJV "aliugua rohoni, akafadhaika roho yake, NRSV "Alijawa na huzuni na kufadhaika moyoni" TEV "Moyo wake uliguswa na kusogea upesi” NJB "Yesu alihuzunika sana, na kushusha pumzi kwa nguvu" Hili kihalisia lilikuwa neno “alipumua katika roho.” Nahau hii kwa kawaida ilitumika kuonyesha hasira (kama vile Dan. 11:30 [LXX]; Marko 1:43; 14:5). Lakini katika mazingira haya, tafsiri zinazoonyesha hisia hazina budi kupewa nafasi (kama vile Yohana 11:38). Ingawa baadhi ya watoa maoni wanaziona hisa hizi zenye nguvu, bila shaka yaweza kuwa hasira iliyopelekea katika kifo, Yesu alikuwa na hisia za kweli za kibinadamu kiukweli (kama vile Yohana 11:33,35,36,38) na kuzionyesha hapa kwa marafiki zake. 11:35 "Yesu akalia machozi" Hii ni sentensi fupi sana kuliko zote katika Biblia. Kifo hakikuwa mapenzi ya Mungu katika Sayari hii. Ni matokeo ya uasi wa mwanadamu. Yesu anajihisi maumivu kwa kupotea kwa mpendwa wake. Anajihisi hivyo kwa uzoefu wa maisha ya wafuasi Wake wote! Kilio cha Yesu kilikuwa cha kimya, cha aina ya kibinadamu, si kilio cha watu wote kinachotajwa katika Yohana 11:33. 11:37 Swali hili linatarajia jibu la "ndiyo".Haya yalikuwa maoni ya Martha katika Yohana 11:21 na ya Mariamu katika Yohana 11:32

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 11:38-44 38 Basi Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake. 39 Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne. 40 Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu? 41 Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. 42 Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya

Page 207: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

191

mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma. 43 Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje. 44 Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende

zake. 11:38 "pango" Katika kipindi hiki makaburi ya Wapalestina pengine yalikuwa

1. Mapango ya asili (Baba Bathra 6:8) 2. Mapango yaliyochimbwa ndani ya majabali,na kusilibwa kwa mawe ya mduara yaliyoviringishwa katika

mitaro. 3. Mashimo yalichimbwa ardhini na kufunikwa kwa mawe makubwa

Kutokana na usomaji wa mambo ya kale huko Yerusalemu uchaguzi #1 unafaa zaidi. 11:39 "Liondoeni jiwe" Jiwe kubwa lililoviringishwa kwa desturi, ilikuwa njia liyotumika kusiliba makabiri kuzuia waporaji na wanyama. ◙ "amekuwa maiti siku nne" Hii ni nahau ya Kiyunani kifasihi "mtu wa siku nne." 11:40 "ukiamini" Hii ni sentensi shurutishi daraja la tatu ambayo inamaanisha tendo linawezekana.msitari huu ni swali linalo tarajia jibu la “ndiyo”. ◙ "utukufu wa Mungu" Utukufu wa Mungu ulibainishwa katika matendo ya Yesu (kama vile Yohana11:4). Tazama nukuu kamili katika Yohana 1:14. 11:41"Yesu akainua macho yake juu" Mkao wa kawaida wa uombaji wa Kiyunani ilikuwa ni kuinua macho (kufumba) na mikono juu mbinguni.Hii ni nahau kwa ajili ya maombi (kama vileYohana 17:1).

◙ "kwa kuwa umenisikia" “Yesu"anamsikia" Baba (kama vile Yohana 8:26, 40; 15:15) na Baba "anamsikia" Yeye. Wale ambao “wanamsikia” wana maisha ya milele. Huu ni mchezo endelevu wa kucheza na maneno “kuona” na “kusikia” ni mfanano wa “kupokea” (Yohana 1:12) na "kuamini" (Yohana 3:16). Lazaro "aliisikia" sauti ya Yesu na akarudi katika uzima tena. 11:42 Hii hapa inaaeleza kusudi la maombi ya Yesu na miujiza. Yesu daima alifanya miujiza ili kuhamasisha imani kwa wanafunzi, na katika hali hii kuweza kuanzisha imani kwa Wayahudi kutoka Yerusalemu. Kithiolojia Yesu tena anakuza mamlaka na kipaumbele cha Baba yake katika kazi zake (kama vile Yohana 5:19,30; 8:28; 12:49; 14:10). Muujiza huu unafunua uhusiano wa karibu wa Yesu na Baba. Tazama Mada Maalumu: Kupelekwa (Apostellō) katika Yohana 5:24 11:43 "akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje'"Inasemekana kuwa kama Yesu asingelimtaja Lazaro bayana, wote waliokuwa makaburini wangetoka nje! 11:44 Miili ilitayarishwa kwa maziko kwa kuoshwa na maji, kisha ikazungushiwa kamba za nguo za kitani zenye kuchanganywa na manukato ili kusaidia katika kutoa harufu nzuri. Maiti zilipaswa kuzikwa ndani ya masaa ishirini na nne kwa sababu Wayahudi hawakuwa na dawa za kuitia miili ya waliokufa.

MADA MAALUMU:UTARATIBU WA MAZISHI

I. Mesopotamia A. Mazishi sahihi yalikuwa muhimu sana kwa maisha ya baadae yenye furaha ambayo daima

yalitazamwa kama mwendelezo wa maisha yaliyopo hapa, (tazama Mada Maalumu: Wafu wako wapi?).

Page 208: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

192

B. Mfano wa laana ya watu wa Mesopotamia ni, "Ardhi haiwezi kuzipokea maiti zenu "

II. Agano la Kale A. Mazishi yaliyo sahihi yalikuwa muhimu sana (kama vile Mhu. 6:3). B. Yalifanyika haraka sana(kama vile Sara katika Mwanzo 23 na Raheli katika Mwa. 35:19 na tazama

Kumb. 21:23). C. Mazishi yasiyo sahihi yalikuwa ni ishara ya kukataliwa na dhambi.

1. Kumbukumbu la torati 28:26 2. Isaya 14:20 3. Yeremia 8:2; 22:19

D. Mazishi yalifanyika kama iwezekanavyo, katika vyumba vya familia vya ndani kwa ndani katika maeneo ya nyumbani (yaani, alilala na baba zake").

E. Hapakuwa na mafuta ya kupaka maiti isioze kama ilivyo kuwa Misri. Mwanadamu alitoka mavumbini na atarudi mavumbini (mf. Mwa. 3:19; Zab. 103:14; 104:29 Pia angalia Mada Maalumu: Kuchoma maiti.

F. Katika sheria za dini za Kiyahudi ilikuwa vigumu kuweka usawa wa heshima kamili na kuukabili mwili katika dhana ya kuinajisi sherehe kunakohusishwa na maiti.

III. Agano Jipya

A. Mazishiya haraka yalifuatia kifo, kwa kawaida ilikuwa ndani ya masaa ishirini na nne.Wayahudi kwa kawaida walilinda kaburi kwa siku tatu, wakiamini kuwa nafsi ingeweza kuurudia mwili ndani ya siku hizo (kama vileYohana 11:39).

B. Mazishi yalijumuisha kuosha na kufunika maiti kwa manukato (kama vile Yohana 11:44; 19:39-40). C. Hapakuwa na utofauti katika taratibu za maziko kati ya Wayahudi na Wakristo (au kitu kilichowekwa

kaburini) katika karne ya kwanza huko Palestina.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 11:45-46 45 Basi wengi katika Wayahudi waliokuja kwa Mariamu, na kuyaona yale aliyoyafanya, wakamwamini. 46 Lakini wengine wakaenda zao kwa Mafarisayo, wakawaambia aliyoyafanya Yesu.

11:45 "Basi wengi katika Wayahudi ... wakamwamini" Hii ndiyo dhamira inayotajwa katika Injili (kama vile Yohana 20:30-31). Hiki kifungu kina mpangilio (kama vile Yohana 2:23; 7:31; 8:30; 10:42; 11:45; 12:11,42). Hata hivyo, inapaswa kuelezwa upya kwamba imani katika Injili ya Yohana ina viwango kadhaa na mara nyingine si imani iokoayo (kama vileYohana 2:23-25; 8:30 na kuendelea). Tazama Mada Maalumu katika Yohana 2:23 11:46 "wengine wakaenda zao kwa Mafarisayo, wakawaambia aliyoyafanya Yesu" Inashangaza kiasi cha kuona upofu wa kiroho mbele ya mafundisho ya aina ile na miujiza mikubwa kiasi kile. Hata hivyo Yesu anayagawa makundi yote katika wale waliotokea kumwamini na wale wanaokataa ukweli kumhusu Yeye. Hata muujiza wenye nguvu kama huu hauwapi imani (Yaani Luka 16:30-31).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 11:47-53 47 Basi wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakakusanya baraza, wakasema, Tunafanya nini? Maana mtu huyu afanya ishara nyingi. 48 Tukimwacha hivi, watu wote watamwamini; na Warumi watakuja, watatuondolea mahali petu na taifa letu. 49 Mtu mmoja miongoni mwao, Kayafa, aliyekuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, akawaambia, Ninyi hamjui neno lo lote; 50 wala hamfikiri ya kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, wala lisiangamie taifa zima. 51 Na neno hilo yeye hakulisema kwa nafsi yake; bali kwa kuwa alikuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, alitabiri ya kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa hilo. 52 Wala si kwa ajili ya taifa hilo tu; lakini pamoja na hayo awakusanye watoto wa Mungu waliotawanyika, ili wawe wamoja. 53 Basi tangu siku ile walifanya shauri la kumwua.

Page 209: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

193

11:47 "wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakakusanya baraza” Hii inarejea kwa Wakuu wa Sinagogi, mahakama kuu ya Wayahudi katika Yerusalemu. Ilikuwa na wajumbe maalumu 70. Makuhani wakuu walikuwa washauri wa kisiasa na kidini waliofahamika kama Masadukayo, walioyakubali maandishi ya Musa tu na kuukataa ufufuo .Mafarisayo ndiyo walikuwa maarufu zaidi, kundi la kidini lililokubalika kisheria lambalo lilikiri (1) Agano la Kale zima;(2) kazi ya Malaika;(3)na maisha baada ya kufa. Inashangaza kuwa makundi haya mawili yanayopingana wangeungana kwa sababu hiyo. Tazama MADA MAALUMU: MAFARISAYO katika Yohana 1:24. Angalia Mada Maalumu: Wakuu wa Sinagogi katika Yohana 3:1

◙"Maana mtu huyu afanya ishara nyingi" Maana ya kumwita Yesu "mtu huyu" ni njia ya kumshusha hadhi kwa kutotaja jina Lake. Pia inashangaza kwamba katika kuwepo kwa miujiza hii yote yenye nguvu kama ya kumfufua Lazaro, kwamba mapokeo yao ya awali ya upendeleo yamepofusha macho yao kabisa (kama vile 2 Kor. 4:4). 11:48 "kama" Hii ni sentensi shurutishi daraja la tatu inayomaanisha tendo muhimu.

◙"watu wote watamwamini" Wivu pamoja na kutokukubali mabishano ya kithiolojia ilikuwa ni sababu ya kutomwamini na kumwogopa Yesu. "wote" ingeweza kuwa inamaanisha hata Wasamaria na watu wa mataifa (kama vile Yohana 10:16). Palikuwa pia na suala la kisiasa kwa hofu (yaani, uthibiti wa Warumi).

◙"Warumi watakuja, watatuondolea mahali petu na taifa letu"Hii ndiyo mojawapo ya ule unabii wa kejeli katika injili ya Yohana. Kwa sababu hii ilitimizwa hasa katika enzi ya miaka ya 70 b.k chini ya jenerali wa Kirumi (baada ya mfalme mkuu) Tito. Uhalisia wa kisiasa wa utawala wa Kirumi ulikuwa ni sehemu kubwa ya wakati wa mwisho (kiama) wa matumaini ya Wayahudi. Waliamini kuwa Mungu angetumia mtu wa kidini au kijeshi kama waamuzi wa Agano la Kale, ili kuwaondoa kinguvu kutoka katika Rumi. Baadhi ya wanaojifanya masihi walianza kuanzisha uasi katika Palestina ili kukamilisha tarajio lao hili la kweli kweli. Yesu alidai kuwa ufalme wake haukutawala kisiasa kwa muda (kama vile Yohana 18:36), bali ni utawala wa roho ambao ungekamilishwa katika ulimwengu wote siku za usoni (yaani, Ufunuo). Alidai kukamilisha unabii katika Agano la Kale, lakini sio kiuhalisia katika maana ya Kiyahudi au kitaifa. Kwa maana hii alikataliwa na Wayahudi wengi wa zama hizo. 11:49 "Kayafa, aliyekuwa Kuhani Mkuu mwaka ule" uongozi wa kikuhani ulikusudiwa kuwa nafasi ya maisha yote yaliyorithishwa kutoka kwa mtawala kwenda kwa watoto wake (kama vile. Kutoka 28), lakini baada ya Warumi kuwa washindi iliuzwa kwa wazabuni wakubwa kwa sababu ya biashara ya faida kubwa iliyokuwepo katika Mlima wa mizeituni na katika maeneo ya mahekalu.Kayafa alikuwa kuhani mkuu mwaka wa 18-36 b.k (mkwe wa Anas, Kuhani Mkuu kutoka mwaka wa 6-15 b.k). 11:50-52 Huu ni mfano mwingine wa maneno ya kejeli ya Yohana. Kayafa hufundisha injili! 11:50 "mtu mmoja afe kwa ajili ya watu" Historia ya nyuma katika Agano la Kale kwa haya ni maoni ya Wayahudi kuhusu “mwili." Mtu mmoja (mzuri au mbaya) angeathiri wengine wote (yaani, Adamu/Eva; Akani). Dhana hii inakuja kuwa kibano kwa mfumo wa utoaji sadaka na hasa katika siku ya upatanisho wa Mungu na mwanadamu (Walawi 16), ambapo mnyama mmoja alizaa dhambi ya taifa. Hii inakuwa dhana ya kimasihi katika Isaya 53. Kaika Agano Jipya ufanano wa Adam/Kristo katika Rum. 5:12-21 inaakisi dhana hii. 11:51 NASB, REV, NET "kwamba Yesu alikuwa anaenda kufa" NKJV, NIV, REB "kwamba Yesu angekufa" NRSV "kwamba Yesu alikuwa kariibu afe" NJB "kwamba Yesu alikufa"

Page 210: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

194

NIDOTTE, juzuu. 1, uk. 326, ina maoni mazuri kuhusu matumizi ya thiolojia ya kitenzi mellō ("lazima," "yapasa kuwa," "kuwa na hakika") kinapotumika kwa mapenzi ya Mungu kwa kazi ya ukombozi wa Kristo.

1. Marko 10:32 1. Mathayo 17:22 2. Luka 9:31,44; 24:21; Mdo. 26:23

3. Yohana 7:39; 11:51; 12:33; 14:22; 18:32 Pia linatumika kwa umuhimu wa usaliti wa Yuda 1. Luka 22:23 2. Yohana 6:71; 12:4 Luka, katika Matendo, analitumia kwa utimilifu wa kinabii (yaani, Mdo. 11:28; 24:15; 26:22). Matukio yote ya ukombozi yalikuwa katika mikono ya Mungu (kama vile Mdo. 2:23; 3:18; 4:28; 13:29)! 11:52 "lakini pamoja na hayo awakusanye watoto wa Mungu" Hii inaonekana kuwa ni maoni ya mwandishi wa Yohana ambayo yangekuwa sambamba na Yohana 10:16. Ingeweza kumaanisha

1. Wayahudi kuishi nje ya Palestina 2. Machotara-Wayahudi kama Wasamaria 3. Watu wa mataifa

Chaguo #3 linaonekana bora zaidi. Lolote litakalokuwa, kifo cha Yesu kitaleta umoja kwa wanadamu "wanaoamini" (kama vile Yohana 1:29; 3:16; 4:42; 10:16). 11:53 "Basi tangu siku ile walifanya shauri la kumwua" Hii ndiyo dhamira inayojirudia katika Yohana (kama vile Yohana 5:18; 7:19; 8:59; 10:39; 11:8).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 11:54 54

Kwa hiyo Yesu hakutembea tena kwa wazi katikati ya Wayahudi; bali alitoka huko, akaenda mahali karibu na jangwa, mpaka mji uitwao Efraimu; akakaa huko pamoja na wanafunzi wake.

11:54 "Kwa hiyo Yesu hakutembea tena kwa wazi katikati ya Wayahudi" Yohana 12 ni jaribio la mwisho la Yesu kushughulika na viongozi wa kidini. Neno lililofasiliwa katika Yohana "hadharani" (kama vile Yohana 7:26; 11:54; 18:20) kwa kawaida linamaanisha "kwa ujasiri." Tazama Mada Maalumu: Ujasiri (parrhēsia) katika Yohana 7:4.

◙"mji uitwao Efraimu" Mji huu ungeweza kuwa karibu na Betheli katika Samaria (kama vile 2 Nyak. 13:19).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 11:55-57 55 Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; na wengi wakakwea toka mashambani kwenda Yerusalemu kabla ya Pasaka, ili wajitakase. 56 Basi wao wakamtafuta Yesu, wakasemezana hali wamesimama hekaluni, Mwaonaje? Haji kabisa sikukuu hii? 57 Na wakuu wa makuhani na Mafarisayo walikuwa wametoa amri ya kwamba mtu akimjua alipo, alete habari, ili wapatekumkamata.

11:55-57 Mistari hii inaunganisha Yohana 11 na 12 pamoja. 11:55 "ili wajitakase" Hii inamaanisha haki ya matambiko au ibada ya kujitakasa na kujiandaa kwa pasaka. Bado kuna mjadala juu ya ni kwa mda gani yesu alifundisha, alihubiri, na kazi za kanisa katika Palestina. Injili fupi zimepangwa kwa namna kwamba mwaka mmoja au miwili inawezekana. Hata hivyo, Yohana ana pasaka kadhaa (siku kuu ya mwaka). Kwa uhakika zipo tatu zilizotajwa (kama vile Yohana 2:13; 6:4; na 11:55) ikiwa angalau ya nne iliyokusudiwa kwenye "siku kuu" katika Yohana 5:1. 11:57 Haya ni maoni mengine ya mwandishi kutoka kwa Yohana.

Page 211: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

195

MASWALI YA MJADALA

Huu ni mwongozo wa fasiri, ina maanisha kwamba unawajibika kwa tafsiri zako mwenyewe za Biblia. Kila mmoja wetu lazima atembee katika mwanga tulio nao. Wewe, Biblia, na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Hutakiwi uvitelekeze vitu hivi kwa mfasiri. Maswali ya mjadala huu yanatolewa kukusaidia kufikiri juu ya mambo makubwa ya sehemu za kitabu hiki.

Yanalenga kukuamsha kimawazo na sio kutoa maana

1. Kwanini Yesu aliruhusu kufariki kwa Lazaro?

2. Je! Muujiza ulikuwa umelengwa kwa nani?

3. Nini tofauti iliyopo kati ya ufufuo na kuamusha aliyelala mauti?

4. Kwanini viongozi wa Kiyahudi walitishika sana kwa kufufuliwa Lazaro?

Page 212: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

196

YOHANA 12

MIGAWANYO YA AYA YA TAFSIRI ZA KISASA

UBS4 NKJV NRSV TEV NJB Kutiwa mafuta Kutiwa mafuta Kutiwa mafuta Yesu alitiwa mafuta Kutiwa mafuta Katika Bethania katika Bethania katika Bethania Bethania katika Bethania 12:1-8 12:1-8 12:1-8 12:1-6 12:1-8 12:7-8 Shauri la kumuua Shauri la kumuua shauri la kumuua Lazaro Lazaro Lazaro 12:9-11 12:9-11 12:9-11 12:9-11 12:9-11 Kuingia kwa Kuingia kwa Jumapili ya mitende Kuingia kwa Shangwe Kuingia kwa Masihi Shangwe huko Shangwe Yerusalemu Yerusalemu Yerusalemu 12:12-19 12:12-19 12:12-19 12:12-13 12:12-19 12:14 12:15 12:16 12:17 12:18-19 Baadhi ya Wayunani Mazao mengi ya Huduma ya Yesu Baadhi ya Wayunani Yesu anazungumzia kifo Wanamtafuta Yesu ngano ya wazi wanamtafuta Yesu chake na hatimaye kuhitmisha katika utukufu 12:20-26 12:20-26 12:20-26 12:20-21 12:20-28a 12:22-26 12:27-28a Mwana wa mtu lazima Yesu anatabiri Yesu anazungumzia Ainuliwe juu kifo chake pale Kuhusu kifo chake Msalabani 12:27-36a 12:27-36 12:27-36a 12:27-28a 12:27-28b 12:27-28b 12:29 12:29-32 12:30-33 12:33-36a 12:34 12:35-36a Kutokuamini kwa Nani kaamini kutokuamini Wayahudi Taarifa zetu kwa watu 12:36b-43 12:36b-43 12:36b-38 12:36b Hitimisho: kutokuamini kwa Wayahudi 12:37-41 12:37-38 12:39-40 12:39-40 12:41 12:41 Tembea katika Nuru 12:42-43 12:42-50 Hukumu kwa maneno 12:42-50 Hukumu kwa maneno

Page 213: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

197

Ya Yesu Ya Yesu 12:44-50 12:44-50 12:44-50

MZUNGUKO WA TATU WA USOMAJI KUFUATILIA KUSUDIO LA ASILI LA MWANDISHI KATIKA NGAZI YA AYA Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwatafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Aya ya kwanza 2. Aya ya pili 3. Aya ya tatu 4. N.k

UTAMBUZI WA MUKTADHA MISTARI 1-50

A. Injili zote nne zinaweka kumbukumbu juu ya yule mwanamke kumpaka Yesu mafuta. Kwa hiyo, tukio hili lingechukua sehemu kubwa kwa waandishi wa injili. Hata hivyo, Marko 14:3-9, Mt. 26:6-13, na Yohana 12:2-8 zinamtambua kama Mariam wa mji wa Bethania, dadake Lazaro, wakati Luka 7:36-50 inamtambua kama mwanamke mwovu katika mji wa Galilaya.

B. Yohana 12 inaiongelea huduma ya wazi ya Yesu (kama vile Yohana 12:29). Amejaribu tena na tena

kuwaleta viongozi wa Kiyahudi kwenye imani. Yohana 11 inajaribu kuwaleta watu wa mji wa Yerusalemu kwenye imani.

C. Kuna makundi matano ya watu yaliyotajwa katika aya hii.

1. Kusanyiko la watu lililoshuhudia Lazaro akifufuka, Yohana 12:17 2. Kusanyiko la watu toka Yerusalemu, Yohana 12:9 3. Watu wa hija wakija kwenye Pasaka, Yohana 12:12,18,29,34 4. Yamkini kusanyiko la watu wa mataifa, Yohana 12:20 5. Yamkini kusanyiko la viongozi wa Kiyahudi walioamini katika Yeye, Yohana 12:42

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 12:1-8 1 Basi, siku sita kabla ya Pasaka, Yesu alifika Bethania, alipokuwapo Lazaro, yeye ambaye Yesu alimfufua katika wafu. 2 Basi wakamwandalia karamu huko; naye Martha akatumikia; na Lazaro alikuwa mmojawapo wa wale walioketi chakulani pamoja naye. 3 Basi Mariamu akatwaa ratli ya marhamu ya nardo safi yenye thamani nyingi, akampaka Yesu miguu, akamfuta miguu kwa nywele zake. Nayo nyumba pia ikajaa harufu ya marhamu. 4 Basi Yuda Iskariote, mmojawapo wa wanafunzi wake, ambaye ndiye atakaye kumsaliti, akasema, 5 Mbona marhamu hii haikuuzwa kwa dinari mia tatu, wakapewa maskini? 6 Naye aliyasema hayo, si kwa kuwahurumia maskini; bali kwa kuwa ni mwivi, naye ndiye aliyeshika mfuko, akavichukua vilivyotiwa humo. 7 Basi Yesu alisema, Mwache aiweke kwa siku ya maziko yangu. 8 Kwa maana maskini mnao sikuzote pamoja nanyi; bali mimi hamnami sikuzote.

Page 214: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

198

12:1 "siku sita kabla ya Pasaka" Huu ni utaratibu tofauti ulio katika mtiririko kutoka katika Mt. 26:2. Ni lazima ikumbukwe kwamba kiini hasa cha injili siyo utaratibu uliopangwa, bali ni matendo wakilishi ya Yesu ambayo yanaakisi ukweli na kazi zake. Injili siyo wasifu wa maisha ya mtu bali ni vijitabu vidogo vidogo vya kiinjili kwa kusudi la kuyalenga makundi. 12:2 "wakamwandalia" Hii inaonekana kumaanisha watu wa Bethania, waliompa Yesu chakula cha usiku akiwa na wanafunzi wake kwa heshima ya kumfufua Lazaro. Hata hivyo, katika, Mt. 26:6, jambo hili linafanyika nyumbani mwa Simoni Mkoma. 12:3 "ratli" Hili lilikuwa neno la Kilatini lililomaanisha Ratli ya Kirumi, iliyokuwa sawa na aunzi 12. Kitu hiki cha thamani baadaye kingekuja kuwa mahari katika harusi ya Mariamu. Wanawake wengi ambao hawakuelewa walivaa chombo cha aina hii kilichokuwa na marashi kwenye mashingo yao. NASB "marhamu ya nardo safi yenye thamani nyingi" NKJV "marhamu iliyotengenezwa kutokana na maua ya mti wa Valerian" NRSV "marhamu ya nardo safi yenye thamani nyingi" TEV "Painti nzima ya marashi ya gharama kubwa yaliyotokana na nardo halisi" NJB "chombo cha mafuta magumu ghali yaliyotokana na nardo halisi" Pamekuwa na ubahatishaji mkubwa kuhusu maana ya visifa hivi: (1) halisi; (2) kimiminika; au (3) jina la mahali. Marashi haya yalitokana na mzizi yenye harufu nzuri toka huko Himalaya yaliyokuwa ghali sana kununua. Tazama James M Freeman, Manners and Customs of the Bible, kur. 379-380.

◙ "akampaka Yesu miguu" Injili zingine zinazungumzia tukio hili (bila shaka ni shukurani ya Mariam kwa kumfufua Lazaro, Yohana 12:2) la mwanamke kumpaka yesu mafuta kichwani. Vivyo hivyo Mariam alimpaka mafuta mwili wote kuanzia kichwani kwenda mpaka miguuni pake. Sababu ni kwa nini miguu ya Yesu ilikuwa wazi ni kwamba alikuwa ameegemea kwa kiwiko cha mkono wake wa kushoto kwenye meza fupi. Hii ni mojawapo ya uhusika mara mbili wa Yohana. Kiungo hiki kilitumika kwa kuandaa mwili kwa maziko (kama vile Yohana 19:40). Mariamu angeweza kuwa ameelezwa zaidi ujumbe wa Yesu kuhusu ukaribu wa kifo kuliko wanafunzi walivyo elewa (kama vile Yohana 12:7). Tazama MADA MAALUMU: KUTIWA MAFUTA KATIKA BIBLIA (BDB 603) katika 11:2

◙ "Nayo nyumba pia ikajaa harufu ya marhamu" Ni kielelezo kiasi gani cha ushahidi wa macho (kihariri). Yohana wazi kabisa anakumbuka wakati huo! 12:4 "Yuda Iskariote" Neno "Iskariote" lina uwezekano wa asili mbili (1) Jiji la Yuda (Keriote kama vile Yosh. 15:25) au (2) neno kwa "kisu cha muuaji." Kwa waandishi wote wa injili Yohana ana maneno makali kuliko wote kuhusu Yuda (kama vile Yohana 12:6). Tazama nukuu kamili katika Yohana 6:70-71.

◙ "kumsaliti" Haya ni maoni mengine ya kiuwandishi. Neno hili kwa kawaida halina kidokezo hiki. Kiuhalisia linamaanisha “kukabidhi” au “kutoa” kwa maana ya kisheria au kukabidhi mtu mwingine kitu. Tazama nukuu katika Yohana 18:2. 12:5 "dinari mia tatu" Dinari ilikuwa ujira wa siku moja kwa askari au kibarua kwahiyo hii ilikuwa takribani ujira wa mwaka mzima. 12:6 Mstari huu ni maoni mengine ya kiuandishi. Yohana, zaidi ya wandishi wengine wa injili, anamlaumu Yuda. NASB, NKJV "sanduku la hela" NRSV "pochi ya kawaida"

Page 215: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

199

TEV "mfuko wa hela" NJB "mfuko wa hela wa kawaida” Neno hili linamaanisha "sanduku dogo." Lilitumika zamani na wanamziki kubebea tungo zao.

◙ "akavichukua vilivyotiwa humo" Neno la Kiyunani ni “kubeba” linatumika katika maana mbili tofauti: (1) alibeba sanduku lakini (2) Pia allinyakua vilivyokuwemo ndani ya sanduku. Maneno haya yanaweza kuwa yamejumuishwa kuonyesha kuwa kusudio la Yuda kwa maskini katika Yohana 12:5 lilikuwa hasa ni kisingizio kwa kuiba ili kujinufaisha. 12:7 Huu ni msitari wa kipekee. Ni wazi kuwa unahusianisha kitendo hiki cha kiungwana na kujitoa kwa utaratibu ule ule unafanyika katika maziko ya mtu (kama vile Yohana 19:40). Haya ni maneno mengine ya kinabii ya Yohana. 12:8 "Kwa maana maskini mnao sikuzote pamoja nanyi" Hii inahusiana na Kumb. 15:4,11. Hii siyo kauli ya kuwaumbua maskini bali ni msisitizo juu ya uwepo wa Yesu kama masihi (kama vile Yohana 12:35; 7:33; 9:4). Agano la Kale ni la pekee miongoni mwa fasihi za mashariki ya kale kuhusu haki na mamlaka ya kuwajali maskini.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 12:9-11 9

Basi watu wengi katika Wayahudi walipata kujua ya kuwa yeye yuko huko, nao wakaja, si kwa ajili yake Yesu tu, ila wamwone na Lazaro, ambaye Yesu alimfufua katika wafu. 10 Nao wakuu wa makuhani wakafanya shauri la kumwua Lazaro naye; 11 maana kwa ajili yake wengi katika Wayahudi walijitenga, wakamwamini

Yesu. 12:9 "watu wengi katika Wayahudi walipata kujua ya kuwa yeye yuko huko" Haya ni matumizi yasiyo ya kawaida ya neno “Wayahudi” katika Yohana 11:19, 45; 12:17,. Inaonekana kumaanisha watu wa mji wa Yerusalem waliokuwa marafiki wa Lazaro na walikuwa wamekwenda katika mazishi. 12:10 "Nao wakuu wa makuhani wakafanya shauri la kumwua Lazaro naye" Walitaka kuondoa ushahidi! Sababu zao zilikuwa hofu (kama vile Yohana 11:48) na wivu (kama vile Yohana 11:48; 12:11). Watakuwa walifikiri kuwa kitendo cha Yesu kufufua Lazaro lilikuwa tukio la pekee na nadra sana. Upofu na upendeleo wa viongozi wa Kiyahudi uliashilia giza la wanadamu hawa walioanguka.

12:11 Hii inahusisha kurudi nyuma hadi 1:45. Tazama Mada Maalum: Matumizi ya Yohana ya neno “kuamini” katika Yohana 2:23

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 12:12-19 12 Nayo siku ya pili yake watu wengi walioijia sikukuu walisikia ya kwamba Yesu anakuja Yerusalemu; 13 wakatwaa matawi ya mitende, wakatoka nje kwenda kumlaki, wakapiga makelele, Hosana! Ndiye mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli! 14 Naye Yesu alikuwa amepata mwana-punda, akampanda, kama vile iliyoandikwa, 15 Usiogope, binti Sayuni; tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwana-punda. 16 Mambo hayo wanafunzi wake hawakuyafahamu hapo kwanza; lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka ya kwamba ameandikiwa hayo, na ya kwamba walimtendea hayo. 17 Basi wakamshuhudia wale mkutano waliokuwapo pamoja naye alipomwita Lazaro kutoka kaburini, akamfufua. 18 Na kwa sababu hiyo mkutano walikwenda kumlaki, kwa kuwa wamesikia ya kwamba ameifanya ishara hiyo. 19 Basi Mafarisayo wakasemezana wao kwa wao, Mwaona kwamba hamfai neno lo lote; tazameni, ulimwengu umekwenda nyuma yake.

12:12-19 Hii ni tafsiri ya ushindi wa Yesu kuingia katika Yerusalemu (kama vile Mt. 21:1-11; Marko 11:1-11; Luka 19:29-38).

Page 216: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

200

12:12 "watu wengi walioijia sikukuu" Palikuwa na sikukuu tatu zilizohitajika kwa Wayahudi wa kiume (kama vile. Kut. 23:14-17; Mambo ya Walawi 23; Kumb. 16:16). Tumaini kubwa la Wayahudi katika maisha yao yote walioishi nje ya Palestina (Diaspora) lilikuwa ni kuhudhuria kwenye sherehe ya Yerusalemu. Kwa siku hizi zilizopangwa Yerusalemu ikajaa watu kutoka mara tatu hadi tano ya idadi ya kawaida ya watu. Fungu hili linaaksi idadi kubwa ya mahujaji waliojaa shauku walipomsikia Yesu na wakatamani kumwona (kama vile Yohana 11:56). 12:13 "matawi ya mitende" Hili ni fungu la maneno lisilo la kawaida la Wayunani juu ya matawi ya mitende. Wengine wanaamini kuwa wakati fulani mitende ilistawi katika miteremko ya milima ya mizeituni (yaani, Josephus), wakati wengine wanaamini yaliletwa kutoka Yeriko. Inaonekana kuwa yalikuwa ni alama ya ushindi (kama vile Ufu. 7:9). Yalitumika kila mwaka kwa matambiko ya sanduku la maagano (kama vile Law. 23:40) na passaka (utamaduni katika kipindi cha wafuasi wa kiongozi wa Kiyahudi aliyeitwa Maccabeas.

◙ "wakapiga makelele" Huu ni wakati usio timilifu unaowakilisha (1) kitendo kilichorudiwa katika wakati uliopita au (2) mwanzo wa kitendo kwa wakati uliopita.

◙ "Hosana" Neno hili linamanisha "okoa sasa"au "tafadhari okoa" (kama vile Zab. 118:25-26). Wakati wa matambiko ya pasaka uamsho wa Zaburi za kumsifu Mungu (kama vile Zab. 113-118) ulitokea wakati mahujaji walikuwa wakitembea kuelekea katika hekalu. Mengi ya matendo haya na maneno yalirudiwa kila mwaka wakati wa sikukuu ya pasaka. Lakini kwa mwaka huu walipata maana yao ya ndani kwa Yesu. Umati ulihisi jambo hili!. Mafarisayo walitambua hili.

◙ "Ndiye mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana” Hili ndilo haswa Yesu amekuwa akidai alitumwa Yeye pekee akimwakilisha YHWH. NASB "hata Mfalme wa Israeli" NKJV, NRSV, TEV, NJB "mfalme wa Israeli” Fungu hili la maneno halikuwa sehemu ya Zaburi, lakini iliongezwa na umati. Inaonekana kuwa ni rejea ya moja kwa moja kwa Yesu kama mfalme Masihi aliyeahidiwa katika 2 Samueli 7 (kama vile Yohana 1:49; 19:19). 12:14 "mwana-punda" Punda ndio walikuwa wanyama watiifu waliotumika kupandwa na jeshi katika Israeli (kama vile 1 Fal. 1:33,38,44). Ni mfalme tu alipanda na kuendesha punda, kwa hiyo ilikuwa ni muhimu sana Yesu alipanda juu ya punda ambaye alikuwa hajawahi kuendeshwa (kama vile Marko 11:2). 12:14-15 "kama vile iliyoandikwa" Hii ni kutoka Zek. 9:9. Mwana punda hazungumzia sio tu ufalme wa ki-Masihi lakini pia kuhusu unyenyekevu wa Yesu. Yesu hakuja kama mtu wa jeshi aliyeshinda kwa tegemeo la Wayahudi, bali mtumishi katika mateso katika Isaya 53 akiendeshwa juu ya mwana Punda.

12:16 "Mambo hayo wanafunzi wake hawakuyafahamu hapo kwanza" Huu ni ushahidi mwingine wa macho, maumivu katika fikra za Yohana. Ni dhima inayojirudia (kama vile Yohana 2:22; 10:6; 16:18; Marko 9:32; Luka 2:50; 9:45; 18:34). Ni baada ya kupaa mbinguni na siku ya Pentekoste ambavyo ndiyo macho yao ya kiroho yalifunguka wazi.

◙ "lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka" Hii ilikuwa mojawapo ya huduma za Roho Mtakatifu (kama vile Yohana 14:26 na 2:22). Mstari huu pia unaonyesha kuwa waandishi wa injili waliunda injili zao kutokana na uzoefu binafsi wa Kristo aliyefufuka. Mihitasari ya injili inamweka Yesu katika maendeleo ya kihistoria na kuficha utukufu wake mpaka mwishoni kabisa mwa shuguli zao za maonyesho au uwasilishaji. Lakini Yohana anaandika injili yake yote katika

Page 217: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

201

mwanga wa utukufu wa Masihi. Injili zinazoonyesha kumbukumbu za baadae na mahitaji ya imani kwa jamii ya watu waliovuviwa. Kwahiyo kuna aina mbili za uandishi wa historia (Waandishi wa Yesu na waandishi wa injili).

◙ "alipotukuzwa" Tazama nukuu katika Yohana 1:14. 12:17 Tazama MADA MAALUM: MASHUHUDA WA YESU katika Yohana 1:8. Mtazamo wa ndani wa mazingira, C. 12:19 "Basi Mafarisayo wakasemezana wao kwa wao" Hili ni tukio lingine linalotangulia la kinabii linalohusiana na (1) Wayahudi, Yohana 11:48; 12:11 na (2) Watu wa mataifa, Yohana 12:20-23. Inaashilia uandishi wa aina mbili wa kihistoria wa maisha ya Yesu na kanisa la kwanza.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 12:20-26 20 Palikuwa na Wayunani kadha wa kadha miongoni mwa watu waliokwea kwenda kuabudu kwenye sikukuu. 21 Basi hao walimwendea Filipo, mtu wa Bethsaida ya Galilaya, wakamwomba, wakisema, Bwana, sisi tunataka kumwona Yesu. 22 Filipo akaenda, akamwambia Andrea; kisha Andrea na Filipo wakamwambia Yesu. 23 Naye Yesu akawajibu, akasema, Saa imefika atukuzwe Mwana wa Adamu. 24 Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi. 25 Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza; naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalimisha hata uzima wa milele. 26 Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.

12:20 "Wayunani kadha wa kadha" Usemi huu ulitumika kwa maana ya watu wa mataifa, sio mahususi kwa makabila asilia ya Kiyunani.

◙ "miongoni mwa watu waliokwea kwenda kuabudu kwenye sikukuu" Njeo ya wakati uliopo inamaanisha walikuwa na mazoea ya kwenda katika sikukuu. Walikuwa ama (1) Waogopao Mungu au (2) watu waliokuwa wakibadili imani za watu katika lango. Wa kwanza walikuwa waamini wa siku zote waliokuwa wakiabudu katika Sinagogi na wa pili walikuwa ni wale waliobadilishwa kuwa katika imani ya Kiyahudi. 12:21 "tunataka kumwona" Hii ni tungo ya wakati uliopita usiotimilifu ukimaanisha (1) waliulizia tena na tena au (2) walianza kuulizia. Walitaka kupata mahojiano ya Yesu katika faragha. Ni wazi kuwa hili lilikuwa suala la mwisho la kinabii kabla ya kifo cha Yesu (kama vile Yohana 12:23). 12:22 Filipo (mpenda farasi) na Andrea (mwanaume) walikuwa ni Mitume wawili tu waliokuwa na majina ya Kiyunani. Pengine hii iliwezesha Wayunani hawa (yaani, Watu wa mataifa) kujiona kana kwamba wangeweza kuwasogelea. 12:23 "Saa imefika" Hii ni tungo ya wakati timilifu. Yohana daima alitumia neno “saa" kumaanisha kuangikwa na ufufuo kama matukio ya nyakati maalumu za ujumbe wa Yesu (kama vile Yohana 12:27; 13:1, 32; 17:1). Yesu alisema kuwa amekuja kwa ajili ya kondoo wa Israeli waliopotea (kama vile Mt. 15:24). Sasa ujumbe wake ulikuwa unawafikia watu wa mataifa!

◙ "Mwana wa Adamu" Haya ni maneno ya Kiaramu yaliyomaanisha tu "mwanadamu" (kama vile Zab 8:4; Ezek. 2:1). Hata hivyo linatumika katika Dan. 7:13 likiwa na nyongeza yenye maana nyingine ya Mungu. Hiki ni cheo alichojipa Yesu mwenyewe kinachounganisha asili yake ya mwanadamu na ya Mungu (kama vile 1 Yohana 4:1-3).

◙ "atukuzwe" Kifo cha Yesu siku zote kilimaanisha "Utukufu." Neno "utukufu" limetumika mara kadhaa katika mazingira yake (kama vile Yohana 12:28 [mara mbili]; 32, na 33). Linatumika daima kuonyesha kifo cha Yesu na ufufuo (kama vile Yohana 13:1,32; 17:1). Tazama nukuu katika Yohana 1:14.

Page 218: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

202

12:24 “Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa" Hii ni lugha ya tukio au maelezo kuhusu vitu vinavyotokea katika milango mitano ya fahamu. Punje moja inaweza kuzaa punje nyingi (kama vile Yohana 15:2,4,5,8,16; 1 Kor. 15:36). Kifo chake kiliwaleta watu wengi katika maisha ya kweli (kama vile Marko 10:45).

◙ "nawaambia" Kuna mfuatano wa sentensi shurutishi daraja la tatu katika mazingira haya zinazomaanisha matendo yenye nguvu (kama vile Yohana 12:24,26,32,47). 12:25 "Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza" Huu ni mchezo wa maneno ya Kiyunani psychē, yanayomaanisha umuhimu wa nafsi ya mtu au nguvu ya maisha (kama vile Mt. 10:39; 16:24-25; Marko 8:34-35; Luka 9:23-24). Mara tu mtu anapomwamini Kristo, anapewa uzima mpya. Uzima huu mpya ni zawadi kutoka kwa Mungu kwa ajilli ya huduma, sio kwa matumizi binafsi, waamini ni watumishi wa uzima mpya, tumewekwa huru kutokana na utumwa kwa dhambi na kuwa watumishi wa Mungu (kama vile Rum. 6:1-7:6). Wachungaji wa uongo katika Yohana 10 walijaribu "kuokoa" maisha yao kwa kukimbia lakini Yesu anaweka chini maisha yake, vivyo hivyo, yawapasa waamini kufanya kama alivyo fanya (kama vile 2 Kor. 5:12-15; Gal. 2:20).

◙ "ataiangamiza" Hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo. Neno (tazama Mada Maalum katika Yohana 10:10) linamaanisha “kuharibu," neno lingine lenye maana mbili tofauti hili ni tofauti na "uzima wa milele." Kama mtu hana imani katika Kristo, hii ndilo suluhisho pekee. Uaribifu huu sio angamizo bali ni kupoteza uhusiano binafsi na Mungu (ambacho ndicho kiini cha jehanamu).

◙ "aichukiaye" Hii ni nahau ya Kiebrania ya ulinganifu. Mungu lazima awe kipaumbele (kama vile Wake za Yakobo, Mwa. 29:30,31; Kumb. 21:15; Esau na Yakobo, Mal. 1:2-3; Warumi 10-13; familia ya mtu, Luka 14:26).

◙ "uzima" Hili ni neno la Kiyunani zoē. Linatumika kwa msimamo katika Yohana kumaanisha (1) maisha ya kiroho; (2) uzima wa milele; (3) uzima wa enzi mpya; na (4) ufufuo wa uzima. Maisha ya kweli ni yale yenye uhuru kutokana na udhalimu wa "nafsi,"ambao ndio kiini cha kuanguka. 12:26 "Tena" Hii ni sentensi shurutishi daraja la tatu inayomaanisha tendo lenye nguvu.

◙ "na anifuate" Hii ni kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopo ambapo inazungumzia uhusiano unaoendelea (kama vile Yohana 15). Hili ni suala la kibiblia lililloachwa linalohusu kusitahimili (tazama MADA MAALUM: HITAJI LA USTAHIMILIVU katika Yohana 8:31). Suala hili daima linachanganya kutokana na mvutano wa kithiolojia kati ya Mungu mkuu na ridhaa ya mwanadamu. Hata hivyo ni vizuri zaidi kuona wokovu na uzoefu wa agano. Mungu daima anaanzisha (kama vile Yohana 6:44, 65) na kuweka agenda ya kuzungumza lakini pia hudai kuwa mwanadamu aitikie kwa kupokea kitu alichokitoa kwa kufanya toba na imani (kama vile Marko 1:15; Matendo 20:21), yote mawili kama uamzi wa awali na uwanafunzi wa kudumu . Usitahimilifu ni ushahidi kuwa tunamjua yeye (kama vile Mt. 10:22; 13:20-21; Gal. 6:9; 1 Yohana 2:19; Ufu. 2:7,11,17,26; 3:5,12,21). Mafundisho ya Kikristo, yakiwa katika msingi wa kibiblia, daima yanakuwa kimafumbo, katika jozi zenye mvutano. Fasihi za mashariki zinaainishwa na methali hizi, utofauti uliopo katika mpangilio. Mara nyingi wasomaji wa kisasa wa magharibi wanalazimisha utata huu kuwa ama chaguzi wakati wanamaanisha kuwa Yote mawili ni ukweli. Ili kuelezea maoni yangu kwa mifano nimejumuisha sehemu kutoka katika semina yangu ya kutoka katika Biblia iitwayo utata wa kibiblia: Utata wa Kibiblia

1. Mtazamo huu umekuwa wa msaada mkubwa kwangu binafsi kama mtu ambaye anapendwa na kuamini Biblia kama neno la Mungu. Katika kujaribu kuichukulia biblia kwa mtazamo makini ikaonekana wazi kuwa maandiko tofauti yanayobainisha ukweli katika baadhi ya njia, na siyo mfumo mzima wa njia. Andiko moja lililovuviwa haliwezi kufuta andiko lingine lililovuviwa! Ukweli unapatikana katika kulijua somo lote la Biblia (ni biblia yote na sio sehemu tu zimevuviwa, kama vile 2 Tim. 3:16-17), sio kunukuu habari moja (kuthibitisha andiko)!

Page 219: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

203

2. Ukweli mwingi wa kibiblia (fasihi ya mashariki) umewasilishwa katika upembuzi wa ukweli au jozi zenye utata (kumbuka waandishi wa Agano Jipya isipokuwa luka, ni Waebrania wenye fikra walioandika katika Kiyunani). fasihi za hekima na fasihi za kimashairi zinatoa ukweli katika mistari inayofanana. Ufanano ulio kinyume unatenda kazi kama fumbo. Maneno ambatani yanafanya kazi kama aya zinazofanana. Kiasi fulani zote zina ukweli ulio sawa! Hali hizi za utata zinaumiza kwa utamaduni wetu mzuri! a. Majaaliwa dhidi ya utashi huru wa mwanadamu b. Usalama wa waamini dhidi ya hitaji la ustahimilivu c. Dhambi ya asili dhidi ya dhambi ya hiari d. Yesu kama Mungu dhidi ya Yesu kama Mwanadamu e. Yesu aliye sawa na Baba dhidi ya Yesu kama mtumishi wa Baba f. Biblia kama neno la Mungu dhidi ya umiliki wa mwanadamu g. Kutotenda dhambi (ukamilifu, kama vile Warumi 6) dhidi ya kutenda dhambi kidogo h. Kuhesabiwa haki na utakaso wa awali dhidi ya utakaso endelevu i. Kuhesabiwa haki kwa imani (Warumi 4) dhidi ya kuhesabiwa haki kwa matendo (kama vile Yakobo

2:14-26) j. Uhuru wa Mkristo (kama vile Rum. 14:1-23; 1 Kor. 8:1-13; 10:23-33) dhidi ya wajibu wa Mkristo

(kama vile Gal. 5:16-21; Efe. 4:1) k. Uwezo wa Mungu kupita wote dhidi ya uwepo wake mahali popote l. Kutojulikana kwa Mungu dhidi ya kujulikana kwake katika maandiko na maneno mbadala mbalimbali

kwa wokovu ya Paulo (1) Urithi (2) Utakaso (3) Kuhesabiwa haki (4) Ukombozi (5) kupewa utukufu (6) Kuamuliwa kabla/majaaliwa (7) Maelewano

m. uwepo wa ufalme wa Mungu dhidi ya ukamilisho wa siku zijazo n. Toba kama zawadi ya Mungu dhidi ya toba kama mwitikio wa lazima kwa wokovu (kama vile Marko

1:15; Matendo 20:21) o. Agano la Kale kama kitu cha kudumu dhidi ya Agano la Kale lililopita na isiyo na kitu chochote (kama

vile Mt. 5:17-19 dhidi ya Mt. 5:21-48; Warumi 7 dhidi ya. Wagalatia 3) p. Waamini ni watumishi/watumwa au wana/warithi "

◙ "nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo" dhamira hii inarudiwa katika Yohana 14:3; 17:24; 2 Kor. 5:8; Flp. 1:23; 1 The. 4:17! Ukristo kimsingi ni uhusiano wa Mtu binafsi na Mungu! Lengo ni uhusiano, uwepo wake, na ushirikiano wake! Tuliumbwa ili kuwa na Mungu (kama vile Mwa. 1:26-27). Wokovu ni urejesho wa ushirika ule wa bustani ya Edeni uliovunjika. Yohana anasisitiza kuwa ushirika huu umerejeshwa sasa!

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 12:27-36a 27 Sasa roho yangu imefadhaika; nami nisemeje? Baba, uniokoe katika saa hii? Lakini ni kwa ajili ya hayo nilivyoifikia saa hii. 28 Baba, ulitukuze jina lako. Basi ikaja sauti kutoka mbinguni, Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena. 29 Basi mkutano uliosimama karibu wakasikia, walisema ya kwamba kumekuwa ngurumo; wengine walisema, Malaika amesema naye. 30 Yesu akajibu, akasema, Sauti hiyo haikuwako kwa ajili yangu, bali kwa ajili yenu. 31 Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo; sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje. 32 Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu. 33 Aliyanena hayo akionyesha ni mauti gani atakayokufa. 34 Basi mkutano wakamjibu, Sisi tumesikia katika torati ya kwamba Kristo adumu hata milele; nawe wasemaje ya kwamba imempasa Mwana wa Adamu kuinuliwa? Huyu Mwana wa Adamu ni nani? 35 Basi Yesu akawaambia, Nuru ingaliko pamoja nanyi muda kidogo. Enendeni maadamu mnayo nuru hiyo, giza lisije likawaweza; maana aendaye gizani hajui aendako. 36 Maadamu mnayo nuru, iaminini nuru

Page 220: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

204

hiyo, ili mpate kuwa wana wa nuru.

12:27 "Sasa roho yangu imefadhaika" Hii ni kauli timilifu tendewa elekezi. Wakala (Baba, Shetani, mazingira n.k) ni neno la nguvu llinalotumika katika njia tofauti katika Agano Jipya.

a. Hofu ya Herode (Mt. 2:3) b. Hofu ya wanafunzi (Mt. 14:26) c. Shauku ya Yesu ambayo haijatulizwa (Yohana 12:27; 13:21; pia nukuu

katika Mt. 26:38; Marko 14:34) d. Kanisa katika Yerusalemu (Mdo. 15:24) e. Kuvunjwa kwa kanisa la uongo katika Galatia (Gal. 1:7)

Hii ilikuwa njia ya Yohana ya kuhusisha shughuli za Yesu kwa Wanadamu na ujio wa maumivu katika kuangikwa msalabani (kama vile Marko 14:32 na kuendelea). Yohana hana kumbukumbu ya maumivu makubwa ya Yesu pale Gethsemane, lakini hili ni tukio lile lile.

◙ "uniokoe katika saa hii" Pana mjadala mrefu kuhusiana na maana halisi ya maneno haya. Je hili ni ombi (yaani, Mt. 26:39)? Je hili ni jibu la kushangaza kuhusu kipi hakipaswi kufanyika (NET Biblia ya NET)?

◙ "Lakini ni kwa ajili ya hayo nilivyoifikia saa hii" Maisha ya Yesu yalifunguka kufuatana na mpango wa Mungu (kama vile Luka 22:22; Mdo. 2:23; 3:18; 4:28) ambao Yesu aliuelewa kikamilifu (kama vile Mt. 20:28; Marko 10:45). 12:28 "ulitukuze jina lako" Baba anaitikia katika Yohana 12:28b. Neno hili "utukufu" ni dhaifu laweza kubadilika. Linaweza kumaanisha

1. Utukufu aliokuwepo kabla (kama vile Yohana 17:5) 2. Ufufuo wa Yesu wa Baba (kama vile Yohana 17:4) 3. Kuangikwa kwa Yesu msalabani na kufufuka (kama vile Yohana 17:1)

Tazama nukuu katika Yohana 1:14.

◙ "ikaja sauti kutoka mbinguni" Viongozi wa dini ya Kiyahudi waliita hii a bath-kol. Tangu nyakati za Malaki

hapajawepo sauti ya kinabii katika Israeli. Kama mapenzi ya Mungu yalikuwa yathibitike, yangethibitika kwa sauti kutoka mbinguni. Injili zina kumbukumbu kuwa Mungu alizungumza mara tatu katika kipindi cha maisha ya Yesu.

1. Katika ubatizo wa Yesu, Mt. 3:17 2. Katika mabadiliko, Mt. 17:5 3. Hapa katika msitari huu

12:29 "Basi mkutano uliosimama karibu wakasikia, walisema" Kuna tafsiri mbili kuhusu kilichotokea: (1) ilikuwa radi. Hii ilitumika na Mungu wakati anazungumza katika Agano la Kale (kama vile 2 Sam. 22:14; Ayubu 37:4; Zab. 29:3; 18:13; 104:7) au (2) Malaika akasema nae. Huu ni sawa na mkanganyiko kuhusu uzoefu wa sauli katika Matendo 9:7; 22:9.

12:30 "Yesu akajibu, akasema Sauti hiyo haikuwako kwa ajili yangu, bali kwa ajili yenu" usemi huu ni wa ulinganifu wa kisemitiki. Hii ina maana kuwa haikuwa kwa ajili ya wao tu bali kimsingi kwa ajili ya yao (kama vile Yohana 11:42). 12:31 "Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo" Huu ni muundo wa sentensi ulio sambamba na fungu lifuatalo ("Mtawala wa ulimwengu huu atatupwa nje"). Muda ambao hili lilitokea haufahamiki vyema (tazama Mada Maalumu ifuatayo). Kwa hakika nakubaliana na F. F. Bruce, Answers to Questions (uk. 198), kuwa Yohana 12:31 ni mfano mwingine ambao C. H. Dodd ulioitwa "mambo yajayo yaliyotambuliwa." Kwa Yohana Yesu amekwisha leta vyote

Page 221: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

205

wokovu kwa wanaoamini na hukumu kwa wasioamini kwa maana hiyo ni sawa na kusanifu kusema "Utimilifu wa kinabii." Kile kijacho kina uhakika kuwa kinaelezewa kana kwamba tayari kimetokea!

◙ "sasa mkuu wa ulimwengu huu" Hii inamaanisha nguvu ya uovu wa mtu mwenyewe (kama vile Yohana 14:30; 16:11) ijulikanayo katika Waebrania "Shetani " au "adui" (kama vile Job 1-2) au kwa Kiyunani "ibilisi" au "mzushi" (kama ville Mt. 4:1,5,8,11; 13:39; 25:41; Yohana 6:70; 8:44; 13:2; 2 Kor. 4:4; Efe. 2:2). Majina haya mawili yanafanana katika Mt. 4:1-11 na Yohana 13:2,27. Atatupwa nje kutoka mbinguni ili asiendelee kuwatia hatiani/kuwafanya wafuasi wa Yesu kutenda maovu.

MADA MAALUMU: UOVU BINAFSI

I. SOMO KUHUSU SHETANI NI GUMU SANA

A. Agano la Kale halibainishi adui mkubwa wa (Mungu), bali mtumishi wa YHWH ambaye anawapa wanadamu mbadala na kutuhumu huyu mwanadamu kwa kutokuwa na haki (A. B. Davidson,

A Theology of the OT, kur. 300-306). B. Dhana ya adui mkubwa wa Mungu ulianza wakati wa fasili kati ya Biblia (zisizo na taratibu za

kikanisa) katika kipindi cha dini ya kiislamu iliyoanzishwa na Zoroaster huko Uajemi. Hii kwa namna nyingine, kwa kiwango kikubwa ilisababisha sheria ya dini ya Kiyahudi (yaani, waliokuwa wametengwa na kuishi nje ya Israel yaani Babiloni, na Persia).

C. Agano Jipya linaunda dharura ya Agano la Kale katika ugumu wa ajabu lakini makundi yaliyochaguliwa Kama mtu anaanza kusoma habari za uovu katika mtizamo wa thiolojia ya biblia (kila kitabu au mwandishi au michoro alisoma na kuandika kwa kifupi kwa kutenganisha) basi mawazo mbalimbali kuhusu uovu yangeibuliwa. Hata hivyo, mtu ataanza kusoma kuhusu uovu lakini kwa njia isiyo ya kibiblia au nje zaidi ya biblia mfano dini za kiulimwengu au dini za mashariki, basi sehemu kubwa ya mambo mengi ya maendeleo ya agano jipya yalionyeshwa katika pande mbili za uajemi na tabia za uyunani na kiroma. Kama mtu alidhaniwa kujitoa kwa uwezo wa kiungu neno la Mungu (lama nilivyo!), kwa hiyo mambo ya Agano Jipya lazima yaonekane kama ufunuo endelevu. Wakristo yawapasa wajilinde dhidi ya kuruhusu simulizi za Kiyahudi au fasihi za Kiingereza (yaani, Dante, Milton) kufafanua zaidi dhana hiyo bila shaka miujiza na maana tofauti tofauti katika eneo hili la wokovu. Mungu amechagua kutobainisha mambo yote ya uovu, asili yake (tazama Mada Maalumu: Lusifa), kusudi lake,lakini amebainisha kushindwa kwake!

II. SHETANI KATIKA AGANO LA KALE

Katika Agano la kale neno "Shetani" (BDB 966, KB 1317) au "mshitaki" linaonekana kuhusiana na makundi matatu tofauti.

A. Washtaki wa wanadamu (1 Sam. 29:4; 2 Sam. 19:22; 1 Fal. 5:4, 11:14,23,25; Zab. 109:6,20,29 B. Washtaki wa kimalaika (Hes. 22:22-23; Zak. 3:1)

1. Malaika wa Bwana – Hes. 22:22-23 2. Shetani – 1 Nya. 21:1; Ayubu 1-2; Zak. 3:1

C. Washtaki wa kimapepo (bila shaka shetani) (1 Fal. 22:21; Zak. 13:2) Baadaye katika kipindi cha kuingia agano jipya ibilisi wa Mwanzo 3 alijulikana ni shetani (kama vile.Kitabu cha Hekima 2:23-24; II Enoch 31:3), na hata baadaye ambapo anakuja kuwa chaguo la viongozi wa kidini wa Uyahudi (kama vile. Sot 9b na Sanh. 29a). "wana wa Mungu" wa Mwanzo 6 wanakuwa malaika wa uovu katika I Enoch 54:6. Wanakuwa waanzilishi wa uovu katika thiolojia ya viongozi wa kidini wa Kiyahudi. Nalitaja hili sio kwa kuonyesha usahihi wake wa kithiolojia, bali kuonyesha maendeleo yake katika Agano Jipya, shuguli hizi za Agano la Kale zinachangia katika uovu wa malaika wa nuru (yaani shetani,)katika 2 Kor. 11:3; Ufu. 12:9. Asili ya uovu wa yule aliyejigeuza kuwa malaika wa nuru ni mgumu au haiwezekani (kutegemea

Page 222: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

206

maoni yako) kuupima toka katika Agano la Kale. Sababu moja wapo ni ile imani ya nguvu juu ya uwepo wa Mungu mmoja tu. (kama vile. Kumb. 6:4-6; 1 Fal. 22:20-22; Mhu. 7:14; Isa. 45:7; Amos 3:6). Majeruhi wote walipelekea YHWH kuonyesha kwa vitendo alivyo wa pekee na mkuu (kama vile. Isa. 43:11; 44:6,8,24; 45:5-6,14,18,21,22). Uwezekano wa vyanzo vya habari ni (1) Ayubu 1-2, ambapo shetani ni mojawapo wa wana wa Mungu "mwana wa Mungu" (yaani, malaika) au (2) Isaya 14; Ezekieli 28, ambapo ujivuni karibu na wafalme wa mashariki (Babiloni na Uturuki) wamekuwa wakielezea sifa au ujivuni wa shetani (kama vile 1 Tim. 3:6). Nimechanganya mihemko kuhusu kuliendea suala hili. Ezekieli anatumia bustani ya Edeni kama neno mbadala sio tu kwa mfalme wa Uturuki kama shetani (kama vile. Ezek. 28:12-16), lakini pia kwa ufalme wa Misri kama mti wa maarifa wa mema na mabaya (Ezekieli 31). Hata hivyo, Isaya 14, hasa kurasa 12-14, anaonekana kuelezea uasi wa malaika kupitia majivuno kama Mungu alivyotaka kubainisha kwetu jinsi alivyo hasa na asili ya shetani hii ni njia isiyo elezea moja kwa moja na mahali pa kuifanya (tazama Mada Mada Maalumu: Lusifa). Lazima tujilinde dhidi ya mwenendo wa Theolojia wa kuchukua sehemu ndogo ndogo, tata toka kwenye maeneo yenye maana mbalimbali ya waandishi, vitabu, na kuviunganisha kama vipande vipande vya fumbo la Kiungu.

III. SHETANI KATIKA AGANO JIPYA

Alfred Edersheim (The Life and Times of Jesus the Messiah, juzuu. 2, kiambatisho XIII [kur.. 748-763] na XVI [kur. 770-776]) anasema mafundisho ya sheria za Kiyahudi yameathiriwa wazi kabisa na umiliki wa pande mbili za Uajemi na mtizamo wa kimapepo. viongozi hawa wa kidini sio vyanzo vizuri vya ukweli katika eneo. Yesu kimsingi anakwepa kutoka kwenye mafundisho ya sinagogi. Nafikiri kuwa dhana ya viongozi wa dini ya kiyahudi ya upatanisho wa kimalaika (kama vile.Matendo 7:53) na upinzani katika kutoa sheria za Musa kwenye mlima Sinai ilifungua mlango kwa dhana ya adui mkuu wa YHWH kadhalika na mwanadamu. Palikuwa na Mungu wawili wa pande mbili za Iran (ufuasi wa Zoroaster).

1. Ahura Mazda, baadaye akaitwa Ohrmazd, aliyekuwa mungu muumbaji, mungu mwema 2. Angra Mainyu,baadaye aliitwa Ahriman,roho aangamizaye, mungu mwovu,

Vita juu ya ukuu na dunia ikawa kama uwanja wa vita. Umiliki wa pande mbili ukajengeka ndani ya pande mbili za Kiyahudi zenye ukomo kati ya YHWH na shetani. Hakika kuna mafunuo endelevu katika agano Jipya kama ilivyo kwenye uovu, lakini sio kama ilivyoelezewa kama walimu wa dini ya Kiyahudi wanavyodai. Mfano mzuri wa utofauti huu ni "vita vya mbinguni." Kuanguka kwa shetani (Mwovu) ni mantiki yenye umuhimu, lakini sehemu husika haikutolewa (Tazama Mada Maalumu: Kuanguka kwa shetani na malaika wake). Hata hivyo kile kilichotolewa kimefichika kwenye mafunuo tanzu (k.v. Ufu. 12:4,7,12-13). Ingawa shetani ameshindwa na kutupwa duniani, bado anatenda kazi kama mtumishi wa YHWH (kama vile. Mt. 4:1; Luka 22:31-32; 1 Kor. 5:5; 1 Tim. 1:20). Lazima tuthibiti kiu yetu katika eneo hili. Kuna nguvu binafsi ya majaribu na uovu lakini bado kuna Mungu mmoja tu na mwanadamu bado anawajibika kwa uchaguzi wake. Kuna vita ya kiroho kabla na baada ya wokovu. Ushindi wawezakuja tu na kubakia ndani na kupitia Mungu wa Utatu. Uovu umekwisha shindwa na utaondolewa (kama vile. Ufu. 20:10)!

◙ "atatupwa nje" Hii ni kauli tendewa elekezi ya wakati ujao. Andiko halionyeshi muda maalumu ambao shetani ataanguka toka mbinguni. Shetani anaweza jadiliwa katika kitabu cha Isaya 14 na Ezekieli 28 kwa maana ya mara ya pili. Habari za kinabii zinashughulika na Wafalme wajivuni wa Babeli na Tiro. Mambo yao ya ovyo ya dhambi yanamaanisha ni ya shetani (kama vile Isa. 14:12,15; Ezek. 28:16). Hata hivyo Yesu anasema alimwona shetani akianguka wakati wa safari ya kupeleka ujumbe wa sabini (kama vile Luka 10:18). Kuna mazungumzo yanayoendelea ya shetani katika Agano la Kale lote. Kwa asili alikuwa malaika mtumishi wa Mungu, lakini kwa majivuno na majidai au kiburi chake, akawa ni adui wa Mungu. Mjadala mzuri wa somo la mabishano haya umo katika A. B. Davidson's Old Testament Theology kur. 300-306.

Page 223: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

207

MADA MAALUMU:VITA HUKO MBINGUNI (toka ufunuo 12:7-9)

Pamekuwapo na mjadala mrefu kuhusu tarehe ya makabiliano haya. Yesu anaonekana akitaja vita hii katika Luka 10:18 na Yohana 12:31. Lakini kwa kujaribu kuweka utaratibu wa mtiririko mzuri wa tarehe kuhusu tukio ni vigumu kabisa:

1. kabla ya Mwanzo 1:1 (kabla ya uumbaji) 2. katikati ya Mwanzo 1:1 na 1:2 (nadhari ya nafasi) 3. katika Agano la Kale baada ya Ayubu 1-2 (Shetani mbinguni) 4. katika Agano la Kale kabla 1 Fal. 22:21 (Shetani katika baraza la mbinguni) 5. katika Agano la Kale baada ya Zakaria 3 (Shetani mbinguni ) 6. katika Agano la Kale baada ya Isa. 14:12; Ezek. 28:15 na II Enoch 29:4-5 (Wafalme waanzilishi

walilaumiwa) 7. katika Agano Jipya baada ya majaribu ya Yesu (kama vile. Mathayo 4) 8. katika Agano Jipya wakati wa ujmbe wa sabini (niliona shetani akianguka toka mbinguni, kama vile.

Luka 10:18) 9. katika Agano Jipya baada ya ushindi wa Yesu kuingia katika Yerusalem (mtawala wa ulimwengu huu

anatupwa, kama vile.Yohana 12:31) 10. katika Agano Jipya baada ya ufufuo na kupaa mbinguni (kama vile. Efe. 4:8; Kol. 2:15) 11. wakati wa saa ya mwisho (kama vile. Ufu. 12:7, bila shaka kama tunapaswa kuiona tu kama vita ya

milele kati ya Mungu na mwenyeji wa maovu) kiurahisi tunapaswa kuvitazama kama vita vya ndani kati ya Mungu na wamiliki wa uovu; mtafaruku huu unakwenda kutimilizwa katika kushindwa kwa yule joka na wafuasi wake. Katika ufunuo 20 wameondolewa na kutengwa! Angalia Mada Maalumu:Kuanguka kwa Shetani na Malaika zake (Uf. 12:4)

12:32 “Nami nikiinuliwa juu" Hii ni sentensi shurutishi daraja tatu inayomaanisha juu ya kitendo muhimu chenye uwezekano wa kufanyika. neno hili linaweza kumaanisha

1. kuinuliwa juu (kama vile Yohana 3:14) 2. kuangikwa (kama vile Yohana 8:28) 3. kuinuliwa (kama vile Matendo 2:33; 5:31) 4. Kuinuliwa juu zaidi (kama vile Flp. 2:9)

Kwa fikra za kawaida fungu hili (kama ilivyo zaidi katika Yohana).

◙ "nitawavuta wote kwangu" Hili laweza kuwa ni dokezo kwa upendo wa agano wa Mungu kwa Israeli katika

Yer.31:3 ambao, ni aya juu ya “agano jipya”(kama vile Yer. 31:31-34). Mungu anawatafuta watu wake kwa upendo na kutenda kwa ajili yao. Utumiaji ule ule wa ki-sitiari katika neno hili unapatikana Yohana 6:44 na kuelezewa katika Yohana 6:65. Hapa “wote” ni mwaliko wa kila mmoja na ahadi ya ukombozi (kama vile Mwa. 3:15; 12:3; Kut. 19:5; Isa. 2:2-4; Yohana 1:9,12,29; 3:16; 4:42; 10:16; 1 Timotheo 2:4; 4:10; Tito 2:11; 2 Pet. 3:9; 1 Yohana 2:2; 4:14)! Kuna utofauti wenye muhimu katika kifungu hiki. Neno “wote” laweza kuwa ni “jinsia ya kiume, ambalo laweza kutafasiliwa “wanaume wote” na linapatikana katika machapishi ya kale ya Kiyunani P75 (VID), אi2, B, L, na W, wakati lile lisilo na upande, ambalo laweza kutafasiliwa “vitu vyote” linapatikana katika P66 na א. Ikiwa litakuwa ndio lile lisilo na upande lingaliweza kuongelea juu ya ukombozi wa ulimwengu mzima wa Kristo unaofanana na Kol. 1:16-17, ambao yumkini ungaliaksi pande mbili za imani potofu za mafundisho yaliyo dhahiri katika 1 John. Toleo la UBS4 linaipa jinsia ya kiume alama "B" angalau yenye uhakika). 12:33 "Aliyanena hayo akionyesha ni mauti gani atakayokufa” Haya pia bado ni maoni mengine ya mwandishi kutoka kwa Yohana.Hii inahusiana na Kumb 21:23 ambapo kuangikwa juu ya msalaba ilichukuliwa kama “umelaaniwa na Mungu.” Hiyo ndiyo sababu viongozi wa kidini walitaka Yesu aangikwe msalabani na siyo kupigwa mawe (kama vile Gal. 3:13).

Page 224: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

208

12:34 "mkutano wakamjibu…kristo adumu hata milele" Hii inawezekana ni hisia katika Zab. 89:4,29,35-37. Agano la Kale lilitegemea ujio mmoja wa Masihi na kuanzisha kwake kwa utawala wa Palestina wa ulimwengu wa amani(kama vile Zab. 110:4; Isa. 9:7; Ezek. 37:25 na Dan. 7:14). Kwa "milele” tazama Mada Maalum: Milele katika Yohana 6:58

◙ "Mwana wa Adamu" Makutano (tazama mtazamo wa kimazingira, C) utakuwa umemsikia Yesu akifundisha na /kuhubiri (bila shaka katika Yohana 12:23-24 kwa ajili ya wadhifa na Yohana 12:30-32 kwa ajili ya kitenzi “kuinuliwa”) kwa sababu wanatumia cheo chake cha kipekee alichojipa. Hapa ndipo mahali pekee kinapotumiwa na wengine. Hakikuwa kipimo cha wadhifa au usanifu wa ki-Masihi ndani ya dini za Kiyahudi. 12:35 "Enendeni maadamu mnayo nuru hiyo" Yesu anawahimiza wasikilizaji wake kuitikia haraka kwenye maneno yake. Muda wake katika dunia hii ulikuwa umepungua. Ilikuwa ni wiki yake ya mwisho kuwepo hapa duniani. Saa yake iliyopangwa kabla ilikuwa imewadia (Yohana 12:23). Kwa maana hiki kifungu (kama vilivyo vingi katika Yohana) ina kumbukumbu za kihistoria na kumbukumbu za kuwepo. Kile Yesu alichosema ni kweli kwa kila mmoja wetu aliyesikia injili (yaani, mfano wa udongo). Hii ni maana mbadala ya utumiaji wa neno “tembea” kama mtindo wa maisha (k.v. Efe. 4:1,17; 5:2,15). Hii kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopo, inayoendeleza msisitizo wa Yesu juu ya kuamini kama mwendelezo wa uhusiano na wanafunzi, na sio maamuzi ya awali (kama vile Yoh. 12:44-46). 12:36 Dhamira ya Yesu kama nuru ya ulimwengu ilikuwa ni jambo la msisitizo lililojirudia katika Yohana (kama vile Yohana 1:4,5,7,8,9; 3:19,20,21; 5:35; 8:12; 9:5; 11:9,10;12:35,36,46). Giza na nuru zilikuwa ni kweli za kiroho zilizopingana katika fasihi za Kiyahudi na Magombo ya Bahari ya Chumvi.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 12:36b-43 36bHayo aliyasema Yesu, akaenda zake, akajificha wasimwone. 37 Walakini ajapokuwa amefanya ishara nyingi namna hiyo mbele yao, hawakumwamini; 38 ili litimie lile neno la nabii Isaya alilolisema, Bwana, ni nani aliyezisadiki habari zetu; Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani? 39 Ndiyo sababu wao hawakuweza kusadiki; kwa maana Isaya alisema tena, 40 Amewapofusha macho, Ameifanya mizito mioyo yao; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakafahamu kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya. 41 Maneno hayo aliyasema Isaya, kwa kuwa aliuona utukufu wake, akataja habari zake. 42 Walakini hata katika wakuu walikuwamo wengi waliomwamini; lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakumkiri, wasije wakatengwa na

sinagogi. 43 Kwa maana walipenda utukufu wa wanadamu kuliko utukufu wa Mungu. 12:37 Ni maoni ya kusikitisha kiasi gani. Upofu wa kiroho ni jambo la kutisha (kama vile 2 Kor. 4:4). Fungu hili linaonyesha dhambi isiyosameheka (tazama Mada maalum katika Yohana 5:21). 12:38 "neno la nabii Isaya" Hii imenukuliwa kutoka katika habari kuhusu mtumishi mwenye mateso katika Isaya. 53:1. 12:39-40 Hii ni mistari migumu.Je Mungu anawafanya watu kuwa sugu kiasi kwamba hawawezi kuitikia? Nimeingiza maoni yangu kutoka katika 6:9-10 na Warumi 11:7 (Tazama www.freebiblecommentary.mobi).

Isaya 6:9-10 kwa kuwa YHWH anabainisha kusudi lake kwa huduma ya Isaya, Pia anabainisha kwa mwitikio wa ujumbe wake kwa Yuda.

1. nenda, Isaya 6:9, BDB 229, KB , Qal kauli shurutishi 2. sema, Isaya 6:9, BDB 55, KB , Qal kauli timilifu 3. endelea kusikiliza, Isaya 6:9, Qal kauli shurutishi na Qal kitenzijina huru cha BDB 1033, KB 1570 4. Lakini usitambue, Isaya 6:9, BDB 106, KB 122, Qal isiyo timilifu inatumika kwa maana ya kuamuru,

kama vile. Isa. 1:3; 5:21; 10:13; 29:14 5. Endelea kuangalia, Qal shurutishi na Qal kitenzijina huru cha BDB 906, KB 1157

Page 225: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

209

6. Lakini usielewe, Isaya 6:9, BDB 393, KB 380, Qal isiyotimilifu inatumika katika maana ya kuamuru 7. Fanya mioyo ya watu hawa kutojali (fas. "nono"), Isaya 6:10, BDB 1031, KB 1566, Hiphil shurutishi 8. masikio yazubae yasisikie, Isaya 6:10, BDB 457, KB 455, Hiphil shurutishi 9. na macho yao yakose mwanga, Isaya 6:10, BDB 1044, KB 1612, Hiphil shurutishi

Hizi kauli shurutishi zinafuatiwa na mtiririko (zisizo timilifu tatu za vitenzi vilivyo tumika wakati uliopita, "ona," "sikia," na "tambua"). Mungu anajua (ama kwa maarifa yake ya awali au kwa kufanya mioyo yao kuwa migumu ambayo tiyari ilikuwa imenyooka na fikra zao kuwa hawatapokea na kuokolewa.

1. Endapo watatubu, BDB 996, KB 1427, Qal kauli timilifu kanushi 2. Endapo wataponywa, BDB 950, KB 1272, Qal kauli timilifu kanushi

Isaya atahubiri na ingawa wengine wataitikia wengi wa watu wake au jamii yake hawatapokea (kama vile. Rum. 1:24,26,28; Efe. 4:19) au hawataitikia (kama vile Isa. 29:9, 10; Kumb. 29:4; Mt. 13:13; Rum. 11:8)! Isaya sio mwinjilisti hapa lakini ni nabii wa kutotii matokeo ya jambo husika (kama vile Mt. 13:13; Marko 4:12; Luka 8:10). Ujumbe wake wa matumaini ni kwa siku ijayo, sio siku yake! Warumi 11:7 "waliobaki wote walipumbazwa" Hii ni kauli tendewa elekezi ya wakati uliopita usiotimilifu (kama vile 2 Kor. 3:14). Kinachomaanishwa ni kwamba Mungu aliwapumbaza (kama vile Rum. 11:8-10). Wakala wa kuwapumbaza ni uovu wao (kama vile 2 Kor. 4:4). "kupumbazwa" (pōroō) ni neno la uganga linalomaanisha ugumu au upofu (kama vile Rum. 11:25; 2 Kor. 3:14; Efe. 4:18). Neno hili linatumiwa na mitume katika Marko 6:52. Ni neno tofauti la Kiyunani kutoka Rum. 9:18 (sklērunō) ambalo ni kinyume cha neno huruma (kama vile Ebr. 3:8,15; 4:7). Mstari huu uko wazi na ni ufupisho wa Rum. 11:1-6. Baadhi waliochaguliwa waliamini, wengine ambao hawakuchaguliwa walipumbazwa hata hivyo msitari huu haukuandikwa kwa kutengwa usemi wa kithiolojia.ilikuwa ni sehemu ya mabishano ya kithiolojia yaliyokuwa endelevu, ni mvutano kati ya ukweli uliosemwa wazi kabisa katika msitari huu na wito kwa ulimwengu mzima wa Warumi 10. Kuna muujiza hapa. Lakini jibu sio kukanusha au kupunguza ukali wa tatizo au kikwazo na pia ukali wa utata.

12:39 "Ndiyo sababu wao hawakuweza kusadiki" Hii ni kauli ya kati isiotimilifu (shahidi) elekezi na kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopo. Walikuwa hawawezi kuendelea katika mahusiano ya imani na Yesu. Miujiza Yake ikawavutia lakini haikuwasababisha kupata imani katika yesu kama Masihi. Katika Yohana "imani" ina viwango. Wote hawapati wokovu. Tazama muhtasari katika Yohana 8:31-59.

◙ "kwa maana Isaya alisema tena" Isaya 6:10; 43:8 inarejea kwa Wayahudi kufanywa kuwa na mioyo mizito kuhusu ujumbe wa Mungu kupitia kwa Isaya (kama vile Yer 5:21; Ezek. 12:2; Kumb. 29:2-4). 12:40 "mioyo" Tazama Mada Maalumu ifuatayo.

MADA MAALUMU: MOYO (AGANO JIPYA)

Neno la Kiyunani kardia limetumika katika tafasiri ya maandiko ya kale ya Kiebrania na Agano Jipya kuashiria neno la Kiebrania lēb (BDB 523, KB 513). Limetumika kwa njia tofauti kadhaa (kama vile Bauer, Arndt, Gingrich na Danker, A Greek-English Lexicon,, 2nd ed. kur. 403-404).

1. Kitovu/Kituo cha maisha ya kimwili, neno mbadala kwa mtu (kama vile Matendo 14:17; 2 Kor. 3:2-3; Yakobo 5:5)

2. Kitovu cha maisha ya kiroho (yaani, adilifu) a. Mungu anatujua mioyo (kama vile Luka 16:15; Rum. 8:27; 1 Kor. 14:25; 1 The. 2:4; Ufu. 2:23) b. Imetumika kwa maisha ya kiroho ya mwanadamu (kama vile. Mt. 15:18-19; 18:35; Rum. 6:17; 1

Tim. 1:5; 2 Tim. 2:22; 1 Pet. 1:22) 3. Kitovu cha maisha ya kifikra (yaani, uwezo wa kufikiri, kama vile. Mt. 13:15; 24:48; Matendo 7:23; 16:14;

28:27; Rum. 1:21; 10:6; 16:18; 2 Kor. 4:6; Efe. 1:18; 4:18; Yakobo 1:26; 2 Pet. 1:19; Ufu. 18:7; moyo ni sawa na mawazo katika 2 Kor. 3:14-15 na Flp. 4:7)

Page 226: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

210

4. kitovu cha maamuzi binafsi (yaani, matakwa,kama vile.Matendo 5:4; 11:23; 1 Kor. 4:5; 7:37; 2 Kor. 9:7) 5. Kitovu cha hisia za ndani (kama vile Mt. 5:28; Matendo 2:26, 37; 7:54; 21:13; Rum. 1:24; 2 Kor. 2:4; 7:3;

Efe. 6:22; Flp. 1:7) 6. Mahali pa pekee kwa shughuli za kiroho (kama vile. Rum. 5:5; 2 Kor. 1:22; Gal. 4:6 [yaani,Kristo katika

mioyo yetu, Efe. 3:17]) 7. Moyo ni njia mbadala ya ki-sitiari ya kumrejerea mtu (kama vile. Mt. 22:37, kwa kunukuu Kumb.

6:5). Mawazo, sababu, na matendo vikichangia kikamilifu kwenye moyo kubainisha kikamilifu mtu alivyo. Agano la Kale lina baadhi ya matumizi ya maneno ya kushangaza.

a. Mwa. 6:6; 8:21, "Mungu alihuzunishwa katika moyo," pia tazama Hosea 11:8-9 b. Kumb. 4:29; 6:5; 10:12, "kwa moyo wako wote na nafsi yako yote" c. Kumb. 10:16; Yer. 9:26, "Roho zisizo na tohara" na Rum. 2:29 d. Ezek. 18:31-32, "moyo mpya" e. Ezek. 36:26, "moyo mpya” dhidi ya “moyo wa jiwe” (kama vile Ezek. 11:19; Zak. 7:12)

12:41 "Maneno hayo aliyasema Isaya, kwa kuwa aliuona utukufu wake" Hii inaonyesha kuwa manabii wa Agano la Kale walikuwa wamejulishwa kuhusu Masihi (kama vile. Luka 24:27). Tazama muhutasari juu ya "utukufu" katika Yohana 1:14. 12:42 "Walakini hata katika wakuu walikuwamo wengi waliomwamini" Ujumbe wa Yesu ulizaa Matunda (kama vile Yohana 12:11; Matendo 6:7). Tazama Mada Maalum katika Yohana 2:23

◙ "hawakumkiri" Tazama MADA MAALUM: UKIRI katika Yohana 9:22-23

◙ "wasije wakatengwa na sinagogi" (kama vile Yohana 9:22; 16:2). 12:43 Hii inamaanisha kuwa imani ya kweli inaweza kuwa dhaifu na yakuogopwa, hata injili ya Yohana ambayo haijatangazwa inatumia kuamini (pisteuō) kwa maana mbalimbali kuanzia mvuto wa awali kufikia mwitikio wa mhemko, hadi imani ya kweli inayobakia.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 12:44-50 44 Naye Yesu akapaza sauti, akasema, Yeye aniaminiye mimi, haniamini mimi bali yeye aliyenipeleka. 45 Naye anitazamaye mimi amtazama yeye aliyenipeleka. 46 Mimi nimekuja ili niwe nuru ya ulimwengu, ili kila mtu aniaminiye mimi asikae gizani. 47 Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu. 48 Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho. 49 Kwa sababu mimi sikunena kwa nafsi yangu tu; bali Baba aliyenipeleka, yeye mwenyewe ameniagiza nitakayonena na nitakayosema. 50 Nami najua ya kuwa agizo lake ni uzima wa milele; basi hayo ninenayo mimi, kama Baba alivyoniambia, ndivyo ninenavyo.

12:44 "Yeye aniaminiye mimi, haniamini mimi bali yeye aliyenipeleka" Lengo la imani hatimaye liko kwa Baba (kama vile 1 Kor. 15:25-27). Hii ni dhamira inayojirudia (kama vile Mt. 10:40; Yohana 5:24). Kumjua Mwana ni kumjua Baba (kama vile 1 Yohana 5:10-12). 12:45 Mungu anafananaje? Kumwona Yesu ni kumwona Mungu (kama vile Yohana 14:7-10)! 12:46 Ulimwengu umo katika giza tangu Mwanzo 3 (kama vile Mwa. 6:5,11-12; 8:21; Zab. 14:3; Isa. 53:6; Rum. 3:9-23). 12:47 "Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike" Hii ni sentensi shurutishi daraja la tatu inayozungumzia juu ya kitendo muhimu.Utii unaoendelea ni ishara kwetu ya uhusiano wetu binafsi unaoendelea kwa imani! (tazama

Page 227: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

211

Mada Maalum katika 1 Yohana 5:13) upo katika msingi wa maisha yaliyo badilika na yanayoendelea kubadilika ya utii na ustahimilivu katika imani (tazama Mada Maalum katika Yohana 8:31, kama vile Vitabu vya Yakobo na 1 Yohana 3:17-21). 12:47-48 "maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu" Yesu kimsingi alikuja kuukomboa ulimwengu lakini ukweli kabisa unawasukuma wanadamu kuamua. Kama wanamkataa, wanajihukumu wenyenyewe (tazama Mada Maalum katika Yohana 8:31, kama vile Yohana 3:17-21). 12:49-50 Yesu anazungumza katika mamlaka ya Kimungu, sio ya kwake. 12:50 NASB, NKJV "agizo lake ni uzima wa milele" NRSV, TEV, NET "agizo lake linaleta uzima wa milele" NJB "agizo lake linamaanisha uzima wa milele" REB "agizo lake ni uzima wa milele" NIV "agizo lake linasababisha uzima wa milele" Net (rejeo) "agizo lake ni matokeo ya uzima wa milele" Chaguo la kwanza ni andiko halisi la Kiyunani .Maandiko mengine yanajaribu kutafsiri maana ya maandiko haya. NASB ina Yohana 6:68 kama kifungu kinachofanana, wakati Michael Magill's NT TransLine ina Yohana 17:8. The Jerome Biblical Commentary (uk. 451) ina Yohana ambayo 10:18 ni sambamba.Bila shaka fungu hili lina maana nyingi. Katika Yohana kuna kubadilika badilika kati ya hali ya umoja na wingi wa neno "amri," isiyo na umuhimu wa ufafanuzi wa maandiko.

MADA MAALUMU: "AMRI" KATIKA MAANDIKO YA YOHANA 1. Lilitumika kwa sheria za Musa,Yohana 8:5 2. Amri toka kwa Baba mpaka kwa Yesu

a. Uthibiti juu ya sadaka yake ya ukombozi, Yohana 10:18; 12:49-50; 14:31 b. ulimwengu utaujua upendo wa Yesu kwa Baba yake, Yohana 14:31 c. Yesu alitii amri ya Baba yake,Yohana 15:10

3. Amri kutoka kwa Yesu kwenda kwa waumini a. Kudumu katika upendo Wake,Yohana 14:15; 15:10 b. Pendaneni ninyi kwa ninyi ,kama alivyowapenda ninyi,Yohana 13:34; 15:12,17; 1 Yohana 2:7-8;

3:11,23; 4:7,21; 2 Yohana 5 c. Kutunza amri zake (yaani, b.), Yohana 14:15; 15:10,14; 1 Yohana 2:3,4; 3:22,24; 5:1-3; 2 Yohana 6

4. Amri kutoka kwa Baba kwenda kwa waumini a. Mwamini Yesu, 1 Yohana 3:23 (kama vile Yohana 6:29) b. Pendaneni ninyi kwa ninyi, 2 Yohana 3:23

MASWALI YA MJADALA

Huu ni mwongozo wa fasiri, ina maanisha kwamba unawajibika kwa tafsiri zako mwenyewe za Biblia. Kila mmoja wetu lazima atembee katika mwanga tulio nao. Wewe, Biblia, na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Hutakiwi uvitelekeze vitu hivi kwa mfasiri. Maswali ya mjadala huu yanatolewa kukusaidia kufikiri juu ya mambo makubwa ya sehemu za kitabu hiki. Yanalenga kukuamsha kimawazo na sio kutoa maana.

1. Kwanini Maria dada yake Lazaro alimpaka Yesu mafuta miguuni?

Page 228: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

212

2. Kwanini Mathayo, Marko na Yohana wanatofautiana kwa kiasi fulani katika maelezo yao katika ajali hii? 3. Kwanini palikuwa na umuhimu wa umati ule kukutana na Yesu wakiwa na matawi ya mchikichi na nukuu

kutoka Zaburi 118?

4. Kwanini Yesu alivutika kiasi kile na ombi la Wayahudi la kuzungumza naye?

5. Kwanini nafsi ya Yesu ilifadhaika? (kama vile Yohana 12:27)

6. Eleza kwanini Yohana anatumia neno “kuamini” katika maana kadha wa kadha.

Page 229: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

213

YOHANA 13

MIGAWANYO YA AYA YA TAFSIRI ZA KISASA

UBS4 NKJV NRSV TEV NJB Kuwatawadha miguu Mkuu awe Mtumishi Chakula cha mwisho Yesu anawatawadha kutawadha miguu Wanafunzi wake wanafunzi wake Miguu 13:1-11 13:1-11 13:1-11 13:1 13:1 13:2-6 13:2-5 13:6-11 13:7 13:8a 13:8b 13:9 Nasi hatuna budi 13:10-11 Kutumika 13:12-20 13:12-30 13:12-20 13:12-17 13:12-16 13:17-20 13:18-20 Yesu atabili kusurubiwa Yesu atabili kutabiriwa kwa Yuda kwake kusurubiwa kwake mtunza fedha 13:21-30 13:21-30 13:21 13:21-30 13:22-24 13:25 13:26-29 13:30 Amri mpya Amri mpya Amri mpya 13:31-35 13:31-35 13:31-35 13:31-35 13:31-35 Kukana kwa Petro Yesu anabishiri Yesu anabashiri Kunabashiriwa Petro kumkana Petro kumkana 13:36-38 13:36-38 13:36-38 13:36a 13:36-38 13:36b 13:37 13:38

MZUNGUKO WA TATU WA USOMAJI KUFUATILIA KUSUDIO LA ASILI LA MWANDISHI KATIKA NGAZI YA AYA Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwatafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Aya ya kwanza 2. Aya ya pili 3. Aya ya tatu 4. N.k

UTAMBUZI WA KI-MUKTADHA 13:1-38

A. Injili ya Yohana inahitimisha ishara za Yesu katika Yohana 12.

Page 230: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

214

Sura ya 13 ya Yohana inaanza na wiki ya mwisho ya Mateso ya Yesu.

B. Katika mwongozo wa kujisomea Biblia wa NASB katika nukuu zake unaweka maoni yake vizuri kwa kutumia jina la kiyunani “Agape” (Upendo) na kitenzi “agapoo (penda) vinajitokeza mara nane tu toka sura 1-12 lakini maneno hayo yanajitokeza mara 31 katika sura “13 – 17."

C. Yohana haandiki habari za chakula cha Bwana (Ekaristi) kama ilivyofanyika kwenye mihtasari ya Injili.

Yohana anatoa maudhui ya mjadala usiku ule katika chumba cha orofani (Yohana. 13-17 ambayo ni asilimia muhimu katika Injili ya Yohana. Hivyo basi, lazima iudhihilishe ubinadamu wa Yesu na kazi yake katika njia mpya za nguvu). Baadhi huona kama kuondolewa huku ni jitihada za makusudi katika kudumaza ukuaji wa kanisa la kwanza katika kuhamasisha sakaramenti hii. Yohana kamwe hakuwahi kutoa ufafanuzi juu ya Ubatizo wa Yesu au Chakula cha Bwana.

D. Muktadha wa kihistoria ya Yohana 13 unaweza kuonekana katika Injili ya Luka 22:24. Wanafunzi wa Yesu walikuwa wakibishana juu ya ni nani atakaye kuwa mkubwa miongoni mwao.

E. Mandhari ya Yohana 13-17 ni maandalizi yaliyofanyika chumba cha juu orofani huko Yerusalemu (au

yumkini Yohana 15-17 wakati akiwa njiani kwenda Gethsemane, k.v. Yohana 14:31), huenda Yohana anaonyesha ni nyumbani kwao, usiku ule ambao Yuda alipomsaliti Yesu.

F. Hapo panaonekana tofauti kuu mbili katika kitendo cha Yesu kutawadha miguu

1. Yohana 13:6-11 kuonyesha kazi atakayoifanya kwa niaba yetu pale msalabani 2. Yohana 13:12-20 ina lengo la kufundisha kuhusu unyenyekevu (Angalia Luka 22:24)

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 13:1-11 1 Sasa, kwa sababu alijua kabla ya sherehe ya pasaka kwamba saa yake ya kutoka katika ulimwengu huu kwenda kwa Baba ilikuwa imefika, Yesu, akiwa amewapenda walio wake mwenyewe waliokuwa ulimwenguni, akawapenda mpaka mwisho. 2 Kwa hiyo, mlo wa jioni ulipokuwa ukiendelea, Ibilisi akiwa tayari ameweka ndani ya moyo wa Yuda Iskariote, mwana wa Simoni, amsaliti, 3 yeye, akijua kwamba Baba alikuwa ametia vitu vyote mikononi mwake+ na kwamba alikuja kutoka kwa Mungu na alikuwa akienda kwa Mungu, 4 alisimama kutoka kwenye mlo wa jioni na kuyaweka kando mavazi yake ya nje. Naye akachukua kitambaa, akajifunga kiunoni. 5 Kisha akatia maji ndani ya beseni akaanza kuiosha miguu+ ya wanafunzi na kuikausha kwa kitambaa ambacho alikuwa amejifunga kiunoni. 6 Na kwa hiyo akafika kwa Simoni Petro. Huyo akamwambia: “Bwana, je, unaosha miguu yangu?” 7 Yesu akajibu, akamwambia: “Ninalofanya huelewi sasa, bali utaelewa baada ya mambo haya.” 8 Petro akamwambia: “Hutaosha kamwe miguu yangu.” Yesu akamjibu: “Nisipokuosha, wewe huna sehemu pamoja na mimi.” 9 Simoni Petro akamwambia: “Bwana, si miguu yangu tu, bali pia mikono yangu na kichwa changu.” 10 Yesu akamwambia: “Yule ambaye ameoga hahitaji kuoshwa zaidi ya miguu yake, bali yuko safi mwili wote. Nanyi mko safi, lakini si ninyi nyote.” 11 Kwa kweli, alimjua mtu anayemsaliti. Ndiyo sababu alisema: “Si wote kati yenu walio safi.”

13:1 “Kabla ya sikuu ya Pasaka” Yohana na mihutasari ya Injili haikubaliani ikiwa siku hii ilikuwa ni kabla ya chakula cha pasaka au siku ya Chakula cha pasaka yenyewe. Wote waliandaa chakula siku ya Alhamisi na kusulubiwa kukatokea siku ya Ijumaa (k.v. Yohana 19:31; Marko 15:43; Luka 23:54). Chakula hiki cha pasaka kinawakumbusha Waisrael kufunguliwa kwao kutoka Misri (k.v. Kut. 12). Yohana anadai kuwa ilikuwa siku kabla ya chakula cha kawaida cha Pasaka (Yohana 18:28; 19:14, 31, 42).

Inawezekana kuwa asili ya jamii ya Essene ilitumia kalenda tofauti (k.v. Kalenda ya Jua kutoka katika vitabu vya Jubilii na Enoki, kama njia ya kuonyesha kutokukubaliana kwao na Ukuhani wa wakati huo), jambo ambalo linaiweka siku ya pasaka mapema.

Page 231: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

215

Fasihi ya kibiblia ya Jerome inafupisha utalaamu wa sasa (uk.451) na kudhani kwamba neno la Yohana “siku kabla” ni sahihi na kwamba mihtasari ya injili inadai kuashiria suala la Chakula cha pasaka kama ishara. Hatuna budi kila mara kukumbushwa kwamba Injili siyo za kimagharibi, sababu na matokeo, mtiririko wa kihistoria. Historia imeandikwa katika njia nyingi ambazo siyo sahihi au mbaya, si za kweli au Uongo. Historia ni ufafanuzi wa masuala yaliyopita ili kusaidia masuala yaliyopo/mahitaji na mitizamo. Suala la msingi hapa ni nani na kwa nini aliandika historia hiyo. Mjadala mzuri hapa ni chimbuko la simulizi za kihistoria na Kiinjili ni Gordon Fee na Douglas Sturt, How To Read the Bible For All Its Worth, Uk. 89-126. ◙“Yesu akiisha kutambua kuwa saa yake imekwisha kuwadia” “kutambua” ni kauli timilifu tendaji inayoendelea (kama ilivyo katika Yn 13:3). Yesu alielewa fika upekee wa kimahusiano kati yake na Baba alipokuwa na umri wa miaka kumi na mbili (Lk 1:41-51). Ujio wa Wayunani kuja kumuona Yesu katika Yohana 12:20-23 ulidhihirisha kuwa Yesu saa ya kufa na kutukuzwa kwake imekwisha kufika (k.v. Yohana 2:4; 7:6, 8, 30; 8:20; 12:23, 27; 17:1). ◙ “Kwamba angeondoka katika ulimwengu huu kwenda kwa Baba” Injili ya Yohana inaendelea kusisitiza juu ya umiliki sahihi wa pande mbili, wa juu na toka chini (k.v. Yohana.13:3). Yesu alitumwa (k.v.Yohana 8:42) na Baba na sasa atarudi tena. Ufupisho wa Injili zinamuonyesha Yesu kama fundisho la pande mbili zilizo sambamba na upeo wa vizazi viwili vya Kiyahudi, wa mvutano uliokwisha timia na ambao bado kutimia wa ufalme wa Mungu. Pana maswali mengi juu ya Injili ambayo wasomaji wa siku hizi lazima waielezee, lakini wakati haya yote yakisemwa na kufanyika, maandiko haya yaliyovuviwa yanafunua mwendelezo wa kibiblia katika mtizamo wa kiulimwengu.

1. Kuna Mungu mmoja Mtakatifu. 2. Uumbaji wake wa pekee, binadamu, ameanguka katika dhambi na Uasi 3. Mungu amemtuma Mwana wake wa pekee Mkombozi (Masihi) 4. Binadamu hana budi kuitikia kwa imani, toba, utii na uvumilivu 5. Pana msukumo binafsi wa uovu katika kupingana na Mungu pamoja na Mapenzi yake. 6. Ufahamu wa uumbaji wote utatoa hesabu wa maisha yao kwa Mungu.

Kitenzi “ondoka” (metabainō) kina dokezo katika uandishi wa Yohana kutoka katika wa uwepo anguko la kimwili (kizazi cha kale chenye dhambi na uasi) ndani ya kizazi kipya chenye Roho na Uzima wa milele (k.v. Yohana 5:24; 13:1; 1 Yohana 3:14; isipokuwa kwa matumizi yake katika Yohana 7:3). ◙ “Naye ali amewapenda watu wake” kifungu hiki cha Kiyunani kilitumiwa katika magombo ya huko Misri (Moulton, Milligan, The Vocabulary of the Greek New Testament) kwa “ukoo wa karibu (k.v. Luka 8:19-21). ◙ “waliokuwemo ulimwenguni” Yohana anatumia neno ulimwengu (kosmos) katika fikira mbalimbali tofauti.

1. Sayari hii (k.v Yohana 1:10; 11:9; 16:21; 17:5,11,24; 21:25). 2. Mwanadamu (k.v Yohana 3:16; 7:4; 11:27; 12:19; 14:22; 18:20,37) 3. Uasi wa mwanadamu (k.v. Yohana 1:10,29; 3:16-21; 4:42; 6:33; 7:7; 9:39; 12:31; 15:18; 17:25)

Tazama Mada Maalum: Matumizi ya Paulo kuhusu Ulimwengu (kosmos) katika Yohana 14:17 ◙ “Aliwapenda upeo” Hili ni neno la Kiyunani “telos,” lenye maana ya kusudi lililotimilizwa. Hii inalenga kazi ya Yesu ya ukombozi kwa mwanadamu kupitia msalaba. Umbo la neno kama hili lilikuwa neno la mwisho la Yesu pale msalabani (k.v. Yohana 19:30), “Imekwisha,” jambo ambalo tunajifunza toka kwenye magombo ya kale ya Misri yaliyokuwa na dokezo la neno“kulipwa lote”! 13:2 “Wakati wa Chakula cha jioni” Pana maandiko ya Kiyunani yanatofautiana katika kigezo hiki. Utofauti unaohusika ni kupitia herufi moja katika neno la Kiyunani.

1. ginomenou, wakati uliopo unaendelea (yaani, wakati wa chakula), MSS א, B, L, W 2. genomenou, wakati usiotimilifu endelevu (yaani, baada ya chakula cha jioni ), MSS P66, 2 א, A, D

Toleo la UBS4 inatoa chaguo namba # 1 alama "B" (takriban bila shaka). Hili huenda linamaanisha kuwa; 1. Baada ya chakula cha jioni 2. Baada ya kikombe cha kwanza cha Baraka, wakati utaratibu ulipohitajika wa kunawa mikono.

Page 232: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

216

3. Baada ya kikombe cha tatu cha Baraka

MAALUM MADA:PASAKA (TARATIBU ZA UTUMISHI)

A. Sala B. Kikombe cha divai C. Kuoshwa mikono na mwenyeji na kupitisha beseni kwa wote D. kuchovya kwenye mchuzi mzito na viungo vikali E. Mwana-kondoo na mlo mkuu F. kuomba na kuchovya mara ya pili kwenye mchuzi mzito na viungo vikali G. Kikombe cha pili cha divai kukiwa na kipindi cha maswali na majibu kwa watoto (k.v. Kutok. 12:26-27) H. Kuimba za Zaburi ya kumsifu Bwana 113-114 na sala. I. Mshereheshaji hufanya kitonge kwa kila mtu baada ya kuosha mikono J. Wote wanakula mpaka washibe; kumaliza na kipande cha mwana-kondoo K. Kikombe cha tatu cha diai baada ya kuoshwa mikono L. Kuimba Zaburi za kumsifu Bwana 115-118 M. kikombe cha nne cha divai, ambacho kiliashiria kuja kwa Ufalme

Wengi wanaamini kuwa taasisi ya chakula cha bwana ilitokea katika “K

◙ "Ibilisi amekwisha kumtia Yuda, mwana wa Simoni Iskariote, moyo wa kumsaliti” Hii ni kauli timilifu tendaji inayoendelea. Yesu alimjua Yuda Iskariote toka mwanzo (k.v. Yohana 6:70). Yule mwovu (Angalia Mada maalum katika Yohana 12:31) alikuwa akimjaribu Yuda kwa muda mrefu, lakini katika Yohana 13:27 Ibilisi alichukua umiliki wote juu yake. Tazama Mada Maalum: Moyo katika Yohana 13:27 Angalia nukuu nzima juu ya Yuda katika Yohana 18:2. 13:3 "Naye Yesu, akijua kwamba Baba alikuwa ametia vitu vyote mikononi mwake" Hii ni hali timilifu tendaji endelevu, kama ilivyo katika Yohana 13:1, ikifuatiwa na hali ya wakati uliopita usiotimilifu tendaji elekezi. Hii ni moja ya kauli za Yesu ya kushangaza juu ya uelewa wake mwenyewe na mamlaka (k.v. Yohana 3:35; 17:2; Mt. 28:18). Wakati uliopita usiotimilifu ni muhimu hapa. Baba alimpa Yesu “vyote”kabla ya kuangikwa. Havikutolewa tu kama tuzo kwa ajili ya utiifu wake, bali kwa sababu ambavyo alivyo! Alijua kuwa yeye ndiye na aliwatawadha miguu hao waliokuwa wakibishana ni nani aliye mkuu miongoni mwao! ◙ "ya kuwa alitoka kwa Mungu” Hiki ni cha pili kati ya vitu vitatu vilivyotajwa katika Yohana 13:3 kwamba Yesu alijua.

1. Baba alikuwa amempa vyote mikononi mwake 2. Alikuwa amekuja kutoka kwa Mungu 3. Alikuwa anakwenda tena kwa Mungu (k.v. Yohana 7:33; 14:12,28; 16:5,10,17,28; 20:17)

Mbili za mwisho ni sehemu kati ya hizo hapo juu dhidi ya pande mbili za chini ambazo ni hali ya kawaida kwa Yohana. Kipengele #2 ni fungu la pekee kwa Yohana (k.v. Yohana 8:42; 13:3; 16:28,30; 17:8). Ina vyote hitimisho la awali na mahali (yaani, Uungu toka mbinguni). 13:4 "aliondoka toka chakulani" Kumbuka kuwa walikuwa wameegemea viwiko vya mikono yao na miguu yao ilikuwa nyuma kwa maana waliketi chini na siyo kwenye viti . ◙ "Akayaweka kando mavazi yake" Wingi huu unamaanisha mavazi ya nje ya Yesu, (k.v. Yohana 19:23). Inavutia kwamba KITENZI kile kile kimetumiwa katika Yohana 10:11,15,17,18 kuwa Yesu anayatoa maisha yake (k.v. Yohana 13:37). Hii huenda ikawa mbinu nyingine ya Yohana kutumia uhusika wa aina mbili. Inaonekana kama vile kitendo cha kutawadha miguu kilikuwa zaidi ya somo la unyenyekevu, (k.v. Yohana 13:6-10). 13:5 "Kutawadha miguu ya wanafunzi wake" Hili ni neno la Kiyunani lililotumika kwa "kutawadha sehemu tu za mwili." Neno katika Yohana 13:10 lilitumika kama kuoga mwili mzima. Kutawadhwa miguu ilikuwa ni kazi ya

Page 233: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

217

mtumwa. Hata walimu wa sheria za kiyahudi hawakutazamia hilo kwa wanafunzi wake. Yesu akijua Uungu wake alikuwa radhi kuwatawadha miguu hawa wanafunzi wake wenye wivu na kunia makuu (hata Yuda)! 13:6 Swali la Petro lilikuwa ni swali lililoulizwa pasipo kutazamia jibu baada ya kujaribu kukataa kutawadhwa miguu na Yesu. Mara zote Petro alifikiri kuwa alijua kile ambacho Yesu angetenda na ambayo asingetenda (k.v. Mt. 16:22). 13:7 Mitume, walioishi na Yesu, mara zote hawakuelewa matendo yake pamoja na mafundisho pia (k.v. Yohana 2:22; 10:6; 12:16; 14:26; 16:18). Kushindwa kuelewa huku ndiko kunapelekea kuelezea pande mbili zilizo wima. 13:8 "Hutaosha kamwe miguu yangu” Huu ni mtizamo hasi wenye nguvu ambao unamaanisha kuwa “Kamwe hapana hata kwa namna yoyote ile." ◙“Nisipokuosha, wewe huna sehemu pamoja na mimi” Hii ni tungo shurutishi daraja la tatu. Mstari huu unaonyesha kuwa kuna mengi yalikuwa yakitokea hapa kuliko somo halisi la kivitendo. Yohana 13:6-10 inaonyesha uhusiano kati Yesu na kazi aliyoifanya pale msalabani ya kusamehe dhambi. Fungu la pili laweza kuaksi nahau katika Agano la kale zinazohusiana na urithi (k.v. Kumb. 12:12; 2 Sam. 20:1; 1 Fal. 12:16). Hii ni nahau madhubuti yenye kuondoa. 13:9 Kiambata hasi Chembe cha Kiyunani “Hapana" (MĒ) kinaonyesha ushurutishi wa tendo “tawadha”" 13:10 “Yeye aliyekwisha kuoga” Yesu anaongea ki-stiari juu ya ukombozi. Petro amekwisha kuoshwa (kuokolewa, k.v. Yohana 15:3; Tito 3:5), lakini anahitaji kuendelea kutubu (k.v. 1 Yohana 1:9) ili kuendeleza ushirika wa ndani. Uwezekano mwingine wa kimazingira ni kuwa Yesu anazungumza juu ya Yuda kumsaliti (k.v. Yohana 13:11 na 18). Hivyo sitiari ya kuoga inalenga kusema;

(1) Mwili wa Petro au (2) kundi la mitume.

◙ “Nanyi mko safi, lakini si ninyi nyote” Kiwakilishi “ninyi” kinasimama kuonyesha wingi, kulenga kiini cha ndani cha wanafunzi, isipokuwa kwa Yuda (k.v. Yohana 13:11,18; 6:70). "Safi" inalenga ujumbe wa “Yesu” ambao wameupokea (k.v. Yohana 15:3). Ni wasafi kwa sababu wameamini/wametumaini/wameimanishwa/wamepokea na Yeye aliye safi, yaani Yesu. Katika kifungu “lakini si ninyi nyote.” Angalia Mada Maalum: Uasi (aphistēmi) katika Yohana 6:64 13:11 Biblia za TEV na NET zinaweka mstari huu katika mabano, ili kuonyesha kama moja ya uhariri wa maoni ya mwandishi.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 13:12-20 12Basi, alipokuwa ameosha miguu yao na kuvaa mavazi yake ya nje, akaketi mezani tena, akawaambia: “Je, mnajua jambo ambalo nimewafanyia ninyi? 13 Ninyi huniita, ‘Mwalimu,’ na, ‘Bwana,’ nanyi mnasema sawasawa, kwa maana ndivyo nilivyo. 14 Kwa hiyo, ikiwa mimi, nijapokuwa Bwana na Mwalimu, niliiosha miguu yenu, ninyi pia mnapaswa kuoshana miguu. 15 Kwa maana niliweka kielelezo kwa ajili yenu, ili, kama vile nilivyowafanyia ninyi, ninyi pia mfanye hivyo. 16 Kwa kweli kabisa ninawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake, wala yule aliyetumwa si mkuu kuliko yule aliyemtuma. 17 Ikiwa mnajua mambo haya, wenye furaha ni ninyi ikiwa mnayatenda. 18 Mimi sisemi juu yenu nyote; ninawajua wale ambao nimewachagua. Lakini ni ili Andiko lipate kutimizwa, ‘Yule aliyekuwa akila mkate wangu amekiinua kisigino chake dhidi yangu.’ 19 Kuanzia dakika hii na kuendelea ninawaambia ninyi kabla ya hilo kutukia, ili litakapotukia mwamini kwamba mimi ndiye. 20 Kwa kweli kabisa ninawaambia, Yule anayempokea yeyote ninayemtuma hunipokea Mimi pia. Naye anayenipokea Mimi, humpokea pia yule aliyenituma”

Page 234: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

218

13:12-20 Tofauti na Yohana 13:6-10, hapa Yesu anafafanua utendaji wake kama mfano wa uvumilivu. Mitume walibishana sana juu ya nani atakayekuwa mkubwa (k.v. Luka 22:24). Ni katika muktadha huu Yesu anafanya tendo ambalo linafanywa na mtumwa na kisha anawaeleza nini maana yake na jinsi gani wanapaswa kufanya. 13:14 "Kama" Hii ni tungo shurutishi daraja la kwanza ambayo hudhaniwa kuwa ni kweli kutokana na mtizamo wa mwandishi au kwa kusudi lake. ◙"Bwana na Mwalimu" Tambua kibainishi cha wazi katika Yohana 13:13 na 14. Pia tambua kuwa vichwa vilivyorudiwa. Huyo ndiye ambaye anazungumza kwa mamlaka. Anamdhihilisha Baba na anatutazamia sisi kuwa na utiifu na kutunza viapo vyetu! Lolote alitendalo hawana budi kuliiga (Yohana 13:15). 13:14-15 "Mnapaswa pia kutawadhana miguu yenu kila mmoja na mwenzake” Je kauli hii ina maana kwamba hiki kitendo cha uvumilivu kinamaanisha kuwa kanisa ni sehemu ya tatu ya ibada? Makundi mengi ya kikristo yamesema hapana kwa sababu;

1. Kamwe hakuna kumbukumbu iliyofanywa na kanisa lolote katika Matendo 2. Kamwe haijawahi kutetewa katika Nyaraka za Agano Jipya (Agano Jipya) 3. Kamwe haijawahi kusemwa kiufasaha juu ya yale yanayojili katika ibada kama vile ya Ubatizo (k.v. Mt.28:19) na Chakula cha Bwana (k.v. 1 Kor. 11:17-34)

Hili Halimanishi kuwa hili sio tukio muhimu la kuabudu. “Mfano” Yesu aliwapa siyo tu uvumilivu bali pia huduma ya kujitoa (k.v. Yohana 15:12-13). 1 Yohana 3:16 inafafanua vema! Yesu anapenda mpaka mwisho (k.v. Yohana 13:1), imewapasa kupenda pia katika kipeo cha juu (yaani, maisha ya kujitoa sadaka, kinyume cha anguko) 13:16 "Kwa kweli kabisa ninawaambia ninyi" Kiuhalisia "Amin, amin" (kama vile Yohana 13:20). Huu ni muundo wa Agano la Kale muda wa “Imani” (k.v. Hab. 2:4). Yesu alikuwa peke yake, (katika fasihi yoyote ya Kiyunani), hutumika kufungua fursa. Kwa kawaida husemwa mwishoni mwa (1) Makubaliano ya au (2) kuthibitisha kauli au tendo. Wakati ikitumiwa mwanzoni mwa tungo na kujirudia, inaonyesha mamlaka, umakini wa chombo. Angalia MADA MAALUM: AMINA katika Yohana 1:51 ◙ “mtumwa siyo mkuu kuliko bwana wake" Huu ni utangulizi wa kifungu kueleza ukweli.

1. Yohana 13:16, wala yule aliyetumwa si mkuu kuliko yule aliyemtuma. 2. Yohana 15:20

a. kama walinitesa Mimi, watawatesa ninyi pia b. kama waliyaweka maneno Yangu, watayaweka na yenu pia

3. Luka 6:40 (zinalandana), bali kila mmoja, baada ya kufuzwa kikamilifu atakuwa kama mwalimu wake (k.v. Mt. 10:24)

4. Luka 22:27 (zina landana), bali Mimi niko miongoni mwenu kama anayewatumikia. 13:17 “Ikiwa mnajua mambo haya, wenye furaha ni ninyi ikiwa mnayatenda” Neno la Kwanza “Ikiwa” ni tungo shurutishi daraja la kwanza ambayo inachukuliwa kuwa kweli kutokana na mtizamo wa mwandishi. Neno la Pili “ikiwa” katika mstari huu ni tungo shurutishi daraja la tatu yenye maana ya tendo muhimu. Ikiwa tunajua, tungefanya (k.v. Mt. 7:24-27; Luka 6:46-49; Rom. 2:13; Yakobo 1:22-25; 4:11)! Maarifa siyo lengo, bali kuishi kama Kristo aishivyo. Hili linaakisi kitenzi cha Kiebrania “shema” yaani “sikia kwa maana ya kufanya” (k.v. Kumb. 6:4). 13:18 “ili Andiko lipate kutimizwa" Hili linamlenga Yuda. Hili ni fumbo lenye mwingiliano wa mambo yaliyoamuliwa kabla dhidi ya mapenzi huru ya mwanadamu. Yesu, na wanafunzi wake, waliamini ukweli wa Maandiko ya Mungu! Yalipokuwa yakisemwa kisemwa hapakuwa na budi kuyaamini (k.v. Mt. 5:17-19). Mara nyingi Yohana atoa maoni kwamba “Maandiko yatimizwe" (k.v. Yohana 12:14; 13:18; 15:25; 17:12; 19:24,36). Mara zote maandiko katika Agano la Kale hayaeleweki vizuri hadi pawepo na tukio linalogusa maisha ya Kristo (yaani, Ufanano, Hosea 11:1) au tukio katika Agano Jipya ni mazidisho yatimilizwayo (yaani, Isa. 7:14 au Dan. 9:27; 11:31; 12:11).

Page 235: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

219

◙ "AMENIINULIA KISIGINO CHAKE DHIDI YANGU" Hii ni nukuu toka Zaburi 41:9. Desturi ya kula pamoja ni ishara ya urafiki na agano ambalo linachochea kosa la Yuda. Karibia Mashariki yote kumuonyesha mtu mwingine unyao ilikuwa ni ishara ya dharau. 13:19 Mstari huu unaonyesha kusudi la muujiza wa Yesu ni ishara na utabiri (k.v. Yohana 20:31). Katika Yohana, imani inakua na kuendeleza uzoefu. Yesu kila mara anachochea imani/uaminifu/kuamini kwa mitume wake. Angalia Mada Maalum katika Yohana 9:7 Yesu anachochea imani yao kwa

1. Maneno Yake 2. Matendo yake 3. Hekima na Maono Yake

Yesu alileta msingi mpya wa namna ya kumpendeza Mungu. Msingi huu ulikuwa mtambuka dhidi ya tamaduni na imani za Wayahudi.

1. Yeye, wala siyo Musa, alikuwa na mtizamo 2. Neema, sio utendaji

◙ "Kwamba Mimi ndiye" Hii ni rejea ya Jina la Mungu, “YHWH,” ambalo ni kutoka kitenzi cha Waebrania “kuwa” (k.v. "Mimi" ya Kutoka 3:14). Yesu anakiri wazi wazi hapa kuwa Yeye ndiye Yule Masiha aliyeahidiwa akiwa na dokezo la ki-Uungu (k.v. Yohana 4:26; 8:24,28, 58; 13:19 na 18:5,6,8; Mt. 24:5 na Marko 13:6; Luka 21:8). Angalia MADA MAALUM: MAJINA YA UUNGU katika Yohana 6:20 13:20 Kwa kawaida Yohana anatumia istilahi "amini" (pisteuō), "amini katika" (pisteuō eis) au "amini kwamba" (pisteuō hoti) kuonesha wakristo, (Angalia Mada Maalum: Matumizi ya “Imani” Ya Yohana katika Yohana 2:23), lakini pia alitumia istilahi zingine kama “pokea” au “karibu” (k.v. Yohana 1:12; 5:43; 13:20). Injili ni ukaribishaji wa mtu na ukubarifu wa kweli ya Kibiblia kuhusu mtu huyo, pamoja na kuishi maisha yanayompambanua mtu huyo. ◙ "Yule atakayempokea yeyote Nimtumaye anipokea Mimi" Ni Kauli ya namna gani yenye nguvu ya kugawa madaraka ya Yesu kwa wanafunzi wake. Inaweza kutumika katika hatua mbalimbali.

1. Katika safari za kimishionari za Thenashara (mitume kumi na mbili), (Mt. 10:40) na sabini (Luka 10:16) 2. Mashahidi wa kanisa (k.v. Yohana 17:20)

Ujumbe kuhusu Yesu una nguvu inayobadilisha maisha ambayo haihusiani na hao wanaopiga hukumu. Mamlaka iko katika ujumbe (yaani Injili), siyo katika ujumbe wa kidunia.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 13:21-30 21Baada ya kusema hayo, Yesu akataabika rohoni, naye akatoa ushahidi na kusema: “Kwa kweli kabisa ninawaambia ninyi, Mmoja wenu atanisaliti.” 22 Wanafunzi wakaanza kutazamana, wasijue kabisa alikuwa akisema hilo kuhusu nani. 23 Mmoja wa wanafunzi wake alikuwa ameegama kifuani pa Yesu, naye Yesu alimpenda. 24 Kwa hiyo Simoni Petro akamtolea huyo ishara ya kichwa na kumwambia: “Muulize anasema hilo kuhusu nani.” 25 Kwa hiyo huyo wa mwisho akaegemea nyuma kifuani pa Yesu na kumwambia: “Bwana, ni nani?” 26 Kwa hiyo Yesu akajibu: “Ni yule ambaye nitampa tonge ambalo ninachovya.” Na kwa hiyo, akiisha kuchovya tonge, akalichukua na kumpa Yuda, mwana wa Simoni Iskariote.27 Na baada ya hilo tonge ndipo Shetani akaingia ndani ya huyo. Kwa hiyo, Yesu akamwambia: “Lile unalofanya lifanye upesi zaidi.” 28 Hata hivyo, hakuna hata mmoja kati ya wale waliokuwa wameketi mezani aliyejua amemwambia hili kwa nini.29 Kwa kweli, baadhi yao walikuwa wakifikiri, kwa kuwa Yuda alikuwa akilishika sanduku la pesa, kwamba Yesu alikuwa akimwambia: “Nunua vitu ambavyo tunahitaji kwa ajili ya sherehe,” au kwamba awape maskini kitu fulani. 30 Kwa hiyo, baada ya yeye kulipokea tonge, akatoka nje mara moja, akaenda. Na wakati huo ulikuwa usiku.

Page 236: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

220

13:21 "Yesu akataabika rohoni" Usaliti wa Yuda ulimkasirisha sana Yesu (neno hilo hilo alilitumia Yesu katika Yohana 12:27). Yesu alimchagua Yuda kwa sababu ya ushupavu wake kiroho lakini kamwe haukuzaa matunda (k.v. Yohana 13:18). ◙ "Kweli kabisa" Angalia nukuu katika Yohana 1:51. 13:22 Huu ni mstari wa kushangaza. Wanafunzi wengi walihofu ndani kwa ndani kwamba kauli hii huenda ingewafanya waonekana kama wasaliti, (k.v. Marko 14:19). Hili ndilo tatizo la kuhisi pasipo kuwa na uhakika. Matendo ya Mungu hayapingani na uhuru wa maamuzi wa mwanadamu, bali hutia mkazo na kuhitimisha matokeo yake. 13:23 "naye Yesu alimpenda" Inaonekana huyu alikuwa ni Yohana mwenyewe (k.v. Yohana 13:23,25; 19:26-27,34-35; 20:2-5,8; 21:7,20-24). Yohana 19 na 13:26 zinathibitisha hili. Jina la Yohana halijitokezi katika Injili hii. Yesu alipendelea kitu gani? Kweli, Alikuwa akipendelea zaidi kuwa na (Petro, Yakobo, na Yohana) na pia familia Maalum ya akina (Lazaro, Maria, Martha). 13:25 Mazingira haya yanaaksi uhalisia wa mipango ya kula katika karne ya kwanza kwa Wapalestina. Wanafunzi wa Yesu wangelikuwa wamelala chini katika meza yenye muundo wa kiatu cha farasi, wakiegemea viwiko vyao huku miguu ikiwa nyuma yao, wakila kwa mikono yao ya kuume. Sababu ya mkao huu haikutajwa kabisa katika Maandiko Matakatifu. Yohana akageuka nyuma na kumuuliza Yesu swali. 13:26 “Ni yule ambaye nitampa tonge ambalo ninachovya” Hii ilikuwa ishara ya heshima (k.v. Ruthu 2:14). Yuda alikuwa anajinyoosha upande wa kushoto wa Yesu ambapo pia palikuwa mahali pa heshima. Yesu alikuwa bado ajaribu kumfikia Yuda! Funda lilikuwa ni bakuri lenye mchuzi wenye viungo (Angalia Mada Maalum katika Yohana 13:2). Marko inayofanana (14:20) inasema "kwangu mimi." Huu ni uthibitisho wa ushuhuda wa macho wenye maelezo ya kuchanganya. ◙ "Iskarioti" Angalia Mada Maalum hapo chini kisha nukuu za somo toka Yohana 6:71 na 18:2.

MADA MAALUMU: YUDA ISKARIOTI

Yuda alikwisha sikia, akachunguza, na kufanya ushirika na Bwana Yesu kwa karibu sana kwa miaka mingi, lakini dhahili kabisa hakuwa na ushirika binafsi na Yeye katika imani (k.v.. Mt. 7:21-23). Petro naye alipitia uzito ule ule wa jaribu kama alilolipitia Yuda, lakini yakiwa na matokeo yenye athari kubwa (k.v.Mt.26:75). Majadiliano mengi yalifanyika juu ya mwenendo wa usaliti wa Yuda:

1. Kimsingi yalikuwa ni mambo ya fedha (k.v.Yoh.12:6) 2. Kimsingi yalikuwa ni mambo ya kisiasa (k.v. William Klassen, Judas Betrayer or Friend of Jesus?) 3. Yalikuwa ni mambo ya kiroho (kama vile Luka 22:3; Yoh. 6:70; 13:2,27)

Juu ya somo la ushawishi wa kishetani au kumilikiwa na pepo (angalia Mada Maalumu: hali ya kimapepo katika agano jipya) kuna vyanzo mbali mbali vya kimapato (vilivyo oredheshwa katika mpangilio wa wale ninao waamini)

1. Merrill F. Unger, Biblical Demonology, Demons in the World Today 2. Clinton E. Arnold, Three Crucial Questions About Spiritual Warfare 3. Kurt Koch, Christian Counseling and Occultism, Demonology Past and Present 4. C. Fred Dickason, Demon Possession and the Christian 5. John P. Newport, Demons, Demons, Demons 6. John Warwick Montgomery, Principalities and Powers

Uwe mwangalifu juu ya udanganyifu wa kitamaduni na miiko. Shetani anamwathuri Petro katika Mt. 16:23 kumjaribu Yesu katika njia zile zile-kifo chake mbadala. Shetani anaendelea. Anajaribu kutumia kila liwezekanalo kuzuia kazi ya Yesu ya ukombozi kwa niaba yetu.

Page 237: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

221

1. Jaribu la Yesu, Luka 4 2. Akamtumia Petro 3. Akamtumia Yuda Iskarioti na wakuu wa Sinagogi

Yesu hata anamwelezea Yuda kama shetani katika Yohana 6:70. Biblia haizungumzii somo la kushawishiwa na kumilikiwa na shetani kama inahusiana na waumini. Lakini, waumini wazi kabisa wanaathiriwa na maamuzi binafsi na uovu binafsi (angalia Mada Maalumu: Uovu Binafsi) Asili ya “Yuda Iskarioti” kwa kiasi Fulani haieleweki; hata hivyo, kuna uwezekano mbali mbali:

1. Kerioth, mji wa Yuda (k.v. Yosh. 15:25) 2. Kartan, mji wa Galilaya(k.v. Yosh. 21:32) 3. Karōides, walipomlaki na matawi ya mitende huko Yerusalemu au Yeriko 4. scortea, aproni au begi la ngozi(k.v. Yoh. 13:29) 5. ascara, kujinyonga (Waebrania) toka Mt. 27:5 6. kisu cha kujiulia (Kiyunani), ikimaanisha alikuwa mkereketwa kama simoni (k.v. Luka 6:15)

13:27 "Na baada ya hilo tonge ndipo Shetani akaingia ndani ya huyo" Hapa ndipo mahali pekee ambapo neno ibilisi limetumika katika Injili ya Yohana. Linamaanisha "adui; mshindani." Kwa Kiebrania (k.v. Luka 22:3 na Yohana 13:2). Je Yuda hahusishwi na hili kwa sababu Ibilisi alimuingia yeye? Kuna mvutano mkubwa katika Biblia kati ya matendo yanayotendeka katika Uwepo wa Roho Mtakatifu (Mungu anaufanya Mgumu moyo wa Farao) na wajibu wa mwanadamu katika hali halisi. Wanadamu hakika hawako huru katika chaguzi zao kama wanavyofikiri. Sisi sote kihistoria, kiuzoefu na kiunasaba tunashurutishwa. Ukiongeza katika vigezo halisi viko katika mzunguko wa Kiroho (Mungu, Roho, Malaika, Ibilisi na Mashetani). Huu ni muujiza! Hata hivyo, binadamu siyo mashine; tunawajibika kwa matendo yetu, chaguzi, na kwa matokeo yake pia. Yuda alitenda! Hakutenda peke yake! Bali kimaadili anawajibika kwa matendo yake. Usaliti wa Yuda ulitabiriwa (Yohana 13:18). Ibilisi alikuwa ni mchochezi (Angalia MADA MAALUM: UOVU BINAFSI katika Yohana 12:31). Ni huzuni kuwa Yuda “hakumjua” kiundani au kumwamini Yesu. 13:29 "Yuda alikuwa akilishika sanduku la pesa" Yuda alikuwa mwangalizi na mtunzaji wa fedha zote za kundi (k.v. Yohana 12:6). Angalia nukuu zote katika Yohana 18:2. 13:30 "Na wakati huo ulikuwa usiku" Je huu ni muda wa ishara au tathimini ya kiroho? Yohana mara zote anatumia vifungu hivi tata ambavyo vinaweza kuwa na maana zaidi ya moja (yaani, Nikodemo, k.v. Yohana 3:2; 19:39).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 13:31-35 31Kwa hiyo alipokuwa ameenda, Yesu akasema: “Sasa Mwana wa binadamu ametukuzwa, na Mungu ametukuzwa kuhusiana na yeye. 32 Na Mungu mwenyewe atamtukuza, naye atamtukuza mara moja. 33 Watoto wadogo, nipo pamoja nanyi muda kidogo zaidi. Ninyi mtanitafuta; na kama vile nilivyowaambia Wayahudi, ‘Ninakoenda ninyi hamwezi kuja,’ ninawaambia ninyi pia sasa. 34 Ninawapa ninyi amri mpya, kwamba mpendane; kama vile ambavyo nimewapenda ninyi, ninyi nanyi mpendane vivyo hivyo. 35 Kwa jambo hili wote watajua kwamba ninyi ni wanafunzi wangu, mkiwa na upendo kati yenu wenyewe.” "

13:31-38 Mistari hii inaunda sehemu kubwa ya muktadha wa mtiririko wa maswali kwa wanafunzi wa Yesu (k.v. Yohana 13:36; 14:5,8,22; 16:17-19) aliulizwa katika majibizano kwenye chumba cha juu orofani usiku ule wa chakula cha Bwana. Ni dhahiri kuwa kauli za Yesu kuhusu kwenda kwake kuliwafanya Mitume kujiuliza maswali mengi kulingana na jinsi ambavyo hawakuelewa maneno ya Yesu.

1. Petro (Yohana 13:36) 2. Tomaso (Yohana 14:5) 3. Filipo (Yohana 14:8)

Page 238: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

222

4. Yuda (sio Iskarioti) (Yohana 14:22) 5. Baadhi ya wanafunzi wake (Yohana 16:17-19)

13:31 "Sasa Mwana wa adamu ametukuzwa" Huu ulikuwa ni usanifu binafsi aliouchagua Yesu mwenyewe. Chimbuko lake ni kutoka Ezek. 2:1 na Dan. 7:13. Inahusisha tabia za kibinadamu na ki-Uungu. Yesu alitumia hivyo kwa sababu ilikuwa haijawahi kutumika katika utaalam wa dini ya Kiyahudi, hivyo, haikuwa na madhara ya utaifa au ukijeshi na kuwa iliunganisha asili zake mbili pasina kuleta mkanganyiko (k.v. 1 Yohana 4:1-3). 13:32 Pana maandishi tofauti ya Kiyunani katika mstari huu. Kifungu kirefu zaidi kinapatikana katika Biblia aina za NASB, NKJV, NRSV, TEV, na NJB. Kifungu hiki kinaungwa mkono na maandishi ya אc, A, C2, K, na mapokeo ya kifungu. Endapo Kifungu hiki ("Ikiwa Mungu anatukuzwa ndani yake") kiimeacha nje katika tafsiri ya MSS P66, א*, B, C*, D, L, W, na X. Haya yanaoneka kuwa mpango bora wa maandishi. Lakini huenda inawezekana waandishi walichanganywa na mrandano na wakaamua kukifutilia mbali kifungu hiki cha kwanza. ◙ "atamtukuza" neno limetumika mara nne au mara tano katika Yohana 13:31 na 32—mara mbili au mara tatu katika wakati usiotimilifu na maradufu katika wakati ujao. Inahusu mpango wa Mungu wa ukombozi kupitia kwa kifo cha Yesu na ufufuo (kama vile Yohana 7:39; 12:16,23; 17:1,5). Hapa inarejea matukio yajayo katika maisha ya Yesu. Wao walikuwa na uhakika wa kutokea kwamba yaelezwe kana kwamba yalikuwa matukio ya zamani (wakati usiotimilifu). Tazama muhtasari katika Yohana 1:14. 13:33 "watoto wadogo" Yohana, aliandika kama mtu mzee kutoka mji au eneo la Efeso, hutumia sifa hii ya kuwasiliana na wasikilizaji/wasomaji wake katika 1 Yohana 2:1,12,28; 3:7,18; 4:4; 5:21. Hapa sitiari ni njia nyingine ya kumtambulisha yeye na Mungu. Yeye ni Mungu/Baba, ndugu, mwokozi, rafiki na bwana. Au kwa kuweka njia nyingine, yeye ni Mungu anayeweza kupita uwezo wa mwanadamu ki-Uungu na Mungu mshirika wa asili. ◙ "bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi. . . na kama vile nilivyowaambia Wayahudi" Yesu alikuwa amewambia hili viongozi wa Kiyahudi miezi michache iliyopita (kama vile Yohana 7:33); sasa anawambia mitume wake (kama vile Yohana 12:35; 14:19; 16:16-19). Kwa hiyo, ni dhahiri kuwa kipengele cha wakati kilikuwa hakieleweki ◙ "Mimi niendako ninyi hamwezi kuja" Viongozi wa Kiyahudi hawakuweza kurudi kamwe (kama vile Yohana 7:34,36; 8:21). Wanafunzi wasingelikuwa naye pamoja mpaka kufa kwao. Kifo, au furaha nyingi kupita kiasi, itawaunganisha wafuasi wake pamoja (kama vile Kor. 2. 5:8; 1 The. 4:13-18). 13:34 "Amri mpya nawapa, Mpendane" “mpendaneni" haikuwa amri mpya (kama vile Gal. 19:18; kwa neno "amri" Tazama Mada Maalum katika Yohana 12:50). Ambacho kilikuwa kipya ni kwamba wanaoamini walipaswa kupendana kama Yesu aliyowaapenda (kama vile Yohana 15:12,17; 1 Yohana 2:7-8; 3:11,16,23; 4:7-8,10-12,19-20; 2 Yohana 5). Injili ni mtu wa kukaribishwa, mwili wa ukweli upaswao kuaminiwa, na maisha ya kuishi kwayo (kama vile. Yohana 14:15,21,23; 15:10,12; 1 Yohana 5:3; 2 Yohana 5,6; Luka 6:46). Injili inapokelawa, inaaminiwa, na inakaa nje! Ni kuishi nje katika upendo au haiishi nje! Ninapenda maandiko ya Bruce Corley'skatika makala "Biblical Theology of the New Testament" katika kitabu cha kanuni za ufasiri, Foundations For Biblical Interpretation: "Watu wa kristo wanaainishwa na maadili ya upendo, ambako thamani ya neema imehusishwa kwenye na uhalali wa upendo kupitia kazi ya Roho (kama vile. Gal. 5:6,25; 6:2; Yakobo 3:17-18; Yohana 13:34-35; 1 Yohana 4:7)" (uk. 562). 13:35 "Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu" Upendo ni sifa ambayo Shetani hawezi kufanya udanganyifu. Wanaoamini wanapaswa kuwa na sifa ya upendo (kama vile 1 Yohana 3:14; 4:7-21).

Page 239: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

223

◙ "mkiwa" Hii ni sentensi shurutishi daraja la tatu ikimaanisha kitendo muhimu. Matendo yetu kwa Wakristo wengine yanathibitisha uhusiano wetu na Yesu (kama vile 1 Yohana 2:9-11; 4:20-21).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 13:36-38 36 Simoni Petro akamwambia, Bwana, unakwendapi? Yesu akamjibu, Niendako huwezi kunifuata sasa; lakini utanifuata baadaye. 37 Petro akamwambia, Bwana, kwa nini mimi nisiweze kukufuata sasa? Mimi nitautoa uhai wangu kwa ajili yako. 38 Yesu akamjibu, Je! Wewe utautoa uhai wako kwa ajili yangu? Amin, amin, nakuambia, Jimbi hatawika hata wewe utakapokuwa umenikana mara tatu.

13:36 "Simoni Petro akamwambia" Hili ndilo la kwanza katika mfululizo wa maswali ya wanafunzi kuhusu maneno ya Yesu katika 13:31-35 (kama vile Yohana 13:36; 14:5,8,22; 16:17-19). Ninafurahi sana wanafunzi hawa waliuliza maswali haya na kwamba Yohana aliwakumbuka na kuweka kumbukumbu yao! 13:37 "Mimi nitautoa uhai wangu kwa ajili yako" Petro alimaanisha jambo hili! Lakini inaonyesha ni jinsi gani mwanadamu aliyeanguka ni dhaifu na namna gani Bwana wetu alivyojikabidhisha, na kukifanya hiki. 13:38 "Amin, amin" Tazama muhtasari katika Yohana 1:51. ◙ "Jimbi hatawika hata wewe utakapokuwa umenikana mara tatu" Hili lazima liwe Jimbi la kirumi. Wayahudi hawakuruhusu wanyama ndani ya mji kwa sababu ilikuwa ni ardhi takatifu. Ndio maana watu wengi matajiri walikuwa na bustani (zilizokua zinahitaji mbolea) nje ya kuta za mji kwenye Mlima wa mizeituni. Bustani ya Gethsemane ilikuwa bustani moja. Yesu anatumia utabiri kuhamasisha imani ndani yake.Hata kitu kilichokwenda kinyume kilidhihilisha maarifa yake na udhibiti wa matukio ya baadaye (kama vile Yohana 18:17-18, 25-27; Mt. 26:31-35; Marko 14:27-31; Luka 22:31-34).

MASWALI YA MJADALA

Huu ni mwongozo wa fasiri, ina maanisha kwamba unawajibika kwa tafsiri zako mwenyewe za Biblia. Kila mmoja wetu lazima atembee katika mwanga tulio nao. Wewe, Biblia, na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Hutakiwi uvitelekeze vitu hivi kwa mfasiri. Maswali ya mjadala huu yanatolewa kukusaidia kufikiri juu ya mambo makubwa ya sehemu za kitabu hiki. Yanalenga kukuamsha kimawazo na sio kutoa maana.

1. Kwa nini Yohana hakujali kuweka kumbukumbu ya mzunguko wa mila halisi wa ibada ya bwana? 2. Kwa nini Yesu aliwosha miguu wanafunzi? Je, na sisi tunatakiwa kuoshana miguu? 3. Kwa nini Yesu alimchagua Yuda kuwa mwanafunzi wake? 4. Tunawezaje kujua kweli kwamba yeye ni Mkristo?

Page 240: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

224

YOHANA 14

MIGAWANYO YA AYA YA TAFSIRI ZA KISASA

UBS4 NKJV NRSV TEV NJB Yesu, njia ya kwenda Njia, kweli, na uhusiano wa muumini Yesu, njia ya kwenda Maagano ya kwa baba maisha kwa Kristo wa utukufu kwa baba hotuba (13:31-14:31) 14:1-14 14:1-6 14:1-7 14:1-4 14:1-4 14:5 14:5-7 Baba anafunuliwa 14:6-7 14:7-11 14:8-14 14:8 14:8-21 Maombi yaliyojibiwa 14:12-14 Ahadi ya Roho Yesu ameahidi msaidizi Ahadi ya Roho Mwingine Mtakatifu 14:15-24 14:15-18 14:15-17 14:15-17 Akaaye ndani ya Baba na mwana 14:19-24 14:21 14:22 14:22-31 Zawadi ya amani yake 14:23-24 14:15-24 14:25-31 14:25-31 14:25-26 14:27-31a 14:31b

MZUNGUKO WA TATU WA USOMAJI KUFUATILIA KUSUDIO LA ASILI LA MWANDISHI KATIKA NGAZI YA AYA Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwatafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Aya ya kwanza 2. Aya ya pili 3. Aya ya tatu 4. N.k

HISTORIA YA NYUMA YA YOHANA 14:1-31

A. Hakupaswi kuwepo na mgawanyiko wa sura kutoka kwa Yohana 13 hadi 17 kwa sababu hii ni umoja ya kitendo cha fasihi, majadiliano ya chumba cha juu usiku wa karamu ya Bwana. Ni dhahiri kwamba maneno ya Yesu kuhusu kuondoka aliwafanya wanafunzi wawe na maswali mengi. Muktadha huu umenjengwa juu ya mfululizo wa maswali haya kwa kuzingatia kutokuelewa kwa mitume kwa maneno ya Yesu

1. Petro (Yohana 13:36) 2. Tomaso (Yohana 14:5)

Page 241: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

225

3. Filipo (Yohana 14:8) 4. Yuda (siye Iskarioti) (Yohana 14:22) 5. Baadhi ya wanafunzi wakasome (Yohana 16:17-19)

Kumbuka, Yohana hutumia majadiliano kwa kuongea kweli!

B. Maswali haya bado yanasaidia wanaoamini 1. Walionyesha kwamba hata mitume ambao walikuwa kimwili pamoja na Yesu hawakuwa muda

wote wakimuelewa. 2. Baadhi ya maneno ya Yesu ya thamani zaidi na ya kina husemwa kwa kujibu maswali haya ya

uaminifu ya kutoelewana.

C. Yohana 14 huanza na Yesu kujadili kuhusu "msaidizi" anayekuja 1. Yesu anarejea kwenye Roho Mtakatifu katika mahubiri ya chumba hiki cha juu yanahusiana moja

kwa moja ( na yenye kikomo) kwa uoga wa wanafunzi na wasiwasi kuhusiana na kuondoka kwa Yesu (kama vile Yohana 13:33,36). Michael Magill, New Testament TransLine (uk. 355) ina muhtasari wa utambuzi wa majibu ya muktadha wa Yesu kwa hofu hizi. a. "utakuwa pamoja name siku fulani ambapo nitaenda," Yohana 14:1-11 b. "itakuwa vizuri kwako kwamba ninakwenda," Yohana 14:12-17 c. "nitakuja kwako ambapo ulipo na kujidhihirisha wenyewe kwako," Yohana 14:18-26 d. "nawaachia amani yangu sasa," Yohana 14:27-31

2. Mjadala huu wa huduma ya Roho Mtakatifu una kikomo katika nafasi. Kuna vipengele vingi vya muhimu sana kwa huduma yake ambavyo havijajadiliwa kabisa katika muktadha huu.

3. Kazi ya Roho kama a. mtoaji wa ukweli na b. mfariji binafsi anayesisitizwa

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 14:1-7 1 Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. 2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. 3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. 4 Nami niendako mwaijua njia. 5 Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia? 6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. 7 Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.

14:1 "Msifadhaike" Hii ni kauli tendewa shurutishi ya wakati uliopo ikiwa na kiambata hasi ambayo mara nyingi ikimaanisha kuzuia kitendo ambacho tayari kipo katika mchakato. “Msifadhaike miyoni mwenu.” Nasaha za Yesu kuhusu kuondoka kwake kunaleta mashaka makubwa. ◙ "mioyoni mwenu” tazama hali ya uwingi. Yesu alikuwa anazungumza na wote kumi na wawili. Matumizi ya Kiebrania ya neno "moyo" huwa yanamaanisha mtu mzima: fikra, mapenzi, na hisia (kama vile Kumb. 6:5; Mathayo 22:37). Tazama Mada Maalum: Moyo katika Yohana 12:40 ◙ "mnamwamini Mungu, niaminini na mimi" Hii ama ni kauli mbili tendaji shurutishi za wakati uliopo (NASB, REB) au kauli mbili tendaji elekezi za wakati uliopo au mchanganyiko wa zote mbili (NKJV, NJB na NET Bible inasema ya kwanza ni elekezi na ya pili ni shurutishi).Imani inaendelea na ya kawaida. Muundo wa kisarufi wa uwiano wa Aya hii unaonyesha kwamba Yesu anadai kuwa sawa na Mungu.Pia kumbuka hawa walikuwa Wayahudi ambao walikuwa wamejitolea kwa imani kwamba kuna Mungu mmoja tu (kama vile Kumb. 6:4-6) na bado wakatambua kuhusishwa kwa maneno ya Yesu (tazama Mada Maalum: Utatu katika Yohana 14:26). Ni

Page 242: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

226

jambo moja la kuamini katika mamlaka na ni jambo lingine kuwa Mkristo. Fungu la maneno haya halilengi kanuni za imani ya mafundisho, bali kwa mtu wa Yesu kristo. 14:2 "Nyumbani mwa Baba yangu" Neno "nyumbani" hutumiwa katika Agano la Kale kwa kibanda au hekalu (kama vile Samweli 2.7), hata hvyo, katika muktadha huu ni wazi lina maana ya sehemu ya familia ya Mungu mbinguni au kukaa pamoja naye katika hekalu lake (kama vile Zab. 23:6; 27:4-6). NASB, NRSV "Nyumbani pa kuishi" NKJV "Makao" TEV "Vyumba" NJB "Makao mengi" Tafsiri ya KJV ya neno "makao," ni kudanganya. Neno la Kiyunani lilimaanisha " makao ya kudumu" (kama vile Yohana 14:23) pasipo wazo la utele. Picha ni kwamba wanaoamini watakuwa na vyumba vyao wenyewe katika nyumba ya Baba (kama vile TEV, NJB), kama vile nyumba ya bweni ambapo wote wanakula pamoja kila siku. Pia inafurahisha kwamba hili linatoka kwenye mzizi ule ule wa Kiyunani wa neno “kukaa” ambayo ni dhana Muhimu (kama vileYohana 15) katika Yohana. Kukaa kwetu pamoja na Baba kunakamilishwa na kukaa kwetu katika Mwana. ◙ "kama" Hii ni sehemu ya sentensi shurutishi daraja la tatu ambayo inaitwa “kinyume na ukweli." Kuna vyumba vingi vinavyopatikana. Maneno haya ni vigumu kuyatafsiri. NASB, REB, NIV "kama isingalikuwa hivyo, nisingaliwaambia" NKJV "kama isingalikuwa hivyo, nisingaliwaambia" TEV "nisingaliwaambia kama isingalikuwa hivyo" NJB, NET "vingenevyo ningaliwaambia" Young's literal Translation “na kama hivyo, ningaliwaambia” New Berkley version “kama hii isingekuwa hivyo, nisingaliwaambia” Williams Translation “kama pasingekuwepo, nisingaliwaambia” ◙ "naenda kuwaandalia mahali"Hii haimaanishi kudokeza kwamba mbinguni, kwa maana ya kimwili, haikuandaliwa kabla ya hili, bali kwamba maisha ya Yesu, mafundisho, na kifo huwawezesha wanadamu wenye dhambi kumkaribia na kukaa pamoja na Mungu aliye Mtakatifu. Yesu huenda mbele ya wanaoamini kama mwongozo wao na mtangulizi (kama vile Ebr. 6:20). 14:3 "kama" Hii ni sentensi shurutishi daraja la tatu ambayo inahusiana na tendo muhimu. Yesu amewambia kuwa anarudi kwa baba yake hivi karibuni (yaani, Yohana 7:33; 16:5,10,17,28) na atawaandalia mahali kwa ajili yao. The Help for Translators toka umoja wa Biblia juu ya Yohana na Newman and Wider kinasema kwamba kifungu hiki kinapaswa kueleweka katika maana ya muda ya neno “baada ya kwenda” au “wakati ninapoenda” au “tangu” (uk. 456). ◙"nitakuja tena niwakaribishe kwangu" Hii inarejea kuja kwa mara ya pili au kifo (kama vile 2 Kor. 5:8; 1 Thes 4:13-18). Huu ushirika wa uso kwa uso pamoja na Yesu unaonyesha ushirika wa Yesu na Baba (kama vile Yohana 1:1,2). Wakristo watashiriki katika urafiki wa karibu sana kati ya Yesu na Baba (Yohana 14:23; 17:1 na kuendelea). Kitenzi kilichotumika hapa, kupokea (paralambanō), kinadokeza "kukaribisha mtu.” Mbinguni ni mahali pa ushirika binafsi pamoja na Mungu. Hapa ni tofauti na Yohana 1:12 (lambanō). Ni vigumu kuthibitisha uingizaji wa maana halisi ya maneno haya mawili; mara nyingi ni sawa.

Page 243: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

227

◙ "nilipo mimi, nanyi mwepo" Mbinguni ndipo Yesu alipo (kama vile Yohana 17:24)! Mbinguni ni ushirika wa kweli wa uso kwa uso pamoja na Mungu wa Utatu! Agano Jipya haliliko wazi hasa ni wakati gani ushirika kamili unatokea.

1. wakati wa Kifo , 2 Kor. 5:8 2. wakati wa kuja mara ya pili, 1 Thes. 4:13-18

Biblia inashangaza ukimya juu ya maisha baada ya kifo. Kitabu kizuri kilicho elezea kwa kifupi ni William Hendriksen's, The Bible On the Life Hereafter.

MADA MAALUMU: WALIOKUFA, WAKO WAPI? (SHEOL/HADES, GEHENNA, TARTARUS)

I. Agano la Kale A. Watu wote wanakwenda shimoni (sheol) (hakuna mizizi yenye chanzo kimoja cha neno na asili ya

neno lenyewe haijulikani, BDB 982, KB 1368), ambayo ndiyo ilikuwa njia ya kurejerea mahali pale wafu wanaishi au kaburi, hasa hasa katika kitabu cha Ayubu na Isaya. Katika Agano la Kale ilikuwa ni kivuli, utambuzi, lakini maisha yasiyo na furaha (kama vile Ayubu 10:21-22; 38:17)

B. Tabia za shimoni (sheol) 1. Inahusiana na hukumu ya Mungu (moto), kumb.32:22 2. Gereza lenye vizuizi, Ayubu 38:17; Zab. 9:13; 107:18 3. eneo ambalo huwezi rudi tena, Ayu. 7:9 (sifa ya mkazi wa Akkad kwa ajili ya umauti) 4. Eneo/ulimwengu wa giza, Ayu. 10:21-22; 17:13; 18:18 5. Mahali penye utulivu, Zab.. 28:1; 31:17; 94:17; 115:17; Isa. 47:5 6. panahusiana na mateso hata kabla ya siku ya hukumu, Zab. 18:4-5 7. panahusiana na utelekezaji (maangamizo; angalia Mada Maalumu: Kutelekezwa…Apollyon),

ambapo pia Mungu yupo, Ayubu 26:6; Zab.. 139:8; Amosi 9:2 8. panahusiana na “shimo refu” (kaburi), Zab.16:10; 88:3-4; Isa. 14:15; Ezek. 31:15-17 9. waovu hushuka ndani ya shimo la sheol,Hes. 16:30,33; Ayu. 7:9; Zab.. 55:15 10. mara nyingi hujibadilisha kama mnyama mwenye mdomo mkubwa, Hes. 16:30; Mith. 1:12; Isa.

5:14; Hab. 2:5 11. kule watu huitwa Repha'im (yaani., "roho za mauti"), Ayubu 26:5; Mith. 2:18; 21:16; 26:14 Isa.

14:9-11) 12. Hata hivyo, YHWH yupo hata hapa, Ayubu 26:6; Zab.. 139:8; Mithali. 15:11

II. Agano Jipya A. Kwa Kiebrania Sheol limetafasiliwa kwa Kiyunani kama Kuzimu (ulimwengu usio onekana) B. Tabia za kuzimu (nyingi zinafanana kama za Sheol)

1. Anarejerea mauti, Mt. 16:18 2. Imehusianishwa na mauti, Ufu. 1:18; 6:8; 20:13-14 3. mara nyingi panafanana na mahali pa mateso ya milele (Gehenna), Mt. 11:23 (nukuu toka

agano la kale); Luka 10:15; 16:23-24 4. mara nyingi inafanana na kuwekwa kaburini, Luka 16:23

C. Yumkini imegawanywa na (walimu wa dini ya Kiyahudi) 1. Sehemu ya watakatifu iitwayo Paradiso (ki-ukweli ni jina lingine la Mbinguni, kama vile. 2 Kor.

12:4; Ufu. 2:7), Luka 23:43 2. Sehemu ya waovu iitwayo “kwenye vifungo vya giza”, iliyoko chini kabisa ya kuzimu, 2 Pet. 2:4,

mahali palipowekwa kwa ajili ya malaika waovu (k.v Mwanzo 6; I Enoch). Inahusiana na kutupwa “shimoni” Luk. 8:31; Rum. 10:7; Ufu. 9:1-2,11; 11:7; 17:18; 20:1,3

D. Gehenna 1. inaangazia kwenye kifungu cha agano la kale, “bonde la wana wa Hinnom (kusini mwa

Yerusalem). Palikuwa ni mahali Wafoenike walipoichoma miungu ya, Molech (BDB 574, KB 591), ilikuwa inaabudiwa wakati wa kuwadhabihu watoto (kama vile 2 Fal. 16:3; 21:6; 2 Nya. 28:3; 33:6), ambavyo ilikuwa imekataliwa katika Law. 18:21; 20:2-5.

2. Yeremia alibadili toka sehemu ya ibada ya wapagani kuwa mahali pa hukumu ya YHWH (Kama

Page 244: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

228

vile Yer. 7:32; 19:6-7). Ikajakuwa mahali pa hukumu kali, ya milele katika I Enoch 90:26-27 na Sib. 1:103.

3. Wayahudi wa enzi ya Yesu waliogopeshwa na ushiriki wa wazee wao katika ibada ya kipagani kwa kuwadhabihu watoto, kwamba waliigeuza sehemu hii kuwa sehemu ya kutupa takataka kwa ajili ya Jerusalemu. Mingi ya misemo ya Yesu kwa ajili ya hukumu ya milele ilitokana na sehemu hii iliyojaza (moto, moshi, minyoo, funza,kama vile Mk. 9:44,46). Neno Gehenna limetumiwa na Yesu tu (hasa katika Yakobo 3:6).

4. Matumizi ya Yesu juu ya neno Gehenna a. Moto, Mt. 5:22; 18:9; Mk 9:43 b. Mahali pa milele, Mk 9:48 (Mt. 25:46) c. mahali pa maangamizo (kwa mwili na roho), Mt. 10:28 d. panafanana na Sheol, Mt. 5:29-30; 18:9 e. Panaainisha waovu kama “wana wa Jehanamu” Mt. 23:15 f. Ni matokeo ya hukumu ya kimahakama, Mt. 23:33; Luk 12:5 g. Dhana ya Gehenna inafanana na mauti ya pili (kama vile Ufu. 2:11; 20:6,14) au ziwa la

moto (k.v. Mt. 13:42,50; Ufu. 19:20; 20:10,14-15; 21:8).Yawezekana ziwa la moto pakawa ndo mahali pa watu kuishi milele (wanaotoka kuzimu) na malaika waovu (waliotoka shimoni, 2 Petr. 2:4; Yuda 1:6 au shimoni, kama vile Luk 8:31; Ufu. 9:1-11; 20:1,3).

h. ilikuwa haikusanifiwa kwa ajili ya binadamu, lakini ilikuwa ni kwa ajili ya shetani na malaika wake, Mt. 25:41

E. yawezekana, kwa sababu ya kupishana kwa maneno shimoni (sheol), kuzimu(hades) na Jehanamu (Gehenna) kuwa 1. kiasili watu wote walikwenda shimoni/kuzimu 2. uzoefu wao wa (mema/mabaya) utazidishwa kwenye siku ya hukumu ya mwisho, lakini sehemu

ya watenda maovu itabaki kuwa ile ile (hi indo kwa sababu toleo la KJV linaitafasili kama kuzimu (kaburi) kama Jehanamu .

3. Andiko katika agano jipya linalotaja kuhusu mateso kabla ya hukumu ni pale penye mfano katika Luka 16:19-31 (Lazaro na mtu tajiri). Sheol pia pameelezewa kama mahali pa mateso (kama vile Kumb. 32:22; Zab. 18:1-5). Hata hivyo, mtu hawezi kutengeneza andiko juu ya mfano.

III. Hali ya mwingiliano kati ya mauti na ufufuo A. Agano jipya halifundishi juu ya “zinaa ya nafsi,” ambacho ni moja ya kitu kati ya mitazamo mingi ya

kale juu ya maisha baada ya kufa , ambapo panadaiwa kuwa 1. nafsi ya mwanadamu huwepo hata kabla ya maisha haya ya kimwili 2. nafsi ya mwanadamu ni ya milele kabla na baada ya kifo cha kimwili 3. mara nyingi mwili unaonekana kuwa gereza na mauti inaurudisha kwenye hali uliokuwanayo

kabla B. Agano Jipya linadokeza juu ya hali ya kutoungana kati ya mauti na ufufuo

1. Yesu anaongelea juu ya utengano wa mwili na roho, Mt. 10:28 2. Ibrahamu angeweza tayari kuwa na mwili, Mk. 12:26-27; Luk 16:23 3. Musa na Eliya walikuwa na mwili wa nyama kipindi Yesu anageuka sura, Mathayo 17 4. Paulo anadai kuwa kipindi cha Yesu kurudi mara ya pili, waamini watakuwa na mwili mpya, 1

The. 4:13-18 5. Paulo anadai kuwa waamini watapata mili mipya ya kiroho siku ya kufufuka, 1 Kor. 15:23,52 6. Paulo anadai kuwa waumini hawaendi kuzimu, lakini huwa wamekufa huwa na Yesu, 2 Kor.

5:6,8; Fil. 1:23. Yesu aliyashinda mauti na kuwachukuwa watakatifu akaenda nao mbinguni, 1 Pet. 3:18-22.

IV. Mbinguni A. Neno hili limetumika kwa maana tatu katika Biblia.

1. kwa maana ya anga juu ya dunia, Mwa. 1:1,8; Isa. 42:5; 45:18

Page 245: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

229

2. Mbingu yenye nyota, Mwa. 1:14; Kumb. 10:14; Zab. 148:4; Heb. 4:14; 7:26 3. Mahali pa kiti cha Enzi cha Mungu, Kumb. 10:14; 1 Fal. 8:27; Zab. 148:4; Efe. 4:10; Ebr. 9:24

(Mbingu ya tatu, 2 Kor. 12:2) B. Biblia haifunui mengi kuhusu maisha baada ya kifo, yumkini kwa sababu ya mwanadamu

aliyeanguka hana njia au uwezo wa kuelewa (kama vile 1 Kor. 2:9). C. Mbinguni kumesimama kwa yote ni mahali (kama vile Yn. 14:2-3) na mtu kamili (kama vile 2 Kor.

5:6,8). Mbinguni paweza kuwa ni bustani ya Edeni iliyorejeshwa (Mwanzo 1-2; Ufunuo 21-22). Dunia itatakaswa na kurejeshwa (k.v. Mdo.3:21; Rum. 8:21; 2 Pet. 3:10). Taswira ya Mungu (Mwa. 1:26-27) imerejeshwa katika Kristo. Sasa ushirika ule wa ndani kwenye bustani ya Edeni yawezekana ukarejea tena. Hata hivyo, huu wawezakuwa ni msemo (mbinguni kama mji mkubwa Ufu. 21:9-27) na sio halisi. 1 Korintho 15 inaelezea tofauti kati ya mwili halisi na mwili wa kiroho kama mbegu ya mti uliokomaa. Tena, 1 Kor. 2:9 (nukuu toka Isaya 64:4 na 65:17) ni ahadi kubwa na tumaini! Nafahamu kuwa tutakapomwona Yeye tutafanana naye (kama vile 1 Yoh.3:2).

V. Vyanzo vya kusaidia

A. William Hendriksen, The Bible On the Life Hereafter B. Maurice Rawlings, Beyond Death's Door

14:4 "mwaijua njia" Maneno ya Yesu yalisababisha Tomaso kuendeleza shaka lake juu ya kuijua njia. Yesu alijibu maelezo kwa maneno matatu ambayo mara nyingi hutumiwa katika Agano la Kale. 14:6 "Mimi ndimi njia" Katika agano la kale, imani ya kibiblia ilinenwa katika njia ya maisha (kama vile Kumb. 5:32-33; 31:29; Zab. 27:11; Isaya 35:8). Sifa ya kanisa la kwanza ilikuwa "njia" (kama vile Mdo. 9:2; 19:9,23; 24:14,22). Yesu alikuwa anasisitiza kwamba alikuwa na ni njia pekee ya kwenda kwa Mungu. Hiki ni kiini cha kitheolojia cha injili ya Yohana! Maisha ya kazi nzuri ni ushahidi wa imani binafsi (kama vile Efe. 2:8-9,10),si njia ya haki. Tazama maelezo katika Yohana 8:12. ◙ "kweli" Neno "kweli" katika falsafa ya Kiyunani lilikuwa na kidokezo cha neno "ukweli" dhidi ya "uwongo" au"ukweli" dhidi ya "kiini macho." Hata hivyo, hawa ni wanafunzi wa lugha ya Kiaramu ambao wangalijua Yesu akizungumza katika maana ya ukweli ya Agano la Kale ambayo ilikuwa ni "uaminifu" au "utiifu" (kama vile Zab. 26:3; 86:11; 119:30). Maneno yote "ukweli" na "maisha"huonyesha "njia." Neno "kweli" mara nyingi hutumiwa katika Yohana kuelezea shughuli za Mungu (kama vile Yohana 1:14; 4:23-24; 8:32; 14:17; 15:26; 16:13; 17:17,19). Tazama Mada Maalum: "kweli" (neno) katika Yohana 6:55 na 17:3 ◙ "uzima" Neno "uzima" ni zoā, limetumiwa na Yohana kuelezea maisha ya kizazi kipya. Katika Agano la Kale, imani ya maisha ya wanaoamini inazungumziwa kama njia ya uzima (kama vile Zab. 16:11; Mith. 6:23; 10:17). Zote tatu za haya maneno yanahusiana na imani ya maisha ambayo inapatikana pekee katika mahusiano binafsi pamoja na Yesu kristo. ◙ "mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi" Ni madai ya kutisha! Ni kizuizi sana lakini pia ni dhahiri kwamba Yesu aliamini tu kwamba kupitia uhusiano binafsi pamoja na Yeye mwenyewe mtu anaweza kumjua Mungu (kama vile Yohana 1. 5:10-12). Hii mara nyingi inaitwa kashfa ya pekee ya Ukristo. Hapa hakuna hoja kuu. Kauli hii ni ya kweli au Ukristo ni uwongo! Kwa njia kadhaa hii ni sawa na Yohana 10. 14:7 "Kama" Kuna maandiko tofauti yaliyounganishwa na aina ya sentensi shurutishi. Mashirika ya umoja wa matini ya Biblia ya Kiyunani yanasaidia sentensi shurutishi daraja la kwanza, Kama yalivyoandikwa maandiko ya kale ya Kiyunani P66, א, na D. Hii ingekuwa imetafsiriwa "kama ungalinijua mimi na sasa wanijua,basi ugemjua baba yangu, ambaye unamjua." Inaweza kuwa sentensi shurutishi daraja la kwanza ambayo mara nyingi inaitwa "kinyume na kweli." Tafsiri ingekuwa "kama ungalinijua mimi, ambaye hunijui, basi ungemjua Baba yangu, ambaye humjuii." Hii inasaidiwa na

Page 246: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

230

maandiko, A, B, C, Db, K, L, na X. Hii ni kauli ngumu kwa sababu tunadhani kwamba mitume walikuwa tayari wameamini kwa wokovu katika Yesu kama Masihi aliyetumwa na YHWH. Huu ukweli mpya na kiuhalisia ungalikuwa mgumu kwao kuweza kuuelewa. Injili ya Yohana inaonekana kuzungumzia kiwango cha imani. Mazingira yanaonekana kusaidia sentesi shurutishi daraja la pili. Pia angalia hali hiyo hiyo katika Yohana 14:2 na 28. ◙ "mngalinijua mimi" Yesu anazungumza tena na kikundi chote cha mitume (kama vile Yohana 14:9). Neno “kujua” linatumika katika hisia ya Agano Jipya, ambayo inazungumzia uhusiano wa ndani wa kibinafsi, si tu ujuzi wa utambuzi (kama vile Mwa. 4:1;Yer. 1:5). ◙ "mngalimjua na Baba" kumwona Yesu ni kumwona Mungu (kama vile Yohana 1:14-18; 5:24; 12:44-45; 2 Kor. 4:4; Kol. 1:15; Ebr. 1:3)! Yesu ni ufunuo kamilifu wa Mungu asiyeonekana. Hakuna mtu aliyemkataa Yesu anaweza kudai kumjua Mungu (kama vile 1 Yohana 5:9-12).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 14:8-14 8 Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha. 9 Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba? 10 Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake. 11 Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe. 12 Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba. 13 Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.14 Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya

14:8 "Filipo akamwambia" Inavyoonekana Fillipo (1) alitaka udhihilisho wa Mungu kwa mwanadamu kiasi fulani kama vile Musa, Isaya, au Ezekiel au (2) hakuelewa kabisa maneno ya Yesu. Yesu anajibu kwa kuthibitisha kwamba wakati Filipo alipomwona na kumjua, alikuwa amemwona na kumjua Mungu (kama vile Kol. 1:15; Ebr. 1:3)! NASB "Yatutosha" NKJV "Yatutosha" NRSV "Tutatosheka" TEV "Na hicho ndicho tunachokihitaji" NJB "Hatimaye tutatoshelezwa" Wanafunzi hawa walitaka aina fulani ya uthibitisho kama vile Mafarisayo. Hata hivyo, wanaoamini wanapaswa kutembea kwa imani na wasitegemee kwenye kuona (kama vile 2 Kor. 4:18; 5:7) katika mambo ya kiroho. Kuamini ni suala muhimu! 14:9 "Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote" Angalia hii iko katika hali ya wingi. Filipo aliuliza swali ambalo kila mmoja wao alikuwa analifikiria. ◙ "Aliyeniona mimi amemwona Baba" Hii ni kauli tendaji endelevu ya wakati timilifu na kitenzi tendaji cha wakati timilifu ambacho kinamaanisha "ameona na anaendelea kuona." Yesu anafunua kikamilifu Uungu wake (kama vile. Wakol.1:15; Waebrania 1:3). 14:10 Swali la Yesu katka Kiyunani linatarajia jibu "ndio." Tazama MADA MAALUM: "KUKAA" KATIKA MAANDIKO YA YOHANA katika Yohana 2:10 ◙ "Husadiki. . .hamsadiki" "husadiki" ya kwanza ni umoja, inarejea kwa Filipo. "hamsadiki" ya pili ni wingi, inarejea kwa kikundi cha mitume (kama vile Yohana 14:7,10).

Page 247: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

231

◙ "Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu" Yesu alikuwa anafanya kwa mbadala wa Baba katika mambo yote (kama vile Yohana 14:24; 5:19,30; 7:16-18; 8:28; 10:38; 12:49). Mafundisho ya Yesu sana yalikuwa ni maneno ya Baba (kama vile Yohana 14:24) ◙ “lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake” Ushirika huu kati ya Baba na Mwana (yaani, Yohana 7:14; 8:28; 10:38), ambao unasisitiza katika sala ya kuhani mkuu Yesu kwa Yohana 17, kuwa msingi wa "kudumu” kwa wanaoamini katika Kristo katika Yohana 15. Injili ya Yohana inafunua wokovu kama (1) mafundisho; (2) ushirika; (3) utii; na (4) uvumilivu. 14:11 “Mnisadiki" Hii ni kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopo au kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo (kama vile Yohana 14:1). Kuna utofauti a maandishi ya umuhimu fulani katika maneno ya ufunguzi ya aya hii. Baadhi ya nakala za kwanza za Kiyunani (P66, P75, א, D, L, na W) zina kitenzi tu "kuamini" zikifuatiwa na (hoti) "kwamba," ambazo zina maana kwamba wanatakiwa kukubali ukweli kuhusu umoja wa Yesu na Baba. Matini mengine ya kale (MSS A na B) yameongeza neno la wakati "ndani yangu," likionyesha kitu cha kibinafsi cha imani. Mashirika ya umoja wa Biblia ya wasomi wa Kiyunani wanaamini kwamba chaguo la kwanza lilikuwa la awali (kama vile Bruce M. Metzger's A Textual Commentary on the Greek New Testament, ambalo linatoa chaguo la alama "B" [karibu bila shaka], uk. 244). Tafsiri nyingi za kisasa zinaweka neno "ndani yangu" lakini zinaongeza "kwamba" (ambayo inaonyesha maudhui yua kuaminika). ◙ "Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe" Yesu anawaambia kuamini katika kazi zake (kama vile Yohana 5:36; 10:25, 38). Kazi yake ilikamilisha unabii wa Agano la Kale. Kazi yake ilimfunua Yeye ni nani! Mitume, kama sisi sote, tulipaswa kukua katika imani. 14:12 “Amini, amini" Tazama ukumbusho katika Yohana 1:51. ◙ "Amin. . . atafanya" Kuamini sio shughuli za akili peke yake bali ni neno la kitendo cha kudumu. Maneno "anaweza kufanya mambo makubwa zaidi” ni kauli tendaji elekezi ya wakati ujao ambayo inapaswa kutafsiriwa “atafanya mambo makubwa." Huenda hii inarejea kwa

1. mawanda ya kijiografia (kama vile Mathayo 28:18-20) 2. ujumbe wa mataifa 3. roho huwa pamoja na kila anaeamini 4. maombi ya kusihi ya Yesu (kama vile Waebrania 7:25; 9:24)

Tazama MADA MAALUM: MAOMBI, YASIYO NA UKOMO LAKINI YANA UKOMO katika Yohana 3:22, B.2 Maneno ya mwisho "atafanya" ni muhimu sana kwa Ukristo wa Kibiblia. Kama Baba alivyomtuma Mwana, Mwana akawatuma wanafunzi wake! Kuwa"katika kristo," na kuwa na "uzima wa milele," inamanisha utendaji wa"agizo kuu" moyo na fikra. Ukristo sio kanuni za imani au kitu tunachopokea siku ya mvua. Ni maelekezo mapya ya maisha, mtazamo mpya wa ulimwengu! Unabadilisha kila kitu! Inapaswa kuwa makusudi, kila siku, kuufahamu ufalme, na maisha ya dhabihu. Kanisa lazima kutwaa tena

1. huduma ya kila mwamini 2. kipaumbele cha Agizo Kuu 3. huduma ya kila siku ya isiyo ya makusudi 4. Mfanano wa kristo sasa!

14:13-14 "Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya" Angalia kwamba madai ya Yesu kwamba atajibu maombi yetu yakiegemea kwenye tabia yake. Katika Mdo. 7:59 Stefano aliomba kwa Yesu. Katika 2 Kor. 12:8 Paulo aliomba kwa Yesu. Katika Yohana 15:16 na 16:23 wanaoamini humuita Baba kwa jina na cheo. Kuomba kwa

Page 248: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

232

jina la Yesu hakukuhusisha kanuni ya nguvu za giza, alisema mwisho wa sala zetu, bali kuomba kwa mapenzi na tabia ya Yesu. Huu ni mfano mzuri wa hitaji la kushauriana na vifungu vinavyofanana kabla ya kutoa maandiko yenye kutangazwa kama imani ya kanisa juu ya masomo ya Kibiblia. Moja lazima iwiane pamoja na “chochote tunachouliza”

1. "katika jina langu" (Yohana 14:13-14; 15:7,16; 16:23) 2. "endelea kuomba" (Mathayo 7:7-8; Luka 11:5-13; 18:1-8) 3. "wawili wanakubaliana" ( Mathayo 18:19) 4. "kuamini" (Mathayo 21:22) 5. "bila shaka" (Marko 11:22-24; Yakobo 1:6-7) 6. "sio ubinafsi" (Yakobo 4:2-3) 7. "kushika amri zake" (Yohana 1. 3:22) 8. "kwa mujibu wa mapenzi yake" (Mathayo 6:10; 1 Yohana 5:14-15)

Jina la Yesu linawakilisha tabia yake. Ni njia nyingne ya kurejea kwenye fikra na moyo wa Yesu. Maneno haya yanatokea mara nyingi katika Yohana (kama vile Yohana 14:13-14,26; 15:16; 16:23-26). Zaidi unavyokua kama kristo, ndivyo namna maombi yako yatajibiwa kwa uthibitisho. Jambo baya zaidi Mungu angelilifanya kiroho kwa waamini wengi ni kujibu maombi yao ya ubinafsi, na ya kutaka vitu. Tazama ukumbusho katika 1 Yohana 3:22.

MADA MAALUMU: MAOMBI YA KUMAANISHA

A. Kuhusiana na uhusiano wa mtu binafsi na nafsi za Mungu mmoja 1. Inahusika kwenye mapenzi ya Baba

a. Mathayo 6:10 b. 1 Yohana 3:22 c. 1 Yohana 5:14-15

2. Kukaa ndani ya Yesu Yohana 15:7 3. Kuomba kwa jina la Yesu

a. Yohana 14:13,14 b. Yohana 15:16 c. Yohana 16:23-24

4. Kuomba katika roho a. Waefeso 6:18 b. Yuda 1:20

B. Inahusika na nia ya mtu binafsi 1. Kutokuyumba yumba

a. Yohana 21:22 b. Yakobo 1:6-7

2. Kuomba vibaya Yakobo 4:3 3. Kuomba kwa tama Yakobo 4:2-3

C. Inahusika na uchaguzi wa mtu binafsi 1. Ustahimilivu a. Luka 18:1-8 b. Wakolosai 4:2 c. Yakobo 2. Ugomvi nyumbani 1 Petro 3:7 3. Dhambi

a. Zaburi 66:18 b. Isaya 59:1-2 c. Isaya 64:7

Maombi yote hujibiwa, lakini si maombi yote yanazaa matunda. Maombi ni uhusiano wa pande mbili. Jambo baya kuliko yote ambalo Mungu angalifanya ni kujibu maombi ya waaminio ambayo si sahihi.

Page 249: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

233

MADA MAALUM: JINA LA BWANA

Hiki kilikuwa ni kifungu cha kawaida kwenye Agano la Kale kwa ajili ya uwepo wa Mungu na nguvu za utendaji za Mungu wa Utatu katika kanisa. Ilikuwa sio kanuni ya kimiujiza, lakini ni ombi la tabia ya Mungu kama ilivyoonekana kwa Yesu. Mara nyingi hiki kifungu kinarejerea kwa Yesu kama Bwana (kama vile Fil. 2:11)

1. Kwenye kipawa cha imani ya mtu ndani ya Yesu (kama vile Rum. 10:9-13; Mdo. 2:21,38; 8:12,16; 10:48; 19:5; 22:16; 1 Kor. 1:13,15; Yakobo 2:7)

2. kwenye upungaji pepo (kama vile Mt. 7:22; Marko 9:38; Luka 9:49; 10:17; Mdo. 19:13) 3. kwenye uponyaji (kama vile Mdo. 3:6,16; 4:10; 9:34; Yakobo 5:14) 4. kwenye tendo la huduma (kama vile Mt. 10:42; 18:5; Luka 9:48) 5. kwenye kipindi cha kulionya kanisa (kama vile Mt. 18:15-20) 6. kipindi cha kuwahubiri watu wa mataifa (kama vile Luka 24:47; Mdo. 9:15; 15:17; Rum. 1:5) 7. katika maombi (kama vile Yn. 14:13-14; 15:7,16; 16:23; 1 Kor. 1:2) 8. njia ya kurejerea Ukristo (kama vile Mdo. 26:9; 1 Kor. 1:10; 2 Tim. 2:19; Yakobo 2:7; 1 Pet. 4:14)

Chochote tukifanyacho kama wapiga mbiu, wahudumu, wasaidizi, waponyaji wenye kutoa pepo, n.k.,

tunatenda katika tabia yake, nguvu zake, —katika Jina Lake (yaani., Fil. 2:9-10)!

◙ "kama" Hii ni sentensi shurutishi daraja la tatu ambayo inamaanisha tendo kuu. ◙ "Mkiniomba neno lo lote" Kawaida wanaoamini wanahimizwa kuomba kwa Roho, kupitia kwa Mwana, kwenda kwa Baba. Aya hii ni aya pekee katika injili ya Yohana ambapo Yesu anajielekezea maombi kwake mwenyewe. Hii inaweza kuwa sababu kwa nini maandiko ya kale yamefuta/yametoa neno "mimi" (yaani. MSS, A, D, L, na baadhi ya kilatini cha kale, matoleo la Kilatini, lugha ya kiluturujia ya kanisa la Koptiki, Ethiopia, na Ulaya na Asia). UBS4 inapima viwango vyake vyote pamoja kama "B" (karibu bila shaka).Imejumuishwa katika MSS P66, P75, א, B, W, na baadhi ya kilatini cha kale, na matoleo ya Ki-shamu.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 14:15-17 15 Mkinipenda, mtazishika amri zangu. 16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; 17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.

14:15 "Mkinipenda, mtazishika amri zangu" Hii ni sentensi shurutishi daraja la tatu ambayo inamaanisha tendo kuu. Mapenzi kwa Mungu katika kristo yamelezewa kwa namna ya utii. Neno "Kushika" ni kauli tendaji elekezi ya wakati ujao limetumika kama kauli shurutishi ya wakati uliopo (Friberg, Analytical Greek New Testament, uk. 337). Utii ni muhimu sana (kama vile. Yohana 8:51; 14:21,23-24; 15:10; Yohana 1. 2:3-5; 3:22,24; 5:3; Yohana 2. 6; Luka 6:46). Yohana 14:21, 23, na 24 pia inasisitiza ukweli huo huo. Utii ni ushahidi wa mazungumzo ya kweli (kama vile Yakobo and Yohana 1). NKJV ina kauli shurutishi "shika amri zangu,” ambayo inasaidiwa na MSS A, D, W, toleo la Kilatini, na Wababa wengi wa kanisa. UBS4 inatoa kauli tendaji elekezi ya wakati ujao ya daraja la "C" (vigumu katika kuamua), ambayo imesaidiwa na MSS B, L, na toleo la Koptiki, pamoja na Baba kadhaa wa kanisa. 14:16 "naye atawapa" Tazama ukumbusho katika Yohana 14:26. NASB, NKJV, TEV "Msaidizi mwingine" NRSV "Mtetezi mwingine" NJB "Msaidizi mwingine"

Page 250: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

234

Neno “mwingine” linatafsiri neno la kiyunani (allos) ambalo linamaanisha “mwingine ya aina hiyo hiyo." Roho Mtakatifu anaitwa “Yesu mwingine” (G. Campbell Morgan, tazama Mada Maalum chini). Neno la pili ni neno la Kiyunani "paraklētos" ambalo linatumiwa na Yesu katika 1 Yohana 2:1 (kama kusihi) na kwa Roho mtakatifu katika Yohana 14:26 na 16:7-14. Asili ya neno "moja iliyeitwa kandokando kusaidia," kwa maana ya kisheria. Kwa hiyo neno “faraja” hutafsiri kwa usahihi neno hili. Kanuni ya mzizi huo huo wa Kiyunani wa neno “faraja", (parakalēo), hutumiwa na Baba katika 2 Kor. 1:3-11. Tafsiri ya jina “mtetezi” (paraklētos) inatoka kwenye mfumo wa kisheria wa kirumi. Tafsiri ya neno "mfariji" ilitumiwa kwanza na Wycliffe na inaonyesha matumizi ya kanuni za kitenzi (parakaleō) katika maandiko ya kale ya Kiyunani (yaani., 2 Sam. 10:4; 1 Nya. 19:3; Ayubu 16:2; Zab. 69:20; Wimb. 4:1; Isa. 35:4). Inaweza kuwa kinyume cha Shetani (mshtakiwa). Wote Philo na Josephus walitumia neno kwa maana ya "hisia" au "mshauri."

MADA MAALUM: YESU NA ROHO

Kuna bubujiko kati ya kazi ya Roho na Mwana. G. Campbell Morgan alisema jina zuri la Roho Mtakatifu ni "Yesu mwingine" (hata hivyo, tofauti yao, utu wa milele). Ufuatao ni mlinganisho wa mhutasari wa kazi na wadhifa wa Mwana na Roho.

1. Roho aitwaye "Roho wa Yesu" au maelezo yanayofanana (kama vile Rum. 8:9; 2 Kor. 3:17; Gal. 4:6; 1 Pet. 1:11).

2. Wote wanaitwa kwa maneno sawa a. "kweli"

1) Yesu (Yohana 14:6) 2) Roho (Yohana 14:17; 16:13)

b. "mwombezi" 1) Yesu (1 Yohana 2:1) 2) Roho (Yohana 14:16,26; 15:26; 16:7)

c. "Mtakatifu" 1) Yesu (Marko 1:24; Luka 1:35; Matendo 3:14; 4:27,30) 2) Roho (Luka 1:35)

3. Wote hukaa ndani ya waamini a. Yesu (Mt. 28:20; Yohana 14:20,23; 15:4-5; Rum. 8:10; 2 Kor. 13:5; Gal. 2:20; Efe. 3:17;Kol. 1:27) b. Roho (Yohana 14:16-17; Rum. 8:9,11; 1 Kor. 3:16; 6:19; 2 Tim. 1:14) c. Baba (Yohana 14:23; 2 Kor. 6:16)

Kazi ya Roho ni kutoa ushuhuda juu ya Yesu(kama vile Yohana 15:29; 16:13-15)

◙ "ili akae nanyi hata milele" Kuna kihusishi tofdauti hutumiwa kwa kurejea Roho mtakatifu.

1. "meta" (Yohana 14:16), "pamoja na" 2. "para" (Yohana14:17), "kwa upande" 3. "en" (Yohana 14:17), "katika"

Angalia Roho mtakatifu yuko pamoja nasi, na sisi, ndani yetu. Ni kazi ya kuonyesha maisha ya Yesu ndani ya wanaoamini. Atakaa nao mpaka mwisho wa dahari (kama vile Yohana 14:18; Mt. 28:20). Angalia Roho huitwa "Yeye." Hii ina maana Roho ni nafsi. Mara nyingi katika KJV roho hutajwa na "ni," lakini hii ni kwa sababu neno "roho" katika Kiyunani ni neno la kawaida (kama vile Yohana 14:17,26; 15:26). Yeye ni mtu wa tatu kwenye utatu (tazama Mada Maalum katika Yohana 14:26). Neno utatu sio neno la kibiblia, lakini kama Yesu ni wa Ki-Mungu na roho ni Mtu, basi aina fulani ya umoja wa utatu inahusika. Mungu ni asili moja ya Utatu lakini udhihilisho wa watatu wa kudumu (tazama, kama vile Mt. 3:16-17; 28:19; Matendo 2:33-34; Rum. 8:9-10; 1 Kor. 12:4-6; 2 Kor. 1:21-22; 13:14; Efe. 1:3-14; 2:18; 4:4-6; Tito 3:4-6; 1 Petro 1:2).Kwa "milele" tazama Mada Maalum katika Yohana 6:58

Page 251: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

235

14:17 “Roho wa kweli" "kweli" hapa ina kidokezo kile kile katika Yohana 14:6 (k.v Yohana 15:26; 16:13; 1 Yohana 4:6). Tazama Mada Maalum juu ya "kweli" katika Yohana6:55 a 17:3. Yenye ni kinyume na Shetani, baba wa uongo (kama vile Yohana 8:44). ◙ "ambaye" "Hiki" ni kitenzi kisicho chukua shamrisho kukubaliana pamoja na neno "roho" (pneuma). Hata hivyo, kwingine katika kiyunani kiwakilishi nomino cha kiume kimetumika (kama vile Yohana 14:26; 15:26; 16:7,8,13,14). Roho mtakatifu kweli sio wa kiume au kike; Yeye ni Roho. Ni muhimu kukumbuka kwamba Yeye pia ni mtu tofauti (tazama Mada Maalum: Utu wa roho katika Yohana 14:26). ◙ "ulimwengu hauwezi kumpokea" Roho mtakatifu anaweza kusitahilishwa na wale ambao wana imani katika kristo (kama vile. Yohana 1:10-12). Anatoa kila kitu ambacho anaeamini anahitaji (kama vile Warumi 8:1-11). Ulimwengu usioamini (kosmos tazama tazama Mada Maalum chini) hauwezi kuelewa na kuthamini mambo ya Kiroho (kama. 1 Wakorintho 2:14; 2 Wakorintho 4:4).

MADA MAALUMU: Matumizi Ya Paulo Ya Neno Kosmos (Dunia)

Paulo analitumia neno kosmos kwa njia tofauti tofauti. 1. Mpangilio wa vitu vyote vilivyoumbwa (kama vile Rum. 1:20; Efe. 1:4; 1 Kor. 3:22; 8:4,5) 2. Sayari hii (kama vile 2 Kor. 1:12; Efe. 1:10; Kol. 1:20; 1 Tim. 1:15; 3:16; 6:7) 3. Wanadamu (kama vile Rum. 3:6,19; 11:15; 1 Kor. 1:27-28; 4:9,13; 2 Kor. 5:19; Kol. 1:6) 4. Kuwa pamoja na kutenda kwa wanadamu mbali na Mungu (kama vile 1 Kor. 1:20-21; 2:12; 3:19;

11:32; Gal. 4:3; Efe. 2:2,12; Fil. 2:15; kol. 2:8,20-23). Inafanana na matumizi ya Yohana (yaani., 1Yohana 2:15-17)

5. Muundo wa ulimwengu wa sasa (kama vile 1 Kor. 7:29-31; Gal. 6:14; inafanana na Fil. 3:4-9, mahali ambapo Paulo anaelezea muundo wa Kiyahudi)

Kwa baadhi ya namna huu mwingiliano na ni vigumu kuainisha kila matumizi. Neno hili, kama yalivyo mengi katika mawazo ya Paulo, yaweza elezewa kwa mazingira ya haraka na sio maelezo yaliyotengenezwa awali. Misamiati ya Paulo ilikuwa ni myepesi (cf. James Stewart's A Man in Christ). Hakuwa anajaribu kutengeneza msamiati wa kithiolojia, lakini akimtangaza Kristo.

◙ "mnamtambua….mnamtambua" Huu yumkini ni uhusika mara mbili mwingine wa Yohana. Kidokezo cha kiebrania kinakuwa ndani, uhusiano wa kibinafsi (kama vile Mwa. 4:1; Yer. 1:5). Kidokezo cha Kiyunani kingalikuwa ni maarifa. Injili iko kwenye hali zote kibinafsi na kiutambuzi. ◙ "anakaa kwenu" Kukaa ni dhana muhimu katika maandiko ya Yohana (yaani, Yohana 15, tazama Mada Maalum katika 1 Yohana 2:10). Baba anakaa ndani ya Mwana, roho inakaa ndani ya wanaoamini, na wanaoamini wanakaa ndani ya mwana. Kukaa ni njeo ya wakati uliopo, sio uamuzi uliotengwa au majibu ya kihisia. ◙ "naye atakuwa ndani yenu" Hii inaweza kueleweka kama "miongoni mwenu" (wingi, kama vile NRSV rejeo) au "ndani yako" (wingi, kama vile NASB, NKJV, NRSV, TEV & NJB). Kukaa kwa anaeamini na Mungu ni ahadi nzuri sana. Agano Jipya linaonyesha kwamba watu watatu wote wa utatu wanakaa kwa wanaoamini.

1. Yesu (Mathayo 28:20; Yohana 14:20,23; 15:4-5; Rum. 8:10; 2 Kor. 13:5; Gal. 2:20; Efe. 3:17; Kol. 1:27) 2. Roho (Yohana 14:16-17; Rum,. 8:11; 1 Kor. 3:16; 6:19; 2 Tim. 1:14) 3. Baba (Yohana 14:23; 2 Kor. 6:16)

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 14:18-24 18 Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu. 19 Bado kitambo kidogo na ulimwengu haunioni tena; bali ninyi mnaniona. Na kwa sababu mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai. 20 Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu. 21 Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha

Page 252: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

236

kwake. 22 Yuda (siye Iskariote), akamwambia, Bwana, imekuwaje ya kwamba wataka kujidhihirisha kwetu, wala si kwa ulimwengu? 23 Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake. 24 Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenipeleka.

14:18 "Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu" Yesu alitimiza kila ahadi aliyofanya kwa wanafunzi siku ya jumapili jioni baada ya pasaka katika siku yake ya kwaza kuonekana katika chumba cha juu ghorofani baada ya ufufuo (kama vile Yohana 20:19-31). Baadhi ya maoni wengine, hata hivyo, waliyaona mazingira haya kama yanarejea kwenye kuja kwa Roho Mtakatifu kwenye siku ya Pentekoste (Matendo 2) au kuja kwa mara ya pili (kama vile. Yohana 14:3). 14:19 "Bado kitambo kidogo na ulimwengu haunioni tena; bali ninyi mnaniona" Yohana 14:20 inaonyesha kwamba hii ni rejea ya kuonekana kwa Yesu baada ya ufufuo. Hii ndio kauli ambayo Yuda alichukua katika Yohana 14:22 kumwuliza Yesu swali lingine. Wanafunzi bado walikuwa wanamtarajia Yeye kuanzisha ufalme wa kidunia wa ki-Masihi (yaani, Mt. 20:20-28; Marko 10:35-45) na walikuwa wamechanganyikiwa wakati aliposema, "ulimwengu hautaniona." Jibu la Yesu kwa Yuda (sio yule Iskariote) alilouliza katika Yohana 14:23 na 24 ni kwamba yeye atajidhihirisha mwenyewe katika maisha ya Wakristo binafsi na hivyo ulimwengu utamuona kupitia kwao! ◙ "Na kwa sababu mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai" Ufufuo wa Yesu ulikuwa ni uthibitisho wa nguvu za Mungu na mapenzi ya kutoa uzima (kama vile Rum. 8:9-11; 1 Kor. 15:20-23,50-58). 14:20 "Siku ile" kifungu hiki mara nyingi kimetumika katika maana ya siku za mwisho (tazama Mada Maalum hapo chini), lakini hapa inaweza kurejea uonekano wa Yesu baada ya ufufuo au kuja kwa ukamilifu wa Roho siku ya Pentekoste.

MADA MAALUM: SIKU HIYO

Kifungu, "siku hiyo" au "kwenye siku hiyo," ni namna ya manabii wa karne ya nane kuzungumzia juu ya ujirio wa Mungu (uwepo), kwa ajili ya hukumu na urejesho.

Hosea Amosi Mika

chanya hasi chanya hasi chanya hasi

1:11 1:5 1:14(2) 2:4

2:3 2:16 3:6

2:15 3:14 4:6

2:16 4:5 5:18 (2) 5:10

2:18 5:9 5:20 7:4

2:21 6:2 6:3 7:11(2)

7:5 8:3 7:12

9:5 9:11 8:9 (2)

10:14 8:10

8:13

Kipengele hiki kiuhalisia kinazungumzia juu ya manabii. Mungu anakwenda kutenda dhidi ya dhambi kwa wakati, lakini pia hutoa siku toba na msamaha kwa wale wanaopenda kubadili mioyo na matendo yao (yaani., kupokea roho mpya, mawazo mapya, na roho mpya, kama vile Ezek. 36:22-27)! Kusudi la Mungu la ukombozi na urejesho utatimilizwa! Atakuwa na watu watakaoaksi tabia Zake. Kusudi la uumbaji (ushirika kati ya Mungu na mwanadamu) utatimilizwa!

Page 253: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

237

◙ "mtatambua" Mara nyingi neno "tambua" lina kidokezo cha kiebrania cha ushirika binafsi,uhusiano wa ndani, lakini hapa kinafuatiwa na neno "kwamba" (hoti), ambalo hufafanua maudhui ya utambuzi. Neno hili, "amini," lina maana mbili. Yohana alichagua aina ya maneno kuelezea injili. Wanaoamini kumtambua yeye (kuamini katika yeye), lakini pia kutambua ukweli kuhusu yeye (kuamini kwamba). Tazama Mada Maalum katika Yohana 2:23 ◙ "mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu" Yohana mara nyingi anasisitiza juu ya umoja wa Yesu na Baba (kama vile Yohana 10:38; 14:10-11; 17:21-23). Ameongezea ukweli kwamba kama Baba na Yesu walivyojingamanisha, ndivyo navyo, Yesu na wafuasi wake wamejiungamanisha (kama vile Yohana 17)! 14:21 "Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika" Hizi ni njeo mbili endelevu za wakati uliopo. Utii ni muhimu sana (tazama ukumbusho katika Yohana 14:15). Ni ushahidi wa badiliko la kweli (kama vile Yohana 14:23). Mitume walikuwa Wayahudi na mara nyingi walitumia nahau za lugha ya kisemitiki katika maandiko yao. Maombi ya Wayahudi ambayo yalianza kila ibada yalikuwa Kumb. 6:4-5, yaitwayo shema, yaliyomaanisha "kusikia kwa ajili ya kutenda"! Hili ndio wazo la maoni ya Yohana (kama vile Yakobo 2:14-26). ◙ "na kujidhihirisha kwake" Hii inarejea ama (1) kuonekana baada ya ufufuo (kama vile Mdo. 10:40-41) au (2) kumtuma Roho mtakatifu ili kufunua na kuunda Kristo ndani ya wanaoamini (kama vile Yohana 14:26; Rum. 8:29; Gal. 4:19). ◙ Yesu aliamini na kudai kwamba Yeye ni (1) aliwakilisha; (2) alizungumza kwa niaba ya; na (3) kumfunua Baba. Kwa wanaoamini neno hili la mamlaka lililozungumzwa na Yesu lililohifadhiwa na waandishi wa kitume ni chanzo pekee cha wazi cha habari juu ya Mungu na kusudi lake. Wanaoamini wanathibitisha kuwa mamlaka ya yesu na maandiko (yanafafanuliwa vizuri) ni mamlaka halisi; sababu, uzoefu, na mila ni muhimu, lakini sio ya msingi. Kuna ugiligili kati ya kazi ya Roho na Mwana. G. Campbell Morgan alisema jina bora kabisa kwa Roho ni "Yesu mwingine."Tazama Mada Maalum katika Yohana 14:16 14:22 Tazama ukumbusho katika Yohana 14:19. ◙ "Yuda (siye Iskarioti)” hili lilikuwa jina lingine kwa Thaddaeus (kama vile Mt. 10:3; Marko 3:18). Tazama Mada Maalum katika Yohana 1:45 14:23 "Kama" Hii ni sentensi shurutishi daraja la tatu ambayo inazungumzia juu ya kitendo muhimu. Mapenzi ya wanafunzi kwa Yesu yanaonekana katika upendo wao kwa kila mmoja (kama vile Yohana 14:15,21). 14:24 "wewe" Swali la kifafanuzi ni kwamba“ ni yupi anaerejerewa" Kisarufi, kiwakilishi kipo ndani ya kitenzi, "sikia" (kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo, mtu wa pili katika wingi). Inaweza kurejea kwa

1. Watu wa ulimwengu ambao wamekataa ujumbe wa Yesu 2. Wanafunzi kama waliyokubali maneno ya Yesu kama maneno ya Baba (kama vile Yohana 14:10-11)

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 14:25-31 25 Hayo ndiyo niliyowaambia wakati nilipokuwa nikikaa kwenu. 26 Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia. 27 Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga. 28 Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba, kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi. 29 Na sasa nimewaambia kabla halijatokea, kusudi litakapotokea mpate kuamini. 30 Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu. 31 Lakini ulimwengu ujue ya kuwa nampenda Baba; na kama vile Baba alivyoniamuru; ndivyo nifanyavyo. Ondokeni, twendeni zetu.

Page 254: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

238

14:25 "Hayo ndiyo"Hii inapaswa kurejea kwenye mafundisho ya chumba cha juu (Yohana 13-17, lakini yamewekwa pamoja hasa katika Yohana 14:15:11; 16:1,4,6,25,33). 14:26 "Roho Mtakatifu" Sifa hii ya mtu wa tatu wa utatu inatokea pekee tu katika Yohana 1:33; 20:22, na hapa katika Yohana (tazama Mada Maalum: Aliye Mtakatifu katika 1 Yohana 2:20). Hata hiyo, anaitwa na majina mengine kadhaa katika injili ya Yohana (Msaidizi, Roho wa kweli, roho). Kuna vifungu kadhaa katika Agano Jipya ambavyo vinamrejea Roho katika maneno ya kibinafsi (kama vile Marko 3:29; Luka 12:12; Yohana 14:26; 15:26; 16:7-15, tazama Mada Maalum chini). Kuna maandiko mengine ambako kiwakilishi nomino cha kawaida hutumiwa na Roho kwa sababu neno la kiyunani kwa Roho (pneuma)ni cha kawaida (kama vile Yohana 14:17; Rum. 8:26). Pia, katika hatua hii ni neno kuhusu dhana ya utatu. Neno “utatu” sio neno la kibiblia, lakini katika maandiko kadhaa ufunuo wa binafsi wa Mungu mmoja wa kweli huonekana pamoja (tazama Mada Maalum chini). Ikiwa Yesu ni Mungu na Roho ni ya nafsi, basi kitheolojia kama imani kwamba kuna Mungu mmoja tu (kama vile Kumb. 6:4-6), tunalazimika kuingia katika umoja wa tatu—si onyesho endelevu, bali watu wa milele!

MADA MAALUMU: UTATU

Angalia kazi za watu hawa wote watatu katika mazingira ya pamoja. Neno “utatu,” kwanza lilibuniwa na Tertallian, sio neno la Kibiblia, lakini dhana yake imesambaa sana.

A. Injili 1. Mt. 3:16-17; 28:19 (na nyingine zinazoendana nazo) 2. Yohana 14:26

B. Matendo-Mdo. 2:32-33, 38-39 C. Paulo

1. Rum. 1:4-5; 5:1,5; 8:1-4,8-10 2. 1 Kor. 2:8-10; 12:4-6 3. 2 Kor. 1:21-22; 13:14 4. Gal. 4:4-6 5. Efe. 1:3-14,17; 2:18; 3:14-17; 4:4-6 6. 1 The. 1:2-5 7. 2 The. 2:13 8. Tit. 3:4-6

D. Petro – 1 Pet. 1:2 E. Yuda-kur. 20-21

Uwingi wa Mungu umedokezwa katika Agano la Kale A. Matumizi ya uwingi kumhusu Mungu

1. Jina Elohim liko katika wingi (angalia mada maalumu: majina ya Uungu), lakini linapotumika kumhusu Mungu mara zote unakuta lina kitenzi kilichoko katika umoja.

2. “Sisi” katika Mwa. 1:26-27; 3:22; 11:7 A. “Malaika wa Bwana” (angalia mada maalumu: Malaika wa Bwana) alikuwa mwakilishi wa Uungu

aliyeonekana 1. Mwanzo 16:7-13; 22:11-15; 31:11,13; 48:15-16 2. Kutoka 3:2,4; 13:21; 14:19 3. Waamuzi 2:1; 6:22-23; 13:3-22 4. Zakaria 3:1-2

B. Mungu na Roho wake ni nafsi tofauti, Mwa. 1:1-2; Zab. 104:30; Isa. 63:9-11; Ezek. 37:13-14 C. Mungu (YHWH) na Masiha (Adonai) nao ni nafsi tofauti, Zab. 45:6-7; 110:1; Zak. 2:8-11; 10:9-12 D. Masihi na Roho Mtakatifu ni nafsi tofauti, Zak. 12:10 E. Wote watatu wametajwa katika Isa. 48:16; 61:1

Uungu wa Yesu na nafsi/haiba ya Roho vimesababisha matatizo kwa uhalisia, kwa wale wanaamini uwepo wa Mungu mmoja (angalia mada maalumu: wanaoamini uwepo wa Mungu mmoja), kwa waumini wa awali

Page 255: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

239

1. Tertellian-ilimshusha Mwana kwa Babaye 2. Origin-aliishusha nafsi ya Uungu wa Mwana na Roho 3. Arius-anaukana Uungu wa Mwana na Roho 4. Watawa-waliamini katika ufanisi wa udhihilisho wa matukio ya Mungu mmoja kama Baba, Mwana,

na Roho Utatu ni kanuni anzilishi ya kihistoria iliyoelezewa na maneno ya Kibiblia.

1. Uungu kamili wa Yesu, ambao ni sawa na wa Baba, ulithibitishwa katika mwaka wa 325 B.K na baraza la Nicea (kama vile Yoh.1:1; Fil. 2:6; Tit. 2:13)

2. Nafsi kamili na Uungu wa Roho ambao ni sawa na wa Baba na Mwana ulithibitishwa katika mwaka 381 B.K na baraza la Constantino

3. Mafundisho ya Uungu yameelezewa kiundani katika kazi ya Augustine De Trinitate Hakika kuna muujiza hapa. Lakini Agano Jipya linathibitisha nafsi moja ya Kiuungu (wanaoamini uwepo wa Mungu mmoja) ikiwa na udhihirisho wa nafsi tatu za umilele (Baba, Mwana, na Roho

◙ "ambaye Baba atampeleka kwa jina langu" Kulikuwa na mapigano makubwa katika kanisa la kale (karne ya nne) yaliyohusu kama Roho alitoka kwa Baba (k.v. Yohana 3:34; 14:16; 16:26) au toka kwa Mwana (k.v. Yohana 15:26; 16:7; Luk. 24:49; Mdo. 2:33) . Jambo la kitheolojia katika mjadala wa Arius -- Athanasius lilikuwa ni utimilifu na Uungu wa milele na usawa kati ya Mungu Baba na Yesu Mwana.

◙ "atawafundisha yote" Huyu yampasa kuwa mwenye sifa zote za kitaaluma. Roho hawafundishi waamini katika maeneo yote ya maarifa, bali maeneo yahusuyo kweli za kiroho, hasa katika uhusiano binafsi wa Yesu na kazi, injili (kama vile Yohana 16:13-14; 1 Yohana 2:20,27).

MADA MAALUM: HULKA YA ROHO

Katika kitabu cha Agano la Kale "Roho wa Mungu" (yaani, ruach) ilikuwa nguvu ambayo ilikamilishwa kwa kusudi la YHWH, lakini kulikuwa na dokezo chache kwamba nguvu hii ilikuwa ya kibinafsi (yaani, Mungu mmoja wa Agano la Kale, tazama Mada Maalum: Mungu mmoja). Hata hivyo, katika Agano Jipya nafsi kamili na utu wa Roho unafunuliwa:

1. Anayeweza kukufuliwa (kama vile Mt. 12:31; Marko 3:29) 2. Anayefundisha (kama vile Luka 12:12; Yohana 14:26) 3. Anayeweza kubeba ushuhuda (kama vile Yohana 15:26) 4. Anaye weza kuhakikisha, huogoza (kama vile Yohana 16:7-15) 5. Anaitwa "aliye" (yaani, hos, kama vile Efe. 1:14) 6. Anayeweza kuhuzunishwa (kama vile Efe. 4:30) 7. Anayeweza kuzimishwa (kama vile 1 The. 5:19) 8. Anayeweza kumpingwa (kama vile Matendo 7:51) 9. Ni msaidizi kwa waamini (kama vile Yohana 14:26; 15:26; 16:7) 10. Anamtukuza Mwana (kama vile Yohana 16:14)

Maandiko ya Utatu (hapa kuna matatu kati ya mengi, angalia Mada Maalum: Utatu) pia yanazungumza juu ya nafsi tatu.

1. Mt. 28:19 2. 2 Kor. 13:14 3. 1 Pet. 1:2

Japokuwa neno la Kiyunani "roho" (pneuma) ni TASA, linamrejelea Roho, kitabu cha Agano Jipya mara nyingi kinatumia KIVUMISHI ONYESHI JINSI YA KIKE (kama vile Yohana 16:8,13-14). Roho ameungamanishwa na matendo ya mwanadamu. Matendo 15:28

1. Rum. 8:26

Page 256: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

240

2. Kor. 12:11 3. Efe. 4:30

Mwanzoni sana mwa kitabu cha Matendo, kazi ya Roho inasistizwa (kma katika Injili ya Yohana). Siku ya Pentekoste haikuwa mwanzo wa kazi ya Roho, buli sura mpya. Yesu alikuwa na Roho mara kwa mara. Ubatizo wake haukuwa mwanzo wa Roho, bali sura mpya. Roho ni maana kamili ya kusudi la Baba kwa ajili wa wanadamu wote walioumbwa kwa sura na mfano wake (tazama Mada Maalum: Mpango wa YHWH wa Ukombozi wa Milele)!

◙ "na kuwakumbusha yote niliyowaambia" Makusudi ya Roho ni 1. kuwafanya wanadamu kuona hatia ju ya dhambi 2. kuwaleta wao kwa Kristo 3. kuwabatiza wao katika Kristo 4. kumumba Kristo ndani yao (kama vile Yohana 16:7-15) 5. kuwasaidia Mitume kukumbuka mambo yote aliyozungumza Yesu kwao na kueleza wazi maana zake ili

wachukue kumbukumbu zake katika Maandiko (kama vile Yohana 2:22; 15:26; 16:13) Yesu mwenyewe pia aliwaagiza Mitume baada ya kufufuka Kwake, hasa kuhusiana na namna Agano la Kale linavyomlenga Yeye na lilivyokamilishwa katika Yeye (kama vile Luka 24:13 na kuendelea). 14:27 "Amani nawaachieni; amani yangu nawapa"Amani ya mwamini haihusiani na jambo, utulivu unaoegemea juu ya ahadi za Yesu na uwepo wake (kama vile Yohana 16:33; Flp. 4:7; Kol. 3:15). "amani" neno hili linatumika katika maana ya shamirisho, urejesho toka kwa Mungu, na maana ya kiima, hisia za kiulinzi au usalama katikati ya mambo magumu. Neno hili linaaksi salamu ya Kiyahudi, Shalom, ambalo lilimaanisha vyote kutokuwepo kwa matatizo na kuridhika (kama vile Yohana 20:19,21,26; 3 Yohana 14; Efe. 2:14; Hes. 6:26; Zab. 29:11; Isa. 9:6). Hili linaeleza juu ya zama mpya!

MADA MAALUMU: AMANI (AGANO JIPYA) Hili neno la Kiyunani linarejelea kutokuwepo kwa misigishano, lakini katika tafasiri ya maandiko ya kale ya Kiyunani (LXX), linadokeza amani ya ndani pamoja na Mungu na mtu mwenzako (yaani., Luka 2:14; 10:6). Agano Jipya, kama lilivyo Agano la Kale, linatumia salaam zake,"Amani na iwe kwenu" (yaani., Luka 10:5; Yohana 20:19,21,26; Rum. 1:7; Gal. 1:3) au "kutakiana heri, enendeni kwa amani" (kama vile Mk 5:34; Luka 2:29; 7:50; 8:48; Yakobo 2:16). Hili neno la asili la Kiyunani lilimaanisha "kuunganisha pamoja ushirika uliokuwa kimevunjika" (kama vile Rum. 5:10-11). Zipo njia tatu za kithiolojia ambazo Agano Jipya huzungumzia amani:

1. Kama kuhusu mtazamo wa amani yetu na Mungu kupitia kristo (kama vile Rum. 5:1; Ko. 1:20) 2. Kama dhahania ya mtazamo wa kupatanishwa na Mungu (kama vile. Yohana 14:27; 16:33; Flp. 4:7) 3. Kwamba Mungu ameunganishwa katika mwili mmoja mpya kwa njia ya Kristo, wote Wayahudi waaminio

na Mataifa (kama vile. Efe. 2:14-17; Kol. 3:15). Newman na Nida, A Translator's Handbook on Paul's Letter to the Romans, p. 92, kina hoja nzuri kuhusu "amani." "Katika Agano la Kale na katika Agano Jipya neno “amani” lina maana pana. Kimsingi unaelezea hali nzuri ya maisha ya mtu; uliasiliwa miongoni mwa Wayahudi kama kanuni ya salamu (shalom). Mtajo huu ulikuwa maana ya kina kiasi kwamba ungeweza kutumika na Wayahudi kama maelezo ya Wokovu wa kimasihi. Kwasababu ya ukweli huu ulikuwa na maana ya kina kiasi kwamba ungeweza kutumika na Wayahudi kama maelezo ya wokovu wa kimasihi. Kwasababu ya ukweli huu kuna nyakati inatumika karibu sawa na mtajo peleka “ili kuwa na uhusiano sahihi na Mungu" (uk. 92).

Page 257: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

241

◙ "nawaachieni" Grant Osborne, The Hermeneutical Spiral (uk. 21) anatengeneza mawazo bora sana kuhusu umuhimu wa muktadha katika kutambua maana ya neno. "Muktadha wa Kimantiki

Katika maana halisi, muktadha wa kimantiki ni kigezo muhimu katika utafsiri. Niliyaambia madarasa yangu kuwa kama mmoja wetu akiwa amesinzia na hakulisikia swali nililouliza, kuna nafasi ya asilimia hamsini ya kuwa sahihi kama ataamua kujibu ‘muktadha’. Neno lenyewe linachukuwa vazi kubwa la athari dhidi ya andiko. Haya kwa uzuri yaweza kusanifiwa kama mfululizo wa duara toka kwenye aya yenyewe. Kadri tunavyokwenda kuelekea kwenye kitovu, ahadi juu ya maana ya aya inaongezeka. Kwa mfano, inatambua aina ya fasihi na kumsaidia mfasiri kutambua mfanano , Lakini hizi si kama zenye kuvutia kama maandiko mengine yaliyoko kwenye aya. Kwa mfano, tunaweza kukitambua kitabu cha Ufunuo kama kitabu cha mambo ya siku za mwisho, ingawa mwisho wa Agano la Kale na Mwanzo wa Agano Jipya na Tamaduni za Kiyunani baada ya kifo ha Alexander Mkuu kuhusu mambo ya siku za Mwisho yanaleta mfanano muhimu, nyingi za alama zimechukuliwa toka Agano la Kale. Upande mwingine mwisho wa kipimo, Muktadha wa Baraka ndo huwa suluhisho la mwisho kwa maamuzi ya neno au dhana. Hakuna dhamana ye yote kuwa Paulo atumie neno kwa njia ile ile aliyoitumia katika Wafilipi 1 kama alivyofanya katia Wafilipi. Lugha kiurahisi haitumiki kwa njia hiyo, kwa kila neno, kuna maana nyingi na utumiaji wa mwandishi unategemea juu ya mazingira ya wakati huu kuliko utumiaji wake wa neno hilo katika mazingira ya nyuma. Mfano mzuri ungeweza kuwa matumizi ya neno aphiemi katika Yohana 14:27, "Amani nawaachieni," na katika Yohana 16:28, "tena nauacha ulimwengu."Kwa nadra tungeweza kutafsiri neno moja baada ya lingine, kwa matumizi yake ni kinyume kabisa. Katika kipindi cha kwanza Yesu aliwapa kitu wanafunzi, katika kipindi cha pili Yesu alikiondoa (mwenyewe!) kitu toka kwao. Hata tungelisoma neno kidogo katika matumizi yake ya kawaida (kama katika 1 Yoh. 1:9) kwa maana ya "msamaha." Aya zingine zinatusaidia sisi kuutambua mpangilio wa kimaana (vitu mbalimbali ambavyo vingemaanishwa na neno hilo), lakini muktadha wa moja kwa moja pekee ndio unaoweza kufanya ufinyu wa uwezekano wa maana halisi" (uk. 21).

◙ "Msifadhaike mioyoni mwenu" Hii ni kauli tendewa shurutishi ya wakati uliopo yenye kiambata hasi ambacho kwa kawaida humaanisha "kusitisha tendo ambalo tayari liko katika mchakato,"marudio ya Yohana 14:1. 14:28 "Kama mngalinipenda" Hii ni sentensi shurutishi dalaja la tatu, kama Yohana 14:7, inayoitwa "ki nyume cha ukweli." Itakuwa bora kwamba Yesu alikwenda kwa Baba na kumtuma Roho, hakika, kwa wakati huu hawakutambua.

◙ "kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi" Huu si usemi unaoangalia juu ya kutokuwepo usawa wa Mwana, bali usemi unaoshughulika na kazi zilizo ndani ya Utatu zinazohusiana na wokovu wa mwanadamu (kama vile Yohana 10:29-30). Udogo huu wa Mwana ulikuwa wa kipindi cha wakati tu, akiwa Zake duniani kuutimiza mpango wa ufunuo wa Mungu wa Utatu na ukombozi (kama vile Yohana 17:4-5; Flp. 2:6-11). Hata hivyo, kuna maana ambayo katika hiyo Baba, akiwa mpeleka, ni ya msingi (kama vile Yohana 13:16; 1 Kor. 15:27-28; Efe. 1:3-14). 14:29 "Na sasa nimewaambia kabla halijatokea" Hii ilikuwa kwa ajili ya kuimalisha imani yao Yohana 13:19; 16:4). 14:30 NASB "mkuu wa ulimwengu huu" NKJV, NRSV, TEV "mtawala wa ulimwengu huu" NJB "mfalme wa ulimwengu" Hii inamrejelea Ibilisi, ambaye kazi yake sasa ulimwenguni iko duniani (kama vile Yohana 12:31; 16:11; 2 Kor. 4:4, "mungu wa dunia hii"; Efe. 2:2, "mfalme wa nguvu ya anga"). Bila shaka, Yesu alikuona kuondoka kwa Yuda kama ujio wa Ibilisi (kama vile Yohana 13:27). Tazama Mada Maalumu katika Yohana 12:31

Page 258: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

242

NASB, NKJV "hana lolote Kwangu" NRSV, TEV, NJB "hana nguvu juu yangu" Maana yake ni kwamba Ibilisi hana mashtaka ya msingi, hana nguvu juu yake, au hana mazoea na Yesu hata kidogo (kama vile Ebr. 4:15).

1. James Moffatt alilitafsiri kama "hakuna chochote alichokipata kutoka kwangu" 2. William F. Beck kama "hana dai lolote juu Yangu" 3. New English Bible kama "hana haki juu yangu" 4. the Twentieth Century New Testament kama "hana chochote kinacho tuunganisha"

14:31 "Lakini ulimwengu ujue" Ibilisi yu ndani ya mapenzi ya Baba na amechiliwa kwa kusudi kuu la Mungu katika ukombozi wa mwanadamu. Tazama A. B. Davidson, The Theology of the Old Testament, kr. 300-306.

◙ "na kama vile Baba alivyoniamuru; ndivyo nifanyavyo" Haya yalikuwa mapenzi ya Baba kwamba Yesu afe (kama vile Isa. 53:10a,b; Marko 10:45; 2 Kor. 5:21). Tazama MADA MAALUMU: MATUMIZI YA NENO “AMRI” KATIKA MAANDIKO YA YOHANA katika Yohana 12:50)

◙ "Ondokeni, twendeni zetu" Hii ni kauli shurutishi ya kati ya wakati uliopo. Hii ni aya ngumu sana kwa sababu imejitokeza katika Mathayo na Marko katika Bustani ya Gethsemane pale Yuda na kikosi cha askari walipomkaribia Yesu. Je! kwa nini aya hii inatumika hasa katika muktadha wa chumba hiki cha juu (ghorofani) (Yohana 13-17) mazingira hayadhihirishi. Bila shaka, Yesu aliondoka katika chumba cha juu (ghorofani) na kwenda kufundisha kandokando ya njia ielekeayo Gethsemane (kama vile Yohana 18:1).

MASWALI YA MJADALA

Huu ni mwongozo wa fasiri, ina maanisha kwamba unawajibika kwa tafsiri zako mwenyewe za Biblia. Kila mmoja wetu lazima atembee katika mwanga tulio nao. Wewe, Biblia, na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Hutakiwi uvitelekeze vitu hivi kwa mfasiri. Maswali ya mjadala huu yanatolewa kukusaidia kufikiri juu ya mambo makubwa ya sehemu za kitabu hiki. Yanalenga kukuamsha kimawazo na sio kutoa maana

1. Eeza tofauti iliyopo kati ya Imani inayokiri kuwepo kwa Mungu na mamlaka Yake, Imani inayokiri kuwepo kwa Mungu na kukana Mafunuo Yake na Ukristo unaoegemea juu ya Yohana 14:1.

2. Eleza usuli wa majina matatu ya Agano la Kale yanayopatikana katika Yohana 14:6. 3. Je! mtu anaweza kujenga theolojia ya maombi juu ya Yohana 14:13 pekee? 4. Je! Nini kusudi kuu la Roho Mtakatifu? (kwa wote waliopotea na waliookolewa) 5. Je! Ibilisi yu ndani ya mapenzi ya Mungu?

Page 259: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

243

YOHANA 15

MIGAWANYO YA AYA YA TAFSIRI ZA KISASA USB4 NKJV NRSV TEV NJB

Yesu mzabibu wa mzabibu wa kweli Mpangilio wa maisha Yesu mzabibu wa Mzabibu wa kweli Kweli ya Mkristo anayeamini kweli 15:1-10 15:1-8 15:1-11 15:1-4 15:1-7 Upendo na furaha 15:5-10 Vimekamilishwa 15:9-17 15:11-17 15:11-17 15:12-17 Chuki ya ulimwengu Chuki ya ulimwengu Chuki ya ulimwengu Wanafunzi na Ulimwengu 15:18 – 16:4a 15:18-25 15:18-25 15:18-25 15:18-25 Kutataliwa kunakokuja 15:26-16:4a 15:26-16:4 15:26-27 15:26-16:4a

MZUNGUKO WA TATU WA USOMAJI KUFUATILIA KUSUDIO LA ASILI LA MWANDISHI KATIKA NGAZI YA AYA Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwatafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Aya ya kwanza 2. Aya ya pili 3. Aya ya tatu 4. N.k

UTAMBUZI WA KI-MUKTADHA WA YOHANA 15:1-27

A. Hii ni aya ya ajabu na yenye kusumbua, inawapa waumini hamasa kubwa ya upendo wa Mungu na ahadi za utendaji wa nguvu, lakini pia ina maonyo yenye kuogofya. Desturi za kithiolojia ni ngumu sana kuzijadili kwenye eneo hili; acha nimnukuu mmoja wa wafasiri wangu nimpendaye, F. F. Bruce katika kitabu chake Answers to Questions. Yohana 15: 4, 6. Msemo huu unamaanisha nini “msipokaa ndani yangu” na “kama mtu hakai ndani yangu”katika Yohana 15:4,6? Inawezekana ni kutokukaa ndani ya Kristo? Mafungu kama haya si magumu kama yalivyo; ugumu unaibuka pale tunapojaribu kuyafanya yenyewe pamoja na maandiko mengine yaoane na thiolojia yetu, badala ya kuyatumia kama msingi wa thiolojia yetu. Katika wakati ule ambao Bwana wetu alikuwa anazungumza, palikuwepo na mfano uliokaziwa macho sana wa mtu aliyeshindwa kukaa ndani yake---Yuda Iskariote, ambaye alikuwa amewaacha. Yuda alikuwa amechaguliwa kama vile wenzake kumi na mmoja walivyokuwa wamechaguliwa (Luka 6:13; Yohana 6:70), Ushirikiano wao na Bwana haukuwaletea manufaa ambayo hayakuwa wazi kwake.Mafungu yaliyo wazi ya maandiko yaliyofundisha uvumilivu wa mwisho wa watakatifu hayapaswi kutumiwa visivyo kama kisingizio kuchukulia kwa wepesi mafungu yaliyo wazi yanayozungumzia hatari ya uasi” (71-72)

Page 260: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

244

B. Inashangaza jinsi njeo za wakati uliopita usio timilifu zinavyotumika katika mazingira ambayo mtu

angetarajia kithiolojia njeo za wakati uliopo. Wakati uliopita usio timilifu unaonekana kutumika kwenye maana ya kujumlisha maisha yote ya mtu na kuyatazama kwa ujumla.

C. Migawanyo ya mafungu ya Yohana 15 hayana uhakika, Yohana kama Yohana 1 ni zulia la ukutani lenye

rangi mbalimbali, mipangilio huonekana tena na tena

D. Msemo huu “kukaa ndani yangu” (menō) imetumika katika .Agano Jipya takribani mara 112. Aarobaini ya hii imeonekana katika injili ya Yohana na mara 26 katika nyaraka zake. Huu ni msemo mkuu wa kithiolojia wa Yohana. Ijapokuwa Yohana 15 ni maneno ya hali ya juu ya mamlaka ya Yesu kwamba tuendelee ndani yake, neno hili lina mtazamo mpana katika Yohana

1. Sheria inadumu milele (Mathayo 5:17-18 pia Kristo (12:34) 2. Kitabu cha Waebrania hueleza njia mpya ya Ufunuo, si kupitia kwa mtumishi bali kupitia mwana

aishiye ndani (Waebrania 1:1-3) pia Yohana 8:35 3. Yesu alisema kutoa chakula kidumucho hata milele (Yoh 6:27) na huzaa matunda yadumuyo

(15:16) stiari zote mbili zafafanua ukweli ule ule, uhitaji wetu kwa Kristo: (1) Mwanzoni na (2) Kuendelea (kama vile Yohana 6:53)

4. Yohana mbatizaji alimwona Roho akishuka na kukaa juu ya Yesu katika ubatizo wake (Yohana 1:32)

E. Tazama Mada Maalum: "Kudumu" katika 1 Yohana 2:10.

F. Katika Yohana 15:11-16 wanafunzi wanaahidiwa furaha ya Yesu, ambapo katika 15:17-27 wanafunzi

wanaahidiwa mateso ya Yesu. Mazingira haya ya mateso yanakwenda mpaka Yohana 16:4a. Hata hivyo kupitia kwa hayo wote wanaoamini wanapaswa kupendana wao kwa wao kama vile yeye alivyowapenda.

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 15:1-11 1Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima. 2 Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa. 3Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia. 4Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. 5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. 6 Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea. 7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. 8 Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu. 9 Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu. 10 Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake. 11 Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe.

15:1 “Mimi ndimi mzabibu wa kweli” Huu ni mmoja wa misemo maarufu ya Yesu ya “Mimi ndimi” misemo iliyo katika injili ya Yohana 4:26, 6:35, 8:12, 10, :7, 9,10, 11, 14:11-25; 14:6) Katika Agano la kale mti wa mzabibu ulikuwa alama ya Israeli (Zab. 80:8-16; Isa. 5:1-7; Yer. 2:21; Ezek. 15:19:10; Hos. 10:1; Mathayo 21:33 na kuendelea: Marko 12:1-12; Warumi 11:17 na kuendelea). Katika Agano la Kale mifano hii kila wakati ilikuwa na vidokezo hasi. Yesu anathibitisha kwamba Yeye ndiye alikuwa Mwisraeli halisi (kama vile Isaya 53). Kama vile Paulo alivyotumia mwili wa Kristo, bibi-arusi wa Kristo na akimjengea Mungu kama sitiari ya kanisa, hivyo basi Yohana anatumia mzabibu. Hii inadokeza kwamba kanisa ndilo Israeli ya kweli kwa sababu ya uhusiano wake kwa Yesu, mzabibu wa kweli (kama vile Gal. 6:16, 1 Petro 2:5, 9; Ufu. 1:6) Tazama Mada Maalum katika Yohana 6:55 na 17:3. Tazama vielelezo katika Yohana 8:12.

Page 261: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

245

Baadhi ya watafsiri wamedai kwamba ujumbe wa chumba cha ghorofani unaishia katika injili ya Yohana 14:3;, “tuondokeni hapa.” kama ndivyo, basi Yohana 15-17 ilifundishwa walipokuwa njiani kuelekea Gethsemane. Tena, kama ndivyo, basi inawezekana picha ya “mzabibu” ilikuwa alama iliyoonekana ikiwa imetwaliwa kutoka kwenye mizabibu ya thamani sana juu ya jengo la hekalu wakati Yesu na wale kumi na mmoja walipotembea viwanja vya hekalu usiku ule. ◙ “Na Baba yangu ndiye mkulima” Tena Yesu anakiri uhusiano wake wa karibu sana na Baba na wakati huo huo kujitiisha kwake katika mapenzi ya Baba Yake. 15:2 “Kila tawi ndani yangu lisilozaa matunda, yeye huliondoa ... lile lizaalo matunda” Hii ni kauli tendewa endelevu ya wakati uliopo inatokea maradufu katika aya hii. Matunda ya kuzaa, sio kuota, ni ushahidi wa wokovu (kama vile Mt. 7:16,20; 13:18 na kuendelea; 21:18-22; Luka 6:43-45). Mazingira yanaonyesha kwamba Yesu alikuwa anazungumzia kuhusu (1) usaliti wa Yuda (kama vile Yohana 15:6; 13:10; 17:12 au (2) wanafunzi wa uongo (kama vile (Yohana 2:23-25; 8:30-47; 1 Yohana 2:18; 2 Petro 2). Kuwa viwango vya kuamini katika injili ya Yohana. ◙ “Yeye hupogolea mzabibu” Hii ni sawasawa na “kusafisha.” Neno lilitumiwa na Philo kwa kupogolea mzabibu (BDBD 386). Linapatikana hapa katika Agano Jipya tu. Ni neno lingine lililochaguliwa na Yohana kwa ajili ya vidokezo vyenye umilikiwa vitu viwili (yaani, kupogolea na kusafisha, kama vile Yohana 15:3; 13:10) hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo. Kuteseka kwa makusudi katika maisha ya wanaoamini (kama vile. Yohana 15:17-22). Kunazidisha uzaaji wa matunda, kunafunua wasio wa kweli, kuwafanya wamtegemee Mungu (kama vile Mathayo 13:20-23; Warumi 8:17 1 Petro 4:12-16). Kwa kutumia vitabu vizuri viwili vya utekelezaji kuhusu somo hili gumu, Tazama (1) Principles of Spiritual Growth by Miles Stanford and (2) The Christian's Secret of a Happy Life by Hannah Whithall Smith. Inawezekana kwa sababu ya mazingira yaliyounganishwa ya Yohana 13:17 kuhusiana na huku kusafisha na kuosha miguu katika Sura ya 13. Walikuwa wamekwisha ogeshwa tayari (okolewa) lakini miguu yao ilihitaji kusafishwa (msamaha endelevu). Njeo ya wakati uliopo inawatambulisha wanafunzi kama 1 Yohana 1:9 inavyoonekana kuthibitisha. Sio utii tu unaohitajika katika “kukaa” bali kuendelea kufanya toba pia! Kusudi la mateso katika maisha ya waamini inaweza kuwa na mambo kadhaa

1. Endeleza kufanana kama Kristo. (kama vile Waebrania 5:8) 2. Adhabu ya kidunia kwa ajili ya dhambi 3. Maisha ya kawaida katika ulimwengu ulioanguka

Ni vigumu mara kwa mara kugundua kusudi la Mungu, lakini ndio mara kwa mara tokea liwezekanalo. 15:3 “Ninyi mmekwisha kuwa safi” Neno hili “huwapogolea” (kathairō) katika Yohana 15:2 ni sawa na mzizi wa Kiyunani kama “safisha” (katharos). Muktadha mzima unao ushahidi wa wanafunzi wa kweli. Neno hili “tayari” linasisitizwa katika maandishi ya Kiyunani ambayo yaliwapatia wanafunzi kumi na moja waliosalia ujasiri wa nafasi yao salama ndani ya Kristo (ikilinganishwa na mzizi ule mmoja uliotumika wa Yuda Iskariote katika Yohana 13:10) ◙ “Kwa sababu ya neno lile nililowaambia” (kama vile Yohana 17:17; Waefeso 5:26; Petro 1. 1:23) 15:4 NASB, NKJV “Kaeni ndani yangu na mimi ndani yenu” NRSV “Kaeni ndani yangu kama nikaavyo ndani yenu” TEV “Bakini ndani yangu kama nilivyo ndani yenu” Hii ni kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopita usiotimilifu iliyoko katika hali ya wingi (kama vile Yohana 6:56, 1 Yohana 2:6). Swali la kisarufi ni kama kifungu cha pili ni maelezo au ulinganisho. Mara nyingi katika aya hii mafundisho ya kithiolojia yanayosisitiza juu ya ustahilivu wa mtakatifu wa kweli yana shida (kama vile Yohana 15:4, 5, 6, 7, 9, 10, 14; Marko 13:13; , 1 Kor. 1.15:2; Gal. 6:9; Ufu. 2:7, 11, 17, , 26; 3:5, 12, 21; 21:7, tazama mada maalum katika Yohana 8:31). Wokovu wa kweli ni kwa yote mawili, mwitikio wa pale mwanzo na uendeleaji katika

Page 262: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

246

wokovu. Ukweli huu wa kithiolojia mara nyingi unapuuzwa katika shauku zetu za uhakika binafsi wa wokovu. Uhakika wa Kibiblia umehusishwa na

1. Ustahimilivu katika imani 2. Mtindo wa maisha ya toba 3. Utii unaoendelea (endelevu) (kama vile Yokobo na 1 Yohana) 4. Kuzaa matunda {kama vile Mt. 13:23)

Tazama Mada Maalum juu ya "kudumu" katika 1 Yohana 2:10. ◙ “Tawi haliwezi kuzaa matunda” Hii inaonesha kipaumbele cha ugawaji wa ki-Ungu. Kuhusu “tunda” Tazama malengo kwenye Yohana 15:5 ◙ “Lisipokaa ndani ya”… “msipokaa ndani yangu” hizi ni sentensi shurutishi daraja la tatu, ambazo zinamaanisha kitendo muhimu. Uwezo wetu wa utendaji kiroho unahusianishwa na uendelevu wa uhusiano wetu na Yesu. 15:5 “Yeye akaaaye ndani yangu, nami ndani yake, huzaa matunda mengi” Hii ni kauli tendaji endelevu ya wakati uliopo ikifuatiwa na kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo. Ushirika unaoendelea (yaani, uhusiano wa imani ya mtu binafsi) ni chanzo cha matunda yanayoendelea. Matunda yangeweza kufananishwa na tabia au mtazamo wa wanaoamini sawasawa na matendo (kama vile Mt. 7:17-23, Gal. 5:22-23, 1 Wakorintho 1. 13). Waaminio wameahidiwa matunda yadumuyo yenye matokeo endapo watakaa ndani yake (kama vile Yohana 15:16) ◙ “Kwani pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya lolote” Hii ni kauli iliyoko kinyume yenye nguvu. Huu ni usemi ulioko kinyume kwenye ukweli halisi wa Yohana 15:5 na Wafilipi 4:13. 15:6 “Endapo mtu ye yote anapoacha kukaa ndani yangu hutupwa mbali” Hii ni sentensi shurutishi daraja la tatu. Miti ya mizabibu haikufaa kwa matumizi yoyote ya nyumbani (kuni) kwa sababu iliungua haraka sana na kutoa moto mkali (kama vile Ezekiel 15). Hii inaonekana kuwa rejeo la Yuda na yumkini Israeli. Kama sivyo lazima iwe inafanyiwa rejea kwa imani za uongo (kama vile Mt. 13:41-42, 50; na 1 Yoh. 2:19). Hii kwa hakika ni picha ya siku za mwisho! Kutakuwepo na “siku ya kusanyiko” na “siku ya kuchomwa moto.” Jinsi tunavyoishi inafunua chanzo cha maisha yetu (yaani, Mungu au Shetani). Kwa matunda utawatambua (kama vile Mathayo 7; Gal. 6:7) ◙ “moto” Tazama Mada Maalumu hapa chini.

MADA MAALUM: MOTO (BDB 77, KB 92)

Moto unavyo vidokezo chanya na hasi katika maandiko. A. Chanya

1. Husisimua (kama vile Isaya 44:15; Yohana 18:18) 2. Huwasha nuru (kama vile Isaya 50:11; Mathayo 25:1-13) 3. Hupikia (kama vile Kutoka 12:8; Isaya 44:15:16; Yohana 21:9) 4. Husafisha (kama vile Hes 31:22-23; Mithali 17:3; Isaya 1:25; 6:6-8; Yer 6:29; Malaki 3:2-3) 5. Utakatifu wa Mungu (kama vile Mwa. 15:17; Kutoka 3:2; 19:18; Ezek. 1:27; Waebrania 12:29) 6. Uongozi wa Mungu (kama vile Kutoka 13:21; Hes. 14:14; 1 Wafalme 18:24) 7. Uwezeshaji wa Mungu (kama vile Mdo. 2:3) 8. Ulinzi wa Mungu (kama vile Zekaria 2:5)

B. Hasi 1. Huunguza (kama vile Yoshua 6:24; 8:8; 11:11; Mt. 22:7 2. Huangamiza (kama vile Mwa. 19:24; Walawi 10:1-2) 3. Hasira (kama vile Hes. 21:28; Isaya 10:16; Zek 123:6) 4. Adhabu (kama vile Mwa 38:24; Walawi 20:14; 21:9; Yoshua 7:17

Page 263: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

247

5. Ishara ya mbaya ya siku ya mwisho (kama vile Ufunuo 13:13) C. Hasira ya Mungu dhidi ya dhambi mara nyingi hudhihirishwa kwa tanuru ya moto.

1. Hasira yake huunguza (Kama vile Hos 8:5; Sefania 3:8) 2. Humimina moto (kama vile Nahumu 1:6) 3. Moto wa milele (kama vile Yer. 15:14; 17:4; Mt. 25:41; Yuda aya ya 7) 4. Hukumu ya siku ya mwisho (kama vile Mt. 3:10; 5:22; 13:40; Yohana 15:5; Thes. 2. 1:7; Petro 2. 3:7-

10; Ufu. 8:7; 16:8; 20:14-15) D. Moto mara nyingi huonekana katika tanuru

1. Mwa. 15:17 2. Kutoka 3:2 3. Kutoka 19:18 4. Zaburi 18:7-15; 29:7 5. Ezek. 1:4, 27; 10:2 6. Ebr. 1:7; 12:29

E. Kama sitiari yingi katika Biblia (yaani chachu, simba) moto unaweza kuwa Baraka au kufuatana na mazingira au muktadha.

15:7 “mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu” Hii ni sentensi shurutishi daraja la tatu yenye kumaanisha kitendo muhimu. Maombi hayajibiwi papo kwa papo! Yesu anageuza sitiari kutoka kwake na kukaa ndani ya wanafunzi kwa maneno ya kukaa. Yesu anamfunua Baba na, vinyo hivyo pia, kwenye mafundisho yake. Ni vyanzo vya ufunuo vinavyobadilishana. Injili na mtu na pia ni ujumbe. ◙ “Ombeni lo lote mtakalo na mtatendewa” Hii ni kauli ya kati shurutishi ya wakati uliopita usiotimilifu (kama vile Yohana 15:16). Fungu hili limehakikiwa vibaya. Kuwa mwangalifu kutafuta fundisho la maandiko yote na usisisitize kwenye maandiko yaliyotengwa tu (kama vile maneno ya kukumbuka katika Yohana 14:13) Tazama Mada Maalum: Maombi. Yasiyo na Mipaka Tena yana Mipaka katika 1 Yohana 3:22 15:8 “Baba yangu anatukuzwa/anapewa utukufu” Maisha ya wanaoamini yenye kufanana na Kristo huleta utukufu kwa Mungu na kuthibitisha kwamba wao ni wanafunzi wa kweli. Katika Yohana 13:31-32, 14:13; 17:4 na Mt. 9:8; 15:31 Baba alitukuzwa katika kazi ya mwana na sasa katika kazi ya wanaoamini (kama vile Mt.5:16). Tazama maelezo ya kukumbuka katika Yohana 1:14 NASB, “hivyo thibitisheni kuwa wanafunzi wangu” NKJV, TEV “Iweni wanafunzi wangu” NJB “Muwe wanafunzi wangu” REB “Hivyo muwe wanafunzi wangu” NIV Good speed “Mkijionyesha kuwa wanafunzi wangu” NET Bible “Onyesheni kwamba ninyi ni wanafunzi wangu” JB “Hapo mtakuwa wanafunzi wangu” Tofauti zinasababishwa na mabadiliko ya njeo katika kitenzi.

1. kitenzi tegemezi cha wakati uliopita usiotimilitu, MSS P66, B, D, L 2. kitenzi elekezi cha wakati ujao, MSS N,A

Maisha (matunda) ya wanaoamini yanafunua wao ni nani! Njeo ya kitenzi sio muhimu kama uhalisia wa maisha yaliyobadilika na yenye kuleta matokeo ya upendo, utii, na huduma. Hizi ni alama za waamini wa kweli! Hatuokolewi kwa upendo wetu, utii, huduma (kama vile Efe. 2:8, 9 bali huu ni ushahidi kwamba sisi tu waamini (kama vile Efe. 2:10) Neno “wanafunzi” linatumika katika injili ya Yohana kuwatambulisha wale ambao ni waamini wa kweli na wafuasi ambao wanafanya mapenzi ya Mungu na kuakisi tabia Yake. Yohana hatumii neno “kanisa” (ekklēsia)

Page 264: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

248

hata mara moja, kwa hiyo “wanafunzi” linakuwa njia ya kutambulisha ushirika wa Kikristo na makusanyiko ya Kikristo. Uanafunzi ni maisha ya kila siku ya kizazi kipya wanayoishi kutoka katika kizazi kilichopita. Yanaainishwa kwa kiwango cha juu kwa upendo,nuru, utii na huduma. Kwa haya wengine watawajua kama wanafunzi wa Yesu 15:9 “Kama vile Baba yangu alivyonipenda name pia nimewapenda ninyi” Mfululizo huu wa uhusiano wa upendo unaainishwa kwa tabia ya familia ya Mungu; Baba anampenda mwana, mwana anawapenda wafuasi wake, Wafuasi wake wanapendana kila mmoja na mwenzake. ◙ “Kaeni ndani ya upendo wangu” Hiki ni kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopita usiotimilifu. Wanaoamini wanaamurishwa kukaa ndani ya

1. Maombi (Yohana 15:7; 14:14) 2. Utii (Yohana 15:10, 14, 17, 20,; 14:15, 21, 23, 24) 3. Furaha (Yohana 15:11) 4. Upendo (Yohana 15:12; 14:21, 23, 24)

Haya yote ni ushahidi wa uhusiano wa mtu binafsi na Mungu. Tazama Mada Maalum: "Kudumu" katika Yohana 1 yohana 2:10 15:10 “Mkizishika amri zangu” Hii ni sentensi shurutishi daraja la tatu ambayo inamaanisha kitendo muhimu. Utii ni ushahidi wa wanafunzi wa kweli (kama vile Yohana 8:31; 14:15, 23-24; Luka 6:46) Yesu anatumia ushahidi huu kama mfano wa uaminifu wake kwa Baba yake. ◙ “Upendo” Neno la Kiyunani kwa upendo (agapē) halikutumika daima katika daraja la juu au fasihi ya kabila la kawaida la Kiyunani hadi pale kanisa lilipoanza kutumia katika maana yake maalumu. Lilianza kutumika kama kutojali nafsi yako, na kujitoa dhabihu, uaminifu/utiifu, upendo katika utendaji. Upendo ni kitendo, sio mhemko (kama vile Yohana 3:16. Neno agapē katika Agano jipya kithiolojia ni mfanano katika agano la kale wa neno hesed, lililomaanisha upendo Agano na utii. ◙ “Kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu” Hii ni kauli tendaji timilifu elekezi. Kama Yesu anavyojihusisha na Baba, waamini wanapaswa kujihusisha na Yeye. Kuna umoja kati ya Baba na mwana ambao umekusudiwa kufanywa miongoni mwa wanaoamini (kama vile Yohana 14:23) 15:11 “Furaha yenu ikamilishwe” Wanaoamini lazima wawe na furaha ya Yesu (kama vile Yohana 17:13). Furaha ni ushahidi mwingine wa uanafunzi wa kweli (kama vile Yohana 15:11 [maradufu]; 16:20, 21, 22, 24, 17:13). Ndani ya ulimwengu huu yapo maumivu na machafuko; ndani ya Kristo kuna furaha, furaha kamili, furaha yake. NIDOTTE (New International Dictionary of Old Testament Theology and Exegesis), juzuu. 1, uk. 741, ina maoni mazuri kuhusu ni namna gani “furaha”, na “kukamilishwa” yanavyotumika pamoja katika maandishi ya Yohana. “Katika Yohana na nyaraka za Yohana kuna ushirikiano au muunganiko wa mara kwa mara kati ya → furaha (chara) kama kiima na kitenzi plēroō kwenye aya, kujazwa. Furaha hii ni furaha ya Yesu (kama vile Yohana 15:11; 17:13) ambayo anaileta kupitia kuja kwake (13:29) maneno yake (15:11; 17:13) na kurudi kwake (16:22) kwa wanafunzi wake (15:11; 17:13) inachukua nafasi ya huzuni inayojaza mioyo yao (16:16, 20). Hivyo furaha ya Kristo inakuwa furaha yao (15:11; 16:24; kama vile Yohana 1. 1:4). Furaha hii itadhihirisha tabia ya maisha ya wanafunzi katika kutembea kwao na Yesu; inakuwa kamili (Yohana 3:29; 15:11; 16:24; 17:13; 1 Yohana 1:4; 2 Yohana 12). Kifungu kinathibitisha ukweli kwamba ni Mungu anayekamilisha suala hili.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 15:12-17 12Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi. 13 Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. 14 Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo. 15 Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu. 16Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni. 17 Haya nawaamuru ninyi, mpate

Page 265: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

249

kupendana.

15:12 “Hii ndiyo amri yangu” Yesu alirudia msemo huu mara kwa mara (kama vile Yohana 13:34; 15:17; Yohana 1.3:11, 23; 4:7-8, 11-12, 19-21, 2 Yohana 5) ◙ “Kwamba mnapendana ninyi kwa ninyi” Hii ni kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopo, amri endelevu. Upendo ni tunda la Roho (kama vile. Wag 5:22) Upendo sio hisia, bali ni utendaji. Inafafanuliwa katika maneno ya kiutendaji (kama vile Gal. 5:22-23; 1 Kor. 1. 13) ◙ “Kama vile nilivyowapenda ninyi” Huu ni kauli tendaji elekezi ya wakati uliopita usiotimilifu. Pengine huu ulikuwa msemo wa kitamathari tu uliorejelewa pale msalabani (kama vile Yohana 15:13), Tena ilikuwa namna maalum ya upendo binafsi uliotolewa na Yesu ambao wanaoamini wanapaswa kuonyesha hadharani (kama vile 2 Kor. 5:14-15, Gal. 2:20, 1 Yohana 3:16) 15:13 “Kwamba mtu autoe uhai wake kwa ajili ya rafiki yake” Hii inahusu kujitoa kwa Yesu kama sadaka kwa ajili ya wengine na badala yao (kama vile Yohana 10:11, 15; 17:18; Marko 10:45; Rum. 5:7-8; 2 Kor. 5:21; Isaya 53) Huu ni upendo katika vitendo! Hiki ndicho ambacho wanafunzi wameitwa kukifanya (kama vile 1 Yohana 3:16) 15:14 “Ninyi ni rafiki zangu” Hii ni nomino ya Kiyunani philos, ambayo mara nyingi inahusianishwa na upendo wa kirafiki (phileō). Katika lugha ya kawaida koine maneno "agapaō " na "phileō " haya mara nyinyi ni visawe vya kitenzi kwa ajili ya upendo wa ki-Mungu (ulilinganishwa na Yohana 13:3 [phileō] na 5 [agapaō]); phileō pia linatumika kwa upendo wa Mungu katika Yohana 5:20. ◙ “Mkifanya ninachowaamuru ninyi” Hii ni sentensi shurutishi daraja la tatu ambayo inamaanisha kitendo muhimu. Inatoa sharti la urafiki ambalo ni utii (kama vile Yohana 14:15, 23-24; 15:10; Luka 6:46). 15:15 Yesu anawaarifu wanafunzi juu ya (1) Kweli kuhusu Mungu na (2) Matukio ya mbeleni. Anadhihirisha uwezo wake ili kwamba wanafunzi wake wakue katika imani na tumaini. Aliwashirikisha wanafunzi wake kile alichokuwa amekisikia kutoka kwa Baba (kama vile Yohana 3:32; 8:26, 40; 12:49; 15:15); waliwajibika kuwaeleza wengine (kama vile Mt. 28:20) 15;16 “Hamkunichagua bali Mimi niliwachagua ninyi” Kuna baadhi ya vipengele vya kisarufi vya kimsingi.

1. vitenzi vyote ni kauli ya kati elekezi ya wakati uliopita usiotimilifu – Yesu, mwenyewe, pasipo kujirudia alinawachagua (kama vile Yohana 6:70; 13:18; 15:16, 19)

2. "alla" iliyo na nguvu (lakini) isiyoleta manufaa 3. "ego" enye kusisitiza au maelezo ya “Mimi”

Hapa ndipo penye uwiano kati ya mwitikio wa mwanadamu na uchaguzi. Yote ni mafundisho ya Kibiblia. Mungu kila wakati huanzisha (Kama vile Yohana 6:44, 65; 15:16, 19) lakini wanadamu lazima waitikie (kama vile Yohana 1:12; 3:16; 15:4, 7, 9) Mungu anaposhughulika na wanadamu kila wakati huwa katika uhusiano wa ki-Maagano (ikiwa.. ndipo) Tazama Mada Maalum katika Yohana 3:16 Kitenzi “kuchaguliwa”katika muktadha huu kinarejerea kwa wale kumi na wawili. Neno “kuchaguliwa” lina dokezo la “kuchaguliwa kwa ajili ya huduma” Katika Agano la Kale na katika Agano jipya tu ndipo kuna dhana iliyoongezwa ya “kuchaguliwa kwa wokovu” ikiwa katika kiwango cha elimu maana. Waamini wa Agano jipya wamechaguliwa kwa kufanana na Kristo ambako ni huduma , kutokuwa na ubinafsi, na dhabihu kwa ufalme wa Mungu, mwili wa Kristo kwa manufaa ya mshirika. Ni udhihirisho ulio wazi kwamba ule ubinafsi wa anguko umekwisha kuvunjwa. Ni tabia katika Yohana kwamba kile ambacho Yesu anasema kuhusu wale kumi na wawili kina ushauri na kutumika kwa waamini wote. Wanawakilisha matunda ya kwanza ya kuwa wanafunzi, lakini uhusiano wake ni

1. Kipekee kwenye ushuhuda wake wa macho (kutiwa msukumo) 2. Unatumika kwa wote walioamini kwa Yesu kwamba mapenzi yake kwao ni mapenzi yake kwa wote

wanaoamini na kumfuata.

Page 266: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

250

◙ “Nimewachagua ninyi ili kwamba mwende kuzaa matunda na kwamba matunda yenu yapate kubaki” Hizi ni kauli tatu tendaji tegemezi za wakati uliopo: (1) Nendeni; (2) Zaeni matunda; na (3) Matunda yadumuyo (yakaayo). Waamini wako kwenye kazi maalumu (kama vile Mt. 28:19-20; Luka 24:46-47; Mdo. 1:8) Mwonekano wa kithiolojia wa neno “waliochaguliwa” waweza kuonekana katika Mdo. 20:28; 1 Wakorintho 12:28; 2 Timotheo 1:11. Ilitumika pia kwa kifo cha Kristo kwa niaba ya wanaoamini (kama vile Yohana 10:11, 15, 17-18; 15:13) ◙ “Kwa jina langu” Wanaoamini lazima wazae tabia ya Yesu. Fungu hili lilifanana na “mapenzi ya Mungu” Katika 1 Yohana 5:14. Upendo na maombi yanayojibiwa yamelinganishwa hapa katika Yohana 14:13-15 Tazama Mada Maalum: Jina la Bwana katika Yohana Yohana 14:13-14 15:17 “Hili nawaamuru, kwamba mpendane ninyi kwa ninyi” Tazama maelezo katika Yohana 15:12. Maombi yaliyojibiwa yamelinganishwa na upendo na jukumu maalum.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 15:18-25 18 Wapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi. 19 Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia. 20 Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu. 21 Lakini haya yote watawatenda kwa ajili ya jina langu, kwa kuwa hawamjui yeye aliyenipeleka. 22 Kama nisingalikuja na kusema nao, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa hawana udhuru kwa dhambi yao. 23 Yeye anichukiaye mimi humchukia na Baba yangu. 24 Kama nisingalitenda kwao kazi asizozitenda mtu mwingine, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa wametuona mimi na Baba yangu, na kutuchukia. 25 Lakini litimie lile neno lililoandikwa katika torati yao, Walinichukia bure.

15:18 “Ikiwa” Hii ni sentensi shurutishi daraja la kwanza ambayo inaaminika kuwa ya kweli kutokana na mtazamo wa mwandishi au kwa kusudi lake katika fasihi. Ulimwengu, utaratibu wa kibinadamu ulioanguka, unachukia wafuasi wa Yesu. ◙ “Ulimwengu” Yohana hutumia msemo huu katika njia kadhaa: (1) Sayari, kama sitiari kwa kila mwanadamu (kama vile Yohana 3:16) na (2) Kama jamii ya mwanadamu iliyopangiliwa na kutenda kazi nje ya Mungu (kama vile Yohana 10:8, 1 Yohana 2:15-17). Tazama Mada Maalum katika Yohana 14:17 ◙ “Ukiwachukia” Hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo; ulimwengu unaendelea kuchukia (kama vile Yohana 15:20) ◙ “Mwajua” Hii ni kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopo. Maarifa ya wanaoamini ya kweli ya Agano jipya utawasaidia kupambana na mateso ya ulimwengu ulioanguka. ◙ “Kwamba umenichukia mimi kabla haujawachukia ninyi” Hii ni kauli timilifu tendaji elekezi. Kiwakilishi nomino “Mimi” ni msisitizo (kama vile Yohana 7:7) hii inafunua upinzani wa ulimwengu kwa Mungu, Masihi wake, na watu wake (kama vile Yohana 17:14; 1 Yohana 3:13) Wanaoamini wote ni wamoja katika pendo la Kristo na ni wamoja katika mateso ya Kristo (kama vile Rum. 8:17; 2 Kor. 1:5, 7; Flp. 3:10; 1 Petro 4:13). Utambulisho pamoja na Kristo huleta amani, furaha na mateso, hata kufa! 15:19 “kama” Hii ni sentensi shurutishi daraja la pili iitwayo “kinyume na ukweli.” Hii inapaswa kutafsiriwa “kama ninyi mngekuwa wa ulimwengu, ambavyo sivyo mlivyo, basi ulimwengu ungewapenda, lakini hauwapendi.” 15:20 “kumbuka”Hii ni kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopo, kama Yohana 15:18, au kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo, ikiwezekana pengine ni swali (LB).

Page 267: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

251

◙ “Mtumwa si mkuu kuliko Bwana wake” Mtu anapolinganisha hii Yohana 15:20 pamoja na 13:16, inakuwa dhahiri kwamba Yesu alitumia misemo iliyofahamika katika njia tofauti tofauti. ◙ “Ikiwa wananitesa mimi…kama walilishika neno langu” Hizi ni kauli mbili za sentensi shurutishi daraja la kwanza ambazo zimechukuliwa kuwa za kweli kutokana na mtazamo wa mwandishi. Neno “kuteswa” linamaanisha kama kufukuzia mnyama wa porini. Mateso ni kawaida kwa wafuasi wa Kristo katika ulimwengu ulioanguka (Mt. 5:10-12; Yohana 16:1-3; 17:14; Mdo. 14:22; Rum. 5:3-4; 8:17; 2 Kor. 2. 4:16-18; 6:3-10; 11:23-30; Wafilipi 1:29; 1 The. 1. 3:3; 2 Tim. 3:12; Yakobo 1:2-4; Petro 1. 4:12-16) Hata hivyo tambua kwamba ingawaje wengine watakataa maneno ya mitume na hata kuwatesa, watakuwepo wengine watakaosikia na kuitika! Wao wenyewe ni uthibitisho wa ukweli huu! 15:21 “Hawamjui yeye aliyewatuma” Ni dhahiri kwamba hili linalejerea kwa Baba. Inadokeza kwamba Wayahudi pamoja na mataifa hawamjui Mungu. “Jua” limetumika katika maana ya lugha ya kisemitiki (Agano la Kale) ya uhusiano binafsi (kama vile Mwa. 4:1; Yer. 1:5). Ulimwengu uliopotea uliwatesa wanaoamini kwa sababu (1) wao ni mali ya Yesu ambaye nao pia walimtesa na (2) hawamjui Mungu! 15:22 “Kama nisingalikuja” Hii ni sentensi nyingine shurutishi daraja la pili, ambayo inamaanisha “kinyume na ukweli.” Inapaswa kutafsiriwa “kama nisingerudi na kusema nao, jambo ambalo nililifanya, basi wasingekuwa na dhambi yoyote, ambayo wanayo.” Kuwajibika kunahusiana na kujua (Tazama MADA MAALUM: DHAMBI ISIYOSAMEHEKA katika Yohana 5:21). Katika muktadha huu matawi yasiyo na matunda (yaani, Yuda na Wayahudi) walikuwa na fursa ya ujuzi, zaidi kuliko wale waliokuwa na ufunuo wa asili tu (yaani, mataifa, kama vile Zab. 19:1-6; Rum. 1:18-20 au 2:14-15) 15:23 Kule kuendelea kumpinga Yesu ni kuendelea kumpinga Mungu (kama vile Yohana 15:24). 15:24 “Kama” Hii ni sentensi nyingine shurutishi daraja la pili ambayo inamaanisha “kinyume na ukweli.” Ilipaswa kutafsiriwa “kama nisingefanya kazi miongoni mwenu ambayo mtu mwingine yeyote alizifanya (lakini ambayo nilifanya), bali wasingekuwa na dhambi, ambayo wanayo” Nuru huleta wajibu (kama vile Yohana 1:5; 8:12; 12:35, 46; Yohana 1. 1:5; 2:8, 9, 11; Mt. 6:23). ◙ “Wametuona Mimi na Baba yangu, wametuchukia” Hizi zote ni kauli tendaji elekezi ya wakati timilifu ambayo inaonyesha tabia iliyoafikiwa. Kumkataa Yesu ni kumkataa Baba (kama vile Yohana 1. 5:9-13) 15:25 Inashangaza kwamba msemo huu “sharia” au “torati” umetumika kueleza nukuu kutoka Zab. 35:19; 69:4. Kwa kawaida msemo huu umetumika katika maandishi ya Musa, Mwanzo hadi Kumbukumbu la Torati. Fumbo la uyahudi kumkataa Yesu mbele ya Ufunuo ulio dhahiri kiasi kile lilichukuliwa kama kutokuamini kwa makusudi (kama vile Isa. 6:9-13; Yer. 5:21; Rum. 3:9-18)

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 15:26-27 26 Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia. 27 Nanyi pia mnashuhudia, kwa kuwa tangu mwanzo mmekuwapo pamoja nami.

15:26 “Wakati msaidizi atakapokuja, ambaye nitamleta kwenu” Wote Baba na Mwana humleta Roho (kama vile Yohana 14:16, 26; 15:26; 16:17) Kazi ya ukombozi inawashirikisha nafsi zote za utatu. ◙ “Roho wa kweli”Hii inatumiwa katika habari ya Roho Mtakatifu kama anayemfunua Baba (kama vile Yohana 14:17, 26; 15:26; 16:13) Tazama Mada Maalum juu ya kweli katika Yohana 6:55 na 17:3 ◙ “atashuhudia kunihusu mimi” Jukumu la Roho ni kumshuhudia Yesu na mafundisho yake (kama vile Yohana 14:26; 16:13-15; Yohana 1. 5:7)

Page 268: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

252

15:27 “Mtanishuhudia pia” Neno “ninyi .. pia” ni lenye msisitizo. Hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo. Hii lazima irejelee kwenye uvuvio wa waandishi wa Agano Jipya (yaani, Mitume na rafiki zao) waliokuwa na Yesu wakati alipokuwa katika uhai wake duniani (kama vile Luka 24:48) Tazama Mada Maalum: Mashuhuda wa Yesu na Mada Maalum: Utu wa roho katika Yohana 14:26

MASWALI YA MJADALA

Huu ni mwongozo wa fasiri, ina maanisha kwamba unawajibika kwa tafsiri zako mwenyewe za Biblia. Kila mmoja wetu lazima atembee katika mwanga tulio nao. Wewe, Biblia, na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Hutakiwi uvitelekeze vitu hivi kwa mfasiri. Maswali ya mjadala huu yanatolewa kukusaidia kufikiri juu ya mambo makubwa ya sehemu za kitabu hiki. Yanalenga kukuamsha kimawazo na sio kutoa maana.

1. “Kukaa” kunahusiana na nini? 2. Inakuwaje kama mwamini akikoma kukaa? Inakuwaje ikiwa mwamini hana matunda? 3. Orodhesha ushahidi wa wanafunzi wa kweli 4. Kama kuteseka ndio kawaida kwa Wakristo, hili linasemaje kwetu leo? 5. Elezea Yohana 15:16 kwa maneno yako mwenyewe.

Page 269: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

253

YOHANA 16

MIGAWANYO YA AYA YA TAFSIRI ZA KISASA UBS4 NKJV NRSV TEV NJB

Chuki ya ulimwengu Kukataliwa Wanafunzi na Kunakokuja ulimwengu (15:18 – 16:4a) (15:26-14:4) uhusiano wa Wakristo (15:18-16:4a) (15:18-16:4a) kwa ulimwengu Kazi ya Roho 16:1-4a Kazi ya Roho Kuja kwa Mfariji Mtakatifu 16:4b-11 Kazi ya Roho 16:4b-11 16:4b-11 16:4b-15 Mtakatifu 16:5-15 16:12-15 16:12-15 16:12-15 Huzuni itageuka Huzuni itageuka Huzuni na furaha Yesu kurudi Kuwa furaha kuwa furaha hivi karibuni 16:16-24 16:16-24 16:16-24 16:16 16:16 16:17-18 16:17-18 16:19-22 16:23-24 Nimeshinda Yesu Kristo Ushindi juu ya Ameushinda ulimwengu ulimwengu 16:25-33 16:25-33 16:25-28 16:29-28 16:29-33 16:29-30 16:29-33 16:31-33

MZUNGUKO WA TATU WA USOMAJI KUFUATILIA KUSUDIO LA ASILI LA MWANDISHI KATIKA NGAZI YA AYA Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwatafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Aya ya kwanza 2. Aya ya pili 3. Aya ya tatu 4. N.k

UTAMBUZI WA MUKTADHA WA YOHANA 16:1-33

Page 270: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

254

A. Muktadha wa fasihi hii unaanza kutoka Yohana 15:18-16:4a. Migawanyo ya sura haiweki msukumo na kuongezwa baadaye, kama kuweka aya, kuweka herufi kubwa, kuweka vituo na koma na mgawanyo wa aya.

B. Jukumu la Roho mtakatifu kwa wale waliopotea kiroho limefafanuliwa katika Yohana 16:8-11, jukumu lake

kwa wale walio okolewa liko katika Yohana 16:12-15. Samuel J. Mikolaski ina muhtasari wa kuvutia wa kazi ya Roho Mtakatifu katika Agano jipya kwenye makala yake “thiolojia ya Agano Jipya” katika The Exposition Bible Commentary, juzuu.1: “Mafundisho ya Agano jipya juu ya utakaso, wakati kwa karibu sana yakihusiana na kuhesabiwa haki, hata hivyo yanatofautiana kiundani. Kama ilivyo katika Agano la Kale, utakaso unaelekeza kwanza kwenye utengano – utakatifu wa Mungu unaovuka uwezo wa kibinadamu na pili, kwa ubora wa uadilifu na uhusiano ule unaofanana na Mungu. Utakaso ni kazi ya Roho mtakatifu ambaye humuunganisha mtu na Kristo na kufanya upya maisha yake ya Kiroho. Lugha ya Agano Jipya inahitaji ubatizo katika Roho mtakatifu. (1 Wakorintho 12:13); mhuri wa Roho (Waefeso 1:13, 14; 4:30). Kukaa ndani kwa Roho Mtakatifu (Yohana 14:17; Warumi 5:5; 8:9-11; 1 Wakorintho 3:16; 6:19; 2 Timotheo 1:14), maagizo toka kwa Roho mtakatifu (Yohana 14:26; 16:12-15), kujazwa Roho Mtakatifu (Efeso 5:18) na tunda la Roho Mtakatifu (Wagalatia 5:22, 23). Utakaso unashabihiana na kuhesabiwa haki, ambavyo ndo vitu vya msimamo mbele za Mungu (Waebrania10:10) na inaweza kudhaniwa kuwa maendeleo ndani ya wazo jipya” (MR 474)

C. Yohana 16:17, Warumi 13:36; 14:5, 8, na 22 ni swali jingine la Mitume

D. Wengi wanaamini kwamba neno “tuondoke hapa” la Yohana 14:31 likiunganishwa na 18:1 linaonyesha

kwamba Yesu alikuwa akinena juu ya Sura 15-17 akiwa njiani kuelekea Gethsemane kupitia hekaluni na mitaa ya Yerusalemu, na sio kule ghorofani.

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 16:1-4 1Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa. 2Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada. 3Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi. 4Lakini nimewaambia hayo, ili makusudi saa ile itakapokuja myakumbuke ya kuwa mimi naliwaambia. Sikuwaambia hayo tangu mwanzo, kwa sababu nalikuwapo pamoja nanyi.

16:1 NASB “Ili msiachwe mkakwazwa/mkajikuza” Nkjv “msije sababisha kujikwaa” NRSV “Kuwaepusha na kukwazika/ kukwazana” TEV “ili msije mkaiacha imani ya Yesu NJB “Ili msije mkaanguka mkaenda mbali” Neno hili la Kiyunani (kauli tendewa tegemezi ya wakati uliopita usiotimilifu ya skandalizō, BAGD 752) awali lilitumika kama chambo cha mtego uliowekwa kwa ajili ya kukamata wanyama. Mara nyingi linatafsiriwa kama “kuangukia mbali” (kama vile Mt. 13:21; 24:10; Marko 4:17; 14:27, 29). Matumizi ya ki-sitiari katika muktadha huu yanarejea waumini wasikamatwe bila kujua kwa matendo ya chuki ya Wayahudi wenzao, hata kwa viongozi wa kidini. 16:2 “Watawatenga na masinagogi” Hii inarejea juu kuwatenga na kanisa la dini ya Kiyahudi (kama vile Yohana 9:22, 34; 12:42). Kuna mengi ambayo hayajulikani kuhusu taratibu za kuwatenga watu kutoka ushirika wa dini ya Kiyahudi. Kulikuwepo na kutengwa kwa muda na kutengwa jumla kutoka katika huduma za Sinagogi. Baadaye, baada ya

Page 271: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

255

kuanguka kwa Yerusalemu mwaka wa 70 B.K, pale Jamnia katika Palestina, walimu wa sheria za Kiyahudi walianzisha, “kiapo cha laana” kinachohusiana na Kristo kwa kile ambacho walitamani kuwatenga Wakristo toka kwenye huduma za Sinagogi. Hiki ni kile hatimaye kilicholazimisha kuwepo na mpasuko kati ya wafuasi wa Kristo na watu wa sinagogi wa Kiyahudi. ◙ “Kila anayewaua kudhani kwamba anatoa dhabihu kwa Mungu” Hiki ndicho hasa ambacho viongozi wa Kiyahudi walikifikiri (kama vile Isaya 66:5; Mt. 5:10-12; 10:32). Sauli wa Tarso (Paulo) ni moja ya maelekezo mabaya ya moyo wa kidini (kama vile Matendo 26:9-11; Gal. 1:13-14). 16:3 “Na hayo watawatendea” uaminifu na kujitoa katika mamlaka iliyoko juu haitoshi. Uovu, makosa na kushika sana dini mara nyingi hutokea katika jina la Mungu. ◙ “Kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi” Neno “kujua” linarejea juu ya kidokezo cha wazi kwenye Agano la Kale, na uhusiano binafsi (kama vile Mwa. 4:1; Yer 1:5). Haya ni madai ya nguvu kwamba kumkataa Yesu ni udhihilisho wa kumkataa Mungu (kama vile Yohana 8:18; 15:21; 1 Yohana 5:9-12) Yohana mara nyingi anatetea juu ya upofu wa kiroho na ujinga wa ulimwengu (kama vile Yohana 1:10; 8:19, 55; 15:21; 16:3; 17:25). Hata hivyo kusudi la kuja kwa mwana lilikuwa ni kuokoa ulimwengu (kama vile Yohana 3:16) na kumfunua Baba ili kwamba ulimwengu upate kumjua (kama vile 27:13) kupitia kwa Kristo. 16:4 kutabiriwa juu ya Yesu kulitolewa kwa maana ya kuwatia moyo wanafunzi katika imani/tumaini/kusadiki katikati ya mateso na kukataliwa (kama vile Yohana 13:19; 14:29). “Kutoka mwanzo” inarejea juu ya mwanzo wa huduma ya wazi ya na wito maalum wa wale kumi na wawili.

ANDKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 16:5-11 5Lakini sasa mimi naenda zangu kwake yeye aliyenipeleka, wala hakuna mmoja wenu aniulizaye, Unakwendapi? 6 Ila kwa sababu nimewaambia hayo huzuni imejaa mioyoni mwenu. 7 Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu. 8 Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu. 9 Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi; 10 kwa habari ya haki, kwa sababu mimi naenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena; 11 kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa.

16:5 “Hakuna mtu kati yenu anayeniuliza mimi, unakwenda wapi” inaonekana ya kwamba Petro aliuliza swali hili katika Yohana 16:13; 36, lakini kwa haraka mawazo yake yalikuwa yamechanganyikiwa na uchungu wa Yesu kuwaacha na kisha swali la nini kingeliwatokea (kama vile Yohana 16:6) Yohana 14:1-3 inaelezea kupaa kwa Yesu mbinguni (Matendo 1:9-11) Hapa ni mahali pazuri kutukumbusha kwamba injili si maneno matupu, neno kwa neno, nukuu za mazungumzo ya Yesu. Ni mihtasari iliyofanywa miaka mingi baadaye kwa makusudi ya kithiolojia. Waandishi wa injili, chini ya uvuvio walikuwa na maamuzi ya kuchagua, kupanga na kurekebisha maneno ya Yesu (tazama Gordon Fee na Douglas Stuart, How To Read the Bible For All Its Worth). Siamini kwamba walikuwa na haki ya kuweka maneno kinywani mwa Yesu. Muundo huu wa kithiolojia wa maneno ya Yesu, mafundisho na matendo kwa ajili ya kuhubiri kusanyiko fulani, pengine unaelezea tofauti nyingi miongoni mwa maelezo ya injili! 16:6 “Huzuni imejaa moyo wako” Hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati timilifu. Uzoefu wa chumba cha ghorofani ulikuwa moja ya huzuni (kama vile Yohana 14:1; 16:6, 22). Neno hili “moyo” linatumika kwa maana ya Kiebrania kuhusu hali yote ya fikra, hisia, na mapenzi ya mtu. Tazama Mada Maaalum: Moyo katika Yohana 12:40 16:7 “Ni kwa faida yenu kwamba mimi niondoke” Mwili wa Yesu katika uhalisia waweza kuwa mahali pamoja kwa wakati mmoja, ambacho ni kitu kinachozuia uwezo wake wa kufundisha na kuhudumu kwa wanafunzi wake wote. Pia, wakati wa uhai wake hapa duniani alijielekeza zaidi kwa Israeli (kama vile Mt. 10:6; 15:24). Kuja kwa Roho mtakatifu kungefungua enzi mpya ambayo ingepanua wigo wa huduma (kama vile. Efeso 2:11-3:13). Neno

Page 272: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

256

hili “faida” lilimaanisha “manufaa” na pia limetumika katika Yohana 11:50 na 18:14 likihusianishwa na kifo cha Yesu. Neno “kuondoka” lingeweza kuhusisha matukio yote ya Yesu ya wiki ya mwisho. ◙ “Kwani nisipoondoka, msaidizi hatakuja kwenu” Kuna sentensi mbili shurutishi daraja la tatu kwenye aya hii zinazoonyesha kitendo muhimu.. Yesu alilazimika kuondoka ili kuja kwa utimilifu wa Roho! Neno paraclētos linaweza kutafsiriwa “mtetezi,” “mfariji” au “msaidizi “(kama vile Yohana 14:16, 26; 15:26, tazama maelezo kamili katika Yohana 14:16). Neno hili linaonekana pekee katika maandiko ya Yohana. Lilitumika katika fasihi ya Kiyunani kwa mwanasheria mtetezi aliyeitwa pamoja kutoa msaada. Katika Yohana 16:8-11 Roho alisimama kama mshitakiwa kwa ulimwengu. Hata hivyo, katika Yohana 16:12-15 utetezi wa Roho unaonekana ukiwa kwa niaba ya wanaoamini. Neno hilo hilo paraclētos linatumika kwa mwana katika 1 Yohana 2:1. Mzizi wa neno la Kiyunani laweza kutafsiriwa “fariji”. Kwa maana hii hutumiwa kwa ajili ya Baba katika Wakorintho 2. 1:3-11. ◙ “Nitamtuma kwenu” Roho alikuja kutoka kwa wote Baba na mwana (kama vile Yohana 14:26). 16:8 “Naye atakapokuja atauhukumu ulimwengu” tambua kwamba sehemu zote tatu (dhambi, haki, hukumu) za ushuhuda wa Roho zinahusiana na hitaji la mwanadamu na kazi ya ukombozi ya Yesu Kristo. Neno “kutia hatiani” lilikuwa neno la kisheria kwa ajili ya “udodosaji” G. B. Caird, The Language and Imagery of the Bible, uk. 159, ina uelewa wa kuvutia wa maneno haya matatu. Kuushawishi ulimwengu kwamba

1. Umefanya makosa kumleta Yesu majaribuni na kumuadhibu kifo. 2. Umefanya makosa kuhusu maana ya dhambi 3. Umefanya makosa kuhusu maana ya haki 4. Umefanya makosa kuhusu maana ya hukumu.

Ikiwa ndivyo basi Roho anaifunua injili kikamilifu kupitia utu wa Yesu. Hali yao ya kushika dini haiwezi kuwaokoa. Hukumu inawangojea wale wanaomkataa Yesu! “Dhambi” ni kutokuamini! Yesu ndiye njia pekee ya maisha pamoja na Mungu! Neno “ulimwengu” linarejea kwa mwanadamu, jamii iliyoanguka iliyojiunda na kufanya kazi mbali na Mungu. Tazama Mada Maalumu katika Yohana 14:17 16:9 “kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi” Injili inaanza kwa kutambua hali ya dhambi ya mwanadamu na hitaji la haki kwa Mungu (kama vile Warumi 3:9-18, 23; 6:23; Efeso 2:1-3). Dhambi sio kizuizi kikubwa cha kujikwaa kwenye wokovu katika upande huu wa Kalvari, lakini kutokuamini kwa mwanadamu katika kazi na Utu wa Yesu Kristo (kama vile. Yohana 3:6-21; 8:24, 26). Neno “kuamini” lina vipengele vya utambuzi na kihisia, lakini kimsingi ni kwa hiari (tazama Mada Maalum katika Yohana 2:23). Haikuzingatia thamani ya wanaoamini au utendaji, lakini juu ya imani yao ya toba yenye mwitikio wa ahadi ya Mungu katika Kristo (kama vile Warumi 3:21-30) 16:10 “Kwa habari ya haki” Hii inaweza kurejea kwa

1. Kazi inayofuata ya ukombozi ya kristo katika Kalvari na ufufuo unaoonekana kama umoja(kama vile Yohana 16:10)

2. Wale wanaodhani kwamba wana haki pamoja na Mungu mbali na Kristo ambapo katika uhakika ni Kristo pekee ambaye ana haki pamoja na Mungu, iliyoonekana wakati wa kupaa mbinguni.

16:11 “Kwa habari ya hukumu, kwa sababu mtawala wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa” Kuna siku inakuja ambapo malaika wote walioanguka pamoja na wanadamu walio dhambini watasimama mbele za Mungu mwenye haki (kama vile Wafilipi 2:9-11). Shetani, ingawa bado ana nguvu katika ulimwengu huu (kama vile Yohana 12:31; 14:30; 2 Wakorintho 4:4; Efeso 2:2; Yohana 1. 5:19), tayari ni adui aliyeshindwa (kauli tendewa elekezi ya wakati timilifu) watoto wake (kama vile Yohana 8:44; Mt. 13:38; 1 Yohana 3:8-10) huvuna ghadhabu ya Mungu!

Page 273: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

257

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 16:12-15 12Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa. 13Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. 14Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari. 15Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari.

16:12 “Hamwezi kuyastahimili sasa” neno “kuyastahimili” linatumiwa kwa habari ya mnyama aliyebeba mzigo. Baadhi ya mambo ambayo hawakuweza kuyaelewa yalikuwa

1. Kuteswa kwa Kristo 2. Kufufuka kwa Kristo 3. Jukumu la Kanisa kwa ulimwengu

Wasomaji wa leo lazima wakumbuke kwamba kwa njia nyingi maisha ya Kristo huwakilisha kipindi cha mpito. Mitume hawakuelewa mambo mengi mpaka pale alipojitokeza baada ya kufufuka na kuja kwa Roho kikamilifi siku ya Pentekoste. Hata hivyo, lazima pia tukumbuke kwamba injili ziliandikwa miaka mingi baadaye kwa kusudi la uinjilisti kwa baadhi ya hadhira iiliyolengwa. Kwa hivyo, zinaaksi thiolojia ya baadaye, iliyokomaa. 16:13 “Roho wa kweli” Kweli (alētheia) limetumika katika vidokezo vyake kwenye Agano la Kale kwa maana ya uaminifu na pia baadaye katika maana ya kuwa na imani. Yesu alisema kwamba yeye ndiye alikuwa kweli katika Yohana 14:16. Sifa hii ya Roho Mtakatifu inasisitiza wajibu Wake kama mdhihilishaji wa Yesu (kama vile Yohana 14:17, 26; 15:26; 16:13-14; Yohana 1. 4:6; 5:7).Tazama kielelezo katika Yohana 6:55. ◙ “Atawaongoza kwenye kweli yote” Hii haikurejerea kwenye kweli kamili katika kila eneo, lakini pale tu kwenye ukweli wa kiroho na mafundisho ya Yesu. Hii kimsingi inarejea kwenye uvuvio wa mwandishi wa maandiko ya Agano Jipya. Roho aliwaongoza katika njia ya kipekee, na ya kimamlaka (iliyovuviwa). Katika maana ya pili inahusisha kazi ya Roho ya kuwaangazisha wasomaji wa baadaye kwenye ukweli wa injili. . Tazama Mada Maalum: kweli katika Yohana 6:55 na Utu wa Roho.

MADA MAALUMU: NURU

Mungu ametenda hapo mwanzo ilikujidhihirisha wazi kwa wanadamu. Kithiolojia, huu unaitwa ufunuo. Alichagua watu kadhaa kuweka kumbukumbu na kueleza ufunuo wake huu. Katika thiolojia, huu unaitwa uvuvio. Ametuma Roho kusaidia wasomaji kuelewa neno lake. Katika thiolojia, huu unaitwa mwangaza.Tatizo linatokea pale tunapobisha kuwa Roho anahusika katika kuelewa neno la Mungu- Sasa, kwa nini panakuwa na tafsiri nyingine kiasi hicho? Sehemu ya tatizo ipo kwa uelewa wa nyuma wa wasomaji au uzoefu binafsi. Daima hoja binafsi inaelezwa kwa kutumia Biblia katika uthibitisho wa kimaandishi au mtindo wa kuhakiki. Daima thiolojia inachagua maneno ya kusoma BibliaI ikiruhusu kusoma maneno kadha na kwa njia zilizopendekezwa. Mwangaza hauwezi kulinganishwa na uvuvio ingawa sehemu zote mbili Roho mtakatifu anahusika. Njia rahisi ya kusoma ni kujaribu kufafanua wazo kuu katika aya, na siyo kutafsiri kila neno kwa kina katika maandiko. Ni wazo la juu tu ambalo linapeleka ukweli hasili wa mwandishi wa kwanza. Kudokezea kitabu au sehemu ya kifasihi inasaidia kufuatilia kusudio la mwandishi wa awali aliyevuviwa. Hakuna mfasili aliyevuviwa. Hatuwezi kuzalisha njia ya tafasiri ya mwandishi wa Kibiblia. Tunaweza na lazima tujaribu kuelewa walichokuwa wakisema enzi za nyakati zao na kuwakilisha ukweli huo nyakati zetu. Kuna sehemu za Biblia ambazo ni tata au zimefichika (hadi wakati/kipindi kingine). Daima patakuwapo kutokukubaliana katika baadhi ya maandiko na masomo lakini lazima tuseme wazi kweli halisi na kuruhusu uhuru wa tafsiri binafsi ndani ya mipaka ya kusudio la mwandishi wa mwanzo. Wafasiri lazima watembee ndani ya mwanga walio nao, na siku zote wakiwa tayari kwa mwanga zaidi kutoka katika Biblia na Roho. Mungu atatuhukumu kutokana na kiwango cha uelewa wetu na jinsi tulivyoishi katika uelewa huu.

Page 274: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

258

◙ “Kwa maana hatasema kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena na mambo yajayo atawapasha habari yake” Mambo ambayo yatakuja yatahusu matukio ya haraka ya ukombozi: Kalvari, Ufufuo, Kupaa Mbinguni, na Pentekoste. Hii hairejerei huduma ya Unabii ya kutabiri mambo ya baadaye (yaani Agabo, Matendo 2:10 tazama Mada Maalum: Unabii katika Yohana 4:19 Roho alitapokea ukweli toka kwa Baba, kama Yesu alivyofanya, na kuwapatia waumini kama Yesu alivyofanya. Sio tu maudhui ya ujumbe wa Roho ndio unaotoka kwa baba, bali pia namna ya kutenda mambo (yaani, binafsi, tazama Mada Maalumu katika Yohana 14:26). Baba katika utendaji ndiye mkuu (kama vile 1 Wakorintho 15:27-28). 16:14-15 “Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari” Kazi ya msingi ya Roho ni kumwinua Kristo na kuelezea kwamba Yesu ndiye Masihi (kama vile Yohana 16:15) Roho kamwe hajing’arishi wenyewe, lakini daima humwinua Yesu (Yohana 14:26) ◙ “Mambo yote ambayo anayo Baba ni yangu” Ni madai ya kushangaza (kama vile Yohana 3:35; 5:20; 13:13; 14:10; 17:10; Mt. 11:27. Hii inafanana na Mt. 28:18; Efeso 1:20-22; Wakolosai 2:10; Petro 1. 2:22. Kuna utendaji wa kimpangilio, sio wa kutokuwa na usawa ndani ya Utatu.Yesu alivyomuaksi Baba, Roho anamuaksi Yesu.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 16:16-24 16 Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni; na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona. 17 Basi baadhi ya wanafunzi wake wakasemezana, Neno gani hilo asemalo, Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni, na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona? Na hilo, Kwa sababu naenda zangu kwa Baba? 18 Basi walisema, Neno gani hilo asemalo; hilo, Bado kitambo kidogo? Hatujui asemalo. 19 Yesu alifahamu ya kwamba wanataka kumwuliza, akawaambia, Ndilo hilo mnaloulizana, ya kuwa nalisema, Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni, na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona? 20 Amin, amin, nawaambia, Ninyi mtalia na kuomboleza, bali ulimwengu utafurahi; ninyi mtahuzunishwa, lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha. 21 Mwanamke azaapo, yuna huzuni kwa kuwa saa yake imefika; lakini akiisha kuzaa mwana, haikumbuki tena ile dhiki, kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtu ulimwenguni. 22 Basi ninyi hivi sasa mna huzuni; lakini mimi nitawaona tena; na mioyo yenu itafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleaye. 23 Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu. 24 Hata sasa hamkuomba neno

kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu. 16:16 “Kitambo kidogo” Neno hili linatokea mara kwa mara katika Yohana (kama vile. Yohana 7:33; 12:13; 33:14; 14:19). Kumekuwepo na nadharia mbali mbali jinsi maneno haya ya kinahau yanamaanisha.

1. Kuonekana baada ya kufufuka 2. Kuja mara ya pili 3. Yesu kuingia ndani kupitia Roho Mtakatifu

Katika hali ya uwazi wa kimazingira, namba 1 ndio pekee inawezekana (kama vile Yohana 16:17-18). Wanafunzi walichanganyikiwa kwa kauli hii (kama vile 16:17-18)

16:17 “Baadhi ya wanafunzi wake kisha waliambiana” Hili ni swali jingine kama Yohana 13:36; 14: 5,8,22. Yesu hutumia maswali haya kwa kuwathibitishia na kujifunua mwenyewe. Ni tabia ya Yohana kuutumia mjadala kufunua ukweli. Katika Yohana kuna mijadala ishirini na saba pamoja au inayomuhusu Yesu. Pia ni tabia ya Yohana kwamba wasikilizaji wa Yesu wasiweze kutambua kile alichokisema (kama vile Yohana 16:18) Yeye anatoka juu; wao wanatokea chini. ◙ “Na kwakuwa naenda kwa Baba” Yesu alitamka hili katika Yohana 16:5 kama alivyotamka yale maneno “baada ya kitambo kidogo” kwenye Yohana 16:16. Kwa maana fulani, hii ni rejea maalum ya Kimasihi (kama vile Yohana 13:1, 3; 16:28; 17:24)

Page 275: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

259

◙ “Hamtaniona…..mtaniona” Kuna maneno mawili tofauti kwa neno “kuona” katika Yohana 16:16 na 17. Yanaonekana kuwa na maana sawa. Kama ndivyo basi kuna kipindi kimoja cha muda kinachofanyiwa mrejeo na yumkini kipindi hicho kilikuwa kati ya kifo cha Yesu msalabani na asubuhi ya kufufuka kwake. Wengine wanafikiri vitenzi viwili na vifungu vinarejea juu ya mtazamo wa “kimwili” na mtazamo wa “kiroho”na kwa hiyo kumaanisha (1) muda kati ya kalvari na Jumapili ya maajirio au (2) muda kati ya kupaa mbinguni na kuja kwake mara ya pili Ukweli kwamba kitenzi cha kwanza (theōreō) ni njeo ya wakati uliopo katika Yohana 16:16 na 17 na pili (horaō) ni njeo ya wakati ujao katika Yohana 16:16 na 17 vinaonekana kusaidiana na nadharia ya maneno yanayokaribia kufanana. 16:18 “Hivyo walikuwa wanasema” Hii ni tungo shurutishi ambayo yaweza kumaanisha (1) walikuwa wanasema tena na tena au (2) walianza kusema. ◙ “Hiki ni nini asemacho” wale waliokuwa pamoja naye, waliomsikia na kuona miujiza yake, hawakumwelewa mara zote (kama vile Yohana 8:27, 43; 10:6; 12:16: 18:4). Hivi ndivyo huduma ya Roho itaondolewa. 16:19 “Yesu alijua kwamba walitaka kumhoji” Yesu kila mara alijua mawazo ya watu (kama vile Yohana 2:25; 6:61, 64; 13:11). Ni vigumu kujua kwa uhakika hii ilikuwa (1) asili yake ya ki-Mungu; (2) utambuzi ndani ya watu na hali; au (3) Vyote 16:20 “Amini, amini nawaambieni” Hii kwa uhalisia “Amina, amina” (tazama Mada Maalum katika 1:51). Neno “Amina” Ulikuwa ni usemi wa Agano la Kale (aman, emeth, emunah) kwa maana ya “imani” (Kama vile Habakuki 2:4). Msingi wa chanzo cha elimu ya maneno na vyanzo vyake ulikuwa “kuwa imara” au “kuwa na hakika.” Lilikuja kutumika kitamathali kwa uaminifu wa Mungu ambalo ni usuli kwenye dhana ya kibiblia juu ya imani/uaminifu. Yesu ndiye pekee ambaye alisema sentensi ikiwa na neno hili. Inaonekana kuwa na kidokezo hiki huwa ni maelezo ya muhimu nay a kuaminiwa i.” ◙ “Mtalia na kuomboleza” Hii ilimaanisha kuwa huzuni ya wazi na ambayo ilikuwa ni tabia ya Wayahudi ya kuonyesha kuhuzunika (kama vile Yohana 11:31, 33; 20:11). Mara tatu Yesu alitumia msisitizo wa wingi “ninyi” alipozungumzia huzuni ya wanafunzi (kama vile Yohana 16:20 [mara mbili] na Yohana 16:22). Uongozi unamaanisha

1. Utumishi 2. Kukataliwa na ulimwengu 3. Mateso kama ya Bwana

◙ “Mtapata huzuni kubwa, Lakini huzuni yenu itageuzwa kuwa furaha” ni ahadi kubwa kiasi gani kwa wanafunzi wakiwa katikati ya kuchanganyikiwa kwao na kutokuwa na uelewa. Kila kitu ambacho Yesu aliahidi kundi hili muhimu la wanafunzi lilitimizwa pale Yesu alipotokea mara tu baada ya usiku wa jumapili ya kwanza kufufuka kule ghorofani.

1. Hatawaacha (kama vile Yohana 14:18; 16:16, 19; 20:19) 2. Atawarudia tena (kama vile Yohana 14:18; 16:16, 19; 20:19) 3. Angeliwapa amani (kama vile Yohana 16:22; 20:14) 4. Angeliwapa Roho (kama vile Yohana 15:26; 20:22)

16:21 “Wakati mwanamke akiwa na uchungu” Sitiari ya mwanamke katika kuzaa ni kawaida katika Agano la Kale na Agano Jipya. Kwa kawaida inatumika kusisitiza juu ya huzuni au kutokuweza kuzaa, lakini hapa mtazamo uko juu ya mwelekeo wa mwanamke, kabla na baada. Sitiari hii mara nyingi inaunganishwa na “uchungu wa kuzaa” wa kizazi kipya (kama vile Isaya 26:17-18; 66:7-14; Marko 13:8). Hiki ndicho hasa Yesu alikuwa anarejea na hii ndio sababu haswa kwa nini wanafunzi, ambao walikuwa bado upande mwingine wa msalaba, ufufuo, na kupaa, hawakuyaelewa maneno ya Yesu!

Page 276: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

260

16:23 “Katika siku ile” Haya ni maneno yenye nahau ya Kiebrania (kama kuzaliwa mtoto kama vile Yohana 16:21) ambayo kwa kawaida yanahusishwa pamoja na kuja kwa kizazi kipya (kama vile Yohana 16:20; 16:25,26) ◙ “Ninyi hamtaniuliza mimi jambo lolote” Kuna maneno mawili toauti kwa “swali” au “uliza” katika aya hii (Yohana 16:26). Ya kwanza inadokeza“uliza swali” (kama vile Yohana 16:5, 19, 30) Ikiwa hii ndio tafsiri sahihi, Yesu alikuwa anarejea kwenye maswali yao yote yaliyoulizwa kwenye muktadha wa Yohana 13:17 (kama vile Yohana 13:36; 14:5,8, 22; 16:17-18). Neno la pili basi lingehusu kuja kwa Roho Mtakatifu (kama vile Yohana 14:16-31; 15:26-27; 16:1-15) ambaye atajibu maswali yao yote. Kwa njia nyingine maneno haya yanikumbusha kuhusu ahadi ya Agano Jipya la Yer. 31:31-34 ambapo kuja kwa kizazi kipya kungeleta kujua kikamilifu kwa wale wote wanaoamini. NASB “Ikiwa mtamwomba Baba lolote kwa jina langu” NKJV “Chochote mtakachomwomba Baba kwa jina langu” NRSV “Ikiwa mtaomba lolote kwa jina langu” TEV “Baba atawapeni lolote mtakalomwomba kwa jina langu NJB “Chochote mtakachoomba kutoka kwa Baba atatoa ruhusa kwa jina langu. Hiki ni kishazi husianishi kisicho dhahiri na sio tungo shurutishi. Lazima ieleweke kwamba kuomba kwa jina la Yesu sio tu kumalizia maombi yetu kwa maneno yaliyopangwa kidini, lakini ni kuomba kwa mapenzi, akili, na tabia ya Yesu Kristo (kama vile 1 Yohana 5:13) Tazama muhtasari katika Yohana 15:16 Tazama MADA MAALUM: MAOMBI, YASIO NA UKOMO LAKINI YANA UKOMO katika Yohana 3:22 Kuna utofauti wa maandishi inaohusiana na maneno“kwa jina langu” Je unapaswa kuendelea na neno “omba” au “toa” au mawili yote? Muktadha mzima hapa ni maombi, kwa hiyo, pengine ilipaswa kuendelea na neno “omba” ingawa kwa ukweli, kila kitu kutoka kwa Baba huja kupitia kwa Yesu (“Jina langu” kama vile Yohana 14:13, 14; 16:15, 24, 26) Tazama MADA MAALUM: JINA LA BWANA katika Yohana 14:13-14 16:24 “ombeni nanyi mtapewa” “omba” ni kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopo. Hii inalenga maombi ya wanaoamini kuwa yanaendelea kuwepo na endelevu. Kwa matazamo mmoja wanaoamini wanahitaji kuomba mara moja, kuaminii, lakini katika mtazamo mwingine, maombi ni ushirika wenye kuendelea na matumaini katika Mungu, endelea kuomba (kama vile Mt. 7:7-8; Luka 11:5-13; 18:1-8). ◙ “Ili kwamba furaha yenu itimizwe” Hii ni kauli timilifu tendewa endelevu yenye mafumbo (kama vile 1 Yohana 1:4) Maombi yaliyojibiwa ni sababu ya furaha yetu! Furaha ni sifa ya wafuasi wa Yesu (Kama vile Yohana 15:11; 16:20, 21, 24; 17:13).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 16:25-28 25Hayo nimesema nanyi kwa mithali; saa yaja ambapo sitasema nanyi tena kwa mithali, lakini nitawapa waziwazi habari ya Baba. 26Na siku ile mtaomba kwa jina langu, wala siwaambii ya kwamba mimi nitawaombea kwa Baba; 27kwa maana Baba mwenyewe awapenda kwa kuwa ninyi mmenipenda mimi, na kusadiki ya kwamba mimi nalitoka kwa Baba. 28Nalitoka kwa Baba, nami nimekuja hapa ulimwenguni; tena nauacha ulimwengu; na kwenda kwa Baba.

16:25 “kwa mithali” Mafundisho ya Yesu yalikuwa na matokeo ya pande mbili: (1) yalifungua uelewa na (2) yalifunga uelewa (kama vile Marko 4:10-11; Isaya 6:9-10; Yer. 5:21). Moyo wa wasikilizaji ndio msingi wa kuelewa kwa ufanisi. Hata hivyo, zilikuwepo na kweli fulani kwamba hata waliookolewa hawakuweza kufahamu mpaka baada ya matukio ya wiki ya mateso (kusulibiwa, kufufuka, kuonekana baada ya kufufuka, kupaa mbinguni) na Pentekoste. Kuwatokea watu wawili njiani baada ya kufufuka wakati wakienda Emau (kama vile Luka 24:13-35) kunaweza kutoa kidokezo kwa jinsi gani Yesu alivyofundisha Mitume (kama vile Yohana 16:25-27,29). Yeye mwenyewe katika kuonekana baada ya kufufuka alionyesha jinsi Agano la Kale lilivyotumiwa na kuonyesha kivuli

Page 277: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

261

cha mbele cha huduma yake.Hii inaweka kipengere cha mafundisho ya petro katika Matendo (kerygma, tazama Mada Maalum katika Yohana 5:39). ◙ “Nitawaambia wazi wazi” Tazama Mada Maaalum: Ujasiri (Parrhēsia) katika Yohana 7:4 16:26 “Na siku ile mtaomba kwa jina langu, wala siwaambii ya kwamba mimi nitawaombea kwa Baba” Aya hii inaonyesha ukweli muhimu. Wakristo wengi wa kisasa wanahisi kwamba hawawezi kumkaribia Mungu moja kwa moja! Hata hivyo, Biblia inafundisha kwamba

1. Roho huwaombea wanaoamini (kama vile Warumi 8:26-27) 2. Mwana huwaombea kwa wanaoamini katika Yohana1. 2:1 3. Wanaoamini wanaweza kumkaribia Mungu moja kwa moja katika maombi kwa sababu ya Kristo

16:27 “Kwa kuwa Baba mwenyewe awapenda” Hili neno kwa maana ya “upendo” ni phileō, ambao linatumika pia katika Yohana 5:20 kwa upendo wa Baba kwa Kristo. Ni kauli ya ajabu ambayo inaongeza nguvu katika Yohana 3:16 (ambayo hutumia agapaō). Sio Mungu mkaidi ambaye Yesu huhitaji kumtuliza, lakini ni yule Baba mwenye upendo ambaye Yesu humtendea kazi ili kukamilisha kusudi lao la ukombozi. NASB “hutoka kwa Baba” NKJV, NRSV, TEV, NJB “Kutoka kwa Mungu” Kuna miswada miwili tofauti ya Kiyunani: (1). “Mungu” ama “Baba” na (2). Kuwepo au kutokuwepo kwa kikororo. Neno “Mungu” linaonekana katika MSS P5, אi2, A, and N, ambapo neno “Mungu mwenyewe” linaonekana katika MSS C3 and W. huu unaonekana ni utohoaji mgumu na usio wa kawaida. Ni mojawapo ya upagazi wa ukosoaji wa maandishi (tazama Mada Maalumu: Ukosoaji wa Maandishi) kwamba andiko lililogumu au lisilo la kawaida yumkini ndilo la asili lililokusudiwa na waandishi kulisema. Shirika ya umoja wa Biblia ya Agano Jipya la Kiyunani linatoa daraja la “C” katika kupanga viwango (ngumu katika kuamua). Hata hivyo neno “Baba” linaonekana katika in אi1 na neno “Baba mwenyewe” katika B, C*, D, na L. Linafaa sana kwenye muktadha huu. ◙ “Kwa sababu mmenipenda mimi na kuamini kwamba nilikuja kutoka kwa Baba” Hizi ni kauli mbili tendaji elekezi za wakati timilifu. Upendo na imani katika Yesu vinaweka jukwaa la Ushirika pamoja na Baba. Maelezo katika A Translator's Handbook on the Gospel of John cha Barclay Newman na Eugene Nida ni ya kuvutia sana: “Kauli hii inaashiria kwamba kwa Yohana dhana ya upendo, utii, na imani ni njia tofauti za kuelezea uhusiano wa mtu kwa Mwana” (uk 518). Kwa neno“waaminio” tazama Mada Maalum: Matumizi ya Yohana ya kitenzi "Sadiki." Katika Yohana 2:23 16:28 “Nalitoka na nimekuja” Hii ni njeo ya wakati uliopita usiotimilifu ikifuatiwa na njeo ya wakati timilifu. Yesu alizaliwa Bethlehemu (kuzaliwa kimwili) na matokeo ya kuja kwake yanadumu (yaani, mimi nipo pamoja na ninyi siku zote,” kama vile Mathayo 28:20). Ukweli kwamba Yesu “alikuja kutoka kwa Baba” (kama vile Yohana 16:27, 30; 8:42; 13:3; 17:8) inaonyesha

1. Kuwepo kwake hata kabla ya yote 2. Uungu wake 3. Ufunuo wake mkamilifu wa Baba

◙ “Nauacha ulimwengu nakwenda kwa Baba” Hii inarejea kupaa kwake kulikofuata na mwanzo wa huduma ya “Msaidizi wake” ambaye ni Roho na huduma ya maombezi ya Yesu (kama vile Ebr. 7:25; 9:24; Yohana 1. 2:1). kama kuwepo kwake kabla ya yote kulivyoonyeshwa katika Yohana 1:1, kwa hiyo, kurejeshwa kwa Yesu kwenye utukufu na nguvu kunaonyeshwa katika aya hii (kama vile Yohana 17:5, 24).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 16:19-33 19Yesu alifahamu ya kwamba wanataka kumwuliza, akawaambia, Ndilo hilo mnaloulizana, ya kuwa

Page 278: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

262

nalisema, Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni, na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona? 20Amin, amin, nawaambia, Ninyi mtalia na kuomboleza, bali ulimwengu utafurahi; ninyi mtahuzunishwa, lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha. 21 Mwanamke azaapo, yuna huzuni kwa kuwa saa yake imefika; lakini akiisha kuzaa mwana, haikumbuki tena ile dhiki, kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtu ulimwenguni. 22 Basi ninyi hivi sasa mna huzuni; lakini mimi nitawaona tena; na mioyo yenu itafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleaye. 23 Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu. 24 Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu. 25 Hayo nimesema nanyi kwa mithali; saa yaja ambapo sitasema nanyi tena kwa mithali, lakini nitawapa waziwazi habari ya Baba. 26 Na siku ile mtaomba kwa jina langu, wala siwaambii ya kwamba mimi nitawaombea kwa Baba; 27 kwa maana Baba mwenyewe awapenda kwa kuwa ninyi mmenipenda mimi, na kusadiki ya kwamba mimi nalitoka kwa Baba. 28 Nalitoka kwa Baba, nami nimekuja hapa ulimwenguni; tena nauacha ulimwengu; na kwenda kwa Baba. 29 Basi wanafunzi wake wakasema, Tazama, sasa wasema waziwazi, wala huneni mithali yo yote. 30 Sasa tumejua ya kuwa wewe wafahamu mambo yote, wala huna haja ya mtu akuulize; kwa hiyo twasadiki ya kwamba ulitoka kwa Mungu. 31 Yesu akawajibu, Je! Mnasadiki sasa? 32 Tazama, saa yaja, naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke yangu; walakini mimi si peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami. 33 Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.

16:29 "wasema waziwazi" Tazama Mada Maalum: Ujasiri (parrhēsia) katika Yohana 7:4 16:30 Sentensi hii lazima ieleweke katika mwanga wa Yesu kulijua swali la wanafunzi wake katika Yohana 16:19. Kauli hii kwao inaonyesha kukua kwao, lakini bado hawajakamilika, katika imani. Walikwisha kuona na kusikia mengi; Je! tukio hili (kama vile Yohana 16:19) linafanya kazi kama hatua kubwa ya kurudi nyuma katika ufahamu wao? Kwangu hii inaonekana kama moja ya nia nzuri ya Petro ikiwa imetiwa chumvi katika maelezo (tazama The Jerome Biblical Commentary, ukr. 456). 16:31 “Mnasadiki sasa?” Hii inaweza kuwa swali au maelezo. Tafsiri nyingi za kisasa za kingereza zilielewa kama swali. Hata katika kipindi hiki muhimu imani ya mitume ilikuwa haijakamilika. Waumini wa mwanzo, lakini dhaifu, imani pia inakubaliwa na Mungu pale wanapomkubali Yesu wakisimamia juu ya mwanga walionao. Kupungukiwa imani kwa wanafunzi utakuwa ni ushahidi dhahiri katika kumkataa kwao Yesu wakati wa majaribu yake na kusulubiwa. 16:32 “Ninyi kutawanyika kila mmoja kwenda nyumbani kwake na kuniacha mimi peke yangu” Inavyoonekana Yohana peke yake ndiye alikuwepo wakati wa majaribu na kusulubiwa (kama vile Mt. 26:31 kutoka Zek. 13:7). Yohana 21:1-3 inapendekeza kwamba baadhi ya mitume walikuwa wamerudi kuvua samaki kama kazi yao ya wito. Yesu alikuwa amenyang’anywa ushirika wa kibinadamu (kama vile Mt. 26:38, 40-41, 43, 45), lakini kamwe si ushirika wa ki-Ungu (kama vile Yohana 8:16, 29) hadi kusulubiwa, pale alipobeba dhambi ya ulimwengu wote (kama vile Mt. 27:45-46). NASB “Nyumbani kwake mwenyewe” NKJV “Kwake” NRSV “Nyumbani kwake” NJB “Njia yake mwenyewe” TEV “Nyumbani kwako mwenyewe” REB, NET, NIV “Nyumbani kwake mwenyewe” Toleo la NKJV ni halisia. Tafsiri nyingi za kingereza zinachukulia kwamba inarejerea kwenye nyumba ya mtu. Bultman anadai inarejea kwa “umiliki” au ‘mali” (NIDOTTE, juzuu 2, uk 839), inarejea kwa Yesu kama muumbaji (yaani, Yohana 1:3; Wakorintho 1. 8:6; Wakolosai 1:16; Waebrania 1:2).

Page 279: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

263

16:33 “Ndani yangu mnaweza kupata amani” Hiki ni Kauli tendaji tegemezi ya wakati uliopo (kama vile. Yohana 14:27) amani pingamizi na kandamizi zote zinapatikana na kudumishwa katika Kristo. Tazama Mada Maalum: Amani katika Yohana 14:27 ◙ “Ulimwengu” Yohana anatumia “ulimwengu” katika muktadha huu kama jamii ya mwanadamu iliyojipanga na kufanya kazi mbali na Mungu. Tazama Mada Maalum: Kosmos (Ulimwengu/dunia) katika Yohana 14:17 ◙ “Ninayo mateso” Mateso aliyoyapata Yesu, na wao watayapata (kama vile Yohana 15:18-25; Mathayo 5:10-12; Mdo. 14:22; 1 Wathesalonike 3:3). Mateso (yaani, thlipsis) ni njia ya kuwafunua wanafunzi wa kweli wa Yesu. Katika ufunuo kuna utofautishaji wa kithiolojia kati ya “ghadhabu” na “mateso.” Ghadhabu ya Mungu kamwe haiwaangukii wanaoamini bali wasioamini, lakini hasira ya wasioamini huwaangukia wale wanaoamini. Ulimwengu unajifunua wenyewe kama mwana wa shetani kwa mashambulizi yake juu ya “nuru ya ulimwengu” (kama vile Yohana 1:1-18; 3:17-21)! ◙ “Jipeni moyo” Hii ni kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopo (kama vile Mt. 9:2,22; 14:27; Marko 6:50; 10:49; Mdo. 23:11). Yanasikika kama maneno ya YHWH kwa Yoshua (kama vile Yos. 1:6, 9, 18; 10:25). ◙ “Mimi nimeushinda ulimwengu” Hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati timilifu. Ushindi ulikuwa wa wa uhakika hata kabla ya Gethsemani, kabla ya kalvari; kabla ya lile kaburi tupu (kama vile Warumi 8:37; Wakorintho 1. 15:57; 2 Wakorintho 2:14; 4:7-15)! Hakuna uhakika wa pande mbili, Mungu yupo katika udhibiti. Jinsi Yesu alivyoushinda ulimwengu kwa upendo na utii kwa Baba, wanaoamini pia wanashida kupitia kwake (kama vile 1 Yohana 2:13-14; 4:4; 5:4-5; Ufu. 3:21; 12:11).

MASWALI YA MJADALA

Huu ni mwongozo wa fasiri, ina maanisha kwamba unawajibika kwa tafsiri zako mwenyewe za Biblia. Kila mmoja wetu lazima atembee katika mwanga tulio nao. Wewe, Biblia, na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Hutakiwi uvitelekeze vitu hivi kwa mfasiri. Maswali ya mjadala huu yanatolewa kukusaidia kufikiri juu ya mambo makubwa ya sehemu za kitabu hiki. Yanalenga kukuamsha kimawazo na sio kutoa maana.

1. Kuna uhusiano gani kati ya Yohana 15 na 16? 2. Katika kuhusiana na Yohana 16:5 unaelewaje 13:36? 3. Je! nini huduma ya Roho Mtakatifu kwa ulimwengu uliopotea? 4. Je! nini huduma ya Roho Mtakatifu kwa wanaoamini? 5. Kwa nini Yohana 16:26 ni kweli za muhimu sana inahitajika katika nuru ya mwelekeo wa kisasa wa

kimadhehebu?

Page 280: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

264

YOHANA 17

MZUNGUKO WA TATU WA USOMAJI KUFUATILIA KUSUDIO LA ASILI LA MWANDISHI KATIKA NGAZI YA AYA Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwatafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Aya ya kwanza 2. Aya ya pili 3. Aya ya tatu 4. N.k

UTAMBUZI WA KI-MUKTADHA WA MSTARI WA 1-26

A. Muundo wa Ki-historia 1. Sura hii ni Sala Kuu ya Kikuhani

a. Yeye Mwenyewe (Yohana 17:1-5) b. Wanafunzi wake (Yohana 17:6-19) c. Wafuasi wa baadae (Yohana 17:20-26)

Ilitolewa katika mazingira ya kujiamini, si kujiuzulu (kama vile Yohana 16:33 2. Hii ndiyo sala ya ndefu ya Yesu iliyochukuliwa kumbukumbu

3. Sala hii ni ngumu kuigawa katika masomo kwa sababu vipengele vile vile vimetamkwa mara kwa mara,

ambavyo ni kiainisho cha maandiko ya Yohana. Hii ni kama kuweka utepe wa mpangilio unaojirudia.

Maneno ya ufunguo ni “utukufu” “wapatie” “jua” “kutumia” “jina” “ulimwengu”, na “moja”

4. Hakuna tamko la Roho Mtakatifu katika sura hii. Hii si kawaida kwa sababu ya kujitokeza Kwake katika

Yohana 14:-16.

B. Sifa bainifu za Wanafunzi katika Yohana 16:6-19

1. Wao ni wateule

MIGAWANYO YA AYA YA TAFSIRI ZA KISASA

UBS4 NKJV NRSV TEV NJB Sala ya Yesu Yesu Anajiombea Maombi Makuu ya Yesu Anawaombea Sala ya Yesu Mwenyewe Kikuhani Wanafunzi Wake 17:1-5 17:1-5 17:1-5 17:1-5 17:1-23 Yesu anawaombea Wanafunzi Wake 17:6-19 17:6-19 17:6-19 17:6-8 Yesu Anawaombea 17:9-19 Waamini Wote 17:20-26 17:20-26 17:20-24 17:20-23 17:24-26 17:24-26 17:25-26

Page 281: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

265

2. Wao ni watiifu

3. Wanamjua Mungu na Kristo

4. Wanaikubali kweli

5. Wanaombewa na Yesu

6. Wanaishi ulimwenguni

7. Wanalindwa kwa nguvu Zake

8. Wao ni wamoja kama Baba na Yesu walivyo wamoja

9. Wanayo furaha Yake

10. Si wa ulimwengu huu

11. Wametakaswa kwa ile kweli

12. Wametumwa kama Yeye alivyotumwa

13. Wanapendwa kama vile Baba alivyompenda Yesu

C. Neno “utukufu” katika Yohana

1. Kuna zaidi ya maneno 25 ya Kiebrania yaliyotafsiriwa kwa neno doxa katika Maandiko ya kale ya

Kiyahudi (L X X).Neno kuu la Agano la Kale ni kabod, linalomaanisha “tofauti” “uzani” “uzito” “u-

thamani” “-enye sifa” “heshima” au mwangaza /ubora”

2. Neno la Kiyunani doxa linatokana na kitenzi cha neno “kufikiri” katika fasili ya sifa

3. Zipo maana nyingi tofauti za hili neno katika Yohana

a. utukufu wa ki-Ungu (kama vile Yohana 17:5, 24; 1:14; 12:41; 12:16)

b. ufunuo wa Baba kwa ishara za Yesu, mafundisho,na kazi kwenye Juma la Mateso (kama vile

Yohana 17:4, 10, 22; 1:14; 2:11; 7:18; 11:4, 40)

c. hasa msalaba (kama vile Yohana 17:1, 4; 7:39; 12:23; 13:31-32)

Hakika kuna kiasi cha bubujiko katika matumizi haya. Ukweli mkuu ni kwamba Mungu asiyeonekana amefunuliwa

ndani ya mwanadamu (yaani, Yesu Kristo) kwa Maneno na Matendo Yake.

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 17:1-5 1Maneno hayo aliyasema Yesu; akainua macho yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe; 2kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele. 3Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. 4Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye. 5Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.

17:1 “Maneno hayo aliyasema Yesu” Hii lazima inarejea mazungumzo ya ghorofani ya Yohana 13-16

◙ “Akiinua machoyake kuelekea mbinguni” Huu ulikuwa mkao wa kawaida kwa Wayahudi wakati wa kuomba:

mikono, kichwa na macho yaliyofunguliwa viliinuliwa kuelekea mbinguni kama vile kukiwa na mazungumzo na

Mungu (kama vile Yohana 11:41; Marko 7:34; Luka 18:13; Zab. 123:1), Yesu aliomba mara nyingi. Hili linaweza

kuorodheshwa kwa usahihi kutoka Injili ya Luka 3:21; 5:16; 6:12; 9:18, 28; 11:1; 22:41-45;23:34.

◙ “Baba” Yesu kwa kawaida aliutaja Uungu kwa neno hili (kama vile Yohana 11:41; 12:27, 28; Mathayo 11:25-27;

Luka 22:42; 23:34).Yesu alizungumza Kiaramu. Neno la Kiaramu la Yesu lilikuwa abba, ambalo mtoto alilitumia

Page 282: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

266

kwa baba yake nyumbani “Aba” (kama vile Marko 14:36). Jambo hili lazima litakuwa limewashtua na kuwachukiza

wale ambao hawakuwa wanafunzi wa Yesu.

◙ “Saa imekwisha kufika”Hii inaonyesha kwamba Yesu alilijua kusudi na muda wa huduma Yake (kama vile

Yohana 2:4; 7:6, 8, 30; 8:20; 12:23; 13:1).Yeye hakukumbwa na hali ya mambo yasiyojulikana.

◙ “Mtukuze Mwanao” Hiki ni kitenzi tendaji cha kauli shurutishi. Mara nyingi Yesu alirejerea juu ya kifo Chake kwa maneno yaliyo sawa na yale yaliyo katika Yohana (kama vile Yohana 17:4; 7:39; 12:23; 13:31-32). Neno hili pia linahusiana na Uungu wa Yesu uliokuwepo kabla (kama vile Yohana 1:14 na Yohana 17:5, 24). Matendo ya Yesu yalimtukuza Baba. Kulikuwa kutendeana! Tazama nukuu katika 1:14 kwa mtazamo wa Ndani. Kwa neno “Mwana” tazama Mada Maalumu katika 1 Yohana 3:8 Kuna utofauti ya ki-machapisho yahusianayo na neno “Mwana”

1. Neno Mwana likiwa na kifungu linaonekana katika MSSP60, א, B C*,W

2. Neno Mwana likiwa na kiwakilishi kimilikishi linaonekana katika MSS A, D, C2

UBS4 inatoa muundo wa #1 alama “B” (yumkini ina uhakika)

17:2 “Mamlaka juu ya wote wenye mwili” Hii ni kauli ya ajabu iliyotolewa na selemara mkulima (kama vile Yohana 5:27; Mt. 11:27; 28:18; Luka 10:22). Neno mamlaka (exousia) ni sawa na lile liliotumika katika Yohana 1:12; 5:27; 19:10, 11. Neno hili linaweza kufasiriwa kama “haki ya kisheria” “mamlaka” au “nguvu” Kifungu “wote wenye mwili” kiko katika hali ya umoja (nahau ya Kiebrania inayorejea juu ya mwanadamu,

kama vile Mwa 6:12; Zab. 65:2; 145:21; Isa. 40:5; 66:23; Yoeli 2:28)

◙ “ili kwamba wote ulioumpa” Neno “wote uliompa” hii ni sentensi isiyo na shamirisho iliyo katika hali ya umoja (kama vile yohana 7:24), ambayo ina mtazamo juu ya wanafunzi, mwili wa Kristo, na sio watu binafsi! Kitenzi hiki ni kauli tendaji elekezi ya wakati timilfu ambacho kinazungumzia kipawa cha uvumilivu.Aya hii inathibitisha kujua kitu kabla hakijatokea na kufanya uchaguzi (kama vile Yohana 17:6, 9, 12; 6:37, 39; Warumi 8:29-30; Waefeso 1:3-14).uchaguzi Katika Agano la Kale ulifanywa kwa ajili ya huduma, ambapo katika Agano Jipya ni kwa ajili ya mambo ya kiroho, utunzaji,na wokovu wa milele. Waaminio wameitwa pia kwa ajili ya huduma. Uchaguzi sio tendo la ki-Ungu tu, bali lazima liwe limeunganishwa kimaagano na jukumu la mwanadamu. Halikutazamia katika kifo bali uzima! Waamini wamechaguliwa kwa ajili ya “utakatifu” (kama vile Efe. 1:4), sio kwa msimamo wa kiupendeleo. Kifungu hiki hakipaswi kueleweka kama Baba hutoa baadhi ya watu kwa yesu na wengine huwaacha.

MADA MAALUM: UCHAGUZI/MAJAALIWA NA UHITAJI WA USAWA KITHIOLOJIA Uchaguzi ni fundisho la ajabu. Hata hiyo, si wito ulio na upendeleo, lakini ni wito kuwa njia, chombo, au njia za ukombozi kwa wengine! Katika Agano la Kale neno hilo lilitumiwa hasa kwa ajili ya huduma; katika Agano Jipya linatumika hasa kwa ajili ya wokovu unaohusika katika huduma. Biblia hipatanishi kamwe kupingana kati ya Ufalme wa Mungu na mapenzi huru ya mwanadamu, lakini inathibitisha zote mbili! Mfano mzuri wa mvutano wa kibiblia itakuwa Warumi 9 juu ya uchaguziwa Ufalme na Warumi 10 juu ya majibu muhimu ya wanadamu (kama vile Warumi 10:11,13). Umuhimu wa huu muvatano wa kitheolojia unaweza kupatikana katika 1:4. Yesu ni mwanadamu mchaguzi wa Mungu na wote ni uwezo wa kuchaguliwa ndani yake (Karl Barth). Yesu ni Mungu. Yesu "ndio" kwa mahitaji ya mwanadamu aliyeanguka (Karl Barth). Waefeso 1:4 pia husaidia kufafanua suala hilo kwa kuthibitisha kwamba lengo la majaaliwa si mbinguni tu, lakini utakatifu (mapenzi ya kristo). Mara nyingi sisi huvutiwa na faida za injili na kupuuza majukumu! Wito wa Mungu (uchaguzi) ni kwa wakati pamoja na milelel! Mafundisho huja kuhusiana na ukweli mwingine, sio mmoja tu, ukweli usiohusiana. Hali au tabia nzuri inakuwa ni kundi dhidi ya nyota moja. Mugu hutoa ukweli katika mashariki na sio magharibi, mtindo. Hatupaswi kuondoa mvutano unaosababishwa na jozi za lahaja(fumbo la maneno) za kweli za mafundisho:

Page 283: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

267

13. majaaaliwa/mchaguzi dhidi ya mapenzi huru ya mwanadamu 14. Usalama wa wanaoamini dhidi ya mahitaji ya uvumilivu 15. Dhambi ya asili dhidi ya dhambi ya hiari 16. Kutotenda dhambi dhidi ya kutenda dhambi kidogo 17. Udhihirisho na utakaso wa papo kwa papo dhidi ya utakaso endelevu 18. Uhuru wa Kikristo dhidi ya wajibu wa Kikristo 19. Mungu anayeweza kupita uwezo wa binadamu dhidi ya Mungu wa asili 20. Mungu kama hatimaye isiyojulikana dhidi ya Mungu anayejulikana katika maandiko 21. Ufalme wa Mungu kama sasa dhidi ya kukamilishwa baadaye 22. Kutubu kama zawadi ya Mungu dhidi ya jibu muhimu la Agano la kibinadamu 23. Yesu kama Mungu dhidi ya Yesu kama mwanadamu 24. Yesu ni sawa na Mungu Baba dhidi ya Yesu wa kumtumikia Mungu Baba

Dhana ya kitheolojia ya “agano” inaunganisha Ufalme wa Mungu (ambaye daia huchukua hatua kwa kuweka mswada) pamoja na mamlaka ya mwanzo imani ya kuendelea kutubu kujibiwa kutoka kwa mwanadamu(k.v. Marko 1:15; Mdo. 3:16,19; 20:21). Kuwa mwangalifu wa maandishi ya uthibitisho wa upande mmoja wa fumbo la maneno na punguza kwa mwingine! Kuwa mwangalifu wa kuthibitisha mafundisho yako ya mapenzi tu au mfumo wa thiolojia!

◙ “awape uzima wa milele” Uzima wa milele na kipawa kutoka kwa Mungu kupitia Kristo (kama vile Yohana 5:21,

26; 6:40, 47; 10:28; 1 Yohana 2:25; 5:11). Inamaanisha “uzima wa Mungu,” “maisha ya zama mpya,” au maisha ya

ufufuo.” Kimsingi hii haipimwi kwa idadi, uzito au wingi, bali kwa ubora (kama vile Yohana 10:10)

17:3 “Na uzima wa milele ndio huu” Huu ni ufafanuzi wa neno “uzima wa milele” ulivyoingizwa na Yohana. Mstari

huu unaonyesha kweli kuu mbili za Ukristo: (1) Mungu mmoja (kama vile Kumb. 6:4-6) na (2) Yesu kama Masihi wa

kizazi cha Daudi (kama vile 2 Samweli 7). Huu “uzima wa milele” si kitu kilichotunzwa kwa ajili ya wakati ujao bali

unapatikana sasa katika Kristo.

◙ “Wakujue wewe” Hii ni kauli tendaji tegemezi ya wakati uliopo. Hii hairejerei juu ya maarifa ya kutambua

kuhusu Mungu tu, japo kuna ukweli unaohitajika ili kuthibitika, lakini inatumika katika maana ya lugha ya ki-

Semitiki juu ya uhusiano binafsi. Hata hivyo, ukweli ni kwamba Yesu ndiye Masihi, ufunuo wa Mungu ulio timilifu

na kamili wa yule aliye wa kweli (kama vile Yohana 1:12, 14; Kor.1:5; Ebr. 1:3), na kwamba lazima watu

wamwamini, wampokee, watubu, wamtii na kustahimili katika Yeye.

◙ “Mungu wa pekee wa kweli” Agano la Kale lilikuwa la kipekee katika kutetea kwake uwepo wa yule Mungu

mmoja tu na wa pekee (kama vile Kut. 8:10; 9:14; Kumb. 4:35, 39; 6:4; 33:26; 1 Sam. 2:2; 2 Sam. 7:22; 1 Fal. 8:23;

Isa. 37:20; 44:6, 8; 45:6-7, 14, 18, 21, 22; 46:9; Yohana 5:44; 1 Kor. 8:4,6; 1 Tim. 1:17; 2:5; Yuda 1:25). Katika hii

napaswa kusemwa kwamba, katika Agano la Kale, uwasilishaji wa Mungu Yeye aliye mmoja na wa pekee

umepangwa dhidi ya mazingira ya mtazamo wa ulimwengu wa Mashariki ya kale wenye kuamini viumbe vingi vya

kiroho. Yupo Mungu mmoja, lakini kuna viumbe vingine vya kiroho (kama vile Kut. 15:11; Kumb. 3:24; Zab. 86:8;

89:6).

MADA MAALUM: IMANI KATIKA MUNGU MMOJA

Mwanadamu siku zote amekuwa akihisi kuna zaidi ya ukweli kuliko huu unaoonekana (yaani kuathiriwa na vitu nje ya uwezo, kama vile dhoruba, kupatwa kwa jua na mwezi, kuanguka kwa vimondo, hali ya hewa, matukio, vifo, n.k.). Wataalamu wa sayansi ya binadamu wanatwambia kuwa wanakutana na vitu katika makaburi ya wanyama wa kale waliowahi kuishi ambavyo yumkini ni viashiria ya maisha yajayo, ambayo yanaweza kuonekana kama mwendelezo wa maisha ya baadaye.

Page 284: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

268

Tamaduni ya kwanza kuandikwa ilikuwa ni ya wakati wa kiangazi (Hedekeli Kusini, Mito Yufrati), ilianza miaka ya 10,000 - 8,000 K.K. Waliandika mashairi kuelezea mawazo yao kwa Mungu na namna wanavyojamiiana. Tena, zaidi kama wanadamu pamoja na madhaifu yao yote. Tamaduni zao zilikuwepo katika namna za midomo zamani hata kabla hazijaandikwa. Kulikuwa na kukua kwa kithiolojia kutoka

1. kuabudu wanyama mpaka 2. kuabudu miungu wengi mpaka 3. mungu mkuu (kuabudu miungu wawili)

Dhana ya "Mungu mmoja" (mmoja na mmoja tu binafsi Mungu mwenye maadili asiye na asili ya kike), si tu "mungu mkuu" ya miungu wengi au mungu mzuri kama miungu ye upili ya kiashuru (wafuasi wa Zoroaster), ni pekee kwa israeli (Ibraham na Ayubu, 2000 K.K.). ni mmoja tu wa pekee asiye patikana patikana katika Misri (Amenhotep IV, pia akijulikana kama Akhenaten, 1367-1350 au 1386-1361 K.K., aliyeabudu Aten, mungu jua, kama mungu pekee). Angalia J. Assmann, The Mind of Egypt, kurasa za 216-217. Dhana hii inaelezea katika tungo kadhaa katika Agano la Kale

1. "hakuna kama YHWH wetu Elohim," Kutoka 8:10; 9:14; Kumbukumbu la Torati 33:26; 1 Wafalme 8:23 2. "Hakuna mwingine zaidi Yake," Kumbukumbu la Torati:30; 1 Kor. 8:4,6; 1 Tim. 2:5; Yakobo 2:19 3. "Hakuna kama wewe," 2 Samweli 7:22; Yeremia 10:6 4. "wewe pekee ndiwe Mungu," Zaburi 86:10; Isaya 37:16 5. "Kabla yangu hakukuwa na Mungu na baada yangu hatotokea," Isaya 43:10 adherence 6. "hakuna mwingine; zaidi yangu. . .hakuna mwingine," Isaya 45:5,6,22 7. "Yeye ni chanzo cha vitu vyote," Isaya 45:7 (kama vile Amosi 3:6) 8. "hakuna mwingine, hakuna Mungu mwingine," Isaya 45:14,18 9. "hakuna mwingine isipokuwa," Isaya 45:21 10. "hakuna kama mwingine;. . .hakuna kama mimi," Isaya 46:9

Lazima kukiri kuwa fundisho hili muhimu limefunuliwa katika maendeleo katika njia. Kauli ya mwanzo ingeweza kueleweka "utii kwa mungu mmoja kati ya wengi" au kuabudu mungu mmoja kwa kimatendo (kuna miungu mingine, yani Joshua 24:15; 1 Wafalme 18:21), lakini Mungu mmoja tu kwa ajili yetu (kama vile Kutoka 15:11; 20:2-5; Kumbukumbu la Torati 5:7; 6:4,14; 10:17; 32:12; 1 Wafalme 8:23; Zaburi 83:18; 86:8; 136:1-9). Maandiko ya kwanza ambayo yalianza kuonesha umoja (Hali ya Kifalsafa ya Mungu mmoja) ni mapema (kama vile Kutoka 8:10; 9:14; 20:2-3; Kumbukumbu la Torati 4:35,39; 33:26). Madai yaliyokamili na yashinda nayo yanapatikana katika Isaya 43-46 (kama vile 43:10-11; 44:6,8; 45:7,14,18,22; 46:5,9). Agano la Kale linapunguza miungu ya mataifa kama

1. Uumbaji wa kibinadamu – Kumbukumbu la Torati 4:28; 2 Wafalme 19:18; Zaburi 115:4-8; 135:15-18; Isaya 2:8; 17:8; 37:19; 40:19; 41:7,24,29; 44:10,12; 46:6-7; Yeremia 10:3-5; Ufunuo 9:10

2. mapepo – Kumbukumbu la Torati 32:17; Zaburi 106:37; Isaya 8:19; 19:3c; 1 Kor. 10:20; Ufunuo 9:20 3. ubatili, utupu – KumbuKumbu la Torati 32:21; 2 Wafalme 17:15; Zaburi 31:6; Isaya 2:18; 41:29;

Yeremia 2:5; 10:8; 14:22; Yeremia 2:5; 8:19 4. hakuna miungu – Kumbukumbu la Torati 32:21; 2 Nyakati 13:9; Isaya 37:19; Yeremia 2:11; 5:7; 1 Kor.

8:4-5; 10:20; Ufunuo 9:20 Agano Jipya linaelezea katika Kumbukumbu la Torati 6:4 katika Warumi 3:30; 1 Kor. 8:4,6; Efe 4:6; 1 Tim. 2:5; na Yakobo 2:19. Yesu alinukuu kama amri ya kwanza katika Mt. 22:36-37; Marko 12:29-30; Luka 10:27. Agano la Kale pia kama Agano Jipya, linaelezea ukweli wa viumbe vingine vya kiroho (mapepo, malaika), lakini muumbaji mmoja tu/Mungu mkombozi (YHWH, Mwanzo 1:1). hali ya kuwepo kwa Mungu mmoja kibiblia kunatabia zifuatazo

1. Mungu ni mmoja na wa pekee ((ontology) nadharia inayojishughulisha na asili ya uhai inadhaniwa, haijawekwa bayana)

2. Mungu ni wa binafsi (kama vile Mwanzo 1:26-27; 3:8) 3. Mungu ni mwadilifu (kama vile Mwanzo 34:6; Nehemia 9:17; Zaburi 103:8-10) 4. Mungu aliwaumba wanadamu katika sura yake (Mwanzo 1:26-27) kwa ajili ya ushirika (yaani #2). Ni

Mungu mwenye wivu (kama vile Kutoka 20:5-6)

Page 285: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

269

Kutoka katika Agano Jipya 1. Mungu ana milele tatu, udhihirisho wa nafsi (angalia Mada Maalum: Utatu) 2. Mungu kwa ukamilifu wake amefunuliwa kikamilifu ndani ya Yesu (kama vile Yohana 1:1-14; Kol. 1:15-

19; Ebr. 1:2-3) 3. Mpango wa milele wa Mungu kwa ukombozi wa mwanadamu aliyeanguka ni sadaka ya Mwanawe wa

Pekee (Isaya 53; Marko 10:45; 2 Kor. 5:21; Fil. 2:6-11; Waebrania)

MADA MAALUMU: “KWELI” (NENO) KATIKA MAANDIKO YA YOHANA

1. Mungu Baba a. Mungu ni kweli /Mwaminifu (kama vile Yohana 3:33; 7:18,28; 8:26; 17:3; Rum. 3:4; 1 Thes. 1:9; 1

Yohana 5:20; Ufu. 6:10)

b. Njia za Mungu ni za kweli (kama vile Ufu.15:3) c. Hukumu ya Mungu ni ya kweli (kama vile Ufu.16:7; 19:2) d. Maneno ya Mungu ni ya kweli (kama vile Ufu.19:11)

2. Mungu Mwana a. Mwana ni kweli/mkweli

1) Nuru ya kweli (kama vile Yohana 1:9; 1 Yohana 2:8) 2) Mzabibu wa kweli (kama vile Yohana 15:1) 3) Mwingi wa rehema na ukweli (kama vile Yohana 1:14,17) 4) Yeye ni ukweli (kama vile Yohana 14:6; 8:32) 5) Yeye ni kweli (kama vile Ufu. 3:7,14; 19:11)

b. Ushuhuda wa mwana ni wa kweli (kama vile Yohana 18:37) 3. Inaweza kuwa na maana ya ulinganifu kati ya

a. Sheria ya Musa dhidi ya ukweli na neema ya Yesu (kama vile Yohana 1:17) b. Hema la kukutania kule nyikani dhidi ya Hema la Mbinguni (kama vile Ebr. 8:2; 9:1)

4. Kama ilivyo mara kwa mara katika maandishi ya Yohana neno hili lina vidokezo vingi (Kiebrania na Kiyunani). Yohana anavitumia vyote kuelezea Baba na Mwana, kama watu, kama wanenaji, na kama jumbe zao ambazo zinahitaji kupitishwa kwa wafuasi wao (kama vile Yohana 4:23; 19:35; Ebr. 10:22; Ufu. 22:6).

5. Kwa Yohana vivumishi hivi viwili vinaelezea Baba kama mmoja na pekee Mungu mwaminifu (kama vile 5:44; 1 Yohana 5:20) na Yesu kama ufunuo wake kamili na wa kweli kwa kusudi la ukombozi, sio tu kwa ajili ya utambuzi, jambo la hakika!.

◙ “Na Yesu Kristo uliyemtuma” Hii inaweza kuwa hoja ya kiuandishi ya Yohana. Msisitizo huu juu ya Yesu kama

“aliyetumwa” kutoka kwa Baba ni urudiaji wa mambo mawili yaliyo sahihi katika Yohana (kama vile Yohana

3:17,34; 5:36, 38; 6:29,38,57; 7:29; 8:42; 10:36; 11:42; 17:3,18,21,23,25; 20:21). Waalimu wa sharia za dini za

Kiyahudi walitumia neno apostellō kurejelea juu ya mtu aliyetumwa kama mwakilishi rasmi. Tazama Mada

Maalumu: Kupelekwa (apostellō) katika Yohana 5:24

17:4 “Mimi nimekutukuza duniani” (Tazama nukuu katika Yohana 13:32) Neno “utukufu” linaweza kutumika kwa

maana ya (1) “kumpa utukufu” au (2) “kufunua utukufu wa” .Yohana 17:6 inadokeza #2. Moja ya kazi kuu ya Yesu

ilikuwa ni kumfunua Baba (kama vile Yohana 1:14, 18)

◙ “hali nimeimaliza kazi” Mzizi wa neno la Kiyunani telos, unadokeza “kutimiza kikamilifu” (kama vile Yohana 4:34; 5:36; 19:30). Kazi ilikuwa katika vipengele vitatu.

1. kumfunua Baba (kama vile Yohana 1:14,18)

Page 286: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

270

2. ukombozi wa mwanadamu aliyeanguka (Marko 10:45; 2 Kor. 5:21)

3. mfano wa utu wa kweli (kama vile Yohana 13:31; 1 Pet. 2:21)

4. Pia, kazi ya Yesu ya kutuombea inayoendelea (kama vile 1 Yohana 2:1; Ebr. 7:25; 9:24).

17:5 “unitukuze… utukufu” Mstari huu unasisitiza juu ya uwepo wa Kristo kabla ya kuzaliwa kwake (kama vile

Yohana 1:1, 15; 6:62; 8:58; 16:28; 17:11, 13, 24; 2 Kor. 8:9; Flp. 2:6-11; Kol. 1:17; Ebr. 1:3; 10; 5-8). Yesu

ameufunua “utukufu” kwa wanafunzi kwa ishara na miujiza Yake (kama vile Yohana 1:14; 2:11; 11:4, 40; 12:28).

Sasa “utukufu” dhahili ungekuwa kifo Chake, ufufuo, na kupaa kwake kurudi kwenye “utukufu” wa mbinguni

(kama vileYohana 17:24; Flp. 2:5-6). Kitenzi ni kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopita usiotimilifu kilichotumika

kama ombi kwa Baba. Tazama maelezo kamili juu ya “utukufu” katika Yohana 1:14.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 17:6-19 6Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; walikuwa wako, ukanipa mimi, na neno lako wamelishika. 7Sasa wamejua ya kuwa yote uliyonipa yatoka kwako. 8Kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; nao wakayapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakasadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. 9Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako; 10na wote walio wangu ni wako, na walio wako ni wangu; nami nimetukuzwa ndani yao. 11Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo. 12Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie. 13Na sasa naja kwako; na maneno haya nayasema ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao. 14Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. 15Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu. 16Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. 17Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.18Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni.19Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.

17:6 “Jina lako nimewadhihirishia” Majina ya Kiebrania yalikusudiwa kuakisi tabia (kama vile Yohana 17:11, 12,25-26; Zab. 9:10). Kifungu hiki pia kithiolojia kinadai kwamba kumwona Yesu ni kumwona Mungu (kama vile Yohana 1:18; 12:45; 14:8-11; Kor. 1:15; Ebr. 1:3). ◙ “jina” linafanya kazi muhimu kithiolojia katika mazungumzo kule ghorofani (kama vile Yohana 14:13, 14, 26; 15:16, 21; 16:23, 24, 26; 17:6, 11, 12, 26).Katika Yohana 17 nyadhifa mbili za kipekee zinatumika kwa Mungu.

1. Baba Mtakatifu, Yohana 17:11

2. Baba mwenye haki, Yohana 17:25

◙ “Watu wale ulionipa” Kithiolojia hii inazungumzia juu ya uchaguzi (kama vile Yohana 17:2, 9, 24; 6:37, 39). Hakuna awezaye kuja kwangu isipokuwa

1. Mungu amempa

2. Roho amemvuta (Yohana 6:44, 65)

3. wamepokea (Yohana 1:12); amini (Yohana 3:16)

◙ “neno lako wamelishika” Utii ni muhimu sana (kama vile Yohana 8:51, 55; 14:23; 15:10, 20). Hili limetumika

katika maana iliyo sawa na Agano la Kale “pasipo lawama” (kama vile Nuhu, Mwa. 6:9; Ibrahimu, Mwa. 17:1;

Israeli Kumb. 18:13; Ayubu, Ayubu 1:1) Hii haidokezi juu ya utii mkamilifu ama kutokuwa na dhambi, bali shauku

ya kusikia na kufanya yale yote yaliyofunuliwa, zaidi linahusu imani ya wanafunzi katika Yesu, kuendelea kudumu

ndani ya Yesu,na kupendana wao kwa wao kama Yesu alivyowapenda wao.

Page 287: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

271

17:7 “Sasa wamejua” Hii ni kauli timilifu tendaji elekezi ikifuatiwa na neno “kile” (hoti), ambayo inarejelea juu ya

maudhui ya ujumbe.Kwa matumizi ya Yohana ya neno “hoti” tazama Mada Maalumu katika Yohana 2:23, #4

◙ “ya kuwa yote uliyonipa yatoka kwako” Yesu alisema kile kilichofunuliwa Kwake na Baba (kama vile Yohana

17:8; 7:16; 12:48-49)

17:8 “nao wakayapokea” Waliupokea ujumbe wa Yesu kumhusu Mungu.Hakuna jambo llilotajwa moja kwa moja.

Katika Yohana 1:12. Jambo la moja kwa moja la kukubali/kupokea lilimrejelea Yesu Mwenyewe; hapa, ni ujumbe

unaomhusu Mungu ambao Yesu aliuleta (kama vile Yohana 17:4).Hii inasisitiza mwonekano pacha wa injili

kama(1) mtu na( 2) ujumbe.

◙ “wakayapokea…, wakayasadiki” Hizi ni kauli tendaji elekezi za wakati uliopita usiotimilifu. Kweli hizi zinarejelea

juu ya asili ya Uungu na ujumbe wa Yesu (kama vile Yohana 5:19; 6:68-69; 12:48-49; 16:30; 17:18,21,23,25).

17:9 “Mimi nawaombea hao” Yesu ni Mpatanishi wetu (kama vile 1 Tim. 2:5; Ebr. 8:6; 9:15; 12:24) na Mtetezi

(kama vile 1 Yohana 2:1). Baba pia anahusika katika kazi hizi (kama vileYohana 16:26-27), kama alivyo (kama vile

Rum. 8:26-27).Nafsi zote tatu za Utatu zinahusika katika vipengele vyote vya ukombozi.

◙ “Ulimwengu” Neno Kosmos limetumika mara kumi na nane katika sura hii. Yesu anashughulikia na (1) dunia

(kama vile Yohana 17:5,24) na (2) Uhusiano wa muumini katika anguko lake (kama vile Yohana 1:10;

17:6,9,11,13,14,15,16,17,18,21,23). Katika maandiko ya Yohana neno hili kwa namna ya kipekee linamaanisha

“jamii ya mwanadamu ambayo imepangwa na inatenda kazi mbali na Mungu.” Wakati mwingine inadokeza

kuhusu (1) dunia (2) maisha yote ya ndani ya dunia; au (3) maisha yaliyo kinyume na Mungu. Tazama

17:10 “na wote walio wangu ni wako, na walio wako ni wangu” Hili linaufunua umoja wa Utatu (kama vile

Yohana 7:11,21-23; 16:15).Kuhusu Utatu tazama Mada Maalumu katika Yohana 14:26

◙ “nimetukuzwa ndani yao” Hii ni kauli timilifu tendewa elekezi. Maisha ya mwanafunzi ni kumpa Yesu heshima

kama Yeye alivyompa utukufu Baba.Ni uwajibikaji gani wenye heshima?

17:11 “Wala mimi simo tena ulimwenguni” Hii inahusu (1) Wakati ujao wa papo hapo (kupaa) wakati Yesu

atakaporudi kwa Baba (kama vile Matendo 1:9-10) au (2) huduma ya Yesu kwa watu wote.

◙ “Baba mtakatifu” Neno hili “Mtakatifu” linatumika hapa kwa Baba tu katika Agano Jipya (Pia limetumika katika sifa, “Aliye Mtakatifu” 1 Pet. 1:15) kama ilivyo katika Agano la Kale. Kivumishi hiki (hagios) mara nyingine pia Roho Mtakatifu anapewa sifa hii (kama vile Yohana 1:33; 14:26; 20:22). Mzizi ule ule wa neno la Kiyunani unatumika kwa wanafunzi katika Yohana 17:17 (hagiasmos) na Yesu katika Yohana 17:19 (hagiazō.) Msingi asilia wa neno ni “kutenga kwa ajili ya utumishi wa Mungu” (Yohana 17:17, 19). Linatumika kwa watu, mahali na vitu vilivyotolewa kikamilifu kwa matumizi ya Mungu, linaelezea sifa za Mungu zipitazo vitu vyote (Aliye Mtakatifu wa Israeli) na utofauti wa kimwonekano, kidunia, vitu vilivyoanguka. Yesu alikuwa mtakatifu; kama wafuasi wake wanavyozidi kuwa kama Yeye, zaidi, nao huakisi “utakatifu.” Mzizi wa neno“mtakatifu” unatokana na neno la Kiyunani “takatifu.” Waamini ni watakatifu kwa kuwa wamo ndani ya Kristo, yawapasa kuwa watakatifu kwa kuwa wanaishi kwa ajili Yake, kama Yeye, na katika Yeye.

MADA MAALUMU: MTAKATIFU

I. Agano la Kale (likielezwa kwa zaidi kutoka Isaya) A. Asili ya neno kadosh (BDB 872, KB 1072) halina uhakika, pengine ni Ki-kanaani (yaani, lugha

Magharibi mwa Syria). Inawezekana kwamba sehemu ya mzizi wa neno (yaani, kd) unamaanisha

Page 288: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

272

"kugawanya." Hiki ni chanzo cha ufafanuzi unaofahamika wa neno "tengwa (kutoka kwenye utamaduni wa ki- Kanaani, kama vile Kumb. 7:6; 14:2,21; 26:19) kwa matumizi ya Mungu."

B. Inahusiana na uwepo wa Mungu ndani ya vitu, mahali, wakati, na watu. Halitumiki katika kitabu cha Mwanzo, bali linakuwa la kawaida katika vitabu vya Kutoka, Mambo ya Walawi, na Hesabu.

C. Katika fasihi ya Kinabii (hasa Isaya na Hosea) hali ya kibinadamu ilikuwepo hapo awali, lakini haikuhimizwa kwa ajili ya kutenda kazi (tazama Mada Maalumu: Aliye Mtakatifu). Inakuwa njia ya kueleza asili ya Mungu.(kama vile Isa. 6:3). Mungu ni Mtakatifu. Jina Lake linalowakilisha sifa yake ni takatifu. Watu wake ndio wanaopaswa kuifunua sifa Yake kwa ulimwengu unaohitaji utakatifu (ikiwa watalitii agano katika imani). 1. KIVUMISHI, BDB 872 ׁשקדו, "takatifu," "tukufu" linatumika juu ya

a. Mungu, Isa. 5:16; 6:3 (mata tatu); tazama Mada Maalumu: Aliye Mtakatifu b. Jina Lake, Isa. 40:25; 49:7; 57:15 c. kukaa Kwake ndani, Isa. 57:15 d. Sabato, Isa. 58:13

2. KITENZI, BDB 872 ׁשקד, "kutengwa mbali," "wekwa wakfu" a. sifa ya Mungu, Isa. 5:16; 29:23 b. Mungu, Isa. 8:13; 65:5 c. malaika wa Mungu, Isa. 13:3 d. jina la Mungu, Isa. 29:23 e. sherehe za kidini, Isa. 30:29 f. wanadamu walioweka wakfu, Isa. 66:17

3. NOMINO, BDB 871 ׁש קד, "utengwaji," "uwekwaji wakfu" a. uzao mtakatifu, Isa. 6:13 b. mlima mtakatifu, Isa. 11:9; 27:13; 56:7; 57:13; 65:11,25; 66:20 c. kutengwa, Isa. 23:18 d. njia ya utakatifu, Isa. 35:8 e. mahali patakatifu, Isa. 43:28; 62:9; 64:11 f. mji mtakatifu, Isa. 48:2; 52:1 g. aliye Mtakatifu, Isa. 49:7 (tazama Mada Maalumu: Aliye Mtakatifu) h. mkono mtakatifu, Isa. 52:10 i. siku takatifu, Isa. 58:13 j. watu watakatifu, Isa. 62:12 k. Roha Mtakatifu, 63:10,11 l. Kiti cha enzi cha Mungu, Isa. 63:15 m. sehemu takatifu, Isa. 63:18 n. miji mitakatifu, Isa. 64:10

D. Huruma ya Mungu na upendo havitenganishwi kutoka katika dhana ya theojia ya maagano,haki, na sifa ya muhimu. Humu ndani pana mvutano wa Mungu dhidi ya utu ulioanguka, usio mtakatifu, wenye kuasi. Kuna mada inayotia shauku sana kuhusiana na mahuhusiano kati ya Mungu kama "mwenye huruma" na Mungu kama "mtakatifu" katika kitabu cha Robert B. Girdlestone, Synonyms of the Old Testament, kr. 112-113.

II. Agano Jipya A. Waandishi wa Agano Jipya (isipokuwa Luka) walikuwa Waebrania wenye fikra pana, lakini

waliandika katika lugha ya kawaida ya Koine. Kanisa la Agano Jipya lilitumia fasiri ya Kiyunani kufasiri kitabu cha Agano la Kale. Ilikuwa ni tafasili ya Kiyunani ya Agano la Kale, sio fasihi ya Kiyunani cha daraja la juu, fikra, au dini, iliyodhibiti misamiati yao.

B. Yesu ni mtakatifu kwa kuwa Yeye ni wa Mungu na ni sawa na Mungu (kama vile Luka 1:35; 4:34; Matendo 3:14; 4:27,30; Ufu. 3:7). Yeye ni Mtakatifu na Mwenye Haki (kama vile Matendo 3:14; 22:14). Yesu ni mtakatifu kwa sababu hana dhambi (kama vile Yohana 8:46; 2 Kor. 5:21; Ebr. 4:15;

Page 289: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

273

7:26; 1 Pet. 1:19; 2:22; 1 Yohana 3:5). C. Kwa kuwa Mungu ni mtakatifu (kama vile Yohana 17:11; 1 Pet. 1:156-16; Ufu. 4:8; 6:10), watoto

Wake yawapasa kuwa watakatifu (kama vile Law. 11:44-45; 19:2; 20:7,26; Mt. 5:48; 1 Pet. 1:16). Kwa kuwa Yesu ni mtakatifu, wafuasi Wake yawapasa kuwa watakatifu (kama vile Rum. 8:28-29; 2 Kor. 3:18; Gal. 4:19; Efe. 1:4; 1 The. 3:13; 4:3; 1 Pet. 1:15). Wakristo wameokolewa ili kutumika katika ufanano wa Kristo (wenye utakatifu).

◙“kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa” Yesu anaomba (hii ni kauli tendaji shurutishi cha wakati uliopita usiotimilifu) kwa kuwezesha ulinzi na uwepo binafsi ambao YHWH amempa (kauli timilifu tendaji ekekezi) ili awape wanafunzi Wake (kama vile Yohana 17:12). Hii itawawezesha kuhudumu katika ulimwengu ulioanguka kamaYeye alivyohudumu katika ulimwengu ulioanguka (Kama vile Yoha 17:18). Hii ni moja ya faida za umoja (Yohana 17:21) kati ya

1. Baba 2. Mwana

3. Wanafunzi

◙ “Ili wawe na umoja kama sisi tulivyo” Hii ni kauli tegemezi ya wakati uliopo. Inarejelea juu ya umoja wa

kimahusiano wa Mungu wa Utatu (kama vile Yohana 17:21,22,23; 10:30; 14:10). Pia hili ni ombi la heshima na

wajibu kwa Wakristo! Wito huu unaohusu umoja haupo katika hizi siku zetu (kama vile Efe. 4:1-6).Umoja, na sio

ufanano, ndio njia ya kuliunganisha tena kanisa lililosambaratika.

17:12 “Nilikuwa pamoja nao …nikawatunza” Kitenzi cha kwanza ni njeo ya wakati usiotimilifu na cha pili ni njeo ya wakati uliopita usiotimilifu. Vitenzi hivi vinafanana. Msukumo wa hiki kifungu ni juu ya ulinzi wa Yesu unaoendelea (kama vile 1 Pet. 1:3-9) Katika kitabu chake cha Word study in the new Tesment, Juzuu 1, M.R Vincent anaweka tofauti kati ya

maneno haya miwili.Anasema neno la kwanza (terēō) limaanisha kuhifadhi na la pili (phulassō) linamaanisha

kulinda (uk. 496).

◙ “Wala hakuna hata mmojawapo aliyepotea” Hii inaonyesha nguvu ya Yesu ya ulinzi (kama vile Yohana 6:37,39; 10:28-29). Neno hili (Apollumi) ni gumu kulitafsiri kwa sababu linatumika katika maana mbili tofauti. Katika kitabu chake cha Theolojical Dictionary ofa the New Testament,Juzuu 1, Gerhard Kittel kuhusiana na neno hili, “Kwa ujumla tunaweza kusema kwamba 2 na 4 zinafukia taarifa zinazohusiana na ulimwengu huu kama ilivyo kwenye vidokezo vya injili, ambapo 1 na 3 zinaegamia kwa yale yanayohusiana na ulimwengu wa baadaye, kama Paulo na Yohana uk. 394. Fafanuzi alizozitoa ni:

1. “kuangamiza au kuua” 2. “kupoteza au kupata hasara" 3. “kuangamia” 4. “kupotea”

Neno hili mara nyingi linatumika kutetea fundisho la angamizo, yaani, watu ambao hawajaokolewa hawataendelea kuwepo baada ya hukumu.Hili linaonekana kwenda kinyume na Danieli 12:2. Pia linapungukiwa utofautishaji uliopo kati ya vidokezo vilivyotumika kwenye mihtasari ya Injili dhidi ya Yohana na Paulo, ambaye huvitumia ki-sitiari kama kuisha kiroho, na sio kuangamia kimwili. Tazama Mada Maalumu katika Yohana 10:10 ◙ “ila yule mwana wa upotevu” Hii wazi wazi inahusiana na Yuda Iskariote. Kifungu hiki chenye kufanana

kinatumika katika 2 Thes. 2:3 juu ya “Mwana wa uovu” (wakati wa mwisho wa mpinga Kristo). Hii ni nahau ya

Kiebrania inayomaanisha “yeye aliye kusudiwa kupotea.” Neno la mzaha juu ya neno “kilichopotea” lililotumika

mapema katika mstari huo: “hakuna aliyepotea bali yule aliyekusudiwa kupotea”

Page 290: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

274

Tazama MADA MAALUMU: UASI (APHISTĒMI) katika Yohana 6:64

◙ “ili andiko litimie” Hii inarejelea juu ya Zab. 41:9, iliyonukuliwa katika Yohana 13:18; 6:70-71.

17:13 “Na sasa naja kwako” Hii ingeweza kukurejelea 1. Sala ya Yesu (Yohana 17)

2. Kupaa kwa Yesu (Yohana 17:11; Matendo 1)

◙ “na maneno haya nayasema ulimwenguni” Kifungu hiki kinaweza kutuunganisha huko nyuma kwa 1. 11:42, Yesu husema kwa sauti kubwa ili wengine wasikie

2. 15:11 Maneno ya Yesu yalihusishwa moja kwa moja na “furaha” ya wanafunzi.

◙ “ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao” Hii ni kauli tendaji tegemezi ya wakati uliopo na kauli timilifu

tendewa endelevu. Ni ahadi nzuri kiasi gani (kama vile Yohana 15:11; 16:24). Yohana anatumia kifungu hiki tena

(kama vile 1 Yohana 1:4; 2 Yohana 12).

17:14“Mimi nimewapa neno lako” Istilahi ya “neno lako” hapa ni lagos. Kisawe cha Kiyunani rhēma kinatumika

katika Yohana 17:8. Huu ni uthibitisho kuhusu ufunuo wa ki-Ungu kupitia mafundisho na mfano wa Yesu. Yesu

hutoa neno na yeye ndiye Neno. Neno liko katika utu wa Yesu, mafundisho, na mfano.Yesu anatoa Neno na ni

Neno. Neno ni vyote yaani utu na dhamira ya utambuzi. Tunamkaribisha mtu wa injili na amini ujumbe wa injili!

◙ “Ulimwengu umewachukia” Kukataliwa na ulimwengu ni ishara ya kukubaliwa na Kristo (kama vile Yohana 15:18-20; 1 Yohana 3:13). ◙ “kwa kuwa wao si wa ulimwengu” Waamini wako ulimwenguni, lakini si wa ulimwengu (kama vile Yohana 17:16; 1 Yohana 2;15-17).

◙ "kama mimi nisivyo wa ulimwengu" "Ulimwengu" neno hili linahusiana na enzi ya anguko la mwanadamu na uasi wa malaika(kama vile Yohana 8:23). Huu ni mfano mwingine wa pande mbili za Yohana zilizo sahihi. 17:15 "Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu" Wakristo wanalo jukumu ulimwenguni (kama vile Yohana 17:18; Mt. 28:19-20; Luka 24:47; Matendo 1:8). Si wakati mwafaka kwao kwenda nyumbani! NASB, NKJV "yule mwovu" NRSV "yule mwovu" TEV, NJB "Aliye mwovu" Neno hili halina shamilisho wala jinsia.Kimaandishi haya ni maelezo ya kitu kimoja, nguvu ya mara kwa mara ya uovu wa mtu binafsi (kama vileYohana 12:31; 13:27; 14:30; 16:11), kwa hiyo,mstari huu, kama Mt. 5:37; 6:13; 13:19,38, lazima awe "yule mwovu" (kama vile 2 Thes. 3:3; 1 Yohana 2:13-14; 3:12; 5:18-19). Tazama Mada Maalumu katika Yohana 12:31 17:17 "Uwatakase" Hiki ni kauli tendaji shurutishicha wakati uliopita usiotimilfu kutoka katika mzizi wa neno "takatifu" (hagios). Hii inaweza kumaanisha

1. Waamini wanaitwa ili kufanana na Kristo (kama vile Yohana 17:19; Rum. 8:28-29; 2 Kor. 3:18; 7:1; Gal. 4:19; Efe. 1:4; 4:13; 1 The. 3:13; 4:3,7; 5:23; 1 Pet. 1:15). HIli linaweza kutokea tu kupitia maarifa ya kuijua kweli, ambayo kwa pamoja ni neno liishilo (Yesu, kama vile Yohana 1:1-14) na neno lililoandikwa (Biblia, kama vile Yohana 15:3).

2. "Uwatakase"katika maana ya Agano la Kale, kimsingi linamaanisha kutenga kwa ajili ya kazi ya Mungu. Yohana 17:18 anafafanua kusudi la wao "kutakaswa."

Page 291: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

275

Si swali aidha la #1 au #2 ni kweli. Yote mawili ni kweli. Maisha ya Yesu yalionyesha umuhimu wa yote mawili (kama vile Yohana 17:19). Inawezekana kabisa kwamba Yohana anao wanafunzi “waliotakaswa” kwa ajili ya kazi ya Mungu kama mtiririko wa uzao wa makuhani wa Agano la Kale waliokuwa wametengwa kwa ajili ya kazi ya Mungu. Walihudumu kama wawakilishi wa dhabihu za Agano la Kale, lakini wanafunzi walimtumikia kama wafuasi wa Agano Jipya lililokamilika, wakati dhabihu ilipokuwa kwa wote, Kristo (tazama kitabu cha Waebrania , kinacholinganisha Agano la Kale na Agano Jipya).

◙ “kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli" Kweli inaurejelea ujumbe wa Yesu kumhusu Mungu (kama vile Yohana 8:31-32). Yesu anaitwa kwa yote mawili, ujumbe (Logos, kama vile Yohana 1:1,14) na kweli (kama vile Yohana 14:6) ya Mungu. Mara nyingi Roho anarejelewa kama Roho wa kweli (kama vile Yohana 14:17; 15:26; 16:13). Tambua kwamba waaminio wanatakaswa na kwa hiyo kweli (kama vile Yohana 17:19, kauli timilifu tendewa endelevu) na kwa Roho (kama vile 1 Pet. 1:2). Kwa mjadala kamili juu ya mzizi wa neno la Kiyunani "kweli, kweli" tazama Mada Maalumu juu ya Kweli katika Yohana 6:55 na 17:3 Inawezekana kwamba "Neno lako ndiyo kweli" linaweza kudokeza ama kunukuliwa kutoka LXX ya Zab. 119:142, "Haki yako ni haki ya milele, na sheria yako ni kweli."Kwa hakika inawezekana kwamba Yesu a lionekana kama

1. Musa mpya (Kumb. 18:15) 2. Wanafunzi wake kama makuhani wapya (matumizi ya kitenzi "takasa") 3. Maisha yake kama ufunuo wa kweli wa Mungu mmoja wa kweli 4. umoja wa Mungu wa Utatu na wanafunzi kama kusudi la uumbaji lililokusudiwa (yaani,Mwa. 1:26-27) 5. Yesu kama utimilifu wa Mwa. 3:15

17:18 "Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni" Maisha ya Yesu ya utii na huduma, hata kufikia hatua ya kufa (2 Kor. 5:14-15; Gal. 2:20; 1 Yohana 3:16), yanaweka muundo kwa wanafunzi Wake (kama vile Yohana 17:19). Atawatuma kweye ulimwengu uliopotea kwenda kufanya kazi maalumu kama Yeye alivyotumwa katika Yohana 20:21. Yawapasa kuuhubiri ulimwengu, si kuishi tu kama watawa. Tazama Mada Maalumu: Kupelekwa (Apostellō) katika Yohana 5:24

17:19 "najiweka wakfu mwenyewe" Hii lazima irejelee katika mazingira haya hadi Kalvari! Yesu alipanga mwenyewe kuyafanya mapenzi ya Baba (yaani, Marko 10:45).

◙ "ili na hao watakaswe katika kweli" Hiki ni kishazi cha neno hina (kishazi nia) kikiwa na kauli timilifu tendewa endelevu yenye mafumbo ambacho kinadokeza kwamba matokeo yamekwisha tokea na yanaendela kwa nguvu. Kwa hiyo, hata hivyo, kuna namna ya uwezekano wa jambo kutokea likiegemea juu ya

1. kazi ya Kristo ya baadaye pale msalabani, ufufuo, na kupaa 2. imani ya mwitikio wa toba endelevu kwa Yesu na mafundisho Yake

Tazama Mada Maalumu juu ya Kweli katika Maandiko ya Yohana. 6:55 na 17:3

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 17:20-24

20Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. 21 Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. 22Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja. 23Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katikaumoja;iliulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi. 24Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami po pote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maanaulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu

17:20 "lakini na wale watakaoniamini" Hii ni njeo ya wakati uliopo. Hii inarejea juu ya waumini wote wa baadaye katika Yohana 10:16, hata kwa watu wa mataifa. Tazama Mada Maalumu katika Yohana 2:23

Page 292: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

276

◙ "kwa sababu ya neno lao"Hili ni neno logos. Kwa sababu ya matumizi yake katika Yohana 17:14 na kisawe chake rhēma katika Yohana 17:8, lazima hii irejelee kwa wanafunzi wapitiao ujumbe wa Yesu wa kimafunuo.

17:21 "Wote wawe na umoja" Umoja huu si mwingine zaidi ya ule wa Utatu (kama vile Yohana 17:11, 22,23; Efe. 4:1-6). Hiki ni kipengele kimoja cha mafundisho ya Yesu ambayo wafuasi Wake hawakuyafuata.

◙ "li ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma" Hii ni kauli tendaji tegemezi ya wakati uliopo. Kusudi la umoja ni uinjiisti. Yohana 17:23 takribani ina muundo na msisitizo unaofanana! Kuna mvutano katika maombi ya Yesu. Haombei ulimwengu (kama vile Yohana 17:9), bado anawatuma wajumbe wake ulimwenguni wakiwa na ujumbe wake utakao sababisha mateso juu yao kwa vile Mungu anaupenda ulimwengu (kama vile Yohana 17:21,23; 3:16). Mungu anapenda ulimwengu wote upate kuamini (kama vile 1 Tim. 2:4; Tito 2:11; 2 Pet. 3:9). Mungu huwapenda wale wote walioumbwa kwa mfano wake na kufanana naye. Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu wote. Tazama Mada Maalumu: Upelekwa (Apostellō) katika Yohana 5:24

17:22 "Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao" Hivi zote ni kauli timilifu tendaji elekezi. Utukufu lazima urejee katika ujumbe wa ki-ufunuo. Watalizalisha neno lake katika ulimwengu kama Yesu alivyolizalisha neno la Baba yake. Hili pia litasababisha wao kubeba shutuma zake! A. T. Robertson katika kitabu chake cha Word Pictures in the New Testament, Juzuu V, anasema"Ni utukufu wa Neno lililofanyika mwili (kama vile Yohana 1:14 na 2:11) si utukufu wa Neno la Milele lililonenwa katika Yohana 17:24" (uk. 280). Tazama ufafanuzi kamili juu ya neno "utukufu" katika Yohana 1:14.

17:23 "ili wawe wamekamilika katika umoja" Hiki ni Kishazi cha neno hina kikiwa na kauli timilifu tendewa yenye mafumbo, kama Yohana 17:19. Katika Yohana 17:19, utambuzi wa jambo liliegemea juu ya (1) kazi ya Kristo inayokuja au (2) imani yao endelevu. Kidokezo ni kwamba wamekwisha unganishwa na njia ya utendaji wa Yesu na hilo litabaki! Kusudi la umoja ni uinjilisti.

◙ "ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi" Hii ni ahadi (kama vile Yohana 16:27 na 14:21,23), lakini ina shariti. Mungu hushughulikia watu kwa njia ya maagano ("kama. . .ndipo"). Upendo wa (agapeō) limetokea mara nane katika Yohana 1-12, lakini mara 31 katika Yohana13-17. Mazungumzo ya huko ghorofani yalisistiza sifa ya Mungu Baba iliyofunuliwa kupitia maneno na matendo ya Mwana muda mfupi baadaye, ufufuo, na hasa Pentekoste, kupitia wanafunzi. Mungu ni upendo (kama vile 1 Yohana 4:7-21).

17:24 "wawe pamoja nami po pote nilipo" Yesu anarudi katika utukufu ili kuandaa nafasi kwa ajili ya wafuasi Wake (kama vile Yohana 14:1-3). Ulimwengu huu si makao yetu kama ambavyo hapakuwa Kwake pia! Ni uumbaji Wake (Mwanzo 1-2) na utarejeshwa tena (Ufunuo 21-22).

◙ "wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa" Bila shaka neno "utukufu" katika mstari huu haliwezi kumaanisha kile alichokifanya katika Yohana 17:22. Hapa linaonekana kuwa pamoja na ukuu wa Yesu wa Uungu uliokuwepo kabla.

◙ "kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu" Mungu wa Utatu alikuwa mtendaji katika ukombozi hata kabla ya uumbaji. Kifungu hiki kinatumika mara kadhaa katika Agano Jipya (kama vile Mt. 25:34; Luka 11:50; Efe. 1:4; Ebr. 4:3; 9:26; 1 Pet. 1:20; Ufu. 13:8; 17:8).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 17:25-26 5 2Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua; lakini mimi nalikujua, na hao wamejua ya kuwa ndiwe uliyenituma. 26 Nami naliwajulisha jina lako, tena nitawajulisha hilo; ili pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, nami niwe ndani yao.

Page 293: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

277

17:25 "Baba mwenye haki" Wadhifa huu unaonekana hapa katika Agano Jipya pekee. Ni mfanano wa "Baba Mtakatifu" katika Yohana 17:11 na linatokana na neno la Kiebrania lenye maana ya "tete la kupimia." Mungu ndiye kipimo cha hukumu! Tazama Mada Maalumu katika Yohana 2:29

◙ "ulimwengu haukukujua" Ulimwengu, jamii ya watu ilioungana na kutenda kinyume na Mungu (matumizi pekee ya Yohana), haumjui Mungu (kama vile Yohana 17:25) wala Mwanaye (kama vile Yohana 1:10). Ni kosa na kutenda uovu (kama vile Yohana 3:19-20; 7:7).

◙ "lakini mimi nalikujua" Yesu ndiye mkuu kuliko vyote na chanzo safi cha ujumbe uanao muhusu Mungu (kama vile Yohana 1:18; 3:11).

17:26 "Nami naliwajulisha jina lako" Hili linarejerea juu ya ufunuo wa Yesu kuhusu sifa na mpango wa Baba wa ukombozi kwa mwanadamu (kama vile Yohana 17:6,11,12; Matendo 2:23; 3:18; 4:28). Neno "julisha" limetumika mara tano katika Yohana 7:25-26.

◙ "tena nitawajulisha hilo" Aidha hii inarejerea juu ya (1) ufunuo endelevu wa Yesu kupitia Roho ambaye hufafanua mafundisho Yake au (2) matukio ya wokovu yatakayotokea (Juma la Mateso). Mazingira ya kifungu yanadokeza #1.Wokovu unahusianisha kati ya mtu na ujumbe, maamuzi na mtindo wa maisha, imani asilia na imani endelevu. Wokovu unahusianisha vidokezo vyote viwili vya Kiyunani vya neno "kuwajulisha" na kidokezo kingine cha Kiebrania “kuwajulisha”

MASWALI YA MJADALA

Huu ni mwongozo wa fasiri, ina maanisha kwamba unawajibika kwa tafsiri zako mwenyewe za Biblia. Kila mmoja wetu lazima atembee katika mwanga tulio nao. Wewe, Biblia, na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Hutakiwi uvitelekeze vitu hivi kwa mfasiri. Maswali ya mjadala huu yanatolewa kukusaidia kufikiri juu ya mambo makubwa ya sehemu za kitabu hiki. Yanalenga kukuamsha kimawazo na sio kutoa maana.

1. Kwa nini sala hii ni muhimu sana kithiolojia? 2. Je! Yuda alikuwa mtu aliyeamini au mtu aliyeanguka toka kwenye neema? 3. Nini kusudi la umoja wetu? 4. Kwa nini uwepo wa Yesu kabla ni mihimu? 5. Fafanua maneno muhimu kulingana mazingira haya:

a. "tukuzwa" b. "toa/patia" c. "julia" d. "pelekwa" e. "jina" f. "ulimwengu"

Page 294: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

278

YOHANA 18

MIGAWANYO YA AYA YA TAFSIRI ZA KISASA UBS4 NKJV NRSV TEV NJB

Kusalitiwa na Kusalitiwa na kukamatwa, kukamatwa kwa kukamatwa kwa Kukamatwa kwa kukamatwa kushtakiwa Yesu Yesu Yesu Getsemane kusulubiwa na Kuteswa kwa Yesu (18:1-19:42) 18:1-11 18:1-11 18:1-11 18:1-4 18:1-9 18:5a 18:5b 18:5c-7a 18:7b 18:8-9 18:10-11 18:10-11 Yesu mbele ya Yesu mbele ya Yesu mbele ya Yesu mbele ya Kuhani mkuu kuhani mkuu Anasi Anasi na Kayafa Petro amkana 18:12-14 18:12-14 18:12-14 18:12-14 18:12-14 Kukanwa kwa Petro amkana Petro amkana Yesu na Petro Yesu Yesu 18:15-18 18:15-18 18:15-18 18:1517a 18:15-18 18:17b 18:18 Kuhani amhoji Yesu ahojiwa na Kuhani mkuu Yesu kuhani mkuu amhoji Yesu 18:19-24 18:19-24 18:19-24 18:19-21 18:19-24 18:22 18:23 18 :24 Petro amkana Petro akana Petro amkana Yesu tena mara mbili Yesu tena zaidi 18:25-27 18:25-27 18:25-27 18:25a 18:25-27 18:25b 18:26 18:27 Yesu mbele ya Mahakamani Yesu mbele ya Yesu mbele ya Pilato mwa Pilato Pilato Pilato 18:28-38a 18:28-38 18:28-32 18:28-29 18:28-32 18:30 18:31a 18:31b-32

Page 295: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

279

18:33-38a 18:33 18 :34 18:35 18:36 18:37a 18:37b 18:38a Yesu ahukumiwa Kuchukua nafasi Yesu ahukumiwa Kufa ya Baraba Kufa (18:38b-19:16c) (18:38b-19:16a) 18:38b-19:7 18:38b-19:7 18:38b-39 18:39-40 18:40-19:3

MZUNGUKO WA TATU WA USOMAJI KUFUATILIA KUSUDIO LA ASILI LA MWANDISHI KATIKA NGAZI YA AYA Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwatafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Aya ya kwanza 2. Aya ya pili 3. Aya ya tatu 4. N.k

UTAMBUZI WA KI-MUKTADHA WA 18: 1-40

A. Yohana anaondoa maumivu makali ya Yesu pale Gethsemane (ingawa Yohana 17 yaweza kuwa zinafanana). Hili lilikuwa wazi kwa sababu anasisitiza juu ya tabia ya Yesu ambayo ilikuwa katika udhibiti wa hali zote. Aliyatoa maisha yake (k.v. Yohana 10:11,15,17,18).

B. Utaratibu wa matukio ya aya hii kwa kiasi Fulani ni tofauti toka kwa vidokezo vya injili. Utofauti huu unaonekana kuwa kivumishi angama 1. Asili ya kuhusika kwa shuhuda wa macho 2. Makusudi ya mwandishi kithiolojia

C. Yohana ana utofauti toka kwa dokezo zingine za injili. Ni kwa nini na kwa vipi maswali hayo kitaalamu

hayawezi kujibiwa. Mjadala mzuri niliouona upo katika Gordon Fee, Douglas Stuart, How To Read the Bible For All Its Worth, ambapo inatoa nadharia mbali mbali. Kwa wazi kabisa waandishi wa injili, chini ya uvuvio, walikuwa na uhuru wa 1. Kuchagua 2. Kubadili 3. Kupanga upya Maneno na kazi ya Yesu. Sifikirii kama wangaliweza kuumba maneno na kazi, lakini wangaliweza kubadili kwa kusudi la uinjilisti kweza kumdhihilisha Yesu kwenye makundi mbali mbali ya watu. Kumbuka injili sio historia ya kimagharibi (yaani., sababu na athari na utaratibu wa kupanga matukio), lakini ni historia za kimashariki. Sio wasifu wa mtu lakini ni vijitabu vya mambo ya kiinjili.

Page 296: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

280

D. Kitabu kizuri cha kufanya nukuu katika aya hii, kwa kadri mashitaka ya Yesu yalivyo kisheria (yaani., kwa

wakuu wa sinagogi) ni A. N. Sherwin-White's Roman Society and Roman Law in the NT

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 18:1-11 1 Alipokwisha kusema hayo, Yesu alitoka pamoja na wanafunzi wake kwenda ng'ambo ya kijito Kedroni, palipokuwapo bustani; akaingia yeyeuala hili ni na wanafunzi wake. 2 Naye Yuda, yule aliyetaka kumsaliti, alipajua mahali pale; kwa sababu Yesu alikuwa akienda huko mara nyingi pamoja na wanafunzi wake. 3 Basi Yuda, akiisha kupokea kikosi cha askari na watumishi waliotoka kwa wakuu wa makuhani na Mafarisayo, akaenda huko na taa na mienge na silaha. 4 Basi Yesu, hali akijua yote yatakayompata, akatokea, akawaambia, Ni nani mnayemtafuta? 5 Wao wakamjibu, Ni Yesu Mnazareti. Yesu akawaambia, Ni mimi. Yuda naye aliyemsaliti alikuwa amesimama pamoja nao. 6 Basi alipowaambia, Ni mimi, walirudi nyuma, wakaanguka chini. 7 Basi akawauliza tena, Mnamtafuta nani? Wakasema, Yesu Mnazareti. 8 Yesu akajibu, Nimekwisha kuwaambieni ya kwamba ni mimi; basi ikiwa mnanitafuta mimi, waacheni hawa waende zao. 9 Ili litimizwe lile neno alilolisema, Wale ulionipa sikumpoteza hata mmoja wao. 10 Basi Simoni Petro alikuwa na upanga, akaufuta, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio la kuume. Na yule mtumwa jina lake ni Malko. 11 Basi Yesu akamwambia Petro, Rudisha upanga alani mwake; je! Kikombe alichonipa Baba, mimi nisikinywee?

18:1 "kijito Kedroni"Neno "kijito" lilimaanisha "kijito cha majira ya baridi kali" au "korongo kavu la mto." "Kedroni" (BDB 871) ilimaanisha (1) miti aina ya mkangazi au (2) kitu cheusi. Hili lilikuwa ni korongo ambalo lilikuwa kavu wakati wa kiangazi lakini likatiririsha maji wakati wa masika. Palikuwa ni mahali ambapo damu zilizokuwa zinatolewa kwa ajili ya dhabihu toka Mlima Mori zilikuwa zinakaushwa. Hii yaweza kuwa ndo chanzo cha maelezo ya neno "kitu cheusi." Ilikuwa kati ya Mlima wa Hekaluni na Mlima wa Mzeituni (k.v. LXX 2 Samweli 15:23; 2 Fal. 23:4,6,12; 2 Nya. 15:16; 29:16; 30:14; Yer. 31:40). Kuna utofauti wa maandishi ya Kiyunani katika eneo hili:

1. "ya miti" (kedrōn) katika MSS אc, B, C, L na baadhi ya maandishi mengine yasiyo ya kawaida 2. "ya mti wa sida" (kedrou) katika MSS א*, D, na W 3. "ya Kidroni" (kedrōn) katika MSS A na S

The United Bible Society's toleo la nne #3

◙ "bustani"Sura hii inaruka kabisa mateso ya Yesu pale Gethsemane, lakini inaweka tukio la kukamatwa bustanini, mahali hapa palikuwa mahali alipopapenda zaidi Yesu (kama vile Yohana 18:2; Luka 22:39). Ni dhahiri Yesu alilala hapa wiki yake ya mwisho ya uhai wake (kama vile Luka 21:37). Bustani hazikuruhusiwa Yerusalemu kwa sababu kule kulazimika kuweka mbolea kulisababisha pasiwe safi. Watu wengi matajiri kwa hiyo walimiliki mashamba ya mizabibu na viungo ya miti ya matunda, kwa mfano, kwenye mlima wa mizeituni.

18:2 Hii ni hoja nyingine ya kiuandishi ya Yohana.

◙ "Yuda" Kuna maoteo mengi kuhusu Yuda na nia yake ya kutenda mambo. Anatajwa na kukashifiwa mara nyingi kwenye injili ya Yohana (kama vile. Yohana 6:70-71; 12:4; 13:2,26,27; 18:2,3,5). Msemo wa kisasa wa neno "Yesu Kristo anayeng’ara" unamtambulisha Yeye kama mtu mwaminifu, lakini haukuwapotosha, wafuasi waliojaribu kumlazimisha Yesu kwenye kuitimiza kazi ya agano la kale juu ya Masihi wa Uyahudi- hii ni, kuwapindua Warumi, kuadhibu waovu na kusimika Yerusalemu kama jiji kuu la ulimwengu. Lakini, Yohana anaeleza nia yake kama mtu mlafi na aliyeshawishika kishetani. Tatizo kuu hapa ni la kithiolojia ni juu ya ukuu wa Mungu na uhuru wa kuamua wa mwanadamu. Je Mungu ama Yesu walimghilibu Yuda? Je Yuda anawajibika kwa matendo yake ikiwa shetani alimtawala ama Mungu alikuwa amemkusudia amsaliti Yesu kabla ya uumbaji.Biblia haitamki maswali haya moja kwa moja. Mungu

Page 297: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

281

anatawala historia; Anajua matukio lakini mwanadamu anawajibika kwa uchaguzi na matendo. Mungu ni mwenye haki, si mtawala wa hila. Kuna kitabu kipya kinaachojaribu kumtetea Yuda --Judas Betrayer or Friend of Jesus? Kimeandikwa na William Klassen, Fortress Press, 1996. Sikubaliani na kitabu hiki kwa sababu kinadhalilisha ushuhuda wa Yohana kuhusu Yuda, lakini kinapendeza na mawazo ya kichokonozi.

MADA MAALUM: UCHAGUZI/MAJAALIWA NA UHITAJI WA USAWA KITHIOLOJIA Uchaguzi ni fundisho la ajabu. Hata hiyo, si wito ulio na upendeleo, lakini ni wito kuwa njia, chombo, au njia za ukombozi kwa wengine! Katika Agano la Kale neno hilo lilitumiwa hasa kwa ajili ya huduma; katika Agano Jipya linatumika hasa kwa ajili ya wokovu unaohusika katika huduma. Biblia hipatanishi kamwe kupingana kati ya Ufalme wa Mungu na mapenzi huru ya mwanadamu, lakini inathibitisha zote mbili! Mfano mzuri wa mvutano wa kibiblia itakuwa Warumi 9 juu ya uchaguziwa Ufalme na Warumi 10 juu ya majibu muhimu ya wanadamu (kama vile Warumi 10:11,13). Umuhimu wa huu muvatano wa kitheolojia unaweza kupatikana katika 1:4. Yesu ni mwanadamu mchaguzi wa Mungu na wote ni uwezo wa kuchaguliwa ndani yake (Karl Barth). Yesu ni Mungu. Yesu "ndio" kwa mahitaji ya mwanadamu aliyeanguka (Karl Barth). Waefeso 1:4 pia husaidia kufafanua suala hilo kwa kuthibitisha kwamba lengo la majaaliwa si mbinguni tu, lakini utakatifu (mapenzi ya kristo). Mara nyingi sisi huvutiwa na faida za injili na kupuuza majukumu! Wito wa Mungu (uchaguzi) ni kwa wakati pamoja na milelel! Mafundisho huja kuhusiana na ukweli mwingine, sio mmoja tu, ukweli usiohusiana. Hali au tabia nzuri inakuwa ni kundi dhidi ya nyota moja. Mugu hutoa ukweli katika mashariki na sio magharibi, mtindo. Hatupaswi kuondoa mvutano unaosababishwa na jozi za lahaja(fumbo la maneno) za kweli za mafundisho:

1. majaaaliwa/mchaguzi dhidi ya mapenzi huru ya mwanadamu 2. Usalama wa wanaoamini dhidi ya mahitaji ya uvumilivu 3. Dhambi ya asili dhidi ya dhambi ya hiari 4. Kutotenda dhambi dhidi ya kutenda dhambi kidogo 5. Udhihirisho na utakaso wa papo kwa papo dhidi ya utakaso endelevu 6. Uhuru wa Kikristo dhidi ya wajibu wa Kikristo 7. Mungu anayeweza kupita uwezo wa binadamu dhidi ya Mungu wa asili 8. Mungu kama hatimaye isiyojulikana dhidi ya Mungu anayejulikana katika maandiko 9. Ufalme wa Mungu kama sasa dhidi ya kukamilishwa baadaye 10. Kutubu kama zawadi ya Mungu dhidi ya jibu muhimu la Agano la kibinadamu 11. Yesu kama Mungu dhidi ya Yesu kama mwanadamu 12. Yesu ni sawa na Mungu Baba dhidi ya Yesu wa kumtumikia Mungu Baba

Dhana ya kitheolojia ya “agano” inaunganisha Ufalme wa Mungu (ambaye daia huchukua hatua kwa kuweka mswada) pamoja na mamlaka ya mwanzo imani ya kuendelea kutubu kujibiwa kutoka kwa mwanadamu (k.v. Marko 1:15; Mdo. 3:16,19; 20:21). Kuwa mwangalifu wa maandishi ya uthibitisho wa upande mmoja wa fumbo la maneno na punguza kwa mwingine! Kuwa mwangalifu wa kuthibitisha mafundisho yako ya mapenzi tu au mfumo wa thiolojia!

18:3 NASB "kikosi cha warumi" NKJV "utengano wa vikosi" NRSV "kikosi cha askari" TEV "kikundi cha askari wa kirumi" NJB "kikosi" Hii inahusu kikundi cha kijeshi cha Kirumi ambacho ni moja ya kumi ya kikosi na kingeweza kuwa na hadi watu 600 wakiwa kwenye kituo kwenye ngome Antonio, karibu na Hekalu (kama vile Mdo. 21:31,33). Haitazamiwi kwamba kundi hili kubwa liliitwa. Warumi walikuwa wameandaliwa kwa ajili ya maasi mjini Yerusalemu kwenye

Page 298: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

282

nyakati hizi za sherehe. Wangaliweza kuchukua tahadhari za lazima kwa kuhamisha vikosi kutoka Kaisaria kwa Bahari. Warumi walihusika kwenye mashtaka ya Yesu kwa sababu Wayahudi walimtaka Yesu asulubishwe. Hii kwa kawaida ilichukua siku kadhaa; wangeweza tu kufanya jambo hili kwa ruhusa na ushirikiano wa serikali ya Warumi.

◙"na watumishi waliotoka kwa wakuu wa makuhani"Maaskari wa Hekalu la Walawi waliungana na kikosi cha ulinzi cha Warumi. Walikuwa wamekwisha kushindwa kumkamata Yesu mara moja (kama vile Yohana 7:32,45).

◙"silaha"Panga zilikuwa zimebebwa na askari wa Kirumi na rungu zilikuwa zimebebwa na askari wa Hekalu (kama vile Mt. 26:43; Marko 14:43; Luka 22:52).

18:4 "Basi Yesu, hali akijua yote"Huu ni msisitizo wenye nguvu kuhusu kujua kwake na kutawala kukamatwa kwake, kushtakiwa na kusulubiwa kwake (kama vile Yohana 10:11,15,17,18). Sio kwamba Yesu alisulubiwa ghafla tu (kama vile Marko 10:45; Mdo. 2:23; 3:18; 4:28). Dhamila hii ni kielelezo cha injili ya Yohana na yaweza kuwa sababu kwa nini hanukuu mgongano wa Gethsemane.

18:5 NASB, NJB "Yesu Mnazareti" NKJV, NRSV, TEV "Yesu wa Nazareti" Kumetokea mjadala kuhusu utambuzi wa vyanzo vya maneno na maana zake kwa habari ya neno "Mnazareti." Inawezekana kwamba inaweza kumaanisha (1) Mnazareti; (2) Nazareti (kama vile Hesabu 6); au (3) kutoka Nazareti. Matumizi ya Agano Jipya (kama vile Mt. 2:23) inakazia #3. Baadhi hata wamehusianisha herufi za Kiebrania nzr kwenye cheo cha Umasihi "Tawi" (nezer, kama vile Isa. 11:1; 14:19; 60:21).

MADA MAALUMU: YESU MNAZARETI Kuna maneno mbalimbali ya Kiyunani ambayo Agano Jipya hutumia kumzungumzia Yesu. A. Haya ni maneno ya Agano Jipya

1. Nazarethi – mji katika Galilaya (kama vile Luka 1:26; 2:4,39,51; 4:16; Mdo. 10:38). Mji huu hautajwi katika vyanzo vya wakati huu, bali umekutwa katika kumbukumbu ya maandishi ya baadaye. Kwa upande wa Yesu kuwa alitoka Nazarethi haikujitosheleza (kama vile Yohana 1:46). Alama ya msalaba wa Yesu ambayo imeliweka jina la eneo hili ilikuwa alama ya aibu kwa Wayahudi.

2. Nazarēnos – pia inataja maeneo ya kijiografia (kama vile Luka 4:34; 24:19). 3. Nazōraios – inaweza kuurejea juu ya mji, lakini pia ingeweza kuwa mwaminifu na mtenda haki Masihi

wa Kiebrania "Utanzu" (netzer, BDB 666, KB 718 II, kama vile Isa. 11:1; maana zinazokaribiana, BDB 855, Yer. 23:5; 33:15; Zek. 3:8; 6:12; iliyodokezwa katika Ufu. 22:16). Luka akilitumia hili kumhusu Yesu katika 18:37 na Mdo. 2:22; 3:6; 4:10; 6:14; 22:8; 24:5; 26:9.

4. Iliyohusiana na #3 nāzir (BDB 634, KB 684), ambalo linamaanisha "aliyewakifishwa kwa maana ya nadhiri."

B. Matumizi ya Kihistoria ya neno nje ya Agano Jipya. 1. Lilimaanisha kundi la ausi la Kiyahudi (Mkristo wa awali) (nāsōrayyā ya Kiaramu). 2. Lilitumika katika mzunguko wa Kiyahudi kuwatambulisha waamini katika Kristo (kama vile Matendo

24:5,14; 28:22, nosri). 3. Lilikuja kuwa neno la kawaida katika kumaanisha waamini katika makanisa ya Kisiria (Kiaramu).

"Mkisto" lilitumika katika makanisa ya Kyunani kumaanisha waamini. 4. Wakati mwingine baada ya kuanguka kwa Yerusalemu, Wafarisayo walikusanyika huko huko Jamnia na

walichochea utengano rasmi kati ya sinagogi na kanisa. Mfano wa aina ya maapizo ya mazungumzo dhidi ya Wakristo unapatikana katika "the Eighteen Benedictions" from Berakoth 28b-29a, ambayo "Wanazarethi." "Wanazareti na awaasi waliweza kutoweka kwa muda mfupi; walifutwa kutoka katika kitabu cha uzima na kutoandikwa kuwa walikuwa na imani."

5. Ilitumiwiwa na Justin Martyr, Dial. 126:1, ambaye alitumia netzer ya (Isa. 11:1) kumhusu Yesu.

Page 299: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

283

C. Maoni ya Mwandishi Nashangazwa sana na herufi za maneno, Ingawa nafahamu kwamba hili ni jambo geni kusikika katika Agano la Kale "Yoshua" ina herufi mbalimbali katika Kiebrania. Maelezo yafuatayo yananisababisha kubaki na mashaka kama maana yake dhahiri : 1. kama vile maana yake ya karibu na neno la Kimasihi “tawi” (netzer) au neno lililo sawa nāzir

(aliyepakwa mafuta kwa maana ya nadhiri) 2. vidokezo hasi vya eneo la Galilaya kuyahusu mataifa 3. uchache au kutokuwepo kwa uthibitisho wa fasili za sasa kukusu mji wa Nazarethi katka Galilaya 4. inatoka katika kinywa cha pepo katika maana ya hukumu (yaani, "Umekuja kutuangamiza?").

Kwa wasifu kamili wa masomo ya kundi la neno hili, tazama Colin Brown (ed.), New International Dictionary of New Testament Theology, juzuu. 2, uk. 346 au Raymond E. Brown, Birth of the Messiah, kur. 209-213, 223-225.

◙"Ni mimi" Hili neno kiuhalisia "mimi ni," Kitenzi cha kiebrania "kuwa" (tazama Mada Maalumu katika Yohana 6:20), ambapo Wayahudi wangehusianisha kwa YHWH, jina la Agano la Mungu (kama vile Kut. 3:14 na Isa. 41:4). Yesu alitoa tamko hili lenye hofu lenye kushangaza juu ya uungu kwa njia ileile ya sarufi ngumu (ego eimi) katika Yohana 4:26; 8:24, 28, 58 na 13:19. Imerudiwa mara tatu katika muktadha huu kwa kusisitiza (kama vile Yohana 18:6, 8). Muundo huu wa sarufi ni tofautina unaojulikana wa Yesu "Mimi niko . . .".

◙"Yuda naye aliyemsaliti alikuwa amesimama pamoja nao"Haya ni mengine ya kuhariri ya aliyeshuhudia mwandishi wa injili, Yohana.

18:6 "walirudi nyuma, wakaanguka chini"Yohana alinakiri jambo hili kusisitiza sifa ya Yesu ya nguvu na uwepo. Hii haisababishi mtu apite atoe heshima (kupiga magoti mbele ya mtu), bali hofu.

18:7 "Basi akawauliza tena"Yawezekana Yesu alikuwa anavuta umakini wao kwake usiwe kwa wanafunzi wake. Hili laonekana kushabiana na maudhui yaliyotokea pale pale ya Yohana 18:8.

18:8 "ikiwa"Hii ni sentesi shurutishi daraja la kwanza; walikuwa wanamtafuta.

◙"waacheni hawa waende zao" Hii ni kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopita usiotimilifu. Ni utimilifu wa unabii kutoka Zak. 13:7 (kama vile Mt 26:31; Yohana 16:32).

18:9 "Ili litimizwe lile neno alilolisema" Hii inaonekana kuwa rejea ya Yohana 16:32, lakini Yohana 17:12 imenukuliwa.

18:10 "Basi Simoni Petro alikuwa na upanga, akaufuta, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio la kuume" Petro hakuwa amekusudia sikio, bali kichwa! Hii inaonyesha utayari wa Petro kufa badala ya Yesu. Kitendo hiki chaweza kuwa kimetokana na kuelewa visivyo kauli ya Yesu katika Luka 22:36-38. Luka 22:51 yatueleza kwamba Yesu aliponya sikio la mtu yule kwa kugusa.

◙"mtumwa jina lake ni Malko" Ni Yohana pekee ambaye anataja jina lake kwenye ushauri wa Kiuhariri mwandishi Yohana alikuwa bustanini!

18:11 "Kikombe" Hii ni sitiari iliyotumika kwenye Agano la Kale kama alama ya mwelekeo wa mtu, kwa kawaida kwenye hisia hasi (kama vile Zab. 11:6; 60:3; 75:8; Isa. 51:17, 22; Yer. 25:15,16,27-28). Mfumo wa kisarufi wa swali la Yesu unatarajia kupata jibu la “ndiyo”. Petro anajifanya tena kama mtu ajuaye ni nini kilicho bora zaidi kutenda (kama vile Mt. 16:22; Yohana 13:8). Matumizi ya neno"kikombe" hapa ni tofauti sana na matumizi ya kikombe katika maelezo ya Yesu kuhusu mateso yake ndani ya Gethsemane. Kwenye maelezo ya injili za muhtasari. Kwa Yohana, Yesu utawala kamili wa matukio! Yohana anamtambulisha Yesu kama mwenye kujiamini, sio mwoga (kama vile Yohana 18:4; 13:1,11)!

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 18:12-14 12 Basi wale askari na yule jemadari na wale watumishi wa Wayahudi walimkamata Yesu,

Page 300: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

284

wakamfunga. 13 Wakamchukua kwa Anasi kwanza; maana alikuwa mkwewe Kayafa, yule aliyekuwa Kuhani Mkuu mwaka ule. 14 Naye Kayafa ndiye yule aliyewapa Wayahudi lile shauri ya kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu.

18:12 NASB "Kikosi na Jemadari" NKJV "sehemu ya askari iliyoondolewa kwenye kikosi pamoja na akiongozi" NRSV "maaskari, afisa hao" TEV "maaskari wa Kirumi na mkuu wao" NJB "kikosi na kiongozi wao wa muda mfupi" Majina ya vitengo vya majeshi yanachukuliwa kutoka kwenye idadi ya idadi kamili ya vikosi husika.

1. Kikosi cha askari – chatokana na na idadi ya watu 600 (kama vile Yohana 18:3) 2. Kamanda ni kuanzia namba -- 1,000 (chiliarch,yaani, Mdo. 21:31; 22:24; 23:10; 24:7)

Vyeo hivi haviongelei kuhusu ni ukubwa au au udogo kiasi gani kitengo kilichomkamata Yesu. Katika Palestina #2 ilimaanisha kiongozi wa kundi dogo la askari.

◙ "walimkamata" Hii haiashirii kwamba walikuwa wanamwogopa Yesu, lakini yaonekana kuwa taratibu za kawaida (kama vile Yohana 18:24).

18:13 "Wakamchukua kwa Anasi kwanza" Kuna mjadala mkubwa kuhusu utaratibu wa mashtaka mbele ya Anasi na Kayafa. Injili za muhtasari hazitaji kamwe habari ya kukutana na Anasi. Yohana 18:24 yaonekana kuwa maelezo yaliyowekwa mwishoni mwa ukurasa kwa chini katika Yohana, lakini ni sehemu ya muhimu sana ya injili za muhtasari kuhusu maelezo ya mashitaka ya Yesu (kama vile Mt 26:57; Marko 14:53). Katika Agano la Kale ukuhani mkuu ulikuwa wadhifa wa maisha na kila mtu ilibidi awe wa uzao wa Haruni. Kwa hali yoyote Warumi walikwisha geuza shuguli hii kuwa kazi ya kisiasa yenye mshahara mzuri iliyonunuliwa na familia ya Walawi, kuhani mkuu alitawala na kushugulika na biashara kwenye ukumbi wa wanawake. Yesu aliposafisha Hekalu hii ilichukizwa. Kwa mujibu wa Flavius Josephus, Anasi alikuwa kuhani mkuu kutoka 6-14 B.K. Aliyeteuliwa na Quirinius, mtawala wa jimbo la Shamu na akaondolewa na Valerius Gratus. Jamaa zake (5 wana na 1 wajukuu) walimfuata. Kayafa (18-36 B.K.), Mkwe wake (kama vile Yohana 18:13), ndiye aliye mfuata mara. Anasi ndiye aliyekuwa nguvu halisi nyuma ya ofisi. Ambaye Yesu inapelekwa kwake (kama vile Yohana 18:13,19-22). 18:14 Haya pia ni maoni ya kiuhariri ya Yohana, kama yaliyo ya Yohana 18:15 na 18.

◙ "Kayafa" Kilichomruhusu sana Yohana kwa habari ya Kayafa kilikuwa kwamba alikuwa ametabiri kuhusu kifo cha Yesu bila yeye kujua (kama vile Yohana 11:50). Alikuwa mkwe wa Anasi na alikuwa kuhani mkuu kutoka B.K 18-36. Tazama maelezo kutoka Yohana 11:49.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 18:15-18 15 Wakamfuata Yesu, Petro na mwanafunzi mwingine. Na mwanafunzi huyo alikuwa amejulikana na Kuhani Mkuu, akaingia pamoja na Yesu katika behewa ya Kuhani Mkuu. 16 Lakini Petro akasimama nje mlangoni. Basi yule mwanafunzi mwingine aliyejulikana na Kuhani Mkuu akatoka, akasema na mngoja mlango, akamleta Petro ndani. 17 Basi yule kijakazi, aliyekuwa mngoja mlango, akamwambia Petro, Wewe nawe, je! Hu mwanafunzi mmojawapo wa mtu huyu? Naye akasema, Si mimi. 18 Na wale watumwa na watumishi walikuwa wakisimama, wamefanya moto wa makaa; maana ilikuwa baridi; wakawa wakikota moto. Petro naye alikuwapo pamoja nao, anakota moto.

18:15 "Wakamfuata Yesu, Petro na mwanafunzi mwingine" Kumekuwako mjadala mkubwa kuhusu utambulisho wa mwanafunzi mwingine huyu.

Page 301: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

285

1. Nadharia ya mapokeo imekuwepo kwamba ni mtume Yohana kwa sababu ya msemo wa namna hiyo uliotumika kumruhusu katika Yohana 20:2, 3, 4, na 8. Kadhalika uwezeko mwingine wa uhusiano ni katika Yohana 19:25, ambao unamtaja mama yake Yohana ambaye angeweza kuwa dada yake Mariamu ambayo inamaanisha angeweza kuwa mlawi na kwa hiyo kutoka familia ya kikuhani (kama vile Ushuhuda wa Polycap).

2. Huyu angeweza kuwa mfuasi mwingine ambaye hakutajwa jina kama Nikodemo ama Yusufu wa Arimathaya kwasababu ya uhusiano wao na kuhani mkuu na familia yake (kama vile Yohana 18:15-16).

◙ "Na mwanafunzi huyo alikuwa amejulikana na Kuhani Mkuu" Huu ni msemo wenye nguvu sana wa neno "kufahamiana" na waonekana kumaanisha "rafiki wa karibu" (kama vile Luka 2:44 na 23:49). Ikiwa ni Yohana hii ingehusishwa na shuguli yake ya uvuvi ambayo ingekuwa imeshirikisha familia yake katika kuleta samaki Yerusalemu.

18:17 "Basi yule kijakazi, aliyekuwa mngoja mlango, akamwambia Petro, Wewe nawe, je! Hu mwanafunzi mmojawapo wa mtu huyu" Mtindo huu wa sarufi kama Yohana 18:25, unatarajia jibu la "hapana". Unaonyesha hali ya kudharauliwa kwa wale wahusika kwa kutolitumia jina la Yesu. Anaweza kuwa ameuliza hivi kwa sababu ya (1) Ukaribu wa Petro na Yohana au (2) lafudhi ya Kigalilaya ya Petro.

◙ "Si mimi" Yawezekana Petro alikuwaa ameishajiandaa kufa kwa ajili ya Yesu lakini hakuwa amejiandaa kujibu swali la kijakazi! Kwenye mihtasari ya injili huku kukana mara tatu kumewekwa pamoja, lakini katika injili ya Yohana kumetengwa na maswali aliyokuwa akiulizwa Yesu na Anasi (kama vile Yohana 18:24).Kauli ya Petro "Mimi ni" iko kinyume kabisa na maelezo ya Yesu “Mimi ndimi” (kama vile Yohana 18:5).

18:18 Kisa hiki kimesimuliwa pamoja vielelezo dhahili vya ushahidi wa kuona kwa macho Yohana 18:18 na 25 zote mbili zina kauli zisizotimilifu zenye mafumbo.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 18:19-24 19 Basi Kuhani Mkuu akamwuliza Yesu habari za wanafunzi wake, na habari za mafundisho yake. 20 Yesu akamjibu, Mimi nimesema na ulimwengu waziwazi; sikuzote nalifundisha katika sinagogi na katika hekalu, wakusanyikapo Wayahudi wote; wala kwa siri mimi sikusema neno lo lote. 21 Ya nini kuniuliza mimi? Waulize wale waliosikia ni nini niliyowaambia; wao wanajua niliyoyanena. 22 Basi aliposema hayo, mtumishi mmojawapo aliyesimama karibu alimpiga Yesu kofi akisema, Wamjibu hivi Kuhani Mkuu? 23 Yesu akamjibu, Kama nimesema vibaya, ushuhudie ule ubaya; bali kama nimesema vema, wanipigia nini? 24 Basi Anasi akampeleka hali amefungwa kwa Kayafa, Kuhani Mkuu.

18:19 "Basi Kuhani Mkuu akamwuliza Yesu habari za wanafunzi wake, na habari za mafundisho yake" Hii inahusiana na Anasi na Kayafa. Anasi alikuwa ni mtu mwenye nguvu nyuma ya kiti cha enzi. Alitawala kutoka karne ya 6 hadi 15 b.k. kwa haraka alifuatiwa na mkwe wake na baadaye wanawe watano na mjukuu wa kiume.Anasi aliyemiliki haki za biashara kwenye mazingira ya hekalu pengine alikuwa na shauku ya kumhoji Yule aliyesafisha hekalu (yawezekana mara mbili). Inapendeza kwamba Anasi alitaka kujua habari za wanafunzi wa Yesu pamoja na mafundisho yake.

18:20 Ni ukweli wa uhakika kwamba Yesu alifundisha hadharani lakini, ni kweli pia kwamba mengi miongoni mwa mafundisho yake yalifichwa kwa watu (kama vile Marko 4:10-12). Swala halisi lilikuwa juu ya upofu wa kiroho kwa upande wa wasikilizaji wake. Maneno na namna ya ufundishaji wa Yesu yamenakiliwa tofauti kati ya vidokezo vya na injili ya Yohana. Vidokezo vya Injili havina kauli za "Mimi ndimi. . ." Yesu ufundisha kwa mfano; Yohana anakili mifano. Inaonekana kwamba tofauti zinaweza kufafanuliwa na vidokezo vya injili vikiwa vinanakiri mafundisho ya hadhara ya Yesu na Yohana akinakili vikao vya faragha.

Page 302: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

286

18:21 "Ya nini kuniuliza mimi" Katika Yohana 18:20 Yesu anatetea asili ya wazi juu ya huduma ya mafundisho yake. Yesu alikuwa anamlenga Anasi kwamba maswali yake hayakuwa halali kutokana na sheria za Kiyahudi na pia kwamba yalipaswa kujulikana na watu wote.

18:22 "mtumishi mmojawapo aliyesimama karibu alimpiga Yesu kofi akisema" Msemo huu awali ulimaanisha "kupiga makofi" au "kupiga kwa fimbo." Baadaye ilimaanisha kupiga kwa mkono." Hili ni dokezo moja kwa moja kwa Isa. 50:6. Yesu anadai kwamba kama angekuwa amefanya lolote baya, alistahili kushitakiwa, vinginevyo, kwa nini anapigwa?

18:23 "Kama. . . Kama" Hizi ni sentesi mbili shurutishi daraja la kwanza ambazo zinachukuliwa kuwa kweli kwa taswira ya mwandishi ama kwa makusudi yake ya kimaandishi.Hapa ile ya kwanza ni njia ya kimaandishi ya kutamka kwa msisitizo uhalisia wa uongo.Yesu anampa changamoto Anasi kuleta ushahidi.

18:24 Mpango wa mashtaka haya umegeuzwa katika vodokezo vya injili.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 18:25-27 25 Na Simoni Petro alikuwa akisimama huko, anakota moto. Basi wakamwambia, Wewe nawe, je! Hu mwanafunzi wake mmojawapo? Naye akakana, akasema, Si mimi. 26 Mtumwa mmojawapo wa Kuhani Mkuu, naye ni jamaa yake yule aliyekatwa sikio na Petro, akasema, Je! Mimi sikukuona wewe bustanini pamoja naye? 27 Basi Petro akakana tena, na mara akawika jimbi.

18:26 "Mtumwa mmojawapo wa Kuhani Mkuu, naye ni jamaa yake yule aliyekatwa sikio na Petro, akasema," Kuna baadhi ya utofauti katika injili nne kuhusu ni nani alimuuliza Petro maswali.

1. katika Marko, ni mwana mwali aliyeuliza swali la kwanza (kama vile Marko 14:69) 2. katika Mathayo ni mjakazi (kama vile Mt. 26:71) 3. katika Luka 22:58 ni mwanaume 4. katika Yohana ni mtumwa/mtumishi wa Kuhani Mkuu

Ni dhahiri kutokana na mpangilio wa kihistoria kwamba mtu mmoja aliuliza swali karibu na moto na wengine wakaunga mkono kuuliza (kama vile Yohana 18:18). 18:26 "Mimi sikukuona wewe bustanini pamoja naye” Tofauti na maswali mawili ya kwanza katika Yohana 18:17 na 25, muundo wa kisarufi unatazamia jibu la "ndiyo". 18:27 "Basi Petro akakana tena" Tunaelewa kutoka Marko 14:71 na Mt. 26:74 kwamba Petro alikana kwa kulaani na kuapa.

◙ "mara akawika jimbi" Mpangilio wa maneno kutoka injili zote nne unaonyesha kwamba hili lilitukia kati ya saa 12:00 na 3:00 asubuhi. Wayahudi hawakuruhusu kuku ndani ya mipaka ya mji wa Yerusalemu kwa hiyo yaweza kuwa alikuwa jimbi wa Kirumi. Luka 22:61 Inatamka kama kweli katika hatua hii kwamba Yesu alimtazama Petro. Imechukuliwa kwamba Anasi na Kayafa waliishi ndani ya nyumba moja na walinzi walikua wanamtembeza Yesu kutoka aalipokutana na Anasi kwenda alipokutana na Kayafa na wakuu wa sinagogi.Ilikuwa katika tukio hili ambapo Yesu alimtazama Petro. Hii yote ni kubahatisha kwa sababu hatuma taarifa za kihistoria za kutosha kutoa maelezo kwa uthabiti na kwa mamlaka kuhusu mfululizo wa matukio ya mashtaka ya usiku huo.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 18:28-32 28 Kisha wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa mpaka Praitorio, nayo ikawa alfajiri;lakini wao wenyewe hawakuingia ndani ya ile praitorio,wasije wakanajisika,bali wapate kuila Pasaka. 29 Basi Pilato akawatokea nje, akasema, Ni mashitaka gani mnayoleta juu ya mtu huyu? 30 Wakajibu, wakamwambia, Kama huyu asingekuwa mtenda mabaya, tusingemleta kwako. 31 Basi Pilato akawaambia, Haya! Mtwaeni ninyi,

Page 303: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

287

mkamhukumu kwa ile torati yenu! Wayahudi wakamwambia, Sisi hatuna ruhusa ya kuua mtu. 32 Ili litimie lile neno lake Yesu alilolisema, akionyesha ni mauti gani atakayokufa.

18:28 NASB, NKJV, JB "kwenda Praitoria" NRSV "kwenda makao makuu ya Pilato" TEV "ikulu ya mtawala" Huu ni mtajo wa Kiratini kuhusu makazi rasmi ya mtawala wa Kirumi alipokuwa Yerusalemu. Hapa pangeweza kuwa ile ngome ya Antonio, ambayo ilikuwa jirani na Hekalu ama ikulu ya Herode mkuu.

MADA MAALUM: MLINZI WA MFALME

Kwa asili yake neno, "praetoria," linahusu hema la majeshi ya Kirumi ("hakimu”), lakini baada ya kipindi cha kuangushwa kwa mtawala wa Rumi lilitumika katika dhana ya utawala kuonesha makao makuu ama maskani ya siasa (kama vile Mt. 27:27; Yohana 18:28,33; 19:9; Mdo. 23:35; Flp. 1:13). Hata hivyo kwenye ulimwengu wa kirumi wa karne ya kwanza lilitumika kwa watumishi ambao waliunda kikosi maalumu cha ulinzi wa ufalme. Kundi hili la maaskari waliopewa heshima maalumu lilianziswha na Augustino (27 K.K.) lakini mwishowe lilitiwa mkazo katika Rumi na Tiberia.

1. Kuwa wenye cheo kimoja, kamanda wa karne 2. pokea mshahara mara mbili ya kiwango 3. kuwa na upendeleo maalumu (yaani, walistaajabu baada ya miaka 16 badala ya miaka 25) 4. kuwa wenye nguvu kiasi kwamba uchaguzi wao kwa amiri jeshi mkuu wa ufalme wa Rumi

aliyeheshimiwa Ulipofika muda wa Konstantine ndipo kikundi hiki kilichokuwa kimepewa heshima maalumu chenye nguvu kisiasa mwishowe kilivunjika

◙ "ikawa alfajiri" Twajua kutokana kumbukumbu za Kirumi kwamba maafisa wa Kirumi katika Palestina walikutana kwa ajili ya Mahakama wakati wa mapumziko ya mchana..ionekanavyo ilikuwa mapema wakati baraza la mafarisayo walipokutana ili kutoa mfanano wa kukubalika na uhalali katika mashtaka ya usiku yasiyo halali. Mara tu wakampeleka Yesu kwa Pilato.

◙ "lakini wao wenyewe hawakuingia ndani ya ile praitorio, wasije wakanajisika" Kwa kule kuingia ndani ya makao ya mtu wa mataifa wangenajisika kwa chakula cha Pasaka. Ni jambo la kinyume kwamba walikuwa wepesi sana kuchukizwa na mambo ya sherehe lakini hawakuwa na shaka kuhusu kumhukumu mtu kifo kinyume na sheria. Aya hii ndicho kiini cha mabishano kuhusu kutokukubalina kwa kihistoria kunakoonekana kati ya dokezo za injili zinazoeleza kwamba yesu alikula Pasaka na wanjafunzi wake (kama vile Mt. 26:17; Marko 14:12; Luka 22:1), na Yohana, inayoonyesha kwamba jambo hili lilitendeka siku moja iliyotangulia (Alhamisi), maandalio ya siku ya sikukuu ya Pasaka. Msomi mwenye tabia ya Yohana aliyetambuliwa sana toka Romani Katoliki, Raymond Brown, anaweka maoni yake ndani ya kitabu cha Jerome Biblical Commentary: "Ikiwa matukio ya nyakati kama yalivyoandikwa ndani ya mapokeo yaliyo pamoja yatapendelewa siku zote kwa yale ya Yohana kutokana na mtazamo wa uhalisi wa matukio, Aya ifuatayo –taarifa ya shahidi ambaye hakika aliyajua mapokeo ya pamoja –anatoa baadhi ya matatizo yasiyotatulika. Ikiwa kwa upande mwingine, tunatambua kwamba ushuhuda wa aliye shuhudia kutoka kwa Yohana umekwisha kuundwa mara nyingi uko karibu zaidi na matukio ya kweli endelevu kuliko muhtasari wa kimpango wa aya , inakuwa yakuelekeza zaidi" (uk. 458). Pia kuna uwezekano wa kuwepo tarehe mbili tofauti za kuishika pasaka, Alhamisi na Ijumaa, lipo pia tatizo lililoongezwa kwamba neno “Pasaka" linaweza kutumika kwenye karamu ya siku moja na sherehe ya siku nane (Pasaka ikiunganishwa na mikate isiyotiwa chachu, kama Kutoka 12).

Page 304: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

288

◙ "bali wapate kuila Pasaka" Bado yapo matatizo kuhusu tarehe yenyewe ya chakula cha mwisho.vidokezo vya Injili vinaonekana kuonesha bila kutaja kwamba kilikuwa chakula cha pasaka, Lakini Yohana anataja kwamba ilikuwa siku moja kabla ya chakula rasmi cha pasaka (kama vile Yohana 19:14 na kinyume chake). Jibu laweza kuwa katika

1. ukweli kwamba neno "pasaka" waweza kuhusu juma lenyewe, chakula chenyewe, ama sabato maalumu 2. ukweli kwamba baadhi ya makundi ya Kiyahudi yanayojitenga (yaani, Essene) kufuata kalenda inayofuata

kuandama kwa mwezi kutoka kwenye kitabu cha sikukuu ya ukumbusho (Jubilii) 3. Ukweli kwamba "maana mbili" za Yohana zinamweka Yesu kama mwana kondoo wa Pasaka (1:29),

ambaye alichinjwa siku moja kabla ya Pasaka

18:29 Mungu alitumia nafasi ya Pilato hasa kama alivyomtumia Farao katika Kutoka. Aliteuliwa kuwa liwali wa Yuda katika mwaka 26 b.k na mfalme Tiberio. Alichukuwa nafasi ya Valerius Gratus (aliyemwondoa Anasi kwenye Ukuhani Mkuu). Pontio Pilato alikuwa liwali wa mwisho wa Warumi. Alitawala ufalme wa Archelaus (mwana wa Herode mkuu), ambao ulijumuisha Samaria na Yuda, Gaza, na Bahari ya Chumvi. Habari kuhusu Pilato zatoka kenye mamlaka ya Flavius Josephus.

MADA MAALUMU: PONTIO PILATO

I. Mtu aitwaye Pontio Pilato A. Mahali na wakati alipozaliwa havijulikani B. Wa daraja au tabaka la Equestrian (daraja la juu ngazi ya kati la jamii ya Warumi) C. Alioa, lakini watoto hawajulikani D. Teuzi za kiutawala wa awali (ambazo lazima zilikuwa nyingi) hazijulikani

II. Nafsi ya mtu A. Mitazamo miwili tofauti

1. Philo (Legatio na Gaium, 299-305) na Josephus (Antiq. 18.3.1 na Jewish Wars 2.9.2-4) wanamwelezea mtawala wa ….. asiye na huruma na katili.

2. The NT (Injili, Matendo) linamtoa kama wakili wa Kirumi dhaifu ambaye anaweza kuendeshwa kwa urahisi.

B. Paul Barnett, Jesus and the Rise of Early Christianity, kur. 143-148, kinatoa maelezo yenye kukubalika kuhusu mitazamo hii miwili. 1. Pilato aliteuliwa kuwa wakili mwaka 26 b.k chini ya Tiberia ambaye alikuwa anaunga mkono

Wayahudi (kama vile. Philo, Legatio and Gaium, 160-161). 2. Tiberius alipatwa mateso ya kupotesa nafasi yake ya kisiasa kwa L. Aelius Sejanus, Kiranja wake

wa walinzi wa jumba la kifalme aliyefanyika ngu halisi nyuma ya kiti cha kifalme na aliyewachukia Wayahudi (Philo, Legatio land Gaium, 159-160).

3. Pilato alikuwa mfuasi wa Sejanus na alijaribu kumvutia a. Kuleta viwango vya kirumi kwenye mji wa Yerusalemu (26 B.K), ambavyo mawakiri

wengine hawakuwa wamefanya. Hizi alama za Miungu wa Kirumi iliwachochea Wayahudi (kama vile. Josephus' Antiq. 18.3.1; Jewish Wars 2.9.2-3).

b. Kuchapa sarafu (29-31 B.K.) ambayo ilikuwa na picha za Warumi wakiabudu zimechongwa juu yake. Josephus anasema alikuwa kwa makusudi kabisa anajaribu kupindua sheria za kiyahudi na desturi (kama vile Josephus, Antiq. 18.4.1-2).

c. Kuchukua fedha kutoka hazina ya hekalu kujenga mfereji Yerusalemu (kama vile Josephus, Antiq. 18.3.2; Jewish Wars 2.9.3).

d. kupata Wagalilaya baadhi na kuwaua wa kutoa dhabihu siku ya pasaka mjini Yerusalemu. e. Kuleta ngao za Kirumi mjini Yerusalemu katika mwaka 31 b.k. , mwana wa Herode mkuu

aliyempelekea ombi kwake waondolewe. Lakini asingefanya hivyo walimwandikia Tiberia ambaye aliwataka warejeshwe kaisaria kwa bahari (kama vile. Philo, Legatio na Gaium,

Page 305: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

289

299-305). f. Kupata Wasamaria wengi wachinjwe juu ya mlima Gerizim (mwaka 36/37b.k) walipokuwa

wanalifuta vifaa vyao vitakatifu vya dini yao, ambavyo vilikuwa vimekwisha potea. Jambo hili lilimsababisha mkuu wake Pilato wa mahali pale (Vitellius, Kiranja wa Ashuru) amwondoe kutoka ofisini na kumtuma Roma (kama vile Josephus, Antiq. 18.4.1-2).

4. Sejanus alihukumiwa katika mwaka 31 b.k na Tiberia alirejeshwa kwenye mamlaka ya kisiasa kwahiyo , #a, b, c, na d pengine zilifanywa na Pilato kupata imani kwa Sejanus' ; #e zingeweza kuwa ni majaribio ya kupata imani kwa Tiberia lakini yawezekana yakawa yamelipuka na kuharibika.

5. Ni dhahiri kwa amiri jeshi mfalme anayeunga mkono Wayahudi aliyerejeshwa pamoja na barua rasmi kwa mawakili kutoka Tiberia kuwa mwema kwa Wayahudi (kama vile Philo, Legatio na Gaium, 160-161), kwamba uongozi wa Kiyahudi katika Yerusalemu walichukua fursa ya udhaifu wa kisiasa wa Pilato na Tiberia na wakamrubuni ili amsababishe Yesu kusulubiwa. Nadharia ya Barnett inaleta pamoja mitazamo hiyo miwili ya Pilato katika njia inayoonekana kuwa yenye mantiki.

III. Hatma yake A. Aliitwa tena na alifika Roma mara tu baada ya kifo cha Tiberia (mwaka 37b.k). B. Hakuteuliwa tena. C. Mke wake hajulikani baada ya hili. Kuna nadharia nyingi za baadaye, lakini hakuna kweli zilizo salama.

18:30"Kama huyu asingekuwa mtenda mabaya, tusingemleta kwako" Hii ni sentensi shurutishi daraja la pili mara nyingi huitwa “kinyume na ukweli.” Yesu hakuwa mtenda maovu. Haya yalikuwa maoni ya kejeli ya Pilato ambaye alikataa kujihusisha na "makosa madogo madogo" ya mashitaka ya kidini ya Kiyahudi Kitenzi hiki "kukabidhi" ni neno hilohilo ambalo kwa kawaida hutafsiriwa "salitiwa" linapotumika kwa upande wa Yuda (kama vile Yohana 6:64,71; 12:4; 13:2,11,21; 18:2,5). Mtajo kwa maana ya asilli lamaanisha "kumkabidhi mtu kwa mamlaka" au "kuendeleza desturi au mapokeo." Kwa kumhusisha Yuda, mtajo umeongeza nguvu katika maana miongoni mwa watafsiri wa kiingereza.

18:31 "Sisi hatuna ruhusa ya kuua mtu" Uongozi wa Kiyahudi ulikuwa umemhukumu kwa kukufuru, lakini walitumia shitaka la kuasi serikalini ili ashtakiwe na Warumi. Ilikuwa muhimu kwa viongozi wa Kiyahudi kwamba Yesu asulubiwe kwa sababu ya Kumb. 21:23 (yaani, kusulubiwa kulieleweka na Rabbi wa karne ya kwanza kama kuwa unalaaniwa na Mungu). Yesu alikwisha tabiri jambo hili katika Yohana 18:32; 3:14; 8:28; 12:32,33; na Gal. 3:13.

18:32 "akionyesha ni mauti gani atakayokufa" Kwa nini viongozi wa Kiyahudi walitaka Yesu asulubiwe? Ni dhahiri kutoka Matendo 7 kwamba walitoa adhabu kali kwa kosa la kukufuru kwa kupigwa mawe wakati huo huo. Pengine inakaribiana na laana ya Kiungu Kumb. 21:22-23. Kwanza ilihusika na kuchomwa na kitu kilichochongoka baada ya kufa lakini Rabbi wa wakati ule walitafsiri aya hii katika mtazamo wa kusulubiwa kwa Kirumi. Walitaka Yesu huyu, aliyejifanya Masihi, alaaniwe na Mungu. Huu ulikuwa mpango wa Mungu kwa ukombozi wa mwanadamu aliyekuwa ameanguka.Yesu mwana-kondoo wa Mungu (yaani, 1:29), alijitoa mwenyewe kama fidia (kama. Isaya 53; 2 Kor. 5:21). Yesu akawa “laana" (kama vile Gal. 3:13).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 18:33-38a 33 Basi Pilato akaingia tena ndani ya Praitorio, akamwita Yesu, akamwambia, Je! Wewe ni Mfalme wa Wayahudi? 34 Yesu akamjibu, Wewe wasema hivi kwa nafsi yako, au watu wengine walikuambia habari zangu? 35 Pilato akajibu, Ama! Ni Myahudi mimi! Taifa lako na wakuu wa makuhani ndio waliokuleta kwangu. Umefanya nini? 36 Yesu akajibu, Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa. 37 Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja

Page 306: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

290

ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu. 38 Pilato akamwambia, Kweli ni nini?

18:33 "Praitorio" Tazama Mada Maalumu katika Yohana 18:28

◙ "Je! Wewe ni Mfalme wa Wayahudi" Yesu alishtakiwa kwa uhaini (kama vile Mt. 27:11; Marko 15:2; Luka 23:2 na Yohana 19:3,12,15,19-22).

18:34 "Yesu akamjibu, Wewe wasema hivi kwa nafsi yako, au watu wengine walikuambia habari zangu" Ikiwa Pilato alikuwa anauliza swali hilo kwa kuhusiana na ufalme wa kisiasa Yesu angekataa. Ikiwa wayahudi walikuwa wameshauri hivyo basi ilihusiana na umasihi wake na Yesu angethibitishia Pilato kwa hakika hakuwa tayari kujadili utatanishi wa mawazo ya dini ya Kiyahudi (kama vile Yohana 18:35).

18:35 Swali la kwanza latarajia jibu la "hapana".Pilato anaweka wazi hali yake ya kutoheshimiwa kwa dini ya Wayahudi.

18:36 "Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania"Hii ni sentensi shurutishi daraja la pili iliyoitwa "kinyume na ukweli."Inapaswa kutafsiriwa "Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu na sivyo ulivyo, basi watumishi wangu wangekuwa wanapingana ambavyo hawafanyi hivyo. Kifungu "watumishi wangu" inarejea kwa (1) wanafunzi au (2) malaika (kama vile Mt. 26:53).

18:37 "Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi?" Hii ilikuwa ni kijeli hasa midomoni mwa alama hii ya nguvu ya kidunia (yaani, Rumi), Ikimshambulia Yesu Na ufalme wake wa kiroho. Hili swali hasa jibu la “ndio."

◙"Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni"Kifungu cha kwanza ni tatizo kutafsiri kwa sababu kina maana zaidi ya moja. Ni tamko linalo dhihirisha ukweli likiwa na sifa (kama vile Mt. 27:11; Marko 15:2; Luka 23:3).Yesu alijua alikuwa nani (vitenzi viwili vya njeo timilifu),(kama vile Yohana 13:1,3; Marko 10:45; Luka 2:49; Mt. 16:22 na kuendelea). Pilato hakupata kuelewa!

◙ "Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya"Yesu ananena kuhusu kazi ya kumfufua Baba” (yaani, "kushuhudia juu ya kweli"). Kimsingi kuna sababu tatu za kwa nini Yesu alikuja.

1. Kumfunua kwa utoshelevu na kikamilifu tabia na kusudi la Mungu (kama vile Yohana 1:18; 3:32) 2. Kufa kama mwanakondoo wa Mungu asiye na hatia azichukua dhambi za ulimwengu (kama vile. Yohana

1:29) 3. kuwapa waamini mfano namna gani waishi na kumpendeza Mungu

◙"Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu" Kila wakati mimi nasukumwa na,"kila mmoja," "yeyote," "chochote kile"! Wengi kiasi chochote Ajabu! YHWH anatimiliza Mwa. 3:15 katika Kristo. Yesu urejesha sura ya Mungu iliyoharibiwa katika Anguko (kuzifikia siku za mwisho). Zaidi ya yote macho ya kiroho na masikio (kama vile, Yohana 10:3,16,27; 18:37) unaweza kuelewa ukweli (kama vile Mt. 11:15; 13:9,16,43; Marko 4:9,23; Luka 8:8; 10:23,24; 14:35; Ufu. 2:7,11,17,29; 3:6,13,22). Yesu ni kweli (Yohana 14:6)! Wakati anazungumza na wafuasi wake (kama vile. Yohana 10:1-5). Katika Yohana "ona" au "sikia" ukweli ni theolojia inayorandana na upokeaji wa "uzima wa milele."

18:38 "Pilato akamwambia, Kweli ni nini?" Pilato aliuliza swali hili, lakini inavyoonekana aliondoka kabla hajapata jibu. Pilato alitaka kujihakikishia mwenyewe kwamba Yesu hakuwa tishio kwenye serikari ya Warumi. Alifanya hili. Kisha alijaribu kumfanya Yesu afunguliwe kama ilivyokuwa desturi ya Wayahudi wa siu zile katika msimu wa pasaka (kama vile Yohana 18:39; Mt. 27:15). Yohana ameandika, kama alivyofanya Luka, kuonesha Ukristo haukuwa tishio kwenye utawala wa Kirumi (yaani, Yohana 18:38b; 19:4; Luka 23:4,14,22).

Page 307: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

291

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 18:38b-40 38bNaye akiisha kusema neno hilo akawatokea Wayahudi tena, akawaambia, Mimi sioni hatia yo yote kwake. 39 Lakini kwenu kuna desturi ya mimi kuwafungulia mtu mmoja wakati wa Pasaka; basi, mwapenda niwafungulie Mfalme wa Wayahudi? 40 Basi wakapiga kelele tena kusema, Si huyu, bali Baraba. Naye yule Baraba alikuwa mnyang'anyi.

18:39 "kuna desturi"Hii imeelezwa katika Mt. 27:15 na Luka 23:17 (lakini haijulikani kutoka kwenye nyaraka za kihistoria nje ya Agano Jipya).

18:40 "Basi wakapiga kelele tena kusema, Si huyu, bali Baraba" Ni jambo la kinyume kwamba Baraba alionekana kama mwanachama wa chama cha zealot na, kwa hiyo, mwenye hatia kwenye shitaka lilelile ambalo Yesu alihukumiwa kwalo (kama vile Marko 15:7; Luka 23:19,25). Kundi hili linaonekana kama lilikwisha kuwa linangojea pale kumuunga mkono shujaa wa nyumbani kwao. Mamlaka ya Wayahudi imechukua nafasi kuhakikisha kutiwa hatiani kwa Yesu (kama vile Marko 15:11). Pia ni jambo la kinyume kwamba jina la "Baraba" linamaanisha "mwana wa baba wa kawaida." Yohana anatumia mchezo huu wa maneno kwenye injili yote. Kusanyiko walitaka “mwana wa baba” aachiliwe badala ya “mwana wa baba” Giza limekuja kikamilifu!

MASWALI YA MJADALA

Huu ni mwongozo wa fasiri, ina maanisha kwamba unawajibika kwa tafsiri zako mwenyewe za Biblia. Kila mmoja wetu lazima atembee katika mwanga tulio nao. Wewe, Biblia, na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Hutakiwi uvitelekeze vitu hivi kwa mfasiri. Maswali ya mjadala huu yanatolewa kukusaidia kufikiri juu ya mambo makubwa ya sehemu za kitabu hiki. Yanalenga kukuamsha kimawazo na sio kutoa maana.

1. Kwanini Yesu alikwenda mahali ambapo alijua Yuda angemkuta? 2. Kwanini Yohana ameruka ile sehemu ya mateso pale Gethsemane? 3. Kwanini baraza la Mafarisayo lilimpeleka Yesu kwa Pilato? 4. Kwanini mpangil io wa matukio kati ya Yohana na injili za muhtasari zinachanganya sana? 5. Kwanini Yohana anamweleza Pilato kama anajaribu kumfungulia Yesu?

Page 308: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

292

YOHANA 19

MIGAWANYO YA AYA YA TAFSIRI ZA KISASA

UBS4 NKJV NRSV TEV NJB Yesu anahukumiwa Askari wa mdhihaki Yesu anahukumiwa Yesu mbele ya Pilato kufa Yesu kufa (18:38b-19:16a) (18:38b-19:7) (18:38b-19:16) (18:28-19:11) 18:38b-19:7 18:38b-19:7 18:33-19:3 18:40-19:3 19:1-4 Uamuzi wa Pilato 19:4-5 19:4-7 19:5-16 19:6a 19:6b 19:7 19:8-12 19:8-12 19:8-9a 19:8-11 19:9b-10 19:11 19:12 Yesu anahukumiwa kifo 19:12-16a 19:13-16a 19:13-16a 19:13-14 19:15a 19:15b 19:15c 19:16a Kusulubiwa kwa Mfalme juu ya Yesu anasulubiwa Kusulubishwa Yesu msalaba 19:16b-22 19:16b-25a 19:16b-21 19:16b-22 19:17-24 19:22 Vazi la Yesu linagawanwa 19:23-27 19:23-24 19:23-24 Mtazame Mama Yesu na Mama yako yake 19:25-27 19:25b-27 19:25-26 19:25-27 19:27 Kifo cha Yesu Imekwisha Kifo cha Yesu Kifo cha Yesu 19:28-30 19:28-30 19:28-30 19:28 19:28 19:29-30a 19:29-30 19:30b Kuchomwa kwa Yesu anachomwa Yesu anachomwa Kuchochomwa Yesu ubavuni ubavuni ubavuni ubavuni 19:31-37 19:31-37 19:31-37 19:31-37 19:31-37 Kuzikwa kwa Yesu Yesu azikwa ndani ya Kuzikwa kwa Yesu Mazishi Kaburi la Yusufu 19:38-42 19:38-42 19:38-42 19:38-42 19:38-42

Page 309: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

293

MZUNGUKO WA TATU WA USOMAJI KUFUATILIA KUSUDIO LA ASILI LA MWANDISHI KATIKA NGAZI YA AYA Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwatafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Aya ya kwanza 2. Aya ya pili 3. Aya ya tatu 4. N.k

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 19:1-7 1 Basi ndipo Pilato alipomtwaa Yesu, akampiga mijeledi. 2 Nao askari wakasokota taji ya miiba, wakamtia kichwani, wakamvika vazi la zambarau. 3 Wakawa wakimwendea, wakisema, Salamu! Mfalme wa Wayahudi! Wakampiga makofi. 4 Kisha Pilato akatokea tena nje, akawaambia, Mtu huyu namleta nje kwenu, mpate kufahamu ya kuwa mimi sioni hatia yo yote kwake. 5 Ndipo Yesu alipotoka nje, naye amevaa ile taji ya miiba, na lile vazi la zambarau. Pilato akawaambia, Tazama, mtu huyu! 6 Basi wale wakuu wa makuhani na watumishi wao walipomwona, walipiga kelele wakisema, Msulibishe! Msulibishe! Pilato akawaambia, Mtwaeni ninyi basi, mkamsulibishe; kwa maana mimi sioni hatia kwake. 7 Wayahudi wakamjibu, Sisi tunayo sheria, na kwa sheria hiyo amestahili kufa, kwa sababu alijifanya kuwa Mwana wa Mungu.

19:1 "Pilato alipomtwaa Yesu, akampiga mijeledi" Mwandamano wa muda na idadi ya vichapo vya mijeredi havina uhakika. Wafungwa wote waliokuwa wanahukumiwa kusulubiwa walipigwa mijeledi. Lilikuwa tukio lenye ukatili wa hali ya juu usio kuwa na huruma kiasi kwamba watu wengi walikufa kutokana nalo. Hata hivyo, kufuatana na mazingira, Pilato anaonekana kuwa alimpiga mijeredi Yesu ili kupata huruma kwa kusudi la kumtaka afunguliwe (kama vile Luka 23:16,22; Yohana 19:12). Hii inaweza kuwa ni kutimia kwa Warumi unabii wa Isa. 53:5. Kuchapwa mijeredi kwa Warumi kulikuwa kwa maumivu ya kutisha, adhabu ya kikatili sana bila huruma iliyokuwa imehifadhiwa kwa wasio kuwa Warumi. Mjeredi wa ngozi uliofungiwa kipande vya mfupa ama chuma kilifungwa kwenye mwisho wa kila kamba kilitumika kumchapia mtu aliyekuwa ameinama, Mikono yake ikiwa imefungwa kuelekea chini, Idadi ya vichapo haikutamkwa. kwa kawaida zoezi hili lilifanyika kabla ya kusulubiwa,(kama vile Livy XXXIII:36). Injili zinatumia maneno tofauti kuelezea mapigo hayo mikononi mwa Warumi.

1. Mt. 27:26; Marko 15:15 -- phragelloō, kuchapa mijeledi 2. Luka 23:16,22 -- paideuō, kwa asili kumwadibisha motto (kama vile Ebr. 12:6-7,10), lakini hapa, kama

katika 2 Kor. 6:9, ya pigo 3. Yohana 19:1 -- mastigoō, kwa asili jina la mjeledi, Mt. 10:17; 20:19; 23:34; Mdo. 22:24-25; Ebr. 11:36

Yote yanaweza kuwa na maana inayokaribiana ama yanaweza kuonesha mapigo mawili a. pigo dogo zaidi lililofanywa na Pilato b. kuchapa mjeledi kabla ya kusulubiwa

19:2 "Nao askari wakasokota taji ya miiba, wakamtia kichwani" Hii ilikuwa namna ya mateso ambapo miiba ilikandamizwa ndani ya nyusi za Yesu. Kwa hali yoyote inawezekana kwamba iliwakilisha taji iliyotengenezwa kwa majani ya mchikichi ambayo ilikuwa njia nyingine ya kufanyia dhihaka Yesu kama mfalme (kama vile Mt. 27:27-31; Marko 15:15-20).

Page 310: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

294

Neno la Kiyunani "taji" (stephanos) lilitumika kumvika mshindi wa mbio ama shada la maua ya mti aina ya mdalasini lililovaliwa na mfalme mkuu.

◙ "wakamvika vazi la zambarau" Zambarau (porphyros) ilikuwa iskara ya ufalme, hiyo rangi ya nguo ilikuwa ya ghali sana kwa kuwa ilitengenezwa kutokana na magamba ya kombe. Rangi nyekundu ilikuwa rangi ya mavazi ya maafisa wa Kirumi (Marko 15:17,20). Dawa nyekundu ilitengenezwa kutokana magamba ya wadudu waliopatikana kwenye mti aina ya mwaloni. Joho hili lilikuwa ni kidokezo kwa joho la kifalme la rangi ya zambarawe, lakini katika uhalisia pengine lilikuwa ni joho jekundu la afisa wa kirumi lililopauka (kama vile Mt. 27:28). 19:3 NASB "na walianza kuja kwake na kusema" NKJV "kasha wakasema" NRSV "waliendelea kuja kwake, wakisema" TEV "na wakaja kwake na wakasema" NJB "Waliendelea kuja kwake na wakisema" Hizi ni kauli zisizo timilifu. Yaonekana maaskari walifanya jambo hili mmoja baada ya mwingine. Dhihaka hii ilikuwa inawadhalilisha Wayahudi kwa jumla zaidi ya Yesu mwenyewe. Yawezekana Pilato alitaka hili ili kusababisha huruma kwa Yesu, lakini haikutendeka hivyo. Tena katika maandiko ya Yohana maneno ya kinabii mara nyingi huwekwa ndani ya midomo ya wapinzani. Askari hawa walisema maneno mengi zaidi ya yale walioyajua.

◙ "Wakampiga makofi" Neno kiasili lilimaanisha kupiga "kumchapa kwa fimbo," lakini baadaye lilikuja kutumika kwa “kuchapa kofi.” Hii yawezakuwa ni ishara ya dhihaka ya salamu ya mfalme ambayo ni zaidi ya ukatili wa kupigwa kwa fimbo. 19:4 NASB "Sioni hatia ndani yakee" NKJV "sioni hatia kwake" NRSV "sioni shitaka lolote likimkabili" TEV "Siwezi kupata sababu yoyote ya kumtia hatiani" NJB "Sipati shitaka lolote kwake" Mojawapo ya madhumuni ya Yohana ilikuwa kuonesha kwamba Ukristo haukuwa tishio kwa serikali ya Kirumi na watawala wake. Yohana anaandika kwamba Pilato alijaribu kumfungua Yesu mara kadhaa (kama vile Yohana 18:38; 19:6; Luka 23:4,14,22). 19:5 NASB, NKJV "Tazama, mtu huyu!" TEV, NET "tazama! Hapa kuna Mtu" NRSV, NJB, REB "huyu hapa yule mtu!" Kumekuwepo na njia nyingi za kuielewa aya hii.

1. Yesu anavalishwa kama mfalme wa kudhihakiwa 2. Yesu anapigwa ili kuomba huruma kwa Mungu 3. ni kidokezo kwa Zek. 6:12 (rejeo la ki-Umasihi la neno "Tawi") 4. baadaye unathibitishwa ubinadamu wa Yesu (yaani, kinyume na mafunuo ya Yohana ya siku hizi) 5. inakaribiana na neno la Kiaramu "mwana wa adamu," bar nashā (mfano mwingine wa Masihi

aliyewekewa utaji)

Page 311: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

295

19:6 "walipiga kelele wakisema, Msulibishe! Msulibishe!!" Sababu iliyowafanya viongozi wa Kiyahudi watake Yesu asulubiwe ilikuwa ili kwamba laana iliyoko kwenye kitabu cha Kumb. 21:23 ingetimia. Hii ni sababu moja ambavyo pengine Paulo alikuwa na Mashaka makubwa kuhusu Yesu wa N azareti kuwa Masihi wa Mungu. Hata hivyo tunajifunza kutoka Wagalatia Gal. 3:13 kwamba Yesu alichukua laana zetu juu ya msalaba (kama vile. Kol. 2:14).

◙ "kwa maana mimi sioni hatia kwake" Pilato analisema hili mara tatu (kama vile Yohana 18:38; 19:4). 19:7 "Inampasa afe kwa sababu alijipanga kuwa mwana wa Mungu" Yesu alidai kuwa wamoja na Mungu, mwanaye pekee. Wayahudi, ambao walisikia matamshi/ kauli zake na wakaelewa nia ya kauli hizo, hawakuwa na mashaka kwamba alikuwa anadai kuwa mwenye Uungu (kama vile Yohana 5:18; 8:53-59; 10:33). Shitaka halisi la Wayahudi kumhusu Yesu lilikuwa kufuru (kama vile Mt. 9:3; 26:65; Marko 2:7; 14:64; Luka 5:21; Yohana 10:33, 36). Shitaka la kufuru liliadhibiwa kwa kupigwa kwa mawe (kama vile Law. 24:16). Kama Yesu si aliyefanyika mwanadamu, Mungu aliyekuwepo kabla ya nyakati, alipaswa kupigwa kwa mawe!

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 19:8-12 8 Basi Pilato aliposikia neno hilo, akazidi kuogopa. 9 Akaingia tena ndani ya ile Praitorio, akamwambia Yesu, Wewe umetokapi? Lakini Yesu hakumpa jibu lo lote. 10 Basi Pilato akamwambia, Husemi nami? Hujui ya kuwa mimi nina mamlaka ya kukufungua, nami nina mamlaka ya kukusulibisha? 11 Yesu akamjibu, Wewe hungekuwa na mamlaka yo yote juu yangu, kama usingepewa kutoka juu; kwa hiyo yeye aliyenitia mikononi mwako yuna dhambi iliyo kubwa zaidi. 12 Na tangu hapo Pilato akatafuta kumfungua; lakini Wayahudi wakapiga makelele wakisema, Ukimfungua huyu, wewe si rafiki yake Kaisari; kila mtu ajifanyaye kuwa mfalme humfitini Kaisari.

19:8 "Basi Pilato aliposikia neno hilo, akazidi kuogopa" Mke wa Pilato alikuwa amekwisha kumwonya kuhusu Yesu (kama vile Mt. 27:19), na sasa viongozi wa Wayahudi walikuwa wanadai kwamba alikwisha kutamka kwamba ndiye alikuwa mwana wa Mungu. Pilato, akiwa na imani za kichawi aliogopa sana. Ilikuwa kawaida sana kwa miungu ya Wayunani na miungu ya Warumi kuwaatembelea wanadamu kwenye umbo la kibinadamu. 19:9 NASB, NKJV, NRSV "Wewe umetokapi" TEV, NJB, NIV "Umetokea wapi" Pilato haulizi kuhusu mji ambao Yesu anatokea bali chanzo chake. Pilato anaanza kuhisi umuhimu wa mtu aliye mbele yake. Yesu alijua kutoka kwenye hoja zake katika Yohana 18:38 kwamba Pilato hakuwa na haja na ile kweli bali faida ya kisiasa hivyo hakuitikia. Pilato anajiunga na idadi ya watu wanaomsatajabia Yesu lakini hawaelewi asili yake (kama vile Yohana 4:12; 6:42; 7:27-28,41-42; 8:14; 9:29-30). Hii ni sehemu ya Yohana ya pande mbili zilizo wima. Yesu ni wa kutoka juu na hakuna yeyote chini anaweza kujua/kuelewa/kuona/kusikia bila mguso wa baba (yaani, 6:44,65; 10:29).

◙ "Yesu hakumpa jibu lo lote" Pilato atakuwa amekwisha kukumbuka jibu la Yesu (kama vile Yohana 18:37)! Baadhi waliona hili kama kutimia kwa Isaya Isa. 53:7. 19:10 "nami nina mamlaka ya kukusulibisha" Pilato anatamka kwamba anayo mamlaka kisiasa ya uzima na kifo, bado mbele ya kundi kaidi aliachilia haki hii katika mapenzi yao. Swali la Pilato kisarufi lilitegemea jibu la “ndiyo"

Page 312: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

296

19:11 "Wewe hungekuwa na mamlaka yo yote juu yangu, kama usingepewa kutoka juu" Hii ni sentensi shurutishi daraja la pili iitwayo "kinyume na kweli." Yesu hakuwa amedhalilishwa na Pilato. Alijua yeye ni nani na kwa nini alikuwa amekuja! Biblia inadhihirisha kwamba Mungu yuko nyuma ya mamlaka yote ya binadamu (kama vile Rum. 13:1-7).

◙ "yeye aliyenitia mikononi mwako yuna dhambi iliyo kubwa zaidi" Kwanza unapoisoma inaonekana

kumruhusu Yuda Iskariote (kama vile Yohana 6:64,71; 13:11) lakini wafasihi wengi wanaamini inamhusu Kayafa, ambaye rasmi alimkabidhi Yesu kwa Warumi. Aya hii inaweza kueleweka kiujumla kama inahusiana na (1) Viongozi wa Wayahudi wasio halali (2) Wayahudi wote kwa ujumla (kama vile Mt. 21:33-46; Marko 12:1-12; Luka 20:9-19; Warumi 9-11). 19:12 "Pilato akatafuta kumfungua" Hii ni njeo isiyo timilifu ambayo inamaanisha kitendo kilichorudiwa wakati uliopita. Alijaribu mara kadhaa.

◙ "Ukimfungua huyu, wewe si rafiki yake Kaisari" Hii ni kauli shurutishi daraja la tatu Ambayo ilimaanisha kitendo chenye nguvu isiyo dhihirika. Viongozi wa Kiyahudi walikuwa wanaishia kumshtaki Pilato kwa wakuu wake kule Roma kama hukutimiza matakwa yao na kumhukumu Yesu kifo. Kifungu "rafiki wa Kaisari" ilikuwa lugha inayoakisi cheo cha kutisha kilichotolewa na mfalme wa Warumi (kuanzia kwa Augustino au Vespasian). Kaisari ulikuwa ni wadhifa kwa mtawala wa Warumi uliokuja tokea kwa Jurius Kaisari na kurithishwa kwa Augustus.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 19:13-16 13 Basi Pilato, aliposikia maneno hayo, akamleta Yesu nje, akaketi juu ya kiti cha hukumu, mahali paitwapo Sakafu ya Mawe, au kwa Kiebrania, Gabatha. 14 Nayo ilikuwa Maandalio ya pasaka, yapata saa sita. Akawaambia Wayahudi, Tazama, Mfalme wenu! 15 Basi wale wakapiga kelele, Mwondoshe! Mwondoshe! Msulibishe! Pilato akawaambia, Je! Nimsulibishe mfalme wenu! Wakuu wa makuhani wakamjibu, Sisi hatuna mfalme ila Kaisari. 16 Basi ndipo alipomtia mikononi mwao ili asulibiwe; nao wakampokea Yesu.

19:13 "Pilato, aliposikia maneno hayo, akamleta Yesu nje, akaketi juu ya kiti cha hukumu" Andiko lina maana zaidi ya moja kwamba ni nani hukaa kwenye kiti cha hukumu. Wote wawili William na tafsiri yenye mwenendo mzuri inadai ya kwamba alikuwa NI Yesu, kama mfalme wa wayahudi. Hata hivyo mazingira yanamwonesha Pilato ambaye alikuwa tayari kutoa hukumu. NASB, NKJV, NJB "inaitwa sakafu kwa Kiebrania, Gabatha" NRSV "inaitwa sakafu ya mawe, au kwa Kiebrania Gabatha" TEV "inaitwa sakafu ya mawe (kwa Kiebrania, Gabatha)" Matumizi ya maneno ya Kiebrania/Kiaramu pamoja na fafanuzi zake vinavyoonesha kwamba wasikilizajji aliokuwa amewakusudia Yohana katika injili yake walikuwa watu wa Mataifa (kama vile Yohana 19:17). Hii sakafu ya mawe ilikuwa eneo la matangazo ya kisheria ya Warumi. Neno Gabbatha linamaanisha “mawe yaliyoinuliwa” ama “mahali palipoinuliwa”. 19:14 "Nayo ilikuwa Maandalio ya pasaka" Iko hitilafu ya dhahiri kati ya tarehe za kwenye vidokezo vya injili na tarehe ya Yohana. Kwenye dokezo za injili, Yesu alifuata kanuni za chakula cha Pasaka na wanafunzi kabla ya kukamatwa kwake (kama vile Marko 15:42), Lakini kwenye Yohana chakula kililiwa kwenye siku ya maandalizi kabla ya sherehe. Tazama maelezo kamili katika Yohana 18:28.

◙ "yapata saa sita" Mpangilio wa mashtaka ya Yesu mbele ya Pilato na kusulubishwa kwake ni:

Page 313: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

297

Mathayo Marko Luka Yohana

Hukumu ya Pilato Saa 6 19:14

Kusulubishwa Saa 3 15:25

Giza kuingia Saa 6-9 27:45

Saa 6-9 15:33

Saa 6-9 23:44

Yesu alilia Saa 9 27:46

Saa 9 15:34

Wakati uteuzi wa Muda wa tukio unalinganishwa, chaguzi mbili za tafsiri zinaibuka. 1. Ziko sawa. Yohana alitumia muda wa Kirumi, kuhesabu kuanzia saa, 12:00 asubuhi (kama vile Gleason L.

Archer, Encyclopedia of Bible Difficulties, uk. 364), na injili za muhtasari zinatumia muda wa Kiyahudi, kuhesabu kuanzia 6:00 asubuhi.

2. Yohana anadai muda wa baadaye kwa kusulubiwa kwa Yesu ambao ungekuwa mfano mwingine wa tofauti kati ya dokezo za injili na Yohana

Inaonekana kutoka Yohana 1:39 na 4:6 kwamba anatumia muda wa Kiyahudi na sio muda wa kirumi (kama vile M. R. Vincent, Word Studies, Juzuu. 1, p. 403). Mpangilio wa muda unaweza kuwa alama katika injili zote kwa kuwa zinahusiana kwenye

1. muda wa dhabihu Hekaluni (saa 3 asubuhi na saa 9 mchana kama vile Matendo 2:15; 3:1) 2. mara tu baada ya alasiri ulikuwa muda wa desturi wa kuchinja mwana kondoo wa Pasaka adhuhuri ya

Nisan 14 Biblia ikiwa kitabu cha kale cha mashariki, Haitazami mpangilio wa matukio, kama zinavyofanya taratibu nyingine za kihistoria za kimagharibi za kisasa.

◙ "Tazama, Mfalme wenu!" Kama Yohana 19:5 yaweza kuwa ni rejeo kwa Zek. 6:12, Aya hii yaweza kuwa rejeo kwa Zek. 9:9 (tazama F. F. Bruce, Answers to Questions, uk. 72). 19:14 Sentensi ya kwanza ni oni la kihariri. 19:15 "Mwondoshe! Mwondoshe! Msulibishe!” Aya hii ina maagizo matatu ya kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopita usio timilifu. Mzizi wa neno "kusulubiwa" linamaanisha "kuinua" au "kumwinua"; mtu katika cheo au heshima (kama vile Yohana 3:14; 8:28; 12:32).

◙ "Wakuu wa makuhani wakamjibu, Sisi hatuna mfalme ila Kaisari" Hii kejeli inafadhaisha. Hawa viongozi wa Wayahudi walikuwa na hatia ya kukufuru, shitaka lilelile ambalo wao walimshtaki Yesu. Katika Agano la Kale Mungu pekee ndiye mfalme wa watu wake (kama vile 1 Samweli 8). 19:16 "mwao" Katika Mt. 27:26-27 na Marko 15:15-16 kiwakilishi kinarejea maaskari wa Kirumi. Katika Yohana mwonekano waweza kuwa kwamba Pilato alimkabidhi Yesu katika matakwa ya viongozi wa Wayahudi na umma.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 19:17-22 17 Akatoka, hali akijichukulia msalaba wake, mpaka mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, au kwa Kiebrania, Golgotha. 18 Wakamsulibisha huko, na wengine wawili pamoja naye, mmoja huku na mmoja huku, na Yesu katikati. 19 Naye Pilato akaandika anwani, akaiweka juu ya msalaba, imeandikwa, YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI. 20 Basi anwani hiyo waliisoma wengi katika Wayahudi; maana mahali pale aliposulibiwa Yesu palikuwa karibu na mji; nayo iliandikwa kwa Kiebrania, na Kirumi, na Kiyunani. 21 Basi wakuu wa makuhani na Wayahudi wakamwambia Pilato, Usiandike, Mfalme wa Wayahudi; bali ya kwamba yule alisema, Mimi ni

Page 314: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

298

mfalme wa Wayahudi. 22 Pilato akajibu, Niliyoandika nimeyaandika.

19:17 "akijichukulia msalaba wake" Umbo la msalaba katika Palestina ya karne ya kwanza halina uhakika; lingeweza kuwa ile herufi kubwa ya T, herufi ndogo ya t, au X. Nyakati zingine wafungwa kadhaa walisulubiwa kwenye jukwaa wanaponyongea waharifu. Hata umbile llingekuwaje mfungwa aliyehukumiwa, ambaye alikwisha pigwa mjeledi, alilazimika kubeba sehemu ya chombo cha mbao hadi mahali pa kusulubishwa (kama vile Mt. 27:32; Marko 15:21; Luka 14:27; 23:26).

◙ "mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, au kwa Kiebrania, Golgotha" Maana halisi ya aya hii haina uhakika. Mtajo wa Kiebrania/Kiaramu haukurejerea mlima ulioonekana kama fuvu la kichwa, bali kwenye mlima mfupi usio na watu uliokuwa njia kuu ya kuingilia Yerusalemu. Warumi walisulubisha kama kukatisha tamaa na uasi. Uchimbaji wa kumbukumbu za kale wa siku hizi hauna hakika mahali palipokuwepo kuta za jiji! Yesu aliuawa nje ya ukuta wa jiji mahali palipo wazi kwa shuguli za kiutawala

19:18 “Wakamsulibisha huko” hakuna injili yoyote inayoeleza kwa undani kuhusu usulubishaji wa kirumi. Warumi wamenjifunza kutoka kwa watu wa Kathago, ambao walijifunza kutoka kwa waajemi. Hata umbile halisi la msalaba halijulikani kwa hakika. Tunajua hata hivyo, kwambaa kilikuwa kifo cha ukatili wa hali ya juu bila huruma kilichochukua muda mrefu kutimia! Jambo hili lilianzishwa kumhifadhi mtu hai katika maumivu kwa siku kadhaa. Kifo cha kawaida kilitokea kwa kukosa hewa. Lilimaanisha liwe kitu cha kuepusha kuiasi Roma. ◙“na wengine wawili” Hii ilitimiza unabii wa Isaya 53:9 ulionukuliwa katika Mathayo 27:38; Marko 15:27; na Luka 23:33. 19:19"Naye Pilato akaandika anwani"Pilato anaweza kuwa aliandika kwa mkono anwani (titlon) ambayo mtu mwingine aliandika kwenye kipande cha ubao. Mathayo anaiita “mashtaka” (aitian, kama vile Mathayo 27:37), ambapo Marko and Luka wanayaita maneno yaliyoandikwa kwenye mnara (epigraphē, kama vile Marko 15:26; Luka 23:38). 19:20“nayo iliandikwa kwa Kiebrania, na Kirumi, na Kiyunani” “kiebrania” kinarejelea kiaramu (kama vile Yohana 5:2; 19:13,17;20:16; Josephus, Antiq. 2.13.1). Inapendeza kufahamu tofauti miongoni mwa injili hata katika kuandikwa sawasawa maneno ya shitaka lililowekwa juu ya kichwa cha Yesu pale msalabani.

1. Mathayo 27:37 -- "Huyu ni yesu mfalme wa wayahudi" 2. Marko 15:26 -- "Mfalme wa Wayahudi" 3. Luka 23:38 -- "Huyu ndiye mfalme wa wayahudi" 4. Yohana 19:19 -- "Yesu, mnazareti, mfalme wa Wayahudi, "

Kila moja iko tofauti, lakini kimsingi ni sawa. Hili ni kweli kwenye nyingi miongni mwa tofauti za habari za kihistoria miongoni mwa injili. Kila mwandishi alinakili kumbukumbu zote kwa njia tofauti kidogo, lakini bado ni taarifa za mashahidi walioona kwa macho. Pilato alimaanisha kuwakasirisha viongozi wa Wayahudi kwa kuweka anwani ile ile waliyoogopa kuiweka juu ya msalaba wa Yesu (kama vile. Yohana 19:21-22). 19:22“Niliyoandika nimeyaandika”Hizi ni njeo mbili za kitenzi cha wakati ulio timilifu ambazo zinasistiza ukamilifu na uamuzi wa mwisho wa kile kilichokuwa kimekwisha andikwa.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 19:23-25a 23 Nao askari walipomsulibisha Yesu, waliyatwaa mavazi yake, wakafanya mafungu manne, kwa kila askari fungu lake; na kanzu nayo. Basi kanzu ile haikushonwa, ilikuwa imefumwa yote pia tangu juu. 24 Basi wakaambiana, Tusiipasue, lakini tuipigie kura, iwe ya nani. Ili litimie andiko lile linenalo, Waligawanya nguo zangu, Na vazi langu wakalipigia kura. Basi ndivyo walivyofanya wale askari. 25a Na penye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mamaye, na umbu la mamaye, Mariamu wa Klopa, na Mariamu Magdalene.

Page 315: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

299

19:23“wakafanya mafungu manne, kwa kila askari fungu lake” Maaskari wakazipigia kura nguo za Yesu. Hii inazungumzia mavazi yake ya juu tu. Haina hakika jinsi gani nguo za Yesu zingiweza kugawanywa makundi manne. Hii lazima iwe inahusu viatu vyake, skafu ya maombi (tallith), kikoi na mavazi ya nje. Hakuna hakika kama Yesu aliyevaa kilemba. Wayahudi wangechukizwa kwa ajili ya uchi wa mnyama. Huu pia ni utimiaji wa unabiii ulionukuliwa na Yohana 19:24(kama vile Zab. 22:18). ◙“kanzu" Vazi la nje la Yesu limelejelewa kwa neno la wingi himatia. Nguo yake ndefu ya ndani, inayovaliwa inayogusana na ngozi, ilikuwa kanzu fupi (chitōn). Tofauti miongoni mwa mavazi haya zaweza kuonekana katika Mathayo 5:40 na Luka 6:29. Dorikasi alishona mavazi yote haya (kama vile Mdo. 9:39). Wayahudi wa karne ya kwanza inaonekana walivaa nguo nyingine ya ndani iliyoitwa nguo ya kiunoni. Yesu hakuvuliwa mavazi yote kabisa. Aya ya mwisho ya Yohana 19:23 ni hoja nyingine ya uhariri kutoka kwa Mtu aliyeishi na Yesu. ◙“Basi kanzu ile haikushonwa, ilikuwa imefumwa yote pia tangu juu” Hii yawezakuwa na umuhimu wa kitheolijia. Kazi kama hii haikuwa ya kawaida na yawezekana ilikuwa ya aghali. Inaonekana nje ya tabia ya Yesu kuwa na nguo ambayo ni aghali tofauti na kawaida. Kutoka Josephus (Antiq. 3.7.4), tunajua kwamba kuhani mkuu alivaa joho kama hili, kama desturi ya walimu wa sheria za kiyahudi inayotaja kama Musa alivyofanya. Je, hii ingeweza kuwa rejeo kwa Yesu kama

1. Kuhani mkuu (kama vile Waebrania) 2. Mtoa sheria mpya

Maana mbili kila mara zawezekana katika injili ya Yohana, lakini wafasiri lazima wawe na juhudi kutofanya maelezo yote na matukio kuwa na maana mbili! 19:24“Ili litimie andiko” Zaburi 22 ilitengeneza msingi wa Agano la Kale kwenye kusulubishwa.

1. Zaburi 22:1-2 -- Mathayo 27:46; Marko 15:34 2. Zaburi 22:7-8 -- Mathayo 27:39,43; Marko 15:29; Luka 23:35 3. Zaburi 22:15 -- Mathayo 27:48; Marko 15:36; Luka 23:36; Yohana 19:28,29 4. Zaburi 22:16 --Mathayo 27:35; Marko 15:24; Yohana 20:25 5. Zaburi 22:18 -- Mathayo 27:35; Marko 15:24; Luka 23:34; John 19:24 6. Zaburi 22:27-28 -- Mathayo 27:54; Marko 15:39; Luka 23:47; (Yohana 20:31; Mathayo 28:18-20; Luka

24:46-47; Mdo. 1:8)

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 19:25b-27 25bNa penye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mamaye, na umbu la mamaye, Mariamu wa Klopa, na Mariamu Magdalene. 26 Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, Mama, tazama, mwanao. 27 Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake

19:25 “Na penye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mamaye, na umbu la mamaye, Mariamu wa Klopa, na Mariamu Magdalene”Kuna mjadala mkubwa kuhusu kama kuna majina manne hapa au majina matatu.Inawezekana kwamba kuna majina manne kwa sababu hakutakuwa na wadada wawili waitwao Mariamu. Dada wa Mariamu, Salome, ametajwa katika Marko 15:40 na16:1. Kama hii ni kweli, basi ingemaanisha Yakobo, Yohana, na Yesu walikuwa binamu. Desturi ya karne ya pili (Hegesippus) yasema kwamba Klopa alikuwa kaka yake Yusufu. Mariamu Magdalene mmoja kati ya wale ambao Yesu alifukuza pepo saba, na wa kwanza ambaye alichagua kumtokea baada ya ufufuo wake (kama vile Yohana20:1-2, 11-18; Marko 16:1; Luka 24:1-10).

MADA MAALUMU: WANAWAKE WALIOMFUATA YESU

A. Tamko la kwanza la wafuasi wa Yesu kwa wanawake waliomsaidia na kikundi cha mitume ni Luka 8:13. 1. Maria, aliyeitwa Magdalena (Luka 8:2)

Page 316: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

300

a. Mt. 27:56,61; 28:1 b. Marko 15:40,47; 16:1,9 c. Luka 8:2; 24:10 d. Yohana 19:25; 20:1,11,16,18

2. Yohana, mke wa Kuza (mtumishi wa Herode, Luka 8:3) ameorodheshwa pia katika Luka 24:10 3. Suzana (Luka 8:3) 4. "Pamoja na wegine wengi waliokuwa wanamhudumia kwa mali zao" (Luka 8:3)

B. Kundi la wanawake wanatajwa kama waliokuwepo wakati akisulubishwa 1. Orodha ya Mathayo

a. Maria Magdalena (Mt. 27:56) b. Mariamu mamaye Yakobo na Yusufu (Mt. 27:56) c. Mama yao wana wa Zebedayo (Mt. 27:56)

2. Orodha ya Marko a. Mariamu Magdalena (Marko 15:40) b. Mariamu mamaye Yakobo mdogo wa Yose (Marko 15:40) c. Salome (Marko 15:40)

3. Luka anasema pekee wale "wanawake walioambatana naye kutoka Galilaya" (23:49) 4. Orodha ya Yohana

a. Mariamu mama yake Yesu (Yohana 19:25) b. Dada ya mama yake (Yohana 19:25) c. Mariamu wa Klopa (KJ, Cleophas, hii iingeweza kumaanisha mke wa Klopa au binti wa Klopa,

Yohana 19:25) d. Mariamu Magdalena (Yohana 19:25)

C. Kundi la wanawake linatajwa wakiangalia mahali alipozikwa Yesu 1. Orodha ya Mathayo

a. Mariamu Magdalena (Mt. 27:61) b. Mariamu mwingine (Mt. 27:61)

2. Orodha ya Marko a. Mariam Magdalena (Marko 15:47) b. Mariamu mama wa Yesu (Marko 15:47)

3. Luka anasema tu, "wanawake waliokuwa wamekuja pamoja naye kutoka Galilaya " (Luka 23:55) 4. Yohana hana maelezo ya wanawake wliokuwa wakiliona kaburi

D. Kundi la wanawake waliokuja kwenye kaburi mapema jumapili asubuhi 1. Orodha ya Mathayo

a. Mariamu Magdalena (28:1) b. Mariamu mwingine (28:1)

2. Orodha ya Marko a. Mariamu Magdalena (16:1) b. Mariamu mamaye Yakobo (16:1) c. Salome (16:1)

3. Orodha ya Luka "walikuja kwenye kaburi" (24:1-5,24) a. Mariamu Magdalena (24:10) b. Yoana (24:10) c. Mariamu mamaye Yakobo (24:10)

4. Yohana anaorodhesha Mariamu Magdalena peke yake (20:1,11) E. Wanawake wanatajwa kwamba waliokuwepo kule gorofani (Matendo 1:14)

1. "wanawake" (Matendo 1:14) 2. Maria mamaye Yesu (Matendo 1:14)

F. Uhusiano kamili kati ya wanawake tofauti kwenye orodha hizi hauna hakika Mariamu Magdalenabila

Page 317: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

301

shaka ana wajibu mkubwa. Andiko zuri kuhusu "wanawake" kwenye maisha na huduma ya Yesu linapatikana ndani ya Dictionary of Jesus and the Gospels lilitolewa na IVP, kur. 880-886.

19:26 “yule mwanafunzi aliyempenda” Kwa kuwa Yohana hatamkwi kwa jina kwenye injili, wengi wanachukulia kwamba hii ilikuwa njia yake ya kujitambulisha (kama vile Yohana 13:23; 19:26; 21:7,20). Katika kila moja ya hizi yeye kutumia neno agapaō, lakini katika Yohana 20:2 anatumia aya ile ile lakini ikiwa pamoja na phileō. Neno hili linafanana katika Yohana; linganisha Yohana 3:35, agapaōna 5:20, phileō, ambapo zote mbili zinarejea upendo wa Baba kwa Mwana. 19:27 “Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake”Hii si lazima imaanishe kwamba Yohana pale pale alimchukua Mariamu mpaka nyumbani kwake, ingawa hii ingeweza kuonyeshwa kwa ukweli kwamba yeye hajaorodheshwa pamoja na wanawake wengine katika Mathayo 27:56 na Marko 15:40. Mila inasema kwamba Yohana alimtunza Mariamu hadi kifo chake kisha akaenda Asia ndogo (hasa Efeso) ambapo alikuwa na huduma ndefu na yenye mafanikio.Ni katika kuwaasa wazee wa kule Efeso kwamba Yohana kama mzee, aliandika kumbukumbu zake za maisha ya Yesu ( yaani, Injili ya Yohana).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 19:28-30 28 Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu. 29 Kulikuwako huko chombo kimejaa siki; basi wakatia sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa hisopo, wakampelekea kinywani. 30 Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema, Imekwisha. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake.

19:28 “Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu” Katika uunganishaji wa maneno inaleta utata kutokana na kuwa na maana nyingi kama andiko lililotajwa linahusika na aya “Naona kiu” au “mambo yote yamekwisha kumalizika”. Inachukuliwa katika njia ya kimapokeo, basi “Naona kiu” ni rejeo la Zab. 69:21 19:29 “Kulikuwako huko chombo kimejaa siki” Hii ilikuwa divai ya thamani ya chini, divai iliyochacha. Ingeweza kuwa kwa ajili ya maaskari na kwa waliosulubiwa. Walipewa kiasi kidogo cha kimiminika ili kufanya kusulubiwa kudumu kwa muda mrefu zaidi. ◙ “divai iliyochacha” Hii ni kwa uhalisia “siki.” Hiki kilikuwa kinywaji cha watu maskini. Tambua kwamba Yesu hakuchukua ile divai iliyochanganywa na ulevi ambayo wanawake wa Yerusalemu walimpa (kama vile. Marko 15:23; Mathayo 27:34). Inawezekana sababu iliyomfanya akubali kile kinywaji ilikuwa kutimiza Zab. 22:15. Alikuwa amekaukiwa sana na joto kiasi cha kutoweza zungumza na alikuwa na jambo moja la kusema. ◙ “juu ya ufito wa hisopo” Badhi wanaona hili kama ishara ya tumizi la mmea maalum ambao ulitumika katika huduma ya Pasaka (kama vile Kutoka 12:22). Wengine wanaamini kwamba kumekuwepo na ufisadi kwenye maneno ya zamani yaliofanyika kwenye neno na kwamba katika asili yake lilimaanisha “mkuki” au “fimbo” (kama vile. NEB lakini REB inarudia kwenye hisopo). Mathayo 27:48 na Marko 15:36 zina "mwanzi." Sababu inayowafanya wengi, waone badiliko la maandishi hapa ni kwa kuwa mmea wa hisopo haukuwa na shina refu (ni futi 2 hadi 4),lakini ni lazima ikumbukwe kwamba misalaba haikuwa imeinuliwa kwenda juu kiasi hicho.Picha zetu za kimapokeo za msalaba mrefu zaweza kuwa ni kuelewa vibaya kwetu kwa Yohana 3:14. Miguu ya Yesu ingeweza kuwa ndani ya futi mbili hadi nne kutoka ardhini 19:30"Imekwisha!"Hii ni kauli timilifu tendewa elekezi. Kutoka kwenye vidokezo vya injili tulijifunza kwamba alipolia kwa sauti katika neno hili(kama vile Marko 15:37; Luka 23:46; Mathayo 27:50). Hii inarejea kazi ya ukomboaji uliuomalizika. Muundo huu wa neno (telos) katika mafunjo ya kimisri (Moulton na Milligan) ulikuwa lahaja ya kibiashara kwa neno“imelipia yote”

Page 318: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

302

◙ “Akainama kichwa, akaisalimu roho yake" Huu msemo “Akainama kichwa” ilikuwa nahau ya “kwenda kulala.” Kifo cha Yesu klikuwa muda wa utulivu kwake. Ufahamu ni kwambva katika kifo mtazamo wa kiroho wa mtu unatengwa kutoka kwenye mwili. Hii inaonekana kudai/hitaji hali ya kutoka kwenye mwili kwa wanaoamini kati ya kifo na siku ya ufufuo (kama vile 2 Wakoritho 5; 1 Thes. 4:13-18, tazama William Hendriksen, The Bible On the Life Hereafter). Mlinganisho wa injili katika Marko 15:37 na Luka 23:46 zina “alitoa pumzi yake ya mwisho.” Neno la kiebrania kwa “roho” na “pumua” yako sawa sawa. Punzi yake ya mwisho iliangaliwa kama roho yake ikiuacha mwili (kama vile Mwa. 2:7).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 19;31-37 31 Basi Wayahudi, kwa sababu ni Maandalio, miili isikae juu ya misalaba siku ya sabato, (maana sabato ile ilikuwa siku kubwa), walimwomba Pilato miguu yao ivunjwe, wakaondolewe. 32 Basi askari wakaenda, wakamvunja miguu wa kwanza, na wa pili, aliyesulibiwa pamoja naye. 33 Lakini walipomjia Yesu na kuona ya kuwa amekwisha kufa, hawakumvunja miguu; 34 lakini askari mmojawapo alimchoma ubavu kwa mkuki; na mara ikatoka damu na maji. 35 Naye aliyeona ameshuhudia, na ushuhuda wake ni kweli; naye anajua ya kuwa anasema kweli ili ninyi nanyi mpate kusadiki. 36 Kwa maana hayo yalitukia ili andiko litimie, Hapana mfupa wake utakaovunjwa. 37 Na tena andiko lingine lanena, Watamtazama yeye waliyemchoma.

19:31 “miili isikae juu ya misalaba siku ya sabato” Wayahudi walikuwa macho sana kuhusu miili iliyokufa katika kuinajisi nchi kufuatana na kanuni na mapokeo ya kidini (kama vile Kumb. 21:23), hasa siku ya sabato kuu takatifu ya Pasaka. ◙ “(maana sabato ile ilikuwa siku kubwa)” Hii imekuwa ikitafsiriwa katika njia mbili.

1. chakula cha Pasaka na Sabato viliingiliana kwa mwaka huo wenyewe(Wayahudi walifuata kalenda ya mwezi) (siku 287)

2. Sherehe ya mikate iliyotiwa chachu iliingiliana na sabato mwaka huu. Sherehe ya Pasaka na mikate isiyotiwa chachu (kama vile Kutoka 12) ilikwisha kuwa sherehe ya siku nane. ◙ “miguu yao ivunjwe, wakaondolewe” kusulubishwa kwa kawaida kulisababisha kifo kutokana na kuishiwa/kukosa hewa ndani ya mapafu.Kuvunja miguu kulisababisha umauti kwa haraka kwa vile mtu asingeweza kusukuma juu miguu yake apate kupumua. 19:33 "walipomjia Yesu na kuona ya kuwa amekwisha kufa, hawakumvunja miguu" Hii pia ingeweza kuwa inatimiza unabii unaorudi nyuma hadi Kutoka. 12:46; Hes. 9:12 na Zab. 34:20. 19:34 "askari mmojawapo alimchoma ubavu kwa mkuki; na mara ikatoka damu na maji" Huu ni ushuhuda wa macho wa maelezo ya kitabibu akionesha kwamba kweli alikuwa amekufa na hivyo kuthibitisha ukweli wa ubinadamu wa Yesu masihi. Injili ya Yohana pamoja na 1 Yohana ziliandikwa katika siku za kukua kwa mafunuo yaliyothibitisha Uungu wa Yesu na lakini yalikana ubinadamu Wake. 19:35 Haya ni maoni ya Yohana ambaye alikuwa shahidi aliyeona kwa macho matukio yote, (1) mashtaka ya usiku; (2) mashtaka ya Warumi na; (3) kusulubishwa. Maoni kuhusu kifo cha Yesu ni sawa na 20:30-31, inayoonesha kusudi la kiinjili la Injili (kama vile. Yohana 21:24). Tazama MADA MAALUM: MASHUHUDA WA YESU katika Yohana 1:8 Upo utofauti wa maandishi ya Kiyunani katika kitenzi cha kishazi cha mwisho. Maandiko mengine yana kitenzi cha njeo ya wakati uliopo na nyingine njeo ya wakati uliopita usio timilifu. Kama ilikuwa kiasili cha wakati uliopita usio timilifu inawaelekea wasioamini, kama inavyofanya Yohana 20:30-31. Hata hivyo ikiwa ni wakati uliopo unaoelekea imani inayoendelea na kuleta maendeleo. Injili ya Yohana yaonekana kuelekezwa kwa makundi yote mawili.

◙ "kweli. . . kweli" Tazama Mada Maalum juu ya Kweli katika Yohana 6:55 na 17:3 .

Page 319: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

303

19:36 Hii inaweza kuwa kuzungumzia mwana kondoo wa Pasaka kutoka kitabu cha kutoka.12:46; Hes. 9:12; au Zab. 34:20. Inategemea ni aya ipi inayoorejelewa: (1) kuchomwa ama (2) kuvunjika. Yesu mwenyewe alilionesha kanisa la kwanza maandiko haya wakati wa siku zile 40 alizokaa duniani baada ya kufufuka kwake (kama vile. Luka 24:27; Matendo 1:2-3). Mahubiri ya kanisa la kwanza yanaaksi nabii hizi za Agano la Kale zilizotimia ambazo Yesu aliwaonesha. 19:37 Hii imenukuliwa kutoka Zek. 12:10 ambayo ni moja ya ahadi kubwa kwamba

1. Siku moja Israeli itamgeukia Yesu, Masihi, katika imani (kama vile. Ufu. 1:7) 2. Wayahudi wengi waliokwisha amini tayari walikuwa pale wakiomboleza kifo cha Yesu 3. Hii inarejerea Yule askari wa Kirumi (kama vile Mt. 27:54) akiwakilisha mataifa ya watu wa Mataifa

(kama vile Yohana 12:32) Inapendeza kwamba hii nukuu ni dhahiri inatoka kwenye maandiko ya Waebrania wa (Masoreti), sio kwenye maaandiko ya kale ya Kiyunani ambayo kwa kawaida yanafanyiwa nukuu na maandishi ya Injili. Maandiko ya kale ya Kiyunani yana "dhihakiwa" lakini maandiko ya Masoreti yana "chomwa."

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 19:38-42 38 Hata baada ya hayo Yusufu wa Arimathaya, naye ni mwanafunzi wa Yesu, (lakini kwa siri, kwa hofu ya Wayahudi), alimwomba Pilato ruhusa ili auondoe mwili wake Yesu. Na Pilato akampa ruhusa. Basi akaenda, akauondoa mwili wake. 39 Akaenda Nikodemo naye, (yule aliyemwendea usiku hapo kwanza), akaleta machanganyiko ya manemane na uudi, yapata ratli mia. 40 Basi wakautwaa mwili wake Yesu, wakaufunga sanda ya kitani pamoja na yale manukato, kama ilivyo desturi ya Wayahudi katika kuzika. 41 Na pale pale aliposulibiwa palikuwa na bustani; na ndani ya bustani mna kaburi jipya, ambalo hajatiwa bado mtu ye yote ndani yake. 42 Humo basi, kwa sababu ya Maandalio ya Wayahudi, wakamweka Yesu; maana lile kaburi lilikuwa karibu.

19:38-39 "Yusufu. . . Nikodemo" Watu hawa wawili matajiri wajumbe maarufu wa baraza la Mafarisayo walikuwa wanafunzi wa Yesu Kristo wa siri ambao walijidhihilisha hadharani katika wakati wa mwisho na wa hatari sana. 19:39 "akaleta machanganyiko ya manemane na uudi, yapata ratli mia" Haya yalikuwa manukato yaliyo tumika katika mazishi ya Kiyahudi katika karne ya kwanza. Kiasi chenyewe ni kama matumizi yaliyoptiliza. Wengi wanaona jambo hili kama ishara ya Yesu akiwa anazikwa kama mfalme (kama vile 2 Nya. 16:14). Tazama Mada Maalum: Kutiwa mafuta katika Biblia katika Yohana 11:2 Neno la Kiyunani kwa "mchanganyiko" (migma), lililopatikana katika MSS P66, אi2, A, D, L na sehemu kubwa ya mababa wa kanisa na tafsiri nyingi, imebadilishwa kwa ajabu kuwa "enye kuwekwa pamoja" (eligma) katika MSS .B, W, na baadhi ya nakala za Koptiki. UBS4 inatoa "mchanganyiko” alama "B" (karibu na uhakika) ,*א

MADA MAALUMU: MANUKATO YA MAZISHI

A. Mane mane, gundi yenye harufu nzuri kutoka kwenye miti ya Uarabuni (BDB 600, KB 629; angalia UBS, Fauna na Flora of the Bible, kur. 147-148) 1. Kiungo kimetajwa mara kumi na mbili katika Agano la Kale, hasa katika fasihi ya hekima (kama vile.

Zab. 45:8; 1:13; 4:14; 5:1,5) 2. Ilikuwa mojawapo ya zawadi zilizoletwa na Mamajusi kwa mtoto yesu (kama vile Mt. 2:11) 3. Kuashiria kwake kunachoma

a. Ilitumika kama "mafuta matakatifu ya kupaka" (Kut. 30:23-25) b. Ilitumika kama zawadi kwa mfalme (Mt. 2:11) c. Ilitumika kumpaka yesu kwenye maziko yake (kama vile Yohana 19:39 kama ishara katika Yohana

11:2). Hii ilikuwa kwa mujibu wa desturi za Wayahudi zilivyoelezwa katika Buku la kanuni za Kiyahudi (Talmud) (yaani, Berakhoth 53a).

d. Ilitumika na wanawake Yerusalemu katika kinywaji kilichotolewa kwa watu waliokuwa

Page 320: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

304

wameteswa wakielekea kwenda kusulubishwa (kama vile. Marko 15:23) kupoza mateso B. Aloes, aina fulani ya mbao yenye harufu nzuri (BDB 14 III, KB 19)

1. Imeunganishwa na manukato yenye harufu nzuri (kama vile Hes. 24:6; Zab. 45:8; Mith. 7:17; wimbo ulio bora 4:14; angalia UBS, Fauna and Flora of the Bible, pp. 90-91)

2. Ilitumika, ikichanganywa, na marhamu, na Wamisri kama sehemu ya kuhifadhi mwili wa marehemu.

3. Nicodemo alileta kiasi kikubwa cha hiyo kwenye maziko ya Yesu na kumpaka (kama vile. Yohana 19:39). Hii ilikuwa kwa mujibu wa desturiza Kiyahudi kama ilivyoelezwa katika buku la kanuni za Kiyahudi-Talmud (yaani, Betsah 6a). Tazama Mada Maalumu: Kanuni za Mazishi

19:40 "Basi wakautwaa mwili wake Yesu, wakaufunga sanda ya kitani pamoja na yale manukato" Manukato yalikuwa kwa makusudi mawili: (1) kuua harufu na (2) kushikilia vitu vya kufunikia ule mwili uwe vizuri wakati wa mazishi. 19:41 "Na pale pale aliposulibiwa palikuwa na bustani" Ni muhimu kwamba tunaelewa Yusufu na Nikodemu walifanya kazi kwa haraka kiasi gani. Yesu alikufa mnamo saa tisa alasiri 9:00 alasili na ilibidi awe kaburini inapofika saa 12:00 jioni, muda ambao ulikuwa mwanzo wa sabato ya Pasaka ya Wayahudi.

◙ "kaburi jipya ambalo hajatiwa bado mtu ye yote ndani yake" Hii ni kauli timilifu tendewa endelevu yenye mafumbo tunajifunza kutoka. 27:60 kwamba hili lilikuwa kaburi lake Yusufu mwenyewe. Huu ni utimilisho wa Isaya 53:9 iliyonukuliwa katika Mathayo 27:57.

MASWALI YA MJADALA

Huu ni mwongozo wa fasiri, ina maanisha kwamba unawajibika kwa tafsiri zako mwenyewe za Biblia. Kila mmoja wetu lazima atembee katika mwanga tulio nao. Wewe, Biblia, na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Hutakiwi uvitelekeze vitu hivi kwa mfasiri. Maswali ya mjadala huu yanatolewa kukusaidia kufikiri juu ya mambo makubwa ya sehemu za kitabu hiki. Yanalenga kukuamsha kimawazo na sio kutoa maana.

1. Kwanini maaskari walimchapa na na kumdhihaki Yesu? 2. Kule kurudia rudia kujaribu kumfungua Yesu kulikofanywa na Pilato kuna umuhimu gani? 3. Kwanini maelezo tamko la kuhani wa Wayahudi katika Yohana 19:15 ni kwa kushangaza sana? 4. Kwanini maelezo ya kusulubiwa yanatofautiana toka injili moja kwenda injili ingine? 5. Kumbukumbu 21:23 inahusianaje na kusulubiwa kwa Yesu?

Page 321: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

305

YOHANA 20

MIGAWANYO YA AYA YA TAFSIRI ZA KISASA

UBS4 NKJV NRSV TEV NJB Kufufuka kwa Kaburi tupu Ufufuo Kaburi tupu Kaburi tupu Yesu 20:1-10 20:1-10 20:1-10 20:1-10 20:1-2 20:3-10 Kuonekana kwa Mariamu Magdalena Yesu amtokea Kuonekana kwa Yesu kwa anamwona kristo Mariamu Magdalena Mariamu Magdalena Mariamu Magdalena bwana aliyefufuka 20:11-18 20:11-18 20:11-18 20:11-13a 20:11-18 20:13b 20:14-15a 20:15b 20:16a 20:16b 20:17 20:18 Kuonekana kwa yesu Mitume wanaagizwa Yesu anaonekana kwa Kuonekana kwa kwa wanafunzi wanafunzi wake wanafunzi 20:19-23 20:19-23 20:19-23 20:19-23 20:19-23 Yesu na Tomaso Kuona na kuamini Yesu na Tomaso 20:24-29 20:24-29 20:24-29 20:24-25a 20:24-29 20:25b 20:26-27 20:28 20:18 Kusudi la Kitabu ili uweze Kuamini Kusudi la Kitabu Hitimisho la Kwanza 20:30-31 20:30-31 20:30-31 20:30-31 20:30-31

MZUNGUKO WA TATU WA USOMAJI KUFUATILIA KUSUDIO LA ASILI LA MWANDISHI KATIKA NGAZI YA AYA Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwatafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Aya ya kwanza 2. Aya ya pili 3. Aya ya tatu 4. N.k

Page 322: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

306

UTAMBUZI WA MUKTADHA WA MISTARI YA 1-29

A. Kila ahadi ambayo Yesu aliitoa kwa wanafunzi katika Yohana 14-17 ilitimizwa jioni ya Jumapili ya kwanza

ya kufufuka. Tazama Melezo katika Yohana 16:20

B. Maelezo ya injili yanatofautiana kwenye mzunguko wa ufufuo kwa sababu

1. ni mambo yaliyoshuhudiwa kwa macho

2. miaka ilipita

3. kila mmoja aiandikia kikundi kilicholengwa alisisitiza mambo tofauti (kama vile Mathayo 28; Marko

16; Luka 24)

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 20:1-10 1 Hata siku ya kwanza ya Juma Mariamu Magdalene alikwenda kaburini alfajiri, kungali giza bado; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini. 2 Basi akaenda mbio, akafika kwa Simoni Petro na kwa yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda, akawaambia, Wamemwondoa Bwana kaburini, wala hatujui walikomweka. 3 Basi Petro akatoka, na yule mwanafunzi mwingine, wakashika njia kwenda kaburini. 4 Wakaenda mbio wote wawili; na yule mwanafunzi mwingine akaenda mbio upesi kuliko Petro, akawa wa kwanza kufika kaburini. 5 Akainama na kuchungulia, akaona vitambaa vya sanda vimelala; lakini hakuingia. 6 Basi akaja na Simoni Petro, akaingia ndani ya kaburi; akavitazama vitambaa vilivyolala, 7 na ile leso iliyokuwako kichwani pake; haikulala pamoja na vitambaa, bali imezongwa-zongwa mbali mahali pa peke yake. 8 Basi ndipo alipoingia naye yule mwanafunzi mwingine aliyekuwa wa kwanza wa kufika kaburini, akaona na kuamini. 9 Kwa maana hawajalifahamu bado andiko, ya kwamba imempasa kufufuka. 10 Basi wale wanafunzi wakaenda zao tena nyumbani kwao.

20:1 “Hata siku ya kwanza ya juma” Hii ilikuwa jumapili, siku ya kwanza ya kufanya kazi kufuata sabato ya juu ya wiki ya Pasaka, wakati matunda ya kwanza yalitolewa Hekaluni. Yesu alikuwa tunda la kwanza la waliokufa (kama vile 1 Kor. 15:23). Kuonekana kwa Yesu kwa jumapili tatu mfululizo usiku ilitengeneza hatua kwa wanaoamini kuabudu siku ya jumapili kama vile Yohana 20:19, 26; Luka 24:36 na kuendelea; Matendo 20:7; 1 Kor. 16:2).

◙ “Mariamu Magdalena” Huyu alikuwa mmoja wa wanawake waliomfuata Yesu na mitume. Katika Galilaya Yesu alimkomboa kutoka kwa mapepo kadhaa (kama vile Marko 16:9 na Luka 8:2). Alikuwepo kwenye kusulubiwa. Tazama maelezo katika Yohana 19:25. Ingawa injili ya Yohana haielezi kusudi la ujio wa Mariamu, Marko 16:1 na Luka 23:56 inaeleza kwamba baadhi ya wanawake (kama vile Yohana 20:2) walikuja mapema asubuhi kuupaka mwili wa Yesu manukato. Inaonekana hawakujua habari za Yusufu na Nikodemo kumpaka manukato ingawa ilihitajika kuongezewa.

◙ “kungali giza bado”Inaonekana yeye na wengine walikuwa wameondoka nyumbani kungali giza, lakini wakati walipofika kulikuwa kumepambazuka (kama vile Mt. 28:1; Marko 16:2).

◙ “lile jiwe limeondolewa kaburini” Katika lugha halisi hii ni “kuondolewa” (kauli tendewa endelevu ya wakati timilifu) kutoka pale lilipokuwa (kama vile Mt. 28:2). Kumbuka jiwe lilikuwa limeondolewa ili kuruhusu shahidi wanaoona kwa macho waingie kaburini, sio kumtoa Yesu nje. Mwili wake mpya wa ufufuo haukuwa na vizuizi vya kimaumbile vya mwili wake wa kidunia (yaani, Yohana 20:19,26).

20:2 “Basi akaenda mbio” Inavyoonekana aliacha kaburi lililotupu mapema kuwaeleza wanafunzi kuhusu Yesu kutokuwa pale (kama vile Mt. 28:5).

Page 323: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

307

◙ “mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda” Neno hili la Kiyunani kwa upendo ni phileō ambalo lina mwelekeo wa “upendo wa kindugu” lakini katika Kiyunani cha aina ya Koine (300 K.K.-300 B.K.) lilikuwa linatumika kwa maana ile ile ya agapaō. Mwanafunzi aliyetajwa anaonekana kuwa Yohana, mwandishi wa injili (kama vile Yohana 20:4-8 na 13:23). Hapa anaunganishwa na Petro.

◙ “Wamemwondoa Bwana kaburini” Hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati uliopita usiotimilifu (yaani, kitendo kilichotimilika). Yesu alikuwa ameisha ondoka. Kwenye fikra ya Mariamu, “wao” inarejelea viongozi wa Kiyahudi. Inavyoonekana mitume pamoja na wanafuzi waliokuwa pale ghorofani walishangazwa na ufufuo

◙ “sisi” Hii inamjumuisha Mariamu wa Magdalena, Mariamu Mama yake Yakobo, Salome, Yohana pamoja na wanawake wengine (kamaa vile Mt. 28:1; Marko 16:1; Luka 24:10).

20:4 “na yule mwanafunzi mwingine akaenda mbio upesi kuliko Petro, akawa wa kwanza kufika kaburini” Yohana pengine alikuwa mwenye umri mdogo kuliko wote miongoni mwa mitume (yaani, mapokeo).

20:5 “Akainama” Makaburi ya kipindi hiki yalikuwa na milango mifupi kiasi cha futi 3 hadi 4 kwenda juu. Mtu alilazimika kuinama (kama vile Yohana 20:11) ili kuingia ndani ya pango/ shimoni.

◙ “kuchungulia” Hii kwa maana halisi “kubinya macho ili kuona.” Hii ilikuwa kwa sababu ya kuweka mlinganisho kati ya nuru ya asubuhi na kaburi lililokuwa limetanda giza.

◙ “vitambaa vya sanda vimelala” Mahali na jinsi vitambaa vilivyokuwa haikuelezwa katika maandiko ya kiyunani. Kama mwili ungeibiwa, vitambaa pia vingechukuliwa kwa sababu vilitumika kama gundi!

20:6 “Simoni Petro” Simoni (Kefa) lilikuywa jina lake la kiebrania (kiaramu) wakati Petro (Petros) lilikuwa jina lake la Kiyunani alilopewa na Yesu. Kwa Kiyunani lilimaanisha “jiwe lililoondolewa kutoka mahali fulani au kundi fulani ama jiwe fulani lililofanywa mviringo kutokana na maji au hali ya hewa” (kama vile Mt. 16:18). Katika kiyunani hakuna tofauti kati ya Petros na Petra.

20:7 “leso” Uso ulikuwa umefungwa na nguo zilizotengwa (kama vile Yohana 11:44). Inawezekana kwamba kitambaa hiki kilitumika (1) kufunika uso (2) kufunika uso kwa kuzungusha kichwani (kama vile NJB); au (3) kufunga taya bila kukaza(kama vile TEV).

◙ “bali imezongwa-zongwa mbali mahali pa peke yake” Hii ni kauli nyingine tendewa endelevu ya wakati timilifu ambayo ina maana kwamba umakini mkubwa ulihitajika kwa mtu kuikunja. Inavyoonekana hii ndiyo ilikamata umakini wa Yohana na kuvuta imani (Yohana 20:8).

20:8 “akaona na kuamini” Yohana aliona ushahidi uliodhahiri na akaamini kuwa Yesu alikuwa hai! Kuamini katika ufufuo inakua hoja muhimu sana ya kitheolojia.

1. Warumi 10:9-13 2. Wakorintho 1. 15

1 Wakorintho 15:12-19 ni muhtasari mzuri wa yale yaliyotokea ikiwa Yesu kweli hakuwa hajafufuliwa! Ufufuo ulikuja kuwa kweli kuu ya mahubiri ya kwanza ya mitume katika Matendo huitwa kerygma tazama Mada Maalum katika Yohana 5:39 20:9 “hawajalifahamu bado andiko” Hii pia ni hoja ya kihariri ya mwandishi. Inaweza kurejea Zaburi 16:10, ambayo Petro anainukuu siku ya Pentekoste katika Matendo 2:27. Hata hivyo, ingeweza kurejea Isaya 53:10-12 au Hosea 6:2. Baraza la Mafarisayo waliuelewa utabiri wa Yesu kuhusu kufufuka kwake (kama vile Mt. 27:62-66), ambapo wanafunzi hawakuelewa. Ni Jambo gani la kinyume hili!

Page 324: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

308

Aya hii inaweza kuwa imetumika kitheolojia kuongeza nguvu ya ukweli kwamba Roho alikuwa hajawajilia wanafunzi kwa utimilifu. Roho, akisha tolewa, angesaidia wanaoamini kuyaelewa maneno na matendo ya Yesu (kama vile Yohana 2:22; 14:26).

20:10 Hii inaweza kumaanisha (1) walirudi Galilaya (kama vile Mt. 26:32; 28:7, 10, 16; Yohana 21 anawakuta wakiwa wanavua samaki kwenye Bahari ya Galilaya) au (2) walikwenda nyumbani kwao Jerusalemu. Kwa sababu matukio baada ya kufufuka yalikuwa kule ghorofani, #2 waweza kuwa ndio wenyewe.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 20:11-18 11 Lakini Mariamu alikuwa akisimama karibu na kaburi, nje yake, analia. Basi akilia hivi, aliinama na kuchungulia ndani ya kaburi. 12 Akaona malaika wawili, wenye mavazi meupe, wameketi, mmoja kichwani na mmoja miguuni, hapo ulipolazwa mwili wake Yesu. 13 Nao wakamwambia, Mama, unalilia nini? Akawaambia, Kwa sababu wamemwondoa Bwana wangu, wala mimi sijui walikomweka. 14 Naye akiisha kusema hayo, akageuka nyuma, akamwona Yesu amesimama, asijue ya kuwa ni Yesu. 15 Yesu akamwambia, Mama, unalilia nini? Unamtafuta nani? Naye, huku akidhania ya kuwa ni mtunza bustani, akamwambia, Bwana, ikiwa umemchukua wewe, uniambie ulipomweka, nami nitamwondoa. 16 Yesu akamwambia, Mariamu. Yeye akageuka, akamwambia kwa Kiebrania, Raboni! (Yaani, Mwalimu wangu). 17 Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu. 18 Mariamu Magdalene akaenda, akawapasha wanafunzi habari ya kwamba, Nimemwona Bwana, na ya kwamba amemwambia hayo.

20:11 “akilia” Hii kwa maana halisi ni “omboleza” (kama vile Yohana 11:31). Ni kauli ya wakati usiotimilifu, inayozungumzia kitendo kinachoendelea katika wakati uliopita, taratibu za mazishi ya mashariki kitabia ni ya kihisia sana.

20:12 “malaika wawili” Yohana na Luka (24:23) wanakubaliana kwamba kulikuwepo malaika wawili. Mathayo, ambaye kawaida anahusisha vitu viwili kwa kila kitu (kama vile Yohana 8:28; 9:27; 20:30), ana malaika mmoja tu! Huu ni mfano mmoja wenye tofauti zisizo elezeka miongoni mwa injili. Injili ni tarifa zilizoshuhudiwa kwa macho zinazochagua, rekebisha, na kuunganisha maneno na kazi za Yesu kwa makusudi yao wenywe ya (kutia msukumo) kitheolojia na kundi lililolengwa. Wasomaji wa kisasa mara nyingi huuliza maswali kama (1) ni injili gani miongoni mwa injili mabayo kihistoria ni angalifu/haina makosa au (2) wanatafuta maelezo ya ziadi ya kihistoria kuhusu tukio au fundisho kuliko lilivyoandikwa a mwandishi mmoja wa injili aliyevuviwa. Wanafasihi lazima kwanza watafute kusudi la mwandishi wa kwanza kama ilivyoelezewa kwenye injili binafsi. Hatuhitaji maelezo zaidi ya kihistoria ili kuelewa injili. ◙ “mavazi meupe” Ulimwengu wa Roho au viumbe wa kiroho vinaelezewa kama vilivyovaa weupe.

1. Mavazi ya Yesu pale Yesu alipogeuka sura -- Mt. 17:2; Marko 9:3; Luka 9:29 2. Malaika pale kaburini -- Mt. 28:3; Marko 16:5; Luka 24:4; Yohana 20:12 3. malaika pale Yesu alipopaa -- Matendo 1:10 4. Malaika wakiwa na Kristo aliyetukuzwa -- Ufunuo. 3:4-5,18 5. Wazee (malaika) wakikizunguka kiti cha enzi cha Mungu -- Ufunuo. 4:4 6. Mashahidi chini ya kiti cha enzi cha Mungu -- Ufunuo 6:11 7. Wote waliokombolewa -- Ufunuo. 7:9,13-14 (kama vile Dan. 12:10) 8. Majeshi (ya malaika) mbinguni -- Ufunuo 19:14 9. Picha ya msamaha ya agano la kale -- Zab. 51:7; Isaya 1:18 (ikionyesha ishara ya utakaso wa Mungu,

kama vile Dan. 7:9)

20:14 “asijue ya kuwa ni Yesu” Mariamu Magdalena hakumtambua Yesu. Inawezakana sababu ya jambo hili ni 1. kulikuwa na machozi machoni pake 2. alikuwa anaangalia kutoka giza kuja nuruni

Page 325: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

309

3. Mwonekano wa Yesu ulikua umebadilika kwa kiasi (kama vile Mt. 28:17 na Luka 24:16,37)

20:15 “Bwana” Hili ni neno la Kiyunani kurios. Limetumika hapa kwa maana isiyo ya kitheolojia (kama vile Yohana 12:21) linaweza kumaanisha “Bwana,” “Mheshimiwa,” “Mwalimu,” “Mmiliki,” “Mume,” au “Bwana.” Mariamu alidhani alikua anaongea na (1) mtunza bustani au (2) mmiliki wa busatani. Lakini angalia matumizi yake ya kitheolojia katika Yohana 20:28!

◙ “ikiwa” Hii ni sentensi shurutishi daraja la kwanza ambayo inachukuliwa kuwa kweli kwa mtazamo wa msemaji. Alidhani mtu Fulani alikuwa ameiba mwili.

20:16 “Mariamu. . . Raboni” Mariamu kwa uhalisia ni Miriamu. Maneno yote haya ni Kiaramu (“Kiebrania” ina maanisha Kiaramu, kama vile Yohana 5:2; 19:13,17,20). Inavyoonekana Yesu alisema jina la huyu mwanamke katika namna ya kitabia. Lazima atakuwa alikwisha kufanya kitu cha namna ile ile wakati alipoomba na watu wale wawili njiani wakienda Emau (kama vile Luka 24:30-31). Ile “i” mwishoni mwa "Rabboni" inaweza kuwa inaonyesha/akisi “Rabbi wangu” au “Mwalimu wangu.”

MADA MAALUMU: KUONEKANA KWA YESU BAADA YA UFUFUO Yesu alijionesha kwa watu kadhaa kuthibitisha kufufuka kwake.

1. Wanawake kaburini, Mt. 28:9 2. Wanafunzi kumi na moja kwenye mkutano ulioandaliwa Galilaya, Mt. 28:16 3. Simoni, Luka 24:34 4. Wale wawili njiani kuelekea Emau, Luka 24:15 5. Wanafunzi gorofani, Luka 24:36 6. Maria Magdalena, Yohana 20:15 7. Wanafunzi kumi ghorofani, Yohana 20:20 8. Wanafunzi kumi na moja ghorofani, Yohana 20:26 9. Wanafunzi saba kwenye bahari ya Galilaya, Yohana 21:1 10. Kefa (Petro), 1 Kor. 15:5 11. (Mitume) kumi na wawili, 1 Kor. 15:5 12. Ndugu 500, 1 Kor. 15:6 pamoja na mathayo Mt. 28:16-17 13. Yakobo (mtu wa familia yake), 1 Kor. 15:7 14. Mitume wote, 1 Kor. 15:7 15. Paulo, 1 Kor. 15:8 (Matendo 9)

Bila shaka baadhi ya haya mengine yanarejelea kuonekana kulekule. Yesu alitaka wao wajue kwa hakika kwamba alikuwa hai!

20:17 NASB "acha kuning’ang’ania" NKJV "usining’ang’anie" NRSV "usinishike" TEV "usinishike" NJB "usining’ang’anie" KJV ina "usiniguse." Hii ni kauli ya kati shurutishi ya wakati uliopo ikiwa na kiambata hasi ambayo kwa kawaida humaanisha kukoma kufanya kitendo ambacho kiko tayari kwenye mchakato. Mariamu alikuwa amekwisha kumnyakua na alikuwa amemng’ang’ania! Hii haina onyesho lolote la kitheolojia kuhusu kugusa mwili wa Yesu kabla hajapaa. Katika Yohana 20:27 Yesu anamruhusu Tomaso kumgusa na katika Mathayo 28:9, anamruhusu mwanamke kushika miguu yake.

Page 326: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

310

◙ “kwa maana sijapaa” Hii ni kauli timilifu tendaji elekezi. Yesu hata paa kwenda mbinguni hadi siku 40 baada ya kufufuka kwake (kama vile Matendo 1:9).

◙ “enenda kwa ndugu zangu” Yesu yule aliyefufuka, aliyetukuza anawaita hawa waoga “ndugu zangu” (kama vile Mt. 12:50).

◙ “Ninapaa kwenda” Hii ni kauli ya wakati uliopo. Hili halikutendeka kiuhalisia hadi siku arobaini baadaye wakati walipokuwa kwenye uwepo wake (kama vile Luka 24:50-52; Mdo. 1:2-3). Yohana anaendelea kutumia uwili wa toka wima wa “juu” na “chini.” Yesu ni wa kutoka kwa Baba (kabla ya kuwepo) na anarudi kwa Baba (kutukuzwa)

◙ “kwa Baba yangu naye ni Baba yenu” Hii ni kauli ya nguvu na ya kushangaza kiasi gani! Hata hivyo, lazima ielezwe kwamba hii haina maana kwamba uwana wa wanaoamini kwa Baba unalingana na uwana wa Yesu kwa Baba yake. Yeye ni mwana wa namna maalum kwa Baba (Yohana 3:16), Mungu kamili na Mwanadamu kamili. Wanaoamini wanakuwa wanafamilia kupitia Yeye. Yeye ni kwa vyote Bwana, mwokozi, na ndugu!

20:18 Mariamu pia ni shahidi!

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 20:19-23 19 Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu. 20 Naye akiisha kusema hayo, akawaonyesha mikono yake na ubavu wake. Basi wale wanafunzi wakafurahi walipomwona Bwana. 21 Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi. 22 Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu. 23 Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa.

20:19 “Ikawa jioni, siku ile” Muda wa Wayahudi huanza na kumalizika jioni (kama vile Mwa. 1:5), ambapo hapa ni kama saa 2:00 jioni, jumapili.

◙ “siku ile ya kwanza ya juma” Siku ya jumapili ilikuwa siku ya kwanza katika kazi, kama jumapili yetu. Hii ikawa siku ya kukutanika kanisani kukumbuka kwa njia ya kusherekea ama kufanya matendo ya kidini kwa ajili ya kufufuka kwa Yesu kristo. Yeye mwenyewe aliweka mtindo wa kufuata kwa kuonekana ghorofani jumapili tatu kwenye mstari (kama vile Yohana 20:19, 26; Luka 24:36 na kuendelea; Mdo. 20:7; 1 Kor. 16:2). Kizazi cha kwanza cha wanaoamini kiliendelea kukutana siku ya sabato kwenye masinagogi ya makwao na hekaluni siku za sikukuu zilizowekwa. Hata hivyo, walimu wa sheria za kiyunani walianzisha “kiapo cha kulaani” ambacho kiliwataka wanachama wote wa kwenye masinagogi kumkata Yesu kama Masihi (baada ya 70 B.K.). Katika hatua hii waliacha ibada za sabato, lakini waliendelea kukutana na wanaoamini wengine siku ya jumapili, siku ya ufufuo kusherekea kufufuka kwa Yesu.

◙ “milango imefungwa” Hii ni kauli tendewa endelevu ya wakati timilifu. Neno wingi ina maana kwamba milango yote ya ghorofa ya chini na ghorofa ya juu imefungwa. Hii ilitamkwa ili (1) kusisitiza hali ile ya kuonekana kwa Yesu au (2) kuonyesha hofu ya kukamatwa.

◙ “wanafunzi” Tomaso hakuwepo. Wanafunzi wengine mbali na wale mitume kumi na moja walikuwepo (kama vile Luka 24:33).

◙ “Amani iwe kwenu” Hii inaonyesha mshangao wao, na pengine hofu. Yesu alikuwa ameawahaidi amani (kama vile Yohana 14:27; 16:33).Hii labda inaonyesha/akisi salamu ya Kiebrania shalom. Yesu anairudia mara tatu (Yohana 20:19,21,26).

Page 327: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

311

20:20 “akawaonyesha mikono yake na ubavu wake” Yohana kukazia kule kuchomwa ubavuni mwa Yesu zaidi kuliko injili nyinginezo (kama vile Yohana 19:37; 20:25). Miguu yake haijatajwa isipokuwa katika Luka 24:39 na Zaburi 22:16. Mwili uliotukuzwa na Yesu unabakiza alama za ufufuo wake (kama vile Kor. 1. 1:23; Gal. 3:1).

◙ “Bwana” Sifa hii imetumika hapa katika maana yake kamili ya kitheolijia ambayo inahusiana na YHWH wa Agano la Kale (kama vile Kutoka 3:14). Kutumia sifa hii ya Mungu Baba wa Yesu katika Agano la Kale ilikuwa njia mojawapo kwa waandishi wa Agano Jipya kuthibitisha ukamilifu wa Uungu wa Yesu. Tazama Mada Maalum katika Yohana 6:20

20:21 "kama Baba alivyonituma mimi" Hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati timilifu (kama vile. Yohana 17:18). Kanisa linayo mamlaka ya ki-Uungu (kama vile Mt.28:18-20; Luka 24:47; Matendo 1:8). Wanaoamini wametumwa pia kwenye kazi maalumu kujitoa mhanga (kama vile Kor. 2. 5:14-15; Yohana 1 3:16). Yesu anatumia maneno mawili tofauti kwa "kupelekwa." Katika Yohana hizi zinafanana. Hii inaonekana dhahiri katika Yohana 8, ambapo pempōl imetumika kwa Yesu akiwa ametumwa na Baba (kama vile. Yohana 8:16,18,26,29), bado apostellō limetumika katika Yohana 8:42. Kitu hiki hiki ni kweli katika Yohana 5,6. Tazama Mada Maalum: Kupelekwa (Apostellō) katika Yohana 5:24

20:22 "akawavuvia" Huu ni mchezo wa maneno kwenye neno "alipumua." Neno la Kiebrania ruach na Kiyunani pneuma yanaweza kumaanisha “pumua," "upepo," au "roho." Kitenzi hicho katika Maandiko ya Kale ya Kiyunani kilitumika katika Agano la Kale kwenye shuguli ya Uumbaji wa Mungu katika Mwa. 2:7 na juhudi za nguvu kwa mara nyingine tena kwa Israeli katika Ezek. 37:5,9. Kiwakilishi nomino "wao" kinarejelea kwa kundi kubwa zaidi ya mitume tu (kama vile Luka 24:33).

◙ "Pokeeni Roho Mtakatifu" Hii ni kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopita usiotimilifu. Jinsi gani hili linahusiana na ujio wa Roho mtakatifu siku ya Pentekoste halikuwa dhahiri. Yesu alitimiza kila kitu alichokuwa amewaahidi wanafunzi wake pale alipoonekana mara ya kwanza. Inahusiana na Yesu kuwaandaa kwa ajili ya kazi mpya katika huduma kama vile Roho alivyomwandaa Yeye katika ubatizo wake. Aya hii ilitumiwa katika kanisa la kwanza kwenye vita kuhusu swali Roho huja kutoka kwa Baba ama kutoka kwa Baba na mwana. Katika hali halisi, nafsi zote tatu za utatu zinahusika katika utendaji wote. Katika A Theology of the New Testament, George Ladd anafanya muhtasari wa tafsiri zinazowezekana za aya hii:

"Aya hii inaibua matatizo katika mwanga wa kuja kwa roho mtakatifu siku ya Pentekoste, ambapo yanaweza kutatuliwa katika moja ya njia tatu. Kwamba Yohana hakujua kuhusu Pentekoste na anaweka habari hii mbadala ili kwamba iwe Pentekoste; ama kulikuwepo hasa na vipawa viwili vya roho; au Yesu kuwa pulizia mitume lilikuwa igizo la fumbo la ahadi iliyotarajiwa ya Roho kwenye Pentekoste" (uk. 289).

Maelezo ya chini ya ukurasa #24 (uk. 1965) katika biblia ya NET inayoeleza kwamba hii inakukumbusha Mwa. 2:7 (LXX). Kama uzima wa kimwili ulivyotolewa katika Mwanzo, uzima wa milele unatolewa katika Agano Jipya. Msisitizo huu juu ya “pumzi ya Mungu" unalinganishwa na Ezekieli 37, ambapo YHWH analeta uzima mpya kwa watu wake kwa pumzi ya Roho.

20:23 “Wo wote mtakaowaondolea dhambi" Hizi ni sentensi mbili shurutishi daraja la tatu pamoja na an ambayo kawaida hutimiwa na sentensi shurutishi daraja la pili, sio ean. Hali hii iliyochanganyika hurefusha kile ambacho hakijaonekana kinachoweza kuonekana siku za baadaye kinachohusiana na wote wanaohubiri Injili na wale ambao wanaitikia kwa imani. Mtu mmoja aliye na elimu ya injili anaamua kumshirikisha mtu na mwingine anaisikia na anaamua kuipokea. Mionekano yote miwili inahitajika. Aya hii haitoi mamlaka kwa viongozi wa kanisa, mamlaka isiyofanya maamuzi ya busara bali nguvu inayotoa uzima wa ajabu kwa mashahidi wa waaminio. Mamlaka hii ilishuhudiwa katika safari ile ya wale sabini wakati wa uhai wa Yesu.

◙ “wameondolewa" Muundo huu wa kisarufi ni tendewa kamilifu inayoonesha kauli ya kutendwa inaonesha msamaha wa Mungu upo kikamilifu kupitia kuihubiri injili. Waaminio wanazo funguo za ufalme (kama vile Mt. 16:19) ikiwa tu watazitumia. Ahadi ni kwa kanisa sio kwa watu binafsi. Hili kithiolojia lafanana na "waliofungwa na waliofunguliwa" la Mt. 18:18.

Page 328: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

312

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 20:24-25 24 Walakini mmoja wa wale Thenashara, Tomaso, aitwaye Pacha, hakuwako pamoja nao alipokuja Yesu. 25 Basi wanafunzi wengine wakamwambia, Tumemwona Bwana. Akawaambia, Mimi nisipoziona mikononi mwake kovu za misumari, na kutia kidole changu katika mahali pa misumari, na kutia mkono wangu katika ubavu wake, mimi sisadiki hata kidogo.

20:24 "Walakini mmoja wa wale Thenashara, Tomaso, aitwaye Pacha, hakuwako pamoja nao alipokuja Yesu" Didymus katika Kiyunani linamaanisha “pacha" (kama vile Yohana 11:16). Mara nyingi watu wametumia aya hii kumwita Tomaso anayesitasita lakini kumbuka 11:16. Tomaso anaonekana mara nyingi kwenye injili ya Yohana kuliko injili yoyote ile (kama vile Yohana 11:16; 14:5; 20:24,26,27,28,29; 21:2).

20:25 "Mimi nisipo. . . mimi sisadiki" Neno "Nisipo" ni sentensi shurutishi daraja la tatu ikiwa na hali ya kanushi mbili zenye nguvu , "kamwe sita, hapana kamwe, sitaamini" bila kuona na kugusa Yesu aliheshimu ombi lake. Yesu alitenda kazi kwa imani ya wanafunzi kupitia (1) Miujiza yake na (2) Tabiri zake. Ujumbe wa Yesu kimsingi ulikuwa mpya sana. Aliwapa muda kuelewa na kusimilisha na kuingizwa lawamani kwa injili.

◙ "kovu" Tazama Mada Maalumu hapa chini.

MADA MAALUMU: MUUNDO (tupos)

Neno tupos lina elimu-maana pana. 1. Moulton and Milligan, The Vocabulary of the Greek New Testament, uk. 645

a. Sampuli b. mpango c. Mtindo au namna ya kuandika d. Amri ya serikali ama agizo litolewalo na mtawala e. Sentensi ama uamuzi f. Mfano wa mwili wa binadamu kama sadaka ya kuondoa nadhiri kwa Mungu anayeponya g. Kitenzi kilichotumika kwa maana ya kuongeza agizo au mwongozo wa sheria

2. Louw and Nida, Greek-English Lexicon, juzuu. 2, uk. 249 a. Kovu (kama vile Yohana 20:25) b. Sura (kama vile Matendo 7:43) c. Fanya kwa mfano (kama vile Ebr. 8:5) d. Mfano (kama vile 1 Kor. 10:6; Flp. 3:17) e. Umboasili (kama vile Rum. 5:14) f. Aina (kama vile Matendo 23:25) g. Maudhui (kama vile Matendo 23:25)

3. Harold K. Moulton, The Analytical Greek Lexicon Revised, p. 411 a. Kipigo, chapa, alama (kama vile Yohana 20:25) b. Eleza kinaganaga c. Sanamu (kama vile Matendo 7:43) d. Kanuni, mpango (kama vile Rum. 6:17) e. Muundo, kusudi (kama vile Matendo 23:25) f. Umbo, enye kufanana na kitu kingine (kama vile 1 Kor. 10:6) g. Umbo tarajiwa, aina (kama vile Rum. 5:14; 1 Kor. 10:11) h. Sampuli mfano (kama vile Matendo 7:44; Ebr. 8:5) i. Mfano adilifu (kama vile Flp. 3:17; 1 The. 1:7; 2 The. 3:9; 1 Tim. 4:12; 1 Pet. 5:3)

Kumbuka, msamiati hauweki maana; ni matumizi tu ya maneno kwenye sentensi/aya ndiyo yanaweka maana (yaani, muktadha). Kuwa mwangalifu kugawanya rasmi kundi la fafanuzi kwa neno na kulitumia kila mahali neno hilo linapotumika katika Biblia, muktadha huamua maana!

Page 329: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

313

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 20:26-29 26 Basi, baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwamo ndani tena, na Tomaso pamoja nao. Akaja Yesu, na milango imefungwa, akasimama katikati, akasema, Amani iwe kwenu. 27 Kisha akamwambia Tomaso, Lete hapa kidole chako; uitazame mikono yangu; ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu, wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye. 28 Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu! 29 Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki.

20:26 "baada ya siku nane" Hii ni nahau ya Kiebrania badala ya wiki. Hii ilikuwa Juma pili nyingine jioni. Yesu alionekana kwa wanafunzi wake gorofani (inawezekana katika nyumba ya Yohana Marko) Jumapili tatu zilizofuatana na ndipo wakaweka kitangulizi cha ibada ya Kikristo. Tazama nukuu katika Yohana 20:19.

20:27 "wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye" Hii ni kauli ya kati (shahidi) shurutishi ya wakati uliopo ikiwa na kiambata hasi kwa kawaida humaanisha kukoma kufanya kitendo kilichoko katika mchakato. Waamini wote ni wageni mchanganyiko wa mashaka na imani!

20:28 Ukiri wa Tomaso yaweza kuwa kitheolojia unahusiana na Yohana 20:17. Ukiri wa Tomaso waweza kuwa umepata kitangulizi cha Agano la Kale kwamba wakati wowote vyeo vya YHWH Elohim (yaani, Mwa. 2:4) vilipotokea kwa pamoja, jina linatafsiriwa "Bwana Mungu." Yesu anakubali kikamilifu tangazo hili lenye kushtua na kutisha la Uungu wake. Kutoka Yohana 1:1, Injili ya Yohana inatangaza Uungu wa Yesu wa Nazareti. Yesu alidai Uungu mara kadhaa katika Yohana (kama vile Yohana 8:58; 10:30; 14:9; 20:28) na mwandishi anatamka Uungu wake katika Yohana 1:1,14-18; 5:18. Waandishi wengine katika biblia pia wanatamka waziwazi kwamba Yesu ana Uungu (kama vile Mdo. 20:28; Rum. 9:5; Flp. 2:6-7; Kol. 1:15-17; 2 The. 1:12; Tito 2:13; Ebr. 1:8; 2 Pet. 1:1,11; 1 Yohana 5:20).

20:29 Hii aya ya ufunguzi yaweza kuwa tamko ama swali lenye kutarajia jibu la "ndiyo". Mfumo wa kifasihi una maana zaidi ya moja.

Hii inafanana na zile Baraka katika Yohana 17:20 (kama vile 1 Pet. 1:8).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 20:30-31 30 Basi kuna ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa katika kitabu hiki. 31 Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.

20:30 Yohana 20:30-31 dhahiri ndiyo dhamira na kusudi la injili. Ni kijitabu cha uinjilisti! Waandishi wa injili chini ya uvuvio, walikuwa na haki ya uwezo uliotolewa na Mungu. Kuchagua kupanga na kufanya matendo na maneno ya Yesu yaweze kutumika na kufanya muhtasari wake ili kuwasiliana kwa urahisi na wapokea ujumbe, Wayahudi, Warumi na watu wa Mataifa, Ukweli kuhusu Yesu. Agano Jipya sio kitabu cha kanuni za Kikristo. Carl F. H. Henry, katika somo lake la kufungua lenye kichwa cha somo "mamlaka na uvuvio wa Biblia” katika The Expositor's Bible Commentary, Vol. 1 anasema:

"Biblia haikusudia kutoa matukio kamili kama yalivyofuatana, iwapo inashugulika na simulizi za uumbaji ama historia ya wokovu, ikijumulisha na hali ya kuwa katika mwili. Lakini madhumuni yaliyotamkwa ya maandiko ya biblia ni kumpa mwanadamu chote ambacho ni lazima na cha kutosha kwa ajili ya msaada wa ukombozi wake na huduma ya utii wa muumbaji wake.Ingawa waandishi wa biblia wakati mwingine hutazama kazi hiyo moja ya kuokoa ya Mungu kutokea kona mbalimbali na kwa makusudi tofauti tofauti, kile kile wanachotuambia ni cha kutegemewa na cha kutosha. Mathayo anashusha sehemu kubwa ya mlolongo wa huduma ya Yesu na kuweka mpangilio wa masomo ambao unaweza kuhudumiwa kwa mafundisho. Luka anaacha mambo yaliyo katika Marko katika kile ambacho bado ni mpangilio wa habari zinazoweka ukuta unaozuia mtu kujazwa mafundisho ya kidini (kama vile Yohana 1:4). Yohana wazi wazi

Page 330: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

314

anatoa hoja juu ya uchaguzi kwa uangalifu, wa msingi ambao injili ya nne imesimikwa (20:30,31)" (kur. 27-28).

◙ "ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi" "ishara" hizi zinaweza kueleweka kwa namna nyingi.

1. Ishara kwamba alikuwa hai a. Kugusa kwao vidonda vyake b. Kula pamoja nao (kama vile Luka 24:43)

2. Ishara maalumu ambazo hazikuandikwa zilizofanyika gorofani mbele yao 3. Urejeleo wa kazi ya uhai wake (kutazama wakati uliopita) akiwaandaa ili waandike injili (kama vile Luka

24:46-48) 20:31 NASB, NKJV, TEV, NJB "kwamba mpate kuamini" NRSV "ili mpate kuamini" Baadhi ya machapisho ya Kiyunani, P66, א*, B2, na maandiko yaliyotumiwa na Origen, yana kitenzi tegemezi cha wakati uliopo, ambacho kingeonyesha kwamba Yohana alikuwa anaandikwa kwa wasioamini. (yaani, אi2, A, C, D, L, N, W) yana kitenzi tegemezi cha wakati uliopita usiotimilifu,daraja “C” (vigumu katika maamuzi). Hii aya imesemwa kwa makusudi ya injili. Yohana ni kama injili nyingine, njia ya uinjilisti. ◙ "Kristo" Hii ni tafsiri ya Kiyunani ya neno la Kiebrania "Masihi" ambalo kimsingi ni “aliyepakwa mafuta." Ilikuwa uzao wa Daudi wa Agano la Kale ambaye alikuwa ametabiliwa kuleta kizazi kipya cha haki. Yesu wa Nazareti (kama vile Yohana 1:45) ndiye Masihi wa Kiyahudi (kama vile Yohana 11:27). Cheo cha Yesu kinapatikana mapema katika injili (kama vile Yohana 1:41). Hata hivyo, wadhifa "Bwana," sio "Masihi," ulikuwa wadhifa uliotumika kwa Yesu katika mazingira ya mataifa (kama vile Rum. 10:9-13; Flp. 2:9-11). Dhana ya “Masihi” ilikuwa inahusisha mabo ya kiama (1) Mafarisayo walikuwa na matarajio ya kisiasa, kitaifa na (2) katika fasihi ya Kiyahudi ya maangamizi ya mwisho wa dunia kulikuwa na matumaini katika viumbe vyake, na viumbe vyote vya angani. ◙ "Mwana wa Mungu" Cheo hiki kinatumika kwa unyimifu kwenye injili za Muhtasari (labda kwa sababu ya uwezekano wa kueleweka vibaya na Mataifa), lakini kilitumika mapema katika Yohana (kama vile Yohana 1:14,34,49). Ikiwa njia ya Yohana kutamka uhusiano wa kipekee kati ya Yesu na Baba (kutumia huios). Yohana hutumia sitiari ya kifamilia kwa njia nyingi.

1. cheo 2. Ikiunganishwa na “mwanawe wa pekee" (monogenēs, kama vile. Yohana 1:18; 3:16; 1 Yohana 4:9) 3. Ikiwekwa pamoja na matumizi ya cheo "Baba" (kama vile. Yohana 20:17)

Tazama MADA MAALUM: MWANA WA MUNGU katika 1 Yohana 3:8

MASWALI YA MJADALA

Huu ni mwongozo wa fasiri, ina maanisha kwamba unawajibika kwa tafsiri zako mwenyewe za Biblia. Kila mmoja wetu lazima atembee katika mwanga tulio nao. Wewe, Biblia, na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Hutakiwi uvitelekeze vitu hivi kwa mfasiri. Maswali ya mjadala huu yanatolewa kukusaidia kufikiri juu ya mambo makubwa ya sehemu za kitabu hiki. Yanalenga kukuamsha kimawazo na sio kutoa maana.

1. Nani alikuja kwenye kaburi? Lini? Kwanini? 2. Kwanini wanafunzi hawakutazamia ufufuo? Kuna yeyote aliyeutegemea? 3. Kwa nini Mariamu hakumtambua Yesu?

Page 331: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

315

4. Kwa nini Yesu alimwambia Mariamu asimng’ang’anie? 5. Elezea Yohana 20:22-23 kwa maneno yako mwenyewe. 6. Je ni haki kumwita Thomaso mwenye mashaka? 7. Fafanua neno "amini" kama ilivyoeleweka katika siku za Yesu.

Page 332: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

316

YOHANA 21

MIGAWANYO YA AYA YA TAFSIRI ZA KISASA UBS4 NKJV NRSV TEV NJB

Kujidhihirisha Yesu Kifungua kinywa Hitimisho la kazi Yesu anajidhihirisha kwa Kuonekana kwenye kwa wanafunzi saba penye bahari wanafunzi saba pwani ya Tiberia 21:1-14 21:1-14 21:1-3 21:1-3a 21:1-3 21:3b-5a 21:4-8 21:4-8 21:5b 21:6 21:7-10 21:9-14 21:9-14 21:11-14 Yesu na Petro Yesu anamrejesha Yesu na Petro Petro 21:15-19 21:15-19 21:15-19 21:15a 21:15-19 21:15b 21:15c-16a 21:16b 21:16c-17a 21:17b 21:17c-19 Yesu na mwanafunzi Mwanafunzi Yesu na wanafunzi Mpendwa mpendwa na kitabu wengine Chake 21:20-23 21:20-25 21:20-23 21:20-21 21:20-23 21:22 21:23 Hitimisho la pili 21:24 21:24-25 21:24 21:24 Hitimisho 21:25 21:25 21:25

MZUNGUKO WA TATU WA USOMAJI KUFUATILIA KUSUDIO LA ASILI LA MWANDISHI KATIKA NGAZI YA AYA Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwatafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Aya ya kwanza 2. Aya ya pili 3. Aya ya tatu 4. N.k

Page 333: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

317

UTAMBUZI WA KI-MUKTADHA KWA MISTARI YA 1-25

A. Kumekua na majadiliano mengi kuhusu Yohana 21 kuwa kama ni nyongezeka kwa sababu injili inaonekana kuishia katika Yohana 20:31. Hata hivyo hakuna machapisho ya Kiyunani ambayo huacha sura ya 21.

B. Yohana 21:25 mara nyingi linafikiriwa kuongezewa baadaye kwa sababu katika baadhi ya machapisho

Yohana 7:53-8:11 limeingizwa baada ya 21:24. Pia, katika machapisho ya kale ya biblia ya Kikristo (sinaiticus), mwandishi wa awali aliacha 21:25 na alirudi nyuma na kufuta nembo ya mchapishaji (colophon) ili kuiingiza.

C. Ingawa sio sehemu muhimu ya injili ya Yohana, Yohana 21 hakika ilitoka kwenye mikono ya mtume.

Inajibu maswali mawili ya kanisa la mwanzo. 1. Je! Petro alichomekwa tena? 2. Vipi kuhusu hadithi za kale juu ya uwepo wa muda mrefu wa Yohana?

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 21:1-3 1 Baada ya hayo Yesu alijidhihirisha tena kwa wanafunzi wake, penye bahari ya Tiberia, naye alijidhihirisha hivi. 2 Simoni Petro, na Tomaso aitwaye Pacha, na Nathanaeli wa Kana ya Galilaya, na wana wa Zebedayo, na wengine wawili wa wanafunzi wake, walikuwapo pamoja. 3 Simoni Petro aliwaambia, Naenda kuvua samaki. Nao wakamwambia, Sisi nasi tutakwenda nawe. Basi wakaondoka, wakapanda chomboni; ila usiku ule hawakupata kitu.

21:1 "Bahari ya Tiberia" Tiberia ilikua mji mkuu wa utawala wa kirumi wa Galilaya. Sehemu hii ya maji pia unajulikana kama "Bahari ya Galilaya" (kama vile Yohana 6:1) au "Ziwa la Genesareti" (kama vile Mt. 14:34; Marko 6:53; Luka 5:1) na katika agano la kale kama "Bahari ya kinerethi" (kama vile. hes. 34:11; kum. 3:17; Yoshua 11:2; 12:3; 13:27; 19:35; 1 Wafalme 15:20). ◙ "Naye alijidhihirisha hivi" Kitenzi hiki kina kidokezo "kujionyesha kikamilifu au wazi" (kama vile Yohana 1:31; 2:11; 7:4; 9:3; 1 Yohana 1:2; 2:28; 3:2; 4:9). Katika Mathayo palikuwepo na mkutano huko Galilaya ambao uliokuwa ukifanyika mlimani (kama vile 26:32; 28:7,10,16),kwa ajili ya kuundwa kwa "amri kuu." Katika Yohana Yesu alijidhihirisha kwenye bahari ya Tiberia. Katika kukutana huku Yesu anahusika na maswali mawili ya kanisa la kwanza yaliyopendekezwa.

1. Je, Petro aliwekwa tena kama kiongozi 2. Nini kuhusu hadithi kwamba Yohana hatakufa kabla Yesu kurudi

21:2 "Tomaso aitwaye Pacha" Tazama Mada Maalum: Jedwali la Majina ya Mitume katika Yohana 1:45 Inaonekana dhahiri kabisa Saba kati ya wale kumi na moja walienda kuvua. ◙ "Na wana wa Zebedayo” Hii inamanisha Yakobo (Yakobo) na Yohana (k. v. Mt. 4:21). Sio Yakobo wala Yohana wametajwa kwa majina katika injili ya Yohana.

21:3 “Simoni Petro aliwaambia, naenda kuvua samaki" Hii ni njeo ya wakati uliopo. Kuna nadharia kadhaa kuhusu safari hii ya uvuvi.

1. Ilikua ni safari ya kupumzika ili kupitisha muda mpaka Yesu atakapoitisha kukutana (kama vile Mt. 26:32; 28:7,10)

2. Ilikua ni kwa lengo la kutengeneza pesa 3. Ilikua ni ushawishi uliojirudia wa wito wa Petro katika uvuvi

Sura hii ni sawa na Luka 5.

Page 334: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

318

◙ "Na usiku huo hawakupata chochote" ona kwamba watu hawa, waliokua na uwezo wa kuponya wagonjwa na kuwatoa mapepo, hawakua na nguvu za miujiza kwa wakati wote kwa madhumuni yote. Kitenzi hiki hakitumiki mahali popote katika Agano Jipya kwa ajili ya kunasa samaki. Kawaida hutumiwa kukamata watu.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 21:4-8 4 Hata asubuhi kulipokucha, Yesu alisimama ufuoni; walakini wanafunzi hawakujua ya kuwa ni Yesu. 5 Basi Yesu akawaambia, Wanangu, mna kitoweo? Wakamjibu, La. 6 Akawaambia, Litupeni jarife upande wa kuume wa chombo, nanyi mtapata. Basi wakatupa; wala sasa hawakuweza kulivuta tena kwa sababu ya wingi wa samaki. 7 Basi yule mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda akamwambia Petro, Ndiye Bwana. Naye Simoni Petro, aliposikia ya kwamba ni Bwana, akajifunga vazi lake, (maana alikuwa uchi), akajitupa baharini. 8 Na hao wanafunzi wengine wakaja katika mashua; maana hawakuwa mbali na nchi kavu; ila yapata dhiraa mia mbili; huku wakilikokota lile jarife lenye samaki.

21:4 "Walakini wanafunzi hawakujua ya kuwa ni Yesu" kumekuwepo na nadharia kadhaa ya kutokua na uwezo wa kumtambua Yesu.

1. Kulikuwa na giza sana 2. Alikua mbali sana 3. Walikua wamechoka sana 4. Yesu alionekana kidogo tofauti (k. v. Yohana 21:12; Mt. 28:16-17; Luka 24:13 na kuendelea) 5. Walizuiwa kwa uwezo wa ki-Ungu kuweza kumtambua Yeye (k.v. Luka 24:16)

21:5 “Wanangu" Hii imetumika ki-sitiari. Kuna maneno mawili kwa "watoto wadogo" yanatumika kwa kawaida katika Agano Jipya. Hili moja (paidion) hutumiwa kidogo na ni tofauti na yale mengine ya kawaida (teknion) yaliyotumika katika Yohana na 1 Yohana. Neno hili linaonekana katika injili pekee ya Yohana 4:49; 16:21, na hapa. Maneno haya yanaonekana kama visawe katika 1 Yohana, paidion katika Yohana 2:13, 18, lakini teknion katika Yohana 2:1, 12, 28.

◙ “Mna kitoweo" Neno hili "kitoweo" (prosphagion) kweli linaashiria chakula cha aina yoyote ambacho huliwa na mkate, lakini katika mazingira haya,"kitoweo" kinahitajika. Swali hili linatarajia jibu la "Hapana".

21:6 Yesu alifanya kwa namna ile ile kama alivyofanya wakati alipowaita, Luka 5:1-11. Kama uainishaji wa sura hii (tazama kumbuka Yohana 21:15) maneno mawili tofauti ya Kiyunani hutumika kumaanisha mashua, ploion katika Yohana 21:3 na 6 na ploiaron (mashua ndogo) katika Yohana 21:8. Yohana anaonyesha fasihi yake ya tofauti katika sura mara kadhaa.

21:7 “Basi yule mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda" Hii inahusu mwandishi wa injili, Mtume Yohana (kama vile. Yohana 13:23; 20:2, 3,8; 21:20). Yohana hakutajwa kamwe kwenye injili.

NASB "akajifunga vazi lake (maana hakuwa amelivaa)" NKJV " akajifunga vazi lake (maana alikuwa uchi)" NRSV "alijifunga vazi lake, maana alikua uchi" TEV "alijifunga vazi lake mwilini (maana alikua amelivua)" NJB "Petro akajifunga vazi lake mwilini (maana alikuwa mtupu)" Katika karne ya kwanza watu wa Palestina walivaa vazi la nje na vazi refu la kubana ndani. Petro alikua ameondoa vazi lake la nje/joho na akaviringisha vazi lake la ndani hadi kiunoni. ◙ "Ndiye Bwana" Neno kurios lilikuwa neno la Kiyunani "mheshimiwa," "mzee," "mkuu wa kaya," "mmiliki," au "Bwana." Katika hali fulani ni utambulisho wa heshima tu, lakini kwingine ni uthibitisho wa kitheolojia wa Uungu wa yesu. Katika muktadha huu hawa wavuvi walimtambua mtu huyu kwenye pwani kama aliyetukuzwa, Mungu aliyefufuliwa!

Page 335: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

319

Asili ya utafsiri inatoka kwenye matumizi ya Agano la Kale, ambapo YHWH hutafsiriwa kama Bwana. Hii ilitokea kwa sababu Wayahahudi waliogopa kutamka jina hili la Agano kwa Uungu, kwa hiyo badala yake waliweka neno lingine la kiebrania , Adonai, ambalo linafanana na kurios. Tazama Mada Maalum katika Yohana 6:20 Bwana ni wadhifa ambao ni juu kuliko majina yote katika Efe. 2:9-11. Ilikua ni sehemu ya kukiri kwa kanisa la kwanza kiubatizo, "Yesu ni bwana" (kama vile Rum. 10:9-13).

21:8 "Na hao wanafunzi wengine" Ni dhahili kabisa wanafunzi wakaribu zaidi wa Yesu waliondoka na Petro na Yohana wakirudi kuvua kama njia ya kupata pesa ya kutumia (Hawakuweza tena kutegemea wanawake waliosafiri pamoja na Yesu).

◙ "Jarife lenye samaki" pamoja na muda kwenda Yesu bado aliendelea 1. Kujenga imani yao 2. Kutoa mahitaji yao 3. Kuthibitisha ufufuo wake na mamlaka (juu ya asili)

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 21:9-14 9 Basi waliposhuka pwani, wakaona huko moto wa makaa, na juu yake pametiwa samaki, na mkate. 10 Yesu akawaambia, Leteni hapa baadhi ya samaki mliowavua sasa hivi. 11 Basi Simoni Petro akapanda chomboni, akalivuta jarife pwani, limejaa samaki wakubwa, mia hamsini na watatu; na ijapokuwa ni wengi namna hiyo, jarife halikupasuka. 12 Yesu akawaambia, Njoni mfungue kinywa. Wala hakuna mtu katika wale wanafunzi aliyethubutu kumwuliza, U nani wewe? Wakijua ya kuwa ni Bwana. 13 Yesu akaenda akautwaa mkate, akawapa, na samaki vivyo hivyo. 14 Hiyo ndiyo mara ya tatu ya Yesu kuonekana na wanafunzi wake baada ya kufufuka katika wafu.

21:9 "Moto wa makaa, na juu yake pametiwa samaki, na mkate" madhumuni ya kifungua kinywa cha asubuhi na mapema ilikua kwa ajili ya ushirika wa pamoja na utazamishaji wa kitheolojia. Matokeo ya kithiolojia ni

1. Sehemu hii inahusika na ukanaji wa Petro katika muundo mwingine wa kujipalia makaa ya moto (kama vile Yohana 18:18). Neno hili linapatikana hapa na pale.

2. Injili ya Yohana na 1 Yohana ziliandikwa ili kupambana na mafunuo yenye mafundisho ya uongo yanayokanusha ubinadamu wa kweli wa Yesu, aliye Masihi. Yesu alikula pamoja nao.

21:10 Kuna maneno mawili tofauti ya neno samaki katika aya: (1) katka Yohana 21:9,10, & 13 neno ni opsarion, hii inamanisha samaki wadogo na (2) katika Yohana 21:6,8 & 11 neno ni ichthus, hii inamaanisha samaki wakubwa. Yanaonekana kutumika kwa kubadilishana katika muktadha huu.

21:11 "Mia hamsini na watatu" katika muktadha panaonekana kutokuwepo na maana yeyote ya umuhimu kwa namba hii; ni maelezo ya ushahidi wa macho tu. Hata hivyo, tabia isiyofaa ya kanisa la kwanza kutumia namba zote kutafasili maana iliyojificha na maelezo kuilazimisha aya hii kumaanisha:

1. Cyril alisema 100 walisimama kwa mataifa na 50 walisimama kwa Wayahudi na 3 kwa ajili ya utatu. 2. Agustino anathibitisha kuwa namba hii inahusu amri kumi na karama saba za roho, ambazo ni sawa na

namba kumi na saba. Ikiwa unaongeza kila namba 1,2,3,4 kupitia 17 unapata 153. Agustino alisema hii ilikua ni idadi ya watu wanaokuja kwa kristo kupitia sheria na neema.

3. Jarome alisema kuna aina 153 tofauti za samaki, kwa hiyo, hii nii ishara ya mataifa yote kuja kwa Kristo. Njia hii ya utafasiri kufunua maana iliyojificha inazungumzia ujanja wa mtafsiri na sio kusudi la mwandishi wa awali!

◙ "Na ijapokuwa ni wengi namna hiyo, jarife halikupasuka" Huu yawezekana ni ushuhuda wa kawaida wa macho au miujiza inayojulikana.

21:14 "Hiyo ndiyo mara ya tatu ya Yesu kuonekana na wanafunzi" Hii inapaswa kurejerea uwajibikaji mara mbili katika Yohana 20 iliyoongezewa kwenye hii.

Page 336: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

320

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): YOHANA 21:15-19 15 Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, Je! Simoni wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa? Akamwambia, Naam, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha wana-kondoo wangu. 16 Akamwambia tena mara ya pili, Simoni wa Yohana, wanipenda? Akamwambia, Ndiyo, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Chunga kondoo zangu. 17 Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo zangu. 18 Akasema, Amin, amin, nakuambia, Wakati ulipokuwa kijana, ulikuwa ukijifunga mwenyewe na kwenda utakako; lakini utakapokuwa mzee, utainyosha mikono yako, na mwingine atakufunga na kukuchukua usikotaka. 19 Akasema neno hilo kwa kuonyesha ni kwa mauti gani atakayomtukuza Mungu. Naye akiisha kusema hayo akamwambia, Nifuate.

21:15 “Simoni wa Yohana" Ona hapa kuwa Yesu hakumuita “Simoni Petro;" Mtu huyu hakuwa chochote ila mwamba! Kuna utofauti wa maandiko yanayohusiana na jina la baba yake Simon.

1. Yohana -- אi1, B, C*, D, L W 2. Yona -- A, C2 3. Acha -- א*

Toleo la UBS4 linatoa chaguo #1 alama "B" (aghalabu yenye uhakika) ikifuatiwa na 1:42 (P66, P72, א, B*, L, W). ◙ "upendo. . .upendo. . .upendo" Dhahiri urudiaji wa maneno matatu yaliyo pamaoja ambayo yanaonekana kufanana na ukanaji wa Petro mara tatu katika uga wa kuhani (kama vile Yohana 18:17,25,27). Kuna aina tofauti za kufanana na kutofautiana katika sehemu hii nzima.

1. Upendo wa (phileō) dhidi ya upendo wa (agapaō) 2. Mwana Kondoo dhidi ya kondoo 3. kutambua (ginoskō) dhidi ya kujua (oida)

Kumekuwepo na majadiliano mengi kuhusu kama hii inarejerea aina mbalimbali ya fasihi au kuna tofauti iliyokusudiwa kati ya maneno haya. Yohana mara nyingi hutumia namna mbalimbali, hasa katika sura hii (maneno mawili kwa"mwana," "mashua," na "samaki"). Kunaonekana kuwepo na baadhi ya utofauti kwenye muktadha huu kati ya maneno ya Kiyunani agapaō na phileō, lakini haya hayawezi kutupiliwa mbali kwa vile ni visawe (kama vile. Yohana 3:35; 5:20; 11:3, 5). ◙ “Wewe wanipenda kuliko hawa" Isimu hii ni yenye utata kama kichwa cha swali hili. Wengine wanasema inamaanisha

1. Uvuvi kama wito 2. Maneno ya awali ya Petro kumpenda Yesu kuliko wanafunzi wengne (kama vile Mt. 26:33; Marko 14:29

na Yohana 13:37) 3. Wa kwanza atakua mtumishi wa wote (kama vile Luka 9:46-48; 22:24-27)

◙ “Chunga kondoo zangu" Hii ni kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopo. Maelezo ya maneno yote matatu yako katika muundo wa kisarufi (kama vile Yohana 21:16 na 17), lakini kidogo yakiwa na maneno tofauti (chunga kondoo wangu na angalia kondoo wangu).

21:17 "Bwana, wewe wajua yote" Petro anajifunza kutozungumza kwa haraka. Anaelezea thiolojia nzuri (kama vile Yohana 2:25; 6:61, 64; 13:11; 16:30).

◙ "Wewe umetambua ya kuwa nakupenda" Kuna mabadiliko katika neno la Kiyunani "wajua" kati ya Yohana 21:16 (oida) na Yohana 21:17 (oida na ginoskō). Sababu halisi haijulikani na inaweza kuhusisha aina tofauti.

21:18 “Utainyosha mikono yako" Huenda hii inaweza kuwa nahau ya kiufundi iliyotumika (1) katika kanisa la kwanza na (2) katika fasihi ya Kiyunani ya "kusulubiwa."

Page 337: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

321

21:19 "Akasema neno hilo kwa kuonyesha ni kwa mauti gani atakayomtukuza Mungu" Tamaduni zinadai kwamba Petro alikufa kwa kusulubishwa kichwa chini miguu juu. Katika The Ecclesiastical History, juzuu. 3:1, Eusebius anasema, "Petro aliaminika kuwa amehubiri katika Pontio, Galatia, Bethania, Kapadokia, na Asia kwa mataifa ya Wayahudi. Alipokwenda Roma alisulubiwa kichwa chini kwa ombi lake mwenyewe. "Tazama kumbuka Yohana 1:14.

◙ "Nifuate" Hii ni kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopo, kama ilivyo Yohana 21:22. Hii inahusiana na kufanywa upya na kuhakikishiwa tena kwa wito wa Petro kuwa uongozi (kama vile Mt. 4:19-20).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 21:20-23 20 Petro akageuka akamwona yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu anafuata; (ndiye huyo aliyeegama kifuani pake wakati wa kula chakula cha jioni, akasema, Bwana, ni nani akusalitiye?) 21 Basi Petro akamwona huyo, akamwambia Yesu, Bwana, na huyu je? 22 Yesu akamwambia, Ikiwa nataka huyu akae hata nijapo, imekupasaje wewe? Wewe unifuate mimi. 23 Basi neno hilo lilienea katikati ya ndugu ya kwamba mwanafunzi yule hafi. Walakini Yesu hakumwambia ya kwamba hafi; bali, Ikiwa nataka huyu akae hata nijapo, imekupasaje wewe?

21:20 "Mwanafunzi aliyependwa na Yesu" Hii inarejerea juu ya uwajibikaji unaopatikana katika Yohana 13:25. Kwa nini yeye ateuliwe katika hali ya usiri usiojulikana (kama vile. Yohana 13:23; 19:26; 20:2; 21:7,20). Nadharia zawezekana ni

1. Kitamaduni maana Maandishi ya Kiyahudi ya karne ya kwanza haikutaja jina la mwadishi 2. Yohana alikua bado mdogo sana pale alipoamua kuwa mfuasi wa Yesu 3. Yohana ndiye mtume peke aliyekaa pamoja na Yesu wakati wa kujalibiwa na kusulubiwa

21:22 "Yesu akamwambia, Ikiwa nataka huyu akae hata nijapo, imekupasaje wewe" Hii ni sentensi shurutishi daraja la tatu. Tunapaswa kukumbuka kwamba ni lazima kushughulika na karama zetu na huduma zetu na sio kuhusika na kile ambacho Mungu amepanga kwa ajili ya wengine! Sababu inayowezekana ya kuongeza Yohana 21 ilikua ni kujibu mkanganyiko wa suala hili. Kwa wazi kabisa kunaonekana kuwepo na uvumi wa mapema (yumkini ufunuo) kwamba Yohana alipaswa kuishi mpaka ujio wa mara ya pili wa Yesu (Yohana anasema kuhusu Parousia, kama vile 1 Yohana 3:2).

◙ "Wewe unifuate mimi" Hii aghalabu inafupisha ukaribisho binafsi wa injili ya Yohana (kama vile Yohana 1:43; 10:27; 12:26; 21:19, 22). Hii inasisitiza dhana binafsi ya injili, wakati "aaminiye" inasisitiza dhana ya maudhui ya injili.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA:): YOHANA 21:24 24 Huyu ndiye yule mwanafunzi ayashuhudiaye haya, na aliyeyaandika haya: nasi twajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli.

21:24 “Aliyeyaandika haya” Je! Hii inarejea juu ya (1) Yohana 21:20-23: (2) Yohana 21; au (3) injili nzima? Jibu halijulikani. ◙ "Nasi twajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli" Kikundi maalumu kinarejerewa na kiwakilishi nomino "sisi" ambacho haijulikani. Ni dhahiri kwamba wengine wanaletwa katika uthibitisho wa ukweli wa injili ya Yohana. Huenda hii inawarejerea wazee wa Efeso. Hili lilikua eneno ambalo Yohana aliishi, alihudumu, na kufa. Mila za awali ziandai kuwa viongozi wa Efeso walimuhimiza Yohana aliyekuwa na umri mkubwa kuandika injili yake mwenyewe kwa sababu ya kifo cha mitume wote na ongezeko la mafundisho mengi ya uongo juu ya Yesu. Tazama Mada Maalum: Mashuhuda wa Yesu katika Yohana 1:8.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) YOHANA 21:25 25 Kuna na mambo mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu

Page 338: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

322

usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa.

21:25 Yohana 21:25 Imekuwa ikipingana kwa sababu mbili: (1) katika maandishi kadhaa Yohana 7:53 - 8:11 yanaingizwa kati ya Yohana 21:24 na 25 (2) katika maandishi ya biblia ya kikristo ( א) mwandishi aliondoa nembo ya mchapishaji na kuingiza Yohana 21:25 baadaye. Hii ilionekana kwa kutumia vyombo maalumu vya mionzi kwenye makumbusho ya huko Uingereza. Aya hii inatufahamisha hasa kwamba waandishi wa injili walikua wachaguzi kwa kile walichotaka kukiandika. Daima swali juu ya kanuni za ufasiri ni kuuliza, "kwa nini waliandika hili kwa namna waliyofanya na hawakukimbilia kuziunganisha injili zote nne?" (Tazama Gordon Fee na Douglas Stuart, How To Read the Bible For All Its Worth).

MASWALI YA MJADALA

Huu ni mwongozo wa fasiri, ina maanisha kwamba unawajibika kwa tafsiri zako mwenyewe za Biblia. Kila mmoja wetu lazima atembee katika mwanga tulio nao. Wewe, Biblia, na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Hutakiwi uvitelekeze vitu hivi kwa mfasiri. Maswali ya mjadala huu yanatolewa kukusaidia kufikiri juu ya mambo makubwa ya sehemu za kitabu hiki. Yanalenga kukuamsha kimawazo na sio kutoa maana.

1. Ni kwa namna gani Yohana 21 ni inafanana na Luka 5? 2. Kwanini wanafunzi hawakumtambua Yesu mara moja? 3. Ni yupi mwanafunzi ambaye yesu alimpenda? 4. Kwa nini Yesu alimuuliza Petro mara tatu kuhusu upendo wake kwake? 5. Je! Yesu alidai kwamba Yohana angeishi mpaka atakapokuja tena? 6. Ni nani anarejerewa katika Yohana 21:24? 7. Je! Yohana 21:25 ni ya asili?

Page 339: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

323

UTANGULIZI WA 1 YOHANA

UPEKEE WA KITABU A. Kitabu cha 1 Yohana sio barua ya binafsi wala barua iliyoandikwa kwa kanisa moja kama “Ujumbe Mtulivu

wa sehemu ya kazi kutoka makao Makuu” (barua ya ushirika). 1. Hiki hakina utamaduni wa utangulizi (kutoka kwa nani, kwenda kwa nani). 2. Hiki hakina salamu binafsi au ujumbe wa mwisho.

B. Hakuna majina binafsi yaliyotajwa. Huu ni upekee wa hali ya juu ambao si wa kawaida katika vitabu

vilivyoandikwa kwa makanisa mengi, kama vile Waefeso na Yakobo. Barua pekee katika Agano Jipya ambayo haina jina la mwandishi ni Waebrania. Hata hivyo, ni dhahiri kwamba hii iliandikwa kwa waamini wa sasa wa kanisa la nyumbani wanaokumbana na tatizo la waalimu wa uongo.

C. Barua hii ni kitheolojia maandiko ya yenye nguvu 1. Ukuu wa Yesu

a. Mungu kamili na mwanadamu kamili b. wokovu huja kwa imani katika Yesu Kristo, si uzoefu wa kiroho au maarifa ya siri (waalimu wa

uongo) 2. Hitaji kwa ajili ya maisha ya ki-Kristo (majaribu matatu ya Ukristo halisi)

a. upendo wa kindugu b. utii c. kukataliwa kwa mfumo wa ulimwengu ulioanguka

3. Uhakika wa wokovu wa milele kupitia imani katika Yesu wa Nazarethi (neno “sasa ” limetumika mara 27)

4. Namna ya kuwatambua waalimu wa uongo

D. Maandiko ya Yohana (hasa I Yohana) kwa kiasi fulani ni ki-Koine cha Kiyunani kilicho kigumu kwa mwandishi ye yote yule wa Agano Jipya, bado kitabu hiki, kama ambapo hakuna kitabu kingine, kinachimbua undani wa maana hii na kweli za milele za Mungu katika Yesu Kristo (yaani, Mungu ni Nuru, 1:5; Mungu ni Pendo, 4:8,16; Mungu ni roho, Yohana 4:24).

E. Inawezekana kwamba I Yohana ilimaanisha kuwa barua ya kiliitoshereza Injli ya Yohana. Mapotoe ya uasi wa karne ya kwanza yanaunda mrejesho wa vitabu vyote. Injili hii ina kweli ya kiunjilisti, ambapo I Yohana inaandikwa kwa ajili ya waamini. Mfasiri maarufu Westcott anadai kwamba Injili inaukiri Uungu wa Yesu, ambapo I Yohana inaukiri ubinadamu wake. Vitabu hivi vinaendana!

F. Yohana anaandika katika maneno meupe na meusi (uwili). Hii ni sifa bainifu ya Magombo ya Bahari ya Chumvi na mapotoe ya waalimu wa uongo. Muundo wa fasiri mbili za I Yohana ni wa vitenzi vyote (nuru dhidi ya giza) na mtindo (maelezo hasi hufuatiwa na chanya). Hii ni tofauti kutoka katika injili ya Yohana, ambayo inatumia uwili sambamba (kutoka juu dhidi ya kutoka chini).

G. Ni vigumu kutoa muhtasari wa I Yohana kwa sababu ya Yohana kutumia dhamira zilizojirudirudia. Kitabu kinafanana na pambo la sufi za ukweli zilizofumwa pamoja katika mipangilio inayojirudirudia (kama vile Bill Hendricks, Tapestries of Truth, The Letters of John).

MWANDISHI A. Uandishi wa kitabu cha 1 Yohana ni sehemu ya mjadala juu ya uandishi wa Johannine Corpus —Injili, I

Yohana, II Yohana, III Yohana na Ufunuo.

B. Kuna misingi miwili ya misimamo

Page 340: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

324

1. Utamaduni a. Utamaduni ulikubaliwa kati ya makasisi wa awali wa kanisa kwamba Yohana, mtume aliyependwa,

alikuwa mwandishi wa I Yohana b. Maelezo ya ushahidi wa kanisa la awali

(1) Clement wa Rumi ( 90 B.K.) alifanya vidokezo kwa I Yohana (2) ) Polycarp wa Smirna, Philippians 7 ( 110-140 B.K ) akidondoo 1 Yohana (3) Justin Martyr’s, Dialogue 123:9 ( 150-160 B.K.) akidondoo 1 Yohana (4) Dokezo la I Yohana limefanywa katika maandiko ya

a) Ignatius wa Antiokia (tarehe ya kuandikwa inatia mashaka lakini katika mwanzo wa miaka ya 100 B.K.)

b) Papias wa Hierapolis (aliyezaliwa kati ya 50-60 B.K. na shahidi yapata mwaka 155 B.K.) (5) Irenaeus wa Lyons (130-202 B.K.) aliiona I Yohana kuwa ya Mtume Yohana. Tertullian, mtetezi

wa awali aliyeandika vitabu 50 dhidi ya waasi, mara nyingi aliinukuu I Yohana (6) Maandiko mengine ya kale ambayo yaona uandishi wa Mtume Yohana ni Clement,

Origen na Dionysius wote watatu wa Alexandria, sehemu ya Muratorian (180-200 B.K.) na Eusebius (karne ya tatu).

(7) Jerome (nusu ya pili ya karne ya nne) anathibitisha uandishi wa Yohana lakini anakubali kwamba ulikataliwa na baadhi katika siku zake.

(8) Theodore wa Mopsuestia, Askofu wa Antiokia kutoka mwaka 392-428 B.K. aliukataa uandishi Yohana.

c. Ikiwa Yohana, tunafahamu nini juu ya mtume Yohana? (1) Alikuwa mwana wa Zebedayo na Salome (2) Alikuwa ni mvuvi katika bahari ya Galilaya na ndugu yake, Yakobo (inawezekana walimiliki

mitumbwi kadhaa) (3) Baadhi wanaamini mama yake alikuwa dada yake Mariamu, mama yake Yesu (kama vile

Yohana 19:25; Marko 15:20) (4) Ni dhahiri alikuwa tajiri kwa sababu:

a) Aliajiri wafanyakazi (kama vile Marko 1:20) a) Alikuwa na Mitumbwi kadhaa b) Alikuwa na nyumba katika Yerusalemu (kama vile Mt. 20:20)

(5) Yohana alikuwa na haki ya kuingia katika nyumba ya kuhani mkuu katika Yerusalemu, hii inaonyesha alikuwa baadhi ya mtu mashuhuri (kama vile Yohana 18:15-16)

(6) Alikuwa ni Yohana aliyemtunza Mariamu, mama yake Yesu, alikuwa mwaminifu d. Utamaduni wa kanisa la awali kwa kauli moja unathibitisha kwamba Yohana aliishi zaidi kuliko

mitume wote na baada ya kifo cha Mariamu katika Yerusalemu alihamia Asia ndogo na kuishi Efeso, mji mkubwa katika eneo hilo. Kutoka mji huu alichukuliwa uhamishoni hadi kisiwa cha Patmo (pwani ya bahari) na baadae akaachiliwa na kurudi Efeso (Eusebius anawanukuu Polycarp, Papias na Irenaeus).

2. Elimu ya sasa a. Kundi kubwa la wanazuoni wa sasa wanatambua mfanano kati maandiko yote ya Johannine, hasa

katika tungo, maneno, miundo ya kisarufi. Mfano wake mzuri ni nafasi iliyoachwa ambayo inaelezea maandiko haya: uzima dhidi ya kifo, kweli dhidi ya uongo. Mgawanyo huu wa sehemu mbili zilizo wazi unaweza kuonekana kama maandiko ya siku; magombo ya Bahari ya Chumvi na mwanzo wa maandiko ya mafunuo.

b. Kuna nadharia kadhaa juu ya uhusiano kati ya vitabu vitano vya desturi vinavyodhaniwa kuwa vya Yohana. Baadhi ya makundi yanadai uandishi kwa mtu mmoja, watu wawili, watu watatu, na kadhalika. Inaonekana sehemu ya kukubalika zaidi ni kwamba maandiko yote ya Johannine ni matokeo ya fikra za mtu mmoja, hata kama ilifanywa dhaifu na wanafunzi wake kadhaa.

c. Maelezo yangu mafupi ni kwamba Yohana, miaka ya mtume, aliandika vitabu vitano vyote hadi mwisho wa huduma yake katika Efeso.

3. Hoja ya uandishi ni hoja ya wafasiri wa fasihi, sio uvuvio. Mwisho mwandishi wa maandiko ni Mungu!

Page 341: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

325

TAREHE —Kwa uwazi kabisa hii inahusianishwa na uandishi A. Ikiwa Mtume Yohana aliziandika barua hizi, na hasa I Yohana, tunayoizungumzia wakati mwingine ni

kipindi cha kuhitimisha karne ya kwanza. Hii ingetoa mwanya wa kushamiri kwa mifumo ya mapotoe ya waalimu wa uongo/kifalsafa na pia ingeshabihiana na istirahi ya I Yohana (“watoto wadogo”), ambayo inaonekana kumaanisha mzee kuzungumza na kundi la waamini walio wachanga. Jerome Anasema kuwa Yohana aliishi miaka 68 baada ya kusulibiwa kwa Yesu. Hii inaone kana kushabihiana na utamaduni huu.

B. A.T. Robertson ana fikiri kuwa I Yohana aliiandika barua hii kati ya mwaka 85-95 B.K, ambapo Injili iliandikwa mnamo mwaka 95 B.K.

C. Kitabu cha The New International Commentary Series on I John na I. Howard Marshall mwandishi wa kitabu hiki anadai kwamba tarehe kati ya mwaka 60-100 B.K. i karibu kama wanazuoni wa sasa wangependa kuikadiria tarehe ya maandiko ya Yohana.

WAPOKEAJI A. Utamaduni unaeleza kwamba kitabu hiki kiliandikwa kwa ajili ya Jimbo la Kirumi la Asia Ndogo

(Uturuki magaharibi, pamoja na Efeso kuwa eneo lake la kimakazi.

B. Barua hii inaonekana kuwa imetumwa kwa kudi maalumla makanisa ya Asia Ndogo ambayo yalikuwa yakikumbwa na matatizo ya kukabiliwa na waalimu wa uongo (kama Wakolosai na Waefeso), kwa upekee (1) unyeyekevu wa kimapotoe ambao uliukanusha ubinadamu wa Kristo, lakini huu uliukiri uungu wake na (2) mapotoe ya wenye kuiruhusu anasa waliotenga theolojia toka mwenendo/maadili.

C. Augustine (karne ya nne B.K.) anasema kuwa hiki kiliandikwa kwa ajili ya Parthians (Babeli). Huyu anafuatishwa na Cassiodrus (karne ya sita ya kale B.K.). Huenda hili lilitokana na mkanganyiko wa kifungu “mteule”, na kifungu, “mteule hapa Babeli,” ambacho kinatumika katika I Petro 5:13 na II Yohana 1.

D. The Muratorian Fragment, orodha ya kale ya kisheria ya vitabu vya Agano Jipya vilivyoandikwa kati ya mwaka 180-200 B.K. katika Rumi, vinaeleza kwamba bara hii iliandikwa “baada ya nasaha za wanafunzi wenzakoe na maaskofu” (katika Asia Ndogo).

MAFUNDISHO YA UONGO A. Barua yenyewe kwa uwazi ni mapambano dhidi ya aina ya mafundisho ya uongo (kama vile “Kama

tunasema. . .” 1:6 na kuendelea na “asemaye . ..” 2:9; 4:20 [karipio]).

B. Tunaweza kujifunza baadhi ya kanuni mafundisho ya uasi kwa kutumia ushaidi wa ndani kutoka 1 Yohana. 1. kulipinga umbo mwili la Yesu Kristo 2. kuupinga upekee wa Yesu Kristo katika wokovu 3. kutoyaishi maisha ya Kikristo kwa usahihi 4. mkazo juu ya maarifa (mara nyingi ni ya siri) 5. mwelekeo wa kujienga

C. Mpangilio wa karne hii ya kwanza

Ulimwengu wa Kirumi wa karne ya kwanza ulikuwa wa wakati wa kiuchaguzi kati ya pande za Mashariki na Magharibi. Ile miungu ya Kiyunani na mahekalu ya miungu ya Kirumi vyote hivi vilikuwa na sifa mbaya. Dini za siri zilikuwa maarufu sana kwa sababu ya mkazo wa uhusiano binafsi pomoja na Uungu na maarifa ya siri. Falsafa ya Kiyunani ya kiulimwengu ilikuwa maarufu na kushamiri pamoja na

Page 342: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

326

mitazamo mingine ya kiulimwengu. Katika ulimwengu huu wa uchaguzi baadaye dini ilikuja kuwa mbali na imani ya Kikristo (Yesu ndiye njia pekee ya kwenda kwa Mungu, kama vile Yohana 14:6). Kwa vyo vyote ilivyo historia halisi ya uasi, hii ilikuwa juhudi ya kuufanya Ukristo kuwa katika ufinyo na ukubalifu wa maarifa kwa hadhira Kiyunani Kirumi.

D. Chaguzi yakini za kundi wanamapotoe linalo linaloelezwa na Yohana 1. Mapotoe ya awali

a. Mafundisho ya msingi ya mapotoe ya karne ya kwanza yanaonekana kuwa na mkazo juu ya uwili wa (milele) kithiolojia kati ya roho na jambo husika. Roho (Mungu Mkuu) alikuwa akifikiliwa kuwa mwema, ambapo suala lilikuwa ouvu wa kiurithi. Ukinyume huu unashahabiana na wazo la Plato dhidi ya mambo yanayoonekana, ya kimbingu dhidi ya kidunia, yasiyoonekana dhidi ya yaonekanayo. Pia kulikuwa na mkazo mkali juu ya umuhimu wa maarifa ya siri (neno la siri au mfumo wa sheria uliowekwa ambao uliiruhusu nafsi kupenya katika ulimwengu wa kimalaika [aeons] hadi kwa Mungu mkuu) ulio muhimu kwa ajili ya wokovu.

b. Kuna mifumo miwili ya mapotoe ya awali ambayo kwa uwazi ingekuwa katika historia ya I Yohana (1) Mapotoe ya kiutiifu, yenye kuukana utu wa Yesu kwa sababu ya suala la uovu (2) Mapotoe ya Cerinthian, yenye kumtambua Kristo kama mmoja wa aeons wengi au

viwango vya kimalaika kati ya mungu mwema mkuu na suala la uovu. Huyu ni “Roho wa Kristo” aliyemshukia Yesu wakati wa ubatizo na kumwacha kabla ya kusulibiwa kwake.

(3) wa makundi haya mawili ambayo baadhi yao yalikuwa na uzoefu wa kujinyima anasa (ikiwa mwili unataka, huo ni uovu), wangine ni wale wenye kuruhusu anasa (ikiwa mwili unataka, utimizie). Hakuna ushahidi ulioandkwa kuhusu uendelezaji wa mfumo wa mapotoe katika karne ya kwanza. Hii si hadi katikati mwa karne ya pili ambapo ushahidi ulioandikwa ulionekana. Kwa habari zaidi kuhusu “mapotoe” angalia

(a) The Gnostic Religion na Hans Jonas, kiliochochapishwa na Beacon Press (b) The Gnostic Gospels na Elaine Pagels, kilichochapishwa na Random House (c) The Nag Hammadi Gnostic Texts na Biblia na Andrew Helmbold

2. Ignatius anapendekeza chanzo kingine yakini cha uasi katika maandishi yake kwa the Smyrnaeans iv-v. Hawa uliupinga utu wa Yesu na maisha ya anasa.

3. Bado pamoja na hayo uwezekanao wa chanzo cha uasi ni Meander wa Antiokia, anayejulikana kutokana na maandishi ya Irenaeus, Against Heresies XXIII. Huyu alikuwa mfuasi wa Simon Msamaria na mtetezi wa maarifa ya siri.

E. Mafundisho ya Uongo Siku za leo 1. Hii roho ya uasi ipo katika siku hizi zetu pale watu wanapojaribu kuichanganya kweli ya Kikristo

na mifumo mingine ya mawazo. 2. Hii roho ya uasi I pamoja nasi katika siku hizi zetu pale watu wanapoweka mkazo “sahihi” wa

mafundisho katika kuutenga mbali uhusiano binafsi na maisha ya imani. 3. Hii roho ya uasi ipo katika siku hizi zetu pale watu wanapougeuza Ukristo kuwa katika maarifa ya

wasomi waliojitenga. 4. Hii roho ya uasi ipo katika siku zetu pale watu wanapolibadilisha tendo la kujinyima anasa au

kuruhusu anasa.

KUSUDI A. Huu ulitazamia waamini

1. kuwapa furaha (kama vile 1 Yohana 1:4) 2. kuwatia maoyo ili waishi maisha ya ki-Mungu (kama vile 1:7; 2:1)

Page 343: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

327

3. kuwaamrisha (na kuwakumbusha) kupendana (kama vile 4:7-21) na si ulimwengu (kama vile 2:15-17).

4. Kuwahakikishia juu ya wokovu wao katika Kristo (kama vile 5:13)

B. Huu ulikuwa na mafundisho yaliyowaelekea waamini 1. kuupinga upotofu wa kuutenga Uungu wa Yesu na ubinadamu wake 2. kuupinga upotofu wa kujitenga kiroho katika usomi pasipo kuyaishi maisha ya ki-Mugu 3. kuupinga upotofu kwamba mtu aweza kuokolewa kwa kuwatenga wengine

MZUNGUKO WA KWANZA WA USOMAJI

Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwa tafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri.

Hivyo, soma kitabu kizima cha Kibiblia kwa mkao mmoja. Taja maudhui kuu katika kitabu kizima kwa maneno yako mwenyewe.

1. Dhamira ya kitabu kizima 2. Aina ya fasihi iliyotumika (uwasilishaji)

MZUNGUKO WA PILI WA USOMAJI

Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwa tafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri.

Hivyo, somakitabu kizima cha kibiblia kwa mara ya pili kwa mkao mmoja. Ainisha masomo makuu na elezea somo kwa sentensi moja.

1. Mada ya sehemu ya kwanza ya fasihi 2. Mada ya sehemu ya pili ya fasihi 3. Mada ya sehemu ya tatu ya fasihi 4. Mada ya sehemu ya nne ya fasihi 5. N.k.

Page 344: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

328

1 YOHANA 1:1-2:2

MIGAWANYO YA AYA YA TAFSIRI ZA KISASA*

UBS4 NKJV NRSV TEV NJB Neno la uzima Kile kilichosikika, Utangulizi Neno la uzima Neno lililofanyika Kuonekana na mwili na kushiriki Kuguswa, Baba na Mwana 1:1-4 1:1-4 1:1-4 1:1-4 1:1-4 Mungu ni Nuru Msingi wa ushirika Mtazamo mzuri Mungu ni Nuru Kutembea katika Na Yeye kuhusu dhambi Nuru (1:5-2:28) 1:5-10 1:5-2:2 1:5-10 1:5-7 1:5-7 Sharti la kwanza Kutengana na dhambi 1:8-10 1:8-2:2

* Ingawa hazijavuviwa, migawanyo ya aya ndiyo ufunguo wa kuelewa na kufuatilia kusudio la asili la mwandishi. Kila tafsiri ya kisasa imegawanya na kufanya muhtasari wa aya. Kila aya ina mada kuu, kweli au wazo. Kila toleo limebeba hiyo mada kwa namna yake ya pekee. Unaposoma maandiko ya mwandishi jiulize ni tafsiri ipi inawiana na uelewa wako wa somo na mgawanyo wa mistari. Katika kila sura lazima tusome Biblia kwanza na kujaribu kutambua somo (aya), kisha tulinganishe na matoleo ya kisasa. Ni pale tunapoelewa kusudi la asili la mwandishi kwa kufuata mantiki yake na jinsi alivyojieleza tunaielewa kwa Biblia kiukweli. Ni mwandishi wa asili tu aliyevuviwa —wasomaji hawana haki ya kurekebisha ujumbe. Wasomaji wa biblia wana wajibu wa kutumia ukweli uliovuviwa kwenye siku na maisha yao. Fahamu kwamba maneno yote ya kiufundi na vifupisho vimefafanuliwa kwa kirefu kwenye nyaraka zifuatazo: Maelezo Fasaha Ya Muundo Wa Sarufi Za Kiyunani(Brief Definitions of Greek Grammatical Structure),Uhakiki Wa Tofauti Za Kiandishi(Textual Criticism),Ufafanuzi na Maelezo ya Kimaandiko(Glossary).

MZUNGUKO WA TATU WA USOMAJI KUFUATILIA KUSUDIO LA ASILI LA MWANDISHI KATIKA NGAZI YA AYA Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwatafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Aya ya kwanza 2. Aya ya pili 3. Aya ya tatu 4. N.k

USURI WA KITHEOLOJIA

A. Kifungu hiki chahusiana na utangulizi wa injili ya Yohana (1:1-18, kabla ya uumbaji halisi), ambao unahusiana na Mwa. 1:1 (uumbaji halisi). Lakini, hapa inahusiana na mwanzo wa huduma ya hadhara ya Yesu.

B. Msisitizo upo katika

Page 345: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

329

1. Ubinadamu kamili wa Yesu Kristo a. hali ya kuendelea inayohusiana na mifumo ya mwanadamu, sauti, kugusa (kama vile. 1

Yohana 1:1,3). Yesu alikuwa binadamu kamili na mwenye mwili. b. nyadhifa kamili za Yesu

(1) neno la uzima (kama vile. 1 Yohana 1:1) (2) Mwanaye Yesu Kristo (kama vile. 1 Yohana 1:3)

2. Uungu wa Yesu Mnazareti a. Kuwepo kabla ya uumbaji (1 Yohana 1:1,2) b. Kufanyika mwanadamu (1 Yohana 1:2)

Kweli hizi zinaelekezwa kinyume na mafundisho ya mafumbo ya walimu wa uongo kuhusu mtazamo wa ulimwengu.

SINTAKSIA

A. 1 Yohana 1:1-4 1. 1 Yohana 1:1-3a inaunda sentensi kwa Kiyunani. 2. Kitenzi kikuu "tangaza" kiko katika 1 Yohana 1:3. Msisitizo uko kwenye maudhui ya mahubiri ya kitume. 3. Kuna vishazi rejeshi vinne katika 1 Yohana 1:1 ambavyo vimewekwa mbele ya vishazi vyao kwa

msisitizo. a. "kile kilichokuwa toka mwanzo" b. "kile tulichokwisha kusikia" c. “kile tulichokwisha kuona kwa macho yetu" d. "kile kilichokwisha kukitazama na kukigusa kwa mikono yetu"

4. 1 Yohana 1:2 yaonekana kuwa mabano mengine kwa Kristo kufanyika mwanadamu. Ule ukweli kwamba kisarufi ni gumu unafanya kuvuta umakini!

5. 1 Yohana 1:3 na 4 zinaeleza makusudi ya tangazo la kitume la Yohana: ushirika na furaha. Taarifa za ushahidi wa kuona kwa macho ya mitume zilikuwa moja ya vipimo vya kutoa maamuzi ili kukubalika kama kitu kitakatifu.

6. Angalia mtiririko wa njeo za vitenzi katika 1 Yohana 1:1 a. isiyotimilifu (kuwepo kabla ) b. timilifu, timilifu ( kweli wa kudumu) c. wakati uliopita usio timilifu (mifano dhahiri)

B. 1 Yohana 1:5-2:2

1. Viwakilishi katika 1 Yohana 1:5-2:2 vina maana zaidi ya mbili, lakini nadhani karibu vyote ila 1 Yohana 1:5, vinamruhusu Baba (inafanana na Efe. 1:3-14)

2. "ikiwa" zote ni sentensi shurutishi daraja la tatu zinazozungumzia utendaji usiodhihirika. 3. Iko tofauti yenye umuhimu ya kithiolojia kati ya

a. njeo ya kitenzi ya wakati uliopo dhidi ya wakati uliopita usio timilifu katika kuhusiana na "dhambi" b. hali ya umoja na hali ya wingi, "dhambi" dhidi ya "dhambi nyingi"

MAFUNDISHO YA UONGO

A. Madai ya walimu wa uongo yanaweza kuonekana katika 1 Yohana 1:1:6,8,10; 2:4,6,9. B. 1 Yohana 1:5-10 yafanana na ile hali ya kithiolojia ya kujaribu kutenga kumjua Mungu (theolojia) kutoka

kumfuata Mungu (maadili). Inawakilisha mafundisho yanayosisitiza sana elimu ya Mambo yaliyofichika. Wale wanaomjua Mungu watafichua tabia yake katika matendo ya maisha yao.

C. 1 Yohana 1:8-2:2 lazima ichukuliwe katika uwiano na 3:6-9. Ni pande mbili za sarafu moja. Pengine zinakanusha makosa mawili tofauti: 1. kosa la kitheolojia (hakuna dhambi) 2. kosa la kimaadili (dhambi sio jambo la kujali)

Page 346: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

330

D. 1 Yohana 2:1-2 ni jaribio la kuweka uwiano kati ya kuichukulia dhambi kwa wepesi mno (kinyume na sheria) na tatizo linalojirudia la hali ya kuhukumu kwa Wakristo, kutetea sheria za kiutamaduni, ama kujikana kwa kuachana na aina zote za anasa kwa ajili ya dini).

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) 1 YOHANA 1:1-4 1 Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima; 2 (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu); 3 hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo. 4 Na haya twayaandika, ili furaha yetu itimizwe.

1:1 "Lile" Kitabu kinaanza na kiwakilishi tasa. Kinazungumzia mionekana yenye pande mbili za ujumbe wa Mungu ambayo ni

1. Ujumbe kuhusu Yesu 2. Ubinadamu wa Yesu mwenyewe jinsi mtu atakavyoishi

Injili ni ujumbe, mtu, na jinsi mtu anavyoishi.

◙ “lililokuwako” Hii ni kauli isiotimilifu inayoarifu. Inadhihilisha kuwepo kwa Yesu kabla ya uumbaji yaani ni wazo linalojirudia rudia katika maandiko ya Yohana (yaani, ni wazo linalojirudia katika maandiko ya Yohana, 1 Yohana 1:2; Yohana 1:1,15; 3:13; 8:57-58; 17:5). Hii ilikuwa njia moja ya kudhihirisha Uungu wake. Yesu anamfunua Baba kwa sababu amekuwa pamoja Baba tangu mwanzo.

◙ "tangu mwanzo” Huo ulikuwa ni msemo usio dhahiri uliokuwa wa hakika katika Mwanzo 1 na Yohana 1, lakini

hapa inahusu mwanzo wa huduma ya Yesu ya hadharani (tazama Mada Maalumu: Archē katika Yohana 1:1). Kuja kwa Yesu haukuwa "mpango B." Injili wakati wote ilikuwa mpango wa Mungu wa ukombozi (kama vile Mwa. 3:15; Matendo 2:23; 3:18; 4:28; 13:29). Aya hii katika muktadha huu inahusu mwanzo wa mitume kumi na wawili kukutan na Yesu ana kwa ana. Yohana kutumia dhana ya "mwanzo" (archē) maya nyingi. Matukio mengi zaidi yamegawanyika katika makundi mawili hasa kimsingi. 1. toka uumbaji

a. Yohana 1:1,2 (Yesu pale mwanzoni) b. Yohana 8:44; 1 Fal. 3:8 (Shetani muuaji na mwongo tangu mwanzo) c. Ufu. 3:14; 21:6,12 (Yesu mwanzo na mwisho)

2. Tangu mwanzo wa kufanyika mwili kwa Yesu na huduma a. Yohana 8:25; 1 Yohana 2:7 [mara mbili]; 3:11; 2 Yohana 5,6 (mafundisho ya Yesu) b. Yohana 15:27; 16:4 (pamoja na Yesu) c. 1 Yohana 1:1 (tokea mwanzo wa huduma ya hadhara ya Yesu) d. 1 Yohana 2:13,24 [mara mbili] (toka imani yao katika yesu) e. Yohana 6:64 (toka kumkataa kwao Yesu)

3. Muktadha #2

MADA MAALUMU: YOHANA 1 IKILINGANISHWA NA 1 YOHANA 1

Injili Waraka

Hapo Mwanzo (1:1,2) Neno (logos) (1:1) Uzima (zōē) (1:4)

Kutoka mwanzo (1:1) Neno (logos) (1:1) Uzima (zōē) (1:1,2)

Page 347: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

331

Nuru katika Yesu (1:4) Nuru ilifunuliwa (1:4) Giza (1:5) Ushuh da kwa nuru (1:6-8) Wanadamu waliletwa kwa Mungu (1:7,12-13) Tazama historia yake (1:14)

Nuru katika Mungu (1:5) Nuru ilifunuliwa (1:5) Giza (1:5) Ushuhuda kwa nuru (1:3,5) Wanadamu waliletwa kwa Mungu (1:3) Tazama utukufu wake (1:1-3)

◙ "Sisi” Inadokeza ushuhuda wa Mitume ambao ni wa kiujumla (yaani, waandishi wa Agano Jipya).Ushuhuda huu wa pamoja ni uanishaji wa 1 Yohana. Umetumika zaidi ya mara 50. Baadhi ya watu wanaona hiki kiwakilishi kama kinawarejea wale wenye "desturi za Yohana." Hii ingedokeza kuhusu walinzi au walimu wa mwonekano wa kithiolojia wa kipekee.

◙ "tulilolisikia. . . tulilolitazama" Hapa zote ni kauli timilifu tendaji zinazoarifu ambavyo zinasisistiza matokeo yanayodumu.Yohana alikuwa anathibitisha ubinadamu wa Yesu kwa matumizi ya kurudia rudia ya hali endelevu inavyohusiana na milango mitano ya fahamu katika 1 Yohana 1:1,3. Hapa anadai kuwa shahidi wa macho katika maisha pamoja na mafundisho ya Yesu wa Nazareti.

◙ "tuliloliona . . . ikalipapasa" Hivi zote ni kauli zinazo arifu za wakati uliopita usio timilifu. "Tuliloliona" inamaanisha "uchunguzaji wa karibu" (kama vile. Yohana 1:14), "gusa" inamaanisha "chunguza kwa karibu kwa kugusa" (kama vile Yohana 20:20,27; Luka 24:39). Neno la Kiyunani kwa "kugusa" au "kubeba jambo" (psēlaphaō) linapatikana kwenye aya mbili tu katika Agano Jipya: hapa na katika na Luka 24:39. Katika Luka limetumika kuhusu kukutana na Yesu baada ya ufufuo. 1 Yohana unalitumia kwenye mantiki hiyo hiyo.

◙ “Neno la uzima" Matumizi ya neno logos ulitumika kugusa umakini wa walimu wa uongo wa Kiyunani, kama kwenye utangulizi wa injili ya Yohana (kama vile 1 Yohana 1:1). Neno hili lilitumika kwa upana katika falsafa ya Kiyunani. Pia lilikuwa na msingi dhahiri katika maisha ya Waebrani (kama vile Utangulizi wa Yohana 1, C). Aya hii hapa inahusu kilichomo ndani ya injili pamoja na mtu wa injili pamoja na mtu wa injili. 1:2 Aya hii ni mabano yanayoelezea "uzima."

◙ "uzima" "Zōē" (1 Yohana 1:2 mara mbili) limetumika bila kubadilika katika maandiko ya Yohana kwa maisha ya kiroho, ufufuo wa uzima, maisha ya uzao mpya, au Maisha ya Mungu (kama vile Yohana 1:4; 3:15,36 [mara mbili]; 4:14,36; 5:24 [mara mbili],26 [mara mbili],29,39,40; 6:27,33,35,40,47,48,51,53,54,63,68; 8:12; 10:10,28; 11:25; 12:25,50; 14:6; 17:2,3; 20:31; 1 Yohana 1:1,2; 2:25; 3:14-15; 5:11,12,13,16,20). Yesu alijiita mwenyewe "uzima" (kama vile Yohana 14:6).

◙ "ulidhihirika" Kitenzi hiki kimetumika mara mbili kwenye aya hii na zote ni kauli tendewa elekezi ya wakati uliopita usio timilifu. Irabu tendewa mara nyingi hutumika kuhusu hali ya kuharakisha ya Mungu Baba. Neno hili (phaneroō) hudokeza "kuleta nuruni kile kilichokuwa tayari." Hili lillikuwa neno alilolipenda Yohana (kama avile Yohana 1:31; 3:21; 9:3; 17:6; 1 Yohana 1:2 [mara mbili]; 2:19; 3:5,8,10; 4:9). Njeo ya wakati uliopita usio timilifu unasisitiza Yesu kufanyika mwili (kama vile Yohana 1:14), ambapo walimu wa uongo walipinga.

◙ "twashuhudia" Hii inahusu uzoefu binafsi wa Yohana (yaani, kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo). Neno hili mara nyingi lilitumika kwenye ushahidi katika mahakama. Tazama MADA MAALUMU: USHUHUDA KUHUSU YESU katika Yohana 1:8

Page 348: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

332

◙ "kuwahubiri" Hii inahusu ushuhuda wenye mamlaka wa Yohana (yaani, kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo) uliofunuliwa na kuwekewa kumbukumbu kwenye mahubiri na maandiko yake. Hiki ndicho Kitenzi kikuu cha 1 Yohana 1:1-3. Kimerudiwa mara mbili (1 Yohana 1:2 na 1 Yohana 1:3).

◙ "uliokuwa kwa Baba" kama 1 Yohana 1:1, Huu ni udhihirisho wa Yesu kuwepo kabla ya uumbaji. Uandikaji wa aya ni sawa na Yohana 1:1. Mungu amefanyika kuwa mwanadamu (kama vile Yohana 1:14). Kumjua Yesu ni kumjua Mungu (kama vile Yohana 14:8-11). Huu ni mfano sahihi wa Yohana wa pande mbili. 1:3 "tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi" Hiki ni kishazi rejeshi cha tano, ambacho kinarudia tena wazo la 1 Yohana 1:1 baada ya vibano vya 1 Yohana 1:2. Kinarudiwa Kitenzi cha utambuzi unaopatikana katika 1 Yohana 1:1.

◙ "twawahubiri na ninyi" Hiki ndicho kitenzi kikuu katika 1 Yohana 1:1-3. Ni kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo. Kumjua Mungu kunahitaji kuwa na ushirika na watoto wake!

◙ "ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi" Hiki ni kishazi nia (hina) ikiwa na kauli tendaji tegemezi ya wakati uliopo.

Kusudi la Biblia lililotamkwa lilikuwa kwamba wale ambao hawakumsikia wala kumwona Yesu waweze kuokoka kutokana na ushuhuda wa mitume (kama vile Yohana 17:20; 20:29-31). Ni ushirika huu katika neema ya ufunuo ndipo inaletwa "furaha," "amani," na"uhakika"! kanisa ni jumuiya ya waaminio, mwili wa waaminio! Injili ni kwa ajili ya ulimwengu wote.

MADA MAALUM: KOINŌNIA (USHIRIKA)

Neno "ushirika" (koinōnia) unamaanisha 1. Ushirika wa karibu na mtu

a. na Mwana (kama vile 1 Kor 1:9; 1 Yohana 1:6) b. na Roho (kama vile. 2 Kor. 13:14; Flp. 2:1) c. na Baba na Mwana (kama vile. 1 Yohana 1:3) d. na ndugu wa agano wa kiume/kike (kama vile. Matendo 2:42; 2 Kor. 8:23; Gal. 2:9; Filemoni aya.

17; 1 Yohana 1:3,7) e. usio na uovu (kama vile. 2 Kor. 6:14)

2. ushirika wa karibu na vitu ama makundi a. na injili (kama vile Flp. 1:5; Philemon aya. 6) b. na damu ya Kristo (kama vile 1 Kor. 10:16) c. usio na giza (kama vile 2 Kor. 6:14) d. na mateso (kama vile. 2 Kor. 1:7; Flp. 3:10; 4:14; 1 Pet. 4:13)

3. Zawadi ama changizo zilizotolewa kwa mtindo wa ukarimu (kama vile Rum. 12:13; 15:26; 2 Kor. 8:4; 9:13; Flp. 4:15; Ebr. 13:16)

4. Kipawa cha Mungu cha neema, kupitia Kristo kinachorejesha ushirika wa mwanadamu na yeye na ndugu zake wa kiume na kike

Hii inatangaza uhusiano wa ulalo (mwanadamu kwa mwanadamu) ambao unaletwa kwa uhusiano wa kweli (mwanadamu na muumbaji). Pia unasisitiza hitaji na furaha ya jumuiya ya Kikristo (yaani, Ebr. 10:25).

MADA MAALUM: UKRISTO NI JAMII MOJA

A. Matumizi ya wingi wa sitiari ya Paulo na Petro kwa watu wa Mungu B. Mwili (kama vile. 1 Kor. 12:12-20) C. Shamba (kama vile. 1 Kor. 3:9)

Page 349: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

333

D. jengo (kama vile 1 Pet. 2:4-5) E. Neno "mtakatifu" kila wakati ni wingi (isipokuwa Flp. 4:21, lakini hata pale pia ni kundi) F. Msisitizo wa matengezo wa Martin Luther kuhusu "ukuhani wa aaminiye" (yaani, uwezo wa nafsi) ni

kuchukulia jambo kibiblia. Kiuhalisia Biblia husema juu ya "ukuhani wa waaminio” (kama vile Kut. 19:6; 1 Pet. 2:5,9; Ufu. 1:6).

G. Kila aaminiye amejaliwa kipawa kwa manufaa ya wote (kama vile 1 Kor. 12:7) H. Ni katika kushirikiana tu ndipo watu wa Mungu wanaweza kupata matokeo. Huduma ni kushirikiana

pamoja (kama vile. Efe. 4:11-12).

◙ "na Baba. . . na Mwana" Aya hizi ziko sambamba kisarufi kwenye kihusishi na kibainishi chenye ukomo. Syntaksi hii inathibitisha ulinganifu na Uungu wa Yesu (kama vile Yohana 5:18; 10:33; 19:7). Haiwezekani kuwa na Baba (Mungu wa juu) bila mwana (Mungu aliyefanyika mwanadamu) kama vile walimu wa uongo wanavyoonesha bila kutaja (kama vile 1 Yohana 2:23; 5:10-12). Ushirika huu wa Baba na Mwana unafanana na ile aya ya wote wawili kukaa ndani ya Yohana 14:23. 1:4 "Na haya twayaandika" Hii ingeweza kuhusika na kitabu chote ama hasa hasa kwa 1 Yohana 1:1-3. Utata wa namna hii unaonekana katika 1 Yohana 2:1. Mwandishi anatamka moja ya makusudi yake hapa (kama vile 1 Yohana 2:1).

◙ "ili furaha yetu itimizwe" Hii ni kauli timilifu tendewa tegemezi yenye mafumbo (kama vile Yohana 15:11;

16:20,22,24; 17:13; 2 Yohana 12; 3 Yohana 4). Furaha ya waaminio ilifanywa timilifu kwa ushirika wa Baba, Mwana, na Roho. Hiki kilikuwa ishara iliyoonekana kwa mvurugano wa waalimu wa uongo.Makusudi ya Yohana yaliyo tamkwa ya kuandika kwa kitabu hiki ni:

1. Ushirika wa Mungu na watoto wake 2. Furaha 3. uhakika 4. Kwa upande hasi kusudi lake lilikuwa kuwawezesha waaminio kupambana na thiolojia ya uongo

mafundisho ya mafunuo ya uongo Kuna kuhitilafiana katika Kiyunani kwenye aya hii kati ya

1. "furaha yetu," MSS א, B, L; NASB, NRSV, NJB, REB, NIV 2. "furaha yenu," MSS A, C; NKJV

UBS4 inapendelea #1. Je "yetu" inahusika na ushuhuda wa macho wa mitume ama na waaminio? Kwa sababu ya msukumo wa 1 Yohana kuelekea uhakika wa Ukristo, nachukulia kwamba inaelekezwa kwa waaminio wote.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) 1 YOHANA 1:5-2:2 5Na hii ndiyo habari tuliyoisikia kwake, na kuihubiri kwenu, ya kwamba Mungu ni nuru, wala giza lo lote hamna ndani yake. 6 Tukisema ya kwamba twashirikiana naye, tena tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli; 7 bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote. 8 Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. 9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. 10 Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu.

1:5 "habari tuliyoisikia" Kiwakilishi "sisi" chahusika na Yohana na wasikilizaji na wale walioshuhudia kwa macho na wafuasi wa Yesu kipindi cha uhai wake hapa duniani. Yohana anasema moja kwa moja na wasomaji wake ("ninyi") katika 1 Yohana 2:1, labda anayahusisha makanisa ya Asia ndogo. Kitenzi "kusikia" ni kauli timilifu tendaji elekezi. Hii inaaksi waziwazi neno linalo rudiwa rudiwa linalohusishwa na milango ya fahamu katika 1 Yohana 1:1-4. Kwa namna fulani huyu ndiye Mtume Yohana akithibitisha uwepo wake kwenye vipindi vya mafundisho ya Yesu. Sio yake mwenyewe! Yawezekana pia kwamba kwa namna ya upekee wa kauli "Mimi ndimi" kwenye injili, zilikuwa kumbukumbu za Yohana za mafundisho ya Yesu ya faragha.

Page 350: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

334

◙ "kwake" Toka kwake" ni Kiwakilishi pekee katika sehemu yote ya 1 Yohana 1:5-2:2 kinachomhusu Yesu. Yesu alikuja kumfunua Baba (kama vile. Yohana 1:18). Katika kuzungumza kithiolojia, Yesu alikuja kwa maksudi matatu.

1. Kumfunua Baba (kama vile. 1 Yohana 1:5) 2. Kuwapa waaminio mfano wa kufuata (kama vile. 1 Yohana 1:7) 3. Kufa badala ya mwanadamu mwenye dhambi (kama vile. 1 Yohana 1:7; 2:2)

◙ "Mungu ni nuru" Hakuna Kibainishi.Hii inasisitiza asili ya ya Mungu ya kiufunuo na mwonekano wake kimaadili (kama vile Zab.27:1; Isa. 60:20; Mika 7:8; 1 Tim. 6:16; Yakobo 1:17). Walimu wa uongo waliofundisha uongo kuhusu siku za mwisho walisisitiza kwamba nuru ilihusu elimu, bali Yohana anasisitiza kwmba inahusu pia usafi kimaadili. "Nuru" na "giza" lilikuwa neno lililotumika mara nyingi (kutumia kwa njia mbili kwa neno hili kuilipatikana katika magombo ya Bahari ya Chumvi na katika mafundisho ya mwanzoni kuhusu siku za mwisho. Yalihusisha mwili kati ya wema na uovu (yaani, Yohana 1:5; 8:12; 12:46) yumkini pande mbili za mafunuo ya uongo juu ya roho na umbo. hili ni mojawapo ya matamko ya Yohana ya kithiolojia mepesi lakini ya ndani sana kuhusu uungu. Mengine ni (1) "Mungu ni pendo" (kama vile 1 Yohana 4:8, 16) na (2) "Mungu ni roho" (kama vile Yohana 4:24). Familia ya Mungu, kama Yesu (kama vile Yohana 8:12; 9:5), lazima kuaksi tabia yake (kama vile Mt. 5:14). Maisha haya yaliyobadilika ya upenndo, msamaha, na utakatifu ni mojawapo ya ushuhuda wa kubadilika kwa kweli.

◙ "wala giza lo lote hamna ndani yake" Hii ni kanushi mara mbili kwa ajili ya msisitizo. Tabia ya Mungu isiyobadilika (kama vile. 1 Tim. 6:16; Yakobo 1:17; Zab. 102:27; Mal. 3:6). 1:6 "Tukisema" Hii ni moja ya baadhi ya sentensi shurutishi daraja la tatu ambayo inahusu madai ya walimu wa uongo (kama vile 1 Yohana 1:8, 10; 2:4,6,9). Matamko haya ndiyo ya pekee kutambua matamko ya waalimu wa uongo. Yanaonekana kuwa ya (wapokeaji) wa mwanzo wa mafunuo ya uongo. Mbinu ya fasihi ya anayepaswa kuwa mpinzani inaitwa kupingwa kwa kila jambo. Ilikuwa njia ya kuweka ukweli kwa mtindo wa swali/jibu. Inaweza kuonekana wazi wazi katika (kama vile Mal. 1:2,6,7,12; 2:14,17; 3:7,14) na Warumi (kama vile Rum. 2:3,17,21-23; 3:1,3,7-8,9,31; 4:1; 6:1; 7:7).

◙ "twashirikiana naye" Waasi walidai kwamba ushirika ulikuwa unaruhusu elimu tu. Huu ulikuwa mwonekano wa falsafa ya Kiyunani kutoka kwa Pilato. Lakini, Yohana anatamka kwamba Wakristo lazima waishi maisha ya mfano wa Kristo (kama vile 1 Yohana 1:7; Law. 19:2; 20:7; Mt. 5:48).

◙ "tukienenda gizani" "Kuenenda" ni kauli tendaji tegemezi ya wakati uliopo. Hii ni sitiari ya kibiblia inayoeleza waziwazi mtindo wa maisha ya uadilifu (kama vile Efe 4:1,17; 5:2,15). Mungu ni nuru bila giza. Watoto wake lazima wafanane na yeye (kama vile Mt. 5:48).

◙ "twasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli" Hizi zote ni njeo za vitenzi vya wakati uliopo. Yohana anaita aina kadhaa ya watu wa dini kuwa waongo (kama vile 1 Yohana 1:10; 2:4,22; 4:20; Isa. 29:13). Matendo ya mfumo wa maisha kwa kweli huufunua moyo (kama vile Mathayo 7). Tazama Mada Maalumu: Kweli (dhana) katika maandiko ya Yohana katika Yohana 6:55 1:7 "bali tukienenda nuruni" Hii ni njeo ya wakati uliopo ambayo inayosisitiza kitendo kinachoendelea. "Enenda" ni sitiari ya Agano Jipya kwa maisha ya Kikristo (yaani, Efe. 4:1,17; 5:2,15). Chunguza mara ngapi "enenda" na vitenzi vya wakati uliopo vinahusianishwa na maisha ya Kikristo. Kweli ni kitu kinachoishi. Sio tu kitu tunacho kijua! Kweli ni dhana kuu katika Yohana. Tazama Mada Maalumu: "Kweli" (neno) katika maandiko katika Yohana 6:55 na Yohana 17:3

Page 351: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

335

◙"kama yeye alivyo katika nuru" Waaminio wapaswa kufikiri na kuishi kama Mungu (Kama vile Mt. 5:48). Inatupasa kuaksi tabia Yake kwa ulimwengu uliopotea. Wokovu ni urejesho wa sura ya Mungu (yaani, Mwa. 1:26,27), iliyoharibiwa kwenye anguko la Mwanzo 3.

◙"twashirikiana sisi kwa sisi" Neno ushirika ni mtajo wa Kiyunani wa neno “koinōnia, ambao unamaanisha kushiriki maisha ya Yesu (Tazama Mada Maalumu katika 1 Yohana 1:3). Ukristo umejengwa juu ya mwamini kushiriki maisha ya Yesu. Tukikubali maisha yake katika msamaha, lazima tukubali huduma yake ya upendo (kama vile 1 Yohana 3:16). Kumjua Mungu sio ukweli wa kinadharia tu, bali kuna anzisha ushirika na maisha ya utumwa. Lengo la Ukristo sio mbingu peke yake tunapokufa bali kufanana na Yesu sasa (kama vile. 1 Yohana 4:20-21 pia Mt. 5:7; 6:14-15; 18:21-35)

◙ "damu yake Yesu" Hii inahusisha kifo cha kujitoa sadaka cha Yesu Kristo (kama vile Isa. 52:13-53:12; Marko 10:45; 2 Kor. 5:21). Inafanana na 1 Yohana 2:2, "sadaka ya upatanisho (utulizo) kwa dhambi zetu." Huu ndio msukumo wa Yohana mbatizaji "Tazama mwana kondoo wa Mungu aiondoaye dhambi ya ulimwengu" (kama vile Yohana 1:2a). Asiye na hatia alikufa badala ya mwenye hatia! Watu wa mafunuo ya uongo wa kwanza walikataa ubinadamu wa kweli wa Yesu, matumizi ya Yohana ya "damu" yanatia nguvu ya ukweli wa ubinadamu wa Yesu. Kuna mswada wa Kiyunani ulio tofauti unaohusiana na jina hilo.

1. Yesu -- NASB, NRSV, NJB, REB, NET 2. Kristo -- MSS א, B, C 3. Yesu Kristo -- NKJV

Kuna mfano mmoja uliotumiwa na Bart D. Ehrman, The Orthodox Corruption of Scripture, uk. 153, kuonesha jinsi waandishi wa kale walivyojaribu kufanya maandiko yawe muhimu zaidi ili kupinga waasi wa siku hizi. Uchaguzi #3 lilikuwa jaribio la kupatanisha tofauti ya MSS.

◙ "yatusafisha dhambi yote" Hii ni kauli tendaji yenye kuarifu ya wakati uliopo. Neno "dhambi" ni hali ya umoja

ikiwa na kibainishi. Hii inazungumzia kila aina ya dhambi. Tambua kwamba aya hii haizungumzi utakaso wa wakati mmoja tu (wokovu, 1 Yohana 1:7), bali utakaso endelevu (maisha ya Kikristo, 1 Yohana 1:9). Yote mawili ni sehemu ya uzoefu wa Kikristo (kama vile Yohana 13:10). 1:8 "Tukisema kwamba hatuna dhambi" Hii ni sentensi shurutishi daraja la tatu. Dhambi ni ukweli wa kiroho katika ulimwengu ulioanguka, hata kwa waaminio (kama vile Warumi 7). Injili ya Yohana inaelezea swala hili mara nyingi (kama vile 1 Yohana 9:41; 15:22,24; 19:11). Aya hii inakataa madai yote ya kale na ya siku hizi yanayokataa kuwajibika kwa tabia ya mtu binafsi.

◙ "twajidanganya wenyewe" Aya hii ya Kiyunani inazungumzia juu ya kukataa ukweli kwa makusudi kwa mtu binafsi, sio kutokujua.

◙ "kweli haimo mwetu" Njia ya kukubalika mbele za Mungu mtakatifu sio kukataa, Bali kutambua dhambi yetu na kukubali kile anachokitoa kupitia Kristo (kama vile Rum. 3:21-31). "Kweli" yaweza kuhusu ujumbe juu ya Kristo ama binadamu Yesu mwenyewe (kama vile Yohana 14:6). Tazama Mada Maalumu katika Yohana 6:55 na 17:3 1:8,9 "Tuki" Zote mbili hizi ni sentensi shurutishi daraja la tatu ambazo zinamaanisha utendaji usiodhihirika. 1:9 "ungama" Hili ni muunganikano wa maneno ya Kiyunani kutoka neno "kunena" na "kile kile." Waaminio wanaendelea kukubaliana na Mungu kwamba wamekiuka utakatifu wake (kama vile Rum. 3:23). Ni njeo ya wakati uliopo, ambayo inadokeza kitendo kinachoendelea. Kukili kunadokeza

1. Kutamka dhambi bayana (1 Yohana 1:9) 2. Kukili dhambi hadharani (kama vile Mt. 10:32; Yakobo 5:16) 3. Kuachana na dhambi dhahiri (kama vile Mt. 3:6; Marko 1:5; Matendo 19:18; Yakobo 5:16)

Page 352: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

336

1 Yohana hutumia neno hili mara nyingi (kama vile 1 Yohana 1:9; 4:2,3,15; 2 Yohana 7). Kifo cha Yesu ndio njia ya msamaha lakini wanadamu wenye dhambi lazima waitikie na kuendelea kuitikia kwenye imani ili waokolewe (kama vile Yohana 1:12; 3:16). Tazama Mada Maalumu: Ukiri katika Yohana 9:22-23

◙ "dhambi zetu" Angalia hali ya uwingi. Hii inarejea matendo dhahiri ya dhambi.

◙ "Yeye ni mwaminifu" Hii inahusiana na Mungu Baba (kama vile Kumb. 7:9; 32:4; Zab. 36:5; 40:10; 89:1,2,5,8; 92:2; 119:90; Isa. 49:7; Rum. 3:3; 1 Kor. 1:9; 10:13; 2 Kor. 1:18; 1 The. 5:24; 2 Tim. 2:13). Tabia ya Mungu Baba ya kutobadilika, rehema, uaminifu ndilo tumaini letu la hakika! Aya hii inasisitiza uaminifu wa Mungu kwa neno lake (kama vile. Hebr. 10:23; 11:11).Hii yaweza kuwa inahusu ahadi ya Mungu ya Agano Jipya iliyoahidiwa katika Yer. 31:34, ambayo iliahidi msamaha wa dhambi.

◙ "na wa haki" Neno hili si la kawaida kwenye muktadha unaohusu Mungu Mtakatifu akiwasamehe bure watu

wenye dhambi. Lakini, hili kitheolojia liko sahihi kwa sababu Mungu hujali sana mambo ya dhambi zetu, hivyo ametoa njia za msamaha wetu katika kifo chake Yesu kutufia sisi (kama vile Rum. 3:21-31). Tazama Mada Maalumu katika 1 Yohana 2:29

◙ "atuondolee. . . kutusafisha" Zote mbili ni dhamira tegemezi tendaji za wakati uliopita usio timilifu. Maneno haya mawili yanafanana katika muktadha huu; yote mawili yanahusu wokovu wa waliopotea, kutakaswa kunakoendelea ambako ni kwa lazima kwa ajili ya ushirika na Mungu (kama vile Isa. 1:18; 38:17; 43:25; 44:22; Zab. 103:3,11-13; Mika 7:19). Waalimu wa uongo walioikana injili, walihitaji wokovu. Waaminio wanaoendelea kutenda dhambi wanahitaji urejesho wa ushirika. Yohana anaonekana kuwaambia kundi la kwanza na la pili wazi. 1:10 "Tukisema" Tazama maelezo katika 1 Yohana 1:6.

◙ "hatukutenda dhambi" Hii ni kauli timilifu tendaji elekezi ambayo inaashiria kwamba mtu kamwe hajatenda dhambi huko nyuma wala wakati huu uliopo. Neno "fanya dhambi" katika hali ya umoja inahusu dhambi kwa ujumla, neno la Kiyunani linamaanisha kukosa kulenga lengo hili, inamaanisha kwamba dhambi ni kitendo cha kuacha na pia kulazimika kufanya vitu vilivyo funuliwa katika neno la Mungu. Walimu wa uongo walidai kwamba wokovu ulihusiana tu na elimu, sio maisha.

◙ "twamfanya Yeye kuwa mwongo" Injili ipo kwenye msingi wa hali ya dhambi kwa wanadamu wote (kama vile Rum. 3:9-18,23; 5:1; 11:32). Kati ya Mungu (kama vile Rum. 3:4) ama wale wanaodai kwamba hawana dhambi, wanajidanganya.

◙ "neno lake halimo mwetu" Hii inahusu mtazamo wa pande mbili wa neno "logos," zote zikiwa kama ujumbe na mtu (kam vile 1 Yohana 1:1,8; Yohana 14:6). Yohana mara nyingi huhusisha hili na "kweli." 2:1 "Watoto wangu wadogo" Yohana anatumia maneno mawili ya udogo kwa "mtoto"katika 1 Yohana.

1. teknion (kama vile 1 Yohana 2:1,12,28; 3:7,18; 4:4; 5:21; Yohana 13:33) 2. paidion (kama vile 1 Yohana 2:14,18)

Ni maneno yenye maana karibu sawa bila upekee uliokusudiwa wa kithiolojia. Maneno haya ya upendo labda yanakuja kutokana na umri mkubwa wa Yohana wakati wa kuandika. Yesu alitumia neno "mtoto" kuhusu wanafunzi katikaYohana 13:33.

◙ "nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi" Hii ni kauli tendaji tegemezi ya wakati uliopita usio timilifu. Yohana anaweka tofauti iliyo dhahiri kati ya wakati uliopo, tabia inayoendelea ya mtindo wa maisha wa kutenda dhambi (kama vile 1 Yohana 3:6,9) na vitendo binafsi vya dhambi inayotendwa na Wakristo wanaopambana na waliojaribiwa. Anajaribu kuleta uwiano kati ya viwango vilivyozidi vya

Page 353: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

337

1. Kuchukulia dhambi kwa urahisi (kama vile Rum. 6:1; 1 Yohana 1:8-10; 3:6-9; 5:16) 2. Utoaji wa adhabu kali na ugumu unaovunjika kw urahisi wa Wakristo kuhusu dhambi za mtu binafsi

Viwango hivi vilivyozidi labda vinaaksi fikra mbili tofauti za mafundisho ya watu wenye mafunuo ya uongo. Kundi moja walihisi kwamba wokovu ulikuwa swala la kielimu; Haikuwa inajalisha jinsi mtu alivyoishi kwa sababu mwili ulikuwa wenye uovu.Kundi jingine la watu wa mafunuo ya uongo pia waliamini kwamba mwili ni wenye uovu, na kwa hiyo ulipaswa kuzuiliwa tamaa zake.

◙ "Na kama mtu akitenda dhambi" Hii ni sentensi shurutishi daraja la tatu inayozungumzia juu ya utendaji usiodhihirika. Hata Wakristo hutenda dhambi (kama vile Warumi 7).

◙ "tunaye Mwombezi kwa Baba," Hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo ambayo inahusu maombezi ya Yesu yanayoendelea yakiwa kama mtetezi wetu wa mbinguni (paraklētos). Hili lilikuwa neno lililokuwa halali kwa mwanasheria mtetezi ama aliye kuwa “ameitwa pembeni kusaidia” (kutoka para, pembeni na kaleō, kuita). Limetumika kwenye mazungumzo kule gorofani katika Injili ya Yohana, kwa Roho Mtakatifu, mtetezi anayekaa ndani, wa hapa duniani, (kama vile Yohana 14:16,26; 15:26; 16:7). Lakini hili ndilo tumizi pekee la neno kwa Yesu (ingawa umedokezwa katika Yohana 14:16; Rum. 8:34; Ebr. 4:14-16; 7:25; 9:24). Paulo alitumia dhana hiyohiyo kwa kazi ya Kristo ya maombezi ya Roho Mtakatifu katika Rum. 8:26. Tunaye mtetezi mbinguni (Yesu) pamoja na mtetezi ndani (Roho), wote wawili ambao Baba mpendwa aliwatuma kwa niaba yake.

◙ "Yesu Kristo mwenye haki" Huu uainishaji unatumika kumhusu Mungu Baba katika 1 Yohana 1:9. Waandishi wa agano Jipya wanatumia mbinu za kiuandishi kutamka Uungu wa Kristo.

1. wanatumia nyadhifa zilizotumiwa kwa Mungu, kwa Yesu 2. wanatangaza matendo ya Mungu yaliyofanywa na Yesu 3. wanatumia aya zinazoendana kisarufi kuhusu wote wawili (vishamirisho vya vitenzi au kihusishi)

Inazungumzia kutokuwa na dhambi (utakatifu, kufanana na Mungu) kwa Kristo (kama vile 1 Yohana 3:5; 2 Kor. 5:21; Ebr. 2:18; 4:15; 7:26; 1 Pet. 2:22). Yeye alikuwa njia ya kuleta "haki" kwa watu. 2:2 NASB, NKJV "Yeye mwenyewe kipatanisho kwa dhambi zetu" NRSV "yeye ndiye dhabihu ya upatanisho kwa dhambi zetu" TEV "Kristo mwenyewe ndiye njia ambayo dhambi zetu zinasamehewa” NJB, RSV "Yaye ndiye sadaka ya kufidia dhambi zetu" Neno hilasmos linatumika katika maandiko ya kale ya kiyunani kwa kifuniko cha sanduku la Agano ambalo huitwa kiti cha rehema ama mahali pa upatanisho. Yesu alijiweka mwenyewe mahali pa uovu wetu mbele za Mungu (kama vile. 1 Yohana 4:10; Rum. 3:25). Katika ulimwengu wa Wayunani na Warumi neno hili lilichukua dhana ya urejesho wa ushirika na Mungu ambaye alichukizana na watu kwa njia ya kulipia gharama, lakini neno waandishi wa Agano Jipya [isipokuwa Luka] walikuwa wenye fikra za Kiebrania, wakiandika katika lugha ya kiyunani cha kawaida cha Koine). Ilitumika katika maandiko ya kale na katika Ebr. 9:5 kutafsiri "kiti cha rehema,"ambacho kilikuwa kifuniko cha Agano kikiwa kimewekwa patakatifu pa patakatifu mahali ambapo upatanisho ulinunuliwa katika siku ya upatanisho (kama vile Walawi 16). Neno lazima lishugulikiwe kwa njia ambayo haipunguzi machukio ya Mungu kwenye dhambi, bali inayotamka mtazamo wake chanya kwa wenye dhambi. Mjadala mzuri unapatikana ndani ya kitabu cha James Stewart's A Man in Christ, kur. 214-224. Njia moja ya kukamilisha hili ni tafsiri ya neno lenyewe ili kwamba uaksi kazi ya Mungu katika Kristo: "sadaka ya upatanisho" au "na nguvu ya upatanisho." Tafsiri za kiingereza za kisasa zatofautiana katika jinsi ya kuelewa neno hili la sadaka. Neno "upatanisho" wanadokeza kwamba Yesu alituliza gadhabu ya Mungu (kama vile Rum. 1:18; 5:9; Efe. 5:6; Kol.3:6). Mtakatifu wa Mungu anachukizwa na dhambi ya mwanadamu. Hili linashugulikiwa katika huduma ya Yesu (kama vile Rum. 3:25; 2 Kor. 5:21; Ebr. 2:17).

Page 354: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

338

Baadhi ya wanafunzi (yaani, C. H. Dodd) wanahisi kwamba dhana moja ya wapagani wa (Kiyunani) (ingepooza hasira ya uungu) haipaswi kutumika kwa YHWH, kwa hiyo, wanachagua "kufanya mabadiliko kwa ajili ya uovu uliotendeka" ambapo huduma ya Yesu ilishughulikia uovu wa mwanadamu (kama vile Yohana 1:29; 3:16) mbele ya Mungu na sio hasira ya Mungu dhidi ya dhambi. Hata hivyo yote mawili ni kweli kwa mujibu wa Biblia.

◙ "kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote" Hii inahusu uwezo

wa upatanisho usio na kikomo (kama vile. 1 Yohana 4:14; Yohana 1:29; 3:16,17; 12:47; Rum. 5:18; 1 Tim. 4:10; Tito 2:11; Hebr. 2:9; 7:25). Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi na dhambi za ulimwengu wote (kama vile Mwa. 3:15). Kitu pekee kinachozuia ulimwengu wote usiokoke sio dhambi, bali kutokuamini. Hata hivyo, wanadamu lazima waitikie na kuendelea kuitikia kwenye imani, toba, utii na ustahimilivu!

MASWALI YA MJADALA

Huu ni mwongozo wa fasiri, ina maanisha kwamba unawajibika kwa tafsiri zako mwenyewe za Biblia. Kila mmoja wetu lazima atembee katika mwanga tulio nao. Wewe, Biblia, na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Hutakiwi uvitelekeze vitu hivi kwa mfasiri. Maswali ya mjadala huu yanatolewa kukusaidia kufikiri juu ya mambo makubwa ya sehemu za kitabu hiki. Yanalenga kukuamsha kimawazo na sio kutoa maana.

1. Kwa nini Yohana anatumia vitanzi vingi kiasi hicho kuhusu milango mitano ya fahamu? 2. Orodhesha maneno ya sadaka inayopatikana katika 1 Yohana 1:7 na 9. 3. Eleza imani za waasi ambao Yohana anawashambulia. 4. 1 Yohana 1:9 inahusianishaje na watu wenye mafunuo ya uongo na waaminio? 5. Fafanua na uelezee maana ya "kuungama."

Page 355: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

339

1 YOHANA 2:3-27

MIGAWANYO YA AYA YA TAFSIRI ZA KISASA

UBS4 NKJV NRSV TEV NJB Kristo mtetezi wetu Msingi wa kushiriki Utii Kristo msaidizi wetu Kutembea katika naye mwanga (1:5-2:2) (1:5-2:28) Sharti la kwanza: kuvunja kwa dhambi (1:8-2:3) 2:1-6 Jaribu la kumjua Yeye 2:1-2 2:1-2 Sharti la Pili: Kushika amri hasa ile ya upendo 2:3-11 2:3-6 2:3-6 2:3-11 Amri mpya Upendo kwa kila Amri mpya Mmoja 2:7-14 2:7-11 2:7-8 Hali yao ya Kiroho Mahusiano ya kweli Sharti la Tatu: kwa Mungu katika Mtawala kutoka Kristo 2:9-11 Duniani 2:12-14 2:12-14 2:12-13 2:12-17 Usipende Dunia Tathimini ya kweli ya Dunia 2:14 Mpinga Kristo Udanganyifu wa saa Uaminifu kwenye Adui wa Kristo Sharti la nne: Kua ya mwisho imani ya kweli mlinzi dhidi ya mpinga Kristo 2:18-25 2:18-23 2:18-25 2:18-19 2:18-28 2:20-21 Ruhusu kweli kukaa ndani yako 2:22-23 2:24-27 2:24-25 2:26-27 2:26-27 2:26-27

MZUNGUKO WA TATU WA USOMAJI KUFUATILIA KUSUDIO LA ASILI LA MWANDISHI KATIKA NGAZI YA AYA Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwatafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Aya ya kwanza 2. Aya ya pili 3. Aya tatu

Page 356: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

340

4. N.k.

MTAZAMO WA NDANI KATIKA MISTARI 2:3-27

A. Ni vingumu sana kufafanua Yohana 1 kwa sababu ni dhamira ya kutokea mara kwa mara. Hata hivyo, watoa maoni wengi wamekubali kwamba Sura ya Yohana 2 inaendeleza dhamira ya Yohana1, ambayo ni tabia ya ushirika pamoja na Mungu, yote chanya na hasi.

B. Kuna mfanano wa kimuundo kati ya Yohana 1 na 2. Yohana hutoa ujumbe ulio kinyume na madai ya uwongo ya Mafunuo.

Sura Sura 1. Ikiwa tunasema…. (1 Yohana 2:6-7) 1. Yeye asemaye…. (1 Yohana 2:4-5) 2. Ikiwa tunasema…. (1 Yohana 2:8-9) 2. Yeye asemaye…. (1 Yohana 2:6) 3. Ikiwa tunaseama…. (1 Yohana 2:10) 3. Yeye asemaye…. (1 Yohana 2:8-11)

C. Baadhi ya orodha ya majaribio ya Muktadha huu au ushahidi ambao hufunua muamini wa kweli (1 Yohana 2:3-25) 1. Utayari wa kutubu dhambia (mwanzo na daima) (1 Yohana 1:8) 2. Utii wa Maisha (1 Yohana 2:3-6) 3. Upendo wa Maisha (1 Yohana 2:7-11) 4. Ushidi juu ya uovu (1 Yohana 2:12-14) 5. Telekeza ulimwengu (1 Yohana 2:15-17) 6. Uvumilivu (1 Yohana 2:19) 7. Mafundisho sahihi (1 Yohana 2:20-24; 4:1-3)

D. Dhana muhimu ya kithiolojia (katika 1 Yohana 2:18-19) 1. "saa ya mwisho" (1 Yohana 2:18)

a. Msemo huu na misemo sawa, kama vile “siku za mwisho”, inarejea kipindi na muda kutoka kuzaliwa kwa Yesu katika Bethlehemu hadi kuja kwa mara ya pili. Ufalme umekuja, lakini bado haijawahi kukamilika kikamilifu..

b. Watu wa Israeli wakati wa kipindi cha kibiblia walianza kuamini katika umri miwili. Umri wa uovu wa sasa na umri wa haki uliingizwa ndani na Roho, ambayo ilikuwa bado kwa siku za baadaye. Nini Agano la Kale halikufunua wazi ni kuja kwa Masihi wawili, wa kwanza kama mkombozi na wa pili kama mkamilishaji au mtimizaji. Umri hii miwili inapishana/inalingana kwa mambo mengine. Tazama Mada Maalum katika 1 Yohana 2:17

c. Haya ni matumizi ya kisitiari ya neno "saa" (kairos) kama kipindi cha muda usioainishwa (kama vile Yohana 4:21,23; 5:25,28; 16:2).

2. "mpinga kristo" (1 Yohana 2:18). Yohana peke yake anatumia neno "mpinga Kristo" (kama vile 1 Yohana 2:18,22; 4:3; 2 Yohana 7). Angalia katika 1 Yohana 2:18 nizote Wingi na Umoja (k.v. 2 Yohana 7). a. Kuna marejeleo ya mtu mmoja wa mwisho wa muda katika wandishi wengine wa kiblia.

1) Danieli -- "Mnyama wa Nne" (k.v. Yohana 7:7-8,23-26; 9:24-27) 2) Yesu -- "chukizo la uovu" (kama vile Marko 13; Mathayo 24) 3) Yohana -- "Mnyama atokae baharini" (kama vile Ufunuo13) 4) Paulo -- "Mtu wa dhambi" (kama vile Wathesalonike 2.2)

b. Yohana pia alitofautisha kati ya mtu wa siku ya kiama na Roho inayomrudia mtu au mwenendo uliopo katika dunia (kama vile. 1 Yohana 2:18; 4:3; 2 Yohana 7; Marko 13:6, 22; Mt. 24:5,24).

c. Kihusishi anti katika Kiyunani kinaweza maanisha (1) dhidi ya au (2) badala ya. Hii ni muhimu kama yatumikavyo kwenye hali zote za umoja na wingi katika Yohana 2:18. Historia imetolewa kwa wingi na wale waliokuwa kinyume na Mungu na Kristo 1) Antiochus IV Epifane (pembe ndogo ya Danieli 8; 11:36-45)

Page 357: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

341

2) Nero na Domitian (walidai Uungu lakini sio Umasihi) 3) Ukomunisti wa kukana Mungu 4) Utu wa kidunia

Lakini hii pia inafananishwa na wale ambao hawampingi Kristo, lakini wanadai kuwa Kristo (kutumia #2). 1) Walimu wa uwongo wa Marko 13:6,22 na Mt. 24:5,24 2) Viongozi wa madhehebu ya kisasa 3) Mpinga kristo (Dan. 7:8, 23-26; 9:24-27; 2 Thes. 2:3; na Ufunuo 13)

d. Wakristo katika kila kizazi wote wataona walimu wa uongo ambao walimkana Kristo na Masihi wa uongo ambaye anadai kuwa Kristo. Hata hivyo, siku moja, siku ya mwisho, siku moja maalumu ya kufanyika mwili wa uovu (yaan, Mpinga Kristo) atafanya yote!

3. "Anakaa ndani yako" (1 Yohana 2:19, 24, 27, 28) a. Wainjilisti wengi wa kisasa wanasisitizia juu ya maamuzi binafsi ya awali kwenye

kusadiki/imani/kuamini katika Kristo, na hakika hii ni kweli. Hata hivyo, Biblia inasisitiza sio kwenye maamuzi tu, lakini kwenye uwanafunzi (kama vile Mt. 28:19-20).

b. Mafundisho ya usalama wa muamini lazima yaunganishwe kwenye mafundisho ya Ustahimilivu. Tazama MADA MAALUMU: Hitaji la Ustahimilivu katika Yohana 8:31 Ama sio/au uchaguzi, bali ni yote/na ukweli wa Kibiblia. Kwa ukweli "kuendelea kudumu" ni onyo la Kibiblia (kama vile Yohana 15)!

c. Vifungu vingine juu ya kuendelea kudumu ni Mt. 10:22; 13:1-9,18-23; Marko 13:13; Yohana 8:31; 15:1-27; 1 Kor. 15:2; Gal. 6:1; Ufu. 2:2, 7, 11, 17, 26; 3:5, 12, 21; 21:7. Tazama Mada Maalumu: "kukaa" katika 1 Yohana 2:10.

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) 1 YOHANA 2:3-6 3 Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake. 4 Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. 5 Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake. 6 Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda.

2:3 "Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye" Kiuhalisia hii ni kusema “tunajua kwamba tunamjua yeye.” Hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo inayofuatiwa na kauli timilifu tendaji elekezi inayosisitiza kwamba Wakristo hawa wa makanisa yanayoweweseka wanaweza kupata imani kamili ya wokovu wao katika mwanga wa mafundisho yenye mafunuo ya uongo. Neno “kujua” limetumika katika maana yake ya Kiebrania kwa uhusiano wa kibinafsi (kama vile Mwa. 4:1; Yer. 1:5) na maana yake ya ukweli kwa Kiyunani ikuhusu jambo Fulani au mtu Fulani. Injili ni vyote mtu na mwili wa kweli. Msisitizo katika msemo huu ni

1. tunaweza kumjua Mungu 2. tunaweza kujua nini anataka katika Maisha yetu 3. tunaweza kujua kwamba tunajua! (kama vile 1 Yohana 5:13)

Moja ya imani ya mahusiano yetu pamoja na Mungu inafunuliwa na matendo na nia yetu (kama vile Mathayo 7; Yakobo, Petro 1). Hili ni dhamira ya mara kwa mara ya Yohana (kama vile 1 Yohana 2:3,5; 3:24; 4:13; 5:2,13). Maandiko ya Yohana hutumia maneno mawili ya Kiyunani kwa neno "kujua" (ginōskō na oida) mara nyingi (mara 27 katika sura tano za Yohana 1) na kwa maana sawa. Inaonekana kutokuwepo na utambuzi wa kutofautisha maana kati ya maneno haya katika lugha ya kawaida ya Koine. Uchaguzi ni wa kimtindo.Na pia inavutia kwamba Yohana hajatumia neno gumu epiginōskō. Yohana anaandika ili kuwatia moyo wanaoamini pamoja na waasi. Injili ya Yohana na Yohana 1 hutumia maneno kwa “kujua” mara nyingi kuliko nyingine kwenye vitabu vya Agano Jipya. Yohana 1 ni kitabu cha imani iliyoegemea juu ya maarifa ya injili na kulinganisha upendo na utii kwenye stadi ya maisha (kama vile. Kitabu cha Yakobo).

Page 358: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

342

◙ "ikiwa" Hii ni sentensi shurutishi daraja la tatu ambayo inamaanisha kufanyika kwa kitendo muhimu.

◙ "tunashika amri zake" Angalia kiashilia chenye masharti (kauli tenda jitegemezi ya wakati uliopo). Agano jipya ni lenye kutokuwa na masharti kama zawadi toka kwa Mungu lakini lenye masharti kama imani ya toba kwa mwanadamu na mwitikio wa utiifu (kama vile 1 Yohana 2:3-5; 3:22,24; 5:2,3; Yohana 8:51-52; 14:15,21,23; 15:10; Ufu. 2:26; 3:8,10; 12:17; 14:12). Moja ya ushahidi kwa badiliko la kweli ni utii wa wazi (kwa Yesu na kwa injili, kama vile Luka 6:46). Hata katika Agano la kale utii ulikuwa bora kuliko ibada ya dhabihu (kama vile 1 Sam. 15:22; Yer. 7:22-23). Utii hauleti au kuulinda wokovu, lakini unafanya ushahidi wa wokovu. Hili sio la msingi (kama vile 1 Thes. 2:8-9), lakini ni lile lenye kuleta matunda (kama vile. 1 Thes. 2:10).

2:4 “Yeye asemaye” Hii ni alama ya maandiko ya muundo wa Yohana wa kukemea.

◙ “Nimemjua” Hii ni moja kati ya madai mengi ya walimu wa uongo (kama vile 1 Yohana 1:6, 8, 10; 2:4, 6, 9). Hii ni njia ya kukemea ("Yeye asemaye…..") sawa na Malaki, Warumi, na Yakobo. Walimu wa uongo wanadai kumjua (njeo ya wakati timilifu) Mungu, lakini walijaribu kutenganisha wokovu toka kwenye maisha ya Kimungu. Walikuwa wanatenganisha kuhesabiwa haki toka kwenye utakaso. Walidai kuwa na maarifa ya juu (yaani, siri) kumhusu Mungu, lakini mfumo wa maisha yao ulifunua mienendo yao ya kweli.

◙ “wala hazishiki amri zake" Hii ni kauli tendaji endelevu ya wakati uliopo ambayo inazungumzia juu ya matendo ya kikawaida ya maisha. Maisha yetu yanafunua mwelekeo wetu wa kiroho (kama vile Mathayo 7). 1 Yohana 2:4 inaelezea ukweli kinyume, wakati 2:5 inaelezea ukweli halisia.

◙"ni mwongo" Hakuna kitu kilicho kibaya zaidi kuliko udanganyifu wa kikaidi! Utii ni ushahidi wa badiliko la kweli. Utawajua kwa matunda yao (kama vile Mathayo 7). Yohana aliwaita wacha Mungu wengi (walimu, wahubiri) waongo (kama vile Yohana 1:6; 2:4, 22; 4:20). Ni wacha Mungu lakini hawako sawa na Mungu!

2:5 “Lakini yeye alishikaye neno lake” Hii ni kauli tendaji tegemezi ya wakati uliopo ambayo inazungumzia juu ya kitendo cha kawaida cha maisha. Mwandishi wa UBS’ A Handbook on The Letters of John (Haas, Jonge, na Swellengrebel) hutoa maoni yanayovutia juu ya uundaji wa Kiyunani: "kiwakilishi rejeshi kikiwa na kiambata cha cha Kiyunani, 'an' au 'ean' na kitenzi kifuatacho katika hali ya utegemezi hutokea katika 1 Yohana 3:17, 22; 4:15; 5:15; 3 Yohana 5. Inaonekana kuelezea mazingira yanayotokea kwa ujumla" (uk. 40). Utii ni dhana muhimu ya Agano la imani. Hiki ndicho kiini cha ujumbe wa 1 Yohana na Yakobo. Huwezi sema unamjua Mungu na bado unakataa vyote neno la uzima na maneno yaliyoandikwa kwa mwenendo wa maisha ya dhambi (kama vle. Yohana 13:6, 9)!

◙ "katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli" Hii ni kauli timilifu tendewa elekezi ambayo inazungumzia juu ya kitendo ilichokamilishwa (kama vile. 1 Yohana 4:12, 17, 18). Haijulikani, nikiongea kisarufi, ikiwa KIMILIKISHI kinaongea juu ya

1. Upendo wa Mungu kwetu (kama vile 1 Yohana 4:12) 2. Upendo wetu kwa Mungu (kama vile 1 Yohana 5:3) 3. Upendo wa Mungu tu kwa ujumla katika mioyo yetu

Neno "kamilifu" (telos kama vile. 1 Yohana 4:12, 17, 18) lina maanisha ya kukomaa, kamili, au uwe kamili kwa kazi uliopewa (kama vile 1 Thes. 4:12), sio bila dhambi (kama vile 1 Yohana 1:8, 10).

◙ "Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake" Hapa tena ni msisitizo juu ya uwezo wa waaminio kuwa na imani ya kujiamni katika uhusiano wao na Mungu. Dhana ya sisi kuwa ndani yake (kukaa, kama vile 1 Yohana 2:6) ni dhamira ya mara kwa mara ya uandishi wa Yohana (kama vile. Yohana14:20, 23; 15:4-10; 17:21, 23,26; Yohana 1. 2:24-28; 3:6, 24; 4:13,16).

Page 359: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

343

2:6 “anakaa” Tazama Mada Maalum katika 1 Yohana 2: 10. Agano Jipya pia linadai kwamba wote Baba na Mwana wanakaa ndani yetu (k.v 14:23 na 17:21). Angalia kwamba hata katika kishazi ambacho kinasisitiza juu ya uhakika kinahitajika, na kinadokeza onyo, la “kupaswa” (kama vile 1 Yohana 2:6, kauli isiyo na kikomo ya wakati uliopo, “kukaa ndani Yake "). Injili ni Agano lenye masharti pamoja na haki na wajibu!

◙ “imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda” Huu ni msisitizo mwingne juu ya “imani ya kweli” kama mfumo wa maisha ya imani (kama vile Yakobo 2:14-26). Imani sio maamuzi pekee, lakini ni mwendelezo wa mahusiano binafsi na Yesu ambayo kiuhalisia yanatokea katika maisha ya kila siku ya kufanana na kristo. Uzima wa milele una sifa inayoonekana! Hii inafanana na 1 Yohana 1:7. Lengo la mkristo sio tu kwenda mbinguni wakati tunakufa, lakini kuishi kama kristo sasa (kama vile Rum. 8:29-30; Kol. 2. 3:18; Gal. 4:19; Efe. 1:4; 1 Thes 3:13; 4:3; Petro 1. 1:15)! Tumeokolewa kutumika. Tumetumwa kwa ajili ya kazi maalumu kama Yeye ametumwa kwa ajili ya kazi maalumu. Kama alivyoweka maisha yake rehani kwa ajili ya wengine, kwa kiasi hicho hicho sisi pia, lazima tujione sisi tu watumishi pia (kama vile. 1 Yohana 3:16). "Yeye" ni uhalisia wa "yule," ambayo ni nahau ya kawaida katika maandiko ya Yohana kwa "Yesu" (kama vile. Yohana 2:21; 19:35; 1 Yohana 2:6; 3:3, 5, 7, 16; 4:17). Mara nyingi hutumika katika njia ya kushusha heshima (kama vile. Yohana 7:11; 9:12, 28; 19:21). Ikiwa "yule" inarejea kwa Yesu, basi nani hufanya “ndani yake” ya 1 Yohana 2:6a inamrejea? Yohana mara nyingi hutumia hali ya kuwa na maana nyingi kwenye maana. Inaweza kurejea kwa Baba (kama vile. Yohana 15:1-2,9-10) au Mwana (kama vile Yohana 15:4-6). Utata ule ule unaweza kueleza kwa mifano katika neno “aliye Mtakatifu” kwa 1 Yohana 2:20.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): 1 YOHANA 2:7-11 7 Wapenzi, siwaandikii amri mpya, ila amri ya zamani mliyokuwa nayo tangu mwanzo. Na hiyo amri ya zamani ni neno lile mlilolisikia. 8 Tena nawaandikia amri mpya, neno lililo kweli ndani yake na ndani yenu; kwa kuwa giza linapita na ile nuru ya kweli imekwisha kung'aa. 9 Yeye asemaye kwamba yumo nuruni, naye amchukia ndugu yake, yumo gizani hata sasa. 10 Yeye ampendaye ndugu yake, akaa katika nuru, wala ndani yake hamna kikwazo. 11 Bali yeye amchukiaye ndugu yake, yu katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho.

2:7 “Wapenzi“ Yohana mara nyingi anawaita wasomaji wake kwa maneno ya kirafiki (kama vile 1 Yohana 2:1). Neno lilitumiwa na Baba kumrejea Yesu katika ubatizo wake (kama vile. Mt. 3:17) na wakati wa kubadilika sura (kama vile Mt. 17:5). Ni usanifu wa kawaida wa wale waliookolewa katika Nyaraka za Yohana (kama vile 1 Yohana 3:2,21; 4:1,7,11; na Yohana 3. 1, 2, 5,11). Upokeaji wa maandishi una neno "ndugu" (MSS K, L, NKJV), lakini 1 Yohana hulitumia hili pekee katika 1 Yohana 3:13. "Wapenzi" zinasaidiwa na herufi kubwa za maandiko ya kiyunani ( א, A, B, C, P, na matoleo ya Kilatini na Shamu na Koptiki, na toleo la Armenia (tazama Bruce Metzger, A Textual Commentary On the Greek New Testament, uk. 708). ◙"siwaandikii amri mpya, ila amri ya zamani" Hii ni sifa ya maandiko ya Yohana (kama vile Yohana 13:34; 15:12,17). Amri haikuwa mpya kwa maanaya muda, lakini mpya kwa maana ya ubora. Waaminio wameamriwa kupendana wenyewe kama Yesu alivyowapenda (kama vile Yohana 13:34). Neno “Amri ya zamani" Inaweza kueleweka kwa maana mbili.

1. sheria ya Musa (yaani Mambo. 19:18)

2. mafundisho ya Yesu yalinukuliwa katika injili ya Yohana (yaani, Yohana 13:34; 15:12,17)

◙ "amri ya zamani" Katika 1 Yohana 2:3 neno "amri" ni wingi, lakini hapa ni umoja. Hii inaonekana kuonyesha kwamab upendo unakamilisha amri nyingine zote (kama vile Gal. 5:22; 1 Kor. 13:13). Upendo ni mamlaka ya injili.

◙ "mliyokuwa nayo tangu mwanzo" Hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati usiotimilifu ambayo inarejea msikiaji kwanza anapokabiliana na ujumbe wa injili (kama vile 1 Yohana 2:24; 1:1; 3:11; 2 Yohana 5-6).

Page 360: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

344

◙ “mlilolisikia" Upokeaji wa maandishi umeongezea kifungu “toka mwanzo” (imetumika katika sehemu ya awali ya aya).

2:8 “lililo kweli ndani yake” Jinsia ya kiwakilishi nomino hiki kinabadilika kutoka kwa jinsi ya (KE) katika Yohana 1. 2:7, ambalo linaendana na neno “amri,” na lile lililo HASI, ambalo linaelezea injili yote. Badiliko linalofanana katika kiwakilishi nomino kinapatikana katika Efe. 2:8-9.

◙ “giza linapita" Hii ni kauli ya kati elekezi ya wakati uliopo (kwa mujibu wa A. T. Robertson's Word Pictures in the New Testament, uk. 212). Kwa wale ambao wanamjua Mungu, enzi mpya ilipambazuka na kuendelea kupambazuka katika mioyo na fikra zao (yaani, mambo ya siku za mwisho yaliyofahamika).

◙ "nuru ya kweli imekwisha kung'aa" Yesu ni nuru ya ulimwengu (kama vile. Yohana 1:4-5,9; 8:12), ambayo ni sitiari ya kibiblia kwa ukweli,ufunuo, na usafi wa kimaadili. Tazama kumbukumbu katika 1 Yohana 1:5 na 1:7. Enzi mpya imepambazuka!

2:9 "naye amchukia ndugu yake" Hii ni kauli tendaji endelevu ya wakati uliopo ambayo inazungumzia mwenendo endelevu uliotulia. Chuki ni ushahidi wa giza (kama vile Mt. 5:21-26).

2:10 "Yeye ampendaye ndugu yake, akaa katika nuru" njeo ya vitendo vya wakati uliopo hutawala mazingira haya. Upendo ni ushahidi wa wokovu wa waaminio pamoja na uhusiano binafsi na ujuzi wa kweli na nuru. Hii ni amri mpya, lakini bado ya zamani (kama vile 1 Yohana 3:11, 23; 4:7,11,21).

MADA MAALUMU: "KUKAA" KATIKA MAANDIKO YA YOHANA

Injili ya Yohana inaeleza uhusiano wa kipekee kati ya Mungu Baba na Yesu Mwana. Ni ukaribu wa pande zote mbili uliojikita katika haki na usawa wa Yesu. Katika Injilii nzima, Yesu anazungumzia yale ambayo amekuwa akisikia Baba yake akiyazungumzia, amefanya yale ambayo ameyaona yakifanywa na Baba yake. Yesu hakutenda tendo lolote katika mapenzi Yake, bali katika mapenzi ya Baba (yaani, Yohana 5:19, 30; 8:28; 12:49; 14:10,24). Ushirika huu wa karibu na utumishi unaweka mpangilio wa uhusiano kati ya Yesu na wafuasi Wake. Uhusiano wa karibu haukuwa wa unyonyaji binabfsi (kama katika fikra/wa kubuni), bali wa kimaadili, uliofuata uadilifu wa mtindo wa maisha (kama vile Yohana 13:15; 1 Pet. 2:21). Ushirika ulikuwa

1. utambuzi (mtazamo wa ulimwengu wa injili kama Neno la Mungu) 2. kiuhusiano (Yesu alikuwa Masihi aliyeahidiwa na Mungu aliyepaswa kuaminiwa na kutegemewa) 3. kimaadili (tabia Yake inafanyika ndani ya wale wanaomwabudu Mungu)

Yesu ni mwanadamu aliyekamili, Mwisraeli kamili, aliyeuvumilia ubinadamu. Anakifunua kile ambacho Adam angekuwa nacho, na ilivyompasa kuwa (kuzungumza kibinadamu). Yesu anatimiza "mfano wa Mungu." Anaurejesha ufanano wa Kiungu ulioanguka katika dhambi kuwa katika ubinadamu (kama vile Mwa. 1:26-27) kwa

1. ukamilifu, upekee, na ufunuo wa mwisho wa Mungu (kama vile Yohana 1:18; 14:7-10; Kol. 1:15; Ebr. 1:1-2)

2. kufa kwake kwa ajili yetu (upatanisho uliofanyika kwa niaba yetu, kama vile Marko 10:45; 2 Kor. 5:21)

3. kuwapa wanadamu unaowaasa kuufuata (kama vile Yohana 13:15; 1 Pet. 2:21; 1 Yohana 1:7) Neno "tiifu" (menō) linaakisi kusudi la ufanano wa Ukristo (kama vile Rum. 8:28-30; 2 Kor. 3:18; Gal. 4:19; Efe. 1:4; 4:13; 1 Thes. 3:13; 4:3; 5:23; 2 Thes. 2:13; Tito 2:4; 1 Pet. 1:15), kurejeshwa kwa wale walioanguka dhambini (kama vile Mwanzo 3). Muungano wa Mungu na uumbaji wake wa mwisho, mwanadamu, kwa lengo la ushirika ni wa Mtume Paulo yaani "katika Kristo" na Mtume Yohana"utii ndani Yangu" (yaani, andiko kuu ni Yohana 15).

Page 361: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

345

Nukuu ya matumizi ya Yohana: 1. Utii kati ya Baba na Mwana

a. Baba ndani ya Mwana (Yohana 10:38; 14:10,11; 17:21,23) b. Mwana ndani ya Baba (Yohana10:38; 14:10,11; 17:21)

2. Utii kati ya Mungu na yule aaminiye a. Baba ndani ya yule aaminiye (Yohana 14:20,23; 1 Yohana 3:24; 4:12-13,15) b. mwamini ndani ya Baba (Yohana 14:20,23; 17:21; 1 Yohana 2:24,27; 4:13,16) c. Mwana ndani ya mwamini (Yohana 6:56; 14:20,23; 15:4,5; 17:23) d. mwamini ndani ya Mwana (Yohana 6:56; 14:20,23; 15:4,5,7; 1 Yohana 2:6,24,27,28)

3. Sifa zingine za utii (halisi) a. Neno la Mungu

1) Ukanaji (Yohana 5:38; 8:37; 1 Yohana 1:10; 2 Yohana 9) 2) Uhalisia (Yohana 8:31; 15:2; 1 Yohana 2:14,24; 2 Yohana 9)

b. mapenzi ya Mungu (Yohana 15:9-10; 17:26; 1 Yohana 3:17; 4:16) c. Roho wa Mungu

1) Juu ya Mwana (Yohana 1:32) 2) Ndani ya mwamini (Yohana 14:17)

d. Usikivu ni utii (Yohana 14:15-21,23-24; 15:10; Luka 6:46; 1 Yohana 3:24) e. Upendo ni kutii katika nuru (1 Yohana 2:10) f. Kuyafanya mapenzi ya Mungu ni kutii (1 Yohana 2:17) g. Utii wa kupakwa mafuta (1 Yohana 2:27) h. Kuitii kweli (2 Yohana 2) i. Kumtii Mwana (Yohana 8:35; 12:34)

4. sifa zingine za utii (kanushi) a. Kutokutii ghadhabu ya Mungu (Yohana 3:36) b. kutii gizani (Yohana 12:46) c. kutupwa nje . . .kunyauka (si kutii, Yohana 15:6) d. kutenda dhambi (si kutii, 1 Yohana 3:6) e. kutokupenda (si kutii, 1 Yohana 3:14) f. kutokuua (si utii wa maisha ya milele, 1 Yohana 3:15) g. yeye ambaye hakutii katika kuyaishi maisha ya kifo (1 Yohana 3:14)

NASB, NKJV "wala ndani yake hakuna kikwazo" NRSV "kwake hakuna kikwazo ndani yake" TEV "wala hakuna kati yetu cha kutusababisha tutende dhambi" NJB "hakuna chochote ndani yake cha kumwangusha" Yumkini kuna tafsiri mbili za Aya hii.

1. Muamini ambaye anatembea katika upendo hawezi kujikwa mwenyewe (kama vile 1 Yohana 2:11) 2. Muamini ambaye anatembea katika upendo hawezi kuwafanya wengine kujikwaa (kama vile Mt. 18:6;

Rum. 14:13; 1 Kor. 8:13) Yote ni kweli! Injili ufaidisha muamini na wengine (wengine wote wanaoamini na waliopotea). Katika Agano la Kale “kujikwaa” ni kinyume cha imani (miguu iliyoimalika, mkao imara). Mapenzi ya Mungu na amri vimeelezwa kwa njia nyeupe. Hii ni jinsi gani neno “tembea” linaweza kuwa sitiari kwa mfumo wa maisha. Tazama Mada Maalum: Amini, kusadiki, imani, na uaminifu katika Agano la Kale katika Yohana 1:14

2:11 “Bali yeye amchukiaye ndugu yake, yu katika giza, tena anakwenda katika giza” Kuna kauli tendaji endelevu ya wakati uliopo (amchukiaye) ikifuatiwa na kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo (atembeaye). Chuki ni ishara ya kutokuamini (kama vile 1 Yohana 3:15; 4:20). Nuru na giza, upendo na chuki haviwezi kuishi ndani ya mtu yule

Page 362: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

346

yule. Haya ni maelezo ya wazi ya Yohana. Yeye alieleza wazo! Mara nyingi, hata hivyo, waamini hupambana na dhuluma, kutokua na upendo, na kutojali! Injili huleta vyote mabadiliko ya papo hapo na mabadiliko endelevu.

◙"kwa sababu giza imempotosha macho" Hii inarejea ama kwa asili ya dhambi inayoendelea kwa waaminio (kama vile 2 Petro 1:5-9), au matendo ya Shetani (kama vile 2 Kor 4:4). Kuna maadui watatu wa binadamu (1) mfumo wa ulimwengu ulioanguka; (2) malaika binafsi wa ulaghai, Shetani; na (3) anguko letu wenyewe, asili ya adam (kama vile Efe. 2:2-3, 16; Yakobo 4).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) 1 YOHANA 2:12-14 12 Nawaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya jina lake. 13 Nawaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nawaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mmemshinda yule mwovu. Nimewaandikia ninyi, watoto, kwa sababu mmemjua Baba. 14 Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu.

2:12-14 Vitenzi vyote katika Aya hii (isipokuwa "nawaandikieni" [NASB 1970], "nimewaandikieni" [NASB 1995], UBS4 inatoa chaguo la pili la alama "A" [hakika]) ni njeo ya wakati timilifu, ambayo huzungumza juu ya kitendo katika siku za nyuma ambacho kinajitokeza katika hali mtu inayoendelea. Kama mazingira yanavyoelezea kuhusu walimu wa uongo, mazingira haya yanamwelezea mwamini. Kuna sifa tatu tofauti walizopewa waaminio: "watoto wadogo," "Wababa," na "Vijana." Kifungu hiki hakiwezi kukaa sawa katika mazingira ya ushahidi wa maisha yenye uhakika. Inawezekana kwamba hatufanyi kazi na vikundi vitatu bali chombo cha fasihi kinachofafanua hali ya utulivu ya Wakristo. Kuna mambo manne yaliyoorodheshwa ambayo waaminio wanajua.

1. kwamba dhambi zao zimesamehewa (1 Yohana 2:12) 2. kwamba kupitia kwa Kristo wamemshida ibilisi (1 Yohana 2:13) 3. kwamba wao "wanajua" wana ushirika pamoja na wote Baba (1 Yohana 2:14) na Mwana (1 Yohana 2:13-

14) 4. kwamba wao wana nguvu katika neno la Mungu (1 Yohana 2:14).

Orodha hii imeelezewa kisarufi katika (1) kifungu "nakuandika wewe" na (2) sita hoti (kwa sababu) vishazi.

◙ 2:12 "kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya jina lake" Huduma ya Yesu ni tumaini pekee la mwanadamu kusamehewa (kauli timilifu tendewa elekezi). Katika uelewa wa kiebrania, jina linalingana na tabia na nafsi ya mtu (kama vile 1 Yohana 3:23; 3 Yohana 7; Rum. 10:9-13; Flp. 2:6-11). Kuna mfululizo wa vishazi sita hoti katika 1 Yohana 2:12-14. Vyaweza kuwa vishazi nia (NASB, NRSV, NJB, "kwa sababu") au ni njia tu ya fasihi ya kuwasilisha kauli za kweli (NET, "kwamba").

2:13 "yeye aliye tangu mwanzo" kiwakilishi nomino katika 1 Yohana kina maana nyingi na inaweza kurejea kwa Baba Mungu au Mungu mwana. Katika mazingira hili linarejea kwa Yesu.Ni maelezo ya kuishi kwake kabla, kwa hali hiyo, Uungu wake (kama vile Yohana 1:1,15; 3:13; 8:48-59; 17:5,24; 2 Kor 8:9; Flp. 2:6-7; Kol. 1:17; Ebr. 1:3).

◙ “mmemshinda" Hii ni ahadi na maonyo ya mara kwa mara katika 1 Yohana (kama vile 1 Yohana 2:14; 4:4, 5:4-5, 18-19). Hii imeelezewa katika kauli timilifu tendaji elekezi ambayo inazungumzia juu ya uhitimishaji wa kitendo. Hapa tena, Yohana aliandika katika maneno ya wazi (huu ushindi wa mambo ya siku ya mwisho uliotambulika ni ukumbukaji wa mambo ya kale ya injili ya Yohana). Waaminio ni washindi, lakini bado kwa sababu ya mvutano “ulio tayari lakini bado kutokea” wa ufalme wa Mungu, bado wanakabiliana na dhambi, majaribu, mateso, na kifo.

◙ "yule mwovu" Hii inarejelea kwa Shetani, ambaye ametajwa tena katika 1 Yohana 2:14. 1 Yohana 2:13 na 14 zinafanana.Tazama Mada Maalum katika Yohana 12:31

Page 363: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

347

◙ "kwa sababu mmemjua Baba" Dhana ya kibiblia ya neno “kujua” inahusisha hisia ya kiebrania ya uhusiano binafsi wa moyoni (kama vile Mwa. 4:1; Yer. 1:5) na dhana ya Kiyunani ya “kuhusu ukweli." Injili ni vyote kumkaribisha mtu ndani yako (Yesu), ujumbe (mafundisho) kukubali na kutenda, na maisha ya kuishi kwayo.

MADA MAALUM: KUJUA (kama ilivyoelezewa toka Kumbukumbu la Torati kama Kielelezo)

Neno la Kiebrania “kujua” (BDB 393) lina maana kadhaa (mazingira ya kimaana) katika shina la neno Qal.

1. Kuelewa mema na mabaya - Mwa. 3:22; Kumb. 1:39; Isa. 7:14-15; Yohana 4:11 2. Kujua kwa kuelewa - Kumb. 9:2,3,6; 18:21 3. Kujua kupitia mazoea - Kumb. 3:19; 4:35; 8:2,3,5; 11:2; 20:20; 31:13; Yos. 23:14 4. kufikiri - Kumb. 4:39; 11:2; 29:16 5. kujua kibinafsi

a. mtu - Mwa. 29:5; Kut. 1:8; Kumb. 22:2; 33:9, Yer. 1:5 b. mungu -Kumb. 11:28; 13:2,6,13; 28:64; 29:26; 32:17 c. YHWH - Kumb. 4:35,39; 7:9; 29:6; Isa. 1:3; 56:10-11 d. kizinaa - Mwa. 4:1,17,25; 24:16; 38:26

9. ujuzi wa kujifunza - Isa. 29:11,12; Amosi 5:16 10. kuwa mwenye hekima - Kumb. 29:4; Mit. 1:2; 4:1; Isa. 29:24 11. maarifa ya Mungu

a. kwa Musa - Kumb. 34:10 b. kwa Israeli- Kumb. 31:21

kithiolojia #5 ni wa muhimu. Imani ya kibiblia ni ushirika wa ndani, wa kila siku, unaokua pamoja na Mungu(angalia Mada Maalum: Koinōnia). Sio sheria pekee au maisha ya kiadilifu pekee. Ni imani binafsi ya kiushirika. Hii ndio sababu Paulo alitumia nyumba ya mshirika katika Efe.5:22-6:9 kuelezea upendo wa Kristo kwa ajili ya kanisa.

2:14 “mna nguvu” Angalia kwamba ushupavu wao umeegemea juu ya neno la Mungu kujaa kwa wingi ndani yao. Hii ni sawa na onyo dogo la Paulo katika Efe. 6:10-18. Neno linlokaa kwa wingi ni injili. Ni kwa maana zote za kifikra na kibinafsi, Mungu alianzisha na kupokea mwenyewe, vyote uamuzi na uanafunzi, Wote ukweli na uaminifu.

◙ "Neno la Mungu linakaa ndani yenu" Hii inatoa mfano wa dhana ya neno la Mungu (injili, kama vile 1 Yohana 2:24). Hiki ni kidokezo kwa Yohana 15. Kimetumika kinyume katika Yohana 5:38 na 8:37.

◙ “nanyi mmemshinda yule mwovu" Huu ni msisitizo kwenye uvumilivu kwa watakatifu wa kweli. Unapatikana katika 1 Yohana 2:17, 19, 24, 27, 28; 5:18; na 2 John 9. Mafundisho ya usalama wa muamini yanahitaji kuwa na usawa na kwa ukweli kwamba wale wote ambao wamekombolewa kweli waendelee kushikilia hadi mwisho (kama vile. Ufu. 2:7, 11, 17,26; 3:5,12,21). Tazama Mada Maalum: Hitaji la Ustahimilivu katika Yohana 8:31 Hii haina maana ya kutokuwa na dhambi sasa, ingawa kwamba ni uwezekano wa kinadharia katika kazi ya Kristo iliyokamilishwa (kama vile Warumi 6).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) 1 YOHANA 2:15-17 15 Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. 16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. 17 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.

Page 364: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

348

2:15 “Msiipende” Hii ni kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopo ikiwa na kiambata hasi, ambayo inamaanisha kuzuia kitendo kilichoko kwenye mchakato.. Upendo wa ulimwengu ulihusisha kundi moja la walimu wa mafunuo ya uongo.

◙ "dunia" Neno hili limetumika katika hisia mbili tofauti katika Agano jipya: (1) sayari ya kimwili na/au ulimwengu ulioumbwa (kama vile. Yohana 3:16; 16:33; 1 Yohana 4:14) na (2) jamii ya kibinadamu umeandaliwa na kufanya kazi mbali na Mungu (kama vile. 1 Yohana 2:15-17; 3:1,13; 4:4-5; 5:4-5,19). Ya kwanza inarejea kwa umbaji wa kimwili wa mwanzo (kama vile. Mwanzo 1-2) nay a pili ni kwa uumbaji ulioanguka (kama vile Mwanzo 3). Tazama Mada Maalumu: Kosmos (Dunia) katika Yohana 14:17

MADA MAALUMU: SERIKALI YA KIBINADAMU

I. UTANGULIZI A. Ufafanuzi – serikali ni utaratibu wa kibinadamu wenyewe wa kutoa na kulinda kwa maana ya mahitaji

(yaani, Mwanzo 4 na 11). Binadamu ni jamii ya viumbe hata kabla ya anguko (kama vile Mwa. 2:18).Familia, makabila, mataifa hutupatia jamii.

B. Kusudi – Mungu anapendelea kuwa utaratibu wafaa kwenye utawala huria. 1. Sheria za Musa, hasa amri kumi za Mungu, ni mapenzi ya Mungu kwa wanadamu katika jamii.

Inaleta ulinganifu wa ibada na Maisha. 2. Hakuna mfumo wa muundo wa serikari unatetewa katika maandiko, ingawa Serikali ya kale ya

makasisi wa Israeli ni mfumo tarajiwa wa huko mbinguni. Sio demokrasia wala ubepari ni ukweli wa kibiblia. Wakristo wanapaswa kutenda ipasavyo kwenye mfumo wa serikali yeyote walioikuta. Kusudi la mkristo ni uinjilisti na huduma, sio mapinduzi. Serikali zote ni za mpito

C. Asili ya serikali ya mwandamu 1. Roman katoliki wanadai kwamba serikali ya mwanadamu ni hitaji la asili. Aristotle anaonekana

kwanza kudai wazo hili. Anasema, “mwanadamu ni mnyama wa kisiasa” na kwa hili alimaanisha kwamba serikali “ipo kwa ajili ya msaada wa maisha mazuri.

2. Mprotestanti, hasa Martin Luther, anadai kuwa serikali ya mwanadamu ni ya asili toka kwenye anguko. Anaiita “ufalme wa Mungu wa mkono wa Kushoto.” Alisema kuwa “Njia ya Mungu ya kutawala wanadamu wabaya ni kuweka watu wabaya katika utawala.”

3. Karl Marx anadai kuwa Serikali ndiyo njia ambayo wasomi wachache wanawaweka watu wengi chini ya utawala. Kwa yeye, serikali na dini huwa na jukumu sawa

II. NYENZO ZA KIBIBLIA

A. Agano la Kale 1. Israeli ni mfumo ambao utatumika mbinguni. Katika Israeli ya kale YHWH alikuwa mfalme. Serikali

ya makasisi ni neno linalotumika kuelezea utawala wa Mungu wa moja kwa moja (kama vile 1 Sam. 1. 8:4-9).

2. Utawala wa Mungu katika serikali ya mwanadamu unaweza kuonekana wazi katika kuteuwa kwake. a. wafalme wote, Dan. 2:21; 4:17,24-25 b. Uongozi wa Musa, Dan. 2:44-45 c. Nebuchadnezar (Babeli mpya), Yer. 27:6; Dan. 5:28 d. Koreshi II (Uajemi), 2 Kor. 36:22; Ezra 1:1; Isa. 44:28; 45:1

3. Watu wa Mungu wanapaswa kuwa watiifu na wenye adabu hata kuvamia na kumiliki serikali… a. Danieli 1-4, Nebuchadnezar (Babeli mpya) b. Danieli 5, Belshazzar (Babeli mpya) c. Danieli 6, Dario (Uajemi) d. Ezra na Nehemia (Uajemi)

4. Kurudishwa kwa Yuda kulikuwa ni kuomba kwa Koreshi na kutawala na uzao wake..

Page 365: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

349

a. Ezra 6:10; 7:23 b. Wayahudi walipaswa kuomba kwa mamlaka ya kiraia, Mihnah, Avot. 3:2

B. Agano Jipya 1. Yesu alionyesha heshima kwa serikali ya kibinadamuu.

a. Mathayo 17:24-27, Yeye alilipa kodi ya hekalu (dini na utawala wa kiraia ulikuwa na maaana ya kuwa mmoja,kama ile. Petro 2. 2:17)

b. Mathayo 22:15-22; Marko 12:13-17; Luka 20:20-26, Alitetea nafasi ya kodi ya kirumi na hivyo mamlaka ya kiraia ya kirujmi.

c. Yohana 19:11, Mungu aliruhusu utawala wa kiraia kufanya kazi. 2. Maneno ya Paulo yalihusiana na serikali ya kibinadamu.

a. Warumi 13:1-5, waaminio lazima wawasilishe kwa utawala wa kiraia kwa kuwa walianzishwa na Mungu

b. Warumi 13:6-7, waaminio lazima kulipa kodi na kuheshimu utawala wa kiraia. c. Timotheo 1. 2:1-3, waaminio lazima kuomba kwa utawala wa kiraia. d. Tito 3:1, waaminio lazima kunyenyekea kwa utawala wa kiraia.

3. Maneno ya Petro yalihusiana na serikali ya kibinadamu. a. Matendo 4:1-31; 5:29, Petro na Yohana kabla ya wakuu wa sinagogi (hii inaonyesha kuendelea

mbele kibiblia kwa kutokutii kwa raia) b. Petro 2. 2:13-17, waaaminio lazima wawasilishe kwa utawala wa kiraia kwa mazuri ya jamii na

kwa uinjilisti. 4. Maneno ya Yohana yalihusiana na serikali ya kibinadamu.

a. Ufunuo 17, uzinzi wa Babeli unawakilisha serikali ya wanadamu iliyoandaliwa na kufanya kazi mbali na Mungu.

b. Ufunuo 18, uzinzi wa Babeli umeharibiwa.

III. HITIMISHO A. Serikali ya mwanadamu (katika ulimwengu ulioanguka) imewekwa na Mungu. Hii sio “haki ya kiungu ya

wafalme,” bali kazi ya kiungu ya Serikali (yaani, amri sio machafuko). Hakuna mfumo wa mtu unaotetewa juu ya mwingine.

B. Ni wajibu wa dini kwa waaminio kutii na kuomba kwa mamlaka ya kiraia. C. Ni sawa kwa waaminio kuunga mkono serikali ya wanadamu kwa kodo na mtazamo wa heshima. D. Serikali ya mwanadamu ni kwa lengo la utaratibu wa kiraia. Wao ni watumishi wa Mungu kwa kazi hii. E. Serikali ya mwanadamu sio mwisho. Ina kikomo katika mamlaka yake.Waaminio lazima kutenda kwa

sababu ya dhamiri zao kwa kukataa mamlaka ya kiraia wakati inapita mipaka yake iliyowekwa na Mungu. Kama Augustino alionyesha katika The City of God, sisi ni raia wa falme mbili, moja ya muda na moja ya milele (kama vile. Wafil. 3:20). Tua wajibu kwa wote, lakini ufalme wa Mungu ni mwisho! Kuna yote mwelekeo wa kibinafsi na ushirika katika wajibu wetu kwa Mungu.

F. Tunapaswa kuwatia moyo waminio katika mfumo wa kidemokrasia kushiriki kikamilifu katika mchakato wa serikali na kuutekeleza, wakati ikiwezekana, mafundisho ya maandiko.

G. Mabadiliko ya kijamii lazima kuendelezwa na ubadilishaji wa mtu binafsi. Hakuna tawi halisi la theolojia linalojishughulisha na kifo, hukumu, pepo na jehanam la kudumu katika serikali. Serikali zote za mwanadamu, ingawa lazima na kutumiwa na Mungu, ni maonyesho ya dhambi ya shirika la mwanadamu mbali na Mungu. Dhana hii inaelezewa katika matumizi ya Johannine ya neno

“ulimwengu (yaani, Yohana 1. 2:15-17).

◙ “wala mambo yaliyomo katika dunia" Hii inaonekana kurejea kwenye upendo wa vitu (kama vile 1 Yohana 2:16) au mambo yale ulimwengu unapaswa kuyatoa: nguvu, ufahari, ushawishi, n.k. (kama vile Warumi 12:2; Yakobo 1:27). Mfumo wa ulimwengu ulioanguka unajaribu kukidhi mahitaji yote ya mwanadamu mbali na Mungu. Unatengeneza maisha kiasi kwamba binadamu anaonekana kuwa huru. Inaasisi kuwa sisi wote ni wa maana kwa vile twawezakuwa waabudu sanamu pale watakaporuhusu uhuru toka kwa Mungu. Mifano ni pamoja na: (1)

Page 366: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

350

mfumo wa serikali ya kibinadamu; (2) mfumo wa elimu ya kibinadamu; (3) mfumo wa kiuchumi wa binadamu; (4) mfumo wa matibabu, n.k. Kama Agustino alivyosema vizuri, "Mtu ana uwazi wenye taswira ya Mungu" katika maisha yake. Tunajaribu kuujaza uwazi huo na mambo ya kidunia, bali tunaweza kupata amani pekee na utimizaji katika Yeye! Uhuru ni laana ya Edeni!

◙ "Kama" Hii ni sentensi yenye masharti daraja la tatu, ambayo inamaanisha kuwepo na uwezekano wa kitendo muhimu. Tunachokipenda ni ushahidi wa sisi ni wa nani. . .Mungu au Shetani.

2:16 "tamaa ya mwili" Hii inarejea mwenendo wa utafutaji binafsi wa mwanadamu aliyeanguka (kama vile. Gal. 5:16-21; Efe. 2:3;1 Petro 2:11). Tazama Mada Maalumu: mwili (sarx) katika Yohana 1:14

◙ "tamaa ya macho" Wayahudi walitambua kwamba macho ni madirisha ya Roho. Dhambi huanza katika fikra za za maisha na hufanya njia kutekeleza kitendo. Na kitendo hicho huanza kujimilikisha katika maisha (mf. Mith.23:7).

◙ "na kiburi cha uzima" Hii inarejea kwa kiburi cha binadamu mbali na Mungu (yaani, binadamu huamini katika rasilimali zao wenyewe). Katika The Jerome Bible Commentary, vol. II, Raymond Brown, msomi anayejulikana wa Kikatoliki, anasema maneno, "Hata hivyo, neno alazoneia, linapatika na pia katika Yakobo 4:16, ina maana zaidi ya utendaji kisha kiburi tu: Inaonyesha kiburi,hali ya majivuno, hali ya kuridhika" (uk. 408). Neno maisha ni bios amabalo linarejereamambo ya ki-Dunia, kimwili, maisha ya muda mfupi, kwenye sayari hii (ni kipi mwanadamu anashirikiana na mimea na wanyama, kama vile. Yohana 1.3:17). Hii tabia inaelezea makundi yote ya walimu wa mafunuo mafunuo ya uongo na mwanadamu aliyeanguka ambaye hajarejeshwa. Mungu atusaidie, pia walielezea wakristo wachanga! ◙ "havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia" Kuna sababu mbili zitakazo sababisha wakristo lazima wasipende Dunia.

1. kwamba upendo hautoki kwa Baba (kama vile 1 Yohana 2:16) 2. Dunia inapita (kama vile 1 Yohana 2:17)

2:17 "dunia inapita" Hii ni kauli ya kati elekezi ya wakati uliopo (kama vile Yohana 1. 2:8). Hii inahusiana na enzi mbili za Wayahudi. Enzi mpya na iliyotimilka inakuja; enzi ya kale ya uovu na uasi inapita (kama vile Rum. 8:18-25).

MADA MAALUMU: ENZI HII NA ENZI IJAYO

Manabii wa Agano la Kale waliutazama wakati ujao kama upanuzi wa wakati uliopo. Kwao wakati ujao utakuwa marejesho ya Israeli ya kijiografia. Hata hivyo, hata wao waliuona kama siku mpya (kama vile Isa. 65:17; 66:22). Kwa kwendelea kukataliwa YHWH kwa makusudi na uzao wa Abraham (hata baada ya uhamisho) ni kielelezo kiliicho dhihirika ndani ya hati ya Kiyahudi ya fasili ya mambo ya ufunuo wa matukio ya siku za mwisho (yaani, I Enoch, IV Ezra, II Baruch). Maandishi haya yanatengeneza utofauti kati ya zama hizi mbili: zama za uovu za sasa zinazomilikiwa na Shetani na zama zijazo za haki zinazomilikiwa na Roho na zilizozinduliwa na Masihi (apiganaye mwenyewe mara kwa mara). Katika eneo hili la theolojia (hukumu, kifo na peponi) kuna maendeleo ya dhairi. Wanatheolojia wanalihita hili "ufunuo endelevu." Agano Jipya linakubaliana na ukweli huu mpya wa kiulimwengu wa zama hizi mbili (yaani, nyakati mbili

Yesu Paulo Waebrania (Paulo)

Mt. 12:32; 13:22,39 Warumi 12:2 Ebr.1:2; 6:5; 11:3

Page 367: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

351

Marko 10:30

1 Kor. 1:20; 2:6,8; 3:18

Luka 16:8; 18:30; 20:34-35 2 Kor. 4:4

Wagalatia 1:4

Efe. 1:21; 2:2,7; 6:12

1 Timotheo 6:17

2 Timotheo 4:10

Tito 2:12

Katika thiolojia ya Agano Jipya zama hizi za Kiyahudi zimekuwa zikipishana kwa sababu ya tabiri zisizotarajiwa na ambazo hazikutiliwa maanani zilizohusu kuja kwa Masihi. Kuonekana kwa Yesu katika umbile la mwili kulitimiza unabii mwingi wa Agano la Kale uliohusu utambuzi wa zama mpya (Dan. 2:44-45). Hata hivyo, Agano la Kale pia liliutazama ujio Wake kama Hakimu na Mshindi, bado alikuja kwa mara ya kwanza kama Mtumishi Ateswaye (kama vile Isaya 53; Zek. 12:10), mnyenyekevu na mpole (kama vile Zekaria 9:9). Atarudi katika nguvu ile ile kama Agano la Kale liilivyotabiri (kama vile Ufunuo 19). Utimilifu wa zama hizi mbili ulisababisha Ufalme kuwepo (uliotambuliwa), lakini zile zijazo (hazijatimilika ipasavyo). Huu ni mvutano wa Agano Jipya wa uliopo tayari, lakini bado!

◙ "bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele" Angalia ni kwa jinsi gani uzima wa milele (yaani, kihalisia “kudumu katika enzi") umeunganishwa na upendo wa maisha, sio ukiri wa imani ya zamani (kama vile. Mt. 25:31-46; Yakobo 2:14-26). Tazama Mada Maalumu: Mapenzi ya Mungu (thelēma) katika Yohana 4:34

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): 1 YOHANA 2:18-25 18 Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho. 19 Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu. 20 Nanyi mmepakwa mafuta na Yeye aliye Mtakatifu nanyi mnajua nyote. 21 Sikuwaandikia ninyi kwa sababu hamwijui iliyo kweli, bali kwa sababu mwaijua, tena kwamba hapana uongo wo wote utokao katika hiyo kweli. 22 Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye mpinga Kristo, yeye amkanaye Baba na Mwana. 23 Kila amkanaye Mwana, hanaye Baba; amkiriye Mwana anaye Baba pia. 24 Ninyi basi, hilo mlilolisikia tangu mwanzo na likae ndani yenu. Ikiwa hilo mlilolisikia tangu mwanzo linakaa ndani yenu, ninyi nanyi mtakaa ndani ya Mwana, na ndani ya Baba. 25 Na hii ndiyo ahadi aliyotuahidia, yaani, uzima wa milele.

2:18 "Watoto" Angalia muhtasari katika 1 Yohana 2:1.

◙ "ni wakati wa mwisho" Kifasihi ni "Saa ya mwisho" ikiwa na kibainishi (kinapatikana hapa pekee). Kama "siku za mwisho," hii ni moja ya kifungu kilichotumika katika Agano jipya kuelezea kuja kwa Yesu mara ya pili (kama vile. Yohana 6:39-40, 44). Hii ni dhana muhimu katika Yohana kwa sababu katika siku zetu wakalimani wengi wameathiriwa na C. H. Dodd's "kutambulika kwa mambo ya siku za mwisho" (imani kuu ya kupinga utawala wa Yesu wa miaka 1000). Na kwa hakika ni kweli kwamba Yohana peke yake na kwa nguvu anafundisha kwamba ufalme wa Mungu umekuja kupitia Yesu. Hata hivyo, maandiko haya yanafunua kwamba pia kuna ukamilisho wa baadaye (tukio au wakati). Yote ni kweli. Huu ni ufafanuzi mwingine wa mvutano wa Agano jipya (fumbo la maneno) kati ya "ulimwengu uliokwisha kuwa tayari na ambao bado" (yaani; "unakuja") wa enzi mbili za Wayahudi, ambao sasa imepishanishwa na wakati.

Page 368: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

352

◙ "mpinga Kristo. . . mpinga Kristo" Hivi vifungu vya kuelezeka vyote viko katika hali ya umoja na wingi; hakuna kifungu chenye kibainishi (ikifuatiwa na MSS א*, B, C). Yohana pekee hutumia neno hili katika Agano jipya (kama vile 1 Yohana 2:18,22; 4:3; 2 Yohana 7). Tazama muhtasari kamili katika mtazamo wa ndani wa kimuktadha wa 1 Yohana 2:3-27, D.

◙ "yuaja" Hii ni kauli ya kati elekezi ya wakati uliopo (shahidi wa maandishi). Katika lugha ya kawaida ya Koine baadhi ya miundo mingine ya vitenzi vya kiyunani havikutenda kazi na vingine vilifanikiwa kutenda kazi badala yake. Vitenzi vyenye ushahidi wa maandishi ni irabu ya kati au irabu tendwa katika muundo, lakini hutafsiriwa kama irabu tendaji katika maana. Hapa wakati uliopo unatumika kuelezea uhakika wa tukio la baadaye. Mpinga kristo, hali ya umoja, yuaja na walimu wengi wa uongo au masihi wa uongo sawa na yeye tayari wamekuwepo (mpinga kristo). Yawezekana ni kitheolojia tu kuwa kwa vile shetani hajui kurudi kwa Yesu mara ya pili,ana mtu tayari aliyemwandaa kusimama kama kiongozi wa dunia muda wowote.

◙ "wamekwisha kuwapo" Hii ni kauli timilifu tendaji elekezi. "roho ya mpinga Kristo” tayari ipo sasa na inatenda kazi katika huu ulimwengu ulioanguka (yaani, walimu wa uongo), hata hivyo bado kuna udhihilisho wa baadaye. Baadhi ya watoa maoni wanaelewa kuwa hii inarejea kwa ufalme wa Warumi wa siku za Yohana, wakati wengine wanaona ni ufalme wa ulimwengu wa baadaye wa siku za mwisho. Katika maana nyingi, ni zote! Wakati wa mwisho ulizinduliwa kwenye kufanyika mwili kwa Yesu na utaendelea mpaka siku ya utimilifu (kuja kwa mara ya pili kwa Kristo).

2:19 "Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu" Huu ni mfano kamili wa walimu wa uongo na toba ya uongo ndani ya kanisa (kama vile. Mt. 7:21-23; 13:1-9,18-23,24-30). Kukosekana kwa ukweli, upendo na uvumilivu ni ushahidi tosha kwamba wao sio waaminio. Uasi siku zote unakuja kutoka miongoni mwao! Mwandishi wa 1 Yohana ni muangarifu sana katika uchaguzi wake wa njeo ya kitenzi. 1 yohana 2:19 inaaksi

1. Walimu wa uongo wameondoka (wakati uliopita usiotimilifu) 2. Kamwe hawakuwa sehemu kati yao (wakati usiotimilifu) 3. Ikiwa walikuwa ni sehemu kati yao wasingeweza kuondoka (sentensi shurutishi daraja la pili pamoja na

njeo ya kitenzi cha wakati uliopita ainishi ) Tazama MADA MAALUM: UASI katika Yohana 6:64.

◙"kama" Hii ni sentensi shurutishi daraja la pili ambayo inaitwa kinyume na kweli. Inapaswa kutafsiriwa, "kama wangalikuwa wetu, ambao hawakuwa,basi wangeweza kukaa pamoja nasi, ambavyo hawakufanya."

◙ "wangalikaa pamoja nasi" Hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati timilifu ainishi ambayo inazungumzia kitendo kilichokamilishwa wakati uliopita. Hii ni moja ya baadhi ya marejeleo ya mafundisho ya uvumilivu (kama vile 1 Yohana 2:24, 27,28). Imani ya kweli hubaki na huzaa matuda (kama vile Mt. 13:1-23). Tazama Mada Maalum katika Yohana 8:31

2:20 "Nanyi mmepakwa mafuta na Yeye aliye Mtakatifu" Neno "Nanyi" ni wingi ambalo linasisitizwa katika maandishi ya kiyunani katika ajili ya utofautishaji wa wale ambao wameondoka kwenye ushirika wa Wakristo. Hii inawezekana kwamba mafunuo yalikuwa yameathiriwa na “muujiza” wa dini za Mashariki na kufundishwa utiwaji wa mafuta maalumu ambao huleta ujuzu na utambulisho pamoja na Uungu. Yohana anadai kwamba walikuwa ni waamini, na sio watu wa mafunuo ya uongo, waliotiwa mafuta (sherehe maalumu) kutoka kwenye Uungu.

MADA MAALUMU: ALIYE MTAKATIFU

I. "Aliye Mtakatifu wa Israeli" ni jina la Uungu lililoshamiri katika Isaya (kama vile Isa. 1:4; 5:19; 10:17,20; 12:6; 17:7; 29:19,23; 30:11,12,15; 31:1; 37:23; 40:25; 41:14,16,20; 43:3,14,15; 45:11; 47:4; 48:17; 49:7; 54:5; 55:5; 60:9,14). Kwa sababu Yeye ni "mtakatifu," watu Wake yawapasa kuwa watakatifu (kama vile

Page 369: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

353

Law. 19:2; Mt. 5:48; 1 Pet. 1:16). Jina hili, katika maana, linaeleza mvutano usiowezekana wa wenye dhambi, watu walioanguka kutii na kuingia katika kiwango cha utakatifu. Agano la Musa halikuwa na uwezekano wa kuutunza (kama vile Yos. 24:19; Matendo 15; Wagalatia 3; kitabu cha Waebrania). Agano la kale lilikuwa ni njia ya kuonyesha kutowezekana kwa wanadamu kukitii kiwango cha Mungu (Wagalatia 3), bado alikuwa pamoja nao, kuwaandaa kwa ajili ya jibu Lake katika hali ya kuanguka kwao (yaani, "Agano Jipya katika Yesu"). Akishusha kiwaango Chake, bali alikitoa kupitia Masihi Wake. Agano Jipya (kama vile Yer. 31:31-34; Eze. 36:22-38) ni agano la imani na toba, na si utendaji wa mwanadamu, ingawa linatoa Ufanano wa Kristo (kama vile Yakobo 2:14-26). Mungu anamtaka mtu anaeangaza tabia yake kwa mataifa (kama vile Mt. 5:48).

II. "alivyo mtakatifu" inaweza kurejea juu ya 1. Mungu Baba (kama vile vifungu vingi vya Agano la Kale juu ya "aliye Mtakatifu wa Israeli") 2. Mungu Mwana (kama vile Mk 1:24; Luk 4:34; Yohana 6:69; Matendo 3:14; 1 Yohana 2:20) 3. Mungu Roho (jina Lake, "Roho Mtakatifu" kama vile Yohana 1:33; 14:26; 20:22).

Matendo 10:38 ni mstari ambapo watu wote wa asili ya Mungu wanahusishwa katika kupakwa mafuta. Yesu alipakwa mafuta (kama vile Luka 4:18; Matendo 4:27; 10:38). Dhana imepanuka ili kuwajumuisha waamini wote (kama vile 1 Yohana 2:27). Aliyepakwa mafuta amekuwa mpakwa mafuta! Hii inaweza kuwa sambamba na Mpinga Kristo au wapinga Kristo (kama vile 1 Yohana 2:18). Katika Agano la Kalelilikuwa ni tendo la kiishara la kimwali la kumiminia mafuta (kama vile Kut. 29:7; 30:25; 37:29) inahusiana na wale ambao waliitwa na kuandaliwa na Mungu kwa ajili ya kuifanya kazi yake maalumu (yaani, manabii, makuhani, na wafalme). Neno "Kristo" ni tafsiri ya neno la Kiebrania "aliye pakwa mafuta" au Masihi.

◙ "mmepakwa mafuta" Tazama MADA MAALUM: Kutiwa Mafuta katia Biblia (BDB 603) katika Yohana 11:2

NASB "Nanyi mnajua nyote" NKJV "Nanyi mnajua vitu vyote" NRSV "Nanyi nyote mna maarifa" TEV "Nanyi nyote mnaijua kweli" NJB "Na wote mmepokea maarifa

Hii ilikuwa kauli yenye umuhimu katika uwazi wa mafunuo ya majivuno ya walimu wa uongo wakijidai kuhusu maarifa yao ya siri. Yohana anaonyesha kwamba waaaminio wana msingi wa ujuzi wa Ukristo (Yohana 1.2:27 na Yohana 16:7-14 na Yer. 31:34), sio maarifa kamilifu hususani katika ulimwengu au maarifa mengine (kama vile Yohana 1. 3:2). Kwa Yohana, ukweli ni kwa vyotekifikra na kibinafsi, kama utiaji wa mafuta ambao unaweza kurejerea kwenye injili au Roho. Kuna maandiko tofauti ya Kiyunani katika kifungu hiki. NKJV inafuata maandiko ya herufi kubwa ya A, C, na K, ikiwa na neno panta, uwingi wenye hasi hutumika kama yambwa tendwa , wakati NASB inafuata maandiko א, B, na P, ikuwa na neno pantes, uwingi jinsi ya (ME), ambao unalenga kwenye kishamirisho "ninyi nyote." Katika nuru ya madai ya pekee ya walimu wa uongo, chaguo la mwisho ni bora. UBS4 inaipa alama "B" (karibu na hakika).Utiwaji wa mafuta pamoja na maarifa hutolewa kwa waamini wote, sio kwa wale waliochaguliwa, walio muhimu, wasomi, walio wa kiroho wachache!

2:21 Hii ni moja ya aya nyingi ambazo zinaonyesha kwamba wasomaji wa Yohana wana moyo wa kujiamini wa imani ya ukombozi na kujua ukweli. Katika aya hii imani imeegemea kwenye kutia mafuta toka kwa Roho ambayo huwapa waaminio njaa na maarifa ya injili.

2:22 "Ni nani aliye mwongo" Huu kifungu hiki kina kibainishi wazi, kwa hiyo, Yohana anarejerea ama kwa 1. Mwalimu fulani wa uongo (huenda akawa Cerinthus) 2. "Uongo mkubwa" na kuikana injili (kama vile 1 Yohana 5:10)

Page 370: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

354

Neno "muongo" linafanana na "mpinga Kristo." Roho ya mpinga Kristo ipo sasa katika kila enzi; ufafanuzi wa msingi ni (vidokezo viwili vyenye KIHUSISHI "dhidi ya") ni "mmoja ambaye anakataa kwamba Yesu si Kristo" au "mmoja ambaye anajaribu kushika nafasi ya Kristo."

◙ "Yesu ni Kristo" The Jerome Biblical Commentary, uk. 408, imefanya hatua nzuri, "Mwandishi hakumaanisha tu utimilifu na Yesu kwa Agano la kale na matarajio ya Wayahudi juu ya Masihi. Kristo hapa alikuwa na uelewa kamili kama usanifu wa Agano jipya ulivyopendekeza juu ya Yesu, ambaye maneno yake na matendo yalimtangaza kuwa mwokozi wa ki-Ungu wa mwanadamu' (kama vile Matendo 2:31; Warumi. 1:4)." Yawezekana kwamba uthibitisho huu wa kimafundisho kufanya kazi

1. kama mabishano dhidi ya Mafunuo ya uongo 2. Mfumo wa kanuni za imani ya Wapalestina kwamba kutofautishwa kwa wazi hekalu la kiyahudi kutoka

kwenye kanisa; yaweza kumaanisha kuwa ni mifumo ya laana ya walimu wa dini ya Kiyahudi kwenye mji ulioko katikati ya Israeli (K.K. 70)

3. kama "Yesu ni Bwana," yawezakuwa ni uthibitisho wa kiubatizo ◙ 2:22-23 "Kila amkanaye Mwana" Inavyoonekana kuwa walimu wa mafunuo ya uongo walidai kumjua Mungu, lakini walikataa, waliyaondoa madaraka na waliipunguza thamani nafasi ya Yesu Kristo (kama vile 1 Yohana 4:1-6; 5:11-12; Yohana 5:23). Ikitegemea juu ya maandishi ya mafunuo ya uongo kutoka kwenye karne ya pili B.K., maoni miongoni mwa Agano Jipya, na makasisi wa kanisa la mwanzo, imani zifuatazo zinajitokeza.

1. Mafunuo ya uongo yalijaribu kuozesha ukristo kwa falsafa ya kiyunani (Pilato) na dini za miujiza za mashariki.

2. Walifundisha kwamba Yesu alikuwa wa ki-Ungu lakini sio mwanadamu kwa sababu roho ilikuwa njema, lakini Umbo (mwili) ulikuwa mwovu. Kwa hiyo, kulikuwa hakuna uwezekano wa kupata mwili wa Uungu.

3. walifundisha mambo mawili kuhusu wokovu a. Kundi moja lilidai kwamba maarifa maalumu ya ulimwengu wa kimalaika (aeon) yalileta wokovu wa

roho isiyohusiana na matendo ya mwili juu ya mwili ulio dhahiri. b. Kundi lingine limetia mkazo kwa kujinyima anasa za mwili (kama vile Kol. 2:20-23). Walidai kuwa

kukataa vyote vile ambavyo mwili unataka na kuhitaji ni muhimu kwa wokovu wa kweli.

2:23 Aya hii katika upokeaji wa maandiko, ukifuatia maandiko ya herufi kubwa ya K na L, imepunguza kwa bahati mbaya maandishi ya kiasili kwa kuondoa nukuu inayofanana ya pili kwa Baba, ambayo imeungwa mkono kwa nguvu na maandiko ya kiyunani ya herufi kubwa ya א, A, B, na C.

◙ "amkiriye" Hakika hii ni kinyume kabisa cha “yeyote anayekana” katika 1 Yohana 2:22 [mara mbili] na 23 [mara moja] na 26 [mara moja]. Tazama Mada Maalumu: Ukiri katika Yohana 9:22-23.

◙ "Mwana" Ushirika pamoja na Mungu unapatikana pekee kupitia imani katika Mwana (kama vile 1 Yohana 5:10-12,13). Imani katika Yesu sio kitu cha uchaguzi! Yeye ndio njia pekee kwenda kwa Baba (kama vile Yohana 5:23; 14:6; Luka 10:16).

2:24 "Ninyi basi" Hii inaonyesha mkazo wa utofauti uliopo kati ya wasomaji wa Yohana na walimu wa uongo na wafuasi wao walioondoka (kama vile 1 Yohana 2:27).

◙ "hilo mlilolisikia tangu mwanzo na likae ndani yenu" Hii ni kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopo pamoja na msisitizo wa kisarufi juu ya neno “ninyi” (ambayo ni mwanzo wa kifungu cha kiyunani) katika utofautisho linganishi wa ujumbe wa walimu wa uongo. Injili ni mfano halisi na imeelezewa kama mgeni aishiye ndani. Hii ni sababu ya kwanza kati ya sababu mbili zilizotolewa kwa ushindi wa wakristo juu ya walimu wa uongo (waongo). Ya pili inapatikana katika 1 Yohana 2:20 na 27, ambapo kutia mafuta kwa Roho kumetajwa. Tena, injili ikiwa kwa pamoja kama ujumbe na nafsi imeunganishwa na msemo “kutoka mwanzo” (kama vile 1 Yohana 2:13, 14, 24

Page 371: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

355

[mara mbili]). Neno la Mungu kwa pamoja ni maudhui na ubinafsi, yote yaliyoandika na yanayoishi (kama vile. 1 Yohana 1:8,10; 2:20,24)! Tazama Mada Maalum: "Kukaa" katika Yohana 2:10

◙ "ikiwa" Hii ni sentensi enye masharti daraja la tatu, ambayo inamaanisha kuwezekana kwa kitendo. Hii inaendeleza onyo na kuasa inayohusiana na “kuendelea kudumu.” ukoma unaodumu unadhihilisha kuwa kamwe haukuwa sehemu yake (kama vile 1 Yohana 2:18-19). Ushahidi wa maisha kwa “kukaa” kunaleta imani ya moyo wa kujiamini (kama vile Yohana 15). Kuendelea kudumu ni ujumbe uliosikika na kupokelewa na ushirika pamoja na wote Mwana na Baba (kama vile. Yohana 14:23) amabao umefunuliwa katika chaguo la mfumo wa maisha, yote chanya (upendo) na hasi (kukataliwa kwa ulimwengu).

2:25 "Na hii ndiyo ahadi aliyotuahidia, yaani, uzima wa milele" Tena viwakilishi nomino katika 1 Yohana 2:25 vina utata mwingi sana na inaweza kurejea kwa Mungu Baba au Mungu Mwana. Labda hii ni muhumu sana (kama katika 2 Petro 1). Inavyoonekana kauli hii ni kama Yohana 3:15-16 na 6:40. Tumaini la muumini linakaa katika tabia na ahadi ya Mungu (kama vile Isaya 45:23; 55:11). Ushirika wetu wa ndani pamoja na Mungu wa Utatu unatoka katika tumaini, naam, ahadi ya uzima wa milele (kama vile 1 Yohana 5:13). Uzima wa milele una tabia zinazoonekana.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) 1 YOHANA 2:26-27 26 Nimewaandikia haya katika habari za watu wale wanaotaka kuwapoteza. 27 Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake.

2:26 “wale wanaotaka kuwapoteza" Hii ni kauli tendaji endelevu ya wakati uliopo. Kuna watu wadanganyifu katika kila rika (kama vile Mt. 7:15; 24:11,24; 2 Yohana 7). Mara nyingi hawa ni waumini waaminifu ambao wanahudhuria na hutenda katika mkusanyiko wa Wakristo.

2:27 "mafuta yale" Hii inaonekana kusistiza juu ya matokeo ya kutia mafuta, sio kwa maana (Roho) au viashiria (ukweli wa injili) vilivyohusishwa. Kutiwa mafuta ilikuwa ni dhana ya Agano la kale kwa wito muhimu na kutayarisha mtu kwa kazi aliyopewa na Mungu. Manabii, Makuhani, na Wafalme walitiwa mafuta. Hili neno kiasili linahusianishwa kwenye neno “Masihi.” Hapa inarejea uimara unaotokea ambapo uangazaji wa Roho mtakatifu wa moyo na fikra kuhusu injili inavyofikishwa kwa waaminio. Tazama MADA MAALUMU: Kutiwa Mafuta katika Biblia (BDB 603) katika Yohana 11:2 Walimu wa uongo walidai ufunuo maalumu kutoka kwa Mungu (yaani, kutia mafuta malumu). Yohana anadai kuwa waaminio wote tayari wametiwa mafuta ya kweli wakati wakiamini yule aliyetiwa mafuta, wamejazwa pamoja na Roho wake na kuendelea kukaa katika neno la Mungu.

◙ “yale mliyoyapata” hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo usiotimilifu ambayo inaonyesha kwa baadhi ya kitendo kilichokamilishwa wakati uliopita. Neno “kutia mafuta” ni linafanana na “mmesikia” katika 1 Yohana 2:24. Injili lazima ipokelewe (1) kipekee kwa imani (kama vile Yohana 1:12; 3:16) na (2) kama mwili wa kweli (kama vile 2 Yohana 9-10; 1 Kor. 15:1-4; Yuda 3). Vitendo hivi vyote vimeanzishwa na Roho mtakatifu.

◙ "wala hamna haja ya mtu kuwafundisha" Yohana 1 2:27 ni inafanana na 1 Yohana 2:20 (yaani, Agano jipya, kama vile Yer. 31:34). Yohana anatumia dhamira ya mara kwa mara (1 Yohana2:20, 24, 27). Roho mtakatifu, sio wale walimu wa uongo wa mafunuo, ndiye mwalimu wetu wa mwisho na wa lazima (kama vile Yohana 14:26). Hata hivyo, hii haimaanishi kwamba idara na karama ya mwalimu haikutenda katika kanisa la mwanzo na sasa (kama vile Efe. 4:11; Matendo 13:1; 1Kor. 12:28). Ina maana kwamba vitu muhimu vinavyohusu wokovu huja toka kwa Roho mtakatifu na Biblia, sio kutoka kwa mwalimu wa kibinadamu maalumu, aliyekilimiwa, ingawa mara nyingi huvitumia kama njia.

Page 372: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

356

◙ "lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo" Hii inarejea kwa ukweli wa Roho.Kila Mkristo ana Roho Mtakatifu anayelinda dhamiri yake. Lazima tuwe wepesi kutambua uongozi wa upole wa Roho katika maeneo ya kweli na maadili.

◙ "na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake" Hii ni kauli tendaji yenye masharti ya wakati uliopo. Yohana hutumia dhana ya “kuendelea kudumu” kwa kiasi kikubwa katika nyaraka zake kama ishara ya imani ya moyo wa kujiamini kwa wasomaji wake (kama vile Yohana 15). Imani ya kibiblia ni agano ambalo Mungu anachukua ari na kuweka ajenda, lakini mwanadamu lazima aitikie kwanza na kuendelea (kukaa)! Kuna vyote dhana ya ki-Mungu na dhana ya mwanadamu inayohusishwa katika kuendelea kudumu. Tazama Mada Maalum: "Kukaa" katika 1 Yohana 2:10.

MASWALI YA MJADALA

Huu ni mwongozo wa fasiri, ina maanisha kwamba unawajibika kwa tafsiri zako mwenyewe za Biblia. Kila mmoja wetu lazima atembee katika mwanga tulio nao. Wewe, Biblia, na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Hutakiwi uvitelekeze vitu hivi kwa mfasiri. Maswali ya mjadala huu yanatolewa kukusaidia kufikiri juu ya mambo makubwa ya sehemu za kitabu hiki. Yanalenga kukuamsha kimawazo na sio kutoa maana.

1. Elezea imani ya walimu wa uongo. 2. Toa ushahidi ambao tunaweza kujua kwamba sisi tumekombolewa kweli. 3. Elezea uhusiano kati ya dhambi ya mazoea na vitendo vya kipekee vya dhambi. 4. Elezea uhusiano kati ya uvumilivu wa mtakatifu na usalama wa muamini. 5. Taja na elezea maadui watatu wa mwanadamu/mtu.

Page 373: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

357

1 YOHANA 2:28-3:24

MIGAWANYO YA AYA YA TAFSIRI ZA KISASA

UBS4 NKJV NRSV TEV NJB Wana wa Mungu Wana wa Mungu Utiifu kwa imani ya Adui wa Kristo Kuishi kama watoto Kweli wa Mungu (2:28-3:10) (2:18-20) (2:18-20) 2:29-4:6 2:28-3:3 2:28-3:3 2:28 2:28-29 2:29 Uhusiano wa Mtoto Uelezwao kama Mwaenendo wa haki 3:1-10 3:1-3 Agizo la kwanza la Kuacha dhambi Dhambi na watoto Wa Mungu 3:3-10 3:4-10 3:4-9 3:4-6 3:7-8 3:9-10 Amri ya upendo Kupendana sisi 3:10-15 Kupendana sisi Kupendana sisi Amri ya pili Kwa sisi kwa sisi kwa sisi kuzishika amri hasa Uzima 3:11-18 3:11-18 3:11-12 3:11:24 Mtazamo wa upendo 3:13-18 Ujasiri mbele za 3:16:23 Uhakika wa Msisitizo mbele Mungu Mkristo za Mungu Roho wa kweli 3:19-24 3:19-24 Na Roho wa uovu 3:24-4:6

MZUNGUKO WA TATU WA USOMAJI KUFUATILIA KUSUDIO LA ASILI LA MWANDISHI KATIKA NGAZI YA AYA Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwatafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Aya ya kwanza 2. Aya ya pili 3. Aya ya tatu

Page 374: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

358

4. N.k UTAMBUZI WA KI-MUKTADHA

A. 1 Yohana 2 inaelekea moja kwa moja katika Mafunuo ya waalimu wa uongo (hasa Mafunuo ya Docetic ambaye alipinga kuhusiana na utu wa Yesu).

B. 1 Yohana 3 inaendelea kudokeza juu ya walimu wa uongo ambao waliutenga wokovu (uthibitisho) kutoka katika maadili na uadilifu (utakaso). Bado sura ya 3 pia inajishughulika na mwamini moja kwa moja zaidi.

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) 1 YOHANA 2:28-3:3 28 Na sasa, watoto wadogo, kaeni ndani yake, ili kusudi, atakapofunuliwa, mwe na ujasiri, wala msiaibike mbele zake katika kuja kwake. 29 Kama mkijua ya kuwa yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa kila atendaye haki amezaliwa na yeye. Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana waMungu;na ndivyo tulivyo. 3:1Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye. 2 Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwaatakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo. 3 Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu.

2:28 Kuna majadiliano mengi baina ya watoa maoni kama kifungu kipya lazima kiwe katika 1 Yohana 2:28, 29, au 3:1. Kwa sababu ya kifungu hiki kurudiwa rudiwa kati ya 1 Yohana 3:27 na 28, mgawanyo wa kifungu hiki lazima kwa yakini uwe hapa.

◙ "watoto wadogo" Tazama nukuu katika 1 Yohana 2:1.

◙ "kaeni ndani yake" hii ni kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopo. Hii ni kauli shurutishi ya wakati uliopo inayotumika kuukuza ustahimilivu wa Mkristo (kama vile 1 Yohana 3:15,24). Tazama Mada Maalumu: Hitaji la Ustahimilivu katika Yohana 8:31 na "Kukaa" katika 1 Yohana 2:10. Usuli wa hiki kiwakilishi mara nyingi ni vigumu kuutambua, lakini katika kifungu hiki, uko wazi.

1. " ndani yake," 1 Yohana 3:28b – Yesu 2. " mbele zake," 1 Yohana 3:28b – Yesu 3. " kwake," 1 Yohana 3:28b – Yesu 4. "yeye ni mwenye haki," 1 Yohana 3:29 – Baba 5. " amezaliwa na yeye," 1 Yohana 3:29- - the Father (angalia dokezi 6. " haukumtambua yeye" 1 Yohana 3:1 -- Baba (kama vile Yohana 7. " atakapodhihirishwa ," 1 Yohana 3:2- - Yesu 8. " tutafanana naye," 1 Yohana 3:2 – Yesu 9. " tutamwona," 1 Yohana 3:2 – Yesu 10. " alivyo," 1 Yohana 3:2 – Yesu 11. " katika yeye," 1 Yohana 3:3 – Yesu 12. " kama yeye alivyo mtakatifu," 1 Yohana 3:3 -- Yesu

Muktadha, muktadha, muktadha!

◙ "atakapofunuliwa" Hii ni sentensi shurutishi daraja la tatu, sawa na 1 Yohana 3:29, na pia kifungu cha "Yesu atakaporudi" cha 1 Yohana 3:2. Hii haimaanishi kueleza tukio lisilo na uhakika, bali wakati usio na uhakika (ni sawa na matumizi ya neno "tumaini," katika Agano Jipya kama vile 1 Yohana 3:3).

◙ "mwe na ujasiri" Neno la Kiyunani …"ujasiri" (parrhēsia) linatokana na mzizi wa neno "kuzungumza kwa uwazi." Uhakika ni mtindo wa maisha ya sasa ulioegemea juu ya maarifa ya mwamini na kuamini katika injii ya Yesu Kristo. Tazama Mada Maalumu: Ujasiri (parrhēsia) katika Yohana 7:4

Page 375: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

359

NASB " wala msiaibike mbele zake" NKJV "wala msiaibike machoni pake" NRSV "bila kuwa na sababu ya kujificha kwa aibu siku ya kuja kwake" TEV "wala msijifiche kwa aibu kwa sababu yake NJB "bila msiaibike katika yeye" Hii ni kauli tendewa (shahidi) tegemezi ambayo inamaanisha kwamba kifungu hiki kinaweza kueleweka kama

1. kuaibika kwa mwamini mwenyewe (NASB, TEV, NJB) 2. kuaibishwa kwa mwamini (NRSV)

Waamini yawapasa kuwa waangalifu na kufurahia katika kurudi kwake Kristo, lakini wale walioishi katika ubinafsi, anasa za kidunia hakika watastaajabu na kuaibika siku ya kuja kwake! Siku hiyo kutakuwa na hukumu ya wale waaminio (kama vile 2 Kor. 5:10).

◙ "katika kuja kwake" Huu ni urejeo wa Kurudi Mara ya Pili. Neno hili, Parousia, linatumika kwa upekee katika maandiko ya Yohana na lina maana nyingine ya kuuelekea wito wa uaminifu. Neno hili liko dhahiri "hadi ile Parousia," lenye kumaanisha "uwepo" na lilitumika kwa ajili ya wito wa uaminifu. Maneno mengine ya Agano Jipya yaliyotumika kwa ajili ya kuzungumzia tukio la Kurudi mara ya Pili ni

1. epiphaneia, "kuonekana ana kwa ana" 2. apokalupis, "isiyo badilishwa" 3. "Ile siku ya Bwana" na tofauti ya aya hii

MADA MAALUMU: MANENO YA AGANO JIPYA YAHUSUYO KURUDI KWA YESU

Msistizo wa kitheolojia kuhusiana na ujio wa siku maalumu wakati wanadamu watakapokutana na Yesu (kama Mwokozi na Hikimu) unaenda kwa udhihirisho kadhaa.

1. "siku ya Bwana wetu Yesu Kristo" (kama vile 1 Kor. 1:8) 2. "siku ya Bwana" (kama vile 1 Kor. 5:5; 1 The. 5:2; 2 The. 2:2) 3. "siku ya Bwana Yesu" (kama vile 2 Kor. 1:14; MS א kama ilivyo katika 1 Kor. 5:5) 4. "siku ya Yesu Kristo" (kama vile Flp. 1:6) 5. "siku ya Kristo" (kama vile Flp. 1:10; 2:16) 6. "Siku yake (Mwana wa Adamu)" (kama vile Luka 17:24) 7. "siku ile ambayo Mwana wa Adamu atafunuliwa" (kama vile Luka 17:30) 8. "ufunuo wa Bwana wetu Yesu Kristo" (kama vile 1 Kor. 1:7) 9. "wakati Bwana Yesu atakapofunuliwa kutoka mbinguni" (kama vile 2 The. 1:7) 10. "katika uwepo wa Bwana Yesu katika ujio wake" (kama vile 1 Thes. 2:19)

Kuna njia kama nne ambazo waandishi wa Agano Jipya wazitumia kurejelea tukio la kurudi kwa Yesu. 1. epiphaneia, neno ambalo linarejelea juu ya ung’avu wenye mng’aro ambao ni wa kitheolojia (ingawa sio

wa asili ya neno) unahusiana na neno "utukufu."Katika 2 Tim. 1:10; Tito 2:11 na 3:4 neno hili linaurejelea ujio wa kwanza wa Yesu (yaani, umbile lake la mwili) na Ujio wake wa mara ya Pili. Hili linatumika katika 2 Thes. 2:8 ambapo linajumuisha maneno yote makuu matatu kwa huu Ujio wa mara Pili: 1 Tim. 6:14; 2 Tim. 4:1,8; Tito 2:13.

2. parousia, neno ambalo linalomaanisha uwepo na kwa asilia ya kurejelea juu ya ugeni wa kifalme. Hili ni neno lililotumika kwa mapana zaidi (kama vile Mt. 24:3,27,37,39; 1 Kor. 15:23; 1 The. 2:19; 3:13; 4:15; 5:23; 2 Thess. 2:1,8; James 5:7,8; 2 Pet. 1:16; 3:4,12; 1 Yohana 2:28).

3. apokalupsis (au apocalypsis), ambayo yanamaanisha kutofunuliwa kwa kusudi la ufunuo. Hili ni jina la kitabu cha mwisho katika Agano Jipya (kama vile Luka 17:30; 1 Kor. 1:7; 2 The. 1:7; 1 Pet. 1:7; 4:13).

4. phaneroō, neno ambalo linalomaanisha kuleta mwanga au kufunua dhahiri au kudhihirisha. Hili ni neno linalotumika mara kwa mara katika Agano Jipya katika vipengele vingi vya ufunuo wa Mungu. Hii, ni sawa na neno epiphaneia, ambalo linaweza kurejelea juu ya ujio wa kwanza wa Yesu (kama vile 1 Pet.

Page 376: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

360

1:20; 1 Yohana 1:2; 3:5,8; 4:9) na kurudi kwake mara ya pili (kama vile Mt. 24:30; Kol. 3:4; 1 Pet. 5:4; 1 Yohana 2:28; 3:2).

5. Neno la kawaida sana la "kurudi," erchomai, pia linatumika kwa tukio la Kristo kurudi mara ya pili (kama Mt. 16:27-28; 23:39; 24:30; 25:31; Matendo 1:10-11; 1 Kor. 11:26; Ufu. 1:7,8).

6. Pia neno hili linatumika na aya "siku ya Bwana" (kama vile 1 The. 5:2), ambalo ni jina la kitabu cha Agano la Kale kuhusu siku ya Mungu ya Baraka (ufufuo) na hukumu.

Kitabu cha Agano Jipya kama kitabu kamili kimeandikwa kwa mtazamo wa uliwengu wa Agano la Kale, ambacho kilizungumzia kuhusiana na

a. uovu wa sasa, zama za uasi b. zama mpya za haki zijazo c. zama zinazoletwa na nguvu ya kupitia kazi ya Masihi (Aliyemiminiwa Mafuta)

Wazo la kitheolojia la ufunuo endelevu linahitajika kwa sababu waandishi wa Agano Jipya kwa bezo walibadilisha matarajio ya Israeli. Badala ya majeshi ya wenyeji (Israeli) wa Masihi ajaye, kuna ujio wa aina mbili. Ujio wa kwanza ni umbile la kimwili la Uungu katika kuchukuliwa mimba na kuzaliwa kwa Yesu wa Nazarethi. Yeye alikuja kama asiye kuwa wa kivita, asiye wa kisheria "mtumishi aliyeteseka" wa Isa. 53; pia ni mnyenyekevu aliyepanda mwana punda (si farasi wa vita wala wa kifalme), wa Ezek. 9:9. Ujio wa kwanza unatoa nafasi kwa ajili ya Zama Mpya za Kimasihi, Ufalme wa Mungu juu ya dunia (tazama Mada Maalumu: Ufalme wa Mungu). Katika maana moja Ufalme uko hapa, lakini kwa yakini, mahari pengine huu bado uko mbali. Huu ni mvutano baina ya ujio wa aina mbli za Masihi (tazama MadaMaalumu: Masihi) ambao, katika maana yake, hizi ni zama mbili za Kiyahudi zinazopishana (tazama Mada Maalumu: Zama hizi na Zama Zijazo) ambazo hazikuonekana, au kuwa na unafuu wa kutokuwa sawa, kutoka ndani ya Agano Jipya. Katika ukweli, huu ujio wa mara ya pili unasistiza ahadi ya YHWH ya kuwakomboa wanadamu wote (kama vile Mwa. 3:15; 12:3; Kut. 19:5 na kuhubiri kwa manabii, hasa Isaya na Yona).

Kanisa hallingojei kutimia kwa unabii wa Agano la Kale kwa sababu unabii ulio mwingi unadokeza juu ya ujio wa mara ya kwanza (kama vile How to Read the Bible For All Its Worth, kr. 165-166). Nini waamini wanakingoja ni ujio wa utukufu wa Mfalme wa Wafalme aliyefufuliwa na Bwana wa Mabwana, utimilifu wa kihistoria wa zama mpya za mwenye haki duniani kama ilivyo mbinguni (kama vile Mt. 6:10). Uwasilishaji wa kitabu cha Agano la Kale haukuwa sahihi, lakini pia haukukamilika. Yeye atakuja tena kama manabii walivyotabiri katika nguvu na malaka ya YHWH. Ule ujio wa mara ya pili si neno la kibiblia, bali dhana ya mtazamo wa kiulimwengu na muundo wa Agano Jipya. Mungu atayapangilia yote kwa unyoofu. Ushirika baina ya Mungu na mwanadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wake utarejeshwa. Waovu watahukumiwa na kuondolewa. Kusudi la Mungu halitashindwa, haliwezi, kushindwa! Kanisa la kale liliabudu siku ya Sabato na siku ya kwanza ya juma (yaani, Jumapili, siku ya ufufuo). Masinagogi yalishughilika na kundi la Wakristo lililokuwa katika hatua ya kukua kwa kuwataka washiriki hao kumkana Yesu kama Masihi (yaani, dua kumi na tano). Katika kiwango hiki (yaani 70 B.K.) Wakristo walikutana siku ya jumapili tu.

2:29 "Kama" hii ni sentensi shurutishi daraja la tatu inayomaanisha tendo lenye uwezekano. Hapa aya hii inarejelea juu ya ufahamu wa kusadiki ambao waamini wanaushiriki, lakini walimu wa uongo waweukosa ufahamu huu. ◙ "mkijua" Katika muundo wa kisarufi aidha hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo, ambayo inazungumzia juu ya ufahamu endelevu, au kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopo inayozungumzia juu ya umuhimu wa ufahamu wa mwamini. Matumizi ya Yohana ya neno "kujua" kama umiliki wa wale wote ambao wana Roho na wanaoongozwa kwamba hii ni kauli elekezi.

Page 377: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

361

◙"yeye" Aya hii inamrejelea Yesu (kama vile 1 Yohana 2:1, 28; 3:7. Hata hivyo, kiwakilishi cha mwisho, "amezaliwa na yeye," kinaonekana kumrejelea Mungu Baba kwa kuwa hii aya "amezaliwa kutokana na Mungu" inatumika mara nyingi (kama vile 1 Yohana 3:9; 4:7; 5:1, 4, 18; Yohana 1:13). ◙ "mwenye haki . . . haki" Hii ndiyo sifa ya familia inayotarajiwa!

MADA MAALUM:HAKI

"Haki"ni mada muhimu ambayo mwannafunzi wa Biblia yampasa kufanya ni upanuzi binafsi wa kusoma juu ya dhana yenyewe. Katika Agano la Kale sifa za Mungu zinaelezwa kama "halali" au "haki" (KITENZI, BDB 842, KB 1003; NOMINO JINSI YA KIUME, BDB 841, KB 1004; NOMINO JINSI YA KIKE, BDB 842, KB 1006). Neno la Mesopotamia lenyewe linatokana na "mafunjo ya mto" ambayo yalitumika kama chombo cha matengenezo ya utaalamu wa mlalo ulionyooka na uelekeo wa ukuta na ua. Mungu alilichagua neno lililotakiwa kutumika kistiari juu ya asili Yake mwenyewe. Yeye ni ukingo ulionyooka (kiongozi) ambapo vitu vyote vinatathiminiwa toka kwake. Dhana hii inatetea haki ya Mungu pamoja na Haki Yake ya kuhukumu. Mwanadamu aliumbwa katika mfano wa Mungu (kama vile Mwa. 1:26-27; 5:1,3; 9:6). Mwanadamu aliumbwa kwa ushirika wa Mungu (yaani, Mwa. 3:8). Uumbaji wote ni hatua au mrejesho kwa Mungu na mwingiliano wa wanadamu. Mungu aliutaka uumbaji Wake mkuu, mwanadamu, kumjua Yeye, kumpenda Yeye, kumtumikia Yeye, na kuwa kama Yeye! Uaminifu wa mwanadamu ulipimwa (kama vile Mwanzo 3) na watu hawa wanadoa wa mwanzo walishindwa jaribio. Hii ilileta matokeo ya kuvunjika kwa uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu (kama vile Rum. 5:12-21). Mungu aliahidi kufanya marekebisho na kurejesha ushirika (kama vile Mwa. 3:15; tazama Mada Maalumu: Mpango wa Wokovu wa Milele wa YHWH). Alifanya hivi kupitia mapenzi Yake mwenyewe na Mwanae. Wanadamu hawawezi kurejesha ahadi iliyovunjwa (kama vile Rum. 1:18-3:20; Ufunuo 5). Baada ya Anguko, hatua ya kwanza ya Mungu kuuelekea urejesho ilikuwa dhana ya agano lililojikita katika mwaliko Wake na toba ya mwanadamu, imani, mwitikio wa utii (kama vile Yer. 31:31-34; Eze. 36:22-38). Kwa sababu ya Maanguko yote, wanadamu huwakuweza kujitenga na tendo (kama vile Rum. 3:21-31; Wagalatia 3). Mungu Pekee ilimbidi kuanzisha upya agano lililokuwa limevunjwa na wanadamu. Alifanya hivi kwa

1. kutangaza haki ya mwanadamu kupitia kazi ya Kristo (yaani, haki ya mahakama) 2. kwa kutoa haki huru kwa mwanadamu kupitia kazi ya Kristo (yaani, haki ya kuzuliwa) 3. kumtoa Roho akaaye ndani ambaye huleta haki (yaani, Ufanano na Kristo, urejeshaji wa mfano

wa Mungu) ndani ya mwanadamu 4. kurejesha ushirika wa Bustani ya Edeni (linganisha Mwanzo 1-2 na Ufunuo 21-22)

Hata hivyo, Mungu anahitaji mwitikio wa kimaagano. Mungu hutoa maagizo (yaani, hutoa kwa uhuru, Warumi 5:8; 6:23) lakini yawapasa wanadamu kuitikia na kuendelea kuitika katika

1. Toba 2. Imani 3. Utii kwenye stadi ya maisha 4. Ustahimilivu

Haki, kwa hiyo, ni agano, ni makubaliano kati ya Mungu na uumbaji Wake wa juu, uliyojikita juu ya sifa za Mungu, kazi ya Kristo, na Roho mwezeshaji, ambapo kila mtu kibinafsi anapaswa kuitikia kwa namna ifaavyo.Dhana inaitwa "haki kwa neema kupitia imani" (yaani, Efe. 2:8-9). Dhana inafunuliwa katika Injili, lakini si katika maneno haya. Kimsingi ilielezwa na Paulo, ambaye anatumia neno la Kiyunani "mwenye haki" katika miundo yake mbalimbali zaidi ya mara 100. Paulo, akiwa mwalimu wa sheria aliyefundishwa, anatumia neno dikaiosunē katika maana yake ya Kiebrania ya neno tsaddiq lililotumika katika Tafsiri za Maandiko ya Kale ya Kiebrania, na si kutoka katika fasiri ya Kiyunani. Katika maandishi ya Kiyunani neno linamhusu yule ambaye amethibitisha matarajio ya Mungu na jamii (yaani, Nuhu, Ayubu). Katika maana ya Kiebrania mara nyingi limendwa katika maneno ya kimaagano (tazama Mada Maalumu: Agano). YHWH ni haki, maadili, Mungu mwema. Anawataka watu Wake kuwa viumbe vipya ili kwendana na sifa zake. Mwanadamu aliyekombolewa anakuwa kiumbe kipya (kama vile 2 Kor. 5:17; Gal. 6:15).

Page 378: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

362

Upya huu unaleta matokeo katika mtindo mpya wa maisha ya Kimungu (kama vile Mathayo 5-7; Gal. 5:22-24; Yakobo; 1 Yohana).Tangu Israeli ilipokuwa katika mfumo wa utawala wa kidini hapakuwepo na maelezo sahihi na ya kinagaubaga kati ya ulimwengu (kanuni za kijamii) na Mungu (mapenzi ya Mungu). Utofauti huu unaelezwa katika maneno ya Kiebrania na Kiyunani kuwa ya kutafsirika katika Kiingereza kama "haki" (yakihusiana na jamii) na "mwenye haki" (ikihusiana na dini). Injili (habari njema) juu ya Yesu ni kwamba wanadamu walioanguka wamerejesha ushirika na Mungu. Hii limetimizwa kupitia pendo la Baba, huruma, na neema; maisha ya Mwana, kifo, na ufufuo; na kuugua kwa Roho na kielelezo cha injili. Haki ni tendo huru la Mungu, lakini linapaswa kuwa jambo la kimungu (Mtazamo wa Augustine, ambao unaakisi vyote msistizo wa Mabadiliko mapya juu ya uhuru wa injili na msisitizo wa Kanisa Katoriki juu ya maisha yaliyobadilishwa ya upendo na uaminifu). Kwa waleta mabadiliko neno "haki ya Mungu" ni shamilisho milikishi (yaani, tendo la mwanadamu aliyetenda dhambi kukubaliwa na Mungud [utakaso wa mahali], ambapo kwa Wakatoliki ni kiima milikishi, ambapo ni tendo la kuimarika zaidi kama Mungu [utakaso endelevu na uliozoeleka]. Katika mtazamo wangu, Biblia nzima kutoka Mwanzo 4 – Ufunuo 20 ni maandiko yenye kuonyesha urejesho wa ushirika wa Mungu pale Edeni. Biblia inaanza kati ya Mungu na mwanadamu kuleta ushirika na mpangilio wa dunia (kama vile Mwanzo 1-2) na Biblia inaridhia mpangilio huo huo (kama vile Ufunuo 21-22). Mfano wa Mungu na kusudi lake vitarejeshwa! lli kuthibitisha mjadala wa hapo juu andika vifungu vilivyochguliwa vya Agano Jipya vyenye vielelezo vya kundi la neno la Kiyunani.

1. Mungu ni haki (mara kwa mara imeunganishwa kwa Mungu kama Hakimu) a. Warumi 3:26 b. 2 Wathesalonike 1:5-6 c. 2 Timotheo 4:8 d. Ufunuo 16:5

2. Yesu ni haki a. Matendo 3:14; 7:52; 22:14 (jina la Masihi) b. Mathayo 27:19 c. 1 Yohana 2:1,29; 3:7

3. Mapenzi ya Mungu kwa uumbaji Wakeni ya haki. a. Mambo ya Walawi 19:2 b. Mathayo 5:48 (kama vile 5:17-20)

4. Kusudi la Mungu kutoa na kutoa haki a. Warumi 3:21-31 b. Warumi 4 c. Warumi 5:6-11 d. Wagalatia 3:6-14 e. Iliyotolewa na Mungu

a. Warumi 3:24; 6:23 b. 1 Wakorintho 1:30 c. Waefeso 2:8-9

f. Iliyopokelewa kwa imani a. Warumi 1:17; 3:22,26; 4:3,5,13; 9:30; 10:4,6,10 b. 2 Wakorintho 5:7,21

g. kupitia matendo ya Mwana a. Warumi 5:21 b. 2 Wakorintho 5:21 c. Wafilipi 2:6-11

5. Mapenzi ya Mungu ni kwamba wafuasi Wake wawe wenye haki a. Mathayo 5:3-48; 7:24-27 b. Warumi 2:13; 5:1-5; 6:1-23

Page 379: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

363

c. Waefeso 1:4; 2:10 d. 1 Timotheo 6:11 e. 2 Timotheo 2:22; 3:16 f. 1 Yohana3:7 g. 1 Petro 2:24

6. Mungu ataihukumu dunia kwa haki a. Matendo 17:31 b. 2 Timotheo 4:8

7. Kupitia matendo ya Mwana a. Warumi 5:21 b. 2 Wakorintho 5:21 c. Wafilipi 2:6-11

8. Mapenzi ya Mungu ni kwamba wafuasi wake wawe watakatifu a. Mathayo 5:3-48; 7:24-27 b. Warumi2:13; 5:1-5; 6:1-23 c. Waefeso 1:4; 2:10 d. 1 Timotheo 6:11 e. 2 Timotheo 2:22; 3:16 f. 1 Yohana 3:7 g. 1 Petro 2:24

9. Mungu atauhukumu ulimwengu kwa haki a. Matendo 17:31 b. 2 Timotheo 4:8

Haki ni tabia ya Mungu, iliyotolewa huru kwa wanadamu wenye dhambi kupitia Kristo. Hilo ni 1. agizo la Mungu 2. zawadi ya Mungu 3. tendo la Kristo 4. ni maisha yapaswayo kuishi

Lakini pia ni tendo la kuwa mwenye haki ambapo ni lazima kuwa na juhudi, uaminifu na kuishikilia, kwamba siku moja itatimizwa katika Ujio wa Pili. Ushirika na Mungu unarejeshwa katika wokovu lakini unaendelea katika maisha mazima ili kukutana naye ana kwa ana (kama vile 1 Yohana 3:2) katika kifo au ujio wa pili! Hapa kuna dondoo nzuri ya kuhitimisha mjadala huu. Imechukuliwa kutoka Kamusi ya Paulo na barua zake kutoka IVP "Calvin, zaidi sana kuliko Luther, inasistiza kipengele cha uhusiano wa haki ya Mungu. Mtazamo wa Luther juu ya haki ya Mungu unaonekana kuwa dhana ya kuwa huru. Calvin anasisitiza asili ya ajabu ya mawasiliano au kutuarifu juu ya haki ya Mungu" (uk. 834). Kwangu mimi uhusiano wa waumini na Mungu una vipengele vitatu.

1. injili ni mtu (msistizo wa Kanisa la Mashariki na Calvin) 2. injili ni ukweli (msisitizo wa Augustine na Luther) 3. injili ni maisha yaliobadilishwa (msistizo wa Katoliki)

Yote ni sawa na yanapaswa kuungamanishwa kwa pamoja kwa ajili ya afya, sauti, Ukristo wa kibiblia. Ikiwa ye yote anasisitizwa sana au anapunguza thamani, matatizo yanatokea. Yatupasa kumkaribisha Yesu! Yatupasa kuiamini injili! Yatupasa kuwa na ushawishi juu ya ufanano wa Kristo!

◙"amezaliwa" Hii ni kauli tendewa elekezi ya wakati timilifu ambayo inamaanisha hali iliyotulia ambayo imeletwa na mtu wa nje, Mungu Baba (kama vile Yohana 3:3). Tazama matumizi mengine ya stiari ya kifamilia (kama vile 1 Yohana 3:9) kuutambua Ukristo (hii ni familia). Tazama nukuu katika 1 Yohana 3:1d.

Page 380: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

364

3:1 "Tazameni, ni pendo la namna gani" Maneno yanayohusiana na upendo yaliyotumika hapa na ndani ya 1 Yohana nzima ni agapaō (KITENZI) au agapē (jina, kama vile 1 Yohana 2:5,15; 3:1,16,17; 4:7,8,9,10, 12,16,17,18; 5:3). Neni hili lilitumiwa katika Uyunani ya sasa, lakini si mara kwa mara. Inaonekana kwamba kanisa la kwanza lilitoa maelezo upya yanayohusiana na neno hili katika mwanga wa injili. Neno hili lilikuja kuwakilisha pendo la ndani la kudumu. Si sawa kusema "upendo wa ki-Ungu wa kujitoa mwenyewe" kwa sababu katika Injili ya Yohana neno hili linatumika kwa ufanano na neno phileō (kama vile Yohana 5:20; 11:3,36; 12:25; 15:19; 16:27; 20:2; 21:15,16,17). Hata hivyo, aya hii inatia shauku kwamba mara nyingi neno hili limetumika (katika 1 Yohana) katika mahusiano ya waamini kupendana wao kwa wao. Imani na ushirika kati yetu na Yesu huubadilisha uhusiano wetu na Uungu pamoja na mwanadamu! ◙"alilotupa Baba" HII ni kauli tendaji elekezi ya wakati timilifu. Matumizi ya wakati huu yaliyohusianishwa na kipawa cha Mungu cha wokovu ndani ya Kristo ni ya msingi mmoja wa kibiblia kwa ajili ya mafundisho ya ulinzi wa mwamini (kama vile Yohana 6:35-40; 10:1 na kuendelea; Efe. 2:5,8; 5:1). Tazama MADA MAALUMU: Dhamana ya Mkristo katika Yohana 6:37

MADA MAALUM: USHAHIDI WA AGANO JIPYA WA WOKOVU WA MTU

Imejikita katika Agano Jipya (kama vile Yer. 31:31-34; Ezek. 36:22-38) katika Yesu: 1. Tabia ya Baba (kama vile Yohana 3:16), kazi ya Mwana (kama vile 2 Kor. 5:21), na huduma ya Roho

(kama vile Rum. 8:14-16), na si matendo ya kibinadamu, sio mshahara kwa ajili ya utii, sio amri. 2. Ni kipawa (kama vile Rum. 3:24; 6:23; Efe. 2:5,8-9). 3. Ni maisha mapya, mtazamo mpya wa kiulimwengu (kama vile Yakobo na 1 Yohana). 4. Ni maarifa (injili), ushirika (imani katika na pamoja na Yesu), na mtindo mpya wa maisha (Kufanana na

Kristo kunakosababishwa na Roho) vyote vitatu wala si kimoja kwa peke yake. 5. Angalia jaribu la wokovu wa kweli katika ufahamu wa kimuktadha kwa 1 Yohana 2:3-27, C.

mtandaoni.

◙ "kwamba tuitwe" hii ni kauli tendewa tegemezi ya wakati uliopita usio timilifu ambayo inatumika katika maana ya jina la heshima ("wana wa Mungu") linalotolewa na Mungu. ◙ "wana wa Mungu" Huu ni mtazamo wa 1 Yohana 2:29-3:10. Mtazamo huu unathibitisha uwezo wa Mungu ndani ya wokovu wetu (kama vile Yohana 6:44,65). Yohana anatumia meneno ya kifamilia kuupambanua uhusiano mpya wa muumini na Uungu (kama vile 1 Yohana 2:29; 3:1,2,9,10; Yohana 1:12). Hii inatia shauku kwamba Yohana (kama vile Yohana 3:3) na Petro (kama vile1 Pet. 1:3,23) wanatumia stiari ya kifamilia "kuzaliwa upya" au "kuzaliwa kutoka juu," ambapo Paulo anatumia stiari ya kifamilia ya neno "kuwa" (kama vile Rum. 8:15,23; 9:4; Gal. 4:1-5; Efe. 1:5) na Yakobo anatimia stiari ya kifamilia ya neno "zaliwa" (kama vile Yakobo 1:18) au "kuzaa matunda" kuupambanua uhusiano mpya wa mwamini na Mungu kupitia Kristo. Ukristo ni familia. ◙ "na ndivyo tulivyo" Hii ni kauli elekezi ya wakati uliopo. Aya hii haipatikani katika tafsiri ya the King James Version of the Bible kwa sababu haikuwekwa katika machapisho ya Kiyunani ya baadaye (yaani, K na L) ambapo tafsiri ya KJV imeegamia kauli hii. Hata hivyo, aya hii inaonekana zaidi katika machapisho kadhaa ya Kiyunani (P47, א, A, B, na C). Hii tafsiri ya UBS4 inatoa hitimisho la dalaja "A"(lililo yakini). Tazama Mada Maalumu: Uhakiki wa Kimaandishi. ◙ "ulimwengu haututambui" Hili neno "ulimwengu" linatumika katika nia ya ufanano wa kitheolojia kama 1 Yohana 2:15-17. Ulimwengu linamaanisha jamii ya mwanadamu iliyoungana na kutenda kinyume na Mungu (kama vile Yohana 15:18-19; 17:14-15). Huku kuteswa na kukataliwa na ulimwengu ni uthibitisho mwingine wa nafasi yetu katika Kristo (kama vile Mt. 5:10-16).

Page 381: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

365

◙ "kwa kuwa haukumtambua yeye" Hii inaonekana kumrejelea Mungu Baba kwa sababu katika Injili ya Yohana Yesu anazungumza tena na tena kwamba ulimwengu haumjui yeye (kama vile Yohana 8:19,55; 15:18,21; 16:3). Hivi VIWAKILISHI katika 1 Yohana ni tata (tazama nukuu katika 1 Yohana 2:28). Katika muktadha huu nomino tangulizi ya kisarufi ni Baba, marejeo ya kitheolojia katika 1 Yohana 3:2 ni Mwana. Hata hivyo, katika Yohana huu unaweza kuwa utata wa makusudi kwa sababu kumwona Yesu ni sawa na kumwona Baba (kama vile Yohana 12:45; 14:9).

3:2 "wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa" Hii inazungumzia juu ya kushindwa kwa Yohana kuyabainisha haya matukio ya nyakati za mwisho (kama vile Matendo 1:7) au asili halisi ya mwili uliofufuliwa (kama vile 1 Kor. 15:35-49). Hii pia inaonyesha kwamba 1 Yohana 2:27 haimaanishi ufahamu kamili katika kila eneo. Hata ufahamu wa Yesu kuhusiana na tukio hili ulukuwa na mipaka ambapo yeye alikuwa na umbo la mwili (kama vile Mt. 24:36; Marko 13:22).

◙ "atakapodhihirishwa" Hili neno "atakapo" linaitambulisha sentensi yenye masharti daraja la tatu. Hapa neno hili halitumiki kuuliza swali lihusulo ujio wa Mara ya Pili, bali kueleza juu ya siku ile isiyojulikana. Japo Yohana anasistiza juu ya wokovu kamili sasa, pia anautarajia ujio wa mara ya Pili.

◙"tutafanana naye" Hii inahusisha ukamilifu wetu wa kumfanana Kristo (kama vile 2 Kor. 3:18; Efe. 4:13; Flp. 3:21; na Kol. 3:4). Mara nyingi hiki kitendo huitwa "kutukuza" (kama vile Rum. 8:28-30). Hiki ndicho kilele cha wokovu wetu! Badiliko hili la matukio ya siku za mwisho linahusiana na urejesho kamili wa mfano wa Mungu ndani ya wanadamu walioumbwa kwa ufanano wake (kama vile Mwa. 1:26; 5:1,3; 9:6). Ushirika wa karibu sana na Mungu kwa mara nyingine unawezekana! ◙ "kwa maana tutamwona kama alivyo" Ayubu alikuwa na shauku ya kumwona Mungu (kama vile Ayubu 19:25-27). Yesu anatwambaia kuwa wenye moyo safi ndio watakaomuona Mungu (kama vile Mt. 5:8). Ili kumwona yeye katika ukamilifu wake inamaanisha kwamba tutabadilishwa na kuwa katika ufanano wake (kama vile 1 Kor. 13:12). Hii inarejea juu ya kutukuzwa kwa mwamini (kama vile Rum. 8:29) katika siku ile ya Kuja mara ya Pili. Ikiwa neno "uthibitisho" linamaanisha kuwa huru kutoka katika adhabu ya dhambi na neno "utakaso" maana yake ni kuwa huru kutoka katika nguvu ya dhambi, kisha neno "kutukuzwa" linamaanisha kuwa huru kutoka katika uwepo wadhambi! 3:3 "Na kila" Neno la Kiyunani pas limejitokeza mara saba kuanzia 1 Yohana 2:29 hadi 3:10. Hakuna ukinzano. Yohana anaiwasilisha injili katika hali ngumu, namna za weusi-au-weupe. Aidha mmojawapo ni mwana wa Mungu ama mwana wa Ibilisi (kama vile1 Yohana 2:29; 3:3,4,6 [mara mbili],9,10). ◙ "matumaini haya" Katika Paulo neno hili linairejelea Siku ya Ufufuo (kama vile Matendo 23:6; 24:15; 26:6-7; Rum. 8:20-25; 1 Thes. 2:19; Tito 2:13; 1 Pet. 1:3,21). Hii inaeleza juu ya uyakini wa tukio hili, lakini kwa dalili zenye utata wa wakati. Yohana hazungumzii kuhusiana na "yale matumaini" ya ujio wa mara ya Pili kama marudio kama ilivyo kwa waandishi wa Agano Jipya. Haya ni matumizi pekee ya neno hili katika maandiko yake. Yeye anatazamia juu ya manufaa na majukumu ya neno "kukaa" ndani ya Kristo sasa! Hata hivyo, hii haimanishi kuwa yeye hakuitegemea hukumu ya uovu siku ile ya mwisho (kama vile1 Yohana 2:18) na siku ile ya mwisho ya kutukuzwa kwa mwamini (kamavile 1 Yohana 3:1-3). ◙ "yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu" Hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo. Utakaso ni muhimu (kama vile Mt. 5:8,48). Yatupasa kuungana katika tendo la utakaso (kama vile 2 Kor. 7:1; Yakobo 4:8, 1 Pet. 1:22; 2 Pet. 3:13,14) kama Yohana 1:12 inayozungumzia juu ya ushirika wetu katika tendo la uthibitisho. Mvutano huu unaofanana baina ya upande wa Mungu (ukuu) ndani ya wokovu wetu na upande wetu (mapenzi huru ya mwanadamu) unaweza kuonekana dhahiri kwa kulinganisha Ezek. 18:31 na 36:26-27. Mara nyingi Mungu huchukua fursa (kama vile Yohana 6:44,65), lakini amedai kwamba watu walio ndani ya agano yawapasa kuitikia kwa toba asilia na imani pamoja na toba endelevu, imani, utii, huduma, ibada, na ustahimilivu.

Page 382: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

366

Hii inaweza kudokeza Sala Kuu ya Kikuhani ya Yohana 17, hasa 1 Yohana 3:17,19. Anajitakasa mwenyewe, wafuasi wake hujitakasa wenyewe. Kwa kiasi fulani inastaajabisha kwamba miundo tofauti tofauti ya mizizi ya msingi iliyo sawa imetumika.

1. Yohana 17:17,19 -- hagiazō (hagios, kama vile Yohana 10:36) 2. 1 Yohana 3:3 -- hagnizō (hagnos, kama vileYohana 11:55)

UTAMBUZI WA MUKTADHA WA 3:4-10

A. Kifungu hiki kimekuwa kitovu cha mabishano kati ya ukamilifu wa Mkristo (kama vile Warumi 6), wakati mwingine huu unaitwa utakaso kamili, na dhambi endelevu ya Mkristo (kama vile Warumi 7).

B. Hatupaswi kuziruhusu chuki zetu za kitheolojia kwa ajili ya kutoa fasiri zetu kuhusiana na andiko hili. Pia,

hatupaswi kuyapa nafasi maandiko mengine kwa aili ya kulishawishi andiko hili hadi pale uhuru wetu wa mafunzo kuhusiana na andiko hili utakapokamilika na kuwa tumeyakinisha kile alichokuwa akikisema Yohana katika pande zote mbili yaani, 1 Yohana 3 na katika kitabu kizima cha 1 Yohana!

C. Hili andiko kwa hakika linawasilisha lengo ambalo wakristo wote wamekuwa wakilisubiria, ukombozi wa

moja kwa moja kutoka dhambini. Wazo hili lenye ufanano linawasilishwa katika Warumi 6. Kwa nguvu za Kristo kuna uwezekano wa sisi kuishi bila kutenda dhambi.

D. Kifungu hiki, hata hivyo, lazima kiwe na manufaa katika muktadha iliyopana ya kitabu chote cha1 Yohana.

1. Kukifasiri kifugu hiki bila kujali 1 Yohana 1:8-2:2 (huku wakristo wakiendelea kutenda dhambi) tungekuwa katika hali ya upumbavu.

2. Kukifasiri kifungu hiki katika namna ile ile ni kama kulidhoofisha kwa ujumla kusudi la 1 Yohana, uhakika wa wokovu kati ya madai ya walimu wa uongo ungekuwa upumbavu pia.

3. Kifungu hiki lazima kihusiane na madai ya walimu wa uongo ya kutokuwa na dhambi au dhambi isiyokuwa na maana (dhambi ndogo). Bila shaka 1 Yohana 1:8-2:2 inashughulika zaidi na mmoja wa walimu wa uongo, ambapo 3:1-10 inashughulika na wengine. Kumbuka kwamba kufasiri nyaraka za Agano Jipya ni kama kusikiliza mazungumzo ya simu ya upande mmoja.

E. Uhusiano wa kimafumbo unajitokeza kati ya vifungu hivi viwili. Dhambi katika maisha ya mkristo ni tatizo

la mara kwa mara katika Agano Jipya (kama vile Warumi 7). Hii inaunda mvutano ule ule wa kilahaja kama nadharia ya kwamba wengine watakwenda mbinguni na wengine watakwenda motoni na mapenzi huru au ulinzi na ustahimilivu. Fumbo hili linaleta ulinganifu wa kitheolojia na kuzishambulia nafasi za walimu wa uongo. Walimu wa uongo waliwasilisha makosa katika maeneo yaliyokuwa na dhambi.

F. Huu mjadala mzima wa kitheolojia umeegemea juu ya kutokuelewana kuhusiana na tofauti kati ya

1. nafasi yetu ndani ya Kristo 2. mapambano yetu kwa ajili ya kuikamilisha nafasi hiyo kiuzoefu katika maisha yetu ya kila siku 3. ahadi kwamba ushindi utakuwa wetu siku moja!

Sisi tuko huru kutoka katika adhabu ya dhambi (uthibitisho) katika Kristo, bado tunapambana kwa nguvu hiyo (utakaso endelevu) na siku moja tutakuwa huru kwa uwepo wake (kutukuzwa). Ni kama kitabu hiki kinavyofundisha kwa ukamilifu umuhumu wa kujitoa dhambini na kupambana kuishi maisha yasiyokuwa ya dhambi.

G. Uchaguzi mwingine unatoka katika matumizi ya fasihi ya Yohana yaliyojirudia mara mbili. Yeye aliandika vipengele vya weupe na weusi (hivi pia vilipatikana katika Magombo ya Bahari ….). Kwake yeye mtu alikuwa ndani ya Kristo kwa kuwa mwenye haki, au ndani ya Ibilisi kwa kuwa dhambini. Hapakuwa na kipengele cha tatu. Hii inatumika kama "wito wa uamsho" kuhitimisha, kiutamaduni, ya muda, mazishi pekee, Ukristo pekee wa Pasaka!

Page 383: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

367

H. Baadhi ya marejeleo yanayohusu ugumu wa somo hili: 1. Kwa tasfsiri za tamaduni saba za kifungu hiki tazamae "Waraka wa Yohana" katika kitabu cha The

Tyndale New Testament Commentaries na John R. W. Stott, kilichochapishwa na Eerdman's (kr. 130-136).

2. Kwa utendaji mzuri kuhusiana na nafasi ya Utimilifu tazama kitabu cha Christian Theology, Juzuu II, uk. 440ff na H. Orlon Willie, kilichochapishwa na Beacon Hill Press.

3. Kwa utendaji mzuri kuhusiana na mafundisho ya dhambi endelevu katika maisha ya Mkristo tazama kitabu cha "Perfectionism" na B. B. Warfield kilichochapishwa na The Presbyterian na Reformed Published Company.

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) 1 YOHANA 3:4-10 4Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi. 5 Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake. 6 Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua. 7 Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki; 8 atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. 9 Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu. 10 Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.

3:4 NASB " Kila atendaye dhambi, afanya uasi" NKJV "Ye yote atendaye dhambi huvunja sheria" NRSV "Kila atendaye dhambi anavunja sheria ya Mungu" TEV "Ye yote atendaye dhambi ana hatia ya kuivunja sheria ya Mungu" NJB "Atendaye dhambi, anatenda kwa udhalimu" Hiki kiwakilishi "kila" hapa kinawekwa mbele na katika 1 Yohana 3:6. Muktadha huu unahusiana na wanadamu wote! Hii ni kauli tendaji endelevu ya wakati uliopo na kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo. Hivi ni vitenzi vya wakati uliopo vinavyosistiza hali ya mazoea, hali endelevu, tendo la mtindo wa maisha katika tofati zenye ulinganifu kwa kile kitenzi cha kauli tendaji tegemezi katika 1 Yohana 2:1-2. Hata hivyo, tatizo la kitheolojia la kifungu hiki (linganisha 1 Yohana 1:7-10 na 3:6-9) haliwezi kutatuliwa kwa ukamilifu kwa kitenzi cha nyakati. Hili linaweza kutatuliwa kwa mapangilio wa kihistoria wa aina mbili za Mafunuo ya walimu wa uongo na muktadha wa kitabu kwa ujumla. Utofauti mwingine wa kifungu hiki ni matumizi yake ya aya ya "kuivunja sheria." Hii haizungumzii kuivunja sheria (Sheria ya Musa au desturi za kijamii) kama mtazamowa uasi. Neno hili lenye ufanano linatumika kueleza juu ya yule Mpinga Kristo katika 2 The. 2:3,7. Linaweza kuwa llinakamilisha maelezo yahusuyo maana ya dhambi (kama vile Yohana 9:41; Rum. 14:23; Yakobo 4:17; 1 Yohana 5:17), hiki ni kinyume cha ufanano wa Kristo (kama vile 1 Yohana 3:5), huu si ukiukaji wa utawala au kuegemea upande huo. 3:5 "alidhihirishwa" Hiki ni kitenzi cha kauli tendewa elekezi kinachozungumzia juu ya Yesu kuchukua umbile la kibinadamu (kama vile1 Yohana 3:8; 2 Tim. 1:10). Kitenzi kile kile, phaneroō, kina tumika mara mbili katika 1 Yohana 3:2 kuzungumzia ujio wake wa Mara ya Pili. Kwanza alikuja kama mwokozi (kama vile Marko 10:45; Yohana 3:16; 2 Kor. 5:21), lakini atarudi kama Mkamilishaji! katika fasihi yake,The Letters of John, mmoja wa walimu wangu kipenzi, Bill Hendricks anasema: "Semi mbili zinazopenya zaidi kuhusiana na kusudi la ujio wa Kristo zinapatikana ndani ya mstari huu na katika mstari wa 8. Yeye alitumwa na Mungu ili kuziondoa dhambi (3:5), na alifunuliwa kuziharibu kazi za ibilisi (3:8). Mahali pengine Luka anaandika kwamba kusudi la Yesu katika ujio wake lilikuwa kuwatafuta na kuwaokoa wale

Page 384: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

368

waliopotea (Luka 19:10). Injili ya Yohana inaeleza kwamba Yesu alikuja katika hali ya uana-kondoo ili kuwa na uzima tele (Yohana 10:10). Mathayo anagusia kusudi la ujio wa Kristo katika fasiri yake inayoeleza maana ya jina la Yesu; Yeye atawaokoa watu kutoka katika dhambi zao (Mt. 1:21). Wazo la msingi katika maelezo haya yote ni kwamba Yesu Kristo amefanya jambo fulani kwa ajili ya maisha ya mwanadamu ambalo yeye asingeliweza kufanya kwa ajili yake (kur. 79-80).

◙ "aziondoe dhambi" Hiki ni kitenzi cha kauli tegemezi. Hili tendo ni yakini kwa mwitikio wa mwanadamu (yaani,toba na imani). Usuli wa usemi huu bila shaka ulihusiana na vyanzo viwili.

1. Siku ya Upatanisho (kama vile Walawi 16) ambapo mbuzi wawili wa kafara kwa ishara waliiondoa dhambi toka katika kambi ya Israeli (kama vile matumizi ya Yohana Mbatizaji katika Yohana 1:29)

2. marejeleo ya kile alichokitenda Yesu pale msalabani (kama vile Isa. 53:11-12; Yohana 1:29; Ebr. 9:28; 1 Pet. 2:24)

◙ "na dhambi haimo ndani yake" Hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo. Yesu Kristo kutokuwa na dhambi (kama vile Yohana 8:46; 2 Kor. 5:21; Ebr. 4:15; 7:26; 1 Pet. 1:19; 2:22) ni msingi wa kujitoa kwake, upatanisho wa uwakilishi kwa ajili yetu (Isaya 53). Nukuu kwamba aya "dhambi" ni wingi katika sehemu ya kwanza ya 1 Yohana 3:5 na umoja katika sehemu ya mwisho. Ya kwanza inazungumzia matendo ya dhambi, ya pili sifa yake ya kuwa mwenye haki. Lengo ni kwamba waamini watashiriki aina zote za utakaso yaani utakaso wa mahali na utakaso endelevu wa Kristo. Dhambi ni jambo lisilokuwa na uhusiano na Kristo na wafuasi wake.

MADA MAALUMU: UTAKASO KATIKA AGANO JIPYA

Kitabu cha Agano jipya kinadai kwamba wenye dhambi wanapomgeukia Yesu kwa toba na imani (kama vile Marko 1:15; Matendo 3:16,19; 20:21), huthibitishwa na kutakaswa papo kwa papo. Hii ni nafasi mpya katika Kristo. Haki yake imewekwa ndani yao (kama vile Mwa. 15:6; Warumi 4). Wametangaziwa haki na utakatifu (tendo la ki-Mungu la kumto mtu hatiani).

Lakini Agano Jipya pia linawasistiza waamini kuwa katika utakatifu au utakaso. Hii ni nafasi ya kitheolojia katika kazi ya Yesu Kristo iliyomalizika na wito wa kufanana na Kristo katika mtazamo na matendo katika maisha ya kila siku. Kwa kuwa wokovu ni neema ya bure na gharama ya kila kitu cha mtindo wa maisha, hivyo hata hii, ni utakaso.

Mwitikio wa Awali Ufanano na Kristo Endelevu

Matendo 26:18 Warumi 15:16 1 Wakorintho 1:2-3; 6:11 2 Wathesalonike 2:13 Waebrania 2:11; 10:10,14; 13:12 2 Peter 1:2

Warumi 6:19 2 Kor. 7:1 Waefeso 1:4; 2:10 1 Wathesalonike. 3:13; 4:3-4,7; 5:2 1 Timotheo 2:15 2 Timotheo 2:21 1 Petro 1:15-16 Waebrania 12:14

3:6 "Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi" Kama 1 Yohana 3:4, Hii ni kauli nyingine ya kitenzi tendaji elekezi ya wakati unaoendelea. Kifungu hiki lazima kitofautishwe na 1:8-2:2 na 5:16.

◙ "kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua" Mstari huu una kauli moja ya kutenda endelevu ya wakati uliopo ikifuatiwa na kauli mbli za kitenzi tendaji endelevu cha wakati uliopo. Kutenda dhambi kwa uwazi na katika hali edelevu ni kufunua kwamba hamtambua Kristo na hakumtambua Kristo kamwe. Wakristo watendao dhambi

1. huuzuia wito wa Kristo 2. hulizuia lengo la Ufanano wa Kristo

Page 385: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

369

3. huifunua asili ya mtu kiroho (kama vile Yohana 8:44) 3:7 "mtu na asiwadanganye" Hii ni kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopo ikiwa na kiambata hasi, ambacho mara nyingi kinamaanisha kusitisha tendo ambalo tayari liko kwenye mchakato. Kuwepo kwa walimu wa uongo (kama vile1 Yohana 2:26) kunaweka mpangilio wa hali ya kihistoria kwa ajili ya uelewa kamili wa kitheolojia wa 1 Yohana kama waraka uliyokamilika na 1 Yohana 1:7-10 na 3:4-10 katika upekee. ◙ "atendaye haki yuna haki" Mstari huu hauwezi kutengwa kutoka katika muktadha wa jumla na kuwa katika matumizi ya kutetea au kuishutumu sehemu ya kimafundisho ("matendo ya mwenye haki"). Agano Jipya linadhihirisha kwamba wanadamu hawawezi kumkaribia Mungu Mtakatifu kwa manufaa yao binafsi. Wanadamu hawaokolewi kwa juhudi zao wenyewe. Hata hivyo, wanadamu lazima wawe na mwitikio juu ya neema ya Mungu ya bure kupitia wokovu katika kazi iliyokamilishwa na Kristo. Juhudi zetu sisi hazitosogezi kwa Mungu. Hizi hazionyeshi kwamba tumekutana naye. Kwa usahihi hizi zinaifunua hali yetu ya kiroho (kama vile Ufu. 22:11) na ukomavu baada ya wokovu. Hatukuokolewa "kwa " kazi nzuri, bali "katika" kazi nzuri. Lengo la neema ya Mungu ya bure katika Kristo ni kuwa na wafuasi wenye kumfanana Kristo (kama vile Efe.2:8-9,10). Mapenzi ya Mungu ya milele kwa kila aaminiye si kwenda mbinguni pale anapokufa (uthibitisho wa hukumu), bali kumfanana Kristo (utakaso wa milele) sasa (kama vile Mt. 5:48; Rum. 8:28-29; Gal. 4:19)! Ili kupata neno la kusoma linalohusiana na mwenye haki tazama Mada Maalumu: Mwenye Haki katika 1 Yohana 2:29

3:8 "atendaye dhambi ni wa Ibilisi" Hii ni kauli tendaji endelevu ya wakati uliopo. Wana wa Mungu wanajulikana kwa namna wanavyoishi, kama walivyo watoto wa Ibilisi (kama vile 1 Yohana 3:10; Mt. 7:13; Efe. 2:1-3).

◙ "kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo" Hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo. Ibilisi aliendelea kutenda dhambi tangu mwanzo (kama vile Yohana 8:44). Je! Aya hii inarejea juu ya uumbaji au uasi wa kimalaika? Kitheolojia ni vigumu kueleza ni wakati gani Ibilisi alipoasi dhidi ya Mungu. Kitabu cha Ayubu 1-2; Zekaria 3 na 1 Wafalme 22:19-23 kinaonyesha kwamba Ibilisi ni wa Mungu na ni mmoja wa washauri wa kimalaika. Hii inawezekana (lakini sio aghalabu) kwamba majivuno, kiburi, na tamaa ya wafalme wa mashariki (mwa Babeli, Isa. 14:13-14 au wa Tiro, Eze. 28:12-16) ndivyo vigezo vinavyotumika kueleza kuhusiana na uhasi wa Ibilisi (kwa uthihirisho huyu ni kerubi afunikaye, Eze. 28:14,16). Hata hivyo, katika Luka 10:18 Yesu anasema kuwa alimwona Shetani akianguka kutoka mbinguni kama umeme, lakini hii aya haituelezi kwa sahihi lini. Asili na kuendelea kwa uovu lazima kubaki na utata kwa sababu ya uhaba wa mafunuo. Jihadhari na mifumo na taratibu zinazowekwa, mifumo ya imani iliyojitenga iliyowekwa na kanisa mahususi, yenye utata, maadiko ya kitamathali! Mjadala nzuri zaidi wa Agano la Kale kuhusiana na namna Shetani alivyokuwa akiendelea kutoka katika kiwango cha utumishi wa ki-Mungu hadi kuwa adui wa uovu ni kitabu cha A. B. Davidson's Old Testament Theology, kilichochapishwa na T & T Clark, kr. 300-306. Tazama Mada Maalumu: Uovu Binafsi katika Yohana 12:31 ◙ "Mwana wa Mungu" Tazama Mada Maalumu hapa chini.

MADA MAALUMU: MWANA WA MUNGU

Hii ni moja kati ya nyadhifa kubwa alizopewa Yesu katika Agano Jipya. Ni wazi kabisa ina kidokezo cha Uungu. Inamjumuisha Yesu kama “Mwana” au “Mwana wangu,” pia Mungu anaelezewa kama “Baba” (angalia Mada Maalumu: Ubaba wa Mungu). Linatokea mara 124 katika Agano Jipya. Hata usanifu wa Yesu mwenyewe kama “Mwana wa Adamu” ina kidokezo cha Uungu toka Dan. 7:13-14 Katika Agano la Kale usanifu wa neno “Mwana” ingalirejea kwenye makundi maalumu manne (angalia Mada Maalumu: “Wana wa……..”)

A. Malaika (mara nyingi iko katika hali ya WINGI, kama vile Mwa. 6:2; Ay. 1:6; 2:1) B. Mfalme wa Israel (kama vile2 Sam. 7:14; Zab. 2:7; 89:26-27) C. Taifa la Israel kwa pamoja (kama vile Kut. 4:22-23; Kumb. 14:1; Hos. 11:1; Mal. 2:10) D. Waamuzi wa Israel (kama vile Zab. 82:6)

Page 386: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

370

Ni utumiaji wa mara ya pili ambao unahusianishwa na Yesu. kwa njia hii “Mwana wa Daudi” na “Mwana wa Mungu” semi zote zinahusianishwa na 2 Samwel 17; Zaburi 2 na 89. Katika Agano la Kale neno “Mwana wa Mungu” kamwe halitumiki hasa kwa Masihi, isipokuwa kama ni mfalme wa siku za kiama kama mmoja wa “wapakwa mafuta” wa Israel. Hata hivyo, katika magombo ya bahari ya chumvi wadhifa unaohusiana na Masihi ni wa kawaida (angalia nukuu maalumu katika Dictionary of Jesus and the Gospels, uk. 770). Pia “Mwana wa Mungu” ni wadhifa wa Kimasihi katika miingiliano miwili ya kazi za mafunuo ya Kiyahudi (kama vile II Esdras 7:28; 13:32,37,52; 14:9 na I Enoch 105:2) Mazingira ya nyuma ya Agano Jipya kama inavyorejerea kwa Yesu kwa uzuri imefupishwa kwa namna mbali mbali.

1. Uwepo wake kabla (kama vile Yohana 1:15-30; 8:56-59; 16:28; 17:5; 2 Kor. 8:9; Flp. 2:6-7; Kol. 1:17; Ebr. 1:3; 10:5-8)

2. Kuzaliwa kwake kwa njia ya pekee (kama vile Isa. 7:14; Mt. 1:23; Luk. 1:31-35)

3. Ubatizo wake (kama vile Mt. 3:17; Mk 1:11; Luk. 3:22. Sauti ya Mungu toka mbinguni ikiunganisha ufalme wa kifahali wa Zaburi 2 na mtumishi mwenye mateso wa Isaya

4. Majaribu ya shetani (kama vile Mt. 4:1-11; Mk 1:12,13; Luk 4:1-13. Anajaribiwa kuuwekea mashaka uwana wake au kutimiliza kusudi lake kwa njia tofauti na ile ya msalaba.

5. Uthibitisho wake na wale wakiri wasiokubalika a. Mapepo (kama vile Mk 1:23-25; Luk 4:31-37,41; Mk 3:11-12; 5:7; angalia Mada Maalumu: Pepo

[roho wachafu]) b. Wasioamini (kama vile Mt. 27:43; Mk 14:61; Yohana 19:7)

6. Uthibitisho wake kupitia wanafunzi wake a. Mt. 14:33; 16:16 b. Yohana 1:34,49; 6:69; 11:27

7. Uthibitisho wake mwenyewe a. Mt. 11:25-27 b. Yohana 10:36

8. Utumiaji wake wa stiari ya kawaida ya Mungu kama Baba a. Utumiaji wake wa neno abba kwa ajili ya Mungu

1) Mk 14:36 2) Rum 8:15 3) Gal 4:6

b. Utumiaji wake wa sasa wa jina Baba (patēr) kuelezea uhusiano wake na Uungu. Kwa ufupi, wadhifa wa neno “Mwana wa Mungu” una maana kubwa ya kithiolojia kwa wale waliolifahamu Agano la Kale na ahadi zake, lakini waandishi wa Agano Jipya waliogopeshwa kuhusu utumiaji wao na watu wa mataifa kwa sababu ya mazingira ya nyuma ya wapagani ya “miungu” ikiwachukulia wanawake na matokea ya watoto kuwa “majitu.”

◙"alidhihirishwa" Hili neno la Kiyunani phaneroō, ambalo linamaanisha "kuleta nuruni ili kuyaweka mambo sawa." 1 Yohana 3:5 na 8 zina ufanano na zote zinatumia maneno katika irabu tendewa, ambayo inazungumzia juu ya Kristo kufunuliwa kweli katika kuchukua kwake umbile la kibinadamu (kama vile1 Yohana 1:2). Tatizo kwa hawa walimu wa uongo halikuwa kwamba injili si sahihi kwao, bali hali ya kuwa na agenda zao wenyewe za kitheolojia/ kifalsafa

◙"ili azivunje kazi za Ibilisi" Kusudi la uthihirisho wa Yesu kwa wakati na kuwa katika umbile la mwili lilikuwa"kuzivunja" (kauli tendaji tegemezi ya wakati uliopita usio timilifu luō), inayomanisha "kupoteza," "kufungua," au "kuharibu." Yesu alilifanya hili huko Kalvari, lakini yawapasa wanadamu kuwa na mwitikio kwa kazi yake iliyokwisha na neema ya bure (kama vile Rum. 3:24; 6:23; Efe. 2:8) kwa kumpokea yeye kwa imani (kama vile Yohana 1:12; 3:16).

Page 387: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

371

Ile "iliyo tayari na iliyo bado" mvutano wa Agano Jipya pia unahusiana na kuziharibu kazi zenye uovu. Ibilisi amekwisha ondolewa, lakini bado anaendelea kufanya kazi katika ulimwengu hadi kilele kamili cha Ufalme wa Mungu.

3:9 "Kila mtu aliyezaliwa na Mungu" Hii ni kauli timilifu tendewa endelevu ambayo inazungumzia juu ya hali ya kuishi ambayo imeumbwa kwa nguvu itokayo nje (Mungu).

◙ "hatendi dhambi" Hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo katika utofautisho linganishi wa1 Yohana 2:1, ambapo kile kitenzi cha kauli tendaji tegemezi kinatumika mara mbili. Kuna nadharia mbili kuhusiana na umuhimu wa usemi huu.

1. Hii inahusiana na Mafunuo ya walimu wa uongo, hasa lile kundi dogo ambalo liliushusha wokovu kuelekea dhana za kitaaluma, hivyo kuondoa ule umuhimu wa maadili ya mtindo wa maisha

2. Kile kitenzi cha wakati uliopo kinasistiza uendelevu, hali ya mazoea, kazi ya dhambi (kama vile Rum. 6:1), si matendo ya dhambi yaliyotengwa (kama vile Rum. 6:15)

Huu utofauti wa kitheolojia unazungumziwa katika Warumi 6 (uwezekano wa kutokuwa na dhambi katika Kristo) na Warumi 7 (mapambano ya mwamini asiye na dhambi yanayoendelea). Mtazamo wa kihistoria #1 unaonekana bora, lakini mwingine bado ameachwa na hitaji la kuutumia ukweli huu nyakati hizi, ambapo #2 huzungumzia juu ya huo. Kuna mjadala mzuri wa ugumu wa mstari huu katika kitabu cha Hard Sayings of the Bible cha Walter Kaiser, Peter Davids, F. F. Bruce, na Manfred Brauch, kr. 736-739.

◙ "kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake" Hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo. Kumekuwa na nadharia kadhaa kama uhalisi wa kile ile aya ya Kiyunani, "uzao wake," inamaanisha

1. Augustine na Luther wanasema hii inarejea juu ya Neno la Mungu (kama vile Luka 8:11; Yohana 5:38; Yakobo 1:18; 1 Pet. 1:23)

2. Calvin anasema hii inarejea juu ya Roho Mtakatifu (kama vile Yohana 3:5,6,8; 1 Yohana 3:24; 4:4,13) 3. Wengine wanasema hii inarejea juu ya Asili ya Uungu au mpya kwayo (kama vile 2 Pet. 1:4; Efe. 4:24) 4. Bila shaka hii inarejea juu ya Kristo mwenyewe kama ule "uzao wa Abraham" (kama vile Luka 1:55;

Yohana 8:33,37; Gal. 3:16) 5. Baadhi wanasema hii ni ina ufanano na ile aya ya "amezaliwa kwa ajili ya Mungu" 6. inavyoonekana hili lilikuwa neno lililotumiwa na wana- mafunuo kuzungumzia dalili za ki-Ungu ndani ya

wanadamu wote Namba 4 yumkini ni uchaguzi bora kimuktadha kwa nadharia zote, lakini Yohana anauchagua msamiati kuyapinga Mafunuo ya mwanzo (yaani, #6). 3:10 Huu ni mhutasari wa1 Yohana 3:4-9. Ndani yake kuna kauli mbili tendaji elekezi za wakati uliopo na kauli mbili tendaji endelevu za wakati uliopo, ambazo zinarejea juu ya tendo lililo katika mchakato. Kitheolojia mhutasari huu unafanana na usemi wa Yesu katika hotoba yake pale Mlimani (kama vile Mt. 7:16-20). Ni kwa namana gani mtu huishi kwa kuufunua moyo wa mtu, ni kumwelewa mtu kiroho. Hiki ni kijalizo hasi kwa 1 Yohana 2:29!

◙ "watoto wa Mungu . . . watoto wa Ibilisi" Hii inaonyesha usuli wa Yohana wa Kisemitiki. Kiebrania, aya hii ni lugha ya kale isiyokuwa na KIVUMISHI, aya hii inatumika kama "mwana wa. . ." kama njia ya kutoa maelezo kuwahusu watu.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) 1 YOHANA 3:11-12 11Maana, hii ndiyo habari mliyosikia tangu mwanzo, kwamba tupendane sisi kwa sisi; 12Si kama Kaini alivyokuwa wa yule mwovu, akamwua ndugu yake. Naye alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu ya matendo yake mabaya, na ya ndugu yake yalikuwa ya haki.

3:11 "habari" Hili ni neno la Kuyunani (aggelia, hili mara nyingi hutafsiriwa kama angelia) lilliotumika katika 1 Yohana 1:5 na 3:11pekee. Matumizi ya kwanza yanaonekana kuwa ya kimafundisho, ambapo yale ya pili ni ya

Page 388: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

372

kimaadili. Hii ni katika kuulinda ulinganifu wa Yohana kati ya hivi vipengele viwili vya Ukristo (kama vile 1Yohana 1:8,10; 2:20,24; 3:14).

◙ "mliyosikia tangu mwanzo" kifungu hiki kifasihi ni chombo ambacho kinahusiana na Yesu kama lile Neno hai la Mungu (kama vile Yohana 1:1) na Neno la Mungu lililofunuliwa (kama vile 1 Yohana 1:1; 2:7,13,14,24; 2 Yohana 5,6).

◙ "tupendane sisi kwa sisi" Huu ni uthibitisho ambapo waamini wanaujua yakuwa wameokolewa kiukweli (kama vile1 Yohana 3:10,14). Hiii inayaaksi maneno ya Yesu (kama vile Yohana 13:34-35; 15:12,17; 1 Yohana 3:23; 4:7-8,11-12,19-21).

3:12 "Kaini" Hii historia ya Kaini ameandikwa katika Mwanzo 4. Rejea kamili ni Mwa. 4:4 (kama vile Ebr. 11:4), ambapo sadaka ya Kaini na Abeli inatofautishwa. Matendo ya Kaini yanafunua ushawishi wa mwanadamu aliyeanguka (kama vil Mwa. 4:7; 6:5,11-12,13b). Katika tamaduni zote za Kiyahudi na za Kikristo (kama vile Efe. 11:4; Jude 11) Kaini ni mfano wa uhasi dhalimu.

◙ "alivyokuwa wa yule mwovu" Utunzi huu wa kisarufi ungeweza kuwa hali ya UMOJA JINSIA YA (ME) (Yule mwovu, kama vile 1 Yohana 3:10) au HALI YA UMOJA HASI (wa uovu). Utata huu huu wa kisarufi unapatikana Mt. 5:37; 6:13; 13:19,38; Yohana 17:15; 2 Thes. 3:3; 1 Yohana 2:13,14; 3:12; na 5:18-19. Katika mambo kadhaa ni dhahiri kuwa muktdha unamrejelea Ibiisi (kama vile Mt. 5:37; 13:38; Yohana 17:15).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) 1 YOHANA 3:13-22 13 Ndugu zangu, msistaajabu, ulimwengu ukiwachukia. 14 Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu. Yeye asiyependa, akaa katika mauti. 15 Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake. 16 Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu. 17 Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo? 18 Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli. 19 Katika hili tutafahamu ya kwamba tu wa kweli, nasi tutaituliza mioyo yetu mbele zake,20 ikiwa mioyo yetu inatuhukumu; kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu naye anajua yote. 21 Wapenzi, mioyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu; 22 na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.

3:13 "msistaajabu" Hii ni kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopo ikiwa na kiambata hasi ambayo mara nyingi inamaanisha kustisha tendo ambalo tayari liko katika mchakato (kama vile 1 Pet. 4:12-16). Hili si jambo la kiulimwengu; hivi sivyo Mungu alivyokusudia ulimwengu kuwa! ◙ "Ikiwa" Hii ni sentensi yenye masharti dalaja la tatu ambayo inafikiriwa kuwa kweli kutokana na mtazamo wa mwandishi au kusudi lake la kiuandishi. ◙"ulimwengu ukiwachukia" unamchukia Yesu; vile vile utawachukia wafuasi wake. Hili ni wazo la kawaida katika Agano la Kale (kama vile Yohana 15:18; 17:14; Mt. 5:10-11; 2 Tim. 3:12) na ushahidi mwingine kwamba yule ni mwamini. 3:14 "Sisi tunajua" Hii ni kauli tedaji elekezi ya wakati timilifu (oida yenye muundo uliotimilifu, lakini wenye maana ya wakati uliopo). Hili ni wazo lingine la kawaida. Ujasili wa watoto wa Mungu unahusiana na (1) mabadiliko ya kiakili na (2) mabadiliko ya tendo, ambayo ni mizizi ya maana ya neno "kutubu" katika Kiyunani na Kiebrania.

Page 389: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

373

◙"tumepita toka mautini kuingia uzimani" Hii ni kauli nyingine tendaji elekezi ya wakati timilifu (kama vile Yohana 5:24). Moja ya ushahidi wa kupitia mautini na kuingia uzimani (yaani, uhakika wa Kristo, tazama Mada Maalumu: Dhamana ya Mkristo angalia Yohana 6:37) ni kwamba tupendane sisi kwa sisi. Jambo lingine ni kwamba ulimwengu unatuchukia. ◙ "kwa maana twawapenda ndugu" Hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati. Upendo ni sifa kuu ya familia ya Mungu (kama vile Yohana 13:34-35; 15:12,17; 2 Yohana 5; 1 Kor. 13; Gal. 5:22) kwa sababu ni sifa ya Mungu, Yeye mwenyewe (kama vile 1 Yohana 4:7-21). Upendo si msingi wa uhusiano wa Mungu na mwanadamu, bali ni matokeo. Upendo si msingi wa wokovu, bali ni ushahidi mwingine wa huo.

◙ "Yeye asiyependa, akaa katika mauti" Hiki ni kiambata cha wakati uliopo kinachotumika kama kiima kilicho na kitenzi cha kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo. Kadri mwamini anavyoendelea kukaa ndani ya pendo, wasio amini hukaa ndani ya chuki. Chuki, kama ulivyo pendo, ni ushahidi wa mazingira ya mtu ya kiroho. Kumbuka ugumu wa kitabu cha Yohana, kurudia rudia vipengele; kukaa katika pendo au kukaa katika mauti. Hapa hakuna mazingira ya maelewano. 3:15 "Kila" Yohana anatumia neno hili (pas) mara 8 tangu 1 Yohana 2:29. Umuhimu wa hili andiko ni kwamba hakuna ukinzano juu ya kile Yohana anachokisema. Kuna aina mbili pekee ya watu, wenye upendo na wenye chuki. Yohana anayaona maisha katika namna mbili yaani nyeupe au nyeusi, sio picha za kuchorwa. ◙ "amchukiaye ndugu yake ni mwuaji" Hii ni kauli tendaji endelevu ya wakati uliopo (yaani, inayoendelea, chuki iliyokomaa). Dhambi hutokea kwanza katika mawazo ya maisha. Katika hotuba ya pale Mlimani Yesu alifundisha kwamba chuki ni sawa na mauaji kama tamaa ilivyo sawa na uzinifu (kama vile Mt. 5:21-22). ◙ "nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake" Hii haizungumzi kwamba mtu anayeua hapaswi kuwa Mkristo. Dhambi inasameheka, bali matendo ya mtindo wa maisha yanaufunua moyo. Hii ni kusema kwamba yule mweye kuchukia mara kwa mara hawezi kuwa Mkristo. Upendo na chuki vyote vina utengano! Chuki hundoa uzima, bali upendo huleta uzima. 3:16 "hili tumelifahamu" Hii kauli tendaji elekezi ya wakati timilifu Neno la Kiyunani lililotumika katika 1 Yohana 3:15 lilikuwa oida; hapa ni ginōskō. Maneno haya yanatumika kwa ufanano katika maandiko ya Yohana. ◙ "pendo" Yesu ameuonyesha mfano wa milele kwa namna ya pendo lake lilivyo. Yawapasa waamini kuufatisha mfano wake (kama vile 2 Kor. 5:14-15). ◙ "wa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu" Hiki ni njeo ya wakati uliopita usio timilifu unaorejelea juu ya Kalvari kwa kutumia maneno ya Yesu mwenyewe (kama vile Yohana 10:11,15,17,18; 15:13). ◙ “imetupasa" Waamini wanatembea ndani ya mfano wa Yesu (kama vile 1 Yohana 2:6; 4:11). ◙ "kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu" Kristo ndiye mfano. Kama alivyoutoa uhai wake kwa ajili ya wengine, Wakristo yawapasa kuutoa uhai wao kama ikiwezekana kwa ajili ya ndugu zao. Mauti hadi kujifikiria mwenyewe ni

1. kuwageuza Walioanguka 2. kuurejasha ufanano wa Mungu 3. kwa ushirika ulio mzuri (kamavile 2 Kor. 5:14-15; Flp. 2:5-11; Gal. 2:20; 1 Pet. 2:21)

3:17 "akini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji" Hivi ni vitenzi vya kauli tendaji tegemezi ya wakati uliopo. Jambo la mtu kuutoa uhai wake katika 1 Yohana 3:16 sasa linawekwa katika hali ya uwezekano, utaratibu wa kumsaidia ndugu mwingine. Mistari hii ina uelekeo nzuri kama Yakobo (kama vile Yakobo 2:15,16).

Page 390: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

374

◙ "akamzuilia huruma zake" hiki kitenzi ni kauli tendaji tegemezi. Neno huruma kifasihi linamaanisha "hari ya kuonea huruma," Ni nahau ya Kiebrania kwa ajili ya hisia kubwa. Tena, matendo yetu yanamfunua Baba yetu.

◙ "Upendo wa Mungu" Tena hii ni kishamirishi au kimilikishi tegemezi au utata uliokusudiwa? 1. upendo kwa Mungu 2. upendo wa Mungu kwetu 3. vyote

Namba 3 inaendana na maandiko ya Yohana! 3:18 "tusipende kwa neno" Matendo huzungumza zaidi kuliko maneno (kama vile Mt. 7:24; Yakobo 1:22-25; 2:14-26). ◙ "tusipende kwa neno" Hili neno "ukweli" linastaajabisha. Mwingine angelitarajia maana yenye kufanana ya neno "nia," kufanana "tendo." Neno hili linaonekana kumaanisha uhalisia (NJB) au ukweli (TEV), kama matumizi ya neno "habari" katika 1 Yohana 1:5 na 3:11, ambalo linasistiza vyote mafundisho na mtindo wa maisha, vivyo hivyo "ukweli.” Tendo na nia lazima vitiwe hamasa na upendo wa kujitoa mwenyewe (upendo wa Mungu) na si onyesho la tendo ambalo hufurahisha nafsi ya mpaji au mtoaji. 3:19 "Katika hili tutafahamu" Hii inarejelea juu ya matendo ya upendo yaliyotajwa hapo awali. Hii ni kauli ya kati elekezi (yenye ushahidi) ya wakati ujao, ambayo ni ushahidi mwingine wa badiliko la mtu la kweli. ◙ "ya kwamba tu wa kweli" Mtindo wa maisha ya upendo wa waamini unaonyesha mambo mawili: (1) kwamba wako upande wa ile kweli na (2) kwamba dhamiri za ni safi. Tazama Mada Maalumu: kweli katika Yohana 6:55. 3:19-20 Kuna mkanganyiko mkubwa sana unaohusu ni kwa namna gani andiko hili la Kiyunani la mistari hii miwili litafsiriwe. Moja lenye uwezekano wa tafsiri linasistiza juu ya hukumu ya Mungu, ambapo lingine linasistiza juu ya huruma ya Mungu. Kwa sababu ya muktadha huu, uchaguzi wa pili unaonekana kuwa dhahiri sana. 3:20-21 Mistari hii yote ni sentensi shurutishi dalaja la tatu. 3:20 NASB "ikiwa mioyo yetu inatuhukumu" NKJV "kama mioyo yetu inatuhukumu" NRSV "kwa maana, hata kama dhamiri yetu yatuhkumu" TEV "ikiwa nafsi zetu zatuhukumu" NJB "hata ikiwa hisia zetu zatuhukumu" Waamini wote wamekumbana na huzuni ya ndani ya kutoishi kwa uchangamfu "ukawaida" kwamba wanayajua mapenzi ya Mungu kwa ajili ya maisha yao (yaani, Warumi 7). Maumivu hayo ya dhamiri yanaweza kutoka kwa Roho wa Mungu (ili kusababisha toba) au upendo lakini bado wakaendelea kupambana na dhambi (vyote agizo na uondoaji). Tazama MADA MAALUMU: Moyo katika Yohana 12:40 ◙ "naye anajua yote" Mungu anazijua nia zetu za kweli (kama 1 Sam. 2:3; 16:7; 1 Fal. 8:39; 1 Nya. 28:9; 2 Nya. 6:30; Zab. 7:9; 44:21; Mit. 15:11; 20:27; 21:2; Yer. 11:20; 17:9-10; 20:12; Luka 16:15; Matendo 1:24; 15:8; Rum. 8:26,27). 3:21 "mioyo yetu isipotuhukumu" Hii ni sentensi shurutishi daraja la tatu. Wakristo bado wana pambana na dhambi wao wenyewe (kama vile1 Yohana 2:1; 5:16-17). Wao wanakumbana na majaribu na matendo yasiyo sahihi katika hali mahususi. Mara nyingi dhamiri zao zinawahukumu. Kama ulivyo wimbo wa kumshukuru Mungu "Kule Mbinguni, Kabla ya Jua Kuwako," na Henry Twells anayeeleza:

Page 391: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

375

"Na hakuna, Ee Bwana, aliyebaki mkamilifu, Kwa kuwa hakuna aliye huru kabisa kutoka dhambini; Na wale wapendao wangekutumikia Wewe uliye mwema Ni watambuzi zaidi wa makosa yaliyo ndani yao." Maarifa ya injili, uhusiano mzuri sana pamoja na Yesu, utiifu kwa mwongozo wa Roho na Baba Mwenye kujua yote na kuituliza mioyo yetu ilitoka mavumbini (kama vile Zab. 103:8-14)!

◙ "tuna ujasiri kwa Mungu" Hii inazungumzia juu ya upatikanaji wa wazi na huru wa uwepo wa Mungu. Hili ni neno na dhana ya Yohana inayorudiwa mara kwa mara (kama vile 1 Yohana 2:28; 3:21; 4:17; 5:14; Ebr. 3:6; 10:35, tazama Mada Maalumu: Dhamana ya Mkristo katika 1 Yohana 7:4). Aya hii inawasilisha faida mbili za uhakika

1. kwamba Wakristo wana ujasiri kamili mbele ya Mungu 2. lolote waombalo wanapata toka kwake

3:22 "na lo lote tuombalo" Hii ni kauli tendaji tegemezi ya wakati uliopo na kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo. Hii inaakisi semi za Yesu katika Mt. 7:7; 18:19, Yohana 9:31; 14:13-14; 15:7,16; 16:23; Marko 11:24; Luka11:9-10. Ahadi za Andiko hili ni tofauti sana na uzoefu wa mkristo katika maombi. Mastari huu unaonekana kuahidi maombi yenye majibu yasiyokuwa na kikomo. Hapa ndipo ulinganishaji wa maandiko mengine yaliyo tofauti unaposaidia kuleta ulinganifu wa kithiolojia.

MADA MAALUM: MAOMBI, YASIYO NA UKOMO LAKINI YENYE UKOMO

A. Injili za ufupisho 1. Wanaoamini wanatiwa moyo kustahimili katika maombi na Mungu atawapa “vitu vyema”

(Mathayo, Mt. 7:7-11) na “Roho yake” (Luka, Luka 11:5-13) 2. Katika mazingira ya kanisa wanaoamini wenye nidhamu(mbili) wanatiwa moyo kuungana kwenye

maombi (Mt. 18:19) 3. Katika muktadha wa hukumu ya Wayahudi wanaoamini wanaambiwa waombe kwa imani bila

mashaka (Mt.21:22; Marko 11:23-24) 4. Katika muktadha wa mifano miwili (Luka 18:1-8, hakimu mdhalimu na Luka 18:9-14, Farisayo na

mwenye dhambi) wanaoamini wakahimizwa kuishi tofauti na hakimu mdhalimu na Farisayo mwenye kujihesabia haki. Mungu huwasikia wanyenyekevu na wanaotubu (Luka 18:1-14)

B. Maandiko ya Yohana 1. Katika muktadha wa mtu alieyezaliwa akiwa kipofu ambaye Yesu anamponya, upofu wa kweli wa

Mafarisayo unafunuliwa. Maombi ya Yesu (kama yalivyo ya mwingine yeyote) yanajibiwa kwa sababu alimjua Mungu na aliishi inavyostahili (Yohana 9:31)

2. Mahubiri ya Yohana katika chumba cha orofani (Yohana 13:17) a. Yohana 14:12-14 – waaminio katika maombi wanajulikana kwa

1. Kutoka kwa wanaoamini 2. Kuomba kwa jina la Yesu 3. Kutamani kwamba Baba atukuzwe 4. Kushika amri (Aya ya. 15)

b. Yohana 15:7-10– waaminio katika maombi wanajulikana kwa 1. Kukaa ndani ya Yesu 2. Neno lake kukaa ndani yao 3. Kutamani kwamba Baba atukuzwe 4. Kuzaa matunda mengi 5. Kushika amri (Aya ya. 10)

c. 1 Yohana 15:15-17– waaminio katika maombi wanajulikana kwa 1. Kuchaguliwa kwao

Page 392: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

376

2. Kuzaa kwao matunda 3. Kuomba kwa jina la Yesu 4. Kushika amri, kupendana wao kwa wao

d. Yohana 16:23-24- waaminio katika maombi wanajulikana kwa 1. Kuomba kwa jina la Yesu 2. Kutamani kwamba furaha iwe timilifu

3 Waraka wa kwanza wa Yohana (Yohana 1) a. Yohana 1. 3:22-24 – waaminio katika maombi wanajulikana kwa

1) Kushika amri zake (aya ya. 22,24) 2) Kuishi inavyostahili 3) Kuamini kwa Yesu 4) Kupendana kila mmoja na mwenzake 5) Kukaa ndani yake naye ndani yetu 6) Kuwa na kipawa cha Roho Mtakatifu

b. 1 Yohana 5:14-16– waaminio katika maombi wanajulikana kwa 1. Kuwa na ujasiri kwa Mungu 2. Sawasawa na mapenzi yake 3. Wanaoamini wanaombeana

c. Yakobo 1. Yakobo 1:5-7–wanaoamini wanapambana na majaribu mbalimbali wanaagizwa kuomba

hekima bila mashaka. 2. Yakobo 4:2-3– wanaoamini wanapaswa kuomba kwa nia nzuri 3. Yakobo 5:13-18– wanaoamini wanakabiliwa na matatizo ya afya wanahimizwa

a. Kuomba wazee wawaombee b. Kuomba kwa imani c. Kuomba kwamba dhambi zao zisamehewe d. Waungame dhambi zao wenyewe kwa wenyewe na kuombeana (sawa na Yohana 1.

5:16) Umuhimu wa maombi yenye kuleta matokeo ni kufanana na Kristo. Hii ndio maana ya kuomba kwa jina la Yesu. Jambo lililo baya zaidi ambalo Mungu angeweza kuwafanyia wengi wa Wakristo ni kujibu maombi yao ya ubinafsi! Katika hisia moja maombi yote yanajibiwa. Mtazamo wenye thamani sana wa maombi ni kwamba waamini wametumia muda kukaa na Mungu, kumtumaini Mungu.

◙ "kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake" Tazama katika muktadha huu yale mahitaji mawili kwa ajili ya maombi yenye kujibiwa.

1. Utii 2. kufanya mambo yenye kumfurahisha Mungu (kama vile Yohana 8:29)

1 Yohana ni "ni kwa namna gani" kitabu cha Mristo aishiye kwa manufaa na huduma.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) : 1 YOHANA 3:23-24 23 Na hii ndiyo amri yake, kwamba tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana sisi kwa sisi, kama alivyotupa amri. 24 Naye azishikaye amri zake hukaa ndani yake yeye naye ndani yake. Na katika hili tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa huyo Roho aliyetupa

3:23 "Na hii ndiyo amri yake. . . kwamba tuliamini . . . na kupendana" Tazama neno "amri" Hii ni kauli ya umoja yenye vipengele viwili. Kipengele cha kwanza ni imani binafsi; kile KITENZI, "kuamini," hiki ni kitenzi cha kauli tendaji tegemezi (kama vile Yohana 6:29,40). Kipengele cha pili ni cha kimaadili; kile kitenzi, kupenda, hii ni kauli tendaji tegemezi ya wakati uliopo (kama vile 1 Yohana 3:11; 4:7). Injili ni habari inayopaswa kuaminiwa, mtu wa kuipokea, na namna ya kuiishi!

Page 393: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

377

◙ "kwamba tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo" Hii dhana ya "kuamini" ni muhimu sana katika kuielewa imani ya kibiblia. Hili neno la Agano la Kale aman liliakisi "utii," "utumainiwaji," "utegemewaji," au "uaminifu" (tazama Mada Maalumu juu ya neno la Kiyunani katika 1 Yohana 2:10). Katika Agano Jipya hili neno la Kiyunani (pisteuō) linatafsiriwa kwa maneno matatu ya Kiingereza: amini, imani, au tumaini (tazama Mada Maalumu juu ya neno la Kiyunani katika Yohana 2:23). Hili neno haliakisi sana juu ya matumaini ya Mkristo kama ya ki- Mungu. Hii ni sifa yake, ufunuo, na ahadi, si utiifu au uaminifu wa wanadamu walioanguka, hata wanadamu waliokombolewa katika anguko, kwamba ndio wautengenezao msingi usiotikisika! Hii dhana ya kuamini katika "hili jina" au kuomba "katika hili jina" inaakisi uelewa karibia huko Mashariki ambapo hili jina huwakilisha mtu.

1. Yesu katika Mt. 1:21,23,25; 7:22; 10:22; 12:21; 18:5,20; 19:29; 24:5,9; Yohana 1:12; 2:23; 3:18; 14:26; 15:21; 17:6; 20:31

2. Baba katika Mt. 6:9; 21:9; 23:39; Yohana 5:43; 10:25; 12:13; 17:12 3. Utatu katika Mt. 28:19.

Haya ni maelezo mafupi ya kiufundi kuhusiana mstari huu. Katika kitabu chake cha Word Pictures in the New Testament (uk. 228), A. T. Robertson anayaainisha matatizo ya machapisho ya Kiyunani yanayohusiana na KITENZI "kuamini." Machapisho ya kale ya Kiyunani B, K, na L yana kitenzi cha kauli tendaji chenye utegemezi, ambapo א, A, na C yana kauli tendaji yenye utegemezi. Kauli zote zinaenda sawa na muktadha pamoja na mtindo wa Yohana.

3:24 "Naye azishikaye. . . hukaa. . ." Hizi ni kauli za wakati uliopo. Utii umeungamanishwa na kukaa. Upendo ni unadhihirisho kwamba tulikuwa ndani ya Mungu na Mungu yu ndani yetu (kama vile 1 Yohana 4:12,15-16; Yohana 14:23; 15:10). Tazama Mada Maalumu: "Kukaa" katika 1 Yohana2:10.

◙ "kwa huyo Roho aliyetupa" Yohana anatumia ushahidi dhahiri kuwatathmini waamini wa kweli (kama vile Rum. 4:13; 8:14-16, tazama Utambuzi wa muktadha wa 2:3-27, C). Mambo mawili yanayohusiana na Roho Mtakatifu.

1. kumkiri Yesu (kama vile Rum. 10:9-13; 1 Kor. 12:3) 2. kuishi katika ufanano na Kristo(kama vile Yohana 15; Gal. 5:22; Yakobo 2:14-26)

MASWALI YA MJADALA

Huu ni mwongozo wa fasiri, ina maanisha kwamba unawajibika kwa tafsiri zako mwenyewe za Biblia. Kila mmoja wetu lazima atembee katika mwanga tulio nao. Wewe, Biblia, na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Hutakiwi uvitelekeze vitu hivi kwa mfasiri. Maswali ya mjadala huu yanatolewa kukusaidia kufikiri juu ya mambo makubwa ya sehemu za kitabu hiki. Yanalenga kukuamsha kimawazo na sio kutoa maana.

1. Nini kinaunganisha maudhui ya 1 Yohana 3:11-24? (kama vile 1 Yohana 2:7-11)? 2. Eleza uhusiano wa 1 Yohana 3:16 na 17. Ni kwa namna gani kujitolea maisha yetu kunaweza

kulinganishwa na sisi kuwasaidia ndugu zetu katika mahitaji yao? 3. Je! 1 Yohana 3:19-20 inasistiza utiisho wa hukumu ya Mungu au huruma kuu ya Mungu a mbayo

hutuliza sisi katika woga wetu? 4. Je! Ni kwa namna gani tunahusianisha usemi wa Yohana kuhusu maombi katika 1 Yohana 3:22 na

mazoea yetu ya kila siku? 5. Je! Ni kwa namna gani mtu alinganishe msistizo wa mtazamo wa Yohana wa kimafumbo juu ya uhitaji

wa Mkristo wa kubali na kuungama dhambi na usemi wake wa ukamilifu wa kutokuwa na dhambi? 6. Kwa nini Yohana anaweka msisitizo mzito kama huu juu ya mtindo wa maisha? 7. Eleza ukweli wa kitheolojia unavyohusishwa katika tendo la "kuzaliwa pili." 8. Ni kwa namna gani kifungu hiki kinahusiana na maisha ya Mkristo ya kila siku?

Page 394: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

378

1 YOHANA 4

MIGAWANYO YA AYA YA TAFSIRI ZA KISASA

UBS4 NKJV NRSV TEV NJB Roho wa Mungu Roho wa Kweli na Kupambanua ukweli Roho wa kweli Sharti la tatu kuwa na Roho ya Roho ya na uongo na Roho wa uongo makini kuhusu mpinga Kristo udanganyifu mpinga Kristo na kuwa kinyume na ulimwengu 3:24-4:6 4:1-6 4:1-6 4:1-3 4:1-6 4:4-6 chanzo cha Upendo na imani (4:7-5:13) Mungu ni pendo Kumjua Mungu kubarikiwa ki Mungu ni pendo chanzo cha upendo Kupitia upendo upendo 4:12 4:7-11 4:7-12 4:7-10 4:7-5:4 Kumwona Mungu 4:11-12 Kupitia upendo 4:12-16 4:13-16a 4:13-16a 4:13-16a 4:16b-21 Ukamilifu wa 4:16b-21 4:16b-18 upendo 4:17-19 4:19-21 Utii kwa Imani 4:20-55

MZUNGUKO WA TATU WA USOMAJI KUFUATILIA KUSUDIO LA ASILI LA MWANDISHI KATIKA NGAZI YA AYA Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwatafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Aya ya kwanza 2. Aya ya pili 3. Aya ya tatu 4. N.k

UTAMBUZI WA MUKTADHA WA NDANI WA 4:1-21

A. Yohana 4 ni kitengo cha fasihi kilichofanywa maalum kuhusu jinsi Wakristo wanavyopima na kuthibitisha wale wanaodai kusema kwa niaba ya Mungu. Ibara hii inahusu 1. Hawa manabii wa uongo waitwao wapinga Kristo (kama vile 1 Yohana 2:18-25) 2. Wale wanaojaribu kudanganya (kama vile 1 Yohana 2:26; 3:7)

Page 395: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

379

3. Ikiwezekana wale wanaodai kujua kweli maalum za kiroho (kama vile 1 Yohana 3:24) Ili kuelewa kikamilifu hali ya hatari ya Wakristo wa kwanza mtu lazima atambue kwamba wengi walidai kusema kwa niaba ya Mungu (kama vile 1 Kor. 12:10; 14:29; 1 Thes. 5:20-21; 1 Yohana 4:1-6). Hapakuwa na Agano Jipya katika ukamilifu wake. Kupambanua roho kurishirikisha vipimo vya mafundisho na maisha ya kijamii (kama vile Yakobo 3:1-12).

B. 1 Yohana ni ngumu sana kueleza kwa muhtasari kwa sababu ya mpangilio wa mawazo unaorudiarudia.

Hii hakika ni kweli katika 1 Yohana 4. Yaonekana kwamba sura hii inasisitiza tena kweli ambayo ilikuwa imefundishwa kwenye sura ya awali, hasa hitaji la waaminio kupendana (kama vile 1 Yohana 4:7-21; 2:7-12 na 3:11-24).

C. Yohana anaandika ili kupambana na waalimu wa uongo na kuwatia moyo waaminio wa kweli. Anafanya hivi kwa kutumia vipimo kadhaa:

1. kipimo cha kimafundisho (imani katika Yesu, kama vile 1 Yohana 2:18-25; 4:1-6,14-16; 5:1,5,10) 2. Kipimo cha mtindo wa maisha (utii, kama vile 1 Yohana 2:3-7; 3:1-10, 22-24) 3. Kipimo cha kijamii (upendo, kama vile 1 Yohana 2:7-11; 3:11-18; 4:7-12,16-21; 5:1-2) Sehemu mbalimbali za maandiko zinahusu walimu wa uongo tofauti tofauti. 1 Yohana inatambulisha uasi wa walimu wa mafunuo ya uongo. Tazama utangulizi kwa 1 Yohana, Uasi. Sehemu nyingine za Agano Jipya (kama vile Yohana 1:13; Rum. 10:9-13; 1 Kor. 12:3). Kila mazingira lazima yasomwe tofauti ili kutambua ni kosa gani linazungumziwa. Kulikuwa na kosa kutoka vyanzo kadhaa. 1. Wayahudi washikiliaji mno wa sheria 2. Wanafalsafa 3. Wayunani wenye mtazamo wa kishi kwa neema 4. Wale waliodai ufunuo maalum wa kiroho ama uzoefu.

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) 1 YOHANA 4:1-6 1 Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. 2 Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu. 3 Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani. 4 Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia. 5 Hao ni wa dunia; kwa hiyo wanena ya dunia na dunia huwasikia 6 Sisi twatokana na Mungu. Yeye amjuaye Mungu atusikia; yeye asiyetokana na Mungu hatusikii. Katika hili twamjua Roho wa kweli, na roho ya upotevu.

4:1 "Msiiamini" Hii ni kauli ya yenye masharti ya wakati uliopo ikiwa na kiambata hasi ambayo kwa kawaida humaanisha kuzuia kitendo ambacho tayari kinaendelea. Mwelekeo wa Wakristo ni kukubali heshima nzito, mijadala yenye mantiki ama matukio ya kimuujiza toka kwa Mungu. Inaonekana walimu wa uongo walikuwa wanadai (1) kuongea na Mungu (2) kuwa wamepata ufunuo maalumu kutoka kwa Mungu.

MADA MAALUM: HUKUMU KATIKA AGANO LA JIPYA

Hukumu ni hakika (kama vile Mt. 12:36; Ebr. 9:27; 10:27; 2 Pet. 2:4,9; 3:7). A. Yeye anayehukumu ni

1. Mungu (kama vile Rum. 2:2-3; 14:10,12; 1 Pet. 1:17; 2:23; Ufu. 20:11-15) 2. Kristo (kama vile Yohana 9:39; Mt. 16:27; 25:31-46; Mdo. 10:42; 17:31; 2 Kor. 5:10; 2 Tim. 4:1) 3. Baba kupitia Mwana (kama vile Yohana 5:22-27; Mdo. 17:31; Rum. 2:16)

Hukumu sio somo zuri, lakini ni maudhui ya sasa katika Biblia. Imejikita katika misingi au miamba za kweli

Page 396: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

380

kibiblia. 1. Huu ni ulimwengu wa kimaadili ulioumbwa na Mungu mwadilifu (tunavuna tunachopanda, kama vile

Gal. 6:7). 2. Uanadamu umeanguka; tumeasi. 3. Huu si ulimwengu ambao Mungu alikusudia uwepo. 4. Uumbwaji wote unaojielewa (malaika na wanadamu) tutatoa hesabu kwa muumbaji wao kwa zawadi ya

uzima. Sisi ni mawakili. 5. Milele itaamuliwa kwa kudumu na matendo yetu na chaguzi tulizozifanya katika haya maisha.

B. Je Wakristo wahukumiane wao kwa wao? Jambo hili lazima lishughulikiwe katika namna mbili. 1. waamini wanaonywa wasije wakahukumiana wao kwa wao (kama vile Mt. 7:1-5; Luka 6:37,42; Rum.

2:1-11; Yakobo 4:11-12) 2. waamini waanaonywa kuwatathmini viongozi wao (kama vile Mt. 7:6,15-16; 1 Kor. 14:29; 1 The. 5:21; 1

Tim. 3:1-13; na 1 Yohana 4:1-6)

Baadhi ya vigezo kwa ajili ya tathmini sahihi inaweza kusaidia

1. tathmini lazima iwe kwa kusudi la kukiri (kama vile 1 Yohana 4:1 – "jaribu" ikiwa na mtizamo wa kuthibitisha; angalia Mada Maalum: Kujaribiwa [peirazō na dokimazō])

2. tathmini lazima ifanyike katika upole na unyenyekevu (kama vile Gal. 6:1) 3. tathmini lazima iweke shabaha kwenye upendeleo wa mambo ya kibinafsi (kama vile Rum. 14:1-23; 1

Kor. 8:1-13; 10:23-33) 4. tathmini lazima itambue wale viongozi walio na "sio weza kuvumilia kukosolewa" kutoka ndani ya

kanisa au katika jamii (kama vile 1 Timotheo 3).

◙ "kila roho" Neno"Roho" limetumika kwa maana ya nafsi ya mtu.Tazama maelezo katika 1 Yohana 4:6. Hii inahusu ujumbe uliotarajiwa kutoka kwa Mungu. Uasi huja kutoka ndani ya kanisa (kama vile 1 Yohana 2:19). Manabii wa Mungu walikuwa wanadai kwamba walinena kutoka kwa Mungu. Yohana anadai kwamba kuna vyanzo viwili vya kiroho, Mungu au Shetani, nyuma ya tamko la mwanadamu na matendo.

◙ "bali zijaribuni hizo roho"Hii ni kauli tendaji enye masharti ya wakati uliopo. Hiki ni kipawa cha roho (kama vile 1 Kor 12:10; 14:29) na hitaji la lazima kwa kila muamini, kama yalivyo maombi.Neno hili la Kiyunani dokimazō lina vidokezo vya "Kujaribu kuwepo na tazamio la kuelekea kukubalika." Waaminio wawaze vyema kuhusu wengine hata kama mabaya yakiwa yamethibitika (kama vile 1 Kor 13:4-7; 1 Thes. 5:20-21).

MADA MAALUMU: MANENO YA KIYUNANI YAHUSUYO KUPIMA NA VIDOKEZO VYAKE

Kuna manaeno mawili ya Kiyunani ambayo yana kidokezo kwa ajili ya kumpima mtu kwa kusudi fulani. 1. Dokimazō, Dokimion, Dokimasia

Neno hili ni neno la mtu yule afuaye vyuma kwa ajili ya kujaribu uhalisia wa kitu fulani (yaani, kistiari mtu fulani) kwa moto (tazana Mada Maalumu: Moto). Moto hudhihilisha chuma halisi na huteketeza (yaani, husafisha) dongo la chuma. Kitendo hiki cha kifizikia kinakuwa nahau yenye nguvu kwa Mungu na/au Ibilisi na/au binadamu kuwajaribu wengine. Neno hili linatumika tu katika maana chanya ya kujaribu kwa kuangalia hadi kuufikia ukubalifu (tazama Mada Maalumu: Mungu Huwajaribu Watu Wake [Agano la Kale).

Linatumika katika Agano la Kale kwa ajili ya a. Madume ya ng’ombe – Luka 14:19 b. sisi wenyewe – 1 Kor. 11:28 c. imani yetu – Yakobo 1:3 d. hata Mungu –Ebr. 3:9

Matokeo ya majaribu hayajafikiriwa kuwa chanya (kama vile. Rum. 2:18; 14:22; 16:10; 2 Kor. 10:18; 13:3,7;

Page 397: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

381

Flp. 2:27; 1 Pet. 1:7), hivyo, neno husilisha wazo la mtu aliyepimwa na kuhakikishwa a. kuwa wa thamani b. kuwa wazuri c. kuwa halisi d. kuwa wa maana e. kuwa wa kuheshimiwa

2. Peirazō, Peirasmus Neno hili mara nyingi lina maana nyingine ya kupimwa kwa kusudi la utafutaji au ukataaji. Linatumika katika maana nyingine kwa majaribu ya Yesu nyikani.

a. Linabeba jaribio la kumtega Yesu (kama vile Mt. 4:1; 16:1; 19:3; 22:18, 35; Marko 1:13; Luka 4:2; Ebr. 2:18).

b. Neno hili (peirazōn) linatumika kama wadhifa kwa Ibilisi katika Mt. 4:3; 1 The. 3:5 (yaani, "mjaribu"). c. Matumizi

1) Lilitumiwa na Yesu alipokuwa akiwaonya wanadamu kutomjaribu Mungu (kama vile Mat. 4:7; Luka 4:12, [au Kristo kama vile 1 Kor 10:9]).

2) Pia linamaanisha jaribio la kufanya kitu fulani ambacho kimeshindikana (kama vile Ebr.11:29). 3) Linatumika katika maana nyingine kwa majaribu na masumbufu ya waamini (kama vile 1 Kor.

7:5; 10:9, 13; Gal. 6:1; 1 The. 3:5; Ebr. 2:18; Yakobo. 1:2, 13, 14; 1 Pet. 4:12; 2 Pet 2:9).

◙ "kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani" Hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo (kama vile Yer. 14:14; 23:21; 29:8; Mt. 7:15; 24:11,24; Matendo 20:28-30; 2 Petr 2:1; 1 Yohana 2:18-19,24; 3:7; 2 Yohana 7). Maana ni kwamba wameliacha kanisa (makanisa ya nyumbani), bado wanaendelea kudai kuzungumza kwa niaba ya Mungu. Tazama MADA MAALUM: Manabii wa Agano Jipya katika Yohana 4:19 4:2 "Katika hili mwamjua Roho wa Mungu" Muundo huu wa sarufi waweza kuwa kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo (kauli) au kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopo (amri). Utatanishi huo huo wa muundo ni "kaa ndani ya," 1 Yohana 2:27 na "jua," 2:29. Roho mtakatifu kila wakati humtukuza Yesu (kama vile Yohana 14:26; 15:26; 16:13-15).Jaribio hili hili laweza kuonekana katika maandiko ya 1 Kor. 12:3.

◙ "kila roho ikiriyo"Hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo kwenye kuendelea kukiri tamko la imani la wakati uliopita. Neno la Kiyunani "kiri" ni muunganiko kutoka kitu “kile kile”na “kusema,” Hii ni dhamira inayojirudia rudia katika 1 Yohana (kama vile 1 Yohana 1:9; 2:23; 4:2-3; 4:15; Yohana 9:22; 2 Yohana 7). Neno hili linamaanisha kwa tamko lililo mahususi na hadhara la uthibitisho na kujitoa kwa mtu kwa ajili ya injili ya Yesu Kristo.Tazama Mada Maalum katika Yohana 9:22

◙ "kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu” Hii ni kauli timilifu tendaji endelevu. Hiki ni kipimo muhimu sana cha mafundisho kwa kuwatambua walimu wa uongo (yaani, Mafunuo) ambao Yohana alikuwa anapambana nao katika kitabu hiki. Tamko lake kuu ni kwamba Yesu ni binadamu kamili (yaani, mwili, ambao Mafunuo yalikataa) na pia ni Mungu kamili (kama vile 1 Yohana 1:1-4; 2 Yohana 7; Yohana 1:14; 1 Tim 3:16). Njeo timilifu zinathibitisha kwamba ubinadamu wa Yesu haukuwa wa muda tu, bali wa kudumu. Hili halikuwa swala dogo, Yesu kweli anashiriki ubinadamu na Uungu. 4:3 "Na kila roho isiyomkiri Yesu” Inavutia kitheolojia kwamba toleo la Kilatini la zamani la Agano Jipya waandishi wa Patristic, Clement, Origen wa Iskandria, Irenaeus, na Tertullian yana leui (huru), inayomaanisha "kumtenganisha Yesu," inavyoonekana ndani ya Roho ya mwanadamu na roho ya Kiungu iliyotengwa ambayo ilifananishwa na maandiko ya Mafunuo. Ya karne ya pili lakini huku ni kuongeza maneno halisi ya mwandishi ambako kunaaksi mapambano ya kufa na kupona ya kanisa la kwanza dhidi ya uasi (tazama Bart Erhart, The Orthodox Corruption of Scripture, kur. 125-135).

Page 398: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

382

◙ “roho ya mpinga Kristo" Hapa neno (kama vile 1 Yohana 2:18-25) limetumika kama uhalisia au usahihi wa Kristo, sio jaribio la kumnyanganya nafasi yake.

◙ "ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani" Hii ni kauli tendaji elekezi ya wakatim uliopo inayoonyesha kwamba Yohana alikwisha kujadiliana na jambo hili mapema na kwamba uhusiano wake ulibaki. Katika Kiyunani kiwakilishi "kitu" kinaendana na neno hasi "roho." Kama 1 Yohana 2:18, aya hii inaakisi kwamba roho ya wapinga Kristo tayari imekwisha kuja na inakuja. Hawa walimu wa uongo wa Mafunuo wanaunda mnyororo wa habari za uongo, mifumo ya maisha ya uongo, kukiri kwa uongo katika vizazi mbalimbali kutoka kwa mwovu wa Mwanzo, 3 hadi ushirikisho wa kuwa na mwili wa uovu kwa mpinga Kristo wa siku za mwisho (yaani , 2 Wathesalonike 2; Ufunuo 13). 4:4-6 "Ninyi. . . nanyi. . .Sisi” viwakilishi nomino vyote hivi vimesisitizwa.Kuna makundi matatu yanayo tambulishwa.

1. Waaminio wa kweli (Yohana na wasomaji wake) 2. Waaminio wa uongo (walimu wa Mafunuo na wafuasi wao) 3. Wamisionari wa Yohana na makundi ya kithiolojia

Vitu vitatu vinavyohusiana kama hivi vinaonekana katika Waebrania 6 na 10. 4:4 "mmewashinda"Hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo. Hili linaonekana kuwa rejeo kwa mgongano wa kimafundisho na maisha Ya ushindi ya Kikristo. Ni neno la ajabu la kutia moyo kwao na kwetu! Yohana anahusika na maisha ya Kikristo ya ushindi dhidi ya dhambi na shetani. Anatumia neno hili (nikaō)mara 6 katika 1 Yohana (kama vile 1 Yohana 2:13,14; 4:4; 5:4,5), mara 11 katika ufunuo na mara moja katika Yohana, 16:33). Neno hili “ushindi" ilitumika mara moja tu katika Luka (kama vile Luka 11:22) na mara mbili kwenye maandiko ya Paulo (kama vile Rum. 3:4; 12:21).

◙ “kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia" Huu ni msisitizo juu ya Uungu unakaa ndani. Hapa inaonekana kuwa mrejeo kwa Baba akaaye (kama vile Yohana 14:23; 2 Kor 6:16). Agano Jipya pia linasisitiza (1) kukaa ndani ya Mwana (kama vile Mt. 28:20; Kol. 1:27) na (2) kukaa ndani kwa Roho Mtakatifu (kama vile Rum. 8:9; 1 Yohana 4:13). Roho na Mwana wanatambulika (kama vile Rum 8:9; 2 Kor 3:17; Wag. 4:6; Flp. 1:19; 1 Pet 1:11). Tazama Mada Maalum katika Yohana 14:16 Aya hii "yeye aliye ulimwenguni" inamhusu shetani (kama vile Yohana 12:31; 14:30; 16:11; 2 Kor 4:4; Efe. 2:2; 1 Yohana 5:19) na wafuasi wake. Neno "ulimwengu" katika 1 Yohana kila wakati unao ushauri hasi (yaani, jamii ya binadamu iliyojipanga na kutenda kinyume na Mungu, Tazama Mada Maalum: Kosmos katika Yohana 14:17) 4:5 "Hao ni wa dunia"Huu ni uhusika wa kuondoa wa chanzo. Neno "dunia" linatumika hapa kwa maana ya jamii ya binadamu inayojaribu kujitunzia mahitaji yake yote kinyume na Mungu (kama vile 1 Yohana 2:15-17). Inahusu roho huru ya binadamu kwa pamoja na wale walioanguka! Mfano wake ni Kaini (kama vile 1 Yohana 3:12). Mifano mingine ingekuwa (1) Eliya na Manabii wa Ba'al (1 Wafalme 18) na (2) Yeremia dhidi ya Anania (Yeremia 28).

◙ "dunia huwasikia" Ushahidi mwingine wa dini za Kikristo dhidi ya walimu wa uongo ni kujua akina nani huwasikiliza (kama vile 1 Tim 4:1). 4:6 "Yeye amjuaye Mungu atusikia"hii ni kauli tendaji endelevu ya wakati uliopo. Walio waamini wa kweli huendelea kusikiliza na kukubaliana na kweli ya mitume! Waamini wanaweza kutambua wahubiri/walimu wa kweli kutokana na maudhui ya ujumbe wao na nani husikiliza na kuwaitikia.

◙ “Katika hili twamjua Roho wa kweli, na roho ya upotevu" Hii yaweza kuhusu Roho Mtakatifu (kama vile Yohana 14:17; 15:26; 16:13; 1 Yohana 4:6; 5:7) na roho ya uovu, Shetani.Waaminio lazima waweze kutambua kiini cha ujumbe. Mara nyingi wote hupewa kwa jina la Mungu wakichukuliwa kama wasemaji wa Mungu. Mmoja humwinua Yesu na kwa mfanano wake na mwingine huinua makisio ya kibinadamu na uhuru wa binadamu.

Page 399: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

383

Robert Girdlestone, Synonyms of the Old Testament,kina mjadala wa kuvutia wa matumizi ya neno "roho"katika Agano Jipya.

1. roho ya uovu 2. roho ya mwanadamu 3. Roho Mtakatifu 4. Vitu ambavyo huzaa ndani ya na kupitia roho ya mwanadamu

a. 'sio roho ya utumwa dhidi ya kufanywa wana' - Rum. 8:15 b. 'roho ya upole' -- 1 Kor. 4:21 c. 'roho ya amani' -- 2 Kor. 4:13 d. 'roho ya hekima na ufunuo katika kumjua yeye' -- Efe. 1:17 e. 'sio roho ya uoga bali ya nguvu na ya upendo ya moyo wa kiasi' -- 2 Tim. 1:7 f. 'roho ya upotevu dhidi ya roho wa kweli' --1 Yohana 4:6" (uk. 61-63).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) 1 YOHANA 4:7-14| 7 Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu.8 Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo. 9 Katika hili pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwamba Mungu amemtuma Mwanawe pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kwa yeye. 10 Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu. 11 Wapenzi ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana. 12 Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu. 13 Katika hili tunafahamu ya kuwa tunakaa ndani yake, naye ndani yetu, kwa kuwa ametushirikisha Roho wake. 14 Na sisi tumeona na kushuhudia ya kuwa Baba amemtuma Mwana kuwa Mwokozi wa ulimwengu.

4:7 "mpendane"Hii ni kauli tendaji tegemezi ya wakati uliopo. Mtindo wa maisha, upendo wa kila siku ndio tabia moja inayowahusu wote waaminio (kama vile 1 Kor 13; Gal. 5:22). Hii ni dhana inayojirudia rudia kwenye maandiko ya Yohana na ukamilifu wa kipimo cha uadilifu (kama vile Yohana 13:34; 15:12,17; 1 Yohana 2:7-11; 3:11,23; 2 Yohana 5, tazama Mtindo wa utambuzi, C). Dhamira tegemezi inayoelezea hali ya dharura.

◙ "kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu" Mungu, sio upendo wa mwanadamu juu ya wanadamu, huruma, au mihemko, ndio chanzo cha upendo (kama vile 1 Yohana 4:16). Kimsingi hauko kimhemko bali kitendo kilichokusudiwa (yaani, Baba kumtuma Mwana kufa badala yetu, kama vile 1 Yohana 4:10; Yohana 3:16).

◙ "kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu" vitenzi ni kauli tendewa ya wakati timilifu na kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo. Maneno muhimu ya Yohana kwa mtu kuwa muamini yanahusika na kuzaliwa kimwili (kama vile 1 Yohana 2:29; 3:9; 4:7; 5:1, 4, 18; Yohana 3:3,7). Neno "jua" linaaksi maana ya Kiebrania ya kuendelea ushiriki wa ndani (kama vile Mwa. 4:1; Yer. 1:5). Ndiyo dhana inayojirudia rudia ya 1 Yohana, ikiwa imetumika zaidi ya mara sabini na saba. Tazama Mada Maalum katika Yohana 1:10 4:8 "Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo"Mtindo wa maisha ya upendo ndicho kipimo cha kweli cha kumjua Mungu. Hii ni mojawapo ya matamko mepesi ya msingi wa Yohana; "Mungu ni pendo" linaendana na “Mungu ni nuru" (kama vile 1 Yohana 1:5) na "Mungu na roho" (kama vile Yohana 4:24). Mojawapo ya njia zaidi kutofautisha upendo wa Mungu na ghadhabu ya Mungu ni kulinganisha Kumb. 5:9 na 5:10 na 7:9. 4:9 "Katika hili pendo la Mungu lilionekana kwetu" Hii ni kauli tendewa elekezi ya wakati uliopo usiotimilifu (kama vile Yohana 3:16; 2 Kor 9:15; Rum. 8:32). Mungu amekwisha onesha dhahiri kwamba anatupenda kwa kumtuma mwanawe wa pekee kufa badala yetu. Upendo ni kitendo sio hisia tu. Waamini lazima

Page 400: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

384

wajitahidi kufanya vyema sana hata zaidi kuliko katika maisha yao ya kila siku. (kama vile 1 Yohana 3:16). Kumjua Mungu ni kupenda kama apendavyo yeye.

◙ “Mungu amemtuma Mwanawe pekee ulimwenguni" Hii ni kauli timilifu tendaji elekezi; kufanyika mwili na matokeo yake vinasalia! Manufaa yote ya Mungu huja kupitia Kristo. Neno "pekee" ni monogenēs, ambalo linamaanisha "namna ya pekee," "moja ya namna yake," sio aliyezaliwa kwa namna ya tendo la ndoa. Uzazi wa Maria haukuwa tendo la ndoa kwa Mungu au Mariamu. Yohana anatumia neno hili mara kadhaa kumhusu Yesu (kama vile Yohana 1:14,18; 3:16,18; 1 Yohana 4:9). Tazama maelezo zaidi katika Yohana 3:16. Yesu ni Mwana wa Mungu katika maana (ufahamu wa kipekee) usioweza kuelezeka kiufahamu. Waaminio ni watu wa Mungu tu katika maana ya kuwezeshwa kutoka chanzo husika.

◙ "ili tupate uzima kwa yeye" Hii ni kauli tendaji tegemezi ya wakati uliopo usiotimilifu ambayo inamaanisha uwezekano wa kitu ambacho hakikuweza kufikilika kabla ya mwitikio wa imani kuwa lazima. Kusudi la kufanyika binadamu lilikuwa ni uzima wa milele (kama vile Yohana 10:10). 4:10 "Hili ndilo pendo" Upendo wa Mungu umedhihirishwa wazi wazi katika uhai na kifo cha Yesu (kama vile Rum. 5:6,8).Kumjua Yesu ndio kumjua Mungu. Kumjua Mungu ni kupenda!

◙ “si kwamba sisi tulimpenda Mungu" Agano Jipya ni la pekee miongoni mwa dini za ulimwengu. Kwa uhalisia dini na mwanadamu aliyeanguka! Ukweli wa ajabu na kupendeza sio upendo wetu kwa Mungu, bali upendo wake kwetu. Ametutafuta kupitia dhambi zetu, Kweli ya utukufu wa ukristo ni kwamba Mungu anampenda mwanadamu aliyeanguka na ameanzisha na kuhifadhi uhusiano unaobadili maisha. Kuna utofauti unaohusiana na muundo wa kitenzi.

1. Kuwa na kuendelea kupenda, wakati timilifu --MS B

2. Alipenda,wakati uliopita usiotimilifu -- MS א UBS4 inatoa njeo ya wakati timilifu “B" (karibu hakika).

◙ “akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu" Tazama maelezo katika 1 Yohana 2:2. 4:11 "ikiwa" Hii ni sentensi shurutishi daraja la kwanza ambayo inayochukuliwa kweli katika mtazamo wa mwandishi ama kwa makusudi ya fasihi. Mungu hutupenda sisi (kama vile Rum. 8:31)!

◙ "Mungu alitupenda sisi" Neno"hasa" inapaswa kueleweka kama “kwa namna ambayo," kama katika Yohana 3:16.

◙ "imetupasa na sisi kupendana" Kwa sababu ametupenda sisi ni lazima tupendane (kama vile 1 Yohana 2:10; 3:16; 4:7). Kauli ya asili inaakisi vitendo vinavyo sababisha kuvunja tabia ya walimu wa uongo. 4:12 "Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote" Hii ni kauli ya kati (shahidi wa maandishi) elekezi ya wakati timilifu. Neno hili lina maana ya “kutazama mtu au kitu kwa mda mrefu" (kama vile Kut. 33:20-23; Yohana 1:18; 5:37; 6:46; 1 Tim. 6:16). Inawezekana kwamba walimu wa mafunuo ya uongo, kwa maana Fulani walishawishiwa na dini za siri, mafumbo au miujiza ya mashariki, walidai kupata namna ya maono kutoka kwa Mungu au ya Mungu.Yesu alikuja kumfunua Baba kikamilifu. Tunapomtazama kwa Muda mrefu tunamjua Mungu!

◙ "Tuki" Hii ni sentensi yenye masharti daraja la tatu inayomaaniisha utendaji usiodhihirika.

◙ "Mungu hukaa ndani yetu" Tazama Mada Maalum: "Kukaa" katika 1 Yohana 2:10.

Page 401: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

385

◙ "na pendo lake limekamilika ndani yetu" Hii ni kauli tendewa endelevu ya wakati uliopita enye mafumbo. Wakristo wanaopendana ni ushuhuda wa upendo wa Mungu uliokamilishwa unaokaa ndani (kama vile Yohana 1. 2:5; 4:17).

4:13 "ametushirikisha Roho wake"Hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati timilifu. Roho mtakatifu akaaye ndani yetu (kama vile 1 Yohana 3:24; Rum. 8:9) na athari yake ya kubadilisha watu ni ushahidi wa kutosha wa wokovu wetu (kama vile Rum. 8:16). Inaonekana kwamba 1 Yohana 4:13 ndiye shahidi wa nafsi ya Roho, wakati 1 Yohana 4:14 ni shahidi wa kuhusu ushuhuda wa kitume. Wale watu watatu wa utatu wanaonekana wazi wazi 1 Yohana 4:13-14. Mada Maalum: Utatu katika 1 Yohana 2:10

4:14 "Na sisi tumeona na kushuhudia" vitenzi ni kauli timilifu ya kati (shahidi wa maandishi) elekezi ya wakati

timilifu iliyounganishwa pamoja na kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo. Inazungumzia ushuhuda wa Yohana wa

kuona kwa macho kuhusu ubinadamu wa Kristo, kama tu katika, 1:1-3.

Neno "kuona" ni neno la Kiyunani kama Yohana 1.4:12 linalomaanisha "kukodolea macho kwa mda mrefu kwa

umakini." Tazama Mada Maalum: USHUHUDA WA YESU katika Yohana 1:8

◙ "ya kuwa Baba amemtuma Mwana" Hii ni kauli timilifu tendaji elekezi. Ukweli kwamba Baba alimtuma Mungu Mwana ulimwenguni (kama vile Yohana 3:16) inakanusha mafundisho ya uongo ya watu wa wa mafunuo kuhusu uwili uliotarajiwa kati ya Roho (wema) na jambo (uovu). Yesu alikuwa kwa kweli wa Kiungu na alikuwa ametumwa katika ulimwengu wenye uovu wa dhambi kutukomboa na sisi (kama vile Warumi 8:18-25) kutoka kwenye laana ya Mwanzo 3 (kama vile Gal. 3:13).

◙ “kuwa Mwokozi wa ulimwengu" Ukweli kwamba Baba alichagua kumtumia Yesu kama njia ya wokovu inakanusha mafundisho ya uongo ya Mafunuo kwamba wokovu unapatikana kutokana na elimu ya siri inayohusika na viwango vya kimalaika. Waliviita viwango hivi vya ki-malaika eons au falme za mamlaka ya ki-malaika katikati ya Mungu wa Juu na Mungu mdogo zaidi ambaye aliunda ulimwengu kutokana na mataifa yaliyokuwepo kabla ya mtu kuwepo. Aya ya "Mwokozi wa ulimwengu" ilikuwa (1) cheo kwa miungu (yaani, Zeus) na (2) cheo cha kawaida kwa kaisari wa Kirumi. Kwa Wakristo Yesu pekee ndiye aliyeweza kuchukua vcheo hiki (kama vile Yohana 4:42; 1 Tim 2:4; 4:10). Hiki ndicho kilichosababisha hasa mateso yaliyofanyika na Makaisari wenyeji wa kule Asia Ndogo. Tambua kuwa yote yamejumuishwa. Yeye ndiye mwokozi wa wote (sio baadhi kama tu wataitikia (kama vile Yohana 1:12; 3:16; Rum. 5:18; 10:9-13).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) 1 YOHANA 4:15-21 15 Kila akiriye ya kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu hukaa ndani yake, naye ndani ya Mungu. 16 Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake. 17 Katika hili pendo limekamilishwa kwetu, ili tuwe na ujasiri katika siku ya hukumu; kwa kuwa, kama yeye alivyo, ndivyo tulivyo na sisi ulimwenguni humu. 18 Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo. 19 Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza. 20 Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona. 21 Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake.

4:15 "Kila akiriye ya kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu" Hii ni kauli tendajitegemezi ya wakati uliopo usiotimilifu.Kwa “kukiri” tazama maelzo katika 1 Yohana 4:2. Moja ya majaribu matatu ya Yohana ya Ukristo wa kweli ni kweli kitheolojia kuhusu mtu na kazi ya Yesu (kama vile 1 Yohana 2:22-23; 4:1-6; 5:1, 5). Hii pia ilifanana katika 1 Yohana na Yakobo pamoja na maisha ya upendo na utii. Ukristo ni mtu, mwili wa kweli, na maisha.Tazama Mtindo wa utambuzi, C.

Page 402: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

386

Pamoja na neno “yeyote” ni ukaribisho mkubwa wa Mungu kwa yoyote na kila mmoja kwenda kwake. Binadamu wote wamefanywa kwa sura ya Mungu (kama vile Mwa. 1:26-27; 5:3; 9:6). Mungu aliahidi ukombozi kwa jamii ya mwanadamu katika Mwa. 3:15. Wito wake kwa Ibrahimu ulikuwa ni wito wa kufikia ulimwengu (kama vile Mwa. 12:3; Kutoka 19:5). Kifo cha Yesu kiligawanya pamoja na matatizo ya dhambi (kama vile. Yohana 3:16). Kila mmoja anaweza kuokolewa kama wakiitikia kwenye wajibu Agano wa toba, imani, utii, huduma, na uvumilivu. Neno la Mungu kwa wote ni “njoo” (kama vile Isaya 55).

MADA MAALUM: MPANGO WA UKOMBOZI WA MILELE WA YHWH

Nalazimika kukubali kwako kiongozi kuwa ninao upendeleo juu ya hoja hii. Mpangilio wangu wa kithiolojia sio wa ufuasi wa Calvin au mfumo wa kidini, bali ni agizo kuu la kiunjilisti (kama vile Mt. 28:18-20; Luka 24:46-47; Mdo. 1:8). Naamini Mungu ana mpango wa milele kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu (mf., Mwa. 3:15; 12:3; Kut. 19:5-6; Yer. 31:31-34; Eze. 18; 36:22-39; Mdo. 2:23; 3:18; 4:28; 13:29; Rum. 3:9-18,19-20,21-31),wale wote walio umbwa kwa sura na ufanano wake (kama vile Mwa. 1:26-27). Maangano yote yameunganishwa katika Kristo (kama vile Gal. 3:28-29; Kol. 3:11). Yesu ni fumbo la Mungu, lilijificha ambalo halijafunuliwa (kama vile Efe. 2:11-3:13)! Injili ya Agano Jipya, sio Israeli, ni ufunguo wa maandiko.

Huu uelewa wangu wa kabla unanakshi tafasiri zangu zote za maandiko. Nasoma maandiko kwa kuyapitia yote! Hakika ni upendeleo (walionao watafsiri wote), lakini ni dhahanio za utaarifishwaji wa kimaandiko. Mtizamo wa Mwanzo 1-2 ni YHWH akiandaa mahali ambapo Yeye na Uumbaji wake ulio juu, mwanadamu, waweza kuwa na ushirika (kama vile Mwanzo. 1:26,27; 3:8). Uumbaji wake wa vitu ni hatua kwa ajili ya ajenda ya ki-Ungu kati ya watu wawili.

1. St. Augustine anaunganisha kama tundu lenye muonekano wa ki-Ungu katika kila mtu ambaye anaweza kujazwa tu na Mungu mwenyewe.

2. C.S. Lewis aliita sayari hii "sayari inayoshikika," (yaani., iliyoandaliwa na Mungu kwa ajili ya wanadamu). Agano la Kale lina vidokezo vingi vya ajenda hii ya ki-Ungu.

1. Mwanzo 3:15 ni ahadi ya kwanza kuwa YHWH hatamwacha mwanadamu katika hali tete ya dhambi na uasi. Hii hairejelei kwa Israel kwa sababu hapakuwepo na Israel, wala watu wa agano, mpaka pale Ibrahimu alipoitwa katika Mwanzo 12

2. Mwanzo 12:1-3 ni wito wa awali wa YHWH na ufunuo kwa Abraham ambao ndio ulikuja kuwa watu wa agano, Israel. Lakini hata katika huu wito wa awali, Mungu alikuwa anaangalia ulimwengu wote. Angalia Mwanzo 12:3!

3. Katika Kutoka 20 (Kumbu kumbu la Torati 5) YHWH alimpa Musa sheria ili kuwaongoza watu wake maalum. Tambua kuwa katika Kutoka 19:5-6, YHWH alidhihilisha kwa Musa uhusiano wa kipekee ambao Israel itakuwa nao. Lakini pia tambua kuwa wao walichaguliwa, kama Abraham, kuubariki ulimwengu (kama vile Kut. 19:5, “kwa vile vitu vyote vya Dunia ni mali yangu”). Israel ilipaswa kuwa chombo kwa mataifa kumjua YHWH na kuvutwa kwake. Kwa masikitiko makubwa wakashindwa (kama vile Eze. 36:22-38)

4. Katika 1 Wafalme 8 Sulemani aliliwakfisha hekalu ili wote waje kwa YHWH (kama vile 1 Fal. 8:43,60). 5. Katika Zaburi– 22:27-28; 66:4; 86:9 (Ufu. 15:4) 6. Kupitia kwa manabii wa YHWH kuendelea kudhihilisha mpango wake wa ukombozi kwa watu wote.

a. Isaya – 2:2-4; 12:4-5; 25:6-9; 42:6,10-12; 45:22; 49:5-6; 51:4-5; 56:6-8; 60:1-3; 66:18,23 b. Yeremia – 3:17; 4:2; 16:19 c. Mika 4:1-3 d. Malaki 1:11

Msisitizo huu wa wote umerahisishwa na uwepo wa “agano jipya” (kama vile Yer.31:31-34; Ezek. 36:22-38), ambao unaangazia juu ya huruma ya YHWH, na sio utendaji wa mwanadamu aliyeanguka. Kuna “moyo mpya,” “mawazo mapya,” na “roho mpya.” Utii ni kitu cha muhimu lakini ni cha ndani, na sio mfumo wa nje tu (kama vile Rum. 3:21-31).

Page 403: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

387

Agano Jipya linaimalisha mpango wa ukombozi wa wote kwa njia mbali mbali.

1. Agizo kuu – Mt. 28:18-20; Luka 24:46-47; Mdo. 1:8 2. Mpango wa Mungu wa milele (yaani., ulio amuliwa kabla) – Luka 22:22; Mdo. 2:23; 3:18; 4:28; 13:29 3. Mungu anawataka wanadamu wote waokolewe – Yohana 3:16; 4:42; Mdo. 10:34-35; 1 Tim. 2:4-6; Tit.

2:11; 2 Pet. 3:9; 1 Yn 2:2; 4:14 4. Kristo anaunganisha Agano la Kale na Agano Jipya – Gal. 3:28-29; Efe. 2:11-3:13; Kol. 3:11. Mipaka yote

na tofauti zote za mwanadamu zimeondolewa katika Kristo. Yesu ni “fumbo la Mungu,” lililofichika lakini sasa limedhihilishwa (Efe. 2:11-3:13).

Agano Jipya linaangazia juu ya Yesu, na sio Israel. Injili, sio utaifa wala eneo la kijiografia, ni kitu cha muhimu. Israel ilikuwa ndio ufunuo wa mwanzo lakini Yesu ni hatma ya ufunuo huo (kama vile Mt. 5:17-48).

Natumai utapata wasaa wa kusoma Mada Maalum: kwa nini ahadi za Agano la Kale zinaonekana kuwa tofauti toka ahadi za Agano Jipya. Waweza kupata katika mtandao www.freebiblecommentary.org.

◙ "Mungu hukaa ndani yake, naye ndani ya Mungu" Hii inaonyesha mfumo wa Agano la mahusiano kati ya Mungu pamoja na mwanadamu. Mungu wakati wote huchukua ari, anaweka ajenda na kupatia msingi kwa Agano, lakini binadamu anawajibu wa kujibu kwanza na kuendelea kujibu. Kuendelea kudumu ni hitaji la Agano, lakini pia ahadi ya ajabu (kam vile Yohana 15). Fikiria muumbaji wa ulimwengu, Roho mtakatifu wa Israeli, anakaa pamoja na (yenye kukaa moyoni) mwanadamu aliyeanguka (kama vile. Yohana 14:23)! Tazama Mada Maalumu: "kukaa" katika 1 Yohana 2:10 4:16 "Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini” vitenzi hivi vyote ni kauli timilifu tendaji elekezi. Tumaini la imani ya kujiamini ya waaminio kwa upendo wa Mungu katika Kristo, sio yenye kuhusu maisha na hali, ni msingi wa mahusiano yao. Tazama Mada Maalumu: Dhamana katika 1 Yohana 5:13 ◙ "alilo nalo Mungu kwetu sisi" Hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo inaelezea upendo unaoendelea wa Mungu. ◙ "Mungu ni upendo" Huu ukweli muhimu umerudiwa (kama vile 1 Yohana 4:8). 4:17 "Katika hili pendo limekamilishwa" Hii ni kutoka katika neno la kiyunani telos (kama vile 1 Yohana 4:12). Lina maanisha ukamilifu, ukomavu, na kukamilika, sio dhambi. ◙ "kwetu" kihusishi hiki (meta) kinaweza kueleweka kama “ndani yetu” (TEV, NJB), "miongoni mwetu" (NKJV, NRSV, NIV, REB), au "pamoja nasi" (NASB). ◙ "ili tuwe na ujasiri" Kwa asili hili neno linamaanisha uhuru wa kuongea. Yohana hutumi hili kwa kiasi fulani (kama vile 1 Yohana 2:28; 3:21; 5:14).Inazungumzia kwa ujasiri wetu katika kusogea/kukaribia Roho mtakatifu (kama vile. Waeb.3:6; 10:35).Tazama Mada Maalumu katika Yohana 7:4 ◙"katika siku ya hukumu; kwa kuwa, kama yeye alivyo, ndivyo tulivyo na sisi ulimwenguni humu" Wakristo wapende kama Yesu alivyopenda (kama vile 1 Yohana 3:16; 4:11).Wanaweza kukataliwa na kuteswa kama yeye alivyo, lakini pia wanapendwa na kuendelezwa na Baba na Roho kama yeye alivyo! Siku moja binadamu wote watafikiriwa na Mungu kwa zawadi ya maisha (kama vile. Mt. 25:31-46; 2 Kor. 5:10; Ufu. 20:11-15). Siku ya hukumu haikushika hofu kwa wale walio katika Kristo. 4:18 "Katika pendo hamna hofu" Pale tutakapo kuja kumjua Mungu kama Baba, hatuta muogopa tena kama Hakimu. Wengi, kama sio wote, mazungumzo Ya wakristo yanashirikisha hofu—hofu ya hukumu, ya lawama, ya

Page 404: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

388

Jehannamu. Hata hivyo, kitu cha ajabu hutokea katika maisha ya mwanadamu aliyeokolewa: kinachoanza na hofu uishiwa kusiko na hofu! ◙ "kwa maana hofu ina adhabu" Hili ni neno la nadra hutumia hapa pekee na Mt. 25:46 (mfumo wa kitenzi ni katika 2 Petr. 2:9), ambapo pia ni mpangilio wa tawi la theolojia linalojishughulisha na kifo, hukumu, pepo na Jehannamu. njeo ya kitenzi cha wakati uliopo kinamanisha kwamba hofu ya hasira ya Mungu ni vyote ya maisha (katika muda) na tawi linalojishughulisha na kifo, hukumu, pepo na jehanamu(katika mwisho wa wakati). Binadamu wamefanywa katika picha ya Mungu (kama vile Mwa. 1:26-27) ambayo inashirikisha vipengele vya nafsi, ujuzi, chaguo, na matokeo. Huu ni ulimwengu wa maadili. Binadamu hawavunji sheria za Mungu; wanajivunja wenyewe kwenye sheria za Mungu! 4:19 "Sisi twapenda" Hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo.NKJV inaongeza yambwa tenda baada ya “sisi twapenda.” Chaguo za miswada kwa yambwa tenda ni:

1. katika moja ya miswada ya Herufi kubwa za kiyunani (א) "Mungu" (ton theon) imewekwa 2. katika Ψ "Yeye" (auton) imewekwa (KJV) 3. katikatoleo la kilatini"kila mmoja" imewekwa

Hii yambwa tenda inaweza kuongewa baadaye. UBS4 imeipa kitenzi alama pekee ya "A" (hakika). ◙ "kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza” Kuna msisitizo uliorudiwa wa 1 Yohana 4:10. Mungu wakati wote huchukua uwezo wa kuanzisha (kama vile Yohana 6:44, 65) lakini mwanadamu aliyeanguka lazima kujibu (kama vile Yohana 1:12; 3:16).Waaminio wanaamini katika uaminifu wake na wana imani katika tumaini Lake. Upendo, kutenda, sifa ya imani ya Utatu wa Mungu ni tumaini na imani ya mwanadamu aliyekombolewa. 4:20 "Mtu akisema" Hii ni sentensi yenye masharti daraja la tatu ambayo inamaanisha kuwezekana kwa kitendo kutendeka. Huu ni mfano mwingine wa rejeo la kauli ya Yohana kwa walimu wa uongo ili kufanya uhakika (kama vile 1 Yohana 1:6,8,10; 2:4,6). Hii mbinu ya kifasihi inaitwa tahakiki ndefu yeye machungu, makemeo na matusi (kama vile. Malaki, Warumi, naYohana). ◙ "Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake" Maisha yetu ya upendo yamefunua wazi kama sisi ni Wakristo (kama vile Marko 12:28-34). Mgogoro inawezekana, lakini kukaa chuki sio (njeo ya wakati uliopo).Tazama MADA MAALUMU: Ubaguzi wa kimbari katika Yohana 4:4 ◙ "ni mwongo" Yohana aliwaita baadhi"waliodhaniwa" waaminio waongo (kama vile 1 Yohana 2:4,22; 4:20). Yohana pia alisema kwamba wale ambao wanahubiri ukweli wa uongo wanamfanya Mungu muongo (kama vile. 1 Yohana 1:6,10; 5:10). Hakika kuwa ni waumini binafsi wadanganyifu! 4:21 Aya hii Iinafupisha sura! Upendo sio wa kughushi/kuiga ushahidi kwa muamini wa kweli. Chuki ni ushahidi wa mtoto wa yule muovu. Walimu wa uongo waliwagawanya makusanyiko ya waumini na kusababisha mgogoro. ◙ "ndugu" Ni lazima kukubaliwa kwamba neno” ndugu” lina maana nyingi.Lina weza kumaanisha “mkristo wenzako” au “binadamu mwenzako.” Hata hivyo, Yohana ana matumizi ya mara kwa mara ya neno “ndugu” kwa waaminio inamanisha maana ya kwanza (kama vile 1 Tim 4:10).

MASWALI YA MJADALA

Huu ni mwongozo wa fasiri, ina maanisha kwamba unawajibika kwa tafsiri zako mwenyewe za Biblia. Kila mmoja wetu lazima atembee katika mwanga tulio nao. Wewe, Biblia, na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Hutakiwi uvitelekeze vitu hivi kwa mfasiri. Maswali ya mjadala huu yanatolewa kukusaidia kufikiri juu ya mambo makubwa ya sehemu za kitabu hiki. Yanalenga kukuamsha kimawazo na sio kutoa maana.

1. Orodhesha majaribio matatu makuu ya mkristo wa kweli.

Page 405: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

389

2. Ni jinsi gani mtu anajua anazungumza kweli kwa Mungu? 3. Orodhesha vyanzo viwili vya ukweli (ya kibinafsi na ya kikweli). 4. Ni nini muhimu kuhusu sifa “mwokozi wa ulimwengu”? 5. Orodhesha vitendo vinavyowafunua waongo (yaani, waaminio wa uongo).

Page 406: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

390

1 YOHANA 5

MIGAWANYO YA AYA YA TAFSIRI ZA KISASA

UBS4 NKJV NRSV TEV NJB Imani ni ushindi juu Utii kwa imani Imani yenye ushindi Ushindi wetu juu ya ya ulimwengu ulimwengu 4:20-5:5 5:1-5 5:1-5 5:1-5 Chanzo cha imani Ushuhuda kuhusu Uhakiki wa ushuhuda Ushuhuda kuhusu 5:5-13 Mwana wa Mungu Yesu Kristo 5:6-12 5:6-13 5:6-12 5:6-12 Maarifa ya uzima Hitimisho Uzima wa milele wa milele 5:13-15 Ujasiri na huruma 5:13 5:13-15 Maombi kwa katika maombi wenye dhambi 5:14-17 5:14-17 5:14-17 5:16-17 Kuijua kweli, 5:16-17 Muhtrasari wa kukataa uongo waraka 5:18-21 5:18-21 5:18-20 5:18 5:18-21 5:19 5:20 5:21 5:21

MZUNGUKO WA TATU WA USOMAJI KUFUATILIA KUSUDIO LA ASILI LA MWANDISHI KATIKA NGAZI YA AYA Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwatafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Aya ya kwanza 2. Aya ya pili 3. Aya ya tatu 4. N.k

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) 1 YOHANA 5:1-4 1 Kila mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na kila mtu ampendaye mwenye kuzaa, ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye. 2 Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake. 3 Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito. 4 Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.

5:1 "Kila mtu" (mara mbili) Neno pas limetumika kwa kurudiwa rudiwa katika 1 Yohana (kama vile 1 Yohana 2:29;3:3,4,6 [mara mbili] 9,10; 4:7; 5:1). Hakuna ambaye ameachwa kwenye thiolojia ya wazi ya Yohana. Huu ni

Page 407: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

391

mwaliko wa ulimwengu wote wa Mungu kumkubali Yesu Kristo (kama vile Yohana 1:12; 3:16; 1 Tim. 2:4; 2 Pet. 3:9). Unafanana na mwaliko mkuu wa Paulo katika Rum. 10:9-13.

◙ "aaminiye"Hii ni kauli tendaji endelevu ya wakati uliopo. Hili ni neno la Kiyunani (NOMINO - pistis; kitenzi - pisteuō) linaloweza kutafsiriwa kama "imani," "amini," au "sadiki." Hata hivyo katika 1 Yohana na nyaraka za kichungaji (1 & 2 Timotheo na Tito) mara nyingi zimetumika kwa maana ya maudhui ya kimafundisho (kama vile Yuda 1:3, 20). Kwenye injili na Paulo inatumika kwa imani binafsi na kujitoa, Injili ni vyote kweli ya kuamini na mtu kumtumaini, kama 1 Yohana na Yakobo wanaweka wazi, tuishi maisha ya upendo na huduma. Tazama Mada Maalum katika Yohana 2:23

◙ "kwamba Yesu ni Kristo" Kiini cha makosa ya walimu wa uongo kimejikita kwenye mtu na kazi ya mtu Yesu, ambaye pia alikuwa amejaa uungu (kama vile 1 Yohana 5:5). Yesu wa Nazareti ni yule masihi aliyeahidiwa! Masihi mwenyewe ni wakushangaza (yaani, kutoka Agano la Kale) pia ni wa kiungu. Aya hii ilikuwa kiapo, yumkini katika ubatizo (kama vile 1 Yohana 2:22), pamoja na aya iliyoongezwa "mwana wa Mungu" (kama vile 1 Yohana 4:15; 5:5). Kwa hakika uthibitisho huu wa umasihi wa Yesu unahusiana na watu wenye mazingira ya Agano la Kale (yaani, Wayahudi, wabadili dini na wenye kumhofu Mungu,).

◙ "amezaliwa na Mungu" Hii ni kauli timilifu tendewa elekezi inayosisitiza juu ya ukomo wa kitendo, kilichofanywa na mjumbe kutoka nje (Mungu, kama vile 1 Yohana 5:4,18; 2:29) kuwa kwenye hali ya kudumu ya mwanadamu.

NASB "hupenda mtoto aliyezaliwa naye" NKJV "ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye" NRSV "Hupenda wazazi hupenda watoto" TEV "humpenda Baba humpenda motto pia" NJB "humpenda Baba humpenda mwana" Aya hii yumkini inahusu Baba kumpenda Yesu kwa sababu matumizi ya (1) umoja; (2) njeo ya wakati uliopita usio timilifu; na (3) majaribio ya walimu wa uongo kithiolojia kumtenga Yesu kutoka kwa Baba yake. Hata hivyo ingeweza kuhusu mada inayorudiwarudiwa (kama vile 1 Yohana 5:2) kwasababu sisi sote tunaye Baba mmoja. 5:2 Aya hii pamoja na, 1 Yohana 5:3, inarudia moja ya mada za 1 Yohana. Upendo, wa Mungu unaoendelea (kama vile 1 Yohana 2:7-11; 4:7-21) na utii (kama vile 1 Yohana 2:3-6). Angalia ushuhuda wa mwamini wa kweli.

1. humpenda 2. humpenda mtoto wa Mungu (1 Yohana 5:1) 3. huwapenda watoto wa Mungu (1 Yohana 5:2) 4. utii (1 Yohana 5:2,3) 5. hushinda (1 Yohana 5:4-5)

5:3 "Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake" kimilikishi chaweza kuwa kishamirishi au kitegemezi ama mchanganyiko. Upendo sio hisia za moyoni bali unatokana na vitendo, kwa upande wa Mungu na wetu pia, utii ni lazima(kama vile 1 Yohana 2:3-4; 3:22,24; Yohana 14:15,21,23; 15:10; 2 Yohana 6; Ufu. 12:17; 14:12).

◙ "amri zake si nzito" Agano Jipya lina majukumu (kama vile Mt. 11:29-30, Pale Yesu anatumia neno "nira"; rabbi walilitumia katika sheria za Musa, Mt. 23:4). Zinamiminika toka kwenye uhusiano wetu na Mungu, lakini hazitengenezi msingi wa uhusiano huo, ambao umejengwa kwenye neema ya Mungu, sio kwenye utendaji wa binadamu au matendo mema (kama vile Efe. 2:8-9,10). Miongozo ya Yesu iko tofauti sana na walimu wa uongo, ambao aidha hawakuwa na sheria (tunakwenda kwa neema) ama sheria nyingi kupindukia (ushikaji mno wa sheria)! Lazima mkubali kwamba kwa jinsi ninavyomtumikia Mungu kwa muda mrefu kwa kuwatumikia watu

Page 408: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

392

wake nazidi kuogopa mambo mawili yaliyovuka mpaka ya uhuru wa kupindukia na ushikaji mno wa sheria kupindukia. Tazama Mada Maalum: Matumizi ya "Amri" katika maandiko ya Yohana katika Yohana 12:50 5:4 NASB, NKJV, NRSV "kila kitu kilichozaliwa na Mungu" TEV, NJB "kwasababu kila mtoto wa Mungu"

Maandishi ya Kiyunani yanaweka neno "yote" (pas) mwanzo kwa msisitizo kama katika 1 Yohana 5:1. Umoja tasa (pan) umetumika ambao umetafsiriwa “chochote kile.” Kwa hali yoyote muktadha unahitaji kidokezo binafsi (yaani, dhana ya kundi zima) kwa sababu imeunganika na kauli timilifu tendewa endelevu ya "aliyezaliwa." Anayeushinda ulimwengu (kama vile 1 Yohana 4:4; 2:13,14).

◙ "huushinda ulimwengu" "Washindi" ni kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo ya neno nikaō (kama vile 1 Yohana 2:13,14; 4:4; 5:4,5). Mzizi uleule umetumika mara mbili katika 1 Yohana 5:4.

1. nomino, "ushindi," nikē 2. kauli tendaji endelevu ya wakati uliopita usio timilifu, nikaō, "amekwisha kushinda"

Yesu tayari amekwisha kushinda ulimwengu (kauli timilifu tendaji elekezi, Kama vile Yohana 16:33). Kwasababu waamini wanakaa katika ushirika pamoja naye, wao pia wana nguvu ya kushinda ulimwengu (kama vile 1 Yohana 2:13-14; 4:4). Neno "ulimwengu" hapa linamaanisha" jamii ya wanadamu iliyojiongoza na inafanya shughuli kinyume na Mungu." Tabia ya uhuru ndiyo msingi wa Anguko na uasi wa Mwanadamu (kama vile Mwanzo 3). Tazama Mada Maalum katika Yohana 14:17 ◙ "kushinda" Hii ni nomino kutoka (nikos) ya kitenzi "amekwisha kushinda." Mwishoni mwa 1 Yohana 5:4 wakati tendaji endelevu wa neno lenye mzizi uleule limetumika. Kisha tena katika 1 Yohana 5:5 wakati endelevu mwingine wa neno nikos umetumika. Waamini ni washindi na wanaendelea kuwa washindi katika Kristo nakupitia ushindi wa ulimwengu. Neno "nike," linalopendwa sana kama mtengeneza viatu vya, tenis, ndilo jina la Kiyunani la ushindi.

◙ "imani yetu" Hili ndilo tumizi la pekee la muundo wa nomino ya neno "imani" (pistis) katika mandishi yote ya Yohana! yawezekana Yohana alikuwa na hofu kuhusu msisitizo uliopitiliza kuhusu "theolojia sahihi" (kama mfumo wa imani nyingi) dhidi ya kufanana na Kristo.

1. imeunganishwa na ushindi wa Yesu 2. imeunganishwa na uhusiano wetu mpya 3. imeunganishwa kwenye nguvu ya Roho Mtakatifu aliye ndani yetu

Tazama Mada Maalum katika Yohana 1:7; 2:23 na 1 Yohana 2:10

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) 1 YOHANA 5:5-12 5 Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu? 6 Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo; si katika maji tu, bali katika maji na katika damu. 7 Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli. 8 Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja. 9 Kisha wako watatu washuhudiao duniani], Roho, na maji, na damu; na watatu hawa hupatana kwa habari moja. Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, kwamba amemshuhudia Mwanawe. 10 Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe. 11 Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe.12 Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana

Page 409: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

393

huo uzima.

5:5 "Yesu ni Mwana wa Mungu" Aya hii inaeleza waziwazi maudhui ya imani yetu, ambayo inaelezwa katika 1 Yohana 5:4. Ushindi wetu ni ungamo/kukiri kwetu kwa imani yetu katika Yesu, ambaye ni yote mawili. Mwanadamu kamili na Mungu kamili (kama vile 1 Yohana 4:1-6). Angalia kwamba waamini wanatamka kwamba Yesu ni (1) Masihi (1 Yohana 5:1); (2) mtoto wa Mungu (1 Yohana 5:1); (3) Mwana wa Mungu (1 Yohana 5:5,10); na (4) Uzima (kama vile 1 Yohana 1:2; 5:20). Tazama Mada Maalum katika Yohana 2:23, anatumia Kuamini ambavyo vinaorodhesha VISHAZI vyote vya nenovikiunganikana kwenye KITENZI “kuamini.”

◙ "Mwana wa Mungu" Tazama Mada Maalum katika 1 Yohana 3:8

5:6 "Huyu ndiye aliyekuja" Hii ni kauli tendaji edelevu ya wakati uliopita usio timilifu unaosisitiza Yesu kufanyika mwili (Yesu kama mwanadamu na Mungu) na kifo chake cha kujitoa sadaka, mambo yote mawili ambayo walimu wa uongo waliyakataa.

◙ "kwa maji na damu" Inaonekana kwamba neno "maji" linahusika na kuzaliwa kimwili kwa Yesu (kama vile Yohana 3:1-9) na "damu" linahusu kifo cha kimwili. Katika muktadha wa walimu wa uongo wa kukataa ukweli wa ubinadamu wa Yesu, uzoefu huu wa aina mbili unafanya kwa ufupi na kufunua ubinadamu wake. Chaguo jingine linalohusu waalimu wenye mafunuo ya uongo (Cerinthus) ni kwamba "maji" inahusu ubatizo wa Yesu. Wanatangaza kwamba "Roho ya Kristo" ilikuja juu ya mtu Yesu katika ubatizo (maji) na ikaondoka kabla mtu Yesu hajafa pale msalabani (damu, tazama ufupisho mzuri katika NASB, Biblia ya kujifunzia, ukr. 1835). Chaguo la tatu ni kuhusisha kirai husika na kifo cha Yesu. Mkuki ulisababisha "damu na maji" (kama vile Yohana 19:34) kumwagika. Waalimu wa uongo, yawezekana walidhalilisha kifo cha Yesu kilichotokea badala ya wengine.

◙ "Roho ndiye ashuhudiaye" Jukumu la Roho mtakatifu ni kufunua Injili. Yeye ni sehemu ya utatu ambaye

anahukumu kuhusu dhambi, huongoza kuelekea kwa Kristo, hubatiza katika Kristo, na kumuumba Kristo ndani ya aaminiye (kama vile Yohana 16:7-15). Wakati wote hushuhudia juu ya Kristo, na sio kazi yake mwenyewe (kama vile Yohana 15:26).

◙ "Roho ndiye kweli" (kama vile Yohana 14:17; 15:26; 16:13; 1 Yohana 4:6). Tazama Mada Maalum katika

Yohana 6:55 na Yohana 17:3

5:7 Kuna mpangilio kiasi Fulani kwenye tafsiri za kiingereza kama 1 Yohana 5:6,7, na 8 zinaanzia wapi na kuishia wapi. Sehemu ya 1 Yohana 5:7 inapatikana katika KJV isemayo "mbinguni, Baba, Neno na Roho mtakatifu, na hawa watatu ni mmoja," haipatikani katika machapisho madogo sana mane yaliyopita katika Agano Jipya: Alexandrinus (A), Vaticanus (B), au Sinaiticus (א), wala katika Byzantine family of manuscripts. Inaonekana tu katika machapisho madogo.

1. MS 61, iliwekewa tarehe katika karne ya 16 2. MS 88 iliyowekewa tarehe katika karne ya 12, ambapo aya iliingizwa kwenye nafasi ya pembeni mwa

mwandishi kwa mkono mwingine 3. MS 629, iliyowekewa tarehe katika karne ya 14 au 15 4. MS 635, iliwekewa tarehe katika karne 11, ambapo aya iliingizwa na mkono mwingine

Aya hii inanukuliwa na yeyote kati ya mababa wa kanisa la kwanza hata kwenye midahalo yao ya kidini kuhusu utatu. Haipo kwenye matoleo yote ya kale isipokuwa chapisho moja la familia moja ya kilatini cha zamani Sixto-Clementine). Inaonekana mara ya kwanza kwenye makala yenye kuhusu msds moja, ilinukuliwa na mapadre wa Kilatini wa Afrika ya kaskazini na Italia kwenye karne ya tano 1 Yohana. Fundisho la Biblia la Mungu mmoja (monotheism) lakini na uthibitisho wa watu watatu (Baba, Mwana,na Roho) haiathiliwi na kule kuikataa aya hii. Ingawa ni kweli kwamba Biblia kamwe haitumii neno "utatu," aya nyingi za kibiblia zinazungumzia wote watatu wa Mungu wakitenda kazi pamoja:

Page 410: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

394

1. ubatizo wa Yesu (Mt. 3:16-17) 2. Agizo Kuu (Mt. 28:19) 3. Roho hutumwa (Yohana 14:26) 4. Hotuba ya Petro siku ya Pentekoste (Matendo 2:33-34) 5. Mjadala wa Paulo wa mwili wa Roho (Rum. 8:7-10) 6. Mjadala wa Paulo wa vipawa vya kiroho (1 Kor. 12:4-6) 7. Mipango ya Paulo ya kusafiri (2 Kor. 1:21-22) 8. Dua ya Paulo (2 Kor. 13:14) 9. Mjadala wa Paulo wa utimilifu wa wakati (Gal. 4:4-6) 10. Maombi ya Paulo ya Sifa kwa Baba (Efe. 1:3-14) 11. Mjadala wa Paulo kwa tabia ya awali ya mataifa ya kuwafanya watu kuwa wakali (Efe. 2:18) 12. Mjadala wa Paulo kuhusu umoja wa Mungu (Efe. 4:4-6) 13. Mjadala wa Paulo wa wema wa Mungu (Tito 3:4-6) 14. Utangulizi wa Petro (1 Pet. 1:2)

Tazama Mada Maalum: Utatu katika Yohana 14:26 5:8 "Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja" Katika Agano la Kale mashahidi wawili au watatu walihitajika kuthibitisha jambo (kama vile kumb 17:6; 19:15). Hapa matukio ya kihistoria ya maisha ya Yesu yanatolewa kama ushahidi kwa ukamilifu wa ubinadamu na uungu wake kwenye aya hii, "maji"na"damu" vimetamkwa tena pamoja na “Roho”neno "maji" na "damu" vimetamkwa katika 1 Yohana 5:6. "Roho" yaweza kuhusu ubatizo wa Yesu kwa sababu ya njiwa kushuka. Kuna kiasi fulani cha kutokukubaliana kuhusu kidokezi hasa cha kihistoria aya lazima yahusu waalimu wa uongo kuukataa ukweli wa ubinadamu wa Yesu. 5:9 "Tuki…" Hii ni sentensi shurutishi daraja la kwanza ambayo imechukuliwa kuwa kweli kutokana na mtazamo wa mwandishi ama kwa maksudi yake kiuandishi. Makanisa ambayo Yohana alikuwa anawaandikia yalikuwa yamechanganyikiwa kwasababu inaonekana walikuwa wamesikia mahubiri au mafundisho ya walimu wa uongo.

◙ "Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi" Ushuhuda huu wa kiungu kimuktadha unahusu,

1. Ushuhuda wa Roho mtakatifu 2. Ushuhuda wa mitume kuhusu maisha ya Yesu na kifo chake (mf, 1:1-3)

◙ "kwamba amemshuhudia Mwanawe" Hii ni kauli timilifu tendaji elekezi ikionyesha kitendo cha wakati uliopita ambacho kimefikia kwenye hali ya ukomo na kinaendelea kudumu. Hii inaweza kuwa inahusu uthibitisho wa Mungu aliotamka kwenye ubatizo wa Yesu (kama vile Mt. 3:17) au wakati wa kubadilika kwake sura (kama vile Mt. 17:5;) au kuyaweka katika kumbukumbu Yote mawili kwenye maandiko 5:32,37; 8:18) (yaani, injili). Tazama Mada Maalum: MASHUHUDA WA YESU katika Yohana 1:8 5:10 "anao huo ushuhuda ndani yake" Inawezekana kutafsiri aya hii katika njia mbili.

1. Ushuhuda wa ndani wa ndani ya waaminio unaovumishwa na Roho (kama vile. Rum. 8:16) 2. Ukweli wa injili (kama vile Ufu. 6:10; 12:17; 19:10)

Tazama Mada Maalum: MASHUHUDA WA YESU katika Yohana 1:8

◙ "amemfanya kuwa mwongo" Hii ni kauli timilifu tendaji elekezi nyingine. Wale ambao wanaukataa ushuhuda wa mitume kuhusu Yesu wanamkataa Mungu (kama vile 1 Yohana 5:12) kwa sababu wanamfanya Mungu kuwa muongo.

◙ "kwa kuwa hakuuamini" Hii ni kauli timilifu tendaji elekezi nyingine ambayo inasisitiza hali ambayo haijafanywa upya.

Page 411: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

395

5:11-12 "ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele" Hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati uliopita usiotimilifu unaoongelea kitendo kilichofanyika wakati uliopita ama kitendo kilichokamilika (kama vile Yohana 3:16). Uzima wa milele unaelezwa katika Yohana 17:3. Katika hali fulani aya inahusu Yesu mwenyewe (kama vile 1 Yohana 1:2; 5:20), na katika hali nyingine ni kipawa kutoka kwa Mungu (kama vile 1 Yohana 2:25; 5:11; Yohana 10:28), kinachopokelewa kupitia imani katika Kristo (kama vile 1 Yohana 5:13; Yohana 3:16). Mtu hawezi kuwa na ushirika na Baba bila kuwa na imani katika mwana!

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) 1 YOHANA 5:13-15 13 Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu. 14 Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. 15 Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.

5:13 "mnaoliamini Jina" Hii ni kauli tendaji endelevu ya wakati uliopita, ambao unasisitiza imani inayoendelea. Huu sio utmiaji wa kimiujiza wa jina (kama mafumbo ya Kiyahudi yaliyosimikwa kwenye majina ya Mungu, Kabbalah), bali matumizi ya jina kama mbadala kwa mtu mwenyewe. Tazama Mada Maalum katika Yohana 2:23

◙ "ili mjue ya kuwa" Hii ni kauli timilifu tendaji tegemezi (oida ni wakati timilifu katika muundo, lakini limetafasiliwa kwenye wakati uliopoT). Hakika ya wokovu wa mtu ni ufunguo mkuu, na mara nyingi kusudi linalotamkwa katika 1 Yohana. Kuna visawe viwili vya Kiyunani (oida na ginōskō) vilivyotumika wakati wote kwenye nyaraka/na mahubiri ambazo zinatafsiri "kujua." Ni hakika kwamba kwa sababu ya hali ya mahali wakati huo na maudhui ya kiutamaduni sasa kwamba wapo waaminio wa kweli ambao hawana hakika. Aya hii kithiolojia inafanana na injili ya Yohana inavyomalizia (kama vile 1 Yohana 20:31). Maudhui yanayofunga injili ya 1 Yohana (5:13-20) yanaorodhesha mambo saba ambayo waaminio wanayajua. Kujua kwao injili kunaleta mtazamo wa ulimwengu ambao ukiunganishwa na imani binafsi ya mtu katika Yesu, ni kweli za msingi za uhakika.

1. Waaminio wanao uzima wa milele (1 Yohana 5:13, oida, wakati timilifu tendaji tegemezi) 2. Mungu husikia maombi ya waaminio (1 Yohana 5:15, oida, wakati timilifu tendaji elekezi) 3. Mungu hujibu maombi ya waaminio (1 Yohana 5:14, oida, wakati timilifu tendaji elekezi) 4. Waaminio wamezaliwa na Mungu (1 Yohana 5:18, oida, wakati timilifu tendaji elekezi) 5. waaminio ni wa (watoka kwa) Mungu (1 Yohana 5:19, oida, wakati timilifu tendaji elekezi) 6. waaminio wanajua masihi amekuja na kuwapa kuelewa (1 Yohana 5:20, oida, wakati timilifu tendaji

elekezi) 7. waaminio wanamjua aliye wa kweli –Baba au Mwana (1 Yohana 5:20, ginōskō, kauli tendaji tegemezi ya

wakati uliopo)

MADA MAALUMU: DHAMANA YA MKRISTO

A. Je! Wakristo wanaweza kutambua kwamba wameokolewa (kama vile 1 Yohana 5:13)? Yohana ana majaribio matatu au ushahidi. 1. Kimafundisho (imani, 1 Yohana 1:1,5,10; 2:18-25; 4:1-6,14-16; 5:11-12) 2. Mtindo wa maisha (utii, 1 Yohana 2:2-3; 2:3-6; 3:1-10; 5:18) 3. Kijamii (upendo, 1 Yohana 1:2-3; 2:7-11; 3:11-18; 4:7-12, 16-21)

B. Dhamana imekuwa ni suala la kimadhehebu 1. John Calvin alijikita katika uchaguzi wa Mungu. Amesema kuwa katika maisha haya kamwe

hatuwezi kuwa na uhakika. 2. John Wesley aliegemea juu ya dhamana ya uzoefu wa kidini. Aliamini kuwa tunao uwezo wa kuishi

juu ya dhambi inayofahamika. 3. Waamini wa Kanisa Katoriki na Kanisa la Kristo wanaegemea juu ya Kanisa la kimamlaka. Kundi

Page 412: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

396

alilomo mtu huyu ni jawabu la neno dhamana. 4. Walokole wengi wameweka dhamana zao juu ya ahadi za Biblia, zilizoungamanishwa na tunda la

Roho (kama vile Gal. 5:22-23) katika maisha ya mwamini (yaani, ufanano na Kristo wa kila siku). C. Dhamana ya awali ya waaminio imeungamanishwa na sifa za Mungu wa Utatu

1. Upendo wa Mungu Baba a. Yohana 3:16; 10:28-29 b. Warumi 8:31-39 c. Waefeso 2:5,8-9 d. Wafilipi 1:6 e. 1 Petro 1:3-5 f. 1 Yohana 4:7-21

2. Matendo ya Mungu mwana a. kifo badala yetu

1) Matendo 2:23 2) Warumi 5:6-11 3) Wakorintho 5:21 4) 1 Yohana 2:2; 4:9-10

b. maombi ya kuhani mkuu (Yohana 17:12) c. maombi endelevu ya kusihi

1) Warumi 8:34 2) Waebrania 7:25 3) 1 Yohana 2:1

3. Huduma ya Roho wa Mungu a. wito (Yohana 6:44,65) b. kutia mhuri

1) 2 Wakorintho 1:22; 5:5 2) Waefeso 1:13-14; 4:3

c. hakikisha 1) Warumi 8:16-17 2) 1 Yohana 5:7-13

D. Lakini wanadamu yawapasa kukubali kujitolea kwa Mungu kupiitia agano lake (katika nafasi zote, ya awali na ile endelevu) 1. waamini yawapasa kugeuka kutoka dhambini (toba) na kumwelekea Mungu kupitia Yesu (imani)

a. Marko 1:15 b. Matendo 3:16,19; 20:21

2. waamini yawapasa kukupokea kujitolea kwa Mungu katika Kristo (tazama Mada Maalumu: Je! Kunamaanisha nini "kupokea," "Kuamini," "Kukiri/Kuungama," "Kusihi" a. Yohana 1:12; 3:16 b. Warumi 5:1 (na kwa mfanano 10:9-13) c. Waefeso 2:5,8-9

3. waamini yawapasa kuendelea katika imani (tazama Mada Maalumu: Ustahimilivu) a. Marko 13:13 b. 1 Wakorintho 15:2 c. Wagalatia 6:9 d. Waebrania 3:14 e. 2 Petro 1:10 f. Yuda 20-21 g. Ufunuo 2:2-3,7,10,17,19,25-26; 3:5,10,11,21

E. Dhamana ni ngumu kwa sababu 1. mara kwa mara waamini hutafuta uzoefu fulani ambao haukuhaidiwa katika Biblia

Page 413: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

397

2. mara kwa mara waamini hawaielewi injili kwa ukamilifu 3. mara kwa mara waamini wanaendelea na dhambi kwa makusudi (kama vile Kor. 3:10-15; 9:27; 1

Tim. 1:19-20; 2 Tim. 4:10; 2 Pet. 1:8-11) 4. aina ya mtu fulani (yaani, mtu aaminiye katika kushinda) asiyeweza kamwe kukubali upendo na

ukubalifu usio na masharti wa Mungu 5. katika Biblia kuna mifano ya maungamo ya uongo (kama vile Mat. 13:3-23; 7:21-23; Marko 4:14-20;

2 Pet. 2:19-20; 1 Yohana 2:18-19, tazama Mada Maalumu: Ukanaji wa Imani) Tazama Mada Maalumu: Dhamana ya Mkristo kwa maelezo ya mihtasari tofauti tofauti ya mafundisho haya.

5:14 "ujasiri tulio nao kwake" Hii ni dhamira inayorudiwa rudiwa (kama vile 1 Yohana 2:28; 3:21; 4:17). Inaelezea ujasiri au uhuru tulionao katika kumwendea Mungu (kama vile. Ebr. 4:16). Tazama Mada Maalum katika Yohana 7:4

◙ "kama…" Hii ni sentensi yenye masharti daraja la tatu Inayomaanisha utendaji usiodhihilika.

◙ "tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake" Maelezo ya Yohana yanaonekana kuwa na kikomo katika uwezo wa aaminiye wa kweli. Kwa vyovyote vile katika kuchunguza zaidi, tunatambua kwamba maombi sio kuomba kwa mapenzi yetu, bali kwamba mapenzi ya Mungu katika maisha yetu (kama vile 1 Yohana 3:22; Mt. 6:10; Marko 14:36). Tazama maelezo ya kina 1 Yohana 3:22. Tazama Mada Maalum: Mapenzi ya Mungu angalia Yohana 4:34. Angalia MADA MAALUM: Maombi yasiyo na ukomo, lakini yenye Ukomo katika 1 Yohana 3:22

MADA MAALUMU: MAOMBI YA KUSIHI

I. Utangulizi A. Maombi ni ya muhimu kwa sababu ya mfano wa Yesu

1. Maombi binafsi, Mk 1:35; Luka 3:21; 6:12; 9:29; 22:31-46 2. Kulisafisha Hekalu, Mt. 21:13; Mk 11:17; Luka 19:46 3. Maombi ya kuiga, Mt. 6:5-13; Luka 11:2-4

B. Maombi yanaweka kuamini kwetu kwenye hali ya kugusika kwa mtu, Mungu anayejali ambaye yupo , anayependa na kutenda kwa niaba yetu na kwa ajili ya wengine, kupitia maombi yetu.

C. Mungu binafsi amejizuia mwenyewe kutenda juu ya maombi ya watoto wake katika Nyanja nyingi (kama vile. Yakobo 4:2)

D. Kusudi kuu la maombi ni ushirika na muda wetu kwa Mngu wa Utatu. E. Nafasi ya maombi ni mtu yeyote au kitu chochote kinachohusiana na waumini. Tunaweza

kuomba,kuamini mara moja, au zaidi na zaidi tena kama fikra zinavyojirudia. F. Maombi yanaweza kuhusisha ishara/dalili mbali mbali

1. Sifa na kuabudu kwa Mungu wa Utatu 2. Shukrani kwa Mungu kwa ajili ya uwepo wake, ushirika, na upaji wake 3. Ukiri wetu wa utendaji dhambi, kwa hali zote za siku zilizopita na wakati sasa 4. Ombi la mahitaji yetu muhimu au hamu yetu 5. Usihi wetu pale tunapoyawasilisha mahitaji ya wengine mbele za Baba

G. Ombi la kusihi ni la ajabu. Mungu anawapenda wale tuwaombeao zaidi kuliko tufanyavyo, na bado maombi yetu yasifanye badiliko, uajibikaji, au hitaji lolote, sio tu kwetu binafsi, lakini hata kwao.

II. Taarifa za Kibiblia

A. Agano la Kale 1. Baadhi ya mifano ya maombi ya kusihi

a. Ibrahim aliomba maombi ya kuitetea Sodoma, Mwa. 18:22ff b. Maombi ya Musa kwa ajili ya Israel

Page 414: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

398

1) Kutoka 5:22-23 2) Kutoka 32:9-14,31-35 3) Kutoka 33:12-16 4) Kutoka 34:9 5) Kumbu. 9:18,25-29

c. Samweli akiiombea Israel 1) 1 Samweli 7:5-6,8-9 2) 1 Samweli 12:16-23 3) 1 Samweli 15:11

d. Maombi ya Daudi kwa ajili ya watoto wake, 2 Samweli 12:16-18 2. Mungu anawatafuta waombeaji, Isaya 59:16 3. Dhambi ijulikanayo, usio ikiri, tabia usizozitubia zinaathiri maombi yetu

a. Zaburi 66:18 b. Mithali 28:9 c. Isaya 59:1-2; 64:7

B. Agano Jipya 1. Huduma ya kusihi/kuombea ya Mwana na Roho

a. Yesu 1) Warumi 8:34 2) Waebrania 7:25 3) 1 Yohana 2:1

b. Roho Mtakatifu, Warumi 8:26-27 2. Huduma ya Paulo ya kuombea kwa kusihi

a. Akiomba kwa ajili ya Wayahudi 1) Warumi 9:1ff 2) Warumi 10:1

b. Akiliombea kanisa 1) Warumi 1:9 2) Waefeso 1:16 3) Wafilipi 1:3-4,9 4) Wakolosai 1:3,9 5) 1 Wathesolanike 1:2-3 6) 2 Wathesolanike 1:11 7) 2 Timotheo 1:3 8) Filemon, uk. 4

c. Paulo analiomba kanisa limwombee 1) Warumi 15:30 2) 2 Wakorinthp 1:11 3) Waefeso 6:19 4) Wakolosai 4:3 5) 1 Wathesolanike 5:25 6) 2 Wathesolanike 3:1

3. Huduma ya kanisa ya maombi ya kusihi a. Kuombeana wao kwa wao

1) Waefeso 6:18 2) 1 Timotheo 2:1 3) Yakobo 5:16

b. Maombi yaliyohitajiwa na makundi maalumu 1) Adui zetu, Mat. 5:44 2) Wakristo watembeaji, Waebrania 13:18

Page 415: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

399

3) Watawala, 1 Timotheo 2:2 4) wagonjwa, Yakobo 5:13-16 5) waliorudi nyuma, 1 Yohana 5:16

III. masharti kwa ajili ya maombi yaliyotakiwa kujibiwa

A. Mahusiano yetu kwa Yesu na Roho 1. Kutii ndani yake, Yohana 15:7 2. Katika jina lake , Yohana 14:13,14; 15:16; 16:23-24 3. Katika Roho, Waefeso 6:18; Jude 20 4. Kwa kadri ya mapenzi ya Mungu, Mathayo 6:10; 1 Yohana 3:22; 5:14-15

B. Visababishi 1. Kutotetereka, Mathayo 21:22; Yakobo 1:6-7 2. Unyenyekevu na toba, Luka 18:9-14 3. Kuomba vibaya, Yakobo 4:3 4. Ubinafsi , Yakobo 4:2-3

C. Mitazamo mingine a. Usitahimilivu b. Luka 18:1-8 c. Wakolosai 4:2

1. Endelea kuomba a. Mathayo 7:7-8 b. Luka 11:5-13 c. Yakobo 1:5

2. Kutoelewana nyumbani, 1 Petro 3:7 3. Kuwa huru kutoka katika dhambi zijulikanazo

a. Zaburi 66:18 b. Mithali 28:9 c. Isaya 59:1-2 d. Isaya 64:7

IV. Hitimisho la kithiolojia

A. Ni faida ipi, fursa ipi, shughuli na uwajibikaji upi B. Yesu ni mfano wetu. Roho ni mwongozo wetu. Baba anasubiri kwa hamu. C. Inaweza kukubadilisha wewe, familia yako, rafiki zako na hata dunia

5:15 "kama" Hii ni sentensi shurutishi daraja la kwanza (lakini ina with ean na chenye kuelekeza, tazama A. T. Robertson, Word Pictures in the New Testament, uk. 243) ambayo imechukuliwa kuwa kweli kutokana na mtazamo ama makusudi yake ya kifasihi. Hii ni sentensi isiyo ya kawaida yenye mashariti.

1. Ina has ean badala ya ei (kama vile Matendo 8:31; 1 The. 3:8) 2. Ina ean kikiunganishwa kwenye utegemezi (yaani, omba), ambayo ni uundaji wa kawaida wa sarufi kwa

sentensi yenye masharti daraja la tatu 3. zipo sentensi zenye masharti daraja la tatu katika 1 Yohana 5:14 na 16 4. Thiolojia ya maombi ya Mkristo yameunganishwa na Mapenzi ya Mungu (1 Yohana 5:14) na jina la Yesu (1

Yohana 5:13)

◙ "tukijua" Hii ni kauli timilifu tendaji elekezi ya wakati uliopo, iliyosambamba na 1 Yohana 5:14. Ni hakika ya aaminiye kwamba Mungu husikia na Kuitikia wito wa watoto wake.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) 1 YOHANA 5:16-17

Page 416: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

400

16 Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, ataomba, na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo ya mauti. Iko dhambi iliyo ya mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hiyo. 17 Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti.

5:16 "ikiwa" Hii ni kauli enye masharti daraja la tatu ambayo ina maanisha utendaji usiodhihirika. 1 Yohana 5:16 inasisitiza hitaji letu la kuwaombea Wakristo wenzetu (kama vile Gal. 6:1; Yakobo 5:13-18) ndani ya viwango vilivyopendekezwa (sio kwa dhambi ya mauti) inayoonekana kuhusiana na walimu wa uongo (kama vile 2 Petro 2) ◙ “akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti” Yohana ameorodhesha makundi kadhaa ya dhambi. Baadhi zinahusu (1) ushirika wa mtu na Mungu; (2) ushirika pamoja na waminio wengine; na (3) ushirika na ulimwengu. Dhambi ya mwisho ni kukataa tumani/imani/kuamini katika Yesu Kristo. Hii ndiyo dhambi inakuelekeza kwenye mauti ya milele! W. T. Conners katika Christian Doctrine, anasema “Hii haimaanishi kwa vyovyote, kutokuamini katika mtazamo wa kukataa kukubali fundisho au imani kali. Ni kutokuamini kukataa kwa mtu kuwa mwadilifu na nuru ya kiroho,hasa kwa kuwa nuru imefafanuliwa katika Yesu Kristo. Ni kukataa ufunuo wa mwisho wa nafsi yake kama ulivyofanywa ndani ya kristo. Wakati kukataa huku kunapokuwa dhahiri na kwa kukusudiwa inakuwa dhambi ya mauti (1 Yohana 5:13-17). Hivyo inakua kujiua kinafsi. Ni mtu mwenye kutoa macho yake ya kiroho. Haitokei mpaka pale inapounganishwa na kiwango kikubwa zaidi cha kutiwa nuru. Ni kumkataa Yesu kama ufunuo wa Mungu,, kwa kusudio la uovu huku ukijua kwamba yeye ni ufunuo kiasi hicho. Ni mwito wa makusudi wa wazi’’ (uk. 135-136).

MADA MAALUMU: DHAMBI HADI MAUTI (1 Yohana) Uzingatiaji wa kanuni za ufasiri

1. Utambulisho sahihi unapaswa kuhusishwa na kuiweka vizuri kihistoria ya 1 Yohana a. uwepo wa mafunuo ya walimu wa uongo (angalia Mada Maalum:Mafunuo) katika makanisa

(kama vile 1 Yohana 2:19,26; 3:7; 2 Yohana 7; (angalia Mada Maalum:Mafunuo) 1) “Cerinthian.” Watu wa mafunuo walifundisha kwamba Yesu aliyekuwa mwanadamu

alipokea roho wa Kristo katika ubatizo wake na kwamba roho ya Kristo iliondoka kabla ya kifo chake pale msalabani (kama vile 1 Yohana 5:6-8)

2) “Docetic.” Watu wa mafunuo walifundisha kuwa Yesu alikuwa ni Roho wa Kiungu, na wala si Mwanadamu kamili halisi (kama vile 1 Yohana 1:1-3)

3) Mafunuo yanadhihilisha kuwa katika maandiko ya karne ya pili yaliangazia kuhusu maoni ya aina mbili tofauti kuhusu mwili wa binadamu a) kwa vie wokovu ulikuwa ni ukweli uliobainishwa katika fikra mwili wa mtu haukuwa na

maana katika ulimwengu wa kiroho. Kwahiyo, chochote ungetaka kingekuwa. Haya daima huitwa mafunuo kwa njia ya neema au mafunuo huru.

b) kundi lingine lilihitimisha kuwa kwa vile mwili ulikuwa na uovu wa asili (yaani, wazo la Kiyunani), tamanio lolote la kimwili sharti likataliwe. Hivyo haya uitwa mafunuo ya “kujinyima.”

b. walimu hawa wa uongo walikwisha ondoka kanisani (kama vile 1 Yohana 2:19), lakini athari zao bado zipo!

2. utambulisho mzuri sharti uhusishwe na mazingira ya fasihi za kitabu kizima a. 1 Yohana kiliandikwa ili kupambanisha mafundisho ya uongo na kuwahakikishia waamini wa

kweli b. makusudi haya mawili yanaweza kuonekana katika majaribio ya waamini wa kweli

1) kimafundisho a) Yesu alikuwa mwanadamu halisi (kama vile 1 Yohana 1:1-3; 4:14) b) Yesu alikuwa Mungu halisi (kama vile 1 Yohana 1:2; 5:20) c) wanadamu ni wenye dhambi na wanawajibika kwa Mungu mtakatifu (kama vile 1

Yohana 1:6,10)

Page 417: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

401

d) wanadamu pia wanasamehewa na kufanya kuwa wenye haki kwa i. kifo cha Yesu (kama vile 1 Yohana 1:7; 2:1-2; 3:16; 4:9-10,14; 5:6-8)

ii. imani kwa Yesu (kama vile 1 Yohana 1:9; 3:23; 4:15; 5:1,4-5,10-12,13) 2) Kivitendo (chanya)

a) Mtindo wa maisha wenye utii (kama vile 1 Yohana 2:3-5; 3:22,24; 5:2-3) b) Mtindo wa maisha wenye upendo (1 Yohana 2:10; 3:11,14,18,23; 4:7,11-12,16-18,21) c) Mtindo wa maisha unaofanana na Kristo (hatendi dhambi, kama vile 1 Yohana 1:7;

2:6,29; 3:6-9; 5:18) d) Mtindo wa maisha wenye ushindi dhidi ya maovu (kama vile 1 yohana 2:13,14; 4:4; 5:4) e) Neno Lake linadumu ndani mwao (kama vile 1 Yohana 1:10; 2:14) f) Wana Roho (kama vile 1 Yohana 3:24; 4:4-6,13) g) Hujibiwa maombi (kama vile 1 Yohana 5:14-15)

3) Kivitendo (hasi) a) Mtindo wa maisha ya dhambi (kama vile 1 Yohana 3:8-10) b) Mtindo wa maisha yenye chuki (kama vile 1 yohana 2:9,11; 3:15; 4:20) c) Mtindo wa maisha usio na utii (kama vile 1 Yohana 2:4; 3:4) d) Kupenda ulimwengu (kama vile 1 Yohana 2:15-16) e) kumkana Yesu (kumkataa Baba na Mwana, kama vile 1 Yohana 2:22-23; 4:2-3; 5:10-12)

3. Utambulisho mzuri lazima uunganishwe kwenye kipengele maalumu katika andiko muhimu (kama vile Yohana 5:16-17) a. Je neno “ndugu” katika 1 Yohana 5:16 linahusiana na wale wote watenda dhambi zisizowapeleka

katika mauti na wale watendao dhambi zinazowapeleka katika mauti? b. Ni wapi wakosaji mara moja wanakuwa wanajumuiya ya kanisa (kama vile 1 Yoh.2:19) c. Nini umuhimu wa kimaandiko wa:

1) Hakuna KIFUNGU kinachoafikiana na “dhambi” 2) Kitenzi “anaona” ni kama kilivyo kwenye DARAJA LA TATU SHURUTISHI kikiwa na KAULI

TENDAJI TEGEMEZI YA WAKATI ULIOPITA USIOTIMILIFU? d. Ni kwa namna gani mmoja wa waombaji wa Kikristo (kama vile Yakobo 5:15-16) aweza kurejesha

uzima wa milele, zōē, kwa mwingine pasipo mwenye dhambi mwenyewe kutubu? e. Ni kwa vipi 1 Yohana 5:17 inahusiana na aina hiyo ya dhambi ( mpaka mauti, kutokuyafikia

mauti) A. Matatizo ya kithiolojia

1. Ni lazima mtafasiri ajaribu kuhusianisha andiko hili na a. Dhambi “isiosameheka” kwenye injili (angalia Mada Maalumu: Dhambi Isiyosameheka) b. Dhambi “inayoondoka mara moja” kwenye Waebrania 6 na 10

Muktadha wa 1 Yohana unaonekana kufanana na dhambi isiosameheka ya Wafarisayo katika siku zile za Yesu (kama vile Mt. 12:22-37; Marko 3:22-29) vile vile Wayahudi wasioamini wa Waebrania 6 na 10. Makundi yote haya matatu (Mafarisayo, Wayahudi wasioamini, na walimu wa mafunuo ya uongo) waliisikia injili wazi, lakini wakakataa kumwamini Kristo.

2. Ni lazima maswali ya kisasa ya kimadhehebu yawe kipimo cha kithiolojia cha kuliangalia andiko hili? Uinjilisti umesisitiza mno juu ya uanzishwaji wa mambo ya Ukristo na kuacha ushuhuda wa imani ya kweli juu ya mtindo wa maisha unaoendelea. Maswali ya kisasa ya kithiolojia yangaliwashangaza Wakristo wa karne ya kwanza. Tunataka kitu “Fulani” kinachoendana na “uhakiki wa maandiko” ya Kibiblia yaliyochaguliwa na mapungufu yetu ya kimantiki au upendelea wa kimadhehebu. Maswali yetu ya kithiolojia, vipimo, na makandokando yanatazamisha kutokuwepo kwetu kwa ulinzi. Tunahitaji zaidi habari na maelezo ya kina kuliko yale yatolewayo na Biblia, kwa hiyo mpangilio wetu wa kithiolojia unachukua kipande kidogo cha andiko na kupeperusha mfumo mkubwa wa mantiki za kimagharibi, na mafundisho maalumu! Maneno ya Yesu katika Mathayo 7 yalijitosheleza kwa ajili ya kanisa la mwanzo! Yesu alikuwa akiwatafuta wanafunzi, na sio maamuzi, imani ya muda mrefu ya mtindo wa maisha, na sio imani ya kimhemuko ya muda

Page 418: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

402

mfupi (kama vile Mt. 13:10-23; 28:18-20; Yohana 8:31-59). Ukristo sio kitendo cha nyuma kilichojitenga, lakini ni kitendo cha toba kinachoendelea, imani, utii, na ustahimilivu. Ukristo sio tiketi ya kwenda mbinguni, sio kitu kilichonunuliwa huko nyuma, au bima ya moto iliyochukuliwa kumlinda mtu toka kwenye mtindo wa maisha ya ubinafsi, maisha yasio ya kiungu! Angalia Mada Maalumu: Utume Dhambi mpaka inarejea mauti ya kimwili au mauti ya milele? Yohana ametumia zōē katika mazingira haya kudokeza tofauti iliyopo inayorejerea mauti ya milele. Inawezekana kuwa Mungu anawarejesha nyumbani wana wanaotenda dhambi? Uhusishaji wa mazingira haya ni kwamba (1) maombi ya waumini wenza na (2) toba binafsi ya mtu mkosaji inajumuishwa kurejesha waumini, lakini kama wakiendelea katika mtindo wa maisha ule uletao fedheha kwa jamii inayoamini, ndipo matokeo yanawezakuwa kwenye “muda usio muafaka” au kuondoka mapema katika maisha haya (kama vile When Critics Ask cha Norman Geisler na Thomas Howe, uk. 541)

◙ “Mungu atampa uzima” tatizo la kithiolojia na kimsamiati hapa ni maana ya neno “uhai” (zoē). Kwa kawaida katika maandishi ya Yohana hii inahusu uzima wa milele, lakini kwenye muktadha huu yaonekana kumaanisha urejesho wa afya au msamaha (yaani, sawa na matumizi ya Yakobo ya “okoa’ katika Yakobo 5:13-15). Mtu anayeombewa anaitwa “ndugu” ambayo kwa nguvu inaonyesha muamini (kufuatana na matumizi ya Yohana ya neno hilo kwa wasomaji wake). 5:17 Kila dhambi nimbaya, lakini kila dhambi yaweza kusamehewa kwa kufanyiwa toba (mwanzo, kama vile Marko 1:15; Matendo 20:21; kuendelea, kama vile 1 Yohana 1:9) na imani ndani ya kristo ila dhambi ya kutoamini!

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) 1 YOHANA 5:18-20 18 Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala 402ash mwovu hamgusi. 19 Twajua ya kuwa sisi tu wa Mungu; na dunia yote pia hukaa katika 402ash mwovu. 20 Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele.

5:18 “Twajua” Tazama maelezo kwenye aya ya pili katika 1 Yohana 5:13. ◙ “mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi” Hii ni kauli timilifu tendewa endelevu. Huu ndio uthibitisho wa wazi Yohana 1. 3:6 na 9. Uzima wa milele unazo dalili zinazoweza kutambulika. Mfumo wa maisha wa walimu wa uongo unafunua mioyo yao isiyofanywa upya (kama vile. Mathayo 7)! Yohana alikuwa anawatambulisha makundi mawili tofauti ya walimu wa uongo. Kundi la kwanza waliokataa kuhusika kwa namna yoyote na dhambi (kama vile 1 Yohana 1:8-2:1) na kundi 402asha402ne ambalo lilifanya dhambi kuwa kitu. Chochote (kama vile 1 Yohana 3:4-10 na hapa). Dhambi lazima kwanza iungamwe na iepukwe daima. Dhambi ndiyo tatizo, ni tatizo na tatizo linaloendelea (kama vile 1 Yohana 5:21 Bruce Metzger, A Textual Commentary of the Greek New Testament (uk. 718) inadhihilisha kwamba utofauti wa machapisho imetokana na kile ambacho mchapishaji alidhani kwamba aya “kuzaliwa na Mungu” ilihusu

1. Yesu – 402asha auton linafaa zaidi (A*, B*) 2. waaminio -- kisha eauton linafaa zaidi (א, Ac)

UBS4 inaipa #1alama "B" (karibu hakika). ◙ “bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda” kitenzi cha kwanza ni njeo tendwa endelevu ya wakati uliopita usiotimilifu, ambao unamaanisha kitendo kilichotimilizwa na mtendaji kutoka nje (yaani, Roho kama vile Warumi. 8:11). Hii inahusu kufanyika mwili kwa Yesu. Kitenzi cha pili ni kauli tendaji elekezi ya ya wakati uliopo ikiwana “yeye” (auton). Hii ni nenokwa neno, “yeye ambaye alizaliwa na Mungu huendelea kumlinda.” Hii inarejea kwa Yesu kuendelea kumhifadhi muamini. Tafsiri hii inafuata mswada wa Wayunani wa kale wa herufi kubwa A* na B*. Hii tafsiri inapatikana katika tafsiri za kiingereza NASB, RSV, na NIV.

Page 419: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

403

Mswada א na Ac ina kiwakilishi nomino kingine “hujihifadhi mwenyewe” (eauton) yeye humanisha kwamba yeye aliyezaliwa na Mungu anao wajibu wa kujihifadhi mwenyewe. Kitenzi kilichotumika hapa kwa “alizaliwa” hakitumiki popote tena kwa Yesu. Dhana ya kujirejelea imetumika ya waaminio katika 1 Yohana 3:3 na 5:4. Hii inafuatwa na watafsiri wa kiingereza wa KJVna ASV.

NASB "na yule mwovu hamgusi " NKJV "yule mpinga haki hamgusi " NRSV "yule mwovu hawagusi" TEV "yule mwovu hawezi kuwadhuru" NJB "yule mwovu hawezi kuwashikilia"

Hii ni kauli ya kati elekezi ya wakati uliopo ambayo inamaanisha yule mwovu hawezi kuendelea “kuwashikilia.” Tumizi lingine pekee la neno hili katika maandishi ya Yohana ni katika injili yake, 20:17. Ni hakika kutoka kwenye biblia na uzoefu kwamba wakristo hushawishiwa. Kumekuwepo na nadharia kuu tatu kuhusu maana ya msemo huu.

1. waaminio wako huru kutoka ile hali ya kutiwa hatiani na yule mwovu katika msingi wa kukeuka/kuvunja sheria (kuthibitisha jambo kuwa haki)

2. Yesu hutuombea (kama vile 1 Yohana 2:1; Luka 22:32-33) 3. shetani hawezi kutunyang’anya wakovu wetu kutoka kwetu (kama vile Warumi 8:31-39), ingawa anaweza

kuzuia ushuhuda wa Mungu katika maisha yetu na yawezekana kwa msingi wa 1 Yohana 5:16-17, kumwondoa muamini kutoka katika ulimwengu huu mapema!

5:19 "Twajua ya kuwa sisi tu wa Mungu" Hii ni kuwa na uhakika wa imani ya matumaini,kusudio la ulimwengu la muamini katika Yesu Kristo (kama vile 1 Yohana 4:6). Mengine yote yamesimikwa kwenye ukweli huu wa ajabu (kama vile 1 Yohana 5:13) tazama maelezo katika 1 Yohana 5:13.

◙ "na dunia yote pia hukaa katika yule mwovu" Hii ni kauli ya kati elekezi (chenye aina za vitenzi vya kilatini na kiyunani vyenye kutoa miundo mbalimbali ya vitenzi) vya wakati uliopo (kama vile Yohana 12:31; 14:30; 16:11; 2 Kor 4:4; Efe.2:2; 6:12).Hili liliwezeshwa kupitia (1”) Dhambi ya Adamu; (2) uasi wa shetani; na (3) mchaguzi binafsi wa kila mtu kufanya dhambi.

5:20 "Nasi twajua" tazama maelezo kamili kwenye kifungu cha pili cha 1 Yohana 5:13.

◙ "Mwana wa Mungu amekwisha kuja" Hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo inathibitisha kufanyika mwili kwa mwana wa ki-Ungu. Uungu pamooja na mwili wa binadamu lilikuwa tatizo kubwa kwa walimu wa uongo wa mafunuo ambao walitamka uovu wa jambo.

◙ "naye ametupa akili" Hii ni kauli nyingine tendaji elekezi ya wakati uliopo, Yesu, sio walimu wa uongo wa mafunuo ametoa utambuzi unaohitajika kuhusu Uungu. Yesu amemfunua kikamilifu Baba kwa njia ya uhai wake, mafundisho yake, matendo yake, kifo chake na ufunuo wake! Yeye ndiye neno hai la Mungu; hakuna anayekwenda kwa Baba bila kupita kwake (kama vile Yohana 14:6; 1 Yohana 5:10-12).

◙ "nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele" msemo wa kwanza “ndani yake aliye kweli” inahusu Mungu Baba (tazama Mada Maalum katika 1 Yohana 6:55 na Yohana 17:3), bali mtu aliyerejelewa kwenye msemo wa pili “Mungu wa kweli” ni vigumu zaidi kubaini. Katika mazingira, yaonekana pia kuhusu Baba, bali kitheolojia ingeweza kumuhusu Mwana. Utata wa kisarufi waweza kuwa uliokusudiwa, kwani upo mara nyingi kwenye maandiko ya Yohana, kwani ili mmoja kuwa ndani ya Baba hivyo lazima awe ndani ya Mwana (kama vile Yohana 5:12). Uungu na ukweli (kweli) wa wote wawili Baba na Mwana yaweza kuwa msukumo wa kitheolojia uliokusudiwa (kama vile Yohana 3:33; 7:28; 8:26). Agano Jipya halitamki Uungu kamilifu wa Yesu wa Nazareti (kama vile Yohana 1:1,18; 20:28; Fil. 2:6;

Page 420: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

404

Tito 2:13; na Ebr. 1:8). Kwa vyovyote walimu wa mafunuo wangeweza pia kutamka Uungu wa Yesu (angalau kwa roho ya kiungu iliyokuwa ndani yake).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA): 1 YOHANA 5:21 21 Watoto wadogo, jilindeni nafsi zenu na sanamu.

5:21 NASB “jilindeni nafsi zenu na sanamu"

NKJV, NRSV "jitengeni nafsi zenu na sanamu"

TEV "jiwekeni nafsi zenu salama kutoka kwa miungu wa uongo!"

NJB "kaeni katika kujilinda na miungu wa uongo"

Hii ni kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopo usiotimilifu, ukweli wa jumla wenye msisitizo. Hii inawahusu ushiriki tendaji wa wakristo katika utakaso (kama vile 1 Yohana 3:3), ambao tayari wanafurahia katika Yesu Kristo (kama vile Efe. 1:4;1 Petr. 1:5). Neno sanamu (ambao limetumika mara mbili tu kwenye maandiko ya Yohana, hapa narejea Agano la Kale katika Ufunuo 9:20), aidha inahusiana na mafundisho na mtindo wa maisha ya walimu wa uongo, au kwa sababu Magombo ya Bahari ya Chumvi hutumia neno hili katika maana ya “dhambi,” neno “sanamu”na “dhambi” yanaweza kuwa yanafanana.

MASWALI YA MJADALA

Huu ni mwongozo wa fasiri, ina maanisha kwamba unawajibika kwa tafsiri zako mwenyewe za Biblia. Kila mmoja wetu lazima atembee katika mwanga tulio nao. Wewe, Biblia, na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Hutakiwi uvitelekeze vitu hivi kwa mfasiri. Maswali ya mjadala huu yanatolewa kukusaidia kufikiri juu ya mambo makubwa ya sehemu za kitabu hiki. Yanalenga kukuamsha kimawazo na sio kutoa maana.

1. Orodhesha majaribio makuu matatu ambayo yanawahakikishia waaminio kwamba wako ndani ya Kristo. 2. Ni nini maneno “maji” na “damu” yanayorejewa katika Yohana 1.5:6 na 8? 3. Je, tunaweza kujua kwamba sisi ni Wakristo? Je, kuna baadhi ya Wakristo ambao hawajui? 4. Ni dhambi gani inayoongoza kwa kifo?Je, inaweza kutendwa na muamini? 5. Je, ni nguvu ya kuhifadhi ya Mungu au juhudi zetu wenyewe inayotuokoa kutoka katika vishawishi?

Page 421: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

405

2 YOHANA

MIGAWANYO YA AYA YA TAFSIRI YA KISASA*

UBS4 NKJV NRSV TEV NJB Salaam salaam kwa dada aliye Utambulisho Salaam Chaguliwa Mist. 1-3 Mist.1-3 Mist. 1-2 Mist. 1-3 Mist. 1-3 Mst. 3 Ukweli na upendo Tembea katika maagizo Ukweli na upendo Sheria ya upendo ya Kristo Mist. 4-11 Mist. 4-6 Mist. 4-6 Mist. 4-6 Mist. 4-5 Mst. 6 Kuwa makini na manabii Adui wa Kristo Wa uongo Mist. 7-11 Mist. 7-11 Mist. 7-8 Mist. 7-11 Mist. 9-11 Salaam za mwisho Salaam ya Yohana ya Maneno ya mwisho Kutakiana heri Mist. 12-13 Mist. 12-13 Mst. 12 Mst. 12 Mst. 12 Mst. 13 Mst. 13 Mst. 13

* Ingawa hazijavuviwa, migawanyo ya aya ndiyo ufunguo wa kuelewa na kufuatilia kusudio la asili la mwandishi. Kila tafsiri ya kisasa imegawanya na kufanya muhtasari wa aya. Kila aya ina mada kuu, kweli au wazo. Kila toleo limebeba hiyo mada kwa namna yake ya pekee. Unaposoma maandiko ya mwandishi jiulize ni tafsiri ipi inawiana na uelewa wako wa somo na mgawanyo wa mistari. Katika kila sura lazima tusome Biblia kwanza na kujaribu kutambua somo (aya), kisha tulinganishe na matoleo ya kisasa. Ni pale tunapoelewa kusudi la asili la mwandishi kwa kufuata mantiki yake na jinsi alivyojieleza tunaielewa kwa Biblia kiukweli. Ni mwandishi wa asili tu aliyevuviwa —wasomaji hawana haki ya kurekebisha ujumbe. Wasomaji wa biblia wana wajibu wa kutumia ukweli uliovuviwa kwenye siku na maisha yao. Fahamu kwamba maneno yote ya kiufundi na vifupisho vimefafanuliwa kwa kirefu kwenye nyaraka zifuatazo: Maelezo Fasaha Ya Muundo Wa Sarufi Za Kiyunani(Brief Definitions of Greek Grammatical Structure),Uhakiki Wa Tofauti Za Kiandishi(Textual Criticism),Ufafanuzi na Maelezo ya Kimaandiko(Glossary).

UTANGULIZI WA KI-MUHTASARI

Yohana wa 2 ni dhahili unahusiana na ujumbe na muundo halisi wa Yohana 1. Yumkini zimetoka kwa mwandishi mmoja, zimeandikwa kwa wakati mmoja. Ni uwasilishaji wa nyaraka binafsi za karne ya kwanza katika hicho kilicho andikwa kwacho katika muundo wa pamoja na kuweza kulingana kwenye upande mmoja wa gombo. Kama ilivyo Yohana 1 ilivyokuwa imeandikwa kwa makanisa mbali mbali (kwa maana ya makanisa yote), Yohana wa 2 inaelezea kwa kanisa moja la mahali na kiongozi wake (ingawa, kwa wingi nyaraka binafsi za Agano Jipya zilisomwa kwa kanisa zima). Ni upenyo mdogo ndani ya maisha ya kanisa la karne ya kwanza katika Asia ndogo (Uturuki).

MZUNGUKO WA KWANZA WA USOMAJI

Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwa tafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Dhamira ya kitabu kizima 2. Aina ya fasihi iliyotumika (uwasilishaji)

Page 422: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

406

MZUNGUKO WA PILI WA USOMAJI

Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwa tafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Mada ya sehemu ya kwanza ya fasihi 2. Mada ya sehemu ya pili ya fasihi 3. Mada ya sehemu ya tatu ya fasihi 4. Mada ya sehemu ya nne ya fasihi 5. N.k.

MZUNGUKO WA TATU WA USOMAJI KUFUATILIA KUSUDIO LA ASILI LA MWANDISHI KATIKA NGAZI YA AYA Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwatafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Aya ya kwanza 2. Aya ya pili 3. Aya ya tatu 4. N.k

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) MISTARI YA 1-3 1Mzee, kwa mama mteule na watoto wake niwapendao katika kweli; wala si mimi peke yangu, bali na wote waijuao ile kweli; 2 kwa ajili ya hiyo kweli ikaayo ndani yetu, nayo itakuwa pamoja nasi hata milele. 3 Neema, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Yesu Kristo Mwana wa Baba, zitakuwa pamoja nasi katika kweli na upendo.

Mst. 1 “Mzee” Wadhifa huu (presbuteros) umetumika kutambua mwandishi wa nyaraka zote Yohana 2 na 3. Una uwanda mpana wa maana katika biblia. Maandiko ya Yohana yanaonyesha usanifu wa kiuandishi katika njia tofauti.

1. Injili inatumia kifungu cha siri “wanafunzi wapendwa” 2. Waraka wa kwanza ni siri haujatajwa 3. Waraka wa pili na wa tatu una wadhifa wa “mzee” 4. Ufunuo, usioainisha uandishi wa mambo ya siku ya mwisho, unaorodhesha mwandishi kama “Mtumishi

wa Yohana” Kuna mijadala mingi imeendelea miongoni mwa watoa maoni na wasomi kuhusu uandishi wa maandiko haya. Yote yana ujuzi wa lugha na muundo unaofanana na unaotofautiana. Katika hoja hii hakuna maelezo yanayokubalika kwa walimu wote wa biblia. Ninauthibitisha uandishi wa kitume wa Yohana kati ya wote, lakini hili ni suala la kanuni za kisanifu na sio suala na kivuvio. Kiukweli, mwandishi halisi wa biblia ni Roho wa Mungu

Page 423: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

407

mwenyewe. Ni ufunuo wa kiaminifu, lakini wandishi wa kisasa hawajui au kuelewa mchakato halisi wa uandishi wao.

MADA MAALUM: MZEE

I. Matumizi ya Agano la Kale A. Lilitumika kurejerea malaika wa Mungu waliounda baraza la malaika (BDB 278, KB 278, kama

vile Isa. 24:23). Msamiati huu huu unatumika juu ya viumbe wa kimalaika (kama vile Ufu..4:4, 10; 5:5,6,8,11,14; 7:11,13; 11:16; 14:3; 19:4).

B. Lilitumika kumaanisha viongozi wa kikabila katika Agano la Kale (kama vile Kut. 3:16; Hes. 11:16). Baadaye katika Agano Jipya neno hili linatumika kurejerea kundi la viongozi kutoka Yerusalemu waliotengeneza mahakama ku ya Wayahudi, Baraza Kuu la Sinagogi (kama vile Mt. 21:23; 26:57). Katika siku za Yesu chombo hiki cha watu sabini kiliendeshwa na uhakunani wenye uharibifu (yaani wasiotokana na uzao wa Haruni bali wakinunuliwa kutoka kwa mabwana wa Kirumi).

II. Matumizi ya Agano Jipya A. Lilitumiwa na viongozi wa makanisa ya maeneo ya kanisa la Agano Jipya. Lilikuwa mojawapo ya

maneno matatu yenye visawe (mchungaji, mwangalizi na mzee, kama vile Tito 1:5,7; Mdo. 20:17,28). Petro na Yohana walilitumia kujijumuisha wenyewe katika kundi la viongozi (kama vile 1 Petro 5:1; 2 Yohana 1; 3 Yohana 1).

B. Kuna mbinu ya kimatumizi juu ya neno mzee (presbuteros) katika 1 Pet. 1:1 na 5. Neno kidhahiri linatumika kama jina la uongozi (kama vile mstari wa 1) na maelezo ya umri (kama vile mstari wa 5). Matumizi ya neno hili yanashangaza kwa kuzingatia kwamba ni msingi wa maelezo ya uongozi wa kikabila ya Kiyahudi wakati "askofu" au "mwangalizi" (episcopos) lilikuwa maelezo ya uongozi wa mji wa Kiyunani. 1 Petro anatumia maneno ya Kiyahudi kuhutubia waaminio wa Mataifa. Petro mwenyewe anajiita "mzee mwenza," neno presbuteros pamoja na kihusishi syn, ambalo linamaanisha "ushiriki wa pamoja na." Petro haelezei mamlaka yake ya kitume (kama vile 2 Yohana 1, ambapo Mtume mwingine anajiita "mzee"), lakini anaonya (yaani, "Angalieni," kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo) viongozi wa maeneo ya mahala kutenda na kuishi sawasawa kwa ufahamu wa 1. mfano wa Kristo 2. kwamba yu karibu kuja Makanisa ya mwanzoni hayakuwa na nafasi za kulipwa za uongozi bali walitambua karama za huduma zitolewazo na Mungu na uongozi ndani ya makanisa ya mahali pamoja. Ukiri huu wa karama ulitakiwa kuwianishwa na uthamani wa kijadi kwa "hekima itokanayo na umri," haswa kati ya jamii iaminiyo ya Kiyahudi. Hivyo Petro anawahutubia aina zote za uongozi. Pia tambua kwamba "wazee" is ni wingi. Hii inaweza kurejerea kwa (1) idadi ya viongozi wa makanisa ya nyumbani (kama vile Mdo. 20:17) au (2) karama za Roho tofauti tofauti kati ya kundi la viongozi (kama vile Efe. 4:11), ambayo kwa uwazi kunataja kwamba huduma ni ya waaminio wote. Huu ni ufanano wa dhana ya "ufalme wa kikuhani" (kama vile 1 Pet. 2:5,9).

C. Lilitumika juu ya watu wenye umri mkubwa katika kanisa, sio lazima wawe viongozi (kama vile 1 Tim. 5:1; Tito 2:2).

◙ “Mama mteule na watoto wake” Kumekuwepo na majadiliano mengi kuhusu wadhifa huu. Wengi wamejaribu kudai kuwa hili liliandikwa kwa mama aitwae Electa, toka kwa neno la Kiyunani kuchaguliwa au kusimamishwa

Page 424: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

408

(Clement wa Alexandria) au Kyria, toka kwa neno la Kiyunani mama (Anastazia). Hata hivyo, ninakubaliana na toleo la Jerome kuwa hili lilikuwa linarejea kwenye kanisa kwa sababu zifuatazo.

1. Neno la Kiyunani kwa ajili ya kanisa ni la KIKE ( 2 Yoh.1:1) 2. Katika maandiko ya kale ya Kiyunani(LXX ) ya neno “kusimamisha” linarejea kundi la watu (k.v 1 Petr. 2:9) 3. Hii inaweza kurejerea kanisa kama bibi harusi wa Kristo (k.v. Efe. 5:25-32; Ufu. 19:7-8; 21:2) 4. Kanisa hili lina wana kikundi waliorejerewa kama watoto (k.v. 2 Yoh. 1:13) 5. Kanisa hili lina mama anayeonekana kurejerewa kwenye kanisa lingine la mahali (k.v. 2 Yoh. 1:13) 6. kuna mchezo hapa kati hali ya UMOJA na hali ya WINGI katika kifungu kizima (UMOJA katika 2 Yohana

1:4,5,13; WINGI katika 2 Yohana 1:6,8,10,12) 7. Neno hili linatumika kwa namna ile ile kwa ajili ya kanisa katika 1 Pet. 5:13

◙ “niwapendao katika kweli” Inashangaza kuwa hiki ni kiwakilishi nomino cha kiume kilichoko katika wingi kwa sababu kinamaanisha kuunganisha huenda kwa “mama” ambaye ni jinsia ya KIKE au “watoto” ambao hawako upande wowote. Nafikiri ilikuwa ni njia ya Yohana ya kukifanya kifungu kuwa alama.

◙ “Nawapenda” Yohana anatumia kisawe phileō kikiwa na agapaō katika injili na ufunuo, lakini katika Yohana I, II na 3 Yohana anatumia agapaō tu (k.v. 2 Yoh. 1:3,5,6; 1 Yoh. 3:18). ◙ “Ukweli” Ukweli ni dhamira inayorudiwa mara kwa mara (k.v. 2 Yoh. 1:1[mara mbili],2,3,4). Kifungu “mafundisho haya” katika 2 Yohana 1:9 [mara mbili] na 10 ni kisawe cha neno “ukweli.” Hili neno yumkini linasisitizwa kwa sababu ni mafundisho mafinyu yalioko kinyume ambayo ni dhahili katika waraka huu (k.v. 2 Yoh. 1:4,7-10) kama ilivyo katika 1 Yohana. “Ukweli” inaweza kurejea moja kati ya vitu vitatu (1) Roho Mtakatifu katika Yohana (k.v. Yoh. 14:17); (2) Yesu Kristo Mwenyewe (k.v. Yoh. 8:32; 14:6); na (3) maudhui ya injili (k.v. 1 Yoh. 3:23). Angalia Mada Maalum juu ya Kweli katika Yohana 6:55 na 17:3

Mst. 2 “Ikaayo ndani yetu” Hii ni kauli tendaji endelevu ya wakati uliopo moja ya maneno pendwa ya Yohana kuwaelezea waumini, “kuendelea kudumu.” Angalia Mada Maalum katika 1 Yohana 5:13. Hii inaonekana kurejea Roho Mtakatifu anayekaa ndani yetu (k.v. Rum. 8:9; au Mwana, Rum. 8:9-10). Watu wote watatu katika Utatu pia wanadumu ndani/wakiwa/ kwa waumini (k.v Yoh.14:23) ◙ “Atakuwa pamoja nasi hata milele” Ukweli unadumu ndani na kubaki na waumini wote milele. Ni maelezo gani yenye nguvu ya uhakika! Angalia Mada Maalumu katika Yohana 6:20. Ukweli inasimama katika pande zote za mtu katika injili na ujumbe katika injili. “Ukweli” huu mara zote unatoka katika upendo, upendo wa Mungu. Upendo kwa kaka/dada wa agano, upendo kwa ulimwengu uliopotea (k.v 1 Yoh. 4:7-21) “Milele” kiuhalisia ni “ndani ya enzi”(k.v. Yoh. 4:14; 6:51,58; 8:35,51; 10:28; 11:26; 12:34; 13:8; 14:16; 1 Yoh. 2:17). Tazama Mada Maalum katika Yohana 6:58 Mst. 3 “Neema, na Rehema, na Amani”Ni utangulizi wa kiaina kwa waraka wa Kiyunani wa karne ya kwanza ukiwa na udhuru. Kwanza, yalikuwa ni mabadiliko madogo kuufanya Ukristo wa kipekee. Neno la Kiyunani kwa neno “salaamu” ni chairein. Lilibadilishwa na kuwa charis, likimaanisha “neema.” Utangulizi huu unafanana sana na ule waraka wa kichungaji, 1 Tim. 1:2; 2 Tim. 1-2; maneno mawili kati yao yamerudiwa katika utangulizi wa Paulo kwa Wagalatia na Wathesalonike 1. Mbili, uundaji wa kawaida wa kisarufi ni maombi au kutakiana afya njema. Hata hivyo, 2 Yohana ni maelezo ya ukweli, ahadi ya kusimama na Mungu ikiwa na shauku ya matokeo ya ki-Ungu.

Kithiolojia mtu atashangaa kama kuna mpango wa kimakusudi kati ya maneno haya. Rehema na neema inaaksi tabia ya Mungu inayoleta wokovu wa bure kupitia Kristo kwa mwanadamu aliye anguka. Amani inaaksi upokeaji wa karama za Mungu. Waumini wanafanya mabadiliko kamili. Kama anguko lilivyoathiri dhana nzima za maisha ya binadamu, vivyo hivyo, wokovu unarejesha, kwanza kupitia nafasi (unahesabiwa haki kwa njia ya imani), tena kwa badiliko muhimu katika mtazamo wa kidunia uliowezeshwa na Roho aishie ndani, ambaye husababisha uendelevu wa ufanano na Kristo (utakaso endelevu). Taswira ya Mungu kwa mwanadamu (k.v Mwa. 1:26-27) umerejeshwa!

Page 425: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

409

Uwezekano mwingine unahusiana na hitaji kwa ajili ya maneno haya matatu katika uwazi wa walimu wa uongo. Walitilia mashaka “neema” na “rehema” na kuleta kila kitu lakini sio “amani.” Pia ni hoja nzuri ya kukumbusha kuwa matumizi pekee ya neno “rehema” (eleeōi) katika maandiko yote ya Yohana. Neno “Neema” (charis) linatumika hapa tu, katika injili katika 2 Yohana 1:14,16,17 na Ufunuo (k.v 1:4; 22:21).

The Jerome Biblical Commentary inataja ukweli kwamba maneno haya matatu yana muunganikano wa kimaagano wa agano la kale (uk. 412). Wandishi wa agano jipya (isipokuwa Luka) walikuwa ni wasomi wa Kiebrania, wakiandika katika lugha ya kawaida ya Koine. Misamiati mingi ya Agano Jipya ina asili ya maandiko ya kale ya Kiyunani.

◙ “zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Yesu Kristo Mwana” Nomino zote zina vihusishi (para) ambavyo kisarufi vinakaa katika ulingano. Hii ilikuwa ni njia ya kisarufi kutetea Uungu kamili wa Yesu Kristo.

◙ “Mwana wa Baba” Mwendelezo wa msisitizo katika 1 Yohana ni kuwa mtu hawezi kuwa na Baba pasipokuwa na Mwana (k.v. 1 Yoh. 2:23; 4:15; 5:10). Walimu wa uongo wanadai kuwa na uhusiano wa kipekee na maalumu na Mungu, lakini kithiolojia inashusha utu na kazi ya Mwana. Yohana anarudia tena kuwa Yesu ni (1) ufunuo kamili wa Mungu na (2) njia pekee (k.v Yohana 14:6) kwa Baba.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) MISTARI YA 4-6 4Nalifurahi mno kwa kuwa nimewaona baadhi ya watoto wako wanaenenda katika kweli, kama vile tulivyopokea amri kwa Baba. 5 Na sasa mama, nakuomba, si kwamba nakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo, kwamba tupendane. 6 Na huu ndio upendo: tuenende kwa kuzifuata amri zake. Hii ndiyo ile amri, kama mlivyosikia tangu mwanzo kwamba mwenende katika hiyo.

Mst. 4 “Nalifurahia” Hii ni kauli tendewa (shahidi) elekezi ya wakati uliopita usiotimilifu. Yumkini wazee walisikia kuhusu kanisa hili toka kwa baadhi ya wanajumuiya waliokuwa wakisafiri. ◙ “Nimewaona watoto wako wanaoenenda katika kweli” Hii inarejea huenda kwenye

1. Kimungu, wakiyapenda baadhi ya maisha ya watu kanisani 2. Njia ya kukubari uwepo wa mafundisho yaliyo kinyume katikati ya kusanyiko lililowaongoza baadhi yao

kwenda tofauti. ◙ “kama tulivyopokea amri toka kwa Baba” Hii ni kauli tendaji elekezi ya wakati uliopita usiotimilifu ambayo inarejea kupokea amri ya kupendana kati ya mtu na mwenzake, kama jinsi Yesu alivyowapenda wao (K.V. Yoh. 13:34-35; 15:12; 1 Yoh. 3:11; 4:7,11-12,21). ◙ “Ile tuliokuwa nayo tangu mwanzo” Hii ni kauli tendaji elekezi isiotimilifu ambayo inarejea mwanzoni mwa mafundisho ya Yesu (k.v. 1 Yoh. 2:7,24; 3:11). Maudhui ya amri ni kuimalisha upya kama “kupendana kati ya mtu na mwenzake” (k.v 2 Yoh.1:5) na “kukubari Yesu Kristo alikuja katika mwili” (k.v 2 Yoh.1:7). Angalia maudhui, ya kibinafsi na mtindo wa maisha. ◙ “Tunapendana sisi kwa sisi” Hii ni kauli tendaji tegemezi ya wakati uliopo (kama ilivyo katika kitenzi cha mwisho katika mstari huu, tembea). Ilikuwa ni tabia ya wale waliokuwa kinyume kutojumuishwa na kutopenda. Hii inatengeneza jaribio la kwanza kati ya yale matatu ya Yohana kwa namna gani mmoja anaweza kutambua kuwa yeye ni Mkristo. Katika kitabu cha 1 Yohana majaribu haya matatu ni: upendo, mtindo wa maisha, na mafundisho. Haya majaribu matatu yanarudiwa katika 2 Yohana.

1. Upendo (k.v. 2 Yoh. 1:5; 1 Yoh. 2:7-11; 3:11-18; 4:7-12,16-21; 5:1-2) 2. Utii (k.v. 2 Yoh. 1:6; 1 Yoh. 2:3-6; 3:1-10; 5:2-3) 3. Maudhui ya kimaandiko(k.v. 2 Yoh. 1:7; 1 Yoh. 1:1ikifuatiwa na; 2:18-25; 4:1-6,14-16; 5:1,5,10)

Mst. 6 “Na huu ndiyo upendo” Upendo wa (agapē) ni kitendo kinachoendelea (njeo ya wakati uliopo), na sio fikra. Upendo ni “alama” ya waumini wote wa kweli (k.v. 1 Wakorintho 13; Gal. 5:22; 1 Yoh. 4:7-21).

Page 426: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

410

◙ “Tokea mwanzo” Angalia maelezo katika 1 Yohana 1:1. Nafikiri kifungu kimetumika katika 1 Yohana na 2 Yohana kama nukuu ya huduma ya Yesu ya awali. ◙ “Mwenende katika hiyo” Ukristo ni ahadi ya awali na mabadiliko ya maisha (k.v 1 Yoh. 2:6). Mtindo wetu wa maisha hautuokowi, lakini hauthibitishi kuwa tumeokolewa (k.v Efe. 2:8-9 na 2:10.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) MISTARI YA 7-11 7Kwa maana wadanganyifu wengi wametokea duniani, wasiokiri ya kuwa Yesu Kristo yuaja katika mwili. Huyo ndiye yule mdanganyifu na mpinga Kristo. 8 Jiangalieni nafsi zenu msiyapoteze mliyoyatenda, bali mpokee thawabu timilifu. 9 Kila apitaye cheo, wala asidumu katika mafundisho ya Kristo, yeye hana Mungu. Yeye adumuye katika mafundisho hayo, huyo ana Baba na Mwana pia. 10Mtu akija kwenu, naye haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu. 11 Maana yeye ampaye salamu azishiriki kazi zake mbovu.

Mst. 7 “Kwa maana wadanganyifu wengi” Neno wadanganyifu linatokana na neno la Kiyunani planē, lile tunalopata neno la Kiingereza “sayari.” Katika ulimwengu wa kale mwenendo wa vitu vya mbinguni viliwekwa kwenye ramani na kusomwa (zodiak). Nyota zilifaa kuwepo katika mpangalio ulio imara, lakini baadhi ya nyota (yaa., sayari) zilizunguka visivyo. Watu wa kale waliziita “nyota za kutangatanga.” Hii ki-isitiari ilikua ndani mwa wale wanao tangatanga toka kwenye ukweli. Walimu wa uongo kwa kweli sio wabaya au watu wanao potosha wasio na ufahamu kuhusu injili. Katika maandiko ya Yohana wote mafarisayo na walimu wa uongo waliasi dhidi ya nuru wlioipata. Hii ndio sababu uasi wao unaainishwa kama “dhambi isiosameheka” au “dhambi hata mauti” (angalia maelezo katika 1 Yoh. 5:16). Majanga hapa ni kuwa pia wao walisababisha wengine wawafuate kwenye uharibifu. Agano Jipya wazi linadhihilisha kuwa walimu wa uongo watajitokeza na kusababisha madhara makubwa (k.v. Mt. 7:15; 24:11,24; Marko 13:22; 1 Yoh. 2:26; 3:7; 4:1). ◙ “wametokea duniani” Hapa Ulimwengu ni sayari yetu hii tuliomo. Hawa walimu wa uongo ama wameacha kanisa la Kikristo (k.v. 1 Yoh. 2:19) au wako kwenye majukumu ya Umisionari (k.v 3 Yohana). ◙ “Wasiokiri” Hili ni neno linaloitwa homologeō, ambalo linamaanisha toba ya wazi na ukiri wa imani katika Kristo. Anaglia Mada Maalum: Ukiri katika Yohana 9:22-23 ◙ “Yesu Kristo yuaja katika mwili” Wapotoshaji hawa wanaendelea na mafundisho yao ya uongo kuhusu ubinadamu wa Yesu. Mstari huu unaendelea kutoa onyo juu ya “kuzijaribu roho” katika 1 Yohana 4:1-6, hasa pale unapoongelea juu ya ubinadamu kamili wa Yesu (k.v Yohana 1:14; 1 Tim 3:16). Watu wenye mafunuo ya uongo wanathibitisha kuwa na umiliki mara mbili wa umilele kati ya “roho” (Mungu) na “vitu” (mwili). Kwao, Yesu hawezi kuwa Mungu kamili na Mtu kamili. Kunaonekana kuwepo kwa wastani kuna mielekeo miwili ya kithiolojia ndani ya fikra za kimafunuo.

1. Kukana ubinadamu wa Yesu; alionekana kuwa mtu, lakini alikuwa roho 2. Walikana kuwa Kristo hakufa pale msalabani; kundi hili (Cerithian) linadai kuwa “roho wa Kristo” alikuja

juu ya Yesu mtu wakati wa ubatizo wake na kumwacha kabla ya kufa kwake pale msalabani Inawezekana kuwa njeo ya wakati uliopo, “kuja katika mwili,” ilikuwa ni njia ya Yesu ya kukataa mafunuo ya uongo wa watu wa Korintho na 1 Yohana 4:1-6 katika njia zake za kukataa mafunuo ya uongo ya kukataa ubinadamu wa Yesu na kufa kwa Yesu msalabani.

◙ “Huyu ndiye yule mdanganyifu na mpinga Kristo” Katika 1 Yohana 2:18 kuna utofauti kati ya hali ya uwingi ya neno “mpinga Kristo” na hali ya umoja ya neno “mpinga Kristo.” Uwingi lilikuja katika siku za Yohana na walikuwa wameondoka kanisani (k.v 1 Yohana 2:19), lakini umoja lilijitokeza wakati wa mbeleni (angalia “mtu asiyeshika sheria” katika 2 Wathesalonike 2). Hata hivyo, katika mstari huu, hali ya umoja imetumika, kama hali ya wingi ilivyotumika katika 1 Yohana 2:18-25.

Page 427: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

411

Mst. 8 “Jiangalieni” Hii ni kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopo. Neno “angalia” (blepō), limetumika kiisitiari kwa maana ya kuonya juu ya uovu (k.v. Mt. 24:4; Marko 13:5; Luk. 21:8; Mdo. 13:40; 1 Kor. 8:9; 10:12; Gal. 5:12; Ebr. 12:25). Waamini wanawajibika kutambua makosa kwa sababu

1. Wanaijua injili 2. Wana Roho 3. Wana mwendelezo wa ushirka na Kristo

NASB "Kuwa msiyapoteze mliyoyatimiliza" NKJV "Kuwa msiyapoteze mliyoyatenda" NRSV "Ya kwamba msiyapoteze mlioyoyatenda" TEV "Ya kwamba tusiyapoteze tuliyoyatenda" NJB "Au kazi yetu yote itapotea" Kuna utofauti wa maandishi ya Kiyunani katika mstari huu unaofanana na kiwakilishi cha kwanza: yawezakuwa ni “wewe” (NASB, NRSV, TEV) au "sisi" (NKJV)? Toleo la UBS4 andiko linakubaliana na “wewe,” likimaanisha waamini walioelezewa wasingali timiliza lengo la injili waliyopewa na mashahidi wa kitume.

◙ “Bali mpokee thawabu timilifu” Hii ni kauli tegemezi ya wakati uliopita usiotimilifu ambayo inaelekeza nyuma wakati wa upokeaji wa injili. Dharura ya utegemezi haihusiani na wokovu wao, lakini ukomavu na kuenea kwa injili kupitia kwao (k.v. 1 Kor. 9:27; 15:10,14,58; 2 Kor. 6:1; Gal. 2:2; Flp. 2:16; 1 Thes. 2:1; 3:5).

Mst. 9 NASB "Kila apitaye cheo, asidumu katika mafundisho ya Kristo" NKJV "Yule akosaye, asidumu katika mafundisho ya Kristo" NRSV "Yeyote asiyedumu katika mafundisho ya Kristo" TEV "Yeyote yule asiyekaa katika mafundisho ya Kristo, lakini huenda mbali nayo" NJB "Ikiwa yeyote hatabaki katika mafundisho ya Kristo lakini akaenda mbali nayo"

Kwanza, angalia utumiaji uliokinyume wa neno pas. Mwaliko wa injili ni kwa “wote,” lakini bahati mbaya pia ni muhimu kwa wale wenye mafundisho ya uongo. Haya mafundisho yaliyo kinyume yanaainishwa na kauli mbili tendaji endelevu za wakati uliopo: “kwenda zaidi” na “asiyedumu.” La kwanza “kwenda mbali” ingekuwa ni msemo kwa walimu wa uongo ukimaanisha wanaufahamu ukweli zaidi ya mitume walioshuhudia kwa macho. Waamini wanaainishwa kwa neno la kweli lililodumu ndani yao (k.v Yohana 8:31; 15:7; 1 Yohana 2:14, walio kinyume katika Yohana 5:38; 1 Yohana 1:10). Angalia Mada Maalum: Hitaji la Ustahimilivu katika Yohana 8:31 na Mada Maalum: Uasi (Aphistēmi) katika Yohana 6:64 Kifungu milikishi “cha Kristo” chaweza kurejea kwa

1. Mafundisho ya Kristo 2. Mafundisho kuhusu Kristo 3. Maana mbili za kawaida za Yohana

Vimilikishi ni vingi na haviko wazi! Mazingira tu ndiyo yanaweza amua maana iliyokusudiwa lakini mara nyingi, kama hapa, imepitiliza. ◙ “Yeye hana Mungu” “Mafundisho kuhusu Kristo” na “ukweli” wa 2 Yohana mstari wa 2 vinafanana. Walimu wa uongo na wafuasi wao hawana thawabu (k.v Yohana mstari 8). Wamepotea kiroho na hawako na Mungu kwa vile ili kuwa na Baba ni lazima uwe na Mwana (k.v. 1 Yohana 5:10-12). Utumiaji wa KITENZI “hana” (mara mbili, kauli tendaji elekezi ya wakati uliopo) akiwa na Mungu kinapatikana hapa tu na katika 1 Yohana 2:23. Mst. 10 “Kama” Hii ni sentesi shurutishi daraja la kwanza inayofikiriwa kuwa kweli kutokana na mtazamo wa mwandishi au kwa kusudi la kifasihi. Walimu wa uongo watakuja!

Page 428: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

412

◙ “Msimkaribishe nyumbani mwenu” Hii ni kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopo ikiwa na kiambata hasi ambayo mara nyingi inamaanisha kuzuia kitendo kilichoko katika mchakato (mazingira lazima yaamue). “nyumba” inaweza kurejerea ukarimu wa Mkristo (k.v. Mat. 25:35; Rum. 12:13; 1 Tim. 3:2; Tit 1:8; Ebr. 13:2; 1 Pet. 4:9 or 3 Yohana 5-6), lakini katika muktadha yumkini inarejerea kumkaribisha Mtumishi aliyesafiri kuongea katika nyumba ya ibada (k.v. Rum. 16:5; 1 Kor. 16:19; Kol. 4:15; Filemoni 2). ◙ “Wala msimpe salamu” Hii ni kauli tendaji shurutishi ya wakati uliopo nyingine ikiwa na kiambata hasi. Usijitambilishe mwenyewe kwa hawa wanaoitwa Wakristo. “Dokezo lolote la ushirika lisieleweke kama kama kibari (k.v 2 Yohana 1:11). Maelezo haya ni magumu kuyatumia katika siku hizi za leo. Wengi wanadai kuwa Wakristo. Lakini bado kwa jaribio la kushirikishana nao lazima liwe la kirafiki na kushirikiana nao katika mazungumzo. Bado, viongozi wa Kikristo lazima wawe waangalifu na utambulisho wa imani zilizo kinyume. Hili, hakika, halitumiki katika madhehebu ya Kikristo!

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) MISTARI 12-13 12 Kwa kuwa ninayo mambo mengi, sitaki kuyaandika kwa karatasi na wino; lakini nataraji kuja kwenu, na kusema nanyi uso kwa uso, ili furaha yetu iwe imetimizwa. 13 Watoto wa ndugu yako aliye mteule, wakusalimu.

Mst. 12 “kwa kuwa ninayo mengi” Mstari huu unafanana na ule wa kumalizia katika 3 Yohana 1:13-14. ◙ “ili furaha yetu iwe imetimizwa” Hii ni kauli timilifu tendewa tegemezi yenye mafumbo ya makusudi (kishazinia chenye kuonyesha udharura). Hii ilikuwa ni dhamira ya kawaida katika Yohana (k.v Yohana 3:29; 15:11; 16:24; 17:13; 1 Yohana 1:4). Furaha hii ilisimamia juu

1. Uwepo wa mwalimu 2. Maarifa ya ukweli uliouleta

Yohana anazungumzia “furaha” yake katika 2 Yohana 1:4 katika mwendelezo wa kutembea kwenye upendo na utii. Mst. 13 Mstari huu, kama ulivyo 2 Yohana 1:1, unatumia lugha ya kiisitiari kuongelea juu ya dada mmoja wa kanisa na wanajumuiya wake.

MASWALI YA MJADALA

Huu ni mwongozo wa fasiri, ina maanisha kwamba unawajibika kwa tafsiri zako mwenyewe za Biblia. Kila mmoja wetu lazima atembee katika mwanga tulio nao. Wewe, Biblia, na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Hutakiwi uvitelekeze vitu hivi kwa mfasiri. Maswali ya mjadala huu yanatolewa kukusaidia kufikiri juu ya mambo makubwa ya sehemu za kitabu hiki. Yanalenga kukuamsha kimawazo na sio kutoa maana.

1. taja majaribu matatu yanayopatikana katika 1 Yohana na kujirudia katika 2 Yohana. a. b. c.

2. Waraka huu umeandikwa kwa yule mama au kwa kanisa 3. Unwezaje kujua toka katika waraka huu mfupi kuwa palikuwepo na imani ya kinyume ndani ya kusanyiko? 4. Wapi na akina nani walikuwa walaghai na wapinga Kristo wa 2 Yohana 1:7? 5. Je 2 Yohana 1:10 na 11 ni mkanganyiko kwenye maelekezo ya Agano Jipya kuonyesha ukarimu na upendo

hata katika maadui zetu?

Page 429: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

413

3 YOHANA

MIGAWANYO YA AYA YA TAFSIRI ZA KISASA

UBS4 NKJV NRSV TEV NJB Salaam Salaam kwa Gayo Utangulizi Mahubiri na salaam Mst.1 Mst. 1-4 Mst.1 Mst. 1a Mst. 1-4 Mst. 1b Mist. 2-4 Mist. 2-4 Mist. 2-4 Ushirikiano na Anasifiwa kwa Gayo anasifiwa Upinzani ukarimu Mist. 5-8 Mist. 5-8 Mist. 5-8 Mist. 5-8 Mist. 5-8 Deotrefe na Deotrefe na Uwe makini na Demetria Demetria mifano ya Deotrefe Mist. 9-10 Mist. 9-12 Mist. 9-10 Mist. 9-10 Mist. 9-11 Mist. 11-12 Mist. 11-12 Mst. 11 Kusifiwa kwa Gayo Mst. 12 Mst. 12 Salaam za mwisho Salaam za kutakiana Salaam za mwisho Hitimisho heri Mist. 13-15 Mist. 13-15 Mist. 13-14 Mist. 13-14 Mist. 13-15 Mst. 15 Mst. 15a Mst. 15b

* Ingawa hazijavuviwa, migawanyo ya aya ndiyo ufunguo wa kuelewa na kufuatilia kusudio la asili la mwandishi. Kila tafsiri ya kisasa imegawanya na kufanya muhtasari wa aya. Kila aya ina mada kuu, kweli au wazo. Kila toleo limebeba hiyo mada kwa namna yake ya pekee. Unaposoma maandiko ya mwandishi jiulize ni tafsiri ipi inawiana na uelewa wako wa somo na mgawanyo wa mistari. Katika kila sura lazima tusome Biblia kwanza na kujaribu kutambua somo (aya), kisha tulinganishe na matoleo ya kisasa. Ni pale tunapoelewa kusudi la asili la mwandishi kwa kufuata mantiki yake na jinsi alivyojieleza tunaielewa kwa Biblia kiukweli. Ni mwandishi wa asili tu aliyevuviwa —wasomaji hawana haki ya kurekebisha ujumbe. Wasomaji wa biblia wana wajibu wa kutumia ukweli uliovuviwa kwenye siku na maisha yao. Fahamu kwamba maneno yote ya kiufundi na vifupisho vimefafanuliwa kwa kirefu kwenye nyaraka zifuatazo: Maelezo Fasaha Ya Muundo Wa Sarufi Za Kiyunani(Brief Definitions of Greek Grammatical Structure),Uhakiki Wa Tofauti Za Kiandishi(Textual Criticism),Ufafanuzi na Maelezo ya Kimaandiko(Glossary).

MZUNGUKO WA KWANZA WA USOMAJI Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwa tafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Dhamira ya kitabu kizima 2. Aina ya fasihi iliyotumika (uwasilishaji)

Page 430: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

414

MZUNGUKO WA PILI WA USOMAJI Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwa tafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Mada ya sehemu ya kwanza ya fasihi 2. Mada ya sehemu ya pili ya fasihi 3. Mada ya sehemu ya tatu ya fasihi 4. Mada ya sehemu ya nne ya fasihi 5. N.k.

MZUNGUKO WA TATU WA USOMAJI KUFUATILIA KUSUDIO LA ASILI LA MWANDISHI KATIKA NGAZI YA AYA Huu ni mwongozo kwa kujisomea wa fasiri, ikiwa na maana kuwa unawajibika kwatafsiri yako mwenyewe ya Bibila. Kila mmoja wetu sharti atembee katika mwanga tulionao. Wewe, Bibila na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Usimwachie kazi hii mfasiri. Soma sura katika mkao mmoja. Tambua masomo linganisha mgawanyo wako na tafsiri tano hapo juu. Kuandika ki-aya sio kazi iliyovuviwa, lakini ni mwongozo wa kufuata kusudio la mwandishi wa kwanza ambacho ndicho kiini cha tafsiri. Kila aya ina somo moja tu.

1. Aya ya kwanza 2. Aya ya pili 3. Aya ya tatu 4. N.k

UTAMBUZI WA MUKTADHA WA 3 YOHANA

UTANGULIZI

A. Waraka huu mdogo umeitwa 3 Yohana kwa sababu kidogo ni mfupi kuliko 2 Yohana. Ninafikiri 2 Yohana na 3 Yohana zinatengeneza mlingano wa ujumbe kwa kanisa la mahali, yumkini mahali fulani katika Jimbo la Rumi ya Asia Ndogo, kuelekea karne ya kwanza.

B. 2 Yohana anashughulika na matatizo ya mafundisho yaliyo kinyume, ya wahabiri waliokuwa wakisafiri, wakati 3 Yohana inashughulika na kuonya ili kuwasaidia wahubiri wa Kikristo wanaosafiri.

C. Kuna watu watatu tofauti hasa waliotajwa katika 3 Yohana 1. Gayo (mtu wa Mungu katika kanisa lililompokea)

a. Kuna wakina Gayo watatu waliotajwa sehemu zingine za biblia. Gayo wa Makedonia, Mdo. 19:29; Gayo wa Derbe, Mdo. 20:4; na Gayo wa Korintho, Rum. 16:23; 1 Kor. 1:14

b. Maandiko yalijulikana kama “katiba ya Kitume” ikimtaja Gayo wa 3 Yohana kama Askofu wa Pegamo, aliyeteuliwa na Yohana.

2. Diotrefe (mtu msumbufu asiye wa Mungu katika kanisa alilopokelewa) a. Huu ni mtaji pekee wa mtu huyu katika Agano Jpya. Jina lake ni kati ya majina machache

yanayomaanisha “mhudumiwa wa Zeus.” Ni jambo la kinyume kiasi gani kwa mtu aliyeitwa baada ya “zeus” awe kinyume na wale walio safari wakati “Zeus” alikuwa “mlinzi wa hao wasafiri.”

b. Mienendo yake imewekwa wazi katika 3 Yohana 1:9-10 3. Demetrio (mbebaji wa nyaraka za Yohana kwa kanisa lake la mahali)

Page 431: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

415

a. Inaonekana kuwa alikuwa ni mmoja wa wale wamissionari waliokuwa wakisafiri na mbebaji wa nyaraka toka kwa Mtume Yohana wa Efeso.

b. Utaratibu wa kuita “katiba ya Mitume” ilimtaja Demetrio kama Askofu wa Philadephia, ambaye aliteuliwa na Yohana Mtume.

D. Kanisa la awali liling’ang’ana namna gani ya kutathimini na kuwasaidia wale wahubiri/ walimu/ wainjilisti waliokuwa wakisafiri. Moja ya andiko la kanuni zisizo za kanisa la awali la Kikristo lilizoandikwa mwanzoni mwa karne ya pili kwenye machapisho yaliyoitwa The Didache or The Teaching of the Twelve Apostles yana mwongozo huu:

SURA YA XI-KUHUSU WALIMU, MITUME, NA MANABII

“kwa hiyo, yeyote, ajaye na kuwafundisheni mambo haya yaliyosemwa kabla, mpokeeni. Lakini kama mwalimu mwenyewe atabadili na kufundisha mafundisho yaliyo kinyume na haya, msimsikilize; lakini na kama atafundisha kwa ajili ya kuongeza haki na maarifa ya Mungu, mpokeeni kama Bwana. Lakini kuhusu Mitume na Manabii, kutokana na sheria za injili, kwa hiyo fanyeni: ngojeni kila Mtume ajaye kwenu mmupokee kama mlivyompokea Bwana. Lakini asikae siku nyingi isipokuwa moja; lakini pakiwepo na hitaji la yeye kukaa, akae siku ya pili; lakini akiendelea kukaa hadi siku ya tatu, basi huyo ni nabii wa uongo. Na Mtume akiondoka, basi asichukue kitu chochote, isipokuwa mkate mpaka amelala; lakini akiomba pesa, mjue huyo ni nabii wa uongo” (uk. 380). SURA YA XII-UPOKEAJI WA WAPENDWA

“Lakini, yeyote asemaye katika roho kwamba, nipeni pesa, au kitu kingine, msimsikilize; lakini akisema kwa ajili ya kuwasaidia wengine walio wahitaji, asiwepo mtu wa kumhukumu. Lakini kila mmoja ajaye kwa jina la Bwana apokelewe, na baadaye mtathibitisha na kumjua yeye; kwa vile atatambua kulia na kushoto. Kama yule ajaye ni mpitaji/msafiri, msaidieni kwa kadri muwezavyo; lakini hatatakiwa kubaki na ninyi, isipokuwa kwa siku mbili au tatu, kama kutakuwepo na hitaji la kufanya hivyo. Lakini kama atapenda kubaki na ninyi, akiwa ni mhunzi, ngojeni afanye kazi na kula; lakini akiwa hana biashara ya kufanya, kadri ya uelewa wenu muangalieni, kama Mkristo mwenzenu, asikae na ninyi pasipo kitu cha kufanya. Lakini asipofanya hivyo, basi huyo ni mchuuzi wa injili. Angalieni asifanye urafiki katika hilo” (uk. 381).

USOMAJI WA NENO NA KIFUNGU CHA NENO

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) MSTARI WA 1 1Mzee, kwa Gayo mpenzi, nimpendaye katika kweli.

Mst. 1 “Mzee” Neno mzee ni kisawe cha neno “Mchungaji” na “askofu” (k.v. Tit.1:5,7; Mdo. 20:17,28). Angalia muhtasari katika 2 Yohana 1:1

◙ “Nimpendaye” Hii ni tabia za nyaraka za Yohana (k.v. 1 Yohana 2:7; 3:2,21; 4:1,7,11; 3 Yohana 1,2,5,11), lakini halipatikani kama wadhifa wa mwamini katika injili au ufunuo.

◙ “Gayo” Kumekuwepo na majadiliano mengi iwapo Gayo au Diotrepha ni Mchungaji wa kanisa hili la mahali. Ni vigumu kufanya maelezo yeyote ya kung’ang’aniza kutoka katika taarifa hizi ndogo zilizopo. Kwa sababu ya 3 Yohana 1:9, ambapo “kanisa” na “wao” wametajwa, yawezekana kuwa Diotrefe alikuwa ni kiongozi kanisa moja na Gayo alikuwa ni kiongozi wa kanisa jingine ambayo yalikuwa yanakaribiana, lakini hizi zilikuwa ni tetesi tu.

◙ “Nimpendaye katika kweli” “Upendo na ukweli” unapatikana kwa pamoja mara nyingi katika nyaraka za Yohana (k.v 2 Yohana 1,2,3,4; 3 Yohana 1,3,4,8,12). Ukweli unaweza kurejerea

1. Roho Mtakatifu (k.v. Yohana 14:17) 2. Yesu aliye Mwana (k.v. Yohana 8:32; 14:6)

Page 432: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

416

3. Maudhui ya injili (k.v. 1 Yohana 2:2; 3:23)

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) MISTARI 2-4 2Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo. 3 Maana nalifurahi mno walipokuja ndugu na kuishuhudia kweli yako, kama uendavyo katika kweli. 4 Sina furaha iliyo kuu kuliko hii, kusikia ya kwamba watoto wangu wanakwenda katika kweli.

Mst. 2 “Naomba” Hii haswa inafuatisha ufunguzi wa nyaraka za Kiyunani. Ni maombi kwa mafanikio na afya ya wapokeaji. Ilikuwa ni njia ya kumsalimia mpendwa wako. Hili haliwezi kufanyika kama uhakiki wa andiko kwa ajili ya “afya, ufanisi wa injili” ambayo ni maarufu sana katika America ya kisasa. Tazama Gordon Fee (wasomi wenye kipaji), The Disease of the Health, Wealth Gospel. Kwa mtazamo wangu juu ya uponyaji, tafadhari angalia mihtasari yangu katika Yakobo 5 kwenye mtandao www.freebiblecommentary.org.

◙“ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya” Haya kiuhalisia ni maombi ya ufunguzi katika ulimwengu wa Kiyunani na Kirumi wa karne ya kwanza. Haikuwa ikimaanisha kuwa uhakiki wa maandiko kwa ajili ya neno “afya, utajili, na mafanikio” kwa wahubiri. Maandiko ya biblia yaliyoondolewa katika muktadha huu yanaweza kutumika kutetea kitu chochote. Andiko laweza kumaanisha leo kwa kile ambacho hakikuweza kumaanishwa siku hiyo. Mtu yule tu aliyevuviwa ndiye mwandishi wa awali. Lazima tufuate fikra zake, lakini zisiingiliane na za kwetu!

◙ “roho” Neno hili "psuche" (roho) takribani ni kisawe cha neno "pneuma." Yanatumika kurejerea kwenye kiini cha utu. Hii hairejerei juu ya sehemu ya mwili (mwili, nafsi na roho). Wanadamu ni wamoja (k.v Mwa. 2:7). Sisi ni roho; hatuna roho.

Mst. 3 “Narifurahi mno” (k.v. 2 Yohana 4; Flp. 4:10).

◙“Walipokuja ndugu na kuishuhudia kweli yako” Maneno yote mawili yapo katika kauli endelevu ya wakati uliopo ambayo yanadokeza kuwa

1. Waumini wa kanisa hili walisafiri mara kwa mara kwenda Efeso na kutoa taarifa kwa Yohana 2. Wale wamisionari waliorudi walitoa taarifa za ukarimu wa Gayo

Yumkini Yohana, mwenye umri mkubwa, hakuweza kusafiri kwa urahisi, lakini alipendelea kusikia hali na makuzi ya makanisa. ◙ “Kama uendavyo katika kweli” Kifungu hiki kithiolojia kinafanana na “kutembea katika nuru” (k.v 1 Yohana 1:7). Ukristo kimsingi sio sheria, tambiko, au tasisi ya kujiunga, lakini ni maisha uishiyo kwayo katika mahusiano na Kristo Yesu. Kanisa la awali mwanzoni kabisa liliitwa “Njia” (kwanza na Mungu kupitia Kristo ikisababisha upendo kwa mtu na mwezake) tazama Mada Maalum: Kweli katika Yohana 6:55 na 17:3

Mst.4 “Watoto wangu” Huu ni usanifu wa kawaida katika nyaraka za Yohana (k.v. 1 Yohana 2:12,13,18,28; 3:7,18; 4:4; 5:21). Msisitizo hapa uko kwenye (1) mamlaka ya Kitume ya Yohana (2) neno la Yohana juu ya athari kwenye makanisa na Wakristo wa jimbo la Rumi ya Asia Ndogo (Magharibi mwa Uturuki), mahali alipoitumia siku yake ya mwisho ya huduma.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) MISTARI 5-8 5Mpenzi, kazi ile ni ya uaminifu uwatendeayo hao ndugu na hao wageni nao, 6 waliokushuhudia upendo wako mbele ya kanisa; utafanya vizuri ukiwasafirisha kama ipasavyo kwa Mungu. 7 Kwa maana, kwa ajili ya Jina hilo, walitoka, wasipokee kitu kwa Mataifa. 8 Basi imetupasa sisi kuwakaribisha watu kama hao, ili tuwe watenda kazi pamoja na kweli.

Mst. 5 “Kazi ile ni ya uaminifu” Matendo haya ya Gayo ni tofauti kabisa na yale matendo ya Diotrefe katika 2 Yohana mistari ya 9-10. Tazama Mada Maalum: Kuamini, Imani na Uaminifu katika Yohana 1:7 na Yohana 1:14

Page 433: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

417

◙ “Uwatendeayo hao” Hiki ni kiwakilishi rejeshi kikiwa na ean na kauli ya kati tegemezi ya wakati uliopita usiotimilifu ambacho kinaelezea hali yenye mtizamo wa kutimiliza jambo. Gayo aliweza kuwasaidia wamisionari waliokuwa wakisafiri kila wakati na kwa kila njia iwezekanayo. ◙”hasa hao wageni” Kanisa lingalipaswa kuwakalibisha na kuwawezesha hawa wasafiri wa Kimisionari, lakini kwa sababu ya hali ya kawaida, Gayo pekee ndiyo alikuwa akiwasaidia hawa wapendwa ambao hakufahamu habari zao tofauti na zile wengine walizozijua, za kuokolewa, na kumpenda Yesu Kristo. Mst. 6 “Walioushuhudia upendo wako mbele ya kanisa” Hakika kanisa la mwanzo huko Efeso walikuwa na muda wa kusoma ripoti wakati wa ibada.

MADA MAALUM: KANISA (Ekklesia)

Neno hili la Kiyunana, ekklesia, linatokana na maneno mawili, "nje ya"na "kuitwa." Neno hili linatumika kidunia (yaani., jamii iliyoitwa kwenye kikao, k.v Mdo. 19:32,39,41) na kwa sababu ya utumiaji wa maandiko ya kale ya Kiyunani ya neno hili kwa ajili ya “kusanyiko” la Israel (Qahal, BDB 874, KB 1078, k.v. Hes. 16:3; 20:4; Kumb. 31:30),na matumizi ya kidini. Kanisa la mwanzo walijiona wao kama mwendelezo wa Agano la Kale la watu wa Mungu. Walikuwa Waisrael wapya (k.v. Rum. 2:28-29; Gal. 3:29; 6:16; 1 Pet. 2:5,9; Ufu. 1:6), utimilizo wa kusudi la Mungu kidunia (k.v. Mwa. 3:15; 12:3; Kut. 19:5-6; Mt. 28:18-20; Luka 24:47; Mdo. 1:8; angalia Mada Maalum: Mpango wa Ukombozi wa Milele wa YHWH Neno lililotumika kwa maana nyingi katika injili na matendo.

1. Mikusanyiko ya kidunia , Mdo. 19:32,39,41 2. Watu wa Mungu ulimwenguni katika Kristo, Mt. 16:18 na Waefeso 3. Kusanyiko la waumini wa mahali katika Kristo, Mt. 18:17; Mdo. 5:11 (katika aya hii, ni kanisa huko

Yerusalem); Mdo. 13:1; Rum. 16:5; 1 Kor. 16:19; Kol. 4:15; Filemoni uk. 2 4. Watu wa Israel kwa ujumla, Mdo. 7:38, katika hotuba ya Stephano 5. Watu wa Mungu kwenye Miji, Mdo. 8:3; Gal. 1:2 (Yuda au Palestina)

Kanisa ni watu waliokusanyika, na sio jengo. Hapakuwepo na majengo ya kanisa kwa muda wa miaka mingi. Katika Yakobo (moja ya kitabu cha mwanzoni kabisa cha Wakristo) kanisa lilitajwa kwa neno "synagōgē" (kusanyiko). Neno kanisa limetokea tu kwa Yakobo (k.v. Yakobo 2:2; 5:14).

◙ “Utafanya vizuri” Hii ni nahau ya Kiyunani iliyopatikana kwenye mafunjo ya Misri (angalia Moulton na Milligan, The Vocabulary of the Greek Testament) kwa neno "tafadhali" (k.v. Mdo. 10:33). ◙ “ukiwasafirisha” Hii ni nahau ya kiufundi ya uwezeshaji, kuombea, na utoaji wa mahitaji kwa wamisionari wanaosafiri (k.v. Mdo. 15:3; Rum. 15:24; 1 Kor, 16:6; 2 Kor. 1:16; Tit. 3:13). ◙ “Kama ipasavyo kwa Mungu” Hii inamaanisha njia muhimu, yenye upendo, yenye utele (k.v. Kol. 1:10; 1 Thes. 2:12). Waamini wanapaswa kuwatendea watenda kazi wa injili katika namna iwafaayo waitumikiayo (k.v Efe. 4:1) Mst.7 NASB, REB "walitoka" NKJV "waliondoka" NRSV "walianza safari zao" TEV, NJB "waliondoka" Hiki kitenzi cha kawaida kinatumika kwa

1. Walimu wa uongo walioondoka kanisani katika 1 Yohana 2:19 2. Manabii wa uongo waliotawanyika duniani katika 1 Yohana 4:1

Page 434: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

418

3. Wapotoshaji wengi waliotawanyika duniani katika 2 Yohana 1:7 4. Mashahidi wa kweli wa Kitume waliokwenda duniani kote katika 3 Yohana 1:7

NASB "kwa ajili ya jina hilo" NKJV "kwa niaba ya jina hilo" NRSV "kwa ajili ya Kristo" TEV "katika huduma ya Kristo" NJB "kwa ajili ya jina hilo zima"

Huu ni mfano wa “jina” lililosimama kwa niaba ya mtu na kazi ya Yesu Kristo. Kama waumini wanavyo amini katika jina lake (k.v. Yohana 1:12; 3:18; Rum. 10:9; 1 Kor. 12:3; Flp. 2:9-11), wamesamehewa kupitia jina lake (1 Yohana 2:13), pia wanatenda kwa jina lake (k.v. Mt. 10:22; 24:9; Marko 13:13; Luk. 21:12,17; Yohana 15:21; 20:31; Mdo. 4:17; 5:41; 9:14; Rum. 1:5; 1 Pet. 4:14,16; Ufu. 2:3). NASB "wasipokee kitu kwa mataifa" NKJV "wasichukue kitu toka kwa mataifa" NRSV "wasipokee msaada toka kwa wasio amini" TEV "pasipo kukubali msaada toka kwa wasio amini" NJB "pasipo kutegemea kwa wasio amini kitu chochote" Kifungu hiki kinarejerea kwa mashahidi hawa wanaomwamini Mungu kwa utoaji wake, zaidi kama Yesu kwa wanafunzi wake kumi na wawili katika Mathayo 10:5-15 na wale sabini katika Luka 10:4-7 Huu ni utumiaji wa kale wa karne ya kwanza wa neno “watu wa mataifa” kama dokezo kwa wapagani au wasio amini (k.v. Mt. 5:47; 1 Petr. 2:12; 4:3). Waumini walihitajika kuiwezesha kazi ya injili! Yeye asaidiaye huudhihilisha moyo wake.Katika nyakati za Yohana walimu wengi waliokuwa wakisafiri walifundisha juu ya fedha na kuwa na sifa njema. Walimu/wahubiri/ wainjilisti wa Mungu walisitahili kusaidiwa si kwa maneno yao, lakini kwa sababu ya Bwana wao ambaye kazi yake walijitoa kwayo.

Mst. 8 “imetupasa” Hii ni ile inayorudiwa mara kwa mara, onyo la kimaadili (k.v. Yohana 13:14; 19:7; 1 Yohana 2:6; 3:16; 4:11). Neno opheilō linamaanisha kwa wazi kuwa katika deni la kifedha, lakini linakuja tumika kitamathari kulazimika au kudaiwa na mtu.

◙ “Kuwakaribisha watu kama hao” Ukarimu ulikuwa ni wajibu muhimu katika kanisa la mwanzo kwa sababu ya tabia za kimaadili zisizofaa kwa wengi wa watu waliokuwamo (k.v. Mt. 25:35; Rum. 12:13; 1 Tim. 3:2; 5:10; Tit. 1:8; Ebr. 13:2; 1 Pet. 4:9).

◙ “ili kwamba tuwe watendakazi pamoja na kweli” Kama waumini wanavyo wasaidia Wamisionari, ndivyo wanavyojihusisha katika kazi zao za imani na ukweli. Hii ni kanuni ya injili! Mwongozo wa agano jipya kwa utoaji wa Mkristo unapatikana katika 2 Kor. 8-9.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) MISTARI 9-10 9Naliliandikia kanisa neno, lakini Diotrefe, apendaye kuwa wa kwanza kati yao, hatukubali. 10 Kwa hiyo, nikija, nitayakumbuka matendo yake atendayo, atoavyo upuzi juu yetu kwa maneno maovu; wala hatoshwi na hayo, ila yeye mwenyewe hawakaribishi hao ndugu, na wale watakao kuwakaribisha, huwazuia, na kuwatoa katika kanisa.

Mst. 9 “Naliliandikia kanisa neno” Hii yaweza kurejerea kwa 1 Yohana au 2 au kwa waraka uliopotea, kwa uelekeo wote hii inarejea kwa 2 Yohana. Angalia Mada Maalum: Kanisa (Ekklesia) katika Yohana 1:6

Page 435: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

419

◙ “Diotrefe, apendaye kuwa wa kwanza kati yao” Hii ni kauli tendaji endelevu ya wakati uliopo. Ni neno la pamoja kwa neno “upendo” (phileō) na “kushika wadhifa wa kwanza” (prōteuō). Linatumika tu mahali hapa katika Agano Jipya, lakini neno la pili limetumika katika Wakolosai 1:18 juu ya wadhifa wa juu wa Kristo. Mwanaume huyu ndiye wa kwanza aliyewekewa kumbu kumbu kama “mzuiaji wa nguvu” au “mtu mkubwa wa kanisa” hatufahamu kama alikuwa ni mchungaji au mtu wa kawaida tu. Hata hivyo, hii haionyeshi makusudio yake. Hii tabia ya kujiona kama wewe imekuwepo katika kanisa kwa kila rika! Ikiwa kama alikuwa mwenye mafunuo ya uongo haijulikani wala kuelezewa, lakini yawezekana.

James Dunn, Unity and Diversity in the New Testament, uk. 392, inamwangalia Diotrefe kama mfano wa “Mkatoliki wa awali” "Hasa katika, ubinafsi wa Yohana inawezekana akaeleweka vizuri kama mpingaji dhidi ya aina ya urasimishaji wa mienendo iliyo dhahili katika maisha ya uchungaji (juu kur. 129 ikifuatana. k.v. tena Waebrania na Ufunuo - §§31.2, 3). Vivyo hivyo maaandiko ya Yohana, kama kuna kitu kinachoonekana kupingwa kwa aina ya sakaramenti ambacho tayari kilianzishwa na Mkatoriki wa mwanzo Ignatius ('dawa ya zinaa' - Efe., 20.2) (angalia hapo juu §41). Kitu cha kufurahisha hapa kati ya vyote ni namna ‘mzee’ alivyomshambulia Diotrefe katika 3 Yohana 9 na kuendelea. Diotrefe kwa uwazi kabisa alikuwa katika udhibiti wa kanisa: sio tu alikuwa na uwezo wa kukataa kuwakaribisha Wakristo waliokuwa wakiwatembelea, lakini hata kuwafukuza kanisani wale waliokuwa karibu nao. Diotrefe, kwa maneno mengine, alikuwa akitenda kwa mamlaka ya mtawala mkuu askofu (k.v. Ignatius, Efe., 6.1; Trall., 7.2; Smyrn., 8.1), na ilikuwa kinyume na matamanio haya kwa ajili ya msimamo wa kidini na mamlaka (philoprōteuōn) yale ambayo ‘mzee’ aliandika. Kwa maneno mengine, tukifikiria kuwa 3 Yohana imekuja toka kwenye mazingira yale yale ya 1na 2 Yohana, ni vizuri tukaona kama wajibu wa aina ya mageuzi ya Ukristo, kinyume na urasimishaji na ubinafsi wa kumcha Mungu, ukipinga dhidi ya ushawishi unaoongezeka wa ukatoriki wa mwanzo."

◙ “Hatukubali uyasemayo” Sio tu Diotrefe alikataa mamlaka ya kitume, lakini alikuwa alihusika kishari kukataa sera za kitume na hata kulipiza kisasi kwa wale watakao mgasi! Mst. 10 “kama” Hii ni sentesi shurutishi daraja la tatu ikimaanisha juu ya tendo muhimu. ◙ “Nitayakumbuka matendo yake atendayo” Yohana anahitaji kwa wazi kabisa kuelezea haya makusudio ya mtu (k.v. 3 Yohana 1:9) na matendo (k.v. 3 Yohana 1:10):

1. NASB -- "atoavyo upuuzi juu yetu kwa maneno maovu" NKJV -- "akitupakazia maneno machafu" NRSV -- "akieneza lawama dhidi yetu" TEV -- "akinena vitu vya ajabu kutuhusu na kusema uongo" NJB -- "mashitaka ya uovu yaliyoenezwa dhidi yetu" 2. "Yeye mwenyewe hawakaribishi hao ndugu" 3. "Huwazuia wale watakao kuwakaribisha" 4. "Huwatoa hata kanisani"

Mtu huyu alitaka pawepo na tahadhali na hakushiriki katika kuangalia na mwingine. Pia aliondoa yeyote toka kanisani ambaye hakukubaliana naye. ◙ “Huwatoa hata kanisani” Hiki kitenzi chenye nguvu (ekballō) pia kimetumika katika Yohana 9:34,35 kwa yule mtu kipofu ambaye Yesu alimponya baada ya kufukuzwa hekaluni. Pia kimetumiwa kwa shetani baada ya kufukuzwa katika Yohana 12:31

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) MISTARI 11-12 11 Mpenzi, usiuige ubaya, bali uige wema. Yeye atendaye mema ni wa Mungu, bali yeye atendaye mabaya hakumwona Mungu. 12 Demetrio ameshuhudiwa na watu wote, tena na ile kweli yenyewe. Nasi pia

twashuhudia, nawe wajua ya kwamba ushuhuda wetu ni kweli.

Page 436: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

420

Mst. 11 “Usiuige ubaya” Hii ni kauli ya kati (enye ushahidi) shurutishi ya wakati uliopo ambayo mara nyingi inamaanisha kuzuia kitendo kilichoko kwenye mchakato. Tunapata neno la kiingereza “mimic” toka kwa neno la Kiyunani (mimeomai). Lazima tuchague kwa uangalifu watu wa kuwaiga. Wanastahili kuwa wakristo waliokomaa katika kanisa (k.v. 2 Thess. 3:7,9; Heb. 6:12; 13:7). Demetrio ni mfano mzuri, Diotrefe ni mfano mbaya. ◙ ”Yeye atendaye mema ni wa Mungu” Nyaraka za Yohana zina majaribu matatu ambayo yaweza kumfanya mtu ajijue kuwa ni Mkristo. Hili linarejea kwenye jaribu la utii (kama vile 1 Yohana 2:3-6,28-29; 3:4-10; 5:18; 2 Yohana 6). Pia kuna vidokezo vya mengine mawili (1) mafundisho (3 Yohana 1:3-4) na (2) upendo (3 Yohana 1:1-2,6).

◙ “Yeye atendaye mabaya hakumwona Mungu” Walimu wa uongo walidai kumjua Mungu kwa undani lakini waliishi maisha yasiyo ya Ki-Mungu wala sio ya upendo. Hii inaaksi wale wenye misimamo, wale wasio na mafunuo walio amini kuwa wokovu ulikuwa ni ukweli wa kufikirika uliohitajika kuthibitishwa lakini haukuwa na uhusiano wowote na maisha ya kila siku.

Mst. 12 “Demetrio ameshuhudiwa na watu wote” Hii ni kauli timilifu tendewa inayo arifu. Kiukweli hii inaonyesha kuwa waraka wa mapendekezo wa Yohana kwa Gayo kuhusu Mmisionari Demetrio, ambaye huenda alimkabidhi 3 Yohana kwa Gayo. Kwa mapendekezo ya nyaraka zingine katika Agano Jipya, angalia Mdo. 18:27; Rum. 16:1; 1 Kor. 16:3; 2 Kor. 3: 1; 8:16-24; Kol. 4:10.

◙ “Tena na ile kweli yenyewe” Kweli (angalia Mada Maalum katika Yohana 6:55 na 17:3 na Mada ni mfano halisi mwingine wa kushuhudia ushuhuda mzuri kwa Demetrio

◙ “Nawe wajua ya kwamba ushuhuda wetu ni kweli” Yohana anatetea uaminifu wake binafsi wa ushuhuda kwa Kristo (k.v. Yohana 19:35; 21:24).

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) MISTARI 13-14 13 Nalikuwa na mambo mengi ya kukuandikia, lakini sipendi kukuandikia kwa wino na kalamu. 14 Lakini nataraji kukuona karibu, nasi tutasema uso kwa uso. [15] Amani kwako. Rafiki zetu wakusalimu. Wasalimu hao rafiki zetu, kila mtu kwa jina lake.

Mst. 13 Huu unafanana na 2 Yohana 12.

ANDIKO LA NASB (LILILOBORESHWA) MSTARI 14b 14bAmani kwako. Rafiki zetu wakusalimu. Wasalimu hao rafiki zetu, kila mtu kwa jina lake.

Mst. 14 “Amani kwako” Dhahiri hili ni rejeo toka kwa nahau ya Kiebrania shalom (k.v Luk. 10:5). Yaweza kumaanisha “aisee” au “kwa heri.” Inaelezea sio tu kutokuwepo na matatizo lakini pia kuwepo kwa Baraka za Mungu. Haya yalikuwa ni maneno ya kwanza ya Yesu baada ya ufufuo kwa wanafunzi wake katika chumba cha juu ghorofani (k.v. Yohana 20:19,21,26). Wote Paulo (k.v. Efe. 6:23) na Petro (k.v. 1 Petr. 5:14) waliyatumia haya kama maombi ya kufungia kwa watu wa Mungu. ◙ “Kwa jina lake” Hii ni nahau kwa ubinafsi, mtu binafsi, na kwa upendo. Mara nyingi ilitumika katika mafunjo ya ki-Misri.

MASWALI YA MJADALA

Huu ni mwongozo wa fasiri, ina maanisha kwamba unawajibika kwa tafsiri zako mwenyewe za Biblia. Kila mmoja wetu lazima atembee katika mwanga tulio nao. Wewe, Biblia, na Roho Mtakatifu ni vipaumbele katika tafsiri. Hutakiwi uvitelekeze vitu hivi kwa mfasiri.

Page 437: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

421

Maswali ya mjadala huu yanatolewa kukusaidia kufikiri juu ya mambo makubwa ya sehemu za kitabu hiki. Yanalenga kukuamsha kimawazo na sio kutoa maana

1. Pamekuwepo na nadharia nyingi kwa nini Gayo na Diotrefe hawakuwa pamoja mara kwa mara. Baadhi wanatoa maoni kuwa huenda ni a. kwa sababu ya kithiolojia b. sababu ya kijamii c. sababu ya mambo ya kidini d. sababu ya mambo ya kiuadilifu

Elezea kila moja ya sababu na kwwa namna gani zinaweza husiana na 3 Yohana. 2. Ni kwa vipi 2 Yohana na 3 Yohana zinahusiana? 3. Orodhesha majaribu matatu kwa ajili ya uhakika wa Mkristo yanayopatikana katika 1 Yohana ambayo

yanajirudia katika 2 Yohana na 3 Yohana.

Page 438: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

422

MAELEZO MAFUPI YA ISTILAHI ZA VISARUFI VYA KIYUNANI

Lugha ya kawaida ya Koine mara nyingi inafahamika kama Kiyunani kilichobobea, ilikuwa ni lugha ya kawaida ya

ulimwengu wa Meditarania ilianzishwa na Alexanda mkuu (336-323 K.K) na ikadumu mpaka miaka ya (300 K.K-

500 B.K.). Haikuwa rahisi, Kiyunani kuwa cha daraja la juu, lakini kwa njia nyingi ni dhana ya Kiyunani ambayo

ilikuja kuwa lugha ya pili karibu na mashariki ya kale na ulimwengu wa Mediterania.

Kiyunani cha Agano Jipya kilikuwa ni cha kipekee kwa njia kadhaa kwa watumiaji wake, isipokuwa Luka mwandishi

wa kitabu cha Waebrania, yamkini alitumia lugha ya Kiarama kama lugha ya msingi. Kwa hiyo, uandishi wao

uliathiliwa na dhana ya muundo wa Kiarama. Pia, walisoma na kunukuu wandishi wa maandiko ya kale (tafasiri ya

Kiyunani ya maandiko ya kale) ambayo pia yaliandikwa kwa lugha ya Koine. Lakini maandiko ya kale pia

yaliandikwa kwa wasomi wa Kiyahudi ambao lugha yao ya asili ilikuwa sio ya Kiyunani.

Hii ilisaidia kuwa kama kumbukumbu ambayo haiwezi kulipeleka Agano Jipya kwenye muundo mgumu wa kisarufi.

Ni wa kipekee na bado una mambo mengi yaliyo pamoja na (1) maandiko ya kale (2) maandiko ya kale kama yale

ya Yusufu na (3) mafunjo yaliyopatikana Misri. Kwa hiyo tunakabilianaje na uchambuzi wa visarufi vya Agano

Jipya.

Muundo wa kisarufi wa lugha ya Koine na Agano Jipya la lugha ya Koine ulibadilika. Kwa njia tofauti ulikuwa ni

urahisishaji wa sarufi. Mazingira ndio yatakuwa mwongozo wetu mkuu. Maneno pekee yana maana katika

upanuzi wa mazingira, kwa hiyo, muundo wa kisarufi unaweza tu kueleweka katika mwanga wa (1) aina mahsusi

ya mwandishi, na (2) mazingira mahsusi

Hapana hitimisho la fasiri ya dhana na muundo wa Kiyunani unaowezekana. Kimsingi lugha ya Koine ilikuwa ni

lugha ya maneno tu. Mara nyingi msingi wa utafasiri ni aina na dhana ya maneno. Mara nyingi vishazi vikuu

hutokea kwanza, vikionyesha kushinda vingine vyote. Katika kueleza kitenzi cha Kiyunani, vipande vitatu vya

habari lazima vizingatiwe (1) kiini cha msisitizo wa njeo, sauti na dhamira (tukio au umbo); (2) kiini cha maana

husika ya kitenzi (usawidi kamusi); na (3) mtiririko wa mazingira yenyewe (isimu ya mpangilio wa maneno)

I. NJEO

A. NJEO au sura inajumuisha uhusiano wa VITENZI ili kukamilisha kitendo au kutokamilisha kitendo. Mara

nyingi huitwa “utimilifu” au “utoutimilifu”

1. Njeo timilifu zinaangazia juu ya utoaji wa kitendo. Hakuna taarifa nyingine zilizotolewa isipokuwa ya

kile kilichotokea! Kuanza kwake, mwendelezo au ukomo wake haukueiezwa.

2. Njeo zisizo timilifu zinaangazia juu ya mchakato endelevu wa kitendo. Zinaweza kuelezewa dhidi ya

unasaba wa kitendo, kudumu kwa kitendo, mwendelezo wa kitendo, n.k.

B. Njeo zaweza kugawanywa kwa jinsi mwandishi anavyoona kitendo kinavyoendelea.

1. Kimetokea-KITENZI TIMILIFU

2. Kilivyotokea au matokeo yake-KITENZI CHA WAKATI ULIOPITA

3. Kilivyokuwa kikitokea nyuma na matokeo yake yakastahimili, lakini sio sasa-KITENZI CHA WAKATI

ULIOPITA TIMILIFU

4. Kinatokea –WAKATI ULIOPO

5. Kilikuwa kikitokea- WAKATI USIOTIMILIFU

6. Kitatokea –WAKATI UJAO

Mfano thabiti wa jinsi njeo hizi zinasaidia katika utafasiri ungalikuwa wa neno “okoa.” Lilitumika katika NJEO

nyingi tofauti kuonyesha kwa pamoja mchakato na ukomo.

1. KITENZI CHA WAKATI TIMILIFU- “okolewa” (Rum 8:24)

Page 439: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

423

2. KITENZI CHA WAKATI ULIOPITA- “ameokolewa na matokeo yake yanaendelea” (Efe 2:5,8)

3. KITENZI CHA WAKATI ULIOPO- “anaokolewa” (kama vile 1Kor 1:18; 15:2)

4. KITENZI CHA WAKATI UJAO- “ataokolewa” (kama vile Rum 5:9,10; 10:9)

C. Katika kuzingatia juu ya VITENZI VYA NJEO, mfasiri huangalia sababu za mwandishi wa kwanza alichagua

kuelezea yeye binafsi NJEO fulani. Tarajio la NJEO “hakuna madoido” lilikuwa ni la KITENZI CHA WAKATI

TIMILIFU. Kilikuwa ni muundo wa KITENZI cha kawaida “kisichoainishwa” “kisichotambulika”

“kisichochoka.” Chaweza tumika katika Nyanja pana ambamo mazingira lazima yaelezee. Kwa kawaida

kilikuwa kinaelezea kuwa kitu fulani kimetendeka. Sura ya muda uliopita ulikusudia tu katika DHAMIRA

ELEKEZI. Kama pana NJEO nyingine zilizotumika, uainishaji wa kitu fulani ulikuwa unasisitizwa. Lakini ni

nini?

1. NJEO YA WAKATI ULIOPITA. Hii inaongelea juu ya tendo lililokwisha tendeka na matokeo yakiendelea

kuwepo. Katika namna fulani ilikuwa ni muunganikano wa NJEO ZA WAKATI TIMILIFU na ZA WAKATI

ULIOPITA. Mara kwa mara mlengo ulikuwa juu ya matokeo yalioendelea kuwepo au kumalizika kwa

kitendo. Mfano: Efe 2:5 & 8, “umekuwa na unaendelea kuokolewa.”

2. NJEO YA WAKATI ULIOPITA AINISHI. Hii ilikuwa kama njeo ya WAKATI ULIOPITA isipokuwa matokeo

yalishakoma. Mfano: “Petro alikuwa akisimama nje mlangoni” (Yoh 18:16)

3. NJEO YA WAKATI ULIOPO. Hii inazungumzia juu ya kitendo kisichokiwisha au kisichotimilifu. Mtizamo

mara nyingi ni juu ya uendelezaji wa tukio. Mfano: “kila mmoja ashikamanae ndani yake haendelei

kutenda dhambi”, “kila mmoja aliyesamehewa na Mungu haendelei kutenda dhambi” (1Yoh 3:6 & 9).

4. NJEO YA WAKATI USIOTIMILIFU. Katika njeo hii uhusiano na NJEO YA WAKATI ULIOPO ni mwendelezo

wa uhusiano kati ya WAKATI ULIOPITA na WAKATI ULIOPITA AINISHI. WAKATI USIOTIMILIFU

unaongea juu ya kitendo ambacho hakijaisha kutendeka ambacho kilikuwa kinatokea lakini sasa

kimekoma au mwanzo wa kitendo awali. Mfano: “kwa hiyo Yerusalemu yote waliendelea kumwacha”

au “ Yerusalemu yote wakaanza kumwacha”(Mt3:5)

5. NJEO YA WAKATI UJAO. Hii inaongelea juu ya kitendo ambacho kawaida kilijitokeza ndani ya muda

mwafaka. Inaangazia juu ya umuhimu wa jambo kutokea kuliko utokeaji wa uhalisia. Mara nyingi

unazungumzia juu ya ualakini wa tukio. Mfano: “Heri wale….wata...”(Mt 5:4-9).

II IRABU

A. Irabu inaelezea mahusiano kati ya kitendo cha KITENZI na KIIMA

B. IRABU TENDAJI ilikuwa ni njia ya kawaida, tarajiwa, isiosisitiza utetezi wa kwamba kiima kilikuwa

kikitenda kitendo cha KITENZI.

C. IRABU TENDEWA ina maana kuwa KIIMA kilikuwa kikipokea kitendo cha KITENZI kilichotolewa na mtu

wan je. Mtu wa nje anayetoa kitendo alionyeshwa katika Agano Jipya la Kiyunani kwa mambo na

VIHUSISHI vifuatavyo:

1. Mtu binafsi wa moja kwa moja wa hupo kukiwa na UHUSIKA WA KUONDOA (kama vile Mt 1:22; Mdo

22:30)

2. Mtu binafsi wa kati na dia kukiwa na UHUSIKA WA KUONDOA (kama vile Mt 1:22)

3. Mtu wa kawaida asiyehusika na en kukiwa na UHUSIKA WA JAMBO

4. Wakati mwingine ni mtu binafsi au asiyehusika kukiwa na UHUSIKA WA JAMBO pekee.

D. IRABU YA KATI inamaanisha kuwa KIIMA kinatoa tendo la KITENZI na pia moja kwa moja kinahusishwa

katika kitendo cha KITENZI. Mara nyingi huitwa irabu ya kurefusha matakwa binafsi. Muundo huu

unasisitizia KIIMA cha kishazi au sentesi kwa namna nyingine. Muunganikano huu haupatikani katika

Kiingereza. Una uwezekano mpana wa maana na ufasiri katika Kiyunani. Baadhi ya mifano ya dhana hizi

ni;

Page 440: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

424

1. YENYE KUJIREJEA – kitendo cha moja kwa moja cha kiima chenyewe. Mfano: “kajiangika mwenyewe”

(Mt 27:5)

2. YENYE KUTIA MKAZO- kiima kinazaa kitendo chake chenyewe. Mfano: “shetani mwenyewe anajifanya

kama malaika wa nuru” ( 2Kor 11:14)

3. Kukubaliana – mwingiliano wa viima viwili. Mfano: “walishauliana wao kwa wao” (Mt 26:4)

III. DHAMIRA (au “NAMNA”)

A. Kuna namna nne za DHAMIRA katika lugha ya Koine. Zinaashiria uhusiano wa KITENZI kuwa kweli, haswa

ndani ya wazo la mwandishi mwenyewe. DHAMIRA hizi zinagawanyika katika namna pana mbili: ile

inayoonyesha ukweli (ELEKEZI) na ile inayoonyesha umuhimu (UTEGEMEZI, KUAMURU/KUSHURUTISHA

na HALI Y A UCHAGUZI).

B. DHAMIRA ELEKEZI ilikuwa ni NAMNA ya kawaida ya kuelekeza kitendo ambacho kimekwisha tokea au

kilikuwa kinatokea, haswa kwenye wazo la mwandishi. Ilikuwa namna pekee ya Kiyunani ya kueleza

ukomo wa muda na hata hapa sura hii ilikuwa daraja la pili.

C. DHAMIRA TEGEMEZI kinaelekeza yumkini kitendo kitakachotokea mbeleni. Kitu fulani ambacho

hakijawahi tokea lakini nafasi ya kutokea ingaliwezekana. Ina vitu vingi vinavyofanana na KITENZI CHA

WAKATI UJAO ELEKEZI. Utofauti ni kuwa UTEGEMEZI unaelezea kiwango fulani cha mashaka. Katika

Kiingereza hii mara nyingi inaelezewa na neno “ingalikuwa”, “ingaliweza”, “yawezekana” au “yenye

uwezo”.

D. DHAMIRA YA UCHAGUZI inaelezea utashi ambao kinadharia unawezekana. Ilifikiliwa ni hatua moja mbele

kutoka katika ukweli kuliko HALI YA UTEGEMEZI. HALI YA UCHAGUZI inaelezea uwezekano chini ya hali

fulani. HALI YA UCHAGUZI ilikuwa ni nadra katika Agano Jipya. Utumikaji wake mara nyingi kilikuwa ni

kifungu maarufu cha Paulo. “yawezekana isiwe” (KJV, Mungu anakataza), kimetumika mara kumi na tano

(kama vile Rum 3:4,6,31; 6:2,15; 7:7,13; 9:14; 11:1,11; 1Kor 6:15; Gal 2:17; 3:21; 6:14) mfano mwingine

unapatikana katika Thes 1:38, 20:16, Mdo 8:20 na 1Thes 3:11

E. DHAMIRA SHURUTISHI inasisitizia juu ya amri ambayo iliwezekana, lakini msisitizo ulikuwa juu ya dhamira

ya mnenaji. Inatetea juu ya uwezekano wa hiari na ilishurutishwa juu ya chaguzi za wengine. Kulikuwa na

matumizi ya kipekee ya HALI YA KUSHURUTISHA katika maombi na hitaji la mtu wa tatu. Amri hizi

zinapatikana tu katika WAKATI ULIOPO na njeo ya WAKATI TIMILIFU katika Agano Jipya.

F. Baadhi ya visarufi vinabainisha VIAMBATA kama moja aina ya NAMNA. Ni vya kawaida katika Agano Jipya

la Kiyunani, mara nyingi vikielezewa kama KIVUMISHI CHA TENDO. Vinatafasiriwa kama muunganiko wa

VITENZI vikuu ambavyo vinafanana. Tofauti pana iliwezekana katika utafasiri wa viambata. Ni vizuri

kuzirejea tafasiri nyingi za Kiingereza. The Bible in Twenty Six Translation kilichochapishwa na Baker ni

msaada mkubwa hapa.

G. KITENZI TENDAJI TIMILIFU ELEKEZI kilikuwa ni njia ya kawaida au “kisichotambulika” cha Kuingiza

matokeo. Njeo nyingine, irabu au zilikuwa na ufasiri mahususi ambao mwandishi wa kwanza alihitaji

kuwasilisha.

IV. Kwa mtu ambaye hayuko na uzoefu na lugha ya kiyunani, msaada wa usomaji unaofuata utatoa taarifa inayohitajika;

A. Friberg, Barbara na Timothy. Analytical Greek New Testament. Grand Rapids: Baker 1988

B. Marshall, Alfred. Interlinear Greek-English New Testament. Grand Rapids: Zondervan 1976

C. Mounce, William D. The Analytical Lexicon to the Greek New Testament. Grand Rapids: Zondervan 1993

D. Summer Ray. Essential of the New Testament Greek Nashville: Broadman 1950

E. Kitaaluma mtangamano wa kozi ya lugha ya Koine unapatikana kupitia taasisi ya Moody Bible iliyoko

Chikago II

Page 441: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

425

V. NOMINO

A. Ki-isimu, NOMINO zinaainishwa kwa jambo. Jambo ni lile lililoshurutisha dhana ya NOMINO ambayo

ilionyesha kuwa na uhusiano na KITENZI na sehemu nyingine ya sentesi. Katika lugha ya Koine kazi nyingi

za uhusika zilionyeshwa na VIHUSISHI. Tangu dhana ya uhusika iliweza kutambua tofauti ya mahusiano

mbali mbali, VIHUSISHI vilitokea kutoa utengano mzuri wa kazi hizo.

B. Uhusika wa Kiyunani uliainishwa kwa njia nane zifuatazo;

1. UHUSIKA WA KIIMA ulitumika kwa ajili ya kutaja na kawaida kilikuwa ni kiima cha sentesi au kishazi.

Pia ilitumika kwa NOMINO ARIFU na VIVUMISHI vikiunganishwa na VITENZI “kuwa” au “kufaa”

2. UHUSIKA MILIKISHI ulitumika kwa ajili ya kuelezea na kawaida ulitoa kivumishi au thamani ya

nenolililofanana nalo. Ulijibu swali, “aina gani?” mara nyingi ulielezewa na utumiaji wa KIHUSISHI cha

Kiingereza “ya/za”

3. UHUSIKA WA KUONDOA ulitumia dhana ile ile ya kushurutisha kama ya UMILIKISHI, lakini ulitumika

kuelezea utenganifu. Kawaida ulidokeza utengano wa alama kwenye muda, nafasi, kiini, chanzo au

degrii. Mara nyingi ulielezewa na matumizi ya KIHUSISHI cha Kiingereza “kutoka”.

4. UHUSIKA WA WAKATI ulitumika kuelezea matwaka ya mtu binafsi. Hii ingalidokeza mtizamo chanya

au hasi. Mara nyingi hiki kilikuwa si kitu cha moja kwa moja. Mara nyingi ulielezewa na KIHUSISHI cha

Kiingereza “ya”.

5. UHUSIKA WA MAHALI ilikuwa dhana shurutishi ya WAKATI, lakini ilielezea mahali au eneo kwenye

nafasi, muda au ukomo. Mara nyingi ulielezewa na KIHUSISHI cha Kiingereza “ndani, juu, ni, kati, kwa,

juu ya na mbali na”

6. UHUSIKA WA KUTUMIKA ilikuwa ni dhana shurutishi kama uhusika wa WAKATI na MAHALI. Unaelezea

namna au uhusiano. Mara nyingi ulielezewa na KIHUSISHI cha Kiingereza cha neno “kwa” au “enye”

7. UHUSIKA WA KUSHUTUMU ulihusika kuelezea hitimisho la kitendo. Unaelwzea ukomo. Haswa

utumikaji wake ulikuwa kwenye dhana ya moja kwa moja. Ulijibu maswali “kwa umbali gani” au “kwa

namna gani”

8. UHUSIKA WA KAULI ulitumika kuelezea moja kwa moja.

VI. VIUNGO NA VIUNGANISHO

A. Kiyunani ni lugha sahihi kwa sababu ina viunganishi vingi. Viunganisho fikra ( vishazi, sentesi na aya). Ni

vya kawaida kwamba utouwepo wao mara nyingi unakuzwa. Kama jambo la uhakika, viunganisho na

viungo hivi vinaonyesha muelekeo wa fikra za mwandishi. Mara nyingi ni vya maana kupima ni kipi haswa

anajaribu kukiwakilisha.

B. Hapa pan orodha ya baadhi ya viunganishi na viungo na maana zake (taarifa hizi zimekusanywa haswa

toka kwa H.E Dana na Julius K. Mantery. A Manual Grammar of the Greek New Testament

1. Viunganishi vya wakati

(a) epei, epedē,hopote, hōs, hote, hotan (TEGEMEZI)- “lini”

(b) heōs- “wakati”

(c) hotan, epan (TEGEMEZI)- “kila, wakati wowote”

(d) heōs, achri, mechri (Tegemezi)- “mpaka”

a. priv (kitenzijina)- “kabla”

b. hōs- “tangu”, “lini”, “kama”.

2. Viunganishi venye mantiki

a. Kusudi/dhumuni

1) hina (TEGEMEZI) hopōs (TEGEMEZI) hōs- “ya kwamba”, “kuwa”

2) hōste(KIUNGO SHUTUMU KISICHO NA UKOMO)- “kuwa”

Page 442: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

426

3) pros(KIUNGO SHUTUMU KISICHO NA UKOMO) au eis (KIUNGO SHUTUMU KISICHO NA

UKOMO)- “kuwa”

b. Tokeo (kuna uhusiano wa karibu kati ya kusudio la dhana ya kisarufi na tokeo)

(1) hōste(ISIYO NA KIKOMO, hasa hiki ni cha kawaida)- “ili kwamba”, “hivyo”

(2) hiva(TEGEMEZI)- “ya kwamba”

(3) ara- “kwa kiasi hicho”

c. Chanzo au sababu

1) gar(chanzo/athari au sababu/hitimisho)- “kwa”, “kwa sababu ya”

2) dioti, hotiy- “kwa sababu ya”

3) epei, epeidē, hōs- “tangu”

4) dia(ikiwa na SHUTUMA) na (ikiwa na KIUNGO KISICHO NA UKOMO)- “kwa sababu ya”

d. Maamuzi

(1) ara, poinun, hōste- “kwa hiyo”

(2) dio(KIUNGO HITIMISHO chenye nguvu)- “kwa sababu ipi”, “kwa nini”, “kwa hiyo basi”

(3) oun- “kwa hiyo basi”, “kwa kiasi hicho”, “hatimaye”, “hivyo basi”

(4) tinoun- “kufuatana na”

e. –a kinyume au tofauti

(1) alla( yenye KINYUME thabiti)-“lakini”, “isipokuwa”

(2) de- “lakini”, “ingawa”, “bado”, “kwa upande mwingine”

(3) kai- “lakini”

(4) mentoi, oun- “ingawa”

(5) plēn- “hata hivyo” (haswa katika Luka)

(6) oun- “ingawa”

f. Ulinganifu

(1) hōs,kathōs (ingiza vishazi linganifu)

(2) kata(kwa muunganiko, katho, kathoti, kathōsper, kathaper)

(3) hasos(katika Kiebrania)

(4) ē- “kuliko”

g. Enye mlolongo au mtiririko

(1) de- “na”, “sasa”

(2) kai- “na”

(3) tei- “na”

(4) hina, oun- “kile”

(5) oun- “kasha”(katika Yohana)

3. Matumizi yenye mkazo

a. alla- “kwa hakika”, “naam”, “kwa kweli”

b. ara- “hakika”, agharabu”, “kweli”

c. gar- “lakini kweli”, “agharabu”, “hakika”

d. de- “hakika”

e. ean- “hata”

f. kai- “hata”, “hakika”, “kweli”

g. mentoi- “hakika”

h. oun- “kweli”, “kwa hali zote”

VII.

Page 443: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

427

A. SENTESI SHURUTISHI ni ile iliyo na kishazi kimoja au zaidi. Muundo huu wa kisarufi unaongeza utafasiri

kwa sababu unatoa amri, sababu au chanzo kwa nini kitendo cha KITENZI kikuu kimetokea au

hakikutokea. Palikuwa na aina nne za sentesi shurutishi. Zilitoka kwa zile zilizofikiriwa kuwa kweli toka

kwa mtizamo wa mwandishi au kwa kusudio lake kwa lile alilokuwa na utashi nalo.

B. SENTESI SHURUTISHI DARAJA LA KWANZA ilielezea kitendo au kile kilichofikiliwa kuwa kweli toka kwa

mtimamo wa mwandishi au kusudio lake. Ingawa ilielezewa kwa neno “kama.” Katika mazingira tofauti

lingeweza kutafasiriwa “tangu”(cf. Mt 4:3, Rum 8:31). Ingawa hii haimaanishi kudokeza kuwa MADARAJA

YA KWANZA yote ni ya kweli. Mara nyingi yalitumika kuweka alama kwenye hoja au kuangazia kosa(cf. Mt

12:27)

C. SENTESI SHURUTISHI DARAJA LA PILI mara nyingi huitwa “inayopingana na ukweli”. Inaelezea kitu

ambacho kilikuwa ni cha uongo kwenye ukweli wa kufanya jambo. Mfano:

1. “kama kweli alikuwa nabii, ambapo sio, alikuwa sasa nani na mwanamke wa tabia gani anaye

mng’ang’ania yeye, lakini hawezi (Thess 7:39)

2. Kama kweli Musa, lakini hamkumwamini, mngaliniamini na mimi lakini hamkuniamini (Yoh 5:46)

3. Kama ningalitaka kuwapendezesha wanadamu lakini sivyo, nisingalikuwa mtumwa wa Christo hata

sasa(Gal 1:10)

D. DARAJA LA TATU linaongelea juu ya tukio lijalo ambalo laweza kutokea. Mara nyingi unafikirika

uwezekanao wa kitendo kutokea. Kawaida inaashiria tahadhari. Kitendo cha KITENZI kikuu ni tahadhari

juu ya tendo la kishazi “hiki”. Mfano toka 1Yoh 1:6-10; 2:4,6,9,15,20,21,24,29; 4:20; 5:14,16

E. DARAJA LA NNE ni daraja la mbali lililoondolewa kwenye uhakika. Ni adimu katika Agano Jipya. Kama

jambo la kweli, hakuna SENTESI SHURUTISHI DARAJA LA NNE lililokamilika ambamo pande zote za jambo

zinastahili maelezo. Mfano wa DARAJA LA NNE ni ufunguzi wa kishazi katika 1Pet 3:14. Mfano wa sehemu

DARAJA LA NNE ni katika kuhitimisha kishazi katika Mdo 8:31.

VIII. VIZUIZI

A. KITENZI CHA KUAMURU CHA WAKATI ULIOPO kikiwa na KIAMBATA MĒ mara nyingi (lakini hakitengwi)

kina msisitizo wa kusimamisha tendo ambalo liko kwenye mchakato. Baadhi ya mifano: “msijiwekee

hazina yenu duniani………….”(Mt 6:19); “msisumbukie maisha yenu……….” ( Mt 6:25); “wala msiendelee

kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi…….”(Rum 6:13); “wala msimhuzunishe Yule

Roho Mtakatifu wa Mungu (Efe 4:30) na “tena msilewe kwa mvinyo…………………”(Ef 5:18)

B. KITENZI TEGEMEZI TIMILIFU kina mkazo wa “udhahanifu au mwanzo wa kutenda kitendo” baadhi ya

mifano: “msidhani ya kuwa……..”(Mt 5:17); “msisumbuke………”(Mt 6:31); “msiuonee haya………..”(2Tim

1:8)

C. KITENZI HASI CHENYE JOZI kikiwa na DHAMIRA TEGEMEZI ni chenye msisitizo hasi. “kamwe, katu” au “kwa

hali yeyote ile”. Baadhi ya mifano: “kamwe, hataonja mauti………”(Yoh 8:51); “hakika, kamwe………..”(1Kor

8:13)

XI

A. Katika lugha ya Koine, KIBAINISHI CHA WAZI cha neno “wale, Yule,ile” kina matumizi mfanano na kwenye

Kiingereza. Kazi yake kuu ilikuwa ni ya “muonyeshwaji”, ni njia ya kukamata hisia ya neno, jina au kirai.

Utumiaji unatofautiana kati ya mwandishi na mwandishi kwenye Agano Jipya. KIBAINISHI CHA WAZI pia

chaweza kutenda

1. Kama chombo cha kutofautisha mfano cha kuonyesha

2. Kama alama ya kurejea KIIMA kilichowekwa awali au mtu

3. Kama njia ya kutambua kiima kwenye sentesi kikiwa na KITENZI kinchounganisha. Mfano: “Mungu ni

Roho” Yoh 4:24, “Mungu ni nuru” 1Yoh 1:5; “Mungu ni upendo” 4:8,16

Page 444: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

428

B. Lugha ya Koine haina KIBAINISHI KISICHO CHA WAZI kama ilivyo kwenye Kiingereza cha neno “a” herufi ya

kwanza ya alfabeti au “an” mbadala wa “a” kwenye irabu zinazoanza na herufi kama “e”, “h”.

Kutokuwepo na KIBAINISHI CHA WAZI chaweza kumaanisha;

1. Mlengo juu ya tabia au thamani ya kitu

2. Mlengo juu ya aina ya kitu

C. Waandishi wa Agano Jipya walitofautiana sana kwa jinsi KIBAINISHI kilivyotumiwa.

X NJIA ZA KUONYESHA MKAZO KWENYE AGANO JIPYA LA KIYUNANI

A. Mbinu za kuonyesha msisitizo zinatofautiana toka kwa mwandishi mmoja hadi mwingine kwenye Agano

Jipya. Waandishi waendelezaji na warasimishaji walikuwa ni Luka na mwandishi wa Waebrania.

B. Mwanzo kabisa tumesema ya kuwa KITENZI TENDAJI TIMILIFU ELEKEZI kilikuwa ni kipimo na

kisichoangaliwa kwenye msisitizo, lakini njeo nyingine, irabu au dhamira zina umuhimu wa ufasiri. Hii sio

kumaanisha kuwa KITENZI TENDAJI TIMILIFU ELEKEZI mara nyingi hakikutumika kwenye umakinishaji wa

kisarufi. Mfano: Rum 6:10 (mara mbili)

C. Upangiliaji wa neno kwenye lugha ya Koine.

1. Lugha ya Koine ilikuwa ni lugha ngumu isiyo tegemezi, kama vile Kiingereza, kwenye mpangilio wa

maneno. Kwa hiyo mwandishi angaliweza kutofautiana kwenye mpangilio wa kawaida aliotegemea

kuonyesha.

a. Kile mwandishi alihitaji kusisitiza kwa viongozi

b. Kile mwandishi angalikishangaza kwa viongozi

c. Kile mwandishi alichosikia toka ndani

2. Mpangilio wa kawaida wa neno kwenye Kiyunani bado ni jambo ambalo halijatulia ingawa mpangilio

wa kawaida unaokusudiwa ni

a. Kiunganishi cha VITENZI/Vitenzi unganishi

(1) KITENZI

(2) KIIMA

(3) SIFA

b. VITENZI elekezi

(1) KITENZI

(2) KIIMA

(3) KISHAMILISHI

(4) KISHAMILISHI KISICHO DHAHIRI

(5) KIRAI HUSISHI

c. Virai vya NOMINO

(1) NOMINO

(2) KIVUMISHI

(3) KIRAI HUSISHI

3. Mpanglio wa neno waweza kuwa muhimu mno kwenye upangiliaji wake. Mfano:

a. “walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika” (Gal 2:9) kirai “mkono wa kuume wa

shirika” imegawanyika na kuwekwa mbele kuonyesha umuhimu wake.

b. Pamoja na Kristo (Gal. 2:20), iliwekwa kwanza kifo chake kilikuwa kiini.

c. “ni sehemu nyingi na kwa njia nyingi” (Ebr. 1:1), iliwekwa kwanza. Ilikuwa ni kwa namna Mungu

alivyojidhihilisha mwenyewe kwa tofauti na sio ukweli wa mafunuo.

D. Kawaida kwa kiasi fulani cha degrii ya msisitizo ulionyeshwa na

Page 445: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

429

1. Urudiaji wa KIWAKILISHI ambacho tayari kilikuwepo katika KITENZI kilichonyambulika. Mfano: “mimi

mwenyewe, hakika nitakuwa nawe…….”(Mt 28:20)

2. Ukosekanaji wa KIUNGO tarajiwa, au kitu kingine cha kuunganisha maneno, virai, vishazi au sentesi.

Hii inaitwa (isiofungamana). Kitu unganishi kilikuwa ni

a. Ibada ya kubarikiwa kwa Kristo, Mt 5:3 ff (ikisisitizia orodha)

b. Yohana 14:1 (maada mpya)

c. Rumi 9:1 (kifungu kipya)

d. 2Kor 12:20 ( inasisitizia orodha)

3. Urudiaji wa maneno au virai vilivyomo katika mazingira tajwa. Mfano: “usifiwe utukufu wa neema

yake” (Efe 1:6, 12 & 14). Kirai hiki kilitumika kuonyesha kazi ya kila mtu wa utatu.

4. Utumiaji wa nahau au neno (sauti) unakaa kati ya istilahi.

a. Tasifida- maneno mbadala kwa viima vyenye miiko kama “lala” kwa kifo (Yoh 11:11-14) au

“nyayo” kwa viungo vya uzazi vya kiume (Ruth 3:7-8; 1Sam 24:3)

b. Maneno ya kuzunguka- mbadala wa maneno kwa jina la Mungu, kama “ufalme wa mbingu” (Mt

3:21) au “sauti toka mbinguni” (Mt 3:17)

c. Maumbo ya hotuba

(1) Kutowezekana kuyakuza (Mt 3:9; 5:29-30; 19:24)

(2) Upole wa maelezo (Mt 3:5; Mdo 2:36)

(3) Mfano halisi wa (1Kor 15:55)

(4) Kejeli (Gal 5:12)

(5) Dondoo za kishairi (Flp 2:6-11)

(6) Mvumo unaokaa kati ya maneno

(a) “kanisa”

i. “kanisa” (Efe 3:21)

ii. “Kuitwa” (Efe 4:1,4)

iii. “Kuitwa” (Efe 4:1,4)

(b) “huru “

i. “Mwanamke huru” (Gal 4:31)

ii. “uhuru” (Gal 5:1)

iii. “huru” (Gal 5:1)

d. Lugha ya kinahau- ni lugha ambayo mara nyingi ni ya kitamaduni na lugha bayana

(1) Hii ilikuwa ni matumizi ya kistiari ya neno “chakula” (Yoh 4:31-34)

(2) Hii ilikuwa ni matumizi ya kiistiari ya neno “hekalu” (Yoh 2:19; Mt 26:61)

(3) Hii ilikuwa ni nahau ya Kiebrania ya kuonyesha huruma, ya neno “chukia” (Mwa. 29:31;

Kumb.21:15; Thess 14:36; Yoh 12:25; Rum 9:13)

(4) “wote” dhidi ya “wengi”. Linganisha Isa. 53:6 (“wote”) na 53:11 & 12 (“wengi”). Istilahi hizi

zina maneno sawa kama Rum 5:18 na 19 kama inavyoonyesha.

5. Utumiaji wa kifungu cha isimu moja kwa moja badala ya neno moja. Mfano: “Bwana Yesu Kristo”.

6. Utumiaji maalumu wa neno autos

a. Wakati likiwa na KIFUNGU (nafasi ya kivumishi angama) kilichofasiliwa “sawa”

b. Wakati bila KIFUNGU (nafasi ya kuarifu) kilitafasiliwa kama KIWAKILISHI CHENYE MKAZO CHA

KUJIREJEA- “mwenyewe jinsia ya ME” “mwenyewe jinsia ya KE” au “yenyewe/chenyewe”

E. Wanafunzi wa Biblia wasio weza soma Kiyunani waweza kutambua mkazo katika Nyanja tofauti:

1. Utumiaji wa misamiati ya kichambuzi na andiko nasaba la Kiyunani/ Kiingereza.

Page 446: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

430

2. Mlinganyo wa fasili za Kiingereza, hasa toka kwa nadharia za fasiri zinazotofautiana. Mfano: ufasiri

mlinganyo wa “neno kwa neno” (KJV, NKJV, ASV, NASB, RSV, NRSV) na “mfanano wa karibu” (William,

NIV, NEB, REB, JB, NJB, TEV)

Msaada mzuri hapa ungalikuwa ni ule toka The Bible in Twenty-Six Translation kilichochapishwa na

Baker.

3. Utumiaji wa The Ephasized Bible cha Joseph Bryant Rotherham (Kregel, 1994).

4. Utumiaji wa tafasiri yenyewe.

a. The American Standard Version ya mwaka 1901

b. Young’s Lateral Translation of the Bible cha Robert Young (Guardian Press, 1976)

Usomaji wa kisarufi unachosha lakini unafaa kwa ufasiri mzuri. Maelezo hasa sahihi, maoni na mifano

inahamasisha na kuwaamusha watu wasiojua Kiyunani kutumia mihitasari ya kisarufi iliyotumiwa kwenye juzuu

hii. Hakika maana hizi zimerahisishwa zaidi. Zisingaliweza kutumika katika hali madhubuti nay a kulazimisha, lakini

kama ngazi ya kupandia kwenda kwenye uelewa mkubwa wa isimu za Agano Jipya. Kimatumaini maana hizi

zitawawezesha wasomaji kuelewa maoni ya msaada mwingine wa usomaji kama vile maoni ya kiufundi juu ya

Agano Jipya.

Ni lazima tuweze kuthibitisha ufasiri wetu uliolenga kwenye habari iliyopatikana kwenye maandishi ya Biblia.

Sarufi ni moja ya msaada mkubwa wa vipengere hivi, vipengere vingine vingalijumuisha muundo wa kihistoria,

maandishi ya kifasihi, utumiaji wa neno la wakati ule ule na dondoo zinazorandana.

Page 447: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

431

Uhakiki wa Tofauti za Kiuandishi Somo hili litajikita kwa namna moja kutoa maelezo yanayopatikana katika maoni haya. Mhutasari ufuatao utahusika

I. Vyanzo vya maelezo ya Biblia zetu za Kiingereza A. Agano la Kale B. Agano Jipya

II. Maelezo mafupi ya matatizo na nadharia ya “maoni dhaifu” pia yanaitwa “uhakiki wa maandiko” III. Vyanzo vilivyopendekezwa kwa ajili ya usomaji wa badaye

I. Vyanzo vya maandiko ya Biblia yetu ya Kiingereza

A. Agano la Kale 1. Machapisho ya kale ya Kiebrania ya karne ya kumi na tisa (MT)-maandiko ya konsonanti za

Kiebrania yalipangwa na Rabbi Aquiba miaka 100 Baada ya Kristo. Nukta za irabu na lafudhinukuu za pembeni, vituo vya uandishi na alama za nukta zilizoongezwa katika karne ya sita Baada ya Kristo na vilihitimishwa katika karne ya tisa Baada ya Kristo. Yalifanywa na familia ya wasomi wa Kiyahudi wajulikanao kama Wana-maandiko ya Kale ya Kiebrania. Muundo wa maandiko walioutumia ulikuwa sawa na ule katika Mishnah, Talmud, Targums, Peshitta, na Vulgate.

2. Tafsiri ya Kiyunani ya Agano la Kale la Kiebrania (LXX) –Utamaduni unasema Tafsiri ya Kiyunani ya Agano la Kale la Kiebrania ilitengenezwa na wasomi wa Kiyahudi 70 katika siku 70 katika maktaba ya Alexandria chini ya ufadhili wa Mfalme Ptolemy wa II (285-246 K.K). Tafsiri ilidhaniwa kuwa matakwa ya kiongozi wa Kiyahudi aliyeishi katika Alexandria. Utamaduni huu unatokana na “Herufi Aristeas.” Mara kwa mara Tafsiri ya Agano Kale(LXX) ilijikita katika kutofautiana kwa utamaduni wa maandishi ya Kiebrania kutoka katika maandishi ya Rabbi Aquiba (MT).

3. Mafunjo ya Bahari ya Chumvi (MBC)-Michoro ya Bahari ya Chumvi -iliandikwa huko Ruma kipindi cha K.K(200 Kabla ya Kristo hadi Baada ya Kristo 70) na madhehebu ya Kiyahudi waliojitenga waitwao “ Esene”. Machapisho ya Kiebrania, yalikutwa katika sehemu nyingi kandokando ya Bahari ya Chumvi yakionyesha baadhi ya zile tofauti za machapisho ya familia za Kiebrania nyuma ya Machapisho ya Kale ya Kiebrania (MKK)na Tafsiri za Kale za Kiebrania (70).

4. Baadhi ya mifano ya mahususi ni kwa namna gani ulinganifu wa maandishi haya imewasaidia wakalimani kulielewa Agano la Kale. a. Tafsiri za Kale za Kiebrania zimewasaidia watafsiri na wasomi kuyaelewa maandishi ya Kale ya

Kiebrania. (1) Tafsiri za Kale za Kiebrania za Isa. 52:14, “Kama vile wengi watakavyo shangazwa Naye.” (2) Maandishi ya Kale ya Kiebrania ya Isa. 52:14, “Bado kama vile wengi walivyo staajabishwa

Nawe.” (3) Katika Isa. 52:15 tofauti ya kiwakilishi cha Tafsiri za Kale za Kiebrania imehakikishwa

(a) Tafsiri za Kale za Kiebrania, “hivyo mataifa mengi yatashangazwa naye” (b) Maandishi ya Kale ya Kiebrania, “hivyo yeye ameyatapakaza mataifa mengi”

b. Mafunjo ya Bahari ya Chumvi (DSS) yamewasaidia watafsiri na wasomi kuyaelewa Maandishi ya Kale ya Kiebrania (1) Mafunjo ya Bahari ya Chumvi ya Isa. 21:8, “ndipo akalia Karibu na mlinzi wa mnara nilipo

simama.” (2) Maandishi ya Kale ya Kiebrania (MT) ya Isa. 21:8, “ndipo akalia kama simba, Ee Bwana,

mimi nasimama daima juu ya mnara wakati wa mchana……” c. Tafsiri za Kale za Kiebrania (LXX) na Mafunjo ya Bahari ya Chumvi (DSS) zote zilisaidia kuichuja

Isa. 53:11 (1) Tafsiri za Kale za Kiebrania (LXX) na Mafunjo ya Bahari Chumvi (DSS), “Baada ya kutaabika

sana, mtumishi wangu atafurahi. Kwa kuwajibika kwake kikimilifu, atatosheka na matokeo hayo.’’

Page 448: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

432

(2) Maandishi ya Kale ya Kale ya Kiebrania (MT), “Ataona —ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki Atawafanya wengi kuwa wenye haki.”

B. Agano Jipya 1. Maandishi yapatayo 5,300 yote au sehemu za Agano Jipya la Kiyunani yapo hadi leo. Yapatayo 85

yameandikwa katika karatasi za mafunjo na 268 ni maandishi yaliyoandikwa yote kwa herufi kubwa (maandiko adimu) Baadaye, mnamo karne ya tisa B.K., maandishi yaliyo somwa (madogo sana) yalikuzwa. Maandishi ya Kiyunani yaliandikwa kutoka namba zipatazo 2,700. Pia tunazo nakala zipatazo 2,100 za orodha ya Machapisho ya maandiko Matakatifu yalitumika katika kuabudu ambayo tunaiita misale ya waumini.

2. Machapisho ya Kiyunani yapatayo 85 yaliyokuwa na sehemu za Agano Jipya zilizoandikwa katika karatasi za mafunjo yamejengewa katika makumbusho. Baadhi yao yamewekwa katika kipindi maalumu kutoka karne ya pili B.K., yaliyo mengi ni kuanzia karne za tatu na nne B.K.. Hakuna kati ya machapisho ya kale. Hizi zilizo na Agano Jipya Kamili. Hii ni kwa sababu hizi ni nakala za kale za Agano Jipya hazimaanishi kuwa sio ya kujiendesha yenyewe zina tofauti chache. Zilizo nyingizilinukuliwa kwa kasi kwa matumizi ya kawaida. Utunzaji haukuzingatiwa katika utendaji. Hivyo, zina utofauti mwingi.

3. Kitabu cha miswada ya kale chenye maandishi ya Kale ya Kiyunani ya karne ya nne B.K. kinachojulikana kwa herufi ya Kiebrania א (aleph) au (01), iliyokutwa katika nyumba ya Mt. Katarina juu ya Mlima Sinai na Tischendorf. Tarehe yake imeandikwa kuanzia karne ya nne B.K. iliyokuwa na zote Tafsiri za Kale za Kiebrania (LXX) na za Agano Jipya la Kiyunani. Ni aina ya“Maandishi ya Kialekzandria.”

4. Kitabu cha miswada ya Kale cha Alexandrianus, kijulikanacho kama “A” au (02), machapisho ya Kiyunani ya karne ya tano ambayo ilipatikana katika Alexandria, Misri.

5. Kitabu cha miswada ya Kale cha Machapisho ya Kiyunani cha karne ya nne, kijulikanacho kama “B” au (03), iliyopatika katika maktaba ya Vatikani katika Roma na imeandikiwa tarehe kuanzia katikati ya karne ya nne B.K. Ina zote Tafsiri za Kale za Kiebrania za Agano la Kale na Agano Jipya la Kiyunani. Yalikuwa aina ya “Maandishi ya Kialekzandria.”

6. Kitabu cha miswada ya kale cha Ephraemi, kijulikanacho kama “C” au (02), machapisho ya Kiyunani ya karne ya tano ambayokwa makusudi yaliaribiwa.

7. Kitabu cha miswada ya Kale cha Bazae, kijulikanacho kama “D” au (05), machapisho ya Kiyunani ya karne ya karnre ya tano au sita. Ni mwakilishi mkuu wa kile kinachojulikana kama “Maandishi ya Magharibi.” Ina maongezeko mengi ulikuwa ushahidi mkuu wa tafsiri ya Mfalme James.

8. Agano Jipya la machapisho ya kale yanaweza kuwekwa katika makundi matatu, kadria nne, familia ambazo zimeshiriki sifa fulani. a. Maandishi ya Kialekzandria kutoka Misri

(1) P75,P76 ( yapata 200 B. K.), ambayo inachukua kumbukumbu ya Injili. (2) P46 (yapata 225 B. K.), ambayo ilichukua kumbukumbu ya barua za Paulo (3) P72(yapata 225-250 B. K.), ambayo ilichukua kumbukumbu ya Petro na Yuda (4) Kitabu cha miswada ya Kale B, kiitwacho Viticanus (mnamo 325 B. K), ambacho kimebeba

Agano la Kale zima na Agano Jipya (5) Origen alinukuu kutoka aina hii ya maandiko (6) Machapisho ya kale mengine ambayo yanaonyesha aina hii ya maandishi ni א,C, L, W, 33

b. Maandishi ya Magharibi kutoka Afrika ya Kaskazini (1) alinukuu kutoka wakuu wa kanisa wa Afrika ya Kaskazini, Tertullian, Cyprian, na tafsiri za

Kale za Kilatini (2) yalinukuliwa kutoka Irenaeus (3) ilinukuliwa kutoka Kilatini na tafsri za kale za Kisiria (4) Andiko D la Machapisho ya kale “Bezae” ilifuata aina ya maandishi haya

c. Byzantine Mashariki kutoka Constantinople (1) aina ya maandishi inaakisiwa katika 80% ya 5,300 MSS

Page 449: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

433

(2) ilinukuliwa na kanisa la mapadre wa Antiokia ya Silia, Cappadoceans, Chrisostom, natherodoret

(3) Andiko A la machapisho ya kale, katika Injili tu (4) Andiko E la machapisho ya kale, (karne ya nane) ya Agano Jipya

d. aina ya nne iwezekanayo ni ya “Kikaizari” kutoka Palestina (1) kwanza inaonekana katika Mrko tu (2) baadhi ya shuhuda zake ni P45 na W

II. Matatizo na nadharia ya “ukosoaji dhaifu.”

A. Ni kwa namna gani tofauti zilitokea 1. isio angalifu au bila kukusudia (matukio mengi mno)

a. makosa madogo madogo ya macho katika kunakili kwa mkono ambapo ulisomwa mfano wa pili wa maneno yanayofanana na pale ambapo yanaondoa maneno yote katikati (mfanano wa maneno) (1) makosa madogo madogo ya macho katika kuondoa maneno ya herufi jozi au vifungu

(urudiaji wa maneno) (2) makosa madogo madogo ya kumbukumbu katika kurudia kifungu au msitari wa

maandishi ya Kiyunani (mshabaha ule ule) b. makosa madogo madogo ya masikio katika kunakili maneno ya imla ambapo makosa ya

kiuandishi hutokea (itacism). Mara nyingi makosa ya kiuandishi hudokeza au kutaja herufizenye mfananowa sauti za maneno ya Kiyunani.

c. maandishi ya Kiyunani ya kale hayakuwa na sura au mgawanyo wa mistari, chache au alama za uandishi na hakuna mgawanyo kati ya maneno. Inawezekana kuzigawa herufi katika nafasi kuunda maneno tofauti.

2. makusudi a. mabadiliko yalifanywa ili kufanikisha muundo wa kisarufi wa maandishi yaliyo nakiliwa b. mabadiliko yalifanywa ili kuyaleta maandiko katika ulinganifu na maandiko mengine ya kibiblia

(mlinganyosambamba) c. mabadiliko yalifanywa kwa kuuunganisha masomo mawili au zaidi yaliyokuwa tofauti katika

muungano mmoja wa maandishi marefu (conflation) d. mabadiliko yalifanywa kusahihisha makosa yaliyotambuliwa katika maandishi (kama vile I Kor.

11-27 na I Yohana 5:7-8) e. baadhi ya taarifa za nyongeza kama mpangilio wa kihistoria au ufafanuzi sahihi wa maandishi

uliwekwa pembezoni kwa nakala moja lakini zilihamishiwa katika maandishi kwa kuzinakili mara ya pili ( Yohana 5:4)

B. Mafundisho muhumu ya ukosoaji wa maandiko (mwongozo wa kimantiki ili kubainisha usomaji halisi wa maandishi wakati tofauti inapojitokeza) 1. maandishi ambayo hayakuwa na ustadi zaidi au ambayo hayakuwa muhimu kisarufi yamkini ni

halisi 2. maandishi mafupi zaidi yamkini ni halisi 3. maandishi ya kale yamepewa uzito zaidi kwa sababu ya ukaribu wake kihistoria katika uhalisia, kila

kitu kuwa sawa zaidi 4. Machapisho ya kale ni namna mbali mbali ya kijiografia mara nyingi yana usomaji halisi 5. Kimafundisho maandishi ya wanyonge, hasa yale yanayohusiana na majadiliano makuu ya

kitheolojia ya kipindi cha mabadiliko ya machapisho kama Utatu katika Yohana 5:7-8, yanapaswa kupendelewa.

6. maandishi ambayo yanaweza kuelezea zaidiasili ya tofauti zingine 7. nukuu mbili ambazozinzsaidia kuonyesha usawa katika tofauti zinazotaabisha

a. kitabu cha J. Harold Greenless, Inroduction to New Testament Textual Criticism, “Hakuna mafundisho ya Kikristo yanayoning’inia juu ya maandishi yenye kujadiliwa; na mwanafunzi wa Agano wa Jipya anapaswa kuyatambua maandiko yake anayoyataka kuwa mwenye imani zaidi au kuwa mwenye nguvu kimafundisho kuliko msukumo asilia” (uk. 68).

Page 450: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

434

b. W. A. Criswell alimwambia Greg Garrison ya The Birmingham News ambayo yeye ( Criswell) haamini kila neno katika Biblia ni la kutia moyo “angalau si kila neno ambalo limekwisha kutolewa kwa alaiki ya kisasa kwa karne za watafsiri.” Criswell alisema “Mimi ni mwamini sana katika ukosoaji wa maandishi. Kama vile, Nafikiri, nusu ya sura ya 16 ya Marko ni uasi: haitii moyo, imebuniwa…Unapolinganisha machapisho hayo kwa kurudi huko nyuma, hakukuwa na kitu kama hicho kama lilehitimisho la Kitabu cha Marko. Mtu fulani alikiongeza…” Mababa wa uzao wa SBC wasio wakosaji walidai kuwa “kutia maneno yasiokuwepo katika kitabu” pia ni dhahiri katika Yohana, uwajibikaji wa Yesu katika bwawa la Bethesda. Na alijadili tofauti mbili za uwajibikaji wa kujinyonga kwa Yuda (Mt. 27 na Matendo 1): “Ni maoni tofauti ya kujinyonga,” Criswell alisema “Kama iko katika Biblia, kuna maelezo yake. Na hatia mbili za kujinyonga kwa Yuda ziko katika Biblia.”Criswell aliongeza, “Ukosoaji wa Maandishi nisayansi ya ajabu ndani yake yenyewe. Si ya muda mfupi kupita, si isiyo husiana.Ni yenye nguvu na kuu…”

III. Matatizo ya machapisho (ukosoaji wa maandishi) A. Vyanzo vilivyopendekezwa kwa ajili ya kusoma zaidi

1. Biblical Critcism, Historical, Literary and Textual, na R. H. Harrison 2. The Textual of the New Testmemt: Its Transmission, Corruption and Restoration, na Bruce M. Metzger 3. Introduction to New Testament Txtual Critism, na J. H Greenlee

Page 451: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

435

UFAFANUZI/FAHARASA

Uasilishaji. Hili ni moja kati ya maoni ya kale ya uhusiano wa Yesu na Uungu. Kimsingi inadai kwamba Yesu alikuwa mwanadamu wa kawaida kwa kila namna na alichukuliwa na Mungu kwa kazi maalumu katika ubatizo wake (Mt. 3:17; Marko 1:11) au katika ufufuo Wake (cf. Rum.1:4).Yesu aliyaishi maisha haya kama mfano ambao Mungu, kwa kiasi chake, (ubatizo, ufufuo) uliyomuasilisha Yeye kama “mwana” Wake (Rum.1:4 Flp. 2:9). Hili lilikuwa kanisa la mwanzo na maoni ya watu wa karne ya nane. Badala ya Mungu kuwa mwanadamu (umbo la kibinadamu) akalirejeresha hili na sasa mwanadamu anakuwa Mungu! Ni vigumu kusema namna gani Yesu, Mungu Mwana, Uungu uliokuwepo kabla alivyozawadiwa au kuwa mbadala kwa ajili ya maisha yenye mfano. Kama Yeye alikuwa tayari ni Mungu, ni kwa namna gani Yeye alitolewa kama zadiwa? Kama Yeye alikuwa na utukufu wa Kiungu wa awali ni kwa namna gani Yeye angeliheshimiwa zaidi? Ingawa ni vigumu kwetu sisi kutambua, kwa namna Baba alivyomuheshimu Yesu katika dhana maalumu ya ukamilifu Wake wa kuyatimiza mapenzi ya Baba. Shule ya Alexandria.Njia hii ya ukalimani wa kibiblia ilikuzwa katika Alexandria, Misri katika karne ya pili B.K. Inatumia misingi ya kanuni za ukalimani ya Philo, ambaye alikuwa mfuasi wa Pilato, mara nyingi inaitwa njia ya kiistiari. Ilitawaliwa katika kanisa hadi wakati wa Marekebisho. Watetezi wake zaidi walikuwa Origen na Augustine. Tazama Moisea Silva, Has The church Misred The Bible? (Academic, 1987) Ufuasi wa Iskandria.Haya ni machapisho ya Kiyunani ya karne ya tano kutoka mji wa Alexandria, Misri ikijumuisha Agano la Kale, lililothibitishwa, pamoja na Agano Jipya. Ni moja ya ushahidi wetu mkubwa katika Agano Jipya zima la Kiyunani (isipokuwa sehemu za kitabu cha Mathayo, Yohana, na II Wakorintho). Wakati ambapo machapisho haya, ambayo yanapewa alama “A, na machapisho ya alama “B” (ya Vatican) yanaafiki juu ya usomaji unaofikiriwa kuwa ya mwanzo na baadhi ya wasomi. Istiari. Hii ni aina ya ukalimani wa kibiblia ambayo kiasili ulianzishwa ndani ya dini ya Kiyahudi huko Alexandria. Ilienezwa na Philo wa Alexandria. Msukumo wake wa msingi ni shauku ya kufanya uhusiano wa Maandiko na utamaduni wa mtu au mfumo wa kifalsafa kwa mpangilio wa historia ya Biblia na/ au muktadha wa maandishi. Inatafuta uficho au kweli ya kiroho nyuma ya kila kifungu cha maandiko. Inapaswa kukubaliwa kwamba Yesu, katika Mathayo 13, na Paulo, katika Wagalatia 4, alitumia istiari kuiwasilisha kweli. Kwa hali yoyote, hii, ilikua katika muundo wa taipolojia (uanishi), na si istiari halisi. Uchanganuzi wa misamiati. Hii ni aina ya chombo cha utafiti ambacho kinamruhusu mtu kutambua kila muundo wa Kiyunani katika Agano Jipya. Ni mkusanyiko, katika mpangilio wa alfabeti za Kiyunani, wa kimuundo na maelezo ya msingi. Katika muunganiko kwa tafsiri mbalimbali, unaruhusu usomaji wa wasio Wayunani kuchambua visarufi vya Agano la Kale la Kiyunani kimsamiati na kimuundo. Ushabihiano wa Maandiko. Hiki ni kifungu kinachotumika kueleza wazo kwamba Biblia nzima imefunuliwa na Mungu, na ni, kwa hiyo sio mkanganyiko bali ukamilifu. Ukubalifu wa dhanio hili ni msingi kwa matumizi yanayo fanana na vifungu vya maneno katika kufasiri maandiko ya biblia. Utata.Hii inarejea juu ya mashaka ambayo yanaleta matokeo katika nyaraka zilizoandikwa ambapo kuna maana mbili ziwezekanazo au zaidi au wakati vitu viwili au zaidi vinakuwa vikirejewa kwa wakati mmoja. Inawezekana kwamba Yohana anatumia utata huu kwa makusudi. Elimu ihusuyo tabia ya mwanadamu. Inamaanisha kuwa na “tabia zinazohusiana na wanadamu.” neno hili linatumika kueleza lugha zetu za kidini kumuhusu Mungu. Linatokana na neno la Kiyunani kumuhusu mwanadamu. Inamaanisha kwamba tunazungumza kuhusiana na Mungu kana kwamba Yeye alikuwa mwanadamu. Mungu anaelezwa katika umbo la mwili lionekanalo, kijamii, maneno ya kisaikolojia ambayo yanahusiana na wanadamu (cf. Mwa. 3:8; II Wafalme 22: 19-23). Hii, hakika ni mshabihiano pekee. Hata hivyo maarifa yetu kumhusu Mungu, ingawa ni kweli, lakini yamewekewa mipaka.

Page 452: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

436

Shule ya Antiokia.Hii njia ya ufasiri wa kibiblia ilianzia huko Antiokia, Syria katika karne ya tatu B.K. kama kuonyesha hisia juu ya utaratibu wa kiistiari wa Alexandria, huko Misri. Msingi wa msukumo wake uliangalia maana ya kihistoria ya Biblia. Ilitafasiri Biblia kama fasihi ya kawaida ya mwaadamu. Shule hii ilikuwa imejumuishwa katika ubishi kumhusu Kristo kama alikuwa na asili mbili (mafundisho kuhusu uwili wa Yesu) au asili moja (Mungu kamili na mwanadamu kamili). Ilitambuliwa kama maoni ya kupinga Ukristo kwa Kanisa Katoriki la Rumi na kuhamishiwa Uajemi lakini shule ilikuwa na umuhimu mdogo. Misingi ya kanuni zake za ufasili wa kibiblia baadaye ikawa kanuni za ufasili wa watu walioleta mageuzi kwenye dini ya Kiprostanti (Luther and Calvin). Kutabaini. Hii ni moja miongoni mwa njia tatu za uwasilishaji wa neno uliotumika kudokeza uhusiano kati ya misitari ya ushairi wa Waebrania. Unahusiana na misitari ya ushairi yenye kukinzana kimaana (cf. Mit. 10:1; 15:1). Fasihi ya mafunuo. Hii ilikuwa ni namna tanzu ya Wayahudi wenye nguvu, hata kuonekana ya kipekee. Ilikuwa ni aina ya uandishi wenye mafumbo uliotumika nyakati za uvamizi na umiliki dola yenye nguvu ya Kiyahudi. Inafikiriwa kwamba mtu, muumbwaji aliyekombolewa na Mungu na kuyatawala matukio ya ulimwengu, na kwamba Israeli ina upendeleo maalumu na uangalizi kutoka Kwake. Fasihi hii inahaidi ushindi mkuu na kupitia juhudi pekee za Mungu. Ni ishara kuu na ya ubunifu sana yenye maneno ya mafumbo. Mara nyingi ilieleza ukweli katika rangi, tarakimu, maono, ndoto, upatanishi wa kimalaika, alama za siri za maneno, mara nyingi uwili wa vitu kati ya mema na mabaya. Baadhi ya mifano tanzu hapa ni (1)katika Agano la Kale, Ezekieli (sura ya 36-48), Danieli (sura ya 7-12), Zekaria; na (2) Katika Agano Jipya, Mathayo 24;Marko 13; II Wathesalonike 2 na Ufunuo. Mtetezi.Hili linatoka katika mzizi wa neno la Kiyahudi “ulinzi wa kisheria.” Haya ni mafundisho ndani ya theolojia ambayo yanatafuta kutoa ushahidi na uwiano wa hoja za kifikra kwa imani za Kikristo. Haki ya kutangulia.Kimsingi huu ni ukaribu wa maana ya neno “dhanio.” Inahusisha ufikiliaji wa wa maana za awali zilizokubalika, kanuni au nafasi iliyosadikika kuwa kweli paspo uchambuzi au uchunguzi. Ufuasi wa Arius.Arius alikuwa mhudumu ndani ya kanisa huko Aexandria, Misri katika karne ya tatu na mwanzoni mwa karne ya nne. Alikubali kwamba Yesu alikuwepo hapo kabla lakini si kwa Uungu (si sawa na asili ya Baba), huenda kwa kufuata Mithali8:22-31. Alipingwa na askofu wa Alexandria, ambaye alianza (B.K. 318) mabishano yalidumu kwa miaka mingi. Ufuasi wa Arius ulikuja kuwa kanuni rasmi katika Kanisa la huko Mashariki. Baraza la Nicaea katika 325 B.K.walimshtumu Arius na kuutetea usawa na Uungu kamili wa Mwana. Jamii ya watu wakuu. Alikuwa mmoja wa wanafalsafa wa kale wa Ugiriki, mwanafunzi wa Pilato na mwalimu wa Iskanda Mkuu.Ushawishi wake, hata sasa, umefika maeneo mengi yanayofundisha mafunzo ya kisasa. Hii ni kwa sababu alisistiza maarifa ni kupitia uchunguzi na upambanuzi. Hii ni moja ya itikadi ya njia za kisayansi. Miandiko binafsi. Hili ni jina lililotolewa kwa maandishi ya mwanzo ya Biblia. Maandiko haya asilia yaliyoandikwa kwa mkono yote yamepotea. Baadhi tu ya nakala zimesalia. Hiki ndio chanzo cha utofauti wa maandishi mbalimbali katika machapisho ya Kiebrania na Kiyunani. Maandiko ya asili ya karne ya sita. Haya ni machapisho ya Kiyunani na Kiratini ya karne ya sita B.K. Yanasanifiwa na alama “D.” Imejumuisha Injili na Matendo na baadhi ya Nyalaka za Jumla. Inabainishwa na nyongeza nyingi za maandishi yenye ueledi. Inaunda msingi wa “uundaji wa maandiko”ambayo ni tamaduni za machapisho makuu ya Kiyunani nyuma ya toleo la King James Version. Upendeleo. Hili ni neno linalotumika kueleza maelezo yenye nguvu kuhusiana na jambo au mtazamo fulani. Ni mtizamo ambao uadilifu ndani yake hauwezekani kungalia kitu au maoni Fulani. Ni madhara ya kieneo.

Page 453: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

437

Mamlaka ya Kibiblia. Ni neno lililotumika katika maana maana ya kipekee. Linaelezwa kama uelewa wa kile alichokisema mwandishi asilia katika siku zile zake na kutumia ukweli huu katika siku zetu. Mamlaka za Kibiblia mara nyingi zinaelezwa kuitazama Biblia yenyewe kama kiongozi chetu chenye mamlaka. Hata hivyo, katika hali ya sasa, utafasiri sio sahihi. Nimeweka mipaka juu a dhana ya Biblia kama ilivyotafsiriwa na kanuni za njia ya historia ya kisarufi. Orodha ya vitabu vya Agano Jipya.Hili ni neno linalotumika kuelezea maandishi yanayosadikiwa kuvuviwa kipekee. Limetumika kuangalia maandiko yote ya Agano la kale na Agano jipya. Kristo kama kitovu.Ni neno lililotumika kuonyesha Kristo kama kitovu cha mambo yote. Na lilitumiwa kuunganisha dhana ya kwamba Yesu ni Bwana wa Biblia zote, Mawazo ya Agano la Kale dhidi yake na utimilifu wa malengo yake. Fasiri.Hii ni aina pekee ya utafiti wa kitabu. Inatoa kwa pamoja usuli wa kitabu cha Biblia. Pia inajaribu kuelezea maana ya kila kipengele cha kitabu. Baadhi inatazamisha matumizi, wakati mwiingine zinahusiana na andiko katika hali ya kiufundi. Vitabu hivi ni vya manufaa, lakini lazima vitumike baada ya mtu kufanya uchunguzi wake wa awali. Tafsiri za watoa maoni lazima zisikubalike kuhakiki. Ukilinganisha fasiri nyingi toka kwa mitizamo ya wanathiolojia tofauti utaona inasaidia. Itifaki. Hii ni aina ya chombo cha utafiti kwa usomaji wa Biblia. Inaorodhesha kila utokeaji wa neno katika Agano Jipya na la Kale. Inasaidia katika njia tofauti: (1) kubainisha maneno ya Kiebrania au Kiyunani yaliyoko nyuma ya maneno ya kiingereza: (2) kulinganisha kurasa ambapo neno lile lile la Kiebrania au Kiyunani limetumika: (3) kuonyesha mahali ambapo maneno mawili tofauti ya Kiebrania au Kiyunani yametafasiriwa kwa neno lie lile la kiingereza: (4) kuonyesha mwendelezo wa kutumia maneno fulani katika vitabu fulani au maandishi: (5) inasaidia mtu kupata somo katika Biblia (cf. Walter Clark’s How to use New Testament Greek Study Aids. kurasa za 54-55). Magombo ya Bahari ya Chumvi. Inarejerea mlolongo wa maandiko ya kale yaliyoandikwa katika Kiebrania na Kiarama ambayo yalipatikana karibu na Bahari ya Chumvi mwaka 1947. Palikuwepo na maktaba za kidini ya Kiyunani ya karne ya kwanza. Msukumo wa umilikaji toka Rumi na vita ya kinazi vya miaka ya sitini viliwasababisha wao kuficha magombo yaliyokuwa yamefungashwa ndani ya vyungu kwenye mapango au mashimo. Inatusaidia sisi kuelewa muundo wa kihistoria wa palestina ya karne ya kwanza na kuthibitisha maandiko ya mossoretes kuwa yako sahihi kwa kiasi fulani enzi ya awali kabla ya Yesu B.C. Mambo yaliyofasiliwa. Njia hii ya kimantiki au ufikiliaji inatokana na kanuni ya pamoja ya matumizi maalumu kwa njia ya wazo. Hii ni kinyume toka ufikiliaji wa mambo yaliyofasiriwa, ambayo yanaangazia njia ya kisayansi toka kwenye uchunguzi maalumu kwenda hitimisho la pamoja (nadharia) Mbinu pembuzi.Hii ni njia ya kufikilisha ambapo kile kinachoonekana kuleta mkanganyiko au mafumbo huwekwa pamoja katika hali ya mkazo, ikitafuta jibu la pamoja ambalo linajumuisha pande zote za fumbo. Mafundisho mengi ya Biblia yana upembuzi unaofanana, kuamuliwa kabla-mapenzi huru, ulinzi-ustahimilivu, imani-kazi; uwamuzi-ufuasi; uhuru wa Mkristo-uwajibikaji wa Mkristo Wayahudi waliotawanyika katika mataifa mengine.Hili ni neno la kiufundi la Kiyunani lililotumiwa na wapalestina wa Kiyahudi kuelezea wayahudi wengine walioishi nje ya mipaka ya kijiografia ya nchi ya ahadi. Mlinganyo wa nguvu. Hii ni nadhalia ya ufasili wa Biblia. Tafasili ya Biblia inaweza kuangaliwa kama mwendelezo toka ushirika wa “neno kwa neno”, mahali ambapo neno la Kiingereza lazima liwekwe kwa kila neno la Kiyunani au Kiebrania, kwenye “ufasili” ambapo tu wazo limetafasiliwa kwa angalizo la chini ya neno au kifungu cha awali. Katika nadharia hizi mbili ndipo pana “mlinganyo wa nguvu” unaojaribu kuchukua neno la mwanzo kwa umakini wake, lakini limefasiliwa katika miundo ya visarufi vya kisasa na nahau. Majadiliano mazuri ya kweli ya hizi

Page 454: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

438

nadharia mbali mbali za fasili zinapatikana katika makala ya Fee na Stuart How to Read the Bible For Its Worth, uk. 35 na katika Robert Bratcher’s utangulizi katika Biblia ya TEV. Kutofuata mfumo. Neno hili linatumika katika mahusiano ya uhakiki wa maandiko. Unarejerea kitendo cha kuchagua usomaji toka machapisho tofauti tofauti ya Kiyunani ili kufika kwenye neno linalotakiwa kuwa karibu na maandiko ya mwanzo. Kupotosha maana. Hili neno ni kinyume cha neno fasili ya maandiko. Kama fasili ya maandiko ni “kuondoa” kulingana na kusudio la mwandishi wa awali, basi neno hili litamaanisha “kuingiza” wazo la kigeni. Elimu ya asili na historia ya neno. Hii ni dhana ya usomaji wa neno unaojaribu kuyakinisha maana ya awali ya neno. Kutokana na chanzo cha maana hii, utumiaji wa kipekee unaotambulika kirahisi katika ufasili, elimu ya asili na historia ya neno sio kiini cha mtizamo, mbali na maana ya wakati ule ule na utumiaji wa neno. Fasili ya maandiko. Hili ni neno la kiufundi kwa utendaji wa kutafasili kifungu maalumu. Inamaanisha “uondoaji nje” (wa neno) ukidokeza kwamba dhumuni letu ni kuelewa kusudi la mwandishi wa mwanzo katika uelewa wa muundo wa kihistoria, mazingira ya kifasihi, sintaksi na maana ile ile ya neno. Namna ya Uwasilishaji. Hili ni neno la Kifaransa ambalo limedokeza aina mbali mbali ya fasihi. Msukumo wa neno hili ni mgawanyiko wa miundo ya fasihi katika namna mbali mbali ambazo zinashirikishana tabia za aina moja. Usimuliaji wa kihistoria, mashairi, mithali, ufunuo na uandikishaji. Maarifa ya utambuzi/mafunuo. Zaidi ya maarifa tulionayo kuhusu imani potofu yameletwa toka maarifa ya utambuzi wa maandiko katika karne ya pili. Ingawa mawazo ya awali yalikuwepo katika karne ya kwanza (na kabla). Baadhi ya maelezo ya mafunuo ya kinazi ya Valentino na Cerinthin ni (1) mwili na roho vyote vilikuwepo kabla. mwili ni mwovu, na Roho ni nzuri. Mungu, ambaye ni Roho hawezi kuhusishwa moja kwa moja na mwili mwovu (2) kuna asili (eons au daraja la kimalaika) kati ya Mungu na mwili. Wa mwisho au wa chini alikuwa YAHWE wa Agano la kale, ambaye aliuumba ulimwengu (kosmos); (3) Yesu alikuwa mwanzilishi kama YAHWE lakini akiwa juu ya viwango, karibu na Mungu wa kweli. Wengine walimweka juu zaidi lakini bado yu chini kuliko Mungu na hakika asiye na mwili wa Kiungu (cf. 1:14). Kwa vile mwili ni mwovu, Yesu asingelikuwa na mwili wa kibinadamu na bado akawa na hali ya Kiungu. Alikuwa ni nafsi ya kufikirika (cf. 1Yoh 1:1-3; 4:1-6); na (4) wokovu ulipatikana kupitia imani katika Yesu pamoja na maarifa maalumu, yaliyojulikana na watu maalumu. Maarifa (maneno ya siri) yalihiiitajika kupitia ulimwengu wa kimbingu. Washikiliaji sana wa kisheria za Kiyahudi nao pia walihitaji kumfikia Mungu. Walimu wa uongo wenye maarifa ya utambuzi walitetea miundo miwili kinzani ya kimaadili (1) baadhi ya stadi za maisha hazikuhusiana na wokovu. Kwao wokovu na utakaso ulifumbwa kwenye maarifa ya siri (neno la siri) kupitia ulimwengu wa kimalaika (eons); au (2) kwa wengine stadi ya maisha ilikuwa muhimu katika wokovu. Walisisitiza miundo ya maisha kama kielelezo cha utakaso wa kweli. Kanuni za ufasili. Hili ni neno la kiufundi kwa kanuni zinazoongoza ufasili wa maandiko. Ni seti ya mwongozo maalumu na sanaa/kipawa. Kibiblia, au takatifu, kanuni za ufasili zimegawanyika kwa namna mbili; kanuni za ujumla na kanuni maalumu. Hizi zinahusiana na aina tofauti za fasihi zinazopatikana katika Biblia. Kila aina tofauti (tanzu)zina mwongozo wake wa kipekee lakini zinashirikiana na baadhi ya dhana na namna ya utafasili. Uhakiki juu ya maandiko. Hii ni namna ya utafasili wa kibiblia ambao unatazamisha kwenye muundo wa kihistoria na umbo la fasihi hasa hasa katika kitabu cha Biblia. Nahau. Neno hili linatumika kwenye vifungu vinavyopatikana katika tamaduni tofauti zenye maana maalumu na sio vilivyohusiana na maana ya kawaida ya maneno binafsi. Maana ya mifano ya kisasa ni: “ilikuwa ni vizuri sana” au “umeniua”. Biblia pia inajumuisha aina hizi za vifungu.

Page 455: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

439

Nuru.Hili ni jina lililotolewa kwenye dhana kuwa Mungu aliongea na mwanadamu. Dhana nzima kwa kawaida imeelezewa kwa namna tatu: (1) ufunuo-Mungu ametenda kwenye historia ya binadamu: (2) uvuvio-ametoa utafasili sahihi wa matendo yake na maana yake kwa watu fulani waliochaguliwa kuweka kumbukumbu ya mwanadamu: na (3) nuru –ametoa roho wake kumsaidia mwanadamu kuelewa mafunuo yake. Kudukiza. Hii ni njia ya kimantiki au kufikiria inayotoka sehemu Fulani na kuenea sehemu yote. Ni njia ya kutegemea majaribio ya kisasa. Kimsingi, huu ni mjongeo wa watu wenye hadhi ya juu. Unasaba. Hii ni aina ya chombo cha uchunguzi kinachoruhusu wale wasiojua lugha za kibiblia kuchunguza maana yake na muundo. Inaweka tafasili ya kiingereza kwenye ngazi ya neno kwa neno chini ya lugha ya awali ya kibiblia. Chombo hiki kinajumuishwa na “misamiati ya kiuchunguzi” ambayi inatoa miundo na maelezo ya msingi ya Kiebrania na Kiyunani. Uvuvio.Hii ni dhana ya kwamba mungu aliongea na mwanadamu kwa kuwalinda waaandishi wa kibiblia kwa usahihi na uwazi ili kuweka kumbukumbu ya mafunuo yake. Dhana nzima imeelezewa kwa namna tatu: (1) ufunuo-Mungu ametenda katika historia ya mwanadamu (2) uvuvio-ametoa utafasiri wasahihi wa matendo yake na maana yake kwa watu Fulani waliochaguliwa kuweka kumbukumbu ya mwanadamu: na (3) Nuru-ametoa roho wake kumsaidia mwanadamu kuelewa mafunuo yake. Lugha ya maelezo. Hii inatumika pamoja na nahau pale Agano la Kale lilipoandikwa. Inaongelewa juu ya dunia kwa namna jinsi vitu vinavyotokea kwenye milango mitanmo ya fahamu. Sio maelezo ya kisayansi hata yakamaanisha kuwepo. Ushikiliaji sana wa sheria. Mwenendo huu umeainishwa kwa msisitizo zaidi juu ya sheria au matambiko. Unajaribu kutegemea juu ya utendaji wa mwanadamu kama njia ya ukubalifu kwa Mungu. Unajaribu kushusha uhusiano na kuinua utendaji, mwote ambamo dhana muhimu ya mahusiano ya kimaagano kati ya Mungu mtakatifu na mwanadamu mtenda dhambi. Tafasili sisisi. Hili ni jina jingine la mlengo wa kimaandiko na njia za kihistoria za za kanuni za ufasili toka Antiokia. Ina maana kwamba utafasili unahusika katika maana dhahili za lugha ya mwanadamu, ingawa inaendelea kutambua uwepo wa lugha za kitamathali. Fasihi tanzu. Hii inarejerea kwenye miundo ya utofauti ili kwamba mawasiliano ya uwanadamu yanaweza kuchukuliwa kama vile ushairi au simulizi za kihistoria. Kila aina ya fasihi ina nji/namna yake maalumu ya kanuni ya ufasili kwa kuongezea kwenye kanuni za pamoja kwa fasihi zote zilizoandikwa. Sehemu ya fasihi. Hii inarejerea mgawanyo wa lengo kuu la kitabu cha Kibiblia. Inaweza kuundwa na misitari, aya, au ibara chache. Ni kijumuishi pekee chenye kiini cha somo. Lower criticism- Uhakiki wa kawaida wa maandiko. Maandiko ya asili. Neno hili linahusiana na nakala mbali mbali za Agano jipya la Kiyunani. mara nyingi limegawanyika katika aina tofauti kwa (1) nyenzo iliyotumika kuandikiwa kwayo (mafunjo, ngozi) au (2) muundo wenyewe wa uandishi. Limefupishwa kwa neno “MS” (umoja) au “MSS” (wingi). Andishi la kidesturi la Kiebrania la Biblia ya Kiyahudi. Hii inarejerea karne ya nane A.D. maandiko ya asili ya Kiebrania ya Agano la kale yalitolewa na vizazi vya wasomi wa Kiyahudi ambayo yalijumuisha alama za irabu na mihtasari mingine ya maandiko. Yanatengeneza msingi wa neno kwa Agano letu la kale la Kiingereza.

Page 456: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

440

Mshabihiano wa neno. Huu ni namna ya msemo ambao jina la kitu linatumika mbadala wa kitu kingine kinachofanana nacho. Kwa mfano “ birika linachemka” ki uhalisia inamaanisha “maji yaliyeko kwenye birika yanachemka”. Orodha ya vitabu vya Agano jipya. Hii ni orodha ya vitabu vya sheria za kanisa la Agano jipya. Iliandikwa huko Rumi kabla ya mwaka 200 A.D. Inatoa vitabu ishirini na saba kama vile vile vya Agano Jipya la Waporostanti. Hii wazi kabisa inaonyesha makanisa madogo madogo ya mahali katika sehemu mbali mbali za milki ya Rumi kulikuwa “kiutendaji” pamewekwa sheria za kanisa kabla ya baraza kuu la kanisa la karne ya Nne. Ufunuo wa asili. Hii ni namna ya Mungu mwenyewe kujifunua kwa mwanadamu. Unajumuisha utaratibu wa kiasili (Rum 1:19-20) na dhamila adilifu (Rum 2:14-15). Umeongelewa katika Zaburi 19:1-6 na Warumi 1-2. Unatofautishwa toka kwenye mafunuo maalumu, ambayo kwa mungu mwenyewe ni muhimu kujifunua katika Biblia na mwanae pekee Yesu wa Nazareti. Uangaliaji huu wa kithiolijia unasisitizwa tena na mwenendo wa “dunia ya zamani” kati ya wanasayansi wa Kikristo (cf. maandishi ya Hagh Ross) wanatumia uangaliaji huu kwa kuthibitisha kuwa kweli yote ni kweli ya Mungu. Ulimwengu ni mlango ulio wazi wa maarifa ya kumjua Mungu; ni tofauti toka kwa ufunuo maalumu (Biblia); unawapa wanasayansi uhuru wa kufanya uchunguzi juu ya utaratibu wa kiasili. Kwa maoni yangu , hii ni fursa mpya ya ajabu kushuhudiwa juu ya wanasayansi wa ulimwengu wa magharibi. Ufuasi wa Nestory. Nestory alikuwa ni mkuu wa familia ya Constantino kwenye karne ya tano. Alifundishwa huko Antiokia ya Syria na kuthibitisha kwamba Yesu ana asili mbili, moja ni mwanadamu kamili na nyingine ni Mungu kamili. Maoni haya yalichepushwa toka kwenye mtizamo wa asili wa mtu mmoja wa Orthodox kutoka Alexandria. Kusudio kubwa la Nestory lilikuwa ni cheo cha “mama wa Mungu” alichopewa Maria Magdalena. Nestory alipingwa na Cycil wa Alexandria na, kwa kuwekwa matatani juu ya mafundisho yake huko Antiokia. Antiokia yalikuwa makao makuu ya mtazamo wa kihistoria wa visarufi vya maandiko kwa utafasili wa Kibiblia, wakati Alexandria yalikuwa makao makuu ya shule Nne zilizotengwa kwa ajili ya utafasili. Nestory hatimaye aliondolewa toka ofisini na kukimbilia mafichoni. Mwandishi wa awali. Hii inarejerea wandishi halisi wa maandiko Mafunjo/Magombo. Haya yalikuwa aina mojawapo ya nyenzo toka Misri zilizotumika kuandikiapo maandiko.

Yalitengenezwa kwa majani au magome ya miti. Ni nyenzo ambazo nakala za zamani Agano la Kale la Kiyunani

zilihifaziwapo.

Vifungu Mlinganyo. Ni sehemu ya mtazamo kuwa yote yaliyomo kwenye Biblia yametoka kwa Mungu na, kwa

hiyo, ni ufafili wake mahsusi na mlinganyo wa kweli wa kimafumbo. Hili pia ni la msaada pale mtu anapojaribu

kutafasili kifungu kisicho wazi au kigumu. Pia inamsaidia mtu kupata kifungu kilicho wazi juu ya somo husika vile

vile mtazamo wote wa kimaandiko juu ya somo husika.

Ufafanuzi/fasili. Hili ni jina la nadhalia ya utafali wa Biblia. Utafasili wa Biblia unaweza kuangaliwa kama

mwendelezo wa mahusiano wa “neon kwa neon” ambapo neon la Kiingreza laweza kuweka kwa kila neon la

Kiebrania au Kiyunani kwenye “fasili” ambapo tu wazo limetafasiliwa kwa mtizamo wa kawaida wa neon au

kifungu cha awali. Kati ya nadhalia mbili hizi “mlinganyo wa nguvu” ambao unajaribu kuchukuawa kwa umakini

andiko la awali lakini likatafasiliwa katika muundo wa kisasa wa kisarufi na nahau. Kweli kabisa mjadara mzuri wa

nadhalia hizi mbali mbali za utafasili zinapatikana katika chapisho la Fee na Stuart How to Read the Bible For All Its

Worth, Uk. 35.

Aya. Huu ni msingi wa ufasili wa fasihi moja kinadhalia. Unajumuisha wazo moja kuu na mwendelezo wake.

Tukibaki na musukumo wake mkuu hatutatazama juu ya udogo wake au uzuri wa kusudi la mwandishi wa awali.

Page 457: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

441

Uparokia. Hii inahusiana na mapendeleo yaliyofungiwa kwenye muundo wa tamaduni/ thiolojia ya kawaida.

Haitambui asili ya mapokeo ya kweli yaliyobadilika ya Kibiblia au matumizi yake.

Fumbo. Hii inarejerea kweli zile zinazoonekana kuleta mkanganyiko, nab ado zote zikabaki kuwa kweli, ingawa

bado zinakinzana. Zinaunda kweli kwa kuwakilisha toka pande zilizo kinyume. Kweli nyingi za Kibiblia

zinawakilishwa kimafumbo (au kiupembuzi). Kweli za Kibiblia sio kama nyota zilizotengana, zimetengenezwa kwa

ukilimio wa sehemu za nyota.

Pilato. Alikuwa ni mmoja ya wanafalsafa wa Ugiriki ya kale. Falsafa yake kwa kiasi kikubwa ulisababisha kanisa la

mwanzo kupitia wasomi wa Alexandria, Misri na baadaye, Augustino. Alituma ujumbe kuwa kila kitu duniani ni

kiini macho na ni mfano tu wa kielelezo asili wa vitu vya rohoni. Baadaye wanathiolojia wakasawazisha

“mtizamo/mawazo” ya Pilato na ulimwengu wa kiroho.

Dhanio. Hili linarejerea uelewa wa jambo tulilowaza kabla. Mara nyingi tunaunda wazo au hukumu kuhusu

mambo hata kabla hatujatazamisha maandiko yenyewe. Uelekezaji huu vile vile hujulikana kama upendeleo,

kujitanguliza mbele, kudhania au kuelewa kabla.

Uhakiki wa maandishi. Hiki ni kitendo cha kutafasili maandiko kwa nukuu za kifungu bila kuangalia mazingira ya

haraka au ukubwa wa mazingira katika fahisi moja. Hii inaondoa vifungu toka kwa kusudio la mwandishi wa awali

na mara nyingi unahusha jaribio la kuhakiki maoni binafsi wakati huo likithibitisha mamlaka ya Kibiblia.

Ualimu wa dini ya Kiyahudi. Ngazi hii ya maisha ya watu wa Uyahudi yalianza walipokimbilia Babel (586-538 B.C).

kama ushawishi wa makuhani na hekalu ulivyoondolewa, masinagogi ya kawaida yakawa mtizamo wa maisha ya

Kiyahudi. Hivi vitovu vya kawaida vya tamaduni za Kiyahudi, ushirika, kuabudu na elimu ya Biblia ikawa mtizamo

wa maisha ya kidini kitaifa. Katika siku za Yesu, hii “dini ya wandishi” ilikuwa sambamba na ile ya makuhani. Katika

kuanguka kwa Yerusalem mwaka wa 70 A.D muundo wa kiandishi, ukitawaliwa na mafalisayo, walidhibiti

mwelekeo wa maisha ya kidini ya Kiyahudi. Inachagizwa na utafasili wa kiutendaji, na wa kisheria wa Torah kama

ulivyoelezwa katika tamaduni za Talmud.

Ufunuo. Hili ni jina lililopewa kwenye dhana ya kwamba Mungu amesemezana na mwanadamu. Wazo zima mara

nyingi limeelezewa katika maneno matatu- (1) Ufunuo-Mungu ametenda katika historia ya mwanadamu (2)

Uvuvio-Ametoa tafasili sahihi ya matendo yake na maana yake kwa mtu Fulani aliyemchagua kuweka

kumbukumbu ya mwanadamu (3)Nuru-Amempa Roho wake kumsaidia mwanadamu kuelewa ukaribu wake.

Elimu-maana. Hii imerejerea kipimo halisi cha maana kinachohusiana na neno. Kimsingi ina vidokezo mbali mbali

vya neno katika mazingira tofauti.

Maandiko ya kale ya Kiyunani. hili ni jina lililopewa tafasili ya Kiyunani ya Agano la kale la Kiebrania. Mafundisho

ya zamani yanasema kuwa yaliandikwa kwa siku 70 na wasomi sabini wa Kiyahudi kwa ajili ya maktaba ya

Alexandria, Misri. Tarehe ya kimapokeo ilikuwa 250 B.C (kiukweli yawezekana ilichukua zaidi ya miaka Mia

kumaliza kuandika). Tafasili hii ni muhimu kwa sababu (1)inatupatia andiko la kale kulinganisha na andiko la

Kiebrania (2) inatuonyesha sisi hali ya utafasili wa Kiyahudi katika karne ya pili nay a tatu B.C (3) inatupatia uelewa

wa umasihi wa Kiyahudi kabla ya kumkataa Yesu. Kifupi chake ni “LXX”.

Machapisho ya asili. Haya ni machapisho ya asili ya Kigiriki ya karne ya Nne A.D. Yalivumbuliwa na msomi wa

Kijerumani, Tischendorf, katika nyumba ya mtawa Catheline, kwenye eneo la kimila la mlima Sinai. Maandishi

haya yameundwa na herufi ya kwanza ya Kiebrania ya alfabeti inayoitwa “eleph” (א). Yanajumuisha Agano la Kale

na Agano Jipya kwa pamoja.

Kujitakasa. Hili neno ni kisawe chenye istiari katika maana kuwa linakwenda mpaka kwenye historian a mazingira

ya fasihi ya kifungu na kulifasili katika msingi wa jambo lingine.

Page 458: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

442

Visawe. Hii inarejerea maana yenye kariba au mfano wa maana moja (ingawa kiukweli hakuna maneno mawili

yenye elimu-maana kamili iliyopishana). Kwa karibu sana yanahusiana kiasi kwamba moja linaweza kuwa mbadala

wa lingine katika sentesi bila kupoteza maana. Pia yanatumika kuunda moja kati ya miundo mitatu ya mlinganyo

wa ushairi wa Kiebrania. Kwa maana hii inarejesha mistari miwili ya ushairi ambayo inaelezea kweli ile ile (cf. Zab

103:3).

Sintaksi. Hili ni neno la Kiyunani linalirejeresha muundo wa sentesi. Inahusiana na namna ya sehemu ya sentesi

zinaweza wekwa pamoja kuleta maana kamili.

Usanisi. Hii ni moja ya maneno matatu yanayohusiana na aina ya ushairi wa Kiebrania. Neon hili linaongelea juu

ya mistari ya ushairi uluojengwa juu ya mwingine katika maana moja, wakati mwingine huitwa “taaluma ya

mabadiliko ya hali” (k.v. Zab 19:7-9).

Thiolojia mpangilio. Hii ni hatua ya utafasili ambayo inajaribu kuhusisha ukweli wa Biblia katika hali ya pamoja na

mlingano. Ina mantiki zaidi kuliko historia tupu, ni uwasilishaji wa thiolojia ya Kikristo kwa namna ( Mungu, mtu,

dhambi,wokovu).

Buku la taratibu na kanuni za Kiyahudi. Ni wadhifa uliokuwapo kwa ajili ya upangaji wa simulizi za kanuni na

taratibu za Kiyahudi. Wayahudi wanaamini ulitolewa kwa Musa kwa kusimuliwa na Mungu kwenye mlima Sinai.

Ki-ukweli inaelekea kuwa ni mkusanyiko wa hekima za walimu wa Kiyahudi kwa miaka mingi. Kuna matoleo mawili

tofauti yaliyo andikwa juu ya Talmud: ya Babel na fupi la kiparestina ambalo halikwisha.

Uhakiki wa tofauti za kiuandishi. Huu ni usomaji wa maandiko wa Biblia. uhakiki wa maandiko ni muhimu kwa

sababu hakuna maandiko ya mwanzo yaliyopo na nakala zilizopo zinatofautiana toka moja hadi nyingine.

Unajaribu kuelezea utofauti na kufika (karibu iwezekanavyo) na maneno ya awali kabisa ya miandiko ya Agano la

kale na jipya. Mara nyingi unaitwa “uhakiki wa asili ya neno”.

Upokeaji wa Maandiko. Usanifishaji huu ulianzia kwenye toleo la Elzevir la Agano jipya la Kiyunani katika mwaka

wa 1633 A.D. Kimsingi ni muundo wa Agano jipya la Kiyunani lililozalishwa toka kwenye maandiko machache ya

asili ya Kiyunani na matoleo machache ya Erasmo ya Kilatini (1510-1535), Stephano (1546-1559) na Elzevir (1624-

1678). Katika An Introduction to the Textual Criticism of The New Testament uk. 27 cha A.T Robertson anasema

“andiko la Byzantine kiutendaji ni aina ile ile ya uundaji wa maandiko. Andiko la Byzantine ni la thamani ya chini

kati ya familia tatu ya maandiko ya awali ya Kiyunani (Kimagharibi, Alexandria na Byzantine). Inajumuisha

mkusanyiko wa makosa ya karne nyingi za maandiko na nakala za mkono. Hata hivyo, A.T Robertson alisema

uundaji wa maandiko umetunza kwa ajili yetu andiko sahihi kimalidhawa (uk.21). Mapokeo haya ya maandiko ya

asili ya Kiyunani (hasa Erasmo, toleo la tatu la 1522) yanatengeneza msingi wa toleo la King James la mwaka 1611

A.D.

Sheria za Musa. Hili ni neno la Kiebrania lenye maana ya “ufundishaji”. Lilitokea kuwa wadhifa rasmi wa

maandishi ya Musa (Mwanzo mpaka Kumbu kumbu la Torati). Kwa Wayahudi ulikuwa ni mgawanyo wa kimamlaka

wa kanuni za kanisa la Kiebrania.

Uanishaji. Hii ni aina ya urasimishaji wa wa utafasili. Mara nyingi unahusisha kweli ya Agano jipya inayopatikana

katika vifungu vya kale kwa njia ya analojia. Namna hii ya kanuni za ufasili ilikuwa ni dalili kubwa ya njia za

Alexandria. Kwa sababu ya matukano ya aina hii ya utafasili, mtu lazima aweke ukomo wa matumizi yake kwa

mfano mahsusi ulioandikwa katika Agano jipya.

Maandiko ya Vatican. Haya ni maandiko ya asili ya Kiyunani ya karne ya Nne A.D . Yalipatikana kwenye maktaba

ya Vatican. Uwasili wake unajumuisha vitabu vyote vya Agano la kale, ufunuo na Agano jipya. Hata hivyo, sehemu

zingine zilipotea( Mwanzo, Zaburi, Waebrania, Filemon na Ufunuo). Inasaidia maandiko ya asili kubadilisha

miandiko ya maneno ya awali. Tena yameundwa kwa herufi kubwa “B”.

Page 459: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

443

Tafasili ya Biblia ya Kilatini. Ni jina la tafasili ya Biblia ya Kilatini ya Jerome. Ilikuwa ndio msingi au utafasili wa

“kawaida”wa kanisa Katoriki la Rumi. Lilifanyika mwaka 380 A.D.

Hekima ya Fasihi. Hii ni fasihi tanzu iliyozoeleka enzi za kale karibu na pande za Mashariki (na ulimwengu wa

kisasa). Kimsingi lilikuwa ni jaribio la kuelekeza kizazi kipya juu ya mwongozo wa maisha ya ushindi kupitia ushairi,

mithali, au insha. Ilielezewa zaidi kwa watu binafsi kuliko kwenye jumuiya iliyoungana. Haikutumia viini macho

kuweka historia, lakini ilisimamia uzoefu na uchunguzi wa maisha katika Biblia, Ayubu kupita Wimbo ulio Bora,

anasadiki uwepo na ibada ya YAHWE, lakini mtizamo huu wa ulimwengu wa kidini sio wa wazi kwa uzoefu wa kila

mtu kila wakati.

Picha ya ulimwengu na Mtizamo wa Kidunia. Haya ni maneno mwandani. Yote yana dhana ya kifalsafa kuhusiana

na uumbaji. Neno “picha ya ulimwengu” inarejerea “kwa namna gani” juu ya uumbaji wakati “mtizamo wa

kidunia” unahusiana na “nani.” Maneno haya yote ni muhimu kwenye utafasili pale mwanzo 1-2 inaposhughulika

hasa hasa na nani, na sio kwa namna gani juu ya ulimwengu.

YAHWE/YEHOVA. Hili ni jina la Agano la Mungu katika Agano la kale. Linaelezewa katika kitabu cha Kutoka 3:14.

Ni muundo wa KISABABISHAJI wa neno la Kiebrania “kuwa” ambalo Wayahudi waliogopa kulitamka jina hili ili

wasilitamke bure; kwa hiyo, walitumia jina lingine badala yake yaani “Adonai” likimaanisha “Bwana”. Hivi ndivyo

jina la Agano limetafasiliwa katika Kiingereza.

Page 460: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

444

KAULI YA KIMAFUNDISHO

Mimi siangalii hasa habari za imani au kanuni za imani. Napendelea kuthibitisha Biblia yenyewe. Ingawa,

natambua kuwa habari ya imani itawaleta wale tusiojuana ili kupima mtizamo wa mafundisho yangu. Katika siku

zetu za leo zenye makosa mengi ya kithiolojia na upotofu, natoa muhtsari mfupi wa thiolojia yangu kama

ifuatavyo.

1. Biblia, yote katika Agano la Kale na Agano Jipya, ni neno la Mungu lililovuviwa, lenye uhakika, lenye uzima

na lenye mamlaka. Ni ufunuo pekee wa Mungu ulioandikwa na watu chini ya uongozi wa nguvu za ajabu.

Ni kiini pekee cha ukweli sahihi kuhusu Mungu na Kusudi Lake. Pia ni kiini pekee cha imani na utendaji wa

kanisa lake.

2. Kuna Mungu mmoja tu wa uzima, muumbaji na mkombozi. Yeye ndiye muumbaji wa vitu vyote,

vionekanavyo na visivyo onekana. Amejidhihilisha mwenyewe kama Mungu wa upendo na anayejali

ingawa pia ni Mungu asiye na upendeleo. Amejidhihilisha mwenyewe katika nafsi tatu tofauti: Baba,

Mwana na Roho; haswa wanatengana lakini wanafanya kazi moja.

3. Muda wote Mungu yuko hai kuangalia ulimwengu huu. Kuna mpango wa milelekwa uumbaji wake

usiobadilika na mtazamo wa kipekee unaomfanya binadamu kutenda mapenzi huru. Hakuna kinachoweza

kutokea pasipo ruhusa na maarifa ya Mungu, bado anaruhusu uchaguzi kwa wote malaika na wanadamu.

Yesu ni chaguo la Baba na wote kimanufaa wamechaguliwa katika Yeye. Ufahamu wa mbele wa Mungu

kuhusu matukio hayampunguzii binadamu kubainisha maandiko yaliyoandikwa kabla. Wote tunahusika

kwa mawazo yetu na matendo.

4. Binadamu, japo aliumbwa kwa sura ya Mungu na mbali na dhambi, aliamua kumwasi Mungu. Ingawa

alijaribiwa na kitu chenye nguvu ya ziada. Adamu na Hawa waliwajibika kwa utashi wao wenyewe

kuamua. Uasi wao umeathiri utu wa uumbaji. Watu wote tunahitaji rehema na huruma ya Mungu yote

kwa hali ya ushirika katika Adamu na uasi binafsi wa hiari.

5. Mungu anatoa aina ya msamaha na urejesho kwa binadamu aliyeanguka. Yesu Kristo, Mwana pekee wa

Mungu Baba, akawa mwanadamu, akaishi maisha yasio na dhambi, na kwa kifo chake mbadala, akalipa

malipo ya dhambi ya mwanadamu. Ndiyo njia pekee ya kurejesha ushirika wetu na Mungu. Hakuna njia

nyingine ya wokovu isipokuwa kupitia imani ya kazi yake aliyoimaliza.

6. Kila mmoja wetu binafsi yampasa kupokea ahadi ya msamaha na urejesho katika Kristo. Hilo linatimizwa

kwa njia ya imani ya hiari katika ahadi za Mungu kupitia Kristo Yesu na kugeuka kwa mapenzi huru kwa

dhambi inayojulikana.

7. Sisi sote tumesamehewa jumla na urejesho umelenga juu ya kuamini katika Kristo na toba toka dhambini.

Ingawa, ushahidi wa mahusiano mapya unaonekana katika mabadiliko na badiliko endelevu. Dhumuni la

Mungu kwa wanadamu sio tu kwenda mbinguni siku moja, lakini kufanana na Kristo kwa sasa. Wale wote

ambao wanakombolewa kweli ingawa wakati mwingine wanatenda dhambi, wataendelea katika imani na

toba siku zao zote za maisha.

8. Roho Mtakatifu ni “Yesu mwingine”. Yuko duniani kuwaongoza wale wote waliopotea katika Kristo na

kujenga ufanano wa Kristo katika kuokolewa. Karama za rohoni zinapewa toka kwenye wokovu. Ni

maisha na huduma ya Yesu yaliyogawiwa katika mwili wake, yaani kanisa. Vipawa 358 ambavyo kimsingi

ndio mwelekeo na msukumo wa hitaji la Yesu likihamasishwa na tunda la Roho. Roho yu hai katika siku

zetu kama alivyokuwa katika enzi za Biblia.

9. Baba amemfanya Yesu Kristo aliyefufuka kama mwamuzi w vitu vyote. Atarudi duniani kuhukumu

wanadamu wote. Wale wote walioamini Yesu na majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima cha

mwanakondoo watapata mwili na utukufu ataporudi. Wataishi nae milele. Ingawa, wale wote walioikataa

Page 461: FASIRI YA BIBLIA ISIYOGHARIMIWA UNAWEZA KUIELEWA BIBLIA ... · Fasiri hii humpa mwanafunzi njia ya haraka ya kuchunguza fasiri zake. Hii haina maana kuwa ni ya kumalizia, bali ni

445

kweli ya Mungu watatengwa milele toka katika furaha ya ushirika wa Mungu wa Utatu. Watahukumiwa

pamoja na shetani na malaika zake.

Hii hakika haijaisha au kukamilika lakini natarajia itakupa ladha ya kithiolojia ya moyo wangu,

nafurahia maelezo:

“Katika mambo ya msingi-umoja, mambo yaliyo ukingoni-uhuru, katika mambo yote-upendo.”