33
Sheria Ndogo za Kijiji cha Kashagulu Usimamizi Shirikishi wa Msitu wa Hifadhi ya Kijiji na Hifadhi ya Mazalia ya Samaki ya Ziwa Tanganyika Sehemu ya Kijiji cha Kashagulu 2007 SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA (MAMLAKA ZA WILAYA) NA. 7 YA 1982 SHERIA NDOGO Zimundwa chini ya Kifungu cha 167

SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

  • Upload
    others

  • View
    53

  • Download
    7

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Sheria Ndogo za Kijiji cha

Kashagulu

Usimamizi Shirikishi wa Msitu

wa Hifadhi ya Kijiji na Hifadhi ya

Mazalia ya Samaki ya Ziwa

Tanganyika Sehemu ya Kijiji cha

Kashagulu 2007

SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA

(MAMLAKA ZA WILAYA) NA. 7 YA 1982

SHERIA NDOGO

Zimundwa chini ya Kifungu cha 167

Page 2: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho
Page 3: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Yaliyomo

1. Jina ............................................................................................... 1 2. Tarehe ya Kuanza na Eneo la Kutumika kwa Sheria hii. ............ 1 3. Marekebisho ya Sheria ................................................................ 1 4. Tafsiri ............................................................................................ 2 5. Madhumuni ................................................................................... 5 6. Umilikaji ........................................................................................ 5 8. Kamati ya Mazingira..................................................................... 6 9. Majukumu ya Kamati ya Mazingira .............................................. 7 10. Ulinzi na Ukaguzi wa Msitu wa Hifadhi ya kijiji na Hifadhi ya

Mazalia ya Samaki ya Ziwa Tanganyika Sehemu ya Kijiji cha Kashagulu .................................................................................... 9

11. Walinzi wa Msitu wa hifadhi ya kijiji na Hifadhi ya Mazalia ya Samaki ya Ziwa Tanganyika ...................................................... 10

12. Masharti ya Kuingia msitu wa Hifadhi ya Kijiji na Hifadhi ya Mazalia ya Samaki ya Ziwa Tanganyika Sehemu ya Kashagulu. .................................................................................................... 12

13. Masharti ya Matumizi ya Msitu wa Hifadhi ya Kijiji na Hifadhi ya Mazalia ya Samaki ya Ziwa Tanganyika sehemu ya Kashagulu. .................................................................................................... 13

14. Vitendo Vilivyopigwa Marufuku .................................................. 14 15. Vitendo Vinavyoruhusiwa kwa Vibali na Malipo ........................ 15 16. Kiasi cha malipo ......................................................................... 16 17. Vitendo Vinavyohitaji Kibali bila malipo (Bure) .......................... 17 18. Viwango vya Faini ...................................................................... 18 19. Gharama na Fidia ...................................................................... 20 20. Faini ya wenye Dhamana/ Madaraka ........................................ 20 21. Taratibu za Kushughulikia Wahalifu wa Msitu wa Hifadhi na

Hifadhi ya Mazalia ya Samaki ya Ziwa Tanganyika sehemu ya Kashagulu. ................................................................................. 21

22. Namna ya Kushughulikia Mazao ya Msitu na Ziwa Tanganyika Yaliyokamatwa, Faini Zilizotozwa na Mgawanyo Wake: ........... 23

23. Kuwasilisha Mashauri Mahakamani .......................................... 24 24. Hatua za Mahakamani ............................................................... 24 25. Mapato na Matumizi ya Fedha za Hifadhi ya Msitu na Hifadhi ya

Mazalia ya Samaki ya Ziwa Tanganyika Sehemu ya Kijiji cha Kashagulu. ................................................................................. 25

26. Matumizi ya Fedha za Kamati ya Mazingira .............................. 26

Page 4: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho
Page 5: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Sheria ndogo za Kijiji cha Kashagulu Usimamizi wa Hifadhi ya Msitu na Mazalia ya Samaki Ziwa Tanganyika

1

SHERIA NDOGO

Zimeundwa chini ya Kifungu cha 167

1. Jina

1.1. Sheria ndogo hizi ziitwe“Sheria ndogo za Kijiji cha

Kashagulu (Usimamizi Shirikishi wa Msitu wa Hifadhi

ya Kijiji na Hifadhi ya Mazalia ya Samaki ya Ziwa

Tanganyika Sehemu ya Kijiji cha Kashagulu), 2007”

2. Tarehe ya Kuanza na Eneo la Kutumika kwa Sheria hii.

2.1. Sheria hii ndogo ya kijiji itaanza kutumika baada ya

kupitishwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kwa

kutiwa sahihi na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji

wa Halimashauri ya Wilaya ya Kigoma.

2.2. Sheria hii itatumika ndani ya mipaka ya eneo la Kijiji

cha Kashagulu.

3. Marekebisho ya Sheria

3.1. Halmashauri ya Kijiji cha Kashagulu kwa idhini ya

Mkutano Mkuu wa kijiji inaweza kufanya marekebisho

ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya

kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria

hii itafanyiwa marekebisho na kupitishwa na Mkutano

Mkuu wa kijiji na Kamati ya Maendeleo ya Kata ya

Kalya.

3.2. Mapendekezo ya mabadiliko yanayokusudiwa

kufanywa ni lazima yapelekwe kwa Afisa Misitu/Uvuvi

Wilaya kwa ushauri zaidi.

3.3. Taarifa za mabadiliko haya ni lazima zitumwe kwa

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya

Kigoma.

Page 6: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Sheria ndogo za Kijiji cha Kashagulu Usimamizi wa Hifadhi ya Msitu na Mazalia ya Samaki Ziwa Tanganyika

2

4. Tafsiri

4.1. Katika Sheria hii tafsiri zifuatazo zimekusudiwa:

4.1.1. “Msitu wa Hifadhi ya kijiji” maana yake ni

sehemu ya ardhi ya kijiji yenye msitu iliyotengwa

na kuhifadhiwa, ambayo kwa mujibu wa Sheria hii

utakuwa Msitu wa Hifadhi ya kijiji cha Kashagulu.

4.1.2. “Hifadhi ya mazalia ya samaki ya Ziwa

Tanganyika” maana yake ni mita mia (100) ya

sehemu ya Ziwa Tanganyika toka kingo za ziwa

ambayo ni muhimu kwa mazalia ya samaki.

4.1.3. “Mpango wa Usimamizi Shirikishi wa Msitu

na mazalia ya samaki ya Ziwa Tanganyika”

maana yake ni mpango au utaratibu wa utekelezaji

uliotayarishwa na Kamati ya Mazingira ya kijiji kwa

ushauri wa wataalam wa misitu na uvuvi kwa lengo

la kuelekeza namna ya utekelezaji wa utumiaji,

ulinzi, na uendelezaji wa msitu wa hifadhi ya kijiji

na hifadhi ya mazalia ya samaki ya Ziwa

Tanganyika sehemu ya kijiji cha Kashagulu.

4.1.4. “Kamati ya Mazingira” maana yake ni Kamati

ya Mazingira ya kijiji cha Kashagulu ambayo

imepewa jukumu la kusimamia utumiaji, ulinzi na

uendelezaji wa msitu wa hifadhi ya kijiji na mazalia

ya samaki ya Ziwa Tanganyika sehemu ya

Kashagulu.

4.1.5. “Maeneo yaliyozuiliwa/hifadhiwa” maana yake

ni maeneo yeyote katika msitu wa hifadhi ya kijiji

na Ziwa Tanganyika ambayo kutokana na

umuhimu wake imeamuliwa na Halmashauri ya

kijiji na Kamati ya Mazingira yahifadhiwe /zuiliwe

kwa matumizi fulani kwa wakati husika.

Page 7: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Sheria ndogo za Kijiji cha Kashagulu Usimamizi wa Hifadhi ya Msitu na Mazalia ya Samaki Ziwa Tanganyika

3

4.1.6. “Maeneo ya matumizi” maana yake ni yale

maeneo ndani ya msitu wa hifadhi ya kijiji cha

Kashagulu ambayo Kamati ya Mazingira na

Halmashauri ya kijiji imeamua yaruhusiwe kwa

matumizi mbali mbali endelevu.

4.1.7. “Mlinzi/walinzi wa msitu na ziwa”maana yake

ni mtu au watu waliochaguliwa na Mkutano

Mkuu wa kijiji/Halmashauri ya kijiji kwa ajili ya

kufanya doria za ukaguzi ndani ya eneo la msitu

wa hifadhi ya kijiji na mazalia ya samaki ya Ziwa

Tanganyika sehemu ya kijiji cha Kashagulu.

4.1.8. “Halmashauri ya kijiji”maana yake ni

Halmashauri ya kijiji cha Kashagulu.

4.1.9. “Mkutano Mkuu wa kijiji” maana yake ni

mkutano wa wanakijiji wote wa kijiji cha

Kashagulu. Huu ndio mkutano wenye mamlaka

ya kufanya uamuzi wa masuala yote kijijini.

4.1.10. “Mahakama” maana yake ni Mahakama ya

Mwanzo au ya Wilaya.

4.1.11. “Mwenyekiti wa kijiji” maana yake ni

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijiji cha

Kashagulu.

4.1.12. “Afisa Mtendaji wa kijiji” maana yake ni Afisa

Mtendaji wa kijiji cha Kashagulu

4.1.13. “Afisa Mtendaji wa Kata” maana yake ni Afisa

Mtendaji wa Kata ya Kalya

4.1.14. “Mwenyekiti wa kitongoji” maana yake ni

kiongozi aliyechaguliwa kuongoza kitongoji

chochote katika kijiji cha Kashagulu.

4.1.15. “Afisa Misitu Wilaya” maana yake ni Afisa

Misitu wa Serikali anayesimamia na kuongoza

Page 8: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Sheria ndogo za Kijiji cha Kashagulu Usimamizi wa Hifadhi ya Msitu na Mazalia ya Samaki Ziwa Tanganyika

4

matumizi ya rasilimali ya misitu katika Wilaya ya

Kigoma.

4.1.16. “Kitongoji” maana yake ni kitongoji chochote

cha kijiji cha Kashagulu kinachotambuliwa na

Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.

4.1.17. “Vyanzo vya maji” maana yake ni chemchem,

mito, makorongo, ardhi oevu katika eneo la

msitu wa hifadhi ya kijiji.

4.1.18. “Miteremko mkali” maana yake ni ardhi yeyote

ndani ya msitu wa hifadhi ya kijiji yenye

mwinuko wa nyuzi 30 (300) au zaidi.

4.1.19. “Mazao ya misitu” maana yake ni rasilimali

yoyote inayopatikana kutoka msituni kama vile:

miti, mbao, kuni, mkaa, fito, nguzo, magome,

kamba, unga wa mbao, mizizi, gundi, mbegu,

majani, matunda, mboji, udongo, asali, nta na

mafuta.

4.1.20. “Zana” maana yake ni vifaa vinavyotumika

kihalali au isiyohalali kukatia miti na ni pamoja

na misumeno, shoka, panga, mundu, kisu,

jembe au kifaa kingine chochote kinachoweza

kukata mazao ya misitu. Pia vifaa

vinavyotumika katika kuvulia samaki majini

ikiwa ni pamoja na nyavu, mitumbwi, ndoano na

kokoro.

4.1.21. ‘’Mhalifu” maana yake ni mtu yeyote

atakayekiuka/kuvunja Sheria hizi ndogo, Sheria

Kuu ya Misitu No.14, 2002 na Sheria

zinazosimamia rasilimali ya Ziwa Tanganyika.

4.1.22. “Wanyamapori” maana yake ni jamii ya

wanyama wote wanaopatikana na kuishi

Page 9: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Sheria ndogo za Kijiji cha Kashagulu Usimamizi wa Hifadhi ya Msitu na Mazalia ya Samaki Ziwa Tanganyika

5

kwenye maeneo yao ya asili ndani ya misitu na

mapori yanazozunguka msitu wa hifadhi ya kijiji

cha Kashagulu. Baadhi ya wanyama hao ni

sungura, kongoni, nyati/mbogo, faru, tembo,

swala, fisi, chui, mamba, simba, n.k.

5. Madhumuni

5.1. Sheria hizi ndogo zimeundwa na Halmashauri ya kijiji

na kupitishwa na Mkutano Mkuu wa kijiji kwa lengo /

madhumuni ya kutumia, kulinda na kuendeleza eneo la

msitu wa hifadhi ya kijiji na hifadhi ya mazalia ya

samaki ya Ziwa Tanganyika sehemu ya kijiji cha

Kashagulu kwa kuzingatia taratibu zilizoainishwa katika

Mpango wa Usimamizi Shirikishi wa Msitu wa Hifadhi

ya Kijiji na Hifadhi ya Mazalia ya Samaki ya Ziwa

Tanganyika sehemu ya kijiji cha Kashagulu.

5.2. Sheria hizi ndogo zinatoa madaraka kamili kwa Kamati

ya Mazingira kwa niaba ya Halmashauri ya kijiji

kusimamia matumizi, ulinzi na uendelezaji wa msitu wa

hifadhi ya kijiji na hifadhi ya mazalia ya samaki ya Ziwa

Tanganyika sehemu ya kijiji cha Kashagulu na

itawajibika katika kuthibiti matumizi ya eneo la msitu na

ziwa, na kuwashughulikia watu wanaokiuka Sheria hizi.

6. Umilikaji

6.1. Eneo la Msitu wa Hifadhi ya kijiji cha Kashagulu

linabakia kuwa sehemu kamili ya ardhi ya Halmashauri

ya kijiji cha Kashagulu na eneo la hifadhi ya mazalia ya

samaki ya Ziwa Tanganyika linabakia kuwa ni mali ya

Taifa la Tanzania, hivyo Halmashauri ya kijiji cha

Kashagulu itakuwa msimamizi tu kuhakikisha kuwa

Ziwa Tanganyika linatumika kwa matumizi endelevu.

Page 10: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Sheria ndogo za Kijiji cha Kashagulu Usimamizi wa Hifadhi ya Msitu na Mazalia ya Samaki Ziwa Tanganyika

6

7. Meneja Mteule

7.1. Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki Tanzania ameiteua

Halmashauri ya kijiji cha Kashagulu kuwa Meneja

Mteule wa msitu wa hifadhi ya kijiji cha Kashagulu.

7.2. Halmashauri ya kijiji cha Kashagulu kwa mujibu wa

taratibu za utendaji imeteua Kamati ya Mazingira ya

kijiji kutekeleza jukumu la usimamizi wa msitu wa

hifadhi ya kijiji na hifadhi ya mazalia ya samaki ya Ziwa

Tanganyika kwa niaba yake.

8. Kamati ya Mazingira

8.1. Kamati ya Mazingira iliyopendekezwa na serikali ya

kijiji na kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa kijiji itakuwa

na wajibu wa kutekeleza jukumu la usimamizi wa msitu

wa hifadhi ya kijiji na hifadhi ya mazalia ya samaki ya

Ziwa Tanganyika chini ya serikali ya kijiji

8.2. Kamati ya Mazingira itachaguliwa kila baada ya miaka

mitatu na itakuwa na wajumbe wasiozidi kumi na nne

(14) kwa uwakilishi wa kutoka kila kitongoji. Idadi ya

wajumbe wanawake isipungue 30% ya wajumbe wote

wa Kamati ya Mazingira.

8.3. Kamati ya Mazingira itachagua viongozi wake kutoka

miongoni mwa wajumbe wake. Nafasi za uongozi

katika Kamati ya Mazingira ni Mwenyekiti, Katibu na

Mweka Hazina.Kila mjumbe wa Kamati ya Mazingira

anaweza kupewa jukumu maalumu kama

watakavyoona inafaa.

8.4. Mabadiliko katika uongozi wa Kamati ya Mazingira

yanaweza kufanyika wakati wowote ilimradi uongozi

mpya unachaguliwa kwa uwingi wa kura za wajumbe

wa Kamati ya Mazingira. Ni lazima Serikali ya Kijiji

ijulishwe kuhusu azma ya kufanya mabadiliko hayo.

Page 11: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Sheria ndogo za Kijiji cha Kashagulu Usimamizi wa Hifadhi ya Msitu na Mazalia ya Samaki Ziwa Tanganyika

7

8.5. Kamati ya Mazingira itakutana mara moja kila mwezi

katika hali ya kawaida. Vikaovya dharura vinaweza

kufanyika wakati wowote. Vikao vya Kamati ya

Mazingira vitafanyika iwapo mahudhurio ya wajumbe

wa Kamati ya Mazingira itakuwa zaidi ya nusu ya idadi

ya wajumbe. Katibu wa Kamati ya Mazingira ataandika

mihtasari ya vikaoyenye nakala kwa Afisa Mtendaji wa

Kijiji.

8.6. Kamati ya Mazingira itaandika taarifa yake ya

utekelezaji mara moja kwa mwezi kwa Afisa Mtendaji

wa Kijiji ambaye atawajibika kutoa taarifa hizo kwenye

vikao vya Halmashauri ya kijiji kila mwezi na Mkutano

Mkuu wa kijiji mara nne kwa mwaka yenye nakala kwa

Afisa Misitu (W) mara nne kwa mwaka.

8.7. Iwapo kutakuwa na malalamiko yoyote kuhusu Kamati

ya Mazingira ni lazima Mwenyekiti au Afisa Mtendaji

wa Kijiji achunguze malalamiko hayo kwa kushirikisha

wajumbe wa Halmashauri ya kijiji na kuchukua hatua

zinazostahili kurekebisha dosari zinazolalamikiwa

iwapo zitathibitika.

9. Majukumu ya Kamati ya Mazingira

9.1. Kamati ya Mazingira itakuwa na majukumu yafuatayo:

9.1.1. Kuhakikisha kuwa mipaka yote ya msitu wa

hifadhi ya kijiji na hifadhi ya mazalia ya samaki

ya Ziwa Tanganyika sehemu ya Kashagulu

inaeleweka waziwazi kwa wanakijiji wote wa

Kashagulu.

9.1.2. Kusimamia utekelezaji wa mipango yote

inayohusu utumiaji, ulinzi na uendelezaji wa

msitu na mazalia ya samaki ya Ziwa Tanganyika

sehemu ya kijiji cha Kashagulu.

Page 12: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Sheria ndogo za Kijiji cha Kashagulu Usimamizi wa Hifadhi ya Msitu na Mazalia ya Samaki Ziwa Tanganyika

8

9.1.3. Kwa kushirikiana na Halmashauri ya kijiji na

wanakijiji wengine kutambua na kutenga msitu

katika kanda / maeneo mbalimbali (matumizi

/uhifadhi) kulingana na hali halisi ya msitu.

9.1.4. Kutunza kumbukumbu zote zinazohusu shughuli

za utumiaji, ulinzi, na uendelezaji wa msitu wa

hifadhi ya kijiji. Kumbukumbu hizo ni:-

9.1.4.1 Mihtasari ya mikutano

9.1.4.2 Doria

9.1.4.3 Uhalifu na faini

9.1.4.4 Vibali vilivyotolewa

9.1.4.5 Mapato na matumizi ya fedha za msitu na

hifadhi ya mazalia ya samaki ya Ziwa

Tangnyika

9.1.4.6 Uoteshaji na upandaji miti, pia shughuli

zote za uhifadhi mazingira ndani ya

maeneo ya kijiji

9.1.5. Kuhakikisha kuwa walinzi wa msitu na hifadhi ya

mazalia ya samaki wanatekeleza kazi yao

kikamilifu na kuchukua hatua zinazopasa

kuondoa dosari zinazojitokeza katika kazi ya

ulinzi.

9.1.6. Kufanya ukaguzi wa msitu wa hifadhi na hifadhi

ya mazalia ya samaki ya kijiji angalau mara mbili

kwa mwezi.

9.1.7. Kuhakikisha matumizi endelevu ya msitu na

Ziwa Tanganyika yanazingatiwa kulingana na

kanuni za matumizi zilizowekwa na kukubaliwa.

9.1.8. Kuwashughulikia wahalifu wa msitu na Ziwa

Tanganyika kwa mujibu wa kanuni za adhabu

Page 13: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Sheria ndogo za Kijiji cha Kashagulu Usimamizi wa Hifadhi ya Msitu na Mazalia ya Samaki Ziwa Tanganyika

9

zilizowekwa na kukubalika kwa ushirikiano na

Halmasahauri ya kijiji.

9.1.9. Kwa ushirikiano na Halmashauri ya kijiji,

kuwahamasisha wanakiiji kushiriki katika suala

zima la uhifadhi wa msitu, Ziwa Tanganyika na

mazingira ya kijiji kwa ujumla.

9.1.10. Kutumia na kutunza vitabu vya stakabadhi

vilivyoidhinishwa na Halmashauri ya Wilaya ya

Kigoma.

9.1.11. Kufungua Akaunti Benki ya Kamati ya Mazingira

ya kijiji kwa ajili ya kuweka fedha za mapato ya

msitu na hifadhi ya mazalia ya samaki ya Ziwa

Tanganyika (ushuru na faini).

9.1.12. Kuhakikisha kuwa fedha za Akaunti ya Kamati

ya Mazingira zinatumika kama zilivyokusudiwa

na kuidhinishwa na Halmashauri ya kijiji cha

Kashagulu.

9.1.13. Kuweka utaratibu wa utoaji wa vibali ili

kuhakikisha kuwa vibali vinavyotolewa ni vile

vilivyoko katika mamlaka ya Kamati ya

Mazingira na kwamba utoaji wa vibali

unakwenda sambamba na mahitaji yaliyopo na

sio vinginevyo.

10. Ulinzi na Ukaguzi wa Msitu wa Hifadhi ya kijiji na

Hifadhi ya Mazalia ya Samaki ya Ziwa Tanganyika

Sehemu ya Kijiji cha Kashagulu

10.1. Kila mwanakijiji wa Kashagulu ana jukumu la kulinda

na kutunza hifadhi ya ziwa na msitu wa kijiji. Hili

jukumu litafanyika kwa kutekeleza yafuatayo:

10.1.1. Kutoa taarifa za uhalifu

Page 14: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Sheria ndogo za Kijiji cha Kashagulu Usimamizi wa Hifadhi ya Msitu na Mazalia ya Samaki Ziwa Tanganyika

10

10.1.2. Kutambua na kutoa taarifa za wahalifu wa msitu

na Ziwa Tanganyika, na zana zao haramu.

10.1.3. Kuzuia moto usitokee na kuzima unapotokea.

10.1.4. Kushiriki katika shughuli za uoteshaji miche ya

miti na upandaji wa miti.

10.1.5. Wakazi wa kijiji ambao maeneo yao

yanapakana na msitu wa hifadhi ya kijiji na

hifadhi ya mazalia ya samaki ya Ziwa

Tanganyika sehemu ya Kashagulu wana wajibu

wa ziada wa kuhakikisha kuwa eneo hilo

haliingiliwi na kuharibiwa kwa namna yeyote ile.

10.1.6. Ni wajibu wa wakazi wote wa kijiji cha

Kashagulu kushirikiana katika ulinzi wa msitu

wa hifadhi ya kijijii na hifadhi ya mazalia ya

samaki ya Ziwa Tanganyika sehemu ya kijiji cha

Kashagulu.

11. Walinzi wa Msitu wa hifadhi ya kijiji na Hifadhi ya

Mazalia ya Samaki ya Ziwa Tanganyika

11.1. Doria za ukaguzi katika msitu wa hifadhi ya kijiji na

hifadhi ya mazalia ya samaki ya Ziwa Tanganyika

sehemu ya kijiji cha Kashagulu zitafanywa na

walinzi/wanadoria angalau mara tatu kwa wiki.

11.2. Walinzi wa msitu na hifadhi ya mazalia ya samaki ya

Ziwa Tanganyika watachaguliwa na Halmashauri ya

kijiji na kuthibitishwa na Mkutano Mkuu wa kijiji

kutoka katika vitongoji vyote vya kijiji na idadi yao

haitakuwa chini ya wajumbe kumi (10). Vitongoji vya

Ugalaba, Ubanda na Lufubu vitatoa walinzi wawili

kila kitongoji na vitongoji vingine vitatoa mmoja kila

kitongoji.

Page 15: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Sheria ndogo za Kijiji cha Kashagulu Usimamizi wa Hifadhi ya Msitu na Mazalia ya Samaki Ziwa Tanganyika

11

11.3. Walinzi wa msitu na hifadhi ya mazalia ya samaki ya

Ziwa Tanganyika watakaochaguliwa wanatakiwa

kuwa na tabia zifuatazo:

11.3.1. Awe na tabia na mwenendo mzuri.

11.3.2. Wenye kujituma na mwaminifu.

11.3.3. Mkakamavu na mwenye afya nzuri.

11.3.4. Asiwe mlevi

11.3.5. Awe mkazi wa kijiji cha Kashagulu na raia wa

Tanzania.

11.3.6. Awe na umri wa miaka kumi na nane (18) na

kuendelea

11.4. Walinzi watachagua kiongozi wao (Kamanda) kutoka

miongoni mwao ambaye atawajibika kupanga

utaratibu wa doria kwa kushirikiana na wanadoria

wengine na utoaji taarifa kwa Kamati ya Mazingira.

11.5. Walinzi wa msitu na hifadhi ya mazalia ya samaki ya

Ziwa Tanganyika hawatalipwa mishahara lakini

watapata motisha kama itakavyoamuliwa na serikali

ya kijiji. Aidha walinzi husika wanaweza kupewa 30%

ya faini anayotozwa mhalifu. Vile vile walinzi wa

msitu wa hifadhi ya kijiji na mazalia ya samaki ya

Ziwa Tanganyika wanaweza kusamehewa kazi

nyingine za maendeleo kijijini.

11.6. Mwenyekiti wa vi/kitongoji kinachopakana na msitu

wa hifadhi ya kijiji na hifadhi ya mazalia ya samaki ya

Ziwa Tanganyika sehemu ya kijiji cha Kashagulu

anao wajibu wa kuhakikisha kuwa ulinzi wa msitu wa

hifadhi ya kijiji na mazalia ya samaki unafanyika

ipasavyo kwa kushirikiana na walinzi na

wanakitongoji wake.

Page 16: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Sheria ndogo za Kijiji cha Kashagulu Usimamizi wa Hifadhi ya Msitu na Mazalia ya Samaki Ziwa Tanganyika

12

11.7. Afisa Mtendaji wa Kata anao wajibu wa kutoa

msukumo katika ulinzi wa msitu wa hifadhi wa kijiji na

hifadhi ya mazalia ya samaki ya Ziwa Tanganyika

katika Kata yake.

11.8. Afisa Misitu/Uvuvi/Nyuki/Wanyamapori (W) anao

wajibu wa kukagua maeneo ya msitu wa hifadhi ya

kijiji na hifadhi ya mazalia ya samaki ya Ziwa

Tanganyika sehemu ya Kashagulu wakati wowote na

kusaidia kazi ya ulinzi pale inapohitajika kufanya

hivyo.

12. Masharti ya Kuingia msitu wa Hifadhi ya Kijiji na

Hifadhi ya Mazalia ya Samaki ya Ziwa Tanganyika

Sehemu ya Kashagulu.

12.1. Mkazi yeyote wa kijiji cha Kashagulu, Afisa

Misitu/Uvuvi au mtu yeyote aliyeruhusiwa wanaweza

kuingia msitu wa hifadhi ya kijiji na hifadhi ya mazalia

ya samaki ya Ziwa Tanganyika sehemu ya

Kashagulu.

12.2. Afisa Misitu/Uvuvi/Nyuki/Wanyamapori yeyote wa

Idara ya Misitu na Nyuki, Wanyamapori na Uvuvi

wakati wowote anaweza kuingia ndani ya msitu wa

hifadhi ya kijiji na hifadhi ya mazalia ya samaki ya

Ziwa Tanganyika sehemu ya Kashagulu aidha akiwa

peke yake au kwa kushirikiana na Kamati ya

Mazingira ya kijiji kwa lengo la kufanya ukaguzi na

kutoa ushauri kwa Kamati ya Mazingira ambao

unapaswa kupokelewa na kufanyiwa kazi kwa lengo

la kuboresha uendelezaji wa eneo hilo la msitu/ziwa.

12.3. Sio ruksa kwa mtu yeyote kuingia msitu wa hifadhi ya

kijiji na hifadhi ya mazalia ya samaki ya Ziwa

Tanganyika sehemu ya Kashagulu bila kibali kutoka

Page 17: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Sheria ndogo za Kijiji cha Kashagulu Usimamizi wa Hifadhi ya Msitu na Mazalia ya Samaki Ziwa Tanganyika

13

kwa Kamati ya Mazingira isipokuwa walinzi wa msitu,

Kamati ya Mazingira, Halmashauri ya kijiji na Afisa

Misitu/Uvuvi wanaweza kufanya hivyo bila kibali.

12.4. Wageni wote wenye vibali toka Wizarani, Wilayani au

wafadhili ni sharti wapite kijijini na kuonyesha vibali

vyao kwa Kamati ya Mazingira ya kijiji kabla ya

kuanza kufanya kazi yoyote ndani ya msitu wa

hifadhi au hifadhi ya mazalia ya samaki ya Ziwa

Tanganyika sehemu ya kijiji cha Kashagulu.

13. Masharti ya Matumizi ya Msitu wa Hifadhi ya Kijiji na

Hifadhi ya Mazalia ya Samaki ya Ziwa Tanganyika

sehemu ya Kashagulu.

13.1. Mahitaji yote yanayohusu ukataji miti aina fulani

kwa ajili ya mbao, nguzo na miamba ya nyumba

ndani ya msitu wa hifadhi ya kijiji cha Kashagulu

yanaruhusiwa katika Ukanda wa Bubaja na

Mbebhe kwa kibali kitakachotolewa na Kamati ya

Mazingira ya kijiji. Mbaozitagongwa alama

(nyundo) itakayotolewa na Halmashauri ya Wilaya

ya Kigoma kama ilivyoainishwa katika Mpango wa

Usimamizi Shirikishi wa Msitu wa Hifadhi ya kijiji.

Miti husika itavunwa kwa kiwango ambacho

hakitaathiri lengo la msingi la kuhifadhi msitu

ambalo ni kuhifadhi vyanzo vya maji na uendelevu

wa rasilimali na huduma ya msitu kwa vizazi vya

sasa na vijavyo vya Tanzania na ulimwengu kwa

jumla. Miti aina ya Mninga, Mpilipili, Mzingati,

Mkoma, Mkamba na Mkola haitaruhusiwa kuvunwa

ndani ya maeneo ya matumizi.

Page 18: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Sheria ndogo za Kijiji cha Kashagulu Usimamizi wa Hifadhi ya Msitu na Mazalia ya Samaki Ziwa Tanganyika

14

14. Vitendo Vilivyopigwa Marufuku

14.1. Vitendo vifuatavyo vimepigwa marufuku kufanyika

katika msitu wa hifadhi ya kijiji na hifadhi ya mazalia ya

samaki ya Ziwa Tanganyika sehemu ya Kashagulu:

14.1.1 Kuchoma moto msitu.

14.1.2 Kuchungia mifugo (ng’ombe, mbuzi, kondoo,

punda, n.k) msituni.

14.1.3 Kukata miti au uoto wa asili kwenye vyanzo vya

maji, miteremko mikali na makorongo.

14.1.4 Kuwinda asali (Kukata miti yenye pango ambayo

kuna nyuki)

14.1.5 Kuingilia eneo la msitu na kingo za Ziwa

Tanganyika kwa kilimo na makazi.

14.1.6 Kutengeneza mkaa.

14.1.7 Kukata/kutoa magome miti mibichi kwa ajili ya

kuni (matumizi ya biashara na nyumbani).

14.1.8 Uwindaji wa wanyamapori katika msitu wa

hifadhi ya kijiji kwa kutumia bunduki, mshale,

mbwa na mitego (waya au kamba).

14.1.9 Kupasua mbao miti aina ya Mninga, Mzingati,

Mpilipili, Mkoma, Mkamba na Mkola kwa kuwa ni

michanga.

14.1.10 Kuvua samaki ndani ya Ziwa Tanganyika kwa

kutumia zana haramu kama vile kokoro

(mkwabho), nyavu za macho madogo chini ya

kalamu ya bic, makila chini ya inchi tatu (3),

katuli, kutumia sumu na baruti.

14.1.11 Kuvua samaki kwa kutumia zana yoyote ile

ndani ya hifadhi ya mazalia ya samaki ya Ziwa

Tanganyika

Page 19: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Sheria ndogo za Kijiji cha Kashagulu Usimamizi wa Hifadhi ya Msitu na Mazalia ya Samaki Ziwa Tanganyika

15

15. Vitendo Vinavyoruhusiwa kwa Vibali na Malipo

15.1. Vitendo vifuatavyo vinaweza kufanyika kwenye msitu

wa hifadhi ya kijiji cha Kashagulu kwa kibali na malipo:

15.1.1 Kupasua mbao aina husika ya miti katika

Ukanda wa Bubaja na Mbebhe.

15.1.2 Kukata miti ya ujenzi – nguzo na miamba ya

Mkurungu, Mhongolo na Msongati

15.1.3 Kukata mianzi kwa matumizi ya nyumbani na

biashara.

15.1.4 Kukata ukindu kwa matumizi ya nyumbani na

biashara

15.1.5 Kuchuma dawa za asili ndani ya msitu wa hifadhi

ya kijiji kwa watu toka nje ya kijiji cha Kashagulu.

15.1.6 Utengenezaji wa nyungo na vitunga kutokana na

mianzi.

15.1.7 Wageni kutembelea msitu wa hifadhi ya kijiji na

hifadhi ya mazalia ya samaki ya Ziwa

Tanganyika sehemu ya kijiji cha Kashagulu kwa

dhumuni la utalii, Ziara za mafunzo na watafiti.

15.1.8 Kukata mipini kwa ajili ya biashara tu.

15.1.9 Kukata kamba kwa ajili ya biashara.

15.1.10 Kuuza mbegu za Myovu kwa Wakala wa

Mbegu za Miti Tanzania.

15.1.11 Uwekezaji wa aina yoyote ile ndani ya msitu

wa hifadhi ya kijiji na hifadhi ya mazalia ya

samaki ya Ziwa Tanganyika sehemu ya kijiji

cha Kashagulu utalipiwa kufuatana na thamani

ya mtaji na kusainiwa kwa Mkataba wa

Makubaliano.

15.2. Kibali cha kuruhusu vitendo vilivyotajwa kitatolewa

baada ya maombi ya mhusika kupokelewa na

Page 20: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Sheria ndogo za Kijiji cha Kashagulu Usimamizi wa Hifadhi ya Msitu na Mazalia ya Samaki Ziwa Tanganyika

16

kujadiliwa na Kamati ya Mazingira na kuridhika

kwamba mazao au huduma hizo zinaweza

kupatikana bila kuleta athari kwa eneo husika la

msitu au Ziwa Tanganyika. Kibali kitaonyesha kiasi

cha mazao, tarehe ya mwisho na malipo

yaliyofanyika.

16. Kiasi cha malipo

16.1. Kiasi cha malipo kitakuwa kama ilivyoelezwa kwenye

kiambatanisho Jedwali 1:

Aina ya mazao/huduma ya Msitu

na Ziwa

Kiasi/Idadi Malipo

(Tshs)

Nguzo/Mwamba wa nyumba 1 100

Mianzi kwa matumizi ya nyumbani

na biashara

1 50

Kutengeneza nyungo kutokana na

mianzi

1 50

Kuchuma dawa za asili ndani ya

msitu wa hifadhi ya kijiji

Kila aina ya

mti/mmea

1,000

Mbao 1 300

Mpini kwa ajili ya biashara 1 100

Ukindu kwa matumizi ya nyumbani

na biashara

1 fungu 50

Ziara za mafunzo:

Watanzania

Kikundi kwa siku 15,000

Toka nchi za nje Kikundi kwa siku 30,000

Watalii:

Watanzania

1 kwa siku 1,000

Toka nje- wenye vibali vya

kufanya kazi nchini

1 kwa siku 3,000

Page 21: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Sheria ndogo za Kijiji cha Kashagulu Usimamizi wa Hifadhi ya Msitu na Mazalia ya Samaki Ziwa Tanganyika

17

Aina ya mazao/huduma ya Msitu

na Ziwa

Kiasi/Idadi Malipo

(Tshs)

Toka nje wasiokuwa na vibali

vya kufanya kazi nchini

1 kwa siku 5,000

Watafiti

Wanafunzi vyuo vya elimu ya juu

1 kwa siku 500

Toka nje ya nchi 1 kwa siku 1,000

Wahadhiri Watanzania 1 kwa siku 1,000

Kamba za miti ya miyombo kwa

matumizi ya nyumbani na biashara

1 fungu (puli) 50

Mbegu za Myovu Mapato yote kwa

mkusanyaji

10%

Uwekezaji ndani ya msitu Thamani ya mtaji

na Mkataba wa

Makubaliano

17. Vitendo Vinavyohitaji Kibali bila malipo (Bure)

17.1. Vitendo vifuatavyo vitaruhusiwa kufanyika kwenye

msitu wa hifadhi ya kijiji na hifadhi ya mazalia ya

samaki ya Ziwa Tanganyika sehemu ya kijiji cha

Kashagulu kwa kibali/ruhusa kisicholipiwa (bure):-

17.1.1. Kutumia maji kwa matumizi ya nyumbani,

mifugo na kilimo.

17.1.2. Kuokota kuni kavu kwa matumizi ya nyumbani

na biashara.

17.1.3. Kukata fimbo za kutembelea.

17.1.4. Kuchukua mboga, uyoga na matunda.

17.1.5. Kuchonga mwiko kwa ajili ya matumizi ya

nyumbani na biashara.

17.1.6. Kuchukua udongo dawa kwa ajili ya ukindu na

nyungo

17.1.7. Kufanya matambiko na ibada.

Page 22: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Sheria ndogo za Kijiji cha Kashagulu Usimamizi wa Hifadhi ya Msitu na Mazalia ya Samaki Ziwa Tanganyika

18

17.1.8. Ziara za mafunzo kwa ajili ya wanafunzi

Watanzania wa shule za awali, msingi,

sekondari na vyuo visivyo vya elimu ya juu

17.1.9. Kuchuma dawa za asili kwa njia endelevu

17.1.10. Njia za usafiri kwa miguu na gari (Kashagulu

kwenda Mwese na Rukoma)

17.1.11. Kuchukua nyasi za kuezekea nyumba.

17.1.12. Kutundika mizinga ya nyuki.

17.1.13. Kukata kamba kwa ajili ya matumizi ya

nyumbani.

17.1.14. Kukata mianzi, nguzo na miamba ya nyumba

kwa kaya ambayo imepata matatizo kama vile

ya kuunguliwa moto nyumba.

18. Viwango vya Faini

18.1. Mtu yeyote akikiuka sheria hii atakuwa ametenda

kosa na akithibitika atatozwa faini isiyopungua

shilingi elfu ishirini (20,000/=) na isiyozidi shilingi elfu

hamsini (50,000/=).

18.2. Iwapo kosa lililofanyika litahusu, vitendo vilivyopigwa

marufuku 13(1) mhalifu/mkosaji atatozwa faini

isiyopungua elfu arobaini na tano (Tshs. 45,000/=)

na isiyozidi shilingi elfu hamsini (Tshs. 50,000/=) kwa

kila kosa pamoja na fidia kutokana na tathimini ya

Afisa misitu wa eneo/ Wilaya husika kwa kila kosa

kulingana na kiwango cha uharibifu. Pia mhalifu

atafidia gharama za ukamataji (mgambo). Kwa mtu

kukataa kushiriki katika kuzima moto ndani ya msitu

wa hifadhi ya kijiji cha Kashagulu, faini na adhabu

zilizotajwa hapo juu zitatumika pia.

18.3. Kwa mtu/watu kuzuia Kamati ya Mazingira kufanya

kazi yake barabara, kama vile vitisho kwa

Page 23: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Sheria ndogo za Kijiji cha Kashagulu Usimamizi wa Hifadhi ya Msitu na Mazalia ya Samaki Ziwa Tanganyika

19

wanakamati ya mazingira viwango vya faini

vilivyotajwa hapo juu (Tshs 45,000 – 50,000/=)

vitatumika kwa kila mhusika.

18.4. Iwapo kosa lililotendwa litahusu vitendo vinavyohitaji

kibali na malipo 14(1) basi mkosaji / mhalifu atatozwa

faini isiyopungua fedha za kitanzania elfu ishirini

(Tshs 20,000/=) na isiyozidi elfu arobaini (Tshs

40,000/=) pamoja na fidia ya mazao yaliyoharibiwa

na gharama zitakazojitokeza.

18.5. Iwapo kosa lililotendwa litahusu vitendo

vinavyoruhusiwa kufanyika kwa kibali kisicholipiwa

17.1. (bure) basi Kamati ya Mazingira italiangalia hilo

kulingana na ukubwa wa kosa. Kwa makosa kama

haya mhalifu atazuiliwa kupata huduma hiyo kwa

muda wa miezi sita (6). Hata hivyo katika kuamua

makosa katika kundi hili lazima Afisa misitu wa eneo

/ Wilaya husika ashirikishwe kama yuko karibu.

18.6. Kwa makosa yatakayohusu uchungiaji mifugo

(mbuzi, ng’ombe, kondoo na nguruwe), faini itakuwa

Tshs 2000/= (elfu mbili) kwa kila mnyama. Faini hii

itatumika mara mbili tu kwa mkosaji, yaani kama

mhusika atafanya makosa kuchungia mifugo msituni

mara mbili, zaidi ya hapo yaani mara ya tatu basi

mifugo itataifishwa kwa kutumia Sheria ya Misitu No.

14, 2002.

18.7. Kama mhalifu atakuwa amekiri kosa na hana uwezo

wa kulipa faini na Kamati ya Mazingira ikaridhika,

basi mtu huyo anaweza kupewa kazi za mikono

kama vile kufyeka mpaka, n.k. kwa makosa yale

yatakayoangukia katika kifungu cha 17 (1).

Page 24: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Sheria ndogo za Kijiji cha Kashagulu Usimamizi wa Hifadhi ya Msitu na Mazalia ya Samaki Ziwa Tanganyika

20

19. Gharama na Fidia

19.1. Kamati ya Mazingira inaweza kutoza gharama

nyingine mbali na faini na fidia za uharibifu, kama vile

gharama za ukamataji na kushughulikia wahalifu.

Gharama hizi zitawekwa kufuatana na kila kosa

lililotendwa; kwa mujibu wa Sheria Na. 7 ya 1982

kifungu cha 16 (2), (3) ya Sheria za Serkali za Mitaa.

20. Faini ya wenye Dhamana/ Madaraka

20.1. Iwapo mjumbe yeyote katika Halmashauri ya Kijiji,

Kamati ya Mazingira au walinzi wa msitu na Ziwa

Tanganyika atakiuka taratibu za kiutendaji

kuhusiana na uhifadhi wa msitu wa hifadhi na

hifadhi ya mazalia ya samaki ya Ziwa Tanganyika

sehemu ya kijiji cha Kashagulu, atakuwa ametenda

kosa kwa mujibu wa Sheria hii na atatozwa faini

itakayojulikana kama faini ya wenye dhamana/

madaraka. Faini hiyo itakuwa mara mbili ya faini

zitakazotozwa kwa watu wasiokuwa na madaraka

kijijini/ zilizoainishwa hapo juu.

20.2. Pamoja na faini hizo, makosa ya viongozi hao lazima

yajadiliwe kwenye vikao vya juu katika kijiji na

kuwachukulia hatua kali kama vile barua za onyo la

maandishi, kusimamishwa na kuwaondoa kwenye

nafasi zao baada ya kuidhinishwa na Mkutano Mkuu

wa Kijiji.

20.3. Kwa wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji, Afisa

Mtendaji Kata ataitisha Kikao kujadili hatima ya

kiongozi aliyefanya uhalifu huo.

Page 25: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Sheria ndogo za Kijiji cha Kashagulu Usimamizi wa Hifadhi ya Msitu na Mazalia ya Samaki Ziwa Tanganyika

21

21. Taratibu za Kushughulikia Wahalifu wa Msitu wa

Hifadhi na Hifadhi ya Mazalia ya Samaki ya Ziwa

Tanganyika sehemu ya Kashagulu.

21.1. Hairuhusiwi kwa mwanakijiji, mwanakamati ya

Mazingira, mlinzi au kiongozi yeyote kumtoza faini

mhalifu akiwa peke yake.

21.2. Mazao ya misitu na ziwa yaliyovunwa kinyume cha

utaratibu pamoja na zana zilizotumika katika uhalifu

huo yakikamatwa ni lazima yafikishwe kwenye ofisi

ya kijiji ambapo hatua zaidi itachuliwa na Kamati ya

Mazingira ya kijiji.

21.3. Iwapo itabainika kuwa mtu au watu wamekiuka

taratibu za matumizi ya msitu wa hifadhi ya kijiji na

hifadhi ya mazalia ya samaki ya Ziwa Tanganyika

sehemu ya kijiji cha Kashagulu, mtu huyo au watu

hao watafikishwa mbele ya Kamati ya Mazingira ya

kijiji na suala lao litashughulikiwa kwa utaratibu

ufuatao hapa chini:

21.3.1. Mhalifu/wahalifu watafikishwa katika ofisi ya kijiji

ambapo Afisa Mtendaji wa Kijiji

atamuweka/atawaweka chini ya ulinzi. Afisa

Mtendaji wa Kijiji atawaarifu viongozi wa

Kamati/wajumbe wa Kamati ya Mazingira

angalau wawili ili kuwatoza faini wahalifu iwapo

watakiri/atakiri kosa kwa kuweka sahihi katika

daftari la“Makosa na Faini”.

21.3.2. Iwapo mhalifu/mtuhumiwa atakataa kukiri

kutenda kosa kwa kukataa kuweka sahihi katika

daftari, mtu huyo atatakiwa kupelekwa

mahakamani.

Page 26: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Sheria ndogo za Kijiji cha Kashagulu Usimamizi wa Hifadhi ya Msitu na Mazalia ya Samaki Ziwa Tanganyika

22

21.3.3. Endapo mhalifu/wahalifu watakiri kutenda kosa,

faini yote lazima iwe imelipwa katika muda wa

siku tatu (3) toka siku ya kukiri kutenda kosa

hilo. Hata hivyo mhalifu atalazimika kuwekewa

dhamana na mtu anayekubalika katika kijiji cha

Kashagulu.

21.3.4. Katibu atapokea malipo ya faini iliyolipwa kwa

kuandika stakabadhi ambayo atampatia

mhalifu. Namba ya stakabadhi iliyotolewa

itaandikwa kwenye daftari la “Makosa na Faini”

na kumkabidhi Mweka Hazina azipeleke

kwenye akaunti ya Kamati ya Mazingira ya kijiji.

21.4. Iwapo mtu anayetuhumiwa kutenda kosa atakataa

kukiri kosa mbele ya Kamati ya Mazingira na mbele

ya Mwenyekiti wa Kijiji au Afisa Mtendji wa Kijiji basi

itabidi vyombo hivyo vya utendaji vifikishe shauri hili

mahakamani kwa uamuzi zaidi. Iwapo mhalifu

atashindwa kulipa faini katika kipindi kilichokubaliwa

basi Kamati ya Mazingira au Afisa Mtendaji wa Kijiji

atafikisha suala hilo mahakamani.

21.5. Faini na /au adhabu nyingine zitatozwa kwa

kuzingatia viwango vilivyowekwa, katika kifungu cha

18.1 – 18.7 ya Sheria hii.

21.6. Mashauri yatakayoshindikana kuamuliwa kijijini

itabidi yafikishwa mahakamani na yasimamiwe na

Afisa Misitu wa wilaya, Tarafa au Kata. Afisa

Mtendaji wa kijiji na Kamati ya Mazingira watapaswa

kuwa mashahidi katika kesi hiyo.

Page 27: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Sheria ndogo za Kijiji cha Kashagulu Usimamizi wa Hifadhi ya Msitu na Mazalia ya Samaki Ziwa Tanganyika

23

22. Namna ya Kushughulikia Mazao ya Msitu na Ziwa

Tanganyika Yaliyokamatwa, Faini Zilizotozwa na

Mgawanyo Wake:

22.1. Mazao ya msitu/ziwa yaliyovunwa kinyume cha

Sheria pamoja na zana zilizotumika katika uhalifu

huo vikikamatwa ni lazima vifikishwe kwenye ofisi ya

kijiji ambapo hatua zaidi zitachukuliwa na Kamati ya

Mazingira. Mapato kutokana na mauzo ya mazao ya

msitu/ziwa yaliyokamatwa yatagawanywa kati ya

Halmashauri ya kijiji 95% na Serikali Halmashauri ya

Wilaya ya Kigoma 5%, aidha zana zitachukuliwa na

Halmashauri ya kijiji cha Kashagulu.

(hazitagawanywa kati ya Halmashauri ya Wilaya na

Halmashauri ya kijiji).

22.2. Mazao ya msitu yaliyokamatwa kwa ushirikiano wa

kijiji na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma mapato

yatagawanywa kwa 50% kila mmoja.

22.3. Mazao ya msitu na Ziwa Tanganyika yaliyokamatwa

na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma peke yake

kutokana na kijiji kuzembea, kijiji husika hakitapewa

mgao wa mapato.Hata hivyo, Halmashauri ya kijiji

itaadhibiwa kwa kutozwa faini ya asilimia 30% ya

thamani ya mali iliyokamatwa au kushitakiwa

kutokana na uzembe huo.

22.4. Thamani ya mazao ya msitu na Ziwa Tanganyika

yakikamatwa na kijiji peke yake ni lazima mapato

yagawanye kama 22(1) hapo juu kila mmoja.

22.5. Kama Mahakama itaamua kutumia Sheria kuu ya

Misitu (Sheria Misitu 14, 2002) kifungu 89(1) na

Sheria Kuu ya nchi kutoa maamuzi au adhabu basi

Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma itakuwa

Page 28: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Sheria ndogo za Kijiji cha Kashagulu Usimamizi wa Hifadhi ya Msitu na Mazalia ya Samaki Ziwa Tanganyika

24

Mlalamikaji (Jamhuri) na Kamati ya Mazingira ya kijiji

itakuwa ni Shahidi (informer), kwa hiyo faini

itakayotozwa italipwa mahakamani, hivyo hakuna

mgao wa faini hiyo.

22.6. Endapo kuna mazao ya misitu yatakayorudishwa

wilayani (mlalamikaji), basi mapato yatagawanywa

kama 22(1) hapo juu kati ya Halmashauri ya wilaya

na Halmashauri ya Kijiji.

23. Kuwasilisha Mashauri Mahakamani

23.1. Iwapo mhalifu atashindwa kulipa faini katika kipindi

kilichokubaliwa basi Kamati ya Mazingira na Afisa

Mtendaji wa kijiji atafikisha suala hilo mahakamani

23.2. Iwapo mtu anayetuhumiwa kutenda kosa atakataa

kukiri kosa mbele ya Kamati ya Mazingira na mbele

ya Mwenyekiti wa kijiji au mbele ya Afisa Mtendaji

wa Kijiji basi vyombo hivi vya utendaji vitawakilisha

shauri hilo mahakamani kwa uamuzi zaidi.

23.3. Iwapo mhalifu atashindwa/kukataa kulipa faini suala

hilo litafikishwa mahakamani

24. Hatua za Mahakamani

24.1. Katika kuendesha kesi, Mahakama itakuwa na haki

ya kurejea kwenye Sheria ndogo za kijiji na wakati

mwingine kuamua mhalifu kuadhibiwa kufuatana na

Sheria hizo. Hii ni pamoja na faini, gharama za

usumbufu, fidia za uharibifu zilipwe kwa Kamati ya

Mazingira ya Kijiji cha Kashagulu.

24.2. Kama mahakama itatoa hukumu kufuatana na

Sheria ya Misitu Na. 14 ya 2002, Kamati ya

Mazingira ya Kijiji cha Kashagulu itakuwa kama

Page 29: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Sheria ndogo za Kijiji cha Kashagulu Usimamizi wa Hifadhi ya Msitu na Mazalia ya Samaki Ziwa Tanganyika

25

mtoa taarifa (informer) na itapata nusu ya faini

atakayotozwa mhalifu chini ya kifungu cha 89(1) na

fedha hizo zitawekwa kwenye Akaunti ya Kamati ya

Mazingira ya kijiji cha Kashagulu.

25. Mapato na Matumizi ya Fedha za Hifadhi ya Msitu na

Hifadhi ya Mazalia ya Samaki ya Ziwa Tanganyika

Sehemu ya Kijiji cha Kashagulu.

25.1. Mapato ya Kamati ya Mazingira yatatokana na:

25.1.1. Faini zitakazotozwa wahalifu wa msitu na

hifadhi ya mazalia ya samaki ya Ziwa

Tanganyika.

25.1.2. Malipo ya mazao na huduma ya msitu wa

hifadhi ya kijiji hifadhi ya mazalia ya samaki ya

Ziwa Tanganyika yaliyoruhusiwa kwa kulipia

katika Mpango huu.

25.1.3. Mauzo ya mbegu za miti aina ya Myovu

(Mkangazi) kwa Wakala wa Mbegu za Miti

Tanzania (Morogoro)

25.1.4. Mauzo ya mazao ya msitu na Ziwa Tanganyika

yaliyokamatwa na zana zilizokamatwa katika

ulinzi.

25.1.5. Wafadhili na wasamaria wema watakaotoa

fedha/ msaada kwa ajili ya Usimamizi wa msitu

wa hifadhi ya kijiji na hifadhi ya mazalia ya

samaki ya Ziwa Tanganyika sehemu ya kijiji cha

Kashagulu.

25.2. Mapato yatokanayo na mazao na huduma za msitu

na Ziwa Tanganyika yatagawanywa kati ya

Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma na kijiji cha

Kashagulu kwa uwiano wa 95% Halmashauri ya kijiji

na 5% kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.

Page 30: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Sheria ndogo za Kijiji cha Kashagulu Usimamizi wa Hifadhi ya Msitu na Mazalia ya Samaki Ziwa Tanganyika

26

25.3. Kijiji kitatakiwa kufungua Akaunti ya Benki kwa ajili

ya kuhifadhi fedha za mapato hayo. Kamati ya

Mazingira itahusika na ufunguaji wa akaunti hiyo.

25.4. Watakuwepo watia sahihi watatu kutoka ndani ya

Kamati ya Mazingira. Fedha zinaweza kuchukuliwa

Benki wakiwepo watia sahihi wawili (2), pamoja na

Muhtasari wa kikao cha Kamati ya Mazingira

kuonyesha Mpango wa Matumizi ya fedha husika

ambao umeidhinishwa na Halmashauri ya kijij cha

Kashagulu.

25.5. Mweka Hazina wa Kamati ya Mazingira atawajibika

na upelekaji wa fedha za mapato Benki na uwekaji

wa kumbukumbu katika daftari la fedha.

26. Matumizi ya Fedha za Kamati ya Mazingira

26.1. Matumizi ya fedha za akaunti ya Kamati ya Mazingira

ni lazima yaidhinishwe na Halmashauri ya kijiji baada

ya Kamati ya Mazingira kuomba kutumia fedha hizo

kwa shughuli halali inayohusu maswala ya ulinzi na

uendelezaji wa eneo la msitu wa kijiji na hifadhi ya

mazalia ya samaki ya Ziwa Tanganyika sehemu ya

Kashagulu.

26.2. Maombi ya Kamati ya Mazingira ya kutumia fedha

sharti yaambatane na muhtasari wa kikao halali cha

Kamati ya Mazingira chenye wajumbe wasiopungua

nusu ya wajumbe wote kilichojadili maombi hayo ya

matumizi ya fedha.

26.3. Matumizi ya fedha za Kamati ya Mazingira

yanakusudiwa kuwa katika mambo yafuatayo:

26.3.1. Ununuzi wa vitabu vya kumbukumbu.

Page 31: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Sheria ndogo za Kijiji cha Kashagulu Usimamizi wa Hifadhi ya Msitu na Mazalia ya Samaki Ziwa Tanganyika

27

26.3.2. Ununuzi wa vitabu vya stakabadhi na hati ya

malipo.

26.3.3. Kulipia gharama za kesi zinazohusu uharibifu

wa msitu wa hifadhi ya kijiji, hifadhi ya mazalia

ya samaki ya Ziwa Tanganyika na uharibifu wa

mazingira mahakamani. Gharama hizi zitakuwa

ni nauli, chakula na malazi ya mashahidi kwa

viwango vitakavyoidhinishwa na Halmashauri

ya kijiji.

26.3.4. Kugharamia shughuli za uoteshaji miche ya

miti; kama viriba na mbegu.

26.3.5. Kulipia asilimia mia moja (100%) ya gharama za

matibabu ya walinzi wa msitu walioumia kazini,

baada ya kuthibitishwa na Kamati ya Mazingira.

26.3.6. Kutoa zawadi kwa walinzi waliofanya kazi nzuri

kwa mwaka, kama itakavyopendekezwa na

Kamati ya Mazingira na kuidhinishwa na

Halmashauri ya Kijiji.

26.3.7. Kununua sare na kutengeneza vitambulisho

kwa walinzi wa msitu.

26.3.8. Kutayarisha mabango ya kutoa onyo/ tahadhari

kwa wananchi juu ya matumizi yasiyoruhusiwa

ndani ya msitu wa hifadhi ya kijiji na hifadhi ya

mazalia ya samaki ya Ziwa Tanganyika.

26.3.9. Kulipia gharama za mikutano, mafunzo na ziara

za mafunzo kwa Kamati ya Mazingira, walinzi

wa msitu na wanakijiji wengine kama

itakavyoidhinishwa na Halmashauri ya kijiji cha

Kashagulu.

26.3.10. Kutoa zawadi/motisha kwa wananchi wema

watakaowezesha kutambua wahalifu wa

Page 32: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Sheria ndogo za Kijiji cha Kashagulu Usimamizi wa Hifadhi ya Msitu na Mazalia ya Samaki Ziwa Tanganyika

28

msitu, kukamatwa kwa wahalifu, kukamatwa

kwa mazao ya msitu au yote pamoja. Zawadi

kwa raia wema itakuwa asilimia kumi (10%) ya

faini au thamani ya mazao ya msitu na hifadhi

ya Ziwa Tanganyika yaliyokamatwa na

kuuzwa kabla ya kugawanywa kati ya

Halmashauri (W) na Halmashauri ya kijiji cha

Kashagulu.

26.3.11. Kununua mahema na usafiri kwa ajili ya doria

na ufuatiliaji wa utekelezaji wa“Mpango wa

Usimamizi Shirikishi wa Msitu wa Hifadhi ya

Kijiji na Hifadhi ya Mazalia ya Samaki ya Ziwa

Tanganyika Sehemu ya Kashagulu”.

26.3.12. Kusaidia shughuli zingine za maendeleo kijijini

endapo salio la Akaunti ya Kamati ya

Mazingira litakuwa si chini ya Tshs

1,000,000/= (shillingi milioni moja tu) kwa

wakati huo na itakavyoidhinishwa na

Halmashauri ya kijiji.

26.4. Taarifa ya mapato na matumizi ya fedha za Kamati

ya Mazingira lazima itolewe na Afisa Mtendaji wa

Kijiji katika Mkutano Mkuu wa kijiji mara nne (4) kwa

mwaka yenye nakala kwa Afisa Misitu (W) husika.

Page 33: SHERIA ZA SERIKALI ZA MITAA - BirdLife International · ya Sheria hii bila kuharibu au kukiuka madhumuni ya kimsingi yaliyopelekea kuwepo kwa Sheria hii.Sheria hii itafanyiwa marekebisho

Sheria ndogo za Kijiji cha Kashagulu Usimamizi wa Hifadhi ya Msitu na Mazalia ya Samaki Ziwa Tanganyika

29