31
JARIDA LA MTANDAONI Toleo Na. 1, 2020/21 TANZANIA Limeandaliwa na: Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) PROCUREMENT JOURNAL HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi

HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

  • Upload
    others

  • View
    3

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

Tanzania J A R I D A L A M T A N D A O N I T o l e o N a . 1 , 2 0 2 0 / 2 1

TANZANIA

Limeandaliwa na: Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA)

PROCUREMENT JOURNAL

HALIUZWI

Wadau waKwa

Ununuzi

Page 2: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

NDANI

1. Ujumbe kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu ___________________________________I

2. Maoni ya Mhariri __________________________________________________________ II

3. PPRA yatembelea Mradi wa 'Julius Nyerere Hydro-power project __________ 01

4. Serikali yataka taasisi zote ziungwe kwenye TANePS _____________________ 03

5. Dkt. Mpango aipongeza PPRA ____________________________________________ 05

6. PPRA yazitaka taasisi nunuzi kuzingatia matumizi ya Taneps ______________ 07

KUTOKA KATIKA TAASISI NUNUZI

7. Taneps yaongeza ufanisi kwa taasisi nunuzi ______________________________ 10

8. Serikali yaokoa bilioni 18.55/- kupitia Ununuzi wa pamoja wa nagari ______ 12

9. RAS Iringa: Elimu juu ya ‘force account’ itasaidia kuokoa fedha za umma __ 13

HABARI KATIKA PICHA

10. Kikao cha wafanyakazi _________________________________________________ 16

11. Yaliyojiri katika vyombo vya Habari ______________________________________18

11. Jamvi la Wazabuni ______________________________________________________ 19

12. Je Wajua _______________________________________________________________ 20

13. Kibonzo ________________________________________________________________ 20

KALENDA YA MAFUNZO _______________________________________________________ 22

TANGAZA NASI ______________________________________________________________ 25

Page 3: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

Awali ya yote, napenda kuwafahamisha kwamba Mamlaka imeamua kuendelea kuandaa jarida hili Tanzania Procurement Journal au TPJ kama njia mojawapo ya kuwasiliana nanyi pamoja na umma kwa ujumla.

Jarida hili, linalotolewa kila miezi mitatu, linarithi lile la awali lililokuwa likichapishwa kila wiki na kwa mujibu wa sheria ya ununuzi wa umma iliyokuwa inazitaka taasisi nunuzi kuwasilisha PPRA taarifa kuhusu Tangazo la Jumla la Ununuzi la Mwaka (GPN), matangazo yote ya tenda/zabuni pamoja na tuzo za mikataba ili vyote vichapishwe katika jarida lile na katika tovuti ya Mamlaka. Lakini, kutokana na kuanza kutumika kwa Taneps (www.-taneps.go.tz), Mamlaka iliona ni busara kusitisha uandaaji wa TPJ ya awali ili kupunguza gharama za matangazo kwa taasisi nunuzi.

Hata hivyo, kutokana na umuhimu wa upashanaji wa habari na wadau wake, Mamlaka imeamua kuendelea na TPJ, ambalo litakuwa linaandaliwa kila robo mwaka na kuchapish-wa mtandaoni tu kupitia tovuti ya Mamlaka (www.ppra.go.tz), na kupitia akaunti za mitan-dao ya kijamii ya Mamlaka ikiwemo Facebook, Twitter, na Instagram, ambayo yote inapa-tikana katika anuani ya “ppra_Tanzania”.

UJUMBE KUTOKA KWA AFISA MTENDAJI MKUU

Kwenu wadau wa ununuzi wa umma:

Baada ya utangulizi huo, napenda kuwakaribisha katika toleo la kwanza la jarida letu Tanzania Procurement Journal – TPJ, ambalo limesheheni taarifa za matukio muhimu ambayo PPRA imehusika nayo katika kipindi cha kuanzia tarehe Mosi Julai hadi 30 Septemba, 2020.

Miongoni mwa matukio hayo ni usimamizi wa mfumo Taneps, ambao umefanikisha zaidi ya asilimia 90 ya taasisi nunuzi zote kuunganishwa kwenye mfumo hadi kufikia tarehe 30 Septemba, 2020. Na jumla ya taasisi 440 zilikuwa zimeshaweka kwenye mfumo mipango ya ununuzi ya mwaka (GPN), yenye jumla ya zabuni 27,548 zenye thamani ya shilingi trilioni 11.47, tangu kuanza kwa mwaka wa fedha 2020/21 hadi mwishoni mwa mwezi Septemba, 2020.

Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia Serikali kuendesha shughuli zake za ununuzi wa umma kwa ufanisi zaidi lakini pia utaokoa fedha nyingi zinazotumika kwenye ununuzi wa umma. Ninatambua kuwa bado kuna changamoto kadhaa kuhusu matumizi ya mfumo huu, lakini napenda niwahakikishie kuwa Mamlaka inafanya kila linalowezekana kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo.

Ili kuhakikisha taasisi zinatumia Taneps sawasawa na kuzingatia sheria ya ununuzi wa umma, Mamlaka iliendelea na programu yake ya mafunzo kuhusu matumizi ya mfumo huo kwa taasisi nunuzi na wazabuni. Sambamba na mafunzo, Mamlaka pia imekuwa ikitoa huduma zake, ikiwemo matumizi ya mfumo huo, kwa njia ya simu, barua, barua pepe, na hata kwa baadhi ya wadau ambao wamekuwa wakifika katika ofisi zetu moja kwa moja.

Mamlaka pia imekuwa ikishiriki kwenye maonesho mbalimbali yakiwemo ya Sabasaba, Nanenane, na Siku ya Wahandisi, kwa ajili ya kutoa elimu kwa wadau. Kipekee, napenda niwapongeze wadau wote wa Mamlaka, ikiwamo Wizara ya Fedha na Mipan-go, Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na watumishi wa PPRA, taasisi nunuzi, wazabuni, na watoa huduma, kwa ushirikiano unaoiewezesha Mamlaka kutekeleza majukumu yake.

Mwisho, nawakaribisha wadau ambao wangependa kutoa michango na makala zao zinazotoa elimu kuhusu ununuzi wa umma kwa ajili ya toleo lijalo la Jarida hili na kutuma kwa njia ya barua pepe ([email protected]), kabla ya tarehe 20 Desemba, 2020.

ASANTENI!

Afisa Mtendaji Mkuu - PPRAMhandisi Leonard .S. Kapongo

I

Page 4: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

Tanzania JARIDA LA MTANDAONI Toleo la Kwanza | JULAI – SEPTEMBA, 2020

TANZANIA

Limaendaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA)

PROCUREMENT JOURNAL

HALIUZWI

KwaWadau wa

Ununuzi

MAONI YA MHARIRI

Toleo hili la Tanzania Procurement Journal au TPJ, ni la kwanza katika mambo kadhaa, ikiwemo lugha, maudhui, matumizi ya tekno-lojia katika kulitayarisha, usanifu, na usambazaji wake. Afisa Mtenda-ji Mkuu wa Mamlaka amekwishaeleza katika ujumbe wake, yaliyojiri mpaka uamuzi wa kutoa jarida kwa staili hii ukafanywa. Matokeo ya uamuzi huu ni mema na muafaka, kwani mabadiliko ni pacha wa maendeleo yatamanikayo. Kiandikwacho, hudumu.

Kwa vile hili ni toleo la kwanza la jarida ambalo pia limenipa na mimi safu mahsusi, sina budi kuishukuru kwanza Mamlaka kwa kunipa fursa ya kukalia dawati la uhariri wake, na pia kuipongeza kwa kuona mbali katika kuwawezesha wadau wengi na umma kwa ujumla siyo tu kupata habari za ununuzi wa umma kwa njia nyepesi, lakini pia kumuwezesha kila mmoja wao kusoma toleo lolote kwa wakati anaoutaka yeye.

Kila tukio huwa na muda wake, lakini haitakuwa ajabu kama tutakuja kujua, hapo baadaye, kwamba watu wengi waliokuwa na kiu kwa muda mrefu ya kuchangia mawazo, kutafuta ujuzi na elimu katika taaluma ya ununuzi wa umma, wananufaidika na jarida hili! Mtu huwa alivyo kwa kiasi kikubwa, kutokana na mazingira yake lakini pia elimu na mambo ayasomayo au ayasikiayo mara kwa mara. Kwa wajuao kusoma, njia hii ndiyo huchangia zaidi katika kufanikisha mabadiliko ya mtu katika kujua jambo lolote. Kusoma huchangam-sha ubongo na huleta raha; hata motto anayejua kusoma hupenda ajisomee – tena kwa wakati wake, kile anachoambiwa – kama kime-andikwa.

Lakini raha na umuhimu wa kujisomea katika kuboresha na kuonge-za uelewa wa mtu hutegemea pia na maudhui katika chapisho husika. Kuna wakati kile kilichomo katika chapisho fulani, huweza kuharibu hata kile kidogo alichokuwa nacho mtu aliyekuwa anajari-bu kupanua wigo wa uelewa wake, pale maudhui husika yanapokuwa yametayarishwa na kusambazwa bila umakini au bila kuzingatia lengo halisi la kuchapisha. Katika hali hii, ni bora kuchapisha kurasa chache zinazokata kiu ya habari na taarifa kwa wapendao kujiende-leza na zenye maudhui yanayokidhi viwango vya Mamlaka. Napenda kuwahakikishia wasomaji kwamba, katika nafasi yangu, nitaongozwa na filosofia hii katika kuchagua, kutathmini na kuhariri maudhui pendekezwa.

Naomba ushirikiano wa wadau popote walipo, kwa kutuletea habari na picha zinazohusiana na shughuli za ununuzi wa umma nchini – na hata nje ya nchi, kama zitakidhi viwango tulivyoweka. Aidha, jarida hili litanufaika na mawazo ya kuliboresha, kupitia njia rasmi za mawasiliano na Mamlaka.Karibuni!

MHARIRI

Mhandisi Nestor Ilahuka,S.L.P. 105122,

Dar es Salaam, TANZANIA.Barua pepe: nestor.ilahu-

[email protected]

WAANDISHIBw. Mcharo Mrutu

Afisa Uhusiano Mwandamizi - PPRA

Bw. Joseph MuhoziAfisa Uhusiano - PPRA

II

Page 5: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

TANZANIA PROCUREMENT JOURNAL01

PPRA YATEMBELEA MRADI WA KUFUA UMEME WA JULIUS NYERERE

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa PPRA walitembelea mradi wa kufua umeme Julius Nyerere Hydropower project mkoani Pwani.

Wajumbe hao walitembelea mradi huo ili kujif-unza na kushuhudia utekelezaji wake, ikiwa ni sehemu ya ufuatiliaji na usimamizi wa shughuli za sekta ya ununuzi nchini.

Katika ziara yao, wajumbe walijionea jinsi mradi huo, uliopo kwenye mto Rufiji, ulivyo kichocheo cha ukuaji wa wafanyabiashara wazawa, viwan-da na wataalam wa ndani ya nchi kwa kuwa unatoa kipaumbele katika matumizi ya wataa-lam wa ndani, bidhaa na malighafi zinazozalish-wa ndani ya nchi.

Akitoa maelezo kwa wajumbe hao, mtaalam mshauri wa mradi huo, Mhandisi Kamuhabwa Mshubila, alisema utekelezaji wa mradi huo una manufaa mengi katika ukuaji wa uchumi wa viwanda.

“Mradi huu ukikamilika,utawezesha upatikanaji wa umeme kuwa wa uhakika na kwa gharama nafuu, na pia asilimia kubwa ya malighafi

zinazotumika hapa zinazalishwa na viwanda vyhapa hapa nchini,” alisema Mhandisi Mshubi-la na aliongeza kuwa msisitizo ulitolewa juu ya kuhusisha wataalam wa ndani ili kuwajengea uzoefu.

Akizungumza baada ya ziara hiyo, Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi Leonard Kapongo, alieleza kuridhishwa na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo na jinsi mradi ulivyozingatia matumizi ya bidhaa, malighafi na wataalam wa ndani ya nchi.

Mradi Julius Nyerere Hydropower Project, unat-egemewa kuzalisha Megawatt 2,115, kiasi cha umeme kitakachowezesha sekta nyingi nchini kupata umeme wa uhakika na hivyo kuinua uchumi na kuboresha huduma mbalimbali nchini.

Katika ziara hiyo, iliyofanyika siku moja kabla ya kufanyika kwa Mkutano wa nne wa baraza hilo mjini Morogoro, wajumbe waliambatana na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya PPRA, Mhandisi Sylvester Mayunga.

Page 6: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

TANZANIA PROCUREMENT JOURNAL 02

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Tatu la Wafanyakazi wa PPRA wakifuatilia maelezo kuhusu mradi Julius Nyerere Hydro-power Project

Mhandisi Kamuhabwa Mshubila wa Julius Nyerere Hydro-power Project, akitoa maelezo juu ya mradi huo, kwa Wajumbe wa Baraza la Tatu la Wafanyakazi wa PPRA.

Page 7: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

TANZANIA PROCUREMENT JOURNAL03

Serikali imeitaka PPRA kuhakikisha taasisi zote za umma nchini zimeungwa kwenye mfumo wa ununuzi wa umma kwa njia ya mtandao almaarufu kwa jina Taneps na kuutumia kwa shughuli zote za ununuzi katika mwaka wa fedha 2020/21. Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, alitoa agizo hilo kupitia hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Bw. Michael Ogwari John, kwenye ufunguzi wa Mkutano wa nne wa Baraza la tatu la wafanyakazi wa PPRA, uliofanyika mjini Morogoro tarehe 18 Septemba, 2020. Aidha, Katibu Mkuu, ambaye pia ni Mlipaji Mkuu wa Serikali, aliziasa taasisi zote za umma

SERIKALI YATAKA TAASISI ZOTE ZIUNGWE KWENYE TANEPS

kuutumia mfumo huo, kwani umeonesha mafani-kio makubwa.

“PPRA kama msimamizi mkuu wa shughuli za ununuzi wa umma nchini pamoja na mfumo wa Taneps, ninawahimiza mhakikishe kuwa taasisi zote zinaungwa kwenye mfumo huu na kuanza kuu-tumia kwani umejidhihiri-sha kwamba ni mwarobaini wa kuondoa changamoto ambazo zimekuwa zikilala-mikiwa kwenye michakato ya ununuzi,” alisema Bw. James.

Page 8: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

Katika hotuba yake, Bw. James pia aliipongeza PPRA kwa kufanikisha kutumika kwa mfumo huo, ambapo zaidi ya asilimia 90 ya taasisi zote, ilikuwa imeshaungwa kwenye mfumo huo na nyingi zimekwishaanza kuutumia katika manunuzi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa PPRA, ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi Leonard Kapongo, alieleza kuwa ni taasisi nunuzi takrib-an 30 tu ambazo zilikuwa hazijajiunga kwenye mfumo huo ilipofika mwishoni mwa mwezi Sep-temba 2020.

“Kwa mfano, tangu mwanzoni mwa mwaka wa fedha 2020/21 hadi leo [tarehe 18 Septemba], jumla ya taasisi 440 zilikuwa zimeshaweka kwenye mfumo mipango ya ununuzi ya mwaka yenye jumla ya zabuni 27,548 zenye thamani ya shilingi trilioni 11.47,” alisema Mhandisi Kapongo.

Katika mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa PPRA, pamoja na mambo mengine, wajumbe walipitia Taarifa ya Mipango na Bajeti ya mwaka wa fedha 2020/21, walijadili changamo-to zinazoikabili Mamlaka na walipendekeza jinsi ya kuziondoa. Pia, wajumbe walipata fursa ya kuelimishwa na wataalamu wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) kuhusu bima.

Wajumbe wa Baraza la Tatu la Wafanyakazi wa PPRA wakiwa wameshikana mikono wakati wakiimba wimbo wa mshika-mano wa wafanyakazi kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Nne wa Baraza la Tatu la Wafanyakazi wa PPRA, uliofanyika

Morogoro tarehe 18 Septemba, 2020.

Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi Leonard Kapongo,

akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Michael Ogwari John, akihutubia

wajumbe wa baraza la wafanyakazi wakati akifungua mkutano.

TANZANIA PROCUREMENT JOURNAL 04

Page 9: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

TANZANIA PROCUREMENT JOURNAL05

DKT. MPANGO AIPONGEZA PPRAWaziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameipongeza PPRA na kuelezea kuridhishwa na kazi na huduma zinazofanywa na Mamlaka na kuitaka kuongeza wigo wa kutoa elimu ya ununuzi wa umma kupitia vyombo vya habari.

Mheshimiwa Dkt. Mpango alitoa pongezi hizo alipotembelea banda la PPRA kwenye Maone-sho ya Wakulima maarufu kama “Nanenane”, yaliyofanyika kitaifa mkoani Simiyu kuanzia tarehe 1 hadi 8 Agosti, 2020.

Dkt. Mpango alieleza kuridhishwa kwake na kazi ya ukaguzi wa ununuzi wa umma unaofa-nywa na PPRA na kwamba amekuwa akisoma na kufuatilia ripoti za ukaguzi zinazofanywa na Mamlaka, na kuitaka kuwa sehemu ya utatuzi wa matatizo wanayoyaibua.

“Mnafanyakazi nzuri sana, ripoti zenu ninaziso-ma vizuri sana na mnaniandikia vizuri. Lakini, msiishie kwenye kuibua matatizo tu, muwe pia sehemu ya kuyatatua,” amesema Waziri Mpango.

Miongoni mwa viongozi wengine waandamizi wa Serikali waliotembelea banda la PPRA kwenye maonesho hayo ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Florens Luoga,

ambaye alieleza juu ya kutambua kazi nzuri inayofanywa na Mamlaka hiyo katika usimamizi wa rasilimali za umma, na kuwataka kutopungu-za kasi kutokana na kusifiwa.

“Kweli kazi yenu tunaiona, mnafanya kazi nzuri. Zamani kidogo kulikuwa na changamoto, lakini kwa sasa kazi yenu tunaiona na tunaitambua, kwa hilo ‘we commend you’ (tunawapongeza),” alisema Profesa Luoga.

Akizungumzia maagizo hayo ya viongozi wa Serikali, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Mahusiano kwa Umma, Bi. Winifrida Samba, alimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa pongezi alizozitoa kwa PPRA na kuahidi kuwa Mamlaka itafanyia kazi maagizo yake yote.

Viongozi wengine waliotembelea banda la PPRA ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antho-ny Mtaka, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani, aliyekuwa KatibuTawala wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagin.

Wadau na wananchi mbalimbali walipewa elimu na kuhamasishwa kuwa sehemu ya usimamizi wa ununuzi wa umma, kwa kutoa taarifa PPRA pale ambapo wataona kuna dalili za uvunjifu wa Sheria.

Page 10: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Phillip Mpango, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu PPRA, alipotembelea banda la Mamlaka hiyo kwenye maonesho ya Nanenane, 2020.

Bi. Esther Revenus akitoa elimu kwa akina mama waliotembelea banda la PPRA kwenye maonesho ya Nanenane, 2020.

TANZANIA PROCUREMENT JOURNAL 06

Page 11: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

TANZANIA PROCUREMENT JOURNAL07

PPRA YAZITAKA TAASISI NUNUZI KUZINGATIA MATUMIZI YA TANEPSPPRA YAZITAKA TAASISI NUNUZI

KUZINGATIA MATUMIZI YA TANEPSAfisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi Leon-ard Kapongo, amezitaka taasisi nunuzi zote kuhakikisha zimejiunga na kutumia mfumo wa ununuzi wa umma kwa njia ya mtandao almaarufu kwa jina Taneps.

Mhandisi Kapongo aliyasema hayo kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za Sabasaba za mwaka huu. Aidha Mhandisi Kapongo alielezea kufurahish-wa na namna ambayo wadau wa ununuzi wa umma walivyoupokea na kuutumia mfumo huo, ambao umeongeza uwazi na kupunguza kwa kiasi kikubwa mianya ya rushwa katika ununuzi wa umma nchini.

“Kitu ambacho wengi wamekifurahia, ni kwamba mfumo umewasaidia sana katika kuongeza uwazi kwenye michakato ya ununuzi. Kuna baadhi ya watoa huduma katika kipindi kilichopita, kabla ya uwepo wa mfumo wa ‘TANePS’ walikuwa hawawezi kupata tenda katika taasisi za umma, lakini sasa hivi mrejesho tunaoupata ni kwamba watu wanaofaa kupata

kazi wanapata kazi ilimradi wanakidhi vigezo,” alisema Mhandisi Kapongo.

Aliongeza kuwa, “hii maana yake ni kwamba, yale mambo ya upendeleo, mambo ya ‘mimi namjua Fulani atanifanyia hivi nipate zabuni’, hiyo yote imekwisha. Kwa kweli sisi tunaliona ni mafanikio makubwa na wadau nao wanaliona kama ni jambo la manufaa kwa upande wao. Yaani kama ni haki yako, na kama umetengene-za zabuni yako vizuri na una vigezo, kama ni wa kupata utapata tu.”

PPRA ilishiriki kwenye Maonesho ya Sabasaba na ilitoa elimu ya Sheria ya Ununuzi wa Umma na Mfumo wa Manunuzi kwa Njia ya Mtandao (Taneps) kwa wadau wa ununuzi wa umma wali-otembelea maonesho hayo.

Katika banda la Mamlaka, wazabuni walisajiliwa kwenye mfumo na kupewa elimu ya jinsi ya kuutumia. Lakini pia, wadau walipata nafasi ya kutoa maoni yao na kuuliza maswali mbalimbali kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma.

Page 12: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka, CPA. Hannah Mwakalinga, akiwa pamoja na watumishi wa PPRA, alipotembelea banda la Mamlaka, kwenye maonesho ya Sabasaba, 2020.

Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Bw. Godfrey Mbanyi, alipotembelea banda la PPRA.

TANZANIA PROCUREMENT JOURNAL 08

Page 13: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

TANZANIA PROCUREMENT JOURNAL09

KUTOKA KATIKA TAASISI NUNUZI

Page 14: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

TANEPS YAONGEZA UFANISI KWA TAASISI NUNUZI

Wadau wamesema mfumo wa ununuzi kwa njia ya mtandao – Taneps umeongeza ufanisi na upa-tikanaji wa thamani halisi ya fedha kwenye ununuzi wa umma.

Wadau kadhaa waliotembelea banda la PPRA katika maonesho ya Siku ya Wahandisi yaliyoan-daliwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), yaliyofanyika kuanzia tarehe 3 hadi 4 Septemba, 2020 jijini Dodoma, walisema wameridhishwa na jinsi Taneps inavyofanikisha malengo ya Seri-kali katika ununuzi.

Miongoni mwa wadau hao ni Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) mkoa wa Man-yara, Mhandisi Bashiri Rwesingisa, ambaye alisema Taneps imesaidia katika utekelezaji na ufua-tialiaji wa michakato ya ununuzi.

“Nawapongeza PPRA kwa kutuletea Taneps kwani mbali ya kuokoa muda pia imetuwezesha hata sisi wakuu wa taasisi kufuatilia kwa karibu michakato ya ununuzi tofauti na awali,” alisema Mhandisi Rwesingisa, ambaye alikuwa kati ya washiriki wapatao 3,700 wa maonesho na mkuta-no huo wa siku mbili.

10TANZANIA PROCUREMENT JOURNAL

Page 15: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

TANZANIA PROCUREMENT JOURNAL11

Mdau mwingine, Mhandisi Motta Kyando, ambaye ni meneja wa Tanroads Mkoa wa Kilimanjaro, alisema mfumo huu unarahisisha michakato ya ununuzi na kuokoa muda, na aliiomba PPRA iongeze kasi ya utoaji elimu kwa watumiaji wa mfumo.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi Leonard Kapongo, alisema ushiriki wa Mamlaka kwenye maonesho hayo ulitoa fursa kwa wahandisi, ambao ni wadau wakubwa kwenye ununuzi wa umma, kupatiwa elimu kuhusu sheria ya ununuzi wa umma pamoja na matumizi ya Taneps.

“Wahandisi ni sehemu kubwa katika ununuzi wa umma kwa sababu miongoni mwao wapo makan-darasi, wahandisi washauri, na watoa huduma, hivyo ilikuwa muhimu sana kwetu kuwa kwenye maonesho haya, alisema Mhandisi Kapongo.

Maonesho hayo yalifanyika sambamba na Mkutano wa 17 wa Siku ya Wahandisi, uliokuwa na kaulimbiu “Mapinduzi ya Nne ya Viwanda ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu: Changamo-to na Fursa kwa Wahandisi”.

Kaimu Mkurugenzi wa Kujenga Uwezo na Huduma za Ushauri wa PPRA, Mhandisi Mary Swai, akisalimiana na wadau waliotembelea banda la PPRA wakati wa maonesho ya Siku ya Wahandisi, 2020 jijini Dodoma.

Page 16: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

SERIKALI YAOKOA BILIONI 18.55/- KUPITIA UNUNUZI WA PAMOJA WA MAGARISerikali imeweza kuokoa takribani shilingi bilioni 18.55 katika kipindi cha Serikali ya awamu ya Tano kutokana na huduma ya ununuzi wa pamoja wa magari ya Serikali (bulk procurement of vehicles) inayotolewa na Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA).

Kwa mujibu wa taarifa kwa wadau wa ununuzi wa umma, iliyotolewa hivi karibuni na Afisa Mtendaji Mkuu wa GPSA, Prof. Giraldine Rashe-li, utaratibu huo wa ununuzi wa pamoja wa magari ya Serikali, umezisaidia taasisi za Seri-kali kuepuka gharama za michakato ya ununuzi, ikilinganishwa na gharama ambazo zinagetumia endapo kila taasisi ingenunua yenyewe.

“Wakala umekuwa kituo maalum ‘One Stop Centre’ kwa ajili ya ununuzi wa magari ya Seri-kali. Katika kipindi cha Serikali ya awamu cha tano, kupitia utaratibu huu, Serikali inakadiri-wa kuokoa zaidi ya shilingi bilioni18.55,” ame-nukuliwa Prof. Rasheli katika taarifa ile.

Katika hatua nyingine, Prof. Rasheli amesema GPSA imekuwa ikitoa ushauri wa kitaalam katika Nyanja za ununuzi, ugavi na ugomboaji mizigo, ambapo wakala umeweza kugomboa mizigo kwa niaba ya taasisi za Serikali kwa usalama, uhakika na gharama nafuu, kutokana na uzoefu, weledi na uwekezaji mkubwa katika eneo hilo.

“Katika kipindi cha Serikali ya awamu ya tano, Wakala umeweza kugomboa mizigo takribani 902 yenye thamani ya shilingi bilioni 807.91 na Serikali inakadiriwa kuokoa zaidi ya shilingi bilioni 9.65 kutokana na tozo nafuu ya ugom-boaji pamoja na kuokoa gharama za michakato ya ununuzi,” aliongeza Prof. Rasheli.

Pamoja na mambo mengine, GPSA pia inatoa huduma za kununua, kutunza na kusambaza vifaa mtambuka na mafuta ya magari kwa taas-isi za serikali; pamoja na kuandaa na kutoa orodha ya wazabuni wa vifaa na huduma mtambuka.

12TANZANIA PROCUREMENT JOURNAL

Page 17: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

TANZANIA PROCUREMENT JOURNAL13

RAS IRINGA: ELIMU JUU YA ‘FORCE ACCOUNT’ ITASAIDIA KUOKOA FEDHA ZA UMMA

Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Bi. Hapines Seneda, amesema elimu kuhusu matumizi ya njia ya ‘force account’, itasaidia kuokoa fedha za umma kwani, matumizi yake bado ni chan-gamoto kuu katika mkoa huo.

Bi. Seneda aliyasema hayo alipokuwa akizung-umza na wawezeshaji kutoka PPRA walipom-tembelea ofisini kwake muda mfupi kabla ya kuanza kwa mafunzo ya Sheria ya ununuzi na kanuni zake kwa watumishi wa umma mkoani humo wanaohusika kwenye michakato ya ununuzi, yaliyofanyika kuanzia tarehe 30 Septemba hadi 2 Oktoba, 2020.

Njia hiyo ya ununuzi wa umma, ambayo hutumia wataalamu wa ndani wa taasisi nunuzi au kwa kushirikiana na Taasisi nyingine nunuzi au kushirikiana naTaasisi au watu binafsi, katika zabuni za umma, haijaeleweka ipasavyo katika maeneo mengi nchini.

“Matumizi ya njia ya ‘force account’ bado ni changamoto na elimu kuhusu njia inahitajika sana,”alisema Bi. Seneda.

“Baadhi ya watendaji hawana elimu ya kutosha kuhusu ‘force account’, hivyo wakati mwingine inasababisha kutumia gharama kubwa badala ya kupunguza gharama kama ilivyokusudiwa,” alisema Bi. Seneda.

Aidha, Katibu tawala huyo alisema kuwa kwa kiasi kikubwa changamoto ipo kwenye eneo la ujenzi ambao hutumia kiasi kikubwa cha fedha.

“Mafunzo haya kwa wanaohusika kwenye michakato ya ununuzi ni muhimu sana hapa mkoani kwetu, kuna changamoto kubwa kwenye sehemu ya ujenzi ambayo ndiyo inachukua kiasi kikubwa zaidi cha fedha, na changamoto kubwa ipo kwenye usimamizi wa mikataba,” alisema.

Page 18: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

Naye Afisa Ununuzi Mwandamizi - Mafunzo na Ushauri kutoka PPRA, Bw. Gilbert Kamunde alisema Mamlaka inaamini mafunzo hayo yange-saidia katika kuongeza ukidhi wa Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2011 na Marekebi-sho yake ya mwaka 2016.

Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa, Bi. Juliana Mka-limoto, ni miongoni mwa washiriki zaidi ya 50

waliohudhuria mafunzo hayo, ambaye alieleza Imani yake kuwa yangeongeza ufanisi katika utekelezaji wa shughuli za ununuzi mkoani humo.

Mafunzo hayo, yaliyotolewa bure kwa watumishi wa umma mkoani humo, yalipangwa kufanyika katika mikoa 10 ndani ya kipindi cha Mwaka wa Fedha 2020/2021.

Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Bi. Happines Seneda (wa pili kulia) akiwa na wafanyakazi wa PPRA, walipomtembelea ofisini kwake kabla ya kuanza kwa mafunzo.

Washiriki wa mafunzo ya sheria ya ununuzi wa umma Mkoani Iringa.

14TANZANIA PROCUREMENT JOURNAL

Page 19: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

HABARI KATIKA PICHA

Page 20: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

KIKAO CHA WANFANYAKAZI

Watumishi wa PPRA wakisikiliza mada kutoka kwa Bw. Desderius Muhiye kutoka NHIF.

Watumishi wa PPRA wakifuatilia mambo wakati wa kikao chao cha 15 jijini Dodoma.

16TANZANIA PROCUREMENT JOURNAL

Page 21: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

TANZANIA PROCUREMENT JOURNAL17

Afisa Uhusiano wa PPRA, Bw. Joseph Muhozi, akichangia hoja. Afisa Ununuzi PPRA Bw. Frank Yesaya akichangia hoja.

Afisa kutoka NHIF, Bw. Desderius Muhiye, akiwasilisha mada wakati wa kikao cha 15 cha wafanyakazi wa PPRA.

Page 22: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

YALIYOJIRI KATIKA VYOMBO VYA HABARI

18TANZANIA PROCUREMENT JOURNAL

Page 23: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

TANZANIA PROCUREMENT JOURNAL19

JAMVI LA WAZABUNI

PPAA: Manispaa ya Ilala ilikuwa sahihi kuhusu zabuni ya ukusanyaji taka

Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma (PPAA) imetupilia mbali rufaa iliyowasilishwa na kampuni Hananasif Women Development Investment dhidi ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa pamoja na kampuni Kajenjere Trading Co. Ltd, juu ya zabuni iliyohusu usafishaji, ukusanyaji ada za uondoshwaji taka ngumu na kuzipeleka dampo la Pugu Kinyamwezi.

Katika rufaa hiyo, mlalamikaji alikuwa akipinga madai ya halmashauri kwamba ukidhi wa kigezo cha uzoefu wa angalau miaka mitatu katika kazi kama zile, ndiyo sifa uliyosababisha kampuni Kajenjere Trading Co. Ltd kushinda zabuni hiyo.

Mkata rufaa alilalamika kuwa zabuni yake ilikataliwa kimakosa na kwa kutumia ubaguzi na upendeleo kwani walipuuza historia ya mikataba aliyowahi kuitekeleza na uzoefu wake na pia kwamba bei yake ilikuwa chini ya shilingi milioni sita, wakati ile ya Kajenjere Trading Co. Ltd ilikuwa ya shilingi milioni 8.5.

Pia, mlalamikaji alipinga kitendo cha Halmashauri ya Ilala kusahihisha nyaraka za Kajenjere Trading Co. Ltd.

Katika kujibu malalamiko hayo, Halmashauri ya Ilala walisema mchakato wa zabuni tajwa ulifua-ta matakwa ya sheria na kanuni za ununuzi wa umma na kwamba mshindi alipatikana kwa njia za haki na usawa.

Pia, Halmashauri ya Ilala walieleza kwamba mkata rufaa hakuwa amewasilisha nyaraka za kud-hibitisha uzoefu wake kama ilivyokuwa inatakiwa, na kwamba badala yake, alikuwa amewasili-sha tu mkataba wa kampuni nyingine.

Katika kufikia uamuzi, PPAA iligundua kwamba hakika mlalamikaji alikuwa ameondolewa kwenye mchakato katika hatua ya tathmini ya kiufundi ambapo alikuwa amewasilisha mikataba miwili ya miezi mitatu kila mmoja, na pia mkataba kati ya kampuni Pick Trading Ltd na Manispaa ya Ilala, kama uthibitisho wa uzoefu. Hivyo, kutokana na nyaraka zile, PPAA ilifikia uamuzi kuwa ni kweli mkata rufaa alikosa uzoefu uliohitajika.

Kuhusu malalamiko kwamba mlalamikiwa alirekebisha nyaraka za zabuni za Kajenjere Trading Co. Ltd, PPAA iliamua kuwa ilikuwa sahihi kufanya vile kwa kuwa marekebisho yale yalihusu makosa juu ya utafutaji jumla tu, na kwamba Kajenjere Trading Co. Ltd ilishinda zabuni kihalali.Mwisho, PPAA ilitupilia mbali shauri hilo na kuamuru kwamba kila upande ubebe gharama zake.

Page 24: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

JE WAJUA?HIVI SASA WAZABUNI WANAWEZA KUPATA NYARAKA ZA ZABUNI NA KUSHIRIKI MICHAKATO YA ZABUNI ZA UMMA KUPITIA MFUMO WA TANEPS WAKIWA MAOFISINI MWAO.

20TANZANIA PROCUREMENT JOURNAL

Page 25: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

TANZANIA PROCUREMENT JOURNAL19

KALENDA YAMAFUNZO

Page 26: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

22TANZANIA PROCUREMENT JOURNAL

j

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA MINISTRY OF FINANCE AND PLANNING

PUBLIC PROCUREMENT REGULATORY AUTHORITY

Kambarage Tower, 9th Floor, Jakaya Kikwete Road, P. O. Box 2865, Dodoma, TANZANIA Phone: +0255 026 2963854, Email: [email protected], Website: www.ppra.go.tz

In reply please quote:

Ref. No. FB. 192/247/01/98 26th August, 2020

To all PEs

RE: REVISED TRAINING CALENDAR AND INVITATION TO ATTEND TRAINING ON PUBLIC PROCUREMENT ACT (PPA), REGULATIONS, PROCUREMENT

IMPLEMENTATION TOOLS AND CONTRACT MANAGEMENT FOR FINANCIAL YEAR 2020/2021

Reference is made to the above subject.

2. PPRA has prepared a four-days intensive training programme on the application of

Public Procurement Act, Regulations, implementation tools and contract management for

Accounting Officers, members of Tender Boards and staff from Procurement Management

Units (PMUs), User Departments, Internal Auditors, and Legal Officers in various centres.

This programme has been designed to equip knowledge and skills to staff of the procuring

entities who have responsibilities in handling procurement activities within their entities.

The trainings are conducted from August, 2020 and it is expected to continue through

June, 2021, therefore this calendar will be updated from time to time as need arises.

3. Moreover, PPRA has planned two sessions of Annual Procurement Governance

Workshops whereby the first session will be for AOs, Board Members, Mayors and

Councilors; second session for TB members and staff from Procurement Management

Units, Legal Units, Internal Audits Units and User Departments.

4. The fee for each participant is TZS. 550,000.00 per training session on PPA, PPR,

Implementation Tools and Contract Management while participation fee for Annual

Procurement Governance Workshop is TZS 480,000.00, for the first session and TZS

580,000.00 for the second session.

Page 27: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

TANZANIA PROCUREMENT JOURNAL23

5. The charges will cover the costs of facilitation, venue, training materials and meals

during the training sessions. Each PE should facilitate their participants with

accommodation and transportation costs associated with participation in each session.

6. Confirmation will be through remittance of fee to PPRA through GEPG control

numbers to be requested from [email protected].

7. To facilitate smooth implementation of the program, kindly confirm your willingness

to sponsor participants from your entity to attend this program to the undersigned by

sending the names of staff who will attend, their contact details, training dates and venue

at least two weeks prior to each session by using the attached training registration form.

8. In this regard you are requested to allow and facilitate your staff to attend in any of

the training sessions. Training calendar and other terms are attached with this letter and

are also available in our website: www.ppra.go.tz. The Authority reserves right to modify

the training programme as appropriate as occasions permits to accommodate any specific

requirements for effective training sessions.

9. Thank you for your cooperation.

Yours sincerely,

Eng. A. O. Kasuwi ACTING CHIEF EXECUTIVE OFFICER

Page 28: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

TANZANIA PROCUREMENT JOURNAL 24

j

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA MINISTRY OF FINANCE AND PLANNING

PUBLIC PROCUREMENT REGULATORY AUTHORITY

Kambarage Tower, 9th Floor, Jakaya Kikwete Road, P. O. Box 2865, Dodoma, TANZANIA Phone: +0255 026 2963854, Email: [email protected], Website: www.ppra.go.tz

Training Registration Form

To: Chief Executive Officer,

Public Procurement Regulatory Authority,

P. O. Box 2865,

DODOMA.

RE: TRAINING CALENDAR AND INVITATION TO ATTEND TRAINING ON PUBLIC PROCUREMENT ACT (PPA), REGULATIONS, PROCUREMENT IMPLEMENTATION TOOLS AND CONTRACT MANAGEMENT FOR FINANCIAL YEAR 2020/2021

Please enroll the following person(s) for the training indicated in the last column.

SN

Name of Participant

Mobile No.

Email Address

Date & Venue of Training

Name & Address of Employer:

......................................................................................................................................................

Enclosed is evidence of payment dated ......................... for TZS ........................................

Date:............................... Signature:..................................... OFFICIAL DESIGNATION STAMP

Note: (i) Submit this form together with the copy of original payment evidence to PPRA before

the workshop starts. Original payment evidence should be submitted during the registration.

Page 29: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

TANZANIA PROCUREMENT JOURNAL25

TRAINING CALENDAR ON PUBLIC PROCUREMENT ACT, REGULATIONS, IMPLEMENTATION TOOLS AND CONTRACT MANAGEMENT FOR FINANCIAL YEAR

2020/2021 S/N NAME OF THE TRAINING DATE VENUE Fee (TZS)

1. Training on PPA Cap.410 and Procurement Contract Management for Goods and Services

September, 8 - 11, 2020 Mwanza 550,000.00/=

2. Annual Procurement Governance Workshops for AOs, Board Members, Mayors and Councilors

November 16-17, 2020 Arusha 480,000.00/=

3. Annual Procurement Governance Workshops for TB Members, PMUs, IAs, UDs, LOs etc.

November 18-20, 2020 Arusha 580,000.00/=

4. Training on PPA Cap.410, procurement implementation tools and preparation of procurement contracts to IAs and Legal Officers

December 15-18, 2020 Iringa 550,000.00/=

Issued on 26th August, 2020 by:-

Eng. A. O. Kasuwi ACTING CHIEF EXECUTIVE OFFICER

Page 30: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

WAHI NAFASI

TANGAZA NASI KUPITIA JARIDA LETU LA

MTANDAONI

PPRA inatoa fursa kwa wadau wa ununuzi wa umma, wakiwemo

taasisi nunuzi, wafanyabiashara na makampuni binafsi,

kutangaza huduma na bidhaa zao kupitia Jarida la “Tanzania

Procurement Journal”. Gharama zetu ni nafuu kama

zinavyooneshwa hapa chini.

1. Ukurasa mzima2. Nusu Ukurasa3. Robo ukurasa4. Ukurasa wa nyuma 5. Ukurasa wa mbele chini

500,000350,000250,000650,000500,000

UKUBWA GHARAMA

���������������������������

Page 31: HALIUZWI Wadau wa Kwa Ununuzi · 2021. 1. 22. · Kwa hili napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau wote wa ununuzi wa umma kwa ushirikiano huu ambao naamini kwamba sio tuutaisaidia

Jengo la Kambarage, Ghorofa ya 9, Barabara ya PSPF,

S.L.P 2865, 41104 Dodoma, TANZANIA.

Simu: +255 262 963 854

Barua pepe: [email protected] | Tovuti: www.ppra.go.tz

PPRA TANZANIA