Upload
others
View
18
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
HALMASHAURI YA JIJI ARUSHA.
TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA
FEDHA 2019/20 KWA KUTUMIA MAPATO YA NDANI KWA KIPINDI CHA ROBO
YA KWANZA JULAI– SEPTEMBA 2019
Imeandaliwa na;
Mkurugenzi wa Jiji
S. L. P. 3013,
20 Barabara ya Boma,
23101 ARUSHA,
Barua Pepe: [email protected]
Tovuti: www.arushacc.go.tz
Oktoba, 2019.
i
YALIYOMO.
YALIYOMO....................................................................................................................i
ORODHA YA MAJEDWALI.........................................................................................i
UTANGULIZI …………………………..……………………………..........................1
1.1 Idara ya Fedha na Biashara…………………………………………………………1
1.2 Idara ya Uchumi, takwimu na ufuatiliaji…………………………………………..2
1.3 Idara ya Elimu………………………………………………………………………3
i) Elimu Msingi…………………………………………………………………....3
ii) Elimu Sekondari…………………………………………………………….…..3
1.4 Idara ya Afya……………………………………………………………………….4
1.5 Idara ya Mipango miji……………………………………………………………...4
1.6 Idara ya Ujenzi……………………………………………………………………..5
1.7 Idara ya maji………………………………………………………………………...5
1.8 Idara ya usafi na mazingira……………………………………………………….…5
1.9 Idara ya Maendeleo na Ustawi wa Jamii……………………………………………6
1.10 Idara ya Mifugo na uvuvi………………………………………………………...6
1.11 Idara ya Utumishi na Utawala……………………………………………………6
1.12 Idara ya Kilimo na Ushirika……………………………………………………...6
ORODHA YA PICHA.
1.1 Jengo la Ofisi ya kata lililopo kata ya Sinoni…………………………………………………2
1.2: Picha ya ujenzi wa OPD katika Hospitali ya Wilaya uliopo Njiro, Kata ya
Engutoto……………………………………………………………………………….……3
1. 3 Kikundi cha walemavu kilichopo kata ya Sombetini kilichopewa mikopo na Halmashauri
ya Jiji la Arusha………………………………………………………………………………………4
ORODHA YA JEDWALI.
1.1Utekelezaji wa miradi ya Maendeleo kwa kutumia mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha
2018/19………………….....................................................................................................7-
1
UTANGULIZI.
Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020, Halmashauri imekadiria kukusanya na
kupokea jumla ya Tshs.77,989,077,436 Kati ya makisio hayo, kiasi cha Tshs.
20,700,000,000.00 zinatokana na mapato ya ndani na Tshs.57,289,077,436.00
zinatokana na ruzuku kutoka serikali kuu
Aidha Katika Mpango wa bajeti ya Maendeleo ya mwaka 2019/2020 Jiji la Arusha
lilikisia kutumia Tshs.28,433,887,653.33 /= kwa mchanganuo ufuatao, Tshs.
10,553,521,804.00 mapato ya ndani na Tshs. 264,076,000.00 Ruzuku ya Serikali Kuu,
Wafadhili mbalimbali Tshs.17,616,289,849.33 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya
maendeleo. Hadi kufikia mwezi Septemba, 2019 jumla ya Tshs.9,950,815,366.31
zimetolewa na Tshs. 5,137,927,549.45 kutumika kwa miradi ya maendeleo ya mwaka
2019/2020 kutoka vyanzo mbalimbali. Halmashauri imepokea fedha kutoka serikali
kuu Tshs. 64,076,000 kwa ajili utekelezaji wa miradi kupitia Mfuko wa Jimbo.
Makisio ya mapato ya ndani
27%
Maakisio ya mapato toka serikali kuu
73%
MAKISIO YA MAPATO YA NDANI DHIDI YA MAPATO TOKA SERIKALI KUU
Makisio ya mapato ya ndani Maakisio ya mapato toka serikali kuu
37%, 37%
1%, 1%
62%, 62%
MAKISIO YA MAPATO KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO
2019/2020
Makisio ya Mapato ya ndani kwaajili ya utekelezaji wa Miradi yaMaendeleo 2019/2020
Makisio ya Mapato ya Ruzuku tokaSerikali kuu kwa ajili ya utekelezajiwa Miradi ya Maendeleo2019/2020
Makisio ya Mapato toka kwawafadhili mbalimbali kwaajili yautekelezaji wa Miradi yaMaendeleo 2019/2020
2
1.1 Idara ya Fedha na Biashara.
Katika sekta ya Fedha na Biashara, Hamashauri imetemga jumla ya
Tshs.257,367,116.00 kwa ajili ya shughuli zifuatazo;
Kuwezesha ukusanyaji mapatao kwa kununua 120 POS ili kuongeza mapato
mradi bado haujaanza.
Kuwezesha ujenzi wa maduka 17 Soko Kuu ambapo jumla ya Tshs.
93965400.79 imeshatolewa na kazi inaendelea.
Kuwezesha ujenzi wa soko la samaki Sakina (Olmatejoo) na kutengeneza
miundo mbinu mingine mradi bado haujaanza.
Kuwezesha ujenzi wa Soko Mapunda Kata ya Daraja II mradi bado haujaanza.
1.2 Idara ya Uchumi, takwimu na ufuatiliaji.
Katika sekta ya Uchumi, takwimu na ufuatiliaji.Hamashauri ilitenga
Tshs.1,980,000,000/= kwa ajili ya;
Kuwezesha ujenzi wa jengo la utawala la Halmashauri ya jiji la Arusha awamu
ya kwanza mradi bado haujaanza.
Ujenzi wa Ofisi ya kata ya kati awamu ya tatu mradi bado haujaanza.
Kujenga nyumba ya Mkurugenzi wa Jiji mradi bado haujaanza.
Kukarabati miundombinu ya jengo la Halmashauri ya jiji mradi bado haujaanza.
Kukarabati ofisi ya Kata Moivaro mradi bado haujaanza.
Kuwezesha utoaji wa mchango wa dharura katika miradi mbalimbali ya kijamii
katika kata 25 mradi umeanza
Kuwezesha utoaji wa mchango katika miradi 6 ya uwekezaji na kijamii.
Kuwezesha shughuli za Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Kata 25 mradi bado
haujaanza.
Kuwezesha usimamizi na ufuatiliaji wa Miradi ya maendeleo katika Kata 25
mradi umeanza usimamizi unaendelea
Kununua gari moja ya Mkurugenzi wa Jiji na gari moja kwa Idara ya Uchumi
Kuwezesha wakuu wa idara 18 na madiwani 32 kukagua miradi ya maendeleo
kwa katika Kata 25 mradi umefanyika kwa robo ya kwanza.
1.1 Jengo la Ofisi ya kata lililopo kata ya Sinoni
3
1.3 Idara ya Elimu.
Katika sekta ya Elimu, Hamashauri ilitenga Tshs. 3,000,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa
miundombinu ya madarasa, matundu ya vyoo, ujenzi wa maabara za masomo ya
sayansi, ujenzi wa nyumba za Walimu, ujenzi wa majengo ya Utawala pamoja na
ununuzi wa madawati na viti na meza kwa ajili ya Walimu.
i) Elimu Msingi
Katika mwaka wa fedha 2019/2020 Halmashauri ya Jiji la Arusha bado haijaanza
utekelezaji wa miradi ya elimu msingi kutokana na kuwa na makusanyo madogo ya
mapato ya ndani kwa robo ya kwanza.
ii) Elimu Sekondari
Katika mwaka wa fedha 2019/2020 Halmashauri ya Jiji la Arusha imeweza kutumia
jumla ya fedha Tshs.345,518,700.00 kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali
kwa upande wa elimu Sekondari ambazo ni Ujenzi wa madarasa 8, Ujenzi wa matundu
ya vyoo 14,Maabara 3 na Majengo 7 ya Utawala.
1.4 Idara ya Afya.
Katika sekta ya Afya Hamashauri ilitenga Tshs. 1,800,000,000/= kwa ajili ya ujenzi
wa Hospitali ya Wilaya, Ujenzi wa Miundombinu ya Vituo vya Afya, Zahanati, Ujenzi
wa Nyumba ya Mtumishi, Ununuzi wa Jenereta, Kununua Mashine 3 za kutoa dawa ya
usingizi kwa ajili ya Vituo vya afya na ujenzi wa uzio katika Vituo vya afya. Hadi sasa
kazi zilizofanyika ni ujenzi wa OPD katika Hospitali ya Wilaya,Umaliziaji wa Kituo
cha afya Muriet.
1.2 Picha ya Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Murriet
4
1.5 Idara ya Mipango miji.
Katika sekta ya mipango miji Hamashauri ilitenga Tshs.101,975,000/= kwa ajili
ya;
Kurekebisha miundombinu kwa ajili ya upimaji na urasimishaji wa makazi
Kufanya hesabu za fidia ya ardhi kwa watu 50.
1.6 Idara ya Ujenzi.
Katika sekta ya ujenzi, Hamashauri imetoa na kutumia jumla ya Tshs 1,215,983,994 kwa
ajili ya; Kujenga 1km ya barabara ya Kisongo - Arusha girls kwa kiwango cha Lami
1.7 Idara ya maji.
Katika sekta ya maji, Hamashauri imetoa na kutumia jumla ya Tshs.48,000,000/= kwa ajili ya;
Kufanya utafiti wa Maji na kuchimba kisima 1 katika Shule ya Msingi
Sinon
Kukarabati na kuboresha chemchemi ya Maji katika eneo la Sorenyi.
1.8 Idara ya usafi na mazingira.
Katika sekta ya usafi na mazingira, Hamashauri ilitenga Tshs. 200,000,000.00 kwa
ajili ya kuwezesha Kununua Gari jipya moja la maji taka lenye ujazo wa lita 6,500.
1.9 Idara ya Maendeleo na Ustawi wa jamii. Katika sekta ya Maendeleo ya Jamii, Hamashauri ilitenga Tshs.1,762,170,694,.00 kwa
ajili ya utoaji wa mikopo ya vikundi vya wanawake vijana na Watu wenye Ulemavu.
Kwa kipindi cha julai hadi Septemba 2019 jumla ya vikundi 83 ambapo Wanawake
vilikuwa 66, Vijana 14 na Watu wenye walemavu 3 vilikopeshwa fedha kiasi cha Tshs.
415,000,000/= hii ni pamoja na fedha za marejesho.
1.3 Kikundi cha watu wenye ulemavu kilichopo kata ya Sombetini kilichopewa mikopo
na Halmashauri ya Jiji la Arusha
5
1.12 Idara ya kilimo na ushirika. Katika idara ya kilimo na ushirika Hamashauri ilitenga Tshs. 60,000,000 kwa ajili ya
ujenzi wa mifereji ya umwagiliaji katika Mto Olevarakwi katika kata ya Sinoni. Aidha
kazi ya ujenzi wa mifereji inaendelea baada ya Mkandarasi kukabidhiwa kazi.
MIKAKATI 2019/2020
Halmashauri imeweka mikakati mbalimbali ya kutatua changamoto ili kufikia
malengo kama ifuatavyo;
Kuongeza viwango vya ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kiwango cha juu ili
kuweza kutekeleza miradi mingi.
Kuandaa maoteo ya wanafunzi wanao andikishwa darasa la kwanza, wanafunzi
wanaohitimu darasa la saba ili kuwa na mpango wa uhakika katika madarasa ya
kutosha na miundombinu yake.
Kushirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuweza kuchangia miradi
mbalimbali ya maendeleo kuandika maandiko mbalimbali.
Kushirikisha jamii katika kuchangia miradi ya maendeleo na kuijengea jamii
dhana ya umiliki wa miradi (sense of ownership).
(Aidha jedwali ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa sekta zote
yameambatanishwa pamoja na taarifa hii.)
6
HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA
TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAPATO YA NDANI KWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020 JULAI HADI SEPTEMBA 2019
NA
SEKTA
JINA LA MRADI/ MAHALI ITAKAPOTEKELEZWA
BAJETI
KATA/ENEO MRADI
ULIPO
FEDHA ILIYOTOLEWA. SHUGHULI ZITAKAZOTEKELEZWA
FEDHA ILIYOTUMIKA
HALI YA UTEKELEZAJI
MAONI
HALMASHAURI
WANANCHI
JUMLA
1
FE
DH
A N
A B
IAS
HA
RA
Kuwezesha ujenzi wa maduka 15 katika Soko la Krokon ifikapo Juni 2020
100,000,000 KATA YA LEVOLOSI
100,000,000 0 100,000,000 Ujenzi upo hatua ya ukamilishaji
100,000,000 Ujenzi wa vibanda 25 na matundu ya vyoo 6 upo hatua ya ukamilishaji
Kazi inaendelea
Kuwezesha utoaji wa mchango wa dharura katika miradi mbalimbali ya kijamii katika kata 25 ifikapo Juni, 2020
257,500,000 JIJI LA ARUSHA
47,818,667.34 47,818,667.34 Kuchangia miradi ya TASAF III; Ujenzi wa nyumba ya Mtumishi Zahanati ya Olmot, Uzio Kituo cha Afya Daraja II na Jengo la Utawala Shule ya Sekondari Oloirien umefanyika.
47,818,667.34 Kuchangia miradi ya TASAF III; Ujenzi wa nyumba ya Mtumishi Zahanati ya Olmot, Uzio Kituo cha Afya Daraja II na Jengo la Utawala Shule ya Sekondari Oloirien umefanyika.
Kazi inaendelea
Ujenzi wa Ofisi ya kata ya kati awamu ya tatu.
100,000,000.00
KATA YA KATI
25,101,163.51
25,101,163.51
Kazi imekamilika.
25,101,163.51
Mradi umekamilika na unatumika.
Kazi imekamilika.
7
JUMLA NDOGO. 457,500,000 172,919,830.85
172,919,830.85
172,919,830.85
2 UCHUMI Kuwezesha utoaji wa mchango katika miradi 6 ya uwekezaji na kijamii ifikapo Juni, 2020
300,000,000 JIJI LA ARUSHA
283,333,333.4 0 283,333,333.4 Michango imetolewa
235,991,984 Michango imetolewa
Kazi imekamilika
Kuwezesha usimamizi na ufuatiliaji wa Miradi ya maendeleo katika Kata 25 ifikapo Juni,2020
77,500,000 JIJI LA ARUSHA
64,582,820 0 64,582,820 Michango imetolewa
340,957,037.32 Ununuzi wa mashine kubwa ya photocopy pamoja na usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo umefanyika.
Kazi imekamilika
Kununua gari moja ya Mkurugenzi wa Jiji na gari moja kwa Idara ya Uchumi ifikapo Juni 2020
400,000,000 JIJI LA ARUSHA
245,047,200.42
0 245,047,200.42
Ununuzi wa gari ya Mkurugenzi wa Jiji umefanyika
245,047,200.42 Ununuzi wa gari ya Mkurugenzi wa Jiji umefanyika
Ununuzi wa gari ya Mkurugenzi wa Jiji umefanyika
Kuwezesha wakuu wa idara 18 na madiwani 32 kukagua miradi ya maendeleo kwa katika Kata 25 ifikapo Juni, 2020
60,000,000 JIJI LA ARUSHA
8,000,000 0 8,000,000 Usimamizi na ufuatiliaji wa miradi
100,000,000.00 Ufuatiliaji umefanyika kwa robo ya nne na unaendelea
Ufuatiliaji unaendelea
JUMLA NDOGO. 1,752,500,000 946,803,015.52
946,803,015.52
1,267,835,883.44
8
3
EL
IMU
SE
KO
ND
AR
I Ujenzi wa Jengo la utawala katika Shule ya Sekondari Burka ifikapo Juni,2020
100,000,000 KATA YA OLASITI
50,000,000 0 50,000,000 Mradi upo katika hatua ya manunuzi.
50,000,000 Mradi upo katika hatua ya manunuzi.
Mradi upo katika hatua ya manunuzi.
Kukamilisha ujenzi wa Jengo la utawala katika Shule ya Sekondari Olasiti ifikapo Juni,2020
15,000,000 KATA YA OLASITI
15,000,000 - 15,000,000 Mradi upo katika hatua ya umaliziaji.
15,000,000 Mradi umekamilika kwa awamu ya kwanza na mradi upo hatua ya umaliziaji kwa awamu ya pili.
Mradi upo katika hatua ya manunuzi
Kukamilisha ujenzi wa Jengo la utawala katika Shule ya Sekondari Ngarenaro ifikapo Juni,2020
20,000,000 KATA YA NGARENARO
20,000,000 - 20,000,000 Mradi upo katika hatua ya umaliziaji.
20,000,000 Mradi upo katika hatua ya umaliziaji.
Mradi upo katika hatua ya umaliziaji.
Kukamilisha ujenzi wa Jengo la utawala katika Shule ya Sekondari Naura ifikapo Juni,2020
20,000,000 KATA YA LEMARA
20,000,000 - 20,000,000 Mradi upo katika hatua ya umaliziaji.
40,000,000 Mradi upo katika hatua ya umaliziaji..
Mradi upo katika hatua ya umaliziaji.
Kukamilisha ujenzi wa madarasa 4 katika shule ya sekondari Olmot ifikapo Juni,2020
70,000,000 KATA YA OLMOT
70,000,000 - 70,000,000 Kujenga jengo la utawala
70,000,000 Ujenzi wa jengo la utawala upo katika hatua ya umaliziaji
Mradi upo katika hatua ya umaliziaji.
9
Ujenzi wa jengo la utawala katika shule ya sekondari Muriet ifikapo Juni,2020
100,000,000 KATA YA MURIET
50,000,000 - 50,000,000 Kujenga maabara 3
50,000,000 Ujenzi wa jengo la Utawala upo hatua ya Manunuzi
Ujenzi wa jengo la Utawala upo hatua ya Manunuzi
Kumalizia ujenzi wa jengo la utawala katika shule ya sekondari Themi ifikapo Juni,2020
20,000,000.00
KATA YA THEMI
20,000,000 - 20,000,000 Fedha zimetumwa shuleni kwa utekelezaji.
20,000,000 Fedha zimetumwa shuleni kwa utekelezaji.
Fedha zimetumwa shuleni kwa utekelezaji.
Ujenzi wa madarasa 4 ya ghorofa katika Shule ya Sekondari Arusha Terrat ifikapo Juni,2020
100,000,000.00
KATA YA MURIET
49,518,700.00
- 49,518,700.00
Utekelezaji unaendelea
76,000,000 Madarasa 4 yapo hatua ya umaliziaji.
Utekelezaji unaendelea
Kumalizia ujenzi wa jengo la utawala katika shule ya sekondari Sinon ifikapo Juni,2020
20,000,000 KATA YA SINONI
20,000,000 - 20,000,000 Kuendeleza ujenzi wa jengo la utawala
20,000,000.00 Ujenzi wa jengo la utawala upo katika hatua yaukamilishaji.
Utekelezaji unaendelea
JUMLA NDOGO. 3,970,000,000 2,208,124,731.04
2,208,124,731.04
2,896,671,766.88
4
AF
YA
Kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ifikapo Juni,2020
502,246,140 KATA YA ENGUTOTO
207,282,576 0 207,282,576 Utekelezajiunaendelea
207,282,576 Utekelezajiunaendelea
Utekelezajiunaendelea
10
Kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Moshono ifikapo Juni,2020
200,000,000 KATA YA MOSHONO
200,000,000 0 200,000,000 Utekelezaji unaendelea
200,000,000 Utekelezaji unaendelea
Utekelezaji unaendelea
JUMLA NDOGO. 8,642,246,140 4,823,532,038.08
4,823,532,038.08
6,200,626,109.76
5 MIPANGO MIJI
Kurekebisha miundombinu kwa ajili ya upimaji na urasimishaji wa makazi 1000 ifikapo Juni 2020
31975000 JIJI LA ARUSHA
23,600,000 23,600,000 Kufanya upimaji wa mipaka kwa Shule 20 na Vituo vya afya 4
23,600,000 Utekelezaji unaendelea
Kufanya hesabu za fidia ya ardhi kwa watu 50 ifikapo Juni, 2020
70,000,000 JIJI LA ARUSHA
6,565,6442.7 6,565,6442.7 Eneo limeshafidiwa.
6,565,6442.7 Fidia ya ardhi awamu ya tatu na ya nne kwa ajili ya shule ya msingi ya muriet B na papa king umefanyika
Eneo limeshafidiwa.
JUMLA NDOGO. 17,386,467,280 9,736,320,518.86
9,736,320,518.86
12,490,508,662.22
6
MA
EN
DE
LE
O Y
A J
AM
II
Kutoa mikopo nafuu kutoka mapato ya ndani kwa vikundi vya wanawake 100 ifikapo Juni 2020
484,237,789 JIJI LA ARUSHA
330,000,000 330,000,000 Fedha zimehamishiwa katika akaunti ya deposit kwa ajili ya kutolewa kwenye vikundi 66 vya wanawake
330,000,000 Fedha zimehamishiwa katika akaunti ya deposit kwa ajili ya kutolewa kwenye vikundi 66 vya wanawake
Mradi unaendelea
JUMLA NDOGO. 35,257,172,349 19,802,641,037.72
19,802,641,037.72
25,311,017,324.44
11
JUMLA KUU. 67,465,885,769 19,802,641,037.72
37,690,341,172.07
48,339,579,577.59