16
Kwa usafirishaji salama na sambamba baharini HALMASHAURI YA KENYA YA USIMAMIZI WA SHUGHULI ZA USAFIRISHAJI BAHARINI (KENYA MARITIME AUTHORITY) Sajili ya ISO 9001:2015

HALMASHAURI YA KENYA YA USIMAMIZI WA … Centers/KMA...za bandari, kufanya usafirishaji wa mizigo, kutafsiri nyaraka za mkataba katika biashara ya usafiri wa meli, kufuata mikataba

  • Upload
    others

  • View
    13

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: HALMASHAURI YA KENYA YA USIMAMIZI WA … Centers/KMA...za bandari, kufanya usafirishaji wa mizigo, kutafsiri nyaraka za mkataba katika biashara ya usafiri wa meli, kufuata mikataba

Kwa usafirishaji salama na sambamba baharini

HALMASHAURI YA KENYA YA USIMAMIZI WA

SHUGHULI ZA USAFIRISHAJI BAHARINI

(KENYA MARITIME AUTHORITY)

Sajili ya ISO 9001:2015

Page 2: HALMASHAURI YA KENYA YA USIMAMIZI WA … Centers/KMA...za bandari, kufanya usafirishaji wa mizigo, kutafsiri nyaraka za mkataba katika biashara ya usafiri wa meli, kufuata mikataba

2 Halmashauri ya Kenya ya Usimamizi wa Shughuli za Usafirishaji Baharini

Page 3: HALMASHAURI YA KENYA YA USIMAMIZI WA … Centers/KMA...za bandari, kufanya usafirishaji wa mizigo, kutafsiri nyaraka za mkataba katika biashara ya usafiri wa meli, kufuata mikataba

KUHUSU KMAHalmashauri ya Kenya ya usimamizi wa Shughuli za usafirishaji Baharini (KMA) ilibuniwa kupitia kwa amri ya Rais ya mwaka 2004, kusimamia shughuli za usafiri Baharini kutoka Mamlaka ya Bandari la Kenya (KPA) hadi Shirika Huru la Kiserikali (KMA).

Mnamo mwaka wa 2006, lilihalalishwa chini ya sheria ya Kenya ya shughuli za baharini kifungo nambari 5, na majukumu yake yakiwa kuongoza, kushirikisha na kusimamia shughuli za baharini kote nchini.

Mnamo mwaka wa 2009, mabadiliko zaidi yakafanyiwa sheria hiyo na kuongeza sheria mpya ya Usafiri Baharini, 2009, iliyoidhinishwa, ambayo iliunda mpangilio muafaka na halali wa usafiri kwa meli baharini nchini Kenya. Sheria hiyo inawezesha kutatuliwa kwa maswala ya usalama, mafunzo, pamoja na kuimarisha nafasi za biashara katika uchukuzi wa baharini na viwanda vinavyohusika na shughuli hizo.

HISTORIA Kenya iko katikati ya eneo lenye kutumiwa na meli nyingi zaidi za kimataifa na inakisiwa kuwa wakati wowote meli (50) hupitia hapo. Kati ya hizi, (10) huwa meli zenye kusafirisha mafuta kutoka mataifa ya Mashariki ya Kati yenye utajiri mkubwa wa petroli wa viwango vya kati ya tani 50 hadi tani 250,000.

Pwani ya Kenya iliyo na urefu wa kilomita 600 kutoka Tanzania hadi Kusini mwa Somalia, imekuwa daima katika mstari wa mbele kibiashara tangu karne ya tano wakati meli za kibiashara za Wachina, za Waturuki na baadaye za Wareno zilipokuwa zikitia nanga katika bandari za zamani za Lamu, Malindi na Mombasa.

Kenya pia imekuwa ikiendesha shughuli za usafirishaji katika maziwa yake ya ndani kutoka ziwa kubwa la Victoria, lile la Turkana na mengine madogo katika Bonde la Ufa Na hata Pwani. Utegemeaji wa Utalii katika uchumi wa Kenya na fedha za kigeni pamoja na uvuvi wa samaki kwa biashara na mlo unalazimisha kuwemo kwa muongozo na masharti yatakayowezesha kulindwa kwa mazingara yake kutokana na uharibifu.

Bandari la Mombasa ni muhimu sana katika kuwezesha biashara kati ya nchi za Kiafrika zisizo ukingoni mwa bahari. Nchi hizi ni Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Rwanda, Burundi, Sudan ya Kusini na hata kwa kiwango fulani Ethiopia na Somalia. Uchukuzi katika eneo hili hujulikana zaidi kama “Northern Corridor.”

3Halmashauri ya Kenya ya Usimamizi wa Shughuli za Usafirishaji Baharini

Page 4: HALMASHAURI YA KENYA YA USIMAMIZI WA … Centers/KMA...za bandari, kufanya usafirishaji wa mizigo, kutafsiri nyaraka za mkataba katika biashara ya usafiri wa meli, kufuata mikataba

4 Halmashauri ya Kenya ya Usimamizi wa Shughuli za Usafirishaji Baharini

Page 5: HALMASHAURI YA KENYA YA USIMAMIZI WA … Centers/KMA...za bandari, kufanya usafirishaji wa mizigo, kutafsiri nyaraka za mkataba katika biashara ya usafiri wa meli, kufuata mikataba

5Halmashauri ya Kenya ya Usimamizi wa Shughuli za Usafirishaji Baharini

Page 6: HALMASHAURI YA KENYA YA USIMAMIZI WA … Centers/KMA...za bandari, kufanya usafirishaji wa mizigo, kutafsiri nyaraka za mkataba katika biashara ya usafiri wa meli, kufuata mikataba

JUKUMU

Halmashauri ya Kenya ya usimamizi wa Shughuli za usafirishaji Baharini (KMA) inasimamia sheria za kimataifa zinazohusika na usafiri Baharini pamoja na kuimarisha taasisi na kanuni zake za kisheria.

KMA ina jukumu la kueleza sheria za kimataifa zinazotawala usafirishaji majini kama vile Shirika la Kimataifa la Bahari (IMO) pamoja na Shirika la Wafanyakazi Duniani (ILO) ili ziweze kuafikia viwango vya kimataifa juu ya usalama.

Mipango imewekwa katika sheria ya usafirishaji wa bidhaa Baharini ili kuhakikisha usawa katika huduma kwa wasafirishaji na wafanya biashara wenyeji, wateja, na kutilia maanani uchumi unaotegemea Bandari ya Mombasa.

Hatua kubwa ya KMA inayotekelezwa kwa sasa ni uamuzi wa Serikali ya Kenya pamoja na mataifa jirani kujenga bandari la pili la kimataifa la Lamu ikishirikiana na nchi za Sudan ya Kusini, Ethiopia ambazo hazina pwani. Hatua hii itapanua uchumi katika maeneo ya Afrika Mashariki, Afrika ya Kati hadi ya Magharibi.

Bandari la Lamu-Port South Sudan-Ethiopia Transport Corridor Projects (LAPSSET) itaharakisha mpango wa Kenya wa Maendeleo- Vision 2030 ambao unanuia kupanua uchumi hadi viwango vya kimataifa.

6 Halmashauri ya Kenya ya Usimamizi wa Shughuli za Usafirishaji Baharini

Page 7: HALMASHAURI YA KENYA YA USIMAMIZI WA … Centers/KMA...za bandari, kufanya usafirishaji wa mizigo, kutafsiri nyaraka za mkataba katika biashara ya usafiri wa meli, kufuata mikataba

Kutosheleza wateja

Kufanya kazi pamoja

Ubunifu

Uwazi, Uadilifu, Uwajibikaji na Utaalamu

Kujitolea kulinda mazingira na kuyaendeleza

Kuzingatia Sura ya Haki, Usawa WA Jinsia, Uzalendo na Haki za Binadamu.

MAADILI YA KIMSINGIMAADILI YA

KIMSINGI

Kuhakikisha usafirishaji salama, bora, safi na sawa kwa faida ya washika dau wote kupitia kwa usimamizi bora na sawa.

WITOWITO

Kuwa taifa linaloongoza katika usimamizi wa shughuli za usafirishaji baharini duniani.

MAONOMAONO

7Halmashauri ya Kenya ya Usimamizi wa Shughuli za Usafirishaji Baharini

Page 8: HALMASHAURI YA KENYA YA USIMAMIZI WA … Centers/KMA...za bandari, kufanya usafirishaji wa mizigo, kutafsiri nyaraka za mkataba katika biashara ya usafiri wa meli, kufuata mikataba

MAJUKUMU

Baadhi ya majukumu ya KMA ni:

Kutekeleza muongozo unaohusiana na mambo ya baharini;

Kushauri Serikali kuhusu utekelezaji wa sheria za kimataifa za baharini;

Kufanya utafiti, uchunguzi na kupima maeneo ya baharini;

Kutekeleza majukumu ya mataifa yenye bandari kwa hali ya juu;

Kubuni, kuongoza na kusimamia utekelezaji wa sheria mafuta yanapomwagika pwani na hata kwenye maziwa ya bara;

Kuandika orodha ya meli na kuisimamia vyema;

Kupeana uongozi katika shughuli za utafutaji na uokoaji baharini ikishirikiana na washika dau;

Kutekeleza sheria za usafirishaji wa meli na kuhakikisha sheria za usalama zinazingatiwa vilivyo;

Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa meli ,kuhakikisha usalama na kuzuia uchafuzi baharini;

Kusimamia na kupeana uongozi mwafaka katika masuala ya mafunzo, uajiri na maslahi ya mabaharia;

Kuchunguza ajali za baharini; na

Kusimia usafiri katika maziwa yaliyo ndani ya nchi kavu

8 Halmashauri ya Kenya ya Usimamizi wa Shughuli za Usafirishaji Baharini

Page 9: HALMASHAURI YA KENYA YA USIMAMIZI WA … Centers/KMA...za bandari, kufanya usafirishaji wa mizigo, kutafsiri nyaraka za mkataba katika biashara ya usafiri wa meli, kufuata mikataba

SHUGULI ZA KIMSINGIUsalama Baharini

Majukumu ya usimamizi wa bandari yanahitaji taifa kusimamia meli za kigeni zinazoingia nchini humo kulingana na mikataba ya kimataifa ambayo taifa hilo ni mshirika. Kulingana na hayo, taifa linahitajika kuchunguza asilimia 25% ya meli zote zinazoitembelea ili kuhakikisha usalama.

Na kulingana na usalama wa baharini, KMA mara kwa mara huchunguza utekelezaji wa meli na usalama wa bandari kupitia ‘Port Facilities Security (ISPS) Code’ kama ilivyo katika mkataba wa kimataifa wa usalama baharini (SOLAS) ili kuambatana na matakwa ya taasisi za kimataifa.

Kulinda Mazingira ya Baharini

Ikishirikiana na taasisi na mashirika ya umma, KMA huchukua hatua kuzuia uchafuzi wa bahari na kulinda mazingira. Kunapotokea umwagikaji wa mafuta ama kemikali, KMA huwa katika mstari wa mbele wa kusimamia mpango wa kitaifa wa kupambana na hatari hiyo (NOSRCP).

Shughuli za Biashara Baharini

Ili kuhakikisha mazingira yatakayofaidisha shughuli za biashara baharini, KMA:

Inasimamia utekelezaji wa hali ya juu wa biashara baharini ili kupunguza mipango duni inayoweza kusababisha msongamano wa mizigo bandarini.

Kusaidia wafanya biashara kufahamu gharama, hatari na majukumu ya kimataifa ya biashara (Incoterms 2000); na pia

Kuinua biashara baharani kwa kutumia utaalamu wa hali ya juu miongoni mwa washika dau.

Shughuli za Utafutaji Na Uokoaji (SAR)

KMA ina kituo cha shughuli za Utafutaji na Uokoaji (RMRCC) kinachofanya shughuli za utafutaji na uokoaji katika sehemu za bahari za Kenya, Tanzania, Ushelisheli na Somalia.

Kituo hicho (RMRCC) vile vile hufanya kazi na kituo cha kupambana na maharamia baharini (ISC) kilichotambuliwa na Shirika la Kimataifa la Bahari (IMO) chini ya mkataba wa Djibouti wa kukabiliana na uharamia.

KMA pia hushirikiana na KPA, Kenya Navy na mashirika mengine katika shughuli za utafutaji na uokoaji pwani na hata bara.

9Halmashauri ya Kenya ya Usimamizi wa Shughuli za Usafirishaji Baharini

Page 10: HALMASHAURI YA KENYA YA USIMAMIZI WA … Centers/KMA...za bandari, kufanya usafirishaji wa mizigo, kutafsiri nyaraka za mkataba katika biashara ya usafiri wa meli, kufuata mikataba

10 Halmashauri ya Kenya ya Usimamizi wa Shughuli za Usafirishaji Baharini

Page 11: HALMASHAURI YA KENYA YA USIMAMIZI WA … Centers/KMA...za bandari, kufanya usafirishaji wa mizigo, kutafsiri nyaraka za mkataba katika biashara ya usafiri wa meli, kufuata mikataba

Mafunzo ya Ubaharia au Bandari

Uwezo wa mabaharia ni muhimu katika uendeshaji salama na ufanisi wa meli, na huathiri moja kwa moja usalama wa maisha katika bahari na ulinzi wa mazingira ya baharini. Uwezo wa mabaharia huongeza ujiri wao katika soko la wafanyakazi la kimataifa.

Kuna upungufu wa mabaharia wanaokisiwa kuwa maofisa 150,000 wa majini kufikia mnamo mwaka 2025. Kenya imo katika orodha ya IMO White List kupitia juhudi za KMA ni dhahiri kuwa taifa la Kenya liko tayari kuweka mabaharia kwa soko la kimataifa.

Elimu na Mafunzo ya Maritimu (MET) ni moja ya Mradi wa Halmashauri ya Kenya ya usimamizi wa Shughuli za usafirishaji Baharini (KMA) ya taswira ya mwaka 2030. Kwa kushirikiana na Chuo cha ustawi na Mtaala ya Kenya (KICD) na Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta cha Kilimo na Teknolojia (JKUAT), KMA imezindua mtaala wa kitaifa wa bahari wa kufunza mabaharia wa Kenya kulingana na mkataba wa viwango vya marekebisho, mafunzo na uangalizi (STCW 78).

Mtaala unahusisha mafunzo ya baharini kutoka kwa mtaalamu hadi ngazi za chuo kikuu na inakubaliana na Mkataba ili kuhakikisha kuwa mabaharia waliohitimu wa Kenya wanaajiriwa duniani kote. Kozi za kisanii hufunza hila katika uhandisi wa baharini na nautical sayansi, shahada katika uhandisi wa baharini na nautical sayansi. Pia kuna mipango ya digrii katika uhandisi wa baharini pamoja na kozi za lazima na za juu za STCW. Ili kuwezesha utekelezaji bora wa mtaala, KMA inaendeleza muongozo na vitabu vua kutumia kufundisha wanafunzi wa ubaharia ili kuhakikisha usawa katika taasisi zote za mafunzo zilizokubalika.

KMA ni imara katika kuimarisha miundo na taasisi za Elimu na Mafunzo ya Maritime (MET) ndani ya nchi, kukuza kazi kwa baharini na kuboresha hali kwa ajili ya kuajiri na kuhifadhiwa kwa mabaharia wa Kenya walio hitimu vyeti halisi.

Ili kukabiliana na pengo la ujuzi katika shughuli za msingi za bandari katika sekta ya usafirishaji, KMA imeanzisha pia mtaala wa usafirishaji katika bahari. Kosi za bandari zimeandaliwa kuwawezesha wanafunzi kuwa na ujuzi sahihi, ujuzi na mtazamo wa utendaji wa kazi za makaratasi na usimamizi katika usindikizaji wa nyaraka za kusafirisha, kusimamia shughuli za bandari, kufanya usafirishaji wa mizigo, kutafsiri nyaraka za mkataba katika biashara ya usafiri wa meli, kufuata mikataba ya mazingira, sheria na kanuni, kusimamia vifaa na usafiri wa mizigo na udalali wa meli.

11Halmashauri ya Kenya ya Usimamizi wa Shughuli za Usafirishaji Baharini

Page 12: HALMASHAURI YA KENYA YA USIMAMIZI WA … Centers/KMA...za bandari, kufanya usafirishaji wa mizigo, kutafsiri nyaraka za mkataba katika biashara ya usafiri wa meli, kufuata mikataba

KMA NA MASILAHI YA MABAHARIA Jukumu moja la Halmashauri ya Kenya ya usimamizi wa Shughuli za usafirishaji Baharini (KMA) ni kusimamia mazoezi, uajiri na masilahi ya mabaharia. Tukizingatia haya, kampuni inaendelea kuhamasisha viwango vya mazoezi na uajiri ya mabaharia wa Kenya. Kulingana na mahitaji ya sehemu 118 ya Merchant Shipping Act, Cap 389, kampuni hudumisha sajili ya mabaharia wa Kenya. Kwa hivyo, wanabaharia wanahitaji kujisajili na kupeana rekodi zao kwa KMA. Hivi sasa, kampuni hii inashughulikia mipango ya kuongeza idadi ya mabaharia wa Kenya wanaoajiriwa kwenye meli za kigeni ikizingatia Big 4 Agenda ya taifa na mpango wa Blue Economy.

KMA imekuwa katika mstari wa mbele kwa kukuza elimu na mafunzo ya kibaharia ya vipindi vya bandari na ubaharia.Vipindi hivi vinalenga kufunza Wakenya walio na uwezo wa kuelekeza mpango wa Blue Economy katika bandari na kwa bahari pamoja na kuongeza mauzo na uajiri wa mabaharia wa Kenya na kampuni za meli za kimataifa.

Mamlaka ya Kenya ya Shughuli za Baharini pia huhakikisha kwamba Kenya inafuata mahitaji ya mafunzo na udhibitisho wa mabaharia kulingana na viwango vya mafunzo, udhibitisho na watchkeeping ya mabaharia (STCW Convention, 1978 ilivyorekebishwa) na kwa hiyo namna ya viwango vinadumishwa katika vyuo vya mafunzo vilivyodhibitishwa. Kwa hivyo, kampuni hii imedhibitisha kozi za mafunzo na vyuo vya mafunzo vya mabaharia kuhakikisha kuwa taifa inadumisha cheo chao katika Shirika la kimataifa la bahari (IMO) “White list”. Nchi ya Kenya ilikubaliwa katika White list ya IMO mnamo mwezi wa May 2010 na kufuatia uhuru wa tathmini ya IMO mwaka wa 2016, kamati ya ubaharia na usalama wa IMO katika kipindi chao cha 97th ilikubaliana kwamba Kenya itaendelea kuzingatia barabara viwango vya mafunzo,udhibitisho na watchkeeping ya mabaharia (STCW Convention,1978 ilivyorekebishwa)

Zaidi ya hayo, KMA ina Jukumu la kuhakikisha kuwa viwango vya elimu na mafunzo ya ubaharia nchini Kenya yametegemezwa kulingana na viwango vya kimataifa. Hili ni hakikisho kwa wamiliki meli wenyeji na wa kigeni kuwa mabaharia waliofunzwa nchini Kenya wameajibika ipasavyo kufanya kazi katika meli zao. Ili mabaharia waweze kuajiriwa katika meli za kimataifa wanapswa kuwa na vyeti vya ustadi katika vyeti vya lazima vya STCW pamoja na vyeti vya kadirio la staha au chumba cha injini.

KMA pia inajukuma la kusimamia usajilishaji wa mabaharia kulingana na mahitaji ya Merchant Shipping Act, Cap. 389 na kanuni 1.4 ya Maritime Labour Convention, 2006 (MLC) ilivyorekebishwa. KMA pia yawezesha uajiri wa mabaharia wa Kenya kupitia kanuni ya usajilishaji na mawakala uwekaji wa mabaharia. Hivi sasa, KMA imeidhinisha mawakala wa tano wa usajili kwa majina Mombasa Ocean Agency, Diverse Shipping, Alpha Logistics, East Africa Deep Sea Fishing na Mediterranean Shipping Company (MSC) ship Management Ltd. Uajiri wa mabaharia wa Kenya yatakikana kuengeza mapato ya kigeni nchini, kuongeza mapato ya taifa na pia kutekeleza Big Four Agenda katika ugavi wa chakula kwani mabaharia watakuwa na uwezo wa kutimiza mahitaji yao pamoja na familia zao.

KMA pia inadhibitisha madaktari wanaowapima mabaharia kuhakikisha kwamba wanaafya njema ya kufanya kazi melini. KMA imepitisha taasisi saba za huduma ya matibabu kama

12 Halmashauri ya Kenya ya Usimamizi wa Shughuli za Usafirishaji Baharini

Page 13: HALMASHAURI YA KENYA YA USIMAMIZI WA … Centers/KMA...za bandari, kufanya usafirishaji wa mizigo, kutafsiri nyaraka za mkataba katika biashara ya usafiri wa meli, kufuata mikataba

zifuatazo; Hospitali ya Mombasa, Kliniki ya Bandari, Hospitali ya Watamu, kituo cha mazoezi ya matibabu Mombasa, Kisima Health Facility, Coast X-ray Centre na Masala Healthcare Services Limited.

KMA inaendelea kufanya kazi pamoja na Chama cha Mabaharia cha Kenya (SUK), International Transport Workers Federation and employers kuhakikisha wametekeleza mazingira bora ya kazi na ya kuishi ndani ya meli kulingana na Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO), Maritime Labour Convention, 2006. Hivi sasa KMA imeshirikiana na State Department of Shipping, the Ministry of Labour and Social Protection pamoja na washikadau wengineo katika maendeleo ya kiwango maalum cha mshahara ya mabaharia wa Kenya. Punde mshahara kamili inapoimarishwa, mabaharia wa Kenya watafaidi malipo adili ya kazi sawa katika meli inayosuluhisha utofauti wa mishahara ya mabaharia wa Kenya na wale wa mataifa mengine ambao wameshaimarisha kiwango maalum cha mshahara.

KMA inaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na Chama cha Mabaharia cha Kenya (SUK) katika uajiri na masilahi ya mabaharia pamoja na kusuluhisha mizozo baina ya mabaharia na waajiri kulingana na roho ya ushirikiano kati ya vyama vya mabaharia, waajiri wao na Serikali katika kushughulika na masuala ya ustawi wa baharini kama ilivyotetewa na Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO) na Mkataba wa Kazi ya Maritime, 2006 (MLC). Ni muhimu kwa mabaharia kujiandikisha na Chama halali ili kufaidika na nguvu katika mazungumzo zinazotolewa na wito mmoja wa vyama vya wafanyakazi.

Zaidi ya hayo, KMA imejitolea kuendeleza ustawi wamabaharia. KMA inaendelea kupatanisha migogoro kati ya mabaharia na waajiri wao pamoja na washauri wa mabaharia juu ya makubaliano ya ajira na mashirika. Kupitia Jimbo la Kudhibiti Bandari (Port State Control) na Watazamaji wa Jimbo la Bendera (Flag State Control), KMA inafanya ukaguzi wa meli ambao ni pamoja na mengine, kuchunguza hali ya kazi ya mabaharia ndani ya meli.

Aidha, usalama wa mabaharia wa Kenya unahakikishiwa kupitia uthibitisho wa ushirikiano wa mpango wa vyeti uliofanywa na Majimbo ya Bendera( Flag States) pamoja na Wamiliki wa meli na Makampuni ya Usimamizi wa Meli. KMA pia inathibitisha vyeti vinavyotolewa na Mataifa mengine ya Nchi ili kuhakikisha usalama wa mabaharia ndani ya meli kabla ya utoaji wa Hati ya Kutayarisha mabaharia wa Kenya na Kitabu cha Rekodi.

13Halmashauri ya Kenya ya Usimamizi wa Shughuli za Usafirishaji Baharini

Page 14: HALMASHAURI YA KENYA YA USIMAMIZI WA … Centers/KMA...za bandari, kufanya usafirishaji wa mizigo, kutafsiri nyaraka za mkataba katika biashara ya usafiri wa meli, kufuata mikataba

USAWA WA JINSIA KATIKA SEKTA YA UBAHARIA KMA imejitolea kutekeleza mpango wa shirika la kimataifa la IMO la kuhakikisha wanawake wanaajiriwa kama inavyotakikana na Malengo ya Maendeleo ya Karne hii yanayotaka wanawake kuajiriwa sawa na wanaume.

14 Halmashauri ya Kenya ya Usimamizi wa Shughuli za Usafirishaji Baharini

Page 15: HALMASHAURI YA KENYA YA USIMAMIZI WA … Centers/KMA...za bandari, kufanya usafirishaji wa mizigo, kutafsiri nyaraka za mkataba katika biashara ya usafiri wa meli, kufuata mikataba

HUDUMA ZA HALMASHAURI KWA JAMII (CSR) Halmashauri imejitolea kufanya shughuli zake kwa njia safi yenye kutilia maanani, utaalamu na ulinzi kwa mazingira na jamii kwa jumla. Kwa hivyo, KMA imetilia maanani huduma kwa jamii na inashirikisha jamii, inalinda mazingira, inainua elimu, kutunza afya, michezo, kuboresha miradi mbali mbali ikiwemo usaidizi mashinani.

Halmashauri imejitolea kufanya shughuli zinazoleta ushirikiano na umoja wa jamii, ulinzi wa mazingira la bahari, elimu, afya, michezo, miradi ya usaidizi, usawa wa kijinsia na mipango kwa watu wenye ulemavu miongoni mwa wengine.

15Halmashauri ya Kenya ya Usimamizi wa Shughuli za Usafirishaji Baharini

Page 16: HALMASHAURI YA KENYA YA USIMAMIZI WA … Centers/KMA...za bandari, kufanya usafirishaji wa mizigo, kutafsiri nyaraka za mkataba katika biashara ya usafiri wa meli, kufuata mikataba

KWA MAELEZO ZAIDI: WASILIANA NASI KUPITIA

MKURUGENZI MKUUKENYA MARITIME AUTHORITYSLP 95076- 80104, MOMBASA.

Simu: +254 41 2318398/9, 0724319344, 0733221322Faksi: +254 412318397

Barua pepe: [email protected]; [email protected];Tovuti: www.kma.go.ke

Tutafute kwa kupitia:: @kmakenya

: Kenya Maritime Authority

Sajili ya ISO 9001:2015