8
KAMATI ZA UADILIFU KAMATI ZA UADILIFU HITIMISHO Uanzishwaji wa Kamati za Kudhibiti Uadilifu sehemu za kazi ni hatua muhimu katika kujenga, kusimamia na kukuza maadili ya watumishi wa umma ndani ya Wizara, Idara na Wakala wa Serikali. Jukumu kubwa la watumishi kwa sasa ni kuzingatia maadili. Wananchi nao hawana budi kutoa taarifa za vitendo vya uvunjaji wa maadili vya watumishi wa umma na kuacha kuwa chanzo cha watumishi hao kuvunja maadili hayo kwa kuwashawishi kupokea rushwa. Ni dhahiri kuwa hatua hizi zitaboresha huduma inayotolewa kwa wananchi na kudhibiti vitendo vya rushwa katika utumishi wa umma. Hii itasaidia kuimarisha imani ya wananchi katika utendaji kazi wa Serikali na hivyo kukuza na kuimarisha ushirikiano wao katika shughuli za ujenzi wa taifa ikiwemo mapambano dhidi ya rushwa. Uadilifu wako na wangu utazuia rushwa, kuboresha na kuimarisha utumishi wa umma. Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, S.L.P. 4865, Dar es Salaam, Tanzania. Simu: 022-2150043-6 Nukushi: 022-2150047 Baruapepe: [email protected] Mkuu wa Taasisi - Mkoa S.L.P 6420, Dar es Salaam Simu 022 213 2954 Mkuu wa Taasisi - Mkoa S.L.P 6420, Ilala, DSM Simu 022 286 1088 Mkuu wa Taasisi - Mkoa S.L.P 90397, Kinondoni, DSM Simu 022 217 0852 Mkuu wa Taasisi - Mkoa S.L.P 42325, Temeke, DSM Simu 022 286 3092 Mkuu wa Taasisi - Mkoa S.L.P 1055, Arusha Simu 027 250 3538, 250 7928 Mkuu wa Taasisi - Mkoa S.L.P 1138, Bukoba Simu 028 222 0848, 222 0491 Mkuu wa Taasisi - Mkoa S.L.P 6420, Dar es Salaam Simu 022 213 2954 Mkuu wa Taasisi - Mkoa S.L.P 1175, Dodoma Simu 026 232 2846, 232 2003 Mkuu wa Taasisi - Mkoa S.L.P 1575, Iringa Simu 026 270 1700, 270 0156 Mkuu wa Taasisi - Mkoa S.L.P 30261, Kibaha Simu 023 240 2658 Mkuu wa Taasisi - Mkoa S.L.P 880, Kigoma Simu 028 280 2889 Mkuu wa Taasisi - Mkoa S.L.P 1004, Lindi Simu 023 220 2456, 220 2799 Mkuu wa Taasisi - Mkoa S.L.P 386, Babati Simu 027 253 0256, 253 0255 Mkuu wa Taasisi - Mkoa S.L.P 1419, Mbeya Simu 025 250 3566 Mkuu wa Taasisi - Mkoa S.L.P 845, Mororgoro Simu 023 261 4302, Fax: 023 260 4478 Mkuu wa Taasisi - Mkoa S.L.P 1951, Moshi Simu 027 275 0885 Mkuu wa Taasisi - Mkoa S.L.P 213, Mtwara Simu 023 233 4013 233 3726 Mkuu wa Taasisi - Mkoa S.L.P 377, Musoma Simu 028 262 2024 Mkuu wa Taasisi - Mkoa S.L.P 2599, Mwanza Simu 028 250 0600, 250 0602 Faxi: 028 250 0600 Mkuu wa Taasisi - Mkoa S.L.P 37, Shinyanga Simu 028 276 2630 Mkuu wa Taasisi - Mkoa S.L.P 484, Singida Simu 026 250 2305, 250 2550 Mkuu wa Taasisi - Mkoa S.L.P 926, Songea Simu 025 260 0613, 260 0663 Mkuu wa Taasisi - Mkoa S.L.P 273, Sumbawanga Simu 025 280 0312 280 2426 Mkuu wa Taasisi - Mkoa S.L.P 1055, Tanga Simu 027 264 5186 Mkuu wa Taasisi - Mkoa S.L.P 1020, Tabora Simu 026 260 4030, 260 4311 TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA

HITIMISHO S.L.P 1419, Mbeya S.L.P 845, Mororgoro...HITIMISHO Uanzishwaji wa Kamati za Kudhibiti Uadilifu sehemu za kazi ni hatua muhimu katika kujenga, kusimamia na kukuza maadili

  • Upload
    others

  • View
    8

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: HITIMISHO S.L.P 1419, Mbeya S.L.P 845, Mororgoro...HITIMISHO Uanzishwaji wa Kamati za Kudhibiti Uadilifu sehemu za kazi ni hatua muhimu katika kujenga, kusimamia na kukuza maadili

KAMATI ZA UADILIFU

KAMATI ZA UADILIFU

HITIMISHOUanzishwaji wa Kamati za Kudhibiti Uadilifu sehemu za kazi ni hatua muhimu katika kujenga, kusimamia na kukuza maadili ya watumishi wa umma ndani ya Wizara, Idara na Wakala wa Serikali. Jukumu kubwa la watumishi kwa sasa ni kuzingatia maadili. Wananchi nao hawana budi kutoa taarifa za vitendo vya uvunjaji wa maadili vya watumishi wa umma na kuacha kuwa chanzo cha watumishi hao kuvunja maadili hayo kwa kuwashawishi kupokea rushwa. Ni dhahiri kuwa hatua hizi zitaboresha huduma inayotolewa kwa wananchi na kudhibiti vitendo vya rushwa katika utumishi wa umma. Hii itasaidia kuimarisha imani ya wananchi katika utendaji kazi wa Serikali na hivyo kukuza na kuimarisha ushirikiano wao katika shughuli za ujenzi wa taifa ikiwemo mapambano dhidi ya rushwa.

Uadilifu wako na wangu utazuia rushwa, kuboresha na kuimarisha utumishi wa umma.

Mkurugenzi Mkuu,Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa,

S.L.P. 4865,Dar es Salaam,

Tanzania.

Simu: 022-2150043-6Nukushi: 022-2150047

Baruapepe: [email protected]

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 6420, Dar es SalaamSimu 022 213 2954

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 6420, Ilala, DSMSimu 022 286 1088

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 90397, Kinondoni, DSMSimu 022 217 0852

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 42325, Temeke, DSMSimu 022 286 3092

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1055, ArushaSimu 027 250 3538, 250 7928

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1138, BukobaSimu 028 222 0848, 222 0491

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 6420, Dar es SalaamSimu 022 213 2954

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1175, DodomaSimu 026 232 2846, 232 2003

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1575, IringaSimu 026 270 1700, 270 0156

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 30261, KibahaSimu 023 240 2658

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 880, KigomaSimu 028 280 2889

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1004, LindiSimu 023 220 2456, 220 2799

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 386, BabatiSimu 027 253 0256, 253 0255

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1419, MbeyaSimu 025 250 3566

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 845, MororgoroSimu 023 261 4302, Fax: 023 260 4478

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1951, MoshiSimu 027 275 0885

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 213, MtwaraSimu 023 233 4013 233 3726

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 377, MusomaSimu 028 262 2024

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 2599, MwanzaSimu 028 250 0600, 250 0602Faxi: 028 250 0600

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 37, ShinyangaSimu 028 276 2630

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 484, SingidaSimu 026 250 2305, 250 2550

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 926, SongeaSimu 025 260 0613, 260 0663

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 273, SumbawangaSimu 025 280 0312 280 2426

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1055, TangaSimu 027 264 5186

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1020, TaboraSimu 026 260 4030, 260 4311

TAAsIsI yA KUZUIA nA KUpAMbAnA nA RUshwA

TAAsIsI yA KUZUIA nA KUpAMbAnA nA RUshwA

Page 2: HITIMISHO S.L.P 1419, Mbeya S.L.P 845, Mororgoro...HITIMISHO Uanzishwaji wa Kamati za Kudhibiti Uadilifu sehemu za kazi ni hatua muhimu katika kujenga, kusimamia na kukuza maadili

UTANGULIZIMwaka 2005, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitoa waraka kwa Wizara, Idara na Wakala zake ikiziagiza kuunda Kamati za Kudhibiti Uadilifu kwa lengo la kusimamia na kukuza maadili ya watumishi. Hatua hii ilitokana na kumomonyoka kwa maadili ya baadhi ya watumishi wa umma hali iliyosababisha huduma kutolewa chini ya kiwango. Tafsiri ya maadili, kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu (Toleo la Pili 2004), ni mwenendo mwema. Neno hili pia linamaanisha misingi, taratibu na kanuni zilizokubalika katika jamii kuwa mwongozo wa mahusiano au matendo mema. Inatarajiwa kuwa utendaji kazi wa kamati hizi utawajenga watumishi kimaadili na hivyo pia kudhibiti vitendo vya rushwa katika utumishi wa umma ambavyo ni mwenendo mbaya.

MAJUKUMU YA KAMATI Majukumu ya Kamati za Kudhibiti Uadilifu, kwa mujibu wa waraka wa Serikali wa Septemba 13, 2005 ni yafuatayo:

• Kusimamia na kuwezesha shughuli za kuzuia vitendo vya rushwa katika Wizara, Idara na Wakala wa Serikali.

• Kuongoza na kusimamia zoezi la kuandaa mipango ya kupambana na rushwa na utaratibu wa utekelezaji wake.

• Kuandaa taarifa za utendaji kazi za robo mwaka na kuwasilisha kwa Katibu Mkuu Kiongozi kupitia Kitengo cha Uratibu Utawala Bora (GGCU). Taarifa hizo zinatakiwa kuridhiwa na uongozi wa taasisi husika.

• Kupokea na kushughulikia malalamiko yote yanayohusu uadilifu, ukiukwaji wa maadili na misingi ya utawala bora sehemu za kazi.

• Kutoa mafunzo kwa watendaji waandamizi, wa kati na watendaji wengine kuhusu umuhimu wa kuzingatia kanuni za maadili, nadharia ya mapambano dhidi ya rushwa na hatua za kuchukuliwa kuleta uwazi na uadilifu katika uendeshaji wa shughuli za umma.

• Kuhakikisha kanuni za maadili katika Wizara, Idara na Wakala zinaeleweka na kuzingatiwa na watumishi wote.

• Kuhakikisha kuwa kanuni za maadili hazilengi kuwaadhibu au kuwabugudhi watumishi bali kuwakumbusha juu ya utumishi unaozingatia tabia nzuri, uaminifu, hekima na uwazi.

• Kutoa ushauri kwa uongozi kuhusu hatua za kiutawala zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya mtumishi aliyekiuka maadili.

MUUNDO WA KAMATI Kamati za Kudhibiti Uadilifu katika Wizara, Idara na Wakala wa Serikali zinaundwa na wajumbe wasiozidi wanne ambao huteuliwa na Mtendaji Mkuu wa sehemu husika. Wajumbe hawa wanatakiwa wawe maafisa waandamizi wenye hadhi ya ukurugenzi au nyadhifa zinazokaribia ngazi hii ambao wako kwenye menejimenti na wanaoshiriki vikao muhimu vya maamuzi.Wajumbe walioteuliwa hupewa mafunzo kuhusu majukumu na mipaka ya utendaji kazi wa kamati. Mafunzo haya huendeshwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

UMUHIMU WA KAMATI Kamati za Kudhibiti Uadilifu zina umuhimu mkubwa sana katika kusimamia na kukuza maadili ya watumishi wa umma na kuimarisha misingi ya utawala bora katika maeneo ya kazi. Maadili yakisimamiwa ipasavyo mambo yafuatayo yatatokea:

• Wananchi watajenga imani juu ya uadilifu wa Serikali. Maadili hulinda heshima ya Serikali mbele ya macho ya wananchi.

• Watumishi wa umma watasimamia kwa dhati utekelezaji wa sheria, kanuni na taratibu na kufanya kazi kwa kuzingatia viwango bora.

• Kutakuwa na matumizi mazuri ya fedha za umma na rasilimali nyingine.

• Viongozi na watumishi wengine wa umma watatumia vizuri madaraka waliyopewa katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.

UMUHIMU WA MAADILISheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2002 inaeleza kuwa ili utumishi wa umma uwe wenye ufanisi na unaoheshimika, watumishi wa umma wanapaswa kufuata Kanuni za Maadili ya Utumishi ambazo zinahimiza tabia na mwenendo ufuatao:

• Kutoa huduma bora.• Utii kwa Serikali.• Bidii katika kazi. • Kutoa huduma bila upendeleo.• Kufanya kazi kwa uadilifu.

• Kuwajibika kwa umma.• Kuheshimu Sheria• Matumizi sahihi ya taarifa za ofisi za Serikali.

Mwaka 1996, Kamati ya Nolan ilitoa mapendekezo ya kanuni saba za kufuatwa na watumishi wa umma ili utumishi wa umma uwe wenye ufanisi na unaoheshimika. Hizi pia ni kanuni ambazo hazina budi kuzingatiwa na watumishi wote wa umma nchini kwa lengo la kuboresha huduma inayotolewa kwa wananchi. Hii ni kwa sababu matokeo ya uzingatiaji wa kanuni hizi, kwa namna moja au nyingine, unadumisha na kuimarisha maadili ya watumishi. Kanuni hizo ni zifuatazo:

• Kutokuwa mbinafsi: Watumishi wa umma wanapaswa kufanya maamuzi kwa manufaa ya umma na siyo kwa manufaa binafsi ili kujipata pesa au faida nyingine yoyote kwa ajili yao, familia zao au marafiki.

• Uadilifu: Watumishi wa umma hawapaswi kuwa na wajibu wa kifedha au wajibu mwingine kwa watu au mashirika ya nje ambao unaweza kuathiri utekelezaji wa majukumu yao ya kiofisi.

• Kutoa Huduma bila Upendeleo: Katika kufanya shughuli yoyote ile ya umma ikiwa ni pamoja na kuweka miadi, utoaji wa zabuni au kupendekeza watu wa kupewa zawadi au manufaa, watumishi wa umma wanapaswa kufanya maamuzi kwa kuzingatia sifa.

• Kuwajibika kwa Umma: Watumishi wa umma watawajibika kwa umma kwa maamuzi na matendo yao na watakuwa tayari kwa uchunguzi wowote dhidi ya Ofisi yao.

• Uwazi: Watumishi wa umma wanapaswa kuwa wa wazi kadiri inavyowezekana juu ya maamuzi na hatua wanazochukua. Watatakiwa kutoa sababu kuhusu maamuzi yao na kutosambaza taarifa yoyote pale maslahi ya umma yatakapohitaji ifanyike hivyo.

• Uaminifu: Watumishi wa umma wana jukumu la kutangaza maslahi binafsi yanayohusiana na majukumu yao kwa umma na kuchukua hatua za kutatua mgongano wowote utakaojitokeza katika namna inayolinda maslahi ya umma.

• Uongozi: Watumishi wa umma wanatakiwa kuziendeleza na kuziunga mkono kanuni hizi kwa kuwa mfano na kwa uongozi.

Page 3: HITIMISHO S.L.P 1419, Mbeya S.L.P 845, Mororgoro...HITIMISHO Uanzishwaji wa Kamati za Kudhibiti Uadilifu sehemu za kazi ni hatua muhimu katika kujenga, kusimamia na kukuza maadili

MALIpo yAsIyosTAhILI KwA MTUMIshI wA UMMAMALIpo yAsIyosTAhILI

KwA MTUMIshI wA UMMA

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 6420, Dar es SalaamSimu 022 213 2954

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 6420, Ilala, DSMSimu 022 286 1088

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 90397, Kinondoni, DSMSimu 022 217 0852

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 42325, Temeke, DSMSimu 022 286 3092

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1055, ArushaSimu 027 250 3538, 250 7928

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1138, BukobaSimu 028 222 0848, 222 0491

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 6420, Dar es SalaamSimu 022 213 2954

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1175, DodomaSimu 026 232 2846, 232 2003

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1575, IringaSimu 026 270 1700, 270 0156

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 30261, KibahaSimu 023 240 2658

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 880, KigomaSimu 028 280 2889

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1004, LindiSimu 023 220 2456, 220 2799

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 386, BabatiSimu 027 253 0256, 253 0255

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1419, MbeyaSimu 025 250 3566

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 845, MororgoroSimu 023 261 4302, Fax: 023 260 4478

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1951, MoshiSimu 027 275 0885

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 213, MtwaraSimu 023 233 4013 233 3726

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 377, MusomaSimu 028 262 2024

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 2599, MwanzaSimu 028 250 0600, 250 0602Faxi: 028 250 0600

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 37, ShinyangaSimu 028 276 2630

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 484, SingidaSimu 026 250 2305, 250 2550

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 926, SongeaSimu 025 260 0613, 260 0663

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 273, SumbawangaSimu 025 280 0312 280 2426

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1055, TangaSimu 027 264 5186

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1020, TaboraSimu 026 260 4030, 260 4311

TAAsIsI yA KUZUIA nA KUpAMbAnA nA RUshwA

TAAsIsI yA KUZUIA nA KUpAMbAnA nA RUshwA

Mkurugenzi Mkuu,Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa,

S.L.P. 4865,Dar es Salaam,

Tanzania.

Simu: 022-2150043-6Nukushi: 022-2150047

Baruapepe: [email protected]

kwa mara ya pili kwa kazi ileile, hukataa malipo yoyote ya ziada kwa kazi aliyoifanya na ambayo anajua tayari amepokea malipo yake.

Je, nini kifanyike?Ni wajibu wa mwajiri mmoja kutoa taarifa za mtumishi au watumishi wa umma wanaodai au kupokea malipo ya kazi moja mara mbili kwa waajiri wenzake. Aidha, ni wajibu wa kila mwajiri kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya mtumishi au watumishi wanaothibitika kudai au kukubali kulipwa mara mbili kwa kazi ambayo mwajiri huyo au mwajiri mwingine tayari amemlipa. Hatua za kinidhamu dhidi ya mtumishi au watumishi wa umma wa aina hiyo zitakomesha tabia za aina hiyo na pia kuokoa fedha za umma ambazo zingekuwa zitumike isivyo sahihi. Ikumbukwe kuwa fedha wanazolipwa watumishi wa umma ni fedha zinazotokana na kodi za wananchi na ambazo zinatakiwa kutumika ipasavyo kwa maendeleo ya wananchi wote na si vinginevyo. Matumizi kinyume na maslahi ya umma ni matumizi mabaya na yanayotakiwa kukemewa kwa nguvu zote.

Page 4: HITIMISHO S.L.P 1419, Mbeya S.L.P 845, Mororgoro...HITIMISHO Uanzishwaji wa Kamati za Kudhibiti Uadilifu sehemu za kazi ni hatua muhimu katika kujenga, kusimamia na kukuza maadili

UtanguliziJukumu kuu la Serikali ya taifa lolote duniani ni kuongoza na kuhudumia jamii ya watu wanaounda taifa hilo na wale wanaotembelea au kuishi katika nchi hiyo kwa sababu mbalimbali. Huduma hizo za kijamii, kiuchumi na kisiasa hutolewa kwa niaba yake na waajiriwa wake ambao kwa hapa nchini wanaitwa watumishi wa umma. Kwa kuwa ni waajiriwa wa Serikali, watumishi hao hulipwa ujira wao kwa kazi wanazofanya na Serikali. Hata hivyo, wapo watumishi ambao pamoja na kulipwa na Serikali kwa kazi wanayoifanya, hudai, hulipwa au hupokea malipo mengine kutoka kwa wale wanaowahudumia. Wengine hudai na hulipwa malipo mara mbili kwa kazi moja. Je, hii ni sahihi? Maelezo katika chapisho hili yanafafanua aina na malipo halali anayostahili kulipwa mtumishi wa umma.

Mtumishi wa umma ni nani?Mtumishi wa umma, kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2002, ni mtu mwenye wadhifa au anayefanya kazi katika ofisi ya kutoa huduma kwa umma. Mtu huyo anaweza kuwa mwajiriwa wa Serikali chini ya Wizara, Idara au Wakala zake. Mfano wa wizara ni Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, wakati Idara zinazozungumziwa hapa ni kama vile Taasisi ya Kuzuia na Kampambana na Rushwa na mfano wa wakala ni Wakala wa Majengo Tanzania. Mtumishi wa umma pia anaweza kuwa mwajiriwa wa shirika la umma linalopata ruzuku kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli zake kutoka Serikalini kama vile Shirika la Posta Tanzania na Shirika la Umeme Tanzania.Vilevile mtumishi wa umma ni mwajiriwa yeyote wa Mahakama au Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vyombo ambavyo pamoja na kuwa mihimili ya uongozi wa nchi, uendeshaji wa shughuli zake unategemea fedha zinazotolewa na Serikali.

Aina ya malipo anayostahili mtumishi wa ummaPamoja na tofauti mbalimbali za stahili za

watumishi wa umma zinazotokana na aina ya ajira au vyeo, kila mtumishi wa umma ana haki ya kulipwa mshahara kwa mujibu wa Sehemu ‘E’ ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma (Standing Orders) za mwaka 1994. Malipo hayo ya mshahara yanatajwa pia katika kifungu cha 20 cha Sheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2002. Pia Sehemu ‘E’ ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma ya mwaka 1994, kama inavyoelezwa katika vifungu vya 85-88 vya Sheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2002, inabainisha kuwa mtumishi wa umma anastahili kulipwa mafao ya kustaafu.Mtumishi wa umma, kwa mujibu wa Sehemu ‘L’ ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za mwaka 1994 anastahili kulipwa posho. Posho hizo ni kama vile posho ya kujikimu safarini, posho ya kikao, posho ya kuhama kituo cha kazi au posho inayotokana na kufanya kazi muda wa ziada. Posho nyingine inayoitwa ‘honoraria’ hulipwa kwa mtumishi kwa kufanya kazi maalum. Aidha, mtumishi wa umma, kwa mujibu wa Kifungu cha 33 cha Sheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2002, anastahili kulipwa fidia iwapo ataumia au kufa akiwa anatekeleza majukumu yake ya ofisi ya umma.

Je, malipo stahili ya mtumishi wa umma ni yapi?Mtumishi wa umma, kama ilivyoelezwa hapo juu, anastahili malipo mbalimbali kutokana na kazi anazozifanya. Malipo haya yanaweza kuwa posho ya safari iwapo amesafiri, honoraria iwapo amefanya kazi fulani maalum au mshahara ambao ni ujira wa kila mwezi. Msisitizo hapa ni kuwa lazima mtumishi huyo awe amefanya kazi ndiyo alipwe.

Malipo asiyostahili mtumishi wa ummaMtumishi wa umma, kwa mujibu wa sheria zinazosimamia utumishi wa umma, hastahili kulipwa malipo yafuatayo:

• Malipo ambayo hajayafanyia kazi:

Haya ni malipo ambayo mtumishi anaweza kulipwa wakati hajafanya kazi ambayo inatajwa kuwa ameifanya.

• Malipo mara mbili: Mtumishi wa umma yeyote hastahili kupokea malipo mara mbili kwa kazi moja. Kwa mfano, hakuna mtumishi wa umma anayestahili kulipwa mishahara miwili kwa mwezi mmoja au posho mbili za vikao kwa kikao kimoja. Aidha, ni kinyume na utaratibu kwa mtumishi kudai, kulipwa au kupokea malipo ya posho ya honoraria mara mbili kwa kazi moja kwa yeye kupokea malipo ya mwajiri wake na yale ya Ofisi ambayo pengine ilimwalika kuwasilisha mada.

• Malipo ya ushawishi: Haya ni malipo ambayo mtumishi wa umma hudai kutoka kwa mtu anayemhudumia.

Ukiukwaji wa taratibu za malipo na hatua za kuchukuliwaKimsingi, iwapo mtumishi wa umma atalipwa mara mbili kwa kazi moja anatakiwa arejeshe malipo ya mmoja wa waajiri waliomlipa ama kukataa malipo ya pili na kutoa ufafanuzi kuwa tayari amelipwa kwa kazi hiyo. Kinyume na hapo, mtumishi huyo atakuwa anakiuka Kanuni za Utumishi wa Umma ingawa huu umekuwa ni mwenendo wa baadhi ya watumishi wasiokuwa waadilifu. Aidha, ni kinyume cha maadili na Kanuni za Utumishi wa Umma kwa mtumishi kulipwa na kampuni binafsi ambayo imeingia mkataba na Wizara, Idara au Wakala wa Serikali ambayo anaifanyia kazi au vinginevyo. Hili ni kosa ambalo linatakiwa kushughulikiwa haraka kiutawala ili kukomesha tabia hiyo.

Uadilifu wa mtumishi wa ummaUadilifu ni moja kati ya sifa anazotakiwa kuwa nazo mtumishi wa umma. Ni kanuni muhimu kati ya kanuni za utumishi wa umma zinazopaswa kuzingatiwa na kila mtumishi iwe ameajiriwa na Wizara, Idara au Wakala wa Serikali ama Mahakama na Bunge. Mtumishi wa umma mwadilifu hawezi kudai na kupokea malipo ya kazi moja mara mbili. Mtumishi wa umma mwadilifu pale atakapoandaliwa malipo

Page 5: HITIMISHO S.L.P 1419, Mbeya S.L.P 845, Mororgoro...HITIMISHO Uanzishwaji wa Kamati za Kudhibiti Uadilifu sehemu za kazi ni hatua muhimu katika kujenga, kusimamia na kukuza maadili

JUKUMU LA KILA MwAnAnChI KUpAMbAnA nA RUshwA

JUKUMU LA KILA MwAnAnChI KUpAMbAnA nA RUshwAMkurugenzi Mkuu,

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa,S.L.P. 4865,

Dar es Salaam,Tanzania.

Simu: 022-2150043-6Nukushi: 022-2150047

Baruapepe: [email protected]

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 6420, Dar es SalaamSimu 022 213 2954

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 6420, Ilala, DSMSimu 022 286 1088

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 90397, Kinondoni, DSMSimu 022 217 0852

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 42325, Temeke, DSMSimu 022 286 3092

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1055, ArushaSimu 027 250 3538, 250 7928

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1138, BukobaSimu 028 222 0848, 222 0491

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 6420, Dar es SalaamSimu 022 213 2954

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1175, DodomaSimu 026 232 2846, 232 2003

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1575, IringaSimu 026 270 1700, 270 0156

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 30261, KibahaSimu 023 240 2658

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 880, KigomaSimu 028 280 2889

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1004, LindiSimu 023 220 2456, 220 2799

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 386, BabatiSimu 027 253 0256, 253 0255

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1419, MbeyaSimu 025 250 3566

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 845, MororgoroSimu 023 261 4302, Fax: 023 260 4478

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1951, MoshiSimu 027 275 0885

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 213, MtwaraSimu 023 233 4013 233 3726

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 377, MusomaSimu 028 262 2024

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 2599, MwanzaSimu 028 250 0600, 250 0602Faxi: 028 250 0600

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 37, ShinyangaSimu 028 276 2630

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 484, SingidaSimu 026 250 2305, 250 2550

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 926, SongeaSimu 025 260 0613, 260 0663

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 273, SumbawangaSimu 025 280 0312 280 2426

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1055, TangaSimu 027 264 5186

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1020, TaboraSimu 026 260 4030, 260 4311

TAAsIsI yA KUZUIA nA KUpAMbAnA nA RUshwA

TAAsIsI yA KUZUIA nA KUpAMbAnA nA RUshwA

Page 6: HITIMISHO S.L.P 1419, Mbeya S.L.P 845, Mororgoro...HITIMISHO Uanzishwaji wa Kamati za Kudhibiti Uadilifu sehemu za kazi ni hatua muhimu katika kujenga, kusimamia na kukuza maadili

uuu

JUKUMU LA KILA MWANANCHI KUPAMBANA NA RUSHWA

Ni jukumu la kila mwananchi kupambana na rushwa. Mwananchi mwenye uzalendo wa kweli na anayeipenda nchi yake huwa mstari wa mbele katika kupambana na rushwa, bila woga wowote. Uzalendo ni kuitetea nchi hadi kujitoa kufa kwa ajili yake huku ukitetea haki, utamaduni, mali za nchi pamoja na mambo yote yanayowafanya kuwa wamoja katika taifa. Bila kumnyooshea kidole mtu mwingine mwananchi unatakiwa kuchukua hatua pale unapoona mtu anavunja sheria, kwa kupokea rushwa au kwenda kinyume na maadili ya kazi. Katiba ya nchi Ibara ya 26 (2) “Kila mtu ana haki, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria, kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha hifadhi ya Katiba na sheria za nchi”

JINSI YA KILA MWANANCHI KUSHIRIKI KUPAMBANA NA RUSHWA:-

• Kutoa taarifa za vitendo vya rushwa• Kutoa ushahidi dhidi ya wala rushwa• Kutoa elimu ya rushwa kwa wenzake.• Kutojihusisha na vitendo vya rushwa• Kutii sheria

Kutoa taarifa

Kila mwananchi ana jukumu la kutoa taarifa za vitendo vya rushwa kwa TAKUKURU au kwa vyombo vingine vya sheria au dola. Katiba ya nchi Ibara ya 27 (1) inasema kila mtu anawajibu wa kulinda mali asilia ya Muungano, mali ya Mamlaka ya nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, pia kuheshimu mali ya mtu mwingine.

Ibara ya 27(2) inasema watu wote watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali ya mamlaka ya nchi na ya pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu, na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadae ya taifa lao.Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11/2007 kifungu cha 39 kinamtaka “kila mtu ambaye anafahamu au anafahamu kusudio la kutendwa kwa kosa la rushwa kutoa taarifa kwa afisa wa TAKUKURU”. Taarifa zinaweza kutolewa kwa njia ya simu barua, barua pepe au kufikisha taarifa hizo katika ofisi ya TAKUKURU Makao Makuu au ofisi zilizopo mikoani na wilayani kote nchini.

Kutoa ushahidi

Kutoa tu taaarifa bila kuwa tayari kutoa ushahidi hakutasaidia kuwachukulia hatua za kisheria wala rushwa. Hivyo wewe mwananchi una jukumu la kuwa tayari kutoa ushahidi wa vitendo vya rushwa ulivyoshuhudia katika mahakama au popote pale utakapohitajika kufanya hivyo. Athari za kukataa kutoa ushahidi au taarifa sahihi ni kesi kushindwa mahakamani au kukosa ushahidi wa kufungua kesi.

Kutoa elimu

Mwanachi yeyote una jukumu la kumuelimisha mwananchi mwenzako kuhusiana na suala la rushwa na athari zake kwake yeye na jamii kwa ujumla. Kwa kufanya hivyo utakuwa umemsaidia mwananchi huyo kuepuka kujihusisha na vitendo vya rushwa. Vilevile kwa kushiriki kutoa elimu utakuwa umeunga mkono juhudi za serikali za kupambana na rushwa nchini na kuisaidia kufikia lengo la kuwa na

Tanzania isiyokuwa na rushwa.

Kuacha rushwa

Mwananchi unatakiwa kuichukia rushwa na kuepuka kushiriki vitendo vya rushwa. Rushwa ni kikwazo kikubwa kwa demokrasia, utawala bora, haki za binadamu na ni tishio kwa amani, utulivu na usalama katika jamii. Wewe ndiye unayeathirika zaidi katika kila tendo la rushwa unaloshiriki, hivyo ACHA RUSHWA!

Kutii sheria

Mwananchi, ni lazima uishi kwa kutii sheria, kanuni na taratibu za nchi pamoja na kuunga mkono juhudi za Serikali za kupambana na rushwa. Mwananchi unatakiwa kubadili mawazo na mtazamo kwamba mapambano dhidi ya rushwa ni ya TAKUKURU au vyombo fulani peke yake. Ushirikiano wako na TAKUKURU pamoja na wadau wengine ndio njia pekee itakayosaidia kuleta mafanikio katika kutokomeza rushwa.

Je, wewe ni mzalendo wa kweli wa kusimamia maslahi ya nchi yako?

TIMIZA WAJIBU WAKO, ZUIA NA PAMBANA NA RUSHWA.

Madhara ya rushwa yanamgusa kila mmoja wetu: pambana nayo!

Wasiliana na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa kwa anuani zifuatazo:

Page 7: HITIMISHO S.L.P 1419, Mbeya S.L.P 845, Mororgoro...HITIMISHO Uanzishwaji wa Kamati za Kudhibiti Uadilifu sehemu za kazi ni hatua muhimu katika kujenga, kusimamia na kukuza maadili

JE, KUKATAA KwAKo RUshwA KUnA ThAMAnI?

JE, KUKATAA KwAKo RUshwA KUnA ThAMAnI?

Mkurugenzi Mkuu,Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa,

S.L.P. 4865,Dar es Salaam,

Tanzania.

Simu: 022-2150043-6Nukushi: 022-2150047

Baruapepe: [email protected]

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 6420, Dar es SalaamSimu 022 213 2954

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 6420, Ilala, DSMSimu 022 286 1088

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 90397, Kinondoni, DSMSimu 022 217 0852

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 42325, Temeke, DSMSimu 022 286 3092

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1055, ArushaSimu 027 250 3538, 250 7928

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1138, BukobaSimu 028 222 0848, 222 0491

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 6420, Dar es SalaamSimu 022 213 2954

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1175, DodomaSimu 026 232 2846, 232 2003

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1575, IringaSimu 026 270 1700, 270 0156

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 30261, KibahaSimu 023 240 2658

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 880, KigomaSimu 028 280 2889

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1004, LindiSimu 023 220 2456, 220 2799

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 386, BabatiSimu 027 253 0256, 253 0255

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1419, MbeyaSimu 025 250 3566

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 845, MororgoroSimu 023 261 4302, Fax: 023 260 4478

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1951, MoshiSimu 027 275 0885

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 213, MtwaraSimu 023 233 4013 233 3726

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 377, MusomaSimu 028 262 2024

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 2599, MwanzaSimu 028 250 0600, 250 0602Faxi: 028 250 0600

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 37, ShinyangaSimu 028 276 2630

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 484, SingidaSimu 026 250 2305, 250 2550

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 926, SongeaSimu 025 260 0613, 260 0663

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 273, SumbawangaSimu 025 280 0312 280 2426

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1055, TangaSimu 027 264 5186

Mkuu wa Taasisi - MkoaS.L.P 1020, TaboraSimu 026 260 4030, 260 4311

Sasa ni wakati wako na wangu kutafakari na kutathmini tumefanya nini, tunafanya nini na tutafanya nini ili kuimarisha, kuendeleza na kufanikisha mikakati ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini. Inawezekana kubadilika na kuchukua hatua stahili leo kwa kukataa rushwa kwa faida na maendeleo ya Tanzania. Kukataa kwako rushwa kuna thamani!

Imeandaliwa na Idara ya Elimu kwa Umma ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Makao Makuu.

Wasiliana na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa kwa anwani zifuatazo:

TAAsIsI yA KUZUIA nA KUpAMbAnA nA RUshwA

TAAsIsI yA KUZUIA nA KUpAMbAnA nA RUshwA

Page 8: HITIMISHO S.L.P 1419, Mbeya S.L.P 845, Mororgoro...HITIMISHO Uanzishwaji wa Kamati za Kudhibiti Uadilifu sehemu za kazi ni hatua muhimu katika kujenga, kusimamia na kukuza maadili

mambo yafuatayo:

• Kunajenga jamii isiyokuwa na rushwa. Kila mmoja wetu akiamua kutoshiriki katika vitendo vya rushwa, jamii yetu haitakuwa na rushwa.

• Kunaimarisha mifumo na kuboresha utoaji wa huduma za kijamii kama vile huduma za afya na elimu na hivyo kuhakikisha tunapata huduma bora.

• Kunajenga mazingira ya utawala wa sheria. Jamii huwa na imani na vyombo vya umma vinavyofanya kazi kwa usawa na uaminifu na kulinda haki za binadamu.

• Kunapunguza athari za vitendo vya jinai: Vitendo kama vile uhalifu uliopangwa, biashara ya dawa za kulevya, biashara za magendo, biashara ya kusafirisha na kuuza binadamu na ugaidi vinapungua au kwisha kabisa.

• Kunavutia uwekezaji wa ndani na wa nje ya nchi. Wawekezaji huvutiwa kuwekeza katika nchi pale wanapoona kuwa mitaji yao haitaathiriwa na wala rushwa.

• Kunawezesha maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Miradi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi itafanikiwa iwapo ushuru bandia wa rushwa hautakuwepo. Aidha, wananchi watakuwa kiuchumi kutokana na uchumi na pato la taifa kukua.

• Kunakuza demokrasia. Serikali za nchi zinazopambana na rushwa huonekana kuwa halali zaidi machoni mwa wananchi wake na hivyo kujenga utulivu na imani ya wananchi.

• Kuongeza pato la taifa. Makusanyo ya fedha zinazolipwa kwa njia ya kodi huongezeka na hivyo kuboresha hali ya wananchi.

Je, kukataa kwako rushwa kuna thamani?

‘Rushwa’ siyo neno geni katika masikio yako, yangu au ya jirani yetu. Ni neno tunalosikia au tunalolitaja mara kwa mara na linalodhihirika kupitia mwenendo wako, wangu au wa jirani yetu na hatiamye kuchukuliwa kuwa ni desturi katika jamii yetu.

Jambo la kujiuliza , je, iwapo rushwa imekuwa desturi inayokubalika kwa nini kitendo cha rushwa kinafanyika kwa siri? Pia, tujiulize, iwapo rushwa ni desturi inayokubalika, kwa nini Tanzania na pia mataifa mbalimbali yanaendelea kujiwekea mikakati ya kuzuia na kupambana nayo? Je, mikakati hii ina faida gani?

Rushwa, kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu, toleo la pili la 2004, ni fedha au kitu cha thamani kinachotolewa na kupewa mtu mwenye madaraka ya jambo fulani ili mtoaji apatiwe upendeleo. Aidha, rushwa ni matumizi mabaya ya ofisi au mamlaka kwa manufaa binafsi. Mara nyingi rushwa hutolewa kwa siri kwa sababu ni tendo la fedheha na ni kosa la jinai.

Tafiti zinaonyesha kuwa rushwa imedaiwa na kutolewa katika upatikanaji wa leseni, zabuni, haki za kisheria na katika upatikanaji wa huduma za jamii. Aidha , fedha zinazotengwa kuboresha huduma za kijamii na kiuchumi kama vile dawa bora, makazi bora na miundo mbinu zimefujwa kwa maslahi ya watu wachache.

Matokeo ya vitendo hivi vya rushwa ni kuathirika kwa upatikanaji wa huduma hizo ambazo ni haki ya wananchi ambapo huduma huwa duni au kutopatikana kabisa. Aidha,

miradi ya maendeleo inakuwa na viwango duni kutokana na vitendo vya rushwa. Jambo lililo dhahiri kufuatia kushamiri kwa vitendo vya rushwa ni kwamba vitendo hivyo huwaathiri zaidi wananchi wa kipato cha chini.

Ni nini thamani ya kitendo chako, changu au cha jirani yetu kukataa rushwa? Tuanze kwa kuzungumzia ni kwa namna gani mtu anaweza kukataa rushwa.

Vitendo vya rushwa hufanyika kwa kuhusiaha zaidi ya mtu mmoja. Kuna mtoaji na mpokeaji na ama shuhuda au mshiriki mwenza wa vitendo hivi. Hii ina maana, kila mmoja wetu, wewe na mimi, anaweza kukataa kushiriki vitendo vya rushwa kwa kufanya yafuatayo:

• Kukataa kutoa au kukataa kupokea rushwa.

• Kukemea mtu au watu wanaojihusisha na rushwa kwa kutoa au kupokea.

• Kutoa taarifa za mtu au watu wanaojihusisha au wanaotaka kujihusisha na rushwa.

• Kushiriki katika kuzuia na kupambana na rushwa kwa kushawishi wengine kutojihusisha na rushwa, kukemea au kutoa taarifa za vitendo vya rushwa.

• Kushiriki katika kupambana na rushwa kwa kutoa ushahidi mahakamani.

• Kuelimisha watu wengine jinsi ya kukataa rushwa.

• Kuelimisha watu wengine faida za kuwa na jamii isiyokuwa na rushwa.

• Kujenga na kuimarisha maadili katika jamii yetu.

• Kuheshimu na kutii sheria.

Je, kitendo cha wewe au mimi kukataa rushwa kina thamani? Ndiyo! Thamani ya kukataa kwako au kukataa kwangu kushiriki vitendo vya rushwa kunaweza kuonekana kwenye