Home - TryEngineering.org Powered by IEEE · Web viewDK Eyewitness Series: Electricity (ISBN:...
13
Insulators and Conductors Provided by TryEngineering - www.tryengineering.org SOMO LA 73 : INSULETA NA KONDAKTA Kusudio la Somo Onyesha dhana ya upitishaji na uzuiaji wa kupitishwa kwa umeme. Zingatia: Andalio hili la somo ni kwa ajili ya matumizi ya darasani tu, chini ya usimamizi wa mwalimu mwenye ujuzi juu ya masuala ya umeme. Muhtasari wa Somo Ufanyaji kazi wa Insuleta na kondakta unawapa hamasa wanafunzi kujaribu vifaa mbalimbali vilivyoko darasani na kubaini kuwa vifaa hivyo ni kondakta ama insuleta. Wanafunzi wafanye katika makundi kujaribu makisio yao juu ya kila kifaa, kisha vikundi vilinganishe na kujadili matokeo yao. Ngazi za Umri Kidato cha 1 – 4 Malengo Kujifunza kuhusu tabia za kiumeme za vifaa mbalimbali. Kujifunza namna ambavyo insuleta na kondakta zinavyoonesha muitikio dhidi ya mkondo wa umeme. Kutatua miundo ya kialjebra inayohusisha kipeo na kipeuo cha pili. Kujifunza kufanya madhanio na kuunda hitimisho. Kujifunza kuhusu ushirikiano na kufanya kazi katika vikundi. Matokeo Yanayotarajiwa kwa Mwanafunzi Kutokana na kazi hii, wanafunzi watatakiwa kujenga uelewa katika: Tabia za kiumeme Kondakta na insuleta Sakiti na mkondo wa umeme Kuunda na kuyajaribu madhanio Ufanyaji kazi kwa kushirikiana Shughuli za Somo P a g e 1 | 13
Home - TryEngineering.org Powered by IEEE · Web viewDK Eyewitness Series: Electricity (ISBN: 0751361321) Make Cool Gadgets for Your Room by Amy Pinchuk and Teco Rodriques (ISBN:
Kusudio la Somo
Onyesha dhana ya upitishaji na uzuiaji wa kupitishwa kwa umeme.
Zingatia: Andalio hili la somo ni kwa ajili ya matumizi ya darasani
tu, chini ya usimamizi wa mwalimu mwenye ujuzi juu ya masuala ya
umeme.
Muhtasari wa Somo
Ufanyaji kazi wa Insuleta na kondakta unawapa hamasa wanafunzi
kujaribu vifaa mbalimbali vilivyoko darasani na kubaini kuwa vifaa
hivyo ni kondakta ama insuleta. Wanafunzi wafanye katika makundi
kujaribu makisio yao juu ya kila kifaa, kisha vikundi vilinganishe
na kujadili matokeo yao.
Ngazi za Umri
· Kujifunza namna ambavyo insuleta na kondakta zinavyoonesha
muitikio dhidi ya mkondo wa umeme.
· Kutatua miundo ya kialjebra inayohusisha kipeo na kipeuo cha
pili.
· Kujifunza kufanya madhanio na kuunda hitimisho.
· Kujifunza kuhusu ushirikiano na kufanya kazi katika
vikundi.
Matokeo Yanayotarajiwa kwa Mwanafunzi
· Tabia za kiumeme
· Kondakta na insuleta
· Kuunda na kuyajaribu madhanio
· Ufanyaji kazi kwa kushirikiana
Shughuli za Somo
Wanafunzi wajaribu katika sakiti aina mbalimbali za vifaa kwa lengo
la kubaini kama vifaa hivyo ni insuleta au kondakta. Wanafunzi
wafanye madhanio juu ya kila kifaa na kujadili matokeo katika
vikundi vyao na kisha na darasa zima. Pia, vikundi vya wanafunzi
pia viunde sakiti zao za kujaribia vifaa hivyo kwa kutumia nyaya,
betri, na balbu.
Uhusiano wa Somo na Mtaala
Tazana ukurasa wa Uhusiano wa kimtaala mwishoni mwa somo
hili.
Mahitaji ya vifaa
· Muongozo wa Mwanafunzi (Umeambatanishwa)
Uhusiano wa Somo na Mtaala
Tazama ukurasa wa "Uhusiano wa Somo na Mtaala" ulioambataniswa
mwishoni.
Viunganishi vya Mtandaoni
Taarifa kuhusu vipimo na makosa katika vipimo.
· ITEA Standards for Technological Literacy: Content for the Study
of Technology
· NCTM Principles and Standards for School Mathematics (
http://standards.nctm.org )
Vyanzo vya Maarifa Vilivyopendekezwa(rejea)
· DK Eyewitness Series: Electricity (ISBN: 0751361321)
· Make Cool Gadgets for Your Room by Amy Pinchuk and Teco Rodriques
(ISBN: 1894379128)
· My World of Science: Conductors and Insulators kilichoandikwa na
Angela Royston
(Heinemann Educational Books, ISBN: 0431137269)
Kazi ya Kuandika ya Hiyari
Andika insha(au aya kwa kutegemea umri wa mwanafunzi) kuelezea zao
ambalo halitofanya kazi vizuri pale vifaa tofautitofauti
vitakapotumika katika utengenezaji wa sakiti. Kwa mfano, balbu ya
umeme iliyotengenezwa kwa filamenti ya plastiki haitofanya
kazi.
Kwa ajili ya Mwalimu: Vyanzo vya Mwalimu;
Vifaa
· Mwongozo wa mahitaji ya mwanafunzi na karatasi ya kufanyia kazi
ya mwanafunzi.
· Vipande vitatu(3) vya waya(zikwanguliwe nchani)
· Betri (saizi D)
· pini za kubania karatasi
· Vifaa mbalimbali ambavyo ni kondakta au insuleta; vinavyotosha
kwa kila kikundi kuchagua vitu kumi kutoka kwenye mkusanyiko wenye
angalau vitu 40 (mapendekezo: kibanio cha karatasi cha metali,
karatasi, ufutio, sineri ya alminiamu, peni ya metali, mpira wa
kufungia, penseli, sarafu, kibanio cha nywele, ufunguo)
Hatua
1. Unda muundo wa sakiti ya umeme darasani kwa kutumia nyaya, balbu
na betri. Onyesha tabia ya upitishaji wa umeme na uzuiaji wa umeme
kwa kujaribu aina mbalimbali za vifaa.
2. Mpe kila mwanafunzi nakala za rejea (Zingatio: rejea hizi pia
zinaweza kutolewa kama kazi ya kujisomea kwa usiku mmoja kabla ya
siku ya kazi yenyewe darasani.)
3. Onyesha muundo mmoja ukiwa na insuleta na kisha ukiwa na
kondakta kuonesha namna vizuiavyo na kupitisha umeme.
4. Wagawanye wanafunzi katika vikundi vya watu watatu mpaka
wanne.
5. Sambaza vifaa vinavyohitajika katika kila kikundi kama vile;
nyaya, balbu na betri na uwaagize wanafunzi kuunda mfumo wao wa
kujaribu upitishaji wa umeme katika vitu mbalimbali.
6. Waambie wanafunzi wachague vitu vitano kati ya vitu walivyoleewa
ambavyo wanaamini vitapitisha umeme(tazama orodha ya vifaa).
Vikundi piaGroups will also select five materials they believe will
not conduct electricity. Selected items will be listed on the
Student Worksheet.
7. Vikundi vya wanafunzi vitakabidhi madhanio yao kwa vikundi
vingine kwa ajili ya kuyajaribu na kuyahakiki - hivyo kila kikundi
kitayajaribu makisio ya kikundi kingine.
8. Matokeo yarekodiwe katika ukurasa wa kufanyia kazi wa mwanafunzi
na washirikishane kwenye kikundi.
Muda Unaohitajika
Mawazo ya Nyongeza
Wanafunzi wakusanye vifaa mbalimbali toka nyumbani kwa ajili ya
kujaribiwa ili kujua vifaa hivyo ni insuleta au kondakta.
Zana za Mwalimu: Kondakta na Insuleta ni nini?
Kondakta/Upitishaji wa Umeme
Upitishaji wa Umeme ni uwezo wa kondakta kuruhusu au kupitisha
joto, umeme au sauti. Kondakta ni aina ya vifaa/vitu ambavyo umeme
unaweza kupita kwa urahisi, ambavyo havizuii upitaji wa umeme.
Mfano wa vitu hivyo ni: kopa, Alminiamu, stili, silva, dhahabu, na
electrolaiti. Ubora wa upitishwaji wa umeme haulingani kwa
vifaa/vitu vyote.
Insuleta
Insuleta ni vifaa/vitu ambavyo huzuia upitaji wa umeme, hivyo umeme
haupiti kwa urahisi. Mfano wa vitu hivyo ni plastiki, mbao, ufutio,
nguo, hewa, kioo. Baadhi ya vitu ni vizuizi vizuri vya umeme kuliko
vingine.
Changamoto
Msumari
Insuleta
Kondakta
Insuleta
Kondakta
Kijiko
Insuleta
Sarafu
Kondakta
Insuleta
Kondakta
Chaki
Insuleta
Kondakta
Sakiti Rahisi
Sakiti rahisi huundwa na vitu visivyopungua vitatu ambavyo ndivyo
vinavyohitajika kukamilisha sakiti ya umeme inayofanya kazi: chanzo
cha umeme (betri), njia au kipitisha umeme (waya) na kifaa cha
ukinzani (taa) ambacho ni kifaa chochote kinachohitaji umeme ili
kufanya kazi. Mchoro uliopo hapa chini unaonesha sakiti rahisi
iliyoundwa na betri moja, nyaya mbili na balbu. Uelekeo wa
mtiririko wa umeme ni kutoka ncha chanya kuelekea kwenye ncha
hasi.
Sakiti mfuatano
Mchoro Elekezi wa Sakiti Rahisi
Ufuatao ni mchoro elekezi wa sakiti rahisi ukionyesha alama za
kielektroniki zinazowakilisha betri, swichi na balbu.
Mchoro wa Sakiti Rahisi
Swichi
Ukurasa wa Kufanyia Kazi wa Mwanafunzi: Kazi ya Insuleta na
Kondakta
Hatua
Kiundi chako kitapewa nyaya, balbu na betri. Pangilia sakito ya
kujaribia upitishani wa umeme kama ionekanavyo hapa chini.
Kisha kikundi kitakapokubaliana juu ya vitu vitano ambavyo
wanakikundi wanadhan vitapitisha umeme (kondakta), na vitano
visivyopitisha (insuleta). Orodhesha vitu hivyo katika ukurasa wa
kufanyia kazi wa mwanafunzi. Badilishaneni orodha yenu na kikundi
kingine na kisha kila kikundi kitayajaribu majibu ya wenzao.
Jaribuni kila kifaa kisha mrudishe majibu ya matokeo kwa kikundi
mlichojaribu madhanio yao. Jadilini matokeo hayo katika vikundi.
Je, nini kiliwashangaza?
Mpangilio wa Jaribio la Kondakta
Unganisha hapa kifaa cha kujaribu ili kuona kama kinapitisha
umeme.
Unaweza kuunda mfumo wa kujaribia kondakta yabisi kwa kutumia
betri, nyaya tatu, na balbu kama ionekanavyo hapo juu. Kama kifaa
kinachopitisha umeme kitawekwa kati ya vibanio vya karatasi viwili
vya metali, balbu itawaka. Kama kisichopitosha umeme kitawekwa kati
ya vibanio vya karatasi viwili vya metali, balbu haitawaka. Kwa
kuunganisha kondakta yabisi katika sakiti na kisha ukaiondoa, basi
hapo utakua umeunda swichi rahisi.
Ukurasa wa Kufanyia Kazi wa Mwanafunzi:
Madhanio ya Kikundi cha Kwanza cha Wanafunzi:
Vitu ambavyo Kikundi cha Kwanza cha Wanafunzi Kinadhani kuwa ni
Kondakta
Vitu ambavyo Kikundi cha Kwanza cha Wanafunzi Kinadhani kuwa ni
Insuleta
1.
1.
2.
2.
3.
3.
4.
4.
5.
5.
Jaribu vitu vilivyochaguliwa na kikundi cha kwanza, kisha
viorodheshe katika chumba stahiki cha jedwari.
Kondakta
Insuleta
Maswali:
1. Asilimia ngapi ya madhanio ya kikundi cha kwanza yalikua
sahihi?
2. Kwanini wahandisi na wajenzi wanatakiwa kuwa na uelewa mzuri juu
ya kondakta na insuleta?
Kwa Walimu: Uhusiano wa Somo na Mtaala
Andalio hili la somo limepangiliwa kwa kuzingatia mtaala mpya
unaojikita kwenye uwezo, wa elimu ya sekondari ngazi ya chini
nchini Uganda, ambao umezalishwa na Kituo cha Kitaifa cha Maendeleo
ya Mtaala "National Curriculum Development Centre" (NCDC)
Shabaha ya Mtaala mpya unaojikita kwenye uwezo ni kujenga uelewa
kupitia majaribio, uchunguzi wa kisayansi, na kufikiri
kimantiki.
Wanafunzi wanatakiwa:
· Kuwa na muingiliano na hali halisi ndani na nje ya darasa.
· Kutazama picha au michoro, kudadisi takwimu au kusoma maandishi
kutonga kwenye vyanzo mbalimbali.
· Wao wenyewe kugundua maarifa na fikra.
Kisha wanatarajiwa kueleza haya kwa maneno yao wenyewe, si kwa
kutumia maneno ya mwalimu na kisha waoneshe kuwa wameelewa vyema
walichojifunza.
Andalio hili la somo pia limefungamanishwa na stadi za kawaida
zinazotarajiwa kupatwa na mwanafunzi aliyefunzwa chini ya mtaala wa
sekondari ngazi ya chini nchini Uganda unaojikita katika
ujuzi.
Stadi hizi za kawaida ni pamoja na:
1. Kufikiri kwa umakini na kutatua changamoto
· kupanga na kufanya uchunguzi.
· Kanga na uchanganue habari.
· Kubashiri matokeo na kufanya maamuzi bada ya kufikiri kwa
makini.
· Kufanya tathmini na masuluhisho tofauti.
2. Ubunifu na uvumbuzi
· Kutumia fikira kuchunguza uwezekano.
· Kupendekeza na kuanzisha mbinu mpya kutatua tatizo.
· Kujaribu njia mbadala za ubunifu.
· Kuangalia mifumo.
· Kuongea kwa ujasiri na kueleza mambo kwa ufasaha.
· Kusoma kwa usahihi na kwa ufasaha.
· Kuandika na uwasilisha kwa usahihi.
· Kutumia media anuwai kuwasiliana maoni.
· Kuwasiliana vizuri na wengine.
· Kufanya kazi kwa uhuru na uvumilivu.
· Kusimamia malengo na wakati.
· Kutumia hisabati kuhalalisha na kuunga mkono maamuzi.
· Kutumia teknolojia kuunda, kusimamia na kuchakata habari.
· Kutumia teknolojia ya kushirikiana, kuwasiliana na kusafisha kazi
zao.
Page 11 | 11