HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

  • Upload
    imma

  • View
    538

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    1/38

    HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA

    UPINZANI BUNGENI KATIKA WIZARA YA ELIMU, SAYANSI,

    TEKNOLOJIA NA UFUNDI MHESHIMIWA SUSAN ANSELIM

     JEROME LYIMO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAONI YA

    KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSU

    MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KATIKA

    WIZARA HIYO KWA MWAKA WA FEDHA 2016/1!

    1! UTANGULIZIM"#$"%&%' S%*, awali ya yote napenda kuchukua fursa

    hii, kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutujalia soteuhai na kutuwezesha kuliona Bunge la 11 tukiwa salama. Pili

    napenda kumshukuru kwa dhati kabisa Kiongozi wa Kambi

    asmi ya !pinzani Bungeni, Mheshimiwa "reeman #ikaeli

    Mbowe $Mb% kwa imani kubwa aliyo nayo kwangu kwa

    kuendelea kuniteua kuwa Msemaji Mkuu wa Kambi asmi ya

    !pinzani Bungeni katika &izara ya 'limu, (ayansi, )eknolojiana !fundi kwa *ipindi *itatu mfululizo. +inaahidi kuendelea

    kuchapa kazi kwa bidii, na kwa hakika sitaiangusha Kambi

    asmi ya !pinzani Bungeni katika wajibu huu niliopewa wa

    kuisimamia (erikali katika sekta ya 'limu nchini.

    M"#$"%&%' S%*, naishukuru familia yangu ikiongozwa na

    mume wangu Boni*enture +gowi na wanangu wote. Kipekee

    namshukuru sana +aibu &aziri wangu r. (uleiman #lly -ussuf 

    kwa ushauri wake. ile*ile nawashukuru sana B#/0# Mkoa

    wa kichama wa Kinondoni kwa kunichagua kuwawakilisha hapa

    kama kawaida sitawaangusha.

      M"#$"%&%' S%*, kwa namna ya pekee napenda

    kuwapongeza *iongozi wote wakuu wa *yama *ina*younda

    1

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    2/38

    !moja wa Katiba ya &ananchi $!K#%, kwa kazi kubwa na

    nzuri walioyoifanya ya kuwaongoza watanzania kuchagua

    mabadiliko katika !chaguzi Mkuu wa tarehe 2 3ktoba 412.

    M"#$"%&%' S%*, pamoja na ukiukwaji mkubwa wa haki na

    demokrasia uliofanywa na *yombo *ya dola dhidi ya upinzani

    katika uchaguzi huo, ikiwemo ku*amia, kuwakamata na

    kuwanyang5anya *ifaa *ya kazi wataalamu wa !K#

    waliokuwa wakijumlisha matokeo ya uchaguzi huo, bado

    wananchi walionyesha imani kubwa sana kwa upinzani kwa

    kuupigia kura nyingi6 na kwa mara ya kwanza katika historia ya

    *yama *ingi hapa nchini, upinzani umepata *iti 117 ikiwa ni

    ongezeko la asilimia 8.8 kutoka *iti 9: *ili*yopatikana katika

    uchaguzi Mkuu wa 414.

    M"#$"%&%' S%*, kwa upande wa kura za rais, licha ya

    mbinu zote zilizofanywa na *yombo *ya dola kuchakachuaushindi wa upinzani, bado upinzani kupitia !K# umeongeza

    kiwango chake cha ushindi hadi ku;kia asilimia takriban imla wa

    muda mrefu. 

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    3/38

    M"#$"%&%' S%*,  kuporomoka huku ni matokeo ya wazi

    kabisa kuwa chama hiki kimepoteza m*uto kwa wananchi

    kutokana na kushindwa kuondoa umasikini pamoja na

    kushindwa kusambaza huduma toshelezi za kijamii hasa elimu

    na afya kwa miaka yote ya utawala wake wa miaka 22 sasa.

    M"#$"%&%' S%*,  kutokana na aibu hii ya kushindwa

    kuondoa umasikini kwa wananchi6 na kutokana na hofu ya

    (erikali kuhojiwa na bunge kuhusu utendaji wake6 sasa (erikali

    hii ya awamu ya tano inayojinasibu kwa kauli mbiu ya ‘hapa

    kazi tu’  imeamua kulinyamazisha bunge kwa kupiga marufuku

    *yombo *ya habari kurusha moja kwa moja mijadala

    inayoendelea bungeni kuhusu utendaji wa (erikali na kuhusu

    mgawanyo wa fedha za umma katika bajeti ya serikali. #idha,

    kutokana na hofu ya kukosolewa kutokana na kutojiamini katika

    mambo inayoyafanya6 (erikali sasa imeanza kuingilia hotuba za

    &asemaji &akuu wa !pinzani na kuzifanyia censorhip kinyume

    kabisa na Kanuni za Bunge hili. 

    M"#$"%&%' S%*,  Kanunu ya ::$:% ya Kanuni za Bunge

    toleo la ?anuari, 417, inasema kwamba@  “Baada ya Waziri

    kuwasilisha hotuba ya bajeti kwa mujibu wa fasili ya kwanza;

    Mwenyekiti wa Kamati iliyopitia makadirio husika na Msemaji

    wa Kambi ya pinzani watatoa maoni yao kwa muda usiozidi

    dakika !" kila mmoja#$Kanuni haijaelekeza kwamba watatoa

    maoni yao baada ya kupitiwa na Kamati ya Kanuni. Kwa hiyo

    Mheshimiwa (pika6 kitendo kilichofanyika tarehe 17 Mei, 417

    cha kuiondoa mezani hotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi asmi

    ya !pinzani Bungeni katika &izara ya Mambo ya +dani ya +chi

    ili ikachakachuliwe na Kamati ya Kanuni, ni kinyume kabisa na

    8

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    4/38

    Kanuni za Bunge6 na ni kinyume kabisa na mila na desturi za

    uendeshaji wa mabunge ya ?umuiya ya Madola.

    M"#$"%&%' S%*,  Kambi asmi ya !pinzani Bungeni

    inakemea kwa ngu*u zote na inaitaka (erikali kuacha mara

    moja tabia hii ya kuingilia shughuli za kikanuni za Kambi asmi

    ya !pinzani Bungeni kwa kutumia mgongo wa Bunge!

    2! ELIMU YETU NA HATMA YA TANZANIA

    M"#$"%&%' S%*, dhambi kubwa na mbaya kuliko

    zote kuwahi kufanywa na (erikali hii ya //M ni kuwanyima&atanzania elimu bora6 kupandikiza elimu nyepesi, potofu na

    tegemezi kwa *izazi *ingi *ya taifa hili6 dhambi ya

    kuwachanganya na kuwa*uruga watoto wa )aifa hili kwa sera

    dhaifu, mitaala isiyo na dira na *itabu *isi*yokuwa na tija kwa

    maendeleo yao na ya )aifa lao.

    M"#$"%&%' S%*, +chi yetu ipo hi*i ili*yo kwa sababu ya

    elimu duni. !maskini, ujinga na maradhi *ina*yotesa )aifa hili

     ni matokeo ya elimu mbo*u iliyotolewa na (erikali ya //M kwa

    zaidi ya miaka 22 tangu tupate uhuru. )aifa linalotoa elimu bora

    halifanani hata kidogo na jinsi )anzania yetu ili*yo.

    M"#$"%&%' S%*, hizi ni zama za kuelezana ukweli, hata

    mkitufungia humu Bungeni wananchi wasituone Ai*e5 bado

    !kweli utaendelea kupasua kuta za Bunge hili na kuwa;kia

    &atanzania. Mwanafasihi mashuhuri wa nchi yetu, #frika ya

    Mashariki na Barani #frika, 0ayati (haaban obert,

    katika kitabu chake cha K!(#CKCK# aliandika hi*i, “Msema

    kweli hukimbiwa na Rafki zake, nikipatwa na Ajali kama

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    5/38

    hiyo sitawaonea Wivu wale wanaodumu na marafki zao

    siku zote. Siwezi kuikana weli kwa kuhofa !pweke wa

    kitambo na kujinyima "uraha ya milele inayokaribia

    kutokea baada ya kushindwa kwa !on#o$ mwisho wa

    kunukuu. Maneno haya ndio msimamo wangu na wa Kambi kwa

    ujumla wake, kwani siku zote wabunge wa !pinzani

    tumeonekana kama maadui na kunyanyapaliwa na (erikali hii

    ya //M kwa sababu kusema ukweli kuhusu madhaifu ya

    (erikali.

    M"#$"%&%' S%*, nchi zilizoendelea zinafanya mambo

    mengi ya kimaendeleo kwa kuwatumia wataalam wao wa elimu

    ya juu D !ni*ersity graduates. &ataalam wa *yuo *ikuu

    wanatengenezwa kwa kutegemea pia elimu bora ya msingi na

    sekondari. )anzania nayo ina *yuo *ikuu. akini leo ipo haja ya

    Bunge hili kujiuliza nini hasa maana ya /huo kikuu D E A

    !niversity is an institution o% hi#her learnin# where

     people&s minds are trained %or 'lear thinkin#, %or 

    independent thinkin#, %or analysis and %or problem

    solvin# at the hi#hest level, is the 'entre %or advan'in#

    the %rontiers o% knowled#e(. Kwamba@ /huo Kikuu ni taasisi

    ya elimu ya juu inayoandaa watu kuwa na ;kra pe*u, ;kra huru

    kwaajili ya kuwa na uwezo mkubwa wa kiuchambuzi na kwaajili

    ya kutatua matatizo kwa kiwango cha hali ya juu, ni kituo cha

    kuendeleza maarifa.

    M"#$"%&%' S%*, (erikali imekuwa na Mawaziri wengi tu

    waliopita *yuo *ikuu, lakini bado wameliingiza )aifa hili kwenye

    2

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    6/38

    hasara kubwa kwa maamuzi mabo*u, kwa kuingia mikataba

    isiyojali maslahi ya taifa na kwa utendaji usio na ufanisi. 0i*i

    hawa wana>;t kweli kwenye de;nition hii ya /huo

    KikuuF !kweli ni kuwa hata (erikali yenyewe haiwaamini

    wataalam wake wanaozalishwa na *yuo *ikuu hasa kwenye

    (ekta ya (ayansi na )eknolojia. +a hili lipo wazi6 leo )anzania

    ina madini, gesi na mafuta, lakini wata;ti, wachimbaji na

    wa*unaji wakubwa wa raslimali hizi, wenye mashine kubwa na

    za kisasa, na zenye kutumia teknolojia ya hali ya juu si

    &atanzania.

    M"#$"%&%' S%*, Mwanafalsafa 0erbet (pencer aliwahi

    kusema, namnukuu “)he #reat aim o% edu'ation is not 

    knowled#e but a'tion$ D kwamba Elengo kuu la elimu si

    ufahamu, bali *itendoG.  )a;ti zinaonyesha ni 8:H tu ya

    wahitimu wa *yuo *ikuu wanaajirika kutokana na kile

    kinachoitwa kukosa ujuzi Elack of skillsG. Kambi ya !pinzani

    inauliza hi*i ni lini serikali itawekeza *izuri kwenye elimu katika

    ngazi zoteFII

    +! BAJETI YA UTEKELEZAJI WA ELIMU BURE

    M"#$"%&%' S%*, kupitia (era Mpya ya 'limu na Mafunzoya Mwaka 41

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    7/38

    ushirikiano baina ya serikali pamoja na wazazi. 0ata hi*yo

    upatikanaji wa pesa shuleni ulikuwa wa shida. Mathalani serikali

    iliweza kupeleka wastani wa )sh.

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    8/38

    (hilingi bilioni 1,

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    9/38

    inaweza kuwa chanzo kingine cha anguko kuu la ubora wa

    elimu nchini.

     *edwali + -harama za kufdia ada na ruzuku

    shuleni kwa ajili ya vi%aa, #harama za mitihani na

    #harama za uendeshaji 

    K%$%

    (T$"$)

    I% 7

    '89:%

     J9&-

    Msingi 14,444 9,:9=,481 Bil. :4(ekondari 2,444 1,2=2,2< Bil.

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    10/38

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    11/38

    ualimu ndio kada pekee inayofanya kazi kwa saa

    < hasa nyakati za kutunga na kusahihisha

    mitihani, kupanga matokeo n.k.

    %%! Kujenga *yumba *ya madarasa *ya kutosha naku*iwekea samani za kutosha ili kupunguza

    mlundikano wa wanafunzi darasani na hi*yo

    kuboresha mazingira ya kufundisha na kujifunza.%%%! Kuwapandisha madaraja kwa wakati sambamba

    na kuwapandishia mishahara walimu waliokidhi

    *igezo *ya kupandishwa madaraja ili kuwapa

    motisha wa kufundisha.%C! Kuwe na chombo kimoja cha ajira kwa walimu,

    na kwa maana hiyo6 )ume ya &alimu ianze

    mara moja kazi ya kutatua kero za walimu.C! Muda wa mafunzo kwa *itendo $B)P% kwa

    walimu uzingatiwe ili walimu%wanafunzi waweze

    kupata uzoefu wa kutosha wa kufundisha kulikoina*yofanyika hi*i sasa ambapo mafunzo hayo

    yanafanyika chini ya wiki nane kila mwaka.

    C%! (erikali ishughulikie kero ya &alimu

    wanaostaafu na kutolipwa stahiki zao mapema

    na pia kutorudishwa makwao kwa mujibu wa

    kanuni za utumishi.C%%! (erikali iwalipe walimu posho ya mazingira

    magumu ya kazi ili ku*utia kufanya kazi

    maeneo ya *ijijini.C%%%! #jira mpya ziingizwe kwenye payroll mapema ili

    kuondoa kero ya kucheleweshwa kwa maslahi

    ya walimu kutokana na majina yao kutokuwepo

    kwenye pa73.--!

    11

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    12/38

    ! SERA YA ?ITABU

     M"#$"%&%' S%*,

    Mwaka 1::1 (erikali ya )anzania ilitangaza sera mpya ya

    *itabu iliyoruhusu wachapishaji binafsi $pri*ate publishers%

    kuchapisha *itabu *ya shule na *yuo nchini. !amuzi huo

    ulifanyika baada ya miaka mingi ya ukosefu wa *itabu

    kutokana na kutai;shwa kwa makampuni ya uchapishaji na

    kuanzishwa kwa mashirika ya uma ya uchapishaji $km )P0,

    '#'P% ambayo yalilenga kuchapisha *itabu amba*yo

    *ingeandikwa na )aasisi ya 'limu.

    Mheshimiwa (pika, !amuzi huo wa kuondokana na dhiki na

    mahangaiko ya kukosekana kwa *itabu *ya shule uliwekewa

    utaratibu maalumu wa utekelezaji ukiratibiwa na kitengo cha

    Book Management !nit $BM!%, makao makuu ya &izara ya

    'limu. Baadae &izara ya 'limu iliunda kitengo cha

    kudhibiti ubora wa *itabu kiitwacho, 'ducational Materials

    #ppro*al /ommittee $'M#/%.

    M"#$"%&%' S%*,  )angu 1::1 wachapishaji wazalendo

    wamepiga hatua kubwa katika fani hii. &anachapisha *itabu

    bora *ya kiada *ya ngazi zote za elimu. )atizo la

    kutokuwapo kwa *itabu *ya kiada halipo tena. )atizo sasa ni

    kwamba serikali hainunui *itabu *ya kutosha na kwa muda.

    Pia wachapishaji wanachapisha *itabu *ya hadithi

    mbalimbali kwa ajili ya watoto wa ngazi zote za msingi na

    sekondari D hususan chini ya /BP kwa mfano kuna aina za

    *itabu $titles% zisizopungua 824 za *itabu *ya hadithi na

    1

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    13/38

    rejea pale /BP. Pia wachapishaji hao wametoa machapisho

    mengine kama kamusi, atlasi, chati mbalimbali, n.k.

    S#3 &7 7 C%9 7 &'* 201=

    Mheshimiwa (pika, (era mpya iliyotangazwa na Kamishna

    wa 'limu kupitia &araka wa 'limu +amba < wa mwaka 41<

    inafuta sera ya (erikali ya *itabu ya mwaka 1::1 na

    kurejesha majukumu ya uandishi na uchapishaji wa *itabu

    *ya shule mikononi mwa )aasisi ya 'limu. (era hiyo inadai

    kuwa wachapishaji binafsi wanaweza kuchapisha *itabu *yaziada D amba*yo ana*iita Areference books5.

    M"#$"%&%' S%*, Mwaka jana $412% )aasisi ya 'limu

    iliendesha semina kwa walimu wakuu wa shule za msingi

    nchini kote kuhusu ufundishaji unaotekeleza mitaala mipya

    hususan darasa la kwanza na la pili kwa utaratibu wa

    Kusoma, Kuandika na Kuhesabu $KKK%. &alimu waliopewa

    semina waliahidiwa kupatiwa *itabu *ipya *ina*yokidhi

    mitaala mipya mwezi ?anuari au "ebruari 417 ili waanze

    ku*itumia madarasani. (hule zimesubiri *itabu hi*yo hadi

    sasa, karibu nusu ya mwaka, bila kupatiwa *itabu hi*yo.

    M"#$"%&%' S%*,Cnasemekana *itabu hi*yo *ipya *ya

     )aasisi ya 'limu ha*ifai. Pia tumesikia kuwa baadhi ya

    wafanyakazi waliohusika katika usimamizi wa kazi hiyo

    wamesimamishwa kazi. akini hadi sasa watoto wako

    madarasani wakisubiri *itabu *ipya *ya )aasisi ya 'limu.

    18

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    14/38

    Mheshimiwa (pika, Mwandishi  ni msanii kama ali*yo

    mchoraji, mwimbaji, mchezaji wa ngoma au mwigizaji. Kundi

    hili lina watu wenye *ipaji maalumu. !andishi siyo kazi

    anayoamriwa au kupangiwa mtu kuifanya ila naifanya kwa

    utashi wake. Pia haitegemei elimu ya mtu, kwa mfano,

    (haaban obert alikuwa na elimu ya darasa la C tu lakini

    aliandika *itabu *ili*yo bora sana amba*yo *inatumika hadi

    *yuo *ikuu.

    M"#$"%&%' S%*,  )aasisi ya 'limu ina mwelekeo wa ukuzaji

    mitaala na siyo kuandika na kuchapisha *itabu. Clichukua muda

    mrefu hadi &izara ya 'limu ya miaka ya 1::4 kutambua hi*yo. +i

    heri &izara ya 'limu ikabidhi jukumu la uandishi na usambazaji

    wa *itabu kwa wachapishaji binafsi.

    M"#$"%&%' S%*, K9.* *"% "%% 7 C%9

    *9*.$#* &$"9-#%, Kambi rasmi ya !pinzani

    inapendekeza yafuatayo@

    $a% (erikali irejeshe (era ya itabu ya 1::1 ambayo ina

    mafanikio makubwa

    $b%(erikali iweke pembeni mitaala mipya ya )C' ya 417na badala yake iunde )ume ya 'limu itakayotathmini Mfumo

    na !tendaji wa 'limu nchini na kutoa mapendekezo mapya

    $c% itabu *ili*yopo tangu mfumo mpya wa elimu wa 1::1,

    *iendelee kutumika shuleni hadi tume imalize kazi yake.

    6! UAMUZI WA KISIASA UNA?YOATHIRI UBORA WA

    ELIMU NHINI

    1

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    15/38

    M"#$"%&%' S%*, (erikali ya //M kwa muda mrefu sasa

    imekuwa na tabia ya kufanya uamuzi wakisiasa katika masuala

    ya elimu na kuweka kando uta;ti au ushauri wa kitaalamu

     jambo ambalo limeathiri sana ubora wa elimu nchini.

    M"#$"%&%' S%*,  mifano iko mingi6 kwa mfano mwaka

    41

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    16/38

    kuporomoka kwa elimu nchini. #idha, ili kuondokana na

    maamuzi ya kisiasa kwenye elimu, tunarudia kupendekeza tena

    kwamba (erikali ianzishe chombo cha udhibiti wa 'limu na

    Mafunzo ya !fundi $)anzania 'ducation and )raining egulatory

    #uthority > )')#% kitakachoweka *iwango *ya ubora wa elimu

    kwa mujibu wa mitaala iliyopitishwa na (erikali, kudhibiti

    utungaji, usahihishaji na upangaji wa matokeo ya mitihani,

    kudhibiti gharama za elimu $ada na michango mingine% baina

    ya shule na taasisi nyingine za elimu za uma na binafsi ili kuwa

    na mfumo mmoja wa elimu unaoeleweka kuliko sasa ambapo

    kuna tofauti kubwa za kimfumo baina ya shule na taasisi za

    elimu binafsi na zile za umma. 0aiwezekani &izara hii iwe ndio

    mtungaji ya sera elimu, mtoaji wa elimu, mdhibiti wa elimu,

    mtungaji na msahihishaji mitihani huku ikiwa pia mmiliki wa

    baadhi ya shule. 0aki itatoka wapiFII

    ! UKIUKAJI WA KATAZO LA SERIKALI LA KUONGEZA

    ADA KWA SHULE ZISIZO ZA SERIKALI KWA

    MWAKA WA MASOMO 2016

    M"#$"%&%' S%*  Pamoja na mkanganyiko uliopo kuhusu

    ada elekezi na katazo la (erikali la kuongeza ada kwa shule

    zisizo za (erikali kwa mwaka wa masomo 417, zipo baadhi yashule zisizo za (erikali zimeendelea kuongeza ada kwa mwaka

    huu wa masomo 417 na kwenda mbali zaidi kuwatoza wazazi

    faini ya hadi shilingi laki moja kwa kuchelewa kulipa ongezeko

    hilo ndani ya siku saba.

    M"#$"%&%' S%*, Kambi asmi ya !pinzani Bungeni inazo

    taarifa kwamba shule ya awali ya # M!+)#C !+C3+ +!('-

    17

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    17/38

    (/033 ya ar es (alaam imeongeza ada kutoka shilingi

    1,294,444J mwaka 412 hadi ku;kia shilingi 1,:94,444J

    mwaka 417 sawa na ongezeko la shilingi

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    18/38

    M"#$"%&%' S%*, athari ya kupanga fedha za mikopo katika

    bajeti ya maendeleo ili bajeti ya maendeleo inaonekane kuwa

    kubwa lakini kimsingi fedha inayokwenda kutekeleza miradi

    halisi ya maendeleo ni kidogo sana na hi*yo kutokidhi mahitaji.

    M"#$"%&%' S%*,  Kambi asmi ya !pinzani Bungeni

    inahoji, kama mkopo wa mafunzo ni uwekezaji kwa nini bajeti

    za mafunzo ya mao;sa wa &izara $)raining domestic na

     )raining outside% yako kwenye bajeti ya Matumizi ya KawaidaF

    Mafunzo kwa ajili ya walimu =444 wa sayansi na lugha katika

    kasima uhalisiahakuna maendeleo yenye tija yatakayofanyika kutokana na

    upungufu mkubwa wa fedha za maendeleo.

    M"#$"%&%' S%*, kama (erikali inadai kwamba mikopo ya

    elimu ya juu ni fedha za maendeleo kwa kigezo kwamba huo ni

    uwekezaji kwenye maendeleo ya rasilimali watu6 basi isiwadai

    wanafunzi wanaopewa fedha hizo kugharamia elimu ya juu

    19

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    19/38

    kwa kuwa ni uwekezaji kama uwekezaji mwingine wa miradi ya

    maendeleo ambayo serikali hugharamia bila kudai kurudishiwa

    fedha hizo.

    M"#$"%&%' S%*, Kambi asmi ya !pinzani Bungeni haioni

    sababu ya (erikali kuwadai wahitimu wa *yuo *ikuu kurejesha

    fedha waliyokopeshwa kugharamia elimu waliyoipata kwa

    sababu gharama hiyo watai;dia kupitia kodi ya mapato $Pay #s

     -ou 'arn% pindi watakapoajiriwa. Kodi hiyo itakuwa ndio faida

    $economic returns% ya kuwalipia wanafunzi wa elimu ya juu

    ambayo inachangia moja kwa moja kwenye pato la taifa na

    uchumi kwa jumla. (erikali itambue pia kwamba fedha

    inazowakopesha wanafunzi wa elimu ya juu inatokana pia na

    kodi waliyolipa wazazi wa wanafunzi hao.

    ! HANGAMOTO ZA KIBAJETI ZA UKAGUZI NA

    UHAKIKI WA UBORA WA ELIMU NHINI!

    M"#$"%&%' S%*,ni dhahiri kwamba moja ya sababu

    zinazochangia kushuka kwa *iwango *ya ubora na ufaulu katika

    shule zetu za umma ni kutokuwepo kwa ukaguzi na ufuatiliaji.

    Kwa mujibu wa )akwimu za 'limu )anzania $B'() 412% ni

    asilimia 1:.1 tu ya shule za msingi na asilimia 1.< pekee ya

    shule za sekondari ambazo hukaguliwa kwa mwaka.

    M"#$"%&%' S%*, tafsiri ya takwimu hizo ni kwamba,

    serikali huchukua takribani miaka mitano kukamilisha ukaguzi

    wa shule zote za umma zilizopo. Kwa maneno mengine ni

    1:

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    20/38

    kwamba, shule hukaguliwa mara moja kila baada ya miaka

    mitanoI

    M"#$"%&%' S%*, kwa mfano, katika bajeti ya Mwaka

    417J41=, jumla ya $"%-%4% %-%.% 2=!1 zimetengwa kwa ajili

    ya idara ya ukaguzi na *itengo *yake kwa ajili ya matumizi ya

    kawaida lakini takribani $"%-%4% %-%.% 22 zimetengwa kwa

    ajili ya mishahara na maslahi mengine ya watumishi katika

    matumizi ya kawaida. 0i*yo kiasi cha takribani $"%-%4% %-%.%

    2  pekee ndicho kilichobaki kwa ajili ya shughuli halisi za

    ukaguzi kama ununuzi wa mafuta ya gari, posho za wakaguzi,

    ukarabati wa magari, mawasiliano na programu za mafunzo au

    uelimishaji.

    M"#$"%&%' S%*, Kambi asmi ya !pinzani Bungeni

    inaitaka (erikali kuona umuhimu wa ukaguzi na uhakiki wa

    ubora wa elimu na hi*yo kutenga fungu rasmi katika mwakampya wa fedha 417J1= lenye fedha za kutosha kukagua

    angalau asilimia 94 ya taasisi za elimu zinazostahili kukaguliwa

    hapa nchini.

    10! MWONGOZO WA UTEKELEZAJI WA SERA MPYA

     YA ELIMU

    M"#$"%&%' S%*, Ctakumbukwa kwamba sekta ya elimu

    sasa inasimamiwa na (era Mpya ya 'limu na Mafunzo ya

    Mwaka 41

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    21/38

    na kuhakikisha kuna upatikanaji wa *ifaa stahili *ya kujifunza

    na kufundishia pamoja na kuongeza ubora wa walimu kwa

    kutoa mafunzo, motisha na kuimarisha udhibiti wa taaluma ya

    ualimu.

    M"#$"%&%' S%*, ili (era hii iweze kutekelezwa kwa ufanisi,

    inahitaji itengenezewe miongozo $Luidelines% na Mpango wa

    utekelezaji $(trategy%. 0ata hi*yo pamoja na kwamba baadhi ya

    matamko ndani ya sera hii yamekwishaanza kufanyiwa kazi

    $mfano utoaji elimu bure%, bado mpango wa utekelezaji wa sera

    hii haujakamilika mpaka hi*i sasa.

    M"#$"%&%' S%*,  Kambi asmi ya !pinzani Bungeni

    inaitaka (erikali kutoa maelezo mbele ya bunge hili kwa nini

    mkakati wa utekelezaji wa sera ya elimu haujakamilika na

    kuanza kutumika hadi leo huku baadhi ya matamko yakiwa

    yameanza kutekelezwaF

    11! WANAFUNZI WALIOHAMISHWA KUTOKA ?YUO

    ?YA ST!JOSEPH

    M"#$"%&%' S%*,kwa muda mrefu Kambi asmi ya

    !pinzani Bungeni iliiomba (erikali kuhamisha *ijana hao

    kutokana na mazingira mabo*u ya kujifunzia na kufundishia.

    0ii ni pamoja na ukosefu wa walimu wenye sifa na program

    zisizo na ulinganifu na yuo *ingine. +ilifuatilia jambo hili hadi

    kufanya ziara katika yuo hi*i na kujionea hali mbaya

    isiyokubalika. Baada ya kupiga kelele nyingi humu Bungeni,

    +aibu &aziri aliahidi kwenda pamoja na )/! kuona hali halisi

    katika *yuo hi*yo. ?ambo la kustaajabisha ni kwamba

    walituletea ripoti ya ho*yo na ya kisiasa zaidi na kusema kuwa

    1

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    22/38

    hali ni shwari6 lakini jambo linaloshangaza zaidi ni kwamba leo

    wanafunzi wale wamehamishwa .

    M"#$"%&%' S%*, Kambi asmi ya !pinzani Bungeni

    inaitaka (erikali kutoa majibu ya kina ni kwani nini mwaka jana

    watendaji wa )/! na wa &izara walisema hakuna tatizo na

    watendaji hao hao mwaka huu wameona kuna tatizo la msingi

    na kuwahamisha wanafunzi wa *yuo hi*yoF. ?e, wanafunzi hao

    watalipwa nini kwa muda waliopotezaF. +a ni nini hatma ya

    *yuo hi*yoFF

    M"#$"%&%' S%*, jambo linalokera zaidi ni baadhi ya *ijana

    hawa sasa wamekwama kwenye *yuo walio*yohamia kwa kuwa

    kozi walizokuwa wanasoma zinatofautiana na pia kutokana na

    kuwa na mihula tofauti wengi wao wanalazika kurudia mwaka

    wa masomo ausemista.

    M"#$"%&%' S%*, Kambi asmi ya !pinzani inahoji ni

    kwanini )/! ili*isajili *yuo hi*i na ku*ipa ithibatiF Pili ni kwanini

    *yuo hi*i *ina mihula tofauti na *yuo *ingineF +a pia ni fedha

    kiasi gani zimepotea katika kuwalipia mikopo *ijana hawa na

    sasa hawajui ni lini watahitimu masomo yaoF +i nini hatma ya

    *yuo hi*yo na ni mfumo gani wa elimu yetu unaoruhusu

    wahitimu wa kidato cha nne kujiunga na *yuo *ikuu kwa

    kisingizio cha special programsFII

    M"#$"%&%' S%*, kitendo cha &aziri wa 'limu kui*unja

    bodi ya )/! jana tarehe 2 Mei, 417 kutokana na kudahili

    wanafunzi wasio na sifa kujiunga *yuo *ikuu siku moja kabla ya

    mjadala wa hotuba yake ya bajeti ya 'limu ni kujaribu kwa hila

    kulizuia bunge kujadili kwa kina udhaifu mkubwa wa (erikali

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    23/38

    kupitia )/! katika kusimamia ubora wa 'limu ya juu hapa

    nchini.

    M"#$"%&%' S%*,  Kambi asmi ya !pinzani Bungeni

    inaitaka (erikali kulieleza Bunge hili ni hatua gani za ziada

    itachukuwa kwa wajumbe hao wa bodi kwa kuwa

    wamewaharibia wanafunzi maisha yao na kupoteza fedha za

    umma kutokana na maamuzi yaoF

    12! MABORESHO YA MFUMO WA ELIMU NHINI

    M"#$"%&%' S%*, kwa muda mrefu sasa Kambi asmi ya

    !pinzani Bungeni imekuwa ikitoa angalizo kuwa mfumo wetu

    wa elimu umepitwa na wakati6 hi*yo upitiwe upya na kufanyiwa

    maboresho ili uendane na mabadiliko yanayotokea katika

    nyanja mbalimbali duniani.

    M"#$"%&%' S%*, elimu ya nchi yetu imekumbwa na

    matatizo mengi ya ki>mfumo jambo ambalo pamoja na

    madhaifu mengine limechangia sana kushuka kwa ubora wa

    elimu ya nchi yetu.

    M"#$"%&%' S%*, kwa kuwa matatizo yanayoikumba sekta

    ya elimu hapa nchini yamekuwa yakijirudia rudia6 na kwa kuwa

    mara kadhaa serikali imekuwa ikifanya maamuzi ya kisiasa

    zaidi kukabiliana na changamoto zinayoikumba sekta ya elimu

     jambo ambalo halijatoa ufumbuzi wa kudumu wa kuondokana

    na changamoto hizo6 na kwa kuwa wadau wote wa elimu wana

    matamanio ya kuona ubora wa elimu yetu unaongezeka6 0i*yo

    basi Kambi asmi ya !pinzani Bungeni inaitaka (erikali kwa

    8

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    24/38

    hatua ya sasa kuunda tume ya kitaalamu kwa ajili ya kuupitia

    upya mfumo wa elimu inayotolewa )anzania ili pamoja na

    kukuza ubora wake lakini pia elimu hiyo iweze kwenda

    sambamba na kasi kubwa ya mabadiliko ya kiuchumi duniani.

    1+! DHANA YA UGATUZI KAMILI WA MADARAKA

    (DEENTRALIZATION BY DE?OLUTION) NA

    MKANGANYIKO WA USIMAMZI WA SEKTA YA

    ELIMU NHINI

    M"#$"%&%' S%*,  katika utekelezaji wa dhana ya

    ugatuzi kamili wa madaraka, yani by , huduma nyingi

    za kijamii zikiwemo afya na elimu zimeshushwa katika

    ngazi ya (erikali za Mitaa na &izara za sekta husika

    zimeachwa na jukumu la kusimamia sera za sekta husika

    na kusimamia taasisi chache tu kulingana na

    itaka*yopangwa na wizara husika.

    M"#$"%&%' S%*, pamoja utaratibu huo kutajwa kuwa

    una nia njema ya kuwapa wananchi madaraka zaidi kupitia

    serikali zao za mitaa, lakini utaratibu huo umeleta

    mkanganyiko mkubwa sana katika usimamizi wa sekta ya

    elimu nchini.

    M"#$"%&%' S%*, nasema hi*i kwa sababu tuliona jinsi

    matatizo ya walimu yali*yokuwa yanashindikana

    kutatuliwa kutokana na kuwa na mamlaka nyingi mno

    zinazoshughulika na walimu hadi tuka;kia uamuzi wa

    kupendekeza kwamba kuwe na chombo kimojakitakachoshughulikia masuala ya walimu yani )')# D

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    25/38

     )anzania 'ducation and )raining #uthority, jambo ambalo

    mpaka sasa halijatekelezwa na (erikali. 0ata hi*yo,

    haiwezekani kutokana na mfumo wa by , waziri awe na

    mamlaka tu na *yuo *ya ualimu na *yuo *ikuu na kuacha

    taasisi nyingine zote za elimu na kazi zake katika mamlaka

    nyingine.

    M"#$"%&%' S%*, kutokana na hali hiyo, Kambi asmi

    ya !pinzani inaitaka (erikali kuangalia upya mfumo wake

    wa ugatuzi madaraka ili usilete mwingiliano wa kiutendaji

    katika ya (erikali Kuu na (erikali za Mitaa lakini pia

    kuweka mfumo ambao kutakuwa na chombo kimoja kikuu

    cha kitaifa kitakachoshughulikia kwa ukamilifu masuala ya

    elimu kuliko ili*yo sasa.M"#$"%&%' S%*,  baada ya kuona matatizo ya

    ugatuaji hapa nchini, niliamua kusoma *itabu *ingi

    *ina*yohusu dhana ya ugatuzi na nimegundua kuwa

     )anzania hatutekelezi kabisa dhana ya by bali

    tunachofanya ni by / yaani D##3-%:%. 7

    D#.#3%.  na ndio maana mambo hayaendi,

    0i*yo basi nashauri serikali isome *itabu *ina*yoelezea

    dhana hii ili waielewe kwa undani.

    1=! UBUNIFU KATIKA SAYANSI NA TEKNOLOJIA

    M"#$"%&%' S%*, hakuna )aifa duniani lililoendelea bila

    kuwekeza kwenye (ayansi na )eknolojia. +i ukweli usiopingika

    kuwa, (ayansi na )eknolojia *inachangia sana katika

    maendeleo ya )aifa lolote. Mageuzi ya (ayansi na )eknolojia

    yanaleta hamasa ya ubunifu, pamoja na ku*utia zaidi ushiriki

    2

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    26/38

    wa sekta binafsi katika kuendeleza (ayansi ya )eknolojia na

    ubunifu. +i wazi mageuzi haya yanahitaji fedha nyingi hasa za

    uta;ti. ?ambo la kusikitisha ni kwamba, (erikali haitoi fedha

    kwa ajili ya uta;ti6 kwa mfano, bajeti ya 412J417 sekta hii

    ilikuwa na upugufu mkubwa na hata baada ya agizo la tengeo

    la1H ya pato gha; la )aifa $LP%. Kambi asmi ya !pinzani

    inaitaka (erikali ieleze ni kiasi gani cha pato gha; la )aifa

    limetengwa kwa ajili ya uta;ti katika bajeti ya 417J1=F

    M"#$"%&%' S%*, Cnasikitisha sana kuona /3()'/ ambacho

    ni chombo pekee cha kutoa ushauri kwa (erikali kuhusu uta;ti,

    sayansi na )eknolojia kilichoanzishwa na sheria +amba = ya

    mwaka1:97 lakini bado (erikali haijaweza kuipata )ume hii

    walau 1H ya pato gha; la )aifa. Mathalani kwa mwaka huu

     )ume imetengewa 4.4

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    27/38

    ilishauri (erikali kuainisha )eknolojia hii kama kipaumbele cha

    kufanya uta;ti na hi*yo )anzania kuwa mstari wa mbele ikiwa

    taasisi zake zataitumia. Kambi asmi ya !pinzani Bungeni

    (erikali kulieleza Bunge hili kama ilitekeleza ushauri iliopewa na

    /3()'/ kuhusu teknolojia hiyo.

    M"#$"%&%' S%*, katika Mwaka 412J417 (ekta hii ya

    (ayansi na )eknolojia ilipata fedha kidogo sana huku tukitamba

    tuko kwenye karne ya (ayansi ya )eknolojia. Kwa mfano mwaka

     jana iliyokuwa &izara ya (ayansi na )eknolojia na Mawasiliano

    ilipokea hadi #prili, 412 shilingi bilioni

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    28/38

    ya shilingi $retention of *alue charges%. Kambi asmi ya

    !pinzani bungeni haikubaliani na kiwango kilichowekwa na

    bodi cha kulinda kuporomoka kwa thamani ya shilingi

    $*alue retention fee% ya taktriban asilimia 24 ya deni lote.

    M"#$"%&%' S%*, ufuatao ni mfano wa hati ya madai

    ya marejesho wa mkopo kwa mhitimu wa chuo kikuu.

    Cnasomeka kama ifuata*yo@ “Kindly be informed that the

    deductions for the loans board will be&in e'ecti(ely May)

    *"+, and the deduction -ercenta&e will be ./ from the

    basic salary$

    0f you ha(e a complaint in accordance to this information)

    kindly see from 1234B

    /hek

    no

    Cnd

    eN

    "ull

    name

    Principle

    #mount

    Penalty oan

    #dmin

    fee

    alue

    etention fee

     )otal

    oan

    #mount

    3utstanding

    debt

    6,=6,000

    !

    6=,60

    0

    6,=60 2,5++,+== 10,=+,=0= 10,=+,=0=

    HANZO HESLB

    M"#$"%&%' S%*,  Kambi asmi ya !pinzani Bungeni

    inaitaka (erikali kufuta gharama ya 02alue Rentention "ee1

    inayowatoza wahitimu wanaporejesha mikopo ili kuwapunguzia

    ukali wa maisha wahitimu hao ukizingatia wengi wao bado

    hawajapata ajira na waliopata ajira bado mishahara yao ni

    midogo. #idha, Kambi asmi ya !pinzani Bungeni bado

    inasimamia msimamo wake wa kuitaka (erikali kutowadai

    wahitimu wa elimu ya juu kwa kuwa fedha inayowapatia ni

    bajeti ya maendeleo ya wizara husika kama ili*yo kwa wizara

    nyingine na hi*yo (erikali haipaswi kudai fedha hizo kama

    9

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    29/38

    amba*yo haidai kurejeshewa fedha inazotoa katika miradi

    mingine ya maendeleo.

    16! UNYANYASAJI WA WANAFUNZI WA ?YUO ?IKUU

    WANAOHISIWA KUUNGA MKONO UPINZANI

    M"#$"%&%' S%*,  kumekuwa na tabia mbaya sana ya

    baadhi ya wakuu wa *yuo *ikuu hapa nchini kuwanyanyapaa na

    kuwadhalilisha na hata kudiriki kuwafukuza chuoni wanafunzi

    ambao kwa hisia zao wana;kiri wanaunga mkono harakati za

    *yama *ya upinzani.

    M"#$"%&%' S%*, Kambi asmi ya !pinzani Bungeni inazo

    taarifa kwamba aliyekuwa kiongozi wa (erikali ya &anafunzi

    katika /huo Kikuu cha odoma amesimamishwa masomo kwa

    hisia tu kwamba alikwa mfuasi wa /0#'M#. #idha, aliyekuwa

    makamu wake, tena &$%",  aliamriwa na uongozi wa

    chuo hicho kukabidhi madaraka yake, kwa uongozi mwingine

    wa serikali ya wanafunzi ambao haukuchaguliwa na wanafunzi

    $uliteuliwa na utawala wa chuo% kinyume kabisa na katiba

    inayoongoza (erikali ya &anafunzi wa chuo hicho.

    M"#$"%&%' S%*,  mwanafunzi huyu $msichana% alitakiwa

    kupongezwa na uongozi wa chuo kwa kuthubutu kugombea

    nafasi hiyo na kuonyesha uwezo mkubwa wa uongozi, lakini

    :

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    30/38

    alisakamwa na uongozi wa chuo na kutishiwa maisha, jambo

    lilomfanya afungue shauri mahakamani kupinga kulazimishwa

    kuachia madaraka. 0ata hi*yo, zilipoonekana dalili za yeye

    kushinda, chuo kilimwandikia barua ya kumfukuza chuo kabla

    ya hukumu.

    1! M"#"#$"%&%' S%*, hukumu imetoka na huyo

    mwanafunzi ameshinda kesi. !tawala wa chuo hicho

    umedharau amri ya Mahakama ya kumrejesha na kumpa

    ushirikiano kiongozi huyo halali wa (erikali ya &anafunzi

    kwa nafasi ya Makamu wa ais6 mwanafunzi huyo

    ananyanyapaliwa na uongozi wa chuo kikuu cha odoma

     jambo ambalo kwa *yo*yote *ile litaathiri masomo yake

    ikizingatiwa kwamba zimebaki wiki chache kabala

    hajafanya mtihani wa kuhitimu shahada yake ya kwanza.

    Kambi asmi ya !pinzani Bungeni inaitaka (erikali kutoa

    maelezo mbele ya bunge hili ni kwa nini haijamchulia

    Mkuu wa /huo Kikuu cha odoma hatua za kinidhamu

    kwa kuendeleza unyanyapaa na unyanyasaji wa wazi kwa

    wanafunzi wa chuo hicho kwa hisia zake tu kwamba

    wanafunzi hao ni wafuasi wa /0#'M#J!K#F Cna

    maana !3M ni kwa ajili ya wanafunzi wa //MF TUME YA

    WALIMU (TEAHERS SER?IE OMMISSION)

    M"#$"%&%' S%*,  Kambi asmi ya !pinzani kwa muda

    mrefu imekuwa ikipinga utaratibu wa walimu kuwa chini ya

    mamlaka tofauti za ajira jambo linaloleta mkanganyiko kwao

    hasa pale wanapokuwa na madai mbalimbali kuhusu maslahi

    yao. &alimu walikuwa wakipata tabu kujua ni mamlaka ipi katiya 3;si ya ais D Menejimenti ya !tumishi wa !mma au 3;si

    84

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    31/38

    ya &aziri Mkuu > )#MC('MC, au &izara ya 'limu na Mafunzo ya

    !fundi .

    M"#$"%&%' S%*, B 7 *#-#-# 7%4%, hatimaye

    serikali ilileta muswada wa (heria ya kuanzisha )ume ya

    !tumishi wa &alimu $)eachers (er*ice /ommision% mwezi ?ulai,

    412. +ia ya (erikali kuleta muswada ule ililenga kuwalaghai

    walimu ili waipigie //M kura katika uchaguzi Mkuu wa 3ktoba

    412, na ndio maana uliletwa ?ulai, 412 tena kwa matangazo

    na mbwembwe nyingi hadi ku;kia hatua ya ais wa wakati huo

     ?akaya Mrisho Kikwete kuupigia kampeni kwa /hama cha

    &alimu $/&)% na wadau wengine wa elimu tofauti na njia za

    kawada za Kamati ya Bunge ya 0uduma za ?amii kukutana na

    wadau ili mradi tu ionekane kwamba (erikali ilikuwa inawajali

    walimu sana.

    M"#$"%&%' S%*, Kambi asmi ya !pinzani Bungeniinapenda kuwaarifu walimu wote nchini kwamba (eriakali hii ya

    //M haijawahi kuwa na nia ya dhati ya kutatua kero zake, ila

    inakaa na walimu kimkakati tu kwa malengo ya kubembeleza

    kura zao, na wakishapiga kura hizo matatizo yanaendelea

    kubaki palepale %. & "% -#. &.

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    32/38

    *yote *yenye mapungufu *iweze kufanyiwa marekebisho ili

    sheria hiyo iwe bora na yenye kutatua kero za muda mrefu za

    walimu.

     

    1! KUHAMISHWA KWA MAFUNZO YA WALIMU

    KUTOKA KURUGENZI YA WALIMU YA WEST HADI

    NATE (NATIONAL OUNIL FOR TEHNIAL

    EDUATION)

    M"#$"%&%' S%*, tangu tupate uhuru, nchi imekuwa

    ikifanya mipango na mikakati ya kutoa elimu bora kwa ajili ya

    wananchi wake. (erikali imekuwa inaweka *yombo au taasisi

    mbali mbali kutekeleza jukumu la utoaji ya elimu. Cli

    kuhakikisha tunaenda *izuri, serikali imekuwa inafanya mapitio

    ya utoaji wa huduma hasa elimu. Mapitio hayo $re*iews%

    yamekuwa yanategemea kwanza6 uta;ti wa kisayansi, na pili

    ushirikishwaji mpana wa wadau wote. 

    M"#$"%&%' S%*, ?ambo la kushangaza ni kuwa bila uta;ti

    wowote wa kisayansi wala ushiriki wa wadau wa elimu kwa

    niaba ya wananchi, M#"!+3 -# !#CM! $)eachers 'ducation%

    yamehamishwa kutoka Kurugenzi ya !alimu ya &'() na

    kupelekwa Mafunzo ya 'limu ya !fundi $+#/)'%.

    M"#$"%&%' S%* malengo na makusudi ya mafunzo ya

    walimu yanatofautiana sana na malengo na makusudi ya

    mafunzo yanayotolewa chini ya +#/)'.

    8

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    33/38

    M"#$"%&%' S%*, Makusudi ya 'limu ya !fundi ni

    inayotolewa chini ya +#/)' ni kama ifuata*yo6 naomba

    kunukuu@>

    5echnical 2ducation objecti(e is to prepare &raduates

    for occupations cate&orised as skilled crafts below

    en&ineerin& profession and hence employees are

    called technicians &uided by +66, 7ational 5echnical

    2ducation -olicy$ 78952 :uality controls and re&ulates technical

    education$

    M"#$"%&%' S%*, matokeo ya kufanya uhamisho huu ni

    sawa na kuweka mafunzo ya !alimu kama fani ya ufundi tofauti

    na !alimu kama taaluma inayojitegemea kama sheria, !hasibu

    au ununuzi ambazo zote zina bodi zake.

    M"#$"%&%' S%* Kambi asmi ya !pinzani ina mtazamo

    kwamba, uamuzi huo wa (erikali usipobatilishwa, basi

    /hangamoto zafuatazao zitatokea.

    i. Kuongezeka kwa gharama za uendeshaji kutokana

    kubadilika kwa muundo wa utawala $organizational

    structure%.ii. Kutakuwa na shida ya kupata wanafunzi wa kujiunga

    na *yuo kwa *ile *yuo *ikuu na*yo *inawaangalia

    hao hao kutoa *yeti na diploma.iii. Kutokwepo harmonization kati ya )/! na +#/)' juu

    ya mafunzo ya walimu hasa ubora wake.i*. !gumu wa kuendesha *yuo kwa *ile serikali

    haitapeleka fedha tena.

    88

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    34/38

    *. "alsafa $philosophies% mbali mbali za *yuo *ya

    bainafsi na umma na hi*yo kuongeza kwa

    mkanganyiko.

    M"#$"%&%' S%* Kambi asmi ya !pinzani Bungeni

    inaitaka (erikali kutoa majibu mbele ya Bunge hili juu ya

    maswali yafuatayo@>

    i. Kulikuwa na sababu gani $rationale% ya kuhamisha

    mafunzo ya walimu toka Kurugenzi ya Mafunzo ya

    &izara ya 'limu kwenda +#/)'Fii. ?e, kuna uta;ti gani wa kisayansi uliofanyika

    kuhalalisha mabadiliko hayoFiii. ?e, wadau walihusihwa kuhusu jambo hiliFi*. Kuna faida na hasara gani ya kufanya huu uhamisho

    huoF*. Kuna mikakati gani iliyowekwa kuhakikisha kuwa

    ubora wa elimu hautaathirikaF*i. Kuna mikakati gani iliyowekwa kuhakikisha

    uandiskishaji wa walimu wanafunzi kukidhi mahitaji

    ya *yuo husikaF*ii. yuo hi*i *itawezaji kuwa endele*u bila ruzuku ya

    serikaliF*iii. ?e, mitaala itawezaje kuwa harmonized kwa ajili ya

    *yuo *yoteF15! MAPENDEKEZO YA JUMLA YA KUBORESHA

    SEKTA YA

    ELIMU NHINI

    M"#$"%&%' S%*, kwa kuwa imebainika dhahiri kwamba

    elimu ya )anzania imekuwa inaporomoka kwa sababu ya

    uwekezaji ha;fu katika rasilimali watu katika sekta hiyo D yaani

    8

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    35/38

    taaluma na mafunzo kwa walimu6 na kwa kuwa imebainika pia

    kwamba mitaala mibo*u isiyokidhi *iwango imechangia sana

    kushuka kwa ubora wa elimu hapa nchini6 hi*yo basi , Kambi

    asmi ya !pinzani Bungeni inapendekeza kwa (erikali kufanya

    mambo yafuatayo@

    1. Kuboresha Mitaala elimu ili ishabihiane na mahitaji ya

     jamii na mabadiliko makubwa yanayoendelea kutokea

    duniani katika nyanja mbalimbali.

    . Kuelekeza na kusimamia matumizi ya kitabu kimoja cha

    kiada ili kufanya *ijana wetu wasitofautiane katika

    ufahamu wa mada zinazofundishwa kwani wanafanya

    mitihani mmoja.

    8. Kusimamia utungaji na uchapaji wa *itabu na kuhakikisha

    kuwa *ina ubora wa hli ya juu kwani *itabu ndio kiongozi

    kwa walimu.

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    36/38

    174 tu kati ya shule za sekondari zaidi ya

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    37/38

    wahitimu wanaotokana na elimu duni inayotolewa, iliyogubikwa

    na maamuzi mabo*u ya kisiasa na *itendo *ya u;sadi, ni

    dhahiri kuwa )aifa letu halitaweza kupata *iongozi bora wa

    kuliongoza huko tuendako.

    M"#$"%&%' S%*, wakati wa kuchukua hatua za kunusuru

    elimu yetu ni sasa. +i lazima tubadilike. Matatizo ya nchi hii

    hayataweza kamwe kutatuliwa kwa elimu hii duni

    tunayopandikiza kwa watoto wetu. )unahitaji

    mapinduzi na mageuzi makubwa ya kielimu kuitoa )anzania

    hapa ilipo na kuipeleka kwenye le(el nyingine$ (uala la kuwa

    nchi ya uchumi wa kati, nchi ya *iwanda, litaendelea kuwa ni

    hadithi za Bulicheka tu ikiwa hatutaondoa mapungufu mengi

    yanayokabili mfumo wetu wa elimu.

    M"#$"%&%' S%*,  napenda kumalizia hotuba yangu kwa

    kusema kwamba, sera ya elimu bure ilianzishwa na /0#'M#.

    Cpo katika ilani ya uchaguzi ya /0#'M# chini ya mwa*uli wa

    !K# tangu mwaka 442, 414 na hatimaye 412. engo

    lilikuwa ni kutoa huduma ya elimu bure kwa ukamilifu wake

    kuanzia shule za awali hadi chuo kikuu. Maigizo ya ilani ya

    /0#'M# yaliyofanywa na //M, yameishia kuondoa ada tu na

    michango midogomidogo ya uendeshaji wa shule hadi kidato

    cha nne tu, huku kukiwa na sintofahamu kubwa juu ya ujenzi na

    ukarabati wa miundombinu katika shule hizo. 0ali hii

    inapelekea kuporomoka zaidi kwa elimu.

    M"#$"%&%' S%*, kuna msemo usemao, A5% edu'ation is

    e3pensive try i#noran'e1,  tafsiri yake ni kwamba6 kama

    8=

  • 8/16/2019 HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI -ELIMU

    38/38

    elimuJ kuelimika ni gharama basi jaribu ujinga. )anzania

    tumeamua kujaribu ujinga, kwa kutowekeza *ya kutosha katika

    elimu na ndio maana elimu yetu imeporomoka na ku;kia hapa

    ilipo. 

    M"#$"%&%' S%*, &aziri wa 'limu katika awamu ya kwanza

    Marehemu ?ackson Makwetta alisema kwamba@ “)anzania ni 

    kama mama mjamzito ambaye siku zake za kuji%un#ia

     zimefka lakini haji%un#ui, hivyo )anzania inahitaji 

    mabadiliko vin#inevyo itaendelea kudidimia kielimu na

    kiu'humi.$ Kwa sababu hiyo6 Kambi asmi ya !pinzani

    Bungeni inaitaka (erikali kuutazama upya mfumo wa elimu

    sasa kwa kuunda tume maalum ya kuupitia upya na kutoa

    mapendekezo ili )aifa liweze kuwa na mfumo bora wa elimu

    unaokidhi *iwango *ya kimataifa.

    M"#$"%&%' S%*,   ya kusema hayo, naomba

    kuwasilisha.

    (usan #nselm ?erome yimo $Mb%

    WAZIRI KI?ULI NA MSEMAJI MKUU WA

    KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KATIKA

    WIZARA YA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UFUDI

    7 Mei, 417