Imam Ali (a.s) ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.w) - Juzuu ya Kwanza

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Imam Ali (as) hakuwa kiongozi wa Waislamu tu bali wa wanadamu wote. Maisha na mwenendo wa Imam Ali (as) umewavutia watu wote, marafiki na maadui, hali ambayo imemfanya kuwa kiongozi wa umma. Mtukufu Mtume (saw) alimtangaza mwanzoni kabisa mwa Ujumbe wake katika kile kikao mashuhuri kabisa cha “karamu ya jamaa”, aliposema: “Huyu ni ndugu yangu, wasii wangu, waziri wangu, khalifa wangu na mrithi wangu. Basi msikilizeni na mumtii.” Hili lilikuwa tangazo la mwanzo kabisa alilolitoa Mtukufu Mtume (saw) kwa ajili ya Imam Ali (as) na aliendelea kuwakumbusha Waislamu kuhusu uongozi wa Imam Ali baada yake katika matukio mengi yaliyofuata baadaye, kama vile katika tukio la Ghadir Khum pale aliposema: “Man kuntu mauwahu fahadha Aliyyun mawlahu – Yule ambaye mimi kwake ni kiongozi basi na huyu Ali ni kiogozi wake.” Na mwisho ni tukio la “Karatasi” pale Mtukufu Mtume (saw) alipokuwa ni mgonjwa na maradhi yamemzidi akaomba aletewe karatasi, kalamu na wino, mashuhuri kama “hadithi ya karatasi.”

Citation preview

  • IMAM ALI (A.S.)

    NDUGU YAKE

    MTUME MUHAMMAD (S.A.W.)

    Usahihishaji Upya wa Historia naUtafiti wa Kina wa Madhehebu ya Shia

    JUZUU YA KWANZA

    Kimeandikwa na: Sheikh Muhammad Jawad Chirri

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:34 PM Page A

  • Haki ya kunakili imehifadhiwa na:AL-ITRAH FOUNDATION

    ISBN: 978 - 9987 - 512 - 56 - 0

    Kimeandikwa na: Sheikh Muhammad Jawad Chirri

    Kimetarjumiwa na:Salman Shou

    Kimepangwa katika Kompyuta na:Hajat Pili Rajab

    Toleo la kwanza: Oktoba,2011Nakala: 1000

    Kimetolewa na kuchapishwa na:Alitrah Foundation

    S.L.P. 19701 Dar es Salaam, TanzaniaSimu: +255 22 2110640

    Simu/Nukushi: +255 22 2127555Barua Pepe: [email protected]

    Tovuti: www.ibn-tv-comKatika mtandao: w.w.w.alitrah.info

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:34 PM Page B

  • Yaliyomo

    Utangulizi....................................................................................................2

    SURA YA KWANZA

    Imam wakati wa kipindi cha Utume ...........................................................7

    Nyumba ya mtukufu Mtume (s.a.w.w)........................................................7.Kumbukumbu kuthibitisha ubora wao.......................................................11

    SURA YA PILI

    Watu wa nyumba ya Muhammad..............................................................20

    SURA YA TATU

    Watu muhimu na walazima.......................................................................29

    Ukoo wa Al-Aus na Al-Khazraj................................................................32

    Abu Talib ..................................................................................................32

    Uislamu wa Abu Talib...............................................................................34

    Sote tunawiwa naye...................................................................................39

    SURA YA NNE

    Waislamu wa kwanza................................................................................48

    SURA YA TANO

    Ndugu na Waziri........................................................................................54Hadith zinazopingana................................................................................58

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:34 PM Page C

  • DImam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    Zawadi iliyotolewa....................................................................................61

    Kwa nini zawadi kubwa hivyo kwa ajili ya Ujumbe................................63

    Mtukufu Mtume (s.a.w.w) hakutaka kuwepo na visingizio......................65

    Matokeo ya mkutano wa nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w).............66

    SURA YA SITAMkombozi............................................................................................... 68

    Ukubwa wa kazi yenyewe.........................................................................72

    Umuhimu wa kuwasilisha amana kwa wenyewe......................................73

    Thamani isiyopungua................................................................................74

    SURA YA SABANafasi ya Ali katika kujenga dola ya Kiislamu................................77

    Ushindani wa hoja dhidi kukosa hoja..............................................79

    Ubora kushindana na wingi............................................................80

    Shujaa wa kipekee...........................................................................81

    SURA YA NANEVita vya Badr...................................................................................83

    SURA YA TISAVita vya Uhud..................................................................................86

    SURA YA KUMIVita vya Handaki.......................................................................................97

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:34 PM Page D

  • EImam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    SURA YA KUMI NA MOJA

    Vita vya Khaybar...........................................................................106

    Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alizingira Khaybar............................109

    SURA YA KUMI NA MBILI

    Udugu watangazwa........................................................................119

    SURA YA KUMI NA TATU

    Nafasi ya Ali kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ndani yaQurani .........................................................................................127

    SURA YA KUMI NA NNE

    Maula wa Waislamu.......................................................................134

    SURA YA KUMI NA TANO

    Wasia wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) usiotimizwa........................141

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:34 PM Page E

  • NENO LA MCHAPISHAJI

    Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiingerezakiitwacho, The Brother of the Prophet. Sisi tumekiita, Imam Ali (as) Nduguwa Mtume Muhammad (saw). Kitabu hiki kilitungwa na aliyekuwa mubal-lighi mashuhuri wa dini ya Kiislamu ya Ushia nchini Marekani, MarehemuSheikh Muhammad Jawad Chirri.

    Kitabu hiki ni wasifu wa mtu mkubwa ambaye alikuwa mwanamume wakwanza kuamini Utume wa Muhammad (saw) na wa kwanza kusali nyumayake.

    Imam Ali (as) hakuwa kiongozi wa Waislamu tu bali wa wanadamu wote.Maisha na mwenendo wa Imam Ali (as) umewavutia watu wote, marafikina maadui, hali ambayo imemfanya kuwa kiongozi wa umma.

    Mtukufu Mtume (saw) alimtangaza mwanzoni kabisa mwa Ujumbe wakekatika kile kikao mashuhuri kabisa cha karamu ya jamaa, aliposema:Huyu ni ndugu yangu, wasii wangu, waziri wangu, khalifa wangu namrithi wangu. Basi msikilizeni na mumtii. Hili lilikuwa tangazo la mwan-zo kabisa alilolitoa Mtukufu Mtume (saw) kwa ajili ya Imam Ali (as) naaliendelea kuwakumbusha Waislamu kuhusu uongozi wa Imam Ali baadayake katika matukio mengi yaliyofuata baadaye, kama vile katika tukio laGhadir Khum pale aliposema: Man kuntu mauwahu fahadha Aliyyunmawlahu Yule ambaye mimi kwake ni kiongozi basi na huyu Ali ni kio-gozi wake. Na mwisho ni tukio la Karatasi pale Mtukufu Mtume (saw)alipokuwa ni mgonjwa na maradhi yamemzidi akaomba aletewe karatasi,kalamu na wino, mashuhuri kama Hadithi ya karatasi.

    F

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:34 PM Page F

  • Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wamaendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, nganoza kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tenakatika akili za watu.

    Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamuakukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yakeyaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji waKiswahili.

    Tunamshukuru ndugu yetu, Maalim Dhikir U. Kiondo (ambaye sasa nimarehemu - Allah amrehemu) kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumikitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia mojaau nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake.

    Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni mwanga kwa waso-maji wetu na kuzidisha upeo wao wa elimu ya dini na ya kijamii.

    Mchapishaji:Al-Itrah FoundationS. L. P. 19701Dar-es-Salaam.

    :

    G

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:34 PM Page G

  • BIBLIOGRAFIAUBAINIFU

    Tarehe zilizotajwa kwenye bibliografia hii zimetegemea Kalenda yaKiislamu ambayo ilianza kwa tukio la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuondo-ka Makka na kwenda Madina. Tukio hilo la kuondoka huitwa Hijiriya yaMtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambalo lilitokea mwaka wa 622 Baada yakuzaliwa Isa (a.s.).

    Endapo msomaji anataka kubadilisha tarehe kutoka tarehe za Kiislamu nakuwa kalenda ya Gregory ya Nchi za Kimagharibi, lazima azingatietofauti ya miaka 622 kabla ya Hijiriya. Zaidi ya hayo, mwaka wa mwan-damo wa mwezi ambao Kalenda ya Kiislamu ndio msingi wake, unazosiku 354 tu. Hivyo mwaka huu ni pungufu kwa siku 11 kuliko mwaka wajua. Kila miaka mia moja ya jua inakuwa miaka 103 ya miaka inay-ohesabiwa kwa kuandama kwa mwezi. Miaka elfu moja ya jua ni sawa namiaka 1030 inayohesabiwa kwa mwandamo wa mwezi.

    QURANI TUKUFU

    AMIINI (Sheikh Hussein Ahmad Al-Amiin) Al-Ghadiir (Tangazo lililosimuliwa la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusuImam Ali hapo Ghadiir Khum), chapa ya pili ilifanywa na Al-HaidariPrinting Tehran, 1372 Hijiriya. Al-Amiin ni mwandishi wa historia maaru-fu wa zama za leo.

    ASKARI (Sayyid Murtadha Al-Askari) Abdallah ibn Saba, chapa ya pili ilifanywa na Matabi-a Al-Kitab Al-Arabimjini Cairo, 1381 A.H. Al-Askari ni mwandishi wa historia na theolojia wazama za leo.

    H

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:34 PM Page H

  • ATHIIR (Ali Ibn Muhammad Al-Shaibani, ajulikanaye kama Ibn al-Athiir) Al-Kamil (kilicho kamilika), kitabu maarufu cha historia ya Uislamu, kili-chochapishwa na Al-Azhari Printings 1301 Hijiriya. Pia kimepigwa chapana Dar-Al-Kitab Al-Lubnani (The Lebanese House of Books), 1973 Baadaya kuzaliwa Isa. Nukuu zilizomo humu nyingi zinatoka kwenye chapa yapili. Ibn Al-Athiir alikufa mwaka wa 750 Hijiriya.

    BALADHURI. (AL-Baladhuri).Ansabul-Ashraf (Nasaba za Masharifu). Kitabu maarufu cha historia yaUislamu, kimechapishwa Jerusalem. Al-Baladhuri, ni mwandishimashuhuri wa historia, alikufa mwaka wa 279 Hijiriya.

    BIRR (Yusuf Ibn Abdul-Birr)Al-Istiiab Fi Maarifat al-Asshab (Elimu linganishi kuhusu Masahaba waMtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kitabu maarufu cha historia ya Kiislamu,kimechapishwa na Al-Fajjala Printing, Cairo, mwaka wa 1970 AD. IbnAbdul-Birr ni mwandishi wa historia maarufu, alikufa mwaka wa 463Hijiriya.

    BUKHARI (Muhammad Ibn Ismail, al-Bukhari).Sahih al-Bukhari (Sahih ya Al-Bukhari), mojawapo ya vitabu sita vilivyoSahihi vyenye Hadith zilizoandikwa (Hadith ni tamko lililosimuliwa autendo au uthibitisho wa kimya wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Muhamamds.a.w.w) Kitabu kilichapishwa na Muhammad Ali Subh huko Al-Azhar,Cairo, Al-Bukhari ni mchaguzi na mwandishi wa Hadith mashuhuri, alik-ufa mwaka wa 256 Hijiriya.

    DAWUD (Suleiman Ibn Al-Ashath Ibn Shaddad anayejulikana kama Abu-Dawood)

    Sunan Abu Dawood (Hadith za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) zilizoandika).Mojawapo ya vitabu sita vya hadith zilizoandikwa, kilichochapishwa naMustafa Al-Babi al-Halabi Misri, mwaka 1952 AD. Abu Dawood ni

    I

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:34 PM Page I

  • mkusanyaji na mwandishi wa Hadith mashuhuri alikufa mwaka 275Hijiriya.

    FAIRUZABADI (Sayyid Murtadha Al-Fairuzabadi).

    Fadha-il Al-Khamsah Min As-Sihah Al-Sitta (Fadhila za watu watano, zili-zoandikwa kwenye vitabu Sahihi Sita), chapa ya tatu ilifanywa na Al-Alami Institute of Printing, Beiruti, mwaka 1973 AD, Al-Fairuzabadi nimkusanyaji wa Hadith, mwanatheolojia na mwandishi wa Hadith wa zamaza leo.

    HADIID (Izzud-Din, ajulikanaye kama Ibn Abil-Hadiid).

    Sharh NahjulBalaghah (Maelezo kuhusu Njia ya Ufasaha wa manenoyaliyokusanywa ya Imam Ali), kitabu kinachosomwa kwa wingi sana.Kimechapishwa na Dar Al-Kutub Al-Arabiyah Al-Kubrah (NyumbaKubwa ya Vitabu vya Kiarabu), ya Mustafa Al-Babi, Cairo, Ibn Abil-Hadiid ni mwanatheolojia na mwandishi wa historia maarufu, alikufamwaka 655 Hijiriya.

    HAIKAL (Dk. Muhammad Husein Haikal) Hayat Muhammad (Maisha ya Muhammad), Chapa ya tatu iliyofanywa na Dar Al-Kutub Al-Misriah (The EgyptianHouse of Books) Cairo, mwaka 1358 Hijiriya. Dr. Haikal ni mwandishi wahistoria wa zama za leo.

    HAKIIM (Sayyid Muhammad Taqi Al-Hakim) Al-Madkhal Ila Darasat Al-Fiqh Al-Muqaran (Utangulizi kuelekeakwenye masomo ya Fiqhi linganishi) kilichapishwa na Dar Al-Andalus,Beirut. 1963 AD. Hakiim ni mwanatheolojia wa zama za leo.

    AL-HAKIM. (Muhammad Ibn Abdullah Al-Nissaburi, ajulikanaye kamaAl-Hakim).

    J

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:34 PM Page J

  • Al-Mustadrak Alas-Sahihain (Hadithi ambazo sahihi za Al-Bukhari naMuslaim imziacha). Hadith zilizomo kwenye kitabu hiki zinachukuliwakuwa za kweli na wanachuoni Waislamu, isipokuwa zikataliwe na Al-Dhahabi, ambaye maoni yake yamechapwa pembezoni mwa kitabu cha Al-Mustadrak, kilichochapishwa na Al-Nasr Printing, Riyadh Saudia Arabia,mwaka 1335 Hijiriya. Al-Hakim ni mwanachuo, mwandishi wa Hadith namkusanyaji wa Hadith maarufu, alikufa mwaka 405 Hijiriya.

    HALABI (Ali Ibn Burhanud-Diin Al-Halabi) Al-Siirah Al-Halabiyah (Wasifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ulioandik-wa na Al-Halabi), kilichochapishwa na Al-Maktaba Al-Kubra ya MustafaMuhammad, Cairo, Al-Halabi ni mwandishi wa historia maarufu, alikufamwaka 1044 Hijiriya.

    HANBAL (Ahmad Ibn Hanbal)Musnad Ahmad, kilichochapishwa na as-Sader Printing, Beiruti, mwaka1969AD. Ibn Hanbal ni mmojawapo wa maimam wa matapo ya Kiislamu,alikufa mwaka 241 Hijiriya.

    HISHAMU (Abdul Malik Ibn Hisham) Al-Siirah Al-Nabawiyah (Wasifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kili-chochapishwa na Mustafa Al-Babi Al-Halabi, Misri, mwaka 1955 AD. IbnHisham ni mwandishi maarufu wa historia ya Kiislamu, alikufa mwaka281 Hijiriya.

    HUSEIN (Dk. Taha Husein)Al-Fitnat Al-Kubra (Mgogoro wa Fitna Kubwa katika dini), Kilichapishwana Dar Al-Maarif, Misri mwaka 1953 AD. Taha Husein ni mwanachuo namwandishi wa historia wa zama hizi.

    JALALAIN (Jalalud-Din Muhammad Al-Halabi na Julalud-Din As-Suyuuti)

    K

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:34 PM Page K

  • Tafsiirul-Jalalain (Tafsiri za Jalal mbili kuhusu Qurani Tukufu)

    KHALID (Muhammad Khalid)Fi Rihab Ali (kwenye nyumba ya wageni ya Ali), Khalid ni mwandishi namwanahistoria wa Misri wa zama za leo.

    MAJAH (Muhammad Ibn Majah) Sunnan Ibn Majah (Hadith zilizokusanywa na Ibn Majah). Mojawapo yavitabu sita vilivyo sahih vya Hadith kilichochapishwa na Dar Ihya Al-Kutub Al-Arabiyah (Nyumba ya Uhuishaji wa Vitabu vya Kiarabu) ya IsaAl-Babi, Cairo, 1952 AD. Ibn Majah ni mkusanyaji na mwandishi waHadith maarufu, alikufa mwaka 275 Hijiriya.

    MAQSOUD (Abdul Fattah Abdul-Maqsoud)Al-Imam Ali Ibn Abi Talib (kitabu cha historia ya Imam Ali), kimechapish-wa na Al-Irfan Printing, Beiruti, Abdul-Maqsoud ni mwandishi namwanahistoria wa Misri wa zama za leo.

    MUGHNIYAH (Sheikh Muhammad Jawad Mughniyah).Hadhi Hiya Al-Wahhabiyah (Huu ndio Uwahabbi), Sheikh Mughniyah nimwanatheolojia maarufu wa zama za leo.

    MUHSIN (Sayyed Muhsin Al-Amiin) Aayan Al-Shiah, kitabu chenye maelezo mengi kilichopangwa kwa alfa-beti. Sayyid Muhsin ni mwanatheolojia na mwandishi wa historia maarufuwa zama za leo.

    MUSLIM (Ibn Al-Hajjaj Al-Qusheiri)Sahih Muslim (Ukweli na usahihi wa Muslim). Ni kimojawapo cha Vitabusahihi sita vya Hadith kilichochapishwa na Muhammad Ali Subh Printing,Misri, mwaka 1349 Hijiriyya. Muslim ni mkusanyaji na mwandishi waHadith maarufu sana, alikufa mwaka 365 Hijiriya.

    L

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:34 PM Page L

  • MUTTAQI (Ali Ibn Hussamul-Diin Al-Hindi Al-Muttaqi)Kanzul-Ummal (Hazina ya waja wa Mwenyezi Mungu), mkusanyikomkubwa wa hadith. Hadith zilizomo kwenye kitabu hiki zimewekwa kati-ka mfululizo.

    MUTTAQI (Ali Ibn Hussamul-Diin Al-Hindi Al-Muttaqi)Muntakhab Kanzul-Ummal (hadith zilizoteuliwa kutoka kwenye Kanzul-Ummal) zilizochapishwa pembezoni mwa Musnad Ibn Hanbal, na as-Sader Printing, Beiruti. Al-Muttaqi ni mkusanyaji na mwandishi maarufuwa hadith ambaye aliishi mnamo Karne ya Kumi na Moja, Hijiriya.

    NISABUURI (Ali-Hasan Ibn Ahmad Al-Nisabuuri)Gharaibul - Qurani (fasili juu ya Qurani Tukufu) zimechapishwa pem-bezoni mwa Jami-ul-Bayan ya Al-Tabari (fasili zingine na Al-Tabari) naAl-Matba-ah Al-Meimaneyah, Misri, 1321 Hijiriya. Al-Nasabuuri nimfasili wa Qurani tukufu, alikufa wakati wa karne ya nane Hijiriya.

    NISAI (Ahmad Ibn Shuaib Al-Nisai)Sunnan Al-Nisai (Hadith zilizokusanywa na Al-Nisai), kutoka kwenyeVitabu Sita Sahihi vya hadith vilivyopigwa chapa na Al-Matba-ah Al-Meimaneyah, Misri, 1321 Hijiriya. Al-Nisa-i ni mteuzi na mkusanyaji wahadith maarufu, alikufa 303 Hijiriya.

    RAYYAH (Mahmood Abu Rayyah)Adhwa-a Ala Al-Sunnah Al-Muhamadiyah (miale juu ya hadith za MtukufuMtume (s.a.w.w.) zilizosimuliwa) chapa ya tatu imefanywa na Dar Al-Maarif (Nyumba ya Maarifa), Misri, 1957 AD. Abu Rayyah ni mwandishimaarufu wa zama za leo.

    RAZZI (Fakhrud-Diin Muhammad Ar-Razzi)At-Tafsiir Al-Kabiir (Tafsiri pana za Qurani Tukufu) chapa ya pili ime-fanywa na Al-Matba-ah Al-Sarafiyah, mwaka 1304 Hijiriya. Ar-Razzi nimwanatheolojia na mfasili wa Qurani Tukufu maarufu sana, alikufa

    M

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:34 PM Page M

  • mwaka 606 Hijiriya.

    SAAD (Muhammad Ibn Saad Al-Zuhri, ajulikanaye kama Ibn Saad)Al-Tabaqat Al-Kubra (kitabu maarufu cha historia ya masahaba waMtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wanafunzi wao), kilichapishwa na Dar as-Sader, Beiruti mwaka 1960 AD. Ibn Saad ni mtaalamu wa Historia yaKiislamu maarufu, alizaliwa mwaka wa 168 Hijiriya.

    SHALTUTE (Sheikh Mahmood Shaltute)Tafsiir Al-Qurani (Tafsiri za Qurani Tukufu), kimechapishwa na Dar-Al-Qalam Printing, mwaka 1960 AD. Sheikh Shaltute ni Sheikh maarufumiongoni mwa masheikh wa Al-Azhar).

    SHARAFUD-DIIN (Sayyid Abdul Husein Sharafud-Diin).Al-Murajat (Majadiliano) kilichapishwa na Al-Irfan, Saida, Lebanon,mwaka 1936 AD. Sayyid Sharafud-Din ni mwanatheolojia na mwandishiwa historia maarufu wa zama za leo.

    SHABLANJI (Mumin Ibn Hussam Al-Shablanji)Nurul-Absar (Nuru ya Macho), chapa ya nane ilifanywa na Atif, mwaka1973. AD, Misri. Al-Shablanji ni mkusanyaji maarufu wa Hadith, alizali-wa mwaka 1251 Hijiriya.

    TABARI (Muhammad Ibn Jariir Al-Tabari)History of Messengers and Kings (Historia ya Mitume na Wafalme). Al-Tabari ni mwandishi wa historia, mwanatheolojia na mfasili wa QuraniTukufu maarufu, alikufa 310 Hijiriya. Nukuu zote katika Jz. 2, ambazozilichukuliwa kutoka kwenye historia ya Tabari, zilichukuliwa kutoka Jz.4, chapa ya 4, na Jz. 5, chapa ya 2, iliyochapishwa na Dar Al-Maarif yaMisri.

    TABARI (Muhammad Ibn Jariir Al-Tabari) Jami-ul-Bayan (Ubainifu Mkubwa), Tafsiri ya Qurani Tukufu,

    N

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:34 PM Page N

  • kilichapishwa na Maimaneyah Printing, Misri, mwaka 1321 Hijiriya.

    TABARSI (Ahmad Ibn Ali Ibn Abi Talib At-Tabarsi)Al-Ihtijaji (mazungumzo) kilichapishwa na Al-Naaman Printing, Al-Najaf,Iraq, 1966 AD. At-Tabarsi ni mwanatheolojia maarufu aliyeishi katikakarne ya sita Hijiriya.

    TIRMIDHI (Muhammad Ibn Isa At-Tirmidhi)Sunan At-Tirmidhi mojawapo ya vitabu Sita Sahih vya Hadith. Sehemu yatano ilichapishwa na Al-Fajjalah Printing, Cairo, 1967AD. At-Tirmidh nimteuzi na mwandishi wa hadith maarufu, alikufa 279 Hijiriya.

    WAQIDI (Muhammad Al-Waqidi)Al-Maghazi (uvamizi), kilichapishwa na Oxford Printing. Al-Waqid nimtaalam wa historia Mwislamu maarufu, alikufa mwaka 207 Hijiriya.

    ZUHRAH (Sheikh Muhammad Abu Zuhrah) Al-Imam As-Sadiq, kilichapishwa na Dar Al-Fikr Ak-Arabi (Nyumba yaFikra za Kiarabu zilizoandikwa) Misri. Sheikh Abu Zuhrah ni mwanathe-olojia na mwandishi wa historia wa zama za leo.

    O

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:34 PM Page O

  • UTANGULIZIImam Ali Foundation ilianzishwa kama chama cha kutoa msaada chenyelengo na madhumuni ya kueneza mafundisho ya Uislamu asilia kamaulivyo hubiriwa mwanzo na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kama ulivy-ofafanuliwa na Ahlul-Bait watukufu, watu wa nyumba ya Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) na uzao wake.

    Kitabu hiki Ndugu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni mojawapo yavitabu vizuri vilivyoandikwa na marehemu Muhammad Jawad Chirri.Alifafanua historia ya maisha ya Imam Ali (a.s) na akachanganua masualambali mbali muhimu ya maisha yake, ama wakati wa uhai wa MtukufuMtume (s.a.w.w.) au baada ya kifo chake.

    Imam Ali (a.s) Foundation ilikiona kitabu hiki kuwa na mvuto na manufaakwa wasomaji wa Kiingereza hususan ambapo inafahamika kwambavitabu vichache sana vimeandikwa kuhusu Imam Ali (a.s) kwa lugha yaKiingereza. Tumepata ari ya kukichapisha tena kitabu hiki kama faida yaWaislamu kwa ujumla na pia wasio Waislamu ambao wanataka kujifunzahistoria ya maisha ya mtu wa pili kwa umashuhuri kwenye Uislamu baadaya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

    Toleo la kwanza la kitabu hiki lilikuwa na juzuu mbili zilizo tenganishwa.Ili kurahisisha zaidi namna ya kushika na kusoma, tulipendeleakukichapisha katika juzuu moja.

    Imam Ali (a.s) Foundation inakaribisha maoni yako kuhusu yale yaliyomokwenye kitabu hiki. Kama unataka maelezo zaidi, tafadhali tuandikie.Imam Ali (a.s) Foundation.18th Dhulhija, 1418/16th April, 1998.

    P

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:34 PM Page P

  • KUHUSU MWANDISHI.

    Imam Muhammad Jawad Chirri ni mzalendo wa Lebanon na ni mhitimu(Graduate) wa taasisi ya kidini iliyo maarufu ya Najaf nchini Iraq. Yeye nimwanatheolojia ya Kiislamu, mhadhiri mwandishi na mwanahistoria. Nimwendeshaji wa kipindi cha redio cha kila wiki kiitwacho Islam in Focuskinachotangazwa na WNIC. Katika vitabu vyake vilivyo chapishwa ni:

    Muslim Practice.Islamic TeachingImam Husein, Leader of the Marteyrs.Inquiries About Islam (Maelfu ya maktaba za Marekani wamekitwaakitabu hiki - Kitabu hiki pia kimetafsiriwa katika lugha ya Kiswahili naTaasisi ya Al-Itrah Foundation, kwa jina la Maswali kuhusu Uislamu).Al-Khilafatu Fi Al-Dustous Al Islam (The Calphate in the Islam consti-tution- Arabic).Amiir Al-Muminiin (The leader of Belivers Arabic).

    Imam Chirri alialikwa na Detroit Muslim Community awe kiongozi waowa kiroho. Alisaidia sana katika ujenzi wa Islamic Center of Detroit,mojawapo ya taasisi kubwa sana za Kiislamu - America ya kaskazini. Sasahivi yeye ndiye Mkurugenzi wa Taasisi hii.

    Kazi ya Imam Chirri ilipanuliwa hadi Afrika ya Magharibi. Alipokuwakatika msafara wa kuhadhiri mnamo mwaka 1958, aliweza kuishawishijamii ya Kilebanoni iliyoko Sierra Leone kujenga hospitali ya watoto kamazawadi kwa wazalendo wa nchi hiyo.

    Wakati alipotembelea Mashariki ya kati mwaka wa 1959, mwandishi huyualilishughulikia tatizo la Kiislamu la siku nyingi na kufaulu kupata ufum-buzi wake. Kwa kipindi cha miaka elfu moja, Waislamu walikuwawamegawanyika katika makundi mawili; Sunni na Shiah (wala hakunahata upande moja baina ya hizo pande mbili uliotambua uthabiti wa

    Q

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page Q

  • Rmafundisho ya kundi lingine licha ya makubaliano ya matapo yote mawilikuhusu mafundisho yote ya Qurani Tukufu na hadithi za Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) zilizosimuliwa kwa usahhihi.

    Mwandishi huyu alikutana na marehemu Sheikh mkuu wa Al-Azhar,Sheikh Mahood Shaltut mnamo tarehe 1, Julai, 1959. Alizungumza nayekuhusu suala hilo muhimu. Katika hitimisho la mazungumzo SheikhShaltut alikubali uthabiti wa Tapo la Kiislamu la Shia Jaafariya.Mwandishi huyu alimwomba Sheikh kutangaza usawa baina ya tapo laShia Jaafariya na Sunni. Tangazo (fatwa) hilo lilirushwa hewani nakuchapishwa Julai 7, 1959. Tamko hili lilikuwa la kihistoria na la kwanzala namna yake tangu matapo hayo yalipotengana.

    Moyo wa udugu wa kweli wa Kiislamu unaweza kuwepo tu kwa uelewanowa pande zote miongoni mwa matapo mbali mbali ya Kiislamu. Ni kwamtazamo huu kwamba Mwandishi anawasilisha kitabu hiki, Ndugu yakeMtukufu Mtume (s.a.w.w.). Bila kuwa na haja ya kusema kwambamabishano miongoni mwa matapo mbali mbali ya Kiislamu yanazungukahasa zaidi kwenye historia ya Imam huyu mashuhuri. Ufahamu wa kwelina wa hakika wa nafasi yake katika Uislamu utawafanya Waislamu waele-kee kwenye undugu wa kweli zaidi.

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page R

  • Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 1

  • 2Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume (s.a.w.w.)

    UTANGULIZI.Wamarekani ambao wanatambua Uislamu na Waislamu kwa wastani niwachache, na wale wanaojua wingi wa matapo ya Kiislamu na kwambamiongoni mwa Waislamu wapo Sunni na Shia ni wachache zaidi.

    Hata hivyo, matukio ya mapinduzi ya Iran yaliyotokea mwaka wa 1978-79,yaliweka habari za Waislamu kwa ujumla na hususan Waislamu wa mad-hehebu ya Shia kwenye kurasa za mwanzo za magazeti ya Magharibi naMashariki. Hii ni kwa sababu Waislamu wa madhehebu ya Shia ni wengizaidi miongoni wa Waislamu nchini Iran. Magazeti ya Marekani yal-izungumzia habari kuhusu Shia kwa ufupi, na mara nyingi zilikuwa poto-fu. Hali hii iliimarisha zaidi msimamo wangu wa kuwepo haja ya kitabucha Kiingereza kitakachoshughulikia tapo la Kiislamu la Shia chenyemaelezo ya kina yaliyotegemezwa kwenye utafiti makini.

    Kwa vile hii ni madhehebu ya Imam Ali, mtoto wa Abu Talib, ingefaa kum-chunguza huyu Imam mashuhuri na historia yake ya kisiasa na kidini.Kwani hii tu ndio njia pekee ambayo tunaweza kuelewa msingi wa mad-hehebu hii.

    Kutosheleza haja hii, niliandika kitabu na kukiita Ndugu yake MtukufuMtume (s.a.w.w.). Hii ni lakabu aliyopewa Imam Ali ya kiupekee naMtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambaye alimfanya kuwa ndugu yake kutokamiongoni mwa Waislamu wote. Kamwe hakujichagulia mtu mwingineyeyote kama ndugu yake.

    Lakabu hii ilikuwa ya thamani mno ndani ya moyo wa Imam; kwani kilaalipojitambulisha hadharani alikuwa na desturi ya kutaja udugu wake kwaMtukufu Mtume (s.a.w.w.) baada ya kutamka utumwa wake kwaMwenyezi Mungu Muweza wa Yote. Na ilikuwa ni jambo la kupendezakwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kumuita Ali Ndugu yangu.

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 2

  • 3Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    Waislamu wanakubaliana kwamba Imam Ali alikuwa na sifa bainifuambazo hapana mtu mwingine alikuwa nazo miongoni mwa Waislamu.Yeye kutoka miongoni mwao ndiye tu mtu aliyelelewa na Mjumbe waMwenyezi Mungu tangu siku za utoto wake. Alilelewa naye kufuatana nakiwango cha maadili yake; halafu akamteua yeye kutoka miongoni mwawatu wote kuwa ndugu yake.

    Wanachuoni wa Kiislamu, Sunni na Shia wanakubaliana kwamba Alialikuwa na ujuzi mkubwa sana wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu (Qurani)na mafundisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) miongoni mwa masahabawote. Ali alikuwa hazina kubwa ya chanzo cha hekima na fasaha mno kati-ka kuongea, mlinzi mkubwa zaidi wa Imani, imara zaidi katika kudumishahaki na mwenye kufanya juhudi kubwa katika njia ya Mwenyezi Mungu.Sifa hizi ni kigezo cha sifa bainifu za Kiislamu, kwani Qurani Tukufuimetangaza kwamba Mwenyezi Mungu hupendezwa na wale wanaojitahi-di katika njia Yake kuliko wadumaavu; kwamba wale wajuao na wasiojuahawako sawa, na hutamka kwamba ubora zaidi miongoni mwa watu mbeleya Mwenyezi Mungu ni wale wamchao Mwenyezi Mungu zaidi.

    Hii huweka wazi kabisa kwamba Sunni na Shia si tu wanakubalianakwenye kanuni zote za Kiislamu ambazo zimetajwa kwenye QuraniTukufu au kwenye Hadith sahihi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w) lakini piawanakubaliana kuhusu nafasi ya Imam Ali kidini na kielimu katikaUislamu. Kwa hiyo Sunni na Shia wanapotofautiana hufanya hivyo kisiasatu; kwani hutofautiana kwenye vipengele vya siasass na si nafasi ya ImamAli kidini na kielimu katika Uislamu.

    Wakati wanakubaliana kwamba Ali alikuwa Khalifa mwadilifu ambayealipata mamlaka kwa kuchaguliwa na watu, hawakubali kwa nyongeza yahili iwapo alikuwa ni Khalifa kwa kuteuliwa na Mtukufu Mtume(s.a.w.w.). Wale wasioamini kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimteuaAli kama mrithi wake wanadhani kwamba nadharia ya uteuzi wa MtukufuMtume (s.a.w.w.) wa Imam Ali ni nadharia ya utawala wa kurithiana kupi-

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 3

  • 4Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    tia undugu wa damu. Wale wanaoamini kwamba Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) alimteua Imam kama mrithi wake wanasema kwamba nadhariaya Imam Ali kuteuliwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni kinyume na nad-haria ya utawala wa kurithiana.

    Waislamu pia hawakubaliani juu ya wajibu wake wa kisiasa/kidini katikahistoria ya Uislamu kama mwanasiasa mweledi. Ambapo wanakubalianajuu ya mshikamano wake kwenye kanuni ya haki kamili na uimara wakekatika kutekeleza sheria za Kiislamu kwa moyo wote na kwa makini, nabaadae wakawa hawakubaliani kwenye busara ya msimamo kama huousiopindika.

    Kuna jambo lingine muhimu linalohusu nafasi yake ya kisiasa/kidinikwenye historia ya Kiislamu, yaani; nafasi yake katika kuanzisha dola yaKiislamu. Kipengele hiki hakikutajwa wazi wazi wala hakikuwa suala lamjadala wenye uzito miongoni mwa wanahistoria na wanachuoni wa his-toria.

    Kwa vile Waislamu wanakubaliana kuhusu nafasi ya Imam kamamwanachuo mahiri wa dini, itakuwa ni kuzidisha kiasi mambo yasiyohita-jika kujadili vipengele hivyo vya maisha ya Imam.

    Kwa hiyo, kitabu hiki hakipitii upya historia ya Imam kwa kinaganaga,wala hakizungumzii kuhusu ujuzi wake, ufasaha wake wa kujieleza auhekima yake. Wala hakizungumzii ucha-Mungu wake na msimamo wakekutopenda mambo ya dunia, wala hakizungumzii utendaji wake usiokawaida. Mazungumzo yake yamelenga juu ya nafasi ya Imam ya kisi-asa/kidini katika Uislamu, uhusiano wake wa kiroho na Mtukufu Mtume(s.a.w.w.), na mchango wake katika kuasisi dola ya Kiislamu na kuenezaImani ya Uislamu.

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 4

  • 5Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    Kitabu hiki kinamzungumzia yeye kama Khalifa na kama mwanasiasamweledi. Pia kinazungumzia kile kilichosemwa kuhusu sera yake nauweledi wake kisiasa na sababu zilizosababisha mlundikano wa matatizomengi ambayo yalimzuia kufika kwenye utawala wa amani na wa kudumuzaidi wakati wa siku za ukhalifa wake.

    Hatimaye, kitabu hiki kinazungumzia ukhalifa kama mfumo wa kidini nasiasa, na aina ya ukhalifa ambao unaafikiana na jinsi ulivyo ujumbe waKiislamu. Kwa hiyo, kitabu hiki kina sehemu zifuatazo:

    Imam wakati wa zama za Utume.Imam wakati wa zama za Makhalifa watatu.Imam wakati wa utawala wake mwenyewe.Ukhalifa katika sharia ya Kiislamu, na hitimisho la mjadala.

    Nimejitahidi kugundua uhusiano baina ya matukio ya kihistoria ambayoyalihusisha maisha ya Imam na ambayo yalitokea wakati wa miaka hamsi-ni na tatu tangu kuanza kwa utume hadi mwisho wa ukhalifa wa haki.

    Msomaji anaweza kuona kwamba matukio hayo yaliungana moja nalingine kwa mafungamano imara. Hivyo, yaliunda mlolongo wa sababu naathari, zilizofuatia miongoni mwa hizo ilikuwa ni matokeo ya mfano wake.

    Katika kusimulia matukio ya kipindi kile, sikutegemea tu vyanzo kutokakwenye vitabu vinavyoheshimiwa vya historia, lakini nilijaribu kuongezakwenye vyanzo hivyo, pale ilipowezekana, kile nilichopata kutoka kwenyevitabu vya Sahihi na vitabu vingine vya kutegemewa vya Hadith ambavyovilikuwa na matukio hayo. Hii ni kwa sababu wasomi wengi wa Kiislamuhutegemea zaidi kwenye Hadith kuliko vitabu vya historia, hususan paleambapo Hadith huandikwa kwenye vyanzo sahihi vinavyojulikana, navitabu vingine vinavyotegemewa.

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 5

  • 6Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    Sikujaribu kumzungumzia Imam kama mtu ambaye uhusiano wakemaalum na Mola wake ulimtofautisha yeye na ukamwezesha kufanya miu-jiza na kuleta matukio yasiyo ya kawaida. Bali nilijaribu kumzungumzayeye kama mtu ambaye yupo chini ya kanuni za maumbile, muda namahali, ambaye alijaribu kwa kadiri ya uwezo wake kuhifadhi kanunitakatifu na akaishi kwa kuzizingatia kanuni hizo na kwa ajili ya kanunihizo.

    Ninayo matumanini kwamba kitabu hiki kitachangia kwenye uelewanomzuri na udugu madhubuti miongoni mwa Waislamu. Kwa hakika shaksiaya Imam na historia yake Binafsi ni vitu vinavyotia moyo, na kamaWaislamu wapo tayari kupokea msukumo huo, utawaelekeza kwenyeumoja na mshikamano.

    Kile ambacho kitaandikwa cha kweli kuhusu shaksia ya mtu ambaye ali-teuliwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuwa ndugu yake hakika kitakuwana uwezo wa kuimarisha moyo wa udugu na upendo miongoni mwaWaislamu wote.

    Muhammad Jawad Chirri

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 6

  • 7Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    SURA YA KWANZA.IMAM WAKATI WA KIPINDI CHA UTUME.

    NYUMBA YA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.).

    Waislamu wote huwatukuza watu wa Nyumba ya Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) ambao huitwa Aali Muhammad au Ahlul Bait Muhammad.Msimamo huu ni utekelezaji wa makubaliano kufuatana na maelekezo yaMtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye aliamuru Waislamu kuwaombea watuwa Nyumba yake wakati wowote wanaposwali na kumswalia yeye. Kwakuwaamuru hivyo, kwa kweli aliwataka Waislamu kutenga sehemu kwaajili yao karibu naye. Qurani Tukufu iliagiza kumswalia Muhammad nakumwombea rehema:

    Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamtakia rehma naamani Nabii! Enyi mlioamini, mtakieni rehma na amani kwa wingi.1

    Masahaba wengi walimuomba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) awafundishewao jinsi ya kutekeleza amri hii. Wasimulizi wengi wenye kuheshimikasana (pamoja na Al-Bukhari na Muslim) waliandika kwenye vitabu vyaovijulikanavyo kama Sahih kwamba Kaab Ibn Ujrah alieleza kwambaMtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema Semeni: Mwenyezi Mungu mpeutukufu Muhammad na watu wa Nyumba ya Muhammad, kamaUlivyowapa utukufu watu wa Nyumba ya Ibrahim, Wewe ni Mwenye kusi-fiwa na Mtukufu. Mwenyezi Mungu, Mrehemu Muhammad na watu waNyumba ya Muhammad kama ulivyowarehemu watu wa Nyumba yaIbrahim, kwa hakika Wewe ni Mwenye Kusifiwa na Mtukufu.21 Qurani Tukufu (Sura 33:56).2 Miongoni mwa Wahadith hawa ni: Al-Bukhari, Sahih Al-Bukhari Sehemu ya 6, uk. 101 kwenye kitabu cha fasili yaQurani Tukufu.Muslim, Sahih Muslim, sehemu ya 4, (Kwenye kumswalia Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) baada ya kutangazwa kwa Uislamu). uk. 136.Muhammad Ibn Majah, Sunan Ibn Majah, Juz. 1, hadith na. 904.Al-Tirmidhi, hadith na. 483, sehemu na. I, Hadith zingine zimeandikwa na AbuSaeed, Abu Masood, Talhah na ibn Masood. Wote wanakubaliana na hadith hiyojuu ya Kaab Ibn Ujrah.

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 7

  • 8Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    Alipokuwa anawaelekeza wafuasi wake kuhusu jambo fulani la kidini,Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakuwa akisema kwa matamanio yake yakiBinadamu. Qurani inathibitisha kwamba alikuwa akisema tu yale yaliy-ofunuliwa kwake:

    Wala hatamki kwa matamanio. Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio-funuliwa; Sura ya 53, aya ya 3 -4.

    JE! UTUKUFU HUU NI KWA SABABU YAUNDUGU?

    Inawezekana kuonekana kwamba kujumuisha watu wa Nyumba yaMuhammad katika kumswalia yeye wakati wa Swala ni kwa sababu yauhusiano wao na undugu wa damu. Kama ni hivyo, haitakuwa ni kulinganana mtazamo wa mafundisho ya Kiislamu. Kuwapa wao hadhi ya kipekeenamna hiyo kwa sababu ya uhusiano wao wa kindugu na Muhammad nikutetea ubora wa kifamilia na inapingana na kanuni zifuatazo:

    Mbele ya Mwenyezi Mungu watu wote wapo sawa, kwani Qurani Tukufuilitangaza:

    Hakika aliye mtukufu ziadi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyoaliye mchaMwenyezi Mungu zaidi katika nyinyi. Qurani tukufu,Sura ya 49:13.

    Mwenyezi Mungu hamuadhibu au kumpa thawabu mja wake kwa dhambiau matendo mema ya wazazi wake au ndugu zake wa karibu au wa mbali.

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 8

  • 9Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    Kutoka kwenye Qurani Tukufu:

    Na iogopeni siku ambayo mzazi hatamfaa mwana, wala mwanahatamfaa mzazi lolote. Qurani, Sura 31:33.

    Mwenyezi Mungu hamuadhibu au kumpa thawabu mwanadamu kwa kili-cho nje ya uwezo wake na bila hiyari yake. Kuwa na uhusiano au kutokuwana uhusiano wa damu na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) si jambo la hiyari yamtu Ibnasfi. Hakuna hata mmoja wetu aliyefanya uchaguzi kabla ya kuza-liwa kwetu kuwa na uhusiano au kutokuwa na uhusiano wa kindugu nafamilia maalum, utaifa au jamii. Kwa hivyo, ingekuwa vigumu sana kwaWaislamu kuamini kwamba wawajumuishe ndugu zake Muhammad kati-ka swala kwa sababu tu wao ni ndugu zake.

    Ni kwa Sababu ya Ubora Wao Si kwa Sababu ya Kurithiana Kwao.

    Kuondoa mgongano huu ulio wazi, ni muhimu kujua kwamba neno AaliMuhammad, ambalo linarudiwa mara kwa mara kwenye Swala za kilasiku, halijumuishi ndugu zake wote. Ni idadi ndogo tu miongoni mwandugu zake ambao wamejumuishwa. Kama wote wengejumuishwa,ingekuwa ubaguzi wa kiukoo au kikabila kwa sababu wengi wao hawaku-fuata njia ya Muhammad, na kuwaweka juu ya wengine ni kutetea uborawa kiukoo. Kuwa ndugu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakumaanishikukubaliwa na Mwenyezi Mungu. Wala hakuwapatii nafasi ndugu zakePeponi au kuwahakikishia kwamba hawataadhibiwa na Mwenyezi Mungu.Kwa mujibu wa mafundisho ya Kislamu, Mwenyezi Mungu ameumbaPepo kwa ajili ya yeyote atakayemtii Yeye, na mahali pa adhabu kwa ajiliya yeyote ambaye hatamtii Yeye, bila kujali uhusiano wa kifamilia, utaifaau jamii. Hata Qurani inayo sura ambayo inamsema vibaya Abu Lahab,ambaye alikuwa ami yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 9

  • 10

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    Imeangamia mikono ya Abu Lahab na yeye pia ameangamia.Hayatamfaa mali yake wala alivyovichumaQurani Tukufu, Sura111:2-3.

    Ukweli ni kwamba neno Aali Muhammad maana yake ni walioteuliwa tumiongoni mwa ndugu wa Muhammad. Hawa watu walioteuliwa hawaku-teuliwa au kutukuzwa kwa sababu ya uhusiano wao wa kindugu naMuhammad, bali wameteuliwa kwa sababu ya uadilifu wao.

    Waliishi maisha halisi ya Kiislamu, walifuata maelekezo ya QuraniTukufu na ya Mjumbe, na kamwe hawakuachana na vitu hivyo kwamaneno au vitendo. Mwenyezi Mungu anapotufahamisha sisi kwenyeKitabu Chake kwamba mbora zaidi miongoni mwa viumbe VyakeBinadamu ni wale waadilifu sana, na Mjumbe Wake anatuamuru sisikuwatukuza watu wa nyumba yake wakati tunapomtukuza yeye, tuna-maanisha kwamba wao ndio waadilifu zaidi baada ya Mtukufu Mtume(s.a.w.w.).

    Kama hawangekuwa hivyo, hawangestahiki utukufu kama huo wa pekee,na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hangetuelekeza sisi kuwatukuza wao wakatiwowote tunapolitukuza jina lake. Kufanya vinginevyo haingelingana naQurani Tukufu. Hivyo, kwa kutuamuru sisi kuwaswalia wao wakatiwowote tunapomswalia yeye, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa kwelialikuwa anatufahamisha sisi kuhusu ubora wao wa hali ya juu, kwambawao ni watiifu sana kwa Mwenyezi Mungu na Mjumbe Wake.

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 10

  • 11

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    KUMBUKUMBU HUTHIBITISHAUBORA WAO.

    Waislamu wote wanakubaliana kwamba Ali, Binamu yake MtukufuMtume (s.a.w.w.) ambaye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimteua kuwandugu na mkewe Fatimah (mama wa nuru), mtoto kipenzi cha Mjumbe waMwenyezi Mungu, na watoto wao wawili, Al-Hasan na Al-Husein, wana-tokana na watu walioteuliwa wa Nyumba ya Muhammad na kwambawanajumuishwa katika Swala tunapomswalia yeye. Sifa za kiwango chajuu za ndugu wa Muhammad walioteuliwa ndio sababu kubwa kwa waokupewa utukufu huu wa pekee.

    Imam Ali alisimama juu ya wenzake wote, baada ya Mtukufu Mtume(s.a.w.w.). Alikuwa mfuasi imara sana wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu.Hakusita kujitolea maisha yake kwa ajili ya kutangaza Uislamu. Wasomajiwa historia wanaweza kutambua kwa urahisi kwamba Imam Ali alikuwamtetezi mkuu wa Uislamu na mfuasi imara wa hukumu zake.

    Msimamo wa Imam Ali kuhusu uwezo Binafsi na heshima ulikuwa wapekee. Wakati wowote alipolazimika kuchagua baina ya kushikamana namaadili yake, na starehe za maisha ya dunia, bila kusita alichagua chamwanzo maadili yake. Historia inathibitisha kwamba alipendeleakupoteza uongozi wa Ulimwengu wa Waislamu kuliko kukubali shartiambalo yeye hakuliamini. Alipewa uongozi huu kwa matarajio kwambaangeahidi kufuata Kitabu cha Mwenyezi Mungu, maelekezo ya Mjumbe,na suna za Makhalifa wawili wa mwanzo yakosekanapo maelekezo yaQurani na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Alijibu:

    Nitafuata Kitabu cha Mwenyezi Mungu na maelekezo yaMjumbe Wake; na yakosekanapo mafundisho dhahiri yavyanzo hivi viwili, nitajitahidi kadiri ya ujuzi na uwezowangu.3

    3 Ibn Atheer, Al-Kamil (historia kamili) sehemu ya 3, uk. 35.

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 11

  • 12

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    Ujuzi wake ulikuwa unashangaza kwa kina chake na ukubwa wake.Hotuba na mihadhara na maneno yake yaliyomo kwenye Nahjul Balaghah(njia ya Ufasaha) ni mambo yanayothibitisha uhakika wa taarifa ya usemiwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.):

    Mimi ni Jiji la Elimu, na Ali ni Lango lake, kwa hiyo, yey-ote anayetaka kuingia katika Jiji lazima apitie kwenyeLango.4

    Kumbukumbu ya watu wengine watatu wenye sifa Binafsi wa Nyumba yaMuhammad, Fatimah na watoto wake wawili Hasan na Husein, inaoneshakwamba walikuwa watumishi waaminifu sana wa Uislamu.

    Hadith (nyingi) sahihi zimezungumza kuhusu heshima na sifa zao kamawashirika wa kudumu wa uadilifu na haki. Zayd Ibn Arqam alisema kwam-ba Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alisema kumwambia Ali, Fatimah,Hasan na Husein:

    Niko katika amani na yeyote yule ambaye yuko katikaamani nanyi; na niko katika hali ya uadui na yeyote yuleambaye ni adui yenu.5

    Abu Huraira alisimulia kwamba, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alisema:Yeyote anayempenda Al-Hasan na Al- Husein ananipenda mimi na yuleanayewachukia wao ananichukia mimi.6

    Hubshi Ibn Janadah alisema kwamba alimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)akisema: Ali anatokana na mimi na mimi natokana na Ali na hapana mtuanayeniwakilisha mimi isipokuwa Ali.7

    Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakutaka kumtofautisha Ali kwa sababu tualikuwa na uhusiano wa kindugu naye. Al-Abbas (ami yake) na watu4 Al-Hakim, Al-Mustadrak, sehemu ya 3, uk. 26.5 Ibn Majah, Sunan Ibn Majah, hadith Na. 145.6 Ibid, Hadith Na. 143.7 Ibid, Hadith Na. 119.

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 12

  • 13

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    wengine na ukoo wa Hashim, pamoja na Jafar (ndugu yake Ali) wote nindugu zake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Wote hawa wangekuwa na sifazinazostahiki kumwakilisha yeye. Lakini alisema; Hapana yeyoteanayeniwakilisha mimi isipokuwa Ali.

    Wakati fulani Muawiyah alikuwa anamlaumu Ali mbele ya Saad Ibn AbuWaqass. Saad akamwambia: Nilimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)anamwambia Ali: Wewe kwangu ni kama Haruna alivyokuwa kwa Musa.Lakini hapatakuwepo na Mtume mwingine baada yangu.8

    Hivyo, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimpa Ali nafasi ya karibu baada ya ileyake, kwani nafasi ya Haruna ilikuwa inafuata baada ya ile ya Musa.

    Al-Bukhari ameandika kwenye Sahih yake kwamba Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) alisema: Fatimah ni kiongozi wa wanawake wa Peponi.9

    Hakuna mtu anayeingia Peponi bali kwa wema wake, na yeyote anayein-gia Peponi ni mtukufu mbele ya Mwenyezi Mungu. Kama Fatimah ni kion-gozi wa wanawake wa Peponi, lazima atakuwa ni mwenye wema zaidi namwanamke mtukufu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu.

    Al-Hakim ameandika kwenye Mustadrak yake kwamba Abu Dhar (sahabamashuhuri wa Muhammad ambaye ukweli wake unajulikana kwaWaislamu) alisema kwamba; Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Mfanowa watu wa Nyumba yangu ni kama ule wa Safina ya Nuhu. Yeyotealiyeingia humo alikuwa salama, na yule aliyeshindwa kuingia humo alik-ufa maji .10

    8 Ibn Majah, hadithi Na. 121.9 Al-Bukhari, Sahih Al-Bukhari, sehemu ya 5, (Sura ya utofautishaji wa nduguzake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)) uk. 25.10 Al-Hakim, Sahih Al-Mustadrak, sehemu ya 3, uk. 151.

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 13

  • 14

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliwaamuru Waislamukuwafuata ndugu zake wateule. Kwa hiyo ndugu zake Muhammad wanafa-hamika kuwa kundi la ukweli, lililotofautishwa kwa sababu ya sifa njemana kazi kwa kuwa wanalo daraja miongoni mwa waja waadilifu sana waMwenyezi Mungu.

    KWA NINI WAO WALIKUWA NI BORAKIASI HICHO?

    Kwa nini hawa watu wa Nyumba ya Muhammad waliwazidi watuwengine, walio Waarabu na wasio Waarabu kwa uadilifu?

    Mifano katika historia.

    Kuelewa sababu, tunapaswa tukumbuke kwamba yale yaliyotokea kwenyeNyumba ya Muhammad hayakuwa yasiyowahi kutokea katika historia yaUtume. Yapo matukio mengi ya aina hiyo. Mwenyezi Mungu Muweza waYote alimfanya Haruna kuwa msaidizi wa kaka yake Musa katika ujumbewake wa kimbinguni. Hakumpa mtu yeyote heshima hii kutoka kwa BaniIsrael. Hii ilikuwa ni kwa sababu ya kuwa na sifa stahiki za kiwango chajuu na jibu la ombi la Musa, kama ilivyotajwa kwenye Qurani Tukufu:

    (Musa) akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Nikunjulie kifua changu,na unifanyie wepesi kazi yangu, na ulifungue fundo lililo katika ulimiwangu, wapate kufahamu maneno yangu. Na nipe waziri katika watuwangu, Haruna, ndugu yangu. Kwake yeye niongeze nguvu yangu. Na

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 14

  • 15

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    umshirikishe katika kazi yanguQurani Tukufu, 20:25-32.

    Nabii Ibrahim alimwomba Mola Wake Mlezi kuwafanya baadhi ya uzaowake kuwa ma-Imam wa watu. Mwenyezi Mungu alimkubalia ombi lakena Akaahidi kuwafanya Maimam kutoka kwenye uzao wake bila kuruhusuyeyote aliye muovu kupata cheo hicho cha juu. Kutoka katika QuraniTukufu tunasoma:

    Na tulimtunukia Ibrahim Ishaqa na Yaqub. Na tukajaalia katikadhuriya wake unabii na Kitabu na tukampa ujira wake katika dunia,naye hahika katika Akhera bila ya shaka ni katika watu wema.Qurani Tukufu, 29:27.

    Pia Mwenyezi Mungu amechagua, pamoja na ndugu zake Ibrahim, nduguzake Imran na akawapendelea zaidi ya wengine:

    Hakika Mwenyezi Mungu alimteua Adamu na Nuhu na kizazi chaIbrahim na kizazi cha Imran juu ya walimwengu wote. Ni wazao waokwa wao; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia na Mwenyekujua. Qurani Tukufu, 3:33-34

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 15

  • 16

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    Zakaria aliomba kwa Muweza wa Yote apewe mtoto mwadilifu. MwenyeziMungu alijibu ombi lake, na Malaika wakampa habari njema:

    Pale pale Zakaria akamwomba Mola wake Mlezi, akasema: Molawangu Mlezi! Nipe kutoka kwako uzao mwema. Wewe ndiyeunayesikia maombi. Alipokuwa kasimama chumbani akiswali,Malaika akamnadia: Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria Yahya,atakayekuwa mwenye kusadikisha neno litokalo kwa MwenyeziMungu na ni bwana na mtawa na Nabii kwa watu wema.QuraniTukufu, 3:38-39Kwa mujibu wa aya hizi Utume uliotangulia ule wa Muhammad ulichukuamkondo huo huo. Kutoka miongoni mwa uzao na ndugu zao hawa Mitumewapo watu waliochaguliwa ambao walifika kiwango cha juu sana chauchaMungu na kwa hiyo walistahili kupewa mamlaka na MwenyeziMungu.

    Kwa nini Mwenyezi Mungu Aliwapa Manabii hao Watoto na Nduguwenye sifa bora kama hao?

    Mwenyezi Mungu Muweza wa yote aliwaumba watu miongoni mwandugu na uzao wa Mitume hawa kwa kuitika na kujibu maombi yao aukama zawadi zao kwa jitihada zao katika kueneza ujumbe wa MwenyeziMungu. Kama Mitume wengine, Muhammad (s.a.w.w.) alipewa ndugu nakizazi wasio wa kawaida kama zawadi kwa jitihada zake katika kumtu-mikia Mwenyezi Mungu na majibu kwa maombi yake. Alituamuru sisi

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 16

  • 17

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    tuseme: Mwenyezi Mungu Mtukuze Muhammad na watu wa Nyumbayake, na aliomba katika nyakati kadhaa kwa ajili ya utakaso wa watuhawa wa Nyumba yake.

    Al-Hakim anasimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimfunika Ali,Fatimah, Hasan na Husein kwa nguo na akaomba kwa kusema:Ewe Mwenyezi Mungu, hawa ndio watu wa familia yangu. NinakuombaWewe umtukuze Muhammad na familia ya Muhammad.

    Katika kujibu ombi lake maneno yafuatayo yaliteremshwa:

    Mwenyezi Mungu anataka kuwaondoleeni uchafunyinyi na kuwafanyeni watu wa familia ya Muhammadwasio na dosari.11

    Hivyo, ilikuwa kawaida kuwepo ndugu na uzao wa Muhammad wana-mume na wanawake wenye sifa bora za kiwango cha juu zaidi cha uadili-fu. Kinyume chake kama watu wa aina hii wasingekuwepo miongoni mwandugu zake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ingelikuwa ni jambo lisilo lakawaida kabisa. Mwenyezi Mungu aliwatukuza Ibrahim, Musa Zakaria naMitume wengine, kwa kuwaumbia katika uzao na ndugu zao watu wenyesifa bora zaidi, na kuwapendelea zaidi ya watu wengine. Kwa nini basiasimtukuze Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Wake wa mwisho na wa muhimuzaidi kwa kumuumbia miongoni mwa uzao wake na ndugu zake watu kad-haa wenye sifa bainifu kwa kiwango cha juu zaidi?

    Malipo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)

    Qurani Tukufu inaweka wazi kwamba kuwapenda ndugu zakeMuhammad (s.a.w.w.) ni wajibu wa Kiislamu. Mwenyezi Mungu alimwa-muru Muhammad (s.a.w.w.) kuwaambia Waislamu kumzawadia yeye kwa

    11 Al-hakim, Al-Mustadrak, sehemu ya 3, uk. 148.

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 17

  • 18

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    kuwapenda ndugu zake wa karibu, kwa sababu ya kutimiza ujumbe wakewa kimbinguni,

    Hayo ndiyo aliyowabashiria Mwenyezi Mungu waja wake walioami-ni na wakatenda mema. Sema; Sikuombeni malipo yoyote kwenu ilamapenzi yenu kwa ndugu zangu wa karibu. Na anayefanya wematutamzidishia wema. Hakika Mwenyezi Mungu ni MsamehevuMwenye shukrani.Qurani Tukufu 42:23

    Mwenyezi Mungu anamwambia Muhammad kuwajulisha Waislamu wotekwamba malipo pekee anayoyataka kwa ajili ya kutimiza ujumbe wake wakiMungu ni yale ya Waislamu kuwapenda ndugu zake. Hii ni kwa sababutu kwamba watu hao (ndugu zake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni watiifumno kwa Mwenyezi Mungu na waja Wake wapendwa sana miongoni mwaWaislamu.

    Kwa kumuagiza Mtukufu Mtume Wake (s.a.w.w.) kufanya hivyo, kwakweli aliwaamuru Waislamu kuwatukuza hao ndugu wateule waMuhammad (s.a.w.w.), waweke matumaini yao kwa wateule hao, na kufu-ata njia wanayopita wao.

    Kwa kufuata amri hii ya mbinguni Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaambiawafuasi wake wote kuwapenda wateule hao. Alisema kwamba yeye hanauadui na yeyote asiye adui yao, na kwamba yeye yu vitani na yeyoteanayewapiga vita wao. Aliwafikiria wao kuwa sawa na ile safina ya Nuh.Yeyote aliyepanda humo alisalimika, na yeyote aliyeshindwa kupandahumo aliangamia.

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 18

  • 19

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    Nyumba ya Muhammad (s.a.w.w.) inaweza kuwa njia ya kuwaunganishaWaislamu. Muungano huu unaweza kutambulika pale ambapo Waislamuwatachukua msimamo ambao Mwenyezi Mungu na Mtukufu Mtume Wake(s.a.w.w.) walioutaka wachukue kuhusu wateule hawa. Haingekuwa sahihikwa Waislamu kumtenganisha Muhammad na watu wa Nyumba yakeambapo yeye mwenyewe alitaka kuunganishwa nao. Huu ni uthibitishoulio wazi alipoelekeza kwamba wafuasi wake wanaunganishe jina lake nahao ndugu zake wateule wakati wowote walipomswalia, ama wakati waSwala zao za kila siku au nje ya Swala zao.

    * * * * *

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 19

  • 20

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    SURA YA PILI.WATU WA NYUMBA YA MUHAMMAD.

    Kwa kutegemea juu ya makubaliano ya kimya kimya miongoni mwaWaislamu, tuliwachukulia Imam Ali, mke wake Fatimah na watoto waowawili Hasan na Husein kuwa ni watu wa Nyumba ya Muhammad(s.a.w.w.) iliyobarikiwa. Ushahidi wa kutegemewa zaidi katika jambo hilini maneno ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe alipozungumzakuhusu Ahlul Bait Muhammad au Itrah wake. Taarifa ya maneno yaMtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusu suala hili inaeweza kuainishwa katikanamna mbili:

    Hadith zenye maelezo ambayo yanatofautisha Nyumba ya Muhammad(s.a.w.w.) na wengine ambao wangetenganishwa kwa maelezo hayo hayo.

    Hadith zenye kuwataja watu hawa wateule.

    HADITHI ZENYE MAELEZO.

    Kutoka kwenye aina ya kwanza ni kama ifuatayo:Jabir Ibn Abdullah, sahaba maarufu alisimulia kwamba Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) wa Mwenyezi Mungu amesema:

    Enyi watu, nimewaachieni vitu ambavyo kama mkivifuata, ham-tapotea kamwe; Kitabu cha Allah na watu wa Nyumba yanguambao ni Itrah wangu (ndugu wa karibu na kizazi changu.12

    Zayd Ibn Arqam, sahaba maarufu wa Muhammad, alisimulia kwambaMtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: 12 Al-Tirmidhi; Sunan Al-Tirmidhi, sehemu ya 5, uk. 328 (hadith na. 3874).

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 20

  • 21

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    Nimewaachieni vitu ambavyo kama mkivishikilia hamtapoteabaada yangu. Kitabu cha Mwenyezi Mungu, kamba iliyonyookakati ya Mbingu na Ardhi na watu wa Nyumba yangu ambao niItrah wangu. Hakika, (Kitabu cha Mwenyezi Mungu na watu waNyumba yangu) havitatengana mpaka viungane nami Siku yaHukumu. Tahadharini jinsi mtakavyo jihusisha navyo baadayangu.13

    Zayd Ibn Thabit alisimulia kwamba Mtukufu Mtume Wake wa MwenyeziMungu amesema:

    Ninawaachieni miongoni mwenu warithi wawili: Kitabu chaMwenyezi Mungu; kamba iliyonyooka baina ya Mbingu naArdhi, na watu wa Nyumba yangu (ambao ni Itrah). Hakika, vituviwili hivyo (Kitabu na Itrah) havitaachana hadi Siku yaHukumu.14

    Zayd Ibn Arqam alisimulia tena kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) waMwenyezi Mungu amesema mnamo siku ya Ghadir Khum:

    Hivi karibuni mimi nitaitwa na Mwenyezi Mungu, na nitaitikia wito huo.Hakika, nimewaachieni vitu viwili vya thamani kubwa sana. Kimojawapokati ya vitu hivi ni kikubwa zaidi kuliko kingine: Kitabu cha MwenyeziMungu, na Itrah wangu watu wa Nyumba yangu. Tahadhari jinsimtakavyo jihusisha navyo baada yangu. Havitaacha hadi Siku yaHukumu.

    Halafu akasema:

    13 Al-Tirmidhi, Sunan al-Tirmidhi sehemu ya 5, uk. 329 (hadith Na. 3876).14 Imam Ahmad alisimulia kwenye Musnad yake kutoka vyanzo viwili vyakutegewa, sehemu ya 5, uk. 181.

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 21

  • 22

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    Hakika Mwenyezi Mungu ni Mawla (kiongozi) wangu na mimini Mawla (kiongozi) wa kila muumini. Halafu akanyanyuamkono wa Ali na akasema: yeyote ambaye mimi ni Mawla wakena Ali ni Mawla wake. Mwenyezi Mungu, Mpende yule anayem-penda yeye na mghadhibikie yule anayemfanyia yeye uadui.15

    Kwa hiyo, watu wa Nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni wale ambaowana sifa zifuatazo:

    Kuwa Itrah wa Muhammad. Itrah wa mtu ni ndugu zake wa karibu (kwakuzaliwa) na dhuriya wake. Kwa ufafanuzi huu, wake zake MtukufuMtume (s.a.w.w.) na masahaba wake ambao si wa ukoo wa Hashim wame-tengwa.

    Uadilifu wa kiwango cha juu sana. Watu wa Nyumba ya Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) wameelezewa kwenye hadith hizi kama washirika wa kweli waQurani ambao kamwe hawataachana nayo. Hivyo wanamume nawanawake wasio wacha-Mungu hawastahiki kuwa kwenye Itrah, wawe niBani Hashimu au wasiwe Bani Hashimu.

    Kuwa na kiwango cha juu sana cha ujuzi wa Yale yaliyomo kwenyeQurani Tukufu na Mafundisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Waleambao ujuzi wao wa dini ni mdogo huondolewa, hata kama ni ndugu wakaribu sana wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Wanalazimika kwa kukosakwao ujuzi kuangukia kwenye kutokukubaliana na Qurani Tukufu, kwamakusudi au bila kukusudia. Watu wa Nyumba iliyobarikiwa kwa mujibuwa Hadith, wao wako salama dhidi ya kutokukubaliana na Kitabu chaMwenyezi Mungu. Usalama wa aina hii hauwezi kuwepo bila ya ujuzi wakina wa Qurani na mafundisho yote ya Kiislamu.

    Kukubaliana wenyewe wao kwa wao. Wanapokuwepo watu au makundiya watu yanayopingana yenyewe kwa wenyewe, baadhi yao lazima15 Al-Hakim, kwenye Sahih yake, Al-Mustadrak, sehemu ya 3, uk. 109.

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 22

  • 23

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    watakuwa wamekosea na kutokubaliana na Qurani Tukufu. Kwa vile watuwote wa Nyumba wanakubaliana na Qurani Tukufu, lazima wao wenyewekwa wenyewe wawe katika makubaliano kamili.

    Kuwa na Yakini katika ujuzi wote wa kidini. Kwa hili, wanachuo waKiislamu ambao tunawaita Mujtahidi, ambao wana uwezo wa kuendeshautafiti wa kidini na uundaji wa rai zao, wanaondolewa, hata kama ni waukoo wa Hashim (wanaohusiana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kuelewahili zaidi, nukta chache lazima zitajwe:

    Tunapojaribu kujua hukumu za Kiislamu za matendo ya ibada na yasiyo yaibada, ushahidi wetu mkubwa hutoka kwenye Qurani au kutoka kwenyeHadith za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Wakati tunapokuta maelekezobayana ya Qurani kuhusiana na suala fulani, ujuzi wetu hufikia kiwangocha yakini imma tuwe wanachuoni wa Kiislamu au maamuma. Kama hatu-pati maelekezo ya wazi ya Qurani, tunatafuta kutoka kwenye Hadith zaMtukufu Mtume (s.a.w.w.). Baadhi ya Hadith ziko wazi katika uelekezajiwake na zimesimuliwa na masahaba wengi sana. Tena, ujuzi wetu kupitiakwenye aina hii ya Hadith hupata yakini.

    Tatizo ni kwamba Hadith za aina hii si nyingi sana, na zilizo nyingi zimes-imuliwa na sahaba mmoja au wawili au wachache sana. Kupitia kwenyeHadithi hizi, ujuzi wetu kuhusu hukumu ambazo tunajaribu kuzijua,kamwe hazifikii kiwango cha uhakika kwa sababu sahaba mwasilishajihakuisimulia kwetu moja kwa moja, kwa sababu haishi katika wakati wetu,wala hakuandika Hadith hiyo kwenye kitabu.

    Mtu alipokea Hadith kutoka kwa sahaba. Na yeye akamsimulia mtumwingine na kuendelea hivyo. Baadaye, Hadith hizo ziliandikwa kwenyekitabu baada ya kupita kwenye mikono ya watu wengi. Hivyo, ujuzi wetukupitia Hadith za aina hii, ungekuwa hasa zaidi wa kubahatisha. Kunasehemu zingine ambapo maelekezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yames-imuliwa lakini hayapo bayana au katika njia mbili zinazopingana. Katika

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 23

  • 24

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    hali kama hiyo, hitimisho linaweza kutolewa tu na wanachuo weledi aumujitahidi.

    Hitimisho lililofikiwa na maoni yaliyoundwa na wanachuo kwenye haliyoyote katika hizo zilizotajwa hapo juu zaidi hasa ni la kukisia. Kwakawaida hawafiki upeo wa uhakika wala hawakubaliani kwa yakini naKitabu cha Mwenyezi Mungu.

    Uwezekano wa kutokukubaliana ni mkubwa sana, chukulia tu maoni yaupande mmoja katika kila suala. Kama tukifikiria maoni ya pande mbilizinazopingana za wanachuo wawili, tunakuwa na uhakika kwamba mmojawapo hakubaliani na Qurani Tukufu kwa sababu maoni ya pande mbiliyanapingana, na Qurani haiwezi kukubaliana na rai mbili zinazopingana.

    Kutokana na hili, inakuwa dhahiri kwamba Mujitahid ima wa ukoo waHashim au asiye wa ukoo wa Hashim, hawajumuishwi katika jamaamakhususi wa Nyumba ya Muhammad. Hii ni kwa sababu ujuzi waMujitahid hasa zaidi ni wa kukisia na katika hali nyingi haukubaliani namafundisho halisi ya Qurani, ambapo ujuzi wa watu wa Nyumbaunakubaliana kwa usalama kabisa na Kitabu cha Mwenyezi Mungu.

    Hii ni kwa sababu Hadith zilizotajwa kwenye kurasa za nyuma zinaoneshawazi kwamba ujuzi wa watu wa Nyumba ya Muhammad ni ujuzi wauhakika na sio ujuzi wa kukisia; vinginevyo katika hali nyingi wangeten-gana na Qurani Tukufu. Katika hali hii tunapaswa kumfikiria mujitahid,kama vile Abdullah Ibn Abbas, (Binamu yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.),aliyeko nje ya duru ya Nyumba, licha ya ujuzi wake mkubwa wa dini nakuwa ndugu wa karibu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Masahaba wengineambao hawakuwa ndugu wa karibu wa Muhammad wala hawakufikiakiwango cha Ibn Abbas katika ujuzi ni wazi kwamba wametengwa mbali.

    Vipi itawezekana kwa watu wa Nyumba ya Muhammad kupata Ujuziwa Yakini katika Mafundisho yote ya Kiislamu?

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 24

  • 25

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    Kuwa na ujuzi wa yakini wa mafundisho ya dini iliwezekana sana wakatiwa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ni mantiki kabisa kufikiria kwam-ba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimfundisha mwanafunzi wake, kama vileAli, yote yale yaliyomo kwenye Qurani Tukufu na akamfahamisha sheriazote za Kiislamu ambazo zinaweza kufika idadi ya maelfu kadhaa. Ni sawakufikiria kwamba mwanafunzi wa karibu kama huyo aliwafundisha baad-hi ya wanafunzi wake yote yale aliyoyapokea kutoka kwa Mtukufu Mtume(s.a.w.w.). Mawazo haya yanaungwa mkono na ukweli fulani:

    Ali alikuwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) tangu utoto wake hadi MtukufuMtume (s.a.w.w.) alipofariki. Alikuwa mwanafunzi wake mwaminifu namshirika wake wa karibu. Alikuwa mwanafunzi wake mwenye akili namakini ambaye alihudhuria mafunzo yake ya hadharani na ya faraghani.

    Al-Hasan na Al-Husein (wajukuu wa Muhammad na watoto wa Ali) wali-ishi na baba yao kwa miaka mingi. Walikuwa washirika wake wa karibusana, na Waislamu waliotakasika sana ambao walifanana na mwalimu waona mwalimu wake. Hivyo unaweza kusema kwamba ujuzi wa yakinikuhusu Qurani Tukufu na maelekezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)ulikuwa unapatikana na kuwezekana kwa baadhi ya wanafunzi waMuhammad.

    HADITH MAKHUSUSI:

    Hadith mbali mbali za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ziliwataja watu waNyumba ya Muhammad. Muslim ameandika kwenye kitabu chake Sahihkama ifuatavyo:

    Aya ifuatayo ilipoteremshwa wakati wa mjadala baina ya MtukufuMtume (s.a.w.w.) na Wakristo kutoka Najran: Watakao kuhoji katikahaya baada ya kukufikia ilimu hii waambie: njooni tuwaite watotowetu na watoto wenu, na wanawake wetu na wanawake wenu, na nafsizetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu na tuiweke laana

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 25

  • 26

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    ya Mwenyezi Mungu iwashukie wenye kusema uwongo. (Qurani3:61). Mtukufu Mtume wa Allah alimwita Ali, Fatimah, Hasan na Huseinna akasema: Ee Mola wangu! Hawa ni watu wa familia yangu16

    At-Tirmidh, Ibn Manthur, Al-Hakim, Ibn Mardawaih na Al-Bayhaqikwenye Sunan yake, wote hao waliandika masimulizi ya Ummu Salamah,mke wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambamo alisema:

    Ndani ya nyumba yangu, iliteremka Aya ya Qurani (kutoka kwenye Suraya 33): Hakika Mwenyezi anataka kukuondoleeni uchafu, enyiwatu wa nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na kukutakasenisanasana. Ali, Fatimah, Al-Hasan na Al-Husein walikuwa nyumbanikwangu. Mjumbe wa Mwenyezi Mungu aliwafunika na nguo, kisha akase-ma: Hawa ndio watu wa Nyumba yangu. Ee Mwenyezi Mungu waondoleeuchafu na wafanye watoharifu na bila dosari. 17

    Muslim kwenye Sahih yake aliandika kwamba, Aisha alisema:

    Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alitoka njeakiwa amejifunika shuka pana, lililotengenezwa kwa manyoyameusi. Fatimah, Hasan, Husein na Ali walikuja kwa kufuatana,halafu akawafunika kwa hilo shuka lake na akasema: HakikaMwenyezi Mungu anataka kuwaondoleeni uchafu wote kutokakwenu, nyinyi watu wa Nyumba ya Muhammad na kuwatakaseni,msiwe na dosari.18

    Hadith mbili zifuatazo zimeandikwa kwenye Al-Durr Al-Manthur na Al-Suyuti (kwenye Tafsiir yake ya Qurani):

    Abu Al-Hamza (mmojawapo wa masahaba wa Mtukufu Mtume16 Muslim, Sahih Muslim, sehemu ya 15 uk. 176.17 Al-Tirmidhi, Sunan Al-Tirmidhi, sehemu ya 5, uk. 328 (hadith na.3875).18 Muslim, Sahih Muslim, sehemu ya 15, uk. 194.

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 26

  • 27

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    (s.a.w.w.) alisimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliende-lea kwa miezi minane mfululizo huko Madina, kuja mlangonikwa Ali kila wakati wa Swala ya Alfajiri, akiweka mikono yakemiwili kwenye pande mbili za mlango na kusema: Asalat, Asalat(Swala Swala) hakika Allah anataka tu kukuondoleeni uchafuwote kutoka kwenu, nyinyi watu wa Nyumba ya Muhammad, nakuwatakaseni msiwe na dosari19

    Ibn Abbas alisimulia:

    Tumeshuhudia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa kipindi cha miezi tisaalikuja kila siku mlangoni kwa Ali Ibn Abu Talib, wakati wa Swala yaAlfajiri na kusema: Assalaam Aleikum Wa-Rahmatullah Ahlul Bayt (a.s).Hakika Allah anataka kuwaondoleeni uchafu wote kutoka kwenu, watu waNyumba, na kuwatakaseni nyinyi msiwe na dosari.20

    Hadith hizi zinaonesha wazi kabisa kwamba kila mmojawapo wa watuhawa wanne ni mtu wa Nyumba ya Muhammad. Pia Hadith hizi zinawaon-dosha watu wengine wote waliokuwa hai wakati wa Muhammad, wa ukoowa Hashim halikadhalika na wasio wa ukoo wa Hashim, miongoni mwaWaarabu na wasio Waarabu.

    Wateule waliozaliwa baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

    Tamko hili ambalo hata hivyo limewekewa mipaka, haliwaondoi watuwote wa ukoo wa Hashim ambao walizaliwa baada ya wakati wa MtukufuMtume (s.a.w.w.).

    Kundi la kwanza la Hadith tulizozitaja linaonesha kwamba watu waNyumba yake wataendelea baada ya kifo chake na kupitia nchi nyingi kwa

    19 Al-Suyuuti, Al-Durr Al-Manthur sehemu ya 5, uk. 198 (ilisimuliwa na SayyedTaqi Al-Hameem, Al-Ussul Al-Ammah kwa ajili ya Al-Fiqh Al-Muquram, uk.155-156).20 Ibid (yaani kama na. 28)

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 27

  • 28

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    sababu watu wateule, kwa mujibu wa Hadith wataendelea kuwepo almura-di Qurani nayo inaendelea kuwepo.

    Kwa kuwaamuru Waislamu wafuate Kitabu cha Allah na watu wa Nyumbayake, na kwa kutangaza kwamba Ali, Fatimah, Hasan na Husein ni watuwa Nyumba yake, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa kweli alimweka Ali nawanawe wawili kwenye kiti cha uongozi wa umma.

    Hivyo, watoto wawili wanaume hawakuhitaji kuteuliwa na baba yao, naHusein hakuhitaji kuteuliwa na kaka yake Hasan.

    * * * * * *

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 28

  • 29

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    SURA YA TATUWATU MUHIMU NA WA LAZIMA.

    Tunapopitia matukio muhimu kwa kukumbuka mambo ya zamani, yanay-ohusu historia ya taifa, tunaona kwamba matukio hayo na mabadiliko yaoya mwanzoni hayakutegemea juu ya wengi wa watu binafsi na makundimadogo ya watu ambao waliishi katika wakati huo makhususi. Kuwepo aukutokuwepo kwa mpiganaji huyu au mkulima yule au mfanya kazi aumfanya biashara au mwanasiasa hakukuathiri matukio hayo.

    Kila mtu binafsi, isipokuwa wachache sana, walikuwa si wa lazima au ili-wezakana kumweka mwingine yeyote badala yake ambaye angewezakufanya kazi kama hii. Kama mambo yalivyo, yapo makundi madogo nabaadhi ya watu binafsi ambao hufanya kazi kubwa ambazo watu wenginehawawezi au hawataki kufanya. Makundi haya madogo na watu binafsihawa wachache watakuwa na ulazima wa kuwepo, na kwa hiyo matukiomakubwa yatahusishwa sana na makundi na watu hawa binafsi.

    Kuwepo kwa mtu yeyote anayeweza kufanya kazi ndogo (na hawa ndiowengi katika kila taifa) kuhusiana na tukio muhimu lazima liitwe tukio lakawaida na si la lazima. Tunasema kwamba kuwepo kwa watu kama haoau makundi madogo ni jambo la kawaida na si la lazima kuhusiana na tukiomuhimu kwa sababu tukio hilo lingeweza kutokea kwa kuwepo aukutokuwepo kwa watu kama hao au kundi hilo, kwani kila mmoja waoanaweza kuondolewa na nafasi yake ikashikwa na mwingine.

    Tunapotazama kwa kukumbuka mambo ya zamani tangu mwanzo waimani ya Uislamu na kunea kwake pole pole wakati wa Mtukufu Mtume(s.a.w.w.), tunaona kwamba Uislamu ulihusishwa sana na kuwepo kwaidadi ndogo ya watu na kundi dogo la watu binafsi.

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 29

  • 30

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    Hakuna haja ya kusema kuhusu uhusiano wa imani ya Uislamu na kuwe-po kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwani yeye ndiye aliyepokea wahyi,akachukua ujumbe na akakutana na mambo ambayo hakuna mtu aliyewahikukutana nayo. Ni yeye tu ndiye mtu ambaye sifa zake zilimfanya astahi-ki kupokea wahyi.

    Kwa kuwa imani ya Uislamu ilitegemea juu utu wa Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) katika kuanza kwake na kuendelea wakati wa kipindi chaUtume, tunaona kwamba kuendelea kwa Uislamu wakati wa kipindi hichokulihusishwa sana na kwa ubayana pamoja na makundi madogo matatuambayo yalilinda maisha ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na yakatoamihanga mikubwa kwa ajili ya ulinzi wake.

    UKOO WA HASHIM.

    Kundi dogo la kwanza miongoni mwa hayo makundi madogo lilikuwa niukoo wa Hashim. Ukoo huu ulitoa kile ambacho hakuna ukoo mwinginewa Makka uliofanya hivyo wakati wa miaka ambayo Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) alitumia kati ya mwanzo wa Utume wake na mwanzo wa Hijrahyake. Kundi hili lilipata upendeleo wa heshima ya kumlinda MtukufuMtume (s.a.w.w.) wakati wa miaka hiyo. Hakuna ukoo mwingine waMakka ulioshiriki heshima hii. Koo zingine zilichagua kuwa na msimamowa kiuadui kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ujumbe wake na ukoo wake.Msimamo huo wa uadui ulimtishia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na watu waukoo wake kwa hatari nyingi mfululizo.

    Hivyo, itakuwa ni haki kusema kwamba kuwepo kwa koo zingine zaMakka kuhusiana na maendeleo ya ujumbe wakati wa kipindi hichohaikuwa tu dharura, bali pia ni nguvu hasi, kwani koo hizo hazikufanyalolote kama makundi katika kumsaidia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwanamna yoyote; kwa kweli walikwamisha maendeleo.

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 30

  • 31

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    Baadhi ya wanamume na wanawake wenye uhusiano na hizi koo za Makkawalimuamini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na walitoa mihanga fulani kwaajili yake na ujumbe wake, lakini walifanya hivyo kama watu binafsi.Makundi ambayo kwamba watu hao wanahusika nayo, yalichukua msi-mamo wa uadui kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na yaliwatesa watu haokwa sababu waliacha msimamo wao huo wa uadui.

    Lau kama koo za Umayya, Makhzum, Zuhra, Jumah na koo nyinginezo zaMakka hazingekuwepo, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ujumbe wakeangekuwa salama kutokana na hatari nyingi zilizokuwa zimemkabili.Imam Ali katika mojawapo ya ujumbe wake aliompelekea Muawiya alita-mka yafuatayo:

    Watu wetu (koo za Makka) walitaka kumuua Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) wetu na kuangamiza ukoo wetu. Walifanya njama naukatili dhidi yetu. Walituzuia tusipate maji na walitufunika kwanguo ya woga, walitulazimisha kuishi kwenye mlima wa mawe nawaliwasha moto wa vita dhidi yetu, na Mwenyezi MunguMuweza wa Yote aliamua kwa niaba yetu kuilinda dini Yake nakupigana kwa ajili ya heshima Yake. Muumini wetu alikuwaanatafuta thawabu za Mwenyezi Mungu, na mkanushaji wetualikuwa anatetea hadhi yake. Waislamu wengine wa Kikureishihawakuzongwa na yale yaliyokuwa yanatupata sisi, ama kwamuungano uliowalinda au kwa uhusiano na ukoo ambao ulikuwatayari kuwalinda. Hivyo walikuwa salama dhidi ya mauaji.

    Hapo ambapo vita ilipamba moto na masahaba hawakutakakupigana, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaweka watu waNyumba yake mbele, akiwalinda masahaba wake kupitia kwaokutokana na joto la panga na mikuki.21

    21 Al-Sharif Al-Radhi Muhammad Ibn Al-Husein, Nahjul Balaghah Mkusanyikowa maneno ya Imam Ali, sehemu ya 3, uk. 8-9.

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 31

  • 32

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    UKOO WA AL-AUS NA AL-KHAZRAJ.

    Makundi mengine mawili madogo ambamo muunganiko wa imani yaUislamu ulikuwa umeunganishwa bayana katika hatua nyingine ya maen-deleo ya harakati ya Kiislamu yalikuwa ni makabila mawili ya Al-Khazrajna Al-Aus. Makabila haya mawili yalibahatika kutoka miongoni mwamakabila ya Waarabu yaliyoko nje ya Makka kwa heshima yao ya kumlin-da Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na ujumbe wake baada ya Hijra. Lau kamamakabila mengine yangetaka kugawana heshima hii na makabila hayamawili, yangefanikiwa kuipata; bahati mbaya, makabila hayo yalichaguakuwa wapinzani wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) badala ya kumsaidia.

    Hivyo, kuendelea mbele kwa imani ya Uislamu kuliunganishwa na hayamakundi matatu madogo. Kuwepo kwa makabila mengine na koo zingineilikuwa si muhimu na kuliko ilivyo kawaida kuhusiana na imani yaUislamu katika wakati huo. Kuwepo kwa koo na makabila hayo kulis-ababisha mwelekeo hasi na uliojaa hatari zilizotishia uhai wa MtukufuMtume (s.a.w.w.) na ujumbe wake.

    ABU TALIB.

    Kama tunavyoona haya makundi madogo matatu yaliyounganishwa kwauimara kwenye ujumbe wa Uislamu, historia ya imani hii inawasilishakwetu watu wawili ambao kuwepo kwao ilikuwa lazima na muhimu wakatiwa kipindi cha Utume.

    Mmojawapo wa watu hao wawili alikuwa Abu Talib, ami yake MtukufuMtume (s.a.w.w.), mlezi wake wakati wa siku za utoto wake na mteteziwake mkuu baada ya kuanza Utume wake. Ulinzi wa shujaa huyu kwampwa wake dhidi ya vitisho vya Makureishi (koo za Makka zisizo na uhu-siano na ukoo wa Hashim) ulikuwa kipengele muhimu katika uendelezajiwa maisha ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na ujumbe wake. Koo za Makka

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 32

  • zilikuwa na chuki kubwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na zilikuwa nashauku ya kumuua. Kilichowazuia wasifanye hivyo ni kuwepo kwa AbuTalib, mkuu wa Makka, ambaye aliwaongoza Bani Hashim na akafanyakwa ajili yao na kwa ajili yake mwenyewe ngome isiyovunjika kumzun-guka Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

    Wasomaji wa historia ya Kiislamu wanajua jinsi koo za Kikureishi walivy-otoa makataa (sharti la mwisho) kwa Abu Talib la kumsitisha mpwa wakeasiendelee kuwakashifu baba zao na kuwafedhehesha miungu wao na kud-hihaki akili zao; vinginevyo, wangemkabili yeye na Muhammad kwenyeuwanja wa vita hadi mojawapo ya makundi hayo mawili liangamie. AbuTalib hakuwa na shaka kwamba kukubali kwake changamoto ya Kikureishikulimaanisha kifo chake na kuangamia kwa ukoo wake. Hata hivyo,hakumshinikiza mpwa wake kuacha kampeni yake. Alichofanya ni kumjul-isha tu kuhusu makataa wa Makureishi, na halafu akamwambia kwa upole:

    Niokoe mimi na wewe, mpwa wangu, na usinibebeshe mzigonisioweza kuubeba.

    Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokataa makataa yao ya mwisho alimtamkiaami yake kwamba kamwe hatabadilisha ujumbe wake kwa kupewa milikiya ulimwengu wote, Abu Talib bila kukawia alibadilisha msimamo wakena aliamua kuendelea kuwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hadi mwisho.Alimuita alipogeuza mgongo wake: Njoo rudi, mpwa wangu. MtukufuMtume (s.a.w.w.) aliporudi, ami yake mkuu akamwambia: Wewe mpwawangu endelea. Sema unalotaka kusema, sitakusaliti wakati wowoteule.22

    Abu Talib alitimiza ahadi hii kubwa kwa heshima maalum. Mtu mmoja waMakka alimtupia uchafu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa amerukuu,Abu Talib alikwenda huku akitikisa upanga wake akiwa ameshikilia

    33

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    22 Ibn Hishamu, Wasifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), sehemu ya I, uk. 266.

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 33

  • mkono wa mpwa wake hadi alipofika kwenye Msikiti mtakatifu. Kundi lamaadui lilikuwa limeketi hapo, na baadhi yao walipojaribu kusimama iliwamkabili Abu Talib, aliwaambia:

    Kwa jina la Yule Ambaye Muhammad anamuamini, endapo yey-ote kutoka miongoni mwenu atasimama kunikabili nitamkata kwaupanga wangu. Halafu akawapaka uchafu kwenye nyuso nandevu zao.23

    Kabila la Kureishi liliunda muungano mkubwa dhidi ya Abu Talib na ukoowake na wakaamua kutumia silaha ya njaa, kuzuia wasipate chakula badalaya kukabiliana ana kwa ana. Walitambua kwamba ukoo wa Hashim wange-jibu mapigo endapo wangeshambuliwa; na kwamba hawangeangamizwabila kuwatia hasara kubwa maadui zao. Hivyo, koo za Makka ziliwekavikwazo vya kiuchumi na kijamii dhidi ya ukoo wa Hashim. Hali yavikwazo iliendelea kwa miaka mitatu ambapo watu wa ukoo wa Hashimwalilazimika kuishi kwenye mlima wa mawe ulioitwa Shiab Abu Talib.Ukoo wa Hashim wakati wa kipindi hicho wakati mwingine walilazimikakula majani ya miti kupunguza makali ya njaa.

    Wakati wa kipindi hicho, jambo kuu lililomshughulisha shujaa huyomkongwe lilikuwa kulinda maisha ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katikakipindi cha miaka hiyo, mara nyingi Abu Talib aliwaamuru watu wa famil-ia yake hususan mwanawe Ali kulala kwenye kitanda cha Mtukufu Mtume(s.a.w.w.), kwa lengo la kumlinda asiuawe.

    UISLAMU WA ABU TALIB.

    Baadhi ya wanahistoria na waandishi wa Hadith wametoa taarifa kwambaAbu Talib alifariki dunia akiwa kafiri. Wengine walitoa taarifa kwambaAya: Haimpasi Nabii na walioamini kuwatakia msamaha washiriki-

    34

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    23 Khalid Muhammad Khalid, Fiy Rihab Ali.

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 34

  • na, ijapokuwa ni jamaa zao, baada ya kwisha bainika kuwa hao niwatu wa motoni. (Qurani; 9:113) iliteremshwa kuhusu Abu Talib,kwani Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitaka kumwomba Mwenyezi Mungukumsamehe na Mwenyezi Mungu alimkataza asifanye hivyo.

    Matamshi ya aina hiyo yalibuniwa kama sehemu ya kampeni za kashfaambazo zilianzishwa na ukoo wa Umayya na washirika wao dhidi ya ImamAli. Walijaribu kwa kubuni Hadith hizo ili kuthibitisha kwamba AbuSufyani, baba yake Muawiya alikuwa bora zaidi ya Abu Talib baba yakeAli, wakidai kwamba Abu Sufyani alikuwa Mwislamu na Abu Talib aliku-fa akiwa kafiri.

    Waandishi wa Hadith na historia walizichukua Hadith hizi bila kuzingatiaushahidi wa udanganyifu wao. Hawakujaribu kuzipima Hadith hizi, lakinitarehe ya kuteremshwa kwa Aya hiyo hapo juu inasadikisha kwambahaikuteremshwa kwa sababu iliyomhusu Abu Talib.

    Aya hii ni sehemu ya sura ya Baraa (sura ya 9). Sura hii yote iliteremshwaMadina, isipokuwa Aya mbili za mwisho (129 na 130). Aya ambayo nimaudhui ya mjadala wetu ni ya 113. Sura ya Baraa iliteremshwa wakatiwa mwaka wa 9 A.H. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuamuru Abu Bakrkutangaza sehemu ya kwanza ya sura hii wakati wa siku za kipindi chaHija mwaka huo alipomtuma kama Amir Al-Hajj (kiongozi wa Hijja).Halafu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimpeleka Ali kuchua sehemu hiyo (yaSura hiyo) kutoka kwake na kuitangaza (yeye badala ya Abu Bakr), kwasababu Mwenyezi Mungu alimuamrisha kwamba Sura hiyo isitangazwe namtu mwingine yeyote isipokuwa imma yeye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aumtu kutoka Nyumba yake. Sura inazungumzia matukio ambayo yalitokeawakati wa kampeni ya Taabuk ambayo ilifanyika mwezi wa Rajab wamwaka wa tisa.

    Kwa kuwa Sura hii inayo Aya iliyotajwa hapo juu, Aya hii haingemaanishaAbu Talib kwa sababu alikufa Makka takriban miaka miwili kabla ya

    35

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 35

  • Hijiriya.

    Kumwomba Mwenyezi Mungu kumsamehe makosa mtu ambaye alik-wisha kufa kwa kawaida hufanyika wakati wa dua ya maziko. Maneno yaAya yanaonesha hivyo kwani inassema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) nawaumini hawaruhusiwi kumwomba Mwenyezi Mungu kuwasamehemakafir. Hii inaonesha kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa nawaumini wengine kwenye Swala ya jamaa alipoomba makafiri wasame-hewe.

    Kusema kweli, Swala ya maziko ilikuwa haijaruhusiwa kabla ya Hijiriya.Swala ya kwanza iliyosalishwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa ajili yamaiti ilikuwa Swala yake kwa ajili ya Al-Bura Ibn Maarour wa Madina.

    Upo uwezekano mkubwa kwamba Aya husika iliteremshwa baada yaMtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuswalia maiti ya mmojawapo wa wanafikiwaliokuwa wakijifanya Waislamu na kuficha ukafiri. Inawezekana kabisakwamba Aya hii iliteremshwa wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akiongozaSwala ya kuswalia maiti ya Abdullah Ibn Abu Saluul ambaye alikufawakati wa mwaka wa tisa na ambaye alijulikana sana kwa unafiki wake,chuki yake kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na uadui wake kwa imani yaUislamu. Kuhusu mtu huyu na wafuasi wake, Sura ya Al-Munafiquun(wanafiki) iliteremshwa kabla ya muda huo. Lau kama waandishi wa his-toria na wa Hadith (ambao kwa kutokuwa waangalifu waliandika Hadithya kubuniwa kuhusu ukafiri wa Abu Talib) wangelifikiria kwa kina fulanina kwa mantiki, wasingeweza kufanya kosa hili la kutisha la kihistoria.

    Kusema kwamba Abu Talib alikuwa kafiri ni kusema kwamba alikuwamuumini wa ibada ya masanamu. Lakini imani hii haiwezi kuwa pamojana imani yake katika ukweli wa Muhammad ambaye aliyakana masanamuna aliona kuheshimiwa na kuabudiwa kwao kama Mwenyezi Mungu niuasi kwa Muumba.

    36

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 36

  • Kwa Abu Talib kuamini dini ya masanamu, alikuwa imma aamini kwam-ba Muhammad alikuwa anawapotosha watu kwa makusudi kuhusuMwenyezi Mungu, au alikuwa anapagawa. Kama Abu Talib alikuwa kafiri,na licha ya hivyo akajitolea sana kwa ajili ya Muhammad, basi lazimaalikuwa mwenye wazimu au mpumbavu isivyo kawaida. (MwenyeziMungu aepushilie mbali). Kama angeamini kwamba mpwa wake alikuwamwendawazimu au mpotoshaji wa makusudi kuhusu Mwenyezi Mungu,Abu Talib angemzuia Muhammad na kuwa mpinzani wake imara badala yakuwa mlinzi wake wa kutisha, kwani ujumbe wa Muhammad ulitegemewakuleta uharibifu na kifo cha Abu Talib na ukoo wake.

    Abu Talib aliifungamanisha hatma yake na hatma ya mpwa wake. Hakujalilolote ambalo lingemtokea yeye na ukoo wake. Alishuhudia hatari zili-zomzunguka yeye na ukoo wake na matatizo yaliyokuwa yamelundikanakumzunguka yeye kwa sababu ya ulinzi wake kwa mpwa wake. Licha yayote yaliyotokea kwake na watu wa uko wake, historia haijaandika nenololote kali kutoka kwa Abu Talib kuhusu mpwa wake. Kinyume chake, ali-jitoa mhanga yeye na watu wa ukoo wake kama wakombozi wa mpwawake. Alimfanyia wema kuliko baba yeyote mwenye huruma na upendoalivyomfanyia mwanawe anayempenda sana. Alimwambia:

    Mpwa wangu endela kutangaza ujumbe wako na sema loloteunalotaka kusema. Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sitakuachakamwe kwenye hatari yoyote.

    Abu Talib alikuwa mtu mwenye imani kubwa na itikadi madhubuti katikaukweli wa Muhammad. Aliishi na ujumbe huo kwa takriban miaka kumina moja na matatizo ya Muhammad na yake yaliongezeka jinsi mudaulivyopita. Alikuwa mtu mwenye imani isiyo ya kawaida kuhusu ukweliwa Uislamu. Historia ilishuhudia sahaba mashuhuri wanakimbia palehatari ilipozidi kuongezeka. lakini Abu Talib hakukimbia wala hakupotezaazma yake. Aliendelea kujitoa mhanga kwa ajili ya Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) katika kipindi cha uhai wake.

    37

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 37

  • Hili lingetoa sifa thibitishi kwa yale aliyoandika At-Tabarsi kupitia sanadyake hadi kwa Imam Jafar as-Sadiq (a.s.):

    Wakati Imam Ali alipokuwa ameketi kwenye Ruhbah hukoKufa akiwa amezungukwa na kundi la watu, mtu mmoja alisima-ma na akasema: Ewe Amiri wa Waumini, wewe umo katika wad-hifa huu mkubwa ambao Mwenyezi Mungu amekuweka wakatibaba yako anateseka ndani ya Jahanamu. Imam alijibu kwakusema: Nyamaza! Mwenyezi Mungu na aharibu mdomo wako!Kwa jina la Yule Aliyemtuma Muhammad akiwa na ukweli, kamababa yangu akiwaombea msamaha watenda dhambi wote katikauso wa ardhi, Mwenyezi Mungu angekubali uombezi wake. 24

    Alificha imani yake, na Mwenyezi Mungu amemlipa mara mbili. AbuTalib aliificha imani yake ili tu aweze kumpa ulinzi Muhammad. Lauangedhihirisha imani katika Uislamu, uhusiano wake na Makureishiungekatika. Alitaka kuendeleza mazungumzo kati yake na Makureishi nakuhakikisha kwamba hayasitishwi kwani kinyume chake ni hali ambayoingesababisha mapambano ya silaha kwenye vita vya kuamua mshindi namshindwa ambavyo huenda vingesababisha maangamizi ya ukoo wake.Ngome ya ukoo wa Hashim iliyomzunguka Muhammad ingeanguka namakafiri wa Makka wangemkamata.

    Licha ya kuficha imani yake, Abu Talib zaidi ya mara moja, alidhihirishawaziwazi imani yake. Alipokuwa kitandani dakika chache kabla ya kukataroho, aliwaambia watu wa ukoo wa Hashim:

    Ninawaamuruni muwe watu wema kwa Muhammad. Ni mtupekee wa kuaminika miongoni mwa Kureishi, na mkweli wakatiwote miongoni mwa Waarabu. Alileta ujumbe ambao umekubali-wa na moyo na kukataliwa na ulimi kwa kuogopa uadui. Kwa jinala Allah yeyote anayefuata njia ya Muhammad atakuwa kwenye

    38

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    24 Al-Tabarsi, Al-Ihtijaj, sehemu ya I, uk. 341.

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 38

  • barabara iliyo sahihi na yeyote anayefuata mwongozo wake ata-furahi katika maisha yake yajayo. Kama ningekuwa bado ninamiaka ya uhai hapa duniani ningempa ulinzi dhidi ya hatari naningemlinda dhidi ya maadui.

    Na nyinyi, watu wa ukoo wa Hashim itikieni wito waMuhammad na mwaminini. Mtafuzu na mtaongozwa vema.Msaidieni Muhammad; hakika yeye ni mwongozo kwenye njiailiyonyooka.25

    SOTE TUNAWIWA NAYE.

    Waislamu wote ni wenye kuwiwa kwa Abu Talib, kwani kuendelea kwaujumbe wa Kiislamu ni matokeo ya mwenendo wa maisha ya MtukufuMtume (s.a.w.w.) hadi Mwenyezi Mungu alipokamilisha ujumbe wakekwa mwanadamu. Ulinzi wa Abu Talib kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)ulikuwa kikwazo kikubwa kwa Kureishi.

    Wakati fulani nilitamka maneno haya kwenye semina ya Kiislamu na swalilifuatalo liliulizwa: Kama Mwenyezi Mungu Ndiye Ambaye alitakaujumbe wa Uislamu uendelee na uenee, hakuwa na uwezo wa kuulinda nakuueneza bila ya Abu Talib na ulinzi wake kwa Mtukufu Mtume(s.a.w.w.)?

    Katika jibu langu, nilisema ifuatavyo: Waisilamu wanaamini kwambaMwenyezi Mungu alikuwa na uwezo wa kulinda maisha ya MtukufuMtume (s.a.w.w.), na alikuwa na uwezo wa kuwafanya wana wa Adamuwote kuwa Waislamu na waumini katika Mwenyezi Mungu, Upweke wakena Siku ya Hukumu. Angewafanya wanadamu wote kuwa watiifu washaria za Akhera. Alikuwa na uwezo wa kufanya koo zote za Kureishikumtii Muhammad. Pia Alikuwa na uwezo wa kwafanya watu wote kutiiamri Zake bila hata kumuumba Muhammad.

    39

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    25 Khalid Muhammad Khalid, Fiy Rihab Ali

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 39

  • Lakini, licha ya imani yetu kwa yote haya, tunatambua kwamba MwenyeziMungu hakufanya hivyo. Hakuwafanya watu wote kuwa waumini.Hakuingilia moja kwa moja kubadili fikra na itikadi zao. Alichofanya Yeyeni kuwapa uhuru wa kuchagua. Hii inamaanisha kwamba MwenyeziMungu hakutaka kuendesha matukio ya hapa duniani kimiujiza na kupitiauwezo wa kiMungu. Alichotaka kufanya Yeye ni kuendesha mambo yaduniani kufuatana na jinsi ya kimaumbile na uelekeo wake. Kwa hiyo,Mwenyezi Mungu aliteremsha Wahyi kwa mwanadamu aliyeitwaMuhammad na akaueneza Uislamu kupitia kwa mtu huyo.

    Mweza wa Yote hakuchagua kuwalazimisha Makureishi kuamini aukutokuamini. Makureishi walio wengi waliamua kumpinga Muhammad,na Abu Talib alichagua kuamini ujumbe wake na kumlinda yeye kwa vyoteilivyokuwanavyo; miongoni mwa watu na namna zilizokuwepo. Ulinzihuu wa Abu Talib kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ulikuwa kipengelemuhimu katika kuponya maisha ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kuende-sha ujumbe wake hadi Abu Talib alipoaga dunia.

    Kuhusisha ukafiri kwa mtu kama Abu Talib, ambaye alikuwa msaidizi kwaWaislamu wote kwa kulinda maisha ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwatakriban miaka kumi na moja, ni moja wapo ya utovu wa shukrani mbayasana. Ni zawadi juu ya fadhila kubwa kwa fedheha mbaya.

    Abu Talib alikuwa mtu wa kwanza miongoni mwa watu wawili mashuhuriambao kwamba uendelezwaji wa imani ya Uislamu uliunganishwa kwaokwa uimara, na kuwepo kwao kuhusu uendelezaji wa imani ya Uislamuhakukuwa dharura.

    IMAM ALI (A.S.).

    Mtu mwingine ambaye uendelezaji wa imani ya Uislamu katika kipindicha siku za uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) uliunganishwa kwa uimarani mtoto wa Abu Talib, ambaye alichukua kazi ile ile baada ya kifo cha

    40

    Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

    Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba Dr.Kanju.qxd 7/1/2011 4:35 PM Page 40

  • baba yake, lakini katika kiwango kikubwa.

    Masahaba wengi sana walifanya jitihada kubwa kwa ajili ya Uisalmu nawalimpatia Mtukufu Mtume wa Uislamu (s.a.w.w.) msaada unaostahilikupongezwa. Inatosha kuwataja Makhalifa watatu: Abu Bakr, Umar naUthman sanjari na masahaba wengi wa Makka kama vile: Zubeir, Talha,Abdul Rahman Ibn Auf Abu Ub