20
Toleo Na. 013 Jarida la kila miezi mitatu Januari - Machi, 2013 Jarida la Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar lMaoni ya Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba uk. 4 Ifanye haki Iwe shauku Inaendelea Uk. 3 M AAFISA Mipango wawili wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) walikuwa ni miongoni mwa waangalizi wa kutoka nchi za Afrika walioshiriki katika uangalizi wa uchaguzi wa Kenya uliofanyika tarehe 4 Machi, 2013. Maafisa wawili wa ZLSC walioshiriki katika uchaguzi wa Kenya ni Bi. Jina Mwinyi Waziri kutoka Afisi ya Zanzibar na Mohammed Hassan Ali kutoka Afisi ya Pemba. Walikuwepo Kenya kwa wiki moja kuanzia tarehe mosi hadi saba Machi 2013. Walishiriki baada ya kupewa mwaliko na Asasi isiyo ya Kiserikali inayoshughulika na Masuala ya Katiba na Uchaguzi (the Constitution and Reform Education Consortium) iliyopo Nairobi, Kenya. Maafisa Mipango walishiriki katika uangalizi wa kampeni za uchaguzi, uangalizi ZLSC Yashiriki Uangalizi Uchaguzi Kenya Inaendelea Uk. 3 S PIKA wa Baraza la Wawakilishi (BLW), Mhe. Pandu Ameir Kificho amezindua kitabu cha Elimu ya Katiba kwa Wananchi kilichotayarishwa na Baraza kwa msaada wa kitaalamu uliotolewa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) na kufadhiliwa SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Pandu Ameir Kificho (katikati) akizinduwa Kitabu cha Elimu ya Katiba kwa Wananchi, kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, Profesa Chris Maina Peter, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar na (kulia) Balozi wa Norway Tanzania Ingunn Klepsvik, uzinduzi huo ulifaanyika katika ukumbi mdogo wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar tarehe 22 Februari 2013. Spika Kificho Azindua Kitabu cha Elimu ya Katiba lTaratibu za Kupata Nafuu Ulipaji wa Nauli za Gari za Abiria uk. 12 lHotuba ya Mkurugenzi wa Mashtaka Katika Sherehe ya Siku ya Sheria Zanzibar uk. 14 lTamko la Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) Kuhusiana na Mauaji ya Padri Evarist Gabriel Mushi uk.18 ya li yo mo MIoNgoNI mwa waangalizi kutoka nchi za Afrika wa Uchaguzi Kenya, Bi. Faith wakwanza kulia kutoka Zimbabwe, Jina Mwinyi kutoka Zanzibar, Zipporali Adhiambo kutoka Kenya, Rumbidcai Dube kutoka Zimbabwe na Sheila Kengingo kutoka Uganda wakiwa katika kikao cha kutathmini hali ya uchaguzi tarehe 4 Machi 2013.

Jarida la Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Ifanye haki ... · waliopo katika majimbo yote 50 ya uchaguzi ya Zanzibar. Wasaidizi wa sheria wapo chini ya uongozi wa ZLSC na wanasomeshwa

  • Upload
    others

  • View
    38

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Jarida la Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Ifanye haki ... · waliopo katika majimbo yote 50 ya uchaguzi ya Zanzibar. Wasaidizi wa sheria wapo chini ya uongozi wa ZLSC na wanasomeshwa

1sheria na haki Januari - Machi, 2013

Toleo Na. 013 Jarida la kila miezi mitatu Januari - Machi, 2013

Jarida la Kituo cha Huduma za Sheria ZanzibarlMaoni ya Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba uk. 4

Ifanye haki

Iwe shauku

Inaendelea Uk. 3

MAAFISA Mipango wawili wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) walikuwa ni miongoni

mwa waangalizi wa kutoka nchi za Afrika walioshiriki katika uangalizi wa uchaguzi wa Kenya uliofanyika tarehe 4 Machi, 2013.

Maafisa wawili wa ZLSC walioshiriki katika uchaguzi wa Kenya ni Bi. Jina Mwinyi Waziri kutoka Afisi ya Zanzibar na Mohammed Hassan Ali kutoka Afisi ya Pemba.

Walikuwepo Kenya kwa wiki moja kuanzia tarehe mosi hadi saba Machi 2013. Walishiriki baada ya kupewa mwaliko na Asasi isiyo ya Kiserikali inayoshughulika na Masuala ya Katiba na Uchaguzi (the Constitution and Reform Education Consortium) iliyopo Nairobi, Kenya.

Maafisa Mipango walishiriki katika uangalizi wa kampeni za uchaguzi, uangalizi

ZLSC Yashiriki Uangalizi Uchaguzi Kenya

Inaendelea Uk. 3

SPIKA wa Baraza la Wawakilishi (BLW), Mhe. Pandu Ameir Kificho amezindua kitabu cha Elimu ya

Katiba kwa Wananchi kilichotayarishwa na Baraza kwa msaada wa kitaalamu uliotolewa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) na kufadhiliwa

SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Pandu Ameir Kificho (katikati) akizinduwa Kitabu cha Elimu ya Katiba kwa Wananchi, kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, Profesa Chris Maina Peter, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar na (kulia) Balozi wa Norway Tanzania Ingunn Klepsvik, uzinduzi huo ulifaanyika katika ukumbi mdogo wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar tarehe 22 Februari 2013.

Spika Kificho Azindua Kitabu

cha Elimu ya Katiba

lTaratibu za Kupata Nafuu Ulipaji wa Nauli za Gari za Abiria uk. 12lHotuba ya Mkurugenzi wa Mashtaka Katika Sherehe ya Siku ya Sheria

Zanzibar uk. 14lTamko la Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZlSc) Kuhusiana na Mauaji

ya Padri Evarist Gabriel Mushi uk.18

yaliyomo

MIoNgoNI mwa waangalizi kutoka nchi za Afrika wa Uchaguzi Kenya, Bi. Faith wakwanza kulia kutoka Zimbabwe, Jina Mwinyi kutoka Zanzibar, Zipporali Adhiambo kutoka Kenya, Rumbidcai Dube kutoka Zimbabwe na Sheila Kengingo kutoka Uganda wakiwa katika kikao cha kutathmini hali ya uchaguzi tarehe 4 Machi 2013.

Page 2: Jarida la Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Ifanye haki ... · waliopo katika majimbo yote 50 ya uchaguzi ya Zanzibar. Wasaidizi wa sheria wapo chini ya uongozi wa ZLSC na wanasomeshwa

sheria na haki2 Januari - Machi, 2013

Maoni ya Mhariri

MCHAKATO wa Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unatarajiwa kuingia katika hatua ya

kuunda Mabaraza ya Katiba kwa ajili ya kupitia na kutoa maoni juu ya Rasimu ya Katiba itakayoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Utaratibu wa kuunda Mabaraza ya Katiba ni hatua ya nne ya mchakato wa Katiba.

Hatua ya kwanza ya mchakato wa Mabadiliko ya Katiba ilikuwa ni kutunga Sheria ya Mabadiliko ya Katiba – Sheria

Nam. 8 ya Mwaka 2011 ambayo imefanyiwa mabadiliko. Hatua ya pili ilkuwa ni kuunda Tume ya Mabadiliko ya

Katiba yenye wajumbe 32 (Nusu kutoka Tanzania Bara na nusu ya pili kutoka Tanzania Zanzibar). Tume inaongozwa na Mwenyekiti Jaji Joseph Warioba na Makamo Mwenyekiti Jaji Mkuu mstaafu wa Tanzania Mheshimiwa Augostino Ramadhani.

Hatua ya tatu ya mchakato wa Mabadiliko ya Katiba ilikuwa ni kukusanya maoni kutoka kwa wananchi ikiwa

ni mwananchi mmoja mmoja na taasisi. Hatua ya nne ni kwa mujibu wa Kifungu cha 18 (3) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ni uundaji wa Mabaraza ya Katiba yatakayowashirikisha na kuwakutanisha wananchi katika jamii kwa lengo la kuchambua rasimu ya Katiba ambayo itatayarishwa na Tume na kutoa maoni yao. Hatua zilizobakia katika Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba ni Bunge Maalum la Katiba na Kura ya Maoni.

Kwa mujibu wa Mwongozo kuhusu muundo, utaratibu wa kuwapata wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya umeshatolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Vikao vya kuwachagua wajumbe wa Mabaraza ya Katiba vinatarajiwa vifanyike kati ya tarehe 05 Aprili, 2013 hadi tarehe 17 Aprili, 2013 kwa pande zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nia na madhumuni ya kutumia nafasi hii kuandika kuhusu Mabaraza ya Katiba ni kuwatanabahisha Watanzania wote kutumia nafasi hii adhimu kwa makini na uadilifu mkubwa katika zoezi la kuwachagua wajumbe. Wajumbe watakaochaguliwa ambao 18,169 kutoka Tanzania Bara na 1,198 watakaotoka Zanzibar wafahamu majukumu yao wanayotarajiwa kuyatekeleza katika kupitia Rasimu ya Katiba.

Sifa za msingi za kuwapata wajumbe hao zimeshatolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Kwa kuzingatia hali halisi ya muundo wa jamii zetu, tunawasiwasi baadhi ya vigezo vitatawala mawazo ya wapiga kura. Au baadhi ya taasisi za kijamii, kidini au kiutamaduni au vyama vya siasa zikajitokeza mstari wa mbele kuwashawishi wapiga kura katika kufanya maamuzi.

Tunawanasihi wapiga kura na wote watakaochaguliwa katika Mabaraza ya Katiba kutojengeka na mawazo potofu katika kutekeleza majukumu yao. Watakaogombea nafasi hizo wasitawaliwe na mawazo au tamaa ya posho katika utekelezaji wa majukumu yao. Ni kazi ya kuwasilisha umma na hakutokuwa na malipo yoyote na kinachotarajiwa ni kupata Katiba mpya ya Tanzania itakayoridhiwa na wananchi wote.

Pili, itikadi za siasa au imani za dini zisipewe nafasi katika kuchagua wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ambao watapata fursa ya kuhakiki Rasimu ya Katiba itakayotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Wanasiasa na watu wa dini watapata nafasi yao kutoa maoni yao kuhusu rasimu hii ya Katiba katika hatua nyengine za mchakato wa Mabadiliko ya Katiba.

Vigezo vya msingi vya ziada vya kuzingatiwa ni uwezo wa kujenga hoja na kuchambua malengo ya kila Ibara itakayopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Hapa tunakusudia misingi mitatu ya kutafsiri sheria izingatiwe; yaani maana ya kawaida ya Ibara (plain rule), maana ya mtazamo wa sentensi (golden rule) na maana iliyojificha (mischief rule).

Kutofahamu dhana hizi za msingi itakuwa ni vigumu kujenga hoja kisheria na kufahamu Ibara zitakazopendekezwa na Tume katika Rasimu ya Katiba. Matokeo yake ni kuridhia mambo bila ya kufahamu dhamira ya ndani ya Rasimu ya Katiba. itakuwa ni sawa na wananchi kujitia kitanzi wenyewe.

Tunawatakia Watanzania wote kila la kheri katika kutekeleza majukumu yao ya kuwachagua wajumbe wa Mabaraza ya Katiba. Vile vile tunawatakia kheri wale wote watakaochaguliwa katika Mabaraza ya Katiba kutekeleza kazi zao vyema.

Prof. Chris Maina Peter,Mhariri

Mhariri: Prof. Chris Maina Peter

Mwenyekiti: Bi. Harusi Miraji Mpatani

Wajumbe:Bw. Ali Ahmed UkiBi. Safia Masoud KhamisBi. Jina Mwinyi WaziriBi. Farhat Rashid Omar

Msanifu:Bw. Yussuf Ali Hassan

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa:Simu: 0242233784S.L.P: 3360 ZanzibarFax: 0242234495E-mail: [email protected]: www.zlsc.or.tz

Chake Chake Pemba wasiliana nasiKwa:-Simu: +255 2452936

Ifanye haki

Iwe shauku

W a n a n c h i wote mnaombwa kusoma Jarida hili la Kituo kwa madhumuni ya kujifunza zaidi na kupima maendeleo ya utendaji kazi za Kituo.Tunakaribisha barua za maoni kutoka kwa wasomaji na michango ya makala kwa ajili ya kuelimisha umma.Aidha wote watakaopenda kuchangia au kuleta maoni yao katika Jarida la Sheria na Haki wanatakiwa wajitambulishe kwa majina pamoja na anuani zao ili kuleta ufanisi, ukweli na uwazi katika kuendeleza Jarida hili.Bodi ya Wahariri itakuwa na uwezo wa mwisho wa kuamua au kuhariri habari i t a k a y o c h a p i s h w a kwenye Jarida hili.

Mhariri

ChAgUEni WAjUmbE mAKini WA mAbArAZA YA KAtibA

Page 3: Jarida la Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Ifanye haki ... · waliopo katika majimbo yote 50 ya uchaguzi ya Zanzibar. Wasaidizi wa sheria wapo chini ya uongozi wa ZLSC na wanasomeshwa

3sheria na haki Januari - Machi, 2013

HABARI

Inatoka Uk. 1Inatoka Uk. 1

Mahakama ya Watoto Yazinduliwa ZanzibarJAJI Mkuu wa Zanzibar Mheshimiwa

Omar Othman Makungu amesema kuanzishwa Mahakama ya Watoto

Zanzibar kutasaidia kupunguza mrundikano wa kesi katika Mahakama za Mikoa.

Alisema Mahakama ya Watoto itashughulikia kesi za jinai zinazowahusu watoto walio chini ya miaka 18.

Mheshimiwa Jaji Mkuu alitoa kauli hii alipokuwa akizindua Mahakama ya Watoto Zanzibar. Sherehe za uzinduzi wa Mahakama ya Watoto zilizofanyika katika jengo la Mahakama Kuu, Vuga, Zanzibar.

Mahakama ya Watoto ilianzishwa chini ya Sheria ya Watoto Nam. 6 ya Mwaka 2011. Kabla ya kuanzishwa Mahakama ya Watoto, kesi zinazowahusu watoto zilikuwa zikisikilizwa katika Mahkama ya Mkoa.

Mhe. Jaji Mkuu alisema Mahakama ya Watoto zitaweka mazingira rafiki watoto kuweza kutoa maelezo yanayohusiana na kesi zinazowakabili bila ya woga.

“Mahakama ya Watoto itasaidia haki kupatikana katika kesi zinazowahusu watoto,” alisema Mheshimiwa Jaji Mkuu.

Alisema kumekuwa na ongezeko kubwa la kesi za udhalilishaji wanazofanyiwa watoto Zanzibar.

Akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa Mahakama ya Watoto, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Wanawake na Watoto Zanzibar, Bibi Fatma Gharib alitaka wananchi kuitumia Mahakama

JAJI Mkuu wa Zanzibar Mheshimiwa omar othman Makungu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mahakama ya Watoto Zanzibar iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Watoto Nam.6 ya 2011. Mrajis wa Mahakama Kuu Zanzibar, Mheshimiwa george Kazi akishuhudia zoezi la ukataji utepe.

ya Watoto.“Pelekeni kesi za watoto katika Mahakama

ya Watoto ili haki itendeke,” alisema Katibu Mkuu huyo.

Vile vile, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) Bibi Harusi Miraji Mpatani alisema kwamba

na Ubalozi wa Norway uliopo Tanzania.Spika Kificho alizindua kitabu hicho

tarehe 22 Januari, 2013 katika ukumbi mdogo wa BLW uliopo Chukwani, nje ya Manispaa ya Zanzibar na kuhudhuriwa na baadhi ya wawakilishi na mawaziri.

Sherehe ya uzinduzi wa Kitabu cha Elimu ya Katiba kwa Wananchi ilihudhuriwa na balozi wa Norway nchini Tanzania Ingunn Klepsvik na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya ZLSC Profesa Chris Maina Peter.

Alisema BLW limeanzisha mradi wa Elimu ya Katiba kwa Wananchi kwa madhumuni ya kutoa elimu ili kuwajengea uwezo wananchi kushiriki na kuchangia mjadala wa mchakato wa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Spika Kificho alisema Kitabu cha Elimu ya Katiba kitatoa mchango mkubwa katika mchakato wa Katiba mpya na kitabakia kumbukumbu ya marejeo ya taaluma.

“Kitabu hiki ni kizuri na kimeandikwa kwa lugha nyepesi ya Kiswahili ili kumuwezesha kila msomaji kufahamu

Kitabu cha Elimu ya Katiba Uchaguzi Kenya

ZLSC itawaelimisha wananchi umuhimu wa Mahakama ya Watoto.

Jumla ya dola za kimarekani elfu tano (sawa na 8100,000/-) zimetumika katika ujenzi wa Mahakama ya Watoto chini ya ufadhili wa Sweden .

maudhui yaliyokusudiwa,” alisema Spika Kificho.

Alisema zoezi la utoaji wa elimu ya Katiba kwa wananchi limeendeshwa na BLW kupitia wasaidizi wa sheria waliopo katika majimbo yote 50 ya uchaguzi ya Zanzibar. Wasaidizi wa sheria wapo chini ya uongozi wa ZLSC na wanasomeshwa masomo ya msingi ya sheria ili kutoa msaada wa bure wa sheria kwa watakaohitaji.

Zoezi la utoaji Elimu ya Katiba kupitia wasaidizi wa sheria limeanza tarehe 23 Juni, 2012 na kumalizika tarehe 31 Oktoba, 2012.

Kitabu cha Elimu ya Katiba kwa Wananchi kimegawika katika sura 20 zilizobeba mada zinazohusiana na Katiba.

Miongoni mwa mada zilizomo katika Kitabu cha Elimu ya Katiba kwa Wananchi ni Dhana ya Katiba, Chimbuko la Katiba katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Chimbuko la Katiba katika Zanzibar, Misingi ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na Misingi ya Maadili ya Kitaifa.

wa zoezi la upigaji kura na kuhesabu kura katika Afisi ya Tume ya Uchaguzi na Mipaka.

ZLSC ilikuwa ni miongoni mwa asasi za kiraia zilizoruhusiwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar kuwa watazamaji wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi wa Zanzibar mwaka 1995 tokea baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964. Katika zoezi la utazamaji, ZLSC ilialika watazamaji kutoka ndani na nje ya Afrika.

Maafisa Mipango walijifunza mambo kadhaa katika uchaguzi wa Kenya. Baadhi ya waliojifunza ni matumizi ya teknolojia ya mawasiliano katika zoezi la kuhesabu kura, wananchi kuwa na elimu ya uraia ya kutosha kuhusu demokrasia na haki ya kuchagua kiongozi.

Aidha, mambo mengine waliyojifunza ilikuwa ni kuwepo kwa nidhamu ya kusikiliza viongozi, kuheshimu sheria, kuvumiliana hatua iliyosaidia kuepusha machafuko, wananchi walihamasika kuelewa haki yao ya kupiga kura na kuwepo kwa uhuru wa vyombo vya habari.

Maafisa Mipango waliona changamoto mbali mbali zikiwemo ukosefu wa huduma za choo, msaada mdogo uliotolewa kwa watu wenye mahitaji maalum kama wajawazito, wazee na sehemu za kupigia kura zilikuwa katika viwanja na jua lilikuwa kali.

Page 4: Jarida la Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Ifanye haki ... · waliopo katika majimbo yote 50 ya uchaguzi ya Zanzibar. Wasaidizi wa sheria wapo chini ya uongozi wa ZLSC na wanasomeshwa

sheria na haki4 Januari - Machi, 2013

MAONI yA KATIBA

UtanguliziKituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ni asasi isiyokuwa ya kiserikali ambacho kilianzishwa mnamo mwaka 1992. Shughuli zake kuu ni:

• Kutoa msaada wa kisheria bure kwa watu wasiokuwa na uwezo;

• Kutoa elimu ya sheria na Haki za Binadamu; na

• Kuhamasisha ulinzi na heshima kwa Haki za Binadamu.

Kituo kinazo ofisi mbili, moja katika kisiwa cha Unguja na ya pili huko Pemba. Kituo kinaongozwa na Bodi ya Wadhamini na Mtendaji Mkuu ni Mkurugenzi Mtendaji. Shughuli zote za Kituo zinafanyika chini ya Katiba yake ya mwaka 1992 na Mpango Mkakati wake wa muda mrefu ambao kwa sasa ni wa mwaka 2013 hadi 2017.

Maoni ya Kituo kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba

Katiba ni dhana pana sana. Siyo rahisi kwa kila mwananchi na kila asasi kutoa maoni kuhusu Katiba yote. Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar

kimeamua kutoa maoni na mapendekezo kuhusu sehemu mbili tu za Katiba inayotarajiwa kutayarishwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sehemu hizi ni:

• Hati ya Haki za Binadamu (The Bill of Rights); na

• Mpangilio wa Katiba na Baadhi ya mambo muhimu ya kukumbukwa.

Kwa kufupi maelezo yetu ni kama ifuatavyo: SEHEMU yA KWANZA yA MAONI yA KITUOSURA yA TATU [kwa mfano]Hati ya Haki za Binadamu

(Bill of Rights)YaliyomoUtangulizi

Sehemu ya Kwanza – Haki na Uhuru Usioweza Kupunguzwa Uwezo Wake1. Haki na Uhuru Usioweza Kupunguzwa

Uwezo Wake

Sehemu ya Pili – Haki na Uhuru Muhimu2. Haki ya Kuishi3. Haki ya Usawa

4. Heshima5. Uhuru na Hifadhi ya Usalama6. Haki ya Faragha7. Uhuru wa Kwenda na Kuishi8. Utumwa, Utumikishwaji na Kazi ya Sulubu9. Uhuru wa Fikra na Maoni10. Uhuru wa Dini na Imani11. Uhuru wa Kujieleza12. Uhuru wa Kupata Habari13. Uhuru wa Vyombo vya Habari14. Uhuru wa Kujumuika na Wengine15. Uhuru wa Maandamano16. Uhuru wa Kushiriki Shughuli za KisiasaSehemu ya Tatu – Haki Mbele ya Sheria17. Usawa Mbele ya Sheria18. Haki za Mtuhumiwa

Sehemu ya Nne – Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamadumi19. Haki ya Kumiliki Mali20. Haki ya Kufanya Kazi21. Haki ya Kupata Ujira wa Haki22. Haki ya Elimu23. Haki ya Afya Njema

KITUO Cha Huduma Za Sheria Zanzibar (ZLSC) ni miongoni mwa asasi za kiraia ziliopo Zanzibar zilizopata fursa ya kutoa maoni kuhusu Mabadiliko ya Katiba katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. ZLSC ilitoa maoni yake tarehe 9 Januari, 2013 katika ukumbi wa EACROTANAL mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Maoni na mapendekezo ya ZLSC yalijikita katika sehemu mbili tu za Katiba. Sehemu ya kwanza ni kuhusu Hati ya Haki za Binadamu na sehemu ya pili Mpangilio wa Katiba na Baadhi ya mambo muhimu ya kukumbukwa. ZLSC iliwakilishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Profesa Chris Maina Peter na Mkurugenzi Mtendaji Bi Harusi Miraji Mpatani. yafuatayo ni maoni ya ZLSC.

ZanZibar legal services centre (Zlsc)House No. 37 Migombani (Opposite Migoz Supermarket)P.O.Box 3360 ZanZibar - TanZaniaTel: +255 24 2233784 Fax: +255 24 2234495E-Mail: [email protected]: www.zlsc.or.tz

suB-OfficE: Chake Chake Pemba Tel: +255 24 2452936

Ifanye haki

Iwe shauku

Katibu,Tume ya Mabadiliko ya Katiba,DAR ES SALAAM.

Yah: MAONI YA KITUO CHA HUDUMA ZA SHERIA ZANZIBAR (ZANZIBAR LEGAL SERVICES CENTRE – ZLSC) MBELE YA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA

JENgo la Baraza la Wawakilishi, Zanzibar.

Page 5: Jarida la Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Ifanye haki ... · waliopo katika majimbo yote 50 ya uchaguzi ya Zanzibar. Wasaidizi wa sheria wapo chini ya uongozi wa ZLSC na wanasomeshwa

5sheria na haki Januari - Machi, 2013

MAONI yA KATIBA

24. Haki ya Familia25. Haki za Mlaji26. Haki za Kiutamaduni

Sehemu ya Tano – Haki za Vikundi Maalum27. Watoto28 Watu Wenye Ulemavu29. Vijana30. Wanawake31. Wazee

Sehemu ya Sita – Haki za Pamoja32. Mazingira Bora33. Ulinzi na Usalama34. Rasilimali za Taifa35. Haki ya Maendeleo na Maisha Bora

Sehemu ya Saba – Wajibu Muhimu36. Kuheshimu Sheria za Nchi37. Wajibu wa Kufanya Kazi38. Ulinzi wa Mali za Umma39. Ulinzi wa Taifa

Sehemu ya Nane – Utekelezaji wa Hati ya Haki za Binadamu40. Haki Muhimu na Wajibu wa Jumla

Sehemu ya Tisa – Usimamizi na Utekelezaji wa Haki za Binadamu

41. Tafsiri ya Haki za Binadamu42. Utekelezaji wa Haki

Sehemu ya Kumi – Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu43. Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu

Sehemu ya Kumi na Moja – Mikataba ya Kimataifa ya Haki za Binadamu44. Mikataba ya Kimataifa ya Haki za

Binadamu

Sehemu ya Kumi na Mbili – Utangazaji wa Hali ya Hatari na Haki za Binadamu45. Utangazaji wa Hali ya Hatari na Haki za

Binadamu UtanguliziHati hii ya Haki za Binadamu, ikiwa in pamoja na haki, uhuru na wajibu, itatumika katika nchi nzima ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Haki hizi na Uhuru zitakuwepo bila ya kuwekewa mipaka ya kuzidhoofisha na kuzinyima maana.Sehemu ya Kwanza – Haki ambazo Haziwezi Kupunguzwa Uwezo Wake1. Haki zifuatazo ni muhimu mno kwa binadamu

yeyote ile na kwa hiyo haki hizi haziwezi

kupunguzwa uwezo au kuwepo kwake na Katiba hii au Sheria yoyote ile ya nchi:

(a) Uhuru wa kutoteswa, kuadhabiwa kinyama au kupewa adhabu zinazotweza na kudhalilisha.

(b) Uhuru kutokana na utumwa;(c) Haki ya mashtaka yalio huru na bila upendeleo;

na(d) Haki ya kuomba yeyote aliyeshikiliwa kinyume

cha sheria alitwe mbele ya sheria.

Sehemu ya Pili – Haki na Uhuru MuhimuHaki ya Kuishi2. Kila mtu anayo haki ya kuishi. Haki hii

haitaondelewa kwa namna yoyote ile.

Haki ya Usawa3. Binadamu wote huzaliwa huru, na wote ni

sawa.

Heshima4. Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa

na kuthaminiwa utu wake.

Uhuru na Hifadhi ya Usalama5. (1) Kila mtu ana haki ya kupata kutoka kwa

jamii hifadhi na usalama wa maisha yake.(2) Mamlaka ya nchi itahakikisha kwamba mtu

yeyote yule hatafanyiwa vitu vifuatavyo:(1) hataingiliwa uhuru wake bila kuwepo

sababu;(b) hatazuiliwa bila kuwepo kesi na maamuzi ya

Mahakama;(c) hatakumbana na aina yoyote ile ya ukatili

kutokana na vyombo vya umma au binafsi;(d) hatateswa kwa namna yoyote ile;(e) hatatendewa vibaya, kuadhibiwa, kutendewa

kinyama au kudhalilishwa;

Haki ya Faragha6. Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata

hifadhi kwa nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na unyumba wake, na pia heshima na hifadhi ya maskani yake na mawasiliano yake ya binafsi. Haki ya faragha ni pamoja na:

(a) Haki ya nyumba yake kutokaguliwa au kuingiliwa bila kibali maalumu kilichotolewa na Mahakama.

(b) Haki ya mali yake kutokaguliwa bila kibali maalumu cha Polisi au Mahakama.

(c) Haki ya mawasiliano yake binafsi kutoingiliwa kwa namna yoyote ile.

(d) Haki ya kutopekuliwa kwa kuvuliwa nguo. Itakuwa marufuku kwa mwanaume kukaguliwa na mwanamke au mwanamke

kukaguliwa na mwanaume.

Uhuru wa Kwenda na Kuishi7. (1) Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo

haki ya kwenda kokote katika Jamhuri ya Muungano na kuishi katika sehemu yoyote, kutoka nje ya nchi na kuingia, na pia haki ya kutoshurutishwa kuhama au kufukuzwa kutoka katika Jamhuri ya Muungano.

(2) Haki na uhuru wa mtu kwenda atakako unaweza kupunguzwa tu katika utekelezaji wa hukumu au amri ya mahakama.

(3) Kila raia anayo haki ya kupata kutoka kwenye mamlaka husika pasi na nyaraka nyingine za kumuwezesha kusafiri pale anapohitaji.

Utumwa, Utumikishwaji na Kazi ya Sulubu8. (a) Ni marufuku mtu yeyote kufanywa au

kutendewa kama mtumwa.(b) Ni marufuku mtu yeyote kulazimishwa

kufanya kazi bila hiyari yake.(c) Ni marufuku kwa mtu yeyote kusafirishwa

kwa nia ya kufanyiwa biashara au faida ya mtu mwingine. Biashara ya kusafirisha Binadamu ni haramu nchini Tanzania.

Uhuru wa Fikra na Maoni9. Kila mtu anayo haki na uhuru wa kuwa na

fikra na maoni yake mwenyewe kuhusu jambo lolote lile na pia yuko huru kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.

Uhuru wa Dini na Imani10. (1). Kila mtu ana haki na uhuru wa uchaguzi

katika mambo ya imani na dini, pamoja na uhuru wa mtu kubadilisha dini au imani yake.

(2). Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu ya binafsi, na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi.

(3) Kila palipotajwa neno “dini” katika Katiba hii lifahamike kwa upana wake ikiwa ni pamoja na madhehebu ya dini, na maneno mengineyo yanayofanana au kuambatana na neno hilo nayo yatatafsiriwa kwa maana hiyo.

Uhuru wa Kujieleza11. (1) Kila mtu anao uhuru wa kujieleza ikiwa ni

pamoja na:

JENgo la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Page 6: Jarida la Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Ifanye haki ... · waliopo katika majimbo yote 50 ya uchaguzi ya Zanzibar. Wasaidizi wa sheria wapo chini ya uongozi wa ZLSC na wanasomeshwa

sheria na haki6 Januari - Machi, 2013

MAONI yA KATIBA

(a) Uhuru wa vyombo vya habari;(b) Uhuru wa kupata na kutoa habari na

mawazo;(c) Uhuru wa kisanii na ubunifu; na(d) Uhuru wa kitaaluma na utafiti wa kisayansi.(2) Mamlaka ya nchi itahakikisha kwamba haki

hizi zinapatikana bila ya kuingiliwa.

Uhuru wa Kupata Habari12. Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati

wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii.

Uhuru wa Vyombo vya Habari13. (1) Vyombo vyote vya habari vitakuwa huru

kufanya kazi yake bila ya kuingiliwa. Uhuru wa vyombo vya habari utahusisha kupokea na usambazaji wa habari kuwa kwa njia zote za upashanaji habari bila kujali mipaka ya nchi.

(2) Uhuru wa vyombo vya habari inakwenda sambamba na uhuru wa ubunifu na sanaa na pia uhuru wa kitaaluma na tafiti za kisayansi.

(3) Mamlaka ya nchi itahakikisha kwamba mtu au chombo chochote kinachohusika na utoaji wa habari hakiingiliwi katika kufanya kazi yake.

Uhuru wa Kujumuika na Wengine14. (1) Kila mtu yupo huru kukutana na watu

wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama vya kisiasa, kitaaluma au kijamii au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.

(2) Ni marufuku kwa mtu yeyote kulazimishwa kujiunga na chama chochote, jumuiya au shirika lolote, au kwa chama chochote au cha siasa kukataliwa kusajiliwa kwa sababu tu ya itikadi au falsafa.

Uhuru wa Maandamano15. Kila mtu anayo haki ya kushiriki katika

maandamano ya amani yenye nia ya kuelezea hisia zao kuhusu jambo lolote lile lenye manufaa kwa kikundi chochote au kwa jamii kwa ujumla.

Uhuru wa Kushiriki Shughuli za Kisiasa16. (1) Kila raia yupo huru katika kufanya

uchaguzi katika mambo ya kisiasa ikiwa ni pamoja na haki ya:

(a) Kuanzisha, kushiriki katika uanzishaji chama cha siasa;

(b) Kushiriki katika shughuli kushiriki katika kazi mbalimbali za chama chake ikiwa ni pamoja na kuhamasisha na kuandikisha wanachama na kufanya kampeni kwa ajili ya chama; na

(c) Kuchagua au kuchaguliwa kugombea wadhifa wowote katika chama chochote cha siasa.

(2) Kila raia ana haki ya kusimama kama mgombea binafsi endapo hapendi kujiunga na chama chochote cha siasa.

(3) Kila raia mwenye miaka kumi na minane na kuendelea, awe mwanamke au mwanaume ana haki ya kupiga kura na kupigiwa kura katika wadhifa wowote wa kisiasa.

(4) Kila raia anayo haki ya uchaguzi ulio huru na wa haki na wa mara kwa mara na ambao utashirikisha raia wote wanaostahili na kwamba uamuzi wao utaheshimiwa.

(5) Kila raia mwenye umri wa mtu mzima anayohaki ya kuandikishwa kama mpiga kura na kupiga kura katika uchaguzi huru na wa siri.

(6) Kila raia anayo haki ya kushiriki katika uchaguzi wowote wa kugombea nafasi katika ofisi za umma au chama chake.

(7) Katika chaguzi zote, serikali itahakikisha ushiriki wa makundi yote ya jamii hususani wanawake na watu wenye ulemavu.

(8) Katika ngazi za maamuzi, serikali itahakikisha uwiano kati ya wanaume na wanawake kwa asilimia hamsini kwa hamsini.

Sehemu ya Tatu – Haki Mbele ya SheriaUsawa Mbele ya Sheria17. (1). Watu wote ni sawa mbele ya sheria,

na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria.

(2) Kila mtu ana haki ya kupeleka malalamiko au shitaka lake katika mahakama au chombo kingine cha kutoa haki kudai haki yake.

(3). Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.

(4). Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu na jumuiya ya watu yatalindwa na kuamuliwa na Mahakama na vyombo vinginevyo vya Mamlaka ya Nchi vilivyowekwa na sheria.

(5) Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au

WAANDISHI wa habari wana haki ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na Mabadiliko ya Katiba Mpya ya Tanzania.

katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya Mamlaka ya Nchi.

(6) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara hii neno “kubagua” maana yake ni kutimiza haja, haki au mahitaji mengineyo kwa watu mbalimbali kwa kuzingatia utaifa wao, kabila, pahala walipotokea, maoni yao ya kisiasa, rangi, dini, jinsia au hali yao ya maisha kwa namna ambayo watu wa aina fulani wanafanywa au kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni na kuwekewa vikwazo au masharti ya vipingamizi ambapo watu wa aina nyingine wanatendewa tofauti au wanapewa fursa au faida iliyoko nje ya masharti au sifa za lazima, isipokuwa kwamba neon “kubagua” halitafafanuliwa kwa namna ambayo itaizuia Serikali kuchukua hatua za makusudi zenye lengo la kurekebisha matatizo katika jamii.

(7) Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria, Mamlaka ya Nchi itaweka taratibu zinazofaa au zinazozingatia misingi kwamba:-

(a) wakati haki na wajibu wa mtu yeyote vinahitaji kufanyiwa uamuzi wa mahakama au chombo kinginecho kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa na haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia haki ya kukata rufaa au kupata nafuu nyingine ya kisheria kutokana na maamuzi ya mahakama au chombo hicho kingenecho kinachohusika;

(b) ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo;

(c) ni marufuku kwa mtu kuadhibiwa kwa sababu ya kitendo chohote ambacho alipokitenda hakikuwa ni kosa chini ya sheria, na pia kwamba ni marufuku kwa adhabu kutolewa ambayo ni kubwa kuliko adhabu iliyokuwapo wakati kosa linalohusika lilipotendwa;

(d) kwa ajili ya kuhifadhi haki ya usawa wa binadamu, heshima ya mtu itatunzwa katika shughuli zote zinazohusu upelelezi na uendeshaji wa mambo ya jinai na katika shughuli nyinginezo ambazo mtu anakuwa chini ya ulinzi bila uhuru, au katika kuhakikisha utekelezaji wa adhabu; na

(e) ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha.

(8). Mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa msaada wa sheria kwa ajili ya watu wote wasiokuwa na uwezo wa kuajiri mawakili wa kuwatetea katika mashauri yao.

Haki za Mtuhumiwa18. Mtu yeyote anayetuhumiwa atakuwa na haki

zifuatazo:-(a) Haki ya kukaa kimya(b) Haki ya kuelezwa kosa lake(c) Haki ya kutokulazimishwa kukiri kosa (d) Kufikishwa mahakamani mara moja bila

kucheleweshwa, si chini ya masaa 24 baada ya kukamatwa

(e) Kuwaasiliana au kutembelewa awapo rumande na wafuatao:

(i) mume/mke; watoto wenye umri zaidi ya miaka 16;

(ii) Ndugu wa karibu;(iii) Kiongozi wa dini;(iv) Daktari wake; na(v) Wakili au mwanasheria wake.(f) Itakuwa marufuku kwa mtuhumiwa kuteswa

au kupewa adhabu au kutendewa kwa namna yoyote inayodhalilisha utu wake.

Sehemu ya Nne – Haki za Kiuchumi, Kijamii na KiutamadumiHaki ya Kumiliki Mali19. (1). Kila mtu anayo haki ya kumiliki mali, na

Page 7: Jarida la Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Ifanye haki ... · waliopo katika majimbo yote 50 ya uchaguzi ya Zanzibar. Wasaidizi wa sheria wapo chini ya uongozi wa ZLSC na wanasomeshwa

7sheria na haki Januari - Machi, 2013

MAONI yA KATIBAhaki ya hifadhi kwa mali yake aliyonayo na iliyopatikana kihalali.

(2). Ni marufuku kwa mtu yeyote kunyang’anywa mali yake kwa madhumuni ya kuitaifisha au madhumuni mengineyo bila ya kufuata utaratibu wa sheria na kuwepo amri ya Mahakama kuhusu uhalali wa kitendo hicho na ambayo inaweka masharti na utaratibu wa kutoa fidia inayostahili.

Haki ya Kufanya Kazi20. (1). Kila mtu anayo haki ya kufanya kazi.(2). Kila raia anastahili fursa na haki sawa, kwa

masharti ya usawa, ya kushika nafasi yoyote ya kazi na shughuli yoyote iliyo chini ya Mamlaka ya Nchi.

Haki ya Kupata Ujira wa Haki21. (1) Kila mtu, bila ya kuwapo ubaguzi wa

aina yoyote, anayo haki ya kupata ujira unaolingana na kazi yake, na watu wote wanaofanya kazi kulingana na uwezo wao watapata malipo kulingana na kiasi na sifa za kazi wanayoifanya.

(2) Kila mtu anayefanya kazi anastahili kupata malipo ya haki.

(3) Kila mfanyakazi ana haki ya kupata mazingira mazuri ya sehemu ya kazi.

(4) Kila mfanyakazi ana haki ya kupumzika, kupunguziwa masaa ya kazi na likizo yenye malipo na mapumziko yenye malipo wakati wa sikuu rasmi za kiserikali.

(5) Kila mfanyakazi ana haki ya kuanzisha na kujiunga na chama cha wafanyakazi anachokipenda kwa ajili ya kuhamasisha na kulinda maslahi yake ya kiuchumi na kijamii.

(6). Kila mfanyakazi anayohaki ya kugoma kama njia ya kushinikiza na kupigania haki na maslahi yake.

Haki ya Elimu22. (1) Kila mtu anayo haki sawa ya kupata elimu

na kila raia anao huru kutafuta elimu katika fani anayopenda hadi kufikia upeo wowote kulingana na stahili na uwezo wake.

(2) Kila mtu anayo haki ya kupata elimu ya msingi bure;

(2) Mamlaka ya nchi inao wajibu wa kuhakikisha kwamba watu wote wanapata fursa sawa na za kutosha kuwawezesha kupata elimu na mafunzo ya ufundi katika ngazi zote za shule na vyuo vinginevyo vya mafunzo.

Haki ya Afya Njema23. (1) Kila mtu ana haki ya kupata haki ya afya

njema ikiwa ni pamoja na huduma ya afya na afya ya uzazi.

(2) Kila mtu ana haki ya kupata mahali pazuri pa kuishi na mazingira mazuri.

(3) Kila mtu ana haki ya kuishi maisha yalio huru kutokana na njaa na kupata chakula cha kutosha na kilicho bora.

(4) Kila mtu ana haki ya kupata maji safi na ya kutosha.

(5) Kila mtu anastahili kuwa na kinga ya hifadhi ya jamii na hasa kwa wale wasiojiweza na wanaowategemea ikiwa ni pamoja na bima ya afya.

(6) Mamlaka ya nchi inalojukumu la kuhakikisha kwamba hakuna mtu atakayenyimwa matibabu ya dharura.

(7) Mtumiaji wa bidhaa ambazo zinahusu afya ana haki zifuatazo:

(a) Kupata huduma bora bila kudhuru afya yake (b) Kupata maelezo kamili ya bidhaa hiyo kabla

hajaitumia (c) Kupata fidia endapo atadhurika na bidhaa

kwa uzembe wa mtoa huduma

Haki ya Familia24. (1) Familia ndiyo mzizi na msingi mkuu wa

jamii. Hivyo, mamlaka husika itahakikisha kwamba familia inalindwa kimwili na kiroho. Familia kama mlinzi mkuu wa maadili, mila na utamaduni katika jamii itakuwa na haki ya kusadiwa.

(2) Kila mtu aliyefikia umri wa miaka kumi na nane atakuwa na haki ya kuoa au kuolewa na mtu wa jinsia tofauti na yake kwa hiari yake mwenyewe.

(3) Mume na mke kwa makubaliano ya pamoja watachagua mfumo wa ndoa yao na mahali wanapotaka kuishi.

(4) Mke na mume watakuwa na haki ya kubaki na majina yao ya ukoo, kuyatumia kama wapendavyo, au kutumia kwa pamoja majina ya koo zote mbili la jina la ukoo mmoja tu wanaochagua.

(5) Mwanamke na mume watakuwa na haki ya kubaki na uraia wao au mmoja kuchukua uraia wa mwenzake.

(6) Mwanamke na mwanamume watakuwa na haki sawa kuhusiana na utaifa wa watoto wao.

(7) Mwanamke na mwanamume watachangia kwa usawa kulinda maslahi ya familia, kulinda na kuwaelimisha watoto wao.

(8) Wanandoa watakuwa na haki sawa wakati wa kufunga ndoa, wakati wa ndoa yao na hata wakati wa kuvunjika kwa ndoa hiyo.

(9) Manawake na wanaume watakuwa na haki sawa katika kuomba kutengana, talaka au kubatilishwa kwa ndoa.

(10) Katika suala la kutengana, talaka au kubatilishwa kwa ndoa wanawake na wanaume watakuwa na haki sawa na majukumu sawa kwa watoto wao. Katika hali yoyote maslahi makuu ya watoto yatapewa kipaumbele cha kwanza.

(11) Katika suala la kutengana, talaka au kubatilishwa kwa ndoa wanawake na wanaume watakuwa na haki sawia katika katika machumo ya ndoa yao.

(12) Mwanandoa hatanyang’anywa haki yake ya kurithi mali au kubaki na kulea watoto wa ndoa yao wakati mwanandoa mwenzake amefariki kwa sababu yoyote ile.

(13) Mamlaka husika itaweka utaratibu wa sheria wa kutambua ndoa zilizoingiwa kwa mujibu wa taratibu mbali mbali kama vile mila, dini au serikali.

Haki za Mlaji25. (1) Walaji watakuwa na haki zifuatazo:(a) bidhaa na huduma zilizo bora;(b) taarifa zilizo lazima ili kufahamu kikamilifu ili

WATU wenye Ulemavu wana haki ya kutoa maoni yao kuhusiana na Mabadiliko ya Katiba Mpya kama anavyoonekana bwana Ame Khamis Ame wa Shehia ya Mangapwani Mdodoni akitoa maoni kuhusu Katiba Mpya ya Tanzania.

kuweza kunufaika na bidhaa na huduma;(c) ulinzi wa afya yao, usalama na manufaa ya

kiuchumi; na(d) fidia kutokana na hasara au maumivu

kutokana na bidhaa au huduma hafifu na zenye kasoro.

(2) Mamlaka husika itaweka sheria na kanuni kutoa kinga kwa mlaji na utaratibu wa utangazaji ulio wa haki, ukweli na heshima.

Haki za Kiutamaduni26. (1) Lugha ya Taifa itakuwa ni Kiswahili.(2) Mamlaka husika itahakikisha kwamba

Sheria zote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinaandikwa kwa lugha ya Kiswahili na hapo ikibidi zitatafsiriwa katika lugha nyingine. Mawasiliano yote ya umma yatakuwa katika lugha ya taifa.

(3) Kila mtu ana haki ya kufurahia lugha yake ya asili na kuzungumza, pia kudumisha utamaduni wake bila kumbagua mwingine kwa mujibu wa sehemu hii ya Haki za Binadamu.

(4) Kila mtu anastahili kunufaika, kuamini na kuhamasisha mila, lugha na utamaduni anaoupenda.

(5) Mila na utamaduni unadhalilisha ubinadamu na kuumiza kimwili na kiroho watu wengine zitazuiliwa na kupigwa marufuku.

(6) Kila mtu ana haki ya kutumia lugha anayoipenda na kushiriki katika maisha na utamaduni anaouchagua.

(7) Mtu hatalazimishwa kufuata aina Fulani ya utamaduni ikiwa ni pamoja na kuongea lugha au kufuata mila na sherehe zake.

Sehemu ya Tano – Haki za Vikundi MaalumWatoto27. (1) Kila mtoto atakuwa na haki zifuatazo za

msingi:(a). Kuwa na jina na utaifa tangu wakati wa

kuzaliwa;(b) Matunzo na urithi kutokana na mali za wazazi

wake, awe amezaliwa ndani au nje ya ndoa;(c) Lishe bora, malazi na matibabu;(d) Elimu ya msingi;(e) Kulindwa kutokana na kazi ngumu ambazo

ni hatari kwa afya, elimu na maendeleo yake;

(f). Kukingwa kutokana na mateso na aina nyingine za ukatili au adhabu ambazo zinamdhalilisha na kumtweza;

(g). Kulindwa kutokana na manyanyaso,

Page 8: Jarida la Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Ifanye haki ... · waliopo katika majimbo yote 50 ya uchaguzi ya Zanzibar. Wasaidizi wa sheria wapo chini ya uongozi wa ZLSC na wanasomeshwa

sheria na haki8 Januari - Machi, 2013

kutekelezwa, madhara ya mila potofu na aina nyingine za adhabu za kinyama

(e) kupata matunzo na ulinzi ikiwa ni pamoja na uwajibikaji wa mama na baba katika kutoa matunzo kwa mtoto, wawe wameoana au hawakuoana; and

(f) Kutowekwa kwenye aina yoyote ile ya kizuizi na kama ikibidi hilo lifanyike:

(i) itakuwa kwa muda mfupi sana; na(ii) atatengwa na watu wazima na jinsia yake na

umri vitatiliwa maanani.(2) Maslahi ya mtoto ni muhimu na yatapewa

kipaumbele katika kila jambo linalomhusu mtoto.

(3) Katika Katiba hii na hasa katika Hati hii ya Haki za Binadamu, mtoto maana yake ni mtu yeyote yule ambaye hajafikisha umri wa miaka kumi na minane.

Watu Wenye Ulemavu28 (1) Mtu yeyote mwenye ulemavu anastahili:-(a) Kushughulikuwa kwa heshima na

kutotendewa au kuitwa kwa njia ya kumdhalilisha;

(b) Kuwezeshwa kuingia katika vyuo na sehemu nyingine za elimu na sehemu zote za umma zitawekewa miundombinu itakayomfanya mlemavu aweze kuitumia vizuri kama watu wengine;

(c) Kuwezeshwa kufikia kwa urahisi sehemu zote za umma ikiwa ni pamoja na usafiri wa umma na taarifa na habari muhimu;

(d) Kuwezeshwa matumizi ya lugha ya alama, uchapaji wa wasioona (Braille) na aina nyingine ya mawasiliano; na

(e) Kuwezeshwa kupata nyaraka na vyombo vingine vinavyo mwezesha kuondoa au kupunguza utegemezi wa watu wengine katika maisha yake ya kila siku.

(2) Serikali itahakikisha kwamba polepole inatakeleza sera ya kimataifa ya kuhakikisha kwamba asili mia tano ya wanaochagulia kuchukua nafasi katika vyombo vyote vya umma ni watu wenye ulemavu.

(3) Watu wenye ulemavu watakuwa na haki ya kuishi na familia zao ikiwa ni pamoja na wazazi au walezi wao na watawezeshwa kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii, ubunifu na za kusherehekea.

(4) Ikiwa itabidi mtu mwenye ulemavu anatakiwa kuishi katika sehemu au makazi maalum, hali na mazingira ya sehemu hiyo itatayarishwa ili ilingane na mazingira anayoishi mtu wa kawaida wa umri wa mtu huyo husika.

(5) Mtu mwenye ulemavu hatatendewa tofauti

na watu wengine kuhusu mahali anapoishi au mambo mengine.

(6) Watu wenye ulemavu wote watalindwa dhidi ya aina zozote za unyonyaji, ubaguzi au kudhalilisha.

(7) Katika shauri lolote la mahakama ambapo mtu mwenye ulemavu anahusika, utaratibu wa sheria utatilia maanani hali ya kimwili na kisaikolojia ya mtu huyo.

(8) Nyumba, barabara na aina nyingine ya miundombinu itatayarishwa kwa namna ambayo itahakikisha kwamba watu wenye ulemavu wanaweza kuitumia bila kipingamizi chochote.

(9) Aina mbali mbali za vivutio vitawekwa ili kuwavutia watu wenye ulemavu waweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za biashara na nyingine za kujipatia kipato na katika ajira ya umma serikali itahakikisha kwamba watu wenye ulemavu wengi wanapatiwa ajira.

(10) Sheria zitatungwa kuhakikisha kwamba yaliomo katika sehemu hii ya Katiba yanatekelezwa kikamilifu.

Vijana29. Mamlaka ya Serikali ina wajibu wa kuhakikisha

kwamba vijana wote:(a) Wanapata elimu na mafunzo ya stadi

mbali mbali kufuatana wa maamuzi yao wenyewe;

(b) Wanapata fursa ya kushiriki kikamilifu katika shughuli zote za kisiasa, kijamii na kiuchumi na sehemu nyingine za maisha.

(c) Wanapata fursa ya kufanya kazi; na(d) Wanalindwa kutokana na mila na utamaduni

mbaya na kunyonywa.

Wanawake30. (1) Mamlaka inayohusika itahakikisha

kwamba Wanawake wanapata haki sawa katika jamii.

(2) Wanawake wanaofanya kazi wanapatiwa fursa kabla na baada ya kujifungua kuweza kupumzika na wakati huo utahesabiwa kama likizo yenye malipo kamili.

(3) Wanawake watapatiwa fursa sawa katika mafunzo na kupandishwa cheo bila ya kuwepo aina yoyote ya kikwazo.

(4) Wanawake wote watapewa fursa kamili kuhusu:

(a) Kuamua kuhusu uzazi wao ikiwa ni pamoja na idadi ya watoto watakaowazaa;

(b) Ulinzi na usimamizi wa miili yao;(c) Kutotumika kama vyombo vya uchunguzi wa

kisayansi bila ya ruhusa yao yenye ufahamu.(5) Watoto wote wanaopata mimba wakiwa bado

masomoni wanapatiwa fursa ya kuendelea na masomo yao baada ya kujifungua.

(6) Serikali itahakikisha kwamba ubaguzi wa aina yoyote ile unaondolewa dhidi ya wanawake na kuhakikisha kwamba haki zote na ulinzi wa mwanamke vinakuwepo kama ilivyoainishwa katika mikataba na matamko mbali mbali ya kimataifa.

Wazee31. (1) Wazee wote wana haki ya kupata haki

zifuatazo:(a) Wanashiriki kikamilifu katika shughuli zote za

kijamii;(b) Wanapewa mwanya wa kushughulikia

maendeleo yao binafsi;(c) Wanaishai kwa heshima bila kubughudhiwa;(d) Wanapata matunzo na msaada kutoka kwa

familia zao na kutoka Serikalini;(e). Wanapata matibabu yaliobora na

yanayokwenda na mahitaji wa umri wao bure;

(f). Wanapata pensheni inayotosha na inayokwenda na wakati bila ya kujali kama walikuwa waajiriwa wa Serikali au Sekta binafsi au walikuwa wamejiajiri wenyewe.

(2) Mamlaka ya nchi itahakikisha kwamba haki wazee wote, bila ya ubaguzi wowote wanapata haki hizi.

(3) Kila mzee, bila ubaguzi wowote, anayo haki ya kupata ulinzi na msaada maalum kufuatana na hali yake ya afya na mahitaji yake ya kiroho.

Sehemu ya Sita – Haki za PamojaMazingira Bora32. (1) Kila mtu anayo haki ya kuishi katika

magingira safi na yanayotoshereza kwa ajili ya maisha yake.

(2) Kila mtu ana haki ya kulindwa dhidi ya uchafuzi wa mazingira ikiwemo kutokuishi karibu na taka ngumu na laini toka viwandani, migodini na sehemu nyingine.

(3) Mamlaka husika itahakikisha kwamba:(a) Panakuwepo mazingira mazuri na

yanayolinda afya ya wananchi wote;(b). Uchafuzi wa mazingira na uharibufu wa

ardhi na bioanuai unazuiwa; na(c) inahamasisha utunzaji na uhifadhi wa

mazingira katika uvunaji wa rasilimali za taifa.

(d) Kuna na mazingira salama kwa manufaa ya kizazi kilichopo na vijavyo kwa kupitia sheria na hatua nyinginezo ambazo.

MAONI yA KATIBA

BAADHI ya wananchi wakitoa mchango wao mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba Zanzibar.

Page 9: Jarida la Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Ifanye haki ... · waliopo katika majimbo yote 50 ya uchaguzi ya Zanzibar. Wasaidizi wa sheria wapo chini ya uongozi wa ZLSC na wanasomeshwa

9sheria na haki Januari - Machi, 2013

Ulinzi na Usalama33. (1) Watu wote wana haki ya kuishi kwa

amani na usalama. Mamlaka ya nchi tahakikisha kwamba panakuwepo na amani na itashikiana na jamii ya kimataifa kuweza kudumisha amani hiyo.

(2) Watu wote wanayo haki ya kunufaika na amani inayotokana na ushirikiano na utengamano wa kimataifa. Mamlaka ya nchi itahakikisha kwamba inaingia mikataba ya kikanda na kimataifa kwa manufaa ya nchi na watu wake.

Rasilimali za Taifa34. (1) Raia wote wanayo haki katika umiliki

wa rasilimali zote na utajiri wote wa nchi na mamlaka husika itahakikisha kwamba rasilimali zote za taifa zinatumika tu kwa manufaa ya wananchi wote.

(2) Raia wote wanayo haki ya kufahamu kwa kikamilifu kuhusu mipango, mikataba na utaratibu mwingine wote wa kuhamisha rasilimali za nchi kutoka kwenye milki yao. Mamlaka ya nchi itahakikisha kwamba inalinda rasilimali zote za nchi na kwamba mambo yote yanayohusu rasilimali hizo yanawekwa wazi kwa kila raia kufahamu.

(3) Raia wote wanao wajibu wa kuhakikisha kwamba hakuna rasilimali yoyote ile ya taifa itakayotolewa bila ya kutilia maanani maslahi ya wananchi wote na kama mali hiyo itatolewa mamlaka husika itahakikisha kwamba wananchi kama wenye rasilimali hiyo wanapata fidia inayolingana na rasilimali hiyo.

Haki ya Maendeleo na Maisha Bora35. (1) Watu wote katika makundi wana haki ya

kupata maendeleo endelevu bila ubaguzi.(2) Kila raia atafurahia haki za kiuchumi, kijamii

na kitamaduni ikiwemo haki ya kupata mafunzo ya ufundi na programu mbalimbali zitakazowekwa na Serikali.

(3) Hatua mahsusi zitachukuliwa kuwalinda wanawake, vijana na watoto dhidi ya unyonyaji wa kiuchumi. Ajira zote za kinyonyaji ni marufuku.

(4) Kila mtu ana Haki ya kufurahia maisha katika kiwango cha wastani chenye kuridhisha na kupata mahitaji muhimu ikiwemo chakula cha kutosha, mavazi ya kutosha na malazi yanayoridhisha kwa mtu huyo na familia yake. Serikali itachukua hatua madhubuti kuhakikisha haki hizi zinatimia kwa wananchi wote bila ubaguzi wa kitabaka au namna iwayo yote.

(5) Kila mtu ana haki ya kufurahia mipango madhubuti ya Taifa ya kuboresha uzalishaji mali, upatikanaji wa mitaji na mbinu mbalimbali za kuboresha kilimo na biashara kwa wananchi hususani wenye kipato cha chini.

(6) Kila mtu ana haki ya kufanya tafiti za kisayansi na kiuchumi kwa manufaa ya nchi.

(7) Kila mtu ana haki ya kufahamishwa juu ya hali ya uchumi wa nchi pale anapotaka kufahamu.

(8) Kila mtu ana haki ya kufahamu na kufahamishwa juu ya mikataba yote Serikali inayoingia na wawekezaji kutoka nchi zingine kuhusu rasilimali za nchi.

Sehemu ya Saba – Wajibu MuhimuKuheshimu Sheria za Nchi36. (1) Kila mtu ana wajibu wa kufuata na

kutii Katiba hii na sheria za Jamhuri ya Muungano.

(2) Kila mtu ana haki, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria, kuchukua hatua za

kisheria kuhakikisha hifadhi ya Katiba na sheria za nchi.

Wajibu wa Kufanya Kazi37. (1) Kila mtu anao wajibu wa:-(a) kushiriki kwa kujituma na kwa uaminifu katika

kazi halali na ya uzalishaji mali; na(b) kutimiza nidhamu ya kazi na kujitahidi kufikia

malengo ya uzalishaji ya binafsi na yale ya pamoja yanayotakiwa au yaliyowekwa na sheria.

(2). Hakutakuwapo na kazi ya shuruti katika Jamhuri ya Muungano.

(3) Kwa madhumuni ya ibara hii, na katika Katiba hii kwa jumla, ifahamike kwamba kazi yoyote haitahesabiwa kuwa ni kazi ya shuruti au kazi ya kikatili au ya kutweza ikiwa ni:

(a) kazi inayobidi ifanywe kutokana na hukumu au amri ya mahakama; au

(b) kazi inayobidi ifanywe na askari wa jeshi lolote katika kutekeleza majukumu yao.

Ulinzi wa Mali za Umma38. (1) Kila mtu ana wajibu wa kulinda raslimali

na mali asilia ya Jamhuri ya Muungano, mali iliyo chini ya Mamlaka ya Nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi.

(2) Watu wote watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali ya mamlaka ya nchi na ya pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhilifu, na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao.

(3) Kila mtu ana wajibu wa kuheshimu mali ya mtu mwingine.

Ulinzi wa Taifa39. (1) Kila raia ana wajibu wa kulinda, kuhifadhi

na kudumisha uhuru, mamlaka, ardhi na umoja wa taifa.

(2) Bunge laweza kutunga sheria zinazofaa kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kutumikia katika majeshi na katika ulinzi wa taifa.

(3) Mtu yeyote hatakuwa na haki ya kutia sahihi kwenye mkataba wa kukubali kushindwa vita na kulitoa taifa kwa mshindi, wala kuridhia au kutambua kitendo cha uvamizi au mgawanyiko wa Jamhuri ya Muungano au wa sehemu yoyote ya ardhi ya eneo la taifa na, bila ya kuathiri Katiba hii na sheria zilizowekwa, na hakuna mtu atakayekuwa na haki ya kuwazuia raia wa Jamhuri ya Muungano kupigana vita dhidi ya adui yeyote anayeshambulia nchi.

(4) Uhaini kama unavyofafanuliwa na sheria utakuwa ni kosa la juu kabisa dhidi ya Jamhuri ya Muungano.

Sehemu ya Nane – Utekelezaji wa Hati ya Haki za BinadamuHaki Muhimu na Wajibu wa Jumla40. (1) Kila mtu katika Jamhuri ya Muungano

anayo haki ya kufaidi haki za msingi za binadamu, na matokeo ya kila mtu kutekeleza wajibu wake kwa jamii, kama zilzivyofafanuliwa katika Hati hii ya Haki za Binadamu.

(2) Kila mtu katika Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kupata hifadhi sawa chini ya sheria za Jamhuri ya Muungano.

(3) Raia yoyote wa Jamhuri ya Muungano hatakuwa na haki, hadhi au cheo maalum kwa misingi ya nasaba, jadi au urithi wake.

(4) Ni marufuku kwa sheria yoyote kutoa haki, hadhi au cheo maalum kwa raia yeyote wa Jamhuri ya Muungano kwa misingi ya nasaba, jadi au urithi.

(5) Ili watu wote waweze kufaidi haki na uhuru vilivyotajwa na Katiba hii kila mtu ana wajibu wa kutenda na kuendesha shughuli zake kwa namna ambayo haitaingilia haki na uhuru wa watu wengine.

Sehemu ya Tisa – Usimamizi na Utekelezaji wa Haki za BinadamuTafsiri ya Haki za Binadamu41. (1) Wakati itakapokuwa inatafsiri vipengele

vya sehemu hii ya Haki za Binadamu, Mahakama, Baraza au chombo kingine chochote cha maamuzi ni lazima kitazingatia yafuatayo:

(a) Haki ya usawa, utu na uhuru wa mtu binafsi na

(b) Sheria za kimataifa za Haki za Binadamu (2) Wakati mahakama itakapokuwa inatoa tafsiri

ya sheria zilizotungwa na Bunge, sheria za kimila ni lazima izingatie misingi ya Haki za Binadamu kwa mujibu wa Surah ii ya Katiba.

Utekelezaji wa Haki42. (1) Mtu yeyote anayedai kuwa haki yoyote

katika Katiba hii inakaribia kuvunjwa, inavunjwa au imeshavunjwa na mamlaka au chombo au uamuzi au sheria au sera yoyote; anaweza kwenda katika mahakama na kuomba nafuu stahiki.

(2) Mtu au watu wafuatao wanaweza kufungua kesi ya kudai haki za kikatiba kwa mujibu wa masharti ya ibara hii:

MAONI yA KATIBA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akitangaza majina ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania.

Page 10: Jarida la Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Ifanye haki ... · waliopo katika majimbo yote 50 ya uchaguzi ya Zanzibar. Wasaidizi wa sheria wapo chini ya uongozi wa ZLSC na wanasomeshwa

sheria na haki10 Januari - Machi, 2013

MAONI yA KATIBA/MATUKIO KATIKA PICHA(a) mtu yeyote anayejiwakilisha mwenyewe;(b) mtu yeyote anayemwakilisha mtu ambaye

hawezi kujiwakilisha mwenyewe kwa mujibu wa sheria;

(c) mtu yeyote anayewakilisha kundi la watu au jamii ya watu fulani wenye kuvunjiwa Haki husika;

(d) Mtu yeyote anayewakilisha jamii kwa maslahi ya umma wa watanzania walio wengi; na

(e) Taasisi inayowawakilisha wanachama wake.(3) Sheria yoyote itakayokiuka haki za binadamu

katika katiba hii itakuwa batili kwa kiwango kile ilichokiuka.

(4) Mtu yeyote anayedai kuwa sharti lolote katika Hati hii ya Haki za Binadamu au katika sheria yoyote inayohusu haki yake au wajibu kwake, limevunjwa, linavunjwa au inaelekea litavunjwa na mtu yeyote popote katika Jamhuri ya Muungano, anaweza kufungua shauri katika Mahakama Kuu.

(5) Mahakama Kuu itakuwa na mamlaka ya kusikiliza kwa mara ya kwanza na kuamua shauri lolote lililoletwa mbele yake kwa kufuata ibara hii; na Mamlaka ya Nchi yaweza kuweka utaratibu kwa ajili ya:-

(a) kusimamia utaratibu wa kufungua mashauri kwa mujibu wa ibara hii;

(b) kufafanua uwezo wa Mahakama Kuu katika kusikiliza mashauri yaliyofunguliwa chini ya ibara hii;

(c) kuhakikisha utekelezaji bora wa madaraka ya Mahakama Kuu, hifadhi na kutilia nguvu haki, uhuru na wajibu kwa mujibu wa Katiba hii.

(6) Utaratibu utakaowekwa utakuwa rahisi na ambao haunyimi au kupunguza haki za wahusika.

(7) Sheria yoyote itakayokiuka haki za binadamu katika katiba hii itakuwa batili kwa kiwango kile ilichokiuka.

(8) Endapo katika shauri lolote inadaiwa kwamba sheria yoyote iliyotungwa au hatua yoyote iliyochukuliwa na Serikali au mamlaka nyingine inafuta au inakatiza haki, uhuru na wajibu muhimu zitokanazo na Hati hii ya Haki za Binadamu, na Mahakama Kuu inaridhika kwamba sheria au hatua inayohusika, kwa kiwango inachopingana na Katiba ni batili au kinyume cha Katiba basi Mahakama Kuu itakuwa na uwezo wa kutamka hivyo na kuanzia hapo jambo hilo halitakuwa halali tena.

Sehemu ya Kumi – Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu

43. (1). Kutakuwa na Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu ambayo kazi na majukumu yatakuwa in pamoja na yafuatayo:-

(a) Kuhamasisha na kulinda Haki za Binadamu na kuendeleza utamaduni wa kuheshimu haki hizi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

(b) Kuhamasisha kuwepo kwa usawa wa kijinsia katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuratibu masuala yote yanayohusu haki na usawa.

(c). Kuhamasisha na kusisitiza ulinzi wa haki za bin adamu kwa watu binafsi, makampuni na asasi zote za kiserikali na zisizo za kiserikali.

(d). Kupokea, kufuatilia, kuchunguza na kutoa taarifa juu ya uvunjwaji wa Haki za Binadamu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

(e) Kupokea malalamiko yote ya uvunjwaji wa Haki za Binadamu na kuchunguza na kuchukua hatua madhubuti ya kusikiliza mashauri hayo na kutoa nafuu husika.

(f). Kutoa Elimu ya Haki za Binadamu kwa wananchi katika ngazi zote.

(2) Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu itaundwa na watu wenye uzoefu na rekodi inayofahamika ya ujuzi na tabia ya kupenda, kutetea na kulinda Haki za Binadamu.

Sehemu ya Kumi na Moja – Mikataba ya Kimataifa ya Haki za Binadamu44. Mkataba wowote wa Kimataifa au wa

Kikanda unaohusu haki za binadamu ambao utaridhiwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utakuwa ni sehemu ya sheria za nchi na utatiliwa nguvu na mahakama kama sheria nyingine yoyote ya Tanzania.

Sehemu ya Kumi na Mbili – Utangazaji wa Hali ya Hatari na Haki za Binadamu

45. Mamlaka inayohusika itahakikisha kwamba ikiwa hali ya hatari itatangazwa, hali hiyo haitaathiri haki na uhuru ilioainishwa katika Hati hii ya haki za binadamu.

SEHEMU yA PILI yA MAONI yA KITUO CHA HUDUMA ZA SHERIA ZANZIBARMpangilio wa Katiba na Baadhi ya Mambo Muhimu ya Kukumbukwa na KufikiriwaMaelezo:(a). Alama za Utaifa (National Symbols)

Kuna vitu fulani ambavyo ni muhimu sana kwa kila Taifa. Hivi ni vitu ambavyo hulitambulisha Taifa la Tanzania popote pale hapa duniani. Ni vizuri vitu hivi viwekwe wazi kwenye Katiba ili vitambuliwe vilindwe kikatiba na kisheria.

BAADHI ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania wakifungua mjadala wa kupokea maoni ya Katiba. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Tume Mhe. Jaji Joseph Warioba (wa kwanza kushoto), Prof. Mwesiga Baregu, Bibi Fatma Said Ali na Bw. Ally Saleh.

Vinaweza kutajwa kwa kifupi kwenye sehemu ya mwazo wa Katiba halafu baadaye kuelezewa maudhui yake kuelezewa kwa kirefu na kwa undani kama moja ya Nyongeza katika Katiba mpya.Vitu hivi ambavyo tunaweza kuviita alama za utaifa (National Symbols) katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni pamoja na:

(i). Bendera; (ii). Court of Arms; (iii). Wimbo wa Taifa; na(iv). Lugha ya Taifa. (b). Upangaji wa Katiba

Pamoja na ukweli kwamba kitu muhimu ni yale yaliomo ndani yake, lakini pia ufasaha wa yalioandikwa katika Katiba na mpangilio wa Katiba unasaidia Katiba kueleweka na hivyo kuvuta heshima kwake. Uandishi mzuri wa Katiba na mpangilio mzuri ni njia mojawapo wa Kuiuza (Marketing of the Constitution) na kuipa heshima kubwa. Vile vile mpangilio wake unaweka yote yaliomo katika muktadha wa kihistoria na uhusiano na waandishi wake.Hivyo basi, Kituo cha Huduma za Sheria cha Zanzibar kinashauri kwamba katika kuitayarisha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mambo yafuatayo yatiliwe maanani:

(i). Katiba inanze na kutangaza Sovereignty of the People;

(ii). Ifuatwe na Supremacy of the Constitution;(iii). Ifuatwe na Ulinzi wa Katiba (Pamoja na

kuwepo utaratibu thabiti wa namna ya kubadilisha Katiba);

(iv). Ieleze Mtanzania ni Nani; (v). Uachwe ule utaratibu wa Kikoloni wa kuanza

na Utawala na Vyombo vyake (Executive) na ianze na Wananchi kama Wenyenchi na Uwakilishi wao (Legislature).

Ni matumaini yetu kwamba Kamisheni hii tukufu itayapokea maoni na mapendekezo yetu na kuyatilia maanani wakati wa kutayarisha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 2014.

Hadi sasa uraia umeelezwa katika Sheria lakini siyo katika Katiba. Katika Katiba zote za hivi karibuni, suala la uraia limepewa uzito mkubwa ikiwa ni pamoja na uamuzi wa kutambua au kutotambua Uraia wa Nchi Mbili (Dual Citizenship) ambao umeleta mjadala mrefu na kufanyiwa utafiti wa kina na Tume ya Kurekebisha Sheria (Law Reform Commission).

Page 11: Jarida la Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Ifanye haki ... · waliopo katika majimbo yote 50 ya uchaguzi ya Zanzibar. Wasaidizi wa sheria wapo chini ya uongozi wa ZLSC na wanasomeshwa

11sheria na haki Januari - Machi, 2013

MAONI yA KATIBA/MATUKIO KATIKA PICHA

BAADHI ya Masheha wa Mkoa wa Kusini Pemba wakishiriki katika mafunzo ya Haki za Watoto yaliyofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Huduma za Sheria Chake Chake Pemba ambayo yemefadhiliwa na Shirika la Save the Children Zanzibar tarehe 14-15 Februari 2013.

MWENyEKITI wa Bodi ya Wadhamini Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar. Profesa Chris Maina Peter, akitowa maelezo ya awali wakati wa uzinduzi wa kitabu cha elimu ya Katiba kwa wananchi katika Ukumbi Mdogo wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar tarehe 22 Januari 2013.

d

d

d

AFISA Mipango wa ZLSC Bwana Taki Abdulla Habib akitoa Elimu ya Haki za Watoto katika Mafunzo ya Watoto yaliyofanyika Chake Chake Pemba ambayo yamefadhiliwa na Shirika la Save the Children Zanzibar tarehe 12 -13 Februari, 2013.

Page 12: Jarida la Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Ifanye haki ... · waliopo katika majimbo yote 50 ya uchaguzi ya Zanzibar. Wasaidizi wa sheria wapo chini ya uongozi wa ZLSC na wanasomeshwa

sheria na haki12 Januari - Machi, 2013

MAKALA yA SHERIA

Inaendelea Uk. 13

Na Khalfan A. Mohammed ZLSC Pemba

Utangulizi

WANAFUNZI, watu wenye ulemavu na wazee ni miongoni wa wanaopata

taabu katika kulipa nauli za usafiri wa barabarani. Kanuni za Usafiri Barabarani za mwaka 2004 zinaelezea taratibu zitakazowawezesha makundi maalum ya watu katika jamii kupata nafuu katika kulipa nauli ya usafiri wa barabarani. Makala hii inaaeleza utaratibu wa kupata nafuu ya nauli ya usafiri wa barabarani.

Mamlaka iliyotunga KanuniKanuni zimetungwa chini ya uwezo

aliyopewa Waziri dhamana wa Usafiri wa Barabarani katika Kifungu cha 80 cha Sheria ya Usafiri wa Barabarani, Nam.7 ya 2003. Kanuni ya 86 (1) ya Kanuni za Usafiri wa Barabarani ya mwaka 2004 imesema kwamba kutakuwa na nafuu katika ulipaji wa nauli kwa watu wanaohusika wanaposafiri kwa kutumia gari za abiria.

Kwa mujibu wa kanuni ya 86 (2) ya Kanuni za Usafiri wa Barabarani ya 2004, watu maalum wanaweza kupata nafuu kulingana na hali zao. Wanaostahiki kupata nafuu ni:-

i. Wanafunzi;ii. Watu wenye ulemavu; naiii. Wazee.

Sifa za kupata nafuu ya nauli kwa wanafunzi

Mazingira yafuatayo yanazingatiwa ili mwanafunzi akubalike kulipa nafuu ya nauli. Mazingira hayo ni:a. Mwananfunzi wa chekechekea bila ya

kuzingatia masafa kutoka nyumbani

kwao na skuli,b. Mwanafunzi wa Skuli ya Msingi

ambaye anaishi zaidi ya masafa ya kilomita 1.5 kutoka skuli na nyumbani kwao;

c. Mwanafunzi wa Sekondari ambaye anaishi zaidi masafa ya zaidi ya kilomita mbili kutoka skuli na nyumbani kwao;

d. Mwanafunzi wa Taasisi za Mafunzo ya Amali ambaye anaishi masafa ya zaidi ya kilomita 2.5 kutoka skuli na nyumbani kwao.

Kanuni ya 86 (4) ya Kanuni hii inaeleza kuwa ni muhimu kuwepo kitambulisho cha kupata nafuu kwa mwanafunzi. Kitambulisho hicho kitakuwa ni kwa ajili ya safari baina ya nyumbani na skuli tu. Kitabmbulisho hakitotumika kwa shughuli za nje ya skuli.

Sifa za watu wenye ulemavuKanuni ya 86 (5) ya Kanuni hii inasema kwamba watu wenye ulemavu ambao wanastahiki kupata nafuu ya kulipa nauli ni:-

i. Mtu asiyeona kikamilifu;ii. Kiziwi au bubu;iii. Mtu mwenye matatizo ya akili,iv. Asiye na mikono;v. Asiye na mguu (kiwete)

Sifa za wazeeKanuni ya 86 (6) ya Kanuni hii inasema kwamba wazee wanaostahiki kupata kitambulisho cha kulipa nauli nafuu ni wanawake na wanaume walio na umri wa miaka sitini (60) na zaidi.

Vitambulisho vya nafuu Kanuni ya 87 (2) ya Kanuni hii

kutakuwa na aina tatu za vitambulisho

vya nafuu katika kulipa nauli za gari za abiria ambavyo ni:-

a) Kitambulisho cha rangi nyeupe. Hiki ni kitambulisho kwa ajili ya mwanafunzi;

b) Kitambulisho cha rangi ya kijani isiyokoza kwa ajili ya watu wenye ulemavu; na

c) Kitambulisho cha rangi ya buluu isiyokoza kwa ajili ya wazee.

Matumizi ya vitambulisho vya kupata nafuu katika gari za abiria

Kanuni ya 87 (3) ya Kanuni hii inaeleza kuwa kitambulisho cha kupata nafuu katika gari za abiria kinamruhusu mmiliki wa kitambulisho kulipa nusu nauli kwa kuzingatia mambo yafuatayo:-i. Kwa mwanafunzi, kwa safari za

kutoka nyumbani na kwenda skuli na kurudi;

ii. Kwa watu wenye ulemavu na wazee kwa kila safari zao wakiwa Zanzibar.

Taratibu za uombaji wa vitambulisho vya kupata nafuu katika gari za abiria(a) MwanafunziMwanafunzi ataomba kitambulisho:a. Atakapojiunga na skuli za Chekechea;b. Anapoendelea kutoka Chekechea

kwenda Skuli ya Msingi;c. Anapoendelea kutoka msingi kwenda

skuli ya sekondari;d. Atakapojiunga na Chuo au Taasisi ya

Mafunzo ya Amali;e. Atakapobadilisha jina, skuli au mahali

anapoishi ataomba kibali upya. Kanuni ya 88 (2) ya Kanuni hii maombi ya kitambulisho yatafanywa katika fomu itakayotolewa na Mamlaka husika. Upande wa mwanafunzi, fomu itachukuliwa na mzazi/mlezi wa muombaji na kutoka katika skuli husika ambaye ataijaza na kuisaini ikiwa mwanafunzi yupo chini ya umri wa miaka 16.

Vile vile, Kanuni ya 88 (3) na (4) ya Kanuni hii inaeleza kuwa fomu ya mwanafunzi iliyokamilishwa iambatanishwe na risiti ya malipo ya ada, picha tatu (passport size) za mwanafunzi. Zitarejeshwa skuli ambayo itathibitisha uwepo wa mwanafunzi katika skuli hiyo na sifa za kupata kitambulisho kuangalia kigezo cha masafa. Na baada ya kuthibitisha uwepo wa mwanafuzi na sifa za kupata kitambulisho cha kupata nafuu, skuli itaipeleka fomu hiyoMamlaka ya Usafiri wa Barabarani au jumuiya ya waendeshaji (operators association) ambayo itatoa kitambulisho

taratibu za Kupata nafuu Ulipaji wa nauli za gari za Abiria

BAADHI ya wanafunzi wakijadiliana na kondakta wa gari ya abiria kuhusu ulipaji nusu ya nauli.

Page 13: Jarida la Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Ifanye haki ... · waliopo katika majimbo yote 50 ya uchaguzi ya Zanzibar. Wasaidizi wa sheria wapo chini ya uongozi wa ZLSC na wanasomeshwa

13sheria na haki Januari - Machi, 2013

MAKALA yA SHERIA

Inatoka Uk. 12kwa mwanafunzi baada ya kulipa ada inayotakiwa.

A. Mzee Kanuni ya 88 (5) ya Kanuni hii inaeleza

kuwa maombi ya mzee yakiwa na risiti ya malipo ya ada, picha tatu (passport size) na cheti cha kuzaliwa au hati ya kiapo ya muombaji yatawasilishwa Mamlaka ya Usafiri wa Barabarani au Jumuiya ya Waendeshaji (Operators Association)

B. Watu wenye Ulemavu Vile vile Kanuni ya 88 (6) ya Kanuni hii

inaeleza kuwa maombi ya Mtu mwenye ulemavu yakiwa na risiti ya malipo ya ada, picha tatu (passport size) na cheti cha kuzaliwa au hati ya kiapo ya muombaji yatawasilishwa Mamlaka ya Usafiri wa Barabarani au jumuiya ya uendeshaji (Operators Asociation)

Kwa watu wenye ulemavu na watu wenye umri wa zaidi ya miaka 70 fomu zitachukuliwa Mamlaka ya Usafiri wa Barabarani na muombaji au mtu yeyote kwa niaba yake.

Pia inafaa ifahamike watu wenye ulemavu wa kutoona au mtu asiyoona kikamilifu, kiziwi au bubu na mtu mwenye matatizo ya akili maombi ni lazima yaambatanishwe na cheti cha uthibitisho kutoka kwa daktari wa magonjwa hayo kinachoelezea uwepo wa moja kati ya aina hizo tatu za ulemavu.

Kanuni ya 88 (8) ya Kanuni hii inaeleza ikiwa Mamlaka au jumuiya itajiridhisha juu ya ulemavu au umri wa muombaji itatoa kitambulisho cha kupata nafuu kwa muombaji. Pia inaelezwa kuwa kwa wazee kitambulisho kitatolewa wiki moja baada ya maombi na baada kukamilisha

malipo ya ada.

Uchukuaji wa kitambulishoImeelezwa katika Kanuni ya 89 (1) ya

Kanuni hii kuwa kila mtu ambaye atakuwa na kitambulisho cha kupata nafuu wakati wa kulipa nauli katika gari za abiria atakionyesha kwa kondakta wakati wa kulipa nauli.

Pia Kanuni ya 89 (2) ya Kanuni hii inaeleza kuwa mtu yeyote wakati anaposafiri kwa kutumia usafiri wa umma na kudai kuwa ana sifa za kupata nafuu katika kulipa nauli lakini akashindwa kuonyesha kitambulisho chake atalazimika kulipa nauli kamili ambayo inatakiwa kulipwa na kila mtu.

Kanuni ya 91(3) ya Kanuni hii inaeleza kuwa wakati wa kusubiri kitambulisho chengine, mwanafunzi, mtu mwenye ulemavu au mzee atalipa nauli kamili atakaposafiri kwa kutumia gari za abiria.

Kusimamishwa na kufutwa kwa kitambulisho cha kupata nafuu

Kitambulisho cha mwanafunzi cha kupata nafuu kitasitishwa mpaka siku 20 za skuli au kufutwa ikiwa mwanafunzi atashindwa kufuata kanuni za maadili zitakazoanzishwa na Mamlaka ya Usafiri wa Barabarani.

Kufutwa kwa kitambulisho cha kupata nafuu

Inaelezwa katika Kanuni ya 93 ya Kanuni hii kuwa Mamlaka ya Usafiri au jumuiya ya waendeshaji (Operators Association) inaweza kufuta kitambulisho cha kupata nafuu katika kulipa nauli za gari za abiria pale itakapogundulika kuwa kimetolewa kimakosa au kutokana na uwasilishaji wa taarifa za uongo

uliofanywa na muombaji.

Changamoto i. Wahusika wa kupata nafuu hawajui

kuwepo kanuni;ii. Mamlaka husika kutotoa elimu ya

kutosha kuhusiana na Kanuni hizi;iii. Kanuni haikueleza mtu atatoa kiasi

gani na hivyo maafisa wanaweza kuamua vyovyote na hivyo kutoa mwanya wa rushwa katika utoaji wa vitambulisho;

iv. Kanuni haikutoa adahabu yoyote kwa kondakta au dereva atakayekataa kitambulisho halali kilichotolewa na mamlaka husika kwa mtu anayestahiki kupata nafuu.

Mapendekezo a. Kutolewe elimu kuhusiana na uwepo

wa Kanuni hizi;b. Mamalaka husika zifanye juhudi za

makusudi ili kuwashajihisha watu wanaostahiki kuomba vitambulisho hivi ili waweze kupata nafuu na kuondoa usumbufu kwa wahusika;

c. Madereva na makondakta wapewe elimu juu ya kufuata taratibu zinazohusu kanuni hii.

Hitimisho Uzoefu unaonyesha kuwa wanafunzi,

watu wenye ulemavu na wazee wamekuwa wakisumbuliwa sana kuhusu ulipaji wa nauli. Ni wakati muafaka mamlaka husika kuzitekeleza kikamilifu Kanuni hizi ili kuondoa usumbufu kwa wahusika. Ni bora Mamlaka ya Usafiri kusambaza fomu katika skuli zote za Zanzibar.

taratibu za Kupata nafuu Ulipaji wa nauli za gari za Abiria

KITUo kikuu cha gari za abiria (daladala) katika eneo la Darajani mjini Zanzibar

Page 14: Jarida la Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Ifanye haki ... · waliopo katika majimbo yote 50 ya uchaguzi ya Zanzibar. Wasaidizi wa sheria wapo chini ya uongozi wa ZLSC na wanasomeshwa

sheria na haki14 Januari - Machi, 2013

HOTUBA

Mheshimiwa Mgeni Rasmi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Jaji Mkuu wa Zanzibar,Mheshimiwa Spika wa Baraza la Wawakilishi,Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria,Waheshimiwa Majaji, Mahakimu, Makadhi na Mawakili,Waheshimiwa Viongozi wa Dini,Waheshimiwa Wanasheria wenzangu,Waheshimiwa Wageni Waalikwa,Mabibi na Mabwana,Assalamu Alaykum.

Kwanza napenda nichukue nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia na kutuwezesha sote kukutana hapa leo kwa ajili ya shughuli hii. Pili, natoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Mgeni Rasmi kwa kuweza kuwa na sisi kwa mara nyengine tena. Tatu, naomba nimshukuru pia Mheshimiwa Jaji Mkuu wa Zanzibar kwa jitihada zake kubwa za kuendeleza utamaduni huu wa kutuwezesha wadau wote wa sekta ya sheria na usimamizi wa utoaji haki hapa Zanzibar kukutana kila mwaka kwa ajili ya shughuli hii muhimu. Nne, nawashukuru waandaaji kwa kunipa fursa hii maalum ili niseme maneno angalau machache katika hafla hii.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni kutokomeza unyanyasaji wa kijinsia. Na ni vyema tukakumbuka kwamba kitovu kikuu cha unyanyasaji wa kijinsia ni ubaguzi. Kwa kweli, ubaguzi ni kitendo kisichukubalika hata kidogo na ni kwenda kinyume na Katiba, sheria na maadili ya jamii yetu. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar zote zinakataza ubaguzi wa aina yoyote.

Kwa kawaida unyanyasaji wa kijinsia ni aina ya ubaguzi ambao hutumia visingizio vya jinsi, umri, maumbile au hali ya mtu. Kwa mfano, mara nyingi wanaoathirika na ubaguzi wa unyanyasaji unaofanywa kwa kutumia kisingizio cha jinsi ni wanawake; wanaoathirika kwa unyanyasaji unaofanywa kwa kutumia kisingizio cha umri ni watoto na wakongwe; wanaoathirika kwa unyanyasaji unaofanywa kwa kisingizio cha maumbile yao ni watu wenye ulemavu; na wanaoathirika kwa unyanyasaji unaofanywa kwa kisingizio cha hali zao ni wale watu wenye mahitaji maalum kama vile wale wanaoishi na virusi vya ukimwi ambapo unyanyasaji hujitokeza kwa njia ya kuwanyanyapaa watu hao. Zote hizi ni anuwai za unyanyasaji wa kijinsia ambazo tunawajibika kuzitokomeza.

Utokomezaji wa unyanyasaji wa kijinsia ni lazima uanzie kwenye malezi yanayopatikana kwenye familia zetu. Familia ndiyo chuo kikuu cha malezi ya kimaadili katika jamii yoyote. Familia zikiharibika na jamii nayo huharibika. Tunapaswa kutokomeza aina zote za unyanyasaji wa kijinsia kwanza kwenye famila zetu.

Tusiwadharau wala tusiwavunje moyo watoto wa kike na wanawake kwa ujumla, tusiwajengee viburi na majivuno watoto wa kiume na wanaume kwa ujumla, halikadhalika kusiwepo ukatili dhidi ya watoto wote wa kike na wa kiume na hata dhidi wa wanawake na wanaume kwa ujumla.

Vile vile tunapaswa kulitizama suala hili la unyanyasaji wa kijinsia kuwa ni suala linalohusu uvunjaji wa haki za msingi za binaadamu. Haki inayovunjwa kwa njia ya unyanyasaji wa kijinsia ni ile haki ya usawa wa binaadamu yaani binaadamu mmoja kuwa sawa na binaadamu mwengine. Misingi mikuu ya haki za binaadamu inatamka kwamba kila binaadamu ana haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.

Sehemu ya XV ya Sheria ya Makosa ya Jinai Nambari 6 ya 2004 inahusu makosa mbali mbali dhidi ya maadili, kwa mfano, kubaka, kulawiti, kutorosha watoto wa kike na wa kiume, kunajisi watoto wa kiume au watu wenye ulemavu wa akili, uwekaji wa madanguro, uzinifu, unyanyasaji wa kingono,na kuingilia maharimu.

Yote haya yamekatazwa na yamewekewa adhabu kali kwenye sheria. Sehemu ya XVI ya sheria hiyo inahusu makosa mbali mbali yanayotokea ndani ya ndoa na kwenye mahusiano ya ndani ya nyumba zetu, kwa mfano, ukatili dhidi ya watoto, utelekezaji wa watoto, kutowapatia watoto mahitaji ya lazima na usafirishaji haramu wa watoto na watu wazima. Adhabu kali zimewekwa kwa makosa hayo.

Sheria ya Watoto Nambari 6 ya 2011, Sheria ya Haki na Fursa za Watu wenye Ulemavu Nambari 9 ya 2006, Sheria ya Kuwalinda Wanawari na Watoto Waliozaliwa na Mzazi Mmoja Nambari 4 ya 2005, na Sheria ya Elimu Nambari 6 ya 1982 zote hizo zinakataza waziwazi udhalilishaji wa kijinsia.

Kwa upande wa sheria zetu hapa Zanzibar kwa hakika inadhihirika kwamba sheria zinakataza udhalilishaji wa kijinsia kwenye familia zetu, kwenye taasisi za elimu na katika jamii kwa ujumla. Kwa upande wa sekta ya ajira Sheria ya Ajira Nambari 11 ya 2005 kwenye kifungu cha 10 na kifungu cha 11 inakataza ubaguzi na unyanyasaji wa kijinsia kwenye ajira; Sheria ya Utumishi wa Umma Nambari 2 ya 2011 kwenye kifungu cha 7 (2) (h) (iii) nayo pia inakataza unyanyasaji wa kijinsia kwenye utumishi wa umma.

Hatahivyo, changamoto nyingi zinajitokeza kwenye utekelezaji wa sheria hizo. Kwanza, kuhusu utoaji wa ripoti za matukio ya unyanyasaji wa kijinsia na utoaji wa ushirikiano kwa vyombo husika vya upelelezi. Katika jamii bado kuna watu miongoni mwetu hawajawa tayari kuvunja ukimya dhidi ya matendo ya unyanyasaji wa kijinsia kwani matukio mengi hayaripotiwi kwenye vyombo husika.

Muamko mdogo wa jamii, kukwepa aibu na unyanyapaa, kushuka kwa imani ya baadhi ya watu kuhusu vyombo vya sheria, ucheleweshaji kwenye ufuatiliaji, gharama zinazojitokeza kwenye ufuatiliaji na jamii kupendelea zaidi njia mbadala za usuluhishi kuliko njia za kisheria ni miongoni mwa sababu za changamoto hiyo.

Pili, changamoto kwenye upelelezi wa makosa ya unyanyasaji wa kijinsia ni pamoja na upungufu wa wapelelezi mabingwa waliobobea kwenye fani hiyo na upungufu wa vifaa vya kisasa vya kisayansi vya

HOTUBA YA MKURUGENZI WA MASHTAKA KATIKA SHEREHE ZA SIKU YA SHERIA ZANZIBAR, TAREHE 07/02/2013

MKURUgENZI wa Mashtaka Zanzibar Mhe. Ibrahim Mzee, alipokuwa akitowa hotuba wakati wa sherehe za maadhimisho ya kilele cha Siku ya Sheria Zanzibar katika viwanja vya Victoria garden Mjini Zanzibar tarehe 7 Februari 2013.

Page 15: Jarida la Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Ifanye haki ... · waliopo katika majimbo yote 50 ya uchaguzi ya Zanzibar. Wasaidizi wa sheria wapo chini ya uongozi wa ZLSC na wanasomeshwa

15sheria na haki Januari - Machi, 2013

HOTUBA

kukusanyia ushahidi na kufanyia uchunguzi ushahidi uliokusanywa. Pamoja na mapungufu hayo, tunatoa pongezi kwa Jeshi la Polisi kwa kuanzisha madawati maalum ya kushughulikia kesi za wanawake na watoto kwa kila wilaya. Hiyo ni hatua muhimu katika kukabiliana na tatizo la unyanyasaji wa kijinsia. Aidha, kuanzishwa kwa vituo vya mkono kwa mkono (One stop centres) kwanye hospitali zetu kuu ni mwanzo mzuri kwa uchunguzi wa kesi za unyanyasaji.

Tatu, kwenye uendeshaji wa mashtaka kuna changamoto kubwa ya kwamba bado tunaendelea kutegemea ushahidi wa moja kwa moja wa mtu aliyeona tukio la uhalifu ushahidi ambao hutolewa kwa mdomo (Oral evidence) kwenye kesi hizo za unyanyasaji wa kijinsia. Mara nyingi matendo kama ya ubakaji hufanyika katika mazingira ya siri ambapo huwa hakuna shahidi aliyeona kwa macho yake.

Kwahivyo, hutegemewa zaidi ushahidi wa kimazingira na maelezo ya yule mtu mwenyewe aliyefanyiwa matendo hayo. Hali huwa ngumu zaidi kiushahidi endapo aliyetendewa matendo hayo ni mtoto au ana ulemavu wa akili kwani ushahidi wao hupungua uzito kidogo; kisheria endapo kuna wasiwasi au mashaka kwenye ushahidi anaenufaika ni mtuhumiwa.

Uzoefu wa nchi nyengine ni kwamba wahalifu wengi hutiwa hatiani kwa makosa ya ubakaji kwa mfano kutokana na ushahidi wa kisayansi (forensic evidence) ambao hupatikana kutoka kwenye mwili wa mtuhumiwa au mwili wa aliyebakwa, au kutoka kwenye eneo la tukio ambapo uhalifu ulitendeka.

Kwa upande mwengine, uendeshaji wa mashtaka unakuwa mgumu kwa kesi hizi kwasababu hata katika ushahidi wa mdomo bado wananchi wengi ama kwa hofu au muhali hawapendi wala hawataki kusimama mahakamani kutoa ushahidi.

Kauli mbiu ya Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar inasema hakuna hatia bila ya ushahidi, usikatae wala usidharau kutoa ushahidi. Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka tayari inaanzisha kitengo maalum cha kuwasidia na kujenga ujasiri kwa mashahidi na wale waliofanyiwa vitendo vya uhalifu ili waweze kutoa ushahidi wao mahkamani bila ya hofu.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, (wa tatu kushoto), Jaji Kiongozi wa Mahkama Kuu Tanzania Mhe. Fakih Jundu (kutoka kushoto) na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mhe. Nassor Ahmed Mazrui ambaye alikuwa anakaimu nafasi ya Waziri wa Katiba na Sheria, (kutoka kulia) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi khamis, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Pandu Ameir Kificho na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. omar othman Makungu, wakiangalia Kikundi cha Wasanii cha Black Roots kilipokua kikitumbuiza katika Siku ya Sheria Zanzibar tarehe 7 Februari, 2013.

Nne, changamoto kwenye mahkama ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu muwafaka hasa kwa mahakama za watoto, wingi wa kesi na uchache wa mahakimu unaopelekea ucheleweshaji wa kesi za udhalilishaji wa kijinsia na ukosefu wa mafunzo ya mara kwa mara kwa mahakimu na majaji kuhusu namna bora na za kisasa za kusikiliza kesi hizo. Vile vile, tuhuma za rushwa kwenye utoaji wa dhamana bila ya kufuata utaratibu wa kisheria ambapo washtakiwa hukimbia na hakuna wadhamini wa uhakika wanaoweza kuchukuliwa hatua. Tabia ya baadhi ya mawakili wa utetezi kuwatisha au kuwakasirisha kwa makusudi mashahidi wa upande wa mashtaka ili wasiweze au wababaike kutoa ushahidi; mahkama zetu zimekuwa kimya hazikemei tabia hiyo ambayo inakwenda kinyume na maadili ya kazi ya uwakili.

Tano, asasi za kiraia hususan zile zinazojihusisha na masuala ya sheria zinafanya kazi kubwa ya kutoa msaada wa kisheria kwa njia ya elimu kwa umma na kwa kutoa ushauri wa kisheria kwa mtu mmoja mmoja anaekabiliwa na matatizo ya udhalilishaji wa kijinsia. Hatahivyo, asasi hizo bado hazijachangia sana katika utoaji wa msaada wa kisheria kwenye uendeshaji au utetezi wa kesi za madai zinazowahusu watu waliokumbwa na matukio ya unyanyasaji wa kijinsia kwa kudhulumiwa mali zao ama na wake wao au waume wao.

Mwisho kabisa naomba nisisitize tena kwamba vita vya kutokomeza udhalilishaji wa kijinsia ni vyetu sote kwa pamoja kwani udhalilishaji wa kijinsia una athari kubwa kijamii, kiafya na kisaikolojia na unarudisha nyuma maendeleo ya nchi.

Tuzidishe mashirikiano katika ngazi zote kuanzia kwenye shehia zetu zote 335 za Unguja na Pemba hadi ngazi ya taifa na tuendelee kushirikiana na wenzetu wa Wizara ya Afya na wa Wizara ya Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto na asasi za kiraia katika kutokomeza udhalilishaji wa kijinsia. Kinachohitajika ni kuzuia vitendo hivyo vya udhalilishaji visifanyike, kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wanaotenda vitendo hivyo na kuwasaidia ipasavyo wale wote walioathirika na vitendo hivyo.

Nawashukuruni ahsanteni sana kwa kunisikiliza.

Page 16: Jarida la Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Ifanye haki ... · waliopo katika majimbo yote 50 ya uchaguzi ya Zanzibar. Wasaidizi wa sheria wapo chini ya uongozi wa ZLSC na wanasomeshwa

sheria na haki16 Januari - Machi, 2013

HOTUBA

HOTUBA YA RAIS WA CHAMA CHA WANASHERIA ZANZIBAR KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA ZANZIBAR TAREHE 07-02-2013

KATIKA VIWANJA VYA VICTORIA GARDEN, ZANZIBAR.

Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Jaji Mkuu ,Mheshimiwa Jaji Kiongozi wa Tanzania,Waheshimiwa Majaji wa Mahkama Kuu,Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria,Mheshimiwa Spika wa Baraza La Wawakilishi, Mheshimiwa Kadhi Mkuu ,Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu ,Mheshimiwa Mkurugenzi wa Mashtaka,-Mheshimiwa Mkuu Wa Mkoa Wa Mjini Magharibi,Mheshimiwa Mrajis Wa Mahkama Kuu , Waheshimiwa Mahakimu na Makadhi wote mliohudhuria,-Waheshimiwa Viongozi wa Dini,Waheshimiwa Mawakili wote mliohudhuria, kutokea Afisi ya Mwanasheria Mkuu, Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na Mawakili wa kujitegemea,Waheshimiwa wafanyakazi na watendaji wote wa Mahkama mliohudhuria,Wageni waalikwa,Mabibi na Mabwana,ASSALAM-ALEYKUM,

Awali ya yote hatuna budi kumshukuru Mwenyenzi Mungu, kwa Rehma na Ukarimu wake wa kutujaalia sote uzima na afya njema na kutukutanisha tena katika Maadhimisho Ya Siku Ya Sheria Zanzibar yakiwa ni Maadhimisho ya pili katika historia ya Nchi yetu.

Mhe. Mgeni Rasmi, sisi Chama Cha Wanasheria Zanzibar tukiwa wadau katika maadhimisho haya, tunapenda kutamka furaha yetu kwako kwa kuweza kujumuika nasi katika Maadhimisho haya bila kujali shughuli nyingi ulizonazo za Kitaifa.

Kwa kawaida Maadhimisho haya yanayoashiria kuanza rasmi kwa shughuli za Kimahkama kwa mwaka husika hutoa fursa ya kuwakutanisha

kwa pamoja wanasheria kutoka Taasisi Kuu za Sheria Zanzibar na kuweza kujumuika pamoja na kujadiliana mambo yanayohusiana na tasnia ya sheria kwa ujumla, kuangalia changamoto inazozikabili tasnia hii na kutafuta njia bora za kutatua changamoto hizo.

Mhe. Mgeni Rasmi, kama unavyojua, kauli mbiu yetu katika Maadhimisho haya ni “Kutokomeza unyanyasaji wa kijinsia”. Dhana ya unyanyasaji wa kijinsia ni dhana iliyo pana ikiwa inajumuisha matendo yote yanayolenga kumdhalilisha na kumdunisha mtu na utu wake na hatuna budi juhudi za utokomezaji wake zichukuliwe kufuatana na upana wake. Athari za matendo ya unyanyasaji wa kijinsia haziishii kwa matokeo yaliyo dhahiri ya kimwili na kiheshima tu bali pia huambatana na athari za muda mrefu za kisaikolojia ambazo huwa ni jinamizi linalomuandama muathirika na hata familia yake daima.

Mhe. Mgeni Rasmi, unyanyasaji wa kijinsia si uovu mpya katika jamii yetu. Ni vitendo ambavyo ni vikongwe kama ilivyo jamii yenyewe. Hata hivyo mambo mawili katika eneo hili ndio yanayotulazimu kujipanga upya kama jamii na kuweza kupambana na matendo haya.

Jambo la kwanza ni tabia inayoanza kujengeka ndani ya jamii yetu ya kuyachukulia matendo ya unyanyasaji wa kijinsia kama mtindo wa kawaida katika maisha yetu na hivyo jamii kuyaona kuwa ni jumla ya mambo maovu ya kawaida tu yasiyoshtua wala kuathiri hisia na dhamira zetu. Mambo haya yameanza kuchukuliwa kwa uwepesi na yameanza kuzoeleka.

Tabia hii ikiendelea kuna hatari ya kufikia wakati matendo haya kuonekana ni sehemu ya maisha yetu na yatazagaa katika jamii na

hivyo juhudi za kupambana nayo hazitakuwa na tija yoyote.

Jambo la pili ni kasi ya ongezeko la matendo ya unyanyasaji wa kijinsia. Ongezeko hili sio tu ni la idadi lakini pia ni la ukubwa wa matendo yenyewe. Takriban Taasisi zote zinazojishughulisha na masuala ya unyanyasaji wa kijinsia zinaonesha kuwepo kwa ongezeko kubwa la matendo ya unyanyasaji wa kijinsia. Kwa mfano kwa Mkoa wa Mjini Magharibi pekee kwa mwaka 2011 kesi 464 zimeripotiwa zikihusisha matendo ya unyanyasaji wa kijinsia kama utoroshaji (kesi 103) ubakaji (kesi 57) kulawiti (kesi 32) mimba (kesi 100) ubakaji kwa kundi (kesi 4) matendo ya kashfa (kesi 166) uingiliaji watoto wadogo (kesi 6). Hata hivyo tukumbuke kuwa takwimu hizi ni kwa matukio yaliyoripotiwa tu , na ukweli ni kuwa mengi ya matukio ya unyanyasaji wa kijinsia huwa hayaripotiwi na hivyo takwimu hizi hazitowi taswira kamili ya ukubwa wa tatizo hili.

Mhe. Mgeni Rasmi, katika muktadha huu huu wa ongezeko la vitendo hivi hatuwezi kuhitimisha bila kugusia ongezeko la vitendo hivi kulikosababishwa na ujio wa teknolojia ya mawasiliano ya intaneti na mitandao yenye mnasaba nayo.

Ni jambo la kusikitisha mno kuwa maendeleo katika uwanja wa mawasiliano yanatumiwa vibaya na wale wenye uchu wa unyanyasaji wa kijinsia na wakati wa kutenda uovu wao huamua kuwarekodi waathirika na kusambaza picha zao kupitia mitandao ya aina mbali mbali. Huu ni udhalilishaji usiostahiki chembe ya huruma. Hivi sasa matukio ya aina hii katika jamii yetu yameanza kuibuka kwa kasi. Na baya zaidi baadhi ya watu hushabikia kwa kurushiana picha za matukio ya aina hii. Mh mgeni rasmi kutenda uovu wa unyanyasaji wa kijinsia hususan kwa mtoto aliye chini ya umri ni idhilali isiyo kifani ila kumrekodi na kusambaza matukio hayo ni unyama uliovuka viwango vya udhalilishaji!

Mhe. Mgeni Rasmi, katika kutathmini unyanyasaji wa kijinsia hatuna budi tuangalie vyanzo vinavyopelekea kuwepo na kuongezeka kwa vitendo hivi ili tuweze kubuni njia za kutokomeza uovu huu katika jamii.

Jambo la kwanza lililopelekea kuongezeka kwa vitendo hivi ni kuporomoka kwa Maadili ndani ya Jamii yetu. Ni jambo lililo wazi kuwa njia nyepesi ya kuweza kufanikisha harakati za kutokomeza unyanyasaji wa kijinsia ni kwa Jamii kurudi katika misingi ya maadili yetu.

Jambo la pili lililopelekea ongezeko la vitendo hivi ni kuwepo kwa ulegelege katika kukabiliana na vitendo hivi ikihusisha mambo kadhaa, baadhi yake ikiwa ni kama yafuatayo:

La kwanza, ni tabia iliyojengeka katika jamii yetu ya kuyaficha matendo haya na hivyo

RAIS wa Chama cha wanasheria Zanzibar (ZLS) akitoa hotuba siku ya sheria Zanzibar Tarehe 7, Februari, 2013.

Page 17: Jarida la Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Ifanye haki ... · waliopo katika majimbo yote 50 ya uchaguzi ya Zanzibar. Wasaidizi wa sheria wapo chini ya uongozi wa ZLSC na wanasomeshwa

17sheria na haki Januari - Machi, 2013

HOTUBAkupelekea kuwa kikwazo kikubwa katika kuyatokomeza. Hatuna budi kama Jamii kuanza kubadilika kwa dhati na kuhakikisha matendo haya yanawekwa wazi, yanaripotiwa na hatua kali za kisheria kuchukuliwa dhidi ya wahusika. Mficha ugonjwa mauti humfichua.

La pili, ni utamaduni unaoshika kasi wa kuhalalisha unyanyasaji kwa ama kumuozesha muathirika wa unyanyasaji wa kijinsia kwa mtu aliyemtendea unyanyasaji huo au familia kukubali kupokea fidia hafifu ili mambo yaishe. Jamii isipoepuka mambo haya unyanyasaji utaendelea kushamiri. Unyanyasaji wa kijinsia usipite katika mkondo wa aina unaolenga kuuhalalisha.

Eneo la tatu ni ulegevu katika usimamizi wa hatua za kisheria kuanzia upelelezi, mashtaka hadi hukumu. Eneo hili nalo lina changamoto nyingi. Udhaifu mkubwa unaanzia katika hatua ya upelelezi ambapo yamekuwepo madai kuwa Taasisi zinazosimamia upelelezi hazijatoa umuhimu stahiki kwa kesi za aina hii. Sambamba na hilo hali inakuwa ngumu zaidi pale tukio lenyewe linaporipotiwa baada ya muda mrefu kupita. Udhaifu huu ni moja kati ya sababu zinazopelekea kesi za aina hii kuishia kufutwa au washtakiwa kutotiwa hatiani, jambo ambalo linavunja moyo na kukatisha tamaa waathirika na jamii kwa jumla.

Kwa mfano katika mwaka 2010 kesi za unyanyasaji wa kijinsia 50 zilifunguliwa Mahkamani na kati ya hizo kesi 32 zimetolewa maamuzi ambapo katika hizo ni kesi 2 tu ndizo washtakiwa wametiwa hatiani.

Kwa mwaka 2011 kesi 77 zilifunguliwa, kesi 34 zimetolewa uamuzi na katika hizo ni kesi moja tu ambayo mshtakiwa ametiwa hatiani. Ni wazi kuwa inamsononesha muathirika kuwa baada ya kufanyiwa unyanyasaji na akauripoti huku akibeba madhila yanayoambatana na yeye kutoa ushahidi mwisho wa siku hukumu

inamuachia huru kutokana na kasoro za kiupelelezi au kiuendeshaji mashtaka au udhaifu katika utoaji hukumu.

Hali hii inaashiria kuwepo kwa kasoro kubwa katika kusimamia kesi za aina hii , si ajabu basi katika hali ya kukata tamaa jamii imeona ichukue hatua mbadala ikiwemo kuwaozesha waathirika kwa wanyanyasaji wao!!!

Kwa hali ilivyo kuna haja ya kuzidisha uangalizi na usimamizi katika hatua zote zinazohusisha kesi za unyanyasaji wa kijinsia tokea zinapofikishwa katika vyombo vya sheria ili ushughulikiaji wake katika ngazi zote ufanywe kwa umahiri na umakini mkubwa.

Eneo la nne ni kuwa kesi hizi bado hazijapewa uzito unaostahiki katika sheria zinazozisimamia na utaratibu unaopaswa kufuatwa. Kwa mfano kesi za kujihusisha na madawa ya kulevya ambazo adhabu yake ni kifungo cha miaka 20 mshtakiwa kwa mujibu wa sheria hastahiki kupewa dhamana lakini kesi ya kumuingilia mtoto kinyume na maumbile ambayo adhabu yake ni kifungo cha maisha mshtakiwa ana haki ya kupewa dhamana.

Kesi za unyanyasaji wa kijinsia ni jumla ya kesi ambazo zingestahiki kupewa kipaumbele kisheria ili kuhakikisha zinasikilizwa na kumalizwa kwa haraka na hukumu kutolewa kwa muda muafaka ili athari ya adhabu itimize lengo lake la msingi ambalo ni kutoa onyo kali kwa Jamii mbali na lile lengo la kumuadhibu mshtakiwa.

Kwa mfano adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka 15 kwa mshtakiwa iliyotolewa takriban wiki 2 zilizopita na Mahkama Kuu ya Zanzibar chini ya Jaji Mh Abdulhakim Ameir Issa katika Rufaa ya Jinai No 18/2011 (DPP v. Hamad Bakar Mohd) imetoa onyo kali kwa jamii kwamba sheria kali zipo na vyombo vinavyosimamia viko makini. Kesi

VIoNgoZI wakisimama wakati wimbo wa Taifa wa Zanzibar ukipigwa na Brass Band ya polisi katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar alipowasili Rais wa Zanzibar, Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, aliyekuwa Mgeni rasmi katika hafla hiyo, iliyofanyika viwanja vya Victoria garden Mjini Unguja tarehe 7 Februari 2013.

hii ni kielelezo cha mporomoko wa misingi ya maadili yetu. Mshtakiwa ni Mwalimu mashuhuri wa Madrasa ya Quraan inayoitwa Madrasatul Qadiriya mtu mzima mwenye umri wa miaka 48 ambaye alishtakiwa kwa kosa la kumuingilia kinyume cha maumbile mtoto mdogo mwanafunzi wake mwenye umri wa miaka 11. Pamoja na kuwa kesi hii ilichukuwa muda mrefu - miaka mitatu na wiki moja - lakini hukumu yake imetoa funzo kwa jamii.

Eneo la tano ni kukosekana kwa nyenzo muhimu za kitaalam zinazohitajika katika usimamizi wa masuala haya kama vile mashine ya kuchunguza DNA, madaktari wataalam wa uchunguzi na pia utaalam maalum wa kiuchunguzi wanaostahiki kuwa nao wanaoendesha na kusimamia uchunguzi wa masuala haya (forensic science).

Mhe. Mgeni Rasmi, tukiwa katika maadhimisho haya ya kuashiria kuanza rasmi kwa shughuli za Kimahkama kwa mwaka huu wa 2013 tunapenda kuchukua fursa hii kuzipongeza juhudi zinazochukuliwa na Serikali yako katika kuuimarisha Mhimili wa Mahkama na hasa maboresho katika maslahi ya Watendaji wa Mhimili huu muhimu.

Ni imani yetu kuwa juhudi hizi zinaendelea na kuwafikia Mahakimu wetu wa Mahkama za Mwanzo yaani Primary Court Magistrates ambako huko nako ndiko kiwango kikubwa cha shughuli za utoaji haki zinakofanyika ili kuweza kuwajengea mazingira ya kukwepa vichocheo vinavyoweza kuwafanya waipoteze njia ya haki.

Mheshimiwa mgeni rasmi, naomba nikiwa mwingi wa heshima, kuwasilisha na niwashukuru wote kwa kunisikiliza.

Awadh Ali SaidRais Chama Cha Wanasheria, Zanzibar

Page 18: Jarida la Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Ifanye haki ... · waliopo katika majimbo yote 50 ya uchaguzi ya Zanzibar. Wasaidizi wa sheria wapo chini ya uongozi wa ZLSC na wanasomeshwa

sheria na haki18 Januari - Machi, 2013

TAMKO

Haki ya kuishi ni haki ya msingi ambayo huzaa haki nyengine zote alizonazo binadamu, haki hizo huzipata binadamu kwa sababu ya kuzaliwa kwake pamoja na kuwa hai.

Hivi karibuni kumejitokeza matukio mbali mbali hapa nchini ambayo yana muelekeo mkubwa wa kuvunja haki za binadamu ikiwemo haki ya kuishi na haki ya kuabudu. Hii inathibitika na tukio la mauaji yaliyofanyika siku ya Jumapili tarehe 17 Febuari, 2013 mnamo majira ya saa 12:45 asubuhi, ambapo Kiongozi Mkuu wa Kanisa, Padri Evarist Gabriel Mushi wa Kanisa Katoliki – Parokia ya Beit El-Ras Visiwani Zanzibar, alipouwawa na watu wasiojulikana baada ya kumfyatulia risasi tatu za kichwa akiwa ndani ya gari yake ambapo alikuwa anakaribia mno na Kanisa lake na hatimaye kuuwawa papo hapo.

Padri huyo alikuwa anakwenda Kanisani kwa ajili ya kuongoza sala ya kawaida (misa) kwa waumini wake ambao kwa muda huo walishajiandaa kupokea sala iliyotarajiwa kuongozwa na marehemu.

Aidha siku mbili baadaye mnamo tarehe 19/2/2013 majira ya saa 10 za Alfajiri kuliripotiwa tukio la kuchomwa moto Kanisa la Siloam Ministry International liliopo Kianga – Wilaya ya Kati Unguja.Ilielewa kuwa kundi la watu wasiojulikana walichoma moto Kanisa hilo na kusababisha uharibifu wa mali na kusababisha hasara inayokisiwa Shilingi za Kitanzania Milioni Tatu na Nusu (3,500,000)

Kiini cha matukio hayo ingawa kwa sasa bado hakijajulikana mbali na sababu nyengine zinazohusika moja kwa moja lakini pia hii inatokana na Jeshi la Polisi kuacha waziwazi kufanya upelelezi na kufungua kesi za aina kama hii katika Mahakama ambapo athari hii inasababisha wanajamii kukosa woga na hatimae kuendelea kufanya matukio ya kinyama kama hayo.

Aidha, udhaifu mwengine ni kwa Jeshi la Polisi kushindwa kudhibiti na kuzuia Raia/Wananchi kuweza kuingiza, kumiliki na kutumia waziwazi silaha za moto na hatari nchini. Kitendo ambacho ni kinyume na sheria za nchi.

Kitendo hiki cha mauaji na uchomaji wa Kanisa kimeleta athari kubwa si tu kwa waumini na wanafamilia kumpoteza Kiongozi wao wa kidini, lakini pia kimedhihirisha uvunjifu mkubwa wa Haki za Binadamu na kimevunja haki ya msingi ya kuishi; haki ya kuabudu; na haki ya kumiliki mali ambazo zinalindwa na Katiba za Nchi na kila mtu anatakiwa azipate akiwa pahala popote pale.

Kuhusu haki hizi tatu muhimu zimeainishwa vizuri katika Katiba zetu ambazo zinasema ifuatavyo:-Haki ya Kuishi:I.

Ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inaeleza kuwa:14 Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka kwa jamii hifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria.

Vile vile kifungu cha 13 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kinaeleza kuwa:

13 (1) Kila mtu anayo haki ya kuwa na hifadhi ya maisha yake

(2) Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka kwa jamii hifadhi ya maisha yake kwa mujibu wa sheria.

TAMKO LA KITUO CHA HUDUMA ZA SHERIA ZANZIBAR (ZLSC) KUHUSIANA NA MAUAJI YA PADRI EVARIST GABRIEL MUSHI WA KANISA KATOLIKI LA MTAKATIFU JOSEPH PAROKIA YA BEIT-EL-RAS VISIWANI ZANZIBAR PAMOJA NA UCHOMWAJI

WA KANISA LA SILOAM MINISTRY INTERNATIONAL LILIOPO KIANGA UNGUJA.

ZanZibar legal services centre (Zlsc)House No. 37 Migombani (Opposite Migoz Supermarket)P.O.Box 3360 ZanZibar - TanZaniaTel: +255 24 2233784 Fax: +255 24 2234495E-Mail: [email protected]: www.zlsc.or.tz

suB-OfficE: Chake Chake Pemba Tel: +255 24 2452936

Ifanye haki

Iwe shauku

Page 19: Jarida la Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Ifanye haki ... · waliopo katika majimbo yote 50 ya uchaguzi ya Zanzibar. Wasaidizi wa sheria wapo chini ya uongozi wa ZLSC na wanasomeshwa

19sheria na haki Januari - Machi, 2013

TAMKO

Haki ya KuabuduII. Ibara ya 19 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inasema:

19 (1) Kila mtu anastahiki kuwa na uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu kubadilisha dini au imani yake.

(2) Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari la mtu binafsi, na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi.

Pia Kifungu cha 19 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kinasema kuwa: 19 (1) Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, wa imani na wa uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na

uhuru wa kubadilisha dini au imani yake.

Haki ya Kumiliki Mali III. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ibara ya 24 inatambua haki ya kumiliki mali. Inasema:24 (1) Kila mtu anayo haki ya kumiliki mali, na haki ya hifadhi ya mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria.

(2) Ni marufuku kwa mtu yeyote kunyang’anywa mali yake kwa madhumuni ya kutaifisha au madhumuni mengineyo bila ya idhini ya sheria ambayyo inaweka masharti ya kutoa fidia inayostahili.

Kwa upande za Zanzibar Kifungu cha 17 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kinatoa kinga kutokana na kudhulumiwa mali.

Hivyo, ni wazi kwamba haki hizi zinatambuliwa wazi Kikatiba na zinastahili kupewa uzito unaostahili na kuheshimiwa.

Aidha, matukio hayo ya mauaji ya kiongozi huyo na uchomwaji wa Kanisa siyo tu ni ya kuhuzunisha, kusikitisha, kukasirisha, bali pia yanavunja na kukiuka Katiba na sheria za nchi, matamko pamoja na Mikataba mbali mbali ya kimataifa yanayozungumzia Haki za Binadamu.

Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) kikiwa mdau na msimamizi wa Haki za Binadamu kinatoa Tamko la kulaani vikali matukio hayo kwa sababu linavunja misingi muhimu ya Haki za Binadamu, lakini pia matukio haya yanaweza kuchangia kupandikiza na kuendeleza chuki na uhasama miongoni mwa waumini wa dini zilizopo nchini na hatimae uvunjifu wa amani na usalama nchini unaweza kutoweka.

Hivyo, Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kutokana na athari hizo kinashauri yafuatayo:Serikali inapaswa kuchukua hatua za haraka na za kudumu ili kukomesha vitendo hivyo.1. Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi na upelelezi wa kina ili wanaohusika na matukio haya wabanwe na sheria.2. Jeshi la Polisi kuzuia uingiaji, umiliki na matumizi ya silaha za mtoto kwa wananchi ili kuzuia matukio kama 3. haya kutokea tena nchiniSerikali kupitia viongozi wake ni lazima wachukua juhudi za kivitendo za makusudi na za waziwazi za 4. kushughulikia matukio ya aina hii badala ya kubakia kulaani kwa mdomo tu.Katiba na sheria zote za nchi ziheshimiwe, kufuatwa na kusimamiwa kikamilifu.5. Kudumisha uvumilivu, ustahamilivu, usalama na amani ili kuepuka vitendo vya ulipizaji kisasi kwa wafuasi na 6. waathirika wa matukio hayo.Kituo kinaungana na azima ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete 7. kuomba msaada kutoka nje ya Tanzania kuchunguza chanzo cha mauaji hayo na ikiwezekana kwa uchomaji wa Kanisa uliofanyika sasa na ule uliofanyika mwezi Mei, 2012 ambapo Makanisa matatu yalichomwa.

Mwisho tunatoa pole na salamu za rambirambi kwa familia ya Padri Mushi, Viongozi wa Makanisa yote ya Zanzibar, Tanzania na Waumini wake kwa ujumla. Aidha, Kituo kinawaomba wawe na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu na Mungu awape nguvu na uvumilivu.

Amina

…………………………..Prof. Chris Maina Peter

MwenyekitiBodi ya Wadhamini

Kituo cha Huduma za Sheria, Zanzibar

Imetolewa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, leo Ijumaa tarehe 22 Febuari, 2013.

Page 20: Jarida la Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Ifanye haki ... · waliopo katika majimbo yote 50 ya uchaguzi ya Zanzibar. Wasaidizi wa sheria wapo chini ya uongozi wa ZLSC na wanasomeshwa

sheria na haki20 Januari - Machi, 2013

Jarida la Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar

Toleo Na. 013 Jarida la kila miezi mitatu Januari - Machi, 2013

Ifanye haki

Iwe shauku

MTOTO wa miaka 17 (jina linahifadhiwa) amefikishwa katika

Mahkama ya Mkoa, Pemba akishtakiwa kusababisha kifo cha Bwana Suleiman Seif (60) katika kijiji cha Vumba, Shehia ya Vitongoji, Wilaya ya Chake Chake, Mkoa wa Kusini, Pemba.Alisomewa shtaka la mauaji mbele ya hakimu wa Mahkama ya Mkoa Chake Chake, Pemba, Mheshimiwa Khamis Ramadhani tarehe 18 Februari, 2013.

Amerudishwa rumande na kesi ya Nam. 1/2013 ilipangwa kutajwa tarehe 12 Machi, 2013.

Mwendesha Mashtaka kutoka

JARIDA la Sheria na Haki la Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC)

limetimiza miaka mitatu tokea kuanzishwa. Jarida hutolewa kila baada ya miezi mitatu. Linaelezea shughuli mbali mbali za Kituo,

Mtoto Ashtakiwa Mauaji Pemba

jarida la ZLSC Latimiza miaka mitatu

habari na makala za Sheria kwa lengo la kuelimisha jamii kuhusu sheria.

Mkurugenzi wa ZLSC, Bibi Harusi Miraji Mpatani alisema uchapishaji wa Jarida ulianza tarehe 8 April, 2010 na kuzinduliwa na aliyekuwa

JENgo la Mahkama ya Chake Chake Pemba.

MIoNgoNI mwa Majarida yaliyochapishwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar.

Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka bw. Ali Bilali alidai kwamba mtoto huyo alimpiga kisu cha shingo marehemu Suleiman Seif aliyekuwa amekaa nyumbani pamoja na familia yake.

Ilidaiwa kwamba marehemu alifariki duniani alipokuwa akipelekwa katika hospital ya Chake Chake kwa ajili ya matibabu.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 14 cha Sheria ya Uhalifu Nam. 6 ya Mwaka 2004, Sheria za Zanzibar, mtu aliye chini ya miaka 14 anakuwa hana dhima ya uhalifu mpaka ithibitishwe vyenginevyo.

Waziri wa Katiba, Sheria na Utawala bora, Mheshimiwa Ramadhani Abdalla Shaabani.

Alisema ZLSC imeimarisha Jarida na kuandika hotuba zinazotolewa na viongozi wa ndani na nje ya nchi zinazohusiana na Sheria.

Jarida linasambazwa ndani na nje ya Zanzibar bila malipo. Baadhi ya taasisi za Serikali na binafsi zinapewa nakala ya Jarida.

ZLSC inachapisha nakala 1,000 katika kila toleo.

ZLSC inasisitiza kwa wasomaji kuleta michango na maoni yao ili kumairisha Jarida letu.