6
TANESCO MITANDAONI APRILI 2021 1 “Tunayaangaza maisha yako” Toleo Na 14 Aprili 27, 2021 Jarida la Jarida la TANESCO yetu Tumekuwa na mafanikio makubwa kwenye Sekta ya Nishati, tumeongeza megawati za umeme hadi kufikia 1,602 ambapo mahitaji ya juu ya umeme ndani ya Nchi yetu kwa sasa ni megawati 1,200 SEKTA YA NISHATI YA UMEME IMEKUWA NA MAFANIKIO - RAIS SAMIA Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ZIARA JULIUS NYERERE

Jarida la TANESCO y etu

  • Upload
    others

  • View
    5

  • Download
    2

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Jarida la TANESCO y etu

TANESCO MITANDAONI APRILI 2021 1

“Tunayaangaza maisha yako”

Toleo Na 14 Aprili 27, 2021

Jarida laJarida la

TANESCOyetuTumekuwa na mafanikio makubwa kwenye Sekta ya Nishati, tumeongeza

megawati za umeme hadi kufikia 1,602 ambapo

mahitaji ya juu ya umeme ndani ya Nchi yetu kwa sasa ni megawati 1,200

SEKTA YA NISHATI YA UMEME IMEKUWA NA MAFANIKIO - RAIS SAMIA

Mhe. Samia Suluhu HassanRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

ZIARA JULIUS NYERERE

Page 2: Jarida la TANESCO y etu

TANESCO MITANDAONI APRILI 2021 2

“Tunayaangaza maisha yako”

Akihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Aprili 22, 2021, Rais wa Jamhuri ya Muungano

wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania imekuwa na manufaa makubwa kwenye Sekta ya Nishati kwa kuongeza uzalishaji za umeme hadi kufikia megawati 1,602.

Rais Samia aliongeza kuwa, mahitaji ya umeme nchini kwa hivi sasa yanafikia megawati 1,200 na kuongeza Serikali kupitia TANESCO imefanikiwa kufikisha umeme kwenye Vijiji 10,294 ambayo ni sawa na asilimia 83.3 ya Vijiji 12,317 vilivyopo nchini.

Aliongeza Serikali ya Awamu ya Sita itaendeleza jitihada za kuimarisha upatikanaji wa nishati ya umeme na kufikisha umeme kwenye Vijiji 1,974 vilivyobaki.

“Tumeanza pia utekelezaji wa mradi mkubwa wa umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere utakaozalisha megawati 2,115, mradi huu kwa sasa umefikia asilimia 45 hivyo basi Serikali ya Awamu ya Sita itakamilisha ujenzi wa bwawa la Nyerere” alisema Rais Samia.

Aidha, Serikali inajipanga kuanza utekelezaji wa kuanza miradi ya kuzalisha umeme kwa kutumia maji ya Ruhudji megawati 358 na Rumakali megawati 222, Kikonge megawati 300, pia utekelezaji wa miradi ya umeme wa gesi asilia Mtwara megawati 300, Somangafungu megawati 330, Kinyerezi III megawati 600 na Kinyerezi IV megawati 300.

Rais Samia alisema kutokana na kasi ya mabadiliko ya tabia ya Nchi Serikali

imedhamilia kuchanganya vyanzo vya nishati ili kuwa na uhakika wa nishati ya umeme wakati wote.

“Hivyo basi tutaangalia uwezekano wa kutekeleza miradi ya nishati jadilifu inayotokana na jua, upepo pamoja na joto ardhi, tutafanya hivyo kwa kuwa vyanzo hivi ni endelevu na tunatarajia katika miaka hii mitano kuzalisha megawati 1,100 kupitia vyanzo hivyo” alisisitiza Rais Samia.

Katika hatua nyingine Serikali itaendelea kujenga njia za kusafirisha umeme wa msongo wa kilovolti 400 kutoka kwenye mradi wa Julias Nyerere hadi kituo kikuu cha kupokea na kupoza umeme cha Chalinze pamoja na ujenzi wa njia za umeme zinazoelekea kwenye maeneo ambayo hayajaunganishwa na gridi ya Taifa ili kupunguza gharama za uzalishaji umeme kwa kutumia mafuta na kuokoa asilimia ya umeme inayopotea.

Tutaangalia uwezekano wa kutekeleza miradi

ya nishati jadidifu inayotokana na jua, upepo na jotoardhi, tutafanya hivyo kwa kuwa vyanzo hivi ni

endelevu na tunatarajia katika miaka hii mitano

kuzalisha megawati 1,100 kupitia vyanzo

hivyo.

Mhe. Samia Suluhu HassanRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

HOTUBA YA RAIS BUNGENI

Page 3: Jarida la TANESCO y etu

TANESCO MITANDAONI APRILI 2021 3

“Tunayaangaza maisha yako”

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) amesema Mradi wa Kufua

Umeme kwa maji wa Julius Nyerere Mw 2115 utakamilika kwa wakati mwezi Juni 2022 kama ilivyopangwa.

Mhe. Majaliwa ameyasema hayo Aprili 10, 2021 alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa Julius Nyerere unaotekelezwa katika Mikoa ya Pwani na Morogoro.

Maendeleo ya Mradi yamemridhisha Mhe. Majaliwa na akatoa pongezi kwa Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme TANESCO na Mshauri Mwelekezi TECU kwa usimamizi mzuri.

“Wakandarasi wamenihakikishia kukamilisha ujenzi wa mradi kwa wakati lakini pia katika viwango vinavyotakiwa ili kutuachia mradi ambao utakua na ubora na thamani kama tulivyo kubaliana” alisisitiza Mhe. Majaliwa.

Aidha, amesema Serikali imedhamiria kupeleka Umeme hadi kwenye Vitogoji, ikiwa ni pamoja na vilivyopo visiwani akitolea mfano visiwa vya Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika, na Ziwa Nyasa pamoja na visiwa vilivyopo kwenye ukanda wa Bahari ya Hindi.

Aidha, ameongeza kuwa mradi wa Julius Nyerere unaenda sambamba na ujenzi wa njia kuu ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovolti 400 kutoka Julius Nyerere hadi Chalinze na kuingizwa kwenye gridi ya Taifa.

Ujenzi wa njia hiyo ya kusafirisha umeme unatekelezwa na TANESCO na hadi saa zabuni

imeshatangazwa kwaajili ya kuanza kwa ujenzi huo pamoja na kituo cha kupokea na kupoza umeme wa kilovolti 400 eneo la Chalinze.

Mradi wa kufua umeme kwa Maji wa Julius Nyerere unajengwa na kampuni zenye ubia za Arab Constructor na Elsewedy Electric zote za kutoka nchini Misri.

Mradi huo unatarajiwa kuzalisha Megawati 2,115 ambazo zitaingizwa kwenye grid ya Taifa na kuifanya nchi kuwa na umeme mwingi na wa uhakika.

Mbali na kuliwezesha Taifa kuwa na umeme wa uhakika, pia mradi huo umewezesha kutoa ajira kwa Watanzania zaidi ya 6,000.

Kukamilika kwa utekelezaji wa mradi huo,

kutaiwezesha Tanzania kuzalisha kiasi kikubwa cha umeme kitakachosaidia maendeleo ya viwanda na huduma ya umeme Vijijini na kuweza kuuza umeme wa ziada kwa Nchi jirani.

ZIARA JNHPP

Mradi wa Julius Nyerere kukamilika kwa wakati na kwa viwango stahiki

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akikagua utekelezaji wa Mradi wa Julius Nyerere.

Page 4: Jarida la TANESCO y etu

TANESCO MITANDAONI APRILI 2021 4

“Tunayaangaza maisha yako”

Ujenzi eneo la kuunganisha mitambo ya kufua umeme (erection bay), kabla ya mashine kusimikwa kwenye jengo la kuendeshea mitambo.

Utekelezaji wa mradi wa Julius Nyerere unaendelea kushika kasi ambapo Jengo la mitambo ya kufua umeme kwenye mradi wa Julius Nyerere lina urefu wa zaid mita 300, upana wa mita 60 .

Eneo hili ni kati ya maeneo muhimu kwenye mradi wa Julius Nyerere kwani ndipo itakapo simikwa mitambo tisa ya kufua umeme kila mmoja ukiwa na uwezo wa kufua megawati 235.

Akielezea kazi zinazoendelea kwenye eneo la ujenzi wa jengo la mitambo ya kufua umeme Mhandisi Ujenzi kwenye mradi wa

Julius Nyerere, David Myumbilwa amesema utekelezaji wa eneo hilo umegawanyika katika maeneo makuu manne.

Alizitaja sehemu hizo kuwa ni eneo la kuunganisha mitambo (Erection bay) kabla ya mashine kusimikwa kwenye jengo la mitambo.

Eneo lingine ni Auxiliary building( Eneo la mifumo Saidizi kwa ajili ya mitambo ), eneo la tatu ni jengo itakaposimikwa mitambo (main power house) mitambo tisa ya kufua umeme na eneo la nne ni jengo la kuendeshea mitambo (Control building)

Kazi ya uchimbaji wa eneo la jengo la mitambo imekamilika kwa asilimia 98 na hivi sasa ni ujenzi wa misingi (foundation) inaendelea. Utekelezaji wa kazi zote za ujenzi kwa ujumla wa jengo hili la mitambo umefikia asilimia 44.8.

“Upande wa mtambo wa tisa na wa saba ufungaji wa nondo na umwagaji zege

umeshaanza kwa ajili ya ujenzi wa misingi ya mitambo hiyo, jumla

kutakuwa na mitambo 9 ya kufua umeme pamoja

na transfoma 27 kwa ajili ya kukuza msongo wa umeme uliozalishwa kutoka kilovolti 15.75

hadi kilovolti 400” alisema Mhandisi

Myumbilwa. Mhandisi Myumbilwa aliongza kuwa

umeme utakaokuzwa kwa msongo wa kilovolti 400 utasafirishwa kutoka Julius Nyerere hadi Chalinze ambapo utaingizwa kwenye gridi ya Taifa kupitia kituo cha kupokea na kusafirisha umeme cha Chalinze.

Alimalizia kwa kusema kuwa kukamilika kwa mradi wa Julius Nyerere kutaifanya Nchi kuwa na umeme mwingi na wa uhakika.

UTEKELEZAJI MRADI WA JULIUS NYERERE

Mhandisi David Myumbilwa Mhandisi Ujenzi JNHPP

Page 5: Jarida la TANESCO y etu

TANESCO MITANDAONI APRILI 2021 5

“Tunayaangaza maisha yako”

Maeneo mengine ambayo utekelezaji wa mradi wa Julius Nyerere unaendelea kushika kasi ni eneo la tuta kuu la

kuhifadhia maji, kituo cha kupokea na kusafirisha umeme na daraja la kudumu (permanent bridge).

Tukiangalia hatua za ujenzi wa tuta kuu ukuta umeshainuliwa kwa upande wa kushoto na kulia kwa kimo cha mita 92 na inatarajiwa hadi kufikia mwezi wa 11 ukuta utakuwa umefikia mita 131 ambapo utakuwa tayari kwa ajili ya kuanza kwa zoezi la kujaza maji kwenye bwawa la Nyerere.

Aidha, yameshasimikwa mabomba mawili upande wa kushoto wa tuta kati ya matano ambayo yatatumika kupitisha maji kwenda kwa watumiaji waliopo eneo la chini la mto Rufiji na kwa ajili ya matumizi ya viumbe hai wakati wa zoezi la kujaza maji kwenye bwawa la kufua umeme litakapoanza.

Kazi ya ujenzi wa bwawa la kufua umeme ulianza mwezi Oktoba 2019 katika kipengele cha uchimbaji eneo la bwawa na maandalizi mengine na ujenzi wa bwawa unatatajiwa kukamilika mwanzoni mwa mwaka 2022.

Maeneo mengine ya awali katika ujenzi wa bwawa ambayo yamekamilka ni nji ya uchepushaji maji,

Il i kujenga bwawa, maji yalitakiwa kuchepushwa ambapo uchimbaji wa handaki (Divisional tunnel) ya kuchepushia maji umekamilika kwa asilimia 100 na hivi sasa maji yanapita katika handaki mchepuko.

Aidha, ujenzi kituo cha kupokea na kusafirisha umeme (Switch yard) unaendelea ambapo misingi imeshajengwa na kituo cha kupokea na kusambaza umeme kinatarajiwa kukamilika mwezi Mei 2022

Kwa upande wa daraja la kudumu lina urefu

wa mita 250 likikamilika linatarajiwa kuwa kiunganishi upande wa kushoto na upande wa kulia wa mto rufiji ambapo ndipo jengo la mitambo ya kuzalisha umeme linajengwa.

Daraja hilo lina geti za pembeni mbili (abutments), kulia na kushoto na geti za katikati mbili kushoto na kulia.

Kazi inayoendelea sasa ni ujenzi wa misingi kwa kusimika nguzo za zege zenye kipenyo cha mita 1.2 na kwenda chini kimo cha mita 30, jumla ya nguzo zote zipo 84 na tayari zimesimikwa nguzo(pile) 79

Daraja hili ni muhimu kwakua ndilo litakalotumika kuvusha mitambo yote kwenye jengo la mitambo na pia ndio litakalotumika na wafanyakazi wa mradi kipindi cha uendeashaji mitambo baada ya mradi kukamilika.

Maeneo mengine ambayo utekelezaji wa mradi wa Julius Nyerere unaendelea kushika kasi ni eneo la tuta kuu la

kuhifadhia maji, kituo cha kupokea na kusafirisha umeme na daraja la kudumu (permanent bridge).

Tukiangalia hatua za ujenzi wa tuta kuu ukuta umeshainuliwa kwa upande wa kushoto na kulia kwa kimo cha mita 92 na inatarajiwa hadi kufikia mwezi wa 11 ukuta utakuwa umefikia mita 131 ambapo utakuwa tayari kwa ajili ya kuanza kwa zoezi la kujaza maji kwenye bwawa la Nyerere.

Aidha, yameshasimikwa mabomba mawili upande wa kushoto wa tuta kati ya matano ambayo yatatumika kupitisha maji kwenda kwa watumiaji waliopo eneo la chini la mto Rufiji na kwa ajili ya matumizi ya viumbe hai wakati wa zoezi la kujaza maji kwenye bwawa la kufua umeme litakapoanza.

Kazi ya ujenzi wa bwawa la kufua umeme ulianza mwezi Oktoba 2019 katika kipengele cha uchimbaji eneo la bwawa na maandalizi mengine na ujenzi wa bwawa unatatajiwa kukamilika mwanzoni mwa mwaka 2022.

Maeneo mengine ya awali katika ujenzi wa bwawa ambayo yamekamilka ni nji ya uchepushaji maji,

Il i kujenga bwawa, maji yalitakiwa kuchepushwa ambapo uchimbaji wa handaki (Divisional tunnel) ya kuchepushia maji umekamilika kwa asilimia 100 na hivi sasa maji yanapita katika handaki mchepuko.

Aidha, ujenzi kituo cha kupokea na kusafirisha umeme (Switch yard) unaendelea ambapo misingi imeshajengwa na kituo cha kupokea na kusambaza umeme kinatarajiwa kukamilika mwezi Mei 2022

Kwa upande wa daraja la kudumu lina urefu

wa mita 250 likikamilika linatarajiwa kuwa kiunganishi upande wa kushoto na upande wa kulia wa mto rufiji ambapo ndipo jengo la mitambo ya kuzalisha umeme linajengwa.

Daraja hilo lina geti za pembeni mbili (abutments), kulia na kushoto na geti za katikati mbili kushoto na kulia.

Kazi inayoendelea sasa ni ujenzi wa misingi kwa kusimika nguzo za zege zenye kipenyo cha mita 1.2 na kwenda chini kimo cha mita 30, jumla ya nguzo zote zipo 84 na tayari zimesimikwa nguzo(pile) 79

Daraja hili ni muhimu kwakua ndilo litakalotumika kuvusha mitambo yote kwenye jengo la mitambo na pia ndio litakalotumika na wafanyakazi wa mradi kipindi cha uendeashaji mitambo baada ya mradi kukamilika.

UTEKELEZAJI MRADI WA JULIUS NYERERE

BODI YA UHARIRI:

Mwenyekiti:Dkt. Tito E. MwinukaMkurugenzi Mtendaji TANESCO Mhariri Mkuu: Johary KachwambaMeneja Uhusiano

Wachangiaji:Grace KisyombeYasini SilayoSalama KasamaluSamia Chande

Msanifu wa kurasa:Henry Kilasila

Page 6: Jarida la TANESCO y etu

TANESCO MITANDAONI APRILI 2021 6

“Tunayaangaza maisha yako”

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya Shilingi Milioni 4, katika hospitali ya

Rufaa ya Bombo iliyopo Mkoani Tanga.Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi

Mtendaji, Mshauri Mkuu wa Sheria na Katibu wa Shirika,Wakili Amos Ndegi amesema kuwa Shirika limeona ni vyema kama sehemu ya jamii kuchangia vifaa hivyo muhimu vitakavyowezesha kuwahudumia watoto wawapo hospitalini.

“Watu wengi wanadhani TANESCO ni Shirika la kibiashara, lakini hapana, tupo kihuduma zaidi na ndiyo maana leo tupo hapa tukiwezesha huduma ya watoto hospitalini lakini pia hata bei ya umeme vijijini sasa ni elfu 27 badala ya laki 3 na hi ipo pia kihuduma zaidi ili kuhakikisha wananchi wote wanamudu bei yakuunganisha Umeme” alisema Wakili Ndegi

Akizungumza mara baada ya makabidhiano ya vifaa hivyo, Muunguzi Mfawidhi wa Hospitali hiyo Bi.Beatrice Rimoy amelishukuru Shirika la Umeme nchini TANESCO kwa kuwa na moyo wa kusaidia jamii na hasa msaada wa vifaa tiba vilivyokua vikihitajika sana Hospitalini hapo.

Naye Dkt.Tumaini Mchiiyo ambaye ni Daktari wa wodi ya watoto hospitalini hapo ameishukuru TANESCO na kutoa wito kwa mashirika mengine kuiga mfano huo kwa kuijali jamii na hasa sekta ya Afya na idara ya watoto ambao hupitia changamoto mbalimbali za magonjwa na hivyo kuwezesha watoto kupata tiba iliyobora zaidi wawapo hospitalini.

TANESCO yakabidhi vifaa tiba Hospitali ya Bombo Mkoani TangaVifaa hivyo kutumika kwenye wodi ya watoto

TANGA

Mshauri Mkuu wa Sheria na Katibu wa Shirika, Wakili Amos Ndegi (kulia) akikabidhi vifaa tiba kwa Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Bombo, Beatrice Rimoy. Wakili Amos Ndegi

Mshauri Mkuu wa Sheria na Katibu wa Shirika

Watu wengi wanadhani

TANESCO ni Shirika la kibiashara, lakini hapana

tupo kuhudumia zaidi na ndio

maana leo tupo hapa tukiwezesha huduma ya watoto

Tunayaangaza Maisha Yako

Plot No. 114, Block G, Dar es Salaam Road, P.O.Box 453 Dodoma, Email: [email protected]

SIMU: +255 22 2 194 400/ +255 768 985 100

Whatsup group zipo nchi nzima tanescoyetultd tanescoyetu tanesco_official_page www.tanesco.co.tz