2
Mkahawa Niupendao. Kila ninapopata fikra ya kutaka kujivinjari,ni mkahawa mmoja tu huja akilini mwangu..Jina la kiswahili,mandhari ya uswahili,bila shaka Magharibi ndiyo chaguo langu.katu sichelewi kufika pale kila mara. Lango kuu lenye rangi ya hudhurungi huvutia na kuacha wengi vinywa wazi wakitamani kujionea yaliyo ndani.Mteja aingiapo,tarishi huwa tayari kufungua mlango na kuwaelekeza waingiao vilivyo.Mle ndani,vyumba vya kila aina kama;vya kucheza densi,vya kubugia sharubati,vya kuchoma nyama na pia vya kutazamia michezo huwa vimeandaliwa vilivyo. Chumba cha kwanza ni cha kucheza densi.Sakafu huwa na mkeka maalum wa kuwaezesha wanaojiburudisha kucheza densi bila tatizo.Chumba cha kubugia sharubati na vileo vingine huwa kimejaa kila wakati.Haya yote huendelea huku wengine wakichoma nyama na wengine wakitazama michezo kwenye runinga. Wahudumu katika mkahawa huu,huwa na libasi rasmi za kuvutia.Isitoshe,majina yao huwa yameandikwa kwenye vitambulisho vilivyopachikwa kwenye libasi zao.Hutoa huduma bora kwa tabasamu na ustaarabu.wao huanza kwa kukujulia hali,kukuuliza jina na mwishowe hutumia muda mfupi sana kuwasilisha chochote kiagizwacho. Wapishi wa mkahawa huu wana tajriba pana.Huandaa vyakula vitamu ambavyo huacha wateja wakilamba vidole vyao.Vinywaji huwa tele.Si divai kutoka ufaransa, "whiskey" kutoka urusi na hata sharubati za kiafrika kama "amarula".Waraibu wa vinywaji mseto huandaliwa vinywahivo papo hapo. Kando na vyumba vya burudani,mkahawa huu una bustani lililojaa maua ya kupendeza pamoja na kidimbwi kidogo kilicho na samaki wa maridadi.

Jeremy Mkahawa Niupendao

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Chat

Citation preview

Mkahawa Niupendao.

Kila ninapopata fikra ya kutaka kujivinjari,ni mkahawa mmoja tu huja akilini mwangu..Jina la kiswahili,mandhari ya uswahili,bila shaka Magharibi ndiyo chaguo langu.katu sichelewi kufika pale kila mara.

Lango kuu lenye rangi ya hudhurungi huvutia na kuacha wengi vinywa wazi wakitamani kujionea yaliyo ndani.Mteja aingiapo,tarishi huwa tayari kufungua mlango na kuwaelekeza waingiao vilivyo.Mle ndani,vyumba vya kila aina kama;vya kucheza densi,vya kubugia sharubati,vya kuchoma nyama na pia vya kutazamia michezo huwa vimeandaliwa vilivyo.

Chumba cha kwanza ni cha kucheza densi.Sakafu huwa na mkeka maalum wa kuwaezesha wanaojiburudisha kucheza densi bila tatizo.Chumba cha kubugia sharubati na vileo vingine huwa kimejaa kila wakati.Haya yote huendelea huku wengine wakichoma nyama na wengine wakitazama michezo kwenye runinga.

Wahudumu katika mkahawa huu,huwa na libasi rasmi za kuvutia.Isitoshe,majina yao huwa yameandikwa kwenye vitambulisho vilivyopachikwa kwenye libasi zao.Hutoa huduma bora kwa tabasamu na ustaarabu.wao huanza kwa kukujulia hali,kukuuliza jina na mwishowe hutumia muda mfupi sana kuwasilisha chochote kiagizwacho.

Wapishi wa mkahawa huu wana tajriba pana.Huandaa vyakula vitamu ambavyo huacha wateja wakilamba vidole vyao.Vinywaji huwa tele.Si divai kutoka ufaransa, "whiskey" kutoka urusi na hata sharubati za kiafrika kama "amarula".Waraibu wa vinywaji mseto huandaliwa vinywahivo papo hapo.

Kando na vyumba vya burudani,mkahawa huu una bustani lililojaa maua ya kupendeza pamoja na kidimbwi kidogo kilicho na samaki wa maridadi.

Magharibi bila shaks ni mkahawa wa sampuli ya aina yake.Vinywaji teule,vyakula vyenye ladha na bustani za kisasa humliwaza mteja kiasi cha kumfanya asahau masaibu yake.Magharibi ni Mambo shwari.