17
Matarajio ya desturi ya shughuli za benki kama yalivyokusanywa na chama cha wenye mabenki nchini Kenya Mwongozo wa Mteja katika shughuli za benki nchini Kenya

katika shughuli za benki nchini Kenya Consumer Guide - Kis… · Kanusho: Uhusiano kati ya mteja na Benki yao ni wa mkataba na hivyo Mwongozo huu wa Mteja hauwezi kwa vyovyote vile

  • Upload
    others

  • View
    5

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: katika shughuli za benki nchini Kenya Consumer Guide - Kis… · Kanusho: Uhusiano kati ya mteja na Benki yao ni wa mkataba na hivyo Mwongozo huu wa Mteja hauwezi kwa vyovyote vile

Matarajio ya desturi ya shughuli za benki kama yalivyokusanywa na chama cha wenye mabenki nchini Kenya

Mwongozo wa Mteja katika shughuli za benki nchini Kenya

Page 2: katika shughuli za benki nchini Kenya Consumer Guide - Kis… · Kanusho: Uhusiano kati ya mteja na Benki yao ni wa mkataba na hivyo Mwongozo huu wa Mteja hauwezi kwa vyovyote vile

Mwongozo wa mteja wa KBA | 1

YALIOMOSehemu ya 1Wajibu wetu muhimu kwako 4

Sehemu ya 2Ada za Benki na asilimia ya faida 8

Sehemu ya 3Masharti ya Benki 10

Sehemu ya 4Uendeshaji wa akaunti yako 13

Sehemu ya 5Huduma za mikopo na muamana 16

Sehemu ya 6Upashanaji habari kuhusu mikopo 20

Sehemu ya 7Ulinzi wa mteja 22

Sehemu ya 8Miongozo ya Busara ya Benki 22

Sehemu ya 9 Usaidizi kwa Mteja 23

Sehemu ya 10 Ufafanuzi 24

Mwongozo wa mteja wa KBA, Toleo la pili/Novemba 2012

© Kenya Bankers Association, 2012

All rights reserved

Edited by Nuru Mugambi

Contributions by: Habil Olaka, Bernadette Ngara, Fidelis Muia, William Maiyo, Bhaskar Kalyan, Kariuki Waihenya, Kristopher Kinyanjui, Abdia Dabaso, Hannah W. Ndarwa

Kiswahili translation by Shaban Ulaya

Page design and layout by Conrad Karume

Page 3: katika shughuli za benki nchini Kenya Consumer Guide - Kis… · Kanusho: Uhusiano kati ya mteja na Benki yao ni wa mkataba na hivyo Mwongozo huu wa Mteja hauwezi kwa vyovyote vile

Kanusho: Uhusiano kati ya mteja na Benki yao ni wa mkataba na hivyo Mwongozo huu wa Mteja hauwezi kwa vyovyote vile kusababisha uwajibikaji wa kisheria kati ya mteja na benki yake wala kubadilisha kifungu chochote cha mkataba kati ya mteja na Benki. Aidha, Mwongozo huu hautanukuliwa katika kesi yoyote kati ya mwanachama yeyote wa KBA na mteja au wateja iwe ni sehemu ya au mwongozo wote.

UTANGULIZI

Wanachama wa chama cha wenye mabenki(KBA) wametakiwa wawe na utendaji bora wakati wanapotoa huduma za kifedha, ukiwemo uangalizi wa juu zaidi wanapotoa huduma za benki kwa umma.

Kwa hiyo, lengo la Mwongozo huu wa mteja ni kufafanua viwango vya utendaji bora vya shughuli za benki kwa ajili ya wateja wa benki pamoja na wanachama wa chama cha wenye mabenki.

Toleo la kwanza la Mwongozo huu lilichapishwa na KBA mwaka wa 2001 kama ‘Kanuni za shughuli za Benki’.

Tafadhali fahamu kwamba sio mabenki yote yanayotoa seti yote ya bidhaa na huduma iliyoangaziwa katika Mwongozo huu.

Kuhusu KBAChama cha wenye mabenki(KBA) ni shirika mwamvuli la Mabenki ya kibiashara yenye leseni chini ya Sheria ya Benki Kuu ya Kenya (CBK) kuhusu

shughuli za benki. Chama kinakuza na kuimarisha kanuni endelevu zinazofaa,utendaji na makubaliano na kuchangia ukuaji wa sekta ya benki. Chama pia kinasimamia masuala ya uhusiano mwema yanayohusiana na shughuli za benki kama tasnia ya huduma pamoja na jukumu lake la kujadiliana masharti ya ajira kwa niaba ya wanachama wake. KBA hushughulika kudumisha uratibu na ushirikiano na Benki Kuu ya Kenya, taasisi za kifedha, Chama cha wafanyibiashara, usimamizi na taasisi za elimu, Shirikisho la Waajiri la Kenya, na mashirika mengine kama hayo kwa ajili ya kutimiza lengo la KBA: “ Tasnia Moja . Kubadili Kenya. “

KBA kinamiliki na kuendesha afisi ya kubadilisha hundi za benki yenye mitambo ya kujiendesha. Aidha, KBA hushirikiana na CBK kuhusu uanzilishi wa mipango kama usasa katika mifumo ya malipo( ukiwemo mradi wa kufupisha muda wa kubadilisha hundi za benki), uanzishaji wa vituo vya fedha kote nchini na mpango wa Kenya wa upashanaji (utoaji na utumiaji pamoja) wa habari kuhusu mikopo.

UTANGULIZI

Mwongozo wa mteja wa KBA | 3

Page 4: katika shughuli za benki nchini Kenya Consumer Guide - Kis… · Kanusho: Uhusiano kati ya mteja na Benki yao ni wa mkataba na hivyo Mwongozo huu wa Mteja hauwezi kwa vyovyote vile

Mwongozo wa mteja wa KBA | 5

Sehemu ya 1

1. Kukusaidia kupata chaguo linalofaaMabenki hutoa aina nyingi tofauti za bidhaa na huduma ili kukidhi mahitaji anuwai ya mteja.

Mara nyingi, tofauti kati ya bidhaa za benki, huduma za benki na njia za benki inaweza kutoeleweka. Aidha, wateja wanaweza kuwa hawaelewi ni habari gani wanapaswa kuuliza benki yao kabla ya kuchagua bidhaa au huduma.

Sehemu hii itasaidia kufafanua orodha ya fedha zilizowekwa kwa faida ya benki hiyo na njia tofauti ambazo mteja anaweza kutumia ili kupata yaliyomo katika chaguo lao. Pia inashughulikia habari ambazo benki inatakiwa itoe kabla ya mtumiaji kuwa mteja, pamoja na baadaye.

2. Habari utakayohitajiKabla ya kuwa mteja, benki ni sharti:• ikupemaelezoyajumlakuhusubenkinabidhaa

na huduma inazotoa ili kukidhi mahitaji yako; na

• kukuambia wakati huo habari yote inayotakiwa kutoka kwako ili ufungue akaunti, hiyo itajumuisha stakabadhi zinazohitajika kuambatana na miongozo ya taratibu za benki ku ya Kenya(CBK).

Kabla ya kuchagua bidhaa au huduma, benki ni sharti :•ikupehabarikuhusuakauntizakimsingipamoja

na akaunti zinazokuzwa ili uweze kuzilinganisha na kufanya uamuzi unaokufaa;

• ikupe habari ya wazi yenye maelezo ya sehemu muhimu za huduma na bidhaa

zinazokuvutia;

Kama watoaji huduma za kifedha, Mabenki hutoa bidhaa na huduma ambazo huwawezesha wateja kusimamia na kukuza rasilmali zao za kifedha.

Ili kutimiza hilo, Mabenki hujishughulisha na:A kutenda kwa uweledi, kiungwana na kimaadili

katika shughuli zote na watejaB kuhakikisha kuwa bidhaa zote na huduma

vinavyotolewa viko katika viwango vya KBA ,hata kama mabenki binafsi yanamasharti yao;

C Kutoa habari kwa wateja kuhusu bidhaa na huduma katika lugha iliyo wazi na inayoeleweka kwa urahisi, na kutoa maelezo kama yatakavyohitajika, ukiwemo ushauri kwa wateja kuhusu walivyochagua na kama kuna bidhaa/huduma bora itakayokidhi mahitaji yao;

D kuwasaidia wateja kuelewa athari za kifedha kuhusu bidhaa na huduma , jinsi vinavyofanya kazi ili kumwezesha mteja afanye maamuzi ya busara.

E kuwa na mifumo salama na ya kutegemewa

ya shughuli za benki na malipo ili kuzuia usumbufu.

F kuhakikisha kwamba taratibu zinazofuatwa na wafanyikazi wa benki na mawakala zinaonyesha utendaji mzuri wa shughuli za benki na uangalizi mkubwa wa mteja;

G kutambua sababu ambazo zinaweza kuathiri wateja wa benki, ikiwa ni pamoja na athariri za mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa, na kuwatilia maanani mmoja mmoja au kwa pamoja kupitia KBA kuhusu jinsi ya kuwasaidia wateja wakati wa matatizo ya kifedha;

H kuwa na njia wazi za mawasiliano na wateja, ukiwemo ushughulikiaji wa malalamiko , na kuhakikisha njia hizo zinatangazwa na ni rahisi kupatikana na wateja wote.

I Kushughulikia malalamiko ya wateja katika muda wa kuridhisha, na kuwafahamisha wateja muda utakaochukua kwa malalamiko au maulizo yao kujibiwa na kushughulikiwa; Na

J kuhakikisha kuwa bidhaa zote na huduma vinaafiki kanuni na sheria zilizoko ukiwemo mwongozo wa taratibu za benki Kuu ya Kenya.

WAJIBU WETU WA KIMSINGI KWAKO

utengenezaji / ubadilishianaji wa hundi, uhamishaji wa fedha kieletroniki / RTGS, ushauri, vilabu vya uanachama, taratibu kuu, kituo cha mawasiliano [ushughulikiaji wa maswali na malalamiko ya mteja ] ....

•atm•simuya

mkono,•intaneti,

•simu•tawi•wakala

akaunti ya kibiashara; akaunti ya mkopo; akaunti ya uwekezaji; kadi za mkopo...

BIDH

AA

HUDU

MA

UTOA

JI

Page 5: katika shughuli za benki nchini Kenya Consumer Guide - Kis… · Kanusho: Uhusiano kati ya mteja na Benki yao ni wa mkataba na hivyo Mwongozo huu wa Mteja hauwezi kwa vyovyote vile

Mwongozo wa mteja wa KBA | 7

• ifichue gharama (kiwango cha riba, malipo, ada) au wajibu mwengine wa kifedha mengine ya kifedha kuhusu bidhaa au huduma uliyochagua;ikushauri kuhusu jinsi unaweza kupata faida kubwa kutoka kwa bidhaa au

huduma hiyo, kwa mfano kama kuna huduma ya hisani au ya bure inayohusiana na akaunti hiyo;

• ikupe habari zaidi kuhusu haki zako na majukumu unapofungua akaunti ya pamoja;

Je Wajua?Wateja wengi wa benki hawajinufaishi na bidhaa na huduma za benki kwa sababu hawana habari. Je wajua kuwa na akaunti ya kawaida, mteja anaweza kutoa taratibu kuu kadhaa ((au kusafisha akaunti) ambazo zitasaidia kudumisha bajeti ya kibinafsi ya kila mwezi pamoja na kuwa na uwajibikaji wa kifedha kama kulipa mkopo?

• ikushauri kama kutakuwa na gharama au adhabu wakati unapoendesha akaunti kwa namna ambayo iko nje ya masharti ya akaunti uliyofungua;

• ikuarifu kuhusu malipo,ada au nyongeza ya riba endapo utaamua kusitisha mkataba wowote mapema; na

• ikuruhusu ufanye uamuzi wa mwisho na ikupe taarifa juu ya bidhaa au huduma hiyo ya pekee.

3. Viwango vya RibaKujua kuhusu jinsi benki inaamua kiwango chake cha riba kwa akaunti za uwekaji amana na mkopo ni habari muhimu unayopaswa kuifahamu.

Kabla ya kufungua akaunti ya mkopo au ya kuweka amana, benki ni sharti:• ikupe taarifa juu ya viwango vya riba

vinavyohusiana na akaunti zako; na • ikushauri ni lini itakukata riba au

itakulipa riba

Mbali na mafunzo kwa mteja anayekutana na wafanyikazi wanaoshughulika na akaunti za kuweka amana na za mkopo kuhusu jinsi ya kushughulikia ombi la mteja la kutaka habari kuhusu viwango vya riba, benki ni sharti itoe taarifa za jumla kupitia wavuti wa beki, nambari ya kutoa msaada na, inapolazimu, magazeti kwa kupitia ilani kwa umma.

4. Shughuli za benki kulingana na Shari’ahKila kukicha mabenki hutoa huduma na bidhaa maalum , ili kukidhi mahitaji ya anuwai ya wateja.

Mfano ni Shughuli za benki kuambatana na Shari’ah au shughuli za benki za kiislamu.

Shughuli za benki zinazoambatana na uislamu ni mfumo wa kuendesha biashara na shughuli za benki kulinganga na kanuni za Kiislamu huku shughuli zote zilizopigwa marufuku zikiepukwa kama vile Riba, Gharar, kugharamia(kufadhili) biashara haramu.

Sio shughuli za benki za mfumo wa kukadiria thamani ya pesa na kupata ribakama ilivyo katika mabenki ya kawaida yenye msingi wa riba lakini ni mfumo wa biashara ambapo bidhaa na huduma huuzwa na mtaji kuwekezwa kwa kuchukua dhima(kubahatisha) ili kupata faida halali. Shughuli za benki bila ya riba ni mwelekeo wa dhana ya shughuli za benki za Kiisalmu.

Tofauti kati ya Shughuli za benki chini ya Shari’ah na shughuli za benki za kawaidaTofauti kubwa kati ya shughuli za benki chini ya Shari’ah na shughuli za benki za kawaidani kwamba mafundisho ya Kiislamu yanasema kuwa pesa zenyewe hazina thamani ya asili (ya msingi) na yanakataza watu kupata faida kuzikopesha, bila ya kukubali kiwango cha dhima(hatari ya hasara)-kwa maneno mengine, pesa haziwezi kutozwa Riba.Chini ya sheria ya Shari’ah, utajiri unaweza tu kuzalishwa kupitia biashara halali na uwekezaji. Faida yoyote / faida inayohusiana na biashara hii/ uwekezaji inagawanywa kati ya/wa mtu aliyetoa mtaji na mtu anayetoa utaalamu (Mudharabah)

Page 6: katika shughuli za benki nchini Kenya Consumer Guide - Kis… · Kanusho: Uhusiano kati ya mteja na Benki yao ni wa mkataba na hivyo Mwongozo huu wa Mteja hauwezi kwa vyovyote vile

Mwongozo wa mteja wa KBA | 9

• matangazokatikaukumbiwashughulizabenki;• matangazo kwa umma yaliyochapishwa katika

gazeti; au• KuchapishakatikawavutirasmiwaBenki.

Wateja wanapaswa pia kujua kuhusu mabadiliko hayo kwa kupiga simu benki, kutembelea tawi au kituo cha kuhudumia wateja, au kutembelea wavuti wa benki.

2. Muda wa kutaarifu Ni utendaji bora kwa mabenki kuwaarifu wateja wao angalau siku 30 kabla ya mabadiliko yakinifu ya akaunti kutekelezwa kupitia matangazo magazetini na/ au kupitia wateja kutumiwa barua.

Kwa ongezeko maalumu la ushuru au asilimia ya faida kwa akaunti, benki hiyo itatoa taarifa kuhusu mabadiliko hayo na lini yatafanyika na moja kwa moja kwa wateja walioathirika.

3. Mabadiliko katika Viwango vya RibaWakati benki inapobadilisha viwango vya riba kwa akaunti, watatoa ilani kuambatana na matarajio ya kutaarifu. Ili kusaidia wateja kulinganisha viwango vya riba, kiwango cha zamani ni sharti kipatikane benki.

Kwa akaunti binafsi ,mabenki yataweza:• kuwashauri wateja ndani ya siku 30 kuhusu

mabadiliko hayo, na kufahamisha siku ya utekelezaji; ama

• katikamudawasiku5zakazikuwekamatangazo

kuhusu mabadiliko hayo katika matawi na / au katika magazeti.

Kwa wateja wa shughuli za benki za Kiislamu:• Chini ya mfumo wa benki wa Kiislamu riba

haitambuliwi lakini faida ipo; na • Kulingana na Shari’ah ,pindi mkataba kati ya

benki na mteja umetiwa saini, ha saini, hakuna upande wowote wenye haki ya kubadilisha kiwango cha faida, bila ya kujali kupanda na kushuka kwa viwango vya riba katika soko.

4. Ushuru wa Bidhaa za KadiKadi za mkopo na zile za kutoa pesa kwenye akaunti zenye pesa ni bidhaa ambazo mabenki hutoa kwa wateja ili kurahisisha wapate fedha na kutekeleza shughuli nyengine za benki. Bidhaa hizi zinaweza kutumika kwa kutumia njia mbalimbali, kama vile mitambo ya ATM (mashine za kujiendesha zenyewe katika kutoa na kuweka pesa), vituo vya ununuzi wa rejareja (POS) na kupitia intaneti.

Kutegemea benki na bidhaa za kadi, ada na asilimia ya faida inaweza kutozwa.Aidha, ada zinaweza kutofautiana kulingana na aina ya njia iliyotumika na kama mteja ametumia benki tofauti(benki nyengine mbali na ile iliyompa kadi).

Wateja wanapaswa kupewa ushauri kwa kupata maelezo ya bidhaa kuhusu muundo wa ushuru na ratiba kabla ya benki kuwapa bidhaa hizo.

Sehemu ya 2

Kama ilivyo katika biashara yoyote, mabenki huwatoza wateja bidhaa na huduma wanazotoa.

Malipo haya, yanayojulikana kama ushuru na asilimia ya faida, hutozwa bidhaa na huduma zinazotolewa na benki na sio tu kwa ada zinazotozwa akaunti za biashara bali pia akaunti za mkopo,kadi za mkopo na njia tofauti ambazo mteja hutumia kufanya shughuli ya benki.

Kama ilivyoelezwa katika sehemu za awali, kabla ya mteja kufungua akaunti,benki inatakiwa kumuarifu

mteja kuhusu ushuru wowote wa uendeshaji wa kila siku wa akaunti hiyo.

Pindi mkataba wa kufungua akaunti unapotiwa saini, benki inalazimika kumpa mteja nakala ya makubaliano ambayo ina masharti ya mkataba huo.

1. Njia za kutaarifu(kutoa ilani)Isipokuwa vinginevyo ilivyoelezwa , mabadiliko yoyote ya ushuru yatatangazwa na benki kwa njia ya kutoa taarifa. Hii inaweza kupitia:• barua kutumwa kwa wateja wa benki

walioathirika;

USHURU WA BENKI NA ASILIMIA YA FAIDA

Page 7: katika shughuli za benki nchini Kenya Consumer Guide - Kis… · Kanusho: Uhusiano kati ya mteja na Benki yao ni wa mkataba na hivyo Mwongozo huu wa Mteja hauwezi kwa vyovyote vile

Mwongozo wa mteja wa KBA | 11

Masharti ya bidhaa na huduma za benki yanakusudia kueleza haki za mteja na majukumu.

Masharti (pia yanajulikana kama T’s & C’s) ni lazima:•kuwawazinakatikalughayawaziinayoeleweka

kwa urahisi;•yafungamanenaainayabidhaaauhuduma;na•yatumielughayakiufundiinapohitajika.

Iwapo benki itafanya mabadiliko muhimu na makubwa ya T’s & C’s ya akaunti tofauti inazotafutia wateja, ni iwaarifu wateja mapema.

Ni kawaida kwa marekebisho yasio na maana(kidogo) ya masharti yawasilishwe katika muda wa siku 30 wa mabadiliko.

Unapaswa daima kujisikia huru kuuliza wafanyakazi wa benki au meneja wa tawi la akaunti yako aeleze masharti ambayo hukuyaelewa. Inashauriwa kwamba masharti haya yaeleweke vyema kabla ya kuandika mkataba na benki.

1. Utangazaji na Masoko

Mabenki hushiriki katika shughuli mbalimbali kutafuta soko la bidhaa na huduma za. Shughuli

2. Kipindi cha kutulizanaKipindi cha kutulizana ni muda ambao mteja anaruhusiwa baada ya kusaini mkataba wa benki kufutilia mbali mkataba bila ya kuadhibiwa. Kipindi hiki hutumiwa kwa bidhaa nyingi za benki;hatahivyo kuna baadhi za upekee. Mteja lazima aarifiwe kuhusu muda unaokubaliwa wa kipindi cha kutulizana kabla ya kutia saini mkataba na benki.

3. Bidhaa na Akaunti zilizositishwa

Mara kwa mara benki huanzisha bidhaa na huduma mpya ili kukidhi mahitaji ya mteja yanayobadilikabadilika pamoja na uwezekano wa mabadiliko ya muelekeo wa mkakati wa benki. Hayo yakitendeka,baadhi ya bidhaa za benki na akaunti husitishwa(hukomeshwa), huboreshwa au hubadilishwa na kuwa kivyengine.

Wakati akaunti au bidhaa imesitishwa, benki ni sharti:• itoeilaniyasiku30kwamtejakablayaakaunti

hiyo/huduma kuachwa;• imshaurimtejailikwambakamamtejaanahitaji

kuchukua hatua zaidi kufuatia uamuzi wa benki anaweza kupewa fursa ya kufanya hivyo; na

• Iwajulishe wazi wateja juu ya chaguzi zaombalimbali mbadala zinazopatikana na kuwashauri wahamie kwa bidhaa mbadala au wachukue hatua inayofaa kama inavyotakiwa.

Iwapo tawi litafungwa, benki ni lazima itoe ilani ya muda wa kutosha kwa wateja binafsi na kuhamisha akaunti zao hadi kwa tawi lengine bila ya kumtoza gharama mteja au ieleze wazi taratibu ya kuhamisha akaunti na kusimamia shughuli yote vizuri.

4. Akaunti zisizotumika

Kulingana na masharti ya kufungua akaunti katika kila benki, akaunti zilizofunguliwa zinaweza kutangazwa kuwa hazitumiki.kwa kawaida benki inatakiwa iwaarifu wateja wake kuhusu mabadiliko ya uainishaji kwa kutoa sababu(kwa mfano kutotumika katika kipindi Fulani).

Katika hali hiyo, benki pia itatakiwa itoe ushauri kuhusu masharti ya kutekelezwa ili akaunti hiyo iweze kuanzishwa na kutumika tena.

5. Kufunga au kusimamisha Akaunti

Isipokuwa kama kuna mazingira ya kipekee, benki haipaswi kusimamishaau kufunga akaunti bila ya kutoa ilani ya siku zisizopungua 14 kwa mmiliki wa akaunti. Hatahivyo kama mabenki yatatakiwa yasimamishe akaunti kuambatana na matakwa ya /sheria za nchi,ilani ya baada ya akaunti kusimamishwa inatakiwa itolewe kwa wateja katika muda wa wiki kuanzia tarehe ya kusimamishwa kwa akaunti.

6. Kuhamisha Akaunti

Iwapo mteja anataka kuhamisha akaunti yake hadi benki nyingine, benki anayotumia ni lazima ihakikishe uhamishaji huo unafanyika shwari. Sharti hili huenda likahitaji benki iratibu uhamisho huo kwa kuwasiliana na benki nyengine moja kwa moja.

Wateja wa Benki wanashauriwa watoe ilani ya muda wa kutosha kwa benki yao kwani baadhi ya uhamishaji wa akaunti ya benki moja hadi nyengine huchukua muda,na wakati mwengine hutozwa ada kuambatana na masharti ya akaunti hiyo.

Sehemu ya 3

MASHARTI YA BENKI

Je Wajua?Wateja wana haki ya kubadilisha au kufunga akaunti zao za benki ikiwa mabadiliko ya masharti ya akaunti yanawaathiri sana.

( Fahamu: ada za kusitisha mkataba huenda zikatozwa)

hizo zinajumuisha kampeini za uuzaji na matangazo ya kibiashara.

Sambamba na utendaji bora katika mawasiliano, matangazo ya benki ni sharti:•kuwayawazi,hakinayamaananayasipotoshe

au kuwasilishwa vibaya;•kutiliamaananimahitajiyawalengwa;na•kuonyeshawazikamamashartihayoyanatumika.

Chama cha wenye mabenki kinawataka wanachama wake wafuate utendaji unaofaa wa kutafuta soko kama ilivyofafanuliwa katika sheria ya kumlinda mteja.

Page 8: katika shughuli za benki nchini Kenya Consumer Guide - Kis… · Kanusho: Uhusiano kati ya mteja na Benki yao ni wa mkataba na hivyo Mwongozo huu wa Mteja hauwezi kwa vyovyote vile

UENDESHAJI WA AKAUNTI YAKOSehemu inayofuata ina habari za kimsingi unazohitaji kujua pindi unapotia saini na kuanza kuendesha akaunti yako ya benki.

1. Taarifa Mabenki hutoa taarifa za akaunti ili kumsaidia mwenye akaunti kusimamia akaunti yake. Taarifa hiyo inaweza kutolewa kila mwezi, kila baada ya miezi mitatu au, katika hali yoyote ile, mara moja kwa mwaka. Idadi ya utoaji wa taarifa hutofautiana kutoka benki moja hadi nyengine, na hivyo wateja watakiwa wawe na habari kuhusu ratiba na namna za utangazaji.

Wateja lazima wafahamu kuhusu ukweli kwamba mabenki yanaweza kumtoza mteja gharama ya uchapishaji wa taarifa zaidi.Katika muda wa utoaji wa taarifa rasmi, wateja wanaweza kuona akaunti zao kupitia taarifa ndogo zinazopatikana katika mitambo ya benki ya ATM. Aidha katika mabenki mengi akaunti zinaweza kupatikana kupitia huduma za kuhamishika,intaneti na simu na hivyo wateja wanaweza kuona jinsi shughuli zao za benki zilivyo.

3. Cheques

Kwa miaka mingi, chama cha wenye mabenki,KBA, kimewekeza katika kuimarisha ufanisi na usalama wa hundi ambazo mabenki hutoa kwa wateja

wao. Leo, hundi ni za kisasa nan a zinaweza kuchunguzwa, kusomwa na kuidhinishwa kupitia mitambo inayojiendesha.

3. Kadi na Nambari za siri(PIN)

ATM, kadi za Mikopo na za utoaji pesa kwenye akaunti ni njia rahisi kwa wateja wa benki kufanya shughuli ya benki na/au kupata fedha zao.

Kawaida benki hutoa kadi moja kwa moja kwa wateja katika tawi. Mteja anaweza kuanza kutumia kadi kwa kuchagua nambari yake ya siri iliyo salama (PIN), na wafanyikazi wa benki watamueleza kwa ufupi jinsi na wapi kadi hutumiwa pamoja na

Je Wajua?Kutegemea na akaunti, Mabenki

yatatoa kitabu cha hundi kwa jina la mwenye akaunti. Pindi unapopokea kitabu chako cha hundi unatakiwa uhakikishe kuwa maelezo kamili ya akaunti ni sahihi.

Vilevile ni vizuri kuangalia kila ukurasa wa hundi kuhakikisha kwamba mfululizo wa nambari ni sahihi na ziko katika hali ya mfuatano.

Sehemu ya 4

Mwongozo wa mteja wa KBA | 13

Ushauri kwa mtejaNi muhimu kuwa na mazoea

ya kuangalia taarifa za akaunti ili kuhakikisha yaliyomo kwenye akaunti ni sahihi.

Iwapo kutakuwa na kasoro yoyote katka akaunti yako, ijulishe benki yako haraka

Page 9: katika shughuli za benki nchini Kenya Consumer Guide - Kis… · Kanusho: Uhusiano kati ya mteja na Benki yao ni wa mkataba na hivyo Mwongozo huu wa Mteja hauwezi kwa vyovyote vile

Mwongozo wa mteja wa KBA | 15

CHEQ

UE

PRES

ENTE

D

FUN

DS

AVA

ILA

BLE

Ushauri kuhusu usalama wa kadi

wakati unapoanza kutumia kadi yako, chagua nambari ya PIN ambayo ni salama na unaweza kuikumbuka kwa urahisi

mtu yeyote hata mkeo, ndugu, jamaa na marafiki na nambari yako ya siri (PIN)

Utakapopoteza kadi yako, ijulishe benki haraka ili iorodheshwe haraka na isiweze kutumika. Pia fika katika tawi la karibu la benki ujaze fomu ya kuomba kadi nyengine.

ni afadhali uthibitishe shughuli ulizofanya mara ya mwisho kwa kutumia kadi kabla haijapotea ili kuhakikisha kuwa hakuna shughuli nyengine zozote ambazo hazikuidhinishwa zimefanyika.

wafanyikazi wa benki hawapaswi kukuuliza PIN ya kadi yako, ni wathibitishe akaunti yako kwa kutumia kitambulisho chako cha kitaifa, nambari ya akaunti ya benki na anuwani ya posta. Pia unaweza kuwa na swali la kiusalama ambalo wanatakiwa wakuulize.

umuhimu wa kuitunza na kutotumia pamoja na kutompa mtu mwengine nambari yake ya siri.

4. Huduma za ubadilishanaji wa fedha za kigeniWateja wanaweza kununua na kuuza fedha za kigeni katika benki au katika ofisi ya ubadilishanaji wa fedha za kigeni. Katika benki, huduma ya kubadilisha fedha za kigeni hutolewa kwa wenye akaunti. Mabenki hayo pia hutoa huduma kwa umma lakini katika kiwango tofauti cha ubadilishaji.

Wakati wa ubadilishanaji, Benki ni sharti:• kutoamaelezoyakiwangochaubadilishaji;na• kueleza kabla ya ubadilishaji malipo

yanayotozwa.

5. Uhamishaji wa kimataifa wa pesa Ikiwa unataka kuhamisha fedha nje ya nchi, benki

inaweza kutoa huduma hii kupitia njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na uhamisho kutoka kwa akaunti hadi kwa akaunti, Kieletroniki kama (uhamisho wa papo hapo wa jumla) RTGS au SWIFT, ama kupitia watoaji wengine wa huduma kama Western Union au Moneygram.

Kwa vile una chaguzi mbalimbali ambazo zinatofautiana katika utoaji huduma na gharama, benki ni sharti: • ieleze gharamazotenaadayanayohusianana

chaguzi mbalimbali;• itoe maelezo ya fedha wakati zitatumwa, na

wakati zinatarajiwa kupokewa;• ieleze kiwango cha ubadilishanaji

kitakachotumiwa, kwa kubainisha hasara au faida katika thamani ; na

•ikujulishekamamtuanayepokeaatatakiwaalipeada yoyote au malipo

Page 10: katika shughuli za benki nchini Kenya Consumer Guide - Kis… · Kanusho: Uhusiano kati ya mteja na Benki yao ni wa mkataba na hivyo Mwongozo huu wa Mteja hauwezi kwa vyovyote vile

Mwongozo wa mteja wa KBA | 17

Wakati wa kuamua kuomba au kutoomba mkopo kutoka kwa benki, ni muhimu kwamba mteja awe anajua kuhusu utaratibu wa kutuma maombi, mahitaji ya mkopo pamoja na gharama na wajibu vinavyohusiana nao. Hii habari ni muhimu na inaweza kuamua kama mkopo unahitajika au la.

Kuna sababu tofauti za watu kuomba mkopo. Huku mahitaji binafsi yakitofautiana,kwa ujumla daima ni vyema wakati wa kupata mkopo wa muda mrefu kuutumia kufanya ununuzi ambao thamani yake itaongezeka kadiri muda unavyosonga. Chini ya shughuli za benki za Kiislamu, hii inajulikana kama uwezeshaji wa kifedha.

Ufafanuzi wa MkopoKuna aina mbalimbali za mkopo ambazo mteja anaweza kupata kutoka njia rasmi kama vile benki, taasisi ndogo ndogo za fedha, vyama vya akiba na mikopo ya ushirika (SACCOS) au njia zisizo rasmi yakiwemo makundi madogo ya uwekezaji(Chamas).

Mikopo ambayo mabenki hutoa inaweza kuwa ya muda mfupi au mrefu ikiwemo mikopo isiyokuwa na dhamana,rehani na mikopo ya malipo ya polepole(HP), au kupitia vyenzo vya mikopo kama kadi za mikopo, ovadrafti(deni katika akaunti ya benki)na barua za mikopo.

Mkopo chini ya shughuli za benki za Kiislamu unaweza kutolewa kupitia mifumo tofauti ya fedha

ya kiislamu; inajumuisha njia mbalimbali za faida na hasara tofauti na zile za riba. Mifumo hiyo ni Mudarabaha,Musharaka, musharaka inayopungua na Ijarah.

Aina za Mikopo na Viwango vya Riba

Unapotoa mkopo kwa mteja, benki hutoza gharama inayojulikana kama kiwango cha riba cha mkopo juu ya mkopo. Kiwango hiki hasa hutegemea aina ya mkopo na maelezo mafupi kuhusu hatari ya hasara ya kumpa mkopo mteja.

Kuna aina mbili kuu za viwango vya riba vya mkopo:• Kiwango kisichobadilika- ambapo riba

hujadiliwa na kuamuliwa kuwa kiwango fulani kwa kipindi fulani au muda wote wa kulipa mkopo; ama

• Kiwango kinachobadilika - ambapo kiwango cha riba kitabadilika kutegemea na kiwango cha msingi cha benki

Wakati viwango vya riba katika soko vimebadilika, mikopo iliyofanyiwa mahesabu kwa kutumia kiwango cha riba kisichobadilika, haiathiriwi, ilhali mikopo yenye riba inayobadilika itakuwa na viwango vipya kutegemea na hali ya benki na gharama za uendeshaji.

Kama vile ambavyo kuna aina tofauti za mikopo, mabenki hutumia mbinu tofautiza kufanya mahesabu ya malipo ya mteja ya mkopo. Mbinu hizi kawaida huuweka mkopo katika ratiba ya kutenga fedha kwa ajili ya kulipia deni (yaani malipo ya

MIKOPO YA BENKI NA MIKOPO MINGINE

kila mwezi ambayo hupunguza deni katika muda uliopangwa).

Je mabenki huangalia nini yanapotoa mkopo?

Wakati wa kukopesha, mabenki hutafuta hakikisho kuwa mikopo wanayotoa inalipwa; na zaidi ya hivyo hupendelea malipo yanafanywa kuambatana mkataba rasmi(mkataba wa mkopo).

Wakati wa kuanzisha mazungumzo ya mkopo, pande zote mbili – mteja na benki - hupitia utaratibu wa kufanya maamuzi.

Kwa upande wa benki, mchambuzi wa mikopo atatathmini uwezekano wa mkopo kulipwa kikamilifu kulipwa kama ilivyoainishwa katika

mkataba. Utaratibu huu unajulikana kama uchambuzi wa hatari ya hasara ya kuchukua jukumu na ni pamoja na kutathmini 1) ukweli halisi kumhusu mteja, 2) nafasi ya kampuni na sera,Pamoja na hali za hisia ambazo mchambuzi atatilia maanani kutegemea na uzoefu wake. kama vile 3) • Kwamikopoyakibinafsi,mchambuziwa

mikopo ataongozwa na:

•Ukweli:

1. shughuli za benki na historia kuhus mikopo (Kuamua uwezo wa ulipaji)

2. dau la mteja (kiasi gani cha hatari ya hasara ya kutolipa kitachukuliwa na mkopaji na mtoaji mkopo.

Ukweli Halisi

kumhusu mteja Nafasi ya kampuni

na sera,

hali za hisia/uelewa

wa mambo

Sehemu ya 5

Mchmabuzi wa mikopo anaongozwa na ukweli halisi kumhusu mteja, 2) nafasi ya kampuni na sera,Pamoja na hali za hisia

Page 11: katika shughuli za benki nchini Kenya Consumer Guide - Kis… · Kanusho: Uhusiano kati ya mteja na Benki yao ni wa mkataba na hivyo Mwongozo huu wa Mteja hauwezi kwa vyovyote vile

Mwongozo wa mteja wa KBA | 19

•Uwezowakuelewamamboharaka:

1. tabia ya mteja, uadilifu katika uamuzi uliopita aliofanya

2. ujuzi ulio na mtu binafsi au shirika ni lazima uweze kutekeleza pendekezo ipasavyo

3. je, kuna mpango mwengine wa mteja endapo mpango wa kwanza haukufaulu?

• Kwa mikopo ya kibiashara / biashara,mchambuzi mikopo ataongozwa na:

• Ukweli:

1. fedha za biashara (waraka mizania na taarifa ya mapato ili kutambua uwezo wa kulipa)

2. dau la biashara (kiasi gani cha hatari ya hasara ya kutolipa kitachukuliwa na mteja na mtoaji mkopo)

3. muundo wa usimamizi, uthabiti wake? Mipango ya urithi?

•Uwezowakuelewamamboharaka:

1. uwajibikaji katika biashara, maadili ya biashara

2. ujuzi ulio na mtu binafsi au shirika ni lazima uweze kutekeleza pendekezo ipasavyo

3. Je, kuna mpango mwengine wa biashara endapo mpango wa kwanza haukufaulu?

Mbali na kumfanyia tathmini mteja, mchambuzi wa mikopo atakadiria jinsi mkopo huo utaathiri faida na hasara ya benki hiyo (pia inajulikana kama P & L). Hii ni kubainisha kama mapato ya riba yatakayotokana na mkopo yatalingana na au yatazidi hatari inayochukua benki katika kutoa mkopo. Pia wataangalia upya kama mkopo ni sambamba na sera za benki hiyo na miongozo ya busara ya Benki Kuu ya Kenya (CBK).

FAHAMU: Mbali na hapo juu, Mabenki ya Kiislamu yana wajibu wa kuhakikisha kwamba hayafadhili shughuli ambazo ni kinyume na Shari’ah.

Dhamana ya kutoa mkopo Katika kutoa mkopo, benki itahitaji mteja aweke dhamana ya mkopo. Hii ina maana kwamba benki

Ushauri kuhusu mkopo

Epuka kuchukua mikopo kwa ajili ya mambo usiyohitaji

wakati wote jaribu kuishi kadiri ya uwezo wa mapato yako,na hivyo mikopo itumike kwa ajili ya kuzalisha mapato au mali inayoongezeka thamani kadiri muda unavyosonga

kuwa muaminifu katika kueleza mikopo mingine uliyonayo

Usione haya kuzungumza na mwenye benki yako…hasa unapoona unaweza kushindwa kulipa deni, mabenki mengi yanaweza kubadili mkataba wa mkopo kabla ya deni kutolipwa (ni vugumu kufanya mazungumzo baadaye).

itashikilia mali ya mteja kwa muda wote wa ulipaji wa mkopo. Mali ambayo hushikiliwa na benki ni hati miliki za makaazi au za biashara,magari na stakabadhi za vifaa au pesa taslimu ambazo zimewekwa katika akaunti ya kudumu na benki hiyo. Kuna wakati benki itaweka dhamana ya mkopo wa biashara kwa kutumia thamani ya biashara hiyo (yaani mali kwenye waraka mizania).

Wakati wa kutathmini thamani ya dhamana, benki itakuwa ikiangalia kama:• thamani inafidia ipasavyo hatari ya hasara

iliyoko• inafaakulingananavigezovyabenki/sera• ni rahisi kutambua / kufilisi kulipia gharama

(kwa kutolipa deni)

UdhaminiMbali na mali, benki inaweza kukubali udhamini kama aina ya dhamana. Katika suala hili benki inaweza kufichua kwa mdhamini wako na mshauri wao wa kisheria habari ya siri kuhusu fedha zako. Wakati wa kumdhaminia mtu dhima(deni), daima unashauriwa kwamba mdhamini:• apateushaurihuruwakisheria ili kuhakikisha

kuwa anaelewa wajibu wake na uwezekano wa matokeo ya uamuzi wake; na

• awe anafahamu kikamilifu kwamba kwakumdhamini au kutoa dhamana nyengine anaweza kuwajibika kisheria kulipa deni badala ya,au pamoja na mteja anayeomba mkopo.

Gharama za mkopo unazotarajiwa kulipaMteja anayeomba mkopo ni lazima ajue ada mbalimbali na gharama zinazohusiana na mkopo huo. Baadhi ya gharama hizi ni za mwanzoni, nyengine ni za kujirudiarudia(kama ulipaji wa mkopo) na kuna zile za mwisho wa kulipa mkopo,kutegemea na mkataba.

Kuna gharama nyengine ambazo ziko huru na mkopo kama viwango vya ribaikiwa mikopo imeratibiwa katika kiwango cha kubadilika; ushuru wa hati na ada ya ukadiriaji thamani ikiwa na suala la rahani.

Gharama za Jumla • Adazamaombi• Adayamajadilianoauasilimiayafaida/adaya

utengenezaji/ada ya kuweka katika utaratibu • Malipoyariba• Malipo ya kabla ya adhabu ya muda wa

mkopo(yanaweza kujadiliwa na kuafikiwa) • Malipo ya adhabu yaliyocheleweshwa au riba

ya adhabu• Adayauwajibikaji(katikaovadrafti)• Adayachaguo(hutozwabaadhiyabidhaaza

benki]

Gharama maalumu za bidhaa - Rahani na Ufadhili wa mali isiyohamishika• Adazaukadiriajithamani• Gharamazakisheria• Ushuruwahati• Bimayamali• BimayaMaisha[kwarahani]

Page 12: katika shughuli za benki nchini Kenya Consumer Guide - Kis… · Kanusho: Uhusiano kati ya mteja na Benki yao ni wa mkataba na hivyo Mwongozo huu wa Mteja hauwezi kwa vyovyote vile

Mwongozo wa mteja wa KBA | 21

Wakopaji wengi hufanya juhudi nyingi kulipa mikopo yao, Lakini hawazawadiwi kwa juhudi hizo kwa sababu historia yao nzuri ya kulipa haipatikani katika benki waliyoenda kuomba mikopo mipya.

Kwa upande mwengine, wakati wowote wakopaji wanaposhindwa kulipa mikopo yao, mabenki hulazimika kuwabwagia wateja wengine gharama ya kutolipwa deni kupitia kuongeza viwango vya riba na ada nyengine.

Utoaji wa habari kuhusu waombaji mikopo unaruhusu benki kutofautisha kati ya wakopaji wazuri na wabaya. Mtu ambaye ameshindwa kulipa mkopo wake katika benki moja hataweza kuenda kwa benki nyengine kuomba mkopo mwingine bila ya benki kujua kuhusu hilo.

Baada ya muda wakopaji watarajiwa wenye “Ripoti Nzuri za kulipa Mikopo” au “Historia nzuri ya kulipa Mikopo” wataweza kupata mikopo ya nafuu na kwa urahisi kuliko wale wenye mashaka makubwa ya kutolipa deni.

Manufaa muhimu ya utoaji habari kuhusu mikopo kwa wateja ni: • Kurahisisha wateja kupata mikopo kwa

kutumia ‘rekodi za nyendo zao’ badala ya dhamana ya mali kama ardhi, magari, hisa,vitu vya nyumbani na vyengine;

• Kupunguakwaviwangovyaribakwaniwatejawanaweza kutumia “rekodi ya nyendo zao”

kujadili masharti ya mikopo yanayowafaa; na• kusaidia kudumisha ulipaji mzuri na desturi

nzuri za kukopa

Kujenga historia yako ya mikopo“Historia ya mikopo” ni rekodi rasmi ya rubuni (mikopo) ulolipa katika muda Fulani. Historia hii hutumiwa na benki yako katika kufanya tathmini ya hatari ya hasara iliyoko ya kukupa mkopo. Katika siku zijazo, watoaji wengine wa mikopo kama SACCOS, taasisi ndogo ndogo za fedha, makampuni ya mawasiliano ya simu na makampuni ya huduma za umma pia wanaweza kupata habari hii.

Moja ya vipengele muhimu vya Historia yako ya mikopo ni “Ripoti ya mikopo.” “Ripoti ya Mikopo”

UPASHANAJI HABARI KUHUSU MIKOPO

FAHAMU! Wakati huu, Ofisi inatakiwa ihifadhi habari kuhusu

mikopo isiyolipwa mpaka mwisho wa miaka saba-hata baada ya kuwa imelipwa.Katika siku zijazo, muda huu huenda uka-punguzwa. Hatahivyo, kuwa na alama ya chini kuhusu mikopo ama kuorodheshwa kama mtu asiyelipa madeni katika wakati uliokubaliwa hakumaanishi kuwa hauwezi kupata mikopo katika muda wa miaka saba. Inamaanisha kuwa mkopeshaji ata-chukua tahadhari zaidi na hata atoze vi-wango vya juu vya riba ya mkopo.

inatayarishwa na Ofisi iliyopewa leseni ya marejeo ya mikopo na ina taarifa za kina kuhusu akaunti za mikopo, taflisi na malipo ya kuchelewa, na maulizo ya punde zaidi kutoka kwa watoaji mikopo (mabenki, taasisi ndogo ndogo za fedha zinazoweka amana,na kadhalika).

Katika ripoti Ripoti hii kuna “alama kuhusu Mikopo“, ambazo ni kiwango cha hatari ya hasara ya kutoa mkopo ambacho kinakisiwa kwa kutumia mfumo uliosanifishwa.

Alama chanya ina sifa za bili kulipwa mara kwa mara; ukosefu wa kutolipamasalio; kudumu katika ajira; matumizi yasiyozidi 25% ya mikopoinayopatikana kwa mteja. Kwa upande mwingine, Alama hasi kuhusu mikopo ina sifa za malipo ya kuchelewa; kufilisika; malipo ya udanganyifu/mashtaka ya ulaghai;madai ya kumiliki ama mali kuchukuliwa baada ya mkopaji kushindwa kulipa kwa wakati uliokubaliwa ; na kupoteza ajira.

Haki yako kwa taarifa sahihi & usiriWateja wana haki za kupinga taarifa yoyote kuwahusu ambazo zinahifadhiwa na ofisi ya kumbukumbu za mikopo zikiwemo taarifa ambazo hazijakamilika na zile ambazo si sahihi; na kuna kanuni na sheria za kutatua mizozo hii.

Kama mzozo hautakuwa umetatuliwa katika muda maalumu, taarifa inayozozaniwa itatakiwa itolewe kwenye data za ofisi zote zenye kumbukumbu za mikopo.

Unapaswa kuwasilisha ripoti za mikopo zinazozozaniwa moja kwa moja kwa ofisi ya ya mikopo iliyotoa ripoti yenye makosa. Hali hii huenda ikabadilika karibuni na huenda ukatakiwa uwasilishe malalamiko yako kwa tawi lako la benki. Kwa habari zaidi juu ya hili, tafadhali sakura www.kenyacreditinfo.com.

Je wajua?

Ripoti ya mikopo kukuhusu wewe inatakiwa ipatikane na wakopeshaji au watoaji mikopo pindi tu wanapopata sababu kuambatana na sheria (kimsingi kutambua kustahili kwako kupewa mkopo wakati unapoomba mkopo).

Benki yako inatakiwa ikujulishe kwa kukuandikia barua kupitia posta ikiwa itawasilisha ripoti isiyofaa kukuhusu kwa ofisi ya kumbukumbu za mikopo( yaani ikiwa itakuorodhesha kama mtu

asolipa deni.

ofisi ya kumbukumbu za mikopo inatakiwa kisheria ikupatie bure ripoti oja ya mikopo kila mwaka na vilevile ikupatie bure ripoti ya mikopo kila benki inapotoa uamuzi usiofaa dhidi yako kwa kutumia taarifa kutoka kwa ripoti ya mikopo.

na hivyo unapaswa kutumia fursa ya mahitaji ya kisheria ya kupata bure ripoti za mikopo.

Sehemu ya 6

Page 13: katika shughuli za benki nchini Kenya Consumer Guide - Kis… · Kanusho: Uhusiano kati ya mteja na Benki yao ni wa mkataba na hivyo Mwongozo huu wa Mteja hauwezi kwa vyovyote vile

Mwongozo wa mteja wa KBA | 23

Sehemu ya 7

ULINZI WA MTEJA Kifungu cha 46 cha Katiba ya Kenya 2010 kina sheria na utendaji unaokubalika kuhusu watoaji bidhaa na huduma wanazotakiwa kutumia wakati wanapokuwa na wateja wao.Mbali na Katiba, mswada wa 2012 kuhusu ulinzi wa mteja ulipitishwa ukiwa na ibara kuhusu utoaji wa huduma za kifedha. Na kwa sababu hiyo mabenki yanapaswa yajue sheria hizi sawa na wateja wao.

Sehemu ya 8

MIONGOZO YA BUSARA YA BENKIKenya imetambuliwa kimataifa kwa kuwa na moja ya sekta zinazoendelea zaidi, imara na bunifu katika sekta za benki barani Afrika.Kwa kweli, Kenya imefikiriwa kuwa kitovu cha huduma za kifedha katika eneo la Afrika Mashariki.Ufanisi huu umepatikana kupitia juhudi za pamoja za mabenki katika mazingira mazuri ya udhibiti.Mabenki hupewa leseni na kudhibitiwa na Benki Kuu ya Kenya (CBK).

Katika kusimamia sekta ya benki, CBK hutekeleza sheria mbalimbali kama ilivyoagizwa na Sheria ya Kenya kuhusu shughuli za benki; na inahakikishakuwa mabenki yanatii kanuni kama zilivyoainishwa katika Miongozo ya busara ya CBK.

Miongozo hii inashughulikia miongoni mwa mengine:• Utawala na Usimamizi wa hatari ya kupata

hasara• MahitajiyaTaarifazafedha,ikiwanipamojana

uwiano wa utendajimabenki ya umma na ya kibinafsi.

• Usimamiziwamuendelezowabiashara• Hudumazabenkizikiwemoshughulizabenki

za uwakala• Taarifa za benki zikiwemo za upashanaji

habari kuhusu mikopo na udhibiti wa ofisi za kumbukumbu za mikopo.

Mbali na Miongozo ya busara,mabenki kupitia chama cha wenye mabenki hupigania udhibiti wa ndani kupitia michakato mbalimbali na mipango ambayo husimamiwa na Chama.

Sehemu ya 9

USAIDIZI KWA MTEJA Wateja daima hutiwa moyo wawasiliane moja kwa moja na benki yao kwa habari kuhusu huduma inazotoa.

1. Utatuzi wa mzozo (Ushughulikiaji wa Malalamiko)Wateja wa Benki daima hutiwa moyo kuanzisha uhusiano wa moja kwa moja na wa muda mrefu na mtoaji wao wa huduma za kifedha. Hali hii itasaidia sana pindi kutakuwa na suala ibuka.

Huku ikitambuliwa kuwa mizozo inaweza kuibuka mara kwa mara kati ya mteja na benki yake, chama cha wenye mabenki,KBA, hupigania utaratibu wa ndani ambao utatumika kupata suluhu kati ya benki na mteja.

Afisi ya kwanza kwa mteja kuwasilisha malalamiko yake iwapo kuna mzozo ni ya meneja wa uhusiano au meneja wa tawi.Suluhu inaweza kutafutwa nje na mteja/benki baada ya juhudi zote za ndani kufanywa na kutozaa matunda.

Kulingana na miongozo ya busara ya CBK,benki inapopata malalamiko inatakiwa ikiri kupokea kwa

maandishi(angalau siku saba kuanzia siku iliyopata malalamiko hayo) na ieleze kuwa inashughulikia suala hilo.Kwa sababu hiyo wateja wanapaswa kuipa benki yao muda huo kulichunguza na kulijibu suala lao.

2. Habari za Jumla Mabenki huwapa wateja wao njia mbalimbali za usaidizi rkama vile kupitia matawi yao pamoja na kupitia intaneti na simu.

Njia nyengine za usaidizi ni kupitia:Chama cha wenye mabenki nchiniWasiliana na:Consumer GuideKenya Bankers AssociationS.L.P. 73100 – 00200, Nairobi, KenyaWavuti: www.kba.co.keBarua pepe: [email protected] Afisi ya Kenya ya upashanaji habari kuhusu mikopoWasiliana na:Consumer InformationKenya Credit Information Sharing InitiativeS.L.P. 73100 – 00200, Nairobi, KenyaWavuti: www.kenyacreditinfo.comBarua pepe: [email protected] Benki Kuu ya KenyaBarua pepe: [email protected]: www.centralbank.go.ke

Sehemu yas 7,8 & 9

Page 14: katika shughuli za benki nchini Kenya Consumer Guide - Kis… · Kanusho: Uhusiano kati ya mteja na Benki yao ni wa mkataba na hivyo Mwongozo huu wa Mteja hauwezi kwa vyovyote vile

Mwongozo wa mteja wa KBA | 25

Hizi fasili hueleza maana ya maneno ambayo mara nyingi hutumika benki. Sio sawasawa kabisa na si ufafanuzi wa kisheria au kiufundi.

AmanaFedha iliyowekwa katika akaunti ya benki.

Akaunti iliyositishwani akaunti ambayo:• haifunguliwi tena na wateja(hii inaweza

kutokana na kuwa benki haitoi tena huduma zake au kwa sababu nyengine); ama

• haikupigiwadebeaukukuzwakwawateja

Alama kuhusu MikopoNi mfumo ambao mabenki hutumia katika kufanya maamuzi ya kukopesha fedha. Alama kuhusu mikopo inatoa taswira ya uwezekano wa kama mteja atalipa mkopo kwa wakati uliokubaliwa.

Akaunti zisizotumika kwa muda Akaunti yoyote ambapo kiasi na asili ya shughuli zake imeshuka kwa kiwango ambacho kwamba benki inaona hakistahili kwa akaunti ya aina hiyo.

Akaunti ya Amana ya Muda Maalum

Ni akaunti ambayo inamruhusu mteja kupokea mapato kutoka kwa benki almradi amana yake itasalia kwenye benki kwa muda ulioafikiwa. Akaunti hii kwa kawaida huzalisha kiwango cha

juu cha riba kwa mteja. Hatahivyo huenda kukawa na adhabu ya kusitisha mkataba kabla ya muda wake kumalizika.

Akaunti ya RejarejaNi akaunti inayoendeshwa na mtu kibinafsi (mteja).

Akaunti za Kawaida Akaunti ya kawaida huwa na sifa zifuatazo:• mapatoyanawezakulipwanawaajirimojakwa

moja kwenye akaunti;• hundi na fedha taslimu zinaweza kulipwa

katika akaunti;• pesa taslimu zinaweza kutolewa katika

mashine za fedha au kwenye kaunta• hakuna kutoa pesa zaidi ya zilizoko kwenye

akaunti (ovadrafti). Akaunti hii inaweza isiwe na kitabu cha hundi.

DeniMikopo au malipo yaliyotolewa mapema na mfadhili kwa mteja wake kwa misingi ya mkopo.

Dhamana Ni neno linalotumiwa kuelezea vitu vya thamani kama vile hati miliki za nyumba, vyeti vya hisa, bima za maisha na kadhalika, ambavyo vinawakilisha mali inayotumika kwa ajili ya mkopo.Katika mkopo uliodhaminiwa, mkopeshaji ana haki ya mali iliyowekwa kama dhamana ikiwa mkopo haukulipwa.

Habari nyengine za UsalamaUteuzi wa mambo ya kweli ya kibinafsi pamoja na habari( katika mpango ambao mteja pekee anajua), ambayo hutumiwa kwa ajili ya utambulisho wakati wa kutumia akaunti. Hii huenda ikajumuisha swali la usalama.

Hatari ya Hasara ya MikopoWakati wa kukopesha, mabenki hufanya tathmini ya mambo mbalimbali yanayoathiri mteja, biashara au kiwanda / uwezo wa sekta katika kulipa deni.

Hesabu ya MtoeFedha zilizotolewa kutoka kwa akaunti ya benki.

Hundi iliyopitwa na wakatiNi Hundi ambayo haijalipwa kwa sababu tarehe iliyoandikwa kwenye hundi ni ya zamani sana,kawaida ni ya zaidi ya miezi sita.

Hundi Isiyolipwa

Hii ni hundi, ambayo, baada ya kulipwa katika akaunti ya mtu aliyoandikiwa ,inarudishwa ‘bila kulipwa’ kwa benki ambayo mteja wake alitoa hundi. Na hivyo aliyeandikiwa hundi anasalia bila ya pesa katika akaunti yake. benki itamtoza aliyeandika hundi ada ya adhabu ya hundi iliyorudishwa kwa kutokuwa na fedha za kulipwa na hivyo ni vyema kuthibitisha pesa zilizoko kabla ya kutoa hundi.

Kadi Neno la jumla la kadi yoyote ya plastiki ambayo

mteja anaweza kutumia kulipia bidhaa na huduma au kwa kutoa pesa.

Kadi ya PesaNi kadi, zaidi ya kadi ya malipo au kadi ya mikopo, ambayo inajumlishwa katika mtandao wa ATM.

Kiwango cha Msingi Kiwango cha chini ambacho benki hulipa juu ya amana au kutoa mkopo. Kiwango hiki hutilia maanani gharama za uendeshaji wa benki, lengo lake la mapato, hatari ya hasara ya mikopo na athari nyengine za nje ambazo ni za kiuchumi (kama mfumuko wa bei).

Kiwango cha Benki Kuu au CBR Chombo cha fedha ambacho Benki Kuu ya Kenya itatumia kuashiria kwenye soko mwelekeo wa gharama za fedha. Mabenki hujumuisha CBR pamoja na mambo mengine wakati kufanya mahesabu ya viwango vya kuweka amana na mikopo. Kwa sababu ya hiyo CBR si jambo la kipekee linaloathiri viwango.

Kiwango kisichobadilika Ni kiwango cha riba ambacho kina hakikisho la kutobadilika katika muda uliopangwa.

Mashine ya fedha Ni mashine inayojiendesha yenyewe(ATM) au mashine iliyosimama yenyewe, ambayo mteja anaweza kutumia kadi yako kupata pesa,habari na huduma nyengine.

Sehemu ya 10

UFAFANUZI

Page 15: katika shughuli za benki nchini Kenya Consumer Guide - Kis… · Kanusho: Uhusiano kati ya mteja na Benki yao ni wa mkataba na hivyo Mwongozo huu wa Mteja hauwezi kwa vyovyote vile

Mwongozo wa mteja wa KBA | 27

Mashine ya PDQ ni mtambo unaoshikiliwa mkononi na ambao hutumiwa na muuzaji rejareja ili kukamilishia shughuli ya malipo inayotekelezwa kupitia kadi ya mkopo au muamana.

MizaniaKiasi cha fedha ulichonacho katika akaunti yako ya benki.

MkatabaNi makubaliano ya kubana kati ya mteja na benki. Ni lazima ushirikishe masharti ya makubaliano yakiwemo majukumu ya kila upande.

Mtoaji Mikopo Ni taasisi inayotoa mikopo kwa mteja. mikopo inaweza kuwa fedha (kwa mfano mkopo au kadi ya mikopo), inaweza pia kuwa ni huduma (kwa mfano kama katika huduma za umma kama usafiri au umeme)

Mawakala wa (Afisi za) kumbukumbu za mikopo Mashirika, ambayo yanahifadhi habari kuhusu watu, ambazo ni muhimu kwa wakopeshaji. Mabenkiyanaweza kuwasiliana na mashirika hayo kupata habari ambazo zitayasaidia kufanya maamuzi tofauti, kwa mfano, kama kufungua au kutofungua akaunti au kutoa mkopo au muamana. Mabenki pia yanawezakutoa habari kwa mawakala.

Mapochi ya KieletronikiAina yoyote ya kadi, au matumizi ya kadi, ambayo ina thamani halisi ya fedha katika mfumo wa pesa za kieletroniki, ambayo mtu amelipa kabla. Baadhi ya kadi zinaweza kuongezwa pesa zaidi na zinaweza kutumika kwa makusudio mbalimbali.

Muda usiobadilikaUnatumika kwa bidhaa na huduma, ambavyo vina muda uliopangwa. Mteja anaweza kutozwa gharama iwapo benki itakubali kubadilisha bidhaa au huduma kabla ya muda uliopangwa kumalizika.

Shughuli za Benki za KiislamuNi mfumo wa shughuli za benki ambazo zinalingana na kanuni za sheria ya Kiislamu(Shari’ah).

Nchini Kenya kuna mabenki kamili ya Kiislamu ambayo hutoa huduma pekee zinazoafiki Shari’ah; aidha mabenki mengine maarufu yanatoa bidhaa ambazo zinalingana na Sheria ya Kiislamu. Waislamu na wasiokuwa waislamu,wote wanaweza kupata bidhaa chini ya mfumo wa Shari’ah.

Mazingira ya Kiuchumi Mabenki huathiriwa kwa kiasi kikubwa na mambo ya nje kama vile kiwango cha ukuaji wa nchi ( Pato la Jumla la nchi/GDP), viwango vya mfumuko wa bei, uthabiti wa kisiasa, thamani ya fedha, viwango vya ajira / ukosefu wa ajira pamoja na sera za fedha.

Miongozo ya BusaraNi seti ya miongozo iliyotolewa na Benki Kuu ya Kenya. Miongozo hiyo inajumuisha mahitaji mbalimbali ya utawala na usimamizi wa hatari za hasara ambayo benki ni lazima itekeleze ili ipewe leseni ya kuhudumu nchini Kenya.

Nywila Ni neno au alama ya siri ambayo mteja amechagua ili kumuwezesha kutumia simu au huduma za shughuli za benki kutoka nyumbani. Pia hutumiwa kwa ajili ya utambulisho.

PIN (nambari binafsi ya utambulisho) Ni nambari ya siri inayoruhusu wateja kutoa pesa na kutumia huduma nyingine.

POS au Kituo cha mauzo Mahali ambapo biashara ya rejareja hufanyika panaitwa kituo cha mauzo. Katika maduka makubwa, kituo cha mauzo ni katika mashine ya kuhesabia pesa. Watu wengi wenye maduka ya rejareja wameweka mashine za kujiendesha za kuhesabia pesa na hutumia mashine za POS, zikiwemo zile za PDQ.

RahaniNi mikopo yenye dhamana ambayo hutolewa mahususi kununua au kukarabati nyumba, kwa kawaida katika muda usiopungua miaka mitano. Katika masikizano mengine aina nyengine za mikopo zinaweza kutimiza lengo hili.

Riba Ni neno linalotumika katika shughuli za benki za Kiislamu katika kufafanua riba. Riba ni udhuru au ongezeko. Kitaalamu, ongezeko , katika mkopo au ubadilishanaji wa bidhaa linatokana na mwenyewe(mkopeshaji) bila ya kutoa thamani sawa ya kaunta au fidia kwa mwengine.Inahusu riba katika mikopo ya kibiashara na ya kibinafsi.

Fedha ambayo benki italipa kwa amana uliyoweka (fedha taslimu) au ada ambayo Benki itakulipisha ikikupa mkopo wa pesa. Katika shughuli za benki za Kiislamu hakuna riba ila faida.

Katika suala la amana, riba ni mapato mwenye akaunti atazalisha kutoka kwa benki; Akaunti za amana za muda maalum zitazalisha riba kubwa kwa sababu benki hiyo itajadiliana nawe muda huo na baadaye ikopeshe pesa hizo katika muda ambao wana uhakika watakuwa wanashikilia pesa zako.

Katika suala la mikopo, riba inaweza kutozwa katika kiwango kisichobadilika au kinachobadilika.Mabenki yana mbinu mbalimbali za mahesabu ya kuamua kiasi gani kitakutoza kwa mkopo uliochukua. Kiwango hicho kitashirikisha gharama za uendeshaji shughuli za benki ,mahitaji ya mapato, hatari ya hasara inayohusishwa na mteja na mazingira ya kiuchumi.

Riba Mchanganyiko Hesabu ambayo inajumlisha riba iliyolimbikizana na mtaji. Kisha riba inatokana na jumla ya fedha zilizochanganywa.

Page 16: katika shughuli za benki nchini Kenya Consumer Guide - Kis… · Kanusho: Uhusiano kati ya mteja na Benki yao ni wa mkataba na hivyo Mwongozo huu wa Mteja hauwezi kwa vyovyote vile

Mwongozo wa mteja wa KBA | 29

RTGS au Malipo ya Jumla ya papo hapo Ni mfumo wa kieletroniki unaotumiwa na mabenki kuhamisha au kushughulikia malipo. Hundi za thamani ya zaidi ya shilingi milioni moja(Ksh. 1,000,000) hazishughulikiwi tena na mabenki na kwa sababu hiyo wateja wanapaswa kuomba uhamisho kupitia RTG.

Sera ya Fedha Benki Kuu ya Kenya huandaa na kufafanua sera kwa ajili ya masoko ya fedha. Sera hii huathiri gharama za fedha na upatikanaji wa fedha (inayojulikana kama ukwasi). Wakati CBK inahitaji kupunguza kiasi cha fedha katika mzunguko (ili kukabiliana na mfumuko mkubwa wa bei ) itafanya pesa kuwa ‘adimu’ kwa ‘kuimarisha udhibiti’ katika sera yake; na kinyume chake, wakati inataka kuchochea ukuaji ‘italegeza’ sera yake na kufanya pesa kuwa rahisi kupatikana.

Shughuli za Benki za Jumla Mabenki hutoa huduma mbalimbali kwa watu binafsi pamoja na makampuni. Kwa mashirika makubwa ,benki itakuwa ikifanya mazungumzo ya

kukubaliana ada na asilimia za faida kwa kuzingatia kiasi cha shughuli za biashara. Katika mpango huu, mabenki yatatoa huduma na bidhaa kwa kutumia mfumo wa bei ya jumla.

SWIFTMfumo wa kieletroniki ambao mabenki hutumia kupokea malipo kutoka nchi nyingine au kutuma malipo kimataifa.

Taarifa ya Benki Ni muhtasari wa shughuli za benki katika akaunti maalumu. Unajumuisha deni (utoaji pesa) na muamana(uwekaji pesa) .

UdhaminiAhadi iliyotolewa na mtu aitwaye ‘mdhamini’ kulipa madeni ya mtu mwingine kama mtu huyo hatayalipa.

Page 17: katika shughuli za benki nchini Kenya Consumer Guide - Kis… · Kanusho: Uhusiano kati ya mteja na Benki yao ni wa mkataba na hivyo Mwongozo huu wa Mteja hauwezi kwa vyovyote vile

Chama cha wenye mabenki nchini (Kenya Bankers Association)Orofa la 13, International House, Mama Ngina StreetS.L.P 73100– 00200 NAIROBISimu: 254 20 2221704/2217757/2224014/5Simu ya mkono: 0733 812770/0711 562910Kipepesi: 254 20 2221792Baruapepe: [email protected]