24
Kodi zetu zinaelekezwa kwenye Elimu? Uchambuzi wa Bajeti ya Elimu 2011/2012 Novemba 2011

Kodi zetu zinaelekezwa kwenye Elimu? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Kodi Zetu ZInaelekezwa Kwenye Elimu.pdf · (Chanzo: Vitabu vya bajeti 2011, Juzuu namba ii-iv, randama

  • Upload
    others

  • View
    33

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Kodi zetu zinaelekezwa kwenye Elimu? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Kodi Zetu ZInaelekezwa Kwenye Elimu.pdf · (Chanzo: Vitabu vya bajeti 2011, Juzuu namba ii-iv, randama

Kodi zetu zinaelekezwa kwenye Elimu?

Uchambuzi wa Bajeti ya Elimu 2011/2012

Novemba 2011

Page 2: Kodi zetu zinaelekezwa kwenye Elimu? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Kodi Zetu ZInaelekezwa Kwenye Elimu.pdf · (Chanzo: Vitabu vya bajeti 2011, Juzuu namba ii-iv, randama
Page 3: Kodi zetu zinaelekezwa kwenye Elimu? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Kodi Zetu ZInaelekezwa Kwenye Elimu.pdf · (Chanzo: Vitabu vya bajeti 2011, Juzuu namba ii-iv, randama

Kodi zetu zinaelekezwa kwenye Elimu?

Uchambuzi wa Bajeti ya Elimu 2011/2012

Novemba 2011

Page 4: Kodi zetu zinaelekezwa kwenye Elimu? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Kodi Zetu ZInaelekezwa Kwenye Elimu.pdf · (Chanzo: Vitabu vya bajeti 2011, Juzuu namba ii-iv, randama

Shukrani

Uchambuzi na uandishi wa ripoti hii ulifanywa na Godfrey Boniventura. Shukrani za pekee ziwaendee Tony Baker, Elizabeth Missokia, Mtemi Zombwe, Elisante Kitulo na Pius Makomelelo kwa kuchangia maboresho na kuhariri ripoti hii.

© HakiElimu, 2011 ISBN 978-9987-18-024-0HakiElimu, S L P 79401, Dar es SalaamBarua pepe: [email protected]: www.hakielimu.org

Sehemu yoyote ya kitabu hiki inaweza kutolewa kwa namna yoyote kwa madhumuni ya kielimu na siyo kibiashara, kwa kuzingatia kuwa chanzo kitatajwa na nakala mbili zitapelekwa HakiElimu

Page 5: Kodi zetu zinaelekezwa kwenye Elimu? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Kodi Zetu ZInaelekezwa Kwenye Elimu.pdf · (Chanzo: Vitabu vya bajeti 2011, Juzuu namba ii-iv, randama

1

Yaliyomo

1.0 Utangulizi 2

2.0 Malengo ya Matumizi ya Ripoti 3

3.0 Matokeo ya Uchambuzi 4

3.1 Uhalisia wa Ongezeko la Bajeti ya Sekta ya Elimu 4

3.2 Uwekezaji katika Miradi ya Maendeleo 6

3.3 Ugatuaji wa Madaraka na Upangaji wa Bajeti 8

3.4 Utekelezaji wa Bajeti 9

3.5 Utegemezi katika Miradi ya Maendeleo 11

3.6 Utekelezaji wa MMES II 12

3.6.1 Fedha za Maendeleo 12

3.6.2 Fedha za Ruzuku kwa Mwanafunzi 14

4.0 Mapendekezo 16

5.0 Marejeo 17

Kiambatisho 18

Page 6: Kodi zetu zinaelekezwa kwenye Elimu? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Kodi Zetu ZInaelekezwa Kwenye Elimu.pdf · (Chanzo: Vitabu vya bajeti 2011, Juzuu namba ii-iv, randama

2

1.0 Utangulizi

Maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi yoyote hutegemea sana jinsi serikali ya nchi hiyo inavyowajibika kijamii kuweka mipango ya maendeleo inayozingatia mahitaji ya wananchi wake. Ili mipango izingatie mahitaji ya wananchi ni lazima serikali iwashirikishe wananchi wenyewe kubainisha kwa undani matatizo yanayoikabili jamii, na njia sahihi za kutatua matatizo hayo. Mipango sahihi inaweza kushindwa kuleta maendeleo kama usimamizi utakuwa siyo imara, na kama wasimamizi wa mipango watashindwa kutumia fedha za bajeti vizuri kutekeleza malengo kiufanisi au kupanga bajeti ambayo haizingatii makadirio ya kifedha ya mpango.

“Kama tunataka kupata maendeleo ya kweli, ni lazima watu washirikishwe”(Mwal. Julius Kambarage Nyerere, Uhuru na Maendeleo)

Utekelezaji wa bajeti ni kutumia fedha ili kuleta au kuboresha huduma za jamii. Kwa mfano, bajeti inapotumika kugharamia ujenzi wa miundombinu ya shule, kuajiri walimu na kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia, jamii inapata huduma ya kujifunza ambapo watoto wanasoma na kupata elimu bora kwa ajili ya kuwaletea maendeleo. Kama jamii inahitaji madarasa, walimu na vifaa vya kujifunzia-kufundishia ili kuanzisha shule ni lazima kuwe na fedha ya kutosha. Ikitokea fedha imepangwa ikawa ndogo kiasi cha kutoweza kujenga madarasa yanayohitajika tutakuwa na shule ambayo haijakamilika na hivyo kusababisha watoto washindwe kujifunza na kufundishwa ipasavyo.

Hii ndio hali halisi inayoikabili Tanzania kwani hakuna shule halisi za msingi na sekondari. Takwimu za BEST1 2011 zinaonesha kuwa shule nyingi bado zina upungufu wa walimu ambapo uwiano wa mwalimu kwa mwanafunzi ni 1:53 kwa shule za msingi. Shule za msingi bado zina upungufu wa matundu ya vyoo ambapo uwiano ni 1:54 na 1:51 kwa wasichana na wavulana badala ya 1:20 na 1:25. Uwiano wa darasa kwa wanafunzi ni 1:66, na uwiano wa kitabu kwa mwanafunzi bado ni 1:3 kwa shule za msingi badala ya 1:1. Matatizo haya yameendelea kuathiri mazingira ya kujifunzia na kufundishia. Uduni wa bajeti ya maendeleo ya sekta ya elimu, utekelezaji hafifu wa bajeti ni vyanzo vikuu vinavyosababisha matatizo haya (URT, budget 2009, 2010)

Ripoti hii inatoa uchambuzi wa bajeti ya sekta ya elimu ya mwaka wa fedha 2011/2012 ili kuonesha ni jinsi gani serikali haiwajibiki kijamii katika upangaji na kutumia fedha ili kuleta maendeleo katika sekta ya elimu. Uchambuzi huu unaeleza changamoto za upangaji wa bajeti na utekelezaji wake kwa kuhusisha miaka ya nyuma (2008/2009-2010/2011. Pia ripoti inatoa mapendekezo ya nini kifanyike ili kubadilisha changamoto kuwa fursa zitakazowawezesha watoto wa Tanzania kusoma katika shule bora na hatimaye kupata elimu bora.

1 Basic Education Statistics for Tanzania

Page 7: Kodi zetu zinaelekezwa kwenye Elimu? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Kodi Zetu ZInaelekezwa Kwenye Elimu.pdf · (Chanzo: Vitabu vya bajeti 2011, Juzuu namba ii-iv, randama

3

2.0 Malengo ya Matumizi ya Ripoti

Ripoti hii ni kwa ajili ya wadau wote wa sekta ya elimu ambao wanaweza kuleta mabadiliko ya upangaji na ufanisi katika utekelezaji wa bajeti ya sekta ya elimu ambao ni wabunge, watunga sera, madiwani, wakurugenzi wa wilaya, wahisani wa maendeleo na wananchi. Yafuatayo ni baadhi ya malengo kwa watumiaji wa ripoti hii.

1. Kwa kuwa uwajibikaji jamii unamtaka kiongozi yeyote wa serikali kuwaeleza wananchi wake jinsi alivyotumia fedha za umma kuwaletea wananchi maendeleo au alivyoshindwa kuwaletea maendeleo waliyoyatarajia. Uchambuzi huu unalenga kuwaonesha wananchi hali halisi ya upangaji na utekelezaji wa bajeti ya sekta ya elimu, ili waweze kuihoji serikali na kupata majibu juu ya hali halisi ya mfumo wa bajeti ya sekta ya elimu, hasa kwenye maeneo yenye matatizo.

2. Bunge ni sehemu muhimu sana katika upangaji, upitishaji wa bajeti na usimamizi wa shughuli za serikali, ripoti hii itawapa wabunge picha halisi ya kujua changamoto hizi, na hivyo kutumia fursa ya Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii au Bunge la Bajeti katika mwaka wa fedha 2012/2013 kurekebisha kasoro hizo, na hivyo kuandaa bajeti sahihi pia kusimamia vizuri fedha za umma ambako kutaleta umakini wa kutumia fedha za umma kwenye sekta ya elimu kwa miaka ijayo.

3. Pia watunga sera, na walioaminiwa kutumia fedha kwa manufaa ya wananchi katika ngazi mbalimbali za serikali kuu na serikali za mitaa wataweza kujifunza juu ya changamoto hizi na kurekebisha makosa ili kuboresha elimu hapa nchini.

Page 8: Kodi zetu zinaelekezwa kwenye Elimu? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Kodi Zetu ZInaelekezwa Kwenye Elimu.pdf · (Chanzo: Vitabu vya bajeti 2011, Juzuu namba ii-iv, randama

4

3.0 Matokeo ya Uchambuzi

3.1. Uhalisia wa Ongezeko la Bajeti ya Sekta ya ElimuOngezeko la bajeti ni moja ya ishara ya kuongezeka kwa matumizi ya serikali, na hivyo kuashiria hali chanya ya mabadiliko katika shughuli za kiuchumi na kijamii. Ongezeko la bajeti linaweza kuleta mabadiliko kama tu bajeti iliyopangwa haiwezi kuathiriwa na mfumko wa bei, na pia ongezeko hilo linaweza kuwa na tija kama linaweza kukidhi mahitaji ya jamii husika. Katika mwaka wa fedha 2011/2012, sekta ya elimu imepangiwa Shs. bilioni 2, 283 tofauti na mwaka 2010/2011 ilikuwa Shs.bilioni 2,045. Hivyo, bajeti ya sekta ya elimu imeongezeka kwa Shs. bilioni 238 (ongezeko la asilimia 12%).

(Chanzo: Hotuba ya bajeti ya taifa, 2010, 2011, BEST 2011)

Bajeti ya sekta ya elimu mwaka 2011/2012 inaonekana kuongezeka, lakini uwezo wa ongezeko hili kununua vitu kwa bei ya soko unatia shaka. Uchambuzi unaonesha kuwa kwa kutumia bei halisi ya soko, bajeti ya elimu mwaka 2011/2012 ina thamani ya Shs. bilioni 20832, hivyo ongezeko la bajeti ni Shs. bilioni 7 tu kiuhalisia na si Shs. bilioni 238. Hii inamaanisha kuwa uwezo wa kimanunuzi wa bajeti ya mwaka 2011/2012 ni karibu sawa na ile ya mwaka 2010/2011. Hii ni sawa na mnunuzi aliyekuwa na Shs. 100 mwaka 2010, ambapo ana uwezo wa kununua machungwa mawili kwa Shs. 50 kila chungwa. Kama mwaka 2011 fedha yake ikiongezeka hadi Shs. 150 huku bei ya chungwa ikiongezeka kwa Shs. 75 Kwa chungwa, mnunuzi huyu ataweza kununua machungwa mawili tu kama ilivyokuwa mwaka 2010/20111.

2 Kwa kuhusisha bei ya soko ya mwezi Juni 2010 na mwezi Juni 2011

Page 9: Kodi zetu zinaelekezwa kwenye Elimu? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Kodi Zetu ZInaelekezwa Kwenye Elimu.pdf · (Chanzo: Vitabu vya bajeti 2011, Juzuu namba ii-iv, randama

5

Uwiano wa bajeti ya elimu na bajeti ya taifa umeendelea kupungua hadi kufi kia asilimia 17. Chati 3 inaonesha mwaka wa fedha 2008/2009 uwiano wa bajeti ya sekta ya elimu na bajeti ya taifa ulifi kia asilimia 20, lakini imekuwa ikishuka kila mwaka hadi kufi kia asilimia 17 kwa mwaka wa fedha 2011/2012(BEST 2011). Kushuka kwa bajeti ya elimu kuna ashiria sekta ya elimu kutokuwa kipaumbele cha kwanza katika bajeti ya taifa kama ilivyokuwa miaka mitano iliyopita. Dalili zinaonesha kuwa bajeti hii itaendelea kushuka zaidi kwani ongezeko la bajeti limekuwa likishuka kila mwaka. Mwaka 2008/2009 bajeti ya elimu iliongezeka kwa Shs.bilioni 344, lakini ikaanza kupungua hadi Shs. bilioni 313 mwaka 2009/2010, ikawa Shs. bilioni 302 mwaka 2010/2011 hadi kufi kia Shs. bilioni 238 mwaka wa fedha 2011/2012 (Chati namba 4). Kiwango cha ongezeko cha bajeti ya elimu, hasa cha mwaka 2011/2012 ni kidogo sana. Na ni vigumu kuleta mabadiliko ya kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia katika harakati za kuboresha elimu yetu hapa nchini.

(Chanzo: Hotuba ya bajeti ya taifa, 2008, 2009, 2010, 2011, BEST 2011)

(Chanzo: Hotuba ya bajeti ya taifa, 2008, 2009, 2010, 2011, BEST 2011)

Page 10: Kodi zetu zinaelekezwa kwenye Elimu? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Kodi Zetu ZInaelekezwa Kwenye Elimu.pdf · (Chanzo: Vitabu vya bajeti 2011, Juzuu namba ii-iv, randama

6

3. 2. Uwekezaji katika Miradi ya Maendeleo Bajeti ya kila sekta ina sehemu kuu mbili. Fedha za maendeleo na fedha za matumizi ya kawaida. Fedha/bajeti ya maendeleo ni kwa ajili ya kugharamia miradi mikubwa katika sekta ya elimu kama vile ujenzi wa madarasa, mabweni, maabara, maktaba na nyumba za walimu. Hizi ni fedha zinazolenga kuongeza uwekezaji katika sekta ya elimu, tofauti na bajeti ya matumizi ya kawaida ambayo inatumika kugharamia matumizi kama vile mishahara, posho na safari mbalimbali za ndani na nje ya nchi. Licha ya kuwa sekta ya elimu inakabiliwa na matatizo ya miundombinu, kiwango kinachotengwa katika bajeti ya maendeleo ni kidogo sana huku fedha nyingi zikielekezwa kwenye matumizi ya kawaida (Chati 5).

(Chanzo: Vitabu vya bajeti 2011, Juzuu namba ii-iv, randama 46, 56, 70-89 na 95)

Katika mwaka wa fedha 2011/2012, ni Shs. bilioni 232.86 ambazo ni asilimia 10.2 ya bajeti nzima ya sekta ya elimu imetengwa kutekeleza shughuli za maendeleo za sekta ya elimu. Matumizi ya kawaida ni Shs. bilioni 2,050.14 ambayo ni sawa na asilimia 89.8 ya bajeti nzima ya sekta ya elimu. Licha ya kwamba bajeti ya maendeleo imeongezeka kwa Shs bilioni 33.23 kati ya mwaka 2010/2011 na 2011/2012(Chati 5), bajeti ya maendeleo ya sekta ya elimu bado ni kidogo sana ukilinganisha na nchi jirani za Kenya na Uganda;

Uganda-Bajeti ya maendeleo katika sekta ya elimu ni asilimia 20-24 ya bajeti nzima ya sekta ya elimu kwa mwaka 2009/2010-2010/2011. (Madina et all, 2011).

Kenya-Bajeti ya maendeleo ya sekta ya elimu ni asilimia 14-15 ya bajeti ya sekta ya elimu kwa mwaka 2009/2010-2010/2011(Kenya, PER 2010).

Ukubwa wa bajeti ya matumizi mengineyo kama posho, mafuta, safari, gharama za mikutano na fedha za kukirimu wageni ndio kinachosababisha ongezeko hili la matumizi ya kawaida. Kwa mfano, mwaka

Page 11: Kodi zetu zinaelekezwa kwenye Elimu? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Kodi Zetu ZInaelekezwa Kwenye Elimu.pdf · (Chanzo: Vitabu vya bajeti 2011, Juzuu namba ii-iv, randama

7

wa fedha 2011/2012, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi bila kuhusisha serikali za mitaa itatumia Shs. bilioni 320 kwa matumizi mengineyo ambayo ni zaidi kwa Shs. bilioni 87.14 ya bajeti ya matumizi ya maendeleo ya sekta ya elimu. Tamko la serikali limebainisha wazi dhamira ya kupunguza matumizi mengineyo katika hotuba ya bajeti ya Waziri wa fedha mnamo Juni 9, 2011 mbele ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa;

“Serikali itasitisha ununuzi wa samani za ofi si hususani zile zinazoagizwa nje ya nchi; kupunguza malipo ya posho mbalimbali yasiyokuwa na tija; kupunguza matumizi ya mafuta kwa magari ya Serikali; kupunguza safari za ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na ukubwa wa misafara; na pia kuendelea kupunguza gharama za maonesho na sherehe mbalimbali, na uendeshaji wa semina na warsha isipokuwa pale inapobidi na kwa kibali cha Ofi si ya Waziri Mkuu”.(Hotuba ya bajeti ya taifa 2011/2012, uk 75)

Lakini swali linabaki; Serikali inapunguzaje matumizi ilihali kwenye bajeti hakuna ishara ya kupunguza matumizi? Ishara ya kupunguza matumizi lazima ianze kuonekana kwenye upangaji wa bajeti na sio wakati wa utekelezaji wa bajeti. Kupunguza mishahara sio njia nzuri ya kupunguza matumizi ya kawaida, njia pekee ambayo ni sahihi ni kupunguza matumizi mengineyo ambayo si ya lazima na yasiyo na tija kwa maendeleo ya taifa. Kwa mfano kupunguza asilimia 20% ya matumizi mengineyo tunaweza kupata Shs. bilioni 64 na kuzitenga katika bajeti ya maendeleo. Twaweza kudhani fedha hizi ni kidogo lakini zinaweza kujenga maabara 1,2803

kwa bei ya Shs. milioni 50 kwa mujibu wa Mpango wa pili wa maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES II).

3 Idadi hii ni karibu nusu ya malengo ya MMES ya kujenga maabara 2,350 ili kuondoa tatizo la ukosefu wa maabara kwa shule za sekondari Tanzania

Page 12: Kodi zetu zinaelekezwa kwenye Elimu? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Kodi Zetu ZInaelekezwa Kwenye Elimu.pdf · (Chanzo: Vitabu vya bajeti 2011, Juzuu namba ii-iv, randama

8

(Chanzo: Vitabu vya bajeti 2011, Juzuu namba ii-iv, randama 46, 56, 70-89 na 95)

3. 3. Ugatuaji wa Madaraka na Upangaji wa BajetiHivi sasa serikali inatekeleza sera ya ugatuzi wa madaraka ambapo shughuli nyingi zinatekelezwa na serikali za mitaa ili kuharakisha maendeleo katika wilaya na vijiji. Sera hii inaipa mamlaka serikali za mitaa kutekeleza shughuli za maendeleo. Hii imesababisha fedha nyingi za bajeti ya taifa kuelekezwa serikali za mitaa kuliko serikali kuu4. Chati namba 7 inaonesha kuwa mwaka wa fedha 2010/2011, serikali za mitaa zilipangiwa asilimia 65 ya bajeti ya sekta ya elimu na mwaka wa fedha 2011/2012, serikali za mitaa zimepangiwa asilimia 68 ya bajeti ya sekta ya elimu.

(Chanzo: Vitabu vya bajeti 2009, 2010, 2011, Juzuu namba ii-iv, randama 46, 56, 70-89 na 95)

4 Idadi hii ni karibu nusu ya malengo ya MMES ya kujenga maabara 2,350 ili kuondoa tatizo la ukosefu wa maabara kwa shule za sekondari Tanzania.

Page 13: Kodi zetu zinaelekezwa kwenye Elimu? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Kodi Zetu ZInaelekezwa Kwenye Elimu.pdf · (Chanzo: Vitabu vya bajeti 2011, Juzuu namba ii-iv, randama

9

Licha ya fedha nyingi za bajeti ya sekta ya elimu kupangwa serikali za mitaa, bajeti ya maendeleo ya serikali za mitaa ni ndogo sana tofauti na fedha za maendeleo zilizotengwa Serikali kuu. Chati 8 inaonesha kuwa, mwaka wa fedha 2011/2012, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi pekee inatumia Shs. bilioni 135.5 wakati Serikali za mitaa zitatumia Shs. bilioni 96.7 kwa shughuli za maendeleo. Hii inamaanisha kuwa elimu ya msingi na sekondari ambazo ziko chini ya serikali za mitaa zinapangiwa fedha kidogo za maendeleo tofauti na elimu ya juu, ualimu na ufundi ambazo ziko chini ya Wizara. Elimu ya juu peke yake imepangiwa Shs bilioni 106 kwa ajili ya shughuli za maendeleo kwa mwaka wa fedha 2011/2012.

Sera ya ugatuaji madaraka bado ina changamoto kubwa hasa katika upangaji wa bajeti. Miradi ya maendeleo ya MMEM II na MMES II ni kwa ajili ya kuboresha elimu ya shule ya msingi na sekondari ambazo ziko chini ya serikali za mitaa. Cha kushangaza katika bajeti ya mwaka 2011/2012 jumla ya Shs bilioni 17.2 za MMEM II na MMES II zimepangwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika randama 46, randama ndogo 3001 na 4001. Hii inapingana na lengo la sera ya ugatuaji wa madaraka inayosema serikali za mitaa ndizo zinakuwa mtekelezaji wa shughuli za maendeleo za elimu ya msingi na sekondari, na serikali kuu inabaki kutunga sera, kutoa ushauri wa kitaalam, kufuatilia mipango na sera za maendeleo na kuhakiki ubora wa miradi iliyotekelezwa.

(Chanzo: Vitabu vya bajeti 2011, Juzuu namba ii-iv, randama 46, 56, 70-89, 95)

3. 4. Utekelezaji wa BajetiMoja ya njia za kuleta maendeleo katika jamii ni kuwa na usimamizi imara katika utekelezaji bajeti. Ili fedha za bajeti zilete maendeleo ni lazima zitumike kama ilivyopangwa, kwa sababu bajeti sahihi huzingatia vipaumbele, mipango iliyopo na uwezo wa kukusanya fedha. Kasi ya kupata maendeleo hupungua pale bajeti halisi iliyotumika kuwa ndogo zaidi ya bajeti iliyopangwa na kupitishwa. Hii inaweza kuwa ni ishara ya kupanga bajeti bila kuzingatia uwezo wa kukusanya mapato, kitu ambacho si kizuri katika taifa lolote.

Page 14: Kodi zetu zinaelekezwa kwenye Elimu? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Kodi Zetu ZInaelekezwa Kwenye Elimu.pdf · (Chanzo: Vitabu vya bajeti 2011, Juzuu namba ii-iv, randama

10

Hali hii inaonekana katika bajeti ya maendeleo ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ambayo inatumia fedha kidogo zaidi ya zilizopangwa katika bajeti5. Tatizo hili limekuwa likiongezeka katika kipindi cha miaka mitatu ya fedha iliyopita. Chati namba 9 inaonesha kuwa mwaka wa fedha 2008/2009, Wizara ilitumia Shs. bilioni 85.1 tu ilizopata toka Hazina badala ya Shs. bilioni 128.5 zilizopangwa katika bajeti. Hivyo Shs. bilioni 43.4 hazikutolewa. Mwaka wa fedha 2009/2010 kiasi cha Shs. bilioni 80.5 zilitolewa na hazina kati ya Shs. bilioni 129.3 (Shs. bilioni 48.8 hazikutolewa) na katika mwaka 2010/2011 Shs. 76.8, zilitolewa na Hazina kati ya Shs. 139.7 zilizopangwa.Tatizo hili limeongezeka hadi kufi kia asilimia 45 kwa mwaka 2010/2011 tofauti na ilivyokuwa mwaka 2008/2009 asilimia 34 tu ndizo hazikutolewa

Fedha ambazo zilipangwa na hazikutolewa kwa kipindi cha miaka mitatu (2008/2009-2010/2011 kwa Wizara ni Shs. bilioni 155.1. Fedha hizi zingetosha kujenga nyumba za walimu 3,875 kwa mujibu wa makadirio ya gharama za ujenzi wa nyumba moja kwa Shs. milioni 40 kama ilivyobainishwa na MMES II. Kwa kujenga nyumba hizi tungeweza kupunguza tatizo la walimu kuacha kazi kwa kukosa makazi hasa katika shule za vijijini

(Chanzo: Hotuba ya bajeti, WEMU 2009, 2010, 2011)

5 Hii inasababishwa na kupata fedha kidogo toka hazina zaidi ya zile zilizopangwa katika bajeti.

Page 15: Kodi zetu zinaelekezwa kwenye Elimu? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Kodi Zetu ZInaelekezwa Kwenye Elimu.pdf · (Chanzo: Vitabu vya bajeti 2011, Juzuu namba ii-iv, randama

11

3. 5. Utegemezi Katika Miradi ya MaendeleoWahisani wa maendeleo ni muhimu sana katika kusaidia kuleta maendeleo, hasa kupitia misaada au kuchangia katika mfuko wa bajeti. Ahadi za wahisani zinakuwa na tija kama wanatoa fedha zote walizoahidi ili kuiwezesha bajeti itekelezeke. Wahisani wakishindwa kutoa kiwango cha fedha walichoahidi miradi mingi hukwama na kuathiri hali ya utekelezaji wa mipango mbalimbali. Tofauti na bajeti ya matumizi ya kawaida, bajeti ya maendeleo ya sekta ya elimu imekuwa inategemea fedha za wahisani kwa karibu asilimia 70. Mwaka 2010/2011 utegemezi wa bajeti ya maendeleo ulikuwa Shs. bilioni 139.73 kati ya bajeti nzima ya maendeleo ya sekta ya elimu ya Shs. bilioni 199.6. Utegemezi umeongezeka zaidi mwaka wa fedha 2011/2012 hadi kufi kia Shs. 161.06 ya bajeti nzima ya maendeleo ya Shs. bilioni 232.86 (Chati 11).

Kasumba ya wahisani kuahidi kiwango kikubwa halafu wanatoa kiwango kidogo ni moja ya tatizo linalochangia kukwama kwa mipango mbalimbali ya maendeleo kama vile Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) na Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Sekondari (MMES), ambayo bado inakabiliwa na changamoto ya wahisani kutotoa fedha walizoahidi katika bajeti. Tatizo la wahisani kutotoa fedha kamili walizoahidi si geni katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Tukihusisha miaka miwili iliyopita kwa bajeti ya Maendeleo ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi tu, mwaka wa fedha 2008/2009, wahisani wa maendeleo walitoa Shs. bilioni 27.6 (asilimia 43) ya fedha walizoahidi Shs. bilioni 64. Na mwaka wa fedha 2009/2010 walitoa Shs. bilioni 30.3 (asilimia 48) ya Sh bilioni 63.4 walizoahidi (Chati namba 12). Hili ni funzo kwa serikali kutafuta njia mbadala ya kufadhili kiasi ambacho hakitolewi na wahisani, na njia pekee ni kupunguza matumizi yasiyo na tija ili kuongeza fedha za bajeti ya maendeleo.

Kuna haja ya Tanzania kujifunza toka kwa majirani zetu Kenya na Uganda ambapo Kenya inatumia fedha zake za ndani kwa ajili ya bajeti ya maendeleo ya sekta ya elimu, hii imefanya Wizara ya Elimu na Wizara ya Elimu ya juu za Kenya kuweza kutekeleza bajeti ya maendeleo kwa asilimia 96 (Kenya, PER 2010). Uganda pia inatumia fedha za ndani kwa matumizi ya maendeleo ya elimu ya msingi, sekondari na elimu ya juu. (Madina et all, 2011). Kwa sababu ya uwekezaji mdogo katika elimu, asilimia ya watu

Page 16: Kodi zetu zinaelekezwa kwenye Elimu? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Kodi Zetu ZInaelekezwa Kwenye Elimu.pdf · (Chanzo: Vitabu vya bajeti 2011, Juzuu namba ii-iv, randama

12

wasiojua kusoma na kuandika ya Tanzania ni kubwa kuliko Kenya na Uganda. Tanzania ina asilimia 31 (Kumbukumbu za bunge, 2011), Uganda ina asilimia 27 na Kenya asilimia 13(www. databank.worldbank.org)

(Chanzo: Hotuba ya bajeti, WEMU 2009, 2010, 2011)

3. 6. Utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari Mnamo Januari 2011, serikali ilizindua Mpango wa pili wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES II) ambao utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano (2010-2014). Katika mpango huu, serikali imedhamiria kutoa ruzuku kwa mwanafunzi ya Shs. 25,000 kwa mwaka katika kipindi chote cha utekelezaji ili kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia. Pia MMES II umelenga kuboresha miundombinu kama vile madarasa, maabara, maktaba na kujenga nyumba za walimu. Mwaka wa kwanza (2010/2011) tayari umemalizika. Je, hali ya utekelezaji inaridhisha? Uchambuzi ufuatao unatoa majibu ya swali hili;

3. 6.1 Fedha za Maendeleo za MMES IIHali ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo si ya kuridhisha. MMES II unapangiwa fedha kidogo kwa ajili ya shughuli za maendeleo tofauti na mahitaji yalivyobainishwa katika mpango kwa mwaka. Chati 13 inaonesha kuwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2010/2011, MMES II ulipangiwa Shs. bilioni 68.96 (pungufu kwa Shs. bilioni 58.44) badala ya Shs. bilioni 127.39. Upungufu umeongezeka hata katika mwaka wa fedha 2011/2012 umepangiwa kiasi cha Shs. bilioni 74.7 (pungufu kwa Shs. bilioni 60.69) badala ya Shs. bilioni 135.39 kwa ajili ya kutekeleza shughuli za maendeleo zilizo chini ya MMES II. Hivyo, kwa wastani, serikali imekuwa ikipanga asilimia 50 ya bajeti ya maendeleo ya MMES II kwa

Page 17: Kodi zetu zinaelekezwa kwenye Elimu? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Kodi Zetu ZInaelekezwa Kwenye Elimu.pdf · (Chanzo: Vitabu vya bajeti 2011, Juzuu namba ii-iv, randama

13

mwaka. Hii inamaanisha MMES II unatekeleza nusu ya malengo yake kwa mwaka na kuna dalili za kushindwa kutekeleza malengo ya kujenga mabweni 120, maabara 2,350, Majengo ya utawala 1,200, na kujenga nyumba za walimu 1,800.

(Chanzo: MMES II 2010 na Vitabu vya bajeti 2011, Juzuu namba iv, randama 46, 56, 70-89 na 95)

Miradi mingi imeshindwa kutekelezwa kwa sababu ya uduni wa bajeti kwenye miradi hiyo. Mfano mzuri ni Mpango wa pili wa Maendeleo wa Elimu ya Msingi (MMEM II). Mpango huu umeshindwa kutekeleza malengo yake na hivyo kuendelea kuathiri elimu ya msingi hapa nchini. Baadhi ya Malengo ya MMEM II yaliyoshindwa kutekelezwa ipasavyo ni;

• Madarasa 6,843 (asilimia 15) yamejengwa kati ya madarasa 45,315 yaliyopangwa kujengwa.• Nyumba za walimu 4,742 (asilimia 5) zimejengwa kati ya nyumba 89,927 zilizopangwa kujengwa.• Vyoo 3,193 (2.5) vimejengwa kati ya vyoo 127,956 vilivyopangwa kujengwa.

Page 18: Kodi zetu zinaelekezwa kwenye Elimu? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Kodi Zetu ZInaelekezwa Kwenye Elimu.pdf · (Chanzo: Vitabu vya bajeti 2011, Juzuu namba ii-iv, randama

14

3. 6.2 Fedha za Ruzuku kwa MwanafunziKatika mwaka wa kwanza wa utekelezaji wa MMES II, serikali imefanikiwa kutekeleza lengo lake la kutoa ruzuku ya Shs. 25,082(PER 2011 Uk 131)) kwa mwanafunzi katika mwaka wa fedha 2010/2011, kama ilivyobainishwa katika mpango wa MMES II. Haya ni mafanikio makubwa na hakuna budi ya kuipongeza serikali kwa uwajibikaji huu kwa kutoa ruzuku ambayo ni zaidi ya ile iliyobainishwa katika MMES II ya Shs 25,000. Licha ya mafanikio haya, kuna mashaka kama serikali itaweza kutoa tena kiasi cha Shs 25,000, katika mwaka wa fedha 2011/2012. Mashaka haya yanatokana na utofauti uliopo kati ya maelekezo ya mpango wa MMES II na mwongozo wa bajeti wa mwaka 2011/2012. Mwongozo wa bajeti, Wizara ya Fedha na Uchumi umezielekeza serikali za mitaa kutenga Shs. 20,000 kwa ajili ya ruzuku kwa mwanafunzi kwa shule za sekondari.

MMES II unasema hivi; “Lengo la kifungu hiki ni kutoa fedha za kutosha kwa shule za sekondari ili kuziwezesha kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia (kiasi cha Shs. 25,000 kwa mwanafunzi), pia kuhakikisha fedha hizi zinatolewa katika muda muafaka, na zinafuatiliwa kikamilifu”. (Rasimu ya MMES II-Benki ya Dunia, Kifungu cha 3, Uk 13, Tafsiri ya mwandishi)

Lakini mwongozo wa Bajeti 2011/2012 unaelekeza tofauti;

“Serikali za mitaa zinapaswa kupanga bajeti ya wastani wa Shs. 20,000 kwa kila mwanafunzi kwa mwaka ili zitumike kununulia vitabu, vifaa vya kufundishia, kufanyia ukarabati mdogo wa shule na gharama za utawala” (Mwongozo wa bajeti 2011/2012, Uk 24, Tafsiri ya mwandishi)

Pia, tathmini ya mradi wa MMES II kwa ajili ya kupatiwa fedha na Benki ya Dunia imeelekeza kuwa asilimia 40 ya Shs. 25,000 ambayo ni Shs. 10,000 inapaswa kutolewa mwezi Januari ya kila mwaka wa utekelezaji wa MMES II. Hii inalenga kuziwezesha shule kununua mahitaji muhimu mwanzoni mwa mwaka wa masomo. Kifuatacho ni kifungu cha tathmini ya mradi wa MMES II kilichoshindwa kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2010/2011;

“Ili kuhakikisha shule zinapata fedha za kutosha kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia. Kiwango cha fedha za ruzuku kitakachotolewa Januari (mwanzoni mwa mwaka wa shule) kitakuwa asilimia 40 ya jumla ya fedha inayopaswa kufika shuleni kwa mwaka mzima. Fedha zinazobaki zitatolewa mwisho wa mwezi Aprili, Julai na Oktoba kila mwaka”. (Rasimu ya MMES II-Benki ya Dunia, Kifungu cha 3, uk 12 Tanbihi namba 16, Tafsiri ya mwandishi)

Mwanzo wa mwaka wa shule (Januari hadi Machi) uko katika robo ya tatu (Januari-Machi 2011) ya mwaka wa fedha, ambapo serikali iliweza kutoa kiasi cha Shs. 390 tu kwa kila mwanafunzi badala ya

Page 19: Kodi zetu zinaelekezwa kwenye Elimu? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Kodi Zetu ZInaelekezwa Kwenye Elimu.pdf · (Chanzo: Vitabu vya bajeti 2011, Juzuu namba ii-iv, randama

15

Shs. 10,000. Fedha nyingi za ruzuku Shs 22,592 zilitolewa robo ya nne (chati namba 16) ya mwaka wa fedha ambayo ni nusu mwaka kwa mwaka wa masomo kwa shule za sekondari. Hali hii itaathiri utekelezaji wa MMES II. Sababu ni kwamba kutoa fedha za ruzuku kwa mwanafunzi katikati ya mwaka au mwisho mwa mwaka wa masomo unachelewesha shule kuanza kutekeleza mipango ya kila mwaka, na hivyo kukwamisha upatikanaji wa maendeleo ya elimu kwa shule za sekondari.

(Chanzo: MMES II 2010, www.mof.go.tz, URT, ESR 2011)

Page 20: Kodi zetu zinaelekezwa kwenye Elimu? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Kodi Zetu ZInaelekezwa Kwenye Elimu.pdf · (Chanzo: Vitabu vya bajeti 2011, Juzuu namba ii-iv, randama

16

4. Mapendekezo

Hali halisi ya upangaji na utekelezaji wa bajeti haitoi ishara nzuri kwa maendeleo ya sekta ya elimu. Fedha nyingi bado zinaelekezwa katika matumizi yasiyo na tija. Pia ufanisi wa bajeti bado ni tatizo hasa kwa bajeti ya maendeleo, na hivyo kuendelea kuathiri sekta ya elimu. Ripoti hii inatoa mapendekezo yafutayo;

1. Bajeti ya sekta ya elimu bado ni ndogo hasa bajeti ya maendeleo. Ili kuweza kutatua changamoto za kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia, serikali haina budi kuongeza bajeti ya maendeleo hasa kwa kutumia fedha za ndani kwani wahisani wanatoa asilimia kati ya 40 -50 tu ya fedha walizo ahidi. Serikali inabidi itafute njia mbadala ya kufadhili kiasi ambacho hakitolewi na wahisani, na njia pekee ni kupunguza matumizi yasiyo na tija ili kuongeza fedha za bajeti ya maendeleo. Kama Uganda na Kenya zinatumia asilimia kubwa ya fedha za ndani kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwenye elimu, kwa nini Tanzania ishindwe ilihali mapato ya ndani ya Tanzania ni zaidi ya Uganda. Mfano mzuri ni kujifunza toka kwa majirani zetu Kenya na Uganda ambapo Kenya inatumia fedha zake za ndani kwa ajili ya bajeti ya maendeleo ya sekta ya elimu. Hii imefanya kuweza kutekeleza bajeti ya maendeleo kwa asilimia 96 (Kenya, PER 2010). Uganda pia inatumia fedha za ndani kwa bajeti ya maendeleo ya elimu ya msingi, sekondari na elimu ya juu. (Madina et all, 2011).

2. Fedha za maendeleo kwa shule za sekondari ni muhimu sana kwa ajili ya miundombinu. Hivyo, Serikali inapaswa kutoa fedha zote za maendeleo kama ilivyobainishwa katika MMES II. Si kwamba serikali haina fedha, bali fedha nyingi zinatumika kwa matumizi ambayo hayana tija. Mfano, WEMU pekee inatumia kiasi cha Shs. bilioni 320 kwa matumizi mengineyo kama vile safari, kununua mafuta, posho, chai wakati wa vikao, ununuzi wa magari na ukarimu wa serikali kwa wageni. Hivyo ni muhimu kupanga vipaumbele kwa makini ili fedha kidogo zitumike kwa kufuata vipaumbele na si mradi kutumia tu kwa matumizi yanayowezekana kupunguzwa.

3. Ugatuaji wa madaraka ni muhimu kwa ajili ya kuharakisha upatikanaji wa maendeleo katika ngazi za wilaya na vijiji. Hivyo serikali inabidi kuongeza fedha za bajeti ya maendeleo kwa serikali za mitaa. Hili linapaswa kwenda sambamba na kuwajengea uwezo watendaji wa serikali za mitaa ili wafahamu jinsi ya kupanga mipango sahihi ya maendeleo na kuitekeleza ipasavyo.

4. Kwa kuwa tayari utekelezaji wa bajeti umeanza tangu mwezi Julai 2011, serikali haina budi kuwahimiza watendaji wote wa serikali kufuata taratibu rasmi za manunuzi ya umma kama zilivyobainishwa na sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2004. Hii itasaidia kuleta ufanisi na usahihi katika utekelezaji wa bajeti ya sekta ya elimu mwaka wa fedha 2011/2012.

5. Wananchi wanapaswa kufuatilia ili kubaini kama kiasi chote cha Shs 25,080 kwa kila mwanafunzi wa shule za sekondari za serikali kimefika shuleni na kimetumika ipasavyo. Kumekuwa na ufujaji wa fedha hizi na mara nyingi zinaanza kupungua zinapofika ngazi ya serikali za mitaa kwenda shuleni.(URT, PETS 2009, HakE PETS, 2011)

Page 21: Kodi zetu zinaelekezwa kwenye Elimu? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Kodi Zetu ZInaelekezwa Kwenye Elimu.pdf · (Chanzo: Vitabu vya bajeti 2011, Juzuu namba ii-iv, randama

17

Marejeo

HakiElimu (2011). Is there Effective Accuntability in the Implementation of PEDP II? A Public Expenditure Tracking Survey Report.Madina et al, 2011, Public spending in the education sector in Uganda: Evidence from program budget analysis.MoSP (Kenya), 2011, Public Expenditure Review Report.URT (2011). Hotuba ya Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bungeni, tarehe 15 Februari 2011, Kumbukumbu za Bunge.URT (2009). Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya UfundiURT (2009) Public Expenditure Tracking Survey: Ministry of Education and Vocational TrainingURT (2010a). Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya UfundiURT (2010b). Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Elimu ya SekondariURT (2010c). Hotuba ya Bajeti ya TaifaURT (2010d). Volume II Estimates of Public Expenditure Consolidated Fund Services and Supply Vote (Ministerial), Government Printer, Dar es SalaamURT (2010e). Volume II Estimates of Public Expenditure Consolidated Fund Services and Supply Vote (Regional), Government Printer, Dar es SalaamURT (2010f), Volume IV Estimates of Public Expenditure Development Votes, Government Printer, Dar es SalaamURT (2011a). Hotuba ya Bajeti ya ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya UfundiURT (2011b). Basic Education Statistics of Tanzania 2011URT (2011c). Hotuba ya Bajeti ya TaifaURT (2011d). Volume II Estimates of Public Expenditure Consolidated Fund Services and Supply Vote (Regional), Government Printer, Dar es SalaamURT (2011e). Volume II Estimates of Public Expenditure Consolidated Fund Services and Supply Vote (Ministerial), Government Printer, Dar es SalaamURT (2011f), Volume IV Estimates of Public Expenditure Development Votes, Government Printer, Dar es SalaamWorldbank (2010). Secondary Education Development Program II, APL Project, Project Appraisal.

Page 22: Kodi zetu zinaelekezwa kwenye Elimu? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Kodi Zetu ZInaelekezwa Kwenye Elimu.pdf · (Chanzo: Vitabu vya bajeti 2011, Juzuu namba ii-iv, randama

18

Kiambatisho 1: Utekelezaji wa MMEM II-2007-2011

Mwaka Madarasa Nyumba za walimu Vyoo

Lengo Iliyojengwa Lengo Iliyojengwa Lengo Iliyojegwa

2007 2,303 3,176 2,183 2,961 56,500 9292008 10,753 1,263 21,936 277 17,864 9392009 10,753 929 21,936 709 17,864 7162010 10,753 510 21,936 293 17,864 1172011 10,753 965 21,936 502 17,864 492

Jumla 45,315 6,843 89,927 4,742 127,956 3,193

Page 23: Kodi zetu zinaelekezwa kwenye Elimu? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Kodi Zetu ZInaelekezwa Kwenye Elimu.pdf · (Chanzo: Vitabu vya bajeti 2011, Juzuu namba ii-iv, randama

19

Page 24: Kodi zetu zinaelekezwa kwenye Elimu? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Kodi Zetu ZInaelekezwa Kwenye Elimu.pdf · (Chanzo: Vitabu vya bajeti 2011, Juzuu namba ii-iv, randama

20

Utekelezaji wa bajeti ni kutumia fedha kuleta na kuendeleza huduma za jamii huduma za jamii. Kwa mfano, bajeti inapotumika kugharamia ujenzi wa miundombinu ya shule, kuajiri walimu na kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia jamii inapata huduma ya shule ambapo watoto wanasoma na kupata elimu bora kwa ajili ya kuwaletea maendeleo. Kama jamii inahitaji madarasa, walimu na vifaa vya kujifunzia na kufundishia ili kuanzisha shule ni lazima kuwe na fedha za kutosha. Ikitokea bajeti imepangwa na ikawa ndogo na haiwezi kujenga madarasa yanayohitajika tunaweza kuwa na shule ambayo haijakamilika na hivyo kusababisha watoto washindwe kujifunza na kufundishwa ipasavyo.

Hii ndio hali halisi inayoikabili Tanzania kwani hakuna shule halisi za msingi na sekondari. Takwimu za BEST 2011 zinaonesha kuwa shule nyingi bado zina upungufu wa walimu ambapo uwiano wa mwalimu kwa mwanafunzi ni 1:53 kwa shule za msingi. Shule za msingi bado zina upungufu wa matundu ya vyoo ambapo uwiano ni 1:54 na 1:51 kwa wasichana na wavulana badala ya 1:20 na 1:25. Na pia uwiano wa darasa kwa mwanafunzi ni 1:66, na uwiano wa kitabu kwa mwanafunzi ni 1:3 kwa shule za msingi. Matatizo haya yameendelea kuathiri mazingira ya kujifunzia na kufundishia. Mfumo wa upangaji wa bajeti ya sekta ya elimu, uduni wa bajeti ya maendeleo, usimamizi mbovu wa fedha za umma na utekelezaji hafifu wa bajeti ni vyanzo vikuu vinavyosababisha matatizo haya.

Ripoti hii inatoa uchambuzi wa bajeti ya sekta ya elimu ya mwaka wa fedha 2011/2012 ili kuonesha ni jinsi gani serikali haiwajibiki kikamilifu kwa jamii katika kupanga na kutumia fedha ili kuleta maendeleo katika sekta ya elimu. Uchambuzi huu unaeleza changamoto za upangaji wa bajeti na utekelezaji wake kwa kuhusisha pia miaka ya nyuma (2008/2009-2010/2011. Pia ripoti inatoa mapendekezo ya ya nini kifanyike ili kubadilisha changamoto kuwa fursa zitakazowawezesha watoto wa Tanzania kusoma katika shule bora na hatimaye kupata elimu bora.

Taarifa za ripoti hii zinawalenga wadau wote wa sekta ya elimu ambao wanaweza kuleta mabadiliko ya upangaji na ufanisi katika utekelezaji wa bajeti ya sekta ya elimu ambao ni wananchi, wabunge, watunga sera, madiwani, wakurugenzi wa wilaya, wahisani wa maendeleo na asasi za kiraia. Lakini pia kwa wananchi, ripoti hii inaweza kutumika kuelewa hali halisi na kuweza kuhoji na kushinikiza utekelezaji mzuri na uwajibikaji wa serikali katika kutimiza malengo na hadi na kuwajibika. Kwa wabunge ripoti hii inatoa uchambuzi wa bajeti na matumizi, ili penye mafanikio waweze kupongeza na kuhimiza muendelezo wa mafanikio hayo, penye mapungufu waweze kusimamia na kuhakisha majibu na suluhisho yanapatikana ili kuboresha mipango na matumizi ya bajeti ili kuboresha kiwango cha elimu ya watoto wa Tanzania. Taarifa hii ina lengo la kuibua mjadala na mazungumzo ya wadau wa elimu, ili suluhisho ziweze kupatikana na kuwawezesha watoto kujifunza na kupata ujuzi na maarifa kwa kuwezesha miundo mbinu na fedha ziwafikie walengwa.

Tuandikie, toa maoni yako, maswali na mapendekezo!

HakiElimu inawezesha wananchi kuleta mabadiliko katika elimu na demokrasia

S.L.P 79401 • Dar es Salaam • TanzaniaSimu: (255 22) 2151852/3 • Faksi: (255 22) [email protected] • www.hakielimu.org