Upload
zitto-kabwe
View
266
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
7/28/2019 Maoni KATIBA-Zitto
1/13
MUUNDO WA MUUNGANO NA TAWALA ZA MIKOA
Rasimu ya Katiba imependekeza kuendelea kuwa na Muungano wa
Tanzania kwa kufanya marekebisho makubwa ikiwemo kupunguza
masuala ya Muungano na kuwepo kwa Serikali 3. Mjadala umekuwa
mkali kuhusu Serikali 3 na hata kuzuia mjadala mpana zaidi wa masuala
ya muungano. Rasimu haikushughulika kabisa na Serikali ya Tanganyika
maana Tume inasema wao walipewa hadidu kuangalia Katiba ya
Muungano tu. Kwa hili Tume haikutendea Haki wananchi maana kama
wao wamependekeza kuunda Chombo kipya ilikuwa ni lazima kusema
chombo hicho kinaundwa namna gani bila kuathiri Katiba ya Jamhuri ya
Muungano.
Wakati Mabaraza ya Katiba yanaendelea nchini kote ni vema mjadala
wa aina ya utawala kwa Serikali ya Tanganyika na mikoa yake ikapewa
fursa pia. Ninaamini kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
inapasa kugusia masuala ya msingi ya Katiba ya Serikali ya Zanzibar na
Katiba ya Serikali ya Tanganyika. Nina mawazo kadhaa ambayo
ningependa yaingie kwenye mjadala wa Katiba mpya.
Muundo wa Muungano
7/28/2019 Maoni KATIBA-Zitto
2/13
Kwa vyovyote vile muundo unaonekana kukubaliaka na wananchi
wengi ni ule wa Muungano wa Serikali 3, Serikali ya Jamhuri ya
Muungano, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Tanganyika, japo rasimu
imeiita Serikali ya Tanzania Bara. Hata hivyo wananchi wanapoambiwa
kuwa kutakuwa na Marais 3, wanaguna. Kwa hiyo suala hapa ni namna
gani ya kuhakikisha kuwa tunakuwa na Muundo wa Serikali 3 yenye
dola imara na Mamlaka ya Jamhuri yenye nguvu ilhali kila mshirika wa
Muungano anakuwa na mamlaka kamili ya kutekeleza wajibu wake kwa
Wananchi.
Iwapo tunataka Muungano uwe imara na usitetereke ni lazima tufanye
maamuzi ambayo yatabadili sura nzima ya Muungano na kuweka wazi
wajibu wa kila Mshirika katika Muungano. Ni vema pia kuweka Muundo
wa Serikali ambao utatoa uhuru kwa washirika kutekeleza majukumu
yao bila bugudha lakini pia utatoa fursa kwa Dola kutekeleza majukumu
yake ya kidola kama kuhakikisha ulinzi, usalama na utulivu wa nchi,
kuhakikisha umoja na mshikamano wa nchi na kuhakikisha maendeleo
sawia kwa maeneo yote ya Jamhuri ya Muungano.
7/28/2019 Maoni KATIBA-Zitto
3/13
Napendekeza Muungano wa Serikali mbili za Tanganyika na Zanzibar
zinazoongozwa na Mawaziri Wakuu watendaji na Serikali ya Muungano
inayoongozwa na Rais. Pia napendekeza masuala ya Tawala za Mikoa
kuwa masuala ya Muungano na Wakuu wa Mikoa (Gavana)
wachaguliwe na wananchi moja kwa moja na wawe na mamlaka kamili
kwenye masuala yatakayokabidhiwa kwa Serikali za Mikoa kwa mujibu
wa Sheria itakayotungwa na Bunge la Muungano (Seneti). Napendekeza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania achaguliwe na wananchi
wote kwa kupata zaidi ya nusu ya kura zote halali na sio chini ya
asilimia 25 ya kura kutoka kila upande wa Muungano. Gavana wa Mkoa
pia achaguliwe na wananchi wote wa Mkoa husika.
Nafasi nyingine za kuchaguliwa moja kwa moja ziwe ni pamoja na
Madiwani ambao watachagua Meya/Mwenyekiti wa Halmashauri,
Wabunge wa Mabunge ya Tanganyika na Zanzibar ambapo chama
chenye wabunge wengi au muungano wa vyama wenye wabunge wengi
utatoa Waziri Mkuu kuongoza Serikali za washirika na Maseneta ambao
watachaguliwa na Mikoa kama inavyopendekezwa na rasimu ya Katiba
ya sasa.
7/28/2019 Maoni KATIBA-Zitto
4/13
Rais wa Jamhuri ya Muungano
Napendekeza Rais awe Mkuu wa Nchi, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi na Usalama na Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania mwenye mamlaka kamili kwenye masuala yote ya Muungano
yaliyoainishwa na Katiba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano awe na wajibu wa kikatiba wa
kuhakikisha kuwa kuna ulinganifu wa maendeleo kwa mikoa yote ya
Jamhuri ya Muungano.
Rais awe na Mamlaka ya kukikaribisha chama chenye wingi wa
wabunge kwenye mabunge ya Tanganyika na Zanzibar kuunda Serikali.
Pale ambapo hakuna chama pekee chenye wingi wa wabunge wa
kutosha kuunda Serikali, Rais awe na Mamlaka ya kukipa fursa ya
kwanza chama chenye idadi kubwa ya wabunge kujaribu kuunda
muungano wa vyama ili kuweza kuunda Serikali.
Rais awe na wajibu wa kila mwaka kuongoza kikao cha Mkutano Mkuu
wa magavana wa mikoa yote nchini na pia kuhutubia Baraza la Taifa
(Seneti, Bunge la Tanganyika, Bunge la Muungano na Mkutano wa
Magavana kwa pamoja).
Rais atakuwa na mamlaka ya kuthibitisha kuondolewa madarakani kwa
Waziri Mkuu kufuatia kura ya kutokuwa na imani iliyopigwa na Bunge
7/28/2019 Maoni KATIBA-Zitto
5/13
(Baraza la Wawakilishi) la nchi Mshirika au pale Waziri Mkuu
anapopoteza uwingi wa viti ndani ya Baraza.
Rais atakuwa na mamlaka, kupitia Tume ya Maadili ya Umma,
kusimamia maadili ya viongozi wa Umma.
Bunge la Tanzania
Kuwe na Bunge la Jamhuri ya Muungano lenye sehemu kuu 2, Bunge la
juu (seneti) na Bunge la chini (Bunge la Tanganyika na Bunge la
Zanzibar au twaweza kuita Mabaraza ya Wawakilishi).
Maseneta wachaguliwe kutoka kila mkoa kwa utaratibu kwamba kila
mkoa utatoa maseneta wawili, mwanamke na mwanaume. Kila Bunge la
mshirika (Baraza la Wawakilishi) litachagua wananchi 5 ambao sio
wajumbe wa Bunge hilo kuwa Maseneta. Wananchi hawa watakuwa
wawakilishi wa makundi ya kijamii kama watu wenye ulemavu, vijana
na watu wenye ujuzi maalumu. Kila mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano aliyepata zaidi ya asilimia 5 ya kura za Urais atakuwa
amechaguliwa kuwa Seneta moja kwa moja.
Bunge (Baraza la Wawakilishi) la Washirika wa Muungano
watachaguliwa kwa mujibu wa Sheria zitakazotunngwa na na watatoka
kwenye majimbo ambayo ni Halmashauri za Wilaya/Miji/Manispaa/Jiji.
7/28/2019 Maoni KATIBA-Zitto
6/13
Kila nchi washirika wataweka utaratibu wa kuhakikisha usawa wa
kijinsia kulingana na mazingira ya kijiografia ya nchi hizo isipokuwa sio
chini ya asilimia 40 ya Wawakilishi watakuwa wanawake.
Waziri Mkuu
Atakuwa Mkuu wa Serikali ya nchi mshirika wa Muungano na atakuwa
na mamlaka kamili kwa masuala yote yasiyo ya muungano.
Waziri Mkuu atatokana na chama chenye Wabunge wengi kwenye
Bunge la Nchi mshirika au kama hakuna chama chenye wabunge wengi
peke yake kuweza kuunda Serikali, basi atatoka kwenye muungano wa
vyama kwa mujibu wa makubaliano ya vyama hivyo na kuthibitishwa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano. Waziri Mkuu hatokuwa Mbunge na
Mawaziri wake hawatakuwa Wabunge isipokuwa uteuzi wao
utathibitishwa na Bunge kupitia Kamati maalumu itakayoundwa na
Bunge.
Waziri Mkuu pamoja na Serikali yake watawajibika kwa Bunge (Baraza
la Wawakilishi).
Gavana (Mkuu) wa Mkoa
Atakuwa Mkuu wa Serikali ya Mkoa mwenye mamlaka kamili juu ya
masuala yote yaliyoidhinishwa kwa mujibu wa Sheria itakayotungwa na
7/28/2019 Maoni KATIBA-Zitto
7/13
Baraza la Wawakilishi (Bunge). Mkuu wa Mkoa (Gavana) atachaguliwa
na wananchi wote wa Mkoa husika na atawajibika kwa BARAZA LA
MKOA.
Mkuu wa mkoa (gavana) atateua Kamati tendaji wa Mkoa kutokana na
Idara zitakazoundwa na Baraza la Mkoa kutokana na Sheria ndogo
zitakazotungwa.
Baraza la Mkoa
Baraza la Mkoa litaundwa na Wajumbe wote wa Baraza la
Wawakilishi/Bunge waliomo kwenye mkoa husika, maseneta wote wa
mkoa husika, Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri za Wilaya za mkoa
husika na madiwani 2, mwanamke na mwanaume, watakaochaguliwa
na Baraza la Madiwani la Halmashauri husika.
Baraza la Mkoa litakuwa na mamlaka ya kujadili na kupitisha mipango
ya maendeleo ya mkoa, kushauri na kusimamia kamati tendaji ya mkoa,
kupitisha sheria ndogo za kuendesha mkoa (by laws), kujadili na
kuidhinisha Bajeti ya Mkoa na kuthibitisha mikataba yote ambayo mkoa
unaingia. Baraza la Mkoa pia litakuwa na wajibu wa kupokea na kujadili
na kutoa maelekezo kuhusu taarifa za utendaji za Halmashauri za
Wilaya ndani ya mkoa husika.
7/28/2019 Maoni KATIBA-Zitto
8/13
Mambo ya Muungano
Rasimu ya Katiba imeainisha masuala saba ya muungano. Hata hivyo
masuala haya hayatoi nguvu ya kikatiba kwa Jamhuri ya Muungano
kubakia moja na imara. Masuala kadhaa hayana budi kuongezwa.
Usimamizi wa Hifadhi ya jamii (social security) ni suala linahusu uhai
wa Taifa na wananchi wake. Pia hifadhi ya jamii ni kama Deni la Taifa
(obligation of the State), kwa hiyo ni lazima liwe suala la Muungano. Kila
nchi Mshirika anaweza kuwa na Shirika lake la Hifadhi ya Jamii, lakini
usimamizi wa Sekta ni vema ufanywe na chombo cha Muungano. Vile
vile Usimamizi wa masuala ya Bima na Mabenki kwa sababu haya ni
masuala ya sera za fedha. Monetary policy huko tunakokwenda ni
suala la monetary Union ya Afrika Mashariki, hivyo suala hili halina
budi kuwa suala la Muungano na hakuna mjadala kwenye hilo.
Usimamizi na udhibiti wa Sekta ya Nishati (Mafuta na Gesi Asilia na
masuala ya Atomiki) yanapaswa kuwa masuala ya Muungano. Kila nchi
mshirika anaweza kuwa na kampuni yake ya Taifa ya Mafuta na Gesi
lakini masuala ya usimamizi wa sekta ni vema yawe chini ya chombo
cha muungano ili kuhakikisha kuwa utajiri wa nchi unanyonywa kwa
uendelevu na pia kutoa mamlaka kwa Bunge la Muungano
7/28/2019 Maoni KATIBA-Zitto
9/13
kupitisha/kuidhinisha mikataba ya kuvuna rasilimali hizo za Mafuta na
Gesi. Ni vema pia kuwa na sera moja ya masuala ya atomiki na nyuklia
kwa Jamhuri ya Muungano.
Rasimu ya Katiba imeondoa suala la usimamizi na udhibiti wa anga
kwenye masuala ya Muungano. Nadhani ni vema kuhakikisha kuwa
avition, civil and military yanakuwa ni masuala chini ya mamlaka ya
Jamhuri ya Muungano. Kila nchi inaweza kuwa na Shirika lake la ndege
usafiri wa anga lakini masuala ya usimamizi na udhibiti wa anga
yabakie kuwa masuala ya Muungano.
Hivi sasa Tanzania nzima inatumia nambari +255 kuitambulisha katika
masuala ya mawasiliano ya simu. Rasimu ya Katiba imeondoa suala la
mawasiliano ya simu katika orodha ya masuala ya Muungano. Nadhani
ni makosa makubwa sana. Suala la usimamizi na udhibiti wa
mawasiliano linapaswa kubakia kuwa suala la Muungano na Tanzania
nzima ibakie na +255 chini ya mamlaka ya Jamhuri ya Muungano.
Rasimu itatupelekea kuwa na code nambari nyingine kwa Tanganyika,
nyingine kwa Zanzibar!
Masuala ya biashara ya kimataifa na forodha ni masuala yanayoratibiwa
na Jumuiya ya Afrika Mashariki na hivyo haikuwa sawa kuyaondoa
kwenye masuala ya Muungano. Kwa mfano, hivi sasa Bunge la Tanzania
7/28/2019 Maoni KATIBA-Zitto
10/13
au la Uganda au la Burundi hayana mamlaka kabisa kwenye masuala ya
forodha maana Bunge la Afrika Mashariki ndio lenye mamlaka hayo na
hutunga Sheri ya forodha (Customs Management Act, 2004). Afrika
Mashariki ipo kwenye Umoja wa Forodha na kuelekea Soko la Pamoja,
hivyo kuondoa forodha na biashara ya kimataifa kwenye masuala ya
Muungano ni kutoona mbali.
Kama tunataka kujenga Taifa lenye uwiano sawia kielemu ni vema
kuoanisha sera za Elimu ya juu angalau. Napendekeza kuwa Elimu ya
Juu iwe suala la muungano. Kila nchi washirika inaweza kuwa na vyuo
vikuu vyake lakini ni muhimu kuwa na Chuo Kikuu cha Taifa chini ya
Serikali ya Muungano. Mikoa inaweza kuanzisha vyuo vikuu vyake
isipokuwa SERA ya Elimu ya Juu iwe jambo la Muungano. Usimamizi wa
vyo vya ufundi unaweze kuwa chini ya mikoa. Serikali za nchi washirika
wanaweza kuwa na sera ya jumla ya elimu na mafunzo ya ufundi.
Mapato
Rasimu ya Katiba imependekeza kuwa ushuru wa forodha na mapato
kutoka Mashirika ya Muungano ndiwe fedha za muungano. Ninaamini
kabisa kwamba Tume ya Katiba haikupata ushauri mzuri kuhusu suala
hili. Kwa uzoefu wangu kama Waziri Kivuli wa Fedha, vyanzo hivyo
7/28/2019 Maoni KATIBA-Zitto
11/13
havitoshi kuendesha DOLA. Dola inapasa kuwa na rasilimali za kutosha
na ziada inaweza kugawa kwa washirika na mikoa katika wajibu wa
kuhakikisha maendeleo yanawiana. Dola pia inaweza kuwa na miradi ya
Muungano. Vile vile, hayo Mashirika ambayo Tume inasema ni yepi
maana muungano umependekezewa masuala saba tu. Kuna haja ya
kuangalia kwa umakini mkubwa suala hili kama kweli kuna nia ya dhati
ya kuendelea kuwa na Muungano.
Mapato ya Muungano
1. Ushuru wa Forodha2. Mrahaba wa uvunaji wa Rasilimali ambapo 25% itabaki kwenye
mkoa wenye rasilimali na 75% itatumika na Serikali ya Muungano
kugawa kwenye mikoa kwa mujibu wa formulae
itakayokubaliwa kwa kuzingatia idadi ya watu, kiwango cha
umasikini na ukubwa wa kijiografia.
3. Ushuru wa Bidhaa ambapo 60% itagawiwa kwa nchi washirikakwa ajili ya miradi maalumu.
4. Mapato kutoka kwenye kampuni za kibiashara za Serikali yaMuungano na gawio la Benki Kuu ya Tanzania.
7/28/2019 Maoni KATIBA-Zitto
12/13
Mapato ya Washirika
1. Kodi ya Mapato ya watu binafsi na Makampuni2.
Kodi ya Ongezeko la Thamani au kodi kama hiyo
3. Tozo mbalimbali zitakazotungwa kwa mujibu wa sharia4. Mapato yasiyo ya kikodi kutoka idara na Wizara za Serikali.
Mapato ya Mikoa
1. 25% ya Mrahaba kutokana na uvunaji wa Rasilimali/maliasiliinayopatikana katika mkoa husika
2. 10% ya makusanyo ya kodi ya mapato ya watu binafsi namakampuni kutoka katika mkoa husika
3. Mgawo kutoka Serikali ya Muungano4. Mgawo kutoka Serikali ya Washirika5. Tozo mbalimbali zitakazoanzishwa kwa mujibu wa sharia ndogo
ndogo.
Deni la Taifa
Napendekeza kuwa Deni la Taifa lisimamiwe kikamilifu na Jamhuri ya
Muungano. Akaunti ya Deni la Taifa iwe chini ya hazina ya Jamhuri ya
Muungano, Jamhuri ya muungano itakopa kwa niaba ya Washirika wa
7/28/2019 Maoni KATIBA-Zitto
13/13
muungano baada ya mikopo hiyo kuthibitishwa na Baraza la
wawakilishi (Bunge ) la nchi mshirika na Seneti. Jamhuri ya Muungano
pia itadhamini mikopo ya ndani na ya nje ya Mikoa na Halmashuri za
Wilaya.