49

Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

  • Upload
    others

  • View
    0

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab
Page 2: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

MASHAIRI YA MASAIBU YA

KERBALA

Kimetolewa na:

AHLUL BAYT (A.S) ASSEMBLY OF TANZANIAS.L.P 75215

DAR ES SALAAM

Page 3: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

Haki ya kunakili imehifadhiwa na:Ahlul Bayt (A.S.) Assembly of TanzaniaP.O. Box 75215, Dar es Salaam, Tanzania

ISBN 9987 633 03 X

Chapa ya Kwanza 1998: Nakala 5,000Chapa ya Pili 2009: Nakala 500

Kimechapwa na:Bilal Muslim Mission of Tanzania

Page 4: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

YALIYOMO

Dibaji . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 1

NAUHA - MATAM

1. Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 22. Yaa Husain . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 93. Allahu Akbar . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .114. Yaa Abbas . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 125. Waa Husainan . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .136. Yaa Lailatal Ashri Tuul . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .147. Ya Shahida Karbala . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .158. Mzuri sana Husaina . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 16

UTENZI

9. Husain Akafahamu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 1710. Ya Husaini Bin Ali . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 1911. Ya Aliy ya Aliy ya Abal-Huseina . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 2312. Machozi yamiminika . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 2413. Hussein Amefariki . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 2614. Kwa Mwezi wa Muharram . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 2715. Husseini Mwana wa Ali . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 2816. Sifa za Imam Hassan na Imam Husain (a.s.) . . . . . . . . . . . . . . . . . 3717. Mtoto wake Husseini . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 3818. Ya Sayyidna Huseini . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 40

Page 5: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.) ASEMA:

1. Ee Allah! Hawa (Ali, Fatima, Hassan na Husain) ndio Ahlul-Bait wangu, basi watoharishe kwa tohari kamili.

2. Husain anatokana na mimi na mimi ninatokana na Husain...

3. Hao (Hassan na Husain) ni maua yangu katika dunia.

4. Ewe Mwanangu (Husain)! Mwili wako ni mwili wangu na damu yako ni damu yangu;

5. (Ewe Husain), wewe u Sayyid, mwana wa Sayyid, na ndugu wa Sayyid; wewe u uthibitisho (wa Mwenyezi Mungu), mwana wa uthibitisho (wa Mwenyezi Mungu) na ndugu wa uthibitisho (wa Mwenyezi Mungu); na baba wa uthibitisho tisa ambao wa tisa wao ni Qaim wao ambaye atakuwa al-Mahdi.

6. Hassan na Husain ni Masayidi wa Vijana wa Peponi.

7. Ewe Mola wangu! Mpende yule ampedae Husain.

8. Adhabu atakayoipewa yule mwuaji wa Husain huko Motoni itakuwa sawa na nusu (nzima) ya adhabu yote watakayoipewa wenye dhambi waulimwengu.

9. ...... Allah hujirafikisha na wale wajirafikishao na Husain na yu adui wa wale walio maadui zake.

10. Yeyote awapendaye Hassan na Husein amenipenda, na yeyote anayewachukia amenichukia.

Page 6: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

1

DIBAJI

Ahlul Bayt (A.S.) Assembly ya Tanzania (ABATA), inayo furaha kwa kutoa Kitabu hiki cha Mashairi kwa watu wazungumzao Kiswahili. Ilikuwa mapendekezo ya Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi, Mwenyekiti wa ABATA, kwamba tuchapishe vitabu vya Majlis na Mashairi (Nauha na Utenzi) juu ya “Masaibu ya Karbala.” Kwa hiyo mwezi Aprili, 1998 tulichapisha Kitabu cha Majlis kinachoitwa, “Maombolezo ya Kifo cha Imam Husain (a.s.)” ambacho kimetokea kupendwa sana Afrika ya Mashariki. Alhamdulillah.

Sayyid Murtaza Rizvi na Sheikh Abdul-Majid Nassor, kwa ushauri wa Mwenyekiti wa ABATA, wameyakusanya Mashairi haya kutoka sehemu mbalimbali, wakayapanga na kupata kitabu kiitwacho “Mashairi ya Masaibu ya Karbala” ambacho unacho mkononi mwako hivi sasa.

Hiki ni Kitabu cha tatu ambacho kimetolewa na Ahlul-Bayt (A.S.) Assembly ya Tanzania; na tunayo furaha kubwa kutoa kitabu cha Mashairi va Karbala kwa Kiswahili ambacho ni cha kwanza katika lugha ya Kiswahili.

Allah Subhanahu wa Ta'ala atoe malipo yake kwa mtunzi, mfasiri na wale wote ambao wamesaidia katika kuchapisha kwake kwa njia yoyote.

Wa ma Tawfeeqi illa Billah

S.L.P. 75215 F.A. HameerDar-es-Salaam Katibu MkuuTanzania Ahlul-Bayt (A.S.) Assembly24 Februari, 1999 ya Tanzania

Page 7: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

2

SALAAM SALAAM, IMAMU SAYYIDNA HUSEIN

Limetungwa na:Maallim Abdul Qahari bin Said,

(wa Mtama, Lindi - Tanzania)

UTANGULIZI

Marehemu Maallim Abdul Qahari bin Saidi mwanachuoni mashuhuri wa Madhehebu ya Sunni (Shafii) ndiye aliyeandika shairi hili.

Kwa sauti kubwa na shangwe alilisoma shairi hili katika azimisho la Siku ya Imamu Husain (a.s.) iliyofanyika huko Mtama (Lindi, Tanzania) mnamo tarehe mosi Julai mwaka 1961.

Lilirekodiwa katika “Tape Recorder” na kusikilizwa katika miji mingi mingineyo Barani Afrika.

Vile vile liliwahi kuchapishwa mara mbili na “Imamia Mission”, ya Lucknow, India.

SHAIRI

Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

1. Bismilah nitajayo, Ni jina la Mola wangu, Rahmani isemwavyo, Ya akhera na ulimwengu, Rahimi isimuliwavyo, Akhera ya wacha Mungu, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

2. Alhamdu ni sifa za Mola, Lillahi jina Ia Hadhiya, Namwalia Rasula, Salaam na neema pia, Waalaalihi liula, Zienee kwa wote pia, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

Page 8: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

3

3. Baada ya kumaliza, Sasa natunga shairi, Naanza kujituliza, Nitaje kisa na maamuri, Kidogo nitatambaza, Si sababu ya kujitafakhari, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

4. Ilahi kamtuma Rasuli, Muhammadi Liamini, Awe mtetezi kamili, Aidhihirishe dini, Nae kakubali, Kuwa kiongozi wa dini, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

5. Kisa ninacho eleza, Maendeleo yaamini, Agizo alitimiza, Aliyemtuma Manani, Hakuna la kumtatiza, Mwislamu moyoni, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

6. Wakati wa maisha yake, Muhamedi Rasuli, Alimzaa mtoto mke, Fatumati Libatuli, Kamuoza binamiyake, Imamu Sayyidna Ali, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

7. Mola mjuwa falagha, Alli akamzaa Husein Mwenyezi Mungu Kawapanga, Wajukuu zake amini, Dunia ikawa na mwanga, Wakafurahi Malaika mbinguni, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

8. Siku nyingi zikapita, Mustafa akatawafu, Ndipo kuanza matata, Shamu mambo machafu, Nakuzitangaza vita, Kuazimu ushupavu, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

9. Dini ikatimiya, Kwa vitendo vya Yazidi, Amani zikapotea, Maasi yakazidi, Kidogo wafuatao njia, Ya Nabii Muhamadi, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

Page 9: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

4

10. Ikawa nyakati hizo, Zikapunguka imani, Ikakithiri michezo, Amani ya Shaitwani, Wachache wafuatao nguzo, Nakuthibiti imani, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

11. Na hali hapo zamani, Nabii alitamka, Ya Husein minni, Waana ilaika, Ndipo kasimama Husein, Naamri akazishika, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

12. Haki ikasimama, Na batili zikaondoka, Mpaka siku ya Kiyama, Dini zitabadilika, Fahimma hata Fahhama, Uislamu utatajika, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

13. Na kifo chake kwa kamili, Ni fidia ya UisIamu, Mfano wa Ismaili, Kwa Nabii Ibrahima, Dini leo ni kamili, Imesimama salama, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

14. lmamu alipo sikia, Ilivyo badilika Shamu, Aamuruvyo bini Muawiya, Mambo mengi yaharamu, Na dini imepotea, Anadai na Uimamu, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

15. Imamu moyo ukasita, Akifikiri tarafa, Yazidu anazo zipita Bila ya amali nadhifu, Akasema hai hata, Ila nende zangu Kufa, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

16. Tarekhe ishirini na Nane, Akaondoka Madina, Kwenda kulitufu Kaaba, Shariya iliyo bayana, Yazidi Kakutubu kitaba, Kujisainisha laana, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

Page 10: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

5

17. Barua ya kutoka Shamu, Ikafika mjini Makka, Karifiwa hakimu, Husein muuwe haraka, Husein alipofahamu, Ikambidi kuondoka, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

18. Imamu Husein hashirafu, Baada hayo kufahamu, Akasema Makka ni tukufu, Kutiya damu haramu, Hicho ni kitendo dhaifu, Kakataza Rabi Karimu, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

19. Ikawa tarehe pili, Ya mwezi wa mfunguo nane, Karbala akawasili, Kiasi cha saa nane, Majeshi ya wakatili, Yakazuia maji wasione, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

20. Mpaka tarehe saba, Mtoni kuna hatari, Maadui wameziba, Na maneno ya jeuri, Maji na heri kunywa simba, Na nguruwe na makafiri, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

21. Islamu Kataharaki, Kooni kulikauka, Kila akiwalahiki, Maji yao kuwa taka, Wao kuzidi hamaki, Huruma imewatoka, Salaam Salaam, Imamu Savyidna Husein.

22. Mama mtoto taabani, Maziwa yamekauka, Hamna tone kifuani, Mtoto anahangaika, Kayabisika midomoni, Damu zina mdondoka, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

23. Wamezuiya hayo maji, Watu elfu tano, Wengi mno walindaji, Wa mishale bila mifano, Ingawaje anawahitaji, Wala hawana mapatano, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

Page 11: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

6

24. Ikafika siku tatu, Tangu waponyimwa maji Wameshikana hao watu, Kwa hali ya uziwiyaji, Wakaona hiyana si kitu, Wana nia ya uuwaji, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

25. Tarehe tisa ilipofika, Walitaka waanze vita, Imamu Husein aliwataka, Ruhusa ya kuswali wakapata, Amuabudu Rabuka, Bila kumfika matata, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

26. Mkuu wa jeshi la Yazidi, Ana moyo mughaladha, Omar bini Saadi, Ameajiriwa kwa fedha, Akisha timiza ahadi, Hataki kwa Mungu Karadha, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

27. Asubuhi tarehe kumi, Vita ikaumuka, Ndipo kuanza uvumi, Mishale kuipachika, Omari mtaka dami, Mshale ukamtoka, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

28. Ndiye mwamrishaji, Vita kuamrisha, Hakuna tena mkaaji, Muda wao umekwisha, Hakuna tena kuhoji hoji, Kawamalizeni maisha, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

29. Ikawa hekaheka, Hali ya vita ni kali, Islamu kateseka, Maji yamewawiya mbali, Yamradi wana mashaka, Hawanywi wala hawali, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

30. Alipofika mkatili, Mlaanifu mwingi wa balaa, Na kisu chake kikali, Yuna kwitwa Shimer, Imamu aliomba aswali, Hakupenda amalize swala, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

Page 12: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

7

31. Alipotaka amuuwe, Alitamka Imamu, Ebu nikuchungue, Nikujue mjirimu, Amuene uso wa Nguruwe, Mara alimfahamu, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

32. Aliambiwa zamani, Uhai wa babu yake, Ataye muuwa Husein, Atabadilika sura yake, Awe mnyama wa mwituni, Nguruwe kwa jina lake, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

33. Ikaja nyingi tufani, Ikatokea kusini, Jua likazama mbinguni, Kukawa giza azimu, Ikashuka mvua mbinguni, Maji mekundu ya damu Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

34. Wakati walipo mchinja, Adui walifurahi, Mwili waliuacha, Ili upondwe na ngamia, Na mtoto wakamchinja, Bila ya kumhurumia, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

35. Wanawake wakachojoa, Shungi zao za kichwani, Kipita akiwasumbua, Wakatembezwa uriani, Kwa ukatili wa kuuwa, Ataulipiza Manani, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

36. Kile kichwa ikabidi, Kama si kichwa cha mtu, Kikapelekwa kwa Yazidi, Akakanyage kwa Fimbo, Fikara za mkaidi, Si kama fikara za utu, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

37. Yazidi aliona vema, Hajui ameangamia, Ndani ya Jahanama, Ndiko aliko ingia, Na maji yaja hima, Ndiyo anaumiya, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

Page 13: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

8

38. Hapa ninahitimu, Shairi nimekomesha, Ingawaje nina hamu, Yakutaka kuzidisha, Rabbi unirehemu, Kwa haya yangu maisha, Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

39. Na kila msikiaji, Mwenye roho ya mahaba, Rabi mwondolee balaji, Mpokelee kila toba Yarabi utufariji, Kwa baraka ya Habiba Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

MUIENUDDIN CHISHTI AJMERI ASEMA:

Shah ast Husain Badshah ast HusainDin ast Husain Din Panah ast Husain

Sar dad, Na dad dar daste YazidHaqqa ke Binae Iailah ast Husain.

Maana yaka:

Husain ni Mfalme (ni Bwana) Husain ni Mfalme wa Wafalme (ni Bwana wa Mabwana)

Husain ni Dini Husain ndiye mhifadhi wa Dini.kichwa alikitoa, bali hakutoa mkono kuuwake juu ya mkono

wa Yazid.Hakika Husain ndiye msingi wa La ilaha illallah.

Page 14: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

9

YAA HUSAIN

1. Yaa Husain, yaa Husain kullu yawmin Aashura Kullu ardhin Karbalaa yaa abal Ahraar x 2

2. Yaa Salilul ambiyaa, anta Imamul atqiyaa Yaa abal ahraar x 2

3. Yaa Kahfil mustajirrin, yaa shariul mudhini biin Yaa abal ahraar x 2

4. Yaa ilma fikulli waad, yaa imama filjihadi Yaa abal ahraar x 2

5. Laa ilaha illa llah, yawmi twaffi-laa nansaa x 2 Yaa abal ahraar x 2

6. Yaa sar khata thairin, Haihata annastakini x 2 Yaa abal ahraar x 2

7. Ya kahfa wal muutamad, amta zaadi wa sanaad x 2 Yaa abal ahraar x 2

8. Salmali man salamakum, Harbali man haraba kum x 2 Yaa abal ahraar x 2

9. Aaala rabbul kainati, fajrana hatma liat x 2 Yaa abal ahraar x 2

10. Yaa min haja filhayat, yaa qudwata bil abat x 2 Yaa abal ahraar x 2

Page 15: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

10

11. Yaa man jismuhu saliib, yaaman shaibu hu khatib x 2 Yaa abal ahraar x 2

12. Yaa madhlumu yaa dhaman, abkaitalinsi wal jani x 2 Yaa abal ahraar x 2

13. Yaa mantabkiika ssamaa, yaa sayyida shuhadaa x 2 Yaa abal ahraar x 2

14. Yaa safinatu nnjaat, antamuhyii fil mamat x 2 Yaa abal ahraar x 2

15. Yaa imamal muttaqin, farrat bil haqil mubini x 2 Yaa abal ahraar x 2

16. Nahjuka nahjurrasuul, saatwiu yahdil anam x 2 Yaa abal ahraar x 2

17. Amta baaki lantazul, Haadiu Nahju rrasuli x 2 Yaa abal ahraar x 2

Page 16: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

11

ALLAHU AKBAR

1. Allahu Akbar Allah yaa Husain ya Hussein Allahu Akbar Allah yaa Husain ya Hussein

2. Aliyu yandubu wayakulu yaa Husain ya Husain x 2

3. Alhassani yandubu wayakulu yaa Husain ya Husain x 2

4. Rasulu yandubu wayakulu yaa Husain ya Husain x 2

5. Azzahra tandubu watakulu yaa Husain ya Husain x 2

6. Fatima tandubu watakulu yaa Husain ya Husain x 2

7. Sakina tandubu yaa Husain ya Husain x 2

8. Jibrilu yandubu wayakulu yaa Husain yaa Husain x 2

9. Al-ardhu Yandubu wayakulu yaa Husain yaa Husain x 2

10. Assamaa tandubu watakulu yaa Husain yaa Husain x 2

Page 17: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

12

YAA ABBAS

1. Yaa Abbas yaa Abbas Ya madhulum fii Karbalaa x 2

2. Yaa Madhulumaa fii Karbalaa Yaa man mata wahuwa atshan Ya madhulum fii Karbalaa x 2

3. Bakati Sakina ladaa Karbalaa Wa Muhammadahu banatuka-sabaya Yaa madhulum fii Karbalaa x 2

4. Bakati ssamaa’u liqatilil-Husain Wa sibtwahu ladaa Karbalaa Yaa madhulum fii Karbala x 2

5. Yaa madhulum fii Karbalaa Wa nazifaahu fii Karbalaa Yaa madhulum fii Karbalaa x 2

6. Raasuhu Husain fawqaa rrimahi Sibtu Nnabiyyi muqattalaa Yaa madhulum fii Karbalaa x 2

7. Sibtu Rrasuli muqqattalaa Waa sibtwahu fii Karbalaa Yaa madhulum fii Karbalaa x 2

Page 18: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

13

WAA HUSAINAN

1. Waa Husainan waa Husainan waa Husainaa x 2 Waa Husainan Swaha Jibriilu Hazinaa

2. Ya srakhul kawnu bukaa’an wa aninaa

3. Qad Qadha ssibtu ghariban fii tufuur Wahdahu haafat bihi tilka sufuuf Min rimahin au nibalin au siyuuf Thumma dhulman Qatwau minhul watiina

4. Waidha bii ssibtwi fii twaffi gharib Jismuhu saa haati fii harbi saliib Maahu rahtul ubati swabirinaa

5. Masaqawhul-maa’fii Yawmil-fajii’li Huwa dham aanin yunadi sama uuh Maata atshanan walam yusqal mainaa

6. Innahum Lam yarhamu hataa rradhii Wa Husseinu ssibtwi kassaddil-manii Nah’wu qawmil ghadri maa maddal yamiinaa

7. Maata alul wahyi walkhatbijaliil Ma baqaa minhum siwaa shakhu su alii Wanhisaauu thakila tuu fil-awiil Qad faqadnal ahla dhulman mal baninaa

Page 19: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

14

YAA LAILATAL ASHRI TUUL

1. Yaa Lailatal-ashri tuul Qad zaada Fiiki nnuhuul Wadidtu min Qibali kuumi Yaa hunu waq rrahiil

2. Bikar balaa mudh-nazalnaa Alimtu inda nnuzuul Biannana sawfa nabqaa Bila hami wwakafiil

3. Wadhaaka aadhamu thatwabi Min zamani jaliil Yumsil Hussein Qatiilaa Wa Yaalahu mun katiil

4. Fayaa dumuiya siilii Alayhi kulla masiil Thumma nthanat bintu twaha Bi-Ibrati wa awiil

5. Tukhatibu-llayla laakim Khitwabuha an dhuhuul Taqulu la tubdi subhaa Wadha minal mustahiil

Page 20: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

15

YA SHAHIDA KARBALA

1. Tunasikitika sana kwa kifo chako Husain Ewe Husain ya shahida Karbala x 2

2. Mal-uni alofika kukuua ya Husain Na Mungu atayaweka makazi yake motoni Ewe Husain ya shahida Karbala x 2

3. Mbingu zilitikisika kwa kifo chako Husain Majabali kupasuka kwa khofu na kwa huzuni Ewe Husain ya shahida Karbala x 2

4. Upanga uliushika ili kutetea dini Kuchezewa yetu dini Husain hukuridhika Ewe Husain ya shahida Karbala x 2

5. Tarehe za tuonyesha kwa kifo chako Husain Husain umeondoka umeacha pengo kubwa Ewe Husain ya shahida Karbala x 2

6. Tunamuomba Manani amiani mal-uni Amlani hayawani Yazidi na jeshi lake Ewe Husain ya shahida Karbala x 2

Page 21: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

16

MZURI SANA HUSAINA

Mzuri sana Husaina Wallahi na kuapiaGiza ilitueneya hapo ulipouliwa

1. Ee mwema mwana amani, umekufa kishahidi Kunusuru hasa dini, ya wetu Mola wadudi

2. Umejitolea muhanga, ewe mwana wa Hashima Ili kuhifadhi mwanga, Nuru kubwa ya Karima

3. Kila lote la azizi, kwa Rabuna umetoa Bila kujali ajizi, hadi kufa kuokoa

4. Wanao wenye tohara, Nduguzo waso kifani Masahaba we imara, umetoa uwanjani

5. Kunusuru haki kweli, mfano wako kuiga Ujabali wenye dhili, kupambana bila woga

6. Kuishi na madhalimu, kamwe neema hapana Ni kudhili jahanamu, maisha hayana maana

Kiit

ikio

ALLAMAH SAYYID SAEED AKHTAR RIZVI ASEMA:

Imam Hassan na Imam Husain (a.s.) wameuhurisha Uislamu kutokana na utumwa wa Wafalme na hivyo basi, wameuhifadhi kutokana na uharibifu daima. Wafalme watakuja, na Wafalme watakwenda, lakini Uislamu utadumu milele. Kwa Uislamu, majina matakatifu ya Hassan na Husain yataangaza milele.

Page 22: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

17

HUSAIN AKAFAHAMU

Husein akafahamu Ikawa hakuna budiMauti yake metimu Dhiki imeshawazidiNa kweli yake damu Wazee kwa auladiAdul watachezea Roho zikiteketea

Adui pasi kuchoka Kiu ilo kubwa mnoWaka mwandama mpaka Joto lisilo kifanoKarbala wakafika Vijana wazi midomoKusudi wa mwandamia Maji wanahitajia

Furati wakaushika maji wanywayo wanyamaPasi nafasi kutoka punda, farasi na kimaMto wakauzunguka Mjukuu wa HashimaNa maji wakijinywea Adui wakazuja

Kiu ikazidi sana Dhiki ilipo wazidiNa joto likawabana Akamuona waladiImamu na wakewana Asifanye ukaidiDhiki ikiwazidia Adui akawendea

Kile kijana swaghiri Kijana kikalalamaImam wetu Amiri Chembe kimeshika nyamaTamaa hakuikata Na damu mwili mzimaYa maji kumpatia Mikononi akafia

Adui wasikubali Mikononi mwa ImamuJapo lau tone mbili Yote ikajaa damuMuhali wakaratili Na roho yake ghulamuPasi Imani kuingia Ikaiaga dunia

Page 23: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

18

Alipo akikariri Ukazidi ukaidiImamu akihubiri Na jeshi la mafisadiAlipata takiswiri Ikawa hapana budiChembe wakamrushia Roho zikiangamia

Waliondoka huruma Basi huu ndio mwanzoWakawa kama wanyama Wakazidisha mkazoPasi kujali dhuluma Pasiwe hata pumbazoRoho zikiteketea Vitoto vikiumia

IMAM HUSAIN (A.S.) ASEMA:

Imam Husain (a.s.) alipokuwa safarinikwenda Karbala alisema:

“Kama Dini ya (Mtume) Muhammad (sa.w.w.)haiwezi kuendelea ila kwa kukitoa

mhanga kichwa changu, basi upangana uje ukichukue.”

Page 24: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

19

YA HUSAINI BIN ALI

1. Kwa jina lako Jalali nasema yenye ukweli Ya Husaini Bin Ali niwe nikihadithia

2. Mama yake ni Fatima, na babu yake Hashima Na Madina mji mwema, ndiko aliko zaliwa

3. Na Sayyidi na Husain, kaka yake ni Hasan Akiwapenda amini, kisha akiwa sifia

4. Mtume amebaini, ya kama huyu Husaini Na mwingine ni Hasani, Peponi wataingia

5. Yaani wao ni mabwana, wa peponi vijana Subhana maulana, wote amewaridhia

6. Ni mwezi wa Shabani, alozaliwa Husain Na siku yake yakini, ni jumanne sikia

7. Mwaka wa nne Hijira, Ndio kazawa mbora Na siku ya saba mara, kamwakikiya Nabia

8. Mtume kamwadhinia, sikioni la kulia Kinywa kamsugulia, kwa mate alafunua

9. Alikuwa ni mzuri, wa umbo la kunawili Sura kama ya Bashiri, kwani kamshabihia

10. Akipigania dini, kwa udhati moyoni Hajali nini na nini, ila dini ya jalia

11. Husaini akiwa Makka, aliupata waraka Kuwa aende haraka, Iraqi kum-baiya

Page 25: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

20

12. Watu wangu simameni, Twende Iraqi mjini Aliwambia Husseini, Nao wakafuatia

13. Husseini aliambiwa, Huko acha kuendea Twakusihi kusikia, Huko hapatakufaa

14. Abdallah wa Abasi, Kasema kinga nafusi Zao japo wafuasi, Japo na watoto pia

15. Wende wewe peke yako, Sio na ahali zako Bwana kwa hisani yako, Shika ninayo kwambia

16. Bwana Husseini kasema, Kwenda huko ni lazima Litalonipata nijema, Mimi nimesafi nia

17. Nikenda wakiniuwa, Peponi nitaingia Kwani nimesafi nia, Dini kuisimamia

18. Liwalo lote na liwe, Iraqi ni paendewe Sio mimi niofie Niache kupaendea

19. Hapo Seyyidi Husseini, Katoka Makka mjini Na watu wake sabini, Wote wakamfatia

20. Wenye farasi yakini, Walikuwa thalathini Wengine arubaini, Kwa miguu ilikuwa

21. Alipokuwa njiani, Wakazidi yakini Mia moja khamsini, Ndio waliozidiya

22. Hao miya khamsini, Walirudia njiani Hawakumfata Husain, Hadi Iraqi sikiya

23. Husseini na watu wake, Ni Iraqi Wapafike Na taabu iwafike, Kwa humo Karbala

Page 26: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

21

24. Mto ulio karibu, Nae Husseini Muhubi Alizuiwa ajabu, Na maadui kutumia

25. Maji wakazuiliwa, Wasiwe wayatumia Kambi akajipigia, Bwana Husseini sikia

26. Akawa maji anyimwa, Huku kiu Chawauma Watoto wanalalama, Kwa vile wanaumia

27. Husseini na watu wake, Ati wao wateseka Na maji yasitumike, Kunywewa na watu hawa

28. Hapo Husseini hakika, Vikali aliteseka Watoto walalamika, Baba! Baba! twaumia

29. Jeshi hilo lilikuwa, Kabisa lamzuia Husseini kukaribia, Maji yale kutumia

30. Watoto waliumia, Kwa kiu kuwazidia Kati yao alikuwa, Mtoto mdogo pia

31. Mtoto huyu ni Ali, Alizidiwa kikweli Zeinabu binti Ali, Sanasana alilia

32. Machozi yalimtoka, Mengi yakatiririka Akayafonza hakika, Mtoto kujimezeya

33. Zeinabu binti Ali, Ni shangazi lake Ali Kwa ala kulihali, Machozi maji yakawa

34. Hata ile siku ya ashura, Kwa mwezi kumi dhahira Muharamu ndio mara, Wakaanza kuuwawa

35. Kwanza wafuasi wake, Kisha wa nyumbani kwake Alibaki ye na chake, Kijitoto kikilia

36. Umri miezi sita, Hivyo hanavyo matata Hivyo maji angepata, Yangali msaidia

Page 27: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

22

37. Mtoto mchanga yule, Wakampiga mishale Na mtoto pale pale, Aliiaga dunia

38. Kisha wakamzunguka, Husseini mwenye baraka Wakamuuwa hakika, Nae kaaga dunia

39. Baada ya kumuuwa, Hema moto walitia Hata wakawachukua, Banati zake Nabiya

40. Wakawafanya mateka, Kisha wakawapeleka Huko Kufa kupafika, Bila kuwahurumia

41. Ni kwa Ibni Ziyadi, Ndiko iliko wabidi Gavana wake Yazidi, Yeye ndie alikiuwa

42. Hivyo watu wa Iraqi, Walikataa haki Kumuuwa mwenye haki, Kipenzi chake Nabia

43. Kuuwawa kwa Husseini, Ni jambo lenye huzuni Katu haiwezekani, Machozi kuyazuia

44. Machozi shuti kutoka, Na watu kuhuzunika Kwa kipenzi msifika, Kinyume alofanyiwa

45. Ewe Seyyidi Husseini, Ulotoka duniani Kwa kupigania dini, Peponi wenda ingia

46. Umekufa ni shahidi, Hivyo ni kama zawadi Allahu Mola wadudi, Shahidi kakwandikia

47. Waswalatu wa Salamu, Zimfikie Hashimu Na Husseini Muadhamu, Na walio bakiya

Na: Saidi MusaZANZIBAR

Page 28: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

23

YA ALIY YA ALIY YA ABAL-HUSEINA

1. Vikali mmeteswa Na pepo mtaingia Na waliowatesa motoni wataingia

2. Aliy Bunal Hussaini kauwawa Karbala Mishale pia vyuma vyote kuwa juuye

3. Aliomba ruhusa kwenda kupigania Akapigwa mshale na Ibn Fadhili Kichwani mwake huyo Aliy Ibunil Husaini

4. Ashahidul Abasi kauwawa vibaya Mikono ilikatwa yote miwili pia

5. Imam wetu Husein Kauwawa Karbala Mikuki na mishale vyote kuwa juuye

6. Kadhulumiwa Husaini huo mji Karbala Humo usoni mwake mawe alirushiwa

7. Vitoto vililalama midomo ilikauka Maji wahitajia adui wamezuiwia

8. Midomo ilipasuka damu pia zilitoka Akina mama pia maziwa hayakutoka

9. Imamu wetu Husaini alichinjwa kinyama Na hao maluuni Fii ardhi Karbala

10. Ya Aliy ya Aliy ya Abal-Huseina Kutilal-Husaina Fii ardhi Karbala Fii ardhi Karbala Kutilal-Hussaina

Page 29: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

24

MACHOZI YAMIMINIKA

1. Kwa Jina la Rahmani Na Anza nudhumuhini

Na Muhammad AminiKwa Machungu na Kuliya

2. Siku hizi za Ashura Kwa kubwa mno hasara

Twazitaja kila maraMaadui walotiya

3. Kiswache cha tuumiza Hatuwezi kunyamaza

Na roho kutuunguzaMashingo kuvumiliya

4. Twadhihirisha Majonzi Na nyoyo zina simanzi

Kwa Imamu na kipenziKwa haya yalotokea

5. Twakumbuka siku hini Ya kuuwawa Huseini

Ya vilio na huzuniMjukuu wa Nabiya

6. Wallahi Tunakatika Mitilizi inashuka

Machozi ya miminikaHatuna budi kuliya

7. Huseini kudhulumiwa Kanyimwa maji kupewa

Kwa machungu kuuliwaYeye na wake dhuriya

8. Hata watoto wachanga Kwa mishale kuwadunga

Wasibali kuwanyongaNa maji kuwazuwiya

9. Wakamchinja Huseini Mjukuu wa Amini

Bila kite na imaniPasina kuzingatiya

10. Na kicha kukitundika Kwa mizozo na dhihaka

Kwa shangwe wakizungukaKwa kipenzi cha Nabiya

Page 30: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

25

11. Tuliye kiliyo gani Kwa kiongozi wa dini

Tudhihirishe ImaniHuyu walo tuuliya

12. Walomuuwa Imamu Hao ndio madhalimu

Wakashika yake damuTarikhi inatwambiya

13. Bila shaka yupeponi Owe nao makhaini

Yeye na tumwa AminiHuseini kutuuliya

14. Kula alo muumini Kwa kifo chake Huseini

Atajawa na huzuniKipenzi cha Hashimiya

15. Na mengi tukiyaeleza Ya akili kushangaza

Maovu ya kuchukizaNa moyo kutosheya

16. Tumefika kikomoni Atupe nyingi Imani

Tushukuru MananiYa dini kusimamiya

17. Muliyoko Hadhirani Rabi atiye auni

Amina kikieniDini kuipiganiya

Umetungwa na:

Sheikh Ahmed Sheikh NabhanyP.O. Box 86876

Mombasa, Kenya

Page 31: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

26

HUSSEIN AMEFARIKI

1. Hakika ni ujahili Kuuwa pasi kujali

Uovu na ukatiliBila ya kuzingatia

2. Asikiyae Hakika Ma machozi yatatoka

Moyo utasikitikaBila yakufikiria

3. Kwa huyu mtoto wake Muda kiu imshike

Hussein kina chakeMaji akihitajia

4. Kufika kwa makafiri Na mwana huyu saghiri

Hussein alopojiriMaji alimuombea

5. Maadui wasijibu Mmoja wao kajibu

Kwa kuwazidi ghadhabuMshale kuutumia

6. Jibu lake ni mshale Akafia pale pale

Kumfunma mwana yuleKifo cha kukusudia

7. Hapo ndipo Hussein Akaingia vitani

Kwa uchungu wamoyoniBila tena kungojea

8. Hussein akapigana Akauwa wengi sana

Kishujaa kukazanaKwa nguvu zake jalia

9. Naye mwisho kifo chake Akafa hali yu pweke

Afanyeje peke yakeShahidi akajifia

10. Hussein amefariki Na hao ni yao dhiki

Hali yukatika hakiWalomtenda ubaya

Page 32: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

27

KWA MWEZI WA MUHARRAMNaanziliza kauliNa Swalawati Rasul

Kwa Jina Lake JalaliNa-ali zake pamoja

Mswiba ulo adhimuDhuriya zake Hashimu

Kwa mwezi wa MuharramuKarbala wakingiya

Hadithi imetuwambiyaWapendwa wake dhuriya

Rasuli ameuswiyaKinyume wakatumiya

Umati walibadiliIkawa ni kuwadhili

Mahabba yao kwa AliNa maji kuwaziwiya

Yasitoshe walofanyaDhuluma wakamuonya

Ya Mtume kuyakanyaVijana kumuuliya

Hawakujali hishimaVijana waliye wema

Ya Sayyidati FatimaWa Haidari Aliya

Sina budi nitaliaIwe kwetu mazoweya

Kukosa kuwateteaAshura ikingiliya

Hadithi walisahauWakawauwa na kiu

Mapenzi wakadharauFurati wakangaliya

Walikunwa KauthariPamoja na Answari

Maji mema ya fakhariDini waloitetea

Yalopita tayakidhiNa kwa Mungu ni fawidhi

Kwa Tumwa nipate radhiNa Aya kiisomeya

INNA LILLAHI WA INNA ILAIHI RAJEUN

Sharif Mohammed Ahmed Al-HuseiniJomvu Station, Mombasa

Page 33: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

28

HUSSEINI MWANA WA ALI

Naanziliza kwajinaMola asiye kijana

Lake yeye SubhanaWala mke asiliye

Ndie watangu natanguMuumba nchi na mbingu

Kabula ya ulimwenguMilele Atabakiya

Asie na mshirikaAmeketi pasi shaka

Na wala hakuzalikaEnzie imetimiya

Sasa penda kuwelezaNa moyo nitaukaza

Kisa kenye kuchukizaHadi mwisho kufikiya

Ni rafiki wa RasuliHusseini mwana wa Ali

Muhammadi mur saliNa Fatuma Hashimiya

Kipenzi chake NabiyaUhai wake sikia

Kuliko viumbe piyaHusseini akimwambiya

Wewe mtu wa peponiApendae kubaini

Huna shaka asilaniNamtizame Husseini

Baada kufa RasuliNa Alii mjamali

Muda ulipotawiliAlipoaga duniya

Kukazidi wasiwasiPasiwe mwenye nafasi

Ulimwengu ukahisiMatumbo kupiganiya

Baada yote kufikaWaso haya wakatoka

Na damu zikimwaikaVita wakaandaliya

Vikaandaliwa vitaUmbea nausalata

Na mengi mno matataVigaro vikatimiya

Page 34: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

29

Vigaro vya mahasidiChini ya yeye Yazidi

Nyoyo zenye ufisadiVitani wakaingia

Husseini yuko ndianiKuwapinga mashetani

Kutaka ihami diniNakuituza duniya

Kwa moyo uso imaniNa damu waitamani

Majeshi yakawa kaniYa Husseni na dhuriya

Wakawa wajikatakataNaimamu washamwita

Watakayo washapataMjini kwao kungiya

Habari hiyo hanayoKumbe mambo sasa siyo

Amekaza wake moyoMauti yamngojea

Yunjiani enda zakeWaume na wanawake

Akaweta watu wakeNa radhi akawiliya

Kuwajuza kwa yakiniPasipo matumaini

Hila zote kwa makiniIraqi kufikiliya

Kawambiya kimbieniEla mini niwacheni

Atakae samahaniNimuhali kukimbiya

Baada yeye kukuliKama vile mafahali

Wengi hawakuhimiliNyumbani wakarudia

Akabakiya HusseiniNa baadhi ikhiwani

Na dhuriya wa nyumbaniAkali wakasaliya

Alipofika IraqiFuraha na kujinaki

Jamii ya halaikiJeshi likamwingilia

Akawa hana namnaPamwe na wake vijana

Pande zote amebanwaWapi watakimbiliya

Page 35: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

30

Akasema kwa lafudhiAdui kuwapa radhi

Ka fasaha na mahadhiKuwatajia Jalia

Akawaonya mifanoBarua zilizo nono

Hati zao za mkonoWalizo kumwandikia

Kayesha yote manenoYote yasiwe ni neno

Wala pasipo usonoYao wakashikilia

Wakamuonya adhabuZimewaingia ghadhabu

Na nyingi mno sulubuBila sababu ya njia

Adui pasi kuchokaKarbala wakafika

Wakamwandama M-makaKusudi wa mwandamiya

Furati wakaushikaMto wakauzunguka

Pasi nafasi kutokaNa maji wakijinyweya

Kiu ikazidi sanaImamu na wake wana

Najoto likawabanaDhiki ikawadhidiya

Ikawa hakuna budiWazee kwa auladi

Dhiki imeshawazidiRoho zikiteketea

Kiu ilo kubwa mnoVijana wazi midomo

Joto lisilo kifaniMaji wanahitajiya

Maji wanywayo wanyuaMjukuu wa Hashima

Punda farasi na kimaAdui akawendeya

Akenda kwao salamaAbdallah anawana

Karibu roho kutemaKwa kiu kumzidiya

Kile kijana swaghiriTamaa hakukasiri

Imamu wetu AmiriYa mali kumpatiya

Page 36: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

31

Adui wasikubaliMahali wakaratili

Japo lau tone mbiliPasi imani kuingiya

Mipo akikaririAlipata takisiri

Imamu akihubiriChembe wakamrushiya

Wakamba ha ndiyo majiMnyweshe yamfereji

Katu huyaonji majiNi leo mtatubiya

Kijana kikalalamaNa damu mwili nzima

Chembe limeshika nyamaMikononi kikafiya

Mikononi mwa ImamuNa roho yake ghulamu

Yote ikajaa damuIkaiaga duniya

Katu wakamba aduiMtayaona jamii

Maji yetu situmaiKanwani hamtotiya

Ukazidi ukaidiIkawa hapana budi

Kwa jeshi la mafisadiRoho zikiteketeya

Basi huu ndiyo mwanzoPasiwe hata pumbazo

Wakazidisha mikazoVitoto vikiumiya

Kajaribu kwa upoleMaji yote yako tele

Kuwaeleza walo paleJapo tone kutumiya

Akenda huko karibuAlipotaka jaribu

Kiu ilimughilibuChembe kikamuingiya

Kikamwingia ImamuMdomoni kikadumu

Chembe chao mahasimuNa damu ikamweneya

Huku kiu imemshikaMsiba umemfika

Damu ikichirizikaHana pakukimbiliya

Page 37: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

32

Kakishika kakizuwaKamshukuru Moliwa

Kwa nguvu akakitowaMuumba wa waja piya

Zikazidishwa sulubuRafikize wakaghibi

Mno na nyingi taabuMauti kuyandamiya

Rafiki wakaangukaNa damu zikimwaika

Imamu kumzungukaAkawa aogeleya

Katikati kwenye damuKatu yako hayatimu

Adui wakakalimuMauti yakungojea

Mauti yenye taabuYatakufika karibu

Usumbufu na adhabuKaa ukiliadhania

Ni leo, leo ni leoNa wote hao watu

Utaiona kwa leoWote tutawalemeya

Kakalimu muungwanaNa Molawe kalingana

Kamshukuru RabanaNa dua kujiombeya

Akatamka HusseiniKwako wewe shukrani

Kamwambia Mola mananiNyoyo zimefurahiya

Hatuna katu huzuniMauti twayatamani

Kwa ulio yasainiKuliko kuangukia

Vita vikauma sanaNa Imamu akawana

Pasipo kusemeyanaPasi nyuma kurejeya

Lakini ifae niniNa ziyada ilondani

Kwa adui elfeniHusseini akalegeya

Akalegeya kwa dhikiAsimpate rafiki

Aloikuta hilakiHuruma kumuonea

Page 38: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

33

Ukweli ulodhihiriHaikuweko ni siri

Ikakabili ni shariShida zikawachachiya

Kutamka kwa upoleSahibuze kuwambile

Pasipo nyingi keleleAtakaye kukiribiya

Usiku huo gizaniNamimi radhi moyoni

Kawambia kimbiyaniNa dua nawaombea

Jamii wakakataaKuliko kuyakimbia

Heri kwao kujifiaMauti wakaridhiya

Adui likadhihiriNa upesi ikaswiri

Moyo umetahayariImamu kumjiliya

Mtoto wake HusseiniKaruka pasi makini

Naye alipobainiAmie kumteteya

Pasi khofu wala shakaNa maneno katamka

Adui akamshikaMsihaya kamwambiya

Kamwambiya huna hayaUtaikuta hizaya

Bure wayatenda hayaMbele ya Mola jaliya

Adui likazungukaHusseini akimtaka

Mtoto akamshikaKijana kumuusiya

Huku mepiga pambajaNa huku akiwapiga

Na adui huko wajaMpaka mwisho kufikiya

Yakamzidi machunguAkaaga Ulimwengu

Akamsabihi MunguMjukuu wa Nabiya

Ghafula akijiliwaAdui lake Moliwa

Roho yake ikatwawaImamu akamwendeya

Page 39: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

34

Akamwendeya kwa dhatiJiadui afiriti

Akamendesha mautiDharuba kumwemezeya

Alipokufa HusseiniNa tatu yaliyo ndani

Yalitimu thelathiniMafumu yalowingiya

Kuna tena thethiniPanga za hao wahuni

Na nne mwake mwiliniMwilini zimesaliya

Mbali mengi majarahaMoyo hauna furaha

Kuyataja ni karahaKwa Imamu kujifiya

Ndio huo mwisho wakeCha Imamu tusichoke

Hiki ndicho kisa chakeMilele kujisomeya

Walipokwisha sainiSasa hii ni yakini

Adui wakabainiUshindi umewajiya

Wakendewa majohariMatekani wakaswiri

Mabanati wa AmiriHuku wakiwachezeya

Pasi haya za usoKuwatia taabani

Wakaona ni kifaniJamaa zake Nabiya

Wakazidisha jeuriNa kichwa chake Amiri

Wala pasipo na siriFumoni wakakitiya

Huku wakikichezeyaPasi imani kuwaingia

Na huku wakiimbiyaWote wamefurahiya

Njiani walikipitaZimekwisha jaa vita

Nyoyo zao mezipataShetwani amewaingia

Alipopata habariYazidi akaamuri

Kwa ambayo yamejiriIli kwehwa kumwiliya

Page 40: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

35

Furahani vibarakaKwa Yazidi kikafika

Haraka kukipelekaMeyowe kufurahiya

Akawa kukitozeyaHuku akimbiliya

Na vijiti kukitiyaChini kukiumbiriya

Msihaya wake diniUchunguwe wa moyoni

Yazidi akatamaniUtatowa kwa duniya

Na huku akikigotaUovu na usalata

Meno akiyaambataHakuna alodhaniya

Ajabu hii ajabuKumfikiya ikabu

Kwa kijanache swahibuWala pasipo hatiya

Muili ukiwa mbaliWakawachiwa mahuli

Kijana cha MurisaliNa nyama kukitezeya

Basi haya ni mautiLakini kwao laiti

Walotenda asheratiMilele wamejutiya

Walitenda pasi hayaYa Mola kuyachezeya

Dini kutotegemeyaPasi nyuma kurejeya

Yapasa tuyalilieIslamu natulie

Mauti yake HusseiniKwa kifo chake Husseini

Hapa napenda kukomaBali mengi sikusema

Hadithie kuisomaDhiki nikiisikiya

Kisomoni waungwanaMpate jua maana

Majumbani na vijanaMambo yaliyo tukiya

Yatupasa IsilamuKumliliya Imamu

Machozi hadi ya damuKwetu imetupasiya

Page 41: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

36

Rabi atamtukuzaKuzidi akimjaza

Peponi kum-bakizaNeema kumshushiya

Hapa naweka kalamuWala mbele siyo tamu

Nimefikiya makamuHapa nitakomeleya

YAPASA TUYALILIE MAUTI YAKE HUSSEIN

Na: Masoud Abdallali Muh’d,Mombasa - Kenya

IMAM SHAFII ASEMA:

1. Hussein! aliuliwa shidi pasi na makosa yoyote na kanzu yake ikatapakazwa wekundu.

2. Ikiwa dhambi zangu ni kuwapenda watoto wa Mtume Mohammad (s.a.w.) basi ni dhambi ambazo sitatubiya.

3. Kwa sababu ya Ahlil-Beit wa Mtume (s.a.w.) Ulimwengu mzima ulitetema na majabali na milima ilikaribia kuyeyuka.

4. Ni nani atakayemfikishia Hussein ujumbe wangu na hata kama nyoyo zatukia?

Page 42: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

37

SIFA ZA IMAM HASSAN NA IMAM HUSAIN (A.S.)

Nawapa na taarifa Walikuwa wana sifa

Japo kuwa walikufaNjema ilotimilia

Walikuwa watukufuWalo na njema sharafu

Tena ni waaminifuAlowajazi Jalia

Walikuwa MaimamuMashujaa walotimu

Kuongoza IsilamuDini kuipigania

Walikuwa watu wemaAkiwapenda Hashima

Vijana wenye heshimaWajukuu wa Nabiya

Walikuwa wenye diniNa nyingi mno imani

Maovu hawathaminiNyoyoni ilowangia

Walikuwa na hurumaToka kwa watu wazima

Isilamu wenye himaNa vijana wote pia

Walikuwa wasifikaTena waliyoumbia

Duniani kutukukaKwa uzuri na tabia

Walikuwa makarimuKisha ni wenye ilimu

Huwezi kuwalaumuYa dini na ya dunia

Walikuwa wafalumeMashujaa wenye tume

Wajukuu wa MtumeVitani kushambulia

Sifa zao ni kathiriWala hazina akhiri

Tena zote ni nzuriWallahi zimezidia

Page 43: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

38

MTOTO WAKE HUSSEINI

Jambo jengine ni hili Hiki si kisa cha piliNi cha kijana rijali

La majonzi ikhiwaniAmbacho ni cha huzuniMtoto wake Husseini

Kadhulumiwa Husseini Na wake mwana mchanga

Naye kafa madhulumuMuovu huyo KhasimuBure kaimwaga damu

Kijana wa mikononiAdui aso imaniYa kijana maskini

Kadhulumiwa Husseini Na wake mwana mchanga

Kifo chake ni dhulumaAdui aso hurumaKwa mshale kamfuma

Kijana huyu yakiniAso Imani moyoniUkamwingia mwilini

Kadhulumiwa Husseini Na wake mwana mchanga

Mshale ulimdungaIkawa hapana kingaAkafa mwana mchanga

Mtoto wake HusseiniYa kuiyepuka zaniKiumbe cha Rahamani

Kadhulumiwa Husseini Na wake mwana mchanga

Ovu liso wezekanaKiumbe chake rabanaWalimu-uwa kijana

Kupata chake kifaniKilo safi cha peponiBila kosa asilani

Kadhulumiwa Husseini Na wake mwana mchanga

Page 44: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

39

Huyo ni wake uweleAlomdunga mshaleNaye piya vile vile

Alo mughuri shetaniKipenzi chake aminiAtaingia motoni

Kadhulumiwa Husseini Na wake mwana mchanga

Kwa kumuuwa kijanaHata akatubu sanaAdhabu yake ragana

Malaika kwa yakiniHaipati samahaniKwake haiwezekani

Kadhulumiwa Husseini Na wake mwana mchanga

IMAM HUSAIN (A.S.) ASEMA:

“Kufa kwa heshima ni bora kuliko kuishi kwa aibu”.

Page 45: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

40

YA SAYYIDNA HUSEINI

Kukuomba sina budi Ili utimu mradi

Ya razaku ya wadudiYote nalo kusudia

Sikutaka kusimamaNi mambo kunisukuma

Mengi mno kuyasemaNi lazima kuelezea

Natokeza hadharaniYalomfika Husseini

Kwa ufupi nibainiYa Rabbi niafikia

Yale ni mambo adhimuSina shaka mwafahamu

Yalomfika ImamuNami tawahadithia

Ule mwaka wa sitiniKaondoka duniani

Wahijira sikianiMuawiya kajifiya

Yazidi alitangazaDini ataiongoza

Nchi zote kaenezaIli watu kumbaiya

Barua aliandikaKwa walioikafika

Madina kaipelekaNae akimwelezea

Kwa makini isomeniKahitaji kura zenu

Mfahamu yalo ndaniIsilamu wote pia

Nazidi kuyabainiNi kura yake Husseini

Yalio mwangu moyoniUfike kumwelezea

Husseini kastakimuHuyo ni mtu dhwalimu

Akasema yakatimuKidini hakutimiya

Kama mimi ni haramuSitaki wake msemu

Kukubali ya dhwalimuMwambiye sitoridhia

Page 46: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

41

Kwanza yeye nakiburiKajaa kila fujuri

Ni mlevi hana siriNyote mnamtambua

Sitokuwa chini yakeTaji hilo silo lake

Hapa na pale afikeHata yeye yamwelea

Mtume alibainiNi Maimamu yakini

Kwa Hassani na HusseiniKila mtu kasikia

Alifu kumi na mbiliKwa mjukue Rasuli

Barua ziliwasiliIraq Zilitokea

Barua ZilimtakaUkhalifa kuushika

Husseini huko kufikaDini kuisimamia

Yazidi si mtu mwemaNa haya tunayosema

Sisi sote twafahamiaWewe twakushtakia

Husseini hakutwawiliIli kujua ukweli

Katuma Ibn AkiliWa mambo yalomfikiya

Alipokewa vizuriWalimfanya safiri

Wadogo hatakibariWa Husseini Msifiwa

Kisha mambo ligeukaMapanga wakayashika

Balozi walimwepukaMuslimu kumuwa

Mwezi nane kutimiaHusseini kashika njia

Mfungo tatu sikiaIraqi kaelekea

Naswaha zilimfikaIraqi usije fika

Twakuomba kutotokaWatu wakakukimbia

Husseini aliwambiyaNitakwenda nadhuria

Hayo yote nasikiaMtume kani uswiya

Page 47: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

42

Wakiniuwa sijaliKua hayo majangili

Aliniambiya RasuliDhulima watatumia

Alipofika njianiNi hayuko duniani

Ilimaka yakiniMuslim kauwawa

Iraq waligeukaHivi waja kukushika

Unafiki wakashikaHusseini aliambiwa

Ule msiba adhimuYeye na wake kaumu

Ulomfika ImamuNakizaziche pamoja

Hapa ni pahali ganiNi Karbala jangwani

Niambiyeni jamaniHuseini aliambiwa

Ibn Saad OmariMaudhi na ujeuri

Najeshile waliswiriImamu wamfanyia

Unyama walifanyiwaNa maji kuzuiliwa

Na kiu iliwauwaHayo yote watendewa

Kauwawa AkbariNa hao watu mashari

Pia hata AsghariMungu yuwashuhudia

Asghari ni kijanaNa kiu ilimbana

Ni mdogo tena sanaKwa chembe walimuua

Husseini aliuuiizaKosa gani tulifanza

Fikirini mukiwazaKutendewa kama haya

Himambo yenye huzuniNashindwa kuyabaini

Alotendewa HusseiniUkumbuni ngatokea

Yangu haki mumetwaaNa leo mwanisumbua

Ya ukhalifa sisawaNilipi mwafikiria

Page 48: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

43

Au hamkusikiaHapo akiwauswia

Usemi wahashimiaKuhusu wake dhuria

Mama yangu ni BatuliNa baba yangu ni Ali

Binti yake RasuliWaswii wake Nabia

Ya Husseini walimwagaWalijifanya wajinga

Damu yake bila wogaUfasiki mewashika

Kijukuu cha RasuliAchinjwa kama ghazali

Ni Husseini bin AliWallahi twakulilia

Alipewa kila dhuliAteswa na majangili

Mwanao ewe BatuliWaso dini sikiya

Walisahau ahadiNa wote ni mashahidi

Ya Mtume MuhammadiMtume akiwauswia

Alimchinja HusseiniNa Mungu si Athumani

Bila khofu na huzuniNae atamlipia

Ni kifo chenye kutishaWallahi chahuzunisha

Tena kina babaishaKila kinapo tolewa

Na Mungu si AthmaniWa kesho wenda motoni

Twalipa dunianiAdhabu yawangojea

Hapo ndipo nitafikaKwa huzuni lonishika

Kalamu chini nawekaSiwezi kuendelea

Mola atupe ImaniTuwe nae na peponi

Yakumpenda HusseiniDua zetu zipokea

Kisha Swala na SalamuNa alize Mainwnu

Zende hadi kwa HashimuHasidi angachukia

Page 49: Mashairi ya Masaibu ya Karbala - Shia Maktab

ISBN 9987 633 03 X

kimetolewa naAHLUL-BAYT (A.S.) ASSEMBLY OF TANZANIA

S.L.P. 75215DAR ES SALAAM

TANZANIA