24
WAZALENDO SACCOS LTD Namba ya Kuandikishwa. 2065 S.L.P 474, MOSHI Barua Pepe: [email protected] MASHARTI YA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA NA MIKOPO WAZALENDO (WAZALENDO SAVINGS AND CREDIT COOPERATIVE SOCIETY LTD) Agosti, 2013

MASHARTI YA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA …...cha chini cha umiliki wa hisa ni kama ilivyoainishwa katika sera ya Hisa, Akiba na Amana. (g) Mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa

  • Upload
    others

  • View
    36

  • Download
    2

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: MASHARTI YA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA …...cha chini cha umiliki wa hisa ni kama ilivyoainishwa katika sera ya Hisa, Akiba na Amana. (g) Mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa

WAZALENDO SACCOS LTD

Namba ya Kuandikishwa. 2065

S.L.P 474,

MOSHI

Barua Pepe: [email protected]

MASHARTI YA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA NA MIKOPO

WAZALENDO (WAZALENDO SAVINGS AND CREDIT COOPERATIVE

SOCIETY LTD)

Agosti, 2013

Page 2: MASHARTI YA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA …...cha chini cha umiliki wa hisa ni kama ilivyoainishwa katika sera ya Hisa, Akiba na Amana. (g) Mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa

ii

Yaliyomo

Ukurasa

Yaliyomo .................................................................................................................................................... ii

Utangulizi .................................................................................................................................................. 1

SEHEMU YA KWANZA ......................................................................................................................... 1

1 TAFSIRI ............................................................................................................................................ 1

1.1 Akiba .............................................................................................................................................. 1

1.2 Amana ............................................................................................................................................ 1

1.3 Bodi ................................................................................................................................................ 1

1.4 Chama ............................................................................................................................................ 1

1.5 Huduma za kifedha ........................................................................................................................ 1

1.6 Kamati ya Usimamizi ..................................................................................................................... 1

1.7 Kanuni za Sheria ya Ushirika ........................................................................................................ 1

1.8 Masharti ......................................................................................................................................... 1

1.9 Mikopo ............................................................................................................................................ 1

1.10 Mkutano Mkuu .............................................................................................................................. 2

1.11 Mwanachama ................................................................................................................................. 2

1.12 Sera ................................................................................................................................................. 2

1.13 Sheria ya Ushirika ......................................................................................................................... 2

1.14 Watumishi ...................................................................................................................................... 2

SEHEMU YA PILI ................................................................................................................................... 2

2 JINA NA MAELEZO MUHIMU YA CHAMA ............................................................................. 2

2.2 Dira ya Chama ................................................................................................................................ 3

2.3 Maarubu/Mwelekeo ....................................................................................................................... 3

SEHEMU YA TATU ................................................................................................................................ 3

3 MADHUMUNI .................................................................................................................................. 3

Page 3: MASHARTI YA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA …...cha chini cha umiliki wa hisa ni kama ilivyoainishwa katika sera ya Hisa, Akiba na Amana. (g) Mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa

iii

3.1 Madhumuni Mahususi ................................................................................................................... 3

3.2 Shughuli za Chama ........................................................................................................................ 3

SEHEMU YA NNE ................................................................................................................................... 4

4 UANACHAMA ................................................................................................................................. 4

4.1 Sifa za Mwanachama ..................................................................................................................... 4

4.2 Kujiunga Uanachama .................................................................................................................... 4

4.3 Kusimamishwa au Kuachishwa Uanachama ................................................................................ 5

4.4 Ukomo wa Uanachama .................................................................................................................. 5

4.5 Wajibu na Haki ya Mwanachama ................................................................................................. 5

4.5.1 Wajibu wa Mwanachama ........................................................................................................... 6

Ufuatazo utakuwa wajibu wa mwanachama ............................................................................................... 6

4.5.2 Haki za Mwanachama ............................................................................................................... 6

SEHEMU YA TANO ................................................................................................................................ 7

5 HISA ZA WANACHAMA ............................................................................................................... 7

SEHEMU YA SITA .................................................................................................................................. 7

6 MTAJI WA CHAMA ....................................................................................................................... 7

SEHEMU YA SABA ................................................................................................................................. 7

7 FEDHA NA MALI ZA CHAMA ..................................................................................................... 7

SEHEMU YA NANE ................................................................................................................................ 8

8 DHIMA YA MWANACHAMA ....................................................................................................... 8

SEHEMU YA TISA .................................................................................................................................. 8

9 UONGOZI NA USIMAMIZI WA CHAMA ................................................................................... 8

9.1 Vyombo vya Maamuzi .................................................................................................................... 8

9.1.1 Mkutano Mkuu wa Mwaka ........................................................................................................ 9

9.1.2 Mkutano Mkuu wa Kawaida ...................................................................................................... 9

Page 4: MASHARTI YA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA …...cha chini cha umiliki wa hisa ni kama ilivyoainishwa katika sera ya Hisa, Akiba na Amana. (g) Mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa

iv

9.1.3 Mkutano Mkuu Maalum .......................................................................................................... 10

9.2 Taratibu za Kuitisha Mkutano Mkuu .......................................................................................... 10

9.3 Bodi ya Uongozi ........................................................................................................................... 11

9.3.1 Sifa za Wajumbe wa Bodi ........................................................................................................ 11

9.3.2 Majukumu ya Bodi ................................................................................................................... 12

9.3.3 Majukumu ya Mwenyekiti wa Bodi ......................................................................................... 13

9.3.4 Majukumu ya Makamu Mwenyekiti wa Bodi .......................................................................... 13

9.3.5 Mikutano ya Bodi ..................................................................................................................... 13

9.3.6 Kuacha au Kusimamishwa ujumbe wa Bodi ........................................................................... 13

9.4 Kamati ya Usimamizi ................................................................................................................... 14

9.4.1 Sifa za Wajumbe wa Kamati ya Usimamizi ............................................................................. 14

9.4.2 Majukumu ya Kamati ya Usimamizi ........................................................................................ 14

9.4.3 Kamati ya Mikopo .................................................................................................................... 14

9.4.5 Majukumu ya Wajumbe wa Kamati ya Mikopo ...................................................................... 15

9.5 Wajumbe wa Uwakilishi............................................................................................................... 15

9.5.1 Majukumu ya Mwakilishi wa Bodi .......................................................................................... 15

9.5.2 Majukumu ya Mwakilishi wa Wanachama ............................................................................. 15

9.6 Menejimenti/Meneja .................................................................................................................... 16

9.6.1 Kazi za Meneja zitakuwa ni; .................................................................................................... 16

SEHEMU YA KUMI .............................................................................................................................. 16

10 TARATIBU ZA UWEKAJI WA HISA, AKIBA, AMANA NA UTOAJI MIKOPO ............. 16

SEHEMU YA KUMI NA MOJA ........................................................................................................... 16

11 MGAO WA ZIADA .................................................................................................................... 16

SEHEMU YA KUMI NA MBILI .......................................................................................................... 17

12 UHASIBU .................................................................................................................................... 17

Page 5: MASHARTI YA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA …...cha chini cha umiliki wa hisa ni kama ilivyoainishwa katika sera ya Hisa, Akiba na Amana. (g) Mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa

v

SEHEMU YA KUMI NA TATU ........................................................................................................... 17

13 KUHIFADHI AKIBA NA FEDHA NYINGINE ZA CHAMA ................................................ 17

SEHEMU YA KUMI NA NNE .............................................................................................................. 17

14 MAHUSIANO NA ASASI ZINGINE ZA KIFEDHA NA MITANDAO ................................ 17

SEHEMU YA KUMI NA TANO ........................................................................................................... 18

15 KUFUTWA KWA CHAMA ...................................................................................................... 18

SEHEMU YA KUMI NA SITA ............................................................................................................. 18

16 MENGINEYO ............................................................................................................................. 18

Page 6: MASHARTI YA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA …...cha chini cha umiliki wa hisa ni kama ilivyoainishwa katika sera ya Hisa, Akiba na Amana. (g) Mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa

1

Utangulizi

Mamlaka ya Kutengeneza Masharti ya Chama

Masharti haya yametengenezwa na wanachama wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo

Wazalendo (Wazalendo SACCOS Ltd) kwa mamlaka ya kisheria chini ya kifungu cha 45 cha

Sheria ya Vyama vya Ushirika ya mwaka 2003 na Kanuni namba 9 ya Kanuni za Vyama vya

Ushirika ya mwaka 2004.

SEHEMU YA KWANZA

1 TAFSIRI

1.1 Akiba

Kiasi cha fedha ambacho mwanachama atakitumia kama kigezo cha kukopa.

1.2 Amana

Kiasi cha fedha za aina ya akiba ya mlaji ambayo hakitumiki kukopeshea bali ni kama akaunti ya

akiba benki ambapo wakati wowote mwanachama ataweka na kuchukua fedha kiasi chochote.

1.3 Bodi

Chombo kilichopewa dhamana ya uongozi na Mkutano Mkuu wa wanachama kusimamia, kwa

niaba ya Wanachama shughuli zote za uendeshaji na utoaji huduma za kifedha kwa Wanachama.

1.4 Chama

Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Wazalendo (Wazalendo Savings and Credit

Coooperative Society Ltd) ambao ni muungano wa hiari wa watumishi wa Chuo Kikuu Kishiriki

cha Ushirika na Biashara (MUCCoBS) wenye nia ya kusaidiana na kuweza kutatua matatizo ya

kijamii na kiuchumi.

1.5 Huduma za kifedha

Huduma za kifedha za Akiba, Amana, Hisa, Mikopo na majanga.

1.6 Kamati ya Usimamizi

Chombo kilichopewa dhamana na Mkutano Mkuu, ya kukagua shughuli zote za uendeshaji wa

Chama na kutoa ushauri katika Mkutano Mkuu.

1.7 Kanuni za Sheria ya Ushirika

Kanuni za Vyama vya Ushirika za mwaka 2004.

1.8 Masharti

Kanuni na misingi inayoongoza mahusiano baina ya Chama , Wanachama, na Wadau wengine

kwenye sekta ya Ushirika na sekta ya Fedha kulingana na maelekezo ya Sheria ya Vyama vya

Ushirika Namba 20 ya mwaka 2003 pamoja na Kanuni za Vyama vya Ushirika za mwaka 2004.

1.9 Mikopo

Kiwango cha fedha ambacho mwanachama anachoweza kupata kutokana na akiba alizonazo kwa

kuzingatia sera ya mikopo na Kanuni za Ushirika.

Page 7: MASHARTI YA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA …...cha chini cha umiliki wa hisa ni kama ilivyoainishwa katika sera ya Hisa, Akiba na Amana. (g) Mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa

2

1.10 Mkutano Mkuu

Chombo cha juu chenye dhamana ya kufanya maamuzi yote yahusuyo shughuli za utoaji

huduma za kifedha za Chama.

1.11 Mwanachama

Mtu yeyote anayemiliki Hisa katika Chama na mwenye dhamana ya kutoa maamuzi ya namna

bora ya kuendesha Chama.

1.12 Sera

Kanuni ndogondogo zinazotumika kufanikisha utekelezaji wa miongozo kama ilivyoanishwa

kwenye Masharti.

1.13 Sheria ya Ushirika

Sheria ya Vyama vya Ushirika ya mwaka 2003.

1.14 Watumishi

Watu walioajiriwa na Chama kwa mujibu wa sera ya utumishi ya Chama.

SEHEMU YA PILI

2 JINA NA MAELEZO MUHIMU YA CHAMA

(a) Jina la Chama ni: CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA NA MIKOPO

WAZALENDO [WAZALENDO SACCOS LIMITED]

(b) Anwani ya Chama ni: S. L. P. 474, Barabara ya Sokoine, Moshi, Kilimanjaro Tanzania.

(c) Mfunganamo wa Uanachama ni Utumishi katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na

Biashara Moshi (MUCCoBS)

(d) Eneo la shughuli za Chama litakuwa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara

Moshi na Vituo vyake vilivyoko Mikoani. Makao Makuu ya Chama yatakuwa Chuo

Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara, Barabara ya Sokoine, Moshi, Kilimanjaro.

(e) Mwaka wa Fedha wa Chama utaanza JANUARI na kuishia DESEMBA yaani utaanzia

01/01 na kuishia 31/12 ya kila mwaka.

(f) Tarehe ya kuandikishwa: 22 Septemba, 1971 kwa Hati namba 2065.

(h) Shughuli Kuu za Chama ni kutoa Huduma za kifedha kwa wanachama ambazo ni:

(i) Huduma za Kifedha za Akiba na Amana

(ii) Huduma za Kifedha za Mikopo

(iii)Huduma za Kifedha za Bima ya Mikopo na Majanga

Page 8: MASHARTI YA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA …...cha chini cha umiliki wa hisa ni kama ilivyoainishwa katika sera ya Hisa, Akiba na Amana. (g) Mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa

3

2.2 Dira ya Chama

Wazalendo SACCOS Ltd kuwa Asasi ya kifedha inayoendeshwa kwa njia shirikishi yenye

biashara pana na mfiko kwa wanachama kwa kuzingatia falsafa, kanuni na maadili ya Ushirika.

2.3 Maarubu/Mwelekeo

i. Kutumia fursa zilizopo kupanua vyanzo vya huduma za kifedha na kuhamasisha

wanachama kuweka hisa na akiba ili ziweze kujenga mtaji wa uhakika wa kuwahudumia

wanachama.

ii. Kuwahudumia wanachama kikamilifu na kwa uwazi na kukidhi mahitaji yao kwa wakati.

iii. Kujenga uhusiano bora miongoni mwa wanachama ndani ya Asasi na wanachama wa

vyama vingine vya Ushirika wa Akiba na Mikopo.

iv. Kuwa na uongozi bora na utawala mzuri wa fedha ili kujenga imani kwa wanachama.

v. Kujenga uwezo wa chama wa kifedha ili kumudu mahitaji ya kifedha kwa wanachama bila

kuwa tegemezi.

SEHEMU YA TATU

3 MADHUMUNI

3.1 Madhumuni Mahususi

Madhumuni mahususi ya Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Wazalendo ni;

(a) Kuinua na kuimarisha hali ya kiuchumi na kijamii ya wanachama kwa kufuata Sheria,

Kanuni, Sera, na Taratibu za Vyama vya Ushirika.

(b) Kutafuta vyanzo vya fedha ili kujenga na kuimarisha Mtaji wa Chama kwa ajili ya kutoa

mikopo kwa Wanachama kwa masharti na riba nafuu.

3.2 Shughuli za Chama

Kufikia na kufanikisha madhumuni yake, Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Wazalendo

kitafanya yafuatayo:-

(i) Kupokea na kuzihifadhi kwa usalama Hisa, Akiba na Amana kutoka kwa Wanachama.

(ii) Kuhamasisha wanachama kujenga tabia ya kujiwekea Akiba na Amana mara kwa mara.

(iii)Kuwapa Wanachama Elimu ya Ushirika itakayowajasirisha ili kuwajengea uwezo na

kuwawezesha kujenga tabia ya kukopa kwa busara, kutumia na kutunza vizuri fedha kwa

ajili ya kuinua hali zao za maisha ya kijamii na kiuchumi.

(iv) Kuwashauri Wanachama kuaandaa mipango yao ya maendeleo katika kuwekeza mitaji

kwenye miradi ya kiuchumi na huduma za kijamii.

(v) Kutafuta vyanzo vya fedha vya nje vyenye riba nafuu kwa kulinganisha na benki na isiwe

juu ya riba inayotozwa na Chama ili kuweza kumudu mahitaji ya mikopo ya wanachama

endapo vyanzo vya ndani ( makusanyo ya Hisa na Akiba kutoka kwa wanachama)

havitoshelezi kumudu mahitaji ya mikopo ya wanachama kwa wakati.

(vi) Kuanzisha huduma za kifedha za majanga zenye kuwawezesha wanachama kukabiliana

na majanga mbalimbali ya kijamii kwa njia shirikishi.

Page 9: MASHARTI YA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA …...cha chini cha umiliki wa hisa ni kama ilivyoainishwa katika sera ya Hisa, Akiba na Amana. (g) Mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa

4

(vii) Kuweka usalama wa fedha za Chama na wanachama kwa kutumia huduma za bima za

fedha zinazofaa.

(viii) Kuanzisha na kuendeleza shughuli zozote za kiuchumi na kijamii kwa manufaa ya

Wanachama na Chama kama itakavyokubaliwa na Mkutano Mkuu na

kuidhinishwa na Mrajis wa Vyama vya Ushirika.

SEHEMU YA NNE

4 UANACHAMA

4.1 Sifa za Mwanachama

Mtu yeyote anaweza kuwa Mwanachama akiwa na sifa zifuatazo:

(a) Awe mtumishi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara Moshi (MUCCoBS)

au Taasisi inayofanyakazi katika eneo la Chama.

(b) Uanachama unaweza kuwa wa mtu binafsi au Taasisi zinazofanya kazi katika eneo la

Chama.

(c) Awe ametimiza umri wa miaka kumi na nane (18). Hata hivyo, mtu mwenye umri wa

miaka 15 anaweza kuwa mwanachama isipokuwa hataruhusiwa kugombea nafasi

yoyote ya uongozi au kukopa mpaka atakapotimiza umri wa miaka kumi na nane (18).

(d) Awe na akili timamu na tabia njema.

(e) Awe tayari kushiriki kikamilifu katika shughuli zote za Chama.

(f) Asiwe na shughuli binafsi za kiuchumi na kijamii zinazofanana na shughuli za Chama.

4.2 Kujiunga Uanachama

Masharti ya kujiunga na Chama ni haya yafuatavyo:-

(a) Mtu anayetaka kuwa mwanachama atajaza fomu ya maombi ya uanachama na kuiwasilisha

katika ofisi ya Chama.

(b) Ombi litajadiliwa na Bodi na kutolewa pendekezo la kukubaliwa au kukataliwa

kutegemeana na sifa zilizotajwa katika masharti haya na kwa mujibu wa Sheria ya

Ushirika, Kanuni za Ushirika. Mkutano Mkuu pia utaidhinisha wale wote

waliopendekezwa kuwa Wanachama.

(c) Mwombaji atakapokubaliwa na Bodi atatakiwa kulipa kiiingilio, Hisa na akiba. Baada ya

kupokelewa na Mkutano Mkuu atatakiwa kutia saini yake au kuweka dole gumba katika

Daftari la Wanachama, mbele ya wajumbe wawili wa Bodi na atapewa kitambulisho cha

uanachama.

(d) Mwanachama atakapojiunga na Chama atalipa Kiingilio cha shilingi elfu ishirini tu

(20,000/=), Hisa kumi (10) zenye thamani ya shilingi elfu kumi (10,000/=) kila moja.

(e) Meneja wa Chama atarudisha kiingilio na Hisa zote zilizopokelewa kutoka kwa waombaji

waliokataliwa uanachama na Mkutano Mkuu. Ada ya fomu ya maombi ya uanachama

haitarudishwa.

(f) Mwanachama aliyekamilisha kulipia Hisa zote atapewa hati ya kumiliki Hisa. Kiwango

cha chini cha umiliki wa hisa ni kama ilivyoainishwa katika sera ya Hisa, Akiba na Amana.

(g) Mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa na haki ya kulipwa hisa na faida

zozote za Chama baada ya kufariki. Mrithi yeyote hatakuwa mwanachama moja kwa moja

isipokuwa baada ya kutuma maombi na kukubaliwa na chama kulingana na Masharti haya.

Page 10: MASHARTI YA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA …...cha chini cha umiliki wa hisa ni kama ilivyoainishwa katika sera ya Hisa, Akiba na Amana. (g) Mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa

5

Mwanachama atakuwa na haki ya kubadilisha jina la mrithi. Kila uteuzi wa mrithi

utaandikwa katika daftari ya wanachama na utatiwa saini na mwanachama.

(h) Chama kitakuwa na daftari la uanachama lenye maelezo muhimu ya kila mwanachama.

4.3 Kusimamishwa au Kuachishwa Uanachama

Mwanachama anaweza kuachishwa au kusimamishwa uanachama kwa ajili ya:

(a) Kukutwa na hatia ya kosa la jinai linalohusisha kutokuwa mwaminifu au kuhukumiwa

kifungo.

(b) Kushindwa kulipa kiasi chochote cha fedha kwa Chama katika muda ulioruhusiwa pasipo

kuwa na sababu yoyote inayokubalika na wajumbe wa Bodi.

(c) Kufanya kitendo chochote ambacho Wajumbe wa Bodi na Mkutano Mkuu wataridhia

kuwa ni cha kutokuwa mwaminifu au ambacho ni kinyume na madhumuni au malengo

ya Chama.

(d) Kwa sababu nyingine yoyote iliyoainishwa katika kifungu cha 26(1) cha Kanuni za

Ushirika.

4.4 Ukomo wa Uanachama

Uanachama utakoma kutokana na sababu mojawapo kati ya hizi zifuatazo;

(a) Kifo

(b) Kichaa kilichothibitishwa na Daktari.

(c) Kuacha kuwa na Hisa kwa mujibu wa masharti haya.

(d) Kujiuzulu baada ya kutoa taarifa ya siku sitini (60) ya maandishi kwa Bodi ya Chama.

(e) Kutenda kosa lolote ambalo limetajwa katika Sheria ya Ushirika na Kanuni za Ushirika.

(f) Kufukuzwa na wanachama katika Mkutano Mkuu kwa idadi ya wanachama wasiopungua

theluthi mbili (2/3) ya waliohudhuria na kupiga kura baada ya kupewa nafasi ya kujitetea.

(g) kutoshiriki katika shughuli za Chama kwa muda wa miaka mitatu.

(h) Kuhama katika eneo la shughuli za Chama.

(i) Kuthibitika kuwa amefilisika.

Hata hivyo:

(i) Mwanachama aliyejiuzulu au kufukuzwa uanachama atalipwa haki zake zote baada ya

kuthibitika kwa haki hizo katika kipindi kisichozidi siku tisini (90) kuanzia siku ya

kukoma uanachama.

(ii) Mwanachama hatahamisha Hisa zake ila kwa chama au kwa mwanachama au kwa mtu

ambaye maombi yake ya uanachama yamekubaliwa na Bodi au kama Hisa zake

zimekuwa katika chama kwa muda usiopungua miaka mitano.

(iii)Mwanachama aliyejiuzulu/aliyefukuzwa anaweza kukubaliwa na kupokelewa tena

kujiunga na Chama baada ya kulipa madeni yote aliyokuwa anadaiwa wakati anakoma

kuwa mwanachama na kutuma maombi kwa kufuata masharti haya.

4.5 Wajibu na Haki ya Mwanachama

Mwanachama yeyote atakuwa na wajibu na haki kama ifuatavyo:

Page 11: MASHARTI YA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA …...cha chini cha umiliki wa hisa ni kama ilivyoainishwa katika sera ya Hisa, Akiba na Amana. (g) Mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa

6

4.5.1 Wajibu wa Mwanachama

Ufuatazo utakuwa wajibu wa mwanachama

(a) Kubeba dhamana ikiwa janga lolote litatokea.

(b) Kulipa madeni yake kwa wakati uliopangwa.

(c) Kulipa mkopo alioudhamini endapo mdhaminiwa/mkopaji atashindwa kulipa mkopo

wake.

(d) Kuwa na angalau kiwango cha chini cha amana na hisa kwa mujibu wa Masharti na Sera.

(e) Kuweka Hisa na Akiba mara kwa mara ili kujenga uwezo wa kimtaji wa Chama.

(f) Kushiriki kikamilifu katika shughuli za Chama na kuhudhuria mikutano yote

inayohusika.

(g) Kushiriki katika kutoa uamuzi wa mambo mbalimbali katika Mikutano Mikuu.

(h) Kufuata Sheria na Kanuni za Ushirika, Masharti na Sera za Chama na maamuzi ya

Mikutano Mikuu.

(i) Kutoa michango mbalimbali katika kuendeleza madhumuni ya Chama.

(j) Mwanachama atakuwa na wajibu mwingine wowote kama ulivyoainishwa katika Kanuni

ya 18 ya Kanuni za Ushirka.

4.5.2 Haki za Mwanachama

Zifuatazo zitakuwa haki za mwanachama.

(a) Kushiriki katika shughuli zote za Chama kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa.

(b) Kuhudhuria na kutoa maoni yake katika mikutano ya Chama.

(c) Kuchaguliwa kuwa mjumbe/kiongozi na kuchagua wajumbe/viongozi wa Chama.

(d) Kupiga kura chini ya misingi ya mtu mmoja kura moja bila kujali idadi ya hisa anazo

miliki.

(e) Kuwa na haki sawa kuhusu mali ya chama na kudhibiti ipasavyo matumizi yake.

(f) Kuweka na kutoa amana, akiba na hisa zake kwa kufuata kanuni za Chama.

(g) Kupewa kitabu cha mwanachama kinachoonyesha aina zote za huduma za kifedha

zinazotolewa na Chama.

(h) Kupatiwa mkopo kwa ajili ya kuongeza tija na maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

(i) Kupewa aina yoyote ya huduma ya kifedha ya mkopo wakati wowote kwa kuzingatia

misingi na taratibu kama zilivyoanishwa kwenye sera ya mikopo ya Chama.

(j) Kuwa mdhamini wa mkopo wa mwanachama mwingine kwa kuzingatia sera ya mikopo

(k) Kukagua masharti, mizania, mihtasari ya Mikutano Mikuu na nyaraka nyingine za

Chama wakati wowote wa saa za kazi.

(l) Kuitisha Mikutano Mikuu ya wanachama kwa mujibu wa Masharti haya na kwa

kuzingatia Sheria na Kanuni za Ushirika.

(m) Kuchagua mrithi anayemtaka.

(n) Kupewa hati ya hisa baada ya kumaliza kulipia hisa zake.

Page 12: MASHARTI YA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA …...cha chini cha umiliki wa hisa ni kama ilivyoainishwa katika sera ya Hisa, Akiba na Amana. (g) Mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa

7

(o) Kusikilizwa.

(p) Kujulishwa mambo yote yahusuyo mwenendo wa Chama.

(q) Kujua mapato na faida/hasara iliyopatikana kutokana na shughuli za Chama.

(r) Kushiriki katika kufanya marekebisho ya Masharti na Sera za Chama.

(s) Kujitoa uanachama kwa kufuata taratibu za kisheria.

(t) Kuanzisha uchunguzi wa mwenendo wa Chama.

(u) Kukata rufaa.

SEHEMU YA TANO

5 HISA ZA WANACHAMA

(a) Kila hisa moja itakuwa na thamani kama ilivyoainishwa kwenye Sera ya Hisa, Akiba

na Amana.

(b) Hakuna mwanachama atakayeruhusiwa kuwa na hisa zaidi ya moja ya tano (1/5) ya

hisa zote za Chama kwa mujibu wa Sheria ya Ushirika.

(c) Kwa mujibu wa Kanuni ya Ushirika, mwanachama anayetaka kuchukua hisa zake zote,

atatakiwa kutoa taarifa ya maandishi ya siku sitini (60).

(d) Mwanachama hataruhusiwa kuchukua wala kupunguza hisa zake hadi atakapokoma

kuwa mwanachama.

SEHEMU YA SITA

6 MTAJI WA CHAMA

Mtaji wa chama utatokana na:-

(a) Hisa za wanachama.

(b) Tengo la Ziada halisi.

(c) Akiba ya lazima na malimbikizo mengine.

(d) Akiba inayobakizwa.

(e) Michango maalum, ruzuku, na misaada.

SEHEMU YA SABA

7 FEDHA NA MALI ZA CHAMA

Fedha na Mali za Chama zitajumuisha yafuatayo:-

(a) Hisa za Uanachama.

(b) Viingilio, ruzuku na misaada.

(c) Ada ya maombi ya uanachama.

Page 13: MASHARTI YA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA …...cha chini cha umiliki wa hisa ni kama ilivyoainishwa katika sera ya Hisa, Akiba na Amana. (g) Mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa

8

(d) Riba juu ya Mikopo ya Wanachama.

(e) Ziada halisi kutokana na shughuli na miradi ya kiuchumi ya Chama.

(f) Nafuu za Kibiashara.

(g) Fedha ya Akiba ya lazima na Malimbikizo.

(h) Fedha ya huduma za Bima ya Mikopo na Majanga.

(i) Asilimia kumi ya Akiba zote kwa kila mwaka.

(j) Mikopo kutoka Mabenki na Taasisi zinazotambulika, baada ya kupata idhini ya Mkutano

Mkuu na Mrajis wa Vyama vya Ushirika. Hata hivyo, kiasi kitakachokopwa hakitazidi

nusu (1/2) ya rasilimali ya Chama.

(k) Mapato mengineyo na yasiyotarajiwa.

(l) Fedha Taslimu na Fedha Benki.

(m) Mawekezo katika Taasisi za Kibiashara.

(n) Vifaa na zana zote zinazohusiana na shughuli za chama.

(o) Majengo na mali zingine za Chama kama zilivyoanishwa kwenye mizania ya chama.

SEHEMU YA NANE

8 DHIMA YA MWANACHAMA

Dhima za chama zitakuwa kama ifuatavyo:-

(a) Dhima ya mwanachama kwa ajili ya madeni ya Chama haitazidi kiwango cha hisa

anazopaswa kulipia katika Chama.

(b) Dhima ya mwanachama aliyeacha uanachama kwa madeni ya Chama yaliyokuwepo

wakati wa kuacha uanachama itaendelea kwa muda wa miaka mitatu (3) baada ya kuacha

uanachama.

SEHEMU YA TISA

9 UONGOZI NA USIMAMIZI WA CHAMA

Mikutano Mikuu ya Wanachama

Mikutano hii itajuimuisha; Mkutano Mkuu wa Mwaka, Mkutano Mkuu wa Kawaida na Mkutano

Mkuu Maalum.

9.1 Vyombo vya Maamuzi

Chama kitakuwa na vyombo mbalimbali vya maamuzi kama ifuatavyo;

a) Mikutano Mikuu ya Wanachama

b) Bodi ya Uongozi

c) Kamati ya Usimamizi

d) Kamati ya Mikopo

e) Menejimenti

Page 14: MASHARTI YA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA …...cha chini cha umiliki wa hisa ni kama ilivyoainishwa katika sera ya Hisa, Akiba na Amana. (g) Mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa

9

Mchoro ufuatao unaonesha uhusiano wa vyombo vya maamuzi katika Chama

MKUTANO MKUU

KAMATI YA USIMAMIZI

BODI

KAMATI YA MIKOPO

MENEJA

9.1.1 Mkutano Mkuu wa Mwaka

(a) Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama utafanyika kila mwaka katika kipindi kisichozidi

miezi tisa (9) baada ya kufunga hesabu za mwaka za Chama. Hata hivyo Mkutano huu

unaweza kufanyika baada ya kipindi cha miezi tisa (9) kwa idhini ya Mrajis.

(b) Shughuli zitazofanyika katika Mkutano Mkuu wa Mwaka ni pamoja na;

(i) Kupokea na Kusoma na kuthibitisha mambo ya Mkutano Mkuu uliopita na

yatokanayo.

(ii) Kujadili Taarifa ya hesabu za mwaka na taarifa ya ukaguzi.

(iii) Kupokea na kujadili makisio ya mapato na matumizi kwa mwaka.

(iv) Kupokea na kujadili Taarifa ya Bodi na Kamati ya Usimamizi

(v) Kujadili namna ya kugawana ziada kwa kuzingatia Masharti ya Chama, Sheria

na Kanuni za Ushirika.

(vi) Kuidhinisha ununuzi au uuzaji wa mali za Chama.

(vii) Kuamua kiwango cha honoraria kwa ajili ya Wajumbe wa Bodi.

(viii) Kuidhinisha kiwango cha riba na faida juu ya akiba, hisa na amana.

(ix) Kuidhinisha idadi ya hisa na thamani ya hisa moja.

(x) Kuidhinisha Mpango Mkakati na Mpango wa Biashara wa Chama na program ya

utekelezaji.

(xi) Kujadili na kuidhinisha marekebisho katika Masharti na Sera kwa mujibu wa

Sheria ya Ushirika.

(xii) Kuzungumzia mambo mengine yanayohusu maendeleo ya Chama kwa ujumla

na kutoa maelekezo ya utekelezaji kwa Wajumbe Bodi.

9.1.2 Mkutano Mkuu wa Kawaida

a) Mkutano Mkuu ya kawaida unaweza kufanyika angalau mara moja kwa mwaka

ambapo utafanyika wakati wowote katika mwaka wa fedha wa Chama.

Page 15: MASHARTI YA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA …...cha chini cha umiliki wa hisa ni kama ilivyoainishwa katika sera ya Hisa, Akiba na Amana. (g) Mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa

10

b) Shughuli zitazofanyika katika Mkutano Mkuu wa Kawaida ni pamoja na;

(i) Kusoma na kuthibitisha muhtasari wa mkutano uliopita na yatokanayo.

(ii) Kupokea na kujadili taarifa za maendeleo ya utekelezaji kutoka Bodi na

Kamati ya Usimamizi.

(iii) Kuamua idadi ya wajumbe Bodi.

(iv) Kuthibitisha makisio ya mapato na matumizi ya mwaka unaofuata.

(v) Kuthibitisha kuingizwa na kufukuzwa kwa wanachama.

(vi) Kuweka ukomo wa madeni kwa mujibu wa Sheria ya Ushirika.

(vii) Kuchagua, kuwasimamisha au kuwafukuza wajumbe wa Bodi.

(viii) Kuchagua wajumbe wa kuwakilisha chama katika vyama na taasisi nyingine

zinazohusika na maendeleo ya Chama.

(ix) Kuidhinisha makubaliano na mikataba.

(x) Kuzungumzia mambo yote yanayohusu maendeleo ya chama kwa jumla na

kutoa maelekezo ya utekelezaji kwa Bodi.

Hata hivyo shughuli zitakazofanyika katika Mkutano huu zinaweza zikafanyika katika Mkutano

Mkuu wa Mwaka.

9.1.3 Mkutano Mkuu Maalum

(a) Mkutano Mkuu Maalum utafanyika pale ambapo theluthi moja (1/3) ya wanachama

itaonesha nia ya kutaka kuitishwa kwa mkutano huo, kwa maandishi na kutuma nakala

kwa Mrajisi wa Vyama vya Ushirika. Hata hivyo huo ni lazima uwe na agenda moja (1)

tu.

(b) Mkutano Mkuu Maalum unaweza kuitishwa na Mrajis wa Vyama vya Ushirika au mtu

aliyepewa mamlaka naye. Mkutano huo utakuwa na nguvu sawa na mikutano mingine ya

Chama iliyoitishwa kwa mujibu wa Masharti ya Chama.

(c) Bodi inaweza kuitisha Mkutano Mkuu Maalum kujadili jambo la dharura ikiwemo

kujadili Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu ili kuwapa fursa Wanachama kujadili kwa undani

na kuchambua vizuri taarifa za ukaguzi kwa mwaka husika wa fedha.

9.2 Taratibu za Kuitisha Mkutano Mkuu

(a) Matangazo ya mikutano yatabandikwa katika ofisi ya chama na kwenye mbao za

matangazo za eneo la Chama.

(b) Tangazo hilo ni lazima lioneshe wazi tarehe ya mkutano, mahali pa mkutano, saa na

jambo/mambo yatakayozungumzwa.

(c) Muda wa matangazo ya mkutano:

i. Mkutano Mkuu wa mwaka si chini ya siku 21.

ii. Mkutano Mkuu wa kawaida si chini ya siku 21.

iii. Mkutano Mkuu Maalum si chini ya siku 7.

(d) Mahudhurio katika mikutano ya Chama ni lazima kuwa zaidi ya nusu (½) ya wanachama

wote au wanachama mia moja (100).

Page 16: MASHARTI YA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA …...cha chini cha umiliki wa hisa ni kama ilivyoainishwa katika sera ya Hisa, Akiba na Amana. (g) Mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa

11

(e) Kwa Mkutano Mkuu Maalum ulioitishwa na Mrajis au Afisa aliyeteuliwa na Mrajis,

utafanyika kwa idadi yoyote ya wanachama waliohudhuria na yote yatakayopitishwa

yatakuwa ni halali na yatawabana wanachama wote.

(f) Kwa Mikutano Mikuu ya mwaka na kawaida ikiwa mahudhurio hayotoshi baada ya saa

moja na nusu ya saa zilizopangwa, Mkutano utaahirishwa kwa siku saba (7), na Mkutano

utakaofuata mambo yatakayozungumzwa ni yale yale ya Mkutano ulioahirishwa. Iwapo

mahudhurio hayatoshi tena Mkutano huo utafutwa.

(g) Kwa Mkutano Mkuu Maalum ulioitishwa na wanachama, Mkutano utafutwa kabisa

iwapo mahudhurio hayatatosha baada ya kupita saa moja nusu.

(h) Mwenyekiti wa Bodi ataendesha mikutano yote isipokuwa ule Mkutano Mkuu Maalum

ulioitishwa na Mrajis ambapo Mrajis au mtu yeyote atakayemteua atakuwa Mwenyekiti.

(i) Iwapo Mwenyekiti hayupo, Makamu wake atendelesha Mkutano Mkuu wa Mwaka au

wa Kawaida. Iwapo wote hawapo kwa muda wa dakika 30, mwanachama yeyote katika

waliohudhuria tachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa muda na ataongoza Mkutano huo.

(j) Hata hivyo uitishwaji wa Mikutano Mikuu itazingatia Sheria na Kanuni za Ushirika.

9.3 Bodi ya Uongozi

Bodi ya Chama itakuwa na uwezo wa kusimamia Chama kwa mujibu wa Sheria na kanuni za

Ushirika, Masharti na Sera za Chama.

Kutakuwa na Wajumbe wa Bodi saba (7) ambao watachaguliwa na Mkutano Mkuu baada ya

kujaza fomu za maombi kwa kuzingatia taratibu zilizoanishwa kwenye Sheria na Kanuni za

Ushirika.

Hakuna mjumbe wa Bodi atakaye kuwa na haki ya kudai malipo ya mshahara au posho

isipokuwa kama ilivyoelekezwa katika masharti haya na kupata idhini ya Mkutano Mkuu.

Wajumbe wa Bodi hii watashika madaraka kwa muda wa miaka mitatu (3) na ataweza

kuchaguliwa tena kwa kipindi kipindi kimoja (1) cha miaka mitatu. Mjumbe

atakayechaguliwa kushika nafasi ya mjumbe aliyeondolewa, aliyefariki au kujihuzuru

atashika madaraka kwa kipindi kilichobaki cha mjumbe huyo.

9.3.1 Sifa za Wajumbe wa Bodi

Mjumbe wa Bodi anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:

(i) Awe na elimu ya kutosha angalau astashahada inayotambulika na mamlaka za elimu

nchini ili kumwezesha kusimamia shughuli za chama kikamilifu.

(ii) Awe mwadilifu na mwaminifu.

(iii) Awe na uwezo wa kuongoza.

(iv) Awe amelipa hisa chamani kwa mujibu wa Masharti haya.

(v) Awe hajawahi kupoteza sifa za uongozi katika ngazi yoyote ya Chama cha Ushirika.

(vi) Awe hajawahi kuwa mjumbe wa Bodi iliyoshindwa kusimamia vizuri shughuli za

Chama na kikapata hasara.

(vii) Awe anashiriki kikamilifu katika shughuli zote za Chama.

(viii) Awe hajawahi kusababisha hasara katika chama chochote cha Ushirika.

(ix) Asiwe na deni alilolipata nje ya utaratibu.

(x) Asiwe na tabia ya kulaza madeni.

Page 17: MASHARTI YA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA …...cha chini cha umiliki wa hisa ni kama ilivyoainishwa katika sera ya Hisa, Akiba na Amana. (g) Mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa

12

9.3.2 Majukumu ya Bodi

Bodi hii itakuwa na wajibu wa kufanya mambo yafuatayo:

(a) Kusimamia shughuli zote za kiuchumi za Chama na kuhakikisha kuwa zinaendeshwa

ipasavyo.

(b) Kutekeleza kikamilifu maazimio na maelekezo ya mikutano mikuu.

(c) Kutunza hesabu za Chama kwa usahihi.

(d) Kutunza kwa usahihi daftari la wanachama na kumbukumbu za mihtasari ya

Mikutano Mikuu na Mikutano ya Bodi.

(e) Kuhakikisha kuwa lakiri ya chama inakuwepo na inatumika ipasavyo

(f) Kuchukua uamuzi ikingojea uithibitisho wa Mkutano Mkuu, juu ya kupokelewa

wanachama wapya, kujiuzulu wanachama na kusimamishwa kwa wajumbe wa Bodi.

(g) Kubuni na kutayarisha Sera na kanuni za Uendeshaji chama zinazohusu fedha,

biashara, utawala, mikopo na bohari ili kufanikisha madhumuni ya Chama.

(h) Kuwasilisha kwenye Mkutano Mkuu wa wanachama taarifa ya hali ya uchumi na

maendeleo ya Chama pamoja na hesabu ya mapato na matumizi, mizania

iliyothibitishwa kwa mwaka uliopita na makisio ya mapato na matumizi kwa mwaka

unaofuata.

(i) Kupokea na kujadili taarifa za Kamati ya Mikopo na kamati ya Usimamizi..

(j) Kupitia na kujadili maombi ya mikopo kutoka kwa Wajumbe wa Bodi, wajumbe wa

Kamati ya Mikopo na wajumbe wa Kamati ya Usimamizi.

(k) Kuteua mwanachama atakayeshika nafasi iliyoachwa wazi katika Kamati ya Mikopo.

(l) Kumwezesha mtu aliyeidhinishwa kukagua vitabu vya Chama na kuhakikisha kuwa

hatua zinachukuliwa kutokana na taarifa ya ukaguzi.

(m) Kuhakikisha kuwa wanachama wanafuata na kuzingatia Sheria na Kanuni za

Ushirika, masharti ya Chama, Sera, mikataba na taratibu mbalimbali za Chama.

(n) Kufungua akaunti Benki na kuhakikisha kuwa fedha zote za Chama zinatunzwa

katika Benki.

(o) Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa mpango mkakati na mpango wa biashara wa

Chama.

(p) Kuhakikisha kwamba Chama kinawakilishwa katika mashitaka yoyote.

(q) Kuhakikisha kuwa mali, bidhaa, vifaa na nyaraka/Hati za Chama zinahifadhiwa vizuri

na kwa usalama.

(r) Kuamua idadi, uwezo na sifa za watu ambao wanaweza kuajiriwa kuendesha shughuli

za Chama.

(s) Kuteua wajumbe watakaotia saini kwenye hundi za Chama.

(t) Kuajiri kwa niaba ya wanachama Meneja/Katibu, Mhasibu au watumishi wengine

ambao wataendesha shughuli za kila siku za Chama.

(u) Kuingia mikataba mbalimbali kwa niaba ya Chama baada ya kupata idhini ya

Mkutano Mkuu na Mrajis.

(v) Kuhakikisha kuwa wakopaji wanalipa madeni yao kama walivyoahidi, kuwachukulia

hatua za kisheria wakopaji wasio waaminifu na kupendekeza kwa Mkutano Mkuu

ufutaji wa mikopo mibaya ambayo haiwezi kulipwa kabisa.

(w) Kupendekeza kwenye Mkutano Mkuu mabadiliko au viwango vya riba au masharti

ya ulipaji mikopo na/au mgawanyo wa mikopo.

Page 18: MASHARTI YA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA …...cha chini cha umiliki wa hisa ni kama ilivyoainishwa katika sera ya Hisa, Akiba na Amana. (g) Mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa

13

(x) Kuandaa mapendekezo ya marekebisho ya Masharti ya Chama pale itakapobidi na

kuwasilisha kwenye Mkutano Mkuu.

(y) Kutekeleza majukumu mengine ya Bodi ni pamoja na;

(i) Kuandikisha mikataba yote ya kibiashara kwa Mrajis wa Vyama vya Ushirika.

(ii) Kuchunguza mara kwa mara shughuli za Chama kwa kumtaka Meneja/Katibu

atoe taarifa ya matokeo ya uendeshaji wa shughuli za Chama.

(iii)Kutayarisha/kuchapisha Hati za kumiliki hisa kwa ajili ya wanachama.

(iv) Kufanya mambo mengine yote ambayo yataoneakana ni lazima katika

kutimiza Sheria na Kanuni za Ushirika, Masharti na Sera za Chama.

9.3.3 Majukumu ya Mwenyekiti wa Bodi

Mwenyekiti wa Bodi atakuwa na kazi zifuatazo:-

(a) Kuongoza Mikutano Mikuu yote isipokuwa Mkutano Mkuu maalum ulioitishwa na

Mrajis.

(b) Kuongoza mikutano yote ya Bodi ya Chama.

(c) Kuitisha Mikutano Mikuu yote na ya Bodi kwa mujibu wa Masharti haya.

(d) Kuweka saini kumbukumbu za Mikutano Mikuu na Mikutano ya Bodi ambayo

ameiongoza.

(e) Kuweka saini kwa niaba ya chama kumbukumbu zote ikiwa ni pamoja na zinazohitaji

kuwekwa lakiri na/au muhuri wa Chama.

(f) Kuwa msemaji Mkuu wa Chama, kama haitaamriwa vinginevyo na Bodi au Mkutano

Mkuu wa wanachama.

9.3.4 Majukumu ya Makamu Mwenyekiti wa Bodi

Makamu Mwenyekiti atafanya kazi zote za Mwenyekiti wakati Mwenyekiti hayupo.

9.3.5 Mikutano ya Bodi

(a) Mikutano ya Bodi itaitishwa na mwenyekiti wa Chama kwa kushauriana na Meneja.

(b) Bodi itapaswa kufanya mikutano angalau minne (4) kwa mwaka. Mahudhurio ya zaidi

ya nusu yatahitajika ili kuendesha Mkutano. Iwapo Mwenyekiti na Makamu

Mwenyekiti hawapo, kikao kitachagua mwenyekiti wa muda miongoni mwa wajumbe

waliopo.

(c) Kila mjumbe wa Bodi atakuwa na kura moja. Iwapo kura zitalingana, Mwenyekiti

atakuwa na kura ya ziada.

(d) Mambo yote yaliyozungumzwa katika mkutano yataandikwa ndani ya kitabu cha mambo

ya mikutano ya Bodi na kuwekwa saini na Mwenyekiti na Meneja/Katibu.

9.3.6 Kuacha au Kusimamishwa ujumbe wa Bodi

(a) Mjumbe wa Bodi ataacha madaraka kwa sababu yoyote kama zilivyoainishwa katika

Kanuni za ushirika.

(b) Mjumbe wa Bodi atakayeshindwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo bila sababu

inayokubalika anaweza kusimamishwa Uongozi hadi Mkutano Mkuu utakaofuata.

Page 19: MASHARTI YA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA …...cha chini cha umiliki wa hisa ni kama ilivyoainishwa katika sera ya Hisa, Akiba na Amana. (g) Mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa

14

9.4 Kamati ya Usimamizi

(a) Kutakuwepo na Kamati ya Usimamizi ya watu watatu nje ya wajumbe wa Bodi.

(b) Wajumbe wa Kamati ya Usimamizi watachaguliwa na Mkutano Mkuu.

(c) Mjumbe yeyote wa Bodi au mtumishi yeyote wa Chama hatastahili kuchaguliwa kuwa

mjumbe wa kamati hii.

(d) Wajumbe wa Kamati hii watashika madaraka kwa muda wa miaka tisa (9), na theluthi

moja (1/3) ya wajumbe wataondolewa kila baada ya miaka mitatu.

(e) Wajumbe wa Kamati hii watatengeneza utaratibu wa kutekeleza kazi zao, pia watachagua

mwenyekiti na mwandishi/katibu miongoni mwao. Mwandishi/katibu atatengeneza na

kuhifadhi kumbukumbu zote pamoja na hatua zinazochukuliwa na kamati hii.

9.4.1 Sifa za Wajumbe wa Kamati ya Usimamizi

Zifuatazo ni sifa za Mjumbe wa Kamati ya Usimamizi.

(a) Awe na elimu angalau stashahada ya kumuwezesha kusimamia shughuli za chama kwa

ufanisi. Angalau wajumbe wawili (2) wawe na uelewa wa utunzaji wa vitabu vya hesabu

au wa uhasibu au ukaguzi na uongozi/usimamizi wa fedha na sheria.

(b) Awe mwadilifu na mwaminifu.

(c) Awe na uwezo wa kuongoza.

(d) Awe amelipa hisa chamani kwa mujibu wa Masharti ya Chama.

(e) Awe hajawahi kupoteza sifa za uongozi katika ngazi yoyote ya chama cha Ushirika.

(f) Awe hajawahi kuwa mjumbe wa Bodi iliyoshindwa kusimamia vizuri shughuli za

Chama na kikapata hasara.

(g) Awe anashiriki kikamilifu katika shughuli zote za Chama.

(h) Awe hajawahi kusababisha hasara katika chama chochote cha Ushirika.

(i) Asiwe na deni alilolipata nje ya utaratibu.

(j) Asiwe na tabia ya kulaza madeni.

9.4.2 Majukumu ya Kamati ya Usimamizi

Yafuatayo ni majukumu ya Kamati ya Usimamizi:-

(a) Kusimamia fedha na mali zote za Chama kwa niaba ya wanachama.

(b) Kusababisha kufanyika japo mara moja katika miezi mitatu (3), uchunguzi wa

shughuli za Chama pamoja na ukaguzi wa vitabu na kutengeneza au kuamuru

utengenezaji wa taarifa itakayotolewa katika Mkutano Mkuu kwa maandishi.

(c) Kufuatilia maendeleo ya miradi mikubwa ambayo imepatiwa mkopo na Chama

mpaka wahusika wanapomaliza marejesho.

(d) Kutayarisha taarifa ya maandishi juu ya hali ya fedha na huduma zitolewazo kwa

wanachama na kuiwasilisha kwenye Mkutano Mkuu, na nakala kutumwa kwa Afisa

Ushirika wa Wilaya na Mrajis Msaidizi kila baada ya miezi mitatu (3).

(e) Kusimamia ukaguzi wa ndani na kupokea taarifa ya mkaguzi wa ndani

atakapoteuliwa.

(f) Kusikiliza malalamiko ya wanachama na kuyatafutia ufumbuzi kwa kushirikiana na

Bodi.

9.4.3 Kamati ya Mikopo

(a) Kamati itaundwa na wajumbe kati ya wajumbe wa Bodi.

Page 20: MASHARTI YA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA …...cha chini cha umiliki wa hisa ni kama ilivyoainishwa katika sera ya Hisa, Akiba na Amana. (g) Mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa

15

(b) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bodi hawatakuwa wajumbe wa kamati ya

mikopo.

(c) Kamati itakuwa na wajumbe watatu (3).

(d) Kamati itafanya mkutano angalau mmoja kila mwezi, lakini inaweza kufanya mkutano

wa dharura wakati wowote. Mkutano utaweza kuendeshwa endapo theluthi mbili (2/3)

ya wajumbe wa kamati watahudhuria. Taarifa ya mikopo itatolewa kwa wanachama

katika mikutano mikuu.

9.4.4 Sifa za Wajumbe wa Kamati ya Mikopo

Mbali na sifa zilizotajwa katika nafasi ya ujumbe wa Bodi, angalau mjumbe mmoja (1) wa

kamati hii awe na elimu ya fedha na shughuli za kibenki.

9.4.5 Majukumu ya Wajumbe wa Kamati ya Mikopo

Majukumu ya Kamati ya Mikopo ni haya yafuatayo:-

(a) Kusimamia/kutekeleza sera za mikopo zilizopitishwa na mkutano Mkuu.

(b) Kupanga na kutekeleza shughuli zote za mikopo.

(c) Kupokea maombi ya mikopo, kuchambua na kutolea maamuzi.

(d) Kuhakiki shughuli/hesabu za wakopaji.

(e) Kufuatilia mikopo iliyopita muda wa kurejeshwa.

(f) Kushiriki katika ukusanyaji wa mikopo iliyocheleweshwa.

(g) Kutathmini shughuli zote za mikopo.

(h) Kutoa taarifa ya shughuli za mikopo kwa bodi na Mkutano Mkuu.

9.5 Wajumbe wa Uwakilishi

Kutakuwepo na wajumbe wawili (2) wa uwakilishi. Mjumbe mmoja (1) atatokana na wajumbe

wa Bodi na mmoja nje ya wajumbe wa Bodi (toka kwa wanachama).

9.5.1 Majukumu ya Mwakilishi wa Bodi

Majukumu ya mwakilishi wa Bodi ni haya yafuatayo:-

(a) Kuwakilisha Bodi kwenye masuala yote ya nje pale ambapo uwakilishi huu hauhitaji

Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti.

(b) Kutoa taarifa kwa Bodi juu ya yale yote yaliyofanyika anapokuwa kwenye uwakilishi.

(c) Kufanya ziara za mafunzo na kutoa ushauri kwa Bodi juu ya mambo ya kuboresha

Chama kinapotoa huduma za kifedha kwa wanachama.

9.5.2 Majukumu ya Mwakilishi wa Wanachama

Majukumu ya Mwakilishi wa wanachama ni haya yafuatayo:-

(a) Kutafuta habari kutoka kwa wanachama na kuzifanyia kazi ili zilete ufanisi wa kiutendaji

katika kutoa huduma za kifedha kwa wanachama.

(b) Kuwawakilisha wanachama kwenye masuala yote yanayohusu wanachama.

(c) Kuhudhuria vikao vya Bodi kama mjumbe aliyekaribishwa ili kuwasilisha hoja za

wanachama kadri anavyozipokea na kufuatilia utekelezaji wake.

(d) Kuhudhuria vikao vya Kamati ya Mikopo ili kushiriki na kuona kama hakuna

wanachama wanaopendelewa wakati wa kutoa mikopo.

Page 21: MASHARTI YA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA …...cha chini cha umiliki wa hisa ni kama ilivyoainishwa katika sera ya Hisa, Akiba na Amana. (g) Mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa

16

(e) Kutoa taarifa katika Mkutano Mkuu juu ya hoja ambazo zitakuwa zimefanyiwa kazi na

ambazo hazijafanyiwa kazi.

9.6 Menejimenti/Meneja

Chama kitaajiri Meneja atakayewajibika kwa Bodi na ambaye atasimamia shughuli zote za

uendeshaji za kila siku kwa niaba ya Bodi.

9.6.1 Kazi za Meneja zitakuwa ni;

Zifuatazo ni kazi za meneja.

(i) Kulinda Ukwasi wa Chama kulingana na Vyanzo vya fedha na misingi ya fedha iliyopo.

(ii) Kuandaa na Kutekeleza Mpango Mkakati na Mpango wa Biashara wa Chama ili

kuwezesha Chama kutoa huduma bora za kifedha kwa wanachama.

(iii) Kuandaa makisio ya mapato na matumizi ya Chama na kuyawasilisha kwa Bodi na

Mkutano Mkuu kwa ili kuidhinishwa.

(iv) Kubuni, kuandaa na kuuza bidhaa za huduma za kifedha zinazokidhi mahitaji ya kifedha

ya wanachama.

(v) Kuhamasisha wanachama kuweka Hisa, Akiba na Amana pamoja na kutafuta fedha

kutoka vyanzo vya nje ili kuweza kumudu mahitaji ya mikopo kwa wanachama.

(vi) Kusimamia shughuli zote za kiuendeshaji na kiutawala za Chama.

(vii) Kuainisha na kusimamia utekelezaji wa majukumu ya watumishi wengine

anaowasimamia

(viii) Kuandaa na kuwasilisha kwenye Bodi taarifa za uendeshaji kila mwezi, zinazohusu utoaji

huduma za kifedha kwa wanachama.

(ix) Kuhakikisha kuwa taarifa za hesabu za kila mwaka za Chama zinaandaliwa, kukaguliwa

na kuwasilishwa kwenye Mkutano Mkuu, kwa wakati na kwa mujibu wa Sheria na

Kanuni za Ushirika.

(x) Kutoa tathmini ya kiutendaji wa ofisi kwenye Bodi kwa kipindi cha robo mwaka.

(xi) Kufuata kanuni zote za fedha na uendeshaji wa ofisi zenye kuzingatia utawala bora.

(xii) Kufanya kazi zingine kadri atakavyoelekezwa na Bodi.

SEHEMU YA KUMI

10 TARATIBU ZA UWEKAJI WA HISA, AKIBA, AMANA NA UTOAJI MIKOPO

Taratibu za uwekaji hisa, akiba, amana na utoaji wa mikopo utazingatia Sera ya Huduma za

Kifedha za Hisa, Akiba, na Amana, na Sera ya Mikopo.

SEHEMU YA KUMI NA MOJA

11 MGAO WA ZIADA

(a) Kila mwaka chama kitatenga kiasi kisichopungua asilimia ishirini (20%) kutokana na

faida halisi kwa ajili ya akiba ya lazima ili kukiendeleza Chama. Akiba ya lazima

itabakia kuwa ni mali ya Chama na haitaweza kugawanywa isipokuwa kama kinavunjwa.

(b) Chama kitatenga asilimia kumi na tano (15%) kwa ajili ya mfuko wa kukombolea hisa,

za walioacha uanachama lakini kiasi hicho kisizidi asilimia kumi na tano (15%) ya hisa

zote.

Page 22: MASHARTI YA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA …...cha chini cha umiliki wa hisa ni kama ilivyoainishwa katika sera ya Hisa, Akiba na Amana. (g) Mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa

17

(c) Asilimia kumi na tano (15%) ya faida halisi itatengwa kwa ajili ya kinga ya madeni

mabaya. Lakini kiasi hicho kisizidi asilimia kumi na tano (15%) ya madeni yote.

(d) Chama kitatenga asilimia kumi (10%) ya faida kwa ajili ya fungu la vitega uchumi.

(e) Bodi inaweza mara kwa mara kupendekeza katika Mkutano Mkuu kuongeza mifuko

mingine kwa ajili ya maendeleo ya baadaye ya Chama iwapo ina faida halisi ya kutosha.

(f) Ziada itakayobaki baada ya matengo ya kisheria kufanyika, itagawanywa kama

itakavyoamuliwa na Mkutano Mkuu wa wanachama na kwa mujibu wa Sheria na Kanuni

za Ushirika.

(g) Hisa zitakazostahili kulipwa ziada ni zile zilizokamilika na ambazo zilichangwa miezi

mitatu (3) kabla ya mwaka fedha unaohusika na ziada itakayogawanywa. Mkutano Mkuu

unaweza kuidhinisha wanachama warejeshewe sehemu ya faida juu ya mikopo yao. Hii

itafanyika kwa uwiano, kwa wakopaji ambao walitumia huduma ya mikopo kwa mwaka

huo.

SEHEMU YA KUMI NA MBILI

12 UHASIBU

Chama kitafuata miongozi ya uandaji wa hesabu wa kimataifa na mfumo wa uhasibu

ulioidhinishwa na Mrajis wa Vyama vya Ushirika katika kutunza vitabu vya hesabu na

kumbukumbu zingine.

SEHEMU YA KUMI NA TATU

13 KUHIFADHI AKIBA NA FEDHA NYINGINE ZA CHAMA

(a) Fedha za Chama zitahifadhiwa katika benki na kuwekeza katika taasisi za kifedha

ikiwa ni pamoja na kununua dhamana za Serikali.

(b) Mahitaji ya mikopo ya wanachama yakishatoshelezwa fedha ambayo itazidi inaweza

kuwekwa benki katika akaunti za amana za muda maalum ili zipate faida kubwa.

(c) Fedha yote ya chama isipokuwa ile inayohitajika kwa matumizi madogo madogo

itahifadhiwa benki.

(d) Bodi inaweza kuruhusu Meneja awe na taslim kiasi kitakachoamuliwa na kuingizwa

katika masharti kwa ajili hiyo.

(e) Malipo yote yatafanyika kwa njia ya hundi.

SEHEMU YA KUMI NA NNE

14 MAHUSIANO NA ASASI ZINGINE ZA KIFEDHA NA MITANDAO

(a) Chama kinaweza kuwa na mtandao wa kutoa huduma za kifedha kwa wanachama wake kwa

kushirikiana na Asasi nyingine za kifedha na kuweza kunufaika na utaratibu wa

kukopeshana kwa Vyama vya Akiba na Mikopo vyenyewe kwa vyenyewe.

(b) Chama kinaweza kuridhia kuwa sehemu ya mtandao wa Asasi za kifedha baada ya kuridhika

kuwa mtandao huo ni wa manufaa kwa wanachama.

Page 23: MASHARTI YA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA …...cha chini cha umiliki wa hisa ni kama ilivyoainishwa katika sera ya Hisa, Akiba na Amana. (g) Mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa

18

(c) Mahusiano haya yataandaliwa na kuchambuliwa na Kamati ya Usimamizi ili yasiathiri

shughuli za kifedha za chama na kuleta athari kwa wanachama.

SEHEMU YA KUMI NA TANO

15 KUFUTWA KWA CHAMA

(a) Chama kinaweza kufutwa kwa amri ya Mrajis wa Vyama vya Ushirika au kwa maombi

ya wanachama wasiopungua robo tatu (3/4) ya wanachama wote.

(b) Kufutwa kwa Chama kutafuata utaratibu wa kisheria uliowekwa katika Sheria na Kanuni

za Ushirika.

SEHEMU YA KUMI NA SITA

16 MENGINEYO

(a) Hakuna Mjumbe yeyote wa Bodi au mfanyakazi wa Chama atakayeidhinisha au kutoa

maamuzi ya maombi ya fedha ikiwa anahusika na maombi hayo kwa namna yoyote.

(b) Wajumbe wa Bodi, wajumbe wa Kamati ya Usimamizi, watendaji wakuu na watumishi wa

Chama watatunza siri kuhusu kumbukumbu zote za mwanachama.

(c) Vitabu vya hesabu na kumbukumbu nyingine za Chama zinaweza kuchunguzwa wakati

wowote na wajumbe wa Bodi.

(d) Kiasi fedha kinaweza kutolewa na Mkutano Mkuu kama honoraria kwa mtu yeyote

aliyejitolea na kuteulewa Bodi kufanyakazi maalum za Chama.

(e) Mgogoro au malalamiko yoyote kuhusu masharti au huduma za Chama kati ya mwanachama

au wanachama na watu wanaodai kupitia wanachama, na wajumbe wa Bodi au Afisa yeyote,

au kati ya Chama na chama kingine cha ushirika, yatapelekwa kwa Mrajis wa Vyama vya

Ushirika.

(f) Masharti haya yanaweza kurekebishwa pale itakaonekana inafaa kwa kupitishwa katika

Mkutano Mkuu na kupata idhini ya Mrajisi.

(g) Masharti haya yatanza kutumika mara baada ya kuwekwa saini na Wajumbe wa Bodi na

Mrajis wa Vyama vya Ushirika.

Page 24: MASHARTI YA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA …...cha chini cha umiliki wa hisa ni kama ilivyoainishwa katika sera ya Hisa, Akiba na Amana. (g) Mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa

1

Wajumbe wa Bodi.

Na. Jina Kamili Wadhifa Saini

1. Tito Bartholomew Haule Mwenyekiti

2. Ndenengo Exaud Mwende Makamu Mwenyekiti

3. Tumaini Hashimu Yarumba Mjumbe

4. Mwanahawa Mhina Mjumbe

5. George Ntakimanzi Mjumbe

6. Martin Mwangalimi Mjumbe

7. Martha Lyimo Mjumbe

Mrajis wa Vyama Vya Ushirika................................................................

Saini............................................................................................................

Tarehe.........................................................................................................