MBEYA POLYTECHNIC COLLEGE –TUKUYU CAMPUS POLYTECHNIC... · A. UFUGAJI WA KUKU (KIENYEJI NA KISASA) - Chuo kinaendesha mafunzo ya kozi ndefu na fupi kwa ajili ya kuwapa wanachuo

Embed Size (px)

Citation preview

  • MBEYA POLYTECHNIC COLLEGE TUKUYU CAMPUS

    MAELEZO YA CHUO (COLLEGE PROFILE)

    NACTE REGISTRATION NUMBER: REG/SAT/015P

    MBEYA POLYTECHNIC COLLEGE TUKUYU CAMPUS P.O BOX 497 TUKUYU Website: www.mbeyacollege.ac.tz Email: [email protected]

  • YALIYOMO:

    1. Ufugaji wa Samaki

    2. Usimamizi wa Uvuvi

    3. Usimamizi wa Misitu

    4. Ufugaji wa Nyuki

    5. Kilimo cha Bustani

    6. Ufugaji wa Wanyama Mbalimbali

    7. Tehama katika Kilimo na Maliasili

    8. Mfumo elekezi wa mafunzo kuanzia Cheti hadi Udaktari wa Falsafa.

    9. Kozi zinazofundishwa

  • UFUGAJI WA SAMAKI (Aquaculture au aquafarming),

    UFUGAJI WA SAMAKI ni kilimo cha viumbe vinavyoishi majini, kwa mfano samaki, konokono na mimea ya majini. Aquaculture inahusisha kilimo cha viumbe vinavyoishi kwenye maji baridi na vile vinavyoishi kwenye maji ya chumvi katika mazingira ya kuhudumiwa,

    Katika kozi ya Aquaculture Chuo kinafundisha elimu ya ufugaji wa samaki, ikiwa ni pamoja na utengenezaji wa mabwawa, utotoleshaji wa vifaranga vya samaki, namna salama ya kusafirisha vifaranga vya samaki, namna ya kuwapanda na kuwahifadhi samaki katika mabwawa na pia usimamizi wa mabwawa (ikiwa ni pamoja na kujifunza magonjwa mbalimbali ya samaki na tiba zake).

    USIMAMIZI WA UVUVI (Fisheries management):

    Usimamizi huu hujikita zaidi katika sayansi ya uvuvi wa samaki ili kutambua njia sahihi za kulinda maliasili samaki na uvunaji wake uwe wenye mafanikio na endelevu.

    Sayansi ya Uvuvi wa Samaki ni taaluma inayohusu uelewa na usimamizi wa uvuvi. Ni sayansi yenye upana katika nyanja za elimu ya maji baridi (mito, mabwawa, visima, n.k.; na maji chumvi ya bahari (limnology, oceanography, freshwater biology, marine biology, conservation, ecology, population dynamics, economics na management),

    Chuo kinamtayarisha mwanachuo katika usimamizi na utunzaji wa maliasili samaki kwa kufanya shughuli za uvuvi katika mito, maziwa na bahaari. Halikadhalika Chuo kinamfundisha mwanachuo matumizi ya vifaa vya uvuvi, utengenezaji wa vyombo vya kuvulia, :.nyavu za kuvulia n.k. Pia Chuo kinamfundisha mwanachuo mbinu bora za uvuvi na usimamizi wa uhifadhi wa maliasili samaki kulingana na sheria na kanuni za kitaifa na kimataifa.

  • USIMAMIZI WA MISITU (Forestry)

    Somo la Misitu ni sayansi ya upandaji miti, utunzaji, utumiaji, na uhifadhi endelevu wa misitu na maliasili zilizomo katika misitu ili kufikia malengo, na mahitaji kwa faida ya mwanadamu na mazingira.

    Chuo kinampa mwanachuo elimu ya upandaji na uhifadhi endelevu wa misitu, usimamizi wa mimea, wanyama na ndege walio katika hatari ya kutoweka. Pia chuo kinampa mwanachuo elimu bora ya uvunaji endelevu wa miti na mazao yake yanayohitajika kukidhi mahitaji ya jamii, kama vile matumizi ya mbao za kujengea nyumba, mitumbwi, miti ya dawa asilia, matunda na mizizi.

    UFUGAJI NYUKI (Apiculture)

    Ufugaji Nyuki ni somo linalohusu utunzaji wa makundi ya nyuki katika mizinga unaofanywa na wanadamu. Mfugaji wa nyuki huwatunza nyuki kwa ajili ya kuvuna asali na mazao yatokanayo na nyuki, kama vile nta, vitoto vya nyuki, na pia uuzaji wa makundi ya nyuki kwa wafugaji wengine.

    Chuo kinamfundisha mwanachuo ujuzi na mbinu endelevu za utengenezaji wa mizinga ya kisasa ya nyuki, upandaji na utunzaji wa miti inayozalisha maua kwa ajili ya chakula cha nyuki, utunzaji wa vyanzo vya maji kwa ajili ya nyuki, uvunaji wa kisasa wa asali, usindikaji na uuzaji wenye tija wa asali na mazao mbalimbali ya asali.

  • KILIMO CHA BUSTANI (Horticulture)

    Kilimo cha Bustani ni tawi la kilimo mazao kinachojikita katika uzalishaji na utunzaji kisayansi na kiteknolojia wa mimea. Kinahusika na ukulima wa mimea inayoliwa (kama vile mimea tiba, matunda, mbogamboga, karanga, mbegu za mafuta, uyoga, mwani, cauliflower), na mimea isiyoliwa (mfano nyasi, miti ya mapambo na maua). Pia kinahusika na uhifadhi wa mimea, usawazishaji na urutubishaji wa udongo na ubunifu wa kupanda mimea katika bustani. Kilimo hiki kinalimwa sana na wakulima wadogowadogo, wa kati na pia wakubwa wenye nafasi pana ya uwekezaji. Ukweli ni kwamba mazao ya bustani ndiyo yanayotumika sana kila siku kuliko mengine katika jamii.

    Chuo kimeuona umuhimu huu na ndiyo maana kinatoa mafunzo katika fani hii kwa wanachuo. Wanachuo wanapewa elimu juu ya utumiaji wa sehemu ndogo ya ardhi kwa bustani inayotoa mazao mengi yenye kipato kikubwa. Wanachuo wanaelimishwa matumizi ya mfumo usiohitaji udongo mwingi na kutumia vyanzo mbadala wa udongo mfano pumba, mboji itokanayo na maranda ya mbao, majani ya miti na makuti, n.k.

    Wanachuo wanaelimishwa elimu ya kuunganisha vikonyo vya miche na kupata mimea chotara (grafting). Pia wanachuo wanajifunza mbinu za upandaji mimea ya bustani kwa kutumia mashina ya migomba.

    Wanachuo halikadhalika wanapewa elimu na ujuzi wa kutafuta masoko ya ndani na nje ya nchi kwa mazao yanayotokana na bustani.

  • UFUGAJI WA WANYAMA MBALI MBALI

    A. UFUGAJI WA KUKU (KIENYEJI NA KISASA)

    - Chuo kinaendesha mafunzo ya kozi ndefu na fupi kwa ajili ya kuwapa wanachuo ujuzi na

    utaalam rahisi wa kufuga kuku hawa kwa faida.

  • - Yafuatayo yanazingatiwa:

    1.0 UTANGULIZI 1.1 Faida za Ufugaji wa Kuku

    (i) Faida za kuku wa Kienyeji

    (ii) Faida za kuku wa Kisasa

    1.2 Aina ya Kuku wafugwao

    (a) Nje ya nchi

    (b) Ndani ya nchi

    2.0 Aina ya Ufugaji 2.1 Huria

    2.2 Kufungiwa katika majumba, senyenge n.k.

    2.3 Ufugaji kuku wa Mayai au wa Nyama

    3.0 Uzalishaji wa Kuku

    4.0 Ulishaji wa Kuku 4.1 Vifaranga

    4.2 Kuku wanaokua

    4.3 Kuku wakubwa

    4.4 Aina ya Vyakula vya Kuku

    5.0 Magonjwa Muhimu, Kinga na Tiba ya Kuku

    6.0 Uvunaji wa Mazao ya Kuku 6.1 Ukusanyaji na Utunzaji wa Mayai

  • 6.2 Uuzaji wa Kuku wa Nyama

    6.3 Masoko ya Mazao ya Kuku (Mayai na Nyama)

    7.0 Mazoezi ya ujenzi wa mabanda bora ya kuku, uchanganyaji wa vyakula vya kulisha vifaranga na kuku wakubwa, usafi wa mabanda na vyombo vya kulishia, ukusanyaji salama wa mayai, n.k.

    B: UFUGAJI WA WANYAMA KWA AJILI YA KUZALISHA MAZIWA

    - Chuo kinaendesha mafunzo ya kozi ndefu na fupi kwa ajili ya kuwapa wanachuo ujuzi na

    utaalam rahisi wa kufuga wanyama wanaozalisha maziwa kwa faida.

    1.0 UTANGULIZI

    1.1 Faida za Ufugaji wa Wanyama wa Maziwa

    (a) Faida za Ngombe wa Maziwa

    (b) Faida za Mbuzi wa Maziwa

    1.2 Aina ya Wanyama Wafugwao kwa Ajili ya Maziwa

    (a) Nje ya nchi

    (b) Ndani ya nchi

    2.0 Aina ya Ufugaji 2.1 Huria, Kienyeji

    2.2 Kufugwa ndani ya mabanda, senyenge

  • 3.0 Uzalishaji wa Ngombe na Mbuzi wa Maziwa

    4.0 Ulishaji wa Ngombe na Mbuzi wa Maziwa 4.1 Ndama wanaonyonya

    4.2 Ndama baada ya kuachishwa kunyonya

    4.3 Wanyama balehe (Animals at Puberty)

    4.4 Wanyama wakubwa

    4.5 Aina ya Vyakula na Umuhimu wake

    5.0 Magonjwa, Kinga na Tiba 5.1 Magonjwa yaambukizwayo na Bakteria

    5.2 Magonjwa yaambukizwayo na Virusi

    5.3 Magonjwa muhimu ila siyo ya kuambukiza

    5.4 Uzuiaji (Kinga) na Tiba

    6.0 Uvunaji Bora wa Maziwa na Wanyama Hai 6.1 Ukamuaji bora na wenye tija

    6.2 Ukusanyaji wa maziwa kama zao

    6.3 Usafi wa Vyombo, Vyumba vya kutunzia Maziwa

    6.4 Masoko ya Zao la Maziwa

    6.5 Uuzaji wa Wanyama Hai kwa ajili ya Kufugwa na wengine

    7.0 Mazoezi ya ukamuaji na usafi wa vyombo, ulishaji wa ndama, na usafi wa mabanda, uchanganyaji wa vyakula vya kulisha wanyama wakubwa na wadogo, ujenzi wa kibano cha wanyama (crush), n.k.

  • C: USINDIKAJI WA MAZAO YATOKANAYO NA MAZIWA

    - Chuo kinaendesha kozi ndefu na fupi juu ya usindikaji wa Mazao yatokanayo na maziwa ili wafugaji waweze kujiongezea lishe na kipato chenye tija na faida

    - Yafuatayo yanazingatiwa:

    1.0 Utangulizi 1.1 Aina ya Mazao yatokanayo na maziwa

    2.0 Usindikaji wa Kila zao

  • 3.0 Utunzaji wa Kila Zao Kabla ya kuliwa au kuuzwa kwa wateja

    4.0 Masoko ya Kila Zao

    5.0 Mazoezi ya usindikaji kama vile maziwa mgando, siagi, samli, jibini, n.k.

    D: UPANDAJI NA UZALISHAJI WA MALISHO BORA YA WANYAMA

    - - Chuo kinaendesha mafunzo ya kozi ndefu na fupi kwa ajili ya kuwapa wanachuo ujuzi na utaalam rahisi wa kulima, kupanda na kuzalisha malisho bora ya kulisha wanyama wafugwao kwa faida.

    - Yafuatayo yanazingatiwa:

    1.0 Utangulizi 1.1 Faidaza Uzalishaji wa Malisho Bora

    1.2 Aina ya Malisho yafaayo kwa wanyama

    (a) Nyasi za Kienyeji, Nyasi bora

    (b) Mikunde

    (c) Miti Malisho

    (d) Masalio ya Mazao Shambani na Viwandani

    2.0 Upandaji na Ustawishaji wa Malisho 2.1 Utayarishaji shamba

    2.2 Utayarishaji wa Mbegu

    2.3 Namna ya Kupanda Malisho (Nyasi, Mikunde n.k.)

    2.4 Utunzaji wa Mimea baada ya kuota

    3.0 Uvunaji na Ulishaji wa Malisho baada ya Kukomaa 3.1 Wanyama Kuchunga katika Malisho

  • 3.2 Kukata na Kulisha (Cut and Carry System)

    3.3 Utunzaji na Uhifadhi

    (a) Saileji

    (b) Nyasi za Kukausha (Hay)

    4.0 Ulishaji wenye Tija 4.1 Virutubisho vilivyomo katika Malisho mbali mbali

    4.2 Uchanganyaji wa Vyakula vya Wanyama

    4.3 Ulishaji kulingana na Makundi mbali mbali wa Wanyama katika Zizi

    (a) Ndama, Mitamba n.k.

    (b) Wanyama wakubwa wenye Mimba au wasio na Mimba

    (c) Wanyama wakamuliwao maziwa

    (d) Madume

    5.0 Uuzaji wa Malisho ya Ziada Kupata Kipato

    6.0 Mazoezi ya utayarishaji wa shamba la kupanda nyasi, utayarishaji wa mbegu kabla ya kupanda, upandaji, uvunaji na utunzaji wa nyasi, n.k.

  • TEHAMA KATIKA KILIMO NA MALIASILI

    1.0 UTANGULIZI:

    Kozi hii ambayo humtayarisha mwanafunzi kwenye ajira katika sekta za Kilimo na sekta za Maliasili, pia

    inamuandaa mwanafunzi kujiajiri mwenyewe na wanafunzi wengine wanaandaliwa kuendelea na

    masomo ya juu zaidi katika fani hii.

    Wote tunafahamu kuwa Dunia sasa inapita kwenye kipindi cha Utandawazi na nyenzo kuu ya

    Utandawazi ni Teknolojia hii ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)

    2.0 UMUHIMU WA TEHAMA KATIKA KILIMO NA MAISHA YA KILA SIKU:

  • Somo la TEHAMA limeingizwa kwenye mtaala wa Kilimo na Maliasili ili kumwezesha mwanafunzi

    kujiandaa kwenye huu Ulimwengu wa Utandawazi.

    Je nini umuhimu wa TEHAMA kwa maisha ya binadamu ya kila siku? Kwa kawaida binadamu

    anapambana na mambo ya msingi kila siku katika kujiendeshea maisha yake. Ajira, elimu, manunuzi na

    masuala ya kibenki yanaweza kuwa ni mambo machache tu ambayo binadamu anapambana nayo kila

    siku. Kabla ya ugundunduzi wa TEHAMA ilikuwa ni ngumu sana kuweza kukabiliana na mambo haya kwa

    sababu ilihitaji mtu kusafiri hata mamia ya kilometa ili kuweza kufanya lolote katika hayo yaliyotajwa

    hapo juu. Leo mtu hahitaji kutembea hata mita moja kuweza kutatua matatizo yake. Yote haya

    yamewezeshwa na TEHAMA.

    TEHAMA imebadili maisha ya kila siku, kwa mfano kuandika barua ambayo inakwenda umbali mrefu na

    kuchukua siku tano au sita hadi kufika huko inakokwenda, sasa tunatumia Barua Pepe ambazo

    zinachukua chini ya dakika moja kufika kwa mpokeaji popote pale alipo duniani, kununua bidhaa leo

    popote zilipo huhitaji kwenda zinapouzwa kwa sababu teknolojia inakuwezesha kuagiza na kupata bila

    kutoka nje ya mahali unapoagizia. Sasa hivi siyo lazima uende Maktaba kwenda kujisomea vitabu na

    majarida mbali mbali kwani unaweza kusoma vitabu hivyo na majarida mbali mbali kwa kujisomea

    kupitia TEHAMA!

    Mifano hiyo michache inaonesha kuwa hata wanafunzi wetu hawawezi kukwepa matumizi ya TEHAMA

    na ndiyo maana wataalamu wetu waliamua kuliweka somo hili ndani ya mtaala wa Kilimo na Maliasili.

    Tunapoongea Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) tuna maana ni mkusanyiko mkubwa wa

    aina mbali mbali za Teknoljia hii, kuanzia redio, televisheni, simu za mkononi na hizi za kisasa (smart

    phone), kompyuta na vifaa vyake mtambuka, progamu mbalimbali na pia mawasiliano ya setilaiti.

    3.0 TEHAMA KATIKA KUMWANDAA MWANAFUNZI:

    Somo letu la TEHAMA limejikita katika mambo matatu katika kumwandaa mwanafunzi. Kwanza kabisa ni

    katika kuboresha na kuongeza uzalishaji wa kilimo, pili ni uboreshaji wa masoko yatokanayo na bidhaa

    za kilimo na mwisho kuwajengea uwezo wadau wa kilimo wakiwemo wakulima ambao ndiyo msingi

    mkubwa wa kilimo chenyewe.

    4.0 TEHAMA KATIKA KUBORESHA KILIMO NA MASOKO YA MAZAO:

    Ni namna gani uongezaji na uboreshaji wa kilimo unafanyika? Ni kufanya ufuatiliaji katika kuongeza

    ubora wa uzalishaji na udhibiti wa mazao kwa wakulima wadogo kwa kuwezesha upatikanaji wa taarifa

    muhimu za wadudu na udhibiti wa wadudu hao, ikiwemo kutoa taarifa mapema, kama kuna wadudu na

    magonjwa mapya, aina mpya za kukabiliana na wadudu hao. Pia kutoa sheria na taratibu husika katika

    kupambana na wadudu na madawa yake ili kulinda mazingira pia.

    Uboreshaji wa masoko. Hili limesimama kwenye ufuatiliaji katika kuangalia masoko mapya, bei katika

    masoko hayo, usimamizi katika wa maamuzi katika kufikiria mazao mapya yanayokubalika katika soko,

    wakati mzuri na mahali pazuri pa kuuza bidhaa za kilimo. Uhuishaji wa taarifa za masoko, bei za bidhaa

    na watumiaji.

  • 5.0 UELIMISHAJI KWA WAKULIMA:

    Hili ni muhimu sana kwani linawapa uwezo katika uwakilishi hasa linapokuja suala la majadiliano

    yanayohusu bidhaa zao za kilimo na utaalamu pia wa teknolojia mpya.

    6.0 UMUHIMU WA TEHAMA KATIKA MASUALA YA MALIASILI.

    Ukweli ni kwamba nchi masikini zipo kwenye changamoto kubwa sana katika kupambana na uchafuzi wa

    mazingira. Ongezeko la watu pia ni changamoto nyingine. Teknolojia sasa inawezesha kukusanya

    takwimu bila kuzunguka eneo lolote la dunia. TEHAMA inaweza kutumika katika kuboresha namna bora

    ya utunzaji wa Ardhi na Maji! Ipo mifumo ya kitehama inayotumika kwa mfano GIS (Geographical

    Information System) katika ukusanyaji wa takwimu mbalimbali.

    7.0 UMUHIMU WA SOMO LA TEHAMA KUFUNDISHWA KATIKA CHUO CHETU:

    Kwa maelezo haya unaweza ukaona namna somo la TEHAMA linavyomuwezesha mwanafunzi wetu

    kwenda kukabiliana na changamoto mara tu anapotoka chuoni na kupata ajira, au kujiajiri. Ukweli ni

    kwamba TEHAMA imefanya dunia sasa kuwa ni kijiji na sisi Watanzania hatuwezi kuikwepa kwa

    kujifanya ni kisiwa kwani hili litaturudisha nyuma na kufanya hali zetu kuwa duni.

  • MFUMO ELEKEZI WA MAFUNZO KUANZIA CHETI HADI UDAKTARI WA FALSAFA

    NGAZI YA NTA UMAHIRI WA MAFUNZO MAJUKUMU ATAKAYOFANYA

    4 (Basic Technician Certificate)

    Umahiri wa kutumia ujuzi na maarifa katika stadi za kazi za kila siku

    Uwezo wa:

    Kufanya kazi mwenyewe au na wengine kwa kazi ya kuongozwa

    Kufanya kazi mwenyewe au na wengine kwa usimamizi wa karibu

    5 (Technician Certificate)

    Umahiri wa kutumia ujuzi na maarifa katika stadi za kazi kadhaa, ambazo baadhi yake si kazi za kila siku

    Uwezo wa:

    Kufanya kazi mwenyewe au na wengine kwa kazi ya kuongozwa

    Kufanya kazi chini ya uangalizi na ufanisi bora

    Kufanya kazi na kuwa na wajibu wa kuwaongoza wengine

    6 (Ordinary Diploma)

    Umahiri wa kutumia ujuzi na maarifa katika aina nyingi za kazi, ambazo baadhi yake si kazi za kila siku

    Uwezo wa:

    Kufanya kazi mwenyewe au na wengine katika kundi kwa kiwango fulani cha kujitegemea

    Kufanya kazi kwa kusimamiwa na kukaguliwa ubora

    Kufanya kazi kwa kuwajibika kwa matokeo ya uzalishaji wa kutosha na bora

    Kusimamia rasilimali chache za uzalishaji bila ufujaji

    Kufanyakazi kwa kuwajibika kwa matokeo ya kazi za wengine

    7 (Higher Diploma)

    Umahiri wa kutumia ujuzi na maarifa katika aina nyingi tata za kazi, wajibu binafsi wa hali ya juu wa kutenda kazi na wajibu wa kusimamia kwa kiasi kazi za wengine

    Uwezo wa:

    Kufanya kazi mwenyewe au na wengine kwa kujituma

    Kufanya kazi kwa kusimamiwa na kukaguliwa ubora

    Kufanya kazi kwa kuwajibika kikamilifu kwa matokeo ya

  • uzalishaji wa kutosha na bora

    Kufanyakazi kwa kuwajibika kwa matokeo ya kazi za wengine zilizopo katika maeneo maalum

    Kutenda kwa ubunifu bila msaada kazi maalumu za kitaaluma

    8 (Barchelor Degree)

    Umahiri wa kutumia ujuzi na maarifa katika aina nyingi za kazi zisizotabirika zikihusisha wajibu binafsi wa hali ya juu kutenda kazi na wajibu wa kusimamia kazi za wengine, na upangaji wa raslimali, kubuni, kutekeleza na kutathmini sera

    Uwezo wa:

    Kufanya kazi mwenyewe au na wengine kwa kujituma na pengine kutumwa

    Kufanya kazi chini ya miongozo mipana

    Kufanya kazi kwa kuwajibika kikamilifu kwa aina na matokeo ya uzalishaji wa kutosha na bora

    Kufanyakazi kwa kuwajibika kikamilifu kwa kupata matokeo ya kazi za makundi

    Kufanya kazi kwa kuwajibika kikamilifu juu ya ugawaji rasilimali, usimamizi wa sera, mipango, utekelezaji na tathmini.

    Kutenda kwa ubunifu bila msaada kazi maalumu za kitaaluma

    Kugawa majukumu kwa watumishi wa ngazi za chini

    9 (Masters Degree)

    Umahiri uliobobea kumudu eneo tata na maalumu la ujuzi na maarifa kuweza kufanyakazi za taaluma ya hali ya juu.

    Uwezo wa:

    Kuwa mwanzilishi, mbunifu na mwajibikaji binafsi

    Kutekeleza kwa hali ya juu ya wajibu na ubunifu kazi za kitaaluma na zinazofanana nazo

    Kuwa na wajibu wa

  • kusimamia majukumu ya kazi maalum za wengine

    Kusimamia wajibu na majukumu yako na ya wengine katika kutenda na kutathmini kazi.

    Kufanya shughuli za kitaaluma kulingana na taaluma na maadili ya kisasa

    Kutimiza uhalisia na ubunifu katika kutumia maarifa, uelewa na uzoefu

    10 (Doctorate Degree)

    Umahiri uliobobea kumudu eneo tata na maalumu la ujuzi na maarifa kuweza kufanyakazi za taaluma na tafiti za hali ya juu.

    Uwezo wa:

    Kutekeleza kwa hali ya juu wajibu na ubunifu wa kazi za kitaaluma

    Kudhihirisha uongozi na uhalisia wa kutatua matatizo ya kitaaluma

    Kushughulikia maadili na taaluma tata na kutoa maamuzi sahihi juu ya masuala yasiyo husiana na taaluma ya sasa.

  • A. KOZI ZINAZOFUNDISHWA (PROGRAMS OF STUDY):

    Tick to choose

    COURSE LEVEL DURATION NACTE AWARD

    ( ) Agriculture & Natural Resources Management

    NTA Level 4 1 year Basic Technician Certificate

    ( ) Agriculture & Natural Resources Management

    NTA Level 5 1 year Technician Certificate

    ( ) Agriculture & Natural Resources Management

    NTA Level 6 1 year Ordinary Diploma

    B. MODULES PER SEMESTER/LEVEL

    a. LEVEL 4

    i. SEMESTER 1

    S/N Module Code Module Name Hours CREDIT

    1. ANT04101 Environmental management and assessment 7 10

    2 ANT04102 Environmental Land use and planning 7 9

    3 GST04113 Basics of Mathematics Applications 2 3

    4 GST04114 Agricultural Biology (Zoology and Botany) 3 4

    5 GST04115 Agricultural Chemistry (Biochemistry and Physical Chemistry 2 3

    6 GST04116 Principles of Agro physics 2 3

    7 GST04117 Communication Skills 2 3

    ii. SEMESTER 2

    1 ANT04203 Principles of Crop Production 8 10

    2 ANT04204 Agriculture and Environment 7 9

    3 ANT04205 Small Scale Irrigation 7 8

    4 ANT04206 Basic Animal Production 7 10

    5 ANT04207 Animal Breeding 5 8

    6 ANT04208 Field Crops Production 5 8

    7 ANT04209 Animal Anatomy and Physiology 4 6

    8 ANT04210 Aquaculture and Fisheries Management 7 11

    9 ANT04211 Production of Seed Crops 5 6

    10 ANT04212 Farm Practical 5 7

    11 GST04218 Computer Applications 2 3

    12 GST04219 Farm Records and Record Keeping 3 4

  • b. LEVEL 5 i. SEMESTER 1

    1. ANT 05101 Pasture Production 5 7

    2. ANT 05102 Monogastric Animal Production and Management 5 8

    3. ANT 05103 Farm structure and Facilities 4 6

    4. ANT 05104 Soil and Water Conservation 5 8

    5. ANT 05106 Community Based Natural Resources Management 6 9

    6. ANT 05107 Livestock Diseases, Control and Treatment 5 8

    7. ANT 05109 Ruminant Animal Production and Management 5 8

    8. GST 05105 Dissemination of Crop and Livestock Technologies 3 4

    9. GST 05108 Entrepreneureship Development 2 3

    ii. SEMESTER 2

    1. ANT 05210 Management of Horticultural Crops 4 6

    2. ANT 05211 Principles of Ecology 5 8

    3. ANT 05212 Sustainable Agro Forestry Management and Beekeeping 6 9

    4. ANT 05213 Crop Protection 6 9

    5. ANT 05215 Harvest and Post Harvest Handling 5 7

    6. ANT 05216 Handling Care and Processing of Livestock Products. 5 7

    7. GST 05217 HIV/AIDS, Gender and Development 2 3

    8. GST 05214 Agribusiness 3 4

    9. ANT 05218 Field Practical 7 7

    c. LEVEL 6

    i. SEMESTER 1

    S/N Code Module name Semester

    1 2

    1 GST06101 Field Data Management 5 7

    2 GST06102 Agro-Forestry Economy 5 8

    3 GST06103 Farm Mechanization 5 8

    4 GST06104 Research Methods 5 7

    6 ANT06106 Animal Nutrition and Feeding 7 10

    7 ANT06107 Plantation Crops 6 9

    8 ANT06108 Land Surveying and Mapping 6 9

    9 GST06113 Agricultural Extension 5 8

  • ii. SEMESTER 2

    1 ANT06209 Meat Hygiene and Inspection 6 9

    2 ANT06210 Agricultural Marketing 5 8

    3 ANT06211 Project Planning, Monitoring and Evaluation 5 8

    4 ANT06214 Field practical 7 10

    5 GST06215 Industrial Internship 3 5

    6 GST06205 Crop and Livestock Experimentation 5 8

    7 ANT06212 Ecosystems and Environmental Management 7 11