4
MAANDALIZI YA TIMU YA BANANA KWA LIGI YA WILAYA Jarida litolewalo na Banana Investments Limited, Toleo Na.11, Oktoba—Desemba 2008 Timu ya mpira wa miguu ya Klabu ya Ba- nana inazidi kuimarika baada ya kukumbana na mikikimikiki ya mashindano mbalimbali ili kuji- weka kwenye nafasi ya kufanya vizuri kwenye ligi ya wilaya ya Arusha iliyoanza wiki ya pili ya No- vemba 2008. Kunako mwezi Septemba mwaka huu uon- gozi wa wa klabu uliandaa ligi ya “KOMBE LA MBUZI” ili kujipima nguvu kabla ya ligi ya wilaya kuanza. Jumla ya timu kumi na mbili zilishiriki na kutoa ushindani mkubwa. Timu ya mpira wa miguu ya Klabu ya Banana ilifanikiwa kuingia robo fainali lakini haikuwa miongoni mwa timu zilizoshinda zawadi. Hata hivyo, kushiriki kwao kulisaidia sana kuwanoa wachezaji na matunda yake yameanza kuonekana timu iliposhinda mechi ya kwanza ya ligi ya wilaya kwa kishindo. Mashindano ya KOMBE LA MBUZI yali- malizika vizuri na washindi kupatikana bila utata. Timu iliyokuwa mshindi wa kwanza, Lemara Boys FC, ilizawadiwa mbuzi mwenye thamani ya TZS 50,000/=. Timu ya Hardrock FC ilikuwa mshindi wa pili nayo ikazawadiwa TZS 25,000/= Kadhalika timu iliyokuwa mshindi wa tatu, Tanga- nyika Packers FC, ilizawadiwa TZS 15,000/=. Mfungaji bora katika ligi hiyo, ndugu John Mas- sawe aliyeifungia timu ya Hardrock FC jumla ya magoli tisa, alizawadiwa TZS 10,000/=. Washiriki wa ligi hiyo walishukuru sana uongozi wa Banana Sports Club kwa kuandaa ligi hiyo kwa mafanikio. Katika hatua nyingine, timu ya mpira wa miguu ilishiriki katika mashindano ya “CHEZA SALAMA CUP” yaliyoratibiwa na P.S.I, tawi la Arusha. Kati ya timu nane zilizoshiriki mashindano hayo timu ya Banana ilikuwa mshindi wa nne. Mshindi wa kwanza wa mashindano hayo ni Baptist FC huku Tanganyika Packers wakiwa nafasi ya pili. Nafasi ya tatu ya ushindi ilichukuliwa na Gymkana FC. Mwishoni mwa mwezi Oktoba 2008, uon- gozi wa klabu kwa kushirikiana na Kampuni ya Ba- nana waliandaa hafla fupi kwa ajili ya kuiwezesha timu ya mpira kujinunulia mahitaji muhimu. Kwa wingi washiriki wa hafla hiyo walikuwa ni viongozi na wafanyakazi wa Kampuni ya Banana. Jumla ya TZS 730,000/= zilikusanywa na timu ikaweza kununua mahitaji mbalimbali zikiwemo jezi, mipira na viatu. Imeandikwa na Adrian Anthony Mwaka huu wanachama wa Klabu ya Michezo ya Banana walifanya safari mbili kutembe- lea mbuga za wanyama na vivutio vingine vya utalii. Hii iliku wa mojawapo ya burudani kwa washiriki na ni mfano hai wa Watanzania kuchangia katika kuendeleza utalii wa ndani wa nchi yao. Safari ya kwanza ilikuwa ni ya kutembelea kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Manyara, safari iliyodhaminiwa na Kampuni ya Banana kupitia kinywaji cha RAHA Alcoholic Beverage na kipenga cha kuanza safari kilipulizwa na kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Banana, Bibi Alphoncina A. Olomi. Mbali na kufurahia kuona na kujivunia mandhari nzuri ya asili ya nchi yao, wanamichezo hao walijikuta wakichanganyika na watalii wa ku- toka nje ya nchi, jambo lililoleta hamasa kubwa kwa pande zote mbili. Watalii hao wa kigeni walifurahia sana kinywaji cha RAHA hata baadhi wakaomba kuondoka na chupa chache. Kwa msaada wa safari hiyo, baadhi ya wanamichezo walipata fursa ya kuanzisha urafiki na wageni kutoka nje ya Tanzania. Ziara ya pili ya wanamichezo wa Klabu ya Banana ilikuwa ya kutembelea Ziwa Duluti. Kwa kuwa ziwa hili liko karibu na Arusha wanamichezo walichangia gharama za safari hiyo bila ya kuomba ufadhili. Wanamichezo walipata habari mbalimbali kuhusu ziwa hilo la ajabu ambalo halipungui au kuongezeka kina kwa majira yote na wakahitimisha safari hiyo kwa kushiriki pamoja chakula cha jioni na kucheza muziki kabla ya kurejea Arusha. Ziara ya tatu ya utalii wa ndani iko mbioni kwani maandalizi ya safari ya kupanda Mlima Meru mwishoni mwa mwezi Novemba yanakaribia ku- kamilika. Imeandikwa na Adrian Anthony WANACHAMA WA KLABU YA BANANA WASHIRIKI UTALII WA NDANI Wanamichezo wakiwa na watalii Manyara Toleo la 11 Oktoba—Desemba 2008 5 SERA YA KAMPUNI KUHUSU MAFUNZO 3 7 AJIRA MPYA YA WAFANYAKAZI ROBO MWAKA YA PILI 2008 4 8 TIMU YA MPIRA WA MIGUU YA BANANA KUSHIRIKI LIGI YA WILAYA 4 3 MAONYESHO YA SABA SABA 2008 2 6 SHEREHE YA WAFANYAKAZI 2008 3 4 MAADHIMISHO YA WIKI YA MAZINGIRA 2 Banana Investments Limited KAMATI YA UHARIRI Augustine S. Minja—Mwenyekiti Beatha A. Massawe– Katibu Patrick S. Mushi—Mjumbe Philbert A. Muhindi – Mjumbe Gerald Limo—Mjumbe 1. SALAAM ZA MKURUGENZI MTENDAJI 2 2. SURA MPYA YA MBIU YA BANANA 2 3. MIKAKATI YA BANANA SACCOS KUJIKWAMUA KIUCHUMI 3 5. MOYO WA KUTHUBUTU KUTENDA: BARACK OBAMA VS BIL 4 6. KAMPUNI YA BANANA INAVYOSAIDIA KUINUA KIPATO CHA WATANZANIA 5 10. AJIRA MPYA KAMPUNI YA BANANA 7 11. MAANDALIZI YA TIMU YA BANANA KWA LIGI YA WILAYA 8 12. WANACHAMA WA KLABU YA BANANA WASHIRIKI UTALII WA NDANI 8 9. WAKAZI WA OLOIRIEN WAPATIWA SEMINA YA UKIMWI 6 8. UTEKELEZAJI WA SERA YA ELIMU YA KAMPUNI YA BANANA WAANZA 6 4. NAMNA YA KUTIBU MNING’INIO 3 7. KIBONZO 5 YALIYOMO Banana Investments Limited MAWASILIANO [Banana Investments Limited] Makao Makuu: Oloirien Village, SLP 10123 ARUSHA, Simu 027 250 6475, 075 422 4440, 075 488 8470. Fax 027 250 1549. Email [email protected] …………………………………………………………………………………………………………… Dar es Salaam Depot: Ubungo Kibangu, karibu na Kituo cha Poilisi cha Ubungo Kibangu, SLP: 79407 Dar es Salaam, Simu: 022 277 4276, 075 670 7983. …………………………………………………………………………………………………………… Tanga Depot: Barabara ya 4, karibu na Stendi ya Mabasi ya TAWAKAL, S.L.P. 5150 Tanga, Simu: 027 264 6134. For more details, please visit our website on (http://www.banana.co.tz)

MBIU YA BANANA TOLEO LA 11 FN · Ndugu wasomaji wa Mbiu ya Banana, viongozi, wafanyakazi, wateja na watumiaji wa bidhaa zetu: 1. Napenda kuchukua nafasi hii kuwatakia heri ya

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: MBIU YA BANANA TOLEO LA 11 FN · Ndugu wasomaji wa Mbiu ya Banana, viongozi, wafanyakazi, wateja na watumiaji wa bidhaa zetu: 1. Napenda kuchukua nafasi hii kuwatakia heri ya

MAANDALIZI YA TIMU YA BANANA KWA LIGI YA WILAYA

Jarida litolewalo na Banana Investments Limited, Toleo Na.11, Oktoba—Desemba 2008

Timu ya mpira wa miguu ya Klabu ya Ba-nana inazidi kuimarika baada ya kukumbana na mikikimikiki ya mashindano mbalimbali ili kuji-weka kwenye nafasi ya kufanya vizuri kwenye ligi ya wilaya ya Arusha iliyoanza wiki ya pili ya No-vemba 2008.

Kunako mwezi Septemba mwaka huu uon-gozi wa wa klabu uliandaa ligi ya “KOMBE LA MBUZI” ili kujipima nguvu kabla ya ligi ya wilaya kuanza. Jumla ya timu kumi na mbili zilishiriki na kutoa ushindani mkubwa. Timu ya mpira wa miguu ya Klabu ya Banana ilifanikiwa kuingia robo fainali lakini haikuwa miongoni mwa timu zilizoshinda zawadi. Hata hivyo, kushiriki kwao kulisaidia sana kuwanoa wachezaji na matunda yake yameanza kuonekana timu iliposhinda mechi ya kwanza ya ligi ya wilaya kwa kishindo. Mashindano ya KOMBE LA MBUZI yali-malizika vizuri na washindi kupatikana bila utata. Timu iliyokuwa mshindi wa kwanza, Lemara Boys FC, ilizawadiwa mbuzi mwenye thamani ya TZS 50,000/=. Timu ya Hardrock FC ilikuwa mshindi wa pili nayo ikazawadiwa TZS 25,000/= Kadhalika timu iliyokuwa mshindi wa tatu, Tanga-nyika Packers FC, ilizawadiwa TZS 15,000/=.

Mfungaji bora katika ligi hiyo, ndugu John Mas-sawe aliyeifungia timu ya Hardrock FC jumla ya magoli tisa, alizawadiwa TZS 10,000/=. Washiriki wa ligi hiyo walishukuru sana uongozi wa Banana Sports Club kwa kuandaa ligi hiyo kwa mafanikio. Katika hatua nyingine, timu ya mpira wa miguu ilishiriki katika mashindano ya “CHEZA SALAMA CUP” yaliyoratibiwa na P.S.I, tawi la Arusha. Kati ya timu nane zilizoshiriki mashindano hayo timu ya Banana ilikuwa mshindi wa nne. Mshindi wa kwanza wa mashindano hayo ni Baptist FC huku Tanganyika Packers wakiwa nafasi ya pili. Nafasi ya tatu ya ushindi ilichukuliwa na Gymkana FC. Mwishoni mwa mwezi Oktoba 2008, uon-gozi wa klabu kwa kushirikiana na Kampuni ya Ba-nana waliandaa hafla fupi kwa ajili ya kuiwezesha timu ya mpira kujinunulia mahitaji muhimu. Kwa wingi washiriki wa hafla hiyo walikuwa ni viongozi na wafanyakazi wa Kampuni ya Banana. Jumla ya TZS 730,000/= zilikusanywa na timu ikaweza kununua mahitaji mbalimbali zikiwemo jezi, mipira na viatu.

Imeandikwa na Adrian Anthony

Mwaka huu wanachama wa Klabu ya Michezo ya Banana walifanya safari mbili kutembe-lea mbuga za wanyama na vivutio vingine vya utalii. Hii iliku wa mojawapo ya burudani kwa washiriki na ni mfano hai wa Watanzania kuchangia katika kuendeleza utalii wa ndani wa nchi yao.

Safari ya kwanza ilikuwa ni ya kutembelea kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Manyara, safari iliyodhaminiwa na Kampuni ya Banana kupitia kinywaji cha RAHA Alcoholic Beverage na kipenga cha kuanza safari kilipulizwa na kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Banana, Bibi Alphoncina A. Olomi.

Mbali na kufurahia kuona na kujivunia mandhari nzuri ya asili ya nchi yao, wanamichezo hao walijikuta wakichanganyika na watalii wa ku-toka nje ya nchi, jambo lililoleta hamasa kubwa kwa pande zote mbili. Watalii hao wa kigeni walifurahia sana kinywaji cha RAHA hata baadhi wakaomba kuondoka na chupa chache. Kwa msaada wa safari hiyo, baadhi ya wanamichezo walipata fursa ya kuanzisha urafiki na wageni kutoka nje ya Tanzania.

Ziara ya pili ya wanamichezo wa Klabu ya Banana ilikuwa ya kutembelea Ziwa Duluti. Kwa kuwa ziwa hili liko karibu na Arusha wanamichezo walichangia gharama za safari hiyo bila ya kuomba ufadhili. Wanamichezo walipata habari mbalimbali kuhusu ziwa hilo la ajabu ambalo halipungui au kuongezeka kina kwa majira yote na wakahitimisha safari hiyo kwa kushiriki pamoja chakula cha jioni na kucheza muziki kabla ya kurejea Arusha.

Ziara ya tatu ya utalii wa ndani iko mbioni kwani maandalizi ya safari ya kupanda Mlima Meru mwishoni mwa mwezi Novemba yanakaribia ku-kamilika.

Imeandikwa na Adrian Anthony

WANACHAMA WA KLABU YA BANANA WASHIRIKI UTALII WA NDANI

Wanamichezo wakiwa na watalii Manyara

Toleo la 11

Oktoba—Desemba 2008

1 TUSAIDIANE KUENDELEZA JARIDA HILI 2 2 MKUTANO WA LEON H. SULLIVAN WAFANYIKA ARUSHA. 2

5 SERA YA KAMPUNI KUHUSU MAFUNZO 3

7 AJIRA MPYA YA WAFANYAKAZI ROBO MWAKA YA PILI 2008 4 8 TIMU YA MPIRA WA MIGUU YA BANANA KUSHIRIKI LIGI YA WILAYA 4

3 MAONYESHO YA SABA SABA 2008 2

6 SHEREHE YA WAFANYAKAZI 2008 3

4 MAADHIMISHO YA WIKI YA MAZINGIRA 2

YALIYOMO

Banana Investments Limited

BODI YA WAHARIRI

KAMATI YA UHARIRI

Augustine S. Minja—Mwenyekiti

Beatha A. Massawe– Katibu

Patrick S. Mushi—Mjumbe

Philbert A. Muhindi – Mjumbe

Gerald Limo—Mjumbe

1. SALAAM ZA MKURUGENZI MTENDAJI 2 2. SURA MPYA YA MBIU YA BANANA 2 3. MIKAKATI YA BANANA SACCOS KUJIKWAMUA KIUCHUMI 3

5. MOYO WA KUTHUBUTU KUTENDA: BARACK OBAMA VS BIL 4 6. KAMPUNI YA BANANA INAVYOSAIDIA KUINUA KIPATO CHA WATANZANIA 5

10. AJIRA MPYA KAMPUNI YA BANANA 7 11. MAANDALIZI YA TIMU YA BANANA KWA LIGI YA WILAYA 8

12. WANACHAMA WA KLABU YA BANANA WASHIRIKI UTALII WA NDANI 8

9. WAKAZI WA OLOIRIEN WAPATIWA SEMINA YA UKIMWI 6 8. UTEKELEZAJI WA SERA YA ELIMU YA KAMPUNI YA BANANA WAANZA 6

4. NAMNA YA KUTIBU MNING’INIO 3

7. KIBONZO 5

YALIYOMO

Banana Investments Limited

MAWASILIANO [Banana Investments Limited]

Makao Makuu: Oloirien Village, SLP 10123 ARUSHA, Simu 027 250 6475,

075 422 4440, 075 488 8470. Fax 027 250 1549. Email [email protected]

……………………………………………………………………………………………………………

Dar es Salaam Depot: Ubungo Kibangu, karibu na Kituo cha Poilisi cha

Ubungo Kibangu, SLP: 79407 Dar es Salaam, Simu: 022 277 4276, 075 670 7983.

……………………………………………………………………………………………………………

Tanga Depot: Barabara ya 4, karibu na Stendi ya Mabasi ya TAWAKAL,

S.L.P. 5150 Tanga, Simu: 027 264 6134.

For more details, please visit our website on (http://www.banana.co.tz)

Page 2: MBIU YA BANANA TOLEO LA 11 FN · Ndugu wasomaji wa Mbiu ya Banana, viongozi, wafanyakazi, wateja na watumiaji wa bidhaa zetu: 1. Napenda kuchukua nafasi hii kuwatakia heri ya

Ndugu wasomaji wa Mbiu ya Banana, viongozi, wafanyakazi, wateja na watumiaji wa bidhaa zetu:

1. Napenda kuchukua nafasi hii kuwatakia heri ya Krismas na mafanikio kwa mwaka mpya 2009. Pia ninatoa shukrani zangu za dhati kwa ushirikiano mliotupa mwaka unaoisha kwa msaada wenu katika kuiwezesha kampuni kufikia malengo yake.

2. Ninafurahi kuwafahamisha kuhusu baadhi ya maendeleo yaliyofanyika hadi sasa:

2.1 Mwaka huu mwanzoni tulifunga Bohari ya Tarakea na kuhamishia bohari ya Dar es Sa-laam Ubungo Kibangu kwa sababu za kiufundi. Bohari ya Dar es Salaam iliongeza mauzo na kuendelea kuhudumia mkoa wa Morogoro.

2.2 Kulikuwa na ongezeko la mauzo nchi nzima kwa vipindi vyote vya mwaka ikilinganishwa na mwaka uliopita. Sehemu kubwa ya usafirishaji na usambazaji wa bidhaa ulifany-ika kwa kutumia magari ya kampuni.

2.3 Mazingira ya uzalishaji yaliboreshwa na machine kuchukua sehemu kubwa ya usindikaji wa bidhaa na ufungashaji.

2.3.1 Mashine za ufungashaji ziolizoagizwa mwaka huu zimeanza kuwasili kiwandani na zinatarajiwa kufungwa na kuanza uzalishaji mapema mwakani.

2.3.2 Ubora wa bidhaa umedumishwa na hatujapokea malalamiko au bidhaa duni kurejeshwa kutoka kwa wateja.

Mwisho ninawaomba muendelee na ushikiano huo mwakani ili tuweze kuendelea kufanya kazi na bi-ashara pamoja.

Asanteni sana.

A.R. Olomi

MKURUGENZI MTENDAJI

Jarida litolewalo na Banana Investments Limited, Toleo Na.11, Oktoba—Desemba 2008

SALAAM ZA MKURUGENZI MTENDAJI

SURA MPYA YA MBIU YA BANANA Ndugu wasomaji, Natumaini mmeona na kutambua kuwa toleo hili la 11 la Mbiu ya Banana limeboreshwa na kuwa na kurasa nane badala ya nne tulizozoea. Hii ni hatua nzuri ya maendeleo ambayo kila msomaji ataifurahia. Hata hivyo naomba ikumbukwe kuwa kuongezeka kwa kurasa za jarida hili kunahitaji makala nyingi kuzijaza, ndiyo maana ninarejea tena ombi la kupata makala kutoka kwa wasomaji—wafanyakazi, wateja na watumiaji wa bidhaa zinazozalishwa na Kampuni ya Banana. Motisha itaendelea kutolewa kwa kila makala itakayochapishwa katika jarida hili bila kujali ni hadithi, vichekesho, habari na hata vibonzo. Kwa niaba ya kamati ya wahariri ninawapon-geza sana ndugu Gerald Lyimo na Ndugu Elipidi J. Urassa kwa kutuanzishia SAFU YA WASOMAJI ukurasa wa 4. na 5. Wamekuwa na moyo wa kuthu-butu kutenda nawakafanikiwa kwa pigo moja tu. Ni-nawaomba waendelee kutuletea makala na pia wawa-himize wasomaji wengine kufanya hivyo.

Baadhi ya wajumbe wa kamati ya uhariri wameondoka na wengine wapya kushika nafasi zao. Napenda kuwapongeza wajumbe wa kamati wanaoon-doka, ambao ni ndugu Michael Bessa, Adolf Mlay na Ibrahim Shigella, kwa ushirikiano waliotoa kuanzisha na kuendeleza jarida hili la Mbiu ya Banana. Pia nawakaribisha wajumbe wapya, ndugu Philbert A. Muhindi na Gerald Lyimo, kwa mategemeo ya kupata ushirikiano wao na hasa mchango wa mawazo mapya. Kuhusu mawasiliano anwani za posta na simu muhimu za Kampuni ya Banana zinaonekana ukurasa wa mbele wa kila toleo la jarida hili, Pia rejea tuvuti (http://www.banana.co.tz). Ninawatakieni Heri ya Krismas na Mwaka Mpya 2009 wenye baraka na mafanikio mengi. Augustine S. Minja Mhariri Mkuu

Jarida litolewalo na Banana Investments Limited, Toleo Na.11, Oktoba—Desemba 2008

SOMA Mbiu ya Banana KILA MARA

Richard Emanuel - Muhudumu wa Uzalishaji.

Bw. Geofery Sakware – Dereva Mauzo

Bw. Allen Festo Ngalo – Fundi.

Omary Mwenda – Muhudumu wa Uzalishaji

Bw. Oswald Jacob Salla – Dereva Mauzo.

Jarida litolewalo na Banana Investments Limited, Toleo Na.11, Oktoba—Desemba 2008

Bw. Jullius Mallya – Dereva Mauzo.

Bi. Joyce Lyimo - Karani wa Mahesabu

Ndani ya kipindi cha miezi mitatu hadi sita iliyopita kampuni imeona umuhimu wa kuajiri wafanyakazi wapya katika nafasi mbalimbali kama ifuatavyo:

AJIRA MPYA KAMPUNI YA BANANA

Bw. Nicholaus Shayo - Dereva Mauzo Bw. Himid Mailla - Dereva Mauzo

Bw. Philbert A. Mhindi - Meneja Utawala

Bw. Thobias Motika - Fundi Umeme Bw. Deogratius A. Mhindi - Fundi Umeme wa Magari

Philbert ana stashahada ya Utawala wa Jamii (Advanced Diploma in Public Administration) ya Chuo cha Mzumbe na uzoefu wa miaka kumi na moja katika fani ya Utawala.

Geofrey ana elimu ya kidato cha sita, na uzoefu wa miaka mitatu akiwa dereva wa mauzo.

Betty ana elimu ya kidato cha sita na stashahada ya computa programs ya Digital Equipments Co. A/S Nairobi. Pia ana cheti cha NABE. (National Business Examinations) uzoefu wa miaka 10 akiwaKatibu Mu-htasi.

Oswald ana elimu ya kidato cha nne na cheti cha ufundi wa magari.

Deogratius ana elimu ya kidato cha nne, cheti cha ufundi umeme cha VETA na uzoefu wa miaka mitatu akiwa fundi

Allen ana cheti cha ufundi wa kuchomelea vyuma mbalimbali na uzoefu wa mwaka mmoja katika fani hii.

Richard ana elimu ya kidato cha nne cha ufundi na uzoefu wa miaka miwili katika fani hii ya uzalishaji.

Omary ana uzoefu wa miaka miwili katika fani hii ya uzalishaji

Joyce ana elimu ya kidato cha nne na cheti cha computa programs ikiwepo cha Accounting packages. Ana uzoefu wa miaka 5 kama katibu muhtasi na karani wa mahesabu.

Bi. Beatha A. Massawe - Afisa Mahusiano

Bi. Betty G. Mboya - Katibu Muhtasi

Beatha ana shahada ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Himidi ana elimu ya kidato cha nne, cheti cha udereva cha Chuo cha Taifa cha Usafirishaji Dar es Salaam, na uzoefu wa miaka 18 akiwa dereva.

Julius ana stashahada ya Uongozi wa Bi-ashara na uzoefu wa miaka sita akiwa ofisa mauzo.

Nicholaus ana elimu ya kidato cha nne, cheti cha Tour Guide & International Languages, na uzoefu wa miaka 3 akiwa dereva mauzo.

Thobias ana cheti cha Ufundi umeme kutoka Arusha Technical College na uzoefu wa miaka 2 akiwa fundi umeme.

Bw. Evance P. Ngowi - Mechanical Attendant Evance ana cheti cha ufundi na uzoefu wa miaka 2 akiwa mechanical attendant.

Living amehitimu kidato cha IV Uchira Secondary School na ana leseni ya udereva ya Kibo Driving School.

Imeandikwa na Patrick S. Mushi

Happy amehitimu kidato cha IV Kiman-dolu Secondary School na amekuwa mhudumu wa uzalishaji kwa mwaka mmoja.

Happy Mosses Mollel– Mhudumu wa Uzalishaji

Living Alois Olomi– Dereva wa Mauzo

Page 3: MBIU YA BANANA TOLEO LA 11 FN · Ndugu wasomaji wa Mbiu ya Banana, viongozi, wafanyakazi, wateja na watumiaji wa bidhaa zetu: 1. Napenda kuchukua nafasi hii kuwatakia heri ya

UTEKELEZAJI WA SERA YA ELIMU YA KAMPUNI YA BANANA WAANZA

Pamoja na jitihada za Kampuni ya Banana kuajiri watu wenye sifa kwa nafasi mbalimbali za kazi, mwaka huu kumekuwa na jitihada za ziada katika kutekeleza sera ya kampuni ya mafunzo. Mbali na wafanyakazi wanaojiendeleza katika muda wao, kam-puni imegharamia mafunzo ya wafanyakazi kama ifuatavyo: 1. Rogath Saleko Alijifunza udereva MODERN DRIVING SCHOOL kwa mwezi mmoja.

2. Julius Mallya Alijifunza udereva KIBO DRIVING SCHOOL kwa mwezi mmoja.

3. John Thomas Anasoma kozi ya “Stock Keeping & Stock Control” Chuo cha Tropical Institute Arusha kwa miezi mitatu.

4. Emmanuel Nevava Anasoma kozi ya “Materials Management” Arusha Commercial Collage kwa miaka miwili.

5. Patrick Mushi. Alichukua kozi ya Sheria Mpya za Kazi Chuo cha Usimamizi wa Mahakama, Lushoto kwa wiki moja. 6. Asantiel Moshi Alichukua kozi ya “Boiler Mechanics & Pipe Fitting Level III” Chuo cha Ufundi ,VETA Moshi, kwa miezi miwili. 7. Bruno Mlay Alijifunza Udereva Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (National Institute of Transport—Dar-es Salaam) kwa wiki tano. 8. Joseph Mushi Alijifunza udereva Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (National Institute of Transport—Dar-es- Salaam) kwa wiki tano. 9. Augustine S. Minja Kampuni ya Banana imemlipia ada ya Uanachama, Institute of Brewing & Distilling, London UK, 2008/2009.

Imeandikwa na Patrick S. Mushi

Jarida litolewalo na Banana Investments Limited, Toleo Na.11, Oktoba—Desemba 2008

WAKAZI WA OLOIRIEN WAPATIWA SEMINA YA UKIMWI.

Kuanzia mwaka jana Kampuni ya Banana imekuwa ikiandaa semina kuhusu UKIMWI kwa ajili ya wafanyakazi wake na kwa ajili ya wakazi wa maeneo yanayozunguka kiwanda. Semina hizo zime-kuwa zikiandaliwa na Banana Foundation kwa ushirikiano na Ofisi ya Kata ya Oloirien na Tumaini VTC, Njiro, Arusha.

Kwa kuwa semina hizo zilikuwa zikifany-ikia kiwandani, ni majirani wachache waliojitokeza kuhudhuria semina hizo. Ni baada ya kugundua ud-haifu huo ndipo uongozi wa Kampuni ya Banana, kupitia taasisi ya Banana Foundation, ukaandaa semina iliyofanyika Oktoba 11, 2008 katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Oloirien.

Katika semina hiyo wakazi 73 wa Kata ya Oloirien walielimishwa kuhusu athari za ugonjwa wa UKIMWI. Mbali na kuelimishwa kuhusu dalili za UKIMWI, washiriki wa semina walifundishwa namna ya kujikinga katika maisha ya kawaida na pia katika dharura mbalimbali, ikiwa pamoja na wan-apotoa huduma kwa waadhirika wa UKIMWI na inapobidi kuhudumia majeruhi wa ajali. Washiriki walikumbushwa kuhusu kuzingatia ngono salama kwa kutumia condom kila mara, kuwa waaminifu kwa wapenzi wao na kupima afya mara kwa mara.

Wanasemina walielimishwa kutumia gloves kila watakapolazimika kuhudumia waadhirika wa UKIMWI au majeruhi wa ajali. Tahadhari ni sharti ichukuliwe pale mhudumu anapokuwa na kidonda kilicho wazi. Kidonda ni sharti kifungwe mathubuti kuepuka kidonda kugusana na damu au maji maji kutoka mwili wa muathirika.

Semina ilikuwa ya mafanikio makubwa kwani washiriki 66, sawa na 90.4%, ya washiriki wote walijitokeza kupima UKIMWI kwa hiari.

Imeandikwa na

Beatha Anthony

NENDA UKAPIME AFYA YAKO

Wanasemina wa Ukimwi Kata ya Oloirien

Jarida litolewalo na Banana Investments Limited, Toleo Na.11, Oktoba—Desemba 2008 Jarida litolewalo na Banana Investments Limited, Toleo Na.11, Oktoba—Desemba 2008

MIKAKATI YA BANANA SACCOS KUJIKWAMUA KIUCHUMI

Wengi wetu tumekuwa tukisikia watu mbalimbali wakilalamika kuwa wana mning’inio baada ya kunywa vinywaji vikali kwa wingi. Baadhi ya dalili za mning’inio ni mwili kuchoka na kichwa kuwa kizito na mtu kushindwa kwa kiasi fulani kufikiri sawasawa. Kwa kuzingatia usemi “Kinga ni bora kuliko tiba” ninapenda kuwaletea njia muhimu kujikinga au kushinda mning’inio. Ni muhimu kupata lishe bora yenye asili ya protini na mafuta, kwa mfano nyama, karanga na jib-ini kabla ya kunywa vinywaji vikali. Kazi ya protini na mafuta ni kupunguza kasi ya ufyonzaji wa kilevi kwenye damu kwa kufanya tabaka kwenye njia ya chakula. Kwa ajili hiyo, ufyonzaji wa kilevi kuingia kwenye damu huwa wa kasi ndogo na mnywaji halewi upesi. Mning’inio inapomkabili mnywaji, njia rahisi ya kuikabili ni kunywa maji mengi. Inashauriwa muathirika wa mning’inio anywe glasi 1 hadi 2 kwa kila glasi ya pombe kwa kutegemea kipimo cha ulevi wa kinywaji kilichonywewa. Maji husaidia kuondoa ulevi na vitu vingine kwenye damu kupitia njia ya mkojo na jasho. Matunda na maboga nayo ni tiba ya mning’inio. Muathirika wa mning’inio hupata nafuu kama aki-tumia matunda kwa mfano ndizi na apples. Vile vile hupata

nafuu akitumia maboga kwa mfano matango au tikiti maji. Matunda na maboga huifanya mishipa ya damu kuwa huru kutokana na kuchoshwa na kilevi mwilini. Supu moto ya nyama, hasa supu ya kuku, humsaidia muathirika wa mning’inio kuepukana na kichefuchefu na kutapika. Pia humpatia madini ya potashi na chumvi ambazo ni muhimu sana katika mwili. Hewa safi ni muhimu kwa mtu mwenye mning’inio. Mara kwa mara matembezi kwenye fukwe za bahari ni tiba bora ya mning’inio. Muathirika wa mning’inio anashauriwa kulala muda wa kutosha. Hakuna dawa za kutibu mning’inio ingawa Asprin inaweza kutumiwa kwa ushauri wa daktari. Matumizi ya dawa za tiba bila maelekezo ya daktari huweza kuadhiri ini na ni hatari kwa maisha yako. Unashauriwa kupiga mswaki kusafisha kinywa meno na ulimi ili kuondoa harufu mbaya ya kilevi. Baada ya kuhakikisha usafi wa meno na kinywa muathirika wa mning’inio anashauriwa kuoga maji moto na sabuni yenye kuondoa harufu mbaya mwilini.

Imeandikwa na Michael Emanuel

Mwaka huu Chama cha Akiba na Mikopo cha Banana kilitimiza miaka kumi na mmoja tangu kiliposajiliwa 1997. Chama kina idadi ya wanachama 89 tu, wanaume 67 na wanawake 22. Idadi hii ndogo ya wanachama inatokana na mfungamano wa wanachama (common bond) inamtaka mtu awe mfan-yakazi wa kudumu wa Kampuni ya Banana ndipo aweze kusajiliwa kuwa mwanachama wa Banana SACCOS Ltd. Katika mkutano mkuu wa chama uliofanyika Oktoba 4, 2008 mikakati mbalimbali ya kuongeza mapato ya chama ilijadiliwa. Mojawapo ya mikakati iliyopitishwa na mkutano huo ni ule wa kuongeza viwango vya chini vya akiba na hisa kuwekezwa na kila mwanachama kwa mwezi. Fedha hizo zimeanza kukatwa kutoa mishahara ya wanachama kuanzia Ok-toba 31, 2008. Mkutano mkuu uliwataka wanachama waendelee kukopa kwa busara na kurejesha mikopo kwa wakati muafaka.

Njia nyingine ya kujipatia mapato iliyopitishwa na mkutano mkuu ni kuwekeza fedha zitokanazo na hisa za wanachama kwenye taasisi za fedha zinazoende-shwa kwa faida. Hata hivyo ilionekana kuwa si busara kuwekeza fedha zote kwa taasisi moja. Ilikubaliwa pia kuwa chama kiendelee kununua viwanja na kuwauzia wanachama kwa faida. Chama kitakopa fedha pale kitakapokuwa hakina budi kufanya hivyo, hasa kwa mahitaji ya ku-kopesha wanachama. Ni kwa ajili hiyo mkutano mkuu ulipitisha maombi ya ukomo wa madeni kwa mwaka 2009 kama yalivyowasilishwa, bila ya mabadiliko. Mkutano Mkuu uliagiza Bodi iongeze juhudi kufuatilia madeni mabaya na ikakubaliwa kutumia wafilisi wa mali kama hatua ya mwisho kufuatilia wadaiwa sugu.

Imeandikwa na Augustine S. Minja

NAMNA YA KUTIBU MNING’INIO

Page 4: MBIU YA BANANA TOLEO LA 11 FN · Ndugu wasomaji wa Mbiu ya Banana, viongozi, wafanyakazi, wateja na watumiaji wa bidhaa zetu: 1. Napenda kuchukua nafasi hii kuwatakia heri ya

Jarida litolewalo na Banana Investments Limited, Toleo Na.11, Oktoba—Desemba 2008

MOYO WA KUTHUBUTU KUTENDA:

BARACK OBAMA VS BIL

Katika hotuba ya kuwashukuru wananchi wa

Marekani kwa kumchagua kuwa Rais wa 44 wa

Marekani, Seneta Barack Obama alimsifu sana bibi

yake, Madelyn Dunham, ambaye ndiye aliyemlea.

Hakika kwa mtu mweusi kuchaguliwa kuwa Rais wa

taifa kubwa kama Marekani baada ya miaka 200 ya

uhuru haikuwa kazi rahisi.

Obama alisema kuwa bibi yake huyu mzaa

mama ndiye aliyekuwa nguzo kuu ya mafanikio yake.

Alisema kuwa tangu utotoni bibii huyu alimjenga

kuwa na moyo wa kuthubutu kutenda na kwamba kila

jambo linawezekana. Kila mara alikuwa akimsistizia

kuwa na ari ya kufanya jambo lolote analoamini

kuwa ni nzuri bila ya kuogopa kushindwa. Alielezea

jinsi bibi yake huyu alivyothubutu kutenda na ku-

panda kutoka karani katika Benki ya Hawaii hadi

kufikia kuwa Makamu wa Rais wa benki hiyo baada

ya miaka ishirini na nne. Kwa mwanamke wa nyakati

hizo hili halikuwa jambo rahisi hasa ikizingatiwa

mfumo dume uliotawala enzi hizo.

Nilikuwa nikitafakari mafanDuikio ya Kam-

puni ya Banana ya sasa kulinganisha na ilivyokuwa

miaka minane iliyopita ndipo wazo la Barack Obama

likanijia. Hakika mafanikio haya yametokana na

kuwa na moyo wa kuthubutu kutenda na kule

kuamini kuwa kila jambo linawezekana. Ni waku-

rugenzi wa kampuni waliothubutu kutenda na, kwa

ushirikiano na uongozi na wafanyakazi, wameweza

kufanya Kampuni ya Banana kuwa kampuni kubwa

kuliko zote zinazotengeneza mvinyo wa ndizi. Ni-

nawapongeza kwa hilo.

Hivyo basi, fundisho tunalopata kutoka kwa

Rais Mteule Barack Obama na Kampuni ya Banana

ni kuwa kila jambo linawezekana; kinachotakiwa ni

bidii na kuthubutu kutenda. Ni bahati mbaya sana

Bibi Madelyn Dunham hakuishi kushuhudia mjukuu

wake akitangazwa kuwa Rais wa 44 wa Marekani

kwani alifariki akiwa na umri wa miaka 86 Novemba

2, 2008, siku mbili kabla ya uchaguzi mkuu. wa

Marekani.

Imeandikwa na

Gerald Lyimo

Barack Obama (katikati) akiwa na wazazi wa mama yake

PICHA KULIA: Maendeleo ya ujenzi wa matenki yenye ujazo wa lita 60,000 kila moja kwa ajili ya kuivishia na kuhifadhi vinywaji kiwandani, Banana Investments Limited

Jarida litolewalo na Banana Investments Limited, Toleo Na.11, Oktoba—Desemba 2008

KAMPUNI YA BANANA INAVYOSAIDIA KUINUA KIPATO CHA WATANZANIA

KIBONZO

Kampuni ya Banana ni moja kati ya makam-puni machache hapa nchini yanayozalisha bidhaa bila ya kuagiza mali ghafi kutoka nje. Mahitaji makubwa ya ndizi kwa ajili ya uzalishaji yamewezesha waku-lima wengi kujiongezea kipato baada ya bei ya ndizi kuongezeka. Pia sekta ya kilimo imeajiri watu wengi zaidi ili kukidhi mahitaji makubwa ya ndizi kwa ajili ya kiwanda cha Banana kilichoko Manispaa ya Arusha. Pamoja na hayo, sekta ya usafirishaji imeajiri watu wengi kusafirisha mali ghafi , hasa ndizi am-bazo hutumika kwa wingi katika uzalishaji wa viny-waji mbalimbali vya banana. Sekta hiyo huajiri watu wengi pia kuwafikishia wateja vinywaji ambavyo ni RAHA Banana Alcoholic Beverage na mvinyo aina ya Malkia na Meru. Nafasi nyingi za kazi hupatikana mashambani wakati wa kulima, kupalilia hadi kuvuna ndizi. Ndizi huhitaji uangalifu mkubwa wakati wa kuziivisha hadi kuziandaa na kuzifikisha kiwandani. Vifaa vinavyotumika hununuliwa hapa hapa nchini hivyo kuwapatia wananchi kipato pia. Tangu Kampuni ya Banana ilipoanzishwa 1993 idadi ya wafanyakazi wake imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka, hivyo kusaidia kwa kiasi fulani kuondoa kero ya ukosefu wa ajira kwa Watanzania. Kampuni ya Banana imeajiri wafanyakazi wengi katika ki-wanda chake kilichoko Arusha na hali kadhalika katika bohari zake zilizoko Dar es Salaam na Tanga. Mbali na kutoa ajira ya moja kwa moja, kampuni hii

inatoa fursa nyingine za ajira kupitia ununuzi wa mali ghafi za hapa nchini na usambazaji wa bidhaa zake kutoka kiwandani hadi kumfikia mlaji. Sekta ya usafirishaji nayo ina nafasi kubwa ya kuajiri Watan-zania kupitia huduma ya kufikisha mali ghafi kiwan-dani na kusafirisha bidhaa za banana kutoka kiwan-dani hadi kumfikia mlaji. Wenye magari hupata faida kutokana na kukodisha magari yao na huku mader-eva, wapakiaji na wapakuaji wakipata ajira kupitia njia hiyo. Njia nyingine inayowapatia Watanzania kipato ni matumizi ya masalia ya uzalishaji kwa ajili ya kulishia mifugo. Mpaka sasa wafugaji walio jirani na kiwanda hupewa mabaki hayo bila ya kutozwa malipo yo yote. Changamoto: Hapa kuna fursa nzuri ya kufanya

utafiti kwa ye yote anayetaka kujua idadi kamili ya ajira zinazozalishwa na Kampuni ya Banana.

Karibu, itumie fursa hiyo!

Imeandikwa na Elipidi Joseph Urassa Mobile: 0784 341270.

Jarida litolewalo na Banana Investments Limited, Toleo Na.11, Oktoba—Desemba 2008 Jarida litolewalo na Banana Investments Limited, Toleo Na.11, Oktoba—Desemba 2008

Art by RICHY 2008

Imeandikwa na Richard Emanuel

Ina maana siku ile wewe ulikunywa nini? Siku nyingine ukifika pale ulizia RAHA. Kwanza inaleta hamu ya kula; vile vile ni kinywaji bora baada ya chakula

Bila shaka unakumbuka pale tulipokuwa tukinywa juzi; siku hizi kuna kinywaji aina ya RAHA, tena kilichothibitishwa na TBS