25

MBIU YA AFYA MAGAZIN - sailvega.com projects/pdf/MBIU YA AFYA MAGAZIN.pdf · Halo, hapo ni kwa DCCO? Ndio, nikusaidie nini? Pamekuwa na uhaba wa vifaa katika nchi nzima kwa kipindi

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: MBIU YA AFYA MAGAZIN - sailvega.com projects/pdf/MBIU YA AFYA MAGAZIN.pdf · Halo, hapo ni kwa DCCO? Ndio, nikusaidie nini? Pamekuwa na uhaba wa vifaa katika nchi nzima kwa kipindi
Page 2: MBIU YA AFYA MAGAZIN - sailvega.com projects/pdf/MBIU YA AFYA MAGAZIN.pdf · Halo, hapo ni kwa DCCO? Ndio, nikusaidie nini? Pamekuwa na uhaba wa vifaa katika nchi nzima kwa kipindi

GAZETI HILI LIMETENGENEZWA NA MRADI WA CHANJO WA TAIFA (EPI), WIZARA YA AFYA TANZANIA, AFRICA VISION TRUST NA WASANI WA KINGO

TAHARIRIMwezi uliopita ulikuwa na kazi nyingi! Pamoja na

kampeni ya siku za chanjo kitaifa na maandalizi yakampeni ya surua kwa hakika kulikuwa hakuna hata

dakika ya kufikiri!.Lakini hiki ni kipindi cha mwaka nilichokifurahia.

Nadhani kwa kazi zote hizi utajihisi umepata mafanikiofulani. Hata hivyo hiyo haitufanyi tuweze kupumzikamiezi mingine ya mwaka. Chanjo za kawaida nimuhimu zikiendelea.

Usalama ni jambo muhimu ambalo limekuwa kati-ka mawazo yangu hivi sasa. Katika wiki chache zilizo-pita tumekuwa na matatizo na sterilaiza yetu na imeni-pa hofu sana kama utoaji wa sindano ulikuwa salamana kwa kiasi gani. Kwa bahati nzuri tulikuwa na TSTspots mpya, hivyo tungeweza kuthibitisha kamailikuwa inafanya kazi vizuri. Hakika hatutaki kabisakusababisha hatari kwa watoto!

Lakini hiyo siyo hatari pekee ninayoihofia. Niliwahikujichoma na sindano nilipojaribu kurudishia kifunikochake mara baada ya kuitumia. Mbali ya kuwa na jer-aha baya kuna hatari kubwa ya kuambukizwamagonjwa kama vile ukimwi, hivyo nina himiza asiwe-po mtu yeyote wa kituo cha afya anayerudishia vifu-niko vya sindano. Sasa tuwe tunazitupa moja kwamoja kwenye maboksi ya usalama.

Maboksi ya usalama ni muhimu sana! Kama hatu-na maboksi maalumu ya EPI, tutengeneze yetu. Nirahisi na salama zaidi. Nimewahi kushuhudia baadhiya wafanyakazi wa afya wakiacha sindano zilizotumi-ka zikizagaa nje ya vituo. Fikiria! kama tunaishi jiranina kituo cha afya tunapaswa kuwa wangalifu zaidi kwakuhifadhi vizuri sindano zilizotumika katika maboksi ndani ya kliniki hadi tunapokuwa tayari kuya-choma moto. Watoto wangu wamekuawakubwa na hupenda kuchezea vitu mbalimbali zikiwemo sindano zilizotumika!. Niathari gani itakayowapata? Siku zote kati-ka kazi zetu tujaribu kuboresha usalamakwa watoto wetu na jamii nzima.

yal iyomo

HADITHI ZA

PICHA NA

KATUNI

Usalama Kwanza uk. 2Bastola ya Maji uk. 13Katuni uk. 24

HabariNjemauk. 12

MAKALA naSIMULIZI

Ujue ugonjwa waHepatitis B uk. 10

Tupa Salama uk. 20

VICHEKESHO uk. 9

BBC uk. 22

JISHINDIEREDIO uk. 22-23

Chemcha Bongo uk. 24

JJIISSHHIINNDDIIEE

RREE

DDIIOO

!!!!!!

Page 3: MBIU YA AFYA MAGAZIN - sailvega.com projects/pdf/MBIU YA AFYA MAGAZIN.pdf · Halo, hapo ni kwa DCCO? Ndio, nikusaidie nini? Pamekuwa na uhaba wa vifaa katika nchi nzima kwa kipindi

USALAMA KWANZA2

Mama Tobi, itabidi umrudishe mtotobaada ya wiki nne kwa sindano

nyingine.

Sofia, vipi tena? Ah, nasikia kichefuchefu nakizunguzungu.

Furaha ya wanakijiji wa “MWEMBE TAYARI” ilikamilika mwaka juzi pale Serikali ilipowajengea kituo cha afya na kuon-dokana na adha ya kutembea maili 15 kufuata huduma za afya.Pamoja na kituo hicho bado kuna tahadhari inayopaswa

kuchukuliwa.

USALAMA KWANZA...

Page 4: MBIU YA AFYA MAGAZIN - sailvega.com projects/pdf/MBIU YA AFYA MAGAZIN.pdf · Halo, hapo ni kwa DCCO? Ndio, nikusaidie nini? Pamekuwa na uhaba wa vifaa katika nchi nzima kwa kipindi

USALAMA KWANZA 3

Hebu lete hiyo sindano niiweke kwenyemaji. Vipi unajisikiaje?

Nasikia kizunguzungu na kichefuchefu. Watu ni wengi na sindanozimetuishia. Itabidi tuahirishe kutoa chanjo mpaka kesho.

Inabidi tuanze

kuziandaa

sindano

sasa hivi.

Unaona!, unoaji wa sin-dano unaweza kukus-ababishia maambukizi!

Mtuwie radhi kina mama. Tumeishiwa sindano zilizochemshwa.Tafadhali njooni kesho tutaendelea kutoa chanjo.

Sindano zimeanza

kuwa butu. Ngoja nzi-

noe kidogo.

Sofia ngoja,usi........

Ni rahisi kujikwangua au kujichoma wakati

unaponoa sindano na hivyokuhatarisha afya yako kwa

maambukizi ya maradhi tokakwa mtu aliyedungwa na sin-

dano hiyo.

U S I N O E S I N D A N O ,N I H ATA R I !

AAAAUU UU UU CC HH !!

Page 5: MBIU YA AFYA MAGAZIN - sailvega.com projects/pdf/MBIU YA AFYA MAGAZIN.pdf · Halo, hapo ni kwa DCCO? Ndio, nikusaidie nini? Pamekuwa na uhaba wa vifaa katika nchi nzima kwa kipindi

USALAMA KWANZA4

...na kama ndivyo, basi tutawatu-

mia mara moja.

Zaidi ya mwaka, una uhakika? Ngoja niangalie kwenye lejaya vifaa.

Kituo cha afya cha MWEMBE TAYARI tumeishiwa - hatujaletewa sindano na akiba ya vifaa kwa zaidi ya mwaka sasa.

Halo, hapo ni kwaDCCO?

Ndio, nikusaidie nini?

Pamekuwa na uhaba wa vifaa katika nchi nzima kwa kipindikilichopita. Hata hivyo Serikali imejitahidi sana kumaliza tatizo

hilo. Pamoja na hayo ni jukumu lako kuhakikisha vifaa vyakuchemshia sindano viko kwenye hali nzuri. Endapo kifaa fulani

ni kibovu toa taarifa kwa DMO haraka!

TA H A D H A R I K A B L A YA WA K AT I !

Page 6: MBIU YA AFYA MAGAZIN - sailvega.com projects/pdf/MBIU YA AFYA MAGAZIN.pdf · Halo, hapo ni kwa DCCO? Ndio, nikusaidie nini? Pamekuwa na uhaba wa vifaa katika nchi nzima kwa kipindi

USALAMA KWANZA 5

Halafu hii sindano yako haina kipimo cha dozi inayohitajika.

Sawa, lakini unahakika gani kama

sindano uliyonunua mtaani

ni salama?

Aka babu wee, sindano zenu ni butu. mwezi uliopita mliniumiziamwanangu. Leo nimeleta sindano yangu.

Usiogope tumeletasindano mpya.

Mna bahati, juzi tu tumepokea shehena mpyaya vifaa toka mkoani!, saini hapa!

Page 7: MBIU YA AFYA MAGAZIN - sailvega.com projects/pdf/MBIU YA AFYA MAGAZIN.pdf · Halo, hapo ni kwa DCCO? Ndio, nikusaidie nini? Pamekuwa na uhaba wa vifaa katika nchi nzima kwa kipindi

USALAMA KWANZA6

Kwa hiyo ni rahisi kutoa zaidi au pungufu yakipimo kinachohitajika.

Alaaa kumbe!

Mwingine!

Mara hii umerudi, nilikuambiaumrudishe mtoto baada ya wiki

nne.

Angalieni sehemu mliyomchoma, sindanoilivyovimba na

kubadilika.

Du!, labda kapata ambukizo,tumpeleke kwa mganga.

Sasa naogopa, mara ya pili hii tunaletewa uvimbe wa sin-dano katika mwezi huu, pengine sterilaiza yetu ina kasoro,

ikague.

Page 8: MBIU YA AFYA MAGAZIN - sailvega.com projects/pdf/MBIU YA AFYA MAGAZIN.pdf · Halo, hapo ni kwa DCCO? Ndio, nikusaidie nini? Pamekuwa na uhaba wa vifaa katika nchi nzima kwa kipindi

USALAMA KWANZA

Tubadilishe vyote,gasketi na valvu

mara moja.

Aah, ndio maana, hebu ona mpira wasterilaiza ulivyochakaa.

Umesahau kwenye she-hena ya vifaa vipya kuna

lebo za TST. Funguatubandike moja.

Lebo ya TST?

Weka kidogo, akiba yamafuta

imepungua. Inabidituagize Wilayani

mapema.

Ha ha ha, hata wewe msomaji hujui lebo za TST kama Sofia!TST ni lebo ya doa dogo lenye

rangi ya njano ambayo hubandikwa ndani ya sterilaiza kabla ya uchemshaji wa sindano. Kazi yake ni kuhakik-

isha mzunguko wa mvuke na joto ndani ya sterilaiza. Kama mzun-guko umefanyika sawa sawa katika dakika 20 za uchemshaji wa

sindano, doa hilo hubadilika rangi na kuwa rangi ya zambarau.

RRiiiiiiNNGG!!!!!!BBRRRRRRiiNNGG!!!!!!

7

Page 9: MBIU YA AFYA MAGAZIN - sailvega.com projects/pdf/MBIU YA AFYA MAGAZIN.pdf · Halo, hapo ni kwa DCCO? Ndio, nikusaidie nini? Pamekuwa na uhaba wa vifaa katika nchi nzima kwa kipindi

USALAMA KWANZA8

Naona umevutiwa na habari zausalama wa sterilaiza.

Haa, mwanangu, miezi michache ijayo utakuwa mikononi mwangu. Sote tuhakik-ishe Mariam anavyotupa sindano salama.

Haaa, rangi ya TST-spot imebadilika toka njano hadi zam-

barau!Tena hizi lebo tuwe tunazibandika kwenye hiki kitabu ili kufuatilia utendaji

wa sterilaiza.

Safi, ikiharibika,

isitushitukize.

Page 10: MBIU YA AFYA MAGAZIN - sailvega.com projects/pdf/MBIU YA AFYA MAGAZIN.pdf · Halo, hapo ni kwa DCCO? Ndio, nikusaidie nini? Pamekuwa na uhaba wa vifaa katika nchi nzima kwa kipindi

Vichekesho!! 9

NILIYOYASIKIAYANANITOSHA:

Bibi yetu mzaa Baba,yaani Lusia, amezee-ka sana kiasi kwambaanaanza kuwa kiziwi.

Madaktari walipen-dekeza afanyiwe upasuaji

wa masikio lakini yeyealipinga vikali wazo hilo.“Tangu nizaliwe sasa ninaumri wa miaka 94, halafubado mnataka nini?, kwaumri huu niliyoyasikia

yananitosha”, alijibu Bibi.

KWA JINSI NINAVYOKOHOA:

Siku zote nimekuwa najiuliza ni kwa vipi

Kaka yangu ambaye ni daktari hawashawishi

wagonjwa wake waache kuvuta sigara. Yeye

huvuta pakiti mbili za sigara kwa siku na nil-

iamini ushauri wake hauwezi kuzingatiwa.

“Hawataacha kuvuta kwa sababu ya

kuwashauri”, aliniambia.

“Wataacha kutokana na jinsi ninavyokohoa

wakati nawaambia”.

KIJOGOO:Akiwa kwenye genge la walevi,jamaa mmoja alianza kutamba;“Habari za wanawake wote wa

mtaa huu niulizeni mimi. Mfanoyule Fatuma unene wa bure tu,kiuno chake saizi inchi 23 tu...,

anashindwa hata na ka-Chausiku.Kenyewe bwana kanavaa inchi30!”, walevi wote kwenye baawaligeuka kumsikiliza jamaa.

“Lakini mtaa mzima kwa kiunokikubwa ni Mama Kidawa

anaongoza, halafu kwa maziwamakubwa Mama Cheupe

anashika namba moja; sidiriayake saizi....”. Kufikia hapo

kundi la welevi wenye hasiralikamzunguka na chupa za bia

mikononi.“Kumbe wewe ndiye kijogoo chawake zetu tunapokuwa makazinisio!, sasa tuambie umejuaje?”.

Huku jamaa akinyoosha mikonojuu, akasema;

“Aka mwaya, tusiuane bure,mimi ni fundi cherehani.Nitawashoneaje nguo bila

kuwapima?”.

AMEKWENDA KUUZIMAULE MSHUMAA:

Mke na mume walikuwa na shauku yakupata mtoto, hivyo wakaenda kwa Kasisi

ili wakaombewe.“Nina safari ya kwenda Roma kwa ajili ya

hija, hivyo nikiwa huko nitawawashiamshumaa wa baraka nanyi mtapata watoto

lukuki”, alisema Kasisi. Miaka mitatubaadaye Kasisi aliporudi kutoka Roma

aliwatembelea mke na mume huyo nyum-bani kwao na kumkuta mwanamke akiwa

mjamzito na huku anawahudumiamapacha wake.

“Yuko wapi mumeo, nataka niwapehongera”, alisema Kasisi.

“Ooho!, mmepishana, amekwenda Romakuuzima ule mshumaa uliotuwashia, ali-

jibu mwanamke.

ASINGEKUWA WANGU

NISINGEKUWA

NAMPELEKA

NYUMBANI:

Askari polisi mmoja alis-

hangazwa na kitendo cha

mwanamke mmoja aliyem-

beba mtoto wake aliyekuwa

analia na kupiga makelele.

Akiwa ameingiwa na huru-

ma, yule polisi akamuuliza

huyo mwanamke.

“Mama huyo ni mtoto

wako kweli?”,

“Asingekuwa wangu,

nisingekuwa nampeleka

nyumbani”, alijibu huyo

Mama.

KAZI YA WITO:Kwa kawaida nesi mmoja ait-

waye Salama huwachoma sin-

dano wagonjwa kumi tu kwa siku

na kuondoka kazini akiacha watu

wakilalamika. Lakini juzi aliweza

kuwachoma sindano wagonjwa

arobaini bila kulalamika kuwa

mkono wake unauma.

Dokta John alishangaa sana na

alipomuuliza kwanini anajituma

sana siku hiyo, Salama alimjibu;

“Tangu nianze kazi miaka kumi

iliyopita, leo nimetambua kuwa

uuguzi ni kazi ya wito!”.

VIC

HEKESH

O!!

Page 11: MBIU YA AFYA MAGAZIN - sailvega.com projects/pdf/MBIU YA AFYA MAGAZIN.pdf · Halo, hapo ni kwa DCCO? Ndio, nikusaidie nini? Pamekuwa na uhaba wa vifaa katika nchi nzima kwa kipindi

Hepatitis B10

UGONJWA WA INIWENYE VIRUSI VINAVYOUA

Hepatitis B ni ugonjwa hatari wa ini unaoenezwa na virusi

vijulikanavyo kama Hepatitis B’.Virusi hivi vina nguvu

kubwa ya kushambulia mara 100 zaidi ya virusi vya

ukimwi!. Mtu anapopata uambukizo, virusi huvamia na kuanza

kuathiri chembe chembe hai za ini na

matokeo yake ni dalili kama ugonjwa wa

mafua, kuumwa kichwa, homa, kuhara,

kutapika na ugonjwa wa ngozi. Aidha

macho hubadilika na kuwa ya man-

jano.Hali hii inaweza ikaendelea kwa

muda wa wiki tatu au miezi kadhaa.

Ugonjwa huu wa Hepatitis B mara nyingi

huenezwa kati ya mtu na mtu kwa kugusana

na damu ya mtu aliyeambukizwa. Lakini

virusi hivi hupatikana pia kwenye mate,

shahawa, majimaji yatokayo kwenye sehe-

mu ya siri ya mwanamke, jasho na hata

kwenye machozi. Njia kuu ya uambukizaji

hasa ni damu, shahawa, na majimaji katika

uke.

Maambukizo mengi hutokea kwa watoto

wenye umri chini ya miaka mitano hasa

watoto wanyonyao. Watu wazima hasa wale

ambao wanafanya kazi kwenye mazingira

ya kugusana na damu au maji-maji ya

mwilini ya watu wengine kwenye

shughuli za sherehe kama vile michezo hasa

ile ya kugusanagusana na kushikana,

wanaweza kuambukizwa.

Maambukizo haya hupatikana

tangu utotoni na yanazuilika kwa

chanjo ya mama mjamzito karibu

ya mtoto kuzaliwa. Baadhi ya watu

huwa hawaponi kutokana na

ugonjwa huu na virusi vinaweza

kuendelea na kuathiri ini na hata

kuleta sarakani ya ini na hatimaye

kifo. Maambukizo ya Hepatitis B ni

janga kwa watoto kwa sababu

wazazi wao wengi hufariki na

kuwaacha wakiwa wadogo kiasi

cha kutoweza kujitegemea.

Watu wengi huwa hawana dalili

za ugonjwa huu na hata hawafa-

hamu kwamba wana ugonjwa huo hali ambayo husababisha

kuambukiza wengine wengi bila ya wao kujua.

Dalili za ugonjwa wa Hepatitis B zaweza kujitokeza wakati

wowote kati ya wiki sita na miezi sita tangu mtu apate ambukizo

la virusi, lakini kwa wastani huchukua muda wa miezi mitatu.

Kwa kuwa ugonjwa huu hauna tiba , njia muhimu ya kujikinga

ni kutumia chanjo. Moja ya chanjo dhidi ya ugonjwa huu ni

mchanganyiko wa chanjo ya DPT na chanjo dhidi ya ugonjwa wa

ini (HB). Chanjo hiyo ni DPT-HB.

Njia za kujikinga na ugonjwa huu ni pamoja na kuepuka matu-

mizi ya damu isiyopimwa virusi vya Hepatitis B, kutotumia

mabomba na sindano zisizotakaswa na kuepuka uasherati.

Ugonjwa huu ni hatari sana na umeenea karibu dunia nzima

ingawa idadi kubwa ya wagonjwa wapo katika mabara ya Afrika,

Asia, na Amerika ya kusini. Matarajio ya chanjo ya Hepatitis B

katika Afrika ni makubwa sana. Lakini kukosekana kwa mpango

wa chanjo maeneo mengi, mamilioni ya watoto wanaweza kufa

kutokana na ugonjwa huu ambao hujitokeza kwa kasi ukubwani.

Page 12: MBIU YA AFYA MAGAZIN - sailvega.com projects/pdf/MBIU YA AFYA MAGAZIN.pdf · Halo, hapo ni kwa DCCO? Ndio, nikusaidie nini? Pamekuwa na uhaba wa vifaa katika nchi nzima kwa kipindi

Hepatitis B 11

LISEMWALOLIPO..!J

ohn na Sara ni marafiki wapenzi wa muda mrefu. Siku zote

wamekuwa makini sana katika uhusiano wao. Wamekuwa

wakitumia njia zote muhimu za kujikinga na magonjwa na

hasa ukimwi ambao wamekuwa wakiuchukulia kuwa ndio

ugonjwa ulio hatari zaidi ya magonjwa mengine. Matarajio yao ni

kufunga ndoa wakiwa salama.

Siku moja walihudhuria mazishi ya jirani yao mmoja ait-

waye Rose ambaye ilivumishwa alikufa kwa ukimwi. Rose

alikuwa ameolewa na aliacha mume na watoto wawili. Wakati

wa mazishi, ilitolewa historia fupi ya marehemu kuanzia

kuzaliwa kwake hadi kifo. Kilichowagusa watu wengi ni historia

ya ugonjwa wake. Marehemu Rose alianza kuumwa mafua

kwa mudamrefu na kisha kuharisha. Halafu macho yake

yalibadilika rangi yakawa ya manjano.

Alipopimwa akagundulika kuwa alikuwa

anaumwa ugonjwa wa ini unaojulikana

kwa jina la kitalaamu “hepatitis B”. Kwa

kuwa Rose alikuwa amekonda sana

watu walidhani alikuwa na ukimwi.

Msemaji wa wafiwa aliendelea kusema

kuwa, ugonjwa huo wa ini huambuk-

izwa kwa njia kama zile zile za ukimwi

na kupitia mate, jasho, hata machozi na

hasa kujamiana.

Waliporudi nyumbani,

John na Sara walijawa

na mawazo mengi.

Habari za ugonjwa huo

wa ini (hepatitis B) zili-

wanyima raha kabisa.

Sio tu kwamba

hawakuwahi kupata

chanjo ya ugonjwa huo bali pia hawakuwahi hata kusikia

habari zake kabla. Sasa walimua kwenda hospitali kupimwa ili

wajue mapema kama wanao ugonjwa huo au la. Walifurahi

sana majibu yalipoonyesha kuwa hawakuwa na ugonjwa huo.

John na Sara ni mfano wa wanajamii wote wanaopenda kuishi

maisha ya kujihami ambayo ni bora zaidi hasa kwa magonjwa

yasiyokuwa na tiba kama Hepatitis B.

Page 13: MBIU YA AFYA MAGAZIN - sailvega.com projects/pdf/MBIU YA AFYA MAGAZIN.pdf · Halo, hapo ni kwa DCCO? Ndio, nikusaidie nini? Pamekuwa na uhaba wa vifaa katika nchi nzima kwa kipindi

Habari njema12

HA

BA

RINN

JJEEMM

AA!!!!

!!Habari njema 1● Shukurani kwa msaada maalum kutokaGAVI (Ushirika wa Kimataifa wa Chanjona Kinga ). Tanzania inatarajia kuanzishachanjo dhidi ya ugonjwa wa Hepatitis Bkatika mpango wa utoaji chanjo unaotaraji-wa kufanywa kwa watoto wachanga wotekuanzia mapema mwaka ujao (2001).

Habari njema 2● Wakati chanjo hii mpya itakayokuwaimechanganywa na DPT italeta mabadilikoyenye unafuu kwa wafanyakazi wa afyakina mama na watoto. Chanjo mpyaitakayochanganywa DPT/Hepatitis Bitakuwa inatolewa katika utaratibu ule uleunaotumiwa kwa chanjo ya DPT. Isitoshe,chanjo hii mpya itatoa kinga madhubutizaidi kwa watoto wachanga wote dhidi yavirusi hivi hatari.

Habari njema 3● Pamoja na uanzishwaji wa chanjompya, Tanzania imeamua kufanyamabadiliko kwa kuacha kutumia mabombana sindano za kuchemsha na kuanzakutumia bomba maalum ‘linalojifunga’baada ya kutumika kwa ajili ya chanjo zotezinazotumia sindano. Unaweza ukawaunalifahamu bomba la aina hii lililowahikutumika kwenye kampeni za ugonjwa wa

surua.

Watumishi wengi wa afya tulioongea naowameyapokea mabadiliko haya ya kutu-mia bomba hili la ‘kujifunga’. “Uchemshajiwa sindano ni kazi ndefu na hatuwezikumudu kuwa na vifaa vya kutosha sikuzote. Lakini sindano hizi mpya ni rahisikuzitumia na kisha unaziweka moja kwamoja ndani ya boksi la usalama. Ni rahisina salama zaidi!”, alisema Muuguzi mmojawa MCH kutoka Zanzibar.

Utajulishwa mabadiliko haya na mafunzomaalum yatatolewa karibu na kipindihicho.

BOMBA LENYE MTUTU UNAOJIFUNGA

B omba lenye mtutu unaojifungabaada ya kutumika ni salama. Maratu mtutu unaposukuma dawa

hauwezi kurudishwa nyuma tena. Hiiinafanyaisiwezekane kutumika tena, nahivyo kunakuwa hakuna hatari ya maam-bukizo kutoka kwa mgonjwa mmojakwenda kwa mwingine.

I sitoshe bado kuna hatari ya kujichomana sindano. Unapaswa uzitupe zotekwa usalama! Maboksi maalum ya

usalama yametolewa kwa kusudio hili.Tupa bomba na sindano iliyotumika mojakwa moja ndani ya boksi la usalamamara tu baada ya kuitumia. Weka boksimahali pa usalama ndani ya kliniki hadiutakapokuwa tayari kwa kulichoma moto.

Page 14: MBIU YA AFYA MAGAZIN - sailvega.com projects/pdf/MBIU YA AFYA MAGAZIN.pdf · Halo, hapo ni kwa DCCO? Ndio, nikusaidie nini? Pamekuwa na uhaba wa vifaa katika nchi nzima kwa kipindi

BASTOLA YA MAJI 13

BASTOLA YA MAJI

Page 15: MBIU YA AFYA MAGAZIN - sailvega.com projects/pdf/MBIU YA AFYA MAGAZIN.pdf · Halo, hapo ni kwa DCCO? Ndio, nikusaidie nini? Pamekuwa na uhaba wa vifaa katika nchi nzima kwa kipindi

BASTOLA YA MAJI14

Page 16: MBIU YA AFYA MAGAZIN - sailvega.com projects/pdf/MBIU YA AFYA MAGAZIN.pdf · Halo, hapo ni kwa DCCO? Ndio, nikusaidie nini? Pamekuwa na uhaba wa vifaa katika nchi nzima kwa kipindi

BASTOLA YA MAJI 15

Page 17: MBIU YA AFYA MAGAZIN - sailvega.com projects/pdf/MBIU YA AFYA MAGAZIN.pdf · Halo, hapo ni kwa DCCO? Ndio, nikusaidie nini? Pamekuwa na uhaba wa vifaa katika nchi nzima kwa kipindi

BASTOLA YA MAJI16

Page 18: MBIU YA AFYA MAGAZIN - sailvega.com projects/pdf/MBIU YA AFYA MAGAZIN.pdf · Halo, hapo ni kwa DCCO? Ndio, nikusaidie nini? Pamekuwa na uhaba wa vifaa katika nchi nzima kwa kipindi

BASTOLA YA MAJI 17

Page 19: MBIU YA AFYA MAGAZIN - sailvega.com projects/pdf/MBIU YA AFYA MAGAZIN.pdf · Halo, hapo ni kwa DCCO? Ndio, nikusaidie nini? Pamekuwa na uhaba wa vifaa katika nchi nzima kwa kipindi

BASTOLA YA MAJI18

Page 20: MBIU YA AFYA MAGAZIN - sailvega.com projects/pdf/MBIU YA AFYA MAGAZIN.pdf · Halo, hapo ni kwa DCCO? Ndio, nikusaidie nini? Pamekuwa na uhaba wa vifaa katika nchi nzima kwa kipindi

BASTOLA YA MAJI 19

Page 21: MBIU YA AFYA MAGAZIN - sailvega.com projects/pdf/MBIU YA AFYA MAGAZIN.pdf · Halo, hapo ni kwa DCCO? Ndio, nikusaidie nini? Pamekuwa na uhaba wa vifaa katika nchi nzima kwa kipindi

TUPA SALAMA20

Hatua za utupaji salama wa bomba na sindano lililokwisha/zilizokwisha tumika

Utengenezaji wa boksi la kuhifadhia bomba na sindano zilizokwisha tumika Kama utakuwa hujapata boksi maalum la EPI.

2. Usirudishie kifuniko chake kwenye

sindano kabla ya kutupakwenye

boksi

3. Tunza boksikwenye sehemu

ambayo ni salama mpaka likijaa robo tatu.Hakikisha hujazi boksi

mpaka juu

4. Likishajaa kufikia robo tatu lipelekekwenye eneo lililotengwa

kwa uteketezaji wa sindano hizo.Choma mara moja boksi likiwana sindano ndani yake na

uchafu mwingine

uliopo

5. Simamia zoezi hilola uchomaji. Usimwachie

kazi hii muhimu

mhudumu wa

usafi

6. Mara moto ukizima fukia

mabaki kwa udongo

Tafuta boksi lenyekuta nene

Funga boksi kwausalama. Funga juu na

chini kwa kutumia gundiau tepu au pini imara

Tengeneza kishimokidogo juu ya boksikitakachowezesha

sindano na bomba lake kupita bila

matatizo

1. Tumbukiza sin-dano iliyokwisha tumika

kwenye boksi mara baada ya kutumia

TUPA

SSAA

LLAAMM

AA!!

Page 22: MBIU YA AFYA MAGAZIN - sailvega.com projects/pdf/MBIU YA AFYA MAGAZIN.pdf · Halo, hapo ni kwa DCCO? Ndio, nikusaidie nini? Pamekuwa na uhaba wa vifaa katika nchi nzima kwa kipindi

Ikiwezekana weka uzio ( mfano wa miti) kuzunguka shimo hilo la taka.

Choma boksi hilo natakataka zingine zilizopo

mara kwa mara. Unawezaukahitaji kiasi kidogo chamafuta ya taa kwa ajili ya

kuwashia moto.Moto ukisha

zima fukia mabaki kwa

udongo

TAH

AD

HA

RI

TUPA SALAMA 21

TUPA

SSAA

LLAAMM

AA!!

Na kama hunasehemu maalumya kuteketezeabomba, sindanona vifaavilivyokwishatumika basi:

Kama boksi ni jembamba kuna hatari ya sindano kuchomoza kupitiakwenye kuta za boksi hilo.

Hivyo zingatia:

● Zuia ubebaji wa boksi hilo usio wa lazima. Tafuta sehemu maalum katika chumba cha sindano ambapo unaweza ukalihifadhi boksi hilo. Hakikisha liko karibu na sehemu unayotolea sindano.

● Litunze boksi katika sehemu hiyo mpaka litakapokuwa tayari kuliteketeza kwa moto.

● Uwe mwangalifu unavyolibeba boksi kwenda kwenye eneo lililotengwa kwa uteketezaji.

● Usimwachie mhudumu wa usafi afanye kazi hii.

Tafuta na chaguasehemu kwenye eneo

hilo hilo la hospitali lililombali kidogo na majengo

ya hospitali kadiri inavyowezekana

Chimba shimoangalau lenye urefu wamita moja kwenda chini

Hakikisha uchafu unatupwa ndani

ya shimo na sio pembenimwa shimo

Tupa boksi, bila kutoasindano kutoka kwenye

boksi

hilo.

Page 23: MBIU YA AFYA MAGAZIN - sailvega.com projects/pdf/MBIU YA AFYA MAGAZIN.pdf · Halo, hapo ni kwa DCCO? Ndio, nikusaidie nini? Pamekuwa na uhaba wa vifaa katika nchi nzima kwa kipindi

BBC/JISHINDIE REDIO!!!22

Ningependa kuanza kwa kuwafa-hamisha kuwa tuna makala maalum

juu ya afya ambayo imeanzishwa mapemamwaka huu. Makala hii hurushwa hewanikila jumatatu jioni ili kuwafahamishawasikilizaji wetu juu ya masuala yahusuyoafya katika mitazamo tofauti.

Kila inapowezekana tunazungumza nawataalam wa afya kutoka Afrika, hasa

tukizingatia kuwa wasikilizajitunaowatangazia ni kutoka barani humo.Na mada ikiwa juu ya suala linalohusianazaidi na nchi zilizoendelea au inapokuwavigumu kumpata mtaalam wa Kiafrika wamasuala hayo basi huwa tunawatumiawataalamu wa hapa hapa Uingereza.

Mara nyingi huwa tunazungumziamasuala ambayo ndio kwanza yana-

jitokeza na huwa tunafuatilia taarifa hizokwa karibu. Kwa mfano, tuliwafahamishawasikilizaji wetu wakati zilipotolewa taari-

fa juu ya athari za matumizi ya simu zamikononi, au wakati ilipotolewa taarifa juuya utafiti kuhusiana na uyoga unaowezakusaidia katika tiba ya maradhi ya mifupa,au kwa lugha ya kigeni arthritis na kadhali-ka.

Wakati mwingine huwatunazungumzia matatizo ya afya

yanayojitokeza katika maeneo ambakomatangazo yetu yanasikika. Kwa mfano,tuliweza kutangaza kuhusu operesheni yakuwatenganisha watoto mapacha waTanzania waliozaliwa huku wakiwa wame-unganika kwenye uti wa mgongo, upasuajihuo uliofanyika huko Afrika Kusini. Nahivi karibuni tu tuliweza kutangazamakala mbili kuhusiana na kampeni inay-oendelea nchini Tanzania ya kukabilianakuudhibiti na kuutokomeza kabisa ugonjwawa macho wa Trakoma, au kama unavyofa-hamika na wengi Ugonjwa wa Vikope,makala yaliyotayarishwa na kutangazwa na

mwenzangu Vicky Ntetema aliyetembeleamaeneo yaliyoathirika zaidi na maradhihaya katika mkoa wa Dodoma.

Kwa hakika ningependa kuongezakuwa BBC ina uwezo wa kuzipata

habari hizo muhimu za afya kutoka popotepale duniani, iwe kutoka kwenye mikutanoya kimataifa juu ya afya, utafiti juu yamaradhi na tiba mpya au kuzuka kwamaambukizo ya magonjwa mbali mbali.

Hivi karibuni tuliweza kuwatangaziawasikilizaji wetu kwa undani sana juu

ya mkutano wa kimataifa kuhusu janga laugonjwa wa UKIMWI uliofanyika DUR-BAN, nchini Afrika kusini..

Ni matarajio yangu kuwa Makala hayaya AFYA, kutoka Idhaa yetu ya

Kiswahili ya BBC yatakuwa na upeo waaina yake katika kukuelimisha na kukufa-hamisha mengi juu ya afya yako wewe najamii kwa ujumla.

Unaweza kusikiliza kipindi hicho cha Afya, kila siku ya Jumatatu jioni, kwenye mita bendi 19, 25 na 41. Vile vile kwenyemasafa ya FM - Dar es salaam 101.4 FM, Radio 5 Arusha kwenye 105 FM na Radio Free Africa katika 89.8 FM.

IDHAA YA KISWAHILI YA BBC YAKULETEA MAKALA YA AFYA NA MTAYARISHI - HAFSA MOSSI

JJIISSHHIINNDDIIEE

RREE

DDIIOO!!!!!!

Tunataka kujua kwa yakiniunafikiri nini kuhusu jarida hili. Endelea kuwa mwaminifu!

Maoni na mapendekezo yakoyatatusaidia kubuni jarida

bora zaidi siku zijazo.

Kama hutataka kuliharibu jaridaunaweza kunakilimajibu yako kwenyekaratasi na kutuma kwetu.Unaweza pia kututumia kivuli

chake (photocopy).Lakini kama unataka kushinda zawadi usisahau kuandika

jina na anuani yako!

Redio IsiyotumiaBetri !!!

Page 24: MBIU YA AFYA MAGAZIN - sailvega.com projects/pdf/MBIU YA AFYA MAGAZIN.pdf · Halo, hapo ni kwa DCCO? Ndio, nikusaidie nini? Pamekuwa na uhaba wa vifaa katika nchi nzima kwa kipindi

JISHINDIE REDIO!!! 23

1. UNALIFIKIRIAJE JARIDA?

■n a. Nimefurahishwa nalo sana.

■n b. Nimefurahishwa nalo kabisa.

■n c. Ninadhani liko sawa.

■n d. Sikufurahishwa nalo.

2. NI RAHISI KULIELEWA?

■n a. Ndio, yote yaliyokuwemo yalikuwa rahisi kueleweka.

■n b. Mengi kati ya hayo yalikuwa rahisi kueleweka

■n c. Baadhi yake yalikuwa rahisi kueleweka

■n d. Sidhani kama yalikuwa yanaeleweka kwa urahisi

3. HATUA ZIPI ULIZOANZA KUCHUKUA BAADA KUSOMA JARIDA HILI?

.........................................................................

.........................................................................

4. NAKALA NGAPI ZA JARIDA HILI ULIZOPOKEA KATIKA KITUO CHAKO CHA AFYA?

Moja ■n ❙ Mbili ■n ❙ Tatu au zaidi ■n

5. WANGAPI MMESOMA JARIDA HILI?

1 ■n ❙ 2 ■n ❙ 3 ■n ❙ 4-nazaidi ■n6. UNAHUSIKA MOJA KWA MOJA NA ZOEZI LA CHANJO?

■n Ndio ❙ ■n Hapana

7.UNGEPENDAKUSOMA NAKALA YATOLEO LIJALO?

■n Ndio ❙ ■n Hapana

8. UNAFANYA KITUO KIPI CHA AFYA?

■n Dispensari

■n Kituo cha afya

■n Hospitali ya Wilaya

■n Hospitali ya Mkoa

■n Kliniki ya binafsi / hospitali

9. Ipi ni kazi yako?

■n Auxilliary/assistant ❙ ■n Muuguzi wa kituo cha afya

■n Muuguzi / mkunga ❙ ■n Cold chain Officer ❙ ■n MCH aide

■n Meneja au Msimamizi ❙ ■n Nyingine (tafadhali fafanua)

.........................................................................

10. Mapendekezo mengine yoyote?

.........................................................................

.........................................................................

.........................................................................

Ni m

akal

a ga

ni

3 ul

izof

urah

ishw

a

nazo

?

Ni m

akal

a 3

zipi

ziliz

okuf

urah

isha

kido

go?

Mak

ala

3 zi

pi

ziliz

okup

asha

haba

ri z

aidi

?

Mak

ala

3 zi

pi

ziliz

okuw

a na

upun

gufu

?

Kumbuka zawadi zitapatikana kwakuchezesha DRAW. Baada ya

DRAW hiyo majina mananeya kwanza yatapewa

ushindi.

11. 12. 13. 14.

a. Usalama kwanzab. Vichekeshoc. Hepatitis Bd. Lisemwalo lipo!e. Habari njema!f. Bastola ya majig. Tupa salamah. Makala ya afya ya BBCi. Maswali ya kushindania/uthibitishoj. Chemsha bongok. Wanasemaje kuhusu chanjo?

ANDIKA JINA NA NWANI KAMILI ILI UWEZEKUJISHINDIA REDIO........................................................................................................................................................................................................................................................................................

FOMU YA KUTHIBITISHA

Wasiliana na: “JISHINDIE REDIO”, EPI, World Health Organization, P.O.Box 9292, Dar es Salaam

Page 25: MBIU YA AFYA MAGAZIN - sailvega.com projects/pdf/MBIU YA AFYA MAGAZIN.pdf · Halo, hapo ni kwa DCCO? Ndio, nikusaidie nini? Pamekuwa na uhaba wa vifaa katika nchi nzima kwa kipindi

CHEMSHA BONGO24

KEHOMAKYTNDUIK

AIJANUZIUAOJIM

OTFTKIBOFUUCAB

YUZUORWOAUHNPK

ASMOABOMHWAAIO

KOAWRKKJAAWCWK

DIYFAUOIPTHEUA

SCDDUKDOSOEHTV

EUNOJRLAMUANSI

DORHNIAIFRKJDP

DFGUODZBIIIAUE

UKOMAYASDPKMRA

KIFAFAHCUEUGUI

MLTOMALARIAOHE

Ndani ya jedwali hili kuna majina yamagonjwa hatari ya kuambukizayanayoleta athari kwa watoto wadogo.Yanasomeka kwa mielekeo ya pandembali mbali:Tafadhali yaonyeshe yalipo kishauyaandike hapa chini:

(a) ..............................................(b) ..............................................(c) ..............................................(d) ..............................................

C H E M S H A B O N G O N a . 1 C H E M S H A B O N G O N a . 2

Katika chemsha bongo hii, jaribu kutambua kama maelezo yaliyoandik-wa hapo chini ni ya kweli au siyo ya kweli. Kama ni kweli chukua heru-fi iliyoko upande wa “ndio” kulingana na namba za pembeni na kuiandi-ka sehemu ya “uchaguzi wako”.Kama siyo kweli fanya vivyo hivyo kwakuchukua herufi iliyoko upande wa “hapana” na kuiandika upande wauchaguzi wako.Ukimaliza kujaza kwa usahihi, utapata neno lenyeujumbe maalum.

1. Siyo vibaya kuichomoa sindano kwenye bomba lake kwa mkono baada ya kutumika.

2. Je, kabla ya kuzitupa sindano zilizotumika ni lazima kuziweka kwenye maboksi maalum?

3. Ugonjwa wa pepopunda huwapata watu wa rika zote na huambukizwa kwa njia ya hewa?

4. Kurudisha kifuniko cha sindano ni hatari kwani mtu anaweza kujichoma na kuambukizwa ugonjwa.

5. Ni kweli kwamba dalili mojawapo ya ugonjwa wa kifua kikuu ni kuvimba mwili?

6. Mabomba ya sindano yaliyotolewa sindano yanaweza kutupwa kama takataka nyingine zinavyotupwa.

7. Sindano iliyochemshwa vizuri haiwezi kumdhuru mchomwaji.

8. Siyo vibaya kumdunga mgonjwa sindano isiyo chemshwa kama kuna haraka ya kuokoa maisha ya mgonjwa.

9. Ugonjwa wa ini (Hepetitis B) hauna tiba. Isipokuwa unaweza kuuzuia kwa dawa ya chanjo tu.

10.Mtu hawezi kupata ugonjwa wa pepopunda kwa kuchomwa na sindano iliyotumika.

Na. Ndio Hapana Uchaguziwako

1.

2.

3.

4.

5.

6.

7.

8.

9.

10

P

E

T

O

C

H

D

N

N

O

K

A

O

A

M

E

A

P

J

A

MAJIBU: *Chemsha bongo na. 1:(a)Surua (b)Polio (c)Dondakoo (d)Kifaduro. *Chemsha bongo na. 2: “PATACHANJO”