Upload
others
View
18
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
MKATABA W A H U D U M A K W A W A T E J A
WeweUna Umuhimu
Kwetu
CS-CHARTER2019 KISWAHILI.indd 1 8/14/19 12:32 PM
2
YA
LI
YO
MO Sisi Ni Nani
Jukumu Letu
Maadili Yetu ya Kimsingi
Mkataba wa Huduma kwa Wateja
Wateja wetu wa Kudhaminiwa
Huduma Zetu za Kimsingi
- Huduma za Baharini
- Uchukuzi wa Mizigo
Viwango Vya Huduma Zetu
Dhamira Yetu Kwako
- Haki Zako
Matarajio ya Wateja
Ufuatiliaji wa Mkataba
- Kushughulikia Malalamiko
Kuwasiliana Nasi
3
4
5
7
8
9
10
11
12
14
15
CS-CHARTER2019 KISWAHILI.indd 2 8/14/19 12:32 PM
3
SISI NI NANI
Mamlaka ya Bandari za Kenya (KPA) ni shirika lililobuniwa kisheria chini ya Wizara ya Uchukuzi, Miundo Msingi, Nyumba, Maendeleo ya Miji na Ujenzi kwa mujibu wa sheria iliyopitishwa na bunge mnamo tarehe 20 Januari, 1978. Mamlaka haya yana jukumu la kuendesha na kusimamia bandari zote, mito na vituo vya makasha hapa nchini Kenya kukiwa na ofisi ya shirika mijini Kampala, Kigali na Bujumbura ambazo zinahudumia kanda ya maziwa makuu.
CS-CHARTER2019 KISWAHILI.indd 3 8/14/19 12:32 PM
4
JUKUMU MAONO
UJUMBE
Kutayarisha, kusimamia, kuendesha, kuboresha na kuthibiti bandari zote zilizoratibiwa katika ufuo wa pwani na maziwa ya Kenya
Bandari bora ya kimataifa
Kutoa huduma za bandari zilizo bora na nafuu ili kufanikisha biashara ya kimataifa
CS-CHARTER2019 KISWAHILI.indd 4 8/14/19 12:32 PM
5
MAADILI YETU YA
KIMSINGI
Huduma kwa Wateja: Kufanikisha huduma ni jambo muhimu katika shughuli zetu ili tuweze kutosheleza kikamilifu matarajio ya wateja
Uadilifu: Tunadumisha haki, uaminifu, ujuzi na uwazi katika shughuli zetu
Umoja Kazini: Sisi hufanya kazi kama timu moja katika shughuli zetu zote
Ubunifu: Sisi ni wabunifu na tunazidi kuongeza thamani kwa wateja wetu
Kujali: Tunajali maslahi ya wafanyikazi, jamii zilizo karibu nasi na tunazingatia uhifadhi wa mazingira
CS-CHARTER2019 KISWAHILI.indd 5 8/14/19 12:32 PM
7
MKATABA WA HUDUMA KWA WATEJA Mkataba huu ni azimio letu la kuendelea kuboresha huduma zetu na kutimiza matarajio
yako. Hii inafafanua ahadi yetu ya kukuhudumia wewe kwa viwango vilivyo wazi ili kuhakikisha uwasilishaji wa huduma bora, zenye ufanisi.
CS-CHARTER2019 KISWAHILI.indd 7 8/14/19 12:32 PM
8
Wateja wetu ni watu binafsi, shirika lolote tunalolihudumia pamoja na wenye nia na huduma zetu. Wao ni:WATEJA
WETU WA KUTHAMINIWA
Wateja wa Kimsingi
• Makampuni ya usafiri wa meli
• Waagizaji bidhaa kutoka nchi za nje
• Wauzaji bidhaa nje ya nchiWateja wa Ngazi ya Pili
• Mawakala wa usafiri wa meli
• Mawakala wa kusimamia na kushughulikia mizigo
• Wasafirishaji mizigoWadau Wengine
• Wahusika katika nyanja ya uchukuzi wa mizigo
• Umma kwa jumla
CS-CHARTER2019 KISWAHILI.indd 8 8/14/19 12:32 PM
9
HUDUMA ZETU ZA
KIMSINGI
KPA inatoa huduma zifuatazo:
Huduma kwa meli: Kuongoza na kuegesha meli
Huduma za Mizigo:
Kupakua na kupakia mizigo bandarini
CS-CHARTER2019 KISWAHILI.indd 9 8/14/19 12:32 PM
10
Tunaahidi kutekeleza:Kwa ujumla
• Kutoa huduma za bandari masaa 24 kwa siku, siku saba kwa wiki, isipokuwa mnamo tarehe 1 Mei na tarehe 25 Disemba ya kila mwaka
• Kujitambulisha kwa kuonyesha beji zenye majina yetu
• Kukuhudumia kwenye mazingira ya kazi yaliyo salama
Shughuli za Bandari
• Kuhakikisha kuwa vifaa vya kuelekeza meli vipo kwa 100% wakati wote
• Kutoa huduma za kuongoza (Usaidizi kuegesha meli) na kupakia ndani ya dakika 30 baada ya kuitishwa
• Kuanza shughuli za kupakua/kupakia ndani ya muda wa saa moja baada ya kuwasili meli bandarini ama gari moshi katika kituo chetu cha ICD – Embakasi
• Kuwasilisha makasha yako ndani ya masaa 5 baada ya kuingia yadi ya kuhifadhi makasha
• Kupakia mizigo ya moja kwa moja ndani ya masaa 2 ya kuingia bandarini kwa kutegemea kuwepo kwa mizigo melini.
Ushughulikiaji wa Hati
• Kutayarisha ankara ndani ya dakika 30 pindi tupokeapo agizo la Pick Up Order au Pre – Advice yako
Mawasiliano
• Kujibu barua pepe ndani ya masaa 24
• Kuthibitisha kupokea na kujibu barua zako ndani ya siku 5 za kazi na iwapo ni maswala magumu, kukufahamisha muda unaokadiriwa kuchukua ili kukujibu kikamilifu
Simu
• Tuko imara kupokea simu zako masaa 24 kila siku
• Tutajibu simu zako ndani ya milio mitatu
• Tutakutambulisha idara uliyopigia simu na jina la afisa
anayepokea simu.
VIWANGO VYA HUDUMA ZETU
CS-CHARTER2019 KISWAHILI.indd 10 8/14/19 12:32 PM
11
• Tutakuhudumia kwa ufanisi, bidii na utaalamu
• Utahudumiwa kwa heshima na wafanyikazi wetu watakusaidia ili kuhakikisha mashaka yako yameshughulikiwa kwa upesi
• Tutatekeleza huduma zetu kwako kwa uaminifu mkubwa na kwa siri
• Tutauliza mashirika husika, maswala tata yanayohitaji umakini ili kuwezesha utatuzi
Haki zako Uko na haki ya:
• Kuuliza au kulalamika iwapo hujaridhika na kiwango cha huduma iliyotekelezwa
• Kupeleka lawama zozote kuhusu huduma duni kwa afisa wa daraja la juu, iwapo hukutosheka na majibu au suluhisho ulilopewa
• Kutoa maoni yako yatakayowezesha mamlaka kutoa huduma bora zaidi
• Kushughulikiwa kwa heshima na uangalifu unapoamiliana nasi
• Kupata majibu ya masuala yanayokuathiri
• Huduma bora bila ya kusumbuliwa
AHADI YETU KWAKO
CS-CHARTER2019 KISWAHILI.indd 11 8/14/19 12:32 PM
12
Ili kutuwezesha kuwahudumia kwa njia bora, tunawatarajia: • Kutoa habari sahihi, kwa wakati ufaao na kukamilisha hati zote
• Kuwa na busara na heshima kwa wafanyikazi wa KPA
• Kutoa habari mpya kuhusu shirika lako na mahitaji yake
• Kudumisha uadilifu na utaalamu katika shughuli zako na KPA
• Kutoa maoni juu ya ubora wa huduma zinazotolewa
• Kupendekeza njia mwafaka za kuboresha huduma zetu
MATARAJIO YETU KWA WATEJA
CS-CHARTER2019 KISWAHILI.indd 12 8/14/19 12:32 PM
14
Tutaendelea kuchunguza na kutathmini viwango vya huduma zetu tunazotoa kama ilivyo katika mkataba huu na kwa mashauriano na wadau wetu. Kuufanyia ukariri kila baada ya miaka 3 kulingana
na mabadiliko katika mazingira ya biashara.
Kushughulikia Malalamiko
Malalamiko ya wateja yatashughulikiwa katika vituo husika vya huduma. Tafadhali tazama nambari za mawasiliano katika ukurasa unaofuata ili kujua sehemu mwafaka za kupata huduma.
Iwapo bado unahisi hujaridhika, tafadhali tutumie barua pepe kwa anwani [email protected] ukitoa maelezo kamili kuhusu malalamiko yako ili tuweze kuyasuluhisha.
UCHUNGUZI NA KUCHANGANUA
MATOKEO YA MKATABA HUU
CS-CHARTER2019 KISWAHILI.indd 14 8/14/19 12:32 PM
15
Makao Makuu
Namba za Simu +254 - 41-2112999/3999
+254 - 709-092999/709-093999
+254 - 730-653999
Depo ya Makasha ya Nairobi (ICD)
+254 - 20-6931000
+254 - 723-786759/60
OFISI YA KPA YA KAMPALA
+256 - 414-346221/2
OFISI YA KPA YA KIGALI +250 - 735-401198
OFISI YA KPA YA BURUNDI +257 - 22-278723
WASILIANA NASI
CS-CHARTER2019 KISWAHILI.indd 15 8/14/19 12:32 PM
KWA MAELEZO ZAIDI Masuala ya kawaida/maelezo: [email protected] Mapendekezo, Malalamiko na heko: [email protected] Makao Makuu ya KPA, Kipevu Road,P. O. Box 95009-80104, Mombasa, Kenya.
TOLEO LA 2018
CS-CHARTER2019 KISWAHILI.indd 16 8/14/19 12:32 PM