7
BODI YA UAINISHAJI FILAMU NCHINI KENYA BODI YA UAINISHAJI FILAMU NCHINI KENYA Mkataba Wa Utoaji Huduma Kwa Raia

Mkataba Wa Utoaji Huduma Kwa Raia - kfcb.co.kekfcb.co.ke/wp-content/uploads/2016/07/KFCB-Service-Charter-swahili-revised.pdf · Bodi ya uaninishaji filamu nchini Kenya ni taasisi

  • Upload
    others

  • View
    22

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Mkataba Wa Utoaji Huduma Kwa Raia - kfcb.co.kekfcb.co.ke/wp-content/uploads/2016/07/KFCB-Service-Charter-swahili-revised.pdf · Bodi ya uaninishaji filamu nchini Kenya ni taasisi

BODI YA UAINISHAJI FILAMU NCHINI KENYABODI YA UAINISHAJI FILAMU NCHINI KENYA

Mkataba Wa Utoaji Huduma Kwa Raia

Page 2: Mkataba Wa Utoaji Huduma Kwa Raia - kfcb.co.kekfcb.co.ke/wp-content/uploads/2016/07/KFCB-Service-Charter-swahili-revised.pdf · Bodi ya uaninishaji filamu nchini Kenya ni taasisi

Mkataba Wa Utoaji Huduma Kwa Raia KFCB Mkataba Wa Utoaji Huduma Kwa Raia KFCB 1

KITANGULIZI

Mkataba wa utoaji huduma kwa raia wa bodi ya uainishaji filamu nchini Kenya imeundwa kwa lengo la kutambua wadau wetu, wateja, huduma na viwango madhubuti.

Mkataba huo unanuia kuboresha utoaji huduma kwa kutoa habari kuhusu bodi hiyo. Tumeweka vigezo vya huduma tunazotoa ili wateja wetu wafahamu watakayotarajia watakapohitaji huduma kutoka kwetu. Huduma zikitolewa, mteja ataweza kutathmini ikiwa tumefikia viwango vinavyostahili kama ilivyo kwenye mkataba.

Ikiwa huduma hizo hazifikii viwango vilivyowekwa, mkakati wa utaratibu wa marekebisho upo ili tuendelee kuimarisha huduma zetu na kutosheleza mahitaji ya mteja.

MAMLAKA

Bodi ya uaninishaji filamu nchini Kenya ni taasisi ya kisheria yenye jukumu la udhibiti katika sehemu ya III sheria ya filamu na tamthilia, kifungu cha 222 ya sheria za Kenya. Sheria hiyo inaipa bodi hii mamlaka ya kudhibiti ubunifu, upeperushaji, usambazaji na maonyesho ya filamu. Ili kutimiza malengo ya mamlaka haya, bodi hii hutekeleza shughuli zifuatazo:

1. Kuhakikisha kwamba filamu na mabango yote nchini yanachunguzwa na kuainishwa kabla ya kuonyeshwa, kukodishwa, kuuzwa au kupeperushwa kwa njia za maonyesho ya video, sinema jukwaani, kuuzwa na wachuuzi au kupeperushwa katika stesheni mablimbali.

2. Kuratibu masuala yote yanayohusiana na uainishaji na maonyesho ya filamu nchini.

3. Kuhakikisha kuwa vyeti vya kutoa idhini vinatolewa kwa filamu zilizowasilishwa ili kuainishwa.

4. Kutunga muongozo mwafaka wa sera kwa serikali kuhusu maonyesho ya filamu na usambazaji nchini.

5. Kutekeleza na kuimarisha utafiti kuhusu uaninishaji wa filamu kwa kuzingatia maslahi ya wadau wote.

6. Kuhakikisha kwamba orodha ya uainishaji inatolewa kwa wanaosambaza na kuonyesha filamu.

7. Kukagua na kutoa leseni kwa maduka na kumbi za wanaosambaza na kuonyesha filamu nchini.

8. Kuhakikisha kwamba ukiukaji wa kipengee chochote cha sheria hiyo unashtakiwa.

Page 3: Mkataba Wa Utoaji Huduma Kwa Raia - kfcb.co.kekfcb.co.ke/wp-content/uploads/2016/07/KFCB-Service-Charter-swahili-revised.pdf · Bodi ya uaninishaji filamu nchini Kenya ni taasisi

MAONO

Kuwa wadhibiti wa maudhui ya filamu wenye kiwango cha kimataifa.

WADAU WETU

Wateja na wadau wetu wanahusisha:

● Maonyesho ya video, maktaba za video, maduka ya video, mikahawa na wasimamizi wa kumbi za sinema

● Stesheni za upeperushaji vipindi● Wabunifu wa filamu ● Taasisi za serikali● Mashirika yasiyo ya kiserikali ● Taasisi za kidini● Umma ● Wafanyakazi ● Bodi ya wakurugenzi

MALENGO

Kulinda maadili ya kitaifa na kanuni kwa njia mwafaka na mahsusi za utoaji huduma za udhibiti wa filamu.

MAADILI YA MSINGI

♦ Utaaluma.♦ Haki na kutopendelea♦ Ubora wa huduma♦ Uadilifu♦ Utuzwaji wa talanta♦ Uaminifu♦ Usimamizi bora♦ Uwajibikaji na uwazi♦ Timu ya kazi♦ Uboreshaji na ubunifu

MALENGO HALISI

♦ Kuchunguza na kuainisha filamu mpya, vidokezo na mabango.♦ Kuendeleza miongozo ya uainishaji wa filamu.♦ Kudhibiti maudhui ya maonyesho ya filamu kwa umma.♦ Kuwezesha ukaguzi wa video na maduka ya sinema.♦ Kufuatilia maudhui ya vipindi vinavyopeperushwa

Mkataba Wa Utoaji Huduma Kwa Raia KFCB Mkataba Wa Utoaji Huduma Kwa Raia KFCB 32

Page 4: Mkataba Wa Utoaji Huduma Kwa Raia - kfcb.co.kekfcb.co.ke/wp-content/uploads/2016/07/KFCB-Service-Charter-swahili-revised.pdf · Bodi ya uaninishaji filamu nchini Kenya ni taasisi

BAADHI YA HUDUMA

Sisi hutoa huduma mbalimbali zikiwemo:

1. Kuchunguza na kuainisha filamu mpya kulingana na kifungu cha 222 cha filamu na uigizaji cha sheria za Kenya na sheria ya Habari na Mawasiliano kifungu cha 411A.

2. Ufuatiliaji wa usambazaji wa filamu ili kuhakikisha kwamba hakuna filamu au aina ya filamu inasambazwa, kuonyeshwa au kupeperushwa, iwe hadharani au faraghani, bila bodi kuichunguza na kutoa cheti cha kidini

3. Kufuatilia upeperushaji wa filamu na vipindi ili kuhakikisha maudhui yanayowalenga watu wazima hayapeperushwi katika muda uliowekwa wa saa 11 asubuhi na saa nne usiku.

4. Kutoa vyeti na leseni kwa wasambazaji na wanaoonyesha filamu.5. Kupendekeza miongozo itakayotumika kuchunguza na kuainisha

filamu.6. Kutoa maagizo mara kwa mara wa utaratibu wa kutoa leseni ya

wanaoonyesha na kusambaza filamu.

Mkataba Wa Utoaji Huduma Kwa Raia KFCB Mkataba Wa Utoaji Huduma Kwa Raia KFCB 54

● Kuafikia viwango vyetu vya utoaji huduma;● Kufanya kazi kwa kujitolea katika kuyapa kipaumbele mahitaji ya

wateja;● Kuwasiliana kwa ufanisi kwa kutumia lugha fasaha;● Kutoa ushauri thabiti na sahihi kuhusu huduma zetu;● Kutoa taarifa za kutosha kuhusu huduma zetu katika njia ya wazi;● Kudumisha viwango vya uwezo na maadili ya utendakazi;● Kuzingatia masuala ya jinsia na ulemavu katika kushughulika na

wateja wetu na wadau;● Kuhakikisha kwamba hakuna mtu atakayebaguliwa kwa misingi ya

hali yake ya afya;● Kukuza sera ya kutotoa rushwa katika ngazi zote;● Kuweka mazingira bila dawa za kulevya kwa wateja wetu na

wadau;● Kuendeleza mifumo ya ufuatiliaji na tathmini ili kutuwezesha

kufuatilia utendakazi;● Kukuza utamaduni wa kuwepo mazingira bora;● Kuchukua hatua ya kurekebisha ulegevu unaoweza kutokea katika

mifumo yetu;● Kuendeleza mabadiliko na ubunifu kwa njia ya kuendelea

kuboresha mifumo na michakato;● Kutumia raslimali zetu kwa busara ili kutuwezesha kutoa huduma

7. Toa lengo la kuwazuia kina mama na watoto dhidi ya unyanyasaji wa kingono katika utoaji filamu na kwenye mtandao wa Internet,

KANUNI KUU ZA UTOAJI HUDUMA

Tutasambaza habari kuhusu huduma zetu iwezekanavyo kwa kutumia majukwaa ya vipeperushi, majarida, tovuti na vyombo vya habari vya kijamii. Mara kwa mara, tutaendelea pia kuboresha viwango vya utoaji huduma kulingana na mahitaji ya wateja na kuendelea kupata maoni tukiahidi :-

Page 5: Mkataba Wa Utoaji Huduma Kwa Raia - kfcb.co.kekfcb.co.ke/wp-content/uploads/2016/07/KFCB-Service-Charter-swahili-revised.pdf · Bodi ya uaninishaji filamu nchini Kenya ni taasisi

zinazopatikana kwa urahisi na zilizoimarika; na● Kuheshimu na kulinda usiri wa habari zinazotolewa na wateja.

Vigezo vya Utendakazi

Tuna madhumuni ya kutoa huduma bora kama ilivyoratibishwa katika vipengee vifuatavyo vya utendakazi:

1. Mkakati wa mpango wa Bodi ;2. Mpango wa kila mwaka wa KFCB;3. Mkataba wa utendakazi wa KFCB;4. Rasimu ya ubora ya KFCB na ISO 9001:20085. Sheria ya Filamu na Michezo ya kuigiza, Sura ya 222 ya sheria za

Kenya;6. Kanuni ya 2009 za Upeperushaji wa Mawasiliano; na7. Kifungu cha 411 cha Sheria ya Kenya ya Habari na Mawasiliano

na sheria zingine husika.

VIWANGO

● Kutoa video na leseni za sinema dakika kumi na tano (15) baada ya maombi;

● Kutoa vibandiko vya uainishaji kabla dakika kumi na tano (15);● Kuidhinisha na kutia muhuri mabango ya sinema ndani ya dakika

kumi (10);● Kuchunguza na kuainisha filamu kwa siku moja (1);● Kusanifisha orodha ya uainishaji filamu kila wiki;● Kufanya ukaguzi wakati wowote wa maeneo ya wahusika kila wiki;● Kuandaa hati za malipo ndani ya siku mbili (2) za kazi;● Kutekeleza malipo ya huduma ndani ya (7) ya siku saba za kazi;

● Kufanya elimu ya wadau na mipango ya uhamasishaji kila mwaka;● Kufanya utafiti wa kuridhika kwa wateja kila mwaka;● Kujibu maswali ya wateja na wadau mara moja;● Kuwasilisha nakala ya video inayoshukiwa kabla ya siku; na● Kushughulikia malalamiko ya wateja na wadau ndani ya siku kumi

na tano (15) siku za kazi.

Mkataba Wa Utoaji Huduma Kwa Raia KFCB Mkataba Wa Utoaji Huduma Kwa Raia KFCB 76

WAJIBU WA MTEJA

● Jifahamishe na huduma zetu;● Toa habari kamili na sahihi kutuwezesha kutenda ipasavyo;● Toa maoni juu ya huduma zetu;● Shiriki katika miradi yetu;● Jifahamishe na sheria na taratibu za serikali;● Bainisha maeneo ya udhaifu katika utoaji wetu wa huduma na

kuwasiliana nasi;● Pendekeza njia za kuboresha huduma zetu; na● Kutotoa vishawishi kwa njia ya zawadi au neema kwa wafanyakazi

au kutendewa vivyo hivyo kwa ajili ya huduma.

MFUMO WA MAREKEBISHO Umma na pia wadau wetu wanahimizwa kutoa mapendekezo ya kweli, pongezi na malalamiko kibinafsi, kwa njia ya posta, simu au barua pepe.

Page 6: Mkataba Wa Utoaji Huduma Kwa Raia - kfcb.co.kekfcb.co.ke/wp-content/uploads/2016/07/KFCB-Service-Charter-swahili-revised.pdf · Bodi ya uaninishaji filamu nchini Kenya ni taasisi

MAONI

Maoni yanaweza kutumwa kwa :

Afisa Mkuu Mtendaji,Kenya Film Classification Board,

Uchumi House 15th Floor,S. L. P 44,226-00,100,

NAIROBI.

Simu :020 2250600 / 2241804Simu ya mkononi: 0711 222 204, 0773 753 355

Barua pepe: [email protected]

Tovuti: www.kfcb.co.ke

Malalamishi : [email protected]

www.facebook.com / kfcb.officialpage

www.twitter.com / InfoKfcb

Mkataba Wa Utoaji Huduma Kwa Raia KFCB Mkataba Wa Utoaji Huduma Kwa Raia KFCB 98

Bodi ina kitengo cha kutoa malalamiko ambayo ni wajibu wa kushughulikia malalamiko ya wateja. Mara kwa mara, Bodi itawasiliana na Tume ya Utawala wa Sheria kwa ajili ya kujifahamisha na masuala ya malalamiko

Tunahakikisha usiri na faragha ili kulinda kitambulisho cha mlalamikaji. Ingawa walalamikaji wanaweza kuchagua kutotambuliwa, tunawahimiza walalamikaji kutambua wenyewe ugumu uliopo ikiwa watatoa malalamiko bila kujitambulisha.

MAREJELEO YA MKATABA

Kulingana na kadri mambo yanavyobadilika, tutaurekebisha mkataba huu kwa azimio la kuendelea kuimarisha huduma zetu.

Page 7: Mkataba Wa Utoaji Huduma Kwa Raia - kfcb.co.kekfcb.co.ke/wp-content/uploads/2016/07/KFCB-Service-Charter-swahili-revised.pdf · Bodi ya uaninishaji filamu nchini Kenya ni taasisi