74
MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA WALIMU WA MADARASA YA MWANZO Moduli ya Kwanza: UTARATIBU WA KUANDAA MAZINGIRA YALIYOSHEHENI MACHAPISHO Moduli ya Mwalimu

Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

  • Upload
    others

  • View
    63

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA WALIMU WA MADARASA YA MWANZO

Moduli ya Kwanza: UtaratibU Wa KUandaa Mazingira

YaliYosheheni Machapisho

Moduli ya Mwalimu

Page 2: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 2

Page 3: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 3

MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA WALIMU WA MADARASA YA MWANZO

Moduli ya Kwanza: UtaratibU Wa KUandaa Mazingira

YaliYosheheni Machapisho

Moduli ya Mwalimu

Page 4: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 4

Moduli hii imetayarishwa kwa ushirikiano na:

Wizara ya elimu na Mafunzo ya Ufundi Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Taasisi ya Elimu Tanzania Chuo Kikuu cha Dodoma

Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania

Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa eQUip-tanzania

Moduli hii imewezeshwa kwa ushirikiano na:

C.C.U Butimba C.C.U Bustani C.C.U Tabora c.c.U ndala C.C.U Kasulu

C.C.U Kabanga c.c.U bundaC.C.U Tarime

c.c.U shinyangaC.C.U Mpwapwa

Page 5: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 5

Maelekezo na taswira katika moduli

Kuna picha na michoro mingi katika moduli. Baadhi zinajirudia mara nyingi kwa sababu zinamaanisha jambo mahususi linalotokea. Chini kuna mfano wa taswira mbalimbali ambazo zinapatikana katika moduli pamoja na kile ambacho zinawakilisha:

Jadili na mwenzako: Wakati wote wa kusoma moduli, walimu wataelezwa kufanya kazi pamoja na mwalimu mwingine juu ya maswali au kazi.

Fikiri– Wawili wawili – Shirikishana: Kama ilivyo katika maelezo ya hapo juu, hapa vilevile walimu wanafanya kazi wakiwa wawili wawili. Japokuwa, hapa walimu wanatafakari mmoja mmoja kwanza juu ya swali au tatizo, halafu wanafanya kazi mwalimu mwenzake na mwishoni wanawasilisha katika kundi lote.

Jadiliana katika kikundi: Wakati mwingine walimu wataelekezwa kutafakari au kujadili maswali mbalimbali katika kikundi.

Soma: Katika kila moduli kuna “dhana kuu” ambayo kwa kawaida huwasilishwa kwa kirefu katika maelezo.

Andika: Moduli itawahamasisha walimu kuchukua maelezo na kuandika fikra zao na majibu.

Igizo: Baadhi ya mazoezi yatahitaji walimu kuigiza kazi ya kufundisha wakati wengine watapaswa kuigiza kama wanafunzi.  

Page 6: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

6Mwongozo wa Kitaifa wa Ujuzi wa Uongozi Mahiri Katika Shule - Tanzania

Mafunzo ya Walimu Kazini ngazi ya shule kwa walimu wa madarasa ya mwanzo

Moduli ya Kwanza: Utaratibu Wa Kuandaa Mazingira Yaliyosheheni Machapisho

MAUDHUI YA MODULI:

Moduli hii inamsaidia mwalimu kuandaa mazingira yaliyosheheni machapisho katika darasa na kuanzisha utaratibu wa kufundisha kwa kurudia rudia ili kuimarisha uwezo wa wanafunzi kujifunza kusoma kwa ufanisi.

DHANA KUU:

Mazingira yaliyosheheni machapisho: Humaanisha darasa lenye picha, kadi za maneno, majina ya wanafunzi, chati ya alfabeti, michoro na machapisho mengine yanayofanana na hayo. Mazingira yaliyosheheni machapisho ni muhimu kwa sababu wanafunzi wanahitaji kuona herufi na maneno mara kwa mara ili wajifunze kusoma kwa ufanisi.

MALENGO YA MODULI:

Baada ya kumaliza moduli hii kila mwalimu ataweza:• Kuandaa utaratibu wa kufundisha kwa kurudiarudia ili kuwajengea wanafunzi tabia ya

kujisomea.• Kubainisha vifaa muhimu vya kuandaa ili darasa liwe na zana zinazotosheleza.• Kuwezesha ujifunzaji wa kusoma Kiswahili kwa kutumia mbinu rahisi kama vile ”ujumbe wa

kila asubuhi”, ”herufi ya siku” na ”wimbo wa alfabeti”.

MAANDALIZI YA KIPINDI:

Mara zote uwe na Moduli yako ya Mafunzo ya Walimu Kazini na kalamu

TARATIBU ZA KUJIFUNZA KWA KILA KIPINDI:

1. Kutana katika sehemu tulivu yenye ubao kama inavyoonekana katika picha 2. Panga madawati/meza ili kuwezesha washiriki wote waonane na kuongea pamoja 3. Kuwa huru kuuliza maswali kama hujaelewa 4. Kuwa wa msaada kwa wenzako 5. Kuwa mbunifu na fikiria jinsi dhana unazojifunzazinahusiana na darasa lako 6. Weka simu yako katika hali ya mtetemo

Page 7: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 7

UTANGULIZI

Chunguza chumba (dakika 15)

Kwa kushirikiana na mwenzako tazama sehemu ya madarasa mawili hapa chini.

Darasa A Darasa B

Jadili maswali yafuatayo pamoja na mwenzako na andika majibu:

Umegundua nini kuhusu madarasa haya? Andika mambo yanayofanana? Andika mambo yanayotofautiana?

Yanayofanana: Yanayotofautiana:

Unafikiri darasa lipi linamwezesha mwanafunzi kuwa na uwezo wa kujifunza kusoma kwa ufanisi? Kwa nini unafikiri hivyo?

Page 8: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 8

Wanafunzi hujifunza kusoma kwa haraka wanapokuwa kwenye mazingira yaliyosheheni machapisho kama vile vitabu, chati ya alfabeti, kadi za herufi darasani. Kwa kadri wanavyoona machapisho kwa wingi kila siku ndivyo akili zao hutaka kujifunza kusoma mambo mengi zaidi.

Darasa lenye ‘mazingira yaliyosheheni machapisho’ ni darasa linalotosheleza mahitaji ya wanafunzi katika kuona na kujifunza maudhui yaliyokusudiwa. Mazingira yaliyosheheni machapisho yana manufaa yafuatayo: 1) Huchochea stadi ya kuongea, kusikiliza, kusoma na kuandika kwa uhalisi; 2) Huwavutia wanafunzi kwa sababu ya matumizi ya rangi ambayo hufanya herufi na maneno yaliyoumbwa vizuri kupendeza ; 3) Darasa lenyewe huwa zana ya kufundishia; 4) Ni rahisi kulitumia kulingana na utaratibu wa darasa.

Kubandika majina ya vitu darasani, kutundika chati ya alfabeti na kuandika taarifa mbalimbali ubaoni ni njia muhimu ya kuwawezesha wanafunzi kujifunza msamiati mwingi zaidi. Darasa lenye kadi nyingi za maneno na picha huwawezesha wanafunzi kujizoesha kuhusianisha herufi moja moja na utamkwaji wake, muunganiko wa herufi na utamkwaji wake, na pia maneno na maana zake. Hii hutokea wanafunzi wanapoangalia kadi na picha hizo katika kila kona ya darasa au wanapoelekezwa na mwalimu ambaye hutumia kadi na picha hizo za kufundishia na kujifunzia.

Kujenga mazoea ya kutumia zana hizi, kunaimarisha kujifunza usomaji halisi wa kila siku na matumizi mbalimbali ya herufi na maandishi darasani. Kwa mfano, endapo mwalimu atabandika chati ya alfabeti darasani anaweza kuitumia kuimbisha wimbo wa alfabeti na kumtaka mwanafunzi aoneshe herufi zinazoimbwa, au akatumia maneno yaliyobandikwa darasani yakasaidia katika kusoma maneno mengine kama hayo kwenye vitabu.

Kujifunza kusoma kwa ufanisi ni muhimu sana kwa ajili ya mafanikio ya baadaye. Kwa sababu hiyo, mwalimu anapaswa kuhakikisha wanafunzi wanatumia muda wao mwingi inavyowezekana katika madarasa ya mwanzo kuona maandishi mengi, kubaini maneno mapya na kuandika wenyewe. Uzoefu unaonesha kuwa ufundishaji wa jumla wa herufi za alfabeti na dhana za maandishi darasani hautoshelezi. Ikumbukwe kuwa kila mwanafunzi anajifunza kwa uwezo unaotofautiana. Kwa hivyo, kila mmoja apewe fursa ya kutosha kujifunza kwa kuzingatia uwezo wake.

Unaweza kufanya mengi kuleta mabadiliko ya haraka na rahisi katika mazingira ya darasani yaliyosheheni machapisho ili kuendeleza ujifunzaji wa wanafunzi. Fanya jitihada zote kuhakikisha kuwa darasa lako lina “mazingira yaliyosheheni machapisho,” yaani darasa zima liwe limejaa picha, kadi za maneno, majina ya wanafunzi, chati ya alfabeti, michoro na machapisho mengine yanayofanana na hayo.

Jadiliana katika kikundi (dakika 10)1

1. Kwa kuzingatia matini uliyosoma hapo juu, taja ni sehemu gani ya matini ambayo unafikiri ni muhimu, haieleweki au ni mpya kwako?

1. Mwalimu mmoja anaanza kusoma kwa sauti. Baada ya kukamilisha aya anamwita mwalimu mwingine kwa jina asome aya inayofuata.

2. Wakati unaposoma:

- Weka alama ya mshangao (!) katika sehemu ambayo unaona ni muhimu

- Weka alama ya (?) katika sehemu ambayo huelewi au hukubaliani nayo

- Weka mduara katika maneno ambayo ni mapya.

DHANA KUU

Umuhimu wa Mazingira Yaliyosheheni Machapisho (dakika 15)

Page 9: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 9

Fikiri peke yako kisha washirikishe washiriki katika kikundi (dakika 10)

1. Fafanua kwa mifano dhana ya mazingira yaliyosheheni machapisho :

2. Taja njia tatu (3) unazoweza kutumia ili kulifanya darasa lako lisheheni machapisho:

a)

b)

c)

3. Jadili umuhimu wa mazingira yaliyosheheni machapisho:

ZOEZI

Kujenga utaratibu wa kufundisha na kijifunza katika mazingira ya darasa yaliyosheheni machapisho (dakika 25)

Ni muhimu kuwa na taratibu zinazoongoza utendaji darasani. Taratibu hizi zinaweza kujengwa kwa kurudia rudia shughuli wanazofanya walimu na wanafunzi. Shughuli hizo zaweza kuwa maandalizi ya awali, kusalimiana, chemsha bongo, maswali na majibu na tathmini. Taratibu za darasani zinazojirudia rudia huweza kuwasaidia wanafunzi kuimarisha stadi ya kuzungumza na kuandika. Kwa mfano, mwalimu anaweza kutumia salamu ya maandishi ubaoni badala ya kuzungumza. Salamu hii huitwa ‘Ujumbe wa Siku’ kama inavyofafanuliwa hapa chini

Ujumbe wa siku

Ujumbe wa siku ni wazo ambalo mwalimu huandika ubaoni kwa wanafunzi siku inapoanza. Ujumbe unaweza kuundwa na sentensi ambazo hutoa ujumbe wa:1. salamu2. Picha ya jumla kuhusu shughuli za siku3. Maelezo ya maudhui ya somo linalokusudiwa katika kipindi husika4. Swali linalohusu tukio muhimu lililotokea jana

Page 10: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 10

5. Swali linalohusu tukio muhimu linalotarajiwa 6. Dhana au jambo lenye kufurahisha ambalo limetendeka

Utaratibu wa kuandika ujumbe wa siku

Mwalimu unatakiwa kuandika ujumbe wa siku kabla wanafunzi hawajaingia darasani. Kwa wanafunzi wa darasa la kwanza ambao hawajajua kusoma, mwalimu unatakiwa kusoma ujumbe wa asubuhi kwa kuonesha maneno unayoyasoma kwa kutumia ncha kionesheo. Wakati unasoma, onesha kwa vitendo taratibu za ku-soma ambazo ni 1) kusoma kwa kuanzia kushoto kwenda kulia; 2) kuanzia juu kushuka chini.

Ufuatao ni mfano wa Ujumbe wa siku:

Njia nyingine ya kufundisha utaratibu zinazojirudiarudia ambao unaweza kuimarisha stadi ya kuzungumza na kuandika ni ufundishaji wa ‘Herufi ya Siku’ ’

Herufi ya siku

Fanya kazi hii kwa dakika 5-10 kila siku kulingana na uwezo wa wanafunzi wako ili kuwasaidia wanafunzi kufanya mazoezi ya kubaini herufi. Endelea na utaratibu huu unaojirudia rudia hadi utakapomaliza herufi zote.

1. Andika herufi za siku ubaoni.

2. Andika neno ambalo herufi ya siku inaanza mwanzo wa neno, mwisho wa neno na katikati ya neno (Tumia maneno ambayo yanafahamika vizuri kwa wanafunzi).

3. Wagawe wanafunzi katika makundi ya wanafunzi 3-5 kisha waongoze kundika maneno mengi yenye herufi ya siku kadri wanavyoweza. Kama darasa lina wanafunzi wengi, waongoze wanafunzi kufanya kazi na jirani aliye upande wa kushoto au kulia ili wasitumie muda mrefu kutengeneza makundi.

4. Kwa darasa la kwanza waongoze wanafunzi kubungua bongo maneno ambayo herufi ya mwanzo inawakilisha herufi ya siku.

5. Waongoze wanafunzi wa darasa la 2 na la 3 kuandika maneno ambayo yanaanza na herufi ya siku.

6. Kama una muda wa ziada, waongoze wanafunzi waje mbele na kuandika maneno sahihi ubaoni kama haya.

7. Anza na maneno yenye silabi mbili kwa darasa la kwanza na kisha maneno yenye kuundwa na silabi tatu kwa darasa la pili

Hamjambo watoto wazuri.Leo ni Jumatatu, siku ya kwanza ya juma.

Leo katika somo la Kiswahili tutajifunza kusoma herufi ’m’.Kisha tutajifunza kusoma maneno mapya.

Karibu tufurahie somo la leo.

Page 11: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 11

Njia nyingine inayojirudia rudia katika ufundishaji darasani ambayo inaweza kuimarisha stadi ya kuzungumza kwa wanafunzi ni wimbo wa alfabeti.

Wimbo wa Alfabeti

Kuimba wimbo wa alfabeti ni tendo la kufurahisha ambalo huweza kuwa rahisi katika kulifanya liwe la kujirudia rudia. Ni muhimu wakati unapoimba wimbo pamoja na wanafunzi, tamka kwa usahihi majina na sauti ya herufi ili wanafunzi wahamasike na kukuiga. Ni muhimu pia kuonyesha kila herufi kama unavyoiimba. Ni vema kuandika herufi ubaoni ili iwe rahisi kuonesha ni herufi gani wanayoimba.. Jaribu kufuatilia mabadiliko baada ya tendo hili.

1. Simama mbele ya chati ya alfabeti au andika herufi ubaoni.

2. Imba wimbo wa alfabeti pamoja na wanafunzi.

3. Tumia fimbo au kionesheo/kilichochongoka kuonyesha kila herufi unayoiimba

4. Imba tena wimbo, safari hii badilisha kasi. Kwa muda imba polepole na muda mwingine imba kwa haraka

5. Mwite mwanafunzi yeyote aje mbele kuliongoza darasa kuimba kwa njia ileile.

6. Mwelekeze mwanafunzi anayeimba kuonesha kila herufi anayoiimba.

Sasa ni wakati wa kujifunza taratibu hizi kwa kutumia igizo dhima.

Igizo (dakika 20)

Kila mwalimu atachagua utaratibu mmoja kati ya tatu tuliojifunza katika moduli hii ambao ni ‘ujumbe wa siku, ‘herufi ya siku’ na ‘wimbo wa alfabeti’. Utakuwa na dakika 10 za kuandaa igizo dhima ambapo wewe utakuwa mwalimu na washiriki wenzako watakuwa wanafunzi wa darasa la 1-3

Mwalimu atakayechagua utaratibu wa ‘Ujumbe wa siku’ lazima afikiri ujumbe mpya ambao utaandikwa ubaoni na utasomwa kwa pamoja (mwalimu na wanafunzi).

Mwalimu atakayechagua ‘herufi ya siku’ lazima abainishe maneno ambayo yanaanza na herufi ya siku, yanaishia naherufi ya siku na katikati ya neno kuna herufi ya siku.

Mwalimu atakayechagua wimbo wa alfabeti lazima aandike herufi ubaoni na kuzionesha herufi wakati wanafunzi wanaimba wimbo wa alfabeti.

Neno linaloanza na herufi ’a’

andazi

Neno linaloishia na herufi ’a’

baba

Bainisha herufi ’a’ katika neno

nazi

Page 12: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 12

Jadiliana katika kundi kubwa (dakika 5)

1. Je, ni wakati gani utaratibu uliochagua hapo juu unaweza kuwa muhimu zaidi darasani kwa-ko? (Utaratibu huu unaweza kuwa tofautina ule uliochaguliwa na mwalimu mwenzako).

2. Unawezaje kuboresha taratibu hizi na kuzitumia darasani?

KUPANGA MKAKATI

Kuandaa ‘Kipindi cha Kusoma na Kuandika’ (dakika 15)

Katika kuimarisha uwezo wa wanafunzi kujifunza kusoma na kuandika, ni muhimu mwalimu kuwa na mpango unaomwezesha kutumia maarifa mapya aliyojifunza wakati wa mafunzo ya walimu kazini kwa vitendo. Aidha ni muhimu kwa wanafunzi kupata muda zaidi wa kujifunza kusoma na kuandika. Kwa mantiki hii, ni muhimu kwa mwalimu kuandaa kipindi cha saa moja cha kusoma na kuandika mara moja kwa wiki. Kwa darasa la kwanza na la pili inaweza kuwa rahisi kupanga kipindi cha kujifunza kusoma na kuandika, ila kwa darasa la tatu ni vema kumshirikisha mwalimu mkuu na mwalimu wa taaluma ili kutoleta mkanganyiko katika ratiba ya masomo.

Soma kwa makini kanuni za kufundisha darasani hapo chini na kisha panga namna nzuri utakavyozitekeleza wakati wa kipindi cha ‘kusoma na kuandika’

Matumizi ya kanuni ya kwanza: Wimbo wa alfabeti

Utangulizi:

1. Andika herufi za alfabeti kwenye ubao

2. Uliza maswali rahisi yanayohusu alfabeti. Kwa mfano kuna herufi ngapi kwenye alfabeti? Ni herufi ipi ya mwanzo au ya mwisho? Ni herufi gani inayotangulia kabla ya herufi ‘m’? Herufi ipi inayotangulia kabla ya herufi ‘d’? Herufi ipi inafuata baada ya herufi ‘s’?

Vitendo:

3. Imba wimbo wa alfabeti pamoja na wanafunzi. Tumia kionesheo ili kuonesha kila herufi inayoimbwa. Kumbuka kutamka herufi kwa uwazi. Imba wimbo tena ila mara hii imba kwa haraka kidogo. Kisha badilisha utaratibu kwa kuimba pole pole na wakati mwingine imba kwa haraka. Ita mwanafunzi mmoja kusimama mbele ya darasa na aimbe wimbo wa alfabeti kwa kufuata utaratibu ulioanza nao. Kumbuka kuwaongoza wanafunzi kuonesha herufi wanayoitamka wakati wa kuimba wimbo.

Upimaji:

4. Futa herufi ubaoni na kisha waambie wanafunzi waandike herufi katika daftari zao za mazoezi (Kwa watoto wa darasa la kwanza wanaweza kuanza kuandika hewani, kisha kwenye mchanga baada ya hapo kwenye daftari zao.

5. Zunguka katika darasa kukagua wanafunzi wanavyoandika herufi kwenye daftari zao na kuwapa msaada wale wanaopata changamoto ya kuandika.

6. Andika orodha ya alfabeti ubaoni . Anza na herufi ‘a’ kisha chagua mwanafunzi mmoja mmoja kuandika herufi moja ya alfabeti.

7. Toa msaada kwa wanafunzi wanaopata ugumu wa kufanya zoezi hili.

Page 13: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 13

Matumizi ya kanunu ya pili: Ujumbe wa siku

Utangulizi:

1. Andika ujumbe wa siku kabla ya wanafunzi hawajaingia darasani

2. Kwa ujumla unaanza na salaam,kisha kutaja jina la siku, hali ya hewa ya siku hiyo na wakati mwingine unaweza kuanza kwa kuzungumzia tukio maalumu kwa mfano jaribio au ugeni wa mtu maarufu hapo shuleni.

Vitendo:

3. Mara baada ya wanafunzi kuketi waambie kuangalia ujumbe wa asubuhi ulioandikwa ubaoni

4. Waambie wanafunzi kila mmoja amulize jirani yake kama kuna neno katika ujumbe wa siku analoweza kulitambua.

5. Waulize wanafunzi kushirikishana maneno wanayoyatambua.

6. Wasomee ujumbe wa siku wanafunzi kwa sauti lakini polepole. Tumia kidole kuonesha maneno unayoya-soma kwenye ujumbe wa siku.

7. Soma ujumbe wa asubuhi kwa pamoja na wanafunzi huku ukionesha kila neno linalosomwa

Upimaji:

8. Rudia kusoma ujumbe wa siku. Wakati huu chunguza mwanafunzi anayepata ugumu wa kubashiri neno linalofuata wakati wa kusoma ujumbe wa asubuhi.

Jadili na mwenzako (dakika 15)

Ukiwa na mshiriki mwenzako, jadilianeni jinsi mnavyoweza kuingiza taratibu hizi za kufundisha katika andalio lako la somo na katika kipindi cha wiki cha kusoma na kuandika. Onesha kwa vitendo namna utakavyoweza kutumia kwa ufanisi taratibu hizi kwa darasa la kwanza, la pili, na la tatu. Kisha wasilisha mawazo yako kwenye kikundi.

Page 14: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 14

Mwisho (dakika 10)

Jibu maswali yafuatayo

Mada ya kipindi:

Ni kwa namna gani umenufaika na malengo ya somo? Kipi kimekusaidia?

Ni mambo gani utapenda kujaribu kwenye darasa lako ndani ya mwezi mmoja ujao?

Kipi umekipenda katika kipindi cha leo?

Je kuna lolote linaloweza kufanyika kwa ajili ya kuboresha kipindi kijacho?

Andika taarifa ya kipindi kijacho:

Mada:

Tarehe na Muda:

Mahali:

Page 15: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 15

Kupima Utendaji Kazi (dakika 5)

Tafadhali tafakari jinsi mratibu wa MWK alivyofanya kazi leo. Jaza fomu ifuatayo kwa ajili ya tathmini yako. Fomu hii itakusanywa na Timu ya Wilaya ya MWK kwa ajili ya kuwasaidia waratibu wa MWK.

Mwongozo wa Usahihishaji kwa ajili ya Waratibu wa MWK:Alama 0:

Hajaweza kabisa

Alama 1:

Ameweza kidogo

Alama 2:

Ameweza kiasi cha kuridhisha

Alama 3:

Ameweza vizuri sana Mratibu wa MWK hajaweza kufanya yale yaliyoorodheshwa

Mratibu wa MWK ameweza kidogo kufanya yale yaliyoorodheshwa

Mratibu wa MWK ameweza kufanya kwa kiwango cha kuridhisha yale yaliyoorodheshwa

Mratibu wa MWK ameweza kufanya vizuri sana yale yaliyoorodheshwa

Yale yaliyofanywa wakati wa kipindi cha MWK:

0 1 2 31. Maandalizi: Mratibu wa MWK amejiandaa kwa kipindi – amesoma vizuri

moduli na ameandaa vifaa vyote vya kufundishia

2. Uwezeshaji: Mratibu wa MWK anasimamia vizuri majadiliano – anajua jinsi ya kuwafanya watu wajieleze na namna ya kupata majibu

3. Uwezeshaji: Mratibu wa MWK anajua namna ya kusimamia makundi – anahakikisha kuwa walimu wanatoa ushirikiano, wanashirikiana na wana hamasika

4. Ufundishaji na ushauri: Mratibu wa MWK anajua jinsi ya kuwahamasisha walimu – anafuatilia kujua waliokosa vipindi au kuchelewa na kutukumbusha kwanini MWK ni muhimu kwetu

5. Ufundishaji na ushauri : Mratibu wa MWK anatoa ushirikiano – anafuatilia maendeleo yetu kujua kama tunatumia mbinu mpya darasani na anatusaidia pale anapoona tuna tatizo

Alama za jumla:

/15 x 100% = ________

Page 16: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 16

Page 17: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 17

Page 18: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 18

Page 19: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA WALIMU WA MADARASA YA MWANZO

Moduli ya Pili:Usimamizi Fanisi wa Darasa

Moduli ya Mwalimu

Page 20: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 2

Page 21: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 3

MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA WALIMU WA MADARASA YA MWANZO

Moduli ya Pili:Usimamizi Fanisi wa Darasa

Moduli ya Mwalimu

Page 22: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 4

Moduli hii imetayarishwa kwa ushirikiano na:

wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Taasisi ya Elimu Tanzania Chuo Kikuu cha Dodoma

Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania

Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa EQUIP-Tanzania

Moduli hii imewezeshwa kwa ushirikiano na:

C.C.U Butimba C.C.U Bustani C.C.U Tabora C.C.U ndala C.C.U Kasulu

C.C.U Kabanga C.C.U BundaC.C.U Tarime

C.C.U shinyangaC.C.U Mpwapwa

Page 23: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 5

Maelekezo na taswira katika moduli

Kuna picha na michoro mingi katika moduli. Baadhi zinajirudia mara nyingi kwa sababu zinamaanisha jambo mahususi linalotokea. Chini kuna mfano wa taswira mbalimbali ambazo zinapatikana katika moduli pamoja na kile ambacho zinawakilisha:

Jadili na mwenzako: Wakati wote wa kusoma moduli, walimu wataelezwa kufanya kazi pamoja na mwalimu mwingine juu ya maswali au kazi.

Fikiri– Wawili wawili – Shirikishana: Kama ilivyo katika maelezo ya hapo juu, hapa vilevile walimu wanafanya kazi wakiwa wawili wawili. Japokuwa, hapa walimu wanatafakari mmoja mmoja kwanza juu ya swali au tatizo, halafu wanafanya kazi mwalimu mwenzake na mwishoni wanawasilisha katika kundi lote.

Jadiliana katika kikundi: Wakati mwingine walimu wataelekezwa kutafakari au kujadili maswali mbalimbali katika kikundi.

Soma: Katika kila moduli kuna “dhana kuu” ambayo kwa kawaida huwasilishwa kwa kirefu katika maelezo.

Andika: Moduli itawahamasisha walimu kuchukua maelezo na kuandika fikra zao na majibu.

Igizo: Baadhi ya mazoezi yatahitaji walimu kuigiza kazi ya kufundisha wakati wengine watapaswa kuigiza kama wanafunzi.  

Page 24: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 6

 

 

Moduli  ya  Pili:  Usimamizi  Fanisi  wa  Darasa      MAUDHUI  YA  MODULI:  Moduli  hii    ni  kuhusu  usimamizi  fanisi  wa  darasa.  Kwako  mwalimu,    inamaanisha  kujifunza  mbinu  mbalimbali  za  kuwa  na  mazingira  rafiki  darasani  pamoja  na  njia  ambazo  walimu  hutumia  kuwafanya  wanafunzi  waelekeze  fikra  zao  katika  kujifunza,    wasikilize  na  kushiriki  kikamilifu  katika  kujifunza  wakiwa  darasani.          DHANA  KUU:    

Usimamizi  fanisi  wa  darasa:  mbinu  na  njia  mbalimbali  ambazo  walimu  wanaweza  kutumia  kuwafanya  wanafunzi  waelekeze  fikra  zao  katika  kujifunza,  kusikiliza  na  kushiriki  kikamilifu  katika  kujifunza  darasani.    

Mazingira  rafiki:  mazingira  hapa  yanaweza  kuwa  mahali  pa  kuishi  au  kujifunzia.  Mazingira  rafiki  ni  hali  ya  kutokuwa  na  vitisho,  hofu,  chuki  au  adhabu,  hasa  ya  kuchapa  fimbo,  kuzaba  makofi,  kupiga  konzi,  kufinya  au  kuvuta  masikio.  Mazingira  rafiki  yanaboresha  ufundishaji  na  ujifunzaji  kwa  sababu  wanafunzi  wanapata  fursa  ya  kujieleza,  wanaweza  kujiamini  na  kuaminiana.      

 MALENGO  YA  MODULI:  Hadi  mwisho  wa  moduli  hii,  washiriki  waweze:  

Kuelewa  maana  ya  “Usimamizi  fanisi  wa  darasa”  na  umuhimu  wa  kufanya  hivyo;     Kubaini  angalau  mbinu  kati  ya  4  hadi  5  zinazowasaidia  walimu  kuwafanya  wanafunzi  waweze  kuzingatia  

kinachofundishwa  darasani,  kusikiliza  na  kushiriki  katika  kujifunza,  hasa  kwa  madarasa  yenye  wanafunzi  wengi;    

Kufanya  mazoezi  ya  mbinu  rahisi  za  kuyaweka  mazingira  ya  darasa  yawe  rafiki  na  kuweza  kuzitumia  mbinu  hizo  wakiwa  madarasani.      

MAANDALIZI  YA  KIPINDI:      Mara  zote  uwe  na  Moduli  yako  ya  Mafunzo  ya  Walimu  Kazini  na  kalamu    

 TARATIBU  ZA  KUJIFUNZA  KWA  KILA  KIPINDI:    

1. Kutana  katika  sehemu  tulivu  yenye  ubao  kama  inavyoonekana  katika  picha  

2. Panga  madawati/meza  ili  kuwezesha  washiriki  wote  waonane  na  kuongea  pamoja    

3. Kuwa  huru  kuuliza  maswali  kama  hujaelewa  4. Kuwa  wa  msaada  kwa  wenzako    5. Kuwa  mbunifu  na  fikiria  jinsi  dhana  unazojifunzazinahusiana  

na  darasa  lako    6. Weka  simu  yako  katika  hali  ya  mtetemo  

   

 Weka  simu  yako  katika  hali  ya  mtetemo  

Page 25: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 7

TAFAKARI            Katika  moduli  iliyopita  ulifanya  kwa  vitendo  mada  iliyohusiana  na  uanziswaji  wa  kanuni  katika  madarasa  yaliyosheheni  machapisho  hususan  matumizi  ya  ujumbe  wa  siku,  herufi  ya  siku  na  kuimba  wimbo  wa  alfabeti.  Orodhesha  mafanikio  uliyoyaona  pamoja  na  changamoto  ulizokabiliana  nazo  wakati  wa  kufundisha  maudhui  ya  moduli  hiyo  darasani  kwako    

 Andika  peke  yako  (dakika  5)  Tafadhali   andika   kwenye   visanduku   mafanikio   na   changamoto   ulizokutana   nazo   wakati   wa   kutekeleza  mikakati  hii  katika  darasa  lako.  

Mafanikio  (Elezea  utaratibu  uliotumia  na  fafanua  jinsi  ulivyofanikiwa)  

         

 Changamoto    

(Elezea  utaratibu  uliotumia  na  fafanua  changamoto  zake)      

 Jadiliana  katika  kikundi  (dakika  10)  

Shirikisha  wenzako  kwenye  kundi  mojawapo  ya  uzoefu  huo.       Kwa  kila  changamoto,  pendekeza  namna  ya  kukabiliana  nayo.   Wakati  wa  majadiliano,  andika  ufumbuzi  unaoendana  na  changamoto  ulizobainisha.  

                     

   

           

Njia    Muhimu  za  Ufumbuzi  (Mawazo  muhimu  mahususi  kwa  wenzetu)  

 

Page 26: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 8

UTANGULIZI          Zoezi  binafsi  la  kujikumbusha  (dakika  5)    

Ukiwa  peke  yako  soma  maelezo  yafuatayo  na  andika  kama  unakubali  au  hukubali.  Tafadhali  jibu  kulingana  na  uelewa  wako.  Hutakiwi  kumshirikisha  mwenzako  majibu  yako  na  hakuna  atakayekuhukumu  kutokana  na  majibu  uliyotoa.      

Maelezo     Nakubali/Sikubali    Haiwezekani  kuwafanya  wanafunzi  kwenye  darasa  kubwa  wakakusikiliza  na  kuwa  kimya  bila  ya  kuwachapa  (au  kuwatishia  kuchapa)      

Kukiwa  na  wanafunzi  wengi  darasani  si  rahisi  kuunda  makundi  haraka  na  bila  ya  kelele      

Ikibainika  kuwa  wanafunzi  wamedanganya,  kuiba  au  kufanya  jambo  baya,  lazima  waonywe  kwa  kuchapwa,  la  sivyo  watarudia  tena      

Kama  wanafunzi  watakosa  umakini  darasani,  kuwachapa  ndiyo  njia  pekee  ya  kuwafanya  wawe  makini  darasani      

Kutembea  na  fimbo  katika  maeneo  ya  shule  ni  sawa  tu  kwani  inawafanya  wanafunzi  wawe  na  adabu  (hata  kama  sitaitumia)      

Wanafunzi  watawaheshimu  walimu  wao  ikiwa  wanawaogopa      

   

 Kuandika  Tafakuri  Binafsi  (dakika  10)        

Baada  ya  kumaliza  zoezi  hili,  tafadhali  jaza  fomu  ifuatayo  kwa  kuzingatia  yafuatayo:    1) Kumbuka  miaka  ya  nyuma  ulipokuwa  mwanafunzi  wa  shule  ya  msingi  2) Tafadhali  orodhesha  adhabu  zote  ulizowahi  kupata,  kama  vile  kuchapwa  fimbo,  kuzabwa  makofi,  

kuvutwa  masikio,  kuchuchumaa,  kulala  na  kujinyanyua  kwa  mikono  (push  up),  nk.  3) Tafadhali  taja  sababu  zilizokufanya  upate  hiyo  adhabu  (na  kama  hakukuwa  na  sababu  yoyote  andika  pia)    4) Tafadhali  andika  ulivyojisikia  baada  ya  kupata  hizo  adhabu.  Tafadhali  sema  ukweli  (je  zilikusaidia?  Je  

zilikufanya  uogope,  uwe  na  hasira  au  mwenye  huzuni?)    5) Baada  ya  kumaliza,  jadili  mawazo  yako  katika  kikundi.    

 Ni  adhabu  zipi  ulipewa  ulipokuwa  

shule  ya  msingi?    Kwanini  ulipewa  adhabu  hizo?     Ulijisikiaje  baada  ya  kuadhibiwa    

     

   

     

   

     

   

     

   

     

   

 

Page 27: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 9

1. Mwalimu  mmoja  anaanza  kusoma  kwa  sauti.  Baada  ya  kukamilisha  aya  anamwita  mwalimu  mwingine  kwa  jina  asome  aya  inayofuata.      

2. Wakati  unaposoma:    -­‐Weka  alama  ya  mshangao  (!)  katika  sehemu  ambayo  unaona  ni  muhimu    -­‐Weka  alama  ya  (?)  katika  sehemu  ambayo  huelewi  au  hukubaliani  nayo    -­‐Weka  mduara  katika  maneno  ambayo  ni  mapya.  

 

DHANA  KUU      

 Mbinu  fanisi  za  kusimamia  darasa  (dakika  20)        

                         Utafiti  unaonyesha  kuwa  kuchapa  viboko  kunaweza  kuwa  na  athari  mbaya  kwa  wanafunzi  (kumbuka  jinsi  ulivyojisikia  baada  ya  kuadhibiwa  ulipokuwa  mdogo).  Kwa  mfano,        

1) Kunasababisha  madhara  ya  kimwili,  kiakili  na  kihisia;    2) kunamfanya  mwanafunzi  awachukie  au  awaogope  walimu  wake,  kitendo  kinachopunguza  uwezo  wao  wa  

kujifunza;  3) Wanafunzi  hawawezi  kujirekebisha  kutokana  na  makosa  yao,  badala  yake  wanajifunza  mbinu  za  kukwepa  

adhabu;    4) Hofu  ya  wasichana  kuadhibiwa,  pamoja  na  kudhalilishwa  na  walimu  na  wanafunzi  wenzao  wa  kiume,  

huwafanya  washindwe  kujieleza  vizuri  darasani.  Hali  hii  ya  wasichana  ya  kutokuwa  wepesi  wa  kujieleza  darasani  ndio  mara  nyingi  huwafanya  waonekane  wameumbwa  wenye  aibu  au  wapole.  

5) Huwafanya    wavulana  wenye  uwezo  mdogo  darasani  wasitoe  ushirikiano  darasani  (hali  inayowafanya  wazidi  kuchapwa)  au  kuwa  watoro/kuacha  masomo  (ili  kuachana  kabisa  na  vichapo  zaidi)    

 Kwa  kuzingatia  matatizo  haya,  walimu  wanakuwa  na  wakati  mgumu  sana  kwa  kuwa  wanakabiliwa  na  madarasa  yenye  wanafunzi  wengi  kuliko  uwezo  wao  huku  wakipata  msaada  kidogo.  Walimu  wengi  wanahisi  kuwa  mazingira  haya  magumu  ndiyo  huwalazimisha  waamue  kuwachapa  wanafunzi.  Mwaka  2010,  walimu  65  kutoka  mkoa  wa  Arusha  walihojiwa  kuhusu  maoni  yao  juu  ya  adhabu  ya  viboko.  Walimu  wengi  waliohojiwa  walieleza  kuwa  hawapendi  kuchapa,  lakini  hawakuwa  na  njia  nyingine  zaidi  ya  kuchapa.  Kwa  mfano  mwalimu  Dora  kutoka  shule  iliyoko  maeneo  ya  vijijini  alisema,      “Sipendi  kuwachapa  kwa  kuwa  lengo  si  kuwachapa.  Lengo  ni  kuwaelimisha  na  kuwafanya  waelewe.  Lakini  kutokana  na  darasa  kuwa  na  wanafunzi    wengi,  inakuwa  vigumu  kuwadhibiti,  ndio  maana  wakati  mwingine  nalazimika  kutumia  fimbo.”    Maelezo  haya  yanadhihirisha  ugumu  walimu  wanaokabiliana  nao  kwa  kuwa  hawapendi  kutumia  adhabu  ya  kuchapa  viboko    ila  wanalazimika  kutumia  adhabu  hiyo  kwa  ajili  ya  kutawala  darasa.  Na  Mwalimu  Grace  kutoka  shule  iliyoko  nje  ya  mji  alieleza,      

“Serikali  inatuzuia  kutumia  fimbo,  hata  hivyo  tunaendelea  kuwachapa  hata  kama  hairuhusiwi.  Tumezuiwa  kabisa  kuchapa.  Lakini  bila  kuwachapa  watoto  hawasikii.”      Kuna  tafsiri  tofauti  za  walimu  wakuu  kuhusu  sheria  ya  adhabu  ya  viboko.  Baadhi  wanaifuata  na  kuwazuia  walimu  kuchapa  wanafunzi,  lakini  wapo  wengine  wanawaruhusu  waendelee  kuwachapa  wanafunzi.  Walimu  wakuu  wengi  wapo  njia  panda.  Hii  inadhihirisha  ugumu  ambao  walimu  wanakabiliana  nao  –  wanajua  kabisa  hawapendi  kuchapa  au  hatakiwi  kuchapa  lakini  bado  wanaona  ndio  njia  pekee  ya  kutumia  kwa  ajili  ya  kuweka  nidhamu  ndani  ya  darasa.    Mwalimu  Amani  kutoka  shule  iliyo  nje  ya  mji  alisema:    

Page 28: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 10

 «  Najaribu  kuwaambia  wanafunzi  wangu,  tafadhali  ninapokuwa  humu  darasani  nikifundisha,  sipendi  kumwona  mwanafunzi  akiongea,  sipendi  kumwona  mwanafunzi  anayetembea  huku  na  kule  …  pengine  nafundisha  hisabati  halafu  wewe  unasoma  Kiswahili.  Sipendi  kabisa  tabia  hiyo.  Unatakiwa  kusikiliza  kwa  makini  kwa  sababu  baada  ya  kipindi  nitawauliza  maswali.  Hamtaweza    kufanya  vizuri  maswali  nitakayowapa  kwa  sababu  hamkunisikiliza  vizuri  wakati  nafundisha.  Na  hicho  ndicho  ninachochukia  sana.  Ndio  maana  wakati  mwingi  nawachapa  fimbo.  »    Hii  inaonyesha  jinsi  inavyotokea  kwa  mwalimu  hadi  kulazimika  kutumia  adhabu  kwa  nia  ya  kuwasaidia  wanafunzi  wake,  lakini  bado  hawamsikii,  wanaongea  darasani,  wanazunguka  huku  na  kule  ndani  ya  darasa,  au  kufanya  zoezi  la  somo  jingine.      Mwalimu  Omari  aliongelea  kuhusu  kuwachapa  wanafunzi  ili  wawe  na  tabia  nzuri  ambayo  itawafanya  wakubalike  na  jamii.      Hii  adhabu  ya  kuchapa  ilikuja  kwa  lengo  la  kuwaadhibu  wanaochelewa  shule,  walio  na  sare  chafu  au  wasio  na  madaftari  ya  somo  husika  au  vifaa  vya  kujifunzia.  Kwa  kauli  yake  mwalimu  Omari,          «  Tunawanyoosha  tu  wanafunzi  kwa  kuwachapa  fimbo  moja  moja  mkononi.  Hii  itawafanya  wasirudie  tena  makosa  kama  hayo.  »    Nukuu  hizi  zote  zinadhihirisha  kuwa  hata  kama  walimu  hawapendi  kuchapa,  wengi  hulazimika  kufanya  hivyo.  Adhabu  ya  kuchapa  hutoa  suluhisho  la  haraka  na  jepesi  la  kuwafanya  wanafunzi  wawe  na  adabu,  lakini  inaweza  kusababisha  matokeo  mabaya  hapo  baadaye  (kama  vile  tabia  ya  wanafunzi  kukwepa  masomo,  kuchukia  masomo,  walimu  au  tabia  yoyote  mbaya).  Walimu  wasiopenda  kutumia  adhabu  hii  hujikuta  wakichoka  kimwili  na  kiakili.  Lakini  huenda  hii  inatokea  kwa  sababu  walimu  hawajui  njia  nyingine  za  kuwawezesha  kudhibiti  nidhamu  ya  darasa,  kuwafanya  wanafunzi  wakae  kimya,  wanafunzi  wawe  wasikivu,  au  kuzuia  uchelewaji.  Huenda  walimu  wangekuwa  na  mbinu  nyingine  za  kuweka  mazingira  rafiki  ya  madarasa  yao,  na  zikathibitika  kuwa  na  ufanisi,  wasingekimbilia  kutumia  sana  adhabu  ya  kuchapa.        

Jadiliana  katika  kikundi  (dakika  10)      

1) Ni  mambo  gani  katika  matini  ya  hapo  juu  ambayo  unaona  ni  ya  muhimu,  hayaeleweki  au  mapya?    

2) Je  unaweza  kuhusianisha  kile  walichosema  walimu  waliohojiwa  na  maisha  yako?  Kama  ndiyo,  je  ni  katika  hali  zipi?      

3) Kama  ungepata  mbinu  nyingine  mbali  ya  kuchapa,  je  utapenda  au  hutapenda  kuzitumia?  Kwanini  utapenda?  Kwanini  hutapenda?        

ZOEZI            

Chunguza  jedwali  lifuatalo,  kisha  shirikiana  na  mwenzako    kuoanisha  kila  tatizo  na  ufumbuzi  wake    (dakika  20)    

Tafadhali  zingatia  kuwa  matatizo  mengine  yanaweza  kuwa  na  majibu  zaidi  ya  moja,  kwa  hiyo  andikeni  majibu  yote  mnayohisi  ni  sahihi  kwa  tatizo  husika.  Pia  kama  kuna  njia  nyingine  kwa  ajili  ya  kutatua  kila  tatizo,  tafadhali  andika  njia  hizo.  Baada  ya  kumaliza,  washirikishe  majibu  yenu  wenzenu  kwenye  kundi.                

Page 29: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 11

MATATIZO      UFUMBUZI  WA  MATATIZO      

1. Darasa  ni  kubwa  na  ni  vigumu  kuwafanya  wanafunzi  wawe  wasikivu,  na  walio  tayari  kujifunza.      

A. Mwalimu  anaweza  kuanzisha  mchezo  kwa  kuwaambia  wanafunzi:  “Nikiinua  mkono,  mnyamaze  na  muinue  mikono  yenu  ”.  Wanafunzi  wote  wataanza  kuinua    mikono  na  wale  wa  mwisho  (wanaoongea  au  ambao  hawajawa  tayari)  watajisikia  vibaya.  Kasha  watafuata  wanavyofanya  wenzao.  

 B. Wanafunzi  hujibu  vizuri  maswali  yenye  manufaa  kwao.  Tumia  dakika  15  

kuwauliza  wanafunzi  ni  tabia  zipi  wanadhani  ni  njema;  kisha  wasaidie    wakubaliane  (kama  vile  kuwa  tayari  kusikiliza,  kufanya  mazoezi  ya  somo  jingine,  kutocheza  darasani,  n.k.).  Waambie  kuwa  atakayeweza  kuzingatia  vyote  hivyo  atakuwa  ‘Mwanafunzi  bora  wa  siku’,  ukimaanisha  kuwa  kesho  yake  utamtangaza  mwanafunzi  bora  wa  siku  na  kumvisha  nishani  au  alama  ya  ushindi    (unaweza  kutengeneza  shada  kwa  kutumia  karatasi  na  uzi).    Ukiwa  unachagua  mwanafunzi  bora  wa  siku  ni  vema  kuwachagua  wale  wanaohitaji  

motisha  na  kuhamasishwa  waendelee  kubadilika.      

C. Tembea  darasani  huku  ukifundisha  halafu  simama  pembeni  ya  wanafunzi  wanaoongea.  Simama  pembeni  yao  halafu  weka  mikono  yako  juu  ya  mabega  yao  huku  ukiendelea  kufundisha.  Hii  itawafanya  wanafunzi  wajue  kuwa  unajua  wanachokifanya  na  hivyo  wataacha  kuongea.    

 

D. Ukiona  wanafunzi  waIioko  nyuma  ya  darasa  wanaongea  na  si  wasikivu  wahamishie  mbele  kwa  muda  na  wabadilishane  na  waliokaa  mbele  ya  darasa.      

Njia  zinazoweza  kutatua:  Kwa  mfano,    A    

Njia  nyingine:    

 

 

 

 

 

 

 

2. Wakati  nafundisha  kuna  wanafunzi  wanaongea,  hasa    wanaokaa  nyuma  ya  darasa.      

Njia  zinazoweza  kutatua:__________  

Njia  nyingine:    

 

 

 

 

 

 

 

3. Kuna  wanafunzi  wengi  ndani  ya  darasa  na  hivyo  inakuwa  vigumu  kuunda  vikundi  kwa  muda  mfupi    na  kwa  utulivu.  

Page 30: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 12

 

Njia  zinazoweza  kutatua:___________  

 

E. Tumia  dakika  15  kuwapanga  katika  vikundi.  Waweke  katika  vikundi  kadiri  ya  mahitaji  tofauti  (kwa  mfano  kundi  la  kusoma  pamoja  kitabu,  kundi  la  kuwachanganya  wenye  uwezo  tofauti),  na  waelekeze  wachague  kiongozi.  Waambie  kila  kundi  lichague  jina  lake  (kwa  mfano  jina  la  mnyama,  matunda  nk).  Waambie  ukifika  wakati  wa  makundi  itabidi  wajikusanye  kadiri  ya  makundi  (kiongozi  wao  atawasimamia).  Waambie  kuwa  ni  mashindano  ya  kuona  kundi  lipi  litakuwa  la  kwanza  kujipanga  mapema  zaidi.  Baada  ya  makundi  kuwa  tayari  watangazie  washindi  watatu  wa  mwanzo,  andika  majina  yao  ubaoni  na  wanafunzi  nwenzao  wawapigie  makofi.  

   

 alichofanya  haikuwa  sahihi,  fafanua  ili  mwanafunzi  aelewa  kuwa  alichofanya  haukuwa  uamuzi  sahihi  huku  ukijiridhisha  kuwa  mazingira  ya  nje  ya  shule  hayachangii  mwanafunzi  kuwa  na  tatizo  hilo  la  nidhamu.  Hatua  ya  pili,  mwambie  kuwa  kwa  kosa  alilofanya  hataweza  kwenda  kupumzika  na  wenzake  wakati  wa  mapumziko  badala  yake  atafanya  tafakari  aidha  kwa  maandishi  au  kwa  maneno  kwanini  alichokifanya  ilikuwa  ni  utovu  wa  nidhamu  na  atafanya  nini  asirudie  kosa  hilo  tena.  

 

 

 

 

           

 

 

 

 

 

   

kwenye  kundi  ameonyesha  tabia  mbaya,  alama  za  kundi  zitapunguzwa.  Waruhusu  wanafunzi  waorodheshe  mifano  mingine  ya  ‘tabia  mbaya’  (kwa  mfano,  mwanafunzi  si  mtulivu,  anaongea  wakati  wa  kipindi,  au  anafanya  kazi  ya  

Njia  nyingine:    

 

 

 

 

 

 

4. Akibainika    mwanafunzi  akidanganya,  akiiba,  au  kufanya  jambo  fulani  vibaya.  Ipi  ni  njia  nzuri  ya  kumuadhibu  ili  ajue  alichofanya  ni  kibaya?  

 

Njia  zinazoweza  kutatua:___________  

Njia  nyingine:    

 

 

 

 

 

 

 

5. Kuna  wanafunzi  wanaochelewa  kuja  shuleni,  wakiwa  wachafu  au  hawana  vifaa  vya  kujifunzia  kama  vile  madaftari    na  kalamu.  Ninafanyaje  kuzuia  tabia  hii  isijirudie?      

 

F.  Kwa  wanafunzi  wenye  matatizo  makubwa  ya  kinidhamu  unaweza  kutumia  mbinu  inayoitwa  ‘muda  wa  tafakari’.  Hatua  ya  kwanza  unaongea  na  mwanafunzi    kwanini  anafikiri  kuwa  

G.  Wanafunzi  watashiriki  vizuri  katika  somo  lako  kama  utalifanya  liwe  na  mvuto.  Jaribu  kutumia  michezo  –  wanafunzi  wanaweza  kuwa  wasikivu  kama  watapata  nafasi  ya  kucheza.  Ni  muhimu  pia  kuwachagua  wale  ambao  wanaonyesha  kutokuwa  wasikivu  washiriki  kwenye  michezo.        

H.    Ligawanye  darasa  katika  makundi  kama  una  darasa  lenye  wanafunzi  wengi.  Kama  una  safu  tatu  za  madawati  basi  unda  kundi  kwa  kila  safu.  Waache  wanafunzi  watoe  majina  ya  makundi  yao.  Watangazie  kuwa  kila  kundi  lina  alama  100  na  waambie  kuwa  kama  kuna  mwanafunzi  toka    

Page 31: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 13

Njia  zinazoweza  kutatua:___________  

somo  jingine).  Endelea  kupunguza  alama  wakati  unafundisha  na  baada  ya  kipindi  tangaza  kundi  lililoshinda  

I.  Kama  wanafunzi  wanachelewa  kuja  darasani  au  wanakuja  wakiwa  hawajajiandaa,  kwanza  kabisa  waulize  kwanini  wamechelewa  au  hawajajiandaa.  Kama  kuna  tatizo  kubwa  jaribu  kuwapa  ushauri.  Kama  hawana  sababu  ya  maana,  waambie  kuwa  unawapa  onyo  mara  mbili  kabla  hawajawekwa  kwenye  ‘kifungo  cha  ndani’  (ukimaanisha  kuwa  hawataweza  kwenda  mapumziko).  Ukiona  wanarudi  mara  ya  tatu,  jaribu  adhabu  ya  ‘kifungo  cha  ndani’  (tazama  njia  namba  F).                  

Njia  nyingine:    

 

 

 

 

 

   

Jadiliana  katika  kikundi  (dakika  10)      

1) Je  unafikiri  njia  hizo  zinaweza  kusaidia  vya  kutosha?  Kwa  nini  zinasaidia?  Kwa  nini  hazisaidii?        2) Njia  ipi  inafaa?  Ipi  haifai?  Na  kwanini?    3) Njia  zipi  utapenda  kuzijaribu  darasani  kwako?  Utaziboreshaje?    4) Unafikiri  mwalimu  mkuu  anaweza  kutumia  mbinu  hizi?  Kama  hawezi,  kwanini?    

     TATHMINI  BINAFSI      

 Tathmini  Binafsi  ya  Mbinu  za  Kusimamia  Darasa  (dakika  5)    

ANGALIZO:  Tathmini  hii  ni  binafsi  hulazimiki  kumshirikisha  mshiriki  yeyote.  Ni  njia  ya  kutathmini  uwezo  wako  wa  kubainisha  maeneo  ya  kuboresha  ili  kuimarisha  mbinu  za  usimamizi  wa  darasa.    

Mbinu  fanisi  za  kusimamia  darasa   Sielewi     Naelewa  lakini  huwa  sifanyi    

Huwa  nafanya  lakini  nahitaji  kuboresha  zaidi    

Nafanya  vizuri  sana      

Natumia  ishara  (kama  vile  kumkodoloIea  macho,  kusimama  karibu  na  mwanafunzi,  kunyoosha  mkono)  kuwafanya  wanafunzi  wawe  wasikivu.    

       

Kwa  mwanafunzi  mwenye  tatizo  kubwa  la  kinidhamu  ninapanga  kuwa  na  muda  wa  tafakari  wakati  wa  mapumziko  .    

       

Napanga  kuwa  na  mchezo  darasani  ili  kulifanya  somo  langu  liwe  la  kuvutia          

Natumia  motisha  chanya  kuwafanya  wanafunzi  wangu  wawe  na  nidhamu          

 

Page 32: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 14

   Mawazo  kuhusu  Usimamizi  wa  Darasa  (dakika  5)  Jaza  tena  chati  ifuatayo  ambayo  uliijaza  wakati  wa  kujikumbusha.  Linganisha  majibu  yako  ya  mwanzo  

wakati  wa  zoezi  la  kujikumbusha  na  majibu  yako  ya  sasa.  Je  majibu  yako  yamebadilika?        

Maelezo     Nakubali/  Sikubali    Haiwezekani  kuwafanya  wanafunzi  kwenye  darasa  kubwa  wakakusikiliza  na  kuwa  kimya  bila  ya  kuwachapa  (au  kuwatishia  kuchapa).      

Kukiwa  na  wanafunzi  wengi  darasani  si  rahisi  kuunda  makundi  haraka  na  bila  ya  kelele  .    

Ikibainika  kuwa    wanafunzi  wamedanganya,  kuiba  au  kufanya  jambo  baya,  lazima  waonywe  kwa  kuchapwa,  la  sivyo  watarudia  tena.      

Kama  wanafunzi  watakosa  umakini  darasani,  kuwachapa  ndiyo  njia  pekee  ya  kuwafanya  wawe  makini  darasani.    

Kutembea  na  fimbo  katika  maeneo  ya  shule  ni  sawa  tu  kwani  inawafanya  wanafunzi  wawe  na  adabu  (hata  kama  sitaitumia).      

Wanafunzi  watawaheshimu  walimu  wao  ikiwa  wanawaogopa.      

 KUANDAA  MPANGO  KAZI      

     Kupanga  ‘Kipindi  cha  Kusoma  na  Kuandika’  (dakika  10)  

   

Katika  kuimarisha  uwezo  wa  wanafunzi  kujifunza  kusoma  na  kuandika,  ni  muhimu  mwalimu  kuwa  na  mpango  unaomwezesha  kutumia  maarifa  mapya  aliyojifunza  wakati  wa  mafunzo  ya  walimu  kazini  kwa  vitendo.  Aidha  ni  muhimu  kwa  wanafunzi  kuwa  na  muda  zaidi  wa  kujifunza  kusoma  na  kuandika.  Kwa  mantiki  hii,  ni  muhimu  kwa  mwalimu  kuandaa  kipindi  cha  saa  moja  cha    kusoma  na  kuandika  mara  moja  kwa  wiki.      Ingawa  kazi  zifuatazo  hazina  uhusiano  wa  moja  kwa  moja  ila  mbinu  zifuatazo  zinaweza  kutumika  kusimamia  darasa    lolote    na  katika  somo  lolote.  Aidha,  zitakuwa  na  msaada  wakati  kwa  kufundisha  kusoma.  Ni  vema  kuandaa  namna  utakavyoingiza  mbinu  hizi  wakati  wa  kipindi  cha  wiki  cha  kusoma  na  kuandika.        Matumizi  ya  mbinu  ya  kwanza:  Uundaji  shirikishi  wa  kanuni  za  darasani      1. Andika  kanuni  za  darasani  ubaoni.      2. Jadili  na  wanafunzi  umuhimu  wa  kuwa  na  kanuni  za  darasa  ambapo  kila  mwanafunzi  atashiriki  na  kujifunza  

kutoka  kwa  wengine.  3. Waulize  wanafunzi  ni  aina  gani  ya  kanuni  wanafikiri  ni  muhimu.  Ungependa  ushirikiane  na  wenzako  kwa  namna  

gani?  Ungependa  kushirikiana  na  mwalimu  wako  kwa  namna  gani?  Ungependa  mazingira  ya  darasani  yawe  katika  hali  gani?    

4.  Waongoze  wanafunzi  kujibu  maswali    5. Andika  ubaoni  majibu  yao    6. Kama  baadhi  ya  wanafunzi  wanapata  ugumu  kujibu  maswali  waulize  kwa  kutumia  mifano  na  ikiwezekana  wape  

ushauri  wako:   Fikiri  kabla  ya  kutenda     Zingatia    muda    

Page 33: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 15

Shirikiana  –  Lakini  omba  unapotaka  kutumia  kitu  cha  mwanafunzi  mwingine     Kuwa  msikivu  mwenzako  anapoongea     Weka  mazingira  ya  darasa  katika  hali  ya  usafi    

7. Baada  ya  kubungua  bongo  kuhusu  kanuni  za  darasa  na  wanafunzi,  wape  muda  mchache  wa  kusoma  kwa  sauti.      8. Fafanua  umuhimu  wa  wanafunzi  wote  kuridhia  kanuni  za  darasani.    9. Baada  ya  kila  mmoja  kuridhia  andika  kanuni  kwenye  ubao  wa  darasa  au  andika  kwenye    karatasi  na  unaweza  

kuwaonesha  wanafunzi  unapotaka  kuwakumbusha  kuhusu  kanuni  za  darasa      Matumizi  ya  mbinu  ya  pili:  Kusimamia  vikundi      1. Ligawe  darasa  katika  vikundi,  kila  safu  inaweza  kuunda  kikundi.  2.  Waambie  kila  kikundi  kichague  jina  la  kikundi  (kama  vile  rangi,  majina  ya  viongozi  mashuhuri,  matunda  au  

wanyama)    3. Watangazie  kuwa  kila  kikundi  kinazo  alama  10  za  kuanzia.  4. Andika    jina  la  kila  kikundi      ubaoni  na  weka  alama  kumi  chini  ya  kila  jina  la  kikundi    5. Waambie  wanafunzi  kuwa  ikiwa  mmoja  wenu  katika  kikundi  akitenda  kosa  la  kinidhamu  alama  moja  itatolewa  

kwenye  alama  10.    6. Jadili  na  wanafunzi  maana  ya  nidhamu  isiyofaa    (mfano,  mwanafunzi  anaongea  bila  ruhusa  wakati  wa  somo,  

mwanafunzi  anawasumbua  wenzake  wakati  wa  somo,  au  siyo  msikivu  wakati  mwalimu  anafundisha    7. Waambie  wanafunzi  wachangie  kwa  kutoa  mifano  maana  ya  neno  ‘nidhamu  isiyofaa’.  8. Punguza  alama  kwa  wasio  na  nidhamu  wakati  unapofundisha;  na  mwisho  wa  kipindi  watangazie  wanafunzi  ni  

kikundi  kipi  kimeshinda  kwa  kubaki  na  alama  nyingi  .  9. Kikundi  kilichoshinda  kinaweza  kupata  upendeleo  wa  kutoka  mapema  kwenda  mapumziko  au  kupewa  majukumu  

ya  kufanya  darasani  kama  vile  kuwa  kiongozi  wa  darasa  n.k.    

 Jadili  na  mwenzako    (dakika  15)  

 Kwa  kushirikiana  na  mwenzako  jadili  namna  unavyoweza  kuingiza  mbinu  za  kusimamia  darasa  katika  andalio  la  somo  kwa  ajili  ya  kipindi  cha  wiki  cha  kusoma  na  kuandika.  Andika  kwenye  daftari  lako  namna  utakavyotumia  mbinu  hizi  kwa  darasa  lako  (Darasa  la  kwanza,  darasa  la  pili,  darasa  la  tatu).    ___________________________________________________________________________    ___________________________________________________________________________    ___________________________________________________________________________    ___________________________________________________________________________      ___________________________________________________________________________        

___________________________________________________________________________  

       

Page 34: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 16

 Mwisho  (dakika  5)      Jibu  maswali  yafuatayo    

   Mada  ya  kipindi:  

 

Ni  kwa  namna  gani  umenufaika  na  malengo  ya  somo?  Kipi  kimekusaidia?      

 

Ni  mambo  gani  utapenda  kujaribu  kwenye  darasa  lako  ndani  ya  mwezi  mmoja  ujao?      

 

Kipi  umekipenda  katika  kipindi  cha  leo?    

 

 

Je  kuna  lolote  linaloweza  kufanyika  kwa  ajili  ya  kuboresha  kipindi  kijacho?    

 

 

   

 Andika  taarifa  ya  kipindi  kijacho:      

Mada:    

 

 Tarehe  na  Muda:  

 

 Mahali:  

 

                                       

Page 35: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 17

 

   Kupima  Utendaji  Kazi  (dakika  5)  

 Tafadhali  tafakari  jinsi  mratibu  wa  MWK  alivyofanya  kazi  leo.  Jaza  fomu  ifuatayo  kwa  ajili  ya  tathmini  yako.  Fomu  hii  itakusanywa  na  Timu  ya  Wilaya  ya  MWK  kwa  ajili  ya  kuwasaidia  waratibu  wa  MWK.          Mwongozo  wa  Usahihishaji  kwa  ajili  ya  Waratibu  wa  MWK:  

Alama  0:    

Hajaweza  kabisa          

Alama  1:  

 Ameweza  kidogo                

Alama  2:  

Ameweza  kiasi  cha  kuridhisha      

Alama  3:  

 Ameweza  vizuri  sana      

Mratibu  wa  MWK  hajaweza  kufanya  yale  yaliyoorodheshwa    

Mratibu  wa  MWK  ameweza  kidogo  kufanya  yale  yaliyoorodheshwa    

Mratibu  wa  MWK  ameweza  kufanya  kwa  kiwango  cha  kuridhisha  yale  yaliyoorodheshwa  

Mratibu  wa  MWK  ameweza  kufanya  vizuri  sana  yale  yaliyoorodheshwa    

 

 

Yale  yaliyofanywa  wakati  wa  kipindi  cha  MWK:    

0  

 

1  

 

2  

 

3  

1. Maandalizi:  Maratibu  wa  MWK  amejiandaa  kwa  kipindi    –  amesoma  vizuri  moduli    na  ameandaa  vifaa  vyote  vya  kufundishia          

       

2. Uwezeshaji:  Mratibu  wa    MWK  anasimamia  vizuri  majadiliano      –  anajua  jinsi  ya  kuwafanya  watu  wajieleze  na  namna  ya  kupata  majibu        

       

3. Uwezeshaji:    Mratibu  wa  MWK  anajua  namna  ya  kusimamia  makundi    –    anahakikisha  kuwa  walimu  wanatoa  ushirikiano,  wanashirikiana  na  wana  hamasika        

       

4. Ufundishaji  na  ushauri:    Mratibu  wa  MWK  anajua  jinsi  ya  kuwahamasisha  walimu  –  anafuatilia  kujua  waliokosa  vipindi  au  kuchelewa  na  kutukumbusha  kwanini  MWK  ni  muhimu  kwetu        

       

5. Ufundishaji  na  ushauri  :  Mratibu  wa  MWK  anatoa  ushirikiano  –  anafuatilia  maendeleo  yetu  kujua  kama  tunatumia  mbinu  mpya  darasani  na  anatusaidia  pale  anapoona  tuna  tatizo        

       

Alama  za  jumla:                      /15  x  100%  =  ________  

 

Page 36: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 18

Page 37: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA WALIMU WA MADARASA YA MWANZO

Moduli ya Tatu: TaThmini ya Wanafunzi na msaada kWa Wanafunzi Wanaojifunza kWa shida

Moduli ya Mwalimu

Page 38: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 2

Page 39: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 3

MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA WALIMU WA MADARASA YA MWANZO

Moduli ya Tatu: TaThmini ya Wanafunzi na msaada kWa Wanafunzi Wanaojifunza kWa shida

Moduli ya Mwalimu

Page 40: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 4

Moduli hii imetayarishwa kwa ushirikiano na:

Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Taasisi ya Elimu Tanzania Chuo Kikuu cha Dodoma

Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania

Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa EQuiP-Tanzania

Moduli hii imewezeshwa kwa ushirikiano na:

C.C.U Butimba C.C.U Bustani C.C.U Tabora C.C.u ndala C.C.U Kasulu

C.C.U Kabanga C.C.u BundaC.C.U Tarime

C.C.u shinyangaC.C.U Mpwapwa

Page 41: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 5

Maelekezo na taswira katika moduli

Kuna picha na michoro mingi katika moduli. Baadhi zinajirudia mara nyingi kwa sababu zinamaanisha jambo mahususi linalotokea. Chini kuna mfano wa taswira mbalimbali ambazo zinapatikana katika moduli pamoja na kile ambacho zinawakilisha:

Jadili na mwenzako: Wakati wote wa kusoma moduli, walimu wataelezwa kufanya kazi pamoja na mwalimu mwingine juu ya maswali au kazi.

Fikiri– Wawili wawili – Shirikishana: Kama ilivyo katika maelezo ya hapo juu, hapa vilevile walimu wanafanya kazi wakiwa wawili wawili. Japokuwa, hapa walimu wanatafakari mmoja mmoja kwanza juu ya swali au tatizo, halafu wanafanya kazi mwalimu mwenzake na mwishoni wanawasilisha katika kundi lote.

Jadiliana katika kikundi: Wakati mwingine walimu wataelekezwa kutafakari au kujadili maswali mbalimbali katika kikundi.

Soma: Katika kila moduli kuna “dhana kuu” ambayo kwa kawaida huwasilishwa kwa kirefu katika maelezo.

Andika: Moduli itawahamasisha walimu kuchukua maelezo na kuandika fikra zao na majibu.

Igizo: Baadhi ya mazoezi yatahitaji walimu kuigiza kazi ya kufundisha wakati wengine watapaswa kuigiza kama wanafunzi.  

Page 42: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 6

   

 

Moduli  ya  Tatu:  Tathmini  ya  Wanafunzi  na  Msaada  kwa    Wanafunzi  Wanaojifunza  kwa  Shida    

   MAUDHUI  YA  MODULI:    Moduli  hii  inamwongoza  mwalimu  kutathmini  kwa  haraka  kiwango  cha  kujifunza  cha  wanafunzi  wakati  wa  somo  ili  kupima   kwa   kiasi   gani   wanafunzi   wanafikia   malengo   ya   somo.   Vilevile   inajadili,   mwalimu   afanye   nini   iwapo  wanafunzi  wanashindwa  kuelewa  dhana  mpya.            DHANA  KUU:      

Tathmini  –  mchakato  wa  kupima  uelewa  wa  wanafunzi  katika  somo  au  dhana.  Inaweza  kufanywa  wakati  wote  wa  somo  au  mwisho  wa  kipindi  au  kwa  muda  maalumu.    

Utofautishaji  –  kurekebisha  sehemu  ya  somo  ili    ilingane  na  uwezo  tofauti  wa  wanafunzi  katika  kujifunza.        

 MALENGO  YA  MODULI:    Washiriki  wakifika  mwishoni  mwa  moduli  hii,  waweze:  

Kupanga  na  kutoa  tathmini  rahisi  ya  shughuli  za  wanafunzi  ambayo  itasaidia  kupata  uelewa  na  ufahamu  wa  wanafunzi      

Kutekeleza  mikakati  ya  kusaidia  wanafunzi  walio  na  matatizo  ya  kujifunza        

MAANDALIZI  YA  KIPINDI:     Tafuta  changarawe  au  jiwedogo  uje  nalo  katika  kipindi.    

 UTARATIBU  ZA  KUJIFUNZA  KWA  KILA  KIPINDI:    

1. Kutana  katika  sehemu  tulivu  yenye  ubao  kama  inavyoonekana  katika  picha  

2. Panga  madawati/meza  ili  kuwezesha  washiriki  wote  waonane  na  kuongea  pamoja    

3. Kuwa  huru  kuuliza  maswali  kama  hujaelewa  4. Kuwa  wa  msaada  kwa  wenzako    

Kuwa  mbunifu  na  fikiria  jinsi  dhana  unazojifunza  zinahusiana  na  darasa  lako    

5. Weka  simu  yako  katika  hali  ya  mtetemo    

• Mara zote uwe na Moduli yako ya Mafunzo ya Walimu Kazini na kalamu• Tafuta changarawe au jiwe dogo uje nalo katika kipindi

Page 43: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 7

TAFAKARI        Kipindi  kilichopita  tulijifunza  kuhusu  mikakati  ya  usimamizi   fanisi  wa  darasa.  Sasa  kila  mmoja  aandike   jambo  moja  alilofanikiwa  na  moja   ambalo   lilikuwa   changamoto   katika   kutekeleza  mikakati   hiyo  darasani  wakati  wa   vipindi   vya  kusoma  na  kuandika.    

         Andika  peke  yako  (dakika  5)  Tafadhali   andika   kwenye   visanduku   mafanikio   na   changamoto   ulizokutana   nazo   wakati   wa   kutekeleza  mikakati  hii  katika  darasa  lako.  

                                 

Jadiliana  katika  kikundi  (dakika  10)   Shirikisha  wenzako  kwenye  kundi  mojawapo  ya  uzoefu  huo.       Kwa  kila  changamoto,  jaribu  kutoa  suluhisho  lako  kwa  ajili  ya  kutatua  changamoto  za  

wenzako.   Wakati  wa  majadiliano,  andika  ufumbuzi  unaoendana  na  changamoto  ulizobainisha.  

                                   

Ufumbuzi    Unaowezekana    (Mawazo  muhimu  kwa  wenzetu)  

   

Mafanikio  (Elezea  utaratibu  uliotumia  na  fafanua  jinsi  ulivyofanikiwa)  

 

Changamoto    (Elezea  utaratibu  uliotumia  na  fafanua  changamoto  zake)  

 

Page 44: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 8

UTANGULIZI      

     Zoezi  la  Kuchangamsha  (dakika  10)  

 Kalamu   na   Changarawe:   Weka   kalamu   na   changarawe   yako   juu   ya   meza   yako.   Sikiliza   kauli   zinazosomwa   na  mwezeshaji  wako.      

Kama  kauli  ni  ya  kweli  kamata  kalamu  yako  na  uinyanyue  juu  (tazama  picha  hapo  chini).     Kama  kauli  sio  ya  kweli  kamata  changarawe  yako  uinyanyue  juu  .  (tazama  picha  hapo  chini)    

      �

     Fikiri  –Wawili  wawili  –  Shirikishana  (dakika  10)  Jadili  maswali  yafuatayo  na  mwenzako.  Baadaye  tutashirikishana  katika  vikundi.    

     

1. Katika  zoezi  hili  mlitakiwa  kufanya  nini?    2. Mratibu  wa  Mafunzo  anaweza  kupima  nini?  3. Kazi  hii  inaweza  kuwa  na  manufaa  kwa  mwalimu?  Kwanini?  4. Je,  unaweza  kuliboresha  zoezi  hili  lifae  kutumika  darasani  kwako?    

                                       

Page 45: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 9

1. Mwalimu  mmoja  anaanza  kusoma  kwa  sauti.  Baada  ya  kukamilisha  aya  anamwita  mwalimu  mwingine  kwa  jina  asome  aya  inayofuata.      

2. Wakati  unaposoma:    -­‐Weka  alama  ya  mshangao  (!)  katika  sehemu  ambayo  unaona  ni  muhimu    -­‐Weka  alama  ya  (?)  katika  sehemu  ambayo  huelewi  au  hukubaliani  nayo    -­‐Weka  mduara  katika  maneno  ambayo  ni  mapya.  

 

DHANA  KUU        

 Umuhimu  wa  tathmini  endelevu  wakati  wa  kufundisha  (dakika  10)    

                     Tathmini  ya  wanafunzi  inasaidia  walimu  kujua  kama  wanafunzi  wamefikia  lengo  lililowekwa  la  kusoma  na  kuandika.  Kama  wanafunzi  hawajafikia  lengo  ina  maana  kwamba  bado  hawajaelewa  yaliyofundishwa  katika  somo  hilo.  Vilevile    tathmini  ya  wanafunzi  inasaidia  walimu  kuchukua  hatua  ili  kuweza  kujiandaa  vyema  zaidi  na  kuandaa  vipindi  muhimu  vya  kupitia  yale  waliyofundisha.        

Je  kutathmini  wanafunzi  kunamsaidiaje  mwalimu?  

Walimu  wanaweza:  -­‐ Kufahamu  kama  wanafunzi  wameweza  kufikia  

lengo  la  somo;  -­‐ Kuthibitisha  ufahamu  wa  wanafunzi  katika  somo;  -­‐ Kuthibitisha  jinsi  wanafunzi  wanavyofanikiwa  na  

kwa  kiwango  gani;  -­‐ Kupima  idadi  ya  wanafunzi  wanaofahamu  dhana  

zilizofundishwa  na  idadi  ya  wale  wanaohitaji  mazoezi  na  msaada  zaidi.  

-­‐ Kuandaa  masomo  ya  kufundisha  kwa  wakati  ujao.    

 

   

Je,  tathmini  zinamsaidiaje  mwanafunzi?  

Wanafunzi  wanaweza:  -­‐ Kufahamu  ni  makosa  gani  wanayofanya;  -­‐ Kupima  uelewa  na  ufahamu  wao  wenyewe  na  

kutambua  maeneo  wanayohitaji  msaada  ;  -­‐ Kuinua  ubora  na  kasi  ya  kuelewa  dhana  

zinazofundishwa.  -­‐ Kujijengea  hali  ya  kujiamini  kulingana  na  uwezo  

wao;  -­‐ Kusaidia  wenzao  wenye  matatizo  ya  kujifunza  .  

 

   Tathmini  za  Wanafunzi  siyo  lazima  ziwe  za  kufanya  majaribio  ya  kuandika  kwenye  karatasi  mwishoni  mwa  kila  sura  ya  kitabu   cha   kiada.   Tathmini   za   mwanafunzi   zinaweza   na   zinapaswa   kufanyika   wakati   wote   kwa   kila   somo  unalofundisha.  Kuna  aina  kuu  mbili  za  tathmini  unazoweza  kutumia  wakati  wa  kufundisha:                                                                                                                                                                                                  

Page 46: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 10

                                                                                                                                                                                           

                                                           TATHMINI-­‐UFAFANUZI                                                            

Tathmini  Endelevu  

Ni  mchakato  wanaoutumia  walimu  wakati  wa  kufundisha  ili  kupata  mrejesho  wa  kuwezesha    kurekebisha  ufundishaji  unaoendelea  ili  kuinua  uwezo  wa  wanafunzi    kufikia  malengo  ya  kujifunza.  

Tathmini      Tamati  

Shughuli  rasmi  za  tathmini  ambazo  zinaonesha  hatua  waliyofikia  wanafunzi  katika  kipindi  maalumu    

 Baada  ya  kupima  kiwango  cha  wanafunzi  cha  kujifunza  kutokana  na  tathmini  endelevu,  walimu  wanaweza  kurekebisha  mikakati  yao  ya  ufundishaji  kulingana  na  mahitaji.  Mfano,  ikiwa  tathmini  endelevu  inaonesha  kuwa  wanafunzi  hawaelewi  dhana  fulani,  inabidi  mwalimu  ajaribu  kuelezea  dhana  hiyo  kwa  kutumia  njia  nyingine  au  atumie  mifano  mingine  mipya.  Vilevile  mwalimu  anaweza  kutumia  tathmini  endelevu  kubaini  wanafunzi  wenye  shida  zaidi  katika  kujifunza  na  kuwapa  msaada  stahiki.        

 Jadiliana  katika  kikundi  kikubwa  (dakika  5)  

                                                         Ni  sehemu  gani  katika  matini  ya  hapo  juu  ambayo  unaona  ni  ya  muhimu,  haieleweki  au  mpya?        

 Zoezi  (dakika  5)    Zungushia   duara   aina   ya   tathmini   iliyo   sahihi   (tathmini   endelevu,   tathmini   tamati,   au   zote   mbili)  

kulingana  na  maelezo  ya  aina  za  tathmini  katika  jedwali  hapo  chini.    Mara  baada  ya  kuzungushia  duara,  ukiwa  katika  kikundi,  jadili  majibu  na  kutoa  maelezo  ya  kina  zaidi.        

 

Maelezo  ya  aina  za  Tathmini     Aina  ya  Tathmini  

1) Inatathmini  rasmi  uwezo/maarifa  kwa  kipindi  maalumu  (mfano:  mwishoni  mwa  sura  au  mwishoni  mwa  nusu  mhula  n.k)    

Tathmini  Endelevu  

Tathmini  ya  Tamati  

Zote  mbili  

2) Inawapa  walimu  taswira  ya  ufahamu  wa  wanafunzi  wakati  wote  wa  somo.    

Tathmini  Endelevu  

Tathmini  ya  Tamati  

Zote  mbili  

3) Inawapa  wanafunzi  fursa  ya  kuonesha  ufahamu  wao.     Tathmini  Endelevu  

Tathmini  ya  Tamati  

Zote  mbili  

 

ZOEZI        

   Mikakati  ya  Tathmini  Endelevu  (dakika  10)    

 Kuna  njia  nyingi  za  haraka  za  kutathmini  ujifunzaji  wa  wanafunzi  wakati  somo  linaendelea.  Ifuatayo  ni  mikakati  minne  ambayo  unaweza  kutumia  hata  katika  madarasa  makubwa:        

ZOEZI

Page 47: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 11

Kalamu  na  Changarawe-­‐  Waambie  wanafunzi  kila  mmoja  aje  na  changarawe  moja  darasani.  Waambie  waweke  kalamu  zao  na  changarawe  katika  madawati  yao.  Waambie  wanafunzi  kuwa  utasoma  kauli  zinazotokana  na  somo  unalofundisha.    Kama  wanafikiri  kauli  hiyo  ni  ya  kweli,  washike  kalamu  zao  mkononi  na  kuinua  juu.  Kama  wanafikiri  kuwa  usemi  huo  siyo  kweli,  wachukue  changarawe  zao  na  wainue  juu.    Mfano,  baada  ya  kujifunza  siku  za  juma,  unaweza  kutengeneza  kauli  ifuatayo:  “Jumatano  ni  siku  ya  kwanza  ya  juma”.  Kama  ilivyo  katika  shughuli  uliyofanya  mwanzoni  mwa  moduli,  aina  hii  ya  mkakati  wa  tathmini  inasaidia  kupima  kama  wanafunzi  wanaelewa  dhana  ambazo  umekuwa  ukifundisha.    

   

Mchezo  wa  kulala-­‐  Waambie  wanafunzi  waweke  viganja  vya  mikono  yao  usoni  na  wainamishe  vichwa  vyao  kwenye  madawati  wakiwa  wamefumba  macho  kama  vile  wamelala  (waambie  wasifumbue  macho!)  Waambie  wanafunzi  utatamka  semi  ambazo  zinauhusiano  na  somo  unalofundisha.  Kama  wanafikiri  kauli  hiyo  ni  ya  kweli,  wainue  mikono  yao  (wakiwa  wameweka  vichwa  vyao  chini).  Kama  wanafikiri  kuwa  usemi  huo  siyo  kweli,  wasiinue  mikono  yao.  Mchezo  wa  kulala  unafanana  na  ule  wa  Kalamu  na  Changarawe,  lakini  mchezo  huu  unawapa  wanafunzi  fursa  ya  kujibu  kwa  uaminifu  bila  kuangalia  wenzao  kupata  jibu  sahihi.  

   

Mchezo  wa  Nioneshe  -­‐  Kuhakiki  kama  wanafunzi  wanaelewa  unachofundisha,  waambie  wanafunzi  kuwa  utauliza  swali  la  haraka  na  wanatakiwa  kuandika  jibu  katika  karatasi  (au  nyuma  ya  daftari  zao).  Wakimaliza  wainue  karatasi  zao  juu  uzione.  Mfano,  ikiwa  unafundisha  silabi,  unaweza  kuuliza,  “Andika  silabi  ba."    Kisha  wanafunzi  wakuoneshe  majibu  yao.  Unaweza  kuendelea  na  mchezo  huu  kwa  kusema,  “Sasa  andika  silabi  bo”      

  Okota  kwa  Kubahatisha      Wanafunzi  waandike  majina  yao  katika  vitu  vya  kudumu  kama  vile,  vipande  vya  

makasha  (kutoka  makasha  yaliyotupwa),  kifuniko  cha  chupa  au  hata  kipande  cha  jiwe  kilicho  na  uso  laini.  Weka  vitu  vyote  katika  mkoba,  kasha  au  ndoo  na  uwe  navyo  katika  kila  somo.  Wakati  unapouliza  swali,  chomoa  kwa  kubahatisha  kitu  kimojawapo  kutoka  katika  mkoba,  kasha  au  ndoo  na  mwanafunzi  ambae  jina  lake  lipo  katika  kitu  hicho  ajibu  swali.  Mbinu  hii  inasaidia  kuchagua  wanaojibu  kwa  njia  ya  kubahatisha.  Hii  ina  maana  kuwa  wanafunzi  ambao  wananyoosha  mikono  mara  kwa  mara  hawatawali  majadiliano  ya  darasani  (na  tathmini).  Vilevile  inasaidia  kupata  majibu  zaidi  ya  yale  

ya  ndio  au  hapana.        

   Igizo  (dakika  20)    

Kila  mwalimu  achague  mojawapo  kati  ya  mikakati  minne  ya  tathmini  endelevu  iliyoelezwa  hapo  juu  (Kalamu  na  Changarawe,  Mchezo  wa  Kulala,  mchezo  wa  Nioneshe    na  Kuokota  kwa  Kubahatisha).  Kila  mwalimu  aandae  igizo  dhima  ambapo  yeye  ni  mwalimu  na  walimu  wengine  ni  wanafunzi  wake.  Tumia  mkakati  wako  wa  tathmini  uliochagua  kutathmini  ujifunzaji  wa  wanafunzi  katika  mada  unayofundisha  katika  somo  la  Kiswahili,  kama  vile,  herufi,  rangi,  siku  za  juma  au  mada  nyingine  katika  muhtasari.  Mfano,  kama  ukichagua  kutathmini  wanafunzi  kuhusu  uelewa  wao  wa  rangi  na  umechagua  kutumia  mkakati  wa  Mchezo  wa  Kulala,  andika  semi  ambazo  ni  kweli  au  siyo  kweli  ambazo  wanafunzi  wanaweza  kuchagua  jibu  (kama  vile,  ‘majani  ya  mti  ni  ya  zambarau’).      Una  dakika  10  kujiandaa.  Baada  ya  hapo  kila  mwalimu  ataonesha  igizo  lake  kwa  kupokezana.    

Page 48: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 12

     Fikiri  –Wawili  wawili-­‐  Shirikishana    (dakika  5)    

  Ni  kwa  namna  gani  kila  mkakati  umesaidia  kutathmini  uelewa  wa  wanafunzi?     Utawezaje  kutekeleza  mikakati  hii  darasani  kwako?     Kwa  namna  gani  utaitumia  hiyo  mikakati?     Kuna  mikakati  mingine  ya  tathmini  endelevu  ambayo  imekujia  kichwani  kwako  wakati  ukiwa  sehemu  ya  igizo  

dhima?          

   Mikakati  ya  Kusaidia  Wanafunzi  Wanaopata  Shida  Kujifunza  (dakika  15)    

     Unapotathmini  wanafunzi  wakati  wote  wa  somo,  unaweza  kuona  wanafunzi  wengi  ambao  hawajaelewa  dhana  fulani.    Katika  hali  kama  hii  inabidi  ufundishe  upya  maudhui  ya  mada  husika,  utumie  njia  bora  zaidi  ya  kuelezea  maudhui  hayo  au  kutoa  mifano  zaidi.  Hata  hivyo,  pamoja  na  kwamba  wanafunzi  wengi  watakuwa  wamefikia  malengo  yaliyowekwa,  bado  wapo  wanafunzi  wachache  ambao  watakuwa  na  shida  ya  kujifunza.  Unatakiwa  kuhakikisha  kuwa  wanafunzi  hawa  wanaopata  shida  kujifunza  wanakuwa  na  mwelekeo  chanya  na  hawakati  tamaa  pamoja  na  kwamba  wako  nyuma  ya  wenzao.  Ifuatayo  ni  mikakati  ya  kusaidia  wanafunzi  wanaopata  shida  kujifunza:        

Kazi  Zilizotofautishwa:    Kama  unafahamu  kwamba  mwanafunzi  anayepata  shida  kujifunza  hataweza  kukamilisha  zoezi,  panga  marekebisho  rahisi  katika  ufundishaji  wako  ili  wanafunzi  wa  aina  hii  waweze  kukamilisha  kazi  wanazopewa.  Mfano,  Kama  wanafunzi  wa  Darasa  la  2  wanaandika  matini  kuhusu  walichofanya  mwisho  wa  juma,  wanafunzi  wanaopata  shida  kujifunza  wanaweza  kuchora  picha  kwanza  na  baadaye  wajikite  tu  katika  kuandika  maneno  ya  msingi,  ‘kaka,’  kuku’,  ‘chipsi’.    

  Wawili  Wawili  Kimkakati-­‐  Wanafunzi  wanaopata  shida  kujifunza,  mara  nyingi  hujifunza  kujenga  stadi  zao  kutoka  kwa  wenzao  ambao  wako  mbele  katika  kujifunza.  Kuweka  mkakati  wa  kuchagua  mwenzao  anayeweza  kusaidia  mwanafunzi  anayepata  shida  kujifunza,  ni  fursa  nzuri  ya  kuwapa  msaada  binafsi  ambao  wasingeupata  wakiwa  katika  darasa  kubwa.  Mfano,  baada  ya  mwanafunzi  anayepata  shida  kujifunza  kuandika  maneno  ya  msingi  kuhusu  mwisho  wa  juma  (kaka,  kuku,  chipsi),  mwenzake    anaweza  kumsaidia  kuandika  maneno  yaliyorukwa  kukamilisha  sentensi  (‘Kaka  yangu  amepika  kuku  na  chipsi’).      

  Mpangilio  wa  Kukaa-­‐  Wakati  mwingine  wanafunzi  wanaopata  shida  katika  somo,  utakuta  wana  uono  hafifu.  Jaribu  kuweka  wanafunzi  wa  aina  hii  mbele  ya  darasa  kupunguza  vikwazo  na  kuwarahisishia  kuona  maudhui  ya  somo  na  vifaa.    Hakikisha  unawaambia  wanafunzi  kwamba,  kukaa  mbele  ya  darasa  ni  upendeleo  na  siyo  kwa  sababu  ya  kutoelewa.  .      

Msaada  wa  ziada-­‐  Ikiwa  darasa  linafanya  mazoezi  binafsi,  unaweza  kutoa  msaada  wa  ziada  wa  pamoja  kwa  wanafunzi  wengi  kwa  kuwaketisha  karibu  karibu.  Mfano,  waketishe  wanafunzi  wenye  shida  ya  kujifunza  mbele  ya  darasa  (kwa  mara  nyingine  waeleze  kwamba  ni  upendeleo)  ili  kuwapa  msaada  wa  karibu  wanapofanya  mazoezi.    

 

Page 49: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 13

Muda  wa  kusubiri-­‐unapowaita  wanafunzi  wenye  shida  ya  kujifunza  kujibu  maswali  darasani,  wape  muda  mrefu  wa  kufikiria  maswali.  Unaweza  kuhesabu  kichwani  mwako  taratibu  kuanzia  moja  hadi  tano  kuhakikisha  kuwa  umetoa  muda  wa  kutosha  wa  kufikiria  na  kutoa  jibu.  Mara  nyingi  ni  vigumu  mwalimu  kutoa  muda  huu  wa  kusubiri,  lakini  unaweza  kuwa  wa  thamani.  Vile  vile  ni  muhimu  kufafanua  maswali  au  kuwapa  maelekezo  zaidi.  Ni  muhimu  kwa  wanafunzi  wenye  shida  ya  kujifunza  kukuza  uwezo  wa  kujiamini.  Hakikisha  unawasaidia  kufikia  jibu  sahihi.                

 Jadili  katika  kikundi  (dakika  5)    

Kwa  wastani,  kuna  wanafunzi  wangapi  wanaopata  shida  ya  kujifunza  darasani  kwako?     Unafikiri  ni  mikakati  ipi  kati  ya  hiyo  inaweza  kuwasaidia  kufanya  vizuri?    

Je,   kuna   mikakati   mingine   unayoweza   kutumia   kusaidia   wanafunzi   wanaopata   shida   kujifunza?  Jadiliana  na  walimu  wenzako.      

TATHMINI  BINAFSI      

   Andika    (dakika  5)    

Tafadhali  kamilisha  tathmini  binafsi  ifuatayo.  Weka  X  katika  nafasi  husika  kuonesha  kwa  kiasi  gani  unatumia  mkakati  huo  KATIKA  DARASA  LAKO.      ZINGATIA:    Tathmini  hii  binafsi  ni  ya  kwako  mwenyewe  (huhitaji  kumshirikisha  mtu  yeyote)  na  ni  njia  ya  kujichunguza  kuona  uwezo  ulionao  na  ni  maeneo  gani  unahitaji  kujiimarisha  katika  utendaji  wako.      

Tathmini  na  Mikakati  ya  Kusaidia      Sielewi   Naelewa  lakini  sifanyi  

 Nafanya  lakini  naweza  

kufanya  vizuri  zadi  

 Nafanya  vizuri  sana  

Natengeneza  na  kutoa  aina  mbalimbali  za  tathmini  tamati  kufuatilia  uelewa  wa  wanafunzi.    

       

Natengeneza  na  kutoa  aina  mbalimbali  za  tathmini  endelezi  kufuatilia  uelewa  wa  wanafunzi.    

       

Narekebisha  ufundishaji  wangu  kulingana  na  matokeo  ya  tathmini  na  ninarudia  kufundisha  maudhui  ya  mada  inapobidi.    

       

Natoa  muda  wa  ziada  wa  kusubiri  kwa  wanafunzi  wanaopata  shida  kujifunza  wakati  wanapojibu  maswali  au  wanapokamilisha  kazi.    

       

Najitahidi  kujenga  uwezo  wa  kujiamini  wa  wanafunzi  wanaopata  shida  ya  kujifunza  ili  wasijione  ni  wajinga.    

       

Wakati  wa  kuuliza  maswali  darasani,  nachagua  wanafunzi  tofauti  tofauti  na  siyo  lazima  wale  wanaonyoosha  mikono  yao  kwanza.    

       

Nabaini  wanafunzi  wanaopata  shida  kujifunza  na  kuweka  mikakati  ya  kuwasaidia.                

Page 50: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 14

KUPANGA  MKAKATI        

     Kupanga  ‘Kipindi  cha  Kusoma  na  Kuandika’    (dakika  15)      

Ili  kuimarisha  uwezo  wa  wanafunzi  wa  kusoma,  ni  muhimu  walimu  waweze  kutumia  mbinu  mpya  za  kusoma  na  kuandika  ambazo  wamejifunza  katika  MWK.  Vile  vile  ni  muhimu  wanafunzi  wapate  muda  maalumu  wa  kusoma.  Hii  ndiyo  maana  ni  muhimu  kuwa  na  kipindi  cha  kusoma  na  kuandika  mara  moja  kwa  juma  (kando  ya  kipindi  cha  Kiswahili).  Pamoja  na  kuwa  shughuli  zinazofuata  hazina  uhusiano  mahususi  katika  kusoma  na  kuandika  (zinaweza  kutumika  kutathmini  na  kusaidia  wanafunzi  katika  darasa  lolote  na  somo  lolote)  lakini  zitasaidia  katika  kufundisha  wanafunzi  kusoma.  Tafadhali  jaribu  kutumia  shughuli  hizi  katika  kipindi  chako  cha  kusoma  na  kuandika.    

   

Kitendo  cha  Matumizi  #1:  Tathmini  ya  Kuokota  kwa  Kubahatisha      Maandalizi    

1) Kabla  ya  siku  ya  somo,  waagize  wanafunzi  walete  vitu  vidogo  vilivyoandikwa  majina  yao  (kifuniko  cha  chupa,  kipande  cha  kasha,  au  kipande  cha  jiwe  chenye  uso  laini).  Vitu  vya  kudumu  vinaweza  kutumika  mwaka  mzima  lakini  karatasi  zinaweza  kutumika  vile  vile.    

2) Tafuta  mkoba,  kasha  au  ndoo  kwa  ajili  ya  kuwekea  vitu  vya  wanafunzi.    3) Tayarisha  orodha  ya  maswali  ya  kutathmini  ujifunzaji  wa  wanafunzi  katika  mada  ambayo  unafundisha  au  

ambayo  umeifundisha  karibuni.  Jiandae  kuuliza  wanafunzi  maswali  yapatayo  10-­‐20.      

Kitendo  Muhimu  cha  Ufundishaji      

1) Waambie  wanafunzi  kwamba  kutakuwa  na  mapitio  ya  kujifunza.  Waeleze  kuwa  utaokota  jina  kwa  kubahatisha,  na  mwanafunzi  mwenye  jina  hilo  lazima  ajibu  swali  atakalopewa.  Wasisitizie  kuwa  yeyote  anaweza  kuitwa  jina  kwa  hivyo  wasikilize  kwa  makini  wakati  wote.    

2) Anza  kitendo,  lakini  hakikisha  unawapa  wanafunzi  sekunde  chache  za    kusubiri  kabla  ya  kujibu  swali.  Kama  wanashindwa  kupata  jibu,  angalia  kama  unaweza  kuwadokezea  ili  wafikie  jibu  sahihi.    Vile  vile  unaweza  kuchagua  mwanafunzi  mwingine  adokeze  jibu.    .  

3) Baada  ya  swali,  tumia  dakika  chache  kuelezea  jibu  sahihi.  Hii  ni  nafasi  nyingine  ya  kujifunza  maudhui  kwa  wanafunzi  wanaopata  shida  kujifunza.        

 Matendo      

1) Katika  vikundi  vidogo  (au  dawati  kwa  dawati)  wanafunzi  wafanye  kwa  pamoja  kitendo  cha  kuokota  kwa  kubahatisha.  Kila  mmoja  aandike  jina  lake  katika  kikaratasi.  Baada  ya  hapo  wanabadilishana  kuwa  ‘mwalimu’  na  kuokota  jina  la  kujibu  mojawapo  ya  maswali  ya  mapitio.  Wanaweza  kurudia  maswali  ya  mwalimu  au  kufikiria  maswali  yao  mengine  ya  mapitio.        

2) Zunguka  darasani  kufuatilia  wanafunzi.  Weka  kumbukumbu  ya  mada  ambazo  zinaonekana  zina  utata  kwa  wanafunzi  wengi  na  ambazo  zitahitaji  kufundishwa  upya.    

                 

KUPANGA MKAKATI

Page 51: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 15

Kitendo  cha  Matumizi  #  2:  Wawili  wawili  Kimkakati      Maandalizi    

1) Waambie  wanafunzi  kwamba,  lengo  la  somo  la  leo  ni  kuwafanya  wanafunzi  kufanya  kazi  katika  jozi  (wawili  wawili)  na  mwenzake  ambaye  hawafahamiani  vizuri.  Lengo  lingine  ni  kujenga  timu  nzuri  ambapo  mmoja  wao  anaweza  kusaidia  mwenzake  inapohitajika.      

2) Mwalimu  utaanza  mchakato  wa  kuwaweka  wanafunzi  wawili  wawili.  Anza  kwa  kuwaweka  mbele  ya  darasa  wanafunzi  wanaopata  shida  kujifunza.  Hii  itahakikisha  kwamba,  wanaona  ubao  vizuri  na  kusikia  maelezo  vizuri.  Baada  ya  hapa,  waweke  pia  wanafunzi  wanaojiweza  mbele  ya  darasa  na  kuhakikisha  kila  jozi  ina  mwanafunzi  anayejiweza  na  mwanafunzi  ambaye  anapata  shida  kujifunza.        

3) Baada  ya  kupata  jozi  hizo,  wanafunzi  wengine  wakae  katika  jozi  na  wenzao  ambao  hawafahamiani  vizuri  au  kukaa  pamoja.    

4) Waeleze  wanafunzi  wote  kwamba,  lengo  ni  kusaidia  wenzao  wakati  wa  somo.  Hata  hivyo,  wawasaidie  wenzao  pale  inapohitajika.    

 Kitendo  muhimu  cha  ufundishaji:    

1) Waambie  wanafunzi  kwamba,  utafundisha  mtoto  wa  shule  ya  awali  kupiga  mswaki  meno  yake.  Kwa  hivyo  itabidi  utoe  maelekezo  fasaha  na  kueleza  namna  ya  kufanya  kwa  usahihi.      

2) Waambie  wanafunzi  kwamba,  hatua  ya  kwanza  wakati  wa  kupiga  mswaki  meno  yako  ni  kuchukua  mswaki.    Kisha  andika  sentensi  hiyo  katika  ubao  wakati  unasema  kila  neno  unavyoendelea  kuandika.  Mfano:      

   

3) Waulize  wanafunzi  wakueleze  hatua  inayofuata.  Andika  hatua  hiyo  ubaoni.        

             4)  Endelea  kuuliza  wanafunzi  hatua  inayofuata  na  andika  kila  hatua  katika  ubao.                5)  Baada  ya  kuandika  hatua  zote  katika  ubao,  soma  maandiko  hayo  kwa  sauti  mbele  ya  darasa  wakati  huo  huo  unaonesha  kila  neno  unalosoma.        Matendo  Binafsi      

1) Wanafunzi  wa  Darasa  la  1:      Waambie  wanafunzi  wasome  maelekezo  katika  ubao  pamoja  na  wenzao  katika  jozi.  Baada  ya  hapo  watachora  picha  kwa  kila  hatua  (Mfano,  picha  ya  kwanza  itaonesha  mtoto  akichukua  mswaki).  Waambie  wanafunzi  kwamba,  wanaweza  kuwaomba  wenzao  kuwasaidia  kuelewa  hatua  yeyote  iliyoandikwa  katika  ubao  kama  hawawezi  kusoma  ubaoni  au  hawakumbuki.      

 2) Darasa  la  2:  Futa  neno  moja  katika  kila  sentensi.  Waambie  wanafunzi  waandike  upya  maelekezo  katika  

madaftari  yao  na  kuweka  maneno  yanayokosekana.  Waambie  wanafunzi  kwamba,  wanaweza  kuomba  msaada  kwa  wenzao  katika  jozi  kuandika  au  kukumbuka  maneno  yeyote  ambayo  yanawatatiza.    

 3) Darasa  la  3:    Futa  hatua  zote.  Waambie  wanafunzi    waandike  upya  maelekezo  wanayoyakumbuka.  

Waambie  wanafunzi  kwamba  wanaweza  kuomba  msaada  kwa  wenzao  katika  jozi  kukumbuka  hatua  yeyote  au  kutamka  herufi  moja  moja  katika  neno  lolote.    

2. Weka dawa ya mswaki katika mswaki.

 

1. Chukua mswaki  

Page 52: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 16

     Jadili  na  mwenzako    (dakika  15)  

 Wewe  na  mwenzako,  jadili  namna  unavyoweza  kuingiza  vitendo  hivyo  viwili  katika  andalio  lako  la  somo  katika  vipindi  viwili  vijavyo  vya  kusoma  na  kuandika.  Tafadhali  andika  mawazo  yako,  hasa  namna  utakavyotumia  vitendo  hivyo  kulingana  na  kiwango  cha  darasa  lako  (  darasa  la  1,  2  au  3).  Baada  ya  majadiliano,  wasilisha  katika  kikundi  cha  wote.      _____________________________________________________________________________________________________    _____________________________________________________________________________________________________    _____________________________________________________________________________________________________    _____________________________________________________________________________________________________    _____________________________________________________________________________________________________    _____________________________________________________________________________________________________    _____________________________________________________________________________________________________    _____________________________________________________________________________________________________    _____________________________________________________________________________________________________    

   Mwisho    (dakika  5)  

Jibu  maswali  yafuatayo  mwenyewe.        Mada  ya  kipindi  cha  mafunzo:    Ni  kwa  namna  gani  umenufaika  na  malengo  ya  somo?  Kipi  kimekusaidia?          Ni  mambo  gani    utapenda  kujaribu  kwenye  darasa  lako  ndani  ya  mwezi  mmoja  ujao?          Kipi  umekipenda  katika  kipindi  cha  leo  cha  mafunzo?          Je  kuna  lolote  linaloweza  kufanyika  kwa  ajili  ya  kuboresha  kipindi  kijacho  cha  mafunzo?            

Page 53: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 17

 

Andika  taarifa  ya  kipindi  kijacho  :    

Mada:      

Tarehe  na  Muda:    

Mahali:    

                 

 Kupima  Utendaji  Kazi  (dakika  5)    

Tafadhali  tafakari  jinsi  mratibu  wa  MWK  alivyofanya  kazi  leo.  Jaza  fomu  ifuatayo  kwa  ajili  ya  kumbukumbu  ya  upimaji  wako.    Fomu  hii  itakusanywa  na  Timu  ya  Wilaya  ya  MWK  kwa  ajili  ya  kuwasaidia  waratibu  wa  MWK.          Mwongozo  wa  kutoa  alama  kupima  utendaji  kazi  wa    Waratibu  wa  MWK:  Alama  0:    Hajaweza  kabisa          

Alama  1:    Ameweza  kidogo                

Alama  2:  Ameweza  kiasi  cha  kuridhisha      

Alama  3:    Ameweza  vizuri  sana      

Mratibu  wa  MWK  hajaweza  kufanya  yale  yaliyoorodheshwa    

Mratibu  wa  MWK  ameweza  kidogo  kufanya  yale  yaliyoorodheshwa    

Mratibu  wa  MWK  ameweza  kufanya  kwa  kiwango  cha  kuridhisha  yale  yaliyoorodheshwa  

Mratibu  wa  MWK  ameweza  kufanya  vizuri  sana  yale  yaliyoorodheshwa    

   Kazi  zilizotekelezwa  wakati  wa  kipindi  cha  Mafunzo  Kazini:    

0    1  

 2  

 3  

1. Maandalizi:  Mratibu  wa  mafunzo  amejiandaa  kwa  kipindi    –  amesoma  vizuri  moduli    na  ameandaa  vifaa  vyote  vya  kufundishia          

       

2. Uwezeshaji:  Mratibu  wa    mafunzo  anasimamia  vizuri  majadiliano      –  anajua  jinsi  ya  kuwafanya  watu  wajieleze  na  namna  ya  kupata  majibu        

       

3. Uwezeshaji:    Mratibu  wa  mafunzo  anajua  namna  ya  kusimamia  makundi    –    anahakikisha  kuwa  walimu  wanatoa  ushirikiano,  wanashirikiana  na  wana  hamasika        

       

4. Kuelekeza    na  kushauri:    Mratibu  wa  mafunzo  anajua  jinsi  ya  kuwahamasisha  walimu  –  anafuatilia  kujua  waliokosa  vipindi  au  kuchelewa  na  kutukumbusha  kwanini  mafunzo  kazini    ni  muhimu  kwetu        

       

5. Kuelekezana  kushauri  :  Mratibu  wa  mafunzo  anatoa  ushirikiano  –  anafuatilia  maendeleo  yetu  kujua  kama  tunatumia  mbinu  mpya  darasani  na  anatusaidia  pale  anapoona  tuna  tatizo        

       

Alama  za  jumla:                        /15  x  100%  =  ________  

   

Page 54: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 18

Page 55: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa
Page 56: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 20

Page 57: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA WALIMU WA MADARASA YA MWANZO

Moduli ya Nne: Kuongeza usawa wa

Kijinsia na ushiriKi

Moduli ya Walimu

Page 58: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 2

Page 59: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 3

MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA WALIMU WA MADARASA YA MWANZO

Moduli ya Nne: Kuongeza usawa wa

Kijinsia na ushiriKi

Moduli ya Walimu

Page 60: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 4

Moduli hii imetayarishwa kwa ushirikiano na:

wizara ya elimu na Mafunzo ya ufundi Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Taasisi ya Elimu Tanzania Chuo Kikuu cha Dodoma

Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania

Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa EQUIP-Tanzania

Moduli hii imewezeshwa kwa ushirikiano na:

C.C.U Butimba C.C.U Bustani C.C.U Tabora C.C.u ndala C.C.U Kasulu

C.C.U Kabanga C.C.u BundaC.C.U Tarime

C.C.u shinyangaC.C.U Mpwapwa

Page 61: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 5

Maelekezo na taswira katika moduli

Kuna picha na michoro mingi katika moduli. Baadhi zinajirudia mara nyingi kwa sababu zinamaanisha jambo mahususi linalotokea. Chini kuna mfano wa taswira mbalimbali ambazo zinapatikana katika moduli pamoja na kile ambacho zinawakilisha:

Jadili na mwenzako: Wakati wote wa kusoma moduli, walimu wataelezwa kufanya kazi pamoja na mwalimu mwingine juu ya maswali au kazi.

Fikiri– Wawili wawili – Shirikishana: Kama ilivyo katika maelezo ya hapo juu, hapa vilevile walimu wanafanya kazi wakiwa wawili wawili. Japokuwa, hapa walimu wanatafakari mmoja mmoja kwanza juu ya swali au tatizo, halafu wanafanya kazi mwalimu mwenzake na mwishoni wanawasilisha katika kundi lote.

Jadiliana katika kikundi: Wakati mwingine walimu wataelekezwa kutafakari au kujadili maswali mbalimbali katika kikundi.

Soma: Katika kila moduli kuna “dhana kuu” ambayo kwa kawaida huwasilishwa kwa kirefu katika maelezo.

Andika: Moduli itawahamasisha walimu kuchukua maelezo na kuandika fikra zao na majibu.

Igizo: Baadhi ya mazoezi yatahitaji walimu kuigiza kazi ya kufundisha wakati wengine watapaswa kuigiza kama wanafunzi.  

Page 62: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 6

 

 Moduli  ya  Nne:  Kuongeza  Usawa  wa  Kijinsia  na  Ushiriki    

       

 

 MAUDHUI  YA  MODULI:    Moduli    hii  inamwelekeza    mwalimu    ufundishaji  na  ujifunzaji  unaozingatia  jinsia.  Walimu  wanaozingatia  jinsia  wanasahihisha  kwa  vitendo  kuegemea  upande  mmoja  wa  jinsia  na  ubaguzi  wa  kijinsia  darasani.  Mfano,  wanahakikisha  kwamba  lugha  inayotumika  haichochei  mwelekeo  hasi  wa  kijinsia,  wavulana  hawatawali  darasa  na  vifaa  vya  kufundishia  na  kujifunzia  havina  masuala  ya  kijinsia  ambayo  ni  ya  mazoea.  Moduli  hii  itamsaidia  mwalimu  kutumia  misingi  ya  usawa  wa  kijinsia  ili  wanafunzi  wote  wapate  fursa  sawa  za  kujifunza  kufikia  kiwango  chao  cha  juu.          DHANA  KUU:       Usawa  wa  kijinsia:  Kutoa  huduma  kwa  usawa,  matumizi  ya  vifaa  kwa  usawa  na  kutoa  fursa  sawa  kwa  

wasichana  na  wavulana.  Katika  utoaji  wa  elimu  inahusu  kuhakikisha  kwamba  wasichana  na  wavulana  wanapata  fursa  sawa  kuandikishwa  shuleni,  wanafundishwa  kwa  usawa  na  wanapata  vifaa  na  fursa  zingine  za  kielimu  kwa  usawa.  

Ufundishaji  na  ujifunzaji  unaozingatia  jinsia:  Hii  inahusu  walimu  kusahihisha  kwa  vitendo  kuegemea  upande  mmoja  wa  kijinsia  na  ubaguzi  wa  kijinsia  ili  kuhakikisha  usawa  wa  kijinsia  kupitia  mchakato  mzima  wa  ufundishaji  na  ujifunzaji.      

Ushiriki  wa  wanafunzi:  Wanafunzi  kushirikishwa  kikamilifu  katika  kutoa  mrejesho  na  taarifa  kwa  walimu.    

MALENGO  YA  MODULI:        Mwisho  wa  moduli  hii,  walimu    wawe  wameweza:  

kueleza  namna  jinsia  inavyoweza  kuathiri  ujifunzaji   kubainisha  maeneo  ya  ufundishaji  na  ujifunzaji  unaozingatia  jinsia     Kutumia  mbinu  za  kufundishia  ambazo  zinawafanya  wanafunzi  wote  kushiriki  vizuri,  hasa  katika  madarasa  

makubwa.      

MAANDALIZI  YA  KIPINDI:        Mara  zote  uwe  na  Moduli  yako  ya  Mafunzo  ya  Walimu  Kazini  na  kalamu      TARATIBU  ZA  KUJIFUNZA  KWA  KILA  KIPINDI:    

1. Kutana  katika  sehemu  tulivu  yenye  ubao  kama  inavyoonekana  katika  picha  

2. Panga  madawati/meza  ili  kuwezesha  washiriki  wote  waonane  na  kuongea  pamoja    

3. Kuwa  huru  kuuliza  maswali  kama  hujaelewa  4. Kuwa  wa  msaada  kwa  wenzako    5. Kuwa  mbunifu  na  fikiria  jinsi  dhana  unazojifunza  

zinahusiana  na  darasa  lako    6. Weka  simu  yako  katika  hali  ya  mtetemo  

 

Page 63: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 7

TAFAKARI          Kipindi  kilichopita  tulijifunza  kuhusu  mikakati  ya  Tathmini  fanisi  ya  Wanafunzi.  Muda  huu  kila  mmoja  aandike  jambo  moja  alilofanikiwa  na  moja  ambalo  lilikuwa  changamoto  katika  kutekeleza  mikakati  hiyo  darasani  wakati  wa  vipindi  vya  kusoma  na  kuandika.    

 Andika  peke  yako  (dakika  5)  Tafadhali  andika  kwenye  kisanduku  mafanikio  na  changamoto  ulizopata  wakati  wa  kutumia  mbinu  hizo  darasani  kwako.    

                                     

Jadiliana  katika  kikundi  (dakika  10)    Elezea  mojawapo  ya  uzoefu  huo  kwenye  kundi.     Kwa   kila   changamoto,   jaribu   kutoa   ufumbuzi   wako   kwa   ajili   ya   kutatua   changamoto   za  

wenzako.   Wakati  wa  majadiliano,  andika  ufumbuzi  unaoendana  na  changamoto  ulizobainisha.  

   

                                     

Ufumbuzi  Unaowezekana  (Mawazo  muhimu  kwa  wenzetu)  

 

 

 

 

Mafanikio  (Elezea  utaratibu  uliotumia  na  fafanua  jinsi  ulivyofanikiwa)  

 

(Elezea  utar              

             

Page 64: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 8

UTANGULIZI        

     Fikiri  –Wawili  wawili  –  Shirikishana  (dakika  15)    

 

Mawazo  kuhusu  majukumu  ya  wanaume  na  wanawake  katika  jamii  yanaweza  kuchochewa  na  taswira  katika  vitabu  vya  kiada.  Angalia  picha  zifuatazo  ambazo  zimechukuliwa  katika  kitabu  kimoja  cha  kiada  na  angalia  shughuli  au  mwonekano  wa  jinsia.  Kisha  jibu  maswali  yanayofuata  chini  yake.  

 

       1. Wanaume  wana  majukumu  gani?    2. Wanawake  wana  majukumu  gani?    3. Mazoea  gani  ya  kijinsia  yanayooneshwa?    4. Unafikiri  ni  muhimu  kubadilisha  vielelezo  hivi?  Kwa  namna  gani?                                                                        

Page 65: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 9

  1. Mwalimu  mmoja  anaanza  kusoma  kwa  sauti.  Baada  ya  kukamilisha  aya  anamwita  mwalimu  mwingine  kwa  jina  asome  aya  inayofuata.      

2. Wakati  unaposoma:    -­‐Weka  alama  ya  mshangao  (!)  katika  sehemu  ambayo  unaona  ni  muhimu    -­‐Weka  alama  ya  (?)  katika  sehemu  ambayo  huelewi  au  hukubaliani  nayo    -­‐Weka  mduara  katika  maneno  ambayo  ni  mapya.  

 

DHANA  KUU      Ufundishaji  na  Ujifunzaji  Unaozingatia  Jinsia    (dakika  15)    

                   Uchunguzi  wa  utendaji  darasani  unaonesha  kwamba,  ufundishaji  na  ujifunzaji  kwa  kiasi  kikubwa  umeegemea  upande  mmoja  wa  jinsia.  Walimu  wengi  wanatumia  njia  na  mbinu  ambazo  haziwapi  wasichana  na  wavulana  fursa  sawa  kushiriki.  Vile  vile  walimu  wanatumia  vifaa  vya  kufundishia  na  kujifunzia  ambavyo  vinaendeleza  mazoea  ya  kijinsia.  Kutokana  na  hali  hii.  Kuna  haja  ya  kufanya  haraka  kuanzisha  ufundishaji  na  ujifunzaji  unaozingatia  jinsia.        

Jinsia  inahusu  uhusiano  na  majukukumu  ya  wanawake  na  wanaume  ambayo  yamepangwa  na  jamii.  Majukumu  haya  yamekuwa  yakirithishwa  kutoka  kizazi  kimoja  hadi  kingine.  Pamoja  na  kwamba  urithi  huu  unabidi  kuthaminiwa,  lakini  ni  muhimu  majukumu  ya  kijinsia  yasiingilie    ujifunzaji  wa  watoto.  Mawazo  ambayo  hayahojiwi  kama  vile,  ‘wasichana  ni  mahiri  katika  usafi’  au  ‘wavulana  ni  mahiri  katika  michezo,”  yanaweza  kukatisha  tamaa  mojawapo  ya  jinsia    kushiriki  hata  kabla  ya  shughuli  kuanza.  Vile  vile  watoto  wanaweza  kufanyiwa  mzaha  kwa  kufanya  vizuri  katika  jambo  ambalo  ‘limehifadhiwa  ‘kwa  ajili  ya  upande  mmoja  wa  jinsia.  Zifuatazo  ni  dhana  ambazo  zinatumika  sana  wakati  wa  kujadili  masuala  ya  jinsia:      

1. Ubaguzi  wa  kijinsia:  Kuwanyima  fursa  na  haki  au  kutoa  upendeleo  kwa  watu  kulingana  na  jinsia  yao.      

2. Mazoea  ya  Kijinsia:  Kuweka  taswira      mara  kwa  mara  ya  wanawake  au  wanaume  wakiwa  katika  majukumu  ya  kijadi  au  mgawanyo  wa  kazi  (katika  vyombo  vya  habari,  mazungumzo,  utani  au  vitabu).  Katika  vitabu  vya  kiada  vya  wanafunzi,  kwa  mfano,  wanawake  wanaonekana  kama  wafanya  usafi,  walezi  na  wauguzi,  na  wanaume  wanaonekana  kama  madereva,  madakatari  na  viongozi.    

3. Usawa  wa  kijinsia:  Kutoa  huduma  kwa  usawa,  matumizi  ya  vifaa  kwa  usawa  na  kutoa  fursa  sawa  kwa  wasichana  na  wavulana.  Katika  utoaji  wa  elimu  inahusu  kuhakikisha  kwamba  wasichana  na  wavulana  wanapata  fursa  sawa  kuandikishwa  shuleni,  wanafundishwa  kwa  usawa  na  wanapata  vifaa  na  fursa  zingine  za  kielimu  kwa  usawa.        

4. Ufundishaji  na  ujifunzaji  unaozingatia  jinsia:  Hii  inahusu  walimu  kusahihisha  kwa  vitendo  kuegemea  upande  mmoja  wa  kijinsia  na  ubaguzi  wa  kijinsia  ili  kuhakikisha  usawa  wa  kijinsia  kupitia  mchakato  mzima  wa  ufundishaji  na  ujifunzaji.      

 Katika  darasa  ambalo  linazingatia  jinsia,  wavulana  na  wasichana  wanahudumiwa  kwa  usawa,  wanapewa  fursa  sawa  za  kujieleza  na  kushiriki  kikamilifu.  Walimu  wanaozingatia  jinsia  wanahakikisha  kwamba  vifaa  vya  kujifunzia  wanavyopewa  au  mazoezi  yanahaririwa  ili  kurudisha  usawa  wa  kijinsia.  Mfano,  wakati  wa  kuandika  maswali  ya  zoezi,  walimu  wanaozingatia  jinsia  wanapinga  mazoea  ya  kijinsia  kwa  kuandika,  ‘Kaka  anapika’  badala  ya  ‘Mama  anapika’.  Zaidi  ya  yote,  walimu  wanaozingatia  jinsia  wanahakikisha  shughuli  za  darasani  kama  vile  kazi  za  vikundi  

Page 66: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 10

na  majadiliano  yanaongozwa  kwa  usawa  kati  ya  wavulana  na  wasichana.        

 Jadiliana  katika  kikundi  kikubwa  (dakika  10)  

 

1. Sehemu  zipi  za  matini  uliyosoma  ni  muhimu,  haieleweki  au  ni  mpya?    2. Unafikiri  unatumia  njia  za  kufundishia  na  kujifunzia  zinazozingatia  jinsia?    3. Unawezaje  kufanya  ufundishaji  na  ujifunzaji  uzingatie  jinsia  zaidi?      

 

 

Mshirikishe  mwenzako  katika  kuoanisha  hali  ya  ufundishaji  na  mikakati  ya  uwajibikaji  wa  kijinsia  kwa  kujaza  kwenye  karatasi  ya  maswali  na  majibu  (dakika  15)  

   .  Jihadhari,  wakati  mwingine  kuna  majibu  zaidi  ya  moja.  .  Pia,  kama  kuna  njia  nyingine  kwa  ajili  ya  kutatua  tatizo  mojawapo,  tafadhali  andika  njia  hizo.  Baada  ya  kumaliza,  Kila  kikundi  cha  watu  wawili  kisome  majibu  katika  darasa    

Hali  ya  Ufundishaji   Mikakati  ya  Uwajibikaji  wa  kijinsia  

1. Mpangilio  wa  darasa      Njia  zinazoweza  kutatua:____  Njia  nyingine:  

 

 A. Epuka  misemo  ambayo  itawafanya  wavulan  au  wasichana  

kujisikia  wao  ni  bora  au  duni  kuliko  wengine.  Mfano,  wavulana  wasifanywe  kujisikia  wanaposhindwa  michezo  wanakuwa  kama  wasichana  au  wasichana  wanaoongea  kwa  sauti  kubwa  au  wanaopenda  kuongoza  wasikatishwe  tamaa  kufanya  hivyo.            

B. Kuwa  msikivu  kwa  mahitaji  yanayogusa  hisia  za  wanafunzi.  Weka  ‘sanduku  la  matatizo’  katika  dawati  lako.  Au,  waeleze  wanafunzi  wako  kwamba  wanaweza  kukuona  wakati  wowote  wakijisikia  hawakutendewa  haki.        

C. Hakikisha  kwamba  wasichana  na  wavulana  wanapata  fursa  sawa  ya  kukaa  mbele  ya  darasa,  hasa  wasichana  wenye  aibu  ambao  wanaweza  kuhitaji  msaada  kuweza  kushiriki  vizuri  katika  somo.        

D. Panga  wavulana  na  wasichana  kwa  kupokezana  unapowapa  majukumu  kama  vile,  ,  kiranja  wa  darasa,  kiranja  mkuu,  kiranja  wa  zamu  n.k        

E. Tumia  mifano  na  mazoezi  ambayo  yanapinga  mazoea  ya  kijinsia.  (mfano,  ‘Baba  anasafisha  nyumba’).      

2. Usafi  wa  darasa    Njia  zinazoweza  kutatua:____  Njia  nyingine:  

   3. Kuepuka  kukuza  ubaguzi  wa  kijinsia    Njia  zinazoweza  kutatua:____  Njia  nyingine:  

   

4. Kuwahamasisha  wanafunzi  kuwaheshimu  wenzao,  walimu  na  jamii  nzima  

 Njia  zinazoweza  kutatua:____  Njia  nyingine:  

   

Page 67: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 11

5. Wavulana  na  wasichana  kupewa  fursa  sawa  za  majukumu  ya  uongozi  

 Njia  zinazoweza  kutatua:____  Njia  nyingine:  

   

F. Unapoona  mvulana  anamnyanyasa  msichana,  mwalimu  anaweza  kuonesha  kuguswa  na  suala  hilo  kwa  kumrudi  mhalifu  lakini  hakikisha  darasa  zima  linaona  umuhimu  wa  heshima.  Mfano,  mwalimu  anaweza  kusisitiza  kwamba  wavulana  na  wasichana  ni  sawa  na  hivyo  ni  lazima  waheshimiane.      

 G. Hakikisha  wasichana  na  wavulana  wanafanya  usafi  kama  

timu,  au  wanapeana  zamu  mara  kwa  mara  kati  ya  jinsia.  Wape  hamasa  wavulana  na  wasichana  kuweka  darasa  lao  safi.  .    

H. Kuwa  makini  na  masuala  ya  kijinsia  yaliyowekwa  kwa  mazoea  katika  vitabu  vya  kiada  na  kuwafanya  wanafunzi  nao  kutambua  uwepo  wa  mazoea  hayo.  Kisha  jadili  jinsi  mambo  haya  yanavyoweza  kuathiri  uelewa  wetu  wa  uwezo  wa  wavulana  na  wasichana.        

6. Kuhakikisha  kwamba  wanafunzi  wanatoa  taarifa  ya  uchokozi  unaohusisha  unyanyasaji  wa  kijinsia  kwa  walimu  na  uongozi  wa  shule  

 Njia  zinazoweza  kutatua:____  Njia  nyingine:  

       Jadiliana  katika  kikundi  kikubwa  (dakika  10)    

1. Kati  ya  hizi  ni  ipi  ambayo  unajisikia  kujiamini  kutekeleza  au  ambayo  umeshatekeleza?      2. Kati  ya  hizi  ni  ipi  ina  changamoto  zaidi,  au  itahitaji  msaada  kutoka  katika  uongozi?  Gani?  bainisha  3. Ni  mikakati  ipi  ambayo  unafikiri  walimu  wote  wanapaswa  waitekaleze?      4. Je,  inawezekana  kujadili  na  walimu  wote?  Lini?    

     

VITENDO      

 Kuhakikisha  Usawa  wa  Kijinsia  na  Ushiriki  wa    Wanafunzi    (dakika  5)      

Kupendelea  sauti  ya  wanafunzi  wote,  mawazo  yao  na  ushiriki  wao  darasani  ni  muhimu.  Kama  kundi  moja  la  wanafunzi  halihamasishwi  kushiriki,  utu  wao  na  hamasa  yao  pamoja  na  ujifunzaji  wao  vinadidimia.  Walimu  wanaweza  kutumia  mikakati  shirikishi  ambayo  itasaidia  wanafunzi  wote  kushiriki  na  kujisikia  kuthaminiwa.  Mikakati  hii  inahusisha,  kazi  za  wanafunzi  wawiliwawli  ,  maigizo  dhima,  na  majadiliano  katika  vikundi.  Pamoja  na  kwamba  mikakati  hii  inaongeza  ushiriki,  lakini  hakuna  hata  mkakati  mmojawapo  ambao  ni  kwa  ajili  kuzingatia  jinsia.  Katika  hali  hii  wavulana  wana  uwezekano  wa  kutawala  mchakato  wa  kujifunza  na  kuwatenga  wasichana.  Kwa  hivyo,  ni  muhimu  walimu  kuhakikisha  kwamba  mikakati  shirikishi  inajali  pia  jinsia.  Mfano:    

1. Toa  mazoezi  ambayo  yatahamasisha  wanafunzi,  hasa  wasichana  kuwa  na  hamasa  na  kuwa  na  malengo.    2. Wape  hamasa  wasichana  na  wavulana  kuwasilisha  kazi  zao  katika  makundi.  3. Hakikisha  makundi  yote  yana  mchanganyiko  wa  wasichana  na  wavulana.  4. Hakikisha  wavulana  na  wasichana  wanashiriki  kama  wanakikundi  na  viongozi  wa  vikundi.  .    5. Toa  nafasi  sawa  kwa  wasichana  na  wavulana  kujibu  maswali.    6. Ongeza  ari  kwa  wote,  wavulana  na  wasichana.    7. Tunga  maswali  na  mifano  ambayo  inaakisi  usawa  wa  kijinsia-­‐  tumia  uwakilishi  wa  wasichana  na  wavulana  

katika  muktadha  na  majukumu  anuwai.    .    

Page 68: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 12

   

 Jadili  na  mwenzako  (dakika  15)  

Hapa  chini  kuna  mikakati  mitatu  ambayo  imekusudiwa  kuwafanya  wanafunzi  washiriki  kikamilifu  kwa  vitendo  katika  masomo.  Katika  jozi,  soma  mikakati  hiyo  na  fikiri  namna  utakavyohakikisha  kwamba  kitendo  hicho  kinazingatia  jinsia.  Unaweza  kutumia  mawazo  yaliyopo  hapo  juu  au  ukafikiria  ya  kwako.        

   

1. Fikiri-­‐  Wawiliwawili-­‐  shirikishana:  Uliza  swali  kwa  wanafunzi  na  waache  kwanza  wafikirie  wenyewe,  kisha  washirikiane  na  jirani  yao  katika  kujadili  majibu  yao.  Wakati  wanafunzi  wanajadili  mwalimu  anazunguka  darasani  na  kusikiliza  kutoelewana  na  kutoa  maswali  ya  ziada  inapobidi.  Baada  ya  hapo,    mwalimu  anachagua  baadhi  ya  wanafunzi  kuwasilisha  majibu  yao.      

 Utachukua  hatua  gani  kuhakikisha  kwamba  majadiliano  yanazingatia  jinsia?  __________________  

 _____________________________________________________________________________________    _____________________________________________________________________________________  

   

2. Igizo  dhima:  Wanafunzi  wanaigiza  jambo  ambalo  linaonesha  kujifunza.  Mfano,  ikiwa  unafundisha  kusalimiana,  wanafunzi  wanatengeneza  igizo  fupi  kwa  kusalimia  kwa  usahihi.  Kama  unafundisha  rangi,  wanafunzi  wanaweza  kufanya  kazi  pamoja  kutengeneza  wimbo  unaohusu  rangi.    

             Utachukua  hatua  gani  kuhakikisha  kwamba  maigizo  yanazingatia  jinsia?  ___________________    _____________________________________________________________________________________    _____________________________________________________________________________________  

   

3. Michezo  ya  Darasa  zima:  Michezo  inasaidia  sana  katika  vitendo  vya  kujifunza  vya  darasa  zima  ambavyo  vinaweza  kutumika  kama  muda  wa  kujifunza  na  kufurahisha.  Mfano  wa  mchezo  wa  darasa  zima  unaitwa,  ‘Mwalimu  Anasema.’  Katika  mchezo  huu,  mwanafunzi  mmoja  anasimama  mbele  ya  darasa  kama  kiongozi  na  kutoa  maelekezo  kwa  kikundi.  .  Mfano,  ‘Mwalimu  anasema  inua  mkono  wako.’  Mwalimu  anasema  chora  herufi  B  hewani  kwa  kidole  chako.’    Wanafunzi  wanafuata  maelekezo  ya  kiongozi.      Hata  hivyo,  kama  kiongozi  haanzi  na  maelekezo  ya  ‘Mwalimu  anasema’  basi  wanafunzi  hawafuati  maelekezo  ya  kiongozi.  Mfano,  kama  kiongozi  akisema,  ‘Msalimie  rafiki  yako,’  wanafunzi  hawasalimiani.  Kama  mwanafunzi  anafanya  kitendo  bila  ya  maelekezo  ya  ‘Mwalimu  anasema’  mwanafunzi  huyo  anakaa  chini.  Wanafunzi  watakaobaki  wamesimama  ndio  washindi.      

 

Utachukua  hatua  gani  kuhakikisha  kwamba  michezo  ya  darasa  zima  inazingatia  jinsia?____________________      ___________________________________________________________________________________          

Page 69: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 13

TATHMINI  BINAFSI      

 Tathmini  Binafsi  ya  Mikakati  inayozingatia  Jinsia  (dakika  5)    Baada  ya  kujifunza  kujali  jinsia,  tafadhali  kamilisha  tathmini  binafsi  ifuatayo.  Weka  alama  ya  X  katika  

nafasi  husika  kuonesha  kwa  kiwango  gani  unatumia  mkakati  huo  katika  darasa  lako.    

 ZINGATIA:    Tathmini  hii  binafsi  ni  ya  kwako  mwenyewe  (huhitaji  kumshirikisha  mtu  yeyote)  na  ni  njia  ya  kujichunguza  kuona  uwezo  ulionao  na  ni  maeneo  gani  unahitaji  kujiimarisha  katika  utendaji  wako.  

 Mikakati  inayozingatia  Jinsia     0   1   2   3  

Nahakikisha  kwamba  wasichana  na  wavulana  wanapata  fursa  sawa  katika  majukumu  ya  uongozi.      

       

Nawapa  wasichana  na  wavulana  wajibu  kwa  usawa.  (rejea  mkakati  wa  kwanza  hapo  juu)      

       

Nahakikisha  kwamba  wanafunzi  wanatoa  taarifa  za  kunyanyaswa  au  kuonewa,  zikiwemo  zile  za  kijinsia.      

       

Nahakikisha  kwamba  darasa  linasafishwa  na  wasichana  na  wavulana.            

Naepuka  kuendeleza  mazoea  ya  kijinsia.            

Nawahamasisha  wanafunzi  kuheshimu  wenzao,  walimu  na  wanajumuiya  wote.    .            

                                                     

Page 70: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 14

KUANDAA  MPANGO  KAZI    

 

                                       Kuandaa  ‘Kipindi  cha  Kusoma  na  Kuandika’(dakika  15)      

Ili  kuimarisha  uwezo  wa  wanafunzi  wa  kusoma,  ni  muhimu  walimu  waweze  kutumia  mbinu  mpya  za  kusoma  na  kuandika  ambazo  wamejifunza  katika  MWK.  Vile  vile  ni  muhimu  wanafunzi  wapate  muda  maalumu  wa  kusoma.  Ndiyo  maana  ni  muhimu  kuwa  na  kipindi  cha  kusoma  na  kuandika  mara  moja  kwa  juma  (kando  ya  kipindi  cha  Kiswahili).  Pamoja  na  kuwa  shughuli  zinazofuata  hazina  uhusiano  mahususi  katika  kusoma  na  kuandika  (zinaweza  kutumika  kutathmini  na  kusaidia  wanafunzi  katika  darasa  lolote  na  somo  lolote)  lakini  zitasaidia  katika  kufundisha  wanafunzi  kusoma.  Tafadhali  jaribu  kutumia  shughuli  hizi  katika  kipindi  chako  cha  kusoma  na  kuandika.      

KITENDO  CHA  MATUMIZI    #1:    NITAKAPOKUWA  MKUBWA    

1. Kwa  kutumia  mkakati  wa  Fikiri-­‐  Wawiliwawili-­‐  Shirikishana,  waulize  wanafunzi  wanataka  kuwa  nani  watakapokua.  Sisitiza  ukweli  kwamba  wavulana  na  wasichana  wanaweza  kufanya  kazi  yeyote  ya  kitaalam.    

2. Wakati  wanafunzi  wanashirikishana  majibu,  andika  ndoto  zao  za  kazi  katika  ubao.    3. Kisha  waeleze  wanafunzi  kuwa  wataandika  hadithi  ya  ndoto  zao  za  kazi.  4. Andika  sentensi  ya  mfano  katika  ubao  kuonesha  aina  ya  sentensi  wanayopaswa  kuandika.  Hakikisha  

sentensi  ya  mfano  inazingatia  jinsia  na  inakazia  wazo  la  wasichana  kuwa  na  kazi  ya  kifahari.  Mfano,      

Juma atakuwa mpishi.

Amina atakuwa rais

5. Kisha  elekeza  wanafunzi  kuanza  kuandika.  Darasa  la  1  wanaweza  kuchora  picha  za  ndoto  zao  za  kazi  na  pengine  wakaandika  neno,  fungu  la  maneno  au  sentensi  kuhusu  picha  hiyo.  Wanafunzi  wa  Darasa  la  2  na  3  wanaweza  kuandika  sentensi  moja  au  zaidi  kuhusu  ndoto  zao  za  kazi  na  pengine  kwa  nini  wanataka  kufanya  kazi  hiyo.    

6. Mwisho  wa  somo,  wasichana  na  wavulana  wasimame  na  kusoma  sentensi  zao  kwa  sauti  au  kuonesha  michoro  yao    kwa  wenzao.    

 

KITENDO  CHA  MATUMIZI  #2:    MWALIMU  ANASEMA    

Kitendo  hiki  ni  cha  darasa  zima  kushiriki  katika  mchezo  ambao  unaweza  kutumiwa  wakati  wa  somo  la  msamiati,  wakati  wa  kupitia  upya,  utendaji  na  vitendo  vya  tathmini  

1. Waambie  wanafunzi  kwamba  watacheza  mchezo  unaoitwa  ‘Mwalimu  anasema.’    2. Waeleze  kanuni  kwa  kusema  ‘Mchezo  huu  sio  rahisi,  unahitaji  kusikiliza  kwa  MAKINI.      3. Onyesha  jinsi  ya  kufanya  kwa  kusema  ‘Mwalimu  anasema  shika  sikio  lako’  –  kisha  shika  sikio  lako.  Inayofuata,  

‘Mwalimu  anasema  inua  mkono  wako’  –kisha  inua  mkono  wako.  Mwisho,  sema  ‘Shika  aridhini’  –  onesha  itakavyokuwa  ukiwa  umesimama  tuli.    

4. Eleza  kwamba  kama  ulisema  ‘shika  kidole  cha  mguu’  badala  ya  ‘Mwalimu  anasema  shika  kidole  cha  mguuni’  ….wanafunzi  hawapaswi  kushika  kidole  chao  cha  mguuni.  Wanapaswa  kusimama  na  kungojea  maelekezo  mengine.    

5. Fanya  majaribio  kuona  kwamba  kila  mmoja  ameelewa  na  yupo  tayari  kucheza.  6. Cheza  ‘Mwalimu  anasema’  kwa  kutumia  msamiati  unaohusu  viungo  vya  mwili  (Uso,  midomo,  pua,  nywele,  

mkono,  bega,  tumbo,  mguu,  kanyagio,  kidole  cha  mguuni….)  7. Waalike  wanafunzi  kucheza  mchezo  ‘Mwalimu  anasema’  katika  vikundi  vidogo  vya  wanafunzi  4,  mahali  

ambapo  kila  mwanafunzi  atapata  nafasi  ya  kucheza  nafasi  ya  kiongozi  na  wengine  wamfuate.    8. Zunguka  kwenye  chumba  kusaidia  vikundi  vidogo.        

Page 71: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 15

   Jadili  na  mwenzako  (dakika  15)  

 Wewe  na  mwenzako,  jadili  namna  unavyoweza  kuingiza  vitendo  hivyo  viwili  katika  andalio  lako  la  somo  katika  vipindi  viwili  vijavyo  vya  kusoma  na  kuandika.  Tafadhali  andika  mawazo  yako,  hasa  namna  utakavyotohoa  vitendo  hivyo  kulingana  na  kiwango  cha  darasa  lako  (darasa  la  1,  2  au  3).  Baada  ya  majadiliano,  wasilisha  katika  kikundi  cha  wote.      _________________________________________________________________________    _________________________________________________________________________    _________________________________________________________________________    _________________________________________________________________________    _________________________________________________________________________    _________________________________________________________________________  

______________________________________________________________________________________________  _________________________________________________________________________  

_________________________________________________________________________  

_____________________________________________________________________________________________  

______________________________________________________________________________________________  

______________________________________________________________________________________________  

                                 

Page 72: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 16

 Mwisho  (dakika  5)      Jibu  maswali  yafuatayo    

 

Mada  ya  kipindi:  

 

Ni  kwa  namna  gani  umenufaika  na  malengo  ya  somo?  Kipi  kimekusaidia?    

 

 

Ni  mambo  gani    utapenda  kujaribu  kwenye  darasa  lako  ndani  ya  mwezi  mmoja  ujao?    

 

Kipi  umekipenda  katika  kipindi  cha  leo?    

 

 

Je  kuna  lolote  linaloweza  kufanyika  kwa  ajili  ya  kuboresha  kipindi  kijacho?    

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

     

Page 73: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 17

Andika  taarifa  ya  kipindi  kijacho:      

Mada:  

 

 

 

Tarehe  na  Muda:  

 

 

Mahali:  

 

 

 

 

 

 

 

   Kupima  Utendaji  Kazi  (dakika  5)  

 Tafadhali  tafakari  jinsi  mratibu  wa  MWK  alivyofanya  kazi  leo.  Jaza  fomu  ifuatayo  kwa  ajili  ya  tathmini  yako.  Fomu  hii  itakusanywa  na  Timu  ya  Wilaya  ya  MWK  kwa  ajili  ya  kuwasaidia  waratibu  wa  MWK.        Mwongozo  wa  Usahihishaji  kwa  ajili  ya  Waratibu  wa  MWK:  

Alama  0:    

Hajaweza  kabisa          

Alama  1:  

 Ameweza  kidogo                

Alama  2:  

Ameweza  kiasi  cha  kuridhisha      

Alama  3:  

 Ameweza  vizuri  sana      

Mratibu  wa  MWK  hajaweza  kufanya  yale  yaliyoorodheshwa    

Mratibu  wa  MWK  ameweza  kidogo  kufanya  yale  yaliyoorodheshwa    

Mratibu  wa  MWK  ameweza  kufanya  kwa  kiwango  cha  kuridhisha  yale  yaliyoorodheshwa  

Mratibu  wa  MWK  ameweza  kufanya  vizuri  sana  yale  yaliyoorodheshwa    

 

 

Yale  yaliyofanywa  wakati  wa  kipindi  cha  MWK:    

0  

 

1  

 

2  

 

3  

1. Maandalizi:  Mratibu  wa  MWK  amejiandaa  kwa  kipindi    –  amesoma  vizuri  moduli    na  ameandaa  vifaa  vyote  vya  kufundishia          

       

2. Uwezeshaji:  Mratibu  wa    MWK  anasimamia  vizuri  majadiliano      –  anajua  jinsi  ya  kuwafanya  watu  wajieleze  na  namna  ya  kupata  majibu        

       

3. Uwezeshaji:    Mratibu  wa  MWK  anajua  namna  ya  kusimamia  makundi    –    anahakikisha  kuwa  walimu  wanatoa  ushirikiano,  wanashirikiana  na  wana  hamasika        

       

4. Ufundishaji  na  ushauri:    Mratibu  wa  MWK  anajua  jinsi  ya  kuwahamasisha  walimu  –  anafuatilia  kujua  waliokosa  vipindi  au  kuchelewa  na  kutukumbusha  kwanini  MWK  ni  muhimu  kwetu        

       

5. Ufundishaji  na  ushauri  :  Mratibu  wa  MWK  anatoa  ushirikiano  –  anafuatilia  maendeleo  yetu  kujua  kama  tunatumia  mbinu  mpya  darasani  na  anatusaidia  pale  anapoona  tuna  tatizo        

       

Alama  za  jumla:                        /15  x  100%  =  ________  

   

Page 74: Moduli ya Mwalimu · Chuo Kikuu cha Dodoma Morogoro Chuo cha Ualimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ... C.C.U Kasulu C.C.U Kabanga c.c.U bunda C.C.U Tarime c.c.U shinyanga C.C.U Mpwapwa

Moduli ya Mwalimu 18