Upload
others
View
4
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
Msaada wa Matibabu kwa Wakimbizi
MWONGOZO WA KUTUMIA Imeanza kutumika tar. 1 Mei 2018
®
Kampuni ya Unified Administrators, LLC
MISSOURI
Utangulizi
Kwa zaidi ya miaka 100 Kamati ya Kuwashughulikia Wakimbizi na
Wahamiaji Marekani (USCRI) imetetea haki na maisha ya watu walio
hamishwa makwao kwa lazima au kwa hiari. USCRI inawapa wakimbizi
na watu wengine fursa ya kutimiza uwezo wao wote wakiwa Marekani.
Uzima wa mwili na hisia, pamoja na kupata huduma za afya, ni
muhimu katika kufanikiwa kuanza maisha upya nchini Marekani. USCRI
ina mpango wa Msaada wa Matibabu kwa Wakimbizi (RMA) kwa
wageni ambao kwa sababu ya hali yao ya uhamiaji hawastahiki katika
mipango mingine ya Medicaid. RMA ina manufaa sawa ya matibabu
ya kawaida, meno na dawa kama ilivyo Medicaid. Mwongozi huu
unakupa maelezo ya jinsi ya kupata manufaa ya mpango wa RMA.
Manufaa ya RMA yanasimamiwa na Point Comfort Underwriters, Inc. (PCU).
Msaada wa Matibabu kwa Wakimbizi
Je, ninastahiki kupata Msaada wa Matibabu kwa Wakimbizi (RMA)? Ili ufahamu kama unastahiki kupata RMA, ni
sharti ujaze ombi la kujiunga na RMA.
Msimamizi wa shauri katika shirika
linalowapa wakimbizi makazi mapya mahali
ulipo anaweza akakusaidia kutuma ombi.
Kwa ujumla, ikiwa umetimiza vigezo
vifuatavyo, basi unastahiki:
1. Wewe ni mkimbizi au kikundi kingine
kinachostahiki.
2. Una hati zinazotakiwa za utambulisho
kwa wahamiaji.
3. Unatimiza kima kilichowekwa cha mapato
na rasilimali.
4. Huna hadhi ya kujiunga na mpango wa
Medicaid, Mpango wa Bima ya Watoto
au bima nyingine yoyote ya umma au ya
binafsi.
3
Je, ninaweza kupata ulinzi kwa muda gani chini ya RMA? Manufaa yako ya RMA huisha moja kwa moja
baada ya miezi 8 tangu unapowasili Marekani,
isipokuwa kama wewe ni mkimbizi ambaye
hajatimiza utu uzima na huna watu wazima walio
nawe (URM). Ikiwa wewe ni mkimbizi ambaye
hajatimiza utu uzima na huna watu wazima (URM),
unaweza kupata manufaa ya RMA mpaka
unapofika miaka 23. Zungumza na msimamizi wa
shauri lako katika shirika linalowapa wakimbizi
makazi mapya mahali ulipo ili akupe maelezo zaidi
kuhusu hali yako.
Kumbuka kwamba ukihama jimbo la Missouri,
manufaa yako ya RMA huisha mara moja.
Utatakiwa utume ombi la kupata manufaa ya
matibabu katika jimbo lako jipya.
KADI YA UTAMBULISHO WA RMA
Kadi ya Utambulisho wa RMA ni nini? Watu wote wanaosajiliwa kwenye mpango wa RMA
hupokea vitambulisho vyao binafsi vya RMA.
Unaweza ukapata kitambulisho chako kutoka kwa
wakala wa kuwapa wakimbizi makazi mapya mahali
ulipo. Pia unaweza kuomba kadi yako ya kitambulisho
cha RMA kutoka kwa PCU. Piga simu kwa PCU au
uwatumie barua pepe [email protected].
Kitambulisho chako cha RMA kina jina lako, namba
yako ya utambulisho na taarifa nyingine kuhusu
manufaa ya RMA. Ni muhimu kuwasilisha Kitambulisho
chako cha RMA kila wakati unapopata huduma. Ikiwa
zaidi ya jamaa mmoja kwenye familia yako
amesajliwa kwenye RMA, basi kila mmoja wao
atapata kitambulisho chake tofauti. Mtu ambaye jina
lake limeandikwa kwenye kadi ndiye pekee
anayeweza kuitumia. Usiazime wala kumpa mtu
mwingine kitambulisho chako.
Je, nitumie vipi kadi yangu ya utambulisho wa RMA? Unafaa kuwa na kitambulisho chako cha RMA kila wakati. Wasilisha kadi yako kwa daktari,
hospitali, daktari wa meno au
duka la dawa kila wakati unapotaka
kuhudumiwa. Wanaokupa huduma watatumia
kitambulisho chako kuthibitisha ustahiki wako
kupata manufaa ya RMA na kupata taarifa
muhimu kuhusu atakayetozwa kulipia huduma
unazopokea. Kukosa kuwasilisha kitambulisho
chako kunaweza kuchelewesha madai ya malipo
na unaweza pia kukosa manufaa yako.
Itakuwaje nikipoteza kitambulisho changu cha RMA? Unaweza ukapata kitambulisho kingine kutoka kwa PCU. Unachotakiwa kufanya ni kuwasiliana
na PCU kupitia [email protected].
Huenda ukaomba kutoa taarifa za binafsi ili PCU
ithibitishe kwamba ni wewe kabla kukupa kadi
mpa ya utambulisho.
4
5
HUDUMA ZA AFYA
Je, ninaweza kutumia watoa huduma gani wa afya? Unaweza ukatumia mtoa huduma yeyote wa afya
ambaye anakubali malipo yanayolingana na
viwango vya Medicaid. Unaweza ukapata orodha
ya watoa huduma ambao wamekubali viwango
hivyo hapa rma.pointcomfort.com, au upige simu
kwa PCU ili upate usaidizi. Ikiwa ungependa
kupata huduma za mtoa huduma ambaye
hajaorodheshwa hapa, unatakiwa kufanya hivi:
1. Pata jina kamili, anwani na namba ya simu ya
mtoa huduma ambaye ungependa kupata
huduma zake.
2. Wasilisha taarifa hizo kwa PCU.
PCU itawasiliana na mtoa huduma huyo kwa lengo la kumtaka akubali kutoa huduma kwa viwango vya
malipo vilivyowekwa. PCU itakufahamisha kuhusu
matokeo ya mazungumzo hayo.
Kumbuka, unafaa kwenda kwenye Kituo cha Dharura
kilicho karibu kabisa na wewe wakati wa dharura.
Je, ni huduma zipi za matibabu zinagharimiwa? RMA hugharimia huduma nyingi za matibabu ikiwa huduma hizo ni muhimu kwa afya na
hazipiti kiwango fulani cha malipo kilichowekwa.
Baadhi ya huduma zinazolipiwa ni pamoja na:
HUDUMA ZA HOSPITALI • Malipo ya huduma za kila siku na malazi
pamoja na huduma za uuguzi katika
chumba cha wagonjwa wachache au wadi
• Malipo ya huduma za kila siku na malazi
pamoja na uuguzi katika Kitengo cha
Uangalizi Maalum (ICU)
• Utumiaji wa vyumba vya upasuaji, matibabu
na kupata nafuu
• Vifaa vya kufunga au kushonea vidonda,
pamoja na vitu vingine ambavyo hupewa
wagonjwa ambao hawajalazwa
• Matibabu ya Dharura (lazima iwe dharura)
• Dawa unazoandikiwa ukiwa umelazwa
• Huduma za rediolojia, maabara na tiba kwa
kutegemea mawimbi ya sauti
• Matibabu ya Viungo, Tiba kwa Vitendo na matibabu ya Kunena wakati wa kulazwa
• Huduma za kitaalamu zikiwemo za madaktari
HUDUMA ZA KUTIBIWA NA KUONDOKA
HOSPITALINI/UPASUAJI NA KUONDOKA • Huduma za kitaalamu zikiwemo za madaktari
• Vifaa vya kufunga au kushonea vidonda,
pamoja na vitu vingine ambavyo hupewa
wagonjwa ambao hawajalazwa
KUWAONA MADAKTARI NA KWENDA KLINIKI • Madaktari na wataalamu
• Matibabu ya Viungo, Tiba kwa Vitendo na
matibabu ya Kunena wakati wa kulazwa
• Wataalamu wa Tabia/Afya ya Akili walio na kibali
• Huduma za rediolojia, maabara na tiba kwa
kutegemea mawimbi ya sauti
HUDUMA NYINGINE ZINAZOGHARIMIWA • Usafiri wa ambulensi kwa dharura mahali unapoishi
• Zana za kudumu za kimatibabu
• Huduma za afya nyumbani
• Huduma za faraja
• Matibabu ya mionzi
• Tibakemikali
• Usafishaji damu kwa mashine ya figo
• Huduma za oksijeni na gesi nyinginezo
• Huduma za nusu kaputi
• Ukaguzi 1 wa Macho na kupewa miwani 1
http://rma.pointcomfort.com/
Ni huduma zipi za afya hazigharimiwi? • Gharama za ujauzito na watoto wachanga
• Bidhaa za binafsi zisizo za lazima
• Kupata ushauri kwa njia ya simu au kukosa kuhudhuria agizo la lililowekwa
• Mabadiliko yoyote yanayofanywa
kwenye mwili ili kuboresha mwonekano,
au kuliwaza akili au mawazo
• Mipango ya mazoezi, iwe
imependekezwa na daktari au la
• Upasuaji wa urembo au usio wa kimatibabu
• Matibabu ya utasa, ugumba au nguvu za kufanya mapenzi
• Huduma au dawa ambazo ni za
uchunguzi, majaribio au za utafiti
• Upasuaji wa macho ili kurekebisha
tatizo la kutoona karibu au mbali au
makengeza
• Matibabu ya mrejesho wa kiasili, tiba burudani,
tiba usingizi au tiba muziki
• Huduma au bidhaa unazopewa na mtu wa ukoo wako au mtu yeyote anayeishi na wewe
• Huduma au bidhaa unazopewa bila malipo
• Ada za kusafiri au malazi
• Matibabu ya kukuza nywele, iwe umeandikiwa na daktari au la
• Matibabu ya kuzuia upara
• Matibabu ya matatizo ya usingizi
• Huduma au bidhaa yoyote
ambayo Si ya Lazima Kimatibabu
• Huduma au bidhaa nyingine ambazo
manufaa au malipo yake unaweza kuyapata
chini ya mkataba au bima nyingine
• Tiba ya kurekebisha maungo
• Tiba maalum ya miguu
• Kujidhibiti kisukari
• Huduma za afya nyumbani
• Huduma za kurejesha hali ya ukawaida nje ya hospitali
• Usaidizi wa tabibu
6
DAWA ZA KUANDIKIWA
Ninaweza kutumia maduka
gani ya dawa? Unaweza kupata dawa unazoandikiwa na daktari kupitia mtandao wa maduka ya dawa ya MagellanRx
Management. Mtandao huo unajumuisha maduka
makuu kama vile Walmart na CVS pamoja na
maduka na wauzaji wengine wa mahali ulipo. Ni
sharti uwasilishe kitambulisho chako kwa mfamasia kila
wakati unapotaka dawa uliyoandikiwa. Mfamasia
atathibitisha kwamba wapo kwenye mtandao huo na
kwamba unastahiki kupata dawa unazoandikiwa.
Ni dawa zipi za kuandikiwa na daktari hazigharimiwi? • Dawa asili wakati kibadala chake kipo
• Dawa yoyote unayoandikiwa lakini ni ya
huduma ya afya isiyogharimiwa
• Dawa unazoweza kununua bila kuandikiwa na
daktari
• Unaweza kupata dawa za hadi siku 30
MATIBABU YA MENO
Ninaweza kutibiwa na daktari yupi wa meno? Unaweza ukatibiwa na daktari yeyote wa meno aliye
katika mtandao wa DenteMax Unaweza ukapata
orodha ya madaktari walio katika DenteMax kwenye
www.dentemax.com/findadentist, au kwa kuwasiliana
na PCU. Madaktari walio katika mtandao wa DenteMax
pekee ndio walio na kibali cha kutoa tiba ya meno chini
ya RMA. Ni shaeri uwasilsihe kitambulsiho chako cha RMA
kwa daktari wa meno kila wakati unapotaka matibabu ya
meno.
Ni matibabu gani ya meno yanagharimiwi? • Matibabu ya dharura ya meno
yanayolenga kumaliza maumivu au
kuzuia maambukizi
• Matibabu ya dharura ya meno
yanayotokana na ajali
• Matibabu 1 ya kawaida ya meno ikiwemo
eksirei
• Kung'oa meno, kujaza, tiba ya fizi pamoja na eksirei, upasuaji na nusu kaputi husika.
Si lazima kuwe na thibitisho la awali kwa
matibabu ya dharura.
RMA hugharimia matibabu mengi ya meno ikiwa matibabu hayo ni muhimu kwa afya na
hayapiti kima fulani cha malipo. Hii ni orodha ya
baadhi tu ya huduma zinazogharimiwa.
Wasiliana na PCU kwa maelezo zaidi.
7
http://www.dentemax.com/findadentist
8
KIBALI CHA AWALI
Je, ni huduma zipi sharti ziwe na kibali cha awali? Huduma nyingi zinazogharimiwa sharti zipate kibali cha awali. Hii ina maana kwamba sharti upate
idhini ya PCU kabla ya kutibiwa. Matibabu
yafuatayo lazima yapate kibali cha awali:
• Huduma za kulazwa
• Upasuaji wowote
• Huduma katika kituo cha huduma za muda mrefu
• Huduma za faraja
• Huduma za afya nyumbani
• Tiba ya kurekebisha maungo
• Tiba ya viungo
• Matibabu kwa vitendo
• Matibabu ya kunena
• Kupima mzio
• Zana za kudumu za kimatibabu
• Tiba ya Akili/Tabia
• Miguu/mikono bandia
• Huduma za viungo saidizi
• Upimaji kwa kutumia kompyuta (CAT Scan)
• Upigaji picha kwa nguvu ya sumaku (MRI)
• Upachukaji wa Viungo/Tishu
Nifanyeje ili nipate Kibali cha Awali? Mara tu anapojua kwamba utaenda kutafuta huduma inayohitaji Kibali cha Awali, unatakiwa uwasiliane na
PCU kupitia [email protected] au kwa
simu. Utatakiwa utaje jina lako, namba yako
kitambulisho, jina la mhudumu ambaye unapanga
kumtembelea, anwani yake na maelezo ya matibabu
unayopanga kupokea. Mara nyingi PCU hutoa kibali
cha awali mara moja; hata hivyo kuna nyakati
ambapo kupata cheti upya huchukua hadi saa 48 ili
kukamilika. Ndiyo maana ni muhimu uwasiliane na PCU
mara tu unapojua kwamba utaenda kutibiwa.
Si lazima upate Kibali cha Awali kwa matibabu ya
dharura; hata hivyo ni sharti utoe taarifa haraka
iwezekanavyo.
Kwa kawaida, anayekupa huduma atakuanzishia
mchakato wa kupata Kibali cha Awali. Atahijati
maelezo yaliyo kwenye kitambulisho chako cha
RMA.
Unafaa kuwasilisha kitambulisho chako cha RMA
kila wakati unapotafuta huduma.
Itakuwaje nikitibiwa bila kupata Kibali cha Awali? Ikiwa umepokea matibabu yaliyotaka upate Kibali cha Awali lakini ulikosa kutoa taarifa, basi
gharama ya matibabu hayo yatakuwa yako.
mailto:[email protected]
9
KUKATA RUFAA
Itakuwaje nisipokubaliana na uamuzi wa Kibali cha Awali au kuhusu madai? Unatakiwa uanze mchakato wa Kukata Rufaa mara moja kwa kufuata hatua hizi:
1. Piga simu au uwaandikie PCU ukiwapa
maelezo kamili kuhusu rufaa yako ndani ya
siku 30 tangu siku ulipoomba Kibali cha
Awali au siku ambapo uliambiwa kwamba
utagharimia matibabu yako. Ni sharti
ujumuishe majina na maelezo ya
mawasiliano ya wahudumu wote
waliohusika.
2. Ndani ya siku 10, PCU itathibitisha kwamba
imepokea rufaa yako na kuweka muda
wa kukamilisha uchunguzi wowote
unaotakikana.
3. Ndani ya siku 30, PCU itakupa majibu
kwa maandishi kuhusu maamuzi juu ya
rufaa uliyokata.
FARAGHA
Kila wakati unapotibiwa, daktari wako huandika kilichofanyika na kuiweka kwenye faili yako. Faili
hii huwekwa siri. Daktari wako anaweza kuwapa
watu wengine faili hiyo ikiwa utakubali.
PCU inatakiwa iweke faragha taarifa zinazohusu
huduma za matibabu unazopokea kwa. PCU
inaweza tu kuwapa watu wengine taarifa zako
ikiwa utakubali.
Una haki ya kupokea nakala za rekodi zako za
matibabu kutoka kwa watoa huduma na PCU.
Unaweza ukaomba marekebisho yafanywe
kwenye rekodi zako ikiwa kuna jambo lisilo sahihi.
Unaweza ukatakiwa kumlipa mtoa huduma au
PCU ada za kunakili rekodi unazotaka.
10
ANWANI ZA HUDUMA ZAKO ZA RMA
Maswali kuhusu ustahiki au manufaa: [email protected] 1-844-210-2010
Maswali kuhusu mitandao ya watoa huduma: Matibabu ya Kawaida na Meno
[email protected] 1-844-210-2010 rma.pointcomfort.com
Dawa za Kuandikiwa na Daktari:
[email protected] 1-800-424-0472
Kubali cha Awali: [email protected] 1-844-210-2010 rma.pointcomfort.com
Hali ya Dai: [email protected] 1-844-210-2010 claims.pointcomfort.com
Kukata Rufaa: [email protected] 1-844-210-2010
MASHIRIKA YA KUWAPA WAKIMBIZI MAKAZI MAPYA
Usimamizi wa RMA:
USCRI Missouri
3401 Arsenal
St Louis, MO 63118
Mashirika ya kuwapa
wakimbizi makazi mapya:
International Institute of Saint Louis
3401 Arsenal
Saint Louis, MO 63118
(314) 773-9090
International Institute –
Southwest Missouri
334 East Commercial Street #212
Springfield, MO 65804
(417) 720-1552
Jewish Vocational Service
4600 Paseo Blvd
Kansas City, MO 54110
(816) 471-2808
Della Lamb Community Services
500 Woodland Ave
Kansas City, MO 64106
(816) 842-8040
Catholic Charities of Central and
Northern MO
201 W Broadway, Bldg. 3
Suite G Columbia, MO 65203
(573) 442-7568
11
mailto:[email protected]:[email protected]://rma.pointcomfort.com/mailto:[email protected]:[email protected]://rma.pointcomfort.com/mailto:[email protected]://claims.pointcomfort.com/mailto:[email protected]
®
Kampuni ya Unified Administrators, LLC