17
M W O N G O Z O W A U Z A L I S H A J I W A M B E G U Z A D A R A J A L A K U A Z I M I W A U B O R A ( Q u a l i t y D e c l a r e d S e e d s ) KITINI NAMBA 7: November, 2019

MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA DARAJA ......Mzalishaji anashauriwa kuzalisha mbegu wakati wa mvua za msimu. Kwa mfano, mbaazi za muda mfupi hustawi zaidi ukanda wa chini na ni

  • Upload
    others

  • View
    16

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA DARAJA ......Mzalishaji anashauriwa kuzalisha mbegu wakati wa mvua za msimu. Kwa mfano, mbaazi za muda mfupi hustawi zaidi ukanda wa chini na ni

MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA DARAJA LA KUAZIMIWA UBORA

(Quality Declared Seeds)

KITINI NAMBA 7:

November, 2019

Page 2: MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA DARAJA ......Mzalishaji anashauriwa kuzalisha mbegu wakati wa mvua za msimu. Kwa mfano, mbaazi za muda mfupi hustawi zaidi ukanda wa chini na ni
Page 3: MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA DARAJA ......Mzalishaji anashauriwa kuzalisha mbegu wakati wa mvua za msimu. Kwa mfano, mbaazi za muda mfupi hustawi zaidi ukanda wa chini na ni

2

YALIYOMO 1.0 UTANGULIZI .................................................................................................................................................... 3

1.1 Mbegu za daraja la kuazimiwa ubora ............................................................................................... 3

2.0 UZALISHAJI WA MBEGU BORA ZA JAMII YA MIKUNDE, MAFUTA NA NAFAKA .......... 3

2.1. Sifa za ziada katika uzalishaji mbegu ............................................................................................ 4

2.2. Utenganisho wa shamba .......................................................................................................................... 4

3.0. UTAYARISHAJI WA SHAMBA ................................................................................................................ 5

4.0. CHANZO CHA MBEGU .............................................................................................................................. 5

5.0. UPANDAJI ....................................................................................................................................................... 6

5.1. Wakati wa kupanda ..................................................................................................................................... 6

5.2. Kiasi cha mbegu ...................................................................................................................................... 6

5.3. Nafasi ya kupanda .................................................................................................................................. 7

5.4. Matumizi ya mbolea .............................................................................................................................. 7

6.0. KUSAJILI SHAMBA LA MBEGU ............................................................................................................. 8

7.0. UDHIBITI WA WADUDU /WANYAMA WAHARIBIFU NA MAGONJWA ............................ 8

8.0. UKAGUZI WA SHAMBA LA MBEGU .................................................................................................. 12

9.0. UVUNAJI NA UHIFADHI WA MBEGU ............................................................................................... 12

9.1. Kupima ubora wa mbegu ......................................................................................................................... 12

9.2. Kufungasha na kuweka nembo yenye taarifa za mbegu ......................................................... 13

MBINU MUHIMU ZILIZOFUNDISHWA KATIKA SOMO HILI: .........................................................14

Page 4: MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA DARAJA ......Mzalishaji anashauriwa kuzalisha mbegu wakati wa mvua za msimu. Kwa mfano, mbaazi za muda mfupi hustawi zaidi ukanda wa chini na ni

3

1.0 UTANGULIZI

1.1 Mbegu za daraja la kuazimiwa ubora

Mbegu ni sehem ya mmea ambayo hutumika kuzalisha/kuotesha mmea mwingine, yaweza

kuwa ni zao la ua au sehem ya mmea iliyokomaa na kuwa tayari kuendelea kuoteshwa tena,

mfano vipando vya muhogo

Mbegu ni mojawapo ya pembejeo muhimu katika kilimo. Mbegu za daraja la kuazimiwa ubora

(QDS) ni mojawapo wa vyanzo bora vya mbegu vya kutegemewa na wakulima. Mfumo wa

uzalishaji wa mbegu bora za kuazimiwa ubora ulianzishwa na shirika la kilimo na chakula

duniani (FAO) mwaka 1993 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2006.

Mbegu hizi ziliingizwa kwenye mfumo rasmi wa kuzalisha mbegu katika sheria ya mbegu ya

mwaka 2003, pamoja na kanuni, miongozo na taratibu zake za uzalishaji za mwaka 2007. Mbegu

hizi huzalishwa na mkulima mmoja mmoja au kikundi cha wakulima kilichosajiliwa na kupata

mafunzo kwa ajili ya kuzalisha mbegu kwa matumizi yao binafsi na/au kuuza kwa wakulima wa

maeneo ya jirani. Ni muhimu nasaba/asili ya mbegu hiyo ijulikane na hivyo mbegu ya msingi au

iliyothibitishwa kuwa ndizo pekee zinazotumika katika uzalishaji ili kuhakikisha ubora wa

mbegu.

Hapa nchini mbegu zilizopevushwa kiasili (OPV) ambazo zinapatikana katika orodha ya taifa ya

mimea ndizo zinazoweza kutumika katika uzalishaji wa mbegu za daraja la kuazimiwa ubora na

siyo mbegu za kizazi cha kwanza cha mbegu chotara (F1 Hybrids). Mfumo wa mbegu za daraja la

kuazimiwa ubora huwawezesha wakulima kupata mbegu bora kwa gharama nafuu na kwa

wakati. Mfumo huu wa QDS upo si kwa nia ya kuubadili mfumo rasmi wa uzalishaji mbegu

zilizothibitishwa ubora ila kujaza pengo lililoachwa na mfumo rasmi. Ni mfumo unaowahusu

wakulima wadogo wadogo walio kwenye vikundi kwa matumizi yao ndani ya wilaya husika.

2.0 UZALISHAJI WA MBEGU BORA ZA JAMII YA MIKUNDE, MAFUTA NA NAFAKA

Mbegu za jamii ya kunde, mafuta na nafaka zinatumiwa na wakulima wengi kwa ajili ya kuzalisha

chakula kwa matumizi ya binadamu na mifugo. Mbegu hizi hustawi kwenye udongo wa aina

tofauti kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali.

Page 5: MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA DARAJA ......Mzalishaji anashauriwa kuzalisha mbegu wakati wa mvua za msimu. Kwa mfano, mbaazi za muda mfupi hustawi zaidi ukanda wa chini na ni

4

Jedwali 1: Aina ya udongo unaofaa

Aina ya mbegu Udongo unaofaa

Mbaazi Udongo wa aina mbalimbali kuanzia ule wenye mchanganyiko wa

kichanga na tifutifu na mfinyanzi na tifutifu. Lakini hufanya vizuri

zaidi kwenye udongo wa tifutifu

Alizeti Udongo wa aina mbalimbali lakini hukua vizuri zaidi kwenye

udongo wa tifutifu usiotuamisha maji

Mahindi Udongo wa tifutifu usiotuamisha maji

Choroko Udongo wa tifutifu usiotuamisha maji

Mpunga Udongo wa tifutifu nchi kavu na mabondeni

Kunde Udongo wa aina mbalimbali pia huweza kustawi vizuri kwenye

udongo wa kichanga

Maharage Udongo wa tifutifu usiotuamisha maji

Angalizo: Epuka kupanda mbegu za aina tofauti kwa misimu miwili inayofuatana

2.1. Sifa za ziada katika uzalishaji mbegu

Inashauriwa kuwa shamba la kuzalisha mbegu liwe msimu uliopita halikulimwa mbegu husika

ili kuepuka magonjwa yanayoweza kutokea.

2.2. Utenganisho wa shamba

Utenganisho wa mashamba ya mbegu unafanywa ili kuzuia vyanzo vyote vinavyoweza kuchafua

mbegu wakati wa kukua. Inahakikisha kwamba uchavushaji mtambuka (cross pollination) wa

chavua (pollen) kutoka kwenye aina nyingine za mimea au kutoka kwenye mimea ya daraja duni

na dhoofu hautokei. Pia inahakikisha kuwa hakuna uchanganyikaji wa mbegu wakati wa kuvuna

au uambukizi wa wadudu kutoka kwa mazao sawa au mazao mbadala.

Kuna aina kuu mbili za utenganisho wa shamba.

a. Utenganisho wa umbali

Shamba la mbegu linatakiwa kutengwa kutoka shamba lingine la aina hiyo hiyo ya mbegu kwa

umbali uliopendekezwa kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali lifuatalo:

Page 6: MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA DARAJA ......Mzalishaji anashauriwa kuzalisha mbegu wakati wa mvua za msimu. Kwa mfano, mbaazi za muda mfupi hustawi zaidi ukanda wa chini na ni

5

Jedwali 2: Utenganisho wa umbali wa shamba

Aina ya zao Utenganisho wa umbali kwa kila daraja la mbegu (mita)

Msingi Certified 1 Certified 2 QDS

Mahindi (OPV) 400 200 200 190

Maize (chotara) 400 200 200 190

Mtama 400 200 200 100

Uwele 300 300 300 100

Mpunga 5 5 5 3

Choroko 20 20 20 20

Karanga 3 3 3 3

Maharage 10 10 10 10

Kunde 5 5 5 5

Mbaazi 50 50 50 50

Alizeti 200 200 200 200

b. Utenganisho kwa kutumia nyakati

Uchafuzi unaweza kudhibitiwa kwa kupanda mimea/mbegu kwa nyakati tofauti. Hii inaweza

kuzuia utoaji wa maua na uchavushaji kwa wakati mmoja.

Zingatia

Epuka kulima mbegu zilizotajwa hapo juu kwenye mabonde yenye kutuamisha maji.

3.0. UTAYARISHAJI WA SHAMBA

Tayarisha shamba mapema ili kutoa nafasi ya manyasi kuoza na hatimaye kuongeza mboji

kwenye udongo. Kama shamba linalotumika ni la zamani hakikisha limetifuliwa vizuri kwa

kutumia aidha wanyama kazi, jembe la mkono au trekta na mabonge ya udongo yapigwe ili

kupata udongo laini. Kama shamba linalotumika ni jipya, hakikisha kuwa visiki na mawe

yameondolewa ili kuwezesha matumizi ya trekta na wanyama kazi katika uandaaji wa shamba.

4.0. CHANZO CHA MBEGU

Mbegu zitakazotumika katika uzalishaji zisiwe chotara. Mkulima atumie mbegu ya daraja la

msingi, au kuthibitishwa ama QDS 1. Mbegu ya msingi na iliyothibitishwa hupatikana katika

mashamba ya wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seed Agency - ASA). Vilevile mbegu za

Page 7: MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA DARAJA ......Mzalishaji anashauriwa kuzalisha mbegu wakati wa mvua za msimu. Kwa mfano, mbaazi za muda mfupi hustawi zaidi ukanda wa chini na ni

6

daraja la kuthibitishwa hupatikana katika makampuni ya mbegu, kupitia kwa wakala wao au

maduka ya pembejeo.

Mkulima anaruhusiwa kutumia mbegu ya QDS 1 iliyopatikana kutoka kwa mkulima wa mbegu

aliyesajiliwa na TOSCI, kama chanzo cha mbegu, lakini ajue ya kwamba, akishavuna hawezi

kuitumia kama mbegu tena.

Baadhi ya aina ya mbegu zinazopendekezwa na Wizara ya Kilimo ni kama zilizoonyeshwa

kwenye jedwali lifuatalo:

Jedwali 3: baadhi ya aina za mbegu zinazopendekezwa

Zao Baadhi ya mbegu zinazopendekezwa

Mahindi Kilima, staha, Katumani, Kito, Cholima 1, Lishe K1, Stuka- 2

Alizeti Rekodi

Karanga Mnanje, Red mwitunde, Nyota, Johari, Pendo 98, Sawia 98

Mbaazi Komboa, Mali, Tumia

Choroko Nuru, Imara

Kunde Tumaini, Fahari, Vuli -1, vuli - 2

Maharage Kabanima, Uyole 84, Uyole 90, Uyole 98, Seliani 90, Seliani

97, Jesca, Wanji

Angalizo

Kwa mkulima anayeanza kuzalisha mbegu, anashauriwa kutumia mbegu ya daraja la msingi.

5.0. UPANDAJI

5.1. Wakati wa kupanda

Mzalishaji anashauriwa kuzalisha mbegu wakati wa mvua za msimu. Kwa mfano, mbaazi za

muda mfupi hustawi zaidi ukanda wa chini na ni vyema zikapandwa mwishoni mwa mwezi wa

Februari kwani hukomaa katika muda wa siku 120.

5.2. Kiasi cha mbegu

Kiasi cha mbegu kwa ekari moja hutegemea aina ya mbegu kama inavyoonyeshwa kwenye

jedwali lifuatalo:

Page 8: MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA DARAJA ......Mzalishaji anashauriwa kuzalisha mbegu wakati wa mvua za msimu. Kwa mfano, mbaazi za muda mfupi hustawi zaidi ukanda wa chini na ni

7

Jedwali 4: Kiasi cha mbegu kwa ekari

Aina ya mbegu Kiasi kwa ekari moja (kg)

Mbaazi Muda mrefu 2

Muda mfupi 3

Alizeti 6

Mahindi 8-10

Choroko 8-10

Kunde 6 - 10

Maharage 10

5.3. Nafasi ya kupanda

Panda mbegu kwa kuzingatia nafasi iliyopendekezwa kati ya mche na mche na kati ya mstari na

mstari kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali lifuatalo:

Jedwali 5: Nafasi inayopendekezwa ya upandaji

Aina ya mbegu Utenganisho

kati ya mstari

na mstari (cm)

Utenganisho kati

ya mche na mche

(cm)

Kina (cm)

Mbaazi 20 50 5

Alizeti 90 25 4 - 6

75 30 4 - 6

Mahindi 75 30 4 – 5

75 60 4 - 5

Choroko 50 10 4 - 5

Karanga 50 10 2.5 - 5

50 15 2.5 - 5

Kunde 75 20 3 – 4

Maharage 50 15-20 2.5 - 3

5.4. Matumizi ya mbolea

Wakati wa kupanda mkulima anashauriwa kutumia mbolea mboji/vunde na/au samadi

kulingana na rutuba ya udongo iliyopo kwenye eneo husika. Mkulima azingatie ushauri wa

wataalam kuhusu matumizi ya mbolea zinazopendekezwa katika kilimo ikolojia.

Page 9: MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA DARAJA ......Mzalishaji anashauriwa kuzalisha mbegu wakati wa mvua za msimu. Kwa mfano, mbaazi za muda mfupi hustawi zaidi ukanda wa chini na ni

8

6.0. KUSAJILI SHAMBA LA MBEGU

Mzalishaji wa mbegu analazimika kusajili shamba lake kwenye Taasisi ya Udhibiti wa ubora wa

mbegu (TOSCI) muda usiozidi siku 30 baada ya kupanda. Uasjili hufanyika katika vituo vya

Morogoro, Mwanza, Njombe, Arusha na sasa Mtwara. Usajili unatoa nafasi kwa Taasisi kupanga

utaratibu wa ukaguzi.

Kung’oa mimea isiyofaa

Hakikisha kuwa shamba lako linabaki safi wakati wote. Ondoa mimea yote ambayo ina

magonjwa, mimea iliyoharibiwa na wadudu. Kwenye alizeti ondoa mimea yenye vichwa vingi.

Zingatia: Shughuli ya kuondoa mimea isiyofaa ifanyike kwa kushirikiana na afisa ugani aliye

karibu.

7.0. UDHIBITI WA WADUDU /WANYAMA WAHARIBIFU NA MAGONJWA

Baadhi ya wadudu waharibifu wanaoshambulia mbegu zikiwa shambani na namna ya

kuwadhibiti ni kama ilivyoonyeshwa katika jedwali lifuatalo.

Jedwali 6: Baadhi ya wadudu wanaoshambulia mimea na udhibiti wake

Zao Mdudu anayeshambulia Udhibiti

Mbaazi Pod borer, spotted pod borer, podfly,

plumemoth, blue butterfly, pod bug na

blister beetles

Tifua ardhi kwa kina kipindi cha

kiangazi ili kuwaibua wadudu

funza wa wadudu waliojificha

ardhini. Tumia kilimo

mchanganyiko cha

mtama/mahindi. Weka mitego ya

limbwata (pheromone traps) na

pulizia dawa za asili. Kuwaua

blister beetle kwa kutumia mitego

na/au kuwakamata na

kuwaharibu.

Alizeti Sunflower Beetles (Mbawa kau wa

alizeti)

Funza wakatao miche, panzi, minyoo

ya ardhini (cutworms) na funza wa

vitumba (sunflower borers)

Hakikisha shamba linakuwa safi

wakati wote kabla na baada ya

kupanda. Pulizia dawa za asili kwa

mchanganyiko maalum kama

ilivyoelekezwa na wataalam wa

Page 10: MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA DARAJA ......Mzalishaji anashauriwa kuzalisha mbegu wakati wa mvua za msimu. Kwa mfano, mbaazi za muda mfupi hustawi zaidi ukanda wa chini na ni

9

kilimo ikolojia kama vile

mwarobaini, pilipili za kuwasha,

majivu, maziwa mabichi, majani

ya mpapai n.k.

Mahindi Maize stalk boarer Ili kudhibiti bungua, tumia mfumo

wa kilimo wa fanya juu fanya chini

(push-pull) kwa kupanda mstari

mmoja wa majani jamii ya

mikunde ya Desmodium

(silverleaf au greenleaf) kila baada

ya mistari mitatu ya mahindi. Pia

panda mistari isiyopungua mitatu

ya Napier grass katika ukingo wa

shamba. Desmodium inatoa

harufu ya kuwafukuza wadudu na

Napier inatoa ute mzito ambao

hunasa larvae na kufa.

Unga wa mwarobaini

Choroko 1) Wadudu wanaoshambulia mabua

(stem feeders)

(2) Wadudu wanaoshambulia majani

(foliage feeders: leaf folder,

caterpillars)

(3) Wadudu wanoshambulia mbegu

(pod feeders)

Matumizi ya mbegu bora

zinazotoa ukidhani dhidi ya

mashambulizi ya wadudu.

Kurekebisha tarehe za kupanda,

matumizi ya aina ya sugu na

kupanda mazao mchanganyiko

(choroko na mahindi) au mazao ya

mtego yanaweza kufuatiwa

kulingana na upatikanaji na

ufanisi katika eneo fulani.

Kutengeneza mandhari ya

shamba (farmscaping) ambayo ni

mbinu ya kiikolojia ya usimamizi

wa wadudu; ikiwa ni pamoja na

matumizi ya safu za miti

Page 11: MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA DARAJA ......Mzalishaji anashauriwa kuzalisha mbegu wakati wa mvua za msimu. Kwa mfano, mbaazi za muda mfupi hustawi zaidi ukanda wa chini na ni

10

zinazofanya ua (hedgerows),

mimea ya wadudu, mazao

yanayofukina ardhi, na mabwawa

ya maji ili kuvutia na kusaidia

viumbe wenye manufaa kama vile

wadudu, popo na ndege wa

mawindo.

Karanga Vidukari (mafuta) Dhibiti kwa kupanda mapema na

kwa nafasi iliyopendekezwa.

Tumia dawa za asili za utupa,

pilipili, mwarobaini n.k.

Inzi wa karanga Panda mapema na pia pilizia dawa

za asili za utupa, pilipili,

mwarobaini n.k.

Mchwa Bomoa vichuguu ambavyo ni

mazalia ya mchwa.

Kunde Aphids/vidudu mafuta Panda aina za mbegu zinazotoa

ukinzani dhidi ya wadudu hao.

Shamba liwe safi lisiwe nan a

magugu na vichuguu vya mchwa.

Pia fanya kilimo mzunguko,

badilisha tarehe za upandaji,

mitego ya wadudu.

Maharage Foliage beetles, flower thrips, pollen

beetles, pod borers, pod bugs, and sap

suckers kama vile aphids

Wadudu hawa wanaweza

kudhibitiwa kwa kutumia mbinu

shirikishi (IPM) ambazo

zinahusisha: kupanda kwa wakati,

kilimo cha mazao mchanganyiko,

kilimo mzunguko.

Baadhi ya magonjwa yanayoshambulia mbegu ni kama yalivyoonyeshwa kwenye jedwali

lifuatalo.

Page 12: MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA DARAJA ......Mzalishaji anashauriwa kuzalisha mbegu wakati wa mvua za msimu. Kwa mfano, mbaazi za muda mfupi hustawi zaidi ukanda wa chini na ni

11

Jedwali 7: Baadhi ya magonjwa yanayoshambulia mimea na udhibiti wake

Zao Magonjwa Udhibiti

Mbaazi Mnyauko Ng’oa na kutupa nje ya shamba

Alizeti Madoa ya majani, kuoza

mizizi, kuvu ya majani

na ukoma

Tumia mbegu zilizothibitishwa ambazo

zinastahamili magonjwa

Mahindi Virusi vya milia (maize

streak vírus), Fugwe (

smut disease)

Ng’oa na kufukia mimea ilyoathirika. Tumia

viuatilifu vya asili kudhibiti wadudu.

Choroko Kuoza mizizi na majani,

kutu

Choma mimea iliyoathirika na ugonjwa.

Pulizia mafuta ya muarobaini.

Karanga Ugonjwa wa kuoza

(aflatoxin), , ukoma,

maganda matupu.

Zuia mikwaruzo wakati wa kuvuna, karanga

zikaushwe vizuri na kuhifadhiwa kwenye

magunia na siyo viroba katik sehemu isiyo

na unyevu.

Kuoza majani na kutu Kupanda mapema, kuondoa maotea, kilimo

cha mzunguko na kutumia mbegu

zinazostahimili magonjwa

Ukoma Panda mapema na kwa nafasi, palilia

mapema, ondoa maotea na panda mbegu

bora

Maganda matupu Ongeza virutubisho vya chokaa na tumia

mbegu za muda mfupi

Kunde Kuoza kunde (Cowpea

rot and damping),

Kukauka majani

(Southern blight) ,

unyaufu wa mmea

kuanzia majani ya chini

(cowpea mosaic vírus),

Mnyauko fusari/Ukoma

(cowpea fusarium wilt)

Kuondoa mimea iliyoathiriwa na virusi,

kudhibiti magugu na kupanda mbegu

zilizothibitishwa zinazotoa ukinzani dhidi ya

magonjwa.

Page 13: MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA DARAJA ......Mzalishaji anashauriwa kuzalisha mbegu wakati wa mvua za msimu. Kwa mfano, mbaazi za muda mfupi hustawi zaidi ukanda wa chini na ni

12

Maharage Chule (anthracnose),

baka jani (halo blight),

mnyauko bakteria

(bactérial wilt), unyaufu

wa mmea kuanzia

majani ya chini (bean

common mosaic virus)

Tumia mbegu zilizothibitishwa ambazo

hazina vimelea vya magonjwa

Ili kuepuka magonjwa haya mkulima anashauriwa kutumia mbegu zilizothibitishwa ambazo

zinastahimili magonjwa.

8.0. UKAGUZI WA SHAMBA LA MBEGU

Ili kuhakikisha kuwa taratibu zote zinazotakiwa kufuatwa kwa ajili ya kuzalisha mbegu

zimefuatwa shamba la mbegu ni lazima likaguliwe. Ukaguzi unafanywa na wataalam kutoka

taasisi ya kudhibiti ubora wa mbegu (TOSCI) na mkulima. Mkaguzi ataangalia kama utenganisho

wa umbali umezingatiwa. Pia ataangalia kama kuna mimea mingine ambao haitakiwi kuwepo

shambani, magonjwa na hali ya ujumla ya mazao. Kwa uchache ukaguzi utafanyika mara mbili

kabla ya mimea kutoa maua na kabla ya kuvuna.

9.0. UVUNAJI NA UHIFADHI WA MBEGU

Vuna kwa kuangalia dalili za kukomaa kwa mbegu.

Safisha mbegu kwa kuondoa uchafu, vumbi, mbegu zilizopasuka na mbegu zisizokomaa.

Mbegu ihifadhiwe sehemu iliyo safi, kavu na yenye mzunguko mzuri wa hewa.

Hakikisha kuwa vyombo vya kuhifadhia kama vile gunia zinapewa kitambulisho.

9.1. Kupima ubora wa mbegu

Kabla ya mbegu kuhurusiwa kuuzwa ni lazima ipimwe ubora wake kwa mfano; uotaji, usafi,

unyevu n.k. Upimaji unafanyika kwenye maabara ya mbegu katika Taasisi ya kudhibiti ubora wa

mbegu (TOSCI). Afisa wa TOSCI au wakala Wake huchukua sampuli ya mbegu na kuzipeleka

maabara ya mbegu ya TOSCI kwa ajili ya kuthibitisha ubora Wake.

Ubora wa mbegu

Mbegu ikithibitika kama ina ubora unaotakiwa inaweza kuuzwa.

Page 14: MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA DARAJA ......Mzalishaji anashauriwa kuzalisha mbegu wakati wa mvua za msimu. Kwa mfano, mbaazi za muda mfupi hustawi zaidi ukanda wa chini na ni

13

9.2. Kufungasha na kuweka nembo yenye taarifa za mbegu

Weka mbegu katika mifuko ya ujazo wa kilo 2, 5 na 10 kulingana na mahitaji ya mteja. Ikiwa

mbegu itabaki kwa kipindi kitakachozidi miezi sita ni lazima mbegu ichukuliwe sampuli nyingine

na kupelekwa TOSCI ili ikafanyiwe tena uchunguzi.

Page 15: MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA DARAJA ......Mzalishaji anashauriwa kuzalisha mbegu wakati wa mvua za msimu. Kwa mfano, mbaazi za muda mfupi hustawi zaidi ukanda wa chini na ni

14

MBINU MUHIMU ZILIZOFUNDISHWA KATIKA SOMO HILI:

1.1 Mbegu za daraja la kuazimiwa ubora

2. Uzalishaji Wa Mbegu Bora Za Jamii Ya Mikunde, Mafuta Na Nafaka

3. Sifa za ziada katika uzalishaji mbegu

4. Utenganisho wa shamba

5. Utayarishaji wa shamba

6. Chanzo cha mbegu

7. Upandaji

7.1 Kiasi cha mbegu

7.2 Aina ya mbegu

7.3 Kiasi kwa ekari moja (kg)

7.4 Nafasi ya kupanda

8. Kusajili shamba la mbegu

9. Udhibiti wa wadudu /wanyama waharibifu na magonjwa

10. Ukaguzi wa shamba la mbegu

11. Uvunaji na uhifadhi wa mbegu

12. Kupima ubora wa mbegu

13. Kufungasha na kuweka kitambulisho

Page 16: MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA DARAJA ......Mzalishaji anashauriwa kuzalisha mbegu wakati wa mvua za msimu. Kwa mfano, mbaazi za muda mfupi hustawi zaidi ukanda wa chini na ni
Page 17: MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA DARAJA ......Mzalishaji anashauriwa kuzalisha mbegu wakati wa mvua za msimu. Kwa mfano, mbaazi za muda mfupi hustawi zaidi ukanda wa chini na ni

SHUK RANI

Kitini hiki cha “ Mwongozo wa uzalishaji wa mbegu za daraja la kuazimiwa ubora” kimeandaliwa

na shirika la Tanzania Alliance for Biodiversity (TABIO) kwa ushirikiano na SWISSAID Tanzania.

Kitini hiki kimepitiwa na kuidhinishwa na wawakilishi wa O�si ya Kilimo ya Mkoa wa Mtwara,

Ministry of Agriculture Training Institute (MATI) Naliendele, Sustainable Agriculture Tanzania

(SAT), Tanzania Organic Agriculture Movement (TOAM), Tanzania Alliance for Biodiversity

(TABIO), Tanzania O�cial Seed Certi�cation Institute (TOSCI-Mtwara), Shirika la Uhifadhi

Misitu Asilia Tanzania (TFCG), wawakilishi wa wakulima na SWISSAID Tanzania katika

warsha iliyofanyika tarehe 25 – 27 September 2019 katika Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara. Pia,

msaada wa kifedha kutoka Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Liechtenstein Development

Service (LED) na Swiss Agency for Development and Cooperation (SDC) umefanikisha kwa

kiwango kikubwa katika kugharamia uandaaji, kupitia na kukamilisha uchapishaji wa kitini hiki.

“Kitini hiki cha mafunzo kipo chini ya hati miliki ya kimataifa nambari 4.0 (CC BY-NC-DC 4.0), hairuhusiwi kuuzwa ama kunakiriwa pasipo idhini ya mmiliki.”

"This training manual is licensed under a Creative Commons Attribution-Non Commercial-NoDerivatives 4.0 International (CC BY-NC-ND 4.0) license"