32
i Machi 2011 Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? Ripoti ya utafiti kuhusu Uhusiano wa Ubora wa Mitaala na Utoaji Elimu Bora

Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

  • Upload
    others

  • View
    75

  • Download
    15

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

i

Machi 2011

Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini?

Ripoti ya utafiti kuhusu Uhusiano wa Ubora wa Mitaala na Utoaji Elimu Bora

Page 2: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

ii

Shukrani

Utafiti huu ni jitihada za pamoja kati ya HakiElimu na Idara ya Saikolojia ya Elimu na Mafunzo ya Mitaala ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kwa ushirikiano na Wafanyakazi wa HakiElimu Dk. Kitila Mkumbo aliandaa muundo wa utafiti na kutoa mafunzo kwa wafanyakazi kuhusu njia za ukusanyaji wa taarifa. Pia alisimamia mchakato mzima wa utafiti.

Wafanyakazi wafuatao walifanya kazi ya utafiti kwa kutembelea maeneo ya utafiti kwa lengo la kukusanya data: Elizabeth Missokia, Daniel Luhamo, Charles Mtoi, Robert Mihayo, Glory Mosha, Fausta Musokwa, Naomi Mwakilembe, Tony Baker, Boniventura Godfrey, Lilyan Omary, Anastazia Rugaba, Frederick Rwehumbiza, Nyanda Shuli, Vicent Mnyanyika na Esther Mashoto.

Ripoti hii iliandikwa na Dk. Kitila Mkumbo. Uhariri, tathmini pamoja na ushauri kuhusu ripoti ulitolewa na Elizabeth Missokia, Mtemi Gervas Zombwe, Robert Mihayo na Nyanda Shuli.

Ripoti ya utafiti huu isingefanikiwa bila ya ushirikiano wa wanafunzi, wazazi, wajumbe wa kamati za shule, walimu pamoja na wafanyakazi katika katika ofisi za wilaya ambao tulifanya nao mahojiano. Tunawashukuru sana kwa michango yao pamoja na utayari wao kufanya kazi nasi.

© HakiElimu 2011, ISBN: 978-9987-18-008-0HakiElimu, S.L. P 79401, Dar es Salaam, TanzaniaSimu: (255 22) 2151852/3, Faksi: (255 22) 2152449

Sehemu yoyote ya ripoti hii inaweza kunukuliwa kwa ajili ya matumizi ya elimu na si ya kibiashara, ili mradi tu chanzo kitatajwa na kwamba nakala mbili zitatumwa HakiElimu.

Page 3: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

iii

Yaliyomo

Orodha ya Michoro iv

Sura ya Kwanza: Utangulizi na Njia ya Utafiti 1

1. Utangulizi 1

1.1 Madhumuni na Malengo ya Utafiti 3

1.2 Je, mtaala hujumuisha mambo gani na huathiri vipi ujifunzaji? 3

1.3 Mbinu za utafiti 4

Sura ya Pili: Matokeo ya Utafiti. 6

2.1 Utangulizi 6

2.2 Maoni ya walimu na wanafunzi kuhusu ubora wa mtaala 6

2.2.1 Utangulizi 6

2.2.2 Maoni ya walimu kuhusu ubora wa mtaala 6

2.2.3 Matokeo ya utafiti kutoka kwenye maswali ya dodoso na

majadiliano ya vikundi kuhusu ubora wa mtaala 9

2.3 Ushiriki wa jamii katika maendeleo na utekelezaji wa mtaala 16

2.4 Tathmini kutoka kwenye baadhi ya vitabu vinavyotumika kufundishia masomo

mbalimbali 16

Mfano dhahiri: Kitabu cha Nne cha Hisabati kinachotumika kufundishia Shule za Sekondari Tanzania kilichochapishwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) na kile kilichochapishwa na

Kampuni ya Uchapishaji ya NNP

Sura ya Tatu: Muhtasari , Hitimisho na Mapendekezo 22

3.1 Muhtasari wa matokeo ya utafiti na hitimisho 22

3.2 Mapendekezo 23

Marejeo 26

Page 4: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

iv

Orodha ya Michoro

Mchoro 1: Kiwango cha ufaulu katika mitihani ya taifa 2005-2009 2

Mchoro 2: Asilimia ya walimu walioripoti kwamba wanaifahamu 7 Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na MKUKUTA

Mchoro 3: Asilimia ya walimu ambao waliripoti kwamba wao pamoja na 8 wadau wengine wanayaelewa malengo ya elimu ya taifa

Mchoro 4: Asilimia ya walimu na wanafunzi walioripoti kwamba mtaala 9 unafaa katika kuandaa wahitimu wenye kujiamini, wanaotimiza wajibu wao, wenye kuleta tija na wenye ujuzi unaofaa.

Mchoro 5: Maoni ya wanafunzi kuhusu ufundishaji wa walimu wao 12

Mchoro 6: Asilimia ya wanafunzi walioripoti kwamba wanaridhishwa na 13 uwezo wa walimu wao katika kufundisha pamoja na uwepo wa nyenzo za kufundishia

Mchoro 7: Maoni ya walimu kuhusu kufundisha kwa kutumia aina moja 15 ya kitabu au vitabu vingi

Page 5: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

1

Sura ya Kwanza:

Utangulizi na Mbinu za Utafiti

1.0 UtanguliziKatika kipindi cha miongo miwili iliyopita kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wazazi, serikali, sekta binafsi na asasi za kiraia juu ya ‘kushuka’ kwa ubora wa elimu nchini Tanzania. Kuna vigezo viwili vinavyotumika katika kupima kiwango cha ubora wa elimu. Kwanza kabisa, wasomi hutazama ufaulu wa wanafunzi katika stadi za msingi kama vile kuandika, kusoma na stadi hesabu (kujumlisha na kutoa). Pili, wasomi hutazama kiwango ambacho wanafunzi wameweza kupata stadi za msingi zitakazowawezesha kuukabili ulimwengu wa ajira. Wakati mwingine vigezo hivi hugawanywa katika nyanja za matokeo ya kitaaluma na stadi za ufundi katika mfumo wa elimu. Kigezo cha uwezo wa kitaaluma kimelenga katika kumwandaa mhitimu ili awe mwanazuoni ambaye uwezo wake wa kufikiri, kuchangia mijadala, kuuliza maswali, kufanya uchunguzi na kupeleleza ni wa hali ya juu zaidi (Pring, 2004).

Kutokana na hayo, wanazuoni wengi husisitiza kwamba elimu bora ni ile itakayowawezesha wanafunzi kufikia vigezo viwili, elimu itakayowawezesha wanafunzi kuwa na uwezo kitaaluma ambao huendana na kufikiri kwa mantiki, kutambua tatizo na kulitafutia ufumbuzi wake na kushiriki katika mijadala ya kitaaluma. Pia wanazuoni wanasisitiza kwamba elimu bora ni ile itakayowaandaa wanafunzi kuwa na uwezo wa kupambana katika ulimwengu wa kazi; elimu ambayo itampatia mwanafunzi stadi za kitaalamu kama vile stadi za mawasiliano na kazi husika.

Kwa kawaida, ubora wa elimu umekuwa ukipimwa zaidi kwa kutumia kigezo cha ufaulu wa wanafunzi. Kwa maana hiyo, wanazuoni na wadau wengine wa elimu hutazama ufaulu wa wanafunzi katika mitihani mbalimbali ili kupima ubora wa elimu ambao wanafunzi wameupata. Kwa kuzingatia kigezo hiki, kwa mfano, katika miaka ya hivi karibuni ufaulu wa wanafunzi katika mitihani ya taifa umekuwa ukishuka, hii ikiwa na maana kuwa ubora wa elimu umekuwa ukishuka pia. Kwa mfano, idadi ya wanafunzi ambao wanafaulu mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi imekuwa ikishuka kwa kasi tangu mwaka 2005. Kwa mfano, kiwango cha ufaulu kimeshuka kutoka asilimia 70.5 katika mwaka 2006 na kufikia asilimia 54.2 katika mwaka 2007, asilimia 52.7 katika mwaka 2008 na kufikia asilimia 49.4 katika mwaka 2009 (Jamhuri ya Muungano wa Tanzania [URT], 2010).

Tathmini ya matokeo ya mitihani ya shule za sekondari pia inaonyesha kuwa ufaulu wa wanafunzi umekuwa ukishuka. Kwa mfano, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, kati ya mwaka 2005 na 2009, asilimia ya watahiniwa wanaopata Daraja la I na II katika mitihani ya Kidato cha IV imeshuka kutoka asilimia 12 katika mwaka 2005 hadi kufikia asilimia 6 katika mwaka 2009 (tazama mchoro 1). Kwa hakika, kama Mchoro 1 unavyoonyesha, idadi kubwa ya watahiniwa (zaidi ya asilimia 50%) imekuwa ikipata Daraja la IV katika mitihani ya kuhitimu Kidato cha IV. Kupata Daraja la IV ni kama kufeli kwa kiwango cha Tanzania kwa sababu mtahiniwa aliyepata Daraja la IV hupata shida katika kusajiliwa kwenye taasisi zinazotoa elimu ya juu.

Page 6: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

2

Kwa kuzingatia ufaulu wa wanafunzi katika mitihani, ubora wa elimu katika ngazi ya msingi na sekondari umekuwa ukishuka. Pia ubora wa ufundishaji mashuleni ni wa kutiliwa mashaka. Utafiti uliofanyika hivi karibuni umeonyesha kwamba karibu asilimia 50 ya watoto wanaomaliza elimu ya msingi hawawezi kusoma habari kwa Kiingereza wala kwa Kiswahili na hali ni mbaya zaidi katika maeneo ya vijijini (Uwezo, 2010). Ubora wa elimu inayotolewa katika mashule yetu unahitaji kufanyiwa uchunguzi ili kubaini sababu zinazofanya hali hii iendelee kuwepo na hii itasaidia kukabiliana na tatizo.

100%

56%

22% 24%

12% 11%

17%

10%12%

6%

56%57% 55%

90%80%70%60%50%40%30%20%10%

0%2005 2006 2008 2009

Daraja la I na la IIDaraja la III

Daraja la IV

Mchoro 1: Kiwango cha ufaulu katika mitihani ya taifa ya kidato cha nne 2005-2009

Sababu nyingi ambazo huathiri ubora wa elimu zimebainishwa. Sababu kubwa inayotajwa inaendana na upatikanaji wa nyenzo za kufundishia na kujifunzia (Chonjo, 1994) pamoja na uongozi wa shule ulio imara na wenye tija (Mosha, 1988). Ubora wa elimu huambatana na upatikanaji wa walimu wenye uwezo bila kusahau uongozi bora (Oduro, Dachi & Fertig, 2008). Oduro et al., wamekuwa wakibainisha kuwa mabadiliko ya elimu katika Afrika yamekuwa yakizingatia zaidi kuongeza idadi ya wanafunzi wakati suala la ubora wa elimu inayotolewa limekuwa likipewa nafasi finyu. Kwamba, wakati tukitambua na kupongeza ongezeko katika usajiri wa wanafunzi katika shule za sekondari miaka ya hivi karibuni, ni muhimu kujiuliza maswali magumu iwapo watoto wote waliopo shuleni wanasoma.

Ingawa kuna sababu nyingi zilizobainishwa na kufanyiwa tathmini kuhusiana na ubora wa elimu katika ngazi ya msingi na sekondari, hakuna tafiti zilizofanyika ili kuchunguza ni kwa namna gani ubora wa mtaala huathiri ubora wa elimu. Kutokana na mapungufu haya, HakiElimu, shirika linalojishughulisha na kuhakikisha kuwa, kunakuwa na usawa, ubora, haki za binadamu na demokrasia katika elimu kwa kuziwezesha jamii kuzibadili shule na sera katika elimu, lilimpa mtaalamu wa elimu kazi ya kufanya utafiti ili kuchunguza uhusiano uliopo kati ya ubora wa mtaala na utoaji elimu bora nchini Tanzania. Ripoti hii inaelezea matokeo ya utafiti.

Page 7: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

3

1.1 Madhumuni na Malengo ya UtafitiMalengo makubwa ya utafiti huu ni kuchunguza jinsi mtaala wa shule katika shule za Tanzania unavyoathiri ubora wa elimu. Utafiti umetilia mkazo malengo manne yafuatayo:

i) Kutathmini ubora wa mtaala wa elimu ya msingi katika utoaji wa elimu boraii) Kutathmini athari za kutumia kitabu cha aina moja au nyingi katika utoaji wa elimu boraiii) Kutathmini ushiriki wa jamii katika kuhakiki ubora wa mtaalaiv) Kupata maoni ya wadau wa elimu kuhusu namna ya kuboresha mtaala ili kutoa elimu bora

kwa wanafunzi wetu

1.2 Je, mtaala hujumuisha mambo gani na kwa namna gani huathiri ujifunzaji?Waandishi wengi wanakiri juu ya ugumu uliopo katika kuelezea maana ya dhana mtaala. Neno mtaala linatokana na lugha ya Kilatini, likimaanisha ‘kuendesha kozi’. Kwa kuzingatia maana ya asili ya neno lenyewe, Oliva (1997, uk 4) anaelezea maana ya mtaala kwa kuzingatia mambo 12.

• Kile kinachofundishwa shuleni• Seti ya masomo• Maarifa• Programu ya masomo• Seti ya vitu vya kujifunza• Orodha ya kozi• Seti ya malengo ya ufanyaji kitu• Kozi ya kujifunza• Kila kitu kinachoendelea shuleni, ukijumuisha mambo yanayofanyika nje ya darasa,

usimamizi, na uhusiano kati ya mtu mmoja na mwingine• Kila kitu kinachopangwa na wafanyakazi shuleni • Mjumuiko wa uzoefu mbalimbali anaoupata mwanafunzi awapo shuleni• Kile ambacho mwanafunzi hukipata kikiwa ni matokeo ya kuwa shuleni

Kwa kuzingatia dhana ya mtaala kama ilivyoelezewa na Oliva, mtaala unaweza kutazamwa kama orodha ya maarifa ambayo mwanafunzi anatarajiwa ayapate na jinsi maarifa haya yalivyopangiliwa. Ni orodha ya fursa za kujifunza zinazotolewa kwa wanafunzi wanapojifunza maarifa fulani (Egan, 2003). Kwa hiyo, mtaala na ujifunzaji ni vitu vinavyoenda pamoja na hii ikimaanisha kwamba mtaala mbovu unaweza kuathiri ubora wa elimu kwa kiwango kikubwa. Mtaala ni kitu kinachofikirika kwa kuwa katika uhalisia si rahisi kuona ‘orodha ya fursa za ujifunzaji’. Tunavyoweza kuviona ni vitu vinavyotokana na mtaala pamoja na athari za mtaala, na si mtaala wenyewe. Kwamba, mtaala hupatikana katika namna nyingi ambazo tunaweza kuziona na ambazo huchukuliwa kama viashiria vya nia zetu katika kutekeleza mtaala huo. Viashiria hivi vinajumuisha kwa mfano:

• Malengo na nia ambazo mtu anazitarajia au matarajio ya wanafunzi katika kujifunza yanayopatikana katika nyaraka rasmi za elimu

• Mlolongo wa shughuli za darasani zinazolenga kutekeleza malengo na nia hizo

Page 8: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

4

• Vitabu na nyanja zingine za ujifunzaji zinazosaidia katika kufanikisha fursa za ujifunzaji• Maandalio ya somo yanayobainisha mada na muda wa ujifunzaji na ufundishaji

Kwamba, katika kufanya tathmini ya mtaala, ni muhimu kuchagua vitu na athari ambazo zinahitaji kubainishwa katika mtaala unaohusika. Utafiti huu umechambua vitu vitatu vifuatavyo vya kuzingatia katika mtaala

i) Uzoefu wa walimu na wanafunzi katika ufundishaji na ujifunzajiii) Ubora wa mada kama ulivyobainishwa kwenye mihtasari ya masomo na vitabu vya kiadaiii) Maoni ya watunga sera na wadau wa elimu kuhusu ufanisi wa mtaala wetu katika kufanikisha

ubora wa ujifunzaji

1.3 Mbinu za utafitiMbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu mchanganyiko ambapo mbinu ya utafiti inayohusisha takwimu na ile isiyohusisha takwimu zilitumika katika ukusanyaji wa data. Kulikuwa na umuhimu wa kutumia mbinu hii ya utafiti ili kupata idadi kubwa ya washiriki katika utafiti. Wakati mbinu ya utafiti wa kitakwimu ilitumika ili kupata idadi kubwa ya washiriki kadri iwezekanavyo. Mbinu ya utafiti isiyohusisha takwimu ilitumika ili kupata hisia za washiriki katika kuelezea dhana ya ubora wa mtaala pamoja na ubora wa elimu hapa nchini Tanzania.

Maswali dodoso yalitumika ili kupata data zinazohusu tathmini ya walimu na wanafunzi katika utekelezaji wa mtaala katika shule zao. Vikundi vya majadiliano vilitumika ili kupata maoni ya walimu na wanafunzi kuhusu ubora wa mtaala pamoja na athari zake katika utoaji wa elimu bora. Vikundi vya majadiliano vilifanyika kwa wazazi pia ili kupata maoni na ushiriki wao katika maendeleo na utekelezaji wa mtaala. Mahojiano yalifanyika kwa watunga sera katika ngazi za mikoa na wilaya ili kupata maoni yao kuhusu ubora wa mtaala na jinsi gani unaathiri ubora wa elimu.

Sera za elimu na mada kama zinavyobainishwa katika mihtasari ya masomo na vitabu vya kiada vilifanyiwa tathmini ili kubaini ni kwa namna gani vinashabihiana na athari zinazoweza kujitokeza kwenye ubora wa elimu inayotolewa kama ilivyobainishwa kwenye matarajio ya ujifunzaji kwa wanafunzi.

Washiriki katika utafiti huu wametoka katika mikoa ya Arusha, Iringa, Tanga, Mwanza, Tabora na Shinyanga. Wilaya moja katika mikoa hii ilichaguliwa kutoka kwenye sampuli ya utafiti, na wilaya zilizochaguliwa ni hizi zifuatazo: Monduli (Arusha), Mufindi (Iringa), Pangani (Tanga), Misungwi (Mwanza), Uyui (Tabora) na Bukombe (Shinyanga). Katika kila wilaya, shule nne zilichaguliwa-mbili za msingi na mbili tena za sekondari. Shule zilichaguliwa kwa kuzingatia ufaulu katika Mitihani ya Kuhitimu Elimu ya Msingi na Mitihani ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari.

Shule moja ya msingi yenye kiwango cha juu katika ufaulu na shule moja ya sekondari yenye kiwango cha juu katika ufaulu zilichaguliwa. Vivyo hivyo, shule moja ya msingi yenye kiwango cha chini katika ufaulu ilichaguliwa na vilevile shule moja ya sekondari yenye kiwango cha chini katika ufaulu ilichaguliwa kwa kila wilaya.

Page 9: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

5

Katika kila shule, wanafunzi waliochaguliwa ni wale wa Darasa la Tano na la Sita katika shule za msingi, wakati katika shule za sekondari wanafunzi waliochaguliwa ni wale wa Kidato cha Tatu na Nne. Sampuli ilichukuliwa kwa kufuata vigezo maalumu na wakati mwingine haikufuata. Katika kuwapata wanafunzi wa kujaza dodoso wavulana na wasichana walichaguliwa kwa uwiano karibu sawa.

Katika kila kundi, yaani kundi la wasichana na wavulana, wanafunzi waliombwa wahesabu 1 na 2, ambapo wanafunzi waliohesabu 2 walichaguliwa kwa upande wa wavulana na wale waliohesabu 1 walichukuliwa kwa upande wa wasichana. Wanafunzi waliojaza dodoso waliombwa pia washiriki katika vikundi vya majadiliano na hivyo wanafunzi tisa walichaguliwa kwa ajili ya kushiriki katika vikundi vya majadiliano.

Walimu wote waliokuwepo siku utafiti unafanyika waliombwa wajaze dodoso na pia kushiriki katika vikundi vya majadiliano.

Data zinazohusisha takwimu zilichambuliwa kwa kutumia programu ya SPSS toleo la 16.0 ambapo takwimu zilitolewa kuonyesha idadi ya washiriki na uzoefu wao katika utekelezaji wa mtaala. Data ambazo hazihusishi takwimu zilirekodiwa kama zilivyo. Majadiliano ya vikundi na mahojiano yalirekodiwa, yalichapwa na kuhifadhiwa kwenye kompyuta.

Yalichapishwa na kurudiwa kusomwa hadi kilichodhamiriwa kilipoanza kuonekana. Malengo ya mazungumzo yalibainishwa kutoka kwenye mazungumzo yaliyorekodiwa na yalichukuliwa kama kigezo katika uchambuzi. Mazungumzo yaliyorekodiwa pamoja na nukuu husika vilitumika katika kufafanua zaidi matokeo ya dodoso.

Ruhusa ya kufanya utafiti huu ilitolewa na Mkurugenzi wa Utafiti Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Ruhusa ya kufanya utafiti katika mashule ilitolewa na Makatibu Tawala wa Wilaya na Mikoa. Maadili yote ya utafiti katika shule za Tanzania yalizingatiwa na hii ikiwa ni pamoja na uhuru wa mtu kushiriki katika utafiti, kutunza siri na mambo ya faragha yanayowahusu washiriki. Utayari wa wanafunzi katika kufanya utafiti ulipatikana kupitia walimu na wanafunzi wenyewe.

Page 10: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

6

Sura ya Pili

Matokeo ya Utafiti

2.1 UtanguliziUtafiti huu umegawanyika katika sehemu mbili kuu: Sehemu ya kwanza imefanya tathmini kuhusu maoni ya walimu, wanafunzi na wadau wengine wa elimu kuhusu ubora wa mtaala pamoja na utekelezaji wake. Hii imefanyika kwa kutumia takwimu na maelezo yasiyohusisha takwimu. Sehemu ya pili ya utafiti huu imefanya tathmini ya ubora wa vitu vinavyowezesha mtaala wenyewe ambapo vitu hivi vinajumuisha vitabu vya kiada vinavyotumika katika kufundishia masomo mbalimbali. Matokeo ya utafiti katika sehemu ya kwanza yametolewa yakifuatiwa na matokeo ya sehemu ya pili.

2.2 Maoni ya walimu na wanafunzi juu ya ubora wa mitaala

2.2.1 UtanguliziWalimu na wanafunzi walijaza dodoso lenye sehemu tatu ambalo lilikuwa na lengo la kutathmini maoni yao kuhusu ubora wa mtaala na jinsi unavyohusiana na ubora wa elimu inayotolewa kwa wanafunzi. Idadi ya walimu waliojaza dodoso ilikuwa ni 233 ambapo idadi ya wanafunzi ambao walijaza dodoso ilikuwa ni 1325. Uwiano wa kijinsia wa walimu waliojaza dodoso ulikuwa kama ifuatavyo: asilimia 50.4 walikuwa ni wanaume ambapo asilimia 49.6 walikuwa ni wanawake wakati asilimia 54.2 ya wanafunzi waliojaza dodoso walikuwa ni wasichana. Umri wa wastani wa walimu waliojaza dodoso ulikuwa ni 34.4 (Uwiano wa tofauti = 2.61) na umri wa wastani wa wanafunzi waliojaza dodoso ulikuwa miaka 15 (Uwiano wa tofauti = 10.31).

Mbali na kujaza dodoso, walimu, wanafunzi, wazazi, viongozi wa jumuiya na wadau wengine wa elimu walishiriki katika majadiliano ya vikundi na kwenye mahojiano ambayo malengo yake yalikuwa kuongezea taarifa za kitakwimu zilizokusanywa.

2.2.2 Maoni ya walimu kuhusu ubora wa elimu

2.2.2.1 Uelewa wa walimu kuhusu sera muhimu zinazoelezea mtaalaIli kufanya tathmini juu ya maoni ya walimu kuhusu ubora wa mtaala, walimu waliulizwa aina tatu za maswali. Maswali yaliyokuwa yamewekwa katika kundi la kwanza yalilenga kupima uelewa wao kuhusu sera muhimu za taifa ambapo kutokana za sera hizo ndipo tunapata malengo ya elimu. Kwa hakika, mtaala wa elimu huongozwa na dira na mwelekeo wa nchi katika masuala ya kijamii, kiuchumi na kisiasa na kwa maana hiyo ni muhimu kwa walimu kuelewa baadhi ya sera. Nchini Tanzania, kuna sera mbili kuu zinazoelezea mwelekeo wa nchi nazo ni Dira ya Maendeleo ya Taifa na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA). Kwa hali hiyo, Sera ya Elimu pamoja na mtaala ni muhimu kuzingatia vitu hivi. Walimu waliombwa waeleze ni kwa kiwango gani wanazielewa sera hizi kuu. Kati ya walimu waliohojiwa ni asilimia 47 tu ndiyo ambao wamesikia kuhusu Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025

Page 11: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

7

na kati ya hao ni asilimia 34.4 tu ndiyo wanaoelewa kuhusu dira hii. MKUKUTA ulikuwa unafahamika vyema kwa walimu waliohojiwa, kwamba asilimia 75 ya walimu waliohojiwa wamewahi kusikia kuhusu MKUKUTA na kwamba kati ya walimu hao asilimia 72.2 waliripoti kwamba ‘wanaulewa vyema’ au ‘wanaelewa’ kuhusu MKUKUTA (tazama mchoro 2).

Mchoro 2: Asilimia ya walimu waliosema kwamba wanaelewa Dira ya Tanzania 2025 na MKUKUTA

2.2.2.2 Uelewa wa walimu kuhusu malengo ya elimu ya TanzaniaNi muhimu kwa walimu kuelewa malengo ya elimu kwa kuwa ndiyo msingi wa kutekeleza mtaala wa elimu. Kwa kuzingatia umuhimu huu, walimu waliulizwa ili kuelezea ni kwa kiwango gani wanayaelewa malengo ya elimu ya taifa. Idadi kubwa ya walimu (asilimia 86.8) waliripoti kwamba wanayaelewa malengo ya elimu vizuri zaidi, na walimu(asilimia 13.2) wanayaelewa kiasi malengo ya elimu ya Tanzania.

Walipoulizwa ni kwa kiwango gani wadau wa elimu wanayaelewa malengo ya elimu, idadi kubwa ya walimu (asilimia 64.2) ilidhani kwamba wadau wa elimu wanayafahamu malengo ya elimu. Kwa kuongezea asilimia 83.9 ya walimu waliripoti kuwa walijifunza kuhusu malengo ya elimu shule za msingi na sekondari walipokuwa vyuo vya ualimu. Hivyo, ni dhahiri kuwa walimu na wadau wengine wa elimu wanayaelewa malengo ya elimu ya taifa (tazama mchoro 3).

100%90%80%

34%47%

75% 72%

70%60%50%40%30%20%10%

0% Waliowahi kusikia Wanaoelewa

Dira ya Tanzania 2025MKUKUTA

Page 12: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

8

Mchoro 3: Asilimia ya walimu waliosema kwamba wao pamoja na wadau wengine wanayaelewa malengo ya

elimu ya taifa

2.2.2.3 Maoni ya walimu na wanafunzi kuhusu ufanisi wa mtaala wa elimu wa Tanzania Walimu na wanafunzi waliombwa kuonesha ni kwa kiwango gani mtaala wa elimu wa Tanzania unafaa katika kutoa wahitimu mahiri, wenye kujiamini, wanaowajibika na wenye ujuzi unaohitajika ambapo matokeo yameonyeshwa kwenye Mchoro 4. Kama mchoro 4 unavyoonyesha, idadi kubwa ya washiriki, walimu na wanafunzi, walikuwa na maoni kwamba mtaala wa elimu wa Tanzanian hauna uwezo wa kutoa wahitimu mahiri katika nyanja mbalimbali. Kwa mfano, ni asilimia 35 tu ya walimu na asilimia 26 ya wanafunzi ndiyo walioripoti kwamba mtaala unafaa katika kuandaa wahitimu mahiri na wenye kujiamini.

Mbali na hiya, ni asilimia 39 tu ya walimu na asilimia 26 tu ya wanafunzi ndiyo walioripoti kuwa mtaala unafaa katika kutoa wahitimu wanaowajibika katika jamii. Ni asilimia 36 tu ya walimu na asilimia 28 tu ya wanafunzi waliokuwa na maoni kwamba mtaala unafaa katika kutoa wahitimu wanaoweza kuisaidia jamii. Kwa upande wa wanafunzi ni idadi kubwa ya wanafunzi iliyokuwa na maoni kuwa mtaala unafaa katika kutoa wahitimu wenye ujuzi unaohitajika ambapo asilimia 70 ya wanafunzi iliripoti kwamba mtaala unafaa katika kutoa wahitimu wenye ujuzi unaohitajika.

100%90%80%

88%

60%70%60%50%40%30%20%10%0%

Wadau wengine wa elimuWalimu

Page 13: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

9

Mchoro 4: Asilimia ya walimu na wanafunzi waliosema kwamba mtaala unafaa katika kutoa wahitimu

wanaojiamini, wanaowajibika, wenye tija na wenye ujuzi unaohitajika.

2.2.3 Matokeo ya utafiti kutoka kwenye vikundi mjadala kuhusu ufanisi wa mitaalaMaoni yalitolewa na washiriki kutoka kwenye vikundi maalumu vya majadiliano kuhusu ufanisi wa mtaala yanakaribiana na maoni yaliyotolewa kutoka kwenye dodoso. Washiriki walikuwa na maoni kwamba mtaala uliopo haujitoshelezi katika kutoa wahitimu wenye uwezo wa kujitegemea. Walibainisha kwamba elimu iliyokuwa ikitolewa katika miaka ya 1980 na 1990 ilikuwa ikimwezesha mhitimu kuwa na mawazo ya kujitegemea katika ngazi yoyote ya elimu aliyofikia, na walibainisha pia kwamba elimu inayotolewa siku hizi inamfanya mhitimu ategemee zaidi ‘kuajiriwa na kufanya kazi za ofisini’. Hii inatokana na mtaala wenyewe wa sasa ambao unatilia mkazo zaidi katika taaluma badala ya kutilia mkazo katika stadi za maisha. Kwa mfano, mmoja wao kati ya Maafisa wa Elimu wa Wilaya alikuwa na haya ya kusema katika mahojiano tuliyofanya naye:

Kuna mkazo mkubwa katika kuhakikisha kwamba watoto wanafaulu mitihani na watoto wanafundishwa ili mradi tu wafaulu mitihani badala ya kuwafundishwa jinsi ya kujitegemea. Hawaandiliwi kukabiliana na ulimwengu wa kazi. Kama wakifeli mitihani yao maana yake maisha yao ya baadaye yanakuwa yameathirika pia.

Mkuu mmoja wa shule katika shule tulizofanya nazo mahojiano alikuwa na mawazo yanayofanana na yale aliyotoa Afisa Elimu. Kwa mtazamo wake, wanafunzi wanapendelea kukariri ili wafaulu mitihani yao na siyo kwamba wapate maarifa na stadi ambazo zitawasaidia katika maisha ya baadaye. Mkuu huyo wa shule alikuwa na haya ya kusema:

Mwanafunzi anajifunza maana ya Fizikia na maana ya Bailojia na si namna ya kutumia dhana hizo walizojifunza darasani katika maisha halisi. Hali hii inakera sana kwa kweli!

100%90%80% 70%

44%

28%36%

26%39%

26%35%

70%60%50%40%30%20%10%0%

Wahitimu wenyekujiamini

Wahitimuwanaowajibika

Wahitimuwanaoweza

kusaidia jamii

Wahitimuwenye ujuzi

WalimuWanafunzi

Page 14: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

10

Mmojawapo wa Maafisa Elimu ambaye alishiriki katika mahojiano aliukosoa mtaala wa sasa, akibainisha kwamba mtaala wa sasa hauendani na mahitaji ya sasa ya jamii. Alisema:

Si rahisi kwa wahitimu wetu kuweza kujitegemea. Kilichopo kwenye mtaala wa sasa kwa uhalisia hakina mantiki kwa kuwa hakiendani na mazingira ambayo wanafunzi wanaishi.

Maoni yaliyotolewa na wanafunzi hayakutofautiana na yale yalitolewa na walimu wao. Walibainisha kwamba elimu yetu inatilia zaidi mkazo katika kufaulu mitihani na kuweka mkazo kidogo kwa masuala yaliyo nje na muktadha wa darasa. Kwa mfano wakati wa majadiliano wanafunzi walitoa maoni yafuatayo:

..........elimu yetu haisaidii sana. Hii ni kutokana na kwamba si ya vitendo sana. Kwa hiyo ni vigumu kuvitumia vile ambavyo tumejifunza shuleni.

Sidhani kama kile tulichojifunza shuleni kitanisaidia mara nimalizapo masomo yangu. Vijana wengi waliomaliza elimu ya sekondari wapo mitaani na wasijue la kufanya. Serikali ni sharti ichukue hatua madhubuti ili kuboresha elimu yetu ili iendane na mazingira ya sasa.

Mtaala wa sasa hauendani na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanayotokea duniani kwa sasa. Je, utajifunzaje kuhusu kutumia kompyuta bila ya kuiona kompyuta yenyewe?

Walimu walizungumzia masuala mawili kuhusu maendeleo na mchakato wa mtaala nchini Tanzania. Walimu walikuwa na maoni kwamba kuna mabadiliko mengi sana kwenye mtaala ambayo yamefanywa kwa muda mfupi, na kwamba walimu na wadau wengine hawashirikishwi katika kufanya mabadiliko hayo. Baadhi ya maoni ya walimu yamenukuliwa hapo chini.

(i) ‘Kuna mabadiliko mengi mno ya mitaala’

Mabadiliko mengi sana ya mtaala ambayo yamefanywa katika kipindi cha miaka kumi iliyopita. Hali hii ilisababisha mkanganyiko kwa wadau. Wadau wengi walikosoa mabadiliko ya mtaala ambayo yamefanywa kwa haraka. Walimu waliikosoa serikali kwa kuanzisha mtaala ambao hauendani na mahitaji ya watu. Pia waliukosoa mwenendo wa serikali katika miaka ya hivi karibuni ambapo imekuwa ikifanya mabadiliko ya mtaala bila ya kuwahusisha wadau ukijumuisha walimu na wanafunzi. Kwa mfano, Afisa Elimu wa Wilaya alikuwa na haya ya kusema kuhusu mabadiliko ya mtaala:

Nadhani tumekuwa tukifanya mabadiliko ya mtaala kiasi cha kuwachanganya walimu wetu. Kabla ya walimu hawajauzoea mtaala mpya, mabadiliko yanafanyika.

Mwalimu mkuu mmojawapo katika shule zilizoshiriki katika utafiti alilaumu mabadiliko ya mara kwa mara yanayofanywa katika mtaala, ambapo alisema “hakuna mtaala maalum kwani mabadiliko ya mara kwa mara yamekuwa yakifanywa kwenye mtaala na hali hii huwachanganya walimu”.

Page 15: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

11

(ii) ‘Walimu hawahusishwi katika kufanya mabadiliko ya mtaala’

Utengenezaji wa mtaala ni mchakato wa pamoja ambapo inafaa uwahusishe wadau wote muhimu. Mabadiliko katika mtaala ni sharti yazingatie mahitaji ya jamii inayohusika. Wakati wa majadiliano na mahojiano tulibaini kwamba mchakato wa utengenezaji wa mtaala nchini Tanzania siyo shirikishi. Kwa mfano, walimu wengi walikuwa wakilalamika kwamba mabadiliko kwenye mtaala yanaamuliwa na uongozi wa juu, hasahasa Wizara inayohusika na elimu bila ya maelezo kwa nini mabadiliko hayo yamefanyika. Pia, washiriki walikuwa na maoni kwamba mabadiliko katika mtaala hayaendani na mabadiliko katika nyenzo za kufundishia na kujifunzia. Hali hii inafanya kuwa na ugumu katika kutekeleza mabadiliko hayo. Mmoja kati ya Maafisa wa Elimu wa Wilaya alikuwa na haya ya kusema:

Mabadiliko ya mtaala yanapofanyika, hatupewi muda wa kutosha kuyaelewa kabla ya utekelezaji kuanza. Mara nyingi mabadiliko haya yanafanywa bila ya kuwahusisha wadau. Vilevile vitabu na vifaa vingine muhimu vya kufundishia na kujifunzia huwa havifiki kwa wakati pindi mabadiliko yanapofanyika. Kwa mfano tangu mabadiliko katika mtaala wa Darasa la Sita yamefanyika, miaka miwili iliyopita, hakuna mabadiliko yoyote katika vitabu na vifaa vingine vya kufundishia na kujifunzia ambayo yamefanyika ili kuendana na mabadiliko katika mtaala. Je, unategemea walimu wafundishe vipi?Mtaala ni mpya ila vitabu ni vya zamani, hali hii inawezekana vipi?

Akitilia mkazo mkazo suala la utengenezaji wa mtaala na kutohusishwa kwa walimu katika mchakato huo, Afisa Elimu mwingine wa Wilaya alikuwa na haya ya kusema:

Kwa jinsi ninavyouelewa mchakato wa uandaaji wa mtaala, mabadiliko yoyote katika mtaala ni sharti yaanzie katika ngazi ya chini kuliko kuanzia ngazi ya juu. Wadau wote ni sharti wahusishwe katika mabadiliko ya mtaala na kwamba mabadiliko yoyote ya mtaala yafaa yaanzie kwa mwalimu anayefundisha darasa husika na kuishia ngazi za juu za uongozi. Kwa bahati mbaya hali hii haifanyiki.

Mwalimu mkuu katika shule ya msingi alikuwa na maoni yanayofanana na hayo yaliyotolewa hapo juu ambapo alisema:

.....sisi ni watekelezaji tu wa mabadiliko ya mtaala. Hatushiriki katika kuleta mabadiliko haya, tunaletewa tu! Mbaya zaidi, huwa hatupewi mafunzo kuhusu mabadiliko haya. Tunachotakiwa kufanya ni kutekeleza maagizo tu.

Mwalimu mkuu katika shule zilizoshiriki katika utafiti alikuwa na maoni yanayofanana ambapo alisema kwamba, mabadiliko katika mtaala huwa hayaendani na mahitaji ya nyenzo za kufundishia na kujifunzia. Alibainisha kwamba:

Mabadiliko mengi katika mtaala hayaendani na mahitaji ya nyenzo za kufundishia na kujifunzia. Hali hii hujitokeza zaidi hasa katika masomo ya sayansi.

Page 16: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

12

Kitu kingine cha msingi kilichozungumzwa na washiriki kuhusiana na mabadiliko ya mtaala ni ukosefu wa mafunzo kwa walimu. Walimu walibainisha kwamba pale mabadiliko ya mtaala yanapofanyika programu za mafunzo kwa ajili ya walimu ili kuuelewa na kuutekeleza mtaala mpya huwa hazitolewi.

2.2.2.4 Uzoefu wa wanafunzi katika mchakato wa ufundishaji na ujifunzajiUbora wa mtaala unabainishwa na jinsi wanafunzi wanavyouchukulia mchakato wa ujifunzaji na ufundishaji. Kwa hiyo, ni muhimu kutathmini maoni ya wanafunzi kuhusu uzoefu wao katika mchakato wa ujifunzaji na ufundishaji ili kutathmini ubora wa mtaala uliopo. Kwa maana hiyo, wanafunzi walipewa maswali mengi kwa lengo la kutathmini uzoefu wao katika mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji.

Maswali haya yanaweza kugawanywa katika nyanja tatu, uwezo wa walimu, upatikanaji wa nyenzo za kujifunzia na upatikanaji wa vitabu vya kiada. Matokeo yanaelezewa kwa muhtasari katika Jedwali la 1 na Mchoro na 3. Kama Jedwali 1 linavyoonyesha, idadi kubwa ya wanafunzi walikuwa wakiridhishwa na uwezo wa walimu wao kwa kuwa waliwapa alama za juu kwa kila nyanja iliyoulizwa. Kwa mfano, asilimia 88.1 ya wanafunzi waliripoti kwamba walimu wao walikuwa na uwezo mzuri katika kuelezea dhana mbalimbali darasani. Asilimia 60 ya wanafunzi waliripoti kwamba ufundishaji wa walimu wao ni wa kufurahisha (tazama Mchoro 5).

Mchoro 5: Maoni ya wanafunzi kuhusu ufundishaji walimu wao

Maswali yalipogawanywa katika nyanja tatu kama ilivyoelezewa hapo juu, kwa wastani wanafunzi walikuwa wanafurahishwa na uwezo wa walimu wao, lakini hawakuridhishwa kabisa na upatikanaji na ubora wa nyenzo za kufundishia na kujifunzia. Kwa mfano, ni asilimia 37.3 tu ya wanafunzi na asilimia 36.4 waliripoti kwamba kulikuwa na nyenzo za kutosha za kufundishia na kujifunzia pamoja na vitabu vya kiada. Asilimia 70.8 ya wanafunzi waliripoti kwamba walimu wao walikuwa na ufanisi

100%90%80%

88%

60%70%60%50%40%30%20%10%

0%Uwezo wa walimu katika ufundishaji

uliokuwa ni mzuriWalimu walikuwa na uwezo mzurikatika kueleza dhana mbali mbali

darasani

Page 17: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

13

katika kufundisha pamoja na kuwezesha tendo la ujifunzaji. Lakini ni asilimia 37.3 tu ya wanafunzi ndiyo walioripoti kwamba kulikuwa na nyenzo za kutosha za kufundishia na kujifunzia; vilevile, ni asilimia 36.4 tu ya wanafunzi ndiyo walioripoti kwamba kulikuwa na vitabu vya kutosha vya kiada kwa masomo waliyokuwa wakijifunza (tazama Mchoro 6).

Mchoro 6: Asilimia ya wanafunzi walioripoti kwamba walikuwa wameridhishwa na uwezo wa walimu wao pamoja na

upatikanaji wa nyenzo za kujifunzia.

100%90%80% 71%

36% 37%

70%60%50%40%30%20%10%

0%Ufanisi wa walimu Upatikanaji wa Vitabu Upatikanaji wa nyenzo

za kufundishia

Page 18: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

14

Maelezo

Walimu wangu ni wazuri katika kuelezea dhana mbalimbali darasani.Walimu wangu wameyafanya masomo yawe ya kupendeza.Walimu wangu wanafundisha kwa moyoMasomo niliyojifunza yameongeza uelewa wangu katika maswala mbalimbali ya taaluma.Walimu wangu mara nyingi wamekuwa wakipatikana ninapohitaji msaada wao.Nimekuwa nikifanya mazoezi ya kutosha darasani.Vigezo vinavyotumika katika kufanya tathmini vimekuwa vikieleweka kwangu.Usahihishaji wa kazi za wanafunzi umekuwa ukifanyika kwa haki.Muda uliotengwa kwenye muhtasari kwa ajili ya kufundisha somo fulani unatoshaDhana zinazofundishwa zinaeleweka waziwazi.Mpangilio wa mada zinazofundishwa ni mzuri na unaeleweka waziwazi.Dhana inayofundishwa ni muhimu na inakidhi mahitaji yangu.Dhana inayofundiswa inafaa na inakidhi mahitaji yangu ya kitaaluma.Nakubaliana na dhana ya kutumia kitabu kimoja kwa shule zote.Nakubaliana na dhana ya kutumia vitabu vya aina mbalimbali kwa shule mabalimbali.Kuna vitabu vya kiada vya kutosha kwa kila somo.Kitabu ninachotumia kina ubora unaohitajika.Kuna nyenzo za kutosha za kujifunzia shuleni kwetu.

Namba

1290

1302

13021306

1314

1314

1305

1300

1308

1300

1305

1318

1290

1298

1294

1310

1301

1314

% MajibuSD4.5

14.8

12.63.5

13.9

8.6

10.5

18.2

11.9

7.3

8.2

7.8

9

26.2

23.1

37.5

15.1

35.4

D5.6

17.1

13.46.3

14.4

10.2

13.4

13.5

16.7

11.8

12.6

10.5

11.3

14.1

12

21.1

14.8

21.1

Na Maoni1.9

8.1

143.4

4.2

2.4

11.9

7.1

7.0

6.1

12

7

8.3

11.4

9

5.1

8.1

6.2

A28.8

27

24.627

25.2

25.1

26.8

19.5

26

31.1

29.3

28.4

28.2

16.5

18.5

12.7

24.9

16

SA59.3

33.1

35.459.8

42.3

53.7

37.4

41.8

38.4

43.8

37.9

46.4

43.2

31.8

37.4

23.7

37.1

21.3

Jedwali 1: Maoni ya Wanafunzi kuhusu Ufanisi katika kufundisha na kujifunza katika Shule zao

Tanbihi: SD=Kutokubaliana Kabisa; D=Kutokubaliana; SA=Kukubaliana Kabisa; na A=Kukubaliana.

Page 19: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

15

2.2.2.5 Maoni ya walimu kuhusu matumizi ya kitabu kimoja cha kiada au vingiVitabu vya kiada ni vitu muhimu sana katika maendeleo ya mwanafunzi kwa namna mbalimbali. Vitabu vya kiada ni muhimu katika kushadidia stadi nne za ujifunzaji ambazo ni kuongea, kusikiliza, kusoma na kuandika (Moulton, 1997). Miongoni mwa mijadala mizito iliyopo katika elimu kwa sasa ni iwapo shule zote zitumie vitabu vya kiada vinavyofanana ama shule ziruhusiwe kutumia vitabu tofautitofauti vinavyopatikana katika mazingira husika.

Sera ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliyopo kwa sasa ni kwa kila shule kutumia vitabu tofautitofauti kwa masomo mbalimbali. Vitabu ni sharti viidhinishwe na Kamati ya Uidhinishaji wa Vitabu (EMAC) ndipo vitumike. Japokuwa kumekuwa na mawazo tofautitofauti kuhusu sera ya kutumia vitabu tofautitofauti, shule mbalimbali Tanzania bado zinatumia vitabu tofautitofauti pamoja na kwamba shule zote zinatekeleza mtaala mmoja. Utaratibu huu umeibua hisia tofautitofauti miongoni mwa wadau wa elimu.

Katika utafiti huu, tuliwaomba walimu watoe mawazo yao iwapo wanapendelea matumizi ya vitabu vya aina moja vya kiada au vitabu vya aina mbalimbali. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba asilimia 79.9 ya walimu wanapenda kutumia vitabu vya kiada vya aina moja katika shule zote na asilimia 20.5 ya walimu wanapenda kuendelea na sera ya sasa ambapo vitabu vya kiada vya aina mbalimbali hutumika katika kufundishia (tazama Mchoro 7).

Mchoro 7: Maoni ya walimu kuhusu kutumia vitabu vya kiada vya aina moja au aina mbalimbali

Wakati wa kufanya mahojiano na majadiliano, walimu wengi walionesha kupendezwa na matumizi ya vitabu vya kiada vya aina moja kuliko kutumia vitabu tofautitofauti. Wale waliokuwa wakipendelea matumizi vya vitabu vya kiada vya aina moja walikuwa na maoni kwamba hali hiyo itawafanya wanafunzi nchi nzima wajifunze mada zinazofanana bila ya kujali tofauti zao za kijiografia.

90%80%

80%

21%

70%60%50%40%30%20%10%0% Napenda kutumia virabu

vya kiada vya aina mojaNapenda kutumia virabu

vya kiada vya aina mbali mbali

Page 20: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

16

Vilevile walipendekeza kwamba usambazaji wa vitabu ungefanywa na vyombo vya serikali badala ya kuwaachia watu binafsi kufanya kazi hiyo. Baadhi ya maoni ya washiriki yamenukuliwa hapo chini:

Sikubaliani na matumizi ya vitabu vya aina tofautitofauti. Hali hii siyo nzuri. Inafaa kuwepo na kitabu kimoja cha kiada kwa kila somo kitachotumika nchi nzima. (Mwalimu Mkuu, Monduli).

“Nadhani kwamba kitabu kimoja cha kiada kitumike katika kufundishia kwa shule zote nchi nzima. Hii ni kwa sababu matumizi ya vitabu vya aina mbalimbali vya kiada yanaweza kuwachanganya wanafunzi pamoja na walimu na matokeo yake ujifunzaji utakosa mantiki. Wanafunzi watajifunza dhana tofautitofauti wakati wanategemewa wafanye mitihani ya aina moja. (Mwanafunzi, Misungwi)

“Nakubaliana kabisa na matumizi ya vitabu vya kiada vya aina moja kwa shule zote, kuanzia mkoa wa Kilimanjaro hadi mkoa wa Pwani. Mwisho wa siku wanafunzi hufanya mtihani wa taifa unaofanana. Matumizi ya vitabu vya kiada vya aina tofautitofauti unaweza kuwa wa manufaa kwa baadhi ya wanafunzi wakati baadhi ya wanafunzi wanaweza wasinufaike na mfumo huo. (Mwanafunzi, Pangani).

Hata hivyo, kulikuwa na watu wachache waliokuwa wakiunga mkono matumizi ya vitabu vya aina mbalimbali kutokana na sababu mbalimbali. Walikuwa wakibainisha kwamba matumizi ya vitabu vya aina mbalimbali huwapatia walimu uhuru na fursa ya kuchagua vitabu kulingana na mazingira yao. Pia waliongezea kwamba matumizi ya vitabu vya aina mbalimbali humjengea mwanafunzi uelewa mpana zaidi wa masuala au mada zinazofundishwa. Kwa mfano, mwanafunzi mmoja wa shule ya sekondari katika Wilaya ya Bukombe alikuwa na haya ya kusema:

“Kwa maoni yangu matumizi ya vitabu vya aina tofautitofauti vya kiada yanafaa kwa kuwa huwapatia walimu na wanafunzi uhuru na fursa ya kuelewa dhana kwa upana zaidi na kuzitumia katika kuelezea masuala mabalimbali”. (Mwanafunzi wa sekondari katika, Mufindi).

Baadhi walikuwa na maoni kwamba matumizi ya vitabu vya aina mbalimbali yanafaa kwa kuwa yanafanya ujifunzaji uwe wa vitendo zaidi kwa kuwa vitabu vinaweza kuandikwa kwa kuzingatia mazingira ya eneo fulani. Hali hii itakifanya kitendo cha kujifunza kilete maana na hivyo kuendana na mazingira ya wanafunzi. 2.3 Ushiriki wa jamii katika maendeleo na utekelezaji wa mtaalaUmuhimu wa ushiriki wa jamii katika maendeleo na utekelezaji wa mtaala hauwezi kupuuzwa. Ushahidi unaonyesha kwamba kadri familia na jamii inavyoshirikishwa zaidi ndipo mafanikio ya wanafunzi yanavyopatikana zaidi (Niemiec, Sikorskim na Walberg, 1999). Mtaala mzuri ni sharti uendane na matarajio na mahitaji ya jamii iliyolengwa. Kwa hiyo, jamii pamoja na wazazi yafaa washirikishwe

Page 21: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

17

katika kupanga mtaala ili mahitaji ya jamii yaweze kubainishwa katika mtaala. Katika utafiti huu, tumelenga kutathmini nafasi ya wazazi na ushiriki wao katika maendeleo na mchakato wa utekelezaji wa mtaala. Hii ilifanyika kwa kukusanya maoni ya walimu kwa njia ya mahojiano pamoja na majadiliano yaliyofanywa kupitia vikundi vya majadiliano kati ya wazazi na kamati za shule.

Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba wazazi na jamii kwa ujumla wanahusishwa kwa kiwango kidogo sana kwenye michakato ya utengenezaji wa mtaala. Matokeo haya yalitarajiwa kwa kuwa hata walimu ambao ndiyo watekelezaji wa mtaala wenyewe hawahusishwi kwa kiwango cha kutosha katika maendeleo na utekelezaji wa mtaala. Kwa ujumla wazazi pamoja na jamii japokuwa walikuwa wanauelewa kuhusu masomo ambayo watoto wao hujifunza shuleni, ilionekana kuwa hawana uelewa juu ya nini hasa watoto wao hujifunza shuleni.

Ilidhihirika kuwa idadi kubwa ya wazazi walikuwa hawana uwezo wa kuwasaidia watoto wao kwa kuwa walikuwa hawana maarifa na ujuzi wa kutosha kuweza kufanya hivyo. Hali hii inajidhihirisha kwa wazazi ambao watoto wao wanasoma katika shule za sekondari. Wazazi hawa walishindwa kuwasaidia watoto wao kutokana na kikwazo cha lugha. Wazazi wengi walilalamika kuwa masomo mengi ya sekondari yanafundishwa kwa Lugha ya Kiingereza ambayo wazazi walikuwa hawaimudi.

Baadhi ya maoni ya wazazi na wanajamii kuhusu ushiriki wao katika maendeleo na utekelezaji wa mtaala yameonyeshwa hapo chini.

...kwa kweli hatufahamu ni kwa kiwango gani watoto wetu wanajifunza. Wanaenda shule, wanarudi na vitabu, je nitajuaje wanachojifunza wakati mimi mwenyewe sikwenda shule (Mzazi, Malangali).

Hapana, hakuna mtu aliyewahi kuniuliza kuhusu nini watoto wangu wanajifunza shuleni. Nadhani hiyo ni kazi ya walimu, wao ndiyo wanaopaswa kufahamu kuhusu kile watoto wetu hujifunza shuleni [mtaala] . (Mazazi, Bukombe).

Ninachofahamu ni vitabu na vifaa vya shule ambavyo watoto wangu hubeba wanapoenda shule. Huwa naona wakibeba mabegi ya shule. Ninachofahamu ni kwamba kuna madaftari, vitabu na vitu vingine vya shule ambavyo hubeba. Lakini kusema kwamba nafahamu wanachofundishwa shuleni nitakuwa nadanganya (Mzazi, Ushirombo).

...Kwa hakika nafahamu masomo ambayo watoto wangu wanajifunza shuleni............Jiografia, Hisabati, Historia, na vitu kama hivyo. Lakini hakuna mzazi aliyewahi kuulizwa ili atoe maoni yake kuhusu kile ambacho watoto wanapaswa kufundishwa (Mzazi, Malangali).

Page 22: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

18

Ni vigumu kujua kile ambacho watoto wangu wanafundishwa kwa kuwa kila kitu kimeandikwa kwa lugha ya Kiingereza. Na hata unapouliza iwapo nawasaidia watoto wangu katika masomo yao, nitawasaidieje wakati masomo yao yapo katika lugha ya Kiingereza? (Mzazi, Mufindi).

2.4 Tathmini ya baadhi ya vitabu vinavyotumika kufundishia masomo mbalimbaliMfano halisi: Kitabu cha Hisabati Kidato cha Nne kilichochapishwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) na kitabu kimoja kinachotumka katika shule za sekondari kilichochapishwa na Kampuni binafsi ya Uchapishaji ya NN (NNP)

Vitabu vya kiada ni nyenzo muhimu katika utekelezaji wa mtaala. Kwamba, vitabu vilivyochaguliwa vilifanyiwa tathmini ili kubaini ufanisi wake katika kufanikisha na kuendeleza mtaala katika ngazi mabalimbali za ufundishaji na ujifunzaji. Uchambuzi wa vitabu hivyo vya kiada ulizingatia vigezo vitano (5) ambavyo ni pamoja na:

i) Jinsi vinavyosomekaii) Uwasilishaji wa madaiii) Jinsi vinavyoendana na muhtasariiv) Matumizi ya mifano na mazoeziv) Lugha iliyotumika kwenye kitabu

Kwa kuwa vitabu vinatarajiwa kutumiwa na wanafunzi wa ngazi inayofanana ya elimu na kwa kuwa inaaminiwa kwamba vimefuata muhtasari unaofanana, vitabu hivi vinatofautiana katika mpangiliano na uwasilishaji wa mada. Pia kuna tofauti katika kiwango cha uelezeaji na mpangilio wa mada. Katika sehemu hii, tunaelezea tofauti hizi kwa kutumia Kitabu cha Kiada cha Hisabati Kidato cha Nne.

Vitabu vyote vinatumika kama vitabu vya kiada katika shule za sekondari, ambapo baadhi ya shule hutumia vitabu vilivyotolewa na TIE wakati shule zingine hutumia vitabu vilivyotolewa na mchapishaji binafsi (NNP) aliyechaguliwa kutoka kwenye sampuli ya wachapishaji binafsi. Baadhi ya sifa za vitabu hivi zimeelezewa hapo chini.

(i) Kueleweka

Kitabu kilichotolewa na TIE kinaonekana kueleweka zaidi kuliko kile cha mchapishaji binafsi. Pia kitabu cha TIE kimetumia lugha ya Kihisabati katika kanuni za kihisabati bila kusahau herufi wakati kile cha mchapishaji binafsi kinatumia lugha ya kawaida. Pia, karatasi za kwenye kitabu cha TIE ni pana na zenye ubora wa juu ukilinganisha na zile za mchapishaji binafsi. Kwamba, kitabu kilichotolewa na TIE kinaeleweka zaidi ukilinganisha na kile kilichotolewa na mchapishaji binafsi.

Page 23: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

19

(ii) Uwasilishaji wa mada

Vilevile, katika uwasilishaji wa mada kitabu kilichochapishwa na TIE kimewasilisha mada zake vizuri zaidi ukilinganisha na kile cha mchapishaji binafsi. Mada zilizopo katika kitabu kilichochapishwa na TIE zimefafanuliwa na kuelezewa kwa undani zaidi na zimejumuisha mada zingine nyingi zaidi ukilinganisha na kile kilichotolewa na mchapishaji binafsi. Kwa mfano, katika uwasilishaji wa mada kuhusu maumbo ya perimeta ya kawaida, kitabu cha TIE kinaelezea kwa usahihi zaidi dhana ya umbo tenge wakati kitabu cha mchapishaji binafsi hakielezei maana ya dhana hii muhimu katika hisabati. Vilevile dhana ya majira ya nukta (vekta) inaelezewa kwa upana zaidi na kwa kutumia vielelezo na mifano katika kitabu cha TIE kuliko inavyoelezewa kwenye kitabu kilichochapishwa na mchapishaji binafsi.

(iii) Kuendana na muhtasari wa somo

Uwasilishaji wa mada katika kitabu cha mchapishaji binafsi kilichochaguliwa kutoka kwenye sampuli unaendana na muhtasari ukilinganisha na kitabu kilichotolewa na TIE. Kwa mfano, muhtasari unapendekeza kwamba fomula ya duara inatokane na kanuni ya pembe ya kampaundi, kitabu cha mchapishaji binafsi kinaelezea vizuri sana hapa ukilinganisha na kitabu kilichotolewa na TIE. Kwa ujumla uwasilishaji wa mada katika vitabu vyote unaendana na mwongozo ulitolewa kwenye muhtasari wa somo la Hisabati katika shule za sekondari.

(iv) Matumizi ya mifano na mazoezi

Inapendekezwa kwamba ni sharti vitabu vya kiada vitumie mifano mingi na viwe na mazoezi mengi ili kurahisisha ufundishaji na ujifunzaji wa dhana muhimu. Vitabu vyote vina mifano na mazoezi ya kutosha ijapokuwa kitabu cha TIE kinaonekana kuwa na mifano na mazoezi mengi zaidi ukilinganisha na kile kilichotolewa na mchapishaji binafsi. Vilevile muundo wa majibu unafanana kwa vitabu vyote na hivyo kuvifanya vitabu hivyo vifanane pia.

(v) Matumizi ya lugha na uwasilishaji

Tathmini ya kina ilifanywa kwenye mada katika vitabu vyote ili kubaini usahihi wa lugha iliyotumika na iwapo lugha hiyo ni ya kihisabati. Hili ndilo eneo linaloleta changamoto zaidi kwenye sera ya kutumia vitabu vya aina mbalimbali katika shule tofautitofauti. Tathmini yetu ilibaini makosa mengi ya lugha katika kitabu kilichochapishwa na kampuni binafsi ukilinganisha kile kilichotolewa na TIE. Baadhi ya makosa ya lugha na dhana yanayopatikana yameainishwa hapo chini:

Page 24: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

20

Makosa ya lugha

• Baadhi ya sentensi hazijakamilika. Kwa mfano, katika ukurasa wa 178 (kitabu cha mchapishaji binafsi), ‘imeandikwa, mstari unaounganisha sehemu mbili umelalia hasa’...Sentensi hii siyo sahihi.

• Katika ukurasa huohuo, sentensi moja imeandikwa kwa makosa kwamba ‘urefu upande mmoja badala ya ‘urefu katika upande mmoja.’

• Katika ukurasa wa 204, kikiripoti utafiti mmoja kitabu kimeandikwa kama ifuatavyo: ‘data zifuatazo zilirekodiwa kutoka kwenye shule moja ya sekondari [ilitakiwa iwe kutoka kwenye shule nyingi za sekondari] katika mkoa wa Dar es Salaam zikielezea mahudhuria ya wanafunzi kwa siku mbili. Vilevile sentensi katika kitabu cha mchapishaji binafsi ni ndefu na hazieleweki. Dhana ya pyramidi pia imechanganywa na haieleweki kwenye kitabu cha mchapishaji binafsi. Hali hii inawachanganya wanafunzi ukizingatia kwamba lugha ya Kiingereza ni lugha ngeni kwao kwa kiwango kikubwa.

Masuala ya dhana

• Kuna makosa ya dhahiri kabisa. Kwa mfano kitabu cha mchapishaji binafsi kinaelezea dhana ya mstari sambamba kuwa “iwapo mistari miwili au zaidi itakuwa imelala kwa usawa kuelekea upande wa hasi au chanya katika uelekeo wa mhimili kama inavyoonekana hapo chini, mistari hiyo huchukuliwa kuwa ni sambamba. Maelezo haya hayakidhi katika kuelezea dhana ya mistari sambamba. Kwa lugha rahisi mistari sambamba inaweza kuwa ‘mistari miwili au zaidi ambayo haiwezi kukutana inapochorwa’. Kitabu pia kimesahau ukweli kwamba kuna uwezekano kwa mistari sambamba kuvuka mhimili na bado ikawa ni mistari sambamba.

• Kosa jingine la dhahiri ni jinsi mchapishaji binafsi anavyoelezea dhana ya mabadiliko ya kompositi. Kitabu kinaelezea dhana ya mabadiliko ya kompositi kama ‘mabadiliko yanayojitokeza kwenye mchoro mmoja badala ya mabadiliko katika michoro mingi’.

• Katika ukurasa wa 24, mchapishaji binafsi ametumia dhana ya ‘kanuni ya utaratibu maalumu’, dhana ambayo ni ya zamani. Neno linalotumika ‘ukokotoaji wa pamoja wa hisabati zinazoendana’.

• Katika ukurasa wa 67, swali linasomeka, ‘tafuta perimeta ya umbo tenge 1 kutoka kwenye mduara wa kipenyo sentimeta 12. Hili pia ni kosa kwa kuwa hakuna umbo tenge lenye upande mmoja.

Page 25: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

21

2.4.1 MuhtasariUchambuzi wa vitabu vya hisabati uliofanywa hapo juu umeonesha kwamba matumizi ya vitabu vya kiada vya aina mbalimbali unaathari ubora wa elimu wanaoupata wanafunzi. Ni ukweli ulio dhahiri kwamba wanafunzi hupewa vitabu vyenye ubora na uwingi mbalimbali wa dhana kutoka kwenye vitabu mbalimbali ambavyo vinalenga darasa fulani. Kwa mfano, uchambuzi unaonesha kwamba vitabu mbalimbali vinaweza kutofautiana katika upande wa kueleweka, uwasilishaji wa mada na usahihi wa taarifa zinazopatikana katika kitabu husika. Kwa ufupi, ubora wa elimu unatofautiana katika vitabu viwili vilivyochambuliwa, wakati vitabu vingine vikitoa elimu bora vingine vinatoa elimu dhaifu.

Kwa uchambuzi uliofanyika hapo juu, kitabu kilichotolewa na TIE ni sahihi zaidi ukilinganisha na kile kilichochapishwa na mwandishi binafsi. Mapungufu yalijitokeza katika kitabu cha mchapishaji binafsi si madogo kwa kuwa yanahusisha uharibifu na upotoshaji wa dhana na taarifa. Hali hii inaibua maswali kuhusu Uidhinishaji Vitabu vya Kiada na jinsi Kamati ya Uidhinishaji wa Vitabu inavyofanya kazi zake.

Page 26: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

22

Sura ya Tatu

Muhtasari, Hitimisho na Mapendekezo

3.1 Matokeo ya utafiti kwa muhtasari na hitimishoUtafiti huu umezungumzia malengo makuu matatu. Kwanza, utafiti umefanya tathmini kuhusu athari za mtaala katika kutoa wahitimu bora. Pili, utafiti umefanya tathmini kuhusu athari za matumizi ya vitabu vya aina mbalimbali katika kutoa elimu bora. Tatu, umefanya tathmini kuhusu ushiriki wa jamii katika mchakato wa maendeleo na utekelezaji wa mtaala.

Mambo mengi yameibuka kutokana na matokeo ya utafiti. Kwanza, kwa mtazamo wa walimu na wanafunzi, mtaala uliopo haufai katika kufanikisha ujifunzaji pamoja na kutoa wahitimu wenye ubora unaohitajika. Washiriki walikosoa ufanisi wa mtaala uliopo kwa kuwa walikuwa na mashaka iwapo mtaala huo unaweza kutoa wahitimu mahiri na wenye ubora unaohitajika. Idadi kubwa ya washiriki walikuwa na maoni kwamba mtaala wa sasa hauna ufanisi wa kutoa wahitimu mahiri, wenye uwezo wa kujitegemea na wenye kutoa mchango muhimu katika jamii. Wadau pia walikuwa na maoni kwamba mabadiliko ya mtaala ambayo yamefanyika yamekuwa hayazingatii mahitaji ya jamii. Pia jamii imekuwa haishirikishwi katika michakato ya maendeleo na utekelezaji wa mtaala. Mabadiliko mengi katika mtaala yanaanzishwa na kutekelezwa na watunga sera kutoka katika ngazi za juu na kwamba mabadiliko hayo ya mtaala huwa hayawahusishi wadau wengine kama vile walimu, wanafunzi na wazazi.

Pili, matokeo ya utafiti yanaonyesha kwamba wanafunzi wengi wanaridhishwa na uwezo wa walimu wao katika kufanikisha mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji. Lakini idadi kubwa ya wanafunzi walikosoa ukosefu wa nyenzo za kufundishia na kujifunzia. Ukosefu wa vitabu bora vya kiada pamoja na nyenzo muhimu za kujifunzia kama vile vifa vya kufundishia pamoja na maabara za sayansi. Vyote hivi vimekuwa ni kikwazo kikubwa katika upatikanaji wa elimu bora mashuleni.

Tatu, athari za matumizi ya vitabu vya kiada vya aina mbalimbali zimeelezewa. Uchambuzi wa vitabu viwili uliofanywa umeonesha kwamba wanafunzi wa ngazi moja na darasa moja wanaweza kufundishwa mada za aina tofautitofauti ambazo zinatofautiana kwa uwingi na ubora. Hili ni tatizo kubwa ukizingatia kwamba wanafunzi wa Kitanzania wanafanya mitihani ya aina moja nchi nzima bila ya kujali tofauti za kijiografia. Kwa kuwa wanafunzi wanafanya mtihani wa aina moja ilikuwa inafaa pia wanafunzi wafundishwe mada zinazofanana. Matumizi ya kitabu cha kiada cha aina moja au nyingi pia yameibua hisia kubwa miongoni mwa wadau. Wadau wengi walipendekeza matumizi ya aina moja ya kitabu cha kiada nchi nzima. Kama ilivyoonekana hapo awali, bila shaka utaratibu huu unafaa ukizingatia kwamba nchi yetu inatumia mtaala wa elimu wa aina moja na kwamba wanafunzi wote wanatarajiwa kujifunza mada zinazofanana na pia wanatarajiwa kufanya mtihani wa aina moja. Matumizi ya vitabu

Page 27: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

23

vya aina tofautitofauti yanawafanya wanafunzi wajifunze mada zinazotofautiana na hii inaathari katika matokeo ya ujifunzaji kwa ujumla na hasa katika ufaulu kwenye mitihani.

Nne, utafiti huu umegundua kwamba kwa ujumla wadau wanahusishwa kwa kiwango kidogo sana katika michakato ya maendeleo na utekelezaji wa mtaala. Hii inatokana na ukweli kwamba wazazi na wanajamii hawashirikishwi katika maendeleo ya mtaala.

Tano, Matumizi ya Kiingereza kama lugha ya kufundishia pia yalionekana kama ni kikwazo kwa wazazi na wanajamii katika kushiriki kikamilifu kwenye utekelezaji wa mtaala. Pia ilibainika kwamba, nyenzo nyingi za kujifunzia zimeandikwa kwa lugha ya Kiingereza, lugha ambayo ni ya kigeni na haifahamiki kwa wazazi na wanajamii walio wengi. Kutokana na kikwazo hiki, wazazi waliowengi hawana uwezo wa kufuatilia kikamilifu kile ambacho watoto wao wanajifunza shuleni na kwa maana hiyo hawana uwezo wa kuwasaidia kwa kiwango kinachohitajika watoto wao.

3.2 Hitimisho/MapendekezoUpatikanaji wa elimu bora unategemea uwepo wa nyenzo bora za kufundishia na kujifunzia pamoja na ushiriki wa wadau muhimu katika michakato ya maendeleo na utekelezaji wa mtaala. Utafiti huu umebaini kwamba shule nyingi hapa nchini hazina nyenzo bora za kufundishia na kujifunzia. Ili kuboresha michakato ya maendeleo na utekelezaji wa mtaala, mapendekezo yafuatayo yametolewa.

i) Mfumo wa matumizi ya vitabu vya aina nyingi hauna tija kwa kuwa unawafanya wanafunzi wajifunze dhana zinazotofautiana wakati wakitarajiwa wafanye mtihani wa aina moja. Kwa mfano iwapo kitabu kimoja kitasema, ini ni sehemu ya ubongo na kitabu kingine kikasema ini linapatikana tumboni maana yake ni kwamba watoto watakuwa wanachanganywa. Hii ni kuwadanganya watoto ukizingatia ukweli kwamba upatikanaji wa vitabu hivi hauko sawa (baadhi watapata A, wengine watapata B), lakini wote wanatarajiwa kufanya mtihani wa aina moja na wanatarajiwa kutoa majibu sahihi.

ii) Raia wengi, wazazi, walimu na wanafunzi walipendekeza matumizi ya vitabu vya aina moja na kwa hiyo serikali inapaswa kuliangalia hili kwa faida ya wote na ili kuhakikisha kuwa kunakuwa na elimu bora. Kwa hiyo, kuna haja ya kuifanyia marekebisho sera ya matumizi ya vitabu vya kiada iliyopo kwa sasa ili iwe kama ilivyokuwa zamani ambapo kitabu cha aina moja kilikuwa kinatumika nchi nzima.

iii) Wakati soko huria la utengenezaji na usambazaji wa vitabu lililenga kupunguza upungufu mkubwa wa vitabu kuna haja ya kudhibiti ubora wa vitabu ili kuhakikisha kuwa vitabu vinavyopendekezwa kutumika mashuleni vinakuwa na ubora unaohitajika. Kwa sasa kama utafiti huu unavyoonesha, vitabu vinavyochapishwa na wachapishaji mbalimbali vinatofautiana sana kwa ubora na kwamba baadhi ya vitabu havina ubora unaohitajika. Ushiriki wa wazazi

Page 28: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

24

na wanajamii katika katika maendeleo na utekelezaji wa mtaala ni suala muhimu katika kufanikisha kitendo cha ujifunzaji kwa wanafunzi. Kwa sasa ushiriki wa wazazi na wanajamii katika maendeleo na utekelezaji wa mtaala ni mdogo hapa nchini, hali hii inawafanya wazazi na wanajamii na hali hii inawafanya wazazi na wanafunzi wasishiriki kikamilifu katika kufanikisha ujifunzaji wa watoto wao. Kwa hiyo, kuna haja ya kuchukua hatua madhubuti, kwanza kuwahamasisha wazazi na viongozi katika jamii juu ya umuhimu wa ushiriki wao katika maendeleo ya watoto wao. Pili, suala la mabadiliko ya mtaala ni sharti lizingatie maoni ya wadau wote muhimu ukijumuisha wazazi, walimu, wanafunzi na wanajamii wengine.

iv) Matumizi ya Kiingereza kama lugha ya kufundishia katika shule za sekondari inaonekana kama kikwazo kikubwa katika ushiriki wa wazazi katika kuwasaidia watoto wao kwa kuwa wazazi wengi hawaimudu lugha hiyo. Suala la lugha ya kufundishia limekuwa likiibua mijadala mizito na kwamba mwafaka umekuwa haufikiwi katika suala hili. Kuna haja kwa Serikali kuchukua hatua madhubuti katika kuongoza majadiliano kuhusu lugha ya kufundishia katika mfumo wetu wa elimu ili kufikia muafaka. Watoto hujifunza vizuri zaidi iwapo wataimudu lugha ya kufundishia. Suala hili linapaswa kutazamwa kwa makini zaidi ili kuhakikisha kuwa lugha ya kufundishia inafahamika vyema kwa walimu na wanafunzi.

v) Ukosefu wa nyenzo na vifaa vya kufundishia na kujifunzia ulionekana kama kikwazo katika utekelezaji wa mtaala. Tatizo hili ni kubwa zaidi kwa vitabu vya sayansi. Ukosefu wa nyenzo hizi za kufundishia na kujifunzia hauwezi kupuuzwa kwa kuwa umebainishwa pia kwenye tafiti zilizopita. Kuna haja kwa wasimamizi katika sekta ya elimu kutilia mkazo suala la upatikanaji wa nyenzo za kutosha za kufundishia na kujifunzia katika shule zetu kwa kuwa bila upatikanaji wa nyenzo hizo muhimu ufanisi katika utekelezaji wa mtaala hautakuwepo.

vi) Utekelezaji wenye ufanisi katika mtaala hutegemea mazingira bora ya kujifunzia. Wanafunzi wengi walioshiriki katika utafiti walikosoa mazingira ya ujifunzaji. Japokuwa walimu walipongezwa na wanafunzi wengi, bado mazingira yao ya kazi ni magumu kwa kuwa wanafundisha madarasa makubwa, kuna ukosefu wa nyenzo za kufundishia, nyumba zao za kuishi siyo bora, mishahara yao ni midogo na hawapati mafunzo ya mara kwa mara. Kuna haja kwa wadau wa elimu kuchukua hatua madhubuti ili kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto na hatimaye kuwafanya watoto wawe na furaha, wawe salama. Shule inapaswa kuwa sehemu ambayo itawafanya watoto wafanikiwe kitaaluma na kijamii.

vii) Cha kusikitisha idadi kubwa ya walimu walionekana kutofahamu vyema sera muhimu ambazo agenda ya elimu imejikita hapo. Sera ambazo idadi kubwa ya walimu walionekana kutozielewa ni kama vile MKUKUTA na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025. Kuna haja ya walimu kufahamishwa kuhusu sera hizi pamoja na kupewa mafunzo ya mara kwa mara ili kupanua uelewa wao. Suala hili ni muhimu ukizingatia kwamba mtaala wa elimu huwa haufanyi kazi

Page 29: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

25

peke yake bila kuhusisha sera zingine. Mtaala huakisi na unatengenezwa kwa kufuata mwelekeo wa sera na Dira ya maendeleo ya nchi.

viii) Mtaala wa sasa wa elimu unasemekana kwamba umelenga kumjengea mwanafunzi ujuzi maalumu katika ngazi fulani ya elimu na hili kwa kiwango fulani linaonekana kwenye njia za kufundishia zilizopendekezwa kwenye mihtasari ya masomo. Hata hivyo, utafiti huu haukuchunguza iwapo ufundishaji unaofanyanyika darasani unalenga kumfanya mwanafunzi apate ujuzi unaohitajika katika ngazi fulani ya elimu. Kuna haja ya kufanya utafiti ili kutathmini iwapo ufundishaji wa walimu unalenga kuwafanya wanafunzi wapate ujuzi unaohitajika katika mazingira ya sasa.

ix) Kuboresha maslahi ya walimu pamoja na kuwapatia mafunzo ni jambo muhimu katika upatikanaji wa elimu bora. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inapaswa kuhakikisha kwamba shule zinakuwa na walimu wa kutosha na wenye sifa ambao watapatiwa vifaa bora vya kufundishia na ambao watapewa mafunzo muhimu yanayohitajika pamoja na motisha ili kuwafanya wawe na moyo wa kufundisha kwa ufanisi. Kuwaweka walimu na wanafunzi kwenye shule ambazo hazina vifaa vya kutosha na kuwa na walimu wenye mafunzo hafifu na ambao hawana uwezo wa kutoa elimu bora ni kukiuka haki za watoto. Kibaya zaidi, hali hii ina athiri taifa zima hapo baadaye. Suala la mtaala bora na unaoendana na mazingira na upatikanaji wa walimu bora ni mambo ambayo hayawezi kuepukika katika mkakati wa taifa wa kutokomeza umasikini. Wakati umefika ambapo upatikanaji wa elimu bora na inayofaa inabidi upewe uzito wa pekee katika nchi hii ili kuwasaidia Watanzania kukabiliana na changamoto zilizopo na zinazolikabili taifa na mtu mmoja mmoja.

x) Kwa kuwa Kamati ya Uidhinishaji wa Vitabu vya Kiada (EMAC) ndiyo chombo kikuu katika kuhakikisha ubora wa vitabu katika shule zetu, kamati hiyo inapaswa ifanyiwe maboresho. Hii ni kwa sababu vitabu vingi vya kiada ambavyo vimepitishwa na kamati hiyo vina makosa ambayo yanawapotosha walimu na wanafunzi. Utafiti uliofanywa na HakiElimu (2010) kutathimini ubora wa vitabu vya Hisabati vya shule za msingi umebaini makosa mengi kwenye vitabu ambavyo vimeidhinishwa na EMAC. Kwa hiyo, EMAC ni muhimu iboreshwe. Uadilifu na uwajibikaji unafaa ndiyo uwe mwongozo katika kamati hiyo ili kuhakisha kuwa vitabu vinavyoidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya shule vinatathminiwa kwa uangalifu zaidi ili kuhakikisha kuwa vinakuwa na ubora unaohitajika. Kama EMAC inapitisha vitabu vibovu nchi itakuwa na wasomi wabovu na hatimaye kuwa na jamii ya wasomi bandia ambao hawataweza kusukuma guruduma la maendeleo la nchi. Na tutaendelea kubaki kwenye umaskini wa kutupa.

Page 30: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

26

Marejeo

Chonjo, P.N. (1994). The quality of education in Tanzanian primary schools: An assessment of physical facilities and teaching learning materials. Utafiti, 1(1), 36-46.

Egan, K. (2003). What is curriculum? Journal of the Canadian Association for Curriculum Studies, 1(1), 9-16.

Mosha, H.J. (1998). A re-assessment of the indicators of primary education quality in developing countries: Emerging evidence from Tanzania. International Review of Education, 34(1), 17-45.

Moulton, J. (1997). How do teachers use textbooks: A review of the research literature. Washington D.C: Academy for Educational Development.

Niemiec, R., Sikorski, M., & Walberg, H. (1999). Designing school volunteer programs. NASSP Bulletin, 83, 114-116.

Oduro, G.K.T., Dachi, H., & Fertig, M. (2008). Educational leadership and quality education in disadvantaged communities in Ghana and Tanzania. Paper presented at the Commonwealth Council for Educational Administration and Management Conference, Durban, South Africa, 8th-12th September 2008.

Oliva, P. (1997). The curriculum: Theoretical dimensions. New York: Longman.

Pring, R. (2004). Philosophy of Education: Aims, theory, common sense and research. London: Continuum.

Voorhees, R.A. (2001). Competence-based learning models: A necessary future. John Wiley & Sons, Inc.

Page 31: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

27

Page 32: Nani huamua Watoto wetu Wajifunze nini? - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/HakiElimu - Nani Huamua watoto wetu... · Mbinu za utafiti zilizotumika zinajumuisha mbinu

28