13
Ndoa na Nyumba Diocese-Based Leadership Training Program Mennonite Churches of East Africa (KMC/KMT) Joseph and Gloria Bontrager Theological Education Coordinators, ©2016

Ndoa na Nyumba - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level2/Ndoa-na-Nyumba.pdf · Agano linazidi mkataba. Agano linakaa juu ya uhusiano, kusudi ni kulinda uhusiano. Mkataba

  • Upload
    others

  • View
    66

  • Download
    5

Embed Size (px)

Citation preview

Ndoa na Nyumba

Diocese-Based Leadership Training Program Mennonite Churches of East Africa (KMC/KMT)

Joseph and Gloria Bontrager Theological Education Coordinators, ©2016

Ndoa na Nyumba, uk. 2

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania Produced by Joseph and Gloria Bontrager, Theological Education Coordinators ©2016

Yaliyomo

Somo Ukarasa

1. Mpango wa Mungu kuhusu Ndoa 3

2. Misingi ya Ndoa Imara 4

3. Ndoa ni Agano: Mfano wa Upendo wa Kristo kwa Kanisa 5

4. Kuimarisha Ukaribu na Uaminifu katika Ndoa 6

5. Majukumu katika Ndoa ya Kikristo 7

6. Kuwajibika katika Ndoa 8

7. Watoto – Baraka ya Mungu katika Nyumba 9

8. Madhara katika Ndoa 10

9. Usimamizi na Matumizi ya Pesa 11

Mapendekezo kuhusu matumizi ya pesa 12

10. Mapambano na Maumivu katika Ndoa 13

Hakuna msingi mwingine mtu anaweza kuuweka isipokuwa ule uliokwisha kuwekwa, yaani Yesu Kristo. 1 Wakorintho 3:11

Ndoa na Nyumba, uk. 3

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania Produced by Joseph and Gloria Bontrager, Theological Education Coordinators ©2016

Somo la 1. Mpango wa Mungu kuhusu Ndoa

Soma Mwanzo 1 – 2

Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na

mwanamke aliwaumba. Mwanzo 1:27

1. Mungu aliwaumba mume na mke kwa sura yake. Mume na mke pamoja huonyesha

mfano wa Mungu kwa ukamilifu kuliko mtu peke yake. Mungu ni upendo, na upendo ni

uhusiano. Ndoa ni uhusiano wa umoja na upendo kati ya mume na mke (Mwanzo 2:24).

Je, ni nani aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu? Mwanaume? Mwanamke? Wote

wawili?

Kwa vipi ndoa inaonyesha mfano wa Mungu?

2. Mzaidizi wa kufanana naye kwa Adamu. Adamu aliwaita wanyama wote kwa majina

yao na wote walikuwa na mwenzake aliyefanana naye. Ila hakuonekana wa kumsaidia

Adamu aliyefanana naye. Mungu alisema, Si vema huyo mtu awe peke yake. Adamu

alihitaji mwenzi kwa kushirikiana naye na kushirikisha maisha yake. Mungu alifanya

mwanamke na kumletea mwanaume (Mwanzo 2:18-22).

Je, Adamu alisemaje alipomwona huyo mwenzi Mungu aliyemfanyia? (Mwanzo

2:22-23)

Maneno gani yanaeleza uhusiano kati ya Adamu na Hawa? (Mwanzo 2:24-25)

3. Mungu aliwabariki wote wawili na kuwaagiza wote wawili sawa, Zaeni, mkaongezeke,

mkaijaze nchi, na kuitiisha (Mwanzo 1:28).

Uhusiano kati ya Adamu na Hawa ulihusisha pia Mungu, Mtoaji wa Uzima na Baraka. Ni

mpango mkamilifu wa Mungu kwa ndoa. Na Mungu alisema, “ni chema sana” (Mwanzo

1:31). Adamu na Hawa waliumbwa wawe pamoja, kumbatana, kuwa mwili mmoja, uchi,

wala hawakuona haya (Mwanzo 2:24-25). Uumbaji wa mume na mke ulitimiza mpango

na mapenzi wa Mungu (Ufunuo 4:11).

4. Adamu na Hawa walimwasi Mungu na mpango mkamilifu wa Mungu ulivunjika.

Wakati Adamu na Hawa walipokula kwa mti wa ujuzi wa mema na mabaya, uhusiano

mkamilifu na Mungu na wao kwa wao ulivunjika. Waliona haya na hofu (Mwanzo 3:7-

10) na walianza kushtakiana kuhusu uasi wao (Mwanzo 3:12-13).

Dhambi ilifanyaje uhusiano wao na Mungu? Kati ya Adamu na Hawa?

Dhambi alifanyaje uumbaji wote? (Mwanzo 3:17)

Dhambi ya Adamu ilitufanyaje sisi? (soma Warumi 5:18-19)

Maswali ya Kujadiliana:

1. Sisi binadamu tunaonyeshaje mfano wa Mungu?

2. Kwa njia gani wanaume na wanawake wanatofautiana katika kuonyesha mfano wa

Mungu?

3. Soma Ufunuo 4:11. Je, Mungu alikuwa na kusudi gani katika kumwumba binadamu?

4. Eleza maana ya maneno “kuwa mwili mmoja,” katika Mwanzo 2:24-25. Eleza maana ya

“kuacha,” “kuambatana,” na “uchi, wala hawakuona haya.”

5. Je, unavyoona, Adamu na Hawa walifurahia maisha yao ya pamoja? Eleza jibu lako.

6. Je, unataka kuuliza maswali gani zaidi kuhusu kusudi ya Mungu kwa ndoa?

Ndoa na Nyumba, uk. 4

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania Produced by Joseph and Gloria Bontrager, Theological Education Coordinators ©2016

Somo la 2. Misingi ya Ndoa Imara

Mungu asipojenga nyumba, waijengao wafanya kazi bure.

Bwana asipoilinda nyumba, ailindaye akesha bure. Zaburi 127:1

1. Kusudi ya Mungu kwa Ndoa. Ili ndoa zetu ziwe imara, tunategemea hekima na uongozi

wa Mungu katika kusudi ya ndoa na jinsi ya kuweka msingi imara. Msingi imara wa ndoa

huanza kwa kuelewa mpango wa Mungu, jinsi ulivyokuwa kabla ya binadamu kufanya

dhambi. Ni uhusiano ya watatu, ambao ni Mungu, mume, na mke. Uhusiano kati ya

mume na mke ni imara ukiwa na Mungu pia.

Dhambi ya Adamu ha Hawa ilisababisha aibu (7), kutengwa na Mungu (8), hofu (10),

kushtakiana (12); kuzaa kwa uchungu; kutaka kutawala (16); na ardhi kulaaniwa (17).

2. Nguzo nne za ndoa imara – kutoka Mwanzo 1:27-28; 2:18

Kila nguzo uliharibika kwa sababu ya kutomtii Mungu. Lakini nguzo zote nne ni muhimu

kwa ndoa imara.

1) Mfano wa Mungu (Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, mume na mke. 1:27)

▪ Mpango wa Mungu: Ndoa ni mfano wa upendo, uaminifu, na umoja wa Mungu.

▪ Dhambi iliharibu mfano wa Mungu – roho, akili, uchaguzi, na mwili (kifo).

2) Kujenga uzima katika jamaa na jamii (Zaeni, mkaongezeke. 1:28)

▪ Mpango wa Mungu: Watoto kuleta furaha na huduma.

▪ Dhambi ilisababisha uchungu katika kuzaa; Kaini na Habili washindana (4:8)

3) Kuimarisha utawala wa Mungu (mkaijaze nchi, na kuitiisha. 1:28

▪ Mpango wa Mungu: Ndoa huleta uzima kwa njia ya imani na utii.

▪ Dhambi: Ardhi ililaaniwa; Adamu na Hawa kutolewa katika Edeni.

4) Uhusiano imara kati ya mume na mke (Si vema huyo mtu awe peke yake 2:18)

▪ Mpango wa Mungu: Ndoa unajengwa kwa uaminifu kati ya mume na mke.

▪ Dhambi: Adamu na Hawo walishtakiana, na kutaka kutawala mwenzake.

3. Ukombozi hujenga tena nguzo zilizoharibika

Kurejesha Mfano wa Mungu, nafsi, roho, na mwili. 1 Wathesalonike 5:23

Kufanya jamaa kuwa mahali malezi katika amani, adabu na maonyo. Waefeso 6:4

Kuleta Ufalme wa Mungu wa haki, amani, na furaha. Warumi 14:17

Ndoa kuimarishwa kwa utakatifu na ukweli. Waefeso 4:24-25

Laana juu ya ardhi na uchungu kwa Adamu na Hawa hazikuwa hukumu ya Mungu. Ni

matokeo ya binadamu kujitenga na Mungu. Mungu ni chanzo cha Uzima na Baraka, na

tukitenganishwa na Chanzo wa Uzima na Baraka, tokeo ni mauti na uchungu. Ndoa iwe

mfano wa ukombozi, kurejesha mpango wa Mungu wa kuleta baraka.

Kwa mazungumzo:

1. Ndoa ya kwanza ilifungwa lini? Ndoa na kusudi ya ndoa ni nini? Mwa 2:24-25; 4:1

2. Katika ndoa yako na ya wengine, kuna mambo gani yanajenga uhusiano? Ni mambo

gani yanaharibu uhusiano?

3. Je, kwa vipi ndoa ni mfano wa Utatu Mtakatifu wa Mungu?

4. Lini mume alianza kumtawala mke? Je, utawala huo ulikuwa mpango wa Mungu?

5. Je, agizo katika Mwanzo 2:24, “kuacha baba na mama na kuambatana na mkewe”

linafaa katika ndoa za kiafrika?

6. Eleza mawazo yao juu ya tabia ya uhusiano imara kati ya mume na mke.

Ndoa na Nyumba, uk. 5

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania Produced by Joseph and Gloria Bontrager, Theological Education Coordinators ©2016

Somo la 3. Ndoa ni Agano: Mfano wa Upendo wa Kristo kwa Kanisa

Kwa sababu Muumba wako ni mume wako. Isaya 54:5

Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa. Waefeso 5:25

1. Agano. Katika Agano la Kale, Mungu alionyesha uaminifu wake kwa watu wake teule

kwa njia ya agano. Eleza namna ya maagano katika mistari inayofuata:

Mwanzo 9:8-11

Mwanzo 17:1-8

Agano linazidi mkataba.

Agano linakaa juu ya uhusiano, kusudi ni kulinda uhusiano.

Mkataba ni mapatano, kusudi ni kutimiza masharti ya mapatano.

2. Kristo na kanisa. Waandishi wa Biblia walieleza ndoa kama mfano wa uhusiano kati ya

Mungu na watu wake katika Agano la Kale, na kati ya Kristo na kanisa katika Agano

Jipya. Jinsi tunavyoelewa upendo wa Mungu kwa Israeli na kwa kanisa, ndivyo

tunavyoweza kuelewa mpango wa Mungu kwa ndoa. Na ndoa ni mfano na kueleza

uhusiano wetu na Mungu. Soma mistari ifuatayo kwa jinsi inavyohusu ndoa:

Yohana 3:16. Nini ilimfanya Mungu kutoa Mwanawe ili kuokoa ulimwengu?

Yohana 13:34. Yesu alitoa amri gani mpya kwa wanafunzi wake?

Yohana 15:12-13. Ni nini Yesu aliwaambia wanafunzi ni ishara kuu ya upendo?

1 Petro 2:9-10, 21. Kama watu wateule wa Mungu, tumeitwa kufanya nini? (mst.9)

3. Ndoa ni agano kati ya mume na mke, ni uhusiano wa upendo na uaminifu kati yao. Yesu

ni mfano wetu wa upendo, unyenyekevu, na utumishi. Mistari inayofuata inaeleza mfano

wa Yesu ambao sisi tumeitwa kuufuata.

Wafilipi 2:1-8. Kuna tabia gani za Yesu zinatajwa katika mistari hii?

Waefeso 5:1-2. Je, kwa njia gani tunafuata mfano wa Kristo?

Waefeso 5:21. Eleza maana ya kunyenyekeana katika ndoa.

Waefeso 5:24. Je, vipi kanisa linamtii Kristo? Vipi mke atamtii mume wake?

Waefeso 5:25-27. Je, Kristo alionyeshaje upendo wake kwa kanisa? Upendo wa Yesu

unatuonyeshaje jinsi waume wapaswa kuwapenda wake zao?

Kama washiriki katika mwili wa Kristo, tunajitoa kwa kanisa, kupendana, kuheshimiana, na

kuhudumiana kwa unyenyekevu.

Hivyo katika ndoa zetu inatubidi kushika agano tulilofanya kwa tabia za upendo, heshima,

unyenyekevu, na kuhudumiana.

Maswali ya kujadiliana:

1. Wengine wanaelewa ndoa kama mkataba kati ya watu wawili. Je, kuna tofauti gani kati

ya mkataba na agano? Je, agano laweza kuvunjwa?

2. Eleza jinsi upendo wa Kristo kwa kanisa ni mfano wa mume kumpenda mke wake.

3. Je, kuna tofauti gani kati ya ndoa ya kikristo na ndoa ya kimila? Je, Mungu anaziona ndoa

hizo tofauti?

4. Je, kuna faida gani katika kufunga ndoa ya kikristo?

Ndoa na Nyumba, uk. 6

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania Produced by Joseph and Gloria Bontrager, Theological Education Coordinators ©2016

Somo la 4. Kuimarisha Ukaribu na Uaminifu katika Ndoa

1. Ndoa ni agano kati ya watu wawili, ni ahadi kujitoana kwa maisha yote. Kuona ndoa

kama agano ni kutambua thamani ya uhusiano kati mwetu na kuimarisha ndoa. Tutaacha

ubinafsi na kuona mke au mume wetu ni baraka ya thamani kutoka Mungu, kama hazina

inayotupasa kuilinda (1 Petro 3:7).

Kuhusu ukaribu. Mungu ametuumba kuhitaji na kutamani ukaribu. Watu wengi

wanaelewa ukaribu kama uhusiano wa kimwili tu. Lakini ukaribu wa kimwili tu hauwezi

kuridhisha haja yetu ya ukaribu. Msingi wa ukaribu wa kimwili au wa kingono

unaoridhisha ni ukaribu wa kiroho.

Kuna ukaribu wa namna mbalimbali kufuatana na mahusiano mbalimbali, kwa mfano

mzazi na mtoto, mume na mke, marafiki na wenzi, wengine wanaume na wengine

wanawake. Katika kila uhusiano kuna matendo yanayoruhusiwa na yasiyoruhusiwa,

tunayaita mipaka. Kwa mfano, jinsi tunavyohusiana na rafiki ni tofauti na jinsi

tunavyohusiana na mume au mke, au mtoto.

2. Ukaribu wa kweli ni kumkaribia na kumfahamu mtu mwingine, na kumwelewa kwa

ndani. Ukaribu unaanza kama urafiki na kushinda muda pamoja. Ni kuona thamani yake

na kuweza kushirikisha wazi mawazo yako, matumaini na hofu zako. Unapoweza

kumwamini mtu bila hofu ya kukataliwa, mtaweza kushirikiana furaha na uchungu, na

kuzidi kushiriki imani na matumaini ya maisha. Ukaribu ni kukua pamoja na kufurahia

ushirikiano kati mwenu. Ukaribu ni kuacha familia ya asili na kujitolea kwa mke au

mume kama uhusiano wa kwanza. Ukaribu wa kweli ni kuungana roho, nafsi, na mwili.

3. Ukaribu wa kingono ni baraka kutoka kwa Mungu, ikiwa katika agano la ndoa. Ni

mpango mkamilifu wa Mungu kwa binadamu, iliyotolewa kabla ya dhambi kuingia

duniani. Agizo la Mungu “zaeni na kuongezeka” ni kufurahia ukaribu wa kingono.

Mithali 5:18-20; Wimbo Ulio Bora 4:10; Waebrania 13:4. Mistari hiyo inaelezaje

uzuri wa ukaribu wa kingono?

1 Wakorintho 6:13b-20; 7:1-5. Mistari inafundisha nini kuhusu ngono halali na isiyo

halali?

Wengine wanaamini kwamba tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya lilikuwa

ngono. Lakini tunda la ni mfano wa jinsi binadamu anavyofuata tamaa zake na kutegemea

akili zake (mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, na kutamanika kw maarifa.

Mwanzo 3:6).

Ngono katika ndoa ni baraka kutoka Mungu, kwa furaha zetu na kuzaa watoto. Ila,

matendo ya ngono nje ya ndoa, yaani uzinzi na uasherati, huleta aibu na hofu.

Maswali ya kujadiliana:

1) Soma Waebrania 13:4. Kwa nini ndoa haiheshimiwi kama ilivyoheshimiwa wakati wa

nyuma, na ngono imekuwa jambo la kuficha badala ya lisilo na lawama wala aibu?

2) Zungumzia namna mbalimbali za ukaribu katika dunia yetu. Kwa kila namna ya

ukaribu, ni maadili (mipaka) gani yanafaa? Je, kuna faida gani katika kuweka mipaka

kwa mwenendo?

3) Je, Mkristo anaweza kuwa na umoja wa kweli na mtu asiyemwamini Mungu?

4) Zungumzia mambo yanayozuia ukaribu wa kweli.

Ndoa na Nyumba, uk. 7

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania Produced by Joseph and Gloria Bontrager, Theological Education Coordinators ©2016

Somo la 5. Majukumu katika Ndoa ya Kikristo

Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba,

mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mwanzo 1:27

1. Mungu alimwumba binadamu kwa mfano wake, mume na mke. Kama wanaume na

wanawake walivyo tofauti kimwili, ndivyo walivyo tofauti kwa tabia. Wanawake wana

mwili wa kuzaa, na tabia ya kulea, huruma na ukarimu, na wanajali na kulinda

mahusiano. Tabia ya wanaume huwa ni nguvu, uongozi, uamuzi, kujenga na kuimarisha,

na wanajali na kulinda kazi. Tabia hizo kwa kawaida ni kweli kwa wanawake au

wanaume, na wakati mwingine wanazishiriki. Lakini tabia hizo zote ni muhimu kwa

uzima na kuimarisha familia, jamii, na kanisa.

Mwanaume na mwanamke waliumbwa sawa kwa hali na kazi. Katika tamaduni nyingi,

wanawake wanahesabiwa kuwa chini ya wanaume. Yesu alianza kuvunja desturi hiyo

kwa kuheshimu wanawake. Paulo aliandika kwamba katika Kristo, hapana mtu mume

wala mtu mke (Wagalatia 3:28). Katika ukombozi, Mungu anarejesha hali ya usawa.

2. Tangu mwanzo, kusudi ya Mungu ni wanaume na wanawake kushiriki kazi na hivyo

kukamilishana. Ila kwa sababu ya dhambi, watu wanashindana na kutafuta utawala juu ya

mwenzake. Yesu alituita kutumikiana (Mathayo 20:25-28). Waume na wake wanaitwa

kunyenyekeana (Waefeso 5:21).

Mungu alimwumba Hawa kuwa msaidizi wa kufanana naye Adamu (Mwanzo 2:18).

Katika lugha ya asili, neno msaidizi linaeleza pia Mungu msaada wetu, anayetuwezesha

(Zaburi 70:5; 121:2). Hivyo, msaidizi si mtumishi wa hali ya chini, bali anayetukaribia na

kutembea nasi ili kutuwezesha katika huduma au hali ngumu. Hawa aliumbwa ili kufanya

pamoja na Adamu kama mwenzake, na kumkamilisha.

3. Katika ndoa imara, mume na mke wanahudumiana na kuhudumia jamaa yao, kila

mmoja kufuatana na uwezo na tabia yake. Majukumu katika ndoa yanafuata uwezo wa

kimwili, kazi iliyopo, mila, desturi za kidini, au mapenzi ya mtu mwenyewe.

1 Timotheo 5:8. Je, jukumu gani la muumini wa Kikristo linatajwa?

1 Timotheo 5:10, 14. Je, wajane katika kanisa walipaswa kushika majukumu gani?

Kumbukumbu 6:6-8. Je, Mungu alitoa agizo gani kwa wazazi?

1 Wathesalonike 2:11-12. Je, kufuatana na mfano wa Paulo, majukumu ya baba kwa

watoto wake ni mambo gani?

Maswali ya kujadiliana:

1. Eleza namna ya uhusiano katika ya wanaume na wanawake katika mila na desturi za

kiafrika.

2. Katika mila na mazoea ya dunia yetu, je, ni majukumu gani hayafai kwa wanawake?

Majukumu gani hayafai kwa wanaume? Toa mifano.

3. Taja majukumu mbalimbali katika nyumba na jamaa. Majukumu gani ni kwa mume

na mke pamoja? Na majukumu gani ni ya mume au mke tu?

4. Mithali 31:1-31. Majukumu gani ya mke yanatajwa katika mistari hiyo?

5. Warumi 12:4-8. Roho Mtakatifu anagawa vipawa kwa huduma kanisani. Je, ni

vipawa vingine kwa wanaume tu? Vingine ni kwa wanawake tu?

6. Injili itatusaidiaje kujua majukumu ya kila mtu katika ndoa?

Ndoa na Nyumba, uk. 8

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania Produced by Joseph and Gloria Bontrager, Theological Education Coordinators ©2016

Somo la 6. Kuwajibika katika Ndoa

1. Matarijio ya ndoa. Katika mafundisho ya kikristo na mazoea ya kimila, ndoa ni ahadi

kati ya watu wawili inayoshuhudiwa na jamii. Ndoa huanzisha uhusiano mpya katika

watu wawili, ni mwanzo wa mji mpya, na jamaa mpya watakapozaa watoto. Jamaa, jamii,

na kanisa wanaonyesha uthibitisho wao kwa njia ya maneno ya baraka, maombi, mahari,

na zawadi. Ushuhuda huo kutoka kanisa au jamii unathibitisha uhalali wa ndoa mbele ya

watu. Na jamii wanatarajia kwamba waliounganishwa katika ndoa watawajibika kushika

masharti ya ndoa.

Taja matarajio ya kawaida kwa watu wawili waliofunga ndoa (kwa mfano, wanakaa

pamoja katika nyumba moja, watakuwa na watoto, n.k.).

Mwanzo 2:24-25. Adamu alipewa maagizo gani alipopokea mke?

1 Wakorintho 7:2-5. Eleza mafundisho ya kanisa la awali kuhusu wajibu muhimu ya

waume na wake. Ni wajibu gani? (kuhusu haja na furaha za kimwili za mwenzake).

1 Wakorinto 6:13-20; Waebrania 13:4. Je, Agano Jipya linasema nini kuhusu

kujamiiiana nje ya ndoa?

2. Kujenga imani kati ya mume na mke. Uhusiano wa ndoa ni kiumbe kilicho hai,

usipolishwa na kutunzwa, utakuwa dhaifu na mwisho itakufa. Lakini ukilishwa na

kutunzwa vizuri, utazidi kuwa na nguu na kuzaa matunda. Jambo la muhimu katika

kuimarisha ndoa ni kujenga imani kati ya mume na mke. Imani inajengwa na uaminifu,

kushirikiana wazi, na kushika ukweli katika njia zote.

Waefeso 4:15. Mstari huu unashauri nini ili kujenga imani?

Warumi 13:8. Mstari huu unataja jukumu gani kwa waumini?

Maswali ya kujadiliana:

1. Je, majukumu katika ndoa yanatofautiana vipi katika mazingira au mila mbalimbali?

2. Muumini wa kikristo akaaye kati ya mila na tamaduni ya asili , je, atajuaje ni

majukumu gani anapaswa kuyashika? Kwa mfano, mahari, mitara, uaminifu kwa mke

mmoja, na kushiriki pesa.

3. Je, katika ndoa, mume na mke wanapaswa kila mmoja awe na majukumu yake tofauti,

au kuna majukumu mengine wanaweza kushiriki? (kwa mfano, kupika, kulima, kulea

watoto, kufanya kazi ya mshahara, n.k.)

4. Katika mila fulani, uaminifu wa kingono ni jukumu la mke tu. Je, kuna shida gani

katika desturi hiyo?

5. Je, kujamiiana nje ya ndoa kunaleta madhara gani?

6. 1 Timotheo 5:8. Kuzaa watoto na kuwatunza ni jukumu la kawaida katika ndoa. Je,

wataamuaje wakitaka watoto wengi lakini pia wanahitaji kuwatunza vizuri?

7. Je, utaweza kufanya nini ili kujenga imani kati yenu katika ndoa?

Ndoa na Nyumba, uk. 9

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania Produced by Joseph and Gloria Bontrager, Theological Education Coordinators ©2016

Somo la 7. Watoto – Baraka ya Mungu katika Nyumba

“Hapa Afrika, watoto ni dalili ya ndoa imara” Gladys Mwiti, Christian Counseling

1. Watoto ni baraka kutoka Mungu. Agizo la kwanza la Mungu kwa Adamu na Hawa ni

“zaeni na kuongezeka” (Mwanzo 1:28). Kila mtoto anayezaliwa ni baraka kutoka Mungu,

ni ishara ya neema ya Mungu. Wengine wanaona watoto watasaidia kuzalisha chakula

kwa ajili ya familia. Au watoto wanapewa majina ya mababu, ili kuendeleza ukoo. Katika

makundi mengine, utasa ni sababu ya mume kutafuta mke wa pili.

Soma Zaburi 127 na 128. Maneno gani yanaeleza kwamba watoto ni ishara ya

baraka ya Mungu?

2. Majukumu ya wazazi kwa utunzaji wa watoto. Katika mistari hapo chini, kuna

majukumu gana yanatajwa:

Mithali 22:6.

Mithali 29:17.

Kumbukumbu 6:6-9.

Waefeso 6:4.

Nyumba ni mahali pa malezi, pa kujifunza imani, maadili na mwenendo kupitia mfano na

mafundisho ya wazazi (2 Timotheo 1:5). Nyumba si jengo tu mnapokaa, ni mahali pa

faraja, starehe, na kushiriki amani na furaha. Wazazi wanaomheshimu Mungu wanajenga

msimamo na kulea watoto wenye uzima na ni baraka katika jamaa na kwa wengine.

Soma Waefeso 6:1-3. Maagizo makuu mawili kwa watoto ni nini?

Utasa mara nyingi ni shida ya kimwili iliyo changamoto katika ndoa. Shida inaweza

kuwa kwa mume au kwa mke, na huenda inaweza kutibiwa na madaktari.

Utasa hausababishwi na laana. Katika Biblia, wanawake walioshindwa kuzaa wakati

mwingine walizaa baadaye mtoto aliyekuwa muhimu katika kazi ya Mungu (kwa mfano

Isaka, Samweli, Yohana Mbatizaji). Akina mama hawa (Sara, Hana, Elisabeti) walikuwa

waaminifu kwa Mungu licha ya utasa, na Mungu aliwabariki.

Mungu anatumia na kuwabariki watu waaminifu hata kama hawana watoto . Wanandoa

katika hali ya utasa watafute ushauri kuhusu matibabu pamoja na kuomba na kuombewa

ili waone mapenzi ya Mungu. Huenda Mungu anawaandaa kwa kazi au huduma maalum.

Isaya 54:1-5. Mke tasa anaandaliwa kwa kusudi maalum na kubarikiwa na wengi

ambao ataweza kuwaita watoto wake.

Zaburi 113:7-9. Bwana anawainua wanyonge, maskini, na aliye tasa.

Zaburi 27:14. Katika hali ya shida, upige moyo konde, umngoje Bwana.

Maswali ya kujadiliana:

1. Zaburi 128:3-4 inasema watoto ni baraka ya Mungu kwa mtu amchaye Bwana. Je,

vipi mtu asiyemcha Bwana lakini anazaa watoto?

2. Je, watoto waasi pia wanaweza kuhesabiwa baraka kutoka Mungu?

3. Kufuatana na gharama ya elimu na kulea watoto, je, inabidi wazazi kubadilisha

mawazo yao kuhusu idadi ya watoto?

4. Kwa ndoa yenye hali ya utasa, je, msaada ni mitara tu, au kuna njia nyingine?

Ndoa na Nyumba, uk. 10

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania Produced by Joseph and Gloria Bontrager, Theological Education Coordinators ©2016

Somo la 8. Madhara katika Ndoa

Upendo wa Kristo kwa kanisa ni mfano wa ndoa imara. (Waefeso 5:28-32). Mambo

matatu yanayoharibu ndoa ni mawasiliano yanayodhuru, ushawishi kutenda maovu, na

uasherati.

1. Mawasiliano yanayodhuru. Mawasiliano kati ya mume na mke ni lazima kwa ndoa

imara. Imesemwa kwamba mawasiliano ya kila siku ni gundi inayounganisha mtu na

ukweli, pia na mwenzake. Maneno yanabariki au kulaani (Yakobi 3:9-10). Maneno

yanageuza hasira au kuichochea (Mithali 15:1). Maneno yanachoma kama upanga au

kuleta afya (Mithali 12:18; 16:24).

Kusikiliza ni sehemu muhimu ya mawasiliano. Ili kumwelewa mwenzetu, inatubidi

kwanza kusikiliza anayosema. Maneno yetu yawe na neema siku zote (Wakolosai 4:6), ya

kufarijiana na kujengana (1 Wathesalonike 5:11).

Amosi 3:3. Je, wawili wanaotaka kutembea pamoja wafanyeje?

Wakolosai 3:8-9. Mistari hii inataja maneno gani ya madhara?

Wakolosai 3:16-17. Je, mazungumzo yetu yawe namna gani?

Yakobo 1:19. Mstari huu unasemaje kuhusu kusikiliza?

2. Ushawishi kufanya maovu. Mungu aliumba ndoa iwe msaada na nguvu. Lakini mume

au mke anaweza kumshawishi mwenzake kumwasi Mungu. Mifano miwili ni Adamu na

Hawa, na Abramu na Sarai.

Mwanzo 3:1-6. Nyoka alimshawishi Hawa kumwasi Mungu, Hawa alileta tunda kwa

Adamu, naya alikula. Ingalikuwaje kama wangaliongea kabla ya kula kuhusu

ushawishi wa nyoka?

Mwanzo 12:10-19. Abramu alifanya nini kumshawishi Sarai kutomtii Mungu?

Aidha, umoja kati ya mume na mke unaweza kutia nguvu katika kumtii Mungu,.

Waebrania 10:24. Ushauri wa kuhimizana katika upendo na kazi nzuri.

Matendo 18:24-26. Akila na Prisila walitiana nguvu kwa vipi? Walitumikia kanisa

kwa huduma gani?

3. Uasherati. Katika Agano la Kale, uzinzi ulikataliwa katika Amru Kumi (Kutoka 20:14).

Tunaitwa kuishi kwa usafi na utakatifu (1 Wakorintho 6:9-11). Tunaagizwa kumtukuza

Kristo na kuwa safi, kwa sababu mwili wetu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani

yetu. Uzinzi ni dhambi juu ya mwili wetu, na juu ya Roho wa Kristo ndani yetu (1

Wakorintho 6:15-20).

Je, zinaa inaweza inaleta dhara gani kwa mwili? Kwa roho? Kwa mahusiano na mke

au mume, familia, na watoto?

Je, uasherati na zinaa zinaleta dhara gani kwa kanisa?

Soma 1 Wakorintho 7:1-5. Paulo alitoa ushauri gani kuhusu kutawala tamaa za

ngono?

Maswali ya kujadiliana:

1. Je, unakubali usemi, “Matusi yanaumiza sawa na mapigo ya kimwili”?

2. Kwa nini waume au wake wanatoka nje ya ndoa ili kuridhisha tamaa zao za kimwili?

3. Je, mawasiliano yenye afya yanawezaje kuzuia madhara katika ndoa?

Ndoa na Nyumba, uk. 11

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania Produced by Joseph and Gloria Bontrager, Theological Education Coordinators ©2016

Somo la 9. Usimamizi na Matumizi ya Pesa

1. Matumizi ya pesa ni chanzo cha matatizo katika ndoa nyingi. Watu waliolelewa

katika jamaa tofauti wanaweza kutofautiana kuhusu namna ya kusimamia mji na kuhusu

matumiza ya pesa. Huenda wanaweza kutofautiana kuhusu pesa wanazopata kwa ajira au

biashara yao. Wasipotoa nuru kuhusu pesa zao, na pesa zinapungua kwa utunzaji wa

jamaa, inaweza kusababisha ugomvi na shida katika uhusiano.

2. Biblia inaeleza mengi kuhusu pesa. Katika mafundisho yote ya Yesu, maneno 15 kwa

mia (15%) yanahusu pesa. Kwa nini Yesu alifundisha kuhusu pesa? Yesu alijua pesa ina

nguvu katika maisha ya mtu binafsi na katika mahusiano. Maandiko yafuatayo

yanafundisha nini kuhusu pesa?

Mathayo 6:24

2 Wakorintho 9:8

1 Timotheo 6:6-10

1 Timotheo 6:17-19

3. Utunzaji wa familia. Katika kanisa la Agano Jipya, waumini wengine walifurahia uhuru

wao wa kiroho, na wakaacha kutunza jamaa zao. Wengine waliamini Yesu atarudi

karibuni, kwa hiyo si muhimu kufanya kazi na kutunza familia. Paulo aliwakemea kwa

maneno makali kwa jinsi ambavyo hawawajibiki.

1 Timotheo 3:4; 5:8. Paulo alifundishaje kuhusu utunzaji wa familia?

1 Wathesalonike 4:11-12. Kuna faida gani katika kufanya kaza kwa mikono yao?

2 Wathesalonike 3:6-13. Paulo alikuwaje mfano kwa waumini? Paulo alisemaje

kuhusu mtu asiyefanya kazi (mst. 10)?

4. Sadaka na fungu la kumi. Katika Agano la Kale, Mungu aliwaagiza watu wake kuleta

sadaka zao. Fungu la kumi ni sehemu moja kwa kumi ya mavuno na wanyama

waliozaliwa kwao.

Kumbukumbu 14:28-29. Nani alisaidiwa na fungu la kumi la Waisraeli? Nani

alipokea baraka?

Mathayo 6:1-4. Yesu alifundishaje kuhusu namna ya kutoa sadaka zetu?

1 Wakorintho 16:1-2. Paulo alishauri nini kuhusu matoleo?

2 Wakorintho 8:1-5. Nini iliwahamasisha waumini wa Makedonia kutoa sadaka? Je,

walitoa katika hali ya utajiri au katika hali ya umaskini?

Maswali ya kujadiliana:

1. Je, umewahi kuona jinsi pesa inavyotumiwa kwa nguvu katika ndoa? Eleza.

2. Kwa njia gani pesa inaweza kutawala maisha yetu na kuchukua nafasi ya Mungu?

3. Kama Mungu anatupatia mahitaji yetu katika hali zote, je, kwa nini tusimwombe

Mungu na kuamini ukarimu wake tu, bila kufanya kazi?

4. Shida ya uvivu ni nini?

5. Wengine wanasema, Fedha ni shina la mabaya ya kila namna. Lakini Biblia inasema,

Kupenda fedha ni shina la mabaya ya kila namna (1 Timotheo 6:10). Je, kuna tofauti

gani kati ya maneno hayo mawili?

6. Umeona madhara gani katika ndoa kutokana na matumizi mabaya ya pesa?

7. Je, unakubali kwamba jukumu la matumizi ya pesa katika ndoa linamhusu mume?

Eleza mawazo yako.

Ndoa na Nyumba, uk. 12

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania Produced by Joseph and Gloria Bontrager, Theological Education Coordinators ©2016

Mapendekezo kuhusu matumizi ya pesa:

2. Njia bora kushughulikia mambo ya pesa katika ndoa ni kuelewana kabla ya kufunga

ndoa.

Ongealea namna ya kutunza familia.

Ongealea jinsi mtakavyosimamia pesa zenu, mtakavyotumia mishahara, kama

mtashiriki mishahara, na mtakavyowekea pesa kwa mahitaji ya mbele.

Kama mmefunga ndoa tayari na matatizo ya pesa yanawatisha, kaa pamoja na

kuongea wazi na kwa ukweli kuhusu matatizo, na kufanya mpango jinsi

mtakavyoendesha mambo yenu. Matumizi ya pesa katika ndoa ni kazi ya pamoja na

kuhitaji mawasiliano, uwazi, na ukweli.

3. Ni muhimu kuandika taarifa ya mapato na matumizi ya pesa. Hivyo mnaweza kujua kiasi

cha pesa kinachopatikana na jinsi mnavyotumia pesa mnazopata. Ukijua matumizi ya kila

siku, na wiki, na mwezi, manaweza kufanya mpango ili mapato yatatosha matumizi.

Mpango huo unaitwa bajeti. Mpango utakusaidia kujua kama unatumia pesa visivyo

lazima, na jinsi ya kupunguza matumizi ili pesa zaidi ipatikane kwa matumizi ya lazima.

Mnaweza kuongelea faida ya akaunti ya kujiwekea ili kuwa na pesa kwa matumizi

maalum, au elimu, au mambo ya dharura kama matibabu ya kiafya, mazishi, au usafiri.

Ndoa na Nyumba, uk. 13

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania Produced by Joseph and Gloria Bontrager, Theological Education Coordinators ©2016

Somo la 10. Mapambano na Maumivu katika Ndoa

Ndoa kamilifu ni watu wawili wasio kamilifu wakivumilia na kukataa kuachana.

1. Ndoa imara ni ambayo mume na mke wamejifunza namna ya kukabiliana na matatizo.

Ndoa ni muungano wa maisha mawili tofauti katika maisha ya pamoja, hivyo haikosi

kuleta magumu na mashindano. Lakini tokeo la kusuluhisha tofauti ni kuimarisha

uhusiano. Ndoa ni safari ya kujifunza jinsi ya kutembea pamoja katika furaha na huzuni,

katika uzima na ugonjwa.

2. Unyenyekevu, ukweli, na msamaha. Uzima katika ndoa unatokea kwa kujifunza na

kuelewa tofauti zetu, na kujitoa kutumia tofauti hizo ili kuimarisha uhusiano wetu. Lakini

kiburi na kudai haki, maneno ya hasira and mabishano yanatia madhara katika uhusiano

wa ndoa.

Je, mistari ifuatayo inatoa ushauri gani kuhusu namna ya kuimarisha ndoa?

Waefeso 4:25-27, 29-32. Nini tokeo la kushika hasira moyoni? (mst. 27)

Wakolosai 3:12-15. Tuwe na tabia gani katika mahusiano yetu?

Waefeso 4:32. Eleza maana ya “iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma,

mkasameheane.”

Je, tunaweza kufuata maneno hayo ya ushauri hata ikiwa mume au mke ametenda dhambi

juu yetu na juu ya ndoa yetu?

3. Jenga juu ya msingi imara. Kinga bora kuliko tiba.

Kama hujaoa, anzisha ndoa kulingana na mpango wa Mungu. (rudia masomo ya 1, 2)

Ishi maisha ya ukweli na uaminifu. Waefeso 4:1-3

Jifunzi namna ya mawasiliano ya uwazi na ukweli. Mathayo 18:15-17

4. Tafuta kupatana na kusuluhisha.

Ongea pamoja, jaribu kupatana.

Mwenzako akikataa kuongea, shirikisha na ndugu au dada unayemwamini, akushauri

na kukuombea. Uovu hupenda siri, lakini hushindwa nuruni. Yohana 3:19-21

Mwenzako akiwa mgumu, itakubidi kuvumilia na kuendelea mwenyewe.

Kuna hatari ya kuumizwa kimwili, huenda bora kuachana, ili kujilinda.

5. Kuhusu talaka.

Marko 10:2-12. Yesu alifundisha kwamba ndoa isivunjwe. Talaka iliruhusiwa na

sheria ya Wayahudi kwa sababu ya “ugumu wa mioyo” yao. Talaka inasababisha

kuzini.

1 Wakorintho 7:10-16. Asiyeamini akikubali kukaa na muumini, wasitengane.

Huenda anaweza kuamini (mst. 16).

Maswali ya kujadiliana:

1. Mambo gani yanasababisha mabishano na ugomvi katika ndoa?

2. Ongelea desturi za kimila, kwa mfano mahari, kurithi mjane, na mitara. Kanisa liwe

na msimamo gani, kulingana na mafundisho ya Biblia?

3. Katika ndoa yenye mashindano, je, “upendo” utakuwa na sura gani?

4. Ni katika hali gani wanandoa washauriwe kuachana au kutafuta talaka?

5. Kufuatana na Biblia, tunawezaje kujenga na kuimarisha ndoa iliyovunjika?