2
1 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI (WCF) UCHANGIAJI NA MAFAO YATAKAYOTOLEWA NA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni Taasisi ya Serikali chini ya Wizara ya Kazi na Ajira iliyoanzishwa kwa mujibu wa Kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Na. 20 ya mwaka 2008 kwa madhumuni ya kutoa fidia kwa Wafanyakazi kutokana na ulemavu au vifo vinavyosababishwa na ajali au magonjwa yatokanayo na kazi sambamba na kukuza mbinu za kuzuia matukio ya ajali mahali pa kazi. Mfuko umeanza kazi rasmi tarehe 1 Julai 2015 baada ya kuteuliwa kwa Mkurugenzi Mkuu na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini. Mkurugenzi Mkuu ndiye Mtendaji Mkuu na anafanya kazi chini ya Bodi ya Wadhamini. Mfuko umeanzishwa kutokana na nia ya Serikali kukabiliana na changamoto za ulipaji wa fidia kwa Wafanyakazi katika mfumo wa utoaji fidia uliokuwepo awali. Changamoto hizo ni pamoja na kiwango kidogo cha malipo ya fidia (kiwango kisichozidi shilingi 108,000 kwa ulemavu wa kudumu na shilingi 83,000 kwa wategemezi endapo kifo kitatokea kwa Mfanyakazi husika), uchache wa mafao na urasimu kwa baadhi ya Waajiri katika utoaji wa fidia. Kwa mujibu wa Kifungu cha 2 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi, Na.20/2008, Mfuko huu unawahusu Waajiri na Wafanyakazi wote katika sekta ya Umma na sekta Binafsi, Tanzania Bara. Uchangiaji katika Mfuko umeanza rasmi tarehe 1 Julai 2015 kama ilivyoelekezwa katika Tangazo la Serikali Na. 169 la Mei, 2015. Katika mwaka wa fedha 2015/16, viwango vya uchangiaji kwa kila mwezi ni asilimia moja (1%) ya mapato ya Wafanyakazi kwa Waajiri wa Sekta Binafsi na asilimia sifuri nukta tano (0.5%) ya mapato ya Wafanyakazi kwa Waajiri wa Sekta ya Umma. Aidha michango hii ni gharama ya Mwajiri na haipaswi kukatwa kwenye mapato ya Mfanyakazi.

Press Release 2015 o8 14 - Dg - Mwisho1

Embed Size (px)

DESCRIPTION

PRESS_RELEASE_2015_O8_14__-_DG_-_MWISHO1

Citation preview

Page 1: Press Release 2015 o8 14 - Dg - Mwisho1

1

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI (WCF)

UCHANGIAJI NA MAFAO YATAKAYOTOLEWA NA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni Taasisi ya Serikali chini ya Wizara ya Kazi na Ajira iliyoanzishwa kwa mujibu wa Kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Na. 20 ya mwaka 2008 kwa madhumuni ya kutoa fidia kwa Wafanyakazi kutokana na ulemavu au vifo vinavyosababishwa na ajali au magonjwa yatokanayo na kazi sambamba na kukuza mbinu za kuzuia matukio ya ajali mahali pa kazi.

Mfuko umeanza kazi rasmi tarehe 1 Julai 2015 baada ya kuteuliwa kwaMkurugenzi Mkuu na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini. Mkurugenzi Mkuu ndiye Mtendaji Mkuu na anafanya kazi chini ya Bodi ya Wadhamini.

Mfuko umeanzishwa kutokana na nia ya Serikali kukabiliana na changamoto za ulipaji wa fidia kwa Wafanyakazi katika mfumo wa utoaji fidia uliokuwepo awali. Changamoto hizo ni pamoja na kiwango kidogo cha malipo ya fidia (kiwango kisichozidi shilingi 108,000 kwa ulemavu wa kudumu na shilingi 83,000 kwa wategemezi endapo kifo kitatokea kwa Mfanyakazi husika), uchache wa mafao na urasimu kwa baadhi ya Waajirikatika utoaji wa fidia.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 2 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi, Na.20/2008, Mfuko huu unawahusu Waajiri na Wafanyakazi wote katikasekta ya Umma na sekta Binafsi, Tanzania Bara.

Uchangiaji katika Mfuko umeanza rasmi tarehe 1 Julai 2015 kama ilivyoelekezwa katika Tangazo la Serikali Na. 169 la Mei, 2015. Katika mwaka wa fedha 2015/16, viwango vya uchangiaji kwa kila mwezi niasilimia moja (1%) ya mapato ya Wafanyakazi kwa Waajiri wa Sekta Binafsi na asilimia sifuri nukta tano (0.5%) ya mapato ya Wafanyakazi kwa Waajiri wa Sekta ya Umma. Aidha michango hii ni gharama ya Mwajiri na haipaswi kukatwa kwenye mapato ya Mfanyakazi.

Page 2: Press Release 2015 o8 14 - Dg - Mwisho1

2

Mwajiri ana wajibu wa kuwasilisha michango kupitia akaunti za Mfuko zilizopo katika benki ya NMB (Akaunti Na. 20110016403, tawi la Bank House) na CRDB (Akaunti Na. 0150237547300, tawi la Holland House) kwa njia ya Mtandao (Electronic money transfer), Hundi (Cheque payments), Fedha Taslimu (Cash payments) au njia nyingine inayokubalika na Benki Kuu ya Tanzania. Ucheleweshaji wa malipo ni kosa linalostahili adhabu kwa mujibu wa vifungu vya 75 (2), (3) na (4) vya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi, Na. 20 ya mwaka 2008.

Uwasilishaji wa nyaraka zinazohusu malipo ya michango utazingatia utaratibu uliowekwa na Mfuko. Mwajiri atawasilisha nakala mbili za fomuWCP1 zilizojazwa, viambatishi vyake na uthibitisho wa malipo. Fomu na kiambatishi chake vinapatikana Ofisi za Mfuko na pia katika tovuti ya Mfuko (www.wcf.go.tz), tovuti ya Wizara ya Kazi na Ajira (www.kazi.go.tz) na Ofisi za Kazi zilizopo mikoani na wilayani.

Mafao yatakayotolewa na Mfuko huu ni huduma ya matibabu, malipo ya ulemavu wa muda, malipo ya ulemavu wa kudumu, malipo kwa anayemhudumia mgonjwa, huduma za ukarabati na ushauri nasaha, gharama za mazishi na malipo kwa wategemezi wa marehemu.

Kipindi kati ya Julai 2015 na Juni 2016 ni cha mpito na Waajiri wataendelea kushughulikia malipo ya fidia kwa Wafanyakazi kwa taratibu zilizopo. Mfuko utaanza kupokea madai ya fidia kwa Wafanyakazi tarehe 1 Julai 2016.

Mfuko wa Fidia utasaidia kuboresha mazingira ya kazi, kulinda nguvu kazi ya Taifa, kuimarisha ustawi wa Wafanyakazi, kuwaongezea ari ya utekelezaji wa majukumu na hivyo kuwezesha ongezeko la tija na kukua kwa uchumi wa Taifa.

Imetolewa na Mkurugenzi Mkuu,

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI (WCF)

GEPF House, Barabara ya Bagamoyo, Regent Estate

Tafadhali uliza mapokezi, Ghorofa ya 9.

Simu Na.: +255 22 2110877

Simu Na.: +255 22 2926107

16 Agosti, 2015