36
Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Lindi Septemba 2016

Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report 2016pg.pdfMkataba wa Banjul (Afrika) na Mkataba wa Kimataifa wa haki za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni unaofa- ... wa

  • Upload
    others

  • View
    35

  • Download
    4

Embed Size (px)

Citation preview

Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)

Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

Lindi

Septemba 2016

Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)

Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

Lindi

Imeandaliwa na Timu ya SAM

Septemba 2016

i

Kukamilika kwa ripoti hii ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii, kwa lugha ya Kiingereza ikijulikana

kama Social Accountability Monitoring (SAM) katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi kumetokana na

ushirikiano mkubwa kutoka kwa wadau mbalimbali katika sekta ya afya. Timu ya SAM Lindi inatambua

na kuthamini kwa kiasi kikubwa cha juhudi kilichofanywa na wadau hao.

Shukrani za dhati ziwaendee Sikika, hususani kwa wawezeshaji wa mafunzo haya ambao ni Scholas-

tica Lucas, Joshua Nkila, Maria Kayombo na Clemence Mombeki, kwa kuratibu mchakato mzima wa

mafunzo, uchambuzi na ufuatiliaji. Tunawashukuru pia kwa kuratibu ziara ya uhakiki wa shughuli mbal-

imbali zilizohitaji uhalalisho, uthibitisho, ufafanuzi na uboreshaji kama zilivyoainishwa katika ripoti hii.

Timu inatoa shukrani za pekee kwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Lindi kwa kutambua umuhimu wa zoezi

hili na kulisimamia tangu mwanzo hadi mwisho, na hatimaye kukamilika kwa ripoti hii. Pia timu ya SAM

inatoa shukrani kwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi hususani Idara ya Afya

kwa ushirikiano mkubwa uliowezesha timu kupata nyaraka mbalimbali muhimu kwa ajili ya uchambuzi.

Timu ya SAM inapenda kuwashukuru watendaji wote wa vituo vya huduma za afya vya Manispaa ya

Lindi kwa kutoa ushirikiano wakati timu ilipotembelea kujionea huduma na miradi mbalimbali inay-

otekelezwa katika maeneo yao.

Shukrani za pekee ziwaendee wajumbe wa Timu ya SAM wa Manispaa ya Lindi kwa kushiriki katika zo-

ezi zima la SAM; Ndugu Christopher Kumpanga, Zuhura Abdalah, Khalfani Mohamedi, Hassan Kalla,

Ratifa Saidi, Swalehe Ahmad, Fadhili Ngongorowe, Imani Ligau, Mohamedi Lueana, Asha Bilali, Hawa

Kipara, Milembe Lyogohya na Mohamedi Kanile.

Asanteni sana

Ndugu Frank Magari

Mwenyekiti wa Timu ya SAM

SHUKRANI

ii

YALIYOMO

SHUKRANI i

YALIYOMO ii

ORODHA YA VIFUPISHO iii

SEHEMU YA KWANZA 1Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii 11.0 Utangulizi 11.1 Lengo la Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii 1

1.2 Uchaguzi wa Wajumbe wa Timu ya SAM 1

1.3 Mafunzo ya Utekelezaji wa SAM 2

1.4 Uchambuzi wa Nyaraka 2

1.5 Njia Zilizotumika Kupata Ufafanuzi 2

1.6 Taarifa ya Zoezi la SAM kwa Wadau wa Afya 2

SEHEMU YA PILI 3Matokeo ya Uchambuzi wa Nyaraka Mbalimbali 32.0 Utangulizi 32.1 Mipango na Mgawanyo wa Rasilimali 3

2.2 Usimamizi wa Matumizi 6

2.3 Usimamizi wa Utendaji 11

2.4 Usimamizi wa Uadilifu 19

2.5 Usimamizi wa Uwajibikaji 20

SEHEMU YA TATU 213.0 Hitimisho 21Viambatisho 22

Kiambatisho1: Wajumbe wa Timu ya SAM 22

Kiambatisho 2: Maazimio ya Kuboresha Huduma 23

Kiambatisho 3: Hotuba ya Mkuu wa Wilaya 26

iii

ORODHO YA VIFUPISHO

CAG Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali

CCHP Mpango Kabambe wa Afya wa Halmashauri

CHF Mfuko wa Afya wa Jamii

CHMT Timu ya Utawala ya Afya ya Halmashauri

CTC Vituo vya Ushauri Nasaha na Upimaji

DMO Mganga Mkuu wa Wilaya

EGPAF Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation

HFGC Kamati ya Usimamizi ya Kituo cha Afya

HBC Huduma Zitolewazo Majumbani

OC Matumizi Mengine

SAM Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii

WEO Afisa Mtendaji wa Kata

WAVIU Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

MSD Bohari Kuu ya Dawa

MRDT Upimaji wa Malaria kwa Njia ya Haraka

TIKA Tiba kwa Kadi

THC Kituo cha Afya cha Mjini

NHIF Bima ya Taifa ya Afya

MTEF Mpango wa Muda wa Kati wa Matumizi ya Serikali

iv

MUHTASARIMchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring” (SAM) ni zoezi lenye

lengo la kuiwezesha jamii kushiriki katika kupanga, kufuatilia na kuchambua utekelezaji wa mipango kuan-

zia ngazi ya jamii mpaka halmashauri. Lengo kuu la SAM ni kuhimiza ushirikishwaji, ufuatiliaji na uwajibikaji

wa watendaji/watoa huduma ikiwemo huduma za afya ili kuwapa wananchi haki zao za msingi kama ilivy-

oainishwa katika sheria za nchi na mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhia. Sheria na mikataba

hiyo ni pamoja na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) Ibara za (11), (12), (14) – (28),

Mkataba wa Banjul (Afrika) na Mkataba wa Kimataifa wa haki za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni unaofa-

hamika kwa lugha ya Kiingereza kama “International Covenant for Economical, Social and Cultural Rights

(ICESCR, 1976)”, ambayo yote imejikita katika kuhakikisha uwajibikaji katika kufikia upatikanaji na utoaji

wa haki za binadamu na mahitaji ya msingi ya jamii.

Tangu mwaka 2012, Sikika imekuwa ishirikiana na halmshauri mbalimbali katika kuendesha zoezi la SAM

kwa kuunda timu katika halmashauri hizo. Timu hizi za SAM zinajumuisha wananchi wa makundi yote,

wajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa dini na wa madiwani. Timu

ya SAM imepewa nafasi ya kushiriki katika kupanga na kufanya uchambuzi wa taarifa mbalimbali pamoja

na kufuatilia utekelezaji wa mipango na miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali. SAM pia inalenga

kuiwezesha jamii kuhoji uwajibikaji wa wasimamizi na watoa huduma za umma ili waweze kutoa huduma

zinazokidhi mahitaji muhimu na ya msingi kwa jamii kama vile afya, elimu, maji, chakula na makazi.

Sikika imekuwa ikiendesha zoezi katika wilaya zaidi ya 10 zikiwemo Mpwawa, Kondoa, Ilala, Kibaha, Singi-

da vijijini, Kilolo, Simanjiro, Kiteto, Kilwa, Temeke na Kinondoni. Katika wilaya ambazo zimewezeshwa kuwa

na timu ya SAM, ufutuatiliaji na uwajibikaji katika upatikanaji wa huduma za afya umeongezeka, ikiwemo

uboreshaji wa miundo mbinu katika vituo vya huduma za afya, na vilevile katika kupanga bajeti yenye ku-

fuata vipaumbele sambamba na matumizi yenye tija.

SAM katika wilaya ya Lindi imefanyika mwaka 2016, ikiwa ni moja ya Wilaya mpya ambazo Sikika imeanzia

kutekeleza mpango mkakati wake wa mwaka 2016 -2020.

Baadhi ya matokeo ya uchambuzi yaliyotokana na zoezi hili ni pamoja na halmashauri kushirikisha wadau

wa afya katika kupanga mpango kabambe wa afya, jambo ambalo ni jema kwa maendeleo ya sekta katika

wilaya. Kwa upande mwingine, kumeonekana kuwa na upungufu wa wafanyakazi katika vituo vya kutolea

huduma, upungufu wa vifaa tiba ikiwemo vitanda, magodoro, vitendanishi, mikasi, mashine za kupima

mgandamizo wa damu, na vitakasa vifaa.

Pia kumeonekana kuwa na majengo machakavu, vyoo vichache na visivyokidhi mahitaji ya wagonjwa,

upungufu wa nyumba za wafanyakazi, miundo mbinu isiyokidhi mahitaji ya walemavu, na upungufu wa

vichomea taka. Kutokana na matokeo hayo Timu ya SAM na uongozi wa Halmashauri ya Lindi umeweka

mkakati wa kuhakikisha masuala hayo muhimu yaliyoibuliwa yanafanyiwa kazi kwa ushirikiano na wadau

wa afya wa wilayani na wananchi kwa ujumla.

1

1.0 UtanguliziMchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii ulikusudia kuiwezesha Halmashauri ya Manispaa ya Lindi kuboresha utoaji wa huduma za kijamii, hususani huduma za afya ili wananchi wanufaike na huduma hizo kama mojawapo ya haki zao za msingi. Sikika iliiwezesha Timu ya SAM kupata mafunzo na kufanya ufuatiliaji kwa kufuata miongozo sahihi ya kisheria za nchi na mikataba ya kimataifa am-bayo Tanzania imeridhia na imejikita katika kuhakikisha uwajibikaji katika kufikia upatikanaji na utoaji wa haki za binadamu na mahitaji ya msingi ya jamii.

1.1 Lengo la Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa JamiiLengo la mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii “Social Accountability Monitoring” – (SAM) ni kuijengea uwezo jamii kushiriki na kufanya uchambuzi wa taarifa mbalimbali pamoja na kufuatilia utekelezaji wa mipango na miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali. SAM pia inalenga kuiweze-sha jamii kuhoji uwajibikaji wa wasimamizi na watoa huduma za umma ili waweze kutoa huduma zinazokidhi mahitaji muhimu na ya msingi kwa jamii kama vile afya, elimu, maji, chakula na makazi.

1.2 Uchaguzi wa Wajumbe wa Timu ya SAMUtekelezaji wa mchakato wa SAM katika Manispaa ya Lindi ulifuata hatua mbalimbali. Hatua za mwan-zo kabisa zilikuwa kutoa ufafanuzi kwa viongozi wa manispaa, madiwani pamoja na wadau wengine wa afya juu ya dhana ya SAM. Hatua hii pia ilihusisha uchaguzi wa washiriki wa timu ya SAM uliofan-ywa kupitia mikutano mbalimbali kuanzia ngazi ya jamii.

Mikutano ya awali ni ile ya wananchi katika kata, ambapo ililenga kutoa elimu kwa wananchi juu ya SAM na kisha kupata uwakilishi kutoka pande mbalimbali za Manispaa ya Lindi. Katika mikutano hii walipatikana wawakilishi wanne (4).

Mkutano wa pili ni ule wa Baraza la Madiwani, ambao ulichagua wawakilishi wawili kwa ajili ya timu ya SAM. Mbali na kupata wawakilishi kutoka katika kundi la madiwani, mkutano huu na Baraza la Madi-wani ulilenga kutoa elimu ya SAM kwa madiwani ili waweze kuitumia katika mchakato wa mipango na bajeti katika ngazi ya halmashauri pamoja na kusimamia uwajibikaji wa watoa huduma.

Mkutano wa tatu ulifanyika katika ngazi ya Manispaa ambao ulijumuisha viongozi na watendaji wakuu wa halmashauri wakiwemo Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Katibu Tawala, Timu ya Uendeshaji wa Shughuli za Afya za Halmashauri (CHMT), watoa huduma za afya vituoni, watendaji wa kata, bodi na kama-ti za afya, wawakilishi wa wananchi (wananchi waliochaguliwa kutoka katika kata), wawakilishi wa wananchi wenye mahitaji maalumu (WAVIU na malemavu), wawakilishi wa asasi za kiraia pamoja na viongozi wa dini. Katika mkutano huu wawakilishi wengine wa timu ya SAM walichaguliwa kuwakilisha makundi mbalimbali ya wadau wa afya na kufanya jumla ya wajumbe wa timu ya SAM kuwa 15. Hivyo, timu ya SAM ya Manispaa ya Lindi iliundwa na wawakilishi kutoka katika makundi ya wananchi, madi-

SEHEMU YA KWANZA

wani, CHMT, bodi na kamati za afya pamoja na watendaji wa kata.

1.3 Mafunzo ya Utekelezaji wa SAMMafunzo ya SAM yalitolewa na wawezeshaji wa Sikika kwa kuipa mafunzo maalum timu ya SAM yali-yojikita katika nguzo kuu tano za mchakato wa SAM, ambazo ni Mipango na Mgawanyo wa Rasilimali, Usimamizi wa Matumizi, Usimamizi wa Utendaji, Usimamizi wa Uadilifu, na Usimamizi wa Uwajibikaji. Mafunzo ya SAM yalienda sambamba na uchambuzi wa taarifa mbalimbali za manispaa, na baadaye kufanya uhakiki wa utekelezaji wa mipango kwa kutembelea vituo vya huduma za afya ili kupata ufa-fanuzi. Lengo la uhakiki ni kujiridhisha iwapo yaliyomo kwenye taarifa ya utekelezaji yanaendana na hali halisi vituoni.

1.4 Uchambuzi wa NyarakaTimu ilichambua nyaraka mbalimbali zikiwemo Mpango Mkakati wa Halmashauri (2012/2013-2016/2017); Mpango Kabambe wa Afya wa Halmashauri (CCHP) 2014/2015; ripoti za utekelezaji za mpango kabambe wa afya wa Halmashauri kwa kila robo 2014/2015; Mpango wa Muda wa Kati wa Matumizi ya Serikali, kwa Kiingereza “Medium-Term Expenditure Framework” (MTEF) 2014/2015-2018/2019; mihutasari ya taarifa za vikao vya baraza la madiwani 2014/2015; ripoti za ukaguzi za mkaguzi wa ndani 2014/2015; ripoti ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) 2014/2015. Taarifa zote hizi zilisaidia kuijenga timu kwa kila hatua ya mchakato wa SAM. Timu ilitakiwa kupitia taarifa am-bazo zinaendana na hatua husika ili kupata mtiririko mzuri wa mchakato mzima wa SAM. Na mwisho, timu iliandaa taarifa kwa kufuata mtiririko wa hatua tano za mzunguko wa SAM kama ilivyoainishwa katika sehemu ya pili ya ripoti.

1.5 Njia Zilizotumika Kupata UfafanuziMara baada ya mafunzo na uchambuzi wa nyaraka, timu ya SAM iliandaa dodoso lenye hoja zilizotoka-na na uchambuzi wa nyaraka ili kuhakiki katika vituo vya huduma za afya. Jumla vituo 12 vilitembelewa na timu kwa uhakiki na kupata ufafanuzi wa taarifa zilizopatikana katika uchambuzi wa nyaraka. Baada ya kumaliza ziara vituoni, timu iliandaa taarifa yenye hoja za vituo pamoja na uchambuzi wa nyaraka na kuipeleka katika ofisi ya mkurugenzi ili kupata ufafanuzi wa maandishi. Baada ya manispaa kutoa ufafanuzi wa hoja hizo, timu ilikutana na Kamati ya Afya ya Halmashauri (CHMT) katika mkutano wa ndani ili kutoa taarifa ya zoezi la SAM pamoja na kupata ufafanuzi wa kina wa taarifa zilizochambuliwa kutoka katika nyaraka, pamoja na taarifa ya ziara katika vituo vya huduma za afya.

1.6 Taarifa ya Zoezi la SAM kwa Wadau wa AfyaBaada ya timu ya SAM kupata ufafanuzi kutoka CHMT wa mambo yaliyoibuliwa katika uchambuzi wa nyaraka pamoja na ziara za vituo vya huduma za afya, ilikutana na wadau wa afya wa manispaa ili ku-toa mrejesho wa zoezi zima la SAM. Mkutano ulijumuisha watendaji wakuu wa halmashauri wakiwemo Mkuu wa Wilaya, Katibu Tawala, Waheshimiwa madiwani, CHMT, Watendaji wa Kata, wawakilishi wa bodi na kamati za afya, wawakilishi wa wananchi (wananchi wa kawaida, WAVIU, asasi za kiraia pamo-ja na viongozi dini).Matokeo ya Uchambuzi wa Nyaraka Mbalimbali

2

3

SEHEMU YA PILI Matokeo ya Uchambuzi wa Nyaraka Mbalimbali

2.0 UtanguliziSehemu hii imejadili kwa undani uchambuzi wa nyaraka mbalimbali zilizotumika katika mafunzo kwa timu ya SAM ya manispaa. Zaidi ya hayo, sehemu hii imejumuisha hoja zilizoibuliwa wakati wa ucham-buzi wa nyaraka na hali halisi iliyoonekana katika vituo vya huduma za afya pamoja na ufafanuzi uliot-olewa na timu ya Uendeshaji wa Shughuli za Afya ya Halmashauri juu ya hoja hizo. Mtiririko wa hoja na ufafanuzi umegawanywa katika hatua tano za SAM kama ilivyoainishwa katika vipengele vinavyofuata.

2.1 Mipango na Mgawanyo wa RasilimaliMipango na mgawanyo wa rasilimali ni moja ya hatua ya kwanza ya mfumo wa uwajibikaji jamii inayo-lenga kuboresha mipango na mgawanyo wa rasilimali. Hatua hii inahusisha mafunzo na uchambuzi wa mipango ya Manispaa na mgawanyo wa rasilimali kulingana na vipaumbele vilivyoainishwa. Timu ya SAM ya Manispaa ya Lindi ilipitia na kuchambua mpango mkakati wa manispaa wa miaka mi-tano kuanzia 2012/13 mpaka 2016/17 na kuangalia dira, malengo ya utekelezaji, muda wa utekelezaji na makadirio ya bajeti kwa miaka mitano. Pia timu iliweza kuchambua mgawanyo wa rasilimali unavy-oendana na vipaumbele vilivyoainishwa.

Pongezi: Timu inaipongeza manispaa kwa uandishi mzuri wa mpango mkakati wenye dira, dhamira na bajeti zinazoeleweka na kutekelezeka. Timu pia inatoa pongezi kwa manispaa kwa kuan-daa mpango mkakati kwa lugha ya Kiswahili inayoeleweka na wananchi.Pamoja na uchambuzi wa mpango mkakati wa manispaa, timu ilifanya uchambuzi wa mpango ka-bambe wa afya (CCHP) 2014/2015 kwa kuangalia masuala mbalimbali yaliyojumuisha ushiriki wa wananchi katika kuandaa mpango, malengo makuu ya mpango, vyanzo vya rasilimali fedha kwa ajili ya kuutekeleza, mgawanyo wa rasilimali fedha kulingana na vipaumbele na kubaini masuala mbalimbali. Zifuatazo ni hoja zilizoibuliwa na timu ya SAM kutoka katika nyaraka:

Hoja namba 1: Timu ya SAM imegundua kuwa manispaa imekuwa ikichangia kidogo sana kwa bajeti ya afya. Kwa mfano; kwa mwaka wa fedha wa 2013/14 manispaa haikuchangia kabisa katika bajeti ya afya wakati mwaka 2014/15 manispaa iliahidi kuchangia SH. 14,200,000/-, ambayo ni sawa na asilimia 0.8 ya vyanzo vyote vya bajeti ya afya vilivyoainishwa katika CCHP, kama ilivyoainishwa katika uk. 60, jedwali namba 14. Hata hivyo, katika ripoti ya utekelezaji ya mwaka (huo), manispaa inaonekana haikutoa fedha zozote kama inavyoonyesha katika ripoti ya utekelezaji 2014/15, jedwali namba 1. Timu iliomba ufafanuzi wa manispaa kushindwa kuchangia sehemu kubwa ya bajeti ya afya, na sababu ya kutotoa fedha iliyoahidi kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za afya kwa mwaka 2014/2015.

Ushauri: Timu inaishauri manispaa kuipa idara ya afya kipaumbele kikubwa katika mgawanyo wake wa rasilimali ili kupunguza idadi kubwa ya vifo vitokanavyo na uzazi ambavyo moja ya sababu kub-

4

wa inayochangia ni upungufu wa bajeti. Kwa mfano, CCHP uk. 32, imetoa takwimu za idadi ya vifo vitokanavyo na uzazi kwa manispaa dhidi ya takwimu za nchi nzima, ambapo Manispaa ya Lindi im-eonekana kuchukua asilimia 45% ya vifo vya wamama wajawazito vinavyotokea nchini, asilimia 88% ya vifo vya watoto wachanga, asilimia 51% ya vifo ya watoto chini ya mwaka na asilimia 7% ya vifo vya watoto chini ya miaka 5. Takwimu hizi zimetolewa katika ripoti ya manispaa ya mwaka (Januari – Disemba 2013).

Majibu ya Menejimenti: Kwa mwaka wa fedha 2014/2015 halmashauri ilitumia mapato yake ya ndani kwa kujenga nyumba Mganga wa Zahanati ya Mnali ili kumwezesha Mganga au Muuguzi kukaa karibu na zahanati ili aweze kuhudumia akina mama wajawazito wakati wote. Lengo ni kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka 5. Menejimenti pia iliahidi kuufanyia kazi ushauri uliotolewa na timu ya SAM.

Hoja namba 2: Mpango wa CCHP uk 3 unaonesha matumizi ya kawaida yamepangiwa kiasi cha shilingi 791,310,217/- sawa na asilimia 43.85 ya bajeti nzima ya mwaka 2014/15, na mishahara kiasi cha shilingi 1,013,479,200/- sawa na asilimia 56.15 ya bajeti yote ya afya 2014/15. Timu iliishauri idara kuongeza kiasi cha fedha za kawaida ili kukidhi mahitaji ya vipaumbele vilivyowekwa. Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto kama vilivyooneshwa katika uk wa 32 wa CCHP ambavyo vimeonekana kukithiri katika manispaa yetu ukilinganisha na takwimu za kitaifa.

Majibu ya menejimenti: Ushauri umepokelewa na utazingatiwa.

Hoja namba 3: Timu ya SAM ilibaini kuwa, mpango wa CCHP katika uk. 1 umeainisha maeneo matatu ya changamoto kuu za afya zinazotarajiwa kutatuliwa ambazo ni vifo vitokanavyo na uzazi na malaria, masuala ya usafi na uhaba wa maji safi na salama na 54% eneo la mwisho ni masuala ya kiutawala na miundombinu kama vile uhaba wa wataalam wa afya kwa 40%. Ukurasa wa 3 katika CCHP umeonesha malengo manne yaliyoainishwa kutokana na changamoto kama yalivyoainishwa ukurasa wa kwanza, ambayo ni: kupunguza vifo vya wamama wajawazito kutoka 203/100,000 mpaka 196/100,000; kupunguza vifo vya watoto wachanga kutoka 93 mpaka 60; kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa malaria kutoka asilimia 33 hadi 23 pamoja na kuongeza kasi ya ukusanyaji taka ngumu kutoka asilimia 54 hadi 70. Timu ya SAM imebaini kuachwa kwa malengo muhimu mengine ambayo ni kupunguza uhaba wa wataalam wa afya ambao upo kwa asilimia 40 pamoja na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama, hivyo timu iliomba kupatiwa ufafanuzi wa sababu ya kuachwa kwa malengo hayo.

Majibu ya menejimenti: • Lengo la kupunguza uhaba wa watumishi - kada ya afya halijasahaulika, kwa kuwa ni len-

go endelevu katika mikakati ya ngazi ya halmashauri, idara na mkoa kwa ujumla kwa kushirikiana na wadau wetu BMAF na GIZ katika kusomesha wazawa wa Lindi mas-omo ya afya, na baada ya kumaliza kurudi kufanya kazi katika maeneo haya. Vilevile ba-

5

jeti ya mishahara ya kila mwaka ya watumishi na mapendekezo ya ajira yanatolewa kulin-gana na Ikama ya Idara ya Afya ilivyopangwa ambayo inafanywa na Ofisi ya Utumishi.

• Mpango wa kuwezesha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi upo kwenye MTEF ya Halmashauri kupitia Idara ya Maji, na ipo miradi mbalimbali ya maji inayoendelea kujengwa.

Hoja namba 4: Timu pia ilipenda kufahamishwa iwapo orodha ya vipaumbele vilivyopo katika CCHP uk 13 imepangwa kulingana na ukubwa wa vipaumbele, na kama mgao wa rasilimali umefanyika kulin-gana na uzito wa vipaumbele hivyo. Kwa mfano, kipaumbele namba moja ndio chenye uzito mkubwa zaidi ya kipaumbele cha mwisho (13).

Majibu ya menejimenti: Vipaumbele vilivyowekwa kwenye mpango vimetengenezwa kutokana na muongozo wa uandaaji wa CCHP. Havikuwekwa kulingana na umuhimu wake, mfano kipaumbele namba 8 kinaweza kuwa cha muhimu zaidi hata kama kimewekwa kuwa cha 8.

Hoja namba 5: Moja ya changamoto zilizoainishwa katika mpango wa CCHP uk 30 inasema hakuna ushiriki wa wananchi katika kuboresha huduma za afya, hii inakinzana na kipengele namba 1.1.9 ush-iriki wa wananchi (CCHP uk 23-24). Timu iliomba kufahamu nini maana ya kuandika hivyo. Je, ni kweli kwamba hakuna ushiriki wa wananchi katika shughuli za afya katika manispaa?

Majibu ya menejimenti: Changamoto mojawapo iliyotajwa kwenye mpango wa CCHP 2014/2015 ni “No community health based initiative activities” maana yake ni kwamba hakuna shughuli iliyonzishwa na wananchi wenyewe. Ushiriki wa jamii katika shughuli za kuendeleza na kuboresha afya kwa jamii ni kwa kiwango kidogo sawa na mpango wa CCHP kipengele 1.1.9 (community involvement). Eneo hili linaonesha uibuaji wa mipango ya idara unatoka kwa wananchi mpaka ngazi za juu, ila ilikuwa ngumu kwa jamii kushiriki kujitolea kubeba mawe, matofali, maji na vinginevyo licha ya kukuhamasishwa kwa muda mrefu kujenga nyumba ya mganga zahanati ya Mnali. Huu ni moja ya mfano wa ushiriki wa jamii katika kutekeleza yale yaliyopangwa kwa pamoja.

Hoja namba 6: Timu imeona mpango haukuipa kipaumbele cha juu uhamasishaji wa uboreshaji afya (health promotion- kipaumbele cha 11: uk 13 wa CCHP) na hivyo kupatiwa mgao mdogo sana (Sh 2,599,401/-). Mbali ya ufinyu wa bajeti hiyo, fedha iliyopangwa haikutolewa yote, kwa mujibu wa ripoti ya utekelezaji, jedwali namba 3 (Sh 1,760,150/-) timu inafahamu kuwa kinga ni bora kuliko tiba, na kama idara itaweka mkazo katika kinga basi manispaa itapunguza ukubwa wa maradhi na vifo. Hivyo timu inaishauri idara kuipa kipaumbele cha juu kabisa “health promotion” katika ugawaji wa rasilimali ili kuboresha afya na kupunguza gharama.

Majibu ya menejimenti: Ushauri tumeupokea na tutauzingatia kwa bajeti zinazofuata.

Hoja namba 7: Timu ilibaini kuwa mpango wa CCHP na ripoti zake za utekelezaji zipo katika lugha ya Kiingereza, kitu ambacho si rahisi kwa mwananchi wa kawaida kuzisoma na kuzielewa. Timu iliiomba

6

idara ya afya kutoa taarifa zake kwa lugha ya Kiswahili kama ilivyo katika mpango mkakati wa manis-paa, mihutasari ya baraza la madiwani pamoja na ripoti za mkaguzi wa ndani.

Majibu yamenejimenti: Kutokana na mfumo unaotumika katika kuandaa taarifa ya idara ya afya (Plan Rep3 version 20) ya mwaka na ya kila robo, mfumo upo katika lugha ya Kiingereza ambapo huwasilishwa Wizara ya Afya na Tamisemi, ingawa inawezekana kutafsiri kwa lugha ya Kiswahili. Hata hivyo taarifa ya utekelezaji ya kila robo inayowasilishwa kwenye vikao vyote vya halmashauri ipo katika lugha ya Kiswahili ambapo taarifa hii inakuwa imetoholewa kutoka kwenye taarifa ya CCHP ya idara ambayo ni ya Kiingereza.

2.2 Usimamizi wa MatumiziHoja namba 8: Bajeti ya kipaumbele cha 2 (Afya ya mama na mtoto) inayoonekana CCHP uk. 13 (sh.152,559,713/-) inatofautiana na ile inayoonekana katika ripoti ya utekelezaji katika Jedwali namba 3 (sh. 219,125,750.10). Timu iliomba ufafanuzi wa utofauti uliopo.

Majibu ya menejimenti: Maelekezo/mwongozo wa serikali wa ukomo wa kupanga matumizi ya fed-ha za kugharamia malipo ya kuitwa kazini ilitufikia wakati kitabu cha mpango cha CCHP kilikuwa tayari kimetayarishwa. Kiwango cha malipo hayo cha shilingi 100, 800,000/- kilipofika kilikwa kwenye kipaumbele namba 2 na 8 kwenye mfumo wa Plan Rep. Na taarifa ya utekelezaji inaundwa kutoka kwenye mfumo wa Plan Rep ndiyo maana kuna utofauti huo kati ya mpango wa CCHP na ripoti ya utekelezaji.

Hoja namba 9: Ripoti ya utekelezaji ya mwaka 2014/2015 katika ukurasa wa utangulizi imeonesha bakaa au salio ishia kuwa ni shilingi 18,916,790/- kiwango ambacho kinakinzana na salio ishia lililoone-shwa katika Jedwali namba 1 katika ripoti hiyo hiyo ya utekelezaji (Sh. 22, 205,610.90), timu ilipenda kufahamu chanzo cha utofauti huu.

Majibu ya menejimenti: Taarifa ya utekelezaji ya mwaka (Annex 11): Muhtasari wa hali ya kifedha ya mwaka 2014/2015 unaonyesha salio ishia au bakaa kuwa shilingi 18, 916,790/- Na Jedwali namba1 inaonyesha hivyo hivyo shilingi 18,916,790/- kadri ya mfumo wa Plan Rep. Naambatisha taarifa ya utekelezaji wa mwaka 2014/2015 kwa uthibitisho zaidi kutoka kwenye mfumo wa Plan Rep.

Hoja namba 10: Katika uchambuzi wa jumla kuu ya matumizi kwa kila robo (Kiambatisho 5) timu ili-baini kuwa salio ishia (bakaa) ya robo ya pili (2) hailandani na salio anzia la robo ya tatu (3). Takwimu hizo zimejirudia katika robo ya tatu, salio ishia halikulingana na salio anzia katika robo ya nne, hivyo kupelekea timu kuomba ufafanuzi kuhusu suala hilo.

Majibu ya menejimenti: Taarifa ya awali ya robo ya kwanza hadi ya nne zilikuwa hazilingani kati ya taarifa na kwenye mfumo wa EPICA, hivyo taarifa hizo zilipitiwa tena mwezi Julai 2015 Dodoma na kurekebishwa. Hivyo naomba kuwasilisha taarifa za mwisho baada ya marekebisho zinavyosomeka kwenye mfumo wa Plan Rep kwa uthibitisho zaidi.

7

Hoja namba 11: Mpango wa CCHP (uk. 1) hauoneshi salio anzia kutoka mwaka uliopita yaani 2013/2014 lakini salio anzia linaonekana katika ripoti ya utekelezaji ya mwaka kwenye ukurasa wa utangulizi na Jedwali namba 1 (sh.81,233,347.60). Timu inaishauri idara kuonesha taarifa zote muhimu katika mpango ili iwe rahisi kufanya ufuatiliaji.

Majibu ya menejimenti: Ushauri umepokelewa na utafanyiwa kazi kwenye taarifa zijazo.

Hoja namba 12: Uchambuzi wa timu ya SAM umebaini fedha zitokanazo na uchangiaji zimekuwa hazitolewi zote kama zinavyopangwa. Timu inatambua kuwa hizi ni fedha zinazokusanywa na vit-uo, hivyo timu ilitegemea fedha hizi zitumike kwa ukamilifu kulingana na mpango. Mfano, ripoti ya utekelezaji (Jedwali namba 1) inaonesha kuwa, fedha kutoka tiba kwa kadi (TIKA) zimetolewa shil-ingi 8,332,519/- tofauti na lengo la shilingi 8,952,500/- fedha za papo kwa papo zimetolewa shilingi 25,638,500/- badala ya shilingi 34,560,000/- zilizopangwa na Bima ya Afya ya Taifa (NHIF) zimetolewa shilingi 19,725,919/- badala ya shilingi 24,000,000/-. Timu iliomba kufahamishwa sababu za kutokufikia lengo katika upatikanaji na matumizi ya fedha hizo za uchangiaji.

Majibu ya menejimenti: Kwa mwaka wa fedha 2014/2015 idara ya afya ilipanga makisio ya kupokea kiasi cha pesa tajwa hapo juu kutoka katika vyanzo vyake vya mapato kama vile TIKA, NHIF na papo kwa papo, tulishindwa kufikia lengo kwa sababu zifuatazo;• Uelewa mdogo wa wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), lakini hao wanaopatikana

wanajiunga kwa elfu kumi (10,000/-) tu kwa kaya moja yenye watu 6 kwa mwaka.• Makusanyo ya NHIF yanategemea uwepo wa wagonjwa kwenye vituo vya kutolea huduma za

afya.• Makusanyo ya papo kwa papo pia hutegemea kiasi cha wagonjwa wanaotibiwa kwenye vituo vy-

etu vya kutolea huduma za afya.• Uwepo wa misamaha kutokana na sera zinazotolewa na serikali, kwa mfano; wazee wenye umri

zaidi ya miaka 60, watoto chini ya miaka 5, akina mama wajawazito na wenye magonjwa sugu hutibiwa bure.

Hata hivyo, menejimenti imekubali ushauri wa timu ya SAM wa kuhamasisha wananchi kujiunga na TIKA. Ushauri uliohimiza: Elimu na uhamasishaji uendelee kutolewa; Mfumo wa kieletroniki utumike katika kukusanya mapato; Timu ya SAM ishirikishwe katika kuhamasisha wananchi kujiunga na TIKA; Wanaojiunga na TIKA wapewe kipaumbele katika huduma zinazotolewa; HBC pia washirikishwe katika mchakato wa kuhamasisha wananchi kujiunga na TIKA; Kiasi cha kumuona daktari kiongezeke kwa huduma za papo kwa papo. ziongezeke kutoka sh 3,000/- hadi 5,000/- kwa zahanati na kituo cha afya iongezeke kutoka 4,500/- hadi 6,500/- ili kuongeza idadi ya wanufaika wa bima za afya. Hoja namba namba 13: Timu ilibaini kuwa, bajeti iliyopitishwa katika mpango wa CCHP- uk 3 (sh. 1,804,790,500/-) inatofautiana na ile inayoonekana katika ripoti ya utekelezaji – Jedwali namba 1(sh. 1,905,589,417.97). Utofauti pia unaonekana katika ukokotoaji wa jumla za bajeti zilizopitishwa kulin-gana na mihula (1-4) ambayo ni jumla ya kiasi cha shilingi 1,951,089,719.73. Timu iliomba kupata

8

ufafanuzi wa tofauti hizo.

Majibu ya menejimenti: Utofauti huo ulionekana kwenye taarifa ya awali (first draft) lakini baada ya marekebisho yaliyofanyika kwenye Plan Rep Dodoma mwezi Julai 2015 taarifa za mwisho hazina tofauti kati ya CCHP na taarifa ya utekelezaji (naambatanisha taarifa za robo ya kwanza hadi ya nne kwa uthibitisho zaidi).

Hoja namba 14: Timu ya SAM ilipenda kufahamu kama pesa za ruzuku kutoka serikali kuu “Local Gov-ernment Block Grant” zilivyoandikwa katika mpango wa CCHP humaanisha matumizi mengine (OC). Ikiwa jibu ni ndio, timu imebaini utofauti wa bajeti iliyopitishwa katika CCHP uk 3 (sh.109,412,000/-) na ile iliyopo katika ripoti ya utekelezaji jedwali namba 1 (sh. 210,211,999.80/-) ambapo kuna utofauti wa kiasi cha shilingi 100,799,999.8/-. Timu iliomba kupatiwa ufafanuzi wa utofauti huu.

Majibu ya menejimenti: Ni kweli local Government block Grant kama ilivyoandikwa katika mpango wa CCHP ina maana OC kwenye mpango wa CCHP ulionyesha kuna kiasi za cha fedha shilingi 109, 412,000/- na kwenye taarifa ya utekelezaji (Jedwali 1) inaonyesha fedha shilingi 210,211,999.80/-, ziada ni shilingi 100, 799,999.80 hii imetokana na ongezeko la fedha za “on call allowance” ambazo zilikuja baada ya mpango kupitishwa. Hivyo kutakiwa kutolea taarifa kwenye taarifa ya utekelezaji wa kila robo mwaka.

Hoja namba 15: Bajeti iliyopangwa kwa kipaumbele cha 8 (kuboresha watumishi wa afya) katika CCHP uk 13 ni (sh.1,058,730,200/-) ambayo ni tofauti na jinsi inavyoonekana katika ripoti ya utekelezaji (Jedwali namba 3) ambayo ni shilingi 1,092,964,163/-. Timu iliomba ufafanuzi katika hili.

Majibu ya menejimenti: Kwenye kipaumbele namba 8 kwenye mpango wa CCHP ilipangwa shilingi 1058, 730,200/- lakini baada ya kupewa ‘ceiling ya On call allowance’ shilingi 100,800,000/- fedha hizo ziliingizwa kwenye mfumo wa Plan Rep kwenye vipaumbele viwili yaani kipaumbele namba 8 shilingi 34,233,963/- na kipaumbele namba 2 shilingi 66,566,037/- hivyo kufanya kipaumbele namba 8 kuone-ka kwenye taarifa ya utekelezaji shilingi 1,092,964,163/-

Hoja namba 16: Mpango wa CCHP katika ukurasa wa 3 umeainisha kiasi cha michango kitaka-chochangiwa na kila taasisi ambazo ni Benki ya Dunia na shirika la Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation (EGPAF). Ripoti ya utekelezaji (jedwali namba 1) inaonesha kupatikana kwa pesa hizo kwa ujumla wake na sio kuainisha kuwa kila taasisi imetoa shilingi ngapi. Timu iliomba kupatiwa taarifa ya kila mmoja aliweza kutoa kiasi gani kulingana na bajeti zao katika mpango.

Majibu ya menejimenti: Mpango wa CCHP unaonyesha kiasi cha fedha kitakachotolewa na mdau yoyote wa maendeleo, lakini kutokana na mabadiliko ya namna ya utoaji wa taarifa kwa kutumia Plan Rep hauruhusu kutoa mchanganuo huo ila unaweza kufuatilia shughuli zilizofanyika kwenye taarifa ya utekelezaji ya kila robo kwa kila chanzo cha fedha. Pesa za EGPAF ambazo zilipokelewa zinaonekana ila Benki ya Dunia hawakuleta pesa kama walivyoahidi.

9

Hoja namba 17: Timu ilibaini kuwa Mpango wa CCHP, uk 129, shughuli C07SO1, ripoti ya utekelezaji robo ya 4 uk.5 unaonesha kuwa, matengenezo ya Zahanati ya Narunyu yalipangiwa kiasi cha shilin-gi 20,096,553/- na kupangwa kutekelezwa katika robo ya 4 (CCHP). Hata hivyo ripoti ya utekelezaji robo hiyo ya 4 inaonesha kiasi cha pesa kilichopokelewa na kutumika kuwa ni shilingi 4,995,200/- na kutofautiana na kiasi kilichoripotiwa kupokelewa na kutumika kwenye taarifa ya utekelezaji ya mwaka, ambapo imeripotiwa jumla ya kiasi cha shilingi 13,400,200/- kilitumika na matokeo yake kuripotiwa ukarabati wa nyumba mbili badala ya zahanati. Timu iliomba ufafanuzi wa utofauti wa pesa zilizoripoti-wa kutumika katika robo ya 4 na ripoti ya utekelezaji ya mwaka; utofauti unaoonekana vile vile kwenye matokeo ya utekelezaji wa shughuli hii.

Majibu ya menejimenti: Tulipanga kutumia shilingi 20,096,553/- kwa mwaka lakini mpaka robo ya nne tulipokea shilingi 4,995,200/- na kiasi hicho kutumika chote katika robo husika kwa 100%. Utofauti wa pesa na matokeo vinavyoonekana kwenye ripoti ya robo ya nne ya mwaka tutarejea nyaraka na kutoa ufafanuzi.

Hoja namba 18: Timu ilibaini utofauti wa bajeti katika shughuli namba CO8S 01 baina ya CCHP na ripoti ya utekelezaji (Ripoti ya robo 3 na 4 uk 10 na CCHP uk 125) ambapo fedha iliyoainishwa kwa shughuli ilikuwa ni shilingi 12,600,000/ kwa kila robo wakati fedha iliyopokelewa na kutumika kwa robo 3 na 4 ikiwa ni shilingi 16,800,000/- kwa kila moja. Timu iliomba kupata ufafanuzi wa ongezeko la fedha iliyotumika tofauti na bajeti iliyoidhinishwa.

Majibu ya menejimenti: Katika bajeti ya robo iliyopita palikuwa na bakaa hivyo katika utekelezaji wa robo uliyofuata fedha ziliweza kutumika zaidi. Pia ukumbukwe si kila fedha zikipokelwa ni lazima utumie zote kwa robo hiyohiyo.

Hoja ya 19: Timu ilibaini kuwa mpango wa CCHP uk 126 katika shughuli ya CO4S 01 ulionesha kuwe-ka mfumo wa maji bomba katika kituo cha afya mjini, ambapo kiasi cha shilingi 2,000,000/- kilipangwa kutekeleza shughuli hiyo katika robo ya nne. Ripoti ya utekelezaji ya mwaka na ile ya robo ya nne zinaonesha kuwa kiasi cha pesa kilichopokelewa na kutumika kuwa ni shilingi 880, 000/-. Shughuli iliripotiwa kukamilika kwa asilimia 100 na matokeo ya shughuli hiyo kuripotiwa kuwa ni matengenezo ya mashine ya fotokopi badala ya shughuli iliyoainishwa kwenye CCHP. Timu iliomba kupata ufafanuzi wa kwa nini utekelezaji wa shughuli hii upo tofauti na mipango ya awali.

Majibu ya menejimenti: Japo tulipanga kukusanya shilingi 2, 000,000/- kwa chanzo cha malipo ya papo kwa papo kwa shughuli hiyo, tulipata shilingi 880,000 /- kutokana na upungufu wa mapato. Ilitu-pasa kutumia tulichopata.Hoja namba 20: Mpango wa CCHP uk 128 umeainisha kupanga kutekeleza shughuli namba CO-7SO2 (ukarabati wa nyumba ya mfanyakazi, zahanati ya Kineng’ene) katika robo ya nne. Ripoti ya utekelezaji robo ya nne imeonesha kuwa shughuli hii ilitengewa kiasi cha shilingi 3,489,675/- ingawa hakuna pesa iliyopokelewa wala kutumika wakati ukarabati ukiripotiwa kukamilika kwa asilimia 100.

10

Ripoti ya utekelezaji ya mwaka nayo imeonesha kiasi hicho hicho kupokelewa chote na utekelezaji kukamilika kwa asilimia 100. Timu ya SAM ilipenda kupata ufafanuzi wa jinsi gani utekelezaji ulifanyika tena kwa asilimia 100 katika robo ya nne wakati hakuna pesa iliyopokelewa.

Majibu ya menejimenti: Ukarabati wa nyumba ya mganga wa zahanati ya Kineng’ene ulifanywa katika robo ya pili badala ya robo ya nne kutokana na unyeti wa tatizo lilivyokuwa kwa wakati huo. Ilionekana mtumishi hakuwa na mahali pa kuishi, tukatekeleza hilo kwa bajeti ya shilingi 3,489,675/-.

Hoja ya 21: Uchambuzi wa timu umebaini utofauti wa bajeti katika shughuli namba COIS 01 ambapo bajeti iliyopangiwa shughuli hii kulingana na CCHP (uk 122) ni shilingi 1,500,000/- kwa robo. Ripoti za utekelezaji za robo zinaonesha bajeti tofauti ambayo ni shilingi 1,991,875/- wakati ripoti ya utekelezaji ya mwaka inaonesha shughuli hii kupangiwa kiasi cha shilingi 7,967,500/-. (Robo ya kwanza uk. 12 inaonesha pesa iliyopangwa ni shilingi 2,289,600/- ambapo hakuna kilichopokelewa wakati fedha iliyotumika ikionekana ni shilingi 2,054,000/- robo ya tatu uk 11 inaonesha bajeti iliyotumika ni shilingi 3,291,000/- na robo ya nne ikionesha fedha iliyopokelewa ni shilingi 3,315,250/- na iliyotumika ni shil-ingi 3,545,250/-. Timu ya SAM iliomba ufafanuzi wa jinsi gani shughuli moja kupangiwa bajeti tofauti, na pia kujua kiasi kilichotumika katika robo ya kwanza kilitoka wapi wakati pesa haikupaikana. Vilevile kupata ufafanuzi wa fedha ya ziada iliyotumika katika robo ya nne.

Majibu ya menejimenti: Shughuli namba COIS01 ilikuwa na bajeti ya shilingi 7,967,500/- kwa ajili ya kutekeleza zifuatazo: a. Posho za kufanyia uchunguzi maiti “Postmortem allowance” shilingi 1,500,000/- b. Posho ya kuhama “Moving expenses allowance” shilingi 5,481,000/- c. Gharama za mazishi shilingi 1,247,500/-Jumla 7,967,500/-

Hata hivyo, fedha iliyotumika robo ya 1 ni bakaa la bajeti ya 2013/2014 ambapo jumla ilikuwa shilingi 18,070,548/-, na shughuli namba C04S01 OC ilipangwa kutumia shilingi 2, 289,600/-. Naambatanisha “carried forward activities” kutoka 2013/2014. Fedha ya ziada iliyotumika katika robo ya nne ilitokana na bakaa ya fedha 2013/2014, pia tulipokea fedha za OC 2014/2015.

Hoja namba 22: Katika uchambuzi wa CCHP 2014/2015, timu ilibaini upungufu mkubwa wa vifaa tiba katika vituo. Mfano, Kituo cha Afya (town health center) kimeonekana kuwa na upungufu kama ifuatavyo (CCHP uk 55). • Mzani (Salter scale) - hakuna kabisa• Kidney dish - hakuna kabisa• Kipimia mapigo moyo wa mtoto tumboni (featal scope) - hakuna kabisa• Kitanda cha uchunguzi (examination bed)- kipo kimoja • Kiti cha huduma za meno (dental chair) - hakuna kabisa• Kitanda cha kujifungulia (delivery bed) - hakuna kabisa• Mikasi (scissors) - hakuna kabisaTimu iliomba kupatiwa ufafanuzi wa jinsi gani kituo cha afya ambacho ndicho kinachotumika kama

11

hospitali ya wilaya kuwa na upungufu wa vifaa hivi muhimu (Je huduma zilikuwa zinatolewaje pasipo vifaa hivyo?)

Majibu ya menejimenti: Kwanza niombe kukanusha takwimu zilizotajwa hapo juu. Siyo za kweli kuwa kituo cha afya cha manispaa kina uhaba huo wa vifaa. THC ndiyo tegemeo kubwa kwa wakazi wa Lindi hivyo ina vifaa vya kukidhi kutoa huduma za afya kama takwimu ninavyoonyesha hapa chini.• Mizani ya kupimia - zaidi ya 3• Kidney dish zipo zaidi ya 8• Kipimio cha mapigo ya mtoto tumboni wanatumia doppler machine ambayo ni kisasa zaidi.• Vitanda vya kuzalia vya akina mama wajawazito vipo 2.• Vitanda vya uchunguzi (examination bed) vipo 3 yaani kila chumba cha daktari.• Kiti cha kutolea meno (dental Chair) kipo 1 ila kutokana na changamoto ya nafasi ya kituo cha Afya

cha Manispaa kiti hicho tulipeleka zahanati ya Polisi.• Kituo cha afya kina mikasi ya kukidhi kutoa huduma ndiyo maana kinaweza kuzalisha akina mama

wajawazito na hata kutoa huduma ya upasuaji mdogo.Timu haikuridhika na majibu yaliyotolewa na menejimenti na kuomba ufafanuzi zaidi wa hoja hii kwa kuwa timu ilizipata takwimu hizo kutoka katika CCHP 2014/15 uk 55 (katika sehemu ya situation anal-ysis). Hivyo katika kikao cha ndani na CHMT, waliweza kufafanua kuwa kulikuwa na tatizo la uchapaji (typing error) katika waraka huo.

2.3 Usimamizi wa UtendajiBaada ya uchambuzi wa nyaraka, timu ya SAM ilipata fursa ya kutembelea vituo vya huduma za afya ili kufanya ulinganifu wa taarifa zilizochambuliwa na hali halisi ya huduma zitolewazo. Jumla ya vituo vya huduma vya afya 12 vilitembelewa ambavyo ni: Kituo cha Afya (THC), Zahanati za Narunyu, Ki-tumbikwela, Mingoyo, Mnali, Kineng’ene, Tulieni, Nachingwea, Chikonji, Mbanja, Mitwero na Ng’apa. Katika ziara hiyo, timu iliweza kubainisha maeneo ambayo yalionekana kuwa na ufanisi mzuri wa utendaji na kutoa pongezi. Baadhi ya maeneo ambayo yalionekana kufanya vizuri ni pamoja na:• Vituo vya Mnali na Chikonji vina miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu.• Vituo vyote vina umeme. Timu ya SAM inashauri vituo vitumie umeme huo kuboresha huduma.

Mfano, ni vema kutumia sterilizer za umeme badala ya jiko la gesi. • Kituo cha Mingoyo hutumia rasilimali zake kutengeneza stoo ya dawa na kuweka mazingira mazuri

ya huduma za CTC. Zahanati zingine ziige mfano huo.• Masuala ya usafi wa mazingira kwa kituo cha afya, zahanati ya Mingoyo, Nachingwea na Ki-

neng’ene. • Zahanati ya Kineng’ene kuwa na maji safi na salama na ya kutosha kurahisisha utoaji wa huduma,

hivyo wengine pia waige mfano.• CHMT imefanya usimamizi mzuri (supportive supervision) kutokana na maoni chanya kutoka ka-

tika vituo.• Kituo cha afya cha mjini kina vyoo vya kisasa na visafi.• Manispaa imefanikisha ujenzi wa nyumba za kisasa za watumishi katika vituo vya Mnali, Chikonji,

Kineng’ene, Mbanja, Nachingwea, Mingoyo. Timu ya SAM inaomba hili liendee katika vituo vyote.

12

Mbali na pongezi, timu ya SAM pia ilibainisha changamoto za jumla kwa vituo vyote ambazo ni:• Vituo vyote 12 vya kutolea huduma za afya vina umeme wa Tanesco lakini vyote vina tumia gesi

kuchemshia vifaa tiba badala ya kutumia ‘sterilizer’ za umeme, kitu ambacho timu iliona inaon-geza gharama za uendeshaji.

• Zahanati zote hazina uzio (hii ni hatari kwa usalama). • Zahanati zote isipokuwa Kitumbikwela, Nachingwea, Kineng’ene na Chikonji zina uhaba wa

matundu ya vyoo. Vyoo vingi si salama na vina matundu mawili yanavyotumiwa na wa tumishi na wagonjwa kwa pamoja bila kujali jinsia.

• Zahanati karibu zote zina majengo machakavu sana.• Zahanati zote kasoro Mingoyo na Kitumbikwela hazina vyumba vya maabara.• Vituo vyote kasoro Mnali na Chikonji havina miundombinu rafiki kwa ajili ya watu wenye ulemevu.• Zahanati zote 11 zina uhaba wa watumishi. • Vituo vyote vina uhaba wa nyumba za watumishi, zilizopo, nyingi hazikidhi mahitaji ya familia

(zina chumba na sebule tu).• Vituo vyote vina uchache wa wanachama wa TIKA (nguvu zaidi ya uhamasishaji inahitajika).• Vituo vyote vina changamoto katika matumizi ya masanduku ya maoni. Vituo na kamati za afya

hazina mamlaka ya kuratibu masanduku hayo.• Tatizo la kutokupandishwa kwa madaraja na mishahara kwa watumishi. Watumishi wanakaa

miaka mingi bila kupandishwa madaraja huku wakiwa wanafanyiwa tathmini ya OPRAS kila mwaka. Pia ucheleweshaji wa malipo ya muda wa ziada.

Pamoja na changamoto za jumla, timu ya SAM ilibani pia changamoto ama hoja maalumu kwa kila kituo ambazo ziliwasilishwa kwa timu ya CHMT kwa ajili ya kupata ufafanuzi, uthibitisho na hatua za kuchukua katika kukabiliana na changamoto hizo. Zifuatazo ni hoja maalum kwa kila kituo na majibu ya timu ya afya ya wilaya (CHMT).

Baadhi ya nyumba za watumishi katika zahanati ya Mnali na Ng’apa.

13

Zahanati ya Mingoyo • Kituo hakina uzio, jambo ambalo ni hatari. Hii ilipelekea sanduku la maoni kuvunjwa na watoto

wanaoingia kituoni kucheza. • Vyumba havina usiri kutokana na kutokuwa na dari ‘ceiling board’. Pia vyumba ni vidogo sana,

havina hewa ya kutosha. Hii ni hatari kwa afya ya watumishi na wagonjwa wanaowa hudumia. • Kituo hakina shimo la kutupia kondo la uzazi. Wanatupa katika kichomea taka.• Uhaba wa vifaa tiba. Mfano, mashine ya kupima CD4 ipo moja, wanahitaji moja zaidi; mzani wa

watoto haupo katika hali nzuri, kituo kinatumia ‘featal scope’ ya kizamani sana ambayo majibu yake yanaweza kuwa si sahihi.

• Timu inakipongeza Kituo cha Mingoyo kwa kutumia rasilimali zake kutengeneza stoo ya dawa na kuweka mazingira mazuri ya huduma za CTC. Zahanati zingine ziige mfano huo.

Zahanati ya Mnali• Kituo kina tundu moja tu la choo nalo halipo katika hali nzuri. Tundu hili linatumiwa na wagonjwa

na watumishi bila kujali jinsia. • Kituo hakina kichomea taka wala shimo la kutupia kondo la uzazi. Wanatumia tundu la choo

kutupia kondo la uzazi. • Kituo kina miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu. • Kituo hakina maji, ingawa timu imeshuhudia bomba la maji kupita nje ya kituo huku kituo

kikinunua maji kutoka katika bomba hilo. • Utunzaji wa mali za kituo. Timu ilishuhudia kitanda cha uchunguzi kikiwa nje ya zahanati kwa

muda mrefu na kupelekea kuharibika kwa sababu ya kunyeshewa na mvua kikiwa nje.

Uchakavu wa jengo: Moja ya jengo chakavu katika zahanati ya Mingoyo.

14

Zahanati ya Kitumbikwela• Kituo ni chakavu sana mpaka kupelekea dari katika chumba cha dawa kuanguka. Pia dari katika

sehemu ya kusubiria huduma kwa wagonjwa linaning’inia. • Kituo kina nyumba mbili tu, ambazo pia zina changamoto. Nyumba ya mfawidhi ni chakavu sana

na haijakamilika, nyumba nyingine haitoshelezi mahitaji ya familia kwa kuwa ina chumba kimoja tu cha kulala na sebule.

• Kituo kina uhaba wa mikasi. Ipo mikasi miwili tu inayofanya kazi.

Zahanati ya Kineng’ene • Kituo hakina sanduku la maoni. • Kituo hakina shimo maalum kwa ajili ya kutupa kondo la uzazi.• Uchakavu wa miundo mbinu, dari la kituo

Uchakavu wa majengo: Moja ya nyumba ya Mganga Mfawidhi katika zahanati ya Kitumbikwela.

Moja ya kitanda kilichosahaulika nje ya zahanati ya Mnali.

15

Zahanati ya Tulieni• Chumba cha kuhifadhia dawa hakina dirisha. • Kamati ya zahanati haijapatiwa mafunzo ya uendeshaji na usimamizi.• Hakuna sehemu ya kutupia kondo la uzazi na kupelekea kutumika kwa choo kama mbadala.• Hakuna choo cha watumishi badala yake watumishi wamekuwa wakitumia vyoo vya wagonjwa.• Kina matanki ya kuhifadhia maji na kimekuwa kikivuna maji ya mvua. • Watumishi wanajaza OPRAS.• Kuna sanduku la maoni ingawa limekuwa halitumiki jinsi ipasavyo na watumia huduma.

Zahanati ya Nachingwea • Hakuna shimo la kutupia kondo la uzazi.• Kichomea taka hakina uzio na kinatoa moshi ambao unaleta athari za kiafya kwa jamii.

Moja ya dari linalokaribia kuanguka katika moja ya vyumba vya zahanati ya Kineng’ene.

Kichomea taka ambacho hakina uzio katika zahanati ya Nachingwea.

16

Zahanati ya Narunyu • Kituo hakina mashine ya kupimia CD4. • Kituo kina uhaba wa mikasi. Ipo mikasi miwili tu na ina kutu. • Kituo kina matundu mawili tu ya vyoo na moja halina kikanyagio. • Kituo hakina maji. Maji hununuliwa ndoo tatu kwa shilingi 1,000/- hivyo huathiri usafi wa kituo

kwa ujumla.• Kituo hakina shimo la kutupia kondo la uzazi.• Kuna uhaba wa vyumba vya kutolea huduma. Chumba kimoja hutumika kama stoo ya dawa,

chumba cha kuzalishia, kupumzikia mama na mtoto.• Vyumba vya kituo ni vidogo sana, na havina hewa ya kutosha. Vile vile majengo ni chakavu

sana.

Baadhi ya wa vifaa tiba vilivyochakaa (kushoto), kulia ni moja ya tundu la choo lenye kanyagio moja katika zahanati ya Narunyu.

Moja ya dari (Kushoto) la vyumba vya zahanati ya Narunyu lililoharibika kwa kuliwa na mchwa, kulia ni uchakavu wa miundombinu sehemu ya mapokezi.

17

Zahanati ya Ng’apa• Kuna upungufu mkubwa wa mikasi. Ipo mikasi

mitatu tu na ina kutu. Viwembe hutumika kama mbadala wa mikasi.

• Vyumba vya kituo ni vidogo sana hususani • chumba cha kujifungulia. Pia miundombinu ni

chakavu sana.• Kituo kina tundu moja tu la choo, ambalo pia ni

bovu. • Hakuna maji, hali inayoathiri usafi wa zahanati. • Eneo la kituo ni dogo sana. • Hakuna shimo la kutupia kondo la uzazi.

Zahanati ya Chikonji• Kituo hakina mashine ya kupimia CD4. • Kituo hakina stoo maalum ya dawa. Dawa zinahifadhiwa maeneo tofauti, kama chumba cha

mganga, chumba cha kutolea dawa na wodi ya wazazi. • Vyumba vya kituo ni vidogo sana na havina hewa ya kutosha. • Hakuna maji. • Kituo hakina kichomea taka, hivyo hutumia shimo ambalo pia halina wigo, kitu ambacho ni hatari

kwa wapita njia na hasa watoto. • Hakuna shimo la kutupia kondo la uzazi hutumia choo kama mbadala.

Choo kinachotumika katika zahanati ya Ng’apa.

Shimo linalotumika kama kichomea taka katika zahanati ya Chikonji.

18

Zahanati ya Mbanja• Hakuna shimo la kutupia kondo la uzazi

wala kichomea taka. Linatumika shimo lililo wazi kama kichomea taka.

• Choo cha kituo kina nyufa hatarishi.• Hakuna mashine ya kupimia CD4.• Kituo kina maji na umeme ingawa hakuna

mbadala wa umeme unapokatika wala matanki ya kuhifadhi maji.

• Kituo kina nyumba za watumishi mbili zenye uwezo wa kuishi familia nne.

• Sanduku la maoni limewekwa ndani ya chumba cha mganga (hii huweza kusababisha wananchi kushindwa kutoa maoni kwa kuhofia kujulikana).

Zahanati ya Mitwero• Timu ya SAM ilifanikiwa kutembelea kituo hiki lakini haikufanikiwa kuonana na mganga

mfawidhi wa kituo (hakukua na mtumishi yeyote siku timu ilipotembelea).• Timu ilipokwenda siku ya pili, ilifanikiwa kuonana na mtumishi wa kujitolea aliyekuwa ana

toa huduma peke yake bila kuwa na msimamizi mwajiriwa, hivyo timu ilishindwa kufanya mahojiano naye.

Kituo cha Afya (THC)• Kichomea taka kipo karibu na wodi (moshi unaweza ukawa kero kwa wagonjwa).• Kituo hakina chumba cha upasuaji. Timu inaona kwamba kituo kingekuwa nayo basi ingepungu-

za usumbufu na adha kwa wagonjwa kwenda mbali kutafuta huduma hiyo. Pia changamoto hii inaweza kuchangia ukosefu wa mapato kwa kituo.

• Eneo la kituo ni dogo sana. • Kituo kina mashine ya kupimia CD4 ingawa timu ilibaini uwepo wa changamoto kama vile ukose-

kanaji ama uhaba wa vitendanishi zinaokwamisha kutumika kwake.• Kituo kina sanduku la maoni.• Huduma za maji na umeme zinapatikana kituoni.

MAJIBU YA MENEJIMENTI KWA HOJA ZA VITUO • Halmashauri inaendelea kuomba watumishi kupitia bajeti ya mishahara “PE” ili kupunguza tatizo la

uhaba wa watumishi lakini pia kusambaza watumishi (re-distribution) kutoka kituo chenye watumi-shi wengi kwenda vituo vyenye uhaba zaidi.

• Halmashauri inaendelea kuweka bajeti ya kufanya ukarabati wa nyumba za watumishi na mae-neo ya kutolea huduma za afya kadri ya upatikanaji wa fedha. Kwa mwaka wa fedha 2016/17 idara imepanga kiasi cha shilingi 31,000,000 kwa ajili ya ukarabati na umaliziaji wa nyumba. Pia

Shimo linalotumika kama kichomea taka katika zahanati ya Mbanja.

19

halmashauri inaendelea kuweka bajeti kupitia vyanzo vyake vya mapato ya ndani na wafadhili mbalimbali ili kupunguza tatizo la uhaba wa nyumba za watumishi kama vile ujenzi wa nyumba ya mganga zahanati ya Kineng’ene ambao unaendelea na maeneo mengine.

• Ushauri wa kujenga miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu umepokelewa na utazingatiwa hasa kwa zile zahanati zinazoendelea kujengwa sasa, ili ziwe na mazingira rafiki kwa walemavu kama vile zahanati ya Nandambi n.k. Pia kulingana na upatikanaji wa fedha, halmashauri itakara-bati zahanati zenye changamoto hii.

• Vituo vyote vina masanduku ya ukusanyaji wa maoni ya mteja na wenye mamlaka ya kukusanya maoni hayo kutoka kwenye masunduku hayo yapo chini ya dawati linaloshughulikia kero mbalim-bali. Lakini pia idara inapata mrejesho wa huduma zitolewazo kupitia sauti ya mteja. Idara imeahidi kukaa na mkurugenzi ili kuona ni jinsi gani watatatua tatizo la uratibu wa masanduku ya maoni.

• Kuhusu uhaba wa maabara katika zahanati, idara ilieleza kuwa huduma za afya zinatolewa kwa kufuata miongozo kwa maana kila ngazi ya kituo kuna huduma stahiki zinazotakiwa kuwepo ku-tokana na miongozo. Kwa sasa zahanati zote zina uwezo wa kupima Malaria kwa kutumia MRDT (Malaria Rapid Diagnostic Test).

• Tayari halmashauri imejiwekea mikakati ya ujenzi wa vyoo kupitia makusanyo yake ya ndani, na vilevile halmashauri imeingia makubaliano ya ujenzi wa vyoo bora na kampuni ya SES ambayo itajenga vyoo zahanati ya Mbanja, Ng’apa, Chikonji, Mnali.

• Idara inaendelea kufanya uhamasishaji wa wananchi kujiunga Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kupitia matangazo ya radio Mashujaa, mikutano mbalimbali kama vile vikao vya madiwani na wanasiasa wengine. Timu ilishauri pia HBC watumiwe pamoja na timu ya SAM ili kuhamasisha wananchi kujiunga na bima za afya.

• Idara inatambua umuhimu wa ujenzi wa vichoma taka na mashimo ya kuhifadhia kondo la uzazi kwenye zahanati zake zote na tumeanza ujenzi wa vichoma taka zahanati za Ng’apa, Mingoyo, Kitumbikwela, Tulieni, THC na Kineng’ene. Na tumeweka kwenye bajeti ya kumalizia ujenzi wa vichoma taka vingine katika zahanati zilizobakia.

2.4 Usimamizi wa UadilifuTimu ilieweza kubaini mapungufu mbalimbali katika utekelezaji wa shughuli za afya za manispaa. Timu iliwasilisha rasimu ya ripoti yenye hoja kwa timu ya uendeshaji wa huduma za afya ya manispaa (CHMT). Lengo lilikuwa kupata ufafanuzi, uhalalisho na uthibitisho wa hoja zilizotokana na uchambuzi wa nyaraka mbalimbali pamoja na ziara ya vituo vya huduma za afya.

Timu ya uendeshaji (CHMT) ilipata fursa ya kujibu hoja (kwa maandishi) kama zilivyoainishwa hapo juu kama hatua ya uwajibikaji kwa wananchi. Mbali na kujibu hoja kwa maandishi, timu ya SAM ilipata fursa ya kukutana na timu ya uendeshaji/usimamizi wa shughuli za afya (CHMT) ya Manispaa ya Lindi na kujadili ana kwa ana hoja zilizokuwa mezani. Tunaipongeza timu ya usimamizi wa shughuli za afya ya Manispaa ya Lindi (CHMT) kwa kuahidi kuchukua hatua za marekebisho (katika baadhi ya maeneo) ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi. Katika zoezi hili, timu ya SAM imeweza kujengewa uwezo wa kusimamia uadilifu wa umma kwa kuhoji watoa huduma juu ya uwajibikaji wao kwa jamii, na kudai kufanyika kwa hatua za marekebisho katika

20

maeneo ambayo watoa huduma hawakufanya maamuzi sahihi.

Timu ilipata fursa ya kupitia ripoti za ukaguzi (ndani na nje) pamoja na mihutasari ya baraza la madi-wani ili kuweza kuona dondoo za mapungufu ya kiutendaji kama yalivyobainishwa na taasisi hizi ikiwa ni pamoja na mapendekezo yake na hatua za marekebisho zilizochukuliwa na Halmshauri ili kubore-sha utendaji. Kwa kupitia ripoti hizi, timu ya SAM imeweza kubaini kwa undani zaidi kiwango cha uadil-ifu wa watumishi wa umma, hususani katika sekta ya afya ambayo timu ilikuwa ikifuatilia, hasa hatua za masahihisho zilizochukuliwa. 2.5 Usimamizi wa UwajibikajiKatika kuangalia ni jinsi gani uwajibikaji unasimamiwa ndani ya manispaa, timu ya SAM ilipitia nyar-aka za ukaguzi zikijumuisha ripoti za mkaguzi wa ndani, mkaguzi mkuu wa hesabu wa serikali na mihutasari ya baraza la madiwani ikiwa na adhma ya kuangalia ni kwa jinsi gani watendaji wamekuwa wakifanyia kazi mapendekezo ya vyombo hivi vya usimamizi ikiwemo vyombo venyewe kuyafanyia kazi kwa wakati ili kuleta maboresho na usahihisho.

Hata hivyo, kupitia uchambuzi wa mihutasari ya baraza la madiwani timu ilibaini kuwa agizo la wa-heshimiwa madiwani katika muhtasari wake LMC/KF/MUHT.NA; 25/2014/15 uk. 24 wa robo ya pili 2014/15 la kurekebisha kichomea taka katika zahanati ya Nachingwea halikufanyiwa kazi hivyo kutoa rai kwa watendaji kushirikiana na wasimamizi wa huduma za jamii kushirikiana kwa pamoja kutatua changamoto katika huduma za afya.

Kwa kupitia mikutano na timu ya uendeshaji/usimamizi wa shughuli za afya manispaa, timu ya SAM iliweza kuhoji juu ya uwajibikaji wa watoa huduma kwa wananchi/jamii na kupata ufafanuzi, uhalalisho na uthibitisho wa mambo mbalimbali yahusuyo utekelezaji wa miradi/shughuli mbalimbali za afya. La-kini pia, kupitia mkutano wa wadau wote wa afya na uongozi wa Manispaa ya Lindi, timu ya SAM na wananchi kwa pamoja waliweza kuzijadili hoja na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya afya katika manispaa. Mkutano huu ulipelekea kufikia muafaka juu ya hatua zitakazochukuliwa katika kuboresha utoaji wa huduma za afya katika manispaa.

Katika mikutano ya mwanzo kabisa ya zoezi hili la uwajibikaji kwa jamii, wawakilishi wa Sikika walifan-ya mkutano na Baraza la Madiwani, lengo kuu likiwa ni kuwajengea uwezo juu ya dhana ya uwajibikaji jamii. Madiwani ni nguzo muhimu katika usimamizi wa uwajibikaji kwa kuwa wana mamlaka ya moja kwa moja ama kupitia kamati zao kupitisha mipango na bajeti za manispaa na pia kuhoji juu ya matumi-zi yake. Madiwani wana wajibu wa moja kwa moja wa kusimamia uwajibikaji hususani katika kufikia maamuzi sahihi ya matumizi ya rasilimali za umma. Timu SAM kama moja ya nguzo za usimamizi wa huduma za jamii, hususani huduma za afya, kwa kushirikiana na taasisi zingine za usimamizi, itafanya ufuatiliaji wa maazimio yote yaliyofikiwa kupitia mchakato mzima wa SAM ili kuboresha huduma za afya katika Manispaa ya Lindi.

3.0 HitimishoKazi ya ufuatiliaji wa uwajibikaji kwa jamii iliyotekelezwa na timu ya SAM imeibua hoja mbalimbali

ambazo tunaamini ni chachu ya mabadiliko katika Manispaa ya Lindi, hususan Idara ya Afya. Timu

inaamini kuwa, mchakato huu wa SAM una manufaa makubwa kwa jamii na halmashauri kwa ujumla.

Pamoja na kutoa mafunzo maalumu na kuwajengea uwezo wananchi wa kushiriki katika kuboresha

huduma za afya, bado mchakato huu umeweza kubainisha changamoto zinazoikabili halmashauri.

Jambo hili ni msaada mkubwa katika kuleta mabadiliko, hususan kwenye Idara ya Afya na utoaji wa

huduma za afya kwa ujumla.

Ni imani kubwa ya timu kuwa, ili halmashauri iweze kuwajibika ipasavyo kwa jamii, ni muhimu kwa zo-

ezi hili kufanyika kwa idara zote mara kwa mara. Hivyo basi, kwa imani hiyo, timu inashauri manispaa

kushirikiana na Sikika na wadau wengine kuiwezesha timu iwe endelevu na iweze kufuatilia uwajibikaji

kwa jamii katika idara nyingine zote za halmashauri. Lengo ni kufikia haki za binadamu na kukidhi ma-

hitaji ya jamii.

SEHEMU YA TATU

21

22

ViambatishoKiambatisho1: Wajumbe wa Timu ya SAMNa. Jina Jinsi Nafasi1 Frank Magari ME Mwenyekiti2 Khalfani Mohamedi Issa ME Katibu

3 Hassani Maliki Kalla ME Mjumbe4 Hawa Kipara KE Mjumbe5 Mohamedi Kachele ME Mjumbe6 Zuhura Abdallah Stahamili KE Mjumbe

7 Ratifa Saidi Mtimbe KE Mjumbe

8 Milembe Lyogohya ME Mjumbe 9 Fadhili Ngongorowe ME Mjumbe 10 Mohamedi Zuberi Luhena ME Mjumbe 11 Imani Ligau ME Mjumbe 12 Christopher Kumpanga ME Mjumbe 13 Swalehe Ahmad Mohamed ME Mjumbe

14 Asha Bilali KE Mjumbe 15 Mohamedi Kanile ME Mjumbe

Kiambatisho 2: Maazimio ya Kuboresha Huduma SN HOJA MAAZIMIO MUHUSIKA1 Tatizo la masanduku ya maoni

vituoni: Kutokuwekwa maeneo ya faragha kwa wananchi kutumia kwa uhuru.Kuwa wazi muda wote (kutokutumika).Kutofunguliwa kwa wakati (mfunguaji ni dawati maalum la kero la manispaa ambalo huwa halivishirikishi vituo katika ufunguaji).

• Vituo visivyokuwa na masanduku viwekewe.

• MMO atafute njia ya kurahi-sisha ufunguaji wa masan-duku unaoshirikisha vituo.

• Ofisi ya MMO• Waganga wa

vituo

2 Uchakavu wa miundombinu ya vituo na nyumba za watumishi.

• Idara kufanya ujenzi na ukarabati wa zahanati. Upanuzi wa zahanati ya Kitumbikwera ili kuongeza wodi ya wazazi, ujenzi wa zahanati ya Ruaha, Mkanga pamoja na kumalizia ujenzi wa zahanati ya Nandambi.

• Idara kutenga bajeti ya ku-fanya ukarabati wa zahanati chakavu pamoja na nyum-ba za watumishi.

• Pia idara itaaangalia suala la kuweka mazingira rafiki kwa watu wenye ulemevu kwa vituo vipya vitakavyo-jengwa.

• Ofisi ya MMO• Manispaa

23

3 Ubovu na upungufu wa vyoo pamoja na vichomea taka kati-ka vituo vya huduma.

• Idara kupitia kampuni ya SES itatekeleza ujenzi wa vyoo katika zahanati za Mnali, Mbanja, Ngapa na Chikonji.

• Halmashauri kutafuta fedha kutoka vyanzo vya ndani ili kukarabati na kujenga vyoo kwenye zahanati zilizobaki.

• Idara kutekeleza ujenzi wa vichomea taka katika za-hanati za Ng’apa, Mingoyo, Kitumbikwela, Tulieni, Ki-nengene na THC; na ujenzi huu utakamilishwa ndani ya mwaka huu wa fedha (2016/17).

• Idara kumalizia ujenzi wa vichomea taka katika za-hanati zilizobaki kwa bajeti ya mwaka 2017/18.

• Ofisi ya MMO• Manispaa

4 Upungufu wa watumishi. SAM iligundua kuwa vituo vyote vina upungufu wa watumishi pamo-ja na watumishi kutokuwepo kabisa vituoni katika baadhi ya vituo.

• Halmashauri kufanya re-distribution ya watumishi kutoka kwenye vituo vyenye watumishi wengi kwenda kwenye vituo vyenye upun-gufu mkubwa

• Halmashauri itaendelea kuomba watumishi kupitia PE hili kukabiliana na tatizo hili.

• Idara kutekeleza mkakati wa kutembelea vituo vyote (surprise visits) hata nyakati za usiku ili kuhakikisha wa-tumishi wanakuwepo vituoni muda wote

• Wajumbe wa SAM kufanya ufuatiliaji wa uwepo wa watumishi vituoni na kutoa taarifa kwa ofisi ya MMO.

• Manispaa• Ofisi ya MMO• Waganga wa

vituo• Timu ya SAM

5 Tatizo la vituo kutokuwa na uzio pamoja na maeneo ya vituo kutopimwa.

• Manispaa kufanya tathmini ya vituo vyote ili kutoa hati kwa vituo ambavyo maeneo yake bado hayajapimwa na hayana hati.

• Idara kuhakikisha vituo vinawekewa uzio ili kuwe-ka mazingira salama kwa mali za vituo, watumishi na wagonjwa.

• Manispaa• Ofisi ya MMO

24

25

6 Tatizo la uchache wa wanan-chama wa bima za afya (TIKA) pamoja na uwingi wa misa-maha (zaidi ya asilimia 60 ya wagonjwa ni wa misamaha).

• Idara kuendeleza uhama-sishaji kwa wananchi kujiunga na TIKA kwa kushirikiana na viongozi wa mitaa pamoja na vyombo vya habari, mfano kwa kutumia radio Mashujaa. Lengo ni kufikia asilimia 90 ya wanufaika.

• Wajumbe wa SAM kusaidia kuhamasisha wananchi kujiunga na TIKA.

• Ofisi ya MMO• Wajumbe wa

SAM

7 Tatizo la uwazi na upatikanaji wa taarifa, hususani taarifa za mapato na matumizi, pamoja na maendeleo ya vituo katika mbao za matangazo ya vituo.

• Vituo vitoe taarifa za mapa-to na matumizi, maendeleo ya vituo pamoja na huduma zinazotolewa vituoni. Taarifa hizi zibandikwe kwenye mbao za matangazo vituo-ni. Taarifa ziwe zinaeleweka kwa wananchi wote kwa lengo la kufanya ufuatiliaji wa huduma zinazotolewa.

• Wataalamu wa manispaa pia watoe taarifa kwa wananchi bila ya kuulizwa au kuombwa. Hii ni njia mojawapo ya kupima uwa-jibikaji.

• Mstahiki Meya• Ofisi ya MMO• Wajumbe wa

SAM• Waganga wa

vituo

8 Ufinyu na uchache wa bajeti ya kawaida inayotumika ku-tekelezea miradi ya maendeleo pamoja na vipaumbele vya afya vya manispaa.

• Idara iongeze bajeti ya kawaida ili kukidhi malengo ya vipaumbele vya afya vya manispaa.

• Pia idara iipe kipaumbele shughuli ya uhamasishaji afya (health promotion) katika ugawaji wa rasilimali katika bajeti zinazokuja. Hii itasaidia kuboresha afya na kupunguza gharama.

• Ofisi ya MMO• Manispaa• Mstahiki meya

9 Tatizo la ukosekanaji wa huduma ya maji safi na salama katika baadhi ya zahanati.

• Idara ihakikishe zahanati zote zinakuwa na mfumo wa kudumu wa maji safi na salama kuanzia mwaka wa fedha 2017/18.

• Ofisi ya MMO

10 Utunzaji wa vifaa na vifaa tiba katika vituo.

• Vituo kutunza vifaa na vifaa tiba.

• Waganga wa vituo

• Ofisi ya MMO

26

Kiambatisho 3: Hotuba ya Mkuu wa Wilaya

– HOTUBA – MKUTANO WA WADAU WA AFYA WA KUHIMIZA UFUATILIAJI WA UWAJIBIKAJI JAMII

TAREHE 25/10/2016UKUMBI WA COETC

Mstahiki Meya,

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri,

Mkurugenzi wa Sikika,

Hitifaki imezingatiwa

Awali ya yote napenda kutumia fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kutukutanisha leo

wote tukiwa na afya njema. Kwa dhati ninashukuru kujumuika nanyi leo katika mkutano huu muhimu

katika Manispaa yetu ya Lindi, ambao umeandaliwa na shirika la Sikika, niwapongeze sana.

Kipekee niwashukuru viongozi wa halmashauri; Mstahiki Meya wa manispaa, na Mkurugenzi mtendaji

kwa ushirikiano mkubwa mliouonesha kwa shirika la Sikika tangu walipofika katika manispaa yetu

mpaka kufanikisha mkutano huu, tena leo tukiwa na Timu yetu ya kufuatilia uwajibikaji walio ijengea

uwezo. Huu ndio uwajibikaji na utumishi wa umma.

Ni imani yangu kuwa lengo kuu la mkutano huu ni kuhimiza Utawala Bora katika kuimarisha mifumo

ya utoaji huduma bora za afya hapa katika manispaa yetu, hili ni jambo jema na la kuungwa mkono na

wadau wote tuliopo hapa. Uwajibikaji unaanzia kwa mtu binafsi, wananchi kwa ujumla, watendaji wa

serikali na wasio wa serikali, pamoja na sisi viongozi wenye dhamana. Sisi kama serikali hili ni suala la

kipaumbele, katika kufanikisha adhma hiyo serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama Sikika

tunaendelea kuimarisha misingi ya utawala bora nchini.

Jitihada hizo kwa serikali zipo wazi, wote ni mashuhuda jinsi serikali hii ya awamu ya tano inayoon-

gozwa na Mh. Rais John Pombe Magufuli imeonesha umadhubuti wa kuimarisha misingi ya utawala

bora hasa Uwajibikaji, Ushiriki wa Jamii na Uwazi. Shime kwetu sasa kuendelea kuimarisha misingi ya

utawala bora katika nchi yetu kuanzia ngazi ya msingi hadi ngazi kuu ya uongozi wetu.

Tunashukuru kasi hiyo ya Mh. Rais inaungwa mkono kikamilifu na wadau mbalimbali hasa shirika la

Sikika, kwani programu zao na hasa zoezi la Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii yaani Social Account-

ability Monitoring (SAM) ni kielelezo tosha na cha wazi kinachoakisi mchango wao katika utekelezwaji

wa Dira ya Taifa, sera ya afya, mkakati wa kupunguza umaskini, na mpango mkakati wa nne wa sekta

ya afya.

Jitihada hizi ni muhimu sana kwa serikali hususani kwetu viongozi wenye dhamana pamoja na wadau

wote kwa nafasi zetu pale tulipo.

Niwahakikishie kuwa, serikali ipo bega kwa bega nanyi kuhakikisha kuwa masuala ya uadilifu, uwa-

jibikaji na uwazi yanapewa kipaumbele cha kwanza ili kuleta maendeleo kwa wananchi, na katika

kuzingatia umuhimu huo serikali imeridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa ili kuimarisha dhana ya

uendeshaji wa shughuli za serikali kwa misingi ya utawala bora.

Dhana ya Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (SAM) au Social Accounatability Monitoring (SAM), inayotekele-

zwa na Sikika kwa mara ya kwanza imetambuliwa na serikali kwa kuingizwa katika mpango mkakati

wa nne wa sekta ya afya (uk. 69 - Kuhusu Uwajibikaji Jamii). Lengo kubwa la utekelezwaji wa dhana

hii kwa serikali ni kuimarisha mifumo ya utoaji huduma bora za afya kwa kushirikisha wananchi katika

kushiriki na kufuatilia uwajibikaji.

Ni vema tukumbuke kwamba, serikali imepewa dhamana kubwa sana na wananchi ya kusimamia na

kutumia rasilimali mbalimbali ili kuwahudumia wananchi. Rasilimali hizi zinatokana na wananchi wetu

hivyo hatuna budi kukumbuka kwamba, rasilimali hizi ni lazima zitafsiri maisha na ustawi wa wananchi.

Tutafanya hivyo kwa kuwashirikisha kikamilifu kwa kuwapa fursa ya kuhoji matumizi yake kupitia vion-

gozi wao.

Tunatambua kuwa Sikika inafanya kazi katika manispaa yetu ya Lindi kwa kipindi cha miaka mitano

2016-2020. Hivyo tutajifunza mengi na kufanikisha mengi kwa mujibu wa malengo yao.

Tarehe 16/09/2016, wadau wa afya hapa katika manispaa yetu ya Lindi waliunda timu ya SAM chini

ya uratibu wa Sikika ambapo leo Timu imeiva kwa kupatiwa mafunzo na kujengewa uwezo. Tupo hapa

kupata mrejesho wa kazi tuliyowatuma wananchi wetu na kuweka maazimio ya kuboresha upatikanaji

wa huduma za afya katika manispaa yetu. Kukamilika kwa hatua ya leo ni sehemu ya utekelezaji wa

mpango mkakati wa nne wa sekta ya afya. Tujadili hoja za Timu na tuunge mkono mapendekezo ya

maboresho yatakayotokana na mjadala wa kikao hiki.

Aidha, nitoe rai kwa Sikika kuendeleza kutekeleza shughuli zao hasa zoezi hili la SAM kwa uadilifu

mkubwa ili yale yote watakayoyafanya yawe na tija kwa wananchi na Manispaa.

Naamini kuwa mafanikio ya kikao hiki yatakuwa chachu ya kukuza UWAJIBIKAJI NA UWAZI katika

manispaa yetu. Nawatakia kikao na majadiliano mema yenye mafanikio makubwa.

Kikao hiki nimekifungua rasmi.

Asanteni Sana kwa Kunisikiliza

27

“Sikika inafanya kazi ya kuhimiza uboreshaji wa mifumo ya afya na

usimamizi wa fedha kupitia uwajibikaji jamii na uraghibishi

katika ngazi zote za serikali”

Nyumba Na.69Ada Estate, Kinondoni Barabara ya Tunisia Mtaa wa WaverleyS.L.P 12183Dar es Salaam, Tanzania.Simu: +255 22 26 663 55/57

Nyumba Na. 340 Mtaa wa Kilimani S.L.P 1970 Dodoma, Tanzania. Simu: 0262321307 Nukushi: 0262321316

Ujumbe mfupi: 0688 493 882 Nukushi: +255 22 26 680 15Barua pepe: [email protected] Tovuti: www.sikika.or.tzBlog: www.sikika-tz.blogspot.com Twitter: @sikika1Facebook: Sikika1Instagram: Sikika Tanzania