18
Umuhimu wa Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira Ushiriki wa Wananchi, Nguzo ya Maendeleo

Ushiriki wa Wananchi, Nguzo ya Maendeleo Booklet -Swahili Version.pdfutekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo. Muundo wa uwajibikaji kwa kuanzia ngazi ya chini ya maamuzi ni

  • Upload
    others

  • View
    18

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Ushiriki wa Wananchi, Nguzo ya Maendeleo Booklet -Swahili Version.pdfutekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo. Muundo wa uwajibikaji kwa kuanzia ngazi ya chini ya maamuzi ni

Umuhimu wa Huduma ya Maji na Usa� wa Mazingira

Ushiriki wa Wananchi, Nguzo ya Maendeleo

Page 2: Ushiriki wa Wananchi, Nguzo ya Maendeleo Booklet -Swahili Version.pdfutekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo. Muundo wa uwajibikaji kwa kuanzia ngazi ya chini ya maamuzi ni

1

Ushiriki wa Wananchi, Nguzo ya Maendeleo

Umuhimu wa Huduma ya Maji na Usa� wa Mazingira

Kimetayarishwa na: Mtandao wa asasi za Maji na Usa� wa Mazingira Tanzania (TAWASANET)

Shukrani: Kwa Mratibu wa Taifa wa Mtandao Ndugu Emmanuel Jackson na Ndugu Darius Mhawi, A�sa Sera na Utetezi katika O�si ya Sekretarieti kwa uandishi wa Kitabu hiki.

Kimehaririwa na: George Frank Kinyashi (Daktari-Fani ya Mipango) Mhadhiri wa Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Dodoma Tanzania

Mchoraji Katuni: Rashid Mbago (MG Graphics) Kimefadhiliwa na: Danish People’s Aid (DPA)

Toleo la Kwanza 2016

ISBN: 978-9976-9953-0-5

Kimesani�wa na Kupigwa Chapa na: Vilex Enterprises, Dar es Salaam

Page 3: Ushiriki wa Wananchi, Nguzo ya Maendeleo Booklet -Swahili Version.pdfutekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo. Muundo wa uwajibikaji kwa kuanzia ngazi ya chini ya maamuzi ni

2

YaliyomoUtangulizi.......................................................................................................................3Serikali za Mitaa ni nini?............................................................................................4Ugatuaji wa Madaraka...............................................................................................5Ushiriki wa Wananchi Kama Nguzo ya Maendeleo.........................................7Muundo wa Uwajibikaji katika Upangaji wa Ngazi ya Serikali za Mitaa..7Kwanini ni muhimu kwa Wananchi kushiriki?...................................................9Mchakato wa Upangaji wa Mipango katika Serikali za Mitaa Tanzania...9Huduma ya Maji na Usa� wa Mazingira.............................................................12Umuhimu wa Maji na Usa� wa Mazingira.........................................................13Matumizi ya Maji........................................................................................................13Usa� wa Mazingira.....................................................................................................14Madhara ya Kukosekana kwa Huduma za Maji na Usa� wa Mazingira..14Upangaji wa Miradi ya Maji na Usa� wa Mazingira Tanzania.....................15Hitimisho.......................................................................................................................15Vitabu vya Rejea.........................................................................................................16

Page 4: Ushiriki wa Wananchi, Nguzo ya Maendeleo Booklet -Swahili Version.pdfutekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo. Muundo wa uwajibikaji kwa kuanzia ngazi ya chini ya maamuzi ni

3

UtanguliziKitabu hiki kimeandaliwa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa pamoja baina ya Mtandao wa Asasi za Kiraia zinazojihusisha na masuala ya Huduma ya Maji na Usa� wa Mazingira nchini ijulikanayo kwa lugha ya Kiingereza Tanzania Water and Sanitation Network (TAWASANET), asasi inayojihusisha na masuala ya Maendeleo wilayani Karatu (Karatu Development Association - KDA), na Shirika la Misaada la Watu wa Denmark ( Danish People’s Aid - DPA); chini ya Mradi wa Kuzijengea Uwezo Asasi za Kiraia katika utawala bora na kuimarisha uwezo wa Serikali wa kutoa huduma, hususani katika sekta ya Maji na Usa� wa Mazingira.

Ikiwa ni sehemu ya kutoa elimu kwa wananchi, kitabu hiki kimeandaliwa kwa lugha nyepesi. Lengo ni kusaidia kukuza uelewa wa wanan-chi na viongozi katika ngazi mbalim-bali kuhusu masuala ya Maji na Usa� wa Mazingira. Msisitizo mkubwa umewekwa katika kuelewa kwa ujumla juu ya faida, hasara, na changamoto za ukosefu wa maji na huduma ya usa� wa mazingira katika maisha ya kila siku kwa wananchi.

Aidha sehemu nyingine ya kitabu hiki inatoa fursa kwa msomaji kujif-unza umuhimu wa ushiriki wa wananchi katika mchakato wa upangaji wa mipango ya maendeleo. Kwa kawaida mchakato huu wa upangaji humilikiwa na wananchi kuanzia hatua ya awali ya kuibua miradi hadi hatua ya usimamizi na ufuatiliaji.

Serikali za Mitaa zimepewa mamlaka ya kuongoza mchakato wa kuwawezesha wananchi kuamua aina ya miradi itakayosaidia kuondoa au kupunguza changamoto na vikwazo mbalimbali vya kijamii ili waji-letee maendeleo yao wenyewe.

Page 5: Ushiriki wa Wananchi, Nguzo ya Maendeleo Booklet -Swahili Version.pdfutekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo. Muundo wa uwajibikaji kwa kuanzia ngazi ya chini ya maamuzi ni

4

Dhamira kuu ya kuandaa kitabu hiki ni kusaidia kuhamasisha na kujenga ujasiri wa wananchi kubaini fursa ya kujipangia maendeleo yao na kuwa-saidia kujua kalenda ya mchakato mzima wa kuandaa mipango katika Ser-ikali za Mitaa. Hii itasaidia kuondoa au kupunguza malalamiko dhidi ya watendaji katika sekta ya umma na serikali kwa ujumla wake.

HIKI KITABU YAANI KINAELEZEA KABISA MAMBO YA USHIRIKI WA WANANCHI KATIKA MIPANGO YA KIMAENDELEO...

YAANI, DHAMIRA KUU YA KITABU HIKI NI KUSAIDIA KUHAMASISHA NA KUJENGA UJASIRI WA WANANCHI KUBAINI FURSA YA KUJIPANGIA MAENDELEO...

KWAKWELI SASA TUTA SHIRIKI KUPANGA MIPANGO YA MAJI NA USAFI KATIKA ENEO LETU

Serikali za Mitaa ni nini?Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali za Mitaa (SM) ni vyombo vya haki na vyenye mamlaka ya kushiriki na kushirikisha wananchi katika kupanga na kutekeleza shughuli za maende-leo na utoaji wa huduma katika maeneo yao ya utawala. Vyombo hivi vinawajibu wa kuimarisha Demokrasia na vinapaswa kuwajibika kwa wananchi katika kutoa huduma na kuchochea maendeleo.

Serikali za Mitaa ziko karibu zaidi na wananchi. Kwa mfumo wa Tanzania zinapaswa kuwa kielelezo na nguzo imara ya “Madaraka au nguvu ya Umma”. Kwa vile ni vyombo vinavyotokana na chaguzi za kidemokrasia, vinatarajiwa kuendeshwa na wananchi wenyewe kwa manufaa yao, chini ya kanuni za utawala bora.

Page 6: Ushiriki wa Wananchi, Nguzo ya Maendeleo Booklet -Swahili Version.pdfutekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo. Muundo wa uwajibikaji kwa kuanzia ngazi ya chini ya maamuzi ni

5

WANANCHI, NI WAJIBU WENU KUAMUA NI MRADI GANI AMBAO MNATAKA KUANZA NAO HAPA KIJIJINI..

TUANZE NA UJENZI WA VYOO VYA SHULE

HAPANA, TUANZE MRADI WA MAJI.

MH! KWELI. NI BORA TUANZE NA MAJI, KISHA VYOO VYA SHULE..TUANZE NA MADAWATI...

Ugatuaji wa MadarakaUgatuaji wa madaraka ni mchakato wa Serikali Kuu kuweka utaratibu wa kimfumo unaowezesha Serikali za Mitaa, Sekta Binafsi, Asasi Zisizo za Kiserikali, na Wananchi kuwa na uwezo wa kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo inayowahusu. Sehemu hii imejikita zaidi katika kuelezea ugatuaji wa madaraka kwenda Serikali za Mitaa, na wajibu wake kuwashirikisha wananchi katika kupanga mipango ya maendeleo yanayowahusu.

Mchakato wa ugatuaji Madaraka kutoka Serikali Kuu kwenda Serikali za Mitaa ambako ndiko Wananchi waliko umesaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa urasimu wa Serikali Kuu. Urasimu huu, huwa ni chanzo cha wananchi kushindwa kushiriki kikamilifu katika kubuni, kupanga na kutekeleza shughuli za maendeleo. Hivyo basi ugatuaji ukifanywa kwa ufanisi utaondoa urasimu wa aina zote na kuwawezesha wananchi kuamua nini wanataka kitokee katika maeneo yao.

Page 7: Ushiriki wa Wananchi, Nguzo ya Maendeleo Booklet -Swahili Version.pdfutekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo. Muundo wa uwajibikaji kwa kuanzia ngazi ya chini ya maamuzi ni

6

Katika mazingira au mfumo wa ugatuaji, Serikali Kuu imebaki na jukumu la kusimamia na kugawanya rasilimali kwa kuzingatia mfumo uwiano sawia na kwa kiasi kikubwa kubeba jukumu la kusimamia na kufanya ufua-tiliaji wa matumizi ya rasilimali. Kikubwa katika mfumo wa ugatuaji, ni Ser-ikali Kuu na Serikali za Mitaa kuendesha shughuli zao kama wawezeshaji. Dhana ya wajibu wa Serikali wezeshi inajumuisha Serikali kuiona jamii kama walengwa wa maendeleo na kuwatambua kuwa ni wananchi wenye haki ya kujiletea maendeleo yao.

Serikali inapaswa kutimiza wajibu wezeshi kwa kuweka mazingira ra�ki na wezeshi kwa wananchi kushiriki. Miongoni mwa mambo mengine mazin-gira ra�ki na wezeshi ni pamoja na kutunga sheria, kanuni na taratibu za kuongoza ushiriki wa wananchi, kuhakikisha ulinzi na usalama wa watu na mali zao, na kuwa kamisaa au msimamizi wa mchakato wa maendeleo. Kuwa kamisaa wa mchakato wa maendeleo ni kitendo cha Serikali iwe Kuu au za Mitaa, kusimamia kwa makini sheria, kanuni, na taratibu zina-zoongoza ushiriki wa wananchi na taratibu za maisha ya watu ya siku kwa siku.

Page 8: Ushiriki wa Wananchi, Nguzo ya Maendeleo Booklet -Swahili Version.pdfutekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo. Muundo wa uwajibikaji kwa kuanzia ngazi ya chini ya maamuzi ni

7

Ushiriki wa Wananchi Kama Nguzo ya MaendeleoUshiriki wa wananchi iwe kama mtu binafsi, Jumuiya za Kiraia, Asasi Zisizo za Kiserikali, au kama jamii; ni wajibu na haki ya Kikatiba. Wajibu na haki hii vimetolewa baada ya kutambua kuwa mchakato wa maende-leo unahitaji juhudi za wadau wengi. Serikali na/au Asasi Zisizo za Kiser-ikali pekee haziwezi kusababisha maendeleo ya mahali fulani yapati-kane. Zaidi sana uzoefu umeonesha kuwa matokeo ya shughuli za maendeleo (kwa mfano kuwepo kwa mabomba ya maji sa� kijiji fulani) yatakayodumu kwa muda mrefu, ni yale yaliyobuniwa na kutekelezwa kwa ushiriki wa wananchi. Hii inaonesha kuwa ushiriki wa Wananchi katika hatua mbalimbali za upangaji wa Mipango ni muhimu. Suala la ushiriki na ushirikishwaji wa wananchi ni moja ya kanuni muhimu zinazozingatiwa katika dhana ya utawala bora; ambayo ina-sisitiza wananchi kupewa fursa ya kushiriki na kuamua kwa kuzingatia miongozo mbalimbali ndani ya muundo wa uwajibikaji katika mchakato wa upangaji mipango ngazi ya Serikali za Mitaa.

Muundo wa Uwajibikaji katika Upangaji Ngazi ya Serikali za MitaaMamlaka ya Serikali za Mitaa inao Muundo wa Uwajibikaji kuanzia ngazi ya chini hadi ngazi ya juu ya kufanya maamuzi. Muundo huo huainisha majukumu na wajibu wa kila ngazi katika dhana ya maamuzi na utekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo.

Muundo wa uwajibikaji kwa kuanzia ngazi ya chini ya maamuzi ni kama ifuatavyo:1.

2.

Kijiji/Mtaa – Kijiji au Mtaa kwa upande wa mijini, ndio ngazi ya msingi yenye mamlaka ya kuandaa mipango ya maendeleo. Kwa tafsiri Kijiji au mtaa ni muunganiko wa Vitongoji kadhaa.

Kata – Ni muunganiko wa Vijiji au /Mitaa kadhaa. Tukiongelea ma- mlaka ya kupanga maendeleo, kimsingi ngazi ya Kata haina mam- laka ya kuandaa mipango ya maendeleo. Badala yake ngazi hii inawajibu wa kutoa ushauri, kuratibu, na kuunganisha mipango ya maendeleo iliyoandaliwa na Vijiji au Mitaa ndani ya Kata husika.

Page 9: Ushiriki wa Wananchi, Nguzo ya Maendeleo Booklet -Swahili Version.pdfutekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo. Muundo wa uwajibikaji kwa kuanzia ngazi ya chini ya maamuzi ni

8

3.

Kila ngazi katika muundo huo wa upangaji inayo mamlaka ya kimaamuzi ambayo huongozwa na kiongozi wa kuchaguliwa au kuteuliwa (Jedwali namba. 1)

Muundo ulioainishwa kwenye Jedwali namba 1, una maana sana katika mchakato wa uandaaji wa mipango ya maendeleo katika jamii hususani kwenye ngazi za vijiji/Mitaa na Kata ambako mipango yote ya maendeleo huanzia mchakato wake katika upangaji na hatimaye utekelezaji wake kufanyika katika vijiji au mitaa husika.

Ili kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi Serikali inaendeshwa katika ngazi kuu mbili ambazo ni Serikali Kuu na Serikali za Mitaa. Rais wa Jam-huri ya Muungano wa Tanzania ndiye Kiongozi Mkuu wa Ngazi zote mbili.

Jedwali Namba 1: Uchambuzi wa Muundo wa ngazi za Kimaamuzi Na Ngazi ya

Uwajibikaji Mamlaka ya Maamuzi

Kiongozi/Mtendaji Mkuu

Kiongozi/Mtendaji anavyopatikana

1

Kitongoji Kamati ya Kitongoji

Mwenyekiti wa Kitongoji

Kuchaguliwa

2 Kijiji/Mtaa Serikali ya Kijiji/Mtaa

• Mwenyekiti wa Kijiji/Mtaa

Kuchaguliwa

• Afisa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa

Kuteuliwa

3

Kata

Kamati ya Maendeleo ya

Kata

• Diwani

Kuchaguliwa

• Afisa Mtendaji Kata Kuteuliwa 3

Halmasha-uri

Halmashauri

• Mwenyekiti/Meya wa Halmashauri

Kuchaguliwa

• Mkurugenzi wa Halmashauri

Kuteuliwa

Halmashauri za Wilaya, Manispaa, na Majiji – hii ni ngazi ya pili yenye mamlaka ya kuandaa mipango ya maendeleo katika ngazi ya Serikali za Mitaa. Ngazi hii huundwa na muunganiko wa Kata mbali mbali katika eneo fulani.

Page 10: Ushiriki wa Wananchi, Nguzo ya Maendeleo Booklet -Swahili Version.pdfutekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo. Muundo wa uwajibikaji kwa kuanzia ngazi ya chini ya maamuzi ni

9

Kwa nini ni muhimu kwa Wananchi kushiriki?Zipo sababu nyingi na za msingi za wananchi kushiriki katika mchakato wa kupanga mipango ya maendeleo kwa njia shirikishi. Baadhi ya sababu hizo ni;o Kutambua nafasi ya wananchi kama ndio watumiaji wakuu wa huduma mbalimbali za kiuchumi na kijamii zinazo tolewa na serikali yaoo Kutambua kuwa wananchi ndio wenye ufahamu wa aina ya huduma wanazozihitaji na ambazo wanauwezo wa kuzisimamiao Kusaidia kubaini na kufanya utambuzi wa matatizoo Kutekeleza dhana ya utawala bora kupitia kanuni ya demokrasiao Kuisaidia Serikali katika utoaji huduma kwa kuzingatia mgawanyo wenye uwiano sawia na kubainisha mahitaji ya kiuchumi na kijamii ya wananchi.o Kujenga hamasa ya umiliki wa miradi inayopelekwa kwa wananchi kwa ajili ya utekelezaji.

Mchakato wa Upangaji Mipango katika Serikali za Mitaa TanzaniaIli kuunganisha matakwa ya Wananchi katika upangaji wa mipango endelevu, Serikali za Mitaa zinao utaratibu unaotambulika na kutu-mika katika kuendesha zoezi la upangaji mipango. Mchakato huo hujulikana zaidi kama "Mchakato wa fursa na vikwazo vya maendeleo"

O�si ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), imeandaa vitini viwili vinavyoainisha hatua za mchakato hatua za mchakato wa fursa na vikwazo vya maendeleo. Kitini cha kwanza hujulikana kama “fursa na vikwazo-mchakato wa vijijini” na cha pili ni “fursa na vikwazo-mchakato wa mjini”. Vitini hivi vimeonesha kwa undani nini kinapaswa kufanywa tangu siku ya kwanza hadi siku ya mwisho katika zoezi la kupanga mipango ya maendeleo kwa kuzingatia ushiriki wa wananchi.

Page 11: Ushiriki wa Wananchi, Nguzo ya Maendeleo Booklet -Swahili Version.pdfutekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo. Muundo wa uwajibikaji kwa kuanzia ngazi ya chini ya maamuzi ni

10

Kwa wale wenye ujuzi wa kutumia mtandao wa intaneti wanaweza kuvi-pata kwa urahisi vitini hivi na kuweza kupata ufahamu zaidi juu ya hatua zinazofuatwa katika mchakato huu kwa maeneo yote mawili, yaani vijijini na mijini.

Jambo la muhimu katika mchakato wa fursa na vikwazo vya maendeleo, ni kwa Halmashauri; Serikali za Vijiji; na Wananchi kutochukulia zoezi hili kama fursa ya kukusanya takwimu na kuibua vipaumbele na miradi itakayoingizwa kwenye mipango mikakati ya Halmashauri tu. Maana kufanya hivyo ni kuendekeza ukiritimba wa Serikali, tofauti tu ni kuwa kabla ya ugatuaji ukiritimba ulikuwa ngazi ya Serikali kuu na sasa utakuwa umehamia Serikali za Mitaa.

Ili kuufanya mchakato wa fursa na vikwanzo uwe wa msaada na wa ufa-nisi katika kusababisha maendeleo endelevu; ni vyema wadau wote wa maendeleo katika eneo husika watumie mchakato huu kama jukwaa ambamo kila mdau anaenda akiwa amefumbua macho kuona fursa zita-kazomsaidia kuibua mradi au miradi atakayoitekeleza yeye binafsi. Kwa maneno mengine, Serikali za Vijiji kama wadau wa maendeleo ziingie kwenye mchakato wa fursa na vikwazo zikiwa zimefumbua macho kubaini fursa ambazo zinaweza kuandaa mipango ya miradi itakay-otekelezwa na Serikali zao, kwa kutumia nguvu za wananchi,michango ya hiari, na tozo zinazotozwa na Serikali zao. Vivyo hivyo, Jumuiya za Kiraia na Asasi Zisizo za Kiserikali zialikwe kushiriki mchakato; nazo ziingie kwenye mchakato zikiwa na nia iyo hiyo ya kubaini fursa ambazo Serikali ngazi za Vijiji na Halmashauri zitaonesha hazina uwezo wa kuzifanyia kazi.

Mwisho, lakini sio kwa umuhimu; ni ushiriki wa sekta binafsi, ambapo ni vyema nayo pia ikishiriki kikamilifu. Nayo inapaswa kushiriki ikiwa imefumbua macho kubaini fursa ambazo zinaweza kuwa maeneo mazuri ya kuwekeza na kujipatia faida, kutengeneza ajira mpya, na hivyo kukuza uchumi wa eneo husika.

Page 12: Ushiriki wa Wananchi, Nguzo ya Maendeleo Booklet -Swahili Version.pdfutekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo. Muundo wa uwajibikaji kwa kuanzia ngazi ya chini ya maamuzi ni

11

Kwa muktadha huu, Serikali Kuu na Serikali za Mitaa zinapaswa kuandaa utaratibu madhubuti wa kuufanya mchakato wa fursa na vikazo kuwa jukwaa la kuwawezesha wadau wote kushiriki kikamilifu katika kutimiza wajibu wao wa Kikatiba wa kujenga nchi yao.

Kwa ufupi kalenda ya mchakato wa upangaji mipango katika Serikali za Mitaa nchini Tanzania unasura iliyooneshwa kwenye Jedwali namba 2 hapo chini:

Jendwali Namba 2: Kalenda ya Mchakato wa Upangaji wa Mipango Ngazi ya Serikali za Mitaa Hatua Kipengele cha Mchakato Kipindi/Muda Mhusika/Wahusika

Kwanza

Maandalizi ya Mwongozo wa Mipango na Bajeti

Agosti hadi Oktoba

Wizara ya Fedha na Mipango

Pili

Mwongozo wa Mchakato hutolewa na kupokelewa na Halmashauri za Wilaya/Miji/Manispaa/Majiji

Novemba

• TAMISEMI • Halmashauri

Tatu

Kupeleka taarifa ya mwelekeo na kuanza kwa mchakato wa upangaji mipango

Novembe hadi Desemba

Halmashauri ya Wilaya/Mji/Manispaa/Jiji

Nne

Kuandaa mpango na kupitisha katika ngazi ya Kijiji kwa kuzingatia mwongozo na kuendesha mchakato wa fursa na vikwazo (Kubainisha vipaumbele)

Desemba hadi Januari

• Wananchi • Serikali ya Kijiji

Tano Kuunganishwa kwa Mipango ya Vijiji Januari • Kamati ya Maendeleo ya Kata (KaMaKa)

Sita

Kupitia Mipango ya Vijiji/Kata na kutoa mapendekezo ya Kitaalamu

Januari hadi Februari

• Timu ya Wataalamu ya Halmashauri

Kupitia Mpango wa Halmashauri na kutoa mapendekezo

Januari / Februari • Kamati ya Ushauri ya Wilaya Januari / Februari • Kamati ya Ushauri ya Mkoa

Saba

Mpango wa Halmashauri kujadiliwa na kupitishwa rasmi na Wawakilishi wa Wananchi katika Halmashauri husika

Februari

• Baraza la Madiwani

Nane

Mpango wa Halmashauri kuwasilishwa katika ngazi ya Wizara

Machi

• TAMISEMI

• Wizara ya Fedha na Mipango

Tisa Kupitia na Kupitisha Mipango na Bajeti za Kisekta

Machi • Kamati za Bunge za Kisekta

Kumi

Bajeti kujadiliwa na kuptishwa na Wawakilishi wa Wananchi Bugeni

Aprili hadi Juni

• Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kumi na Moja

Mchakato wa Kupatikana kwa Fedha kwa ajili ya Utekelezaji wa Mipango

Juni na Julai

• Halmashauri • Wizara ya Fedha na Mipango

Page 13: Ushiriki wa Wananchi, Nguzo ya Maendeleo Booklet -Swahili Version.pdfutekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo. Muundo wa uwajibikaji kwa kuanzia ngazi ya chini ya maamuzi ni

12

Huduma ya Maji na Usa� wa Mazingira Ule msemo maarufu usemao kuwa maji ni uhai hauwezi kuwa dhahiri kama hakuna huduma za maji au kama huduma hizo ni duni. Ili maji yawe uhai ni lazima yawepo, na ili maji yawepo ni lazima huduma za maji zitolewe na wadau mbali mbali. Ni muhimu kujua kuwa huduma za maji zina uhusiano mkubwa na huduma za usa� wa mazingira. Mahali penye shida ya maji ni lazima usa� wa mazingira utaathirika kwa kiasi kikubwa.

Takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa kiwango cha upatikanaji wa maji salama kimekuwa kikishuka kwa sababu kushidwa kufanyia maten-genezo mifumo ya maji iliyoko, na ukosefu wa fedha za kujenga mifumo mipya. Pia takwimu zinaonesha kuwa katika kila kaya mia moja zilizoko vijijini sehemu ya Tanzania bara zaidi ya kaya 55 hutembea umbali wa zaidi ya dakika 30 kila siku kufuata maji. Kama hali ya upatikanaji wa maji iko hivi, ni dhahiri kuwa hali ya usa� wa mazingira nayo itakuwa sio nzuri.

Page 14: Ushiriki wa Wananchi, Nguzo ya Maendeleo Booklet -Swahili Version.pdfutekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo. Muundo wa uwajibikaji kwa kuanzia ngazi ya chini ya maamuzi ni

13

Umuhimu wa Maji na Usa� wa Mazingira Miradi ya Maji na Usa� wa Mazingira ina umuhimu mkubwa kwa maen-deleo ya nchi na watu wake. Inahitaji kupewa kipaumbele cha kwanza kwa kuwa inagusa maisha ya kila siku ya watu. Umuhimu wake hujielekeza katika kutekeleza huduma kadhaa wa kadha za kibina-damu na kimaendeleo, zikiwemo zifuatazo:

Matumizi ya Majio Kunywao Kupikiao Ujenzi wa nyumba na miundo mbinu mbali mbalio Kufanya usa�o kunywesha mifugoo umwagiliaji mazao ya kilimoo kusa�sha vyombo, nguo nko kuhudumia viwanda vidogo na vikubwao Huduma za afyao Usa�ri, usa�rishaji nk

Page 15: Ushiriki wa Wananchi, Nguzo ya Maendeleo Booklet -Swahili Version.pdfutekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo. Muundo wa uwajibikaji kwa kuanzia ngazi ya chini ya maamuzi ni

14

Usa� wa MazingiraHuduma za usa� wa mazingira zinajumuisha upatikanaji wa vyoo sehemu mbali mbali, kama vile: sehemu za makazi; maeneo ya umma kama stendi; na sehemu za taasisi kama vile mashuleni na sehemu za ibada. Huduma nyingine zinazohusu usa� wa mazingira ni uzoaji na uhifadhi wa taka ngumu na taka maji.

Kwa kuangalia huduma hizi ni dhahiri kuwa huduma hizi zikikosekana au zikiwa duni ni rahisi afya ya jamii kutetereka; na pale ambapo afya ya jamii itatetereka ushiriki wa jamii hiyo katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo utakuwa wa kiwango cha chini sana. Hivyo basi, huduma za usa� wa mazingira ni muhimu sana kwa kuwa husaidia katika mambo yafuatayo:o Uhifadhi na Uharibifu wa taka ngumu na taka lainio Uzoaji wa maji taka na kinyesio Utunzaji na uhifadhi wa chakula

Madhara ya Kukosekana kwa Huduma za Maji na Usa� wa MazingiraKukosekana kwa mojawapo au zote kati ya huduma za Maji na Usa� wa Mazingira huleta madhara makubwa kwa mtu mmojammoja, familia na Taifa kwa ujumla. Baadhi ya madhara hayo ni pamoja na;o

o Kupoteza hadhi ya utu kutokana na ukosefu wa chooo Kutokuwa na uhakika wa maji sa� na salama kwa ajili ya kunywa o

Kuibuka kwa mlipuko wa magonjwa mbalimbali kama vile; kipindipindu, kuhara na kuhara damu, kichocho, homa ya matumbo, magonjwa yanayoambatana na athari ya hedhi kwa wasichana na wanawake.Watoto wa kike (Wasichana) kushindwa kuhudhuria darasani ipasavyo na kusababisha kushindwa kumudu na kutimiza malengo yao ya kielimu

Kupoteza fedha nyingi kugharamia matibabu inayosababishwa na magonjwa yanayoepukika

Page 16: Ushiriki wa Wananchi, Nguzo ya Maendeleo Booklet -Swahili Version.pdfutekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo. Muundo wa uwajibikaji kwa kuanzia ngazi ya chini ya maamuzi ni

15

o Kuongezeka kwa vitendo viovu kama vile ubakaji kwa wan awake wanaosa�ri umbali mrefu kutafuta majio Kuongezeka kwa idadi ya ndoa zinazovunjika - talakao Ukosefu wa huduma bora ya afya katika zahanati, vituo vya afya na hospitali kwa sababu ya ukosefu wa maji

Upangaji wa Miradi ya Maji na Usa� wa Mazingira TanzaniaPamoja kutambua kuwa huduma za maji na usa� wa mazingira ni muhimu na hazipo za kutosha nchini Tanzania, hali halisi inaonesha kuwa ubunifu, upangaji na utekelezaji wa miradi ya Maji na Usa� wa Mazingira umekosa nguvu na shinikizo la kutosha kutoka ngazi zote zenye mamlaka ya kupanga. Hali hiyo husababisha miradi ya Maji na Usa� wa Mazingira kutopewa kipaumbele na wananchi na viongozi wakati wa kuandaa mipango ya maendeleo.

Kimsingi ni sahihi kusema kuwa, kwa wadau wa maendeleo kuacha kuipa miradi ya maji na usa� wa mazingira kipaumbele; ni sawa na kukata tawi walilolikalia wenyewe. Wadau wanahitaji kuwaza vingi-nevyo, Serikali za Vijiji/Mitaa na wananchi katika Mitaa yao na Vijijini ambako mipango ya maendeleo huanzia wanapaswa kukumbuka kuipa miradi hii kipaumbele cha juu. Wawakilishi wa wananchi waki-wemo Waheshimiwa Madiwani na Wabunge, Jumuiya za Kiraia, na Asasi Zisizo za Kiserikali zinapaswa kuhamasisha na pengine kushinikiza Ser-ikali na Wananchi kuipa miradi hii kipaumbele cha juu. Aidha Sekta Bin-afsi inaweza kujipatia fursa ya uwekezaji na kuongeza ajira hasa katika miradi ya usa� wa mazingira, kama vile kuwekeza katika miradi ya vyoo vya kuhamisha hamisha.

HitimishoKitabu hiki kinaongelea mambo makuu mawili, ushiriki wa wananchi katika mchakato wa kupanga mipango ya maendeleo na umuhimu wa huduma za maji na usa� wa mazingira. Katika suala la ushiriki wa wananchi, imeoneshwa kuwa ushiriki wa wananchi unaweza kuwa katika sura mbali mbali: kama mwananch binafsi (sekta binafsi), kama Jumuiya za Kiraia, na kama Asasi Zisizo za Kiserekali. Vile vile imeoneshwa kuwa kushiriki ni haki na wajibu wa Kikatiba,

Page 17: Ushiriki wa Wananchi, Nguzo ya Maendeleo Booklet -Swahili Version.pdfutekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo. Muundo wa uwajibikaji kwa kuanzia ngazi ya chini ya maamuzi ni

16

ambapo wadau hasa Serikali imeaswa kuacha kuwaona wananchi kama walengwa wa maendeleo; badala yake iwaone kama wananchi wenye haki ya kujiletea maendeleo yao wenyewe. Hapa Serikali inawajibu wa kuweka mazingira wezeshi kwa kutunga sheria, taratibu, na kanuni zitakazo ongoza uendeshaji wa michakato mbali mbali ya maendeleo; na kudhibiti tabia na mienendo ya watu na taasisi zenye mrengo wa kukizanzana na michakato cha maendeleo.

Muhimu sana ni kuacha kuona mchakato wa fursa na vikwazo kuwa ni zoezi la kukusanya takwimu zitakazotumika kuandaa mpango mkakati wa Halmashauri, badala yake mchakato uwe ni jukwaa la wadau wote wa maendeleo ikiwemo sekta binafsi kuona fursa za uwekezaji na utoaji huduma. Wadau wote waende jukwaani wakiwa wamefumbua macho kuona fursa, wasiiachie Serikali peke yake.

Kwa suala la huduma za maji na usa� wa mazingira, inaweza kuhitimishwa kuwa; hali inayoendelea sasa ya kutokutoa kipaumbele cha juu kwa huduma za maji na usa� wa mazingira wakati wa kupanga mipango ya maendeleo; ni ishara mbaya. Ikiachwa kuendelea hivyo, afya za wananchi zitadorora hali ambayo itaathiri maendeleo ya mahali husika na Taifa kwa ujumla, kwasababu ushiriki wa wananchi wenye afya mgogoro katika miradi ya maendeleo utakuwa hauna tija.

Vitabu vya RejeaJamhuri ya Muungano wa Tanzania (2005): Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2013): Taarifa ya Wizara ya Maji Juu ya Ramani ya Vituo vya Maji Tanzania Bara ya Mwaka 2013 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania O�si ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (2007): Uandaaji wa Mipango Shirikishi Jamii kwa Mfumo wa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo: Kiongozi cha Mchakato wa Mjini Jamhuri ya Muungano wa Tanzania O�si ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (2007): Uandaaji wa Mipango Shirikishi Jamii kwa Mfumo wa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo: Kiongozi cha Mchakato wa Vijijini The United Republic of Tanzania (2016): Guidelines for the Preparation of Annual Plan and Budget for 2016/17 in the Implementation of the Five Year Development Plan II 2016/17-2020/21, Issued by: Ministry of Finance and Planning.

Page 18: Ushiriki wa Wananchi, Nguzo ya Maendeleo Booklet -Swahili Version.pdfutekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo. Muundo wa uwajibikaji kwa kuanzia ngazi ya chini ya maamuzi ni

Kitabu hiki kimeandaliwa kwa lengo la kusaidia kuongeza uelewa wa makundi mbalimbali ya kijamii hususan viongozi na wananchi wa kawaida juu ya nafasi yao na umuhimu wa kushiriki mchakato wa kupanga mipango ya maendeleo ambapo hutoa fursa kwa kila mwananchi kupitia mfumo maalum ulio wazi.

Kitabu pia kimegusia kwa ufupi na kwa ujumla kuhusu ufahamu na um-uhimu wa masuala ya Huduma ya Maji na Usa� wa Mazingira, athari zake na pia kuihamasisha jamii kuchukua hatua kwa kuyapa masuala hayo kip-aumbele katika mchakato wa upangaji ili kupunguza au kuondoa kabisa athari zinazosababishwa na ukosefu wake.

Ni imani ya waandaaji kuwa maudhui yaliyomo katika kitabu yataongeza uelewa na kusaidia kuimarisha jamii ya Watanzania kuzingatia uboreshaji wa huduma zilizopo na kutambua nafasi yao katika ujenzi wa Taifa lao kwa

Kimetayarishwa na; Mtandao wa Asasi za Maji na Usafi wa Mazingira Tanzania (TAWASANET) kwa ufadhili wa Danish Peoples Aid (DPA)

Brovejen 4 DK-4800 Nykøbing Falster Denmark Simu: + 45 70 220 230

Barua Pepe: [email protected]

Mtaa wa Mbutu, Eneo la Sinza (Kwa Remmy), Geti namba 13 S.L.P 33410, Dar es Salaam Simu +255 22 2 462 065,

Barua Pepe: [email protected] / [email protected] Tovuti: www.tawasanet.or.tz