Upload
others
View
212
Download
36
Embed Size (px)
Citation preview
Mwongozo wa kusali
Rozari ya Bikira Maria
Melkisedeck Leon Shine Katoliki.ackyshine.com
ROZARI YA MAMA MARIA MELKISEDECK LEON SHINE
ROZARI YA MAMA MARIA
JINSI YA KUSALI ROZARI YA MAMA BIKIRA MARIA
Anza kusali Rozari kwa kuibusu miguu ya Bwana Yesu katika taswira
(picha) yake Msalabani kisha fanya Ishara ya Msalaba ukiwa
unasema “Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu,
Amina”.
Taja kwa ufupi nia za Rozari hii. Tangaza nia hizo kwa sauti kama
mnasali wengi kwa pamoja, Mfano, “Tusali kuombea amani katika
ROZARI YA MAMA MARIA MELKISEDECK LEON SHINE
ROZARI YA MAMA MARIA
nchi yetu na ulimwenguni kote, na tuunganishe nia hizo na nia zetu
sisi wenyewe, nk) .
Baada ya Sala ya Nasadiki pamoja na ya Baba Yetu, tunamwomba
Mungu (Utatu Mtakatifu) fadhila za Imani, Matumaini na Mapendo,
zikiambatana na Salamu Maria tatu.
Mojawapo ya maneno yafuatayo huweza kutumika:
“Mungu Baba utuongezee Imani. Salamu Maria, …… Mungu Mwana
utuongezee matumaini, Salamu Maria, …… Mungu Roho Mtakatifu
washa nyoyo zetu kwa mapendo yako, Salamu Maria, …..” Au;
“Utuongezee Imani ee Bwana, Salamu Maria,…. Utuongezee
matumaini ee Bwana, Salamu Maria,…. Uwashe nyoyo zetu kwa
mapendo yako ee Bwana, Salamu Maria, …..” Au;
“Salamu e uliyechaguliwa na Mungu Baba, Salamu Maria,….. Salamu
e Mama wa Mungu Mwana, Salamu Maria,….. Salamu e Mchumba wa
Mungu Roho Mtakatifu, Salamu Maria,……”
Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu, kama mwanzo na
sasa na siku zote, na milele, Amina.
Ee Yesu wangu, utusamehe dhambi zetu, utuepushe na moto wa
milele, ongoza roho zote mbinguni, hasa za wale wanaohitaji huruma
ROZARI YA MAMA MARIA MELKISEDECK LEON SHINE
ROZARI YA MAMA MARIA
yako zaidi.
Tuwasifu milele, Yesu, Maria na Yosef.
Kisha endelea na sala zinazofuata kama mpangilio unavyoonyesha
hapo juu.
Kila baada ya Tendo moja na makumi ya Salamu Maria…,
“Atukuzwe..”, “Ee Yesu wangu…” na “Tuwasifu milele…” kama muda
unatosha wimbo ufaao wa Bikira Maria uimbwe (kama muda ni mfupi
basi angalau ubeti mmoja mmoja uimbwe kila baada ya makumi
hayo). Baada ya Wimbo, Tendo linalofuata litangazwe kwa sauti
pamoja na tafakari fupi au ombi linaloambatana na Tendo husika
kama inavyoonyeshwa hapa chini.
MATENDO YA ROZARI TAKATIFU
MATENDO YA FURAHA (Jumatatu na Jumamosi)
Tendo la kwanza; Malaika Gabrieli anampasha habari Maria kuwa
atakuwa Mama wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie unyenyekevu.
Tendo la pili; Maria Mtakatifu anakwenda kumtembelea Elizabeti.
Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani.
ROZARI YA MAMA MARIA MELKISEDECK LEON SHINE
ROZARI YA MAMA MARIA
Tendo la tatu; Yesu anazaliwa Betlehemu. Tumwombe Mungu atujalie
moyo wa ufukara
Tendo la nne; Yesu anatolewa hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie
usafi wa moyo.
Tendo la tano; Maria anamkuta Yesu hekaluni. Tumwombe Mungu
atujalie kuwatii wakubwa wetu.
MATENDO YA UCHUNGU (Jumanne na Ijumaa)
Tendo la kwanza; Yesu anatoka jasho la damu kwa ajili yetu.
Tumwombe Mungu atujalie sikitiko la dhambi.
Tendo la pili; Yesu anapigwa kwa mijeledi kwa ajili yetu. Tumwombe
Mungu atujalie kuacha dhambi za uchafu.
Tendo la tatu; Yesu anatiwa miiba kichwani kwa ajili yetu.
Tumwombe Mungu atujalie kushinda kiburi.
Tendo la nne; Yesu anachukua Msalaba kwa ajili yetu. Tumwombe
Mungu atujalie kuvumilia taabu.
ROZARI YA MAMA MARIA MELKISEDECK LEON SHINE
ROZARI YA MAMA MARIA
Tendo la tano; Yesu anakufa Msalabani. Tumwombe Mungu atujalie
kuwapenda Yesu na Maria.
MATENDO YA UTUKUFU (Jumatano na Jumapili)
Tendo la kwanza; Yesu anafufuka. Tumwombe Mungu atujalie
kugeuka watakatifu.
Tendo la pili; Yesu anapaa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie
kwenda mbinguni.
Tendo la tatu; Roho Mtakatifu anawashukia Mitume. Tumwombe
Mungu atujalie bidii katika dini yetu.
Tendo la nne; Bikira Maria anapalizwa mbinguni. Tumwombe Mungu
atujalie kufa vizuri.
Tendo la tano; Bikira Maria anawekwa Malkia mbinguni. Tumwombe
Mungu atujalie kudumu katika njia njema.
MATENDO YA MWANGA (Alhamisi)
Tendo la kwanza; Yesu anabatizwa Mto Jordani. Tumwombe Mungu
atujalie uaminifu kwa ahadi zetu za ubatizo.
ROZARI YA MAMA MARIA MELKISEDECK LEON SHINE
ROZARI YA MAMA MARIA
Tendo la pili; Yesu anageuza maji kuwa divai huko Kana. Tumwombe
Mungu atujalie kuukoleza ulimwengu kwa chachu ya enjili.
Tendo la tatu; Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu. Tumwombe
Mungu atujalie kupokea Ufalme wake kwa toba ya kweli.
Tendo la nne; Yesu anageuka sura. Tumwombe Mungu atujalie
neema ya kuung’arisha ulimwengu kwa uso wa Yesu.
Tendo la tano; Yesu anaweka Sakramenti ya Ekaristia. Tumwombe
Mungu atujalie neema ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine.
LITANIA YA BIKIRA MARIA
Bwana utuhurumie
Bwana utuhurumie
Kristo utuhurumie
Bwana utuhurumie
Bwana utuhurumie
Kristo utusikie
Kristo utusikilize
Mungu Baba wa Mbinguni,…… Utuhurumie
ROZARI YA MAMA MARIA MELKISEDECK LEON SHINE
ROZARI YA MAMA MARIA
Mungu Mwana Mkombozi wa dunia ……… Utuhurumie
Mungu Roho Mtakatifu …….. Utuhurumie
Utatu Mtakatifu Mungu Mmoja …….. Utuhurumie
Maria Mtakatifu ………. utuombee
Mzazi Mtakatifu wa Mungu …….. utuombee
Bikira Mtakatifu Mkuu wa Mabikira …….. utuombee
Mama wa Kristo ……… utuombee
Mama wa Neema ya Mungu ………….. utuombee
Mama Mtakatifu sana ……… utuombee
Mama mwenye usafi wa Moyo ……….. utuombee
Mama mwenye ubikira ……….. utuombee
Mama usiye na doa ……….. utuombee
Mama mpendelevu ………. utuombee
Mama mstajabivu ………. utuombee
Mama wa Muumba ………. utuombee
Mama wa Mkombozi ………….. utuombee
Mama wa Kanisa……….. utuombee
Bikira mwenye utaratibu ………….. utuombee
Bikira mwenye heshima ………….. utuombee
ROZARI YA MAMA MARIA MELKISEDECK LEON SHINE
ROZARI YA MAMA MARIA
Bikira mwenye sifa ………….. utuombee
Bikira mwenye uwezo ………….. utuombee
Bikra mweye huruma ………….. utuombee
Bikra mwaminifu………….. utuombee
Kioo cha haki ………….. utuombee
Kikao cha hekima ………….. utuombee
Sababu ya furaha yetu ………….. utuombee
Chombo cha neema ………….. utuombee
Chombo cha kuheshimiwa ………….. utuombee
Chombo bora cha ibada ………….. utuombee
Waridi lenye fumbo ………….. utuombee
Mnara wa Daudi ………….. utuombee
Mnara wa pembe ………….. utuombee
Nyumba ya dhahabu ………….. utuombee
Sanduku la Agano ………….. utuombee
Mlango wa Mbingu ………….. utuombee
Nyota ya asubuhi ………….. utuombee
Afya ya wagonjwa ………….. utuombee
Kimbilio la wakosefu ………….. utuombee
ROZARI YA MAMA MARIA MELKISEDECK LEON SHINE
ROZARI YA MAMA MARIA
Mtuliza wenye huzuni ………….. utuombee
Msaada wa waKristo ………….. utuombee
Malkia wa Malaika ………….. utuombee
Malkia wa Mababu ………….. utuombee
Malkia wa Manabii ………….. utuombee
Malkia wa Mitume ………….. utuombee
Malkia wa Mashahidi ………….. utuombee
Malkia wa Waungama dini ………….. utuombee
Malkia wa Mabikira ………….. utuombee
Malkia wa Watakatifu wote ………….. utuombee
Malkia uliyepalizwa Mbinguni ………….. utuombee
Malkia wa Rozari takatifu ………….. utuombee
Malkia wa amani ………….. utuombee
Mwanakodoo wa Mungu uondoaye dhambi za
dunia,…………..Utusamehe ee Bwana.
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za
dunia,…………..Utusikilize ee Bwana
ROZARI YA MAMA MARIA MELKISEDECK LEON SHINE
ROZARI YA MAMA MARIA
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za
dunia,…………..Utuhurumie.
Utuombee, Mzazi Mtakatifu wa Mungu,…………..Tujaliwe ahadi
za Kristo.
Tuombe
Ee Bwana Mungu, utujalie sisi watumishi wako afya ya roho na mwili
siku zote; na kwa maombezi matukufu ya Maria Mtakaatifu Bikira
daima, tuopolewe na mashaka ya saa, tupate na furaha za milele.
Kwa Kristo Bwana wetu, Amina.
ROZARI YA MAMA MARIA MELKISEDECK LEON SHINE
ROZARI YA MAMA MARIA
MWANDISHI: Melkisedeck Leon Shine
Copyright © All Rights Reserved, Ackyshine
Tembelea katoliki.ackyshine.com Kupata majarida mengine