28
COUNSENUTH Information series No. 1 Toleo la Pili, January, 2004 Vidokezo Muhimu kwa Washauri Nasaha ULISHAJI WA MTOTO ALIYEZALIWA NA MAMA MWENYE VIRUSI VYA UKIMWI:

ULISHAJI WA MTOTO A L I Y E Z A L I W A NA MAMA ...counsenuth.or.tz/sites/default/files/Ulishaji wa Mtoto...kunyonya maziwa ya mama. Hii hupunguza hatari ya magonjwa ya kuhara kwani

  • Upload
    others

  • View
    24

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: ULISHAJI WA MTOTO A L I Y E Z A L I W A NA MAMA ...counsenuth.or.tz/sites/default/files/Ulishaji wa Mtoto...kunyonya maziwa ya mama. Hii hupunguza hatari ya magonjwa ya kuhara kwani

COUNSENUTH

Information series No. 1

Toleo la Pili, January, 2004

Vidokezo Muhimukwa Washauri

Nasaha

ULISHAJI WA MTOTO

A L I Y E Z A L I WA NAMAMA MWENYE

VIRUSI VYAU K I M W I :

mtoto mwenye virusi.qxd 1/7/05 3:10 PM Page 1

Page 2: ULISHAJI WA MTOTO A L I Y E Z A L I W A NA MAMA ...counsenuth.or.tz/sites/default/files/Ulishaji wa Mtoto...kunyonya maziwa ya mama. Hii hupunguza hatari ya magonjwa ya kuhara kwani

2

mtoto mwenye virusi.qxd 1/7/05 3:10 PM Page 2

Page 3: ULISHAJI WA MTOTO A L I Y E Z A L I W A NA MAMA ...counsenuth.or.tz/sites/default/files/Ulishaji wa Mtoto...kunyonya maziwa ya mama. Hii hupunguza hatari ya magonjwa ya kuhara kwani

3

UTANGULIZI

Kijitabu hiki kinatoa maelekezo ya kumlishamtoto aliyezaliwa na mama mwenye virusivya UKIMWI. Hili ni toleo la pili ambalolimefafanua na kuboresha taarifa zilizopokwenye kijitabu “Ulishaji wa Mtoto Mchangakwa Mama mwenye virusi vya UKIMWI:Vidokezo Muhimu kwa Washauri Nasaha,COUNSENUTH Information series No.1”.

Ni dhahiri kuwa mama anayeishi na virusi vyaUKIMWI anaweza kumwambukiza mtotowake kupitia maziwa yake. Lakini ni muhimupia kuelewa faida za kunyonyesha maziwa yamama. Taarifa ambazo zimewekwa kwenyesura hii kuhusu ulishaji wa mtoto wakatimama ana virusi vya UKIMWI ni zakumwezesha mtoa huduma kupata mwangaau kuelewa kwa kiasi hali hiyo ya ulishaji wamtoto kama mama ana virusi vya UKIMWI.

Kijitabu hiki hakitoshi kumfanya mtoahuduma au mshauri nasaha kuwa na stadi nautaalamu wa kutosha utakaomwezesha kutoahuduma kamilifu kwa mama mwenye virusivya UKIMWI kuhusu ulishaji wa mtoto. Mtoahuduma au mshauri nasaha anahitaji mafunzozaidi kama itakavyokuwa imeelekezwa nasekta ya Afya. Aidha mtoa huduma ambayehajapata mafunzo ya kutosha atahitajikuwafahamu watoa huduma ambaowamepata mafunzo hayo, ili wawezekushirikiana kwa kutoa rufaa kwa mama iliapate huduma kamilifu.

Kwa wanawake ambao hawana virusi vyaUKIMWI, wale ambao hawajui hali yao yauambukizo na wale waliopima lakinihawakuchukua majibu, wanakuwa katikakundi moja la kushauriwa kumlisha mtotokama kawaida na kufuata taratibu za kawaidaza kunyonyesha.

mtoto mwenye virusi.qxd 1/7/05 3:10 PM Page 3

Page 4: ULISHAJI WA MTOTO A L I Y E Z A L I W A NA MAMA ...counsenuth.or.tz/sites/default/files/Ulishaji wa Mtoto...kunyonya maziwa ya mama. Hii hupunguza hatari ya magonjwa ya kuhara kwani

4

UAMBUKIZO WA VIRUSI VYAUKIMWI KUTOKA KWAMAMA KWENDA KWA

MTOTO

Kwa kawaida sio wanawake wote wenyevirusi vya UKIMWI huambukiza watoto wao.Inakadiriwa kuwa kiasi cha asilimia 60 – 70 yawatoto wanaozaliwa na wanawake wenyevirusi vya UKIMWI hawaambukizwi kabisavirusi vya UKIMWI na asilimia 30 – 40 yawatoto huambukizwa virusi vya UKIMWI.

Mambo yanayochangia kuongeza

hatari ya maambukizi ya virusi

vya UKIMWI kutoka kwa mama

kwenda kwa mtoto

• Mama kuambukizwa virusi vya UKIMWIwakati wa ujauzito au wakati wak u n y o n y e s h a: Nyakati hizi mama anavirusi vya UKIMWI vingi kwenye damu nahivyo uwezekano wa kumwambukizamtoto ni mkubwa;

• Mama kuwa na UKIMWI: Uwezekano wakumwambukiza mtoto ni mkubwa kwanimama atakuwa na virusi vya UKIMWIvingi mwilini mwake;

• Mama kuwa na maambukizi yamagonjwa ya ngono wakati wa ujauzito:

Katika asilimia 30 - 40 ya watotowatakaoambukizwa virusi vya.UKIMWI na mama zao:• Asilimia 5 – 10 wataambukizwa

wakati wa ujauzito;• Asilimia 10 – 20 wataambukizwa

wakati wa kujifungua; na • Asilimia 5 – 20 wataambukizwa

wakati wa kunyonyesha.

mtoto mwenye virusi.qxd 1/7/05 3:10 PM Page 4

Page 5: ULISHAJI WA MTOTO A L I Y E Z A L I W A NA MAMA ...counsenuth.or.tz/sites/default/files/Ulishaji wa Mtoto...kunyonya maziwa ya mama. Hii hupunguza hatari ya magonjwa ya kuhara kwani

5

Magonjwa ya ngono husababisha vidondavidogo ukeni ambayo huongeza hatari yamaambukizi ya virusi vya UKIMWI;

• Taratibu zinazotumika wakati mamaa n a p o j i f u n g u a: Kwa mfano kuongeza njiaya uzazi, uchanaji mapema wa utandu,kumnyonya mtoto uchafu baada yakuzaliwa n.k;

• Hali ya lishe ya mama: Mama mwenyehali nzuri ya lishe ana mfumo thabiti wakinga na hivyo kuchelewesha mama huyokupata UKIMWI;

• Hali ya matiti ya mama: Matiti yenyevidonda au michubuko, chuchu zinazotoadamu na majipu ya titi huongeza hatari yamama kumwambukiza mtoto wake iwapomtoto atanyonyeshwa;

• Muda wa kunyonyesha: Hatari yauambukizo huongezeka iwapo mamamwenye virusi vya UKIMWIatamnyonyesha mtoto wake kwa zaidi yamiezi sita;

• Kuchanganya maziwa ya mama navinywaji au vyakula vingine:Kuchanganya maziwa ya mama navinywaji kama maziwa mbadala, maji,chai, uji, maji ya matunda n.k. huwezakusababisha mikwaruzo kwenye utumbowa mtoto na hivyo kutoa mwanya kwamaambukizi ya virusi vya UKIMWI;

• Hali ya kinywa cha mtoto: Vidonda vyakinywani au kooni na utandu mweupekinywani kwa mtoto huweza kuongezahatari ya maambukizi ya virusi vyaUKIMWI kupitia sehemu hizo zenyev i d o n d a .

Ikumbukwe kuwa njia kuu ya kuzuia mtoto kupatavirusi vya UKIMWI ni wazazi kuzuiawasiambukizwe virusi hivyo. Jukumu hili ni lababa na mama.

mtoto mwenye virusi.qxd 1/7/05 3:10 PM Page 5

Page 6: ULISHAJI WA MTOTO A L I Y E Z A L I W A NA MAMA ...counsenuth.or.tz/sites/default/files/Ulishaji wa Mtoto...kunyonya maziwa ya mama. Hii hupunguza hatari ya magonjwa ya kuhara kwani

6

ULISHAJI WA MTOTOMCHANGA ALIYEZALIWA NAMAMA MWENYE VIRUSI VYA

UKIMWI

Tamko rasmi lililotolewa na mashirika yakimataifa (WHO/UNAIDS/UNICEF) linasisitizamambo muhimu yafuatayo:

• Mama mwenye virusi vya UKIMWIaelekezwe kikamilifu kuhusu hatari yakuambukizwa mtoto kupitia maziwa yamama na njia nyingine;

• Wanawake wahimizwe na wapewehuduma za ushauri nasaha na kupimavirusi vya UKIMWI kwa hiari (VCT);

• Mwanamke mwenye virusi vya UKIMWIapewe taarifa muhimu na zilizo sahihi,kumwezesha kufanya uamuzi wa njia yakumlisha mtoto wake, iwe ni kunyonyeshakwa maziwa yake au kutumia maziwam b a d a l a .

Vipengele muhimu vya kuzingatia

wakati wa kutoa ushauri nasaha

Ikumbukwe kuwa kwa kusoma kijitabu hikitu, mshauri nasaha hawezi kuwa na stadi zakutosha kumsaidia mama mwenye virusi vyaUKIMWI kuhusu ulishaji wa mtoto wake.

Mshauri nasaha azingatie vipengele vifuatavyokatika kumshauri mama mwenye virusi vyaUKIMWI kabla ya kupata mimba, wakati waujauzito au akishajifungua:

• Ni vizuri mshauri nasaha awafahamuwashauri nasaha waliopewa mafunzo yakutosha kuhusu ulishaji wa mtoto kamamama ameambukizwa virusi vya UKIMWIili washirikiane;

• Kila mama apewe ushauri nasaha pekey a k e ;

mtoto mwenye virusi.qxd 1/7/05 3:10 PM Page 6

Page 7: ULISHAJI WA MTOTO A L I Y E Z A L I W A NA MAMA ...counsenuth.or.tz/sites/default/files/Ulishaji wa Mtoto...kunyonya maziwa ya mama. Hii hupunguza hatari ya magonjwa ya kuhara kwani

7

• Mama aelezwe njia zinazowezakumwambukiza mtoto ikiwa ana virusi vyaUKIMWI, ikiwemo unyonyeshaji maziwaya mama;

• Mama afahamishwe kiwango cha hatariiliyopo ya maambukizi ya virusi vyaUKIMWI kupitia maziwa ya mama na njian y i n g i n e ;

• Mama ana haki ya kuelezwa kwa ufasahanjia zote ambazo zinaweza kutumikakumlisha mtoto mchanga katika hali kamahii; pia faida na athari za kila njia yau l i s h a j i ;

• Mama afahamishwe pia kwamba watotowasionyonya maziwa ya mama wanahatari kubwa zaidi ya kupata magonjwakama vile ya kifua, masikio, kuharisha,mzio (allergies) na kupungukiwa kingaambayo watoto wanaonyonya huipatakwenye maziwa ya mama;

• Mama asaidiwe ili aweze kujipima uwezowake, kuona kama anaweza kumudu njiaaliyoichagua kiuchumi (kama kununuamaziwa na vifaa), kimazingira (upatikanajiwa maji safi na salama na hali ya usafi) nahuduma za afya;

• Mama asaidiwe aweze kupima iwapokutakuwa na athari zozote kwa familiayake kutokana na njia atakayoichagua;

• Ni muhimu kuendelea kumpima mtotokliniki kama kawaida ili kufuatilia ukuajiwake na hali yake ya afya;

• Mama aelezwe umuhimu wa kuishirikishafamilia yake hasa mume au baba wa mtotokuhusu uamuzi wake, na ikiwezekanamume au baba wa mtoto ashirikishwekwenye hatua zote za kufanya uamuzih u o ;

mtoto mwenye virusi.qxd 1/7/05 3:10 PM Page 7

Page 8: ULISHAJI WA MTOTO A L I Y E Z A L I W A NA MAMA ...counsenuth.or.tz/sites/default/files/Ulishaji wa Mtoto...kunyonya maziwa ya mama. Hii hupunguza hatari ya magonjwa ya kuhara kwani

8

• Mama aelekezwe mahali anapowezakupata ushauri zaidi wa njia aliyoichagua,hasa kama kuna mama wengine wenyeuzoefu zaidi;

• Mama asiyejua hali yake ya uambukizo wavirusi vya UKIMWI, ashauriwekunyonyesha maziwa yake kama kawaida.Pia ashauriwe kwenda kupimwa ili ajuehali yake.

Njia zinazoweza kutumika

kumlisha mtoto mchanga tangu

anapozaliwa mpaka miezi sita

Kumbuka kuwa katika miezi sita ya mwanzoya maisha ya mtoto, maziwa ndiyo chakulapekee na ni muhimu sana. Maziwa hayoyanaweza kuwa ya mama au maziwamengine. Ikiwa mtoto hanyonyeshwi maziwaya mama basi apate maziwa mengine kiasicha ml. 150 za maziwa kwa kila kilogramumoja ya uzito wake kwa siku. Kwa mfanomtoto mchanga mwenye kilogramu tanoanahitaji mililita (ml) 750 za maziwa (yaani ml.150 x kilo 5) kwa siku, kiasi hiki kinawezakugawanywa katika milo mitano au zaidi kwasiku. Ni muhimu kutumia kikombe kumlishamtoto badala ya chupa ya kunyonya iwapomtoto analishwa kwa njia ambayo siokunyonya maziwa ya mama. Hii hupunguzahatari ya magonjwa ya kuhara kwani ni rahisikusafisha kikombe kuliko chupa.

Kuna njia kuu mbili zinazoweza kutumikakumlisha mtoto aliyezaliwa na mama mwenyevirusi vya UKIMWI. Njia hizi ni kutumia

Ni muhimu kuhakikisha kwamba wanawakewasio na virusi vya UKIMWI wanaendeleakushauriwa kunyonyesha maziwa yao kamakawaida, na wasishawishike kutumia maziwamengine kwa sababu tu ya kuwaona wenginewakitumia maziwa hayo.

mtoto mwenye virusi.qxd 1/7/05 3:10 PM Page 8

Page 9: ULISHAJI WA MTOTO A L I Y E Z A L I W A NA MAMA ...counsenuth.or.tz/sites/default/files/Ulishaji wa Mtoto...kunyonya maziwa ya mama. Hii hupunguza hatari ya magonjwa ya kuhara kwani

9

maziwa ya mama na matumizi ya maziwam b a d a l a .

KUTUMIA MAZIWA YA MAMA

Mama aliyeamua kuchagua kutumia maziwayake tu ana njia kuu tatu ambazo anawezakuamua ni ipi itakayomfaa yeye na mtotowake. Njia hizi ni:-

• Kunyonyesha maziwa ya mama pekeetangu mtoto anapozaliwa hadi miezi sita

• Kunyonyesha maziwa ya mama kwamuda mfupi

• Kutumia maziwa ya mamayaliyokamuliwa na kuchemshwa

Kunyonyesha maziwa ya mamapekee tangu mtoto anapozaliwa

hadi miezi sita

Tafiti zimeonyesha kuwa unyonyeshaji wamtoto kwa maziwa ya mama pekeeunapunguza uwezekano wa mtoto kupatamaambukizi ya virusi vya UKIMWI kutokakwa mama yake ukilinganisha nakumnyonyesha mtoto na wakati huo huokumpa maziwa mengine, vinywaji au vyakulavingine. Iwapo mama atachagua njia hiia n a s h a u r i w a : -

• Kumnyonyesha mtoto wake maziwa yakepekee kwa miezi sita ya mwanzo bila yakumpa mtoto kitu kingine chochote hatamaji. Kumpa mtoto maziwa mbadala,vinywaji au vyakula vingine kutawezakuongeza hatari ya uambukizo wa virusivya UKIMWI kwa mtoto. Vinywaji auvyakula hivyo huweza kusababishamichubuko kwenye utumbo wa mtoto nahivyo kuruhusu virusi vya UKIMWIkupenya kwa urahisi;

mtoto mwenye virusi.qxd 1/7/05 3:10 PM Page 9

Page 10: ULISHAJI WA MTOTO A L I Y E Z A L I W A NA MAMA ...counsenuth.or.tz/sites/default/files/Ulishaji wa Mtoto...kunyonya maziwa ya mama. Hii hupunguza hatari ya magonjwa ya kuhara kwani

10

• Kuhakikisha anamnyonyesha mtoto kilaanapohitaji, usiku na mchana;

• Kumpakata na kumweka mtoto vizurikwenye titi ili kuzuia matatizo ya matitiyanayoweza kujitokeza, kama chuchukupata mipasuko au michubuko. Matatizohayo huongeza hatari ya uambukizo wavirusi vya UKIMWI kutoka kwa mamakwenda kwa mtoto;

• Kuhakikisha matatizo kinywani kwa mtotoyanatibiwa mapema, kwa mfano utandumweupe kwani huongeza hatari yamaambukizi ya virusi vya UKIMWI kwam t o t o ;

• Kuacha kabisa kumnyonyesha mtotobaada ya miezi sita. Wakati huo mamaanaweza kukamua na kuchemsha maziwayake huku akimpatia mtoto vinywaji navyakula vingine.

Picha (b):

Inaonyesha njia ambayo sisahihi ya kumshika mtoto.Hapo mtoto hatawezakuingiza titi kinywani vizuri.

Picha (a):

Inaonyesha njia sahihi yakumshika mtoto ili afikie titivizuri. Tumbo la mtotolimemwelekea mama na usoumeangalia na umesogeleat i t i

mtoto mwenye virusi.qxd 1/7/05 3:10 PM Page 10

Page 11: ULISHAJI WA MTOTO A L I Y E Z A L I W A NA MAMA ...counsenuth.or.tz/sites/default/files/Ulishaji wa Mtoto...kunyonya maziwa ya mama. Hii hupunguza hatari ya magonjwa ya kuhara kwani

11

Kunyonyesha maziwa ya mama

kwa muda mfupi

Kumwachisha mtoto kunyonya maziwa yamama yake mapema husaidia kupunguzauwezekano wa mtoto kuambukizwa virusivya UKIMWI kutoka kwa mama kupitiamaziwa kwani kwa kufanya hivyo muda wamtoto kuwa kwenye hatari ya maambukizi yavirusi vya UKIMWI hupungua. Iwapo mamamwenye virusi vya UKIMWI atachagua njia hiia n a s h a u r i w a : -

• Kuacha kumnyonyesha mtoto wakemapema iwezekanavyo kabla ya miezisita. Muda halisi wa kuachakumnyonyesha mtoto utaamuliwa namama mwenyewe kwa kuzingatiauwezekano wa kupata maziwa mbadala;

• Kukumbuka kumnyonyesha mtotomaziwa yake pekee bila kumpa maziwambadala, vinywaji au vyakula vingine

Picha (a):

Inaonyesha mtoto ambaye titilimeingia vizuri mdomoniyaani chuchu pamoja nasehemu nyeusi inayozungukachuchu imeingia kinywani.Midomo iko wazi na kidevukimegusa titi. Mtotoatanyonya vizuri.

Picha (b):

Inaonyesha mtoto ambayehakuingiza titi vizurikinywani. Mtoto huyuananyonya chuchu tu,midomo haikufunguka vizurina kidevu kiko mbali na titi.Mtoto hataweza kunyonyav i z u r i .

Chuchu yote, na sehemu kubwa ya eneo jeusilinalozunguka chuchu iingie kinywani kwa mtoto

mtoto mwenye virusi.qxd 1/7/05 3:10 PM Page 11

Page 12: ULISHAJI WA MTOTO A L I Y E Z A L I W A NA MAMA ...counsenuth.or.tz/sites/default/files/Ulishaji wa Mtoto...kunyonya maziwa ya mama. Hii hupunguza hatari ya magonjwa ya kuhara kwani

12

vyovyote. Uchanganyaji wa maziwa yamama na maziwa mbadala, vinywaji navyakula vingine huongeza hatari yamaambukizi ya virusi vya UKIMWI kwam t o t o ;

• Mama anapoamua kuacha kumnyonyeshamtoto wake ashauriwe kufanya hivyomara moja. Ili kuweza kuzuia hatariambazo zinaweza kujitokeza katika kipindihicho cha mpito au kutokana namabadiliko ya ghafla kama utapiamlo,mama ashauriwe kuanza kukamua maziwayake katika wiki mbili kabla yakumwachisha mtoto na kumnyweshamtoto maziwa hayo kwa kutumiakikombe. Hii itamwezesha mtoto kuwezakuzoea kutumia kikombe;

• Kumpakata na kumweka mtoto vizurikwenye titi ili kuzuia matatizo ya matitiyanayoweza kujitokeza;

• Mtoto aliyeachishwa kunyonya maziwa yamama yake kabla ya miezi sita apewemaziwa mbadala au mama akamuemaziwa yake na kuyachemsha kabla yakumpa mtoto. Mtoto anyweshwe maziwahayo mara tano au zaidi kwa siku;

• Mama anayenyonyesha akiwa na halimbaya, hasa anapopata magonjwanyemelezi na akawa mgonjwa sana nivyema aache kunyonyesha;

• Mama anayeamua kuacha kumnyonyeshamtoto wake mapema anapaswa kusaidiwakufanya hivyo kwa ufanisi na usalama ilikuepusha madhara yoyote yanayowezakutokea kwa mtoto.

Maziwa ya mamayaliyokamuliwa na kuchemshwa

Virusi vya UKIMWI vilivyoko kwenye maziwaya mama vinaweza kuharibiwa kwakuchemsha maziwa hayo yaliyokamuliwa.

mtoto mwenye virusi.qxd 1/7/05 3:10 PM Page 12

Page 13: ULISHAJI WA MTOTO A L I Y E Z A L I W A NA MAMA ...counsenuth.or.tz/sites/default/files/Ulishaji wa Mtoto...kunyonya maziwa ya mama. Hii hupunguza hatari ya magonjwa ya kuhara kwani

13

Tafiti zimeonyesha kuwa virusi vya UKIMWIvilivyoko kwenye maziwa ya mama hufa bilakuharibu kingamwili zilizopo kwenyemaziwa iwapo yatapashwa moto kati ya nyuzijoto 56°C – 63°C kwa muda wa dakika 20.Lakini katika mazingira ya kawaida sio rahisikupima nyuzi joto hizo hivyo inashauriwakuacha maziwa hayo mpaka yachemke. Maratu yakichemka yaipuliwe. Kwa kuchemshamaziwa hayo baadhi ya kingamwili navirutubishi vilivyomo huharibika. Ni muhimumama apate ushauri wa daktari au mtaalamuwa afya kuhusu virutubishi vya nyongeza vyakumpa mtoto.

Iwapo mama ataamua kutumia maziwa yakealiyoyakamua na kuyachemsha ili kuua virusivya UKIMWI, yafuatayo ni muhimu:

• Mama aelekezwe njia rahisi ya kukamuamaziwa yake bila ya kusababishamaumivu kwa titi lake;

• Maziwa hayo yaipuliwe pindi tuyanapoanza kuchemka;

• Maziwa hayo yapoozwe kwa haraka aidhakwa kutumbukiza chombo chenye maziwandani ya maji baridi au kuweka ndani yaj o k o f u ;

• Mtoto anyweshwe maziwa hayo kwakutumia kikombe;

• Ikumbukwe kuwa maziwa ya mamayaliyokamuliwa yanaweza kukaa bilakuharibika kwa saa 8 kwenye joto lakawaida na saa 72 kwenye jokofu.

• Mama anapochagua njia hii kama ilivyokwa njia nyingine anapaswa kupataushauri nasaha na kusaidiwa.

Maziwa ya mama yaliyokamuliwa nakuchemshwa bado ni bora kuliko maziwam b a d a l a .

mtoto mwenye virusi.qxd 1/7/05 3:10 PM Page 13

Page 14: ULISHAJI WA MTOTO A L I Y E Z A L I W A NA MAMA ...counsenuth.or.tz/sites/default/files/Ulishaji wa Mtoto...kunyonya maziwa ya mama. Hii hupunguza hatari ya magonjwa ya kuhara kwani

14

KUTUMIA MAZIWA MBADALA

Maziwa mbadala yanaweza kutumikakumlisha mtoto aliyezaliwa na mama mwenyevirusi vya UKIMWI. Maziwa mbadala nipamoja na maziwa yaliyotengenezwamaalumu kwa watoto wachanga, maziwayanayotayarishwa nyumbani kutokana namaziwa ya wanyama kama ng’ombe au mbuzina maziwa yanayotayarishwa nyumbanikutokana na maziwa yaliyokaushwa (driedmilk powder) au maziwa yaliyochevushwa( e v a p o r a t e d ) .

Jinsi ya kukamua maziwa ya

mama

Ni muhimu kila mama ajifunze au aelekezwenjia rahisi ya kukamua maziwa bila yakusababisha maumivu.

Yafuatayo ni maelezo muhimu:

- Shika sehemu nyeusii n a y o z u n g u k achuchu kwa kuwekavidole vinne upandewa chini na kidolegumba upande wajuu, kisha bonyezakwa kugandamizak i f u a .

- Bonyeza sehemunyeusi ya titi kati yavidole vinne nakidole gumba.

- Bonyeza pia sehemuza pembenikuhakikisha maziwayote yanatoka.

mtoto mwenye virusi.qxd 1/7/05 3:10 PM Page 14

Page 15: ULISHAJI WA MTOTO A L I Y E Z A L I W A NA MAMA ...counsenuth.or.tz/sites/default/files/Ulishaji wa Mtoto...kunyonya maziwa ya mama. Hii hupunguza hatari ya magonjwa ya kuhara kwani

15

Wakati wa kumpa mama ushauri wa njia yakumlisha mtoto wake, mshauri nasahaakumbuke, ili kutumia maziwa mbadala nimuhimu kuhakikisha kuwa hatari ya mtotokufa kwa kutumia maziwa mbadala ni ndogokuliko hatari ya mtoto kufa kwa UKIMWIkupitia maziwa ya mama.

Maziwa yaliyotengenezwamaalumu kwa watotowachanga (Infant Formula)

Maziwa hayo hutengenezwa kutokana namaziwa ya ng’ombe, mbuzi au soya na yanavirutubishi vinavyokaribiana sana na vilevilivyoko kwenye maziwa ya mama. Kwakawaida huwa yameongezwa vitamini nam a d i n i .

Iwapo mama ataamua kutumia maziwa hayokumlisha mtoto wake, ni muhimu kufahamuvipengele vifuatavyo:

• Mama anahitaji wastani wa makopo 40yenye uzito wa nusu kilo (gramu 500) ilikuweza kumlisha mtoto wake kwa miezisita ya mwanzo;

• Maziwa kwa ajili ya mtoto yanapaswayachaguliwe kulingana na umri wake;

• Maelekezo yaliyoandikwa kwenye kopoyanapaswa kuzingatiwa na kufuatwa;

• Ni muhimu kutumia vikombe wakati wamatayarisho kwa vile uoshaji wake nir a h i s i ;

• Mama amlishe mtoto kwa kutumiakikombe huku akiwa amempakatakaribu naye ili kujenga uhusiano wak a r i b u ;

• Ni vizuri kuepuka matumizi yaC h u p a .

mtoto mwenye virusi.qxd 1/7/05 3:10 PM Page 15

Page 16: ULISHAJI WA MTOTO A L I Y E Z A L I W A NA MAMA ...counsenuth.or.tz/sites/default/files/Ulishaji wa Mtoto...kunyonya maziwa ya mama. Hii hupunguza hatari ya magonjwa ya kuhara kwani

16

• Usafi wa mtayarishaji, mazingira na vifaavya kutayarishia uzingatiwe;

• Mama ahakikishe muda wa kutumikamaziwa hayo haujamalizika (expiry date);

• Mama anapaswa kuwa mwangalifu sanana kupata msaada unaotakiwa ili mtotoasipate magonjwa ya kuambukiza hasa yak u h a r i s h a ;

• Maziwa yaliyokwishatengenezwayasiwekwe kwa matumizi ya baadaye.Wapewe watoto wakubwa auyachanganywe kwenye chakula chao;

• Ni muhimu mtoto apelekwe kliniki ilikufuatilia ukuaji wake kwa karibu naaonwe na daktari pale inapobidi.

Maziwa ya ng’ombe au mbuzi

Iwapo mama ataamua kumlisha mtoto wakekwa kutumia maziwa ya ng’ombe au mbuzivifuatavyo ni vipengele muhimu:

• Kila mililita (ml) 100 za maziwa yang’ombe au mbuzi ziongezwe ml. 50 zamaji na sukari vijiko vidogo viwilivisivyojazwa sana (kijae bapa);

• Mchanganyiko huo uchemshwe mpakauchemke vizuri;

• Mtoto apewe maziwa hayoyaliyopoozwa kwa kutumiak i k o m b e ;

• Kwa siku mtoto apewe kiasi cha ml.150 kwa kila kilo ya uzito wake;

• Mtoto huyo aonwe na daktari au mtaalamuwa afya atakayetoa ushauri wa madini navitamini atakazohitaji mtoto kamanyongeza kwani maziwa hayo yanawezakuwa na upungufu wa madini ya chuma,zinki, folic acid na vitamini A;

mtoto mwenye virusi.qxd 1/7/05 3:10 PM Page 16

Page 17: ULISHAJI WA MTOTO A L I Y E Z A L I W A NA MAMA ...counsenuth.or.tz/sites/default/files/Ulishaji wa Mtoto...kunyonya maziwa ya mama. Hii hupunguza hatari ya magonjwa ya kuhara kwani

17

• Usafi wa vifaa vya kutengenezea maziwa,maji safi na salama pamoja na mazingiramasafi ni muhimu sana.

Lifuatalo ni jedwali linaloonyesha mfano wamahitaji ya siku kwa mtoto kwa kutumiamaziwa ya ng’ombe au mbuzi.

mtoto mwenye virusi.qxd 1/7/05 3:10 PM Page 17

Page 18: ULISHAJI WA MTOTO A L I Y E Z A L I W A NA MAMA ...counsenuth.or.tz/sites/default/files/Ulishaji wa Mtoto...kunyonya maziwa ya mama. Hii hupunguza hatari ya magonjwa ya kuhara kwani

18

Maziwa ya unga yenye mafuta (driedfull cream) au yale yaliyopunguzwamaji (evaporated)

Maziwa haya yanaweza kutumika kamamaziwa ya aina nyingine hayapatikani. Iwapomaziwa haya yanatumika, yafuatayo nim u h i m u :

• Maziwa yatengenezwe kwa kutumia majiyaliyochemshwa na kufuata maelekezokwenye paketi au kopo lake. Hapounapata maziwa kama ya ng’ombe. Baadaya hapo fuata maelekezo yaliyotolewahapo juu ya kutengeneza maziwa yang’ombe ili kumfaa mtoto mchanga;

• Mtoto huyo aonwe na daktari au mtaalamuwa afya atakayetoa ushauri wa madini navitamini za nyongeza atakazohitaji mtotokwani maziwa hayo yanaweza kuwa naupungufu wa madini na vitamini;

• Usafi wa vifaa vya kutengenezea maziwa,maji safi na salama pamoja na mazingiramasafi ni muhimu sana.

KUMBUKAMaziwa ndiyo chakula pekee kwa mtoto chiniya umri wa miezi 6.

Namna ya kumlisha mtoto

mchanga kwa kutumia kikombe

Kumlisha mtoto kwa kikombe kunapunguzahatari ya uambukizo ambao unawezakutokana na kutumia chupa. Kikombe nirahisi kuosha, na anayemlisha mtotoinalazimu ampakate vizuri, na hivyo kujengaupendo na ukaribu zaidi kati ya mtoto namzazi au mlezi. Zingatia yafuatayo:

• Mpakate mtoto na muweke nusu wima(kama ameketi);

• Shikilia kikombe cha maziwa kwenyemidomo ya mtoto mchanga;

mtoto mwenye virusi.qxd 1/7/05 3:10 PM Page 18

Page 19: ULISHAJI WA MTOTO A L I Y E Z A L I W A NA MAMA ...counsenuth.or.tz/sites/default/files/Ulishaji wa Mtoto...kunyonya maziwa ya mama. Hii hupunguza hatari ya magonjwa ya kuhara kwani

19

• Kikombe kikae kwenye mdomo wa chiniya mtoto mchanga na kingo za kikombeziguse mdomo wa juu. Kikombekiinamishwe ili maziwa yatiririke polepolekwenye kinywa cha mtoto mchanga;

• Mtoto mchanga huonyesha kuwa tayarikwa kufungua mdomo na kuchangamka.Mtoto mchanga aliyezaliwa na uzitopungufu atachukua maziwa kwenyekinywa na ulimi, lakini yule aliyezaliwa nauzito wa kutosha atafyonza maziwa;

• Usimimine maziwa kwenye kinywa chamtoto mchanga bali shikilia kikombe tukwenye mdomo naye atafyonza;

• Kama mtoto mchanga amekunywamaziwa ya kutoshaatafunga mdomona hatakunywazaidi. Ikibainikakuwa mtotom c h a n g ahakunywa maziwakiasi cha kutosha,aidha atakunywazaidi wakatimwingine au inashauriwa kumnyweshamara kwa mara. Unashauriwa kupimakiasi cha maziwa aliyokunywa mtotobaada ya saa 24 na siyo baada ya mlom m o j a .

Vyakula na maziwa yasiyofaa

kumlisha mtoto mwenye umri

chini ya miezi sita

• Maziwa yaliyotolewa mafuta (skimmedmilk) na yale yaliyopunguzwa maji nakuongezwa sukari (sweetened, condensedm i l k ) ;

• Maji ya matunda au maji ya sukari;

• Maziwa yaliyoganda (mtindi);

• Chai ya rangi au uji.

mtoto mwenye virusi.qxd 1/7/05 3:10 PM Page 19

Page 20: ULISHAJI WA MTOTO A L I Y E Z A L I W A NA MAMA ...counsenuth.or.tz/sites/default/files/Ulishaji wa Mtoto...kunyonya maziwa ya mama. Hii hupunguza hatari ya magonjwa ya kuhara kwani

20

FAIDA ZA MAZIWA YA MAMA

Maziwa ya mama ndiyo bora kwa mtotomchanga kuliko maziwa mengine yoyote.Kunyonyesha maziwa ya mama kunampamama pamoja na mtoto faida nyingi, kamainavyoelezwa hapa chini:

• Humpatia mtoto virutubishi vyoteanavyohitaji kwa uwiano sahihi kwaukuaji wake kiakili na kimwili kwa miezisita ya mwanzo;

• Humpatia mtoto kinga dhidi ya maradhimbalimbali kama kuharisha, magonjwa yanjia ya hewa na masikio;

• Maziwa ya mamah u m e n g ’ e n y w a( h u y e y u s h w a )kwa urahisitumboni mwamtoto na hivyoh u s h a r a b i w a(hufyonzwa) nakutumiwa mwilinikwa ufanisi;

• Ni safi, salama na hupatikana muda wotekatika joto sahihi kwa mtoto na hayahitajim a t a y a r i s h o ;

• Gharama yake ni ndogo ikilinganishwa namaziwa mbadala;

• Hayaharibiki ndani ya titi na hatayakikamuliwa huweza kukaa saa 8 katikajoto la kawaida na saa 72 kwenye jokofubila kuharibika;

• Hayaleti matatizo ya mzio (allergies) kamapumu na magonjwa ya ngozi;

• Huleta uhusiano mzuri na wa karibu katiya mama na mtoto na pia imeonekanakwamba watoto walionyonyeshwa

mtoto mwenye virusi.qxd 1/7/05 3:10 PM Page 20

Page 21: ULISHAJI WA MTOTO A L I Y E Z A L I W A NA MAMA ...counsenuth.or.tz/sites/default/files/Ulishaji wa Mtoto...kunyonya maziwa ya mama. Hii hupunguza hatari ya magonjwa ya kuhara kwani

21

maziwa ya mama huwa na mwenendomzuri kitabia;

• Kwa mama, kunyonyesha husaidia tumbola uzazi kurudi katika hali ya kawaidam a p e m a ;

• Kunyonyesha pia humsaidia mamakupunguza damu inayotoka baada yakujifungua, hivyo huzuia upungufu wawekundu wa damu;

• Kunyonyesha hupunguza uwezekano wamama kupata saratani ya mfuko wa uzazina matiti;

• Kunyonyesha hupunguza uwezekano wamama kupata ujauzito katika miezi sita yamwanzo iwapo mama atamnyonyeshamtoto maziwa yake tu kwa zaidi ya mara10 kwa siku na pia kama hajapata hedhikatika miezi sita ya mwanzo.

KUMLISHA MTOTO WA MIEZI SITA

HADI MIAKA MIWILI

Mtoto anapofikisha umri wa miezi sitaanahitaji vyakula vingine ikiwa ni pamoja namaziwa. Iwapo mama ana virusi vya UKIMWIyafaa mtoto huyo asiendelee kunyonyeshwana yafuatayo ni muhimu:-

• Mtoto apewe maziwa ya aina nyingineyoyote angalau mara tano kwa siku nawakati huu maziwa ya ng’ombe au mbuzihayahitaji kuchanganywa na maji.

• Maziwa ya mama yaliyokamuliwa nakuchemshwa yanaweza pia kutumika.

• Pamoja na maziwa, mtoto pia apewechakula cha familia kilicholainishwa, maratano au zaidi kwa siku.

• Chakula cha mtoto kiwe na mchanganyikowa angalau chakula kimoja kutoka katikamakundi yafuatayo:

mtoto mwenye virusi.qxd 1/7/05 3:10 PM Page 21

Page 22: ULISHAJI WA MTOTO A L I Y E Z A L I W A NA MAMA ...counsenuth.or.tz/sites/default/files/Ulishaji wa Mtoto...kunyonya maziwa ya mama. Hii hupunguza hatari ya magonjwa ya kuhara kwani

22

- Nafaka na vyakula vitokanavyo na mizizina ndizi (mahindi, ulezi, mchele, mtama,viazi vya aina zote, mihogo, ndizi n.k).

- Vyakula vitokanavyo na wanyama namikunde kama mayai, maziwa, samaki,maini, nyama, dagaa, maharagwe,kunde, karanga, njegere, choro k o ,dengu, mbaazi n.k.

- Mboga-mboga kama mboga za kijani,k a roti, maboga n.k.

- Matunda kama mapapai, machungwa,maembe ndizi, nanasi n.k.

- Mafuta na sukari. Mafuta ni pamoja nambegu zitoazo mafuta kama; alizeti,ufuta, karanga n.k. Sukari ni pamoja naasali na sukari.

• Vyakula vya mtoto viwe laini ila visiwevyepesi sana. Ongeza vyakula kamamafuta, sukari, siagi, asali, mbegu zitoazomafuta kama karanga au korosho, kweme,tui la nazi au maziwa ili kufanya chakulakiwe laini. Kimea pia chaweza kutumikakulainisha uji ulio mzito.

• Mtoto aanze kwa kupewa chakula chaaina moja katika mlo na si kuchanganyavyakula vingi kwa mara moja. Hii itasaidiakuzoea kwa urahisi na kujua vyakulavinavyoweza kumletea mtoto matatizo yamzio (allerg i e s ) .

• Mtoto aongezewe kiasi cha chakulataratibu kadiri anavyoendelea kukua.

• Mtoto mwenye umri zaidi ya miezi 6anaweza kutumia maziwa mengine yoyoteyakiwemo maziwa ya mgando (mtindi).

• Chakula cha mtoto kinaweza kutayarishwakutoka katika chakula cha familia.

mtoto mwenye virusi.qxd 1/7/05 3:10 PM Page 22

Page 23: ULISHAJI WA MTOTO A L I Y E Z A L I W A NA MAMA ...counsenuth.or.tz/sites/default/files/Ulishaji wa Mtoto...kunyonya maziwa ya mama. Hii hupunguza hatari ya magonjwa ya kuhara kwani

23

Watoto wadogohula pole polena kiasi kidogo.Ni muhimumtoto atengewechakula chakemwenyewe ilikujua kamaamekula vyakulavyote muhimuna kiasi chak u t o s h a .

Mara nyingi,mtoto mdogoa n a h i t a j ikulishwa aukusaidiwa iliaweze kulachakula chak u t o s h a

HITIMISHOInasisitizwa kwamba, mshauri nasaha atumiembinu zake za msingi za kusikiliza kwamakini na kutafuta taarifa zilizo sahihi kutokakwa mteja na pia kumpa mteja taarifa zilizosahihi. Njia yoyote mama atakayochaguakutumia kumlisha mtoto, apewe msaadaunaowezekana au kupatikana ili awezekufanikisha njia hiyo kwa usahihi na usalamai w e z e k a n a v y o .

mtoto mwenye virusi.qxd 1/7/05 3:10 PM Page 23

Page 24: ULISHAJI WA MTOTO A L I Y E Z A L I W A NA MAMA ...counsenuth.or.tz/sites/default/files/Ulishaji wa Mtoto...kunyonya maziwa ya mama. Hii hupunguza hatari ya magonjwa ya kuhara kwani

24

LISHE BORA KWA MAMA

MJAMZITO NA

ANAYENYONYESHA

Mama mjamzito na anayenyonyesha nimuhimu kuwa na lishe bora. Inashauriwamama huyo:

• Ale mlo kamili angalau mara tatu kwa sikuna asusa (snack) kati ya milo hiyo;

• Ale vyakula mbalimbali vya mchanganyikovipatikanavyo kwa urahisi sehemua n a y o i s h i ;

• Ale matunda na mboga za majani kila siku,ikiwezekana katika kila mlo;

• Matunda ya njano na mboga za kijani aunjano ni bora zaidi;

• Anywe maji ya kutosha kila siku, sio chiniya lita moja na nusu (glasi 8);

• Ajiwekee muda wa kupumzika kila sikuwakati wa mchana angalau saa moja;

• Asinywe chai au kahawa wakati wa mlo ilikuwezesha madini chuma yatokanayo namimea kusharabiwa (kufyonzwa) vizuri;

• Asitumie pombe au sigara wakati waujauzito na kunyonyesha kwani hivihuathiri mtoto.

mtoto mwenye virusi.qxd 1/7/05 3:10 PM Page 24

Page 25: ULISHAJI WA MTOTO A L I Y E Z A L I W A NA MAMA ...counsenuth.or.tz/sites/default/files/Ulishaji wa Mtoto...kunyonya maziwa ya mama. Hii hupunguza hatari ya magonjwa ya kuhara kwani

25

VYANZO

1 . U N I C E F / U N A I D S / W H O / U N F PA, HIV andInfant Feeding: A Guide for Health CareManagers and Supervisors (Final Draft),S e p t e m b e r, 2003.

2 . I B FAN Africa, Infant Feeding Options inHIV/AIDS: Information for HealthWorkers. Mbabane, Swaziland, May, 2002.

3 . FAO/WHO, Living well with HIV/AIDS: Amanual on nutritional care and support forpeople living with HIV/AIDS, Rome, 2002.

4 . U N I C E F / U N A I D S / W H O / U N F PA, HIV andInfant Feeding: Guidelines for DecisionMakers (Final Draft), September, 2003.

5 . Food and Nutrition Technical Assistance( FA N TA), HIV/AIDS: A Guide for Nutrition,C a re and Support. Academy forEducational Development, Wa s h i n g t o nDC, 2001.

6 . COUNSENUTH, Unyonyeshaji bora wamaziwa ya mama: Vidokezo muhimu kwajamii. COUNSENUTH Information SeriesNo. 5, June, 2003

7 . COUNSENUTH, Nutritional Care for PLHA:Training and Reference Manual (DRAFT),S e p t e m b e r, 2003.

mtoto mwenye virusi.qxd 1/7/05 3:10 PM Page 25

Page 26: ULISHAJI WA MTOTO A L I Y E Z A L I W A NA MAMA ...counsenuth.or.tz/sites/default/files/Ulishaji wa Mtoto...kunyonya maziwa ya mama. Hii hupunguza hatari ya magonjwa ya kuhara kwani

26

SHUKRANI

COUNSENUTH inatoa shukrani kwaWA M ATA, SHDEPHA+, MATI-Uyole, SUA nawatu binafsi ambao wameshiriki katikak u b o resha kijitabu hiki.

Shukurani za pekee kwa RFE kwa ufadhili.

VIJITABU VINGINE KUHUSULISHE NA VIRUSI VYA UKIMWI

VILIVYOTOLEWA NACOUNSENUTH:

1 . Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Vi r u s ivya UKIMWI: “Vidokezo Muhimu”COUNSENUTH information series No. 2,Toleo la Pili, January, 2004.

2 . Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wa n a o i s h ina Virusi vya UKIMWI: “Vy a k u l av i n a v y o b o resha uyeyushwaji wa chakulana ufyonzwaji wa virutubishi mwilini”:COUNSENUTH information series No. 4,M a rch, 2003.

3 . Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wa n a o i s h ina Virusi vya UKIMWI: “Majibu ya MaswaliYanayoulizwa Mara kwa Mara”COUNSENUTH information series No. 3,Toleo la Pili, January, 2004.

mtoto mwenye virusi.qxd 1/7/05 3:10 PM Page 26

Page 27: ULISHAJI WA MTOTO A L I Y E Z A L I W A NA MAMA ...counsenuth.or.tz/sites/default/files/Ulishaji wa Mtoto...kunyonya maziwa ya mama. Hii hupunguza hatari ya magonjwa ya kuhara kwani

27

mtoto mwenye virusi.qxd 1/7/05 3:10 PM Page 27

Page 28: ULISHAJI WA MTOTO A L I Y E Z A L I W A NA MAMA ...counsenuth.or.tz/sites/default/files/Ulishaji wa Mtoto...kunyonya maziwa ya mama. Hii hupunguza hatari ya magonjwa ya kuhara kwani

ISBN 9987-8936-4-3

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:M k u r u g e n z i

Kituo cha Ushauri Nasaha, Lishe na Afya

( C O U N S E N U T H )S . L . P. 8218, Dar es Salaam,

Ta n z a n i aSimu: (22) 2152705 au 0744 279145

Fax: (22) 2152705

Kijarida hiki kimetolewa na:The Centre for Counselling, Nutrition and Health Care

( C O U N S E N U T H )United Nations Rd./ Kilombero Str.

Plot No. 432, Flat No.3P.O. Box 8218, Dar es Salaam Ta n z a n i a .

Kimefadhiliwa na:

Rapid Funding Envelope for

HIV/AIDS (RFE)

Designed & printed by:

Desktop Productions Limited

P.O. Box 20936, Dar es Salaam, TanzaniaContact: 0748 387899, Email: [email protected]

mtoto mwenye virusi.qxd 1/7/05 3:10 PM Page 28