Upload
others
View
17
Download
1
Embed Size (px)
Citation preview
CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
SERA YA MFUKO WA MAZISHI YA CHUO KIKUU
CHA DAR ES SALAAM
JANUARY, 2016
i
YALIYOMO
UTANGULZI .............................................................................................................................................. II
VIFUPISHO ................................................................................................................................................ V
SURA YA KWANZA ..................................................................................................................................1
1.0 HISTORIA FUPI YA SERA YA MFUKO WA MAZISHI .....................................................1
1.1 MAELEZO YA AWALI .................................................................................................................1
1.2 MFUKO WA MAZISHI ................................................................................................................2
1.2.1 AWAMU YA KWANZA: KABLA YA 1993 ...........................................................................2
1.2.2 AWAMU YA PILI: BAADA YA 1993 ....................................................................................3
1.3 SIHA YA MFUKO ..........................................................................................................................8
1.4 HALI ILIVYO HIVI SASA .........................................................................................................8
SURA YA PILI........................................................................................................................................... 11
2.0 UMUHIMU WA SERA, DIRA, DHIMA NA MALENGO YA SERA ................................. 11
2.1 UMUHIMU WA SERA YA MFUKO WA MAZISHI YA CHUO KIKUU CHA DAR ES
SALAAM ..................................................................................................................................................... 11
2.2 DIRA YA SERA YA MFUKO WA MAZISHI YA CHUO KIKUU CHA DAR ES
SALAAM ..................................................................................................................................................... 11
SURA YA TATU ........................................................................................................................................ 13
3.0 MALENGO NA MATAMKO YA KISERA ............................................................................... 13
3.1 LENGO NAMBA 1 ........................................................................................................................ 13
3.2 LENGO NAMBA 2 ....................................................................................................................... 14
3.3 LENGO NAMBA 3 ....................................................................................................................... 15
3.4 LENGO NAMBA 4 ....................................................................................................................... 15
3.5 LENGO NAMBA 5 ....................................................................................................................... 16
SURA YA NNE .......................................................................................................................................... 18
4.0 MUUNDO WA KISHERIA NA KIUONGOZI WA SERA YA MFUKO WA MAZISHI
YA WAFANYAKAZI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM ............................................... 18
4.1 MUUNDO WA KISHERIA ........................................................................................................ 18
ii
4.2 MUUNDO WA KIUONGOZI .................................................................................................... 18
SURA YA TANO ....................................................................................................................................... 20
5.0 HITIMISHO NA MAPENDEKEZO ......................................................................................... 20
5.2 MAPENDEKEZO ......................................................................................................................... 20
KANUNI ZA MFUKO WA MAZISHI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM ................. 25
KIAMBATISHO A .................................................................................................................................... 38
KIAMBATISHO B .................................................................................................................................... 41
ii
Majedwali
Jedwali Namba 1: Mafano yaliyokuwa yakitolewa ............................................................ 5
Jedwali Namba 2: Viwango vipya vya Mafao ..................................................................... 7
Jedwali namba 3.1: Mchanganuo wa Mafao ya Mazishi kama Mchango wa
Mwanachama utakuwa Tshs. 3,000/= .............................................................................. 21
Jedwali Namba 3.2: Mchanganuo wa Mafao ya Mazishi kama Mchango wa
Mwanachama utakuwa Tshs. 4,000/= .............................................................................. 22
Jedwali Namba 3.3: Mchanganuo wa Mfao ya Mazishi kama mchango wa
Mwanachama utakuwa Tshs. 5,000/= .............................................................................. 23
Jedwali Namba 3.4: Ongezeko/pungufu kwa mwaka ikizingatia mchango wa
Mwanachama na kiasi cha malipo kwa Mfiwa .................................................................. 24
iii
UTANGULZI
Kwa barua ya tarehe 10 Machi, 2015 Naibu Makamu Mkuu wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam, Utawala, aliteua Kamati ya Kuandaa Sera ya
Mfuko wa Mazishi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kamati ilipewa
hadidu za rejea zifuatazo:
1. Kupitia upya Rasimu ya Sera ya Mazishi ya 2014 iliyowasilishwa
kwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Utawala) pamoja na kanuni
zake ili kupendekeza malipo ya ziada ambayo mfiwa atapewa kutoka
katika Mfuko wa Chuo wa Sera ya Mzishi.
2. Kupendekeza jambo jingine lolote ambalo kamati itaona linafaa
kuhusishwa, kuingizwa au kufanyiwa kazi, ili kuboresha Sera ya
Mazishi, kwa maslahi ya wafanyakazi na Chuo kwa ujumla.
Kamati ilitakiwa kuwasilisha rasimu ya Sera ya Kanuni zake ifikapo
tarehe 31 Machi, 2015.
Katika kikao chake cha kwanza Kamati ilichambua hadidu za rejea ili
kujiridhisha na upana na upeo wa kazi. Kamati ilizielewa hadidu za rejea
kama ifuatavyo:
1. Kwamba Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitatekeleza majukumu
yake ya kisheria kuhusiana na mazishi ya mfanyakazi wake.
Utekelezaji huo kumhusu mfanyakazi una nguvu ya kisheria tokana
na Agizo la Serikali 2009 (Public Service Standing Orders, 2009),
Kanuni namba Q.7. Agizo hilo ni sehemu ya sheria za Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam kwa kunukuliwa katika “UDSM Staff Regulations,
2013” kanuni namba 70.
2. Kwa kuwa sera ya Mazishi iliyopo inahusisha Chuo Kikuu kama
mwajiri na wafanyakazi, uelewa wa Kamati hapo juu (1) una maana
kwamba sera ya Mfuko wa Mazishi ambayo Kamati inabidi iiandae
ni sera ya Mfuko wa Mazishi ya Wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam.
iiii
3. Kwa kuwa majukumu ya kisheria yatatekelezwa na majiri, yaani
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, sera ya Mfuko wa Mazishi ya
Wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam itajazilisha pale
ambapo yanaishia majukumu ya kisheria ya Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam.
Kutokana na maelezo ya hapo juu Kamati imeelewa inatakiwa
kufanya yafuatayo:
(a) Kupitia upya Rasimu ya Sera ya Mazishi ya mwaka 2014 kwa
mtizamo ulioainishwa hapo juu.
(b) Kuangalia maeneo ambayo hayataguswa na majukumu ya
kisheria ya Chuo Kikuu.
(c) Kuangalia mambo mengineyo ambayo itaona yanafaa kwa
maslahi ya wafanyakazi na Chuo kwa ujumla.
Kamati ilifarijika pale Naibu Makamu Mkuu wa Chuo alipouafiki
uelewa huo kwa barua yake ya tarehe 26 Machi, 2015.
Kamati ilifanya kazi yake kwa bidii; ilikutana mara tano na kuweza
kuandaa Sera ya Mfuko wa Mazishi ya Wafanyakazi wa Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam na pia Kanuni zake baada ya kupitia rasimu ya
Sera ya Mazishi ya mwaka 2014, kuyatambua maeneo ambayo Chuo
Kikuu hakihusiki katika kumzika mfanyakazi wake au mtu yule
anayetambulika kisheria. Mwishoni Kamati imetoa mapendekezo
yake.
Kamati inasikitika kwamba kwa uzito wa kazi iliyopewa haikuweza
kuiwasilisha hiyo rasimu na kanuni zake ilipofika tarehe 31 Machi,
2015.
iiv
Rasimu ya Sera ya Mazishi na Kanuni za Mfuko wa Mazishi
ziliwasilishwa na kujadiliwa katika Kamati ya Ajira ya CKD tarehe
22 Desemba 2015. Kamati iliridhishwa na Rasimu ila ilitoa
mapendekezo, ambayo tayari yamefnyiwa kazi katika Rasimu hii
inayowasilishwa kwenye Baraza la CKD.
Mapendekezo hayo yalikuwa:
1. Kwamba wastaafu waliokuwa wanachama wachangiaji nao
wajumuishwe kama wanachama ili waweze kupata mafao. Kwa
sababu ya pendekezo hilo jina la Sera na Mfuko ilibidi liangaliwe
upwa na pendekezo la sasa ni kwamba jina la Sera liwe Sera ya
Mfuko wa Mazishi ya CKD na jina la mfuko liwe Mfuko wa Mazishi
wa CKD.
2. Kiwango cha mafao kiwe walau TShs. 1,000,000/= (Milioni Moja)
Tu.
3. Ulazima wa kuwa na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wanachama
wote uangaliwe upya
iv
VIFUPISHO
Vifupisho vifuatavyo vimetumika katika rasimu hii na kanuni zake na
vinanyumbulishwa kama inavyoonekana hapa chini –
CKD - Chuo Kikuu Dar es Salaam
CoICT - College of Information and Communication Technology
RAAWU - Researchers, Academicians and Allied workers Union
SJMC - School of Journalism and Mass Communications
UDSAS - University of Dar es Salaam Acadmic Staff Assembly
1
SURA YA KWANZA
1.0 HISTORIA FUPI YA SERA YA MFUKO WA MAZISHI
1.1 Maelezo ya awali
Mnamo mwezi Novemba 1993 Baraza la Chuo Kikuu Dar es
Salaam (CKD) liliamua kuwe na Sera ya Mfuko wa Mazishi ya
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Sera ya Mfuko ilianzishwa na
kuanza kutumika mwaka 1994. Kila mfanyakazi wa CKD
(wakiwemo wastaafu wenye mikataba ya ajira) ilibidi ajiunge
na kuchangia kupitia makato ya mishahara ya kila mwezi.
Aidha mwajiri (CKD) alichangia kiasi sawa na cha mfanyakazi
anachochangia.
Sera ya Mfuko wa Mazishi ya CKD ulikuwa ni mwongozo wa
mfumo wa CKD wa kulipia gharama za mazishi kwa
wafanyakazi na familia zao, wazazi au walezi na wanafunzi.
Gharama hizi za mazishi zilikuwa ni pamoja na matayarisho ya
mwili, matanga, rambirambi na usafiri.
Kabla ya kuanzishwa kwa mfuko huu, CKD kilikuwa kinafuata
mwongozo wa “Amri za Serikali na Kanuni za Mashirika ya
Umma” (Public Service Standing Orders). Mwongozo huo
uliainisha wajibu wa mwajiri, taratibu na vitu vya kugharimia
wakati mfanyakazi wake au mtegemezi wa mfanyakazi
anapofariki. Waraka huu pia ulifafanua juu ya wategemezi
wanaopaswa kuhudumiwa na mwajiri wanapofariki.
Mwongozo uliagiza kuwa pale:
Mfanyakazi anapofariki, Mwajiri alitakiwa kugharimia
matayarisho ya mwili, sanduku, sanda, kaburi, shada na
mapambo pamoja na kuusafirisha mwili wa marehemu
2
kutoka sehemu alipofia kwenda mahali yeye alichagua (au
wawikilishi wake walichagua) kuzikiwa.
Huduma za mazishi pia ziliwahusisha familia ya mfanyakazi
hususan Mke au Mume na Watoto na gharama zote zililipwa
kwa kutumia fedha za umma.
Kila Taasisi au Shirika ilitakiwa kuwa na mfumo wake wa
kusaidia gharama wakati wa msiba (kwa maana ya gharama
za matanga na rambirambi).
Katika utekelezaji wa mwongozo huu wa Serikali matatizo
yalijitokeza. Malalamiko mengi yalihusu upendeleo katika
kuhudumia misiba ambapo viwango vya gharama za mazishi
vilivyotolewa kwa wafiwa vilitofautiana. Kutatua matatizo hayo
CKD kilipendekeza kuundwa kwa Sera ya Mazishi ambayo
ilianzishwa mwaka 1993 na kuanza kutumika mwaka 1994. Sera
hii ilipoanza kutumika haikuwa na kanuni.
1.2 Mfuko wa mazishi
Historia ya Mfuko wa Mazishi inaweza kugawanywa katika
sehemu kuu mbili ambazo ni kabla na baada ya kuazishwa kwa
Sera ya Mazishi; yaani kabla na baada ya 1993.
1.2.1 Awamu ya kwanza: kabla ya 1993
Katika awamu hii ya kwanza CKD hakikuwa na Sera ya Mazishi
na pia hakikuwa na Mfuko wa Mazishi. Malipo yote ya gharama
za mazishi ya mfanyakazi na familia yake yalikuwa yakitolewa na
CKD kwa kufuata mwongozo wa Amri za Serikali na Kanuni za
Mashirika ya Umma (Public Service Standing Orders)
ulioainisha aina ya mafao na viwango vya mafao kwa
3
wafanyakazi wa Serikali na Mashirika ya Umma pamoja na
familia zao.
Mwongozo uliainisha yafuatayo kuhusu aina ya mafao au
gharama ambazo mfanyakazi na familia yake walistahili
palipotokea kifo cha mfanyakazi au mwana-familia yake. Malipo
yalitolewa kulipia gharama za kaburi, sanduku au mbao na
mkeka, sanda, chumba cha kuhifadhi maiti, shada la maua
pamoja na usafiri kwa mwili wa marehemu kutoka mahali mauti
yalipomkuta hadi kwenye kituo chake cha kuzikiwa.
Mwongozo haukutaja gharama za usafiri wa mwili wa marehemu
kutoka kituo cha kazi hadi nyumbani kwake wala aina au
kiwango cha msaada uliokuwa ukitolewa kwa familia ya
marehemu.
Kwa kuzingatia mahitaji halisi na uwezo, Mashirika ya Umma na
Taasisi za Serikali zilikuwa zikitoa huduma ya usafiri wa mwili
wa marehemu hadi nyumbani kwake kwa kutumia fedha za
umma.
Mwongozo haukuwahusisha wazazi (au walezi) wala wanafunzi.
Kwa kutoweka wazi viwango vya mafao stahili kwa mfanyakazi
na familia yake, ilipelekea kutolewa kwa malipo tofauti ya
kulipia gharama za mazishi, usafiri na rambirambi.
Kutofautiana kwa malipo kulizaa malalamiko halali kutoka kwa
wafanyakazi na vyama vya wafanyakazi. CKD hakikuwa na budi
kutafuta ufumbuzi wa kudumu.
1.2.2 Awamu ya pili: Baada ya 1993
Baada ya malalamiko ya wafanyakazi na vyama vya wafanyakazi
kuwa mengi, Uongozi wa CKD uliainisha changamoto zote
zilizoukabili, malalamiko ya wafanyakazi na mapendekezo na
4
kuliomba Baraza la CKD ushauri. Changamoto zilizoainishwa
zilionyesha kuongezeka maradufu kwa malipo ya gharama za
mazishi yaliyokuwa yakilipwa kutokana na vifo vingi vya
wafanyakazi na wanafamilia zao, ufinyu wa bajeti na kukosekana
kwa viwango halisi.
Baada ya kuzingatia changamoto hizo Baraza la CKD, katika
kikao chake cha 50 kilichofanyika tarehe 2 Desemba 1982, liliipa
mamlaka ya Uongozi wa CKD kutekeleza masuala yote
yanayohusu ulipaji wa gharama za mazishi kwa wafanyakazi na
familia zao. CKD kikapendekeza aina mbili za utekelezaji wa
malipo kama ifuatavyo:
(i) Kwenye kifo cha Mfanyakazi Chuo kitoe sanda, jeneza
au ubao na mkeka, gharama za kuhifadhi maiti, kaburi,
shada, usafiri hapa Dar es Salaam, chakula wakati wa
matanga hapa Dar es Salaam na usafiri hadi alikozaliwa
marehemu.
Chuo pia kilipendekeza usafiri na fedha za kujikimu kwa
wafanyakazi wawili - mmoja kutoka Utawala na mwingine
kutoka Chama cha Wafanyakazi kusindikiza mwili wa
marehemu na kuwakilisha CKD kwenye mazishi.
(ii) Kwenye kifo cha mke/mume, mtoto au mzazi wa
mfanyakazi Chuo kitoe usafiri wa hapa Dar es Salaam na
gari kwa mfanyakazi aliyefiwa isipokuwa alipie gharama za
mafuta ya gari na posho ya dereva.
Ili kutatua matatizo mengi yaliyokuwa bado yanalalamikiwa,
CKD kilipendekeza kuanzishwa kwa Sera ya Mazishi ambayo
Baraza la CKD iliipitisha mwezi Novemba 1993 na ilianza
kutumika rasmi mwezi Novemba 1994. Sera hii ilielekeza
kwamba kila mfanyakazi wa CKD alipaswa kuchangia Shs.
5
2,400/= kama kiingilio na baada ya hapo Shs. 200/= kila mwezi
kwa muda wote wa uanachama wa mfanyakazi. CKD kilichangia
Shs. 14,000,000/= kila mwaka. Wanafunzi hawakuhusishwa
moja kwa moja na Sera hii hapo awali. Jukumu la huduma za
wanafunzi waliachiwa waajiri au wafadhili wao.
Pale ambapo mfanyakazi au mtegemezi wa mfanyakazi alifariki
mafao yaliyotolewa yalikuwa kama yalivyoonyeshwa kwenye
jedwali hapo chini:
Jedwali Namba 1: Mafano yaliyokuwa yakitolewa
Tabaka la
Uanachama
Kundi la Mafao Kiwango Jumla
Mfanyakazi * Gharama za Mazishi 150,000
235,000 Rambirambi 35,000
Gharama za Matanga 50,000
Mke au
Mume
* Gharama za Mazishi 150,000
180,000
Rambirambi 30,000
Gharama za Matanga --
Mtoto * Gharama za Mazishi 150,000
170,000 Rambirambi 20,000
Gharama za Matanga --
Mzazi * Gharama za Mazishi 150,000 150,000
*Gharama za mazishi zilijumuisha gharama za Kuhifadhi
maiti, Sanda, Jeneza au Ubao na Mkeka, Kaburi na Shada.
Utekelezaji wa Sera ya Mazishi na uendeshaji wa Mfuko wake
ulipata changamoto nyingi kwa vipindi tofauti. Uongozi wa CKD
haukuwa na budi isipokuwa kutafuta ufumbuzi wa changamoto
6
zilizojitokeza hivyo ililazimika kuunda Kamati ya Sera ya
Mazishi ili kusimamia masuala ya mfuko. Kamati hii ilikuwa ya
watu sita (6) na Wajumbe wake walikuwa:-
i) Katibu wa Baraza la Chuo - Mwenyekiti
ii) Mwakilishi wa UDASA - Mjumbe
iii) Mwakilishi wa RAAWU - Mjumbe
iv) Afisa Bima Mkuu - Mjumbe
v) Msarifu - Mjumbe
vi) Afisa Tawala Mwandamizi - Mjumbe
Kamati hii ilipewa mamlaka ya kushughulikia masuala yote
yakiwemo yale yaliyokuwa na utata katika utekelezaji wa sera
nzima ya mazishi. Kamati hii pia ilipendekeza kwamba viwango
vya gharama viainishwe ili kila mfanyakazi apate huduma sawa
na mwingine. Ndipo kamati ndogo ya Sera ya Mfuko wa Mazishi
iliundwa ambayo ilishughulikia mambo yafuatayo:
i) Kuangalia gharama halisi ya sanduku, sanda, maua,
kaburi, huduma za matanga, usafiri n.k.
ii) Kulinganisha matukio ya vifo kati ya wakati wa kuanzisha
mfuko na sasa (2002).
iii) Kushauri juu ya viwango vya sasa vya michango ya
wanachama kulingana na gharama halisi.
iv) Kushauri juu ya uanachama wa wanafunzi ambao
hawachangii mfuko huo.
v) Kushauri jinsi ya kuboresha uendeshaji wa mfuko
wenyewe.
vi) Kushauri juu ya swala lolote linaloweza kuboresha mfuko
huo.
7
Kamati tajwa hapo juu ilitoa ripoti yake ambayo ilijadiliwa na
vyombo husika vya jumuiya ya CKD. Mapendekezo yote ya
Kamati hiyo yalikubalika na viwango vipya vya mafao na ada
vilipitishwa na vilianza kutumika mwaka 2005/06. Kutokana na
mapendekezo hayo akaunti ya mfuko ilifunguliwa na fedha
zilizokuwa zimechangwa kabla zilihamishiwa kwenye hii
akaunti.
Mfuko huu uliendelea kufanyiwa maboresho ambayo yalitokana
na tathmini zilizokuwa zikifanyika. Kwa mfano viwango vipya
vifuatavyo vya mafao vilipendekezwa na kupitishwa:
Jedwali Namba 2: Viwango vipya vya Mafao Viwango Vipya vya
mafao: Tabaka
Kundi la
Mafao
Kiwango Jumla
Mfanyakazi Gharama za
Mazishi
200,000/- 500,000/- +
Gharama halisi za
usafiri Rambirambi kwa familia 100,000/-
Gharama za Matanga 200,000/-
* Gharama za Usafiri * 400,000/-
Mke au
Mume
Gharama za
Mazishi
200,000/- 500,000/- +
Gharama halisi za
usafiri Rambirambi kwa familia 100,000/-
Gharama za Matanga 200,000/-
* Gharama za Usafiri * 400,000/-
Mtoto Gharama za
Mazishi
200,000/- 500,000/- +
Gharama halisi za
usafiri Rambirambi kwa familia 100,000/-
Gharama za Matanga 200,000/-
* Gharama za Usafiri * 400,000/-
Mzazi Gharama za
Mazishi
200,000/- 500,000/-
HAKUNA
huduma ya Rambirambi kwa familia 100,000/-
8
Gharama za Matanga 200,000/- usafiri
* Gharama za Usafiri HAKUNA
Mwanafunzi Gharama za
Mazishi
200,000/- 300,000/- +
Gharama halisi za
usafiri Rambirambi kwa familia 100,000/-
Gharama za Matanga HAZILIPIWI
* Gharama za Usafiri * 400,000/-
Mfuko huu ulisaidia sana kuondoa malalamiko mengi
yaliyokuwepo hapo awali. Mfuko ulikuwa ni chombo ambacho
kiliweza kutoa mafao ya haraka kwa wafiwa na kuhakikisha
kwamba kila mfiwa alipata haki stahili bila ya ubaguzi wowote
na kwa haraka. Pia gharama za uendeshaji wa Mfuko huu
zinaonekana kuwa ni ndogo sana ukilinganisha na faida
iliyopatikana kwa kuwa na utaratibu huu wa mfuko.
1.3 Siha ya mfuko
Tangu Kamati ya Sera ya Mazishi ya CKD ikabidhiwe
majukumu ya kuongoza, Mfuko uliweza kukua kutoka limbikizo
la takriban shilingi milioni 79.0 mwaka 2004/05 hadi kufikia
shilingi milioni 584.7 mwaka 2011/12. Hii ilikuwa ni hatua
kubwa.
1.4 Hali ilivyo hivi sasa
Viwango vipya vilivyopitishwa na Baraza la CKD vya mwaka
2004 vilianza kutumika 2005/06 kama inavyoonekana hapo
juu. Viwango hivyo vinaendelea kulipwa hadi hivi sasa
2014/2015. (Rejea jedwali Namba 2, hapo juu).
9
Sasa hivi kuna changamoto kadhaa zinazougusa mfuko wa
mazishi, zikiwemo:
Vifo vingi kutokea;
Gharama za mazishi kuendelea kupanda; na
Gharama zinazolipwa kuonekana kuwa ndogo.
Kwa sababu ya changamoto hizi Uongozi wa CKD uliteua
Kamati nyingine iliyopewa jukumu la kufanya tathmini ya
mfuko na kupendekeza viwango ambavyo vingetumika na
kuachana na hivi vinavyotumika sasa.
Hadidu za rejea za Kamati zilikuwa ni pamoja na kuangalia:
a) Gharama halisi za mazishi anayopewa mwanachama
akipatwa na msiba na kushauri juu ya viwango vya malipo
vya sasa kama vinakidhi;
b) Huduma ya usafiri kwa mazishi yanayofanyika Dar es
Salaam;
c) Kupitia viwango vya michango ya sasa ya
wanachama (wafanyakazi na wanafunzi); na
d) Namna ya kuboresha uendeshwaji wa kazi za Kamati.
Kamati iliyoteuliwa ilifanya kazi yake na kuwasilisha ripoti kwa
Uongozi wa Chuo kwa ajili ya kupitishwa kwa viwango vipya
vilivyopendekezwa vianze kutumika 2014. Wakati huo huo
kulizuka hoja kuhusu wajibu wa CKD kumzika mfanyakazi wake
kama ilivyoainishwa katika sheria.
Baraza la CKD, katika kikao chake cha Januari, 2015, baada ya
kupitia sheria husika, yaani “Public Service Standing Orders” ya
2009, kifungu Q. 7 na “University of Dar es salaam Staff
Regulations” kifungu namba 70, liliona ni wajibu wa kisheria
kwa CKD kubeba majukumu yake ya mazishi ya wafanyakazi,
10
wenzi wao na watoto hivyo kukiagiza Chuo kutekeleza
majukumu hayo ya kisheria.
Baada ya maagizo hayo ya Baraza la CKD, uongozi wa Chuo kwa
barua ya tarehe 10/3/2015 uliteuwa kamati mpya kuangalia kwa
upya mfuko wa sera ya mazishi. Kamati hiyo ilipewa hadidu za
rejea zifuatazo:
Kupitia upya Rasimu ya sera ya Mazishi ya 2014
iliyowasilishwa kwa Naibu Mkuu wa Chuo Utawala pamoja
na Kanuni zake ili kupendekeza malipo ya ziada ambayo
mfiwa atapewa kutoka katika mfuko wa Chuo wa sera ya
Mazishi.
Kupendekeza jambo jingine lolote ambalo kamati ingeona
linafaa kuhusishwa, kuingizwa au kufanyiwa kazi ili
kuboresha Sera ya Mazishi kwa maslahi ya Wafanyakazi wa
Chuo kwa ujumla.
Kamati ilizifanyia kazi hadidu za rejea baada ya kujiridhisha
kwamba ilitakiwa kufanya yafuatayo:
a) Kupitia upya Rasimu ya Sera ya Mazishi ya Mwaka 2014
kwa mtizamo kwamba ingewahusu wafanyakazi tu wa
CKD;
b) Kuangalia maeneo ambayo hayataguswa na majukumu
ya kisheria ya Chuo Kikuu;
c) Kuangalia mambo mengineyo ambayo itaona yanafaa
kwa maslahi ya wafanyakazi na Chuo kwa ujumla.
11
SURA YA PILI
2.0 UMUHIMU WA SERA, DIRA, DHIMA NA MALENGO YA
SERA
2.1 Umuhimu wa Sera ya Mfuko wa Mazishi ya Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam
Umuhimu wa sera yoyote ile iwe ya Elimu au Afya ni kwamba
inaonyesha mfumo/mhimili au njia (framework) inayoeleweka
kwa walengwa wa sera hiyo ya nini kifanyike linapotokea jambo
fulani.
Sera ya Mfuko wa Mazishi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni
muhimu kwa sababu zifuatazo:
(a) kumhudumia mwanachama, pale ambapo majukumu ya
CKD kisheria yanaishia.
(b) kumhudumia mwanachama pale ambapo CKD hakihusiki
2.2 Dira ya Sera ya Mfuko wa Mazishi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
2.2.1 Dira (vision) ni maono au uwezo wa kuona mbali/mbele. Dira ya
Sera ya mfuko wa Mazishi ya CKD ni kuwa “Mfuko unaotoa
rambirambi bora kuliko mfuko wowote wa mazishi ulio kwenye
Tasisi na Mashirika ya Umma Tanzania”.
2.2.2 Dhima (mission) ni jukumu au wajibu au daiwo. Dhima ya Sera ya
Mfuko wa Mazishi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni kuweza
kutoa rambirambi inayokidhi gharama halisi za mazishi kwa
wakati husika pindi mfanyakazi anapofariki au mwenza wake au
mtoto/watoto wake (biological child/children) au mzazi wake
(biological parents) au mlezi aliyemlea akiwa chini ya umri wa
12
miaka 18 au mstaafu ambaye alikuwa mwanachama kabla ya
kustaafu.
2.3 Malengo ya Sera ya Mfuko wa Mazishi ya Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam
2.3.1 Malengo (objectives) ni madhumuni, au makusudio. Malengo ya
Sera ya Mfuko wa Mazishi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni:-
a) Kuunda Mfuko wa Mazishi wa CKD ili kujazia pale ambapo
majukumu ya kisheria ya Mwajiri, CKD, yanapoishia katika
mazishi ya mwanachama wa Mfuko na wale wamhusuo chini
ya Kanuni za Mfuko.
b) Kuwafanya wafanyakazi wote wachangiaji katika Mfuko
kuwa wanachama.
c) Kumhudumia mwanachama pale ambapo majukumu ya CKD
kisheria yanapoishia, kwa mfano kugharimia matanga na
rambirambi.
d) Kumhudumia mwanachama pale ambapo CKD hakihusiki
kabisa kisheria, kwa mfano kugharimia mazishi ya mzazi au
mlezi wa mfanyakazi mwanachama, kama ilivyoainishwa
katika Kanuni za Mfuko.
e) Kuhakikisha wanachama wote wanatimiza wajibu wao,
isipokuwa kwa mstaafu aliyekuwa mwanachama kabla ya
kustaafu, na kupata stahiki zao.
13
SURA YA TATU
3.0 MALENGO NA MATAMKO YA KISERA
3.1 Lengo namba 1
Kuunda Mfuko wa Mazishi wa CKD ili kujazia pale ambapo
majukumu ya kisheria ya Mwajiri, CKD, yanapoishia katika
mazishi ya mfanyakazi wake au wale wanaohusika na mfanyakazi
wake kisheria.
Maelezo
CKD kinayo majukumu ya kisheria ya kumzika mfanyakazi wake,
mume au mke wa mfanyakazi na watoto wa mfanyakazi. Jukumu
hili limeainishwa katika “Public Service Standing Orders, 2009”,
kanuni Q.7 na kunukuliwa katika kifungu 70 cha “University of
Dar es Salaam Staff Regulations, 2013”. Katika hayo majukumu
ya kisheria CKD hakihusiki na maeneo kadhaa ambayo Mfuko wa
Mazishi utahusika nayo kulingana na Kiambata B.
Tamko namba 1
Wafanyakazi wa CKD, kwa baraka za uongozi wa CKD, wanaunda
Sera hii ya Mfuko wa Mazishi na kuanzisha Mfuko wa Mazishi ili:
a) kujazia pale ambapo majukumu ya kisheria ya CKD
yanaishia; maeneo ya kujazia ni kama rambirambi na
gharama za matanga (chakula, viti, mahema na mapambo)
b) kugharimia pale ambapo CKD hakiwajibiki; kwa mfano
mazishi ya mzazi au mlezi wa mfanyakazi/mwanachama au
mstaafu ambaye alikuwa mwanachama mchangiaji kabla ya
kustaafu.
14
3.2 Lengo namba 2
Kuwafanya wafanyakazi wote wachangiaji katika Mfuko wa
Mazishi wa CKD [Kampasi ya Mlimani ya Mwalimu J.K. Nyerere,
Shule Kuu ya Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC) na
Kampasi ya Infomatiki na Teknolojia ya Mawasiliano (CoICT)]
kuwa wanachama wa Mfuko.
Maelezo
Mfuko wa Mazishi wa Wafanyakazi wa CKD utakuwa ni wa
wafanyakazi wote wachangiaji wa CKD, Kampasi ya Mlimani ya
Mwalimu J.K. Nyerere, Shule Kuu ya Habari na Mawasiliano ya
Umma (SJMC) na Kampasi ya Infomatiki na Teknolojia ya
Mawasiliano (CoICT). Nia ya Mfuko ni kuwanufaisha
wafanyakazi kwa kutoa mafao stahiki kwa mfanyakazi au
wategemezi wake kama Kiambata B kinavyooshesha. Mfuko pia
utawahudumia wastaafu ilimradi walikuwa wanachama
wachangiaji kabla ya kustaafu.
Tamko namba 2
Wafanyakazi wote wachangiaji wa CKD, Kampasi ya Mlimani ya
Mwalimu J.K. Nyerere, Shule Kuu ya Habari na Mawasiliano ya
Umma (SJMC) na Kampasi ya Infomatiki na Teknolojia ya
Mawasiliano (CoICT) watakuwa wanachama wa Mfuko wa
Mazishi.
Mfanyakazi mwanachama asiyelipwa kupitia “payroll” ya
“Lawson” ya CKD (kwa mfano yule ambaye yuko katika likizo bila
malipo, n.k.) atalazimika kuhakikisha kuwa anachangia kila
mwezi ili kuendelea kuwa mwanachama wa mfuko.
15
Mstaafu aliyekuwa mchangiaji kabla ya kustaafu hataendelea
kuchangia baada ya kustaafu, lakini atastahili kupewa mafao;
hata hivyo mafao hayo hayatahusu mke au mume au watoto au
mlezi wa mstaafu huyo.
3.3 Lengo namba 3
Kumhudumia mwanachama pale ambapo wajibu wa CKD,
kumzika mfanyakazi wake, mume au mke au watoto, unapoishia
kisheria.
Maelezo
Sheria imeainisha wazi majukumu ya CKD katika kumzika
mfanyakazi wake au mke au mume wa mfanyakazi wake au
watoto wa mfanyakazi wake. CKD hakiwajibiki kutoa rambirambi
wala kugharimia matanga (chakula, viti, mahema au mapambo).
Mfuko huu utagharimia matanga na kutoa rambirambi.
Tamko Namba 3
Mfuko utamhudumia mwanachama pale ambapo wajibu wa CKD,
kumzika mfanyakazi wake, mume au mke au watoto, unapoishia
kisheria.
3.4 Lengo Namba 4
Kumhudumia mwanachama pale ambapo CKD hakihusiki
kisheria.
Maelezo
Sheria inatamka wazi kwamba wajibu wa CKD ni kumzika
mfanyakazi wake au mke au mume wa mfanyakazi na watoto wa
mfanyakazi. Wazazi au walezi hawatambuliwi na sheria husika.
16
Ukweli ni kwamba mwanachama akifiwa na mzazi au mlezi,
kwake hilo ni pigo kubwa na huwa anahitaji sana msaada na
faraja. Mfuko utamhudumia mwanachama anayefiwa na mzazi
au mlezi kulingana na gharama halisi za mazishi kwa wakati
husika mradi mfuko utakuwa na uwezo wa kufanya hivyo.
Tamko namba 4
Mfuko utamhudumia mwanachama aliyefiwa na mzazi au mlezi
kama ilivyoainishwa katika Kanuni za Mfuko. Hata hivyo
mwanachama ambaye ni mstaafu aliyekuwa akichangia kabla ya
kustaafu hatapata mafao kwa kufiwa na mke au mume, mtoto au
mlezi.
3.5 Lengo namba 5
Kuhakikisha wafanyakazi wote wanatimizi wajibu wao na kupewa
stahiki zao
Maelezo
Wafanyakazi wote wa CKD, Kampasi ya Mlimani ya Mwalimu
J.K. Nyerere, Shule Kuu ya Habari na Mawasiliano ya Umma
(SJMC) na Kampasi ya Infomatiki na Teknolojia ya Mawasiliano
(CoICT) wakiwa wanachama wa Mfuko wa Mazishi, watakuwa na
wajibu na stahiki zao.
Wajibu wa wanachama utakuwa ni pamoja na:
a) Kujaza fomu za uanachama (Kiambata A)
b) Isipokuwa kwa mwanachama mstaafu aliyechangia kabla
ya kustaafu, kulipa kiingilio kilichokubaliwa na michango
ya kila mwezi kama ilivyoainishwa kwa kukatwa mshahara.
c) Kutoa taarifa sahihi katika ujazaji wa fomu ya usajili.
17
d) Kutoa taarifa na vielelezo sahihi kuhusu kifo.
Stahiki za mwanachama zitakuwa ni pamoja na:
a) Kupewa kijazilisho stahiki pale ambapo majukumu ya
kisheria ya CKD yanapoishia
b) Kumhudumia mwanachama pale ambapo CKD hakihusiki
c) Kupewa nakala ya ripoti ya utekelezaji wa Mfuko wa
Mazishi.
d) Kuhudhuria na kushiriki katika Mikutano ya Wanachama
wote.
Tamko namba 5
5.1 Kila mwanachama wa Mfuko wa Mazishi atatekeleza wajibu
wake na kupewa stahiki zake kama ilivyoainishwa katika Sera
hii na Kanuni zake.
5.2 Stahiki za mwanachama ambaye amefariki dunia au amefiwa
na mume/mke au mtoto zitakuwa ni kama zinavyoainishwa
katika Kanuni za Mfuko wa Mazishi na Kiambata B.
5.3 Stahiki za mwanachama ambaye amefiwa na mzazi au mlezi
zitakuwa ni kama zinavyoainishwa katika Kanuni za Mfuko wa
Mazishi na Kiambata B.
5.4 Stahiki za mwanachama mstaafu aliyechangia kabla ya
kustaafu zitakuwa kama zilivyoainishwa katika Sera hii na
Kanuni zake.
18
SURA YA NNE
4.0 MUUNDO WA KISHERIA NA KIUONGOZI WA SERA YA MFUKO
WA MAZISHI YA WAFANYAKAZI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES
SALAAM
4.1 Muundo wa kisheria
Sera ya Mfuko wa Mazishi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(CKD) imeanzishwa kwa mujibu wa Mwongozo wa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Public Service Standing
Orders, 2009), Kanuni Q. 7 (3), inayotoa uhuru kwa Taasisi na
Mashirika ya umma kuanzisha mfumo wake wa ndani kusaidia
gharama za msiba za mfanyakazi wake au mtegemezi
anapofariki. Mfuko huu pia umeanzishwa kwa mujibu wa Sheria
ya Ajira ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ya mwaka 2013
(University of Dar es Salaam Staff Regulations, 2013) kifungu
cha 70 (3).
Baada ya CKD kuamua kuchukua majukumu yake ya kisheria
pale ambapo mfanyakazi wake au mtu ambaye ameainishwa
katika sheria kufariki dunia, Sera ya Mfuko wa Mazishi ya CKD
ilibidi irekebishwe na kuwa Sera ya Mfuko wa Mazishi ya
Wafanyakazi wa CKD na wategemezi wao tu.
4.2 Muundo wa kiuongozi
Mfuko wa Mazishi ya Wafanyakazi wa CKD
Utakuwa ni mfuko unaojitegemea (self-accounting unit)
katika CKD.
Utaongozwa na Kamati ambayo itakuwa na wajumbe
wafuatao ambao watateuliwa na Naibu Makamu Mkuu wa
19
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Utawala. Baadhi ya
Wajumbe watateuliwa kwa nyadhifa zao.
(i) Mwenyekiti atakayeteuliwa na Naibu Makamu
Mkuu wa CKD, Utawala
(ii) Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala
(iii) Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya, CKD
(iv) Mawakilishi wawili kutoka chama cha Wafanyakazi,
CKD
(v) Mkurugenzi Huduma za Jamii
(vi) Naibu Msarifu
Wajumbe watamchagua Katibu wa Mfuko kutoka miongoni
mwao.
Wajumbe wa Kamati hii (isipokuwa wale walioteuliwa kwa
nyadhifa zao, ambao ni Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala,
Mganga Mkuu na Naibu Msarifu) wataongoza mfuko kwa muda
wa miaka mitatu na wanaweza kurudia kwa awamu nyingine
mara moja tu.
Ofisi ya Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala ndiyo
itakayohusika na shughuli za siku hadi siku zihusuzo Mfuko wa
Mazishi.
Kutakuwa na Mkutano Mkuu moja wa mwaka wa Wanachama
wote wa Mfuko ambao utagharamiwa na Mfuko.
Mfuko utakuwa unatoa taarifa zake za utendaji zikiwemo za fedha
katika vikao vya Baraza la Wafanyakazi na Kamati ya Mipango na
Fedha ya CKD kila baada ya miezi mitatu.
20
SURA YA TANO
5.0 HITIMISHO NA MAPENDEKEZO
5.1 Hitimisho
Kamati inawasilisha rasimu ya Sera ya Mazishi na Kanuni za
Mfuko wa Mazishi kwa hatua zinazostahili.
Kamati imependekeza jina la sera liwe ni Sera ya Mfuko wa
Mazishi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa sababu zifuatazo:
Wanufaika na Mfuko wa Mazishi si tu wafanyakazi
wanachama, bali pia wastaafu ambao walikuwa
wachangiaji wa Mfuko kabla ya kustaafu.
CKD, kama mtu kisheria, kina wajibu wa kuwazika
wafanyakazi wake, wake au waume wa wafanyakazi au
watoto wa wafanyakazi.
CKD kinahusika na Sera na Mfuko huu kwa sababu wadau
wa Sera na Mfuko ni wafanyakazi wake wote. Na kwa
mantiki hiyo CKD kinaombwa kikubali kuchukua
majukumu yanayoainishwa katika Sera hii ya Mazishi na
Kanuni za Mfuko.
5.2 Mapendekezo
Katika kuandaa Sera ya Mazishi na kuunda Mfuko wa Mazishi
Kamati inatoa mapendekezo yafuatayo:
Mafao ya wanachama yawe TSh. 1,000,000/= (Milioni Moja) tu;
ikiwa anafariki mfanyakazi, mke au mume wa mfanyakazi, mtoto
wa mfanyakazi au mzazi au mlezi wa mfanyakazi, au mstaafu
aliyekuwa mwanachama mchangiaji kabla ya kustaafu, kama
Jedwali la mchanganuo wa mafao hapo chini linavyojieleza
(Jedwali namba 3).
21
Mchanganuo wa mafao kama unavyooneshwa kwenye jedwali
namba 3 umefanywa kwa kuzingatia kwamba sera hii inawahusu
wafanyakazi tu. Kwa mantiki hiyo wanafunzi hawakuhusishwa.
Vilevile mchangunuo huu umetumia takwimu za miaka mitatu.
Kwa mfano wastani wa idadi ya wafanyakazi na vifo kwa mwaka
ni 2,249 na 110, kwa mtiririko huo.
Jedwali namba 3.1: Mchanganuo wa Mafao ya Mazishi kama Mchango
wa Mwanachama utakuwa Tshs. 3,000/=
Maelezo
Wastani
wa vifo
kwa
mwaka scenario 1 scenario 2 scenario 3 scenario 4
Kiasi cha kulipwa
mfiwa
500,000 800,000 1,000,000 1,500,000
Mapato kwa mwaka kwa
wafanyakazi
2, 249
80,964,000
80,964,000 80,964,000 80,964,000
Gharama za
nyongeza za msiba kwa
mwaka 110
55,000,000
88,000,000 110,000,000 165,000,000
Gharama za Benki 531,500 531,500 531,500 531,500
Gharama za
mikutano ya Kamati n.k
2,600,000 2,600,000 2,600,000 2,600,000
Jumla ndogo
matumizi
58,131,500 91,131,500 113,131,500 168,131,500
Ongezeko/ pungufu
kwa mwaka
22,832,500 - 10,167,500 -32,167,500 -87,167,500
22
Jedwali Namba 3.2: Mchanganuo wa Mafao ya Mazishi kama Mchango
wa Mwanachama utakuwa Tshs. 4,000/=
Maelezo
Wastani
wa Vifo
kwa
mwaka scenario 1 scenario 2 scenario 3 scenario 4
Kiasi cha kulipwa mfiwa
500,000
800,000 1,000,000 1,500,000
Mapato kwa mwaka kwa
wafanyakazi
2, 249
107,952,000
107,952,000
107,952,000
107,952,000
Gharama za
nyongeza za msiba kwa
mwaka 110
55,000,000
88,000,000 110,000,000 165,000,000
Gharama za Benki 531,500 531,500 531,500 531,500
Gharama za
ikutano ya Kamati n.k
2,600,000 2,600,000 2,600,000 2,600,000
Jumla ndogo
matumizi
58,131,500
91,131,500 113,131,500 168,131,500
Ongezeko/ pungufu
kwa mwaka
49,820,500 16,820,500 -5,179,500 -60,179,500
23
Jedwali Namba 3.3: Mchanganuo wa Mfao ya Mazishi kama mchango wa
Mwanachama utakuwa Tshs. 5,000/=
Maelezo
Wastani
wa Vifo
kwa
mwaka scenario 1 scenario 2 scenario 3 scenario 4
Kiasi cha kulipwa mfiwa
500,000
800,000 1,000,000 1,500,000
Mapato kwa mwaka kwa
wafanyakazi
2, 249
134,940,000 134,940,000 134,940,000 134,940,000
Gharama za
nyongeza za msiba kwa
mwaka 110
55,000,000
88,000,000 110,000,000 165,000,000
Gharama za Benki 531,500 531,500 531,500 531,500
Gharama za
mikutano ya Kamati n.k
2,600,000 2,600,000 2,600,000 2,600,000
Jumla ndogo
matumizi
58,131,500
91,131,500 113,131,500 168,131,500
Ongezeko/ pungufu
kwa mwaka 76,808,500 43,808,500 21,808,500 -33,191,500
24
Jedwali Namba 3.4: Ongezeko/pungufu kwa mwaka ikizingatia mchango
wa Mwanachama na kiasi cha malipo kwa Mfiwa
Jedwali namba 3.4 linaonesha kwa ujumla ongezeko au pungufu kwa
mwaka kwa viwango mbalimbali vya mchango wa mwanachama na kiasi
cha malipo kwa mfiwa. Mchanganuo huo unaonesha kuwa kiwango cha
sasa cha uchangiaji wa Tsh. 3,000 hakitatosheleza kama tutaamua
kuongeza kiasi cha kulipwa mfiwa. Aidha, mchango wa mwanachama
ukiongezeka hadi Tsh. 4,000 mfiwa ataweza kulipwa hadi Tsh. 800,000
bila mfuko kuyumba. Hata hivyo maboresho zaidi ya malipo ya mfiwa
yanawezekena kuongezeka kufikia Tsh. 1,000,000 ikiwa mchango wa
mwanachama utakuwa Tsh. 5,000.
Mchango wa mwanachama (Tsh)
Kiasi cha malipo
kwa mfiwa (Tsh) 3000 4000 5000
500,000 22,832,500 49,820,500 76,808,500
800,000 -10,167,500 16,820,500 43,808,500
1,000,000 -32,167,500 -5,179,500 21,808,500
1,500,000 -87,167,500 -60,179,500 -33,191,500
25
KANUNI ZA MFUKO WA MAZISHI WA CHUO KIKUU CHA
DAR ES SALAAM
1.0 UTANGULIZI
1.1 Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni Kuu za
kuendesha/kufafanua shughuli za Mfuko wa Mazishi wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam za mwaka 2015 na zitatumika kutekeleza
yale yote yanayotamkwa na Sera ya Mfuko kuhusu uendeshaji wa
shughuli na majukumu pamoja na mahitaji ya Wanachama.
1.2 Kanuni hizi zinatoa tafsiri mahsusi ya Sera ya Mfuko wa Mazishi ya
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kutekeleza matakwa ya
Mwongozo wa Utumishi kwa Mashirika ya Umma ya mwaka 2009
sehemu ya Q.7 (3) na Sheria ya Ajira ya Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam sehemu 70 (3) ya mwaka 2013.
1.3 Kanuni hizi ni sehemu ya Sera ya Mfuko wa Mazishi na zitasomwa
sambamba na Sera hiyo.
1.4 Kanuni hizi zitaanza kutumika baada ya kuidhinishwa na vyombo
husika vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
1.5 Mwenye mamlaka ya kuzitunga na kuzirekebisha kanuni hizi ni
Wanachama wenyewe kupitia Baraza la Wafanyakazi na kuridhiwa
na mkutano wao Mkuu wa Mwaka.
2. UFAFANUZI
Katika Kanuni hizi isipokuwa pale ambapo imefafanuliwa
vinginevyo “maneno”au “misemo” ifuatayo itakuwa na maana
iliyotolewa ndani ya Sera:
CKD – ni kifupisho cha neno “Chuo Kikuu cha Dar es Salaam”
Mfanyakazi – ina maana ya Mwajiriwa au mtu yeyote aliyeingia
katika Mkataba/Makubaliano na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(mwajiri) kwa kulipwa mshahara.
26
Mwanachama – ina maana ya
(i) Mwanachama wa Mfuko wa Mazishi ambaye ni Mfanyakazi
yeyote aliye katika ajira ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na
ambaye ametoa kiingilio na kutoa michango ya kila mwezi
kwa kukatwa mshahara,
(ii) Mstaafu aliyekuwa mwanachama kabla ya kustaafu.
Baraza la Wafanyakazi – ina maana ya chombo
kinachowashirikisha Wafanyakazi katika uongozi wa pamoja
mahali pa kazi.
Mfuko – ina maana ya “Mfuko wa Mazishi wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam.”
Serikali – ina maana ya "Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania" au Chombo chenye madaraka ya utawala kwa eneo
husika
Mwenyekiti – ina maana Mwenyekiti wa Kamati ya Mfuko wa
Mazishi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye ndiye pia
msemaji mkuu wa Mfuko na ambaye pia atakuwa mwenyekiti
wa Mkutano Mkuu wa wanachama wote.
Mwanachama mfanyakazi asiyelipwa mshahara kupitia
“payroll” ya “Lawson” ya Chuo - ni yule ambaye yuko katika
likizo bila malipo, au ameazimwa Serikalini, n.k.
3. JINA LA MFUKO
Mfuko huu utaitwa Mfuko wa Mazishi wa Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam
27
4. MADHUMUNI MAKUU YA MFUKO
Madhumuni Makuu ya Mfuko yatakuwa yafuatayo:
4.1 Kujazia pale ambapo majukumu ya kisheria ya CKD kumzika
mfanyakazi wake, mke au mume wa mfanyakazi au watoto wa
mfanyakazi, yanaishia au kugharimia pale ambapo CKD
hakiwajibiki.
4.2 Kuwafanya wafanyakazi wote wachangiaji katika Mfuko wa
CKD (Kampasi ya Mlimani ya Mwalimu J.K. Nyerere, Shule
Kuu ya Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC) na Kampasi
ya Infomatiki na Teknolojia ya Mawasiliano (CoICT) kuwa
wanachama wa Mfuko.
4.3 Kumhudumia mwanachama pale ambapo wajibu wa CKD,
kumzika mfanyakazi wake, mume au mke au watoto, kisheria
unapoishia.
4.4 Kumhudumia mwanachama pale ambapo CKD hakihusiki
kisheria.
4.5 Kumhudumia mstaafu aliyekuwa mwanachama mchangiaji
kabla ya kustaafu kama inavyoainishwa katika Sera ya Mfuko
wa Mazishi ya CKD.
4.6 Kuhakikisha wafanyakazi wote wanatimizi wajibu wao na
kupewa stahiki zao
5.0 UANACHAMA
5.1 Uanachama ni wa lazima kwa kila Mfanyakazi wa Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam Kampasi ya Mlimani ya Mwalimu J.K.
Nyerere, Shule Kuu ya Habari na Mawasiliano ya Umma
(SJMC) na Kampasi ya Infomatiki na Teknolojia ya
Mawasiliano (CoICT). Kila mwanachama mfanyakazi
28
atalazimika kujaza fomu maalum (“Kiambatisho A”). Taarifa
zote ziwe za kweli na ziambatane na nakala za vithibitisho
halali ambavyo ni cheti cha ndoa, vyeti vya kuzaliwa vya
watoto, hati ya kutohoa/kuasili (adoption certificate), n.k.
5.2 Taarifa zote za wanachama zitawekwa kwenye “data base”
ambayo itakuwa inafanyiwa marekebisho ya mara kwa mara
anapoajiriwa mfanyakazi mpya, kunapotokea msiba au
anapozaliwa mtegemezi mpya. Taarifa hizi ndizo
zitakazotumika kuhakiki taarifa za mfanyakazi na wategemezi
wake.
5.3 Mstaafu ambaye alikuwa mwanachama mchangiaji
atalazimika kujaza fomu maalum kama ilivyoainishwa katika
kifungu 5.1.
6.0 FEDHA ZA MFUKO
Fedha za Mfuko zitakusanywa kwa madhumuni ya
kuuwezesha Mfuko kufanikisha kugharimia maeneo
yafuatayo:-
(a) Kulipia gharama pale ambapo wajibu wa kisheria wa
CKD katika kumzika mfanyakazi wake, mume au mke
wa mfanyakazi au mtoto wa mfanyakazi unapoishia;
(b) Kulipia gharama pale ambapo CKD hakihusiki kisheria.
29
7.0 MICHANGO, VIWANGO, MAFAO NA NAMNA
MWANACHAMA ANAVYO NUFAIKA NA MFUKO
7.1 Kiingilio
7.1.1 Kiingilio cha uanachama, ambacho kinafafanuliwa katika
Sera ya Mfuko kitatolewa na Mwanachama kwa madhumuni
ya kupatiwa usajili katika mfuko na kwamba malipo haya
yatafanywa mara moja tu.
7.1.2 Kwa kuwa kuna wazo la kutumia Akiba iliyopo kama sehemu
ya Sera hii, na kwa kuwa hapatakuwa na ubaguzi (Preferential
treatment) ya waanzilishi wa mfuko na wanachama wapya,
ingefaa wanachama wapya kulipa kiingilio chenye kutambua
uwepo wa Akiba (Reserve).
7.2 Ada ya kila Mwezi
7.2.1 Kila mwanachama mfanyakazi atalazimika kulipa mchango wa
kila mwezi ambao utakuwa unakatwa kutoka kwenye mshahara
wa mfanyakazi wa kila mwezi kulingana na makubaliano ya
wanachama. Aidha, Mwanachama ataendelea kutoa mchango
huu ilimradi yupo kwenye ajira ya Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam na kulipwa mshahara/ujira.
7.2.2 Kiwango cha mchango kitakuwa kile kinachotumika kwa
wakati huo. Kwa hivi sasa, kiwango cha mchango pendekezwa
ni TSh. 5,000/=tu kwa mwezi.
7.2.3 Mwanachama mfanyakazi asiyelipwa kupitia “payroll” ya
“Lawson” ya Chuo (k.m. yule ambaye yuko katika likizo bila
30
malipo, n.k.) atalazimika kuhakikisha kuwa mchango wake wa
kila mwezi unapelekwa kwenye Mfuko; la sivyo uanachama
wake katika Mfuko utakoma.
7.3 Mafao ya Mfuko
Mafao ya mfuko ni yale ambaye yameainishwa katika sera ya
mazishi na yatatolewa pale anapofariki dunia:
7.3.1 Mwanachama yaani mfanyakazi
7.3.2 Mke au Mume wa mwanachama
7.3.3 Mtoto wa mwanachama. Kwa mtoto aliyezaliwa "bahati -
mbaya" (kazaliwa hai na kufariki punde baada ya kuzaliwa au
kafia tumboni wakati wa kujifungua) itabidi uthibitisho utolewe
kupitia Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha CKD.
7.3.4 Mzazi au Mlezi wa mwanachama mfanyakazi.
7.3.5 Mstaafu aliyekuwa mwanachama kabla ya kustaafu.
7.4 Viwango vya Mafao
Viwango vya mafao vitakuwa kama vilivyopendekezwa katika
“Kiambata B”.
7.5 Unufaikaji wa Mwanachama
Kutokana na utoaji michango hiyo, Mwanachama atanufaika
kwa kupata haki zifuatazo:-
7.5.1 Kupewa mafao stahiki na kwa wakati muafaka mara taarifa ya
tukio la kifo inapofika kwenye ofisi husika. Kijazilisho hiki
kitatolewa kwa mafao ambayo yameainishwa kwenye mfuko
pale ambapo majukumu ya kisheria ya CKD yanapoishia.
7.5.2 Kupewa nakala ya Sera ya Mfuko wa Mazishi.
7.5.3 Kutoa mapendekezo ya sehemu za kuwekeza pesa za mfuko ili
uweze kupanuka na kuwa endelevu.
31
7.5.4 Kupewa ripoti ya fedha ya mwaka.
32
8.0 UTUNZAJI WA FEDHA ZA MFUKO
8.1 Uwekezaji na Udhibiti wa Fedha za Mfuko
8.1.1 Uwekezaji
(a) Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Utawala baada ya kushauriana
na Kamati ya Mfuko wa Mazishi pamoja na Msarifu atakuwa
ndiye mwenye mamlaka ya kuingia mikataba inayohusu
masuala ya uwekezaji wa fedha za Mfuko.
(b) Bila kuathiri utekelezaji wa Sera ya Mfuko, shughuli za
kusimamia na kudhibiti fedha ya Mfuko zitafanywa na Kamati
ya Mfuko wa Mazishi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa
kuzingatia miiko ya taratibu za fedha ya CKD.
8.1.2 Udhibiti wa fedha za Mfuko
Fedha ya Mfuko zitatolewa tu kulipia shughuli zilizoidhinishwa
katika Sera na Kanuni za Mfuko.
Taratibu za fedha za Mfuko zitakuwa kama ifuatavyo:
(a) Fedha yote ya kiingilio na michango itakayokatwa kutoka
kwa wanachama itapelekwa benki.
(b) Waweka saini kuhusiana na fedha iliyo katika akaunti za
benki watakuwa ni Viongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam.
(c) Hati za Malipo zitaandaliwa na Ofisi ya Rasilimali Watu na
kuidhinishwa na Wanakamati wa Mfuko.
8.2 Uthibitisho wa Madai
Mwanachama atalipwa mafao husika mapema iwezekanavyo
baada ya kuwasilisha taarifa rasmi ya msiba kwenye ofisi husika
33
na atatakiwa kuwasilisha mojawapo ya taarifa zifuatazo kwa
maandishi kama uthibitisho ndani ya miezi mitatu (3):
(a) Uthibitisho wa kifo husika kutoka kwa daktari au
hospitali;
(b) Cheti cha kifo kutoka kwa Msajili wa Vizazi na Vifo;
(c) Barua kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji au
Mtaa yenye anuani, simu na muhuri wa ofisi kwa ajili ya
kuthibitisha;
(d) Kadi ya kliniki kwa mtoto aliyezaliwa "bahati-mbaya" kwa
ajili ya uthibitisho
34
9.0 MKUTANO MKUU
9.1 Kutakuwa na Mkutano Mkuu wa mwaka ambao
(a) kila mwanachama atawajibika kuhudhuria;
(b) utafanyika kabla ya kumalizika kwa mwaka wa fedha wa
CKD;
(c) utagharamiwa na fedha za mfuko.
9.2 Majukumu ya Mkutano Mkuu yatakuwa ni pamoja na:
(a) kupokea, kujadili na kutolea uamuzi au mwongozo
mambo yatakayoletwa na Kamati ya Mfuko wa Mazishi.
(b) Kuridhia maamuzi ya Kamati ya Mfuko wa Mazishi hasa
kuhusiana na:
(i) mabadiliko katika Kanuni za Mfuko;
(ii) mabadiliko katika uongozi wa Mfuko wa Mazishi;
(iii) uwekezaji wa fedha za ziada za Mfuko;
(iv) taarifa za fedha za mfuko pamoja na ukaguzi wa
mahesabu yake
(v) mambo mengine ambayo yatahitaji kupelekwa kwenye
Mkutano Mkuu
(c) Mwenyekiti wa Mkutano huo atakuwa mwenyekiti wa
Kamati ya Mfuko wa Mazishi.
(d) Katibu wa Kamati ya Mfuko wa Mazishi atakuwa Katibu
wa Mkutano Mkuu.
35
10. UONGOZI WA MFUKO
10.1 Viongozi wa Mfuko
Viongozi wa Mfuko watakuwa wale ambao wameainishwa
katika Sera ya Mfuko wa Mazishi (Sura ya nne, kifungu namba
4.2) ambao ni:
(a) Mwenyekiti ambaye atateuliwa na Naibu Makamu Mkuu
wa Chuo, Utawala;
(b) Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala
(c) Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya, CKD
(d) Mwakilishi mmoja kutoka chama cha Wafanyakazi, CKD
(e) Mwakilishi, UDASA
(f) Naibu Msarifu
(g) Mwakilishi mmoja, Ofisi ya Rasilimali Watu
(h) Mwakilishi wa Waanzilishi wa Mfuko.
10.2 Wajumbe watamchagua Katibu kutoka miongoni mwao
36
11.0 UKOMO WA UANACHAMA
11.1 Uanachama utakoma kwa:
(a) mwanachama kuacha kazi CKD kwa hiari yake
mwenyewe,
(b) Bila kuathiri vipengele vingine vya Kanuni hizi, kustaafu,
(c) Kufukuzwa, au
(d) kufariki dunia.
11.2 Aidha, Mwanachama mfanyakazi ambaye mshahara wake
haupitii kwenye “payroll” ya “Lawson” ya CKD na ambaye
atashindwa katika kipindi cha siku 90 kuufikisha mchango
wake wa kila mwezi katika Mfuko atakoma kuwa mwanachama
na hatastahili kurudishiwa michango yake ya nyuma.
12. KINGA
Iwapo mwanachama atabainika na kuthibitika kutoa taarifa za
uongo, vithibitisho visivyo halali au kuchelewesha kuwasilisha
vithibitisho husika, miezi mitatu tangu malipo yafanyike hatua
zifuatazo zitachukuliwa dhidi yake:
(a) Atapewa onyo la kimaandishi kutoka kwa Naibu
Makamu Mkuu wa Chuo - Utawala
(b) Atachukuliwa hatua za kinidhamu, ikiwa ni:
(i) makato ya mshahara kufidia malipo yaliyotolewa; na
(ii) makato ya ziada ya asilimia 50% ya malipo
yaliyotolewa.
13. TATHMINI YA MFUKO
Kamati ya Mfuko wa Mazishi utafanya tathmini ya Mfuko kila
baada ya miaka 3 na kupendekeza viwango vipya vya malipo ya
37
mafao pamoja na ada ya mwezi. Mapendekezo hayo
yatawasilishwa kwenye Mkutano Mkuu kwa ajili ya kuridhiwa.
14. MAMBO MENGINE YA KUZINGATIA
(a) Mavazi ya msiba yawe ya rangi nyeusi.
(b) Fedha za ziada za mfuko ziwekezwe katika maeneo
yasiyo hatarishi ili kuutunisha mfuko.
38
KIAMBATISHO A
Fomu ya Usajili / Registration Form
Taarifa Binafsi / Personal Particulars
Jina la Ukoo / Surname or Family-name:
JIna la mwanzo / First-name:
Majina mengine / Other names:
Tarehe ya kuzaliwa / Date of Birth:
Jinsi / Sex:
Taarifa za Ajira / Employment Particulars
Chuo / College
Shule Kuu / School
Idara / Department
Tarehe ya kuajiriwa / Date of
Employment
Namba ya Muajiriwa / Employee Number
Anuani za Mawasiliano
Contact Address
Posta / Postal:
Simu / Tel.:
Faks / Fax:
Barua Pepe / Email:
Anuani ya Nyumbani - Makazi ya
kudumu
Permanent Home Address/Place of
Domicile
Posta / Postal:
Mkoa / Region:
Wilaya / District:
Mji / Town:
Kijiji / Village:
Taarifa za Ndugu (wakati wa dharura)
Next of Kin (for notification in case of emergency)
Jina kamili / Full Name:
39
Uhusiano (Kaka, Dada, n.k.)
Relationship (Brother, Sister, etc.)
Anuani za Mawasiliano
Contact Address
Posta / Postal:
Simu / Tel.:
Faks / Fax:
Barua Pepe / Email:
Taarifa za Ndoa / Marital Status
Hujaoa - Hujaolewa / Single Mtalakwa / Divorced
Umeoa - Umeolewa / Married Mjane / Widowed - Widow
Jina kamili la Mke - Mume / Spouses Full Name:
*Namba ya Cheti cha Ndoa / Marriage Certificate No : * Ambatanisha nakala halali ya cheti cha ndoa / Attach CERTIFIED
copy of original marriage certificate
Taarifa za Watoto / Particulars of children
Jina kamili
Full name:
Namba ya Cheti cha
kuzaliwa
Birth Certificate
Number
Jinsi
Sex
* Ambatanisha nakala halali za vyeti vya kuzaliwa
* Attach CERTIFIED copies of birth certificates
Taarifa za Baba Mzazi / Father’s Particulars
Jina Kamili / Full Name:
Yuko hai / Alive
Amefariki / Deceased Tarehe / Date: ________________________
40
Taarifa za Mama Mzazi / Mother’s Particulars
Jina Kamili / Full Name:
Yuko hai / Alive
Amefariki / Deceased Tarehe / Date: ________________________
Taarifa za Mlezi / Guardian’s Particulars
Jina Kamili / Full Name:
Yuko hai / Alive
Amefariki / Deceased Tarehe / Date: ________________________
Je, ulishawahi kulipwa mafao kutoka Mfuko wa Mazishi?
Ndiyo Hapana (chagua mojawapo)
Have you ever received financial support from the UDSM Funeral
Support Fund?
Yes No (tick one)
Kama NDIYO - tafadhali ainisha lini na kwa ajili ya nani.
If YES - please state when and for whom.
1.__ ___________________________________________
2.______________________________________________
3.______________________________________________
*** *** *** *** *** *** *** *** *** *** *** ***
Nathibitisha kuwa taarifa zote nilizotoa hapo juu ni sahihi na kweli
I hereby declare that all information provided is true to the best of my
knowledge.
Tarehe / Date:___________Saini / Signature: _____________
41
KIAMBATISHO B
Mafao kutoka Mfuko wa Mazishi ya Wafanyakazi wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam
Mfuko utatoa mafao yafuatayo iwapo mwanachama, mke au mume wa
mwanachama, mtoto au mzazi au mlezi wa mwanachama anafariki
dunia. Gharama ya kila fao imeonyeshwa.
Fao: Gharama
1. Rambirambi TSh. 400,000.00
2. Turubai TSh. 100,000.00
3. Chakula TSh. 300,000.00
4. Viti TSh. 100,000.00
5. Mapambo TSh. 100,000.00
Jumla TSh. 1,000,000.00
Jumla ya gharama ya mafao yote itakayotolewa itakuwa ni TSh.
1,000,000.00 (Shilingi za Kitanzania milioni moja) tu na itatolewa
mapema iwezekanavyo baada ya taarifa kupelekwa kwenye ofisi husika.