8
2 Shule za umma za kata ya Fayette Darasa la 2 Mwongozo wa Familia wa Kujifunza Muhtasari wa yale watoto wanastahili kufahamu na kuweza kufanya na njia za familia kuongeza masomo nyumbani. “Tunaamini familia ni wenzetu. Niwa kwanza na waelimishaji wa watoto wenye nguvu zaidi . Pamoja tutahakikisha mafanikio ya wanafunzi wote.” - Mrakibu Emmanuel Caulk, Shule za umma za kata ya Fayette

Shule za umma za kata ya Fayette Mwongozo wa Familia wa ... Guides/Swahili...Shule za umma za kata ya Fayette 2 Darasa la 2 Mwongozo wa Familia wa Kujifunza Muhtasari wa yale watoto

  • Upload
    others

  • View
    38

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Shule za umma za kata ya Fayette Mwongozo wa Familia wa ... Guides/Swahili...Shule za umma za kata ya Fayette 2 Darasa la 2 Mwongozo wa Familia wa Kujifunza Muhtasari wa yale watoto

2Shule za umma za kata ya Fayette

Darasa la 2

Mwongozo wa Familia wa Kujifunza

Muhtasari wa yale watoto wanastahili kufahamu na kuweza kufanya na njia za familia kuongeza masomo

nyumbani.

“Tunaamini familia ni wenzetu. Niwa kwanza na waelimishaji wa watoto wenye nguvu zaidi . Pamoja

tutahakikisha mafanikio ya wanafunzi wote.”

- Mrakibu Emmanuel Caulk, Shule za umma za kata ya Fayette

Page 2: Shule za umma za kata ya Fayette Mwongozo wa Familia wa ... Guides/Swahili...Shule za umma za kata ya Fayette 2 Darasa la 2 Mwongozo wa Familia wa Kujifunza Muhtasari wa yale watoto

Darasa la 22

Kuhusu mwongozo wetu wa kujifunza:

Mwongozo huu unawakilisha baadhi ya vitu muhimu mtoto wako anapaswa kujuana kuweza kufanya kufikia MWISHO wa mwaka wa shule katika usanaa wa lugha yaKiingereza (ELA) na Hesabu. Malengo ya kujifunza inasaidia familia na walimu kujualini wanafunzi wanahitaji msaada zaidi na lini wanahitaji changamoto zaidi.

Familia zinaweza kufanya nini?

Kuna mengi ya kufanya kumsaidia mtoto wako kujifunza na kusaidia kuwatayarishakwa maisha yao ya mbeleni. Haya ni mambo machache ambayo yatawasaidiawanafunzi kufanikiwa:

1. Shiriki na mtoto wako jinsi masomo yalivyo muhimu kwako. Waambie elimu inastahili, kwamba ni msingi wa mafanikio.

2. Fanya shule iwe kipaumbele kwa kumpeleka mtoto wako shuleni kwa wakati kila siku.

3. Hudhuria mikutano ya mzazi-mwalimu na shughuli zingine za shule inapowezekana.

4. Shiriki na shule kujenga kuheshimiana. 5. Mtoto wangu yuko kwa ama juu ya matarajio ya masomo? Kama ndivyo, nini

kingine shule inaweza kutoa? Naweza kufanya nini nyumbani? 6. Jadiliana na mtoto wako kuhusu nini kinatendeka shuleni. 7. Wasiliana mara kwa mara na walimu wa mtoto wako kuhakikisha mtoto

wako anafanya maendeleo kwa mwaka mzima. 8. Una haki ya kujua jinsi mtoto wako anavyoendelea; usisite kuwasiliana na

mwalimu wake kama una mswali.

Kuzungumza na Mwalimu wa Mtoto wako

Ni muhimu kuwasiliana na mwalimu wa mtoto wako na shule mara kwa mara kuhusumaendeleo ya mtoto wako kuhusu malengo ya masomo. Hapa kuna mifano yamaswali ya kuuliza:

■ Mtoto wangu ana nguvu wapi na ni wapi anahitaji kuboresha? ■ Maendeleo ya mtoto wangu yanapimwa vipi katika mwaka mzima? ■ Naweza kuona mifano ya kazi za mtoto wangu? Vipi wanafikia ama hawafikii

malengo ya masomo? ■ Mtoto wangu yuko njiani kufikia malengo ya kiwango cha darasa? Kama

sivyo, misaada gani shule itatoa? Naweza kufanya nini nyumbani? ■ Mtoto wangu yuko kwa ama juu ya matarajio ya masomo? Kama ndivyo, nini

kingine shule inaweza kutoa? Naweza kufanya nini nyumbani? ■ Umesoma IEP ya mtoto wangu? Ni makao gapi yanayofanyiwa mtoto

wangu? ■ Mtoto wangu anajifnuza Kiingereza. Kukua kwa lugha ya mtoto wangu

kunasaidiwa vipi shuleni?

Page 3: Shule za umma za kata ya Fayette Mwongozo wa Familia wa ... Guides/Swahili...Shule za umma za kata ya Fayette 2 Darasa la 2 Mwongozo wa Familia wa Kujifunza Muhtasari wa yale watoto

Shule za umma za kata ya Fayette 3

Kuzungumza na Mtoto wako

Hii inasikika kama kawaida? “Shule ilikuwaje leo?” “Sawa” “Ulifanya nini?” “Hakuna” Hiyo ni sawa, endelea kuuliza!

Wanafunzi ambao wazazi wao wanazungumza nao kuhusu shule hufanya vizurikimasomo katika shule. Hapa kuna njia unaweza kumhusisha mtoto wako na usaidiemafaniko yao:

■ Teua wakati kila siku kuzungumza na mtoto wako kuhusu shule.■ Uliza mtoto wako akueleze jambo moja walisoma leo. Nini mtoto wako

anafaikiri kuwa inavutia sana? Nini inaonekana ngumu?■ Tizama ama pitia makaratasi na miradi ambayo mtoto wako analeta

nyumbani kutoka shuleni. Uliza mtoto wako: unajuaje hivo? Unadhani nini? Unatambua nini? Kwa nini uliifanya vile ama hivi? Kuna njia nyingine ya

kupata jawabu hilo?■ Pongeza mtoto wako kwa kazi ngumu na bidii, sio tu kwa “majibu sahihi”.■ Uliza maswali kuhusu mtoto wako anafikiria nini: Unajuaje? Unafikiri nini?

Unatambua nini? Uliifanya hivyo kwa nini? Kuna njia nyingine ya kupata jawabu hilo?

Kusaidia kujifunza mbali na nyumbani

Kujifunza hakusimami wakati wanafunzi wanatoka shuleni. Hapa kuna njia ambazounaweza kusaidia kujifunza nje ya darasani:

■ Somea mtoto wako, soma na mtoto wako, na uhimize wakati wa familia wa kusoma—katika lugha ambayo unajisikia starehe.

■ Tengeneza mahali patulivu na starehe na uunde ratiba ya kila mara kwa wanafunzi wako kufanya kazi za shuleni za kufanyia nyumbani ama shughuli nyingine.

■ Hakikisha wewe na mtoto wako mko na kadi ya maktaba na mnahudhuria shughuli za kusoma kwa familia nzima.

■ Jaribu kuanzisha ratiba ya mara kwa mara ya kufanya homework ama shughuli zingine za kujifunza.

■ Mtoto wangu yuko kwa ama juu ya matarajio ya masomo? Kama ndivyo, nini kingine shule inaweza kutoa? Naweza kufanya nini nyumbani?

Page 4: Shule za umma za kata ya Fayette Mwongozo wa Familia wa ... Guides/Swahili...Shule za umma za kata ya Fayette 2 Darasa la 2 Mwongozo wa Familia wa Kujifunza Muhtasari wa yale watoto

Darasa la 24

Nini mwanafunzi wako anapaswa kujua na kuweza kufanyakatika sanaa ya Lugha ya Kiingereza (ELA):

Lugha□ Rudia tena habari muhimu ama mawazo kutoka kwa mjadala ama hadithi

zilizosomwa kwa sauti. □ Tambua maana sawa ya neno lililo na maana tofauti kulingana na mazingira

ambayo neno limetumika. Kwa mfano: tumia sehemu nyingine yote ya sentensi ama aya kuamua ikiwa neno “saw” (kuona) inamaanisha kifaa ama wakati uliopita wa kuona.

□ Fikiria maana ya neno jipya wakati prefiksi ya kawaida inaongezwa kwa neno lijulikanalo. Kwa mfano:

Kusoma na Fasihi□ Fanya utabiri kuhusu yaliyomo katika kitabu kisicho cha uongo ukitumia ufahamu

wa awali na mambo ya vitabu kama vile sehemu ya yaliyomo, vichwa, maelezo, na maneno muhimu.

□ Eleza tena hadithi aliyesoma kwa kujibu maswali ya nani, nini, wapi, lini na vipi.□ Linganisha na kufananisha mateleo tofauti ya hadithi hiyo.□ Amua funzo ama maadili ya hadithi, hadithi, na ngano.

Kuandika□ Andika maoni kuhusu hadithi ambaye ameisoma, mambo muhimu kutoka kwa

kitabu kuunga mkono maoni hayo.□ Andika maelezo ya wazi ambayo yanaelezea mchakato ama taratibu, kama vile,

jinsi ya kupanga meza kwa chakula ama kucheza mchezo wa kadi uupendao.□ Andika hadithi zenye kueleweka mwanzom katikati, na mwisho na utume miundo

sahihi ya sentensi, herufi kubwa, nafasi, na alama.

Page 5: Shule za umma za kata ya Fayette Mwongozo wa Familia wa ... Guides/Swahili...Shule za umma za kata ya Fayette 2 Darasa la 2 Mwongozo wa Familia wa Kujifunza Muhtasari wa yale watoto

Shule za umma za kata ya Fayette 5

Jinsi ya Kuhimiza Kujifunza ELA Nyumbani

□ Soma na kujifunza kuhusu vitabu pamoja. Baada ya kusoma maandishi ya nonfiction, zungumza kuhusu nini mtoto wako amejifunza na shiriki jambo ulilojifunza. Baada ya kusoma maandishi ya fiction, himiza mtoto wako kuzungumzia kuhusu nini kinatendeka mwanzo, katikati, na mwisho wa hadithi.

□ Tafuta maneno yenye tofauti mbili ama zaidi ya maana (kama vile kimbia, ona, na bluu). Zungumzia jinsi maneno yaliyomo yanatufundisha kuelewa maana ipi ya neno inatumia. Himiza mtoto wako kutafuta mifano ya maneno iliyo na maana tofauti anaposoma.

□ Saidia mtoto wako kuandika mafundisho ya resepi iliyo viungo hatua-kwa-hatua kutengeneza chakula mkipendacho. Kwa mfano: jinsi ya kutengeneza siagi ya njugu karanga na sandwichi ya jeli na saladi yamatunda.

□ Uliza maktaba yako mtaani kupendekeza vitabu ama hadithi ambazo ziko na tofauti ya hadithi ya fairy tale azipendazo. Soma hadithi kwa sauti pamoja na mtoto wako na jadilianeni jinsi zinafanana ama jinsi zinatofautiana.

□ Uliza mtoto aandike noti ya asante ama barua kwa jamaa wa familia ama marafiki.

Tafadhali ungana na mwalimu wa mtoto wako na uulize kuhusu rasilimali za masomoya nyumbani zinazohusika na programu za kipekee za kusoma na kuandika.

Page 6: Shule za umma za kata ya Fayette Mwongozo wa Familia wa ... Guides/Swahili...Shule za umma za kata ya Fayette 2 Darasa la 2 Mwongozo wa Familia wa Kujifunza Muhtasari wa yale watoto

Darasa la 26

Nini mwanafunzi wako anapaswa kujua na kufanya katikahesabu:

□ Tilia maanani na suluhisha hesabu za kuongeza na kuondoa ukitumia mbinu ya ufanisi na zana.

□ Elewa na utumie uhusiano kati ya kuongeza na kuondoa. Kwa mfano: kuna apple 30, apple kumi na sita zipo mezani, na zingine zipo kwenye mfuko. Ni apple ngapi zipo kwenye begi? Ninaweza kujumuisha ili nitatue: 16 + ? = 30. Kuna apple 14 kwenye mfuko!

□ Tumia ukweli wa taarifa inayohusiana kuongeza na kuondoa ili kutatua matatizo. Kwa mfano: kama 8 + 6 = 14, basi 80 + 60 + 140.

□ Kiakili ongeza na kuondoa na jumla ya 20 ama chache haraka na kwa ufanisi.

□ Pima na ukisie urefu katika kwango cha (inches, fiti, klipu za karatasi) vitengo.

□ Tambua nambari za kawaida (1/2, 1/3, na ¼) ukitumia zana za hesabu na vitu halisi vya maisha.

□ Kiakili ongeza na uondoe 10 ama 100 kwa nambari iliyopeanwa 100-900.

□ Wakilisha na fanya maana ya data. Kwa mfano: tengeza picha, chati ama grafu ambayo inaonyesha ni mifuko mingapi wanafunzi wanavaa leo?

□ Husika na muda na fedha. Kwa mfano, “Ni 7:30. Wakati wako wa kulala ni kwa dakika 30 zijazo. Wakati wako wa kulala ni muda gani?” “Niko na $16.00. Nakupa $4.00 kunua kitabu katika haki ya vitabu (book fair). Nimebaki na pesa ngapi?”

Page 7: Shule za umma za kata ya Fayette Mwongozo wa Familia wa ... Guides/Swahili...Shule za umma za kata ya Fayette 2 Darasa la 2 Mwongozo wa Familia wa Kujifunza Muhtasari wa yale watoto

Shule za umma za kata ya Fayette 7

Jinsi ya Kuhimiza Kujifunza kwa Hesabu Nyumbani

Tafuta vitu vinavyokuja kwa vikundi, kama vile miguu miwili kwa mtu ama tairi nne kwenye gari. Uliza mtoto wako afikiri watu nane wana miggu mingapi ama tairi ngapi ziko kwa magari matano?

Tumia hali za kila siku kutafuta na kutumia hesabu za fraksheni za kawaida, kama vile 1/2, 1/3, na 1/4 ya kitu kizima. Kwa mfano: Kata sandwichi katika nusu mbili ama kunja gazeti kwa nusu au sehemu nne.

Uliza watoto wahesabu na kuweka akiba ya pesa ili kulipia vitu katika duka ama soko.

Uliza mtoto wako kufikiri kuhusu nusu moja ya kikundi cha vitu. Kwa mfano: ikiwa mtoto wako ana kadi 24 za besiboli kugawanya kisawa na rafiki, kila mmoja atapata ngapi?

Pamoja na mtoto wako, tumia rula ama vitu vingine vya kupima kutafuta urefu wa vitu tofauti katika nyuma yenu. Wacha mtoto wako alinganishe urefu wa vitu hivi.

Tafadhali ungana na mwalimu wa mtoto wako na uulize kuhusu rasilimali za masomo yanyumbani zinazohusika na programu za kipekee za hesabu.

Page 8: Shule za umma za kata ya Fayette Mwongozo wa Familia wa ... Guides/Swahili...Shule za umma za kata ya Fayette 2 Darasa la 2 Mwongozo wa Familia wa Kujifunza Muhtasari wa yale watoto

FAYETTE COUNTY PUBLIC SCHOOLS1126 Russell Cave RoadLexington, KY 40505

859-381-4100 www.fcps.net

Brosha hii imechapishwa na shule za umma za kata ya fayette.

Ilitengenezwa Fall 2016