2
Zantel yatoa msaada wa kisima cha maji kwa watoto yatima wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania Dar es Salaam, 19 June, 201! Kampuni ya simu ya Zantel leo imetoa msaada wa kisima cha maji kwa watoto yatima wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania,ikiwa na lengo la kumaliza tati maji na kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa takribani watoto 70 wa kituo Tatizo la maji ni moja ya matatizo sugu katika mkoa wa !ar es salaam pamoja na Tanzania ujumla hi"yo msaada huu ni wa muhimu kwa watoto wa kituo hicho Kisima hicho kilichokabidhiwa leo kitatoa maji safi na salama na yaliyotayari kwa matumi ambayo yatawasaidia watoto kuepukana na maradhi yanayosababishwa na maambukizi ya maji yasiyo salama na machafu #kizungumza wakati wa makadhiano, $kurugenzi $tendaji wa Kampuni ya Zantel, % &hose alisema kampuni ya Zantel imekuwa siyo tu ikitoa huduma bora na zenye unafuu kwa wateja wake bali pia imekuwa ikifanya jitihada za kusaidia maendeleo ya kijamii na kiuch kwenye jamii inayoizunguka 'Kampuni yetu inalenga kugusa maisha ya wananchi wanaotuzunguka, na ndio maana tumeamua kutoa msaada huu wa kisima ili kiweze kukisaidia kituo hiki kumaliza matatizo yaliyokuwa yanawakabili kwa muda mrefu( alisema %ratap )aye $kuu wa Wilaya ya Kinondoni, $heshilmiwa %aul $akonda, ambaye alikuwa $ge *asmi katika shughuli ya makabidhiano, aliipongeza kampuni ya Zantel kwa msaada akisema ni ishara inayofaa kupongezwa '+stawi wa watoto na "ijana ni jambo muhimu katika jamii, hi"yo nakipongeza kituo hiki k kubwa wanayofanya, na pia kampuni ya Zantel kwa kulikumbuka kundi hili muhimu katika jam na ninatoa wito kwa makampuni mengine kushiriki na kusaidia kituo hiki( alisema $akonda Kituo cha Watoto Wetu Tanzania kilianzishwa mwaka 00-, kwa lengo la kuhakikisha watoto wasio na wazazi au walezi wanapata matunzo na elimu bora #kitoa neno la shukurani $kuu wa Kituo cha Watoto Wetu Tanzania,."ance Tegete alisem awali kituo kilikuwa na tatizo kubwa la maji, lakini sasa shukrani kwa Zante limemalizika '#walitulikuwa tunategemea maji kutoka !#W#/ 1 ambayo upatikanaji wake si wa uhakika,tunawashukuru Zantel wameweza kutusaidia kutatua tatizo hili( alisema Tegete

Swahili Release

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Swahili Release

Citation preview

Zantel yatoa msaada wa kisima cha maji kwa watoto yatima wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania

Dar es Salaam, 19 June, 2015: Kampuni ya simu ya Zantel leo imetoa msaada wa kisima cha maji kwa watoto yatima wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania,ikiwa na lengo la kumaliza tatizo la maji na kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa takribani watoto 70 wa kituo hicho.Tatizo la maji ni moja ya matatizo sugu katika mkoa wa Dar es salaam pamoja na Tanzania kwa ujumla hivyo msaada huu ni wa muhimu kwa watoto wa kituo hicho.Kisima hicho kilichokabidhiwa leo kitatoa maji safi na salama na yaliyotayari kwa matumizi ambayo yatawasaidia watoto kuepukana na maradhi yanayosababishwa na maambukizi ya maji yasiyo salama na machafu.Akizungumza wakati wa makadhiano, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Zantel, Pratap Ghose alisema kampuni ya Zantel imekuwa siyo tu ikitoa huduma bora na zenye unafuu kwa wateja wake bali pia imekuwa ikifanya jitihada za kusaidia maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwenye jamii inayoizunguka

Kampuni yetu inalenga kugusa maisha ya wananchi wanaotuzunguka, na ndio maana tumeamua kutoa msaada huu wa kisima ili kiweze kukisaidia kituo hiki kumaliza moja ya matatizo yaliyokuwa yanawakabili kwa muda mrefu alisema Pratap.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mheshilmiwa Paul Makonda, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika shughuli ya makabidhiano, aliipongeza kampuni ya Zantel kwa msaada huo akisema ni ishara inayofaa kupongezwa.

Ustawi wa watoto na vijana ni jambo muhimu katika jamii, hivyo nakipongeza kituo hiki kwa kazi kubwa wanayofanya, na pia kampuni ya Zantel kwa kulikumbuka kundi hili muhimu katika jamii, na ninatoa wito kwa makampuni mengine kushiriki na kusaidia kituo hiki alisema Makonda.Kituo cha Watoto Wetu Tanzania kilianzishwa mwaka 2001, kwa lengo la kuhakikisha watoto wasio na wazazi au walezi wanapata matunzo na elimu bora.Akitoa neno la shukurani Mkuu wa Kituo cha Watoto Wetu Tanzania,Evance Tegete alisema awali kituo kilikuwa na tatizo kubwa la maji, lakini sasa shukrani kwa Zantel tatizo hilo limemalizika.Awali tulikuwa tunategemea maji kutoka DAWASCO ambayo upatikanaji wake si wa uhakika,tunawashukuru Zantel wameweza kutusaidia kutatua tatizo hili alisema Tegete.