68
Nani Mwenyezi Mungu? Imefasiria na(translated by): Abdiin Hussein Kifea HARUN YAHYA 1

Nani mwenyezi mungu. swahili (kiswahili)

Embed Size (px)

Citation preview

NaniMwenyezi Mungu?

Imefasiria na(translated by):Abdiin Hussein Kifea

HARUN YAHYA

1

Neno la Mfasiri (Translator’s Note)

Tangu zama za zama, watu wamekuwa wakiutafakari Ulimwengu na chanzo cha uhai na wametoa mawazo yao mbali mbali juu ya suala hili. Tunaweza kuyagawa mawazo hayo katika makundi mawili. Mosi, yale yanayofafanuwa Ulimwengu kwa mtazamo wa kukanusha uumbaji na pili yale yanayoona kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Aliyeumba maada na Ulimwengu kutokana na Ombwe Tupu na kuupangiya utaratibu. Viumbwa vyote hai na visivyo hai, vinavyoonekana na visivyoonekana, vilitokana na kazi ya Mwenyezi Mungu. Wanadamu, Majini, Wanyama, Mimeya, Magimba (galaksi), Nyota, Sayari, miyezi na vimondo vyote vimeumbwa na Mwenyezi Mungu. Usanii bora, mahesabu, urari, mizaniya, uwiyano na mpangiliyo unaoonekana katika Ulimwengu na kwa viumbwa hai ni vielezeo vya Imani hii.

Kwa wakanushaji, wao wanadai kuwa sayansi na mantiki viko upande wa itikadi isiyoamini Mungu. Wameshikilia kuwa Mwenyezi Mungu hayupo kwa sababu hatambulikani kwa milango yetu mitano ya fahamu. Wameiendeleza hoja hii kwa kudai kuwa Ulimwengu unatokana na maada na kwamba maada ndiyo kitu pekee kilichopo. Wanadai kuwa bahati nasibu ndiyo iliyosababisha Ulimwengu ujiunde wenyewe na uhai kutokea kwa kujianzisha wenyewe kidogo kidogo kutokana na vitu visivyo na uhai. Kwa maneno mengine, viumbwa vyote hai Ulimwenguni viliibuka tu kutokana na vyanzo vya asili na bahati nasibu kwa kanuni ya kila tukiyo na sababisho lake. Yakiwa ni matokeo ya ngano hiyo, dhanna ya kumkana Mungu huchukuliwa kama ndiyo “jambo la kawaida”, yaani jambo lisilohitaji jitihadi za kiakili kwani halihitaji uthibitisho. Ni muumini anayebebeshwa dhima hiyo, ambaye anahitajika kuthibitisha imani yake na hivyo ndiye anayejitahidi kujihami. Muumini anapotafuta jawabu ya maswali haya anakutana na nadhariya kem kem au hiyana za wanafalsafa ambazo ndizo zijengazo imani za watu wanaomkanusha Mwenyezi Mungu wakiwemo wanasayansi. Mtazamo wa falsafa ya ukanushaji unashikilia kuwa Ulimwengu na maumbile yake hayakuumbwa bali ni wa milele na unajiendesha pasi na haja ya kuwa na Muumba.

Ama kwa Waumini, wao ithibati yao ni kwamba Mungu Muumba ndiye Aliyeumba Ulimwengu kwa Kun -Fayakun, yaani kukitaka kitu kiwe na kikawa! Aidha utendaji kazi usiyo na dosari wa kila kitu ni kielezeo chao cha uwezo mkubwa kabisa wa kuumba Alionao Mwenyezi Mungu. Kokote na popote mtu ageukiapo, anakutana na ishara zinazobainisha wazi wazi kuwapo kwa Muumba. Kwa hakika hakuna uwezekano wowote wa Ulimwengu na vilivyomo kutokea kwa bahati nasibu.

Kwa min-ajiri hiyo, kitabu hiki kinachambua kwa kina maumbile ya angani, kuonesha maajabu yake ili kujibu maswali ambayo tangu zama za awali za maisha ya Mwanaadamu hapa Duniani, kila Mwanaadamu amevutwa nayo na kuyatafakari; kwamba ni namna gani Ulimwengu tunaoishi ulivyotokea, ni kwa jinsi gani mpangiliyo, uwiano na utaratibu

2

madhubuti ulivyojitokeza na ukiendelea kudumu kama ulivyo ukidhibiti maumbile yote? Na ni namna gani Dunia tuishiyo ilivyowiana na viumbwa inavyovibeba pamoja na maumbile mengine yaliyo nje yake hivyo kuifanya Dunia kuwa makazi munasibu yenye kuwezesha maisha ya viumbwa vyenye uhai. Majibu maridhawa yapatikanayo ndani ya kitabu hiki yanaoana na hitimisho la Wanasayansi na Wanafalsafa wakweli kwamba ulinganifu huu na utaratibu madhubuti ni ushahidi toshelevu wa kuwapo kwa Muumba ambaye ndiye mtawala wa Ulimwengu na vyengine vyote ambaye akili ya Mwanaadamu ni muhali kuweza kumdiriki. Kwamba ni Muumba huyo, Mweledi, Hodari Aliyewezesha kuwepo hayo yote ambaye sifa zake za kiungu ni pamoja na kutokuwa na mwanzo wala mwisho kinyume na ilivyo kwa viumbwa.

Hiki ni kitabu cha Tawhiid ambacho makusudio yake siyo tu kuwanufaisha wanafunzi bali wote watakaochukua taabu kukisoma kwa mazingatio, ambao kwa Taufiiq ya Mwenyezi Mungu, wamedhamiria kujenga imani thaabiti juu ya Muumba wao. Kwa ajili hiyo, maudhui ya kitabu hiki yatakuwa na manufaa zaidi iwapo wasomaji watayasoma kifamilia au kivikundi ili kwa pamoja, waweze kutafakari na kujadili mada hii muhimu kwa maslaha ya maisha yao ya hapa Duniani na maisha ya baada ya kifo, akhera.

Tunataraji, kwa msaada wake Mwenyezi Mungu, ujumbe huu utawafikia walengwa kwa namna ile iliyokusudiwa na Waandishi. Matarajio hayo ni pamoja na kuona wasomaji wakibadili tabia na mienendo yao baada ya kukiri kuwa wao ni viumbwa vyenye kutegemea mwongozo na maelekezo ya Muumba katika maisha yao yote.

Abdiin Hussein KifeaDar es SalaamTanzania

3

Utangulizi

Wengi miongoni mwa watu, kwa kujidhani kuwa hawana wanayepaswa kuwajibika kwake katika maisha yao ya kila siku, wameshindwa kutafakari juu ya muujiza na maajabu ya ukubwa wa Ulimwengu wanaoishi. Lakini hata kama wangaliweza kufanya hivyo, wasingaliweza kuuzingatia ukubwa huo ingawa kutafakari kwao kungaliwafikisha kuukiri ukweli unaojidhihirisha katika umbile la Ulimwengu kuwa umeumbwa na Muumbaji Hodari, Fundi, Mwenye uwezo usiyomithilishwa, na Hekima iliyopindukia uwezo wa kufikiri alionao Mwanaadamu.

Tuchukue upana wa mji mkubwa mmoja ambao watu wanaishi, tuuangalie kutoka upande mmoja hadi mwingine. Itatudhihirikia kuwa upana huu ni mkubwa mno. Labda tutumie njia nyingine katika kuelewa jambo hili. Tujaalie tumeweza kusafiri kutoka upande mmoja wa nchi yetu hadi mwingine, yaani kutoka mashariki hadi magharibi, hiyo piya haitaweza kutusaidia bali tutashangazwa tu na ukubwa wa eneo la nchi! Huu ni mfano mdogo wa kututia fikirani. Yawezekana wengi kama si wote, wameshasafiri kwa magari ya mabarabarani au ya relini kwenda sehemu za mbali ndani au nje ya nchi. Hebu zivutwe fikira juu ya suala moja muhimu, nalo ni hili. Hivi kuweza kusafiri kuzunguka sehemu zote za Dunia kwaweza kusaidia kuuhisi ukubwa wa Ulimwengu? Jawabu litakuwa hapana. Hiyo ni kwa sababu ukubwa wa Dunia unachukua nafasi iliyo sawa na vumbi kwa kulinganisha na ukubwa wa Ulimwengu huu ambao nao ni sehemu tu katika vile vilivyoumbwa na Mwenyezi Mungu. Ametukuka Mwenyezi Mungu, Mbora wa kuumba!

Sayari hii ya Dunia ni kijitone tu ikilinganishwa na ukubwa wa Ulimwengu wote. Mazingatio yetu yaende pia kwenye umbile la ardhi yetu hii ambayo nayo ni kama kijivumbi tu katika Ulimwengu huu. Wanaadamu wanaendesha mambo yao wakiwa katika kijitone hiki kilichopo Ulimwenguni. Barabara zipitazo zimejengwa kwenye duara hili linalojizungusha lenyewe na kulizunguka jua kwa kasi kubwa sana. Dunia inapojizungusha yenyewe hupatikana usiku na mchana katika saa ishirini na nne. Na inapolizunguka jua kwa muda wa siku 365, unapatikana mwaka mmoja. Iwapo mtu atachukua mawe au ‘matoi’ ya magari kisha akayaweka juu ya mpira aangalie iwapo mawe au ‘matoi’ hayo ya magari yataweza kutuliya hapo juu, kwa hakika atabaini kuwa hayataweza kukaa, yataanguka. La kuzingatia hapa ni jinsi wanaadamu, wanyama na viumbwa vyengine vinavyoweza kukaa siku nzima, juma zima, mwezi mzima, mwaka na miaka juu ya duara hili la sayari ya Dunia lenye kuzunguka kwa kasi kubwa isiyoelezeka, viumbwa hivyo vikiendesha shughuli mbali mbali na kwa furaha bila hata kuanguka! Kwa kweli hayo ndiyo maajabu yenyewe. Je ni namna gani jua linatoa mwanga. Mwanga unaoonekana usingalikuwepo bila ya kuwepo duara hili kubwa ajabu mfano wa yai. Je, bila ya jua ingaliwezekana kufanya shughuli mbali mbali? Kwa kweli isingaliwezekana! Isingaliwezekana kufanyika chochote kwa sababu bila ya jua, kusingekuwa na kitu chochote

4

chenye uhai katika sayari hii ya Dunia. Si mimea, miti, ndege, au mauwa yapendezayo bali hata baba, mama, mtoto, kaka, dada, ndugu, jamaa na marafiki wasingalikuwepo katika Dunia hii.

Mifano hii miwili ya Jua na Dunia yaonesha umuhimu wa maumbile yaeleayo angani katika maisha yetu. Ipo mifano mingi mizuri ya aina hii itakayotolewa katika mada za somo letu hili refu na zuri. Ni somo lenye kuvutia kwa kuwa limelenga kuujua Ulimwengu, limelengwa kumuwezesha msomaji kumjua Muumba Aliyeumba. Ili kuweza kufaidi zaidi, ingefaa maudhui haya yasomwe kwa pamoja baba, mama na marafiki kwa kuwa ni maudhui ambayo mbali ya kusisimua sana, pia yanahitaji mjadala na tafakuri ya pamoja. Kadiri maudhui haya yatakavyosomwa kwa makini zaidi, ndivyo Mwenyezi Mungu, Muumba, Atakavyofahamika Yeye ni nani na ndivyo utakavyofahamika uumbwaji wa Ulimwengu wetu huu na viumbwa vingine. Pia itafahamika lilivyoumbwa jua, mwezi, Dunia na kila kilichomo Ulimwenguni. Somo hili limelengwa kujibu maswali Nani Mwenyezi Mungu, vipi na kwa nini aliumba ili kuchochea mazingatio. Tukiyazingatia kwa makini tutakayojifunza katika maudhui ya kitabu hiki, mienendo yetu itabadilika kwa kuwa itaongozwa na Mwenyezi Mungu katika kila hatua na kwa hivyo itafanya Wanaadamu waishi kwa furaha na amani wakifuata mfumo wa maisha wa Mwenyzi Mungu.

Harun YahyaMwandishi

5

Sura ya Kwanza

UumbajiTunajifunza nini tunapotumia neno “uumbaji” wakati tukielezea kitu kinachoitwa

kuwepo kutokana na kisichokuwepo. Tunachojifunza kuwa, ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye anayekifanya kitu kiwepo kutokana na kutokuwepo. Ingawa inafahamika kuwa watu nao kadhalika huweza kuunda kitu kisichokuwepo kikawepo kama vile kuchora picha za watu na wanyama, wakaweza kuunda meli na majahazi na wanaunda magari, hata hivyo wanafanya hayo kwa kutumia taswira au malighafi inayopatikana katika Ulimwengu huu na kwa kuigiza vitu ambavyo tayari vipo. Kwa mfano, wanatengeneza nguo wakitumia malighafi ya pamba au sufu za wanyama. Au wanaunda magari, meli na ndege wakitumia malighafi ya vyuma ambavyo madini yake ipo tayari, kadhalika wanaigiza miundo ya vyombo hivyo kutokana na maumbile ya wanyama, ndege na wadudu ambao tayari Mwenyezi Mungu alikwisha waumba. Kwa hakika mwanaadamu haumbi ila anaunda,yaani anaunganisha na kuigiza vilivyopo.

Kuumba ni kukifanya kitu kiwepo kutokana na kutokuwepo, bila ya kuigiza mahali. Bila ya kuigiza mahali, Mwenyezi Mungu Ameumba Ulimwengu ikiwemo hii Dunia na vyote. MwenyeziMungu Amemuumba mtu wa kwanza kabisa Adamu bila ya kuigiza chochote. Alimuumba kwa udongo ambao tayari alikwishauumba. Mwanaadamu ni kiumbe aliyeumbwa baadaye sana, ni baada ya viumbwa vyote kuumbwa,kama tunavyofahamishwa katika Qur’an:

“Hakika ulipita muda mrefu sana Mwanaadamu hakuwa kitu kinachotajwa”. (76:1)

Wanadamu wanaiga tu katika vile ambavyo tayari Mwenyezi Mungu Amekwishaviumba, hata wanapochora picha huigiza picha za vile vilivyokwishaumbwa. Watu wanapochora picha basi picha hizo zitakuwa ama juwa, milima, miti, bahari au watu, hawawezi kuchora kitu kisichokuwepo. Isingaliwezekana kuchora picha ya mti iwapo mchoraji hangekuwa ameuona mti tangu azaliwe. Mtu asiyeona kabisa tangu azaliwe si aghlabu kuchora kwa kuwa hana taswira ya maumbile kichwani kwake. Atakachokijua ni labda jua ambalo hulisikia kuwa ni la duara lenye mwanga wenye joto kubwa. Yeyote yule ambaye hajapata kuona tangu azaliwe itokee ghafla macho yake yafunguke aone, kwa kweli hataweza kuwajua kwa sura hata ndugu zake wa karibu mpaka labda wazungumze asikiye sauti zao. Iwapo watakaa kimya hataweza kuwajua sura licha ya kuwa amekuwa akikaa, kuongea au kucheza nao siku zote. Kwa nini, kwa sababu hakuwa akiwaona. Vivyo hivyo mtu hawezi kuvijua vitu ambavyo hajaviona kabisa, kwa sababu hiyo hataweza kuchora picha zake. Lazima kwanza ziwepo taswira kichwani ndipo mtu aweze kuchora. Kwa mifano hii tunaona kuwa ni Mwenyezi Mungu tu mwenye uwezo wa kuumba kitu bila kuigiza chochote.

Katika mada hii tumejifunza:

6

Kumbe hapakuwa na Ulimwengu kabla ya Mwenyezi Mungu hajauumba. Mwenyezi Mungu ndiye Aliyeumba kila kitu bila ya kuigiza mahali. Wanaadamu hawaumbi ila huunda, yaani huigiza katika vile ambavyo tayari Mwenyezi

Mungu Ameviumba.Mwenyezi Mungu ameufanya Ulimwengu uwepo kutoka kwenye ombwe tupu

aliloliumba.

Mbingu saba ni nini?

“Basi akazifanya Mbingu saba katika siku mbili, na kila uwingu akaufunulia kazi yake. Na tumeupamba uwingu wa karibu yenu huu kwa mataa na kuulinda. Hiki ndicho kipimo cha Mwenye nguvu, Mwenye kujuwa(41:12).

Wengi hustaajabishwa na uzuri wa anga lenye nyota na miezi inayong’ara. Kwa uzuri huo, wengi wamekuwa wakidadisi juu ya umbile hilo. Neno Mbingu ambalo limetumika katika aya nyingi, moja ya maana zake ni anga. Neno hilo pia lina maana ya maumbile makubwa ambayo Mwanaadamu hajafikia kiwango cha elimu ya kuyajua zaidi, ambayo kwa mujibu wa Qur’an yameumbwa kimatabaka moja likiwa juu ya jiingine. Matabaka yote yamelifunika duara la Ulimwengu:

“Ambaye Ameumba Mbingu saba zilizo tabaka tabaka..(67:3).

“Na tukajenga juu yenu saba madhubuti”(78: !2)

Na bila shaka sisi tumeipamba Mbingu ya karibu kwa pambo la nyota. Na kuilinda na kila shetani asi(37:6-7)

Ulimwengu ni mkubwa ajabu, umekusanya maumbile mengi ambayo ni pamoja na miezi, vimondo, nyota zenye mkia, sayari ikiwemo Dunia na angahewa yake, nyota kubwa zenye kuwaka na zisizowaka, matrilioni ya Magalaksi(Magimba) na mengineyo tusiyoyajuwa:

“Ameumba Mbingu saba kwa siku mbili...” (Surat Fussilat 12).

...Na tumeupamba uwingu wa karibu yenu huu kwa mataa na kuulinda...(41:12)

Anga linaloizunguka ardhi huitwa angahewa nalo lafahamika kama Mbingu ambapo utafiti umeng’amua kuwepo kwa matabaka saba yaliyoizunguka ardhi na vilivyomo ndani yake. Kwa kutumia tafsiri hii, anga la Dunia ambalo huitwa angahewa, nalo lina tabaka saba:

7

“Mwenyezi Mungu ni yule ambaye ameziumba Mbingu saba na ardhi kuwa mfano wa hizo. Amri zake zinashuka humo ili mjuwe kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu, na kwamba amekizunguka kila kitu kukijuwa”(65:12).

Kuumbwa kwa UlimwenguMaumbile yaonekanayo angani yote yana uhusiano mkubwa yakiwa yamedhibitiwa

katika mtandao mmoja unaoitwa Ulimwengu. Ulimwengu huu ni sehemu tu ya maumbile ya Mwenyezi Mungu kama zilivyo Mbingu saba, Arshi, Pepo, Moto, viumbwa na maumbile mengine mengi anayoyajua Mwenyewe Mwenyezi Mungu yaliyo nje ya duara la Ulimwengu huu:

“Vinamuomba Yeye kila vilivyomo Mbinguni na Ardhini; muda wote Yeye yumo katika mambo(mengine mengine)”(55: 29).

Duara hili tuishilo lenye umbile mithili ya yai ni kichembe tu cha maumbile mengi na makubwa yaliyomo Ulimwenguni. Hii ni sayari iitwayo Dunia au ardhi ambayo ni ndogo sana kuliko hata baadhi ya sayari zilizo karibu yake. Kwa mfano kimpangilio, sayari zilizo katika mfumo wa jua letu hili, kutoka Dunia, inafuata sayari ya Maazi, halafu sayari ya Jupita. Hii sayari ya Jupita ni kubwa kwa zaidi ya mara 318 kuliko Dunia, ikiwa na kipenyo chenye kulizidi umbile la Dunia kwa mara 11. Ukubwa wa sayari hii ya Jupita si wa bure bure tu, bali kwa ujuzi mkubwa alionao Mwenyezi Mungu, sayari hiyo husababisha uvutano kati yake na njia ipitayo Dunia yetu katika kulizunguka jua, mzunguko ambao hutupatia miaka. Uvutano kati ya mduara huo wa njia ya Dunia na duara la Jupita, hufanya Dunia isitoke nje ya mzunguko wake. Kadhalika, kwa utaratibu wa uumbaji wa Mwenyezi Mungu, jua ndilo liwezeshalo kuwepo kwa uhai katika maisha haya ya Dunia. Inafahamika kuwa bila ya jua hakitawezekana chochote katika sayari hii. Kwa hiyo, Mwenyezi Mungu Ameumba maumbile yote kwa uwiano na ulingano uliofungwa chini ya mtandao mmoja wa kila umbile au kiumbwa kimoja kutegemea kingine kwa namna ya ajabu kabisa. Ametukuka Mwenyezi Mungu Muumba wa Ulimwengu na vyote. Yawezekana kila mtu akawa ameshajiuliza maswali kadhaa yenye kustaajabia Ulimwengu huu usio na mwisho ulivyotokea? Namna gani Dunia, jua, mwezi na nyota zing’arazo usiku zilivyotokea kwa mara ya mwanzo kabisa? Hivi anafahamika yule Aliyeumba Ulimwengu huu wenye maumbizi mengi mazuri pamoja na jua hili, Dunia na mwezi wake? Hivi inafahamika nguvu na uwiano uliopo katika Ulimwengu huu unaowezesha kuwepo maisha katika sayari hii ya Dunia?

Hapo kabla hapakuwa na Ulimwengu!Katika zama za kale sana, Mwanaadamu hakuwa na elimu ya kutosha juu ya mambo ya

anga. Vifaa vilivyohitajika kufanyia uchunguzi wa anga vilikuwa duni, havikuwa bora kama ilivyo hivi sasa. Kwa hiyo wakati mwingine watu walipojaribu kuelezea chanzo cha Ulimwengu, walijenga fikira na mawazo ya ajabu kabisa. Kulikuwa na mawazo yaliyodai kuwa

8

Ulimwengu huu ni wa milele. Kabla ya mwanaadamu kupata viona mbali na vifaa vya kuchunguzia anga, baadhi ya watu walikua wakieneza mawazo yaliyodai kuwa Ulimwengu huu hauna mwanzo na utaendelea kuwa hivyo milele!

Mawazo hayo yalikuwa hayo kwa wakati huo! Mtu anaweza kujiuliza hivi nyumba wanayoishi watu au shule wanayosoma wanafunzi ilijengwa lini? Majibu yatakuwa, ilijengwa muda, tarehe au kipindi fulani. Hata misitari hii inayosomwa katika somo hili iliandikwa muda fulani. Vivyo hivyo, kila mmoja wetu alizaliwa siku fulani ndiyo maana baadhi ya watu husherehekea siku zao za kuzaliwa kwao. Miaka inayotumika hivi sasa kwa kufuata mwendo wa jua inanasibishwa na uzawa wa Nabii Isa(a.s), kwa hiyo Isa(a.s) alizaliwa ingawa uzawa wake si ule wa kawaida wa kuhusisha maingiliano ya wazazi wawili, bali yeye alizaliwa na mama tu bila ya baba. Nabii Adamu aliumbwa, hakuwa na baba wala mama, bali aliumbwa na Mwenyezi Mungu kwa udongo kisha akapuliziwa Roho kuwa kiumbe hai(mtu). Mtume Muhammad(s.a.w), alizaliwa kutokana na wazazi wawili, baba na mama, alisherehekea siku ya kuzaliwa kwake kwa kufunga saumu. Mtume(s.a.w) alizaliwa siku ya jumatatu, kwa hiyo kila jumatatu alikuwa akifunga saumu ya Sunna. Waislamu hupaswa kumuiga Mtume Muhammad kwa kufunga funga ya sunna siku ya jumtatu. Kwa kuwa Mtume Muhammad (s.a.w) aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa, maana yake Mtume (s.a.w.) aliumbwa kama Wanaadamu wengine na kama viumbwa vyote vya Mwenyezi Mungu. Hiyo ina maana kwamba chochote kionekanacho chenye uhai na kisicho na uhai kilikuja wakati fulani, si kwamba kimekua hivyo bila ya mwanzo. Kwa hiyo, mawazo kwamba Ulimwengu hauna mwanzo kwa sababu umekuwa hivyo, si sahihi. Mifano ifuatayo ni muhimu kwa mazingatio.

Jaalia wakati fulani asubuhi wanafunzi fulani walikwenda shule kwa kupita njia tafauti na ile wanayopita siku zote, ghafla wakaona kinyago. Je, mawazo gani watakayo kuwa nayo juu ya kinyago au sanamu hiyo? Kwa kweli wazo litakalowajia ni kwamba yupo aliyekitengeneza kinyago au sanamu hiyo, na yupo aliyeweka sanamu hiyo hapo. Sasa ikitokea mtu akasema “hapana, kinyago hicho kimekuwepo hapo wakati wote, hakuna aliyekitengeneza, watu watamfikiriaje mtu huyo!” Kwa kweli atakuwa amemshangaza kila mtu na huenda akadhaniwa mpuuzi na mjinga! Kila kazi ya usanii imefanywa na msanii, kwa hiyo kinyago kimetengenezwa na kuwekwa hapo na msanii mchonga vinyago! Wale wanaodai kwamba Ulimwengu umekuwa hivyo ulivyo bila ya kuwepo Muumba, ni watu wenye fikira finyu na upeo mdogo. Wameshindwa kujitafiti na kujitafuta walikotoka. Kinyago ni kipande tu cha mti au jiwe, lakini Ulimwengu unakusanya maumbizi yote ya anga yaliyo chini ya utaratibu maalumu na mifumo mizuri na milinganifu yenye kutatanisha sana kuliko sanamu au kinyago ambacho inaaminika kuwa kimetengenezwa na kuwekwa hapo kilipo na mtu au watu fulani. Watafiti na wachunguzi wa mambo ya anga wa leo wameweza kugundua maajabu makubwa ya anga na kisha kukiri kwamba yule anayesema Ulimwengu huu hauna Muumbaji wake ni mchache wa fikira na mtovu wa shukurani.

9

Sura ya Pili

Mlipuko Mkubwa ulioumba Ulimwengu(‘the Big Bang’)

Kabla Mwenyezi Mungu hajaumba Ulimwengu, hapakuwepo umbile lenye jina hilo katika yale yaliyokwishaumbwa wakati huo. Tumeona pia kuwa ni Mwenyezi Mungu Aliyeumba kila kitu bila ya kuigiza mahali. Na tukaona kuwa Wanaadamu hawaumbi ila huunda, yaani huigiza katika vile ambavyo tayari Mwenyezi Mungu ameviumba. Mwenyezi Mungu Ameufanya Ulimwengu uwepo kutoka kwenye ombwe tupu. Je tukio hilo kubwa na la ajabu la kuumbwa Ulimwengu lilitokeaje.

Mabilioni ya miaka iliyopita, Ulimwengu ulikuwa kiduara kidogo. Sasa ni namna gani kijiduara hicho kilivyotokea na kupanuka kufikia Ulimwengu huu tulionao. Watu wanaweza kuvuta fikira juu ya mlipuko wa kitu chochote kile. Kwa mfano, muwindaji anajaribu kukiwinda kijidudu kidogo pengine mfano wa kunguni. Katika uwindaji huo akajaribu kutega bomu kwenye nyumba ili kuweza kukidhibiti kijidudu hicho. Katika utegaji huo, ifikiriwe ni nini kitatokea iwapo bomu hilo litalipuka. Ni wazi udongo utasambaa huku na kule, matofali kurushwa mbali, kwa hakika hapatapatikana kitu.Tunafahamu kuwa kabla ya mlipuko huo, matofali na udongo huo vilikuwa pamoja. Lakini baada ya bomu kulipuka vyote vitasambaa huko na kule mbali kabisa. Hivi ndivyo tunavyofahamu mlipuko wowote ule unapotokeya.

Mabilioni ya miaka huko nyuma kabisa, Ulimwengu huu ulifanyika baada ya mlipuko wa aina hiyo. Chembe chembe nyingi na ndogo sana zilitokea kutokana na mlipuko huo. Kama ilivyokuwa katika ile nyumba ya muwindaji, chembe chembe hizi zikasambaa huku na kule. Lakini la kustaajabisha kabisa, baada ya mlipuko na kusambaa huko, chembe hizo zikaanza kujikusanya na kuunda nyota, sayari mbali mbali na maumbile mengine makubwa yanayoonekana Ulimwenguni hivi sasa. Mlipuko ulioanzisha uumbaji wa Ulimwengu huu unajulikana na wajuzi wa elimu ya anga (wanaastromia) kama ‘The big Bang’ yaani Mlipuko Mkuu.

Ulimwengu haukutokea kwa bahati nasibu kama wasemavyo baadhi ya mabobwe ila umefanyika kutokana na mlipuko huu mkubwa ambao asili yake anaijua Mwenyezi Mungu. Ulimwengu huu unaojiendesha kwa utaratibu madhubuti tangu mizunguko ya chembe chembe hadi mizunguko ya sayari, unatokana na mitawanyiko ya chembe chembe na nguvu ambayo ilikadiriwa ijiwekee mpango maalumu kuanzia pale ulipotokea mlipuko mkubwa. Muda mlipuko huo ulipotokea, Ulimwengu ulianza kujiweka katika umbile duara lililokusanya

10

mabilioni na mabilioni ya maumbile mfano wa hilo, ambao kwa pamoja ukiendelea kukua na kutanuka hadi leo.

1. Matrilioni ya miaka nyuma kabisa huko hakukuwa na Ulimwengu2. Ulimwengu umetokea baada ya mlipuko wa umbile moja.3. Baada ya mlipuko huo, idadi isiyohesabika ya maduara madogo yalitokea yakafanya

Ulimwengu, wakati huo huo, maduara hayo yalianza kuelekea mbali ya pale yalipotokea huku yenyewe yakijikimbiza na kujiweka mbali mbali.

4. Duara la Ulimwengu huu limekuwa likipanuka mithili ya puto au mpira ujaao upepo kadiri maumbile yaliyomo yanavyosonga mbele zaidi.

Huu ni ushahidi wa uwezo wa Mwenyezi Mungu usio na ukomo. Hata wanaadamu wakijikusanya wote kwa pamoja, hawawezi kuumba Ulimwengu wala kuuhisi ukubwa wake. Hata kama vifaa vinavyopatikana katika ardhi hii vitakusanywa pamoja, mwanaadamu hataweza kuiga mfano wa mlipuko mkubwa sawa na ule wa Mlipuko Mkuu wa uumbaji. Uwezo wote ni wa Mwenyezi Mungu, Aliyeumba kila kitu. Inaeleweka kuwa mlipuko wowote ule hauwezi kutoa utaratibu na mpangilio wenye nidhamu nzuri bali kinyume chake ambapo husambaratisha na kuharibu kila kitu. Mlipuko huangamiza kila kilicho karibu yake. Mlipuko mkubwa kabisa wa bomu huharibu majengo na kuyafanya yasiwepo kabisa. Bomu lenye nguvu sana Ulimwenguni ni bomu la Atomiki. Bomu hili likilipuliwa mahali, huangamiza kabisa kila kitu. Kwa mfano bomu la Atimiki lilipoangushwa katika miji ya Hiroshima na Nagasaki Japan wakati wa vita kuu ya pili miaka ya 1939-1945, liliharibu kila kitu na kuwaacha vilema wale wote walionusurika na mlipuko huo wa bomu hilo baya. Hadi leo vizazi bado vinaathirika. Kubwa linalojitokeza hapa na lenye kustaajabisha ni jinsi mlipuko mkubwa kabisa, zaidi ya mara mabilioni ya bomu la Atomiki ulivyotokea. Mlipuko huo badala ya kuangamiza ulitengeneza, ulitoa matokeo tafauti na yale anayoyajua mwanaadamu kuhusiana na mlipuko wa aina yoyote. Mlipuko huo ulianzisha utaratibu madhubuti wa Ulimwengu. Hivyo, Ulimwengu huu tunaoujua uliopangwa vizuri mno kutuwezesha sisi kupata kila tunachokihitajia, unatokana na mlipuko huo mkubwa. Kwa nini Mlipuko huu uweke utaratibu huo madhubuti badala ya kuangamiza?

Kwa hakika ni Mwenyezi Mungu Aliyeumba Ulimwengu kutoka pasipokuwa kitu kwa njia hii ya mlipuko mkubwa. Na ni Yeye aliyeweka utaratibu madhubuti unaoendesha Ulimwengu kwa namna ya ajabu kabisa bila ya migongano. Hivyo, yeyote anayejaribu kutoa jawabu ya uumbaji wa Ulimwengu huu wa ajabu kinyume na hili, kwa hakika hana jawabu sahihi ila kujaribu kuwazuga Wanaadamu kwa manufaa yake binafsi ya kidunia. Kwa mfano, mtu anayedai Ulimwengu huu umetokea tu wenyewe na kujiweka hivyo ulivyo bila ya Muumba kwa kweli ni mwongo pengine hana akili timamu. Kusema kwamba Ulimwengu huu wenye utaratibu eti umetokea kwa bahati nasibu baada ya mlipuko wa awali, maneno hayo si ya akili kabisa. Ni nini kitakachotokea katika mchanga iwapo bomu litaangushwa mahali hapo?

11

Kwa hakika chembe chembe za mchanga zitaruka na kusambaa ovyo huku na kule. Je, atatazamwaje yule ambaye atasema nyumba imezuka mtaani baada ya bomu kuangushwa? Kwa kweli ataonekana ni mtu wa ajabu sana. Vivyo hivyo huonekana ni kichaa mtu anayedai kuwa mpangilio na utaratibu madhubuti unaoendesha maumbile ya Ulimwengu umejifanyiza wenyewe!

Ipo mifano mingi ya ulingano, uhusiyano na uwiano madhubuti katika Ulimwengu huu. Mifano hiyo hatuwezi kuilinganisha na ile nyumba ya mtaani ambayo kamwe haiwezi kuzuka baada ya milipuko tunayoijua katika maisha yetu. Mwezi septemba tarehe 11, 2001 ndege ziliyalipua majengo ya kituo cha biashara cha Dunia(World Trade Centre) na Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon. Majengo hayo yaliharibiwa vibaya sana.

Katika kuhitimisha mada hii, tumalizie na kauli kwamba, ukamilifu, umadhubuti na mpangilio uliopo, unathibitisha ukweli kwamba Ulimwengu haukutokea au kujifanyiza wenyewe. Ulinganifu, uwiano na mpangilio wa kila kitu uliofungwa chini ya mtandao mmoja uitwao Ulimwengu ni alama ya busara isiyo na ukomo ya Mwenyezi Mungu Muumba. Ametukuka kweli kweli Mwenyezi Mungu, Muumba wa Mbingu na Ardhi na vyote vilivyomo.

Katika mada hii ya mlipuko ulioumbisha Ulimwengu:

-Tumejifunza kuwa kumbe Ulimwengu ulifanyika pasipo chochote kabla yake.-Tumejifunza kuwa Aliyeasisi Mlipuko huo na hatimaye maumbile yaliyotokea baada ya

mlipuko huo ni Mwenyezi Mungu. -Tumejifunza kuwa wanaastronomia yaani wanaanga wanauita Mlipuko uliyoumba

Ulimwengu kuwa ni Mlipuko Mkuu, -Tumejifunza piya kuwa tangu mlipuko mkubwa, Ulimwengu unazidi kutanuka, ulianza

mdogo, sasa umepanuka na kuwa mkubwa zaidi na bado unaendelea kuwa mkubwa zaidi na zaidi.

Mafundisho ya Qur’an juu ya kuumbwa Mbingu na ArdhiQur’an ni Kitabu Kitukufu cha Mwenyezi Mungu kilichoshusha kuwaongoza watu.

Kitabu hiki ndicho kinachotoa maelezo sahihi kabisa juu ya mambo mbali mbali. Maelezo ya kitabu hiki ni sahihi kwa sababu kila neno lililomo limetoka kwa Mwenyezi Mungu mwenyewe Muumbaji na Mjuzi wa kila kitu. Wakati Qur’an ikiteremshwa kwa Mtume Muhammad(s.a.w), Ulimwengu ulikuwa bado haujapiga hatua kubwa kisayansi na kitekinolojia. Kwa hiyo baadhi ya maelezo yaliyomo kwenye Qur’an hayakuweza kufahamika wala kufanyiwa utafiti. Hivi leo yamepatikana maendeleo makubwa ya kisayansi na kiteknolojia, hivyo mafundisho na maelezo mengi ya Qur’an yameweza kufahamika vizuri zaidi. Mfano mmojawapo ni kuwa Qur’an inatufahamisha kwamba Mbingu na Ardhi zilikuwa kitu kimoja, baadaye vikaachanishwa:

12

“Je hawaoni wale waliokufuru kuwa Mbingu na Ardhi vilikuwa kitu kimoja, kisha tukaviachanisha.”(Suratil Anbiyaa aya 30).

Kwanza, neno Mbingu linawakilisha anga na vilivyomo katika eneo hilo. Pili, Kauli kwamba, Mbingu na Ardhi vilikuwa kitu kimoja inafahamisha kwamba mwanzo maumbile yote ya Ulimwengu yalikuwa katika duara moja lililoshikamanishwa. Hatimaye kauli kwamba, “Tukaviachanisha” inaweka wazi kuwa duara hilo lililipuliwa na mlipuko uliyoliachanisha katika mapande mapande mengi. Chochote kinachopingana na mafundisho ya Qur’an si sahihi na cha kutupiliwa mbali.

Katika maelezo tuliyoyaona, tunafahamu kuwa Qur’an ndiyo inayotoa maelezo ya hakika zaidi kwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa Ulimwengu na ndiye aliyeiteremsha Qur’an, kwa hiyo, Yeye anajua zaidi Alivyoumba na Alichokiumba.

UlimwenguJua, Dunia na Mwezi ni maumbile tunayo yafahamu. Yapo maumbile mengine mengi

katika anga la Ulimwengu huu ambayo hayaonekani. Anga lililo juu ya upeo wa macho lina nyota nyingi, sayari na vimondo vinavyoweza kuonekana katika picha ya kimawazo. Maumbile yanayoitwa ya angani yanajiweka pamoja chini ya mikusanyiko maalumu inayoitwa mifumo ya Jua ambayo nayo imekusanywa katika mikusanyiko mikubwa sana inayoitwa Magalaksi.

Maumbile ya angani ni makubwa mno. Ili mtu aweze kujua ukubwa wa maumbile hayo hana budi kujua kuwa sayari yetu hii ya Dunia ni katika maumbile madogo sana yakilinganishwa na maumbile mengine ya angani yaliyokusanywa na Ulimwengu. Hata hivyo, licha ya udogo wa umbile la Dunia katika maumbile yaliyoko angani, kwetu ni kubwa lenye kutosha kuwakusanya wanaadamu wote, wanyama, milima, viumbwa vingine vyote vinavyonekana na visivyoonekana (mfano majini) na kila kitu kisichoweza kukifikirika. Ametukuka Mwenyezi Mungu Muumba wa Mbingu na Ardhi.

13

Sura ya Tatu

MagalaksiMabilioni ya nyota zilizojikusanya pamoja, wataalamu wa mambo ya anga huita

Magimba au galaksi. Tunafahamishwa ya kuwa, gimba au galaksi moja kubwa kabisa linakusanya nyota trilioni tatu. Na galaksi la ukubwa wa wastani linakusanya nyota biliyoni 200 mpaka 300, wakati ambapo galaksi ndogo kabisa lina mkusanyiko wa nyota bilioni 100. Bilioni moja ni kitu gani? Kuelewa bilioni ni kitu gani, iandikwe namba moja kisha iwekwe sifuri mbili, hiyo itakuwa 100. Ikiongezwa sifuri moja mbele ya 100, itakuwa elfu, 1,000. Ikiongezwa sifuri nyingine mbele ya 1000 hiyo ni elfu kumi, 10,000. Zikiongezwa sifuri mbili katika ile 10,000, itakuwa milioni moja, 1,000,000. Zikiongezwa sifuri tatu zaidi katika hiyo 1,000,000, hapa itakuwa imefikia bilioni moja, 1,000,000,000. Na mwisho, zikiwekwa sifuri mbili zaidi baada ya namba 1,000,000,000, hapa itakuwa imefikia bilioni mia moja(100,000,000,000) ambayo ni idadi ya nyota zilizokusanyika katika galaksi iliyo ndogo kabisa. Galaksi zenye idadi hii ya nyota, nazo ziko nyingi sana. Galaksi ambamo ulimo mfumo wetu wa jua ambayo wataalamu wa mambo ya anga wanaiita “milky way” ni miyongoni mwa galaksi zenye ukubwa wa wastani.

Mpaka hapa tumeweza kuuona ukubwa wa Ulimwengu. Ni Mwenyezi Mungu Aliyeumba Ulimwengu mkubwa kiasi hicho. Mwenyezi Mungu Ameumba Ulimwengu mkubwa sana ambao hapana yeyote katika wanaadamu awezaye kuudiriki katika fikira na mawazo yake. Ulimwengu ni mkubwa sana, wanaadamu ni vijiumbile vidogo sana katika maumbile yaliyomo, ni kwa sababu hii Mwenyezi Mungu anatuuliza ili tuweze kutafakari:

“Je, nyinyi ni wenye umbo la nguvu zaidi au Mbingu? Yeye amezijenga”(Surat Anaziat aya ya 27).

Pamoja na kuumba Ulimwengu mkubwa kiasi hicho ambao nao ni sehemu tu ya maumbile yake mengi, Mwenyezi Mungu amekizunguka kila kitu Alichokiumba anakijua vyema na Amekikadiria na Analijua kila linalopitikana humo pamoja na shughuli ya kila kitu. Katika Qur’an, Mwenyezi Mungu Anatufahamisha hili:

“Na ni vya Mwenyezi Mungu tu vyote vilivyomo Mbinguni na Ardhini. Na Mwenyezi Mungu ndiye aliyevizunguka vitu vyote (4:126).

Uwezo wa Mwenyezi Mungu usiyodirikika na usiyo na Ukomo unaelezwa piya katika aya ifuwatayo:

14

“Sema: kama mkificha yaliyomo vifuwani mwenu au mkiyadhirisha, Mwenyezi Mungu anayajuwa; anayajuwa yaliyomo Mbinguni na yaliyomo Ardhini; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye Uweza juu ya kila kitu”(Al Imran aya ya 29).

Kwa yale magalaksi yenye ukubwa wa wastani au makubwa zaidi, katikati yake kipo kiini ambacho wanaanga hukiita “galactic centre” yaani kitovu cha Galaktiki. Kuzunguka “kitovu cha Galaktiki”, ipo mikondo ambayo wanaanga huiita “mikono” ambayo inazunguka kwa kasi kubwa sana. Mikondo au “mikono” hiyo imefanyika kwa mikusanyiko ya nyota, hewa na mawingu ya vumbi. Yakiwa na “mikono” na viini vyake, magalaksi ndiyo maumbile makubwa kabisa katika maumbile ya anga. Mfumo wa jua, unakusanya Jua lenyewe ambalo ni nyota na sayari zake, Sayari nazo zina miyezi, kwa mfano sayari ya Dunia ina mwezi mmoja unaoonekana uking’ara wakati wa siku za mbaamwezi. Kisha hii mifumo ya jua nayo kwa mabiliyoni inaunda galaksi moja na kuna mabilioni ya magalaksi yenye ukubwa tafauti. Galaksi kubwa kabisa linakusanya nyota zaidi ya trilioni tatu, wakati ambapo galaksi ndogo inakusanya takribani nyota biliyoni 200.

Tuliyojifunza katika mada hii ni:

Kwanza, tumeona kuwa magalaksi ni mikusanyiko ya mabilioni na hata Matrilioni ya nyota,

Pili, tukaona pia kuwa yale magalaksi makubwa au yale yenye ukubwa wa wastani yana vitu sehemu ya kati vinavyoitwa viini yaani “vitovu vya galaktiki”.

Tatu, tumeona pia kuwa “mikono au mikondo ya galaksi imefanywa kwa nyota, hewa na wingu zito la vumbi”. Na tumeona mikono hii inakizunguka kiini cha galaksi kwa kasi kubwa sana.

Tuzingatie kuwa galaksi lenye nyota bilioni moja ni galaksi dogo sana, hapa haijatajwa kuwa kila nyota ya ukubwa wa wastani ni sawa na hili jua letu. Zipo nyota zilizo kubwa kulizidi jua letu hili. Mbali ya hivyo, katika nyota hizo kuna mfuatano wa sayari nyingine zenye ukubwa sawa au kuizidi Dunia yetu.

Mabilioni haya ya nyota yaliyojiweka katika utaratibu huo wa ajabu yalikutana pamoja kwa bahati nasibu? Nyota zingeweza kwa ghafla kujiunda zenyewe na kujiweka katika utaratibu huo ambao hauna migongano kati yake na maumbile mengine?

Kwa nini, kwa mfano, Dunia yetu haijapata kugongana na sayari nyingine au kugongana na huu mwezi unaoonekana kuwa jirani yake hasa ikizingatiwa kwamba Dunia na maumbile mengine ya anga yanazunguka kwa kasi kubwa sana. Haya yote yanadhihirisha kwamba yupo Muumbaji Ambaye ni Mwenyezi Mungu aliyepanga utaratibu huo wa maumbile na kuuweka katika mpango mzuri kabisa.

15

Mwenyezi Mungu huumba bila mfanoWanaanga wamefanya kazi nzuri sana ya kuichunguza anga, hivyo wametupatia maelezo

mazuri kabisa. Utafiti wa anga umesaidia sana kuonesha ujinga wa wale wanaodai kuwa Ulimwengu huu haukuumbwa ila umetokea tu wenyewe! Kutoka wapi? Hawana jibu. Kwa kweli uvumbuzi wa Wanaastronomia pia umeonesha kuwa Ulimwengu huu umeumbwa kama kilivyoumbwa kila kiumbe. Mtu wa kwanza kabisa kuubaini ukweli huo miongoni mwa Wanaanga tukiwaacha mitume na manabii wa Mwenyezi Mungu, inaelezwa kuwa ni Bwana mmoja aliyeitwa Edwin Hubble. Mtu huyo akitumia viona mbali vyenye nguvu sana, aliweza kushuhudia nyendo za nyota. Ilikuwa mwaka 1929 Mwanaanga huyo alipobaini hilo. Mwendo wa nyota alioushuhudia Bwana Hubble haukuwa huu wa kawaida tunaouona bali aliona jinsi nyota zinavyosonga mbele mbali zaidi na sisi. Zaidi ya hivyo aliweza kuona jinsi nyota moja inavyosonga mbele na kujiweka mbali zaidi na nyingine. Kwa hiyo kutokana na kusonga mbele zaidi kwa nyota, Ulimwengu wetu huu unaokusanya kila kitu unakua mkubwa zaidi kadiri siku zinavyosonga mbele. Ni miaka isiyozidi 100 tu iliyopita tangu watu walijue hilo. Wanasayansi wote wamebaini sasa kuwa kumbe nyota zinakimbiana na kujiweka mbali zaidi, na vile vile zimeendelea kuwa mbali zaidi na Dunia yetu. Mwendo huu wa nyota ni habari muhimu sana kwa mnasaba wa kuumbwa kwa Ulimwengu huu. Ukweli huu wa nyota kuendelea kusonga mbele kutoka mahali zilipokuwa, unadhihirisha kwamba, katika wakati fulani zote hizo zilikuwa kitu kimoja. Wanasayansi hao wanakadiria kwamba zaidi ya miaka bilioni 15 iliyopita maumbile yote yaliyomo Ulimwenguni, yalikuwa kitu kimoja katika umbile mithili ya ncha ya sindano. Kwa hiyo Ulimwengu wetu ulitokea kutokana na mlipuko wa umbile hilo moja.

Tulivyoviona katika mada yetu hii:

Kwanza, tumefahamu kuwa nyota zinakwenda daima.Pili, kila nyota moja inajiweka mbali zaidi na nyingine na kujiweka mbali zaidi na Dunia

yetu hii.Tatu, iwapo itatokea zijirudishe nyuma zilikotoka tungaliweza kuona nyota hizo zikirudi

hadi kufikia kuwa kitu kimoja.Nne, hivi ndivyo itakavyoendelea hadi kufikia Ulimwengu wote kuwa kitu kimoja.

Tano, tukisonga mbele zaidi tutaona kuwa kitu hicho kimoja nacho kitafikia kutokuwepo. Kwa hiyo hii ina maana kuwa Ulimwengu wetu umetokea kwa kuumbwa na Mwenyezi Mungu. Ametukuka kweli kweli Muumba wa Ulimwengu na vyote.

Ni dhahiri kuwa sasa, itakuwa imeeleweka kuwa nini maana ya Ulimwengu kutokea pasipo kuwepo kitu. Maswali mepesi ya kujibu ni kama yafuatayo:

1. Ulikuwa na umri gani mwaka mmoja uliyopita?Huenda jibu likawa ni miaka pungufu mwaka mmoja ya miaka ya sasa.

16

2. Iwapo mtu atahesabu miaka yake kinyumenyume mwaka mmoja mmoja atapata miaka mingapi mwisho wa kuhesabu huko?

Jibu ni mwaka mmoja tu. Mwaka mmoja tu baada ya mtu kuzaliwa alikuwa na umri wa mwaka mmoja. Na wakati anazaliwa hakuwa na umri wowote. Hapa tunaweza kusema alikuwa na umri sifuri.

3. Je mwaka mmoja kabla hajazaliwa alikuwa na umri gani? Alikuwa wapi wakati huwo? Jawabu hapa ni kwamba hakuwepo katika Ulimwengu huu.

4. Na mwili wa mtu ukirudishwa kinyumenyume utaonekana ukipungua kidogo kidogo na mwisho wake utakuwa umepotea kabisa. Kila mwaka mwili utapungua kuwa mdogo zaidi na zaidi, mpaka mwisho utarejea kuwa mtoto anayesimama dede, atarejea kutambaa, atarejea kukaa, atarejea katika uchanga wa kurusharusha miguu kitandani, ukirudi nyuma tena atakuwa hawezi hata kurusharusha hiyo miguu, amekuwa kichanga kisichojimudu, kidogodogo hatimaye atapotea kabisa katika Ulimwengu, watu watakuwa hawamjui.

Mtu amfikirie nduguye aliyekufa kabla ya yeye kuzaliwa, nduguye ambaye ameona picha yake. Mtu huyo hamjui kwa kuwa hakuwepo wakati yeye akiwepo na pengine awe aliishi katika nyumba hiyo hiyo anayoishi na labda alikuwa akilala kitanda hicho hicho alicholala. Jambo muhimu hapa si kwamba umri umerudi kinyumenyume bali waliokufa waliishi na kukamilisha muda wao kwa kadiri siku zilivyokuwa zikienda. Siku moja inaposonga mbele mtu ajue muda wake wa kuishi Duniani nao unapungua, yaani anaisogelea siku ya kufa kwake, kama ilivyokuwa siku ya kuzaliwa. Kwa hiyo hapakuwa na Ulimwengu kabla ya Mwenyezi Mungu hajauumba. Iwapo tutarudisha nyuma wakati, tutaona jinsi Ulimwengu unavyorudi hadi kuwa mchanga kama ulivyokuwa awali. Utaendelea kuwa mdogo, mdogo na mwisho utapotea kabisa, utakuwa haupo. Yote haya yanadhihirisha kuwa Ulimwengu umeumbwa.

Katika mada hii tumejifunza:

- Kuna maumbile ya anga yaitwayo Galaksi- Kumbe haya magalaksi ni mkusanyiko wa mifumo ya nyota yenye umbile la mduara- Wanajimu wanakadiria kuwepo kwa magalaksi zaidi ya bilioni 300- Kumbe galaksi yetu ni katika zile zenye ukubwa wa wastani - Kumbe yako magalaksi makubwa yenye kukusanya mifumo ya nyota zenye idadi

kubwa isiyoweza kuhesabika- Mfumo wetu wa jua uko katika kiini cha galaksi yetu ukizunguka na kukamilisha

mzunguko wake kwa muda wa miaka bilioni 220.

17

Sura ya Nne

Nyota zing’arazo AnganiNyota na sayari, kama ilivyo kwa maumbile mengine, zimekuwepo kutokana na

kutokuweko kufuwatia mkandamizo wa ujazo wa gesi na vumbi vumbi katika eneo ambalo Wanaastronomia huliita “nebulae”. Nebulae au unyenyezi, ikiwa ndicho chanzo cha maumbile ya angani, ina jukumu kubwa katika Ulimwengu huu. Nyota zilizo kwenye “Nebulae” hazina mwanga kama zilivyo nyota nyingine, kwa hiyo ni vigumu sana kuziona. Nyota zilizoko kwenye Nebulae huonekana pale tu zinapoakisi mwanga kutoka nyota nyingine. Pia tunaweza kuziona pale zinapopitiwa na vyanzo vyengine vya mwanga. Nyota zina joto, mwanga na nishati. Mbali ya zile nyota ndogo ndogo, zipo nyota kubwa sana. Katika kundi hilo la nyota kubwa, jua letu nalo ni nyota lakini halimo. Jua letu limezidiwa ukubwa na nyota nyingi. Nyota nazo huishi na kufa licha ya kwamba zenyewe hazina uhai. Kama ilivyo kwa viumbwa vyenye uhai, nyota nazo huzaliwa, huishi na hatimaye hufa. Nyota hutoka kwenye unyenyezi unaotokana na Nyota kubwa iliyoishi umri mrefu ambayo baadaye hulipuka na malighafi yote iliyotumika kuumbisha nyota hiyo husambaratika kule na huko. Kutokana na msambaratiko huo hutokea vipande vipande ambavyo huzaa viasili yaani elementi ambazo hujikusanya tena kuunda nyota ndogo na sayari. Wataalamu wanatwambia kuwa mabilioni ya miaka iliyopita, Jua letu na sayari zake, ambamo ndani yake mna hii Dunia yetu, limetokea kufuwatia mlipuko wa nyota kubwa inayotoka katika kundi la unyenyezi.

Baada ya kuona asili ya nyota, hebu sasa tuingie kuutazama kwa undani kidogo mfumo wetu wa jua.

Mfumo wa JuaKatika mfumo wetu wa jua, kuna sayari nane(kabla ya watafiti wa anga kuiondolea

Pluto ilifahamika ziko tisa) ambazo kwa ujumla zina miezi 54 na vijiumbile vingine vidogo visivyo idadi. Maumbile yote hayo yanazunguka umbile moja kubwa linaloitwa jua. Juwa likiwa kubwa zaidi linalozivuta sayari zote hizo, limewekwa katikati ya mfumo huu. Ndiyo maana mfumo huu unaitwa mfumo wa jua. Sayari zote nane ambazo ni sehemu ya mfumo wa jua, hujizungusha zenyewe wakati zikilizunguka jua katika utaratibu uliopangwa vizuri. Sayari tisa zilizo katika mfumo wa jua tukianza na ile iliyo jirani kabisa na juwa; ni Mekyure, Venasi, Duniya, Maazi, Jupita, Satuni, Uranasi na Neptuni ( kabla ya utafiti mpya ya mwisho ilikuwa Pluto). Katika mpangilio huo, Dunia yetu ni sayari ya tatu kutoka kwenye jua. Hata hivyo, hayo si kwamba ndiyo majina halisi ya sayari hizo bali yametolewa na wanajimu. Kila sayari iliyo katika mfumo wa jua ina hali tafauti na nyingine. Wakati halijoto katika baadhi ya sayari hizi iko juu sana kiasi cha kuweza kuyeyusha chuma, hali ya hewa katika sayari nyingine, ni ya barafu iliyozingira sayari yote. Sayari nyingine zimezingirwa na gesi. Zaidi ya hivyo baadhi ya sayari ni ndogo sana kama ulivyo mwezi. Kuna uhusiano mkubwa baina ya umbile kubwa na

18

mfuasi wake. Kwa mfano, Dunia ni mfuasi wa jua na mwezi ni mfuasi wa Dunia. Hii ina maana kuwa Dunia inalizunguka jua na mwezi unaizunguka Dunia na kwa pamoja maumbile hayo mawili yanalizunguka jua bila ya kuachana. Kisha jua, sayari na miezi yake kwa pamoja yanazunguka kiini cha galaksi. Urari wa uvutano kati ya Dunia na mwezi ndiyo unaofanya sayari isitoke katika njia yake licha ya kuzunguka kwa kasi kubwa sana. Kwa mfano, iwapo mwezi utazunguka kwa kasi ndogo, utakuwa umeachwa na Dunia kwa kasi kubwa. Na ikitokea hali hii huu ndiyo utakuwa mwisho wa uhai katika Dunia. Kadhalika mwezi ukizunguka kwa kasi inayozidi Dunia utakuwa umekwenda mbali ya Dunia na hautakuwa tena mfuasi wa sayari hii.

Tumejifunza yafuatayo katika mada hii:- Mfumo wa jua una sayari tisa, miongoni mwa hizo ni hii Dunia- Pamoja na sayari hizo pia kuna miezi na maumbile madogo yasiyo na hisabu.

Umbile la Jua Jua ndilo umbile kubwa zaidi katika maumbile yanayounda mfumo wa juwa. Jua ni

kubwa mara 1000 ya ukubwa wa sayari ya jupita ambayo nayo ni kubwa kuliko Dunia kwa mara 318, yaani Dunia ziwe 318 ndiyo Jupita moja. Kwa hiyo Jua ni kubwa mara zaidi ya 300,000 kuliko Dunia. Yaani dunia ziwe laki tatu ndiyo ukubwa wa jua moja. Kipenyo chake tu ni kikubwa zaidi ya sayari hii ya dunia kwa mara zaidi ya 21. Jua lina joto kali lisilomithilika, vile vile lina gesi. Kwa mujibu wa wataalamu wa mambo ya anga, Jua lina kipenyo chenye upana unaokadiriwa kuwa kilometa1, 400, 000, ambao ni mara 10 ya sayari ya Jupita. Upana wa kipenyo cha Jua ni mara nne ya umbali wa kutoka Duniyani hadi kwenye Mwezi. Mzingo wa umbile la Juwa una kilometa milioni nne. Kuweza kusafiri eneo lote hili kwa ndege yenye kasi ya mara tatu ya sauti, itachukuwa miyezi miwili kukamilisha safari hiyo! Karibu asilimia 99.9 ya chembe chembe za Jua ni haidrojeni na Hiliamu. Kila sekunde ya hali ya Juani hutokea milipuko mikubwa inayolizidi bomu la Atomu kwa mara matrilioni. Milipuko hiyo hutoa macheche makubwa yanalolizidi umbile la Duniya kwa zaidi ya mara 40 mpaka 50. Juwa ni mithili ya umbile la mpira ambalo usoni mwake hutowa mwanga na joto kali na mwanga unaoziangazia sayari zote zilizo katika mfumo wake. Kwa ajili hiyo, wanaanga wanakadiria kuwa kasi ya mzunguko wa Jua katika njia yake ni ya chini kulinganisha na kasi za sayari inazoziangaziya. Kasi ya Jua kuzunguka katika Obiti yake ni kilometa 220 kwa dakika, kadhalika kasi ya jua kujizungusha lenyewe katika muhimili wake ni ndogo, huchukuwa siku 24 za dunia kukamilisha mzunguko wake mmoja.

Kama jua lisingalikuwepo, katika Dunia yetu hii, muda wote kungekuwa ni usiku au kiza totoro na Dunia yote ingalikuwa imezingirwa na barafu. Na kubwa zaidi kusingalikuwa na uhai katika ardhi. Anga ni eneo ombwe lenye kiza kikubwa. Dunia yetu ni ya umbile linaloelea katika eneo ombwe tupu hilo, kubwa na lenye kiza, ambapo hakuna umbile lolote lililo jirani lenye kuimulika, kulipa joto na mwanga mbali ya jua. Mwanga unaotoka kwenye jua ni mkali

19

sana, usiyoweza kutazamika na macho ya kawaida. Katika kipindi cha joto, miyonzi na miale ya juwa ni mikali zaidi. Hata hivyo, juwa lipo umbali mkubwa sana kutoka Duniani. Ni mamilioni ya kilometa na ni sehemu moja tu kati ya mionzi ya joto 2000 itolewayo na jua ambayo huweza kuifikia Dunia. Pamoja na umbali lilipo jua, hali ya hewa ya Dunia ni ya joto linalotosheleza.

Wanasayansi wamejaribu kufanya makadirio mbali mbali juu ya maumbile ya anga na hali iliyopo angani. Hata hivyo haiwezekani kufananisha halijoto ya juwa kwa kulinganisha na halijoto ya kitu chochote tunachokijuwa katika Dunia hii, ingawa joto lililopo katika kiini cha ndani kabisa ya dunia, linalizidi joto la uso wa juu wa Jua. Hali joto iliyopo kwenye kiini cha tabaka la ndani kabisa ya Dunia ni nyuzi za sentigredi 7,500(13,500 F). Halijoto iliyopo katika uso wa jua ni nyuzi za Sentigredi 6000 (au faranihait 11, 000), katika kiini cha kati cha tabaka la ndani la umbile la jua halijoto hufikia hadi nyuzi za sentigredi 12,000,000(21,000,000 F). Hakuna joto la kitu chochote kijulikanacho katika maisha haya, linaloweza kulinganishwa na joto hili. Mtu hushindwa kuvumilia kuweka kidole chake katika maji yachemkayo sana ambayo joto lake halizidi nyuzi za Sentigredi 50 tu (120 F). Hata katika kipindi cha joto sana, halijoto ya Dunia hufikia nyuzi 40 hadi 50(105-120 F) tu. Mfano huu unaonesha jinsi Mwenyezi Mungu alivyokadiria umbali kati ya Dunia na Jua kwa namna ya ajabu kabisa. Iwapo juwa lingalikuwa karibu kidogo na Dunia yetu, kila kitu kingaliyeyuka, kukauka kabisa na kubaki majivu. Na kama Dunia yetu ingalikuwa mbali zaidi ya hapa ilipo, kila kitu kingaliganda na kukauka kwa barafu. Na kwa hakika uhai usingalikuwepo. Maeneo ya pola ambayo hupokea mwanga na joto dogo kutoka kwenye jua yanazingirwa na barafu kali. Eneo la kati ya Dunia au lenye kupitiwa msitari wa kufikirika, unaogawa Dunia sehemu mbili, hufikiwa na miyonzi mingi ya juwa, lina joto sana. Mwenyezi Mungu Ameumba maeneo haya kama mfano kwetu. Maeneo mengine yana hali inayoimarisha uhai wa mwanaadamu. Hii inaonesha jinsi Rehema ya Mwenyezi Mungu ilivyo juu yetu. Hiyo ni kwa sababu, kama Mwenyezi Mungu asingaliuweka umbali huu kati ya Jua na Dunia ingekuwa vigumu kwa Mwanadamu kuweza kuishi. Na kwa hakika kusingekuwa na uhai ila kwa kutaka Mwenyezi Mungu.

Kama ilivyoelezwa awali, Mwenyezi Mungu Ameumba Juwa na Mwezi ili kuwezesha maisha ya Wanadamu katika sayari hii. Katika Qur’an Mwenyezi Mungu Anatufahamisha kwamba Jua na Mwezi vinakwenda na kuogelea kwa Amri yake:

“Mwenyezi Mungu ndiye aliyeziinua Mbingu bila ya nguzo mnazoziona hivi. Kisha Akatawala juu ya Arshi. Na Akaliitisha juwa na mwezi. Na kila kimoja kinaendeleya mpaka muda uliowekwa. Yeye ndiye anayeliendesha kila jambo. Anazipambanuwa aya hivi ili mpate yakini ya kukutana na Mola wenu”. (13:2).

Katika mada hii tumeona:- Umbile la jua, ukubwa na joto lake lisilo na mfano.

20

- Joto la jua ni kali mno kuweza kuyeyusha au kugeuza hata jivu kuwa na hali nyingine tafauti.

- Umbali kati ya jua na sayari iliyo jirani yake umeifanya sayari hiyo kuitwa sayari nyekundu kutokana na mwanga unaotoka kwenye jua.

-Ukali wa jua ni wa kutisha kwa sababu sayari yetu hii ya Dunia iko mbali sana na jua lakini ina joto ambalo mahali pengine huweza kuathiri.

Nguvu ya uvutano ya juaNguvu ya uvutano ya jua inazivuta sayari zote zilizo katika mfumo wa juwa. Maumbile

ya angani yasiyo na idadi yanaogelea katika utaratibu uliopangwa vyema bila ya mgongano. Mwenyezi Mungu ameweka njia maalumu zinazopitiwa na maumbile hayo ambazo wanajimu yaani wataalamu wa mambo ya anga huziita Obiti. Obiti ni njiya ambazo sayari na nyota yenye mkia hupita katika mwendo wao wa kulizunguka jua. Hakuna sayari inayoweza kupita nnje ya Obiti yake kuelekeya mahali pengine angani. Hiyo ni kwa sababu sayari zote zipo chini ya milki ya nguvu ya uvutano ya juwa. Dunia yetu inazunguka katika njia yake kwa kasi ya kilometa 108, 000(maili 70,000) kwa saa kulizunguka jua. Mifano michache yaweza kusaidia kuelewa kasi hii: Kasi ya mwisho kabisa ya gari ni kilometa 200(maili 125) kwa saa. Hii ina maana kwamba kasi ya Dunia kujizungusha yenyewe wakati ikilizunguka jua ni mara 540 zaidi ya kasi ya gari. Risasi inakwenda kasi ya kilometa 1,800 (maili 1,100) kwa saa. Kasi ya Dunia kulizunguka jua ni mara 60 ya kasi ya risasi.

Kwa sababu ya kasi hii kubwa ya mwendo wa Dunia, nguvu ya uvutano ya juwa ni muhimu sana. Iwapo jua litalegeza nguvu hiyo ya uvutano, wanaadamu watajikuta wamerushwa mbali nje ya Dunia wakiachwa wakiogelea katika anga kama ziogeleavyo sayari na maumbile mengine ya anga hali ambayo itafanya uhai usiwepo tena Duniani. Kwa upande mwingine, iwapo jua litaongeza zaidi nguvu ya uvutano, Dunia yetu pia itavutwa jirani na jua na itaungua tiki tiki pamoja na vilivyomo. Na kwa hivyo itakuwa mwisho wa uhai katika Dunia. Zaidi ya hivyo, nguvu ya uvutano ya jua vile vile hudhibiti sayari ziendelee kubaki kwenye njia zake (Obiti), zisitoke nje ya hapo na hivyo kusababisha kugongana zenyewe. Hivi jua bila ya uumbaji uliotukuka wa Mwenyezi Mungu lingeweza lenyewe peke yake kuzivuta na kuzimiliki sayari zake kwa nguvu yake ya uvutano?

Jibu la swali hilo li wazi. Ni Muumba, Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu na uwezo usiyo na mipaka, Ambaye Ameumba na kuweka vipimo vinavyoendelea kuweka urari asilia wa maumbile. Mbali ya hilo, si jua pekee lenye nguvu inayovuta bali Sayari zilizomo kwenye mfumo wa jua letu nazo kadhalika zina nguvu za uvutano . Kwa mfano, nguvu ya uvutano ya Dunia inauvuta na kuudhibiti mwezi. Kwa sababu ya nguvu hii ya uvutano, mwezi umedhibitiwa kukaa umbali maalumu. Kwa namna hii, Dunia haiwezi kugongana na mwezi. Bila shaka, yote haya hayawezi kujifanyiza yenyewe bali ni Muumba aliyeweka mpango huu na kuudhibiti kwa sheria na kanuni za kimaumbile alizoziweka. Ni Mwenyezi Mungu Anayeuzuia

21

mwezi usianguke juu ya Dunia na si Mwezi unaojizuia kwa kujiwekea wenyewe kanuni hizo! Ipo nguvu nyingine inayovuta ifananayo na hiyo ya Jua, iliyowekwa kuwawezesha Wanaadamu kuishi. Hiyo ni nguvu iliyomo ndani ya ardhi inayowapa wanaadamu uzito. Nguvu ya uvutano inayowapa uzito, huwafanya wabaki katika hii Ardhi, kuwawezesha kutembea na kukimbia kwa urahisi bila ya kutoka katika eneo la Ardhi.

Hebu tujaaliye, tumeshika mipira mikononi mwetu; kisha tuwe tumeiyachia mipira hiyo. Tujiulize nini kitatokea? Kwa hakika mipira hiyo itaanguka chini kwa sababu kuna uvutano unaoelekeza kila kitu kurejea chini katika ardhi. Lakini, ukitoka nje ya duara ya sayari hii ya Dunia ukiwa umeshika mpira huo kisha ukauwachia, hautaanguka chini bali utaelea kwa kuwa kuna nguvu ndogo ya uvutano. Kuwepo kwa nguvu ya uvutano ndani ya ardhi ni muhimu sana kwetu. Lipo jambo jengine muhimu la kuzingatiya. Nguvu ya uvutano haitakiwi ipungue au izidi hii iliyopo. Iwapo itakuwa ndogo, wanaadamu watakuwa wakitembea hewani na hawataweza kuigusa Ardhi kwa miguu yao. Hawataweza kutembea wanavyotaka, watakuwa wakienda kwa kurukaruka kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Vivyo hivyo, nguvu ya uvutano ya Dunia ingalikuwa kubwa zaidi ya hii, watu wasingaliweza kutembea kwa sababu wangaligandamizwa chini Ardhini. Kitu ambacho wangeweza kufanya pengine, ni kusota na kujiburuza kwenye udongo. Hayo yote hayawezi kutokea ila ni kwa sababu ya Rehema ya Mwenyezi Mungu, Muumba ambaye Ameumba na kukadiria nguvu zinazowezesha maisha yawezekane katika Dunia hii. Ili kulifahamu vyema somo hili, hebu tuchukuwe mfano ufuatao: Mwezi, kama Dunia, una nguvu ya uvutano. Hata hivyo, nguvu hii ya mwezi ni ndogo kuliko ile ya Dunia. Kwa sababu hiyo haiwezekani kwa mwanaadamu kuishi katika mwezi. Katika ile picha ya Apollo 11, wanaanga waliotua mwezini mwaka 1969, wanaonekana jinsi wanavyotembea kwa kunyata na kurukaruka wakilazimika kutembea kwa hatua ndogo. Iliwalazimu wanaanga wale kutembea hatuwa ndogo sana tena kwa taratibu sana ili wasiruke ruke zaidi. Ni vipi Wanaadamu wangaliweza kuishi katika mazingira hayo bila ya idhini ya Mwenyezi Mungu?

Katika mada hii tumeona:

- Nguvu za uvutano kati ya jua na sayari na kati ya sayari na miezi jinsi zinavyofanya mpango wa maumbile hayo uende kama ulivyopangwa bila ya kutokeya mgongano wowote.

- Ni Mwenyezi Mungu aliyeweka urari asilia wa maumbile ya anga unaoyawezesha kuogelea katika Obiti zao bila ya kwenda mbali ya hapo.

- Sayari ni maumbile ya anga yanayojizungusha yenyewe katika mihimili yake na wakati huo huo kuzunguka nyota kubwa zilizo katikati yao.

- Juwa ni nyota kubwa inayozungukwa na sayari pamoja na jumla ya miezi zaidi ya 54 iliyopo katika sayari zote zilizomo katika mfumo wetu wa jua.

22

Sura ya Sita

Sayari zinazozunguka kwenye mfumo wetu wa juwa

PlutoMfumo wetu wa jua ni kama duara. Kwa hiyo, jua ndilo lililo katikati. Katika maduara

hayo, Pluto inakuwa katika duara ya mwisho kabisa mithili ya mizunguko ya chembe za Elektroniki inayofanya maduwara katika chembe za Atomu. Pluto ambayo awali ilifahamika kama sayari kabla ya utafiti mpya kuiondoa katika kundi hilo, ni umbile dogo kabisa na lililo mbali zaidi kutoka kwenye Jua. Kuweza kuichunguza Pluto imekuwa vigumu sana kwa Wanaanga kwa kuwa hata ile darubini kubwa kabisa ya Mwanaanga Hubble iliweza kuonesha sehemu tu ya umbile hilo dogo. Pluto imezingirwa na baridi kali sana inayoifanya iwe barafu kabisa. Kipimo cha halijoto yake kinakadiriwa kuwa nyuzi hasi za sentigredi 238 (ambayo ni sawa na nyuzi hasi 396 za Faranihait). Katika kipindi cha baridi ambapo halijoto ya Duniani hushuka hadi nyuzi hasi mbili au tatu Sentigredi( ambayo ni sawa na nyuzi hasi 28 au 26 za Faranihait), Pluto huganda kabisa. Nyuzi hasi 238 za sentigredi ni hali ya baridi kali kuizidi mara 100 ile hali ngumu kabisa ya baridi ya Duniya ambayo watu huweza kuihimili nyakati za baridi. Hali ya hewa iliyopo kwenye umbile la Pluto ikijitokeza hata kwa sekunde chache tu hapa Duniani basi hapatakuwa na uhai. Kutokea nje, Pluto inaonekana kama mpira uliosilibwa au kuzingirwa na barafu. Pluto iko mbali zaidi katika mfumo wa jua. Hapana kiumbe hai kinachoishi katika Pluto. Mwenyezi Mungu ndiye ajuaya zaidi.

NeptuniKutoka Pluto kulielekea jua, tunakutana na sayari iitwayo Neptuni. Sayari hii vile vile

ina hali ya hewa ya barafu ambapo uso wake una halijoto ya nyuzi hasi za sentigredi 218( nyuzi hasi za Faranihait 360). Angahewa yake imekusanya gesi za sumu kwa uhai wa wanaadamu. Hii ni mbali na yale matufani mabaya sana yenye ukubwa unaofikia kilometa 2000 (Maili 1250) ambayo huanguka juu ya uso wa sayari hiyo kila baada ya saa moja. Kwa hiyo hakuna uwezekano wa kuwepo uhai katika sayari hiyo ila kwa yale ayajuayo Mwenyezi Mungu.

UranasiKutoka sayari ya Neptuni kusonga mbele kidogo kulielekea jua katikati ya duara hili la

mfumo wa jua, tunakutana na Sayari ya Uranas. Uranas ni sayari ya tatu kwa ukubwa katika mfumo wetu wa jua. Halijoto ya angahewa yake inakaribia nyuzi hasi za sentigredi 214(sawa na nyuzi hasi 353 za Faranihait), hii ina maana kuwa hali ya hewa ya sayari hii vile vile ni baridi kali kuweza kumfanya Mwanaadamu agande kwa muda wa sekunde moja tu. Angahewa

23

yake imekusanya gesi za sumu ikionesha dhahiri kuwa hakuna kiumbe hai kinachoweza kuishi katika sayari hiyo, kwa kiwango cha ujuvi wa mwanaadamu.

SatuniTukiendelea mbele zaidi kulielekea jua kutoka Sayari ya Uranasi, tunaikuta Sayari ya

Satuni. Kipenyo chake ni kilometa 120,500. Ukubwa wake ni sawa na maumbile 95 yenye ukubwa wa Dunia. Hii ni sayari ya pili kwa ukubwa katika mfumo wetu wa jua. Ni sayari ya aina yake kwa kuwa imezungukwa na liduara kubwa lenye umbile la taili la baiskeli. Duara hilo lililozunguka Sayari ya Satuni limefanyika kwa gesi, majabali na barafu. Halijoto katika sayari hiyo vile vile haiwezeshi kuwepo uhai wa Mwanaadamu na viumbwa vinavyofanana na yeye. Ina nyuzi hasi za sentigredi 178 (sawa na nyuzi hasi 288 za Faranihait).

JupitaTukisogea mbele kulikurubia jua kutoka sayari hiyo ya Satuni, tunaikuta Sayari kubwa

zaidi katika mfumo wetu wa jua inayoitwa Jupita. Kipenyo cha sayari ya Jupita ni kilometa 143,000. Kipenyo hiki kinaizidi cha Dunia kwa mara 11. Hata hivyo kipenyo cha Jupita kinazidiwa na kile cha Jua kwa mara 10 zaidi. Ukubwa wa Jupita ni sawa na maumbile 318 ya ukubwa wa Dunia. Nayo Jupita inaingia mara 1000 kwa juwa. Hali ya hewa katika sayari hii vile vile haioneshi uwezekano wa kuwepo uhai kwa Mwanaadamu na viumbwa afafananavyo ila kwa alitakalo Mwenyezi Mungu. Ina hali ya hewa ya baridi kali mno.

MaaziKutoka Sayari ya Jupita kuelekea kwenye Jua, inafuata Sayari ya Maazi. Maazi ni Sayari

yenye ukubwa wa baina ya ukubwa wa sayari za Venasi na Dunia. Ni sayari iliyokufa isiyoweza kufananishwa sana na Dunia. Utafiti wa hivi karibuni ambao umewezesha kufikisha chombo cha anga kwenye sayari hiyo umeweza kuchimbua mchanga wake na kujaribu kuuoanisha na ule wa dunia, hata hivyo walichoweza kusema watafiti wa mradi huo ni kwamba kama udongo huo ungalikuwa na hali ya hewa ya dunia basi ungaliweza kuotesha maboga na jamii ya mamung’unya. Aidha wako katika kufikiria kubadilisha usemi wa “kuwepo uhai” badala yake kuangalia uwezekano iwapo ardhi hiyo inaweza kuruhusu mwanaadamu kuishi kwenye uso wake. Sayari ya Maazi haina uhai huu tuujuao kwa elimu zetu za maumbile. Sababu, Mosi, angahewa yake ina mchanganyiko wa sumu na hewa nyingi ya Kaboni dayoksaidi, pili, sayari hiyo haina sehemu kubwa ya maji yaliyotuwama, kupwa na kujaa au yatiririkayo kama ilivyo katika sayari ya Dunia. Tatu, halijoto katika Sayari ya Maazi inafikia nyuzi hasi za sentigredi 53(ambayo ni sawa nyuzi hasi 63 za Faranihait). Mwisho, ina kipindi kirefu cha upepo mkali wenye dhoruba na tufani za michanga, ambacho huisha baada ya miezi kadhaa. Hali ya hewa ya sayari ya Maazi haitabiriki hubadilika ghafla. Hata hivyo, kwa kuwa Maazi ni sayari inayoikaribia Dunia, zimekuwepo jitihada za Wanasayansi wa mambo ya angani, kujaribu kujuwa kulikoni kwenye Maazi, pengine kuangalia iwapo kuna uwezekano wa mtu kutoka Duniyani kwenda kuishi kwa masiku kadhaa katika sayari hiyo. Watafiti wa taasisi

24

ya NASA tayari wameshatuma chombo ambacho baada ya safari ndefu ya Kilomita miliyoni 106 kilitua katika sayari hiyo na tangu wakati huo kimekuwa kikifanya uchunguzi, uchimbuzi na kurejesha taarifa Duniani kupitiya taasisi hiyo. Baadhi ya taarifa zilionesha kuwepo kwa hali ya unyevunyevu na mvuke ukiashiria pengine kuwepo maji hapa na pale. Hata hivyo kwa mujibu wa uchunguzi uliofanyika awali, ilionekana kuwa maji yaliyoko katika angahewa ya Maazi yangeligandishwa kuwa barafu basi yangelifikia ujazo wa mchemraba wa kilometa moja kwa upande mmoja kulinganisha na yaliyoko katika angahewa ya Duniani yenye kufikia ujazo wa mchemraba wa Kilometa 1000 kwa upande mmoja.

DuniaKutoka Maazi kulielekea jua, inafuata sayari ya urujuwani iitwayo Dunia. Kipenyo cha

Dunia kinazidiwa kwa mara 11 na kile cha Jupita ambapo kipenyo cha Jupita kinazidiwa na cha jua kwa mara 10. Tutaitazama kwa urefu sayari hii katika sura ya mwisho ya kitabu hiki. Hata hivyo, hebu tujikumbushe nukta moja tu muhimu sana kuhusu sayari ya Dunia. Dunia yetu ndiyo sayari pekee yenye hali ya hewa na mazingira yanayowezesha viumbwa hai kuishi.

VenasiKutoka sayari hiyo ya Dunia ambamo Wanaadamu na viumbwa vyengine vinaishi

kulielekea jua kidogo, utafiti unatupeleka hadi kwenye sayari inayoitwa Venasi ambayo ni sayari ing’arayo sana katika mfumo wetu wa jua baada ya Jua lenyewe na Mwezi. Kwa mng’aro huo, tangu zama za kale watu wameweza kuigundua sayari hiyo. Japo ipo mbali sana kama ilivyo Sayari ya Satuni ambayo watu wameweza kuifahamu vyema nyakati zote za historia ya Mwanaadamu, sayari ya Venasi imejulikana zaidi kwa ule mng’aro wake nyakati za asubuhi na jioni angani. Kinyume na sayari nyingine, hali ya hewa ya Venasi ni joto sana. Halijoto katika uso wake ni nyuzi za sentigredi 450(sawa na nyuzi 840 za Faranihait), ambayo inatosha kabisa kuyeyusha chuma. Jiografia nyingine ya sayari ya Venasi ni angahewa lake lenye tabaka zito la hewa ya Kaboni dayoksaidi. Mbali ya hilo, angahewa ya Venasi ina matabaka mengine ya asidi kilometa kadhaa katika kina chake. Hakuna kiumbe chochote kinachoweza kusalimika japo kwa sekunde moja katika mazingira haya. Kwa hiyo hali ya Sayari hii haiwezeshi kuwepo uhai kama unavyojulikana na elimu ya maumbile aliyojaaliwa mwanaadamu.

MekyureKutoka katika sayari ya Venasi, kuna sayari ya Mekyure, sayari iliyo jirani na Jua.

Mzunguko katika muhimili wake ni wa pole pole sana kutokana na ukaribu wake na Juwa ambapo Sayari hiyo huweza kujizungusha mara tatu tu kikamilifu katika mizunguko yake miwili ya kulizunguka Jua. Hii ndiyo sababu, upande mmoja wa sayari hiyo kuwa na joto kali sana na upande mwingine kuwa na baridi kali sana. Tafauti ya hali ya hewa kati ya usiku na mchana katika Sayari ya Mekyure ni nyuzi za sentigredi 1,000(sawa na nyuzi 1800 za faranihait). Mazingira hayo kwa hakika hayawezi kuruhusu kiumbe kilicho hai kuishi ila kwa

25

elimu ya Mwenyezi Mungu. Utafiti kuhusu sayari hizi zilizopo angani katika mfumo wetu wa jua, unaonesha kuwa kumbe ni sayari ya Dunia tu yenye kuwezesha uhai kwa viumbwa. Sayari zote zilizobaki hazina uhai na ni maumbile yasiyo na shughuli zinazofanana na hizi za Duniani. Ni maumbile yaliyo kimya kabisa. Dunia yetu ina kila kinachohitajiwa kwa uhai wa Mwanaadamu. Ina misitu ya kijani na kirujuwani katika bahari, chanikiwiti katika mimea na nyasi. Kwa hiyo kutokeya mbali inaonekana kuwa eneo maridhawa. Wanaanga wa mwanzo kabisa kwenda mwezini walishangazwa na uzuri wa Dunia kwa jinsi walivyokuwa wakiitazama kutokea huko ikionekana yenye rangirangi za kung’ara.

Katika mada hii tumeona kuwa:

- Sayari zilizo katika mfumo wa jua kuanziya Pluto hadi Mekyure.- Sayari hizo ziko chini ya himaya ya juwa zikizunguka katika njiya zao huku kila moja

ikiwa na hali ya hewa na mazingira tafauti na nyingine. - Sayari zote zilizoitangulia Dunia, zina halijoto kali sana, hivyo haiwezekani kuwepo

uhai katika mazingira yake. - Sayari zote zinazoifuwatiya Dunia, zina hali ya hewa ya baridi kali sana na nyingine

kuzingirwa kabisa na barafu.

26

Sura ya Saba

Maumbile mengine ya angaMaumbile mengine ya anga yaliyo katika mfumo wetu wa jua ni pamoja na nyota yenye

mkia, vijiumbile vidogo vinavyoitwa asteroyid na vimondo. Hayo ni maumbile ya anga yaliyoendelea kuwepo yakitokana na unyenyezi ambao mfumo wetu pia ulitokana nao miaka inayokadiriwa na Wanaastronomia kufikia bilioni sita iliyopita . Hii ni kwa mujibu wa hesabu zetu za Dunia.

Nyota yenye mkiaNyota zenye mkia zimeumbwa kwa gesi iliyoshikamana barabara na vumbi. Njia zao

huzifanya zipite karibu zaidi na juwa. Kadiri Nyota hiyo inavyolikurubia juwa ndivyo uso wake unavyotoa mvuke zaidi kutokana na mwanga mkali wa jua. Mvuke huu huifanya ing’are zaidi. Duara kubwa la gesi na vumbi hujitokeza zaidi katika kiini chake. Duara hili la gesi na vumbi, wanajimu, huliita Koma. Pia kuna mkia ambao nao umeumbwa kwa gesi, ukiwa umetokezeshwa nyuma ya umbile hilo.

AsteroyidiAsteroyidi ni vijabali vidogo vinavyokwenda kasi na kuanguka huku vikitoa mwanga

mkali. Vingi ya vijabali hivi huonekana katika eneo lililo kati ya sayari za Maazi na Jupita. Baadhi ya vijabali hivyo vina ukubwa unaofikia kilometa 1000(maili 620).

Vimondo Hivi ni vijiumbile vigumu vinavyoanguka katika angahewa yetu kutoka anga za mbali.

Vipande vipande vya vijabali ambavyo ni mchanganyiko wa chuma, hujitenganisha kutoka kwenye nyota na vimondo vikubwa. Wakati mwingine Dunia inapopita kwenye wingu la vumbi masalio yatokanayo huungua katika angahewa yetu. Huungua yanapoingia katika angahewa ya Dunia na kupita kasi yakiacha msitari mrefu wa mwanga yanapoelekea kuanguka. Mara nyingi hali hii hushuhudiwa nyakati za usiku. Hivi ndivyo vimondo. Wakati mwingine visipoungua kikamilifu, vimondo hivi huweza kuanguka Duniani. Vimondo vinavyoanguka katika angahewa ya Dunia wanajimu huviita Aeroliti na Meoriti. Kwa kawaida, Vimondo vinavyoingia katika angahewa ya Dunia huweza kuanguka Ardhini. Vikianguka huweza kusababisha uharibifu kulingana na ukubwa wa kimondo chenyewe. Dunia yetu imezungukwa na hatari ya kulipuliwa na Vimondo kila baada ya dakika moja, lakini Mwenyezi Mungu ameyaumba maumbile hayo kwa namna ambayo huungua na kuharibika yakiwa katika angahewa, hivyo hayawezi kusababisha hatari yoyote. Hii inaonesha ni kwa kiasi gani Rehema ya Mwenyezi Mungu ilivyo juu yetu. Ni Mwenyezi Mungu aliyeyaumba maumbile hayo na kuyadhibiti yawe makubwa au madogo, na anayeyaendesha yote na kwa muda wote kwa mpango na utaratibu maridhawa kabisa.

27

Katika mada hii mafunzo tuliyoyapata ni:

-Maumbile mengine ya anga yakiwemo vimondo, nyota yenye mkia na vijiumbile vingine vidogo.

- Majina yanayotumika kufahamisha sayari yanatokana na lugha ya kigiriki.- Kwa mkosi mkubwa sana Wagiriki walizinasibisha sayari hizi na majina ya miungu

yao. - Zamani, Wagiriki walikuwa watu wanaoamini miungu mingi kila mungu

wakimnasibisha na jukumu fulani. - Sayari ya Mekyure ilinasibishwa na biashara. Kwa hiyo Mekyure ni mungu wa

Kiroma anayehusika na mambo ya biashara kwa Warumi wa jadi hizo. - Venasi ni mungu wa mapenzi. Maazi mungu wa vita, Neptuni ni mungu anayetawala

bahari, Pluto ni mungu wa chini ya Ardhi, - Jupita ni Mfalme wa miungu yote ya Kigiriki, ama Satuni na Uranusi majina ya

miungu ya kale kabisa ya wahenga wa kigiriki.

28

Sura ya Nane

Sayari ya Dunia Mpaka karne ya 16, miaka 500 iliyopita, watu wengi walikuwa hawafahamu kuwa

Dunia ni sayari. Hata hivyo utafiti na uvumbuzi wa mambo ya anga uliokuja kufanyika baadaye, ukawafahamisha wanaadamu wengi kuwa kumbe Dunia nayo ni sayari. Katika karne ya 20, wanaadamu mbali ya kujua Dunia pia ni sayari waliweza kubaini mahali ilipo na mkao wake katika mfumo huu wa jua wenye sayari tisa. Dunia ni Sayari ya tatu kutoka kwenye Jua na ni sayari ya tano kwa ukubwa katika Sayari hizo nane, kipenyo chake kinadiriwa kuwa cha ukubwa wa kilometa 12, 756. Kwa mujibu wa Wanaastronomia, Dunia inazunguka katika njia yake kwa kasi ya maili 70,000 kwa saa moja, maili 1166 kwa dakika moja na maili 19 kwa sekunde moja. Hii ni kasi kubwa mno mtu kuweza kuihisi lakini hata hivyo wanaadamu wanaendesha maisha yao katika Sayari hii inayokwenda kwa kasi hiyo kali bila ya kuhisi kama wanasafirishwa! Vile vile Wanasayansi wanaamini kwamba Dunia ina kiini chenye madini ya chuma ambacho halijoto yake ni nyuzi za sentigredi 7, 500(ambazo ni sawa na nyuzi za faranihait 13,500). Joto hili ni kubwa sana zaidi ya lile la uso wa juu wa jua. Hata hivyo kwa sababu haiwezekani kuhisi japo chembe ya joto hili kubwa sana la kiini cha Dunia, ndiyo maana watu wanaweza kuishi na kuendesha shughuli zao za kila siku bila ya kuhisi ukubwa wa joto hilo. Hii inatokana na gamba la Dunia kuwakinga na kuwahami na joto hilo kubwa ambalo lingeweza kuwayeyusha mara moja. Ni kutokana na Rehema za Mwenyezi Mungu, Dunia imeumbwa na gamba hilo liwezalo kukinga nguvu ya joto ya kiini cha Dunia isiweze kupenya na kuwafikia wanaadamu. Mwenyezi Mungu Ameumba angahewa inayoendana na maumbile ya wanaadamu. Kadhalika Ameifanya mimea iwe na hali inayoweza kutoa na kuhifadhi hewa ya Oksijen kwa ulingano wenye urari na ile ya Kaboni Dayoksaidi. Umbile hili la Dunia na urari wake huo maridhawa unabainisha ya kwamba umeumbwa kwa namna inayowawezesha wanaadamu kuishi. Angahewa na jiografia yake, tangu umbali wa kutoka kwenye Jua mpaka katika aina zote za uwiyano katika mivutano yake, Dunia inathibitisha kuwa imeumbwa makhsusi kuwezesha maisha ya Wanaadamu na viumbwa vyengine alivyoumbiwa avitumiye:

“Yeye Ndiye aliyefanya Ardhi iwe inatumika kwa ajili yenu. Basi nendeni katika pande zake zote na kuleni katika riziki zake, na kwa yeye ndiyo marejeo”(67:15).

Ili kuelewa hilo vyema, tuchukuwe mfano wa tangisamaki ili kutazama uwezekano wa uhai wa wanaadamu katika sayari hii ya Dunia. Ili tangisamaki liweze kuhifadhi samaki, mimea mingine ya bahari pamoja na viumbwa vyengine, lazima liwe na hali inayoendana na maumbile ya samaki au viumbwa kama hivyo. Kwa mfano iwe na themostati yaani kirekebishi cha joto chenye kazi ya kutunza halijoto katika maji yanayoweza kuhifadhi uhai wa viumbwa hivyo. Katika tangisamaki hilo pia kuwe na mota yenye kuingiza na kutoa hewa na mchanga chini yake. Pia kutahitaji kuwekwa tembe maalumu katika maji hayo. Pia pawepo na gamba la

29

kulikinga tangisamaki hilo, mfumo wa uchujaji wa maji yanayoingia na kutoka humo na pia kiwepo chakula muda wote. Yote hayo ndiyo yenye kuwezesha samaki kuishi katika tangisamaki hilo. Hata hivyo, samaki waliyomo humo hawatakuwa na khabari na mazingira hayo ya kuigiza. Muda wote watakuwa wakijihisi wako katika mazingira yale yale ya asili, mazingira yanayoonekana kana kwamba yamezuka tu ghafla. Hawafahamu kuwa jamaa mmoja ametengeneza tangisamaki lenye kirekebishijoto na kuweka sawa viwango vya maji. Vile vile kuwe na mota inayowezesha kuingia kwa hewa na kutoka kwa kiwango kinachoendana na maumbile yao. La kuzingatia hapa ni kuwa samaki hawa wafugwao huku wakielea huko na kule katika matangisamaki hawajui nani aliyewawekea vyakula vinavyoonekana katika kina cha maji yaliyomo. Kwa mfano huu, itakuwa imeeleweka kuwa, chanzo cha vyote hivyo ndani ya tangisamaki hilo, ni yule anayewafuga samaki hao akiwapa kila wanachokihitajia.

Kwa hiyo, ni wazi kuwa maisha katika Dunia hii yanahitaji mifumo makini zaidi kuliko ile ya tangisamaki. Mwanaadamu mwenye busara hawezi kuendesha maisha yake katika Dunia hii kwa ujinga kama ule wa samaki katika tangisamaki. Anajua kuwa ardhi iko pale tayari ikiwa imeumbwa kwa ajili yake, huku akimzingatia yule Aliyeiumba na kuimiliki kama vile yeye anavyoweza kumiliki lile tangisamaki lenye samaki wanaoishi wakiogelea huku na kule, wakivuta hewa na wakila chakula kilichomo, vyote vikiwa vimewekwa na mwenye tangisamaki hilo. Mwenyezi Mungu Ameumba Dunia na maumbile mengine akaweka mizani makini na kuweka utaratibu na mpango madhubuti katika maumbile hayo kuwezesha kuweko uhai katika Dunia hii.

Mtu mwenye akili timamu lazima atataka kumjua Mwenye kumiliki vyote hivi akijaribu kujisaili kuwa nini angepaswa kumfanyia Muumba huyo. Katika Qur’an, Mwenyezi Mungu Anataka watu wamjue Yeye na wayajue yale yanayotarajiwa wayafanye. Muumba ameweka mizania na utaratibu makini unaofanya uhai uwezekane katika sayari hii:

“Na Mbingu Ameziinua juu na Ameweka humo mizani” (Suratil Rahman :7)

“Na Tukaweka katika Ardhi milima ili isiwayumbishe na Tukaweka humo mabonde yawezeshayo njiya za kuwaongoza. Tukaifanya Mbingu kuwa dari iliyohifadhiwa...(Suratil Anbiyaa 31-32).

Uwiano unaofanya maisha yawezekane DunianiMambo ambayo tumeyataja mpaka sasa ni machache tu katika uwiano ambao ni muhimu

kwa maisha hapa Duniani. Tukiichunguza Dunia, tunaweza kutengeneza orodha ndefu ya “vigezo muhimu ili kujaribu kuonesha uwezekano wa maisha” katika Dunia. Mwanaanga wa Kimarekani Hugh Ross aliandaa orodha yake ndefu ya mambo yenye kuonesha mpangilio na uwiano madhubuti unaowezesha maisha:

30

1. Uvutano katika uso wa dunia -Ungekuwa na nguvu zaidi: angahewa lingehifadhi gesi ya nyingi ya ammonia ambayo ni

sumu isiyowezesha maisha katika Dunia

-Ungekuwa dhaifu zaidi: angahewa la duniya lingepoteza maji mengi kupita kiasi

2. Umbali kutoka kwenye Jua-Ungekuwa mkubwa sana: Dunia ingekuwa baridi mno-Ungekuwa mdogo sana:Dunia ingekuwa na joto mno

3. Unene wa gamba la Dunia;-Lingekuwa nene sana:Oksijeni nyingi zaidi ingehamishwa kutoka kwenye angahewa

kwenda kwenye gamba.

-Lingekuwa jembamba sana:Volkeno na matetemeko yangekithiri.

4. Kipindi cha Mzunguko;-Kingekuwa kirefu sana: Tafauti za jotoridi wakati wa mchana ingekuwa kubwa zaidi.-Kingekuwa kifupi sana: Msukumo wa pepo za angahewa ungekuwa mkubwa sana

5. Muingiliano wa nguvu za uvutano na mwezi;-Ungekuwa mkubwa: Athari za mawimbi kwenye bahari, angahewa na kipindi cha

mzunguko kingekuwa kikubwa mno.-Ungekuwa dhaifu: Mabadiliko ya nafasi ya Obiti yangesababisha kutotengamaa kwa

majira na misimu.

6. Eneo la uvutano wa sumaku-Lingekuwa na nguvu sana: Dhoruba za elekromagnetiki(Umeme -sumaku) zingekuwa

kali sana.-Lingekuwa dhaifu: Kusingekuwa na ulinzi wa kutosha wa kuzuia ‘miale’ mikali kutoka

kwenye jua na nyota nyingine.

Uwiano wa mwanga unaoakisiwa na kiasi chote cha mwanga kinachoangaza kwenye uso wa Dunia:

-Ungekuwa kubwa: vipindi virefu vya barafu vingetokea -Ungekuwa pungufu: “athari za greenhouse ” zingetokea

7. Uwiyano wa Oksijeni na Naitrojen kwenye angahewa;-Ukiwa mkubwa: Mpangilio wa maisha ungekwenda kwa haraka-Ukiwa mdogo: Mpangilio wa maisha ungekwenda taratibu.

31

8. Kiwango cha tabaka la Ozoni katika angahewa:-Kingekuwa kikubwa: jotoridi katika uso wa Dunia lingekuwa chini mno.-Kingekuwa pungufu: jotoridi katika uso wa Dunia lingekuwa juu sana.Mitetemo ya ardhi -ingekuwa mikubwa: Maisha yangeharibika-Ingekuwa pungufu: viinilishe vya chini ya bahari visingezungushwa mabarani kote

kupitia mitetemo.

Haya ni baadhi tu ya mambo yenye kuonesha mpangilio wa lazima ili maisha yawezekane na kuendeleya Duniani. Vigezo hivi vinatosha kuthibitisha kwamba dunia haikutokea kwa bahati nasibu wala kwa mtiririko wa matukio ya kubahatisha. Mwenyezi Mungu ameweka mpangilio, uwiano, mizania na urari unaowezesha kila kiumbwa kuendana na chengine chini ya mtandao mmoja. Kila anayebaini ukweli huu lazima aamini kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, uwezo wake usiyo na ukomo na kwa hivyo awe mwenye kushukuru kwa vyote alivyopewa. Kushukuru huko ni kumcha Yeye katika mzunguko wote wa maisha ya mtu ya kila siku.

Katika mada hii tumejifunza:

- Katika karne ya 20, wanaadamu mbali ya kujua kuwa Dunia ni sayari, piya waliweza kubaini mahali ulipo mkao wake katika mfumo huu wa juwa wenye sayari tisa.

- Piya walibaini kuwa Dunia ni Sayari ya tatu kutoka kwenye Jua na ni Sayari ya tano kwa ukubwa katika Sayari hizi tisa.

- Umbile la Dunia na urari wake huwo maridhawa unathibitisha kwamba umeumbwa kwa namna inayowawezesha Wanaadamu kuishi.

- Tangu angahewa na jiografia yake, umbali wa kutoka kwenye Jua hadi kwenye aina zote za uwiano katika mivutano yake, Dunia inathibitisha kuwa imeumbwa makhsusi kuwezesha maisha ya Wanaadamu.

32

Sura ya Tisa

Mahali ilipo Dunia katika Ulimwengu Swali ambalo kila mwenye kutafakari juu ya maumbile ya angani hangekosa kujiuliza ni

hili; je ingekuwaje kama Dunia ingekuwa jirani kidogo na Jua? Jibu la swali hili li wazi. Kila mtu anajua ya kwamba joto la Jua ni kali mno na lenye kuweza kuyeyusha kila kichopo katika ardhi hii. Kwa hakika kama Dunia ingekuwa jirani na Juwa ingefanya angahewa kutokuwepo pamoja na bahari zote. Halijoto ingekuwa ya juu sana kiasi kwamba maji yote ya Dunia yangetokota kwa mchemko. Kwa maana hiyo kusingalikuwa na saliyo la maji katika ardhi. Kwa hiyo, hali ya Dunia yote ingekuwa kavu kama ile ya jangwani. Kwa mfano tumeona kuwa sayari ya Venasi iko jirani na juwa kuliko sayari yetu. Kwa hiyo, halijoto ya sayari ya Venasi ni ya juu zaidi kuliko ya Duniya. Kwa nyakati nyingine, hali hii ya joto ya Sayari ya Venasi hupanda na kufikiya nyuzi za sentigredi 475 (sawa na nyuzi za Faranihait 885). Ili kuweza kuhisi kiasi cha joto kubwa kinachoelezwa na nyuzi hizo za sentigredi, hebu mazingatio yapelekwe kwenye sifuriya lenye maji yaliyobandikwa jikoni yakachemka na kufikiya nyuzi 100 za sentigredi.

Hebu sasa piya tufikirie kinyume chake. Je kama Duniya hii ingekuwa mbali sana kutoka kwenye jua? Kwa jinsi hii, Dunia yetu ingepokeya joto dogo sana. Mtu anaweza kuhisi iwapo ingekuwa hivi, sehemu kubwa ya Dunia ingaliganda na kugeuka barafu. Uso wa Dunia nao ungekuwa hauna kitu ukifanana na ule wa sayari ya Maazi iliyo mbali kidogo kutoka kwenye jua kulinganisha na Dunia. Kwa maelezo hayo tunaweza kuhitimisha kwamba: Dunia yetu iko mahali ambapo ndipo hasa palipokadiriwa na kukusudiwa iwepo. Kama hivyo ndivyo, je yaweza kufikiriwa hili lilitokeyaje? Je mpango huu maridhawa waweza kutokea kwa bahati nasibu? Dunia yetu iwe imejiweka mahali hapo ilipotakiwa iwepo kuwezesha viumbwa kuishi ndani yake? Kwa hakika bahati nasibu haiwezi kupanga utaratibu huwo. Dunia ni umbile au sayari isiyojitambua. Kwa hiyo isingaliwezekana kwa umbile hilo lisilojitambua kuweza kujiweka lenyewe mahali lilipo kwa usahihi mkubwa kiyasi hicho. Ukweli ni kwamba mkao wa Dunia mahali hapo ni alama tosha ya uumbaji wenye ukamilifu wa Muumba:

“Yeye Ndiye aliyefanya Ardhi iwe inatumika kwa ajili yenu. Basi nendeni katika pande zake zote na kuleni katika riziki zake, na kwa yeye ndiyo marejeo”(67:15).

Utafiti wa kinajimu wa hivi karibuni unaonesha umuhimu wa sayari nyingine kwa ajili ya kuwepo kwa Dunia. Kwa mfano, ukubwa wa Sayari ya Jupita na pale ilipo katika mfumo wa juwa ni hali inayoshangaza hasa kwa sababu ya jinsi ilivyo kubwa sana katika mfumo wa juwa. Ukubwa huo wa Jupita huifanya Dunia ibaki katika njia yake licha ya kuwa na mwendo wa kasi katika mzunguko wake wa kulizunguka juwa. Iwapo kusingalikuwa na sayari yenye ukubwa wa Jupita mahali pale ilipo, Dunia ingekuwa angukiyo la vimondo vinavyopukutika

33

kwa maelfu kutoka anga za mbali. Kwa ufupi, Jupita ni kama mlezi na mlinzi anayeilinda Dunia kutokana na hatari ya kuangukiwa na vimondo vyenye madhara. Jupita ingalikuwa katika Obiti tafauti na pale ilipo, Dunia na vilivyomo visingalikuwepo. Mwanaadamu anayejua yote haya, hana budi kukiri kwamba hapana chochote katika Ulimwengu huu kilichoumbwa bila ya kuwa na lengo. Ufahamu wa namna hii ndiyo unaoelezwa na Qur’an kama ifuwatavyo:

“Katika kuumbwa kwa Mbingu na Ardhi na kupishana kwa usiku na mchana, zipo alama(za kuonesha uumbaji wa Mwenyezi Mungu) kwa watu wenye akili (Surat Al Imran aya 190).

Kama aya inavyoeleza, maumbile ya angani na Ardhini yawe mazingatio kwa Wanaadamu wenye kutafakari.

Halijoto ya DuniaHalijoto ya wastani ya anga za juu ni ngapi? Ni nyuzi hasi za sentigredi 270(sawa na

nyuzi hasi 455 za Faranheit). Hiyo ni halijoto isiyowezesha uhai kuwepo. Halijoto ya wastani ya Dunia yetu ni kati ya nyuzi 15 - 20 za sentigredi(ambazo ni sawa na nyuzi 60 - 70 za Faranihaiti). Halijoto hutafautiana kulingana na jinsi mtu anavyozidi kwenda juu katika tabaka za angahewa. Kwa mfano, Bara la Afrika lina hali ya joto. Je yawezekana kutengeneza sanamu la theluji Afrika? Ili mtu aweze kutengeneza sanamu hilo anahitajika kwanza kuwa na theluji . Kwa hiyo kwa kuwa ni vigumu kupata theluji katika mazingira ya joto, hivyo hakuna uwezekano wa kutengeneza sanamu la aina hiyo. Itawezekana tu kufanya hivyo kwa kupanda mlima wa Kilimanjaro ambao ni mrefu zaidi kuliko yote barani Afrika. Kilele cha Mlima Kilimanjaro ambacho kiko juu ya usawa wa bahari, muda wote kimezingirwa na theluji. Hii ni kwa sababu kadiri mtu anavyokwenda juu kutoka Ardhini ndivyo halijoto inavyopungua. Halijoto hushuka zaidi hadi kufikia nyuzi hasi za sentigredi 50(sawa na nyuzi hasi za 58 Faranihaiti) inapofikia katika eneo tabaka la angahewa ambalo Wanaanga wanaliita kwa jina la “Angastrato” . Mbele zaidi ya hapo halijoto hupanda tena. Hata hivyo kwa Ulinzi wa Mwenyezi Mungu, Dunia yetu haina halijoto kubwa zaidi. Utengenezwaji wa kiwango hiki cha halijoto unahusiana na kiasi cha miale ya joto ya jua iangazayo umbali kati ya Dunia na Jua. Katika mada za sura zilizopita, tuligusia mada hii. Hebu sasa tuichambue zaidi. Kwa mujibu wa ukokotozi wa mahesabu ya anga, kupungua kwa asilimia 10 tu kwa nishati itolewayo na jua huweza kusababisha uso wa Dunia kuzingirwa na mita nyingi za matabaka ya barafu. Vivyo hivyo iwapo nishati ya jua itaongezeka kidogo, viumbwa vyote hai vitanyauka na kufa ila kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Kasi ya gurudumu la Dunia husaidia pia kuweka urari katika mgawanyo wa halijoto. Juwa hukamilisha mzunguko wake mmoja katika mhimili wake katika muda wa saa 24. Kwa sababu hii, vipindi vya usiku na mchana huwa ni vifupi. Kwa sababu hii ya ufupi, tafauti za halijoto kwa usiku na mchana nazo pia ni ndogo. Umuhimu wa hili unaonekana katika mfano dhahiri tunaoupata kutoka kwenye Sayari ya Mekyure, ambayo mchana wa siku moja tu hudumu kwa zaidi ya mwaka unaohesabika kwa vipimo vya Dunia,

34

wakati huo huo tafauti ya halijoto kati ya mchana na usiku takriban ni nyuzi za sentigredi 1,000(Sawa na nyuzi 1,800 za Faranihait).

Jiografia ya Dunia vile vile husaidiya kugawanya joto kwa uwiano uliyo sawa. Kuna tafauti ya nyuzi 100 za sentigredi(sawa na nyuzi 212 za Faranihaiti) katikati ya maeneo ya ncha ya Dunia na yale ya ukanda wa Ikweta. Iwapo tafauti ya halijoto hiyo itaendelea kuwepo kwa kiwango kamili, matokeo yake ni kusukumiliwa mbali kwa kila kitu kilichopo eneo husika. Badala yake, Dunia ina vizuwizi vya kijiografia vinavyozuia mwendo kasi mkubwa wa hewa ambao ungesababishwa na tafauti hizo za halijoto. Vizuwizi hivyo ni pamoja na milima kama ile iliyoshikamanisha mashariki na magharibi ikianzia kwenye milima ya Himalaya iliyopo China na kuendeleya hadi Milima ya Taurasi iliyopo Anatolia na Apsi barani Ulaya.

Mpaka hapa tumejifunza jinsi Dunia inavyojiwekea, kujigawia na kujidumishiya halijoto ya kiyasi chake ingawa wakati ikifanya hivyo, anga za juu zina halijoto inayofikia nyuzi hasi za sentigredi 270(sawa na nyuzi hasi 455 za faranihaiti). Kama halijoto ya Dunia ingekuwa baridi au joto sana, kiyasi cha kuhatarisha maisha ya wanaadamu, uhai usingaliwezekana katika Dunia. Kwa hiyo, kiwango sawia cha halijoto ya Duniya kinaonesha Rehema ya Mwenyezi Mungu juu ya watu, mimea, wanyama na viumbwa vyengine.

Jinsi umbile la Dunia linavyolindwa na khatari ya maumbile mengineTukilinganisha umbile la Dunia na sayari nyingine kwa kigezo cha ukubwa, umbile la

Dunia ni mfano wa punje ya njegere. Kwa mfano huu, sayari ya Mekyure kama punje ya ufuta, sayari ya Venasi kama ilivyo Dunia, sayari ya Maazi ni sawa na mbegu ya tikiti, sayari ya Jupita ionekane yenye umbile lenye ukubwa mithili ya chungwa, sayari ya satani kama chenza, sayari za Uranasi na Neptuni kama ndimu na umbile la Pluto liwe mithili ya ufuta kama ilivyo Mekyure. Kando ya sayari hizi, Jua linatazamika kama umbile kubwa la duara sawa na mpira wenye ukubwa unaozidi ule wa mpira wa kikapu ikilinganishwa na umbile la Dunia linalofananishwa na punje ya njegere. Je, ukubwa huu wa umbile la Dunia kulinganisha na sayari nyingine, umetokea kwa bahati nasibu? Au umewekwa hivyo kwa makusudiyo maalumu?

Umbile la Dunia likichunguzwa vyema, kwa urahisi sana litafahamika kuwa limekadiriwa ukubwa ambao ndiyo hasa uliotakiwa kuwa. Iwapo Dunia ingekuwa ndogo kuliko umbile lake la sasa, nguvu ya uvutano ingekuwa dhaifu na nyepesi zaidi kuweza kuhimili angahewa iliyoizunguka. Bila ya angahewa, Dunia ingekuwa ikiangukiwa mara kwa mara na vimondo au kufikiwa na mionzi mibaya itokayo anga za juu. Mbali ya hayo, Oksijeni yote ingetoweka na hivyo kufanya uhai usiwezekane katika sayari hii. Iwapo Dunia ingekuwa kubwa zaidi ya umbile la sasa, nguvu ya uvutano ingeongezeka kwa namna ya ajabu kabisa na kuigeuza angahewa kuwa mchanganyiko mbaya kwa kuwa tangu hapo ina aina nyingi ya hewa

35

za sumu. Mbali ya ujazo wake, vile vile umbile la Dunia ndani yake limewekwa kwa namna maalumu. Matabaka, kutokea kiini cha kati ya Dunia, kila moja linazunguka jingine na mizunguko hii ndiyo inayotengeneza nguvu ya sumaku. Nguvu hii ya sumaku ni muhimu sana katika kuhifadhi uhai katika Dunia. Ikiwa imeanzia mbali kabisa ya uso wa Dunia, nguvu hii huilinda ardhi kutokana na athari ya miyonzi mibaya itokayo anga za juu. Tafiti nyingine za kisayansi zinaonesha kwamba Ulimwengu haukutelekezwa. Kwa hakika Mwenyezi Mungu, Muumba na Mola wa Ulimwengu anauendesha na kuudhibiti. Kwa uwezo wake, Ameumba Magimba(magalaksi), nyota na sayari na kuzifanya zijiendeshe kwa kanuni Alizoziweka. Sayari ya Dunia ambayo wanaadamu wanaishi, ni uumbaji maalumu wa Mwenyezi Mungu. Katika Qur’an, Mwenyezi Mungu Ameelezea uumbaji huu wa ajabu kama Anavyobainisha:

“Ameumba kila kitu na Akakikadiria kipimo chake”(25:2).

Aya nyingine nyingi zinafahamisha kwamba katika sayari hii, Mwenyezi Mungu ameweka kila linalohitajika na Wanaadamu.

Sehemu kubwa ya uso wa Dunia ni maji!Takribani asilimia 71 ya uso wa ardhi umefunikwa na maji. Zipo dhana kuwa huenda

katika sayari ya Jupita mkawemo maji yenye hali ya kumiminika, hata hivyo mpaka sasa utafiti unaonesha ni Dunia pekee yenye maji yaliyo katika hali ya kumiminika. Sayari nyingine zina barafu zilizogandamana muda wote. Katika Sayari ya Dunia, maji yamekusanyika katika maziwa, mito na vijito na kisha katika bahari ambalo ni eneo kubwa lililo wazi lenye kina kirefu, maji ambayo ni muhimu kufanya uhai uwepo katika sayari hii. Kwa mfano, maji yanazuia mabadiliko ya ghafla ya halijoto ya angahewa hivyo kuwezesha viumbwa kuishi katika halijoto ya kiwango kinachoendana na maumbile yao. Vile vile hulainisha hewa kuwa nyevunyevu. Kwa upande mwingine, maji ya bahari husawazisha mkondo wa bahari kupitia mmomonyoko na kupwa kwake. Mfumo huu haupo katika sayari yoyote. Zaidi ya hivyo, bahari hutupa samaki na vyakula vyengine vya bahari. Kula kwetu vyakula vitamu vya bahari, kuogelea na kusafiri kwa maboti, yote hayo ni katika rehema za Mwenyezi Mungu zinazopatikana kupitia neema ya maji. Mwenyezi Mungu Ameumba kila kitu tunachokihitajia kwa ukamilifu wa hali ya juu. Kwa hakika, mbali ya vitu vizuri, pia kuna hatari nyingi kama vile Volkeno zinazofoka ambazo hata hivyo, muda mwingi hua zimetulizana.

Milima Kwa sababu ya magma(ujiuji mzito) au miamba laini iliyo katika kiini cha ardhi,

Volkeno iliyo katika umbile la umajimaji hujichomozesha kupitia nyufa za kiini hicho na hivyo kufoka kwa hasira. Kutokana na mpasuko mkubwa, mara nyingi volkeno hutoa tani za mchanga na takataka katika angahewa. Aina hii ya mpasuko hutengeneza wingu zito la kiza angani. Kisha magma huanza kutiririka katika uso wa ardhi kumwagikia kwenye misitu na miji iliyo jirani. Magma inayotiririka kutoka kwenye volkeno huitwa Lava (Chemchem moto).

36

Baada ya muda, chemchem hii hupowa na kutulizana katika uso wa Dunia kisha hugandamana na kutengeneza miamba. Katika historiya yote, miji mingi imekuwa ikiharibiwa na majanga ya volkeno zilizo hai ambazo hufoka. Kwa mfano, mnamo karne ya mwanzo, mlipuko wa volkeno uliharibu mji wa Pompeii na kisha, Roma wakati huo ukiwa mji mzuri. Chemchem moto iliufikia mji wa Pompeii ambao ulijulikana kwa jinsi wakazi wake walivyokuwa waovu zama hizo wakikiuka wazi wazi makatazo ya Mwenyezi Mungu na kutenda maovu kwa sherehe na kujipongeza. Ulikuwa mlipuko wa ghafla ambao uliwafudikiza, kuwaunguza na kuwauwa watu kabla hawajajiyokowa. Watu hao walikufa mara moja. Tukiyo hilo ambalo halikuweza kuepukika, liliangamiza uhai wa watu wa mji huwo. Chemchem hiyo, inafanana na ile iliyoelezwa katika Qur’an kama ifuatavyo:

“...basi tuliwapelekeya kimbunga cha changarawe, na miongoni mwao wako waliotolewa roho kwa ukelele na miyongoni mwao wako tuliowadidimiza Ardhini, na miyongoni mwao wako tuliowagharikisha..”(29:40).

Aya hizi zinabainisha kuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye uwezo juu ya kila kitu, huweza kukiharibu chochote kile pale anapotaka. Hakuna anayeweza kujiokoa na adhabu yake. Hata hivyo Mwenyezi Mungu ni Msamehevu na Mrehemevu kwa waja wake. Katika vitabu vya Mwenyezi Mungu kuna mifano ya dhahiri inayoonesha urehemevu wa Mwenyezi Mungu usiyo na ukomo. Kutokea mara chache kwa milipuko ya Volkeno ni Rehema nyingine ya Mwenyezi Mungu tunayopaswa kuizingatia.

Angahewa ni muhimu kwa maisha ya DuniaMaana ya neno Mbingu ambalo limetumika katika aya nyingi, ni anga. Tafsiri nyengine

ya aya ya Qur’an juu ya Mbingu saba ni matabaka saba ya angahewa:

““Mwenyezi Mungu ni yule ambaye ameziumba Mbingu saba na ardhi kuwa mfano wa hizo..”(65:12)

Vile vile, neno hilo hufasiriwa kuwa ni lile anga wazi lililo juu ya sayari ya Duniya. Neno Mbingu pia kama tulivyoona kurasa za nyuma lina maana ya maumbile makubwa ambayo Mwanaadamu hajawa na elimu wala teknolojia ya kuyajua kwa wakati huu ambayo kwa mujibu wa aya yamekaa kimatabaka moja likiwa juu ya jingine yakiwa yamelifunika duwara la Ulimwengu:

“Ambaye Ameumba Mbingu saba zilizo tabaka tabaka..(67:3)

Kwa kutumia tafsiri ya kwanza, Duniya na anga lake liitwalo angahewa, limezungwa na matabaka saba mithili ya mkao wa Mbingu zilivyoufunika Ulimwengu kwa matabaka saba moja juu ya jingine:

37

“Mwenyezi Mungu ni yule ambaye ameziumba Mbingu saba na ardhi kuwa mfano wa hizo. Amri zake zinashuka humo ili mjuwe kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu, na kwamba amekizunguka kila kitu kukijuwa”(65:12)

Tabaka saba za angahewa la Dunia

Sifiyatropo: Hili ni tabaka la mviringo la angahewa lililo jirani na uso wa Dunia. Wembamba wa tabaka hili hushabihiana na hali ya hewa iliyopo katika anga letu. Halijoto yake huyeyuka na kutengeneza umajimaji kadiri mwinuko unavyoongezeka kutoka usawa wa bahari. Halijoto katika mwinuko uliyo juu zaidi huwa kati ya nyuzi hasi za sentigredi 51(sawa na nyuzi hasi 60 za Faranihaiti) hadi nyuzi hasi za sentigredi 79( sawa na nyuzi hasi 110 za Faranihaiti).

Sifiyastrato: Hili ni tabaka la angahewa mviringo lililo juu ya Sifiyatropo. Halijoto yake hupanda kadiri mtu anavyoelekea juu.

Sifiyameso: Hili ni tabaka mviringo lililo juu ya Sifiyastrato. Halijoto yake hushuka hadi kufikia nyuzi hasi 73 za sentigredi(sawa na nyuzi 100 za Faranihait).

Sifiyathemo: Hili ni tabaka lililo juu ya Sifiyameso. Halijoto yake hupanda kwa kasi ndogo. Tafauti ya halijoto ya hapa kati ya usiku na mchana ni zaidi ya nyuzi za sentigredi 100(sawa 212 za Faranihait).

Sifiyaeksosi: Ni tabaka anga linaloanzia kwenye mwinuko wa zaidi ya kilometa 500(maili 310) juu kutoka uso wa Dunia.

Sifiyaiyonosi: Jina la tabaka hilo iyoni hutokana na aina ya gesi yake ambayo hubadilika kuwa iyoni.

Sifiyamagneto: Kuwepo kwake kwenye eneo lenye sumaku, tabaka anga hili huitwa Sifiyamagneto. Tabaka hili, ambalo hufanya kazi ya ulinzi, lipo kati ya Kilometa 3,000 na 30, 000(Maili 1,850 na 18, 500) juu ya uso wa Dunia. Tabaka hili huilinda Dunia kutokana na mionzi hatari inayotoka angani, ambayo huitwa ukanda wa Vanaleni.

Ili kuweza kufahamu vyema umuhimu wa angahewa, tutafiti sayari nyingine, hasa Sayari ya Mekyure ambayo haina angahewa. Tumekwisha ona umuhimu wa angahewa katika maisha yetu na tumekwishaeleza umuhimu wa gesi katika angahewa kama vile Oksijeni au hali ya usumaku iliyopo katika tabaka la angahewa ya Sifiyamagneto inavyolitulinda na hatari za miale na mionzi mibaya. Vile vile katika angahewa ndipo unapopatikana uzito wa kila kitu ambao ni muhimu kwa uhai. Angahewa imetengenezwa kwa hewa nyepesi. Hata hivyo hii

38

haina maana kuwa angahewa haina uzito. Kwa hakika tabaka hizi za hewa zilizo juu kilometa nyingi, zina uzito mkubwa sana.

Kwa mujibu wa utafiti uliyofanyika, angahewa lina uzito wa tani nyingi zikimsukuma kila mmoja wetu. Huu unaitwa msukumo wa hewa. Iwapo tunasukumwa na angahewa vipi hatugongani? Hatugongani kwa sababu miili yetu imeumbwa na nguvu ya kujishikiza na uzito wa angahewa. Hatuwezi kufanya lolote au hata kuishi iwapo mazingira yetu yatakuwa na msukumo mdogo wa angahewa. Hiyo ni kwa sababu, bila ya msukumo, mzunguko wa haraka wa damu katika miili yetu ungekuwa mkubwa mno katika mishipa yetu. Ni kutokana na uwiano huo kati ya miili na angahewa ndiyo maana tunaweza kuishi, vinginevyo mishipa yetu ingalipasukia mbali kutokana na msukumo mkubwa wa damu. Kwa hiyo haiwezekani kwa mwanaadamu kuweza kuishi katika mazingira kama yale ya sayari ya Mekyure yasiyo na angahewa. Katika sayari ya Venasi, ipo angahewa lakini msukumo wake ni mara 90 zaidi ya ule wa angahewa ya Dunia, kwa hivyo sayari hiyo haina mazingira yanayoweza kuruhusu uhai kwa wanaadamu na viumbwa wengine wa Dunia hii.

Kutokana na maelezo hayo, sasa inafahamika kuwa hakuna uhai unaoweza kuwepo katika sayari ya Venasi kwa kuwa katika mazingira ya msukumo mkubwa zaidi ya mara 90 ya ule wa Dunia, viumbwa vyote vitakuwa vikijigonga ovyo na kutapanyika.Tukirejea nyuma kidogo katika ile nukta ya awali, tunaona kuwa Angahewa ni moja ya viwezeshi muhimu vya maisha ya wanaadamu hapa Ardhini. Angahewa ina kazi nyingi, mojawapo ni kuwezesha kuwepo gesi ambazo nazo huwezesha uhai wa mwanaadamu katika sayari hii. Iwapo angahewa isingalikuwepo, gesi isingekuwepo, hivyo viumbwa visingeweza kupumua na kwa hivyo kusingalikuwa na uhai katika Dunia ila kwa idhini yake Mwenyezi Mungu. Kazi nyingine ya angahewa ni kuilinda Dunia na hatari zinazotoka anga za juu kama vile vimondo. Angahewa huzuwia vimondo vinavyoungua kwa maelfu visiangukie Duniani na kusababisha majanga. Angahewa vile vile huzuwiya mionzi hatari kupenya katika eneo la uso wa Dunia. Kutokana na kuzuiliwa na angahewa, ni asilimia saba tu ya miyonzi hiyo mibaya ambayo hupenya na kuufikia uso wa Dunia. Hata hivyo kuhusiana na asilimia hii saba ya mionzi hatari inayopenya na kuufikia uso wa Dunia pana fundisho jingine kubwa hapa. Mionzi hiyo ambayo huwezesha uhai katika ardhi ni ile tu ambayo Dunia inaihitaji. Na kwa kadari ya Mwenyezi Mungu umbali kati ya Dunia na jua ni ule uliohitajika; si mbali sana na si karibu sana. Kwa hiyo ile asilimiya saba ya miyonzi khatari inakuwa sehemu ya miyonzi inayohitajika katika uhai wa Dunia. Je angahewa hii ambayo ni muhimu sana kwa maisha yetu imetokeya tu yenyewe kwa bahati nasibu?

Ulinganishi mzuri unaoonesha kutokuwezekana kwa uhai kutokea kwa bahati nasibu ni huu ufuatao: Hebu tuyapeleke mawazo yetu kwenye keki tulazo majumbani. Nini kinachozipa keki hizi ladha tamu? Hapana shaka, utamu huo ni kwa sababu keki hizo zimepikwa na kuwekwa viungo na vionjo vilivyomo katika ule unga wa ngano ambao ulichanganywa na

39

kuokwa kwa joto munasaba. Je, mpishi aliyepika keki hizo hahitajiki? Kwamba keki hizo zaweza kujipika zenyewe? Kwa hakika mawazo hayo yatakuwa ni ya ajabu sana.

Je, angahewa iliyozunguka ardhi yenye matabaka saba kama yalivyoonekana, yaweza kuwa imetokea yenyewe kwa bahati nasibu? Kwa kweli haiwezekani kutokea kwa bahati nasibu. Iwapo Mwenyezi Mungu asingeumba angahewa, uhai katika Dunia usingaliwezekana ila kwa siri zake Mwenyewe. Dunia ingalikuwaje kama Mola wetu asingaliilinda ambapo vimondo vikubwa vingeishambulia na kuiharibu kabisa. Kwa kweli Mwenyezi Mungu ni mwenye uwezo wa ajabu kabisa. Kwa hiyo mazingatio kwa angahewa ni moja ya njia ya kuujua uwezo Mtukufu wa Mwenyezi Mungu.

“Je hamuoni jinsi Mwenyezi Mungu Alivyoziumba Mbingu saba kwa utaratibu- tabaka tabaka(71:15).

Kufaa kwa angahewa kwa uhai wa DuniaAnga ya Dunia imesheheni aina zote za nyuso za kijiografia. Hebu tutazame umbile

maalumu la angahewa yetu. Angahewa ya Dunia ina asilimia 77 ya gesi ya Naitrojeni, asilimia 21 ya gesi ya Oksijeni na asilimia moja ya Kaboni dayoksaidi na gesi nyingine.

Hewa ya OksijeniHewa ya Oksijeni ni muhimu kwa maisha ya wanaadamu na wanyama. Kwa kuwa,

nishati inayohitajika kwa uhai wa viumbwa inapatikana kupitia hatua za kikemikali ambazo nyingi ya hizo hutokana na Oksijeni, hiyo ndiyo sababu mara kwa mara Oksijeni yahitajika, kwa kuwa inatuwezesha kupumua. Kiwango cha Oksijeni kilichopo katika angahewa ndicho kinachohitajika kwa uhai. Iwapo kiwango hicho kingeongezeka, badala ya asilimia 21 ikawa 22, hiyo ingetosha kusababisha mmuliko mmoja wa radi kuunguza misitu yote. Iwapo kiwango hicho kingekuwa kama asilimia 25, moto mkubwa ungeliunguza Dunia yote kwa kuwa Oksijeni ni gesi inayoshika moto kwa haraka. Ni muhimu kujisaili swali lifuwatalo: Ingetokeya nini iwapo Oksijeni iliyopo katika angahewa ingekuwa imetumika yote?

Licha ya uchafuzi wa hewa uliofanyika karne iliyopita, hiyo haijawa tishio kwa kuwa zaidi ya asilimia 80 ya Oksijeni inayozalishwa katika Dunia yetu inatokana na viumbwa vidogo vya bahari visivyoonekana ila kwa darubini kubwa. Hivyo kwamba, iwapo misitu yote ingetoweka bado Oksijeni ingaliendelea kuwepo. Ni mfumo madhubuti unaodumisha na kudhibiti kiyasi cha Oksijeni katika angahewa. Mfumo huu unaitwa mfumo mzunguko. Wanyama na wanaadamu wanavuta Oksijeni na kutoa nje hewa ya Kaboni dayoksaidi. Mimea kwa upande mwingine, inavuta Kaboni dayoksaidi na kutowa nje Oksijeni . Mimea imekuwa ikidumisha na kuendeleza uhai kwa kubadili Kaboni dayoksaidi kuwa Oksijeni. Kila siku mabilioni ya tani za Oksijeni yanazalishwa kutoka kwenye mimea na kutawanywa kwenye angahewa.

40

Jambo moja yafaa lizingatiwe. Kwa nini iwe ni mimeya tu ndiyo inayozalisha hewa ya Oksijeni. Je isingaliwezekana kwa viumbwa vyote kuweza kuzalisha Oksijeni? Hapa jibu lisilo shaka wala utata ni hapana, kwa kuwa uhai usingelikuwa mwepesi zaidi iwapo kila kiumbe kingalikuwa kikitoa hewa ya Oksijeni. Kinyume chake, iwapo wanyama na wanaadamu vile vile wangalikuwa wakizalisha hewa ya Oksijeni, kiasi cha Oksijeni katika angahewa kingalikuwa kikubwa zaidi kiasi kwamba angahewa ingaligeuka kuwa yenye kutatarika kwa muda mfupi. Kwa hivyo, cheche ndogo tu ingaliweza kusababisha moto mkubwa wa ajabu.

Kwa upande mwingine, iwapo viumbwa vyote hai, ikiwemo mimeya, vingalikuwa vikizalisha hewa ya Kaboni dayoksaidi, hewa ya Oksijeni iliyopo kwenye angahewa ingalifyonzwa na kutoweka kwa haraka na kwa hivyo viumbwa hai kwa idadi kubwa sana vingalianza kufa kutokana na kugugumiya kwa kukosa hewa kutokana na mkandamizo wa hewa inayotakikana katika kupumuwa. Mbali ya kuwalinda Wanaadamu, angahewa huhifadhi Oksijeni inayohitajika katika upumuaji. Nchini Kwa Rehema yake, Mwenyezi Mungu Ameumba mifumo mingi inayoingiliana ili kuwezesha Oksijeni ibaki katika kiwango kinachotakiwa. Wanadamu wanatakiwa kuzingatia kwa kila pumzi wanayopumua. Hiyo ni Rehema ya Mwenyezi Mungu kwa wanaadamu. Iwapo Mwenyezi Mungu asingehiyari hivyo, kusingekuwa na angahewa wala Oksijeni na kwa hivyo viumbwa wasingekuwepo katika Dunia hii. Ndiyo maana Muumini anapotaka kufanya jambo hana budi kuanza kwa kulitaja jina la Muumba, Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mrehemevu.

Mada yetu imezungumziya juu ya:

- Angahewa ya Dunia yenye asilimia 77 ya gesi ya Naitrojeni, asilimia 21 ya gesi ya Oksijeni na asilimia moja ya Kaboni, Agoni na gesi nyingine.

- Umuhimu wa hewa ya Oksijeni kwa maisha ya wanaadamu na wanyama unatokana na nishati yake inayohitajika kwa uhai wa viumbwa.

- Tunahitaji Oksijeni kwa ajili ya kupumuwa. Bila ya kuwepo Oksijeni wanaadamu hawataweza kupumuwa na kwa hivyo uhai hautakuwepo katika sayari hii.

41

Sura ya Kumi

Mawingu yapeperukayoTuangaliapo angani, wakati fulani tunaona mirundi sawa na milima inayofanana na

moshi wenye rangi nyeupe au njano, wakati mwingine meusi tii. Wakati fulani mirundi hiyo hufanana na maumbile fulani. Hayo ni mawingu. Kila mmoja kwa wakati wake yawezekana ameshawahi kutafakari juu ya namna gani mawingu yalivyotokea. Kila siku joto la juwa husababisha maji yaliyoko kwenye uso wa Dunia kupata hali ya joto joto yaani uvuguvugu. Aina hii ya maji au uvuguvugu unaposambaa katika hewa hubadilika kuwa mvuke. Hewa inayokuja jirani na ardhi huwongeza mvuke huo. Hewa hii ya joto hupanda kusafirisha mvuke huo mpaka angani. Huko angani, mvuke uliyo ndani ya hewa yenye joto hukabiliana na hewa baridi, hivyo hubadilika kuwa manyunyu na kisha vijiwe vya barafu.

Maji ya bahari ambayo kiasili yana chumvi na yale ya maziwani ambayo huwa na madini mbali mbali, nayo husafirisha vijichembe vya chumvi mpaka angani. Vijichembe hivi vya chumvi ni vidogo mno visivyoweza kuonekana na macho ya kawaida. Kwa siku, upepo husafirisha angani vinyunyu vilivyokusanya mamilioni ya tani za chumvi. Chumvi hizi hutengeneza viini katika matone ya mvua inayotarajiwa. Kutokea Ardhini, mawingu angani huonekana kama vifurushi vya pamba vinavyopeperuka, kiasi cha kuashiria mrundikano mkubwa mno, bila ya uzito. Lakini, kwa hakika ni mafuwele ya maji yanayoonekana kama vifurushi vya pamba vinavyobadilika na kuwa mvua, hapo ndipo tunaposhuhudia tani za maji yanayonyesha Ardhini. Kwa wastani mawingu hukusanya tani 300,000 za maji (tani moja ni sawa na kilogramu 1,000 (ambayo ni sawa na paundi 2,200). Tani 300,000 ni sawa na kilogramu milioni 300(sawa na paundi milioni 660). Ikizingatiwa kuwa uzito wa mtu mzima mmoja ni kati ya kilogramu 60-70(Paundi 130-150), basi kwa wastani uzito wa mawingu ni mkubwa sana, ni zaidi ya tani 300,000 zinazopeperushwa angani. Mwenyezi Mungu huteremsha mvua kutoka katika mawingu makubwa ili kuhuisha ardhi iliyo kame. Kwa namna hii, kila kona ya ardhi hupata mvuwa ya kutosha kulingana na wakati wake. Katika Qur’an, Mwenyezi Mungu:

Je, huoni ni ya kwamba Mwenyezi Mungu Anayaendesha mawingu, kisha huyaambatanisha pamoja, kisha huyafanya mirundi? Basi utaona mvuwa ikitoka katikati yake; Naye huteremsha kutoka juu katika milima ya mawingu-mvuwa ya mawe, akamsibisha nayo amtakaye na kumuepusha nayo Amtakaye; hukurubia muwanga wa umeme wake kupofowa macho(24:43).

Mbali ya hilo, Mwenyezi Mungu anayavuta mazingatio yetu katika usafi na utwahara wa maji anayoyateremsha kutoka mawinguni.

42

...Na tunayateremsha maji safi kutoka Mbinguni(Surat al Furqan 48).

Kama aya inavyoeleza, maji yanayoteremshwa Ardhini ni safi na twahara yakiwa yamechujwa vyema na kubakisha kiyasi kidogo sana cha chumvi na madini. Hii ni rehema kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu; udongo nao hupokeya kiyasi cha chumvi inachokihitaji kutoka katika mvuwa. Iwapo mvuke uliyotoka baharini na wenye kiyasi kikubwa cha chumvi ungeshuka kwa njia ya mvua katika hali yake ya asili, ni wazi ungekuwa na madhara kwa uhai katika sayari hii. Iwapo maji ya mvua yangalikuwa na chumvi chumvi, yangaliharibia mbali udongo na mimea, hali ambayo ingesababisha vifo kwa viumbwa hai katika ardhi. Kwa kifupi, uhai katika ardhi ungalikoma. Hata hivyo hili halitokei kwa sababu Mwenyezi Mungu ni mwingi wa Rehema kwa watu. Mwenyezi Mungu analibainisha hilo katika aya ifuatayo:

“Je mnayatafakari maji mnayoyanywa”. Je? Mumeyateremsha nyinyi mawinguni au Sisi ndiyo tunaoyateremsha? “Tungalitaka Tungaliyafanya ya chumvi, basi mbona hamshukuru?(56:70).

Maelezo yanayopatikana kutoka katika aya hizi yanaweka wazi kwamba Mwenyezi Mungu Ameumba kila kitu kwa ajili maalumu ya kuwezesha uhai kwa wanaadamu. Kama tulivyoona, Mwanaadamu hana uwezo wa kupata kila analolihitajia kwa ajili ya maisha yake. Ni kwa ridhaa ya Mwenyezi Mungu ndiyo maana anaweza kuishi katika ardhi hii. Kwa sababu hiyo, kila dakika anatakiwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu aliyemuumba, kwamba yeye ni Muumba wa kila kitu na kwa hivyo mara kwa mara Amshukuru.

Katika mada hii tumejifunza:

- Jinsi maji yanavyotengenezwa mvuke, namna mawingu yanavyotengenezwa na baadaye kugeuzwa mvua.

Mvua yenye kipimo maalumuMvua hunyesha kwa kipimo maalumu kilichokadiriwa na Mwenyezi Mungu. Tafiti za

hivi karibuni zimekuja kugundua kipimo hiki. Mahesabu ya tafiti hizo yamegundua kwamba ni tani zisizopungua milioni 16 za mvua, hudondoka kwa njia ya matone kwa kila sekunde ya muda ule mvua inaponyesha. Kwa mwaka, tani hizi hufika trilioni 505. Kwa hivyo mvua inyeshayo kila mwaka katika uso wa Dunia ni kipimo cha tani trilioni 505. Na kwa mujibu wa tafiti hizo, tani hizo hulingana katika mwaka mmoja hadi mwingine. Ukweli huu uliokuja kubainika wazi na sayansi za kileo, umeelezwa kwa ufasaha katika Qur’an ya Mwenyezi Mungu tangu kuumbwa kwa Ulimwengu.

43

“...Na ambaye Ameteremsha maji mawinguni kwa kipimo maalumu”(Surat az Zukhruf 11).

Ni jambo la kufurahisha sana kwamba Mwenyezi Mungu ametaja kipimo maalumu cha mvua anayoiteremsha kutoka mawinguni. Ugunduzi wa hivi karibuni unaonesha kuwa kiasi cha mvua kinachonyesha kila mwaka ni kile kile. Kiasi cha maji kilichoelezwa hapo juu ambacho ni mzunguko wa maji, hudumisha na kuendeleza uhai hapa Ardhini. Kama kipimo hicho kingalikuwa cha kubahatisha isingaliwezekana kudumisha hali hiyo hata kama ingalitumika teknolojia ya kileo. Mabadiliko madogo tu katika mzunguko wa maji yaweza kusababisha mvurugiko mkubwa kwenye maumbile katika kipindi kifupi sana. Na huo utakuwa ndiyo mwisho wa uhai ardhini. Hata hivyo, hilo kamwe halitatokea, uso wa ardhi kwa muda wote hupokea maji kwa kiwango kile kile cha mvuwa.

“Mwenyezi Mungu huteremsha maji Ardhini kwa kiwango maalumu.”

Alhamdulillah, imefahamika kuwa Mwenyezi Mungu ndiye anayedhibiti kiwango cha ushukaji wa maji Ardhini. Vinginevyo, isingaliwezekana kuwepo kiasi cha mvua kinachofanana kwa kila mwaka Ardhini. Mwenyezi Mungu ndiye Mola wa Ulimwengu, na kila kitu kinakwenda kulingana na utashi wake.

Upinde wa mvuaBila shaka kila mmoja ameshapata kuuona upinde wa mvua. Na kama yupo ambaye

hajapata kuuona basi walau ameona picha ama kwenye kitabu au kwenye runinga. Upinde wa mvua ni duara kubwa la rangi saba angani. Kuonekana kwa upinde wa mvua kwa kweli kunastaajabisha, kwa vile umbile hilo na rangi zake, linapendeza mno. Hivi mazingatio yetu yameshawafikisha wanaadamu walio wengi katika kuhoji rangi hizo zilivyotokeya?

Upinde wa mvua mara nyingi hujitokeza kipindi ambacho Jua huchomoza mara baada ya mvua kunyesha. Ni mtiririko wa elektroni hewani inayoyeyusha na kuunga metali) lenye rangi saba zilizojiweka kitabaka moja juu ya nyingine. Upinde wa mvua huonekana kama taji la mauwa, lenye kuvutia sana. Upinde wa mvua kwa hakika ni zao la miale itokanayo na rangi saba zitokanazo na mwanga wa jua. Kwa hakika, mionzi myeupe ya jua kiasili ina rangi mchanganyiko. Rangi hizi zinazotokana na jua zina mpangilio maalumu wa taswira zitokanazo na miali ya mnunurisho. Rangi za msingi za spektra ni nyekundu, rangi ya chungwa, njano, kijani, samawati, na urujuwani. Weupe wa mwanga wa jua hujitengeneza pale rangi hizo zinapojichanganya. Mara tu mwanga wa jua unapopenya katikati ya tone la mvua, rangi inayotengenezwa hujitokeza. Hiyo ni kwa sababu maji hupindisha au hutenganisha rangi kutoka kwenye mwanga. Rangi hizi zilizotenganishwa hupita kwenye matone ya maji na kujiainisha katika pande tafauti. Ili kuweza kupata mfano wa rangi hizi, mtu achukuwe glasi ya maji na aimulike mwanga mkali ndani yake. Hapa glasi ya maji itakuwa mfano wa uwazi wa tone la

44

maji. Kisha itaonekana pale glasi hiyo itakapowakiwa na mwanga huo mkali, kiupinde kidogo cha maji kitajitokeza pembezoni mwake. Upinde wa mvua kwa kawaida huonekana kama ni nusu duara, hivyo sivyo. Upinde wa mvua, kwa hakika ni duara kamili lakini haiwezekani kuliona duara lote kwa upande mmoja wa ardhi. Ndiyo maana, mara kwa mara huonekana kama nusu duwara. Ni pale mtu anapokuwa kwenye ndege angani ndipo huweza kuliona duwara lote la upinde wa mvuwa. Katikati ya duara la upinde wa mvua aghalabu huwa ndipo katikati pa duara la jua. Pale jua linapojitokeza zaidi, upinde huo vile vile hujitokeza zaidi ili kuendelea kubaki katika kiwango kile kile cha jua.

Mwenyezi Mungu Ameumba rangi hizi mchanganyiko zenye kupendeza machoni ili wanaadamu waweze kukiri uwezo na sifa zake. Mwenyezi Mungu ana uwezo wa kuumba idadi ya vitu vizuri isiyo na ukomo. Kwa hiyo, maumbile haya yawashawishi Wanaadamu katika kuukiri uwezo wa Mwenyezi Mungu ili wawe wenye kushukuru kwa kumuabudu katika kila hatua ya maisha yao.

Mbaamwezi ing’arayo usikuMwezi hufanana na jiwe kubwa lenye umbile la mpira linalozunguka Dunia. Nyakati za

usiku anga likiwa jeupe, mwezi hung’ara vizuri. Mwanga wa mwezi hautokani na mwezi wenyewe. Ni kama kioo, kinachoakisi mwanga wa jua. Hali ya Mwezi imeelezwa vizuri katika Qur’an kama ifuwatavyo:

“Ametukuka kweli kweli yule Aliyejaaliya mkusanyiko wa nyota angani na Akaweka humo taa itowayo mwanga na mwezi ung’arao(Surat al Furqaan).

Kwa kawaida wanaadamu wanaona upande mmoja tu wa mwezi kwa kuwa unajizungusha wenyewe na wakati huo huo ukizunguka Dunia kila baada ya siku 29. Tuangaliapo angani, nyakati za usiku, wakati fulani huonekana duara kamili na wakati mwingine nusu duwara. Kwa kadiri Mwezi unavyozunguka Dunia, sura yake huchukua maumbile tafauti. Dunia na Mwezi kila moja humvuta mwenziwe, lakini nguvu ya uvutano ya Dunia huzidi ile ya mwezi kwa mara sita zaidi. Licha ya kuzidiwa hivyo kiuvutano na Dunia, Mwezi nao huivuta Duniya na kusababisha kupwa na kujaa kwa bahari kwa kiwango kile kile kinachobaki katika usawa wa eneo la bahari. La kuzingatia kuhusu uweza wa Mwenyezi Mungu katika uumbaji ni kwamba kama isingalikuwa nguvu ya uvutano wa mwezi na Dunia na katikati yake kuwepo angahewa ya Dunia inayodhibiti na kukibakisha mahali pake kila kilichopo katika ardhi; basi Dunia katika kujizungusha kwake kwa kasi katika muhimili wake na katika kulizunguka jua, ingesababisha maji ya bahari kutotuwama yakikupwa na kujaa na kubaki yalivyo bila ya kumwagika. Ukichukua chombo kilichojaa maji kisha ukakiinamisha chini juu ni wazi kuwa maji yatamwagika. Lakini tunaona licha ya Dunia kuzunguka kwa kasi, maji ya bahari hayamwagiki kwa sababu Mwenyezi Mungu Ameumba angahewa kwa kuiambatanisha na Dunia ambayo hukivuta na kukibakisha chini kila kilicho juu ya uso wa

45

Dunia. Kama nguvu ya uvutano ya Mwezi ingalikuwa kubwa zaidi ya hii ya sasa, kupwa na kujaa kwa maji kungesababisha kiwango cha maji kuongezeka na hatimaye kufurika na kutawanyikia nchi kavu. Katika mazingira hayo, maeneo yaliyo jirani na bahari yangalikuwa na mafuriko nyakati zote. Hata hivyo, wakati wa kupwa na kujaa, maji ya bahari hubaki katika kiwango cha kawaida kwa sababu Mwenyezi Mungu amekadiria vilivyo nguvu ya uvutano ya mwezi na Dunia kuweza kuyalinda maji ya bahari yabaki kama yalivyo ili kuwahifadhi wanaadamu na janga la mafuriko makubwa.

Nyakati za usiku na majiraWakati ikijizungusha yenyewe katika muhimili wake, Dunia yetu hubetuka kidogo

kutoka katika njiya yake. Hali hiyo ndiyo hufanya kuwepo kwa majira; masika, kiangazi na kipupwe. Mwenyezi Mungu angalitaka angaliweza kuifanya Dunia ibaki katika njia yake bila ya kujibetuwa, hivyo kusingalikuwa na majira. Halijoto ingalikuwa moja Duniani kote. Kwa hivyo tangu chakula tulacho na hewa tuvutayo, aina ya maisha tuishiyo na mazingira kwa jumla yangalikuwa tafauti na haya ya sasa. Usiku na mchana unapatikana vipi katika anga linaloonekana kiza tupu. Ardhi yetu ambayo inaogelea katika anga hilo, inajizungusha yenyewe katika mhimili wake hivyo kuna kutafautiana baina ya usiku na mchana. Nyakati za asubuhi, wanaadamu huamka juwa likiwapa mwanga na usiku unapoingia huwa kiza. Dunia inapokuwa katika mwendo wake wa kasi katika njiya yake vile vile hujizungusha yenyewe katika muhimili wake. Kwa hiyo kadiri inavyojizungusha, upande unaolielekea juwa huwa ndiyo wenye mwanga. Tafauti na Sayari ya Dunia, Sayari ya Uranasi hujizungusha katika pande zake kama vile inaanguka. Hii husababisha Sayari hiyo kubiringika mithilli ya pipa wakati ikizunguka jua ikiwa katika njia yake. Msitari wa kati wa Uranasi hulielekea juwa kwa nyuzi 98 kutoka kwenye Obiti, kwa hivyo kila ncha ya sayari hiyo hulikabili jua vilivyo kwa karibu kila sehemu ya mzunguko huo. Kwa hivyo huchukua miaka 84 ya Dunia kwa Uranasi kulizunguka jua. Kwa muda wote huo, kila ncha ya Uranasi hupokea mwanga wa Jua au huwa na kiza kwa mfululizo.

Nini kingalitokea iwapo Dunia nayo ingalikuwa na mwendo kama wa sayari ya Uranasi ambapo mchana ungalikuwa upande mmoja kwa muda wote na usiku ungalikuwa kama hivyo hivyo pia. Bila ya shaka, kwa muda wote wa miaka 84, watu wangalizaliwa na kuishi hadi kufa bila ya kuona mchana au usiku. Kwa hiyo kama hali ingalikuwa ni hiyo watu wasingalikuwa na muda maalumu wa kulala. Kila mmoja angalijiamulia mwenyewe kwenda kulala au kuwa macho kwa nyakati tafauti. Hivi ingalikuwa mchana tu wanaadamu wangaliweza kulala na kukoroma? Hata hivyo, wasingaliweza kuuona mwezi na nyota ambazo huonekana usiku wakati wa kiza. Vivyo hivyo kama ingalikuwa usiku tu wanaadamu wangalikuwa wakiishi kwenye kiza tu. Kwanza wasingaliweza kuliona jua, anga zuri la samaa au maumbile mengine mazuri yanayoonekana nyakati za mchana. Hakuna anayejua ni vipi muda wa kulala ungalikuwa au ungeanzaje. Wangalikuwa wakifanya shughuli zao nyakati za kiza na kupumzika wakiwa kizani. Kilicho muhimu zaidi ni jinsi mimea inavyohitaji nyakati zote mbili kuweza kusitawi. Kwa hali hiyo mimea isingalikuwepo. Na kwa hivyo Ulimwengu huu

46

ungalikosa uhai. Mwenyezi Mungu Ameumba usiku na mchana ili kurahisisha maisha. Kwa kuumba usiku na mchana, Ameyaweka maisha katika utaratibu maalumu. Sababu za kuumbwa usiku na mchana zimeelezwa katika Qur’an kama ifuwatavyo:

“Na Yeye ndiye Aliyekufanyieni usiku kuwa nguwo na usingizi kama kufa, na Akaufanya mchana uwe kama ndiyo kufufuka”(Surat Furqan).

Wakizingatia kwamba kila siku uvumbuzi na ugunduzi wa kisayansi hufanyika, lakini hakuna hata moja kati ya hizo umepata kitu kipya mbali ya vile ambavyo tayari vipo katika maumbile. Hakuna uvumbuzi wowote ambao ulifanya Dunia ijizungushe yenyewe katika mhimili wake ili upatikane usiku na mchana. Ni Mwenyezi Mungu peke yake Aliyefanya hivyo kwa kuwa Ndiye Muumba wa Mbingu, Ardhi na vyote vilivyomo. Wanaadamu wanapaswa kuleta mazingatio kwamba iko siku ambayo Mwenyezi Mungu Aliyeumba usiku na mchana, ataviondoa siku moja. Ikifikia hapo, maisha ya wanaadamu yatakuwa katika hamkani kubwa na zaidi ya hivyo viumbwa hawataendelea kuwepo tena.

Katika Qur’an, Mwenyezi Mungu Anabainisha kwamba Angalipenda angaliweza kuufanya usiku au mchana uwe wa kuendelea:

“Iwapo Mwenyezi Mungu Akiufanya usiku uwe wenye kuendelea mpaka siku ya kiyama, ni Mungu gani asiyekuwa Mwenyezi Mungu atakayekuleteeni mwanga?(28:71).

“Iwapo Mwenyezi Mungu Akiufanya mchana uwe wenye kuendelea mpaka siku ya kiyama, ni Mungu gani asiyekuwa Mwenyezi Mungu atakayekuleteeni usiku?(28: 72).

Aya hizi zinabainisha wazi kuwa si usiku wala mchana ambao ungaliweza kuwepo bila ya Mwenyezi Mungu kutaka. Ulimwengu huu tunaouona na maumbile mengine yaliyo nje ya Ulimwengu huu tusiyoweza kuyadiriki kwa milango yetu ya fahamu na kila kitu vyote vimeumbwa na Mwenyezi Mungu. Ni Mwenyezi Mungu aliyewaumba wanaadamu kwa umbo kamilifu kabisa na ndiye Aliyeumba kila kitu.

HitimishoKatika kitabu hiki, yameshuhudiwa maajabu ya uumbwaji wa Ulimwengu. Wasomaji

wameona ya kwamba uko utaratibu wa hakika wenye uwiano na ulinganifu wa ajabu kabisa. Wameona kwamba, Dunia ni sayari iliyoumbwa kwa makusudi kabisa kuwezesha viumbwa kuishi. Watu wametokeya baada ya miaka mingi kupita baada ya kuumbwa Dunia na maumbile mengine. Kama ingalikuwa wanaadamu hawakuumbwa na Muumba mmoja mweledi, wasingalikuwa na maumbile yanayowiana na hali au mazingira ya Dunia waliyoyakuta baada ya muda mrefu wa wao kutokuwepo.

47

“Hakika zilipita dahari(karne) nyingi Mwanadamu hakuwa kiumbe kinachotajwa”(76:1).

Katika kuhitimisha, hebu tuchukuwe mfano mmoja tu kutoka katika mwili wa Mwanaadamu kuonesha muungano na uwiano wa ajabu unaothibitisha kuwapo kwa Muumba mweledi, mfano huu ni ule Mfumo wa mawasiliano mwilini.

Wengi wetu twaijua minara mirefu ya mawasiliano na wengi wetu pia tumeiona mitambo ya kurushia taarifa na habari katika Televisheni. Taswira inayotujia kichwani ni ile ya mtambo uliojaa antena na vifaa tata vya umeme. Taswira hii ni sahihi kwa sababu, ili kuvijua vifaa vya teknolojia iliyotumika katika ufungaji wa mitambo hiyo, mtu lazima awe na utaalamu wa uhandisi katika mambo ya elektroniki na mawasiliano. Aidha karibu sote tunakubali kuwa nyenzo hizi ni muhimu mno katika kutuwezesha kupata mawasiliano na watu mbalimbali katika sehemu mbalimbali za Ulimwengu.

Sasa hebu fikiria; hali itakuwaje iwapo minara yote ya mawasiliano pamoja na vituo vya mawasiliano vitafungwa kwa muda mfupi tu? Hapana shaka kuwa hali hiyo itasababisha vurugu na wasiwasi. Hata hivyo, hata kama hali hiyo itasababisha hasara kubwa ya mali lakini bado hasara hiyo inaweza kufidiwa. Lakini endapo mawasiliano baina ya seli zetu Trilioni 100, au mawasiliano ndani ya seli moja tu yatakatika kwa muda mchache sana na hivyo taarifa zisifike katika vituo vyao, matokeo yake ni kifo. Mifumo ya sasa ya mawasiliano inatengenezwa kwa kutumia nyenzo za elektroniki na zana zenye Teknolojia za hali ya juu lakini teknolojia ya mifumo ya ndani ya mawasiliano ya seli, ambayo pia ni tete mno wanaadamu kuielewa yenyewe inajengwa kwa nyenzo zitokanazo na protini. Ndani ya protini hakuna njia za umeme au hata vyombo vya kupokea umeme kama vile vilivyomo katika nyenzo za kawaida. Humo mna Atomu tu za Kaboni, Haidrojeni, Oksijeni na Naitrojeni. Inakisiwa zipo takribani Protini 30,000 za aina mbalimbali katika kiwiliwili cha mtu na kati ya hizo, ni asilimia mbili (2%) tu ya protini hizo ndiyo ambayo kazi yake inafahamika kikamilifu. Kazi ya Protini nyingi zinazofanya kazi katika mwili kwa kiasi kikubwa bado haijafahamika.

Mfumo wa mawasiliano miongoni mwa seli kwa namna fulani unafanana na mifumo inayotumiwa na binadamu. Kwa mfano juu ya kiwambo au utando wa seli kuna “Antena” ambazo zinaziwezesha seli hizo hupokea taarifa zinazozifikia. Chini kidogo tu ya Antena hizi kuna vituo ambavyo vinatafsiri taarifa zilizotumwa kwenye Seli. Antena hizi zipo juu ya utando wa seli wenye upana wa Milimita Miamoja elfu unaozingira Seli. Kipokezi hiki cha mawasiliano ambacho hujulikana kama “tyrosine kinase” kina sehemu kuu tatu: Antena, Bodi na mkia. Umbile la sehemu ya Antena inayotoka kwenye utando wa seli linafanana na Antena ya Dishi inayotumika kukusanya taarifa za Satellite. Kila Antena moja ya dishi hukusudiwa kupokea mawasiliano fulani ya Setellite, vivyo hivyo kuna vipokezi tafauti ambavyo huelewa lugha ya taarifa zinazobebwa na molekuli mbalimbali za homoni. Taarifa zitokeazo katika seli/ homoni mbalimbali huingia katika Antena juu ya utando wa seli, lakini kila antena hukusudiwa

48

kupokea taarifa moja tu. Huu ni mfumo wa aina yake ambapo hata mara moja taarifa haiwezi kupelekwa kimakosa katika Seli nyingine.

Uwiano mkubwa uliopo baina ya homoni na Antena unaoonekana katika kila kazi ya kibailojia waweza kulinganishwa na uhusiano kati ya funguo na kitasa. Kwamba, ni ule ufunguo sahihi tu ndio unaoweza kufungua kitasa husika. Hii ni kusema kuwa, ni ile seli husika tu ndiyo itakayohusika na ujumbe uliotumwa, ambapo kwa seli nyinginezo ujumbe huo hauna maana kabisa. Pale homoni inapoifikia seli, huufanya mfumo huu mzima wa ajabu uwe katika harakati. Kupitia mfumo maalumu wa mawasiliano, ujumbe unaokwenda kwenye seli hupelekwa kwenye DNA ya Seli hiyo. Kisha seli hiyo huingizwa katika utendaji kazi kwa mujibu wa ujumbe huo. Ili kuelewa jinsi utendaji huu wa kazi ulivyo wa ajabu, hebu jaribu kulifikiria tukio ambalo mtu yeyote anaweza kukutana nalo katika maisha ya kila siku . Taarifa hutumwa kupitia mtandao wa Intaneti na kumfikia yule ambaye kompyuta yake imeunganishwa katika mtandao wa Intanent katika kompyuta nyingine.Taarifa inayotumwa kwenye kompyuta husambazwa katika sehemu nyingine, kwa mfano katika kichapishio (Printa) ambapo printa nayo huuweka ujumbe katika karatasi. Watu wamekuwa wakitumia kompyuta tangu miaka ya themanini:

Kompyuta imekuwa ikitumika majumbani na makazini, na tangu miaka ya tisini, mtandao wa intanet umekuwa sehemu ya maisha ya watu. Iwapo siku moja itatokea kusoma habari katika gazeti kuwa kametengenezwa ka ngamiza (kakompiyuta) kadogo mno ambako hakaonekani kwa macho na kwamba kompyuta hako kana mawasiliano na kompyuta nyingine, jawabu lako litakuwa tafauti kabisa. Pengine hutaamini kuwa tekinolojiya hii ya mawasiliano yaweza kufanyika kwa kompyuta ya saizi hiyo. Hata hivyo, katika maisha halisi; kuna mfumo wa mawasiliano wenye teknojiya ya hali ya juu zaidi unaofanya kazi katika eneo dogo mno lisiloonekana kwa macho. Ule ukweli kwamba ujumbe unaotoka katika antena za seli husambazwa kwa kasi kubwa kwenye mzingo wa seli na kwamba teknolojiya hiyo ya hali ya juu hutumika katika mchakato wa mawasiliano, ni wa ajabu kabisa kuliko kijikompyuta kidogo kisichoonekana kwa macho matupu. Hii ni kwa sababu seli ni pande la nyama na kiwiliwili chako kizima, kuanziya macho yako unayosomeya gazeti hili hadi mikono yako unayoshikiya gazeti hili hujengeka kwa seli zinazofanya kazi pamoja.

Katika mwili wa kila mmoja wetu kuna chembe ndogo ndogo zipatazo Trilioni mia moja ambazo zina mfumo wa hali ya juu wa mawasiliano. Katika awamu ya mwisho ya karne ya ishirini kulikuwa na hatua nyingi za maendeleo ya kisayansi katika nyanja ya mawasiliano ya seli. Hatua kubwa zilipigwa katika ugunduzi wa mitandao ya mawasiliano ndani kabisa ya miili yetu. Kwa mfano tukiangalia tuzo za nishani ya nobeli zilizotolewa katika miaka kumi na miwili iliyopita, tuzo zipatazo sita zilizotolewa katika fani ya tiba, zilitolewa kwa ajili ya ule utafiti uliofanywa katika eneo la mawasiliano. Ni umbali gani tulifikia katika mwaka 2003? Je ni hatua gani mbele ulimwengu wa sayansi unatakiwa kupiga? Jibu la swali hili ni muhimu

49

kweli kweli kwa sababu majibu tutakayoyatoa yatatusaidia kuelewa kuwa mfumo wa mawasiliano ya seli ni ajabu kubwa ya maumbile.

Katika nchi mbali mbali duniani kuna Taasisi nyingi ambazo zinatumia bajeti ya mamilioni ya Dola kufanya utafiti wa jambo hili. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2000, Shirika la mawasiliano ya seli (Alliance for Cellular Signaling- AFCS) lilianzishwa. Vyuo vikuu vipatavyo ishirini pamoja na mamia ya wanasayansi wa shirika hili, na Muwasisi wake, Alfred Gilman walizawadiwa nishani ya Nobel mwaka 1994 kwa ile kazi juu ya mawasiliano ya seli, Prof. Gilman alikuwa na haya ya kusema kuhusiana na suala hili:

“Iwapo ubongo unahitaji sukari, Ini lazima liizalishe. Kama misuli inahitaji damu zaidi, Moyo lazima udunde kwa kasi zaidi. Mamia ya Sigino tafauti za kikemikali hutiririka mwilini mzima kutoka kwenye seli moja, kushajiisha kazi za seli nyingine. Daima Seli humiminikiwa na idadi kubwa ya Sigino za kikemikali ambazo huziambia nini cha kufanya na vipi zitende kazi zao.Tatizo kubwa na ambalo ni gumu zaidi kulitafiti ni namna zote hizi zinavyofanyakazi pamoja”.

Wapo Wanasayansi wanaolizungumzia suala hili kwa uwazi na ukweli. Mmoja wao ni yule mshindi wa mwaka 1999 wa tuzo ya Nobeli, Gunter Blobel ambaye alifanya utafiti wa mfumo wa maalumu “zip code” katika seli. Profesa huyu mashuhuri duniani alisema yafuatayo katika mahojiano juu ya jambo hili:

“Inatahayarisha kuona jinsi tunavyoelewa kidogo sana juu ya namna seli inavyofanya kazi na hiyo itachukuwa muda mrefu na mrefu mno kuitafiti. Karne ya ishirini na moja, kufuatia maendeleo ya sayansi, imetuwezesha kujua zaidi maajabu yasiyo kifani ya mawasiliano ndani ya seli zetu”.

Kwa mtu mwenye kuelewa yaani mtu mwenye akili, kila mfumo unaogunduliwa huwa

ishara kwake ya hekima na uweza mkubwa wa Mwenyezi Mungu na ni ishara ya kutuwaidhi kuwa yeye ndiye Mola pekee anayestahiki kutukuzwa na kushukuriwa.

Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Muumbaji, Mtengenezaji, Mfanyaji wa sura; Mwenye majina mazuri. Kinamtukuza kila kilichomo mbinguni na ardhini. Naye ni Mwenye nguvu, Mwenye Hikima. (59:24)

Tulichokiona katika maudhui ya kitabu hiki hakika kinathibitisha kwamba si Ulimwengu, Dunia wala maumbile ambayo yangaliweza kuwepo kutokana na mfuatano wa utukiaji wa pole pole wa maumbile katika hali ya kubahatisha kama wanavyoeleza watu wasiyojua. Yote haya yanabainisha ukweli kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye uwezo usiyo na ukomo, Mwenye

50

kudra, Ameumba Ulimwengu, nyota, sayari, milima na bahari kwa ukamilifu, na amevipa uhai vitu vyote vinavyoishi. Uumbaji huu wenye ukamilifu unaelezwa katika Qur’an:

“Je, nyinyi ni wenye umbo la nguvu zaidi au Mbingu? Yeye amezijenga? Akainua kimo chake na akazitengeneza vizuri. Akautia kiza usiku wake na Akautokezesha mchana wake. Na ardhi baada ya hayo Akaitandaza. Akatowa ndani yake maji yake na malisho yake. Na milima akaisimamisha kwa ajili ya kukustarehesheni nyinyi na mifugo yenu(Surat Naziat 27:33).

Muda wote, wanaadamu wanatakiwa wazingatie kwamba Mwenyezi Mungu Ameumba ulimwengu na maumbile, Amewaumba wao na kila kitu walichonacho. Kila wanachokimiliki ni Rehema kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kwa ajili hiyo wanapaswa kuzingatiya ukweli wa kimaumbile kwa kuvuta fikira juu ya Rehma na Neema walizopewa, kisha wawe wenye kumshukuru Muumba kwa kutekeleza maamrisho na kuacha makatazo yake katika kila hatua ya maisha yao ya kila siku na kisha waseme kama walivyosema Malaika:

“Utakatifu ni wako!Hatuna ilimu isipokuwa ile uliyotufundisha;

bila shaka Wewe ni Mjuzina Ndiwe Mwenye hikima”

(2:32).

51