1
Mamlaka ya Mapato Tanzania inapenda kuwataarifu waajiriwa wapya waliopangiwa kazi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hivi karibuni baada ya mchakato wa ajira kupitia Sekretarieti ya ajira kukamilika kuwa, wanatakiwa kuripoti Chuo Cha Kodi (ITA) kilichopo Mikocheni “B”‘Industrial Area’ siku ya Jumamosi tarehe 8 Juni, 2019, ambapo kutakuwa na mchakato wa ukamilishwaji wa taratibu za ajira kwa siku ya tarehe 8 na 9 Juni, 2019 kuanzia saa 2.00 asubuhi na baadaye mafunzo kuanzia tarehe 10 –19 Juni, 2019. Ili kukamilisha zoezi hilo, kila mwajiriwa mpya anatakiwa afike na nyaraka zifuatazo:- 1. Barua ya kupangiwa kituo cha kazi kutoka Sekretarieti ya Ajira. 2. Nyaraka zote muhimu za taarifa binafsi ziwe na majina matatu, mfano cheti cha kuzaliwa na vyeti vya taaluma. Endapo jina mojawapo halipo katika vyeti basi utahitaji kuwa na kiapo kilichothibitishwa na msajili wa Hati (Deed poll) kutoka Wizara ya Ardhi. 3. Endapo umebadilisha majina utatakiwa kuwasilisha kiapo kilichothibitishwa na Msajili wa Hati (Deed poll) kutoka Wizara ya Ardhi. 4. Vyeti vya Elimu na Taaluma:- (i) Nakala halisi na (ii) Nakala ambazo zimethibitishwa na mwanasheria (Certified copies). 5. Kwa waliosoma nje ya nchi kwa elimu ya sekondari na vyuo wawasilishe nakala za uthibitisho kutoka NECTA, NACTE na TCU. 6. Cheti cha kuzaliwa (Birth Certificate) (i) Mwajiriwa–(Nakala 3 zilizothibitishwa na Mwanasheria) (ii) Wategemezi (Watoto/Mke)- Nakala 3 zilizothibitishwa na Mwanasheria 7. Cheti halisi cha ndoa na nakala 2 zilizothibitishwa na Mwanasheria 8. Nakala 1 ya Kitambulisho cha Taifa , iliyothibitishwa na Mwanasheria 9. Picha (Passport size) (i) Mwajiriwa nakala 8 (ii) Wategemezi nakala 1 10. Wasifu binafsi (Curiculum Vitae) Imetolewa na; Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala KNY: KAMISHNA MKUU TAARIFA KWA WAAJIRIWA WAPYA WALIOPANGIWA KAZI TRA 4 Juni, 2019 Dara es Salaam.

TAARIFA KWA WAAJIRIWA WAPYA WALIOPANGIWA KAZI TRA · vyeti vya taaluma. Endapo jina mojawapo halipo katika vyeti basi utahitaji kuwa na kiapo kilichothibitishwa na msajili wa Hati

  • Upload
    others

  • View
    2

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: TAARIFA KWA WAAJIRIWA WAPYA WALIOPANGIWA KAZI TRA · vyeti vya taaluma. Endapo jina mojawapo halipo katika vyeti basi utahitaji kuwa na kiapo kilichothibitishwa na msajili wa Hati

Mamlaka ya Mapato Tanzania inapenda kuwataarifu waajiriwa wapya waliopangiwa kazi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hivi karibuni baada ya mchakato wa ajira kupitia Sekretarieti ya ajira kukamilika kuwa, wanatakiwa kuripoti Chuo Cha Kodi (ITA) kilichopo Mikocheni “B” ‘Industrial Area’ siku ya Jumamosi tarehe 8 Juni, 2019, ambapo kutakuwa na mchakato wa ukamilishwaji wa taratibu za ajira kwa siku ya tarehe 8 na 9 Juni, 2019 kuanzia saa 2.00 asubuhi na baadaye mafunzo kuanzia tarehe 10 –19 Juni, 2019.

Ili kukamilisha zoezi hilo, kila mwajiriwa mpya anatakiwa a�ke na nyaraka zifuatazo:-1. Barua ya kupangiwa kituo cha kazi kutoka Sekretarieti ya Ajira.2. Nyaraka zote muhimu za taarifa binafsi ziwe na majina matatu, mfano cheti cha kuzaliwa na vyeti vya taaluma. Endapo jina mojawapo halipo katika vyeti basi utahitaji kuwa na kiapo kilichothibitishwa na msajili wa Hati (Deed poll) kutoka Wizara ya Ardhi. 3. Endapo umebadilisha majina utatakiwa kuwasilisha kiapo kilichothibitishwa na Msajili wa Hati (Deed poll) kutoka Wizara ya Ardhi. 4. Vyeti vya Elimu na Taaluma:- (i) Nakala halisi na (ii) Nakala ambazo zimethibitishwa na mwanasheria (Certi�ed copies).5. Kwa waliosoma nje ya nchi kwa elimu ya sekondari na vyuo wawasilishe nakala za uthibitisho kutoka NECTA, NACTE na TCU. 6. Cheti cha kuzaliwa (Birth Certi�cate) (i) Mwajiriwa–(Nakala 3 zilizothibitishwa na Mwanasheria) (ii) Wategemezi (Watoto/Mke)- Nakala 3 zilizothibitishwa na Mwanasheria7. Cheti halisi cha ndoa na nakala 2 zilizothibitishwa na Mwanasheria8. Nakala 1 ya Kitambulisho cha Taifa , iliyothibitishwa na Mwanasheria9. Picha (Passport size) (i) Mwajiriwa nakala 8 (ii) Wategemezi nakala 110. Wasifu binafsi (Curiculum Vitae)

Imetolewa na;Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala

KNY: KAMISHNA MKUU

TAARIFA KWA WAAJIRIWA WAPYA WALIOPANGIWA KAZI TRA

4 Juni, 2019 Dara es Salaam.