8
HOTUBA YA KATIBU MKUU KIONGOZI KWENYE MAKABIDHIANO YA HATI YA HISA NA NYARAKA HUSIKA ZA UNUNUZI WA HISA 26% ZA GENERAL TYRE INTERNATIONAL COMPANY - CONTINENTAL AG KATIKA KAMPUNI YA GENERAL TYRE EAST AFRICA LIMITED, OFISI ZA MSAJILI WA HAZINA, DAR ES SALAAM, 21 AGOSTI, 2015 ______________________________ 1.0 UTANGULIZI 1.1 Kiwanda cha General Tyre East Africa Limited (GTEA) kilianzishwa mwaka 1969 kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania (mmiliki wa 74% ya hisa) na kampuni ya General Tire International Company (GTIC) ya Marekani (26%). Lengo lilikuwa kuzalisha na kuuza aina mbalimbali za matairi ya magari kwa kutumia nembo ya “General” ya ‘General Tyre Brand’ kwa kuzalisha matairi 320,000 kwa mwaka. Uzalishaji ulianza rasmi mwaka 1971 na mwaka 1987 hisa zote za GTIC zilinunuliwa na Continental Arktiengesellschaft Germany (Continental AG). 1.2 Uzalishaji uliendelea hadi 2007 ambapo matatizo mbalimbali yalianza kujitokeza ya kujiendesha kutokana na sababu mbalimbali na mojawapo ikiwa usimamizi hafifu wa kiwanda hicho na hatimaye kufungwa kabisa mwaka 2009 hadi hivi sasa. 1

Talking Points.generaltyre1

Embed Size (px)

DESCRIPTION

talking points.generaltyre1

Citation preview

Page 1: Talking Points.generaltyre1

HOTUBA YA KATIBU MKUU KIONGOZI KWENYE MAKABIDHIANO YA HATI YA HISA NA NYARAKA HUSIKA ZA UNUNUZI WA HISA

26% ZA GENERAL TYRE INTERNATIONAL COMPANY - CONTINENTAL AG KATIKA KAMPUNI YA GENERAL TYRE EAST

AFRICA LIMITED, OFISI ZA MSAJILI WA HAZINA, DAR ES SALAAM, 21 AGOSTI, 2015______________________________

1.0 UTANGULIZI

1.1 Kiwanda cha General Tyre East Africa Limited (GTEA)

kilianzishwa

mwaka 1969 kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania (mmiliki

wa 74% ya hisa) na kampuni ya General Tire International

Company (GTIC) ya Marekani (26%). Lengo lilikuwa

kuzalisha na kuuza aina mbalimbali za matairi ya magari

kwa kutumia nembo ya “General” ya ‘General Tyre Brand’

kwa kuzalisha matairi 320,000 kwa mwaka. Uzalishaji

ulianza rasmi mwaka 1971 na mwaka 1987 hisa zote za

GTIC zilinunuliwa na Continental Arktiengesellschaft

Germany (Continental AG).

1.2 Uzalishaji uliendelea hadi 2007 ambapo matatizo

mbalimbali

yalianza kujitokeza ya kujiendesha kutokana na sababu

mbalimbali na mojawapo ikiwa usimamizi hafifu wa kiwanda

hicho na hatimaye kufungwa kabisa mwaka 2009 hadi hivi

sasa.

1.3 Serikali ikiwa na hisa nyingi pamoja na mipango madhubuti

ya

kuendeleza viwanda iliamua kwa dhati kuwa kiwanda hiki

kifufuliwe mara moja. Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na 1

Page 2: Talking Points.generaltyre1

Biashara Mwezi Mei 2012 iliikabidhi NDC jukumu la kufufua

kiwanda na kuandaa mazingira bora ambayo yatavutia

sekta binafsi kushiriki katika kufufua na kupanua kiwanda

hiki.

1.4 Lengo la Serikali ni kufufua kiwanda hiki cha matairi na

kuanza

kuzalisha matairi yenye ubora ambayo yatahimili ushindani

katika soko la ndani na ukanda wa Afrika Mashariki.

2.0 HATUA ZILIZOFIKIWA ZA UFUFUAJI WA KIWANDA

2.1 Serikali kupitia Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) chini ya

Wizara

ya Viwanda na Biashara, ilifanya tathmini ya hali ya

kiwanda ilivyokua kwa wakati huo na kutayarisha ‘Concept

Note’ ambayo ilionesha dira ya kufufua kiwanda hicho.

2.2 NDC inaendelea kutayarisha mazingira bora ya uwekezaji ili

kuweza kuvutia wawekezaji watakaoshirikiana nao katika

kukamilisha kufufua, kupanua na kuweka miundombinu

bora ya kuongeza uzalishaji wa matairi. Juhudi za ufufuaji

zimefanyika katika maeneo yafuatayo:

2.3 Ukarabati wa awamu ya kwanza wa jengo la utawala, jengo

la mtambo wa mvuke, na kubadilisha mabati katika sehemu

ambazo zilikuwa zinavuja kwenye paa la kiwanda;

2.4 Tathmini ya kiufundi iliyohusisha ukaguzi wa mashine,

mitambo pamoja na miundombinu ya kiwanda, ili kujua

ukubwa wa kazi na kiasi cha fedha kinachohitajika katika

kufufua mitambo hii;

2

Page 3: Talking Points.generaltyre1

2.5 Uandaaji wa Mpango wa Kibiashara (Business Plan) wa awali

wa ufufuaji wa kiwanda na kuhusisha mali ghafi ya mpira

unaopatikana nchini na nchi jirani;

2.6 Ukarabati wa mfumo wa umeme na vifaa husika

unaendelea;

2.7 Utafiti wa soko la matairi nchini na Afrika Mashariki ambao

kwa ujumla ulibaini kuwa soko lipo ingawa limetawaliwa na

matairi kutoka Mashariki ya mbali;

2.8 Kubaini wafanyakazi muhimu waliokuwepo mpaka wakati

kiwanda kinasitisha uzalishaji;

2.9 Ukarabati wa mitambo ya kuzalisha matairi utafanyika

baada ya kukamilika ukarabati wa mfumo wa umeme;

2.10 Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Mahesabu (Internal Auditor

General) alishakamilisha tathimini ya mali na madeni ya

Kampuni ya GTEA;

2.11 Mkataba wa Ununuzi wa Hisa asilimia 26 kutoka Continental

AG katika GTEA ulisainiwa tarehe 30 April 2015 na malipo

ya hisa hizo yalifanyika 30 Julai 2015 ndani ya siku 90 kwa

mujibu wa mkataba;

3.0 MPANGO WA KUFUFUA KIWANDA

3

Page 4: Talking Points.generaltyre1

3.1 Serikali imekuwa ikifanya juhudi zote kuhakikisha kuwa

masuala yote ya kisheria na umiliki wa kiwanda

yanatatuliwa ili kusiwepo na migongano wakati wa kuingia

ubia na wawekezaji ambao tutashirikiana nao kuendeleza

kiwanda hiki.

3.2 Kuhamisha mali za GTEA kwenda NDC ili kuipa nguvu ya

kisheria ya kutafuta mbia wa kushirikiana naye katika

kuendeleza kiwanda.

3.3 Kukamilisha ukarabati wa mfumo wa umeme wa kiwanda ili

kufanya majaribio ya mitambo na miundombinu husika

kuwezesha NDC kufanya majaribio ya uzalishaji wa matairi.

3.4 Kutafuta mbia/mwekezaji mahiri, ambaye atashirikiana na

NDC kuendesha na kupanua kiwanda hiki kwa kutumia

teknolojia ya kisasa ili kuongeza uzalishaji na ubora wa

matairi.

3.5 Kuhamisha milki ya mashamba ya mpira kwenda NDC ili

nayo yafufuliwe na kutoa malighafi ya kutosha kwa

kiwanda.

4.0 MAKABIDHIANO YA NYARAKA

4.1 Kama ilivyosemwa hapo juu, Serikali imeshanunua hisa

asilimia 26, hivyo, kwa sasa, kiwanda cha Matairi cha

Arusha kinamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100.

4.2 Sasa tunashuhudia makabidhiano ya nyaraka muhimu za

umiliki wa hisa hizo kutoka kwa General Tire International

Company/Continental AG kwenda Serikalini.4

Page 5: Talking Points.generaltyre1

4.3 Hatua hii iliyofikiwa ni mwanzo mzuri wa kuanza uzalishaji

wa matairi nchini.

4.4 Hii itapunguza mzigo mkubwa kwa taifa wa kuagiza matairi

kwa kutumia fedha za kigeni na ikiwa ni mikakati mahususi

ya kufufua viwanda nchini.

4.5 Unatangazia Umma wa Watanzania kwamba sasa Kiwanda

cha kuzalisha Matairi cha Arusha ni mali ya Serikali na

hakuna mbia mwenza yeyote.

5.0 SHUKRANI

5.1 Mafanikio haya yametokana na juhudi kubwa za watu wengi

na taasisi nyingi.

5.2 Namshukuru sana Rais, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho

Kikwete, ambaye binafsi alitusukuma sana tuhakikishe

kiwanda hiki kinarudi mikononi mwa Serikali kwa asilimia

mia moja na kwamba tunakifufua kwa kutambua umuhimu

wake kwa maendeleo ya Taifa, na kwa ajira na uchumi wa

Jiji la Arusha.

5.3 Nashukuru sana Mwansheria Mkuu wa Serikali na Wataalam

wa Ofisi yake kwa ushauri uliotuwezesha kufika hapa.

5.4 Namshukuru Waziri wa Viwanda, Katibu Mkuu, Bodi na

Watendaji wa NDC kwa juhudi zao kubwa.

5

Page 6: Talking Points.generaltyre1

5.5 Ninaishukuru Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa

Kimataifa, akiwemo Balozi na Ubalozi wa Tanzania, Berlin,

Ujerumani katika kufanikisha majadiliano na aliyekuwa mbia

wetu.

5.6 Ninaishukuru timu ya Serikali iliyofanya majadiliano, (yaani

Government Negotiating Team) kwa kazi nzuri.

5.7 Naishukuru Kampuni ya Continental AG ya Ujerumani

ambao ndio walikuwa wabia wetu kwa ushirikiano wao hadi

tulipokamilisha kurejesha hisa zao mikononi mwa Serikali.

5.8 Mwisho, kwa kutajwa lakini si kwa umuhimu, ni shukrani

nyingi kwa Wizara ya Fedha, na Msajili wa Hazina, ambao

bila mchango wao, na bila wao kutoa fedha za kununua hisa

hizo, tusingefika hapa.

6