TANGAZO LA KAZI 1 JULAI 2014 NAO

Embed Size (px)

DESCRIPTION

pata ajira sasa

Citation preview

  • 5/23/2018 TANGAZO LA KAZI 1 JULAI 2014 NAO

    1/3

    1

    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAOFISI YA RAISSEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

    Kumb. Na EA.7/96/01/G/27 1 Julai, 2014TANGAZO LA NAFASI ZA KAZISekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwamujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwana Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombohiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazizinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi yaWatanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi 100 kwa ajili ya Mdhibiti naMkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

    NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.

    i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingiliakatika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi zakazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hilikutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenyeanwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)watatu wa kuaminika.vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vyakidato cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya2

    kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanishohivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.

    - Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.

    - Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI

    - Computer Certificate

    - Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)

    - Picha moja Passport size ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.vii. Testmonials, Provisional Results, Statement of results, hati matokeo zakidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)HAVITAKUBALIWA.

    viii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa nakuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuombaisipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia waliokokatika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezoyaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za

  • 5/23/2018 TANGAZO LA KAZI 1 JULAI 2014 NAO

    2/3

    kisheria.xii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 15 Julai, 2014xiii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajiraHAURUHUSIWI.xiv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwekupitia posta kwa anuani ifuatayo.Katibu, AU Secretary,Sekretariati ya Ajira katika Public Service RecruitmentUtumishi wa Umma, Secretariat,SLP.63100, P.O.Box 63100Dar es Salaam. Dar es Salaam.

    1.0 MKAGUZI WA HESABU DARAJA LA II (AUDITOR GRADE II) - NAFASI 1001.1 MAJUKUMU YA KAZI Kukagua nyaraka za matumizi, maendeleo, amana, wakala, mfuko, miradimaalum na mapato ya Serikali. Kushiriki kuandaa na kusimamia utekelezaji wa mpango wa kazi za ukaguzi wakila mwaka.

    3

    Kushiriki kufanya tathmini ya mpango wa kazi na kupendekeza mabadilikoinapobidi kulingana na tathmini ya taarifa ya utekelezaji ya mpango wa kazi. Kuhakikisha kuwa hoja na barua za ukaguzi zinatolewa na kushughulikiwa kwawakati unaotakiwa. Kushiriki kutayarisha na kutekeleza mpango wa ukaguzi (Audit Programme). Kushiriki kupanga na kuratibu mpango wa kazi za ukaguzi. Kutayarisha hoja na barua za ukaguzi. Kutunza daftari za kumbukumbu mbalimbali za hesabu katika kituo chake kwamaelekezo ya kiongozi wake mahali pa kazi.

    1.2 SIFA ZA MWOMBAJI

    Kuajiriwa wenye Shahada ya Biashara/Sanaa yenye mwelekeo wa uhasibu auStashahada ya juu ya Uhasibu (advanced Diploma in Accounting) kutoka vyuoau taasisi yoyote inayotambuliwa na Serikali. Wenye uzoefu wa kazi za ukaguzi wa hesabu kwa muda usiopungua mwakammoja (1) watafikiriwa kwanza.1.3 MSHAHARA

    Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D Kwamwezi.X.M. DAUDIKatibuSekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

  • 5/23/2018 TANGAZO LA KAZI 1 JULAI 2014 NAO

    3/3