6
Taarifa kwa vyombo vya habari Novemba 18,2015 Familia 30,000 zanufaika na umeme wa jua wa Mobisol nchini Tanzania na Rwanda -Mobisol yasherehekea mafanikio hayo kwa kutoa msaada wa nishati katika zahanati ya kijiji cha Ngasamo wilayani Simiyu Kampuni ya Mobisol yenye makao yake makuu mjini Berlini nchini ujerumani ambayo inajihusisha na uzalishaji wa umeme wa jua tayari imewaunganisha wateja wapatao 30,000 nchini Tanzania katika kipindi cha miaka 2 tangia ianze kutoa huduma hizi barani Afrika. Kasi hii ya ongezeko la wateja wanaotumia umeme nishati ya jua kutoka kampuni hii inadhihirisha kuwa uwekezaji wake unaendana sambamba na kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania za kupunguza tatizo la upatikanaji nishati ya umeme nchini.

Umeme Release Swahili

Embed Size (px)

DESCRIPTION

umeme release-swahili

Citation preview

Page 1: Umeme Release Swahili

Taarifa kwa vyombo vya habari

Novemba 18,2015

Familia 30,000 zanufaika na umeme wa jua wa Mobisol nchini Tanzania na Rwanda

-Mobisol yasherehekea mafanikio hayo kwa kutoa msaada wa nishati katika zahanati ya kijiji cha Ngasamo wilayani Simiyu

Kampuni ya Mobisol yenye makao yake makuu mjini Berlini nchini ujerumani ambayo inajihusisha na uzalishaji wa umeme wa jua tayari imewaunganisha wateja wapatao 30,000 nchini Tanzania katika kipindi cha miaka 2 tangia ianze kutoa huduma hizi barani Afrika.

Kasi hii ya ongezeko la wateja wanaotumia umeme nishati ya jua kutoka kampuni hii inadhihirisha kuwa uwekezaji wake unaendana sambamba na kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania za kupunguza tatizo la upatikanaji nishati ya umeme nchini.

Katika kuadhimisha mafanikio ya kufikisha idadi ya wateja 30,000 Mobisol imetoa msaada wa kuinganisha na umeme wa nishati ya jua zahanati ya serikali ya kijiji cha Ngasamo kilichopo Simiyu ambapo anatokea mteja aliyejiunganisha na umeme wa kampuni hiyo akiwa anakamilisha idadi ya wateja 30,000 katika nchi hizi mbili za Tanzania na Rwanda ambako inatoa huduma zake.

Akiongea wakati wahafla ya kutoa msaada huo iliyofanyika katika zahanati hiyo,Meneja Masoko wa Mobisol, bwana Nkora Nkoranigwa amesema kuwa kampuni hiyo imejizatiti kuondoa tatizo la giza nchini na

Page 2: Umeme Release Swahili

kuaikisha iawapatia wananchi umeme wa nishati ya jua wa uhakika kwa kutumia teknolojia ya kisasa na gharama nafuu.

“Sote tunaelewa kuwa nishati ya umeme inahitajika katika kuleta maendeleo ya haraka na kuwaongezea vipato hususani wakazi wa vijijini.Tutahakikikisa tunaunga mkono jitihada za serikali za kuzalisha na kusambaza umeme kwa kwa wananchi hususani wanaoisi maeneo ya vijijini kwa gharama nafuu ii uwasaidia katika itihada zao za kujiendelea kimaisha”.Alisema

Bwana Nkoranigwa Alisema umeme ikipatikana utasaidia wananchi kuachana na matumizi ya vibatari na kufurahia matumizi ya vifaa vya kisasa kama jokofu,feni ,kuchaji simu na viginevyo na kuwezesha watoto kujisomea katika mazingira mazuri wawapo majumbani na mashuleni hali ambayo itasaidia kuongeza kiwango cha ufaulu katika masomo yao.

Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Bwana Patrick Onyango alishukuru kwa msaada huo na kusema kuwa utawaondolea kero ya kukosa nishati ya umeme waliokuwa nayo kwa muda mrefu na itarahisisha utoaji wa huduma za matibabu kwa wagonjwa na aliahidi kuwa watahakikisha wanatunza vizuri vifaa vya nishati hiyo walivyozawadiwa “Kuna msemo kuwa akufaaye kwa dhiki ndio rafiki wa kweli”.Tunaishukuru kampuni ya Mobisol kwa msaada huu wa kusaidia wananchi wengi”Alisema.

Naye Afisa Utawala wa Wilaya hiyo Bwana Rabani Mageja kwa niaba ya serikali alishukuru kwa zahanati hiyo kupatiwa msaada wa nishati na aliongeza kuwa serikali wilayani humo itazidi kuunga mkono wawekezaji wanaokuja na miradi ya kusaidia kuleta maendeleo katika jamii kama ulivyo mradi wa nishati wa Mobisol.

Page 3: Umeme Release Swahili

Kwa upande wake mteja wa 30,000 wa kampuni ya Mobisol ambaye alisababisha hafla hiyo kufanyika kijijini hapo na zahanati kupatiwa msaada Bwana Kichoro alisema kuwa amefurahi kuona kampuni imemuenzi kwa kuleta msaada wa nishati kwenye zahanati wa kuwanufaisha wananchi wote.

Akiwa ni mteja wa umeme unaozalishwa na kampuni hiyo alisema ni wa uhakika na gharama nafuu na unafanya maisha kuwa rahisi na kisasa na kuwataka wanakijiji wajiunge kwa aili ya kuishi maisha ya kisasa na kuweza kuanzisha miradi midogo midogo ya uzalishaji kwa utumia nishati hiyo.

Mwisho

For further information contact

Seth Mathemu

Marketing Team Leader

Mob +255 755 94 92 81

[email protected]

Note to the editor

About Mobisol

Mobisol’s aim is to provide clean, affordable and reliable electricity to millions of households in low-income communities – stimulating economic and social development while simultaneously contributing to global environmental protection. Mobisol combines generating power from solar energy sources with

Page 4: Umeme Release Swahili

innovative mobile technology and IT solutions, as well as a comprehensive customer service plan.

The low-cost, high-tech solar systems can be paid for through convenient instalments for as low as 50 cents a day via mobile phones in a 36-month instalment plan. In this way customers circumvent the problem of high initial investment costs of solar home systems. Clients fully own their personal electricity source after three years. Mobisol customers enjoy an extended warranty and comprehensive service plan including customer education, remote monitoring of each system and free maintenance within 48 hours for three years.

Mobisol SHS’s are available in four different sizes ranging from 80 to 200 Watt. The smallest unit can e.g. illuminate a medium-sized home with ten LED bulbs as well as power a radio, charge various mobile phones and run a TV for some hours during the day. The largest system powers multiple lights, consumer appliances such as a laptop/TV, a DC refrigerator and charges up to ten mobile phones simultaneously. Mobisol also offers a “Business out of a Box” feature, which enables entrepreneurial customers to set-up income generating activities such as barbershops as well as phone and solar lantern charging stations.