1
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA TAARIFA KWA UMMA RATIBA YA MAZISHI YA MAREHEMU MHE. CELINA KOMBANI Kufuatia kifo cha aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ulanga Mashariki (CCM) Morogoro, Marehemu Mhe. Celina Kombani kilichotokea Alhamisi tarehe 24 Septemba, 2015 katika Hospitali ya Apollo iliyopo Nchini India alikokuwa anapata matibabu, Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia yake wanapenda kutoa taarifa ya awali ya mazishi kama ifuatavyo: Zoezi la kuaga na kutoa Heshima za Mwisho kwa Mwili wa marehemu Celina Kombani litafanyika kesho Jumatatu tarehe 28 Septemba, 2015 katika Viwanja vya Karimjee, Jijini Dar es Salaam kuanzia saa Nne Asubuhi na linatarajiwa kukamili Saa Nane Mchana. Baada ya zoezi hilo kukamilika, mwili Marehemu wa ulisafirishwa kwenda Morogoro kwa Njia ya Barabara na kupokelewa Nyumbani kwa Marehemu Maeneo ya Forest Hill na Viongozi wa Mkoa, Maafisa wa Serikali na Bunge Siku ya Jumanne tarehe 29 Septamba, 2015, ibada ya Mazishi itafanyika nyumbani kwake ikifuatiwa na Zoezi la kuaga na kutoa Heshima za Mwisho kwa Mwili wa marehemu Celina Kombani kabla ya Mazishi yatakayofanyika Shambani kwake Lukobe Nje kidogo ya Mji wa Mrorogoro. Pamoja na taarifa hii, taarifa zaidi juu ya msiba huu zitaendelea kutolewa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na Serikali na familia kadri zitakapopatikana ikiwa ni pamoja na ratiba nzima ya zoezi la Kuaga na Mazishi. “Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina lake Lihimidiwe” Imetolewa na: Ofisi ya Bunge, Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano DAR ES SALAAM 27 Septemba 2015

Updates - Kifo Cha Mhe. Kombani

Embed Size (px)

DESCRIPTION

UPDATES - KIFO CHA MHE. KOMBANI

Citation preview

Page 1: Updates - Kifo Cha Mhe. Kombani

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA

TAARIFA KWA UMMA RATIBA YA MAZISHI YA MAREHEMU MHE. CELINA KOMBANI Kufuatia kifo cha aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ulanga Mashariki (CCM) Morogoro, Marehemu Mhe. Celina Kombani kilichotokea Alhamisi tarehe 24 Septemba, 2015 katika Hospitali ya Apollo iliyopo Nchini India alikokuwa anapata matibabu, Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia yake wanapenda kutoa taarifa ya awali ya mazishi kama ifuatavyo:

• Zoezi la kuaga na kutoa Heshima za Mwisho kwa Mwili wa marehemu Celina Kombani litafanyika kesho Jumatatu tarehe 28 Septemba, 2015 katika Viwanja vya Karimjee, Jijini Dar es Salaam kuanzia saa Nne Asubuhi na linatarajiwa kukamili Saa Nane Mchana.

• Baada ya zoezi hilo kukamilika, mwili Marehemu wa ulisafirishwa kwenda Morogoro kwa Njia ya Barabara na kupokelewa Nyumbani kwa Marehemu Maeneo ya Forest Hill na Viongozi wa Mkoa, Maafisa wa Serikali na Bunge

• Siku ya Jumanne tarehe 29 Septamba, 2015, ibada ya Mazishi itafanyika

nyumbani kwake ikifuatiwa na Zoezi la kuaga na kutoa Heshima za Mwisho kwa Mwili wa marehemu Celina Kombani kabla ya Mazishi yatakayofanyika Shambani kwake Lukobe Nje kidogo ya Mji wa Mrorogoro.

Pamoja na taarifa hii, taarifa zaidi juu ya msiba huu zitaendelea kutolewa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na Serikali na familia kadri zitakapopatikana ikiwa ni pamoja na ratiba nzima ya zoezi la Kuaga na Mazishi.

“Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina lake Lihimidiwe” Imetolewa na: Ofisi ya Bunge, Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano DAR ES SALAAM 27 Septemba 2015