8
mbegu bora za soya Uzalishaji wa Kwa maelezo zaidi, wasiliana na: Maruku Agricultural Research Institute, S.L.P. 127, Bukoba, Tanzania Simu/Fax +255 732 983258; Barua pepe: [email protected]

Uzalishaji wa mbegu bora za soya - Home | Cabi ASHCafricasoilhealth.cabi.org/wpcms/wp-content/uploads/2014/05/207-ARI-Maruku-Soybean...Kwa kufuata kanuni bora za uzalishaji mbegu bora

  • Upload
    others

  • View
    13

  • Download
    6

Embed Size (px)

Citation preview

1

mbegu bora za soyaUzalishaji wa

Kwa maelezo zaidi, wasiliana na:Maruku Agricultural Research Institute, S.L.P. 127, Bukoba, TanzaniaSimu/Fax +255 732 983258;Barua pepe: [email protected]

2

1. Kuchagua mbegu

Chagua mbegu bora zinazoshauriwa kitaalamu (k.m. Uyole soya 1 na Uyole soya 2).

Fahamu uotaji wa mbegu kwa kupanda mbegu 30. Iwapo mbegu 25 au zaidi zitaota, mbegu hizo zinafaa kupandwa.

3

2. Kutayarisha eneo

Ondoa majani na magugu yote.

Tifua eneo kwa kina kirefu.

Sawazisha eneo vizuri ili kulaininisha udongo.

Eneo liwe na udongo wenye kima kirefu na usiotuwamisha maji.

4

4. Kuweka vichochezi vya rutuba

Changanya mbegu na vichochezi vya rutuba ya udongo kulingana na maelezo yaliyoko kwenye pakiti ya vichochezi vya rutuba ya udongo.

Tandaza mbegu zilizochanganywa na vichochezi vya rutuba ya udongo kwenye turubai au karatasi safi la nailoni kwenye kivuli kwa muda wa dakika 20 hadi 30.

Unashauriwa kupanda mbegu zote zilizochanganywa na vichochezi vya rutuba ya udongo siku moja.

5

4. Kupanda

Panda mapema mara tu mvua inaponyesha.

Tumia mfuko mmoja wa DAP ya kilo 50 kwa kila ekari (nusu kizibo cha soda kwa kila shimo).

Tia DAP kwenye shimo la kupandia halafu changanya na udongo ili kuondoa athari za mbolea kwenye uotaji wa mbegu.

6

5. Kutunza shamba

Punguza mimea ibaki 2 kama iliyoota ni zaidi ya mimea 2.

Ng’oa mimea yote ambayo haifanani na mbegu zilizopandwa.

Tumia Folicur ili kuzuia ugonjwa wa kutu ya majani.

Madawa aina ya Cypermethrin au Lambda (Karate) huzuia wadudu wanaoshambilia majani ya mimea (leaf rollers na leaf eaters).

7

6. Kuvuna

Vuna mimea mara tu mifuko ya maharage ya soya yanapogeuka kuwa ya rangi ya kahawia.

Weka mimea iliyovunwa kwenye jua kwa siku 3-5 kutegemea kiasi cha jua.

Ondoa mbegu kwenye mimea kwa kupiga mimea kwenye turubai safi lililotandazwa chini. Pepeta kuondoa uchafu kisha chambua mbegu ili kuondoa mbegu zilizoharibika na zenye magonjwa.

8

Kwa kufuata kanuni bora za uzalishaji mbegu bora za soya utapata mavuno kiasi cha tani 2 hadi 3 kwenye hektari 1 (ekari 2½ )

7. Kuvuna na kuhifadhi

Kausha mbegu kwa kufikia kiwango cha unyevu wa 11-12%. Kiasi hiki cha unyevu itafikiwa iwapo ukiuma mbegu kwa meno zitakuwa ngumu na kutoa sauti.

Weka mbegu za soya kwenye mifuko ya nailoni (mifuko ya salifeti) inayopitisha mwanga.

Hifadhi magunia ya mbegu za soya juu ya chanja kwenye chumba chenye hewa ya kutosha kisichopitisha jua.