24
COUNSENUTH Information series No. 2 Toleo la Pili, January, 2004 ULAJI BORA KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI Vidokezo Muhimu

Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 1 ULAJI BORA ...counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Ulaji-bora...Kundi hili hushirikisha mahindi, ulezi, mchele, ngano, mtama, uwele,

  • Upload
    others

  • View
    0

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 1 ULAJI BORA ...counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Ulaji-bora...Kundi hili hushirikisha mahindi, ulezi, mchele, ngano, mtama, uwele,

COUNSENUTH

Information series No. 2

Toleo la Pili, January, 2004

ULAJI BORAK WA WAT U

WANAOISHI NAVIRUSI VYA

U K I M W I

Vidokezo Muhimu

Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 1

Page 2: Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 1 ULAJI BORA ...counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Ulaji-bora...Kundi hili hushirikisha mahindi, ulezi, mchele, ngano, mtama, uwele,

2

UTANGULIZINi muhimu kwa watu wote na hasa wanaoishina virusi vya UKIMWI kufuata ulajiunaotakiwa kwa ajili ya lishe na afya bora.Lishe bora hufanya kinga ya mwili kuwa imarazaidi na hivyo kufanya maisha kuwa borazaidi.

Kutokana na umuhimu wa lishe bora kwawatu wanaoishi na virusi vya UKIMWI, toleohili la pili limeboresha taarifa zilizoko katikakijitabu “Ulaji bora kwa watu wanaoishi nav i rusi vya UKIMWI: Vi d o k ezo muhimu”COUNSENUTH “Information series No. 2”na kuongeza vidokezo na mambo menginemuhimu ya kuzingatia katika kuboresha lishena afya ya watu hao.

Kijitabu hiki kinaweza kutumiwa na watuwanaoishi na virusi vya UKIMWI, washaurinasaha, wahudumu wa afya na watu wenginewanaowatunza.

UMUHIMU WA CHAKULA NALISHE

Binadamu wote wanahitaji chakula chenyekukidhi mahitaji ya kilishe ya miili yao.Chakula huupatia mwili viru t u b i s h imbalimbali kwa ajili ya afya bora, ambayo nipamoja na:

• Ku b o resha kinga ya mwili dhidi yamagonjwa mbalimbali;

• Kutengeneza na kurudisha seli za mwilizilizokufa, zilizochakaa au kuharibika;

• Ukuaji wa kiakili na kimwili; na

• Kuupa mwili nguvu, joto na uwezo wakufanya kazi.

Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 2

Page 3: Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 1 ULAJI BORA ...counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Ulaji-bora...Kundi hili hushirikisha mahindi, ulezi, mchele, ngano, mtama, uwele,

3

Lishe bora ni muhimu zaidi kwa watuwanaoishi na virusi vya UKIMWI, kwanimahitaji ya miili yao kilishe yameongezekakwa sababu ya maambukizi ya virusi vyaUKIMWI. Vilevile magonjwa mengiy a n a yoambatana na virusi vya UKIMWIhuathiri ulaji, uyeyushwaji, usharabu( u f yozwaji) na utumikaji wa viru t u b i s h imbalimbali mwilini na hivyo kumuweka mtuanayeishi na virusi vya UKIMWI katika hatariya kupata matatizo yanayoambatana na lisheduni.

Ulaji bora wa vyakula mbalimbali huwezakuboresha afya na lishe ya mtu anayeishi nav i rusi vya UKIMWI na hivyo huwez akuongeza muda wa kuishi. Lishe bora pia nimuhimu katika kusaidia dawa zinazotumikakuweza kufanya kazi vizuri. Ni muhimu kwawatu wanaoishi na virusi vya UKIMWI kulamlo ulio kamili. Mlo ulio kamili husaidiak u b o resha lishe na afya, na pia huwez akuboresha kinga ya mwili.

MLO ULIO KAMILIMlo kamili huwa na chakula mchanganyikona cha kutosha na unatakiwa kuwa na chakulaangalau kimoja kutoka katika makundiyafuatayo ya vyakula:-

• Nafaka, mizizi na ndizi

Vyakula hivi huchukua sehemu kubwa ya mlona kwa kawaida ndio vyakula vikuu. Kundihili hushirikisha mahindi, ulezi, mchele,ngano, mtama, uwele, viazi vikuu, viazivitamu, viazi mviringo, mihogo, magimbi,ndizi n.k.

Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 3

Page 4: Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 1 ULAJI BORA ...counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Ulaji-bora...Kundi hili hushirikisha mahindi, ulezi, mchele, ngano, mtama, uwele,

4

• Vyakula vya mikunde na vyenye asiliya wanyama

Vyakula vilivyoko kwe n ye kundi hili nipamoja na kunde, njegere, maharagwe, njugum a we, fiwi, soya, karanga,dengu, choroko, aina zote zanyama, mayai, maziwa, dagaa,samaki, jibini, na waduduwanaoliwa kama kumbikumbina senene.

• Mboga-mboga

Kundi hili lina aina zote za mboga za majanikama matembele, mchicha, majani yamaboga, majani ya kunde, kisamvu,figiri, spinachi, sukuma wiki,mnafu, mchunga pia mboganyingine kama karo t i ,biringanya, bamia, maboga,matango, pilipili hoho, nyanyachungu, mlenda, bitiruti n.k.

• Matunda

Kundi hili lina matunda aina zote kamamapera, machungwa, maembe, mapapai,karakara (pesheni), malimao, machenza,zambarau, mananasi, mafenesi, mastafeli,pichesi, topetope n.k. Pia yale matunday a n a yoliwa ambayo hayalimwi nawakati mwingine huitwa matundapori, ubora wake ni sawa namatunda mengine na penginekuzidi. Matunda hayo nikama ukwaju, ubuyu,mabungo, embe ng’ o n g’ o ,mavilu, mikoche n.k.

Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 4

Page 5: Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 1 ULAJI BORA ...counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Ulaji-bora...Kundi hili hushirikisha mahindi, ulezi, mchele, ngano, mtama, uwele,

5

• Mafuta na Sukari

Mafuta na sukari ni muhimu na vinatakiwavitumike kwa kiasi. Mafuta yanawez akutokana na mimea kama nazi, mawe s e ,mbegu zitoazo mafuta kama karanga, koroshoalizeti, ufuta, mbegu za maboga, kweme, napia yale mafuta yatokanayo na wanyama kamasiagi na samli. Sukari ni pamoja na miwa, asali,sukari n.k.

Maji

Japo maji sio kundi la chakula, ni sehemumuhimu ya mlo. Maji ni muhimu kwakurekebisha joto la mwili na kusaidia mfumowa chakula. Ni muhimu kunywa maji angalaulita 1.5 (glasi 8) kwa siku. Ni pamoja nakunywa maji safi na salama, madafu, maji yamatunda au maji yaliyochemshwa na viungo.

KUMBUKAPunguza au epuka vinywaji vyenye

kafeini kwa wingi kama chai, kahawa, nasoda na vyenye kilevi kama aina

mbalimbali za pombe kwani hufanyamwili kupoteza maji zaidi

KUMBUKAMlo kamili unaweza kutayarishwa kwakutumia vyakula vinavyopatikana kwa

urahisi katika jamii

UTAYARISHAJI BORA WACHAKULA

Ni muhimu chakula kitayarishwe katika haliambayo ni bora, rahisi na salama kuliwa. Ilikukifanya chakula kiwe bora na rahisi kulaunaweza kufanya yafuatayo:

• Ponda na saga vyakula kila inapowezekana

Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 5

Page 6: Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 1 ULAJI BORA ...counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Ulaji-bora...Kundi hili hushirikisha mahindi, ulezi, mchele, ngano, mtama, uwele,

• Ongeza vyakula vyenye virutubishi kwawingi katika chakula kama vile karangazilizosagwa, mbegu mbalimbali za mafutaau tui la nazi. Vyakula hivi vinawez ak u o n g ezwa katika uji au vyakulav i l i v yopondwa kama vile wali, ndizi,mihogo, mboga za majani n.k.

• Tumia viungo mbalimbali katika chakulakama vile vitunguu saumu, tangawizi,papai bichi, mdalasini au iliki. Viungohuongeza hamu ya chakula na husaidiakatika uyeyushwaji wa chakula. Baadhi yaviungo pia huweza kusaidia kuimarishakinga ya mwili. Inashauriwa kutumiaviungo kwa kiasi.

• Tumia vyakula vilivyo c h a c h u s h w a(fermented) kama vile togwa na maziwa yamgando. Vyakula hivi huongeza ubora wachakula na usharabu (ufyonzwaji) wavirutubishi mwilini.

• Kupika baadhi ya vyakula kwa mvukehusaidia vyakula hivi viweze kuyeyushwana virutubishi kufyonzwa mwilini kwaurahisi. Kupika kwa mvuke pia husaidiakuhifadhi virutubishi vilivyopo kwe n yechakula.

• Inapowezekana tumia mbegu zilizooteshwa(kimea) ili kuboresha chakula. Unga wakimea unaweza kutumika kufanya vyakulavyenye asili ya wanga kuwa vyepesi narahisi kumeza. Mbegu nyingine huwezakuoteshwa na kutumika katika mapishimbalimbali. Mbegu hizo ni kama mahindi,mtama, ulezi, uwele, choroko, kunde,maharagwe, njegere au karanga. Angaliachati inayo o n yesha jinsi ya kuoteshambegu mbalimbali.

6

Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 6

Page 7: Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 1 ULAJI BORA ...counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Ulaji-bora...Kundi hili hushirikisha mahindi, ulezi, mchele, ngano, mtama, uwele,

7

Jinsi ya kuotesha mbegumbalimbali

Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 7

Page 8: Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 1 ULAJI BORA ...counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Ulaji-bora...Kundi hili hushirikisha mahindi, ulezi, mchele, ngano, mtama, uwele,

8

USAFI NA USALAMA WACHAKULA NA MAJI

Mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI yukok we n ye hatari ya kupata maambukizimbalimbali ambayo yatadhoofisha afya yake.Hivyo basi ni muhimu kwa mtu huyo aumtayarishaji wa chakula kuzingatia yafuatayoili kufanya chakula na maji viwe safi na salamakwa mtumiaji:

• Vyombo vinavyotumika kutayarishia nakupakulia chakula viwe safi. Vyo m b ov i o s h we vizuri kwa sabuni kabla yakutumia. Majivu yatumike pale ambapohakuna sabuni.

• Sehemu zote za kutayarishia chakula ziwesafi.

• Funika vyakula na maji na hifadhi katikahali ya usafi kuzuia wadudu hasa inzi.

• Hakikisha chakula kimepikwa na kuivavyema, na pia kiliwe kingali cha moto.

• Osha matunda na mboga-mboga kwa majiya kutosha, ikiwezekana yaliyochemshwa.

• Sehemu zenye michubuko katika mbogana matunda zikatwe na kutupwa.

• Epuka kutumia vyakula vilivyo s i n d i k w aa m b a v yo muda wake wa kutumiaumekwisha.

• Epuka nafaka au vyakula vilivyo o t aukungu.

• Hakikisha kuwa nyama, samaki na mayaivinapikwa na kuiva vizuri ili kuepukamaambukizo ya magonjwa (vyakula hivikamwe visiliwe vikiwa vibichi).

• Vyombo na vifaa vinavyo t u m i k akutayarisha nyama mbichi, samaki wabichi

Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 8

Page 9: Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 1 ULAJI BORA ...counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Ulaji-bora...Kundi hili hushirikisha mahindi, ulezi, mchele, ngano, mtama, uwele,

9

na mayai mabichi vioshwe vizuri kwasabuni kabla ya kuvitumia kwa matumizimengine. Majivu yatumike pale ambapohakuna sabuni.

• Vyakula vilivyokaa zaidi ya saa mbili baadaya kupikwa au viporo, ikibidi kuliwavipashwe moto vizuri kabla ya kuliwa hatakama bado vina uvuguvugu.

• Epuka mgusano wa vyakula vibichi na vilevilivyopikwa, hasa nyama mbichi, samakiwabichi na mayai mabichi.

• Hakikisha maji ni safi, chemsha maji naacha yaendelee kuchemka kwa muda wadakika 5 hadi 10.

• Tunza maji katika chombo safi chenyemfuniko.

• Iwapo unahitaji kutumia barafu hakikishamaji yaliyotumika kutengenezea barafuyamechemshwa.

Usafi na usalama binafsi wakati wakutayarisha chakula

• Osha mikono yako kwa sabuni na maji yakutosha kabla, wakati, nabaada ya kutayarisha chakula.Majivu yatumike pale ambapohakuna sabuni.

• Nawa mikono mara baada yakutumia choo au kujisaidia,kupiga chafya, kufuta kamasiau kuzoa taka.

• Zingatia usafi wa mwili na nguo.

• Funga vidonda vya mkononi ili kuzuiasibiko (contamination) wakati wakutayarisha chakula.

• Tumia vitambaa kushikilia sufuria navyombo vya moto.

Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 9

Page 10: Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 1 ULAJI BORA ...counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Ulaji-bora...Kundi hili hushirikisha mahindi, ulezi, mchele, ngano, mtama, uwele,

10

• Tumia ubao kukatia vyakula kuepukakujikata.

• Jihadhari kujitoboa au kujikataunapotumia vitu vikali na vyenye nchakali.

LISHE NA ULAJI WAKATIWA MATATIZOMBALIMBALI

YANAYOAMBATANA NAVIRUSI VYA UKIMWI

Vyakula mbalimbali vinaweza kutumikakupunguza ukali wa baadhi ya matatizoyanayompata mtu anayeishi na virusi vyaUKIMWI. Hata hivyo ni muhimu kumuonadaktari iwapo tatizo litaendelea kwa mudam refu. Yafuatayo ni baadhi ya matatizoyanayoambatana na hali ya kuishi na virusivya UKIMWI na ushauri wa ulaji unaofaa.

Kukosa hamu ya kulaTatizo hili linaweza kutokea mara kwa marakwa mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI.Maambukizi mbalimbali, msongo, uchov u ,maumivu ya kinywa au koo na kutokula kwamuda mrefu huweza kusababisha hali hii.

Mambo ya kufanya:

• On g eza viungo kama tangawizi, limao,mdalasini, kotimiri au iliki kwe n yevinywaji au vyakula mbalimbali; hivihusaidia kuongeza hamu ya kula.

• Kula milo midogo midogo mara nyingikwa siku.

• Ik i wezekana usitayarishe vyakulamwenyewe au kukaa jikoni ama karibu na

Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 10

Page 11: Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 1 ULAJI BORA ...counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Ulaji-bora...Kundi hili hushirikisha mahindi, ulezi, mchele, ngano, mtama, uwele,

11

jiko kwani harufu za vyakula hupunguzahamu ya kula.

• Jaribu kunywa vinywaji na kula vyakulaunavyovipenda.

• Ikiwezekana usile peke yako, kula pamojana familia au marafiki.

• Usinywe na kula wakati mmoja kwani hiiitasababisha tumbo kujaa haraka. Kunywakati ya mlo mmoja na mwingine.

• Ongeza aidha karanga, maziwa au mafutakwenye vyakula mbalimbali ili kuviboreshana kuvifanya viwe rahisi kumeza.

• Jaribu kubadili ladha na aina ya vyakulakwani hii huongeza hamu ya kula.

• Fanya mazoezi mbalimbali kama kutembeaharaka haraka na mengine ili kuongezahamu ya kula.

• Ikibidi, jilazimishe kula, kwani chakula nimuhimu sana kwa afya.

Rudia vyakula vya kawaida mara tu tatizolinapokwisha

Kichefuchefu au kutapika

Kichefuchefu hupunguza hamu ya kula.Kichefuchefu kinaweza kusababishwa nabaadhi ya vyakula, njaa, magonjwambalimbali, ukosefu wa maji ya kutoshamwilini na pia baadhi ya madawa.

Jaribu yafuatayo unapokuwa na kichefuchefuau kutapika:

• Epuka vyakula vye n ye viungo vingi,mafuta mengi au sukari nyingi.

• Epuka pombe na vyakula vyenye kafeinikama chai na kahawa.

Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 11

Page 12: Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 1 ULAJI BORA ...counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Ulaji-bora...Kundi hili hushirikisha mahindi, ulezi, mchele, ngano, mtama, uwele,

12

• Jaribu kula vyakula vikavu na vye n yechumvi kama mkate, kwani hii hupunguzakichefuchefu.

• Kunywa maji, supu na vinywaji vya viungokidogo kidogo na endelea na vyakula laini.

• Jaribu kula vyakula vilivyopoa.

• Jaribu juisi ya limao au ndimuiliyochanganywa kwenye kikombe cha majiya moto kwani huweza kusaidiakupunguza kichefuchefu.

• Jaribu kula milo midogo midogo mara kwamara (si chini ya mara 5 hadi 6 kwa siku).

• Kula wakati umekaa wima au jiegemezekidogo kwe n ye mto. Us i j i l a ze mara tubaada ya kula (subiri dakika 30 hadi saa 1baada ya kula).

• Jaribu vyakula vichachu au vyenye chumvi.

• Usikae muda mrefu bila kula au kunywachochote.

• Usile haraka, jaribu kula taratibukupunguza kichefuchefu au kutapika.

• Muone daktari tatizo likizidi.

KuharishaKuharisha huweza kusababisha upotevu wamaji na virutubishi mwilini. Kuharisha piah u weza kusababisha usharabu duni( u f yonzwaji) na uyeyushwaji duni wavirutubishi na wakati mwingine kutokuwa nahamu ya kula. Kuharisha mara nyingikunasababishwa na maambukizi mbalimbalikwenye mfumo wa chakula, minyoo na baadhiya dawa kama kiua vijasumu (antibayotiki).

Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 12

Page 13: Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 1 ULAJI BORA ...counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Ulaji-bora...Kundi hili hushirikisha mahindi, ulezi, mchele, ngano, mtama, uwele,

13

Jaribu kufanya yafuatayo unapoharisha:

• Kunywa maji safi na salama kwa wingikuzuia upotevu wa maji mwilini (zaidi yalita 2 kwa siku).

• Kunywa vinywaji vya maji-maji kwa wingizaidi kama maji ya mchele, madafu, togwa,supu, juisi ya matunda na maji ya sukari nachumvi (ORS).

• Kula matunda kama embe,papai, ndizi mbivu na mboga-mboga zilizopikwa kamak a roti, maboga, spinachi,mchicha n.k ili kuru d i s h amadini na vitaminiz i n a zopotea kutokana nakuharisha.

• Kula milo midogo midogo mara nyingi ilik u rudisha virutubishi vinavyopotea nakukidhi mahitaji ya kilishe ya mwili.

• Tafuna kwa muda mrefu au kula vyakulav i l i v yolaini kwani ni rahisi kumez a ,k u yeyushwa na virutubishi kufyo n z w amwilini.

• Kula vyakula vyenye uvuguvugu na sio vyamoto sana au baridi sana.

• Epuka vyakula vye n ye mafuta mengi,viungo vingi au pilipili nyingi.

• Jihadhari kutumia matunda yasiyo i vavizuri au ye n ye uchachu mkali kamanyanya, machungwa, machenza, limaokwani wakati mwingine huweza kuongezatatizo.

• Epuka vyakula na vinywajivinavyosababisha gesi kwa wingi tumbonikama maharagwe, kabichi na soda.

Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 13

Page 14: Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 1 ULAJI BORA ...counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Ulaji-bora...Kundi hili hushirikisha mahindi, ulezi, mchele, ngano, mtama, uwele,

14

• Epuka vinywaji vyenye kafeini kama chaina kahawa, kwani hivi husababishaupotevu wa maji zaidi.

• Epuka matumizi ya pombe kwani huzuiabaadhi ya virutubishi kufyonzwa nahuongeza upotevu wa maji.

• Epuka maziwa mabichi kamayanasababisha kuharisha na jaribu mtindi.

• Epuka vyakula vyenye nyuzinyuzi (dietaryfibre) nyingi kama nafaka zisizokobolewaau vyakula vya mikunde vyenye maganda,kwani haviyeyushwi kwa urahisi na hivyohuongeza kuharisha.

• Ponda vitunguu saumu na changanyakwenye vinywaji kama supu na vinginevyovilivyochemshwa.

• Muone daktari kuharisha kukiendelea.

Kupungua uzitoKupungua uzito kwa watu wanaoishi na virusivya UKIMWI huweza kusababishwa nao n g ezeko la mahitaji ya viru t u b i s h imbalimbali mwilini, ulaji duni, uyeyushwajina ufyonzwaji duni wa virutubishi mwilini.

Kupungua uzito kunaweza kudhibitiwa kwa:

• Kuongeza aina, kiasi cha chakula na idadiya milo kwa siku.

• Kuongeza karanga, mafuta, siagi, maziwa,sukari au asali n.k. kwe n ye vyakulambalimbali.

• Kula vyakula vya nafaka kwa wingi kamamahindi, mchele, ngano, mtama, ulezi,uwele, viazi na pia aina za nyama, samakina mikunde

Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 14

Page 15: Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 1 ULAJI BORA ...counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Ulaji-bora...Kundi hili hushirikisha mahindi, ulezi, mchele, ngano, mtama, uwele,

15

• Kutumia asusa (snacks) mara kwa marakati ya mlo na mlo kama karanga,matunda, mtindi n.k.

• Kuweka viungo katika chakula ili kuongezahamu ya kula na kusaidia uyeyushwajiwake.

• Kutumia vyakula vilivyochachushwa kamamtindi na togwa ili kusaidia uyeyushwajina usharabu.

• Kufanya mazo ezi kunaongeza hamu yakula na kujenga misuli.

Vidonda kinywani au kooni, nautandu mweupe kinywani

Vidonda vya kinywani au kooni na utandumweupe kinywani (fangasi) huweza kufanyaulaji wa vyakula kuwa mgumu na hivyokupunguza kiasi cha chakula anachoweza kulamtu anayeishi na virusi vya UKIMWI.

Yafuatayo huweza kusaidia:

• Kula vyakula laini kama mtindi, uji auvyakula kama parachichi, papai, ndizi n.k.

• Epuka vyakula vyenye viungo au ladha kali.

• Epuka vyakula vya moto au vyenye pilipilikali.

• Epuka vyakula vyenye sukari nyingi.

• Sukutua kinywa kwa kutumia majiyaliyochemshwa yenye kitunguu saumu aumdalasini. Rudia kila baada ya saa 3 hadi 4.

• In a p owezekana, tumia mrija wakati wakunywa au kula.

• Jaribu kumung’unya barafu kamainapatikana (iliyo t e n g e n ezwa kwa majiy a l i yochemshwa) kwani huwez akupunguza maumivu ya kinywa.

Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 15

Page 16: Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 1 ULAJI BORA ...counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Ulaji-bora...Kundi hili hushirikisha mahindi, ulezi, mchele, ngano, mtama, uwele,

16

• Jaribu maziwa ya mgando au embe bichikwani hivi hutuliza maumivu na kusaidiakupona.

• Tumia mtindi kwani huzuia ukuaji wautandu mweupe kinywani.

Kukosa choo au kupata chookigumu

• Kunywa maji mengi yaliyo c h e m s h w aangalau lita 2 kwa siku.

• Tumia vyakula vinavyotokana na nafakaambavyo havijakobolewa kama dona, ungawa ngano usiokobolewa n.k.

• Jaribu kufanya mazo ezi kwani husaidiachakula kusagwa na kuyeyushwa.

• Tumia papai, parachichi au embe kwanivimeonekana kusaidia kulainisha choo.

• Kula matunda na mboga mboga kwawingi.

• Jipe muda wa kutosha chooni wakati wakujisaidia.

Kifua kikuuKifua kikuu ni mojawapo ya magonjwanyemelezi kwa watu wanaoishi na virusi vyaUKIMWI na wenye UKIMWI. Kifua kikuuhuathiri mapafu na sehemu nyingine za mwilikama figo, uti wa mgongo na mfumo mzimawa njia ya chakula. Ufuatao ni ushauri wa lishekwa mwenye kifua kikuu:-

• Kula chakula mchanganyiko na chakutosha.

• Kwa vile dalili za kifua kikuu ni pamoja nahoma za mara kwa mara, kikohozi,

Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 16

Page 17: Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 1 ULAJI BORA ...counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Ulaji-bora...Kundi hili hushirikisha mahindi, ulezi, mchele, ngano, mtama, uwele,

17

kichefuchefu, kutapika, kuharisha, kukosahamu ya kula na kupungua uzito, dalili hizizikabiliwe kama ilivyoshauriwa hapo awalikatika kudhibiti dalili hizi.

• Kwa vile dawa zingine za kutibu kifuakikuu zinaweza kuingilia matumizi yavitamini B mwilini, inashauriwa kula kwa

wingi vyakula vyenye wingi wa vitamini hiikama vile viazi vitamu, maharagwe ,mahindi, parachichi, kabichi, nyama, nasamaki.

• Kula vyakula vyenye protini kwa wingi,kama vile aina zote za nyama, samaki,wadudu wanaoliwa kama senene nakumbikumbi. Pia maziwa mabichi, mtindi,jibini, mayai na jamii ya mikunde kama,soya, maharagwe, kunde n.k.

• Kula matunda kwa wingi.

• Pata muda wa kupumzika.

• Kumbuka kuendelea na matibabu kamainavyoshauriwa.

Mafua na kikohoziMafua na kikohozi ni maambukiziyanayowapata pia watu wanaoishi na virusi vyaUKIMWI na we n ye UKIMWI. Wa k a t imwingine mafua na kikohozi husababishahoma. Mara nyingi magonjwa haya hutowekapengine bila hata dawa.

Jaribu yafuatayo:

• Kunywa maji yakutosha au vinywajivingine na upumzike.

• Tengeneza vinywaji vyalimao, tangawizi,

6

Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 17

Page 18: Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 1 ULAJI BORA ...counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Ulaji-bora...Kundi hili hushirikisha mahindi, ulezi, mchele, ngano, mtama, uwele,

18

kitunguu maji, nanaa n.k. Un a wez akuvitumia wakati wote unapokuwa namafua au kikohozi.

• Jifukize kwa kutumia mvuke wa maji yamoto.

• Changanya limao na asali na tumia marakwa mara katika kipindi chote chaugonjwa.

• Kikohozi kikizidi muone daktari ili kupataushauri.

HomaHoma husababishwa na maambukizimbalimbali yanayompata mtu anayeishi navirusi vya UKIMWI au mwenye UKIMWI.

Jaribu yafuatayo:

• Kunywa vinywaji kwa wingi mara kwamara kupunguza joto la mwili.

• Kula milo midogo midogo mara nyingi ilikukidhi ongezeko la mahitaji ya mwili.

• Punguza nguo nzito mwilini.

• Oga kwa maji ya uvuguvugu.

• Muone daktari ili kupata ushauri namatibabu.

Upungufu wa wekundu wadamu

Upungufu wa wekundu wa damu huwezakusababishwa na ulaji duni hasa wa vyakulav ye n ye madini ya chuma kwa wingi aumagonjwa kama malaria na minyoo. Mtuanayeishi na virusi vya UKIMWI huathirikakiafya haraka zaidi kama ana tatizo laupungufu wa wekundu wa damu.

Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 18

Page 19: Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 1 ULAJI BORA ...counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Ulaji-bora...Kundi hili hushirikisha mahindi, ulezi, mchele, ngano, mtama, uwele,

19

Upungufu wa wekundu wa damu huwezakukabiliwa kwa:-

• Kula vyakula vyenye madini chuma kwawingi, kama vile samaki, nyama,maini, mboga za kijani (kamamchicha, spinachi, kisamvu,matembele, majani yamaboga), maharagwe, njegere ,choroko, dengu, mbaazi, karangana mbegu za aina nyingine.

• Kula matunda kwa wingi wakati wa mlohasa matunda yenye vitamini C kwawingi ili kusaidia usharabu(ufyonzwaji) wa madini ya chumamwilini. Matunda kama mapera,machungwa, machenza, karakara(pesheni), nanasi, mabungo,ubuyu, ukwaju, nyanya n.k.yana vitamini C kwa wingi.

• Epuka vinywaji vyenye kafeini wakati wamlo.

• Tafuta ushauri wa daktari kuhusumatumizi ya vidonge vya madini ya chumana kutibiwa magonjwa kama vile malariana minyoo.

Matatizo ya ngoziMa t a t i zo ya ngozi pia huwapata watuwanaoishi na virusi vya UKIMWI au wenyeUKIMWI. Baadhi ya matatizo hayohusababishwa na upungufu wa baadhi yavitamini kwa mfano vitamini A na B Ingawaje magonjwa haya yanaweza kuhitajimatibabu, ulaji wa vyakula vyenye vitamini Ana/au vitamini B kwa wingi unawez akupunguza au kuzuia magonjwa hayo.Vyakula vye n ye vitamini A kwa wingi nimboga zenye rangi ya kijani, mawese, maini,

6

6.

Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:03 PM Page 19

Page 20: Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 1 ULAJI BORA ...counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Ulaji-bora...Kundi hili hushirikisha mahindi, ulezi, mchele, ngano, mtama, uwele,

Matumizi ya virutubishi vya nyongeza ni kitumuhimu kwa mtu anayeishi na virusi vyaUKIMWI. Ikumbukwe kwamba virutubishihivi sio badala ya chakula na wala siomatibabu ya UKIMWI, bali ni nyo n g ez ai n a yosaidia kuboresha lishe na afya. Nimuhimu kutumia rasilimali uliyo n a yokununua kwanza chakula cha kutosha ndipoununue virutubishi vya nyo n g eza. Mu o n edaktari au mtaalamu wa afya ili kupata ushaurizaidi kuhusu aina ya virutubishi unavyohitaji.

20

mayai, maziwa, jibini, papai, karoti namaboga. Vyakula vyenye vitamini B kwawingi ni kama maharagwe, mboga za kijani,karanga, mahindi, nyama na parachichi.

Matumizi ya virutubishi vya nyongeza

HITIMISHONi muhimu kwa watu wanaoishi na virusi vyaUKIMWI kuzingatia ulaji wa chakula chamchanganyiko na cha kutosha. Na zaidi yahayo ni kuongeza idadi ya milo, kufanyamazoezi, kutibu magonjwa nyemelezi mapemana kuzingatia usafi na usalama wa chakula namaji wakati wote.

6

Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:03 PM Page 20

Page 21: Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 1 ULAJI BORA ...counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Ulaji-bora...Kundi hili hushirikisha mahindi, ulezi, mchele, ngano, mtama, uwele,

21

ZINGATIA YAFUATAYO:• Ishi kwa matumaini na furaha

• Tumia huduma za ushauri nasaha

• Kula chakula cha mchanganyiko na chakutosha

• Kula chakula mara kwa mara

• Tibu maradhi yote mapema

• Jiepushe na magonjwa ya ngono

• Maji ya kunywa, yakutengeneze avinywaji au ya barafu yachemshwe vizuri

• Zingatia usafi wa chakula, maji,mazingira na usafi wa mwili

• Fanya mazoezi mara kwa mara

• Epuka matumizi ya pombe

• Epuka matumizi ya sigara, tumbaku,ugoro au madawa ya kulevya

• Pima afya yako mara kwa mara

VYANZO1. Bijlsma, M., Nutritional care and support

for people with HIV: Review of literature,initiatives and educational materials in sub-sahara Africa, and recommendations fordeveloping national programmes. Reportto FAO, July, 2000.

2. Bijlsma, M., Living Positively: Nutritionguide for People with HIV/AIDS, MuntareCity Health De p a rtment, Zi m b a bwe ,Second Edition, 1997.

3. FAO/WHO, Living well with HIV/AIDS:A manual on nutritional care and supportfor people living with HIV/AIDS, Rome,2002.

Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:03 PM Page 21

Page 22: Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 1 ULAJI BORA ...counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Ulaji-bora...Kundi hili hushirikisha mahindi, ulezi, mchele, ngano, mtama, uwele,

22

4. The Network of African people living inHIV/AIDS (NAP+). Food for peopleliving with HIV/AIDS, July, 1996.

5. Food and Nutrition Technical Assistance( FA N TA), HIV/AIDS: A Guide forNutrition, Care and Support. Academy forEducational De velopment, Wa s h i n g t o nDC, 2001.

6. Friis, H. “The possible effect ofm i c ronutrients in HIV infection. SCNNews, United Nations Systems Forum onNutrition, Number 17, December, 1998.

7. Food and Nutrition Technical Assistance( FA N TA), Food and Nu t r i t i o nImplications of Antiretroviral Therapy inRe s o u rce Limited Settings (DRAFT) .Academy for Educational Development,Washington DC, June, 2003.

8. COUNSENUTH, Nutritional Care forPLHA: Training and Reference Manual(DRAFT), September, 2003.

SHUKRANI

COUNSENUTH inatoa shukrani kwaWA M ATA, SHDEPHA+, MATI-Uyole, SUA nawatu binafsi ambao wameshiriki katikak u b o resha kijitabu hiki.

Shukurani za pekee kwa RFE kwa ufadhili.

Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:03 PM Page 22

Page 23: Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 1 ULAJI BORA ...counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Ulaji-bora...Kundi hili hushirikisha mahindi, ulezi, mchele, ngano, mtama, uwele,

23

VIJITABU VINGINE KUHUSULISHE NA VIRUSI VYA UKIMWI

VILIVYOTOLEWA NACOUNSENUTH:

1 . Ulishaji wa mtoto aliyezaliwa na mamamwenye virusi vya UKIMWI: “Vi d o k e z omuhimu kwa washauri nasaha”.COUNSENUTH information series No. 1,Toleo la Pili, January, 2004.

2 . Lishe na Ulaji bora kwa watu wanaoishi navirusi vya UKIMWI: “Majibu ya MaswaliYanayoulizwa Mara kwa Mara”COUNSENUTH Information Series No. 3,Toleo la Pili, January, 2004.

3 . Lishe na ulaji bora kwa watu wanaoishi navirusi vya UKIMWI: “Vy a k u l av i n a v y o b o resha uyeyushwaji wa chakulana ufyonzwaji wa virutubishi mwilini”:COUNSENUTH information series No. 4,M a rch, 2003.

Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:03 PM Page 23

Page 24: Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:02 PM Page 1 ULAJI BORA ...counsenuth.or.tz/wp-content/uploads/2017/10/Ulaji-bora...Kundi hili hushirikisha mahindi, ulezi, mchele, ngano, mtama, uwele,

ISBN 9987-8936-5-1

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:M k u r u g e n z i

The Centre for Counselling, Nutrition and

Health Care ( C O U N S E N U T H )

Reprinting facilitated by VSHP TUMAINI, a pro g r a mimplemented by the Strategic Alliance made up of

CARE, COUNSENUTH, FHI, HEIFER, HST and MUCHS,in partnership with the Government of Tanzania and

Funded by USAID

Kijarida hiki kimetayarishwa na: The Centre for Counselling, Nutrition and

Health Care ( C O U N S E N U T H )United Nations Rd./Kilombero Str.

Plot No. 432, Flat No. 3P. O. Box 8218, Dar es Salaam, Ta n z a n i a

Tel/Fax: +255 22 2152705, Cell: 0744 279145

Kimefadhiliwa na:

Rapid Funding Envelope for HIV/AIDS (RFE)

Designed & printed by:Desktop Productions Limited

P.O. Box 20936, Dar es Salaam, TanzaniaContact: 0748 387899, Email: [email protected]

Reprinted July 2004

Vidokezo Muhimu.qxd 1/7/05 3:03 PM Page 24