5
WARAKA WA UPUMBAVU NA ULOFA KATIKA DEMOKRASIA Rai ya Mtanzania Na Prof Handley Mpoki Mafwenga Ph.D (finance -COU), MSc (finance -Strathclyde), MBA (Mg.Eco -ESAMI/MsM), LLM (taxation- UDSM), LLB (Tudarco), PGD tax mgt (IFM), AD tax mgt (IFM)] Nikiwa katikati ya mji ghafla namuona Edward Lowasa anapanda Daladala siamini macho yangu Napata kizunguzungu ghafla naanguka mithiri ya mgonjwa wa kifafa napoteza fahamu. Mara namuona Mwalimu Nyerere ameshika kisu kinadondosha damu, mkono wa kulia kashika Katiba ya Tanzania imejaa damu, kisu chake kina maandishi madogomadogo ya aina mbili “Wapumbavu,…….. Malofa”. Ananipa Katiba anaamrisha niipekue mara nakutana na picha ya Fredrick Sumaye imezungukwa na maneno "Wapumbavu…Malofa” picha imeambatana na Waraka ananipa niwape Watanzania na viongozi wetu Ben Mkapa, Edward Lowasa na Fredrick Sumaye yenye ujumbe ufuatao; Wanangu Watanzania yumkini hamjui maana hata ya majina ya viongozi wenu; kabla ya kuwalaumu kwa matamshi yao yafaa mjue maana ya majina yao. Majina huumba tabia, ukimwita mwanao “Chuki”atakuwa na “Chuki”; “Chausiku atakuwa mtu wa kutoka usiku’”Shida”atakuwa mwenye shida daima n.k Mini Baba yenu wa Taifa nilichagua Rais kwa maana ya jina liendalo na matakwa ya mazingira ya wakati huo; leo mna jina la Edward maana yake hutokana na asili ya Kiingereza likitoholewa kutokana na jamii ya Wajerumani wa asili ya Angeln na Saxony ambao walihamia Uingereza baada ya kuanguka kwa Dola la Roma Miaka 410 Baada ya Kristo hao huitwa Anglo-saxion. Ni jina lijulikanalo kwa asili kama Ēadweard, likiundwa na maneno mawili Eadlikiwa na maana ya Mali, Utajiri, Bahati, Matumaini na neno Weardlikiwa na maana ya Mlinzi au Mdhibiti. Kwa mujibu wa jina lake siyo ajabu kumsikia anachukia sana Umaskini na anapenda sana Watanzania wote wawe matajiri kama Mengi na Bhahresa. ila Kauli hiyo si ya kweli kwani hata nchi zilizoendelea zina Maskini na Tajiri. Lakini kwa vile anatamani muombeeni kauli zake ziumbe ndoto zake ziwe kweli. Jina Edward linavumisha sifa ya mtu mwenye nguvu na anayenuwia jambo. Huwa anapenda kuwa kiongozi pale bahati inapomwangukia ingawa wakati mwingine angependa kuwa kimya awapo kiongozi na kuwa Mfano wa wengine pale anapoamini hafikiwi na watu. Ni mtu mwenye nidhamu kwa kiwango kikubwa ambapo hawezi kukubali kuwa mtu wa kawaida na kufanya mambo ya bandia. Nguvu zake ni dhana ya kujiamini na kupania mambo, huwa na mvuto wa asili ya Mamlaka na kipaji cha kupangiliza mambo na kuwa na Uandilifu, Uwezo, Uimara na dhana kuu ya Haki. Kwa upande mwingine mapungufu yake ni mtu wa kujiona kwa kulingia Ujuzi wake na kuwa mtu mwenye msimamo kitu kinachomfanya awe mzito kubadilika kutokana na mazingira, hasira alizonazo na kushindwa

WARAKA WA UPUMBAVU NA ULOFA KATIKA DEMOKRASIA

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: WARAKA WA UPUMBAVU NA ULOFA KATIKA DEMOKRASIA

WARAKA WA UPUMBAVU NA ULOFA KATIKA DEMOKRASIA

Rai ya Mtanzania

Na Prof Handley Mpoki Mafwenga Ph.D (finance -COU), MSc (finance -Strathclyde), MBA (Mg.Eco -ESAMI/MsM), LLM (taxation- UDSM), LLB (Tudarco), PGD tax mgt (IFM), AD tax mgt (IFM)]

Nikiwa katikati ya mji ghafla namuona Edward Lowasa anapanda Daladala siamini macho

yangu Napata kizunguzungu ghafla naanguka mithiri ya mgonjwa wa kifafa napoteza

fahamu. Mara namuona Mwalimu Nyerere ameshika kisu kinadondosha damu, mkono wa

kulia kashika Katiba ya Tanzania imejaa damu, kisu chake kina maandishi madogomadogo

ya aina mbili “Wapumbavu,…….. Malofa”. Ananipa Katiba anaamrisha niipekue mara

nakutana na picha ya Fredrick Sumaye imezungukwa na maneno "Wapumbavu…Malofa”

picha imeambatana na Waraka ananipa niwape Watanzania na viongozi wetu Ben Mkapa,

Edward Lowasa na Fredrick Sumaye yenye ujumbe ufuatao;

Wanangu Watanzania yumkini hamjui maana hata ya majina ya viongozi wenu; kabla ya

kuwalaumu kwa matamshi yao yafaa mjue maana ya majina yao. Majina huumba tabia,

ukimwita mwanao “Chuki”atakuwa na “Chuki”; “Chausiku atakuwa mtu wa kutoka

usiku’”Shida”atakuwa mwenye shida daima n.k

Mini Baba yenu wa Taifa nilichagua Rais kwa maana ya jina liendalo na matakwa ya

mazingira ya wakati huo; leo mna jina la Edward maana yake hutokana na asili ya Kiingereza

likitoholewa kutokana na jamii ya Wajerumani wa asili ya Angeln na Saxony ambao

walihamia Uingereza baada ya kuanguka kwa Dola la Roma Miaka 410 Baada ya Kristo hao

huitwa Anglo-saxion. Ni jina lijulikanalo kwa asili kama Ēadweard, likiundwa na maneno

mawili “Ead” likiwa na maana ya Mali, Utajiri, Bahati, Matumaini na neno “Weard” likiwa

na maana ya Mlinzi au Mdhibiti. Kwa mujibu wa jina lake siyo ajabu kumsikia anachukia

sana Umaskini na anapenda sana Watanzania wote wawe matajiri kama Mengi na Bhahresa.

ila Kauli hiyo si ya kweli kwani hata nchi zilizoendelea zina Maskini na Tajiri. Lakini kwa

vile anatamani muombeeni kauli zake ziumbe ndoto zake ziwe kweli.

Jina Edward linavumisha sifa ya mtu mwenye nguvu na anayenuwia jambo. Huwa anapenda

kuwa kiongozi pale bahati inapomwangukia ingawa wakati mwingine angependa kuwa

kimya awapo kiongozi na kuwa Mfano wa wengine pale anapoamini hafikiwi na watu. Ni

mtu mwenye nidhamu kwa kiwango kikubwa ambapo hawezi kukubali kuwa mtu wa

kawaida na kufanya mambo ya bandia. Nguvu zake ni dhana ya kujiamini na kupania

mambo, huwa na mvuto wa asili ya Mamlaka na kipaji cha kupangiliza mambo na kuwa na

Uandilifu, Uwezo, Uimara na dhana kuu ya Haki. Kwa upande mwingine mapungufu yake ni

mtu wa kujiona kwa kulingia Ujuzi wake na kuwa mtu mwenye msimamo kitu

kinachomfanya awe mzito kubadilika kutokana na mazingira, hasira alizonazo na kushindwa

Page 2: WARAKA WA UPUMBAVU NA ULOFA KATIKA DEMOKRASIA

kuwa mvumilivu. Huwa ni mtu mwenye tabia ya usumbufu na kufuatilia mambo ya watu.

Lakini kumbuka ni pale tu anapoamini yeye ni sahihi muda wote. Ni mtu wa kupania mambo

ambaye ana kila nafasi ya kuishi kwa umoja na raha. Anapokuwa katika umri mdogo huwa

makini, muwajibikaji, na mwenye kuathiriwa zaidi na mazingira ya familia yake. Jina la

Edward hutoa sifa ya kupenda kuwa Mfano kwa jamii na mtu anayeogopa sana kueleweka

vibaya ndani ya jamii

Mnaye kijana wangu Benjamin Mkapa, Mwanahabari aliyebobea masuala ya Diplomasia

enzi zangu alinisaidia sana. Jina Benjamin maana yake “Kijana wa Mkono wa Kuume” ni

jina lililotumika pia na mtoto wa Mwisho kati ya Watoto 12 wa Yakobo. Jina hili lina maana

pia ya “Kijana wa Kusini” na pengine huwa na maana ya “Kijana wa Uzao wa Uzeeni” ni

Jina lenye asili ya Kiebrania na maana yake ni “Kijana wa Mkono wa Kiume” au “Bahati”.

Ni jina linalotamkwa Ben-Ja-Men. Kama nilivyobainisha, ni mtoto wa Yakobo na Raheli na

mjukuu wa Isaka. Rahel alikufa alipokuwa akimzaa na kumwita jina la “Benon” yaani

“Mtoto wa Uchungu Wangu” Baadaye jina hili likabadilishwa na Yakobo kuwa Benjamin.

Watu wenye Jina la Benjamin ni watu wenye hisia kubwa ya kuwa na Msimamo, wanapenda

familia zao na Jamii kwa ujumla na wanahitaji sana kufanya kazi na watu wengine na zaidi

hupenda kushukuriwa. Watu wa Jina hili wanapenda sana Mabadiliko, kufanya Maajabu na

kuwa Mwanaharakati. Ni wepesi kubadilika kutokana na Mazingira, Wana Mtazamo mpana

na Busara, wanauwezo wa kuweka mazingira mazuri ya kutumia uhuru uliopo. Wanapenda

kupambana na Sheria na Kanuni zinazowazuia kufanya kazi. Ni wepesi pia kubadilishwa

wanachokiamini kwani ni wasikivu, kutopumzika na kuwa wana Mapinduzi halisi.

Kuna kijana huko kwenu tumemsikia akiwa ana enzi dhana yangu ya “Kazi ni Kipimo cha

Utu” nasikia mnamwita Jembe; hii inanikumbusha enzi zangu za Chama kimoja ambapo

wagombea Ubunge niliwagawia uhuru wa kuchagua Jembe au Nyumba. Nilipata Wabunge

wengi wenye alama ya Jembe kuliko Nyumba. Na Jembe ilikuwa ishara ya uwakilishi wa

Wakulima wakati nyumba ilikuwa kwa Wafanyakazi. Sijaelewa tafsiri yenu lakini pengine

inaendana na jina lake. Jina la John maana yake ni “Rehema ya Mungu” lina asili ya

Kiebrania maana yake “Yehova ni Mwenye Rehema, ameonyesha Upendeleo”. Katika Biblia

jina hili lilitumiwa na Yohana Mbatizaji aliyembatiza Yesu Kristo katika Mto Jordan.

Watu wenye jina hili wanapenda sana kuwa na Msimamo, wanapenda familia zao na jamii

kwa ujumla na wanapenda kufanya kazi na watu wengine na kushukuriwa. Watu wenye jina

hili wanahurka ya kuwa wakimya, wenye kushirikiana na wenzao, wenye kujali wenzao,

wenye upendo kama wanavyojipenda wenyewe, wepesi kuishi nao, hawayumbi kwenye

maamuzi na wakati mwingine hupenda kuonea watu soni. Ni watu wenye Uaminifu wa hali

ya juu, wanaheshimu hali ya kujiamini ya watu wengine, na wana diplomasia ya hali ya juu,

wapatanishi na wanapenda kushirikiana na watu. Mara kwa mara ni wabunifu, wanapenda

maelezo ya kina yenye ukweli na sheria na wakati wote wanaona mabadiliko yanapaswa

kuangaliwa kwa umakini. Wanapenda sana kuwa na dhana ya kujiona siyo salama hivyo siyo

watu wa kupumzika.

Lakini pia anatumia jina la Joseph ambalo ni jina la kilatini aina ya Kigiriki kilichoanzia kwa

Waebrania maana yake “Ätaongeza” Jina hili pia mbali ya Mume wa Mariah mama wa yesu

lilitumika na Mtoto wa kumi na moja wa Yakobo kipenzi wake ambaye kaka yake Rubeni

alimuuza Misri na kumwambia baba yake kuwa ameuwawa kwa kumuokoa kuuwawa na

ndugu zake na ndiye alikuwa mshauri wa mfalme wa faraoh aliyewokoa Uzao wa Yakobo

wakati wa Njaa.

Page 3: WARAKA WA UPUMBAVU NA ULOFA KATIKA DEMOKRASIA

Jina la Fredrick ni jina la asili ya Uingereza lenye asili zaidi ya Ujerumani likiwa na maana

“Mtawala wa Amani” likijumuisha maneno frid yaani Ämani”na ric yaani “Mtawala”. Jina

hili lilikuwa maarufu sana kwenye ukanda wa lugha ya Ujerumani likitumiwa zaidi na Dola

la Kiroho la Roma, Ujerumani, Austria, Scandinavia, na Prussia. Watu wenye jina hili

huchukuliwa kuwa ni watu wenye mtazamo chanya (extrovert), wenye akili nyingi, na wenye

ubunifu wa hali ya juu. Watu hawa huwa wajasiriamali wenye kupenda mafanikio na hutumia

akili zao katika kujenga dhana ya ukweli. Watu hawa huwa na mvuto wawapo katika kundi la

watu na wenye kujipenda sana. Huchukuliwa kuwa ni Watawala kwenye familia zao,

marafiki, na hupendwa kwa upekee sana.

Nimesikia kuwa mnalalamika Ben amewatukana, nadhani hamjujui Ben kama ninavyomjua

mimi; Ben mmesahau kuwa ni mzee wa Uwazi na Ukweli na ndiyo maana enzi zake zilikuwa

ni za Uwazi na Ukweli; lakini pia tatizo lenu Watanzania wangu mmezoweshwa kwa muda

wa miaka kumi mkiwa na Rais Jakaya ambaye ni mcheshi, mpole na anatabasamu hata na

adui zake na hata kuwapungia mikono; hamjui kwanini anafanya hivyo ngoja niwaeleze

mambo yalivyo;

Kipindi cha utawala wangu nilikuwa kwa muda mrefu lakini ikabidi niwe nabadilisha

uongozi kutokana na mazingira ya wakati; kuna muda nilihitaji Waziri Mkuu mpole kama

Rashid Kawawa, na pale nilipohitaji Waziri Mkuu wa kupambana na kasi ya Uchumi wa

Kimataifa nilimhitaji Cleopa David Msuya; wakati wa kuwa na Nguvu Kazi na Kuweka

Ukali kwenu nilimtumia Edward Sokoine. Kipindi cha Utawala wa Mzee Mwinyi ilibidi

tukubali kuwa na Utawala wa Upole sana kwavile tulikuwa na hali duni kiuchumi suala la

Uwaziri Mkuu haikuwa tatizo sana ilikuwa lazima uwe na mtu kama Joseph Warioba

mwenye Busara, na alipomaliza ikabidi tuwe na mtu Mwenye Busara katika watu watano

kuliko wote Duniani ndugu Samuel Malecela. Lakini mwishoni mwa Miaka ya tisini tulihitaji

Busara itumike kidogo na hivyo kulazimika kumtumia Augustine Mrema nadhani

mnakumbuka alivyowaendesha Wananchi wangu hadi alipozidisha zaidi Matakwa yetu

ikabidi tumlazimishe ajiuzuru katika Serikali ya awamu ya pili.

Kipindi cha Ben kilikuwa cha Uwazi na Ukweli, ilibidi tumtumie Fredrick Sumaye ambaye

ukweli anayemjua sana ni Ben kwani alikaa naye miaka kumi. Wengi walifikia kusema

Fredrick asingefaa kuwa Waziri Mkuu ndani ya Serikali lakini akazidi kumtumia miaka yote

kumi; najiuliza kama Fredrick pamoja na wenzie aliokaa nao leo ameitwa Mpumbavu na

Lofa na bosi wake wa ndani ya Ikulu nyie Watanzania wangu mnashtuka nini? Kipindi cha

Ben kilikuwa cha kusimamia Maadili walikuwa hawacheki na kutabasamu; Mkumbuke Omar

Mahita, Robbert Mboma, Upson Mwangónda, na Kamanda Banzi, hii ilikuwa safu ya

Unidhamishi. Kijana wangu Ben bado ni wa Uwazi na Ukweli na Mnidhamishi kamwe

hajatukana bali ametoa sifa za watu. Katika siasa kuna hekima na Maarifa, ili uweze kujua

Hekima, Wazimu Na Upumbavu mtambue ni sawa na kujilisha upepo; kwani wingi wa

hekima mna wingi wa huzuni sielewi mnalalamika nini? Mnafaa kujitathmini ili hekima yenu

isiwe na huzuni. Na Mfahamu ya kuwa mgombea Urais anayeongezeya Maarifa huongeza

masikitiko.

Mnashtuka kwasababu mmejaa Ukikwete; Kipindi cha Jakaya ni cha Diplomasia, Upole,

Kufurahi na kuwaunganisha kama ndugu; Jakaya hufurahi na maadui na hata kuwapungia

mkono wa heri; kwani anajua “Heri Wenye Moyo Safi Maana Hao Wataitwa Wana Wa

Mungu”. Watu wanaomtukana Jakaya kwenye Mitandao watamkumbuka kwa kutoa machozi

yasiyofutika kamwe na ni laana. Safu yake imejaa wenye upole na ndiyo maana Edward

mambo yalimshinda miaka miwili tu ya Utawala wake; ikabidi akae Mizengo ambaye muda

wote mlimuonea, mkumbuke Alhaj Mwema, Gen Davis, na sasa Ezekiel; hivyo sioni ajabu

mkishtuka kauli za Unidhamishi kutoka kwa Ben. Na hata Jakaya alipomtumia Harrison

Page 4: WARAKA WA UPUMBAVU NA ULOFA KATIKA DEMOKRASIA

Mwakyembe na John Magufuli, wawili hawa walionekana kama ni timu tofauti kabisa maana

haikuwa muda wao muafaka.

Mioyo yenu iwaongoze kwa hekima jinsi ya kushikana na Upumbavu ambao Ben

amewaambia, ili myaone mema ya kuwafaa Watanzania. Kwani naamini kuwa Edward ni

bidhaa inayopendwa lakini haiuziki ndani ya medani ya soko la siasa wakati John Magufuli

ni bidhaa inayouzika lakini haijapendwa sana ndani ya medani ya soko la siasa. Ben

anapofoka anavaa Ubaba katika Taifa lenu msikilizeni, muulizeni Baba una maana gani

badala ya kulalamika.

Mimi Mwalimu nikageuka kuwaletea Mabadiliko ya Uongozi wa kupokezana kwa heshima

tofauti na Mataifa mengine ili kupambanua Hekima, Wazimu, na Upumbavu. Hata Ben

ameweza kutambua Upumbavu baada ya kuona watu wamegeuka. Nikaona kuwa kweli

Hekima hupita Upumbavu kwa kadri Makada wa CCM wanavyowazidi Makada wa vyama

vingine. Nafahamu kuwa macho yake mwenye hekima yamo ndani ya Ilani zenu za vyama,

lakini Mpumbavu huenda bila Sera wala Dira, naomba mtathmini hayo. Kwani

mmechanganya nyama ya Samaki na nyama ya Mbuzi yaani CCM-Edward na CUF-Duni

iangalieni Ilani ya CHADEMA na siyo kutangaza UKAWA mnauwa CHADEMA

aliyoianzisha ndugu yangu Edwin Mtei na niliisifu sana Katiba yake Mwaka 1992.

Huku kuzimu nikatambua kuwa ni tukio la tarehe 25 Oktoba, 2015 litakalowapata wote

sawasawa kushinda au kushindwa. Hata mimi Mwalimu nilipata kuwaambia kuwa mnaacha

yaliyo mema tuliyoyafanya mnachukua ya Kipumbavu; yumkini kusema yalikuwepo ya

kijinga pia; sioni kama Ben amekosea kutoa hisia zake na kuwajulisha anavyowafahamu

baadhi ya watu. Nikaichukua kazi yangu yote toka nilipopigania Uhuru na ni vyema iachwe

kwa mwenye hekima na siyo Mpumbavu, na atawale yangu yote niliyoshughulika kwa faida

ya Watanzania. Mnalipoteza kaburi la TANU na ASP kwa kupoteza neno la Mapinduzi ndani

ya chama changu CCM kwa dhana ya kujifanya mnataka Mabadiliko? Kabla ya kufanya

Mabadiliko ni vyema mtathmini ni Mabadiliko yapi mnayoyataka. Nimefahamu huku kuzimu

Edward na Regina ni Watanzania wa Kwanza Kuhiji Israel na kwenda Nigeria kwa TB

Joshua baada ya kujiuzuru Mwaka 2008; kijana huyu nasikia ameokoka na sasa ananyoosha

mkono wa kutoa Mbaraka mithiri ya Mpakwa Mafuta; CHADEMA mmesahau hata vidole

viwili vya Amani na Upendo.

Mpumbavu huikunja mikono yake naye hula chakula chake mwenyewe na si kwa ajili ya

Watanzania.Edward anajua hilo ndiyo maana hakunji mikono; John Magufuli ndiyo haswa

ananikuna kwani tafsiri ya mikono siyo mikono ya mwili kiroho, mikono ni kauli zenye

mshiko zitokazo kwenye ulimi wenye Upako. Kama Edward ana Upako wa nywele nyeupe

basi John Magufuli ana Upako kwenye Ulimi wake; naomba Muwatathmini. Ndoto za

kwenda Ikulu huja kwa shughuli nyingi na sauti ya Mpumbavu kwa njia ya wingi wa

maneno. Kazi yote ya Mwanasiasa ni kwa Ilani ya Chama chake; kwa maana mwenye

hekima hupata faida gani kuliko Mpumbavu?. Heri kusikia laumu ya mwenye hekima kama

Ben ndani ya vyama vyenu kuliko mtu kusikia wimbo wa Wapumbavu. Lakini pia CCM

msiwe na jeuri kwa vile mna hekima kwani jeuri hupumbaza mwenye hekima. Heri mwisho

wa Kampeni zenu kuliko mwanzo wake, msilaumu neno mwanzo wa Kampeni, huenda

likawa na maana sana mwisho wake na historia ikageuka kuwahukumu wakati Ben

akipumzika. UKAWA msifanye haraka kukasirika rohoni mwenu; maana hasira hukaa

kifuani mwa Wapumbavu na ndipo Ben atakapoonekana alikuwa sahihi. Siku ya kufanikiwa

furahini na siku ya mabaya fikirini.

Maneno ya wenye hekima kama Ben yanenwayo taratibu husikiwa zaidi ya mlio wake

atawalaye katikati ya Wapumbavu. Hekima ya kusema ni bora zaidi kuliko silaha za vita.

Upumbavu haba ni mzito kuliko hekima na heshima. Moyo wake mwenye hekima upo

Page 5: WARAKA WA UPUMBAVU NA ULOFA KATIKA DEMOKRASIA

upande wa kuume na ndiyo maana niliwapa maana ya Benjamin kuwa ni Mtoto wa mkono wa

Kuume, bali moyo wake Mpumbavu upo mkono wa kushoto. Mpumbavu aendapo njiani

hupungukiwa fahamu zake angalieni UKAWA msije mkapungukiwa ufahamu kabla ya

kufika Ikulu, kwani pia mmenichanganya ni CHADEMA inaenda Ikulu, Edward au

UKAWA?Angalieni Wanangu UKAWA isije ikawa UKIWA.

Edward anafahamu sana kuwa maneno ya kinywa cha mwenye hekima kama Ben yana

neema; na ndiyo maana aliwaomba kuwa kama mnadhani Ben ametukana msameheni kwani

anajua pia kuwa midomo ya Mpumbavu itammeza nafsi yake mwenye Upumbavu; Edward

asingependa nafsi zenu zimezwe kwani mwanzo wa maneno yenu ni upuuzi na mwisho wa

usemi wenu ni wazimu wenye hatari.

Nisingependa kuingilia Uhuru wenu wa kuchagua viongozi lakini chagueni atakaye enzi Sera

zangu hususan atakayejali Kazi kwani Kazi ni kipimo cha Utu wa Mtanzania. Na Maendeleo

yoyote huletwa na Kazi. Ikumbuke Imani niliyowaachia “Nitasema Kweli Daima Fitna

Kwangu Mwiko”.

Mara nikazinduka na nikajikuta niko Muhimbili Hospitali ambayo zamani iliitwa St Magreth

nimelazwa nasikia John Magufuli yuko Nkasi, Edward Uwanja wa Fisi Toobaah.

MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI AFRIKA