85
Huduma ya Afya katika Uislamu Kimeandikwa na: Jopo la Wataalamu la Taasisi ya Balagha Kimetarjumiwa na: Al-Hajj Hemedi Lubumba Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page A

Huduma ya Afya katika Uislamu

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Afya ya mwili kwa mwanadamu ni kitu muhimu sana. Ili mwanadamu aweze kuyajenga maisha yake na kuwa bora kimwili, lazima awe na afya bora, na sio tu kwa ajili ya kuendesha maisha yake, bali pia bila afya nzuri mtu hawezi kutekeleza ibada zake sawasawa jinsi inavyotakiwa kuifanya. Hivyo, kama Uislamu ulivyo kwamba ni dini na ni mfumo kamili wa maisha, umeelezea kwa kina huduma ya afya, yaani mtu akiwa nini ili ajipatie afya njema. Waandishi wa kitabu hiki wameelezea mambo mbalimbali ambayo yanapaswa kufanywa kwa ajili ya afya ya mtu binafsi na ya jamii kwa ujumla. Katika maelezo yao wamezingatia Qur’ani Tukufu, Sunna pamoja na mafundisho ya Maimamu Watukufu.

Citation preview

Page 1: Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afyakatika

Uislamu

Kimeandikwa na:Jopo la Wataalamu la Taasisi ya Balagha

Kimetarjumiwa na:Al-HHajj Hemedi Lubumba

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page A

Page 2: Huduma ya Afya katika Uislamu

©Haki ya kunakili imehifadhiwa na:AL-ITRAH FOUNDATION

ISBN: 978 - 9987 - 17 - 011 - 1

Kimeandikwa na:Jopo la Wataalamu la Taasisi ya Balagha

Kimetarjumiwa na:Al-Hajj Hemedi Lubumba

Kimepangwa katika Kompyuta na:Hajat Pili Rajab

Toleo la kwanza: Julai,2011Nakala: 1000

Kimetolewa na kuchapishwa na:Alitrah Foundation

S.L.P. 19701 Dar es Salaam, TanzaniaSimu: +255 22 2110640

Simu/Nukushi: +255 22 2127555Barua Pepe: [email protected]

Tovuti: www.ibn-tv.comKatika mtandao: www.alitrah.info

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page B

Page 3: Huduma ya Afya katika Uislamu

YALIYOMO

Afya na umbile la mwanadamu.........................................................3

Kuujali mwili na kuutunza.................................................................6

Maradhi ya Kisaikolojia na Athari zake katika Afya ya mwili.........21

Maradhi na kukamilika kwa Nafsi..................................................32

Maumivu na fidia.............................................................................41

Maradhi na Taklifu za Kisheria........................................................46

Mamlaka ya mgonjwa.....................................................................49

Matibabu na Mwanamke Ajinab.................................................... 52

Utabitu ni wajibu wa kutosheleza...................................................55

Kumtembelea mgonjwa...................................................................66

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page C

Page 4: Huduma ya Afya katika Uislamu

D

Huduma ya Afya katika Uislamu

NENO LA MCHAPISHAJI

Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya Kiswahili ya kitabu chaKiarabu kiitwacho, ar-Ri’ayatu ‘s-Swihiyyah Fi ‘l-Islam kilichoandikwana Jopo la Wataalamu la Taasisi a Balagha. Sisi tumekiita, Huduma yaAfya katika Uislamu.

Afya ya mwili kwa mwanadamu ni kitu muhimu sana. Ili mwanadamuaweze kuyajenga maisha yake na kuwa bora kimwili, lazima awe na afyabora, na sio tu kwa ajili ya kuendesha maisha yake, bali pia bila afya nzurimtu hawezi kutekeleza ibada zake sawasawa jinsi inavyotakiwa kuifanya.Hivyo, kama Uislamu ulivyo kwamba ni dini na ni mfumo kamili wamaisha, umeelezea kwa kina huduma ya afya, yaani mtu akiwa nini ili aji-patie afya njema.

Waandishi wa kitabu hiki wameelezea mambo mbalimbali ambayo yana-paswa kufanywa kwa ajili ya afya ya mtu binafsi na ya jamii kwa ujumla.Katika maelezo yao wamezingatia Qur’ani Tukufu, Sunna pamoja namafundisho ya Maimamu Watukufu.

Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wamaendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, nganoza kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tenakatika akili za watu.

Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamuakukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yakeyaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji waKiswahili.

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page D

Page 5: Huduma ya Afya katika Uislamu

E

Huduma ya Afya katika Uislamu

Tunamshukuru ndugu yetu, Hemedi Lubumba kwa kukubali jukumu hilila kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshirikikwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake.

Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni changamoto kubwakwa wasomaji wetu.

Mchapishaji:Al-Itrah Foundation

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page E

Page 6: Huduma ya Afya katika Uislamu

F

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page F

Page 7: Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 1

Page 8: Huduma ya Afya katika Uislamu

2

Huduma ya Afya katika Uislamu

Kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe vyote.Rehema na amani zimwendee Muhammad na aali zake watoharifu naSahaba zake walio wema.

Kanuni na taaluma za kibinadamu zimeamiliana na mwanadamu kwamsingi wa mahitaji ya kimwili pekee, hivyo zikajali na kutilia umuhimumasuala ya kimada tu na zimepuuzia mahitaji yake ya kiroho, jambo amba-lo limefanya utatuzi wake ushindwe kuzaa matunda yoyote kwani kilawanapojaribu kutatua upande huu upande ule nao huharibika. Hiyo ni kwasababu mwanadamu tangu mwanzo ni roho na mwili na bado ndivyoalivyo, na ukweli huo haujakanushwa ila na yule aliyejitenga, na bila shakaaliyekanusha hajabadili chochote katika ukweli wake halisi.

Mkabala na mtazamo huo tunazikuta dini za kimapokezi – zisizokuwaUislamu – kutokana na mageuzi na mabadiliko yaliyozifika katika historiazinaamiliana na mwanadamu kwa mtazamo mwingine usiokuwa sawajapokuwa ni kwa namna nyingine, pale walipopuuzia mahitaji yamwanadamu ya kimwili na mahitaji yake ya kimada hivyo wakaifanya dinikuwa ni ibada tu za kiroho, na hatimaye wameyafunga mafanikio ya mtukwenye hali ya kujitenga na dunia na kuacha ladha na yote aliyohalalishaMwenyezi Mungu.

Uislamu ulipambana na hali hizo zote mbili tangu pale tu ulipoteremka.Mwenyezi Mungu anasema: “Na uruhubani wameuzusha, sisihatukuwaandikia” (Sura Hadid: 27). Kwani dini ilikuja ili kunadhimumaisha ya kweli ya mwanadamu, na mweka sheria ni Yule Mjuzi wa vilealivyoviumba Naye ni Mpole kwa waja wake. Hivyo hawezi kuipuuziadunia na hali ameiumba kwa ajili ya waja wake. Amesema: “Sema: Ninani aliyeharamisha mapambo ya Mwenyezi Mungu ambayo amewa-tolea waja wake na vitu vizuri vya riziki” (Sura Aaraf: 32).

Kama ambavyo roho ina mchango mkubwa katika afya ya mwanadamu nausalama wa fikra zake, ndivyo hivyo hivyo mwili nao ulivyo na mchango

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 2

Page 9: Huduma ya Afya katika Uislamu

3

Huduma ya Afya katika Uislamu

mkubwa kwa mwanadamu katika kutekeleza jukumu lake maishani, kati-ka kujenga utu wake na kujenga jamii yake. Kwa ajili hiyo Uislamu ume-jali sana kanuni za afya ambazo zinawezesha sehemu kubwa ya ibadakutekelezwa na pia zinazohusu miamala mbalimbali.

Kama ambavyo Uislamu umeweka sheria zinazohalalisha, zinazowajibishana kuharamisha ili kudhamini usalama wa mtu na roho yake, pia una she-ria nyingi zinazodhamini usalama wa mwili wa mwanadamu na kulindaafya yake. Anayesoma hazina adhimu ya Uislamu katika mchepuo huu naule bila shaka atafikia ukweli kwamba dini hii ni dini ya wastani katika kilakitu ikiwemo mahitaji ya roho na mwili, dunia na Akhera.

Tunafuraha katika maudhui hii kutoa uchambuzi tulionao ambaounakamilishwa na uchambuzi uliotangulia kuhusu Afya ya mwili katikaUislamu, tunataraji utarejea huko ili kufaidika zaidi.

Taufiki ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu.Muasasatul-Balagha.

AFYA NA UMBILE LA MWANADAMU

Mwenywezi Mungu amesema ndani ya Kitabu Chake kitukufu:

“Ewe mwanadamu! Ni nini kikudanganyacho na Mola wako MleziMtukufu. Aliyekuumba na kukutengeneza, kisha akakulinganishasawa. Katika sura yoyote aliyoitaka amekutengeneza.” (Sura al-Infitar: 6 – 8).

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 3

Page 10: Huduma ya Afya katika Uislamu

4

Huduma ya Afya katika Uislamu

Akasema pia:

“Ndio sanaa ya Mwenyezi Mungu aliyekitengeneza kila kitu.” (SuraNamlu: 88).

Akasema tena: “Bila shaka tumemuumba mtu katika hali nzuri sana.”(Sura Tini: 4).

Imepokewa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.w) - kwamba alisema:“Neema mbili hazithaminiwi: Amani na afya.”

Kila kilichomo ndani ya ulimwengu huu kinathibitisha hekima na ufanisiwa muumba wake, na mwanadamu ni sehemu ya ulimwengu huu wa kima-da, ameumbwa kutokana na udongo wa ardhi hii na umbile lake la kimwililimenadhimika kulingana na mpangilio wa kinidhamu wenye kushangaza.Mwili wa mwanadamu ni mfumo wa kipekee wa uhai katika ulimwenguwa viumbe, hufanya kazi ndani yake chembechembe hai, viungo namashine kwa umakini na mpangilio makini.

Asili katika mpangilio wa umbile ni afya, ukamilifu na ufanisi, kwa ajilihiyo imepokewa hadithi toka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwambaalisema katika kuitambulisha dosari: “Ni ile iliyozidi juu ya umbile.” Yaanikila kisichokuwa katika asili ya umbile ni dosari.

Mwenyezi Mungu amemuumba mwanadamu hali kasalimika na dosari,maradhi na upungufu. Bali maradhi humpata mwanadamu kutokana nakuvurugika mpangilio wa mwili kwa sababu ya visababishi na viathiri vyanje kuvuruga mpangilio wa umbile, kwa ajili hiyo tunaiona Qur’aniTukufu inamkumbusha mwanadamu neema za Mwenyezi Mungu juuyake, umakini uliopo kwenye sanaa, hekima na ufanisi uliopo katikaviumbe. Tunalisoma hilo kwa uwazi katika kauli Yake:

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 4

Page 11: Huduma ya Afya katika Uislamu

5

Huduma ya Afya katika Uislamu

“Aliyekuumba na kukutengeneza, kisha akakulinganisha sawa.”(Sura al-Infitar: 6 ).

“Ndio sanaa ya Mwenyezi Mungu aliyekitengeneza kila kitu.” (SuraNamlu: 88).

“Bila shaka tumemuumba mtu katika hali nzuri sana.” (Sura Tini: 4).

Hivyo kuanzia chembechembe hai hadi kiungo katika mwili wamwanadamu kinafanya kazi kwa umakini na ufanisi ndani ya mipangiliona harakati zenye kuungana zilizokamilika. Chembechembe hai zinampangilio wake makhususi katika mwili, kiungo kina mpangilio wakemakhususi na mshipa una mpangilio wake makhususi, na yote ipo chini yampangilio mmoja na muungano mmoja wa kimajukumu uliokamilika, napindi mpangilio wa mwili unapopatwa na mvurugiko au dosari ndipomwanadamu huugua, ndio maana ugonjwa ukatambulishwa kuwa ni:Kutoka nje ya unyoofu makhususi wa mwanadamu.1

1 Muujamu Mufradati Alfadhil-Qur’ani cha ar-Raghib al-Isfihaniy.

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 5

Page 12: Huduma ya Afya katika Uislamu

6

Huduma ya Afya katika Uislamu

KUUJALI MWILI NA KUUTUNZA

Miongoni mwa fikra na sheria ya Uislamu ni ulingano na uwiano na usawakati ya mwili, akili, roho na nafsi. Kuujali kwake mwili na kutunza afya yamwili ni kwa hali ya juu mno, kwa ajili hiyo umeuwekea mwili haki zakimaada ambazo umeziwajibisha juu ya mwanadamu mwenyewe, na juuya dola na jamii pindi mtu binafsi mwenyewe anaposhindwa kuutekelezeamwili wake haki zake. Mwili una haki ya chakula, kinywaji, mavazi, tibana makazi, achilia mbali mapumziko, usingizi na kinga.

Qur’ani imezungumzia chakula, mlo na kujali mahitaji ya mwili,inathibitisha kwamba kupata usalama wa kichakula ni haki ya mwanadamuna kwamba ni sehemu ya mpangilio wa uwepo wa ulimwengu. Aya Tukufuimebainisha maana hii kwa maandiko yake ambayo yanazungumzia ardhina riziki, Mwenyezi Mungu amesema: “Na akapima humo chakulachake katika hatua nne, ni sawa kwa waulizao.” (Sura Haa Mim: 10).Na katika sehemu nyingine ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu tunakutaufafanuzi wa ukweli huu kwa Adam baba wa wanadamu wote, anasemaMwenyezi Mungu:

“Hakika hutakuwa mwenye njaa humo wala hutakuwa uchi. Na kwahakika hutapata kiu humo wala hutapata joto.” (Sura Twaha: 18 –19).

Ameweka hayo yote na ameweka kanuni na mpangilio wa lazima ilikutimiza haja ya chakula kwa mwanadamu, kama vile sheria ya Zakaambayo imefaradhishwa katika vyakula, ngano, shairi, tende, zabibu, kon-doo na mbuzi, ng’ombe na ngamia, kama ambavyo pia imefaradhishwakatika pesa na ikawa ni sunna katika mbegu na matunda yaliyobakia.

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 6

Page 13: Huduma ya Afya katika Uislamu

7

Huduma ya Afya katika Uislamu

Na Qur’ani ikawalaumu wale wanaolimbikiza dhahabu, fedha na malihuku wakiwakosesha wengine kustarehe na yale wenye haja nayo mion-goni mwa chakula na vinywaji, na ikawaita mafakiri kwamba niwaliokoseshwa, ikawasifu wale ambao katika mali zao wametenga fungukwa ajili ya kutatua matatizo ya waliokoseshwa, ikasema: “Na katikamali zao kuna haki ya mwenye kuomba na anayejizuia.” (SuraDhariyat: 19).

Na ili walafi na maadui wa ubinadamu wasichezee chakula cha tabakafakiri Uislamu umeharamisha kulangua chakula, na umeipa dola, waamr-ishaji wa mema na kukataza mabaya na wenye kufanya kazi katika sektaya uhasibu haki ya kuzuia ulanguzi na kumlazimisha mwenye kulanguakukipeleka sokoni chakula kilicholanguliwa ili bidhaa za chakulazipatikane, na bei zishuke kutokana na wingi wa chakula masokoni.

Na katika kusoma maelekezo ya kiafya na umuhimu wa chakula tunagun-dua jinsi sheria na fikra ya Uislamu ilivyojali elimu ya chakula na maleziya kiafya, hivyo tunakuta inahimiza kula vyakula na milo ambayo itaweze-sha mwili kukua katika hali ya afya na kuutimizia kinga imara dhidi yamagonjwa na dhidi ya sababu za udhoofu.

Tunaweza kufupisha mfumo wa afya katika Uislamu na kujali kwake afyaya mwili kwa haya yafuatayo:

Kwanza - Chakula bora:

Uislamu umejali chakula bora na umewahimiza wazazi hasa mwanamkemjamzito na mwenye kunyonyesha kula baadhi ya vyakula ili kulinda afyaya mimba na kuipatia sifa ya uzuri. Na umetilia msisitizo katika kujalichakula cha mtoto kutokana na chakula kilivyo na athari katika afya yamimba na usalama wa makuzi ya mwili na uzuri wa sura.

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 7

Page 14: Huduma ya Afya katika Uislamu

8

Huduma ya Afya katika Uislamu

Tunaweza kuuona ukweli muhimu wa kielimu, nao ni kwamba kitendo chaUislamu kutilia umuhimu sheria ya chakula si chini ya kitendo chake chakutilia umuhimu sheria ya ibada na nidhamu ya jamii, hilo tunalikuta kwauwazi kabisa katika riwaya na hukumu zake. Kati ya riwaya hizo ni ileiliyopokewa toka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Chakulacha kwanza kwa mwanamke anayekaribia kujifungua kiwe ni tende laini,kwani hakika Mwenyezi Mungu alimwambia Mariam: ‘Na litikise kwakoshina la mtende, litakuangushia tende nzuri, zilizoiva.’”2

Akasema tena: “Wanawake wanaokaribia kujifungua hawana tiba mfanowa tende laini, kwa sababu Mwenyezi Mungu alimlisha Mariam tende laininzuri wakati wa uchungu wake.”3

Utafiti wa kielimu unaonyesha kwamba tende humtengenezeamwanadamu uwiano wa chakula kati ya sukari, protini, wanga, mafuta,madini na vitamini.

Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Wanywesheni wanenu uji wa ngano na shairiudogoni mwao, kwani hakika (chakula) hicho huotesha nyama na kuko-maza mifupa.”4

Imam Ali bin Musa ar-Ridha (a.s.) amesema: “Hakuna Nabii yeyote ilaalimwombea mwenye kula shairi na kumbariki.”5

Imam Ja’far as-Sadiq (a.s.) amesema: “Mlisheni mwenye ugonjwa watumbo la kuachia mkate wa mchele, hakuna kitu kiingiacho katika tumbola mwenye tumbo la kuachia chenye manufaa kushinda wenyewe.”6

2 Muujamu Mufradati Alfadhil-Qur’ani cha ar-Raghib al-Isfihaniy, Uk. 134.3 Muujamu Mufradati Alfadhil-Qur’ani cha ar-Raghib al-Isfihaniy, Uk. 134.4 Biharul-An’war Juz. 104, Uk. 105.5 Biharul-An’war Juz. 17, Uk. 4.6 Biharul-An’war Juz. 104, Uk. 5.

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 8

Page 15: Huduma ya Afya katika Uislamu

9

Huduma ya Afya katika Uislamu

Imam Musa bin Ja’far (a.s.) amesema: “Nyama huotesha nyama.”7

Akasema tena: “Kuleni komamanga na maganda yake hakika husafishautumbo.”8

Na kutoka kwa Ibrahim bin Abdul-Hamidi amesema: Nilimsikia Abul-Hasan akisema: “Jitahidini kula samaki, ukimla bila mkate atakutosheleza,na ukimla na mkate atakunufaisha.”9

Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Nabii miongoni mwa Manabii waMwenyezi Mungu alimlalamikia Mwenyezi Mungu upungufu wa kizazi.Akasema: Kula nyama na mayai.” 10

Na pia amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa akilaasali na kusema: Ina Aya nyingi toka katika Qur’ani.”11

Imam as-Sadiq (a.s.) alikuwa akisema: “Watu hawakupewa tiba mfano waasali.”12 Na akisema: “Walisheni watoto wenu komamanga, kwani ndilolililo jepesi zaidi kwa ujana wao.”13 Na pia akisema kuhusu mwanamkemjamzito anayekula pera: “Hakika mtoto atakuwa mwenye harufu nzuri narangi ya kuvutia.”14

Na kuna maelekezo lukuki yanayousia kula matunda, mboga mboga naaina za nyama na mboga za majani, pia yanatoa wito wa kutilia umuhimuchakula cha mwili na kulinda uwiano wa chakula na mwili.7 Biharul-An’war Juz. 104, Uk. 12.8 Biharul-An’war Juz. 104, Uk. 16.9 Biharul-An’war Juz. 104, Uk. 53.10 Biharul-An’war Juz. 104, Uk. 57.11 Biharul-An’war Juz. 104 Uk. 63.12 Biharul-An’war Juz. 104 Uk. 73.13 Biharul-An’war Juz. 104 Uk. 105.14 Wasailus-Shia Juz. 7 Uk. 133, chapa ya Daru Ihyaut-Turathil-Arabiy

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 9

Page 16: Huduma ya Afya katika Uislamu

10

Huduma ya Afya katika Uislamu

Pili: Kutokula baadhi ya vyakula:

Uislamu umeharamisha baadhi ya vyakula, vinywaji na vitendo vyenyekudhuru afya ya mwili, na huenda mfano ulio kinara katika mfumo waUislam na sheria ya afya kwa ajili ya kulinda afya na kuhakikisha usalamawa kiafya ni kuharamisha kwake baadhi ya vyakula na vinywaji na viten-do vinavyodhuru mwili.

Uislamu umeharamisha pombe, madawa ya kulevya, zinaa, kulawiti,kusagana, ukuwadi, damu, nyama ya nguruwe na mengineyo mengi, kamaulivyoharamisha kila ambalo asili yake ni kudhuru mwili, ikifuata kanuniisemayo: “Hakuna kudhuru wala kujidhuru,” Ambayo imepatikana katikakauli ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.).

Katika jibu la Imam al-Baqir (a.s.) alilolitoa kwa mtu mmoja aliyemuuliza,tunapata ufumbuzi wa kielimu wa hekima ya uhalali na uharamu, muuliza-ji alisema: Kwa nini Mwenyezi Mungu aliharamisha pombe, mzoga,nyama ya nguruwe na damu? Akasema: “Hakika Mwenyezi Mungu haja-haramisha hayo kwa waja wake na akawahalalashia yasiyokuwa hayo kwakutamani yale aliyowahalalishia na wala si kwa kutohitaji yale aliyowa-haramishia, lakini aliumba viumbe na akajua yale yanayojenga miili yao nayanayowafaa wao, hivyo akawahalalishia na kuyaruhusu kwao, na akajuayanayowadhuru hivyo akawakataza hayo, kisha akahalalisha kwa yulealiye katika dhiki katika wakati ambao hakuna cha kuusaidia mwili wakeila hicho.”

Hivyo kipimo cha uhalali ni “yale yanayojenga miili yao na yanayowafaawao, hivyo akawahalalishia.” Na kipimo cha uharamu ni “yanayowadhuruhivyo akawakataza hayo.” Sayansi na uchunguzi wa kielimu umethibitishakwamba magonjwa yaliyo hatari sana hivi sasa kwa afya ya mwanadamusababu yake ni pombe, ngono ya kinyume na maumbile na ngono iliyo njeya sheria, kama vile zinaa na mengineyo miongoni mwa aina za uharibifuwa kitabia. Na huenda janga la Ukimwi ndio janga baya mno lenye kutishalinalotishia maisha ya mwanadamu na ambalo sababu yake kuu ni ngono

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 10

Page 17: Huduma ya Afya katika Uislamu

11

Huduma ya Afya katika Uislamu

zisizo za kisheria.

Ama magonjwa yasababishwayo na pombe na madawa ya kulevya nayenye kuidhuru afya huzingatiwa kuwa ndio aina kubwa mno yamagonjwa na hatari zaidi kwa afya na usalama wa jamii. Magonjwa hayohayaidhuru afya tu bali yanadhuru pia hali ya uchumi na usalama. Kesinyingi za jinai za mauwaji na uporaji, ubakaji na ajali za barabarani sababuyake ni pombe na madawa ya kulevya. Ni mali nyingi kiasi gani hutolewana dola na serikali katika kutatua bila mafanikio madhara yasababishwayona pombe na madawa ya kulevya?

Tatu: Kutofanya ubadhirifu:

Uislamu umekataza kufanya ubadhirifu, na miongoni mwa vitendo hatarijuu ya afya ya mwili ni kufanya ubadhirifu katika chakula, vinywaji nangono. Maradhi mengi ya mwili sababu yake ni kuendekeza na kufuatamatamanio ya mwili, ubadhirifu wa kupindukia katika kula na kunywa,kwa ajili hiyo Qur’ani imekataza kufanya ubadhirifu katika chakula navinywaji na mengineyo. Mwenyezi Mungu amesema: “Kuleni na kuny-weni wala msifanye ubadhirifu.” Mtume Mtukufu amesema:“Mwanadamu hakujaza chombo shari kushinda tumbo lake.” Kamaalivyosema tena: “Utumbo ni nyumba ya magonjwa, na kujithamini nikinara wa dawa.”

Kwa sheria hizi za afya na kumwelimisha mwanadamu madhara ya ubad-hirifu na kumkataza kufanya hivyo Uislamu umetoa wasia wa mbelekabisa wa kuilinda afya, nao ni wasia wa Kinga dhidi ya Maradhi, kwakuifanyia kazi hekima mashuhuri: “Kinga ni bora kuliko tiba.”

Nne: Kufuata kanuni za usafi:

Kwa kuweka sheria ya tohara na kutoa wito wa usafi Uislamu unakuwaumeweka mfumo mpana wa kumuhami mwanadamu na mazingira dhidi yauchafuzi na uchafu na vyanzo vya madhara ya kiafya. Tunaweza kufupisha

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 11

Page 18: Huduma ya Afya katika Uislamu

12

Huduma ya Afya katika Uislamu

mfumo wa Uislamu katika sekta hii katika mambo mawili ya msingi, nayoni:

i. Uislamu umezingatia kwamba baadhi ya vitu ni najisi na ukalazimishakujitenga navyo. Na najisi hizi ndio chanzo kikuu na kikubwa cha vijiduduna bakteria wa maradhi, kama vile haja kubwa na haja ndogo na kinyesicha wanyama wengi, mizoga, damu, manii na vitu vingine vilivyonajisikakwa najisi hizo. Vinyesi hivyo na vitu hivyo hutengeneza chanzo cha ucha-fu na kupatwa na maradhi. Hivyo kwa kujitoharisha na kujikinga dhidi yavitu hivyo tunakuwa tumejenga msingi muhimu katika kujikinga namaradhi na kuilinda afya.

ii. Usafi: Usafi hutengeneza sura ya wazi miongoni mwa sura zamwanadamu aliyestaarabika ambaye anajali afya yake, akili yake namwonekano wake. Uislamu umekuja ili kutimiza masilahi na kuondoauharibifu, na kinara wa masilahi hayo ni kulinda afya ya mwanadamu nakuipa heshima akili yake na mwamko wake katika afya na ustaarabu.

Hivi leo vipaumbele vya mwanadamu na tafiti zake za kielimu hasahasahuwa ni katika kuyalinda mazingira na kuyahifadhi dhidi ya uchafu navyanzo vya uchafuzi ambavyo vimekuwa ni miongoni mwa matatizo yasasa. Kwa kufuata mfumo wa Uislamu katika usafi na tohara unatuhakik-ishia ulinzi wa mazingira na kuhifadhi afya na kuokoka dhidi ya maradhiambayo hutokana na kupuuza usafi na kueneza uchafu. Umekuja msisiti-zo juu ya usafi na wito wa kujiepusha na uchafu, tunalipata hilo wazi wazikatika ubainifu wa Qur’ani Tukufu:

“Mwenyezi Mungu hapendi kukutieni katika taabu, lakini anatakakukutakaseni na kutimiza neema yake juu yenu ili mpate kushukuru.”(Sura Maida: 6).

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 12

Page 19: Huduma ya Afya katika Uislamu

13

Huduma ya Afya katika Uislamu

Tukiichunguza Aya hii ya tohara tunaikuta Qur’ani imezingatia kujitohar-isha na uchafu ni kutimiza neema za Mwenyezi Mungu juu ya mwanadamuambazo zinastahiki shukrani. Hiyo ni kwa sababu tohara ni moja ya vyan-zo vya afya, na afya ni moja ya neema mbili ambazo Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) amemkumbusha kwazo mwanadamu: “Neema mbilihazithaminiwi: amani na afya.”

Na katika maelekezo ya Nabii tunapata wito wa kujiepusha na uchafu natakataka, na kuhakikisha usafi katika mavazi, nyumba na mwili. Hayoyamekuja kwa kauli yake (s.a.w.w.): “Jisafisheni, hakika Uislamu nimsafi.” “Hakika Mwenyezi Mungu huchukia uchafu rafurafu.” “Ni mjambaya aliyoje! Yule aliye mchafu.”

Tano: Michezo:

Michezo ni mkusanyiko wa vitendo na mazoezi ambayo hukuza uwezo wamwanadamu na nguvu yake na kumhakikishia mwanadamu uwiano wakimwili, kama vile kuogelea, upandaji wa ngamia, kutembea kwa miguu,mieleka na mengineyo miongoni mwa mazoezi mingine. Michezo kama hiiya kimazoezi hukuza nguvu za mwili katika kufanya kazi na uzalishaji,kama ambavyo huuongezea mwili uwezo wake wa kupambana na marad-hi na mazingira ya afya ambayo huzorota kwa kuleta maradhi. Uislamukatika mfumo wake wa kiroho umesisitiza kuujali mwili na kuulinda mwilikwa mazoezi ili kukuza uwezo wa mwanadamu na nguvu zake, ili ujengekizazi chenye miili imara na roho imara. Miongoni mwa kanuni hizo ni ileiliyokuja katika kauli ya Mwenyezi Mungu kuhusu jihadi na kutetea she-ria, nchi na masilahi ya kisheria: “Na waandalieni nguvu muwezavyo, nakwa farasi waliofungwa..” (Surat Anfal: 60). Kanuni hiyo ambayoMtukufu Mtume aliifasiri katika kauli zake nyingi na vitendo vyake, kamakauli ya Mtume: “Wafunzeni wanenu shabaha, uogeleaji na upandajingamia.” Na miongoni mwa tafsiri zake ni kushiriki kwake mwenyewekatika mashindano ya ngamia na mieleka, bali alikuwa akiweka zawadikwa wenye kushinda katika mbio za ngamia na akiwashajiisha kufanya

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 13

Page 20: Huduma ya Afya katika Uislamu

14

Huduma ya Afya katika Uislamu

hivyo. Mtume alishindana zaidi ya mara moja na akashinda kama ambavyongamia wake alishindwa mara moja.

Na katika maadhishi ya Sharia ya Uislam tunapata hukumu makhsusi zina-zohusu mashindano ya mbio, shabaha na zawadi ili kunadhimu mazoezihaya.

Kama alivyoshiriki yeye mwenyewe (s.a.w.w.) katika mashindano naakahimiza kushiriki na akaweka zawadi kwa wenye kushinda pia aliingiakatika shindano la mieleka pamoja na Rukana bin Yazid, na huyu alikuwani mwanamieleka mashuhuri lakini Mtume akamshinda. Kama alivyokuwahodari wa mieleke, mbio za ngamia pia alikuwa anajua kuogelea, alijifun-za hilo katika bwawa la Bani Adiy tangu angali mdogo.

Na lililo wazi katika kanuni za sheria ya Uislamu ni kwamba Mtume waMwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ni kigezo katika kila kitu, na pindi anapo-fanya kitu huwa kwa hali hiyo amethibitisha sheria kwa mwanadamu namfumo wa matendo, maadamu tu kitendo hicho si makhususi kwaMtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Sita: Kujishughulisha na kuacha kujibwetesha:

Mwenyezi Mungu anasema: “Yeye ndiye aliyefanya ardhi laini kwa ajiliyenu, basi nendeni katika pande zake na kuleni katika riziki zake, nakwake ndio marejeo.” (Sura Mulki: 15). Katika Aya hii tukufu Qur’aniimemsisitizia mwanadamu kujituma ardhini kwa ajili ya kutafuta riziki nakipato cha halali, na kujituma ni kufanya harakati na kufanya kazi, naharakati na kazi ni vyanzo viwili muhimu vya uchangamfu na nguvu.Imekuja kauli kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Ibada ina sehemusabini, iliyo bora kushinda nyingine ni kutafuta halali.” Na pia akasema:“Mwenyezi Mungu humchukia mja asiyejishughulisha mwingi wa kulala.”

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 14

Page 21: Huduma ya Afya katika Uislamu

15

Huduma ya Afya katika Uislamu

Kazi haitoi faida za kiuchumi na kipato tu, bali pia humhakikishiamwanadamu faida ya afya, kwani kazi ni juhudi za mwili, hukuza uwezowa mwanadamu na nguvu zake za kimwili, humpa afya, uhai na nguvu zamwili ambazo katika baadhi ya nyakati hushinda mazoezi na harakati zakimichezo. Kama ambavyo kazi ina athari chanya katika kuujenga mwilina kuupa kinga ya afya pia ina athari za kisaikolojia katika nafsi yamwanadamu. Matatizo mengi ya kisaikolojia ya mwanadamu sababu yakeni kujibwetesha na kutojishughuliasha, na hivyo hali ya maradhi namachungu ya kisaikolojia hugeuka na kuwa machungu na maradhi yakimwili. Na kama ambavyo kazi ni chanzo miongoni mwa vyanzo vyanguvu na uchangamfu wa kisaikolojia na kimwili, kujibwetesha na kuto-jishughulisha ni chanzo miongoni mwa vyanzo vya kudhoofika kwa mwilina kupotea nguvu zake.

Saba: Kinga na tiba:

Hakika sheria na maelekezo ambayo yanazungumzia afya, kinga, tiba nahaki za mwili yanatengeneza uwanja mpana katika Fiqhi, elimu na mafun-zo ya Uislamu. Kanuni na wasia wa Uislamu vimetilia mkazo mpakakiwango cha wajibu kuujali mwili, kuilinda afya na kutibu maradhi, kwanimaradhi hayatibiki ila kwa matibabu, kwa ajili hiyo Uislamu umezingatiakwamba matumizi ya mwanadamu ya mwaka anayoyahitajia katikakugharamia matibabu na huduma za afya kwa ajili yake mwenyewe nawanafamilia yake yamesameheka kodi ya wajibu ya Zaka na Khumsi.

Na kwa ajili ya Uislamu kutilia mkazo matibabu na dawa sheria yaUislamu imezingatia kwamba upatikanaji wa dawa, maabara na taasisi zatiba katika jamii ni wajibu wa kujitosheleza, kama ambavyo umezingatiamatibabu kuwa ni wajibu wa mtu binafsi juu ya tabibu mtoa tiba ambayeyuko peke yake iwapo hapatikani mwingine. Ikiwa wajibu wa kuhakikishamaabara za tiba zinapatikana ni wajibu wa wanajamii wote basi kujitibu nakugharamia matibabu ya lazima ni wajibu kwa mtu binafsi ili awezekujitibu na kumtibu yule ambaye kisheria matumizi yake yako juu yake,

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 15

Page 22: Huduma ya Afya katika Uislamu

16

Huduma ya Afya katika Uislamu

kama vile mke, watoto wadogo, wazazi wawili wasioweza kujihudumia.Akiwa hana uwezo wa kufanya hivyo hupewa fungu toka katika mapato yakisheria ili agharamie dawa na matibabu. Zaidi ya hapo ni kwamba dolainawajibika kuwatimizia wananchi wake wasiojiweza huduma ya mati-babu na yote yanayoambatana na matibabu hayo.

Uislamu katika wajibu wa matibabu umeanzia kwenye kanuni ya msingikatika kuifahamu afya, maradhi na tiba, na katika mtazamo wake wakiitikadi na nadharia yake ya kifalsafa kuhusu uhai na maisha. Hivyo fikraya Uislamu inaamini kuwa ulimwengu wote ni ulimwengu umesimama juuya msingi wa kanuni ya sababu na falsafa ya uwepo wa uhusiano baina yavitu, hivyo ulimwengu ni mnyororo wa sababu na matokeo, hivyo ugonjwani matokeo ya sababu na ila, na kwamba tiba huja kuondoa sababu hizo naila hizo kupitia sababu nyingine na ila nyingine. Na kwamba uhusiano katiya ugonjwa na tiba ni sehemu ya mpangilio wa mvutano uliopo katikaulimwengu wa mada na viumbe na katika wigo wa mwili wa mwanadamu.Ugonjwa katika hali zake nyingi ni sehemu ya mvutano huu, hivyo tibahuenda kulingana na mpangilio wa mvutano na kanuni ya sababu nakisababishwa. Fikra hii ya kielimu tunaisoma katika maelekezo ya kitabibualiyoyatoa Mtukufu Mtume, na kutoka katika amri zake za kuamrisha tiba.

Hakika kukimbilia kwenye matibabu kunaafikiana na imani ya Uislamuambayo inakusanya baina ya kuamini kanuni ya sababu na mada na bainaya kumtegemea Mwenyezi Mungu. Hiyo ni kwa sababu ila na sababu zakimada hufuata nguvu za Mungu na msaada wake, hivyo sababu na ilakama alivyoeleza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni sehemu ya uwezo waMwenyezi Mungu. Hivyo umekuja msisitizo juu ya matibabu na kutumiadawa, na umekuja ufafanuzi wa uhusiano uliopo baina ya sababu za kimat-ibabu na uwezo wa Mungu.

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira, kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.)kwamba alisema: “Mwenyezi Mungu hakuleta ugonjwa ila aliushushia

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 16

Page 23: Huduma ya Afya katika Uislamu

17

Huduma ya Afya katika Uislamu

tiba.”15 Na kutoka kwa Jabir bin Abdillah al-Ansariy amesema Mtume(s.a.w.w.) alisema: “Kila ugonjwa una dawa, dawa ikiupata ugonjwahupona kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.”16

Na imekuja katika habari kwamba: Hakika Musa bin Imran (a.s.) aliugua,wana wa Israil wakaingia kwake na wakautambua ugonjwa wake.Wakamwambia: Ungetumia dawa fulani ungepona. Akasema: Situmiidawa mpaka Mwenyezi Mungu anipe afya njema bila dawa. NdipoMwenyezi Mungu akampelekea wahyi: “Naapa kwa nguvu Zangu nautukufu Wangu, sikuponyeshi mpaka utumie dawa waliyokutajia.”Akawaambia: Nipeni dawa mliyoitaja. Wakampa dawa naye akapona.Akaingiwa na khofu nafsini mwake kwa hilo, ndipo Mwenyezi Munguakampelekea wahyi: “Ulitaka kuvunja hikima yangu kwa tawakuli yakokwangu, basi ni nani asiyekuwa mimi aliyeweka katika mti wa Aqaqirimanufaa ya vitu!”17

Ahmad bin Hanbali ameandika katika Musnad yake kwamba Usama binSharik alisema: Nilikuwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ndipo wakajamabedui na kusema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Tutumie dawa?Akasema: “Ndio enyi waja wa Mwenyezi Mungu tumieni dawa, hakikaMwenyezi Mungu hajaleta ugonjwa ila una tiba ila ugonjwa mmoja.”Wakasema ni upi? Akasema: “Ukongwe.”18

Kama alivyobainisha matibabu na utumiaji wa dawa pia alibainisha kwam-ba kila maradhi yana tiba isipokuwa ni kwamba sisi hatuijui, hivyo akawa-jibisha kufanya utafiti na kuitafuta ili kuigundua, hilo limekuja katika kauliyake (s.a.w.w.): “Hakika Mwenyezi Mungu hajaleta ugonjwa ilaaliteremsha dawa yake, elimu yake ni toka katika Ujuzi Wake na hajaijuaasiyeijua.”

15 Sahih Bukhar Juz. 7, Uk. 12.16 Sahih Muslim, Mlango wa tiba.17 Jamius-Saadat, chapa ya tatu, Juz. 3, Uk. 228.18 Musnad Ahmad bin Hanbal, Mlango wa tiba.

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 17

Page 24: Huduma ya Afya katika Uislamu

18

Huduma ya Afya katika Uislamu

Bali sheria ya Uislamu imezingatia kuficha maradhi na kutoyaeleza kwatabibu ili ayatibu kwa ufanisi ni kuufanyia khiyana mwili, hivyo imepoke-wa Hadithi toka kwa Imam as-Sadiq (a.s.) kwamba: “Atakayemfichatabibu maradhi yake ameufanyia khiyana mwili wake.”

Na ili kufafanua uhusiano uliyopo baina ya sababu za kimatibabu na bainaya uwezo wa Kimungu tusome aliyoyapokea Abu Khuzama, Hadithi yaMtume ambayo alizingatia matibabu kuwa ni sehemu ya uwezo waMwenyezi Mungu. Alisema: Nikamwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu:Unaona hirizi tunazotumia, dawa tunazotumia na kinga tunazoweka, jezinapingana na chochote katika uwezo wa Mwenyezi Mungu? Akasema:“Hayo ni sehemu ya uwezo wa Mwenyezi Mungu.”19

Hivyo ndivyo sheria ya tiba katika Uislamu inavyothibitisha wajibu wakulinda mwili na kuupatia matibabu na usalama wa kiafya. Mafunzo hayaya kisheria na fikra hii ya kielimu vimeleta mfumo wa kielimu wa utafitiwa kitiba, na hivyo tiba ikaendelea sana mikononi mwa ulamaa wa kiisla-mu, na ikapanda hadi mustawa wa utafiti wa kielimu na mfumo wakimaabara, zikagunduliwa nadharia za kitiba katika magonjwa, matibabu,mpangilio wa mwili na umbo lake.

Nane: Utatuzi wa matatizo ya kisaikolojia:

Uislamu umeweka mfumo wa afya ya kinafsi, kwani uhai wa mwanadamukatika sekta zake zote za kisiasa, uchumi, usalama, akida, afya ya mwili naya kisaikolojia, mahusianio ya kijamii na kifamilia, zote zimekamilika nazinaathiriana zenyewe kwa zenyewe na kuathirika. Afya ya kisaikolojiaambayo ndio msingi wa wema wa mwanadamu na uovu wake huathiri haliya mazingira yote ya mwanadamu. Ufakiri, ukosefu wa kazi, ugaidi wakisiasa, ukosefu wa amani na matatizo ya familia, yote hayo ni sababuzinazoathiri afya ya saikolojia upande wa hasi na chanya.

19 Sahih Ibnu Majah, Mlango wa tiba.

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 18

Page 25: Huduma ya Afya katika Uislamu

19

Huduma ya Afya katika Uislamu

Mfumo wa Uislamu ni mfumo wa kielimu uliokamilika ulioweka ufanisikatika sekta zake mbalimbali na katika utatuzi wake mbalimbali, na kwanamna ambayo unamhakikishia mwanadamu afya na utulivu wa nafsi.Zaidi ya hapo ni ule mfumo wake wa kimalezi katika sekta ya kuhifadhiusalama wa hali ya kisaikolojia dhidi ya mifundo na maradhi ya nafsi.Uislamu katika sehemu kubwa ya fikra zake na sheria yake umetiliaumuhimu suala la kuihami hali ya kisaikolojia dhidi ya khofu, huzuni,hikdi, umimi, husuda na wivu kwa mwanamke. Kwa ajili hiyo umeichoreanafsi ya mwanadamu msitari wa kupita na mfumo wa kufuata ambao utai-hami nafsi na maradhi ambayo huipata na kuiangamiza yenyewe na mwiliwake.

Tisa: Kutokomeza ufakiri:

Ufakiri ni sababu hatari miongoni mwa sababu za maradhi na ukosefu waafya bora ya kinafsi na kimwili. Pamoja na maendeleo ya kielimu na yakiviwanda bado ufakiri umekuwa ni tatizo kubwa kwa mwanadamu, hiyoni kwa sababu maendeleo ya kielimu na kiviwanda hayajachangia cho-chote katika kuutengeneza ubinadamu na tabia za mwanadamu, hivyo kilahali ya kiuchumi inavyokua kwa mwanadamu mjeuri ndivyo hali yake yakinafsi inavyoporomoka na kumong’onyoka kimaadili, na hapo huzidishadhulma, ulafi, kupenda mali na kuhodhi vyanzo vya mwanadamu dhaifu,jambo ambalo huwazidishia mafakiri tatizo na kupanuka uwanja waufakiri.

Na huenda maradhi mabaya mno kati ya maradhi ya ufakiri ni uduni wachakula na ukosefu wa chakula kinachowiana na afya ya mwanadamu.Mwili mahitaji yake ni protini, vitamini, wanga, sukari na mafuta, hivyomwili unapokosa mahitaji ya kivyakula hupatwa na magonjwa mbalimbalina udhaifu wa kupambana na maradhi na hatimaye ni kuporomoka kwaafya na nguvu. Litakapotatuliwa tatizo la ufakiri tutaweza kuyatokomezamaradhi haya ya kifakiri. Kama ambavyo ufakiri moja kwa moja huletamaradhi yasababishwayo na chakula kutokana na uduni wa chakula pia

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 19

Page 26: Huduma ya Afya katika Uislamu

20

Huduma ya Afya katika Uislamu

husababisha kudhoofika kwa taasisi na sera za kinga, upatikanaji wamaisha ya afya njema na kukosekana kabisa.

Uislamu ulipoweka mfumo wake wa uchumi ulizingatia hali ya kum-timizia mwanadamu mahitaji yake ya chakula, makazi, mavazi na dawa, nakumwokoa mwanadamu na ufakiri. Na la kuzingatia katika mfumo wauchumi wa Uislamu ni kwamba faradhi ya Zaka imejikita katika bidhaa zavyakula, kama vile ngano, tende, shairi, zabibu na wanyama, ukiongezeapesa, jambo ambalo huhakikisha uwepo wa usalama wa kichakula nahusaidia kutokomeza maradhi yatokanayo na chakula duni.

Kumi: Mapumziko na kulala:

Mwili ni ala hai iliyojaa harakati, utendaji na uchangamfu, hivyo hupatwana uchovu na mchoko, na kama hautapata mapumziko na maandalizi yanishati ya harakati mpya hupatwa na maangamizi, mmong’onyoko namaradhi. Mwenyezi Mungu amekadiria mpangilio wa usingizi kuwamapumziko ya fikra, nafsi na mwili, na ili kupangilia uhai wamwanadamu. Kama ambavyo pia ameweka kwa namna ya uwiano ilekanuni ya kielimu ya kazi, kutoa juhudi na kupumzika, Mwenyezi Munguamesema: “Na tukaufanya usingizi wenu ni mapumziko. Na tukau-fanya usiku vazi. Na tukaufanya mchana kufufuka.” (Sura Nabai: 9 –11). Kwa Aya hizi amegawa wakati baina ya mapumziko, kazi, harakati nauchangamfu.

Na katika maelekezo ya Mtume (s.a.w.w.) kuna msisitizo wa kupunguzakuuchosha mwili, thamani ya mapumziko na kujiwekea udhibiti dhidi yasababu za tamaa na ulafi ambazo humpelekea mwanadamu kuuchakazamwili wake, fikra zake na nafsi yake. Kuuchakaza mwili ni sababu mion-goni mwa sababu za kuyaharibu maisha ya mwanadamu na kudhoofikakwa nyama za mwili na zaidi ya hapo ni kuudhuru mwili. Kama ambavyousingizi na mapumziko ni njia bora kati ya njia za kutibu misuli ya mwilina kuupa mwili fursa ya kuirejesha nishati yake. Maelekezo hayo

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 20

Page 27: Huduma ya Afya katika Uislamu

21

Huduma ya Afya katika Uislamu

tunayakuta katika kauli ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Fanyeni wastanikatika kutafuta, kwani hakika Roho Mtakatifu aliniambia: Nafsi haitakufampaka iwe imechukua riziki yake yote.”

Kwa mpangilio huu na ugawaji huu wa wakati baina ya mapumziko, juhu-di na kazi, Uislamu umeweka mfumo makini wa kielimu ili kuuhifadhimwili, nafsi na fikra dhidi ya uchakavu na maradhi.

MARADHI YA KISAIKOLOJIA NAATHARI ZAKE KATIKA AFYA YA MWILI

Hakika miongoni mwa mambo yanayokubalika kimsingi ndani ya fikra zaUislamu ni kwamba kila kimoja kati ya roho, akili na nafsi kina umbolake, mpangilio wake na kazi yake makhususi, kwamba vitu hivi huathiri-ana vyenyewe kwa vyenyewe na kuathiriwa. Katika somo letu hili fupitutajaribu kutoa utambulisho mwepesi wa maradhi ya kisaikolojia na uhu-siano wake na maradhi ya kimwili, na pia za maradhi hayo na ugumu wautibikaji wake hata baada ya kuwa zimeanza nadharia za uchambuzi wakisaikolojia na majaribio ya kutaka kugundua chanzo cha maradhi na tati-zo la kisaikolojia. Pia tutabainisha hali za maradhi ambayo humsumbuamwenye maradhi ya kisaikolojia, na tutabainisha thamani ya kumwaminiMwenyezi Mungu na athari zake katika kuilinda nafsi ya mwabnadamu natatizo hilo na maradhi hayo, na uwezo wake (huko kumwamini MwenyeziMungu) katika kuyatatua na kuyatibu maradhi hayo. Nafsi ya mwanadamukama unavyoelekeza uchambuzi wa ulamaa wa kiislamu ni umbolisilokuwa na sifa za kimaada, ni ni chombo chenye kujitergemea, nachombo hiki ni kama mwili, wakati mwingine huwa katika afya njema nahupata pia maradhi na hutibika.

Hebu tumsikie mwanafalsafa wa maadili, Sheikh Muhammad Mahdi an-Naraqiy mmoja wa ulamaa wa maadili wa kiislamu, hapa anazungumzia

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 21

Page 28: Huduma ya Afya katika Uislamu

22

Huduma ya Afya katika Uislamu

nafsi, mwili na maadili, na yale yanayokisibu kila kimoja kati ya mwili nanafsi miongoni mwa maradhi na mvurugiko katika mpangilio wao.Amesema:

“Tambua kwamba mwanadamu ana ndani na nje, roho na mwili,na kila kimoja kati ya hivyo viwili kina mambo yasiyooana nachona yanayooana nacho, machungu na matamu, yenye kuangamizana yenye kuokoa. Yasiyooana na mwili na ambayo ndio machun-gu yake ni maradhi ya kimwili, na yanayoona nao ni afya njema naladha za mwili. Na elimu yenye dhamana ya kubainisha ufafanuziwake na matibabu yake ni elimu ya tiba. Ama yasiyoona na rohona ambayo ndio machungu yake ni maadili machafu ambayohumwangamiza mwanadamu na kumsababishia mashaka, amaafya yake njema ni kurejea kwenye maadili mema ambayo yatam-pa wema na kumwokoa na kumfikisha karibu na watu waMwenyezi Mungu na walio karibu Kwake, elimu yenye dhamanaya kubainisha maadili machafu na kuyatibu ni elimu ya tabianjema. Kisha ni kwamba mwili ambao ni mada ni wenye kutowe-ka, na roho ambayo haina mada ni yenye kubakia.”20

Akasema tena: “Hakuna shaka kwamba nafsi haina mada na ni yenyekubaki baada ya kuachana na mwili.”21

Akafafanua kwa kusema: “Kutokuwa na mada kwa nafsi ni kule kwa asilina si sasa, kwa sababu sasa inahitaji mwili na nyenzo, hivyo utambulishowake ni: Yenyewe ni chombo cha juu chenye kuutumikisha mwili katikahaja zake, na chenyewe ndio mwanadamu mwenyewe. Viungo na nguvu ninyenzo zake ambazo huzitegemea katika utendaji wake, na yenyewe inamajina mbalimbali kulingana na kigezo, huitwa roho kwa kuwa uhai wamwanadamu huitegemea yenyewe, na huitwa akili kwa sababu huyadirikimambo ya kiakili, na huitwa moyo kwa sababu ya kugeuka kwake katika

20 Jamius-Saadat Juz. 1, Uk. 5.21 Jamius-Saadat Juz. 1, Uk. 5.

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 22

Page 29: Huduma ya Afya katika Uislamu

23

Huduma ya Afya katika Uislamu

mawazo.”22

Hivyo ndivyo uchambuzi wa kifikra wa ulamaa wa kiislamu unavyocham-bua mambo yanayoambatana na nafsi ya mwanadamu, nayo ni:

Hakika nafsi ya mwanadamu ni umbo lisilo na sifa za kimada, kamaambavyo nguvu kwa wazo la elimu ya fizikia inatofautiana na mada.

Hakika nafsi ndio mwanadamu mwenyewe, na ndio huitwa “mimi”,mwanadamu asemapo: “mimi” hukusudia nafsi. Umbo hili lisilo na madaambalo huhisi utamu na uchungu, hudiriki na kufikiri, huchukia na kupen-da, hukhofu na kuhuzunika, hughadhibika na kuridhia, na hutaka nakukataa.

Hakika mwili ni nyenzo ya kutekelezea mahitaji ya nafsi, kile ambachonafsi inakitaka na kukipenda huenda kujitimizia kwa njia ya kubadili suraya kifikra kwenda kwenye msimamo wa kutaka na tabia ya kimatendo.Hivyo hakika nafsi huathiri mwili kama ambavyo mwili huathiri nafsi, nakutoka katika unyenzo huu hisia nyingi na taswira nyingi hubadilika nakuwa hali za kimaradhi, kama vile huzuni, khofu, kupenda na kuchukia, nahivyo huathiri taathira ya mabadiliko na hapo mwili hupokea mabadilikohayo mapokezi ya kifiziolojia, na baadhi ya wakati huacha athari zake zakimaradhi kwenye mwili.

Hakika nafsi hupatwa na maradhi kama mwili unavyopatwa na maradhi, namaradhi ya nafsi ni kule kukengeuka msitari wa unyoofu ambao wanafal-safa wa maadili huuita msitari wa kati na uwiano, na hapo mwanadamuhupatwa na huzuni, khofu, hikdi na kuhisi upungufu. Na maradhi hayahuleta mabadiliko kwa kubadilika na kuwa maradhi ya kimwili. Matokeoya uchunguzi wa kielimu yamethibitisha kwamba asilimia kubwa yamaradhi ya kimwili sababu yake ni mabadiliko ya kisaikolojia, kama vile

22 Jamius-Saadat Juz. 1, Uk. 28

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 23

Page 30: Huduma ya Afya katika Uislamu

24

Huduma ya Afya katika Uislamu

maradhi ya kisaga chakula, vidonda vya tumbo, usagaji mbaya wa chaku-la na uvimbe wa utumbo, kama pia maradhi ya mishipa, kutowiana kiwan-go cha sukari, maradhi ya maumivu ya kizazi na kuumwa kwa kichwa, namengineyo.

Maradhi mengi huanza kisaikolojia na baadaye hugeuka na kuwa maradhiya kimwili. Taarifa na uchambuzi wa kisaikolojia unasisitiza kwambamaradhi mengi ya kimwili sababu zake ni maradhi ya kisaikolojia, nakwamba uhusiano kati ya hayo mawili mara nyingi ni wa kubadilishanakati ya mwili na nafsi katika afya njema na maradhi.

Hebu sasa tusome yaliyopatikana katika ripoti ya afya inayozungumziauhusiano wa maradhi ya kimwili na maradhi ya kisaikolojia. Imekujahumo: “Matokeo ya uchunguzi katika nchi za Kimagharibi ambazo humo imee-nea elimu ya afya ya saikolojia na ambazo humo nyenzo za matibabu yakisaikolojia zimeendelea, yanathibitisha kuenea sana kwa maradhi yakisaikolojia na kiakili kwa watu. Mfano Marekani, matokeo yanaonyeshakwamba nusu milioni ya Wamarekani hupata matibabu katika hospitalikutokana na maradhi haya, kama ambavyo hospitali za Marekani hupokeakila mwaka wagonjwa wapya 150000 wa maradhi haya. Na baadhi yamatokeo yanaonyesha kwamba asilimia kumi ya Wamarekani wakokwenye hatari ya kupatwa na maradhi haya muda mchache tangu kuanzauhai wao.”23

“Ukweli ni kwamba matokeo waliyoyapata yanawafikiana kabisa na nad-haria ya tiba ya kisasa inayohusu umuhimu wa kionjo cha saikolojia kati-ka tiba ya kisasa. Matokeo ya kina yameonyesha kwamba asilimiathamanini ya wagonjwa wa maradhi mbalimbali katika miji yote yaMarekani maradhi yao sehemu kubwa hutokana na sababu za kisaikolojia.23 Sayajmunda Farid Uk. 13. Huu ni utangulizi wa Dr. Muhammad UthmanNajatiy, Mtaalamu wa masuala ya saikolojia.

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 24

Page 31: Huduma ya Afya katika Uislamu

25

Huduma ya Afya katika Uislamu

Hembu chunguza ni sababu zipi za msingi ambazo husababisha maradhi yamishipa? Hakika miongoni mwa sababu za msingi za maradhi haya nikuhisi dhambi, kosa, hikdi, khofu, mashaka, hasira, kubabaika, shaka,ghera na kuchoka. Na linalosikitisha ni kwamba wengi wanaojishughulishana matibabu ya saikolojia wanaweza kufaulu katika kutibu sababu zamihangaiko ya kisaikolojia ambayo husababisha maradhi, lakiniwanashindwa kutibu mihangaiko hii, kwa sababu wao katika matibabu yaohawakimbilii katika kupeleka imani ya kumwamini Mwenyezi Mungukatika nafsi za wagonjwa. Na juu ya hilo ni lazima tujiulize kuhusumihangaiko hii na mabadiliko haya na sababu ambazo husababisha marad-hi hayo, hiyo ndio mihangaiko yenyewe ambayo dini zimekuja kutukom-boa nayo…..”24

Uchambuzi wa kisaikolojia wa sasa unaafikiana na uchambuzi wa ulamaawa tabia njema wa kiislamu kuwa nafsi ya mwanadamu hupatwa namaradhi, na kwamba yenyewe hupatwa na hali ya afya njema na maradhikama inavyoupata mwili. Mmoja wa maprofesa waliobobea katika elimuya saikolojia anaandika ukweli huu kwa kusema:

“Hakika siha ya saikolojia na maradhi ya kisaikolojia ni pande mbili za haliza kisaikolojia ambazo inapasa elimu ya siha ya kisaikolojia inapasa kutil-ia mkazo katika kuzisoma, kwa kuujua upande mmoja tutaweza kuzamakwa kina katika kuujua upande mwingine na kuweza kujua kiwango chaukaribu wetu au umbali na pande zote mbili, nazo ni kama mikono miwiliya mizani moja, kwayo tunakuwa na uhakika wa maarifa yetu ya jinsimwenendo unavyokuwa, unavyotikisika au kuchambuka ..…”25

Anaendelea kusema: “Na kwa upande wa kimatendo tunaweza kuzingatiauhai kuwa ni mnyororo wa mivutano ambayo mtu hufaula pale anapoishin-da na hapo hujengeka siha ya kisaikolojia, au hushindwa na hapo huwa ni

24 Allahu Yatajala Fi Asril-Ilmi, Uk. 136, cha Dr. Paulo Artost Adolof.25 Ilmus-Sihatun-Nafsiyah, Uk. 35 – 36, cha Dr. Mustafa Khalil Sharqawiy.

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 25

Page 32: Huduma ya Afya katika Uislamu

26

Huduma ya Afya katika Uislamu

maradhi ya kisaikolojia. Na maana ya hilo ni kwamba siha ya kisaikolojiahaiwezekani kuifahamu ila kwa mwangaza wa maradhi ya kisaikolojia. Natunaweza kusema kwamba maradhi ya kisaikolojia uhalisia wake ni kulekushindwa kukusanya na kutimiza na kutekeleza sifa za mwenendo wasiha ya kisaikolojia, kama ambavyo kuyasoma maradhi ya kisaikolojia,kuyasimulia na kuchambua sababu zake kuna athari kubwa katika kuain-isha sifa ambazo kwa mujibu wake unaweza kuhukumu na uwepo wa sihaya kisaikolojia.”26

Kisha anakomea kwenye kauli: “Kuna sehemu mbili za msingi, nazo ni‘Sehemu ya siha ya kisaikolojia’ nayo inakusanya hali ya kutokuwa namaradhi ya kisaikolojia. Nayo ndio hali ya chini kabisa kati ya hali za sehe-mu hii, ambapo iliyo juu yake ni hali ya usalama wa kisaikolojia ambayohuwa katika kilele cha hali ya siha ya kisaikolojia. Na mkabala na sehemuhiyo ni ‘Sehemu ya maradhi ya kisaikolojia,’ nayo inakusanya hali ya mtik-isiko na mabadiliko, hali ambayo huzingatiwa kuwa ni ya chini kabisa katiya hali za maradhi ya kisaikolojia ni hali ya maradhi ya saikolojia ya mwili,kisha ni maradhi ya mishipa na mwisho ni ubongo, ambao huwakilisha halimbaya zaidi ya ulemavu wa kiakili.”27

Hivyo ndivyo zinavyopatikana mbele yetu hali mbili zenye kukabiliana,nazo ni sura ya siha ya kisaikolojia na sura ya maradhi ya kisaikolojia,zinapambana juu ya nafsi ya mwanadamu na wala hakuna wema kwamwanadamu ila kwa kujipatia siha ya kisaikolojia na nafsi kutokuwa namaradhi na mabadiliko ya kimaradhi.

Na kama ambavyo ulamaa wa kiislamu wameweka wazi, hakika yalewaliyoyaita tabia njema (hali za siha ya kisaikolojia) na kutokuwa na yalewaliyoyaita tabia mbaya (hali za maradhi ya kisaikolojia) yenyewe nimiongoni mwa kanuni za msingi za kujenga utu wa kiislamu, hivyo

26 Ilmus-Sihatun-Nafsiyah, Uk. 46, cha Dr. Mustafa Khalil Sharqawiy.27 Ilmus-Sihatun-Nafsiyah, Uk. 48, cha Dr. Mustafa Khalil Sharqawiy.

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 26

Page 33: Huduma ya Afya katika Uislamu

27

Huduma ya Afya katika Uislamu

tunamkuta Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) anatamka kwa sauti:“Hakika nimeletwa kuja kukamilisha tabia njema.”28

Na katika kauli nyingine anatuchambulia uchambuzi wa kielimu kwambatabia mbaya huakisi maradhi juu ya nafsi, anasema: “Ambaye tabia yake nimbaya ameiadhibu nafsi yake.”29 Kuiadhibu nafsi si kesho Akhera tu, balini hata katika adhabu ya mashaka na matatizo ya dhamiri miongoni mwamashaka, ghamu, huzuni, hali ya umimi, ghera na husuda ambazo hujikitandani ya kina cha nafsi na kumfikisha mwenye nayo kwenye moto wadaima.

Imam Ali (a.s.) ametoa sura nzuri ya hali ya kisaikolojia kwa mwanadamuhasidi, naye ni yule mwenye umimi ambaye hawatakii wengine kheri, nahuumia kuona wengine wanafanikiwa kushinda yeye, na hutamani ajitumeili kuwaepusha na mafanikio hayo na kuwakosesha kheri waliyonayo,hivyo huishi katika chuki, hasira na tamaa ya kuwaadhibu, ambaye maranyingi hubadilika na kwenda katika hali za kujiuwa na kujinyonga, aukuwateta wengine au kuwashushia heshima zao na kujitahidi kuwaan-gusha. Amirul-Muuminina amesema kweli alipoisawiri picha hii kwa kuse-ma: “Ole wako hasadi! Ni adilifu ilioje! Imemwanza mwenye nayo na hati-maye imemuuwa.”30

Matokeo ya uchunguzi na uchambuzi wa kisaikolojia yanaonyesha kwam-ba mashirika ya kijamii na mifumo ya kimalezi na nadharia za kunadhimumwenendo wa mwanadamu zimeshindwa kutibu maradhi ya kisaikolojiana kumwokoa mwanadamu dhidi yake. Bali ripoti na matokeo ya uchun-guzi vinathibitisha uwepo wa ongezeko la wapatwaji wa magonjwa yakisaikolojia, na ukosefu wa siha ya kisaikiolojia ni matokeo ya maisha yakimada yenye matatizo na yenye kumpa mashaka mwanadamu. Ugaidi wa

28 Kanzul-Ummal, Hadithi ya 5217.29 Biharul-An’war: 78 Uk. 246.30 Ghurarul-Hikam Wadurarul-Kalim.

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 27

Page 34: Huduma ya Afya katika Uislamu

28

Huduma ya Afya katika Uislamu

kisiasa ni kwa sababu ya tofauti za mawazo au siasa, au utawala wakidikiteta. Ukosefu wa amani wa mtu mmoja mmoja au wa jamii nzimakatika nchi nyingi za ulimwengu ndio msiba mkubwa wa mwanadamu.Khofu ya kutokea vita na magomvi, kutokuwa na utulivu juu ya hali yasasa na mustakbali, mashaka dhidi ya kudidimia kwa hali ya maisha, kuhisiukosefu wa maana halisi ya maisha na kukata tamaa dhidi ya uwezo wakipato cha kiuchumi, kukosekana maridhiano na uwelewano baina ya watuna jamii, kusambaratika kwa familia, kukosekana mapenzi, huruma naupendo, kutapakaa kwa hali ya kufukuzwa na upotevu, hisia za kudha-rauliwa na kutokuwepo mwenye kumjali mwanadamu aliyefukuzwa. Halihizi zote zimekuwa miongoni mwa matatizo ya sasa na sumu za maendeleoya kiuchumi ambayo yamemwingiza mwanadamu katika majuto na kus-ababisha kuenea kwa maradhi ya saikolojia ambayo yamemkoseshamwanadamu ladha ya maisha na raha yake.

Hatuna kimbilio mbele wala mwokozi ila Uislamu, ambao mfumo wakeumekusanya kinga ya nafsi na kumlinda na maradhi ya kisaikolojia kwakumwamini Mwenyezi Mungu na ulimwengu wa Akhera, ukafanya kazi yakuzitakasa nafsi na kuzisafisha dhidi ya hikdi na umimi, ukazihami nakhofu na mashaka, kwa kusalimisha mambo kwa Mwenyezi Mungu nakuridhia maamuzi Yake na makadara Yake pindi mwanadamu anapokum-bana na hali za kisaikolojia zisizo za kawaida, na ukaiwekea ngome nafsidhidi ya kupatwa na maradhi ya kisaikolojia kwa kutumia malezi na kwakuyatimiza mazingira ya kifamilia na kijamii na kisiasa na kikanuni,mazingira ambayo yatampa mwanadamu utulivu, upendo na heshima yautu wake na kuuthamini.

Na msingi wa kielimu ambao mfumo wa Uislamu unautegemea katika kui-hami nafsi dhidi ya maradhi ya kisaikolojia ni kule kuamini kwambaumbile la mwanadamu ni umbile safi lililo salama dhidi ya maradhi yakisaikolojia. Mwenyezi Mungu anasema:

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 28

Page 35: Huduma ya Afya katika Uislamu

29

Huduma ya Afya katika Uislamu

“Basi uelekeze uso wako kwa dini iliyo sawasawa ndio umbileMwenyezi Mungu alilowaumba watu. Hakuna mabadaliko katikamaumbile ya viumbe wa Mwenyezi Mungu, hiyo ndio dini iliyo hakilakini watu wengi hawajui.” (Sura Rum: 30).

Bila shaka siha ya kisaikolojia inaonekana kwa kuhifadhi umbile hili nakulihami na uchafu na uendaji kinyume kwa kulizowezesha malezi memaya maadili mema, na kuleta mazingira na hali ya kijamii ambayo itasaidiaumbile hili kusafika na kubakia salama katika ukuaji na ukamilifu uliombali na maadili machafu na mabaya, baada ya kuwa Uislamu ume-haramisha kumwogopa mwanadamu na kudharau utu wake, na umaweta-ka wazazi na wanafamilia na jamii kupendana na kusaidiana na kuheshimi-ana, na ukawajibisha kuleta amani ya kisiasa na kimaisha, na ukahimizakwamba nafsi yenye kifundo ikimbilie kwa Mwenyezi Mungu na imtakemsaada Yeye, kwa hayo mwanadamu atakuwa huru dhidi ya khofu, dharauna umimi.

Na kanuni nyingine miongoni mwa kanuni za kuilinda nafsi na maradhi yakisaikolojia ni kuamini Siku ya Mwisho na kutoweka kwa vitu vyote nakudumu kwa kheri na matendo mema, ili yawe msingi wa malipo naneema, na hivyo kuituliza nafsi na kuipa utulivu kwa kuisalimisha namashaka na khofu, adui wa mwanadamu na sababu ya huzuni yake naadhabu ya nafsi yake katika maisha.

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 29

Page 36: Huduma ya Afya katika Uislamu

30

Huduma ya Afya katika Uislamu

Mwenyezi Mungu anasema:

“Jueni ya kwamba maisha ya dunia ni mchezo na upuuzi na pambo nakujifakharisha baina yenu, na tamaa ya kuzidiana katika mali nawatoto. Kama mvua ambayo huwafurahisha wakulima mazao yake,kisha yanakauka ukayaona yenye rangi ya manjano, kisha yanakuwayenye kuvunjika vunjika, na katika Akhera ni adhabu kali na msama-ha wa Mwenyezi Mungu na radhi yake na maisha ya dunia siyo ila nistarehe idanganyayo tu. Uendeeni upesi msamaha wa Mola wenuMlezi na Pepo ambayo upana wake ni kama upana wa mbingu naardhi, iliyowekewa wale waliomwamini Mwenyezi Mungu na Mitumewake, hiyo ni fadhila ya Mwenyezi Mungu, humpa amtakaye naMwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kuu. Hautokei msiba katika

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 30

Page 37: Huduma ya Afya katika Uislamu

31

Huduma ya Afya katika Uislamu

ardhi wala katika nafsi zenu ila huwamo Kitabuni kabla hatujauum-ba, kwa hakika hilo ni rahisi kwa Mwenyezi Mungu. Ili msihuzunikejuu ya kitu kilichokupoteeni, wala msifurahi kwa alichokupeni. NaMwenyezi Mungu hampendi kila ajivunaye, ajifakharishaye.” (SuraHadiid: 20 – 23).

Aya hizi tukufu zilizobarikiwa zimechukua jukumu la kutoa ufafanuzi wamaana ya uhai na kifo ili kumwelimisha mwanadamu na kumjengea fikrasalama ya uhai na uhusiano wake salama, hivyo zikatoa taswira sahihi yauhai kwa namna iliyo karibu na ufahamu wa mwanadamu na uwelewawake, ili kung’oa vyanzo vya mashaka na huzuni ya nafsi iliyojikita kati-ka khofu dhidi ya kupitwa na vitu na kuvipoteza, na katika khofu yakedhidi ya vile anavyotarajia kutokea na vile ambavyo amedumbukia. PiaMwenyezi Mungu amefafanua ukweli wa uhai na akaushabihisha na uhaiwa shamba, na anawataka kwamba wasiitii khofu dhidi ya kipato chamaisha na wala kisimpe mashaka. Kila kitu kimekadiriwa na kinakwendakufuatana na makadara. Pia anamfafanulia mwanadamu kwamba kukim-bilia kwa Mwenyezi Mungu ndio ufunguo wa furaha na utulivu, ili aji-fungamanishe na Mwenyezi Mungu mbali na mashaka, hivyoanamwambia:

“Wale walioamini na zikatulia nyoyo zao kwa kumkumbukaMwenyezi Mungu, sikilizeni kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu,nyoyo hutulia.” (Sura Ra’d: 28).

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 31

Page 38: Huduma ya Afya katika Uislamu

32

Huduma ya Afya katika Uislamu

MARADHI NA KUKAMILIKA KWA NAFSI

Darasa na uchunguzi wa saikolojia ya maadili unasisitiza kwamba siha yakisaikolojia ndio chanzo cha furaha ya mwanadamu, utulivu wa jamii nakulinda nidhamu yake. Hivyo jamii ambayo watu wake wanastarehe kwasiha ya kisaikolojia na kwa mwenendo sahihi hujenga nidhamu ya kijamiiambayo itakuwa nadra kuwa na makosa, mmong’onyoko, matatizo namigogoro ya kisiasa, kiuchumi na amani, na itasalimika na tabia zakiuadui. Mwanadamu kwa malezi mema, utashi, mazingira ya tiba namazoezi ya kinafsi anaweza kuokoka na hali za kimaradhi, kama vileumimi, hikdi, kiburi, ujeuri, kujiona na ulafi. Na yenyewe kama ilivy-oelezwa na Qur’ani Tukufu ipo katika hatari ya kupatwa na maradhi yakiburi, dhulma na majivuno juu ya wengine. Ili sura hii iwe wazi kwakobasi tusome sehemu tu ya ufafanuzi wa Qur’ani na uchambuzi wake.Mwenyezi Mungu amesema:

“Hautokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu ila huwamoKitabuni kabla hatujaumba, kwa hakika hilo ni rahisi kwa MwenyeziMungu. Ili msihuzunike juu ya kitu kilichokupoteeni, wala msifurahikwa alichokupeni. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila ajivunaye, aji-fakharishaye.” (Sura Hadiid: 22 – 23).

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 32

Page 39: Huduma ya Afya katika Uislamu

“Ama wale walioamini na kufanya vitendo vizuri, basi atawapamalipo yao na atawazidishia katika fadhila yake. Ama wale walioonaunyonge na kufanya kiburi, basi atawaadhibu adhabu yenye kuumiza,wala hawatapata kiongozi wala msaidizi yeyote badala ya MwenyeziMungu.” (Sura Nisaa: 173).

“Kwa hakika wale wanaobishana katika Aya za Mwenyezi Mungupasipo dalili yoyote iliyowafikia. Hamna nyioyoni mwao ila kiburi,lakini hawataufikia, basi jikinge kwa Mwenyezi Mungu, kwa hakikayeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” (Sura Muumin / Ghafir:56).

“Kwa hakika tumevifanya vilivyoko juu ya ardhi view mapamboyake, ili tuwajaribu ni nani katika wao mwenye vitendo vizuri zaidi.”(Sura Kahfi: 7).

33

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:25 PM Page 33

Page 40: Huduma ya Afya katika Uislamu

“…Na haukuwa uhai wa ulimwengu ila ni raha ya udanganyifu.Hapana shaka mtapata misukosuko katika mali zenu na nafsi zenu.”(Sura Aali Imran: 185 – 186).

“Na Ayubu, alipomwita Mola wake Mlezi ya kwamba imenigusa dharanawe ndiye unayerehemu kushinda wote wanaorehemu. Basitukamkubalia na tukamwondolea dhara aliyokuwa nayo na tukampawatu wake na mfano wa pamoja nao ni rehema kutoka kwetu, naukumbusho kwa wafanya ibada.” (Sura Anbiyai: 83 – 84).

“Ambao anapotajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hutetemeka, nawanaovumilia juu ya yale yanayowapata na wanaoshika Sala na kati-ka vile tulivyowaruzuku wanatoa.” (Sura Hajji: 35).

“Ambaye ameniumba, naye ananiongoza. Naye ndiye anayenilisha nakuninywesha. Na ninapougua, basi yeye ananiponya” (Sura Shua’raa:

34

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 34

Page 41: Huduma ya Afya katika Uislamu

78 – 80).

Hivyo ndivyo Qur’ani inavyozungumzia mambo makubwa ya ulimwenguwa mwanadamu, tunaweza kutaja muhimu kati ya hayo:

Hakika nafsi ya mwanadamu ipo katika hatari ya kupatwa na maradhi yakisaikolojia, kama vile kiburi, majivuno, jeuri na kujidai, ambayo nimatokeo ya nguvu na kujiona amejitosheleza bila kumhitaji MwenyeziMungu wala watu, na ili kuficha hali ya kuhisi upungufu uliomo ndani yakina cha akili ya ndani. Watu wengi miongoni mwa majeuri na wenyemajivuno huhangaika na ugonjwa wa kuhisi upungufu, na kwa ajili hiyobila kujua hukimbilia kwenye njia za kiburi. Hakika maradhi hayo ambayohujiakisi kwenye maadili ya jamii hudhihirika kwenye muamala na mahu-siano ya kibinadamu katika sura tofauti za kijamii na kisiasa. Na hakikamaradhi haya ya kisaikolojia na kimaadili ndio msiba mkubwa wamwanadamu na ndio chanzo cha taabu zake na adhabu yake duniani naAkhera, hivyo Qur’ani imelibainisha hilo kwa kusema:

“Wala usitembee katika ardhi kwa maringo, hakika wewe huwezikuipasua ardhi, wala huwezi kufikia urefu wa milima.” (Sura Israil:37).

“..Ama wale walioona unyonge na kufanya kiburi..” (Sura Nisaa: 173).

“..Hamna nyoyoni mwao ila kiburi.” (Sura Ghafir / Muumin: 56).

35

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 35

Page 42: Huduma ya Afya katika Uislamu

“Basi Adi walitakabari katika ardhi bila ya haki na wakasema: Ninani aliye na nguvu zaidi kushinda sisi?” (Sura Fusilat/ Haa Miim:15).

Hivyo ndivyo mfundo ulivyo chanzo cha ukafiri, dhuluma na uharibifu wakijamii, kisiasa na kiuchumi, kama ambavyo ndio chanzo cha utovumwingine wa maadili ya mtu.

Hakika kupatwa na maradhi aina mbalimbali ikiwemo maradhi ya kimwilini moja ya njia za kimalezi na kimafunzo ambazo humhisisha mwanadamuudhaifu wake na haja yake ya kumtegemea Muumba wake, kama ambavyohuchukua nafasi ya adhabu kwa wakosaji, wajeuri na waovu. Kishayenyewe ni somo na nasaha kwa wengine ambao hushuhudia muovu najeuri na mwenye majivuno kauwawa kwa maradhi, yamemdhalilisha nakumkosesha afya na fursa ya kustarehe na maisha. Ulamaa wa theolojia nawanamaadili wa kiislamu wamezungumzia sana maradhi haya na atharizake katika kuikamilisha nafsi na kuifunza, hivyo wamegawa somo hilosehemu mbili:

Sehemu moja ni adhabu, kisasi, kuwaadabisha na kuwazuia wakosaji.

Na sehemu nyingine ni mafunzo na kafara ya madhambi na kukuza hali yaukamilifu kwa mwanadamu. Maradhi humfanya mwanadamu ahisi udhai-fu mbele ya Muumba wake, ahisi uhitaji wake wa rehema zake, msamahawake na hisani yake, na pia humhisisha upole na huruma kwa wengine, nahumzuia na ujeuri, kiburi na kuwadhulumu wengine, hali ambazo huzal-ishwa na hali ya kujiona ana nguvu na ubora juu yao.

Qur’ani tukufu imemtaka mwanadamu ambaye hajapatwa na masaibu namisukosuko ikiwemo maradhi, avute subira na kushukuru msiba nakupambana nayo kwa ushujaa na utashi imara na bila kukata tamaa yakupona, kwani hakika ponyo imo mikononi mwa Mwenyezi Mungu, dawana matibabu si chochote ila ni njia tu ya kupatia taufiki na utashi wa

36

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 36

Page 43: Huduma ya Afya katika Uislamu

Mwenyezi Mungu.

Hakika Mwenyezi Mungu huwapa wenye subira kitu mbadala badala yamatatizo na maradhi ya miili yao. Qur’ani imeonyesha mifano mingi tu yamajaribu ya maradhi ya kimwili, subira na kustahiki rehema na kitumbadala. Imeonyesha maradhi yaliyomsibu Nabii Ayubu (a.s.), naimezungumzia kisa cha maradhi yake na urefu wa muda wa maradhi yake.Kutokana na uzoefu huu toka kwa Nabii mwanadamu hujifunza kuvutasubira juu ya maradhi, na kuelekea kwa Mwenyezi Mungu kwa duaambayo humpeleka upande wa ukamilifu kwa nguvu ya nafsi, na husisiti-za maana ya unyenyekevu, huja na mwelekeo kwa Muumba wa ulimwen-gu na mgawaji wa kheri na neema.

Qur’ani imefichua ukweli uliokuwa mbali na watu wengi ambao huamil-iana na matukio kwa muamala usio wa kina, hivyo hulitizama kila jamboambalo linawaumiza na kuudhi nafsi zao au kwenda kinyume na utashiwao kuwa ni shari ambayo ni lazima kujiokoa nayo. Qur’ani inasahihishamakosa haya, na inasisitiza kwamba mengi kati ya mambo ambayomwanadamu hudhani kuwa ni shari kwake kwa kweli ni kheri tupu kwake,na inaikataa fikira hii ambayo ni sawa na fikira ya mtoto mdogoanayeikana dawa kwa sababu ya uchungu wake. Kwa kupitia kanuni hiikuu ya kimafunzo na kimawazo Qur’ani inabainisha wazi hekima yamaradhi na falsafa yake katika maisha, inamfahamisha mwanadamukwamba upatikanaji na uwepo wa maradhi ni dharura ya kimaumbile na nidharura ya maisha ya mwanadamu.

Qur’ani imebainisha ukweli huu kwa kusema: “Mmelazimishwa kupi-gana vita ingawa mwaichukia, huenda mkachukia kitu nacho ni kherikwenu, na huenda mkapenda kitu nacho ni shari yenu. Na MwenyeziMungu anajua, na nyinyi hamjui.” (Surat al-Baqarah: 216).

37

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 37

Page 44: Huduma ya Afya katika Uislamu

Kama alivyobainisha falsafa ya adhabu za mahakama ya kiislamu kwakusema: “Na mnao uzima katika kisasi, enyi wenye akili ili msal-imike.” (Surat al-Baqarah: 179).

Ijapokuwa kupigana vita na adhabu za kimahakama ni vitu vyenye mau-mivu na kuchukiwa na nafsi lakini bado ni moja ya njia za upatikanaji wausalama na amani katika jamii ya mwanadamu. Hivyo hivyo viwili nimiongoni mwa vyanzo muhimu kabisa vya furaha na utulivu. Na kwamsingi wa kanuni hii inapatikana hikima ya maradhi ya kimwili ambayohuwa kizuizi cha maradhi ya kisaikolojia na nyenzo ya kuelimisha nakuadabisha. Hivyo tunakuta uwazi wa hikima ya maradhi unaonekana kati-ka hadithi na maelezo ya Mtume (s.a.w.w.), huku mwingine ukija toka kwaMaimamu wa nyumba ya Mtume (a.s.) ambao unazungumzia maradhikama moja ya nyenzo za majaribu na mitihani, na mwingine ukizungumziamaradhi kama moja ya njia ya ukamilifu na kusafisha moyo wamwanadamu dhidi ya maradhi ya kisaikolojia.

Katika kundi la kwanza tunasoma kauli ya Mtume (s.a.w.w.): “MwenyeziMungu Mtukufu alisema: Hakuna mja nitakaye kumuingiza peponi ila nilazima nitamjaribu kwa maradhi mwilini kwake, hiyo huwa ni kafara yadhambi zake, na la sivyo humbana katika riziki yake, hiyo nayo huwa nikafara ya dhambi zake, la sivyo humkazia kifo mpaka anijie na hali hanadhambi, kisha humwingiza peponi.”31

Imam as-Sadiq (a.s.) akasema: “Muumini hapitiwi na siku arubaini bilaMwenyezi Mungu kumjaribu, ima kwa maradhi katika mwili wake na imakwa msiba ambao Mwenyezi Mungu atamlipa kwawo.”32

38

Huduma ya Afya katika Uislamu

31 Mishkatul-An’war Uk. 291.32 Mishkatul-An’war Uk. 292.

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 38

Page 45: Huduma ya Afya katika Uislamu

Na akasema tena: “Bila shaka mja hupata cheo mbele ya MwenyeziMungu, lakini hakipati ila kwa moja ya sifa mbili: Ima kwa kuondokewana mali yake au kwa maradhi katika mwili wake.”33

Imam Ali Ibni Husain Sajjad (a.s.) anazungumzia maradhi kwa kusema:“Mimi nachukia mtu kupewa afya njema duniani bila kupatwa na kitu katiya misiba yake.”34

Mtume (s.a.w.w.) anafafanua kiwango cha mafunzo na athari za kimareke-bisho za maradhi ya kimwili na pale mwanadamu anaposibiwa na majaribuya maradhi. Anafafanua athari za maradhi kwa mujibu wa maadili na tibaya hali za kisaikolojia za mgonjwa, na jinsi harakati za kisaikolojiazinavyokua kupita na kushinda athari nyingine za kimarekebisho ambazohuachwa na matendo mengine mema pindi utakapoamua kuzilinganisha najinsi maradhi yanavyoacha athari za kina na mabadiliko ya kina ndani yanafsi. Hayo yote anayafafanua Mtume kwa hikima yake pale anapoongeana masahaba zake kwa kusema: “Anayependa kwamba awe na afya njemabasi asiugue.” Tukabutwaa na kusema: Ewe Nabii wa Mwenyezi Mungutueleze hilo litawezekanaje? Akasema: “Hivi mnapenda muwe kama pundaaliyepotea?” wakasema hapana ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.Akasema: “Hivi hampendi kuwa watu wa majaribu na kafara. Naapa kwayule Ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake, hakika Mwenyezi Munguhamjaribu muumini kwa majaribu yoyote aliyompa ila ni kwa ajili yakumkirimu, hakika Mwenyezi Mungu anakuwa amemweka nafasi ambayoamali yake yoyote isingeweza kumfikisha hapo bila ya kufikwa namajaribu ambayo yameweza kumfikisha nafasi hiyo.”35

Na tunasoma ufafanuzi wa kina wa Imam Muhammad al-Baqir (a.s.) wahikima za maradhi na athari zake ambazo hufanya kazi ya kuiimarishanafsi na kusahihisha mwenendo wake wa kimaadili, na kutibu hali yake ya

39

Huduma ya Afya katika Uislamu

33 Mishkatul-An’war Uk. 298.34 Mishkatul-An’war Uk. 295.35 Mishkatul-An’war Uk. 301.

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 39

Page 46: Huduma ya Afya katika Uislamu

kimaradhi, yeye anafafanua kwamba maradhi ya kimwili hutibu maradhiya kisaikolojia. Ufafanuzi huo umeletwa ndani ya maandiko yafuatayo:“Mwili usipougua huwa shari mbaya mno, na wala mwili wenye sharihauna kheri.”36

Hivyo ndivyo maandiko ya Qur’ani na Sunna yanavyotoa utatuzi wa kima-tendo wa kadhia hatari sana inayomkabili mwanadamu katika maisha yake,nayo ni kadhia ya maradhi ya kimwili na kisaikolojia, na ili kujua kwaundani kuhusu suala zito katika kadhia hii, ni kwamba nyingi kati ya haliza maradhi ya kimwili ndio tiba ya maradhi ya kisaikolojia. Na kwambamaradhi ya muumini ambayo humpata toka kwa Yeye Mwenyezi, huwa sikwa uzembe wake, bali hata maradhi ambayo humfika mwanadamu kwasababu ya uzembe wake bado humpa uzoefu wa kinga ya maradhi, nahumhisisha neema ya siha njema aliyoweza kumneemesha, hivyo maradhikama maandiko yasemavyo ni malezi kwa mwanadamu mwislamumuumini, na ni kukuza harakati za ukamilifu wa nafsi yake kutokana nasubira dhidi ya maumivu, kuimarisha utashi, kuridhia makadara yaMwenyezi Mungu na majaliwa yake, kupambana na chembechembe hai zakiburi, ujeuri na majivuno. Baada ya hapo hayo huwa ni kafara ya mad-hambi, kwani maradhi yanayomfika muumini kwa makadara ya MwenyeziMungu huwa ni maumivu, na maumivu haya yana fidia yake toka kwaMwenyezi Mungu.

Fidia hii ni maghfira, na msamaha mzuri. Hii haimaanishi kwambamwanadamu ajitafutie maradhi na asipambane nayo, bali ni kwambaUislamu umemwajibisha mwanadamu kujilinda dhidi ya kila aina ya mad-hara na ukaharamisha kujidhuru, kama ambavyo pia umewajibisha kujitibuna maradhi ambayo hayaondoki ila kwa tiba. Hivyo sheria ya Uislamuimezingatia kwamba gharama za matibabu ya mke ni sehemu ya matumiziyaliyo wajibu juu ya mume. Bali pia umetueleza kwamba kuficha maradhina kutokwenda kwa tabibu ili ayafanyie uchunguzi na kuyatibu ni kuu-

40

Huduma ya Afya katika Uislamu

36 Mishkatul-An’war Uk. 280.

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 40

Page 47: Huduma ya Afya katika Uislamu

fanyia khiyana mwili. Imam Ali (a.s.) amesema: “Mwenye kuwafichamatabibu maradhi yake bila shaka ameufanyia khiyana mwili wake.”

Maelekezo ya Uislamu yanaamiliana na hali za kisaikolojia za mgonjwakwa kumpa utatuzi wa kielimu wenye manufaa, kati ya huo ni kwambabaadhi ya wagonjwa huhisi makosa na uzembe mbele ya nafsi zao, muum-ba wao na jamii yao, isipokuwa ni kwamba baada tu ya maradhi kuondo-ka na afya kuboreka haraka sana husahau mawaidha haya na kusahau fad-hila za Mwenyezi Mungu juu yao, hivyo maelekezo hayo yanaamiliananao kwa kuwapa mwamko, ukumbusho na kusahihisha mienendo yao natabia zao ili kuweza kuwavua toka kwenye tatizo hili la kimaadili.Maelekezo hayo unayapata katika kauli ya Sayidina Ali (a.s.): “Usiweanayetarajia Akhera bila matendo, akiugua hushinda katika majuto, naakipata afya njema hujiaminisha kwa kusahau. Anajivuna anapopewa afyanjema na anakata tamaa anapojaribiwa kwa maradhi.”

MAUMIVU NA FIDIA

Hakika miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu na ukarimu Wakemkubwa ni mwanadamu kuhisi maumivu na raha na kupatikana raha namaumivu, hali ambayo ni msukumo wa asili wa mwenendo wamwanadamu. Mwanadamu kwa asili yake hupokea lile linalompa raha nahuliepuka lile linalomletea maumivu, hivyo yeye huchukia maumivu nahupenda raha.

Allama al-Hilli alitambulisha maumivu na raha kuwa ni: “Maumivu nikudiriki usiyoyataka, na raha ni kudiriki unayoyataka.”37

41

Huduma ya Afya katika Uislamu

37 Kashful-Murad Fisharhi Tajridul-Iitiqad Uk. 295 – 296.

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 41

Page 48: Huduma ya Afya katika Uislamu

Akasema tena: Jua kwamba raha na maumivu hufuata hali ya kiafya, rahani kustawi kwa hali ya kiafya, na maumivu ni kudorora kwa hali ya kiafya,na maana hizi mbili zinasihi kwenye miili.”38

Wataalamu wa elimu ya saikolojia wakatambulisha maumivu kwamba ni:Kuhisi hatari, hivyo maumivu ni kengele ya kumzindua na kumhisishamwanadamu uwepo wa hatari inayomtishia usalama, na hali hii ndio aliy-oieleza Allama al-Hilli kwa kusema: ni kudiriki usiyoyataka. Na maumivujinsi yalivyo hugawanywa sehemu mbili, nazo ni: Maumivu ya kimwili namaumivu ya kisaikolojia.

Kila kimoja kati ya vigawanyo hivyo kina sifa zake makhususi, athari namatokeo yake. Kama ambavyo maumivu ya kisaikolojia yanaathiri uten-daji wa mwili, harakati zake na uwezo wake, ni hivyo hivyo kwamba mau-mivu ya kimwili huiathiri nafsi na aghlabu kuiachia sura yenye kuumiza.Maumivu ya kisaikolojia hubadilika na kuwa maumivu ya kimwili, namaumivu ya kimwili hubadilika na kuwa maumivu ya kisaikolojia. Basikutokana na kuamini na kukubali kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenyehikima, hafanyi kitu ila kwa hikima na chenye masilahi kwa waja wakeduniani na akhera, ijapokuwa hikima hiyo hawataiona, na kwamba viten-do vyake vina shabaha na lengo maalumu, basi kutokana na hayo yotetunaamini kwamba maradhi yanayomsibu mwanadamu toka kwaMwenyezi Mungu yana lengo, shabaha na hikima inayorudi kwamwanadamu mwenyewe. Hikima hii na shabaha hii inapatikana katika:

Mwenyezi Mungu anaweza kumpa maradhi mwanadamu kutokana nahuruma Yake juu yake ili kumwondolea madhara yaliyo makubwa kushin-da maradhi hayo, na kwamba bila maradhi hayo basi mwanadamu huyoangedumbukia ndani ya hatari kubwa zaidi na madhara makubwa zaidi.Mwenyezi Mungu anaweza kumpa maradhi mwanadamu kutokana nahuruma Yake juu yake ili kumtimizia manufaa na masilahi yanayomrudia

42

Huduma ya Afya katika Uislamu

38 Kashful-Murad Fisharhi Tajridul-Iitiqad Uk. 295..

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 42

Page 49: Huduma ya Afya katika Uislamu

yeye mwenyewe au kumrudia mtu mwingine.

Mwenyezi Mungu anaweza kumpa maradhi mwanadamu kwa ajili yakumwadhibu kutokana na kustahili kufanyiwa hivyo. Na kutokana nauadilifu wa Mwenyezi Mungu kwa uadilifu wake humpa mwanadamuhuyu fidia ya yale maumivu ya kimwili au kisaikolojia yaliyompata katikahali mbili za mwanzo. Ama maumivu yanayomsibu mwanadamu katikahali ya tatu yenyewe huwa ni adhabu na wala hayana fidia, hivyo ulamaawa theolojia ya kiislamu wamezungumzia maumivu kama walivy-ozungumzia maradhi na mengineyo yanayomfika mwanadamu kutoka kwaMwenyezi Mungu, na fidia anayostahiki aliyefikwa na hayo.

“Katika fidia, Shia Imamia wanaona kwamba maumivu anayoyawekaMwenyezi Mungu kwa mwanadamu huwa ni ima ni kwa ajili ya kisasi nakumwadhibu, naye hustahiki hilo. Mwenyezi Mungu anasema: “Na kwahakika mmekwishawajua wale walioasi miongoni mwenu katika saba-to, basi tukawaambia: Kuweni manyani madhalili.” (Surat al-Baqarah: 65).

Na akasema: “Je hawaoni kwamba wanajaribiwa kila mwaka maramoja au mara mbili? Kisha hawatubu wala hawakumbuki.” (SuraTawba: 126). Maumivu haya hayana fidia.

Na ima huwa kwa namna ya hisani, na bila shaka hufanywa hisani hiyo naMwenyezi Mungu kwa sharti mbili: Kwanza ni lazima iwe ina masilahifulani kwake mwenyewe yule mwenye kupatwa na maumivu au kwamwingine, na hiyo ni aina ya huruma yake, kwani bila masilahi hayo kiten-do hicho kingekuwa ni mchezo, na Mwenyezi Mungu ametakasika na kilaaina ya mchezo. Pili mkabala na maumivu hayo kuwepo fidia yenyethamani kushinda maumivu, ambayo ataipata yule aliyefikwa na maumivu,kiasi kwamba la aliyepatwa na maumivu ataonywesha maumivu na fidia naakaombwa achague basi atachagua fidia, la sivyo itakuwa ni dhuluma na

43

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 43

Page 50: Huduma ya Afya katika Uislamu

uonevu toka kwa Mwenyezi Mungu juu ya mja wake, kwani kumuumizamwanadamu na kumwadhibu bila dhambi yoyote wala faida ni dhuluma nauonevu, na jambo hilo ni muhali kwa Mwenyezi Mungu.”39

Allama al-Hilli amesema: “Hizi ni aina ambazo kwazo Mwenyezi Munguhustahiki kutoa fidia:

Kwanza: Anaposhusha maumivu kwa mja, kama vile maradhi namengineyo. Tayari tumeshabainisha kwamba fidia ni lazima kwa sababubila fidia hiyo itakuwa ni dhuluma.

Tatu: Kumshushia huzuni, kwa Mwenyezi Mungu kumwekea sababu zahuzuni, kwani huzuni katika akili ni sawa na madhara mengine, hiyo ni bilakujali kwamba huzuni hiyo ni alama ya dharura ya kuteremka msiba aukufikwa na maumivu, au ni dhana inayoonyesha alama za kufikwa na mad-hara au kupitwa na manufaa. Hivyo kwa sababu huzuni hiyo imetokakwake Mwenyezi Mungu basi na fidia huwa ni juu yake. Ama huzuni inay-opatikana kwa mwanadamu mwenyewe bila kutoka kwa MwenyeziMungu, kwa mfano yeye mwenyewe afanye utafiti na kwa kutokana naujinga wake aone kwamba kafikwa na madhara au kapitwa na manufaa,basi fidia si juu ya Mwenyezi Mungu.”40

Hivyo ndivyo somo la theolojia ya kiislamu linavyotuletea uhusianouliopo baina ya uadilifu wa Mwenyezi Mungu na hikma yake na baina yayale yanayomsibu mwanadamu katika maradhi ya mwili au huzuni yanafsi. Na linatufafanulia kwamba maumivu yatokayo kwa MwenyeziMungu kwa hisani yake ni kitu kizuri, kwa sababu yanamnufaishamwanadamu kwa kuwa huwa yana masilaha ya kidunia na fidia yakiakhera. Ama yale yanayomsibu mwanadamu kwa uzembe wake au dhanazake za kimaradhi na hatimaye kujawa na huzuni na mfundo, hayo hayanafidia.

44

Huduma ya Afya katika Uislamu

39 Dalailus-Didqi cha Shaikh Muhammad Hasan Mudhaffar, Juz. 1 Uk. 361.

40 Kashful-Murad Fisharhi Tajridul-Iitiqad Uk. 360.

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 44

Page 51: Huduma ya Afya katika Uislamu

Zimepatikana riwaya nyingi zikizungumzia athari za huzuni na mifundo namashaka katika kuitakasa nafsi na kuitengeneza na kuisafisha dhidi ya kilaaina ya uchafu. Zaidi ya hapo ni kule kustahiki malipo na fidia juu ya huzu-ni hizo.

Mtume anasema: “Madhambi ya mja yanapokithiri na akawa hana amaliyakuweza kumfutia madhambi hayo, basi Mwenyezi Mungu humjaribukwa huzuni ili iweze kumfutia.”41

Pia amesema: “Mwislamu hapatwi na mchoko wala mnyong’onyeo,mashaka wala huzuni, udhia wala mfundo, hata mwiba unaomchoma ila nilazima Mwenyezi Mungu amfutie makosa yake kwa mwiba huo.”42

Abdullah (r.a.) amesema: “Nilimtembelea Mtume wakati wa maradhi yakenaye akiwa ana homa kali. Nikasema: Hakika wewe una homa kali sana,hiyo ni kwa sababu wewe una malipo mawili. Akasema: “Ndio, hakunamwislamu atakayepatwa na udhia ila ni lazima Mwenyezi Mungu atamfu-tia makosa yake kama yanavyopukutika majani ya mti.”43

Hivyo ndivyo Mtume (s.a.w.w.) anavyobainisha kwamba maradhi yamuumini huwa ni kafara ya madhambi yake, kama ambavyo maumivu yakisaikolojia kama vile mashaka, mfundo na huzuni nayo huwa ni kafara yadhambi, hivyo ni juu ya mwislamu awe na subira juu ya yale maradhi namatatizo yanayompata katika mwili wake na nafsi yake. Hivyo Qur’aniimezungumzia malipo ya wale wenye kuvuta subira dhidi ya maradhi namatatizo, ikatoa hali ya Nabii Ayubu kama mfano halisi wa aina hiyo yasubira. Mwenyezi Mungu akasema: “Na Ayubu, alipomwita Mola wakeMlezi ya kwamba imenigusa dhara nawe ndiye unayerehemu kushin-da wote wanaorehemu.” (Sura Anbiyai: 83). Kama ambavyo

45

Huduma ya Afya katika Uislamu

41 Mishkatul-An’war Uk. 281.42 Sahih Bukhari Juz. 7, Uk. 2.43 Sahih Bukhari Juz. 7, Uk. 3.

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 45

Page 52: Huduma ya Afya katika Uislamu

imezungumzia nafasi ya subira katika kuimarisha utashi na azma katikakupambana na matatizo na hatari. Mwenyezi Mungui akasema:

“Na subiri juu ya yale yanayokupata, hakika hayo ni katika mamboyanayoazimiwa.” (Sura Luqman: 16).

“Enyi mlioamini! Ombeni msaada kwa subira na Sala, bila shakaMwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri.” (Surat al-Baqarah:153).

“Na uwakumbushe siku za Mwenyezi Mungu. Hakika katika hayomna mazingatio kwa kila mwenye kusubiri akashukuru.” (SuratIbrahim: 5).

MARADHI NA TAKLIFU ZA KISHERIA

Sheria ya Uislamu imeainisha taklifu za kiibada zilizo wajibu juu yamwanadamu awapo katika hali ya afya njema na awapo katika hali yamaradhi, imezingatia katika hali zote mbili nguvu za mwanadamu nauwezo wake. Hivyo Qur’ani, Sunna ya Nabii na somo la sheria ya Uislamvimezungumzia taklifu ya mgonjwa na hukumu zinazomhusu kwa kufuatamsingi wa majukumu na malipo katika akida ya Uislamu inayofungamana

46

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 46

Page 53: Huduma ya Afya katika Uislamu

na uadilifu wake na huruma yake juu ya waja wake. Mwenyezi Munguamefafanua kanuni kuu ya majukumu kwa kusema:

“Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote, ila iliwezalo” (Sura al-Baqarah: 286).

“Mwenyezi Mungu hamkalifishi mtu yeyote ila kwa kadiri alivyompa”(Surat Talaaq: 7).

“Wala hakuweka juu yenu uzito katika dini” (Sura Hajji: 78).

“Mwenyezi Mungu anataka kuwapunguzieni, na ameumbwamwanadamu hali ya kuwa ni dhaifu.” (Sura Nisai: 28).

Kwa msingi wa kanuni hii Mwenyezi Mungu anasema:

“Na ambaye alikuwa katika nyinyi ni mgonjwa au yuko safarini basiyampasa idadi yake katika siku nyingine. Na wale waiwezayo kwamashaka yawapasa fidia kumlisha masikini.” (Surat al-Baqarah: 184).

47

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 47

Page 54: Huduma ya Afya katika Uislamu

“Si vibaya kwa kipofu, wala si vibaya kwa kilema, wala si vibaya kwamgonjwa..” (Sura Nuru: 61).

Kama ambavyo Qur’ani tukufu inavyozungumzia kanuni ya msingi ya tak-lifu, ikabainisha kwamba miongoni mwa masharti ya mtu kuwajibikiwa nakitu kisheria na kupata malipo yake ni kuwa na uwezo wa kutekeleza kituhicho, sawa iwe uwezo huo unaohitajika ni wa kimwili au kimali au kinaf-si. Kama pia ilivyobainisha pia kwamba waja wameondolewa uzito, naMwenyezi Mungu hamkalifishi mwanadamu taklifi ambayo ita-msababishia uzito, bali Mwenyezi Mungu kwa upendo Wake, huruma Yakena rehema Zake amewasahilishia waja na kuwarahisishia njia ya kufikaKwake. Hivyo taklifi za kiibada kama tohara, Sala, Saumu, Hija na Jihadizimetegemea uwezo wa kimwili.

Kanuni hii inaelezea uadilifu wa Mwenyezi Mungu, upendo Wake nahuruma Zake kwa viumbe. Tunaposoma maandishi ya kifiqhi tunaonasheria ya Uislamu imetofautisha baina ya mtu mgonjwa na mzima kati-ka taklifu. Kwa mfano sheria ya Uislamu imemwajibisha mtu mwenyeafya njema ya kawaida kuoga josho la hadathi kubwa, kama vile jana-ba, hedhi na nifasi, kama ilivyomwajibisha kuchukua wudhu kwa ajiliya Sala. Ama mgonjwa ambaye kuoga kunamdhuru au kuchukua udhukunamdhuru yeye amesamehewa na taklifu hizo, na ni juu yakekuchukua tohara kwa njia mbadala nayo ni kutayamamu, atayamamukwa udongo badala ya kuoga au udhu kwa maji.

Mgonjwa ambaye saumu inamdhuru basi saumu yake haisihi, na nijuu yake kutokufunga na alipe baada ya kupona maradhi yake, au atoefidia, nayo ni kiwango maalumu cha chakula, atatoa fidia ya kila sikumoja kati ya siku alizoshindwa kufunga kwa sababu ya maradhi kwakuwapa chakula hicho mafukara. Mgonjwa ambaye hawezi kutekelezaSala katika hali ya kusimama wima ataitekeleza akiwa amekaa chini,na akishinda hali hiyo basi ni huku akiwa amelala.

48

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 48

Page 55: Huduma ya Afya katika Uislamu

Na ambaye hawezi kuhiji wala kupigana jihadi kwa sababu ya matati-zo ya kimwili basi wajibu na taklifu hiyo huwa imemvuka na husame-hewa majukumu hayo. Kama ambavyo tunaikuta kanuni ya hakunakudhuru wala kujidhuru ni hukumu yenye kuhusika na taklifu zote,inahusika na kila taklifu inayosababisha madhara ya kimwili kwamwanadamu, na kwa kufuata kanuni hii basi kila taklifu inayos-ababisha madhara ya kimwili kwa mtu huwa imemvuka mtu huyomhusika.

MAMLAKA YA MGONJWA

Hakika baadhi ya maradhi yanayomsibu mwanadamu ni maradhi hatariyanayopelekea kukatisha uzima wake na maisha yake na wala hawezikupona maradhi hayo. Wanafiqhi huyaita maradhi kama haya kwa jina la‘maradhi ya kifo’. Kanuni ya Uislamu huamiliana na matumizi ya mali zawagonjwa wa namna hiyo, ili kuihifadhi na kuiweka chini ya vizuizimaalumu, hivyo mgonjwa huzuiliwa kutumia mali kwa matumizi ambayoyatawadhuru warithi baada ya kifo chake. Hiyo ni kwa sababu baadhi yamatumizi yake katika mali yatawadhuru warithi kwa sababu za kisaikolo-jia ambazo huzikimbilia baadhi ya wale waliopatwa na maradhi ya kifo,wale waliokata tamaa ya kupona, kama vile kwa sababu ya kuwapendabaadhi ya jamaa huwapendelea kuliko wengine, au kwa sababu yakuwachukia hutamani na kutaka kuwanyima haki yao ya mirathi. Lakinitambua kwamba kanuni za Uislamu zinazoamiliana na mgonjwa wanamna hii haziangalii nia ya mgonjwa katika hali hii, bali huangalia matu-mizi ya kimali je yanawadhuru warithi au la.

Miongoni mwa matumizi ambayo hukimbilia wale wenye kupatwa namaradhi haya ya kifo ni:

Kutoa au kuomba talaka ili kumnyima mke au mume mirathi.Kutoa zawadi, kifutajasho, kisuluhishi, kijivuo, wakfu, sadaka na mfanowake miongoni mwa matumizi ya kimali ya kisheria, matumizi ambayo

49

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 49

Page 56: Huduma ya Afya katika Uislamu

yatahamishia umiliki wa mali yake kwa watu wengine bila fidia walambadala, na hatimaye kuwasababishia madhara warithi.

Kabla hatujafafanua hukumu inayohusu hali hiyo ya maradhi ya kifo, hatu-na budi kutaja kwamba sheria ya Uislamu haijamruhusu mtu yeyote, sawaawe mgonjwa au mzima, kukabidhi wasia uliozidi theluthi ya mali yake,ila pale tu warithi watakapoafikiana na kukubali ule wasia ambao ni ziadailiyo juu ya theluthi, la sivyo ile ziada haitokubalika kisheria.

Hapa tunanukuu hukumu kwa mujibu wa sheria ya Uislamu juu ya matu-mizi ya mali ya mgonjwa yanayowadhuru warithi, hebu tuone sheria inase-ma nini:Lau aliyepatwa na maradhi ya kifo atatoa tamko la kuwepo kwa deni juuyake au amana ya mtu kwake, sawa huyo mwenye deni na amana awe nimmoja wa warithi wake au la, basi ufanyiwaji kazi wa tamko hilo utatege-mea kuthibiti kwa ukweli wake, kukiwa kuna vielelezo vinavyoonyeshakwamba tamko hili limetoka kwake ili kuwanyima warithi haki yao, au ilikumpendelea mtu huyo na ukweli ni kwamba hakuna deni lolote lililo juuyake wala amana yoyote ya mtu huyo iliyo chini ya dhima yake, basitamko hilo halifanyi kazi ila kwa kadiri ya theluthi ya mali yake. Amaikiwa hakuna vielelezo vinavyoonyesha uwongo wa tamko lake basi tamkolake litafanya kazi na matumizi yake hayo ni sahihi. Na vinapokosekanavielelezo vya kuthibitisha ukweli wake wala kukanusha tamko lake basitahadhari ya mkazo ni kutolitekeleza tamko katika ile ziada iliyozidi juu yatheluthi.44 Bora zaidi ni warithi kujadiliana na huyo aliyetamkwa kwenyetamko.

Akitoa zawadi mali au kuitoa wakfu au akaitumia katika aina yoyote yamatumizi yasiyokuwa na mbadala na ambayo yanawadhuru warithi, ikiwamatumizi haya yanazidi theluthi ya mali yake hayatatekelezwa ila baada yawarithi kuafikiana na hilo. Ama baadhi wakiafiki na wengine kutoafiki basi

50

Huduma ya Afya katika Uislamu

44 Tahrirul-Wasila cha Ima Khomeini, Juz. 2, Uk. 23.

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 50

Page 57: Huduma ya Afya katika Uislamu

ile ziada iliyo juu ya theluthi itatekelezwa kwa kadiri ya uwafiki wa warithihawa baadhi.

Iwapo aliyepatwa na maradhi ya kifo atamtaliki mkewe talaka rejea auisiyokuwa na rejea bado mke atakuwa na haki ya kurithi mpaka upite mudawa mwaka mzima, iwapo atakufa kabla ya mwaka mzima tangu kutoa tala-ka. Lakini iwapo atafariki baada ya mwaka mzima tangu talaka itolewe,mke hatokuwa na haki ya mirathi. Hiyo ni kwa sharti kwamba talaka hiyoisiwe imeombwa na mke mwenyewe, na wala isiwe ya Khluu na Mubarati,na pia asiwe amepona maradhi haya ya kifo, na asiwe ameolewa baada yaeda kuisha, hivyo iwapo ataolewa basi hana mirathi, kama ambavyo iwapotalaka ni ya kuomba yeye mwenyewe basi hana mirathi ila iwapo atafarikindani ya kipindi cha eda katika talaka rejea. Hukumu hii inamhusumgonjwa wa maradhi ya kifo na hata yule asiyekuwa katika maradhi hayo,kama ambavyo pia mume atamrithi mkewe iwapo atafariki ndani ya edahii, hiyo ni kwa sababu aliyetalikiwa talaka rejea huzingatiwa kuwa ni mkemaadamu tu bado yumo ndani ya eda.45

Miongoni mwa hukumu zilizomo ndani ya sheria ya Uislamu ni kwambamwamnamke anastahiki mahari kamili toka kwa mumewe iwapo atajami-iana naye, na anastahiki nusu ya mahari iwapo atatalikiwa, au atafariki aukufariki mumewe kabla ya kujamiiana naye. Lakini iwapo mmoja atafari-ki kabla ya kujamiiana basi aliyebaki hai atamrithi mwenzake, kujamiinasi sharti katika kustahiki mirathi. Lakini hukumu hii haifanyi kazi iwapomume atapatwa na maradhi ya kifo. Kwani iwapo mume huyu atafarikikatika maradhi ya kifo, sawa iwe kwa maradhi haya au kwa sababunyingine kama vile matukio ya ghafla na maradhi mengine, basi hapo ndoahuwa imevunjiaka, na mke huwa hana mirathi wala mahari. Ama akifarikibaada ya kujamiiana naye, hapo mahari huthibiti na mirathi pia.46

51

Huduma ya Afya katika Uislamu

45 Min’hajus-Salihin cha Sayyid Muhsin al-Hakim, Juz. 2, Uk. 316.46 Min’hajus-Salihin cha Sayyid Muhsin al-Hakim, Juz. 2, Uk. 316.47 Min’hajus-Salihin cha Sayyid Muhsin al-Hakim, Juz. 2, Uk. 316.

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 51

Page 58: Huduma ya Afya katika Uislamu

Iwapo aliyepatwa na maradhi ya kifo atafunga ndoa na mwanamke, kishaakafariki kabla hajajamiina naye basi mwanamke huyo hatokuwa na edaya kufiwa na mume.47

MATIBABU NA MWANAMKE AJINABI

Ili sheria ya Uislamu ihifadhi heshima ya mwanamke na utukufu wake,na ili ing’oe mizizi ya uharibifu na ukiukaji wa maadili ikiwa ni mion-goni mwa vitu vinavyochochea vitendo vya ngono, Uislamu uliwa-jibisha sitara juu ya mwanamke. Ukaweka hukumu na maelekezomakhususi juu ya hilo, ambayo yanahusu kumtizama mwanamumeajinabi au kumgusa mwanamke ajinabi. Nasi tukiwa tunazungumziahukumu za kumgusa na kumtazama mwanamke ni lazima tufafanuekwamba hakika sheria ya Uislamu ambayo inatatua suala na maudhuihii, imetofautisha hukumu ya mukallafu kulingana na mazingira halisina hali iliyopo.

1. Katika hali ya kawaida ya mwanadamu: Sheria ya Uislamu ime-haramisha mwanamume kumtizama au kumgusa mwanamke ajinabiawapo katika hali ya kawaida, ila mtazamo wa kwanza usio wa kum-tamani. Ama iwapo atataka kumuoa basi anaruhusiwa kumtizamausoni na mikononi, na amtizame akiwa katika hali ya kutembea nakusimama. Kama Uislamu ulivyoharamisha kwa mwanamume ajinabikumtizama mwanamke ajinabi pia umeharamisha mwanamke ajinabikumtizama mwanamume ajinabi au kumgusa katika hali ya kawaida.Kwa msingi wa kanuni hii ya kisheria hairuhusiwi kisheria mwanamkekumgusa mwanamume ajinabi au kuutazama mwili wake kwa lengo lakumtibu, kama ambavyo hairuhusiwi kisheria kwa mwanamume kuu-gusa mwili wake au kumtizama kwa lengo la kumtibu pindianapokuwepo na kupatikana tabibu wa jinsia yake, mwanamume kwamwanamume na mwanamke kwa mwanamke.

52

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 52

Page 59: Huduma ya Afya katika Uislamu

Mara nyingi mwanamke au mwanamume hutokewa na maradhi na halihakuna tabibu wa jinsia yake au aliye maharimu wake, basi wakati huoinaruhusiwa kisheria kwa kila mmoja kumtizama mwenzake au kumgusakwa lengo la kumtibu, kwa sababu tu ya dharura hii bila kumtamani. Nakama kitendo kimoja kati ya kumtizama na kumgusa kitatosha kusaidiakumtibu, basi hairuhusiwi kisheria kutekeleza na cha pili, kwa mfanoiwapo matibabu yanaweza kukamilika kwa kumtizama tu, basi haijuzukumgusa, na hivyo hivyo kinyume chake.

UTABIBU NI WAJIBU WA KUTOSHELEZA

Miongoni mwa mambo ambayo yanayopatikana tu katika sheria yaUislamu kutokana na utukufu wa malengo yake ya kimaendeleo, na mti-zamo wake wa kibinadamu na kimaadili kwenye majukumu ya kijamii nakwenye thamani ya mali, ni kuweka sheria zinazohusu afya. Tunawezakufahamu utukufu huu wa kimaendeleo wa kiislamu katika sekta hii yasheria kwa kutizama yale yaliyojaa katika masomo ya fiqhi katika mlangowa tiba. Na ili kuonyesha uhusiano uliyopo kati ya maudhui ya maradhi namatibabu au kati ya wajibu wako mbele ya maradhi na usalama wa kiafya,tutaonyesha baadhi ya hukumu na hatua ambazo zimethibitishwa nawanafiqhi katika sekta hii.

Wanafiqhi wamegawa wajibu wa kisheria sehemu mbili:

Wajibu binafsi wa kila mmoja: Nao ni ule wajibu ambao maelekezo namajukumu yanaelekezwa kwa kila aliye mukalafu, kwa sura ya mtu mmojammoja, kama vile sala na saumu.

Wajibu wa kutosheleza: Nao ni ule wajibu ambao maelekezo huelekezwakwa mtu kwa sura ya kundi, na hutakiwa kuutekeleza bila kujali ni naniatakayeutekeleza, na inatosha iwapo baadhi ya walengwa watatekelezaamri hiyo, na hapo wajibu ule huwaondokea waliobaki, kama vilekumtetea aliyedhulumiwa, kumwokoa aliye katika vitisho vya hatari,

53

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 53

Page 60: Huduma ya Afya katika Uislamu

kumzika maiti na kumtibu mgonjwa, na mengineyo.

Fikra na sheria ya Uislamu vimetilia umuhimu sana majukumu ya kijamiiambayo huleta manufaa na kutimiza mahitaji ya wanajamii na jumuia zake,hivyo ikayafanya mambo hayo kuwa ni wajibu wa kutosheleza, kama vileuhandisi, utabibu na fani nyinginezo za kielimu zinazohitajika kijamii.

Hebu hapa tunukuu maandiko ya kifiqhi yanayotufafanulia wajibu wa tibajuu ya mtabibu, wajibu wa kutosheleza. Katika maandiko hayo imeandik-wa: “Pia inajuzu kuchukua malipo lau akimuajiri kwenye wajibumwingine usiokuwa wa kiibada, kama vile kumwandikia dawa mgonjwa,au kumtibu au mfano wa hayo, bila shaka inasihi. Na pia kama atamwajirikatika mambo ambayo yanahitaji utawala, kama vile baadhi ya taalumazinazohusu kilimo, viwanda, utabibu……”48

Sheria hii inamaanisha kuhakikisha uwepo wa yale yanayohitajika na jamiimiongoni mwa matabibu, dawa, vifaa vya tiba, taasisi za uchunguzi watiba na vyuo vya tiba, na kila kinachotakiwa katika kutimiza wajibu huukwa namna ya wajibu wa kutosheleza.

Lakini kutoa matibabu huwa ni wajibu binafsi wa kila mmoja juu ya tabibuiwapo hakuna wa kutimiza hilo ila yeye tu, na hapo huwa ndiye mwenyedhamana na uhai wa mgonjwa, hivyo iwapo akimwacha bila kumtibu kishaakafa kwa sababu ya kuacha kwake, basi yeye ndiye mhusika wa kifohicho.

Ijapokuwa ni wajibu wa kutosheleza lakini tabibu ana haki ya kuombamalipo yanayooana na matibabu, kama maandiko ya fiqhi yaliyotanguliayalivyoeleza. Lakini analazimika kumtibu bila malipo mgonjwa ambayeuhai wake unategemea matibabu haya, hiyo ni iwapo mgonjwa hana uwezowa malipo hayo, na kama atamwacha bila kumtibu kwa sababu ya kushind-wa kulipia matibabu, basi yeye ndiye mwenye kuwajibika iwapo atafariki,

54

Huduma ya Afya katika Uislamu

48 Min’hajus-Salihin cha Sayyid Muhsin al-Hakim, Juz. 2, Uk. 120.

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 54

Page 61: Huduma ya Afya katika Uislamu

kama ambavyo yeye ndiye mwenye kuwajibika na madhara yoyoteyatakayomfika mgonjwa kwa sababu ya yeye tabibu kushindwa kutekelezajukumu lake.

Hebu tunukuu maandiko ya kifiqhi yanayobainisha wajibu wa tabibu naulazima wa kuwajibika iwapo atamsababishia mgonjwa madhara kwasababu ya kushindwa kutekeleza majukumu yake: “Na pia tabibu aliye-husika kutoa matibabu yeye mwenyewe ni mwenye dhamana ya uharibifuiwapo utatokea..”49 yaani ndiye mwenye kuwajibika na madhara yoyoteyatakayompata mgonjwa kutokana na kutotekeleza jukumu lake katika njiaya kutoa matibabu, au kwa sababu ya mtabibu asiye na ujuzi na ugonjwahuo kujitwika kazi hiyo.

Tunaweza kufahamu thamani ya utabibu, malipo yake na thawabu zakekupitia maelezo ya Uislamu ambayo yanalingania huruma na msaada,kupunguza maumivu ya watu, kutoa msaada wa hali na mali kwa wenginena kuwaondolea adha na madhara, thawabu ambazo anastahiki kuzipatatabibu mwenye nia safi na utashi safi, yule mwenye kuwapunguzia watumaumivu na mwenye kuilinda afya yao.

DUA NA PONYO

“Ambaye ameniumba, naye ananiongoza. Naye ndiye anayenilisha nakuninywesha. Na ninapougua, basi yeye ananiponya” (Sura Shua’raa:78 – 80).

55

Huduma ya Afya katika Uislamu

49 Min’hajus-Salihin cha Sayyid Muhsin al-Hakim, Juz. 2, Uk. 120

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 55

Page 62: Huduma ya Afya katika Uislamu

“Na tunateremsha Qur’ani ambayo ni ponyo na rehema kwa wenyekuamini, wala hayawazidishii madhalimu ila hasara tu.” (Sura Israil:82).

“Muombeni Mola wenu Mlezi kwa unyenyekevu na kwa siri, hakikayeye hawapendi warukao mipaka.” (Sura Aaraf: 55).

“Na Mola wenu Mlezi husema: Niombeni nitakujibuni. Kwa hakikawale wajivunao kufanya ibada yangu, wataingia Jahannam wakifed-heheka.” (Sura Muumin: 60).

“Wale walioamini na zikatulia nyoyo zao kwa kumkumbukaMwenyezi Mungu, sikilizeni, kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu,nyoyo hutulia.” (Sura Ra’d: 28).

56

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 56

Page 63: Huduma ya Afya katika Uislamu

“Na waja wangu watakapokuuliza juu yangu basi hakika mimi nipokaribu, nayaitikia maombi ya mwombaji anaponiomba, basi wani-itikie na waniamini, ili wapate kuongoka. (Surat al-Baqarah: 186).

“Na Ayubu, alipomwita Mola wake Mlezi ya kwamba imenigusa dharanawe ndiye unayerehemu kushinda wote wanaorehemu. Basitukamkubalia na tukamwondolea dhara aliyokuwa nayo na tukampawatu wake na mfano wa pamoja nao ni rehema kutoka kwetu, naukumbusho kwa wafanya ibada.” (Sura Anbiyai: 83 – 84).

Maradhi ni jina la kuvurugika mpangilio wa mwili au nafsi na kuharibikautendaji wake, na ili mwili na nafsi virudi kwenye hali yake ya afya namazingira ya kawaida ni lazima kuondoa uvurugikaji huo na uharibikajihuo. Kazi hii ya kuondoa ndio huitwa tiba.

Tiba ya mwili ina vifaa na njia mbalimbali za kielimu, hivyo maradhi yakimwili hutibiwa kwa njia ya vyakula, dawa za kemikali au za asili,mazoezi ya kawaida, utumiaji wa miyonzi, upasuaji, uondoaji wa kiungoau kukibadili au kuitoa ile sehemu yenye kudhuru, na mengineyo.

Na suala la kuathiriana kati ya mwili na nafsi ni mambo yenye ukweli wakielimu uliothibitishwa na uchunguzi wa kitiba, hivyo maradhi mengi yamwili sababu yake ni maradhi na hali za kisaikolojia, kama ambavyomaradhi mengi ya kisaikolojia sababu yake ni maradhi ya kimwili. Hivyomatabibu wanasisitiza kwamba maradhi ya mapafu, mgandamizo wadamu, vidonda vya tumbo, kichwa, kisukari, moyo na mengineyo miongo-ni mwa maradhi yamsumbuayo mwanadamu, chanzo chake ni hali namabadiliko ya kisaikolojia, kisha ni kwamba yaligeuka na kuwa maradhiya kimwili.

Amatekasika Mwenyezi Mungu ambaye alimuumba vilivyo mwanadamu,mwili na nafsi vina uwezo wa kuandaa mazingira ya kawaida na kubadilihali ya kimaradhi. Mwili unamiliki uwezo wa kujitengeneza wenyewe kwa

57

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 57

Page 64: Huduma ya Afya katika Uislamu

kutumia nguvu ya asili au kwa msaada wa chakula au dawa, viharakishi navifaa vyenye kusaidia kuurudishia mwili mpangilio wa kawaida.

Kama ambavyo mwili unaweza kuandaa mazingira ya kawaida ya mwili,yaani ile ghali ya afya, kwa kutumia nguvu ya asili na kwa msaada wa tiba,ndivyo hivyo hivyo nafsi nayo inaweza kubadili na kugeuza kwa kuletamazingira mengine.

Hakika miongoni mwa nyenzo muhimu za kutibia maradhi ya kisaikolojia,ni kazi ya uchambuzi wa kisaikolojia na kugundua sababu za mabadilikoya hali za kisaikolojia, na kujitahidi kuweza kuzidhibiti. Na hakika mion-goni mwa njia bora kabisa za kuyadhibiti maradhi ya kisaikolojia nikumwelimisha mgonjwa na kumfahamisha hali ya ugonjwa baada ya kuu-fafanua, na pia kuondoa mafundo ya ugonjwa na kuinua hali yake yakisaikolojia, na kuweza kulipokea tatizo kama hali ya kawaida, au kamahali ya kawaida inayoweza kuondoka kupitia tiba ya kimada au kisaikolo-jia.

Njia zote hizo za matibabu, sawa ziwe za kutibu maradhi ya kisaikolojia auya kimwili, zote zinategemea msaada wa mwili na nafsi katika kuandaamazingira ya asili yake ya kawaida. Hivyo mtu anapomwelekea MwenyeziMungu kwa dua na moyo wenye ikhlasi, akatenda mema, kama kutoa sada-ka, kutekeleza nadhiri na kuomba maghufira, basi rehema humwelekeayeye, na hapo Mwenyezi Mungu huruhusu mwili na nafsi viandae mazin-gira yake ya asili yake ya kawaida, kwani utashi wa Mwenyezi Munguwenye kutawala na kutiisha vitu vyote ndio sababu yenywe nguvu yenyekutawala ulimwengu huu ambao huenda kulingana na utashi Wake namatakwa Yake.

Kumwamini Mwenyezi Mungu na kumtegemea yeye ndio sababu kubwaya kuitengeneza nafsi na kuitibu na maradhi yake, kwa sababu hali hiyo yaimani ina uwezo wa kuiokoa na mashaka, khofu, huzuni, hasira na hali yamihangaiko ya kinafsi.

58

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 58

Page 65: Huduma ya Afya katika Uislamu

Hivyo Mwenyezi Mungu amembainishia wazi mwanadamu kwambamiongoni mwa Aya za Qur’ani zimo zilizo ponyo la nyoyo na kisafisho chanafsi dhidi ya hali za khofu, mashaka, na hali mbalimbali ambazo hus-ababisha maradhi ya kisaikolojia. Mwenyezi Mungu akasema: “Natunateremsha Qur’ani ambayo ni ponyo na rehema kwa wenyekuamini.” (Sura Israil: 82). Na akasema: “Sikilizeni kwa kumkumbu-ka Mwenyezi Mungu, nyoyo hutulia.” (Sura Ra’d: 28). Nafsi inapoponamaradhi yake ndipo mwili nao unapopona maradhi yake makubwa yakimwili.

Hivi ndivyo dua inavyokuwa sababu ya kupata ponyo:

Kwanza: Ni kutokana na uwezo wake wa kutengeneza hali ya kisaikolo-jia kwa mgonjwa kutokana na kumpa mgonjwa hali ya kumtegemeaMwenyezi Mungu na kuridhia majaaliwa yake na makadara yake, hivyoimani hii inamwokoa na hali ya mfundo, hasira, na mihemuko mingine yakisaikolojia, na hapo athari za imani zinaakisi hali ya kiafya ya mwili nakutoa matokeo mazuri. Hivyo ndivyo kumwamini Mwenyezi Mungukunavyoisaidia nafsi kurejesha hali yake ya kawaida na kuathiri hali yamwili, kwa njia hiyo dua inaingia kama tiba ya kielimu na sababu yenyekuathiri mfumo wa utendaji wa mwili kwa kutoa athari za kawaida.

Pili: Hakika uumbaji na mambo yote yapo chini ya Mwenyezi Mungu nayendiye muweza wa kutenda alitakalo: “Ufalme umo mikono mwake naye niMuweza wa kila kitu.” Hivyo hutoa ponyo na uokovu kwa mgonjwa, nahapo mwili hurudi kwenye hali yake ya kawaida kama alivyouumba ukiwasalama katika maumbile yake, harakati zake na utendaji wake.

Mwenyezi Mungu ametuambia kwamba hujibu maombi ya mwenyekumuomba pindi anapomuomba, na kwamba Yeye ndiye anayemilikiponyo, na Yeye ndiye ambaye rehema Zake zilimfunika Nabii Ayubu (a.s.)baada ya kupatwa na maradhi na kumchosha, hapo akamjibia dua yake naakamrudishia afya njema na usalama.

59

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 59

Page 66: Huduma ya Afya katika Uislamu

Kuna habari na riwaya zimepokewa kutoka kwa Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) kwamba alikuwa akiwakinga Hasan na Husain kwa kuwasomeaSurat Nasi na Surat al-Falaqi. Kama ambavyo alikuwa akiomba dua yakutaka ponyo dhidi ya maradhi na akisisitiza kumwombea dua mgonjwa.Ali (a.s.), Fatima binti wa Mtume (s.a.w.w.) na Fidha mtumishi wa Fatima(a.s.) waliweka nadhiri ya kufunga siku tatu ili kuomba ponyo la ugonjwauliowasibu Hasan na Husein, na hapo Mwenyezi Mungu akawaneemeshana ponyo, na ndipo wakatoa sadaka ile futari yao kwa muda wa siku tatu,na hapo Mwenyezi Mungu akateremsha Surat Dahri akiwapongeza Ali,Fatuma, Fidha, Hasan na Husain (a.s.).

Ili kukamilisha faida hebu tunukuu baadhi ya dua za Mtukufu Mtume zina-zohusu tiba ya maradhi, ili dua hizo ziwe njia ya kuomba fadhila na rehe-ma toka kwa Mola Mlezi na ziwe sababu ya kupona.

Al-Kaf’amiy amepokea kutoka kwa al-Mujahidi kwamba: Anayetafutatiba ya ugonjwa alionao, basi aseme kwenye sijida yake ya pili katika rakaazake mbili za mwanzo za sala ya usiku: “Ewe Mtukufu! Ewe Adhimu! Ewe Rahman! Ewe Rahimu! Ewe Msikivuwa dua! Ewe Mwenye kutoa kheri! Msalie Muhammadi na aaliMuhammadi, na nipe toka katika kheri ya dunia na Akhera yale uyaridhi-ayo wewe, na niepushie toka katika shari ya dunia na Akhera uyachukiayowewe, na niondolee ugonjwa huu (taja ugonjwa) kwani bila shakaumenizidia na umenihuzunisha.” Ataomba dua mara kwa mara bila shakainsha’allah atapatwa na afya haraka iwezekanavyo.

Imepokeawa dua ya maradhi yote kutoka kwa Imam Ridha (a.s.): “Ewe Mteremshaji wa ponyo na muondoaji wa ugonjwa! MsalieMuhammadi na aali zake, na niteremshie ponyo kwenye ugonjwa wangu.”

Sayyid Ibnu Taus katika kitabu al-Muhji amepokea kutoka kwa IbnuAbbasi kwamba alisema: Nilikuwa nimeketi kwa Ali (a.s.) na ndipoalipoingia mtu aliyesawijika rangi, akasema: Ewe Amirul-Muuminina!

60

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 60

Page 67: Huduma ya Afya katika Uislamu

Mimi ni mtu mwenye maradhi, mwingi wa magonjwa na maumivu, naom-ba unifundishe dua itakayonisaidia katika maradhi yangu. Ali (a.s.) akase-ma: “Nitakufundisha dua ambayo Jibril (a.s.) alimfunza Mtume (s.a.w.w.)walipougua Hasan na Husain (a.s.), nayo ni: ‘Ilahi! Kila unineemeshapo neema yoyote, hupunguka shukurani yangukwako juu ya neema hiyo, na kila unaponijaribu kwa mtihani wowote,hupunguka subira yangu kwenye mtihani huo. Ewe ambaye hupungukashukurani yangu juu ya neema yake lakini haninyimi! Na ewe ambayehupunguka subira yangu kwenye mtihani wake lakini hanitelekezi! Na eweambaye aliniona nikiwa katika maasi lakini hajanifedhehesha! Na eweambaye aliniona nikiwa katika makosa lakini hajaniadhibu kwayo! MsalieMuhammadi na aali Muhammadi na nighufirie dhambi zangu na niponyemaradhi yangu, hakika wewe ni Muweza wa kila kitu.”’

Ibnu Abbasi amesema: Baada ya mwaka nikamwona mtu yule akiwa nauso wa kupendeza wenye kung’aa wekundu, akasema: Sikuwahi kuiombana hali ni mgonjwa ila nilipona, wala nikiwa na maradhi ila yalipona, nasikuwahi kuingia kwa mtawala ila alipunguza ujeuri wake, na sikuwahikuisoma ila Mwenyezi Mungu alinikinga naye.”

Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: Mwenye ugonjwa ausomee dua hii maraarubaini kila siku asubuhi: “Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.Kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe wote.Anatutosha Mwenyezi Mungu naye ndio mtegemewa bora. AmetukukaMwenyezi Mungu muumbaji bora kushinda wote. Hakuna ujanja walanguvu ila kwa msaada wa Mwenyezi Mungu Mtukufu Adhimu.”

Imam as-Sadiq amesema: Weka mkono wako juu ya eneo lenye maumivuna useme mara tatu: “Allahu, Allahu, Allahu ni Mola wangu Mlezi kweli, simshirikishi na cho-chote. Ewe Mwenyezi Mungu! Wewe ndiye Mmiliki wake na kilalililokubwa basi yaondowe (maumivu) na unifariji dhidi yake.”

61

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 61

Page 68: Huduma ya Afya katika Uislamu

Imam as-Sadiq amesema: Ni kwa ajili ya maumivu yote:

“Kwa jina la Mwenyezi Mungu na kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, nineema ngapi za Mwenyezi Mungu zimo ndani ya mishipa tulivu na isiyotulivu, juu ya mja mwenye shukurani na asiye na shukurani.”

Na sema mara tatu: “Ewe Mwenyezi Mungu! Niondolee matatizo yangu na niharakishie afyayangu na niondolee dhara langu.”

Imam as-Sadiq amesema: Hakika Ali aliugua, Mtume akamjia nakumwambia: “Sema: “Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika mimi nakuomba kuharakishiwa afyayako, subira juu ya mtihani wako na kutoka kwenye dunia kwenda kwenyerehema yako.”

Na Shahidi (r.a.) alikuwa akimshika mgonjwa mkono wa kulia na kusoma: “Ewe Mwenyezi Mungu! Mwondolee maradhi na magonjwa, na mrudishekwenye siha na ponyo, na mwendelezee kwa kumpa kinga bora na mrud-ishe kwenye afya njema, na fanya maradhi yaliyomsibu nyongeza ya uhaiwake na kafara ya makosa yake. Ewe Mwenyezi Mungu na msalieMuhammadi na aali Muhammadi.”

Imepokewa ndani ya kitabu al-Mujtaba Minaduail-Mujtaba kwambautamsomea mgonjwa: “Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika wewe umesema ndani Kitabu chakiokilichoteremshwa juu ya Nabii wako uliyemtuma: Hakuna msiba wowoteuliowapata ila ni kwa sababu ya yale yaliyochumwa na mikono yenu, naanasamehe mengi, ewe Mwenyezi Mungu msalie Muhammadi na aaliMuhammadi na yaweke maradhi haya miongoni mwa yale mengiunayosamehe na kuponya. Tulia ewe maumivu na ondoka sasa hivi tokakwa mja huyu dhaifu, nimekutuliza na kukuondoa kupitia ambaye vimetu-lia kwa ajili yake vilivyomo usiku na mchana, naye ni Msikivu Mjuzi.”

62

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 62

Page 69: Huduma ya Afya katika Uislamu

Ali (a.s.) amesema: Ni kinga ya kila maumivu ya mwili, atakayeyasemahatodhuriwa na maumivu, nayo ni: “Najilinda kwa nguvu ya Mwenyezi Mungu na uwezo wake juu ya vituvyote. Nailinda nafsi yangu kwa Jabari wa mbinguni na ardhini. Nailindanafsi yangu kwa ambaye jina lake halidhuriwi na ugonjwa wowote.Nailinda nafsi yangu kwa ambaye jina lake ni baraka na ponyo.”

Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: “Mkiwaona waliopatwa ni miti-hani, muhimidini Mwenyezi Mungu na wala msiwasikilizishe kwa kufanyahivyo kutawahuzunisha.”

Imam al-Baqir (a.s.) amesema: “Ukimuona aliyepatwa na mtihani, semamara tatu bila yeye kusikia: Kila sifa njema ni ya Mwenyezi Munguambaye amenipa afya njema dhidi ya yale aliyomjaribu, na lau angelitakaangefanya.”

Dua wakati unapopatwa na msiba:“Na wape habari ya furaha wenye kusubiri. Ambao ukiwafikia msiba, husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na sisi tu wenye kure-jea kwake. Hao juu yao ziko baraka na rehema kutoka kwa Mola waoMlezi, nao ndio wenye kuongoka. Kila sifa njema ni ya Mwenyezi Munguambaye hajafanya msiba wangu ni katika dini. Na kila sifa njema ni yaMwenyezi Mungu ambaye lau angelitaka msiba wangu uwe mkubwakushinda ulivyo angefanya, na kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu juuya jambo ambalo alitaka liwe na likawa.”

Dua ya kuondoa mashaka na huzuni:“Ewe Ambaye Kwake hufunguka mafundo yachukizayo. Ewe Ambayekupitia Kwake makali ya shida huwa butu. Ewe Ambaye huombwa ubari-di wa kuifikia faraja. Magumu yamedhalilika mbele ya nguvu Zako, kwahuruma Zako sababu zimepatikana, kwa nguvu Zako hukumu zimepita nakwa utashi Wako vitu vimekwenda kama ilivyotakiwa. Kwa utashi Wakobila kauli Yako vimewajibika na kwa utashi Wako bila katazo Lako vime-

63

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 63

Page 70: Huduma ya Afya katika Uislamu

jizuia.

Wewe ndiye wa kuombwa wakati wa jambo muhimu na ndio kimbilio lawakati wa shida. Haiondoki isipokuwa ile uliyoiondoa na wala haitatukiisipokuwa ile uliyoitatua. Tayari ewe Mola wangu Mlezi yameshan-iteremkia yale ambayo uzito wake umenielemea na limenishukia jamboambalo uzito wake umenishinda.

Kwa nguvu Zako umelishusha juu yangu na kwa mamlaka Yakoumelielekeza kwangu. Hivyo basi hakuna wa kuondoa ulilolileta, kuzuiaulilolielekeza, wa kufungua ulichofunga wala wa kufunga ulichokifungua,kukifanya chepesi kile ulichokifanya kizito, wala wa kumsaidiauliyemtelekeza. Hivyo msalie Muhammad na Aali zake na nifungulie eweMola wangu Mlezi mlango wa faraja kwa rehema Zako. Vunjilia mbalimamlaka ya usumbufu kwa nguvu Zako. Nipe mtazamo mzuri kwamalalamiko yangu. Nionjeshe utamu wa matendo kupitia yale niliyokuom-ba. Nipe faraja njema na rehema kutoka Kwako. Na nijaalie mwanya wakupenya upesi kutoka Kwako.

Usinifanye nijishughulishe na mengine na kuacha kutekeleza wajibu Wakona Sunna Yako. Nimedhikika kutokana na yale yaliyonishukia Ee MolaWangu Mlezi! nimejawa na huzuni kwa kuyabeba yale yaliyoniteremkia,na Wewe ndiye Mwenye uwezo wa kuondoa yaliyonifika na kuyawekambali niliyoangukia, hivyo nifanyie hayo ingawa sistahiki kupata hayokutoka Kwako ewe bwana wa Arshi adhimu na Mwenye neema uliyeMkarimu, Wewe ni Muweza ewe Mwenye huruma kushinda wote wenyehuruma. Amina ewe Mola Mlezi wa viumbe wote.”

Dua ya kuondoa matatizo:

“Ewe nguzo ya asiyekuwa na nguzo! Ewe akiba ya asiyekuwa na akiba!Ewe egemeo la asiyekuwa na egemeo! Ewe hirizi ya asiyekuwa na hirizi!Ewe hirizi ya wanyonge! Ewe mwenye matarajio makubwa! Ewe

64

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 64

Page 71: Huduma ya Afya katika Uislamu

mwokozi wa aliyezama! Ewe mwokozi wa aliyehiliki! Ewe mwema! Ewemtenda mazuri! Ewe mneemeshaji! Ewe mtenda fadhila! Wewe ndiyeambaye umesujudiwa na giza la usiku, nuru ya mchana, mwanga wamwezi, mionzi ya jua, mvumo wa miti na sauti ya maji. Ewe MwenyeziMungu! Ewe Mwenyezi Mungu! Ewe Mwenyezi Mungu! Hakuna munguila Wewe Mmmoja wa pekee usiye na mshirika. Ewe Mola wangu eweMwenyezi Mungu! Msalie Muhammadi na aali Muhammadi na nitendeemimi yale uyatakayo, nitendee mimi kadha wa kadha. (Hapo utataja hajayako).”

Dua nyingine kutoka kwenye kitabu Kunuzun-Najah, Mtume (s.a.w.w.)alimfunza bintiye Fatima (a.s.) dua hii, nayo ni:

“Ewe Mjuzi wa ghaibu na siri! Ewe Mwenye kutiiwa! Ewe Mwenyenguvu! Ewe Mjuzi! Ewe uliyeyashinda makundi kwa ajili ya Muhammadi!Ewe uliyemtega Firaun kwa ajili ya Musa! Ewe uliyemwokoa Isa tokamikononi mwa madhalimu! Ewe uliyemwokoa Nuhu na gharika! Ewemwenye kutenda kila kheri! Ewe mwenye kuongoza kuelekea kwenye kilakheri! Ewe mwenye kujilisha kila kheri! Ewe mwenye kuamuru kila kheri!Ewe muumba wa kheri! Wewe ndiye Mwenyezi Mungu hakuna mungu ilaWewe, nimetamani kwako yale ambayo wewe umeshayajua, basi nijibukwa fadhila zako, ewe Mwenyezi Mungu! Ewe Mwingi wa rehema.”

65

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 65

Page 72: Huduma ya Afya katika Uislamu

KUMTEMBELEA MGONJWA

Mwenyezi Mungu amesema:

“Enyi watu! Kwa hakika tumekuumbeni kutokana na mwanaume namwanamke, na tumekufanyeni mataifa na makabila ili mjuane, haki-ka aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni aliye mchaMungu zaidi katika nyinyi, kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi,Mwenye khabari.” (Sura Hujrat: 13).

Hakika kuisoma jamii ya kiislamu au namna Uislamu unavyoinadhimujamii ya kibinadamu kunatuonyesha misingi na viunganishi imaraambavyo Uislamu umetumia kujengea mahusiano ya kijamii na heshimaya mwanadamu na utukufu wake. Hakika maadili, kanuni, maelekezo,ibada na fikra za kiitikadi, yote hayo yanachangia katika kujenga umbile lakijamii na kulinadhimu kwa misingi ya upendo, kusaidiana na kuheshimuhisia za mwanadamu, na kusisitiza maana ya ushirikiano wa ubinadamu naupendo na kuleta hisia za huruma. Kitendo cha Uislamu kujali sana sualala maingiliano na muamala wa kijamii na kusisitiza kuendelea kwa mwe-nendo huu kinaakisi kwetu thamani ya maisha ya kijamii na jinsi ulivyojalijamii na adabu zake.

Uzoefu wa kihistoria na kimaendeleo umethibitisha kwamba misingi naviunganishi vya kimali vyenyewe pekee havijengi jamii yenye mshika-mano na wala haviimarishi jamii ya kibinadamu iliyo imara. Na bila shakakusoma na kuchambua jamii ya kimali tuliyonayo sasa kunatufichuliakiwango cha matatizo ya kisaikolojia na kijamii, ukosefu wa huruma,

66

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 66

Page 73: Huduma ya Afya katika Uislamu

kutokuwepo kwa roho ya kibinadamu katika mahusiano na mafungamano,na pia jinsi mwanadamu anavyohisi mashaka, huzuni, mchoko, unyonge,kutokuwa na maana, ugeni na upweke katika jamii hii.

Ni jambo lililo wazi katika masomo ya saikolojia, maadili na maisha yahisia, kwamba jambo la kwanza analolihitaji mwanadamu kabla ya hajazote na lenye athari kubwa katika kumletea furaha ni kushibisha upande wakisaikolojia na wa huruma, ushibishaji salama. Bali ni kwamba furaha yakweli kwake ni utulivu wa kisaikolojia na hisia za ndani ambazohuonekana katika hali ya kuridhia, upendo na utulivu. Mwanadamu katikabaadhi ya hatua za maisha yake anahisi haja ya kujaliwa na wenzake nakupata huruma yao kushinda anavyohisi katika hatua nyingine. Katikahatua ya utoto, uzee, udhaifu, maradhi na matukio ya kuumiza,mwanadamu huhitaji kusaidiwa na msaada wa huruma, kujaliwa nawengine na huduma yao kwake kushinda anavyohitajia mambo hayo kati-ka wakati na mazingira mengine. Na kwa kweli kukosekana kwa hudumahii toka kwa wenzako huathiri vibaya hali ya mwanadamu huyu na hati-maye huakisi uhusiano wake na nafsi yake na jamii yake.

Hakika hisia hatari zaidi ambayo huleta uadui kwa watu wengi ni kulemwanadamu kuhisi kutengwa na wenzake na kutoheshimu utu wake.Misimamo kama hii kutoka kwa wenzake na mfano wa hisia kama hizihutengeneza hali ya maradhi inayoongeza mahangaiko yake na taabu zake,kwa ajili hiyo Uislamu umelingania kusaidiana na huruma, kumjulia haliasiyekuwepo na ukahimiza kutembeleana na ukasisitiza kumtembeleamgonjwa, undugu, ujirani mwema na kuwa na ndugu na marafiki, ilikwamba wanajamii waingie katika mnyororo wa mahusiano ya kiupendona ubinadamu ambayo yatatoa roho ya kusaidiana na kujaliana, na yata-pandikiza hisia za upendo na kuhehimu utu wa mtu, jambo ambalo lita-saidia sana kujenga maadili mema na kuondoa hali za upotofu namkengeuko.

67

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 67

Page 74: Huduma ya Afya katika Uislamu

Hakika kumzuru mgonjwa hupandikiza ndani ya nafsi yake hisia zakupendwa na wenzake na hupunguza machungu ndani ya nafsi yake, nahumhisisha huduma toka kwa ndugu zake, watu wake, marafiki zake najamii yake. Mara nyingi anachokianza mgonjwa aliyepatwa na maradhimakubwa, au ya muda mrefu au yaliyo hatari zaidi kwa uhai wake, maranyingi baada ya kupona huanza mwenendo mpya na mahusiano mengimazuri ya kibinadamu na yaliyo sahihi, hususan anapompata mwenyekumsaidia kwa tiba na ponyo, kwa kumpunguzia maumivu ya kihali namali.

Hivyo tunaikuta Qur’ani tukufu inasisitiza kujuliana hali, kusaidiana nakushirikiana baina ya wanajamii. Katika wosia wa Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) na maimamu waongofu, tunasoma maelekezo na mwongozo wathamani katika maudhui hii. Hapa tutataja zile riwaya zilizopatikanakuhusu kumtembelea mgonjwa na kuhurumiana naye. Mtume (s.a.w.w.)amesema: “Mwislamu akimtembelea ndugu yake kwa ajili ya MwenyeziMungu, Mwenyezi Mungu husema: Umepata mema na umepata makazipeponi.”50

Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Watembeleeni wagonjwa wenu nawaombeeni dua.”51

Al-Barau bin Azib amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ali-tuamuru mambo saba na alitukataza mambo saba: Alituamuru kumtembe-lea mgonjwa, kusindikiza jeneza, kumwombea dua mwenye kutoa chafya,kuitikia salamu, kumvua na tuhuma yule mwenye kuapa, kuitikia mwaliko,na kumsaidia mdhulumiwa. Alitukataza kutumia vyombo vya madini yafedha, kuvaa pete ya dhahabu, hariri……”52

68

Huduma ya Afya katika Uislamu

50 Musnad Ahmad bin Hanbal Juz. 2, Uk. 326.51 Mishkatul-An’war Uk. 280.52 Musnad Ahmad bin Hanbal Juz. 4, Uk. 284.

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 68

Page 75: Huduma ya Afya katika Uislamu

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Hakika mwenyekumtembelea mgonjwa huzama ndani ya rehema, anapoketi humfunika.”53

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Hakuna mtuanayemtembelea mgonjwa na kuketi kwake ila hufunikwa na rehema tokakila upande muda wote atakaokaa kwake. Na atokapo kwake huandikiwamalipo ya funga ya siku nzima.”54

Kama ambavyo wosia na maelekezo ya Uislamu umesisitiza kumtembeleamgonjwa ndivyo hivyo hivyo umesisitiza kumkirimu mgonjwa nakumpelekea zawadi, ili kumhisisha furaha na upendo wa mwenye kumtem-belea. Tunaposoma msimamo wa Imam Ja’far as-Sadiq (a.s.) tunaonaharakati hizi za kimaadili na ambazo zimesisitizwa.

Mfanyakazi wa Imam Ja’far as-Sadiq (a.s.) amesema: “Mmoja wa wafuasiwake aliugua tukatoka kwenda kumtembelea nasi tukiwa na kundi lawafuasi wa Ja’far, ghafla tukakutana na Ja’far njiani, akatuambia:‘Mnaelekea wapi?’ tukasema tunakwenda kumtembelea fulani.Akatwambia: ‘Simameni.’ Tukasimama, ndipo akatuambia: ‘Je mmojawenu ana tufaha, pera au manukato au udi?’ tukasema hatuna chochote.Akasema: ‘Hivi hamjui kwamba mgonjwa hupata raha kwa kila ana-chopelekewa.”55

Hakika riwaya hii inatufichulia alama ya utamaduni wa kiislamu ambaounajali sana upande wa nafsi na kuingiza furaha moyoni mwa mgonjwa,ukiachia mbali ile faida na manufaa ya kimada anayoyapata. Hivyo utaonainasisitiza kumpelekea mgonjwa zawadi za matunda yenye rangi nzuri namanukato mazuri. Kama ambavyo inavyosisitiza udi na harufu nzuri kamaalama ya kuonyesha thamani ya uzuri na hisia za kisaikolojia ambazohuachwa na zawadi ndani ya nafsi ya mgonjwa.

69

Huduma ya Afya katika Uislamu

53 Kanzul-Ummal Juz. 9, Hadithi ya 25169.54 Kanzul-Ummal Juz. 9, Hadithi ya 25184.55 Mizanul-Hikma Uk. 129.

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 69

Page 76: Huduma ya Afya katika Uislamu

Na miongoni mwa mambo muhimu ya kisaikolojia ambayo yametiliwaumuhimu na adabu za kijamii za Uislamu ni kumsikilizisha mgonjwamaneno mazuri, kumuombea dua apone na kumsisitiza kuvuta subira,jambo ambalo huingiza ndani ya nafsi yake hisia za upendo na hisia zakujaliwa na wenzake, na hivyo kuongeza ari yake katika kupambana namaradhi na kupata matumaini na matarajio au kuyaimarisha ndani ya nafsiyake.

Hakika Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anatuelekeza kwenye muamala huu wakuamiliana na mgonjwa, anasema: “Hakika miongoni mwa namna zammoja wenu kutimiza hali ya kumtembelea ndugu yake ni aweke mkonowake juu yake, na amuulize alivyoamka na alivyoshinda.”56

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimtembelea sahaba mtukufuSalman, akasema: “Ewe Salman! Mwenyezi Mungu auponye ugonjwawako, akughofirie dhambi zako na akuafu katika dini yako na mwili wakompaka wakati wa kifo chako.”57

Uislamu katika maadili yake na adabu zake na misingi ya mahusiano yakeunapambika kwa heshima na kuheshimu adabu za kijamii, na kuuheshimuupendo wa nafsi ya mwanadamu, hivyo umetaka tupunguze muda wakumtembelea mgonjwa na kutokurefusha kikao kwa mgonjwa, hiyo ni ilikumpa muda wa kupumzika kimwili na kimawazo na kumpa usalama wakiafya yule mwenye kumtembelea. Kwani hakika baadhi ya watembeleajihumuudhi mgonjwa kwa sababu ya kurefusha ziara na kikao nakukithirisha mazungumzo, hivyo imekuja katika maelekezo ya MtukufuMtume kwamba alisema: “Mtembeleaji mgonjwa aliye bora kushinda woteni yule mwenye kuhafifisha.”58 Na pia alisema: “Kumtembelea mgonjwani kwa kadiri ya mpito wa ngamia.”59

70

Huduma ya Afya katika Uislamu

56 Kanzul-Ummal Juz. 9, Hadithi ya 25195.57 Kanzul-Ummal Juz. 9, Hadithi ya 25200.58 Kanzul-Irfan, Hadithi ya 25139.59 Kanzul-Irfan, Hadithi ya 25155.

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 70

Page 77: Huduma ya Afya katika Uislamu

Bali msisitizo wa kufupisha ziara na kupunguza muda wa kukaa kwamgonjwa unaongezeka pale mgonjwa anapokuwa hapendi kuzongwa,Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Hakika kumtembelea mgonjwa kuliko namalipo makubwa na kule kwa muda mfupi.”60 Na amesema: “Aliye namalipo makubwa kwa Mwenyezi Mungu kushinda wote wenye kumtem-belea mgonjwa ni yule ambaye anapomtembelea ndugu yake mgonjwahupunguza kikao, ila iwapo mgonjwa atapenda hilo au kulitaka, na akawaamemwomba kufanya hivyo.”61

Hivi ndivyo zinavyokamilika kanuni na misingi ya adabu za kijamii katikakumtembelea mgonjwa, adabu ambazo zinaoana na hali za kisaikolojia nakinafsi na ambazo zinatoa matokeo bora ya kijamii kiasi kwamba zina-pandikiza upendo, kujuliana hali na hisia za roho ya undugu na kusaidiana.

Na mwisho wa dua zetu ni kumshukuru Mwenyezi Mungu Mola Mlezi waviumbe wote.

71

Huduma ya Afya katika Uislamu

60 Kanzul-Irfan, Hadithi ya 25149.61 Mizanul-Hikma: Mgonjwa.

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 71

Page 78: Huduma ya Afya katika Uislamu

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NAAL-ITRAH FOUNDATION

1. Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thalathini

2. Uharamisho wa Riba3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza 4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili5. Hekaya za Bahlul6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.)7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.)8. Hijab vazi Bora9. Ukweli wa Shia Ithnaashari10. Madhambi Makuu11. Mbingu imenikirimu12. Abdallah Ibn Saba13. Khadijatul Kubra14. Utumwa15. Umakini katika Swala16. Misingi ya Maarifa17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia18. Bilal wa Afrika19. Abudharr20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu21. Salman Farsi22. Ammar Yasir23. Qur'an na Hadithi24. Elimu ya Nafsi

72

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 72

Page 79: Huduma ya Afya katika Uislamu

25. Yajue Madhehebu ya Shia26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu27. Al-Wahda28. Ponyo kutoka katika Qur'an. 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii30. Mashukio ya Akhera31. Al Amali32. Dua Indal Ahlul Bayt33. Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna.34. Haki za wanawake katika Uislamu35. Mwenyeezi Mungu na sifa zake36. Amateka Na Aba'Khalifa37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s)38. Adhana.39 Upendo katika Ukristo na Uislamu40. Nyuma yaho naje kuyoboka41. Amavu n’amavuko by’ubushiya42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya swala mbili44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya46. Kusujudu juu ya udongo47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s)48. Tarawehe49. Malumbano baina ya Sunni na Shia50. Kupunguza Swala safarini51. Kufungua safarini52. Umaasumu wa Manabii53. Qur’an inatoa changamoto54. as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm55. Uadilifu wa Masahaba

73

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 73

Page 80: Huduma ya Afya katika Uislamu

56. Dua e Kumayl57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume

Muhammad (s)61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili63. Kuzuru Makaburi64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita70. Tujifunze Misingi Ya Dini71. Sala ni Nguzo ya Dini72. Mikesha Ya Peshawar73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu74. Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia

iliyonyooka75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake76. Liqaa-u-llaah77. Muhammad (s) Mtume wa Allah78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 79. Uislamu Ulienea Vipi?80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81. Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 82. Urejeo (al-Raja’a )83. Mazingira84. Utokezo (al - Badau)

74

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 74

Page 81: Huduma ya Afya katika Uislamu

85. Sadaka yenye kuendelea 86. Msahafu wa Imam Ali87. Uislamu na dhana88. Mtoto mwema89. Adabu za Sokoni90. Johari za hekima kwa vijana91. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza92. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili93. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu94. Tawasali95. Imam Mahdi katika Usunni na Ushia96. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu97. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi98. Swala ya maiti na kumlilia maiti99. Shiya na Hadithi (kinyarwanda)100. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu101. Hadithi ya Thaqalain102 Fatima al-Zahra103. Tabaruku104. Sunan an-Nabii105. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza)106. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili)107. Mahdi katika sunna108. Kusalia Nabii (s.a.w)109. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza110. Ujumbe - Sehemu ya Pili111. Ujumbe - Sehemu ya Tatu

75

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 75

Page 82: Huduma ya Afya katika Uislamu

112. Ujumbe - Sehemu ya Nne113. Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa114. Iduwa ya Kumayili.115. Maarifa ya Kiislamu.116. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza117. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili118. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu119. Ukweli uliopotea sehmu ya Nne120. Ukweli uliopotea sehmu ya Tano121. Johari zenye hekima kwa vijana122. Safari ya kuifuata Nuru123. Idil Ghadiri124. Myahudi wa Kimataifa125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza127. Visa vya kweli sehemu ya Pili128. Muhadhara wa Maulamaa129. Mwanadamu na Mustakabali wake130. Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Kwanza131. Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Pili132. Khairul Bariyyah133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi134. Vijana ni Hazina ya Uislamu.135. Yafaayo kijamii136. Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu137. Taqiyya

76

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 76

Page 83: Huduma ya Afya katika Uislamu

138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje?140. Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Kwanza141. Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Pili142. Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah144. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu145. Kuonekana kwa Allah146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt

(Sehemu ya Kwanza)147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili)148. Ndugu na Jirani149. Ushia ndani ya Usunni150. Maswali na Majibu.151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 1153 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 2154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 3155. Abu Huraira156. Kati ya Alama kuu za dini Swala ya Jamaa.157. Mazingatio kutoka katika Qur’an sehemu ya Kwanza158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an sehemu ya Pili159. Mazingatio kutoka katika Uislamu sehemu ya kwanza160. Mazingatio kutoka katika Uislamu sehemu ya Pili161. Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi162. Falsafa ya mageuzi ya Imam Husein (a.s)163. Huduma ya Afya katika Uislamu

77

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 77

Page 84: Huduma ya Afya katika Uislamu

164. Hukumu za Mgonjwa165. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein166. Uislamu Safi167. Majlis ya Imam Husein168. Mshumaa169. Tiba ya Maradhi ya Kimaadili170. Uislam wa Shia

78

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 78

Page 85: Huduma ya Afya katika Uislamu

BACK COVER

Afya ya mwili kwa mwanadamu ni kitu muhimu sana. Ili mwanadamuaweze kuyajenga maisha yake na kuwa bora kimwili, lazima awe na afyabora, na sio tu kwa ajili ya kuendesha maisha yake, bali pia bila afya nzurimtu hawezi kutekeleza ibada zake sawasawa jinsi inavyotakiwa kuifanya.Hivyo, kama Uislamu ulivyo kwamba ni dini na ni mfumo kamili wamaisha, umeelezea kwa kina huduma ya afya, yaani mtu akiwa nini ili aji-patie afya njema.

Waandishi wa kitabu hiki wameelezea mambo mbalimbali ambayo yana-paswa kufanywa kwa ajili ya afya ya mtu binafsi na ya jamii kwa ujumla.Katika maelezo yao wamezingatia Qur’ani Tukufu, Sunna pamoja namafundisho ya Maimamu Watukufu.

Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wamaendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, nganoza kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tenakatika akili za watu.

Kimetolewa na kuchapishwa na:Alitrah FoundationS.L.P. 19701 Dar es Salaam, TanzaniaSimu: +255 22 2110640Simu/Nukushi: +255 22 2127555Barua Pepe: [email protected]: www.ibn-tv.comKatika mtandao: www.alitrah.info

79

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislam check Lubumba final.qxd 7/1/2011 4:26 PM Page 79