24
SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR WIZARA YA BIASHARA NA VIWANDA MKATABA WA UTOAJI WA HUDUMA KWA MTAKA HUDUMA RASIMU YA AWALI APRILI, 2018

WIZARA YA BIASHARA NA VIWANDAtradesmz.go.tz/Downloads/Mkataba.pdfWIZARA YA ARDHI NYUMBA MAJI NA NISHATI MKATABA WA UTOAJI WA HUDUMA. - Septemba, 2018 SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

  • Upload
    others

  • View
    96

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

                                                                       WIZARA  YA  ARDHI  NYUMBA  MAJI  NA  NISHATI    

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

WIZARA YA ARDHI NYUMBA MAJI NA NISHATI

MKATABA WA UTOAJI WA HUDUMA.

- Septemba, 2018

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

WIZARA YA BIASHARA NA VIWANDA

MKATABA WA UTOAJI WA HUDUMA KWA MTAKA HUDUMA

RASIMU YA AWALI

APRILI, 2018

YALIYOMO DIBAJI......................................................................................... 21. MAJUKUMU YA WIZARA .......................................... 41.1 DIRA ............................................................................... 51.2 DHAMIRA....................................................................... 51.3 HUDUMA ZETU ......................................................... 61.4 MADHUMUNI YA MKATABA ................................... 81.5 WATAKA HUDUMA WETU ......................................... 91.6 MAADILI YETU ............................................................ 92. AHADI ZA IDARA KWA WATAKA HUDUMA NA WADAU WETU .............................................................. 102.1 IDARA YA UENDESHAJI NA UTUMISHI .................. 102.1.1 Majukumu ....................................................................... 102.1.2 Ahadi za Idara:................................................................. 112.2 IDARA YA MIPANGO, SERA NA UTAFITI ................ 142.2.1 Majukumu ....................................................................... 142.2.2 Ahadi za Idara ................................................................. 142.3 IDARA YA BIASHARA NA UKUZAJI MASOKO....... 152.3.1 Majukumu ....................................................................... 152.3.2 Ahadi za Idara ................................................................. 152.4 IDARA YA MAENDELEO YA VIWANDA NA UKUZAJI UJASIRIAMALI .......................................... 1724.1 Majukumu........................................................................ 1724.1 Ahadi za Idara.................................................................. 17 3.0 WAJIBU WETU KWA MTAKA HUDUMA .................. 184.0 HAKI NA WAJIBU WA MTAKA HUDUMA................ 194.1 Haki ya Mtaka huduma ................................................... 194.2 Wajibu wa Mtaka huduma............................................... 20

1

DIBAJI

Mkataba wa Huduma kwa Mtaka huduma ni maazimio ya ahadi za Taasisi za utendaji wa ufanisi kwa umma. Kwa kutambua umuhimu wa Mkataba wa utoaji wa huduma kwa Mtaka huduma, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imetambua umuhimu wa kutumia Mkataba wa Huduma kwa Mtaka huduma kama dhana ya kuleta mabadiliko chanya katika uwajibikaji wa watendaji wake kwa umma. Hatua hii ya Serikali kuanzisha mabadiliko ya utendaji kupitia Mkataba wa Huduma kwa Mtaka huduma, ni changamoto kwa vyombo vyote vya umma kuwa na Mkataba wa Huduma kwa Mtaka huduma.

Kwa kuzingatia umuhimu huo, Wizara ya Biashara na Viwanda iliyoanzishwa kwa Tangazo Rasmi la Serikali mwezi Machi, 2018 na kukabidhiwa majukumu ya kusimamia na kuendeleza Sekta ya Biashara na Viwanda, imeamua kuandaa Mkataba wa Huduma kwa Mtaka huduma ili kutoa huduma bora kwa wadau wa sekta za biashara na viwanda.

Mkataba huu unaainisha huduma tunazotoa, viwango vya huduma ambavyo tunaamini wataka huduma wetu wana haki ya kupata, na pia kuelezea jinsi ya kupokea maoni au malalamiko na utatuzi wa matatizo pale yanapojitokeza na njia ya kuwasiliana na sisi.

Ni matarajio yetu kuwa tutatoa huduma bora na kwa wakati kulingana na viwango tulivyoahidi. Tunawashauri wateja na wadau wetu kwa ujumla kuufahamu Mkataba huu na kuutumia ipasavyo.

2

Tunawakaribisha wataka huduma na wadau wetu kutoa maoni katika kuboresha huduma zetu. Tunaamini Mkataba huu wa Huduma kwa Mtaka huduma utaimarisha mahusiano mazuri katika utendaji na utoaji huduma kwa umma.

Sahihi: ………………...............…… Mheshimiwa Balozi: Amina Salum Ali Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Tarehe: 10 Mei, 2018

3

1. MAJUKUMU YA WIZARA

i. Kuandaa Kuendeleza na kusimamia Utekelezaji wa Sera na Mipango mbali mbali za Taasisi zilizomo chini ya Wizara.

ii. Kusimamia na kuwaendeleza Watumishi katika Wizara

iii. Kusimamia Uendeshajii wa Rasilimali watu, Rasilimali fedha na Rasilmali nyengine pamoja na shughuli zote za Ofisi katika Wizara.

iv. Kuweka mazingira mazuri ya biashara na kuwapa moyo wafanyabiashara wa sekta binafsi na sekta ya Umma.

v. Kukuza uhusiano baina ya Serikali na Taasisi binafsi

vi. Kuhakikisha Ushindani Halali wa kibiashara kwa madhumuni ya kumlinda mtumiaji.

vii. Kukuza na kuendeleza Wafanyabiashara Wadogo na Wakati

viii. Kuhakikisha upatikanaji wa Soko la ndani na la nje kwa bidhaa zinazozalishwa nchini.

ix. Kuandaa mazingira mazuri kwa Wawekezaji binafsi katika Sekta ya Viwanda

4

x. Kuendeleza Viwanda Vidogo na vya Kati

xi. Kuhakikisha bidhaa na huduma zinazozalishwa au kuuzwa nchini zinakuwa na kiwango cha Kitaifa na Kimataifa

xii. Kusimamia na kuratibu shughuli za Utafiti zinazohusiana na Biashara, Masoko na Viwanda.

xiii. Kurahisisha usajili wa Biashara na Mali.

1.1 DIRA

Kuifanya Zanzibar kuwa kituo cha biashara na uzalishaji wa bidhaa za viwanda zenye ubora kwa lengo la kuchangia ukuaji wa uchumi endelevu.

1.2 DHAMIRA

Ili kujenga na kudumisha mazingira ya usawa na ushindani wa kibiashara, kilimo cha biashara na maendeleo ya viwanda, Wizara ya Biashara na Viwanda ina dhamira ifuatayo:

i. Kutunga na kufuatilia utekelezaji wa sera na sheria husika za Biashara, Masoko na maendeleo ya Viwanda;

ii. Kuanzisha mifumo ya kitaasisi kwa ajili ya kukuza uwekezaji wa viwanda, na kukuza ubora wa bidhaa katika masoko ya ndani na nje

5

iii. Kuitangaza Zanzibar katika medani ya Kibiashara ya kimataifa.

1.3 HUDUMA ZETU

i. Usajili wa Wafanyabiashara na Wajasiriamali.

ii. Urasimishaji wa Wafanyabiashara na Wajasiriamali

iii. Kutoa vibali vya usafirishaji wa biashara na bidhaa.

iv. Kutoa taarifa na takwimu sahihi za kibiashara

v. Ukaguzi wa maduka maghala na mabekari.

vi. Kuteketeza bidhaa zisizofaa kwa mahitaji ya binadamu.

vii. Kufanya Uhakiki wa Mizani na vipimo.

viii. Ukaguzi wa Vipimo na Bidhaa zilizofungashwa

ix. Kusuluhisha Migogoro ya kibiashara

x. Utoaji wa habari za biashara

xi. Kutoa taaluma na ushauri kwa wazalishaji wadogo wadogo na wa kibiashara

xii. Kutoa usaidizi juu ya maandiko ya miradi

6

xiii. Kufanya ukaguzi wa miradi ya viwanda vidogo vidogo, viwanda/miradi mikubwa na kutoa taarifa.

xiv. Kuweka kumbukumbu za maendeleo ya viwanda

xv. Kutoa usaidizi wa vifaa kwa wazalishaji wa wadogo wadogo

xvi. Kufanya utambuzi wa viwanda

xvii. Kuandaa na kusimamia Jukwaa la Biashara baina ya sekta ya Umma na sekta binafsi.

xviii. Kuandaa na kusimamia Viwango vya Ubora wa Bidhaa mbalimbali.

xix. Kuandaa bajeti ya Wizara.

xx. Kufanya Tafiti kwa Sekta za Biashara, Viwanda na Masoko.

xxi. Kusimamia na kuratibu mfumo wa utoaji wa leseni za Biashara kwa mamlaka za utoaji wa leseni.

xxii. Kusimamia utekelezaji wa Miradi ya Wizara.

xxiii. Kuandaa Miongozo na taratibu zinazopaswa kwa Mamlaka za utoaji leseni kufuatwa.

xxiv. Kuandaa Sera juu ya Usimamizi wa Masuala ya leseni, Ruhusa na Vibali.

7

xxv. Kutoa Ushauri kwa Mamlaka za leseni juu ya kufuata kanuni za Uendeshaji Biashara unaozingatia masuala ya urahisi wa upatikanaji wa leseni.

xxvi. Kuandaa sera, sheria, kanuni na miongozo inayosimamia uendeshaji na usimamizi wa biashara.

xxvii. Kuandaa sera, sheria, kanuni na miongozo inayosimamia uanzishaji, uendeshaji na usimamizi wa viwanda.

xxviii. Kuandaa sheria, kanuni na miongozo inayosimamia uendeshaji wa masoko ya jumla na rejareja.

xxix Kusimamia masuala ya Ushindani halali wa Biashara na Kumlinda Mtumiaji.

1.4 MADHUMUNI YA MKATABA

Madhumuni ya Mkataba huu ni kukuza kiwango cha uelewa wa wataka huduma na wadau wetu kuhusu upatikanaji wa huduma zetu, ubora na viwango vyake. Vilevile, Mkataba huu unalenga katika kuboresha utendaji kazi na unaweka wazi utaratibu wa kupokea na kushughulikia maoni na malalamiko pale ambapo huduma zinazotolewa hazikidhi matarajio ya wataka huduma.

8

1.5 WATAKA HUDUMA WETU

i. Jamii

ii. Mashirika/Taasisi za Umma

iii. Viwanda/ Wasindikaji

iv. Wizara na Idara za Serikali

v. Asasi zisizo za Kiserikali

vi. Sekta Binafsi Ndani na nje ya nchi

vii. Washirika wa Maendeleo

viii. Wanafunzi wa Vyuo vikuu, Wataalam na Watafiti

ix. Wawekezaji

x. Vyombo vya Habari

xi. Wanasiasa

xii. Wavuvi, wafanyabiashara wakulima na wajasiriamali.

xiii. Watumishi wa Wizara.

1.6 MAADILI YETU

i. Kufanya kazi kwa ushirikiano;

ii. Kufanya kazi kwa kujituma;

9

iii. Kufanya kazi kwa kuzingatia muda na mpango kazi;

iv. Kuzingatia maadili ya kitaalam;

v. Kutoa huduma kwa uwazi;

vi. Kutoa huduma kwa uadilifu na uaminifu;

vii. Kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu;

viii. Kuzingatia matumizi bora ya rasilimali za Serikali;

ix. Kujiheshimu na kuheshimiana;

x. Kuwa wabunifu;

xi. Kuzingatia maslahi mapana ya jamii na Taifa; na

xii. Kuzingatia na kutimiza wajibu wa Utumishi wa Umma.

2. AHADI ZA IDARA KWA WATAKA HUDUMA NA WADAU WETU

Ofisi yetu inaahidi kutoa huduma kupitia Idara zake kama ifuatavyo:

2.1 IDARA YA UENDESHAJI NA UTUMISHI

2.1.1 Majukumu Majukumu ya Idara hii ni kuziwezesha Idara na Taasisi za Wizara kufanyakazi zake vizuri kwa kutoa huduma

10

za kiutumishi kama vile kushughulikia ajira, kusimamia rasilimali za Wizara, kuendeleza na kuelimisha rasilimali watu pamoja na kutoa haki na maslahi ya watumishi. Aidha Idara inajukumu la kutunza, kuhuisha, kuhifadhi kumbukumbu na kutoa huduma za kiutawala ili kuhakikisha mazingira mazuri ya kufanya kazi.

2.1.2 Ahadi za Idara:

i. Kutafuta jalada na kuliwasilisha kwa mhusika ndani ya Wizara ndani ya dakika (15) tangu ombi kupokelewa masjala,

ii. Kufanya taratibu za marekebisho ya mishahara ndani ya siku tatu (3) za kazi baada ya vielelezo vyote kukamilika,

iii. Kutoa barua ya maombi ya mikopo kwa watumishi kwenda taasisi ya kifedha ndani ya siku mbili (2) za kazi baada ya kupokea fomu ya maombi,

iv. Kutoa tangazo la wito kwa watumishi waliofanikiwa kujaza nafasi za ajira ndani ya siku tatu (3) za kazi baada ya kukamilika kwa taratibu za ajira,

v. Kutoa barua/madokezo ya watumishi wanaohitaji ufafanuzi wa kiutumishi ndani ya siku tatu (3) za kazi baada ya kupokea barua/dokezo,

vi. Kutoa barua za kupandishwa vyeo, kuthibitishwa kazi, likizo bila ya malipo na kuongezewa muda wa

11

kuendelea na kazi kwa watumishi ndani ya siku saba (7) za kazi baada ya taratibu kukamilika na kuidhinishwa na Tume ya Utumishi Serikalini,

vii. Kujibu barua ya maombi za likizo ndani ya siku mbili (2) za kazi baada ya kupokea maombi yaliyokubalika kutoka kwa Katibu Mkuu,

viii. Kuhifadhi barua za nje kwenye majalada baada ya kutoka kwa Waziri/Katibu Mkuu ndani ya masaa manne (4) ya kazi,

ix. Kuandaa na kusambaza ajenda na mihutasari ya vikao vinavyohusu masuala ya uendeshaji na kuitumishi ndani ya siku mbili (2) kabla ya kikao,

x. Kuandaa na kusambaza maagizo ya vikao mbali mbali ndani ya siku tatu (3) baada ya kikao,

xi. Kutoa barua za maombi ya Pasi za Kusafiria za Utumishi (Diplomatic/Service /Ordinary Passports), kuongezea muda wa pasi za kusafiria na kubadili hadhi ya pasipoti katika muda wa siku tano (5) za kazi baada ya kupokea kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi,

xii. Kupitia matumizi ya Ofisi kabla ya malipo ndani ya siku mbili (2) za kazi,

xiii. Kufanya ukaguzi wa matumizi ya mahesabu kila baada ya miezi mitatu (3),

12

xiv. Kutoa ripoti ya ukaguzi wa hesabu kila baada ya miezi mitatu (3),

xv. Kuandaa Makala na utayarishaji wa vipindi kila baada ya miezi mitatu (3),

xvi. Kutoa taarifa mbali mbali kupitia vyombo vya habari zinazohusiana na shughuli za Ofisi kila inapohitajika,

xvii. Kuaandaa vocha za malipo ndani ya siku moja (1) baada ya kupokea dokezo,

xviii. Kuandaa malipo ndani ya siku moja (1) baada ya kukamilisha zoezi la kupiga vocha kwa “manual” na kuingiza kwenye system (Hazina),

xix. Kufanya malipo ndani ya masaa matano (5) ya kazi baada ya kuvunja hundi,

xx. Kutoa risiti papo hapo baada ya kupokea fedha,

xxi. Kuweka kumbukumbu za kupokea vifaa kutoka kwa msambazaji “Suppliers” ndani ya siku moja (1) baada ya vifaa kuwasili,

xxii. Kutoa mafunzo kwa wafanyakazi kila mwaka kwa kuzingatia mpango wa mafunzo uliotayarishwa na Wizara.

13

2.2 IDARA YA MIPANGO, SERA NA UTAFITI

2.2.1 Majukumu Majukumu makuu ya Idara hii ni kufanya utafiti kwa ajili ya kuendeleza Sekta ya Biashara na Viwanda, kuandaa Sera, Mipango na Mikakati ya Wizara na kuratibu mahusiano na mashirikiano ya Wizara na taasisi nyengine za umma na sekta binafsi pamoja na washirika wa maendeleo.

2.2.2 Ahadi za Idara

i. Kufuatilia utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ya Wizara kwa kila siku ya kazi.

ii. Kutoa ripoti ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ya wizara ndani ya siku saba (7) za kazi baada ya Ufuatiliaji kukamilika.

iii. Kusimamia Mfumo wa Matumizi ya Kompyuta kwa kila siku ya kazi.

iv. Kukusanya Takwimu za Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini za Wizara ndani ya siku thelathini (30) za kazi baada ya kazi au Mradi kumaliza.

v. Kuandaa Tafiti zinazohusiana na sekta ya Biashara na Viwanda ndani ya siku thelathini (30) za kazi baada ya kuidhinishwa na kuthibitishwa Utafiti huo.

vi. Kutoa ushauri kwa jamii kuhusu Tafiti na Takwimu za Wizara kila inapohitajika

14

vii. Kuchambua utekelezaji wa sera za kitaifa na kuzifikisha kwa wadau ndani ya siku saba (7) za kazi baada ya kupokea muongozo kutoka Taasisi husika.

viii. Kuandaa Ripoti za Utekelezaji wa kazi za Wizara kila baada ya kipindi cha robo mwaka.

ix. Kubuni na kuandaa mipango na miradi mipya ya maendeleo kufuatia changamoto za kisekta kila zinapojitokeza.

2.3 IDARA YA BIASHARA NA UKUZAJI MASOKO

2.3.1 Majukumu

Idara ya Biashara na Ukuzaji Masoko ina jukumu la kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara, kusimamia mwenendo wa biashara na kumlinda mtumiaji, kukuza na kuendeleza masoko ya bidhaa na huduma, kufanya ukaguzi wa bei na bidhaa na kukusanya Mapato ya Wizara.Uhakiki na ukaguzi wa mizani na vipimo kwa mujibu wa sheria na kanuni za biashara.

2.3.2 Ahadi za Idara

i. Kupokea maombi ya usafirishaji wa bidhaa kwa muda wowote wa kazi.

ii. Kuzingatia maombi na kutoa majibu ya maombi ya usafirishaji wa bidhaa ndani ya siku tatu (3) za kazi baada kupokea maombi hayo.

15

iii. Kupokea maombi ya ushauri wa kibiashara muda wote wa kazi.

iv. Kutoa ushauri wa kibiashara mara tu baada ya kupokea maombi.

v. Kukusanya na kuzihifadhi taarifa za usafirishaji na uingizaji wa bidhaa kutoka vyanzo vyake kila siku za kazi.

vi. Kukusanya taarifa za uingizaji wa bidhaa muhimu za chakula (Mchele, Unga wa Ngano na Sukari) kutoka nje na ndani ya siku na saa za kazi baada ya Bidhaa kuwasili bandarini

vii. Kufanyia kazi maombi ya Hati ya Usajili wa usafirishaji na uagiziaji wa bidhaa kutoka kwa mfanyabiashara ndani ya siku na saa za kazi baada ya maombi kuwasilishwa.

viii. Kuzingatia maombi na kutoa Hati ya usajili wa wasafirishaji na waagiziaji bidhaa ndani ya siku tatu (3) za kazi baada ya maombi kuwasilishwa na kufanyiwa kazi

ix. Kufanya ukaguzi wa bidhaa madukani na maghalani katika shehia husika ndani ya siku na saa za kazi.

x. Kufanya uangamizaji wa bidhaa zilizoharibika au zisizofaa kwa matumizi ya binaadamu kila baada ya miezi mitatu (3).

16

xi. Kufanya ukaguzi wa Vipimo na Mizani katika Shehia husika ndani ya siku na saa za kazi.

xii. Kufanya uhakiki wa vipimo na mizani kwenye depots vituo nya mafuta na gesi na viwandani.

xiii. Kukagua bidhaa zilizofungashwa.

2.4 IDARA YA MAENDELEO YA VIWANDA NA UKUZAJI UJASIRIAMALI

2.4.1 Majukumu:

Idara hii ina jukumu la kusimamia Sera za kukuza Maendeleo ya Viwanda, Ujasiriamali, na kufanya Ukaguzi wa Miradi ya Viwanda na Uzalishaji. Aidha Idara inajukumu kushajihisha uanzishaji wa viwanda kwa maeneo tengefu Wilayani na kusimamia uendelezaji wa maeneo hayo kwa mujibu wa sera na sheria ya viwanda.

2.4.2 Ahadi za Idara

i. Kupokea maombi ya usaidizi wa kitaaluma na vifaa kutoka kwa wajasiriamali ndani ya siku na saa za kazi kila inapohitajika

ii. Kutoa majibu ya maombi ya usaidizi wa kitaaluma na vifaa kwa wajasiriamali ndani ya muda wa siku tatu (3) baada ya kupokea maombi.

iii. Kufanya ukaguzi kwenye viwanda/miradi na kutoa ushauri ndani ya siku na saa za kazi

17

iv. Kutoa usaidizi wa kuandika Miradi ndani ya siku thelathini (30) za kazi baada ya kupokea maombi.

v. Kutoa taarifa kwa wenye Viwanda/Miradi ndani ya siku saba (7) kabla ya kufanya ukaguzi rasmi.

vi. Kufanya ukaguzi Viwanda Vikubwa na Vidogo na kutoa Ushauri elekezi kila siku na saa za kazi pale inapohitajika.

vii. Kutoa ripoti ya ukaguzi wa Viwanda ndani ya siku saba (7) baada ya kufanya ukaguzi.

viii. Kutoa taarifa za Viwanda kwa watafiti na wanaozihitaji tafiti hizo ndani ya siku saba (7) baada ya kupokea kibali.

ix. Kupitia maombi na kutoa majibu ya usaidizi wa vifaa kwa wajasiriamali wadogo wadogo ndani ya siku siku saba (7) za kazi baada ya maombi hayo kukamilika.

x. Kukusanya taarifa za utendaji za mwaka na robo mwaka kutoka kwa wadau.

3.0 WAJIBU WETU KWA MTAKA HUDUMA

Kuhakikisha kwamba tunakuwa na Mahusiano mazuri na wataka huduma wetu na kutoa huduma zinazozingatia viwango kama ifuatavyo: -

i. Kutoa huduma bora za kitaalam kwa ufanisi katika muda muafaka;

18

ii. Kutoa taarifa sahihi za kuaminika na kwa lugha rahisi inayoeleweka;

iii. Kushirikisha wataka huduma na wadau katika mashauriano ya kuboresha huduma zetu;

iv. Kutumia teknolojia sahihi katika utoaji wa huduma kwa jamii, ikiwemo makundi maalum;

v. Kuzingatia utunzaji na matumizi bora ya rasilimali kwa faida ya jamii;

vi. Kujiepusha kuomba, kupokea na kutoa rushwa;

vii. Kuwa na heshima na kauli nzuri kwa wataka huduma.

4.0 HAKI NA WAJIBU WA MTAKA HUDUMA

4.1 Haki ya Mtaka Huduma

i. Kupewa taarifa sahihi na kwa wakati;

ii. Kupata huduma bora na kwa wakati muafaka;

iii. Kutoa/ kuwasilisha maoni, pongezi au malalamiko; na

iv. Kupata faragha na kutunziwa siri zinazohusu huduma aliyopewa na Wizara.

19

4.2 Wajibu wa Mtaka Huduma

i. Kuwa na heshima na kauli nzuri kwa Watumishi

ii. Kutoa taarifa sahihi na kwa wakati.

iii. Kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika kupata huduma.

iv. Kutokutoa, kutokupokea wala kuomba rushwa kwa Watumishi

v. Kuitikia wito pale anapohitajika.

MAWASILIANO YA TAASISI

Katibu Mkuu,Wizara ya Biashara na Viwanda,S.L.P 601Phone: +255-24-22348443Fax: +255 24 2230605Email: [email protected] Tanzania. Afisa Mdhamini,Wizara ya Biashara na Viwanda,Afisi Kuu Pemba,S. L. P. 199 WETE - PEMBAFax: +255 24 2454149Tel: +255242454149Phone: +255773186448Email: [email protected]– Tanzania

20