16
1 YALIYOMO YALIYOMO ................................................................................................................................... 1 SURA YA KWANZA: MISINGI YA KUFUNDISHIA LUGHA .............................................. 2 Utangulizi: ............................................................................................................................... 2 Lugha ni nini? .......................................................................................................................... 2 SIFA AU TABIA ZA LUGHA ............................................................................................................ 2 i.Lugha ni sauti za binadamu zenye maana ............................................................................. 2 ii. Lugha ni sauti nasibu ........................................................................................................... 2 iii.Lugha ni mfumo maalum wa sauti ...................................................................................... 2 iv Lugha ni mali ya binadamu ................................................................................................. 3 v.Lugha hubadilika .................................................................................................................. 3 vi Lugha huathiri na kuathiriwa............................................................................................... 3 vii. Lugha hupitia mfumo wa kuishi ........................................................................................ 3 Viii .Lugha hufungamana na utamaduni wa jamii fulani ........................................................ 4 DHIMA ZA LUGHA .................................................................................................................. 4 i.Lugha ni chombo cha mawasiliano ....................................................................................... 4 i i Lugha ni kitambulisho ...................................................................................................... 4 iii Lugha ni chombo cha kuunganisha watu ......................................................................... 5 iv Lugha ni chombo cha kurithishia utamaduni wa jamii ................................................... 5 vi Lugha ni chombo cha kutolea elimu na mafunzo ............................................................... 5 KUFASILI LUGHA .................................................................................................................... 6 SIFA ZA MFASIRI BORA .................................................................................................................. 6 MSINGI WA KUJIFUNZA LUGHA..................................................................................................... 6 1Kuchagua ............................................................................................................................... 7 2. Kuyahusisha na maneo mengine ......................................................................................... 7 3. Kupitia ................................................................................................................................. 7 4. Kuhifadhi ............................................................................................................................. 8 5. Matumizi .............................................................................................................................. 8 NJIA ZA KUJIFUNZIA LUGHA ............................................................................................... 8 ............................................................................................ 8 ................................................................................. 8 ................................................................................. 8 SURA YA PILI: .......................................................................................................................... 9 MBINU ZINAZOFAA KUFUNDISHIA ISIMU........................................................................ 9 ISIMU.......................................................................................................................................... 9 Matawi ya Isimu ...................................................................................................................... 9 a)Isimu Fafanuzi/Elezi ............................................................................................................. 9 b)Isimu Historia ....................................................................................................................... 9 c)Isimu Linganishi ................................................................................................................. 10

YALIYOMO · 5 mmoja kati ya watu wa itikadi ipi, jamii ipi au taifa gani. Kwa mfano mtu akiongea Kiswahili awapo katika mataifa mengine hubainika moja kwa moja kuwa ni wa Afrika ya

  • Upload
    others

  • View
    12

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: YALIYOMO · 5 mmoja kati ya watu wa itikadi ipi, jamii ipi au taifa gani. Kwa mfano mtu akiongea Kiswahili awapo katika mataifa mengine hubainika moja kwa moja kuwa ni wa Afrika ya

1

YALIYOMO

YALIYOMO ................................................................................................................................... 1

SURA YA KWANZA: MISINGI YA KUFUNDISHIA LUGHA .............................................. 2

Utangulizi: ............................................................................................................................... 2

Lugha ni nini? .......................................................................................................................... 2

SIFA AU TABIA ZA LUGHA ............................................................................................................ 2

i.Lugha ni sauti za binadamu zenye maana ............................................................................. 2

ii. Lugha ni sauti nasibu ........................................................................................................... 2

iii.Lugha ni mfumo maalum wa sauti ...................................................................................... 2

iv Lugha ni mali ya binadamu ................................................................................................. 3

v.Lugha hubadilika .................................................................................................................. 3

vi Lugha huathiri na kuathiriwa ............................................................................................... 3

vii. Lugha hupitia mfumo wa kuishi ........................................................................................ 3

Viii .Lugha hufungamana na utamaduni wa jamii fulani ........................................................ 4

DHIMA ZA LUGHA .................................................................................................................. 4

i.Lugha ni chombo cha mawasiliano ....................................................................................... 4

i i Lugha ni kitambulisho ...................................................................................................... 4

iii Lugha ni chombo cha kuunganisha watu ......................................................................... 5

iv Lugha ni chombo cha kurithishia utamaduni wa jamii ................................................... 5

vi Lugha ni chombo cha kutolea elimu na mafunzo ............................................................... 5

KUFASILI LUGHA .................................................................................................................... 6

SIFA ZA MFASIRI BORA .................................................................................................................. 6

MSINGI WA KUJIFUNZA LUGHA ..................................................................................................... 6

1Kuchagua ............................................................................................................................... 7

2. Kuyahusisha na maneo mengine ......................................................................................... 7

3. Kupitia ................................................................................................................................. 7

4. Kuhifadhi ............................................................................................................................. 8

5. Matumizi .............................................................................................................................. 8

NJIA ZA KUJIFUNZIA LUGHA ............................................................................................... 8

............................................................................................ 8

................................................................................. 8

................................................................................. 8

SURA YA PILI: .......................................................................................................................... 9

MBINU ZINAZOFAA KUFUNDISHIA ISIMU ........................................................................ 9

ISIMU.......................................................................................................................................... 9

Matawi ya Isimu ...................................................................................................................... 9

a)Isimu Fafanuzi/Elezi ............................................................................................................. 9

b)Isimu Historia ....................................................................................................................... 9

c)Isimu Linganishi ................................................................................................................. 10

Page 2: YALIYOMO · 5 mmoja kati ya watu wa itikadi ipi, jamii ipi au taifa gani. Kwa mfano mtu akiongea Kiswahili awapo katika mataifa mengine hubainika moja kwa moja kuwa ni wa Afrika ya

2

d)Isimujamii........................................................................................................................... 10

SURA YA KWANZA:

MISINGI YA KUFUNDISHIA LUGHA

Utangulizi:

Ili kujifunza vizuri juu ya mada hii yatupasa kujua kwanza maana rasmi ya lugha na sifa

zake.kufanya marejereo ya kina juu ya maana ya rasmi ya lugha, sifa zake na dhima zake katika

jamii.

Lugha ni nini?

Lugha ni mfumo maalum wa sauti nasibu zenye maana ambazo hutumiwa miongoni mwa

binadamu kwa ajili ya kukidhi malengo ya kimawasiliano miongoni mwa watumiaji husika.

Kutokana na fasili hiyo, kwa muhtasari lugha ni sauti nasibu, lugha ni mfumo maalum, lugha

inamhusu binadamu, lugha hutumika kwa ajili ya kuwasiliana. Dhana hizi zitajipambanua zaidi

katika sehemu inayofuata (Sifa za Lugha).

Sifa au tabia za Lugha

i.Lugha ni sauti za binadamu zenye maana

Lugha ni sauti zinazozalishwa na binadamu kwa kutumia ala za sauti kama vile ulimi, midomo

ufizi, kaakaa laini, kaakaa gumu, meno, koromeo na viungo vinginevyo; sauti hizi huanzia kama

irabu na konsonanti. Sauti hizi ili kuitwa lugha lazima ziwe na maana na kueleweka kwa

watumiaji wake. Na hii ndio sifa muhimu kuitofautisha lugha ya binadamu na mawasiliano ya

viumbe hai wengine.

ii. Lugha ni sauti nasibu

Tunasema lugha ni nasibu kwa sababu hizi huzuka kwa nadra tu (bila kukusudiwa) na hazina

uhusiano wa moja kwa moja na mkile kinachorejelewa. Kwa maana nyingine hakuna

makubaliano au mikakati ya pamoja katika kuamua utokeaji wa sauti hizi.

iii.Lugha ni mfumo maalum wa sauti

Hii ni kwa sababu sauti hizi ziitwazo lugha hutokea katika utaratibu maalum unaoanzia kiwango

cha chini mpaka kiwango cha juu zaidi. Sauti hizi huanzia katika upekepeke kama irabu au

konsonanti, kisha huunda neno, kirai (kikundi cha maneno), kishazi na hatimaye sentensi

(tungo). Katika viwango vyote, yaani Kiwango cha Sauti (Fonolojia), Kiwango cha Maumbo

(Mofolojia), Kiwango cha Miundo (Sintaksia), Kiwango cha Maana (Semantiki) na Kiwango cha

Isimu Amali (Pragmatiki) kunakuwa na kanuni maalum.

Page 3: YALIYOMO · 5 mmoja kati ya watu wa itikadi ipi, jamii ipi au taifa gani. Kwa mfano mtu akiongea Kiswahili awapo katika mataifa mengine hubainika moja kwa moja kuwa ni wa Afrika ya

3

iv Lugha ni mali ya binadamu

Hakuna kiumbe kingine zaidi ya binadamu kinachotumia lugha. Licha ya kuwa viumbe wengine

(ambao si binadamu) hawahusiani na huwasiliana, mawasiliano yao si lugha bali ni ishara, sauti

na namna mbalimbali za kuwasiliania lakini hawana lugha. Kwa hivyo lugha ni mali ya kipekee

ya binadamu kwa sababu ndiye kiumbe pekee mwenye uwezo wa kuzalisha lugha kwa kuwa

ndiye mwenye viungo pekee vyenye uwezo huo.

v.Lugha hubadilika

Lugha yoyote hupokea au kupitia mabadiliko kutokana na wakati na mazingira. Mabadiliko haya

hutokea katika viwango vyote vya lugha kama ifuatavyo:

a. Mabadiliko ya kifonolojia

Haya ni mabadiliko ya kanuni au mfumo wa matamshi katika lugha. Mara nyingi yanatokana na

lugha kukopa misamiati ambayo ina sauti zisizopatikana katika lugha inayokopa au mabadiliko

mengineyo.

b. Mabadiliko ya kimofolojia

Hay hutokea pale ambapo lugha fulani hubadilika katika utaratibu wake wa kimaumbo hususani

katika kanuni za uundaji wa maneno.

c. Mabadiliko ya kileksia na kimaana

Haya ni mabadiliko katika leksimu au maana katika lugha husika, kwa mfano kuongezeka kwa

leksimu hutokana na njia au mbinu zote za uundaji wa maneno. Leksimu inapoongezeka na

maana huongezeka kwa kuwa huja na dhana (maana) inayowakilishwa.

d. Mabadiliko ya kisintaksia

Haya ni mabadiliko ya kimiundo ambapo lugha hubadilika katika utaratibu tofauti na ule

uliokuwepo awali.

vi Lugha huathiri na kuathiriwa

Lugha yoyote inaweza kuathiri utaratibu wa lugha nyingine, kadhalika lugha hiyo hiyo inaweza

kuathiriwa na lugha nyingine katika kiwango, viwangu fulani au viwango vyote vya lugha. Rejea

katika sifa ya mabadiliko.

vii. Lugha hupitia mfumo wa kuishi

Lugha hupitia awamu karibu zote za maisha ya viumbe hai kama vile binadamu, wanyama,

mimea na vinginevyo. Hatua hizi ni kama ifuatavyo:

a. Lugha huzaliwa

Hii ni punde lugha inapoibuka.

b. Lugha inakuwa

Lugh iikishazaliwa hukua, na kukua kwake ni pale inapojitanua kwa kujiongezea msamiati na

(au) matumizi.

Page 4: YALIYOMO · 5 mmoja kati ya watu wa itikadi ipi, jamii ipi au taifa gani. Kwa mfano mtu akiongea Kiswahili awapo katika mataifa mengine hubainika moja kwa moja kuwa ni wa Afrika ya

4

c. Lugha ianweza kufa

Kufa kwa lugha ni aple inapokosa watumiaji au kutotumika kwa sababu mbalimbali.

Lugha yoyote ina hadhi sawa na nyingine na hujitosheleza

Lugha zote duniani zina hadhi sawa kwa sababu zinajitosheleza kwa sababu hukidhi mahitaji ya

wtumiaji wake katika nyanja zote za maisha ikiwemo kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na kijamii.

d. Lugha hujizalisha

Lugha yoyote hujiongezea msamiati kupitia njia maalum za uundaji wa maneno/msamiati/istilahi

ikiwemo Kutohoa au Kukopa, Ufupishaji, Ufananishaji wa umbo au sauti, Urudufishaji, na njia

nyinginezo.

Viii .Lugha hufungamana na utamaduni wa jamii fulani

Lugha ni sehemu ya utamaduni wa jamii ya watumiaji wake na ni nyenzo ya kuhifadhia na

kurithisha utamaduni wote kwa ujumla. Kadhalika, lugha hutumika kuendana na kwa kukidhi

shughuli na mambo yote katika maisha ya kila siku.

DHIMA ZA LUGHA

i.Lugha ni chombo cha mawasiliano

Lugha hutumika kupashana habari, kuwasilisha dhana au fikra walizo nazo binadamu, hisia

kama vile furaha, huzuni, hasira, maarifa na uhalisia mwingine wa kimaisha kupitia kutoa na

kupokea ujumbe.

i i Lugha ni kitambulisho

Kupitia lugha tunaweza kumtambua na kumfahamu zaidi mtu au jamii. Utambulisho huo

waweza kuwa katika namna mbili kama ifuatavyo:

a. Utambulisho wa mtu binafsi

Kupitia matumizi ya lugha tunaweza kubaini jinsi ya mtu (ni wa kike au ni wa kiume) hata kama

hatujamuona ana kwa ana, yaani hata kama tunaona alichokiandika. Kwa mfano wanaume kwa

kiasi kikubwa hutumia lugha isiyofasaha ukilinganisha na wanawake, pia wanaume hutumia

ubabe katika mazungumzo hasa majadiliano ikiwemo kumkatisha mzungumzaji mwenzake bila

kumwacha amalize (yaani hukiuka kwa kiasi kikubwa utaratibu wa kuachiana nafasi katika

mazungumzo ukilinganisha na jinsi ya kike). Pia kupitia lugha tunaweza kung‟amua falsafa,

mtazamo, umri, kiwango cha elimu, hulka na tabia nyinginezo. Kwa mfano mtu mwenye tabia ya

unyanyasaji tutambaini katika mazungumzo na kadhalika.

b. Utambulisho wa kikundi cha watu, jamii au taifa

Kupitia lugha tuanweza kufahamu mengi kuhusiana na watu fulani, utaratibu wao, falsafa yao,

itikadi yao na kile wanachokiamini. Hivyo, kupitia lugha tunaweza kufahamu kuwa mtu ni

Page 5: YALIYOMO · 5 mmoja kati ya watu wa itikadi ipi, jamii ipi au taifa gani. Kwa mfano mtu akiongea Kiswahili awapo katika mataifa mengine hubainika moja kwa moja kuwa ni wa Afrika ya

5

mmoja kati ya watu wa itikadi ipi, jamii ipi au taifa gani. Kwa mfano mtu akiongea Kiswahili

awapo katika mataifa mengine hubainika moja kwa moja kuwa ni wa Afrika ya Mashariki

hususani nchini Tanzania au Kenya. Vile vile tunaweza kufahamu kuwa mtu ni wa dini au dhebu

gani, chama gani cha siasa, kabila au taifa gani. Yote ni kwa sababu kundi tunalomuweka

linafanana kwa namna fulani ya lugha.

iii Lugha ni chombo cha kuunganisha watu

Lugha hupatanisha watu na kuwaweka pamoja mtu na mtu, mtu na watu, watu na watu au jamii

na jamii. Kwa mfano kupitia salamu au kauli mbiu ya aina moja watu wanajikia kuwa ni

wamoja, wako pamoja na wenye nia sawa ya kimaisha. Rejea nchini Tanzania, lugha ya

Kiswahili ndio nyenzo pekee iliyotumika kuwaunganisha watanzania kudai uhuru, pamoja na

kuungana kuijenga nchi yao.

iv Lugha ni chombo cha kurithishia utamaduni wa jamii

Lugha hutumika kuendeleza na kudumisha mila, desturi, na amali za jamii kutoka kizazi hadi

kizazi kupitia misemo na nyenzo nyinginezo zitumiazo lugha. Lugha ndio itunzayo

kumbukumbu yamatambiko, miiko pamoja na mila na desturi nyinginezo.

v Lugha ni nyenzo ya kulinda, kuimarisha na kurejesha amani

Lugha hudumisha utulivu, kuheshimiana, kuvumiliana na kuthamiana bila hofu yoyote. Kwa

mfano kupitia kampeni za kuimiza kulinda amani kama vile “Tuilinde Amani ya Nchi Yetu”,

“Tanzania ni Kisiwa cha Amani” na nyingine kama hizo, kauli mbiu kama hizi hutumika

kuimarisha amani katika nchi zetu. Kadhalika, pale inapotokea tishio la kutoweka kwa amani, ni

lugha ndiyo inayotumika kurejesha ikiwemo kutumika kupatanisha makundi asimu, na mamlaka

ya ulinzi wa amani kutoa matumaini kwa watu wake juu ya kurejea tena kwa amani.

vi Lugha ni chombo cha kutolea elimu na mafunzo

Binadamu hutumia lugha kupata elimu na kuuelewa ulimwengu ili kuuishi ipasavyo kupitia

kufundisha na kujifunza.

Athari ya Matumizi Mabaya ya Lugha

Lugha ikitumika vibaya huwa kinyume na dhima mbalimbali tunazozifahamu na hupelekea

yafuatayo (baadhi tu)

i. Lugha inaweza kutumika kukandamiza uhuru wa mtu au taifa

ii. Lugha inaweza kuwatenganisha watu, jumuiya, jamii au taifa (au inaweza kutumiwa kwa

lengo hilo).

iii. Lugha inaweza kuwa chanzo cha kuvuruga amani kama chanzo cha migogoro

iv. Lugha inaweza kuleta utabaka na ubinafsi katika jamii

Page 6: YALIYOMO · 5 mmoja kati ya watu wa itikadi ipi, jamii ipi au taifa gani. Kwa mfano mtu akiongea Kiswahili awapo katika mataifa mengine hubainika moja kwa moja kuwa ni wa Afrika ya

6

v. Lugha inaweza kukwamisha maendeleo ya jamii (pale inapotumika vibaya)

vi. Lugha inaweza kutumika kunyanyapaa, kudunisha na kuwabagua watu wengine.

KUFASILI LUGHA Fasili ni istilahi inayotokana na kitendo cha kufasili; mantiki yake ni kutoa maana, dhana

maelezo au ufafanuzi juu ya jambo fulani, kutoa maelezo ya kuhusu mana ya neno/maneno.

Mfano Kamusi ni mfano mzuri wa matini ianayofasili mismiati ya kiswahili japo pia, Kamusi

inatafsiri misamiati isiyo na asili ya kibantu. kwa hiyo, fasili au kufasili ni kutoa maana au dhana

ya jambo/kitu fulani kinachohitaji ufafanuzi.

Mshindo (2010:2) ansema kufasiri ni kufafanua maana ya matini moja na kutayarisha baadae

matini nyingine inayowiana nayo ambayo huitwa tafsiri na ambayo inawakilisha ujumbe uleule

uliomo katika matini ya awali kwa kutumia lugha nyingine.

Kwa mfano. Kusoma (kiswahili) reading (kiingereza)

Sifa za mfasiri bora

Mfasiri bora anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:

Awe mahiri wa lugha husika, hii ina maana kuwa awe anajua kwa ufasaha lugha zote mbili, yaani

lugha chanzi na lugha lengwa. Hii ni kujua vizuri nyanja mbalimbali za Isimu ya lugha husika

kama vile; Fonolojia-{Matamshi}, Mofolojia-{Maumbo}, Sintaksia-{Muundo} na Semantiki-

{Maana}

Awe na ufahamu mkamilifu wa ujumbe au mada iliyoandikwa katika matini chanzi na uwezo au

jinsi ya kuelezea ujumbe au mada hiyo kwa ufasaha katika lugha lengwa.

Awe mjuzi wa TEHAMA.

Ajue lugha mbili au zaidi.

Awe na tajiriba kubwa ya usomaji wa aina mbalimbali za tafsiri na kujiendeleza kulingana na

mabadiliko ya kijamii.

Afahamu vizuri watu, jamii na utamaduni wa watumiaji wa lugha chanzi na lugha lengwa.

Afahamiane na watu wengi, yaani kujichanganya changanya na watu wa fani au sekta

mbalimbali.

Awe na tabia yakushirikiana na watu wengine katika shughuli za kufasiri.

Msingi wa kujifunza lugha

Ili kuwa na uwezo wa kutumia lugha mpya, binadamu anatakiwa kujifunza. Biadamu hasa mtu

mzima huweza kujifunza lugha vizuri kama tu ataweza kuzingatia yafuatayo

Page 7: YALIYOMO · 5 mmoja kati ya watu wa itikadi ipi, jamii ipi au taifa gani. Kwa mfano mtu akiongea Kiswahili awapo katika mataifa mengine hubainika moja kwa moja kuwa ni wa Afrika ya

7

a) Utayari wake wa kujifunza(kwa mfano, mtu anapenda kujua lugha Fulani lakini hayuko

tayari kujifunza lugha hiyo)

b) Kuwa na utayari wa kujenga hisia za kutafakari

c) Kukazia maarifa katika uhalisia

d) Kufanya Marudio ya alicho jifunza

Kwa mjibu wa kamusi ya uingereza maarufu kama Oxford dictionary, neno kujifunza ni

mapokeo ya ujuzi au elimu baada ya uzoefu ama mafunzo fulani.Hivyo ni bayana ya mambo

tuonayo na kusikia mashuleni hadi majumbani mwetu.

Ili kujifunza lugha mpya na kuitumia vizuri misingi ifuatayo yatakiwa kupewa kipaumbele

1Kuchagua

Ni muhimu kujifunza lugha mpya, uwezo wa kujifunza lugha mpya utatengemeana na jinsi

binadamu huyo anajifunza lugha mpya anavyochagua maneno amabyo atayatumia zaidi na

yanompendeza zaidi.I kumbukwe pia kuwa, kila lugha ina maelufu ya maneno na mengi kati ya

hayo hata hautakuja kuyatumia katika maisha yako yote. Pia , lugha zote zina maneno kuhusu

kila mada, kuanzia wanyama mpaka taaluma.

Kuchagua mneno yanayokuvutia ndio silah yako kubwa katika kuhakikisha unayakumbuk.

Ukichagua maneno yenye maana kwako, haitakuwa rahisi kwako kuyasahau hata baada ya muda

mrefu. Kwa msing huu unaeza kuongeza maneno mapya kirahisi zaidi.

2. Kuyahusisha na maneo mengine

Katika kujifunza lugha mpya ni muhimu sana kujua maneno muhimu. Jambo la msingi hapa ni

kuyahusianisha maneno hayo na mzingira unayoyafahamu. Neon moja unaweza kulihusiansha

na kumbukumbu zako, hisia na mambo mengi tu unayoyajua hivyo kukusaidia zaidi

kulikumbuka kirahisi na kuwezesha ujifunzaji wa lugha kuwa rahisi zaidi.

3. Kupitia

Kufanya marudio na kupitia huwezesha kutosahau mara kwwa mara. Taarifa ambazo

zimerudiwarudiwa huhifadhiwa kwenye kwenye kumbukumbu zako za muda mrefu na bila

shaka utakuwa unzikumbuka kwa maisha yako yote. Hivyo basi ni muhimu kuhakikisha kwamba

unapitia mambo uliyojifunza mara kwa mara kw kipind kirefu.

Page 8: YALIYOMO · 5 mmoja kati ya watu wa itikadi ipi, jamii ipi au taifa gani. Kwa mfano mtu akiongea Kiswahili awapo katika mataifa mengine hubainika moja kwa moja kuwa ni wa Afrika ya

8

4. Kuhifadhi

Kimsingi, unapojifunza lugha mpya ni lazima uyaandike sehemu yoyote ambayo ambayo

unaweza kuisoma baadaye ukihitaji.

Wjerumani hapo awali walikuwa na msemo wao kwamba “ maneno ya kutamka tu huwa

yanasahaulika haraka, lakini yaliyoandikwa yataendelea kukumbukwa”

5. Matumizi

Msingi mwingine mzuri wa kujifunza lugha ni kuitumia mara kwa mara ata kama kuna makosa

unayoyahusisha na matumizi yako ya lugha. Hii inatukumbusha kwamba unavyozidi

kuzungumuza na watu wengine unazidi kiongea lugha kwa ufasaha zaidi na kukumbuka maneno

uliyojifunza mbele ya mtu mwengine. Hii husaidia zoezi la kujifunza liwe jepesi zaidi na

litakuongezea uzoefu wa matumizi ya maneno ambayo umeyakariri.

NJIA ZA KUJIFUNZIA LUGHA

Kutumia muda zaidi na lugha

Jambo muhimu zaidi ni shahada ya kuzamisha katika lugha. Muda zaidi kutumia na lugha, kwa

kasi kujifunza. Hii ina maana ama kuwa kusoma reading au kuandika writing au kusikiliza kwa

listening au kusema speaking au kujifunza maneno na misemo learning words and phrases

katika lugha ya kigeni. Na haina maana wamekaa darasani na kuangalia nje ya dirisha au

kusikiliza wanafunzi wengine ambao bado kujua jinsi ya kuzungumza au kusikiliza kwa maelezo

ya sarufi katika lugha yao wenyewe. Ina maana «pamoja» katika lugha ya lengo.

na kusoma kila siku

Mzigo mchezaji ruwaza hotuba na kuwasikiliza, haraka iwezekanavyo. Kama wewe ni mapya tu

kujifunza lugha, kusoma macho kwamba ni kusikiliza (unaweza kutumia vitabu vya redio au

vitabu vya kiada kisasa, mwishoni mwa ambayo kuna tapescrips Kusikiliza na kusoma, utapata

kutumika kwa lugha. Kusoma saa na vikao kusikiliza ni sawa na masaa kadhaa ya darasani.

Msamiati vocabulary — moja ya mambo mawili ya lugha, bila ambayo unaweza kamwe kusema

(wa pili — sarufi). Makini na maneno mapya na matumizi yao katika hukumu. Kuandika na

kukariri pamoja na maneno jirani collocations Kama wewe ni kusoma kwenye kompyuta yako,

kutengeneza orodha ya maneno katika Word au Notepad. Usijali kama huwezi bado kusema

ufasaha na kuandika, kutumia muda juu ya uteuzi wa neno — hii ni ya kawaida. Lakini wewe

wameanza kupanua msamiati wako.

Kama hawataki kujifunza lugha, una hiyo na wala kujifunza. Kama unataka — kufuatilia

mchakato. Chagua eneo la riba katika ambayo kuelewa au wanataka kuelewa. Angalia kwa

maneno ambayo itasaidia kusikiliza na kusoma. Je, si kusubiri kwa mtu mwingine kufundisha

Page 9: YALIYOMO · 5 mmoja kati ya watu wa itikadi ipi, jamii ipi au taifa gani. Kwa mfano mtu akiongea Kiswahili awapo katika mataifa mengine hubainika moja kwa moja kuwa ni wa Afrika ya

9

lugha. Kuchunguza lugha wenyewe, kuzungumza na kuandika juu yake kama unataka. Mwalimu

haina kufundisha hotuba ufasaha, ili kufanikisha hili tu unaweza.

Msiwe na wasiwasi juu ya nini unaweza na kile hakuweza kukumbuka. Haijalishi. Wewe ni

kujifunza na kufanya maendeleo binafsi. Lugha polepole kuwa wazi, lakini huwezi kudhibiti

mchakato huu. Kukaa nyuma na kufurahia. Lakini kuwa na ufahamu kwamba inazalisha kiasi

cha haki ya ulimi. Kisha mtazamo wako itakuwa chanya na utafiti, ambayo ina athari chanya

katika matokeo, na wewe haraka kufikia mafanikio katika kujifunza!

SURA YA PILI:

MBINU ZINAZOFAA KUFUNDISHIA ISIMU

ISIMU

Isimu ni „taaluma ya uchunguzi wa lugha kisayansi‟. Ipo taaluma kama vile ya Falsafa ambayo

nayo inaweza kujishughulisha na uchambuzi wa masuala ya lugha lakini si kwa kutumia vigezo

vya kisayansi. Wanaisimu huhakikisha kuwa wakati wa kutafiti na hatimae kuwasilisha matokeo

ya utafiti wao wanatumia vigezo vya kisayansi hatua kwa hatua. Kwanza huchunguza na

kukusanya data, Halafu wanafanya malinganisho kabla ya kuunda nadharia na kuzipima nadharia

na kuonyesha matokeo yake. Baadaye hujiundia nadharia na kutoa kanuni ambazo zinapimika.

simu (au "maarifa ya lugha") ni sayansi inayochunguza lugha. Imegawiwa katika matawi

mbalimbali kama ifuatavyo

Matawi ya Isimu

a)Isimu Fafanuzi/Elezi

Tawi hili linaz ingatia umuhimu wa kuchambua au kufafanua vipengele vya lugha jinsi vilivyo.

Huchunguza jinsi lugha inavyozungumzwa wakati fulani na watu fulani. Kimsingi, isimu

fafanuzi inahusika na lugha wakati huohuo wala sio uliopita au ujao. Tawi hili ndilo shina kubwa

la isimu. Isimu fafanuzi haitilii mkazo mabadiliko yaliyotokea katika lugha hata kama

mabadiliko haya yapo. Katika utanzu huu ndipo tunachambua muundo wa sauti za lugha,

muundo wa maneno, muundo wa sentensi, na hata maana za tungo za lugha.

b)Isimu Historia

Isimu historia ni miongoni mwa matawi makongwe zaidi. Tawi hili ndilo linashughulikia

uchunguzi wa maendeleo na mabadiliko ya lugha kiwakati kutoka kipindi kimoja cha kihistoria

hadi kingine, sababu na matokeo ya mabadiliko hayo. Isimu historia hudhihirisha mabadiliko ya

sauti, maumbo ya maneno, sentensi, na maana za maneno kihistoria.

Page 10: YALIYOMO · 5 mmoja kati ya watu wa itikadi ipi, jamii ipi au taifa gani. Kwa mfano mtu akiongea Kiswahili awapo katika mataifa mengine hubainika moja kwa moja kuwa ni wa Afrika ya

10

Isimu historia ni uchunguzi wa mabadiliko ya lugha katika mapito ya nyakati. Inaangaza jinsi

lugha inavyobadilika katika vipindi mbalimbali, sababu za mabadiliko hayo na athari zake katika

lugha hiyohiyo na lugha nyinginezo. Tawi hili pia huangalia hatua mbalimbali ilizopitia lugha

katika kukua kwake.

c)Isimu Linganishi

Hili ni tawi la isimu ambalo linafanya uchunguzi wa lugha mbalimbali ili kuzilinganisha na

kuzilinganua. Wanaisimu huchunguza lugha katika viwango vyote vya fonolojia, mofolojia,

sintaksia na semantiki ili kuonesha na kueleza jinsi lugha hizo zinavyofanana au kutofautiana.

Isimu Linganishi ndiyo imewezesha kubainisha makundi mbalimbali ya lugha. Kwa mfano,

familia za lugha kama vile lugha za ulaya na za kihindi na makundi mbalimbali ya lugha za

kiafrika. Wanaisimu wanapozilinganisha lugha mbalimbali, hufanikiwa kuunda lugha mame ya

lugha hizo. Kutokana na hiyo lugha mame mwanaisimu hubainisha lugha hizo na uhusiano wa

kinasaba na kuonesha jinsi lugha hizo zinavyotofautiana.

d)Isimujamii

Hili ni tawi la isimu linalochunguza uhusiano uliopo baina ya lugha na watumiaji wake au jamii.

Baadhi ya mambo muhimu ambayo huchunguzwa ni pamoja na sera za lugha, lugha sanifu,

usanifishaji, lahaja, rejesta au sajili. Maswali muhimu yanayojibiwa katika utanzu huu ni

pamojana: nani anasema nini, kwa nani au na nani, wakati gani, kuhusu nini. Wanaisimujamii

huamini kwamba umuhimu wa lugha upo katika matumizi yake. Hii ndiyo sababu

wanachunguza lugha katika miktadha yake ya jamii.

Page 11: YALIYOMO · 5 mmoja kati ya watu wa itikadi ipi, jamii ipi au taifa gani. Kwa mfano mtu akiongea Kiswahili awapo katika mataifa mengine hubainika moja kwa moja kuwa ni wa Afrika ya

11

TEACHING ABOUT MEMORUNDUM:

What are memos?

The term memo is a short form for „memorandum‟. The purpose of it is to give information in a

brief or short form.

Memos can be seen as notes or very brief letters. It is usually very short (a few lines or

paragraphs at the most).

Organizations like schools and colleges usually have a recognizable form and layout for all

internal memos.

Most memos are like short advertisement which passes between colleagues, sometimes within

departments or to other departments or other sites.

Remember; the Internet has become a very popular medium for the memo. This is probably due

to its brief format. Email messages can be seen as electronic memos in most business instances.

Memos should have a main heading stating the subject of the message, and sub-headings which

lead into the message sections.

Memos usually bear the generic heading „MEMO‟ at the top of the page. This acts as an

advanced organiser so that the receiver or recipient is without doubt of the document type and

function.

The information in a memo should be set out in order of importance, with the most important

item listed first.

Remember that effective business communication operates on the „punchline first‟ principle.

MAIN PARTS OF A MEMO

A memo should always contain the following information.

The subject of the memo

Page 12: YALIYOMO · 5 mmoja kati ya watu wa itikadi ipi, jamii ipi au taifa gani. Kwa mfano mtu akiongea Kiswahili awapo katika mataifa mengine hubainika moja kwa moja kuwa ni wa Afrika ya

12

The name of the sender

The name of the recipient(s)

The date of posting

The message itself

TYPES OF A MEMO

There are various types of memo. These are the most commonly used.

(i) Information

(ii) Announcement

(iii) Update

I. Information memos

An information memo provides information that is relevant to the recipient, or it replies with

information that has been requested. The memo subject is stated in the title.

Consider the example below:

MEMO

SUBJECT

DATE

TO

FROM

Quote for Budget Projections

18 February 2017

J. Brown, Training Manager

Meshack Addelah

Background

You requested a quote from a printer to use in your budget projections on the current project.

Quote

The cost for printing 1000 dcuments in the dimensions you cited will be approximately Tshs

2,000.

Source

I obtained this information from Streamline Printers.

Page 13: YALIYOMO · 5 mmoja kati ya watu wa itikadi ipi, jamii ipi au taifa gani. Kwa mfano mtu akiongea Kiswahili awapo katika mataifa mengine hubainika moja kwa moja kuwa ni wa Afrika ya

13

Scheduling

Though you did not ask about scheduling, the information manager of Streamline printers stated

unequivocally that you must allow three weeks from the date of delivery of camera-ready copy.

II. Announcement memos

A meeting announcement memo is one sent by an individual or department to other individuals,

departments, or company representatives to advise them of a forthcoming meeting.

These usually contain the date and agenda of the meeting, although, they may simply announce

the date.

Consider the example below:

MEMO

SUBJECT

DATE

TO

FROM

Meeting about Sundeal Hotels

21 March 2017

Members of the Executive Committee

D. Henderson, Chair of Neatfit

Purpose

This meeting will consider a joint venture between Belsize Amusement Parks and Sundeal

Hotels.

Time

The meeting will be held on 26 March at 9.30 am.

Place

The Board Room has been booked and refreshments will be served.

Agenda

The meeting will include two sessions.

General session (10.00 am to 12.00 am)

introductions of board members

AAAP Presentation

financial summary

questions and discussion

Page 14: YALIYOMO · 5 mmoja kati ya watu wa itikadi ipi, jamii ipi au taifa gani. Kwa mfano mtu akiongea Kiswahili awapo katika mataifa mengine hubainika moja kwa moja kuwa ni wa Afrika ya

14

Executive session (1.15pm to 4.00 pm)

fiscal status Sundeal Hotels

decisions and recommendations

Confirmation

Please confirm your attendance by contacting Mary Golding Ext. 234

Attachments

The following documents are attached:

AAAP Annual Report

financial summary

preliminary paper on Joint Venture

III Update memos

Update memos are notes which are transmitted between friends (colleagues) on a regular or

frequent basis.

Because of the nature of the relationship of the authors, these are often quite brief and informal.

These are the sort of office communications that are now largely conducted via email messages.

Example 1

MEMO

SUBJECT

DATE

TO

FROM

Help me out!

12 March 2017

Jean

Jeremiah

Quick! I need a list of all our products containing Zinc.

Sorry to dump on you like this but it‟s more than my job‟s worth to miss the deadline. (Tues)

Let‟s have a coffee later in the week.

Page 15: YALIYOMO · 5 mmoja kati ya watu wa itikadi ipi, jamii ipi au taifa gani. Kwa mfano mtu akiongea Kiswahili awapo katika mataifa mengine hubainika moja kwa moja kuwa ni wa Afrika ya

15

Example 2

MEMO

SUBJECT

DATE

TO

FROM

Staff Outing

19 December 2012

Brian

Trevor

Hi

I went to the Cmmittee Group meeting yesterday and the subject of the staff outing came up.

Could you let me have some ideas for a venue and flesh it out with a bit of detail.

Alton Towers was suggested but I‟d prefer something more adult myself.

Cheers,

T

Example 3

MEMO

SUBJECT

DATE

TO

FROM

Interview Panel

12 October 2013

Brenda

Geoffrey

Dear Brenda

Glad to tell you that; you‟re on the interview panel for the new teaching job.

Interviews start at 9-30 next Wednesday. I‟ve sent you the CVs of those shortlisted and hope you

have time to go through them in time.

Wear your best frock and put them through their paces.

See you then

Page 16: YALIYOMO · 5 mmoja kati ya watu wa itikadi ipi, jamii ipi au taifa gani. Kwa mfano mtu akiongea Kiswahili awapo katika mataifa mengine hubainika moja kwa moja kuwa ni wa Afrika ya

16