Transcript
Page 1: DARASA V KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA … · C. John alisema naweza kufundisha D. John alisema “ nafundisha vizuri [ ] 28. Ingawa walipata shida nyingi njiani ..... walifika

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA APRILI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

DARASA V – KAZI YA NYUMBANI

KISWAHILI

JINA LA MWANAFUNZI: _____________________

MAELEKEZO

1. Kumbuka kuandika majina yako matatu kwa usahihi.

2. Jibu maswali yote kulingana na maelekezo.

3. Soma maswali kwa ufasaha kabla

SHULE YA MSINGI MARTIN LUTHER S. L. P 1786 Dodoma. Simu. +255 26 2395029, +255 784 449098

Fax +255 26 2395030 (www.martinlutherschooldodoma.com)

“Quality Education for the New Generation”

Page 2: DARASA V KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA … · C. John alisema naweza kufundisha D. John alisema “ nafundisha vizuri [ ] 28. Ingawa walipata shida nyingi njiani ..... walifika

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA APRILI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, OFISI YA RAISI

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA SHULE YA MSINGI MARTIN LUTHER

KISWAHILI, KAZI WAKATI WA LIKIZO APRIL, 2020

JINA____________________________________ DARASA LA V ________ MUDA: SAA 1

SEHEMU A: SARUFI

1. Andikawingi wa sentensi hii “ mvua ya masika imeanza”

A. mvua ya masika zaanza B. mvua zimeanza C. mvua za masika zimeanza D. mvua zimeratika [ ]

2. “Shangazi amesema kuwa ataenda mjini leo jioni” hii ni aina gani ya kauli?

A. kauli nzuri B. kauli halisi C. kauli taarifa D. kauli kali [ ]

3. Mjomba wetu anapenda ...... mashari A. kugani B. kuimba C. kughani D. kucheza [ ]

4. Kutokana na maziwa tunapata ?........

A. siagi, ngozi, pembe B. mtindi, damu, kweto C. samli, siagi na jibini D. kwato, sumu, samadi [ ]

5. Huyu .... aliyekuwa anatafutwa A. ndio B. ndiyo C. ndiye D. ndivyo [ ]

6. Kisawe cha neno SHAIBU ni ......... A. barabara B. babati C. ajuza D. buda E kigori [ ]

7. Sikuweza kutambua ni nani amelala kitandani kwa sababu alijifunika shuka .........

A. lote B. gubigubi C. nzima D. zama E. zima [ ]

8. Mchanganyiko wa mboga na matunda unaoliwa bila kupikwa huitwa .........

A. matango B. kabichi C. saladi D. nyanya [ ]

9. “Mchezo mkali ni ule tuliocheza ......... ya timu ya majengo”. A. zidi B. kabla C. dhidi D. thidi [ ]

10. Jane anacheza mpira barabarani “ sentensi hii ikiwa katika hali ya mazoea itakuwa ipi kati ya hizi zifuatazo

A. Jane atacheza mpira barabarani B. Jane hucheza mpira barabarani

C. Jane amecheza mpira barabarani D. Jane anacheza mpira barabarani [ ]

11. Katika sentensi zifuatazo ipi ni sahihi

A. nimekuja hapa tangia jana B. nimekuja hapa tangiapo jana

C. nimekujaga tokea jana D. nimekujaga hapa tangu asubuhi [ ]

12. Maria angalisoma ......... mtihani wake. A. angefaulu B. angasoma C. angalifaulu D. asingalisoma [ ]

13. Sisi ni watoto wadogo. Neno sisi lipo katika nafsi gani?

A. ya kwanza umoja B. ya pili wingi C. ya kwanza wingi D. ya tatu wingi [ ]

14. Neno ughilibu lina irabu ngapi? A. kumi na tatu B. nne C. tatu D. sita [ ]

Page 3: DARASA V KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA … · C. John alisema naweza kufundisha D. John alisema “ nafundisha vizuri [ ] 28. Ingawa walipata shida nyingi njiani ..... walifika

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA APRILI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

15. Msicheze barabarani “ kaka alituambia” hii ni kauli gani

A. kauli halisi B. kauli tekeleza C. kauli taarifa D. kauli tenda [ ]

16. Magrety ni mtoto wa mjukuu wa ngu, Magrety ni nani kwangu?

A. kilembwekeza B. kijukuu C. kitukuu D. kilembwe [ ]

17. Kalamu ........ inavuja wino A. vyangu B. wangu C. yangu D. sangu [ ]

18. “Funga dirisha” hii ni aina gani ya kauli A. kauli taarifa B. kauli tendwea C. kauli halisi D. kauli shirikishi [ ]

19. Kiwanja cha mpira kina magori mangapi A. manne B. matano C. sita D. mawili [ ]

20. Baada ya kufanya kazi nzito siku nzima zawadi alilala A. kifudifudi B. fofofofo C. chali D. fofofo [ ]

21. Shule ......... zimefungwa kwa sababu ya ugonjwa wa Corona A. zote B. wote C. sote D. nyote [ ]

22. Mwalimu ........ ni mzuri sana. A. wetu B. zetu C. wote D. vyote [ ]

23. ........... tulikula wali na nyama A. Kesho B. Jana C. Mwakani D. Hamna jibu [ ]

24. Ili tuvune mazoa bora ....... tulime kwa juhudi na maarifa. A. ni budi B. budi C. hatuna budi D. tunabudi [ ]

25. Alitembea ............ miguu kutoka shuleni hadi nyumbani. A. kwa B. na C. Wa D. cha [ ]

26. Wao watarudi kesho kutwa. Sentensi hii ipo katika nafsi ya ngapi

A. nafsi ya kwanza umoja B. nafsi ya tatu umoja C. nafsi ya pili wingi D. nafsi ya tatu wingi [ ]

27. Badili sentensi hii kuwa kauli halisi “ John alisema kuwa hawezi kufundisha”

A. John hawezi kufundisha B. John alisema “ siwezi kufundisha”

C. John alisema naweza kufundisha D. John alisema “ nafundisha vizuri [ ]

28. Ingawa walipata shida nyingi njiani ...... walifika salama. A. hatimaye B. ingawa C. ingawaje D. hatima [ ]

29. Kinyume cha neno “ adimu ni kipi? A. haba B. ghali C. tele D. potea [ ]

30. Watu wale .................. walimsimamisha Sofia A. ndiye B. ndiwo C. ndio D. ndo [ ]

31. Neno kung’ang’aniwa lina silabi ngapi? A. saba B. sita C. tano D. kumi na tano [ ]

32. “Kimbia haraka” sentensi hii ipo katika kauli gani A. mshangao B. halisi C. kushtuka D. taarifa [ ]

33. Frank huna madaraka ..........ya kunifukuza kazi A. yoyote B. vyovyote C. yotre D. yangu [ ]

34. Kama ungaliniomba kitabu kile........ . A. ningalikupa B. ningelikupa C. ningekupa D. nitakupa [ ]

35. Mpanda ngazi hushuka. Kinyume cha neo “kupanda” katika sentensi hii ni nini?

A. kutopanda B. kusimama C. kushuka D. kuvana [ ]

36. Neno la jumla la maneno MEZA, VITI, KABATI na KITANDA ni lipi?

A. vifaa B. vyombo vya nyumbani C. vifaa vya mbao D. samani [ ]

Page 4: DARASA V KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA … · C. John alisema naweza kufundisha D. John alisema “ nafundisha vizuri [ ] 28. Ingawa walipata shida nyingi njiani ..... walifika

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA APRILI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

37. Mtoto wa kiume wa baba yangu ni .......... A. mwanangu B. kaka yangu C. mjomba wangu D. dada yangu [ ]

38. Maana ya neno “ ughaibuni” ni kipi? A. nchi za mbali B. nchi jirani C. magharibi D. nyumbani [ ]

39. Chakula hiki si kibaya ..... hakina viungo A. kama B. ila C. kwa kuwa D. ingawa [ ]

40. Mimi ninakula chakula . sentensi hii ipo katika nafsi ya ngapi

A. nafsi ya kwanza wingi B. nafsi ya pili wingi C. nafsi ya tatu umoja D. nafsi ya kwanza umoja [ ]

SEHEMU B: MISAMIATI

41. Ng’ombe dume huitwa fahali mbuzi dume huitwa ........ A. masai B. jogoo C. beberu D. kidume [ ]

42. Mume wa dada yangu ni ........... A. wifi B. mke C. shemeji D. mlezi [ ]

43. Neno lenye maana sawa na zeruzeru A. chotara B. suriama C. albino D. yatima [ ]

44. Kinyume cha neno huzuni ni ............ A. fura B. ogopa C. furaha D. kubali [ ]

45. Jua huzama upande wa ........... A. kusini B. kaskazini C. magharibi D. mashariki [ ]

46. Neno jimbi lina maana sawa na A. jogoo B. kuku C. jogoo D. tumbili [ ]

47. Mtu anayetunza vitabu maktaba huitwa A. msomi B. melikebu C. mkutubi D. mtunza vitabu [ ]

48. Nyumba ya nyuki huitwa ....... A. usinga B. chooni C. mzinga D. kana [ ]

49. Angesoma kwa bidii ......... vizuri na kupewa zawadi kubwa

A, angekisoma B. angelifaulu C. angefaulu D. angalifaulu [ ]

50. Baada ya mwizi kushitakiwa kesi yake ilipelekwa A. sokoni B. samba C. mahakamani D. jingo [ ]

Unda neno moja kwa kubadili mpangilio wa herufi za kila neno

51. Audin ................................................................................

52. Ualkam .................................................................................

53. Ocath ................................................................................

54. Neno lenye maana sawa na neno chooni ni A. msaada B. msarani C. msalani D. vyoo [ ]

Andika maneno yafuatayo kwa kiferu

55. Tusojua ............................................................................

56. Jinale ..............................................................................

57. Dalilize .............................................................................

58. Mekuja .............................................................................

59. Lilotuandama ...............................................................................

Page 5: DARASA V KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA … · C. John alisema naweza kufundisha D. John alisema “ nafundisha vizuri [ ] 28. Ingawa walipata shida nyingi njiani ..... walifika

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA APRILI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

60. Babake ..............................................................................

61. Wizara ya kilimo na mifugaji imeanza kutengeneza ........ bora za kilimo

A. zana B. vifaa C. thana D. dhana [ ]

62. .......... ni mahali panapompa mtu nafasi ya kuzungumza kwa siri A. falaga B. faragha C. faragha D. siri [ ]

63. Usipofunga ......... yako vizuri, barua yako itapotea A. anuani B. zahani C. bahasha D. posta [ ]

64. Mtu hodari, jasiri asiyeogopa kupigana wala kufa huitwa? A. jambazi B. Mkaidi C. mpiganaji D. jasiri [ ]

65. Bibi anatumia ..... ili kupata egemeo A. msaada B. mkongojo C. mguu D. maini [ ]

66. Mtu msafi wa mwili na mavazi huitwa .......... A. nazifu B. nasifu C. nadhifu D. mwadilifu [ ]

67. Kinyume cha neno” kustahi” ni ........ A. kusifia B. kipupwe C. kunyanyapaa D. kumbembeleza [ ]

68. Bibi fatma hana meno. Maana yake ni A. anakibyongo B. kibogoyo C. kazeeka D. suriama [ ]

69. Katika neno KATAA ukidondosha irabu moja ya mwisho unapata neno gani

A. karakana B. karata C. kata D. taka [ ]

70. ......... makubwa huingiza hewa na mwanga wa kutosha A. mlango B. taa C. madirisha D. pagala [ ]

71. Ukitazama ....... utajua leo ni siku gani na tarehe ngapi A. mwezi B. Jua C. kalenda D. karenda [ ]

72. “ Baba huvuna asali”; kitendo cha kuvuna asali huitwa A. kuiba B. kuchukua C. kurina D. kupakua [ ]

73. Shangazi aliniandalia ........ fupi baada ya kuhitimu darasa la saba A. msiba B. shida C. tafrija D. karamu [ ]

74. ......... ni kitendo cha kuburudisha wasikilizaji A. Burudani B. Tumbuiza C. Tambulisha D. Chereko [ ]

75. .......... tutarudi kesho kutwa. A. Sisi B. Wewe C. Wao D. Yeye [ ]

76. Mbuzi anamiguu mingapi A. 6 B. 4 C. 5 D. 8 [ ]

77. Mtu anayefua vyuma anaitwa ......... A. mfua nguo B. mfua vyuma C. mhunzi D, mfua dhahabu [ ]

78. Kanchiri huvaliwa sehemu gani ya mwili? A. kichwani B. miguuni C. kifuani D. mkononi [ ]

79. Kitendo cha jua kuzama huitwa A. mawio B. macheleo C. mapambazuko D. machweo [ ]

80. .......... wake wa mwisho anaitwa Paulo A. Binti B. Kijana C. Mwezetu D. Wifi [ ]

81. Tumekula chakula .............. jioni A. za B. cha C. wa D. mwe [ ]

82. Kinyume cha neno rudia ni ........ A. subiria B. rudi C. nenda D. rejea [ ]

83. Kanusha sentensi isemayo” wanaimba vizuri”

A. wanaimba sana B. hawaimbi vizuri C. wanaimba vibaya D. hawaimbi sana [ ]

Page 6: DARASA V KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA … · C. John alisema naweza kufundisha D. John alisema “ nafundisha vizuri [ ] 28. Ingawa walipata shida nyingi njiani ..... walifika

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA APRILI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

Eleza maana ya maneno yafuatayo

84. Kuli ........................................................................................................................................

85. Sonara ........................................................................................................................................

SEHEMU C: METHALI, NAHAU NA VITANDAWILI

Kamilisha methali zifuatazo

86. Ukitaka cha uvunguni .........................................................................................................

87. Haba na haba ....................................................................................................................

88. ...............................................................................................................si chururu

89. .............................................................................................................halimdhuru mwewe

90. Chanda chema .................................................................................................................

91. Dua mbaya ...........................................................................................................................

92. Mwenda tezi na omo ..........................................................................................................

93. .....................................................................................................................hapotei njia

94. Kawia ........................................................................................................................

95. ..............................................................................................................hupasuka msamba

96. ............................................................................................................... si mkulima

97. .................................................................................................................. hasara

98. Mwenda bure ..................................................................................................................

99. Kuvuja kwa pakacha ....................................................................................................................................

Eleza maana ya nahau hizi

100. Fika kwenye neema .............................................................................................................................................

101. Kuwa na jina ........................................................................................................................................................

102. Andika meza ........................................................................................................................................................

103. Kuwa nguzo ..........................................................................................................................................................

104. Unatia chumvi ........................................................................................................................................................

105. Kupiga chuku ............................................................................................................................................................

106. Mnanila kichogo .....................................................................................................................................................

107. Humeza mate ........................................................................................................................................................

Page 7: DARASA V KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA … · C. John alisema naweza kufundisha D. John alisema “ nafundisha vizuri [ ] 28. Ingawa walipata shida nyingi njiani ..... walifika

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA APRILI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

108. Amelikoroga ...........................................................................................................................................................

109. Kuwa popo ..............................................................................................................................................................

110. Fuata nyayo .............................................................................................................................................................

Tegua vitendawili vifuatavyo

111. Mgeni kachungulia dirishani .......................................................................................................................................

112. Popoo mbili zavuka mto .............................................................................................................................................

113. Kwetu sisi sote ni weusi ..............................................................................................................................................

114. Nyumba yangu ndogo imejaa askali tele .................................................................................................................

115. Hakika sirudi tena kwa mjomba .................................................................................................................................

116. Toa fimbo nami nitoe tucheze ngoma ya kwetu .......................................................................................................

117. Wali wa mama mtamu ...............................................................................................

118. Napigwa faini kosa silijui .............................................................................................

119. Hachagui wala hashauriwi ...................................................................................................................................................

120. Chini ugali, katikati kuni na juu mboga .......................................................................................................................

121. Boma la machozi baridi ........................................................................................................................................

122. Mwanangu amenitia aibu mbele ya wageni .................................................................................................................

123. Ukiona njigi utadhani njege

124. Njoo hapa nije hapo ...............................................................................................................................

SEHEMU D: UTUNGAJI.

Umepewa sentensi tano zilizoandikwa bila kufuata utaratibu mzuri wa mawazo, zipange sentenzi hizo katika

mtiririko unaofaa kwa kutumia herufi A, B, C, D ili kuleta maana sahihi ya habari

125. Dakika chache baadaye tuliona msafara wa magari ukiingi [ ]

126. Gari hilo lilifuatwa na gari lingine lililojaa askari wa kuzuia fujo, kisha lilifuata gari la Rais [ ]

127. Mnamo saa saba hivi tuliona pikipiki ya askari wa usalama barabarani ikija mbio kama mshale [ ]

128. Mbele ya msafara huo kulikuwa na pikipiki nne zilizofuatiwa na gari la polisi lenye king’ora. [ ]

Umepewa sentensi tano zilizoandikwa bila kufuata utaratibu mzuri wa mawazo, zipange sentenzi hizo katika

mtiririko unaofaa kwa kutumia herufi A, B, C, D, E ili kuleta maana sahihi ya habari

129. Ili mpate kuyajua ni lazima mjifunze kwa bidii na maarifa muweze kufaulu mitihani yenu [ ]

Page 8: DARASA V KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA … · C. John alisema naweza kufundisha D. John alisema “ nafundisha vizuri [ ] 28. Ingawa walipata shida nyingi njiani ..... walifika

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA APRILI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

130. Ninyi ni vijana wadogo bado wenye matumaini ya kupata maendeleo katika maisha yenu ya baadaye [ ]

131. Endeleeni kusoma na kujifunza kwa bidii kwani elimu ni bahari haina mwisho [ ]

132. Elimu ndiyo itakayoweza kuwafungulia njia za kupata maendeleoe hayo katika safari hii ya kuelimika zaidi [ ]

133. Katika safari hiyo ya kuelimika zaidi utagundua kuwa yapo mambo mengi muhimu ambayo hamyajui [ ]

Panga sentensi zifuatazo ili zilete mtirirko unaofaa kwa kuzipa herufi A, B, C, D, E

134. Kumbe basi hilo ndilo alilosafiria rafiki yangu [ ]

135. Kulipopambazuka nilioga harakaharaka nikavaa upesi na kuelekea kituo cha mabasi [ ]

136. Baada ya kuangaza huko na huko nikaona basi la kwanza likiingia pale kituoni [ ]

137. Aliposhuka nikamlaki kwa kufurahi na kuendekea naye nyumbani [ ]

138. Ingawaje sikuchelewa lakini nilijawa na wasiwasi pale kituoni [ ]

Panga sentensi zifuatazo ili zilete mtirirko unaofaa kwa kuzipa herufi A, B, C, D, E

139. Wanyama wote waliishi kijiji kimoja [ ]

140. Wanyama wote walihudhulia mkutano huo [ ]

141. Mwenyekiti wao alikuWa simba [ ]

142. Hapo zamani za kale [ ]

143. Siku moja aliitisha mkutano mkubwa [ ]

Panga sentensi zifuatazo ili zilete mtirirko unaofaa kwa kuzipa herufi A, B, C, D, E

144. Maombelezo yalikuwa baada ya miezi miwili,Jane alirudi tena kazini [ ]

145. Ndugu, jamaa walifika kutoa rambirambi zao kwa familia ya baba Jane [ ]

146. Alikuwa kama amepagawa kwa muda mpaka alipoulizwa na mumewe [ ]

147. Jane alipata taarifa za kifo cha baba yake [ ]

148. Ikiwa yapata saa tatu na robo asubuhi [ ]

Panga sentensi zifuatazo ili zilete mtirirko unaofaa kwa kuzipa herufi A, B, C, D, E

149. Kila usomaji unaenda na mwendo wake katika kusoma [ ]

150. Upo usomaji wa aina nyingi [ ]

151. Mathalani usomaji wa kiada ni wa makini [ ]

152. Kuna usomaji wa kimya na wa sauti [ ]

Page 9: DARASA V KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA … · C. John alisema naweza kufundisha D. John alisema “ nafundisha vizuri [ ] 28. Ingawa walipata shida nyingi njiani ..... walifika

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA APRILI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

153. Kusoma kwa kuzingatia mambo kunahitaji umakini, ufahamu wake ni wa juu [ ]

Umepewa insha yenye sentensi tano zilizochanganywa zipange sentensi hizo ili zilete maana sahihi ya habari kwa

kutumia herufi A, B, C, D, E

154. Lakini walipiga moyo konde [ ]

155. Safari haikuwa mabaya wala nzuri [ ]

156. Walikutana na wanyama wakali [ ]

157. Wakaendelea na safari yao [ ]

158. Na hata watu wenye sura za kutisha [ ]

Panga sentensi zifuatazo kwa kuzipa herufi A, B, C, D na E ili ziweze kuleta mtiririko mzuri wa mawazo

159. Wengine husema ni homa za mbu [ ]

160. Neno malaria ni lugha ya kigeni [ ]

161. Mara nyingine ugonjwa huu unaitwa bandama, degedege au homa [ ]

162. Kwa mfano watu wengine wanasema kuwa malaria ni homa [ ]

163. Hapa kwetu tunayo majina mbalimbali ya ugonjwa huu [ ]

SEHEMU E: UFAHAMU

Soma shairi lifuatalo kisha jibu swali la (165 – 169)

Kiswahili nikafanya, nikafanya kwa makini,

Mtima nikaukanya, utulie kifuani,

Mawazo nikakusanya, tena kwa kujiamini

Jagina wa kiwahili, Kiswahili lugha yangu

Maswali

164. Neno mtima limetumika badala ya neno lipi? .................................................................................................

165. Shairi hili lina beti ngapi ....................................................................................................................................

166. Vina vya ubeti wa kwanza ni ..................................................... na .................................................................

167. Taja mizani iliyopo katika ubeti wa kwanza mstari wa kwanza .........................................................................

168. Kituo cha shairi hili kinasema ............................................................................................................................

Soma habari ifuaatayo kwa makini kisha jibu swali la (170 – 174)

Makum bi ni kijiji kinachopatikana katika wilaya Ujiji mkoani Kigoma , kijiji hiki kimebarikiwa kuwa na watu wa aina

mbalimbali wenye kazi zao, kundi la kwanza ambao ndiyo wengi zaidi katika katika kijiji hiki ni wakulima na wafugaji,kundi

la pili ni wafanyakazi kama vile walimu, madaktari, manesi na wafanyakazi wengine, kundi la tatu ni la watu

ambao Wamejiajiri kama vile waganga wa kienyeji, fundi mWashi, fundi seremala, wasusi kutokana na juhudi zao

wanakijiji hawa wamefanikiwa kuwa na uchumi mzuri kuliko vijiji vyote vilivyopo mkoani Kigoma.

Page 10: DARASA V KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA … · C. John alisema naweza kufundisha D. John alisema “ nafundisha vizuri [ ] 28. Ingawa walipata shida nyingi njiani ..... walifika

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA APRILI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

Maswali

169. Makumbi ni kijiji kinachopatikana katika wilaya gani? .....................................................................................................

170. Kuna makundi mangapi katika kijiji cha Makumbi ..........................................................................................................

171. Watu ambao wamejiajiri ni kama vile ........................................., ......................................., ..........................................

172. Mtu anaye hudumia wagonjwa huitwa ............................................................................................................................

173. Kundi la kwanza katika kijiji ni ...................................................................... na ..............................................................

Soma habari ifuatayo kisha ujibu swali la 175 – 179

Siku moja Adili na kikundi chake kilichofahamika kwa jina la simba mtoto ambacho kilikuwa hatari sana sehemu za kabwe

walivamia nyumbani kwa mzee Mwanjoka mfanyabiashara mkubwa hapo jijini Mbeya muda wa saa saba usiku.

Mzee Mwanjoka alistuka kutoka usingizini na kuchukua bastola yake na kuanza kunyata kuelekea sebuleni mara, aliwaona

vijana wanne wakitoka sebuleni kuelekea nje huku wakiwa wamebeba television, deki, redio, pamoja na vifaa vingine

walivyovikuta sebuleni hapo mzee alianza kuwakimbiza huku akipiga kelele wezi! Wezi! Wezi! vijana wale walianza

kukimbia. Mzee Mwanjoka aliwaamrisha wasimame la sivyo atafyatua risasi, lakini sikio la kufa halisikii dawa vijana wale

hawakutii onyo lile kweli siku za mwizi ni arobain mzee mwanjoka alifyatua risasi iliyompata adili mguuni. Wenzake

walifanikiwa kutoroka wakati yeye akiugulia maumivu makali pale chini huku akilia kwa uchungu.

Maswali

174. Pendekeza kichwa cha habari uliyosoma ...................................................................................................................

175. Kikundi cha adili kilijulikana kwa jina la ...................................................................................................................

176. Taja methali mbili zinazopatikana kwenye habari uliyosoma

a. ...............................................................................................................................

b. ...............................................................................................................................

177. Ni nani aliyefyatuliwa lisasi mguuni ? ........................................................................................................................

178. Nyumba ya mzee nani ilivamiwa ...............................................................................................................................

Soma kwa makini habari ifuatoyo kisha jibu maswali 180 – 184 yafuatayo

Uuzaji wa mazao ni tendo la kubadilisha mazao kwa fedha, mkulima anampa mtu mwingine mazao yake ili apewe fedha,

uuzaji huu unaweza kufanywa na mkulima mwenyewe au dalalikituo kikubwa cha kuuzia mazao haya ni soko au gulio ,

selikali huwa inawashauriwakulima kuanzisha vyama vya ushirika vyama hivi vitakuwa na kazi ya kununua mazao ya

wakulima na kuyauza ndani na nje ya nchi tatizo kubwa la vyama vya ushirika ni ile tabia ya kukopa mazoa kwa wakulima

halafu kuyauza ndipo ipatikane fedha ya kuwalipa wakulipa wakulima mfumo huu unatakiwa uwe unaratibiwa vizuri na

wakulima kwani mali bila daftari hupotea bila habari

Siku hizi kuna soko huria watu binafsi hujitokeza kununua mazao kwa bei nzuri na hulipa fedha kwa wakati huo huo kwa njia

hii huwasaidia wakulima kupata soko la mazao yao, hata hivyo wakulima wanapaswa kuwa makini kwa kuwa wanunuzi

wengi wamekuwa na ni matapeli mashambenga huwa hufanya hila kwa kutumia mizani zisizo sahihi na hivyo wakulima

huambulia fedha kichele tu, hali hii huwaletea simanzi wakulima lakini pamoja na masononoko hayo kwa kuwa walanguzi

Page 11: DARASA V KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA … · C. John alisema naweza kufundisha D. John alisema “ nafundisha vizuri [ ] 28. Ingawa walipata shida nyingi njiani ..... walifika

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA APRILI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

hutoa pesa papo kwa papo wakulima huona bora kuwauzia wakalanguzi kuliko kukopesha serikali wahenga walisea heri

kenda kuliko kumi nenda uje

Maswali

179. Kichwa cha habari kinachofaa kwa habari uliyosoma ni kipi

A. soko la mazao B. mazao na walanguzi C. biashara iliyosahii D. biashara ya mazao [ ]

180. Vyama vya ushirika vinahitaji kuwa na nini

A. pesa taslimu B. utalatibu mzuri C. utunzaji kumbukumbu D. udhibiti mzuri [ ]

181. “Fedha kichele” nahau hii ina maana ipi

A. fedha kidogo B. utaratibu mzuri C. utunzaji ndogo ndogo D. udhibiti mzuri [ ]

182. Neno lipi kati ya yafuatayo ni kinyume cha neno “ hila”

A. udanganyifu B. ughalobu C. uungwana D. ujanja [ ]

183. Funzo muhumi zaidi ulilolipata katika habari uliyosoma linawakilishwa na methali ipi ?

A. mali bila daftari hupotea bila habari B. biashara haigombi

C. baniani mbaya kiatu chake dawa D. bandu likikushinda jenga kibabda [ ]

Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali 185 – 189

Wakati wa kutambua, majira kuangazia,

Masika yenye mvua, hali ya hewa sawia,

Kiangazi chenye jua, na vuli iso udhia,

Tuyafahamu majira, pia na hali ya hewa

Kipupwe baridi kali, baridi iliozidia,

Usiku kamwe hulali, isipojifunika

Si ubavu wala chali, baridi hukusumbua

Tuyafahamu majira, pia na hali ya hewa

Maswali

184. Shairi hili lina beti ngapi ...................................................................................................................................

185. Shairi hili lina mizani mingapi kwa kila mstari ..................................................................................................

186. Kipi ni kituo/ kibwagizo katika beti hizo ..............................................................................................................

187. Hivi sasa tupo katika majira gani .......................................................................................................................

188. Wewe unapendelea mazingira gani ......................................................................................................................

Soma habari ifuatayo kisha jubu swali la 189 – 192

John ni Joani ni watoto wanaosoma katika shule ya msingi Uhafiwa Joini nai mwanafunzi wa darasa la tano na Joani ni

mwanafunzi wa darasa la nne. Joni na Joani ni watoto wa Mzee Materu Joni ni kaka yake Joani, na Joani ni dada yake .Joni.

Kipindi cha kuwapo nyumbani huwasaidia wazazi waokazi za nyumbani kama, kupika, kufua, kuchota maji, kutunza mifugo

Page 12: DARASA V KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA … · C. John alisema naweza kufundisha D. John alisema “ nafundisha vizuri [ ] 28. Ingawa walipata shida nyingi njiani ..... walifika

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA APRILI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

na kufanya usafi wa ndani, pia huwa na muda wa kujisomea na kujibu maswali mbalimbali waliyopewa na walimu wao, hiyo

imewafanya wapendwe sana na wazazi wao.

Maswali

189. Andika kichwa ambacho ungetamani kiandikwe kuhusu habari ya hapo juu

A. maisha ya Joni na Joani B. maisha ya Mzee materu C. kazi za Joni na Joani D. kazi za nyumbani [ ]

190. Baba yao Joni na Joani anaitwa A. Joni B. Joani C. Materu D. Uhafawa [ ]

191. Kaka yake Joani ni A. Joni B. Materu C. Grace D. Neema [ ]

192. Nje na kazi zingine za nyumbani, Joni na Joani hufanya nini

A. hujisomea na kujibu maswali waliyopewa na walimu wao B. huenda kucheza

C. huenda mjini D. huanza kumsalimia baba yao [ ]

Soma shairi ifuatayo kisha ujibu maswali 193 – 200

Shairi

Nyumbani kwako kuzuri, japokuwa ni pangoni,

Nyumba yako ni Johari, ya mwenzako siatamani,

Hata pawe pa tajiri, hapafai maishani,

Nyumbani kwako johari, kwingine uzitamani,

Uipende nyumba yako, utaona raha yake,

Kisha penda ndugu yako, kwako apaone kwake,

Dunia mahangaiko, usipende peke peke

Nyumbani kwako johari kwingine usitamani

Maswali

193. Kichwa cha shairi kinachofaa ni kipi

A. Johari na nyumba B. nyumbani si pangoni C. tuthamini kwetu D. tupende marafiki [ ]

194. Kituo katika shairi hili ni kipi ......................................................................................................................................

195. Vina vya kati na vya mwisho katika ubeti wa pili ni ................................................................................................

196. Neno “ Johari” kama lilivyo tumiwa na mtunzi lina maana gani .............................................................................

197. Beti zote zina jumla ya mishororo mingapi? ............................................................................................................

198. Tunapata funzo gani katika shairi hili ........................................................................................................................

199. Kila mstari una mizani mingapi ...................................................................................................................................

200. Kituo katika shairi hili jumla ya mizani mingapi ..........................................................................................................

“Elimu ni uzima wangu” (Mithali 4:13)


Recommended