1
������� ���
Fataawa Za Wanachuoni
´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
[20]
Imefasiriwa Na Kutayarishwa Na:
Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush
©
2
Dibaji:
Hizi ni Fataawa za wanachuoni mbali mbali ambazo nimezikusanya ili
kuweza kuwasahilishia ndugu zetu Waislamu na khaswa wale watafutaji
elimu. Fataawa ni mchanganyiko kuhusiana na masuala mbali mbali ya
Tawhiyd, ´Aqiydah, Manhaj, Fiqh na mengineyo.
Hivyo, ninamuomba Allaah (´Azza wa Jalla) ziweze kuleta faida kwa ndugu
zetu Waislamu, na ninamuomba Allaah (´Azza wa Jalla) Ajaalie kazi hii niwe
nimeifanya kwa kutafuta Radhi Zake (Subhaanahu wa Ta´ala), na Amlipe kila
Aliyeisambaza kwa ndugu mwengine na Awalipe ndugu wasomaji wote kwa
jumla.
Tanbihi: Fataawa zote hizi tumezifasiri kwa njia ya Video na zinapatikana
Youtube waweza kusoma na huku wasikiliza. Kwa mwenye kutaka hizo
Fataawa za Video aende Alhidaaya au Youtube kwa juu sehemu ya kutafuta
aandike au kukopi kichwa cha habari cha Fatwa (kama ilivyo hapo chini kwa
kila Fatwa ina kichwa chake cha habari) na atafute itajitokeza In Shaa Allaah.
Jazaakumu Allaahu Khayra
Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad , na ahli zake na
Maswahabah zake na watakaowafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah.
3
Fataawa zilizomo:
1. Nini Maana Ya ´Ilmaaniyyah?
2. ´Aaliym Ni Katika Majina Ya Allaah (´Azza wa Jalla)
3. Allaah (Ta´ala) Alipomuumba Aadam Alimuongelesha Lugha Ipi?
4. Mtume Na Maswahabah Hawakufanya Khuruuj Wafanyazo Jamaa´at-
ut-Tabligh
5. Kuswali Nyuma Ya Imamu Mshirikina
6. Ni Kina Nani Wahaabiyyah?
7. ´Allaamah al-Luhaydaan Kuhusu Sigara
8. ´Allaamah al-Luhaydaan Kuhusu Shaykh Al-Albaaniy (Rahimahu
Allaah)
9. Hakuna Mjinga Mkubwa Katika Dini Kama Huyu!
10. Ifanye Swalah Ni Jambo Muhimu Zaidi Maishani Mwako
11. Khitmah Ni Bid´ah
12. Da´wah Kuifanyia Biashara
13. Hukumu Ya Dhikr Ya Pamoja (Kikundi)
14. Haijuzu Kumpa Wasia Mwenye Kurithi
15. Uadilifu Kwa Mwenye Mke Zaidi Ya Mmoja
16. Hukumu Ya Kusema Allaah Akimponyesha Mgonjwa Wangu
Nitamshukuru
17. Mwenye Kusema Ya Kwamba Dunia Imeumbwa
Kwa Ajili Ya Muhammad
18. Kutibu Uchawi Kwa Kutumia Uchawi
19. Radd Kwa Mwenye Kupinga Kustaawa Kwa Allaah Juu Ya ´Arshi Yake
20. Tasbiyh Ni Bid´ah
21. Kuswali Swalah Ya Usiku Jamaa´ah Nyumbani
22. Anaeswali Faradhi Anaweza Kuswali Nyuma Ya Anaeswali Sunnah?
23. Kukithirisha ´Amali Njema Kunaweza Kufuta Dhambi Kubwa?
24. Maiti Husikia Du´aa Za Wanaomuombea?
25. Mwanafunzi Katika Nchi Ya Ugenini Kuoa Kwa Nia Ya Talaka
26. Ni Lazima ´Aqiyqah Ifanywe Katika Mji Mtu Anapoishi
27. Hukumu Ya Kujiita Majina Ya Makafiri
28. Kumfunza Mke Wa Kaka Na Mke Wa Mjomba
29. Kumsusa Mubtadi´
30. Kunyanyua Mikono Wakati Wa Du´aa Baada Ya Darsa
31. Kuongea Kwenye Simu Msikitini
4
32. Kupewa Udhuru Kwa Ujinga
33. Kurudi Katika Mji Wa Kikafiri Kuwatendea Wema Wazazi
34. Kuswali Janaza Ya Shahidi Iliopita Miaka Mingi
35. Kusema "Sayyidna" Katika Tashahhud
36. Kusoma Qur-aan Makaburini
37. Kumsomea Maiti Suurat Yaasiyn
38. Kukabiri Baada Ya Kila Swalah Siku Ya Idi
39. Kutokwa Na Upepo Katikati Ya Twawaaf
40. Kuuza Maji Ya Zamzam
41. Allaah Hatomwangalia Mwenye Kuburuta Nguo Yake Kwa Kiburi
42. Muislamu Kupewa Udhuru Katika ´Aqiydah
43. Msafiri Wa Kunuia Kukaa Zaidi Ya Siku 3 Haruhusiwi Kufupisha Wala
Kujumuisha Swalah
44. Muziki Na kuvaa Mavazi Mafupi
45. Vitu Vimtokavyo Mwanamke Baada Ya Kukoga Janaba
46. Kufanya Bid´ah Kwa Kutokujua Kisha Mtu Akatubia Baada Ya Kujua
47. Du´aa Ya Shaykh Kwa Asiyekuwa Na Uzazi
48. Nasaha Za Shaykh al-Luhaydaan Kwa Wanandoa
49. Swahiyh al-Bukhaariy Na Muslim Hamna Hadiyth Dhaifu
50. Nyimbo Na Muziki Ni Haramu
51. Wanaume Kupiga Dufu
52. Wanawake Kumswalia Maiti
53. Wapeni Watoto Majina Ya Salaf-us-Swaalih
54. Watu Wa Peponi Hawatotatizika Katika Kumuona Allaah (Ta´ala)
55. Mjinga Kumsimamishia Hoja
5
Bismillaahi Rahmaani Rahiym
1. Nini Maana Ya ´Ilmaaniyyah?
Swali:
Ni nini ´Ilmaaniyyah? Na je, ni katika makundi 72?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Watu wanaposema ´Ilmaaniyyah wanachokusudia ni kwamba kusiwepo Dini,
bali watu wote wawe ni kama kitu kimoja. Kwa mfano asli ya mtu ni
mwarabu, kusiwepo tofauti ya Mnaswara na asiyekuwa Mnaswara, au
mshirikina na asiyekuwa mshirikina. ´Ilmaaniyyah yaani mtu asiamini Dini
yoyote. Ni katika mambo machafu mno yaliyozushwa ambayo
yamewadanganya watu wengi, wakapoteza mambo mengi ya Dini yao, na
huenda hata baadhi yao au wengi wao wakapotea (kutoka) katika Dini yao.
2. ´Aaliym Ni Katika Majina Ya Allaah (´Azza wa Jalla)
Swali:
Je, ´Aaliym ni katika Majina ya Allaah (´Azza wa Jalla), mtu akaitwa "´Abdul-
´Aaliym"?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Ndio. Allaah ni Muta´aaliy. Mtu aitwe ´Abdul-Muta´aaliy.
6
3. Allaah (Ta´ala) Alipomuumba Aadam Alimuongelesha Lugha Ipi?
Swali:
Wakati Allaah (Ta´ala) Alimuumba Aadam (´alayhis-Salaam), kwa lugha ipi
Alimuongelesha?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Sijui nini utafaidika (kwa kuuliza swali hili)? Alimuongelesha Allaah (Jalla wa
´Alaa) kwa alichomuelewa Aadam kutoka kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa).
Yasemekana Allaah (Jalla wa ´Alaa) Alimuongelesha Aadam kwa lugha ya
kiarabu. Lakini hili linahitajia uthibitisho.
4. Mtume Na Maswahabah Hawakufanya Khuruuj Wafanyazo Jamaa´at-ut-
Tabligh
Swali:
Yapi maoni yako kuhusu kutoka na Jamaa´at-ut-Tabliygh?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Sionelei hivyo. Na hili ni kutokana na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam):
"Atakayezusha katika amri yetu hii lisilokuwemo litarudishwa."
Katika upokezi mwingine:
"Atakayefanya ´amali isiyokuwa humo amri yetu, atarudishiwa."
7
Maswahabah ambao ni watu wenye hima na wao ni katika karne bora katika
Ummah huu, je walikuwa wakifanya hivi? Je, walikuwa wakitoka siku yoyote,
au katika wiki, au katika mwezi, au siku arubaini, je walikuwa wakifanya yote
hayo? Au walikuwa wamepitwa na kheri au kughafilika? Hapana!Kwa hivyo,
ni juu ya Ummah zilizokuja nyuma wafuate yale waliyoyafuata watu wa
kwanza wa Ummah huu. Na Kasema Imaam Maalik bin Anas:
"Hautofaulu Ummah wa mwisho huu isipokuwa kwa yale waliyofaulu kwayo
wa kwanza wao."
Kwa kheri wako nayo, na wana baadhi ya mambo yanayokwenda kinyume,
lakini yatosheleza kuwa ni ´amali ambayo haikufanya Mtume wa Allaah
(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Na wala hakuna dalili ya kwamba
alielekeza hilo. Kwa hivyo, vipi hizi karne bora zitaghafilika ambazo Mtume
(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kazitolea ushahidi wa kwanba ni karne
bora. Kumepita karne ya kwanza, ya pili, ya tatu, maimamu wa nne na
wanafunzi wao na karne nyingi zimepita na hawakujua katika hayo lolote ila
si chini ya miaka mia ya nyuma tu. Tunamuomba Allaah Atusamehe sisi na
wao, lakini ni juu ya Muislamu kuangalia njia aipitayo kama inaafikiana na
Shari´ah kwa kuwa Dini yote imetimia tokea uhai wa Mtume (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam) na imekamilika. Na kutokana na hili ndio maana Mtume
alitahadharisha Bid´ah, akasema:
"Tahadharini na mambo ya kuzusha, kwa hakika kila kitakachozushwa ni
Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu."
Na katika upokezi mwingine
"... na kila upotevu ni Motoni."
Ukweli ni kwamba, si kila mwenye kutaka kheri huafikiwa kuipata kheri hiyo.
Lazima kwa mwenye kutaka kufanya kheri, awe na dalili ya kheri hiyo.
5. Kuswali Nyuma Ya Imamu Mshirikina
Swali:
8
Ipi hukumu ya kuswali nyuma ya Imamu ambaye anajifunza uchawi na
anahudhuria walima zinazofanywa kwenye makaburi na wanayaadhimisha?
Pamoja na kujua ya kwamba ni Msikiti mmoja katika mji...
´Allaamah al-Luhaydaan:
Ikiwa mna uhakika ya kwamba anajifunza uchawi na kuufunza, hukumu ya
mtu huyu iko wazi katika Qur-aan Kariym kutokana na kisa cha Haruut na
Maaruut.
���ر � � �ن �� � � ��و� إ و�� � ����ن �ن أ�د ���
"Na (hao Malaika wawili) hawamfundishi yeyote mpaka wamueleze: “Hakika
sisi ni fitnah (mtihani), basi usikufuru (kufanya uchawi).” (02:102)
Kujifunza uchawi haijuzu. Wala sionelei akaachwa kuwa Imamu
anayewaongoza watu naye yuko na sifa kama hii. Na ikiwa anahudhuria
walima zinazofanywa kwenye makaburi, hili halijuzu. Kwa nini? Je, kichinjo
kinachinjwa kwa ajili ya aliye ndani ya kaburi? Bila shaka kitendo hichi ni
upotevu. Ikiwa kumechinjwa nyama kwa ajili ya maiti, hii ni Shirki kubwa.
´Allaamah al-Luhaydaan:
Bila ya shaka, kufanya Maulidi ni Bid´ah. Kwa hakika haya Maulidi
hayajulikani kuwepo kwake katika uhai wa Mtume Muhammad (Swalla
Allaahu ´alayhi wa sallam), wala katika uhai wa Maswahabah (Radhiya
Allaahu ´anhum), wala katika uhai wa Taabi´iyn, wala katika uhai wa
maimamu wanne, wala uhai wa wanafunzi wao. Hayakujulikana katika
ulimwengu wa Uislamu kitu kinachoitwa Maulidi kabisa. Sehemu ya kwanza
yalipopatikana ni Misri, yalizusha na Faatwimiyyuun, dola iliyokuwa chafu
ya maovu; al-Baatwiniyyah. Na yalipoanza kusambaa, katika watu wa Ahl-us-
Sunnah mtu wa kwanza aliyeanza kuyasambaza ni mfalme aitwae Irbel Iraaq
kutokana na ujinga wake wa kuwaiga Manaswara ambao na wao
wanaadhimisha siku ya ´Iysa (´alayhis-Salaam). Wakakataza wanachuoni hilo.
Yakaendelea kukua mpaka yakaenea leo katika ulimwengu wa Uislamu.
Maulidi yanaingia katika maneno ya Mtume:
9
"... na tahadharini na mambo ya kuzua, kwa hakika kila kitakachozushwa ni
Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu."
Na yanaingia katika maneno ya Mtume:
"Atakayefanya ´amali isiyokuwa humo amri yetu, atarudishiwa."
Mtu asijikurubishe kwa kitu anachokizingatia kuwa ni utiifu na kujikurubisha
kwa Allaah isipokuwa kwa dalili. La sivyo atarudishiwa mwenyewe. Na
kuichukulia siku hii kama Idi, na pengine kukafanywa makubwa zaidi ya
yanayofanywa katika Idi. Mtume alipoenda Madiynah na walikuwa Answaar
na siku ambazo wanasherehekea, akawaambia:
"Allaah Amewapa badala ya sikukuu za Kijaahiliyyah, Amewapa Idi al-Fitwr
na Id-ul-Adhhaa."
6. Ni Kina Nani Wahaabiyyah?
Swali:
Ni kina nani Wahaabiyyah? Na yapi madhehebu yao?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Neno Wahaabiyyah lilizusha maadui wa Da´wah ya Salafiyyah ambayo
ilihuishwa katika karne ya kumi na mbili Najdiy na Shayk-ul-Islaam
Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab na akasaidiwa na Muhammad bin Su´uud.
Kukakusanyika elimu pamoja na mfalme na dola ikawa dola ya Tawhiyd
kutokana na fadhila za Allaah (Jalla wa ´Alaa) kisha kwa sababu ya Da´wah
hii. Wakafanya kampeni maadui wa haki na kuiita Da´wah hii na
wanayoinusuru "Wahaabiyyah". Vinginevyo ni kwamba Shaykh na wafuasi
wake wote wako katika madhehebu na yale aliyokuwemo Imaam Muhammad
bin Hanbal na wafuasi wake. Na kuhusu ´Aqiydah yuko juu ya yale
aliyokuwemo Salaf wa Ummah huu kama Imaam Ahmad na wafuasi wake,
Shaafi´iy, Maalik na wafuasi wao. Na katika Da´wah hii hakuna
10
(hawakuunda) mfumo maalum na madhehebu maalum, bali madhehebu yao
ni kufuata madhehebu ya Imaam Ahmad. Isitoshe, haya madhehebu sio
lazima kwa mtu ashikamane na madhehebu yoyote, kwa hakika wanachuoni
unakuta mmoja wao mwanzoni wake yuko katika madhehebu ya Imaam
fulani, kisha anahama kwenda katika madhehebu mengine. Na kutokana na
hili kuna wanachuoni wengi maarufu (ambao hawakuwa na madhehebu
yoyote), kama mfano wa Ibn Daqiyq al-´Iyd ambaye alikuwa ni maarufu
katika karne ya saba Hijriyyah (hakuwa na madhehebu yoyoye).
7. ´Allaamah al-Luhaydaan Kuhusu Sigara
Swali:
Ipi hukumu ya kuvuta sigara?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Bila ya shaka ni katika Haramu. Kwa hakika Allaah (Ta´ala) Kawahalalishia
waja wake vitu vizuri katika riziki, na Akawaharamishia vitu vibaya. Na
siamini ya kwamba kuna mtu wa akili - hata kama mtu huyo atakuwa anavuta
- anaweza kusema sigara ni katika vitu vizuri. Si katika vitu vizuri sawa kwa
harufu yake, uchafu wake katika mwili, kuharibu mali bila ya faida yoyote ya
mwili; siamini ya kwamba kuna mtu wa akili ambaye anaweza kusema sigara
ni katika vitu vizuri (vilivyohalalishwa na Allaah). Bali hili ni katika majaribio.
Bila ya shaka ni katika vilivyoharamishwa. Mtu anapoteza mali yake bure bila
ya faida, mtu anafanya nazo maasi na maasi hayaji kwa kheri. Ni wajibu wa
kila Muislamu kujiepusha na yanayomdhuru.
8. ´Allaamah al-Luhaydaan Kuhusu Shaykh Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah)
11
Swali:
Kumekithiri maneno kuhusu Shaykh wetu Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah)
kwamba ana Itikadi ya Irjaa´. Je, una maneno yoyote ya kutuwekea wazi
manzila ya mwanachuoni huyu mkubwa?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Jambo la kwanza ni kuwa mtu huyu kishafariki (Allaah Amrehemu). Watu
wanatakiwa wajiepushe kwa kuwaudhi waliohai na waliokufa, isipokuwa tu
kama kutakuwepo maslahi. Na mtu huyu ana juhudi ambazo zinatakiwa
kushukuriwa (Rahimahu Allaah). Na hakulindwa na madhambi. Waliolindwa
na madhambi ni Mitume peke yao. Wengine wote, yanachukuliwa maneno
yao (yakiafikiana na haki) na yanaachwa (yakienda kinyume na haki); kama
alivyosema Maalik bin Anas.
9. Hakuna Mjinga Mkubwa Katika Dini Kama Huyu!
Swali:
Ipi hukumu ya mwenye kujuzisha kujenga Misikiti kwenye makaburi, na
anamtuhumu mwenye kukhalifu kauli hii kuwa ni mjinga haelewi nususi za
Dini?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Ikiwa huyu si mjinga, basi ntakuwa sijui mjinga wa nususi za Dini. Mtume
(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliomba Allaah Asiifanye kaburi lake kuwa
sanamu linaloabudiwa, na akawalaani Mayahudi na Maswara kwa
waliyokuwa wakiyafanya - kuyaabudu makaburi ya Mitume na watu wao
wema. Kisha kunajitokeza mtu na kusema makatazo haya si sahihi?
Je, Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walikuwa wakijenga kwenye
makaburi? ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anhu) na wengi katika Maswahabah
12
waliobashiriwa kuingia Peponi Madiynah waliyabomoa (majumba)
yaliyokuwa yamejengwa kwenye makaburi. Na si hao tu bali Maswahabah
wengi walifanya hivyo. Na ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu) alipokalifishwa na
mtu Abu al-Hiyaaj al-Asadiy na kumwambia:
"Je nikutume kwa alichonituma Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa
sallam); usiiache kaburi hata moja iliyoinuliwa isipokuwa uiweke sawa (na
zingine), wala usiache picha (sanamu) isipokuwa uiteketeze."
Maneno mfano wa haya hakuna haja wa kuyapiga Radd, yaani huyu
anayesema ya kwamba watu hawa hawafahamu Dini - kwa haya
wanayoyakataza.
10. Ifanye Swalah Ni Jambo Muhimu Zaidi Maishani Mwako
Swali:
Nimepitwa na Swalah ya Dhuhr na ´Aswr. Je, niswali kwanza ´Aswr au
Dhuhr?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Hapana, anza kuswali Dhuhr. Lakini jitahidi usiwe ni mwenye kupitwa na
Swalah na badala yake kuswali kila Swalah kwa wakati wake. Lifanye jambo
la Swalah ni jambo muhimu zaidi kwako, huko ni kumuiga Mtume (Swalla
Allaahu ´alayhi wa sallam). Kimbilia pia kuinufaisha nafsi yako.
11. Khitmah Ni Bid´ah
Swali:
13
Katika mji wetu baada ya kuzikwa maiti, linakusanyika kundi la wanafunzi
katika nyumba ya maiti na wanasoma Qur-aan kwa nia ya kumtumia maiti
thawabu. Ipi hukumu ya hilo?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Bila ya shaka, haya ni katika mambo yaliyozushwa. Mambo ya kuzushwa
yanatofautiana athari yake, kwa ujumla yote ni Bid´ah. Maswahabah (Radhiya
Allaahu ´anhum) walikuwa wakifiwa na watoto, baba, na mama zao na
hawakuwahi kukusanyika katika nyumba ya yeyote na kusoma Qur-aan.
Wala kumueka mtu mmoja aje kusoma Qur-aan nyumbani kwa kumnufaisha
maiti wao. Kila kilichozushwa katika kujikurubisha kwa Allaah (Jalla wa
´Alaa), kinaingia katika Hadiyth ya ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha) iliopo
katika Swahiyhayn, pale (Mtume) alipotahadharisha mtu kufanya ´amali
katika Dini hii isiyokuwa ndani yake na amri ya Mtume (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam). Mizani imara ya matendo yetu, ni Hadiyth:
"Atakayefanya ´amali ambayo hamna humo amri (Dini) yetu atarudishiwa
mwenyewe."
Huu ndio mzani wa ´amali zetu. Na
Hadiyth:
"Hakika ya ´amali hulipwa kutegemea kwa nia."
Mi mizani ya ´amali za moyoni.
12. Da´wah Kuifanyia Biashara
Swali:
Ipi hukumu ya kuchukulia ujira; vitabu, makala, sahifu na magazeti vya
kidini?
14
´Allaamah al-Luhaydaan:
Inajuzu kwa mtu kuvichukulia vitu hivi ujira. Lakini kule kutoviuza kwake na
akawa Anatafuta ujira kutoka kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) hili ni bora zaidi.
Hivi ni vitu vya Kishari´ah vya kheri. Inatakikana kwa kitu mtu akiweza
avifanye kwa kutafuta Wajh wa Allaah, atosheke na fadhila atazopata kutoka
kwa Allaah nazo ni bora zaidi na wala havilingani baina ya ujira huu
Ataoupata kwa Allaah na baina ya atakayempa ujira ima wa kidini au
kidunia.
13. Hukumu Ya Dhikr Ya Pamoja (Kikundi)
Swali:
Ipi hukumu ya kufanya Dhikr ya pamoja (kikundi) kwa sauti moja?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Maswahabah walikuwa hawafanyi hivyo. Bali ilikuwa kila mmoja (Allaah
Amuwie radhi) anamuiga Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa
kufanya Adhkaar zilizowekwa. Hivyo jambo hili ni uzushi katika Dhikr.
14. Haijuzu Kumpa Wasia Mwenye Kurithi
Swali:
Je, inajuzu kwa mrithi kumuusia mmoja wa warithi? Je, wasia naweza kumpa
mmoja wa watoto wangu?
15
´Allaamah al-Luhaydaan:
"Hakuna wasia kwa mrithi, hakika Allaah Kampa kila mwenye haki haki
yake, hakuna wasia kwa mwenye kurithi."
Haijuzu kumpa wasia mmoja wa warithi kwa chochote; si mtoto wala
asiyekuwa mtoto.
15. Uadilifu Kwa Mwenye Mke Zaidi Ya Mmoja
Swali:
Kuwafanyia uadilifu wake ni katika makazi peke yake?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Anatakiwa kufanya uadilifu kwa (yote) ayawezayo katika haki za mke. Na
Allaah Anajua mwenye kuwa na uwezo na asiyekuwa na uwezo. Mtume
(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema kwa yule mwenye mke zaidi ya
mmoja na asiwafanyie uadilifu atakuja siku ya Qiyaamah na bega lake
limepinda; yaani atakuwa ni mwenye fedheha mbele ya watu. Uadilifu ni
jambo kubwa. Watu wanapaswa kuwa waangalifu kwa hili katika mambo
yote; awe ni muadilifu kwa kuhukumu, awe ni muadilifu kwa anachowapa
watoto na wake zake.
16. Hukumu Ya Kusema Allaah Akimponyesha Mgonjwa Wangu
Nitamshukuru
Swali:
Mtu kusema:
16
"Allaah Akimponya mgonjwa wangu nitamshakuru Allaah."
Je, huku ni kuweka nadhiri?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Subhaana Allaah. Na ikiwa Hakumponya hatomshukuru Allaah? Hii ni
nadhiri dhalimu. Ana azima chafu. Kwa kuwa inavyofahamika ni kwamba
ikiwa mtu huyu Allaah Hakumponyesha mgonjwa wake hatomshukuru
Allaah. Huku ni kuweka nadhiri kwa shari. Sio nadhiri bali ni shari.
17. Mwenye Kusema Ya Kwamba Dunia Imeumbwa
Kwa Ajili Ya Muhammad
Swali:
Ipi hukumu ya mwenye kusema ya kwamba dunia imeumbwa kwa ajili ya
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?
Allaah Anasema:
و�� )��ت ا"&ن� وا$ س إ�� "� !دون
"Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi." (51:56)
Kisha anasema huyu mjinga mpumbavu ya kwamba imeumbwa kwa ajili ya
Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ametakasika Allaah. Ni
ajabu ilioje ya maneno haya na uongo wake. Allaah Anasema:
و�� )��ت ا"&ن� وا$ س إ�� "� !دون
"Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi." (51:56)
Hakuumba (kitu) chochote kwa ajili ya mwengine.
17
18. Kutibu Uchawi Kwa Kutumia Uchawi
Swali:
Huyu anauliza hukumu ya kutibu uchawi kwa kutumia uchawi?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Allaah Hakufanya kwa Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa
sallam) dawa ya Haramu kiasi ambacho kukawa hakuna dawa nyingine
isipokuwa kwa kutumia tu dawa hiyo ya Haramu... yaani yawezekana
ikaponyesha dawa hii ya Haramu, lakini kuna dawa zingine zisizo za
Haramu. Sahihi ni kwamba si Halali kujitibu kwa kutumia uchawi. Isitoshe, ni
nani aliyekwambia kuwa maradhi haya ni uchawi? Je, ni mchawi? Wao sio
wakweli. Je, ni yule ambaye anatumia majini? Wao pia sio wa kweli. Ni nani
ambaye ni muaminifu na ni muadilifu ambaye ametoa ushahidi kuwa huu ni
uchawi?
19. Radd Kwa Mwenye Kupinga Kustaawa Kwa Allaah Juu Ya ´Arshi Yake
Swali:
Ipi hukumu ya mwenye kusema Allaah Hayuko juu ya ´Arshi na wala
Hayuko kila mahala bali Allaah hana mahala? Ipi Radd kwa kauli hii?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Ikiwa hana mahala, yuko wapi sasa? Asli ya maneno haya ni kwamba
anakanusha ya kuwa hakuna mungu kabisa. Bila ya shaka huyu ni upotevu
mkubwa. Allaah Anasema:
ن ,�� ا" رش ا*�وى ـ �� ا"ر�
18
"Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rahmah) juu ya ‘Arsh Istawaa (Yuko juu kwa
namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah)." (20:05)
Kisha anasema huyu mjinga "hapana" si kweli. Au akajikalifisha nafsi yake
mwenyewe na (badala ya kusema Kastawaa juu ya ´Arshi Yake) yeye akasema
Katawala. Na je, kabla ya wakati huyo alikuwa Hajatawala juu ya ´Arshi? Mtu
husema "fulani katawala kitu filani" ikiwa kabla ya hapo hajatawala kwa kitu
hicho wala hana neno lolote juu yacho. Madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-
Jamaa´ah katika Qadhiya hii ndio ya haki na nususi za kutegemewa kama
ilivyokuja kutoka kwa Allaah na kwa Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi
wa sallam). Hii ndio Manhaj ya watu wa haki.
20. Tasbiyh Ni Bid´ah
Swali:
Muulizaji anauliza hukumu ya Tasbiyh?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Tasbiyh sio katika Sunnah. Ataeichukulia kuwa ni Sunnah, basi (ajue kuwa) ni
Bid´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akimsabihi Allaah
kwa vidole vya mikono yake. Na alipoambiwa ´Abdullaah bin Mas´uud ya
kwamba kuna watu wanaleta tasbihi kwa mawe, na walikuwa ni katika
wanafunzi wa ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhu), na kwamba
wanakusanyika mahala. Watu katika wakati huo hawakuwa na Tasbiyh.
Akatoka (Ibn Mas´uud) na kukaa nao. Kulikuwa mmoja wao anayesema
"Semeni mia", basi wanamsabihi Allaah mara mia na wakiendelea kufanya
vivyo hivyo. Alipohakikisha hilo (Ibn Mas´uud), akawaambia "Je, nyinyi ni
waongofu zaidi kuliko Maswahabah wa Mtume Muhammad au mmetuletea
tu Bid´ah? Tendeni ´amali zenu zitahifadhiwa. Atawakataza na akachukulia
hilo ni katika Bid´ah. Wamesema hili wanachuoni walioandika vitabu kuhusu
Bid´ah na baadhi yao ni katika wanachuoni wa Maalikiyyah wa Indonesia.
19
21. Kuswali Swalah Ya Usiku Jamaa´ah Nyumbani
Swali:
Je, inajuzu kuswali Qiyaam-ul-Layl (Swalah ya usiku) nyumbani usiku?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Ndio, inajuzu.
22. Anaeswali Faradhi Anaweza Kuswali Nyuma Ya Anaeswali Sunnah?
Swali:
Inajuzu kutofautiana nia ya maamuma na Imamu katika Swalah?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Ndio, inajuzu. Inajuzu mwenye kuswali Swalah ya faradhi kuswali nyuma ya
mwenye kuswali Swalah ya Naafil (Sunnah), au kinyume chake. Na wala
hakuna neno kufanya hivyo In Shaa Allaah.
23. Kukithirisha ´Amali Njema Kunaweza Kufuta Dhambi Kubwa?
Swali:
20
Je, dhambi kubwa inaweza kufutwa kwa kufanya ´amali njema?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Ndio linawezekana. Lakini elimu yake iko kwa Allaah, sisi hatuwezi kujua
hilo. Mtu akifanya ´amali nyingi na akatubia kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa),
inakuwa ni Tawbah (katubia kwa Allaah) isipokuwa tu kama kuna haki ya
waja (umechukua), hili halikafiriwi kwa Tawbah. Tawbah inapokelewa kwa
yale ambayo ni baina yako wewe na Allaah (Jalla wa ´Alaa). Ama haki za
waja, ni lazima kuzirudisha. Isipokuwa tu kama mtu huyo atakusamehe, au
Akakuridhia Allah (Jalla wa ´Alaa).
24. Maiti Husikia Du´aa Za Wanaomuombea?
Swali:
Je, maiti husikia Du´aa za watu wanaowaombea walio hao?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Ndio wanasikia. Kafiri anasikia yanayomuudhi na kumbughudhi, na
muumini anasikia yanayomfurahisha na kumridhisha. Lakini hawezi kujibu.
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) siku ya Badr alipowaita waliouawa
katika vita vya Badr. Akamwambia ´Umar "Vipi utawaita watu wasiosikia?"
Akasema "Wanasikia mnayowaambia, lakini hawawezi kujibia." Waumini
wanasikia Du´aa za waumini wanazowaombea, lakini hawawezi kujibia.
25. Mwanafunzi Katika Nchi Ya Ugenini Kuoa Kwa Nia Ya Talaka
21
Swali:
Mimi ni kijana naishi katika mji wa kikafiri kwa ajili ya masomo. Je, inajuzu
kwangu kuoa kwa nia ya Talaka kwa kujizuia na fitina?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Kuoa kwa ni ya Talaka kunakurubiana na Mut´ah ambayo ameiharamisha
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) iliyokuwa inaruhusiwa katika
Jaahiliyyah. Kisha ikaharamishwa kama lilivyothibiti hilo katika upokezi
mwingi wa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) ´Aliy na wengine. Kuoa
kwa nia ya Talaka, mtu akanuia ni kwa Mut´ah tu na akawa na azima ya
kutokuwamke wake, hili ni katika mambo wamekhitilafiana wanachuoni. Na
bila ya shaka kauli ya sahihi ni kwamba ni Haramu. Ikiwa umelazimika kuoa,
oa na weka nia na uazimie kwamba ikiwa atakuwa mwema, atakuwa mke
wako; na ikiwa hakuwa mwema Allaah Kajaalia kwa yule mambo
yamemkuwia mazito ataliki. Lakini asioe kwa kunuia kutaliki. Jambo hili
linakwenda kinyume na misingi iliyowekwa ya ndoa na Allaah (Jalla wa
´Alaa) kwa watu.
26. Ni Lazima ´Aqiyqah Ifanywe Katika Mji Mtu Anapoishi
Swali:
Nimepata mtoto wa kiume na niko na pesa kidogo. Je, inajuzu kwangu
kumfanyia ´Aqiyqah katika mji wa Kiislamu usiyokuwa wangu ambapo
kunaruhusiwa kufanya ´Aqiyqah?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Hakuna ubaya kufanya hivyo. Muhimu tu kufanywe ´Aqiyqah.
22
27. Hukumu Ya Kujiita Majina Ya Makafiri
Swali:
Ipi hukumu ya mwenye kujiita kwamajina ya baadhi ya makafiri?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Akiitwa kwa majina ya baadhi ya makafiri, dogo tuwezalo kusema ni kwamba
hii ni aina ya kujifananisha nao. Na Mtume Anasema:
"Mwenye kujifananisha na watu, basi yeye ni katika wao."
Tunamuomba Allaah Atukinge. Kipi kinachomkataza kuitwa majina ya
Kiislamu na waislamu. Na lau angeenda katika vitabu angepata majina mengi
sana. Hakuitwa majina ya baadhi ya makafiri isipokuwa ni kwa sababu
amevutika nao.
28. Kumfunza Mke Wa Kaka Na Mke Wa Mjomba
Swali:
Je, inajuzu kumfunza mke wa kaka au mke wa mjomba?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Ama kubainisha tu kitu, hakuna ubaya kufanya hivyo. Ama kukaa pamoja
naye na kumfunza, kufanya darsa kabisa na pengine hata wakawa ni wao
peke yao hili halijuzu. Ama kule kumueleza tu Halali na Haramu, hakuna
ubaya kufanya hivyo.
23
29. Kumsusa Mubtadi´
Swali:
Ni ipi dhawabiti ya kumsusa Mubtadi´?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Ukiweza kumnasihi na kumuelekeza na kumuonesha haki, fanya hivyo. Na
ikiwa hatokubali, achana naye.
30. Kunyanyua Mikono Wakati Wa Du´aa Baada Ya Darsa
Swali:
Je, inajuzu kwangu nitapokutana darsa Msikitini niombe baada ya darsa na
kunyanyua mikono yangu na wanyanyue wasikilizaji mikono yao?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Hakuna ubaya kufanya hivyo. Kwa hakika kunyanyua mikono wakati wa
Du´aa, ni sababu ya kukubaliwa Du´aa kama ilivyo katika Hadiyt ilioko katika
Swahiyh. Na ninakumbuka ya kwamba as-Suyuutwi (Rahimahu Allaah)
kaandika Risaalah kuhusu kunyanyua mikono wakati wa Du´aa. Na anasema
Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah:
"Hakika ni katika Sunnah kunyanyua mikono wakati wa kuomba Du´aa."
Lakini kunyanyua mikono, isiwe ni kama wanavyofanya baadhi ya watu
wanapotoa Salaam wananyanyua mikono kuomba Du´aa moja kwa moja na
wamemaliza. Akitaka kuomba Du´aa hakuna ubaya akanyanyua mikono,
24
isipokuwa tu wakati wa Du´aa kuitikia "Aamiyn" katika Khutbah ya siku ya
Ijumaa. Inatakiwa kwa msikilizaji kutulia na kukaa kimya, hakuna neno
akaitikia Aamiyn kwa sauti ya chini asijishawishi mwenyewe na wenye
kuswali.
31. Kuongea Kwenye Simu Msikitini
Swali:
Ipi hukumu ya kuongea kwenye simu ndani ya Msikiti?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Kule kuongea tu hakuna ubaya, ikiwa sio maongezi mabaya. Kama jinsi
anavyoweza kuongea na mtu, inajuzu kwake kuongea na swahibu wake kwa
simu, bila ya kuwashawishi watu.
32. Kupewa Udhuru Kwa Ujinga
Swali:
Je, mtu anaweza kupewa udhuru katika mambo ya ´Aqiydah?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Shirki kubwa hapewi udhuru yeyote. Mwenye kumuabudu asiyekuwa Allaah
(Jalla wa ´Allaa), hakuna yeyote awezae kumpa udhuru na kusema ni mjinga.
Je, huyu anayemuabudu anaona kuwa anamiliki kunufaisha na kudhuru,
kupatikana kwa kitu na kukosena, kutajirisha na kufukarisha? Ama baki ya
25
´amali ambazo sio ´Ibaadah na sio Shirki, yule ambaye hajui uhakika wake na
kwa mtu kama yeye inawezekana kweli akawa hajui, Allaah Kasema:
! ث ر*ول � !�ن ��� �� � ذ � و�� �
"Na Hatukuwa Wenye kuadhibu (yeyote) mpaka Tupeleke Mjumbe
(kuwaonya)." (17:15)
Na ni lazima kumsimamishia hoja. Lakini asibaki mtu katika ujinga na
kusema mimi ni mwenye kupewa udhuru. Akafanya apendacho na kusema
mimi sijui kuwa ni Haramu, hapana! Ni lazima aulize na ajifunze. Ama
kuhusu Shirki:
3 � 2��ر أن 5�رك !3 و2��ر "ك "�ن �5�ء إن� ا"�ـ� �� دون ذ
"Hakika Allaah Haghufuri kushirikishwa; na Anaghufuria yasiyokuwa hayo
kwa Amtakae." (04:48)
Ni lazima kwa mja kujiepushe na kila kitachomuingiza Motoni. Moto wa
duniani ambao ni dhaifu mara mia kuliko Moto wa Aakhirah, yatosha kuwa
onyo, vipi kwa Moto wa Aakhirah?
33. Kurudi Katika Mji Wa Kikafiri Kuwatendea Wema Wazazi
Swali:
Je, inajuzu kwa aliyefanya Hijrah kurudi katika mji wa kikafiri ili kuwatendea
wema wazazi wake?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Ikiwa kurudi kwake hawezi kudhihirisha Dini yake, haijuzu kwake kurudi.
Na ikiwa kurudi katika mji wake ataweza kuidhihirisha Dini yake na wala
haitomtatiza na wazazi wake ni Waislamu, arejee kwa kuwa kuwatendea
wema wazazi na kuwaangalia ni aina ya Jihaad.
26
34. Kuswali Janaza Ya Shahidi Iliopita Miaka Mingi
Swali:
Mimi naishi mji wa mbali, jeinajuzu kwangu kuswali Swalah ya Janaza
kuwaswalia mashahidi waliokufa katika vita ya Uhud?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Hapana waombee maghfirah. Swalah ya Janaza, haiswaliwi Janaza ambayo
imeshapita miaka 1.400 na zaidi ya miaka 20. Na hili halikufanywa na Mtume
(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wala Maswahahah wala Taabi´uun.
Isitoshe waliokufa katika Uhud, asli ni kwamba haswaliwi anaekufa katika
Jihaad.
35. Kusema "Sayyidna" Katika Tashahhud
Swali:
Kusema "Sayyidna Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)" katika
Tashahhud ndani ya Swalah inajuzu au hapana?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Hapana haijuzu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwafunza nini
watachosema Maswahabah katika Swalah zao na Tashahhud zao, walikuwa
wakisema:
"Allaahumma Swalli ´alaa Muhammad" kama ilivyo katika Hadiyth ya Ibn
Mas´uud. Hakukuthibiti neno "Sayyidna" (Bwana wetu). Bila shaka yeye ni
bwana wa wanaadamu wote. Lakini tukomeke katika ´Ibaadah zetu kwa yale
27
tuliyojifunza. Mtume alipoambiwa "Tufunze ni vipi tutakuswalia". Hakusema,
semeni "Allaahumma Swali ´alaa Sayyidna Muhammad." Kawafunza ni vipi
watamswalia na ndio Swalah bora kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam); Swalah hizo ambazo watu walijifunza kutoka kwake nazo
ni Hadiyth Swahiyh. Kwa hivyo, mtu asiseme katika Swalah yake "Ashhadu
anlaa ilaaha illa Allaah, wa ashhadu anna Sayyidna Muhammad RasuuluLlaah",
hapana akomeke na aliyosema Mtume wa Allaah. Mtume wa Allaah ni mjuzi
zaidi wa haki ya ´Ibaadah hii kuliko kiumbe mwengine yeyote.
36. Kusoma Qur-aan Makaburini
Swali:
Je, inajuzu kusoma Qur-aan kwenye kaburi? Kuna baadhi ya Mahanafiy
wanadai ya kwamba kuna Hadiyth 23 zinatoa dalili kujuzu kusoma Qur-aan
kaburi na kwamba ni Hadiyth Swahiyh.
´Allaamah al-Luhaydaan:
Haikuthibiti ya kwamba Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum)
walipokuwa wakienda makaburini walikuwa wakisoma Qur-aan. Na Mtume
(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuamrisha kisomo [kwenye makaburi].
Na kusema kwake kwamba [kuna Hadiyth Swahiyh], lau angetutajia Hadiyth
moja tu katika Hadiyth hizi ilituiangalie ukweli wake.
37. Kumsomea Maiti Suurat Yaasiyn
Swali:
Ipi hukumu ya kusoma Suurat Yaasiyn kwenye kaburi?
28
´Allaamah al-Luhaydaan:
Haijuzu. Haijuzu kwa mtu kwenda makaburini ili kusoma Qur-aan huko.
Qur-aan inasomwa Misikitini na majumbani. Ama makaburini, lililothibiti ni
waliohai kuwatolea Salaam waliokufa:
"Assalaam ´alaykum daara qawmin mu-uminiyn."
Awaombee maghfirah, na wala asiwasomee Qur-aan.
38. Kukabiri Baada Ya Kila Swalah Siku Ya Idi
Swali:
Siku za ´Iyd-ul-Adwhaa tunakabiri kwa sauti baada ya kila Swalah. Je, hili
linajuzu?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Inajuzu. Watu walikuwa wakikabiri hata Mina, alikuwa ´Umar akikabiri na
watu nao wakikabiri na wakipandisha sauti. Lakini si kwa Takbiyra sauti ya
pamoja. Kila mmoja akabiri...
39. Kutokwa Na Upepo Katikati Ya Twawaaf
Swali:
Mwenye kufanya ´Umrah akitokwa na upepo katikati ya Twawaaf yake. Je,
atoke ili atawadhe kisha arudi au akamilishe atapomaliza?
29
´Allaamah al-Luhaydaan:
Hapana atoke. Mtume (´alayhis-Salaam) kasema kwamba kutufu katika
Ka´abah ni Swalah, na Swalah imeshurutishwa kuwa na Twahara. Anatakiwa
kutoka atawadhe kisha akirudi akamilishe pale alipokuwa ameishia.
40. Kuuza Maji Ya Zamzam
Swali:
Je, inajuzu kuuza maji ya zamzam?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Atakayechukua maji ya mzamzam, inakuwa ni yeye ndiye mwenye
kuyamiliki. Akitaka kuyauza inajuzu.
41. Allaah Hatomwangalia Mwenye Kuburuta Nguo Yake Kwa Kiburi
Swali:
Vipi kuvaa Isbaal?
´Allaamah al-Luhaydaan:
"Allaah Hatomwangalia mwenye kuburuta nguo yake kwa kiburi."
"Kilichoko chini ya kongo mbili za miguu ni Motoni."
30
Kunaingia humo kubuta nguo ikiwemo na suruwali. Nguo ya muumini
inapaswa kuwa katikati ya mguu, na wala hakuna ubaya ikiwa itafika mpaka
kwenye kongo mbili za miguu. Na kilichoko chini ya kongo mbili za miguu ni
Motoni. Na kumekuja Hadiyth nyingi kuhusiana na hili.
"Allaah Hatomwangalia mwenye kuburuta nguo yake kwa kiburi."
42. Muislamu Kupewa Udhuru Katika ´Aqiydah
Swali:
Baadhi ya Madu´aat katika nchi ya Urusi wanasema mwenye kuishi Urusi
wao wako na udhuru kwa ujinga katika ´Aqiydah. Vipi kuwaradi?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Ujinga ambao hakukupatikana sababu ya kuuondoa, yawezekana ikawa ni
kweli. Lakini kumshirikisha Allaah, hakuna mtu yeyote anayepewa udhuru.
Kwa mfano mtu hawezi kuabudu sanamu na kaburi na kusema kuwa alikuwa
hajui kuwa haijuzu, kwa kuwa angelifirikia kwa akili yake ataona kuwa
anayemuabudu badala ya Allaah hamiliki si mauti, uhai wala ufufuo. Ama
mambo ambayo hayafikiwi isipokuwa mpaka kwa elimu na akakosa mtu
mwalimu wa kumfunza, kwa mfano kazaliwa katika mji wa kikafiri na wala
hakupata wa kumfunza Swalah, idadi yake, wakati wake; anasema kuwa ni
Muislamu lakini hakuna yeyote wa kumfunza, huyu anapewa udhuru kwa
hili lakini hapewi udhuru kwa kuabudu asiyekuwa Allaah.
43. Msafiri Wa Kunuia Kukaa Zaidi Ya Siku 3 Haruhusiwi Kufupisha Wala
Kujumuisha Swalah
31
Swali:
Ikiwa mtu ni msafiri na akafika Madiynah anapoenda. Je, inajuzu kwake
kujumuisha Swalah muda ataokuwepo hapo?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Ikiwa Madiynah anapokwenda hakunuia kubaki zaidi ya siku nne, bali kanuia
kukaa siku tatu na siku ya nne kurudi, kauli ya sahihi ni kwamba hairuhusiwi
kwake kujumuisha wala kufupisha. Kwa kuwa asli ya kubaki ni kwamba mtu
asifupishe Swalah wala kujumuisha na nyingine isipokuwa tu kwa haja.
Kinachoruhusiwa katika safari ni kufupisha Swalah, ama kujumuisha ni
ruhusa [dharurah] imewekwa kwa mwenye kuihitajia. Kauli ya jamhuri ya
wanachuon ni kwamba kuchukua ruhusa ya safari, haiwi kwa mtu ambaye
amenuia kukaa zaidi ya siku nne. Wamechukua kwa yale wayajuayo kwa
yakini kwamba Mtume alifasiri akafupisha na hilo ilikuwa ni wakati wa Hajj
peke yake, ama kabla ya hapo haijulikani kama alikuwa anajua lini safari yake
itaisha.
44. Muziki Na kuvaa Mavazi Mafupi
Swali:
Kumeenea kukithiri kwa muziki na [wanawake wanaovaa] mavazi mafupi
yanayokhalifu haya. Ipi nasaha kwa watu hawa?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Twatumai - In Shaa Allaah - hapa Msikitini hakuna mmoja katika watu hao.
Na tunamuomba Allaah Awaongoze.
32
45. Vitu Vimtokavyo Mwanamke Baada Ya Kukoga Janaba
Swali:
Ipi hukumu ya kutokwa na "saail" (ni maji maji yanayotoka kwenye tupu ya
mwanamke) baada ya kukoga janaba na kuendelea kutoka huku hata wakati
wa kuswali faradhi?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Ikiwa yataendelea kumtoka, hukumu yake ni kama hukumu ya mwenye
maradhi ya kutokwa hovyo na mkojo. Sio wajibu kukoga... Ikiwa yanaendelea
kumtoka, hukumu yake ni kama ya mwenye maradhi ya kutokwa hovyo na
mkojo. Atatawadha katika kila Swalah ya faradhi.
46. Kufanya Bid´ah Kwa Kutokujua Kisha Mtu Akatubia Baada Ya Kujua
Swali:
Je, husamehewa mwenye kufanya Bid´ah kwa kutokujua na alikuwa na nia
nzuri?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Hapana. Kwanza Bid´ah ni upotofu. Na Hadiyth:
"Na kila Bid´ah ni upotofu."
Katika lafdhi nyingine:
"Na kila upotofu ni Motoni."
Njia ya kuingia Motoni haiwi sababu ya kusamehewa, isipokuwa ikiwa njia
hii ya Motoni mtu alijirejea na ikawa mja huyu kila anapokumbuka
33
alichokifanya anatubia upya na kuomba msamaha... Bid´ah mtu hasamehewi
kwayo. Lakini akijuta au akajua kisha akatubia, atasamehewa kwa Tawbah
yake.
47. Du´aa Ya Shaykh Kwa Asiyekuwa Na Uzazi
Swali:
Niombee kwa Allaah afya mimi sina uzazi?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Tunamuomba Allaah Akupe afya na Amponye kila mgonjwa katika
wagonjwa wa Waislamu. Awape afya nzuri kwenye miili yao na roho zao na
akili zao. Na Ummah wa Kiislamu aupe hali nzuri kwa sasa na katika
Mustaqbal.
48. Nasaha Za Shaykh al-Luhaydaan Kwa Wanandoa
Swali:
Mimi nataka kuoa, waniusia nini?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Ninakuusia kumcha Allaah (Jalla wa ´Alaa) na kumshukuru kwa
Aliyokukadiria katika ndoa hii. Umhimize mke wako kuhifadhi Swalah tano
kwa wakati wake, kuwa na heshima na kujisitiri, kusaidiana na kuishi kwa
34
wema. Ninamuomba Allaah Awape watoto wema na mapatano katika maisha
yenu ya ndoa, na afanye iwe hivyo kwa kila wanandoa.
49. Swahiyh al-Bukhaariy Na Muslim Hamna Hadiyth Dhaifu
Swali:
Je, katika Swahiyh al-Bukhaariy na Muslim kuna Hadiyth dhaifu?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Hapana. Swali hili halina maana. Wakusudia nini, wataka kusema kwamba
kuna mwanachuoni yeyote anayesema kwamba katika al-Bukhaariy kuna
Hadiyth dhaifu? Ummah mzima umekubaliana kwa Swahiyh al-Bukhaariy na
Muslim kuwa ni Hadiyth Swahiyh. Maswali kama haya hayana kheri.
50. Nyimbo Na Muziki Ni Haramu
Swali:
Ipi hukumu ya kusikiliza nyimbo na muziki?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Kusikiliza nyimbo zenye ala ya taarabu, bila ya shaka ni Haramu.
51. Wanaume Kupiga Dufu
35
Swali:
Hukumu ya wanaume kupiga dufu?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Dufu kawaruhusu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati wa
harusi kwa wanawake. Wanaume wanatakiwa kujiepusha nayo.
52. Wanawake Kumswalia Maiti
Swali:
Ipi hukumu ya wanawake kumswalia maiti Jamaa´ah nyumbani?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Ikiwa maiti yuko katika nyumba ambapo kuna wanawake, na wakamswalia
[maiti] kabla hajatolewa nje kwenye Muswalla, hakuna ubaya kufanya hivyo.
53. Wapeni Watoto Majina Ya Salaf-us-Swaalih
Swali:
Nimeruzukiwa mtoto, unaninasihi nimwite vipi?
´Allaamah al-Luhaydaan:
36
Mpe jina mojawapo la wanawake wa Salaf-us-Swaalih (wema waliotangulia);
mwite Khadiyjah, Ruqayyah, Faatwimah, ´Aaishah, Zaynab. Majina ni mengi.
54. Watu Wa Peponi Hawatotatizika Katika Kumuona Allaah (Ta´ala)
Swali:
Je, watu wa Peponi wanatofautiana katika kumuona Allaah (´Azza wa Jalla)?
Kuna ambao watakuwa wakimuona kila siku, wengine kila baada ya siku
mbili, wengine kila wiki.
´Allaamah al-Luhaydaan:
Hapakuja kitu chochote kuhusiana na hayo katika Hadiyth. Lililothibiti ni
kwamba watamuona Allaah (Jalla wa ´Alaa), na kwamba hawatosongamana
katika kumuona, na hawatotatizika katika kumuona, na kwamba watamuona
kama wanavyoona mwezi mweupe usiku wa Badr.
55. Mjinga Kumsimamishia Hoja
Swali:
Vipi mtu atapata kumsimamishia hoja mjinga?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Kwa kumsimamishia hoja.
37
Chanzo:
http://www.alharamain.gov.sa/index.cfm?do=cms.scholarsubject&schid=309
81&subjid=31339&audiotype=lectures&browseby=speaker
Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad , na ahli zake na
Maswahabah zake na watakaowafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah.