1
SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
WIZARA YA MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO
HOTUBA YA MAKADIRIO YA MAPATO NA
MATUMIZI YA WIZARA YA MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO KWA MWAKA WA FEDHA
2014/2015
JUNI 2014
2
YALIYOMO UKURASA
I UTANGULIZI ............................................................. 4
II. UTEKELEZAJI WA KAZI ZA KAWAIDA NA MAENDELEO
KWA MWAKA 2013/2014 NA MALENGO YA MWAKA
2014/201………………………………………………………………………….6
IIa) OFISI KUU PEMBA ..................................................... 8
IIb) UTAWALA NA SERA ................................................... 9
(i) IDARA YA MIPANGO, SERA NA UTAFITI ....................... 10
(i-1) MIRADI YA MAENDELEO ............................................. 11
(i-1.1) MIRADI YA UJENZI WA BARABARA ………………………11
(i-1.1.1) Mradi wa Barabara Tatu za Kaskazini Pemba ........... 12
(i-1.1.2) Mradi wa Barabara ya Wete-Chake ......................... 13
(i-1.1.3) Mradi wa Barabara ya Ole-Kengeja ......................... 14
(i-1.1.4) Mradi wa Barabara za Vijijini Kaskazini Pemba: ........ 14
(i-1.1.5) Mradi wa Barabara Zinazoingia Mjini Unguja ........... 15
(i-1.1.6) Mradi wa Barabara 3 za Vijijini Unguja .................... 16
(i-1.1.7) Mradi wa Barabara 6 za Vijijini Unguja .................... 16
(i-1.2) MIRADI YA SEKTA YA USAFIRI WA ANGA .................. 17
(ii) IDARA YA UTUMISHI NA UENDESHAJI ........................ 26
IIc. SEKTA YA USAFIRI WA NCHI KAVU. .......................... 28
3
(i) IDARA YA UJENZI NA UTUNZAJI WA BARABARA ........... 29
(ii) IDARA YA USAFIRI NA LESENI ................................... 34
IId) SEKTA YA MAWASILIANO ......................................... 37
(i) IDARA YA MAWASILIANO ........................................... 38
IIe) SEKTA YA USAFIRI WA ANGA ................................... 41
(i) MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE ZANZIBAR ............ 41
IIf) SEKTA YA USAFIRI WA BAHARINI ............................. 48
(i) MAMLAKA YA USAFIRI BAHARINI .............................. 48
(ii) SHIRIKA LA BANDARI ................................................ 52
(iii) SHIRIKA LA MELI NA UWAKALA. .............................. 57
III HITIMISHO. .............................................................. 60
IV. MAOMBI YA FEDHA KWA MWAKA 2014/2015 .............. 62
KIAMBATANISHO NAMBA 1: ............................................ 63
KIAMBATANISHO NAMBA 2: ............................................ 67
KIAMBATANISHO NAMBA 3: ........................................... 70
KIMBATANISHO NAMBA 4: ............................................ 725
KIAMBATANISHO NAMBA 5: .......................................... 933
KIAMBATANISHO NAMBA 6: .......................................... 988
KIAMBATANISHO NAMBA 7: ........................................ 1033
KIAMBATANISHO NAMBA 8: ....................................... 10909
4
I: UTANGULIZI
1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba
Baraza lako likae kama Kamati, ili liweze kupokea,
kujadili na hatimae kupitisha Mpango na Makadirio
ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano, kwa kazi za kawaida
na maendeleo kwa mwaka wa fedha 2014/2015.
2. Mheshimiwa Spika, naomba nianze kwa
kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uhai na kutuwezesha kukutana tena leo kujadili maendeleo ya Sekta ya Usafiri na Mawasiliano na ya Taifa kwa
ujumla.
3. Mheshimiwa Spika, napenda vile vile nimpongeze na kumshukuru kwa namna ya pekee Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein kwa ushauri na miongozo anayoitoa kwa Wizara katika kuendeleza Sekta ya Usafiri na
Mawasiliano na kuendelea kuiongoza vyema nchi yetu.
4. Mheshimiwa Spika, niruhusu pia nitumie fursa hii kuwashukuru Makamo wa Kwanza wa Rais, Mhe.
Maalim Seif Sharif Hamad, pamoja na Makamo wa Pili wa Rais, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, kwa uongozi wao
imara na wa mfano ambao umesaidia sana Wizara hii katika utekelezaji wa majukumu yake.
5. Mheshimiwa Spika, naomba nimalizie kwa pongezi
zifuatazo: kwanza kwako wewe binafsi Mhe. Spika,
5
Naibu wako, na Wenyeviti wa Baraza kwa kuendelea kuliongoza Baraza letu kwa staha, uvumilivu mkubwa
na bila kuyumba katika kusimamia kanuni tulizojiwekea. Pili, Mawaziri wenzangu na Wawakilishi
wote kwa kazi nzuri wanayofanya na kwa ushirikiano mzuri wanaonipa katika kutekeleza majukumu yangu kama Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano. Tatu,
na mwisho familia yangu na wapiga kura wa Jimbo la Uchaguzi la Ziwani ambao wameendelea kunionyesha
upendo na ushirikiano mkubwa hata pale ninapokuwa nimebanwa na majukumu ya kitaifa nje ya Jimbo langu
la uchaguzi.
6. Mheshimiwa Spika, hotuba hii imezingatia kikamilifu maudhui yaliyomo kwenye Hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora, anayesimamia
Tume ya Mipango Mhe. Dkt. Mwinyihaji Makame Mwadini; na Waziri wa Fedha Mhe. Omar Yussuf Mzee,
zilizowasilishwa katika Baraza lako Tukufu tarehe 14 Mei, 2014. Naomba kuwashukuru na kuwapongeza kwa hotuba zao zilizotoa ufafanuzi wa kina kuhusu
utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwa mwaka 2013/2014 na mwelekeo wa shughuli za Serikali na
dira ya Bajeti ya Serikali katika mwaka 2014/2015.
7. Mheshimiwa Spika, naomba kuishukuru Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi ya Mawasiliano na
Ujenzi chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Mahmoud Mohamed Mussa, Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni kwa kazi nzuri na kubwa ya uchambuzi wa kina wa
6
Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Sekta katika mwaka 2013/2014 na Mapendekezo ya Mpango na
Bajeti ya Wizara kwa mwaka 2014/2015. Pamoja na kuipongeza Kamati kwa kazi nzuri, Wizara pia
itazingatia maoni na ushauri wa Kamati katika kuimarisha utendaji wa Sekta ya Usafiri na Mawasiliano nchini.
II: UTEKELEZAJI WA KAZI ZA KAWAIDA
NA MAENDELEO KWA MWAKA 2013/2014
NA MALENGO YA MWAKA 2014/2015
8. Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo ya awali, niruhusu sasa nifanye mapitio ya utekelezaji wa kazi za kawaida na maendeleo za Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano kwa mwaka 2013/2014 na kutoa maelezo kuhusu Malengo na Makadirio ya
bajeti ya Wizara kwa mwaka 2014/2015. Utekelezaji wa kazi za kawaida na maendeleo kwa mwaka 2013/2014 ulizingatia: Dira ya Taifa ya Maendeleo ya
mwaka 2020, Malengo ya Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUZA II), ahadi na maagizo
ya Serikali, pamoja na Sera na Mipango ya Kisekta, Kitaifa na Kimataifa.
9. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2013/2014 Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano
ilikadiriwa kutumia jumla ya TZS bilioni 5.192 kwa kazi za kawaida. Kati ya fedha hizo TZS bilioni 3.26 ikiwa ni
7
mshahara na TZS bilioni 1.93 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo. Kwa upande wa kazi za maendeleo Wizara
ilipanga kutumia jumla ya TZS bilioni 14.90. Aidha, Wizara ilipangiwa kukusanya jumla ya TZS milioni
406.2. Hadi kufikia mwezi Machi 2014, fedha halisi
zilizopatikana ni TZS bilioni 3.362 kwa matumizi ya kazi za kawaida, sawa na asilimia 64.75. Kati ya hizo TZS
bilioni 2.709 ni mshahara sawa na asilimia 83 na TZS milioni 652.368 ni matumizi mengineyo sawa na
asilimia 33. Aidha, jumla ya TZS bilioni 4.376 zilipatikana kwa kazi za maendeleo sawa na asilimia 35.70 ya makadirio ya mwaka 2013/2014. Wizara pia,
ilikusanya jumla ya TZS milioni 314.248, sawa na asilimia 77. (Kiambatanisho Namba 1).
10. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano inatekeleza majukumu yake ya kisekta
kupitia Idara, Mamlaka na Mashirika yaliomo ndani ya Wizara, taasisi binafsi na baadhi ya taasisi za
Muungano kama ifuatavyo:-
i) Ofisi Kuu Pemba
ii) Utawala na Sera
Idara ya Mipango, Sera, na Utafiti,
Idara ya Uendeshaji na Utumishi.
iii) Sekta ya Usafiri wa Barabara
8
Idara ya Ujenzi na Utunzaji wa
Barabara,
Idara ya Usafiri na Leseni.
iv) Sekta ya Mawasiliano
Idara ya Mawasiliano.
v) Sekta ya Usafiri wa Anga:
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (ZAA),
vi) Sekta ya Usafiri wa Baharini
a. Mamlaka ya Usafiri Baharini (ZMA).
b. Shirika la Meli na Uwakala (SHIPCO).
c. Shirika la Bandari (ZPC).
IIa) OFISI KUU PEMBA
11. Mheshimiwa Spika, Ofisi Kuu Pemba inaratibu na kusimamia shughuli za Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano kwa upande wa Pemba. Katika kipindi cha 2013/2014 Ofisi Kuu Pemba
imeendelea kutekeleza kazi mbali mbali za uratibu wa shughuli za Wizara kwa upande wa Pemba.
12. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hicho Ofisi Kuu
Pemba ilikadiriwa kutumia jumla ya TZS bilioni 1.277
kwa kazi za kawaida na kukusanya jumla ya TZS milioni 50.2 kutoka kwenye vianzio vyake vya mapato.
9
Kati ya fedha hizo TZS milioni 877 ni mshahara na TZS milioni 400 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo.
Hadi Machi 2014 fedha zilizoingizwa ni TZS milioni
858.724 sawa na asilimia 67. Kati ya hizo TZS 733.06 sawa na asilimia 83.5 ni mshahara na TZS milioni 125.664 sawa na asilimia 31 ni kwa ajili ya matumizi
mengineyo. Ofisi Kuu Pemba imekusanya jumla ya TZS milioni 44.550 sawa na asilimia 89.
MALENGO YA MWAKA 2014/2015
13. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2014/2015 Ofisi
Kuu Pemba itaendelea kuratibu na kusimamia kazi za
Wizara za kawaida na maendeleo kwa upande wa Pemba. Malengo yote yanasimamiwa na Idara husika
na Ofisi Kuu Pemba inaratibu malengo hayo kwa kila Idara. Katika kipindi hicho, Ofisi Kuu Pemba inakadiriwa kukusanya jumla ya TZS milioni 62 na
inaombewa jumla ya TZS bilioni 1.362 kwa matumizi ya kazi za kawaida. Kati ya hizo TZS bilioni 1.081 ni
mshahara na TZS milioni 280.78 ni matumizi mengineyo.
IIb) UTAWALA NA SERA
14. Mheshimiwa Spika, Kazi za uratibu wa Sera,
Mipango na Miradi ya Maendeleo ya Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano zinasimamiwa na Idara
10
ya Mipango, Sera na Utafiti. Aidha, masuala ya uendeshaji, utumishi na utawala hutekelezwa kupitia
Idara ya Uendeshaji na Utumishi.
(i) IDARA YA MIPANGO, SERA NA UTAFITI
15. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha 2013/2014 Idara ya Mipango, Sera na Utafiti iliendelea na kazi za uratibu na kusimamia utekelezaji wa Sera na Mipango
ya sekta ya Usafiri na Mawasiliano ikiwemo kubuni, kutayarisha na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya
maendeleo na kufanya maandalizi ya utafiti wa kisekta. HATUA ZA UTEKELEZAJI (2013/2014)
16. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha 2013/2014,
Idara iliendelea kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Sera ya Usafiri Zanzibar, Sera ya Mawasiliano pamoja na Mpango Mkuu wa Taifa wa Usafiri wa Zanzibar
(Zanzibar Transport Master Plan).
Idara kupitia programu ya mageuzi ya mfumo wa taasisi inayoendelea inakamilisha Mpango wa
utekelezaji wa mageuzi ya taasisi za Wizara ikihusisha maandalizi ya Mpango wa Uendeshaji Kibiashara (Business Plans) kwa kila Taasisi itakayohusika na
mageuzi hayo pamoja na Sheria zinazohusiana na taasisi hizo.
11
Idara pia, imeratibu na kufuatilia taratibu za uanzishwaji wa vyuo vya ubaharia na urubani. Kwa
upande wa uanzishwaji wa chuo cha ubaharia, Wizara imefanya mazungumzo na kampuni ya Rom Solution
ambayo imewasilisha mapendekezo ya mradi wa uanzishwaji wa Chuo cha Ubaharia kwa kuanzia na Upembuzi yakinifu ikiwemo uhakiki wa kisheria,
kuandaa malengo ya muda mfupi na muda mrefu, kuandaa mpango wa mafunzo na mitaala pamoja na
kuandaa mahitaji ya majengo ya Chuo hicho.
(i-1) MIRADI YA MAENDELEO
17. Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa uratibu na
usimamizi wa miradi ya maendeleo, jumla ya Miradi ya Maendeleo 14 ya ujenzi wa miundombinu ya barabara,
viwanja vya ndege na bandari pamoja na mradi wa Mageuzi ya mfumo wa taasisi (Kiambatanisho Namba 2) imetekelezwa kama ifuatavyo:-
(i-1.1) MIRADI YA UJENZI WA BARABARA
18. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia programu ya ujenzi wa barabara, iliendelea kutekeleza jumla ya miradi saba (7) ya ujenzi wa barabara katika kipindi
cha 2013/2014. Taarifa za utekelezaji wa miradi hiyo kwa kipindi kilichopita na fedha inazoombewa kwa
mwaka 2014/15 ni kama ifuatavyo:
12
(i-1.1.1) Mradi wa Barabara Tatu za Kaskazini Pemba
19. Mheshimiwa Spika, Mradi huu unaogharamiwa kwa mkopo kutoka Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Afrika (BADEA) na Mfuko wa Maendeleo wa Saudi
Arabia (Saudi Fund) pamoja na fedha za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar unazihusisha barabara za Wete
– Konde (kilomita 15) na Wete – Gando (kilomita 15) kwa awamu ya kwanza umefikia hatua mbali mbali za
kifusi.
Mheshimiwa Spika, Mradi huu ulisita kwa muda
kutokana na Mkandarasi kusimamisha ujenzi kwa sababu ya kuchelewa kulipwa na Wafadhili na Serikali.
Hata hivyo, baada ya Wizara kufuatilia kwa kina Mkandarasi alilipwa jumla ya Dola za Kimarekani milioni 2.74 ikiwa ni malipo kutoka kwa Wafadhili.
Kwa upande wa Serikali, Mkandarasi huyo amelipwa
deni lake lote la TZS bilioni 2.855 alilokuwa akidai kwa barabara hizi kwa kipindi cha Julai hadi Septemba 2013. Kwa ujumla Mkandarasi amelipwa jumla ya TZS
bilioni 6.079 hadi kufikia mwezi Septemba 2013. Aidha, Mkandarasi amelipwa USD milioni 3 alizokuwa akidai
Serikali kwa mradi wa ujenzi wa barabara ya Amani - Dunga, Mfenesini - Bumbwini na Madaraja ya barabara ya Mahonda - Donge - Mkokotoni.
13
Baada ya kufanyika malipo hayo, Mkandarasi alikubali kuendelea na kazi za ujenzi na kuanza kazi rasmi
mwezi wa Aprili 2014. Kwa sasa kazi za ujenzi wa barabara hizo zinaendelea vizuri na kutarajiwa
kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.
20. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa fedha
2014/2015 mradi unaombewa jumla ya TZS bilioni 2.425 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu.
(i-1.1.2) Mradi wa Barabara ya Wete-Chake
21. Mheshimiwa Spika, ujenzi wa barabara hii yenye
urefu wa kilometa 22 umepangwa kufanyika katika
awamu ya pili ya Mradi wa Barabara Tatu za Kaskazini Pemba ambapo jumla ya USD milioni 23 zinatarajiwa
kutumika. Tayari Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeshatiliana saini ya mkopo wa USD milioni 10 na benki ya BADEA kwa ajili ya ujenzi wa barabara
hii. Juhudi za kukamilisha taratibu za kusaini mkopo wa USD milioni 10 na Mfadhili wa pili (SAUDI Fund)
zinaendelea.
22. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha
2014/2015 Wizara inakusudia kuanza taratibu za kumpata Mshauri wa kufanya mapitio ya usanifu wa
barabara na usimamizi wa ujenzi baada ya kukamilika kwa taratibu za mkopo kutoka Saudi Fund. Jumla ya TZS milioni 100 zinaombwa kwa ajili ya malipo ya fidia.
14
(i-1.1.3) Mradi wa Barabara ya Ole-Kengeja
23. Mheshimiwa Spika, Mradi wa Barabara ya Ole-Kengeja unagharamiwa kwa mkopo kutoka Jumuiya ya
Nchi zinazosafirisha Mafuta kwa Wingi Duniani (OPEC) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar una lengo la kuijenga kwa kiwango cha lami barabara inayoanzia
Ole hadi Kengeja yenye urefu wa kilomita 35. Hatua za kumpata Msimamizi wa Mradi zimekamilika na kazi ya
upimaji wa barabara hiyo zimeanza ambapo jumla ya kilomita saba (7km) zimeshapimwa na taratibu za
manunuzi ya zana za ujenzi zinaendelea kupitia fedha za Mfadhili. Jumla ya TZS milioni 20 zimepatikana kutoka Serikalini kwa mwaka wa fedha 2013/2014.
Kwa mwaka wa fedha 2014/2015 Serikali inakusudia
kuendelea na matayarisho ya ujenzi wa barabara hii na jumla ya TZS milioni 500 zinaombwa kwa ajili ya malipo ya fidia.
(i-1.1.4) Mradi wa Barabara za Vijijini Kaskazini Pemba:
24. Mheshimiwa Spika, Mradi huu uliogharamiwa kwa
kutumia ruzuku kutoka Serikali ya Marekani kupitia Mfuko wa Changamoto ya Milenia (MCC) na fedha za
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ulikuwa na lengo la kujenga kwa kiwango cha lami barabara 5 za Kaskazini Pemba zenye jumla ya kilometa 35. Mradi huo ambao
ulihusisha barabara za: Mzambarauni-Pandani-Finya
15
(kilometa 7.9), Bahanasa-Daya-Mtwambwe (kilometa 13.6), Chwale-Kojani (kilometa 1.9), Kipangani-
Kangagani (kilometa 8.9) na Mzambarauni-Mapofu (kilometa 8.9) umekamilika na kuzinduliwa rasmi
mwezi Machi mwaka huu. Hadi kufikia mwezi Machi 2014, jumla ya TZS milioni 40 zimepatikana sawa na asilimia 27 ya makadirio.
(i-1.1.5) Mradi wa Barabara Zinazoingia Mjini Unguja
25. Mheshimiwa Spika, lengo la mradi huu ambao bado haujapata mfadhili ni kuzitanua na kuzifanyia matengenezo makubwa barabara 7 zenye urefu wa
kilometa 83 zinazoingia katika mji wa Zanzibar. Barabara zenyewe ni Bububu-Mtoni-Kinazini-Malindi
Port (kilometa 19), Creek road-Mkunazini-Mnazi Mmoja (kilometa 1.28), Tunguu-Fuoni-Magomeni-Kariakoo-Mkunazini (kilometa 13.3), Welezo-Amani-Ngambo-
Kariakoo (kilometa 3.5), Mtoni-Amani-Kiembesamaki (kilometa 8.5), Uwanja wa Ndege-Kiembe Samaki-
Kilimani-Mnazi Mmoja (kilometa 7) na Bububu-Mahonda-Mkokotoni (kilometa 31). Juhudi za kutafuta fedha za ujenzi wa barabara hizi zinaendelea na hadi
kufikia mwezi Machi 2014 hakuna fedha iliyopatikana kutoka kwa Wafadhili kwa ajili ya mradi huo.
Kwa mwaka wa fedha 2014/2015, Wizara itaendelea na juhudi za kutafuta fedha kwa njia ya msaada au
mkopo kutoka kwa Washirika wa Maendeleo kwa ajili
16
ya utekelezaji wa mradi na unaombewa jumla ya TZS 50 milioni.
(i-1.1.6) Mradi wa Barabara 3 za Vijijini Unguja
26. Mheshimiwa Spika, mradi huu unaoendelea
unagharamiwa kwa mkopo kutoka Benki ya Kiarabu ya
Maendeleo ya Afrika (BADEA) na fedha za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar unazijumuisha barabara za
Kizimbani-Kiboje (kilometa 7.2); Koani-Jumbi (kilometa 6.3); na Jendele-Cheju-Kaebona (kilometa 11.7). Hadi
kufikia mwezi wa Machi 2014, jumla ya TZS milioni 405 zimepatikana ambapo jumla kilometa 11.7 zimeshawekwa kifusi cha tabaka la chini kwa barabara
ya Jendele-Cheju-Kaebona na kilometa 4.2 za barabara ya Koani – Jumbi zimesafishwa. Pamoja na
changamoto za ulipaji fidia mradi unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu kwa mujibu wa mkataba.
Kwa mwaka wa fedha 2014/2015, Wizara inakusudia
kuendelea na utekelezaji wa mradi huu na unaombewa jumla ya TZS 1.6 bilioni kwa ajili ya malipo ya fidia na mchango wa Serikali.
(i-1.1.7) Mradi wa Barabara 6 za Vijijini Unguja
27. Mheshimiwa Spika, mradi huu una lengo la
kufanya upembuzi yakinifu, usanifu na utayarishaji wa
zabuni wa barabara 6 za vijijini Unguja zenye urefu wa
17
kilometa 62.6 unagharimiwa kwa mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB). Barabara hizo ni:
Matemwe-Muyuni (kilometa 7), Kichwele-Pangeni (kilometa 4.8), Njianne-Umbuji-Uroa (kilometa 11),
Jozani-Charawe-Ukongoroni-Bwejuu (kilometa 22.2), Fuoni-Kombeni (kilometa 8.5), na Mkwajuni-Kijini (kilometa 9.1). Hatua za utekelezaji wa mradi huu ni
kukamilika kwa uchambuzi yakinifu wa awali wa mradi huu.
Kwa mwaka wa fedha 2014/2015, Wizara itakamilisha
upembuzi yakinifu na matayarisho ya zabuni za mradi huo kwa kutumia fedha za Mfadhili.
28. Mheshimiwa Spika, kwa jumla, kwa mwaka wa fedha 2014/2015 Wizara itaendelea na utekelezaji wa
miradi niliyokwishakuieleza kwenye sekta ya usafiri wa barabara ambapo jumla ya TZS bilioni 4.975 zinaombwa kutoka Serikalini. (Kiambatanisho
Namba 2)
(i-1.2) MIRADI YA SEKTA YA USAFIRI WA ANGA
29. Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa sekta ya
usafiri wa anga Wizara ilipanga kutekeleza jumla ya
miradi 4 ya ujenzi wa miundombinu ya viwanja vya ndege vya Unguja na Pemba katika mwaka 2013/2014.
Utekelezaji wa miradi hiyo kwa kipindi kilichopita na
18
fedha zinazoombwa kwa mwaka ujao wa fedha ziko kama ifuatavyo:-
(i-1.2.1) Uendelezaji Ujenzi wa Uzio.
30. Mheshimiwa Spika, Mradi huu unalengo la kujenga uzio wenye urefu wa kilometa 11.9 katika kiwanja cha
ndege cha kimataifa cha Abeid Amani Karume. Hadi kufikia mwezi Machi, 2014 jumla ya kilometa 8.59 za
uzio zimeshajengwa sawa na asilimia 73.5 ya lengo. Kwa mwaka wa fedha 2014/2015 Wizara inakusudia
kuendelea na mradi huu kwa kutumia fedha za maendeleo.
(i-1.2.2) Ujenzi wa Jengo Jipya la Abiria Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume
31. Mheshimiwa Spika, Baada ya mradi huu kusita
kwa muda, mnamo mwezi wa Juni 2013 Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano ilitoa ruhusa kwa
mkandarasi kuendelea na ujenzi kwa kuzingatia marekebisho yalioyopendekezwa na Mshauri Mwelekezi
kampuni ya ADPi ya Ufaransa. Marekebisho hayo yatabadilisha mfumo wa uegeshaji wa ndege kubwa kutoka mbele ya jengo (airside) na badala yake
kuegesha upande wa kusini ya jengo, kuongeza ukubwa wa jengo kutoka mita za mraba 17,800 hadi
23,000, kuongeza eneo la kuegeshea ndege kutoka
19
mita za mraba 23,000 hadi mita za mraba 37,300, kuongeza urefu wa jengo kwa upande wa kusini kwa
mita 36 na upana mita 75 na kuongeza sehemu ya mbele (lobby) ya jengo kwa mita 18.
32. Mheshimiwa Spika, napenda kuliarifu Baraza lako
tukufu kuwa kazi za ujenzi wa jengo jipya zinaendelea
kwa kukamilisha uwekaji wa vyuma (steel structure) eneo liloongezeka upande wa kusini na sehemu ya
mbele (canopy/lobby). Kwa eneo liloongezeka kwa upande wa kusini tayari limefikia asilimia 75. Ujenzi
wa sehemu ya mbele (canopy/lobby) tayari imefikia asilimia 80. Pia ujenzi wa ngazi za jengo unaendelea kwa kuchimba misingi kulingana na marekebisho ya
michoro.
33. Mheshimiwa Spika, Mkandarasi pia anaendelea kukamilisha ujenzi wa makazi na ofisi mpya ambayo iko katika hatua za mwisho ambapo baadhi ya maeneo
tayari yanatumika. Aidha vifaa vya ujenzi kama kokoto, saruji na nondo kwa ajili ya kuweka zege ya ghorofa
ya kwanza ya jengo zimefika kwenye eneo la ujenzi. Pia kazi ya kufunga nondo kwenye ghorofa ya pili zimeanza kwa mataarisho ya kuweka zege.
34. Mheshimiwa Spika, kuhusu kazi za ukamilishaji na
uthibitishaji wa michoro (Usanifu na Uhandisi), Mshauri Mwelekezi anaendelea kupitia michoro iliyowasilishwa na inayosubiri kuthibitishwa na Wizara kwa mfano,
20
mfumo wa uingiaji na utokaji wa abiria, mizigo, wafanyakazi pamoja na utoaji wa takataka ndani ya
jengo. Pia, ADPi wamekamilisha kupitia michoro mbali mbali ikiwemo ya Usanifu (“architectural drawings”),
Uhandisi (Engineering Drawings) “Plumbing drawings” and michoro ya mfumo wa vipoza joto (Heat, ventilation and Air Condition). Mkandarasi pia
amewasilisha marekebisho ya mpangilio wa matumizi ya vyumba vya jengo na ripoti ya usalama wa moto
(fire safety report). Taarifa zote hizi kwa sasa zinapitiwa na Mshauri Mwelekezi kabla ya kuishauri
Wizara ili kuthibitishwa.
35. Mheshimiwa Spika, Naomba pia ifahamike
kwamba awamu hii ya uthibitishaji michoro, haimzui Mkandarasi kuendelea na kazi za Ujenzi, kwa maana
hatua hii ya kuendelea na marekebisho ya michoro ni suala la kawaida katika taratibu za Ujenzi. Ni matarajio ya Serikali kwamba Mradi huo utakamilika kabla ya
mwisho wa mwaka 2015.
36. Mheshimiwa Spika, Hadi kufikia mwezi Machi 2014
jumla ya TZS milioni 807.798 zimepatikana sawa na asilimia 59 ya makadirio.
Kwa mwaka wa fedha 2014/2015 Mradi unaombewa
jumla ya TZS bilioni 1.950 kwa ajili ya huduma ya Ushauri na Usimamizi wa Mradi.
21
(i-1.2.3) Ujenzi wa Maegesho na Njia ya Kupitia Ndege uwanja wa ndege wa Kimataifa.
37. Mheshimiwa Spika, Mradi huu una lengo la
kujenga sehemu ya maegesho ya ndege (apron) na kuimarisha njia za kupitia ndege (taxiways) katika Kiwanja cha Ndege cha kimataifa cha Abeid Amani
Karume. Mradi huu unagharamiwa kwa mkopo kutoka Benki ya Dunia na fedha za Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar. Hadi kufikia mwezi Machi 2014, ujenzi wa njia tatu za kupitia ndege
umekamilika na ujenzi wa njia mbili mpya unaendelea na uimarishaji wa njia moja. Aidha, kazi za uwekaji wa kifusi na lami kwenye eneo jipya la
maegesho ya ndege zinaendelea na jumla ya TZS milioni 75 zilipatikana kutoka Serikalini sawa na
asilimia 3 ya makadirio.
Kwa mwaka wa fedha 2014/2015 jumla ya TZS milioni 975 zinaombwa kwa ajili ya kugharamia ujenzi
wa uzio.
(i-1.2.4) Uimarishaji wa huduma za Uwanja wa Ndege Pemba
38. Mheshimiwa Spika, Mradi huu unagharamiwa na Serikali ya Mapinduzi pekee na
una lengo la kuweka taa katika barabara ya kurukia na kutulia ndege na kufanya upembuzi
yakinifu na usanifu wa huduma mbali mbali katika
22
kiwanja hicho. Hadi kufikia mwezi Machi 2014, hakuna kazi iliyofanyika kutokana na ukosefu wa
fedha. Katika kulipatia ufumbuzi wa kudumu suala la uimarishaji wa Kiwanja hicho, Serikali imefanya
maamuzi rasmi ya kutekeleza Mradi huo kwa njia ya mkopo kutoka Benki ya Exim ya Uturuki kupitia Kampuni ya Renaisance ya nchi hiyo.
Makubaliano ya awali ya kazi yalifanyika mwishoni mwa mwaka 2013 baina ya Serikali kupitia Wizara
ya Fedha na Kampuni ya Renaisance ya Uturuki. Baada ya makubaliano hayo kampuni hiyo ilipeleka
wataalamu wake Pemba kwa ajili ya kupata taarifa zaidi ya uwanja huo. Rasimu ya Upembuzi Yakinifu wa Kifedha na Kimazingira imekamilishwa na
kuwasilishwa Wizarani kwa ajili ya kupata maoni ya kitaalamu. Aidha, gharama za awali kwa ajili ya
kazi za ujenzi zimewasilishwa na zinaendelea kufanyiwa mapitio ya kina.
39. Mheshimiwa Spika, Uimarishaji wa uwanja
huo utajumuisha jengo jipya la abiria, kuongeza urefu wa njia ya kutulia na kurukia ndege kutoka
mita 1,500 hadi mita 2,300, ujenzi wa uzio kuzunguka uwanja mzima, uwekaji wa taa za kuongozea ndege wakati wa kuruka na kutua,
kulikarabati jengo la abiria liliopo pamoja na huduma nyengine za kiwanja hicho. Lengo la
ongezeko hilo ni kukiwezesha Kiwanja hicho kuweza kutua ndege kubwa zaidi ya sasa ikiwemo Boeing 737 – 200.
23
40. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2014/2015 Wizara inakusudia kuendelea na
utekelezaji wa mradi huu kwa mkopo kupitia Benki ya Exim ya Uturuki.
41. Mheshimiwa Spika, kwa ujumla kwa mwaka wa fedha 2014/2015 Wizara inakusudia kuendelea na utekelezaji wa miradi ya usafiri wa Anga na
jumla ya TZS bilioni 2.925 zinaombwa kutoka Serikalini (Kiambatanisho Namba 2)
MRADI WA UJENZI WA BANDARI YA MPIGADURI
42. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa uimarishaji miundombinu ya bandari, Wizara tayari
imekamilisha kazi ya Upembuzi Yakinifu ya Ujenzi wa Bandari mpya ya Mpigaduri. Aidha Wizara
imetiliana saini makubaliano ya ujenzi wa Bandari hiyo kati yake na Kampuni ya China Harbour Engineering Company (CHEC) baada ya kukamilika
kwa kazi za Upembuzi Yakinifu. Aidha, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania tayari imewasilisha rasmi maombi ya mkopo wa ujenzi wa Bandari hiyo kutoka Benki ya Exim ya China kupitia Serikali
ya nchi hiyo.
24
Kwa mwaka wa fedha 2014/2015 Jumla ya TZS milioni 500 zinaombwa kwa ajili ya utekelezaji wa
mradi huo.
MRADI WA UJENZI WA MELI MPYA YA ABIRIA NA MIZIGO YA SERIKALI.
43. Mheshimiwa Spika, Utekelezaji wa ahadi ya Serikali ya kujenga meli mpya ya abiria na mizigo
kupitia bajeti yake wenyewe unaendelea. Katika utekelezaji wa ahadi hiyo, mnamo tarehe 10
Julai, 2013 Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilitiliana saini na Kampuni ya DAEWOO
International ya Korea Kusini ya ujenzi wa meli hiyo. Napenda kuchukua fursa hii kuliarifu Baraza lako Tukufu kwamba ujenzi wa meli hiyo
unaendelea kwa kukamilisha kazi za usanifu na uandaaji wa michoro ya meli hiyo. Aidha, zoezi la
ukataji wa vyuma vya meli hiyo (steel cutting) zimezinduliwa rasmi mwezi Machi 2014 na kazi za ulazaji wa mkuku (keel laying) zinatarajiwa
kufanyika ifikapo mwezi Julai 2014 baada ya kukamilika kwa kazi za usanifu. Ni matumaini yetu
kuwa ujenzi wa meli hiyo utakamilika mapema mwaka 2015 kwa mujibu wa ratiba ya ujenzi wa meli hiyo.
44. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014 Idara ya Mipango, Sera na Utafiti ilipangiwa
kutumia jumla ya TZS milioni 288 kwa matumizi
25
ya kazi za kawaida. Hadi Machi 2014, fedha zilizopatikana kwa kazi za kawaida ni TZS 83.137
sawa na asilimia 29 ya makadirio.
MALENGO YA MWAKA 2014/2015
45. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2014/2015, Idara ya Mipango, Sera na Utafiti itaratibu na
kutekeleza mambo yafuatayo:-
Maandalizi ya Sheria, Kanuni na Mpango
Mkakati wa utekelezaji wa Sera ya TEHAMA; Kufanya tafiti mbali mbali zinazohusiana
na sekta ya usafiri na mawasiliano kwa lengo la kuongeza ufanisi na tija katika
kazi za ujenzi wa miundombinu; Kuratibu na kusimamia mpango wa
Serikali wa kuanzisha Chuo cha Ubaharia na Urubani;
Kukusanya na kuchambua takwimu za maendeleo ya Sekta na kuweka mpango
bora wa utunzaji wa kumbukumbu; Kuratibu mashirikiano ya kisekta baina ya
taasisi za ndani, kikanda na nje ya nchi.
46. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka 2014/2015 Idara ya Mipango, Sera na Utafiti inaombewa jumla ya TZS milioni 200 kwa matumizi ya kazi za
kawaida.
26
(ii) IDARA YA UTUMISHI NA UENDESHAJI
47. Mheshimiwa Spika, Idara ya Uendeshaji na Utumishi inajukumu la kutekeleza kazi zifuatazo:-
Kusimamia na kuratibu majukumu ya
kiutumishi ikiwemo ajira, na upandishaji wa vyeo kwa watumishi wa Wizara.
Kuwaendeleza wafanyakazi wa Wizara kwa
kuwajengea uwezo kielimu na kusimamia
maslahi yao. Kusimamia na kuhakikisha kuwa sheria ya
utumishi wa Umma na sheria ya manunuzi na uondoshaji wa mali chakavu za Serikali
zinasimamiwa vizuri na zinafuatwa. Kusimamia shughuli za uendeshaji wa kazi
za ofisi za kila siku kwa kuimarisha mazingira mazuri ya utendaji wa kazi kwa kuhakikisha vitendea kazi vinapatikana kwa wakati.
Kusimamia na kuimarisha mawasiliano ya
habari na ofisi nyingine.
48. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha
2013/2014 Idara imetekeleza na kusimamia masuala ya kiutumishi na uendeshaji ya Wizara
kwa ujumla. Idara imewapatia mafunzo mbali mbali jumla ya wafanyakazi 94. Kati ya hao, wafanyakazi 48 walipatiwa mafunzo ya muda
27
mrefu na wafanyakazi 46 walipatiwa mafunzo ndani ya muda mfupi. (Kiambatanisho Namba
3). Aidha, Wizara iliajiri wafanyakazi wapya 42 pamoja na kustaafisha wafanyakazi 34 na
kuwapatia mafao yao. Idara pia, kwa kushirikiana na Wizara ya Kazi na
Utumishi wa Umma imewapandisha vyeo wafanyakazi wote wanaostahili ikihusisha
wafanyakazi wenye uzoefu wa muda mrefu na kuhakikisha kuwa wanalipwa mishahara yao kwa
mujibu wa mabadiliko ya mishahara ya watumishi kama yalivyotolewa na Serikali mwezi Februari 2014.
Vile vile, Wizara kupitia Idara hii imeratibu na
kusimamia ujenzi wa Jengo Jipya moja na ukarabati wa majengo mengine manne (4) katika eneo la Kisauni ambayo hivi sasa yanatumika
kama Makao Makuu ya Wizara.
49. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa fedha 2013/2014 Idara ya Uendeshaji na Utumishi ilipangiwa kutumia jumla ya TZS milioni 501.4 kwa
matumizi ya kazi za kawaida na jumla ya TZS bilioni 2.082 kwa mishahara ya watumishi wote wa
Wizara. Fedha halisi zilizotolewa katika kipindi cha Julai 2013 hadi Machi 2014 ni TZS milioni 217.946 sawa na asilimia 43.47 kwa matumizi ya kawaida
28
na TZS bilioni 1.798 sawa na asilimia 86 kwa matumizi ya mishahara.
MALENGO KWA MWAKA 2014/2015
50. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2014/2015
Idara itaendelea kutekeleza majukumu yake ya
uendeshaji wa ofisi na utumishi kama ilivyopangiwa. Aidha, Wizara kupitia Idara hii
itaendelea kushirikiana na Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma kuratibu maelekezo na
miongozo yote kuhusiana na masuala ya kiutumishi kama yatakavyotolewa.
51. Mheshimiwa Spika, ili kuongeza ujuzi, ufanisi na tija kwa wafanyakazi wa Wizara, katika
mwaka 2014/2015 Idara imepanga kuwapatia mafunzo jumla ya wafanyakazi 12 kwa Unguja na wafanyakazi 9 kwa Pemba kwa mujibu wa
mpango wa mafunzo wa Wizara.
Katika mwaka 2014/2015, Idara ya Uendeshaji na Utumishi inaombewa jumla ya TZS milioni 376.936 kwa matumizi ya kazi za kawaida na TZS milioni
2.892 kwa mishahara ya wafanyakazi wa Wizara.
IIc. SEKTA YA USAFIRI WA NCHI KAVU.
52. Mheshimiwa Spika, Sekta ya Usafiri wa Nchi Kavu ni muhimu katika kuchangia ukuaji wa
29
uchumi wa nchi yetu na ustawi wa jamii kwa kusafirisha wananchi mijini na vijijini na bidhaa za
wakulima.
Katika kipindi cha mwaka 2013/2014, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano kupitia Idara ya Ujenzi na Utunzaji Barabara na Idara ya Usafiri na
Leseni imeendelea kuimarisha miundombinu ya barabara na huduma za usafiri wa barabara kwa
kuendeleza kazi za ujenzi na utunzaji wa barabara, madaraja na kusimamia masuala ya usalama
barabarani.
(i) IDARA YA UJENZI NA UTUNZAJI WA BARABARA
53. Mheshimiwa Spika, kazi za ujenzi na utunzaji wa barabara zinafanywa kupitia Idara ya Ujenzi na Utunzaji Barabara. Hadi kufikia mwezi Machi 2014
Wizara kupitia Idara hii imezifanyia matengenezo barabara mbali mbali mijini na vijijini (Unguja na
Pemba) na kufanya usafi wa barabara za lami kadhaa zenye urefu wa kilometa 249
(Kiambatanisho Namba 4) kwa kutumia fedha zinazotolewa na Mfuko wa Barabara chini ya Makubaliano Maalum ya Utekelezaji (Performance
Agreement) kati ya Wizara na Mfuko huo.
54. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2013/2014, Idara ya Ujenzi na Utunzaji wa
30
Barabara ilipangiwa kukusanya jumla ya TZS milioni 10 kutokana na mapato mengineyo na
ilitengewa jumla ya TZS milioni 250 kwa ajili ya matumizi ya kazi za kawaida. Hadi Machi 2014
jumla ya TZS milioni 3.48 zimekusanywa ambazo ni sawa na asilimia 35 na fedha zilizotolewa kwa kazi za kawaida ni TZS milioni 81.28 sawa na
asilimia 33 ya makadirio.
MATENGENEZO YA BARABARA
55. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha 2013/2014, Wizara kupitia programu ya
matengenezo ya barabara, iliendelea kutekeleza jumla ya miradi 5 ya ujenzi wa barabara kwa kutumia bajeti ya Serikali pekee. Kwa mwaka
2014/2015 Wizara inakusudia kuendeleza miradi hiyo kama ifuatavyo:-
(i) Barabara ya Mgagadu - Kiwani
56. Mheshimiwa Spika, Mradi huu unagharamiwa na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar na una lengo la kuijenga barabara ya Mgagadu-Kiwani yenye jumla ya kilometa 7.6.
Hadi kufikia mwezi Machi 2014 jumla ya kilometa 7.6 zimekamilika kwa hatua ya kifusi tabaka mbali mbali. Kutokana na kutopatikana kwa fedha za
31
Mradi kutoka Serikalini, Wizara ilifanya juhudi ya kupata fedha kupitia Mfuko wa Barabara kwa ajili
ya ujenzi wa daraja katika kijiji cha Mbaoni.
Kwa mwaka wa fedha 2014/2015, Mradi unaombewa jumla ya TZS milioni 300 kwa ajili ya kuendelea na kazi za ujenzi wa barabara hii.
(ii) Barabara ya Mkanyageni-Kangani
57. Mheshimiwa Spika, Mradi huu una lengo
la kuijenga barabara inayoanzia Mkanyageni hadi Kangani yenye urefu wa kilomita 6.5 kwa kiwango cha lami. Mradi huu mwanzoni
ulipangwa kutekelezwa baada ya kukamilika kwa barabara ya Mgagadu-Kiwani na
unagharamiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Hata hivyo, kwa mwaka huu wa fedha Wizara imepanga kujenga daraja moja la
tasini ambapo jumla ya TZS milioni 180 zimetengwa kupitia Mfuko wa Barabara. Aidha
ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha kifusi utafanywa kupitia mradi wa MIVARF
unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kupitia Wizara ya Kilimo unaotarajiwa kuanza robo ya kwanza ya mwaka 2014/2015.
32
(iii) Barabara ya Amani-Mtoni (Benjamin Mkapa)
58. Mheshimiwa Spika, huu ni mradi unaoendelea ambapo Wizara ilipanga
kukamilisha ujenzi wa sehemu ya pili ya barabara hiyo yenye jumla ya urefu wa
kilometa 2.4 kwa kiwango cha lami, ujenzi wa mtaro wa maji ya mvua mita 200, kalvati ndogo ndogo 6 na kulipia fidia za nyumba kwa ajili ya
kuruhusu ujenzi wa barabara hiyo.
Hadi kufikia mwezi Machi 2014 ujenzi wa kilometa 1.6 kwa kiwango cha lami umekamilika. Aidha,
kazi za ujenzi wa mtaro kwa mawe na saruji wenye urefu wa mita 120, ujenzi wa kalvati ndogo
mbili (2) pamoja na ujenzi wa kingo za zege (curbstones) zenye urefu wa kilometa 1.4 zimefanyika.
Kutokana na uhaba wa fedha za kulipia fidia,
ujenzi wa barabara hii ulisita kwa sababu ya kutolipwa fidia ya nyumba eneo lenye urefu wa
kilometa 0.8 ili kukamilisha ujenzi wa barabara yote. Hata hivyo, Wizara inaendelea na taratibu za malipo ya fidia ya eneo hilo baada ya kupata
fedha kupitia Mfuko wa Barabara ili kuruhusu kazi za ujenzi kuendelea. Kazi za ujenzi wa barabara hii
33
unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Oktoba 2014.
59. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha
2014/2015 Wizara inakusudia kukamilisha ujenzi wa sehemu ya barabara iliyobakia kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara.
(iv) Barabara ya Ole-Konde.
60. Mheshimiwa Spika, Mradi huu mpya una lengo la kuifanyia matengenezo ya muda maalum
(Periodic maintenance) barabara inayoanzia Melitano hadi Madenjani kwa urefu wa kilometa 12.3.
Hadi kufikia mwezi Machi 2014 taratibu za
kumpata Mkandarasi atakaefanya kazi hiyo zinaendelea kufanyika.
61. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa fedha 2014/2015 Wizara inakusudia kutekeleza mradi
huu kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara.
(v) Barabara ya Njianne-Umbuji
62. Mheshimiwa Spika, Mradi huu una lengo la kuifanyia matengenezo ya muda maalum (Periodic maintenance) kwa kiwango cha lami barabara
inayoanzia Njianne hadi Umbuji yenye urefu wa
34
kilometa 5. Hadi kufikia mwezi wa Machi 2014 jumla ya kilometa 3 za barabara hiyo zimejengwa
kwa kifusi.
Kwa mwaka wa fedha 2014/2015 Wizara itaendelea kutekeleza mradi huu kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara.
MALENGO YA IDARA (2014/2015)
63. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha
2014/2015 Idara itaendelea kuzifanyia matengenezo barabara mbali mbali zenye jumla ya urefu wa kilometa 697 Unguja na Pemba ili
ziendelee kutumika kwa wakati wote kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara. (Kiambatanisho
Namba 4). Idara inatarajia kukusanya jumla ya TZS
10,000,000 na inaombewa jumla ya TZS milioni 165.488 kwa matumizi ya kazi za kawaida.
(ii) IDARA YA USAFIRI NA LESENI
64. Mheshimiwa Spika, Idara hii inasimamia usalama wa watumiaji wote wa barabara, kuendesha shughuli za ukaguzi wa vyombo vya
moto, kusimamia mafunzo ya udereva, upasishaji madereva wanafunzi na walimu wa skuli za
35
udereva, utoaji huduma za usafirishaji abiria na mizigo kwa njia ya barabara pamoja na kutoa
vitambulisho vya utingo na madereva. Aidha, Idara inasimamia na kuendesha Karakana Kuu ya
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyoko Chumbuni na sehemu ya mitambo iliyoko Pemba.
HATUA ZA UTEKELEZAJI (2013/2014)
65. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Idara hii imeendelea kusimamia utekelezaji wa Kanuni
mbali mbali za Sheria ya Usafiri Barabarani ya mwaka 2003 ili kusaidia kuimarisha usalama wa usafiri barabarani kwa kufanya ukaguzi wa
vyombo vya moto na kutoa leseni za usafirishaji.
66. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi wa Machi 2014 jumla ya vyombo 27,731 vimekaguliwa ukilinganisha na vyombo 28,067 vilivyokaguliwa katika kipindi cha mwaka 2012/2013. Aidha, ruhusa za usafirishaji kwa njia
ya barabara ziliendelea kutolewa ambapo katika kipindi hicho Idara imetoa ruhusa za njia na
usafirishaji 1,896 kwa magari ya biashara mbali mbali Unguja na Pemba ukilinganisha na ruhusa 2,015 zilizotolewa katika kipindi cha Julai 2012
hadi Machi 2013 ikiwa ni pungufu ya aslimia 5.9.
36
67. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hicho Idara imewafanyia jumla ya madereva wanafunzi 5,721
mitihani ya nadharia na vitendo na kutoa leseni za madereva wanafunzi 7,218. (Kiambatanisho
Namba 5) Idara pia, imeendesha vipindi mbali mbali kuhusiana na usalama barabarani (elimu kwa umma) kwa kutumia vyombo vya habari.
68. Mheshimiwa Spika, Idadi ya magari
yaliofanyiwa matengenezo katika Karakana Kuu na Sehemu ya Mitambo Pemba iliongezeka kwa
asilimia 40. Jumla ya magari 628 yalifanyiwa matengenezo katika kipindi cha Julai 2013 hadi Machi 2014 ukilinganisha na magari 447
yaliofanyiwa matengenezo katika kipindi kilichopita.
69. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha
2013/2014 Idara ilipangiwa kukusanya jumla ya
TZS milioni 346 na kutumia jumla ya TZS milioni 300 kwa kazi za kawaida. Hadi kufikia Machi 2014,
Idara ilikusanya jumla ya TZS milioni 266.218 sawa na asilimia 77 na iliingiziwa jumla ya TZS milioni 64.298 kwa kazi za kawaida sawa na
asilimia 21 ya makadirio.
MALENGO YA IDARA (2014/2015)
37
70. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2014/2015, Idara itaendelea kusimamia
matumizi bora ya barabara kwa ajili ya kuimarisha usalama wa watumiaji wa barabara kwa
kuendelea kutoa elimu ya usalama barabarani na kuimarisha ukaguzi wa vyombo vya moto.
Juhudi zitaendelea kuchukuliwa ili kuhakikisha kuwa Karakana Kuu ya Unguja na Sehemu ya
Mitambo Pemba zinaimarishwa kwa kupatiwa vifaa vya kisasa na wafanyakazi wenye ujuzi ili ziweze
kufanya kazi zake ipasavyo. 71. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2014/2015
Idara ya Usafiri na Leseni inatarajia kukusanya jumla ya TZS milioni 364 na inaombewa jumla ya
TZS milioni 200.585 kwa matumizi ya kazi za kawaida.
IId) SEKTA YA MAWASILIANO
72. Mheshimiwa Spika, Sekta ya Mawasiliano imeendelea kutoa mchango mkubwa katika ukuaji
uchumi na huduma za kijamii katika nchi yetu na inajumuisha utoaji wa huduma za mawasiliano kwa njia ya posta, simu na huduma za teknolojia
ya habari na mawasiliano. Lengo na Sekta hii ni kuharakisha matumizi ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano katika sekta ya umma na binafsi, ili
38
wananchi wa Zanzibar wanufaike na teknolojia mpya za TEHAMA zinazovumbuliwa ulimwenguni.
(i) IDARA YA MAWASILIANO
73. Mheshimiwa Spika, Idara hii ina jukumu la
kusimamia huduma za mawasiliano na masuala ya
Taasisi za Mawasiliano za Serikali ya Jamhuri ya Muungano zilizopo Zanzibar. Idara pia, ina jukumu
la kuratibu na kusimamia uwekaji wa miundombinu ya mawasiliano na kuhakikisha
kuwepo kwa nyenzo za mawasiliano zilizo bora zitakazorahisisha ukuwaji wa uchumi na biashara kitaifa na kimataifa.
HATUA ZA UTEKELEZAJI (2013/2014)
74. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka 2013/2014
Idara ilikamilisha Sera ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar na kutoa mchango wa kiufundi katika masuala ya teknolojia ya habari na
mawasiliano, ushauri na muongozo katika uwekaji wa miundombinu ya mawasiliano kama vile
mkonga wa taifa na ujenzi wa minara ya simu. Aidha, Idara ilifanya ukaguzi na usimamizi wa utumiaji wa minara ikiwemo ya simu na mtandao.
Jumla ya minara 229 kutoka makampuni mbalimbali. Idara pia, iliratibu na kusimamia
39
mabadiliko ya teknolojia na uwekaji wa Anuani za Makaazi (post code).
MATUMIZI YA MKONGA WA MAWASILIANO
75. Mheshimiwa Spika, Mkonga wa mawasiliano
ni miundombinu ya mawasiliano iliyotandikwa
chini ya ardhi, yenye uwezo mkubwa wa kusafirisha habari data, habari picha, habari video
kwa kasi kubwa zaidi. Miundombinu ya mkonga wa mawasiliano imegawanyika katika sehemu kuu
tatu:-
1- Backabone Network
2- Distribution Network
3- Last mile Network
Hivyo basi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
imeweka miundombinu hiyo kwa hatua ya
"Backbone Network" tu ambayo ina uwezo
mkubwa sana wa kusafirisha mawasiliano. Pia,
Serikali kwa kushirikiana na Kampuni ya Zantel
inaendelea kuweka miundombinu ya "last mile"
katika taasisi mbali mbali za Serikali. Jumla ya
taasisi 84 tayari zimeshafikiwa na "fiber optic"
na ili kuziwezesha ofisi hizo kupata huduma za
mtandao wa nje duniani kote (internet) na
mtandao wa ndani ya nchi (intranet).
40
MALENGO YA IDARA (2014/2015)
76. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa fedha 2014/2015 Idara itaendelea kuratibu na kufuatilia
utekelezaji wa Sera ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hapa Zanzibar, kwa kuandaa Sheria
na Kanuni za TEHAMA na Mpango Mkakati wa TEHAMA kwa mashirikiano na Idara ya Mipango, Sera na Utafiti.
Idara itaandaa kanuni za miundombinu ya
mawasiliano ili tuweze kusimamia, kudhibiti na kukusanya mapato kupitia minara na mikonga ya mawasiliano kwa wanaomiliki.
Idara pia, itasimamia mkonga wa taifa wa
mawasiliano kwa kushirikiana na Kampuni ya Zantel kwa upande wa matumizi ya Serikali na Taasisi binafsi.
77. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka 2013/2014,
Idara ya Mawasiliano ilipangiwa kutumia jumla ya TZS milioni 255.6 na hadi kufikia Machi, 2014 fedha iliyopatikana ni TZS milioni 80.039 sawa na
asilimia 31.31 ya makadirio.
Kwa mwaka wa fedha 2014/2015 Idara inaombewa jumla ya TZS milioni 179.527 kwa ajili
ya kazi za kawaida.
41
MASHIRIKIANO YA IDARA NA TCRA
78. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Miundombinu
na Mawasiliano kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inaendelea na
mchakato wa mradi wa uwekaji wa simbo za posta na anuwani za makaazi (postcode). Hivi sasa, tayari mzabuni ameshapatikana ambapo kampuni
ya Mwananchi Supply Ltd ya Zanzibar ndio iliyoshinda kwa hatua ya majaribio kwenye shehia
nne zifuatazo: Mombasa na Chukwani Unguja, na Limbani na Selemu kwa upande wa Pemba.
IIe) SEKTA YA USAFIRI WA ANGA
79. Mheshimiwa Spika, sekta ya usafiri wa anga inajumuisha huduma za viwanja vya ndege na
udhibiti wa usalama wa usafiri wa anga. Huduma hizi zinatolewa kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar kwa mashirikiano na taasisi mbali
mbali za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sekta binafsi.
(i) MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE ZANZIBAR
80. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha
2013/2014 Mamlaka ya Viwanja vya Ndege imesimamia, kuendesha na kuendeleza viwanja
vya ndege vya Unguja na Pemba kwa kuzingatia
42
miongozo na kanuni za Kitaifa na Kimataifa. Aidha, Mamlaka imetekeleza miradi mbali mbali ya
uimarishaji huduma za ndege, abiria na mizigo katika viwanja vya ndege vya Zanzibar ili kukidhi
haja na matakwa ya watumiaji kwa kiwango kinachokubalika.
HATUA ZA UTEKELEZAJI KWA MWAKA 2013/2014.
81. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha mwaka
wa fedha 2013/14 Mamlaka ya Viwanja vya Ndege imehudumia jumla ya safari za ndege 45,801 ikilinganishwa na safari 43,339 zilizohudumiwa
katika kipindi kama hicho cha mwaka 2012/2013, sawa na ongezeko la asilimia 5.7. Kati ya safari
hizo safari za ndege 38,453 zilihudumiwa katika kiwanja cha Kimataifa cha Abedi Amani Karume na safari za ndege 7,348 zilihudumiwa katika
kiwanja cha Pemba.
82. Mheshimiwa Spika, Idadi ya abiria waliohudumiwa iliongezeka kutoka abiria 649,724
mwaka 2012/2013 na kufikia abiria 727,151 Julai 2013 hadi Machi 2014 sawa na asilimia 11. Kati ya abiria hao, abiria 668,804 walihudumiwa katika
kiwanja cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume na abiria 58,347 walihudumiwa katika kiwanja cha
Pemba. Aidha, abiria waliopita (Transit) wamefikia
43
76,680. Ongezeko hili la abiria limetokana na kuongezeka kwa shughuli za utalii, biashara na
kijamii. Idadi ya abiria wa nje ni 302,479 na abiria wa ndani ni 424,672. (Kiambatanisho Namba
6). Kwa upande wa mizigo (freight) jumla ya tani
1,396 zilihudumiwa katika viwanja vya Unguja na Pemba ikilinganishwa na tani 850 zilizohudumiwa
katika kipindi kilichopita ikiwa ni ongezeko la asilimia 64. Ongezeko hili limetokana na
kuongezeka kwa idadi ya ndege maalum za mizigo.
MAPATO NA MATUMIZI KWA MAMLAKA.
83. Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar kwa mwaka wa fedha wa 2013/14
ilipanga kukusanya jumla ya TZS bilioni 4.7 kutoka vyanzo vyake vya mapato ya ndani.
Hadi kufikia mwezi Machi 2014 Mamlaka imekusanya mapato halisi ya TZS bilioni 3.1
kutoka ada ya utuaji wa ndege, kodi za ofisi, faida ya biashara (concession fees), huduma za kumbi
za watu mashuhuri, ada za kuegesha magari na mapato mengineyo, sawa na asilimia 65.2 ya makadirio. Aidha, jumla ya TZS bilioni 3.4 sawa na
asilimia 67 ya makadirio ya matumizi zilitumika katika kipindi hicho.
44
UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO 2013/2014.
84. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha
2013/2014, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar iliendelea kuimarisha usalama katika
viwanja vya ndege kwa kuongeza mitambo na mfumo wa kufuatilia mienendo ya shughuli za
usalama na uendeshaji wa kiwanja (CCTV) na mashine za upekuzi kwa kiwanja cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume kupitia miradi ifuatayo:
Ujenzi wa ukumbi (business arrival lounge)
85. Mheshimiwa Spika, Mradi huu ulikusudia
kujenga ukumbi mpya wa kufikia abiria (business arrival lounge) tayari umemalizika kwa asilimia 100 na uko tayari kwa matumizi. Jumla ya TZS
milioni.225.69 zimetumika.
Ujenzi wa kituo cha biashara (business centre)
86. Mheshimiwa Spika, Mradi wa ujenzi wa kituo
cha biashara uliokuwa na lengo la kujenga ofisi za wadau, sambamba na kutoa fursa za ajira kwa vijana pamoja na kuongeza mapato kwa
Mamlaka, ujenzi wa mkahawa pamoja na ujenzi wa ofisi kwa awamu ya mwanzo umekamilika na
jumla ya ofisi saba (7) zimeshajengwa. Hatua inayoendelea sasa ni ukamilishaji wa awamu ya
45
pili ya ujenzi wa ofisi saba (7) zilizobakia. Mradi huu umegharimu TZS milioni 249.44.
Ununuzi wa mashine za ukaguzi (x-rays
machines)
87. Mheshimiwa Spika, Mradi huu ulikusudia kununua mashine nne (4) za ukaguzi kwa ajili ya
kuimarisha hali ya usalama katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Abeid Amani Karume (AAKIA). Mzabuni wa kampuni ya (HISCO
SECURITY DETECTION PRODUCTS) tayari ameshapatikana na hatua iliyobakia ni kutiliana
saini mkataba wa utekelezaji mradi huo. Mradi huu umegharimu TZS milioni 960.
Uwekaji kipaza sauti (public address system)
88. Mheshimiwa Spika, Mradi huu ambao
uliokuwa na lengo la kufunga kipaza sauti kwa ajili ya kuwaondolea usumbufu abiria tayari
umekamilika tayari kipaza sauti hicho kinatumika. Mradi huu umegharimu jumla ya TZS milioni 24.4.
89. Mheshimiwa Spika, kwa ujumla miradi yote imegharimu TZS bilioni 1.49.
46
MALENGO YA MAMLAKA KWA MWAKA 2014/2015.
90. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/2015
Mamlaka ya Viwanja vya ndege kupitia viwanja vya ndege vya Unguja na Pemba inatarajia
kuhudumia jumla ya ndege 48,091 na abiria 763,508.
Mamlaka pia, itaendelea kuvifanyia matengenezo viwanja vyake vya ndege na kuimarisha utoaji wa
huduma mbali mbali za abiria, ndege na mizigo ili kukuza mahitaji ya Usafiri wa Anga kupitia miradi
ifuatayo ambayo kwa ujumla wake inatarajiwa kugharimu TZS milioni 400:-
i. Ufungaji wa mkanda wa mizigo (conveyor belt) kwa ajili ya kuhudumia mizigo katika
kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume katika eneo la kuwasili abiria.
ii. Ujenzi wa kipaa (canopy) eneo la kuwasili
abiria hadi eneo la maegesho ya magari kwa ajili ya kujenga mazingira mazuri kwa wananchi wanaosubiri wageni wao katika
eneo la maegesho.
iii. Kufanya matengenezo ya sehemu ya kuondokea abiria wa ndani katika jengo la
huduma (service building).
47
iv. Kufanya Upembuzi yakinifu wa uwekaji wa kifaa cha kuongozea ndege (ILS) kwa ajili ya
kumuwezesha rubani kuweza kuona vizuri uwanja katika kipindi cha mvua na hali ya
mawingu na hivyo kuhakikisha usalama wa ndege na abiria.
91. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa fedha
2014/2015 Mamlaka inakadiria kukusanya jumla ya TZS bilioni 4.9 na kutumia jumla ya TZS bilioni 4.9 kwa kazi za kawaida na maendeleo. Kati ya
hizo TZS 4.5 ni makusanyo yatokanayo na vianzio vya mapato vya Mamlaka na TZS milioni 400
zitatokana na "safety fee". MASHIRIKIANO NA TAASISI ZA MUUNGANO
92. Mheshimiwa Spika, katika mwaka
2013/2014, Wizara iliendelea kushirikiana na taasisi za Muungano zilizopo hapa Zanzibar (Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) katika utoaji wa huduma na usimamizi wa Sekta ya
Usafiri wa Anga. Mashirikiano na taasisi hizi yamechangia kwa kiasi kikubwa katika upatikanaji
wa huduma na usimamizi mzuri wa sekta hii.
48
IIf) SEKTA YA USAFIRI WA BAHARINI
93. Mheshimiwa Spika, Sekta ya Usafiri Baharini inajumuisha huduma za bandari, huduma za
usafiri wa baharini na udhibiti wa usalama wa usafiri baharini. Huduma za bandari na usafiri wa baharini zinatolewa kupitia Shirika la Bandari,
Shirika la Meli na Uwakala pamoja na sekta binafsi. Aidha, udhibiti wa usalama wa usafiri
baharini unasimamiwa na Mamlaka ya Usafiri Baharini.
(i) MAMLAKA YA USAFIRI BAHARINI
94. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Mamlaka ya Usafiri Baharini iliendelea kusimamia udhibiti
wa usalama wa usafiri wa baharini kwa kuzingatia Sheria ya Usafiri Baharini ya mwaka 2006 na Kanuni zake pamoja na itifaki na mikataba mbali
mbali ya kimataifa iliyoridhiwa na nchi yetu.
HATUA ZA UTEKELEZAJI (2013/2014) Usimamiaji wa usalama wa usafiri baharini
95. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014
Mamlaka ya Usafiri wa Baharini iliendelea kusimamia usalama wa vyombo vya baharini vya
49
abiria na mizigo. Katika kipindi hichi Mamlaka iliandaa Kanuni moja ya „‟Training and Certification
„‟ na kufanya mapitio ya kanuni za Sheria ya Usafiri Baharini na kuzifanyia marekebisho. Aidha,
Mamlaka kwa kutumia kanuni za kusimamia makampuni na taasisi zinazotoa huduma katika bandari na meli, iliendelea na hatua za kuwapatia
leseni waendeshaji wa huduma hizo na kudhibiti shughuli zao.
96. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha
2013/2014 Mamlaka ilisajili jumla ya meli 15 zenye uzito wa ujazo (GRT) 9,127 kwa usajili wa ndani (Tanzania Zanzibar Registry ) na meli 62 zenye
uzito wa ujazo (GRT) 343,653 kwa usajili wa nje (Tanzania Zanzibar International Registry).
(Kiambatanisho Namba 7). Aidha, vyombo vidogo vidogo 112 vilisajiliwa pamoja na kutolewa vitabu vya mabaharia (Discharge Books) 676 na
vitambulisho vya kimataifa vya mabaharia 19. Mamlaka pia imetoa leseni za manahodha (Boat
Master Licences ) 92 na Boat Engineer 12. Vile vile, Mamlaka ilikagua jumla ya meli 52 zenye
uzito wa ujazo (GRT) 41,626 na kuthibitisha mikataba 262 ya mabaharia wanaosafiri na meli za
nje kupitia kampuni ya DANAOS.
50
97. Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Usafiri Baharini imefanya vikao mbali mbali vya wadau
wa sekta ya usafiri baharini ikiwemo vikao vya ushirikiano na SUMATRA, Kamati za Ulinzi na
Usalama za Mikoa na Wilaya zote na Wakuu wa Madiko Unguja na Pemba kuhusiana na masuala ya usalama wa vyombo vidogo vidogo
kuzitumia bandari zisizo rasmi. Jumla ya vikao 14 na wadau hao wa sekta ya usafiri baharini
vimefanyika. Aidha, Mamlaka imefanya zoezi maalum la kuhakiki utaratibu wa udhibiti wa
uuzaji wa tiketi za magendo na utumiaji wa vitambulisho wakati wa ununuzi wa tiketi na uingiaji bandarini.
Vile vile, Mamlaka ya Usafiri Baharini na SUMATRA zimeendelea kushirikiana katika
masuala yanayohusu ukaguzi na uhakiki wa ubora wa vyombo vya usafiri wa baharini, taratibu za utafutaji na uokozi na kubadilishana
taarifa muhimu.
98. Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Usafiri Baharini kwa mwaka 2013/2014 ilikadiria kukusanya jumla ya TZS bilioni 1.738 na kutumia
jumla ya TZS bilioni 1.625 kwa matumizi ya kawaida.
Hadi kufikia mwezi Machi 2014, jumla ya TZS milioni 872.66 zimekusanywa sawa na asilimia
51
51 ya makadirio na kutumia jumla ya TZS milioni 792.27 sawa na asilimia 49 ya makadirio.
MALENGO YA MAMLAKA KWA MWAKA
(2014/2015). 99. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa fedha
2014/2015, Mamlaka itaendelea kusimamia masuala ya usafiri baharini kwa kufanya ukaguzi
na kutoa leseni za vyombo vya baharini, utoaji wa leseni za manahodha na kukuza vyanzo vyake vya
mapato pamoja na kukamilisha kanuni tano za Sheria ya Usafiri Baharini ili ziendelee kutumika. Aidha, Mamlaka itaendelea kudhibiti shughuli za
makampuni na taasisi zinazotoa huduma katika bandari na meli na kuwapatia leseni. Vile vile,
usajili wa meli za kimataifa utafanywa na Mamlaka ya Usafiri Baharini yenyewe na kuondokana na uwakala.
100. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa fedha
2014/2015 Mamlaka imepanga kukusanya jumla ya TZS bilioni 1.380 na kutumia jumla ya TZS bilioni 1.359 kwa matumizi ya kazi za kawaida
ikiwemo ruzuku ya TZS milioni 300 ya mishahara ya Mamlaka.
52
Huduma za Bandari
(ii) SHIRIKA LA BANDARI
101. Mheshimwa Spika, Shirika la Bandari lina jukumu la kutoa huduma za uingizaji na utoaji
meli katika bandari za Unguja na Pemba, ufungaji na ufunguaji wa meli kwenye gati, uangalizi wa alama za kuongozea usafiri wa meli (minara na
maboya), uteremshaji na upakiaji wa bidhaa kwenye meli pamoja na vyombo vyengine vya
usafiri wa baharini. Vile vile, Shirika lina wajibu wa kuhifadhi mizigo na utunzaji wake katika Bandari pamoja na kuvifanyia matengenezo madogo
madogo vyombo mbali mbali vya usafiri wa Baharini kwa kutumia Karakana yake ya Malindi.
HATUA ZA UTEKELEZAJI (2013/2014)
102. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka
2013/2014 Shirika lililenga kuhudumia meli za kigeni 180 zenye uzito wa ujazo (GRT) 2.6
milioni. Hadi kufikia mwezi Machi 2014 jumla ya meli za Kigeni 152 zenye uzito wa ujazo (GRT)
2.27 milioni zimehudumiwa sawa na asilimia 84 ya lengo. Aidha, meli za ndani zipatazo 2,913 zimehudumiwa pamoja na vyombo vya kienyeji
4,617 kati ya vyombo 4,100 vilivyokadiriwa. Shirika pia, limehudumia jumla ya tani 49,363
ukilinganisha na tani 53,245 za mizigo
53
mchanganyiko zilizohudumiwa katika kipindi kilichopita. Vile vile, Shirika limehudumia jumla
ya makontena 44,276 ikilinganishwa na makontena 38,341 yaliohudumiwa katika kipindi
kama hicho kilichopita.
Kwa upande wa abiria jumla ya abiria 1,776,101 wa ndani na abiria wa nje 2,654
wamehudumiwa kupitia bandari za Unguja na Pemba.
Kazi za Kiufundi:
103. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Julai 2013 hadi Machi 2014 Karakana kuu ya
Shirika ilifanya kazi ya ubadilishaji wa Maboya matatu (3) yanayotumia taa za nguvu ya jua
(Solar Power) katika Bandari ya Mkoani na Boya moja (1) katika Bandari ya Wete.
104. Mheshimiwa Spika, Shirika kupitia
karakana yake hiyo pia, imeyafanyia matangenezo maboya manne (4) ya Solar
pamoja na kuunda maboya saba (7) bubu ambapo maboya mawili (2) ni kwa ajili ya Meli za mafuta katika Bandari ya Wesha na matano (5)
kwa ajili ya kuongozea vyombo vya baharini katika Bandari hiyo.
54
UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO
105. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Julai 2013 hadi Machi, 2014 Shirika limetekeleza
miradi ifuatayo:-
i. Matengenezo ya sakafu ya eneo la
kuhifadhia makontena bandarini Malindi. Kazi za kuchimbua, kujaza kifusi na kushindilia eneo hilo zimefanyika. Jumla
ya TZS milioni 164.01 zimetumika kugharamia mradi huu.
ii. Ujenzi wa jengo la Afisi bandarini. Mradi
huu umeshakamilika na kukabidhiwa
Shirika katika mwezi wa Aprili 2014 ambapo jumla ya TZS milioni 958.74
zimetumika.
iii. Ununuzi na Ufungaji wa Taa za Solar
katika minara yote mikubwa ya kuongozea Meli iliopo Unguja na Pemba. Taa hizo tayari zimenunuliwa na
zimeshafungwa katika minara yote mikubwa minane (8) ya Unguja na Pemba
na zinafanya kazi kama ilivyokusudiwa. Jumla ya USD 221,700 zimetumika.
iv. Ununuzi wa tagi kubwa kwa ajili ya
ufungaji na ufunguaji wa meli katika
55
bandari ya Malindi. Taratibu za manunuzi zimekamilika na Shirika limetiliana saini
Mkataba wa matengenezo ya Tagi hiyo katika mwezi wa Machi, 2014 na
Mkandarasi aliyeshinda Zabuni. Ujenzi wa chombo hicho utaanza mara tu Shirika litakapofanya malipo ya awali (Down
Payment) na unatarajiwa kuchukua miezi sita (6). Mradi huu utagharimu jumla ya
Euro milioni 4.4 ambapo kwa sasa jumla ya Euro milioni 1.32 zimeshalipwa sawa
na TZS bilioni 3.05.
v. Uchimbaji wa Mchanga (Dredging) katika
Gati ya Malindi. Mradi huu haujaanza kutokana na hali ya kifedha kwa hivi
sasa. Hata hivyo Shirika limekusudia kuutekeleza mradi huo mara tu hali itakaporuhusu.
MAPATO NA MATUMIZI YA SHIRIKA
106. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Julai 2013 hadi Machi, 2014 Shirika lilikadiria
kukusanya jumla ya TZS bilioni 12.81. Hadi kufikia mwezi wa Machi, 2014 jumla ya TZS bilioni 14.60 zilikusanywa ikiwa ni sawa na
asilimia 114 makadirio ya kipindi hicho cha miezi tisa. Aidha, Shirika lilipanga kutumia
jumla ya TZS bilioni 10.63 na hadi kufikia
56
Machi 2014 jumla ya TZS bilioni 10.47 pia zimetumika kwa kazi za kawaida sawa na
asilimia 98.51.
MALENGO YA SHIRIKA KWA MWAKA
2014/2015
107. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka
2014/2015 Shirika la Bandari linatarajia kuhudumia jumla ya meli 185 za kigeni zenye uzito (GRT) wa Tani 2.7 milioni, Meli za ndani
zipatazo 3,500 na Majahazi 5,000 pamoja na kuhudumia tani 86,140 za mzigo mchanganyiko
na makontena 59,116.
108. Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa miradi ya maendeleo Shirika linatarajia kuendelea na uimarishaji wa huduma na
rasilimali zake kwa kuikamilisha miradi iliyoanzishwa mwaka wa Fedha unaomalizika
kama ilivyoelezwa hapo juu pamoja na kuendelea na awamu ya tatu ya mradi wa ununuzi wa vifaa vya kunyanyulia mizigo
bandarini.
Kwa mwaka wa fedha 2014/2015 Shirika la Bandari limekadiria kukusanya jumla ya TZS bilioni 19.81. Aidha katika kutekeleza malengo
yake Shirika limepanga kutumia jumla ya TZS bilioni 16.22 kwa kazi za kawaida.
57
(iii) SHIRIKA LA MELI NA UWAKALA.
109. Mheshimiwa Spika, Shirika la Meli na Uwakala limeendelea kutoa huduma za usafiri
wa baharini baina ya visiwa vya Unguja na Pemba kwa kutumia meli ya MV Maendeleo. Aidha, Shirika limekodisha meli ya MT
Ukombozi kwa kampuni ya GAPCO. Changamoto kubwa inayoikabili Shirika ni
uchakavu wa meli zake. Ili kukabiliana na changamoto hii Shirika liliendelea na utaratibu
maalum wa “preventive maintenance” kwa ajili ya kupunguza matumizi makubwa yatokanayo na matengenezo ya meli. Utaratibu huu
ulianzishwa mwaka jana kupitia ajira za mkataba za Wahandisi bingwa wa
matengenezo ya meli kutoka Kenya. Wataalamu hao kwa kushirikiana na Wahandisi wetu wameweza kuzifanya meli za Shirika
ziendelee kufanyakazi vizuri.
HATUA ZA UTEKELEZAJI KWA MWAKA 2013/2014)
110. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai
2013 hadi Machi 2014 meli ya MV. Maendeleo
imefanya safari 100 kwa kusafirisha abiria na mizigo katika visiwa vyetu. Kwa upande wa
abiria na mizigo, jumla ya abiria 82,980
58
walisafirishwa kwa kutumia meli hiyo na shehena ya mizigo tani 17,218.986. Aidha,
Shirika limehudumia meli za kigeni zipatazo 128 zilizoingia nchini kwa kutumia bandari zetu.
MAPATO NA MATUMIZI YA SHIRIKA.
111. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha
Julai 2013 hadi Machi 2014 Shirika lilikusanya
jumla ya TZS bilioni 4.315 sawa na asilimia 79 ya makisio ya mwaka 2013/2014. Kati ya hizo
TZS bilioni 1.26 zilitokana na meli ya MV Maendeleo na TZS bilioni 1.24 kutoka meli ya MT. Ukombozi na TZS bilioni 1.28 kwa Uwakala
wa meli za kigeni.
Kwa upande wa matumizi, jumla ya TZS 4.314 bilioni sawa na asilimia 85 ya makisio ya
mwaka 2013/2014 zilitumika. MALENGO YA SHIRIKA KWA MWAKA
2014/2015
112. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/2015 Shirika linategemea
kukusanya jumla ya TZS bilioni 6.63 kutokana na vianzio vyake vya mapato na kutumia jumla ya TZS bilioni 5.761 kwa matumizi ya kazi za
kawaida.
59
113. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2014/2015 Shirika litaendelea kutekeleza
majukumu yake ya uendeshaji wa meli za Serikali kwa kusafirisha abiria na mizigo kwa
kutumia meli ya MV Maendeleo. Aidha, Shirika litaendelea na utaratibu maalum wa “preventive maintenance” ulioanzishwa mwaka jana kwa
ajili ya kupunguza matumizi makubwa yatokanayo na matengenezo ya mara kwa
mara ya meli na kuzifanya meli zetu ziendelee kufanya kazi vizuri hadi pale taratibu za
upatikanaji wa meli mpya zitakapokamilika.
Vile vile, Shirika litaendelea na taratibu za kuajiri kwa mkataba wahandisi kwa kazi za
melini (Sign-on/Sign- off) na kuendelea kutoa huduma za uwakala wa meli za kigeni
zinazoingia nchini kwa kutumia bandari zetu.
60
III: HITIMISHO.
114. Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Wizara
ya Miundombinu na Mawasiliano, napenda kuwashukuru kwa dhati wale wote
walioshirikiana nasi katika kipindi cha mwaka wa fedha 2013/2014 katika utekelezaji wa majukumu yetu. Shukurani za pekee ziwaendee
Washirika wa Maendeleo walioendelea kushirikiana nasi katika kutekeleza programu na
mipango yetu ya uimarishaji miundombinu ya usafiri na mawasiliano. Washirika hao ni
pamoja na Jamhuri ya Watu wa China, Norway, Japan, Saudi Arabia, India, Marekani, Ujerumani, Oman na UAE. Mashirika ya
Kimataifa ni pamoja na Benki ya Dunia (World Bank), China Exim Bank, Jumuiya ya Nchi za
Ulaya (EU), Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Afrika (BADEA), Mfuko wa Umoja wa
Maendeleo ya Kimataifa wa Nchi Zinazosafirisha Mafuta kwa Wingi ulimwenguni (OPEC Fund),
SAUDI Fund, NORAD, Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya UNDP, IMO na ICAO.
115. Mheshimiwa Spika, nitakuwa mchoyo wa
fadhila nisipowashukuru viongozi wenzangu na nikianza na Mhe. Issa Haji Ussi Gavu, Naibu
Waziri, Dkt. Juma Malik Akil, Katibu Mkuu, Nd. Tahir M.K. Abdullah na Wakurugenzi wote.
61
Aidha, nawashukuru Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya
Wizara, Wakuu wa Vitengo pamoja na wafanyakazi wote wa Wizara ya Miundombinu
na taasisi zake kwa kuendelea kujituma kwa juhudi na maarifa katika kutekeleza malengo na majukumu ya Wizara yetu.
116. Mheshimiwa Spika, tunawashukuru wadau wote wa sekta ya usafiri na mawasiliano
na hasa sekta binafsi ambao wametupatia ushirikiano wa kutosha katika kuendeleza sekta
hii. Shukurani zangu za pekee nazitoa kwa Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali na wafanyakazi wote wa Ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali
kwa kuchapa vizuri hotuba hii.
62
IV: MAOMBI YA FEDHA KWA MWAKA 2014/2015
117. Mheshimiwa Spika, kwa madhumuni ya
kuiwezesha Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano kutekeleza majukumu yake na malengo yaliyoelezwa katika hotuba hii, naomba kutoa hoja kwamba, Baraza lako
Tukufu liidhinishe jumla ya TZS bilioni 14.077 kwa ajili ya matumizi ya Wizara kwa mwaka wa
fedha 2014/2015. Kati ya fedha hizo, TZS bilioni 5.677 ni kwa ajili ya kazi za kawaida na
TZS bilioni 8.40 ni kwa ajili ya kazi za maendeleo.
Aidha, naliomba Baraza lako Tukufu kuruhusu
Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano kukusanya mapato ya jumla ya TZS
436,000,000 kutokana na vianzio mbalimbali vilivyomo ndani ya Wizara hii.
118. Mheshimiwa Spika
Naomba kutoa hoja.
63
KIAMBATANISHO NAMBA 1:
SEHEMU A: MUHTASARI WA MAKADIRIO YA FEDHA KWA KAZI ZA KAWAIDA, MAENDELEO NA MAPATO KWA KIPINDI CHA
JULAI 2013 HADI MACHI 2014 NA MAKISIO YA MWAKA 2014/2015
KASMA
MATUMIZI
HALISI
2012/2013
MAKADIRIO
2013/2014
FEDHA HALISI Julai 2013-Machi 2014 Asilimia Makisikio
Mishahara/
Maposho
Matumizi
Mengineyo
Jumla
%
2014/2015
0301 PEMBA 1,074,213,708 1,277,000,000 733,060,300 125,664,000 858,724,300 67% 1,362,501,000
0401 MIPANGO 108,007,210 288,000,000 0 83,137,770 83,137,770 29% 200,585,000
0501 MAMLAKA YA USAFIRI BAHARINI. 0 238,000,000 178,560,000 0 178,560,000 75% 300,000,000
0701 UUB 1,271,433,402 250,000,000 0 81,282,842 81,282,842 33% 165,488,000
0801 LESENI 447,121,180 300,000,000 0 64,298,000 64,298,000 21% 200,585,000
64
KASMA
MATUMIZI
HALISI
2012/2013
MAKADIRIO
2013/2014
FEDHA HALISI Julai 2013-Machi 2014 Asilimia Makisikio
Mishahara/
Maposho
Matumizi
Mengineyo
Jumla
%
2014/2015
0901 UENDESHAJI 1,135,464,070 2,583,400,000 1,798,064,362 217,946,860 2,016,011,222 86% 3,269,114,000
0110 MAWASILIANO 104,294,460 255,600,000 0 80,039,000 80,039,000 31% 179,527,000
JUMLA 4,140,534,030 5,192,000,000 2,709,684,662 652,368,472 3,362,053,134 5,677,800,000
65
Kiambatanisho 1: Inaendelea……………….
SEHEMU B: MAPATO
KASMA
MAPATO
HALISI
2012/2013
MAKADIRIO
2013/2014
FEDHA
ZILIKUSANYWA
JULY-MACHI
2013/2014
ASILIMIA %
MAKISIO
2014/2015
0301 PEMBA 47,882,500 50,200,000 44,550,559 89% 62,000,000
0701 UUB 6,650,000 10,000,000 3,480,000 35% 10,000,000
0801 LESENI 339,833,650 346,000,000 266,218,300 77% 364,000,000
JUMLA 394,366,150 406,200,000 314,248,859 77% 436,000,000
66
Kiambatisho 1: Inaendelea……………….
SEHEMU C: KAZI ZA MAENDELEO
KASMA
MATUMIZI
HALISI
2012/2013
MAKADIRIO
2013/2014
FEDHA
ZILIZOPATIKANA
JULY-MACHI
2013/2014
ASILIMIA % MAKISIO
2014/2015
0301 PEMBA 2,501,829,904 4,723,356,000 3,120,000,000 66 3,325,000,000
0401 MIPANGO 897,270,096 7,976,644,000 822,798,204 10 3,325,000,000
0701 UUB 1,609,544,000 2,200,000,000 433,532,436 20 1,750,000,000
JUMLA 5,008,644,000 14,900,000,000 4,376,330,640 96 8,400,000,000
67
KIAMBATANISHO NAMBA 2:
MIRADI YA MAENDELEO ILIYOPANGWA/KUTEKELEZWA 2014/2015
NA. UJENZI UREFU (km) MFADHILI BAJETI YA SMZ
(Tsh)
RUZUKU/
MKOPO (Tsh)
1. Ujenzi wa barabara 3 za Pemba
Wete – Gando (13.6)
Wete – Konde (15.1)
Wete – Chake (24)
52.7 SMZ/BADEA
/SAUD FUND 2,425,000,000 11,999,998,000
2 Ujenzi wa barabara 3 za Pemba
Wete – Chake (mradi mpya) 24 SMZ/BADEA
/SAUD FUND 100,000,000 0
3. Ujenzi wa barabara ya Mgagadu- Kiwani 7.6
SMZ
300,000,000
0
4. Ujenzi wa barabara ya Mkanyageni - Kangani
6.5 SMZ 0 0
5. Ujenzi wa barabara ya Ole – Kengeja
35 SMZ /OPEC 500,000,000 4,392,000,000
68
NA. UJENZI UREFU (km) MFADHILI BAJETI YA SMZ
(Tsh)
RUZUKU/
MKOPO (Tsh)
6
Upembuzi yakinifu wa barabara za vijijini-Unguja
(Matemwe –Muyuni, Kichwele-Pangeni, Njia nne-
Umbuji-Uroa, Jozani-Charawe-Ukongoroni-Bwejuu
naMkwajuni-Kijini) (mradi mpya)
65.2 AfDB 0 1,754,456,000
7. Ujenzi wa Barabara ya Amani – Mtoni (Benjamin
Mkapa) 4 ROAD FUND 0 0
8 Barabara zinazoingia mjini
77.9 50,000,000 0
9
Ujenzi wa barabara 3 Vijijini -Unguja
Barabara ya Koani – Jumbi (6.3)
Barabara ya Kizimbani – Kiboje (7.2)
Barabara ya Jendele – Cheju – Kaebona (11.7)
25.2
SMZ/BADEA
1,600,000,000
7,500,000,000
JUMLA NDOGO 4,975,000,000 25,646,454,000
- -
10
Ujenzi na utanuzi wa maegesho na njia za kupitia
ndege.
SMZ/WB 975,000,000 14,600,000,000
11 Ujenzi wa jengo jipya la abiria A.AKIA SMZ /EXIM 1,950,000,000 110,840,000,000
69
NA. UJENZI UREFU (km) MFADHILI BAJETI YA SMZ
(Tsh)
RUZUKU/
MKOPO (Tsh)
CHINA
12 Uimarishaji huduma uwanja wa ndege wa Pemba
SMZ 0 0
13 Ujenzi wa bandari mpya Hubport - Maruhubi SMZ 500,000,000 0
14 Mfumo wa mageuzi ya taasisi (Institutional reform) ADB 0 654,456,000
JUMLA NDOGO 3,425,000,000 126,094,456,000
JUMLA KUU 8,400,000,000 151,740,910,000
70
KIAMBATANISHO NAMBA 3:
WAFANYAKAZI WALIOPATA MAFUNZO KWA KIPINDI CHA MWAKA 2013/2014.
IDARA MASTERS PG/DIPLOMA DEGREE
ADV.
DIPLOMA DIPLOMA CHETI JUMLA
MKE MME MKE MME MKE MME MKE MME MKE MME MKE MME
UENDESHAJI NA UTUMISHI
1
11 1 1 1 15
MIPANGO,SERA NA UTAFITI 1 3
1
5
IDARA YA MAWASILIANO
1 1
IDARA YA USAFIRI NA LESENI
1
1
3 1
6
IDARA YA UTUNZAJI BARABARA
1 1
3 1
2 8
AFISI KUU PEMBA
1
1 1 1
1 2 1 2 3 13
JUMLA 1 5
1 4 3
1 19 4 3 7 48
71
MASOMO YA MUDA MFUPI
IDARA W/WAKE W/ME JUMLA
UENDESHAJI NA UTUMISHI 2 7 9
MIPANGO,SERA NA UTAFITI 3 5 8
IDARA YA MAWASILIANO 1 8 9
IDARA YA USAFIRI NA LESENI
3 3
IDARA YA UTUNZAJI BARABARA 2 7 9
AFISI KUU PEMBA 1 7 8
JUMLA 9 37 46
72
KIMBATANISHO NAMBA 4:
BARABARA ZILIZOFANYIWA MATENGENEZO KUPITIA MFUKO WA BARABARA KWA MWAKA
WA FEDHA 2013/2014
Matengenezo ya kawaida ya barabara za lami (Routine maintenance for paved roads)
Kazi zilizofanywa na wafanyakazi wa idara ya barabara (Force account contract)
(Ukataji wa majani, kusafisha misingi na kuziba mashimo)
SNO JINA LA BARABARA
UREFU (KM)
UNGUJA
1 Tunguu- Makunduchi 34.00
2 Kaebona-Kaepwani 6.00
3 Kibuteni-Kizimkazi Mkunguni 6.00
4 Mkwajuni-Matemwe 7.00
5 Mshelishelini-Pwanimchangani 7.50
6 Mwanakwerekwe-Tunguu 30.00
7 Mchinamwazo-Nyumbambili 1.20
8 Soko la mboga –Buyu 1.20
73
SNO JINA LA BARABARA
UREFU (KM)
9 Paje-Michamvi 17.82
10 Mtegani-Mtende 5.50
11 Dunga-Chwaka 14.40
12 Paje-Makunduchi 18.40
Jumla ndogo 149.02
PEMBA
1 Chake-Wete 30.00
2 Kilindini-micheweni 6.00
3 Konde-Kiuyu kwa Manda 3.50
4 Mkoani-Makombeni 5.00
5 Bogoa-Michenzani 3.00
6 Chanjaani-M/manne 4.00
7 Mbuguani-Mkoani Port 2.00
8 Mkoani-Shindi 2.20
74
SNO JINA LA BARABARA
UREFU (KM)
9 Mkoani-Ng'ombeni school 0.50
Jumla ndogo 56.20
75
KIAMBATANISHO 4: INAENDELEA……………..
Matengenezo ya sehemu korofi - uwekaji wa lami
SNO JINA LA BARABARA UREFU KM MAELEZO
UNGUJA
Kazi zimeanza
1 Upenja-Kiwengwa 1.30
2 Mkwajuni-Matemwe (sehemu ya Kilimani) 0.17
3
Uwekaji wa taa za nguvu za jua (Sola) za kuongozea magari na CCTV sehemu ya
makutano ya barabara Malindi, Mkunazini na Kwamchina mwanzo
4 Mwanakwerekwe-Tunguu ( Sehemu
yaTunguumwisho ) 6.00
JUMLA 7.47
76
Matengenezo ya muda maalum (Periodic maintenance)
SNO JINA LA BARABARA UREFU KM MAELEZO
UNGUJA
1 Kikwajuni-Kisiwandui via Wireless (kiwango cha
lami) 0.50
Mkandarasi anafanya
matayarisho 2 Buyu-Chukwani (Kiwango cha lami) 0.70
3 Fuoni-Kibondemzungu (Kiwango cha kifusi) 2.00
4 Amani-Mtoni (uwekaji wa kingo za zege awamu
ya kwanza katikati ya barabara)- 1.6km Kazi zimekamilika
5 Njia nne-Umbuji (Kiwango cha lami) 5.00 Kazi zinaendelea
6 Kivunge-Mkokotoni (Uwekaji wa lami) 3.30 Kazi zimekamilika
7 Mkwajuni-Mshelishelini (Uwekaji wa lami) 2.00 Kazi zimekamilika
8 Kwaabasi Hussein-Kilimahewa (Kiwango cha lami) 0.30 Kazi zimekamilika
JUMLA NDOGO 13.80
PEMBA
1 Barabara ya Mtaa wa Kilo road (Kiwango cha
kifusi) 0.40
Kazi zinaendelea
2 Barabara ya Mtaa wa Selemu (Kiwango cha 0.80
77
SNO JINA LA BARABARA UREFU KM MAELEZO
kifusi)
3 Barabara ya Msitu wa Ngezi (kwa kiwango cha
Saruji na udongo) 1.20 Kazi zimekamilika
4 Melitano-Madenjani (Kiwango cha lami) 12.30 Taratibu za manunuzi
zinaendelea
5 Chake-Wesha (Kiwango cha lami) 1.00 Kazi zimekamilika
6 Melitano-Machomanne(Kiwango cha lami) 2.20 Kazi zinaendelea
JUMLA NDOGO 17.90
JUMLA KUU UNGUJA NA PEMBA 31.70
78
KIAMBATANISHO 4: INAENDELEA……………..
Matengenezo ya dharura
SNO AINA YA KAZI/JINA LA BARABARA UREFU KM MAELEZO
UNGUJA
1 Uchimbaji wa mtaro wa maji-Kwamchina mwanzo
(barabara ya Jang'ombe) kwa awamu ya kwanza 0.23 Kazi zimekamilika
2 Matengenezo ya sehemu korofi sehemu ya Sogea 0.60 Kazi zinaendelea
PEMBA
1 Ujenzi wa mtaro sehemu ya Kwachangawe
barabara ya Mkoani-Chake 0.12 Kazi zimekamilika
79
Matengenezo/ Ujenzi wa kalvati na mitaro
SNO JINA LA BARABARA IDADI/KM MAELEZO
PEMBA
Kazi zinaendelea
Ujenzi wa kalvati (No)
1 Mgagadu-Kiwani 2
2 Konde –Kiuyu 2
JUMLA 4
Ujenzi wa mitaro (Km)
Ole-Konde 0.20
Chake-Mkoani 0.40
JUMLA 0.60
80
KIAMBATANISHO 4: INAENDELEA……………..
MALENGO KWA MWAKA WA FEDHA 2014/2015 KWA KUTUMIA FEDHA ZA MFUKO WA
BARABARA - ZANZIBAR.
Matengenezo ya kawaida barabara za lami (Routine maintenance for paved roads) zilizopangwa
kufanywa na Idara ya barabara (Force account contract)
(Ukataji wa majani, kusafisha misingi na kuziba mashimo)
UNGUJA
Ref JINA LA BARABARA UREFU (KM)
T3 Tunguu-Makunduchi 34.00
R107 Kaebona-Unguja Ukuu 6.00
T8 Paje - Makunduchi 18.00
R109 Mtegani-Mtende 5.50
T002 Dunga - Chwaka 14.42
R108 Kibuteni-Kizimkazi 5.50
R115 M/shelini - P/Mchangani 7.50
R113 Mkwajuni - Matemwe 7.43
81
Ref JINA LA BARABARA UREFU (KM)
T7 Pongwe - Matemwe 20.40
R Mfenesini- Bumbwini-Mangapwani 13.82
T8 Paje - Michamvi 17.00
T3 M/kwereke - Tunguu 30.00
F448 Kwamchina mwanzo -Mbuyu mnene/nyumbambili 2.80
U220 Mazizini-Chukwani/U/ndege 9.00
Jumla 191.37
Matengenezo ya kawaida barabara za lami (Routine maintenance for paved roads) zilizopangwa
kufanywa na Idara ya barabara (Force account contract)
(Ukataji wa majani, kusafisha misingi na kuziba mashimo)
82
PEMBA
Ref JINA LA BARABARA UREFU (KM)
T31
Chake Chake - Wete 30
R199 Konde - Kiuyu cha Manda 3.5
T31 Chanjaani - M/Manne 4
T31 Mbuguani - Mkoani Port 2
T32 Kilindini - Micheweni 6
U301 Mkoani Port- Ngo'mbeni school 0.5
R161 Mkoani - Makombeni 5
F503 Bogoa - Michenzani 3
F502 Mkanyageni - Shidi 2.2
Jumla 56.20
83
KIAMBATANISHO 4: INAENDELEA……………..
Matengenezo ya kawaida barabara za lami (Routine maintenance for paved roads) zilizopangwa
kufanywa na wakandarasi/vikundi vya jamii (Contract account contract) (Ukataji wa majani, kusafisha
misingi na kuziba mashimo)
UNGUJA
Ref JINA LA BARABARA UREFU (KM)
1 Lot. 1
R119 Bububu - Mndo 3.94
F401 Kwanyanya-Mkanyageni 3.08
R102 Regezamwendo-Mfenesini 14.27
2 Lot.2
F402 Kitundu-Ndagaa 5.50
T2 Amani -Dunga 12.74
F403 Koani - Machui - Kitumba 5.50
R103 Kidimni- Kitope 19.00
3 Lot.3
84
Ref JINA LA BARABARA UREFU (KM)
T6 Kinyasini - Tunguu 26.76
T1 Mkwajuni - Nungwi 19.00
4 Lot.4
R114 Upenja - Kiwengwa 8.31
T7 Kipilipilini - Pongwe 14.00
T1 Mahonda - D/Mkokotoni 13.52
R104 Njianne - Bambi 6.50
5 Lot.5
T1 Kwanyanya - Mahonda 19.00
T1 Mahonda-K/Mkokotoni 15.00
6 Lot. 6
T4 Mazizini - Fumba-Kwabakharesa 19.82
R110 Kitogani - Paje 11.60
Lot.7
T1 Malindi jctn-Kwanyanya 10.00
T5 Mnazimmoja - U/ndege 3.00
85
Ref JINA LA BARABARA UREFU (KM)
U201 Mtoni- Amani - K/samaki 9.00
Jumla 239.54
86
KIAMBATANISHO 4: INAENDELEA……………..
Matengenezo ya kawaida barabara za lami (Routine maintenance for paved roads) zilizopangwa
kufanywa na wakandarasi/vikundi vya jamii (Contract account contract) (Ukataji wa majani, kusafisha
misingi na kuziba mashimo)
PEMBA
Ref JINA LA BARABARA UREFU (KM)
1 Lot.1
T32 Ole - Konde 25.50
T32 Madenjani - M/Takao 5.50
2 Lot.2
T31 Chajaani - Mbuguani(Mkoani) 27.50
R163 Mtuhaliwa - Chokocho 8.80
3 Lot.3
R178 Machomane - Vitongoji 7.00
R177 Chanjaani - U/Ndege 5.50
R179 Chake Chake - Wesha 8.00
87
Ref JINA LA BARABARA UREFU (KM)
4 Lot.4
R164 Mtambile - Kangani 6.4
R174 Chanjamjawiri - Tundauwa 11.0
R175 Chanjaani - Pujini 5.0
R169 Kenya - Chambani 3.2
R165 Mtambile - Mwambe 9.4
R202 Mizingani - Wambaa 9.4
5 Lot.5
R187 Bahanasa-Uondwe (Mtambwe) 10.36
R188 M/takao-Pandani-M/karim 13.44
R190 Kipangani-Kangagani 2.7
R195 Chwale-Likoni 1.9
R198 Mapofu-Finya Bahraini 5.5
R200 Daya-Makongeni 3.65
Jumla 169.75
88
Matengenezo ya kawaida barabara za kifusi (Routine maintenance for unpaved roads)
zilizopangwa kufanywa na Idara ya barabara (Force account contract)
UNGUJA
Ref JINA LA BARABARA UREFU (KM)
F413 Kwakisasi via Mwanyanyanya-Bububu school 3.8
F440 Donge- Mwanda 2
F412 Kama-KMKM 2.5
F421 Kijitoupele-Nyarugusu 2.5
F416 Fuoni-Kwarara 0.6
Jumla 11.4
89
KIAMBATANISHO 4: INAENDELEA……………..
Matengenezo ya sehemu Korofi (Spot improvement)
PEMBA
Ref JINA LA BARABARA UREFU (KM)
Mkoani- Chake sehemu ya Kwachangawe 1.20
Matengenezo ya muda maalum (Periodic Maintenance)
Ref JINA LA BARABARA UREFU (KM)
UNGUJA
R101 Bumbwini-Kiongwe School (kwa kiwango cha kifusi) 4.3
T2 M/kwerekwe Makaburini-Fuoni (kwa kiwango cha lami) 1.7
Tomondo Magereza - Mchina mwisho (kiwango cha lami) 1.5
Michenzani- Mtendeni (Kiwango cha lami) 0.7
T1 Kikobweni-Mshelishelini (Kiwango cha lami) 5.28
Jumla 13.48
PEMBA
90
R199 Melitano-Madenjani (kiwango cha lami) 12.3
Pandani - Mlindo (Kiwango cha kifusi) 2.5
Jumla 14.8
Jumla yote (Unguja na Pemba) 28.28
Matengenezo ya Madaraja/Kalvati Kasha na Mitaro
Ref JINA LA BARABARA IDADI
Ujenzi wa kalvati kasha Unguja na Pemba
T1 Bububu-Mahonda- Ujenzi wa daraja kasha la Kitope 1No
R164 Kangani-Mkanyageni - Ujenzi wa kalvati kasha 1No
Jumla 2No
Ujenzi wa Mitaro barabara za Pemba
T32 ChakeChake-Mkoani road 0.4km
T32 Chake chake -Wete road 0.4km
Jumla 0.8km
91
KIAMBATANISHO 4: INAENDELEA……………..
Uwekaji wa alama za barabarani na mipaka ya miliki ya barabara
Ref JINA LA BARABARA IDADI
UNGUJA
Uwekaji wa alama za miliki ya barabara (Road reserve posts)
U204 Amani-Dunga road (10km) 100No
T1 Bububu - Mahonda (21km) 210No
Jumla 310No
92
Uwekaji wa alama za usalama barabarani (Road signs)
U204 Amani-Dunga road (10km) 60No
T1 Bububu - Mahonda (21km) 10No
Jumla 70No
Uchoraji wa mistari kwenye barabara (Road marking)
U201 Barabara ya Amani-Mtoni road (4km-4lines) 12,000m2
Jumla 12,000m2
93
KIAMBATANISHO NAMBA 5:
UKAGUZI WA VYOMBO VYA MOTO JULAI 2013 HADI MACHI 2014:
AINA YA
VYOMBO
IDADI YA VYYOMBO VYA MOTO VILIVYOKAGULIWA
JUMLA
UKAGUZI WA
KAWAIDA
UKAGUZI WA
SHAKA
UKAGUZI WA
AJALI
UNGUJA PEMBA UNGUJA PEMBA UNGUJA PEMBA
GARI 12,573 1,050 75 13 548 33 14,292
MOTORCYCLE 11,274 1,912 22 3 221 7 13,439
JUMLA 23,847 2,962 97 16 769 40 27,731
94
Kiambatanisho 5: Inaendelea……………….
RUHUSA ZA NJIA NA USAFIRISHAJI
MAHALI
ZILIPOTOEWA
AINA YA HUDUMA ILIOTOLEWA
Daladala Shamba P/Hire Taxi Mizigo School Staff H/Drive Jumla
UNGUJA 369 301 342 205 280 22 27 00 1,546
PEMBA 29 201 12 18 90 00 00 00 350
JUMLA 398 502 354 223 370 22 27 0 1,896
95
Kiambatanisho 5: Inaendelea……………….
TAKWIMU ZA MADEREVA WALIOJARIBIWA KUENDESHA VYOMBO VYA MOTO:
AINA YA
MADEREVA
WALIOJARIBIWA
KUENDESHA
WALIOFAULU
KUENDESHA
WALIOFELI
KUENDESHA
Gari M/c Jumla Gari M/c Jumla Gari M/c Jumla
UNGUJA 2,443 1,473 3,916 1,775 1,301 3076 633 207 840
PEMBA 918 887 1,805 868 381 1,249 346 210 556
JUMLA 3,361 2,360 5,721 2,643 1,682 4,325 979 417 1,396
96
Kiambatanisho 5: Inaendelea……………….
UTOAJI WA LESENI KWA MADEREVA WANAFUNZI
DARAJA M A B1 B C1 C D1 D E G JUMLA
UNGUJA 34 2,511 2,646 6 453 290 968 308 2 0 7,218
PEMBA 0 478 251 75 43 13 51 74 0 0 985
JUMLA 34 2,989 2,897 81 496 303 1,019 382 2 0 8,203
97
Kiambatanisho 5: Inaendelea……………….
UKUSANYAJI WA MAPATO
S/No Aina ya mapato Unguja Pemba jumla
1 Majaribio ya madereva 41,288,500 7,478,500 48,767,000
2 Ukaguzi wa vyombo 156,270,000 16,569,500 172,839,500
3 Fomu za maombi 32,971,400 8,370,000 41,341,400
4 Kadi za njia 26,298,900 1,840,000 28,138,900
5 Mapato mengineyo 9,390,000 10,292,559 19,682,559
Jumla 266,218,800 44,550,559 310,769,359
98
KIAMBATANISHO NAMBA 6:
IDADI YA NDEGE ZILIZOHUDUMIWA KATIKA KIPINDI CHA JULAI 2013 HADI MACHI 2014
AINA YA
NDEGE
IDADI YA NDEGE
2012/2013
JUMLA
IDADI YA NDEGE
2013/2014
JUMLA
UNGUJA PEMBA UNGUJA PEMBA
SCHEDULE 22,369 6,096 28,465 21,977 7,014 28,991
CHARTER 13,568 236 13,804 15,257 268 15,525
CARGO 4 - 4 124 - 124
PRIVATE 663 - 663 421 - 421
MILITARY 54 - 54 38 - 38
OTHERS 281 68 349 636 66 702
JUMLA 36,939 6,400 43,339 38,453 7,348 45,801
99
Kiambatanisho 6: Inaendelea……………….
IDADI YA ABIRIA WALIOHUDUMIWA KATIKA KIPINDI CHA JULAI 2013 HADI MACHI 2014
KIWANJA IDADI YA ABIRIA
2012/2013
JUMLA IDADI YA ABIRIA
2013/2014
JUMLA
International Domestic International Domestic
UNGUJA 256,637 343,468 600,105 302,460 366,344 668,804
PEMBA 37 49,582 49,619 19 58,328 58,347
JUMLA 256,674 393,050 649,724 302,479 424,672 727,151
100
Kiambatanisho 6: Inaendelea……………….
KAMPUNI ZA NDEGE ZILIZOTUMIA KIWANJA CHA NDEGE CHA ABEID AMANI KARUME KWA
MWAKA 2013/2014
S/N JINA LA KAMPUNI VITUO NCHI INAYOTOKA
1 Precision Dar, Kilimanjaro, Mombasa,
Nairobi
Tanzania
2 Coastal Travel Zanzibar, Dar, Arusha,Tanga Tanzania
3 Zan Air Zanzibar, Pemba, Dar, Arusha Tanzania
4 Auric Air Dar, Zanzibar, Pemba Tanzania
5 Flight Link Dar, Zanzibar, Pemba Tanzania
6 Air Advanture Zanzibar, Dar, Arusha Tanzania
7 As Salam Air Dar, Zanzibar, Pemba,Tanga Tanzania
101
S/N JINA LA KAMPUNI VITUO NCHI INAYOTOKA
8 Pelican Air Dar, Zanzibar Tanzania
9 Regional Air Dar, Zanzibar Tanzania
10 Safari Air Link Dar, Zanzibar Tanzania
11 Shine Aviation Dar, Zanzibar Tanzania
12 Tanzan Air Dar, Zanzibar Tanzania
13 Tropical Air Dar, Zanzibar, Pemba ,Arusha Tanzania
14 Zenith Aviation Dar, Zanzibar, Pemba Tanzania
15 Twin Wing Dar, Zanzibar Tanzania
16 Air Excel Zanzibar, Dar, Arusha Tanzania
17 Fast Jet Kilimanjaro, Zanzibar Tanzania
18 Ethiopian Airline Addis- Ababa Ethiopia
19 540 Aviation Mombasa, Nairobi Kenya
20 Kenya Airways Mombasa, Nairobi Kenya
102
S/N JINA LA KAMPUNI VITUO NCHI INAYOTOKA
21 Meridian Fly Milan, Malpensa Italy
22 Condor Frankfut, Mombasa Germany
23 Tui Airline Brussels Belgium
24 Travel Service Budapest Hungary
25 Neos Air Milan Italy
26 Oman Air Muscat Oman
27 Livingstone Milan, Mombasa Italy
28 Arkefly Amsterdam, Huhgada, Mombasa Netherlands
29 Alitalia Milan, Mombasa Italy
30 Mango Johannesburg South Africa
31 Xl Airways France France France
103
KIAMBATANISHO NAMBA 7:
ORODHA YA MELI ZILIZOSAJILIWA CHINI YA USAJILI WA NDANI ( LOCAL REGISTRY )
KIPINDI CHA
JULY 2013 – MACHI 2014
S/N JINA LA MELI UZITO (GRT)
1. FATMAH-ZEHRA 341.38
2. COMARCO 185 629
3. CORMACO 186 629
4. CORMACO 184 629
5. NGATI HAKA 258
6. BERKAT MENJALA N0. 23 587
7. SEMUDERA PACIFIC NO. 3 498
8. ALRABEE1 1515
9. FATIMA (EX TORGELOW) 299.48
10. MUNEERA ( EX SEMLOW) 299
11. TANYA 1295
12. MEISA 949
104
S/N JINA LA MELI UZITO (GRT)
13. SVS GUARDSMAN 168
14. SVS AVERY 168
15 MARTIAL 863
JUMLA 9,127.86
105
Kiambatanisho 7: Inaendelea……………….
MELI ZILIZOSAJILIWA CHINI YA USAJILI KUPITIA ‘ TANZANIA ZANZIBAR
INTERNATIONAL REGISTER OF SHIPPING’’ KIPINDI CHA JULY 2013 – MACHI 2014
S/N Name of Vessel UZITO (GRT)
1 RANYRAN 479
2. CANTE 13,322
3. ARABIAN SUN 2 412
4. SEA BIRD 1 215
5. SEA BIRD 3 248
6. AURIGA 55,962
7. TABUN 26639
8. SAN JOSE 168
9. MED STAR 3,909
10. MEGAH CEMENT 6,774
11 PENTA 387.24
12. SYMPHONY 44190
13. BARAWATI 55042
106
S/N Name of Vessel UZITO (GRT)
14. PERGIWO 23496
15. RODE 20818
16. SEA BREEZE 5306
17. AL KHALEEJ 1 359
18. Vare 17183
19. Danhaibianmao 171 125
20. Danhaibianmao 187 125
21. Danhaibianmao 189 125
22. Shuang Yang 199
23. SSE Angelina 158
24. Hai Jie 198
25. Harmony Liverstock 2062
26. SSE Rhonica 30
27. Pendora 49.6
28. Roula 11506
29. Kathy 203
30. Hamza 5 224
31. Sulaiman 161
107
S/N Name of Vessel UZITO (GRT)
32. Capricorn 2187
33. Quality 712
34. Falcon 1 861
35. Onassis 671
36. Friendship I 683
37. Al Khaleej 4 205
38. Santa Cruz 179
39. Revana 1288
40. Crystal Sun 4722
41. Zheng Ying 168
42. Grann. St. Anne 1048
43. Lampunchai 1381
44. Mandalay 420
45. Hao Xiang 66 1967
46. Malak 1040
47. New Falcon 4066
48. Rahma 1473
49. Ang Quan 11042
108
S/N Name of Vessel UZITO (GRT)
50. Heng Yang 77 375
51. Delta 1 2867
52. Revana I 1332
53. Al Wakra 3423
54. Hong Yuan 643
55. Gulf Trader 1197
56. Chang Da 124
57. Chun Hing N0. 1 177
58. Sea Sul I 2472
59. SL-D10 958
60. Hamal 422
61. Munsu 675
62. Victoria Star 1485
JUMLA 343,653.84
109
KIAMBATANISHO NAMBA 8:
HUDUMA ZA MELI
S/NO
AINA YA MELI
KIPINDI
ONGEZEKO/
PUNGUZO (%) JULAI, 2012 –
MACHI, 2013
JULAI 2013 –
MACHI, 2014
1. Meli za Nje 133 152 14.29
2. Uzito wa Meli (GRT) 1,929,141 2,227,955 15.49
3. Meli za Ndani 4,050 2,913 (28.07)
4. Mjahazi 4,456 4,617 3.61
110
Kiambatanisho 8: Inaendelea……………….
HUDUMA ZA MIZIGO
S/NO AINA YA MIZIGO
KIPINDI ONGEZEKO/ PUNGUZO
(%) JULAI, 2012 –
MACHI, 2013
JULAI, 2013 –
MACHI, 2014
1. Mzigo Mchanganyiko 53,245 49,363 (7.29)
2. Makontena 38,341 44,276 15.48
3. Mafuta 26,711 40,133 50.25
4. Mzigo wa Majahazi 83,785 116,802 39.41
5. Abiria wa Ndani 1,641,849 1,776,101 8.18
6. Abiria wa Kigeni 2,053 2,654 29.27